Simulizi : Je Haya Ni Mapenzi!!
Sehemu Ya Tano (5)
Jeff alitoka nyumbani kwao na kuelekea kwakina Sabrina ambapo aliwakuta baba na mama Sabrina pamoja na mdogo wa Sabrina.
Akawasalimia pale kisha akaomba kuongea nao,
"Mmh una ujumbe gani kwetu Jeff?"
"Ujumbe huu unahusu kilichotokea baina yangu na Sabrina"
"Hebu tueleze"
Wakatulia kumsikiliza,
"Ukweli ni kwamba wale watoto wa Sabrina yani Cherry na Sam ni watoto wangu"
"Watoto wako kivipi?"
"Wale watoto ni damu yangu na mimi ndio baba yao mzazi"
Mara Sam akaingia na kufanya wote kushtuka na kumtazama kwani hata mlango hakugonga.
Jeff alitoka nyumbani kwao na kuelekea kwakina Sabrina ambapo aliwakuta baba na mama Sabrina pamoja na mdogo wa Sabrina.
Akawasalimia pale kisha akaomba kuongea nao,
"Mmh una ujumbe gani kwetu Jeff?"
"Ujumbe huu unahusu kilichotokea baina yangu na Sabrina"
"Hebu tueleze"
Wakatulia kumsikiliza,
"Ukweli ni kwamba wale watoto wa Sabrina yani Cherry na Sam ni watoto wangu"
"Watoto wako kivipi?"
"Wale watoto ni damu yangu na mimi ndio baba yao mzazi"
Mara Sam akaingia na kufanya wote kushtuka na kumtazama kwani hata mlango hakugonga.
Sam alionekana wazi kuwa na hasira sana kwani hata macho yake yalikuwa yakicheza cheza huku akimtazama Jeff kwa ghadhabu sana kisha akasema,
"Rudia uliyoyaongea yote Jeff"
Jeff alikaa kimya kwani moyo wake uligubikwa na uoga usio kifani, ila Sam nae aliwekea msisitizo ile kauli yake kwa Jeff kuwa arudie yote aliyokuwa akiyasema.
Mara Jeff akajishtukia akipata ujasiri wa haraka sana na kujikuta akisema kwa kujiamini,
"Nimewaambia kuwa Cherry na Sam ni damu yangu"
Sam akamuuliza Jeff,
"Una uhakika kuwa ni damu yako?"
"Ndio nina uhakika"
"Una uhakika kuwa ni damu yako?"
Sam akarudia tena swali na kumfanya Jeff uoga umshike tena, ambapo Sam alipomuona Jeff kuwa kashindwa kujiamini akajikuta naye akipata ujasiri na kuita,
"Cherry, Cherry mwanangu"
Mara wakamuona Cherry akitokea chumbani kwa Sabrina na kumkimbilia Sam.
Kitendo hicho kiliwaogopesha hata wazazi wa Sabrina kwani walijikuta wakitetemeka tu.
Cherry alipokuwa amemkimbilia Sam, ni hapa Sam akatumia nafasi hii kumuuliza,
"Nani baba yako kati ya mimi na huyo ndorobo?"
Cherry naye akajibu kwa ujasiri mkubwa,
"Wewe ndio baba yangu"
Kisha akamkumbatia Sam ambapo Sam alimnyanyua na kumbeba begani kisha akamwambia Jeff,
"Kama una uhakika kuwa hii ni damu yako nifuate"
Halafu Sam akatoka na yule Cherry na kuondoka naye.
Mule ndani walibaki na viulizo visivyokuwa na majibu.
Kwanza kabisa ulitawala ukimya wa hali ya juu, baada ya muda kidogo mama Sabrina akawa wa kwanza kuuliza swali,
"Jamani, huyu mtoto kaja muda gani humu ndani?"
Baba Sabrina nae akashangaa vizuri sasa,
"Na kweli, huyu Sabrina si amekuja mwenyewe na yule mtoto wa mgongoni tu? Na wakati ule amefika si akapiga kelele kuwa kamuona mwanae chumbani! Ni nini hiki jamani?"
Akili ikawajia haraka haraka na kuamua kuinuka ili wakamuangalie Sabrina chumbani kuwa anaendeleaje.
Waliingia chumbani kwa Sabrina na kumkuta kalala tu kitandani, ni hapa walipoamua kumuamsha sasa ila walitumia muda mrefu kumuamsha bila ya Sabrina kuamka na kuwafanya wahisi kuwa kazimia ikabidi wachukue maji na kummwagie ili azinduke.
Na walipommwagia yale maji tu na kweli Sabrina akazinduka ila alipiga kelele sana wakati wa kuzinduka kwake huku akitaka kuinuka na kukimbia ila wazazi wake walifanya kazi ya ziada kwa kumshika ili asikimbie.
Kwakweli Jeff nae alikuwa kimya tu kwani akili yake ilipoteza uelekeo tu na alikuwa kajiinamia kwenye kochi pale kwakina Sabrina huku machozi yakimtoka kwani yeye alikuwa akilaumu sana kitendo chake cha kufanya siri kwani alihisi kuwa ndio kitu pekee kinachomtesa kwa wakati huo.
Sam aliondoka na yule Cherry hadi kwenye nyumba yake ya awali kwani alijua wazi kuwa asingeweza kwenda nae kule kwake kupya kutokana na ule uwepo wa mama yake.
Kama kawaida ya nyumba yake hii palikuwa na mlinzi getini ambaye alifungua geti na kuwakaribisha.
Mlinzi huyu alimuangalia sana Sam na huyu mtoto wake ila kwavile yeye ni mlinzi tu basi hakuweza kuhoji jambo lolote lile.
Sam aliingia na Cherry ndani huku bado akiwa na hasira ya kisasi dhidi ya Jeff ila aliamua kwanza azungumze na mtoto huyo ili ajue cha kufanya kabla ya kufanya anachokiwaza yeye.
Sam alikaa na huyu Cherry sasa ili angalau apate cha kufanya.
Cherry alionekana kuwa na jazba sana kwani aliongea kwa hasira na ukali,
"Yule mama yako umfukuze pale"
"Hilo sio tatizo ila tatizo kwangu ni huyu Jeff kwakweli amenikera sana yani pale ilibaki kidogo tu ningemfanya kitu kibaya"
Cherry akacheka na kusema,
"Hivi unajua kama mimi amenikera zaidi? Basi mchagulie adhabu nikampe sasa hivi kwani najua unajua ninachoweza kufanya"
Sam akafikiria kidogo na kupatwa na huruma kwa mbali dhidi ya Jeff kwani alikuwa na uhakika kabisa kuwa chochote atakachosema basi huyo anauwezo wa kuharibu.
Akamuomba Cherry asubiri kidogo ili afanye maamuzi,
"Kabla ya kufanya maamuzi yako, nataka chakula."
"Chakula, hakuna shida twende tu hotelini ukale"
"Unasemaje? Umeshasahau chakula changu au? Nahitaji chakula, na uzingatie kwamba mmenikera sana kipindi hiki. Nahitaji chakula, yani siku ya leo isipite tafadhari"
Sam alielewa moja kwa moja kile alichoagizwa kwa muda huo na kuahidi kuwa anaenda kukifanyia kazi.
"Basi nitakuacha hapa kwa muda ili nikafanyie kazi hilo swala"
"Sawa hakuna tatizo ila kumbuka kuwa ulipo nipo. Na huyo Sabrina asifikirie kwamba simuoni, muda wowote nikitaka kwenda naenda"
Sam akamuacha huyo Cherry ndani kisha yeye akatoka na kuondoka na gari yake.
Jeff naye alihisi kuchanganyikiwa kwakweli kwani aliona kama mambo yapo ndivyo sivyo, aliamua kuinuka pale kwakina Sabrina ili aweze kurudi kwao.
Ila alipotoka nje alijikuta akizua safari mpya kabisa, alitaka kwenda kuonana na baba yake mzazi ili aweze kumueleza mustakabali mzima na kuona kama anaweza kumsaidia kwa mawazo ingawa anajua wazi mzozo uliotokea baina yao kutokana na kifo cha dada yake Amina ila bado alijipa moyo wa kwenda kuzungumza na baba yake huyo.
Akiwa njiani, kuna mdada alimfata akiwa na mtoto mgongoni.
Mdada huyo alionekana kuchoka sana yani ukimtazama tu unaweza ukagundua kuwa maisha yamempiga kiasi cha kumfanya kama mgonjwa.
Huyu mdada alimsogelea Jeff na kujaribu kumuomba msaada,
"Nisaidie kaka yangu, yani unavyoniona hapa mimi na mwanangu hatujala chochote tangu jana. Naomba msaada wako"
"Dada, mimi mwenyewe unaponiona hapa ni msaada maana maisha yangu ni shida tupu. Kwani baba mtoto yuko wapi?"
"Aliniacha, alienda kuwa na mwanamke mwingine. Maisha yangu yamekuwa ndio haya kila siku"
"Ila dada, hilo liwe fundisho kwako na kwa wengine. Sio kila mwanaume ni wa kuzaa nae au kulala nae, jifunzeni wadada. Mi mwenyewe hapa shida tupu labda nikusaidie hii miatano ila ndio mjifunze"
Jeff akatoa miatano na kumkabidhi yule dada kisha yeye akaondoka zake.
Jeff alipofika mbele akasikia sauti ikimwambia,
"Jeff kaka yangu, yule dada ungemsaidia kwa kumpeleka mahali sahihi ila pale ulipomuacha anaenda kuhangamia kama mimi dada yako"
Jeff akashtuka sana kwani hii sauti alipoisikiliza vizuri aligundua wazi kuwa ni sauti ya dada yake Amina na kumfanya Jeff ashtuke sana na kugeuka nyuma.
Akamuona yule dada na mwanae wakiingia kwenye gari kisha ile gari ikaondoka na alipoiangalia vizuri akagundua kwa haraka sana kuwa ile gari ni ya Sam.
Kwakweli Jeff alijihisi kutetemeka sana, na alipoangalia tena mbele akamuona Amina akiwa na sura ya unyonge sana.
Jeff alijihisi kuchanganyikiwa zaidi na kugeuka kwa haraka kisha akaanza kurudi alipotoka kwani akili yake ilionekana kutokuwa sawa kwa muda huo.
Wazazi wa Sabrina, walimkongoja Sabrina mpaka sebleni na kukaa nae ili waweze kuzungumza yale yanayomsibu na yale waliyozungumza na Jeff.
"Kwani Sabrina hebu tueleze vizuri, unajua wazazi wako hatuelewi kitu. Mfano mzuri mimi mama yako yani ndio sielewi kabisa, umekuja hapa ukiwa na mwanao mdogo mgongoni ukaenda chumbani kwako na kupiga kelele tukaja kukuangalia. Cha kushangaza ulipolala kaja Jeff hapa na kutupa habari za kushangaza, mara Sam nae akaja na kumuita Cherry ambaye alitokea chumbani kwako. Ni muda gani ulikuja na huyo mtoto Sabrina? Hebu tueleze ukweli mwanangu"
Sabrina alikuwa akiwaangalia tu kama mtu anayewashangaa kwani hata yeye mwenyewe hakuelewa vizuri ila akataka kuongea yale aliyokumbana nayo yeye ila kabla hajaanza kuongea gafla alianguka na kuanza kuweweseka.
Wazazi wa Sabrina walistaajabu sana huku wakijaribu kumpa huduma ya kwanza.
Jeff alirudi nyumbani kwao huku akiwa amevurugika kabisa kwenye akili yake kwani hakujua kuwa ni wapi aanzie na wapi aishie.
Alimkuta yule binti wa kazi akiendelea kumuhudia mama yake ila alipoingia yeye yule binti alimfata na kumsalimia kisha akamwambia,
"Kaka, unajua mwezi huu hujanipa mshahara wangu?"
"Natambua hilo, nitakulipa tu"
"Nyumbani kwetu kuna matatizo ndiomana nimekukumbusha ili unipatie hiyo pesa niwatumie nyumbani"
"Sawa nimekuelewa Keti nitakupa tu"
Kisha Jeff akaelekea chumbani kwake na kukaa akitafakari kwani vitu vingi sana walikuwa wakitegemea toka kwa Sam na kwajinsi mambo yalivyoharibika kwa kipindi hiko aliona ni ngumu kwa yeye kupata msaada hapo.
Mama mdogo wa Sam aki wa na Cherry ndani, alishangaa kuona muda ukipita bila ya Sam kurejea.
"Khee ni usiku tayari na huyu Sam alisema kuwa nisipike tutaenda kula hotelini, sasa hadi muda huu hajafika hata simu hajapiga kweli!! Ila natumaini yupo salama"
Kisha mama huyu akaamua kwenda jikoni na kupika ili aweze kula na mjukuu wake.
Alipomaliza kupika alikaa na mjukuu wake wakala ambapo muda kidogo kupita huyu Cherry akawa amelala tayari, ikabidi aende kumlaza kisha yeye amsubirie kidogo Sam ila alipoona kuwa muda unakwenda ndipo alipoamua kulala na yeye.
Usiku sana aliposhtuka akasikia mlango ukifunguliwa na moja kwa moja akahisi kuwa ni Sam na kuamua kuamka ila alipofika sebleni hakuona mtu.
Akili yake ikampeleka moja kwa moja kuwa ni nguvu za giza na kuanza kukemea kwa maombi.
Huyu mama alikuwa pale sebleni kwa Sam akifanya maombi kwa masaa mawili mfululizo.
Kisha akarudi zake kulala na kuona wazi kuwa ile nyumba ya Sam imetawaliwa na nguvu za giza.
Asubuhi na mapema huyu mama alikuwa sebleni na mjukuu wake, ndipo Sam nae aliporudi muda huu ila alionekana kuwa na hasira sana tena bila ya kumsalimia mama yake alianza na hoja moja tu,
"Kwakweli mama naomba urudi Arusha"
"Kheee ndio salamu hiyo jamani Sam! Arusha ni kwangu na nitarudi tu ila sio kwa staili hiyo unayosema wewe. Na kwanini unaanza na swala la kurudi Arusha? Nini tatizo?"
"Mama, nimelalamikiwa na majirani. Unaomba usiku kucha, unafanya watu washindwe kulala kwakweli wamelalamika sana. Kwahiyo mama nakuomba urudi Arusha"
Huyu mama akacheka kwanza na kusikitika pia kisha akamwambia Sam,
"Kwakweli Sam acha kunichekesha, labda useme jambo lingine ila sio kuhusu maombi. Hebu angalia hii nyumba yako ilivyokubwa tena na madirisha ya vioo sasa kwa sauti gani nitoe iwasumbue majirani? Kwanza nyumba yako iko mbali na nyumba zingine, je hao ninaowasumbua ni wakina nani? Hivi unajua kama nyumba yako inamapambano mazito sana? Hivi unajua kwanini nimeshtuka usiku na kuomba? Sikushangai mwanangu, utakuwa unasumbuliwa na mapepo"
"Sina mapepo mama, ila maombi yako naomba upunguze au uache kabisa lasivyo urudi Arusha"
Kisha Sam akaelekea chumbani kwake.
Kwakweli huyu mama alimsikitikia sana mtoto wake na kuona wazi kuwa kuna kitu ambacho kinamsumbua mtoto wake huyo.
Kwa upande wakina Sabrina, wazazi wake waliamua kuwa nae karibu sana kwani waliona kuwa kufanya hivyo kunaweza kukamsaidia Sabrina na kumrudisha katika hali yake ya kawaida.
Ila waliogopa kumuuliza swali la kuhusu watoto wake kwani ilikuwa kila akitaka kujibu anaanza kuweweseka.
"Yani Sabrina mwanangu kwasasa utulie tu, Mungu atakusaidia uweze kurudi kwenye hali yako ya kawaida."
Baba Sabrina nae akajisikia kumuuliza mkewe,
"Hivi mama Sabrina, zile mbwembwe zako za kusali sali ziliishiaga wapi? Maana nakumbuka zamani ulikuwa na moto balaa"
Mama Sabrina akamuangalia mumewe kwani haya maneno yalimchoma haswa,
"Unajua uvivu mbaya sana, yani mimi uvivu na maswaibu yangu ila umenikumbusha kitu cha muhimu sana. Yani kipindi kile nilikuwa nina imani ya ajabu hadi mi mwenyewe nilikuwa najiogopa ila siku hizi sasa hata sijui nina matatizo gani. Kwakweli Mungu anisamehe tu"
"Sio akusamehe, mrudie Mungu wako labda yote haya tunapigwa kofi kwa kumsahau"
"Wewe mwenyewe mbona husali? Mmh waniona mimi tu"
Walikuwa wakishushuana pale ila Sabrina alikuwa kimya kabisa akitafakari maswaibu yake yote yaliyompata.
Jeff nae alipojiandaa kutoka, wazo lake lilikuwa ni juu ya mtoto wake Cherry tu na hapo akapata wazo la kwenda nyumbani kwa Sam ili akaonane nae na waongee kiume.
"Kwakweli sitaki kukubaliana na hili swala kabisa, yule mtoto ni damu yangu. Hata wanifukuze ila nitaendelea kuifatilia damu yangu."
Kwahiyo hakutaka kupoteza wakati na moja kwa moja akaanza safari ya kuelekea kwa Sam.
Sam nae hakukaa sana pale nyumbani kwake kwani muda kidogo alitoka na kuona kisha pale akabaki mamake mdogo na mtoto Cherry.
Muda kidogo alifika mgeni na kumfanya mama huyu kumfungulia mlango na kumkaribisha.
Mgeni alikuwa ni Jeff ambapo alipomuona Cherry na huyo mama alifarijika sana bila hata ya kumjua kuwa huyo mmama ni nani.
Ila alimshangaa sana Cherry kwani alionekana kuwa ni mtoto wa kawaida sana.
Mama wa Sam akajitambulisha kwa Jeff kisha akatulia ili kumsikia kilichomleta,
"Kwanza samahani mama hata sikujua kama wewe upo, kwani kilichonileta ilikuwa ni kuja kumchukua huyo mtoto"
"Mmh umchukue uende nae wapi? Huyu yupo kwa bibi yake hapa na sitaki aende popote kwani hata baba yake tu nilimkatalia"
Ikabidi Jeff awe mpole kiasi kwani aliona kama akitoa ukweli kwa huyo mama atazidi kumchukiza Sam kwahiyo akaamua kuaga na kuondoka.
Jeff alirudi kwao moja kwa moja, ila alipofungua mlango wa ndani kwao moja kwa moja akabambana na mtoto Cherry akiwa amekaa kwenye kochi huku akitabasamu.
Jeff alirudi kwao moja kwa moja, ila alipofungua mlango wa ndani kwao moja kwa moja akabambana na mtoto Cherry akiwa amekaa kwenye kochi huku akitabasamu.
Jeff akashtuka sana ila huyu mtoto akamuuliza,
"Unashtuka nini sasa wakati ulinifata mwenyewe!"
"Ndio nilikufata, ila nani kakuleta?"
"Baba kanileta"
Jeff akatulia kimya kwa muda kwani alikuwa kama haelewi elewi kile kinachoongelewa na huyo mtoto, kisha akamuita mdada wa kazi wa mule ndani kwao ambaye alifika pale sebleni na kumshangaa Jeff na Cherry wakiwa pale.
Kisha Jeff akamuuliza huyu mdada,
"Keti, nani kaja na huyu mtoto?"
"Si umekuja nae wewe au?"
"Inamaana hujui aliyekuja nae?"
"Hapana nashangaa hilo swali maana mie umeniita hapa ndio nakuona wewe na huyo mtoto sasa nitajuaje aliyekuja nae"
Jeff akatulia kidogo akimuangalia huyu mtoto, kuna kitu kilikuwa kikimwambia moyoni mwake ila akakipuuzia kisha akamsogelea huyu Cherry ili aweze kumuhoji vizuri kuwa amefikaje fikaje hapo, ila yule mdada wa kazi aliondoka zake na kuwaacha.
"Hebu niambie ukweli mwanangu, umefikaje hapa"
"Khee tena ukome, mimi sio mwanao"
Jeff akashtuka kwani mtoto huyu aliongea kama mtu mzima kabisa,
"Kwani una matatizo gani jamani?"
"Matatizo unayo wewe, mtu gani wewe usiyesikia unayoambiwa. Tena mshukuru sana Sam kwa anavyokuhurumia maana bila hivyo wangeongea mengine"
"Unajua sikuelewi, mbona unaongea kama mtu mzima?"
Cherry akacheka na kusema,
"Sasa ulitaka niongee kama mtu aliyekufa? Au niongee kwa huruma kama marehemu dada yako Amina? Na kwa taarifa yako yule mdada wa jana na mtoto wake wameshaenda kusalimia akhera kwahiyo wewe tunavyokukalia kimya usidhani tunakuogopa."
Jeff alianza kupatwa na mashaka sasa na kujikuta akitetemeka kwani maneno ya huyu mtoto yalikuwa makali sana ila huyu mtoto akaendelea kuongea,
"Tena kwa taarifa yako, unanihitaji sana mimi kwani maisha ya mama yako yapo mikononi mwangu. Acha tabia yako ya kunifatilia"
Kisha kile kitoto kikasimama na kumnasa kibao Jeff kilichompa kizunguzungu halafu yule mtoto akatoweka na kumfanya Jeff aanguke na kuzimia.
Nyumbani kwakina Sabrina nako hali haikuwa shwari kwani Sabrina bado alionekana kuwa na tatizo kubwa sana.
Mdogo wake aliamua kuwa nae karibu sana ili aweze kumdokeza kuhusu ukweli wa maneno aliyoyaongea Jeff,
"Dada, ongea na mimi mdogo wako. Je ni kweli hawa watoto wako ni watoto wa Jeff?"
Sabrina alikuwa kimya v na kumfanya mdogo wake azidi kumshawishi ili aweze kuupata ukweli wa mambo,
"Niambie dada yangu, mimi ni mdogo wako na hapa tupo wawili tu. Mapenzi hayachagui dada, hayaangalii dini kabila wala umri. Ilimradi tu watu mnapendana kwa dhati mnaweza kuwa pamoja bila ya kujali chochote. Na wala sitakushangaa dada yangu ukiwa na mahusiano na Jeff kwani naye ni mwanaume kama wanaume wengine. Niambie ukweli sasa dada yangu, na kumbuka kuwa ukweli umweka mtu huru. Je hawa watoto baba yao ni Jeff kweli?"
Sabrina akaitikia kwa kichwa kwani haya maneno ya mdogo wake yalimuingia, ila alipoitikia tu kwa kichwa akamwambia mdogo wake,
"Ila usimwambie baba na mama"
"Sabrina dada yangu, tafadhari kuwa na imani na mimi. Nakupenda sana dada yangu, pia napenda maisha yako, napenda kuona ukifurahi. Nilijaribu kufatilia maisha unayoishi na Sam nimeona huridhishwi nayo kabisa, dada ulikuwa na mwili mzuri sana ila siku hizi unazidi kukonda dada yangu. Sababu kubwa ni kuwa huishi na furaha yako, hakuna wa kukucheka dada yangu ikawa Jeff ndiye mwanaume pekee anayekupa furaha basi hunabudi kuishi naye bila ya kujari maneno ya walimwengu. Nakupenda dada yangu, amini maneno yangu na uwe na amani kabisa"
Kisha akainuka na kumuaga dada yake kuwa badae atarudi wazungumze tena mawili matatu.
Sam alikuwa na mawazo sana kwani aliona mama yake mdogo akikwamisha mambo yake mengi sana.
Akawaza namna ya kufanya ili aondoke pale nyumbani kwake.
Wazo likamjia kichwani, kisha akarudi nyumbani kwake kuzungumza nae.
Alifika na kumkuta kama kawaida akicheza na mjukuu wake na kiukweli kwa hizo siku chache huyu mtoto alionekana kuchangamka na kuwa kama watoto wengine.
Sam alikaa na kuanza kuzungumza na mama yake,
"Mama, nimepata safari ya gafla ya kikazi ya kwenda Arusha. Sasa nimefikiria na kuona ni vyema tukaenda pamoja mama yangu"
Huyu mama akakaa kimya kwa muda kidogo huku akitafakari mambo ma wili matatu hadi pale ambapo Sam alimshtua tena,
"Vipi mama, mbona kimya tena? Au hutaki kusafiri na mimi jamani?"
"Sio kwamba sitaki, ila kuna kitu nilikuwa nafikiria kwanza"
"Kitu gani tena mama?"
"Nina ombi moja mwanangu, ukinitekelezea tu tutaondoka wote"
"Ombi gani hilo mama yangu?"
"Nahitaji kwenda kuonana na wazazi wa Sabrina pamoja na Sabrina ili nizungumze nao kidogo halafu tutasafiri pamoja"
"Hilo sio tatizo mama yangu, kesho jiandae nikupeleke. Ingekuwa leo muda haujaenda sana ningekupeleka mama"
Sam hakuona kama kuna tatizo kufanya hivyo kwani yeye kitu pekee ambacho hakukitaka kwa kipindi hicho ni huyo mama yake kuendelea kuwa hapo kwani aliona kama akimuharibia mambo yake mengi sana.
Kisha akaongea nae pale na kuamua kwenda chumbani kwake kwa lengo la kulala.
Mdogo wa Sabrina akaenda kwakina Jeff sasa kwa lengo la kuzungumza na Jeff.
Alipoingia kwakina Jeff alishangaa kumuona Jeff chini, ikabidi aite mtu aliyekuwepo mule ndani ambapo mdada wa kazi wakina Jeff akatoka huku nae akiwa anashangaa tu,
"Vipi tena?"
"Unaniuliza mimi mgeni? Nyie vipi mbona mstaarabu wa humu ndani kwenu haueleweki? Mlango mmeacha wazi na mtu anaonekana kuanguka hapa chini. Hebu kalete maji"
Yule dada akaenda kuleta maji kisha mdogo wa Sabrina akajaribu kummwagia Jeff ambapo akazinduka baada ya kumwagiwa yale maji.
Akawa kama mtu anayetaka kukimbia ila mdogo wa Sabrina akamshika vizuri ili asikimbie kisha akaongozana nae kuelekea chumbani kwake ambapo alimsaidia kukaa kitandani na kumuacha kimya kwa muda kisha akamuuliza kilichompata,
"Vipi ndugu yangu, nini tatizo?"
"Dah yani hata sijielewi, kumbe ukubwa ndio shida kiasi hiki? Dah!"
"Pole sana Jeff, kwani umepatwa na nini?"
"Acha nikae kimya Sam, anaweza akarudi hapa"
"Hawezi sababu mimi nipo"
Mdogo wa Sabrina aliongea kanakwamba anaelewa kuwa ni kitu gani kinaendelea kwa Jeff, kisha kimya kidogo kikatawala halafu mdogo wa Sabrina akaanzisha maswali yake kwa Jeff pia,
"Hivi Jeff ni kiasi gani wampenda Sabrina ?"
"Nampenda sana ila nisingependa kuongelea habari hizo muda huu"
"Usiogope Jeff, nina lengo zuri sana kwako wewe na kwa dada yangu Sabrina. Sipendi mapenzi yenu yawe ya siri kama mlivyoyaweka. Hebu jaribu kutazama moyo wako vizuri kama haya mapenzi ya siri yanapendeza"
Mdogo wa Sabrina akatulia kimya kidogo kisha akaendelea kuongea,
"Sikia Jeff, wewe ni mwanaume tena ninaamini kuwa ni mwanaume shupavu. Hutakiwi kuacha penzi lako likiteketea eti sababu ya kuogopa macho ya watu kwani hiyo kitu haitakusaidia zaidi ya kukuumiza tu"
"Ni kweli uyasemayo Sam, tena naumia zaidi ya ufikiriavyo. Kwakweli nampenda sana Sabrina, laiti kama angekubali ni siku nyingi sana ningejionyesha machoni pa watu wengi wanifahamu. Tatizo Sabrina alikuwa akiona aibu kuwa na mimi, pia hakuweza kuwa na mimi kwavile sikuwa na pesa kama yule Sam ila ukweli ni ukweli tu kuwa mimi ndiye mwanaume pekee ninayempenda Sabrina. Umri kwangu si chochote wala lolote, umri ni namba tu ila ukweli nampenda Sabrina na wala sioni aibu kusimama hata kwenye umati wa watu na kusema ukweli wa moyo wangu"
"Sasa mbona ukawa kimya siku zote hizi?"
"Sikutaka kuwa kimya Sam ila Sabrina hakutaka mapenzi yetu yawe wazi kwani aliona aibu kuwa na kijana mdogo kama mimi ila kiukweli nampenda sana na ndiomana nilikuwa nafanya vile anavyotaka yeye ili nisimkwaze ingawa leo hii kitu ndio inayonitesa"
"Pole sana Jeff ila mimi najitolea kuwa sauti yenu, ninaamini kuwa kila kitu kitaenda sawa kabla mambo hayajaharibika zaidi. Nimejikuta nikipatwa na huruma sana haswaa juu ya mtoto wako Cherry"
"Mmh Sam tafadhari, naomba usimtaje huyo mtoto. Unajua mara nyingi mwanamke anavyobeba mimba huwa hajui amebeba kitu gani. Wengine wanatuletea wezi, makahaba, majambazi hata wachawi. Ila hiki alichokizaa Sabrina hata sijui ni kitu gani kwakweli"
"Hapana Jeff usiseme hivyo, wanawake wote huwa wanazaa watoto sawa kabisa na wote wakiwa na lengo jema tatizo ni jamii inayotuzunguka ndio inayoharibu watoto wengi sana. Usifikirie kuwa kuna mtu yeyote aliyezaliwa ili awe mwizi sijui kahaba au mchawi. Jamii ndio inayoharibu watoto hawa, kwa imani yangu huyu mtoto atarudi kwenye hali ya kawaida tu."
Wakashauriana pale mawili matatu kisha mdogo wa Sabrina akainuka na kumuaga Jeff huku akimuahidi kuonana nae tena kesho yake.
Mdogo wa Sabrina alikuwa na mawazo mengi sana, alikuwa akitafakari namna ya kuisaidia familia yake, alitafakari namna ya kumsaidia Sabrina pamoja na Jeff na kitu pekee alichoona kuwa kinaweza kuwasaidia ni ukweli tu uliofichika baina ya hao wawili kwahiyo akapanga apumzike kwanza ili kesho yake akae na wazazi wake na azungumze nao kwa undani zaidi dhidi ya kinachoendelea kati ya Sabrina na Jeff.
Kisha akarudi kwao na kwenda chumbani kwake kupumzika.
Sam aliamua kulala nyumbani kwake siku hiyo ili kesho yake amalizane na mama yake kwani aliona kama akimpotezea mambo yake tu.
Ila alikuwa akitafakari mambo mengi sana ukizingatia akiwa hapo nyumbani kwake kwa kipindi hicho hakuweza kuzungumza chochote na mtoto wake Cherry kwahiyo aliona kuwa mama yake akimzibia mambo mengi sana.
Alitaka tu pakuche haraka ampeleke mama yake huyo kisha asafiri nae na kwenda kumuacha Arusha.
Sabrina akiwa amelala usiku wa manane, akahisi kama kuna mtu pembeni yake.
Aliposhtuka akashangaa kumuona mwanae Cherry, kwakweli Sabrina akaanza kupatwa na uoga kisha yule Cherry akamwambia,
"Hivi hadi leo hujanizoea tu? Hivi unajua nimekukinga na mangapi hadi leo? Kwakweli hutakiwi kuniogopa ila nakushangaa unavyoshtuka kila ukiniona. Hivi unajua kitu cha kuniondoa mimi ni nini?"
Sabrina alitingisha kichwa kuwa hajui chochote.
Huyu mtoto akacheka na kumwambia,
"Cha kuniondoa mimi ni damu, tena damu ya mtu"
Sabrina akawa anatetemeka tu kwani hata hakujielewa.
"Narudia tena, ni damu yani ni damu tu tena damu ya mtu ndio kitu pekee cha kuniondoa mimi. Kesho nitashughulika na Sam maana leo kanikimbia. Halafu mwambie mdogo wako asifikirie kuwa simuoni namuangalia tu ila kiherehere chake kitamponza"
Sabrina akawa anatetemeka tu na kushindwa hata kulala ila huyu mtoto alimpulizia kitu Sabrina na kujikuta akilala kabisa.
Kulipokucha mdogo wa Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka na kuanza kufanya kazi zake kidogo kisha akawaita wazazi wake ili azungumze nao kwani hakuweza kukaa na jambo hilo moyoni mwake.
Wazazi wao walitulia na kumsikiliza kwa makini ambapo aliwaeleza kwa kina kile alichoelewa yeye,
"Kheee kwahiyo ni kweli kuwa wale watoto ni wa Jeff?"
"Ndio ni kweli"
Baba Sabrina akainuka mikono juu na kusema,
"Asante Mungu imekuwa kweli maana nilikuwa na mawazo sana yani sikuwa na raha. Sasa kwanini walificha mapenzi yao kwa kipindi chote hiki?"
Mdogo wa Sabrina akawaelezea sababu ya wao kuficha na jinsi Jeff anavyotamani kuishi na Sabrina.
Kwakweli wazazi wa Sabrina hawakuwa na tatizo juu ya hili ingawa ni maswali machache yaliyowasumbua.
Sam na mama yake mdogo kama ambavyo walivyopanga, walijiandaa kisha safari ya kuelekea kwakina Sabrina ikaanza huku huyu mama akiwa amemshika mtoto Cherry.
Wazazi wa Sabrina pamoja na mdogo wa Sabrina wakiwa sebleni ikabidi wamwambie mdogo wa Sabrina akamuite Sabrina ili waweze kupanga mkakati wa kufanya kuhusu kile walichozungumza.
Mdogo wa Sabrina akaenda kumuita Sabrina, muda kidogo akaja nae sebleni.
Walipokuwa sebleni ndio huo muda ambao Sam alifika na mama yake pamoja na Cherry.
Ila Cherry alipomuona Sabrina tu alimkimbilia kumkumbatia ila Sabrina alimsukuma yule mtoto na kumfanya aanguke chini na kubamiza kichwa.
Wazazi wa Sabrina pamoja na mdogo wa Sabrina wakiwa sebleni ikabidi wamwambie mdogo wa Sabrina akamuite Sabrina ili waweze kupanga mkakati wa kufanya kuhusu kile walichozungumza.
Mdogo wa Sabrina akaenda kumuita Sabrina, muda kidogo akaja nae sebleni.
Walipokuwa sebleni ndio huo muda ambao Sam alifika na mama yake pamoja na Cherry.
Ila Cherry alipomuona Sabrina tu alimkimbilia kumkumbatia ila Sabrina alimsukuma yule mtoto na kumfanya aanguke chini na kubamiza kichwa.
Wote mule ndani wakamshangaa Sabrina kwa kile kitendo, mama mdogo wa Sam alikuwa wa kwanza kumuokota yule mtoto pale chini ambapo alitoa kilio kikali cha gafla na kuwa kimya.
Kwakweli kile kitendo kiliwaumiza wote mule ndani na kumuhurumia yule mtoto.
Mama mdogo wa Sam hakutaka kuongea sana ila alikuwa akifanya maombi tu dhidi ya yule mtoto kisha Sam akamuomba mama yake kuwa wampeleke mtoto hospitali kwani hata yeye huruma ilimuingia dhidi ya mtoto huyo kutokana na kile kilichofanywa na Sabrina.
Safari ya kumpeleka Cherry hospitali ikaanza huku Mama Sam akiwa kambeba Cherry mikononi huku akiambatana na baba Sabrina pamoja na mdogo wa Sabrina.
Mama Sabrina ndiye aliyebaki mule ndani huku akiendelea kumshangaa mwanae kwakile alichokifanya, kisha akamuuliza kwa masikitiko sana,
"Sabrina mwanangu, kwanini umefanya vile kwa mtoto wako mwenyewe? Unajua kama akifa yule damu yake itakulilia maisha yako yote!"
Sabrina alikaa chini huku akitetemeka kwani hata yeye binafsi uoga ulimshika kwa kile kitendo, kisha akajiuliza alikopata ujasiri wa kumsukuma yule mtoto.
Mama yake nae alikazana kumdadisi ili aweze kujua mbivu na mbichi.
"Una matatizo gani kwani Sabrina? Umeanza kuchanganyikiwa au ni kitu gani jamani? Umepata wapi ujasiri wa kumsukuma mtoto kiasi kile? Nani kakupa huo ujasiri mwanangu!"
Sabrina alikuwa kimya tu kwani hata machozi yalionekana kumtoka pale chini.
"Ongea Sabrina, una matatizo gani?"
Sabrina alijibu huku akilia,
"Sielewi mama, yani sijielewi kabisa hata sijui nina matatizo gani mama yangu. Simuelewi huyu mtoto mama ananichanganya kwakweli"
"Anakuchanganyaje mtoto wako mwenyewe Sabrina?"
"Mama, ni kweli huyu mtoto nimemzaa mwenyewe ila simuelewi. Huyu mtoto sio binadamu wa kawaida mama yangu"
"Kheee Sabrina, hebu acha hayo maneno mwanangu yani mtoto mdogo yule unasema sio binadamu wa kawaida kweli! Sasa ni binadamu gani kama sio wa kawaida ni mchawi au ni nini? Na hata kama ni mchawi, sasa huo uchawi kautoa wapi? Hata hivyo mtoto mdogo kama yule atakuwaje mchawi? Sabrina mwanangu, damu ya yule mtoto itakulilia kila siku inayoitwa leo, tumuombe tu Mungu yule mtoto apone awe mzima kabisa. Si jambo jema kumchukia mtoto uliyemzaa mwenyewe au kwavile baba yake amekukosea basi ndio umchukie mtoto. Hapana kwakweli, haipaswi kuwa hivyo."
"Najua wote mtaongea vibaya kuhusu mimi ila ni kwavile tu hamjui kinachoendelea juu yangu, hamjui ni mambo gani hunitokea juu ya yule mtoto. Kwakweli kitendo nilichofanya kinaniuma sana tena sana kwani kiukweli nimefanya bila ya kudhamilia yani imetokea tu na kujikuta nikifanya vile. Mungu amsaidie mwanangu ingawa sielewi kwanini mtoto huyu ananitenda hivi"
Sabrina alionekana kuingiwa na moyo wa huruma sana hata mama yake alimuhurumia pia na kuona ni wazi kuwa mtoto wake amechanganyikiwa kwa kipindi hiko.
Walifika hospitali na moja kwa moja walienda kwa daktari ambapo alimpima mtoto na kumpiga picha ya ubongo.
Majibu waliambiwa kuwa damu inaonekana kuvilia na vitu vimechanganyika kwenye ubongo, daktari akawaambia
"Huyu mtoto inaonekana amebamiza sana kichwa, kwakweli hali ikiendelea hivi anaweza akawa tahira ila mshukuru Mungu tu kuwa amepona maana bila ya hivyo ingekuwa habari nyingine hapa"
Mama mdogo wa Sam akadakia,
"Naimani na Mungu ninayemuomba, huyu mtoto atapona kabisa"
Daktari nae akasema kwa kebehi,
"Kama una imani mbona umekuja hospitali? Kwanza huyu mtoto wenu labda tumfanyie operesheni ndio apone"
Baba Sabrina akashangaa sana,
"Kheee operesheni ya kichwa?"
"Ndio, ulijua ni ya mguu!"
Sam hakupendezewa na majibu ya huyu daktari kisha akawaomba kuwa waende hospitali nyingine ambapo wote walikubaliana na hilo na kutoka.
Ila walipokuwa kwenye gari, mama mdogo wa Sam alionekana kuomba kwa uchungu sana dhidi ya yule mtoto kwani hata yale majibu ya yule daktari yalimuumiza na kumfanya apatwe na uchungu zaidi.
Muda kidogo wote wakashangaa kumuona Cherry akiamka na kukaa tena alionekana kuwa mzima kabisa.
Mama mdogo wa Sam alikuwa na kauli moja tu mdomoni mwake kwa muda huo, neno la kumshukuru Mungu tu.
Wote walikuwa wakishangaa mtoto kuonekana mzima kabisa.
Ingawa mama mdogo wa Sam aliwaomba kuwa warudi nyumbani ila bado Sam hakuwa na imani kuwa yule mtoto kapona kweli na moja kwa moja akaendesha gari kuelekea hospitali nyingine.
Sabrina akiwa na mama yake, aliamua kuinuka sasa na kuelekea chumbani kwake.
Aliingia vizuri na kukuta mwanae wa kiume ameamka huku akicheza cheza kitandani kanakwamba kuna mtu anacheza naye.
Sabrina alimuangalia mwanae huyo kisha akaenda kukaa nae pembeni ila alipoangalia mbele yake alimuona Cherry akitabasamu na kufanya ashtuke sana kisha Cherry akamwambia,
"Nilikwambia nizoee mama ukawa mbishi, unaona sasa ulichokifanya leo? Mimi huwezi kunifanyia vile, siku yoyote utakayopata ujasiri wa kunipiga au kuniua jua kwamba utakuwa umemdhuru mwanao na sio mimi. Kamwe huwezi kupata ujasiri wa kunidhuru mimi, unionavyo mimi ni zaidi ya unijuavyo kwahiyo kuwa makini sana."
Sabrina alikuwa akitetemeka tu kwani hata raha ya maisha kwake ilitoweka gafla, ila huyu Cherry aliendelea kuongea,
"Unatakiwa unizoee Sabrina. Nizoee mimi ila leo nina hamu ya kula tena hamu yangu ni ya kula damu. Kwavile kuna mtu kajiweka kuliwa basi sina budi kwenda kummalizia. Ila kuwa makini, huenda akawa mwanao au wewe mwenyewe"
Huku akicheka sana, Sabrina hakuweza kustahimili na kutaka kukimbia ila akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Walienda hospitali nyingine sasa tena kwa daktari moja kwa moja, wakamuelezea daktari huyu kama walivyomuelezea daktari wa mwanzo kuwa yule mtoto alianguka.
Kisha daktari akampima huyu mtoto vipimo vile vile alivyopimwa akiwa hospitali ya mwanzo.
Ila majibu ya huku yalikuwa tofauti kabisa hata picha ya huku ya ubongo ilikuwa tofauti kabisa,
"Mnasema kuwa huyu mtoto alianguka?"
"Ndio na kuna hospitali tumetoka daktari kasema labda afanyiwe operesheni."
"Jamani, huyu mtoto anaonyesha kutokuwa na jeraha lolote lile. Na picha hii hapa, angalieni ubongo wake unaonekana kuwa sawa kabisa. Hana tatizo kabisa huyu mtoto jamani"
Ilibidi wakubaliane na daktari kuwa huyu mtoto ni mzima kama ambavyo walivyoambiwa.
Kisha wakarudi kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani.
Kwakweli hata baba Sabrina nae alionekana kushangazwa sana na kile kilichotokea siku hiyo,
"Jamani kwakweli Mungu mkubwa sana mmh haya mambo ya leo haya duh."
Kila mmoja alimshukuru Mungu, hata Sam alijikuta akimuangalia mama yake na kumwambia,
"Mama, kumbe Mungu anaweza kufanya chochote!"
"Mungu ni mkubwa mwanangu, tunatakiwa tumtumainie yeye"
Baada ya hilo jibu, Sam akaamua kubadilisha mada kwani alimfahamu vizuri mama yake huyo kuwa angeanza mahubiri hapo muda sio mrefu.
Mama Sabrina akiwa ametulia, alifika Jeff na kumkaribisha.
"Karibu sana Jeff"
"Asante mama"
"Kheee sio bibi tena!! Ila hakuna tatizo, usiwe na shaka yoyote Jeff tutakuwa nawe bega kwa bega hadi mwisho ilimradi tu tumeujua ukweli wa mambo yote kwahiyo usiwe na wasiwasi"
Jeff akatabasamu tu kwani alipendezwa na yale maneno ya mama mkwe ukizingatia alianza kukata tamaa ya mapenzi yake kwa Sabrina.
Ila mama Sabrina aliendelea kumdadisi Jeff,
"Ila unampenda sana Sabrina?"
"Ndio mama, nampenda sana"
"Ila usingekuwa na uwezo wa kumtolea mahali kipindi kile, shukuru Mungu Sam amekusaidia kuficha aibu yako"
"Ila Sam ni kaka yake na Sabrina"
"Kwa mfano asingekuwa kaka yake ungefanyaje?"
Jeff alikaa kimya kwa muda kidogo kwani hata yeye hakujua kuwa ingekuwa si kaka yake angefanyaje ila alipotulia kidogo akajaribu kujibu,
"Sijui ningefanyaje ila nampenda sana Sabrina"
"Sikia Jeff, katika maisha kila kitu hutokea kwasababu fulani kwahiyo yote yaliyotokea yalikuwa na sababu. Ila kwanini siku zote hizi umekuwa ukituficha? Kwanini hukutaka kusema ukweli?"
"Nilitamani sana kusema ukweli ila sikuweza kwavile sikutaka kumkwaza Sabrina kwavile ni kweli nilikuwa na mapenzi ya dhati kwake. Ilinifanya nikubali kile alichokitaka yeye"
"Na kwanini yeye hakutaka tujue?"
"Alikuwa anasema kuwa ni aibu na hakujua vile ambavyo mngechukulia baada ya kujua ukweli"
"Ila ni kweli, hata sijui tungemchukuliaje pale mwanzoni mmh!"
Mama Sabrina na Jeff leo walijikuta wakiongelea mambo mbali mbali haswa ya kuhusu mahusiano ya Jeff na Sabrina.
Daktari aliyekuwa anashushuana na wakina Sam, akiwa amekaa ofisini kwake akafika mgonjwa wa kike na kupanda kitandani.
Daktari akamshangaa yule mgonjwa ni vipi kapanda kitandani bila ya kuambiwa,
"Vipi wewe mdada unafika tu na kupanda kitandani, nani kakwambia sasa."
Ila yule mdada alimuangalia tu daktari na kutabasamu, kitendo hicho kilimkera daktari na kumuamuru yule dada atoke nje ila gafla yule dada akabadilika sura na muda huo huo akawa Cherry pale kitandani na kumfanya daktari ashtuke sana.
Kisha yule Cherry akamwambia daktari,
"Njoo unifanyie hiyo operesheni nimekuja sasa"
Daktari akaogopa sana na kutaka kukimbilia nje ila alipojaribu kufungua mlango akagundua kuwa umefungwa na kumfanya azidi kutetemeka.
Cherry aliinuka na kumsogelea karibu, kisha akamgusa na kumfanya yule daktari aanguke pale na kuwa kimya kabisa.
Nesi wa kwanza kuingia kwenye kile chumba cha daktari baada ya tukio alipata mshtuko na kuita watu ila yule daktari alipopimwa iligundulika kuwa tayari amesha kufa kitambo sana.
Mama Sabrina akiendelea kuzungumza na Jeff pale ndipo Jeff alipoulizia uwepo wa Sabrina,
"Kuna makubwa yametokea hapa Jeff yani hata hayaelezeki, hata Sabrina tulikuwa nae hapa sebleni"
"Makubwa gani hayo tena?"
"Kwakweli ni makubwa, hata kama nikijaribu kukuelezea najua nitakuchanganya tu akili yako ila jua kwamba yaliyotokea hapa ni makubwa."
Jeff alihitaji sana kujua kilicho tokea hivyo alikazana kumuuliza mama Sabrina kilichotokea ila mwisho wa siku mama Sabrina aliamua kumueleza ukweli Jeff na kumfanya ashtuke sana.
Wakina Sam wakiwa wanarudi, Sam aliamua kupitia kwanza kwenye ile hospitali ya awali ili akamshushue yule daktari kwa yale majibu ambayo aliwapa.
Ila walipofika pale hospitali hakuna aliyetaka kushuka kwani mtoto alishapona ila Sam alishuka na moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha yule daktari.
Akashangazwa kuona watu wamejaa eneo lile na alipouliza moja kwa moja alijibiwa kuwa yule daktari amekufa.
Kwakweli Sam akashtuka kisha akaona kama taswira ya Cherry ikikatisha kwenye hospitali ile moja kwa moja akapata jibu ya juu ya kile kilichompata yule daktari.
Kwahiyo Sam akarudi kimya kimya kwenye gari, kitu hicho kilifanya wamuulize kile kilichotokea,
"Vipi tena mbona kama umenyong'onyea?"
"Yule daktari kauwawa"
Wote wakashtuka na kuuliza kwa mshangao,
"Kauwawa?"
"Ndio"
"Kivipi?"
"Sijui ila nimeambiwa kuwa amekufa"
Wakatazamana kwa zamu, kisha Sam akatoa gari eneo hilo na kuelekea kwakina Sabrina.
Walipofika kwa kina Sabrina wakamkuta mama Sabrina akimsimulia Jeff juu ya kile kilichotokea ila alipowaona alifurahi sana kwani ilikuwa kama muujiza kwake kwa mtoto kurudi mzima kabisa kwa siku hiyo.
Waliingia na kukaa ila kwa furaha ile mama Sabrina aliamua kwenda chumbani kwa Sabrina ili akamuite kuwa mtoto kapona.
Ila alipoingia tu chumbani kwa Sabrina alishangaa kumuona yupo chini.
Na alipojaribu kumgeuza, alimkuta Sabrina damu zikimtoka mdomoni.
Walipofika kwa kina Sabrina wakamkuta mama Sabrina akimsimulia Jeff juu ya kile kilichotokea ila alipowaona alifurahi sana kwani ilikuwa kama muujiza kwake kwa mtoto kurudi mzima kabisa kwa siku hiyo.
Waliingia na kukaa ila kwa furaha ile mama Sabrina aliamua kwenda chumbani kwa Sabrina ili akamuite kuwa mtoto kapona.
Ila alipoingia tu chumbani kwa Sabrina alishangaa kumuona yupo chini.
Na alipojaribu kumgeuza, alimkuta Sabrina damu zikimtoka mdomoni.
Mama Sabrina akashtuka sana na kuanza kupiga kelele, kitendo kile kiliwafanya wote wakimbilie kule chumbani na wote wakastaajabu kumuona Sabrina pale chini.
Wakati wakitaka kufanya harakati za kumkimbiza Sabrina hospitali, kuna kitu kiliongea kwenye akili ya mama Sam na kuwaomba wamuache amuombee nao walifanya hivyo ingawa kwa imani hafifu sana.
Walirudi sebleni huku wakiwa na mawazo juu ya Sabrina, na muda kidogo mama mdogo wa Sam alirudi na Sabrina pale sebleni na kufanya wazidi kushangaa huku wakimshukuru, ila akawaambia
"Hapana, hampaswi kunishukuru mimi ila mnapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu wa mbinguni aliyeniongoza mimi."
Wakatulia kimya na kumsikiliza ambapo aliendelea kuongea,
"Hii nyumba inaonekana kuwa na mapambano sana, hii nyumba ni nzito kwakweli"
Kisha akamtazama mama Sabrina na kumwambia,
"Wewe mama, unaonekana ulikuwa ni mwombaji mzuri sana, kipi kimekurudisha nyuma? Nini tatizo jamani? Niangalieni mimi, nimepitia vingi sana sikuwa mtu mwema ila tangu nimetambua kuwa yote ninayofanya hayana faida kwangu ndipo nilipoamua kumrudia Mungu wangu, hadi sasa. Haijalishi nimekumbwa na mangapi haijalishi watu wananisema vipi ila ninachojali ni Mungu ananionaje mimi. Unatakiwa kumrudia Mungu wako, usijibweteke dada yangu haya maisha tunapita tu."
Mama Sabrina alikuwa kimya kabisa kwani yote aliyoambiwa yalimuingia kwenye akili yake na yalikuwa ni maneno yenye ukweli mtupu kwani akifikiria alivyokuwa mwanzoni na alivyosasa ni kweli alikuwa amebadilika tena amebadilika sana kwani swala la kuomba kwake lilimpitia kushoto kabisa kwa kipindi hiko.
Sam nae alipoona mahubiri yamenoga ikabidi aingilie kati ili aweze kumkatisha mama yake mdogo huyo kwani hata muda nao kiukweli ulikuwa umeenda kutokana na mambo yaliyofanyika siku hiyo,
"Inatosha mama, muda nao umeenda sana. Bora tufanye kilichotuleta kisha tuondoke."
"Usinikatishe Sam tafadhari, hii ni kwaajili ya faida ya watu wote hapa. Kila mmoja hapa anatakiwa kujua umuhimu na uwepo wa Mungu wetu"
Sam akawa anapatwa na hasira tu kwani mama yake alikuwa ndio kama vile anachochewa kuongea, ikabidi Sam aongee tena
"Mama, ila kumbuka kuwa kesho tunatakiwa kusafiri. Tafadhari tumalizie kilichotuleta tuondoke"
"Sam, siwezi kuondoka mwanangu. Haya mambo yanatakiwa tuwekane sawa. Najua ni Mungu tu aliyeamua haya niyagundue mimi. Na kama nisipoyasema mimi unadhani ni nani atakayeweza kusema!"
Sam akainuka sasa kwani aliona ni longo longo tu, kisha akamwambia mamake mdogo
"Ukimaliza kuwahubiria hapo utanipigia simu"
Kisha akatoka nje na kuondoka, wote walimtazama tu bila ya kumuuliza chochote kile.
Sam aliondoka pale na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwake ambapo alimkuta Cherry ndani na kumfanya atabasamu,
"Nilijua tu kuwa lazima utarudi"
"Nisingeweza kumsikiliza yule mwanamke na hoja zake"
"Na ana bahati sana, namuonea huruma kumdhuru sababu ni mama yako"
"Kheee hadi yule kumbe unamuweza?"
"Kwanini nimshindwe sasa? Hakuna ambaye simuwezi ila sijamuamulia tu, namuonea huruma kwavile ni mama yako"
"Kwakweli hata mimi ananikera jamani ila ndio hivyo ni mama. Unajua nilishangaa ulivyohama na nyumba kwaajili yake, nikajua umemuogopa. Yani bado kidogo niungane na imani yake"
"Ukithubutu kufanya hivyo jua kwamba utakufa, yule nimemuhurumia tu kwani muda wowote nikihitaji nammaliza. Umeona nilichofanya kwa daktari?"
"Nimeona ndio, kwisha habari yake"
"Si nilikwambia lakini kuwa mimi nina uwezo mkubwa sasa, ila ni bora ukiwa unaniona hivi kwa umbo la mtoto wenu ingawa yule mama amemshikilia yule mtoto"
Sam aliongea na huyu Cherry huku akijiaminisha kwa kila kitu alichoongea nae kwani alimuona yupo sahihi sana.
Ila alimuomba jambo moja.
"Naomba ukasambaratishe kile kikao chao basi"
"Hilo tu! Hakuna tatizo ila kabla sijafanya hivyo nenda kanitafutie damu"
"Hakuna tatizo pia"
Kisha Sam akatoka na kuondoka zake.
Pale kwakina Sabrina, yule mama mdogo wa Sam aliendelea kuwahubiria na kuwaambia kile anachokihisi kuwa kipo kwenye nyumba hiyo,
"Kwanza hii nyumba imetawaliwa na roho ya mauti, yani msipokuwa makini na kusimama imara basi mtajishangaa mkiteketea. Mnajua si kitu kizuri kumkuta mtu ameanguka chini bila sababu tena huku damu ikimtoka. Kwahiyo mnatakiwa kuwa makini sana."
Sabrina nae akadakia,
"Kwakweli hata mimi sitaweza kuendelea kuishi humu ndani kwani nako napaona pabaya kama nyumba niliyotoka"
Mama Sabrina akamuuliza mwanae kwa mshangao,
"Sasa utaenda kuishi wapi mwanangu?"
Jeff akadakia,
"Bora akaishi kwetu maana kwetu ni salama"
Mama Sam akawaangalia na kuendelea kuwaambia,
"Kukimbia nyumba si tatizo, ila tatizo ni kuwa hamumkaribishi Mungu katika maisha yenu."
Akamuangalia tena mama Sabrina na kumwambia,
"Wewe mama, rudi kwenye mstari wako wa mwanzo. Rudia tabia yako ile ya mwanzo, rudi kwa Mungu wako ili uokoe familia yako. Jamani mimi naomba niendelee kuwa karibu na huyu mtoto kwani moyo wangu ni mgumu sana kumuacha popote"
Sabrina akasema,
"Ila huyo mtoto ndio tatizo"
"Hapana, huyu mtoto si tatizo ila tatizo ni hayo mawazo yenu yanayowaza kuwa huyu mtoto ni tatizo, au labda mimi ndio sielewi kitu. Hebu jaribuni kunielewesha kuwa kwanini mseme kwamba huyu mtoto ni tatizo"
Sabrina alitulia kidogo na kupata ujasiri wa kujibu,
"Yani kwanza hapo, siwezi hata kumshika ingawa ni mtoto wangu mwenyewe kwani nahisi kamavile atanigeukia"
Kisha Sabrina akawaeleza jinsi ambavyo huwa akitokewa na mtoto huyo kwenye mazingira ya kutatanisha na jinsi ambavyo huwa akiongea.
Wote walisikiliza maelezo ya Sabrina na kustaajabu sana kwani hakuna aliyeweza kufikiria kwa haraka haraka kuwa hali imefikia kiasi kile hata mama mdogo wa Sam nae alishangaa na kuona kuwa hali hiyo ni ya utata,
"Mnajua nini, hata dada yangu kule Arusha alinieleza hayo ila tangu nimefika na kuishi na huyu mtoto nimemuona ni wa kawaida tu. Ila kwa maelezo yako inaonekana kuwa kuna nguvu za giza kali sana zimetawala kwenye maisha yenu, haswaa maisha yako wewe Sabrina. Kiuhalisia saizi ni usiku sana ila nina uhakika kuwa hakuna anayetamani kulala baada ya maelezo yote haya. Sasa kwa faida yetu na kwa usiku huu, kama mjuavyo kuwa usiku huwa na mapambano makali sana. Nawaomba jamani tuombe kwa pamoja"
Wakatazamana kwa zamu ila kila mmoja alishindwa kukataa kwavile walishaingiwa na hofu ila walimuacha mama mdogo wa Sam aombe yeye mwenyewe kwanza.
Sam akiwa anaelekea kwenye hoteli ili akaangalie wa kumlaghai kwa usiku huo, na kwa bahati alimkuta binti njiani aliyeomba lifti naye akampakiza.
Ila akiwa anaelekea mahali sasa akakamilishe adhma yake, simu yake ikaita.
Akaangalia mpigaji, alikuwa ni mama yake mdogo.
Kidogo sura ya Sam ikabadilika kwani aliona kuwa muda umeenda sana sasa kupigiwa simu na huyo mama yake akaona kama ni kumuharibia mipango yake tu, ila akaipokea
"Njoo unichukue sasa"
"Kwahiyo umeshamalizana nao hapo?"
"Ndio njoo unichukue"
Sam ikabidi awe mpole tu na kuamua kuelekeza gari yake kule pa kumfata mama yake.
Akamuangalia yule binti na kumuona kuwa ni wazi kaponea kwenye tundu la sindano,
"Nitakushusha hapo mbele ila nitakupa pesa upande gari ya kukodi uelekee huko kwenu"
"Nashukuru sana kaka yangu na Mungu akubariki"
"Na usipende kuomba omba lifti, kuna watu wengine ni wabaya na wanaweza kukufanyia vitu vibaya"
Sam akasimamisha gari na kumpatia yule dada pesa ili achukue usafiri wa kukodi ambapo yule dada alimshukuru sana Sam kisha kumuomba mawasiliano yake.
Sam akatoa kadi yake ya biashara na kumkabidhi yule dada,
"Asante sana, nikikupigia nitajitambulisha kwa jina la Emmy. Nashukuru sana kaka yangu"
"Haya Emmy kwaheri"
Yule dada akaondoka huku Sam akifanya safari ya kwenda kumfata mama yake mdogo huku akimtafakari yule mdada jinsi alivyopata bahati ya kuachiwa bila ya jereha lolote lile wakati alikuwa kwenye hatua ya mwisho kumaliziwa.
Ila kwavile yule dada alichukua mawasiliano ya Sam, moja kwa moja Sam akatambua wazi kuwa lazima huyo mdada atamtafuta tu na ataingia kwenye mtego wake.
Mama mdogo wa Sam alimalizia kuagana na wale ndani baada ya kusikia gari ya Sam nje,
"Jamani kesho nitakuja kuongea nanyi tena"
"Ila si tulisikia kama Sam anasema kuwa unasafiri?"
"Ni kweli nilitaka kusafiri ila naona kuwa bado kuna umuhimu wangu wa kuzungumza nanyi"
Kisha Sam alisogea pale karibu na kumwambia mama yake kuwa muda umeenda aache maongezi na waondoke.
Huyu mama alimbeba yule mtoto Cherry kwani alikuwa amelala sasa kisha wakapanda gari na safari ya kuelekea kwa Sam ikaanza.
Ila huyu mwanamke aliweza kuisoma akili ya Sam kwa haraka sana,
"Unajua Sam una matatizo wewe, ila kwanini hutaki kuniambia? Kwanini hunielezi ukweli? Je kuna mtu uliyempata wa kumueleza siri zako? Napaswa kujua mengi sana kuhusu wewe"
"Utayajua tukifika Arusha"
Huyu mama hakutaka kuongea zaidi kwani aliweza kugundua akili ya Sam kuwa kuna kitu kinasumbua akili hiyo.
Nyumbani kwakina Sabrina, bado Sabrina alishikilia wazo lake la kutokulala humo.
Naye Jeff akakazania kuwa akalale nyumbani kwao kwani alipaona ni salama zaidi ila kiuhalisia hata yeye alikumbuka siku ambayo alimkuta Cherry kakaa sebleni ila alimkazania Sabrina kuwa akalale kwao ili angalau apate kampani.
Kwavile Sabrina aling'ang'ania basi wazazi wake hawakuwa na pingamizi lolote juu ya hilo na kuwaruhusu tu.
Kisha Sabrina akambeba yule mwanae mdogo mgongoni na kuelekea kwakina Jeff.
Walipofika, Jeff alifungua mlango kwa mashaka ila hapakuwa na mtu kwani wengine walilala na hata yule wa mauzauza hakuwepo pia.
Kwakweli Jeff akapumua kwa hilo kisha akaelekea na Sabrina chumbani kwake ambako nako palikuwa salama.
Jeff akatabasamu tena kwani moyoni mwake katika siku ambazo alikuwa na furaha basi ilikuwa ni siku hiyo kwani ni siku aliyoitamani siku zote katika maisha yake.
Siku ya kuweza kulala na Sabrina huku wakimuweka mtoto wao katikati yao.
Na jambo la kwanza kulifanya alipoingia na Sabrina chumbani ilikuwa ni kumkumbatia Sabrina ambapo Sabrina alijihisi kusisimka mwili mzima. Kisha Sabrina akamwambia Jeff,
"Tafadhari tujihadhari tusijeleta mtoto wa tatu tena"
Jeff nae akajibu kwa ujasiri,
"Hata akija hakuna tatizo, ila uzuri ni kwamba nitakuwa huru na wewe tofauti na mwanzo. Nakupenda sana Sabrina"
Kisha Jeff akamkumbatia tena Sabrina, halafu wakaelekea kulala.
Jeff hakutaka kuipoteza ile furaha kwa kumsumbua Sabrina kwani alihitaji ile furaha kuwa iwe ndio furaha yao ya siku zote.
Sam alifika na mama yake nyumbani na kuingia nae ndani, kisha kwa usiku ule ule akamwambia mama yake
"Kesho safari si ndio mama"
"Hapana Sam, bado sijamaliza mambo yangu"
"Mambo gani hayo mama? Unajua sitaki kukuacha kwani najua mwisho wa siku utanilaumu. Kwanini hupendi kunisikiliza mama jamani!"
"Basi ni vyema tukasikilizana kesho juu ya hilo. Ila kwa saizi naomba tuombe kwa pamoja ili tukalale kwa amani"
"Aah mambo gani hayo? Omba mwenyewe"
Kisha Sam akaelekea chumbani kwake na kumuacha mama yake pale mwenyewe na mtoto ambapo aliomba kisha akaenda kulala na mtoto huyo.
Kulipokucha Jeff alikuwa wa kwanza kuamka na moja kwa moja macho yake yalielekea kumtazama Sabrina aliyekuwa amelala huku kamkumbatia yule mtoto wao mdogo na kumfanya Jeff atabasamu.
Ila gafla akajihisi kuwa hata yeye kamkumbatia mtoto, alipotahamaki na kumuangalia mtoto aliyemkumbatia yeye alikuwa ni Cherry.
Kulipokucha Jeff alikuwa wa kwanza kuamka na moja kwa moja macho yake yalielekea kumtazama Sabrina aliyekuwa amelala huku kamkumbatia yule mtoto wao mdogo na kumfanya Jeff atabasamu.
Ila gafla akajihisi kuwa hata yeye kamkumbatia mtoto, alipotahamaki na kumuangalia mtoto aliyemkumbatia yeye alikuwa ni Cherry.
Jeff alishtuka sana ambapo hata yule Cherry naye aliamka halafu akakaa huku akimuangalia Jeff na kutabasamu kisha akamuuliza,
"Unashtuka nini? Hujafurahia kulala pembeni na mtoto wako wa kwanza?"
Jeff hakuweza kujibu kwani hofu kubwa ilimtawala moyoni mwake, akataka kumuamsha Sabrina ila huyu Cherry alicheka na kumwambia,
"Huyo unayetaka kumuamsha hapo alipolala hawezi kuamka bila ridhaa yangu, ninachotaka ufanye sasa ni uchukue simu yako na umpigie simu Sam"
Jeff akashtuka kuwa atampigiaje simu Sam na ampigie amueleze nini.
Jeff akawa kama ameganda na kutamani ile iwe ni ndoto.
Alijikuta akimuangalia tu huyu Cherry bila ya kufanya chochote ambapo huyu Cherry alichukua simu ya Jeff na kumkabidhi kisha kumuamrisha tena kuwa ampigie simu.
Jeff akiwa anatetemeka, akachukua ile simu ila kabla ya kupiga akamuuliza Cherry,
"Nimwambie nini?"
Cherry akacheka na kusema,
"Mwambie kuwa leo umelala na Sabrina"
Jeff akazidi kukosa raha na kushindwa hata kufanya chochote ambapo mtoto huyo alimuita tena Jeff kwa kumshtua,
"Jeff!"
Jeff alishtuka sana na kukosa hata ujasiri wa kumtazama tena huyu Cherry kisha akamwambia,
"Hivi unajua kama maisha ya mama yako yapo mikononi mwangu? Unajua kuwa nina uwezo wa kuamuru chochote dhidi ya mama yako na kikafanyika? Nisikilize mimi, fanya ninachosema mimi ufurahi, kiuka ninachosema ulie maisha yako yote. Haya mpigie simu Sam muda huu, hili si ombi bali ni amri"
Jeff aliamua kupiga ile simu ambapo iliita kwa mara ya kwanza bila ya kupokelewa na kuamua kuipiga tena.
Muda huu Sam alikuwa bafuni akioga huku akitafakari cha kufanya ili aweze kumshawishi mama yake ili amsafirishe kwani pale aliona akimzuia mambo mengi sana.
Wakati simu yake ikiita alikuwa bado akioga na kuona ni vyema amalize kwanza kuoga ndipo akaipokee simu hiyo.
Alipomaliza alivaa na kuchukua simu yake kisha akaangalia mpigaji, akaona kuna simu kama tano ambazo hazikupokelewa.
Moja wapo ilikuwa ni namba mpya na zingine zilionekana kuwa ni za Jeff,
"Aah huyu dogo anafanya matatizo halafu anaanza kunitafuta, ngoja nianze na namba mpya kisha nitampigia badae."
Sam alianza na ile namba mpya aliyoikuta kwenye simu yake ambapo aliipiga na ule upande wa pili ilipokea sauti ya kike,
"Hallow Sam, Emmy anaongea hapa"
"Emmy! Emmy yupi?"
"Ulinikuta usiku njiani, nilikuwa na shida ukanipa lifti. Wakati wa kushuka ukanipa namba yako."
"Aah nimekukumbuka tayari, mambo vipi?"
"Poa tu, samahani tunaweza kuonana?"
"Bila samahani Emmy, hilo halina tatizo niambie ulipo nikufate"
Basi Emmy akampa maelekezo Sam kisha wakaagana kwenye simu na kukata ile simu.
Sam alitabasamu kwani aliona jambo lake likiwa limetiki tena bila ya jasho,
"Nilijua tu kuwa huyu binti lazima anitafute tena, mimi ndio Sam bhana hakuna mwingine. Na huyu binti lazima atimize azma yangu kwani bila ya hivyo sitakuwa na cha kumjibu Cherry"
Sam akajiandaa kutoka na kusahau kabisa swala la kumpigia simu Jeff kwani mawazo yake kwa muda huo yalikuwa ni juu ya huyo Emmy tu na ukizingatia kamtafuta mwenyewe basi akaona ndio njia rahisi ya kumpata.
Sam alipotoka sebleni alimkuta mama yake mdogo akiwa pale amekaa akamsalimia kisha akamuaga,
"Mama, tutaonana badae"
"Mungu akutangulie uendako mwanangu"
"Mmh mama nawe kila kitu Mungu Mungu, kwakweli umezidisha sasa."
"Lakini Mungu ndio tegemeo letu mwanangu, Mungu ana upendo, ana huruma na na anatujali"
"Aah huyo Mungu angekuwa na huruma si angekupa mtoto"
Mama mdogo wa Sam akasikitika sana na kumwambia Sam,
"Usiseme hivyo kila kitu Mungu hufanya kwa makusudi yake, hatupaswi kumkufuru"
"Aah unanichosha na porojo, jiandae kesho safari"
Hapa sasa Sam hakutaka hata kujua kuwa mama yake atasema nini tena kwani alitoka na kuondoka.
Huyu mwanamke alimsikitikia Sam kwani alimuona ni mtu anayefanya kitu bila kujua ubaya wake.
Alijikuta akiomba msamaha kwa niaba ya Sam,
"Eeh Mungu msamehe huyu maana hajui atendalo"
Ila roho yake iliumia sana kwani alitamani Sam aamini vile ambavyo yeye anaamini.
Jeff alikuwa bado kwenye misukosuko na huyu Cherry kwani alijaribu kujitetea vile hali halisi ilivyo kuwa anampigia simu Sam ila Sam hapokei simu zake.
Na mara ya mwisho kumpigia alikuta simu ya Sam ikiwa inatumika.
Huyu Cherrya alikuwa na hasira sana na kumwambia Jeff,
"Nadhani wote hamnijui vizuri, ila huyu Sam ananielewa vilivyo na anafanya makusudi. Nikiamua kufanya kitu mimi nawaambia hakuna wa kupona hapa, Sam kaenda kinyume na masharti yangu. Ila leo nahitaji umpate uzungumze nae ndipo nikuachie la sivyo nipo hapa hapa"
Jeff hakuweza kumtazama Cherry ila akaomba jambo,
"Basi niruhusu nimfate huko kwao. Nakuomba tafadhari, nikweli sikujui ila cha kufanya pia sina. Niruhusu nimfate"
"Nakuruhusu"
Kisha huyu Cherry akapotea.
Jeff akatetemeka sana kisha akainuka pale kitandani kama kichaa, akajaribu kumuamsha Sabrina ila hakuamka.
Jeff alivaa na kutoka, akajaribu kumuita mdada wao wa kazi nae hakuitika na kumfanya agundue kuwa bado amelala.
Ila Jeff hakutaka kupoteza muda kwani alijua hata kulala kwao ni kwasababu ya yule yule mtoto.
Jeff alipanda daladala huku akitetemeka sana kwani jibu lililokuwepo kichwani mwake kwa muda huo ni kuwa yule ni jini,
"Mungu wangu, nimeongea na jini. Mungu nisaidie mimi. "
Jeff alikuwa kama mtu asiyejielewa kabisa kwa muda huo.
Sam alifika eneo ambalo alikubaliana kukutana na yule mdada, alimuona akitabasamu mbele yake kisha akasogea na kumsalimia ambapo yule mdada alionekana kumchangamkia sana Sam,
"Aah ndio Emmy eeh!"
"Ndio ni mimi Emmy"
Kisha wakaelekea mahali pa kuweza kukaa na kuzungumza, Sam alikuwa akimuangalia tu huyu dada kwani aliona kama leo amebadilika tofauti na alivyomuona usiku.
Alionekana ni binti mzuri, mrembo, mpole na mstaarabu.
Walifika na kukaa ila macho ya Sam hayakuweza kubanduka kutoka kwa huyu mdada hata ikamfanya huyu mdada atambue hilo na kutabasamu ambapo Sam alizidi kuona uzuri wa huyu dada kwa lile tabasamu lake.
Kisha huyu dada akamuuliza Sam,
"Mbona unaonekana kuniangalia sana?"
Sam hakuweza kuvunga na moja kwa moja akamjibu huyu dada,
"Naangalia huo uzuri wako, tabasamu lako. Kwakweli kuna watu mliumbwa na mkaumbika kweli"
Huyu dada alitabasamu zaidi kwa zile sifa alizopewa na Sam kisha akamwambia,
"Asante, ila pindi ukinizoea utaniona wa kawaida tu. Mimi nipo kawaida ila kikubwa namshukuru Mungu kwa hivi alivyoniumba"
Kisha Sam nae akatabasamu kwani hata yeye alitoa saluti kwa uumbwaji wa yule dada kisha Sam akamuita muhudumu na wakaagiza vinywaji ambapo muhudumu alipoondoka Sam akamuuliza huyu dada,
"Mbona umeagiza juisi? Je hutumii bia au kilevi chochote? Agiza tu usihofu nitalipia"
"Hapana, mimi sio mtumiaji wa kilevi"
"Kwanini sasa?"
"Basi tu huwa situmii"
Sam akajua kuwa hii ni janja ya wanawake kujifanya hawatumii kilevi ili waonekane ni watulivu ila akamuacha atumie kile alichoamua.
Jeff aliposhuka stendi ili aelekee kwakina Sam kwa lengo la kumfata Sam, kuna kitu kwenye akili yake kikamzuia kwenda na kumfanya asimame kwa muda kama mtu anayejifikiria kufanya jambo ila kuna sauti nyuma yake ikamwambia,
"Nenda Jeff , usiache nenda tu."
Sauti hii ikamfanya ashtuke kidogo na kugeuka nyuma ili ajue ni nani.
Na alipogeuka akamuona mdada amemuelekezea mgongo, Jeff akaogopa kumshtua kisha akageuka tena na kuendelea kwenda.
Ila alipofika mbele alijikuta bado akitamani kumtambua yule mdada na kumfanya ageuke tena, alipomuangalia yule mdada alionekana kutabasamu kisha kugeuka kama anaondoka.
Jeff alishtushwa sana na yule mdada na kumfanya hata yeye ageuke nyuma kwa haraka.
Sura ikamjia kichwani na kugundua kuwa ni Amina, uoga ukamshika Jeff na kumfanya ajiulize kuwa kwanini Amina anamfatilia.
"Mungu wangu si amekufa huyu? Nikoje mimi siku hizi au ndio nimekufa ila sijijui?"
Jeff hakutaka tena kugeuka nyuma ila aliendelea mbele tu.
Sam na Emmy waliletewa vinywaji na kuendelea na mazungumzo, kwa mawazo ya Sam ilikuwa ni lazima yule Emmy ametokea kuvutiwa nae na ndiomana hata akaamua kumuita hapa na alijua nia yake ni kutaka kufunguka juu yake, lakini cha kushangaza huyu Emmy alionekana kuleta stori zingine ambazo zilimchanganya kidogo Sam na kumchefua.
"Samahani Sam, kuna kitu kilichofanya niombe kuonana na wewe siku ya leo"
"Bila samahani, niambie tu tatizo ni nini. Nipo tayari kukusikiliza na kukusaidia."
Emmy akatabasamu na kuendelea,
"Jana usiku nimeota ndoto mbaya sana kuhusu wewe"
Hapa palimfanya Sam amshangae huyu Emmy na kumuuliza kwa umakini,
"Ndoto? Kumbe unataka kuniletea habari za ndoto!"
"Ni ndoto ndio ila najua nimeota ili nikusaidie wewe, nimeota kuwa kuna jini lipo kwenye maisha yako yani kila unachokifanya liko pembeni"
Sam akaonyesha kubadilisha sura yake kwani ile mada ilishamchefua tayari,
"Wee binti umetumwa? Nakuuliza umetumwa? Kamwambie aliyekutuma hiki ni kisiki cha mpingo"
Sam akataka kuinuka, ila Emmy akamshika mkono Sam na kumfanya akae tena kwani mguso ule wa mkono wa Emmy ulimfanya Sam asisimke mwili mzima.
Sam alimuangalia machoni Emmy na kumuuliza,
"Una nini Emmy?"
"Sina kitu ila nahitaji kukusaidia"
"Mbona mikono yako ipo hivyo yani kama umenigusa na shoti!"
Emmy akatabasamu na kusema,
"Hapana Sam ila nahitaji unisikilize"
Sam alipomuangalia Emmy machoni alijikuta akinyong'onyea sana kwani kila kilichopo kwa Emmy kilimvutia na kufanya ajiulize moyoni mwake,
"Je nimependa tena?"
Kumbe aliongea kwa sauti bila ya kujigundua, naye Emmy akamjibu
"Ni kweli umenipenda ndiomana umepata uwezo wa kusisimka hivyo, ila huwezi kuwa na mimi bila ya kunisikiliza"
Ndipo Sam alipomuuliza tena Emmy,
"Kwamaana hiyo naweza kuja kuwa mpenzi wako!"
Emmy akatabasamu na kumjibu,
"Ila hautaniua kama wale"
Sam akainamisha macho chini huku akijiuliza kuwa imekuwaje huyu Emmy kuonekana akiyajua mambo mengi yanayomuhusu? Hakupata jibu, akainua tena macho na kumtazama
"Natambua lengo lako usiku lilikuwa ni nini? Ila lisingewezekana kwani mimi nilitakiwa kukutana na wewe ili niweze kufahamu mengi yanayokuhusu"
"Umewezaje kuyafahamu?"
Sam alimuuliza huyu Emmy kwa mashaka kidogo kwani alipenda kujua ni vipi huyu Emmy kafahamu kuhusu yeye.
"Kupitia ndoto Sam, ndoto imefanya nitambue mambo mengi sana kuhusu wewe."
"Ndoto ya usiku mmoja? Na ile usiku ulipatwa na nini hadi ukaomba lifti kwangu Emmy?"
Emmy akatabasamu kisha akamshika bega Sam ambapo Sam alihisi damu ikienda mbio mwilini kwa msisimko alioupata na kujikuta akiuliza swali lingine tena kwa sauti yenye uoga kwa mbali,
"Nitakuwa wako kweli Emmy?"
"Ndio ila ukifanya kile ninachotaka mimi na kunisikiliza"
Sam akamtazama Emmy ambaye naye pia alimtazama, hapa Sam alijihisi akiwa kwenye msisimko zaidi kwa yale macho ya Emmy.
Jeff alifika hadi kwakina Sam ambapo alipogonga mlango alifunguliwa na mama mdogo wa Sam na kukaribishwa ndani.
Jeff aliingia akiwa na wasiwasi sana kitu kilichomshangaza hata mama mdogo wa Sam,
"Mbona unaonekana kuwa na mashaka kiasi hicho?"
"Hapana ila nina shida na Sam"
"Shida na Sam ndio wima wima hivyo! Karibu ukae kisha tuzungumze ili kama yupo nikuitie"
Ikabidi Jeff aende kukaa sasa.
Mama Sam akainuka na kuelekea jikoni ili angalau amletee hata maji na kumtota ule uoga aliokuwa nao.
Muda huo Cherry nae aliamka, na kwavile mlango ulikuwa wazi alishuka kitandani na kuelekea moja kwa moja sebleni.
Jeff kumuona Cherry akapiga kelele na kuinuka ili akimbie ila alipofika mlangoni alijikwaa na kuanguka.
Ikabidi Jeff aende kukaa sasa.
Mama Sam akainuka na kuelekea jikoni ili angalau amletee hata maji na kumtota ule uoga aliokuwa nao.
Muda huo Cherry nae aliamka, na kwavile mlango ulikuwa wazi alishuka kitandani na kuelekea moja kwa moja sebleni.
Jeff kumuona Cherry akapiga kelele na kuinuka ili akimbie ila alipofika mlangoni alijikwaa na kuanguka.
Cherry alisimama tu akimshangaa kwa uoga, na zile kelele za Jeff pamoja na kishindo cha kuanguka zilimfanya mama mdogo wa Sam kutoka jikoni kwa haraka sana ili kuweza kushuhudia kinachoendelea.
Alimshangaa Jeff pale akiugulia maumivu na kumsaidia kumuinua.
"Vipi tena? Nini tatizo?"
Akamsaidia kumuinua na kwenda kukaa nae karibu kwenye kiti huku akiendelea kumuuliza, ila Jeff aliomba kuondoka
"Naomba kuondoka, siwezi kukaa humu"
"Sababu kubwa ni nini?"
"Huyo mtoto"
"Mtoto ana nini? Jamani hebu acheni uchizi wenu jamani, jana mmetupa hekaheka kubwa ya kuhangaika na huyu mtoto mahospitalini huko leo na wewe unaleta habari zako. Kwani hukuwepo jana wakati nawaelimisha? Mtoto ana nini huyu? Ni malaika wa Mungu huyu mtoto jamani, hebu acheni kumpandikiza mambo ambayo hayapo"
Kisha mama mdogo wa Sam akamuangalia Cherry na kumuita kwani alikuwa amesimama kwa uoga sana,
"Njoo mjukuu wangu mwaya"
Cherry alisogea kisha akamuinua na kukaa nae, halafu akamwambia Jeff
"Hebu muangalie kwa makini huyu mtoto, muangalie kama ana dosari yoyote. Jana bila ya Mungu kutusaidia ingekuwa ni hadithi nyingine kuhusu huyu mtoto kwani tungekuwa tumempoteza kwakweli. Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa kuweza kuendelea kumuona huyu mtoto kwa macho yetu tena akiwa mzima kabisa. Haya na wewe mtu mzima eti unamkimbia huyu mtoto na kutaka hata kuvunja miguu hapa kisa nini jamani? Sam hayupo unadhani kama hospitali ningekupelekaje mimi?"
Jeff alikaa kimya kwa muda na kumtazama huyu mtoto sasa kwani hata yeye alimshangaa kumuona akiwa na muonekano wa kawaida kabisa.
Kisha mama mdogo wa Sam akamkabidhi Jeff yule mtoto ili aweze kuondoa uoga zaidi dhidi ya mtoto.
"Hebu mshike kwanza, mtoto yupo kawaida kabisa huyu"
Jeff alimchukua yule mtoto kwa uoga na kumuweka mapajani mwake huku akimuangalia kwa umakini sana.
Kimya kidogo kilitawala kwani bado Jeff alikuwa akijiuliza vingi kuhusiana na yule mtoto.
Wazazi wa Sabrina nao kama kawaida ya siku zote waliamka na kuandaa mambo mbali mbali ila walishangaa bila ya Sabrina kurudi.
"Ni lazima angerudi maana nguo zote za mtoto zipo huku"
"Sasa imekuwaje hajarudi hadi muda huu?"
"Hapo ndio sielewi"
Kwavile walielewa alipoenda kulala ikabidi mama Sabrina amuagize mdogo wa Sabrina kwenda kumuangalia dada yake,
"Maana mambo mengi na hatuwezi kujua kilichotokea huko, hebu nenda kawaangalie basi"
Mdogo wa Sabrina hakupinga bali alitoka mahali pale na kuanza kuelekea kwakina Jeff ili kuwaangalia.
Alipofika kwakina Jeff alishangaa kukuta nyumba ikiwa kimya kabisa na akajaribu kugonga lakini hakuna ambaye alimfungulia mlango, moja kwa moja mdogo wa Sabrina akatambua kwamba hapakuwa na mtu mule ndani ila hakuweza kupata jibu kuwa watakuwa wapi.
Akajaribu kupiga simu zao ila hakuna iliyopatikana na kumfanya arudi kwao na kuwapa taarifa kuwa hawapo,
"Kheee watakuwa wameenda wapi sasa? Hivi Sabrina anaweza kuondoka bila hata ya kja kuaga kweli!"
"Pengine wamepata safari ya gafla, hata hivyo tusiwe na wasiwasi sana mama. Tuamini kuwa watarudi tu"
"Sawa, lakini hiyo hali imenishangaza kwakweli. Yani Sabrina naye aondoke tu bila ya kuja kuniaga! Mmh haiwezekani"
Mdogo wa Sabrina akaongea mawili matatu pale kisha akamuaga mama yake na kuondoka.
Kwa upande wa Sam leo alijiona kamavile kakutana na jini mahaba maana kwa msisimko aliokuwa anaupata haikuwa kawaida kabisa ila Emmy naye alijaribu kutulia kwa muda ili kuifanya akili ya Sam iwe sawa.
Baada ya kimya kidogo, Emmy akamuuliza Sam
"Unaweza kunipeleka kwenu?"
"Sio tatizo hilo Emmy"
"Je nikitaka unipeleke mahali ninapotaka mimi utanipeleka?"
Sam akakaa kimya kwa muda kisha akajibu kuwa nalo sio tatizo,
"Basi mimi nataka unipeleke kule ambako yule mganga alikupa lile jini"
Sam akashtuka sana na kuuliza,
"Mbona unajua mambo mengi kuhusu mimi? Umeyajuaje?"
"Ni ndoto Sam, ndoto imenijulisha yote haya. Unaniona mimi nilivyo"
Sam akaitikia kuwa anamuona vizuri sana,
"Mimi ni msichana mrembo sana na vijana wengi huvutiwa na mimi. Ila tatizo lako halina tofauti na langu"
"Ni kweli wewe ni mrembo ila kivipi tatizo lako linafanana na langu?"
"Wewe ni kijana na una pesa, umeweza kuwashawishi wasichana wengi na kwa kutumia pesa zako umeweza kuwaangamiza ili kutimiza adhma ya huyo anayekuzunguka. Mimi ni mwanamke tena mrembo, vijana wengi wametumbukia kwangu sababu ya urembo wangu na kwa hakika nimewaangamiza wengi sana. Hakuna aliyepona pindi tu alipolala na mimi. Tunafanana Sam, ulitumia pesa zako nami nilitumia urembo wangu"
Sam akamuangalia kwa makini Emmy na kumuuliza,
"Kwahiyo ulikuwa unajiuza?"
Emmy akatabasamu na kujibu,
"Ndio, na nisipofanya hivyo kwa muda mrefu nilikuwa naumwa. Sam, unatakiwa utoke kwenye hiyo hali sio nzuri kwako. Maisha ya nje na hiyo hali ni matamu sana Sam, najua hujawahi kufurahia tendo sababu ya hiyo hali kwani unajua ukimaliza basi umeua ila uwezekano wa kutoka upo. Huku nje ni kutamu zaidi Sam"
Kisha Emmy akamshika bega Sam kama kutaka kumpa msisitizo ila Sam alisisimka kupita maelezo na kushindwa hata kuongea ambapo Emmy alimuuliza kwa sauti ya upole sana,
"Upo tayari Sam?"
Sam aliitikia kwa kichwa kwani hakuwa na sauti ya kujibu kwa msisimko alioupata.
Mama mdogo wa Sam aliendelea kuzungumza na Jeff ili aweze kumuweka kwenye mstari ulionyooka.
"Niliwaambia kuwa muwe mnamuomba Mungu je umefanya hivyo leo?"
"Mmh majanga tu kwakweli majanga ila siku ukifika nyumbani kwetu na kuona hali ya mama yangu utaelewa kwanini nachanganyikiwa. Maisha kwangu yamekuwa mtihani mzito sana"
"Pole, maisha ndivyo yalivyo ila muamini Mungu ni muweza wa yote. Chochote uombacho kwa kuamini basi atatenda"
"Nashukuru ila je kuna uwezekano wa Sam kurudi leo?"
"Sijui ila Sam huwa haelewekagi, anaweza akarudi ila akachelewa sana"
"Basi akirudi mwambie anipigie simu"
"Kwahiyo unataka kuondoka?"
"Ndio"
"Hutaki tuzungumze zaidi kidogo? Huwezi jua, maneno yangu yanaweza kukusaidia ufahamu wako"
"Nitakusikiliza siku nyingine, acha nirudi nikaiangalie familia yangu kwanza"
Kisha Jeff akamshusha Cherry na kuaga na kuondoka zake.
Mama mdogo wa Sam alimuangalia tu kwani si rahisi kumlazimisha mtu kufanya kile anachotaka yeye.
Kisha akamchukua mjukuu wake na kuendelea kufurahi nae.
Mama Sabrina hakuwa na imani na majibu ya mwanae hivyo akaamua kwenda yeye mwenyewe kwakina Jeff.
Na alipofika pale palitawala ule ukimya, nae akagonga bila ya kufunguliwa.
Akajaribu na kuita majina lakini hakuitikiwa, ikabidi tu akubaliane na hali halisi kuwa mule ndani hakuna mtu.
"Yani huyu Sabrina huyu ndio hata bila kuaga kweli? Ameanza kuwa na akili za huyo Jeff sasa."
Mama Sabrina hakupendezewa na ile hali kabisa kwahiyo alirudi nyumbani kwake akiwa amechukia huku akipanga kuwasema wakirudi.
Alipofika nyumbani kwake alimkuta mtu ambaye hakumtarajia kabisa.
Alimkuta Cherry amekaa sebleni, mama Sabrina akashtuka sana
"Kheeee!"
"Unashangaa nini?"
Hakuweza kujibu ila alizidi kushangaa tu, gafla akapatwa na kizunguzungu na kuanguka chini.
Sam alikuwa na wakati mzuri kadri muda ulivyozidi kwenda mbele.
"Tukiachana hapa, tafadhari Sam nenda moja kwa moja nyumbani kwako yani usipite popote pale."
"Nimekusikia Emmy"
"Halafu kesho nitapenda unipeleke kule nilipokwambia"
"Ni mbali sana Emmy"
"Haijalishi ila inatakiwa iwe hivyo, Sam unatakiwa kuwa huru kwasasa. Tafadhari usifikirie pesa na magari, kwa muda huu naomba unifikirie mimi na ukubaliane na mimi"
Sam alitikisa kichwa kwani alikubaliana na yote aliyoambiwa na huyu dada.
Kisha wakafurahi pamoja na kuagana,
"Ukifika usiache kunijulisha kwenye simu Sam"
"Hilo halina tatizo Emmy"
Kisha Emmy akamkumbatia Sam na kumuaga.
Kwakweli Sam muda huu alijihisi kama kaganda kwenye barafu kwa lile kumbatio alilolipata toka kwa Emmy.
Sam alipanda kwenye gari yake akirudi nyumbani kwake ila mawazo yake kwa muda huo yalikuwa kwa Emmy tu.
Aliwaza uzuri wa Emmy, aliwaza jinsi anavyosisimka akiguswa nae na jinsi alivyomkumbatia.
Alijikuta akijiuliza,
"Mmmh mapenzi gani haya? Ni mapenzi kweli haya? Mmh moyo wangu mimi, moyo umechanganyikiwa kabisa. Mapenzi yanafanya umpende mtu kuanzia mwili hadi akili? Mmh ndio mapenzi haya? Je yale niliyokuwa nayo kwa Sabrina ni nini?"
Sam alijiuliza maswali mfululizo kwani kila kilichotokea mbele yake alipokuwa na Emmy kilikuwa cha kumshangaza.
Mdogo wa Sabrina aliporudi kwao alishangaa kumkuta mama yao chini akiwa amepoteza fahamu, ikabidi amuite baba yao aliyekuwa chumbani bila ya kujua kilichoendelea sebleni.
Wakajitahidi kumuinua na kuanza kumpa huduma ya kwanza kwani alionekana kuwa na tatizo lililompelekea kuanguka chini.
Muda kidogo alizinduka ila hakukumbuka kilichotokea nyuma, hakukumbuka kilichomfanya aanguke.
Jeff akiwa njiani alimtafakari mtoto aliyempakata ambaye hakuonekana kuwa na mbwembwe zozote kama za yule wa nyumbani na hii kitu ikamfungua akili kuwa huyu wa huku ndiye mtoto wao kweli ila tu hakuwa na la kufanya.
Alipanda kwenye daladala na kushuka kwenye kituo cha kuelekea kwao, ila njiani akapatwa na maswahibu leo kwani alijikuta akitembea bila ya kufika kwao na mwisho wa siku giza nalo likaingia.
Jeff alikuwa amechoka sana, muda kidogo akaiona nyumba yao na kuingia ndani huku akiwa amechoka vya kutosha.
Alimkuta mama yake pamoja na Keti pale sebleni.
Akamsalimia Keti kisha akapitiliza chumbani kwake ili aweze kulala.
Alipoingia chumbani akamkuta Sabrina akiwa amelala, hakukumbuka tena kuwa alimuacha akiwa amelala ila alichokifanya Jeff kwa muda huo ni yeye kupanda kitandani pia na kulala.
Sam alifika nyumbani kwake akiwa amejaa tabasamu na kama kawaida alimkuta mama yake mdogo pale sebleni na mada zake zikiwa zile zile kuwa Sam amrudie Mungu.
"Mama ukimrudia wewe inatosha na ukiomba wewe inatosha. Wengine huyo Mungu atatupiga vibao kwakweli tukijifanya kumuomba omba"
Mama mdogo wa Sam alikuwa akimsikitikia tu Sam ingawa bado aliendelea kumuombea.
Sam alienda chumbani kwake na kukaa huku akijifikiria kuwa huenda akikubaliana na matakwa ya Emmy vipi kuhusu mali zake na utajiri wake.
Akakumbuka kauli ya Emmy kuwa kwa muda huo asifikirie mali bali amfikirie yeye,
"Mmh nitaishije? Nitawezaje?"
Sam hakuwa na jibu.
Keti akiwa pale sebleni na Sakina, gafla akatokea Cherry na kumfanya Keti ashtuke kwani hakumtarajia.
"Usishtuke"
Keti akamuuliza kwa uoga,
"Umekuja na nani?"
"Nimekuja na baba"
Keti akamuangalia huyu mtoto kama dakika mbili hivi bila ya kuongea chochote, ila huyu Cherry akamwambia Keti
"Mimi naweza kumponya huyu"
"Unaweza kumponya? Kivipi?"
"Unabisha? Fumba macho uone"
Keti kwa uoga kiasi akafunga macho yake.
Baada ya muda kidogo akaambiwa fungua ila cha kushangaza hakumuona tena Cherry mbele yake ila tu ni mama Jeff ambaye aliinuka na kujishangaa,
"Khee nilikuwa wapi mimi? Mbona sielewi?"
Keti alimuangalia tu kwani ilikuwa maajabu kweli ukizingatia muda mfupi uliopita alikuwa hawezi hata kuongea na alikuwa kama tahira.
Ila Sakina bado alizidi kujishangaa na kuuliza,
"Yuko wapi mwanangu?"
"Yupo chumbani kwake"
Hapa Keti aliamua kumjibu, na moja kwa moja Sakina akaelekea chumbani kwa Jeff.
Alifika na kufungua mlango, akashangaa kumuona Jeff akiwa amelala na Sabrina huku wamekumbatiana.
Ila Sakina bado alizidi kujishangaa na kuuliza,
"Yuko wapi mwanangu?"
"Yupo chumbani kwake"
Hapa Keti aliamua kumjibu, na moja kwa moja Sakina akaelekea chumbani kwa Jeff.
Alifika na kufungua mlango, akashangaa kumuona Jeff akiwa amelala na Sabrina huku wamekumbatiana.
Sakina aliwaangalia kama dakika tano hivi kisha akawashtua,
"Nyie"
Ila inaonyesha walikuwa kwenye usingizi mzito sana, hivyobasi Sakina aliamua kwenda kuwatingisha ambapo wote wawili walishtuka kwa pamoja na kumuangalia Sakina huku wakiwa kama wanashangaa hivi.
Sakina akawauliza,
"Mambo gani haya? Hebu nielewesheni"
Jeff alimuangalia vizuri mama yake na kugundua kuwa mama yake amepona na amerudiwa na fahamu na ndiomana ameweza kuongea na hata kuuliza lile swali.
Ikabidi Jeff ainuke pale kitandani ili ajaribu namna ya kumuelezea mama yake,
"Mama, ngoja nikakueleze ukweli wa mambo"
"Ukweli gani? Kwamba umeamua kutembea na Sabrina? Umeamua kuwa na mahusiano na Sabrina? Si ulizoea kumuita mamdogo huyo imekuwaje sasa? Niwaelewaje mimi?"
"Mama, punguza jazba na unisikilize mwanao. Hivi unajua matatizo uliyokuwa nayo mama yangu? Unajua ni mambo gani yaliyotokea hapo kati? Huwezi kuyajua sababu ulikuwa na matatizo, basi tulia mama yangu nikueleze nikwambie kilichotokea"
"Siwezi kujua ndio sababu sikuwepo"
Kisha Sakina akamuangalia Sabrina pale kitandani akiwa amekaa na kuinamisha macho chini,
"Hivi Sabrina na wewe una akili kweli? Huyu si mtoto uliyekuwa ukimuangalia, kumlisha na hata kumvalisha nguo. Eti leo ni mpenzi wako sijui nani yako huko, una akili kweli wewe? Unawezaje kuongozana na huyu Jeff? Si kitoto kabisa hiki! Kweli nimeamini, mtoto ni yule unayemzaa mwenyewe kwani akiwa mtaani kila mmoja anamuona mkubwa mwenzie. Ndiomana wale wanawake wa Jeff ulikuwa unawapiga vita kila siku. Hivi na wewe Jeff kabisa hujaona mtu mwingine yeyote zaidi ya huyu! Mke wa mtu tena ana watoto wawili, Jeff mwanangu una akili kweli wewe?"
Jeff na Sabrina walimuacha aongee kwanza ili apunguze dukuduku lake kabla ya wao kumwambia hali halisi kwani walimuona kuwa ameshapaniki tayari, na kweli Sakina alikuwa amepaniki kwani hakuelewa yaliyotokea katikati.
"Siwezi kukubaliana na huu upuuzi maana huku ni kudhalilishana na kufedheheshana. Sabrina wewe ni kama mdogo wangu na nikakupa dhamana ya mwanangu umuone kama mwanao ila wewe kumbe umeenda kumuona kama mumeo kweli? Nilikutafutia kaka yangu ukamkataa kumbe ulikuwa unangoja mwanangu akue kue kidogo umdake! Hizo tabia za kuvizia ni za wanaume kumbe na wewe mwanamke unafanya hivyo. Kwakweli Sabrina umeusononesha moyo wangu, Sabrina umeniumiza na kunidhalilisha. Tena bila ya aibu umeamua kuja kumfata mwanangu hapa nyumbani ili mfanye uchafu wengu kwenye nyumba yangu! Sabrina ni mwanamke gani wewe uliyekosa mshipa wa aibu? Kwanini umeshindwa kuwa hata na chembe ya aibu Sabrina?"
Sakina hakunyamaza hata na kumfanya Sabrina ainame huku machozi yakimtoka, Jeff akaona sasa inatosha kwani hakupenda kuwe na mapenzi ya siri tena baina yake na Sabrina.
Aliamua kuongea ili kumkatisha mama yake na waweze kuongea wao wawili tu kwani ulikuwa ndio muda wa kuweza kuanza kumtetea Sabrina.
"Mama, tafadhari. Nakuheshimu mama yangu na kukupenda pia. Hupaswi kuongea maneno yote hayo dhidi ya Sabrina, unatakiwa kuniuliza mimi mwanao kuwa imekuwaje"
Kisha akamshika mama yake mkono na kutoka nae nje.
Sabrina akiwa amekaa pale kitandani alijikuta akiwaza mambo mengi sana kwani aliona hata kilichotokea ni kati ya yale aliyoyawaza awali kuwa endapo itagundulika kuwa ana mahusiano na Jeff.
"Leo yametimia yote niliyokuwa nikiyafikiria"
Akashtuka kidogo na kujaribu kukumbuka muda ambao alitoka kwao na kuja huku kwakina Jeff,
"Ila si nimekuja leo mimi? Yani leo leo ndio napatwa na majanga. Halafu huyu Sakina nae imekuwaje maana hata sielewi, yani kapona gafla na gafla hiyo hiyo kaja humu chumbani"
Mara gafla akasikia kicheko cha Cherry kilichomfanya ashtuke kwakweli na kuanza kuangalia kila mahali mule ndani, ila alichoshtukia ni kumuona Cherry mbele yake kitu kilichomuogopesha sana,
"Nilishakwambia usiniogope, wewe unapaswa kunizoea yani nizoee tu. Na kwa taarifa yako hapa hujaja leo bali ulikuja jana usiku ila kilichokutokea ni kuwa leo kutwa nzima nilikufanya ulale usingizi hapo bila kushtuka"
Sabrina alikuwa akishangaa tu,
"Tena na huyo Sakina nimemponya mimi mwenyewe, nilitaka aje awashuhudie akiwa na akili zake timamu. Mimi nina uwezo wa kufanya chochote ninachokitaka, nilimpa kazi huyo Jeff ila hakufanya kazi yangu ipasavyo, naye nikampa adhabu ya kutembea kwa muda mrefu hadi alipochoka ndio nikamuonyesha kwao aweze kulala. Mimi ninao uwezo wa kubadilika nitakavyo"
Mara akaanza kubadilika, Sabrina hakuweza kuvumilia bali alianguka na kuzimia.
Jeff alijaribu kuzungumza na mama yake pia akajaribu kumtetea Sabrina dhidi ya mama yake.
"Nampenda Sabrina mama, na sijaanza kumpenda leo wala jana. Kuhusu hili swala usimlaumu Sabrina mama bali nilaumu mimi kwani mimi ndiye chanzo hata cha kuvunja ndoa yake mapema sana kwa mapenzi niliyonayo kwake."
"Mwanangu, kupenda sio tatizo ila kwanini umpende huyo Sabrina na sio mwingine? Mwanangu huenda umewekewa dawa hujui tu"
"Hebu kumbuka mama, uliwahi kunisimulia kuwa kipindi una ujauzito wangu ulikuwa ukimpenda sana Sabrina. Tena ulinisimulia mwenyewe kuwa ulikuwa huwezi kufanya chochote bila uwepo wa Sabrina hata kulala ulikuwa unapenda kulala na Sabrina hadi mama yake na Sabrina alikuwa anachukizwa na hilo. Je umesahau mama?"
"Hapana sijasahau"
"Tena ukanisimulia kuwa hata uliponileta duniani nilikuwa napenda kubebwa na Sabrina, napenda kulishwa nae ingawa hakuwa mkubwa sana wa kufanya hivyo ila alikuwa anafanya kwaajili yangu. Hiyo ni dhahiri kuwa mimi nilianza kumpenda Sabrina kabla sijazaliwa yani tangu nipo tumboni kwako nilikuwa nampenda Sabrina, kwamaana hiyo Sabrina ndio chaguo langu na ndio mwanamke wa maisha yangu"
Sakina akapumua kidogo kisha akajiuliza,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa ndio mapenzi gani haya? Hebu nenda Jeff tutazungumza kesho"
"Sawa mama ila ninachomshukuru Mungu kwasasa ni kupona kwako"
Kisha Jeff akaondoka pale na kumuacha mama yake ambaye moja kwa moja alienda chumbani kwake na kulala.
Jeff nae aliporudi chumbani kwake na kumkuta Sabrina akiwa chini, wazo lililomjia kwa haraka haraka ni kuwa Sabrina amelia sana na kuanguka hivyo akamuinua na kumpandisha kitandani ambapo Sabrina alikuwa kama mtu aliyelala.
Jeff alimuangalia Sabrina kwa jicho la huruma na upendo kisha akasema,
"Pole sana Sabrina najua upendo wangu ndio uliokufanya udhalilike ila tambua kwamba nitakupenda daima. Sijali chochote, sijali lolote nitakupenda siku zote za maisha yangu. Wewe ndio mwanamke pekee unayenifaa katika maisha yangu. Na jamii yote itajua na kutambua kuwa ni kiasi gani nakupenda"
Kisha akamsogeza karibu na mtoto wao halafu akawakumbatia wote wawili na kulala.
Kulipokucha, Sakina alikuwa wa kwanza kuamka.
Alijikuta akikaa na kutafakari yaliyotokea usiku ila hakuweza kuelewa kitu.
Kwanza kabisa alijiuliza alipokuwapo kabla ya ile usiku hakupata jibu,
"Hivi nilisafiri au nilikuwa wapi?"
Akatafakari na kukumbuka kuwa mara ya mwisho alikuwepo nyumbani kwa Sam kisha akarudi huku nyumbani kwake ila kilichotokea hapo hakukumbuka mpaka tukio aliloliona usiku.
Kisha akatafakari kuhusu Sabrina na Jeff kisha akajiuliza,
"Je haya ni mapenzi?"
Akawaza sana,
"Mapenzi gani haya?"
Akainuka, akaenda kuoga kisha akatoka na kumkuta yule Keti sebleni ambapo alimuaga kuwa anakwenda nyumbani kwakina Sabrina.
Keti alimuitikia tu ingawa alikuwa na mshangao wa kila aina ukizingatia mtu huyu jana tu alikuwa hoi tena asiyejiweza kabisa ila vipi leo? Yani ile kupona tu usiku wa jana, kesho yake kashapata nguvu ya kuzunguka nyumba kwa nyumba.
Keti alimshangaa tu na kuzidi kushangaa maajabu ya ile nyumba haswa maajabu ya yule mtoto wa usiku ambaye ni Cherry.
Nyumbani kwakina Sam kama kawaida ya yule mama yake mdogo alikuwa akimsisitiza swala moja tu nalo ni maombi ila hilo swala lilikuwa ni zito sana kwa upande wa Sam na ukizingatia kipindi hiko akili yake haikuwa na majibu kamili kwani kukutana kwake na Emmy kulishamchanganya sana.
Ila leo Sam alienda kukaa sebleni na mama yake mdogo na kuzungumza nae kidogo,
"Kuna binti nimekutana nae ila kiukweli hadi sasa namtafakari kwamaana simuelewi"
"Humuelewi kwanini?"
"Nahisi anataka kuharibu maisha yangu. Labda huko kuomba mama uombe juu ya huyu dada apotee kwangu"
"Sikia Sam, ninachokuomba mimi ni umlete kwanza huyo dada hapa nyumbani hapa. Mlete nimuone na nizungumze nae"
Sam akafikiria kidogo, akamfikiria Emmy kisha akakumbuka maneno aliyoambiwa na huyo Emmy na kujikuta akinyamaza kimya kama kwa dakika tano hivi.
"Vipi tena mbona kimya? Mlete huyo mwanamke nizungumze naye"
"Usijali mama nitamleta"
Muda kidogo simu ya Sam ikaita na kumfanya aichukue, kuangalia mpigaji alikuwa ni Emmy ikabidi aipokee ila ile sauti ya Emmy kwenye salamu tu ilimfanya Sam asisimke mwili mzima na kukosa hata pozi za kuendelea kuzungumza pale mbele ya mama yake mdogo hivyo aliinuka na ile simu na kwenda kuzungumza nayo chumbani.
"Naomba tuonane tafadhari Sam au umesahau kile tulichoongea"
"Bado natafakari Emmy"
"Unatafakari nini sasa, fanya maamuzi haraka ili tumalizane na haya mambo mapema."
"Kwahiyo unataka tuonane leo"
"Ndio leo, tena ukitoka huko kwenu naomba uje moja kwa moja huku yani usipitie popote pale"
"Sawa Emmy nimekuelewa"
Kisha Sam akakata ile simu na kupumua kiasi kwani kile kitendo cha kuzungumza na Emmy kwenye simu kilikuwa ni kitu cha kumpa msisimko sana tangu alipoonana nae jana yake katika muonekano wa kumvutia na ndiomana ikawa ngumu sana kwa yeye kukataa kile alichoambiwa na Emmy ingawa kwa upande mwingine kila akifikiria aliona ikimgharimu sana maisha yake.
Sakina alienda moja kwa moja nyumbani kwakina Sabrina ambapo mama Sabrina alipomuona alimpokea kwa mshtuko na furaha kwani hakutegemea kumuona mzima vile.
Wakasalimiana pale, halafu Sakina akamuuliza mama Sabrina
"Inamaana nilikuwa naumwa sana kiasi kwamba mnanishangaa kiasi hicho?"
"Ni kweli Sakina, umeumwa sana yani tulikuwa tukimuomba Mungu tu akuponye"
Ila Sakina aliacha kwanza mada za kuhusu ugonjwa wake na kuanza kuzungumzia mada iliyomleta ambayo ni ya Jeff na Sabrina,
"Hivi mama umewezaje kuruhusu hili litokee? Hivi Sabrina kwa Jeff si sawa na mama kwa mtoto jamani"
"Punguza munkali Sakina, mapenzi hayachagui. Hata mimi nilishtushwa kama wewe mwanzoni ila badae nilitafakari na kuelewa. Umri, dini, kabila, rangi, kimo na umbo si kitu kwenye mapenzi ya kweli. Zamani ilikuwa kama sheria kuwa ni lazima mwanaume awe amempita mwanamke ila kuna kipindi ukiangalia unaona wazi haikuwa sawa. Mfano mzuri wewe hapo, yule mumeo alikupita miaka mingapi na mbona mmeachana?"
Sakina akafikiria kwa muda kisha akajibu,
"Hilo sio tatizo mama, ila jambo linalonipa mawazo ni moja. Jeff anadai alianza kumpenda Sabrina toka alipokuwa tumboni, je hayo ni mapenzi?"
"Kwanini yasiwe mapenzi?"
"Hapana mama hayo si mapenzi, kwanza ni kawaida kwa mwanamke mjamzito kupenda baadhi ya vitu na kuchukia baadhi. Mimba yangu kumpenda Sabrina halikuwa tatizo kwani ni hali ya mimba tu, inamaana wamama wote walipokuwa wajawazito na kuwapenda watu fulani ndio lazima watoto wao wawe na mapenzi kwa hao watu? Hii hali si ya kawaida kabisa, Jeff anaongea kwa ujasiri kuwa alianza kumpenda Sabrina tangia tumboni inawezekanaje? Itakuwa mwanangu alirogwa labda ili awapende watu wazima"
"Sakina hebu acha vituko kwanza, kaa chini tafakari jinsi ulivyokuwa ukimpenda Sabrina kisha tafakari na hayo maneno ya mwanao kisha nipe jibu"
Sakina alijikuta akiwa kimya kwa muda akitafakari lile swala.
Sam alitoka na kumuaga mama yake mdogo,
"Sam uwe unakumbuka kitu kikubwa kimoja tu kwenye safari zako, maombi. Mkumbuke Mungu mwanangu, sala ni muhimu"
Sam akatoka zake kwani hizi kauli za mama yake zilikuwa ni marudio sana.
Alipanda gari yake na kuanza safari ya kuelekea kwa Emmy ila njiani akakumbuka kitu kwenye ile nyumba yake nyingine hivyo akageuza gari na kuelekea huko.
Alifika kama kawaida na kuingia ndani.
Na alipoingia tu ndani akamkuta Cherry akiwa na hasira sana siku hiyo,
"Sam nilikutuma nini na umefanya nini? Sasa leo nitakuonyesha kuwa mimi naweza kubadilika na kuwa mbaya hata kwako muda wowote"
Sam alishtushwa na hii kauli na kumfanya aanze kuogopa kwani hakuwahi kumzoea akiwa hivi.
"Nilikwambia nataka damu umenipuuza, umeenda kupanga mipango ya kunitokomeza mimi sasa mimi leo nitakutokomeza wewe kabla yangu."
Uoga ukamshika Sam na kujikuta akipiga magoti ili kujaribu kumuomba msamaha.
Na alipoingia tu ndani akamkuta Cherry akiwa na hasira sana siku hiyo,
"Sam nilikutuma nini na umefanya nini? Sasa leo nitakuonyesha kuwa mimi naweza kubadilika na kuwa mbaya hata kwako muda wowote"
Sam alishtushwa na hii kauli na kumfanya aanze kuogopa kwani hakuwahi kumzoea akiwa hivi.
"Nilikwambia nataka damu umenipuuza, umeenda kupanga mipango ya kunitokomeza mimi sasa mimi leo nitakutokomeza wewe kabla yangu."
Uoga ukamshika Sam na kujikuta akipiga magoti ili kujaribu kumuomba msamaha.
Ila kabla hajazungumza chochote alishtukia akipigwa kibao kilichompa kizunguzungu hadi akaanguka kisha yule Cherry akaanza kucheka kwa nguvu sana.
Sam nae hakuwa na nguvu yoyote pale chini kutokana na kibao alichopigwa hata kuinuka hakuweza, kisha yule Cherry akamuinua Sam kwa kumkunja na kumwambia sasa,
"Chagua moja, ninyonye damu yako na nikumalize muda huu ili mchezo wa wewe na mimi uishe au nikupe adhabu ya mwisho katika maisha yako"
Sam alikuwa akitetemeka tu kwani hakujua hata hiyo adhabu ingekuwa ni nini ingawa kwa upande mwingine aliogopa kufa ukizingatia kuna wengi aliosababisha vifo vyao.
Sam aliomba kupewa adhabu kwani kifo kilikuwa ni tishio kubwa sana kwake.
"Kwahiyo unataka adhabu ila adhabu yangu usipoitekeleza ndani ya siku mbili nakumaliza wewe mwenyewe"
"Sawa nimekuelewa"
"Cha kwanza kabisa sitaki uonane na yule dada uliyeonana nae. Umenisikia"
Sam akatikisa kichwa kuashiria kwamba anasikia,
"Pili, kwa siku hizi mbili nataka unipatie damu ya wadada kumi na tano"
Sam akashtuka kidogo kwani hiyo idadi ilikuwa kubwa sana na ukizingatia siku zenyewe mbili tu.
"Yani hapa namaanisha hadi kufikia kesho usiku uwe tayari umeshatimiza idadi hiyo. Haya sasa kazi ianze"
Sam akataka kujaribu kumuomba Cherry ampunguzie adhabu ila ilikuwa tayari kashapotea mbele yake.
Kwakweli Sam alijiona yupo kwenye mtihani mgumu sana hata akasahau kilichompeleka hapo kwake kwani alitoka na kuondoka kimya kimya.
Sakina bado alikuwa akitafakari na kujiona wazi kuwa upendo aliokuwa akimpenda Sabrina pindi alipokuwa mjamzito haukuwa wa kawaida.
Alijiuliza kuwa huenda alirogwa kipindi hicho na kama alirogwa ndio kusema mambo yote yamerejea kwa mwanae akiwa mkubwa.
Akakumbuka jinsi alivyokuwa karibu na Sabrina hata siku ya kujifungua alikuwa na huyo huyo Sabrina porini.
Akamuangalia mama Sabrina na kumuuliza,
"Unajua mama kuna maswali najiuliza ila majibu sipati, hivi imewezekanaje? Imekuwaje hadi mambo kuwa hivi? Nashangaa sana. Mama huyu Sabrina si alikuwa anamuita Jeff mwanae, na huyu Jeff si alikuwa akimuita Sabrina mamdogo sasa imekuwaje hadi wakapendana na kuwa wapenzi? Wameanzia wapi wazo la mapenzi kati yao? Hebu jaribu kunijibu ili nipate kuelewa maana nawaza ila sielewi"
"Sasa hayo maswali nenda kawaulize wenyewe huko maana ukiniuliza mimi kazi bure. Mi sijui walipoanzia kupendana, ila nilichokuwa najua ni upendo wa ndugu ila kilichonishangaza ni kuwa hata hawa watoto wa Sabrina wote baba yao ni huyo Jeff"
Sakina akashangaa zaidi hapa baada ya kusikia kuwa watoto wa Sabrina wote baba yao ni Jeff,
"Kheee inamaana wameanza siku nyingi! Uwiii nilikuwa nafichwa mimi tu"
Kisha akakumbuka siku ambayo Sabrina alijifungua huyu mtoto wake wa pili, akakumbuka alichosema daktari na kile alichosikia kwa manesi.
Pia akakumbuka walivyomuuliza Jeff na jinsi alivyowazuga.
"Sasa nimeanza kuelewa ila natumai nikizungumza vizuri na huyu Jeff ndio nitajua vizuri"
"Ndio hivyo, usiwe na hasira wala nini. Ilimradi wamependana basi tuwaache waendelee na mapenzi yao"
"Na vipi kuhusu Sam"
"Najua hukumbuki ila kuna mengi sana yametokea hapa kati"
Kisha Mama Sabrina akaanza kumueleza Sakina kuhusu undugu wa Sam na Sabrina.
Jeff alipoamka, alimuamsha na Sabrina ambaye aliinuka huku akijishika shingo kwani alikuwa na maumivu makali sana ya shingo pia njaa ilikuwa ikimuuma sana.
Ikabidi Jeff ainuke na kwenda kubandika uji ili Sabrina na mwanae wapate kunywa kwani mtoto huyu nae alionekana kulia sana sababu ya njaa.
Uji ulipokuwa tayari, Sabrina alianza kunywa huku Jeff akimnywesha yule mtoto wao.
Ndipo Jeff alipopata wazo la kuulizia alipo mama yake.
Keti akamjibu vile alivyoagwa,
"Mmh huyu mama yani kupona tu tayari kiguu na njia ila awe tu amepona kweli maana mmh. Hivi Keti kwani ilikuwaje?"
"Hata sielewi kwakweli ila ninachokumbuka ni kuwa jana uliporudi na kwenda kulala nilikuwa hapa na mama akiwa mgonjwa vile vile, mara akaja yule mtoto wa kike yule wa kule kwa kaka Sam akitokea humo chumbani kwako akaniambia kuwa anaweza kumponya mama nikashangaa tu akasema kama siamini nifumbe macho. Nikafumba ila nilipofumbua nilimkuta mama kashanyanyuka huku akijishangaa na kuanza kukuulizia wewe halafu yule mtoto sikumuona tena"
Jeff na Sabrina wakatazamana kisha Sabrina nae akaamua kumueleza Jeff jinsi na yeye alivyotokewa na yule mtoto.
Keti alikuwa akiwashangaa tu, ndipo na yeye alipouliza,
"Kwani yule mtoto kuna nini kipo katikati yake mbona yupo tofauti na watoto wengine?"
Jeff akamjibu,
"Ni kweli yupo tofauti na watoto wengine ila kwa usalama wako nakuomba uachane na habari za huyo mtoto kwani unaweza kujikuta ukiumia bure na kujijutia"
Ikabidi Keti akae kimya kwani hata akifatilia ni kazi bure ukizingatia ni mambo yasiyomuhusu.
Sabrina na Jeff wakarudi chumbani sasa kwani Sabrina alikuwa akijianaa ili arudi nyumbani kwao.
Kisha Jeff akamwambia Sabrina,
"Unajua nini Sabrina, nahisi kuwa yule mtoto aliyekuwepo kwa mama wa Sam ndio mtoto wetu halisi kwani hata ukikaa nae unaona kabisa kuwa umekaa na mtoto, kwakweli yule ndio mtoto wetu wa ukweli ila huyu anayetutokea tokea sio mwanatu huyu ingawa kamponya mama yangu"
"Sasa itakuwaje kuhusu huyo wetu wa kweli?"
"Nadhani tungemuacha kwanza pale maana pale yupo kwenye mikono salama"
"Ila natamani kumuona yule mwanangu wa ukweli"
"Usijali, kwasasa yupo kwenye mikono salama. Naimani yule mama anamlea vyema sana"
Wakati wanaongea hayo akatokea yule Cherry mbele yao na kuwafanya washtuke sana kisha akawaambia,
"Kwahiyo sasa mmenikataa rasmi kuwa mimi sio mtoto wenu!"
Kisha akaanza kucheka na kusema tena,
"Ni kweli mimi sio mtoto wenu na pia mimi sio mtoto kama mnavyofikiria kwahiyo hata undugu nanyi sina. Ila kwa huruma yangu ndio iliyofanya nimponye mama yenu. Hebu tulieni kwanza msiwe na papara sina nia yoyote mbaya kwenu tena nawataarifu kuwa naenda kupumzika leo na kesho sasa kuanzia kesho kutwa mnatakiwa kuwa makini sana kwani hamuwezi jua kama nitakuwa na furaha au nitakuwa na hasira"
Kisha akapotea mbele yao na kuwaacha na mshtuko mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo ila kwasasa Jeff alimsogelea Sabrina na kumkumbatia ili kujaribu kuiondoa hofu iliyotawala kwenye akili zao.
Kwa upande wa Sam sasa hakujielewa kabisa, akapanda kwenye gari yake huku akifikiria hiyo idadi ya wadada kumi na tano ambao ataenda kuwamaliza.
Akakumbuka kipindi cha nyuma jinsi alivyokuwa katili, jinsi gani alivyokuwa akiwamaliza.
Akafikiria sana ila moyo wake na dhamira yake ilikuwa ikimsuta moyoni na kufanya asikie kama sauti ikimwambia,
"Tafadhari Sam, umeshaua wengi sana huu ni muda wako wa kupumzika na kutubu sio muda wa kuendelea kuongeza idadi ya marehemu. Fikiria hilo"
Sam hakuwa na raha kabisa ukizingatia aliogopa adhabu ya kifo chake ila ilikuwa sawa kwa vifo vya wengine.
Akajivika moyo wa ujasiri na kwenda kwenye baa ili aweze kuanza na wahudumu watakaojipendekeza kwake na wale watakaoonekana kuvutiwa na pesa zake.
Kwa upande wa Sakina sasa ukawa muda wa kurudi nyumbani kwake.
Aliamua kuridhishwa na majibu aliyopewa na mama Sabrina kwahiyo alirudi nyumbani kwake huku akiwa na maswali machache sana.
Alipofika kwake alipishana na Sabrina kwani na yeye alikuwa akitoka kuelekea nyumbani kwao.
Kwahiyo alichokifanya Sakina ni kumuita tu mwanae ili azungumze nae kwani hata kama akiendelea kumchukia Sabrina haitasaidia kitu chochote kile.
Jeff alikuwa tayari kumuelekeza mama yake kilichopo baina yake na Sabrina ili angalau mama yake huyo apate kuelewa kinachoendelea.
"Kwakweli mama nampenda sana Sabrina, na katika hili hupaswi kumlaumu Sabrina hata kidogo bali nilaumu mimi mwanao ambaye sikuweza kukubali ile hali halisi ya kuona Sabrina akiolewa. Hata Sam anatambua hili na ndiomana kabla ya harusi yao Sam alilazimika kunisafirisha. Nampenda sana sana Sabrina"
"Kwahiyo ni kweli kuwa wale watoto wa Sabrina ni wako?"
"Ndio ni kweli tena ukweli mtupu wale ni wanangu ni damu yangu"
"Kwamaana hiyo upo tayari kuishi na Sabrina na kujitangaza mbele za watu kuwa ndiye mkeo?"
"Nipo tayari mama, mtu pekee aliyekuwa akinipa mashaka siku zote ni wewe ila kwakuwa umeshajua basi sinabudi kuijulisha jamii nzima kuwa ni jinsi gani nampenda Sabrina"
"Hivi Jeff ni akili zako kweli kabisa hizo?"
"Nimempenda Sabrina nikiwa na akili timamu na ninayatamka haya nikiwa na akili timamu. Na pia nitaishi na Sabrina kwa akili yangu kabisa na nitaijulisha jamii kuwa mapenzi hayachagui na mapenzi ni upofu"
"Mmh hapa kweli kazi. Ni kweli usemayo kuwa mapenzi hayachagui na ni upofu ila wako wewe umeangukia pabaya mno ingawa wewe mwenyewe unajiona upo sawa. Sina pingamizi juu yenu ingawa bado najiuliza maswali mengi sana kuwa mnaitanaje humo ndani na mtaishije? Ila yote mnajua nyie wenyewe"
"Cha msingi umenielewa mama yangu, nashukuru kwa kunielewa"
Kisha Jeff akamsogelea mama yake na kumkumbatia ingawa ilionyesha wazi kuwa mama huyu kakubali mdomoni ila moyoni ilionyesha kuwa bado ana kinyongo dhidi ya kile kilichotokea.
Sabrina nae alifika kwao ambapo mama yake akamueleza kuhusu Sakina na waliyozungumza,
"Kwakweli mama siwezi hata kumtazama Sakina usoni, jana usiku aliongea maneno makali sana dhidi yangu"
"Yule asikubabaishe mwanangu, muache ataelewa taratibu. Mi nimemwambia hapa kuwa maswali yote akamuulize mwanae. Mimi sina kinyongo chochote dhidi yenu maana ndio maisha mliyoyachagua. Sikujua yaliyokuwepo miyoyoni mwenu siku zote hizi kama mlikuwa mnapendana"
"Mama, ila mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Nakumbuka nilikuwa namuona Jeff kama mdogo wangu, na hivi nilizoea kumuita mwanangu ndio kabisa. Mwanzoni sikumpenda Jeff kimapenzi ingawa nilitamani angekuwa mkubwa. Sikujua kilichokuwepo kwenye akili yake kwa siku zote hizi yani laiti ningejua basi ningefanya chochote kuwa mbali nae. Pia nadhani tatizo langu ndio limekuwa chanzo kikubwa cha kufanya niangukie kwenye mapenzi na Jeff"
"Tatizo gani hilo?"
Leo kwa mara ya kwanza Sabrina alijitoa kumueleza mama yake dhidi ya tatizo alilokuwa nalo zamani, tatizo la kamba, tatizo ambalo lilimzuia kukutana kimwili na mwanaume yoyote yule ila mwanaume aliyefanikiwa kufanya hivyo ni Jeff na alifanikiwa kwa kumpa madawa Sabrina kitu ambacho ilikuwa ni kumbaka.
Haya maelezo ya Sabrina yalimshangaza sana mama yake.
Mama mdogo wa Sam kwa upande wake akiwa pale nyumbani alihisi kuwa Sam ana matatizo ila je anamsaidiaje? Akaona msaada pekee ni kufanya maombi juu yake ila anamuombeaje mtu ambaye hataki kuombewa? Maana Sam hakutaka kusikia chochote kinachohusiana na maombi na siku zote alimwambia mama yake huyu kuwa aombe mwenyewe.
Huyu mwanamke akaelewa wazi kuwa kuna kitu kinachomfunga Sam na kumfanya awe kama hivi alivyo ila na yeye hakuacha kumuombea kwa muda wowote anaohisi kuwa mtoto wake huyo ana matatizo kwani huyu mama aliamini kuwa maombi ndio silaha pekee ya ushindi kwenye maisha.
Sam akiwa baa kwa muda mfupi kabisa, alifanikiwa kuwashawishi wadada tofauti tofauti ila alitaka kuondoka na mmoja mmoja toka baa tofauti tofauti ili atimize kwa haraka ile idadi yake.
Muda huu alianza kuondoka na mwanadada aliyeitwa Mwajuma ambaye kwa jina maarufu hapo aliitwa Mwajy.
Wakati anaingia kwenye gari yake na mwanadada huyo, akasikia sauti ya kike ikimuita.
Kugeuka nyuma akamuona Emmy ambaye alionekana kumuangalia kwa jicho la upole na huruma sana.
Sam akiwa baa kwa muda mfupi kabisa, alifanikiwa kuwashawishi wadada tofauti tofauti ila alitaka kuondoka na mmoja mmoja toka baa tofauti tofauti ili atimize kwa haraka ile idadi yake.
Muda huu alianza kuondoka na mwanadada aliyeitwa Mwajuma ambaye kwa jina maarufu hapo aliitwa Mwajy.
Wakati anaingia kwenye gari yake na mwanadada huyo, akasikia sauti ya kike ikimuita.
Kugeuka nyuma akamuona Emmy ambaye alionekana kumuangalia kwa jicho la upole na huruma sana.
Sam hakufurahishwa na kile kitendo cha kuitwa na Emmy kwani ilikuwa kama ni kukiuka maagizo aliyopewa.
Kwahiyo akageuka tena na kujifanya kama hajamuona wala hajamsikia huku akitaka kuingia kwenye gari yake ili aondoke na yule Mwajuma.
Ila Emmy akamwambia,
"Hapana Sam usifanye hivyo, najua umeniona na unanisikia. Tafadhari nisubiri tuongee."
Sam hakutaka kugeuka nyuma tena bali akaingia kwenye gari na kujiandaa kuondoka.
Emmy alipoona vile aliamua kukimbilia mbele ya gari ya Sam na kumfanya Sam azuie kwa muda kuliondoa, kisha akafungua kioo na kumwambia Emmy,
"Tafadhari Emmy naomba uondoke hapo mbele"
Emmy nae akamjibu,
"Nimalize kwanza mimi kabla ya kwenda kummaliza huyo wa kwenye gari"
Mwajuma nae kusikia neno la kumalizwa akashtuka, ikawa kama akili yake imemrejea kidogo na kumfanya akumbuke stori za kusimuliwa kuhusu vijana wanyonya damu.
Hofu ikamshika Mwajuma na kumuomba Sam kuwa ashuke,
"Naomba kushuka"
"Kushuka uende wapi?"
Jicho la Sam lilionekana kuwa jekundu sana na hata sura ilibadilika na kuonekana kuwa mwanaume katili.
Hali ile ikazidi kumtisha Mwajuma ambapo alijikuta akitetemeka kwa uoga.
Emmy nae aliendelea kumwambia Sam,
"Mwache ashuke huyo, tangia hapo umeshakosea masharti uliyopewa tayari"
Sam akakumbuka kuwa hakutakiwa kuzungumza na Emmy, kile kitendo kilimchanganya zaidi.
Akafungua mlango wa gari na kumsukumia Mwajuma kwa nje.
Ingawa Mwajuma aliumia ila aliinuka na kuondoka bila hata kuangalia nyuma kwani hofu ilimtawala tayari.
Kisha Emmy akaingia kwenye gari ya Sam ambapo Sam aliondoa gari bila ya kuongea kingine zaidi na Emmy.
Mwajuma alirudi ndani ya baa huku akitetemeka sana na kufanya wenzie wamuulize kulikoni.
Akawaeleza kilichotokea,
"Jamani, nadhani leo ilikuwa naenda kuchunwa ngozi si kwa jicho lile aliloniangalia nalo yule mkaka. Tamaa mbaya jamani"
"Mmh na wewe umezidi, hapo haikuwa kuchunwa ngozi wala nini yule mwanamke alikuonea wivu tu"
Mwenzao mwingine ndio akawafungua macho,
"Ila tujifunze jamani, nilitamani kumuita Mwajy wakati anaondoka na yule baba ila sikuweza. Jamani yule mbaba sio mara ya kwanza kumuona, huwa anachukua wanawake hivyo hivyo na hawarudi tena kwani huwa wanakufa hata sijui huwa anawafanya nini. Muwe makini jamani, tena wewe Mwajuma nenda ukamshukuru na Mungu wako kabisa maana ndio ingekuwa mwisho wako"
"Kwahiyo ulitaka nihangamie kweli? Mbona mna roho mbaya hivyo?"
"Mtaongea sababu hamumfahamu vizuri yule, niliogopa kwakweli ila nenda kamshukuru Mungu"
Mwajuma hakuwa na hamu hata ya kuendelea na kazi kwa siku hiyo hivyo ikamlazimu kurudi nyumbani kupumzika.
Mama Sabrina alimuhurumia sana mwanae kwa yale maelezo aliyompa.
"Pole sana mwanangu, na kwanini ulikuwa umenificha siku zote hizi?"
"Mama, mimi ni mtoto wako pekee wa kike ila sikuweza kuwa huru kwako na kukwambia chochote kinachonisibu. Mtu pekee kwangu alikuwa ni Sakina, yeye ndiye alinifahamu kwa kila kitu kwani nilimwambia kila jambo lililokuwa likinitokea hata kwa baadhi ya waganga nilienda nae. Na katika watu walioshtuka baada ya kusikia kuwa nina ujauzito basi ni Sakina, na mpaka sasa najua anamawazo yale ya mwanzoni kuwa kama ningekuwa na tatizo lile basi ningemmaliza mwanae ila tu hajajua kama mwanae ndio kawa daktari wa tatizo langu. Sikuwa na sababu za kumpenda Jeff ila kwasasa nina sababu za kutosha kumpenda Jeff na ninakwambia leo mama kuwa nampenda Jeff"
Mama Sabrina alimuangalia mwanae na kumuona kuwa kweli ameamua juu ya hilo kwani siku zote alipokuwa akiulizwa kuhusu Jeff alikaa kimya ila leo kafunguka wazi kuwa anampenda Jeff.
Sam aliendesha gari kwa hasira na alipofika mbele akasimama kisha akamuangalia Emmy na kumuuliza,
"Hivi Emmy unanitakia nini mimi? Kitu gani unataka kutoka kwangu ili nikupatie uniache niwe huru"
"Ninachotaka toka kwako ni kimoja tu, nataka uondoke utumwani. Huko ulipo hapakufai Sam, hebu jaribu kufikiria ni damu za watu wangapi umemwaga, ni wangapi wamelia kwasababu yako? Sam unatakiwa kuwa binadamu huru kama wengine, angalia maisha yako, angalia ndugu zako, angalia wazazi wako halafu fikiria kuwa wewe ndio mmoja kati ya wale uliowaua kimakusudi kabisa. Hebu jaribu kufikiria, mimi nitakuacha uwe huru endapo utachagua uhuru wa kweli"
Sam alimuangalia kwa jicho la hasira sana Emmy kwani maneno yake nayo yalizidi kumchukiza na kumfanya atamani hata kumfanya kitu kibaya Emmy.
Hilo jambo Emmy aliligundua mapema sana kwahiyo akajaribu kufanya njia ambayo aliona ni rahisi kumtuliza Sam.
Emm alimsogelea karibu, kisha akamshika kwa kiganja cha mkono wake kwenye mkono ulioshikilia usukani halafu akamuangalia machoni.
Sam akapumua kidogo na kujikuta zile hasira alizokuwa nazo juu ya Emmy zikinywea kwani ulaini wa kiganja cha Emmy ulimfanya asisimke hata sauti yake sasa ikapoteza makali ya ukali wa mwanzo.
Kisha kwa upole kabisa Sam akamuuliza Emmy,
"Unataka twende wapi Emmy?"
"Nataka twende nyumbani kwako"
"Unataka twende kule kwa mama au kule kwingine?"
"Twende kule kwingine"
Sam akainamisha macho chini kwani alijikuta akifikiria yale masharti aliyopewa.
Emmy nae alishamwelewa, hivyobasi akazungusha kiganja chake kingine cha mkono na kushika shingo ya Sam kwa nyuma kitu kilichofanya Sam asisimke zaidi, kisha akamwambia
"Sam usiogope, ukiwa na mimi usiogope chochote. Najua masharti yake yanakutisha ila mimi najua cha kufanya, niamini mimi Sam. Wakati wa kufanya ni sasa."
Kisha akamsogelea na kumbusu ambapo Sam hakuwa na neno la ziada zaidi ya kugeuza gari lake na kuanza kuelekea nyumbani kwake.
Muda kidogo Jeff nae alifika nyumbani kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa pale kwenye mazungumzo na mama yake ambapo mama Sabrina alimkaribisha Jeff bila ya kinyongo chochote kile.
"Karibu sana Jeff"
Jeff alisalimia pale kisha akaeleza kilichompeleka,
"Nimeona ni vyema twende tukamuone mtoto wetu wa ukweli."
Sabrina alikubali kwani ni kitu alichohitaji wafanye toka mwanzo.
Kisha ikawapasa kutoa maelezo kwa mama Sabrina ambaye hakujua kilichoendelea na alibaki kushangaa tu na kuwauliza,
"Hivi jana mlikuwa wapi?"
Akawaeleza muda wote aliofika pale kugonga bila hata ya kufunguliwa mlango.
Jeff akamweleza pia alichokijua yeye,
"Mimi pekee ndio sikuwepo ila nadhani kuna kitu kilitokea mule ndani maana wote hawa walikuwa ndani ingawa cha kushangaza wakati naondoka asubuhi nilimuacha Sabrina akiwa amelala na niliporudi jioni sijui ndio usiku ule hata sielewi ila nilimkuta amelala vile vile. Kuna mambo mengi yanatokea kati yetu bila ya sisi wenyewe kujua chochote ila naamini yataisha tu"
Mama Sabrina alimuelewa ila kwa yale waliyomsimulia akaona ni vyema waende wao ila mtoto wamuache ambapo Sabrina alienda kujiandaa kisha mtoto akamuachia mama yake halafu yeye akaondoka na Jeff.
Sabrina na Jeff kwa wakati huu walionekana kuwa na furaha ya kuongozana pamoja maana hicho kitu kimekuwa adimu sana kati yao.
Sabrina alionekana kuwa na macho ya kuibia kumtazama Jeff kwani bado alikuwa na maswali kichwani mwake dhidi ya uchaguzi wake wa kuwa na Jeff ila ilionyesha Jeff nae kutambua mashaka ya Sabrina,
"Usihofu Sabrina, amini kuwa upo kwenye chaguo sahihi. Kwanini uubane moyo wako kwa mtu unayempenda? Kuwa huru mama, hili ni chaguo sahihi kwako."
Sabrina akatabasamu kisha safari yao ikaendelea hadi walipofika nyumbani kwa Sam.
Waligonga na kama kawaida walifunguliwa na yule mama wa Sam ambapo alikuwa ameambatana na Cherry ila Cherry alipomuona Sabrina alijificha nyuma ya mama huyu huku akilia na kumfanya huyu mama amnyanyue na kumuweka mabegani kisha akawakaribisha ila Cherry alionekana kutokutaka kumuangalia kabisa Sabrina hadi wanaingia ndani.
Mama mdogo wa Sam alikaa nao na kujaribu kuwaelewesha kuwa kwanini mtoto anawaogopa, kilichotokea ni kuwa mtoto huyu mtoto bado alikuwa na kumbukumbu za kusukumwa na Sabrina na ndiomana hakuweza hata kumtazama mama yake huyu.
Kwakweli Sabrina alijisikia vibaya kwa kile kitendo cha mtoto wake, ila mama mdogo wa Sam alijaribu kuongea nao na kuwaelimisha.
"Unajua nini Sabrina, huyu ni mtoto na kumbukumbu za mtoto hudumu miaka yote cha msingi ni wewe kumuonyesha upendo kwasasa ili uweze kumsahaulisha yale yaliyopita"
"Ila sasa je tunaweza kuondoka nae?"
"Hapana, siwezi kuwaruhusu kwa hilo kwakweli. Natakiwa kuwa karibu sana na huyu mtoto kushinda hata mnavyofikiri. Huyu mtoto amekuwa kamavile mtoto aliyetengwa kwahiyo anahitaji upendo wa karibu sana kama ninaompa mimi. Labda cha kukusaidia ni wewe kuja hapa ili uwe karibu na mimi"
Ikabidi wakina Sabrina wamueleze huyu mama yale yanayotokea na kwajinsi yule mtoto alivyowatokea na alivyowaambia,
"Yani nyie mnazidi kunifungua macho kuwa hapa kuna jambo ambalo ni zito sana, kwakweli hapa kuna mapambano inatakiwa tupambane"
Jeff akauliza,
"Sasa tunapambanaje na mtu wa ajabu kiasi kile? "
"Hapa silaha yetu ni moja tu, jamani maombi ni ya muhimu. Tunatakiwa kumuomba sana Mungu, ila mimi huwa nahisi kuwa kuna vingi Sam anajua kuhusu huyu mtoto ila anatuficha maana mapambano ni makali. Msinione hivi mimi, yani hapa huwa nakesha kwa maombi hii nyumba ni nzito sana hata sijui Sabrina ulikaaje humu bila maombi ila mimi napigana na Mungu kwakweli ananipigania na kunilinda"
Maneno ya huyu mama yaliwaingia sana hata Sabrina kwa leo alitamani angeishi tu na huyu mama kwani kila muda anaoishi kwao alijiona kuwa na maruweruwe.
"Ila basi nisaidie kitu kimoja mama, naomba huyu mwanangu asahau kile kitendo nilichomfanyia, haikuwa kusudio langu hata moyo wangu unaniuma kwa kitendo hicho, nisaidie kwa hilo tafadhari"
Sabrina aliongea kwa upole sana, Jeff nae alikuwa na ombi lake kwa huyu mama,
"Mi naomba nisaidie nijue kuomba kama wewe, kwakweli yule mtoto anatutesa na ametuambia kuwa atakaporudi tena tujiandae kwamaana hatujui kama atarudi akiwa na furaha au hasira. Nifundishe kuomba tafadhari maana kwa waganga nilipozunguka waligoma kunisaidia. Tafadhari tunakuomba kwa hilo maana naona maisha yangu na ya Sabrina yapo hatarini zaidi"
"Sawa nimewaelewa, ila kuhusu kuomba ni vyovyote vile unavyoweza kumuomba Mungu ila tu uwe na imani kuwa atafanya. Kitu kingine cha kuwasaidia, kwanini msije hapa tukawa pamoja na tuweze kupambana kwa pamoja dhidi ya huyo mtu"
"Mmh Sam atakubali?"
"Huyo Sam mwenyewe ni wa kumuombea jamani maana kila siku napatwa na ndoto mbaya dhidi yake."
Hili wazo la wao kuja kukaa pamoja hapo Jeff aliona kuwa ni swali jema ila je familia zao wanaziachaje nyumbani ikiwa yote yanawahusu kwa pamoja?
Akafikiria kidogo, kisha akawa na ombi moja kwa huyu mama
"Nina ombi moja la mwisho"
"Niambie tu wala usijali"
"Naomba kwasasa hivi twende wote kwetu ili ukaangalie na yale mazingira tunayoishi tafadhari usikatae nakuomba kisha tutarudi wote"
Mama mdogo wa Sam hakupinga juu ya hili, aliamua kwenda kujiandaa ili waondoke.
Sam alifika na Emmy hadi pale kwenye nyumba yake, kwanza wakasimama mlangoni kama dakika kumi hivi kwani Sam alikuwa akisua sua kuingia ndani ila Emmy akamshawishi hadi wakaingia ndani.
Sam alienda moja kwa moja kukaa kwenye kochi ambapo Emmy nae alikaa huku akimtazama Sam.
Mara gafla ikasikika sauti ya mtu akikohoa na kumfanya Sam ashtuke sana, muda kidogo ile sauti ya kikohozi ikageuka kuwa sauti ya kicheko na gafla mbele yao akatokea Cherry.
Kwakweli Sam alishtuka sana na kujua kuwa muda wake umefika.
Huyu Cherry aliongea sauti iliyopigana na mwangwi,
"Umekiuka masharti yangu, subiri uone nitakachofanya"
Akatoweka mbele yao na kumuacha Sam akiwa anatetemeka sana.
Mama Sabrina akiwa nyumbani na yule mjukuu wake mdogo, muda kidogo Sakina alienda tena pale kwa mama Sabrina na kumkuta akiwa nje na mjukuu wake.
Akamsalimia tena,
"Yani kwangu hapakaliki hata sijui napaonaje mama"
Mama Sabrina aliamua kuzungumza nae ili kumpa moyo.
Kwavile huyu mtoto mdogo wa Sabrina alikuwa ni mtoto anayetambaa kwa kipindi hicho, na ile hali ikamfanya awe mtundu kwahiyo mama Sabrina alimuacha acheze cheze.
Wakati wenyewe wakizungumza pale nje, huyu mtoto alielekea ndani.
Muda kidogo ukapita bila ya huyu mtoto kutoka, ikabidi mama Sabrina ainuke ili akamchungulie.
Alijikuta akipiga kelele baada ya kuingia ndani kwani alimuona mtoto akiwa chini yani kama ameanguka halafu puani vilimtoka vitu kama utumbo.
Wakati wenyewe wakizungumza pale nje, huyu mtoto alielekea ndani.
Muda kidogo ukapita bila ya huyu mtoto kutoka, ikabidi mama Sabrina ainuke ili akamchungulie.
Alijikuta akipiga kelele baada ya kuingia ndani kwani alimuona mtoto akiwa chini yani kama ameanguka halafu puani vilimtoka vitu kama utumbo.
Zile kelele za mama Sabrina zilimshtua na Sakina na kumfanya nae akimbilie mule ndani.
Wote kwa pamoja walijikuta wakishangaa na kuogopa muonekano wa mtoto huyu,
"Jamani kapatwa na nini?"
"Sielewi kitu, Mungu wangu"
"Na vile vitu puani ni vinini? Haya mambo mbona makubwa jamani"
Hakuna aliyeelewa cha kufanya na mtoto wakati ule kwani hata kwenda kumnyanyua uoga uliwashika ila mama Sabrina akajivika ujasiri na kwenda kumuinua yule mtoto ambapo alikuwa kalegea viungo vyote na alionekana wazi kuwa ni mtu aliyekufa huku yale mavitu yaliyokuwa yakimtoka puani kama utumbo mbo nayo yaliendelea kutoka huku mengine yakianguka chini.
Kwakweli hali ilikuwa mbaya sana na kuwafanya watetemeke kwa uoga.
Jeff na Sabrina wakiwa wameambatana na mama mdogo wa Sam wakielekea nyumbani kwakina Jeff, walipokuwa wanakaribia kufika tu njiani mama wa Sam akasita kidogo kisha akawaambia,
"Tuelekee kwanza kwakina huyu"
Akimaanisha kwakina Sabrina ambapo Jeff akamuuliza,
"Kwanini kwakina Sabrina wakati kwetu ndiko ambako hujawahi kufika?"
"Ni kweli sijawahi kufika kwenu ila roho yangu inaniambia kuwa kuna tukio baya kwakina Sabrina"
Ikabidi wakubaliane nae na kuanza kuelekea kwakina Sabrina kwanza.
Huku mama Sabrina na Sakina wakiwa na hekaheka dhidi ya yule mtoto, wakapata wazo kuwa wamkimbize hospitali ingawa Sakina nae alikuwa na wazo lake ambalo ni wazo alilopenda kulitumia mara nyingi sana,
"Hivi mama kwanini tusimpeleke kwa mtaalamu?"
"Yani Sakina na kuumwa kote kule bado una mawazo ya wataalamu!"
"Mama, hiki kitu sio cha kawaida. Tukienda hospitali tutampoteza huyu, hebu muangalie jamani ni kurogwa huku"
Ila mwisho wa siku ikabidi wakubaliane tu kumpeleka hospitali na kumpigia simu dereva ambapo walivyokata simu tu dereva alisema yupo nje.
Mama Sabrina na Sakina wakatazamani,
"Mmh huyu dereva hatari, hebu tumuwahishe hospitali."
Hawa wawili walikuwa kama hawajielewi hata mambo waliyoyafanya kwa haraka haraka hawakuyaelewa kwa muda huo.
Wakatoka nje na yule mtoto mikononi, na kweli wakaona gari ikiwa pale nje ikiwasubiri.
Wakaisogelea ile gari ili wapande.
Gafla wakasikia sauti ya kuwazuia,
"Hapana msipande humo"
Mama Sabrina na Sakina wakashtuka na kufanya waangalie alie wakataza, walipotazama wakamuona Sabrina, Jeff pamoja na mama mdogo wa Sam na aliyekuwa akiwakataza alikuwa ni mama mdogo wa Sam.
Waliposhusha tena macho ili waangalie lile gari halikuonekana tena mbele yao na kuwafanya washtuke sana kisha kurudi nyuma yani kama wanakimbilia ndani hivi huku wakiwaangalia wakina Sabrina ambapo Sabrina alipofika eneo lile alikuwa wa kwanza kumdaka mwanae huku akiangua kilio kwani hakujua kuwa mtoto wake kapatwa na nini.
Ikabidi mama mdogo wa Sam atumie busara kwa kuwarudisha tena ndani ili wasije wakajaza watu pale maana kile kilio cha Sabrina na ile hali ya mtoto ingesababisha pale pajae watu ambao wangefika kushangaa kuwa kuna nini.
Walirudi ndani huku Sabrina akilia sana ila mama mdogo wa Sam aliamua kumbembeleza kwa busara ili aweze kumtuliza bila ya kujaza watu.
Waliingia ndani, kisha mama mdogo wa Sam akaomba apewe yeye yule mtoto ambapo Sabrina alimkabidhi huku akilia kimya kimya kwani kwasasa hakupayuka na kilio kama cha mwanzo.
Kisha mama mdogo wa Sam akawauliza kilipo chumba cha kulala nao wakamuonyesha ambapo huyu mama akainuka na huyu mtoto ili kumpeleka kwenye chumba hicho.
Cherry nae hakuweza kubaki na yeyote kati ya wale waliokuwepo pale sebleni kwani alimshikilia huyu mama na kwenda nae hadi chumbani ambako walikaa humo kama dakika tano kisha huyu mama Sam na Cherry wakatoka.
Wote pale sebleni walitulia wakingoja kauli toka kwa huyu mama ambaye alisimama na kuongea kwa kifupi kwanza,
"Jamani, mimi sio Mungu ila Mungu ananionyesha maono. Kuna kitu kimetokea dhidi ya yule mtoto, si kitu cha kawaida ila ni mambo ya nguvu za giza. Basi nawaomba kwa pamoja tusimame na tuombe kwa Mungu amponye, tuwe na imani na Mungu atafanya"
Hakuna aliyebisha dhidi ya hili, kisha wakashikana mikono na kila mmoja akaomba kwa imani yake.
Baada ya dakika chache, mama mdogo wa Sam akakatisha haya maombi na kuwaambia tena
"Jamani, kila mmoja aombe Mungu. Tuombe kwa imani na Mungu atafanya"
Kisha akamuangalia Sakina na kumwambia,
"Tafadhari kuwa na imani, waganga wa kienyeji hawawezi kutusaidia kwa hili zaidi wataongeza tatizo juu ya tatizo. Weka imani yako kwa Mungu, achana na mawazo ya waganga wa kienyeji"
Sakina kidogo akaogopa kwa hili kwani ni kweli mawazo yake yalikuwa ni kuhusu waganga tu, hivyo kutetemeka kule kulimfanya ashindwe kuendelea na maombi yale hivyobasi mama mdogo wa Sam akamuomba atoke nje kwanza naye akafanya hivyo.
Sakina alipokuwa nje bado alikuwa hana imani na kile ambacho walikuwa wakifanya ndani,
"Yani hawa wanachekesha kweli, yule mtoto ndio tunampoteza hivi tunamuona. Yani alipokuja mwanzo huyu mama na sera zake za kutukataza tusipande lile gari halafu tumeliangalia limepotea nikajua ni mtu muhimu sana, sasa badala afanye mandingo eti anataka tuombe loh yani hapo wataomba hata bahari ikauke lakini hawataweza. Hapo huyo mtoto ni wa kupelekwa kwa mtaalamu tu"
Kwakweli alikuwa pale nje akiwasikitikia na kuwaona kuwa wanapoteza muda tu kwakile ambacho walikuwa wakikifanya.
Akatoka kabisa nje ya nyumba ile, mara akaona gari kama lililokuja mwanzo kuwafata.
Kwavile ni muoga, na hapa uoga ukamshika tayari.
Ila kwenye lile gari akashuka kijana na kumsogelea ambapo alitaka kukimbia na hata kupiga kelele kwa uoga.
Na kadri yule kijana alivyokuwa akisogea ndipo Sakina nae uvumilivu ulivyozidi kumshinda na kujikuta akipiga kelele kweli.
Kelele za Sakina zilifika ndani na kuwashtua wote kasoro mama mdogo wa Sam, ambapo wote walikimbilia nje na kumuacha yule mama akiwa mwenyewe ndani na yule Cherry.
Mama mdogo wa Sam alisikitishwa na hiki kilichotokea ila aliamua yeye mwenyewe kubeba mzigo wa yule mtoto peke yake kwahiyo aliingia tena kwenye kile chumba alichomlaza yule mtoto akiwa ameambatana na Cherry, na sasa alianza mwenyewe kutubu kwanza mbele za Mungu kwani maombi ya mwanzo ilikuwa kama ni mchezo ukizingatia aliozungukwa nao walikuwa na imani haba.
Huyu mama alimuomba Mungu kwakweli huku akisaidiwa na mjukuu wake pembeni kwa maombi.
Wale walipotoka nje wakamkuta Sakina akiendelea kupiga zile kelele zake ikabidi wamshtue na wamuulize vizuri ambapo aliwaonyesha yule kijana mbele yake nao wakamuangalia na kumuhoji kuwa kulikoni.
"Hata mimi mwenyewe namshangaa, maana nimefika hapo nikawa nasogea ili kumuuliza nashangaa anapiga kelele"
Mama Sabrina akamuangalia vizuri huyu kijana na kugundua kuwa ndio yule aliyempigia simu kuwa aje awafate, mama Sabrina alimuangalia kwa mshangao na kumuuliza,
"Si nilikupigia simu utufate wewe na ukatufanyia mazingaombwe hapa!!"
"Mazingaombwe kivipi mama, niliongea nawe kwenye simu na nikakwambia kuwa nipo mbali. Na kweli nilikuwa mbali ila kwavile simu yako haipatikani tena nikaona ni vyema nije kuangalia kama mmepata usafiri au la ili niwachukue"
Mama Sabrina akashangaa kwani maongezi yake na huyu kijana hakusikia hilo neno la nipo mbali zaidi ya kuambiwa nipo hapa nje tokeni.
Mama Sabrina alimuangalia sana na kushindwa hata kuongea kwani aliona kamavile ni mambo ya ajabu kwa yaliyotokea mwanzoni.
Akamuangalia tena kisha akaliangalia lile gari lake ambalo lilikuwa vile vile kama lililokuja mwanzo na kumfanya hata mama Sabrina na yeye apatwe na mashaka kiasi juu ya kile kilichotokea.
Ila yule kijana alipoona kuwa mambo hayaeleweki hapo ikabidi awaage na kuondoka zake.
Walibaki pale nje wakiulizana maswali kadhaa bila ya majibu kisha wakashauriana kurudi ndani ila kabla ya kurudi Sakina alimuuliza mama Sabrina,
"Ila mmeishiana vipi na hayo maombi?"
"Ooh Mungu wangu, sisi wanadamu ni wadhaifu sana kelele zako zilifanya tushindwe kustahimili pale ndani na hata sijui huyu mama anatufikiriaje"
"Mmh! Hivi kwa mtazamo wako yule mtoto atapona kweli kwa hayo maombi?"
"Sijui ila tumuachie Mungu"
Sabrina akashikwa na hofu tena pale nje baada ya kukumbuka kuwa wamekimbilia nje na kuacha kumuangalia mtoto na kusaidiana kwa hayo maombi.
Wakajikuta wote kwa pamoja wakirudi ndani huku wakiwa wamenyong'onyea.
Kwenye ile nyumba ya Sam bado Sam alikuwa akitetemeka sana dhidi ya kile alichoambiwa kuwa kuna kitu kibaya kinaenda kufanyika.
Uoga ulikuwa umemjaa, akamuangalia Emmy na kuwa kama mtu anayeomba msaada juu ya hili
"Emmy nisaidie tafadhari, nakuomba nisaidie Emmy nishakosea tayari na sina msaada popote. Tafadhari Emmy nisaidie"
"Tatizo la msaada wangu kwako kwa muda huu lazima uwe na madhara juu yake je upo tayari?"
"Madhara gani?"
"Tatizo lako ndio hilo, Sam narudia tena. Ulishafanya makosa tayari kwahiyo usipendelee kuendelea kufanya makosa, unatakiwa uwe tayari kwa chochote ili niweze kukusaidia. Ukijibu tu kuwa upo tayari basi nitakusaidia"
Kwavile Sam ilikuwa maji ya shingo yamemfika na ukizingatia masharti aliyopewa alishayakosea ikabidi akubaliane na madhara aliyoambiwa na Emmy kuliko kuuwawa kwa kukosea masharti aliyopewa.
"Kwahiyo upo tayari?"
Akaitikia kwa kutikisa kichwa,
"Hapana, nataka unijibu kwa sauti yako Sam. Upo tayari?"
"Ndio nipo tayari"
Lile jibu lilifanya Cherry atokee mbele yao huku akiwa na hasira sana.
Emmy nae akamwambia kwa ujasiri,
"Tafadhari njoo na sura yako halisi, acha kutumia umbo la mtoto mdogo asiye na hatia"
Yule Cherry akatoweka tena na kumfanya Sam azidi kutetemeka kwani alijua wazi kuwa umbo halisi la hiki kiumbe ni umbo la kutisha sana hata akamshangaa Emmy kuwa kapata wapi ujasiri wa kuweza kuongea hayo na kumwambia kuwa huyu kiumbe aje na umbo lake halisi.
Wakina Sabrina waliporudi ndani walishangaa kumkuta mama mdogo wa Sam akiwa na watoto wote wawili pale sebleni tena wakiwa salama kabisa.
Walijikuta wakiwa kimya na kuanza kumshukuru kwa aibu,
"Haipaswi kunishukuru mimi ila mshukuruni Mungu, hivi iko wapi imani yenu dhidi ya Mungu aliyewaumba? Ni kweli sisi wanadamu ni dhaifu ila kwanini kuachia udhaifu utawale hivi katika maisha yetu. Hivi mnaamini uwepo wa Mungu kweli? Na je mnaamini kuwa Mungu ndiye aliyetenda haya?"
Wakaitikia kwa pamoja kuwa wanaamini,
"Na kama mnaamini ni kwanini mmefanya migumu miyoyo yenu? Kwanini hamtaki kuamini kuwa Mungu atatenda? Wakati tunafika hapa, nikawaona mnataka kuingia kwenye jeneza"
Mama Sabrina na Sakina wakashtuka na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,
"Jeneza?"
"Ndio, ila nyie mlikuwa mnaona kuwa lile ni gari. Halikuwa gari lile ndugu zangu lilikuwa ni jeneza na wote mngeishia huko kwa siku ya leo. Ila mnatakiwa kushukuru sana, mshukuruni Mungu kuwa anawapenda. Shukuruni sababu inatupasa kushukuru kwa kila jambo na ukizingatia kama hili kubwa lililotokea leo. Huyu mtoto ilikuwa ndio tunampoteza hivi ila Mungu ni mwema na anatupenda sana."
Sabrina akamchukua mwanae na kumuangalia, alikuwa kama mtu asiyeamini juu ya uzima aliouona kwa mwanae kwa muda huo kwani mtoto alionekana kamavile hakuna chochote kibaya kilichompata.
Ila huyu mama mdogo wa Sam aliwaomba kuwa aondoke na hawa watoto wote kwa pamoja.
"Hapana kwakweli labda na mimi twende wote"
"Hata na mimi pia"
"Mmh nani atabaki hapa?"
Walikuwa kimya kwani kila mmoja aliona ni vyema kuishi na huyu mama karibu.
Emmy alimshika Sam mkono na kumuomba watoke nje, Sam hakupinga ukizingatia muda huo alikuwa kama mtu asiyejielewa.
Walipofika nje, gafla nyumba ya Sam ikalipuka kamavile ilitegeshewa bomu ndani.
Sam nae alikuwa kama kapatwa na maruweruwe na kujikuta akimponyoka Emmy na kukimbilia kwenye mlipuko.
Emmy alimshika Sam mkono na kumuomba watoke nje, Sam hakupinga ukizingatia muda huo alikuwa kama mtu asiyejielewa. Walipofika nje, gafla nyumba ya Sam ikalipuka kamavile ilitegeshewa bomu ndani.
Sam nae alikuwa kama kapatwa na maruweruwe na kujikuta akimponyoka Emmy na kukimbilia kwenye mlipuko.
Kwakweli hili tukio lilikuwa la gafla sana kwahiyo muda ambao Emmy aligundua tayari Sam alikuwa ndani ya moto.
Kwa bahati gari la zima moto lilifika na kufanikiwa kumuokoa Sam ingawa tayari alikuwa na majeraha ya moto.
Kilichofanyika kwa wakati huo ni kumkimbiza Sam hospitali kwani hakuwa na fahamu yoyote ile.
Familia ya Sabrina wakiwa bado wanabishana juu ya nani ataenda na mama wa Sam kule nyumbani kwake, maongezi yao yakakatishwa na mlio wa simu ya Jeff ambapo alisogea pembeni kidogo na kuipokea simu hiyo.
Muda kidogo Jeff akarudi pale walipokaa wakina Sabrina huku amenyong'onyea na kufanya Sabrina kuwa wa kwanza kuuliza kuwa kuna tatizo gani,
"Jamani, Sam kalazwa"
Wote wakashtuka kwani hakuna aliyeelewa moja kwa moja imekuwaje hadi amelazwa sababu hata taarifa aliyopewa Jeff ilikuwa ni juu ya kulazwa kwa Sam na hospitali aliyolazwa bila ya kuambiwa chanzo, hivyobasi Jeff akawaomba kuwa yeye aende kwanza halafu awaletee taarifa,
"Kwanini tusiende wote?"
"Sabrina, tulia kwanza. Mambo mengine si ya kukurupuka ukizingatia ujaji wa hizi taarifa kwanza. Angalia tuna matatizo kwasasa kwahiyo hatutakiwi kukurupuka, hebu jiulize hapo Sam kalazwa na kwanini mimi niwe wa kwanza kupewa taarifa? Kwanini asipigiwe simu mama yake hapo? Kwasasa tuna mapambano kwahiyo inatakiwa tuwe makini kwa kila ujumbe tunaopokea"
Sabrina alionekana kuelewa kiasi ila wakati wote huo wakijadiliana, mama mdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa mpaka pale alipomuona Jeff akitoka napo alimwambia neno moja tu,
"Mungu akutangulie."
Jeff akatoka na kuondoka akielekea kwenye hospitali aliyoelekezwa.
Nyumbani kwakina Sabrina, mama mdogo wa Sam aliwaomba watulie na wajitahidi kumuombea Sam kwa lolote lililompata.
"Naomba mnisikilize, mimi ni mama mdogo wa Sam ila huyu Sam ni kama mwanangu wa kumzaa, ni mtoto wa dada yangu kwahiyo na mimi ni damu yangu. Kwa maana hiyo najua mnaelewa ni kiasi gani nimepatwa na mshtuko na uchungu kwa hizi taarifa. Ila nawaomba tumuombe Mungu atutie nguvu na atuepushe na mabaya yote yanayotunyemelea kwasasa. Mimi ni mwanadamu kama nyie, nina uchungu, nina mawazo pia maana najua hapa wengine mnajiuliza kuwa kwanini kama nina uchungu sijapapalika kwenda kumuona! Jamani yatupasa kuomba sana, tunatakiwa kuomba kwa yote yaliyo mbele yetu ikiwa yametokea au yanatarajia kutokea. Sina silaha yoyote mimi zaidi ya maombi, naomba tusaidiane jamani hili tatizo ni letu sote. Najua wote tumeshtushwa na habari hii, basi hatuna budi tuombe jamani"
Wote walikuwa wametulia na ilionyesha wazi kuwa haya maneno yamewaingia na kuwagusa kabisa na kufanya wawe wapole na wamuombe Mungu kweli kwani matukio ambayo yalikuwa yakiwatokea kwa kipindi hiki yaliwashangaza sana.
Jeff alikaribia hospitali aliyoelekezwa ila akasita kidogo kwani gafla kwenye lile eneo hakuona jengo la hospitali.
"Mmh! Hospitali waliyoitaja si huwa ipo hapa? Imekuwaje tena haipo?"
Mashaka yakamjaa na kujikuta akikimbia eneo lile ila kabla hajafika mbali alikutana na mdada ambaye alimshika mkono na kubadilisha nae njia.
Jeff hakuelewa kitu na wala hakumuelewa yule mdada ila kwavile alikuwa hajielewi aliona ni vyema kufatana na huyu mdada.
Walipofika mbele, huyu mdada akiwa kamshikilia mkono Jeff alisimama sasa na kumwambia.
"Pole sana"
"Hebu nieleweshe basi, unanifahamu? Je unafahau kilichokuwa kikiendele?"
"Sikufahamu na wala wewe hunifahamu ila kuna mtu kati yetu anakufahamu wewe na ananifahamu mimi. Twende tukakae pale kwanza tuzungumze vizuri"
Jeff hakupinga ingawa bado alikuwa hamwelewi huyu dada.
Wakaondoka nae kabisa lile eneo, wakafika mahali karibia na hospitali nyingine.
Wakaingia kwenye hiyo hospitali na kukaa kwenye benchi lililokuwepo nje ya ile hospitali kisha huyu dada akajitambulisha kwa Jeff,
"Mimi naitwa Emmy, vipi wewe waitwa nani?"
"Mimi Jeff, hebu nieleze vizuri maana kiukweli sikufahamu"
"Ndio hunifahamu hata mimi sikukufahamu kwa kukuona bali nilikufahamu mawazoni"
"Mmh kivipi?"
"Kwanza niambie imekuwaje hadi ukafika pale?"
Ikabidi Jeff amueleze vile alivyopigiwa simu kuhusu Sam na jinsi alivyoelekezwa hospitali aliyolazwa Sam.
Emmy akatingisha kichwa kutokana na mawazo aliyokuwa nayo,
"Sasa nimeelewa, kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa sana kushinda nilivyofikiri"
"Kwani vipi? Hebu nieleweshe dada"
"Ni kweli Sam amelazwa na hali yake sio nzuri kwani ameungua sana"
Jeff akashtuka na kushangaa,
"Imekuwaje hadi ameungua? Nini kimempata kwani? Je ni wewe uliyepiga simu kunitaarifu?"
"Swala la kuungua ni maelezo marefu kiasi ila kwa kifupi ni kuwa nyumba yake imeungua na kila kitu ndani yani hakuna kilichopona, sasa na yeye alikimbilia ndani ili kujaribu kuokoa baadhi ya vitu. Ila swala lingine, mimi sikuwa na mawasiliano ya ndugu yeyote wa Sam kwahiyo hakuna niliyempigia simu"
Jeff akafikiria kitu kidogo, kwanza akafikiria hali ya Sam kwa wakati ule pia akafikiria nyumba ya Sam aliyoambiwa kuwa imeungua na hakuna kilichookolewa toka kwenye nyumba hiyo, pia akafikiria juu ya mtu aliyempigia simu yeye kumpa taarifa,
"Sasa ni nani aliyenipigia simu?"
"Nadhani ni yule aliyeteketeza nyumba ya Sam"
"Nani huyo?"
"Tusimzungumzie tafadhari"
"Basi niambie, wewe umejuaje na kunifata pale?"
"Mimi nilikuwa hapa hospitali, gafla moyo wangu ukaanza kuuma, na mara nyingi moyo ukiniuma huwa najua wazi kuna tukio baya linataka kutokea. Nikatulia kwanza na kujiuliza kuwa kuna nini? Kuna kitu kiliniambia moyoni kuwa kuna mtu wa karibu na Sam anataka kuteketezwa. Ni hapo nilipoomba niongozwe kumsaidia mtu huyo.
Niliondoka hapa hospitali na kufika eneo lile, nikakuona upo ukingoni mwa bahari halafu unataka kukimbilia baharini na ndiomana nikaja na kukushika mkono ili tuondoke pamoja, kwa bahati nzuri nawe umekuwa msikivu"
Jeff akajikuta tena akipatwa na mawazo, moja kwa moja akahisi kuwa huenda mtu huyo alikuwa ni yule Cherry wa ajabu kwani alijaribu kukumbuka tukio ambalo yeye alilazimishwa kumpigia simu Sam kwahiyo akawaza kuwa lazima kuna mtu alilazimishwa kumpigia simu yeye na ndiomana ikawa vile ilivyokuwa. Akajikuta akipumua kidogo na kusema,
"Asante Mungu kwa kunisaidia"
Kisha akamuomba Emmy ampeleke alipolazwa Sam ili aweze kumuona.
Emmy aliinuka na Jeff pale, kisha moja kwa moja akampeleka chumba alicholazwa Sam.
Kwakweli Jeff alisikitika sana kwani hali ya Sam ilikuwa mbaya na alionekana kuungua karibia kila sehemu ya mwili wake.
Jeff alijikuta akijiuliza maswali kadhaa kwani hali ya Sam ilikuwa ni mbaya kwakweli, akamuangalia Emmy na kumuuliza
"Inamaana wakati nyumba inaungua huyu Sam alikuwa ndani yake?"
"Hapana, yani ilitokea v gafla Sam akaenda ndani ambako nyumba inaungua ila kwa bahati zima moto na waokoaji nao walifika mapema yani hali ya Sam ni mbaya kwakweli. Tuombe tu apone na arejee kwenye hali ya kawaida."
Jeff akawaza jinsi ya kuwapa taarifa wale aliowaacha nyumbani ila kwavile muda nao ulikuwa umeenda akaona si vyema kuwashtua kwa muda ule ili wasiwe na hofu.
Ila wakati anawaza hayo, simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia na kukuta mpigaji ni Sabrina ikabidi amuulize kwanza Emmy kuwa kama awaambie ukweli wa hali halisi au afanyaje.
"Waambie kuwa ukirudi utaenda kuwaeleza vizuri"
Naye Jeff akasema kama alivyoagizwa na Emmy.
Alipomaliza kuongea akamuuliza kwanini ameamua kuwa asiseme ukweli,
"Unajua usiku umeingia, halafu usiku una mambo mengi. Sasa kwa hali halisi ilivyo nimeona si vyema ukawaambia ukweli kwani hujui watapaniki vipi na mwisho wa siku watake kuja usiku usiku. Naona ni tatizo, na ukizingatia kwa hali ya mgonjwa ilivyo haitakiwi azungukwe na watu wengi. Jamani mie nipo hapa kwahiyo msiwe na shaka kabisa, na tena uwaambie hali halisi kesho asubuhi ili hiyo kesho ndio waje wamuone mgonjwa"
Jeff alikubaliana na Emmy kisha kumuaga ili aweze kurudi nyumbani na aweze kujipanga namna ya kuwaeleza wakina Sabrina.
Jeff alikawia kufika na kwakweli wote pale kwakina Sabrina walikuwa wakimsubiria afike ili awaeleze alichokutana nacho huko alipokuwa.
Ila bado hakuwasili, ikabidi Sabrina ampigie tena Jeff simu ambapo alidai kuwa amesharudi kwao.
"Jamani, hivi huyu Jeff nae ana akili timamu kweli?"
Sakina akauliza kuwa kwanini mwanae asiwe na akili timamu,
"Hivi muda wote tunamsubiri hapa atupe majibu eti kumbe amepitiliza nyumbani na tena ananiambia kuwa ameshalala"
"Mmh! Huyu Jeff akili zake ni mbili kasoro huyu, na mimi siwezi kurudi kule kwangu usiku huu kwahiyo itabidi tu nilale hapa hapa"
Sakina aligoma kuelekea nyumbani kwake, ila kwavile hapo vyumba vilikuwepo basi wakaona ni vyema alale hapo.
Hata mama mdogo wa Sam nae isingewezekana kurudi kule kwa Sam kwani usiku ulikuwa wa kutosha.
Ikabidi wajikusanye wakalale ambapo kwa matukio yaliyopo Sabrina aliona vyema yeye alale pamoja na mama mdogo wa Sam na wale watoto wake.
Wakajipanga halafu wakaenda kulala.
Wakiwa wamelala, Sabrina alijikuta akimfikiria Jeff na kujawa na wivu juu yake.
Akakumbuka kuwa kwakina Jeff kuna binti wa kazi aitwaye Keti, hofu ikamjaa kuwa pengine Jeff amefanya vile ili apate nafasi ya kuwa na huyo Keti ukizingatia hata mama yake alilala huko kwao, kwahiyo kwenye ile nyumba walibaki wawili tu yani Jeff na Keti.
Kwakweli Sabrina usingizi ukakata kwa wivu kwani alijikuta akimfikiria sana Jeff kuwa anasalitiwa.
Akatamani hata aende ili akashuhudie kama kweli anasalitiwa ila ule usiku ulivyo mkubwa ulikuwa ukimuogopesha kwani ni ngumu kujua kuwa nje utakutana na kitu gani.
Akakaa akijifikiria, mama mdogo wa Sam alishtuka usingizini na kumuona Sabrina jinsi alivyokaa na mawazo,
"Vipi Sabrina! Mbona umejiinamia kwa mawazo? Kila kitu muombe Mungu akupe amani naye atakupigania"
Sabrina akamsikiliza huku akijiuliza kimoyo moyo,
"Na kusalitiwa nako nimuombe Mungu! Mmh ili afanyaje? Amzuie asinisaliti?"
Mama Sam alimuangalia tu Sabrina, ingawa hakumsikia chochote ila akamwambia,
"Kila kitu kinawezekana mbele za Mungu, cha muhimu ni kuomba amani kwanza."
Kisha akamsihi Sabrina kuwa arudi kulala, ingawa Sabrina alirudi kulala ila mawazo yake yote kwa muda huo yalikuwa ni juu ya Jeff, huku akitamani pakuche mapema.
Palivyokucha tu, Jeff akawa wa kwanza kufika na kuwagongea mlango ambapo mtu wa kwanza kuamka alikuwa ni mama Sabrina.
Kisha akamkaribisha Jeff ndani,
"Ila ulichofanya jana hakikuwa sawa Jeff, kwanini uamue tu kwenda kwenu wakati unajua fika tulikuwa tunakungoja huku?"
"Kwavile nilichelewa kurudi nikajua mtakuwa mmelala na ndiomana nami nikapitiliza nyumbani tu"
"Haya, vipi hali ya mgonjwa maana taarifa ya jana ilitutisha sana"
"Ile ile taarifa niliyoacha mimi au kulikuwa na taarifa nyingine?"
"Wakati umeondoka, kuna mtu alimpigia simu Sabrina na akasema kuwa Sam yupo kwenye hali mbaya sana yani tufanye juu chini twende tukamuone hata wawili wawili. Baada ya ile simu, Sabrina akatueleza ila mama Sam akatugomea kuwa tusiende hadi tuwasiliane na wewe halafu wewe unapigiwa simu unasema utatueleza ukifika. Hivi unafikiri tungewezaje kulala bila maelezo? Na ndiomana tukakungoja utueleze halafu ndio unatuletea hoja kuwa umelala yani wewe kwakweli hufai."
Wengine nao wakaamka na kuwakuta Jeff na mama Sabrina wakiwa pale sebleni ambapo Jeff akawasalimia ila kwa upande wa Sabrina hata hakujisikia kuzungumza na Jeff kwani bado alikuwa amekabwa na donge la wivu kooni.
Kisha Jeff akawaeleza hali halisi ya Sam iliyofanya wote kushtuka na kuingiwa na huruma kwa kile kilichoelezwa.
Mama mdogo wa Sam aliumia kwakweli ila alijitahidi kujikaza ili aweze kwenda kumuona huyo Sam.
Wakajiandaa wote, kisha wakafunga nyumba na kuondoka kwani kwa kipindi hiko hakuwepo baba wa Sabrina wala kaka yake kwani walisafiri siku za nyuma.
Walifika hospitali na kumkuta Emmy ambaye aliwapa habari kwa ufupi kuhusu Sam kisha ikatakiwa kwenda kwa awamu kumuona mgonjwa kwani kutokana na hali yake haikutakiwa kwenda wote kwa pamoja.
Walikaa pale nje ya hospitali na kujadiliana mawili matatu ila wakaona ni vyema wakachukue pesa nyumbani ili kuendeleza matibabu ya Sam kutokana na ile hali waliyomkuta nayo.
Mama mdogo wa Sam akatoa funguo na kumkabidhi Jeff ambapo walikubaliana kuwa Jeff na Emmy ndio waende nyumbani kwa Sam kwaajili ya kuchukua fedha zilizomo mule ndani.
Jeff na Emmy wakawaaga pale kisha wakaondoka zao kuelekea huko nyumbani kwa Sam.
Njiani, Emmy alionekana kuwa na mashaka kiasi ila alijipa moyo wa kuendelea.
Jeff nae hakuwa akijiamini ukizingatia alishasimuliwa mengi na Sabrina kuhusu Sam, ila kwavile aliambatana na mdada aliyemuokoa jana aliona ni vyema ajiamini tu.
Walifika nyumbani kwa Sam na kufungua milango kama kawaida, ila nyumba ilionekana kuwa kimya sana.
Hilo halikuwatisha ukizingatia ni kweli mule ndani hapakuwa na mtu yeyote.
Wakaambizana kuwa moja kwa moja wakaangalie chumbani kwa Sam ili kama wakikosa pesa basi watafute kazi zake ili kama ana kadi ya huduma za afya na aendelee kutibiwa kwa kadi na wasiingie gharama zitakazowashinda.
Na kweli walipoingia chumbani, walikuta kadi zote za Sam zikiwa kitandani hadi zile kadi zake za benki, hii kitu ikawapa matumaini zaidi kisha wakazichukua.
Jeff akaenda kufungua droo na kukuta pesa nyingi sana zikiwa zimefungwa kimaburungutu, ni hapa akamwambia Emmy
"Tatizo la kifedha limeshaisha Emmy"
Wakachukua begi ili wazipakie humo, ila kabla hawajafanya hivyo wakasikia harufu ya chakula yani ilikuwa kama mtu yupo jikoni kwenye hiyo nyumba ya Sam akipika.
Wakati wanasikilizia vizuri, wakasikia na sauti na vyombo vikigongana yani kanakwamba huko jikoni kuna mtu zaidi ya mmoja.
Jeff akaenda kufungua droo na kukuta pesa nyingi sana zikiwa zimefungwa kimaburungutu, ni hapa akamwambia Emmy
"Tatizo la kifedha limeshaisha Emmy"
Wakachukua begi ili wazipakie humo, ila kabla hawajafanya hivyo wakasikia harufu ya chakula yani ilikuwa kama mtu yupo jikoni kwenye hiyo nyumba ya Sam akipika.
Wakati wanasikilizia vizuri, wakasikia na sauti na vyombo vikigongana yani kanakwamba huko jikoni kuna mtu zaidi ya mmoja.
Haya mambo yaliwafanya kusita kidogo kwani ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwa nyumba ambayo haikuwa na watu zaidi ya wao wenyewe.
Jeff akajikuta akimuuliza Emmy,
"Inawezekana ikawa nini?"
Emmy akaweka kidole mdomoni kama ishara ya kutaka awe kimya.
Naye Jeff akatulia kimya huku moyo wake ukiwa umejaa mashaka ya kutosha.
Walivyotulia kwa muda, wakasikia sauti za watu kama wakizungumza sebleni, ikabidi waambizane ili wachungulie kuwa ni wa kina nani.
Kwavile waliambizana kwa ishara, ikabidi Jeff ajipe ujasiri wa kwenda kuwachungulia.
Alichungulia na kushtuka, kisha akarudi nyuma na kumnong'oneza Emmy,
"Nimemuona Sabrina na mama yake, wamefikaje na wameingiaje?"
Emmy akaweka mikono kichwani na kusema kwa sauti ya chini kabisa tena ile ya kujihami,
"Mungu wangu tumekwisha"
Jeff akapatwa na uoga na kumuuliza,
"Kwani ni nini? Na tunafanyaje?"
Emmy alikaa kimya kwa muda kama akitafakari kitu kingine.
Hospitali nako, mama mdogo wa Sam alionekana kutokuwa na furaha hata kidogo na ilionyesha kuwa anafikiria mambo mengi sana.
Ikabidi mama Sabrina awe nae karibu akimuuliza,
"Unaonekana kuwa na mawazo sana, kwanini? Kumbuka wewe ndiye tunakutegemea kwa sasa, wengine imani zetu zilikufa siku nyingi sana ila bado naamini kuwa Sam atapona. Na vipi wewe unaonekana kuwa na mawazo hivyo?"
"Mapambano ni makubwa sana, sikujua kama Sam amepitia kwenye mambo ya ajabu kiasi hiki. Kuna vitu naviona, kuna mambo nayaona hata sijui nianzie wapi katika maombi yani kila sehemu ni tatizo, kila mahali kuna ngome ngumu imewekwa. Sijui Sam alifikiria nini hadi akaamua kuwa vile alivyokuwa. Kwakweli Mungu atusaidie na atupe ujasiri."
Mama Sabrina alikuwa akijitahidi na yeye kuongea maneno ya kuleta amani ili kidogo wawe na amani.
Kwa upande wa Sabrina alikuwa na mawazo mbali mbali, katika mawazo hayo alikumbuka hadi siku ya kwanza kukutana na Sam akiwa kwenye hoteli yake Arusha.
Akakumbuka jinsi Sam alivyokuwa mkarimu kwake hadi kufikia hatua ya kumpeleka nchi za mbali kusoma.
Kwakweli kwa muda huu alikuwa akikumbuka mema tu aliyofanyiwa na Sam na kuona kuwa ni mengi kuliko yale mabaya machache.
Alijipa imani na yeye na kumuombea Sam kuwa apone kwani hali yake ilikuwa mbaya sana na huwezi kumfikiria kuwa ndio yule kijana aliyekuwa tajiri mwenye mali nyingi.
"Mungu msaidie Sam, nakuomba umponye. Msamehe kwa yote aliyokosea, na wote aliowakosea wamsamehe kwaajili yangu"
Hapo akakaa kimya kwa muda na kujikuta akiwakumbuka wadada waliokufa sababu ya Sam haswaa alimkumbuka Neema na ile barua yake ya mwisho.
Akakumbuka pia alivyosimuliwa na Sam jinsi alivyoenda kwa mganga kwaajili ya kuwakomesha wanaomchukia na kumfanya awe tajiri.
Katika kufikiria hayo akaona ni muhimu awaeleze na hawa wazazi wao ili wajue na wafikirie kuwa ni jinsi gani ya kumsaidia Sam.
Aliwafata na kuwauliza muda watakaorudi nyumbani, ila kwavile mama mdogo wa Sam aliona ni vyema wakatulie na maombi basi hata yeye akashauri kuwa warudi tu maana Emmy na Jeff walikawia kurudi na hawakutoa taarifa yoyote.
Mama Sabrina nae akawashauri kuwa warudi wote kule kule nyumbani kwake, kisha wakafanya hivyo.
Walipofika nyumbani waliingia ndani, muda kidogo wakapata mgeni ambaye alikuwa ni shangazi wa Sabrina.
Walimkaribisha na kusalimiana nae,
"Hii ni mara ya pili nafika, mwanzoni nilikuta mmefunga nikaamua niende kwanza kwa huyo (akimaanisha Sakina) ila nae sikumkuta ila alikuwepo mdada mmoja akanikaribisha vizuri tu ila saizi nikasema ngoja nije kuwachungulia. Vipi kuondoka nyumba nzima! Kuna tatizo mahali?"
Ikabidi wamueleze hali ya Sam,
"Kheee sijaja huku siku nyingi jamani, amepatwa na nini tena?"
"Amepatwa na majanga ya moto"
Wakawa wanajadiliana pale kama walikuwepo kwenye chanzo cha huo moto ila Sabrina akawakatisha na kuwaomba kuwaeleza kitu kuhusu Sam,
"Jamani kuna kitu nataka kuwaambia kuhusu Sam, hiki kitu Sam aliniambia mimi tu kwavile ya upendo wake aliokuwa nao kwangu. Ila naona nyie ni watu muhimu na mnapaswa kulifahamu hili labda itasaidia kujua jinsi ya kumsaidia Sam"
Walitulia kimya wakimsikiliza Sabrina ila Sabrina nae akanyamaza kimya kwa muda akikumbuka kuwa Sam alimwambia yeye tu kwavile ana muamini sana je akisikia kawaeleza hawa atajisikiaje? Si atamuona kuwa ni msaliti?
Mama Sabrina akamshtua Sabrina na kumwambia,
"Tumetulia hapa tukisikilizia hiko unachotaka kutuambia halafu wewe umenyamaza kimya unataka tukueleweje sasa?"
Mama mdogo wa Sam naye akamwambia,
"Kama kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia ni vyema ukatueleza tu ili tujue tunaanzia wapi na kuishia wapi maana mambo mengine unaweza sema nifanye hivi kumbe jambo liko vile. Tafadhari tueleze tu hata usiwe na mashaka"
Sabrina akatulia tena kidogo kisha akajitoa muhanga na kuwaeleza ukweli wa mambo kulingana na vile alivyoelezwa na Sam.
Emmy alipofikiria kwa muda akachukua lile begi na kuweka baadhi ya hela na vile vitambulisho vya Sam halafu akalivaa mgongoni, kisha akamshika Jeff na kumwambia kuwa watoke ila Jeff alishangaa kuwa kwanini ameacha pesa karibia zote ila Emmy alimjibu kuwa aachane nazo.
Walipofika sebleni ni kweli wakawakuta wale wale ambao Jeff aliwaona na kumfanya Jeff atetemeke zaidi kwani ilikuwa ni kitu cha maajabu na kuogopesha yani watu muwaache hospitali, muingie ndani na kufunga mlango ila muwakute sebleni.
Jeff alikaa kimya tu ambapo Emmy akiwa kamshika vile vile mkono wakaenda mpaka mlangoni na kufungua mlango ila kabla hawajatoka wakaulizwa na mmoja wapo pale sebleni aliyekuwa na sura ya Sabrina,
"Kwahiyo mnatoka hamsalimii wala hamuagi!"
Emmy ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kujibu,
"Tunawaaga vipi wakati hampo katika maumbo yenu?"
Ikasikika sauti ya kicheko iliyomfanya Jeff atetemeke hadi mkojo ukamtoka.
Mara akatokea sasa yule Cherry mdogo,
"Umbo gani unalolitaka wewe? Hivi unajua kama wewe ndiye unayemuweka matatizoni huyo Sam? Maumbo yetu unaweza kustahimili wewe?"
"Ndio naweza ndiomana nimewaambia mje na maumbo yenu"
"Subiri"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wote wakayeyuka. Emmy akamshikilia mkono Jeff zaidi hadi wakatoka nje.
Walipofanikiwa kuwa nje kabisa, Emmy akamuomba Jeff asigeuke nyuma na wakaanza kuondoka eneo lile.
Kufika mbele kidogo Jeff akashtuka,
"Aah nimesahau simu yangu"
"Achana nayo"
"Sasa watu wakinipigia?"
"Achana nayo, kwanza shukuru Mungu tumetoka na usithubutu kugeuka nyuma"
Kwavile tayari Jeff alishajawa na uoga hivyo ikawa ni ngumu sana kwake kugeuka nyuma.
Walienda mbele tu hadi walipofika stendi ya daladala na kupanda daladala kuelekea hospitali.
Ile habari waliyosimuliwa na Sabrina iliwashangaza na kuwatisha sana,
"Kwahiyo Sabrina siku zote unaishi na Sam na unajua wazi kuwa ana matatizo hayo! Umewezaje?"
Mama Sabrina alimuuliza mwanae kwa mshangao sana, na leo akajua ni jinsi gani mwanae alivyokuwa na roho ngumu tena ya kijasisi kwani si rahisi mtu kuficha mambo ya hatari kiasi hicho.
Sakina nae akafikiria kitu na moja kwa moja akajiwa na kumbukumbu ya maneno aliyoyasikia kipindi cha nyuma wakiwa hotelini pia akajikuta akikumbuka na kifo cha Amina, hapo moja kwa moja akapata jibu kuwa hata kile kifo kilisababishwa na Sam, alijikuta akijiuliza mambo mengi na kujijibu mwenyewe, mwisho akaamua tu kumuuliza Sabrina,
"Inamaana yule Amina alikufa baada ya kutembea na Sam eeh!!"
Sabrina akaitikia kwa kutikisa kichwa, kisha Sakina akamuuliza tena
"Kwanini hukuniambia Sabrina?"
Ikabidi shangazi wa Sabrina aingilie kati,
"Jamani huu sio muda wa kuulizana kwanini, tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuhusu huyo Sam. Yani kwa maelezo ya Sabrina hapa kafanya nikumbuke mambo mengi sana"
Mama mdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa akiwasikiliza huku akitafakari mambo mbali mbali.
Shangazi wa Sabrina ndiye pekee aliyejikuta na ufafanuzi wa mambo mbali mbali,
"Jamani kwa maelezo hayo naona kabisa Sam ana jini, na hilo jini ndio linalolinda mali zake. Sasa inahitajika umuhimu sana wa kwenda kuangalia mali za Sam ila inahitajika umakini wa hali ya juu maana bila ya hivyo itatugeukia sisi wenyewe. Na kuhusu moto uliomuunguza ilikuwaje?"
"Ni nyumba yake ndio iliyoungua na yeye ndio akaungua"
Ilabidi warudie yale maneno Waliyomwambia mwanzoni ambavyo huyu shangazi wa Sabrina alikuwa akishangaa tu ila mama mdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa na ilionyesha wazi kuwa kuna vitu vingi vinavyomfanya awe kimya akivifikiria kwa undani zaidi kabla na yeye hajatoa tamko lake.
Emmy na Jeff walienda moja kwa moja hospitali ila wakashangaa kwa kutokuwakuta wakina Sabrina,
"Inawezekana wameenda nyumbani na inawezekana walijaribu kupiga labda wakakuta haipatikani na hivi nimeiacha kule inawezekana kabisa"
"Basi tukubali tu kuwa wamerudi nyumbani ila walitakiwa kutusubiri kama makubaliano yetu yalivyokuwa."
Kisha wakaongozana tena kwenda kumuangalia Sam ambaye kwa wakati huu hali yake ilionekana kidogo afadhari,
"Mungu amsaidie Sam apone tu ili nikatimize naye kile nilichokubaliana nae"
"Kipi hicho?"
"Huwezi kujua, haya ni mazungumzo baina ya mimi na Sam"
Jeff alivyokaa kidogo akajisikia harufu ya mikojo na kukumbuka kuwa mikojo ilimtoka kule nyumbani kwa Sam kwa uoga, hivyobasi akaamua kumuaga Emmy na kuondoka zake ili akaweze kubadili nguo.
Kwahiyo akaagana na Emmy pale kisha akaondoka zake.
Emmy alibakia mwenyewe sasa pale hospitali, alitoka nje na kukaa kwenye benchi huku akijiuliza maswali mbalimbali, muda kidogo akasikia sauti ikimuongelesha kana kwamba huyo mtu amekaa nae karibu pale,
"Sam anaendeleaje?"
Emmy akakaa kimya kidogo kisha naye akauliza hiyo sauti,
"Unauliza wewe kama nani kwa Sam?"
Ile sauti ikacheka na kumuuliza tena,
"Kwani wote wanaoulizia hali ya mgonjwa wana undugu naye?"
Emmy akakaa kimya kwani kila akipepesa macho pembeni hapakuwa na mtu kabisa ila ile sauti jinsi ilivyokuwa ikiongea ilionyesha wazi kuwa huyo mtu yupo pembeni yake.
Akili ya Emmy ikacheza kwa haraka na kugundua kuwa hiyo ni michezo ya yule mtu wa ajabu kwahiyo Emmy akaamua kuwa makini sana juu ya hilo.
Mara akasikia ile sauti ikimwambia tena,
"Wewe unajifanya mjanja sana ila tutakuwa bega kwa bega na yule uliyekuja nae"
Ile sauti ikatoweka na kumfanya Emmy afikirie moja kwa moja kuhusu Jeff na hapo akapata wazo la kuwasiliana na Sabrina kwavile Jeff ameaga kwenda kwao akajua kwa vyovyote vile lizima watamsubiria kule kwao.
Kwavile yeye alishapitia mambo kama haya, ikawa ngumu sana kwa wao kumdhuru yeye moja kwa moja na ndiomana walikuwa wakitumia njia za pembeni.
Sabrina alipokea simu kutoka kwa Emmy na akapewa maelekezo,
"Kwahiyo nimsubiri akija?"
"Ndio ila uwe makini akifika tu jitahidi uwe nae karibu kisha usimwache awe peke yake."
Ile simu ilivyokatika tu, Sabrina akaambizana na Sakina pale kisha wakawaaga pale ndani kwao kuwa wanaenda kwa Sakina kwa muda halafu wakaondoka.
Mama mdogo wa Sam nae aliamua kutumia muda huu huku akimsisitiza mama Sabrina na shangazi wa Sabrina kuwa wakazane kumuomba Mungu.
Jeff alivyofika kwao, alimkuta Keti akiwa pale sebleni. Akamsalimia na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake ambapo alioga kwa haraka na kubadilisha nguo, wakati akitaka kutoka akajikuta akiamua kutazama zile nguo zake chafu.
Akashtuka kuona simu yake juu ya zile nguo, Jeff akaogopa sana ukizingatia ile simu ndiyo aliyoiacha kwa Sam.
Kwakweli Jeff aliamua kutoka ndani kwa uoga, alipofika sebleni akamuona Sabrina na mama yake.
Hofu ikamjaa na kujikuta akikumbuka kule nyumbani kwa Sam, kitu alichokifanya Jeff kwa muda huo ni kuanza kukimbia bila hata ya kufikiria.
Kwakweli Jeff aliamua kutoka ndani kwa uoga, alipofika sebleni akamuona Sabrina na mama yake.
Hofu ikamjaa na kujikuta akikumbuka kule nyumbani kwa Sam, kitu alichokifanya Jeff kwa muda huo ni kuanza kukimbia bila hata ya kufikiria.
sabrina na Sakina walijikuta wakitazamana kwani hawakujua ni kitu gani kimempata Jeff ila wakapata wazo kwa haraka la kumfatilia kwa nyuma kanakwamba watakimbia nae ila kile kitendo cha wao kumfata Jeff nyuma kilimpa mashaka zaidi Jeff na kumfanya aongeze mbio kwani aliona kama vile hatari inamkaribia.
Ikabidi Sakina na Sabrina wasimame huku wakijiuliza,
"Kwani imekuwaje? Kaingiwa na nini huyu jamani?"
"Hebu twende nyumbani kabisa tukawaeleze kuhusu hili maana si swala la kawaida."
Wakakubaliana kurudi nyumbani kwakina Sabrina ambapo waliwakuta waliowaacha na kuanza kujadiliana nao kuhusu swala la Jeff.
Mama Sabrina akawauliza,
"Kwahiyo amekimbilia wapi?"
"Hata hatuelewi, maana sie tunaingia na yeye alikuwa anatoka chumbani ila alipotuona tu akatimua mbio hizo balaa yani hata hatuelewi alipokimbilia"
"Au inawezekana kaelekea tena kule hospitali?"
"Labda"
Kisha wakajaribisha kupiga simu ya Jeff ambayo iliita tu bila ya kupokelewa.
Sakina na Sabrina wakashauriana kuwa waende hospitali kwanza kumuangalia ukizingatia hawakuweza kumpigia simu Emmy kwavile hawakuwa na mawasiliano yake.
Wakati Sabrina na Sakina wanataka kutoka, shangazi wa Sabrina akawazuia kwanza.
"Naona kama msiende huko"
"Kwanini shangazi?"
"Sijui kwanini ila roho yangu inanikataza nyie kwenda huko"
"Mmh sasa tutajuaje alipo?"
"Ila kama mmeamua kwenda basi nendeni"
Walishukuru kwa kauli hii na wala hawakutaka kumsikiliza zaidi kwani walijua wazi kuwa kwa vyovyote vile kama ataendelea kuongea basi atawazuia tu.
Sakina na Sabrina wakaondoka pale kwao na kuanza kuelekea hospitali.
Njiani wakakutana na Francis ambaye alikuwa ni rafiki wa zamani sana wa Sabrina ambapo walisalimiana nae na mwisho wa siku wakamueleza hali ya Sam ambapo Francis alionekana kupatwa na huruma sana kutokana na alivyoelezwa, kisha akampa pole Sabrina kwani alijua wazi kuwa lazima Sabrina ndiye mwenye uchungu zaidi ukizingatia ni mume wake.
"Pole sana Sabrina, ila atapona tu dah"
Kisha akaamua kuongozana nao kuelekea huko hospitali alipolazwa Sam.
Jeff alikuwa kama kachanganyikiwa kwa muda huo, mbio zake zilienda kuishia nyumbani kwa rafiki yake ambaye alipomuona Jeff alishangazwa sana na ujio wake na jinsi alivyokuwa,
"Kheee Jeff, vipi ndugu yangu una tatizo gani? Leo umekuja kwangu ni maajabu kwakweli ila cha ajabu zaidi unavyohema, nini tatizo?"
"Ommy wee acha tu, kuna majanga yamenikuta mwenzio hadi nimekuwa sijielewi yani sijielewi kabisa"
"Majanga gani hayo?"
Ikabidi Jeff ajibalaguze kwani aliona aibu kumueleza ukweli rafiki yake juu ya yale yanayomsibu kwa kipindi hicho.
Ila kwavile hakutaka kusema ukweli hata rafiki yake hakutaka kumlazimisha kwani alimjua fika Jeff kuwa ni msiri,
"Najua una matatizo Jeff tena yatakuwa makubwa tu, ila kwavile umeshazoea kufa na tai shingoni hata sikulazimishi kuniambia ndugu yangu"
Kisha akaenda kumletea kikombe cha maji ili ashushie kwani kwa jinsi alivyokuwa anahema ilionyesha ni mtu aliyechoka sana na mwenye uhitaji wa hayo maji.
Sabrina na Sakina wakiwa wameongozana na Francis walifika hospitali ila hawakumkuta Emmy wala Jeff ikabidi wajiongeze tu kuwa huenda Emmy nae ameenda kupumzika maana tangia jana si mchezo.
Kisha wakaongozana na Francis kwenda kumuona Sam, kwakweli Francis alimuhurumia Sam zaidi maana kwa ile hali aliyomuona nayo matumaini ya kupona yalikuwa hafifu sana.
Akajikuta tu akisema,
"Dah! Ama kweli hujafa hujaumbika, yani huyu ndio Sam kweli? Sam ndio kawa hivi jamani dah! Mungu amsaidie apone"
Sabrina na Sakina wakatazamana kwani hata na wao walikuwa na mshangao kidogo kwenye hali ya Sam,
"Mbona kama saizi ndio ameongezeka vidonda?"
"Hata mimi nashangaa, unajua asubuhi hakuwa hivi kabisa sijui hata imekuwaje jamani"
Machozi yaliwatoka tu kanakwamba wanamtazama marehemu.
Kisha wakatoka kwenye kile chumba na kwenda hadi mapokezi ambapo walienda kwa daktari moja kwa moja,
"Eti dokta, mbona kama mgonjwa wetu vidonda vinazidi jamani wakati asubuhi hali yake ilikuwa afadhari"
"Msiwe na mashaka jamani, tunajitahidi kwa uwezo wetu wote tuhakikishe anapata nafuu na kisha anapona kabisa"
Kisha daktari akatoka nao na kuwaacha pale mapokezi halafu yeye akaenda kumuangalia mgonjwa.
Wakati wapo pale kwenye mabenchi ya hospitali, Francis aliinuka na kwenda msalani. Halafu muda kidogo Emmy nae akawasili na kuwakuta Sakina na Sabrina mahali pale.
Wakasalimiana na kumueleza habari za mgonjwa kwanza kabla ya habari za Jeff,
"Tumefika kumuona mgonjwa kwakweli amezidiwa sana halafu vidonda navyo vimeongezeka, hivyo tumeenda kumwambia daktari ndio kaenda kumuangalia"
Emmy akasikitika na kusema,
"Dah ndiomana sikutaka kuondoka jamani sababu ya haya haya mambo"
Kisha akainuka na kuanza kuelekea kule kwa mgonjwa na kuwaacha Sakina na Sabrina pale kwenye benchi.
Emmy alimkuta daktari akiwa anaandaa sindano ya kumchoma Sam, ni hapo alipomzuia dokta kufanya hivyo ila dokta akafoka kwanza.
"Si nimewaambia mnisubiri jamani! Vipi tena unaingia kwenye chumba na kumzuia daktari kufanya kazi yake?"
"Nina maana yangu daktari na wala sina nia mbaya"
"Maana yako ni ipi? Kama mngeweza kumtibia huyu mgonjwa wenu wenyewe si msingemleta hospitali? Mmemleta hospitali ili tumtibie iweje uingilie kati tiba zetu?"
Kwavile daktari alishaonekana kupaniki kutokana na alivyokatazwa na Emmy dhidi ya kumchoma sindano mgonjwa huyo ikabidi Emmy atumie njia ya ziada katika kumtuliza daktari huyo.
Emmy akamsogelea daktari na kumuangalia usoni, macho ya Emmy yalimfanya daktari anywee kiasi. Kisha Emmy akamshika bega daktari ambapo daktari alikusanya vile vifaa vyake na zile sindano zake na kumuomba Emmy wakazungumze ofisini ambapo Emmy hakupinga hilo ila alimuomba daktari atangulie.
Daktari akatangulia na kuelekea ofisini, Emmy alimuangalia Sam kwakweli alionekana kuwa na hali mbaya zaidi ila Emmy akatambua wazi kuna mchezo umechezwa kwa Sam na dawa pale si sindano kwani alihisi wazi kuwa sindano ingemmaliza Sam ila dawa pale ilikuwa ni mitishamba tu, swali kwake likawa je ni nani atampeleka porini kwenda kuchimba dawa hiyo?
Kwa akili ya haraka haraka akawaza kupelekwa na Jeff ila uoga wa Jeff ulimtia mashaka kwa kiasi fulani.
Kisha akatoka pale na kwenda kwenye ofisi ya daktari.
Jeff akiwa bado kwa rafiki yake Ommy, baada ya muda kidogo rafiki huyu alimuomba Jeff akamsalimie bibi yake.
"Kabla hujaondoka Jeff twende ukamsalimie bibi, amekuja tangia juzi"
Jeff hakuona tatizo juu ya hilo kisha wakainuka na kwenda bustanini ambako huyo bibi alikaa chini ya mti na mkeka wake akivuta ugoro.
Kwakweli Jeff alimshangaa sana huyu bibi kwani ule ugoro alikuwa anavuta kama ndio pumzi yake vile.
Kwahiyo walikaa wakimsalimia ila Jeff alikuwa akimshangaa tu huyu bibi ambapo baada ya muda kidogo bibi akamuuliza Jeff,
"Kwanini unaongozana na viumbe wabaya?"
Jeff akashtuka sana na kufanya ajiangalie kila mahali kuwa hao viumbe wako wapi.
Bibi akamuuliza tena,
"Unafikiri utawaona? Huwezi kuwaona kwa kuwaangalia hivyo ila muda utakaowaona hutapenda tena kuongozana nao"
Ikabidi Jeff ajikaze kuongea,
"Ila mi sipendi kuongozana na hao viumbe"
"Kwani unawajua?"
Jeff akatikisa kichwa kuwa hawajui.
"Na kama huwajui kwanini umesema hupendi?"
"Kwasababu wewe umeniambia ni viumbe wabaya"
"Unataka niwafukuze?"
"Ndio bibi wapotelee kabisa."
"Haya sema maneno haya"
Jeff alikuwa makini kumsikiliza huyu bibi na kufatisha maneno yake.
"Enyi viumbe wabaya, siwahitaji katika maisha yangu, sitaki muongozane na mimi, sina chochote cha kwenu. Poteleeni mbali kabisa. Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"
Kisha bibi akachukua ugoro wake na kuupuliza pembezoni mwa Jeff kisha akamwambia,
"Washaondoka ila muda wowote unapohisi hali tofauti sema eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"
Kisha Jeff akamshukuru huyu bibi hapa kisha akaaga kwaajili ya kuondoka ambapo rafiki yake aliamua kumshindikiza.
Njiani Jeff aliona vyema kumsifu yule bibi kwani kwasasa alikuwa na amani sana,
"Ommy huyu bibi yako kiboko, yani anavyovuta ugoro kiasi kile sikutegemea kama angekuwa na maono kama vile yani sasa nina amani za kutosha."
Ommy akacheka na kusema,
"Ndio wazee wa zamani wale wana mizimu sana yani bibi yangu hata kama umerogwa ukimsogelea tu anakwambia umerogwa yani bibi yetu ni hatari. Anaitwa bi. Hamida yule tushamzoea wenyewe"
Jeff akatamani hata angekuwa anaishi na bibi huyu karibu.
Kisha wakaagana na rafiki yake na kuondoka.
Emmy akiwa ofisini kwa daktari aliweza kuongea nae kwa ushawishi wa hali ya juu hadi daktari akashawishika kuwa atakuwa anatoa dozi zote za sindano chini ya uangalizi wa Emmy.
Daktari alikuwa akimuangalia tu Emmy na kwakweli tamaa ya kimapenzi ilimuingia juu ya Emmy naye Emmy alilitambua hilo na kutumia kama njia pekee ya kumshawishi huyu daktari kufanya vile atakavyo yeye.
"Unajua wewe ni msichana mrembo sana?"
Emmy akamjibu daktari huku akimrembulia macho yake,
"Naelewa daktari, ila ukifanya vile ninavyotaka mimi basi utafurahi sana maana nitakupa utakacho"
Hili neno la mwisho lilimuingia vilivyo daktari huyu na kujikuta akitabasamu tu, kisha Emmy akamuaga na kutoka huku huyu daktari akimuangalia Emmy hadi mwisho.
Emmy alirudi tena pale walipokuwa wamekaa wakina Sabrina, akawashangaa kuwaona wakiwa wamekaa na kijana wa kiume ambapo moja kwa moja akajiuliza kuwa yule kijana ni nani.
Ila aliposegea tu, Francis nae akainuka kichwa na kumuona Emmy ambapo aliinuka na kumshangaa,
"Emmy ni wewe!!"
"Kheee kumbe ni Francis!"
Wakasogeleana na kukumbatiana ambapo Sabrina na Sakina walikaa kimya tu wakishangaa kuwa kumbe Emmy na Francis wanafahamiana ambao baada ya kukumbatiana walienda pembeni kuzungumza.
Emmy aliona kuwa ni huyu huyu Francis ndio anafaa kwenda nae porini kutafuta dawa kwahiyo alivyomvutia pembeni alikuwa anamuomba kuwa amsindikize huko porini, ambapo Francis hakuwa na pingamizi lolote
"Hakuna tatizo Emmy, wewe mtu wangu wa karibu sana. Twende tu nikupeleke huko."
Walivyokubaliana wakarudi kuwaaga wakina Sabrina na kuondoka.
Sabrina na Sakina wakatazamana, na muda huo huo wakaanza kumsengenya Emmy.
"Kale kasichana kamalaya kale hakana lolote"
"Kumbe na wewe umekaona eeh dada, yani ni kamalaya kweli na usikute hata Sam alikuwa anamtaka"
"Si unaona mwenyewe alivyomkumbatia Francis hapa mmh! Kidogo wakaenda pembeni kuzungumza mara wanaaga, watakuwa wanaenda nyumba za wageni huko"
Sabrina akawaza kidogo na kusema,
"Ooh maskini Jeff wangu, hawezi kumshawishi kweli huyu? Halafu leo muda wote walikuwa pamoja mmh! Nina mashaka"
"Na jana pia walikuwa pamoja au umesahau, ila Jeff hana ujinga huu. Haka kadada hakafai tunakaangalia tu, eti kanajivunia uzuri wake. Hebu tuondoke zetu sie"
Wakaona ni vyema waondoke zao tu maana kila wakiendelea kumfikiria Emmy vichwa viliwauma tu.
Wakati wanataka kutoka, daktari akawaita na kuzungumza nao.
"Jamani, kwasasa mkija kumuona mgonjwa muwe chini ya uangalizi wa yule ndugu yenu Emmy"
Sabrina na Sakina wakaangaliana kisha wakamuitikia daktari na kuondoka zao.
Walitoka nje ya hospitali na kusimama getini huku wakipiga umbea.
Jeff alipanda daladala akijiuliza kuwa aende hospitali au aende nyumbani. Ila wazo la nyumbani akalipinga kutokana na yale aliyokutana nayo na kwavile yule bibi akamwambia kuwa anaongozana na viumbe wa ajabu ndio kabisa yani.
Akaona ni vyema aende hospitali ili hata akaweze kuzungumza na Emmy kuhusu yule bibi na kuangalia jinsi gani atawasaidia.
Jeff alipofika hospitali akashtuka sana kumuona Sakina na Sabrina pale getini na kuona sasa mwisho wake umefika.
Akageuka ili aanze kukimbia, ila ile anavuka barabara tu akagongwa.
Jeff alipanda daladala akijiuliza kuwa aende hospitali au aende nyumbani. Ila wazo la nyumbani akalipinga kutokana na yale aliyokutana nayo na kwavile yule bibi akamwambia kuwa anaongozana na viumbe wa ajabu ndio kabisa yani.
Akaona ni vyema aende hospitali ili hata akaweze kuzungumza na Emmy kuhusu yule bibi na kuangalia jinsi gani atawasaidia.
Jeff alipofika hospitali akashtuka sana kumuona Sakina na Sabrina pale getini na kuona sasa mwisho wake umefika.
Akageuka ili aanze kukimbia, ila ile anavuka barabara tu akagongwa.
Kitendo cha kugongwa kwa Jeff kilikuwa cha gafla sana hata Sakina na Sabrina hawakuelewa kuwa ni nani aliyegongwa kwani hawakuwa na wazo kabisa kama Jeff alitokea eneo hilo.
Kwahiyo na wao wakasogea eneo la ajari kama watu wengine walivyosogea kushangaa.
Walipoona kuwa ni Jeff wakapatwa na mshtuko wa hali ya juu sana na kujikuta wakilia lia hovyo tu huku wasamalia wema wakiwasaidia na haikuwa ngumu sana kwavile walikuwa karibu na hospitali.
Emmy akiwa na Francis kwenye kapori kadogo ambako aliamini kuwa ataweza kupata dawa, alijikuta akishtuka sana na kumfanya hata Francis nae ashtuke.
"Vipi Emmy una tatizo?"
"Sina tatizo ila kuna jambo baya limetokea"
"Kheee sasa tutafanyaje?"
"Tushachelewa tayari, ngoja tu niangalie hiyo dawa kisha tuondoke"
Francis alimuangalia Emmy kwa huruma sana kwani alionekana kuwa na mawazo sana kwa muda huo.
Emmy alitambua jinsi gani alihurumiwa na Francis ila aliona ni vyema afanye kile kilichompeleka kwenye kipori hicho.
Wakatembea kidogo, kisha wakafika mahali na kusimama, Emmy akamwambia Francis kuwa amsubirie eneo hilo.
"Hapana Emmy, siwezi kukuacha uingie mwenyewe porini. Ukipata matatizo je?"
"Nina maana yangu Francis, hata hivyo nasogea hapo kidogo tu kwenye mti ule ndiomana nakwambia unisubirie. Mi siwezi kudhulika humu ila wewe unaweza ukadhurika. Tafadhari nisikilize"
"Hapana Emmy, sihafikiani na wewe kwa hilo swala kabisa"
Kisha Emmy akaanza kuelekea anapopasema huku Francis akimfata kwa nyuma.
Na kweli Emmy akaiona dawa anayoitaka chini ya huo mti, ikabidi ainame na kuichuma.
Wakati Emmy anaichuma dawa hiyo, Francis alikuwa kasimama pembeni tu akimuangalia.
Gafla akahisi kuna kitu kimemdokoa, kuangalia ni nyoka. Kwakweli Francis alijikuta akiruka juu kwa kelele huku yule nyoka akikimbia.
Emmy ikabidi aache alichokuwa anafanya na kusogea karibu kumuangalia Francis ambapo damu zilikuwa zikimtoka, ikabidi Emmy achukue mtandio wake na kumfunga Francis mguuni kama njia ya kumpa huduma ya kwanza ili sumu ya yule nyuka isisambae mwilini.
Hapo tena ilibidi tu kumuwaisha Francis hospitali, ambapo Emmy alichukua ile dawa kisha akaanza kukongojana na Francis ili waweze kutoka kwenye kale kapori.
Walipofanikiwa kutoka, Emmy akaona mti ambao majani yake husaidia kukata sumu ya nyoka.
Ikabidi ayachume na kuyatafuna mdomoni kama ishara ya kuyaponda ponda kisha akampaka Francis kwenye kidonda na safari ya kuelekea hospitali ikaendelea.
Mama Sabrina na shangazi wa Sabrina walikuwa wanashangazwa tu na ukimya wa Sabrina na Sakina kwani hawakupigiwa simu kupewa taarifa zozote halafu na giza nalo lilianza kuingia.
Ila kila walipojaribisha simu zao kwa muda huo ilikuwa hazipatikani.
"Mmh au wamepatwa na matatizo jamani?"
"Inawezekana maana si kwa ukimya huu"
Ila pia walishangazwa na mama mdogo wa Sam ambaye alionekana kuwa kimya muda wote kamavile mtu aliyekata tamaa.
Ikabidi mama Sabrina amuulize kuwa ana tatizo gani.
"Vipi mzazi mwenzangu mbona kimya hivyo? Hebu tushirikishe basi ili na sisi tujue."
Akatulia kidogo kisha akawajibu,
"Jamani, msione nimetulia hivi kwakweli kuna mambo mengi sana yamezunguka kichwa changu. Namuona Sam akiwa kwenye matatizo makubwa zaidi. Yani simuoni hospitali ila namuona mahali akiteseka. Halafu kitu cha kunitisha zaidi ni kuwa muda mfupi uliopita nimemuona Jeff akiwa ndani ya tatizo. Yani namshukuru Mungu kwa kuweza kunionyesha mambo mbali mbali ila je nafanyaje kupambana na haya ninayoyaona jamani?"
Wote wakatazamana kwa zamu zamu, kisha mama Sabrina akajibu
"Ni maombi tu."
Hii kauli ya mama Sabrina ilimfanya mama mdogo wa Sam apate moyo wa kuendelea na aliyokuwa akiongea,
"Ni kweli, inatakiwa tufanye maombi jamani maana hiki ninachokiona ni kigumu sana. Na mapambano ya hapa sisi kama sisi hatuwezi, ni Mungu tu awezaye kutusaidia"
Ikabidi wakubaliane pale hata shangazi wa Sabrina nae akagairi kuondoka ili wawe pamoja kwenye hayo maombi.
Emmy alienda na Francis kwenye hospitali ya karibu kwahiyo alikaa hapo kusubiria apate hiyo huduma ukizingatia alijiona wazi kuwa yeye ndiye mwenye makosa, akatamani hata arudishe muda nyuma ili amzuie zaidi Francis kuongozana nae kwani pale ni wazi kuwa vile vitu vibaya vinavyosumbua kwa Sam ndio vilivyomfatilia na yeye hadi mwisho wa siku kutumia vitu vya kumdhuru Francis.
Alijifikiria sana ila ndio hivyo ilishatokea tayari.
Francis alipomaliza kuhudumiwa hata giza nalo lilikuwa tayari limeshaingia mahali pale.
Walipotoka, Emmy alimuomba Francis aelekee nyumbani tu ili akaendelee na dozi na apate muda wa kupumzika.
Akaagana nae pale halafu kila mmoja akashika njia yake.
Francis aliona vyema aelekee kwa bibi yake kwani licha ya dawa aliyopakwa na Emmy na zile walizompa hospitali bado hakuwa na matumaini thabidi, akaona ni vyema akafikie kwa bibi yake na kumueleza kwavile bibi yake huyo kidogo alikuwa na uzoefu wa dawa za kienyeji.
Alimkuta bibi yake akiwa anajiandaa kwenda kulala na kuamua kukaa nae kidogo wazungumze,
"Vipi huo mguu kwanza mbona unachechemea?"
"Nimeng'atwa na nyoka bibi"
"Nyoka! Wapi huko? Imekuwaje? Je umepata dawa?"
Francis akamueleza bibi yake kuwa ameshapewa dawa hospitali ila angehitaji za kienyeji.
"Ila hebu nijuze vizuri, huyo nyoka imekuwaje kuwaje? Ulikuwa mashambani?"
Francis akamueleza kwa kifupi tu kuwa alikuwa porini ila bibi yake akaguna kidogo na kumuahidi kumtafutia dawa kesho yake.
Emmy alifika hospitali na moja kwa moja kwenda kwenye chumba alicholazwa Sam, kwavile yeye alikuwa na kibali kwahiyo hakuna nesi aliyemzuia.
Alichukua ile dawa yake aliyoichuma akaifikicha kwa mikono kisha akampaka paka Sam mwilini kisha akamfunika na kuinama pale kwa dakika kadhaa halafu akatoka.
Akatamani kujua walipo Sakina na Sabrina ila hakujua na hakuwaona akahisi wazi watakuwa wamerudi nyumbani tu, na kwavile hata yeye alichoka akaamua kutoka na kuondoka ili angalau akapumzike na kusahau kabisa kuwa alipatwa na wazo kwamba Jeff kapatwa matatizo.
Basi akatoka pale na kuelekea anapoishi.
Emmy akarudi kwao moja kwa moja kwani kwa wakati huo hakutaka kuwa na wazo lolote la ziada.
Ila alipofika kwao akaoga na kupumzika, kisha akalala.
Akajiwa na ndoto ambayo ilionyesha tukio zima la ajali wa Jeff.
Kwakweli Emmy alijikuta akishtuka sana toka usingizini huku akiombea kuwa isiwe vile alivyoota.
Ila jambo lilikuwa tayari limeshatokea.
Akafikiria sana, ila kwenye ile ndoto aliona vitu vya ajabu kabla ya ajali ya Jeff akaweza kuelewa wazi kuwa ajali ile ilitengenezwa makusudi kwa lengo la kuwaumiza ila bado akawa na imani kuwa haijatokea na akapanga kuwahi mapema kesho ili aweze kuzungumza na Jeff na wajue ni jinsi gani wataepukana na hilo.
Kulipokucha, nyumbani kwakina Sabrina bado hawakupata mawasiliano yoyote toka kwa Sabrina ila walipokaa pamoja na kuzungumza ilionyesha kuwa hata mama mdogo wa Sam alipata ndoto kuwa Jeff amepata ajali.
"Jamani, lile tatizo la jana nililosema kuhusu Jeff ni kuwa amepata ajali"
Wakashtuka na kuulizana,
"Inamaana huyo Jeff atakuwa wapi na wakina Sabrina nao watakuwa wapi?"
"Inawezekana kabisa wapo hospitali, kwahiyo twendeni huko ili tuweze kupata habari kamili"
Ikabidi wawaandae wale watoto wa Sabrina na kuwabeba kisha kuondoka nao kuelekea huko hospitali.
Emmy alishafika hospitali na kabla ya kwenda kumuona Sam aliamua kwenda moja kwa moja kwa daktari kwanza huku akiamini kuwa wakina Jeff lazima watakuja siku hiyo.
Alisalimiana na dokta, kisha dokta akampa pole Emmy
"Poleni jamani kwa majanga yaliyowakuta"
"Kheee daktari kuna mengine au?"
"Kwani hujui? Si yule ndugu yenu mwingine aliletwa jana hapa amepata ajali hapo nje"
Emmy akashtuka sana na kuona wazi kuwa mawazo yake yalikuwa nyuma sana ya wakati.
Ikabidi amuulize daktari vizuri maana hakuelewa kitu,
"Hebu nieleweshe daktari, amelazwa wapi sasa?"
"Hali yake haikuwa nzuri kwakweli, tulimtibia hapa na kumpa uhamisho wa kwenda hospitali kubwa zaidi kwaajili ya mifupa maana inaonyesha amevunjika ndani kwa ndani."
Emmy akauliza kuhusu hospitali aliyopelekwa Jeff, daktari akamuelekeza halafu Emmy akainuka na kumuaga kisha akatoka.
Kwa muda huo hakutaka tena kwenda kumuangalia Sam, kwahiyo alichokifanya ni kutoka hapo ili aweze kuelekea hospitali aliyoelekezwa.
Emmy alipotoka nje ya hospitali akaonana na ndugu wa Sabrina wakija hapo ikabidi azungumze nao na awaeleze kile alichoambiwa na daktari kisha wakaungana na kuanza kuelekea kwenye hospitali waliyoelekezwa.
Walipofika kwenye hiyo hospitali waliwakuta Sakina na Sabrina ambao walisogea na kuwakumbatia.
"Eti jamani imekuwaje tena? Na huyo Jeff je tunaweza kumuona?"
"Hapana kwasasa maana muda wa kuona wagonjwa umepita, sisi wenyewe tunangoja mchana hapa tukamuone tena"
Sabrina aliwajibu huku akiwa na uchungu sana.
Kisha wakatulia ili waelezwe ilivyokuwa, ikabidi Sabrina aeleze ilivyokuwa tangu nyumbani Jeff alivyowaona na jinsi alivyoanza kukimbia na jinsi walivyoshangaa pale hospitali akipata ile ajali.
Hapo hapo ikamfanya Emmy aelewe vizuri zaidi kilichosababisha Jeff apate ajali,
"Jamani Jeff alikuwa anawakimbia nyie ndiomana imekuwa hivyo"
"Sawa, ila je kwanini alikuwa anatukimbia? Je kuna kitu gani hapo?"
Ikabidi Emmy awaeleze kuhusu walichokutana nacho kwenye nyumba ya Sam na kufanya wote washangae.
Sabrina akauliza kwa mshangao sana,
"Kwahiyo walivaa sura zetu?"
"Ndio, wale viumbe ni wabaya sana jamani wanafanya chochote tu na kupambana nao inahitajika tuwe na nguvu ya ziada."
Sabrina akakumbuka na yeye alivyomsukuma mwanae akijua ni yule kiumbe wa ajabu kumbe alikuwa mwanae ukweli.
Alijikuta anakuwa mpole sana na kuuliza,
"Tufanyeje sasa jamani ili tuepukane na hili?"
Emmy akawaeleza kwa kifupi anachofahamu yeye
"Hapa ni uzima wa Sam kwani ndiye anayeelewa alipoyatoa yale madude"
Sabrina akauliza tena,
"Inamaana tatizo likiendelea kwa Sam na sisi tutaendelea kuteseka?"
"Tatizo ni kwamba hapa tulipo karibia wote tulitumia mali ya Sam hata kama kwa kidogo sana na ukizingatia sisi ndio ndugu zake wa karibu kwahiyo lazima tujitahidi apone ili tuweze kuondokana na haya matatizo."
Wakajadiliana pale huku wakipeana mawazo mbali mbali ila kama kawaida mama mdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa.
Bibi wa Francis alimtafutia Francis dawa ya kunywa na ya kupaka kisha akampa onyo mjukuu wake huyu,
"Tafadhari Francis, hebu achana na ile familia. Kila siku nakwambia, unaona kipindi cha kati kati hapo umeishi vizuri tu bila ya tatizo lolote. Ile familia haifai mjukuu wangu utapotea bure"
"Umejuaje bibi kama nilikuwa huko?"
"Mie ni mtu mzima ninaona mengi, toka siku ya kwanza nilikwambia kuwa yule mdada familia yake haifai ila kwa kiburi chenu hadi nduguyo akawa kipofu. Haya sasa mmeshakuwa wakubwa halafu bado mnafatilia ile familia ya nini? Hebu achaneni nayo jamani"
Ikabidi Francis aitikie ili kuweza kumpa moyo bibi yake huyo kuwa hatoifatilia tena ile familia ya kina Sabrina.
Muda wa kuangalia wagonjwa ulipofika walienda kumuangalia Jeff ambaye miguu yake ilitundikwa juu juu kwaajili ya jiwe la kuweza kuweka sawa mifupa na alionekana kuumia kwakweli.
Ila kwavile alikuwa kalala kutokana na dawa ya usingizi aliyopewa, daktari akawashauri wakamtengenezee chakula mgonjwa wao ili jioni aweze kula.
Walipotoka pale wakakubaliana wengine warudi nyumbani na wengine wakamuone Sam.
Kwakuwa shangazi wa Sabrina hakumuona Sam ikabidi aende kumuona Sam na kwavile nyumbani nako walihofia kukutana na mambo ya ajabu ikabidi Sabrina na Sakina waongozane na mama mdogo wa Sam kurudi nyumbani.
Wakaagana kwenye stendi ya daladala ambapo mama Sabrina, Emmy pamoja na shangazi wa Sabrina walielekea hospitali na wengine kwenda nyumbani.
Wakina Emmy walipofika hospitali moja kwa moja wakaenda alipolazwa Sam ila cha kushangaza hawakumkuta pale kitandani na kuwafanya washtuke na kwenda kumfata daktari.
"Mgonjwa wetu yuko wapi?"
"Alikuwepo pale pale kitandani"
"Hayupo"
"Haiwezekani"
Ikabidi daktari aongozane nao hadi alipolazwa Sam.
Kufika pale hata yeye mwenyewe akashangaa kwa kutokumuona Sam pale kitandani.
Wakina Emmy walipofika hospitali moja kwa moja wakaenda alipolazwa Sam ila cha kushangaza hawakumkuta pale kitandani na kuwafanya washtuke na kwenda kumfata daktari.
"Mgonjwa wetu yuko wapi?"
"Alikuwepo pale pale kitandani"
"Hayupo"
"Haiwezekani"
Ikabidi daktari aongozane nao hadi alipolazwa Sam.
Kufika pale hata yeye mwenyewe akashangaa kwa kutokumuona Sam pale kitandani.
"Inamaana amepelekwa wapi?"
"Ndio tukuulize wewe daktari maana hatuelewi kabisa"
Ikabidi daktari amtafute nesi wa zamu na kumuuliza kuhusu Sam, ila hata yule nesi alishangaa tu na kujikuta akiuliza na yeye
"Kwani hayupo?"
"Ndio hayupo"
"Kheee, mi nilimuacha hapo hapo kitandani"
Emmy akatazamana na ndugu wa Sabrina kwa mshangao huku kila mmoja akijaribu kutoa wazo lake, shangazi wa Sabrina akauliza
"Au ameenda chooni?"
"Hawezi kwenda mwenyewe ndiomana tukamuwekea mirija ya haja"
Ila hiyo mirija nayo haikuonekana na ikaonyesha wazi kama amepotea basi kapotea na mirija yake.
Hakuna aliyeweza kuamini kwakweli, ikabidi daktari awaite wauguzi wote na kuwauliza iwapo kuna yeyote kamuamisha mgonjwa huyo, na wote wakakataa na kusema kuwa hawafahamu chochote kwani hata wao walikuwa wakishangaa tu.
"Sasa jamani tufanyaje?"
Daktari akawaambia kuwa wavute subira ili ufanyike uchunguzi.
Nao wakatoka pale na kwenda kukaa mapokezi huku wakijaribu kujadiliana yaliyojili.
Mama mdogo wa Sam pamoja na wakina Sabrina walienda moja kwa moja nyumbani kwakina Sabrina.
Kwavile watoto walikuwa wamelala ikabidi wakawalaze kisha Sakina na Sabrina wakamuaga mama mdogo wa Sam kuwa waende sokoni kwaajili ya kununua mahitaji ya mgonjwa, kisha wakaondoka.
Mama mdogo wa Sam alibaki pale kwakina Sabrina huku akitafakari mambo mengi sana bila ya majibu, alibaki akisema tu,
"Mungu tusaidie"
Kwakweli hakuelewa vitu vingi na alijikuta akitafakari bila mwisho kwani kila akifikiria kinachoendelea alikosa majibu kabisa.
Akakumbuka walichoelezwa na Emmy juu ya kwanini Jeff aliwaogopa Sakina na Sabrina.
Akawaza jinsi alivyosimuliwa waliyoyakuta kwenye nyumba ya Sam.
"Mmh haya mambo mbona hayakutokea wakati mimi nipo pale? Je ni kitu gani hiki? Kwakweli sielewi ila Mungu nakuomba utusaidie."
Aliamua kuingia kwenye maombi sasa.
Sakina na Sabrina walipomaliza kununua mahitaji yao sokoni, wakati wanatoka kuna mtu akamwita Sabrina na alipogeuka akamuona kuwa ni Fredy ikabidi wasimame na kumsalimia.
Fredy alimuangalia sana Sabrina kwani hakuwa kama zamani, leo alionekana kuwa mchafu mchafu sana.
Fredy alimpa pole kwanza na moja kwa moja Sabrina akatambua kuwa Fredy atakuwa ameelezwa na Francis,
"Asante, ila tumepatwa na majanga mengine tena"
"Yapi hayo?"
"Jeff kapata ajali na sasa yupo hospitali"
"Kheee poleni sana, ila familia yenu ina majanga sana, yani Francis nae karudi na majeraha ya kung'atwa na nyoka"
Sakina na Sabrina wakaangaliana kwani hawakuelewa kuwa imekuwaje hadi huyo Francis nae ang'atwe na nyoka, ikabidi Fredy awaeleze kwa kifupi vile anavyofahamu yeye,
"Sijui alienda na ndugu yenu gani huko porini ndio akang'atwa na nyoka."
Sabrina akashangaa kisha akasema,
"Ndugu yetu!! Sio ndugu yetu yule ila ni mwanamke tu tena anafahamiana nae sijui ni mpenzi wake hata hatuelewi ila mpe pole sana."
Basi wakaachana hapo kweni iliwabidi wao wawahi kupika.
Fredy aliwaangalia sana bila ya kuwamaliza.
Hadi walipofikia kuvuka barabara, Fredy akaona kitu na kufanya ashtuke na kuwaita ambapo waligeuka huku wakiona kama anawapotezea muda tu ila wakasimama hivyo hivyo wamsikilize.
Fredy akasogea ila sio karibu sana na wao, kisha akawauliza,
"Mmebeba nini kwenye mfuko huo?"
Sabrina akajibu,
"Ni ndizi kwani vipi?"
"Hapana sio ndizi hizo"
"Kheee utasemaje sio ndizi wakati tuliobeba ni sisi? Na kama sio ndizi ni nini?"
Sabrina akataka kuufungua ule mfuko ila Fredy akamkataza kwa haraka sana,
"Hapana usifungue, ila utupe chini"
"Kheee nitatupaje chini chakula!"
Sabrina akaufungua ule mfuko, yani ikawa kama kufumba na kufumbua kwani alirukiwa na vitu kama maji usoni kisha akapiga kelele na kuutupa ule mfuko.
Ilikuwa ni kitendo cha haraka sana ila wakashuhudia nyoka akitoka kwenye ule mfuko huku Sakina na Fredy wakiwa na mshangao na baadhi ya watu waliokuwa karibu kuanza kukimbia.
Ila yule nyoka hakujulikana alipoelekea, ikabidi Sakina na Fredy kumuinua Sabrina pale chini na kujaribu kutafuta usafiri wa kumkimbiza hospitali kwani macho yake yalikuwa yanawasha halafu na hakuweza kuona chochote.
Walifika hospitali na moja kwa moja Sabrina akapelekwa kwenye chumba cha matibabu.
Nje wakabaki Fredy na Sakina ambapo Sakina akamuuliza Fredy kwani hakuweza kuelewa kitu kwakweli.
"Unajua sielewi mpaka sasa hivi, wee umejuaje kama ule mfuko haukuwa salama?"
"Wakati mnaondoka, mimi nilikuwa nawaangalia kwakweli nikashangazwa na jinsi mfuko ulivyokuwa ukicheza cheza na ndiomana nikaja kuwauliza mmebeba nini"
"Yani sielewi jamani, tumeenda sokoni na kununua ndizi ili tukampikie Jeff, sasa zile ndizi zimegeuka nyoka! Mambo gani haya?"
"Ni majanga, ila mara nyingine tujifunze si kila unayemuona sokoni ni muuzaji kweli au ni mnunuaji kweli. Haya ni majanga tena majanga haswaa"
"Sasa nitamjuaje asiye muuzaji kweli? Yani sisi tununue ndizi halafu tukute nyoka kweli? Na kwanini huyo nyoka amtemee mate Sabrina? Mi ndiomana naendaga kwa waganga kwakweli hii hali imezidi sasa."
Muda huo huo Sakina akamuomba huyu Fredy amsindikize kwa mganga kwani aliona hata kubaki pale hospitali ni kupoteza muda tu wakati waganga wa kienyeji wapo.
Fredy hakupinga, wakaenda kumuaga daktari kuwa wanaenda nyumbani mara moja ili awe makini na mgonjwa wao kisha wakaondoka.
Huku hospitali kwa upande wa wakina Emmy bado walikuwa wakijiuliza juu ya kupotea kwa Sam kwani hakuna hata aliyepata wazo au hisia kuwa Sam anaweza akawa mahali gani.
"Sasa tufanyeje? Turudi nyumbani au tufanyeje?"
"Sasa tukirudi nyumbani ndio itasaidia kwani? Maana mtu katoweka na haijulikani alipo sasa huko nyumbani tutafanya nini?"
"Jamani, hata na hapa tunafanya nini maana mambo hayaeleweki. Tuchukueni tu mawasiliano ya daktari ili atupe taarifa"
Ila shangazi wa Sabrina aliamua kuwaaga kwani na yeye tangu alipoondoka jana na kuiacha familia yake hakurudi.
"Jamani, ngoja na mimi nikawaone nyumbani ila kwa chochote kile mnipe taarifa"
Kisha akaondoka zake.
Mama Sabrina na Emmy waliamua kwanza kwenda hospitali aliyolazwa Jeff kisha ndio waende nyumbani kwani na wao walikuwa hata hawajielewi kwa muda huo.
Na ukizingatia kuwa mambo yameenda ndivyo sivyo.
Sakina alifika na Fredy kwa mganga wa kienyeji, ila hawakukuta watu wengi sana na kuwafanya wapate nafasi ya haraka kuonana nao.
Moja kwa moja Sakina alimueleza matatizo yanayowakabili, yule mganga akamueleza
"Nikikuahidi kuwa nitakutibia itakuwa ni uongo tu kwani matatizo yenu yapo kwenye hali mbaya"
"Tusaidie jamani mtaalamu"
"Nawasaidiaje kwa hali hii? Mngewahi kabla matatizo hayajakomaa kiasi hiki ningewasaidia ila kwasasa ni ngumu sana kuwasaidia."
"Jamani mtaalamu tuhurumie, mwanangu amepata ajali, mdogo wangu kawa kipofu. Hali ni mbaya, tusaidie tafadhari. Nakuomba sana tusaidie"
Huyu mganga hakuongea neno tena ila alikuwa kimya na akajifunika shuka.
Ukimya wa huyu mganga uliwatisha sana Sakina na Fredy hadi wakajikuta wakipatwa na uoga wa hali ya juu kwani ukimya wa huyu mganga haukuwa wa kawaida.
Muda ukapita, wakajikuta wakiambizana kuwa waondoke ila kwa upande mwingine Sakina alihitaji kusubiria zaidi.
Wakasubiri tena, ikapita nusu saa wakasikia kicheko toka kwa yule mganga na kisha akaanza kuongea,
"Kumbe ni wajasiri na wavumilivu kiasi hiki? Kwa hakika dawa nitakayowapa mtaifanyia kazi vilivyo"
Sakina aliposikia neno dawa alifurahi sana kwani kwa wakati huo ni watu wawili tu ndio aliwawaza sana kwenye akili yake yani Sabrina na Jeff.
Kwahiyo sasa wakatulia zaidi kusikiliza maelekezo ya dawa, ingawa sauti ya mganga ilibadilika kwa muda huo yani ilikuwa tofauti na ya mwanzo ila iliwapa matumaini kuwa sasa wanaenda kupata ufumbuzi wa tatizo lao.
Huyu mganga alitoa dawa aina ya unga unga wa kijivu kisha akawaambia,
"Utachukua hii dawa utaenda kuiweka mlangoni kwakina Sabrina kwa mstari"
Walishangaa kidogo kwa huyu mganga kutambua jina la Sabrina ila kwavile alikuwa ni mganga hawakuwa na shaka nae.
Kisha akaendelea kuwaeleza,
"Ukishaweka, usiingie humo ndani kwa muda huo sawa!"
Sakina akaitikia kwa kichwa, kisha akampa kitu kingine kama jiwe na kumwambia,
"Hili utachimba pembe ya kwanza ya nyumba yao na kufukia ila usiingie ndani. Kisha hii ya unga itakayobaki utaichanganya na hii"
Akampa dawa nyingine yenye rangi nyekundu,
"Kisha uende nayo nyumbani kwako, inyunyuzie mlangoni, halafu subiria kama nusu ndipo uingie nyumbani kwako, sawa!"
"Sawa"
Sakina aliitikia kwa haraka zaidi kwani aliona kuwa yale masharti sio magumu sana kusema atashindwa kuyatekeleza. Tena aliyafurahia kwani aliona hiyo kazi kuwa rahisi zaidi.
Kisha yeye na Fredy wakainuka na kuondoka eneo lile.
Walipokuwa nje ikabidi Fredy aende hospitali kumuangalia Sabrina halafu Sakina arudi nyumbani kutimiza masharti ya dawa alizopewa.
Fredy alienda moja kwa moja hospitali na kwakweli hali ya Sabrina haikuwa nzuri hata daktari alikiri wazi kuwa huenda wakashindwa kumsaidia huku Fredy nae akijaribu kudadisi zaidi,
"Sasa jamani ndio atakuwa kipofu?"
"Tunapenda apone na arudi kwenye hali ya kawaida ila tatizo ni kuwa tukiyachunguza macho yake na kuyapima tunaona hayana tatizo lolote ila yeye mwenyewe analalamika kuwa yanauma na hawezi kuona na ndiomana tumemchoma sindano ya usingizi ili atulie kiasi"
"Kwakweli nashangaa hapa hata nakosa la kusema, kwahiyo hasaidiki jamani!"
"Sio kwamba hasaidiki, bado tunajitahidi ila hali ni tete"
Fredy alitulia akijipa moyo kuwa huenda dawa aliyopewa Sakina na yule mganga itawasaidia pia kwa tatizo la Sabrina moja kwa moja ila kidogo akajiuliza kuwa kwanini zile dawa ni za milangoni na si za kupaka mgonjwa,
"Mmh labda kwavile wanaangalia chimbuko la tatizo."
Ikabidi atulie tu kimya akingoja majibu zaidi kwa daktari.
Emmy na mama Sabrina walishangazwa walipofika hospitali aliyolazwa Jeff kuwa hadi muda huo mgonjwa hakupelekewa chakula.
Ikabidi wakanunue chakula na kumuomba daktari ili mgonjwa aweze kula ambapo daktari aliwaruhusu na moja kwa moja wakaenda kumpa chakula Jeff huku wakiulizana kuwa wakina Sabrina wamekwamishwa na kitu gani.
Kwavile Jeff alikuwa na ufahamu muda huo akaweza kuzungumza nao mambo mengi ambapo hata Emmy alishangaa kuwa Jeff aliikuta simu yake nyumbani kwao.
"Yani mimi nilihisi tu kuwa ulipata kiwewe kuwaona tena. Pole sana, haya mambo sijui hata yataisha lini."
Alipomaliza kula ikabidi watoke na kuondoka huku safari yao ikiwa ni kwenda nyumbani kuwaangalia wakina Sabrina.
Sakina alifika kwakina Sabrina na moja kwa moja akafanya maelekezo aliyopewa kuhusu zile dawa. Ya kufukia akafukia na ya kunyunyuzia kimstari mlangoni akanyunyuzia kisha akaenda nyumbani kwake.
Muda ambao Sakina anatoka kwakina Sabrina ilipita kama dakika tano ambapo Emmy na mama Sabrina nao waliwasili pale nyumbani.
Ila mama Sabrina alipotaka kuingia, Emmy akamshika mkono kumrudisha nyuma.
Mama Sabrina akamshangaa Emmy na kumuuliza,
"Mbona umenivuta! Kwani kuna nini?"
"Hapo mlangoni si salama"
"Si salama kivipi?"
"Subiri kidogo nipate jibu ila si salama"
"Kumbuka kuna watu ndani!"
"Naelewa, ila wao wanaweza kuwa salama kushinda wewe utakayevuka hapo"
Mama Sabrina alikuwa akishangaa tu na kuamua kubaki pembeni.
Sakina aliweka ile dawa na nyumbani kwake kama alivyoambiwa, kisha baada ya nusu saa akaingia ndani.
Alipofika tu sebleni akashtuka sana kumuona Sam amekaa kwenye kochi pale ndani kwake.
Sakina aliweka ile dawa na nyumbani kwake kama alivyoambiwa, kisha baada ya nusu saa akaingia ndani.
Alipofika tu sebleni akashtuka sana kumuona Sam amekaa kwenye kochi pale ndani kwake.
Sakina alishangaa sana na kujikuta akishindwa hata kuongea kwani ni jambo la ajabu kwa Sam aliyemuona jana yake akiwa hoi tena akiwa hana ufahamu kabisa halafu saa hizi yupo ndani mwake.
Akajikuta kwa haraka akikumbuka alichosimuliwa na Emmy kuwa walipoenda kwa Sam waliwakuta wao sebleni.
Hofu ikamjaa na kuhisi kuwa huenda waliyoyakuta Emmy na Jeff ndio yamemgeukia yeye.
Muda huo huo akageuka na kutaka kukimbia, ila wakati anatoka mlangoni akajikwaa na kuanguka kama mzigo.
Kwavile hili tukio lilikuwa la gafla sana, ikamfanya Keti nae aliyekuwa jikoni kuja kwa haraka, ila alishangaa ile hali na pia alimshangaa Sam kwa kumwangalia tu Sakina bila ya kumsaidia.
Akamshangaa, huku akielekea yeye mwenyewe kwenda kumsaidia ila gafla akakatazwa na Sam,
"Mwache hapo hapo"
"Kwanini?"
"Na wewe utaanguka hivyo hivyo, nenda kaendelee na shughuli zako. Atazinduka mwenyewe tu huyo"
"Kheee!!"
Keti hakubisha zaidi kwani bado alimuheshimu Sam kama bosi wake.
Emmy na mama Sabrina bado walikuwa pale mlangoni huku mama Sabrina akiwa haelewi bado ile sababu ya yeye kuzuiliwa kuingia ndani.
"Nimekwambia hapa mlangoni kuna dawa, usiwe mbishi mama. Utapotea, narudia tena utapotea"
Ikabidi mama Sabrina awe mpole sasa na kuuliza tena,
"Tufanyaje sasa?"
"Hebu nisubirie kidogo nikaangalie hapo kama nitapata ndulele huenda zikasaidia kiasi, ila yeyote atakayekuja usimruhusu kuingia humo ndani kwako"
Mama Sabrina akatulia tu, huku Emmy akienda mahali ambako kulikuwa na majani na miti miti mifupi.
Mama Sabrina alimuangalia sana Emmy na kwa haraka haraka akamuona kuwa ni mtu anayependa mambo ya kishirikina na ndiomana anaamini kuwa kila mahali ushirikina umehusika.
"Yani huyu angeishi na Sakina wangepatana sana maana mambo yao yanafanana kabisa. Najua wazi kuwa Sakina nae akitulia kidogo tu ataanza zile safari zake za kwenda kwa waganga."
Muda kidogo, Emmy akawa amerudi na ndulele tatu.
Moja akaitoboa na kijiti na kuweka pale pale mlangoni halafu nyingine akampa mama Sabrina na nyingine akabakia nayo yeye, kisha akamwambia mama Sabrina afatishe kile anachokisema yeye.
Wakati wanasema hayo maneno, mbele yao akatokea yule Cherry wa ajabu na kumfanya mama Sabrina aogope sana, kwani kwa yeye ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kumuona huyu Cherry wa ajabu maana kwa kipindi kingine alimuona akiwa ndani ya Cherry wa kawaida na kumfanya asimfahamu vizuri ila utokeaji wake wa leo ule wa kimaajabu ulimfanya aogope sana na kuanza kutetemeka.
Emmy akamuangalia mama Sabrina na kumwambia,
"Usiogope"
Hii kauli ikamchekesha Cherry wa ajabu kwani ilimfanya acheke sana kisha akamuangalia Emmy kwa hasira na kusema,
"Wewe ndio unajifanya jasiri sana? Ila mimi hunifahamu vizuri, nina uwezo wa kukufanya nitakavyo."
Emmy nae akamjibu kwa kujiamini,
"Fanya sasa"
"Unajua ulichokifanya hapo, kwahiyo unahisi sitaweza. Ila nitakupa pigo ambalo hutokaa usahau maisha yako yote. Na siku zote ukiiangalia hii familia utakumbuka pigo nililokupa"
Kisha akatoweka.
Kile kitendo kilimtetemesha zaidi mama Sabrina na kumfanya akose raha kabisa.
Emmy akamuangalia mama Sabrina na kumwambia kuwa wanaweza kuingia ndani kwasasa.
Wakati wanaingia mama Sabrina akataka kuitupa ile ndulele ila Emmy akamkataza,
"Hapana, usiitupe sasa. Kaa nayo tu"
Kisha wakaingia ndani.
Fredy alikaa sana hospitali akisubiri kurejea kwa Sakina lakini Sakina hakurudi, ikabidi aamue kuondoka tu kwani hata hali ya Sabrina nayo haikuwa nzuri akaona hata yeye kuendelea kubaki hapo bado haiwezi kumsaidi Sabrina kuwa apone.
Akatoka pale hospitali akiwaza kuwa aende kwakina Sabrina ili ajue kama Sakina amefanikisha au arudi tena kwa yule mganga kumuulizia vizuri.
Wazo la kurudi kwa yule mganga likamkaa sawa, ingawa muda ulikuwa umeenda sana ila alienda hivyo hivyo.
Alipofika akamkuta hata yule mganga amepumzika na familia yake kwa maana hiyo kwa huo muda kazi ya uganga alipumzika.
Ila Fredy alimsalimia na kumsogelea kumueleza shida yake hivyo hivyo,
"Nina shida mzee"
"Muda wangu wa kazi umeisha hivyo sitaweza kukusaidia kwa muda huu."
"Hata kama hautanisaidia kwa muda huu, ila naomba unisikilize kwanza"
"Lakini muda wa kazi umeisha"
Fredy aliona watazungushana nae tu, hivyo basi akaenda na hoja ya msingi moja kwa moja na kumueleza walivyokuja mchana na dawa alizowapa.
"Nakumbuka ndio mlikuja mchana ila hakuna dawa niliyowapa"
"Ulitupa dawa mzee na tena ukatupa na masharti, ukasema tukitimiza basi matatizo yetu yatakwisha kabisa."
"Hivi wewe kijana akili yako ni timamu kweli? Inamaana umesahau kuwa niliwafukuza! Si niliwaambia kuwa siwezi kuwatibia hayo matatizo yenu, inamaana umesahau?"
Fredy akamshangaa huyu babu kuwakana wakati ni yeye aliyewapa dawa na masharti.
Fredy akajaribu hata kuelezea hali halisi ilivyokuwa, ila yule mganga aliendelea kukana kuwa hajawapa dawa yoyote wala masharti yoyote bali aliwafukuza tu.
Ikabidi Fredy akubali tu na kuaga kisha akaondoka zake.
Fredy aliondoka huku akimshangaa sana huyu mganga ukizingatia ni kweli aliwapa dawa na masharti.
Kwavile muda nao ulikuwa umeenda akaona ni vyema arudi nyumbani kwao tu kisha kuahidi kufatilia kesho habari za wakina Sabrina na ndugu zake.
Aliporudi kwao tu, akamkuta Francis akiwa yupo tu akiangalia mguu wake aliong'atwa na nyoka.
Ikabidi amueleze yaliyojili,
"Kuwa makini ndugu yangu yasije yakakukuta
yaliyonikuta mimi, tatizo kuna mambo mengi sana yamejificha kwenye ile familia, cha muhimu kwasasa jiangalie wewe na uachane na habari za hao waganga."
Fredy akamuitikia ndugu yake ingawa anaelewa wazi kuwa maneno yake hatoyafanyia kazi.
Ila baada ya hapo aliamua pia kumuelezea hali halisi ya Sabrina ambapo kwa haraka Sam ilimgusa sana.
Emmy na mama Sabrina wakaenda moja kwa moja kisha wakaingia sebleni na kumkuta yule mama mdogo wa Sam akiwa na wale watoto wa Sabrina.
Wakasalimiana nae kisha wakamueleza yaliyojiri mlangoni,
"Khee hii nyumba nayo ina makubwa, hata nilikuwa sijui ingawa nilihisi kuwepo kwa uzito wa nyumba kumbe kuna vitu vya ajabu! Inapaswa tukemee jamani, tatizo wenzangu hamna ushirikiano na mimi"
Mama Sabrina aliamua kujitetea,
"Sio kwamba hatuna ushirikiano ila haya mambo yanazidi uwezo wetu"
"Ni kweli yanazidi uwezo wetu na ndiomana inatakiwa tuombe, yani kwa kifupi hakuna la kutusaidia zaidi ya maombi"
Emmy alikuwa kimya kwa muda huu na alionekana kuwa na mawazo mengi sana kwa wakati huo.
Ikabidi mama Sabrina amshtue kidogo,
"Vipi, nini tatizo?"
"Hapana, ila kuna mawazo mabaya sana yananijia"
Ndipo mama mdogo wa Sam alipotoa hoja yake ya kukazana kuomba ila hawa wawili walionekana kuwa na mawazo na kushindwa kuendelea na mengine.
Giza liliingia bila ya Sakina na Sabrina kurudi na kuwafanya wapatwe na hofu zaidi, hata Emmy hakutaka kuondoka ili kujua walipoishia Sakina na Sabrina.
Kwavile giza tayari lilishaingia huku Sakina akiwa pale pale mlangoni, kwakweli Keti alionekana kumuhurumia sana na kumuuliza tena Sam kama wanaweza kumtoa kwa muda huo.
"Hapana, mwache tu"
"Sasa huo mlango hatuufungi?"
"Wewe mwache tu na mlango utafungwa"
Keti akaamua kwenda tena jikoni huku akiwa na mawazo sana.
Muda kidogo akarudi sebleni, akamuona Sakina amelazwa kwenye kiti halafu ule mlango umerudishiwa.
Keti akamuangalia Sam na kumuuliza,
"Umeamua kumnyanyua mwenyewe?"
Sam akatabasamu bila ya kujibu chochote.
Keti akamuangalia sana Sam, kidogo hofu ikamuingia mwilini na kuelekea chumbani kwake ambapo alijilaza kitandani huku akiwa na mawazo sana.
Usiku wa manane, Keti akiwa chumbani akagongewa mlango na kwa haraka haraka akajua Sakina amezinduka.
Akainuka na kwenda kufungua mlango ambapo moja kwa moja aliingia Sam na kwenda kukaa kwenye kitanda cha Keti kisha akamuuliza,
"Ni nani aliyekuita kufanya kazi?"
"Ni wewe bosi"
"Na kwanini unafanya kazi?"
"Nafanya kazi ili nipate pesa itakayoniwezesha kuishi na kusaidia familia yangu"
"Kwenye hii kazi ni nani anakulipa?"
"Ni wewe bosi"
"Sawa, basi nataka unifanyie kazi moja tu na utayapenda maisha yako baada ya hapo"
Uoga kiasi ukamshika Keti kwani alishawahi kuwasikia Sakina na Sabrina wakizungumzia matatizo ya Sam ingawa hakuwa na uhakika nayo, uoga ulimshika kwavile hakujua ni kazi gani anataka kupewa kwa muda huo wa usiku.
Alisimama tu vile vile na kuogopa hata kukaa ila Sam alimuomba asogee karibu ili akae nae kwa ukaribu zaidi na hilo swala la ukaribu ndio lililomtisha zaidi Keti na kujikuta machozi yakimtoka.
Sam alipomuona Keti analia aliamua kumuuliza,
"Vipi tena, nini kinakuliza?"
Keti aliongea huku akilia,
"Nihurumie bosi, nafanya kazi kwaajili ya maisha yangu tafadhari usinikatishie maisha. Mimi ni masikini, sina uwezo wowote wa kupingana na wewe ila pia sistahili adhabu unayotaka kunipa"
"Nani kakwambia kuwa nataka kukupa adhabu Keti? Usifikirie chochote kibaya na kama ningetaka kufanya hivyo basi ningefanya tu. Ninachotaka mimi kwa muda huu ni kimoja tu"
Keti alitulia huku akitetemeka na kumsikiliza Sam anachokitaka.
"Naomba ufanye jambo moja, nenda pale sebleni nilipokuwa nimekaa mimi. Nenda kakae pale na usinzie pale pale hadi kutakapokucha halafu mimi nitalala humu chumbani kwako"
Keti hakupinga ingawa hakujua ni kwanini Sam amesema vile, kwahiyo alichokifanya kwa muda huo ni kwenda mahali ambako Sam alikaa kisha Sam alibaki mule chumbani kwa Keti na kulala.
Emmy alilala nyumbani kwa wakina Sabrina kwa siku hiyo ila hadi panakucha hawakuwaona Sakina wala Sabrina na pia hawakupata mawasiliano yoyote ya sehemu waliyokuwepo.
Hakuna aliyekuwa na jibu la moja kwa moja hivyo asubuhi hiyo Emmy aliamua kuondoka ili aweze kurudi nyumbani kwanza.
Kufika njiani akakutana na Francis, wakasalimiana pale na kuendelea na maongezi mengine,
"Na huo mguu vipi asubuhi yote hii?"
"Naenda kumuona Sabrina hospitali"
"Sabrina hospitali! Sabrina gani huyo?"
"Kwani hujui?"
Emmy akatingisha kichwa kuashiria kuwa hajui chochote ndipo Francis alipoanza kumueleza alichoelezwa na Fredy hadi kuhusu mganga ambaye Fredy na Sakina walienda.
Emmy alibaki kushangaa na kuamua kuahirisha safari ya kuelekea kwao na kuanza hiyo safari ya kuelekea hospitali aliyolazwa Sabrina.
Keti hakulala kwa raha pale sebleni kwani muda wote alikuwa na mawazo na kushtuka shtuka huku akihisi kuwa amewekwa kama chambo ila kulipokucha Sakina nae alizinduka huku akijiangalia na kujishangaa, kisha akamuuliza Keti kuwa amepatwa na nini,
"Kitu gani kimenipata Keti?"
"Pole mama, ulianguka"
"Niliangukaje? Na kwanini nianguke?"
"Mi sijui ila ulianguka"
"Hivi dawa niliweka kweli?"
"Dawa gani?"
Sakina alikumbuka dawa za mganga bila matukio mengine yoyote kwani alimuuliza huyu Keti ambaye hata haelewi huo uwepo wa dawa.
Akatulia kidogo na kuinuka huku akitaka kutoka nje kwanza ila Keti alimzuia,
"Usitoke kwanza mama"
"Kwanini nisitoke?"
"Ndio maagizo niliyopewa"
"Nani huyo kakupa maagizo hayo?"
Sakina alikuwa anamuangalia Keti kwa makini sana huku akingoja jibu la swali lake ila kabla hajajibu, Sam alitoka ndani na kumwambia
"Ni mimi niliyempa maagizo hayo"
Sakina alijikuta akitetemeka kwa uoga na kushindwa hata kuongea zaidi ila Sam ndio akaendelea kuongea,
"Dawa uliyopewa jana haikuwa salama, umeiweka hapo mlangoni. Kutoka kwako ndio kudhurika kwako"
Sakina akajipa kidogo nguvu ya kuongea na kumuuliza Sam,
"Umewezaje kutoka hospitali? Na mbona unaonekana kuwa mzima kabisa wakati ulikuwa umeungua sana?"
Sam akacheka, tena akacheka sana na kusema,
"Ni historia ndefu ila ni ngumu kuitambua, ninayemuhitaji kwa muda huu ni Sabrina tu"
Sakina akamjibu Sam,
"Sabrina huwezi kumpata kwa muda huu, yupo hospitali na ana hali mbaya sana. Umesema tusitoke, kwahiyo itakuwa ngumu kwako kumuona Sabrina."
Sam akatabasamu kisha akamwambia Sakina,
"Geuka nyuma"
Sakina alipogeuka nyuma akamuona Sabrina na kumfanya ashtuke sana.
Sakina akajipa kidogo nguvu ya kuongea na kumuuliza Sam,
"Umewezaje kutoka hospitali? Na mbona unaonekana kuwa mzima kabisa wakati ulikuwa umeungua sana?"
Sam akacheka, tena akacheka sana na kusema,
"Ni historia ndefu ila ni ngumu kuitambua, ninayemuhitaji kwa muda huu ni Sabrina tu"
Sakina akamjibu Sam,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sabrina huwezi kumpata kwa muda huu, yupo hospitali na ana hali mbaya sana. Umesema tusitoke, kwahiyo itakuwa ngumu kwako kumuona Sabrina."
Sam akatabasamu kisha akamwambia Sakina,
"Geuka nyuma"
Sakina alipogeuka nyuma akamuona Sabrina na kumfanya ashtuke sana.
Kwakweli Sakina aliishiwa nguvu kabisa na kujikuta akianguka na kuzimia.
Sabrina alikuwa amesimama tu akishangaa huku akimuangalia Sam aliyekuwa akitabasamu kisha Sam akamwambia Sabrina,
"Karibu sana Sabrina, karibu sana mwanamke niliyekupenda kuliko wanawake wote duniani"
Keti aliinama chini kumuangalia Sakina huku akimuangalia Sam kama kuna chochote atakisema ila Sam hakusema chochote kile, ikabidi Keti amwambie
"Tusaidiane kumnyanyua basi tumweke kwenye kochi"
"Mwache hapo hapo"
Hizi kauli za Sam zilimshangaza sana Keti ila hakuwa na la kusema zaidi ya kukubaliana nae tu.
Kisha akakaa pale pale pembeni ya Sakina huku akimuangalia Sam na Sabrina ingawa hata yeye hakuelewa kuwa Sabrina ameingiaje mule ndani.
Emmy na Francis walifika hospitali ambayo Francis alielekezwa na Fredy kuwa Sabrina amelazwa hapo.
Wakaenda mpaka wodi waliyoelekezwa ila hawakukuta mtu, wakatazamana na kuulizana,
"Au sio hospitali hii?"
"Ni hii hii nimeelekezwa labda kama kabadilishwa wodi"
Ikabidi waende mapokezi kuulizia vizuri.
Wakapewa maelekezo ya wodi ile ile na namba ya kitanda,
"Tumemuangalia hayupo"
"Hayupo kivipi?"
Ikabidi huyu nesi amuite mwenzie ili aongozane na wakina Emmy kwenda alipo Sabrina.
Walifika na kukuta vile vile kuwa hakuna mtu pale hata huyu nesi alishangaa tu,
"Sasa atakuwa kaenda wapi?"
Francis akatoa hoja yake,
"Au mmemuhamisha wodi?"
"Angehamishwa tungejua tu, ila ngoja nijaribu kuangalia vizuri"
Huyu nesi akaenda kuangalia wodi zingine na baada ya muda akarudi na jibu lile lile kuwa hayupo.
Emmy akauliza,
"Au mmemruhusu kutoka?"
"Kwa hali yake ilivyokuwa tusingeweza kumruhusu na hata hivyo bado bili zake hazijalipwa"
Nesi akawaomba Francis na Emmy wamsubirie hapo kidogo nao wakaitikia.
Huyu nesi alipoondoka, akili zikawacheza na wakaona kwa vyovyote vile wataletewa bili wakati hata mgonjwa wao hawajamuona.
Ikabidi watumie ujanja wa kutoka hapo na kuondoka.
Walipokuwa nje, Emmy na Francis walijikuta wakijadiliana sasa na ndipo Emmy alipomueleza Francis juu ya Sam pia kutoweka hospitali katika mazingira ya kutatanisha.
"Nadhani kilichompata Sam ndio kilichotokea kwa Sabrina, sasa swali langu ni je watakuwa wapi?"
"Hapo sasa ndio pagumu jamani"
Francis alimueleza pia alivyoelezwa na Fredy kuhusu kwenda kwao kwa mganga kwaajili ya kupata dawa na jinsi mganga alivyomkana Fredy, moja kwa moja Emmy akaelewa kuhusu ile dawa aliyoikuta mlangoni kwakina Sabrina na pia akatambua kuwa huenda imemdhuru huyo Sakina pia kama aliweka na mlangoni pake.
"Uwiiii huyu dada jamani anapenda kwenda kwa waganga dah! Anatusababishia matatizo mengine yasiyo na kichwa wala mguu. Yani kwa vyovyote vile nina uhakika kaweka na kwake na amedhurika. Hata sijui tuanzie wapi sasa!"
Wakatazamana tu na Francis kwani hawakuelewa kuwa waanzie wapi na kuishia wapi.
Wakaona ni vyema waende kumuona na Jeff kwanza ili wajue na yeye imekuwaje ndipo waendelee na mengine.
Mama Sabrina na mama mdogo wa Sam nao walikuwa wakijadiliana cha kufanya kwa wakati huo.
Mama Sabrina alionekana kukata tamaa kabisa ila mama mdogo wa Sam aliendelea kumpa moyo,
"Ni marufuku kukata tamaa, hatutakiwi kukata tamaa kwamaana tunapokata tamaa ndipo shetani anakuja kwa karibu zaidi ili kukuvuruga na kukuharibia. Yani haitakiwi kukata tamaa kabisa."
"Unajua nini, yani Sabrina anafanya kichwa kiniume kwakweli maana sijui alipo"
"Yote tumuachie Mungu na tuombe"
Mama mdogo wa Sam alianza kuomba huku mama Sabrina nae akiomba kwa kujikaza tu.
Emmy na Francis sasa walifika hospitali aliyolazwa Jeff na moja kwa moja wakaenda kwenye wodi na kumkuta Jeff akiwa yupo macho ila mguu ukiwa umening'inia juu ila walipojaribu kuzungumza nae hakuwajibu chochote, nesi akawafata na kuwaomba wamuache mgonjwa apumzike.
Emmy na Francis wakatoka na kwenda kukaa mapokezi huku akijiuliza sababu za Jeff kutokuongea,
"Yani jana jioni hapo tumekuja, tukampa chakula na kuongea nae kabisa sasa iweje leo ashindwe kuongea?"
"Labda leo anaumwa zaidi"
"Hapana, leo inaonyesha ameanza kupona kabisa sasa kwanini ashindwe kuongea?"
"Mimi na wewe hatujui, nadhani ni vyema tuwaachie madaktari waendelee na shughuli zao."
Ikabidi wakubaliane hivyo ili wasiendelee kuhoji vitu wasivyovijua.
Nyumbani kwa Sakina ilionekana wazi kuwa Sabrina alikuwa akijishangaa na hakujielewa kabisa.
Muda kidogo, Sakina nae akaonekana akizinduka na kukaa pale pale chini huku akitazama pande zote mule ndani na haswaa akamtazama Sabrina kisha akamuuliza,
"Umefikaje fikaje hapa?"
"Hata sijui kwakweli, najishangaa tu hapa. Sielewi nimefikaje"
"Na vipi kuhusu macho yako?"
"Macho hayana tatizo lolote yani kwa kifupi niko mzima na wala hayaniumi ila tu sielewi imekuwaje hadi niwe hapa"
Sakina akamtazama Sam kisha akamuuliza pia,
"Na wewe ilikuwaje?"
"Kama ilivyokuwa kwa Sabrina"
Majibu ya Sam yalikuwa yakimchanganya Sakina tu kwani hakuweza kumuelewa hadi na kumfanya afikirie kuwa hayupo mahali salama.
Alijiona kama vile yupo mtegoni, aliwatazama tena ila hakuwa na jibu la maswali yake.
Akawatazama kwa zamu zamu Sabrina na Sam ila hakuwa na ujanja wowote kwani mwili wake ulichoka kupita maelezo ya kawaida.
Emmy alimuomba Francis amsindikize kwao,
"Kwahiyo hujaenda kwenu tangu lini?"
"Toka juzi mbna jana nililala kwakina Sabrina kwasababu tulikutana na matatizo mengine"
"Matatizo gani tena?"
Emmy akamuelezea jinsi ilivyokuwa pale kwakina Sabrina na jinsi zile dawa alizoweka Sakina zilivyoonekana kuwa na nguvu zaidi, ni hapa Francis alipomkumbushia na yale maneno aliyoambiwa na Fredy kuhusu yule mganga ndipo akili ya Emmy ilipomkaa sawa na kuona ni vyema atangulie huko kwakina Sakina.
"Basi twende kwanza huko kwakina Sakina ili isije ikawadhuru watu wengi zaidi"
Wakakubaliana na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Sakina.
Mama Sabrina na mama mdogo wa Sam nao walipoona muda unaenda bila ya taarifa yoyote kuhusu Sakina na Sabrina ikabidi mama Sabrina atoe ushauri wa yeye kwenda kwa Sakina kumuuliza hata yule mfanyakazi wao kama kuna taarifa yoyote amepata ila alipokuwa anaondoka mama mdogo wa Sam akamzuia kwanza na kumuuliza,
"Je, una imani na unapoenda?"
"Kwanini nisiwe na imani nako?"
"Mie nakushauri uombe kwanza ndio uende"
"Kwanini? Kwani napo si salama? Ila wewe si utaniombeaga!"
"Penda sana kujiombea kuliko kuombewa, narudia omba kwanza kabla hujaenda huko"
"Basi twende wote"
"Hapana, mimi siwezi kwenda na wala sitaenda kwa wakati huu. Na ukifika utajua kwanini mimi siwezi kwenda maana siwezi kufanya vitu vinavyokinzana"
Mama Sabrina hakumuelewa kabisa huyu mama mdogo wa Sam kuwa vitu vinavyokinzana kivipi ila kwavile alishajipanga kwenda kwa Sakina ikabidi atoke na kuelekea huko kwa Sakina.
Emmy na Francis walipokuwa njiani walikutana na mtu aliyeonekana kumfahamu sana Emmy ambapo alimsimamisha na kumsalimia kisha akamwambia,
"Huruma yako itakuponza Emmy na sio itakuponza swala ni kwamba imeshakuponza"
"Kivipi mbona sikuelewi?"
"Utanielewa tu muda utakaorudi kwenu ila pole sana najua utairaumu sana huruma yako"
Kwakweli ilikuwa ngumu kwa Emmy kumuelewa kwani hakuwa na wazo lolote la kuhusu nyumbani kwao, kwahiyo akaishia kushangaa tu kisha akwamwambia Francis kuwa waendelee na safari yao ila Francis alipatwa na hofu kiasi
"Ila ameniogopesha huyu, sijui kutakuwa na nini huko kwenu!"
"Usijali, kilichopangwa kimepangwa twende tu tulikopanga kwenda."
Ikabidi Francis amuitikie na kuendelea na safari yao.
Mama Sabrina alifika nyumbani kwa Sakina, alishangaa tu kwa ukimya ule ila kilichomshangaza zaidi ni kuona kuna uyoga umeota pembezoni mwa mlango wa kuingilia kwa Sakina ila kilichomshangaza zaidi ni kuwa ule uyoga ulikuwa na rangi nyekundu.
Ni hapa alipoyakumbuka maneno ya mama mdogo wa Sam kuwa sehemu anayoenda si salama na kumfanya ashikwe na hofu kiasi huku akijiuliza kuwa huenda asogee akagonge au afanye kitu gani.
Akajiuliza sana na ikapita kama nusu saa akijiuliza jambo lile lile kuwa akagongea au afanyaje.
Kwa gafld likamjia wazo kuwa akang'oe vile viuyoga vilivyojiotea pale, akakubaliana na wazo lake hilo na kusogea karibu, halafu akainama ili ang'oe ule uyoga ila kabla hajaung'oa akashtuliwa na sauti ya Emmy ikimkataza ikabidi aache mara moja,
"Mbona unapenda kujitafutia matatizo mama angu, hivi huoni kama hiko kitu ni cha tofauti jamani!"
Mama Sabrina alikuwa kimya tu kwani hata yeye hakuielewa ile akili iliyomuelekeza kuwa ang'oe ule uyoga, hivyo akarudi nyuma kwa uoga.
Emmy akamwambia kuwa asifanye chochote pale.
Kisha akamuangalia Francis na kumwambia,
"Ndio hiki alichokifanya huyo Sakina, kaja kujiharibia na nyumba yake mwenyewe"
"Tutafanyaje sasa?"
"Subirini"
Emmy akatoka kidogo na kuwaacha pale Francis na mama Sabrina ambapo mama Sabrina alimuuliza Francis,
"Hivi huyu Emmy unamuelewa?"
"Namuelewa sana"
"Hivi alitaka kuwa mganga wa kienyeji au ana dalili za uganga?"
"Kwanini unauliza hivyo?"
"Kwani wewe huoni kama yupo tofauti na wengine, huoni kama anagundua mambo ya ajabu?"
"Lakini ndio anasaidia hivyo"
Mama Sabrina akaguna na kutulia kwa muda.
Wakati Emmy anachuma majani ambayo anaamini kuwa yatawasaidia, yule kiumbe wa ajabu akamtokea kwenye lile lile umbo la mtoto wa Sabrina yani Cherry kisha akamwambia Emmy,
"Unachokitafuta utakipata, endelea tu na hayo mambo ila nakwambia hutonisahau kamwe"
Akatoweka, ila Emmy hakuwa na uoga wowote kwani alitambua kwamba kile kiumbe kinafanya kumtishia tu ili aache kuwasaidia wale halafu yeye aendelee kuwatesa.
Emmy alirudi na majani ambayo aliyafikicha kidogo na kumpaka mama Sabrina kwenye paji la uso, kisha akampaka Francis na kujipaka na yeye halafu akamwambia mama Sabrina aangalie tena ule uyoga.
Mama Sabrina alipoangalia alishtuka sana kuona kuwa haukuwa uyoga bali alikuwa ni nyoka, kwakweli mama Sabrina alitetemeka mwili mzima na kujiuliza kuwa angeshika ingekuwaje.
Emmy alichukua majani mengine na kuyatupia pale, gafla yule nyoka akatoweka na kumfanya mama Sabrina asisimke zaidi.
Emmy akawaambia kuwa sasa wanaweza kugonga mlango ila hakuna aliyethubutu kusogea mlangoni, ikabidi Emmy mwenyewe asogee na kugonga.
Kwa waliokuwa ndani sasa walishtushwa sana na aliyegonga mlango kwani wote hawakudhania kuwa kuna mtu atafika kugonga muda ule, hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kufungua zaidi ya Sam ambaye alisogea pale mlangoni na kufungua.
Emmy alishtuka sana kumuona Sam, na kwa uoga kiasi aliokuwa nao akarudi nyuma.
Ikabidi Sakina nae ainuke kuwakaribisha, kidogo Emmy akapatwa na akili kuwa wale ni watu na kuwaambia mama Sabrina na Francis wote waingie ndani ila swala lililomchanganya Emmy kwa muda huo ni kuwa Sam imekuwaje hadi amepona vile na amewezaje kuwa nyumbani, Sam nae alielewa mshtuko wa Emmy na kumwambia,
"Najua unashtuka kuniona mimi ila kwakweli mimi nimepona Emmy, hebu niangalie vizuri, je kuna mahali popote nina kovu?"
Emmy akatingisha kichwa maana Sam alionekana kuwa mzima kabisa.
Kisha Emmy akamtazama Sabrina waliyeambiwa kuwa amelazwa,
"Na huyu imekuwaje?"
Sakina ndiye aliyejibu,
"Shangaeni nyie maana mimi nimeshangaa hadi nimechanganyikiwa kwakweli kwa kushangaa"
Wakakaa chini sasa ili kujaribu kujadiliana na kujua kilichotokea ili wajue cha kufanya.
Ila kwavile Sam alikuwa amepona, Emmy aliona ndio wakati sasa wa wao kutokomeza kile kiumbe.
Ila wakati wanaulizana mawili matatu, kengele ya hatari ikalia kwa Emmy kuhusu familia wake hivyo akajikuta akiwaomba wote kwa pamoja wamsindikize nyumbani kwao.
"Kwani kuna nini Emmy?"
"Sielewi ila naona kuna hatari, naomba niende nyumbani na Sam na Francis wengine mbakie tu"
Hawakutaka kupoteza muda na kuondoka.
Pale ndani alibaki Keti, Sabrina, Sakina na mama Sabrina huku kila mmoja akiwa na mashaka kuwa Sam aliyekuwepo pale hakuwa mtu wa kawaida kutokana na vile walivyomuona hospitali, na wakati huo huo Sakina nae alikuwa na mashaka na Sabrina kutokana na jinsi alivyofika mule ndani.
Emmy akiwa ameongozana na Sam pamoja na Francis, walipofika kwao walishangaa kuona watu wamejaa sana na ndugu wa Emmy walipomuona Emmy walimpokea kwa vilio na kumfanya Emmy aulize kwa mshangao,
"Kuna nini hapa?"
"Mama amekufa Emmy"
Emmy hakuweza kuamini kabisa na kujikuta akianguka chini na kuzimia.
Emmy akiwa ameongozana na Sam pamoja na Francis, walipofika kwao walishangaa kuona watu wamejaa sana na ndugu wa Emmy walipomuona Emmy walimpokea kwa vilio na kumfanya Emmy aulize kwa mshangao,
"Kuna nini hapa?"
"Mama amekufa Emmy"
Emmy hakuweza kuamini kabisa na kujikuta akianguka chini na kuzimia.
Ikabidi Francis na Sam wasaidiane kumuinua na kumbeba hadi sehemu nzuri kiasi kwani pale ilikuwa chini kabisa kwenye mchanga.
Walikaa pembeni yake huku vilio vikiendelea na kufanya wakina Francis kuulizia vizuri kuwa huyo mama amekumbwa na nini,
"Eti alikuwa anaumwa au imekuwaje?"
"Kwakweli hajaumwa ila kwa maelezo ya haraka ni kuwa juzi alikuwa analalamika kuwa anaona majeneza. Jana ameamka vizuri kabisa, tumekaa vizuri hapa sasa kwenye jioni jioni hivi akaanza kulalamika kuwa moyo unamuuma sana gafla akaanza kusema kuwa anamuona mtu mfupi mbele yake kama mtoto ila ni mtu mzima yani muda huo huo akaanguka na kufa hapo hapo."
Sam na Francis walitazamana kwani kifo hiki kiliwashangaza kidogo huku wakijiuliza huyo mtu mfupi ndio Israel mtoa roho au ndio kitu gani! Hawakuelewa ila ndio vilio vilikuwa vimeenea hapo na wala Emmy hakuzinduka kwa muda huo.
Nyumbani kwa Sakina bado walikuwa wakimshangaa Sabrina huku Sakina akijaribu kumueleza mama Sabrina ilivyokuwa kwa Sabrina hadi walipompeleka hospitali ila yeye Sabrina hakuelewa kitu chochote hata walipokuwa wakimuuliza maswali hakuweza kuwajibu jambo lolote na kuishia kujibu kuwa sijui.
"Mmh mbona makubwa haya"
"Tena makubwa si kidogo yani sijawahi kuona vitu hivi maishani mwangu"
Wakatazamana kisha mama Sabrina akauliza pia kuhusu Sam,
"Hivi na huyu Sam na yeye imekuwaje maana nimeshangaa kumuona jamani tena akiwa hana jeraha lolote, imekuwaje kwani?"
"Kwakweli huyo hata mi mwenyewe sijui kitu, nimemkuta tu hapa ndani"
"Unajua mi na Emmy tulienda hospitali kumuangalia na kumkosa yani tumetafuta wodi zote hata madaktari nao wamestaajabu kuwa imekuwaje na amepelekwa wapi, tumewaacha waendelee na uchunguzi eti leo namkuta huku loh maajabu haya!"
Mama Sabrina alikuwa akishangaa tu, ikabidi Sakina amuulize vizuri Keti maana muda wote yupo mule ndani,
"Eti Keti, huyu Sam amefikaje fikaje humu kwangu?"
"Ilikuwa mchana siku hiyo nilikuwa nimelala, nikasikia mlango ukigongwa nilipofungua nikamuona bosi Sam basi nikamkaribisha na kumpa pole, akaniambia kuwa amepona kabisa na akasema kuwa alienda kule kwakina Sabrina na kukuta kufuri ndio akaamua kuja hapa kwahiyo mimi sikuelewa chochote na nilimuona kuwa wa kawaida tu kwani hakuwa na tatizo lolote. Nilimpa chakula na akala"
Sakina akawatazama wenzie kwa maelezo haya kisha akili ikamkaa sawa na kukumbuka maelezo ya yule mganga wa kienyeji na kuwaeleza wenzie.
Mama Sabrina akaelewa haraka kwani ndicho walichokutana nacho mlangoni akiwa na Emmy,
"Una balaa wewe Sakina! Madawa uliyopewa huko yalikuwa ni madawa ya kutudhuru yani tushukuru tu alikuwepo yule Emmy kwakweli Sakina una mabalaa na waganga wako hao"
Sakina akawa kimya huku Mama Sabrina akimueleza jinsi walivyohangaika kupambana na yale madawa.
Haya maelezo yalimfanya Sakina kushtuka na kukumbuka kuwa mwanae Jeff yupo hospitali amelazwa.
"Mungu wangu, jamani mwanangu Jeff nae sijui anaendeleaje"
Ndipo alipomwomba mama Sabrina aende nae kumuona, hilo halikuwa tatizo ila walipotoka pale mama Sabrina alirudi na Sabrina na kumuacha nyumbani kisha wao kuondoka zao.
Sabrina aliingia ndani na kumkuta mama mdogo wa Sam, ambapo alipotazamana nae machoni tu Sabrina alianguka kwahiyo mama mdogo wa Sam akapata kazi ya kumuombea Sabrina pale kwani kule kuanguka haikuwa hali ya kawaida.
Sabrina aliombewa pale huku akitapatapa kamavile mtu mwenye mashetani ila mama mdogo wa Sam hakuacha kumuombea mpaka pale alipoona ameanza kurudi kwenye hali ya kawaida, ndipo alipoanza kuimba nyimbo mbali mbali ili angalau Sabrina ajione kuwa yupo mahali salama kwani alitambua akili yake ilikuwa ndio inarudi sasa.
Sabrina aliinuka na kukaa huku akijishangaa sana na kumtazama mama mdogo wa Sam kisha akamuuliza,
"Nipo wapi hapa?"
"Upo nyumbani Sabrina tena upo mahali salama kabisa"
Sabrina akatulia kwa muda kisha akauliza tena,
"Ndipo walipo wanangu hapa?"
"Ndio"
Mama mdogo wa Sam akamuonyesha Sabrina watoto wake ambao alikuwa amewalaza kwenye kochi, Sabrina aliwafata akawashika na kuwabusu yani ilikuwa kamavile mtu asiyeamini yale anayoyaona kwa muda ule.
Sakina na mama Sabrina, walifika hospitali na moja kwa moja wakaenda alipolazwa Jeff ila hawakumkuta na kumuita nesi ambaye nae alishangaa ila akawaambia,
"Jamani na nyie ndugu wa huyu mgonjwa mna roho mbaya jamani, chakula hamumletei wala pesa za matibabu hamjaleta na mnajua kabisa kuwa kavunjika mguu"
"Ila nesi huu si wakati wa kulaumiana, tuambie kwanza mgonjwa wetu yuko wapi maana na sisi tuna matatizo ndiomana unaona hivi"
Huyu nesi nae akajaribu kuulizia kwa wenzie hakuna aliyemuona wala aliyemtoa na kwa haraka ilikuwa ni ngumu sana kusema kuwa Jeff ameondoka mwenyewe sababu ya ile hali aliyokuwa nayo.
Wakatazamana wale manesi lakini hakuna hata mmoja aliyetambua kuwa Jeff ameenda wapi.
Sakina na Sabrina wakasogea pembeni na kuambizana,
"Huenda kilichompata Jeff ndicho kilichompata Sam na Sabrina"
"Kwamaana hiyo inawezekana Jeff naye yupo nyumbani?"
"Inawezekana kabisa si unaona hata manesi hawajui alipo!"
Sakina na mama Sabrina wakakubaliana kuwa warudi nyumbani kwani kwa vyovyote vile walikuwa na uhakika kuwa Jeff atakuwa nyumbani tu.
Waliwaacha manesi wakibishana pale kisha wao wakaondoka zao kuelekea nyumbani.
Nyumbani kwakina Emmy bado Emmy hakuzinduka, ikabidi wamtengee chumba maana kila mtu aliyefika msibani hapo alionekana moja kwa moja akienda kumshangaa Emmy.
Muda nao ulikuwa umeenda sana ila Francis na Sam hawakuondoka ukizingatia wao ndio waliompeleka Emmy pale nyumbani kwao.
Emmy alipoingizwa chumbani na wao kubaki nje, muda wote Sam alionekana kuinamisha kichwa chini kwani alihofia kuonana na watu wanaomfahamu au watu aliomaliza ndugu zao kwani alijua wazi kuwa kwa vyovyote vile watu hao watakuwa na hasira sana na yeye.
Sam akiwa kainama tu kama kawaida, kuna mdada alifika na kumsalimia kisha akamuuliza,
"Samahani, hivi wewe ni bosi Sam?"
Sam hakutaka hata kumuangalia huyu dada bali alitingisha kichwa na kukataa kuwa siye,
"Kheee mmefanana hadi sauti"
"Duniani wawili wawili"
"Ila hata mi nilishangaa kumuona bosi Sam bila ya kuona gari yoyote ya kifahari hapo nje."
Yule dada akainuka na kwenda zake sehemu ya wanawake.
Sam akabaki kujihoji moyoni kuwa yule dada alitaka kumwambia nini ila kila alipoitafakari sauti yake akagundua kuwa ni sauti ya Eliza ambaye ni mfanyakazi wake pale kwenye kampuni yake ila Sam aliona vyema kuwa kimya ili asitambulike na yeyote yule.
Mama Sabrina na Sakina walirudi moja kwa moja nyumbani kwa Sakina na kumkuta Keti yupo pale, ikabidi Sakina amuulize Keti
"Hivi Jeff hajafika huku?"
"Jeff!! Hajafika, kwani alisema anakuja huku?"
"Sio kwamba alisema ila nae alikuwa mgonjwa kalazwa hospitali ndio muda ule tumeenda ila hatujamkuta pale hospitali na hata manesi hawajui alipo ndiomana tumehisi yupo huku kama ilivyotokea kwa Sam na Sabrina"
"Mmh jamani Jeff sijamuona huku kabisa, na kama angekuja basi angegonga hodi maana mlango nilifunga"
"Inamaana atakuwa wapi sasa? Mbona haya ni makubwa zaidi jamani, mbona sielewi haya mambo?"
Wakakaa chini wakitafakari kwani kila mmoja hakujielewa kwa muda huo kuhusu Jeff wakabaki wakitazamana tu huku wakiulizana cha kufanya.
"Sasa tutafanyaje? Turudi hospitali tukaulizie vizuri au iweje?"
Wakaona wazo la kurudi hospitali ni bora zaidi kwani huko ndipo alipopotelea.
Wakajipanga kurudi hospitali kwanza ila muda nao ulikuwa umeenda na giza nalo lilianza kuingia na kuwafanya washauriane vizuri sasa,
"Tukifika huko hospitali si itakuwa tayari ni usiku, sasa itakuwaje?"
"Kwahiyo twende asubuhi! Nitaweza kulala kweli bila ya kujua hatma ya mwanangu jamani!"
"Sasa utaenda kukesha hospitali ndugu yangu! Hebu kuwa mvumilivu jamani, tutajua tu Jeff alipo maana kukesha kwako hospitali hata hakutasaidia kitu"
Mama Sabrina akaona ni vyema aende na Sakina nyumbani kwake maana kumuacha hapo alihofia kuwa anaweza akaamua kwenda mwenyewe hospitali.
Hivyo akamuomba na kuondoka nae kwa muda huo na kwenda nae nyumbani kwake na mama Sabrina.
Walipofika walimkuta mama mdogo wa Sam akiwa na Sabrina na alionekana kumueleza Sabrina baadhi ya mambo.
Walipofika nao walitulia kwani waliona wazi ni mambo ambayo yatakuwa yanawahusu pia.
Kwa muda huu walimkuta mama mdogo wa Sam akimuuliza Sabrina kwa makini mahali ambako alikuwepo,
"Kwakweli nakumbuka wazi yaliyonipata mara ya mwisho"
Naye akaelezea kile kitendo cha kutemewa mate na nyoka na kupelekwa hospitali,
"Nakumbuka nilivyokuwa hospitali macho yalikuwa yakiniuma sana na nilikuwa nikilalamika macho yananiuma huku nikilia. Kwa mara ya mwisho alikuja daktari na kunichoma sindano ya usingizi, sasa kutoka hapo sikuelewa kitu ila nilijikuta tu nikishangaliwa nyumbani kwa Sakina. Kwakweli sikujielewa na wala nilikuwa sielewi chochote na ndiomana hata walipokuwa wananiuliza sikuweza kuwajibu cha maana sababu sikuelewa chochote ila nilipofika hapa nyumbani na kuingia ndani kichwa changu kilikuwa kizito sana na kujikuta nikianguka ila kwasasa najisikia mzima kabisa"
Mama mdogo wa Sam akamtazama Sabrina na kuwatazama hawa wengine kisha akawaambia,
"Mnaona nguvu za giza zinavyotenda kazi? Huyu karudishwa na nguvu za giza ila maombi yamefanya awe mzima na akili yake iwe sawa. Jamani hizi nguvu za giza ni kali sana na tusipokuwa makini tutapotea wote"
Mama Sabrina akamueleza mama mdogo wa Sam kuhusu uwepo wa Sam pia,
"Inamaana napo ni nguvu za giza?"
"Ndio, tena hamjui jinsi gani napambana kuhusu Sam. Kwa nje mnamuona kuwa ni mzima amepona ila bado Sam hajapona na tusipokuwa makini anaweza akafanya kitu cha ajabu sana ambacho hatukifikirii wala kukitarajia"
"Sasa tufanyeje?"
"Napenda wote tungekuwa na lengo moja, kama maombi ni maombi tu tatizo letu tumegawanyika. Wengine wanaamini kwa waganga wa kienyeji na wengine kwenye ushirikina kwakweli hilo ni tatizo kubwa sana."
Kisha akamuangalia Sakina na kumwambia,
"Ulienda kwa mganga ndugu yangu, ila kwakweli yule uliyekuwa ukizungumza nae hadi akakupa dawa hakuwa mtu ila alitaka kuwateketeza"
"Umejuaje?"
"Nilionyeshwa, jamani tuwe na umoja"
"Mwanangu nae kapotea hospitali, niangalizie basi alipo"
"Sakina, mimi sio mganga wa kienyeji useme kwamba ukiongea kitu basi nichukue tungule nione hapana, ila mimi naingiza jambo kwenye maombi halafu Mungu akiona kuna umuhimu wa kunionyesha basi atanionyesha"
Sakina akatulia kwa muda na kuwa kamavile mtu anayejifikiria kwanza, kisha akafanya kama anaomba ushauri,
"Basi niambie cha kufanya, niende tena hospitali kumuangalia au nifanyeje?"
"Cha kufanya ni tuungane kwenye maombi, tuombee yote yanayoendelea na hilo la mwanao ila kwenda wewe hospitali kwa muda huu hakutasaidia chochote kwani tayari mmeshaambiwa kuwa kule hayupo na kwa vyovyote vile zitakuwa ni nguvu za giza tu sasa hatuwezi kupambana nazo hivi, tunatakiwa kufanya maombi"
Sakina alikuwa mpole na kukubaliana na maneno ya mama mdogo wa Sam kisha wakashikana mikono kwa lengo la kufanya maombi.
Francis na Sam waliona vyema waingie ndani wakamuone Emmy ili iwe kama wanamuaga waende wakatoe taarifa kwa wengine waelewe kuwa Emmy kafiwa. Walipoingia kwenye kile chumba, Emmy alikuwa kwenye hali ile ile ambapo kwa haraka ilimpa Francis mashaka na kuona kuwa labda wangempeleka hospitali, akawakilisha wazo lake kwa Sam ila Sam alipingana na wazo hilo.
Kisha Sam akasogea alipolala Emmy na kumbusu kwenye paji la uso kama ishara ya kumuaga ila kabla hajaondoka akashtuka akishikwa mkono na Emmy, ikamfanya Sam ashtuke kidogo na kumtazama Emmy usoni na kumuona Emmy kafungua macho kisha akakaa.
Francis nae akasogea karibu ili kumpa pole Emmy kwani ni muda mrefu sana tangu kazimia.
Emmy hakuitikia zile pole na kuwa kimya tu, kisha wakamuuliza kuwa anaendeleaje,
"Nipo salama"
"Pole sana Emmy, tukuletee chakula?"
"Hapana"
"Unajua ni muda mrefu sana umezimia"
"Sikuzimia mimi"
Francis na Sam wakatazamana kwa kauli za Emmy ambapo muda kidogo akawashtua na kauli yake nyingine,
"Mapambano sasa yameanza"
Hawakumuelewa ila gafla walishangaa akianza kubadilika rangi ya mwili wake.
Francis na Sam wakatazamana kwa kauli za Emmy ambapo muda kidogo akawashtua na kauli yake nyingine,
"Mapambano sasa yameanza"
Hawakumuelewa ila gafla walishangaa akianza kubadilika rangi ya mwili wake.
Kisha Emmy akasimama, gafla umeme nao ukakatika na kufanya kuwe na giza kiasi mule ndani. Emmy akawaambia Sam na Francis,
"Nifateni"
Wakaanza kumfata nyuma huku wakiwa na mashaka kiasi.
Kwavile giza lilishaingia nje na umeme nao haukuwepo ikafanya watu wa pale wasiweze kumuona Emmy na ule mbadiliko wa rangi ya mwili wake.
Emmy akatoka nje akiwa ameambatana na Sam pamoja na Francis huku akiwaacha ndugu zake wakihangaika kutafuta taa ya chemli pamoja na mishumaa kwaajili ya kupata mwanga.
Emmy hakuwaangalia kabisa ndugu zake hao na aliendelea kwenda mbele ya safari tu.
Emmy pamoja na wakina Sam wakapotea kabisa kwenye lile eneo la nyumba ya kina Emmy na hakuna aliyewaona wakiondoka kwahiyo hawakugundua kuwa Emmy hayupo ndani.
Walipomaliza kuwasha mishumaa yao na chemli, kabla hawajaweka sawa na umeme nao ukarudi na kumfanya kila mmoja kuwa kwenye hali ya kawaida huku wakizima zima ile mishumaa na kuiweka mahali ambapo hata kama umeme ukikatika tena basi iwe rahisi kwa wao kuipata na kuiwasha.
Dada wa Emmy sasa akaingia chumbani kule alipo Emmy ili kuangalia kuwa anaendeleaje, alipoingia akashangaa kutokumkuta Emmy ikabidi awaite wadogo zake wengine na kuwauliza juu ya Emmy,
"Jamani imekuwaje mbona Emmy hayupo humu?"
"Ameenda wapi kwani maana nakumbuka mara ya mwisho nimekuja kumchungulia alikuwa bado yupo kitandani yani alikuwa bado hajazinduka"
"Mmh inawezekana vipi au kazinduka halafu kaondoka bila kuaga?"
"Mmh haiwezekani jamani lazima tungemuona, ila nakumbuka mara ya mwisho nilipokuja kumuona wakati natoka wakaingia wale wakaka wawili waliokuja nae na walisema kuwa wamekuja kumuaga wanaondoka. Sasa nashangaa hili swala jamani, mi sikuweza kufatilia kwavile muda kidogo ndio umeme ukakatika"
Ikabidi watulie wakishauriana kuhusu Emmy huku wakiambizana na kushauriana kuhusu mahali ambako wanahisi kuwa anaweza akawepo ila wakakubaliana kuwa mpaka kesho wasipompata wakatoe taarifa kwenye kituo cha polisi kwani walikuwa na mashaka na watu aliofika nao Emmy ambao ni Francis pamoja na Sam.
Nyumbani kwa kina Sabrina palikucha salama bila ya kupata taarifa kuhusu wakina Sam wala Emmy ila kwa haraka haraka wakahisi kuwa hata kama wamerudi basi watakuwa wameenda nyumbani kwa Sakina ingawa wao na Sakina mwenyewe walikuwa hapo kwa kina Sabrina.
Walipokaa vizuri sasa, Sakina akakumbushia tena lile swala la kwenda hospitali kuangalia kama imeshajulikana alipo Jeff, basi mama Sabrina akajiandaa tena ili yeye ndio aongozane na Sakina kwani kwake yeye ilikuwa rahisi kuliko kumuachia Sabrina afanye hivyo.
Walipomaliza walitoka na kuanza kuelekea kule hospitali alipolazwa Jeff.
Nyumbani kwakina Emmy bado hawakujua mahali Emmy alipo hivyo basi wakaona ni vyema kwenda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi, na washtakiwa ilikuwa Sam na Francis kwani wao ndio waliohisiwa kuondoka na Emmy.
Ilikuwa ni machungu na majonzi zaidi kwao ukizingatia walipanga siku hiyo ndio iwe siku ya mazishi.
Walipotoka kituo cha polisi kushtaki, ikabidi warudi nyumbani na kujadiliana kama familia ili kujua hitimisho ya mipango yao ya mazishi kwa siku hii,
"Sasa itakuwaje jamani! Je tutazika bila kuwepo kwa Emmy?"
"Emmy alivyokuwepo ilikuwa ni vizuri zaidi ila kumbukeni Emmy hakuonekana hapa kwa muda gani na bado tukapanga leo kuwa siku ya mazishi. Sidhani kama ni jambo jema kuendelea kumkalisha marehemu wakati tulishapanga siku ya mazishi kuwa ni leo. Kwahiyo naona vyema tukiendelea na taratibu zetu za mazishi kisha baada ya hapo tuendelee na swala la kumtafuta Emmy. Sijui mnalionaje swala langu!"
Asilimia kubwa ya ndugu wa Emmy wakakubaliana na hili swala kwahiyo taratibu za mazishi zikaendelea huku wengine wakipangwa kwenda kuchukua mwili wa marehemu hospitali ili wapeleke kwenye makaburi kwaajili ya ibada na mazishi.
Waliopangwa kwenda hospitali wakajiandaa kufanya hivyo na wengine kuendelea na taratibu za pale nyumbani kwao.
Mama Sabrina na Sakina walifika hospitali huku wakitumaini kuwa Jeff kasharudishwa pale kitandani, wakaenda moja kwa moja kwenye ile wodi ila pale kitandani bado hapakuwa na mtu, ikabidi waende tena kwa daktari ili waweze kujua hatma ya mgonjwa wao ila bado daktari nae alikuwa na majibu ya kujiuma uma tu kwani kiukweli hakuelewa kabisa alipo huyo mgonjwa ukizingatia hata katokaje tokaje ilikuwa ngumu kuelezea.
Sakina alikuwa amepaniki kwakweli ukizingatia Jeff ndio mtoto wake wa pekee,
"Kwakweli daktari leo hatuwaelewi jamani, mgonjwa anapoteaje kwenye mikono yenu? Mie siwaelewi yani siwaelewi kabisa na leo siondoki hadi nijue alipo mwanangu. Kama amekufa niambieni kuliko hivi jamani, yani mwanangu amepotelea hospitali! Haiwezekani kwakweli"
Ikabidi daktari awapooze kidogo na kuwaambia wakasubirie pale mapokezi kwa lengo la uchunguzi zaidi.
"Uchunguzi gani huo toka jana? Maana mlituambia hivi hivi inamaana hamkufanya huo uchunguzi wenu au mnanifanyia makusudi tu kuhusu mwanangu! Inaniuma sana jamani, inaniuma kwakweli"
"Tunaelewa mama ila lawama hazitasaidia, inatakiwa mtulie jamani ili na sisi tujue cha kufanya"
Ikabidi mama Sabrina amtulize Sakina kwavile tayari alishaonekana kupaniki kupita maelezo ya kawaida kwahiyo ikabidi yeye ndio amtulize kisha wakaenda mapokezi na kukaa huku Sakina akionekana kunung'unika na kulalamika muda wote,
"Usipaniki sana Sakina, mimi naimani tutajua tu alipo Jeff yani tutampata tu hata usikate tamaa Sakina"
Mama Sabrina alifanya kazi ya kumbembeleza tu Sakina mahali pale.
Wakiwa pale hospitali kwenye mida ya mchana hivi wakaona kuna watu wamefika kama watano hivi na kuwapita pale ila kuna mmoja wapo aliangaliwa sana na mama Sabrina ambapo huyu mama akamshtua Sakina na kumwambia,
"Umemuona yule mdada kati ya waliopita alivyofanana na Emmy!"
"Ndio hata mi nimemuona nikataka nikushtue, yawezekana ni ndugu yake au ndio yale ya duniani wawili wawili"
"Yani asingekuwa mnene na asingekuwa na kiremba kile kichwani ningesema ni Emmy duh wamefanana sana ila nina hisi kuwa huenda ni ndugu wa Emmy"
"Ngoja wakirudi tena tujaribu kumsimamisha na kumuuliza"
Wakakubaliana hivyo kuwa wale watu watakavyokuwa wanarudi basi wamsimamishe yule dada na kumuuliza.
Muda kidogo wakamuona mmoja kati ya wale watu akipita pale mapokezi na kuelekea kwa daktari kisha akatoka na daktari huku wakiongozana kwa kubishana.
Ikafanya mama Sabrina na Sakina kutazamana na kuulizana,
"Au na wenyewe hawajamuona mgonjwa wao?"
"Inawezekana maana hii hospitali nayo haiaminiki kabisa hata nashangaa ile hospitali ya mwanzo tuliyompeleka Jeff kutuhamishia huku na kusema kuwa huku ndio hospitali bora wakati wagonjwa wanapotea kwenye mazingira ya kutatanisha"
Walikuwa wakiilalamikia hii hospitali tu na kusahau kuwa hata hospitali walizolazwa Sabrina na Sam nao walipotea kwenye mazingira ya kutatanisha.
Walisubiri pale kwani waliamini kuwa muda kidogo watasikia zogo kutoka kwa wale watu walioingia mahali pale.
Na kweli kama mategemeo yao yalivyokuwa, kuna baadhi ya watu kama wawili kati ya waliokuja walitoka kule na kwenda kukaa kwenye zile benchi za pale mapokezi huku mmoja akionekana kulia na mwingine akimbembeleza, aliyeonekana kulia ni yule mdada mnene waliyemfananisha na Emmy.
Mama Sabrina na Sakina wakatazamana tena kisha Sakina akamwambia mama Sabrina,
"Si unaona wamemkosa ndugu yao hao yani hata mimi hapa nimekaa kimya sababu ya ujasiri tu kwani ilitakiwa nilie kama hivyo"
"Hata ukilia haitasaidia Sakina, cha muhimu tusubiri tu jibu lao la mwisho kwetu"
Ingawa walikuwa wanaendelea na maongezi mengine ila bado walitamani kujua zaidi kuhusu wale watu.
Ile hali ya kutamani kujua zaidi ikawafanya wasogee karibu na wale watu na kujaribu kuuliza amcpo yule mwingine aliyekuwa akimbembeleza mwenzie ndio aliyewajibu,
"Tumepatwa na matatizo jamani kwakweli ni huzuni"
"Matatizo gani tena? Maana hata sisi tuko hapa sababu ya kupotelewa na mgonjwa wetu huko wodini yani hata hatuelewi alipo mpaka sasa, ila tulivyowaona tukahisi kama yanaendana na sisi"
"Kwani ndugu yenu kapoteaje?"
Sakina akawaeleza kwa kifupi juu ya upotevu wa mgonjwa wao na kuwafanya na wao kufunguka kuhusu yaliyowasibu
"Jamani, kwa upande wetu sisi ni hivi; tumefiwa wenzenu na mama yetu, huyu anayelia hapa ni mwanae na mimi huyu marehemu ni mtoto wa dada yake, kwakweli inauma sana kwani alikufa gafla sana, tukamkimbiza huku hospitali na wakatuthibitishia kuwa amekufa na wakampeleka monchwari pamoja na sisi tulienda nao. Tumerudi nyumbani huko na kupanga habari za mazishi yani leo ikawa ndio siku ya mazishi kwahiyo tumekuja kumuandaa marehemu na kumchukua kwaajili ya mazishi ila cha kushangaza kule machwari hayupo yani maiti ya mama haipo kwakweli hata hatuelewi imekuwaje na imeenda wapi ikiwa sisi ndio wahusika? Na kama kuna watu wamechukua maiti yetu kwanini hata hospitali hawajui lolote jamani!"
Sakina na mama Sabrina wakashangaa na kuona kuwa hii hospitali inamaajabu zaidi kwani jambo la kupotea kwa maiti liliwastaajabisha zaidi ya kawaida.
Muda huu huyu dada aliyekuwa analia akainua kichwa kidogo na kulia kwa kuongea sasa,
"Jamani mdogo wangu nae jamani sijui yuko wapi ajishuhudie haya yanayotendeka jamani, maisha gani haya? Mitihani gani hii imetukumba sisi? Uko wapi Emmy jamani! Uko wapi mdogo wangu Emmy?"
Sakina na mama Sabrina wakaangaliana tena baada ya kusikia jina la Emmy, na kuwafanya wawe makini zaidi kwenye kusikiliza na kuuliza,
"Samahani, ni Emmy yupi huyo mnayemtaja?"
Huyu ndugu aliyekuwa akimbembeleza dada wa Emmy akawaelezea kuhusu Emmy aliyekuwa akiongelewa na jinsi alivyopotea kwenye mazingira ya kutatanisha,
"Jana alikuja na wakaka wawili ambapo mmoja alijitambulisha kwa jina la Sam na mwingine Francis, kwavile Emmy alizimia kwahiyo wale vijana badae wakasema kuwa wanataka kumuaga na walipoingia kumuaga ndio hatuelewi yuko wapi hadi sasa"
Ndipo Sakina na mama Sabrina kujibu kwa haraka kuwa wanawafahamu hao watu bila ya kujua kuwa wanazaa tatizo juu ya tatizo.
Huyu ndugu mmoja akainuka kidogo pale na kuwaacha wakiwa wamekaa na yule dada wa Emmy.
Muda kidogo yule dada akarudi akiwa ameambatana na ndugu wengine ambao waliomba kwenda kuzungumza na Sakina pamoja na mama Sabrina,
"Ila jamani itakuwa vyema kama tukienda kuzungumzia kwenye gari"
Hawakupinga hilo na kuondoka nao hadi kwenye gari.
Ila hapakuwa na mazungumzo yoyote bali gari ilianza kuendeshwa hata wao wakashangaa na kufanya waulize,
"Vipi tena jamani?"
"Tulieni tu"
Wakatazamana huku wakikosa jibu kabisa, ile gari ilienda mpaka kituo cha polisi ambapo waliitiwa askari na wakaamriwa kushuka ambapo waliingia kituoni hapo na kuambiwa kuwa wataisaidia polisi ili kuwapata Sam na Francis.
Kwakweli ilikuwa ni mtihani mwingine kwa upande wa Sakina na mama Sabrina,
"Jamani sisi mnatuonea tu, haya kapotea huyo Emmy mmetukamata sisi je na hiyo maiti iliyopotea mtamkamata nani? Au kwavile wengine hatuna uwezo wa kujieleza jamani! Yani mmeacha hata kushughulikia pale hospitali kuhusu marehemu wenu eti mnapata nguvu kutukamata watu tuliosema tunawafahamu tu! Huu ni uonevu kwakweli"
Hakuna aliyewasikiliza kwa makini, wakaandikishwa maelezo kisha kuruhusiwa kuondoka ambapo waliamua kurudi nyumbani tu kwani ilikuwa ni ngumu kwao kurudi tena hospitali.
Walipokuwa njiani kurudi nyumbani, kuna gari ilifika na kusimama mbele yao kisha ikawapigia honi na kuona wazi kuwa ni mtu anayewafahamu, ikabidi wasogee pale iliposimama ile gari ambapo mlango wa mbele ulifunguliwa.
Walishtuka sana kuona anayeendesha ile gari kuwa ni Jeff.
Walipokuwa njiani kurudi nyumbani, kuna gari ilifika na kusimama mbele yao kisha ikawapigia honi na kuona wazi kuwa ni mtu anayewafahamu, ikabidi wasogee pale iliposimama ile gari ambapo mlango wa mbele ulifunguliwa.
Walishtuka sana kuona anayeendesha ile gari kuwa ni Jeff.
Kwakweli Sakina na mama Sabrina walishikwa na uoga na kujikuta hawawezi hata kusogea mbele wala kurudi nyuma yani ilikuwa kama wameganda vile. Ila Jeff mwenyewe alikuwa kawaida kabisa na kuwaambia,
"Pandeni twende"
Hakuna aliyeweza kunyanyua mguu wake kuwa apande kwenye ile gari ila kati yao ni mama Sabrina tu aliyepata ujasiri na kumwambia Jeff kuwa aende tu,
"We nenda, sie tunakuja wenyewe"
Jeff nae hakuonekana kuwalazimisha kwani alifunga mlango wa ile gari na kuondoka zake.
Sakina na mama Sabrina walicki wakitazamana, kisha Sakina akamuuliza mama Sabrina,
"Hivi ni kweli au ndoto?"
"Kwakweli mimi ndio nimechanganyikiwa kabisa yani hata sielewi, sielewi kitu chochote. Ni mambo gani haya jamani? Mbona maajabu!! Hebu turudi nyumbani kwanza labda wenzetu watatusaidia kimawazo."
Wakaamua kuendelea na safari yao ya kurudi nyumbani huku wakiwa na mawazo yasiyo na mwisho.
Walifika nyumbani na ilikuwa jioni tayari imeingia, waliwakuta waliowaacha pale nyumbani na kuanza kuwasimulia yaliyowakuta huko hospitali,
"Kwahiyo inamaana mama yake Emmy amekufa?"
"Ndio hivyo, eti na Emmy amepotea ndio tumeanza kushikiliwa sisi jamani hadi kituo cha polisi si maajabu haya mmh kisa tu tunamfahamu Sam na Francis. Ila njiani tumepatwa na maajabu mengine"
"Yapi hayo?"
Wakaanza kuelezea jinsi walivyokutana na Jeff, kwakweli hata Sabrina alishangaa hii hali.
"Kheee hayo makubwa jamani, hata kama huyo mliyekutana nae ni Jeff, swali langu ni kuwa hilo gari kalitoa wapi au katoka nalo wapi?"
"Hapo hata sisi wenyewe tumekosa jibu yani hadi hapa bado sijielewi maana haya mambo mengine ni kama ndoto jamani yani najiona kama nipo ndotoni"
Mama mdogo wa Sam alikuwa kimya ila naye aliamua kuongea,
"Jamani, hata mimi nimekutana na vituko vingi sana katika maisha yangu ili hivi vya hii familia vimenishinda kwakweli. Ni mambo gani haya? Sielewi, huwa natamani nirudi zangu Arusha ila najua naweza acha mambo makubwa zaidi huku nyuma, jamani haya maisha ya huu mji kwakweli nimeshindwa kuyaelewa. Mungu atusaidie tu"
Mama Sabrina aliamua kujitetea,
"Ila dada, tulikuwa tunaishi salama kabisa yani haya majanga yameletwa na huyu Sam"
Sabrina nae akaongezea,
"Mama usingenishawishi kuolewa na Sam basi yote haya yasingetukuta"
"Sio nisingekushawishi kuolewa na Sam, sema usingefanya majanga yaliyofanya tukimbilie Arusha basi tusingeonana na Sam na yote haya yasingetukuta"
"Ila sio muda wa kulaumiana jamani, mambo yametokea basi tujue jinsi ya kukabiliana nayo. Majuto ni mjukuu"
"Ni kweli dada majuto ni mjukuu ila chanzo cha yote ni huyu mtoto (huku akimnyooshea kidole Sabrina) huyu mtoto katusumbua dada, na yote hayo ni mapenzi alichanganya wanaume huko mwisho wa siku zinaletwa kesi hadi alipelekwa rumande huyo usimuone hivyo, mapenzi ndio yamesababisha yote haya yani hata sijui alikuwa na moyo gani wa kupenda penda"
Sabrina akanuna kwa hizi kauli za mama yake na kumfanya ainuke akielekea chumbani kwake huku mama mdogo wa Sam akiendelea kumshauri mama Sabrina kuwa sio wakati wa kulaumiana.
Sabrina alienda chumbani kwake na kujilaza kitandani, akajiwa na mawazo mengi sana ya maisha yake ya nyuma yaliyomfanya akumbuke toka siku ya kwanza anakutana na Francis ambaye alikuwa ni mwanaume wa kwanza yeye kumpenda, akakumbuka pia alipompindua Francis kutokana na tabia yake na kuamua kuwa na nduguye Fredy. Akajisikitikia kidogo na kujiona hapo ni kweli alikuwa na makosa ila je kosa lake ni nini wakati walimpenda wenyewe? Na wote walionyesha kuwa wanampenda kweli, akakumbuka hadi siku aliyokutana na John na kuamua kumpindua kwa kutoka na Japhet aliyekuwa rafiki yake na ni kaka wa Sia, mwisho wa siku huyu Japhet ndiye aliyemsababishia matatizo.
Kwakweli Sabrina alijikuta akikumbuka vingi sana kwa wakati mmoja. Kisha akasema,
"Ningeweza kurudisha siku nyuma basi ningeyafuta yale yote yaliyotokea kwenye maisha yangu, ila chanzo cha yote walinipenda wenyewe na je kwanini walikuwa wananipenda halafu wananiumiza kiasi cha mimi kumfikiria mwingine? Ila yote ni kwavile sikujua kuwa wangu alikuwa hajakua vizuri ilipaswa nimsubiri, Jeff ndiye mtu sahihi kwangu"
Akatulia tena, katika mawazo yake akakumbuka maelezo aliyopewa na Sam juu ya jini linalofatilia maisha yake, kwa hapo akaogopa kiasi kisha akainuka na kwenda dirishani ambapo alifunua pazia na kuchungulia nje, gafla akaona mtu kwa nje akimfanyia ishara kama ya kumuita ila Sabrina hakumtambua mtu huyo, akarudishia pazia kisha akatoka chumbani kwake na kutaka kutoka nje ila mama mdogo wa Sam akamshtua kwa kumuuliza,
"Unaenda wapi Sabrina?"
"Naenda hapo nje mara moja"
"Unaenda kufanya nini?"
Sakina alimshangaa huyu mama kumuuliza Sabrina maswali kama mtoto mdogo vile. Ila Sabrina alijibu tu,
"Kuna mtu kaniita"
"Unamjua?"
"Hapana simjui"
Sakina akaamua kuongea,
"Ila jamani, huyu Sabrina ni mtu mzima na anaelewa anachokifanya, hayo maswali sasa mmh kama Cherry vile anavyoulizwa"
Mama mdogo wa Sam hakujali hoja za Sakina kwani anamjua kuwa ni mtu wa kupinga hata vitu vya ukweli, kwahiyo mama huyu aliendelea kumuongelesha Sabrina,
"Subiri twende wote"
Mama mdogo wa Sam akainuka na kumfata Sabrina pale mlangoni kisha wakatoka wote nje na kuzunguka nyuma ambako Sabrina alisema kuwa huyo mtu aliyemuita yupo ila cha kushangaza hakuonekana mtu yeyote yule yani kwa kifupi hapakuwa na chochote kinachoonyesha uwepo wa mtu eneo hilo.
"Haya, huyo mtu yuko wapi?"
"Hata mi mwenyewe nashangaa simuoni"
"Sabrina, tupo kwenye mapambano sasa kwahiyo usikubali chochote kivuruge akili yako, hata siku nyingine kabla hujafanya jambo jiulize kwanza. Huyu mtu kwanini akuitie huku nyuma? Je ameshindwa kuzunguka na kugonga mlango ili akuulizie? Tunatakiwa kuwa makini sasa ili tusiumie na tusiteseke bila mpango wowote. Tusitafute matatizo ya kujitakia, najua tusingetoka wote huenda ungepatwa na matatizo maana bado hujasimama vizuri katika maombi, kuwa makini Sabrina"
Kisha wakaanza kurudi ndani, ila wakati wanazunguka Sabrina akasikia kama sauti ikimuita kwa jina lake, kisha akamwambia mama mdogo wa Sam,
"Mbona nasikia kama mtu akiniita kwa jina?"
"Ikatae hiyo sauti tena uikatae kabisa kabisa, twende ndani na tuombe kwaajili ya hili"
Sabrina hakupingana na huyu mama, ambapo wakarudi ndani kwa lengo la kufanya maombi sasa.
Kwa upande wa ndugu wa Emmy walirudi nyumbani na kuhairisha mazishi kwa siku hiyo kwani hadi jioni inafika haikujulikana hiyo maiti iko wapi kwani hata hospitali nako walikuwa hawajui kilichotokea.
Kikao cha familia kikawekwa ili kujua kuwa endapo hiyo maiti isipopatikana hadi kesho yake wafanye nini,
"Na kweli jamani inapaswa tufikirie kuhusu hilo swala maana watu wamekusanyika hapa wakingoja mazishi tunatakiwa kujua kabisa tutakachofanya"
"Jamani mimi naona ni vyema tukawaambia watu ukweli, na pengine tuahirishe mazishi mpaka pale marehemu atakapopatikana"
"Na asipopatikana je?"
"Itabidi tuzike mgomba jamani maana itakuwa tumejiwekea uchuro wenyewe"
"Na kwanini asipatikane jamani?"
"Huenda kuna watu wamechanganya maiti ya ndugu yao"
"Hilo haliwezekani jamani yani haiwezekani kabisa, pale hospitali wenyewe wanashangaa ukizingatia kile chumba kilikuwa na maiti nne tu, zingine zote zipo kasoro ya kwetu kwanini?"
Moja kwa moja wengine wakaingiza maswala ya ushirikina kwani haikuwa kitu rahisi vile kusema tu kuwa maiti imepotea tena kwenye mazingira yasiyoeleweka.
Wakakubaliana kuwaambia watu ukweli wa mambo ili kila mmoja aelewe kuwa kwanini ratiba ya mazishi imehairishwa kwa siku hiyo.
Kwakweli kwa upande wa majirani nao kila mmoja aliongea lake huku wengine wakiwashauri wale ndugu kuwa waende kwa mganga wa kienyeji.
Wakiwa ndani wakina Sakina, muda huu Sakina aliamua kumkumbusha mama Sabrina kuhusu Jeff kisha wakajipa ujasiri wa kwenda kumuangalia nyumbani kwani Sakina alikuwa na uoga wa kutembea peke yake ingawa muda mfupi uliopita alimsema Sabrina kuwa ni mtu mzima na anaelewa anachofanya ila kwa upande wake yeye alikuwa na uoga wa kutosha kabisa.
Mama Sabrina akainuka na kutoka na Sakina wakielekea huko nyumbani kwa Sakina ambapo walifika na kugonga mlango halafu Keti aliwafungulia na kuwakaribisha.
Swali la kwanza toka kwa Sakina kwenda kwa Keti ilikuwa,
"Hivi huogopi unavyobaki peke yako?"
"Niogope nini mama?"
"Kwahiyo wewe unaona kawaida tu kuwa mwenyewe wala huoni tatizo lolote?"
"Ndio, mi naona kawaida tu kwani kazi yangu huwa inafanya mara nyingi sana niachwe mwenyewe ndani kwahiyo huwa siogopi chochote"
"Duh! Wewe ni jasiri sana, hongera kwa hilo"
Keti akatabasamu tu, kisha wakamuuliza tena
"Je, Jeff amekuja huku?"
"Ndio alikuja"
Wakatazamana na kusema kwa pamoja,
"Kumbe ni kweli alikuwa ni yeye!"
Kisha wakamuuliza tena Keti,
"Amefanya nini alipokuja na ameenda wapi?"
"Alikuja hapa akagonga nikamfungulia na akanisalimia kisha akaelekea chumbani kwake, kwakweli huko ndio sielewi alienda kufanya nini ila muda kidogo alitoka na kuondoka ila hajasema kuwa anaenda wapi"
"Kheee, hajasema kuwa amekutana na sisi?"
"Hapana hajasema"
"Eeh alivaaje?"
Keti akawaeleza alivyokuwa amevaa ambapo ilikuwa ni nguo zile zile ambazo walimuona nazo.
Sasa Sakina na mama Sabrina wakakaa kwani walikuwa wameshapata uhakika kuwa yule waliyekutana nae ni kweli alikuwa Jeff ila je ni kitu gani kimempata na je imekuwaje kuwaje bado hawakuelewa kuhusu hilo kabisa.
Giza nalo lilikuwa limeshaingia na kufanya mama Sabrina ahitaji kurudi nyumbani kwake,
"Ila mama sidhani kama ni vyema kuwa urudi huko kwani, mi nadhani leo tungelala wote hapa hapa si unajua usiku ulivyombaya halafu na giza hili mmh!"
Sakina aliamua kuongea maneno ya kumtisha kidogo mama Sabrina huku akijaribu kumuwekea stori zingine ili asiondoke.
"Hivi kwanza umejaribu kujifikiria kuwa huyo Emmy atakuwa wapi?"
"Sio Emmy tu, vipi kuhusu huyo Francis na Sam? Haya mambo mmh sijui hata watakuwa wapi na kwanini wamekuwa kimya kiasi hiki!"
"Yani bora mchana mama maana usiku ni majanga zaidi"
Mama Sabrina nae akashikwa na mashaka ya kutembea kwa muda huo na kuona ni vyema tu walale hapo.
Wakina Sabrina walipoona muda unaenda bila ya wale kurudi wakajua tu lazima wameamua kulala huko huko, Sabrina nae akaamua amkumbushe kitu mama mdogo wa Sam,
"Na hivi wamekutana wote waoga, hawawezi kurudi na giza hili"
Mama mdogo wa Sam akacheka na kumuuliza Sabrina,
"Je wewe ungeweza?"
"Zamani ningeweza ila kwa kipindi hiki, thubutu yangu hunitembezi usiku hata kwa bakora"
Muda kidogo wakasikia mlango wa pale sebleni ukigongwa na kumfanya Sabrina ashtuke sana kwa uoga,
"Kheee kweli wee Sabrina nae muoga, ndio kushtuka kiasi hiko mmh!"
Mama mdogo wa Sam akainuka na kwenda kufungua, akamkaribisha ndani alikuwa ni baba Sabrina ambapo Sabrina nae alipomuona alimkaribisha kwa furaha, kisha huyu mzee akawauliza
"Siku hizi hamfungi lile geti la pale nje?"
"Ni mama katoka tukajua hatokawia kurudi ndiomana hatukufunga"
Sabrina alijitetea hivyo wakati ilikuwa ni kawaida yao kutokufunga kwa kipindi hicho.
Ikabidi aeleze alipokwenda mama yake kwani aliulizwa pia.
Deo alipojiridhisha na majibu ikabidi awaage na kwenda kumfata mke wake kwani alijua wazi kuwa yeye ndiye wa kumuandalia anachohitaji kwa muda huo kama ni chakula au maji ya kuoga.
Kwa upande wa nyumbani kwa Sakina waliposikia hodi walishtuka sana na aliyekuwa na ujasiri wa kwenda kufungua alikuwa ni Keti tu ambaye alifungua na kumkaribisha baba Sabrina ndani.
Aliingia na kusalimia kisha kuongea mawili matatu na kuomba kuondoka na mama Sabrina ila Sakina aliwaomba wamsubiri ili waondoke wote.
Sakina aliamua kwenda chumbani kwake ili angalau akachukue nguo za kubadilisha, ila alipoingia chumbani alishtuka sana na kuanza kupiga kelele.
Kwa upande wa nyumbani kwa Sakina waliposikia hodi walishtuka sana na aliyekuwa na ujasiri wa kwenda kufungua alikuwa ni Keti tu ambaye alifungua na kumkaribisha baba Sabrina ndani.
Aliingia na kusalimia kisha kuongea mawili matatu na kuomba kuondoka na mama Sabrina ila Sakina aliwaomba wamsubiri ili waondoke wote.
Sakina aliamua kwenda chumbani kwake ili angalau akachukue nguo za kubadilisha, ila alipoingia chumbani alishtuka sana na kuanza kupiga kelele.
Zile kelele za Sakina ziliwafanya wale waliokuwa sebleni nao washtuke sana na kufanya wakimbilie alipokuwa ila walimkuta ametoka kwenye korido huku akihema sana, wakataka kwenda kuingia ili kujua kuna nini ila Sakina aliwazuia na kuwaomba kabisa kuwa wasiingie humo chumbani.
Alikuwa akihemea juu juu na kuwaomba sana wasiingie,
"Tafadharini sana tuondokeni, msiingie humo kabisa"
"Kwani kuna nini?"
"Naogopa kusema ila kwa usalama wenu msiingie humo"
Wakatazamana ila bado Sakina alisisitiza kauli yake kuwa wasiingie mule chumbani, ikabidi wamsikilize na kukongojana nae hadi sebleni ambapo aliwaambia kuwa waondoke.
Mama Sabrina akamuuliza,
"Vipi unaenda bila hizo khanga tena?"
"Haiwezekani kwenda kuchukua khanga mule, bora tuondokeni tu"
"Kwani kuna kitu gani cha tofauti?"
"Siwezi kusema ila hapa ni hapana kabisa, twendeni"
Keti akaamua nae aulize kwani alikuwa anamsikia tu Sakina akisema hapo si salama je vipi usalama wake yeye anayebaki hapo ndani,
"Jamani vipi kuhusu mimi? Naulizia usalama wangu mimi kwani mkumbuke kuwa mnaniacha hapa peke yangu!"
Baba Sabrina nae akachangia kuhusu hilo,
"Na kweli jamani, tunamuachaje mtu wakati inaonyesha kuna matatizo humu ndani!"
"Ni kweli kuna matatizo ila huyu Keti si muoga na ndiomana ameweza kuishi siku zote humu ndani peke yake bila kuhofia chochote labda tu cha kumuonya ni kuwa asiingie chumbani kwangu"
Keti alitulia tu kimya huku akisikilizia kama kuna yeyote wa kumsaidia kwa hilo ila tu baba Sabrina akasema,
"Kama ni kawaida kwenu basi sawa, sina la ziada na tunaweza kwenda."
Kwakweli Keti walimuacha hapa huku hofu kubwa ikiwa imemtanda moyoni mwake kwani uoga ulimjaa na ukizingatia hakujua kinachoendelea humo chumbani kwa Sakina.
Waliondoka huku wakiambizana mambo mbali mbali njiani ila kabla hawajafika mbali wakapishana na mtu ambaye ilikuwa kama wanamfahamu ila alikuwa kwenye muonekano wa ajabu sana.
Aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Sakina,
"Jamani, sio Emmy huyu tuliyepishana nae?"
"Kama yeye ila mbona yupo kama kichaa?"
Baba Sabrina akaona hawa wataanza na mada zingine hivyo akaamua kuwakatisha yale mazungumzo ili watembee kwa amani,
"Yani nyie wanawake mkitoka hili mnaingia lile, mwisho wa siku mtachanganyikiwa bure nashindwa hata kuwaelewa. Hebu tutembee kwa amani. Mpo njiani mnaogopa je mwenzenu mliyemuacha nyumbani peke yake je afanyeje? Hebu twendeni"
Wakafika kwakina Sabrina na kuingia ndani ambapo walimkuta Sabrina akiwa na yule mama mdogo wa Sam kwenye maombi, nao wakajiunga pamoja hadi walipomaliza ambapo kule kumaliza tu, mama mdogo wa Sam akamuuliza Sakina,
"Umeona nini?"
Sakina akaogopa kiasi na kutetemeka halafu akashindwa kujibu, ambapo mama mdogo wa Sam akamwambia tena,
"Sakina usiogope tupo kwaajili ya kusaidiana na ndiomana nakuuliza umeona nini?"
Sakina nae akauliza kama vile haelewi anachoulizwa,
"Kuona nini wapi?"
"Huko nyumbani kwako, kule chumbani kwako umeona nini!"
Hapa sasa pakamfanya Sakina amshangae zaidi mama mdogo wa Sam kwani lile swali ilikuwa kamavile alimuona alivyokuwa akipiga kelele kule nyumbani kwake.
Sakina alikaa kimya kwa muda bila ya kujibu chochote tena na kumfanya mama mdogo wa Sam kumuuliza tena,
"Umeona nini chumbani kwako?"
Sakina akajiminya minya mikono huku kisha akasema,
"Naogopa kusema"
"Usiogope Sakina, sema ukweli ili uwe huru, halafu ukweli wako utawaokoa wengine"
"Nimeona vitu vya ajabu sana"
"Vinini vitaje!"
"Maiti"
Wengine wakashtuka sana ila Sakina aliposema hivyo tu alianguka na kuanza kuweweseka.
Wakina Sabrina wakataka wamuinue pale chini ila mama mdogo wa Sam aliwaambia wamuache tu na atakuwa salama.
Kwa muda huo karibia wengine wote walishikwa kwa uoga kiasi haswaa mama Sabrina kwani aliogopa hata kwenda chumbani kwake peke yake kwa uoga aliokuwa nao.
Baada ya muda kidogo mama mdogo wa Sam akawaambia kuwa wanaweza kwenda kulala,
"Na huyu Sakina hapo chini je?"
"Msijali atakuwa salama, ni dhana mbaya waliyompandikiza ndio inatoka na kama asingesema kweli basi leo asingeweza kulala ila Mungu ni mwema sana ndiomana amenishuhudia jambo hili"
Baba Sabrina ingawa alikuwa hajamfahamu sana huyu mwanamke ila aliweza kugundua kuwa ni jinsi gani alikuwa na imani.
Kisha baba Sabrina akainuka na kuwa wa kwanza kuelekea chumbani kwani wengine walionekana kujawa na uoga.
Ni hapo ambapo mama Sabrina nae akapata ujasiri wa kunyanyuka na kuelekea chumbani alipo mume wake.
Pale sebleni walibaki wale wale ambapo mama mdogo wa Sam akamwambia Sabrina kuwa amemruhusu akalale,
"Aah mimi bado kwakweli"
"Kwahiyo unaogopa?"
"Hapana"
"Sasa tatizo ni nini wakati nimekuruhusu, nenda kalale na watoto huyu ataamka tu na wala hatofanya chochote kwavile na mie nitakuwepo hapa, msiwe na mashaka yoyote yale"
Sabrina nae akainuka na kuelekea chumbani walipokuwa watoto wake.
Sabrina alifika chumbani na kulala pembeni ya watoto wake huku akiwaza kuwa kwanini mama mdogo wa Sam abaki mwenyewe na Sakina pale sebleni? Akawaza kuwa lazima kuna namna kwani hakuona kuwa ni kitu cha kawaida ukizingatia jinsi alivyokuwa anawaambia kuhusu kulala.
"Mmh nina mashaka sana, au huyu mama anatudanganya kuwa ni mwanamaombi ila kumbe ni mshirikina? Maana kwanini abakie nae peke yake?"
Sabrina aliwaza bila ya kupata majibu huku akitamani kwenda kuchungulia ili aone kinachoendelea ila tu alihofia kuwa atachungulia mpaka saa ngapi.
Mawazo haya yalimfanya Sabrina achukue muda mrefu sana kupata usingizi, na muda kidogo akamsikia mama mdogo wa Sam akiomba ila kwa haraka haraka Sabrina akahisi kuwa huyu mama atakuwa anazuga,
"Na ukizingatia anajua kama nipo macho kwani anajifanya anaona kila kitu, lazima anazuga tu. Itabidi kesho nijadiliane na mama kuhusu hili swala kwani naona wazi tukipigwa changa la macho hapa"
Muda kidogo akapata usingizi na kulala ila alilala akiwa na mawazo haya haya.
Moja kwa moja akajiwa na ndoto kuwa mama mdogo wa Sam anatambika, akamuona kwenye ndoto akizunguka nyumba yao huku akifukia dawa kila pembe ya nyumba halafu akaona yupo na kundi kubwa la watu wakijadiliana hususani kuhusu familia yao wakina Sabrina.
Alikuja kushtuka huku jasho likimtoka sana na tayari ilikuwa pameshakucha na kukuta hata wanae wameshaamka, huku mwanae mkubwa akidai anataka kwenda kwa bibi yake huyo.
Moja kwa moja Sabrina akahisi kuwa huyu mama mdogo wa Sam alishafanya kitu kwa mwanae pia na ndiomana mwanae kila siku anamdai yeye,
"Huyu mama nina mashaka nae sana, usikute kashavuruga akili za watoto wangu na mwisho wa siku huyu mama kwa nimuonavyo anaweza akabeba wanangu na kwenda kutokomea nao huko Arusha, cha msingi niwe makini sana. Hebu nijiulize, kama huyu mama ni mtu wa maombi kweli mbona mambo ya ajabu bado yanatokea? Kwakweli hapa kuna namna tu, halafu anajifanya anaona kila kitu na kwanini anashindwa kuzuia? Na usikute hata hiyo maiti chumbani kwa Sakina ni yeye mwenyewe kaiweka"
Aliposema hilo neno la mwisho, uoga ukamshika kidogo na kumfanya aamke kabisa na kutoka kwenda sebleni.
Alipofika sebleni alimkuta mama yake, mama mdogo wa Sam pamoja na Sakina wakiwa wamekaa mahali pale wakiongea mawili matatu na kumfanya agundue kuwa Sakina alishazinduka.
Ila Sabrina alifika na kukaa bila ya kumsalimia yeyote kati yao ila watoto wake walienda moja kwa moja kwa mama mdogo wa Sam kamavile ishara ya kuwasalimia.
Mama Sabrina alimshangaa sana mwanae kuwa kwanini amefanya vile yani kwanini hajasalimia watu na kumfanya amuulize kwa mshangao,
"Kheee Sabrina, siku hizi ukiamka ndio husalimii mwanangu!"
"Kwani salamu ni lazima mama?"
"Khee umeamka na kisirani leo nini? Salamu ni lazima ndio, haya tuambie umeamkaje?"
Mama mdogo wa Sam akachangia,
"Sio ameamkaje tu, muulize ameotaje hadi ameamka akiwa amenuna? Na amewezaje kuota hivyo? Je alikuwa anawaza nini kabla?"
Haya maswali ya mama mdogo wa Sam yakamshtua Sabrina na kumfanya moja kwa moja aamini mawazo yake na ndoto zake, na ndio hapo aliporopoka,
"Wewe mmama kweli nimeamini wewe ni mchawi tena ni mchawi wa wachawi wewe, haiwezekani ukajua mawazo yangu na ndoto zangu. Vinakuhusu nini mpaka ujue?"
Mama Sabrina alimshangaa sana mwanae kwa yale maneno aliyokuwa akiyasema,
"Wee Sabrina wewe, hebu muogope Mungu na uache huo ujinga wako. Huyu mama angekuwa mchawi si angeshatudhuru mwanangu jamani!"
"Kheee mama nadhani huelewi ila humu ndani mimi ndio muelewa, wachawi ndio zao kujifanya watakatifu ili tuwakumbatie na mambo yao. Kama kweli huyu mama ni wa maombi muulize kwanini hana mtoto hadi leo nadhani Sam atakujibu kuhusu hili, huyu mama ni mchawi huyu. Ndiomana watoto wangu kutwa kucha wanamganda yeye kwa uchawi wake. "
Sakina nae akaingilia kati,
"Sabrina! Kweli unathubutu kusema hayo maneno dhidi ya huyu mama? Amakweli nimeamini tenda wema uende zako usingoje shukurani, kumbuka huyu mama ana mambo yake mengi sana ya kufanya huko Arusha ila hadi leo yuko hapa sababu yetu, hivi umeshawahi kujiuliza kuwa asingekuwepo huyu mama tungekuwa tunafanya nini? Hebu mara nyingine ujifikirie Sabrina, je umefanya mambo mangapi ya kijinga kwa hayo mawazo yako? Unakumbuka ulivyomsukuma mwanao mwenyewe hata leo unashangaa kuwa kwanini wanao wanampenda huyu mama? Hebu uwe na akili muda mwingine jamani"
"Jamani na nyie msinichanganye, kwa kifupi ni kuwa huyu mama hafai tena hafai kabisa ni mchawi wa kudumu. Endeleeni kufuga maradhi ila kifo kitawaumbua"
Mama mdogo wa Sam alikuwa akiwasikiliza tu, mama Sabrina alimuangalia mama huyu na kumuomba msamaha,
"Tusamehe sisi ndugu yetu"
"Wala msijali, tambueni ya kwamba hii hali wala haijanishtua kwani nilionyeshwa kabla. Kwenye maisha makwazo hayanabudi kutokea na kwenye maisha si kila uombacho lazima upokee kwa wakati uombao, Mungu anamakusudi yake na hutoa kitu kwa wakati wake. Kama ukiulizia maisha yangu ya nyuma na sasa ni vitu viwili tofauti ila nashukuru Mungu kwa kunipa moyo wa kupambana na changamoto za maisha"
Kabla hata hajamaliza vizuri maneno yake, Sabrina aliibuka na hoja
"Kwa kifupi yani sitaki kumuona huyu mama humu ndani bora aondoke yeye au niondoke mimi. Huyu mama ni mchawi na alikuwa anatambika kwenye nyumba yetu siku zote hizi ili atutoe kafara, jamani nimemshtukia huyu mama"
"Sabrina, nitaondoka ila jua kwamba wanapenda sana kukutumia wewe si akili zako hizo ila unatumiwa tu na ndiomana hata mimi inaniwia vigumu kufanya maamuzi ila hata mimi ni binadamu wa kawaida mwenye maumivu kama wengine. Nitaondoka tu"
"Ndio, bora uondoke"
Sakina akaongezea,
"Kuliko kuondoka ni bora uje kwangu kukaa kwa muda hadi haya mambo yatakapotulia"
Mama Sabrina nae alikuwa akimbembeleza kuwa aendelee kuwa hapo kwao,
"Usiondoke hapa jamani mambo yataharibika"
"Kwa hapa si rahisi sana ila tatizo ni kwa huyo binti yako kwani anaweza akafanya mambo yarudi kule yalipotoka."
Sakina akaona na yeye ndio kapata nafasi ya kumkaribisha huyu mama nyumbani kwake hivyo akaendelea na hoja ile ile ya kumshawishi aende nae angalau kwa siku hiyo tu.
"Nadhani haya yametokea ili niende huko kwako"
Sakina akafurahi ila mama Sabrina hakufurahia na kuuliza,
"Na hapa je?"
"Hapa nitarudi sababu ya hawa watoto ila naamini akili ya Sabrina nayo itakuwa sawa kwani wanaomtumia nawatambua na najua ni kwanini wamefanya hivyo. Kwani lengo lao kubwa ni moja tu, nikirudi nitawaambia"
Mama mdogo wa Sam akainuka na kumwambia Sakina kuwa yupo tayari kwenda nae huko kwake.
Mama Sabrina alimuangalia sana mwanae na kumuona kama mtu mwenye matatizo ya akili.
Wakati wakina Sakina wanatoka, huyu mama aliwabusu watoto wa Sabrina na kukaa nao kimya kama dakika tano kisha wakaaga na kutoka na Sakina. Sasa Sabrina alibaki na mama yake na kuanza kumsimulia ndoto aliyoota siku hiyo,
"Yani Sabrina mwanangu hadi leo bado unaamini hizo ndoto zako? Pole sana mwanangu ila kuna muda akili itakukaa sawa, huyu mama kanifundisha vitu vingi sana kwakweli anastahili pongezi kwani mimi kwa hasira zangu nisingekubali uongee vile wakati nipo kwaajili yenu. Jitafakari Sabrina, utapata jibu la hayo mawazo yako na ndoto zako finyu"
Mama Sabrina aliinuka na kwenda kuendelea na mambo mengine kwani mumewe alishatoka asubuhi sana.
Sasa Sabrina alibaki mwenyewe na kujiuliza kuwa kwanini hakuna anayemsapoti.
Mama mdogo wa Sam na Sakina walifika nyumbani kwa Sakina ila kadri mama huyu alipoisogelea nyumba ya Sakina akaelewa kwanini imemuwia vigumu sana yeye kufika mahali hapo.
Walifika na kugonga ila hakuna aliyefungua, ndipo Sakina alipojaribisha kufungua na kukuta mlango upo wazi na kuingia ndani.
Wakashangaa kumuona Keti akiwa chini huku povu likimtoka mdomoni kamavile mtu aliyekunywa sumu.
Mama mdogo wa Sam na Sakina walifika nyumbani kwa Sakina ila kadri mama huyu alipoisogelea nyumba ya Sakina akaelewa kwanini imemuwia vigumu sana yeye kufika mahali hapo.
Walifika na kugonga ila hakuna aliyefungua, ndipo Sakina alipojaribisha kufungua na kukuta mlango upo wazi na kuingia ndani.
Wakashangaa kumuona Keti akiwa chini huku povu likimtoka mdomoni kamavile mtu aliyekunywa sumu.
Sakina alishtuka zaidi na uoga ulimuingia juu ya mtoto wa watu na kumfanya akumbuke vile ambavyo jana alisema kuwa anamuachaje peke yake wakati amesema kuwa mule ndani pana matatizo.
Sakina alijikuta machozi ya uoga yakimtoka huku akisema,
"Nisamehe Keti jamani, nisamehe mimi sikujua kama ingekuwa hivi bora tungeondoka wote."
Alikuwa akilia huku akitaka kumsogelea Keti pale chini ili hata angalau amshike ila mama mdogo wa Sam akamrudisha nyuma na kumkataza kumshika.
Sakina akanyamaza kwanza na kumuangalia huyu mama kisha akamuuliza kuwa kwanini amemkataza.
Mama mdogo wa Sam hakujibu ila alimvuta Sakina na kukaa nae kwenye kochi kisha akamwambia,
"Nyumba yako ndio kituo chao kwasasa, yatupasa kuomba sana"
Neno lile la nyumba yake kuwa ndio kituo lilimpa uoga sana Sakina hata mama mdogo wa Sam akatambua hilo na kujaribu kumpa maneno ya kuondoa uoga ili waweze kuwa kwenye maombi.
"Usitetemeke sana Sakina, inatakiwa tuombe kwani sina imani juu ya hiko kiumbe hapo kama ni mtu"
Akimaanisha yule Keti pale chini, kwasasa Sakina akamshangaa tu kwani yeye alikuwa anaumia kuona Keti yupo kwenye hali ile wakati mama huyu alisema kuwa hana imani kama kile kiumbe ni mtu.
Huyu mama kabla ya maombi yoyote yale alianza kwa kuimba imba ambapo Sakina alikuwa akimfatisha tu ila huku moyoni alikuwa na hali ya uoga balaa.
Nyumbani kwakina Sabrina, muda huu Sabrina alibaki mwenyewe akitafakari maneno aliyomwambia mama mdogo wa Sam, kwa upande mwingine alijiona kuwa amefanya sawa ila kwa upande mwingine alijiona ni mkosaji.
Aliwaza sana, akaona ni vyema hata akatoka nje ili aweze kupunga kidogo upepo na kumfanya atafakari zaidi.
Alitoka kabisa nje ya nyumba yao na kuangalia baadhi ya wapita njia ila pale kwao hapakuwa njia inayotumiwa na watu wengi kwahiyo wapita njia walikuwa wachache sana.
Muda kidogo kupita, akamuona mtu kama Jeff na kumfanya ashtuke kisha akajaribu kumuita,
"Jeff, Jeff, Jeff"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila huyu mtu hakugeuka nyuma, Sabrina akahisi kuwa huenda ameamua kuuchuna tu, hivyo akainuka na kumkimbilia kwa nyuma.
Alipomkaribia akamshika bega ambapo mtu yule aligeuka nyuma.
Sabrina akashtuka sana na kugeuka pia huku akikimbia kwani mtu yule hakuwa Jeff ila alikuwa ni mtu mwenye sura ya ajabu sana kwani sura yake haikufanana na binadamu yeyote yule.
Sabrina alikimbilia kwao ila kabla hajaingia getini alimkuta mtu yule akiwa amesimama pembeni mwa geti lao, Sabrina akazubaa kwa uoga huyu mtu akamnasa Sabrina kibao kilichompeleka hadi chini ila na yeye akakumbuka maneno ya kusema kama kuomba msaada kwa Mungu, akajikuta akiomba Mungu amsaidie.
Gafla kidogo yule mtu akapotea, Sabrina aliinuka pale chini na kuingia ndani kwao huku amejishika shavu kwani kibao alichopigwa ilikuwa si kibao cha kawaida.
Mama yake akamuona pale ndani na kumuuliza,
"Vipi tena Sabrina umepatwa na nini?"
Sabrina alimjibu mama yake ila kwa shida kutokana na maumivu ya kile kibao alichopigwa.
Akatulia kidogo akisikilizia kile kibao kisha akaanza kumuelezea mama yake yaliyomtokea,
"Kheee Mungu wangu, pole sana mwanangu. Mbona makubwa haya!"
"Yani mama wee acha tu, nashukuru Mungu kwa kunifanya nikumbuke maombi aliyokuwa akiyafanya mama Sam yani yamenisaidia hadi kile kiumbe kimetoweka ndio nimeweza kuingia ndani. Mdomo wote unaniuma mama"
"Pole sana mwanangu"
Ikabidi mama yake amchukulie dawa za maumivu na kumpatia kwani alimuona jinsi alivyokuwa akipata shida wakati wa kuongea.
Sabrina alikunywa ile dawa, kisha mama yake akamwambia
"Yatupasa kumtumainia Mungu mwanangu maana yaliyopo mbele yetu ni makubwa mno, bila ya Mungu hatuwezi kitu chochote."
"Ni kweli mama"
"Yani mimi nakumbuka jinsi nilivyokuwa napiga maombi zamani ila maisha yalifanya nirudi nyuma, ndiomana nashukuru sana ujio wa huyu mama Sam kwani amefanya niweze kusimama tena"
"Kweli kabisa mama, huyu mama amefanya hata tupumzike kwenda kwa waganga wa kienyeji"
Muda huu Sabrina alikuwa akimsifia mama mdogo wa Sam na kusahau kuwa muda mfupi uliopita alimuita mchawi na mshirikina na kumwambia hataki hata kumuona.
Ila kwa maumivu ya mdomo aliyoyapata alijikuta akimkumbuka yule mama mdogo wa Sam na kusema kuwa kama angekuwepo pale kwao basi angemkataza kutoka nje kwa muda huo na kumfanya asikumbwe na yaliyomkumba.
Mama mdogo wa Sam akaanza kufanya maombi sasa, gafla vikasikika vitu vya ajabu sana vikitoka mule ndani na kumfanya Sakina apatwe na uoga kupita maelezo ya kawaida ila mama mdogo wa Sam aliendelea na maombi tu.
Muda huyu mama alipomaliza maombi na kuanza kuimba, Sakina aliangalia pale chini walipomkuta Keti ila hakumuona tena na kumfanya amsogelee karibu zaidi mama mdogo wa Sam kwa uoga huku akimshikilia.
Muda kidogo huyu mama alimaliza kuimba na kuwa kimya kwa muda kisha kukaa kwenye kochi ambapo Sakina alikaa pembeni yake huku akitaka kumwambia kuwa Keti pale chini ametoweka ila kabla hajasema chochote akamuona Keti akitokea koridoo na kuja pale sebleni.
Sakina akashtuka sana ambapo Keti nae akashtuka kiasi kuwaona kanakwamba hakuwategemea.
Akafika na kuwasalimia huku akiwa amejishika shingo kuonyesha kwamba alikuwa na maumivu ya shingo hiyo.
Mama mdogo wa Sam akampa pole,
"Pole sana"
"Asante"
Sakina ndio hakuweza kuongea chochote kabisa kwani alikuwa na uoga bado.
Keti akawauliza,
"Mmefika muda mrefu eeh!!"
Mama mdogo wa Sam ndiye aliyekuwa anajibu na kuuliza,
"Tumefika muda mrefu ndio, ulikuwa wapi kwani?"
"Hata sielewi jamani ila mambo yaliyotokea usiku wa jana nadhani ndio yaliyosababisha yote haya hata sijielewi, nimejikuta tu chini chumbani halafu shingo inaniuma sana"
Hapo ndipo Sakina nae alipomuuliza,
"Mambo gani hayo yaliyotokea usiku Keti?"
"Jana mlipoondoka, muda kidogo nikasikia hodi na kufungua nikamkuta Emmy ila akiwa amebadilika sana, hakuongea na mimi ila aliingia moja kwa moja ndani huku akinusa nusa kwakweli sikuweza kumuelewa na moja kwa moja akaenda chumbani kwako ambako ulisema nisiingie ila na mimi niliposogelea kile chumba chako ikawa kama macho yangu yamepigwa upofu na sikuweza kuona chochote. Wakati napapasa papasa nikajikuta nimegonga ukuta na kuanguka chini kwakweli sijajielewa tena hadi muda huu nilipojikuta chini chumbani tena shingo nayo ikiniuma sana. Kwakweli sielewi chochote hapa nilipo."
Moja kwa moja Sakina akaelewa kuwa yule waliyemuona jana na kumuhisi kuwa ni Emmy ni kweli alikuwa Emmy, akili yake ikampeleka moja kwa moja hospitali ambako ndugu wa Emmy walikuwa wakilalamika kupotelewa na maiti ya mama yao halafu akakumbuka jinsi alivyoona maiti chumbani kwake, hapo moja kwa moja akili yake ikahisi wazi kuwa ile maiti aliyoiona chumbani kwake ndio maiti ya mama yao na wakina Emmy, hapa kidogo uoga kiasi ukamshika.
Baada ya kimya cha muda mfupi, mama mdogo wa Sam akamshtua kidogo Sakina,
"Vipi Sakina unawaza nini?"
"Nawaza kuwa ile maiti chumbani kwangu iliwekwa na nani? Na je huyo Emmy ndio alikuja kuichukua au ni nini?"
"Usiwaze sana kuhusu hayo mambo Sakina unaweza ukachanganyikiwa bure, cha msingi umshukuru Mungu kwa kila kitu cha sasa"
Sakina akatulia kimya huku akiwa na mawazo bado ila akamuomba mama mdogo wa Sam kuwa aende nae chumbani kwake kwani anaogopa na hakiamini tena chumba chake.
"Kwa maombi tuliyofanya hakuna kinachoweza kuendelea kuwa hapa ila twende"
Wakainuka na kuelekea chumbani kwa Sakini ambako palikuwa kawaida kabisa kamavile hapakuwa na chochote kibaya kilichoweka mahali hapo, kisha mama mdogo wa Sam akafanya nao maombi tena kidogo mule chumbani ambapo Keti alianguka kama mtu mwenye mapepo ndipo huyu mama alipohamia kumuombea Keti sasa.
Nyumbani kwakina Sabrina wakapata mgeni na kumkaribisha, mgeni huyo alikuwa ni Francis ambaye ujio wake uliwashtua kiasi ila walimkaribisha vizuri tu kama kawaida.
"Karibu sana"
"Asante"
Baada ya salamu, ni mama Sabrina ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuuliza swali huyu Francis,
"Nasikia wewe na Sam ndio mnahusika na kupotea kwa Emmy"
"Si kweli mama"
Kisha akawasimulia kile kilichotokea kwakina Emmy na jinsi walivyoondoka na huyo Emmy,
"Mama, Emmy alibadilika kabisa yani hakuwa yule Emmy tuliyemzoea yani mimi na Sam tulichukuliwa tu yani ilikuwa ni wafata mkumbo ambapo Emmy alitupeleka mpaka makaburini. Kufika pale aliongea maneno ambayo sikuyaelewa kwakweli, yani muda wote nilikuwa nimejawa na uoga mama yangu. Tulipotoka hapo akatupeleka mahali kulikuwa na mti mkubwa sana ambapo alitoka na kibuyu kimoja na kumkabidhi Sam ambapo aliongea maneno na Sam ila sikuelewa chochote kisha akafanya kitu na kumfanya Sam atoweke kabisa yani hadi leo sijui huyo Sam yuko wapi. Halafu nikabaki nae, akaniambia anaitaka maiti ya mama yake. Basi kwa siku zote hizi tunahangaika kuitafuta hiyo maiti ilipo, kwakweli nikachoka na kumwambia kuwa siwezi kuendelea tena. Sijui akafanya kitu gani, jana nikajishtukia nipo nyumbani. Jamani huyu Emmy sio mtu wa kawaida kabisa huyu, yani sio mtu wa kawaida jamani"
Mama Sabrina na Sabrina walishangaa tu hayo maelezo ya Francis na kuwafanya wajiulize kuwa huyu Emmy ni mtu wa aina gani mpaka anaweza kufanya mambo ya ajabu kiasi hicho? Ndipo mama Sabrina alipomuuliza tena Francis,
"Sasa hiyo maiti mlikuwa mnaitafutia wapi na je mlikuwa mnaitafuta ili iweje?"
"Kwanza tulianyia hospitali ambako ilionekana wametuwahi na kuihamisha, ndipo tulipoanza kutafuta sehemu mbali mbali"
Mama Sabrina akawakumbuka na wale ndugu wa Emmy waliokuwa wanafatilia hiyo maiti bila ya matumaini yoyote,
"Mambo mengine mbona ya ajabu jamani mmh! Sijawahi kuyahisi haya mambo kwakweli. Sasa huyu Emmy ana nguvu za aina gani kuweza kufanya mambo kama hayo?"
"Mi nadhani Emmy atakuwa na majini maana yale aliyokuwa anayafanya kwa hakika kabisa hayawezi kufanywa na mtu wa kawaida ila yeye ameweza kuyafanya yani hadi sasa sijui huyu Emmy nimuweke
kwenye kundi gani"
"Kwahiyo na huyo Sam haijulikani alipo!"
"Haijulikani ndio kwani hata mimi mwenyewe sijui aliambiwa nini na hata alipotoweka sijui alielekea wapi. Mi ninachoshukuru ni kuwa nimepona na sidhani kama nitajihusisha tena na mambo haya kwakweli"
Walitulia kwa muda huku Francis akijaribu kuwaelezea kuhusu muonekano wa Emmy kwa jinsi alivyobadilika.
Mama mdogo wa Sam alipomaliza kumuombea Keti alikuwa sawa kwa muda huo na kurudi nae sebleni ambapo alijikuta akiongea mambo mengi sana,
"Kwakweli najiona kuwa mwepesi, sikujua kama nina mizigo kwenye moyo wangu"
"Ulikuwa na mashetani Keti"
"Ni kweli kabisa hata siwabishii, nilipewa na bibi yangu alikuwaga mganga kwahiyo kabla hajafa akaniambia ananiachia walinzi ila kwa masharti ambapo mwanzoni sikuona kama ni tatizo ila kadri siku zinavyokwenda ndipo niliona kuwa ni tatizo ila sikujua ni kwa jinsi gani naweza kupambana na hili tatizo"
Sakina akamuuliza,
"Kwani alikupa masharti gani?"
"Hayakuwa masharti kihivyo ila ndio ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu. Mimi ni mtu mzima sasa, natamani niwe na mume, watoto yani niwe na familia yangu ila bibi aliniambia kuwa kwa walinzi alionipa sitaweza kuolewa kamwe na wala sitakuwa na uwezo wa kumtamani mwanaume wa aina yoyote. Na huo ndio ukweli kwangu, sijawahi kumtamani mwanaume yoyote na hakuna mwanaume hata mmoja aliyewahi kujitokeza kuwa anataka kunioa au ananipenda hadi leo"
"Kweli hilo ni tatizo Keti, ni tatizo haswaa"
"Usijali yataisha"
Muda kidogo mlango uligongwa, na kwasasa ni huyu mama mdogo wa Sam ndiye aliyeenda kufungua.
Na alipofungua tu akamkuta anayegonga ni Jeff ambapo Jeff alipomuona mama huyu gafla akageuka na kuanza kukimbia.
Muda kidogo mlango uligongwa, na kwasasa ni huyu mama mdogo wa Sam ndiye aliyeenda kufungua.
Na alipofungua tu akamkuta anayegonga ni Jeff ambapo Jeff alipomuona mama huyu gafla akageuka na kuanza kukimbia.
Ila huyu mama alisimama tu pale pale mlangoni kisha akarudi ndani na kuacha mlango wazi ambapo Sakina akamuuliza kuwa itakuwaje juu ya mwanae ambapo mama mdogo wa Sam akamjibu kwa kifupi tu kuwa,
"Usijali atarudi tu"
Wakakaa kimya tu, baada ya muda mfupi wakashangaa kumuona Jeff akirudi tena kwa kukimbia na alipofika pale ndani alianguka chini na kuzimia.
Mama mdogo wa Sam akawaambia watulie na wafanye maombi tu ambapo maombi yake yeye kwa muda huo yalikuwa ni kumuombea Jeff ili aweze kurudi kwenye hali ya kawaida.
Wote walikuwa wakimuombea Jeff kwa imani zao mpaka pale walipomuona mama mdogo wa Sam akiwa kimya kwani nao walinyamaza na kumuangalia ambapo mama huyu alisogelea mlango wa kutoka nje na kuufunga kwa sasa.
Wote walikuwa wakimuangalia huku Jeff akiwa bado pale pale chini.
Mama mdogo wa Sam aliporudi alikaa kwenye kiti akiwa kimya tu ila aligundua kwa haraka sana kuwa Sakina na Keti wana mashaka kiasi hivyo akaamua kuongea ili kuwatoa hofu waliyokuwa nayo.
"Jamani msiwe na shaka, Mungu ni mwema na aminini kuwa tulichokiomba kitafanikiwa."
Alivyoongea hivi ilikuwa kamavile amewapa matumaini kiasi.
Sabrina na mama yake muda huu walikaa pamoja huku wakipeana moyo kwa yaliyotokea na kukumbushana yale maneno ambayo mama mdogo wa Sam amekuwa akiwaambia mara kwa mara.
Muda kidogo wakasikia hodi, kwa muda huo ilikuwa ni afadhari mama Sabrina ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kufanya jambo lolote hivyo ni yeye aliyeinuka na kwenda kufungua mlango, hapo moja kwa moja akamuona mtoto wake James, kwakweli alifurahi sana kwana mtoto wake huyu ni siku nyingi hajaonana nae.
Akamkaribisha mwanae ndani huku akimuuliza maswali mbali mbali kuwa kwanini amewatenga kiasi kile,
"Utafikiri mimi sio mama yako jamani James? Kwanini hivi lakini? Kwanini kukaa kimya kiasi hiki!"
"Nisamehe sana mama ila huwezi amini huwa nakuja mara kwa mara siwakuti na mara nyingi simu zenu hazipatikani. Nakumbuka hadi kuna siku nikampigia simu yule Sam tena mara nyingi tu ila ilita bila ya kupokelewa kabisa na wala hakuwahi kunipigia tena"
"Ni matatizo mwanangu, yani tuna matatizo mengi sana tena yanaibuka usiku na mchana"
"Kweli naona kuna matatizo maana kwa niliyokutana nayo leo huko njiani ni khatari"
Ikabidi wamsikilize kwa makini ili wajue amekutana na kitu gani kwani moja kwa moja walihisi kuwa ni yale mauzauza ambayo huwa yanawatokea wao kila siku.
"Hebu tuelezee James, ni mambo gani hayo"
"Nimekutana na Sam njiani ila alionekana kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nilimuita kumsalimia ila alinikimbia na kuanza kuniita mimi chizi, kwakweli sikuweza kumfatilia ila bado sijamuelewa kuwa kwanini amekuwa vile"
Mama Sabrina alikuwa akishangaa tu kwa hayo ambayo mwanae amemueleza kuhusu Sam huku moja kwa moja akimfikiria mume wake kuwa atakuwa kwenye hali gani akipata habari hizo,
"Sasa huyo Sam ameingiliwa na nini tena jamani mbona mapya haya!"
Ilikuwa ni kushangaa tu hali waliyoelezwa ya huyo Sam.
Muda kidogo ilipokuwa inakaribia mida ya jioni Jeff alizinduka na alikaa huku akijishangaa sana, mama mdogo wa Sam alielewa kuwa ni kwanini Jeff aliinuka na kujishangaa ni kwavile anajiona tofauti na yupo nyumbani ambako hakupategemea.
Na kweli muda kidogo Jeff akauliza,
"Nimefikaje hapa na imekuwaje jamani?"
Mama mdogo wa Sam ikabidi ainuke na kama kumsaidia Jeff kusimama kisha akaenda nae kwenye kochi na kukaa.
Alijaribu kumuelezea mambo mbalimbali na jinsi walivyoteseka kuhusu yeye, kwakweli Jeff nae alijikuta akielewa kwa haraka sana kwani akili yake nayo haikuchukua muda mrefu kuelewa.
"Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta ila tunamshukuru sana Mungu kwakweli ametenda makubwa sana katika haya maisha yetu"
Wote wakaonekana kumsapoti mama mdogo wa Sam na waliongea mengi hadi muda wa kulala ulipofika na kwenda kulala.
Nyumbani kwa kina Sabrina kwavile muda ulienda, James nae aliwaaga na kumuahidi mama yake kuwa atamletea wajukuu zake awaone jinsi walivyokuwa kwasasa.
Wakaagana nae pale ni kisha kuondoka.
Muda kidogo baba Sabrina nae akarudi nyumbani hivyo wakafanya shughuli za hapa na pale hadi muda wa kulala ulipowadia.
Wakaenda kulala huku Sabrina akiwa na wanae kama kawaida.
Bado kwa usiku wa leo akajifikiria sana kitendo alichofanya kwa mama mdogo wa Sam kwa siku hiyo huku akijiuliza kuwa yale mawazo ya jana usiku na zile ndoto alizokuwa anaota zilitokea wapi kwani ilikuwa ni kitu kilichomshangaza tu kwa wakati wote.
Aliwaza sana ila mwisho wa siku akalala, na moja kwa moja ikamjia ndoto ya maisha aliyokuwa akiishi yeye na Sam kama mke na mume na jinsi mambo yalivyokuwa kwa kipindi hicho.
Alijikuta akiota vitu vingi sana vya mambo yaliyowahi kutokea awali na jinsi Sam alivyokuwa akimueleza ukweli wa maisha yake.
Katikati ya ile ndoto akaona kitu kinachomsumbua Sam, kisha akamuona Emmy kama akimuita Sam huku akiwa ameshika chupa ambapo gafla akamuona Sam akiwa mdogo kabisa ndani ya ile chupa ambayo Emmy aliibana na kuitupia baharini kisha akamuna Emmy akirudi peke yake bila ya Sam.
Sabrina akashtuka hapo kutoka usingizini huku akiogopa sana, akatamani kwenda kuchungulia dirishani ili aangalie giza la nje kama kuna karibia kukucha ila kwa leo alijikataza mwenyewe ili kujiepusha na yale matatizo ya kujitakia.
Ila ndio alikaa kitandani na kuwaza muda wote mpaka pale kulipokucha na alipomsikia mama na baba yake wakiongea sebleni ndipo na yeye alipotoka chumbani kwake.
Kwa upande wa nyumbani kwa Sakina kulipokucha, Sakina na mama mdogo walikuwa wa kwanza kuamka na moja kwa moja mama mdogo huyu alihitaji kurudi kwa kina Sabrina,
"Sasa kwanini uende asubuhi hii?"
"Huu ndio muda sahihi kabisa kwenda, nataka kwenda kuwaona wajukuu na vile vile kuzungumza na Sabrina"
"Basi ni vyema tukaenda wote"
Sakina alijiandaa na kumuaga Keti kisha yeye na mamdogo wa Sam wakaondoka na kuwaacha pale ndani.
Wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwakina Sabrina ikabidi Sakina amkumbushe huyu mama kuhusu yale maneno yaliyosemwa na Sabrina jana yake, ila mama mdogo alionekana kutokuyajari kabisa na kumwambia Sakina,
"Yale ni maneno ya mkosaji, na mimi nilikuwa naelewa tangu panaanza kukucha ndiomana sikushtushwa nayo sana ingawa kiuanadamu kawaida yanaumiza moyo cha muhimu katika maisha ni kuwa mvumilivu, jasiri na ujue jinsi ya kupambana na changamoto mbali mbali. Kama ningekuwa ni mtu wa kuchukia basi ni muda mrefu tangu nipo hapa jijini ningemchukia mwanangu Sam. Yani ujue mtoto yule nimemlea mwenyewe na kuhangaika nae ila huwezi amini kuwa naye alishawahi kuthubutu kunyanyua ulimi wake na kuniambia kuwa ndiomana sina kizazi eti ndio sababu ya kuachika kwangu, amesahau kuwa yeye ndiye alikuwa sababu kubwa ya mume wangu wa kwanza kuniacha. Ila namshukuru Mungu kwavile kuna ujasiri ndani yangu unaofanya nivumilie mengi sana"
Sakina alimuangalia sana huyu mama na kumuona kuwa ni wa tofauti sana katika wamama wengi aliokutana nao kwani kwa haraka haraka angekuwa ni yeye basi kwa yale maneno ambayo Sabrina aliyasema jana ingefanya asiongee tena na Sabrina kwavile yeye huo moyo wa uvumilivu hana kabisa.
Walipofika waligonga hodi na aliyewafungulia na kuwakaribisha alikuwa ni Sabrina tena alionekana kuwafurahia sana huku upande mwingine wa sura yake ukionekana kujutia yale maneno yake ya jana.
Watoto wa Sabrina nao walipomuona mama huyu wakamfurahia sana kwani kumkosa kwa siku moja tu iliwafanya wanyong'onyee.
"Yani hawa watoto jana yote hawakuwa na raha kabisa kwakweli wameshakuzoea mama. Naomba unisamehe kwa yake yote niliyoyasema jana"
"Wala usijari Sabrina wewe kuwa na amani tu"
Kisha wakakumbatiana, mama Sabrina nae alipokuja wakasalimiana nae halafu moja kwa moja mama mdogo huyu alihitaji kitu kimoja tu ambapo alihitaji Sabrina amueleze kuhusu ndoto aliyoiota usiku wa kuamkia leo.
Sabrina alimueleza kila kitu kwa yale aliyoyaota jana ila ile sehemu kuwa Sam aliwekwa kwenye chupa na kutupwa baharini kwakweli wote walisikitika huku wakitamani kuwa iwe ni sehemu ya ndoto tu.
Sabrina akamuuliza huyu mama kuwa kwanini amekuja kumuuliza kuhusu hiyo ndoto,
"Mtajua tu sababu ya mimi kuuliza kuhusiana na hii ndoto ila yatupasa kuomba sana"
Wakaamua sasa kuendelea na mambo mengine.
Nyumbani kwa Sakina, moja kwa moja Keti akaenda kumgongea mlango Jeff kwani ilionekana kuwa bado hajaamka.
Jeff alitoka chumbani kwake na kumsalimia Keti huku akimuangalia sana, kisha Keti akamwambia,
"Chai tayari, nimekuwekea mezani karibu"
Jeff hakumjibu Keti bali alikazana kumuangalia tu hadi Keti nae akamshangaa kidogo na kumuuliza,
"Mbona hunijibu unaniangalia tu?"
"Unajua nakushangaa!!"
"Unanishangaa nini?"
"Hivi ni wewe Keti au mwingine?"
"Ni mimi kwani vipi?"
"Mbona leo umebadilika!"
"Nimebadilikaje?"
"Umekuwa msafi"
Keti akacheka na kuuliza,
"Kwani siku zingine huwa ni mchafu?"
"Hebu wewe mwenyewe jiangalie vizuri leo ulivyo, unaonekana umeoga, umechana nywele, umepaka mafuta na umependeza wakati siku zingine unakuwaga rafu kabisa ila leo duh!"
Kisha Jeff akatoka na kwenda huko mezani kunywa chai.
Keti akajiuliza maswali mfululizo juu ya muonekano wake wa siku hiyo ila na yeye akajiona wazi kuwa ni kweli kabadilika.
Jeff alipomaliza kunywa chai alienda kukaa sebleni huku akitafakari mambo mbali mbali yaliyotokea katika maisha yake, ndipo Keti nae alipoenda kukaa pale pale sebleni akimtazama Jeff, kwa hakika Jeff nae alitambua jinsi alivyokuwa akitazamwa na Keti hivyobasi akaamua kumuuliza,
"Mbona wanitazama hivyo Keti? Je kuna lolote unataka kuniambia?"
"Hapana ila nakutazama tu jinsi ulivyo kijana mzuri"
Jeff akacheka na kumuuliza,
"Huo uzuri umeonekana leo? Au na mimi nimebadilika kama wewe?"
Keti akatabasamu huku akimtizama Jeff kwa jicho la aibu sasa.
Jeff akamuuliza tena,
"Una nini kwani leo? Unajua sio kawaida yako Keti? Yani unafanya vitu ambavyo sikuelewi kwa haraka haraka"
"Ni ngumu kunielewa Jeff, siku zote nilikuwa nimefungwa na kushindwa kuona uzuri wako, kwakweli leo najikuta tu nikikushangaa ingawa najua siwezi"
"Huwezi nini?"
Keti akakaa kimya hapo halafu muda kidogo akanyanyuka na kuelekea jikoni.
Keti akiwa jikoni kwa mara ya kwanza alijikuta sura ya Jeff ikicheza kwenye akili yake hadi yeye mwenyewe akashangaa, ni hapa alipoelewa kuwa kwanini mtu mzima kama Sabrina amemng'ang'ania Jeff, alikuwa akijisemea tu,
"Amakweli huyu Jeff ni kijana mzuri sana tena anavutia sana, Sabrina anakila sababu ya kumng'ang'ania huyu kijana ila ni kwanini Jeff nae anampenda sana Sabrina ingawa anajua wazi ni mkubwa kwake? Inamaana Sabrina ndio mwanamke mzuri kuliko wote?"
Akatoka jikoni na kuelekea chumbani kwake kisha akachukua kioo na kujiangalia,
"Mbona na mimi ni mzuri? Je kwenye haya mabadiliko yangu Jeff hajaweza kuona uzuri nilionao? Uuh mawazo yangu haya hayana kichwa wala miguu ila najikuta tu nikitamani hata kwenda kumsogelea Jeff angalau nimshike na kumbu...."
Akakaa kimya kwa muda na kupumua kiasi.
Nyumbani kwakina Sabrina bado walikuwa wakielezana na ndipo Sakina alipoeleza kuhusu kurudi kwa Jeff na jinsi ilivyokuwa.
Hii habari ilikuwa njema sana kwa upande wa Sabrina kuliko habari zote zilizopita kwani hii aliiulizia kwa makini sasa,
"Eeh sasa anaendeleaje Jeff?"
"Anaendelea vizuri ila asubuhi hii tumemuacha amelala"
"Aah itabidi nikamuone"
Moja kwa moja Sabrina akaenda chumbani kwake kujiandaa ila hakuna aliyemshangaa kwani kwasasa kila mmoja alishaelewa kilichopo baina ya Jeff na Sabrina.
Muda kidogo Sabrina alimaliza kujiandaa na kutoka akiwaaga, na kama kawaida mamdogo wa Sam alimwambia kuwa awe makini sana njiani na huko aendako.
Hilo la umakini halikuwa tatizo kubwa kwa Sabrina na pia alishalizoea kutoka kwa mama huyo.
Keti alitoka chumbani kwake na kurudi tena sebleni, safari hii alienda kukaa karibu zaidi na Jeff kisha akamuuliza,
"Je mimi si mzuri?"
"Mbona wewe ni mzuri sana Keti haswa leo umekuwa mzuri sana"
Keti akatabasamu kisha akamshika bega Jeff huku akitetemeka kwa uoga flani hivi, halafu akamsogelea kama anataka kumbusu mdomoni.
Gafla mlango wa sebleni ukafunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sabrina ambaye alibaki na mshangao.
Keti akatabasamu kisha akamshika bega Jeff huku akitetemeka kwa uoga flani hivi, halafu akamsogelea kama anataka kumbusu mdomoni.
Gafla mlango wa sebleni ukafunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sabrina ambaye alibaki na mshangao.
Sabrina akauliza kwa ukali,
"Nini kinaendelea hapa?"
Keti akajigeleza na kumkaribisha Sabrina,
"Karibu dada, Jeff ana uvimbe mdomoni ndio nilikuwa namuangalia"
"Uvimbe mdomoni wakati nimewaona kabisa mlichotaka kufanya!"
Ikabidi Jeff nae aingilie kati ingawa kiukweli hata yeye mwenyewe hakumuelewa Keti kabisa kuwa alikuwa na lengo gani au alikuwa anataka kitu gani.
"Hakuna kitu Sabrina usipende kuwa na mawazo mabaya"
Kisha akainuka na kumshika mkono Sabrina na kuelekea nae chumbani kwake ili apate kumtulize kidogo.
Keti alibaki pale sebleni huku akitabasamu kwa mbali na huku uoga nao ukimtawala kwa mbali ila alitamani sana lile lengo lake la kumbusu Jeff lingetimia muda ule kwani wazo lake juu ya Jeff lilikuwa gumu sana kutoka kwenye akili yake.
Jeff na Sabrina walipoingia chumbani kwanza kabisa Jeff akamkumbatia Sabrina ili angalau kumtoa mawazo mabaya.
Ila bado walipokaa Sabrina alikumbushia mada ile ile,
"Amakweli wanaume ni sawa, yani Jeff wa kutaka kutembea na msichana wenu wa kazi duh.!"
"Unanifikiria vibaya bure Sabrina, mimi siwezi kabisa kufanya hicho unachofikiria, kwanza jua kabisa ni jinsi gani nakupenda, ni mangapi nimevumilia ili nikupate wewe! Yani sasa hivi naona kabisa muelekeo wa kuwa nawe upo kwenye mstari halafu nifanye ujinga? Siwezi Sabrina, kama wanaume wote ni sawa basi mwanaume mimi nipo tofauti na hao wanaume wenzangu na yote hiyo ni sababu nakupenda sana Sabrina"
Maneno ya Jeff siku zote huwa yanamuingia sana akilini Sabrina kwahiyo akaanza kuwa mpole na kuuliza maswali kwa kipole.
"Nilimuona kama anataka kukubusu jamani, halafu hicho kidonda alichokuwa anakuangalia kiko wapi mbona huna kidonda?"
"Tuachane na hayo mambo Sabrina, hebu niambie watoto wanaendeleaje?"
Hapo mada ikabadilika na wakaanza kuongelea habari za watoto kwa muda huo.
Nyumbani kwa wakina Sabrina kwavile Sabrina alitoka ikabidi wajadiliane kuhusu huyu Sabrina na aliyeanzisha mjadala alikuwa ni Sakina,
"Kwahiyo mama unamuachia kabisa Sabrina awe na Jeff!!"
"Sasa Sakina unataka nifanyaje? Na wewe unakumbuka wazi kipindi tunawauliza walivyotujibu au umejisahaulisha mwenzangu?"
"Sijajisahaulisha ila cdo napata maswali sana, yani Sabrina niliyekuwa namwita mdogo wangu leo hii awe mkwe wangu!!"
"Sasa wewe wasiwasi wa nini tena, jiulize huyo Sabrina anamwitaje Jeff kwasasa. Yani hayo mashaka ya kuitana inabidi wawe nayo wao na sio wewe. Sisi tutulie tu na tutauona mwisho wao, yani mi hata hawanitii presha kabisa maana mara nyingine nikifikiria huwa naona kama ni ndoto tu"
Sakina akawa kimya kwa muda kwanza akijitafakarisha kuhusu haya mahusiano ya Jeff na Sabrina ila mama Sabrina akamwambia kuwa ni bora aachane na hayo mawazo ili asije akajiumiza bure bila ya sababu za msingi.
Keti alikuwa anawaza ni jinsi gani Sabrina anafaidi kuwa na Jeff kwakweli alijiona wazi akipatwa na wivu dhidi ya penzi la Jeff na Sabrina mpaka akajiuliza,
"Au kwavile Jeff ndio amekuwa mwanaume wa kwanza machoni mwangu? Kwanini iwe hivi? Kwanini nimtamani Jeff na si mwanaume mwingine ila kwakweli Jeff anavutia sana"
Akainuka pale na kuelekea chumbani kwa Jeff mlangoni ili aweze kuwasikilizia kuwa wanazungumza mambo gani au akiweza awachungulie kuwa wanafanya nini, ila alipokuwa anakaribia mlango nao ukafunguliwa na kumfanya ashtuke sana kwani aliyetangulia kutoka alikuwa ni Sabrina ambapo alimuuliza Keti kwa kumshangaa sana,
"Una matatizo gani wewe? Mbona umekuwa hivyo wewe!!"
Keti alikuwa kimya kwa aibu kwani hakuweza hata kujitetea, hivyobasi akaondoka kwa aibu tu.
Sabrina akatoka na Jeff pale kwani lengo lake ilikuwa ni kumsindikiza.
Walipotoka nje, Sabrina akamwambia Jeff
"Yani huyu Keti ananipa mashaka sana"
"Mashaka ya nini Sabrina?"
"Hivi wewe huoni matendo yake niliyomkuta nayo? Ninahofia sana, unaweza ukaingia mtegoni wewe"
"Hata usiwe na shaka juu ya hilo, yani wewe jua tu kuwa ni kitu kisichowezekana. Kwanza hata mi mwenyewe namshangaa leo maana hadi ameoga na kuoga"
"Ndio ameoga ili ajiandae kuwa na wewe"
"Hata kama, mimi siwezi kuwa na yeye hata awe vipi na sio yeye tu ila mwanamke yeyote yule tofauti na wewe siwezi kuwa naye. Mwanamke pekee ninayempenda ni wewe tu Sabrina kwahiyo utambue kabisa hilo kuwa hakuna mwanamke ninayeweza kuwa naye zaidi yako. Nakupenda wewe tu"
Kama siku zote, maneno ya huyu Jeff yalikuwa yakiupoza sana moyo wa Sabrina na kumfanya ajione kuwa mwanamke mwenye bahati kuliko wanawake wengine.
Jeff alimsogelea Sabrina na kumwambia kuwa kabla hawajarudi nyumbani apite nae mahali amuonyeshe kitu ambapo Sabrina alikubali hilo jambo.
Wakiwa ndani na kuendelea na maongezi ya hapa na pale, ikagongwa hodi na kuamua kwenda kufungua ila wote wakashangaa sana kumuona Emmy ila wakamkaribisha hivyo hivyo.
Mama Sabrina ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuuliza Emmy kuwa imekuwaje kwani hata kuja kuja kwake ilikuwa kwa kushtukiza.
"Emmy hebu tueleze vizuri mlipokuwa na hadi leo hapo ulipo"
"Kwakweli ni historia ndefu sana ila ninahofia maisha ya Sam sijui kama anaweza akapona maana amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwasasa."
"Mmh kivipi? Hebu tueleweshe"
"Ni kwamba hapo kati kati yametokea matatizo mengi sana na kiukweli hatukuwa kwenye hali ya kawaida na hamuwezi kuamini ila ukweli ni kwamba mimi na Sam tulisafiri kwenda mbali sana na yote hiyo lengo langu lilikuwa ni moja tu. Nilitaka Sam aepukane na matatizo aliyokuwa nayo na kwa kiasi fulani tulifanikiwa ila tatizo tulivyorudi tulikuta ofisi za Sam zimefungwa na katika kufatilia tukaambiwa kuwa hoja ya kufunga ofisi wamepewa na Jeff na swala ni kuwa waliambiwa ni amri ikabidi watii amri hiyo na kufunga ofisi zote za Sam kwahiyo ni muda sasa ofisi hizo hazifanyi kazi. Hicho kitendo kimemkera sana Sam na kumfanya kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na kaniambia kuwa mtu wa kwanza anayetaka kuonana nae ni huyo Jeff."
"Khee mbona makubwa hayo! Kwahiyo huyo Sam yuko wapi kwasasa?"
"Sijui alipo ila niliachana nae akiwa na hali mbaya ya akili kwakweli na ndiomana nimeamua kuja huku ili nijue kuhusu Jeff kwani huenda hakufanya kwa akili zake bali ni yale madudu yaliyokuwa yakimsumbu."
"Huo ndio ukweli kwamaana Jeff karudiwa na akili zake jana na tumepata nae shida sana"
Sakina aliona ni vyema kumtetea mtoto wake.
Mamamdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa, mara gafla wakamuona kama machozi yakimtoka na kila mmoja kushindwa kumuelewa kuwa tatizo ni nini.
Ila mama Sabrina aliamua kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
"Mbona unatoa machozi dada, tatizo nini?"
"Naambiwa kuwa kuna jambo baya linataka kutokea halafu kupingana nalo siwezi"
Karibia wote wakashikwa na uoga juu ya hilo jambo baya waliloambiwa na huyu mama.
Jeff alimpeleka Sabrina mahali ambako palikuwa na kauchochoro na kumuuliza,
"Je unapakumbuka hapa?"
Kwa haraka haraka ilikuwa ngumu kwa Sabrina kukumbuka eneo lile mpaka pale Jeff alipomkumbusha kuhusu lile eneo.
"Unakumbuka miaka hiyo iliyopita ulitaka kubakwa hapa!"
Moja kwa moja Sabrina akakumbuka hilo tukio ambapo kwa kipindi hicho Jeff alikuwa bado mdogo ila ndiye aliyemuokoa Sabrina toka kwa yule kijana mbakaji.
Sabrina akamuangalia Jeff na kumuuliza,
"Kwanini umeamua kunileta eneo hili?"
"Nimetaka tu ukumbuke hili tukio na pia napenda uniamini"
Sabrina akatabasamu tu kisha yeye na Jeff wakaanza kuondoka eneo lile.
Njiani wakaona kama gari ya Sam tena ikionekana kuwa inaenda nyumbani kwakina Jeff.
Wakatazamana na kuulizana,
"Si gari ya Sam ile!"
"Ndio ni yenyewe"
"Kwamaana hiyo Sam amepona na ameanza tena kuendesha mali zake kama kawaida?"
"Sijui, inawezekana ila je kule nyumbani kwenu atakuwa amefata nini?"
"Sijui ila badae tutajua tu, hebu twende kwanza kwenu halafu nikirudi nitajua alichokuwa amefata pale nyumbani"
Wakakubaliana juu ya hilo ingawa Sabrina alitaka waende pamoja ila kwa upande mwingine akahofia kwavile hakujua ni jinsi gani Sam atakuwa kwa kipindi hiki je ataendelea kukubaliana na penzi la Jeff na Sabrina au ataendelea kulipinga penzi hilo.
Lile gari lilikuwa ni la Sam kweli na aliyekuwa ndani ya gari alikuwa ni Sam na alienda pale kwakina Jeff kwa lengo lake moja tu la kuzungumza na Jeff. Ila alipofika pale aligonga mlango na kufunguliwa na Keti ambaye alimkaribisha vizuri sana ila muonekano wa Keti kwa siku ya leo ulimshangaza Sam pia na kuamua kumwambia,
"Mbona leo umebalika sana Keti?"
Keti akajichekelesha na kuuliza,
"Nimebadilikaje?"
"Umekuwa msafi, mzuri kwa kifupi umependeza sana"
Hizi sifa zilimfurahisha sana Keti na kumfanya atabasamu muda wote kisha Sam akaingia na kukaa, kama lengo lake lilivyokuwa alianza kwa kumuulizia Jeff,
"Yuko wapi Jeff"
"Katoka kidogo ila nadhani atarudi muda sio mrefu"
Keti aliongea hayo huku akimuangalia vizuri Sam na kimoyo moyo aliweza kuona ni jinsi gani Sam nae anavutia na kuzidi kumuona Sabrina kuwa ni mwanamke mwenye bahati sana kwa kupata wanaume wote wanaovutia.
Sam alishtukia jinsi alivyokuwa akiangaliwa na Keti ikabidi amuulize,
"Mbona unaniangalia sana au huamini kama nimerudi? Mimi nimerudi Keti ingawa sina muda mrefu wala maisha marefu"
"Kivipi?"
"Basi tu ila najiona kama mtu anayekaribia kufa"
"Mmh usiseme hivyo boss, huu ni mwanzo wa maisha yako mapya kama maisha yangu mapya kwani natumaini hadi umerudi basi umeshapona na yale matatizo yako."
"Ni kweli nimepona ila mimi siwezi kudumu tena katika maisha haya"
"Kitu gani kimekudhihirishia kuwa umepona?"
"Unamfahamu Emmy?"
"Ndio namfahamu"
"Basi huyu ni mwanamke aliyenidhihirishia kupona kwangu, huyu ndiye mwanamke shujaa wangu ingawa kiukweli mimi si shujaa wake"
Keti akamtazama sana Sam kisha kuna neno akatamani kumwambia ila alikwama nalo njiani, ikabidi Sam amuulize kwa makini kuwa ni kitu gani anachotaka kusema.
Keti akajikaza na kuongea,
"Hata mimi nimepona"
"Kwani ulikuwa na tatizo gani?"
"Nilikuwa siwezi kumtamani mwanaume"
Sam akacheka na kumuuliza,
"Kwahiyo sasa umemtamani mwanaume gani?"
Keti akainama chini na kushindwa kujibu kwa aibu, ikabidi Sam amuulize tena,
"Inamaana umenitamani mimi?"
Keti alijibu kwa aibu huku akitikisa kichwa kuwa ni kweli amemtamani Sam, ni hapa Sam alipomuuliza tena
"Kwahiyo unataka nini toka kwangu?"
"Natamani nipate mara moja tu ili nami nipime kupona kwangu na wala sitathubutu tena kukutamani"
"Hilo sio tatizo kwangu ila tatizo ni kuwa nitakuwa nimemsaliti Emmy"
"Kwa hakika Emmy hatojua jambo hili na wala sitomwambia mtu yeyote yule. Naomba nisaidie kwa hili."
Sam alimuhurumia huyu Keti ingawa alijua wazi kuwa kufanya nae hivyo ni kukiuka masharti aliyopewa na Emmy ila kwavile alimuhurumia Keti ikabidi amkubalie tu kwani hakuona kama ni tatizo kwa upande wake.
Hivyobasi Sam na Keti wakainuka na kuelekea chumbani kwa Keti ili kwenda kumtimizia kile ambacho Keti alikiomba.
Jeff na Sabrina walifika nyumbani kwakina Sabrina ambapo Jeff aliamua kumuagia Sabrina pale pale nje ili aweze kuondoka ila kabla hajaondoka Emmy alitoka ndani na kuwakuta pale nje ambapo walishtuka kiasi na kumuangalia. Ikabidi Emmy awashtue kwa kuwasalimia,
"Jamani yani kama mmeona mzimu vile hadi salamu mnajibu kwa mashaka duh! Poleni"
"Hapana Emmy unajua ni siku nyingi sana, halafu hapo njiani tumeona kama gari ya Sam ikienda nyumbani kwetu yani hapa nataka nirudi nikamuulize"
"Kumbe! Basi twende wote"
Sabrina kusikia ile twende wote ikabidi naye aseme kuwa anawafata ili na yeye akaonane na Sam.
"Mmh Sabrina si tulikubaliana kuwa unarudi wewe"
"Ndio ila nimeshaahirisha tayari"
Basi wakaamua kuongozana wakielekea nyumbani kwakina Jeff.
Walipofika walikuta gari ya Sam ikiwa pale nje ila nyumba ilionekana kuwa kimya sana, wakaingia sebleni na hapakuwa na mtu hapa kidogo hofu ikawashika hasa Sabrina ambaye aliuliza kwa uoga,
"Au yale mauza uza yamerudi tena?"
Emmy alijibu kwa kujiamini,
"Mauza uza yale hayawezi kurudi tena"
Kisha Emmy akamuuliza Jeff kilipo chumba cha Keti maana kitendo cha kutowakuta pale sebleni na vile walivyokuwa wakiitwa bila kuitika ilifanya moja kwa moja Emmy ashikwe na mashaka kuwa watakuwa chumbani.
Walifika chumbani na kufungua mlango ambao ulifunguka bila ya tatizo lolote ila wote walishangaa kumuona Sam na Keti wakiwa kitandani ila walionekana kama watu waliozimia.
Walifika chumbani na kufungua mlango ambao ulifunguka bila ya tatizo lolote ila wote walishangaa kumuona Sam na Keti wakiwa kitandani ila walionekana kama watu waliozimia.
Kitendo hiki kiliwashangaza sana na kuwafanya washtuke na kushikwa na uoga, ila ni Emmy tu aliyeweza kuongea ingawa aliongea kwa kumlalamikia Sam,
"Kwanini Sam? Kwanini umeamua kufanya hivi jamani?"
Emmy aliongea kwa uchungu kanakwamba anaelewa fika kilichofanywa na Sam na Keti.
Hata walipojaribu kuwafunua wakagundua wazi kuwa walikuwa wakifanya mapenzi ila kwanini iwe vile? Ilikuwa ngumu kwa wao kutambua ila iliyobaki ni kuita gari ya wagonjwa mahututi na kuwakimbiza hospitali tu maana hapakuwa na namna nyingine yoyote ile.
Emmy alionekana kuumia bila hata ya majibu ya aina yoyote ile kwani ilikuwa kamavile anaelewa ambacho wataenda kujibiwa hospitali.
Walipokuwa hospitali haikuchukua muda mrefu sana, wakaletewa majibu,
"Jamani poleni sana ila tumewapoteza ndugu zetu"
"Nini dokta?"
"Wenzetu wametangulia mbele ya haki"
Emmy hakuweza kulia bali alikaa chini na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa gafla, wakati huo Sabrina alimkumbatia Jeff kwa kilio cha hali ya juu na kuwafanya madaktari wapate wakati mgumu juu yao.
Kwa bahati alikuwepo daktari anayewafahamu wakina Sabrina vizuri hivyo kuwasaidia kupanda kwenye gari yake na kuwarudisha nyumbani kwao ambako walienda kuwapa taarifa ya msiba.
Waliingia ndani wakiwa kwenye hali ya kilio na hakuna aliyestahimili kulia baada ya kupata habari ya misiba hii yani kwa wakati huu kila mmoja alikumbuka mema ya Sam tu.
Sakina nae alihisi kuchanganyikiwa kwakweli ukizingatia alimuacha Keti asubuhi akiwa mzima wa afya kabisa halafu saizi anaambiwa kuwa amekufa kwakweli Sakina alijikuta akilia hadi kufikia hatua ya kumlaumu Mungu kwa kile ambacho kimetokea.
Hakuna aliyependa kuwa ile hali iwe ni kweli kwani kila mtu alitamani iwe kati ya yale mauza uza yaliyokuwa yakiwatokea siku za nyuma kabla, na hakuna aliyekuwa akiamini kuwa hili jambo ni la ukweli hakuna kabisa kila mmoja alilia kwa uchungu wake.
Hata mama mdogo wa Sam ambaye siku zote alikuwa ni mtu wa kujikaza ila kwa hili machozi yalimtoka na kumfanya aumie moyoni mwake, alijikuta akisema,
"Sam, nilikuja mjini kwaajili yako. Nilikuja kwaajili ya kusaidiana nawe kwenye matatizo yako, yani umeamua kunikimbia mwanangu yani umenikimbia nisikuone tena? Je nilikuwa nakukera sana kukwambia tuombe mwanangu? Keti jamani, nilifanya maombi kwaajili ya kukuokoa na maisha yako kumbe nilikuwa nakuangamiza Keti? Eeh Mungu, kosa langu mimi ni nini kwa watu hawa? Kwanini umeamua iwe hivi Mungu wangu kwanini?"
Alilia sana huyu mama na kuwafanya wengine walie zaidi kwakweli siku yao ilikuwa imeharibika kwa mtindo huo hadi usiku uliingia wakiwa bado wana majonzi.
Baba Sabrina aliporudi nyumbani kwake nae alishangaa kukutana na watu pale kwake, na alipoingia ndani na kukumbuna na habari za msiba alishikwa na uchungu sana na kujikuta machozi yakimtoka na wala hakutaka kuamini kuwa kuna ukweli wowote kwa yale aliyoyasikia kwani aliona kama yupo ndotoni.
Kwakweli hii siku ilikuwa mbaya sana kwa hii familia.
Baba wa Sabrina hakuweza kuendelea kukaa pale sebleni hivyo aliinuka na kuelekea chumbani, alifika kitandani na kujilaza huku akiwa haamini kabisa kile ambacho ameambiwa kuhusu Sam.
Alijaribu kutafakari mambo mengi sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile na muda mwingine kujiona kama mwanaume mwenye makosa kutokana na yale yaliyotokea baina yake na Sam ukizingatia huyu Sam nae ni mwanae.
Kwakweli roho ilimuuma sana na kumfanya atamani sana kuwa walau angepata wasaa wa kuweza kuzungumza na Sam japo mambo mawili matatu ili aweze kumfahamu vyema mtoto wake huyo ila ndio hivyo tena mambo yakawa ndivyo sivyo kwani alikuwa na mawazo sana juu ya kifo cha huyu mtu.
Kulipokucha kila mmoja alitamani kuwa usiku ule uwe ni ndoto tu yani muda pamekucha basi na mambo hayo yote yawe yameisha ila hali ilikuwa vilevile na kuwafanya wakae chini na kujadiliana kuhusu mazishi ya hawa watu ingawa bado ilikuwa ni mtihani mkubwa sana kwao.
"Jamani, hivi itakuwaje? Mbona nazidi kuchanganyikiwa jamani"
"Kwakweli hii hali inachanganya, na kinachochanganya zaidi ni kuhusu huyu Keti. Tunafanyaje kuwapata ndugu zake? Ni nani anayepajua kwao?"
Ikabidi wamuulize Sabrina hilo swali kwani waliamini kuwa ni yeye ndiye atakuwa anajua kwavile hata Sakina alisema hajui chochote kuhusu Keti.
"Kwa upande wangu mimi sielewi chochote kwani nakumbuka kuwa huyu Keti alikuwa akifanya kazi nyumbani kwa Sam. Kipindi naumwa hakuna ninachokumbuka ila nilipopona nilikuwa nae pale nyumbani ila sijawahi kupata hata wasaa wa kuzungumza nae kwani ilikuwa kipindi cha majanga tu hadi hivi amekufa. Dah kweli tunachofikiria wanadamu si mawazo ya Mungu maana sikuwahi kufikiria jambo kama hili juu ya Keti. Wa kumuuliza ni Sabrina tu hapa"
Sakina alionekana kuwa na uchungu sana kutokana na vile alivyokuwa akikumbuka jinsi mwanae alivyomsimulia vile Keti alikuwa akimuhudumia wakati anaumwa.
Sabrina nae akaanza kueleza vile anavyoelewa kuhusu Keti,
"Jamani, mimi Keti sikuwahi kumfahamu vizuri maana aliletwa na Sam ili aweze kunisaidia kazi za ndani, nimeishi nae kwa mtindo huu yani sijui hata anatokea mkoa gani, siwajui ndugu zake wala rafiki zake. Aliyekuwa anamfahamu Keti vizuri ni Sam tu ila ndio hivyo Sam nae hatuponae tena"
Sabrina aliinama na kutokwa na machozi, kwakweli ilikuwa ngumu kwa wote kutambua ndugu wa Keti, hakuna mtu aliyeweza kugundua kuwa Keti ni mtu wa wapi kwahiyo mwisho wa siku hapakuwa na namna zaidi ya kushughulika nae wao wenyewe kwani hakuna mtu aliyekuwa na taarifa yoyote juu yake.
Mchana wa siku hiyo, Emmy alimuomba Sabrina kuwa wakachambue nguo za Keti ili waangalie inayoweza kumfaa kwaajili ya mazishi.
Sabrina alikubali kisha wakaelekea nyumbani kwa Sakina wakiwa wameongozana na Sakina mwenyewe kwani hata yeye alikuwa hajakanyaga nyumbani kwake tangu yale matukio yalipokuwa yametokea yani tangu jana alipoondoka asubuhi.
Walivyoingia tu ndani, Sakina alijikuta akiita jina la Keti na kutokwa na machozi,
"Keti, Keti, nijibu Keti tafadhari. Nilikuwa nikirudi nyumbani kama hivi nakuita Keti nawe ulikuwa unaniitikia kwa upoje kabisa. Keti tulikuwa tunakuacha peke yako hapa ila hujawahi kuchukia wala kukasirika, jamani Keti umeamua kuniacha jamani Keti, Keti itika basi"
Wakina Sabrina ilibidi wambembeleze kwanza Sakina ingawa na wao walikuwa na uchungu kama wake kwani misiba yote hii miwili iliwagusa vilivyo na iliwaumiza kisawasawa ila walijikaza kwa muda.
Kwakweli ilikuwa ngumu kwa Sakina kujikaza ukizingatia ukweli ni kuwa alikuwa amemzoea sana Keti.
Ikabidi Sakina alipotulia wamuacha pale sebleni kisha Emmy na Sabrina kwenda chumbani kwa Keti kuangalia hizo nguo.
Waliingia chumbani kulikuwa na hali ya utulivu sana ambapo kwa haraka haraka iliwatia simanzi kiasi na kujifuta machozi kisha wakafanya kile kilichowapeleka mule ndani.
Wakati wanapekua pekua nguo kwenye begi la nguo la Keti, wakakutana na kadaftari kadogo kalikokuwa kameandikwa na peni na ilionyesha kuwa aliyeandika alikuwa ni Keti ikabidi wakasome ili kuona kama wanaweza kupata ujumbe wowote unaohusu ndugu wa Keti ili waweze kuwapata.
Aliyesoma hili daftari alikuwa ni Sabrina ambapo kwa juu kabisa liliandikwa kwa maandishi makubwa yaliyokolezwa kwa peni na yalisomeka hivi, MAPENZI, Sabrina alianza kusoma kilichoandikwa kwa chini yake,
"Mimi Keti, nimeishi na bibi yangu aliyenipenda sana kwakweli nina kila sababu ya kusema kuwa huyu ndiye aliyekuwa mpenzi wangu wa kweli ingawa naye anakasoro zake. Sijawahi kupata penzi la mama wala la baba kwani hata katika kukua kwangu sikuwahi kuwatia machoni pangu, bibi aliniambia kuwa mama alipopata ujauzito ni hapo baba nae akamkimbia.
Pindi mama alipojifungua mimi akamkimbia bibi kwahiyo hata bibi yangu hakujua mama yangu alipo, ni hapo bibi aliniambia kuwa aliyachukia mapenzi kwani hata yeye alikimbiwa na mume wake, hicho kitu kilimfanya bibi aingie kwenye mambo ya kienyeji. Nilipokuwa mkubwa tu yani siku niliyovunja ungo bibi alinionya na kunisihi juu ya mapenzi, aliniambia kuwa mapenzi ni mabaya sana na akanitaka nisijihusishe na mapenzi kwani nikifanya hivyo nitamsahau yeye. Akanipa dawa ya kunilinda na pia aliniambia kuwa dawa ile itanisaidia mimi nisimpende mwanaume yeyote na wala hakuna mwanaume atakayeweza kunipenda mimi. Kutokana na maelezo ya bibi niliona wazi kuwa ile dawa ilinifaa sana ila nilipozidi kuwa mkubwa na kuona wadada wakiolewa nikatamani na mimi siku moja nivae shela nipendeze kama wao ila hakuna mwanaume aliyewahi kunitongoza wala niliyemtamani.
Nimeandika haya leo kwavile kaja huyu mama na kuniombea ila kwa bahati mbaya aliniambia mimi nisimamie maombi ila sikuweza na kujikuta nikimuwaza huyu kijana humu ndani, na sasa najiuliza je haya ndio mapenzi? Kwanini nimtamani huyu wa ndani na si mwingine wakati najua wazi ana mtu kwanini? Kwanini mapenzi yapo hivi? Ndoto yangu ya kuvaa shela sasa imekuwa kubwa sana, natamani na mimi nivae shela kabla ya kufa kwangu. Kwasasa natamani jambo moja tu, natamani huyu kijana hata anibusu jamani. Kumbe mapenzi ndio yanachanganya hivi? Bibi yangu alikuwa na kila sababu ya kuyachukia mapenzi. Mungu akurehemu bibi yangu, akuweke salamu huko mbinguni nami ipo siku nitakufata ila mapenzi yameshanichanganya bibi, nakukumbuka sana niepushie mbali hili janga bibi yangu ingawa bado nina ndoto ya kuvaa shela"
Sabrina alipomaliza kusoma akamtazama Emmy na kujikuta wakitazamana tu, kisha Emmy akasema
"Keti hakuwa na hatia jamani dah! Dunia hii kweli haina usawa"
Sabrina akakaa kimya kwa muda kisha akamuuliza Emmy,
"Tufanyaje sasa Emmy?"
"Nadhani tutimize ndoto ya Keti, najitolea kwenda kumtafutia shela na tumzike nalo"
Sabrina akaafikiana na hilo kisha wakatoka na kumfata Sakina pale sebleni ambapo walimsomea lile daftari Sakina aliyeonekana kuumia sana na kujiona kama yeye ndiye mwenye makosa ya kumpeleka mama mdogo wa Sam pale aliyemuombea Keti na kumfanya awe katika ile hali aliyoandika kwenye daftari lake.
Wakatoka pale na kurudi nyumbani kwakina Sabrina kulipowekwa ile misiba ya wote wawili.
Walipofika Emmy akawasilisha wazo lake la kwenda kumnunulia Keti shela la kuzikiwa nalo ili tu ajaribu kumtimizia ndoto yake ingawa itakuwa kaburini.
Wakakubaliana na Emmy juu ya hilo ambapo siku hiyo hiyo Emmy alienda kutafuta shela la kumfaa Keti.
Emmy alifanikiwa kupata nguo ambayo aliona wazi kuwa itamfaa Keti ila akamfikiria kidogo Sam kwakweli bado hakutaka kuamini kama Sam amekufa yani hakuamini kabisa kwahiyo muda wote huo alikuwa akijipa matumaini kuwa akienda hospitali basi akute maajabu kama ya wengine yani akute maiti ya Sam imetoweka ila akirudi tena arudi mzima kabisa.
Alipomaliza alirudi na lile gauni pale nyumbani kwakina Sabrina ambapo alikutana na kilio maradufu kwani mama mzazi wa Sam alifika eneo hilo muda huo huo huku akiwa ameongozana na wanawake wengine wawili kutoka Arusha.
Kwakweli mama Sam alilia sana na kuwafanya wengine nao walie kwasababu yake, na alikuwa akilia kwa uchungu kwani alijiona kuwa yeye ndio chanzo cha kumkosesha mwanae huyo mapenzi ya mzazi ukizingatia hakumlea kutokana na vile ambavyo mumewe hakumpenda mtoto huyo.
Kwahiyo huyu mama alijikuta akilia huku akikumbuka mambo mengi sana ambapo rafiki yake wa pembeni aliyekuja nae pia alionekana kujifuta machozi kwa ule uchungu aliokuwa nao mwenzie.
Kilio kikaendelea mahali pale kama kwa nusu saa hizi kisha wakatulia kidogo na kuanza kupeana pole na kuelezana kwa kifupi vile ilivyokuwa.
Mama Sam alishangaa kusikia kuwa kifo cha mwanae kimehusika pia na kifo cha mwingine,
"Jamani kwahiyo tuna misiba miwili!"
"Ndio hivyo, yani tumepatwa na pigo tena pigo kubwa sana"
Huyu mama wa pembeni akachangia kuwa, "Inasikitisha sana"
Wakafarijiana tu na usiku nao ulikuwa umeingia na kufanya waweke mikeka na mito vizuri pale sebleni na kulala.
Emmy alienda kulala chumbani kwa Sabrina akiwa na Sabrina pamoja na wale watoto wa Sabrina.
Wakiwa wamelala, Emmy akajiwa na ndoto. Akamuona Keti katika ndoto akiwa amevaa lile gauni la harusi yani lile shela alilolinunua tena alionekana akitabasamu.
Emmy akashtuka sana, kufumbua macho akamuona mtu akiwa kavaa lile shela na akitabasamu vile vile kama Keti.
Wakiwa wamelala, Emmy akajiwa na ndoto. Akamuona Keti katika ndoto akiwa amevaa lile gauni la harusi yani lile shela alilolinunua tena alionekana akitabasamu.
Emmy akashtuka sana, kufumbua macho akamuona mtu akiwa kavaa lile shela na akitabasamu vile vile kama Keti.
Emmy akashtuka sana kiasi kwamba alijihisi kama kapandwa na presha ila alivyomuangalia vizuri mtu huyo alimuona kuwa ni Sabrina, kwakweli Emmy alichukizwa sana na hili hadi akamuuliza Sabrina kwa ukali kabisa,
"Ndio mambo gani hayo umefanya? Hivi unajua kama unaweza kumuua mtu kwa presha? Kwanini Sabrina unafanya mambo kama mtoto! Kwani hujui kama hilo gauni nimenunua ili tukamvishe marehemu?"
Sabrina akatabasamu kidogo na kujibu,
"Najua"
"Kama unajua ni kwanini umevaa? Hujui kama unajiwekea uchuro lakini Sabrina?"
Emmy alionekana kuchukizwa na kukerwa sana kitu kilichofanya aongee huku akitetemeka. Ikabidi Sabrina awe mpole na aongee kwa ustaarabu ili kumfanya Emmy apunguze hasira alizokuwa nazo,
"Tafadhari Emmy nisamehe, tena nisamehe sana Emmy sikujua kama jambo hili litakukera na wala sikujua kama utawahi kushtuka na kunikuta hivi"
"Sio kunikera tu ila jambo ulilolifanya si sawa kabisa kufanywa na mtu mwenye akili timamu. Hebu livue kwanza hilo gauni na uniambie kwanini ulilivaa"
Sabrina akavua lile gauni, kisha akaenda kukaa kitandani na kumueleza Emmy sababu ya yeye kuvaa lile gauni,
"Sikiliza Emmy, kwanza nisamehe sana kwani najua nimekosa kwa nilichokifanya. Wakati nimelala hapo nimejikuta nikimkumbuka sana Sam, nimejikuta nikikumbuka siku ambayo nilifunga ndoa na Sam. Kwakweli siwezi kuisahau siku ile katika maisha yangu, pia nimeyakumbuka maneno ambayo Keti aliandika kwenye barua yake kuwa anatamani kuvaa shela katika maisha yake. Hata mimi nilivaa shela ila haikuwa sababu ya kunifanya nifurahie ile ndoa kwani ilikuwa ni ndoa yenye masharti na mateso, halafu mwisho wa siku nikaja kugundua kuwa niliolewa na kaka yangu iliniuma sana. Nimejiuliza sana, je kuvaa shela ndio furaha ya maisha? Je ndio furaha ya mwanamke? Au je kuvaa shela ndio mapenzi? Ndipo nilipoinuka na kuchukua hilo shela na kulivaa kwani hata mimi binafsi nimesahau ladha ya shela, nadhani hata Keti mwenyewe hakufikiria kwa makini kuhusu shela. Nilivaa na kutabasamu kwani moja kwa moja kichwani mwangu nilimuwaza Keti na Sam, pia najua hili ni jambo litakalonifanya nisiwasahau kamwe"
"Sabrina sitaki kukulaumu sana kwani akili yako sijaijua vizuri ila siku nyingine usifanye kitu kama hiki bila kuuliza. Kwanza kaa ukijua kuwa ni ngumu sana kuielewa furaha ya mwanamke moja kwa moja na ni vigumu sana kuyaelewa mapenzi. Mimi nimenunua shela ili tu kumfanya Keti aende kwa furaha huko aendako ingawa hakuna anayejua siri ya huko ila usije ukajaribu siku nyingine kufanya kama hiki ulichofanya"
"Hakitojirudia tena Emmy, nisamehe kwa hilo"
Kisha wakaendelea na mazungumzo mengine kwani hawakujisikia tena kulala kwa muda huo.
Kulipokucha, walitoka nje na kuendelea na shughuli za hapa na pale kwaajili ya mazishi kwani siku hiyo ndio waliyopanga kwaajili ya mazishi.
Mama mdogo wa Sam alikuwa karibu na mama yake Sam pamoja na wale wanawake wawili ili kumtia moyo dada yake na kumpa maneno ya ujasiri kwani muda mwingi alionekana akilia tu.
"Dada, usilie hivyo kumbuka kulia sana ni kumkufuru Mungu. Hebu niangalie mimi mdogo wako, unafikiri sijaumia dada? Fikiria nimeishi miaka mingapi na Sam! Fikiria tu hilo, Sam alikuwa mwanangu, furaha yangu yani alikuwa ndio kila kitu kwenye maisha yangu. Nilimpenda sana, alipokuja akilia nilikuwa nalia nae kwani alikuwa ni mtu pekee anayejua uchungu wangu. Ila alipokua na kutaka kujitegemea nilimuacha aende kwani kila jambo na wakati wake, na sasa wakati wake wa mwisho umefika kwakweli nimeumia sana ila sitaki kumkufuru Mungu"
Aliongea haya huku akijifuta machozi kwani ilikuwa wazi kuwa na yeye ana maumivu ya moyo kama waliyokuwa nayo wengine. Tena inawezekana yeye ni zaidi kwani ndiye aliyemlea Sam.
Maneno ya huyu mdogo wake kidogo yakamfanya mama Sam nae anyamaze ingawa alitokwa na machozi kwani kila akikumbuka sababu iliyomfanya ashindwe kumlea mwanae ndio iliyomfanya aumie zaidi.
Hawa wanawake wawili waliokuja na mama Sam nao walikuwa karibu nae sana.
Muda kidogo baba Sabrina akasogea kuwasalimia kwani aliambiwa toka jana kuwa wamekuja ila kwavile na yeye akili yake haikuwa sawa ikafanya asiweze kusogea kuwasalimia ila leo alijikaza na kuwafata.
Kwakweli mama Sam alipomuona huyu baba ndipo machozi yalimtoka zaidi na kujikuta akilia tena ila huyu baba Sabrina alipogeuka ili kumsalimia huyu mwanamke mwingine kati ya walioambatana na mama Sam wakajikuta wakiangaliana na mwanamke huyu kwa muda kidogo ambapo huyu mwanamke alimuuliza baba Sabrina,
"Si Deo wewe!"
Baba Sabrina akawa kimya kwa muda,
"Umenisahau mimi Bahati!!"
"Kheee Bahati kumbe upo!"
"Ulifikiri nimekufa? Nipo ndio, mwanaume mshenzi sana wewe"
Baba Sabrina akaona isiwe tatizo hivyobasi akainuka na kurudi zake ndani.
Mama Sam akamuangalia huyu aliyekuja nae na kumuuliza,
"Bahati, kumbe unamfahamu Deo?"
"Ndio namfahamu vizuri sana mwanaume mshenzi huyu alinikimbia nikiwa na mimba changa kabisa"
"Kheee pole mwaya, mi mwenyewe huyo Sam ndio nilizaa nae"
"Bahati yako kama alikuhudumia"
"Anihudumie wapi? Ni historia ndefu, mtoto mwenyewe kaja kumjua na ukubwa wake tena akiwa kamuoa binti yake"
"Kheee huyu Deo ni kichefuchefu jamani, ptuuu"
Akafanya kama anatema mate na kujikuta wakianza kumjadili Deo wakati huo kwani ilikuwa kamavile kuna mambo ya nyuma kawakumbusha watu hawa.
Baba Sabrina alirudi ndani na kwenda moja kwa moja chumbani, akakaa kitandani na kuanza kujaribu kukumbuka vizuri kuhusu huyu Bahati.
Akakumbuka alipokuwa Singida kikazi ndipo alikutana na huyu Bahati kipindi hicho akiwa ni binti.
Akawa nae kwenye mahusiano ila kama kawaida yake hakumuamini kwani hakuwa na kawaida ya kumwamini mwanamke tofauti na mke wake.
Akakumbuka siku moja Bahati alimtaka wakamtembelee mama yake, naye alikubali na walipofika ndipo bahati akasema mbele ya mama yake kuwa ana mimba ya Deo huyo mama nae hakulaza damu akasema kuwa inatakiwa huyu Deo amuoe Bahati ili mtoto azaliwe ndani ya ndoa kwani ndio mila zao, akakumbuka maneno ya yule mama kuwa iwapo mtoto atazaliwa nje ya ndoa kikwao basi mtoto huyo hawezi kudumu na atakufa tu.
Deo akakumbuka kuhusu hilo swala, pia akawaza kuwa kipindi hicho yeye tayari alikuwa ameshaoa hivyobasi akaona njia bora ni kukubaliana nao ili awakimbie na ndivyo alivyofanya na toka kipindi hicho hakukanyaga tena mji wa Singida.
Alijifikiria sana na kujiambia,
"Ama kweli milima haikutani lakini binadamu hukutana. Kwakweli sikujua kama ipo siku mimi nitakutana tena na huyu mwanamke wa kuitwa Bahati. Ngoja tukimaliza kuzika nimuulize vizuri kuhusu mtoto na je kama alikuwa na mimba kweli au ilikuwa namna ya kunivuta ili nimuoe"
Muda kidogo mkewe akaingia mule chumbani na kumfanya akatishe mawazo yake ya muda huo.
"Baba Sabrina unahitajika huko uongozane na vijana wale kufata maiti hospitali. Si unajua sisi ndio wahusika!"
"Naelewa mke wangu ingawa bado siamini kuwa Sam amekufa"
"Hakuna anayeamini ila ndio hivyo mume wangu, kazi ya Mungu haina makosa. Wanao wengine nao wameshafika nao wanakusubiri uende nao huko hospitali"
"Kwahiyo James na Sam mdogo wamefika?"
"Ndio, wapo nje wanakusubiri"
Ikabidi ajitayarishe kisha akatoka na kukutana na vijana wake ambao walimkumbatia kama ishara ya kumpa moyo baba yao kisha akatoka nao na kuongozana na vijana wengine kwaajili ya kumuandaa Sam kwa mazishi, kisha na wamama nao ambao waliongozana na Sakina na Emmy kwaajili ya kumuandaa Keti kwa mazishi.
Pale nyumbani alibaki Sabrina na watoto wake, mama Sabrina, mama Sam, mama mdogo wa Sam na wale rafiki zake pamoja na watu wengine ambapo mama Sam aliweza sasa kumjulisha yule Bahati kuwa amfahamu mke wa Deo, ni hapo walipoikoleza mada yao tena,
"Unajua wanaume hawa ni tamaa tu zinawasumbua, mbona mkewe mzuri tu! Na kama anajiona kuwa hawezi kuhimili masafa marefu basi angekuwa anasafiri na mke wake"
"Bahati unaongea kamavile wanaume huwajui vizuri, yani mwanaume hata aoe malaika ila kuridhika kwake ni mwiko. Kwa kifupi ni kuwa mwanaume hana kawaida ya kuridhika, atataka tu radha tofauti. Yani mwanaume hata uwe unamuogeshea maziwa hawezi kuridhika"
"Najua ni ngumu ila basi wajiheshimu kidogo, unajua wanatutesa sana! Kwakweli wanaume wanatutesa jamani dah!"
Walimuongelea Deo kwa mabaya tu bila ya kujua kuwa mkewe alimuona Deo kama ndiye mwanaume bora duniani.
Walifika hospitali huku Emmy akitamani kuwa utokee muujiza wowote ule na iwe ni uongo kuwa ndugu zao hawa wawili hawajafa ila waliingia mochwari na kukuta maiti zipo vizuri tu ila bado Emmy alihisi kuwa watu hawa watakuwa bado wamelala.
Waliwatayarisha vizuri kabisa kwaajili ya mazishi.
Emmy alipowakabidhi tu lile gauni la kuvalishwa Keti alitoka nje na kukaa kwenye benchi ambapo machozi yalimtoka kwa kasi sana, katika hali ile ya kulia alijihisi akitaka kutapika na kumfanya kutoka nje kabisa na kwenda kutapika ambapo Sakina alimfata kwa nyuma na kumshika hadi alipomaliza kutapika na kuanza kumpa pole,
"Huenda umepatwa na homa pia Emmy, itabidi tukimaliza mazishi na shughuli hizi za msiba ukapime"
"Hata usijali dada yangu, nadhani ni sababu ya kulia tu ila nitakuwa sawa"
Walikaa pale nje wakiwasubiri waliokuwa wakiandaa marehemu na walipomaliza walitoka nao pamoja huku jeneza za wale marehemu zikipakizwa kwenye gari.
Jambo hili lilimuumiza sana Emmy kwani alizidi kuona dhahiri kuwa Sam na Keti wamekufa na kumfanya atokwe na machozi zaidi.
Wakapanda kwenye gari nyingine huku akiwa analia sana huyu Emmy.
Nyumbani yakaandaliwa mazingira yote ya kuweza kuwaaga hao marehemu pindi maiti zao zikifika na pia wale wachimba kaburi walishafanya hivyo kwenye eneo la makaburi ambalo walielekezwa kwahiyo kilichobaki ni kuwasubiri walioenda hospitali ili kutoa heshima zao za mwisho na kwenda kuzika.
Sabrina alikuwepo tu kamavile mtu asiyejielewa kwani kuna wakati mwingine aliona mambo haya kuwa kama ndoto tu.
Kwavile Jeff nae alikuwepo eneo hilo hivyo akaona vyema kumfata Sabrina na kuzungumza nae kiasi.
"Nakuona ukiwa na mawazo sana Sabrina ila yote haya ni mipango ya Mungu"
"Hata kama Jeff, kwanini iwe sasa? Kwanini Sam asingesubiri kipindi kingine ndio afe, kwanini afe kipindi hiki?"
"Sabrina tusimkufuru Mungu bure, kila kitu anapanga kwasababu na wakati wake. Hakuna anayejua mbele yake kuna nini, punguza mawazo na kuwa makini na watoto"
Jeff akatoka huku akiamini kuwa alichomwambia Sabrina kitamsaidia kwa kiasi fulani.
Jeff alipokuwa nje ya nyumba ya kina Sabrina akamuona baba yake pamoja na watu wengine na kugundua kuwa kumbe baba yake nae alihudhuria msiba huu, ila alimsikia akisema
"Hatimaye kijana aliyesababisha kifo cha mwanangu Amina nae amekwenda na maji, afadhari nitaishi kwa amani sasa"
Hapa Jeff akaona ni jinsi gani kifo cha Sam kimewaumiza wengine na wengine kuwafurahisha.
Pia akatambua kwamba si kila anayehudhuria msiba wako basi ameguswa na msiba huo.
Waliporudi kutoka hospitali, moja kwa moja ikatakiwa kuanza shughuli ya kutoa heshima za mwisho ili waende kuzika.
Ila kabla ya kuaga, Sabrina aliomba aisome tena ile barua iliyoachwa na Keti kwani alihisi kuwa pengine kuna watu wanaweza kusaidiwa na ile barua ingawa kwa kifupi maisha ya Keti yalikuwa ya kusikitisha ingawa waliojua kuwa Keti na Sam walikutwaje wakati wamekufa ni wale wale kati ya waliowakuta na ndugu wa karibu tu.
Sabrina alisoma ile barua, ikawasikitisha wengi kwavile hawakugundulika ndugu wa Keti yani alizikwa ugenini.
Shughuli ya kutoa heshima ya mwisho ilianza ambapo kama kawaida walianza watu wengine kisha ndugu, kila mmoja alipita na kulia kivyake ila alipopita huyu mama aliyekuja na mama Sam yani yule Bahati alionekana kusimama muda mrefu sana kwenye jeneza la Keti, kisha akaonekana kutahamaki na kusema,
"Haiwezekani, haiwezekani kabisa nasema haiwezekani"
Kisha akaonekana kukimbilia ndani, hakuna aliyemuelewa na wote walikuwa wakimshangaa tu.
Muda kidogo akatoka akiwa ameshika picha mkononi na aliwakuta vijana tayari wakitaka kufunika lile jeneza, aliwakataza akachukua ile picha na kuiweka pembeni ya marehemu, mara gafla wakamshangaa akianguka chini.
Muda kidogo akatoka akiwa ameshika picha mkononi na aliwakuta vijana tayari wakitaka kufunika lile jeneza, aliwakataza akachukua ile picha na kuiweka pembeni ya marehemu, mara gafla wakamshangaa akianguka chini.
Ikabidi watu wamuinue pale chini na kwenda kumuweka pembeni ila Emmy alienda kuitoa ile picha kwenye jeneza la Keti kabla hawajalifunika tena.
Aliishika ile picha huku akiangalia jeneza la Sam kwani alitamani utokee muujiza wowote kuwa Sam aamke ila ndio hivyo Sam hakuamka wala nini na kumfanya Emmy aumie moyo zaidi, hadi wanapakia yale majeneza kwenye gari kwaajili ya kwenda kuzika bado Emmy alikuwa haamini amini kuhusu kifo cha Sam na Keti haswa kifo cha Sam.
Emmy nae alipanda kwenye gari kwaajili ya kwenda kuzika huku ile picha aliyoitoa kwenye jeneza la Keti ameiweka kifuani kwani hakutaka kuiangalia kwa muda huo na wala hakutaka kuipoteza kwani alihisi kuwa huenda picha hiyo inamaana kubwa sana.
Nyumbani alibaki mama Sabrina, shangazi wa Sabrina wakiwa karibu na yule mwanamke aliyeanguka na kujulikana kwa jina la Bahati.
Mama Sam alitaka kubaki na huyu aliyeanguka ila hakuweza kwani alitaka kushuhudia kabisa mwanae akizikwa ukizingatia hakuwa na imani kuwa mwanae amekufa kweli kwahiyo alitamani hata utokee muujiza wowote ule mwanae afufuke.
Sabrina nae hakwenda makaburini ila alikuwa amejifungia chumbani na watoto wake akilia kwani hakuamini kabisa kama aliyemuona kwenye jeneza ilikuwa ni Sam kweli.
Sabrina aliwashika hawa wanae wawili akilia kwa uchungu sana kwani alijikuta akimkumbuka Sam na mazuri yake licha ya mabaya aliyomfanyia ila Sabrina kwa siku ya leo aliona mabaya yote ya Sam kuwa ilikuwa ni sehemu ya mapenzi kwani aliwaza ni jinsi gani huyu Sam alimpenda.
"Yani kweli kabisa sitakuona tena Sam wangu? Kweli kabisa! Hivi ni mwanaume gani mwenye upendo kama wako Sam? Hukujua kama mimi ni dada yako ila ulinipenda sana na hukutaka kunidhuru. Nimezaa na mwanaume mwingine, ulichukizwa juu ya hilo ila ukaendelea kunipenda na ukawapenda watoto wangu kama wanao Sam? Hivi hawa watoto nitawasimuliaje kuhusu wewe Sam? Mwanaume mwenye upendo na mapenzi ya kweli, huwa nakukera, unachukia ila hujawahi kuthubutu kunidhuru ingawa uwezo huo unao. Ukanifichia aibu yangu ya kuzaa na Jeff ingawa sasa mambo yapo hadharani, hivi ni nani wa kufanana na wewe Sam? Siwezi kukusahau kamwe katika maisha yangu, mume wangu, rafiki yangu, kaka yangu, mwalimu wangu, siwezi kukusahau Sam"
Sabrina alikuwa akilia kwa uchungu sana huku na yeye akitamani muujiza wowote utokee ili wale walioenda kuzika warudi na Sam akiwa mzima kabisa.
Walifika makaburini na shughuli ya mazishi ikaendelea ambapo ilifanyika sala kidogo kisha wakaanza kuzika.
Kile kitendo cha kutia mchanga kwenye kaburi kilimpa simanzi sana kwani hapo ndipo aliamini wazi kuwa ni mwisho wa yeye kumuona Sam tena katika macho yake na kwakweli alilia sana, kitu ambacho kilifanya watu wamshikilie kwani alionekana kuchanganyikiwa zaidi.
Ikabidi Jeff amshike Emmy na kwenda kumpakiza kwenye gari ili amuondoe eneo lile kwani Emmy alionekana kulia kiasi cha kuanza kuishiwa na pumzi.
Kwakweli Jeff alimuhurumia sana Emmy kwani hata yeye binafsi alijikuta akimkumbuka Sam kwani kwa upande wake Sam alikuwa ni mtu wa pekee sana kwake ukizingatia ni mwanaume gani agundue unatembea na mke wake na bado akuhurumie kukuadhibu au akupe kazi kwenye kampuni yake ili kuendeleza kipato chako? Jeff alifikiria sana na kujiona wazi kuwa hata yeye hawezi kuwa na moyo aliokuwa nao Sam, hii hali ilimfanya Jeff atokwe na machozi kwani hata yeye uchungu ulimshika huku akichungulia kwa mbali jinsi kaburi la Sam lilivyozidi kufukiwa.
Alimshikilia Emmy kwa uchungu kwani wote kwa wakati huo walijikuta wakitokwa na machozi.
Shughuli ya mazishi ilipoisha watu waliagana hapo makaburini kwani hapakuwa na sababu ya kurudi kwa wafiwa na kilichobaki ilikuwa ni tanga ndugu.
Watu wengi waliosikitishwa na msiba wa Sam ni wale waliohudhuria harusi ya Sam na Sabrina kwani walikumbuka vyema jinsi walivyokula na kunywa kwenye sherehe hiyo tena bila ya kuchangishwa michango ya aina yoyote ile.
Wengi hawakuyajua vyema maisha ya Sam na Sabrina kwani walichokijua wao ni mke na mume pia kutokumuona Sabrina makaburini hawakushangaa sana kwani walijua kuwa ameachiwa pigo kubwa sana la ujane na watoto wake kuwa yatima kwahiyo walimuhurumia sana Sabrina.
Safari ya kurudi nyumbani ilimfanya Jeff azidi kuwa karibu na Emmy kwani aliweza kuigundua vyema akili ya Emmy kuwa haipo sawa kwa wakati huo, na aligundua jinsi gani Emmy kapatwa na pigo kubwa juu ya kifo cha Sam kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu sana kuliko wengine.
Walirudi nyumbani na kuanzisha kilio kama ishara ya kuendelea kuwaaga wale marehemu kwani bado waliumizwa sana na kifo cha hawa watu.
Walilia kwa muda kidogo kisha kila mmoja kuanza kumtuliza mwenzie.
Shangazi wa Sabrina alijaribu kuwatuliza huku na yeye akielezea jinsi alivyomfahamu Sam.
"Jamani jinsi tunavyolia sana mjue tunamkufuru Mungu kwa maamuzi aliyoyafanya inatakiwa tushukuru kwa yote. Kwa kipindi nilichomfahamu Sam alikuwa ni kijana mstaarabu sana, kijana ambaye hajawahi kunikosea heshima hata siku moja. Najua tunalia kwa uchungu ila bado tujue kuwa Mungu ni mwema"
Mama wa Sam akadakia kwa kuuliza,
"Kama Mungu ni mwema kwanini amchukue mwanangu mimi? Jamani yule mtoto wangu bado nilihitaji sana kuwa nae karibu kwanini Mungu amchukue?"
Sakina nae akaongezea,
"Licha ya hivyo, kama Mungu ni mwema kwanini aruhusu Keti aombewe ili apatwe na hisia za mapenzi zilizosababisha kifo chake? Kwanini Mungu aruhusu haya kutokea kwa Keti, kwanini amfanyie hivi Keti jamani?"
Muda huu ilikuwa kama wamemuamsha mama mdogo wa Sam azungumze kwani hakuona sababu ya wao kumlaumu Mungu wakati ni watu wengi sana wanakufa,
"Jamani mnapoelekea sasa ni pabaya, naomba mtambue jambo hili kuwa Mungu halaumiwi wala hakosei. Chochote kinachofanywa na Mungu kipo sahihi na hukifanya kwasababu ambazo kwa haraka sisi wanadamu huwa hatutambui sababu hizo. Tunatakiwa kushukuru kwa kila jambo, Mungu ni mwema kwetu. Mimi ni binadamu na nina maumivu kama wengine ila siku zote huwa nakumbuka kwamba Mungu halaumiwi wala hakosei"
Wote walikaa kimya kwa muda kwani maneno ya huyu mama yalionekana kuwaingia kwenye akili zao vilivyo kwahiyo wakajikuta wakiwa kimya tu kamavile watu wanaotafakari maneno yaliyozungumzwa muda mfupi uliopita.
Muda kidogo yule mama aliyeanguka na kuzimia sasa alizinduka.
Aliyekuwa wa kwanza kumuuliza alikuwa ni mama Sam kwani ndio rafiki yake aliyekuja nae na hata yeye hakuelewa kwanini rafiki yake alizimia.
"Unajisikiaje Bahati"
"Sijisikii chochote, yuko wapi Keti?"
Wote wa pale wakatazamana, ni Sakina ndiye aliyemjibu,
"Tumeshamzika Keti"
Huyu mama alipiga tena yowe la kilio,
"Uwiii mwanangu mimi jamani, Keti mwanangu jamani, Keti roho yangu kwanini umenipa adhabu hii? Jamani Keti wangu mimi"
Alilia kwa muda kidogo, mama Sam akamuuliza
"Keti ni mwanao kivipi? Mbona sijawahi kukusikia kuhusu huyo mtoto?"
"Keti ni mwanangu tena ni mwanangu kabisa nilizaa na hilo lishenzi"
Akimnyooshea kidole Deo, wote wakabaki kimya kwani ilikuwa ni kitu cha kuwashangaza na kuwastaajabisha kuwa imekuwaje kuwaje hilo jambo.
Mama Sabrina alimuangalia mumewe kwa jicho la mshangao na kamavile mtu anayemuuliza kama kuna ukweli juu ya lile jambo.
Deo alibaki kimya kwani hata yeye alikuwa kamavile haelewi kinachozungumziwa ila mama Sabrina alimuuliza Bahati ingawa alikuwa akilia ila alipenda kujua ukweli wa alichokisema,
"Ulizaa na huyu kivipi mbona sikuelewi?"
"Nilizaa nae kivipi? Nilizaa nae kama ulivyozaa nae wewe, mwanaume mbwa sana huyu"
Aliongea kwa jazba tena huku akilia, watu wakagundua kuwa huyu mama kapaniki na kuamua kuingia nae ndani ili kujaribu kumtuliza kwanza.
Hakuna aliyemuelewa huyu Bahati kwa wakati huu kwani hata Deo alionekana kimya kabisa, kisha wote wakaingia ndani kabisa ili kuepusha kuwafaidisha watu wengine.
Walipokuwa ndani ndipo Emmy alipoitoa ile picha ambayo huyu mama aliiacha kwenye jeneza la Keti, kisha akaiangalia.
Ni kweli ilionekana kuwa ni picha ya Keti ingawa muonekana wako ulionyesha kuwa ilipigwa kipindi cha nyuma sana kwani Keti alionekana kuwa binti mdogo wa kipindi hiko.
Emmy aliiangalia sana ile picha kisha akawapa wengine ambapo huyu Bahati aliidai picha ya mtoto wake na kisha kumkabidhi mwenyewe.
Muda huu kimya kidogo kikatawala kisha huyu huyu Bahati akaongea tena,
"Yani Sabra nilijua nakuleta kwenye msiba wa mwanao kumbe nakuja kwenye msiba wa mwanangu pia? Jamani Keti hukutaka hata kuniona mama yako jamani! Nisamehe mwanangu, yani ndio sikupati tena? Mama yangu amekufa, na wewe kipenzi changu umekufa nitakuwa mgeni wa nani mimi jamani!"
Ikabidi mama Sam afanyekazi ya kumbembeleza rafiki yake huyu ila mama Sabrina bado hakuweza kuvumilia na sasa akamuuliza mumewe,
"Deo hebu tuweke wazi kumbe Keti nae alikuwa mwanao?"
"Mi sijui"
Bahati akadakia tena,
"Hujui nini? Ulivyoniacha na mimba ulitegemea nimezaa jiwe? Nilijifungua mtoto wa kike ambaye ndiye Keti yani Keti mwanangu mimi katoka tumboni mwangu ndio amekufa bila hata ya kumuona na kuongea nae jamani"
Mama Sabrina akamuangalia shangazi wa Sabrina na kumwambia,
"Haya sasa kipindi kile umenishikilia mimi sijui msaliti sijui nini na nini hadi ukafanya maisha niyaone machungu tena ukumbuke kuwa yote yale yalinipata bila hata kutarajia, haya sara huyu kaka yako unamuweka kwenye kundi gani?"
Kisha mama Sabrina akamuangalia Deo na kumuuliza,
"Hivi ni kitu gani kilikushinda Deo kuwalea hao watoto? Hivi ni laana gani umeweka kwenye familia? Kuwalea watoto wa ndani vizuri wakati wa nje wanateseka si jambo jema na ndiomana kila leo familia inapatwa na matukio ya ajabu ajabu kumbe ni sababu yako Deo, kwakweli hiki kitu kitakutafuna maisha yako yote."
Mama Sabrina alionekana kuongea kwa jazba sana ikabidi shangazi wa Sabrina aingilie kati,
"Jamani huu sio wakati wa malumbano maana jambo kama limetokea basi tuelewe wazi kuwa limeshatokea kwani hata tukilaumiana hatuwezi kupata muafaka wala kurudisha mambo nyuma ili yaanze upya, kama kutokea imeshatokea tayari"
Deo akainuka na kuelekea chumbani.
Sabrina akiwa ni mtoto pekee anayemuelewa baba yake vilivyo alijikuta akimfata ili aweze kuzungumza nae kwani alitambua wazi kuwa baba yake ameshachanganyikiwa ukizingatia hao hao watoto zake waliojulikana kuwa aliwakimbia wote wawili walikufa pamoja.
Pale sebleni, shangazi wa Sabrina alisogea karibu na Bahati ili aweze kuzungumza nae kwa undani zaidi kuhusu Keti.
Sabrina nae alijaribu kuzungumza na baba yake ambaye kwa muda huo alionekana kutotaka kuongea na mtu yeyote yule.
"Baba tafadhari naomba uongee na mimi mwanao Sabrina"
"Je Sabrina mwanangu bado utanipenda?"
"Nakupenda baba yangu, wewe ndio mzazi wangu na sina sababu ya kukuchukia baba. Yote yaliyokutokea ni changamoto za maisha tena wengi sana watajifunza kupitia wewe baba, tafadhari hata usichanganyikiwe kwani tayari yameshatokea na tuyaache yapite"
"Kwakweli kama ni changamoto basi najutia ujana wangu tena najutia sana Kwani ujana ndio uliofanya yote haya ila kikubwa najutia mapenzi yangu tena najutia sana vile nilivyompenda mama yenu"
Sabrina alimuelewa vizuri baba yake hivyo akamtaka apumzike kwanza kisha kumpa maneno ya faraja na kumwambia kuwa watazungumza zaidi.
Kisha Sabrina akatoka mule chumbani na kumuita mama yake kwa pembeni huku akijaribu kuongea nae kuwa asimseme vibaya baba yao.
"Mama tafadhari mama yangu usimseme vibaya baba, tuliowapoteza inatosha mama kwakweli sipo tayari kuona tukimpoteza na baba. Tafadhari mama yangu"
"Sabrina unaongea kamavile hujui uchungu wa mtoto, mimi sitaongea nae vibaya ila kwa kifupi inauma."
Mama Sabrina akarudi kwa wenzie kwani usiku ulishaingia na sasa wakajiandaa kulala huku kila mmoja akiwa na mawazo yake.
Kulipokucha Sabrina akazungumza na Sakina na kuona kuwa ni vyema wakienda kuchukua vitu vya Keti ili wamkabidi yule mama yake.
Hivyobasi wakaondoka mahali pale wakiwa wameongozana Sabrina, Sakina, Emmy na Jeff.
Walifika nyumbani kwa Sakina na hali ya ukimya ikiwa ile ile huku gari ya Sam ikiwa pale pale nje kwani hakuna aliyeitoa gari ile.
Walipoingia ndani ndipo Sabrina alipoona funguo za gari ya Sam zikiwa kwenye kochi.
Wakati Emmy na Sakina wakielekea chumba alichokuwa analala Keti enzi za uhai wake huku wakiambatana na Jeff, wakati huo Sabrina alitoka na zile funguo hadi nje kwenye gari ya Sam.
Alifungua gari hiyo ambapo kwenye kiti cha dereva akaona bahasha kubwa ambayo nje iliandikwa kwa herufi kubwa SABRINA.
Kwakweli Sabrina alishtushwa na bahasha hii, akajikuta akiifungua huku akitetemeka.
Wakati Emmy na Sakina wakielekea chumba alichokuwa analala Keti enzi za uhai wake huku wakiambatana na Jeff, wakati huo Sabrina alitoka na zile funguo hadi nje kwenye gari ya Sam.
Alifungua gari hiyo ambapo kwenye kiti cha dereva akaona bahasha kubwa ambayo nje iliandikwa kwa herufi kubwa SABRINA.
Kwakweli Sabrina alishtushwa na bahasha hii, akajikuta akiifungua huku akitetemeka.
Ile bahasha ndani ilikuwa na karatasi lenye mtindo wa barua.
Sabrina aliifungua na kuanza kuisoma ambapo iliteka hisia zake zote na kugundua kuwa ile barua kweli iliandikwa na Sam.
Ilikuwa ikisomeka hivi,
"Kwako Sabrina, nimeamua kuandika hii barua kwako ili nikueleze yaliyo moyoni mwangu kwani nimeona kwa kuyaongea naweza nisimalize na wala usinielewe chochote.
Kwanza kabisa nakumbuka ahadi niliyokupa ya kukusimulia kuhusu maisha yangu ila baadhi ya mambo nitayaandika humu ila mengine nikipata nafasi ya kuzungumza nawe basi nitakwambia ila sitaki kuzungumza nawe kwanza ndiomana nikaandika hii barua, pia napenda kukupa pole kwa yote uliyopitia kwasababu yangu. Pole sana Sabrina kwani nimefanya uingie kwenye mitihani mikubwa sana ya maisha.
Ila kabla ya yote napenda kukiri wazi kuwa katika maisha yangu hakuna mwanamke niliyewahi kumpenda kama wewe Sabrina kwakweli nakupenda sana tena sana, ila tu nilishangaa siku niliyogundua kuwa wewe ni dada yangu, kwakweli mpaka naandika hii barua bado najiuliza Je haya ndio mapenzi? Na kama ndio mapenzi kwanini nikupende wewe kiasi hiki wakati ni dada yangu? Kwakweli sipo tayari kukuona ukiishi na mwanaume mwingine ndiomana ukaona nikifanya yote yale.
Sikuwa na nia ya kukutesa wala kukuumiza ila tu sikuwa tayari kukuona ukiishi na mtu mwingine. Bado najiuliza kama naweza kuendelea kukubaliana na hali hii kwenye akili yangu.
Nakupenda sana sana Sabrina, sijui hata nieleze vipi ili ujue ni kiasi gani nakupenda mpenzi wangu, mke wangu na dada yangu.
Mwanzoni kabisa nilipogundua kuwa una mimba ya mtu mwingine niliumia sana ila kwavile nilikupenda nikajitolea kukuoa hivyo hivyo na pia nikajitolea kuelea mtoto.
Toka mwanzo niligundua kuwa Jeff ndiye mwizi wangu ila sikuweza kumdhuru kwavile nilijua wazi kuwa nitakuumiza mwanamke nikupendaye, nadhani unaweza kupata picha ni kiasi gani nakupenda Sabrina.
Mtoto wako wa kwanza ambaye ndiye mtoto wetu nilimpa lile jina kwa malengo mahususi kabisa.
Kwanza kabisa tambua kuwa lile jina lilikuwa ni jina la jini aliyekuwa akinilinda mimi, tafadhari usichukie wala usipaniki na wala usimbadilishe mtoto jina.
Utaelewa tu kwanini nilimpa jina hilo, sikuwa na nia mbaya kumpa jina hilo mtoto wetu ingawa lilikuwa ni jina la jini kwani nilikuwa na sababu zangu zingine kabisa kutoa hilo jina ila yule jini alipoona nimempa jina hilo mtoto naye ndio akatumia mwanya huo kuonekana na sikuweza kumzuia kwani ni jini ambaye alikuwa akinisaidia sana na ndiye niliyekabidhiwa kwa yule mganga.
Hata aliponigeuka kwakweli mwenye kosa alikuwa ni mimi kwavile nilikosea masharti ambayo alinipatia.
Kwakweli nakiri wazi kuwa huyu jini amenitesa sana na pia kawatesa na nyie msiokuwa na hatia, kwakweli namshukuru sana Emmy kwani amesaidia kwa kiasi kikubwa sana hadi tumeweza kumtokomeza yule jini, ila shukrani zangu kubwa nazitoa kwa mama yangu mdogo kwakweli huyu mama ni mwanamke wa pekee na tofauti sana kwani nilikuwa nikimwambia maneno machafu ila hakuacha kuniombea na wala hakuacha kunitakia mambo mazuri.
Kwa kifupi ni kuwa Emmy amefanya nipone kabisa na niweze kuwa mwanaume wa kawaida, ila je nitawezaje kuishi na Emmy wakati nikikuangalia wewe ukiishi na Jeff? Ni kweli Emmy ni mwanamke mzuri sana tena ni mwanamke anayevutia ila kwanini nampenda kawaida tofauti na ninavyokupenda wewe? Mapenzi gani haya? Nakumbuka yule mganga aliwahi kuniambia kuwa kwa dawa anazonipa nisithubuu kulala na dada ambaye nimezaliwa nae kwa baba mmoja kwani itasababisha nipotee na huyo dada apotee pia ila nilimwambia mganga asiwe na shaka kwavile mimi sina baba kwahiyo nipo salama kwa hilo.
Kwakweli siku nagundua kuwa wewe ni dada yangu nikakumbuka maneno ya yule mganga kuwa ningekupoteza nami ningepotea.
Kwakweli Sabrina kwasasa nitaamua jambo moja tu, nataka kwenda mbali kabisa na wewe ili nikaanzishe familia huko. Kama Emmy akikubali basi nitaondoka nae, napenda uishi na furaha Sabrina ila sipendi kuona ukiishi na mwanaume mwingine zaidi yangu na ndiomana naamua hivi kwenda mbali kabisa na wewe kipenzi cha roho yangu.
Utawaambia Cherry na Sam kuwa nawapenda sana na kamwe sitoacha kuwapenda kwani kwangu mimi hao bado ni wanangu na siku zote nitawapenda.
Cherry akikua mwambie anisamehe kwani halikuwa lengo langu kumuhusisha na maswala ya majini. Nilipenda awe kawaida tu ila ndio hivyo yule jini alikuwa anajivisha kwenye mwili wa Cherry, nisameheni sana kwa hilo. Nampenda sana Cherry mwanangu tena sana.
Huyo Sam ni kwavile mliniwahi na kumpa jina langu ila mimi ningemuita Jeff ili awe shujaa na jasiri kama Jeff kwa kupigania penzi lake bila ya kujali kuwa mtu anayepigania nae ni mtu wa aina gani.
Ila kama mtapanga kuwa na mtoto mwingine basi mmuite Jeff au Francis kwani huyu Francis nae ni mwanaume wa ajabu sana yani alikuwa akinishangaza vile anavyojitoa kukusaidia mwanamke wake wa zamani.
Nina mengi ya kuandika Sabrina ila yote haya ni sababu ya mapenzi yangu kwako, nakupenda sana Sabrina.
Sasa ngoja nikwambie kikubwa kilichofanya niandike hii barua, sababu kubwa ni kumuhusu Cherry, yani huyu ndiye aliyefanya niandike barua hii na kukwambia hisia zangu. Jambo kubwa hapo ni kuhusu mali zangu.
Sabrina mali zangu zote niliandika mrithi ni Cherry tena hapo ni kabla hajazaliwa yote hiyo ni kwavile nililipenda hilo jina na pia huyo jini alikuwa ni mlinzi wangu mzuri sana.
Nilikuwa na ndoto za kuwa na mtoto na ndiomana niliandika kuwa mrithi wangu ni mtoto wangu Cherry, kwahiyo chochote kitakachotokea katika maisha yangu basi ujue wazi kuwa mrithi wangu si mwingine bali ni Cherry na hati zote za mali zangu pamoja na stakabadhi zipo kwa yule rafiki yangu mwanasheria wangu.
Huyu mtoto Cherry nampenda sana, akikua mwambie nampenda sijui utatumia jina gani kunitambulisha kwake, sijui utamwambia baba au anko ila yote sawa cha muhimu tu umwambie ni jinsi gani nampenda.
Kwakweli katika maisha yangu kuna wadada wengi sana wamekufa kwaajili yangu, kwakweli kama dhambi za damu za watu basi mimi nimezibeba sana Sabrina kwani nimewamaliza wengi sana huku kilio chao kikiumiza masikio yangu na moyo wangu ila asilimia kubwa ya walioangamizwa na mimi ilikuwa ni wale wadada wenye tamaa kwavile ilikuwa ni rahisi sana kwangu kumshawishi mwanamke aliye na tamaa na ukizingatia nilikuwa na pesa za kutosha.
Ila katika wote kifo kilichoniumiza kilikuwa ni kifo cha Neema kwani huyu mdada alikuwa na ujasiri mkubwa sana hata kufa kwake kulikuwa ni kwa ujasiri na kwakweli huyu ni mtu aliyefanya niumie na kufadhaika kwa kitendo cha kinyama nilichokuwa nawafanyia wanawake.
Ila natumaini Sabrina umenisamehe kwa yote haya niliyoyatenda na sasa nimekuwa mtu mpya na sitatenda yale yote. Yule jini ndiye aliyefanya niwe natenda mambo ya kinyama kwa wadada kulingana na yeye alivyotaka, nisamehe sana Sabrina.
Namalizia kwa kusema kuwa nakupenda sana Sabrina, hata Emmy nampenda sana ila upendo wangu kwa Emmy haujafikia hata robo kwako. Kama utaweza basi naomba uniandikie kwa maandishi maana halisi ya neno mapenzi na pia naomba unijibu kuhusu haya mapenzi niliyonayo juu yako, je haya ni mapenzi? Nijibu Sabrina maana jibu sina ila nakupenda sana na siwezi kuacha kukupenda mpenzi wangu, mke wangu na dada yangu.
Kwaheri Sabrina, muda ukipatikana tutaongea zaidi.
Ni mimi mpenzi wako, mume wako na kaka yako Sam"
Sabrina aliisoma hii barua zaidi na kumfanya apumue kwa nguvu kwani aliona wazi kuwa Sam aliandika ile barua kama ishara ya kumuaga pia maneno ya ile barua yalimfanya Sabrina agundue ni kwanini Sam alikufa, ni kwavile alilala na dada yake ambaye ndiye Keti.
"Uwiii kweli Keti alikuwa ndugu yangu jamani dah kweli baba yetu kashindikana"
Pia akafikiria kuwa ingetokea siku angelala na Sam basi ndio ingekuwa mwisho wao.
Akakumbuka kwa mara ya kwanza alipojigundua kuwa anaujauzito wa Jeff na jinsi alivyofanya mbinu za kuweza kulala na Sam ili aweze kumsingizia ile mimba na jinsi Sam alivyomkwepa kulala nae,
"Kwakweli Sam alikuwa ananipenda sana, kwakweli Sam alikuwa na mapenzi ya pekee laiti kama asingekuwa kaka yangu basi huyu ndiye aliyekuwa na mapenzi ya dhati juu yangu. Nami naweza kukiri kuwa alichokuwa nacho Sam juu yangu ndio mapenzi"
Sabrina alikuwa akifikiria na aliyekuja kumshtua kwenye ile gari alikuwa ni Jeff,
"Vipi Sabrina! Na hiyo barua vipi?"
Sabrina akashtuka na kuirudisha ile barua kwenye bahasha kisha akauliza kama tayari wamemaliza kukusanya nguo za Keti ndipo Jeff alipomjibu kuwa wamemaliza kisha Sabrina akawaomba kuwa wapande kwenye lile gari la Sam na waende nalo nyumbani.
"Kwanini umesema hivyo Sabrina?"
"Sasa unafikiri hapa litakuwa linafanya nini? Likizidi kuwa hapa litafanya tuendelee kukumbuka mambo mengi sana"
Wakakubaliana na Sabrina kisha wakapanda kwenye ile gari na kurudi nalo nyumbani kwakina Sabrina ambako waliwakuta wale wengine kama kawaida ila baba wa Sabrina bado alikuwa chumbani.
Sabrina alimuuliza mama yake kama baba yake alitoka,
"Atoke wapi? Amejawa na aibu balaa yupo ndani tu toka asubuhi"
Ikabidi Sabrina akamgongee baba yake ili azungumze nae tena.
Sabrina alimkuta baba yake ambaye bado alikuwa akiyalalamikia maisha kuwa yamemfanyia kitu kibaya sana.
"Kwanza nina mashaka kuwa huenda yule Keti hakuwa mwanangu"
"Usiseme hivyo baba, yule Keti alikuwa ni mwanao"
"Unajua nini Sabrina, naongea haya kwa uchungu jamani. Huyu Bahati na ukoo wake hawakunitakia mema na ndiomana mimi nilikimbia, kumpa mimba mwanamke si lazima umuoe kwani mambo mengine huwa yanatokea kwa bahati mbaya tu, sasa wao walinilazimisha nioe na ndiomana mimi nikakimbia na pia nikahisi ku wa yule Bahati alinidanganya tu kuwa ana mimba ili nimuoe kwakweli sikujua kama kweli ndiomana hata najikuta nikisema kuwa huenda huyo Keti si mwanangu"
Ikabidi Sabrina amueleze baba yake kwa kifupi kuhusu ile barua aliyoiacha Sam, akamuelezea kile kipengele cha mganga ila bado ilikuwa ngumu kwa huyu baba kuelewa.
"Hebu kaniletee hiyo barua nami niisome kwa macho yangu"
Sabrina akafikiria kidogo kisha akainuka na kwenda kumchukulia ile barua baba yake.
Shangazi wa Sabrina siku ya leo naye alijaribu kukaa na huyu Bahati ili aweze kujua zaidi ilivyokuwa kiasi cha kwamba hata mwanae alipo hakujua mpaka hapo msibani.
"Mi naomba unieleze japo kidogo tu maana kuna ile barua ya marehemu aliandika kuwa hamfahamu mama yake wala baba yake yani kwa kifupi walimkimbia je ni kweli ulimkimbia mwanao?"
"Sikumkimbia ila nilienda kutafuta maisha"
"Inamaana uliondoka bila ya kuaga au ilikuwa vipi?"
"Unajua mimi bado nina uchungu sana, maisha kijijini yalikuwa magumu kwakweli. Nikamuomba mama ruhusa ya mimi kwenda mjini akagoma ndio nikaamua kuondoka bila ya kuaga ila haikuwa na maana kuwa nilimkimbia mwanangu"
Akaanza kulia tena, ikabidi shangazi wa Sabrina aanze kumtuliza tena.
Sabrina alichukua ile barua na kumpelekea baba yake ambaye aliifungua na kuanza kuisoma.
Ilipita muda kidogo na kimya kikatawala huku huyu baba akiisoma ile barua.
Muda kidogo huyu baba aliinua kichwa na kumuangalia Sabrina, kisha akamwambia,
"Huenda wewe si mwanangu"
Sabrina alishtuka na kumshangaa baba yake.
Sabrina alichukua ile barua na kumpelekea baba yake ambaye aliifungua na kuanza kuisoma.
Ilipita muda kidogo na kimya kikatawala huku huyu baba akiisoma ile barua.
Muda kidogo huyu baba aliinua kichwa na kumuangalia Sabrina, kisha akamwambia,
"Huenda wewe si mwanangu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sabrina alishtuka na kumshangaa baba yake.
Kisha Sabrina akamuuliza baba yake kwa mshangao ule aliokuwa nao,
"Baba!! Huenda mimi si mwanao kivipi? Imekuwaje hadi uongee hivyo baba yangu?"
"Inawezekana vipi upendwe na kaka yako kiasi hiki? Inamaana huyu Sam hakuona wanawake wengine zaidi yako? Na kwanini aendelee kukupenda ilihali ameshagundua kuwa ni kaka yako? Nina mashaka na wewe kuwa huenda si mwanangu"
"Baba! Sikutegemea kama ipo siku utaongea maneno hayo"
"Mama yenu haaminiki, mimi nilimpenda kwa moyo wote ila yeye kazi yake ni kunisaliti tu. Unafikiri yule James bila kichaa cha dada yangu ningeujua ukweli? Kipindi mnazaliwa nyie dada yangu alishapona kichaa chake unafikiri nitakuwa na uhakika gani kama na wewe ni mtoto wangu"
"Yani baba ndio unaongea maneno hayo kwangu? Unajua ni uchungu gani nilionao juu yako baba yangu?"
"Sio uchungu, kama wewe ni mwanangu kwanini upendane na kaka yako?"
"Sio swali la kuniuliza mimi hilo baba nadhani ungemuuliza muhusika vizuri. Kwanza kabisa mimi na Sam tulikuwa hatufahamiani na ndiomana ikafikia hatua hiyo. Hivi unafikiri ungetulea pamoja ingekuwa hivyo? Na kama ni ngumu kaka na dada kupendana mbona Sam kalala na Keti ambaye ni dada yake hadi kufa? Fikiria mara mbili baba, tena katika swala hili wewe baba ndio mbaya maana umesababisha yote haya. Wewe ndio chanzo, nakuhurumia baba yangu kumbe unahisi mimi sio mwanao dah! Itabidi mama aniambie alipo baba yangu sasa"
Sabrina alijikuta akitokwa na machozi ya hasira kwani hakutegemea kama ingetokea siku ambayo baba yake angeongea maneno kama yale.
Hasira alizoonekana kuwa nazo Sabrina zilifanya mawazo ya baba yake yarudi nyuma. Kwani kiukweli katika watoto wake wote, mtoto aliyeweza kuwa nae karibu alikuwa ni Sabrina tu.
Kwakweli huyu bac aliamua kumuomba mwanae msamaha ila alichokifanya Sabrina ni kuchukua ile barua na kutoka nayo nje ambapo alielekea chumbani kwake moja kwa moja.
Sabrina alipoingia chumbani akamkuta Emmy akiwa mule chumbani kwake amejiinamia tu ila Sabrina alimshtua Emmy na kumuuliza,
"Eti inawezekana vipi baba yako mzazi akakuhisi kuwa wewe si mwanae?"
"Kivipi Sabrina?"
"Baba yangu leo anasema kuwa huenda mie sio mwanae"
"Kwanini aseme hivyo?"
"Eti kwanini Sam alikuwa ananipenda wakati ni kaka yangu"
"Kheee baba yako nae ana visa, hayo mambo si yalishapita kisha wewe na Sam kila mmoja akaendelea na maisha yake, iweje leo akumbushie jamani? Ameanza kupagawa eeeh hajui kama yalishapita hayo? Huna hata sababu ya kulia, wewe tulia tu baba yenu itakuwa kachanganyikiwa kiasi"
Sabrina hakuweza kumwambia Emmy kuhusu ile barua kwani aliogopa kuwa inaweza ikaibua vitu vingine kwa Emmy ila Emmy alimuona nayo mkononi na kumfanya amuulize pia.
"Ni kitu gani hicho?"
"Sio kitu ni karatasi tu"
Kisha Sabrina akaenda kuweka kwenye kabati lake akihofia kuiangusha na pia aliamini kuwa Emmy hatoweza kwenda kuchukua kabatini kwani hana mambo ya kuchunguza vitu vya watu.
Kisha Emmy nae akainuka na kutoka nje.
Emmy alipokuwa nje kabisa akamuona Jeff akiwa nae amekaa nje mwenyewe.
"Jeff niambie"
"Unajua bado natafakari kuwa haya mambo ni ya kweli au ni ndoto! Yani huwa sitaki kuamini kama Sam na Keti hatuponao tena"
"Unatakiwa kuamini Jeff maana kifo ni kama upepo yani kufumba na kufumbua unaweza kuona karatasi imepeperushwa toka sehemu moja kwenda nyingine. Na pia kifo hakina taarifa kwani laiti kama kingetutaarifu basi tungejiandaa mapema sana ila ndio hivi hakuna taarifa. Wao wameenda bado sisi"
"Ni kweli kabisa usemayo Emmy ila kuna vitu vingi sana vinafanya nishindwe kuamini juu ya kifo cha Sam na Keti. Pia kuna muda naona kama Keti ameonewa sana ukizingatia hajayafurahia maisha kiasi kile."
"Ni kawaida tu maana hata watoto nao hufa huku wakiwa hawajui hata nini maana ya maisha"
Kisha kimya kidogo kikatawala halafu Emmy akabadilisha mada kwa kumuuliza Jeff kuhusu Sabrina,
"Hivi Jeff ilikuwaje hadi ukajikuta ukimpenda Sabrina?"
"Kwakweli hata mimi mwenyewe huwa sielewagi kuwa nilianzaje kumpenda Sabrina ila kiukweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana kwani hapa nilipo hata uniulize ni lini nimeanza kumpenda Sabrina sijui ila ninachojua mimi ni kuwa nampenda sana tena nilijaribu mara nyingi kujizuia ili nisimpende ila haikuwa rahisi kwani kadri nilivyojizuia ndivyo nilivyozidi kumpenda"
"Na je unafikiri ni kitu gani kilikuvutia zaidi kwake hadi kufikia hatua ya kumpenda?"
"Sijui ni kitu gani ila kwakweli Sabrina ni mwanamke mstaarabu sana, mpole na pia ana huruma sana. Nakumbuka kipindi nasoma ilikuwa nikigoma kwenda shule basi Sabrina atanibembeleza hadi niende shule na ndiye aliyefanya nisome kwakweli. Na pia mama alinisimulia kuwa nilipokuwa mdogo kuna wakati nilikuwa nagoma kula basi mama anampa Sabrina anilishe nami nilikuwa nakula. Nadhani huyu Sabrina nilianza kumpenda zamani sana tatizo watu wamejiwekea kuwa eti mwanaume akimpita mwanamke miaka basi hamfai ila kiukweli mapenzi hayachagui umri na kama mtu anahitaji mapenzi ya dhati basi asiwe anajiwekea vikwazo mbele yake sijui umri, dini mara kabila lake silipendi, sijui ana rangi mbaya sijui mfupi mara mrefu sana. Ukiweka tu vikwazo vya aina hii ujue kumpata mtu unayependana nae kwa dhati itakuwa ni ndoto kwako na utajikuta ukiishia kuumizwa na kulia kila siku"
"Kwahiyo unaamini kwamba Sabrina ndiye mwanamke pekee atakayekufanya usilie wala usiumizwe na mapenzi?"
"Ingekuwa kuumizwa na mapenzi na Sabrina basi angeniumiza kipindi yupo na Sam ila sio kwasasa. Nampenda sana Sabrina na siku zote nimekuwa nikipigania penzi langu kwake na sasa nimefanikiwa kabisa kwani naamini wazi kuwa Sabrina ndiye mwanamke pekee anayenipenda kimapenzi tena kwa dhati. Namuamini sana sana huyu Sabrina"
"Hongera sana kwa hilo, nakuuliza yote hayo kwavile mtu kama mimi sijawahi kufurahia mapenzi, sio kwasababu ya kuchagua sana wanaume hapana ila ni sababu ya kasoro nilizokuwa nazo ila nashukuru sana kutokea kwa Sam kwenye maisha yangu ingawa furaha yangu imetoeshwa na kifo chake. Kuna kipindi nawaza sana kuwa kwanini kuna mapenzi duniani ambayo baadhi yetu yanatuumiza tu"
"Pole Emmy ila watu wengine huwa mnapatwa na mambo ambayo yanakuwa fundisho kwa wengine ila amini kuwa furaha yako bado ipo na utafurahi zaidi"
Emmy akatabasamu kwani swala la yeye kuwa na furaha ya mapenzi anaona kuwa ni ndoto ukizingatia mwanaume aliyemfanya awe katika hali ya kawaida tena alikuwa ni huyo Sam ambaye tayari alikuwa ni marehemu kwa kipindi hicho.
Kisha Emmy akainuka na kuelekea tena ndani.
Wakati Emmy alipokuwa akielekea ndani ndipo alipopishana na Sabrina kwani nae alikuwa akitoka nje na moja kwa moja akaelewa kwamba anaenda kuongea na Jeff ila Emmy alienda kukaa sebleni karibu na mama mzazi wa Sam huku akimuangalia sana huyu mama, kisha akamuuliza,
"Ni kitu gani ungependa Sam akiache kabla ya kifo chake?"
"Ningependa angalau Sam angeniachia hata mjukuu jamani, unajua nilifurahi sana siku niliyosikia kuwa Sam ana watoto ila nilinyong'onyea pale nilipogundua kuwa wale watoto si wa mwanangu Sam. Kwakweli inauma sana kwani Sam angeacha mtoto basi ningefanya kile ambacho sikufanya kwa Sam kwani mimi sikuwa mama mzuri kabisa kwa mwanangu jamani yani natamani hata kurudisha siku nyuma."
"Pole sana mama yani Sam amekuwa pigo kubwa sana kwetu sote"
"Ni kweli na inaniuma sana wala sitaki kukumbuka yale yote yanayosadikika kuwa Sam aliyafanya. Ninachoamini ni kuwa mwanangu alikuwa ni mtu mwema sana"
Emmy alimuangalia huyu mama kwa jicho la huruma kiasi kisha akamuangalia mama wa Keti aliyeonekana akilalamika kila mara na alionekana kuwa mwanamke asiyeamini kile ambacho kimetokea kwa mtoto wake na muda mwingi alionekana akilalamikia maisha . Kisha Emmy akamwambia mama Sam,
"Mpe pole na mwenzio"
"Huyu ni kama amechanganyikiwa ujue, yani ile picha alikuwa akitembea nayo kwa lengo la kumtafuta mwanae ila ndio hivyo kaja kumkuta mwanae akiwa ni marehemu. Kwakweli inauma sana kwavile hajaishi sana na mwanae zaidi ya kuishi nae alipokuwa mdogo sana kwakweli anahaki ya kuchanganyikiwa"
"Dah! Maisha haya jamani hayana usawa kabisa"
Kisha Emmy akafikiria kiasi na kugundua kuwa hawa wazazi wanajutia vile vitendo walivyofanya kwa watoto wao huku wenyewe wakijua kwamba ndio wanawasaidia watoto wao kumbe ndio walikuwa wakiwaangamiza.
Akakumbuka stori aliyopewa na Sam kuhusu mama yake huyu na kugundua kwamba mama mdogo wa Sam alikuwa na uchungu zaidi juu ya Sam kuliko mama yake mzazi, kisha akainuka na kuelekea tena chumbani kwa Sabrina.
Wakati huu Sabrina alikuwa nje akizungumza na Jeff, na kikubwa alichomuuliza ilikuwa ni juu ya mazungumzo yao na Emmy ambapo Jeff alimueleza Sabrina kile alichokuwa akizungumza na Emmy.
"Unafikiri ni kwanini Emmy amekuuliza maswali hayo?"
"Kwakweli ni ngumu sana kujua ni kwanini ila mimi nimemjibu kulingana na alivyouliza"
"Sawa, ila hata huwezi kufikiria kuwa ni kwanini"
"Kwakweli siwezi"
Muda kidogo akaonekana mama Sabrina na Sakina wakitoka nje ila Sakina alipowaona Jeff na Sabrina akarudi nyuma.
Ikabidi mama Sabrina nae arudi na kumuuliza,
"Vipi Sakina?"
"Kwakweli nashindwa mama, nashindwa kukubaliana na mahusiano ya hawa watu wawili"
"Sakina utakuwa hivyo hadi lini? Hebu achia moyo wako, acha wafurahi na wenyewe. Waliopendana ni wao kwanini wewe uteseke? Halafu mbona muda mwingine unawaona na unakuwa kawaida tu iweje sasa jamani?"
"Muda mwingine huwa najitahidi kuvumilia ila mara nyingine naumia jamani kwani Sabrina ni kama mdogo wangu halafu Jeff ni mwanangu, najua unaelewa kuwa ni kiasi gani naumia mama yangu"
"Hebu kumbuka kuwa Sabrina na Jeff tayari wana watoto, tuliza mawazo yako hayo na tukubaliane na hali halisi ili tusije tukawaathiri wale watoto wadogo kisaikolojia"
"Naelewa mama ila dah naumia sana"
Kisha akarudi ndani tu kwani hakutaka tena kutoka nje.
Kile kitendo cha Sakina kurudi ndani gafla kilifanya Sabrina na Jeff wamshangae kwakweli, ni hapa Sabrina alipomwambia Jeff,
"Inaonekana bado mama yako hakubaliani na mahusiano yangu na wewe"
"Wala asikusumbue akili kwani kuna muda ataelewa tu"
"Mmh anafanya hadi nijihisi vibaya"
"Hata usijihisi vibaya malkia wangu"
Sabrina akatabasamu kisha akainuka ili aweze kurudi tena ndani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Emmy akiwa tena chumbani kwa Sabrina akajikuta akitamani sana kujua kile ambacho Sabrina alificha, yani alikuwa amejawa na shauku juu ya hilo.
Ndipo alipoinuka na kwenda moja kwa moja kabatini halafu akatoka na lile karatasi ambalo aligundua kuwa lilikuwa ni barua.
Emmy akaanza kuisoma kwa umakini sana.
Kwakweli alishangazwa sana na kile ambacho Sam alikuwa amekiandika kwenye ile barua, alijikuta akijiuliza kuwa ni upendo gani ambao Sam alikuwa nao juu ya Sabrina? Pia akaelewa moja kwa moja kuwa baba wa Sabrina aliisoma hii barua ndiomana akafikia hatua ya kusema kuwa Sabrina si mtoto wake.
"Inawezekana vipi kwa kaka kumpenda kiasi hiki dada yake? Kwakweli hii kitu sio ya kawaida jamani."
Muda kidogo mlango ukafunguliwa na Sabrina akaingia na kumshangaa Emmy akiwa na ile barua,
"Jamani Emmy umeanza lini tabia ya kupekua vitu visivyokuhusu?"
Emmy hakujibu kwani alikuwa akitafakari mengi sana juu ya Sabrina, hivyobasi Sabrina akauliza tena swali jingine,
"Kwahiyo umeisoma hiyo barua?"
Emmy hakujibu, na mara gafla akainuka na kukimbilia nje, ikabidi Sabrina amfate kwa nyuma na kumkuta akitapika sana pale nje.
Emmy hakujibu, na mara gafla akainuka na kukimbilia nje, ikabidi Sabrina amfate kwa nyuma na kumkuta akitapika sana pale nje.
Sabrina akamsogelea Emmy na kumuuliza,
"Nini tatizo tena?"
Emmy alikuwa kimya kwani bado aliendelea kutapika.
Ikabidi Sabrina akamletee Emmy maji ambayo aliyatumia kwa kusukutua mdomo kisha akakaa chini sasa ambapo Sabrina alimuuliza tena,
"Niambie Emmy tatizo ni nini?"
"Kwakweli hata sijui nimejishangaa tu gafla nikitaka kutapika"
"Mmh pole sana, je unajisikiaje?"
"Nipo kawaida tu na wala hata siumwi chochote"
"Lakini itabidi uende hospitali"
"Nitaangalia kwanza"
Kisha Emmy akainuka na kwenda sebleni, halafu Sabrina nae akaelekea chumbani kwake na kuchukua ile barua ambayo ilikuwa kitandani na kuirudisha kwenye kabati huku akifikiria ni jinsi gani Emmy amejisikia baada ya kuisoma ile barua.
Alijifikiria sana kwani alihisi wazi ni jinsi gani kuna vipengele kwenye ile barua vilivyomuumiza Emmy na moja kwa moja akahisi kuwa pengine Emmy kapata mshtuko uliopelekea atapike.
Sabrina akajihisi vibaya sana ila mwisho wa siku ikabidi achukulie kawaida tu.
Pale sebleni nako walikuwa wakijadili namna ya kuondoka, ila mama wa Sam akauliza,
"Tunaondokaje bila kujua hatma ya mali za Sam? Inatakiwa tujue kabisa maana Sam alikuwa na mali nyingi sana"
Emmy akaingilia mazungumzo yao na kuwauliza,
"Mnataka kujua hatma ya mali za Sam? Mnataka kugawana mali zake? Laiti mngejua wala msingejisumbua"
"Tusijisumbue kivipi wakati Sam ni mtoto wangu wa kumzaa kabisa kwahiyo nina haki zote za kujua hatma ya mali za mwanangu"
Kimya kidogo kikatawala kwani hata Emmy alijiuliza juu ya huyu mzazi wa Sam ambaye alionekana kuchanganyikiwa kabisa wakati wa mazishi lakini leo amekuwa wa kwanza kuulizia hatma ya mali za mwanae na kujisahau kuwa siku zilizopita ndio aliongoza kwa uchungu mahali hapo.
Ila Emmy aliamua kukaa kimya tu kwani aliona hata kama akiongea ni kazi bure tu ukizingatia kwa ile barua ambayo imeachwa na Sam mwenyewe.
Kwavile tayari ilikuwa ni usiku ilibidi kila mmoja ajiandae na kwenda kulala.
Na kama kawaida ikabidi Emmy aende kulala kwa Sabrina ambako alimkuta Sabrina ameshalala na watoto wake.
Akalala pembeni yao ila ilikuwa ngumu sana kwa yeye kupata usingizi kwani kila alipoifikiria ile barua akaona ni ngumu sana kwake kulala.
Akajikuta akijiuliza kuwa kwanini Sam aliamua kuandika vile kabla ya kifo chake? Akajipa majibu mwenyewe kuwa huenda alihitaji Sabrina ajue ni kiasi gani alikuwa akimpenda, alijiuliza pia kuwa kwanini upendo aliokuwa akimpenda Sabrina asingempenda yeye? Kwakweli Emmy alikuwa na maswali mengi sana yaliyomfanya akose raha kutokana na ile barua.
Usiku wa manane, Sabrina alishtuka kutoka usingizini na kumkuta Emmy akiwa bado macho tena huku amejiinamia kwa mawazo ikabidi amuulize tena ilihali ukweli halisi aliujua kuwa ni kitu gani kilimkosesha raha Emmy.
"Samahani Emmy ila je una matatizo gani?"
"Hapana sina matatizo yoyote"
"Ila mbona unaonekana kuwa na mawazo sana?"
"Hapana sina mawazo"
Kisha Emmy akajilaza tena kitandani na kumfanya Sabrina nae ajilaze kwani hakupewa ushirikiano wa maswali yake ingawa alielewa wazi kuwa chanzo kikubwa ni ile barua ila aliamua kukubaliana na hali halisi kwavile hata huyo Emmy hakumuonyesha ushirikiano wowote.
Kulipokucha kwa siku hiyo aliyekuwa wa kwanza kuamka alikuwa ni Sabrina ambaye moja kwa moja alienda kwenye chumba ambacho Jeff alilala na kumkuta humo kuwa amelala kisha akamuamsha na kuanza kuzungumza nae.
"Unajua Jeff wewe angalau unapatana na huyu Emmy, sasa mimi ningependa uzungumze nae kuwa ni kitu gani kinamsumbua maana namuona hana raha kabisa"
"Yule Emmy anasumbuliwa na mambo mengi tu yani kwa kifupi bado ana mawazo kuhusu Sam"
"Licha ya hivyo Jeff bado kuna vitu vimemchanganya zaidi halafu anaumwa ila kwenda hospitali hataki basi hata uzungumze nae na umshauri kwenda nae hospitali"
"Hilo halina tatizo nitafanya hivyo"
Sabrina akainuka ili atoke ila Jeff akamvuta mkono na kumbusu jambo lililofanya Sabrina atabasamu kisha Jeff nae akainuka na kutoka na Sabrina nje ambapo walikuwa wameongozana.
Muda huu Sakina nae alikuwa ameshaamka na aliwaona wakiwa wameongozana kwakweli aliinamisha kichwa chake chini tu ila hakuongea zaidi kwani alijua wazi kuwa siku hii ya leo atarudi na mwanae huyu nyumbani kwani ndio siku waliyopanga kusambaratika mahali hapo.
Aliwaangalia hadi walipotoka nje kabisa ambapo pale nje Sabrina alimwambia tena Jeff kuwa anaenda kuwaogesha watoto wao.
Jeff akamshika tena mkono Sabrina na kumwambia,
"Unajua nini Sabrina, kilichobaki ni mimi na wewe kufunga ndoa"
Na kumfanya Sabrina atabasamu tena huku akirudi ndani ambapo macho yake yakagongana na macho ya Sakina kisha kila mmoja kati yao akainamisha kichwa chini na kumfanya Sabrina aelewe kuwa ni jinsi gani yeye na Sakina walikuwa wakioneana aibu kutokana na kile kilichoendelea.
Muda kidogo karibia wote mule ndani walikuwa wameamka, na sasa walikuwa wametulia wakinywa chai.
Wakati huu wa chai, Emmy alionekana akitoka nje kwa mbio na kisha alianza kutapika.
Muda huu Jeff alikuwa nje na kumshuhudia Emmy akitapika ikabidi amsogelee karibu na kumsaidia kisha kumpa pole.
Jeff akatumia nafasi hiyo hiyo kumshawishi Emmy aende hospitali,
"Nitaenda tu usijali"
"Emmy, mi nakuomba ujiandae na twende wote huko hospitali muda huu, nipo hapa nakusubiri"
Emmy hakupinga kisha akaenda ndani kujiandaa kwaajili ya kwenda huko hospitali na Jeff.
Wakati anatoka mule chumbani kwa Sabrina akakumbuka kitu na kumfanya arudi na kufungua kabati la Sabrina kisha kuichukua ile barua na kuiweka kwenye mkoba wake halafu akatoka nje na kumkuta Jeff akiwa tayari kisha akaongozana nae kuelekea huko hospitali.
Kufika hospitali, Emmy alienda kwa daktari ambapo alimuelezea tatizo lake kisha daktari akamuandikia vipimo ambapo Emmy aliinuka na kwenda maabara ila kabla hawajamfanyia vipimo vyovyote, Emmy alitoa ile barua na kumpa Jeff aisome kisha yeye akaelekea kwenye vipimo maabara.
Jeff alibaki na ile barua akiisoma sasa na hata yeye aliweza kugundua kuwa hatari gani ingekuwepo endapo Sam asingekufa kwani asingekubali kuona akiishi na Sabrina. Pia alifurahi kuona ni jinsi gani Sam ameweza kuona harakati zake juu ya upendo wake kwa Sabrina ila alimsikitikia Emmy kwani aliona jinsi gani Sam amesisitiza kwenye ile barua yake juu ya upendo wake kwa Sabrina na akaelewa na jinsi gani Emmy atakuwa ameumizwa juu ya hili.
Muda kidogo Emmy nae alirudi kutoka kwenye vipimo na kukaa karibu na Jeff huku akisubiri majibu.
Jeff alimsogelea Emmy na kumshika bega kisha akamwambia,
"Usijali Emmy furaha yako bado ipo"
"Iko wapi furaha yangu Jeff? Mwanzoni nilijipa moyo kuwa Sam atakuwa akinipenda kwani alionekana akivutiwa sana na mimi ila baada ya kusoma hiyo barua nimegundua kwamba Sam hakuwa mwanaume sahihi kwangu ingawa nilifanya yote kwa lengo la kumsaidia tu"
"Emmy usiseme kwamba Sam hakuwa mwanaume sahihi kwako, kwanza kumbuka kuwa Sam na Sabrina ilikuwa na ndugu kwahiyo hapakuwa na namna yoyote ile zaidi ya wao kuachana. Kwakweli usijiumize moyo sana kufikiria juu ya hilo na juu ya hii barua. Unachotakiwa kufanya sasa ni kufikiria kuhusu maisha yako. Naamini kuwa furaha yako bado ipo Emmy yani furaha yako iko pale pale kwani kila kitu duniani hutokea kwa sababu maalumu kwani hakuna cha kuziba furaha yako kati ya vilivyotokea."
Jeff alitumia muda wake kumbembeleza Emmy na kumfanya asijione mpweke juu ya lolote linaloendelea juu yake.
Majibu ya Emmy nayo yalikuwa tayari ambapo Jeff aliongozana na Emmy hadi kwa daktari.
Yule daktari alipowaona alitabasamu kisha akawapa hongera ambapo Emmy na Jeff walishangaa na kutazamana.
Jeff akamuuliza daktari,
"Hongera ya nini tena?"
"Mkeo ni mjamzito"
Huyu daktari alihisi Emmy na Jeff ni familia na ndiomana hakuona tatizo kuwapa hongera.
Emmy nae alishangaa sana kusikia kuwa anaujauzito.
"Inamaana nina mimba? Kivipi?"
"Mbona unashangaa tena dada? Vipimo vinaonyesha hapa kama una ujauzito"
Emmy alionekana kutokuamini kabisa ilibidi Jeff awe nae karibu kwa kumtuliza kisha wakatoka kwenye kile chumba cha daktari.
Wakiwa njiani, Jeff alitumia muda wake kwa kumfanya Emmy asijisikie vibaya,
"Nashukuru kwa moyo unaonipa Jeff ila inakuwaje mimi niwe na mimba?"
"Emmy, wewe ni mwanamke kama wanawake wengine sasa unafikiri huwezi kubeba mimba?"
"Hapana sio hivyo, inamaana kama nina mimba basi mimba hii itakuwa ya Sam"
"Wow, Sam!! Hata yeye akigundua hilo swala atafurahi sana huko alipo. Tafadhari Emmy nakuomba uwe na furaha pia."
Kwakweli ilikuwa ngumu sana kwa Emmy kuamini kama ana mimba hivyo basi akapita kwenye duka la madawa na kununua kipimo cha mimba ili akakishuhudie mwenyewe akiwa nyumbani ambako waliona ni vyema waende nyumbani kwakina Jeff ili kuangalia kipimo hicho.
Kwahiyo safari yao sasa ilikuwa ni moja kwa moja nyumbani kwakina Jeff ili Emmy akajipime mwenyewe.
Walifika kwakina Jeff na kuingia ndani ambapo kulikuwa na ukimya sana.
Emmy hakutaka kupoteza muda, kisha akaenda kufanya kile kipimo kwa kutumia mkojo.
Muda kidogo akapata majibu yake kwani kipimo nacho kilionyesha kuwa Emmy ni mjamzito.
"Uwiii nashindwa kuamini kabisa kuwa imewezekana vipi mimi kupata ujauzito"
"Emmy huu sio wakati wa kushangaa. Nakwambia hivi tena inatakiwa wote pale wajue kama una mimba ya Sam kwa hakika watafurahi sana"
Emmy akaongezea,
"Hasa mama yake Sam, naona atafurahi zaidi"
"Ndio tena atafurahi kweli, basi kwa hilo hunabudi na wewe kufurahi Emmy"
Emmy akatabasamu tu kwani hata yeye alijishangaa na ile mimba.
Nyumbani kwakina Sabrina kwa muda huu walikaa na kuanza kuongelea mali za Sam ambapo walimuita Sabrina awaorodheshee vyote alivyokuwa akimiliki Sam.
Ila Sabrina alionekana kutokujua vitu vingi sana vilipo.
"Jamani, kiukweli kuhusu mali za Sam ninazojua mimi ni kiasi tu kwani kuna mali zingine za Sam ambazo sijawahi kuzifahamu hata zilipo."
"Kwahiyo unadhani ni nani anayeweza kufahamu zaidi kuhusu mali za Sam!"
"Nafikiri anayeweza kufahamu zaidi kuhusu mali za Sam ni Emmy kwani ndiye mtu pekee aliyekuwa nae kwa kipindi kirefu hapa mwishoni"
"Sawa, basi orodhesha unachokifahamu kuhusu Sam"
Ikabidi Sabrina aanze kuandika kile kidogo anachokifahamu kuhusu Sam huku akiamini kuwa hawa ndugu wa Sam watajisumbua tu ukizingatia kuwa mali zote za Sam zipo kwa jina la mtoto wake Cherry kama ndio mrithi halali wa mali hizo kutokana na ile barua ambayo Sam aliiandika.
Sabrina alipomaliza kuorodhesha anachokijua akainuka na kuelekea chumbani kwake huku wao wakiendelea na mjadala wa cha kufanya kwani baba Sabrina nae aliungana nao kwa muda huu ili kusikiliza huo mjadala.
Sabrina alipokuwa chumbani alijaribu kuitafuta ile barua ila hakuipata na moja kwa moja akamuhisi Emmy kuwa kachukua barua hiyo.
Huku sebleni mjadala uliendelea huku baba Sabrina akiwa kimya kabisa kwani aliyeonekana kuuendesha mjadala huo alikuwa ni mama Sam.
"Jamani kule Arusha nako mwanangu Sam ana hoteli yake kama alivyoandika Sabrina hapa nadhani ile itabidi niisimamie mwenyewe maana ndio ilikuwa biashara kubwa sana ya Sam. Mbona hakuna anayenisapoti wala anayetoa mawazo yake zaidi yangu jamani!? Eti mdogo wangu"
Akamuangalia mama mdogo wa Sam ambaye alionekana hana cha kusema,
"Sina cha kusema chochote kile dada yangu, yote mtakayoamua kwangu ni sawa maana naona ni mapema sana kuamua"
Kisha mama Sam akaendelea kuongea kuhusu mali zingine za Sam.
Muda kidogo Jeff na Emmy waliingia na kukatisha mazungumzo ya watu hawa ambapo Jeff aliwaambia kuwa Emmy ana ujumbe wao kisha wote wakamsikiliza Emmy.
"Jamani leo nilienda hospitali kupima na imegundulika kuwa nina mimba ya Sam"
Wote ndani walishtuka ila mama Sam alionekana kushtuka zaidi na kuuliza kwa mshangao,
"Una nini?"
"Nina mimba ya Sam"
"Haiwezekani"
Wote wakamshangaa huyu mama kwa kusema haiwezekani, ikabidi Jeff amuulize,
"Haiwezekani kivipi?"
"Nimesema haiwezekani"
Kisha akainuka kwa hasira na kutoka nje.
Muda kidogo Jeff na Emmy waliingia na kukatisha mazungumzo ya watu hawa ambapo Jeff aliwaambia kuwa Emmy ana ujumbe wao kisha wote wakamsikiliza Emmy.
"Jamani leo nilienda hospitali kupima na imegundulika kuwa nina mimba ya Sam"
Wote ndani walishtuka ila mama Sam alionekana kushtuka zaidi na kuuliza kwa mshangao,
"Una nini?"
"Nina mimba ya Sam"
"Haiwezekani"
Wote wakamshangaa huyu mama kwa kusema haiwezekani, ikabidi Jeff amuulize,
"Haiwezekani kivipi?"
"Nimesema haiwezekani"
Kisha akainuka kwa hasira na kutoka nje.
Hakuna mtu aliyemuelewa kabisa kwani kila mmoja alikuwa yupo mshangaoni.
Ikabidi mama mdogo wa Sam atoke nje kumfata ili amuulize kuwa tatizo ni nini.
Alimkuta akiwa amechukia sana na kumuuliza,
"Dada, nini tatizo kwani?"
"Hakuna tatizo ila nimesema haiwezekani"
"Haiwezekani kivipi dada kwani ulikuwepo wakati wanapeana hiyo mimba?"
"Unajua wewe mara nyingine sijui hata unafikiriaga nini, nadhani kwavile hujawahi kupata mimba ndiomana unakubali kila kitu."
"Kheee dada ndio yamekuwa hayo! Kutokuzaa kwangu si sababu ya kukataa kila kitu, tena yatupasa tumshukuru Mungu maana huu ni kama muujiza kwetu. Sam hatunaye tena ila Mungu ni mwema akaona tusiwe wapweke kaamua kutuletea mjukuu, je huoni kama hili ni jambo la neema katika maisha yetu!"
"Neema! Neema ipi? Hebu nitolee balaa na wewe, eti tumshukuru Mungu yani hadi kwenye ujinga ujinga kama huu tumshukuru Mungu! Nitolee balaa mimi"
Ikabidi mama mdogo wa Sam awe kimya kwa muda kwani alishindwa kumuelewa huyu dada yake kabisa.
Muda kidogo wale waliokuwa ndani wakatoka nje na aliyekuwa wa kwanza kumsogelea mama Sam alikuwa ni Emmy na kumuuliza,
"Kwanini umesema haiwezekani?"
"Nimeshasema haiwezekani na ndivyo ilivyo"
"Kwakweli mama umenisikitisha sana maana katika watu ambao nilikuwa nategemea kuwa watafurahia basi wewe ulikuwa namba moja eti leo ndio unakuwa wa kwanza kupinga loh!"
"Kwahiyo kwavile ulijua nitafurahia ndio ukaamua kuleta habari za uongo kuwa una mimba eeh! Kwanza nifurahie kwa lipi?"
"Habari za uongo kivipi wakati hata vipimo vinaonyesha hivyo!!"
"Wee mtoto wewe usifikirie sisi ni wapumbavu, wadanganye hao hao. Hivyo vipimo siku zote vilikuwa wapi? Umesikia tukijadili mali za marehemu ndio unajishauwa kuwa una mimba yake, kwa taarifa yako sasa kama unajihesabia kwenye mali za Sam basi jua kwamba umeula wa chuya kwa uvivu wa kupembua"
Emmy akatabasamu kidogo na kusogea pembeni ila sio kwamba alitabasamu kwa raha bali alimsikitikia huyu mama anayewaza mali za mwanae badala ya kuwaza kuhusu mwanae.
Akajikuta akijiambia moyoni,
"Kwa stahili hii mtu ukiitwa mchawi unakataaje kwa mfano ikiwa tu matendo yako ni kama matendo ya kichawi"
Akasikitika tena na kurudi ndani peke yake.
Alikaa pale sebleni huku akingoja wengine waingie na aweze kutoa tamko lake kwani kwa upande wake hakuona sababu ya kugombea au kuzungumzia mali za marehemu ilihali anajua wazi kuwa hata kwenye mirathi hayumo, na ndiomana alimshangaa sana mama wa Sam kuzungumzia mali za Sam bila ya kujali mustakabali uliopo kwenye mali hizo.
Mama Sam alipoinuka kurudi ndani ili awaeleze vyema kilichomfanya apinge ile mimba ya Emmy, ndipo wengine wote walipoingia ndani pia.
Mama Sam alikaa sasa na wote kukaa ila kabla ya mama Sam kuongea chochote ni Emmy ndiye aliyeanza kuongea tena,
"Jamani, nilipokuja kuwaambia kuhusu mimba niliyonayo hata sikuwa na nia ya kuvuruga kikao chenu, na pia nilijua hii itakuwa ni habari njema kwa wote kutokana na yale yaliyotupata. Ila kwavile habari hii imepokelewa tofauti na kupelekea mimi kuonekana muongo kwenu napenda niseme haya......"
Kabla hajasema, mama Sam alimkatisha Emmy na kusema,
"Sio kwamba tumekuona muongo Emmy ila kwa kifupi ni kwamba hiyo habari ni uongo, wengine wanaweza kukuamila ila sio mimi. Kumbuka kuwa mimi ni mama mzazi wa Sam kwahiyo namjua Sam vilivyo kushinda wewe umjuavyo, Sam ni mwanangu, nimembeba miezi tisa kwenye tumbo langu hili na kumzaa mwenyewe tena kwa uchungu usioelezeka, sasa unafikiri ni nani wa kumjua Sam zaidi yangu! Hakuna, najua mwanangu hakuwa na uwezo wa kumpa mimba mwanamke yeyote yule, sasa iweje akupe wewe mimba? Najua Emmy umefanya hivyo sababu Sam amekufa na pia unajua ana mali nyingi kwahiyo unatafuta jinsi ya sisi kukupa mali hizo kwakweli kwa hilo umebugi. Sikia, unaweza kweli ukawa na mimba ila hiyo mimba sio ya Sam inaweza ikawa ya mtu mwingine kabisa. Mwanangu namjua jamani, wewe Emmy ni muongo"
Mama Sam akanyamaza kwanza na kumfanya Emmy aongee tena,
"Mama, unasema unamjua mwanao je unavijua hadi vya ndani? Najua utachukia na kuona kama nimekukosea heshima ila kauli yako ndio iliyokukosea heshima. Jamani, mimi kama Emmy sina haja yoyote na mali ya aina yoyote kutoka kwa Sam, laiti mngejua furaha yangu kwenye hii mimba basi msingeongea yote hayo. Hii mimba ni zawadi kubwa sana kwangu, mtoto nitakayemzaa ni urithi tosha kwangu toka kwa Sam, na kama ningekuwa na haja ya mali za Sam basi ningemshikilia kipindi namsaidia kuwa aniandikishe mali zake zote na asingeshindwa kufanya hivyo ila kwavile sikuwa na lengo lingine kwa Sam zaidi ya lengo la kutimiza furaha yangu ndiomana mnaona sina haja ya mali zaidi ya hii zawadi aliyoniachia"
"Hutaki mali wapi jamani tusidanganyane, kama usingetaka mali basi usingekuja kujitangazia hizo habari za uongo."
Kimya kidogo kikatawala, kisha Emmy akainuka na kuelekea chumbani kwa Sabrina.
Pale sebleni nako walikuwa kimya kabisa huku mama mdogo wa Sam akimuangalia dada yake na kumsikitikia kwani alionyesha wazi kuwa ni jinsi gani alivyokuwa na tamaa ya mali kuliko kitu chochote.
Ila huyu mama kwakweli hakumkwepesha dada yake na akampachika swali,
"Hivi dada ndio kwa kiasi hicho unaonyesha jinsi gani unampenda na kumjua mwanao ambaye ulimfukuza nyumbani kwako? Kweli pesa ni shetani"
Baba Sabrina alikuwa kimya tu kwani aliogopa kuongea kuwa huenda akasababisha mengine.
Sabrina pia akaenda chumbani kwake na kumkuta Emmy akiwa amejiinamia huku akilia na kumfanya ashindwe hata cha kuongea nae.
Muda kidogo, Emmy akaonekana kuweka baadhi ya nguo zake kwenye pochi kwa lengo la kuondoka.
"Mmh Emmy kama unataka kuondoka muda umeenda sana ujue, halafu huko njiani utajisababishia matatizo mengine bure."
"Hata usijali Sabrina, msiba umeisha na kama kuzika tumeshazika. Acha tu nirudi nyumbani hata nikaione familia yangu"
"Mmh! Kwanini usiondoke kesho Emmy?"
"Hapana, muda huu ndio unanifaa kuondoka"
"Jamani, basi ngoja nikaongee na Jeff akusindikize"
"Hata usijisumbue kwa hilo"
Sabrina akajua wazi kuwa Emmy anaongea kwa hasira tu, hivyobasi akatoka nje na kwenda kuzungumza na Jeff ambaye hakukataa na alikuwepo pale nje akimsubiri Emmy atoke kisha Sabrina akarudi ndani.
Emmy alipotoka aliwapita pale sebleni na kuwaaga, hakuna aliyeweza kutia neno kwani wengi waliamini kuwa akili ya Emmy imeshavurugika.
Alipotoka nje alimkuta Jeff aliyemwambia kuwa alikuwa akimsubiri ili amsindikize,
"Kwanini unapenda kujisumbua Jeff?"
"Ingekuwa ni kujisumbua basi hata hospitali nisingekusindikiza Emmy"
Kisha wakatoka kabisa na kuondoka.
Njiani Jeff aliweza kuelewa ni kwa jinsi gani Emmy alikuwa na mawazo kwani ilionyesha wazi kuwa kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vikimchanganya akili, kwanza ni ile barua na pili ni maneno ya mama Sam.
Kwahiyo ikabidi Jeff awe karibu na Emmy ili angalau aweze kumtolea mawazo yale.
"Emmy, unajua nini! Mambo kama haya yapo sana kwenye jamii zetu yani kuna watu ukiwaangalia mwanzoni wanaonekana watu kweli ila kwa swala la tamaa wanakuwa mstari wa mbele."
"Unajua yule mama sikumtegemea kabisa kabisa, kwakweli nilijua kuwa atafurahia sana"
"Kwa upande wangu nimefurahi sana Emmy kwani naamini kuwa sasa tumempata Sam mdogo wa ukweli. Halafu yule mama yake Sam usimsikilize wala nini maana ana matatizo tu yule mmama cha msingi wewe angalia mbele tu kwanza hajui yule jinsi gani wewe unafahamu mali za Sam kushinda yeyote yule."
Jeff alionekana kumpa moyo Jeff karibia njia nzima.
Muda kidogo wakiwa njiani wakakutana na Francis ambaye aliwasalimia na kuwapa pole sana kwa kilichotokea,
"Kwakweli hakuna aliyetegemea jamani yani mi mwenyewe nilishtuka sana nilivyoambiwa vile na ilikuwa ngumu kuamini. Hadi siku ya mazishi nilikuwa pale"
Wakamshangaa kwavile hawakuonana nae kabisa tangu kifo cha Sam.
Ila Francis aliwahakikishia kabisa kuwa alikuwepo mahali pale, na alipogundua kuwa Jeff anamsindikiza Emmy nyumbani kwao ndipo na yeye alipoamua kumsindikiza ili wawe pamoja huku njiani wakiongea mambo mbali mbali.
Walipita mahali, Francis akawashtua kidogo na kuwaambia,
"Jamani mmeona hilo nasikia ni godauni la Sam hilo, dah kifo hakina huruma jamani mmh!"
Jeff na Emmy wakatazamana kwani hata na wao hawakujua kama lile godauni ni la Sam.
Walifika nyumbani kwakina Emmy na tayari ilikuwa usiku, Francis kufika hapa akakumbuka ile mara ya mwisho walivyokuja na Sam na kukutana na msiba wa mama yake na Emmy na jinsi mambo yalivyoingiliana hadi kuwapeleka kwenye mapambano ambayo Francis hakuyaweza na akaishia nayo njiani.
Ndipo Francis alipomuuliza Emmy,
"Vipi Emmy mama yako ni mzima?"
"Kwanini umeuliza hivyo Francis?"
"Nakumbuka mara ya mwisho mambo hayakuwa shwari hapa"
"Mama yangu ni mzima tena mzima haswa"
Na walipokuwa wakiingia ndani ni huyu mama Emmy ndiye aliyewakaribisha na kumfanya Francis awe kimya tu.
Walikaribishwa vizuri sana ndani huku huyu mama akimshangaa mwanae maana ni siku nyingi kiasi hajaonekana kwao.
"Tulipatwa na matatizo mama, tulifiwa"
"Kheee mlifiwa na nani tena?"
"Unamkumbuka yule kijana ambaye nilikuja nae kukuona hapa?"
"Yule uliyekuja nae mara ya mwisho?"
"Eeh huyo huyo, basi amekufa mama"
"Kheee amekufa? Alikuwa anaumwa nini tena? Si ndio yule alisema anataka kukuoa jamani? Au mwanangu hujapona yale matatizo yako?"
"Yani mama acha tu, kwakweli kila mtu kasikitishwa na kifo chake. Mama mie yale matatizo nilipona kabisa na yule ndio alikuwa mwanaume sahihi kwangu ila ndio hivyo amekufa"
Emmy akainama akitoa machozi, ikabidi mama yake ambembeleze na kumfanya atambue kuwa ni jinsi gani Emmy alimpenda yule kijana ukizingatia haikuwa tabia ya Emmy kumlilia mwanaume wa aina yoyote ile.
"Pole mwanangu, haikuwa riziki yako"
"Ilikuwa riziki yangu mama kwani hapa nilipo nina mimba yake"
Emmy akazidi kulia, kwakweli mama yake alimuonea huruma sana Emmy na kuona jinsi alivyoumizwa mtoto wake huyo.
Francis nae akaelewa ni kwanini Emmy amepatwa na mawazo kiasi kile, kwani pale alipo ana mimba na aliyempa mimba hiyo tayari alishakufa.
Hata yeye Francis alijitoa na kuanza kumpa pole tena huku akitamani kufahamu zaidi kilichotokea baina ya Emmy na Sam hadi kuishia kupeana mimba.
Nyumbani kwakina Sabrina baada ya kuona mabishano ya mali yakiendelea ndipo baba Sabrina alipoamua kutoa tamko.
"Jamani mama Sam, najua huko una ndugu zako wengi sana na kama ulivyosema kuwa wewe unamfahamu sana mwanao basi sinabudi kukwambia kwamba nenda kwa ndugu zako huko kajadilianeni kuhusu hizo mali za Sam ila sio kwangu hapa. Umemkosesha binti wa watu furaha badala tufurahie kumpata Sam namba mbili eti wewe una nuna na kupingana na hali halisi"
"Kuondoka sio tatizo cha muhimu kwanza mnipe funguo za nyumba ya mwanangu"
"Funguo anazo mdogo wako huyo, nadhani atakupatia ili mkajadiliane huko"
Kwakweli mama mdogo wa Sam hakufurahishwa kabisa na hii hali na kuahidi kumpa dada yake funguo kesho yake kwani usiku nao ulishaingia.
Muda kidogo wakakubaliana na maamuzi yao kisha kila mmoja kwenda kulala.
Kulipokucha, mama Sam alikumbushia kuhusu funguo kisha mdogo wake akamkabidhi na kugoma kwenda nae ambapo ilibidi achukuzane na wale marafiki zake wawili na kuondoka nao.
Mama Sabrina alimshangaa sana huyu mama mdogo wa Sam kutokwenda na dada yake,
"Mbona hujaongozana nae?"
"Huwa sipendi kwenda mahali bila kushauriwa na roho yangu, sikuja hapa kwa lengo la kupambana kuhusu mali za Sam bali kilichonileta ilikuwa ni kumsaidia Sam pamoja na wale watoto wawili ambao napenda kuwaita wajukuu zangu. Bado nipo hapa kwasababu moja tu, kuna mtu namsubiri anitumie nauli niondoke kwani kazi yangu nimeimaliza"
Kwakweli mama Sabrina alimshangaa sana huyu mama mdogo wa Sam na kumfanya azidi kuona tofauti iliyopo ndani yake na wengine ukizingatia mama wa Sam alidai hadi michango ya pale msibani huku akisema kuwa ule msiba unamuhusu yeye.
Mama Sabrina akagundua kuwa ni kwanini Sam alikuwa akimpenda zaidi mama yake mdogo kuliko mama yake mzazi kwani mama huyu alionekana kuongozwa na tamaa zaidi.
Mama Sam na wenzie walifika nyumbani kwa Sam kwakweli wenzie walishangaa ukubwa na uzuri wa ile nyumba.
"Kwakweli ulikuwa una haki zote za kupigania mali za mwanao, kumbe ndio alikuwa tajiri hivi!"
"Mnamchezea Sam eeh mwanangu alikuwa hatari ngoja nifungue geti tuingie"
Akafungua geti na wakaingia na kuwafanya wazidi kushangaa yale magari yaliyopangana.
"Jamani, magari yote haya loh kifo kibaya sana"
"Ila mwanao nae hata kukupa moja mama yake loh!"
"Ndio hivyo ila mwanangu alikuwa tajiri sana"
"Ila kukutembelea ndio alikuwa hapendi"
"Tatizo lake alidanganywa sana na yule mdogo wangu, nilikuwa namkutaga kwake. Yani mdogo wangu yule si mtu mzuri kabisa. Ngoja tuingie ndani"
Mama Sam akafungua mlango wa kuingia ndani, ila kabla hawajaingia gafla wakakubwa na kitu kama moshi kutoka ndani na kuwafanya waanguke chini wote watatu.
Mama Sam akafungua mlango wa kuingia ndani, ila kabla hawajaingia gafla wakakubwa na kitu kama moshi kutoka ndani na kuwafanya waanguke chini wote watatu.
Hakuna aliyeweza kuinuka kwa wakati ule kwani walipoteza fahamu.
Emmy akiwa njiani wakati akiwasindikiza Francis na Jeff kwenda kituo cha daladala kwavile usiku wa jana walilala kwao, gafla walishangaa kumuona Emmy akishtuka kanakwamba kuna kitu amekiona.
Francis na Jeff wakamuuliza kwa mshangao kuwa ni kitu gani kilichomshtua,
"Kuna kitu nakihisi kuwa kimetokea nyumbani kwa Sam"
"Khee nyumbani kwa Sam tena!!"
"Ndio, kule ambako Sam alikuwa akiishi nahisi kuwa kuna kitu kimetokea."
Ikabidi Francis amuulize kwa makini,
"Ni kitu gani hicho Emmy au ndio yale mambo yako yameanza tena?"
"Hapana Francis, yani nahisi kuna kitu kibaya kimetokea kule ingawa sijui ni kitu gani. Aah au basi tuachane na habari hizo"
Francis na Jeff wakaona ni vyema wamuombe huyu Emmy arudi tu nyumbani kwao kwani kwa jinsi walivyomfahamu walihisi wazi kuwa anaweza kubadilisha maamuzi muda huo huo na kutaka kwenda kwa Sam halafu wakaona kwamba huko kwa Sam hapakuwa mahali salama kwake kwa wakati huo.
Wakasimama na kuagana nae, kisha wakamuangalia hadi anaingia nyumbani kwao halafu wakaondoka.
Kwavile Francis alikuwa na maswali mengi, hakusita kumuuliza Jeff baadhi ya maswali yake,
"Kwahiyo Sam alikuwa anatembea na Emmy pamoja na Sabrina?"
"Kivipi?"
"Ninachofahamu ni kuwa Sabrina ndiye alikuwa mke halali wa Sam, halafu jana nimeshangaa kumsikia Emmy kuwa ana mimba ya Sam"
Jeff akatulia kidogo kwani alielewa wazi kuwa Francis haelewi chochote, akatamani kumwambia ukweli ila akasita kidogo kwani anatambua wazi kuwa Francis naye anampenda Sabrina. Hivyobasi aliamua kukwepa swali la Francis kwa kumwambia kuwa akawaulize Sabrina au Emmy kwani ndio wanaujua ukweli wa mambo yote.
Ikabidi Francis akubali kile alichoambiwa na safari yao kuendelea.
Nyumbani kwakina Sabrina, kwa muda huu Sabrina alikuwa na mawazo sana na aliyekuwa akimfikiria kwenye akili yake alikuwa ni Jeff.
Aliwaza kwanini Jeff hakurudi jana, na kwanini achukue maamuzi ya kulala huko huko.
Muda kidogo Sakina akamfata Sabrina na kumshtua toka kwenye yale mawazo.
"Mbona una mawazo hivyo Sabrina?"
Sabrina akacheka kwa kujigelesha na kujibu kuwa hana mawazo.
"Mmh huna mawazo wakati inaonyesha una mawazo"
"Hata usijali kuhusu mimi"
"Eeh Sabrina, huyu Jeff yuko wapi maana namtafuta nirudi nae nyumbani"
Sabrina akaona leo Sakina amejikaza kwani siku zote hizi amekuwa akiumizwa sana na ukaribu wao ila leo amejikaza na kuulizia alipo Jeff, hivyobasi Sabrina akamueleza ukweli kuwa Jeff alitoka jana kwenda kumsindikiza Emmy,
"Kheee kwahiyo ndio hajarudi!"
"Ndio"
"Hajarudi kwanini?"
"Nadhani amelala huko huko"
"Mmh huyu Jeff huyu, alale huko huko kwa misingi gani? Pole mwaya"
Sakina akainuka na kuelekea nje, Sabrina akamshangaa kwa ile pole aliyompa ukizingatia hata yeye hakuwa na mawazo mema dhidi ya Jeff huko alipolala.
Akaamua kuinuka na kuelekea sebleni ambako mama yake pamoja na mama mdogo wa Sam na watoto wake walikuwa huko.
Kama kawaida akawaona watoto wake wakiwa wamekaa karibu na mama mdogo wa Sam na kumfanya aendelee kuuona umuhimu wa mama huyu katika maisha ya watoto wake hawa, wakati huo Sakina nae alikuwa pembeni tu amekaa.
Sabrina alipofika pale akakumbushia swala la mimba ya Emmy kuwa na wao wanaonaje swala hilo.
Aliyekuwa wa kwanza kujibu alikuwa ni mama mdogo wa Sam,
"Jamani, kwa upande wangu hili swala la mimba ya Emmy nimeona kuwa ni swala la kheri sana ukizingatia hatuna ukumbusho wowote wa Sam"
"Ila sasa kwanini mama anakataa?"
Sakina nae akaongezea,
"Na kwanini aseme kuwa mwanae hawezi kumpa mimba mwanamke?"
"Kwakweli hata mimi nimeshindwa kumuelewa dada yangu kwa hilo, pia sijaona sababu ya yeye kukataa. Na kama sababu yake ni hiyo ya kusema kuwa mwanae hawezi kumpa mimba mwanamke kwakweli naikataa kabisa, maana hiyo ingekuwa sababu nzito basi hata hawa watoto wa Sabrina angewakataa. Mbona hawa aliwakubali au kwavile mwenye mali alikuwepo? Sioni sababu ya yeye kukataa kwakweli na hata hivyo sidhani kama Emmy katudanganya kwani Emmy hapa mwishoni alikuwa karibu sana na huyo Sam na kama angekuwa na haja na mali basi kwa hakika angezipata hata kabla ya kifo cha Sam. Ila dada yangu hashauriki kwa sasa maana kama angeshaurika basi ningemshauri waende wakapime ili ajithibitishie mwenyewe na roho yake"
Waliyaelewa vilivyo maneno ya huyu mama.
Muda kidogo pale kwakina Sabrina aliwasili Jeff akiwa ameambatana na Francis na kuwasalimia pale huku wakijaribu kuongea ya hapa na pale ila Sabrina alionekana kuwa kimya kwa wakati huu wote kisha akainuka na kumuomba Jeff nje.
Sabrina akatoka na Jeff nae akatoka,
"Mmh kwahiyo jana ukaona bora ulale huko huko Jeff jamani, ulishindwa nini kurudi?"
Jeff akatabasamu na kumfanya Sabrina achukie zaidi na kumuuliza kwa ukali,
"Kinachokufanya ucheke?"
Jeff akacheka zaidi sasa kisha akamuomba msamaha Sabrina,
"Nisamehe tafadhari haikuwa dhamira yangu"
"Nikusamehe nini wakati mimi nakuuliza unajifanya kucheka"
"Sijacheka kwa ubaya Sabrina ila nimefurahi tu"
"Haya, kilichokufurahisha?"
"Nimefurahi kuona una wivu juu yangu Sabrina"
"Lione vile"
Sabrina akanuna kidogo na kumsonya ila bado Jeff alitabasamu tu, kisha wakarudi tena ndani ambapo Jeff alimuulizia mama Sam maana hakumuona mahali hapo.
"Hayupo, ameondoka na wale wenzie"
"Kheee wameenda wapi? Au ndio wamerudi Arusha?"
"Hapana, wameenda nyumbani kwa Sam"
Jeff akamtazama Francis kwani walikumbuka ile kauli ambayo Emmy aliwaambia wakati anawasindikiza.
Francis aliamua kusema,
"Wakati Emmy anatusindikiza njiani alishtuka sana na kudai kuwa kuna kitu kibaya kimetokea nyumbani kwa Sam"
Wote wakawa kimya kwa muda, kisha Sabrina akauliza
"Inamaana yale mauza uza nyumbani kwa Sam bado hayajaisha? Mmh mbona majanga! Au hicho kitu kibaya anachosema Emmy ni hao kwenda huko kwa Sam?"
Sakina nae akachangia,
"Mmh kazi ipo ndiomana mamdogo kakataa kwenda. Yani mimi sehemu ambayo huyu mama kakataa hata mimi siwezi kwenda hiyo sehemu"
Waliongea pale ila mama mdogo wa Sam alikuwa kimya kabisa akiwasikiliza huku wakiendelea kuhojiana cha kufanya juu ya hilo.
"Sasa tunafanyaje jamani maana hata hatuelewi, je kuna mema au mabaya huko"
Mama Sabrina akasema,
"Mi nadhani tungeenda tu kuangalia"
Sakina akasema huku akimuuliza mama mdogo wa Sam,
"Eti mamdogo twende kule au tusiende?"
Mama mdogo wa Sam akawauliza,
"Kwanini mnaniamini sana mimi? Hata mimi mwenyewe huwa siwezi kuamua jambo kama hilo bila kuingia kwenye maombi. Jamani tuwe na kawaida ya kuweka mambo yetu kwenye maombi"
"Kwahiyo unatushauri tuombe kwanza kabla ya kwenda huko?"
"Ni vyema kumshirikisha Mungu katika mambo yetu yote kabla ya kuyatenda"
Wakamsikiliza pale ila kwa upande wa mama Sabrina alikuwa akitamani sana kwenda kuwaona kuwa wamekumbwa na kitu gani ila kwavile hakuwa na sapoti yoyote ikabidi awe kimya tu.
Nyumbani kwa Sam hawa wamama watatu walivyoanguka ilipita muda kidogo kwa wao kuzinduka, na walipozinduka walijihisi kuwa viungo vyote mwilini vinawauma na hawakuwa na msaada wowote kwa muda huo wala hakuna aliyetamani tena kuingia ndani kwenye nyumba ya Sam.
Wakaanza kuulizana wanavyojisikia ila kila mmoja alilalamika kuhusu viungo vyake, ndipo muda kidogo walipoanza kujivuta kwa lengo la kutoka nje kabisa ya nyumba hiyo.
Walipobahatika kufika nje kabisa, walihangaika kuinuka kisha mama Sam akarudishia lile geti na kusaidia wale wengine kuinuka huku wakitembea kwa taratibu ili kuondoka eneo lile.
Walipofika stendi hawa wenzie wakamuuliza mambo Sam,
"Kwani ile nyumba ya mwanao ina nini? Maana sio kwa mweleka ule tulioanguka"
"Jamani ndugu zangu mnisamehe bure tu, ile nyumba ya mwanangu imekuwa na mauzauza toka enzi za uhai wake ila mi nilifikiri kuwa yale mambo yameshaisha. Nisameheni bure ndugu zangu?"
Hakuna aliyemlaumu sana ila wote walikuwa wakioneana huruma tu kwajinsi vile ilivyokuwa.
Kisha wakaanza kuulizana wanapoelekea sasa baada ya lile tukio la wao kuanguka kwenye mlango wa nyumba ya Sam.
"Haya tupo stendi, ndio tunaelekea wapi sasa?"
"Jamani turudini tu kule tulipotoka ili niwaage halafu ndio kesho tusafiri maana sina hamu tena na hiyo nyumba ya mwanangu."
Wakakubaliana nae kurudi kule walipotoka kwani hawa wenzie hawakuwa na tatizo lolote ukizingatia wao ni kama bendera tu fata upepo.
Nyumbani kwakina Sabrina kila mmoja aliendelea na shughuli zake na hata muda ulipoenda Sakina na mwanae waliamua kurudi kwao ili wakapange nyumba yao v4zuri kwahiyo waliinuka mahali hapo na kuondoka.
Kwa upande wake Francis na yeye aliambatana pamoja na Sakina na mwanae wakaondoka pamoja halafu pale wakawaacha wanafamilia tu ambapo alibaki mama Sabrina, Sabrina, mama mdogo wa Sam pamoja na watoto wa Sabrina kwani hata baba Sabrina nae hakuwepo mahali hapo ukizingatia siku hiyo alitoka asubuhi na mapema kwenda katika mambo yake ya hapa na pale.
Kwahiyo pale kwao walibakia hao tu kwani hata na ndugu wengine pia waliondoka baada tu ya msiba kuisha kwani ile migogoro ya hapa na pale iliwashinda kwakweli haswaa shangazi wa Sabrina kwani hakutaka kabisa kuendelea kubishana na watu hawa.
Wakiwa pale sebleni, muda kidogo wakasikia hodi na walioingia ni wale wamama watatu tena wakiwa wamechoka sana.
Sabrina ilibaki kidogo tu ashikwe na kicheko ila aliwauliza kwanza kulikoni ili waeleze kilichowasibu.
Muelezaji mkubwa alikuwa ni mama Sam,
"Jamani ndugu zetu mtusamehe tu, kwakweli hapa nilipo sina hamu na nyumba ya Sam sina hamu kabisa. Anayeitaka nyumba ile aende tu. Pale tulifika vizuri na kuingia ndani, sasa ile kutaka kuingia ndani kabisa sasa tulipofungua mlango tu yani gafla sijui hata ule moshi ulitokea wapi yani ulitupuliza usoni na kujikuta tukipiga mweleka hadi chini. Tulipoteza fahamu pale pale, kuja kuzinduka sasa yani viungo vyote vinauma kamavile kuna kazi nzito tulikuwa tunafanya. Kwani nimepata tena ujasiri wa kuingia? Thubutu yangu, ilibidi tujikongoje tutoke na kuamua kurudi tu hapa ili kesho tusafiri"
Sabrina alikuwa wa kwanza kuwapa pole,
"Jamani poleni sana, kwakweli ile nyumba ni ngumu sana kuacha kuwa na mauza uza yani mimi ndio nilishasema kabisa kuwa kule siendi tena. Poleni sana"
"Asanteni, na funguo hizi hapa"
Wakamkabidhi funguo mama mdogo wa Sam ambapo aliwauliza,
"Je mlikumbuka kufunga milango?"
"Mmh! Mungu wangu sidhani kama ile milango tumeifunga kwakweli maana kila mmoja alichanganyikiwa. Hebu fikiria toka asubuhi mpaka muda huu jamani, si jioni hii. Yani hapa tumechoka na njaa zinauma balaa"
Sabrina akawahurumia kiasi na kwenda kuwaandalia chakula ila kwa upande mwingine alifurahia kilichowapata ili wajifunze halafu siku nyingine wasirudie upuuzi wao walioufanya kwa ubishi.
Jioni hii Emmy akiwa nyumbani kwao bado mawazo yake yalikuwa kwenye ile nyumba ya Sam na kumfanya ajiulize kama aende au asiende. Ila kila alipofikiria bado mawazo yalikuwa kulekule.
Hivyobasi akaamua kujiandaa ili aende, kwakweli mama yake alipomuona Emmy anataka kutoka kwa siku ya leo mama huyu akamkataza binti yake,
"Jamani mwanangu Emmy ungepumzika kiasi"
"Sina sababu ya kupumzika mama yani hili ninalofikiria ni lazima niende leo"
Kwahiyo Emmy akatoka pale nyumbani kwao na kuelekea kwa Sam bila kujali kuhusu funguo.
Ila alipofika nyumbani kwa Sam alikuta geti limerudishiwa tu, hivyo akasukuma na kuingia.
Na alipofika mlango wa ndani na kujaribu kufungua nao pia ulifunguka.
Emmy akaingia sebleni, akaona kuna karatasi dogo mezani, akalichukua na kusoma.
Liliandikwa kwa maneno machache sana,
"Kwaheri Emmy"
Kwakweli Emmy alishtuka sana.
Ila alipofika nyumbani kwa Sam alikuta geti limerudishiwa tu, hivyo akasukuma na kuingia.
Na alipofika mlango wa ndani na kujaribu kufungua nao pia ulifunguka.
Emmy akaingia sebleni, akaona kuna karatasi dogo mezani, akalichukua na kusoma.
Liliandikwa kwa maneno machache sana,
"Kwaheri Emmy"
Kwakweli Emmy alishtuka sana.
Alijawa na uoga gafla kwani hakujua kuwa lile karatasi limewekwa na nani pale sebleni, akajikuta akiangaza nyumba yote kuangalia kama kuna uwepo wa kitu chochote kibaya ila kabla hajafanya chochote akasikia kicheko na kugundua wazi kuwa kile kicheko kilikuwa ni cha yule jini ambaye alikuwa akimtesa Sam.
Kwakweli Emmy aliogopa ukizingatia aliamini kuwa mambo ya yule jini walishayamaliza alipokuwa na Sam na aliwaahidi kutokuwasumbua tena, sasa iweje asikie kicheko chake!
Emmy akataka hata kukimbia ila kabla hajafanya huo uamuzi wa kukimbia akasikia sauti ya yule jini ikimwambia,
"Usiogope Emmy, sina nia mbaya kwako wala sina nia yoyote ile ya kukudhuru wewe na familia yako. Najua utajiuliza kuwa nilisema sitawasumbua tena na kwanini nimekuja sasa. Jua kwamba kuna vitu vyangu vilikuwemo humu ndani kwa Sam na pia nimerudi kwaajili yako Emmy ila sio kwamba nimerudi kukutesa au kukusumbua hapana, nimerudi kwa muda mchache tu ili niweze kukusaidia. Sikiliza Emmy, mtu wangu hayupo kwahiyo siwezi kurudi kama awali. Pia napenda ujue kwamba kama swala la kumuokoa Sam ningemuokoa endapo msingekuwa mmenifukuza ila kwavile mlijitenga nami, sikuweza tena kuwa karibu na Sam. Dawa alizopewa zilikuwa kali sana, wewe hukufa kwasababu haikuwepo nguvu yangu ya kuwanyonya damu wanawake anaolala nao Sam, ila Sam na nduguye wamekufa kwavile nguvu ya dawa juu ya kulala na nduguye ilikuwa pale pale. Siku zote mimi nilimlinda Sam kutokana na hilo na ndiomana hakuweza kulala na Sabrina kwani tangu mwanzo nilijua kuwa ni ndugu na ukizingatia sikutaka kumpoteza Sam. Hakuna kifo kilichoniuma kama kifo cha Sam, kama ningeweza kumrudisha kwa hakika ningemrudisha. Ila kilichonileta leo ni hiki hapa......."
Mara gafla mbele ya Emmy pakatokea kitu kama sinema na muda kidogo akawaona mama Sam akiwa ameongozana na wenzake wawili wakifungua geti huku wakishangaa shangaa.
Kisha akawaona wakisogelea mlango wa kuingia ndani ila walipofungua wakapuliziwa kitu kama unga na kuanguka chini ila muda huo huo wakainuka kivingine kabisa na kuingia ndani huku kila mmoja akifanya usafi kwenye nyumba ile.
Walionekana wakideki, wakifuta madirisha, wakiosha vyombo na kupanga, wakipanga nguo vizuri kwenye kabati yani wakifanya usafi wote wa nyumba ile. Na walipomaliza usafi wa ndani, walitoka nje na kuanza kuosha magari yote, waliyasafisha vizuri kabisa.
Kisha wakaonekana wakirudi tena pale chini walipoanguka na kulala ila muda kidogo waliamka na kila mmoja kudai kuwa amechoka sana kisha wakaanza kujinyoosha kwa uchovu huku wakijikongoja kutoka nje.
Kwakweli Emmy alishangaa sana ile sinema kwani ilikuwa kamavile anaota.
Ila alipoangalia mazingira ya ile nyumba aliyaona yakiwa tofauti sana kwani yalikuwa masafi kamavile kuna watu wanaishi humo na kumfanya aamini ile sinema aliyoiona.
Kisha ile sauti ikasema nae tena,
"Umeona Emmy!! Nyumba ilikuwa chafu sana hii hata mimi siwezi kustahimili kwenye nyumba chafu ndiomana nilipowaona tu nikasema hawa hawa ndio watakaofanya usafi kwenye nyumba kama unavyoona sasa nyumba yote ni safi. Usinichukie Emmy kwani bado nataka ufahamu biashara za Sam zinazofaa na zisizofaa"
Kimya kidogo kikatawala huku Emmy akiwa bado anamshangao kwani aliyeongea nae hakumuona kabisa zaidi ya kusikia sauti, na kwavile sauti ilikatika gafla ndiomana akabaki na mshangao.
Hakutaka kuogopa zaidi kwani sasa aliamua kukaa kwenye kochi kabisa huku akiendelea kusikilizia kama atazungumza tena.
Baada ya kimya zaidi ikabidi aulize kwani alijua wazi kuwa atasikika tu,
"Kwahiyo hii karatasi hapa mezani umeniwekea wewe?"
Sauti ya kicheko ikasikika tena na kumwambia,
"Ndio Emmy"
"Ulikuwa na maana gani?"
"Nilikuwa na maana ya kukuaga, nakuhakikishia Emmy sitakutenda chochote kibaya na wala sitakuwa karibu na wewe ila kwenye mambo machache nitakayoweza kukusaidia basi nitakusaidia Emmy"
Kwakweli Emmy hakujua ajibu nini ingawa hiki kiumbe hakukitaka kabisa na aliona kama itakuwa kama anavyosema basi itakuwa ni mkosi katika maisha yake ingawa kwa imani yake nyingine aliamini kuwa hiki kiumbe kinaweza kuwa msaada katika maisha yake, kwahiyo ilikuwa ngumu sana kwa Emmy kujibu chochote kile.
Kimya tena kikatawala humu ndani huku usiku nao ukiingia huku Emmy akiwa mule mule ndani ya nyumba kwani alijikuta akiwa na uvivu ambao ulimfanya ashindwe hata kuinuka ili arudi kwao.
Francis nae alivyomaliza kuwasaidia wakina Jeff pale kwao aliamua kurudi tena nyumbani kwakina Sabrina ili kuwaaga vizuri kuwa anaondoka.
Na alivyofika kwakina Sabrina alimuomba Sabrina amsindikize ambapo Sabrina alitoka nae kwa lengo la kumsindikiza kidogo kwani hata giza nalo lilianza kuingia.
Njiani kidogo Francis akasimama na kumuuliza Sabrina,
"Sabrina kuna mambo sielewi"
"Mambo gani?"
"Ni kuhusu wewe, Sam na Emmy. Nimesikia kuwa Emmy ana mimba ya Sam, swali langu ni je Sam alikuwa akitembea na wewe pamoja na Emmy?"
"Hapana haikuwa hivyo"
"Sasa iweje Emmy awe na mimba ya Sam?"
"Ni historia ndefu kidogo ila kwa kifupi ni kuwa Sam alikuwa kaka yangu, tulikuja kugundua hilo kisha ikabidi tutengane na ndipo Sam alipoanzisha mahusiano na Emmy"
"Kheee na wale watoto mliozaa pamoja je?"
"Wale watoto si wa Sam"
"Ni wa nani sasa?"
Sabrina akafikiria kiasi na kuona kuwa mficha maradhi kifo humuumbua kwahiyo akaona ni vyema kumwambia ukweli tu huyu Francis,
"Wale watoto ni wa Jeff"
"Kheee kwahiyo Sabrina umezaa na Jeff!!"
"Ndio kwani kuna tatizo gani?"
"Dah! Acha masikhara Sabrina, si bora hata ungezaa na mimi jamani"
"Ndio nishazaa na Jeff na hilo haliwezi kubadilika"
"Aaah Sabrina, Jeff kijana mdogo huyu nakumbuka kipindi kile anakuita mamdogo mamdogo kumbe leo ndio umezaa nae dah bora hata ungezaa na mimi jamani"
"Ila nyie wanaume ni tatizo jamani, wewe si ulioa wewe halafu ukazaa mtoto mmoja na yule mwanamke kisha ukamuacha. Haya unataka nini sasa?"
"Sikuweza kuishi na yule kwasababu sikumpenda kweli ndiomana niliamua kuachana nae kwani mwanamke ninayempenda kwa dhati ni wewe Sabrina."
"Ngoja niishie hapa Francis kwaheri"
"Ila nakupenda sana"
Kwakweli Sabrina hakutaka kuongea zaidi na Francis kwani alimuaga pale na yeye kuanza kurudi kwao huku akijiuliza ndio mapenzi gani haya ya kila mmoja kujidai kuwa anampenda kwa dhati.
Aliporudi nyumbani kwao akamkuta Jeff kasimama kwenye mlango wao wa nje wa kuingilia.
"Toka umetoka kumsindikiza yule, mimi niliwaona na nikasimama hapa ili nikusubiri utakaporudi ila cha kushangaza mbona umechelewa sana.
Sabrina akamueleza alichokuwa akizungumza na Francis ila hakumwambia kuhusu swala la Francis kumwambia kuwa bado anampenda kwavile hakutaka kuweka bifu baina yao.
Jeff alionyesha kuelewa kiasi kisha akasema na yeye kilichompeleka hapo muda huo.
"Nilikuja kukuona tu Sabrina"
Sabrina akaguna ila Jeff akamvuta karibu Sabrina na kumbusu kisha akamuaga na kuondoka.
Sabrina aliingia ndani kwao huku akiwaza lile busu alilopewa na Jeff na kumfanya atabasamu kwani aliona wazi kuwa mapenzi anayoyahitaji yeye yapo kwa Jeff tu.
Alipoingia ndani kwao wakamshangaa vile alivyokuwa akitabasamu tena mama yake akawa wa kwanza kumuuliza mwanae kuwa mbona ameingia ndani huku akiwa na tabasamu usoni mwake ila bado Sabrina aliwaambia kuwa ameamua tu kuweka tabasamu.
Kisha akaenda zake chumbani kwake kulala na watoto wake.
Aliwakuta tayari wamelala kwahiyo na yeye akalala pembeni yao huku akitabasamu tu na kumfikiria Jeff .
Muda kidogo usingizi ukamchukua na kumfanya aote mambo mbali mbali.
Emmy na yeye alipokuwa amekaa kwenye lile kochi huku uvivu ukiwa umemjaa alijikuta akilala pale pale kwenye kochi.
Moja kwa moja .
Akiwa amelala akajiwa na ndoto, katika ndoto hiyo akaonyeshwa karibia mali zote alizokuwa nazo Sam, tena alikuwa na uwezo wa kuona zile zinatakiwa kuendelezwa na zile ambazo hazipaswi kuendelezwa.
Kwakweli katika ndoto yake hapo aliweza kujua vitu vingi sana.
Pia akaonyeshwa ile ofisi ya Sam na jinsi Jeff alivyoenda pale bila ya kujitambua na kuwasimamisha kazi wafanyakazi wote katika ile kampuni.
Emmy aliweza kuona vitu vingi na mambo mengi sana.
Muda alioshtuka ni pale alipogundua kuwa tayari pamekucha na alipojaribu kuangaza aliweza kugundua mambo mbali mbali.
Ndipo alipoinuka na kwenda kwenye chumba ambacho Sam alikuwa analala yani chumba cha Sam.
Alipoingia aliona ni jinsi gani chumba kilipangwa vizuri na kumfanya akumbuke ile kazi ya usafi ambayo ilifanywa kwenye nyumba hiyo.
Akatabasamu kidogo na kusikitika kwani kufanyishwa kazi bila ya kujua basi unaweza kujikuta ukifanya kazi kupita uwezo wako wa kawaida.
Emmy akaenda na kukaa kitandani kwa Sam huku akitafakari mambo mengi sana ambayo yametokea kiukweli alibaki akiwa kimya tu kisha akainuka bila kupekua popote pale na kuamua kutoka mule chumbani na kurudi sebleni ili aweze kuondoka zake.
Ila alipofika sebleni akajaribu kuangaza tena kwani alitambua wazi kuwa yule kiumbe wa ajabu ni lazima bado yupo mule mule ndani kisha akajaribu kama kuuliza ili aone kama atajibiwa ila aliona kimya, kisha akaona karatasi nyingne mezani imeandikwa,
"Kwaheri Emmy, nikiwepo hapo siku nyingine utajua tu ila nimeondoka."
Ikabidi Emmy atoke na kurudishia ile milango akaangalia gari moja wapo ya Sam ambayo funguo ilikuwa mlangoni na kwenda kupanda gari hiyo na kutoka nayo huku safari yake ikiwa ni kuelekea nyumbani kwakina Sabrina ili kujaribu kuwaulizia kama wanafunguo za nyumba ile na pia kuwaambia kuwa kama kuna yeyote atakayejisikia kuwenda kuishi pale basi amwambie kuwa aende akaishi.
Kwahiyo milango ya pale aliirudishia tu na kuondoka na ile gari.
Huku kwakina Sabrina nao waliamka asubuhi na mapema huku mama Sam na wale wenzie wakijiandaa kwaajili ya safari yao ya kurudi Arusha kasoro mama mdogo wa Sam ndio hakufanya hivyo hata dada yake alimshangaa kwani alikuwa pale kwakina Sabrina kamavile ni ndugu zake kweli kweli.
Dada yake akamuita pembeni,
"Kwahiyo wewe ndio huondoki?"
"Dada, mmenipa nauli ya kusema niende?"
"Khee kwahiyo nauli huna! Mwambie aliyekuleta akupatie urudi"
"Dada jamani, hujui kama aliyenileta ndio huyo marehemu mtoto wetu? Sasa hiyo nauli atanipatia nani?"
"Pole mdogo wangu, nikifika huko na kupata pesa ya kutosha nitakutumia uje. Ngoja kwasasa nisafiri na hawa kwanza niliokuja nao"
"Sawa hakuna tatizo"
Kisha wakarudi ndani na kuaga na wale wenzie kwa pamoja ikabidi wakina Sabrina watoke nao kwa lengo la kuwasindikiza.
Walipofika nje huku wakiagana agana ndipo akaingia Emmy na ile gari ya Sam na kufanya karibia wote pale washtuke kwani wote wanatambua wazi kuwa ile gari ni ya Sam ila kabla hawajaamua chochote walimuona Emmy akishuka toka kwenye ile gari na kuzidi kumshangaa.
Ila Emmy alisogea na kuwasalimia bila ya tatizo lolote.
Moja ya marafiki wa mama Sam akamuuliza mama Sam,
"Hii si ndio ile gari tuliyoikuta jana na gari zingine!"
"Ndio ni hii hii"
Mama Sam akamuuliza Emmy,
"Umeitoa wapi hiyo gari?"
"Nimetoka nayo nyumbani kwa Sam"
"Aah kumbe"
Kisha mama Sam akamsogelea Emmy na kumnasa kibao, kabla ya Emmy hajauliza wala kusema chochote akamnasa tena kibao cha pili kisha akamsukuma na kufanya Emmy aanguke chini.
Mama Sam akamuuliza Emmy,
"Umeitoa wapi hiyo gari?"
"Nimetoka nayo nyumbani kwa Sam"
"Aah kumbe"
Kisha mama Sam akamsogelea Emmy na kumnasa kibao, kabla ya Emmy hajauliza wala kusema chochote akamnasa tena kibao cha pili kisha akamsukuma na kufanya Emmy aanguke chini.
Akataka kumsogelea tena na pale chini ila mama mdogo wa Sam alisogea kwa haraka na kumshika dada yake huyu huku akimuuliza kwa tahamaki,
"Una nini wewe dada?"
Mama Sam akajibu kwa hasira,
"Sina chochote, na aliyemruhusu huyu kuchukua gari ya mwanangu ni nani?"
"Kheee hiyo ndio sababu!!"
"Ndio"
"Hebu acha kunichekesha dada yangu, pale kwa Sam kuna gari ngapi? Jana si mlienda! Mmeshindwa nini kuchukua gari hata moja mkaondoka nalo? Kisa cha kumpiga mtoto wa watu nini? Kwanza sijaona hata cha kugombea hizo mali za Sam"
"Licha ya hivyo unadhani ni nani aliyetupulizia ule moshi kama si yeye?"
Emmy alikuwa kimya tu akiwaangalia na kuona kwamba alichowafanyia yule kiumbe ilikuwa ni saizi yao kabisa kwani walifanya vitu bila hata kufikiria.
Baada ya kimya
kidogo, mama Sam akang'ang'ania kuwa achukue ile gari na wenzie waondoke nalo.
Mdogo wake akacheka na kumuuliza,
"Kwanza hebu usinichekeshe dada yangu, hilo gari umeanza kujifunza lini? Hebu tutolee vituko jamani"
Sabrina nae aliinama pale chini na kumsaidia Emmy kuinuka kisha akasogea nae pembeni na kusema,
"Jamani kuhusu gari hata sio swala la kugombana, gari nyingine ya Sam ipo hapo kwenye gereji nyuma tulienda kwaajili ya kulipaki. Kwahiyo kama mnataka mnaweza mkachukua ile, sioni sababu ya kubishana hapa"
"Sabrina hebu nyamaza, haya magari yanayoongelewa hapa ni magari ya mwanangu, mimi ndio mwenye uchungu wa mtoto huyo na ndio mwenye haki katika mali zake zote. Hakuna mtu yeyote anayepaswa kujimilikisha mali za mwanangu zaidi yangu mimi mwenyewe"
Sabrina na Emmy wakamuangalia huyu mama wakimshangaa tu kwani ilionyesha wazi anaongea vitu bila kujua sheria maana ukiacha undugu bado kisheria Sabrina alikuwa ni mke halali wa Sam na wale watoto wake walitambulika kuwa ni watoto wa Sam pia.
Kwahiyo huyu mama hakuwa na sababu kubwa ya kujimilikisha mali za Sam bila kujiuliza kwanza kuhusu mali hizo.
Huyu mama bado alikomalia swala lake kuwa alikuwa akihitaji gari lile ambalo Emmy amekuja nalo ila Emmy akaongea na yeye sasa,
"Sina haja ya kuwakatalia chochote kile ambacho ni mali ya Sam ila tu sio kwa hili gari mnalolitaka. Kwakweli nawaonea huruma juu ya hili"
"Huruma ya nini kwenye mali za mwanangu? Kama unataka kututishia uchawi basi mimi ni mchawi zaidi yako na wala siogopi kitu"
Emmy akatikisa kichwa kwa ishara ya kusikitika, kisha akawatazama watu wote wa pale na kusema,
"Jamani, namkabidhi huyu mama funguo ila sitapenda mtu yoyote kunisema juu ya chochote watakachokutana nao hawa watu"
Kisha Emmy akampa funguo yule mama wa Sam.
Huyu mama akasema,
"Hapa sasa ndio sawa"
Akawageukia wale wenzie na kuwaambia,
"Twendeni sasa, haya ndio mambo. Hapa ni mwendo hadi Arusha"
Wale wamama walikuwa wamesimama kimya tu wakimuangalia na kumfanya Mama Sam aseme tena,
"Twendeni jamani, usafiri ndio huu hapa ushapatikana"
Ila yule rafiki yake aliyejulikana kwa jina la Bahati, muda huu akaongea,
"Ndugu yangu, rafiki yangu. Tunakupenda sana, tumekuja vizuri huku kwenye msiba na mwishowe nikakutana na habari zingine kuhusu mwanangu Keti. Sina cha kurithi kutoka kwa mwanangu maana hakuwa na chochote, mwenzangu mwanao alikuwa na mali na magari ndiomana unapata hata kiburi za kusema unataka urithi. Swali langu kwako, mwanao Sam na mali zote hizo je amewahi kukwambia kuwa mama chukua hii gari moja hata utembee tembee nalo tu, amewahi? Kama hajawahi jiulize kwanini? Ningekuwa wewe nisingechukua chochote kile zaidi ya kumshukuru Mungu tu, kuzaa si sababu ya kufanya tung'ang'anie hata visivyotuhusu rafiki yangu. Kumbuka uling'ang'ania kwenda kule kwa Sam yakatukuta majanga, saivi unang'ang'ania gari yake mmh mimi sipandi hiyo gari kama hayo majanga yakakupate mwenyewe mi simo ila usiseme kwamba hatukukwambia."
Yule mama mwingine naye akasema,
"Yani Bahati umeongea kile ambacho mimi nilitaka kuongea, hiyo gari aende nayo mwenyewe kwakweli hakuna mtu anayetaka majanga ya kujitakia. Mtu unakatazwa kitu ila bado unang'ang'ania kwakweli nenda mwenyewe ila kumbuka kuwa una watoto zaidi ya Sam wanaokutegemea."
"Kheee kwahiyo ndio mmenisusia eeh!!"
Mama Sam alionekana kuwa mbishi sana ila mama mdogo wa Sam naye akaingilia kati,
"Dada hebu mambo mengine uwe unaachana nayo jamani, kwanini unakuwa hivyo dada yangu. Hebu jaribu kuwa muelewa"
"Kheee na wewe mcha Mungu unaungana nao kwenye imani za kishirikina.? Kweli vya dunia vitamu"
Akatupa ule ufunguo wa gari chini na kusema,
"Haya twendeni tukapande hayo mabasi mliyoamua"
Kisha akaanza kuongoza mbele, hakuna aliyeongeza neno zaidi ya kufatana nae.
Ila Sabrina alibaki na Emmy pale nyumbani kwao.
Kisha Emmy na Sabrina wakaingia ndani, ambapo Sabrina alianza kumuuliza Emmy kuhusu hali yake,
"Hebu niambie kwanza Emmy unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri kabisa Sabrina"
"Unajua nini Emmy, kumekuwa na matatizo mengi mengi sana hapa kati ndiomana imekuwa ngumu hata kuzungumza mambo ya hapa na pale ila kuna jambo nilitaka kukuuliza Emmy"
"Wewe uliza tu Sabrina hata usiwe na shaka"
"Swali langu Emmy ilikuwa ni kuhusu Sam, uliwezaje kumsaidia Sam akapona kutokana na lile tatizo alilokuwa nalo?"
"Nilijua tu Sabrina kuwa lazima utaniuliza kuhusu hilo swala, kwakweli ni historia ndefu labda nikueleze kwa kifupi tu"
"Nieleze hata hiyo kwa kifupi nipate kuelewa hata jambo kidogo"
"Kwanza kabisa siwezi kusahau ile siku niliyoweza kukutana kimwili na Sam, ilikuwa ni Arusha kwenye hoteli yake."
"Niambie basi uliwezaje kupona wewe na yeye? "
"Unajua mwanzoni nilianza kukata tamaa kuhusu kumsaidia Sam na nilitamani kuacha mambo kama yalivyo ila hakuna siku niliyopandwa na kichaa kama siku ambayo nilikuta mama yangu amekufa na watu wamekusanyika pale nyumbani ilihali nilijua wazi kuwa mama yangu hakufa kweli"
"Mmh ulijuaje Emmy kama mama yako hakufa kweli?"
"Unajua mimi hapo kabla nishawahi kuwa na matatizo kama ya Sam sababu kulikuwa na jini ambalo lilinitesa maishani ila mara nyingi nilikuwa najichunga ili nisimalize wanaume wanaonizunguka ukizingatia sikuona kosa. Ile hali yangu ilinisumbua sana na niliikataa kabisa kiasi kwamba nilizunguka kila mahali kwa lengo la kupata tiba. Kiukweli kuna wanaume kama watano waliokufa kwasababu yangu ingawa Sam nilimwambia kuwa ni wanaume wengi sana ili kumvuta akapate matibabu na aone kuwa tatizo lake linatibaka. Wale wanaume watano waliokufa kwaajili yangu kwakweli niliumia sana, haswa huyu wa mwisho aliumiza roho yangu kiasi kwamba nikajitolea maisha yangu kupambana na hali niliyokuwa nayo. Katika kuhangaika kwangu ndio nikapambana na mizimu ambayo imekuwa ikinifatilia sasa mara nyingi hadi nilijihakikishia kupona ila bado sikutaka kulala na mwanaume yeyote hadi nilipokutana na huyu Sam. Kiukweli ile mizimu imekuwa migumu kutoka kwangu ila ndio hunionyesha au kunishtua kuhusu jambo lolote lile ndiomana kuna wakati naonekana nafanya mambo kama ya kiganga"
"Duh! Ndiomana umewakataza kuondoka na ile gari eeh! Hapo inaonyesha umeona kitakacho wapata?"
Emmy akacheka kidogo,
"Sabrina jamani maswali yako loh!"
"Haya basi tuachane na hayo, haya vipi kuhusu kifo ulipogundua ukafanyaje? Je ulimsaidia mama yako kupona au ilikuwaje?"
"Kiukweli hata wakina Sam walijua nimechanganyikiwa au nilikuwa jini, kipindi hiko nagundua nilikuwa na Sam pamoja na Francis. Yawezekana Francis akakueleza mengi zaidi maana mimi nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Ninachokumbuka zaidi ni ule muda niliozimia kwani nilikuwa naonyeshwa mambo mengi sana, sasa nilipozinduka kwakweli sikuwa Emmy mimi kabisa hata Sam mwenyewe alinisimulia kuwa alibaki kunishangaa tu. Francis yakamshinda ikabidi tumruhusu aondoke. Yani lile jini la Sam kwakweli lilitutesa sana, ilitakiwa niupate ule mwili wa mama ili aweze kuwa hai tena. Cha kushangaza sasa, mwili wa mama akaja kuuweka nyumbani kwa Sakina jamani tena chumbani loh!! Nashukuru nilikuwa na ule moyo wa kijasiri, moyo wa Emmy mwingine mbna ningekuwa mimi kwakweli nisingeweza. Keti aliogopa sana ila nikafanikiwa kuupata ule mwili na kuondoka nao, nakumbuka nilimuacha Keti akiwa ameanguka.
Nilikutana tena na Sam kisha tukamtafutia mama dawa na kumfanya azinduke, ila zile hasira ndio zilifanya nifunge safari tena na Sam kwenda kupambana na yule jini huku nikiwa nimejitoa kabisa, kufa na kupona."
"Khee yalikuwa makubwa hivyo mmh! Kwanza mama yako aliwezaje kurudi kwenu?"
"Mama, tulimrudisha wenyewe na kumuacha mlangoni. Ila nasikia nyumbani walishtuka sana na wengine wakidhania kuwa ni mzimu ila mama alikuwa salama kabisa na yupo salama hadi leo."
"Kwakweli mizimu yako ni mikali sana Emmy mmh!! Sasa kuhusu Sam ndio ukaenda nae wapi?"
Kabla Emmy hajaanza kuelezea, mama mdogo wa Sam pamoja na mama Sabrina wakawa wamerudi.
Waliwakuta Emmy na Sabrina wakizungumza pale sebleni ambapo walipoonekana moja kwa moja Sabrina aliuliza kuhusu usafiri kama waliupata wale ndugu wa Sam.
"Ndio wameshapanda gari, kwahiyo jioni utawasikia kuwa wameshafika"
"Mmh ila mama Sam mbishi jamani, ndiomana mule ndani mimi na yeye tulikuwa tukisumbuliwa na lile jini kila siku na mwishowe uzalendo ukamshinda hadi akaondoka. Ila amerudi anafanya maubishi yake na kujifanya kuwa kasahau yale yote yaliyokuwa yakiwatokea"
Mama Sabrina nae akaongezea,
"Ndiomana wamerudi hapa wamechoka balaa eti walizimia mmh kule kuzimia au kubeba zege?"
Ikabidi Emmy awaeleze kwa kifupi aliyoyakuta kwenye nyumba ya Sam, aliwaeleza zaidi kuhusu ile sinema ila tu aliwaficha kuhusu yule jini, ndipo mama mdogo wa Sam alipomuuliza,
"Wewe uliwezaje kuona hiyo sinema?"
"Ilitokea tu"
"Ilitokeaje? Lazima kulikuwa na kitu Emmy ila hata hivyo tuachane na hayo tujadili ya kwetu"
Emmy akainama chini kidogo kwani ilikuwa ni kweli ila aliogopa kuongelea kuhusu lile jini tena akihofia kujenga uoga kwa watu pale ndani haswaa Sabrina kwani alijua wazi kuwa lazima Sabrina ndio ataumiza akili zaidi kwa jambo hilo ingawa karibia wote pale sebleni walitamani kujua kuwa ilikuwaje mpaka kupelekea Emmy akaonyeshwa alivyoonyeshwa.
Ikabidi wabadilishe mada na kuanza kuzungumzia mambo mengine na pia Emmy asingeweza kusimulia alivyomuokoa Sam mbele ya mama mdogo Sam na mama Sabrina kwahiyo muda huu Emmy akaaga kwa lengo la kuondoka ila Sabrina ndio akainuka nae Emmy na kutoka nae nje kisha akamwambia,
"Bado nina mengi ya kuongea na wewe Emmy"
"Naelewa hilo Sabrina"
"Sasa itakuwaje Emmy?"
"Basi kesho nije nikuchukue twende kule nyumbani kwa Sam tukazungumze maana naona leo muda utakuwa umeenda sana"
Ila ni hapa hapa ambapo Emmy akakumbuka kuwa kilichomleta hapo ilikuwa ni funguo za nyumba ya Sam na si kitu kingine chochote, ndipo alipomkumbushia Sabrina ambaye alienda kumwambia mama mdogo wa Sam kuhusu funguo ambapo aliwakabidhi funguo hizo.
Kisha Emmy akamwambia,
"Au twende leo basi?"
"Hapana Emmy, tutaenda kesho"
"Basi sawa, ngoja mimi nikafunge milango kisha nirudi kwetu maana sijaenda tena tangu nilipoondoka jana"
Sabrina akashangaa kidogo maana kwa kumbukumbu zake ni kuwa Emmy alikuwa kwao, sasa jana tena tena akaenda wapi wakati wakina Jeff walihakikisha kabisa kuwa wamemfikisha kwao ila hakutaka kumuhoji sana kwa muda huo zaidi ya kumuaga na kuondoka.
Jioni ya siku hiyo mama Sam na wenzie walishafika Arusha ila mama Sam akawaambia wenzie kuwa waende moja kwa moja kwenye hoteli ya mtoto wake, hilo hawakupinga na wakaenda nae.
Kufika pale moja kwa moja alimuulizia meneja wa hoteli ile ambaye alitoka na kumsikiliza,
"Samahani mwanangu, mimi mnanifahamu?"
"Nakufahamu ndio mama, Sam ameshawahi kututambulisha kuwa wewe ni mama yake."
"Sawa, hapo vizuri sana. Hivi mnajua kama Sam amekufa?"
"Tunajua mama, na tulisikitishwa sana na kifo chake"
"Haya, sasa naomba uniletee nyaraka zote za hii hoteli"
"Za nini tena mama?"
"Za nini? Hamjui kuwa hoteli hii ni mali yangu? Sababu hapo kabla ilikuwa ni mali ya mwanangu"
"Mama, kabla ya kifo cha Sam kutokea huko, siku tatu za nyuma alikuwa huku na kuna mwanamke alikuja nae, kisha kesho yake akatutambulisha kuwa huyo mwanamke ndio mmiliki halali wa hii hoteli yake tena akabadilisha nyaraka zote"
"Unasemaje wewe? Na huyo mwanamke anaitwa nani?"
"Anaitwa Emmy mama"
Pale pale mama Sam akaanguka chini na kuzimia.
"Unasemaje wewe? Na huyo mwanamke anaitwa nani?"
"Anaitwa Emmy mama"
Pale pale mama Sam akaanguka chini na kuzimia.
Ikabidi wale wenzie wasaidiane na meneja kumsogeza pembeni maana ilikuwa ni njiani.
Kisha meneja akachukua gari yake na kusaidiana kumuweka kwenye gari hiyo ili kumuwaisha hospitali.
Ila walipofika njiani huyu mama alizinduka na kuwaomba wampeleke tu nyumbani kwake ambapo yule meneja alifanya hivyo kwa kufatilia maelekezo kutoka kwa wale wenzie.
Walifika na kushuka na kuingia ndani, kisha mama Sam akamshukuru huyu meneja na kumuuliza pia,
"Asante kijana kwa msaada wako, ila ngoja nikuulize"
"Uliza tu mama"
"Unadhani ni halali kwa Sam kumpa hiyo hoteli mwanamke?"
"Kwakweli mama hata mimi sielewi makubaliano yao ila mimi nafatisha vile mwenyewe alivyotaka"
"Je wewe unaweza kumuandika mwanamke kwenye mali zako na kumuacha mama yako?"
"Mmh mama hapo pagumu kidogo, ila kwakweli mimi nampenda sana mama yangu tena sana. Kabla sijaoa, kila nilichomiliki mimi bila kujali ni kidogo cha aina gani nilikuwa nikiweka jina la mama, ila nilipooa na kupata watoto basi wanangu ndio niliwapa kipaumbele ila bado mama alikuwa na nafasi yake kama mama"
"Kwahiyo unapopata watoto, hao watoto ndio wanakuwa na nguvu kuliko mama yako?"
"Mama kiukweli kabisa, mama kama mama ana nafasi yake, mke ana nafasi yake na watoto nao wana nafasi yao. Huwezi kutenganisha sana ila kadri siku zinavyokwenda ndipo unajitahidi kufanya mambo mengi zaidi kwaajili ya watoto wako yani hapo mama yuko pembeni na mke nae yupo pembeni kwani utawatazama zaidi watoto kuwa wataishije, watakula nini na watalala wapi"
"Nashukuru mwanangu, ila hebu tutoe hilo swala la watoto na tuongelee nafasi ya mke na mama"
"Mke na mama hawawezi kufanana maana kila mmoja anakuwa na nafasi yake. Ukiniuliza mimi kuhusu kupenda kati yao basi nitakujibu kuwa nampenda zaidi mama yangu, pia hilo ndio jibu la kila mmoja kwani mama ndio mtu pekee mwenye mapenzi ya kweli kwa mtoto wake"
"Sasa kwanini Sam ampe mwanamke na kumuacha mama yake?"
"Hilo sijui mama ila kama ujuavyo hawa wanawake wa siku hizi, labda kuna vidawa kamfanyia ukizingatia yule hata si mke halali wa ndoa ile ndiye aliyempa hoteli yake. Labda kuna dawa kamfanyia ila mama ndiye mwenye upendo kwa mtoto"
Bahati aliyekuwa pembeni ambaye ni rafiki wa mama Sam akaongezea pia,
"Na mama ndiye mtu pekee ambaye akiamua kufanya roho mbaya basi ni roho mbaya kweli na akiamua kuwa mkatili basi anakuwa katili haswa"
Muda kidogo akaanza kulia huku akitaja jina la mwanae Keti, alionekana kulia sana kiasi kwamba akajaza watu pale nyumbani kwa mama Sam wakijua kuna msiba tena mahali pale.
Huyu meneja ilibidi aage na kuondoka zake kwani tayari ilikuwa ni usiku.
Mama Sam na mwenzie wakaanza kumbembeleza huyu ili anyamaze kwani tayari alifanya watu wajae katika nyumba ile.
Walibembelezana pale mpaka alipotulia kabisa kisha wakamsindikiza na kumpeleka nyumbani kwake, ingawa alipofika kwake pia aliwaita wanae usiku ule ule huku akiwakumbatia na kulia nao.
Hawa watoto walimshangaa mama yao kwavile hawakuelewa anacholilia ila alipotulia akawaambia,
"Hivi mnajua kama mlikuwa na dada yenu?"
Hawa watoto walikuwa watatu tena wa kiume wote, wakatazamana kwani hakuna aliyekuwa akijua kwamba wana dada,
"Unamaanisha nini mama?"
"Dada yenu alikuwa akiishi mjini, ni mwanangu niliyemzaa mimi mwenyewe alikuwa ni mwanangu wa kwanza ila ndio tumeshamzika tayari"
Watoto wakatazamana na kumuuliza tena mama yao,
"Kivipi? Na kwanini hatukumjua siku zote hizi?"
"Nilimuacha kijijini na mama yangu, nilipokuja mjini nikapata mwanaume wa kuishi nae amcye ndiye baba yenu ila sikuthubutu kumwambia kuwa nina mtoto kwavile alijua kuwa mimi bado ni bikra ukizingatia ndivyo nilivyomuongopea, sikutaka kumwambia kuhusu mama yangu wa ukweli kwani ndiye aliyekuwa akiishi na binti yangu. Kwahiyo baba yenu nilimpeleka kwa mama yenu mdogo ambaye alikuwa ni kama rafiki yangu na alinifichia siri zangu zote, ila leo kifo cha mwanangu kimeniumbua mimi mmh kwanini umekufa Keti? Kwanini umekufa bila ya kuniona mama yako?"
Akaangua kilio kingine na kumfanya awe kama mtu aliyechanganyikiwa, kwahiyo muda huu ni hawa wanae waliokuwa wakifanya kazi ya kumbembeleza mama yao kwani hali yake iliwatisha kwa kiasi fulani.
Alipotulia ndipo mama Sam na yule mwenzie nao wakaaga na kuondoka ukizingatia usiku ulikuwa umeingia sana.
Kulipokucha kamavile ambavyo Emmy alimuahidi Sabrina kwani alifika pale asubuhi na mapema kwa lengo la kumchukua Sabrina ili aweze kwenda nae kwa Sam na waweze kuzungumza yale waliyotaka kuzungumza kwa undani zaidi siku ya jana.
Sabrina alipomuona Emmy akamshangaa kidogo kwani ilikuwa ni mapema sana.
"Emmy umekuja mapema!"
"Asubuhi ndio vizuri"
"Vipi umekuja na gari ya jana?"
"Hapana"
"Kwanini sasa?"
"Nimeiacha nyumbani kwa Sam ile jana nilipoenda kufunga milango"
"Ila kwnini umeiacha?"
"Huwa sipendi lawama Sabrina ndiomana nimeamua kuiacha" "Emmy, uliyajali maneno ya yule mama ndugu yangu! Yule hata asikuumize kichwa ndugu. Ngoja nijiandae twende"
Sabrina akaenda ndani kujiandaa na kumuacha Emmy akiwa pale sebleni.
Muda kidogo mama mdogo wa Sam alitoka chumbani na kumkuta Emmy ambapo alimsalimia na kuanza kumuuliza hali yake na anavyojisikia,
"Niko salama tu mama yangu"
"Basi vizuri, ashukuriwe Mungu kwa hilo"
"Ila mama wewe una upendo sana jamani, naamini ipo siku Mungu atakufanikisha na atajibu kilio chako"
"Kilio changu ni kuona nyie mnafurahi kwakweli hiyo ndio furaha yangu"
Sabrina nae akawa ametoka ndani tayari kwa safari, kisha wakaaga pale na kuondoka.
Mama Sam kwa siku ya leo alikuwa akijiuliza kuhusu mtoto wake na mali za mwanae kwani bado aliona kuwa yeye ndiye mwenye haki ya kumiliki mali hizo.
Akaiwaza ile kauli iliyotolewa na meneja wa hoteli ya Sam kuwa huenda Sam kachezewa na madawa, kwahiyo moja kwa moja mama Sam akapata wazo kuwa huenda Emmy kamuwekea madawa Sam kisha akawaza kuwa huenda hata mimba anayosema si kweli.
Mama Sam akafikiria sana swala hili, ndipo alipopata wazo la kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kupata uthibitisho wa mawazo yake kwani hakuamini kabisa kuwa Sam anaweza kufanya vile licha ya kwamba anajua wazi kuna mambo ambayo hayakuwa mazuri yeye kumfanyia Sam.
Akajiandb vizuri na kuelekea kwa mtblamu ambaye alijua ndiye anayeweza kumsaidia tatizo lake.
Ila alipofika pale alikutana na foleni kubwa sana, ikabidi akae kwenye foleni akisubiria zamu yake ya kumuona mtaalamu.
Akiwa pale kwenye foleni, akajikuta amekaa karibu na binti mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema na kuanza kufanya nae mazungumzo ya hapa na pale ambapo huyu binti alimuuliza mama Sam,
"Kwani mama wewe shida kubwa iliyokuleta hapa ni nini?"
Mama Sam akamuelezea kwa kifupi kilichompeleka ingawa anajua wazi kuwa kila mtu pale ameenda kwa matatizo yake binafsi.
Kisha huyu Neema akamwambia mama Sam,
"Kwahiyo hapo unaona mwanao hajakutendea haki, unaona mwanao hakupendi ila jiulize je wewe ukikuwa unampenda mwanao?"
"Ndio nilikuwa nampenda tena sana"
"Kama ulikuwa unampenda kwanini ulimfukuza nyumbani kwako hadi akalelewa na mdogo wako?"
"Kheee umejuaje kama nilimfukuza?"
"Kwa maelezo yako ya awali tu nimejua kama ulimfukuza mwanao ndiomana hata mwanao hakupendi"
"Ila mimi sikumfukuza kwa kupenda, hujui tu. Mwanangu alikuwa na mambo ya ajabu sana yani kuna kipindi alitaka hata kunibaka"
"Mmh mama! Mwanao akubake! Akubake kwasababu gani haswa? Wewe mama lazima una matatizo ndiomana mtoto wako alikuwa hakupendi"
"Nani kakwambia kuwa mtoto wangu alikuwa hanipendi?"
"Sio nani kaniambia, kwanza wewe jua kwamba ndio chanzo cha kumfanya mwanao ajiingize kwenye mambo ya kishetani kwavile alikosa upendo kutoka kwako, yale manyanyaso yako yakamfanya awe vile. Hivi unajua ni wasichana wangapi waliokufa sababu ya mwanao? Basi damu yao wote inakulilia wewe maana wewe ndiye uliyebeba kile kiumbe tumboni mwako. Maana yangu ni kwamba wewe ndiye uliyemzaa yule Sam na kutokana na manyanyaso yako ukafanya mwanao ajiingize katika mambo mabaya halafu mambo hayo yakafanya wasichana wengi sana wafe. Je unafikiri damu zao zinamlilia nani kama si wewe mama yake?"
Mama Sam alimshangb sana huyu binti, kisha akamjibu,
"Kuzaa sio sababu ya mimi kubeba dhambi zake, na yeye kujiingiza kwenye mambo hayo sio sababu ya kunipa lawama mimi , kwakweli kama kuna mtu anawaza kunipa lawama mimi kwa makosa ya mwanangu basi atakuwa ananionea"
"Kupewa lawama hutaki ila mali za mwanao unazitaka, kuzaa sio sababu ya kurithishwa mali na mwanao. Kwanza unajua hizo mali kazitoa wapi? Unajua kafanya nini kupata hizo mali? Kama hujui kwanini unazing'ang'ania? Na kama unajua basi kwanini unakwepa kulaumiwa kuhusu matendo ya mwanao?"
"Kheee wewe binti umetumwa au?"
Huyu dada akaanza kucheka kisha akamwambia,
"Kama hujui mama basi ngoja nikujuze, damu yangu ni kati ya damu zinazokulilia wewe yani mimi ni mmoja wapo wa wanawake waliokufa sababu ya mwanao"
Kisha akacheka tena na kumpa mama Sam uoga, ambapo aliinuka kwa uoga na kuanza kukimbia kwa lengo la kurudi nyumbani kwake.
Sabrina na Emmy walifika nyumbani kwa Sam na palikuwa kimya sana na kuingia ndani, kwakweli hata Sabrina alishangaa usafi uliofanyika kwenye ile nyumba na kumfanya aamini kuwa ni kweli wakina mama Sam walifanyishwa usafi kwenye nyumba hiyo.
Walikaa chini na Emmy na kuanza mazungumzo ya hapa na pale.
"Eeh Emmy niambie sasa jinsi ambavyo Sam alipona"
"Ilibidi twende kwenye kiini cha tatizo ili kuweza kutatua lile tatizo, unajua ubaya ni nini! Ubaya ni kuwa yule mganga aliyempa lile jini alikuwa ni marehemu tayari. Kwakweli ukitaka kuteseka ni upewe kitu na mganga halafu mganga huyo afe kwakweli utatamani kulia maana utakuwa umeachiwa matatizo ya milele ndiomana hata neno la Mungu linasema kuwa amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Ni kweli kabisa yani tena ni laana ya milele. Kwakweli tumepata shida sana mpaka Sam kurudi kwenye hali ya kawaida na hata alipopona bado hakujiamini kuwa amepona kwahiyo nikaamua kujitoa kwenda kulala nae. Ndipo nikaenda nae kwenye hoteli yake Arusha ambapo tulilala na wote tukatoka wazima kabisa. Kile kitendo kilimfurahisha sana Sam ndipo kesho yake alipoamua kubadili umiliki wa ile hoteli na kuniweka mimi kama mmliki, alikuja pale mwanasheria wake na kupitisha hilo"
Kwakweli hapa Sabrina alishtuka kidogo kwani hakujua kama umiliki wa ile hoteli ya Sam tayari ulishabadilishwa na kuona kuwa Emmy amemfanyia Sam vitu adimu sana na kumfanya afikie kwenye maamuzi yale.
"Kwahiyo hoteli ya Arusha ameiweka jina lako?"
"Ndio aliweka jina langu"
"Vitu gani vingine vina jina lako Emmy?"
Sabrina alionekana kupata mashaka kidogo kwani kitu kama ile hoteli kubwa kumfanya Sam abadilishe jina kwa muda mfupi kukamfanya aone kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna vingi ameweza kubadilisha kwa hali hiyo.
Swali la Sabrina lilimfanya Emmy acheke kwani aligundua mawazo yake kwa rahisi sana, kisha akamjibu,
"Unajua nini Sabrina, hata siku ile wakati mama Sam anaongea nilimwambia kwamba kama ningetaka mali za Sam basi ningezipata kwa urahisi sana ila sikuwa na haja na mali za Sam, tena nitaenda kukupeleka kila mahali kwenye mali zake ili iwe rahisi kwako kujua zilipo mali za Sam kwani kuna zinazofaa na zisizofaa basi mimi nitakuonyesha na kukuelekeza"
"Wewe umejuaje zinazofaa na zisizofaa?"
Emmy akacheka kisha akasema,
"Mambo mengine tuachane nayo Sabrina ila twende chumbani kwa Sam tukaangalie baadhi ya vitu"
Emmy akainuka akiwa na Sabrina na kuelekea chumbani kwa Sam ambapo walipakuta pakiwa na utulivu kabisa.
Leo Sabrina aliweza kutulia na kukiangalia vizuri chumba cha Sam ambapo wakati wanapekua pekua, wakaona kitabu kidogo cha Sam na walipokiangalia vizuri wakagundua kuwa ni kitabu chake cha matukio ya kumbukumbu.
Kitabu hiki kiliwafanya Emmy na Sabrina watulie wakikisoma.
Mama Sam alifika kwake huku akiwa anahema sana kwani hakumuelewa kabisa yule binti aliyekutana nae kwa mtaalamu.
Alipoingia sebleni kwake na kukaa ndipo alipogundua kuwa alipokaa kuna mtu amemkalia Alipogeuka kumuangalia mtu huyo akamkuta ni yule binti Neema.
Alipogeuka kumuangalia mtu huyo akamkuta ni yule binti Neema.
Kwakweli mama Sam akashtuka sana na kuogopa kwani huyu binti alikuwa akicheka tu.
Mama Sam akazimia kwa uoga, baada ya muda mfupi akazinduka pale sebleni na kumkuta binti yake akimpepea huku akimpa pole na kumuuliza kuwa anajisikiaje.
"Mwanangu upo hapa tangia muda gani?"
"Toka unaingia mama, mie nilikuwa hapa hapa"
"Hakuna mtu wa ajabu uliyemuona?"
"Sijamuona mtu zaidi yako mama"
Mama Sam akapumua kwa pumzi ndefu sana kwani alikuwa kamavile haamini alichoambiwa na binti yake huyu kuwa hakuna mtu yeyote aliyeonekana zaidi yake, kisha mwanae akamuuliza,
"Kwani tatizo ni nini mama yangu?"
"Yani mwanangu sirudii kwenda kwa mganga mimi sirudii tena"
"Khee mama yani ulienda kwa mganga kumbe!! Ila mama kwanini usingekuwa kama mamdogo tu. Mdogo wako yupo vizuri sana, imani za kishirikina hana kabisa. Ukikaa nae ni habari za Mungu tu. Ungeachana na wewe na hayo mambo ya kuwaamini waganga mama yangu."
"Matatizo mwanangu ndio yanayonipelekaga kwa mganga"
"Matatizo gani tena wakati kila siku hapa ulikuwa unalalamika kuhusu mwanao Sam kuwa sio mtu mzuri na anakufanya uende kwa waganga. Haya sasa huyo Sam ameshakufa, kinachokupeleka kwa waganga ni nini?"
"Ila na wewe ndio huna uchungu jamani, hata hujaumizwa na kifo cha Sam!"
"Naumizwa vipi na mtu aliyesababisha kifo cha dada yangu na rafiki yangu, hata nimekuwa nikikushangaa siku hizi unavyojifanya kuwa umeumizwa na kifo cha Sam sijui eti unampenda, hivi mama unawezaje kumpenda mtoto ambaye umekuwa ukimkana kila siku? Tena kuna kipindi ulisema huenda Sam walikubadilishia, na pia utampenda vipi mtu muuaji kama Sam! Bora na yeye amekufa, na ungejua watu walivyofurahi kusikia huyo mwanao amekufa basi ungekuwa unashangaa tu hapa. Tena mmefanya jambo la maana sana kumzikia huko huko mjini maana huku hata maiti yake ingepigwa mawe. Yule mwanao alikuwa muuaji mama hata sio wa kumsikitikia"
"Yote hayo sijakataa ila yule bado ni mwanangu bila ya kujali chochote alichofanya, sikuhudhuria harusi yake wala sikujishughulisha na chochote ila siku nilipoenda kwa mdogo wangu na aliponieleza kuwa Sam ana watoto ndipo nilipofunga safari kwenda kuwaona watoto hao yote sababu bado nilikuwa nampenda mwanangu"
"Mama, na sisi tunakupenda sana. Tafadhari achana na mambo ya huyo Sam kisha tufanye maisha yetu ya maendeleo maana huyo Sam hakuwa na msaada wowote kwako na wala hawezi kuwa na msaada. Cha msingi tuangalie maisha yetu tu"
Mama Sam alipofikiria kwa kina aliona kama maneno ya binti yake huyu kuwa yana mantiki kwani hata yeye mwenyewe alipokumbuka vizuri aligundua wazi hakuwa akimpenda mwanae huku akifikiria chanzo kikubwa cha yeye kutokumpenda mwanae ni mwanaume aliyempa ile mimba kwani alimjengea chuki ya moja kwa moja katika moyo wake.
Mama Sam alifikiria sana maisha yake ya nyuma na kumfanya alaumu nafsi yake.
Akakumbuka alivyokutana na Deo na jinsi alivyopata ile mimba, akakumbuka jinsi Deo alivyoondoka katika mazingira ya kutatanisha na jinsi alivyojaribu kuitoa ile mimba bila ya mafanikio. Kisha akajiuliza,
"Au mimi ndiye niliyemvika roho ya laana mwanangu kwakule kujaribu jaribu kuitoa ile mimba?"
Akaguna na kukumbuka jinsi tumbo lake lilivyokuwa kubwa na kumfanya afukuzwe nyumbani kwao.
Ila alipojifungua na kupata wazo la kumtupa yule mtoto ndipo mdogo wake aliyekuwa akimtafuta akajitolea kusaidiana nae ili kumlea yule mtoto.
Na akakumbuka jinsi Sam alivyokua kua kidogo na kuwa mchapakazi sana kiasi cha kufanya atamani tena kuishi na mtoto wake huyo hadi pale alipopata mwanaume na kuolewa.
Akakumbuka jinsi mumewe alivyokuwa akimchukia Sam tena huku akimuonyesha chuki za wazi na kumfanya mama Sam amuondoe mtoto wake huyo kwa lengo la kuokoa ndoa yake.
Sam alielekea tena kwa mamake mdogo ambapo mume wa mdogo wake pia hakumtaka Sam na kupelekea mdogo wake pamoja na Sam kufukuzwa na ndipo Sam aliporudi tena nyumbani kwake huku mdogo wake nae akiwa hana makazi na alikuwa akitangatanga tu.
Ila huyu mumewe bado alionyesha chuki za wazi wazi kwa Sam, mpaka pale mama Sam alipohisi kuwa Sam anataka kumbaka ilihali alikuwa na miaka kumi na tano tu.
Ndipo aliposhirikiana na mumewe kumtimua Sam nyumbani hapo.
Ndipo Sam alipoingia maisha ya kutanga tanga kama mamake mdogo kwani ilikuwa kama huyu mdogo wake akipata bwana wa kuishi nae basi alienda na huyu Sam, halafu ikitokea huyu Bwana hamtaki Sam nyumbani basi aliwatimua wote.
Mama Sam akafikiria sana na kuona kiukweli mdogo wake ndiye aliyekuwa na upendo wa kweli kwa mwanae kwani hakujali kutangatanga kwake bali alimjali Sam kwanza.
Akakumbuka mdogo wake alivyomtembelea na kumwambia kuwa amepata kichumba cha kuishi na Sam, pia akakumbuka alivyomtahadharisha mdogo wake huyu kuishi na Sam kwani yeye alimuona kuwa tayari huyu mtoto wake ni kijana mkubwa kwahiyo angeweza hata kumbaka mdogo wake huyu ila ilionyesha kuwa huyu mdogo mtu alimuamini sana Sam na hakuona kama kuna tatizo lolote la kuishi nae.
Akakumbuka baada ya miaka kadhaa jinsi Sam alivyoenda nyumbani kwa mama yake kwa madai kuwa ameenda kusalimia, ndipo alipofanya uharibifu wake kwa kumuua binti mkubwa wa mume wa mama yake na pia akafanya uharibifu kwa kuwamaliza baadhi ya mabinti kisha akaondoka ila karibia sehemu yote pale walimchukia ingawa hawakumuona tena kwani mtu aliyekuwa akimtetea alikuwa ni mama yake mdogo ambaye pia alihama eneo alilokuwa anakaa na haikujulikana anapoishi tena kwa kipindi hicho.
Ndio akakumbuka miaka ya juzi juzi mdogo wake yule alipoenda kumchukua na kumpeleka nyumbani kwake na kumshangaa kuwa ile nyumba nzuri kaitoa wapi naye akamjibu kuwa ile nyumba imejengwa na Sam, ndipo mama huyu alipoamua kujua mengi kuhusu Sam, na ndipo alipogundua kuwa mwanae kwa kipindi hiko alikuwa ni kijana tajiri sana.
"Labda ni kweli kuwa ni mimi niliyesababisha mwanangu aingie katika mambo ya kishetani maana kama ningemlea katika maadili yampendezayo Mungu basi asingekuwa vile alivyokuwa."
Huyu mama alibubujikwa na machozi ya majuto juu ya mwanae.
Emmy na Sabrina walikuwa wametulia kabisa wakikisoma kile kitabu ambacho kilionyesha kuwa aliandika mambo mengi sana, kilianza kwa kusema,
"Mimi Sam, sikuwa mtu mzuri hata kidogo ila ubaya wangu ulitokana na kile nilichokikuta katika ulimwengu huu, sijui kwanini ilitokea watu kunichukia kiasi hiki hadi mama yangu mzazi!! Isipokuwa mama mdogo pekee ambaye hakuwa na bahati ya kuwa na mtoto ila alinipenda mimi kama mwanae kabisa"
Kisha wakaenda ukurasa mwingine ambao Sam aliandika,
"Nakumbuka siku niliyomuwekea dawa baba yangu wa kambo ili nimkomeshe kwa chuki yake dhidi yangu, nilikaa pembeni nikiangalia yule baba atakavyoenda kuoga, cha kushangaza kule bafuni alienda mama kuoga ndipo nilipojitosa mule bafuni na kumwaga yale maji ila mama alitafsiri vibaya kitendo changu hicho kwa kujua kuwa nilitaka kumbaka. Kwakweli niliumia sana kwani nilipigwa sana na yule baba pamoja na mama kisha nikafukuzwa kabisa kuwa nisionekane pale nyumbani. Siwezi kusahau hii siku kwani niliumia sana moyo wangu kisha nikaenda kuungana na mamdogo ambaye hakuacha kulia na mimi huku akiahidi tutakula na kulala popote Mungu atakapotujaalia."
Emmy na Sabrina wakatazamana na kwa kiasi fulani wakagundua ni jinsi gani Sam alikuwa na uchungu katika moyo wake.
Wakafungua kurasa nyingine iliyoandikwa juu kwa herufi kubwa 'MAPENZI NA UMASKINI'
Kisha wakasoma kilichoandikwa chini yake,
"Kwakweli vitu vilivyofanya mimi nijiingize kwenye mambo mabaya ni mapenzi na umaskini.
Niliishi na mamdogo katika maisha ya umaskini yale yaliyopitiliza, hata nilipojaribu kufanya kazi za hapa na pale bado sikupata uwezo wa kujikwamua katika umaskini wangu ukizingatia hata shule sikusoma kwavile mamdogo hakuwa na uwezo wa kufanya nisome.
Iliniuma sana pale nilipokua mkubwa na kuona hakuna mwanamke aliyenikubali sababu ya umaskini wangu na kila mmoja alinitoa kasoro aliyoijua yeye.
Kwakweli mapenzi yanaumiza sana pale unapogundua hakuna anayekupenda, na unapogundua kuwa hawakupendi sababu ya umaskini, ndipo nilipomuaga mamdogo na kufunga safari ya kuelekea kwa mganga aliyebadilisha maisha yangu na kufanya niwe Sam mpya"
Wakatazamana tena na kufungua kurasa nyingine ambayo iliandikwa,
"Baada ya kupata dawa na pesa kiasi, niliamua kuanza na mtoto wa mume wa mama yangu kwani lengo langu kubwa ilikuwa ni kulipa kisasi. Na baada ya hapo ndipo nilipofungulia njia ya kutembea na wasichana nikianzia na wale walionikataa awali wakati sina pesa, yani huu ndio ulikuwa muda wangu wa kuwalipizia"
Wakafungua kurasa nyingine na kusoma,
"Siku hii siwezi kuisahau kwani ni siku ambayo nimekutana na mwanamke, tena ni mwanamke ambaye moyo wangu umempenda kwa dhati. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ya hivi nimeweza kumpenda huyu mwanamke, natamani kama ningekuwa kawaida kama wanaume wengine ili niweze kuanzisha familia na huyu binti. Nipo tayari kujitoa maisha yangu kwaajili yake, nampenda sana Sabrina."
Sabrina akapumua kidogo na kufungua ukurasa mwingine,
"Mwanamke ni kiumbe cha ajabu sana, sijui umpende vipi ili aweze kutulia na kuelewa, huyu Sabrina ana mimba ambayo anatafuta jinsi ya kuweza kunibambikiza ila mimi namuangalia tu. Kwavile nampenda, ipo siku na muda ambao nitamwambia kuwa naujua ukweli wote na kumuomba asijisumbue na chochote kile kwani sina nia yoyote mbaya juu yake ukizingatia nampenda sana"
Sabrina na Emmy wakatazamana tena na kufungua ukurasa mwingine,
"Leo naenda kufunga ndoa na mwanamke nimpendae, kwakweli najiona kamavile namuoa malaika. Huyu mwanamke nampenda kwa hakika kabisa.
Najua atasema ndio mbele za watu na kila mmoja atashuhudia nikiwa karibu na furaha yangu"
Sabrina akapumua kidogo na kukumbuka siku ambayo alikuwa akifunga ndoa na Sam, akakumbuka jinsi ilivyokuwa na jinsi mama yake alivyofurahi kumuozesha, ila Emmy alikuwa kimya kabisa katika kipengele hicho kisha wakafungua ukurasa mwingine,
"Mke wangu kajifungua mtoto wa kike, nimempa jina Cherry. Jina hili lina maana kubwa sana katika maisha yangu, ni ngumu kwa mtu mwingine yoyote kujua maana ya jina hili. Nimempa huyu mtoto hili jina kwa makusudi kabisa kwani ndiye mtoto aliyeweza kunifichia aibu yangu kwani kila mmoja alifuta dhana yake ya kusema kuwa mimi sina kizazi kwavile hawakuona mtoto yeyote ila kwasasa ninatembea kifua mbele nikijiita baba Cherry tena Cherry anayeonekana sio yule anayenisaidia bila kuonekana"
Wakafungua ukurasa mwingine ila Emmy alikuwa akifikiria jinsi furaha ya Sam ingekuwa pale angegundua kuhusu mimba aliyokuwa nayo.
Ule ukurasa uliandikwa,
"Huyu kijana anaitwa Jeff kwakweli anasumbua sana akili yangu, hivi kwanini Sabrina anampenda kijana huyu? Kwanini Sabrina anaonyesha kuridhishwa sana na huyu kijana? Jeff ni kijana mdogo sana na hata haendani na Sabrina ila Sabrina ndio amempenda huyu kijana kwakweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana, yani kwa jinsi ninavyompenda Sabrina nashangaa kuona yeye akimpenda Jeff kijana mdogo sana na kufikia hatua hadi ya kuzaa nae"
Emmy akatulia kidogo na kumuuliza Sabrina,
"Ni liasi gani unampenda Jeff?"
"Nampenda sana"
"Je unadhani ni sahihi kwa wewe kumpenda Jeff?"
Sabrina akawa kimya kidogo, kisha Emmy akamuuliza swali jingine,
"Je kumpenda kwako Jeff unadhani ndio mapenzi?"
Sabrina alionyesha kukasirishwa na lile swali na kujikuta akimwambia Emmy kwa ukali kuwa aache kumuuliza.
Ila kurasa waliyofungua sasa walikuta maandishi yaliyowashtua.
"Je unadhani ni sahihi kwa wewe kumpenda Jeff?"
Sabrina akawa kimya kidogo, kisha Emmy akamuuliza swali jingine,
"Je kumpenda kwako Jeff unadhani ndio mapenzi?"
Sabrina alionyesha kukasirishwa na lile swali na kujikuta akimwambia Emmy kwa ukali kuwa aache kumuuliza.
Ila kurasa waliyofungua sasa walikuta maandishi yaliyowashtua.
Wakatazamana na kuyasoma kwa pamoja, yale maandishi yalikuwa na Swali juu yake na yaliandikwa kwa herufi kubwa kabisa.
JE HAYA NI MAPENZI?
Kisha wakatazamana tena kwani ilikuwa kamavile maswali ambayo Emmy alikuwa akimuuliza Sabrina yaliendana na hiki kilichoandikwa.
Kisha Emmy akasoma kwa sauti kilichokuwa kimeandikwa chini ya maandishi hayo,
"Najiuliza hili swali na sidhani kama naweza kupata jibu, huenda jibu la swali langu nitalipata pindi nitakapokuwa nimekufa.
Je, mapenzi ni nini? Au mapenzi ni kitu gani? Kuna watu wanataka kuniaminisha kuwa mapenzi ya dhati yanapatikana kwa baba na mama. Mbona mimi baba yangu alikataa mimba yangu? Inamaana hakunikubali tangu nipo kwenye tumbo la mwanamke aliyempenda, na kama alimpenda huyu mwanamke mbona akamkimbia? Napata jibu moja kwa moja kuwa sikuwahi kupendwa na baba yangu. Ila kwanini aliponiona na kunitambua ukubwani aliumia sana, inamaana alikuwa akinipenda? Hapana, mapenzi gani haya? Siwezi kuamini kuwa alinipenda wakati alinikimbia.
Kwa upande wa mama yangu mzazi, mama aliyenibeba kwenye tumbo lake kwa miezi tisa na kunizaa kwa uchungu, je hili pekee ndio linaweza kuonyesha kuwa ananipenda? Kama alikuwa ananipenda ni kwanini alimthamini zaidi mume wake hadi kufikia hatua ya kunifukuza mimi! Huyu mama alinipenda kweli? Bado napata utata juu ya upendo wake kwangu ingawa bado nitaendelea kumthamini kama mama yangu mzazi.
Kwa upande wa mama mdogo, yani huyu ndio huwa natamani angekuwa ni mama yangu mzazi maana upendo ambao huwa ananionyesha si upendo wa kawaida yani ni upendo ambao mama mzazi anatakiwa kumpatia mtoto wake, sijui kwanini mama yangu hakuweza kunipatia mimi upendo wa namna hii! Ila swali langu ni kuwa mama mdogo alinipenda kiasi kile sababu hana mtoto? Je angekuwa na mtoto angenipenda kiasi hiki au na yeye angenitenga kama wengine? Nikifikiria hilo huwa nawaza kuwa pengine upendo wake nao ni batili ila kiukweli ni mama mdogo tu ndiye pekee aliyenipenda kwa dhati.
Nikija sasa kwenye upande wa mpenzi ya jinsia mbili tofauti, swali langu ni kuwa kwanini nimempenda sana Sabrina? Na kwanini Sabrina ametokea kuwa dada yangu? Na kwanini hata baada ya kujua kuwa ni dada yangu ila bado nikampenda tena kumpenda kimapenzi kabisa na kisheria inaonyesha kuwa huwezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada yako, ila sasa kama haiwezekani basi kwanini nikampenda Sabrina ambaye ni dada yangu? Tena nampenda kwa dhati kabisa. Mapenzi gani haya ya kukataza kuwa na mahusiano na mtu umpendaye eti sababu ni ndugu yako? Nampenda Sabrina jamani tena nampenda sana.
Ila kwanini yeye Sabrina hanipendi, kwanini yeye kampenda kijana mdogo Jeff! Je hayo ndio mapenzi? Sabrina si aliniambia kuwa Jeff alikuwa kama mwanae tena Jeff alikuwa akimuita Sabrina mamdogo ila mwisho wa siku wamependana na kuzaa kabisa, hivi ndio mapenzi gani haya?
Kwa upande wa Emmy, huyu dada ananipenda jamani yani hata sijui ni kwanini ananipenda kiasi hiki, na kwanini amechelewa kuja katika maisha yangu. Huenda angewahi wala isingetokea mimi kumpenda Sabrina ila tatizo alichelewa.
Emmy ni msichana mzuri sana anayevutia, kwakweli ilikuwa kila nikitazama macho yake nahisi hata kuchanganyikiwa ila kiukweli Emmy nilimtamani na si kumpenda. Au kutamani ndio hupelekea kupenda?
Huyu Emmy jamani amechanganya akili yangu hadi nimejikuta nikimkabidhi hoteli yangu ya Arusha, tena nimempa hoteli ile bila ya kulazimishwa na mtu yeyote yani kwa moyo wangu kabisa nilimuita mwanasheria wangu na kufanya sheria zote za makabidhiano.
Kiukweli nimefanya yote haya kutokana na mahaba aliyonipa Emmy kwani katika maisha yangu sikuwahi kufurahia hili tendo zaidi ya kufanya kwa lengo maalumu na kwa jinsi vile moyo wangu ulivyokuwa unasukumwa kufanya.
Ila Emmy kafanya nione radha ya hili tendo, kumbe huwa kuna raha sana mmh! Tafadhari Emmy usiniache katika maisha yangu.
Niliporudi hapa nyumbani bado niliona ile hoteli niliyomkabidhi haitoshi kwa alichonifanyia na hivyobasi nimeamua kumkabidhi na nyumba yangu hii ninayopendezwa nayo hata kama Emmy akinigeuka kwakweli sijali kitu kwa kile alichonifanyia.
Bado najiuliza, au yale mahaba aliyonipa Emmy ndio mapenzi yenyewe? Ila kwa ile raha niliyoipata nadhani yale ndio mapenzi? Na kama yale ndio mapenzi mbona sikuyapata kwa Sabrina ambaye ni mwanamke wa maisha yangu na ndoto zangu. Mbona hakunipa kile ambacho Emmy amenipa? Kwakweli nakosa jibu, au Sabrina anampenda sana Jeff kwavile mimi sikuweza kumpa kile ambacho Jeff alimpa?
Nadhani kwa mapenzi ya mahusiano kwa mtazamo wangu basi haya ndio mapenzi.
Kwa upande mwingine nilikuwa natamani sana watoto, nilitamani siku moja nipate mtu atakaye niita baba kwakweli Sabrina ameweza kufanikisha jambo hili na kunipatia binti mzuri sana ambaye nilimpa jina la Cherry kwa madhumuni maalumu.
Kuna wengi walinichukia ila si huyu mtoto ambaye ni malaika kwani ananipenda na kila akiniona ananifurahia na kufanya nijivunie kuwa baba.
Nimefurahi kumpata mtoto huyu kwani mali zangu nyingi sana zinasimama kwa jina lake. Nilifanya yote haya nikiwa na matumaini kupata mtoto siku moja kisha nimuite Cherry ili achukue mali zangu zote na awe msimamizi halali wa mali zangu.
Nampenda sana huyu mtoto kwani ameweza kunifichia aibu yangu.
Mambo yangu yakiwa tayari, kuna gari nimeagiza ni kwaajili ya mama yangu mdogo, natumaini atafurahi sana. Sijataka kumpa gari yoyote ambayo nimetumia na ndiomana nimeagiza gari jipya kwaajili yake. Nampenda sana huyu mama.
Ila bado sijapata jibu ya maana halisi ya neno mapenzi kwani kila kitu kinanichanganya juu ya hili neno.
Napendwa sana na Emmy ila mimi nampenda sana Sabrina ambapo Sabrina hanipendi mimi bali anampenda sana Jeff, sijui kwanini ni ngumu kupendwa na umpendae.
Napata shida sana kuelewa mbna halisi ya mapenzi"
Kurasa hii iliishia hapo kisha Emmy akamuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Je hayo uliyonayo kwa Jeff ndio mapenzi?"
Sabrina alikuwa kimya kidogo kisha akaongea kile kinachomfikirisha kwenye akili yake zaidi,
"Hivi unadhani upendo aliokuwa nao Sam juu yangu ndio mapenzi? Na kama kweli Sam alinipenda mimi kiasi hicho yani hata wewe anadai kuwa alikutamani, mbona hakuna hata mahali ambako ametaja kuwa sehemu hii ya mali yangu nimemkabidhi Sabrina kwa upendo wangu juu yake? Hakuna mahali aliposema hayo zaidi ya kukazania kuwa ananipenda sana. Bado kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Sam alikuwa na mapenzi ya dhati kwako. Nami naamini kuwa Jeff ndiye mwenye mapenzi ya dhati kwangu ingawa hana kitu chochote cha kunipatia."
Emmy akawa kimya kidogo, na kufungua kurasa ambayo ilionekana ni ya mwisho kwa maandishi kwani zingine zilizofuata hazikuandikwa chochote.
Walianza kuisoma,
"Leo nina furaha sana maana nimekamilisha ile zawadi niliyopanga kumpatia mama yangu mdogo, nitaondoka na hii gari mpya ambayo nitamkabidhi kama zawadi na pia kabla ya yote nitamkabidhi Sabrina barua ambayo itaeleza hali halisi ya vile ninavyojisikia ila kabla ya yote nitapenda kuzungumza na Jeff kwanza, nitamwambia jinsi ninavyojisikia kumuachia Sabrina mwanamke ninayempenda kwa dhati ya moyo wangu ambapo napenda ajue pia mali nilizomuandikisha mwanangu Cherry na kwavile hata ofisi yangu ya mjini ipo chini ya Cherry basi nitapenda aisimamie kipindi mimi nikiwa nje ya nchi.
Kisha nitaenda kwakina Sabrina na kumkabidhi mama mdogo gari yake ikiwa na stakabadhi zote ndani yake halafu ndio nitampa Sabrina barua yake.
Nikitoka hapo nitaenda kwakina Emmy na kumuomba Emmy akubali ili nikaanzishe nae maisha katika mji mwingine kwani matumaini yangu nadhani kuwa ipo siku nitampenda Emmy kwa dhati, naamini kuwa ipo siku nitampenda Emmy zaidi ya ninavyompenda Sabrina.
Emmy akikubaliana na mimi, hapo sitakawia kutangaza ndoa ili nikaanze maisha mapya kabisa na Mungu anisaidie kumsahau Sabrina na mawazo yangu nihamishie kwa Emmy"
Kwakweli Emmy aliisoma hii kurasa huku machozi yakimtoka kwani alijikuta akitamani sana Sam awe mzima tena. Alitamani uhai wa Sam urudi kisha yale aliyokuwa ameyaandika aweze kuyatimiza kwa muda muafaka.
Ila ndio hivyo tena Sam alikuwa marehemu tayari.
Emmy akamwambia Sabrina,
"Inamaana ile gari aliyoenda nayo Sam pale kwakina Jeff ndio gari aliyopanga kumzawadia mamake mdogo?"
"Itakuwa hivyo tu maana hata ile barua niliikuta kwenye lile gari"
Emmy akasikitika kidogo,
"Yani sijui hata ni kitu gani kimeingilia hapa kati, kwakweli Sam hakustahili kufa ilitakiwa awepo ili atimize yale aliyoyapanga. Ila kwakweli binadamu hatujui chochote katika hatma za maisha yetu ila Sam ni kijana mwenye akili sana"
"Kivipi?"
"Sam alikuwa tajiri na mali nyingi pia nadhani alitambua wazi kuwa ipo siku atakufa, kwakweli kwa kile alichokifanya Sam ni cha kujifunza. Unajua unapokufa kwakweli kila mmoja huwa anajiona kuwa na haki ya mali zako na ndiomana Sam aliamua kuziweka mali zake kwa mtu aliyeona kuwa ni sahihi katika maisha yake ambaye ni Cherry"
"Naomba nikuulize kitu Emmy."
"Uliza tu hakuna tatizo"
"Hivi wewe unaona kuwa ni sahihi kwa Sam kukupa wewe hoteli yake na nyumba yake halafu hajampa chochote mama yake mzazi je ni sahihi kwako?"
Emmy akatabasamu kidogo kisha na yeye akamuuliza swali Sabrina,
"Na je wewe unaona sahihi kwa Sam kumpa mwanao Cherry mali zake zote zilizobaki bila kujali kuwa huyo si damu yake, kisha kutokumpa chochote mama yake je ni sahihi"
Sabrina akawa kimya kwani alijiona kamavile yeye na Emmy wameanza kugombea mali za Sam ukizingatia hata siku zilizopita ndicho kilichotokea nyumbani kwao kwa mama wa Sam kugombea mali hizo na kuambulia patupu.
Baada ya kile kimya cha muda mfupi Emmy akamuomba Sabrina kuwa waondoke tu ili wakawape taarifa wengine kwa walichokipata.
Nyumbani kwa mama wa Sam leo alikaa na wanae wote kuzungumza nao na kuwaambia kuhusu hatma yake kwa Sam na kwenye mali za Sam.
"Jamani wanangu wapendwa, Sam alikuwa ni mwanangu kama mlivyo nyie wote ila nasikitika kwamba mtoto huyu sikumuonyesha upendo wowote kama mtoto kwavile tu niliumizwa sana na baba yake ukizingatia alinikimbia nikiwa na mimba. Napenda kuwaambia wanangu wapendwa haswa wanangu wa kike, mtoto ni mtoto haijalishi baba yake ni wa aina gani. Sisi wanawake tunatakiwa tuwathamini na kuwapenda watoto wetu kwani ndio faraja pekee ambayo mtoto anaipata katika maisha yake. Kwakweli naumizwa sana kwavile nilimchukia mwanangu mwenyewe ila namshukuru sana mdogo wangu kwa kunilelea mwanangu maana bila yeye huenda huyo Sam angekuwa amekufa siku nyingi sana. Nilipatwa na tamaa za mali za mwanangu kwani niliamini kuwa ilikuwa halali yangu, ila nimejiuliza kuwa mwanangu alipata wapi mali zile ikiwa mimi kama mzazi wake nilimuwekea mazingira mabovu? Kwasasa moyo wangu kwa amani kabisa namtakia mwanangu apumzike kwa amani, sina shida wala sitamani mali yake yoyote bali natamani uzima wake maana kama angekuwepo basi kwa jinsi ninavyojisikia ningemuomba msamaha mwanangu. Nawaomba wanangu, wiki ijayo tusafiri pamoja ili wote tupate kuona kaburi la Sam na kuondoa vinyongo vyote tulivyonavyo juu yake. Najua nilimchukia mwanangu ila yeye alinipenda sana na ndiomana alipoonana na mimi cha kwanza kabisa aliniomba nikawaone watoto wake. Najutia yote, ila kwakweli hakuna mzazi anayemchukia mtoto wake ila ni mazingira tu yanatufanya tunakuwa wabaya. Basi kwa pamoja tuungane na tufanye ibada ya pamoja tukijiombea na kuwaombea waliotutangulia"
Mama Sam aliongea kwa simanzi sana na kufanya watoto wake waelewe kuwa ni jinsi gani mama yao ameguswa na swala hilo.
Sabrina na Emmy walipokuwa wanatoka kwenye nyumba ya Sam, gafla wakasikia sauti ikisema,
"Mngejisikiaje kama Sam angekuwa hai tena?"
Wakashtuka na kugeuka nyuma, Sabrina akamuona mtu kama Sam na kumfanya apige kelele na kuanguka.
Sabrina na Emmy walipokuwa wanatoka kwenye nyumba ya Sam, gafla wakasikia sauti ikisema,
"Mngejisikiaje kama Sam angekuwa hai tena?"
Wakashtuka na kugeuka nyuma, Sabrina akamuona mtu kama Sam na kumfanya apige kelele na kuanguka.
Emmy kama kawaida yake bado alikuwa na ujasiri wa hali ya juu na ilionyesha kuwa ni mtu ambaye kutetereka kwake ni swala gumu sana.
Emmy aligundua kwa haraka kuwa lile ni jini ambalo siku zote limekuwa likimtawala Sam kwani hata na lenyewe limeshindwa kukubaliana na kifo cha Sam.
Emmy akaongea kwa ustaarabu kabisa kanakwamba anamuona anayeongea nae,
"Tafadhari usitufanyie hivi, ulivyo wewe ni tofauti kabisa na tulivyo sisi. Kwakweli sisi ni wanadamu tena ni waoga na hatuwezi kustahimili mambo yako. Kwani ni kitu gani ulichobakisha hapa, ungetuambia basi tukupatie kuliko kutufanyia hivi"
Emmy hakujibiwa kwani kimya tu kilitawala na baada ya muda mfupi Sabrina nae alizinduka kisha Emmy akamshika mkono na kutoka naye nje kabisa.
Hata walipokuwa njiani bado Sabrina hakuwa na raha yoyote, kisha akamuuliza Emmy
"Ni nani atakayeweza kukaa nyumba ya Sam yenye miujiza kiasi kile?"
"Usijali Sabrina, kuna suluhisho nalifikiria hapa"
"Suluhisho gani hilo?"
"Nafikiri ile nyumba tuiuze"
"Kheee tuiuze!! Atakayekubali kuinunua ni nani?"
"Hiyo kazi niachie mimi maana bila ya hivyo yule jini hawezi kutuacha kwa amani, ni lazima tufanye jambo gumu tu"
"Mmh haya, mi sina usemi wowote maana kwa upande wangu tu siwezi kufanya kitu kwenye ile nyumba"
"Tena tuuze ile nyumba na lile gari ambalo Sam alimpa Cherry zawadi"
"Mmh na lile gari tuliuze?"
"Nisikilize mimi Sabrina maana kuna vgtu tunatakiwa kujiepusha navyo kabla havijawa na madhara kwetu"
"Sawa basi utaendelea kuniambia na vingine ambavyo unaviona kuwa haviko salama"
"Usijali kwa hilo cha muhimu tuelewane tu"
Kwasasa Emmy na Sabrina walionyesha kuelewana sana kupita mwanzoni walipokuwa ndani kwenye nyumba ya Sam.
Walifika nyumbani kwakina Sabrina na tayari ilikuwa jioni, walimkuta Jeff akiwa pale akiwasubiri.
Ni hapo Emmy alipoaga na kuahidi kuja tena kesho yake.
"Ila Emmy bado kuna mengi ya kuongea"
"Natambua Sabrina ila acha nikatulize kichwa halafu kesho nitakuja na jibu kamili"
Wakakubaliana juu ya hilo kisha Emmy akaondoka zake.
Sasa alibaki Sabrina akiwa na Jeff ambapo Jeff alipenda kujua kilichoendelea kwa Emmy kwavile alitaka kujua mipango ambayo Emmy alikuwa akiongelea.
Ikabidi Sabrina amueleze kwa kifupi kile kilichoendelea na kilichotokea na vile alivyopanga na Emmy,
"Kwahiyo Sabrina umekubaliana kabisa na Emmy kuuza nyumba ile ya Sam pamoja na gari la Cherry?"
"Ndio nimekubaliana nae"
"Mmh mbona mie naona kamavile sio sahihi, hivi unajua kama si vizuri kuuza mali za marehemu?"
"Naelewa kama si vizuri ila unajua kama Emmy anajua mambo mengi zaidi yetu?"
"Najua ila huyu Emmy kwa anapoelekea sasa hashindwi kutuambia kuwa tuuze hadi ofisi ya Sam"
"Mmh huko umefika mbali Jeff, kwakweli kwa upande wa nyumba na lile gari naona ni sahihi kabisa unajua vina maajabu sana vile vitu kwakweli nimemuunga mkono kabisa juu ya hilo."
"Ila badae tusilaumiane juu ya hilo kabisa maana naona kabisa jinsi kunapoelekea lazima na ile ofisi itauzwa kwavile na yenyewe inamaajabu kama vitu vingine"
Sabrina aliamua kubadilisha mada kwani hakuona kama ni jambo la muhimu kwa wao kuanza kujadili kuhusu mali za Sam kwani kwenye mgao wa mali hizo hawapo kabisa zaidi ya binti yao mdogo ambaye ndiye mwenye mgao mkubwa wa mali za Sam.
Walipozungumza mawili matatu Sabrina alirudi ndani kisha Jeff akienda kwao huku akiahidi kwenda kesho yake kumsikiliza huyo Emmy kwa kina zaidi na panapohitaji maelezo basi apewe kwa undani zaidi hayo maelezo kwani Jeff aliamini kuwa wana haki ya kuongea kwa niaba ya mtoto wao Cherry ambapo kwa kipindi hicho yeye asingeweza kujitetea.
Sabrina alimkuta ndani mama yake kama kawaida na mama mdogo wa Sam.
Akatamani kumueleza mama mdogo wa Sam kile kilichojiri ila aliona ni vyema kama Emmy akija kuelezea kesho yake kama alivyoahidi.
Sabrina aliwasalimia tu na kuelekea chumbani kwake ambapo aliwakuta watoto wake wamelala.
Akamuangalia mtoto wake Cherry kakumbuka jinsi alivyopata mimba kipindi hicho na jinsi alivyotaka kuitoa.
Kwa upande mwingine alijiona kamavile yupo upande wa mama Sam jinsi vile alivyokuwa akimtenda mwanae na kufikia hatua ya mtoto kuanza kumuogopa yeye.
Akafikiria sana na kuona huenda hata mama Sam hana hatia ila tu huenda alikuwa na vitu vilivyomsumbua akili kama ambavyo yeye alisumbuliwa kiasi cha kuonekana anamchukia mtoto wake.
"Kwakweli sidhani kama kuna mama anayemchukia mtoto wake ila kuna mambo tu yanaingiliana na kufanya iwe hivyo. Nawapenda wanangu"
Kisha akajilaza pembeni yao na kupitiwa na usingizi.
Ule usingizi ulimpeleka kwenye ndoto moja kwa moja ambapo kwenye ndoto hiyo aliiona nyumba ya Sam, aliona hiyo nyumba ikitokewa na mambo mengi sana kisha akaona kamavile wao wameenda kwa lengo la kuweka suluhisho kwa waliokuwa wakiishi humo ndani ila gafla walivyoingia tu hiyo nyumba nayo ikaripuka kamavile iliwekwa bomu.
Kwakweli Sabrina alishtuka sana na kuamka kabisa huku akikumbuka siku ambayo Sam aliungua kwenye nyumba yake ile nyingine.
Kwakweli alitafakari sana na kuona kuwa maamuzi ya Emmy juu ya kuiuza ile nyumba ni maamuzi sahihi pia akaona kuwa ni njia pekee ya wao kujiepusha na yale majini ambayo yalikuwa pamoja na Sam.
"Natakiwa kuwa makini sana kwa maana hayashindwi kumuingilia mwanangu Cherry"
Kisha akamuangalia na Cherry na kugundua kuwa ameamka tayari ambapo mtoto huyu alimsogelea moja kwa moja Sabrina na kumkumbatia, kwakweli Sabrina leo aliona wazi kuwa penzi la mama na mtoto limerejea kwani kawaida ya huyu mtoto ni kuwa akiamka tu basi huwa anashuka kitandani na kutoka nje kumfata moja kwa moja mama mdogo wa Sam na kumkumbatia kwahiyo kitendo cha kumkumbatia mama yake leo kimemfanya Sabrina ajihisi faraja na amani kisha akainuka na mtoto wake huyo kwa lengo la kwenda kumuogesha na kumbadili nguo.
Emmy alifika hapa nyumbani kwakina Sabrina kamavile ambavyo aliahidi jana yake na kuwakuta kama kawaida Sabrina na familia yake wakiwa sebleni.
Muda kidogo Jeff nae aliwasili ikiwa lengo lake ni kusikia kile ambacho Emmy amepanga kuzungumza.
Emmy nae hakupoteza muda na kuanza pale pale,
"Jamani kuna vitu nilizungumza jana na Sabrina kuhusu mali za Sam, kuna mali baadhi niliongea nae kuwa tuziuze ila kwasasa naomba niseme kuwa swala hili si kwa mali baadhi tu bali ni kwa mali zote ambazo Sam ameziacha"
Wote wakashtuka na kushangaa, wa kwanza wao kuuliza alikuwa ni Jeff,
"Mali zote alizoacha ziuzwe kivipi?"
Kisha akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Si nilikwambia jana, umeona eeh!!"
Sabrina akawa kimya na kuendelea kusikiliza jibu la Emmy kwa swali la Jeff.
"Jamani msinifikirie vibaya wala msiwaze vibaya kuhusu nilichosema. Nia yangu ni njema jamani, hivi mnajua kama hizi mali tukiendelea kuzitumia kama zilivyo zitatutesa wenyewe! Hivi ni nani anayejua vile ambavyo Sam alipata mali hivi? Mi najua kwa kifupi tu. Kwakweli hizi mali nyingi zina vilio vya damu za watu. Simlaumu Sam kwa hili ila ilikuwa ni sehemu yake tu ya kujitafutia maisha"
"Kwahiyo tukishauza ndio tutafanyaje?"
"Kuna mali tutaziuza kisha pesa tutawekeza kwenye biashara zingine ili ziweze kuendeleza kumbukumbu ya Sam. Katika mali zote za Sam, kitu pekee ambacho si cha kuuza ni ile ofisi yake ya mjini na hoteli yake ya Arusha ila vilivyobaki vyote tuuze na tununue vingine"
Sabrina akaamua kuuliza kuhusu lile gari ambalo Sam aliandika kuwa ni la mamake mdogo,
"Vipi na lile gari nalo tunaliuza?"
"Aah nilisahau kidogo, lile gari hapana tusiliuze kwani lile gari Sam amelipigania kihalali kabisa kwaajili ya mama yake"
Jeff akamuuliza tena,
"Kwahiyo uuzaji wa hizo mali ni nani atasimamia?"
"Kwa usalama wenu naomba nisimamie mimi mwenyewe ila nitakachokifanya ni kuwakabidhi pesa halafu mtaamua ni kipi mtafanya. Ila mie nikishauza hizo mali nitasafiri na kwenda nchi nyingine, nikishajifungua ndio nitarudi"
Hakuna aliyempinga kwa wakati huo ingawa kiukweli walikuwa na mashaka na huyu Emmy kwani waliona kamavile anataka mali za marehemu kinguvu.
Baada ya hayo, Emmy alimuomba Sabrina ajiandae kisha amuandae na Cherry halafu aende nao kwa mwanasheria wa Sam ili ajue pa kuanzia na zoezi lake alilohitaji kulifanya. Zoezi lake la kuuza mali za Sam.
Ilipita wiki moja ikiwa tayari Emmy amekamilisha mambo karibia yote aliyoyapanga, na leo alikuwa kuagana na wakina Sabrina kwani walimsindikiza uwanja wa ndege kwaajili ya safari yake.
"Jamani, mbaki salama. Kwakweli ningeweza kubaki ningebaki ila najua ni kitu gani kinaweza kunipata kwa yale niliyoyafanya. Kwahiyo tutaonana tena tu ndugu zangu, Mungu akipenda tutakuwa pamoja tena"
Sabrina alionyesha kusikitishwa sana na kuondoka kwa Emmy kwani hata ongea yake ilikuwa ya masikitiko ila Emmy alimpa moyo na kumwambia kuwa asijali kwani muda utafika na atarejea tu.
Kisha Emmy akawaaga tena na kwenda ndani ya uwanja wa ndege.
Kilichobaki ilikuwa ni wakina Sabrina kurudi nyumbani pia.
Mama mdogo wa Sam naye akawaambia kuwa kesho yake atasafiri,
"Jamani mnazidi kutuongezea upweke"
"Hapana Sabrina sio upweke, sasa tumeshakuwa ndugu kwahiyo ni wakati wenu kwa nyie kuja nyumbani kwangu kutembea pia."
Wakazungumza pale huku wakielekea nyumbani kwakina Sabrina.
Walipofika waliingia ndani na muda kidogo Jeff alifika akiwa ameambatana na wageni nao walikuwa ni mama Sam pamoja na mabinti wawili na kijana mmoja.
Walisalimiana pale ambapo mama Sam aliwatambulisha wale alioenda nao pale kuwa ni ndugu wa Sam na amekuja nao kwa lengo la kwenda kuona kaburi la Sam.
"Kwakweli tulipofika hapa na kukuta milango imefungwa nikawaza sana kuwa nani atatupeleka huko makaburini ila kwa bahati nzuri akatokea huyu kijana na nilipomueleza tu akatupeleka. Asante sana Jeff, sasa ndio tumerudi na kuwakuta wenyeji wake"
Mama mdogo wa Sam aliongea pia na kuwapongeza kwa walichokifanya,
"Kwakweli mmetenda jambo jema sana maana katika maisha inatakiwa kusameheana. Kwahiyo kitendo cha watoto wako wote kukubali kwenda kutembelea kaburi la Sam imeonyesha wazi kuwa mmemsamehe Sam kwa kupenda kabisa, kwakweli hata mimi nafurahi kwa hilo jamani."
"Sawa, ila sisi sio wakaaji sana kwani kesho tutarudi Arusha"
"Basi ni vizuri maana hata mimi nimepanga kurudi Arusha kesho"
Sabrina nae akachangia,
"Tena itakuwa vyema kwani naamini kijana hapa anaweza kuendesha gari, kwahiyo itakuwa rahisi kwa wote kwenda na ile gari yako mamdogo"
Kisha ikabidi mama huyu amueleze dada yake kuhusu hilo gari ili asishtuke sana.
Kisha wakaongea mambo mbali mbali ila mmoja wa mabinti wa mama Sam aliamua kuulizia kuhusu nyumba ya Sam kwani waliambiwa kuwa ni nyumba nzuri ya kifahari na kuwafanya wawe na hamu ya kuiona nyumba hiyo.
Sabrina aliwajibu kuwa nyumba hiyo ilishauzwa. Mama Sam hakuonyesha kushangazwa kabisa wakati siku za mwanzo alikuwa akishtushwa na kushangazwa na kila mali ya Sam.
Kesho yake kabla ya safari kuanza, Sabrina aliamua kuwapa kiasi cha pesa kidogo katika zile pesa ambazo mali za Sam ziliuzwa.
Sabrina alifanya hivyo kwani aliamini kuwa mama Sam alikuwa na haki pia kwa mali za mwanae pia aliamini kuwa hakuna mzazi anayemchukia mtoto wake na wala hakuna mtoto anayemchukia mzazi wake ila tu kuna mambo ambayo huwa yanawaingilia na kuwafanya wanakuwa na chuki ambazo badae huwa ni majuto.
Mama Sam alimshukuru sana Sabrina huku wakiagana pale na kuwakaribisha nyumbani kwao ili wawe wanatembeleana.
Wakaagana kwa masikitiko kwani kwasasa walionana kama ndugu kabisa.
Maisha yalianza upya na kila kitu kilibadilika.
Baba wa Sabrina aliitisha kikao na kuwataka Sabrina na Jeff wakaishi kwa amani na kama watataka kufunga ndoa basi yeye hatokuwa na pingamizi lolote juu yao.
Hata kwa upande wa Sakina pia aliona ni vyema tu kukubaliana na hali halisi kwani hata kama akiendelea kupinga yale mahusiano je atapata faida gani ukizingatia tayari kuna wajukuu ambao ni watoto wa Sabrina na huyo Jeff.
Kisha akasema,
"Jamani, kwa upande wangu mimi sina kinyongo chochote juu yao. Kwakweli nimeamini kuwa mapenzi ni kitu cha tofauti sana, nadhani kama kungetokea watu wenye upendo wa Jeff na Sabrina kwa hakika ndoa nyingi zingedumu. Nilikuwa namuona Sabrina kuwa ni mkubwa sana kwa Jeff na kujaribu kumletea Jeff wasichana wa rika yake ila bado upendo wake ulikuwa kwa Sabrina. Kwa hakika naamini kuwa mapenzi ni upofu, pia mapenzi hayachagui umri, rangi wala maumbile. Kwasasa sina kinyongo chochote, nimemkubali Sabrina kama mdogo wangu na kama mkwe wangu"
Wote wakafurahi juu ya hilo kwani ni Sakina pekee ndiye aliyebaki kuwa na pingamizi juu ya mahusiano ya watu hawa.
Baada ya mwaka mmoja kupita, Emmy alirudi nchini na wakamfanyia sherehe ya kumkaribisha.
Alikuwa na mtoto mdogo wa kiume aliyeonekana kufanana kila kitu na Sam.
Kila mmoja alipenda kujua kuwa Emmy amempa jina gani mtoto huyo kwani alikuwa kamavile ni pacha wa Sam au kamavile Sam kazaliwa tena.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwanza kabisa Emmy aliwashukuru kwa mapokezi waliyomfanyia kisha akawatajia jina la mtoto.
"Huyu mtoto nimempa jina la Deo, naamini kuwa mtoto huyu atakuwa mtii na muaminifu katika maisha. Mazuri yote yaliyofanywa na babu yake atayaendeleza na yale mabaya atayarekebisha"
Kwakweli baba Sabrina alifurahi sana na kuona kuwa huyu binti amempa heshima kubwa sana kwa kumuita mtoto jina lake.
Hii ilikuwa ni siku ya furaha kwao, siku ya kumkaribisha Sam mpya duniani tena ni Sam mwenye jina jipya la Deo.
Mama Sam nae alifurahi sana kwani sasa aliweza kumuona Sam tena ila katika sura ya mtoto mpya.
Kila mmoja alionyesha kumpenda huyu mtoto kama ishara ya kuonyesha shukrani zao kwa Sam na pia kuonyesha kwamba hawakuwa na kinyongo tena na Sam.
Mwisho...........!!!
0 comments:
Post a Comment