Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

THE WORST VALENTINE’S DAY - 5

 







    Simulizi : The Worst Valentine's Day

    Sehemu Ya Tano (5)







    “Samah mimi ndo sababu ya wewe kuwa hai mpaka sasa hivi, haitakusaidia kama utanyamaza kimya na kuendelea kuona watu wakiteseka, niambie nawezaje kujiepusha na hao watu” nilimbembeleza ili aniambie na wakati huo Jamshid na Clara walikuwa kimya.

    “Faith, kundi ulilojiunga halikuwa Freemason” aliongea Samah na kutufanya wote tuliokuwa pale tuangaliane, mimi nilijiunga na kundi la freemason lakini si na kundi jingine lolote kama alivyosema Samah.

    “sijakuelewa unachokisema Samah” nilimuuliza kwa sauti ya upole ili aweze kunielezea kwa undani alichokuwa akimaanisha.

    “Ulijiunga na kundi la SIXTYNINE SIX (696) na sio freemason” alinishtua na hapo ndipo nilipochoka hasa ukizingatia sikuwa nimewahi kulisikia kabla.

    “bado sijawahi kulisikia hilo kundi” niliuliza tena kwa shauku ya kutaka kujua.

    “hili ni kundi la watu wasomi wenye wanaopinga uwepo wa kimungu katika dunia na chanzo cha uwepo wa wanadamu,,ni kundi lililojitoa katika utawala wa kundi la illuminati lililokuwa kundi la siri la lenye watu sawa na kundi la freemason,,kundi hili la 696 ni kundi la siri na hufanya kazi yake kwa kupitia wasomi ambao wengi wanaonekana kuwa hawana imani za kidini” aliongea kwa sauti ya chini.

    “embu kwanza naomba unieleweshe maana naona unanichanganya,,hao illuminati ni nini” niliuliza na sasa ilinibidi nibadilishe mkao na kukaa karibu kabisa huku macho na masikio yangu nikivielekeza kwa Samah.

    “Illuminati ni jina lililopewa makundi ya kweli na kusadikika, ni kundi lililoanzishwa tarehe 1 May mwaka 1776 likiwa na lengo la kupinga imani potofu au kuamini kuwa jambo moja linaweza kupelekea madhara ya kitu kingine bila ya kuwa na ushahidi wa kuonekana,,walipinga uchawi na mambo yasiyo na ushahidi, pia ilipinga juu ya imani ya kidini mbele ya mambo ya umma, kundi halisi la Illuminati lilikuwa linaitwa Bavarian Illuminati lakini kwasasa kuna makundi mengi yanayotumia jina la illuminati ili kuitawala dunia,,wanaingiza mawakala wao katika serikali na mashirika makubwa ili kufanya kazi pamoja na serikali na baadae waje waitawale dunia,,mawakala hawa wako kwenye dini na mahali mbali mbali kama ambavyo imeandikwa kwenye kitabu cha ufunuo japo haikuandikwa kwa undani sana”…….. sikuwa na la kuuliza tena zaidi ya kuendelea kusikiliza, nilihisi kuwa mimi nilikuwa kati ya watu wapuuzi wa hii dunia kwa kujiunga kwenye kundi ambalo sikulifahamu vizuri,,nakumbuka mzee Rorbahcho alipokuja kunitembelea kule Finland na baada ya kunieleza kila kitu juu ya Freemason na pia kwakuwa nilipata muda wa kuwasoma na kuwaelewa vizuri sikuwa tena na shaka juu yao niliamua kujiunga na kundi hilo na tayari vikao kadhaa na sala zao nilianza kuhudhuria,,cha ajabu mwanzoni nilihisi kuwa nikishajiunga basi imani yangu ya kikatoliki itakuwa basi lakini haikuwa hivyo,, niliendelea na imani yangu na hakukuwa na shida wala tatizo lolote katika hilo,,mambo yangu mengine yalienda vizuri na kila kitu kilikuwa sawa kabisa, japo nilikuwa nikihofia sana lakini nilipata moyo pale nilipokuwa nikikutana na wajumbe wengine ambao walikuwa ni wasichana wadogo matajiri na wasomi,,mfano kuna siku nikiwa kwenye mkutano uliofanyika Texas nchini marekani nilikutana na Jesica Kephax msichana mrembo mwenye miaka 25 tu lakini aliyekuwa akimiliki kampuni kubwa sana pale Texas,,alikuwa ni tajiri anayemiliki ndege zake mwenyewe na jumba kubwa la kifahari pale Texas na katikati ya jiji la New York, Jesica alitokea kuwa rafiki yangu mkubwa sana na mara nyingi alikuwa akifunga safari kutoka marekani kuja Finland kunitembelea na kuniletea zawadi mbalimbali,,mimi na Jesica tulikuja kugombana pale nilipokuja kugundua Jesica alikuwa ni msagaji na alikuwa akinitaka, lakini pamoja na kugombana huko Jesica bado alikuwa ni binti wa mfano kwangu.

    “Faith unawaza nini” nilishtuka toka kwenye kisiwa cha mawazo na kurudi tena duniani na sasa niliendelea kumsikiliza Samah.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ kwaiyo hili kundi la 696 lilitokeaje” Jamshid alimuuliza Samah.

    “baada ya baadhi ya wanachama wa kundi la Illuminati kuona kuwa hawakuwa wanakubaliana na baadhi ya mambo ya kundi hilo basi walijitenga na kuanzisha kundi la 696 ambalo ni kundi linalojihusisha na nguvu za giza, sayansi ya vitu vigumu na mambo ya kufikirika, ni kundi ambalo unapojiunga tayari unaingia kwenye imani ya sadaka ya damu kama ishara ya ukomavu na umoja wa kundi hili,,utahusika kwenye ajali na mambo mengine ya kufikirika pasipo wewe kujijua au kwa kujua,,ni kundi ambalo linauwezo mkubwa na maajabu ya kishetani” aliendelea kuhadithia na mimi nilitoka kwenda kuchukua maji ya kunywa, niliporudi simulizi iliendelea;

    “kwahiyo kuna uhusiano gani kati ya freemason na 696” aliuliza Clara.

    “696 ni jamii ya siri,,freemason ni jamii ya wazi,, hivyo 696 huchukua wanachama kwa mgongo wa freemason na pale unapotoa sadaka yako basi unakuja kuhalalishwa kama mwanachama hai wa 696 na kila kitu unapewa lakini utahitajika kuleta watu wengi zaidi,,” aliendelea kuhadithia.

    “unamfahamu Jesica Kephax?” nilimuuliza kwa upole

    “Jesica Kephax ni mjukuu wa Mzee Daniel Kephax ambaye ni moja ya waanzilishi wa 696, na baba yake na Jesica pia alikuwa ni mwanachama wa kundi hili kabla hajafariki,,Jesica anacheo kikubwa sana na ni moja kati ya wasichana matajiri sana wa kundi hili,,ana shahata 23 za 696”…hapo ndipo aliponimaliza nguvu na kutaka kujua zaidi kuhusu yeye kuliko kuhusu mimi.

    “na wewe unashahada ngapi” nilimuuliza tena.

    “ninashahada kumi na 19 na kama nikifanikisha wewe kutoa sadaka nitapata shahada ya 20 na sitafanya tena kazi za kuzunguka” aliongea kwa kujiamini kama vile alikuwa bado anauhakika kuwa atafanikiwa,,nilimtazama machoni nikatamani nimuue palepale ilikazi yake iwe imekwisha.

    “kazi yako imekwisha Samah, utakufa na hizohizo shahada za kishenzi ulizopata” aliongea Jamshid na kumnyanyua kwa hasira,,nilimsihi tena Jamshid amuache;

    “huruma yako itakuponza Faith” aliongea Jamshid na kumuachia Samah.

    “Faith lazima mtakamatwa tu ni bora msingeondoka na mimi” Samah aliongea wakati Jamshid alipomuachia.

    “kwanini unasema hivyo” Jamshid alimuuliza kwa Jazba.

    “kwakuwa kila mmoja aliyefikisha cheo kama changu amewekewa kifaa cha kujua alipo” alituambia vile ili tumuachie aondoke lakini kwa Jamshid mambo hayakuwa hivyo. Alimsogelea mpaka pale alipokuwa na kumkaba;

    “hicho kifaa kipo wapi kilichowekwa kwako?” alimuuliza kwa hasira.

    “kipo sehemu ya juu kabisa ya paja langu kiliwekwa ndani kabisa ya paja huwezi kukiona,,nirudisheni mpaka Dar au hata mkanipandishe gari niondoke kuliko kukaa na mimi hapa nitawaweka mashakani zaidi” aliongea Samah huku akilia.

    “Hautaondoka hapa” Jamshid alimwambia hayo na hapo aliingia chumbani na kuchukua funguo ya gari kisha aliondoka bila kusema anaenda wapi nilimfuata hadi mlangoni na nilipomtazama macho na mwili wake ulikuwa ni mwekundu,,Jamshid alikuwa ni mpole sana lakini kila alipoona kuna jambo lililokuwa likikaribia kunifanya nisiwe na furaha basi alikuwa mkali kulimaliza.

    “unaenda wapi Jamshid” nilimuuliza huku nimemshika shati lake.

    “naenda kumkatia tiketi” alinijibu na kunikamata kisha alinisogeza karibu na kunibusu, aliponiachia alikwenda kuwasha gari na kuondoka. Nilirudi ndani na kumkuta Clara bado aliendelea kuongea na Samah.

    “yani mambo yanazidi kuwa magumu Faith,,itakuwaje kama hawa watu wake watakuwa wameshagundua huyu alipo na wakaamua kuja kumfuata huku,,si tutamalizika mpenzi” aliongea Clara ambaye alionekana kuchanganyikiwa.

    “tutakuwa sawa Clara na utasafiri salama kabisa na Gerald” niliongea huku nikitabasamu.

    “hahaa, wewe ni msichana shupavu sana Faith,,ingekuwa mimi ndio wewe ungekuta nimejitoa uhai mda mrefu sana” aliongea Clara na kunifuata pale nilipo kisha akanikumbatia.

    “Jam kaenda wapi” aliuliza Clara.

    “aahh,,kasema anaenda kumkatia Samah tiketi anataka kesho amsafirishe” nilimjibu na kujitupa kwenye kochi.

    “we Faith huyu mtu atawezaje kusafiri katika hali aliyokuwa nayo hiyo?” aliuliza Clara kwa sauti ya kunong’ona.

    “Nitaweza,,nina nguvu,,niondoeni tu mahala hapa” alidakia Samah. Nilimtazama Samah na kukumbuka kipindi akiwa na mimi bega kwa bega baada ya kifo cha wazazi wangu, alikuwa ni mpole na mwenye kunisaidia sana, pamoja na udhaifu na mabaya yake lakini Samah alikuwa ni msichana mzuri, ukimtazama alionekana kama mwenye miaka 23 lakini katika ukweli halisi alikuwa na miaka 35, alijipenda na hakuna mwanaume angeweza kumpita bila kumtazama mara mbili,,nilijiamini kuwa nilikuwa mzuri lakini si mimi wala Clara aliyemfikia Samah aliyekuwa na asili ya Uarabuni na mchanganyiko wa kiafrika,,alikuwa mweupe na asiye na doa wala kovu lolote lililoweza kuonekana,,,alikuwa na macho mazuri ya mviringo, kiuno chembamba na hipsi zilizofanya hata akivaa hijabu asomeke,,alifungashia vizuri sehemu za nyuma na alikuwa na tumbo dogo ambalo wasichana wengi wangetamani kuwa nalo,,nywele zake za singa zilikipamba kichwa chake vizuri na kumfanya aonekane ni mrembo wa warembo,,ukikutana nae huwezi amini kama ni mmoja wa wauaji, alikuwa na mapaja manene kiasi na meupe yasiyo na chembe ya michirizi bali vinyweleo vidogo vilivyotia nakshi uzuri wa maumbile yake,,,”mh! Nisijeulizwa niliyaonaje mapaja ya Samah”,,nilijisemea moyoni,,nilikuwa nikimuogesha Samah mda wote tuliokaa pale Mikumi hivyo nilipata nafasi ya kumuona vizuri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “eeehee nimekumbuka” nilirudi tena kwenye mazingira ya kawaida na sasa nilimsogelea tena Samah mpaka pale alipokuwa.

    “Nieleze kuhusu baba yangu” nilimuuliza huku nikimtumbulia mimacho.

    “baba yako alikuwa ni mtu wa kundi hili na alibadilika baada ya kuambiwa akutoe wewe kafara na badala yake alidanganya kuwa Magret ndiye mtoto wake wa kwanza ili wamchukue Magret na kukuacha wewe,,lakini baada ya hilo kushindikana aliamua kuachana nao na kisha wakaanza kumsonga na ndipo alipoingia maagano na nguvu za kicha wi ili zimlinde yeye na mali zake na familia yake,,kitu ambacho kilishindikana baada ya wale majini kumgeuka na kutaka damu ya mkewe” alihadithia na huku mwili ukinisisimka niliendelea kumuuliza.

    “wewe ulijuana vipi na baba yangu?” lilikuwa swali lililofata.

    “nilijuana na baba yako kipindi alipojitoa na kuingia kwenye makubaliano na watu wengine ambao ulikuwa ni utawala wa majini na……” alisita kuendelea na ndipo nilipogeuka na kumkazia macho.

    “na nini endelea” nilimsemesha kwa sauti ya ukali.

    “mimi nililetwa kama mpelelezi baada ya mzee Rorbahcho kuonekana alikuwa swahiba mkubwa wa baba yako na asingeweza kabisa kutoa taarifa za namna baba yako alivyokuwa akifanya mambo yake, lakini hata mimi nilishindwa kwa…kwaaakuuu…”alisita tena huku machozi yakimtoka, sikujua kwanini alilia lakini niliendelea kumlazimisha aongee.

    “nieleze ukweli wa kila kitu using’ateng’ate maneno” nilimfuta machozi na hapo akaendelea na masimulizi;

    “nilishindwa baada ya kuingia kwenye mapenzi na baba yako” aliongea na kuanza kulia tena.

    “unasemaje? Ooh mungu wangu, Samah baba yangu hajawahi kumsaliti mama yangu,,stop that nonsense(acha huo upumbavu)”..niliongea hayo japo sikua na uhakika na ukweli kuwa baba yangu alikuwa mwaminifu kwa mama yangu, niliamua kumtetea baba yangu, kwakuwa siku zote za maisha yake alimpenda sana mama yangu na alikuwa ni mwanaume wa familia ambaye mar azote alikuwa akikaa nyumbani na familia yake. “looh wanaume nuksi” nilijisemea moyoni kabla ya kumruhusu Samah aendelee kuongea;

    “nilifanya kazi kwenye kampuni ya baba yako nikiwa kama mwanasheria msaidizi lakini baadaye alinisomesha na baadaye alikuja kunifanya mwanasheria kamili wa kampuni yake,,kila alipokuwa anaenda safari za nje alikuwa akiondoka na mimi,,na taratibu nilianza kuvutiwa na baba yako,,alikuwa ni mtu aliyeijali familia yake na kila mara alikuwa akikaa na kunieleza juu ya familia yake na malengo ya kukufanya uwe mwanamke wa kuheshimika hapa Tanzania na dunia kwa ujumla…malengo ya baba yako na busara yake ndivyo vilivyonivuta kwake na nilifanya kila njia ili niwe nae lakini baada ya muda mrefu sana tuliingia kwenye mahusiano kwa sharti la mimi kuheshimu familia yake na kazi yangu,,kwaiyo na mimi nilifanya hivyo,,japo sikupata muda mrefu sana wa kuwa naonana au kukaa na baba yako kama wapenzi kwakuwa ratiba yake ilikuwa ikijali zaidi kazi na familia yake lakini muda mchache niliopata wa kuwa nae ulikuwa na maana kubwa sana kwangu kwakuwa alinipa faraja kubwa sana,,baba yako alikuwa ni mwanaume wa nguvu,,jasiri na mwenye kujituma katika kazi,,maisha na mapenzi,,alifanya vitu vyake kwa ufanisi mkubwa na sikuzote hakutaka kuona yeyote akiteseka, nilimpenda sana na hata alivyofariki nililia na kuomboleza,,Faith mbali na yote hata baada ya baba yako kuondoka niliendelea kukupenda wewe na chochote kibaya nilichokufanyia nilifanya kwakuwa sikuwa na njia nyingine ya kufanya,,nilifanya kwakuwa nililazimishwa kufanya hivyo” wakati wote huo Samah akiongea ilikuwa kama ametonesha kidonda kilichokuwa kina karibia kupona, nilinyanyuka pale huku nikilia na kutoka nje lakini kabla sijakaribia mlangoni nilihtuka na kugeuka kwa alichokisema Samah.

    “unasemaje Samah” nilimuuliza kwakuwa nilihisi sikuwa nimemuelewa vizuri.

    “Nimezaa na baba yako”,,,ni kauli ambayo sikuwa tayari kutafuta ukweli wake nilikaa chini kwa muda nikitafakari na wakati huo Samah aliendelea kulia pale kwenye kochi, nilinyanyuka na kumfata tena pale alipokuwa;

    “Huyo mtoto yuko wapi” nilimuuliza na sasa machozi yalikuwa hayanitoki tena.

    “yupo Nairob anasoma huko shule ya bweni” alinijibu huku bado akiendelea kusoma.

    “anasoma darasa la ngapi” nilimuuliza tena huku nikimtazama.

    “yuko darasa la kwanza”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “jina lake anaitwa nani” nilimuuliza ikiwa bado nimemkazia macho

    “anaitwaHerman, nilimpa jina hilo kama kumbukumbu ya baba yako baada ya kifo chake,,jina lake la zamani alikuwa akiitwa Hans lakini baada ya kifo cha baba yako nilimbadili jina” aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka.

    “nitamuonaje mdogo wangu,,ni damu yangu nahitaji kumuona,,” kabla sijamaliza kuongea nilimuona Jamshid akiingia huku ameshika kisu kidogo kipya na mkazi na vifaa vingine kama vya hospitali,,alikuwa amevimba kwa hasira na niliogopa kwakuwa sikujua nini kitafata, Samah alianza kulia na kuomba Jamshid asimfanye chochote,,nililia sana kwakuwa niligundua aliyekuwa akiteseka ni mama yangu wa kambo, japo alinitesa lakini kwasasa sikupenda Herman aje kuishi maisha ya uyatima.

    “tafadhali Jamshid naomba usimfanyie chochote, nilianza kumuomba Jamshid huku nikipiga magoti.

    “Faith stay away from me”(Faith kaa mbali na mimi) aliniambia Jamshid kauli iliyoniogopesha na kunifanya ninyamaze kimya kisha alikuja akaniita pembeni.

    “samahani mpenzi najua nimekutolea kauli mbaya,,lakini nahitaji kukulinda kwa namna yoyote ile,,sitamdhuru lakini nipe mda nifanye niwezalo” aliniambia na kunibusu na kabla sijamaliza kuongea aliniachia na kwenda pale alipokuwa Samah.

    “Clara” nilimsikia Jamshid akimuita Clara.

    “Abee”

    “nipe gloves zilizokuwa zimebaki jana” muda si mrefu Clara alikuja pale na zile gloves na wote tulisimama pale ili tuone nini Jamshid alitaka kufanya.

    “usifanye mambo yakawa magumu kuliko yalivyo sasa, sitakuchoma sindano ya ganzi ili usikie uchungu na maumivu na ujifunze maisha,,nionyeshe wapi icho kidude kilipo” aliongea Jamshid huku macho ya hasira yakiwa yamemtoka.

    “Jamshid nakuomba unichome sindano ua ganzi,,tafadhali naomba” alizidi kuomba huku akilia,,nilitokwa na machozi lakini nilipomtazama Clara hakuwa na hata chembe ya chozi.

    “Clara nisaidie kuniombea tafadhali” aliongea Samah.

    “natamani hata akukate mguu kabisa si kukutoa iyo ‘cheap’,,unakumbuka wewe ndiye ulisababisha mpaka sasa ninamkono mmoja tu,,mpuuzi wewe, Jamshid mkate kabisa mkuu huyu mbwa”,,Clara alikuwa na hasira na hapo ndipo nilipogundua kuwa Samah ndiye aliyeenda kumtorosha kwenye ile ajali na ndiye aliyeipanga ile ajali, lakini bado haikuwa sababu ya kumuona akiteseka.

    “Jamshid mchome sindano” nilimuambia Jamshid.

    “Faith, kama huwezi kusimama hapo tafadhali nenda chumbani,,Samah sio mtu wa kumuonea huruma” alimaliza kuongea hapo na hapo alishika ile pajama ya Samah na kuivua yote na kisha alimuacha akiwa na nguo ya ndani tu,,alianza kumkagua kwenye mapaja mpaka alipoonda sehem yenye mshono kwa mbali juu kabisa ya paja,,aliichana ile pajama na kuifanya kama kamba akamfunga Samah mikono na miguu kisha akaingiza kile kisu mpaka kikafika nusu,,Samah alipiga kelele mpaka nilimuonea huruma,,nililia sana na nilijaribu kumuomba Jamshid amchome sindano ya ganzi lakini hakunisikiliza,,alikipenyeza kile kisu na kukata sehemu kubwa kisha alimwaga spirit pale iliyomfanya Samah alie mpaka damu zianze kumtoka tena kwenye kidonda kile cha kooni,,,Jamshid aliingiza ule mkasi na kutoa kibati kidogo kilichokuwa na kitaa kidogo chekundu,, alikitoa na kukitazama kisha alitoka nje na nilipomuangalia kupitia dirishani alikuwa akikiponda kile kibati kwa chuma iliyokuwa pale nje na mpaka kilipopondeka na kumalizika kabisa. Alirudi ndani na hapo alichukua chupa ya dawa na kuvuta dawa kisha alimchoma sindani,,nilipoisoma ile chupa niligundua ilikuwa ni diclofenac, na baada ya kumchoma alimsafisha na kuanza kumshona,,Clara alikuwa pale pembeni kimya akimtazama Samah kama vile alihitaji muda na yeye amtese. Samah alikula na baada ya hapo Jamshid alimchoma sindano ya usingizi na akaishia usingizini. Usiku wa siku hii tulikuwa hatuna la kuongea zaidi ya kumuelezea Jamshid kuhusu yote aliyoniambia Samah wakati yeye akiwa hayupo.

    ****

    KESHO YAKE

    Asubuhi ilikuwa tulivu sana, ndege walikuwa wakiimba na mandhari ya ukungu iliyotanda pale ililifanya eneo lile lionekane kuwa zuri na la kuvutia, Jamshid alikuwa akiandaa chai kama kawaida yake kila siku ambapo yeye huamka saa kumi na moja na kufanya mazoezi mpaka saa kumi na mbili na nusu kisha huingia kuoga na kuanzia hapo huwa anafanya kazi ya kupika chai na vitafunwa,,lakini tulipoamka mambo yalikuwa tofauti,,Jamshid hakuwa amepika chai kama kawaida ila leo alikuwa amepika mchemsho wa kuku kitu ambacho kilitushangaza.

    “Umemtoa wapi kuku mtamu hivi” Clara alimuuliza.

    “haha sio kuku huyo ni kanga,,leo nilipoamka asubuhi kufanya mazoezi nilimkuta anakunywa maji nikaanza kumkimbiza mpaka nikamkamata,,nikakata na ile Ndizi ndogo ilikuwa pale nje ndo nikawatengenezeeni mchemsho hasa ukizingatia leo mpendwa wetu Clara anaondoka na ni lazima ale kitu cha kitanzania kabla hajaondoka”. Hii ilikuwa huzuni nyingine,,sikuwa tayari kuona Clara akiondoka lakini sikuwa na namna,,alihitajika kwenda kulea ujauzito wake lakini pia kwenda kufanyiwa matibabu ya mkono wake na kuwekewa wa bandia.

    Tulipata kifungua kinywa na mida ya saa tano gari aina ya Land cruiser ya kitalii ilikuwa imefika na kupiga honi,,,na Clara alikwenda kufungua nasi pia tulimfata nyuma,,Clara alimrukia yule mwanaume wa kizungu aliyeshuka na niligundua kuwa yule alikuwa Gerald, walikumbatiana na walilia kwa pamoja,,Gerald alimuangalia mkono na hakuamini. Alikuja na kunisalimia huku akinitania kwakuwa alinifahamu toka nikiwa chuoni,,tuliingia ndani na mimi nilielekea chumbani kumsaidia Clara kupaki vitu vichache alivyokuwa navyo kisha na tulimuacha Gerald na Jamshid pale sebuleni wakiongea. Tuliporejea Gerald alisema ametulipia fedha ya kuishi hotelini kwa usiku wa siku hiyo na hivyo tujiandae tuondoke wote,,sikuweza kupinga ila akili yangu ilimuwaza Samah tu,,tungewezaje kuondoka na kumuacha katika hali ile,,Jamshid alienda kumchomekea ile mirija ya chakula na kumchoma sindano nyingine ya diclofenac na ya usingizi kisha tuliondoka na kufungwa milango yote. Baada ya kufika huko tuliwasindikza Clara na Gerald na wao walipanda ndege ndogo ya kukodi ya ile hotel kuelekea Dar.

    USIKU

    Ikiwa ni muda wa miezi mingi sasa toka mara ya mwisho nimekuwa na Jamshid katika ulimwengu wa mapenzi leo hii tulikuwa tunakutana tena nilitamani sana siku ya leo ifungue tena mwanzo wetu na maisha ya ndoa yaanze leo,,lakini moyoni nilijua pengine mambo bado hayajakaa sawa,,Gerald alikuwa ameniachia kiasi cha fedha za kitanzania zilizoweza kuniwezesha mimi na Jamshid kuishi kwa raha kwa muda mrefu sana.

    ****

    “Jamshid stop maji ya baridi bhana” nilikuwa nikimlalamikia Jamshid aliyekuwa akinimwagia maji ya barid,,nilinyanyuka pale na kwenda chini ya hotel hiyo kwaajili ya kuulizia kuhusu jambo fulani na niliporejea nilikuta Jamshid amekwisha oga na mimi niliingia kuoga,,nilipotoka Jamshid alikuwa kama akinisubiri vile pale kitandani,,alitabasamu aliponiona nikitoka na mimi kwa mbwembwe nililiachia lile taulo na kumpa nafasi ya kunitazama kwa undani huku taratiiibu nikikisogelea kitanda, Jamshid hakuwa na subira alinyanyuka na kunifata pale kisha aliileta midomo yake ikakutana na yangu na hapo taulo alilokuwa amejifunga lilidondoka,,,alinisogeza mpaka ukutani taratiibu huku ndimi zetu ziliendelea kupeana salam baada ya kukosana kwa muda mrefu,,sitoacha kusema kuwa Jamshid alijua nitakacho kila nitakapo,,alijua sehemu muhimu kwenye mwili wangu na hakupoteza muda kujaza maji kwenye gunia, siku zote amekuwa akijaza maji kwenye pipa na kushuhudia yakijaa kila alipokuwa akiongeza,,,alicheza na sehemu zilizonipa raha tu nakuacha kupoteza muda na sehemu ambazo hazikuwa na thamani kwa kazi hiyo, aliendelea taratiibu kuiruhusu mikono yake ipate nafasi ya kutalia mwili wangu panapo milima na maponde,,ulimi wake ulifanya kazi kubwa ya kuhakikisha usalama wa furaha yangu,,kwangu Jamshid alikuwa kama computer,,alitumia ulimi wake kucheza na kifua changu huku akimikono yake ikiendelea na kazi nyingine katika kila pande ya mwili wangu,,,na mimi siku nyuma kuhakikisha kuwa namsaidia kusukuma ili liwake,,nilikuja kushtuka nikipiga kelele zilizoashiria kuwa kuna kitu kilikuwa kikileta raha kwenye mwili wangu,,nilipotazama nilikuwa kitandani nimelala na nilipomtazama Jamshid niliona kicha chake kikiwa sehem ya kati ya mwili wangu ile sauti ilizidi na sasa nilisikia kama nilikuwa nikipaa na parachuti… kazi ilienda vizuri na baada ya mchakamchaka wa takribani masaa manne wote tulilala. Tulipoamka kulikuwa kumeshakucha na safari ya kuondoka kurudi nyumbani ilianza,,nilijihisi mwepesi sana na mwenye furaha,,Jamshid alikuwa ni mfalme kwangu,,nilimpenda sana kwa kuwa kumpata mwanaume kama yeye ni mtihani ambao nisingeuweza kama ningekubali kumpoteza,,yeye ni maisha kwangu. Tulipofika nyumbani ile gari iliyotuleta ilituacha pale na tulipoingia ndani ya geti tulishtuka kumuona Samah akiwa amekaa pale kwenye ngazi,,,nilimkimbilia pale alipokuwa;

    “Samah unajisikiaje,,samahani tulikuacha kidogo lakini tulijua tutakuwahi” nilijitetea na ghafla nikajiuliza moyoni kwanini najitetea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Msijali niko sawa na ninajisikia nina nguvu japo mguu wangu bado unauma” alinijibu na nilimkumbatia ila Jamshid alimpita na kabla hajaingia ndani Samah alimuita.

    “Jamshid hutakiwi kunichukia,,kumbuka hata wewe ulikuwa unafanya mambo ya kinyama lakini si kwamba wewe ulikuwa na roho ya unyama, lakini ulifanya mambo kwa kufata maagizo ambayo hata kama uliyapenda au hukuyapenda ilikuwa ni lazima uyafanye” aliongea Samah, maneno ambayo kimsingi yalikuwa ni ya kweli na yalionekana kumgusa Jamshid;

    “lakini kikubwa Jamshid nashukuru kwa kunitoa ile chip,,hapo umeniondoa kwenye utawala wa 696, na sasa naweza kuishi maisha huru kama hamtaniua, lakini hata mkiniua nawaombeni mumlee Hermani,,Faith Herman ni mdogo wako ni damu yako kabisa, kabla ya kufa kwa baba yako aliniomba nikutambulishe kwa Herman huku akisisitiza kuwa umpende na kumlinda mdogo wako” aliongea hayo Samah na kunifanya kutokwa machozi tena,,Jamshid alikuja pale na wote tulikumbatiana,,tulikaa na kula pamoja, majira ya jioni Samah alianza kuumwa ghafla na hapo tulianza kuhangaika namna ya kumtibu,, Jamshid alisema tumpeleke hospitali na hivyo alifungua kwenye chumba cha stoo cha nyumba iyo ili kuangalia kama angeweza kupaka pamba za kumfunga vizuri,,lakini alipofungua alikuta bunduki na vifaa vingine vya uwindaji na bunda kubwa la pamba,,alimfunga kidonda na Samah aliomba asipelekwe hospitali,,Jamshid alimchoma sindano ya usingizi.

    Wakati Jamshid yuko chumbani nilisikia taarifa ya habari ikitangaza jambo la kushtua na hapo ndipo niliongeza sauti na Jamshid alikuja.

    “msichana huyo aliyekamatwa anafahamika kwa jina la Clara na ndiye aliyekuwa mwanasheria wa mtuhumiwa huyo kabla hajatoroka, hivyo jeshi la polisi linamshikilia mwanasheria huyo ili aeleze sehemu alipokuwa mteja wake, japo taarifa zilizotufikia ni kwamba mwanasheria huyo bado amekataa kuongea” ilikuwa ni sehemu ya taarifa hiyo.

    “Jamshid naenda kujisalimisha polisi” nilimwambia jamshid huku nikiwa kama nimechanganyikiwa.

    “hapana, watamuachia kama wakikukosa, hakuna haja ya kukurupuka” aliongea Jamshid kwa sauti ya ukali.

    “hapana Clara ni mjamzito,,Gerald ametoka huko kuja kumchukua alaf aje apate tabu,,ni kwasababu yangu Clara sasa ni kilema,,siko tayari apate shida zaidi” niliongea na kuchukua simu lakini Jamshid alininyang’anya,,nilimng’ata mkono na kumrushia stuli iliyomgonga mguu na kumfanya aka echini na kushindwa kunifata kisha nilipiga simu polisi kuwataarifu kuwa nilikuwa sehemu gani,,wakati huo Jamshid aliendelea kunikataza huku akilia lakini sikuwa tayari,,nilimaliza kuongea na kumuendea Jamshid pale chini alipokuwa bado akiuangalia mguu wake;

    “samahani mpenzi wangu sikuwa namaana ya kukuumiza” niliongea huku nikimsaidia kumuamsha.

    “maumivu haya si kitu kama maumivu ya kuishi bila wewe,,siko tayari,,tuondoke sasa hivi” aliongea Jamshid.

    “nakupenda sana Jamshid lakini katika hili siko tayari,,watu wataendelea kuteseka kwaajili yangu mpaka lini?” kabla sijamaliza kuongea nilisikia geti gari zikiwa nje ya geti na niliona mtu akiruka ukuta na kuja kufungua geti kisha gari nne zenye maaskari wenye silaha waliingia na kuzunguka ile nyumba,,nilimfata Jamshid na kumkumbatia huku sauti ya wale askati kwa kutumia kipaza sauti walikika;

    “Sisi ni jeshi la polisi wa kituo kikuu cha mikumi,,tumepewa amri ya kukukamata Faith Herman kwa kutoroka chini ya ulinzi halali wa polisi,kwa mauaji na kwakudharau mahakama, tunakuamuru utoke nje mikono yako ikiwa juu,lasivyo itatulazimu kutumia nguvu” nilimuachia Jamshid na kuingia mpaka chumba alichokuwepo Samah nilimbusu japo alikuwa usingizini na kutoka nje,,Jamshid alikuwa akinizuia lakini ilishindikana,,,nilipotoka nje nilifungwa pingu na Jamshi alitoka na ile bunduki kisha alianza kuwashambulia wale polisi, wakati nikimsihi Jamshid awaache nilishuhudia risasi ikiachiwa na polisi mmoja na kumpiga Jamshid kisha alianguka na kuanza kutupa miguu huku na kule,,nililia na kurudi pale alipoanguka lakini nilizuiliwa kwa makofi,,wale askari walienda kumgusa na nilimsikia mmoja akimueleza yule mkuu wao;

    “ameshafariki mkuu”





    Sikuweza kulia tena baada ya kusikia kuwa Jamshid amefariki niliomba sana wale askari niende japo nimfumbe macho,,huku wakiwa wamenifunga pingu nilienda mpaka pale na nilipomgusa niligundua ni kweli alikuwa amefariki, nililia sana nikiwa pale chini na ndipo waliponinyanyua na tukaondoka,,maaskari wengine walibaki pale ili kuangalia namna ya kuuondoa mwili wa Jamshid pale.

    Nilifikishwa kituo cha polisi mikumi na baada ya taratibu za awali kufanyika kamanda wa polisi wa mkoa wakiongozana na gari tatu za polisi nikiwa chini ya uangalizi mkali tulianza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam… gari lilikuwa likikimbizwa sana na huku ving’ora vya kuyaamuru magari mengine yakae pembeni vilikuwa vikisikika,,sikujua kwanini polisi walidhani mimi ni mtu hatari kiasi cha kuhitaji ulinzi mkali kiasi kile, hawakujua kuwa mimi sikuwa wa aina hiyo waliyodhani,,sikuwa mtukutu kiasi cha kuhitaji askari wengi kiasi kile,,safari haikuwa ndefu sana kwani baada ya mwendo wa masaa matano tulikuwa tumeshaingia Dar,,,kilichonishangaza ni kundi kubwa la waandishi wa habari waliokuwa wametanda makao makuu ya polisi pale Dar es Salaam, nilishtushwa pia na uwepo wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi eneo lile na baada ya kufikishwa niliingizwa mpaka ndani na baada ya taratibu zao za kipolisi kukamilika niliwekwa kwenye chumba maalumu chini ya ulinzi mkali, lakini nikiwa pale ndani niliweza kusikia sauti ambayo hata hivyo niliwahi kuisikia kabla, ilikuwa ni sauti ya kamanda wa polisi kanda maalum aliyekuwa akiongea na waandishi wa habari kwa pale nje;

    “Jeshi la polisi lipo makini, na niwahakikishie wananchi kuwa wahalifu wote hawataweza kwenda mbali na mikono ya dola na wakatoka salama,,,huyu binti anaitwa Faith nadhani ndugu waandishi wote mnamfaham aliwahi kutoroka akiwa hospitali na anakabiliwa na kesi ya mauaji na video ya namna alivyofanikisha mauaji ya watu wawili akiwemo ndugu yake wote mliiona, lakini akiwa anatibiwa alitoroka baada ya kufanya mbinu zilizopelekea pia askari wetu wawili waliokuwa wakimlinda kufariki,,na pia kuna mauaji ya wazungu wanne waliokuja Tanzania kwa ajili ya utalii yalitokea huko maeneo ya bunju nayo pia alifanikisha yeye na tumefanikiwa kukuta gari ya wazungu wale aina ya Nissan Patrol ikiwa huko alikojificha,,,hata hivyo alikuwa na jambazi mwingine wa kiume ambaye tunaamini alikuwa ni mpenzi wake na katika kurushiana risasi na polisi alipigwa risasi na kufariki,,hivyo tunaomba kwa pamoja kama jeshi la polisi na ninyi ndugu zangu waandishi,,lakini pia waziri yuko hapa nae anamachache ya kuongea” alimaliza yule kamanda na kumkaribisha waziri,,machozi yalinitoka kwakuwa Jamshid aliitwa jambazi,,,mimi ndiye niliyestahili kuitwa jina lolote hapa duniani na si yeye,,hakuwa na kosa lolote,,alifawafyatulia polisi risasi kama njia ya kunilinda mimi na kama ambavyo mwanaume yeyote yule mwenye mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake angefanya,,mimi kwake nilikuwa ndiye kila kitu na kwangu yeye alikuwa ndiyo maisha yangu sikuwa na la kufanya zaidi ya kukaa kimya kwakuwa sasa mambo yalikuwa magumu kuliko mwanzoni..niliendelea kumsikiliza yule waziri akiongea pale ambaye hata hivyo hakuwa na meneno ya tofauti sana na yale aliyokuwa akiongea yule kamanda wa polisi lakini zaidi yeye alifafanua adhabu yangu;

    “,,hivyo sheria ya nchi inafahamika,,na huyu amehusika waziwazi kwenye vifo vya watu nane wakiwamo askari wawili,wazungu wanne na ndugu yake pamoja na mfanyakazi wake tena kwa kudhamiria na kwa unyama mkubwa,, naliagiza jeshi la polisi kwakuwa tayari ushahidi wanao basi wamfikishe mahakamani ili mahakama iamue,,hatutasita kumnyonga kama ataadhibiwa hivyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kiuaji na kijasusi,,huyu binti ni sumu kwa taifa na tabia kama hizi lazima tuzipige vita” alimaliza na hapo waandishi wa habari walitawanyika kwakuwa sikusikia tena hapo nje kama kulikuwa kuna mtu,,,nilikalishwa pale kwa muda mrefu ilia ilipofika mida ya jioni nilisikia lango likifunguliwa na nilifurahi kuona Clara akiingia pale ndani,,alikuwa amekonda kwa muda mfupi aliokamatwa,,nilitamani kumkubatia lakini haikuwezekana kwakuwa kulikuwa na kizuizi cha geti jingine la chuma, Clara alikuwa akilia sana lakini nilimsihi asilie;

    “najua hukuua Faith, najua hukuua” aliendelea kulia na kusema maneno hayo huku nikimsihi anyamaze.

    “usilie Clara,,mimi niko tayari kwa lolote sasa hivi, sina namna nyingine ya kuukabili ulimwengu zaidi ya kukubali kuwa mambo yanatokea and I have to see them happening (na inabidi nione tu yakitokea),,sina namna nyingine Clara” nilimuambia Clara maneno hayo na kabla sijaongea zaidi alikuja kutolewa pale.

    “Clara” nilimuita wakati akiondoka na hapo aligeuka na wale polisi walisubiri.

    “Jamshid amefariki” nilijikaza kumweleza lakini sikuwa na namna ya kumficha.

    “hapana Faith haiwezekani,,haiwezekani kabisa” aliongea Clara huku akilia, huo ulikuwa ukweli ambao sio Clara tu aliyekuwa hayuko tayari kuusikia bali hata mimi sikuwa tayari kuusimulia. Walimuondoa Clara pale na kumpeleka nje na sikusikia tena sauti yake,,baada ya muda si mrefu ule mlango ulifunguliwa tena na askari waliingia na kunifunga kila sehemu kisha nilipakiwa kwenye gari na kuondoka eneo lile huku nikisindikizwa na magari ya polisi waliokuwa wameshika bunduki kama walikuwa wamewakamata Alshabab.

    MWEZIMMOJA MBELE.

    Mwaka ulikuwa umeshaingia mpya na sikuwa na taarifa kwani kule nilikokuwa nimefungiwa sikuweza kuona tena nje,,,nilikuwa kama kichaa kwa muonekano nilianza kukonda na afya yangu ilidhoofika,,nilikuwa nikikohoa sana kutokana na fumbi la mule ndani lakini hakuna aliyejali,,dalili za kansa ya utumbo zilikuwa zimenianza na sasa sikuwa na dawa yoyote nikitumia. Nilijilaza pale sakafuni na kile kipande cha godoro kilichoisha kilisaidia kwa kiasi flani kunipa ahueni ya maumivu yangu.

    ****

    Upepo mkali ulianza kuvuma na kuingia ndani ila sikujua kabisa ulikuwa ukipita sehemu gani, niliamka na kuketi kwenye kona moja ya ukuta huku nikijikunyata, mwanga mkali kutoka kwenye kona ya pili ulinipiga na nilipofungua macho nilishangaa kuona mzimu,,niliamini kuwa ni mzimu kwakuwa kipindi cha nyuma niliwahi kupatwa na hali kama, nilipotazama nilianza kuona sawia na alikuwa ni Jamshid..sikuogopa tena kama mwanzo nilimsogelea nimkumbatie lakini nilishindwa;

    “Jamshid nakupenda mpenzi, nakupenda sana Jamshid na sikuwa na maana ya kukuingiza kwenye matatizo” nililia nikimwambia maneno hayo lakini hata hivyo hakujibu chochote zaidi ya yeye kuzidi kulia na hakuwa anaongea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “tafadhali Jamshid sema chochote,,sema hata unanichukia kwakuwa sikukusikiliza uliponiambia nisipige simu polisi,,nambie Jamshid,,sema baasi Jamshid,,nambie unanichukia mpenzi wangu”,,machozi yalinizidi kiasi kwamba macho hayakuona tena nililia sana kwakuwa Jamshid hakuongea, nilimuona tu akilia na bila kusema chochote aliondoka na kuniachia kikaratasi..baada ya kumaliza kulia nilikiangalia na kukifungua ndipo nilipogundua kuwa ilikuwa ni zile dawa nilizokuwa nikimeza kipindi nikiwa mikumi, nilizichukua harakaharaka na kuzimeza.

    Asubuhi na mapema siku iliyofuata nilichukuliwa mpaka mahakama kuu na leo nilisomewa mashtaka yangu ya zamani na mapya,,nililetewa wakili ambaye sikuelewa kazi yake ni nini kwakuwa alikuwa akikubali kila kitu, baada ya mlolongo mrefu wa kimahakama pale ilifika wakati nikaambiwa nijitetee na mimi nilinyanyuka huku machozi yakinitoka, niliangalia huku na kule nikagundua mahakama ilikuwa imefurika kuliko kawaida,,hakukuwa na nafasi ya kupita mtu na hadi madirishani kote kulikuwa kumejaa watu walioning’inia kusikiliza kesi ya muuaji mimi;

    “ni kweli nimeua,,ni kweli nina husika na kila kitu,,kila kilichoandikwa kwenye jalada la mashitaka ni kweli kabisa,,naomba niadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi” niliongea huku nikitokwa na machozi kabla ya kukatishwa na sauti ya mtu aliyeongea kwa shida;

    “si kweli,,sio yeye aliyeua” ilikuwa sauti ya mwanamke aliyeonekana kutoka katikati ya lile kundi la watu pale mlangoni,,sikuweza kumuona vizuri,,alizidi kujipenyeza huku akiendelea kuongea kwa tabu na mateso kuwa ‘si kweli,,sio yeye aliyeua’,,,alifanikiwa kujipenyeza huku akilia na kuonekana akikuwa mgonjwa kweli kweli alifika mbele na kurudia yale maneno tena kuwa ‘si kweli,,Faith hajaua’,,nilipomtazama vizuri alikuwa ni Samah,,alikuwa amechoka kweli kiafya na uso wake ulikuwa umepauka sana,,alikuwa akichechemea huku hijab aliyokuwa amevaa ikiwa imeloa damu sehem ile ambayo kulikuwa na kile kidonda,,shingo yake ilikuwahaifai kuangalia kwa ulo mchubuko alioupata wakati akipenya pale kwenye lile kundi la watu ilia je mbele na kuyaongea maneno yale ambayo sasa pamoja na kuyasema jaji aliamrisha wale askari wamtoe nje kwakuwa eti alikuwa kichaa,,wakati anatolewa nje kwa nguvu bado alikuwa akiendelea kuongea kwa shida lakini sauti yake ilisikika;

    “mimi sio kichaa ila Faith hakuua,,,mimi najua aliyeua lakini sio faith,,muacheni hana hatia” maneno ya Samah sio tu yalinihuzunisha mimi ila nilishuhudia wamama wengine waliokuwa pale ndani wakitoa machozi,,Samah alikuwa anateseka sana kwa nilivyokuwa nimemuona,,alikuwa anataabika pengine ni kwa yale matatizo ambayo Jamshid alimsababishia.

    *****

    Baada ya hapo mahakama iliahirishwa na kesi yangu ilipanga tena tarehe 2 mwezi wa pili ambayo ndiyo ilikuwa siku ya Hukumu, nilichukuliwa na kurudishwa tena mpaka mahabusu na maisha ya kutoona nje tena kwa muda wa wiki moja , Jamshid aliendelea kuniletea zile dawa lakini hakuwahi kuongea hata siku moja zaidi ya machozi kumtoka,,nilishangazwa na ile hali ila nilifurahi kwakuwa nilijihisi bado niko nae,,maisha ya pale ndani yalikuwa hayana tofauti sana na maisha ya shimoni,,hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika wala hakukuwa na mtu wa kuja kukutembelea,,nilikuwa nikilia na kusali mpaka usingizi uliponipitia, chakula nilikuwa nikipewa lakini sikukielewa kwakuwa hakikuwa chakula cha kumpa binadamu,,kuna muda nilikaa siku mbili bila kula kwakuwa nilishindwa kabisa kula,,,nilitumia muda mwingi sana kukumbuka wakati nikiwa msichana nisiye na matatizo,,nilikumbuka sana kipindi niko nchini Finland jinsi ambvyo nilikuwa mwenye furaha achilia mbali kuwa nilikuwa yatima,,nilikuwa ni moja ya wasichana matajiri pale chuoni ambaye nilikuwa nikitaka kuwa marekani kila wiki sijishauri napiga simu tu nawekewa tiketi ya ndege,,nilikuwa nikienda London nakaa kwenye hotel yenye hadhi ya nyota tano,, nilikuwa na maisha ambayo hayalingani kabisa na haya ninayoishi sasa,, maisha ya kula vyakula vibovu na kuwa mfungwa si maisha yangu lakini bado nilijipa moyo kuwa kila jambo hutokea kwenye maisha na kitakachokusaidia si historia yako ya nyuma bali ni uvumilivu wa nafsi na imani yako ya kimungu, kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja toka nianze kuandamwa na tabu na mahangaiko tayari nilikuwa nimejifunza kumshirikisha mungu kwa kila jambo,,kuachana na mambo ya kuiga lakini pia kuwa mvumilivu na kutolalamika,,,nilikuwa na shida ambazo pengine msichana yoyote mrembo asingeweza kuvumilia na angekuwa akilalamika kuwa mungu amemuacha lakini, kwangu haikuwa hivyo, niliyatathimini matatizo yangu na kwakiasi kikubwa hata kama yamesababishwa na wengi ila mimi nilikuwa mmoja ya watu walioshiriki kunifikisha hapa nilipo,,pengine kwa kuwa sikufikiri sawia wakati nilipohitajika kufikiri au sikufanya maamuzi sahihi wakati nilipohitajika kufanya maamuzi sahihi,,wazazi wangu walichangia pia mimi kuingia kwenye maagano ya ajabu yaliyonifikisha hapo nilipo lakini siwezi kuwalaumu kwakuwa baada ya kifo chao nilikuwa mtu huru na mwenye uwezo wa kuchambua na kuamua kwa matakwa yangu mwenyewe,,nilikuwa nina muda wa kuachana na historia mbaya na kuanzisha historia mpya mbele yangu,,,nilikuwa na msimamo wa kuwachukia wanaume ila sikuwa na msimamo wa kimaamuzi wa maisha yangu lakini hata hivyo siwezi kujilaumu kwakuwa yameshatokea na kama ningekuwa na muda wa kurudi nyuma na kurekebisha nilipojikwaa pengine nisingekuwa kama nilivyosasa lakini itabaki kuwa historia na sitajifunza mimi tu bali ulimwengu wote utakao fahamu hili na ujifunze.

    ****

    Ilikuwa usiku sana siku ambayo kesho yake ndiyo ilikuwa siku ya Hukumu yangu, nilitegemea kumuona Jamshid usiku ule akinipa moyo lakini sikumuona,,badala yake nilimuona bibi Eunice, alikuja akiwa ni mwenye afya na aliketi karibu na mimi na kuniongoza nisali rozari, tulisali rozari nakurudia mpaka niliposhtuka na kukuta hakuwa pale tena na tayari mda wa kuelekea mahakamani ulifika. Nilipakiwa kwenye gari na kufika mahakama kuu, sikuwa na woga kabisa, nilikuwa na uso wenye furaha na sikujua ni kwanini nilikuwa na furaha wakati leo ingekuwa siku mbaya kwangu,,Hukumu ilianza kusomwa saa tatu asubuhi na mimi sikuweza kuisikia vizuri kwakuwa mawazo yangu yalikuwa mbali sana na nilisikia kwa mbali,,,majira ya saa nane mchana kama saa ya pale mahakamani ilivyokuwa ikionyesha ndipo nilishtuka na kusikia jaji akitamka maneno haya;

    “hivyo basi baada ya kupitia ushahidi wote wa upande wa utetezi na ule wa mashtaka, na baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa Faith aliua kwa kukusudia, mahakama hii tukufu INAMUHUKUMU KUNYONGWA MPAKA KUFA..pia nafasi ya kukata rufaa iko wazi” yalimaliza maneno ya hakimu na hapo nilisikia kilio toka kwa wanawake waliokuwa pale mahakamani,,kilichonishangaza ni namna ambavyo kila mtu alikuwa na huzuni.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitolewa pale mahakamani na kupandishwa kwenye gari,,wakati natoka nje ya lango la mahakama niliangalia kwa mbali nikaona mwanamke aliyekuwa amevaa hijab nyeusi na miwani nyeusi,,nilitazama kwa makini na kisha nilimuona akivua ile miwani na alitoa karatasi akaionyesha kwangu, nilifanikiwa kuisoma na maandishi yake yalisomeka ‘FORGIVE ME’ niligeuka kumuangalia na nikagundua alikuwa ni Maysa,,sikuongea chochote, nilipelekwa mpaka magereza na kufungiwa. Kesho yake asubuhi nililetewa karatasi iliyonionyesha tarehe yangu ya kunyongwa na nilionyeshwa orodha ya watu waliotaka kuja kuongea na mimi kabla ya kifo changu,,walikuwa ni wengi wakiwamo wanaharakati na watu wa haki za binadamu lakini nilikubali kuonana na watu watatu tu na wa kwanza alikuwa padre Thomas Mvungi ambaye alisoma seminary moja na marehemu baba yangu. Majira ya saa nne asubuhi alikuja padre na nilifanya sala ya kuungama zambi zangu,, padre alitaka kujua kama ni kweli niliua au la lakini sikuwa tayari kumueleza chochote zaidi ya kukiri kuwa niliua. Baada ya maungamo aliondoka na kuniacha nikitafakari mwisho wangu nilikaa na kulia peke yangu lakini moyoni nilikuwa na furaha kwakuwa nilijua nitaenda kukutana na Jamshid na Magret pamoja na wazazi wangu.

    Siku moja kabla ya kunyongwa alikuja mtu wa pili katika ile orodha ya watu nilikubali waje kuniona, huyu alikuwa ni Samah,,alikuwa amechoka kupita kawaida;

    “Samah pole mama najua unateseka, naomba umsamehe Jamshid,haikuwa dhamira yake kukufanya uteseke, naomba tafadhali” nilimlilia Samah ambaye hata hivyo nae alizidi kulia,,alikuwa amekonda na mabaka kila sehemu kama vile ameungua na maji ya moto.

    “hapana sio Jamshid, baada ya wewe kuondoka kule na mwili wa Jamshid kuchukuliwa, walikuja 696 na kunichoma sindano ya sumu,,nategemea kufa tarehe ambayo wewe utanyongwa Faith”…taarifa hii ilinishangaza lakini pia ilinisikitisha sana na kunifanya nilie,,nilihuzunika kwakuwa nilishaanza kumpenda tena Samah kama mama yangu na mama wa mdogo wangu Herman.

    “pole Samah,,pole sana” nilimshika mikono na wote tulilia pamoja.

    “sumu hii imeshaua maini yangu kwa asilimia kubwa na kinga ya mwili wangu imekwisha kabisa” aliongea Samah na kunyanyuka kisha aliipandisha ile hijabu na kunionyesha kile kidonda alichotolea ile chip,,kilikuwa kikitoa funza na usaha kumaanisha kuwa kilikuwa kimeoza tayari, alifungua na ile hijabu na kunionyesha tena shingo yake iliyokuwa nayo imeoza.

    “baada ya Jamshid kunifunga ile mara ya mwisho vidonda vyote vilishaanza kukauka na nilipata nguvu,,lakini waliponichoma ile sindano ya sumu ndiyo ilikuja kuvuruga kila kitu” nilimuonea sana huruma lakini sikuwa na la kusema zaidi ya kulia tu.

    “na nimekuja na watu wawili nilikuwa nataka ukutane nao” kabla sijasema chochote alinyanyuka na watu wawili waliingia.

    “Faith tafadhali naomba unisamehe’’nimekukosea sana najua hilo” ilikuwa sauti ya Maysa ambaye kwa sasa sikuwa na sababu yoyote ya kutomsamehe, tuliongea nae sana na nilimsamehe,,ila kitu kilichonipa furaha na huzuni kwa pamoja ni huyu mwingine,, alikuwa mtoto mdogo mzuri wa kiume mwenye afya nzuri;

    “Faith huyu ndiye kaka yako Herman,,”alitambulishwa kwangu na Samah yule mtoto mdogo,,nililia sana kwakuwa Herman alikuwa anakwenda kuitwa mtoto yatima,,alikuwa akifanana sawasawa na baba yangu na hata vidole vyake nilipoviangalia vilifanana na vyangu, haipingiki kuwa kweli yule alikuwa ni mtoto wa baba yangu.

    Tuliongea na muda uliisha kisha tuliagana na wote waliondoka,,nilifurahi kuwa ninaondoka duniani lakini nimefanikiwa kumuona mdogo wangu na ninaamini damu ya baba yangu bado itabaki duniani.

    ******* *******

    Mateso yangu leo yamefikisha mwaka toka yalipoanza,,kwangu huu ni mwaka wa mateso,,,leo hii ni tarehe 14 mwezi wa pili mwaka 2005 ni siku ya wapenda nao,,siku ambayo ni mbaya kwangu kwakuwa nahitimisha ngwe yangu ya kuishi hapa dunian kwangu IT’S THE WORST VALENTINE’S DAY, ni mbaya kwakuwa leo hii Herman anakwenda kuwa yatima,,mimi na kwenda kunyongwa na Samah anakwenda kufa,,ni siku mbaya kwakuwa ni siku ambayo naacha yote ya dunia na kuondoka bila kumuona mtoto wa Clara,,lakini siku hii ni nzuri kwakuwa leo nakwenda kupumzika,,japo sijui huko niendako ila nina imani ninakwenda kuondokana na shida na taabu za dunia lakini pia nitakwenda kuonana na familia yangu pamoja na Jamshid.

    “Kwenye orodha ya watu niliopanga waje kunitembelea ulikuwa umebaki wewe tu, na ndiye ambaye nilitaka kuongea na wewe masaa machache kabla ya mimi kuiaga dunia,,nilitaka kuongea na wewe leo ili nikupe ujumbe ambao utahakikisha kuwa kila mtu anausoma,,kawaandikie watu wajue ukweli wa kila jambo na waniombee niendako,,HIYO NDIYO HADITHI YANGU NDUGU MWANDISHI, NILIFICHA KIASI CHA FEDHA KWENYE KIWANJA NAMBA MBZ/KN/123 huko mbezi beach,,nenda utaona mti mkubwa chimba chini ya ule mti utakuta sanduku lifungue,,ndani kuna picha zangu na familia yangu,,pia kuna picha za Magret,,Clara na watu wengine,,kuna kiasi cha fedha milioni 8 zitumie kuandika kitabu UTAKACHOKIPA JINA LA THE WORST VALENTINE’S DAY ukiuze na asilimia 75 ya fedha utakayopata ukawape wajane na watoto yatima na wote wanaoishi kwenye mazingira magumu,,alimia 10 utampa Maysa amuwekee Herman,,utakuta pia hati ya nyumba namba KN/MSK/11 iko masaki hakikisha unafanya namna ya kubadili hati hiyo iwe na jina la Herman,,,Nakuomba kwakuwa nakufahamu na naamini utafanya hivyo”.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    HAYO YALIKUWA MANENO YA MWISHO KUNIAMBIA FAITH BAADA YA KUNISIMULIA HADITHI NDEFU NILIYOWAANDIKIA,,,FAITH ALINYONGWA MASAA MACHACHE BAADA YA KUMALIZA KUNISIMULIA HADITHI HII…KWASASA NI MWAKA 2013 NI MIAKA 8 TOKA FAITH ANYONGWE NA TOKA SAMAH AFE,,LEO HII HERMAN KATIMIZA MIAKA 16 TOKA AZALIWE NA NI MOJA YA WANAFUNZI BORA HAPA TANZANIA LAKINI PIA NI MMLIKI WA SALUNI YA FAITH BEAUTY.

    #HESHIMU WAKATI ULIONAO KWAKUWA WAKATI ULIOPO NI SASA#.



    MWISHO!!!!


0 comments:

Post a Comment

Blog