Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MIMI NI MUAFRIKA (I'M AFRICAN) - 5

  







    Simulizi : Mimi Ni Muafrika (I'm African)

    Sehemu Ya Tano (5)





    Wanawake wa Kiafrika, wazee,watoto,pamoja na askari kumi waliokuwa pamoja nao kudumisha ulinzi,wakiwa juu ya mti wa ubuyu, mti uliokuwa umbali wa takribani mita kumi na eneo la vita, walisikia sauti za risasi, kelele za vilio na machungu zikipenya katika masikio yao, machozi ya huzuni yakawatoka, wakaa kimya, bila kutikisika juu ya mti, huku kila mmoja akiomba kwa mizimu, ndugu zao washinde na kurejea salama …



    “,Twendeni tukawasaidie, twendeni ……”,askari mmoja, kati ya askari kumi waliokuwa juu ya mti, wakiwalinda wanawake, wazee na watoto, aliongea, alikuwa na shauku ya kutaka kutoa msaada kwa wenzake.



    “,Hapana, hatujui wako mahali gani, tunaweza kushuka chini na kushambuliwa, isitoshe, kundi hili kubwa la Waafrika takribani wote, tuna waacha na nani? “,askari wa pili ,askari wa Kiafrika alimjibu mwenzake, akauliza tena swali.



    “,Kweli kabisa, tuombe Mungu tu …”,askari wa tatu, akakubaliana na mwenzake, akaunga mkono, hawakua na haja ya kushuka chini ya mti wao wa maficho, wakatupilia mbali mawazo hayo, ghafla ukimya ukatawala tena msituni kwa mara nyingine tena …

    …………………………………

    Ngome kubwa :3;20pmhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Magari kumi tu ndiyo yalirejea, magari ya askari wa kikoloni waliobakia, maiti zote ziliachwa msituni, zilikuwa nyingi sana, wakaziacha, wakiahidi kuzichukua watakaporejea msituni, wakiwa na kundi kubwa zaidi



    Askari mia moja na hamsini tu ndio walirudi salama,wakiwa na mioyo iliyojaa huzuni, simanzi, pamoja na hasira juuu ya Waafrika.



    “,Wamerudi, they are back! but why, ziko chache sana, zimekufa, they are killed ……”,



    “,Hahahaaaa ……”,



    Kundi la kwanza, kundi lililoenda kuwatafuta Waafrika katika majumba yao, makazi duni, wakawakosa na kushindwa kuwakamata, kisha wakawekwa rumande kwa amri ya gavana, waliongea kwa kejeli, wakacheka kwa dharau, walifurahi sana wenzao kurudi mikono mitupu,jeshi likiwa limepungua, askari wenzao wakiwa wameuawa kikatili …



    “,Vizuri sana Africans, very good!very good! penda nyinyi sana ……”,



    “,Hahaaa, haaaa, haaa …”,



    Wakiwa wamesimama kwenye nondo za magereza yao, nondo ambazo ziliwawezesha kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea nje, waliwazomea, wakawakejeli askari wenzao, waliorudi wakiwa na nyuso za huzuni, huku baadhi wakiwa wamebeba mwili wa malikia wao, maneno ya kejeli na matusi yalipenya katika masikio ya gavana,akachukia, hasira zikampanda,askari wote waliokuwa pamoja naye wakachukia,sura zao zikakunjamana kwa hasira…



    “,Firee them, I say fire them, kill them, uwa jinga yote ……,hypocrite people ……”,gavana Richald Robeni uvumilivu ulimshinda, akanyanyua bunduki yake, akaikoki, akavuta taiga, askari wake, askari waliokuwa pamoja naye, wakatii amri yake, wakageuka mahali yalipokuwa magereza ya wazungu, wakakoki bunduki zao, wakavuta taiga na kuanza kumimina risasi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Paaaa, paaa, paaaa! ”

    “,Aaaaa…ah, you have kill…ed us, mmetu…u…a, ”

    “,paaaah, paaaah “,

    “,Aaa…a…ah “,



    Vilio vilisikika, askari wa kikoloni waliokuwa wamefungwa gerezani walikufa kama nzige,wakapiga kelele za maumivu, hakuna aliyesikia vilio vyao, ndani ya dakika tano tu, wote walikuwa wamepoteza maisha, ukimya ukatawala tena katika ngome ya wakoloni …



    …………………………………

    “,Let’s stop here, mimi choka sana, ”

    “,Au ngoja nikubebe “,

    “,No, no, hata wewe you have to rest, unapaswa kupumzika…”,

    “,Mimi nashauri tupumzike, japo tumebaki wapambanaji arobaini tu, wengine wote wamekufa ……”,

    “,Yes,wamekufa,by using this local guns,upinde na mishale, we can’t win the battle,hatuwezi kushinda kabisa, akili ikitulia, machungu ikipungua kwa moyo wangu, fundisha nyie kutumia guns, no way! I have killed my mum, I didn’t expect that, sikutegemea kabisa, I can’t go back,nikirejea kwa baba I will die, we have to win, tunapaswa kushinda,ili kuwakomboa na mimi jikomboa mwenyewe! “,,„Angel alipiga moyo konde, akajivika roho ya paka, akakubaliana na hali halisi, hakuwa na mama tena, baba yake hakumuhitaji tena, walikuwa maadui kwa sasa, hakua na jinsi zaidi ya kuungana na Waafrika kupigania uhuru kufa na kupona, hakua na jinsi kupigania maisha yake, bila hivyo baba yake pamoja na askari wake wa kikoloni watamuua, alipaswa kuwaua kabla hawajamuua …

    The great fort (ngome kubwa)

    Gavana Richald Robeni alikuwa ameketi katika sebure yake, ndani ya kasri lake kubwa la kifahari, uso wake ulikuwa na huzuni,alikuwa amepoteza watu muhimu katika maisha yake, mke wake alipoteza maisha mbele ya macho yake,baada ya kupigwa risasi na Angel, mtoto wao kipenzi ambaye kwa sasa alikuwa ni adui wake mkubwa.



    “,Africans must pay!, lazima walipe kifo cha mke wangu, nitamuua Angel kwa mikono yangu mwenyewe ……”,Richald Robeni aliongea,akiwa amejipumzisha, mara baada ya kumzika mke wake, alichukua simu yake kubwa ya mkonga, akapiga simu.



    “,Hallow! “,upande wa pili wa simu ulijibu.



    “,Aim Richald Roben, gavana ya Goshani, i need your help, nyie kama jirani yangu, mimi huku pigana na Africans, zimeua askari yangu nyingi sana pamoja na mke yangu,nahitaji msaada yenu, one hundred soldiers inatosha sana …”,gavana aliomba msaada kwa majirani zake,kisiwa cha Gano kilichopatikana bahari ya hindi, kisiwa cha waswahili ambacho kiliongozwa na wakoloni wa kichina.



    “,Oooh,pole sana,wewe rafiki yangu sana, kila siku unaniuzia pembe za ndovu na mkonge, lazima nikusaidie, nusu saa ijayo jeshi langu litafika katika koloni lako……”,gavana wa kisiwa cha Gano aliyejulikana kwa jina la Hwang Lee aliongea,kisha akakata simu.



    Angalau gavana Richald Robeni aliweza kupata faraja, akatabasamu kwa mara nyingine tena, tabasamu ambalo lilificha siri nyingi za uchungu na majonzi.Nusu saa ijayo alitegemea kupokea askari wa kichina mia moja, watakao muongezea nguvu kwenye vita dhidi ya waafrika ambao walitaka uhuru wao,jambo ambalo lilikuwa ni gumu kama samaki kuishi nchi kavu.



    …………………………………

    Angel Richald, mtoto wa gavana, aliamua kusahau kila kitu kilichokuwa kimetokea, alikuwa amejitoa kwa moyo mmoja kumsaidia mpenzi wake Mpuzu pamoja na jeshi lake, waweze kupata ushindi dhidi ya Waafrika.



    “,Kila mtu ajaribu kulenga shabaha,mti ambao nimeuwekea jani la njano,hakikisha mkononi umeshika bunduki, kama ambayo ninayo mimi ……”,Angel aliongea, akanyoosha juu bunduki yake ya smg kila mmoja akaiona,kisha akaikamata vizuri,aweze kuendelea na somo lake.



    “,Hii inaitwa magazini,hii ni taiga,hii ni darubini yako,pakia magazini, shika kwa nguvu bunduki yako,hakikisha umeibana kwa nguvu kwenye kwapa lako,kisha tazama darubini,mlenge adui yako,then vuta taiga,shoot him,mpige adui!”,Angel Richald aliendelea kutoa mafunzo yake kwa vitendo,baada ya kutoa maelezo marefu, alikaa vizuri, akafanya kama alivyowaelekeza, wote wakiwa wanamtazama, akavuta taiga na kuruhusu risasi.



    “,Paaaaa, paaaa, paaaaa! “,alifyatua risasi tatu, akausambaratisha katikati mti mkubwa wa ubuyu uliokuwa umbali wa mita mia mbili, kutoka eneo la kulengea shabaha.

    “,Is it clear?, mmenielewa vizuri? “,Angel aliuliza.



    “,Ndiyo tumekuelewa! “,jeshi la waafrika liliitikia, jeshi ambalo lilibakiwa na askari arobaini tu,likiwa limechanganyikana na vijana, wazee wenye nguvu, mdogo wake Mpuzu aliyeitwa Mwamvua pamoja na Angel mwenyewe.



    “,Kama mmenielewa ,ngoja tujaribu kufanya shambulio, fateni amri yangu …”,Catherine aliongea, akasimama vizuri, akajiandaa kutoa amri,akiwa mtaalamu pekee wa silaha za kizungu katika jeshi la Waafrika,alitambua kuwa silaha za jadi zisingewafikisha mbali katika vita.



    “,Pakia magazini, ikoki bunduki yako,lenga shabaha ya adui wako kwa kutumia darubini,fireeee them, fyatua risasi ……”,Angel alitoa amri, kisha akaruhusu shambulio.



    “,Paaaa, paaaa, paaaa, paaa………”,risasi zilisikika,jeshi la Waafrika lilifanya kama lilivyoelekezwa,walishambulia miti waliyoelekezwa, mahali kulipowekwa alama, miti yote ikapasuliwa, Angel akayaziba masikio yake, mlio ulisikika ulikuwa mkubwa, ukasindikizwa na sauti za mwangwi msituni.



    “,Yeeeeeee, ngwaluna, gwaluna, “(tumeweza, tumeweza) “,walishangilia kwa furaha, wakitumia lugha yao ya asili, wakaluka kwa furaha kama masai wa kule Monduli mkoani Arusha, nchini Tanzania.



    “,Haya sasa, that is over! suala hilo kwisha kabisaa, this is another thing, hiki ni kitu kingine tunapaswa kujifunza,ni rahisi kutumia, sio kama bunduki ……”,Angel aliongea, akachukua mabomu mawili aliyoyakuta katika moja ya maiti za askari wa kizungu, akawaonyesha juu.



    “,What is this? “,Angel aliuliza kwa lugha ya kizungu, kwa muda sasa walikuwa wamekaa naye, alikuwa amefahamu maneno mengi ya kiswahili, wao pia walikuwa wamejifunza maneno mengi ya kizungu.

    “,bomu! “,

    “,Mlipuko, “,

    “,Risasi! “,

    “,kibuyu! “,

    “,Hicho ni kibuyuu! “,



    Kila mtu alitamka neno lake, watu wa mwanzoni walipatia, wengine wakakosea kidogo, lakini watu wawili wa mwisho walikosea na kutaja vitu vya ajabu, Angel akajikuta anacheka, kwa sasa alikuwa na furaha, alijiona mmoja kati ya waafrika, alianza kusahau kuhusu kifo cha mama yake aliyemuuwa kwa mikono yake mwenyewe.



    “,Hili ni bomu dogo, linauwezo wa kuuwa watu takribani ishirini kwa wakati mmoja, hii hapa ni pini, ukiichomoa kwa kuivuta kisha ukawarushia maadui zako, utakua umemaliza kila kitu, litalipuka na kuwaua, ndio silaha pekee inayoua vibaya! “,Angel aliongea kwa kiswahili safi kilicho nyooka, alianza kuongea kiswahili kizuri cha wazawa,kama vile alikuwa amezaliwa Afrika mashariki.



    “,Oneni kwa makini navyofanya!, “Angel aliongea tena, jeshi lake likawa makini kumsikiliza, kwa sasa walimuamini, wakaheshimu mawazo yake, Angel alichomoa pini, kisha akalitupa bomu mita mia moja katikati ya msitu.



    “,Puuuu, puuuuu! “,mlipuko ulisikika, miti ilipasuliwa mingine ikadondoka chini, vumbi zito likatimka,waafrika wote wakabaki midomo wazi, walikuwa hawatambui nguvu za silaha za wazungu.



    “,Chakula, chakula, muda wa chakula,iyeeeee! iyeeee!, muda wa chakula ……”,la mgambo lililia, mmoja kati ya vijana wenye nguvu alipiga kelele, akiwa ameongozana na wenzake sita, walilejea kutoka msituni kufuata chakula,walikuwa na mikungu mitano ya ndizi pamoja na maembe. Jeshi la waafrika wakaahirisha shughuli zao, mafunzo yao yalikuwa yamekamilika, wakaenda kuwapokea ndizi, ndizi zingine zikapelekwa juu ya mti mkubwa wa ubuyu, maficho ya waafrika wote, ndani ya mti huu kulikuwa na matawi pamoja na mapango ambayo yalitumika kama maficho wakati wote wa vita.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,we have to be careful, tuwe makini kabisa, muda wowote watarudi, kama sio leo basi kesho asubuhi, “Angel aliongea, akatazama juu angani, yalikuwa ni majira ya jioni, jua lilikuwa limeanza kuzama.



    “,Usjali mke wangu, muda wowote tuko tayali kupambana ,ulinzi uko salama kabisa…”,Mpuzu aliongea, akamuondoa shaka mpenzi wake wa kizungu aliyemfanya ajiamini na kuanzisha vita hii ya kupigania uhuru, kwa sasa alikuwa amekamatilia bunduki yake iliyojaa risasi.



    “,Wifi usjali, nipo kwa ajili yako …”,Mwamvua, mdogo wake Mpuzu aliongea, akaikoki bunduki yake, akamuhakikishia usalama.



    “,Hahaaa, lakini tuwe makini sana, wale ni askari wazoefu na wamepitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi, kwahiyo wanatuzidi askari, silaha pamoja na udhoefu, cha muhimu ukiua, hakikisha silaha yake unaichukua ……”,Angel aliongea.



    “,Usjali shemeji, mimi nipo kwa ajili ya ulinzi na kutoboa matumbo yao kwa mishale, kwa yoyote yule atakayeisogelea kambi yetu …”,Ishimwe rafiki yake Mpuzu aliongea, akiwa ameshika silaha zote mbili, bunduki pamoja na upinde wake, aliupenda sana, hakuwa tayali kuuacha.



    “„Sawa nimewaelewa, “Angel aliongea,wakakumbatiana, kwa sasa walipendana sana.



    …………………………………

    Gavana Richald Robeni alishtuka, akanyenyuka sebureni kwake, akatoka nje, alikuwa amesikia sauti ya risasi, nje ya ngome yao, baada ya dakika tano, mlipuko wa bomu ukasikika, nje ya ngome yao, moshi mzito ukaanza kuelekea angani, aliuona vizuri sana…



    “,What is that? (ile ni nini) “,aliuliza kwa kizungu.



    “,ni mlipuko, pamoja na risasi kutoka katika msitu wa mikoko …”,mmoja kati ya askari wa kikoloni aliongea, gavana akatafakari, kisha akatikisa kichwa, alikumbuka jambo fulani, akatambua chanzo cha mlipuko huo.



    “,Ndiyo maana askari wetu waliouawa hatujawakuta na bunduki yetu, bunduki yote imechukuliwa na African, but they won’t win this battle, hawatatushindaa! “,gavana alifoka kwa hasira, kisha akarudi zake ndani, akijiandaa kwa vita siku inayofuata.



    Ngome kubwa :6:20pm

    Gavana Richald Robeni aliingia tena ndani kasri lake,alipotaka kuketi kwenye viti vyake,ghafla akasikia muungurumo wa helikopta, muungurumo ulikuwa mkubwa sana, bila shaka zilikuwa helikopta zaidi ya moja, akatoka nje haraka sana, akatazama juu ya anga la ngome yake, akatabasamu, helikopta tano zenye rangi nyeupe iliyopambwa na bendera za kichina,ziliwasili katika ngome yake, alifurahi sana, bila kutambua kuwa alikuwa amejichimbia kaburi yeye mwenyewe.



    “,Welcome, karibuni sana kwenye makazi yetu …”,gavana alitoka nje ya kasri lake, akasogea mpaka kwenye kiwanja chao cha ndege, akawapokea askari wapya, akasalimiana na kiongozi wa jeshi hili wakapigiana saluti za heshima.



    “,Asante, samahani sana kwa kuchelewa …”,kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akaomba samahani,mkononi alikuwa ameshika fimbo yake ya kijeshi, akiipiga piga mkononi.



    “,Ondoeni shaka kabisa,hamjachelewa, kesho asubuhi na mapema tutaelekea vitani, “gavana aliongea.



    “,Ok, can you give me the map of that forest? “,(sawa, unaweza kunipatia ramani ya huo msitu? “,kiongozi wa jeshi la kichina aliuliza, alitaka kuijua ramani, awapangie majukumu vijana wake. Gavana alijishika shika na mikono yake, akapekua mifuko ya nyuma ya suruali yake, hakuona ramani, akapekua mifuko ya shati lake, akaipata ramani katika mfuko upande wa kushoto, akampatia jenerali yule, wakashikana tena mikono, kila mmoja akachukua hamsini zake, gavana alirudi katika kasri lake, kiongozi wa jeshi la kichina akaongozana na vijana wake, mpaka kwenye vyumba vyao vya wageni.

    …………………………………

    Gano :Nusu saa iliyopita

    Hwang lee alitabasamu,muda ambao aliusubili kwa hamu ulikuwa umewadia, alitamani sana kumiliki koloni la nchi ya Goshani, nchi ambayo ilijaa utajiri wa kila aina, madini, pembe za ndovu, ardhi yenye rutuba pamoja na nguvu kazi ya kutosha.



    “,Lazima niwe mtawala wa Goshani,this is the only chance I was waiting for, lazima nitawale Goshani, lazima! “,Hwang lee aliongea yeye mwenyewe, ndani ya ofisi yake, akanyanyua simu ya mkonga, akapiga, baada ya dakika mbili, akakata simu, alikuwa amemaliza kufanya mazungumzo na mtu aliyekuwa anamuhitaji.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Ngo ngo, ngo ngo! “,mlango wa ofisi ya gavana wa kichina uligongwa, gavana katili aliyependa kutawala kila kona za dunia, huku akitumia jeshi lake kueneza utawala wake.



    “,Get in!, ingia ndani ,mlango uko wazi …”,Hwang lee aliongea,mlango ukafunguliwa,kisha ukafungwa tena, mtu aliyekuwa amempigia simu alikuwa amesimama kwa heshima mbele yake, fimbo yake akiwa ameiweka na kuibana kwenye kwapa lake, akapiga saluti ya kijeshi.



    “,Goshani wanapigana vita, waafrika they need to be free, wanataka uhuru wao, tumepigiwa simu na gavana Richald tukatoe msaada, muda mrefu tulitamani kumilika koloni hili, sasa muda umefika, chukua askari mia moja, nenda huko, fanya mbinu yoyote ile, gavana Richald auwawe, halafu uwa na hao waafrika walioanzisha vita! “,gavana Hwang lee alitoa maelekezo.



    “,Sawa mkuu, nimekuelewa, kila kitu kitakwenda sawa,usiwe na shaka! “,jenerali na kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akapiga saluti, kisha akaondoka zake, tarumbeta kubwa ya kijeshi ikapigwa, katika ngome ya gavana, askari wote wakakusanyika..



    “,Tunaenda kwenye vita ya dharula,Goshani inapigana vita, koloni la Waingereza na waafrika, tunaenda kutoa msaada, na kuliweka koloni hili katika himaya yetu!,nahitaji askari mia moja tu wa kuondoka nao”,kiongozi wa jeshi la kikoloni alitoa maelekezo kwa jeshi lake, vijana wake wakaluka juu kwa shangwe, walipenda sana kupigana vitaa.



    “,Iyeeeeee, “zilikuwa ni shangwe za kufurahia vita, askari mia moja wakaingia katika helikopta zao za kivita, bunduki zao zikiwa mikononi, baada ya dakika tano helikopta ikapaa angani,ikaiacha ardhi ya kisiwa cha Gano, ikaelekea bara,nchini Goshani, nchi zote zikipatikana Afrika ya mashariki.



    …………………………………

    Msitu wa mikoko :8:00

    Jeshi la Waafrika lenye askari arobaini tu kwa sasa, hawakulala, waliendelea kujiandaa na mapambano,walitega mitego kama kawaida yao, walichimba shimo lingine katikati ya barabara nyembamba iliyoingia msituni, ndani ya shimo wakaweka miti iliyochongoka kama mikuki, kisha juu ya shimo wakaweka fito dhaifu zenye uwezo wa kukatika, wakatandaza nyasi, wakaweka udongo juu yake,wakasambaza, haikuwa rahisi kuutambua mtego huu,barabara ilisawazishwa vizuri kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kutofautisha mahali penye mtego na pasipokuwa na mtego.



    “,Vuta juu hilo gogo,lazima liwauee tena kama nzige …”,mzee Nyamigo aliongea,Mpuzu akiwa juu ya mti akalivuta vizuri gogo, juu ya mti, usawa wa barabara, gogo ambalo liliunganishwa na kamba mpaka barabarani, kisha kamba ikafukiwa, yoyote yule ambaye angepita barabarani kizembe na kujikwaa kwenye kamba, kamba ingefyatua mtego, gogo likamuangukia na kumuua palepale.



    ” ,Yes, well done, tumemaliza, kwa sasa tusikae kwenye miti, wameshajua mahali tulipojificha mwanzoni, watu ishirini wakae katika vichaka upande wa kushoto, wengine ishirini wakae vichakani upande wa kulia “,Angel Richald aliongea, hakuna aliyemuelewa, wote wakabaki wanamtazama, walikuwa hawajui kusoma, kuhesabu wala kuandika.



    Mwamvua akaifanya kazi hiyo, alikuwa mtundu sana, siku zote alipenda kujifunza, alifahamu kila kitu mpaka lugha ya kizungu, bila hata kwenda shuleni, alijifunza kupitia wakoloni alioishi nao, alikalili kila kitu walichokifanya ambacho aliona kitamsaidia ,baada ya kumaliza kuwahesabu askari wa kiafrika, na yeye akakaa katika kundi moja lenye watu kumi na tisa,kisha wakaingia vichakani, pembeni ya barabara, wakajificha,kusubili vita…

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    …………………………………

    Ngome kubwa :9:30pm

    Kikao cha siri kiliendelea ndani ya vyumba vya wageni,askari wa kichina walipanga mipango yao ya siri kumuua gavana Richald Robeni, kisha waweze kuwa watawala wa Goshani.



    “,Sisi tuna askari mia moja tu, wao wako wengi, japo hawazidi mia mbili, mimi nitaenda na gavana, katika gari moja, nitamteka na kumfunga kamba,mlinzi wake nitamuua, hana uwezo wa kupambana na mimi, kisha jeshi la Waingereza, tutawaambia watii amri zetu, kwenye vita na Waafrika,ili kuyaokoa maisha ya kiongozi wao, mtaenda vitani mkirudi mahali mlipotuacha, nikiwa nimemuweka mateka gavana, mtakuta nimemuua,akiwa ndani ya gari, bila wao kujua kama amekufa,nitawaambia waweke silaha chini kumpata gavana wao,wataweka silaha chini, kisha tutawashambulia kwa risasi, mchezo utaishia hapo! “,jenerali wa kichina alitoa maelekezo na mpango wake wa kufanya shambulio, wote wakamuunga mkono. Baada ya kikao, kila mmoja akajipumzisha kitandani, akiisubili kwa hamu asubuhi, siku inayofuata.



    Msitu wa mikoko:7:00am

    Msafara wa magari hamsini ya kikoloni uliwasili msitu wa mikoko, gari la kwanza likiwa na jenerali wa jeshi la kichina aliyeitwa Liang Xung,alikuwa ameketi viti vya nyuma, ndani ya gari,mbele yake alikuwa ameketi gavana Richald Robeni, pamoja na mlinzi wake ambaye alikuwa akiendesha gari.



    “,Tumefika, msitu ndiyo huu! “,mlinzi wa gavana Richald Robeni aliongea, akasimamisha gari lake,akageuza shingo nyuma,palepale akapigwa na risasi, akafa palepale.



    “,Mikono juu! “,gavana wa kichina aliongea, alikuwa amemnyoshea bastola kichwani gavana wa kiingereza, Richald Robeni na yeye alipitia mafunzo ya kijeshi, akataka kuchukua bastola yake lakini alionekana.



    “,Nitakumaliza kama nilivyomfanya mwenzako, usisubutu kuweka mikono yako mfukoni! “,jenerali wa kichina aliongea, akamtoa nje, akiwa amempiga roba na kumuwekea bastola kichwani.



    “,Wamemkamata gavana yetu, wanataka kufanya mapinduzi na kuchukua koloni letu,tupambane, lets fight ……”,jeshi la waingereza walisikia mlio wa risasi ndani ya gari lililokuwa na gavana wao, wakashuka kwenye magari yao, kabla hawajalisogelea gari, gavana wao akatoka nje akiwa chini ya ulinzi, wakakasilika, makundi yote mawili yakanyosheana silaha,jeshi la kichina pamoja na jeshi la wenyeji ambao ni wazungu wa kiingereza.



    “,Mkifanya lolote nammaliza kiongozi wenu! “,kiongozi wa kichina alizungumza, akaamua kubadili mbinu, jeshi la waingereza walikuwa ni wengi, akaamua kuchukua utawala mapema sana kabla ya kwenda kupigana na Waafrika.



    “,Put downs your guns! (Wekeni silaha zenu chini …)”,jenerali Liang Xung aliongea, jeshi la waingereza wakagoma kuweka silaha chini, kwa sasa makundi yote yalikuwa yametengana, jeshi la waingereza walikuwa wamesimama upande wa kusini, wakati jeshi la wachina wakiwa wamesimama upande wa kaskazini.



    “,Put down your guns , mnataka niuwawe! “,gavana Richald Robeni akafanya kosa lingine tena, likaugharimu utawala wake, alitoa amli, vijana wake wakaitii kwa shingo upande, wakaweka silaha zao chini, askari takribani kumi wa kichina wakakusanya silaha zote za waingereza, wakaziweka upande wao.

    “,Fireeee them, waueee! “,jenerali wa kichina alitoa amli kwa jeshi lake, alikuwa katili kama gavana wake.



    “,What! “,Richald Robeni alishangaa sana, alizani atasamehewa, kumbe sivyo!.



    “,Paaaa,papapa,paaaa,paaaa! !”,jeshi la waingereza walishambuliwa na risasi,wakafa kama nzige, hawakuwa na uwezo wa kujitetea, walijuta kusalamisha silaha zao.



    “,Paaaaaa! “,gavana Richald Robeni na yeye akasambaratishwa ubongo wake, akafa palepale.



    “,Yeeeeee! Goshani is our kingdom!(Goshani ni ufalme wetu) “,askari wa kichina walishangilia,koloni la nchi ya Goshani lilikuwa mikononi mwao,vita iliyokuwa imebakia ilikuwa dhidi ya jeshi la Waafrika, vita ambayo waliiona ni rahisi kuliko vita yoyote ile ambayo walikuwa wamepigana,jenerali wao alikuwa amesimama mbele, msururu mrefu wa askari ukamfuata kwa nyuma, macho yao yalitazama mita mia moja mbele, kulia, kushoto na juu ya miti, walikuwa makini sana tofauti na jeshi la waingereza.



    Msitu ulikuwa mnene, ulijaa vichaka kila kona, ulitisha, jenerali Liang Xung machale yakamcheza,akaogopa kutangulia mbele,akatanguliza vijana wake kumi, yeye akakaa katikati, msafara ukaendelea.



    …………………………………

    Jeshi la Waafrika walishtuka usingizini, milio ya risasi iliwashtua sana, kila mmoja akachukua bunduki yake, akaikoki, akajiandaa kufanya shambulio.



    Umbali wa mita kadhaa walianza kusikia kelele za watu, Angel akasogeza sikio lake juu ya ardhi, ardhi ilikuwa inatetemeka,wote wakatazama juu, makundi ya ndege yalikuwa yanahama kutoka mwanzo wa msitu, kuja katikati ya msitu.



    “,Wanakujaa, jiandaenii, nikitoa amri, shambulia adui! “,Angel aliongea, baada ya dakika tano,jeshi la kichina lilikuwa mbele yao, sare zao zilikuwa na rangi nyeupe pamoja na madoa mekundu, walifanana kwa kila kitu,jeshi la Waafrika wakapigwa na butwaa, askari waliokuwa mbele yao hawakutambua walitokea wapi.



    “,Yaaaaala…aa, nakufa…aa …”,



    “,Paaa,paaa,paaa!”,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askari wa kichina waliokuwa wametangulia mbele walidumbukia ndani ya shimo la mtego,wakachomwa chomwa na miti iliyochongoka ndani ya shimo,wakafa palepale,walikuwa askari kumi,jeshi la kichina wakapiga risasi hovyo,waafrika wakalala chini,alimanusura ziwapate vichakani.



    “,Ni mtego! wamekufa kikatili, shiit! “,jenerali alishangaa sana, kama si machale kumcheza na kurudi nyuma, angekuwa miongoni mwa askari waliopoteza maisha.



    “,Let’s go on, tuendelee na safari but you have to be careful, muwe makini sana! “,jenerali Liang Xung aliongea,msafara ukaendelea, yeye akiwa amesimama katikati, walipiga hatu mbili tu,shambulio lingine likafanyika.



    “,Puuuuuu! “,askari mmoja aliyekuwa ametangulia mbele alijikwaa kwenye kamba ya mtego akajitupa mweleka, gogo likatoka juu na kumpiga tumboni, damu zikamtoka mapuani, mdomoni na masikioni, alikufa palepale. Jeshi la kichina likaogopa, likarudi nyuma, wote wakaogopa kusonga mbele.



    “,Songa mbelee, tumewauaa askari wa kingereza pamoja na gavana wao, hawa weusi ndiyo watushindee?, let’s move on, songa mbelee! “,jenerali wa kichina aliwafokea vijana wake, kila mmoja aliogopa kutangulia mbele, Angel alikasirika sana, baada ya kusikia baba yake ameuawa, japo hakuelewana na baba yake, lakini alikuwa bado anampendaa.



    “,Fireeee them,fireee, piga risasi, shambuliaaa! “,alitoa amli kwa hasira, akarusha bomu lake dogo ambalo lilikuwa mkononi mwake



    “,Puuuuuu ,puuu”,lililipuka na kuuwa askari wa kichina kumi na tano, miili yao ikiwa imekatika vibaya sana, kila kiungo mahala pake.



    “,Paaaaa, paaaa, paaaa, paaa! “,Waafrika walifanya shambulio la ghafla,wakaua askari hamsini wa kichina, wakabaki askari thelathini na tano, wakafyatua tena risasi zikagoma, risasi zilikuwa zimeisha kwenye magazini za bunduki zao, hapo ndipo mwisho wao ulikuwa umefika, walikuwa hawana silaha nyingine yoyote, isipokuwa Ishimwe aliyekuwa na upinde wake pembeni, akauchukua na kuanza kufyatua.



    “,Pyuuuuu! “,Ishimwe alifyatua mshale, alimanusura umpige shingoni jenerali wa kichina, akatazama mahali mshale ulipotokea, akapiga risasi hovyo, askari wote waliobakia wakasambaratisha vichaka na risasi,vikawaka moto.



    “,Puuu, puuuuu! “,mlipuko ulisikika, askari wa kichina walilusha mabomu mawili vichakani, Angel akapigwa na bomu, akafa palepale, Mwamvua akafa palepale, Ishimwe na Mpuzu wakajisalamisha, wakanyosha mikono juu, walikuwa wamebaki wawili tu, machozi yaliwatoka,ndugu zao walikuwa wamekufa kikatili,walipigwa na bomu, kila kiungo kilikuwa mahali pake.



    “,bhanetuuu bhafwaaa, bhanetuuu bhafwaaa, bhagabho bhachuu bhafwaaa! “,(watoto zetu wamekufaa, waume zetu wamekufaaa! “,Waafrika, wanawake, wazee na watoto waliokuwa juu ya miti walilia, jeshi la kichina likasikia kelele zao juu ya mti mkubwa wa ubuyu, askari wakapanda juu ya mti, wakawatoa Waafrika wote, wote wakawekwa chini ya ulinzi,safari ya kutoka msituni ikaanza,Waafrika wakiwa na majonzi,kwa sasa walikuwa chini ya uongozi wa Wachina.



    …………………………………

    Gavana Hwang lee alifika nchini Goshani ,alifurahishwa na taarifa za ushindi,jeshi lake lilimchukia,aliwatesa na kuwaua askari wake mara kwa mara,kwa kosa dogo tu,walimpania muda mrefu kumuua.



    “,Paaaaaa,paaa!”,risasi mbili zilifyatuliwa, moja ilimpiga gavana,nyingine akapigwa kichwani mlinzi wake ,wote wakiwa wanashuka kwenye helikopta kuikanyaga ngome kubwa(great fort), ardhi ya nchi ya Goshanihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,Yeeeeee!aim your governer,now and onwards!”,(mimi ni gavana wenu,sasa na kuendelea)”, jenerali Liang Xung alipiga kelele za shangwe,alikuwa amekamilisha mauaji,askari wake wakamkimbilia na kumnyenyua,walimpenda sana,akawa gavana mpya wa Goshani pamoja na Gano,yaani ni kisasi juu ya kisasi.



    …MWISHO…

    Mpuzu na Ishimwe walipatiwa vyeo jeshini,baadaye wakapigania uhuru,wakashinda,Mpuzu akawa raisi,Ishimwe akawa waziri mkuu,wote walikuwa wazee,Gavana Liang Xung alizaa na mwanamke wa Kiafrika,wakapata Mtoto anaitwa Yuan Liang,Wachina walipofukuzwa Goshani,akarudi china na kuacha mtoto pamoja na mke wake,Yuan liang akawa yatima,soma Yuan Liang ujue mengi zaidii!


0 comments:

Post a Comment

Blog