Simulizi : Mimi Ni Muafrika (I'm African)
Sehemu Ya Pili (2)
9;00pm
Mpuzu pamoja na Ishimwe walianza kukwea ukuta, taa zilizokuwa zikizunguka na kuangaza kila kona zilitulia tuli kama maji mtungini huku zikiangaza sehemu moja tu, wakatumia mwanya huo adimu ili kuvuka ukuta kuingia ndani, wakipitia eneo la giza lisilofikiwa na mwanga, dakika kumi na tano zilitimia,wakafika juu ya ukuta, wakaangaza tena huku na kule, hakuna aliyewaona, wakatumbukiza kamba ndani, wakaitumia kushukia ndani ya ngome, wakajibanza kwenye matanki makubwa ya maji yaliyosambaza maji kila kona katika ngome yote ya wakoloni, Waingereza kama watawala namba moja, kisha Wahindi wakifuatiwa na Waarabu, wote walipatikana katika ngome hii maarufu kama the great fort (ngome kubwa).
“,Sikia nikwambie Mpuzu, nikitupia buyu lote la upupu ndani ya maji,ukautumia mpira huu unaopeleka maji katika bustani za matunda za hawa wazungu, utaweza kuukamata vizuri na kuwamwagia huku mimi nikiwashambulia kwa mishale, “Ishimwe alimshauri rafiki yake Mpuzu, akimnongoneza, wazungu wasisikie na kuwakamata.
“,Kweli kabisa wazo zuri sana,fanya hivyo,”Mpuzu aliongea,Ishimwe akarusha kibuyu,”,Chubwiii!”,sauti ilisikika,kibuyu kilitumbukia ndani ya maji,sauti ya maji kukipokea kibuyu ikasikika.Askari mmoja wa kikoloni akiwa na bunduki yake begani alishtuka,akaangaza huku na kule kwenye matanki ya maji hakuona kitu,akaendeleza kupiga usingizi bila kutambua chochote kile.
Ngome kubwa; 9;45pm
“Tyeee! iityeee! “,Mwamvua alipiga chafya, vumbi lilipenya katika matundu ya pua yake, alizinduka baada ya masaa takribani matano akiwa amepoteza fahamu, “,Wuuuu! wuuuu! “,mbwa walifoka, wakiwa na macho ya hasira kwa Mwafrika huyu aliyekuwa nusu mfu muda uliopita, Mwamvua aligeuka baada ya kusikia kelele za Mbwa, giza nene lilikuwa ndani ya chumba cha gereza, hakuona chochote kutokana na giza kali zaidi ya macho madogo manne ya mbwa, pamoja na meno meupe ya vinywa viwili, bila shaka alitambua idadi kamili ya mbwa hawa, walikuwa ni wawili.
Mapigo ya moyo wake yalimuenda kasi, alikiona kifo mbele yake, alijaribu kunyanyuka akashindwa,akajaribu tena akashindwa! maumivu yalimtapakaa mwili mzima. Akawakumbuka wazazi wake, watu muhimu katika maisha yake, “baba, mama! uko wabi baba?, uko wapi mama?, “Mwamvua alipiga kelele, chozi lilichuruzika usoni mwake, maumivu ya vidonda yakasikika usoni, chumvichumvi za machozi zikatonesha vidonda, akalia tena na tena kwa maumivu, akazidi kujiumiza na kuipandisha hasira yake!
“,Mama, mama! baba, baba! “,Mwamvua akaita tena,akipapasa huku na kule, mikono ikagusa damu iliyoganda, ikapapasa tena mbele, ikagusa kidonda kibichi kilichojaa damu nyingi. “,Yalaaa, “baba yake Mwamvua, mzee Yahimana Yahimana alipiga kelele, maumivu ya kutoneshwa kidonda yalirejesha fahamu yake, akalia kwa uchungu, alipojaribu kujigeuza upande wa pili, akamlalia mke wake,akamfanya na yeye apate fahamu na kuzinduka ghafla kwa mshituko!
“,Humu ni wapi? “,mama yake Mwamvua pamoja na Mpuzu aliuliza.
“,Hata mimi sijui,? “,baba yake Mpuzu, mzee Yahimana Yahimana aliongea, huku akijipapasa mwilini, damu zilimjaa, maumivu yalimuenea mwili mzima, akakumbuka ukatili waliofanyiwa na wazungu, masaa takribani sita yaliyopita.
“,Tumefungiwa katika magereza ya Waafrika, ili tuliwe na mbwa watakapo kata kamba, watule kutibu njaa zao”,,Mwamvua aliongea,roho ya ukatili ikamuingia, ujasiri ukamvaa, kisasi kikamzidi nguvu!,huku wazazi wake wakiangaza kila kona, baada ya kusikia kuhusu hatari ya kuliwa na mbwa.
“,Wuuu! wuuu! “,Mbwa wa kizungu, John na Jacksoni wakabweka tena, huku wakijitahidi kukata kamba, waliuma kamba kwa meno, wakajaribu tena na tena, nyuzi chache zilikua zimesalia kamba kukatika …
“,baba tutoke mahali hapa, muda wowote kuanzia sasa watakata kamba, tutakufa ……!”,Mwamvua aliongea, akiwashuhudia kwa mwanga hafifu sana, mbwa wakijitahidi kukata kamba bila mafanikio. Baba yake akatembea kwa kupapasa, akausogelea mlango, akajaribu kusukuma, mlango wa chuma haukutikisika hata kidogo, kufuri nene lilifungwa kwa nje, hakuna yoyote yule angelifungua zaidi ya ufunguo wake, msumeno au nyundo ya kuvunjia mawe.
“,Hapo hatuwezi kupita, njia pekee ile kule juu! “,Mwamvua aliongea huku akitazama na kunyosha kidole juu, waliliona dirisha dogo lenye nondo tatu, dirisha ambalo liliruhusu mwanga kuingia ndani ya chumba cha gereza bila kutoshereza.
“,wazo zuri mwanangu, lakini tunatokaje? ,tunapandaje kufika juu?,’mzee Yahimana aliongea, wote wakaanza kutafakari, mama yake Mpuzu pamoja na Mwamvua alikuna kichwa, mzee Yahimana akakuna kichwa, wote walitafakari namna ya kulifikia dirisha umbali wa mita kumi na tano kwenda juu.
…………………………………
Nusu saa iliyopita;
Mpuzu na Ishimwe walimaliza kuweka upupu kwenye maji, wakaanza kujadiri kwa ukimya, namna ya kulisogelea gereza la Waafrika wafungwa, kuwakomboa ndugu zao!
“,Sikia Ishimwe, kazi ndio tunaenda kuianza rasmi, kamba tuliyoshukia humu ndani tuiache hapo hapo tutaitumia kurudi, tukawakomboe wazazi wangu, kisha nikamchukue msichana niliyekwambia nampenda na isitoshe atatusaidia sana kudai uhuru! “,Mpuzu aliongea.
“,Kweli kaka nimekuelewa, sasa hivi tutumie upinde kuwashambulia,tukiua mmoja mmoja atakaye leta kimbelembele, “Ishimwe aliongea na kumsapoti Mpuzu.
Wote wakakubaliana, wakashikana mikono ishara ya umoja, wakagonga mikono, wakagonga tena miguu kama kawaida yao.
“,Tunaenda kwa kujibanza kwenye kuta kila baada ya hatua moja, tutapitia chini ya magari yale, tutajificha kwenye mataili, tutapandisha ngazi, tutatokea juu ya dali, mahali ambapo kuna dirisha dogo la kupitisha hewa, tutaanza kuchungulia dirisha moja baada ya jingine kwa umakini na utulivu, mpaka tukitambue chumba walichomo ndugu zangu! “,Mpuzu alitoa maelekezo kwa rafiki yake, ramani yote ya jengo aliifahamu kichwani, usingempoteza ndani ya ngome kubwa tangu afanye juhudi kuikalili asipate taabu wakati wa kumuwinda Angel Richald, mtoto wa gavana wa jimbo la Goshani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Sawa rafiki, nimekuelewa! “,Ishimwe akaongea, wakaanza kutembea kwa kujibanza, walichungulia huku na kule, walipomuona askari amesimama walisubili aangaze upande mwingine, alipogeukia upande mwingine na bunduki yake begani, walivuka haraka na kujibanza kwenye ukuta, sekunde kumi mbele, walikuwa usawa wa malori na magari ya kikoloni yakiwa yamepaki, wakalala chini na kuanza kupita chini ya magari, wakatembelea tumbo na kujiburuza, wakimuona askari wanajibana kwenye taili la gari, wasimolekwe na tochi,askari wa kikoloni alipohakikisha usalama na kuzima tochi, waliendelea na safari, wakafika usawa wa ngazi, wakapandisha ngazi kwa umakini, takribani dakika tano zilitosha, walifika juu ya dali, katika dirisha la chumba cha kwanza cha gereza. Wakachungulia chini, Mungu si Athumani,waliona macho sita yakiwa yanawakodolea kwa juu, Mpuzu alitabasamu, aliyafahamu vizuri macho ya ndugu zake, yalifanana kwa kila kitu …
…………………………………
10;20pm
Mzee Yahimana, Mwamvua, pamoja na mama yake Mpuzu, waliendelea kujadiriana namna ya kufika usawa wa dirisha, wavunje nondo kisha watoke nje. Lakini je watafikaje? hata wakifika, nondo watazivunjaje?, walijiuliza maswali bila majibu yoyote, wakabaki kulitazama dirisha kwa juu, huku mbwa wakibweka nyuma yao, ndimi za mbwa zikiwa nje, udenda ukindondoka kwa hamu ya nyama ya binadamu. …
Ghafla waliona sura mbili zikitokeza dirishani, “Mama,baba, dada, ni mimi Mpuzu, nimekuja na Ishimwe kuwakomboa! “,Mpuzu aliongea, akionekana kuwa na furaha, alisahau kama walikuwa hatarini.
Mzee Yahimana akatabasamu, Mwamvua akatabasamu, mama yake akatabasamu, wote walifurahi kumuona Mpuzu, kwani tayali hofu za kifo juu yake walianza kumohofia kwani siku nzima hakuepo nyumbani na alitafutwa kila kona na askari wa kikoloni bila mafanikio …
Ishimwe alichomoa panga lake gumu alilotumia kuchimbia viazi shambani, akalipenyeza katikati ya nondo, akatumia nguvu nyingi kuzikunja nondo zile, nondo zikazidiwa nguvu na panga la Ishimwe, zikanyongonyea na kujikunja.
Mpuzu akachukua kamba ndefu ya mkonge iliyokuwa begani mwake, akaifunga kwenye nondo zote mbili za dirisha, akairuhusu kushuka chini, ikateremka ndani ya chumba cha gereza, ikafika mikononi mwa mzee Yahimana, baba yake Mpuzu.
“,Aanze kutoka mwanangu Mwamvua,sisi tumekula chumvi nyingi, hata tukifa haina shida, mwanangu atakua salama ………”,Mzee Yahimana aliongea, akampatia kamba Mwamvua, Mwamvua akasita, alitaka wazazi wake watangulie kutoka kabla yake.
“,Chukua mwanangu, panda haraka, sisi hata tukifa lakini mnvi zimetujaa kichwani, wewe hata ungo haujavunja! “,mama yake Mpuzu aliongea, maneno yakamuingia vilivyo mtoto wao Mwamvua, akaipokea kamba kwa unyonge.
“,Fanyeni haraka tutoroke, kabla hawa wapumbavu hawajaamka.! “,Mpuzu alihimiza, huku akimtazama Mwamvua kwa chini, Mwamvua akaanza kupanda, mwili wake ulikuwa mwepesi, ulizoea mazoezi ya serekasi na kufanya kazi ngumu za shambani, dakika tano tu alikua juu, akajipenyeza kwenye dirisha, akatoka nje,Mpuzu akateremsha kamba tena, mama yake Mpuzu akaichukua, alikuwa mwanamke shupavu, licha ya umri wa miaka hamsini na tatu, alipanda na kujivuta kuelekea juu, dakika kumi zilitimia akafika juu, akatoka nje. “,Ewalaa! wewe ni shujaa! “,Mpuzu alimpomgeza mama yake, akateremsha kamba tena, mzee Yahimana akaichukua, akaikunja na kuanza kupanda juu, kwa dakika saba mzee Yahimana alifika juu, “Asante wanangu, mmetuokoa mikononi mwa mbwa wenye njaa kali “,,mzee Yahimana aliongea, akawakumbatia vijana wake kwa furaha.
…………………………………
dakika ishirini nyuma.
Angel aliamka kitandani, wazazi wake walifikiri tayali amelala, kumbe alizuga tu, kope zake zilikuwa bado zinapekua peku peku, macho yalikodoa kila muda kutazama kama wazazi wake wamelala. Hatimaye malengo yake yalitimia, saa nne kamili, mama na baba yake walienda kulala,akasubili dakika kumi mbele kimya kilitawala ndani ya nyumba yao, akavaa suruali,akavaa tisheti, akavaa raba zake nyeusi, akabana nywele zake ndefu na kibanio, akafungua kitasa cha chumba chake polepole,akatoka, akafika sebuleni akatembea polepole kama kinyonga, akafika mlango mkubwa, akafungua komeo taratibu, akatoka nje, akarudisha tena mlango, akabana kwa nje na komeo, akatokea geti la nyumba yao, geti la uwani, akamkuta askari wa zamu kulinda nyumbani kwao akiwa anakoroma, usingizi ulimlemea na kulala fofofo. Angel akamuibia funguo mikononi mwake, akafungua mlango wa geti taratibu, akatoka, akafunga kwa nje, akatokomea na funguo!
…………………………………
‘”Paaa!paaa!risasi zilipigwa juu ya dali,zikawakosa,wakaacha kukumbatiana,furaha ikatoweka,wakati wa kupigania roho zao ulifika ,”tushuke haraka,tushuke,tukimbie,!!”,Mpuzu aliongeaaa,akatangulia mbele akiwa na upinde mkononi,ndugu zake wakafuatia,Ishimwe akiwa nyuma kabisa kudumisha ulinzi.
Wakashuka ngazi,uso kwa uso na Angel,”My love,are you ok?,mimi kuja okoa hawa Afrika,kumbe ndugu yako!”,Angel aliongea baada ya kumtambua Mpuzu,angalau alianza kujaribu kuzungumza kiswahili.
“,Hawa ni wazazi na mdogo wangu,huyu ni rafiki yangu,tumekuja kuwaokoa wazazi wangu baada ya kukamatwa!” ,Mpuzu aliongea huku akitabasamu,alisahau kama tayali askari wa kikoloni walikua nyuma wanawafuata.
“,Papaaaa,paaa!paaa!”,wakashambuliwa tena.
“Tuondoke,twendeni,”Mpuzu aliongea.
“,Mimi enda na nyinyi,siwezi ishi na bad people,my people are killers”,Angel aliongea,Mpuzu akatabasamu,ndio muda sahihi alio usubili kwa hamu.Wazazi wake Mpuzu wakafurahi pia,walitambua msichana huyu angewasaidia kutoa siri nyingi za kuwasaidia kwenye ukombozi,wakaanza kutoroka naye,watoke nje ya ngome.
Askari wote waliokua wamelala waliamka,milio ya risasi iliwashitua usingizini,wakaanza kukimbia kuelekea sehemu sauti za risasi zilitokea.Mpuzu na kundi lake wakalala chini,wakajificha chini ya magari,askari walio washambulia walifika sehemu walipokuwa wamesimama awali,wakaanza kuwatafuta maadui wao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Come on guys,come on!Africans prisoners have escaped……”,(Njooni ,njooni,wafungwa wa Kiafrika wametoroka)Askari mmoja aliongea kwa sauti akiwaita wenzake,filimbi ya hatari ikapulizwa ,pilikapilika kuwasaka maadui wao waliotoroka ikaanza kwa nguvu ya hali ya juu,hasira zikiwa zimepamba nyuso zao.
Ngome kubwa; 11;20
Malikia Magreth alikuwa bado hajapitiwa na usingizi, kwa mbali alisikia hatua za miguu sebureni, akasikiliza kwa makini, akaendelea kusikiliza hatua za miguu, akasikia mlango unafunguliwa, kisha ukafungwa, kimya kikatawala, “baba Angel, my husband!, my husband! “,malikia Magreth aliita, alimgusa begani mume wake, mume wake Richald Robeni alikuwa amelala fofofo.
“,Paaaa! paaaaa! “,milio ya risasi ikasikika nje, gavana Richald Robeni akashtuka usingizini, “kuna nini?, risasi za nini usiku huu? “,Richald Robeni aliongea kwa mshangao, aliamka na kukutanisha macho na mke wake.
“,Hata mimi sifahamu, nimekuamsha muda mrefu hujanisikia, before! nilisikia sauti za viatu ndani kwetu, then after, risasi zikafuatia ……”,malikia Magreth aliongea, alikaa Goshani na mume wake muda mrefu, alikuwa na miaka takribani minne nchini Goshani, hivyo alikimudu kiswahili vizuri sana.
Richald Robeni akashtuka, maneno ya mke wake yalimchanganya sana, “Paaaa,paaaa,paaaa!”,risasi zikasikika tena,kelele na purukushani zikasikika nje ya nyumba yao,wakaamka harakaharaka,wakiwa na nguo za kulalia,Richald Robeni akachukua bastola yake chini ya kitanda,mke wake na yeye akachukua bastola yake kwenye mkoba wake,pembeni ya meza yake ya vipodozi,wakawasha taa,wakatoka ndani ya chumba chao kwa umakini.
“,What!where is our daughter?,where is Angel?(Mtoto wetu yuko wapi?Angel yuko wapi?),Richald Robeni aliongea kwa mshangao,kitanda kitupu kirimkaribisha baada ya kuingia ndani ya chumba cha mwanaye Angel kutazama usalama wake,”Hayupo?,atakua ametoka nje,nilisikia mtu akitoka nje?”,malikia Magreth alimjibu mume wake kwa lugha ya kiswahili,wakatoka ndani ya chumba cha Angel haraka sana,wakausogelea mlango mkubwa wa nyumba yao,”Shit!the door is closed!(shit!mlango umefungwa),”waliongea kwa mshangao,hofu ilijaa ndani ya mioyo yao,hawakujua Angel alielekea wapi.
“,Watch man!watch man!,mlinzi,mlinzi!”,malikia Magreth alianza kumuita mlinzi,aliita tena na tena bila kuchoka,hakuna aliyeitika na kujibu sauti yake,akakasirika,akakunja uso kwa hasira.
…………………………………
Dakika kumi nyuma;
Milio ya risasi ilisikika,mlinzi na askari wa zamu katika nyumba ya gavana Richald Robeni alishtuka,kelele za askari wakikimbia huku na kule zilipenya katika masikio yake,akanyanyuka,akachukua bunduki yake,akalisogelea geti lake,akafungua mlango,mlango ukagoma!,”Where is the keys?,funguo ziko wapi?”,aliongea kwa kingereza, akaongea tena kwa kiswahili,akatafakari, akakumbuka mahali apoziweka jana, akarudi kwenye kibanda chake, mahali alipokuwa ameketi, hakuona funguo, akapekua kila kona, hakuona funguo,akachoka!
Akajipapasa kwenye mifuko ya kaptula yake, hakuziona funguo, akatafakari, akakumbuka wakati analala zilikua mikononi mwake. “Who took the keys?, nani kachukua funguo? “,aliongea kwa kingereza, akamalizia kwa kiswahili kama kawaida yake.
“,Watchman! Watchman!, mlinzi,mlinzi……”,Kwa mbali alisikia anaitwa,akakaa kimya,akaitwa tena kwa kiswahili,akaitambua vizuri sauti ya malikia wake Magreth,akatimua mbio kuusogelea mlango wa nyumba ya gavana.
…………………………………
“,Ameenda wapi?,itakua labda ametoka nje baada ya kusikia risasi,?”,Richald Robeni alimwambia mke wake aliyekuwa amejawa na hasira,wote wakiwa wamesimama mlangoni.Taratibu walianza kusikia sauti za mtu akikimbia,alikimbia kuusogelea mlango,mahali walipokuwa wamesimama.
“,Malikia!nimeitikia wito,?”,mlinzi aliongea.
“,Tufungulie mlango,tumefungiwa kwa nje na hatuna funguo ,Angel hatujui ameenda wapi?”,malikia Magreth na gavana Richald Robeni waliongea kwa Kiswahili.
“,What!,nani amefunga milango?,hata geti kubwa limefungwa kwa nje,na funguo zimeibiwa?”,askari wa kikoloni aliongea,bila shaka alikuwa na muda mrefu nchini Goshani,aliongea kiswahili kwa ufasaha bila kutetereka.Alifungua mlango ukagoma,akafungua tena ukagoma!,akabaki akiwa amepigwa na butwaaa kwa mshangao.
…………………………………
11;40
Baba yake Mpuzu, mzee Yahimama Yahimana alishikilia upanga wa Ishimwe, Mpuzu pamoja na Ishimwe walikua na upinde mikononi, walitembelea tumbo chini ya magari, wakavuka magari mawili, matatu, matano mpaka wakafika mbali,kwenye tenki karibu na ukuta, eneo la mashambulizi ambalo walilipanga, Mpuzu na Ishimwe.
“,Hawa huku kwenye matenki! “,askari aliyekua kwenye banda, juu ya ukuta, alifanikiwa kuwaona Mpuzu na kundi lake, akaisogeza taa yake, ikawaangaza vema, alipigwa na butwaa, akashindwa kushambulia, alimuona Angel akiwa ameongozana na wafungwa wa Kiafrika.
“,Pyuuuu! “,mshale ulitua tumboni mwake, mshale uliyofyatuliwa na Mpuzu Yahimana.
“,Yalaaaa! Stupid, st…u…pi ……”,askari yule wa kuongoza taa alitoa ukelele wa maumivu, akadondoka chini,huku akitukana. “,Puuuuu! “,kishindo cha ardhi kilimpokea,alidondoka chini, akafa papo hapo.
“,Kimbieni, kapandeni kwenye kamba ukutani! “,Mpuzu na Ishimwe waliongea.
“,Paaaa! paaa! “,wakashambuliwa kwa risasi, rundo la askari lilikuwa mita chache, mita mia moja na eneo la tenki.
“,Pandeni, kamba hiyo hapo, sisi tunabaki kushambulia …”,Mpuzu na Ishimwe waliongea, Ishimwe aliwahi mpira wa maji akaukamatilia vizuri, Mpuzu alikuwa ameketi vizuri kwa ajili ya kushambulia.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Yahimana aliisogelea kamba, Mwamvua akaanza kupanda akafika juu, akashuka upande wa pili wa ukuta, akafuatia Angel Robeni, mtoto wa gavana wa kizungu, akaanza kupanda kuelekea juu ya ukuta.
“,Paaaa! paaaa! “,askari wa kikoloni walishambulia, hawakuwa na shabaha nzuri sababu ya giza, isitoshe walikuwa makini wasimdhuru Angel, mtoto wa gavana wao Richald Robeni.
“,Nendeni, wahini mkamzuie kabla hawajamtorosha, atafika juu ya ukuta ………!”,askari mmoja, mwenye mikanda mingi begani mpaka kiunoni aliongea, aliliamrisha jeshi lake la kikoloni, jeshi lake likaanza kukimbia kusogea eneo la tenki ,walikimbia kuwahi kabla Angel hajavuka ukuta wa ngome kubwa.
“,Stupid, what this!, yalaaaa! stupid Africans! yalaaa…a ………!”,askari wa kikoloni walitukana kwa kizungu, waliwashwa mwili mzima,baada ya kumwagiwa maji yenye upupu, walitupa silaha zao, wakaanza kujikuna, wakauawa kwa urahisi na mishale iliyopenya katika matumbo yao, kifo cha kizembe bila kujitetea.
“,Fungua maji mpaka mwisho, ongeza presha!,Mpuzu aliongea, huku akifyatuwa mishale na kuua wakoloni kama nzige…
“,Kill, kill, uwa wazungu, uwaa ……!”,kwa kingereza cha kukalili, kwani aliwasikia wazungu wakitamka mara nyingi, neno kill (uwa),Ishimwe aliongea kwa sura iliyojaa tabasamu, alikamatilia mpira na kuwamwagia maji askari wote wa kikolini waliowasogelea,maji yaliyochanganywa na upupu, wakajikuna, akawacheka, wakapigwa na mishale, wakauawa kirahisi.
Tayali Angel alikua juu ya ukuta akashuka upande wa pili, mama Mpuzu akapanda, dakika ishirini alikuwa tayali upande wa pili, akafuatia mzee Yahimana, dakika kumi, alikuwa ameshapotea ndani ya ngome ya kikoloni.
“Tayali wametoka, tukimbie! “,Ishimwe aliongea.
“,Tangulia, ukiwa unapanda nitakua na kulinda, ukifika juu ya ukuta, nitaanza kupanda huku wewe unanilinda nisipigwe na risasi kwa kuwashambulia na mishale ……”,Mpuzu aliongea, wakafanya hivyo, dakika tano zikapita, kumi, ishirini, wote walikuwa juu ya ukuta, wakashuka kwa pamoja kwa kutumia kamba,wakiwa na furaha kubwa ndani ya mioyo yao.
…………………………………
The great fort (Ngome kubwa); 00;40.
Vilio vilitawala ndani ya ngome kubwa, askari zaidi ya mia mbili walipoteza maisha,askari wengine walikua bize kubeba majeruhi kuwapeleka hospitali. Wote walihuzunika, roho za ukatili na visasi zikawajaa, isitoshe waliuawa na pia mtoto wa gavana kutoroshwa katika ngome yao, askari wa kikoloni walijidharau, walijiona wazembe, walifaa adhabu ya kifo. Wengine walijishika tama, wakisubili amri kutoka kwa gavana,kutoka nje, kuelekea makazi duni ya Waafrika kutoa adhabu,na pia kuwakamata wahusika …
Tabasamu la furaha liliipamba sura ya kila mmoja, Ishimwe alifurahi kutimiza lengo lake la kumsaidia rafiki yake, Mpuzu alifurahi kuwaokoa wazazi wake na kumtorosha msichana mrembo wa kizungu aliyempenda sana, Angel Richald, mtoto wa gavana Richald Robeni.
Penzi lina nguvu, Angel Richald aliisaliti familia yake, akaisaliti rangi yake, akaikimbia ngome kubwa ya kikoloni,ili awe karibu na mpenzi wake Mpuzu Yahimana.
“,Nifuateni!, nitawaelekeza mahali pa kujificha, “Mpuzu Yahimana aliongea, kundi lote likamfuata, licha la giza nene la majira ya saa saba usiku hawakuogopa, walisonga mbele.
“,Hatuendi nyumbani? “,Mwamvua aliongea, akionekana kushangaa njia ya ajabu kuelekea msituni ambayo walikuwa wakipelekwa.
“,Makazi yetu ya Kiafrika sio salama hata kidogo, muda wowote watayavamia kututafuta, Ishimwe peke yake ndiye atarudi katika makazi yetu muda huu, atatangaza hali ya hatari ili ndugu zetu wakajifiche, wenye nguvu,vijana wapigania Ukombozi watakao taka kutuunga mkono watatufuata porini ……”,Mpuzu aliongea.
“,I will help you to fight for your freedom, but we have to get enough weapons, I will teach you on how to use them………”,(Nitawasaidia kupigania uhuru wenu, lakini tunapaswa kupata silaha za kutosha, nitawafundisha jinsi ya kutumia …)”,Angel Richald alitambua malengo ya mpenzi wake Mpuzu pamoja na ndugu zake, alifahamu wasingeweza kulishinda jeshi la kikoloni kwa kutumia silaha za jadi, aliahidi kuwasaidia na kuwafundisha jinsi ya kuzitumia. Aliongea kwa hisia,kwa kutumia lugha ya kizungu, lugha ambayo wengi hawakuielewa,walielewa neno moja moja tu …
“,Speak Swahili, mimi understand you …”,baba yake Yahimana alimjibu Angel kwa kingereza kibovu, huku safari ya kuelekea mafichoni ikiwa imepamba moto. Hawakuelewa kile alichowaeleza, walitaka afafanue kwa kutumia kiswahili …
“,Yes, mimi not elewa you …,speak Swahili ……”,Mpuzu Yahimana alikazia, hata yeye alikuwa hajaelewa.
“,Amesema hivi, tunapaswa kupata silaha za kutosha, silaha za kizungu kama bunduki, atatufundisha namna ya kutumia! “,Mwamvua aliongea, alielezea vizuri sana maneno ya wifi yake mtarajiwa, Angel Richald. Uchu wa kutaka kuikomboa nchi siku moja, vilimfanya Mwamvua kukalili kizungu kila aliposikia kikitamkwa na mzungu, akiwa na miaka kumi na mbili tu, tayali misamiati ya kingereza ilijaa kichwani mwake, akatafsiri kila kona.
“,Exactly, sawa kabisa, wewe iko sahihi, vizuri sana! “,Angel alijaribu kuongea kiswahili, akamsifia Mwamvua, akamkumbatia, kitendo ambacho kiliwashangaza sana, tangu wazaliwe hawakuwahi kuona mzungu mwenye roho nzuri, asiye na roho ya kibaguzi kumgusa Muafrika, kumsalimia Muafrika kwa mikono ilikua ni kama kushika kinyesi kibichi cha binadamu, cha ajabu leo walimshuhudia Angel, mtoto wa kizungu akimkumbatia Mwamvua. Wote wakatabasamu, wakaahidi kumpenda na kumkumbuka popote pale.
“,Nitahakikisha nakulinda popote pale, una roho nzuri na unatupenda Waafrika sio kama ndugu zako “,Mpuzu Yahimana aliongea
“,Nawapenda sana, i will make sure mnapata uhuru,I love you Mpuzu,nitabaki Afrika milele …”,Angel aliongea kwa hisia huku akilitaja jina la Mpuzu, muda wote wazazi wa Mpuzu walikua kimya,wakiendelea kuchapa miguu kuelekea mafichoni, miguuni walitembea peku peku, isipokuwa Angel aliyekuwa amevaa viatu, laba nyepesi zilizomuwezesha kutembea kwa haraka.
“,Endeleeni na safari, nitawakuta huko, ngoja nikatoe taarifa kwa ndugu zetu! “,Ishimwe aliongea,wakiwa wamesimama njia panda, barabara iliyotenganisha njia iliyoelekea katika misitu ya Mikoko, huku njia nyingine ikielekea makazi duni ya Waafrika.
“,Fanya haraka, waambie wakati wa ukombozi umefika, watuunge mkono! “,mama yake Mpuzu aliongea, akamshika kichwani Ishimwe kumpatia baraka, rafiki kipenzi wa mwanae Mpuzu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Usjali mama, nitarudi salama, nikiwa na jeshi kubwa la vijana ,wakubwa kwa wazee waliochoshwa na ubaguzi, manyanyaso na ukatili ……”,Ishimwe aliongea, akautwaa upanga wake kutoka kwa mzee Yahimana,akawakumbatia, kisha akatoweka …
“,Utatukuta kwenye maficho,katikati ya msitu,Mpuzu aliongea,huku rafiki yake akiwa mita kadhaa,akikimbia kuelekea makazi duni ya Waafrika.
…………………………………
Ngome kubwa;2;40pm
Ilikua saa nane usiku,ngome ya wakoloni ilijawa na simanzi,vifo vya ghafla viliwachanganya,hakuna aliyekuwa na hamu ya kulala tena,askari takribani kumi walikuwa bize kusafisha tanki maji,tanki lililowekewa upupu na kuwadhibiti kwa urahisi,askari wengine walikua bize kusikiliza hotuba ya gavana Richald Robeni,pamoja na viongozi wengine wakubwa wenye vyeo vya juu,katika ngome ya kikoloni maarufu kama the great fort.
“,We have to fight, we have to bring back our respect, Europeans are Gods, ………”,(tunapaswa kupambana, tunapaswa kurudisha tena heshima yetu, Waingereza ni Miungu ……),gavana Richald Robeni aliongea, baada ya mirango ya nyumba yake kuvunjwa, akatolewa yeye pamoja na mke wake malikia Magreth, wakiwa hawa amini kilichotokea.
Mtoto wao Angel aliikimbia ngome yao, akaasi, akajiunga na Waafrika, maadui wakubwa wa wazungu.
“,Be strong, ensure that my daughter hates Africans, prove to my daughter that, Africans are bad people ………”,(Kuweni imara, hakikisheni mtoto wangu anawachukia Waafrika, muhakikishieni mwanangu kwamba Waafrika ni watu wabaya ……),Richald Robeni aliendelea kuongea,machozi ya hasira yakamdondoka,akajikaza kisabuni, akatangaza uamuzi wa mwisho!
“,Tomorrow morning go and bring all Africans into our prisons, make sure you demolish all slums ……”,Kesho asubuhi nendeni mlete Waafrika wote katika magereza yetu, hakikisheni mnateketeza makazi yao …)”,gavana Richald Robeni aliongea,akashangiliwa, akatoweka zake yeye pamoja na mke wake, wakarejea ndani.
Mikiki ikaanza, askari wa kikoloni walianza kutayalisha silaha zao,magari yakaandaliwa,walijiandaa kwenda kulipiza kisasi, lazima wakawaue Waafrika jua litakapochomoza.
…………………………………
Slum areas (Makazi duni)
Ukimya ulikuwa umetawala,alifunga breki za miguu yake, alihema na kuvuta pumzi kwa kasi sana,akagonga katika kibanda chao. “,Mama, mama”,Ishimwe aliita, akagonga tena.
“,ngo, ngo, ngo,mama, mama “,Ishimwe aligonga mlango wa bati wa kibanda chao, akamuita mama yake.
Akasikia mama yake akiamka, akaacha kugonga, mlango ukanyenyuliwa, ukasogezwa pembeni. “,Pomweee, (habari)”mama yake Ishimwe aliongea, alitabasamu, alifurahi sana kumuona mwanae akiwa mzima, akamsalimia.
“,Pomweee mayo …(salama mama) “,Ishimwe alijibu, akamshika miguu mama yake kama ishara ya heshima, akanyanyuka tena,akampatia taarifa mama yake.
“,Tumefanikiwa kuwakomboa ndugu zake Mpuzu, wameelekea mafichoni, msitu wa mikoko, muda wa ukombozi umefika, tunapaswa kupiga kelele za hatari muda wowote makazi yetu yanavamiwa na askari, tutauawa, kwasababu kule tumeua askari wengi …”,Ishimwe aliongea, mama yake akamuelewa, hakua na muda wa kupoteza.
“,Pomwee wana Goshani, Waafrika waliochoshwa na uonevu wa watu weupe, muda wowote tunavamiwa na askari wa kikoloni, amkeni tujiandae kupigania uhuru wetu! “,mama yake Ishimwe, akishirikiana na mwanae, alipiga kelele za hatari, kutokana na ukimya uliokuwa umetawala,kelele za hatari zilisikika mpaka kilomita tano, zikawafikiwa Waafrika wengi zaidi.
“,Ukisikia taarifa hii, mjulishe na mwenzako,asogee uwanja wa mikutano ……”,Ishimwe na mama yake waliongea,wakitembea kuusogelea uwanja wa mikutano, majira ya saa tisa usiku.
…………………………………
Makazi duni; uwanja wa mikutano
Waafrika walipeana taarifa, wakafurika katika uwanja wa mikutano, sura zao zilificha huzuni na manyanyaso, walichoka kuteswa, kuonewa, kufanyishwa kazi kwa nguvu, huku wakilipwa senti moja tu ambayo haikutosha hata kulipia kodi ya kichwa.
“,Tumefanikiwa kuwakomboa ndugu zake Mpuzu baada ya kukamatwa mahali hapa leo asubuhi, lakini wamejeruhiwa katika miili yao, kwa sasa wako mafichoni msitu wa mikoko, taarifa nzuri ni kwamba mtoto wa gavana amejiunga nasi, tumetoroka naye kwenye ngome kubwa, yuko tayari kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa askari wetu, walio tayali kujiunga na jeshi letu la ukombozi tuelekee msituni, wengine mkajifiche, wazungu watafika hapa muda wowote, watawakamata na kuwaua, kwani hata sisi tumeua wazungu wengi ……”,Ishimwe aliongea, mbele ya zaidi ya Waafrika elfu tano, wakubwa kwa wadogo.
“,Wote tunaelekea msituni, lazima tukapambane! “,mtoto mdogo wa kiume aliongea, alikuwa na miaka tisa tu, sura yake ilijaa chuki dhidi ya wazungu.
“,Hapa tuache mitego, wakifika wafe wenyewe, sisi tutakua tuko porini tumejificha “,mzee mmoja aliyekula chumvi nyingi aliongea, umri wake yapata miaka sabini.
“,Ndio, tutege wafe,!”,Waafrika walipiga kelele ,wakaitikia kwa fujo.
“,Kweli, tutege wafe wenyewe,tumechoka kunyanyaswa…”,wengine waliitikia.
Slum area(makazi duni)
Mkutano ulifikia tamati,Waafrika wakajigawa makundi, kila kundi likapewa majukumu yake, walichoka na utumwa, utumwa katika ardhi yao wenyewe.
“,Wazee na watoto, mtaongozwa na baadhi ya vijana kuelekea msituni, chukueni vifaa vya kujikinga na baridi pamoja na mvua, vijana wenye nguvu watabaki na mimi kutega mitego kisha tutatoweka mahali hapa kabla jua halijachomoza …”,Ishimwe, kijana shujaa aliongea, licha ya umri wake mdogo, aliheshimika kutokana na uhodari wake katika harakati za kupigania uhuru wa nchi ya Goshani.
“,Vijana kumi wenye nguvu sogeeni kwangu! “,Ishimwe aliongea, dakika tatu mbele, vijana kumi wakiwa kifua wazi,siku zote hawakuvaa nguo zaidi ya kuzuia sehemu za siri na magome ya miti, huku wanawake na wenyewe wakijistili sehemu za maziwa yao pamoja na sehemu zao siri kwa kutumia magome ya miti.
“,Nendeni mchukue mishale, upinde na vifaa vyote vya ulinzi, tangulieni na wazee pamoja na watoto, mkifika msitu wa mikoko, muiteni Mpuzu kwa kutumia filimbi ya Kiafrika “,Ishimwe alitoa maelekezo, wakaanza kuondoka kwenda kuchukua silaha, nyuma yao kundi kubwa la wazee na watoto likiwafuata, huku wamama wenye watoto wakiondoka pamoja na watoto wao, walisalia vijana pamoja na wababa wenye nguvu tele miilini mwao.
“,Tulio salia wote tuna nguvu, tunapaswa kufanya kazi kwa nusu saa tuu”,Ishimwe aliongea.
“,Tuweke mitego ndani ya nyumba, wakifika katika makazi yetu, wakituita tukaacha kutoka, wataingia ndani, huko ndiko watakutana vifo vyao ……”,baba mmoja wa Kiafrika, umri wa takribani miaka therathini na tano aliongea
“,Wazo zuri, lakini tunapaswa kuweka mtego ambao utawajeruhi hata wazungu waliobaki nje, sio watakao ingia ndani tu …”,kijana mmoja umri sawa na Ishimwe aliongea.
“,Ndio, tuweke pombe za kienyeji,pombe zetu zikiguswa na risasi zitaripuka …”,Kijana mwingine aliongea.
“,Rahisi sana, wanapenda kututoa nje kwa risasi, tuweke pombe zetu, ndani ya mabanda yetu,tutawanasa tu, twendeni niwaonyeshe …”,mzee Nyamigo, mzee aliyekula chumvi nyingi aliongea, wengine wakamfuata, aliwaongoza kwenda kutega mitego.
………………………………
Masaa mawili nyuma;
Mpuzu Yahimana alifika msitu wa mikoko, akiwa ameongozana na ndugu zake pamoja na Angel Richald. Aliona mahali sahihi pa kujificha ni katikati ya msitu, katika mti wa ubuyu ulioko pembeni mwa njia ndogo msituni, mti ambao Mpuzu alijificha awali, na kupelekea wazazi wake kukamatwa.
“,Tumefika, pandeni hapa! “,Mpuzu aliongea, akateremsha kamba aliyoitumia kupanda awali, kamba aliyokuwa ameikunja isionekane na mtu yoyote yule..
“,Mwanangu unajua kuchagua, huu mti tunaweza kutengeneza vitanda kabisa, “mama yake Mpuzu aliongea, akiushangaa mti wa ubuyu uliokuwa na matawi mengi juu, kiasi kwamba ni vigumu kutambua kama kuna watu walijificha ndani ya matawi yake.
“,Very creative boy, nakupenda “,Angel Richald alitabasamu, aliyaelewa vizuri maneno ambayo Mpuzu aliambiwa na mama yake. Wakakumbatiana, huku wakimtazama Mwamvua akipanda kuelekea juu ya mti.
“,Acheni maongezi,tupande tupumzike,inawezekana tusipate muda wa kupumzika tena!”,baba yake Mpuzu,mzee Yahimana Yahimana aliongea,huku akiyafikicha macho yake,bila shaka usingizi ulimzidi nguvu.
Dakika kumi baadae, wote walikuwa juu ya mti,mwamvua alikuwa pamoja na wazazi wake kwenye tawi moja, huku Mpuzu akiwa na Angel, wakiwa wamejipumzisha na kuegemea matawi ya mti, kamba waliyotumia kupandia ilifungwa na kukunjwa vizuri,hakuna adui yoyote angetambua uwepo wa watu mahali pale …
Angel alikishangaa kifua cha Mpuzu,aliwahurumia sana kukaa vifua wazi,aliahidi kufanya kila njia,apate nguo za kutosha,awapatie ndugu zake wapya wa Kiafrika,aliwahurumia kwa baridi kali,hakutambua kuwa walikuwa tayali wameshazoea hali hiyo,alijilaza kwenye kifua cha Mpuzu,usingizi ukampitia,wote walikuwa wamechoka na purukushani,kutoroka ngome ya kikoloni bila kupumzika…
…………………………………
Pombe ilikua ni jambo la kawaida kwa raia wa Goshani,walikunywa pombe yao aina ya Kenzoi baada ya majukumu mazito,walitumia kuliwaza akili zao na kuondoa uchovu,pombe yao ilipelekea waishi miaka mingi,kwani ilikuwa na viturubisho muhimu katika mwili wa binadamu,sifa kuu ya pombe hii inaweza kusababisha ajari,inaripuka pale tu inapoguswa na moto,baadhi ya askari wa kikoloni hufa,kwani hutumia bunduki zao kushambulia mitungi ya pombe hii ili kuwahimiza watu wakafanye kazi zao,waachee kulewa muda wa kazi, na pia kuteketeza viwanda vidogo vya Waafrika, na kujikuta wakipata majeraha baada ya pombe hii kuripuka.
“,Kila nyumba wekeni mtungi mmoja sebureni,hatua chache kutoka mlangoni,juu ya mlango wekeni upinde na mshale,huku kamba moja ikitegwa mlangoni,atakaye ingia na kugusa kamba,atafyatua mshale utampiga,wengine wakiona mwenzao kashambuliwa na mshale,watashambulia kibanda,mtungi wenye Kenzoi utaripuka kibanda kikipigwa na risasi,bila shaka askari karibu na jengo wote watakufa ……”,mzee Nyamigo aliongea, vijana na wazee wengine wakampigia makofi, waliunga mkono mawazo yake, wakaanza na kibanda cha kina Ishimwe, mzee Nyamigo akakifungua, akachukua upinde na mshale, akauvuta vizuri mpaka mwisho, kisha akaufunga vizuri na kamba ndefu kidogo,mtungi wa pombe ya Kenzoi ukawekwa ndani, upinde na mshale ukawekwa vizuri juu ya mlango, ukafichwa na nyasi za nyumba usionekane kwa urahisi, wakaipitisha kamba vizuri mlangoni, haikua rahisi kuitambua kama iliwekwa kama mtego, kisha wakanyenyua mlango wa bati, wakafunga vizuri kibanda.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakakisogelea kibanda cha kina Mpuzu, vijana wengine wakasogelea nyumba zingine, wawili wawili kila nyumba,wakafanya kama walivyoelekezwa, waliweka mtungi uliojaa pombe ya Kenzoi sebureni, wakachukua upinde na mishale, wakauvuta vizuri kiasi cha kumuua mtu kama ukifyatuliwa, wakafunga kamba vizuri, wakapitisha mpaka mlangoni, yoyote akigusa kamba tu, angejeruhiwa vibaya mno na mshale, wakafunga milango. Saa moja lilikamilika, saa kumi na mbili ilifika, wakakamilisha kazi, wakachukua silaha zao, wakatoweka haraka eneo la makazi duni, wakaelekea msitu wa mikoko, walikoelekea Waafrika wenzao kwenda kujificha …
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment