Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MIMI NI MUAFRIKA (I'M AFRICAN) - 1






IMEANDIKWA NA : HAKIKA JONATHAN



*********************************************************************************



Simulizi : Mimi Ni Muafrika (I'm African)

Sehemu Ya Kwanza (1)



Mpuzu Yahimana,kijana wa Kiafrika, alipanda ukuta mkubwa uliojengwa kwa mawe, huku akiwa makini asionekane na askari wa kizungu walioizunguka ngome yote ya kikoloni kudumisha ulinzi.Moyo wake ulikosa furaha, macho yake yalitamani kuona sura ya mtoto mrembo wa kizungu kwa mara nyingine tena tangu siku iliyopita. Uvumilivu ulimzidi nguvu, hisia za mapenzi zikamuandama, licha ya ngozi nyeusi aliyokuwa nayo, aliapa kumpata mtoto wa gavana Richald Roben kwa gharama yoyote ile …



“Sijui anajua kiswahili?lakini nitamfundisha, ngoja nichungulie, labda nitamuona tena angalau moyo wangu upate faraja …”!Mpuzu Yahimana aliongea, mikono yake miwili ilikamatilia kwa nguvu mawe ya ukuta imara wa ngome ya kikoloni, moyo wake haukua na hofu juu ya kifo na kunyongwa kikatili iwapo akikamatwa, moyo wake ulimuwaza Angel Richald, mtoto wa kipekee wa gavana wa Kiingereza katika nchi ya Goshani. Mpuzu aliendelea kukwea ukuta, huku kila mara akiangaza mashariki, kutazama kama jua linachomoza, lakini aliambulia wingu la ukungu lililosababishwa na baridi kali majira ya asubuhi.



“Jua lisipochomoza!mtoto wa gavana hatatoka kuota jua sababu ya baridi, lakini inabidi niendelee kupanda juu, muda sahihi ni huu, walinzi wanaamini hakuna Muafrika anayejiamini na kuvuka ukuta huu mkubwa, tena majira haya,bila kujua yupo Muafrika hodari Mpuzu Yahimana, mjukuu wa Yahimana kiongozi mkuu wa Manamba katika koloni hili la Waingereza miaka ishirini iliyopita “,Mpuzu aliongea, kichwa na mwili wake ukitoa mvuke, kutokana na baridi kali ya asubuhi.

Mpuzu alikua tayali kuteseka,kuumia na kufa,sababu ya penzi



.Hatimaye safari ilifika Ukingoni, majumba ya Kizungu yalianza kuonekana,Mpuzu akiwa umbali wa futi hamsini kutoka chini.Tabasamu likaipamba sura yake kufika mwisho wa ukuta, jua nalo lilichomoza ,katika wakati sahihi ambao Mpuzu aliutarajia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ewala! jana alikuwa amekaaa pale kwenye zulia, bila shaka hata leo atakaa pale kuota jua, eee mizimu ya mababu nisaidieni nitimize lengo langu, nitoke salama mahala hapa ………”,Mpuzu aliongea huku akiomba ulinzi wa mizimu ya mababu imlinde, kwani ilikuwa ni kosa la jinai kwa Muafrika yoyote yule kukanyaga ngome ya kikoloni, makazi ya wazungu, waarabu pamoja na wahindi.



…………………………………

The great Fort (Ngome kubwa);

Siku tatu zimepita tangu akanyage Afrika,awali alifikili ni bala tajiri kama Ulaya, kinyume na matarajio yake, Afrika ilijaa mashamba makubwa ya mikonge, mashamba yaliyomilikiwa na wazungu, huku Waafrika wakifanyishwa kazi kwa nguvu na kulipwa senti moja tu kwa masaa kumi na mbili shambani.



Hamu ya kutaka kujua koloni walilotawala wazazi wake ilimwishia, akiwa na siku moja tu, alitaka kuondoka Goshani na kurudi Uingereza.



“Subili mwanangu, wait two weeks to come, i will take you back to British (subili wiki mbili zijazo, nitakurudisha Uingereza) “,ni maneno ambayo Angel aliambiwa, kila alipozungumzia swala la yeye kurudi Uingereza mbele ya baba yake.



Ghafla wazo la yeye kurudi Uingereza likatoweka, fikra mpya zikatawala kichwa chake, moyo wa Angel ukazama katika penzi la kijana wa Kiafrika, kijana Mpuzu Yahimana aliyeingia ngome ya Kikoloni siku iliyopita akiwa na manamba wenzake, wakiwa wameleta mazao ya katani kwenye ghala la kuhifadhia mazao, kabla ya kusafirishwa kwa meli kupelekwa Uingereza.



Usiku hakula chakula, hakuna mtu angemshirikisha tatizo lake akamsaidia, tofauti na kawaida yake, alilala mapema kupumzisha kichwa chake,kichwa kilichojaa mawazo mengi, kwani aliwaza na kuwazua namna ya kuwa karibu na kijana yule wa kiafrika, na mahali pa kumpata bila majibu yoyote yale. Kutokana na badiliko la ghafla, gavana Richald Robeni alifikili mwanae anaumwa kumbe sivyo.



Asubuhi na mapema, jua lilichomoza, Kama kawaida yake, Angel alitoka nje ili aweze kuota jua. Alitoka nje, huku kichwa chake kikitafakali namna ya kumdanganya baba yake, ampatie ruhusa ya kutembelea makazi ya Waafrika, suala ambalo lilikuwa ni gumu mithili ya chatu kummeza tembo.



“,Fliiiiii ,fliiiii ………”,mlio kama filimbi ulisikika, Angel akiwa ameketi kwenye Zulia akiota jua alitazama huku na kule, hakuona chochote kile …



“,What is this? Oooh nothing!”,(Hii ni nini?, ooh hakuna kitu), Angel alizungumza peke yake baada ya kusikia mlio wa filimbi, alipogeuka huku na kule hakuona kitu chochote, akaendelea kuota jua.



“Fliiiii, Fliiiii ……”,filimbi ilisikika tena, Angel akageuka kwa mara nyingine, hakuamini alichokiona, kijana wa kiafrika aliyemkosesha usingizi alikuwa juu ya ukuta akimchungulia, uvumilivu wa mapenzi ukamshinda, hofu ya Mpuzu kudondoka chini ikamuandama Angel, bila kutambua kuwa Mpuzu alikuwa kijana hodari zaidi ya anavyofikilia.



“,Come down please, your not safe over there, you can die ……”,(Njoo chini tafadhali, hauko salama mahala hapo, unaweza kufa), “Kwa lugha ya kizungu Angel alizungumza, lakini Mpuzu hakuelewa chochote kile, jambo ambalo lilipelekea askari wa kizungu kushtuka, kwani Angel alionekana akiongeea na mtu fulani juu ya ukuta na kuhatarisha usalama wake……



“,Paaaaa! paaaa! paaa………”,risasi zilifyatuliwa juu ya ukuta alipokuwa Mpuzu,Mpuzu alimrushia cheni Angel, cheni ambayo Angel aliipokea kwa ustadi mkubwa bila askari yoyote yule wa kikoloni kugundua, huku akiitazama na kuishangaa zawadi ile.



“Paaap! paaaa! ……”,askari wa kikoloni waliendelea kumshambulia Mpuzu bila kumtambua vizuri sura yake ,kwani alikua mbali kabisa juu ya ukuta.



“,Aaaaaaa! “,Mpuzu alitoa ukelele, akalalamika kwa uchungu.



“,Puuuuuh! “,kishindo kilisikika upande wa pili, Mpuzu alidondoka chini ,baada ya kuachia mikono yake miwili, wakati wa kukwepa risasi kuikomboa nafsi yake.



“,Zungukeni, zungukeni upande wa pili,! aletwe hapa, stupid boy! “,askari mmoja wa kikoloni, aliwaamrisha na kuwatawanya wenzake kutoka nje ya ngome kubwa(the great fort), kwenda kumkamata Mpuzu Yahimana.



“,I hate you, I hate you! if you kill him, i will also kill you ………”,(nawachukia, nawachukia!, kama mtamuua na mimi nitawaua ),Angel alifoka kwa hasira na kukimbilia ndani, hakuna aliyejali kelele zake, askari wa kikoloni walipishana kukamata silaha kwenda kumtafuta Muafrika aliyekanyaga ngome yao maarufu kama ngome kubwa (the great fort) na kuichafua.



Mpuzu Yahimana alinyanyuka kwa shida huku akiugulia maumivu, hakuwa tayali kukamatwa na askari wa kikoloni, njia pekee ya kuepuka kifo ni kukimbilia msituni. Safari ya kutokomea mafichoni ilianza haraka haraka ,kabla hawajamkalibia.



…………………………………

Makazi duni; (Slums area)

Magari ya kikoloni yaliingia kwa fujo katika makazi ya Waafrika, askari wa kikoloni walibeba silaha pamoja na mijeledi mikononi, huku sura zao zikikunjamana kwa hasira.



“Mtu yote itoke kwenye slum! sisi tafuta pumbavu moja kuja ingia kwa ngome yetu this morning! “,askari mmoja wa kikoloni alizungumza, akiwa amevalia shati jeupe, pamoja na kaptula, mguuni alivalia viatu vyeusi vilivyong’arishwa na rangi nyeusi,kiunoni alivaa mkanda, mkanda uliounganishwa mpaka mabegani, sare kamili ya jeshi la kikoloni!



“Every family should get out of their slums!, if any member of your family is missing, you will be in trouble all of you ……”,(Kila familia inapaswa kutoka nje ya kibanda chao,kama mtu yoyote katika familia anakosekana,nyote mtakua kwenye matatizo), “askari mwingine alifoka kwa kizungu,huku akitumia mjeledi wake kutoa Waafrika katika vibanda vyao vilivyoezekwa kwa nyasi.



Familia zilipanga mistari,kisha wakubwa kwa wadogo wakachapwa viboko, baada ya mtu mmoja kukosekana. Huku wakihimizwa kutaja mtu aliyekosekana, kwani hakuna manamba wowote waliokuwa tayali wameelekea katika mashamba ya wakoloni.



Kisu cha moto kikachemshwa, wazee wote walitakiwa kukatwa vidole, huku dawa ikiwa ni kumtaja mtu aliyekosekana …



“Mpuzu Yahimana, mwanangu hayupo! msiwahukumu wasio na hatia! “,baba yake Mpuzu alizungumza na kupiga magoti mbele ya askari, pamoja na viongozi wa kikoloni, bila kutegemea, askari walimkamata yeye pamoja na familia yake,walifungwa kamba, kisha wakapakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa gerezani …



The great Fort (Ngome kubwa); 9.45am

Angel machozi yalimtoka, mikononi alishika cheni aliyopatiwa kama zawadi na Mpuzu, cheni ya kiathili iliyotengenezwa kwa kutumia katani, aliitazama kwa uchungu,machozi yakitiririka kwa fujo katika paji lake la uso, aliuona upendo wa kweli kutoka kwa Mpuzu,bila kujali rangi yake, aliapa kumpenda mpaka kifo.



“,They will kill him!, I have to see him by any means …”,(Watamuua, ninapaswa kumuona kwa njia yoyote ile) “,Angel aliongea kwa sauti nzuri iliyojaa hisia kali za mapenzi. Huku akitafakali namna ya kutoroka katika ngome ya kikoloni, ngome iliyo ongozwa na baba yake, gavana wa Kiingereza Richald Robeni.



…………………………………

Saa moja nyuma; Msitu wa mikoko;

Mpuzu Yahimana alijikokota kwa shida,akiburuta mguu wake kuelekea kwenye maficho ya muda, akisubili jua lizame, arudi katika makazi ya Waafrika.



“Mikoko forest “,Kibao kilisomeka, bila kujali hila za wanyama wakali wa msitu huo, aliingia msituni, akaangaza huku na kule, akaona mti mkubwa wa ubuyu, mti uliojaa matawi mengi yaliyofaa kwa maficho. “,Mti huu utanifaa kujificha mpaka machweo, “Mpuzu alizungumza, alitoa kamba ya mkonge ambayo hakuiacha mahala popote pale, akaishika vizuri kwenye mkono wake, akazungusha mkono wake kisha akarusha kamba juu ya mti, akajalibu kuivuta. “,Kama imekaza, bila shaka imenasa vilivyo, “Mpuzu Yahimana aliongea.



Akakwea mti kama nyani, huku akijivuta kwa kutumia kamba, sekunde tano baadaye, alikua tayali juu ya mti, akaivuta kamba, akaikunja ili askari yoyote wa kikoloni au mnyama hatari asiweze kumgundua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“,Jua likizama nitarejea nyumbani, bila shaka natafutwa kwa sasa, sina budi kujificha! “,Mpuzu aliongea, hakujua chochote kile kuhusu kukamatwa kwa wazazi wake, alikaa vizuri juu ya mti huku akiunyosha vizuri mguu wake ulioteguka.



…………………………………

The great fort (Ngome kubwa); 10;10am

Gari dogo aina ya the Roll royce, gari aliyopanda gavana Richald Robeni, iliongoza msafara wa magari kumi aina ya Range rover yaliyojaa askari pamoja na viongozi wachache wa kikoloni. Huku gari moja kati ya kumi,Yahimana Yahimana baba yake Mpuzu,mama yake Mpuzu, pamoja na Mwamvua dada yake Mpuzu walikuwa ndani yake.



“,Baba ,kaka yuko wapi? au wamemuua “,Mwamvua,mtoto wa kike, mdogo wake wa kipekee wa Mpuzu aliongea.



“,Sijui chochote kile, sijui yuko wapi, lakini sina shaka yoyote atakua salama, namwamini! “,Yahimana Yahimana, baba yake Mpuzu, alimjibu mwanae Mwamvua.



“,Usjali mwanangu, kaka yako yuko salama,kua mshirikiane kuleta uhuru wa Goshani, siunaona mateso haya? “,mama yake Mpuzu aliongea, huku akitazama nje kupitia nyavu za madirisha ndani ya gari la wafungwa ,wakiwa wamepakiwa kuelekea katika makazi ya wakoloni.



“,Ndiyo mama, naona mateso haya, tangu baba anisimulie kuhusu biashara ya watumwa, jinsi babu alivyouzwa sokoni kama nguo kutoka mkoa wa Kigoma nchi ya Tanganyika, mpaka kufika nchi hii, sijawahi wapenda wakoloni, nawachukia sana! “,Mwamvua alizungumza kwa hisia kali zilizojaa chuki dhidi ya wazungu.



“,Stupid Africans! you are making noise ,”(Waafrika wajinga, mnapiga kelele) “,sauti ya ukali ilisikika, askari wa kizungu walioendesha gari walifoka upande wa pili.



“,You are very stupid t……”,(nyie ni wajinga pi …)”,Mwamvua alizungumza kwa kingereza cha kukalili, kabla hajamalizia, baba yake alimziba mdomo, asizue balaa zaidi.



…………………………………

11;00am

Geti lilifunguliwa,ngome ikawa wazi kuruhusu msafara kuingia, magari kumi na moja yakaingia katika ngome kubwa ya kikoloni maarufu kwa jila la “The great fort “.



“,Shusha hiyo jinga Africans, peleka chumba ya mateso, mpaka mtoto yao ipatikane! “,gavana Richald Robeni alizungumza,kundi kubwa la askari likawakamata wazazi wa Mpuzu Yahimana, likawapeleka katika chumba cha mateso, kuchapwa fimbo sabini na mbili kila mmoja.



“,Tumefanya nin?i, hatujui kosa letu! “,mama yake Mpuzu alilalamika.



“,Twambieni kosa letu, hatujui chochote! “,baba yake Mpuzu na yeye akalalamika.



“,Shut up! nyamanza! ,toto yenu imekosekana, bila shaka ndiyo jinga African iliyokuja the great fort asubuhi kinyume na sheria”,askari aliyevalia bukta nyeupe, pamoja na mkanda kiunoni, mkononi akishikilia mijeledi alifoka,bila shaka alikuwa na cheo kidogo sana.



“,Usimfokee mama yangu, nitakuua! “,Mwamvua, binti wa miaka kumi na nne alimfokea askari wa kikoloni, huku akimvuta sare yake kumzuia asimburuze mama yake.



“,Puuuuuu! “,mlio wa kitako cha bunduki ulisikika, alimanusura umpate Mwamvua, aliinama akakwepa, ukampata askari mwingine wa kikoloni aliyekuwa amemshika Mwamvua. Askari wa kikoloni akagalagala, damu zikimtoka mapuani, wenzake wakambeba na kumpeleka katika hospitali ya kikoloni.



“,We are going to kill you(tunaenda kuwaua), nyie jinga Africans hamuwezi ua mwenzetu !”,askari aliyempiga Mwamvua kitako cha bunduki akakwepa, alizungumza kwa hasira, akamwacha mama yake Mpuzu, akatembea kumfuata Mwamvua ili amtie adabu.



Alimpiga na kitako cha bunduki, Mwamvua akainama, akakwepa tena kama awali, akatoa pigo moja la teke, akampiga askari yule sehemu za uzazi, “stupid! fuck you! fuck you “,askari yule akiwa na maumivu, alifoka kwa hasira na uchungu, huku akitukana kwa kizungu.



Mamia ya askari walioshuhudia mkasa ule hasira zikawajaa, nyuso zao zikakunjamana, hawakuwa tayali kuaibishwa na ngozi nyeusi, wakiwa na mijeledi, wengine bunduki za SAR, waliwavamia baba na mama yake Yahimana na kupunguza hasira zao kwa kuwachapa mijeledi kila kona ya miili yao, huku Mwamvua akipigwa kipigo kikali zaidi bila kujali umri wake.



“,Peleka mizoga kwa gerezani, peleka ikafie huko iliwe na mbwa “,gavana Richald Robeni alisikia kelele, alirudi akashuhudia mkasa mzima, hakuwa tayali kushuhudia ngozi nyeupe ikidharilishwa, akatoa amri ya mwisho kwa familia ya Yahimana. Wakiwa taabani, miili ikiwa imechanwa chanwa, alama za majeraha zikiwa zimejaa mwilini,amri ya Richald Robeni ikatekelezwa.



Yahimana Yahimana, mke wake, pamoja na binti yao Mwamvua walinyenyuliwa kama wafu, wakatupwa gerezani, gereza lenye mbwa wakali wenye njaa za siku nyingi.



Mbwa ambao walifundishwa kuua na kushambulia Waafrika wanapowekwa katika gereza hilo, siku zote hufungwa kamba za mkonge, wakifanikiwa kukata kamba hizo, wakaonesha uhodari wao kwa kukata kamba, hupata kiu ya njaa yao kwa kula Waafrika wafungwa.



“,John na Jacksoni letea wewe chakula kama fanikiwa kata kamba kula nyama ya Africans! “,askari wakizungu waliwaambia mbwa wa kizungu waliojulikana kama John na Jacksoni, huku miili ya Yahimana na familia yake ikitupwa ndani ya gereza hatari.



…………………………………

Tabasamu liliipamba sura ya Angel mtoto wa Richald Robeni,aliposhuhudia kupiti a dirishani jinsi mtoto mdogo wa kike tena wa Kiafrika,akiwatia adabu askari wa kizungu,lakini ghafla furaha ilitoweka,askari wengi waliwavamia na kuwashambulia Waafrika wale,furaha ikatoweka zaidi aliposhuhudia baba yake mzazi akishiriki ukatili ule na kuamua kuwatupa watu wale kuliwa na mbwa hatari katika gereza la Kikoloni.



“,I have to help them, i hate you dady,(Ninapaswa kuwasaidia,nakuchukia baba)”,Angel aliongea kwa uchungu,ubongo wake ukaanza kutafakali kwa kina,aliapa kutoa msaada kwa Waafrika wale haraka iwezekanavyo,kabla hawajashambuliwa na mbwa wa kikoloni.



…………………………………

Slum area(Makazi duni)4;00 pm

Jua lilianza kuzama, kwa masaa matano akiwa ndani ya msitu wa Mikoko, Mpuzu Yahimana alitoka akiwa na nguvu mpya, aliamini katika makazi ya Waafrika kulikuwa na usalama. Hakuhofu chochote kile, hakutambua lolote lile ambalo liliendelea, laiti kama angejua, bila shaka angekuwa tayali kwenye mapambano kuikomboa familia yake dhidi ya kifo kilichowakabili.



“,yeeee! yeeee! Umbhaye hehe mwanawachu!, (yeyee! yee! ulikuwa wapi mtoto wetu!), “mwanamke wa makamu, jirani na kibanda cha Yahimana Yahimana aliongea, baada ya kukutana uso kwa uso na Mpuzu.



“,Pomwee! mama Ishimwe,nilikua porini kuwinda, lakini sijabahatisha kitu, kwani kuna tatizo? “,Mpuzu alisalimia ,kisha akamdanganya mama wa rafiki yake, aliyeitwa Ishimwe.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Pomwee mwana Wanje! (salama mtoto wangu), wazazi wako wamekamatwa,Waafrika wote wakubwa kwa wadogo tumechapwa kwa ajili yako, bila shaka wazazi wako wako pabaya, wanaweza kufa “,mama Ishimwe alijibu salamu kwa kilugha, kisha akaongea kiswahili, lugha ya taifa ya nchini Goshani.



Mpuzu hakua na muda wa kupoteza, aliingia ndani, akachukua upinde na mishale, kisu alichorithishwa na babu yake, akaanza safari ya kuelekea “the great fort “,ngome ya wakoloni iliyojulikana kama ngome kubwa.



“,Ama zangu ama zao wazungu, naenda kuchukua mke wangu!, naenda kuokoa familia yangu “,Mpuzu aliongea, akidhamiria kabisa kuwaokoa wazazi wake na pia kumtorosha Angel katika ngome ya Wakoloni.



The great fort(ngome kubwa); 05;20pm

Mpuzu Yahimana alikimbia kilomita tatu, miguuni hakuvaa kiatu chochote kile, unyayo wa miguu yake ulikuwa imara, ulistahimili kokoto na miiba, wakati mwingine miiba ilimchoma, hakuhisi maumivu yoyote yale, fikra zake ziliwaza uzima wa ndugu zake.



“,Yanipasa kusubili giza liingie, wametapakaa kila kona katika ngome, nikizubaa nitakamatwa, hapatakua na msaada tena, sisi sote tutakufa ……”,Mpuzu Yahimana aliongea,macho yake yalikodoa kodo kutazama ukuta mrefu mita mia mbili mbele yake, alijibanza kwenye miti, kukwepa taa mbili kubwa zilizozunguka kuangaza kwa zamu kila kona, kudumisha ulinzi.



“,Njaa inauma, tangu asubuhi sijatia kitu kinywani “,Mpuzu aliongea, akaingiza mkono wake mifukoni, akapapasa mavazi yake ya asili huku na kule, akatabasamu, aliupata muhogo wake aliohifadhi tangu jana, akaanza kutafuna, akisubili giza liingie aanze kuingia katika ngome hatali ya wazungu, wakoloni watawala wa nchi ya Goshani.



“,Impomwe imbwe imbwe impomwe imbwe! “,Mpuzu aliimba kwa kilugha, akijipa moyo kwa kazi iliyokuwa mbele yake, kazi iliyo ngumu na ya hatari, lakini alipaswa kuikabili.



………………………………

Slums area (makazi duni);Nusu saa iliyopita

Ishimwe, rafiki kipenzi wa Mpuzu, alirejea kutoka shambani, katika mashamba ya wakoloni. Mkononi alishika senti moja aliyolipwa, huku akiitunza kwa makini, ili atakaporejea siku inayofuata, akamilishe senti mbili kwa ajili ya kulipia kodi ya kichwa. Siku mbili zimepita, hajamtia rafiki yake machoni, hajui chochote kile, alifika nyumbani kwao akiwa amechoka sana, akaketi karibu na mama yake juu ya zulia.



“,Pomweee mayo ……”,(habari mama) “,Ishimwe alisalimia, huku akimgusa miguuni mama yake kwa heshima.



“,Pomwee mwana wanje …”,(salama mtoto wangu), mama yake Ishimwe alijibu. Huku akijiweka sawa kuzungumza jambo, bila shaka alimsubili kwa hamu mtoto wake pekee wa kiume, hodari na shupavu, mwenye nidhamu ya hali ya juu.



“,Wazazi wetu waliuzwa kama bidhaa, wakapigana vita, biashara haramu ya utumwa ikakomeshwa, kuna watu walijitoa kwa wengine, lakini baada ya biashara hiyo, neno ukoloni liliibuka, asubuhi tu tumepigwa viboko, tumeaibishwa mbele yenu! tumewakuza mashujaa mkomboe nchi yenu, rafiki yako kaelekea ngome kubwa ……”,mama Ishimwe aliongea maneno mengi, akamalizia na ujumbe aliokusudia.



” ,Unasemaje? inamaana tangu wazazi wake wachukuliwe hawajarudi? “,Ishimwe aliuliza kwa mshangao.



“,Ndio,ameenda kuwakomboa, peke yake hawezi, kamata upinde na mishale, nenda kamsaidie, wakati sahihi wa nyie kutuepusha na aibu ni huu! “,mama Ishimwe aliongea, sura yake haikua na utani, ilijaa uchungu na hasira ndani yake.



Ishimwe alitikisa kichwa, alikubaliana na mama yake, hakuwa tayali kumkosa rafiki yake Mpuzu, waliapa kufa kifo cha kufanana katika uwanja wa vita wakipigania uhuru wa nchi ya Goshani.



Alichukua panga lake aina ya jambia, panga alilotumia kuchimbia viazi shambani, akachukua kibuyu kitupu, akachukua upinde na mishale, hakuvaa kitu mguuni, alikuwa peku.



“,Nakenda! (nitarudi salama), “alimuondoa shaka mama yake, akainama kwa heshima, akambusu miguu yake, akasimama na kutimua mbio.



“,Mizimu ya Goshani ikulinde …!”,mama Ishimwe aliongea kwa uchungu, chozi likadondoka, hakuwa na hakika kama mwanae atarejea salama, kutoka mikononi mwa wakoloni wasio na roho ya huruma.

Ishimwe, kijana wa miaka kumi na tisa, umri sawa na Mpuzu, alikimbia bila kupumzika, alipaswa kuwahi kutoa msaada, akiwa umbali wa kilomita mbili, aliufikia mti wa upupu pembeni mwa njia, akakwangua upupu wa kutosha, akatia kwenye kibuyu, akafungasha silaha zake, akasonga mbele kuendelea na safari.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

…………………………………

Ngome kubwa; (The great fort) 8:00pm

John na Jacksoni, mbwa wakubwa wa kizungu, sura zao zilijaa hasira, macho mekundu yaliangaza, ndimi zao ziliwatoka kwa nje huku udenda ukiwachuruzika.



Njaa ziliwasumbua, waliendelea kukata kamba zao kwa juhudi,ili waweze kuwa huru na kujitwalia nyama ya binadamu kama zawadi. Robo tatu ya kamba ilikatika, nyuzi chache tu zilisalia ili kamba zote kukatika.



Yahimana Yahimana, mke wake, pamoja na binti yao Mwamvua, hawakutambua chochote kile, fahamu hawakuwa nayo tena, maumivu ya kipigo walichokipata yaliwalemea, walifaa kuitwa wafu walio hai.



Angel Richald alisubili baba yake, pamoja na mama yake waweze kulala,atoroke, akawakomboe Waafrika waliofungwa katika gereza lenye mbwa wenye njaa kali. Lakini muda wa kulala ulikua bado, ndio kwanza saa mbili kamili ilitimia, alikaa akitafakali mbinu ya kutoa msaada alikosa, mtoto wa kike alibaki wa kike tu! msaada wa haraka hakua nao tena …



…………………………………

Giza lilitapakaa aneo lote lililozunguka ngome ya wakoloni, muda sahihi wa kazi ulifika, Mpuzu alinyanyuka alipokuwa ameketi chini ya mti,lakini machale yalimcheza, alihisi hatua za mtu kumnyemelea, alitayalisha upinde kuikabili hatari yoyote mbele yake.



“,Pomweee Mpuzu (habari Mpuzu), “Ishimwe alisalimu, huku akirudisha mahala pake silaha zake,baada ya kutambua kuwa aliyekuwa anamnyemelea hakua adui bali rafiki yake kipenzi.



“,Pomweee Ishimwee! (salama Ishimwe) “,Mpuzu aliitikia, tabasamu likiipamba sura yake, waligonga miguu, kisha wakakumbatiana, wakagonga miguu tena, staili yao ya kipekee waliyoitumia kusalimiana siku zote wanapokutana.



“,Mama kanieleza yote, nimekuja kukusaidia! “,Ishimwe aliongea.



“,Karibu sana rafiki, natumaini kazi itakua rahisi sana ukiwepo! “,Mpuzu alimjibu rafiki yake.



“,Haswaa! tena leo nimekuja na upupu, tukiwatilia kwenye chanzo chao, matanki ya kuogea, pamoja na mavazi yao, hawatapata muda wa kutushambulia na bunduki zao zaidi ya kujikuna “,Ishimwe aliongea, akachomoa kibuyu na kumuonesha rafiki yake.



“,Hahaaaa! “,wote walicheka, wakagonga miguu,wakagonga mikono, ishara yao ya furaha, wakashikana mikono ishara ya umoja wao na upendo, kisha wakaianza safari kwa kujibanza kwenye majani wasionekane, wakaisogelea ngome ya wakoloni.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

…………………………………

Bunduki aina ya SAR zilikua begani wengine mikononi, askari wa kikoloni wakiwa wamevalia bukta zao nyeupe, sare zao za jeshi, waliangaza kila kona kudumisha ulinzi, bila kutambua kuwa walinyemelewa na Mpuzu pamoja na Ishimwe, vijana hodari wa Kiafrika.

“,Let me sleep,all places are safe! (ngoja nilale, maeneo yote ni salama) “,askari mmoja wa kikoloni aliongea, akiwa juu ya kibanda cha ulinzi juu ya ukuta, kuongoza taa kubwa iliyozunguka huku na kule kulinda usalama, aliacha kuzungusha taa ile kubwa, akaketi vizuri kwenye kiti chake, akapiga usingizi. Akatoa nafasi kwa maadui wake Mpuzu na Ishimwe bila kutambua.



…………………………………





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog