Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

JERAHA LA MOYO - 5

 







    Simulizi : Jeraha La Moyo

    Sehemu Ya Tano (5)







    Siku hii alipasa kuiandika katika kumbukumbu zake kama histori ya kupendeza. Alijihisi raha muda wote. Alihisi kupendwa na kufikia hatua ya kujiona hakuna apendwae duniani kama yeye. Alicheka na kufurahi. Alideka na kununa kimadeko. Alijibaraguza na kujikunyata kwenye mwili wa rijali yule. Alijiona ni wa pekee sana katiia ulimengu huu. Pengine ni kutokana na jambo hili alilofanyiwa siku hiyo!.



    Ni katika ufukwe maarufu ulioko ndani ya jiji hilo katika mji mdogo wa Pangani. Almaarufu kama Panga Deco. Rommy na Cecy walikuwa wakifurahia mahala hapo. Wana haki ya kupoteza muda mwingi mahala hapo maana walifika asubuhi na mapema. Hata hivyo hawakupanga kuishia hapo tu. Walipanga wakishatoka hapo watembelee na maeneo ya mji huo wenye historia ya kale.



    Majira ya saa nane mchana baada ya kumaliza kula. Walijiandaa kwenda kutembelea maeneo hayo. Wakatoka wakiwa wao na walinzi wa Rommy mpaka huko sehemu moja inayoitwa Makoma. Huko wakatafuta wenyeji ambao watawaongoza kwenye safari hiyo. Haikuwa tabu kuwapata kwasababu kuna watu maalumu kwaajili hiyo. Wakaelezwa ni kiasi gani wanatakiwa walipe ndipo shuhuli hiyo ifanyike. Baada ya kutajiwa gharama za shuhuli hiyo. Rommy akalipa pale pale ikawa ni wao tu kuwaongoza.



    Waliacha magari yao na kwenda huko kwa kutumia miguu tu. Kabla ya kufikishwa maeneo hayo, kwanza walionyeshwa vivutio vyengine ikiwa ni kuonyeshwa mambo ya kale. Walitumia saa moja kuwa mahala hapo kisha wakaelekea kwenye mapango. Huko walionyeshwa vitu vingi sana mpaka wenyewe wakakiri kwamba sehemu hiyo ilikuwa ni ya kihistoria kweli. Majira ya saa kumi na moja wakawa wameshahitimisha ziara yao.



    Wakarudi walipoacha magari yao kwa mwendo wa taratibu huku wakizidi kupewa historia na watu wale waliokuwa kama viongozi wao kwenye msafara ule. Walipofika sehemu walipoacha magari yao. Wakawashukuru sana wenyeji wao kisha wakapanda safiri zao na safari ya kurudi mjini ikaanza.







    Saa moja kasoro jioni iliwakuta mjini ambapo walikuwa wakiufuata uelekeo wa kupapata makazi ya kina Cecy. Walipofika mahala ambapo Cecy mara nyingi hupendelea kushushwa. Gari zikasimama kwaajili ya kumshusha Cecy. Alimshukuru sana Rommy kwa kuifanya siku yake iende vyema. Akatamani wangekuwa wakitoka kama hivyo kila siku. Mwisho akampiga busu la mdomo kisha akashuka.

    Ni raha ipi aipendayo kama hiyo ambayo tangu awe na Ramah hakuwahi kufanyiwa? Pengine ni kutokana na uwezo mdogo wa kijana huyo. Ila hakufikiri kwamba ni raha kiasi gani kuwa na mtu anaekupenda. Huenda alidhani Rommy ni mwenye kumpenda kama yeye ampendavyo na ndio maana anafanya yote hayo kwaajili ya furaha yake. Hakujua!.



    Siku hiyo ilikuwa poa sana kwa Cecy ambae muda mwingi alionekana ni mwenye kutabasamu kudhihirisha furaha yake. Hata Mama yake pia alishangazwa na vituko hivyo maana alishazoea kumuona mwanae akiwa katika hali ya kawaida. Furaha kidogo na kununa kidogo changanya na kudeka. Sasa ni vipi leo hii awe ni mwenye furaha muda wote? Kwavile alipenda kumuona mwanae huyo wa pekee akiwa na furaha, hakutaka kumuhoji sana akihofia kuipoteza furaha hiyo. Akamuacha!



    Siku hiyo nayo ikapita, ikawadia siku nyengine. Siku ambayo pengine nae Ramah alipaswa kuiandika katika historia ya maisha yake. Ni siku ambayo alipanga kumtafuta Cecy wakae mahali ajue hatma yake. Hatma ya penzi lake kwa mnyange huyo. Tangu siku iliyopita alikuwa akiiwazia siku hiyo tu itakavyokuwa. Hakutaka kumsumbua siku hiyo akitarajia siku inayofuata ambayo ndio hiyo tayari ishajiri kumtafuta Cecy ili wayaongee.



    Asubuhi kulipokucha Ramah alijibaraguza kwa kumtumia ujumbe kwa njia ya simu Cecy. Akimtakia asubuhi njema akitarajia ujumbe wake ujibiwe kwa furaha. Ila ikawa tofauti na alivyotarajia. Ni saa pili sasa linaishia lakini asipokee ujumbe wowote kutoka kwa Cecy. Akafadhaishwa na jambo hilo na kujihisi mnyonge kama kitoto kilichotelekezwa na mamae. Ndio, lazima ajihisi mnyonge si alishazoea anapomtumia ujumbe haichukui hata sekunde umeshajibiwa?.



    Sasa ni kipi afanye tofauti na kumpigia simu ikiwa ujumbe wake haukujibiwa? Akampigia!. Hata pale Cecy alipopokea simu yake. Hakua mchangamfu kama ilivyo ada yake. Aliongea kikawaida sana utafikiri anaeongea nae hamfahamu na hapo alikosea namba tu. Hata zile nguvu za kuhoji kwanini hakujibiwa ujumbe wake Ramah hakuwa nazo. Zaidi alimuomba waonane siku hiyo na Cecy hakutaka kumbishia. Akamuambia asubiri atampa jibu ni wapi wakutane. Ramah kabla hajaongea chochote, simu ikakatwa.



    Akashusha pumzi za fadhaiko huku akiitazama simu yake. Akaingia upande wa picha kwenye simu yeka na kuanza kutazama picha za Cecy nyengine ambazo walipiga wote sehemu mbalimbali. Ule ujasiri aliokuwa nao siku iliyopita, yale maneno yote aliyoshauriwa na Jay. Vyote vilimpotea na unyonge ndio uliotawala muda huo.



    Akaitupa simu yake pembeni kwa hasira na kujilaza kitandani. Mawazo yalimtawala bongoni kwake kiasi ambacho alijihisi yu hospitalini mgonjwa mahututi anaesubiri kutolewa roho na malaika mwenye kufanya kazi hiyo. Alijizuia kutoa machozi lakini moyoni kwake aliuguliwa vilivyo. Akajitahidi kuutafuta usingizi japo apate utulivu wa bongo kuyakimbia mawazo yaliyong'anania kichwani kwake. Japo ilikuwa shida lakini baadae aliupata. Akalala!.



    Majira ya saa kumi na mbili jioni akiwa tayari ameshazinduka kwenye lindi la usingizi muda mrefu. Alipata kuishuhudia simu yake ikiita na alipotazama ni nani mpigaji. Alikuta ni Cecy ndie anaempigia. Akaipokea kwa pupa huku kiroho kikimuenda mbio. Hata pale alipoipokea simu hiyo ni maneno machache tu aliyopata kuyasikia.



    “Njoo muda huu Sizzler Corner” Simu ikakatwa na Ramah akabaki kugugumia ndani kwa ndani. Akajitoa pale alipo na kutoka nje kwaajili ya kwenda kujiandaa.



    Alitoka nyumbani kwao kwaajili ya kuelekea kule alipotakiwa na Cecy. Hakutaka kuipoteza nafasi hiyo ambayo kwake aliona ni ya dhahabu sana kutokana na jinsi Cecy alivyobadilika. Alitafuta usafiri wa bodaboda ambao ungemfikisha kwa haraka eneo hilo.



    Dakika kadhaa akawa amefika, akamlipa bodaboda aliempeleka mahala pale kisha akajongea kuuendea mgahawa ule. Taratibu kabisa mpaka pale alipokuwa amekaa Cecy. Leo hii Cecy alipendeza kileo si mas'hara. Suruali ya jinzi na shati la mikono mifupi la rangi jekundu lenye maua ya rangi ya njano na meupe. Usoni alivalia mawani ya jua nyeusi iliyofananiana kidogo na suruali aliyoivaa. Kichwani akiwa amesuka nywele za kuunga zilizoning'inia mpaka mgongoni. Kwa kumtazama tu haraka haraka alipendeza huku uzuri wake wa sura akiuchagiza na utafunaji Big G kwa madaha.



    Ramah alifika mahala pale na kumpa salamu Cecy ambayo aliitikia kama ni mwenye kujilazimisha tu. Ramah hakujali. Akamsifia kwa kupendeza na Cecy wala asijibu lolote zaidi ya tabasamu hafifu lililomtoka kwa sekunde kadhaa kisha likazima. Akamtazama kwa pozi Ramah kisha akaachia cheko dogo ilhali Ramah akiwa kimya akimtazama yeye.



    “Enhee! Niambie ex wangu” Cecy aliongea kwa dharau kisha akacheka tena. Ramah roho ilimuuma lakini hakuwa na jinsi. Sasa ni nini atafanya zaidi ya kuwa mpole? Mara hiyo akafika muhudumu kwaajili ya kusikiliza shida ya Ramah ikiwa Cecy tayari ana kinywaji chake.



    “Ex, agiza chochote nitalipa” Cecy alionyesha dharau za waziwazi kiasi ambacho mpaka yule muhudumu alielewa kitu. Akamtazama Cecy kwa staajabu kisha akamtazama Ramah kwa mshangao. Ramah aliendelea kuwa mpole japo moyoni alizidi kuumia.



    “Samahani dada yangu, nenda tu nikihitaji nitakuita. Ila samahani sana kwa usumbufu” Ramah aliongea hayo na yule muhudumu aliefika hapo kwaajili ya kusikiliza shida yake, akamuelewa na kuondoka. Ramah akamtazama Cecy aliekuwa akitabasamu kwa kejeli. Ramah hakujua aseme nini maana dharau alizoonyeshwa na binti huyo ambae kipindi cha nyuma aliyaona mapenzi ya wazi wazi juu yake. Ati leo hii anasema hakuwa akimpenda? Hapana kwa kweli, hata kama alikuwa akiigiza lakini sio kwa kiasi kile bwana. Ni dhahiri roho tu imembadilika na tamaa kumuingia mpaka kufikia hatua ya kumsaliti. Na sio kumsaliti tu, pia kumletea dharau ambazo hazikustahili kutolewa na yeye hata kidogo.



    “Umeshindwa kuagiza unachotaka sijui ni kwaajili ya aibu ama sijui ni nini? Ok. Sio mbaya nikikuachia hiki kinywaji changu usindikize maongezi yako” Cecy alisema kisha akaisogeza ile glasi ya plastiki yenye shurubati ya ndimu ndani yake kumsogezea Ramah. Ramah aliitazama ile glasi kwa muda kisha macho yake yakatembea taratibu kwenye mkono wa Cecy ambao ulisogeza ile glasi. Macho ya Ramah yalitembea taratibu kupanda na mkono wa Cecy mpaka alipofika kwenye bega. Huko aliendelea kuusawili mwili wa Cecy mpaka usoni, kisha macho yake yaka komea hapo.



    “Asante. Unaweza kuendelea na kinywaji chako..” akatulia mara hiyo Cecy alitabasamu na kuirudisha ile glasi na kwake. Akaiinua na kunywa kwa madaha kinywaji kile huku akimtazama Ramah kwa jicho la uchokozi kisha akaishusha baada ya kupiga pafu dogo la kinywaji kile.



    “Sijui ni kipi hasa kimekufanya mpaka ukawa hivi leo hii...” Ramah akaipata sauti yake. “Ukawa na dharau, kiburi, jeuri ambazo unazifanya kwa makusudi kunifanyia mimi ukijua kabisa ni jinsi gani vitaniumiza. Cecy mi siwezi nikakulazimisha uwe nami kwasababu mwenye maamuzi ya kumchangua wa kuwa nae ni wewe. Pamoja na kuwa wewe ndie mwenye maamuzi. Lakini pia unapaswa kutafakari maamuzi hayo yananiathiri vipi mimi unaenichukulia. Sihitaji kukukumbusha kwamba nakupenda lakini inabidi nikukumbushe pengine umesahau ni mapenzi kiasi gani ninayo juu yako. Sikatai sawa sina hela kama Ethan lakini naamini mimi nina mapenzi ya dhati kuliko yeye. Sipo hapa kwaajili ya kumponda kwasababu pia ni ndugu yangu. Lakini muda mwengine unapaswa kutafakari kabla ya kuchukua maamuzi. Ethan ni kweli aliwahi kuwa na wewe kabla yangu. Lakini alikuumiza Cecy na akakuacha na maumivu mengi ambayo sidhani kama yameshafutika moyoni mwako mpaka leo. Nakumbuka sana kipindi ambacho nakufuata kwa mara ya kwanza na kukueleza hisia zangu ni vipi najihisi juu yako. Nakumbuka maneno yako uliyoniambia baada ya kukubali ombi langu kwamba hata wewe ulikuwa ukinihusudu sana lakini hukua na njia ya kunieleza. Hata ukafikia hatua ya kumshukuru Mungu kwa kunijalia uwezo wa kukueleza yale ambayo wewe ulishindwa kunieleza mimi. Pengine labda ni kutokana na utamaduni tuliojiwekea watu weusi kwamba, si vyema binti kumueleza kijana hisia zake hata awe anamuhusudu vipi. Lakini pia nayakumbuka maneno yako uliyowahi kuniambia mpaka ukadiriki kutoa machozi ya kwamba. Unahitaji utulivu na faraja kwangu mimi kwasababu huko nyuma ulishaumizwa vibaya. Dah! Sikujua kama ile ahadi niliyojiwekea na kukuambia dhahiri kwamba sintoweza wala kujaribu kuja kukusaliti achilia mbali kukuacha kabisa. Ahadi ile imegeuka upande imekuwa ni kwako sasa unaniacha achilia mbali kunisaliti.

    Hivi kweli Cecy unayakumbuka yote haya ama unapelekwa tu na tamaa za nafsi? Nakupenda Cecy na nipo tayari kuyafuta haya makosa ama kuyabadilisha kuwa mema kwangu....” Ramah akaweka kituo kisha akafuta chozi lililokuwa likitoka kwenye jicho lake moja kisha akameza mate.







    “Tazama Cecy, leo hii nalia kwaajili yako, tena mbele yako. Mbona unataka kulipa jina lako maana mbaya. Cecilia eeeh! Nalia kwaajili yako na wewe unanitazama kama jibwa koko linalokulilia mbele yako likitaka huruma yako ulirushie japo pande la ukoko ili liondokwe na njaa inayoisulubu tumbo lake? Nakumbuka sana maneno ya watu kwamba wanawake mnahuruma nyingi kushinda sisi. Lakini kwako naona tofauti tena kubwa iliyoje. Ama wewe si katika wanawake niwajuao? Nilioelezewa kwamba wanahuruma? Cecy usitake ni kutoe kwenye kundi hilo pengine ni shetani tu anacheza na akili yako na kukusahaulisha mapenzi yangu kwako. Zile ahadi zako ulizoniahidi zote zimepotelea hewani mithili ya moshi wa karatasi. Nakumbuka Cecy uliwahi niambia watamani wewe tuishi katika dunia ya pekeetu ili tuwe mbali na walimwengu wasiopenda mapenzi yetu. Sa ni vipi maneno yako leo yawe kama hatua azipigazo nzige ardhini pindi atokwapo na mbawa zake na kufutwa na upepo? Hapana Cecy sitaki kuamini kama kweli hunipendi kama usemavyo. Sasa kama wewe hunipendi mbona mi nakupenda? Wewe kama hunihitaji mbona mi nakuhitaji? Eeee! Nifanye basi na mimi nisikupende, nisikuhitaji kama wewe usivyonihitaji...”



    Mara hii sasa Ramah macho yote yalimbubujika machozi. Alitia huruma kumtazama! Na ilihitaji moyo wa ujasiri sana kuyakataa maneno yake. Hata Cecy mwenyewe maneno yale yalimuingia na kumchoma mtimani kwake. Lakini ni vipi awe nae tena wakati alishaamua awe na Rommy? Hatari!



    Cecy alikuwa akimtazama kwa macho ambayo hayakuweza kutafsirika kwa haraka. Hayakuonyesha huruma kwa Ramah wala hayakuonyesha kupingana na maneno yake. Nakupenda pia Rafael lakini nimeamua kuwa na Rommy kwasababu yeye ndio wa kwanza kuwa nae. Siwezi! Siwezi Ramah kubadilisha maamuzi tena nitaonekana juha mbele za watu. Acha niwe nae tu japo maneno yako yananiumiza kila uongeapo. Cecy aliwaza kisha akatazama chini. Akainua kichwa baada ya kusikia sauti ya Ramah akiongea.



    “Hata kama umeamua kuniacha, lakini haikuwa kwa staili hii. Ni bora ungenidanganya tu mpaka pale ambapo ningekuja kujua mwenyewe kwamba hunipendi. Ni bora usingenitamkia kwamba hunipendi. Lakini mbona kipindi kile ulinilazimisha nikuambie nakupenda wakati sikuwahi kukuonyesha ishara za kukupenda? Ukauteka moyo wangu taratibu kwa maneno yako na vitendo vyako vya kunijali kila muda. Mpaka ukafanikiwa hilo na hata pale niliposita kukueleza hisia zangu ukanilazimisha sana nikueleza nami bila kusita tena nikakueleza. Ile furaha yako ya kipindi kile ipo wapi sasa? Ulifurahia baada ya kukuambia nakupenda, ila sasa unafurahia wewe kwa kuniambia hunipendi. Mbona imekuwa kinyume? Aargh! Hujui ni maumivu kiasi gani ninayoyapata kila nikiyafikiria maneno yako. Hata sasa nimeumia, naumia unaponionyesha dharau zako. Hujui! Hujui Cecy tani ngapi za maumivu uliyonibebesha moyoni mwangu bila kujali kama ninauwezo wa kubeba ama laa! Ama nipigie siyahi kubwa watu wote watambue kama naumia kwaajili yako? Ama nimfuate mmoja mmoja aliekuwa hapa nimueleze ni kiasi gani naumia kwaajili yako? Eeee! Niambie basi nifanye nini ambacho kitasaidia kuyapunguza haya maumivu niliyonayo. Aaargh!!”



    Ramah aliinama chini baada ya kushindwa kuzungumza. Hisia za maumivu zilionekana kwenye maneno yake na wajihi wake ukachagiza hilo. Maneno aliyoyaongea yata yeye mwenyewe yalimuumiza sana. Akatamani walau Cecy apate uwezo wa kuzama ndani ya moyo wake na kuchungulia kidogo tu maumivu yake. Kisha atoe jibu kwa kuomba msamaha kwa yale aliyomtendea.



    “Sikiliza nikuambie Ramah.....” Cecy aliongea baada ya kimya kifupi. “Moyo wangu unanafasi moja tu ya kupenda. Nilianza kumpenda Ethan kabla yako. Akaondoka na nafasi hiyo ukaipata wewe. Sasa amerejea na nafasi yake bado ipo. Sasa ni vipi nikuongopee kwamba nakupenda ilhali sikupendi? Haki vile nisingeweza. Ningekuambia tu kama ambavyo nimeshakuambia. Sikupendi Ramah nampenda Rommy ndugu yako. Wewe nafasi yako haipo tena na huwa sipendi kulazimishwa ninapochukua maamuzi. Ukilielewa hilo naamini hutonisumbua tena. Chakukushauri sasa hivi. Futa namba yangu, nitoe kwenye fikra zako. Naamini hilo litasaidia kunisahau mimi. Na kama uta...”



    “Noo! Cecy nakupenda usiseme hivyo...”



    Ebwana eee! Ni kitendo cha ghafla sana. Ni baada ya Ramah kumkatisha Cecy kuongea na kupayuka kwa nguvu huku akimshika mikono Cecy. Cecy alijitoa kwenye mikono ya Ramah na kuachia kofi kali lililotua kwenye shavu la Ramah. Kofi ambalo lilitoa sauti kali mfano wa baruti na kumshtua kila mmoja aliekuwa eneo lile. Wote wakageuka kule walipo wakina Cecy huku wakiwa wametaharuki.



    “Niache! Mjinga wewe. Unakuwa kama mototo mdogo huelewi unachoambiwa” Cecy alipayuka hayo kisha akammwagia ile shurubati aliyokuwa akiitumia yeye. Akavuta mkoba wake uliokuwa juu ya meza na kuondoka mahala hapo huku akiachia msonyo mkali. Baadhi ya waliopata kushuhudia kitendo hicho walisikitika huku wengine wakiangua vicheko.

    Ilihuzunisha!.



    Baada ya Cecy kupotea eneo lile. Ramah akabaki akiwa na fedheha kubwa aliyoachiwa. Mwili mzima ulimtetema kwa fadhaha, macho yake hayakuweza kutazama popote zaidi ya kutazama pale alipomwagiwa ile shurubati. Hakika kwake ilikuwa ni aibu ya mwaka aliyowahi kufanyiwa. Hakujua aanze vipi kuinuka mahala pale. Machozi ya uchungu yalimtoka akiwa haamini kama kitendo kile kimefanywa na Cecy mwana wa Ally. Ilitia simanzi si mas'hara!!



    Taratibu kabisa aliinuka huku soni imemjaa kwenye wajihi wake. Hatua ndogo ndogo huku kichwa amekiinamisha chini kama mchawi aliefumaniwa akiwanga. Alitoka mahala pale huku vicheko vikimsindikiza na pole za kwa mbali kwa wale walioguswa na kitendo kile zilisikika. Ama kwa hakika Cecilia umenidhihirishia hunipendi. Aliwaza hayo huku akitoka nje ya wigo wa mgahawa ule.



    Kitendo kile aliona kama kimeshuhudiwa na ulimwengu mzima. Hakuweza kutazamana na yoyote hata wale ambao hawakuwa wameshuhudia hilo. Kwa aibu iliyomvaa akaamua atafute usafiri wa Bajaji ambao alihisi utamsitiri na watu wasimuone kama mwenyewe alivyohisi. Akakwea ndani ya Bajaji bila ya kumjuza mwenye usafiri na kumfanya ashtuke maana alikuwa amesinzia ndani ya usafiri wake.



    “Vipi kaka! Kwema?” Dereva alimuuliza kwa kiroho huku akimtazama kwa hofu.



    “Kwema. Nipeleke Duga. Twenzetu” Ramah alijibu huku akijitahidi asitazamane na dereva Bajaji maana usoni alichafukwa na michirizi ya machozi.



    “Elfu tatu. Utanipa Elfu tatu mpaka huko”Dereva Bajaji alisema huku akimsaili vyema abiria wake aliezama kama mzuka kwenye Kibajaji chake. Ramah akamuambia haina shida na dereva akawasha chombo chake na kutimka eneo lile kuelekea huko alipotaka abiria wake apelekwe.



    “Niache! Mjinga wewe. Unakuwa kama mototo mdogo huelewi unachoambiwa” Kumbukumbu ya maneno ya Cecy yalijirudia tena kichwani kwake. Machozi yaliyokuwa yamekoma kutoka yalianza upya kumtoka. Kilio cha chini chini kilimtoka bila kupenda. Alihisi kuonewa sana kwa vile alivyofanyiwa na Cecy. Ni kweli alipenda lakini haikustahili kufanyiwa vile.



    Dereva akageuza shingo kimbea kumtazama abiria wake baada ya kusikia kilio alichotoa. Ramah alikuwa amejiinamia huku akidondosha machozi, kamasi zilizotaka kupata hewa ya ulimwengu alizivuta ndani baada ya kuchungulia kwenye tundu za pua yake.



    “Anko vipi? Umefiwa ama?” Dereva alimuuliza huku akipunguza kidogo mwendo. Lakini swali lake halikupata kujibiwa. Hata yeye alipoona imeshindika kupatikana jibu. Akakaa kimya lakini kiroho cha kutaka kujua nini kimemkuta abiria wake kikimsukuma kuhoji tena.



    Walifika mwisho wa safari kwa maelekezo ya Ramah. Hata pale Ramah alipofika nyumbani kwao. Akashuka kwenye Bajaji kama vile alivyoingia. Akatoka tu bila kumpatia dereva ujira wake na kumfanya dereva apige kelele kumtaharifu kwamba hakumpatia pesa zake. Ramah akarudi pale alipo dereva, mara hii alikuwa amejitoa ndani ya Bajaji na kusimama nje kwa nia ya kumfuata Ramah. Ramah akaomba samahani na kumpatia shilingi elfu tano kisha akaondoka mahala hapo akimuacha dereva ametoa macho kama alieona kitu cha kuogofya.

    “Rizki ya bure hii” alijisemea kisha akapanda kwenye usafiri wake na kutokomea pasipojulikana.



    Ramah akiwa kwenye mwendo usioeleweka, alimpita kwa kasi mama yake aliekuwa akiandaa chakula cha usiku. Mama yake alibandika sufuria na kumtazama Ramah aliekuwa akipotelea ndani ya chumba chake. “Ana nini huyu mtoto?” Alijiuliza huku akiutazama mlango wa chumba alichopotelea Ramah. Akaguna kisha akaendelea na kuupepea moto.



    Alipofika ndani ya chumba chao. Akafunga mlango na komeo na kukaa kwenye sofa lililokuwa ndani humo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “.... Wewe nafasi yako haipo tena na huwa sipendi kulazimishwa ninapochukua maamuzi. Ukilielewa hilo naamini hutonisumbua tena. Cha kukushauri sasa hivi. Futa namba yangu, nitoe kwenye fikra zako. Naamini hilo litasaidia kunisahau mimi.....”



    Maneno ya Cecy yalizidi kukisumbua kichwa chake. Aliyakumbuka kila mara na yalizidi kumuongezea maumivu ya nafsi. Mara hii sasa ndio alipata uhuru wa kulia vyema. Akalia kimya kimya huku machozi yakimbubujika mithili ya maji kwenye maporomoko. Kamasi zilimtoka na wala hakujisumbua kuziondosha.



    “Eee! Mungu wangu unakubali vipi mja wako dhalili nipitie mateso makali namna hii? Kwanini usingezuia haya yaliyotokea nikabaki na furaha kama ilivyo mwanzo? Hivi ni kweli Cecy hanipendi? Kama kweli ananipenda asingenifanyia haya. Cecy hanipendi Cecy! Na sijui ni kwanini.... Basi kama Cecy hanipendi tena. Mungu nipe ujasiri niyashinde haya, nimsahau yeye na maumivu yanipotee kabisa. Namchukia kuanzia sasa! Simpendi tena!....”







    Ramah aliongea hayo kama mtu aliechanganyikiwa. Akachukua simu yake na kuanza na namba ya Cecy. Akaifuta kisha akahamia kwenye picha, nazo akafuta moja baada ya nyengine. Wakati anafuta picha za Cecy, kuna baadhi alikawia kuzifuta, alibaki akizitazama kwa kitambo huku machozi yakimtoka na mengine kuangukia juu ya kioo cha simu yake. Lakini kwa vile alishaamua kufuta, alifuta zote. Kisha hapo simu akaizima na kuiweka pembeni. Akainamisha kichwa chini na kutulia lakini machozi yasikome kumtoka.



    “Mama hiko chakula saa ngapi aisee! Maana tumbo lalia alamu ile ile” Jay aliyaongea hayo huku akishuka kwenye pikipiki yake aliyofika nayo punde tu hapo na kumkuta mama yake akiwa jikoni akipika chakula.



    “Hayo maneno yako ya kihuni kila siku nakukataza kuniongelea mimi. Ongea na hao hao wahuni wenzako huko na sio mimi. Na kama unataka upikiwe kwa muda unaotaka oa ndio utafanyiwa hivyo” Mama yake aliongea hayo huku akikoroga uji kwenye sufuria.



    “Mama nawe kwani hunizoei tu? Kwanza hapo ndio unaanza, ama mboga tayari?” Jay alimuuliza huku akisogea pale alipo mama yake.



    “Kwani lakini mbona unagubu wewe? Wataka nikuambie mboga tayari ili ukadokoe tu huna lolote wala si njaa ikusumbuayo zaidi ya uroho tu. Kwani nani asiekujua wewe?” Jay alicheka baada ya kusikia maneno ya mama yake. Akavuta kiti na kukaa karibu yake.



    “Kwanza mwenzako ni kipi kimemkuta. Maana kanipita hapa hai hai kama nina ugomvi nae na kupotelea huko chumbani kwenu na sijui ana nini maana hajatoka tangu aingie” Jay akashangazwa na maneno ya Mama yake. Akainuka bila kujibu kitu na kuuendea mlango wa chumba chao. Akajaribu kuufungua na kukuta ukiwa umefungwa kwa ndani. Akagonga huku akimuita Ramah. Mama yao akaacha alichokuwa anafanya na kugeuka kule alipo Jay huku wasiwasi ukimuanza.



    Jay aligonga tarkibani dakika nzima ndipo aliposikia sauti ya komeo likifunguliwa. Akazama ndani na kuurudishia mlango. Akamkuta Ramah akiwa amejiinamia kwenye sofa, sakafu ikilowana kwa maji maji. Alimuita tena huku akimtazama kwa wasiwasi na Ramah akainua sura yake. Ebwana eee! Macho ya Ramah yalivimba na kuwa mekundu mithili ya nyanya mbivu. Aliona na kitu chengine kilichomuogofya. Kwenye shavu la kulia la Ramah kulikuwa na alama za vidole vya mkono vilivyoacha alama ya damu iliyovia. Kutokana na weupe wa ngozi ya Ramah, hilo halikuwa tabu kuonekana.



    “Nini ndugu yangu? Mbona hivi tena?” Jay aliongea kwa hofu huku akikaa karibu yake. Ramah alijaribu kufuta machozi lakini ndio kama alitengeneza njia ya kushuka mengine.



    “Cecy...” Alitamka jina hilo na wala asiweze kuendelea tena kuzungumza.



    “Cecy! Ana nini tena?” Jay aliuliza kwa wahka. Ramah alivuta pumzi ndani na kuzitoa kwa mkupuo. Kisha akavuta na kamasi kwa ndani, akatulia kidogo na kumueleza yote nduguye yaliyomkuta. Jay alishusha pumzi huku akimtazama kwa huruma Ramah.



    “Sikiliza Rafael. Ni dhahiri Cecy hana haja na wewe tena mpaka kufikia hatua ya kukudhalilisha mbele za watu. Achana nae sio mtu yule. Yule ni shetani aliyejivika ngozi ya mbuzi ili aonekane ni mnyama. Ikiwa ameweza kukudhalilisha kiasi hicho. Naamini anaouwezo wa kuutoa uhai wako endapo utaendelea kumfuatilia. Narudia tena achana nae na usijaribu tena kumtafuta. Nakuapia ndugu yangu, haya mateso uliyonayo sasa kwajili yake. Yatamrudia na yeye na atakutafuta tu...” Jay alikatisha maneno yake baada ya kusikia sauti ya mama yake akimuita. Akamuacha Ramah pale na kutoka nje ambapo alimkuta mama yake akiwa amesimama huku usoni akionyesha hofu.



    “Ana nini huyo mwenzako?. Naomba usinifiche” Ndio maneno ya kwanza kutamkwa na mama yake baada ya kumfikia karibu. Alionekana akiwa na shauku ya kutaka kujua ni kipi kimemkuta mwanae. Jay alitazama chini akitafakari ni vipi atamueleza mama yake. Ni wapi ataanzia kumueleza. Akanyanyua uso na kumtazama usoni mama yake. Akakuta mama yake akiwa na uso wa umakini akisubiri kuelezwa. Jay alijitutumua na kumueleza yote mwanzo mwisho. Tangu kisa kilipoanza mpaka hapo kilipofikia. Hakumficha chochote alimueleza yote.



    “Kwahiyo Ethan ndio amemfanyia hivyo mwenzie kwa makusudi kabisa?” Mama yake alimuhoji.



    “Hapana mama. Kwa maelezo ya Ramah sidhani kama Ethan atakuwa anajua chochote. Cecy ndie muasisi wa yote haya” Jay alijibu.



    “Sawa. Lakini mama yake na Cecy anayajua haya?”



    “Hapana, hana anachojua”



    “Haya na huyo mwenzako nae yupo katika hali gani?”



    “Kwasasa hayupo sawa. Ila acha nimtulize ili arejewe na hali yake ya kawaida” Jay alizungumza hayo na mama yake akampa ruhusa. Akaondoka kurudi chumbani kwao huku mama yao akiendelea kuandaa chakula.



    Jay alirudi tena chumbani kwao na kumkuta Ramah akiwa katika hali ile ile. Amejiinamia chini huku akitokwa na machozi. Akakaa tena karibu na kuanza kumfariji nduguye. Lakini ikawa kama kumpigia mbuzi gitaa akitarajia ainue miguu ya mbele aanze kucheza. Haikuwa hivyo, Ramah alikuwa katika hali ile ile mpaka pale Jay alipoitwa na Mama yake kwaajili ya kwenda kuchukua chakula. Alienda na aliporudi alikuwa amebeba chakula, akakiweka mezani na kumuambia Ramah kwamba chakula tayari na anahitajika ale.



    “Endelea mi nitakula baadae” Ramah alijibu hivyo akiwa katika pozi lile lile la kujiinamia.



    “Usiwaze sana mdogo wangu, hayo mambo yapo, wewe sio wa kwanza kutendwa” Jay alisema hayo kisha akavuta sahani yake.



    Jay wakati anaendelea kula taratibu, simu yake ikaita na alipotizama ni nani anaempigia akakuta ni namba ngeni. Hakujisumbua kuipokea maana ndivyo ada yake ilivyo. Hakuwa na kawaida ya kupokea namba ngeni haraka haraka. Akaiacha simu yake ikaita mpaka ikakata. Sekunde hiyo hiyo ikaita tena. Mara hii sasa aliona apokee. Akainyanyua na kuipokea kisha akaiweka sikioni.



    “Halo Jay” Sauti ya kike ilisikika kwenye spika ya simu yake. Akatulia kidogo kuitafakari kama ataweza kumaizi ni nani hasa mwenye kumiliki sauti hiyo. Lakini hakuweza kujua. Akajibu na yeye kwa kusema Halo.



    “Samahani Jay. Jeni hapa nilikuwa na shida na Ramah maana napiga simu yake lakini haipatikani. Yupo wapi kwani?” Mara hii sasa Jay aling'amua kumbe aliempigia simu alikuwa ni Jenifa. Akamtazama Ramah pale alipo. Ramah wala hakuwa na habari yoyote.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ramah ninae hapa lakini sidhani kama ataweza kuongea” Jay alijibu.



    “Ok. Mpe pole mwambie kesho nitakuja hapo nyumbani” Jeni akasema hayo kisha wakaagana na simu ikakatwa.



    Baada ya kumaliza kula. Aliondoa vyombo alivyotumia yeye huku kile chakula cha Ramah akikiacha pale pale kwa minijali ya kwamba, Ramah atakula baadae kama alivyosema. Aliporudi tena ndani. Akapunguza baadhi ya nguo kwenye mwili wake kisha akalala kitandani. Muda huo hakutaka kutoka tena kwasababu azijuazo mwenyewe. Akavuta simu yake na kuanza kucheza nayo. Hakujitambua hata pale alipokumbwa na usingizi huku simu yake akiisaliti kitandani.



    ------------



    Majira ya saa mbili asubuhi. Jay alifumbua macho baada ya kuyafumba kwa muda mrefu alipokuwa usingizini. Alipekecha macho yake yaliyokuwa na mawenge ya usingizi kisha akatafuta ni wapi alipoiacha simu yake. Alipoipata akatazama saa kisha akaiweka kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni ya kitandani.



    Alishangazwa baada ya kumuona Ramah akiwa pale pale kwenye sofa mara hii alikuwa ameegemeza mgongo wake kwenye mto wa sofa huku akiwa anatazama mbele, macho yakiwa wazi bila kupepesa. Alipotazama kwenye meza, alikuta kile chakula ambacho Ramah alisema atakila, kilikuwa vile vile na wala hakikuonekana kuguswa hata kidogo. Akajiinua na kukaa pale kitandani akimtazama Ramah kwa mshangao.



    “Oyaa! Kwahiyo huu msosi haukula? Halafu umelala hapo kwenye hilo sofa...?.” Ramah akamtazama Jay na kugandisha macho yake usoni kwake.



    “Aaaa! Ndugu yangu usiwe hivyo bwana. Unataka kuniambia mawazo ndio yanataka kukuchanganya kiasi hicho? We ni mwanaume unatakiwa kukabiliana na changamoto zinazokuja mbele yako. Sasa ikiwa changamoto hii ndio inakuhenyesha namna hii mi nakushangaa ati.... Subiri nakuja..” Jay aliongea hayo kisha akainuka pale kitandani. Akavuta bukta ndefu na kuivaa, akachukua fulana ambayo ilikatwa mikono na kuivaa. Kisha akatoka nje.



    Dakika tano alirudi akiwa ameongozana na Jeni. Jeni alipomuona Ramah akiwa katika hali ile alihuzunika na kusikikita. Akamtazama Jay kwa muda kisha macho yake akayahamisha kwa Ramah aliekuwa ametazama chini. Haikujulikana kama alitambua uwepo wa Jenifa ama laa! Alikuwa kama bubu asieweza ongea lolote lile.



    “Rafa...!” Jeni alimuita huku akikaa kitandani akiangaliana nae. “Hupaswi kuwa hivyo Rafael we ni mwanaume. Usikubali kuendeshwa na hisia za moyo. Hisia za mapenzi usikubali zikakuteka kiasi hicho kwasababu zitakupelekea kushindwa kufanya mambo yako muhimu...” Akatulia na kujivuta mbele kidogo. “Jana Cecy alinipigia simu akaniambia alichokufanyia. Hata mimi hayakunipendeza kwasababu haikustaili kukufanyia mtu kama wewe. Mtu ambae uliijali furaha yake muda wote. Ulihakikisha unamfurahisha kadri uwezavyo lakini leo hii amekulipa haya. Huwezi amini nusura tuuvunje urafiki wetu baada ya kumuhoji kwanini amekufanyi yale. Nadhani alitegemea ningemuunga mkono kwa alichokufanyia. Alipoona nipo tofauti nae akanijia juu huku akinikashfu. Lakini nakuhakikishia bado sijachoka, nitamtafuta na kumueleza jinsi ulivyo pengine anaweza kurudisha moyo nyuma”



    Jeni aliongea hayo kwa upole kama muuguzi ambembelezapo mgonjwa wake anywe dawa. Machozi yaliyokuwa yamekoma kwenye macho ya Ramah. Yalianza upya kutoka kudhihirisha ni machungu kiasi gani yaliyo moyoni mwake.



    “Usilie Rafael, jikaze we ni mwanaume hupaswi kuwa hivyo” Jeni alisema hayo kisha akatoa kitambara chake na kumfuta machozi Ramah.



    “Acha niwaacheni, nitarejea baadae ama kesho lakini Ramah usiwe hivyo bwana we ni mwanaume hunabudi kujikaza. Amini yatapita haya” Jeni aliongea hayo kisha akatoka chumbani mule akisindikizwa na Jay.



    Safari ya Jane ilikuwa ni nyumbani kwa kina Cecy. Hata pale alipofika alimkuta Cecy akiwa anatoka nyumbani kwao. Akamsalimia Mama yake na Cecy kisha akamfuata Cecy.







    “Naelekea hapo dukani mara moja. Kama vipi nitoe basi” Cecy aliongea hayo kisha Jane akamuambia amsubiri apeleke mkoba wake ndani. Jeni akaingia sebuleni na kuurusha mkoba wake kwenye sofa kisha akatoka nje kuelekea huko Cecy anapoenda. Wakaongozana wote mpaka huko, kisha Cecy akanunua alichokusudia kununua halafu wakarudi tena nyumbani kwao moja kwa moja mpaka chumbani kwa Cecy.



    “Mwenzangu wee! Sijakuelezea tuliyoyafanya juzi mimi na Rommy huko Pangani. Aisee kumbe ule mji ni mzuri balaa, una sehemu za kihistoria kama watu wasemavyo. Tatizo lako wewe hutaki kuwa huru kwa Rommy wakati yule ni shemeji yako. Naamini kama ungekuwa huru nae, tungeenda wote kule maana pia alikuulizia” Cecy alinena kwa furaha akitegemea kuungwa mkono na Jeni kwa kile alichonena. Akashangazwa na ukimya wa Jeni huku sura yake ikiwa ya kawaida tofauti na yeye alivyodhani kwamba atakuwa ni mwenye kutabasamu.



    “Vipi wewe...?” Akauliza kwa mastaajabu huku akimtazama usoni. Tabasamu hafifu likaonekana kwenye wajihi wa Jeni kisha sekunde hiyo hiyo likazama.



    “Unajua Cecy we ni mkubwa. Ninapozungumzia ukubwa namaamisha unayajua mengi na hupaswi kujuzwa kila jambo. Na hakika unalijua lipi baya lipi zuri. Lipi lafaa lipi halifai. Lakini bado nashindwa kuishangaa akili yako ikoje. Sijui ni nani hasa anaeindesha maana nashindwa kuamini kama ni kweli unaiendesha mwenyewe. Hufananiani kabisa na vile nikujuavyo tangu kitambo. Umekuwa wa tofauti ghafla naamini hata mwendawazimu akielezewa vituko vyako lazima atastajabu. Una nini lakini wewe? Umepatwa na nini......? Siwezi kuingilia maamuzi yako ya kuamua uwe na nani, nani uachane nae. Lakini sio kwa Rommy, Cecy! Rommy wewe unamfahamu vyema. Unaufahamu ulaghai wake maana hata kipindi kile alionyesha kukujali kama akuonyeshavyo hivi sasa. Lakini ni kipi mwisho wa mchezo kilitokea? Mtazame Rafael, tangu nimjue, tangu niyajue mapenzi yenu sikuwahi kumuona akiyapunguza hata siku moja zaidi ya kuyaongeza siku hadi siku. Lakini leo hii ni kipi hasa umemlipa zaidi ya maumivu makali mtoto wa watu. Eeee anaelekea kuwa chizi sasa kwa maumivu yako....”



    “Kwahiyo umeamua kunitukana?....” Cevy aliwaka. “Umeniona mimi siwezi kuiendesha akili yangu kwamaana ya kuwa yupo anaeiendesha tofauti na mimi au sivyo? Ukanishusha thamani kwa kunifananisha na mwendawazimu, nakusikiliza tu si kwamba maneno yako nayaelewa vyema. Ukaona haitoshi, kwavile ushaniona sina akili timamu sasa ukataka nichagulia mpaka wakuwa nae. Vyote nakusikiliza...” Akamtazama Jeni kwa hasira.“Nadhani urafiki wetu umeshauchoka na unataka tuwe maadui....”



    “Sivyo Cecy. Tena wala usinifikirie vibaya. Malengo yangu nikukuelewesha tu....”



    “Utamuelewesha nani wewe mjinga tu......” Cecy alipaza sauti kudhihirisha hasira zake. “Shule kwenyewe ulikuwa ukinitegemea mimi nikueleweshe, sasa leo utanielewesha kitu gani ambacho sikuwahi kukuelewesha mimi? Umekuwa ni mtume wewe? Umekuwa ni nabii? Achana na mimi mpuuzi tu wewe na yule mwenzako na kwa taarifa yako nimeshagundua janja yako kwamba unamtaka Rommy na hapa upo kunishawishi ili umteke wewe. Nyoo! Umeshindwa dada labda ukaroge tena. Kama unajifanya kumhurumia sana Ramah si umfuate wewe. Tena toka na usinijue tena, hasidi wewe mchonganishi. Jini kisirani mfuatilia vya watu vyako vya kushinda” Cecy alipayuka kwa sauti kisha akainuka pale alipokaa na kwenda kumvuta mkono Jeni, kisha akaanza kumkokota mpaka nje ambapo mama yake alikuwapo huko akiendelea na shuhuli zake. Akashangazwa na vurumai hilo la marafiki hao wa muda mrefu. Kwa taharuki akasimama akiwatazama huku mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.



    “Sawa Cecy naondoka lakini utakuja kuyakumbuka haya unayoyafanya na utakuwa ushachelewa hata ukihitaji msamaha”



    “Kwendeni huko wachawi tu nyie kwani asiewajua nani? Eti niyakumbuke! Kwa lipi? Tena ondoka usituwangie kwetu mafala nyie...” Cecy aliyaongea hayo kwa kisirani kisha akaingia ndani. Sekunde hiyo hiyo akafungua mlango na kutoka tena. “Nakuapia, haki ya Mungu Jenifa nikikuona tena hapa kwetu jua utatambua kwamba Cecy mwana wa Ally kwanini ameitwa Cecilia. Wajinga nyie!” Akamaliza na hayo kisha akazama tena ndani moja kwa moja mpaka chumbani kwake. Akajifungia mlango huko na kutulia mwenyewe akiwa anatweta kwa hasira.



    “Jeni..! Jenifa. Embu njoo mama. Njoo unieleze nini kimetokea mpaka mkaanzisha vurumai wakati mlikuwa mkicheka wote punde tu”



    Anita mama yake na Cecy alimuita Jenifa aliekuwa anaondoka mahala hapo. Mara hii Jenifa alikuwa akilia baada ya kutukwana na rafikiye wa muda mrefu. Anita alienda kumshika mkono mpaka kwenye mkeka ambao mwanzo Anita alikuwa amejipumzisha hapo. Akamkalisha chini kisha akamuuliza ni kipi hasa kimetokea kwao wawili hao.



    Jeni akiwa bado analia, alimueleza yote Mama yake Cecy kisha akalalamika kwa kusema liwapi kosa lake. Kumuambia ukweli Cecy ndio imekuwa kosa mpaka kufikia hatua ya kumtukana namna ile. Anita hakuwa akiyajua hayo kabla. Akashusha pumzi huku akitazama chini kwa tafakuri. Hata pale alipoinua sura yake juu hakuweza kumuona Jeni mbele yake. Zaidi aliishia kuona nguo aliyoivaa Jeni kwa siku hiyo ikipotea kwenye kona ya nyumba yake. Kizazaa!.



    Anita aliguna kisha akainuka pale kwenye mkeka. Akavaa ndala zake, hatua mosi, hatua pili mpaka nje ya mlango wa chumba cha mwanae. Akajaribu kuufungua lakini haukufunguka ishara ya kuwa umefungwa kwa ndani. Hakuwa na budi kugonga huku akiita jina la mwanae. Mlango ukafunguliwa na yeye akazama ndani. Cecy alikuwa amevimba mithili ya andazi lililokolezwa hamira. Hasira za wazi wazi zilionekana usoni mwake. Anita alimtazama kwa kitambo kisha akakaa kwenye meza kumuelekea.



    “Enheee! Nini kimetokea mpaka ukagombana na mwenzio, tena kwa matusi juu huku ukimuita mwenzako mchawi. Tatizo nini?” Anita alimuhoji kwa utulivu na si kwamba hakumuamini Jeni? La hasha! Bali alitaka kusikiliza na maelezo ya Cecy. Cecy aliuvuta mdomo na pembeni kwa jeuri. Kisha akasema.



    “Unajua Mama huwa sipendi kuingiliwa kwenye amuzi langu. Sasa yeye ni vipi aniingilie? Au kwavile nimempa nafasi ya kuwa rafiki yangu ndio anaona kila kitu anaweza kunipangia. Mi sio wa kihivyo mama yangu. Mi naendeshwa na akili yangu na wala si akili ya mtu yoyote kama anavyohisi yeye”



    “Nimekuelewa. Ila sijaelewa chanzo cha ugomvi wenu ni nini mpaka kufikia hatua ya kutukanana?” Anita alimuhoji tena.



    “Ananipangia kwenye mambo yangu” Cecy alijibu kiufupi.



    “Kivipi? Embu nieleweshe. Halafu naomba usinifiche chochote maana naona unazunguka kunieleza” Anita mara hii alimkazia. Cecy akatulia kimya kama dakika moja, kisha akaongea baada ya kugutushwa na sauti ya Mama yake aliemtaka maelezo.



    “Mama mimi nayakumbuka maneno yako sana, hata sasa nayakumbuka. Ulikuwa ukiniambia mwenye maamuzi ya mwisho ya kuchagua niwe na nani ni mimi mwenyewe. Kwa kipindi chote nilichokaa na Ramah nimegundua kwamba ananipenda sana ila mimi sikuwa nikimpenda...”



    “Unasemaje wewe mtoto?” Anita aliuliza kwa taharuki huku akimkazia macho Cecy. Cecy akaogopa lakini akajivika ujasiri.



    “Ndio Mama, Ramah sikuwa nikimpenda na moyo wangu shahidi wa hilo. Sasa ni vipi nimdanganye? Mi nimemuambia ukweli tu!”



    “Cecy mwanangu nini kimekukuta wewe? Hukuwa wewe wakunilalamikia mimi kwamba Ramah hapokei simu zako kisa umemuudhi? Tena muda mwengine ulikuwa ukinilazimisha niongee nae ili niyaweke mambo yenu sawa? Hivi hukuona kuwa ulikuwa unanidhalilisha? Anhaa! Kukupa uhuru wa kuwa na mwanaume ukiwa na umri huo ndio unahisi tayari nimeshakuoza si ndio? Unafanya mambo yako unavyoamua mwenyewe tena kwa kujinadi ( akabana pua kwa viganja vyake huku akitazama juu akiwa ameikunja sura yake) Huwa siingiliwi kwenye maamuzi yangu na yoyote, nikiamua nimeamua( Mwisho wa kuigiza. Akaendelea kuongea). Umekuwa siku hizi waoga chooni ndio unaniona hata mimi Mama yako mavi tu siwezi kuingilia maamuzi yako..?” Kofi kali likatua kwenye shavu la Cecy. “Pumbavu mmoja wewe!”



    Cecy akajiinamia akiwa ameshika shavu lake huku akilia. Sekunde saba mbele aliinuka kwa kisirani na kutoka chumbani humo akimuacha mama yake akimuita kwa hasira.



    * *



    Tangu alipokula siku iliyopita chakula kile kilichopewa jina ati chakula cha mchana. Ndio mpaka siku hii majira haya haya ya mchana hakuwa ametia chochote kinywani. Nduguye alihangaika kumsemeza na kumbembeleza kila muda kuwa atie chochoto tumboni mwake ili aupe nguvu mwili. Lakini yeye hakuwa ni mwenye kujibu chochote zaidi ya kutulia vile vile kama kiziwi asiesikia lolote au bubu asieweza kutamka akaeleweka.



    Hata pale Jay alipomshirikisha Mama yao kuhusu swala la Ramah kugoma kula, mama yao lilimuumiza sana na kuamua kujaribu yeye bahati yake. Pia alimbembeleza sana lakini hakuwa ni mwenye kujibu lolote. Sasa ni vipi agome kula kwani hakuwa akisikia njaa. Haikujulikana! Lakini sasa ni nini wafanye ikiwa ndugu yao amegoma kula?



    Nusu saa imepita tangu wambembeleze kula. Na si kula tu, hata kunyanyuka pale alipokuwa amekaa aligoma. Dorine hakujua afanye nini juu ya mwanae kutokana na hali iliyomkuta. Machozi ya uchungu wa mwana yalimtoka huku akimtazama mwanae kwa huruma. Alimlaani Cecilia kwa kumfanya mwanae awe katika hali hiyo huku yeye akihisi atakuwa ni mwenye kufurahika huko alipo.



    Kwakuwa mwanae hakupata chakula ikiwa ni siku ya pili hiyo. Hata yeye hakuona umuhimu wa kula ikiwa anajua kabisa kwamba mwanae ana njaa. Chakula alipika yeye ndio lakini raha ya kula ataitoa wapi ikiwa aliepika kwaajili yake aligoma kula? Jay na yeye hakuweza kula chakula kile. Akaungana na wenzake kuyasulubu matumbo yao ilhali chakula kingali kuwapo. Sasa ni vipi ale ilhali wenzake hawakula? Furaha ya kula ataitoa wapi ikiwa hakuna aliekula kati ya nduguze. Yamkini hali ile iliwaumiza wote watatu!.



    Yakiwa ni majira ya saa mbili usiku. Wote waishio kwenye nyumba hiyo wakiwa wamekisusa chakula kwasababu zinazojulikana. Jay akiwa kitandani amejiinamia huku Ramah akiwa kwenye sofa macho yakitazama mbele tu utafikiri ni mwenye kukariri kitu huko atazamapo. Mama yao akiwa chumbani kwake amejilaza kitandani kwake mawazo kibao juu ya wanae.







    Simu ya Jay aliita ikiwa juu ya meza. Akainua kichwa kiuvivu na kuitazama simu yake. Namba ile ile ambayo siku iliyopita ilipiga na kutoipokea kwa haraka. Na hata pale alipoipokea akamaizi ni Jeni ndie mmiliki wa namba ile. Sasa namba ile ilikuwa akipiga tena simu yake. Akajivuta kidogo kuifikiia meza kisha akaichukua simu na kuipokea. Wakasalimiana kidogo kisha Jeni akaulizia hali ya Ramah. Jay hakumficha kitu. Alimuambia kwamba Ramah hali yake haieleweki na zaidi amegoma kula tangu alivyokula siku iliyopita hakula tena mpaka hivi leo.



    “Jamaniii! Kwanini lakini amekuwa hivyo? Ok. Jay nakuja sasa hivi hapo” Hata kabla ya Jay hajajibu lolote simu ikakatwa. Akairudisha simu yake kwenye meza na kuendelea kujiinamia. Hakutaka kutoka ndani mule amuache nduguye akiwa katika hali ile. Alionelea bora abaki nae karibu pengine Ramah anafarijika awapo karibu yake.



    Dakika nane mbele, mlango wa chumba chao uligongwa hodi. Jay aliinua kichwa na kuutazama mlango utadhani unaweza kumuonyesha alieko nje. Akanyanyua kinywa chake na kumkaribisha. Sekunde hiyo hiyo mlango ukafunguliwa na Jeni akaingia ndani humo. Akatazama mazingira ya humo akakuta yakiwa ni yenye kuhuzunisha. Jay hakuwa na sura ya furaha hata kidogo huku Ramah akiwa katika hali ile ile aliyomuacha nayo asubuhi ya siku hiyo.



    Akamsalimu Jay kisha akamgeukia Ramah. Ramah alikuwa bize na kutazama mbele tu na wala hakujishuhulisha kumtazama Jeni. Pia haikujulikana kama aliutambua uwepo wake ama laa! Dakika hiyo hiyo mlango ukafunguliwa na Dorine mama wa wana hao akaingia ndani humo. Jeni alimsalimu na Dorine aliitikia salamu hiyo. Hata yeye wajihi wake haukuwa ni wenye furaha kama ilivyo kwa wanae.



    “Kwahiyo Jay unataka kuniambia Ramah hakuwa amekula tangu jana?” Jeni alimgeukia Jay na kumuuliza. Jay aliitikia kwa kichwa kukubali. Jeni alimtazama tena Ramah kisha akajongea mpaka pale kitandani. Akakaa mahala hapo akiwa anatazamana na Ramah.



    “Rafael..." Jeni akamuita huku akimtazama usoni. Akaendelea. “Nakumbuka kipindi kile tunasoma ulikuwa ukituhusia sana kuwa wajasiri pindi tukutwapo na mitihani hasa hasa ile tuifanyao shule. Na tulikuwa tukikusikiliza kwasababu ulituzidi kidato kimoja na tulijua wewe unajua mengi sana ya kimasomo kuliko sisi. Nakumbuka ulikuwa ukituambia tusiiogope mitihani iliyokuwa mbele yetu ama ile ambayo tulikuwa nao kwa wakati huo. Ukatuambia kuwa mitihani imewekwa ili kupima uwezo wetu kimaarifa na kiakili. Licha ya hivyo, pia tuweze kuwa majasiri zaidi pindi mitihani iishapo na ukutuhusia tusizikimbie zile test za kila mwezi kwasababu zile ndio zitakazo tupatia ujasiri kwenye mitihani mikubwa. Sasa vipi leo hii wewe usiwe jasiri kwenye mtihani huu mdogo uliokuwa nao? Inamaana ulikuwa ukitudanganya sisi? Lakini hapana, mbona tulivyojivika ujasiri tuliifaulu vizuri ile mitihani? Usitake maneno yako yakarudi nyuma na kukuacha wewe usiwe jasiri kwenye mtihani huu mdogo. Ikiwa leo hii unateseka ati kwa vile umeachwa na mwanamke. Je kesho Mama nae akitoweka utakuwa katika hali gani? Si utakuwa mwendawazima kama si kufa kabisa.

    Najua sote unatupenda hapa. Unampenda Mama. Unampenda Jeremiah na hata mimi pia unanipenda. Lakini usituonee huruma sote, muone huruma Mama hapa. Anahuzunika kwaajili yako kwasababu umegoma kula chakula. Sio tu kuhuzunika, pia hakula chakula kwa kuona mwanae hujala bado. Sasa unapenda Mama alale na njaa kisa wewe hujala....?” Jeni aliyaongea hayo kwa sauti ya upole kiasi ambacho wote waliokuwa mahala pale walikuwa kimya hata sauti za pumzi zao hazikusikika pale walipopumua.



    Jeni alifungua bakuli lililokuwa limewekwa chakula kwaajili ya Ramah. Chakula hiki hakikuwa ni kile alichokiacha siku iliyopita. La! Bali kile kiliondolewa baada ya kuwa kimeharibika na hiki kilikuwa ni chengine alichowekewa mchana wa siku hiyo hata pale akagoma kukila. Kilikuwa ni wali uliotandazwa mchuzi wa samaki ulioungwa vyema na kuleta harufu nzuri iliyoingia kwenye pua za wote waliokuwa hapo.



    Jeni akanawa mikono yake na kumega tonge dogo la chakula kile na kulifinyanga kidogo. Kisha taratibu kabisa akalipeleka kinywani mwa Ramah akitarajia labda Ramah anaweza fumbua kinywa na kulipokea. Lakini ikawa tofauti, Ramah hakuweza kufumbua kinywa. Achilia mbali kinywa. Hata macho hakupepesa.



    “Haki vile Ramah hili tonge silirudishi nyuma. Kwanini lakini unamfanya mama asiwe na rahaa? Embu tazama mama anavyokutazama akitarajia utakula chakula hichi ili afurahi na yeye apate kula. Embu mtazame anavyohuzunika kwajili yako!” Jeni mara hii aliongea kwa hisia mpaka Ramah mwenyewe akageuza shingo taratibu na kumtazama Mama yake kwa sekunde kadhaa. Kisha akarudisha macho yake kule alipo Jeni.



    Jeni akajaribu tena kusogeza tonge lile kinywani kwa Ramah. Zikapita sekunde thelathini ikiwa kiganja cha Jeni kilichofinyanga tonge dogo kikiwa karibu kabisa na kinywa cha Ramah. Taratibu kabisa papi za mdomo wa Ramah zikagawanyika. Wa juu ukapanda juu na wa chini ukashuka chini kinywa kikawa wazi. Taratibu kabisa Jeni akapenyeza lile tonge kinywani kwa Ramah na yeye akalipokea vyema japo ilikuwa shida kidogo kuzama kabisa kinywani.



    Wote waliokuwa mahala pale walitabasamu huku Dorine akithubutu kudondosha chozi la furaha baada ya kuona mwanae amekubali kula kwa ushawishi wa Jeni. Ramah alikohoa sana baada ya kumeza tonge lile. Jeni haraka akachukua glasi ya maji na kumimina maji kutoka kwenye jagi. Kisha akamnywesha Ramah taratibu.



    Ramah akayanywa yale maji. Jeni akaongeza tabasamu usoni mwake na kumega tena tonge jengine. Mara hii hakuleta tabu kufumbua kinywa pengine tumbo muda huu ndio lilihisi njaa. Hata hivyo muda mwengine alijisahau kufungua kinywa mpaka pale Jeni alipogusisha tonge kwenye mdomo wake. Jeni aliendelea kumlisha mpaka pale Ramah alipogoma kabisa kufungua kinywa. Hata hivyo walihisi pengine alishatosheka. Akachukua tena glasi ya maji na kumnywesha. Alipokunywa maji yale Jeni akarudisha glasi mezani kisha tabasamu lililoelekea kicheko likaonekana usoni kwake.



    “Huoni mama amefurahi sasa. Naamini leo atalala usingizi mnono pengine kuliko siku zote alizowahi kulala” Jeni aliongea hayo kisha akanawa mikono. Mama yake na Ramah muda wote alikuwa akitabasamu huku moyo wa Jay ukiwa mweupe kwa furaha.



    Jeni akamuuliza maswali lakini Ramah alikuwa akimuangalia tu pasi na kumjibu. Hata hivyo furaha waliyokuwa nayo baada ya kula haikuondoka kwenye mioyo yao. Jeni akawaambia kuwa hali ya Ramah bado haikuwa vyema pamoja na kuwa amekula. Akamuambia Jay amsaidie Ramah kumtoa nje ikiwezekana amfanyie hudumu muhimu ikiwemo kumuogesha. Hilo halikuwa tatizo kwa Jay.



    Baada ya hapo Jeni akawaaga kuwa anaelekea nyumbani kwao majira hayo. Jay ikabidi amsindikize japokuwa hapakuwa na umbali wowote. Wakiwa wanatembea njiani, Jeni alimuhadithia Jay yaliyomkuta siku hiyo alipoenda kwa kina Cecy mpaka kupelekea kugombana wenyewe. Jay alisikitika, zaidi akimsikitikia Cecy kwa kuona anaendeshwa na nguvu ya mapenzi mpaka kufikia hatua ya kugombana na rafiki yake.



    Walipofika karibu na nyumbani kwa kina Jeni, Jay akaomba aishie hapo. Jeni akakubali lakini pia akiomba jukumu la kumlisha Ramah alivae yeye endapo kama atagoma tena kula. Jay hakupinga zaidi alimshukuru kisha wakaagana. Jay akarudi kwao huku akiwa na furaha moyoni kwake kwa kitendo cha Ramah kukubali kula.

    Ndio, lazima awe na furaha kwasababu wote walikata tamaa na hawakujua ni vipi watamshawishi Ramah akubali kula.



    * *



    Wiki moja ikapita hali ya Ramah ikiwa vile vile. Hakuwa ni mwenye kutoka nje ya chumba chao mpaka atolewe. Japokuwa hivi sasa kula aliweza kula mwenyewe lakini Jeni alipenda tu kumlisha, na yeye hakulipinga hilo. Pamoja na yote hayo. Kuongea kwake ilikuwa ni kwa bahati sana kusikika, ni nadra sana kusikika akiongea. Na hata pale alipoongea hakuwa ni mwenye kuongea maneno mengi kabla ya kukata sauti kabisa.



    Kama alivyojiwekea ada kuwa ni lazima atenge muda kwaajili ya kwenda kwakina Ramah kwenda kuzungumza nae na baadae kumlisha chakula. Japokuwa mara nyingi anapomuongelesha Ramah huishia kuitikiwa kwa kichwa tu au hata kwa tabasamu. Hata hivyo hakujali, furaha yake ilikuwa ni kukaa nae karibu.



    Hata leo hii alikuwa mbele yake akimlisha chakula huku akimpigia stori ambazo zilimfanya Ramah atabasamu huku mara kadhaa akimuunga mkono kwa kuitikia kwa kichwa. Hata pale alipomaliza kumlisha baada ya Ramah kutoa ishara kwamba inatosha. Jeni akaacha na kuchukua nafasi hiyo kupiga nae stori. Dakika kadhaa akamuaga kuwa anaelekea nyumbani kwao na atarudi siku inayofuata. Huzuni ilionekana usoni kwa Ramah pindi Jeni alipomuaga kuwa anataka kuondoka. Lakini sasa Jeni abaki nae masaa yote bila kufanya mambo yake mengi?

    Haikuwezekana!.



    Akatoka nje na kuelekea sebuleni ambapo alikuwa Mama Jay na Jay wakiwa wamekaa wakizungumza mambo yao. Jeni alipofika pale Mama Jay alimkaribisha kwa furaha na kumuambia akae. Kisha akamshirikisha Jeni kile walichokuwa wakikiongea. Ilikuwa ni kuhusu hali ya Ramah ni vipi atarudi kwenye hali yake ya kawaida. Jeni akafikiri kidogo kisha akasema.



    “Mama..” Akaita na wote wakawa makini kumsikiliza. Akaendelea.“ Kwa hii elimu yangu ndogo niliyonayo nimegundua kwenye akili ya Ramah kuna kitu na hakitaki kutoka bila tiba maalumu. Simjuvi sana lakini nadhani panatikiwa apatikane mtaalamu wa saikolojia naamini ataweza kuiweka akili ya Ramah vyema. Tungesema tumuache ndio awe vile vile mpaka akili yake itakapokuwa sawa. Lakini itachukua muda sana mpaka kutokea hivyo. Lakini njia rahisi ni hiyo na naamini kwa uwezo wa Mungu lazima Ramah arudi katika hali yake ya kawaida” Jeni akawaeleza hayo. Mama Jay alimtazama Jay na Jay nae alimtazama mama yake.

    Wakatazamana!.



    “Sawa mama nimekuelewa. Lakini sasa huyo mtu tutampata wapi maana mimi kama mimi sina hata moja kwa hayo uliyoaongea. Isitoshe pia sijui itagharimu kiasi gani mpaka mwanangu kupona” Mama Jay alisema.



    “Mama msijali, ilimradi msharidhia. Basi mambo yote niachieni mimi na kesho nitawajia na jibu kamili” Wakakubaliana nae kisha Jeni akaaga na kuondoka mahala hapo.







    Wakati upande huu yakiendelea haya. Upande mwengine wa Rommy ama Ethan mambo yalielekea kubaya kwa mfanyakazi wao Siwema. Ni siku ya tano sasa hakuwa akiielewa hali yake. Uchovu muda wote hata baadhi ya kazi akawa hazifanyi kwa ufasaha. Kichefuchefu na kutapika muda wowote kulimjaa. Kwa umri aliokuwa nao hakuitaji daktari wa kumthibitishia kuwa ni mjamzito. Maana hata siku zake alizisubiria kwa zaidi ya wiki sasa lakini hakuziona japo siku zake za kawaida zilishapita. Sasa kama si mimba ni nini?



    Furaha ikamshika huku moyo ukimuenda mbio mbio kwa shangwe. Ndio, lazima afurahi kuzaa na kijana mdogo mwenye kumiliki mali nyingi. Naamini nikimuambia Rommy swala hili lazima afurahi. Alijiwazia huku akilishika tumbo lake lisiloonyesha ishara zozote za kuhifadhi kiumbe. Sasa kwanini nisiende kumuambia sasa ili na yeye ajue? Afurahi kama nifurahivyo mimi muda huu? Hapana bwana lazima nimshirikishe na yeye furaha hii.



    Akatoka hai hai mpaka sebuleni ambapo alikuwa Rommy na kina Paskali wakicheza gemu muda huo. Akamuita Rommy huku akiwa na tabasamu na kumtaka watoke nje. Rommy akamfuata Siwema kule nje alipotoka huku akiwa haelewi ni kipi hasa akitakacho mwanadada huyo. Huko alimkuta ukutani akiwa ameegemea huku meno yakiwa nje kwa tabasamu. Kufika na kufika tu akamkumbatia Rommy kwa dakika moja kisha akamuachia.

    Huyu mwanamke ana matatizo gani huyu? Ama ni kichaa kinamuanza? Rommy alijiuliza hayo huku akimtazama Siwema usoni kwa mshangao. Siwema hakutaka Rommy ashangae sana badala yake akauvuta mkono wake na kuushikisha kwenye tumbo lake. Hata hivyo Rommy hakuwa ameelewa kitu.



    “Mume wangu unaenda kuitwa baba baada ya miezi kadhaa mbele” Siwema alisema hayo huku akiwa na furaha ya dhahiri usoni mwake. Sura ya Rommy ilitoka katika hali ya mshangao mpaka kwenye kuchukia. Kitendo hicho kilimshangaza Siwema na kuamua kuhoji nini tatizo.



    “We mwanamke unaakili kweli wewe? Umeona wapi bwana akazaa na mbwa wake anaemfuga mwenyewe? Acha hizo wewe hiyo mimba si yangu. Tena kuanzia sasa kusanya kilichochako na utoke ndani humu. Maana unataka kunifanya zoba, mimba wakupachike wengine uje kunibwagia mimi. Toka rudi huko huko walipokuzawadia hiyo mimba” Rommy aliongea kwa ghadhabu huku mishipa ya shingo ikimtutumka mithili ya mti wa muembe uliokomaa.



    Haraka akajitoa pale na kuingia ndani. Hata pale alipoingia ndani, aliwapita wakina Paskali pale ukumbini kwa kasi ya Farasi mpaka chumbani kwa Siwema. Akakusanya nguo zake na kuzitia kwenye begi lake. Kisha akatoka na begi hai hai mpaka sebuleni alipomkuta Siwema akilia kwa uchungu huku akimsisitizia kwamba mimba ni ya kwake.



    “Rommy usifanye hivyo. Haki ya Mungu ni ya kwako, na wala sikuongopei!” Siwema aliongea huku akilia. Hakuwa akiamini kama kweli Rommy anaweza kuikataa mimba yake mwenyewe.



    Furaha yake yote ilififia. Zile ndoto alizokuwa akiziota siku kadhaa nyuma kwamba ataishi kwenye nyumba hiyo kama Malkia na sio kijakazi tena zikapotea. Inamaana Rommy hajui kwamba sikuwahi kutoka nje ya nyumba hii? Pia hakumbuki kwamba alishalala na mimi zaidi ya mara moja? Siwema alijiuliza hayo huku akimtazama Rommy kwa huruma.



    Unadhani Rommy alitaka kusikia lolote? Ama alitaka kumhurumia mwanamke huyo. Alimfukuza Siwema huku akimtukana matusi mazito ambayo haikuwa sawa kuandikwa hapa. Hata pale Siwema alipoleta ubishi kutoka aliishia kupokea kipigo kikali mpaka wakina Paskali wakaingilia kuwaamua.



    “Na utoke humu ndani malaya wewe..!” Aliishia kusema sentensi hiyo na asiweze kuendelea kuongea tena. Akabaki akitweta kwa hasira akiwa mikononi mwa Paskali. Rommy alipoona Siwema bado yupo chini akilia kwa uchungu. Akapaza sauti kumuita mlinzi wa getini ambae alifika kwa kasi eneo lile mithili swala aliekutana na simba macho kwa macho.



    “Sikiliza we ‘Get Man’. Toa hii taka taka nje. Ukishindwa kuitoa hakikisha na wewe unatoka. Harakaaaaa!” Akafoka namna hiyo mpaka mlinzi wa watu akatetemeka kwa hofu. Hima hima akamyanyua Siwema pale chini na kuanza kumkokota kumtoa nje huku akiburuza na begi lake. Ghafla tu, Siwema alijitoa mikononi mwa mlinzi na kumgeukia Rommy.



    “Asante sana Rommy kwa hiki ulichonifanyia. Haki ya mama na shahidi mizimu ya kwetu, lazima yakukute makuu wewe. Na kwa vile nimedhulumiwa na kwa mujibu wa dini yangu, dua ya mwenye kudhulumiwa haina pazia. Basi naamini Mungu wangu atajibu haya” Siwema aliongea kwa ujasiri kisha akampangua mkono mlinzi. Akavuta begi lake na kutoka nje mwenyewe bila ya kushurutishwa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nenda huko malaya mbovu wewe, sitishiwi na mizimu mimi wala huyo mungu wako unaemuabudu. Mjinga wewe na ukoo wenu wote” Rommy alibweka namna hiyo huku na yeye akijitoa mikononi mwa Paskali.



    “Kwani kaka mkubwa tatizo nini?” Paskali alihoji.



    “Mjinga tu yule anajaribu kunizushia mimba mimi. Amefeli sana!” Rommy aliongea hayo kisha akapotelea chumbani kwake. Wote waliokuwa eneo hilo walistaajabu. Ni vipi Siwema awe na mimba halafu inajulikana dhahiri kwamba Rommy alikuwa akifanya nae mapenzi halafu leo hii eti akatae mimba si yake ilhali Siwema alikuwa ni mtu wa ndani tangu aanze kazi hapo? Ajabu hii!.



    Yakiwa ni majira ya mchana ndani ya siku hii mpya. Siku ya Alhamisi saa saba kasoro mchana. Jeni aliingia nyumbani kwa kina Ramah. Alimkuta Mama Ramah akiwa dukani kwake akiendelea na shuhuli zake. Akasimama kumsalimu na Mama Ramah akaipokea salamu hiyo kwa bashasha zote. Kisha hapo akakiendea chumba cha kina Ramah.



    Taratibu alifungua mlango wa chumba hicho. Hakutaka kubisha hodi maana alisikia sauti ya muziki wa gitaa ikisikika ndani humo. Tabasamu zito likajiunda usoni mwake baada ya kumshuhudia Ramah akiwa anacheza na kifaa hicho. Taratibu kabisa alikuwa akicharaza nyuzi za kifaa kile. Japo hakuwa akiimba wimbo wowote lakini alionekana akiwa katika hisia kali.



    Jeni alitulia kimya akimtazama Ramah ambae hakuwa bado amemuona. Dakika tatu mbele baada ya kusikiliza sauti tamu inayotoka kwenye kifaa kile. Jeni alipiga makofi ya hongera ambayo yalimgutusha Ramah alieacha kupiga gitaa na kugeuka kule alipo Jeni. Ramah alipomuona Jeni alitabasamu kisha akatoa ishara ya kumkaribisha. Jeni akaenda kukaa kitandani kisha akamtaka Ramah aendelee.



    Ramah bila ajizi, huku akitabasamu alianza kuvuta nyuzi taratibu na ala tamu ya muziki ikasikika. Jeni akazidisha tabasamu huku akimtazama kijana huyo anavyocharaza gitaa. Baada ya kucheza na kifaa kile kwa zaidi ya dakika moja. Hisia zilipomkolea akaonekana dhahiri ni mwenye kutaka kuimba ila sauti ilimsaliti. Hisia zilizomjaa mtimani mwake zilijionyesha dhahiri kwenye macho yake kwa kutoa machozi.



    Alimtazama kwa huruma huku moyo wake ukiingiwa na ubaridi wa hisia. Akampa ishara ya kuacha kupiga gitaa na Ramah akaacha. Akamtazama Jeni usoni huku machozi yakiwa bado yanamtoka. Jeni akajivuta mbele kumkaribia kisha akapeleka viganja vyake kwenye mashavu ya Ramah. Akafuta machozi yaliyokuwa yakimtoka kisha akamtazama akiwa anatabasamu. Ramah nae akatabasamu.



    “Heshima ya mwanadamu ni kukubali kukosolewa na kufuta machozi kwa yale ya nyuma yaliyomuumiza. moyo wa jasiri hukubali kushauriwa na kufuata yale ya busara aliyosemezwa. Isingelikuwa vyema kutoa machozi kila mara huku ukiusulubu moyo wako kwa kumbukumbu za kuumiza zilizopita. Usidhihirishe maumivu yako mbele ya kadamnasi kwasababu utayaweka wazi madhaifu yako na kukupunguzia heshima kwa wanaokuheshimu. Sitegemei kuona tena machozi kwenye mboni zako zaidi ya furaha na matumaini mapya ya kihisia. Rafael we ni wakipekee sana na mwenye thamani ya juu kwenye mioyo ya watu wanaokuzunguka. Hupaswi kuwa mnyonge namna hii jamii itakutafsiri tofauti.”



    Jeni aliongea kwa hisia akiwa ameikamata mikono ya Ramah huku akimtazama usoni bila kupepesa macho. Ramah alitabasamu baada ya kuyahisi vyema maneno hayo ndani ya moyo wake. Alionekana kutaka kusema kitu ila kinywa kikamsaliti kwa hilo. Akabaki kugugumia kama bubu ndani kwa ndani huku alichotaka kusema akikidhihirisha kwenye mboni za macho yake. Alikuwa akitaka kushukuru. Kumshukuru Jeni kwa hayo anayomfanyia ila ndio hivyo sauti ilikaa mbali nae.



    Jeni alitabasamu huku akitingisha kichwa ishara ya kwamba amemuelewa vyema. Akamuambia kuwa anaenda kuongea na Mama mara moja atarejea tena punde tu. Ramah akatingisha kichwa kukubali. Jeni aliinuka na kuuendea mlango. Lakini aligeuka nyuma aliposikia sauti ya Ramah ikisema.



    “Asante.... Jenifa..” Ramah alitamka hayo kisha akatabasamu. Jeni akataka kurudi lakini akakumbuka kwamba mtu huyo hubahatisha maneno na hapo anaweza asiongee tena. Akatabasamu na yeye kisha akatoka nje. Alimkuta Mama Ramah akiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho ya chakula. Akamsaidia vya kumsaidia kisha akaingia na chakula kule alipo Ramah.



    “Mpendwa nimeleta chakula. Leo kuna zoezi moja nataka tulifanye. Kila siku mimi ndio nakulisha wewe. Sasa leo nataka tulishane” Jeni aliongea hayo huku akiweka chakula kile mezani. Ramah akatabasamu kisha akatingisha kichwa kukubali.



    Jeni akamnawisha mkono Ramah kisha na yeye akanawa. Akakaa kitandani kumuelekea Ramah kisha akamuambia yeye ndio aanze kwasababu kila siku huwa ni yeye ndio anaemuanza. Ramah huku akitabasamu, akamega tonge dogo la ugali na kulifinyanga vyema, kisha akalichomvya kwenye mboga na kumpelekea Jeni kinywani. Jeni akalipokea vyema lile tonge kinywani mwake kisha akacheka huku kinywa chake akikifumba kwa viganja vyake.







    Ramah yeye alikuwa akitabasamu tu mpaka pale Jeni alipoacha kucheka. Akataka kumlisha tena lakini Jeni akakataa na kumuambia kwamba ni zamu yake kumlisha. Jeni nae akamega tonge na kulichomvya kwenye mboga, huku akitabasamu, tabasamu lililoelekea kucheka, akamlisha Ramah. Waliendelea na zoezi hilo mpaka pale walipotosheka. Jeni akatoa vyombo na nje baada ya kuhakikisha meza ameisafisha vyema.



    Kule nje aliwaona Jay na Mama yake Sebuleni wakiwa wanakula. Akawaendea kule kule na kuchukua nafasi kwenye sofa. “Niliona nisikusumbue mama, nikaacha ule na rafiki yako kule” Mama Jay alisema.



    “Hakuna shida mama, maana hata yeye hupenda tule sote” Jeni nae akajibu.



    Kisha Jeni akawaeleza kwamba, amefanikiwa kumpata mwana saikolojia na tayari wameshaongea kila kitu. Imebaki wao tu kumpeleka mgonjwa wao huko. Mama Jay akashukuru kwa juhudi za Jeni kuhakikisha mwanae anapona. Kisha akamuuliza kuhusu gharama na Jeni akamjibu asiwe na shaka kuhusu swala hilo. Ilimradi mgonjwa wao apone ndio jambo la kushukuru.



    “Tena Mama kama ikiwezekana tumpeleke leo ili matibabu yaanze haraka. Hata hivyo hatochukua muda mwingi kwasababu hali yake sio sawa na mwanzo” Jeni akashauri. Wote wakamuunga mkono na ikaonelewa waanze michakato hiyo punde tu watakapo maliza kula.



    Nusu saa mbele walikuwa wakitoka nyumbani hapo kuelekea huko walipopanga kwenda. Muda huo Ramah hakuwa amejulishwa ni wapi anapelekwa. Wakatafuta usafiri utakao wafikisha huko na walipoupata wakazama ndani yake. Mama yao alionelea yeye abaki, hata hivyo alikuwa na biashara yake na hakuwa na wakuamuachia. Jay, Ramah pamoja na Jeni walielekea huko.



    Walipofika walishuka kwenye gari lililokuwa limewapeleka mahala hapo na kuzama ndani ya jengo hilo. Ramah alishangazwa na mambo hayo maana yeye hakujua ni wapi hasa anapelekwa na wanakwenda kufanya nini huko. Kinywa chake kilitetemeka ishara ya kwamba alikuwa anataka kusema kitu. Hata hivyo hakuna aliemuona kwasababu kila mmoja alikuwa akitazama mbele wanapoelekea.



    “Tuna...tunaenda wapi?” Ramah alipoipata sauti yake aliwauliza. Jeni hakuwa na budi kumjuza ili asijihisi mnyonge atakapofika kwa mtaalamu huyo. Akamuambia kila kitu walichopanga na Ramah hakubisha. Moja kwa moja wakazama ndani ya jengo hilo.



    Jeni hakupata tabu sana kujitambulisha kwa ‘secretary’ kwasababu siku iliyopita alifika hapo na kujitambulisha na alieleza shida yake. Hata leo hii alipofika mwanadada yule aliekuwa mapokezi alimkaribisha kwa bashasha tele. Jeni akamuulizia mtu waliemfuata na mwanadada yule akamjibu kuwa wasubiri kidogo kuna mgeni ofisini. Wakakaa kwenye benchi lililokuwa eneo hilo wakisubiri mtu atoke waingie wao.



    Hata hivyo hawakukaa sana kabla ya mwana mama mmoja kutoka katika ofisi ya mwanasaikolojia. Mwanadada wa mapokezi akawapa ruhusu ya kuingia na wao wakanyanyuka pale na kuzama ndani.

    Huko walimkuta mwanaume mtu mzima anaeukaribisha uzee kwenye umri wake. Mwanaume yule alipowaona aliachia tabasamu huku akiivua miwani yake ya macho kisha akawatazama wote na kugandisha macho yake kwa Ramah kwa kitambo kifupi kabla hajawakaribisha kwenye viti.



    “Karibuni. Karibuni vijana, kaeni kwenye viti hapo” Wakakaa baada ya mtu yule kuwakaribisha.



    “Dokta Hamimu tumekuja kama jana nilivyokueleza. Mgonjwa mwenyewe ni huyu hapa kaka angu” Dokta Hamimu akamtazama tena Ramah kisha akatabasamu.



    “Anaonekana tu kwa kumtazama haraka haraka...” Akawatazama Jay na Jeni kisha akasema. “Ningeomba mtupishe kidogo mimi na mgonjwa wangu tunataka kujuana kabla ya mambo mengine kufuatia” Hawakupinga lolote badala yake wakatoka nje. Dokta Hamimu akamgeukia Ramah na kumtazama kwa muda. Kisha akasema.



    “Habari yako kijana?” Ramah akagugumia kinywani mwake akitaka kujibu. Ilimchukua sekunde kadhaa mpaka kujibu salamu hiyo. Hapo Dokta akagundua tatizo jengine kwa Ramah.



    “Unaonekana mtanashati, mtu unaejipenda sana. Hivi unaitwa nani kwanza?” Ramah akataja jina lake.



    “Oooh! Rafael, karibu sana. Mimi niite Dokta Hamimu mkazi wa mji huu. Kwenu mmezaliwa wangapi?” Dokta alijitambulisha na yeye kisha akamuuliza. Ramah akajibu wawili. Alikuwa akijibu kwa sauti japo ilimpa shida kidogo.



    Dokta Hamimu alimuuliza maswali mengi ikiwemo majina ya ndugu zake na majina ya wazazi wake. Akamuuliza umri wake na anapoishi. Ramah yote hayo akayajibu vyema. Akamuuliza kuhusu chakula anachopendelea na kwenye swali hilo Ramah alitabasamu kisha pia akamjibu. Dokta Hamimu akamuomba radhi Ramah na kumuambia amsubiri dakika kadhaa atarejea tena. Kisha akatoka nje akimuacha Ramah akipata muda mzuri wa kukishangaa chumba hicho.



    Alipotoka nje akawataka wakina Jay wamfuate. Wakaongozana wote mpaka nje ya jengo hilo na kuweka kambi mahali fulani.



    “Nimekaa na mgonjwa dakika chache tu lakini kuna vitu nimevigundua kutoka kwake. Kwanza nimeipima akili yake kwa kumtazama tu kama atakuwa na uwezo wa kukumbuka lakini nikaona kumbukumbu zake zipo vyema kabisa hazina tatizo. Ila tu akili yake haipo sawa na inahitajika akae mbali na yale mazingira aliyoyazoea kwa muda mfupi kiasi huku akiendelea na matibabu mengine...” Dokta akameza mate kabla hajaendelea kuongea. “ Kwasababu gani anatakiwa akae mbali na mazingira aliyoyazoea. Sababu ni kwamba ili asiweze kukumbuka yale yaliyomfanya kuwa katika hali ile. Kwasababu kama atakuona wewe( akimaanisha Jeni) atakumbuka yale yaliyomtokea. Au hata Mama yake, marafiki zake, ndugu zake na yoyote yule aliezoea kumuona kumbukumbu ya yale yaliyomkuta haitoondoka. Lakini kama akiwa mbali na watu aliowazoea na kwenda kukutana na watu wapya, mazingira mapya basi hapo akili yake itakuwa ikiwaza haya mazingira mapya kuliko yale aliyotoka....”



    Dokta aliwaeleza mengi yanayotakiwa yafanyike ili hali ya Ramah itengemae. Wakakubaliana nae na wote wakarudi tena ofisini kwa Dokta walipomuacha Ramah. Huko Dokta Hamimu akamueleza Ramah kuwa anatakiwa abaki nae kwa muda fulani kabla ya kurudi nyumbani kwao. Ramah hakuwa na uwezo wa kupinga kwasababu hata yeye hali aliyokuwa nayo haikumpendezea hata kidogo.



    Hapo Dokta aliwapa ruhusu wakina Jay na wao wakashukuru kisha wakainuka kwaajili ya kwenda wakimuacha Ramah mahala hapo. Jeni alimtazama Ramah akiwa anatabasamu kisha akamkonyeza. Ramah nae akatabasamu, Jeni alimfuata pale alipo na kumpiga busu la kwenye paji la uso kisha akamuonyeshea dole gumba. Tabasamu la Ramah likaongezeka uzito. Kisha watu wale wakatoka nje kwaajili ya kurudi nyumbani.



    Upande huu wakiwa wanahangaika Ramah apate matibabu arejee kwenye hali yake ya kawaida. Upande mwengine wapenzi wawili walikuwa wakifurahi kwenye nyumba ya kifahari. Muda huo walikuwa wao wenyewe chumbani wakipiga soga kuhusu mapenzi yao ambayo hayakuwa hata mwezi yamefikisha tangu warejeane.



    Zikutanapo jinsia mbili sehemu ya faragha shetani huwa wa tatu akiwa na kazi moja tu ya kuwashawishi wafenye yale yasompendeza Mungu ikiwa si wanandoa. Rommy alikuwa katika kuunda maneno ya ushawishi ili aiteke akili ya Cecy wafanye ngono.



    “Sasa mpenzi. Kama unanikatalia hivi kila siku mi nitaamini vipi kama unanipenda? Au unataka unikute ule msemo unaosema kwamba nitakula kwa macho? Sio kihivyo bwana, mi nakupenda embu na wewe nithibitishie kama unanipenda basi” Rommy alinung'unika huku Cecy akitabasamu.



    “Hapana Rommy sio kama unavyofikiri. Ni leo tu sijisikii vyema lakini si kwamba ati nakukatalia”



    “Nimeshagundua kitu....” Rommy alibadilika ghafla. “..naomba utoke humu ndani maana hunipendi wewe. Na kama ungekuwa unanipenda wala usingejaribu kufanya hivyo. Nenda na tusijuane siwezi kuishi na mtu asie na faida kwangu”



    Rommy alisema hayo katika hali ya kukasirika. Cecy aliingiwa na fadhaa! Akawa mnyonge ghafla tu. Lakini kwanini nakuwa mgumu kufanya mapenzi na Rommy? Akajiuliza mwenyewe. Hata hivyo unadhani Cecy ni mjinga kiasi gani ati aachane na Rommy kisa tu kufanya mapenzi? Akakubali!.



    Meno ya Rommy yalionekana kwa furaha baada ya kukubaliwa ombi lake. Na kwa vile Cecy amekubali kwa moyo mmoja kumkabidhi mwili wake Rommy. Hakuweza kukataa hata pale Rommy alipoanzisha mbwembwe zake kutalii mwili wake. Walilegezana mpaka pale walipohisi miili yao ikiwa na joto la kufanya kitendo hicho. Wakafanya!.



    “Sasa sijui ni kipi ulichokuwa unakiringia. Mbwembwe zote zile za kunibania nikadhani basi labda utakuwa tofauti na wenzako kumbe ndio kama wale wale tu” Maneno hayo yalimtoka Rommy baada ya kuwa wameshamaliza kufanya kile walichokuwa wakikifanya. Kisha hapo Rommy akajitoa kitandani na kukifuata choo ambacho kilikuwa humo humo. Huku nyuma Cecy aliumia baada ya kuhisi amekejeliwa na kijana huyo.







    Ndio alikejeliwa na hata mwenyewe alilitambua hilo na ndio maana maneno yale yakamchoma. Akabaki kuyafikiria maneno yale kama iwapo yalisemwa na Rommy katika hali ya hasira ama ndio kama alivyohisi.



    Rommy alitoka chooni huku akijifuta maji na taulo. Muda huo Cecy alikuwa akimuangalia tu na asijue aongee nini juu ya kijana huyo. Rommy aliiendea meza ndogo iliyo na vitu vyake vidogo vidogo iliyokaribu na kabati.



    “Vipi wewe? Huendi kuoga tuondoke?” Rommy alimuuliza hayo bila ya kumtazama zaidi akiendelea na kufanya mambo yake.

    Haaa! Mara hii tu baada ya kumaliza mchezo ananitaka niondoke? Cecy alijiuliza hayo huku akimtazama Rommy ambae wala hakuwa na shuhuli nae, zaidi yeye aliendelea na kuupaka mwili wake mafuta kabla ya kuvaa nguo.



    “Ama utaenda hivyo hivyo ukiwa hujaoga?” Rommy alimuuliza hivyo baada ya kugeuka kule kitandani alipokuwa Cecy. Cecy hakujibu kitu alionyesha kukasirishwa na wala Rommy hakujali lolote zaidi ya kuendelea na mambo yake.



    Sasa ni vipi amnunie mtu ambae wala hakuwa akimjali? Akajitoa kitandani kwa kisirani na kuingia chooni huku nyuma Rommy akiwa anatabasamu. Dakika tano Cecy akatoka akiwa tayari ameshaoga. Akaziendea nguo zake na kuzivaa akiwa mdomo wake ameuvuta kwa kisirani. Muda huo Rommy alikuwa akicheza na Laptop yake na wala hakuonyesha kumjali Cecy.



    “Nipeleke nyumbani” Cecy aliongea kwa kisirani na Rommy aliinua shingo kumtazama. Kisha akamuuliza kwa kejeli kwamba ameshamaliza kuvaa nguo zake ilhali alimuona kabisa akiwa ameshavaa. Cecy hakujibu kitu zaidi alifungua mlango na kutoka nje. Rommy aliifunga laptop yake ambayo ilikuwa imezima na pale alifanya kama geresha tu. Akatoka nje kule alipoelekea Cecy. Sebuleni alimuambia Paskali amrushie funguo ya gari na Paskali akafanya hivyo, kisha Rommy akatoka nje.



    Akaliendea moja ya gari na kuzama ndani yake, Cecy nae akaenda mahala pale na kuingia ndani ya lile gari lakini hakukaa nafasi ya mbele badala yake alikaa nyuma. Rommy hakujali!. Taratibu alilitoa gari ndani humo baada ya geti kufunguliwa. Kisha akashika uelekeo wa nyumbani kwa kina Cecy.



    Hata pale walipofika Rommy alisimamisha gari na kutulia kimya. Muda wote Cecy alitegemea labda Rommy atamuomba msamaha kwa yale aliyomfanyia. Lakini ikawa sivyo. Rommy hakuongea kitu zaidi ya kukaa kimya tu kama ambae anasubiri Cecy aongee kitu ili ajibu.

    Cecy akaongea!.



    “Rommy ndio unafanya nini hivi?” Cecy alimuuliza.



    “Kufanya nini kivipi?” Cecy akamtazama Rommy aliekuwa akimtazama yeye kupitia kioo kilichokuwa juu mbele yake. Akataka kuongea kitu ila akawahiwa na Rommy.



    “Samahani Cecy. Ningefurahishwa zaidi kama ungeshuka kwenye gari maana nataka kuwahi nyumbani....”akageuka kule alipo. “si unajua leo nimekuja pekeangu?” Akamalizia. Cecy alimtazama kisha akashuka kwa kisirani na kuubamiza mlango wa gari kwa nguvu mpaka Rommy akashtuka. Kisha akacheka na kuondoa gari mahala hapo.



    Dakika kadhaa akawa amefika, akapaki gari sehemu alipolitoa na kushuka ndani yake. Akauendea mlango na kuufungua kwa pupa kiasi ambacho aliwashtua wakina Paskali waliokuwa sebuleni.



    “Demu mwenyewe hovyo tu haki ya mungu, bora ya Siwema alikuwa akijiweza. Kashaniisha hamu huyu” Rommy aliongea hayo baada ya kuingia ndani.



    “Unataka kutuambia huyu mtoto hakuwa akijiweza kwa lolote?” Zuma alimuuliza.



    “Hamuwezi amini ila ukweli ndio huo. Nimepiga kimoja tu najionea kero. Nikaona bora nimkatae tu” Kicheko kikali kikawatoka wakina Paskali.



    “Hata kama angekuwa mtamu kiasi gani ningemkataa tu vile vile kwasababu sina siku nyingi narudi Nairobi. Sasa mnadhani ningeondoka nae?....” Wakina Paskali wakakubali kwamba angeondoka nae kwasababu walimsifia alikuaa ni mzuri. “Wapii! Huko nimeacha watoto wakisomali wakali zaidi. Sa ndo nije kubabaika na kitoto hichi ambacho hakijiwezi kitandani? Si bora ningepiga masturbate nikajua moja...” Wakacheka tena kiasi ambacho Zuma glasi ya shurubati aliyoishika mkononi mwake ilimponyoka na kupasuka sakafuni. “Wacha nikawasiliane na mzee nimjuze kwamba siku si nyingi nitarejea nyumbani” Rommy aliongea kisha akaingia chumbani kwake.



    ********



    Huo ndio ukawa mwanzo wa manyanyaso ya Cecy kwa Rommy. Siku ile waliyoachana pasi na maelewano mazuri Cecy hakuwa na raha kabisa. Hata pale alipojaribu kumtafuta yeye Rommy kwa njia ya simu baada ya kuona ni muda mrefu umepita bila ya Rommy kumtafuta. Rommy alimjibu vile alivyojisikia yeye. Hakuwa ni mwenye maneno mazuri kama ilivyokuwa siku za nyuma. Hakuwa akibembelezwa tena kama ilivyokuwa siku za nyuma.



    Mambo yote yalibadilika tena kwa ghafla sana. Tena sana zaidi ya sana tofauti na vile ifikiriwavyo. Alishatamkiwa mara nyingi na Rommy kwamba hakuwa akitakiwa lakini yeye aling'ang'ania mpaka kufikia hatua ya kuomba msamaha bila ya kujua ni wapi alipokosea. Ndio, alikuwa na haki ya kubembeleza na kung'ang'ania kwasababu alihisi haya moyoni mwake. Yale aliyokuwa akiambiwa kuhusu mtu huyo na kuwaona watu ni wabaya mpaka kufikia hatua ya kugombana nao. Leo hii alikuwa akiyaamini.



    Wahenga walisema, mwana kulitaka, mwana kulipewa!. Kwani hakuwa akikumbuka yale aliyofanyiwa na kijana huyo miaka ya nyuma? Sasa yale yale yaliyomkuta kipindi cha nyuma ndio hayo hayo yanayomkuta tena kipindi cha sasa. Tena akiwa mtu ni yule yule aliemtesa na kumdhalilisha mbele za watu bila kujali lolote.



    Baada ya kuchoka usumbufu wa Cecy. Rommy siku moja alimuambia afike mahala fulani ambapo yeye alikuwapo. Cecy akiwa na kiroho cha mashaka yaliyochanganyikana na furaha. Maana alihisi ni bahati kuonana na kijana huyo baada kumuomba jambo hilo muda mwingi lakini Rommy alikuwa akimkatalia kwa kisingizio cha kuwa hakuwa na muda wa kuonana nae. Sasa ni vipi siku hiyo aambiwe na kijana huyo afike mahala fulani kwaajili ya kuonana na yeye akatae? Akatoka hai hai mpaka huko alipoitwa.



    Yalikuwa ni maeneo ya shule ya sekondari Mkwakwani. Cecy alifika maeneo hayo na kuliona kwa mbali gari alilokuwa akitemba nalo Rommy likiwa limeegeshwa mahala hapo. Kabla hajaamua nini cha kufanya simu yake ikaingia ujumbe kutoka kwa Rommy aliemtaka aingie ndani ya gari hilo. Kwa mwendo wa haraka alilifuata na kufungua mlango wa nyuma kisha akazama ndani.



    Huko aliwakuta Paskali aliekuwa amekaa siti ya dereva huku Rommy akiwa nyuma siti za pili. Akawasalimu na wote wakaitikia salamu yake. Rommy alimtazama binti huyo kisha akamuambia anampenda. Cecy akatabasamu moyo wake ukiingiwa na ubaridi wa furaha. Na yeye akajibu kwamba anampenda pia.



    “Siamini kama unanipenda mpaka unitimizie jambo moja ndio nitaamini hayo. Na nitakuwa radhi nisirudi chuo niishi na wewe huku kama mume na mke” Rommy aliongea hayo akiwa makini akimaanisha kile alichoongea. Cecy moyo ukamlipuka kwa hofu. Hakujua ni jambo gani hilo akilitimiza Rommy atafanya yote hayo kama alivyoahidi. Akajiapisha kukubali hata kama likiwa ni jambo baya ama gumu kulitekeleza. Akamuuliza ni jambo gani hilo. Rommy akatulia kisha akamtazama Paskali aliekuwa kimya akitazama mbele utafikiri hakuwa akisikia hayo yaliyokuwa yakiongelewa.



    “Nataka tufanye mapenzi....” akamtazama uskoni kusisitiza kile alichoongea. “humu humu garini..” Cecy akashtuka huku akimtazama Rommy kwa mshangao. Mapenzi garini? Akajiuliza. Hata hivyo hakuona tabu yoyote. Lakini iwapo Paskali atawapisha. “Tunafanya mapenzi humu humu ikiwa Broo Paskali akiwapo. Lakini hata hivyo hatoshuhudia chochote kwasababu yeye atakuwa ameangalia mbele. Usihofu kwa hilo”



    Rommy aliongea hayo utafikiri ni jambo rahisi kufanyika. Cecy alishangazwa na Rommy si mas'hara. Akapinga jambo hilo huku akidai hatoweza kufanya hivyo. Maana kwake yeye kufanya hayo ni sawa na kujidhalilisha. Rommy alimtazama usoni kwa muda kisha akamfungulia mlango alioingilia nao ishara ya kwamba atoke nje ya gari.



    “Kama mtihani huu mdogo niliokupa umeishindwa, basi ni dhahiri hata nikiwa na wewe unaweza ukaja kuniacha huko mbele endapo nitapatwa na jambo kubwa. Tafadhali, toka nje na uwende zako na kuanzia sasa usinijue tena”



    “Lakini Rommy mimi nimekubali, ila sio kiivyo. Mi nipo tayari lakini....”



    “Tafadhali Cecy. Naomba ushuke kwenye gari iwapo umeshindwa jambo hili” Rommy mara hii aliongea huku akiwa amekaza sura kumaanisha anachoongea. Cecy akawa mpole kama mwizi alieshikiwa panga.



    “Basi nisamehe. Nimekubali!” Cecy aliongea kinyonge. Rommy akatabasamu kisha akaufunga ule mlango.



    Moyo upendapo mwili huumia. Hii ilikuwa kwa Cecy pia aliekubali kuudhalilisha mwili wake ili aufurahishe moyo wake. Alichokubali alidhamiria kweli. Akiwa na aibu nyingi usoni kwake, Rommy alimvuta karibu yake. Wakanyonyana mate mithili ya njiwa na mwana wake amlishapo chakula. Kisha hapo Rommy akamlaza Cecy kwenye siti na yeye akafuatia juu yake.

    Assalalee!.



    Kilichofanyika hapo hakikuwa kitendo cha kiungwana hata kidogo. Inamaana Cecy amekubali kuudhalilisha mwili wake kisa tu amependa? Sasa anauhakika gani kama na yeye alipendwa kama apendavyo yeye? Ama kipimo kilikuwa ni hicho kufanya ngono garini! Tena kukiwa na vijana wawili ndani yake. Ilihitaji ujasiri kwa mwenye moyo wa kike!.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kitendo kile kilichukua dakika nne tu kabla ya Rommy kujitoa maungoni mwa Cecy. Akapandisha suruali yake Cecy na yeye akaziweka vyema nguo zake. Katika mchezo ule hakukuwa na yeyote aliefika kishindo ila tu Rommy alijitoa kwa Cecy na sababu isijulikane. Alimtazama Cecy aliekuwa na soni nyingi usoni mwake kisha akasikitika Rommy.







    “Ikiwa mwili wako mwenyewe umeshindwa kuuthamini mpaka kufikia hatua ya kufanya ngono garini. Na si garini tu pekee, pia kukiwa na mtu mwengine asiehusika na kitendo hicho, unadhani ni nani mwengine atakaeuthamini mwili wako? Haki leo ndo na uthibitisha ule usemi usemao kwamba wanawake wengi hamna akili na wewe ndio kiongozi wao pasi na shaka. Muone kwanza alivyotahayari! Unadhani kunipa mwili wako garini ndio kutaongeza mapenzi kwenye moyo wangu? Kwanza sikumbuki kama nilishawahi kupenda tangu mama yangu afariki dunia. Malaya wote niliowahi kuwa nao hakika wewe umewazidi umalaya kwa hiki kitendo ulichokifanya leo. Sikuwahi kupenda Cecy na wala usidhanie labda kama nilikuwa nikikupenda! Na hata kama ningekuwa nimewahi kupenda wala nisingekupenda wewe ambae wala huna utu kwenye kupenda. Taarifa zako nimezipata, umemsaliti ndugu yangu kwaajili yangu. Ukamdhalilisha mbele za watu na wala hukujali lolote ilimradi ukidhi matakwa ya moyo wako. Sijui yu hali gani Rafael ila nimesikia yu mgonjwa sana na chanzo ni wewe. Hata nashindwa kwenda kumtazama kwa haya iliyonivaa usoni kwasababu wote watakuwa wakiamini mimi ndio chanzo cha matatizo yote. Dah! Maskini Ramah nisamehe mimi sikuwa najua chochote kuhusiana na haya mpaka kuwa katika hali hiyo uliyokuwa nayo...” Akamzatazama Cecy huku machozi yakimtoka Rommy. “Cecy nilipanga nikudhalilishe kama wewe ulivyomdhalilisha ndugu yangu. Lakini sikuona sawa kukudhalilisha mbele za watu kama ilivyokuwa kipindi kile tunasoma. Lakini nilipanga nikudhalilishe kama hivi sasa. Na kuanzia sasa naomba usinijue na utoke humu ndani kabla sijakufanya kitu kibaya”



    Rommy alimaanisha alichoongea. Cecy akiwa hajui afanye nini, maneno hayo yakiwa yamemuingia vyema kabisa akilini mwake. Alishtukia mlango ukifunguliwa na yeye kusukumizwa na nje. Kisha pale pale gari ikawasha na kuondolewa mahala hapo. Vile vile alivyokuwa Ramah kule mgahawani wakati anamdhalilisha, leo hii imekuwa na kwake.



    Kitendo kile kilipata kushuhudiwa na wanafunzi wa shule hiyo lakini hawakuwa ni wenye kujua lolote. Wakabaki vinywa wazi huku wakimtizama Cecy aliekuwa chini muda huo akijizoazoa kuinuka huku akilia. Hata pale aliposimama wima hakuweza kuiacha sura yake wazi, alijiziba na kitambara chake huku akielekea barabara kubwa kutafuta usafiri utakaomfikisha kwao.



    Hata pale alipofika kwao, alipitiliza mpaka chumbani kwake katika mtindo ule ule wa kujiziba sura yake kitendo ambacho kilimshangaza mama yake na kuamua kumfuata kule kule akajue nini kimemkuta mwanae. Aligonga mlango sana huku akiita jina la mwanae lakini Cecy hakuweza kufungua mlango ni kilio tu ndio kilisikika ndani humo. Anita alihisi kuchanganyikiwa kwa jinsi mwanae alivyokuwa. Hakujua ni kipi kimemkuta mwanae, sasa ni vipi awe katika hali ya kawaida?



    “Cecy una tatizo gani lakini....? Nieleze mimi Mama yako nitakusaidia lakini sio kulia mwenyewe kama hivyo mwanangu” Anita aliongea hayo akiwa nje ya mlango, hiyo ni baada ya kugonga sana mlango wa chumba cha Cecy na wala usifunguliwe.



    Ikiwa imepita wiki moja na siku zake. Majira hayo hayo ya mchana ambayo Cecy alikuwa akiugulia maumivu ya kudhalilishwa na kutukanwa palipo pakubwa. Ilionekana tax ikipaki nje ya wigo wa nyumba ya kina Ramah. Kisha hapo mlango wa siti za abiria ukafunguliwa na Jeni akatoka ndani yake. Akazunguka upande wa pili na kuufungua mlango. Ramah aliekuwa katika tabasamu pana usoni mwake alieonekana kushuka garini humo.



    Tax ile ikaondoka na watu wale wakapata kuonekana vyema. Mama yake na Ramah aliekuwa ndani ya duka lake alipata kuwashuhudia watu wale. Butwaa lilimpata huku akiwa ameganda mahala humo akiwatolea macho ya mshangao. Mbio mbio alitoka na kwenda kumkumbatia mwanae kwa furaha na wote machozi yakawatoka ilhali Jeni akiwa kwenye tabasamu.



    Ilikuwa ni furaha kwa mtu na mwanae hasa kwa Dorine ambae alikuwa halali vyema akikesha kumuombe dua mwanae arudi katika hali yake ya kawaida. Walitoka mahala pale mpaka kwenye sebule ya nyumba hiyo wakaweka makazi mahala hapo. Dorine alimuuliza Ramah kuhusu hali yake na Ramah akajibu yu salama na anamshukuru Mungu wake. Dorine hakuwa akiamini kwamba Ramah huyu ndio yule ambae masiku kadhaa nyuma kuongea kwake ilikuwa shida. Kula kwake ilikuwa mpaka abembelezwe lakini leo hii alikuwa salama kama alivyomtoa kwenye tumbo lake.



    Kwakuwa ilikuwa ni majira ya mchana na palihitajika chakula muda huo. Mama Ramah akawaambia wamsubiri akaandae chakula mara moja. Akatoka na kuwaacha watu hao wenyewe. Ramah alichukua nafasi hiyo kumshukuru sana Jeni na yeye alizipokea shukurani hizo kwa mikono miwili. Kisha hapo Jeni akasema anaenda kumsaidia mama kuandaa chakula, kisha akainuka kwaajili ya kutoka nje.



    “Jenifa...” Ramah alimuita na Jeni akageuka kule alipo. Ramah akainuka pale alipokaa na kumsogelea pale alipo Jeni. Sekunde kadhaa akawa anamtazama Jeni usoni jambo ambalo mnyange huyo alishindwa kuvumilia na kutazama chini kwa haya.



    “Nakupenda Jeni, tafadhali naomba uzipokee hisia zangu kama ulivyopokea shukurani kwa moyo mkunjufu” Ramah alitamka hayo akiwa makini akimtazama mnyange huyo usoni. Mapigo ya moyo wa Jeni yalienda hobwe hobwe baada ya kusikia kauli hiyo. Akabaki mdomo wazi na asijue azungumze nini? Akatae ama akubali?



    “Nimeijua thamani yako kwangu baada ya kunikuta yale yaliyonikuta. Hukutaka kuniacha kama alivyoniacha yule haini. Ulikuwa mfariji wangu muda wote na hakika nakuthibitishia kukulipa upendo wa dhati endapo ukikubali moyo wako useme na wangu ishara moja tu ya mapenzi. Tafadhali Jeni ruhusu hisia zangu ziseme na zako kwasababu tayari zimeshagonga hodi kwenye moyo wako. Narudia tena kukutamkia nakupenda itokayo moyoni na si mdomoni tu”



    Jeni hakuamini anachosikia kutoka kwa kijana huyo. Ramah unanipenda? Akapepesa macho kama mara tatu kisha akamkumbatia Ramah. Tabasamu mwanana likachanua usoni kwake kwa furaha.



    “Huna haja ya kunisisitizia namna hii kwamba unanipenda Ramah. Nimekubali kwa moyo mmoja na hata mimi nakuhakikishia kukupenda kama unipendavyo” Ramah akazidisha kumkumbatia mnyange huyo huku akimuahidi kutomuacha. Jeni alikuwa akitabasamu tu hakuwa na usemi wowote. Sasa aseme lipi wakati ameambiwa anapendwa? Hivi unadhani hakuna asiependa kupendwa? Hasa kwa yule ambae hisia zako zimeelekea juu ya yake?

    Hakuna!.

    Dakika moja wakaachiana kisha Jeni akaondoka mahala hapo akiwa na furaha moyoni mwake iliyojidhihirisha kwenye wajihi wake.



    * *



    Ikiwa ni siku nne zimepita baada ya Ramah na Jeni kuhamia katika sayari nyengine ya mapenzi kutoka katika dunia ya urafiki. Hali ya Cecy haikuwa sawa kwa kipindi hicho. Kutokana na msongo wa mawazo yaliyokataa kutoa makazi kwenye ubongo wake, ilipelekea kuumwa na kichwa. Hali hiyo mama yake hakuweza kuivumilia hata kidogo. Akalazimika kumpeleka Cecy hospitalini akapatiwe matibu japo Cecy alileta pingamizi kubwa.



    Wakiwa hospitalini wakisubiri majibu baada ya vipimo. Waliitwa kwenye ofisi ya Daktari aliemchukua vipimo Cecy na walipofika Dokta aliwataka wakae kwenye viti kwaajili ya kuwapatia majibu yao. Dokta yule aliinua makaratasi yaliyokuwa juu ya meza na kuanza kuyasoma moja moja utafikiri hakuwa ameyasoma kabla. Kisha akainua macho yake kumtazama Cecy kisha Anita.



    “Samahani dada. Huyu binti ni mwanao kabisa wa kumzaa?” Daktari alimuuliza Anita. Anita alimtazama Cecy na Cecy nae alimtazama Mama yake. Kisha Anita akarudisha macho kwa Dokta.



    “Ndio Dokta. Ni mwanangu. Mwanangu kabisa wakumzaa” Anita alijibu. Dokta akatingisha kichwa kuashiria ameelewa kisha akayainua tena yale makaratasi na kuyasoma upya.



    “Sawa. Mgonjwa wetu baada ya vipimo tumegundua ana Malaria kali ambayo inahitajika haraka apate dawa...” Akatulia na kuyatazama tena yale makaratasi kwa kitambo kifupi. Kisha akaendelea. “ Pamoja na kuwa na Malaria, pia tumepata ugonjwa mwengine ambao anao...” Akanyamaza tena na kuwatazama watu hao na kuwakuta wakiwa makini kumsikiliza. “Mgonjwa wetu ana upungufu wa kinga mwilini nikimaanisha analo gonjwa la UKIMWI. Hata hivy....” Dokta hakuweza kumalizia maneno yake kabla ya Cecy kuzimia kwa mshtuko. Haraka haraka akawaita manesi waje kutoa msaada wa kumpeleka Cecy wodini muda huo Anita akiwa hajiwezi kwa kilio.



    Majira ya saa mbili usiku Cecy alishtuka kutoka katika usingizi wa waliopoteza fahamu. Mama yake yupo pembeni yake akiwa analia tu. Hata baada ya kurudisha kumbukumbu zake vyema na kukumbuka kile kilichomsababisha kuwa mahala hapo. Aliungana na mama yake katika kilio. Daktari alifika mahala pale na kuwakuta mama na mwana wote wakiwa wanalia. Akakerekwa baada ya kuona wanaleta kero kwa wagonjwa wengine.



    Akamtaka Anita waongozane ofisini kwake na Anita akanyanyuka pale alipo na kumfuata Dokta. Akamuambia akae kwenye kiti baada ya yeye kukaa. Anita alikaa huku akifuta machozi na kanga yake.



    “Unajua dada watu wengi wanaliogopa hili gonjwa. Lakini hapo hapo hawachukui tahadhari yoyote ya kujilinda nalo. Na mwisho likiwapata basi hujiona hawana thamani tena ulimwenguni. Lakini hayo ni mawazo potofu tu kwasababu ule ni ugonjwa kama ugonjwa mwengine. Muhimu ni kuzingatia sheria za matibabu kwasababu hata Malaria inaua pale mgonjwa asipofuata sheria zake kama kutumia dawa kwa muda pangwa..... Aaaa! Sasa ni hivi. Binti yetu kwa sasa hayupo vyema, kwahiyo nitatoa ruhusa kwasababu hana tatizo lolote kubwa lililompata zaidi ya mshtuko tu na kwasasa hali yake ipo vyema. Kwahiyo baada ya kutoa ruhusa sasa hivi mtaondoka na baada ya siku mbili hakikisha unamrejesha hapa ili tumpe nasaha asije jihisi hana thamani tena duniani” Dokta alimueleza hayo. Anita alishukuru na kunyanyuka kwenye kiti kwenda kumchukua mwanae na kurudi nae nyumbani.







    ENDELEA...



    Haki ya ubongo ni kupata utulivu wa nafsi na moyo. Na mara zote nafsi isononekapo moyo hunung'unika huku akili ikikosa utulivu na kupeperusha maarifa. Kufikiri huwa finyu mithili ya punje ya mchanga na hufanya maamuzi ambayo yatashangaza wengi. Ni hiki ndicho kilichomtokea Cecilia binti wa Ally.



    Ni siku mbili sasa zimepita tangu apatiwe majibu ya kwamba ni muathirika wa gonjwa baya la Ukimwi. Siku zote hizo hakuwa na akili sawa sawa za kufikiri mambo. Alifanya mambo hata yale ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake ilimradi aifurahishe nafsi yake. Alishajaribu kumtafuta Rommy kutaka kumshukuru kwa kumpatia gonjwa hilo hatari lakini akakuta amefungiwa namba yake na kijana huyo. Sasa ni nani mwengine aliempatia gonjwa hilo kama si yeye?



    Akiwa chumbani kwake, akili zikiwa si zake, alihitaji huruma na msamaha kwa yale aliyoyafanya. Akachukua simu yake na kuibofya_bofya kisha akaiweka sikioni. Sekunde kadhaa akaishusha na kuibofya_bofya. Mara hii alichukua muda kidogo kufanya hivyo. Kisha alipomaliza akaiweka pembeni na kutulia vile vile alivyokuwa.



    ----------



    Katika mgahawa wa Sizzler Corner yakiwa ni majira ya jioni. Anaonekana Ramah akiingia ndani humo akiwa amependeza si kawaida. Jinzi ya rangi bluu iliyopauka kwa mbali, tisheti ya mikono mirefu ya rangi nyeupe iliyochanganyikana na rangi nyekunde kwenye mikono. Huku kichwani nywele zake akizibana nyuma mtindo ambao wengi humsifia ya kuwa anapendeza akiziweka hivyo. Machoni mwake alivaa mawani ya jua yenye vioo vyeupe vilivyoonyesha macho yake bila kificho. Chini kabisa akiwa amevalia raba nyekundu aina ya All Star. Alimpendezea kila aliemuona na wengi walimsifu kwa tabasamu walipokutanisha macho huku wengine wakimsifu ndani ya nafsi zao.



    Alijongea kwa hatua fupi fupi mpaka pale alipoifikia meza moja ambayo kwenye viti vyake kimoja wapo alikalia Cecy. Ndio, Cecy huyu huyu aliewahi kuwa mpenzi wake kabla ya kuachana kwa ubaya. Cecy alilazimisha tabasamu japo kinywa chake kiligoma kutoa tabasamu baada ya kumuona Ramah. Akamkaribisha kwa unyenyekevu kijana huyo na Ramah alivuta kiti na kukaa.



    Haya iliyomvaa Cecy haikuwa ndogo hata kidogo. Aliona soni kutazamana na kijana huyo macho kwa macho lakini alijikaza tu ili atimize lengo lake. Ramah hakuwa akitabasamu wala hakuwa amenuna. Alikuwa kawaida sana na wala hakuonyesha kutaka kutabasamu muda huo. Pengine hakuwa tayari kufanya mazungumzo na binti huyo.



    Mgahawa ule ule ambao Cecy alimkataa kwa mara ya mwisho Ramah na kumdhalilisha vibaya. Ndio huo huo aliomuomba siku wakutane. Wakati pale alipokuwa akibofya simu yake siku hiyo, mwanzo alijaribu kumpigia simu Ramah lakini akakuta ikiwa inatumika. Akakata ndipo alipoamua kumtumia ujumbe wa kumuomba wakutane majira hayo sehemu hiyo. Ramah nae bila ajizi alifika!.



    “Ramah...” Cecy aliita. Ramah hakujibu kwa kinywa bali macho yake yalidhihirisha kuitikia wito huo. Cecy akaendelea. “Mwema huomba samahani pale anapokosea. Nami sina budi kukuomba msamaha kwa yale niliyokufanyia. Nakiri kwamba nimekosa na ni shetani tu yule alinipitia kama ulivyowahi kuniambia. Tamaa zilinijaa moyoni huku pepo la usaliti likinivaa rohoni...” Akafuta machozi yaliyoanza kumtoka machoni kwake. “Hazikuwa akili zangu zile mpaka kukutendea yale niliyokutendea. Najuta Ramah! Naijutia nafsi yangu kwa kuniingiza kule pasipo matarajio yangu. Nilitambua kama Rommy ni ndugu yako na niliyakumbuka yale aliyowahi kunitendea nyuma. Lakini sijui ni kipi hasa kilichonifanya nikageuza ule ubaya wake na kuuona ni wema. Huku yale mabaya yake nikikubebesha wewe bila kuujali upendo wako. Rafael, msamaha wako ndio utaniacha mimi huru kwenye kifungo hiki nilichojifungia mwenyewe bila kujua. Nisamehe Ramah, usiponisamehe utaniacha kati hali ngumu sana..” Ramah alimtazama kwa muda kisha akasema.



    “Nimekusamehe Cecy. Usihuzunike sana kuhusu hili”



    Cecy alizidi kulia kwa uchungu akidai kwamba haamini kwa yale yote aliyomfanyia ameamua kumsamehe kirahisi namna hiyo. Ikabidi Ramah amueleweshe vyema kwamba amemsamehe kwa dhati na wala hakuwa na kinyongo nae. Cecy akaonyesha furaha lakini machozi yasikome kumtoka. Pamoja na kusamehewe, lakini hakujua kwamba amesamehewe mpaka kwenye mapenzi yao ama msamaha huo ni kwa yale aliyomfanyia tu. Akiwa na aibu nyingi alijaribu kumueleza Ramah jambo hilo.



    “Ila tambua bado nakupenda Ramah. Pamoja na kunipatia msamaha huo. Sidhani kama nafsi yangu itatulia kama hutorudisha moyo wako nyuma na kuwa wapenzi tena. Tafadhali Ramah naomba ulikubali na hili”



    Ramah alimtazama Cecy kwa muda kisha akatabasamu huku akiinamisha kichwa chake chini. Alipoinua macho yake kumtazama Cecy, tabasamu halikuwapo kama mwanzo kwenye wajihi wake kisha akasema.



    “Nikisema nimekusamehe Cecy haimaanishi eti mpaka kwenye mapenzi turudiane tena. Nimekupa msamaha lakini si kwamba ndio nitakupenda tena. Nafasi yako haipo Cecy! Nafasi yako kwenye moyo wangu haipo tena, kwa sasa inamilikiwa na mtu ambae alikuwa akinijali kipindi ambacho sikuwa sawa. Alikuwa mfariji wangu kipindi ambacho nilihitaji faraja yako. Alinifuta machozi kipindi ambacho sikutambua kama macho yangu yalikuwa yakitoa machozi. Alinimbembeleza, aliniliwaza na kunifariji pale nilipojihisi mpweke. Unajua Cecy nilikupenda sana kiasi ambacho kuna kipindi nikawa sijijali mimi nakujali wewe tu. Lakini umenipa somo kubwa sana kwamba endapo nisipojithamini mimi basi hakuna atakaenithamini. Ndio, na kwako ilikuwa hivyo, hukunithamini kwasababu ulishagundua sikuwa najithamini mwenyewe badala yake nakuthamini wewe. Hujui! Hujui Cecy kama unakosea kusema unanipenda sana. We hunipendi na ushanithibitishia hilo. Na kama ungekuwa unanipenda basi usingeacha niteseke vile. Sikuhisi njaa wakati tumboni sikutia chochote kwa muda mrefu. Jenifa aliekuwa rafiki yako uliegombana nae alipokufuata kukushauri kuhusu Ethan ndio ambae alikuwa akinifanyia yote hayo. Mwanzo sikuwa nikimpenda ila baada ya kuona ameitambua thamani yangu basi moyo wangu ukafunguka kwake. Nampenda na yeye amenijibu ananipenda na sitoacha kumpenda nikurudie wewe ulienitenda niliempenda kipindi ambacho mimi mwenyewe sikuitambua thamani. Nampenda yeye na nikakuambia wazi kwamba nafasi yako imekaliwa na yeye....”



    “No Ramah! Kumbuka tumetoka wapi mimi na wewe. Sasa leo iweje unipe hukumu kubwa kwa kosa dogo tu hili?” Cecy aliongea huku akiwa analia.



    “Usingenisaliti kama ungelitambua hilo...” Ramah akaitazama simu yake iliyokuwa ikiita kisha akatabasamu na kuipokea. Baada ya kusikiliza kwa sekunde kadhaa akataja mahala hapo alipo kisha akatulia tena kabla hajakubaliana kitu na huyo aliekuwa akiongea nae. Akayatua macho yake kwenye wajihi wa Cecy akiwa mkavu bila tabasama, akasema.



    “Samahani, mtu muhimu sana amenipigia simu ananihitaji kwa sasa. Na kwavile sitaki kumuudhi na wala kumsononesha, acha niwahi saa hii” Ramah aliongea hayo kisha akainuka. Cecy nae akainuka haraka na kwenda kumuwahi Ramah miguuni, akapiga magoti akimuomba msamha huku akilia sana. Wateja waliokuwa ndani ya mgahawa huo waliacha shuhuli zao na kuwatazama wao kwa mshangao.



    “Tafadhali Rafael naomba unisamehe nakupenda sana mpenzi wangu. Usiniache pekeangu utaniumiza. Nakiri nimekosa naomba unisamehe hee hee!” Cecy aliongea hayo huku akilia sana. Ramah alimtazama huku akitabasamu kisha akajitoa kwenye mikono ya Cecy iliyoshikilia jinzi lake. Akaondoka mahali hapo huku akimuacha Cecy akimuita jina lake huku akilia sana.



    Ramah alipofika kwenye geti la kutoka nje ya mgahawa huo akasimama. Kisha akageuka kule alipo Cecy, taratibu kabisa kwa hatua ndogo ndogo alienda pale alipo Cecy huku akiivua ile mawani na kuishika kwa mkono wake wa kushoto. Cecy aliekuwa akilia huku ameinamisha kichwa chake chini. Alishangaa kuona miguu iliyovikwa viatu vyekundu ikiwa mbele yake. Akainua sura yake taratibu mpaka pale alipotazama juu kabisa na kumuona Ramah akiwa amesimama mbele yake akimnyooshea mikono kwaajili ya kumuinua.



    Cecy alipigwa na butwaa na kilio kilikata ghafla baada ya kushuhudia kitendo hicho. Amerudi tena kwaajili yangu? Alijiuliza hayo huku akivitazama viganja vya Ramah vilivyokuwa tayari kupokea viganja vyake. Akainua tena shingo kumtazama Ramah usoni akakuta kijana huyo ni mwenye kutabasamu. Taratibu aliinua mkono wake wa kulia na kubandika viganja vyake kwenye viganja vya mkono wa kushoto wa Ramah. Akatulia kwa sekunde kadhaa na kuinua ule wa kushoto na kubandika viganja vyake kwenye viganja vya kulia vya mkono wa Ramah. Kisha hapo Ramah akamuinua taratibu mpaka alipofiki usawa wa kutazamana.

    La haulaa!

    Kilikuwa ni kitendo ambacho hakikutegemewa na yeyote kati ya watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo achilia mbali Cecy mwenyewe







    Kilikuwa ni kitendo ambacho hakikutegemewa na yeyote kati ya watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo achilia mbali Cecy mwenyewe. Cecy mara hii alikuwa chini akigaagaa baada ya Ramah kuachia mikono yake na kumsukumiza maeneo ya kifuani na Cecy akaenda chini na kulalia mgongo. Ramah aliivaa miwani yake na kupangusa mikono yake huku akiondoka mahala hapo akiwaacha watu midomo wazi. Cecy alijizoazoa pale chini na kukaa kitako huku akilia sana kama kitoto kidogo kilichonyimwa sufuria la ukoko wa wali na mamae.



    Ramah majira haya alikuwa ndani ya Nyumbani Hotel. Akashuka chini ya kwenye Hoteli hiyo ghali na kwenda mpaka kwenye magahawa mdogo uliokuwa ndani humo. Kwenye meza zilizokuwa eneo hilo moja wapo alionekana Jeni akiwa amekaa huku akiwa bize na simu yake. Jeni alipomuona Ramah aliinuka haraka na kwenda kumkumbatia. Kisha akajitoa kwenye kumbato hilo na kumsifia Ramah ya kuwa amependeza sana siku hiyo. Ramah akashukuru kwa kusifiwa na wote wakarudi kwenye ile meza na kuweka kambi mahala hapo.



    “Ulikuwa unafanya nini huko ulipotoka mpenzi?” Jenifa alimuuliza Ramah baada ya kuwa wamekwisha kaa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna mtu nilienda kukutana nae mara moja..” Punde tu muhudumu alifika hapo na kuwataka oda watu hao. Ramah akaagiza alivyotaka kuagiza na Jeni nae akafanya hivyo.



    * *



    Hali ya Cecy tangu siku ile alipokataliwa kabisa na Ramah ilibadilika sana. Hakujiweka vyema kama ilivyokuwa mwanzo. Hakuwa msafi wala mwenye kuzungumza lolote kama ilivyokuwa kawaida yake. Hakuwa ni mwenye kutoka nje zaidi ya kushinda chumbani kwake tu. Muda wote alikuwa ni mwenye kutokwa na machozi huku kinywa kikiwa kimefumba. Ni vipi awe na raha wakati aliona maisha yake yameshaharibika? Licha ya kuharibika kwa maisha yake. Hata lile gonjwa alilokuwa nalo lilimchanganya sana na kumvuruga kabisa akili yake. Ni wiki ya pili sasa alikuwa ni wa ndani tu!.



    Na hapa sasa ndio tunapata kisa kamili kilichomfanya Cecy awe katika hali ya uchizi wa fikra kwa mara ya kwanza tulipoanza kumuona wakati Anita Mama yake akimlalamikia ni kwanini amejichagulia maisha hayo ya unyonge.



    “Ni kweli mkosaji lakini sikupaswa kuadhibiwa kukubwa namna hii. Nimekuwa mtumwa wa mawazo kutwa kucha kuiadhibu akili yangu kwa kuwaza ambayo hayana maana yoyote. Nampa shida Mama yangu kwa upumbavu wangu niliojitakia mwenyewe huku wengi wao wakinishauri vyema na mimi nikawapuuzia. Ikiwa nina gonjwa hatari la Ukimwi nasubiri nini sasa duniani? Sitaki kumuadhibu Mama yangu kwa manyanyaso kipindi anbacho nitakuwa hoi kitandani. Mwili wote umeisha nimebaki mifupa. Haja zote nazishusha hapa hapa kitandani huku Mama yangu nikimsulubu kunihudumia kila kitu. Yanini yote haya yanikute? Hapana! Lazima nife! Nife na yule alienisababishia matatizo haya. Hata hivyo nafsi yangu haitoridhia tufe wawili tu. Lazima wafe na wale ambao hawahusiki kwenye huu upumbavu wangu.

    Lazima tufe!”



    Maneno haya Cecy aliyanena kipindi ambacho Mama yake alitoka nje kwenda kuwaandaa wale samaki alionunua muda mfupi tu. ( Sehemu hii ni pale mwanzo wa kisa hiki kilipoanza). Cecy akashuka pale kitandani na kuvaa ndala. Kisha akatoka nje kwa mwendo wa kasi kiasi ambacho alimshangaza Mama yake aliekuwa jikoni.



    Anita alitoka hai hai kumfuata Cecy maana tangu aamue kukaa ndani ni wiki ya pili na siku zake hakuwahi kutoka nje. Na leo ametoka akiwa katika mazingira yasioeleweka. Hata pale alipofika nje, Anita hakuweza kumuona Cecy. Alimtafuta kwanza hapo hapo nyumbani kwake kwa kuzunguka pembe zote za nyumba lakini hakumuona. Ikambidi sasa atoke nje ya wigo wake na kwenda kumtafuta huko.



    Majira hayo yakiwa ni jioni kigiza ndio kinaanza kuingia. Zuma alitaka kutoka akafuatilie mambo yake. Paskali na Zuma wakamuomba kutoka nae ili walau watembee_tembee vya mwisho ndani ya jiji hilo kabla hawajarudi Nairobi siku inayofuata. Wakamuaga Rommy aliekuwa chumbani kwake kwa kumtumia ujumbe kuwa wanatoka mara moja lakini watawahi kurudi, nae akawaruhusu.



    Ni dakika zile zile ambazo wakina Zuma walitoka. Mlinzi wa getini alisikia kengele ya hodi ikigongwa. Akachungulia kwenye kidirisha kidogo kabla ya kufungua mlango alipomtambua mgongaji. Akafungua.

    Alikuwa ni Cecy alieingia ndani humo akiwa katika muonekano wa ajabu uliomshangaza mlinzi. Lakini kwa vile alishazoea kumuona binti huyo mara kadhaa akiwa ndani humo, hakuweza kumzuia wala kumuhoji chochote.



    Cecy alimpita mlinzi kwa kasi na kufungua mlango wa kuingilia sebuleni ambao ulikuwa haukufungwa. Akazama sebuleni na kuyaangalia mazingira ya hapo. Haraka haraka akaangaza macho yake kisha akaliendea kabati lililokuwa mahala hapo. Akalifungua na kuchomoka na kisu kilichokuwa kikimeremeta kwa makali. Akashika uelekeo wa chumba cha Rommy huku akikikaza kisu kile viganjani mwake akiwa anatetemeka vibya.



    Akaufungua mlango kwa pupa na mlango ukatii amri yake. Macho kwa macho na Rommy aliekuwa kitandani amejilaza, pembeni yake kukiwa na mwanamke ambae ki umri alionekana kumzidi Rommy. Rommy akashtuka baada ya kumuona Cecy akiwa ametokea humo kama mzuka wa kuzimu. Mwanamke yule hakuwa akielewa chochote zaidi alizungusha macho kuwatazama watu hao kwa zamu.



    “Utanisamehe Rommy lazima ufe. Umeniharibia maisha yangu. Umezivuruga ndoto zangu, pia ukaona haitoshi ukanizawadia na gonjwa hatari. Lazima ufe Rommy!” Ni maneno pekee aliyosema Cecy baada ya kumtazama Rommy kwa muda. Kisha akaitazama droo iliyokuwa karibu na kabati la nguo. Alikiachia kile kisu na kutua sakafuni kisha kikatulia. Aliiendea ile droo kwa kasi huku Rommy nae akijitahidi kuinuka kuiwahi ile droo. Lakini hata hivyo Cecy ndie aliewahi na kuifungua. Kisha akachomoka na bastola ndogo.



    Rommy akafunga breki na kusimama wima ikiwa mdomo wa bastola umemtazama yeye usoni. Mwili ukaanza kumtetemeka mithili ya kifaranga cha kuku kilicho nyeshewa na mvua. Muda huu hata yule mwanamke aliekuwa amelala na Rommy pale kitandani alianza kutetemeka huku akilikusanya shuka bila kujua.



    “Ce....cecy! Achana na hiyo kitu. Ni hatari! Weka chini tuyazungumze, mi nakupenda Cecy watambua hilo” Rommy aliongea kwa kitetemeshi huku akijaribu kumsogelea Cecy taratibu. Cecy alifanya kama anaishusha ile bastola na alipofika usawa wa paja la Rommy lililokuwa wazi kwa kushindwa kustiriwa ni kipensi kifupi. Ghafla mlio wa risasi ukasikika huku yowe kubwa lililomtoka Rommy lilichagiza huku Rommy mwenyewe akigaagaa chini kwa maumivu huku akishika ile sehemu yenye jeraha. Yule mwanamke pale kitandani alizimia pale pale baada ya mlio wa bastola kusikika.



    “Hiyo ni ya kunisaliti. Subiri nikupe ya kuniambukiza gonjwa lako. Pumbavu wewe!” Cecy aliongea hivyo kisha akafyatua tena risasi iliyoenda kuchangua kichwa cha Rommy. Rommy alitapatapa pale chini na baada ya sekunde kadhaa akatulia kimya. Rommy akapoteza maisha!.



    Cecy alitoka mbio huku bastola ile akiifutika kwenye nguo yake aliyoivaa. Akatoka nje ya jengo hilo na kumkuta mlinzi akiwa ameshika vyema bunduki yake. Cecy roho ilimbadilika. Hakuwa Cecy yule mpole mpenda kudeka kila mara. Cecy huyu wa sasa aliuvaa usheteani huku damu ya mauaji ikitembea nae mwilini.



    Alipoonana ana kwa ana na mlinzi wa nyumba hiyo. Akafyatua tena bastola bila kulenga vyema na risasi ikaenda kutua kwenye bega la mlinzi. Atalenga vipi ikiwa hakuwahi kujifunza kuitumia silaha hiyo zaidi ya kuona kwenye tamthilia za kizungu? Mlinzi yule alipiga yowe la maumivu huku akiachia bunduki lake na kuegemea ukuta. Cecy akapata upenyo mzuri wa kutoka ndani ya nyumba hiyo. Akapotelea nje na kutokomea kusikojulikana.



    Kikiwa kigiza tayari kimeshaingia muda huu. Jeni baada ya kurudi kule Beach alipokuwa na Ramah. ( Sehemu hiyo tuliiona mwanzo wa kisa hiki kabla hatujaingia kwenye kumbukumbu). Majira hayo alikuwa akijiandaa kupika chakula cha usiku. Akiwa amebadilisha yale mavazi aliyotoka nayo matembezini na sasa alikuwa amevaa kanga moja huku juu akiwa na fulana.



    Alikuwa katika maandalizi ya kupika kwasababu alikuwa pekeake nyumbani kwao. Mama yake hakuwepo tangu mwanzo wa siku hiyo. Akiwa katika maandalizi hayo alimuona Cecy akija mahala hapo. Akaacha kile alichokuwa anafanya na kumtazama yeye.



    Cecy alionekana akija mahala hapo akiwa na haraka. Jeni alisimama kumtazama rafiki yake huyo wa zamani kabla hawajatengana kwa ugomvi. Akiwa ametaharuki kwa kumuona Cecy nyumbani kwao kwa mara ya kwanza tangu wakosane.



    Cecy alipofika karibu yake aliichomoa ile bastola na kumuelekezea Jeni huku akimsogelea. Hofu! Jeni aliingiwa na ubaridi wa hofu moyoni mwake baada ya kushuhudia kitendo hicho. Anataka kufanya nini huyu? Alijiuliza kwa taharuki huku akirudi nyuma.



    “Huna makosa Jenifa rafiki yangu. Ila kosa lako kubwa ni kunipokonya mpenzi wangu na kujimilikisha wewe. Utanisamehe sana ni bora tukose wote..” Cecy alitamka hayo kisha akafyatua risasi iliyoenda kuzama moja kwa moja kwenye moyo wa Jeni.



    Jeni alitupwa nyuma kwa msukumo wa risasi ile. Akaanguka chini na kutulia kimya. Maskini ya Mungu Jeni hatunae tena. Mbele yake nyuma yetu. Cecy baada ya kuona ameshafanya yale aliyokusudia. Akajielekeze na yeye ile bastola kichwani na kufyatua. La haula!. Bastola haikuwa na risasi kwenye chemba. Akajaribu kufyatua kwa mara nyengine lakini hakukusikia mlio wowote zaidi ya vyuma vitupu vilivyokuwa vikisuguana ndani ya bastola ile.



    Pale pale akaitupa ile bastola na kutoka mbio mbio mahala hapo huku watu wakianza kujaa eneo lile baada ya kusikia mlio wa risasi. Cecy alikuwa kama mwendawazimu. Sasa alipanga akimbilie kwao kwa mama yake kabla hajakamatwa.



    Assalalee!.







    Nitukio ambalo liliacha historia kubwa na ya kutisha kwa watu waliopata kushuhudia tukio hilo. Cecy hakutazama popote wakati anavuka barabara. Gari la Polisi lililokuwa kasi likiwahi eneo lile iliposikika mlio wa risasi maana kutoka alipokuwa akiishi Jeni na kituo cha Polisi Mabawa hapakuwa na umbali wowote. Gari lile likiwa katika mwendo ule ule wa kasi lilimzoa Cecy na kishindo kizito kikasikika kabla ya kishindo chengine cha gari lile lililoenda kugonga kwenye nguzo ya umeme baada ya dereva wa gari lile alipokuwa akijitahidi kumkwepa Cecy.



    Cecy muda huo alikuwa kando ya barabara chini akiwa kimyaa huku damu zikimvuja mwili mzima baada ya kurushwa vibaya hewani kabla hajatua kwenye jiwe kubwa lililokuwa kando ya barabara hiyo. Watu walijaa eneo hilo kushuhudia ajali hiyo. Wengi wao hawakuweza kuvumilia kuutazama mwili wa Cecy pale chini. Wapo waliotazama mara moja tu kisha wakajitoa eneo lile kwa hofu huku wengine wakiutazama mwili Cecy huku wakimtaja Mungu wao. Ni dhahiri alishakata roho muda mrefu, pia viungo baadhi vya mwili wake vilikuwa vimelegea baada ya kuvunjika.



    Askari walijaa eneo hilo kwa kufuatia matukio mawili. Moja ikiwa ni hiyo ajali na jengine ni lile la kusikika mlio wa risasi eneo hilo. Askari waliokuwa kwenye lile gari la polisi lililosababisha ajali wengi wao waliumia huku wengine wakitoka wazima. Dereva wa gari lile alizimia pale pale. Gari la wagonjwa lilifika mahala pale na kuwakusanya wote waliopatwa na maswahibu yale. Kisha likatimka kuwahi hospitalini.



    Taarifa za kifo cha Cecy, Anita alizipata siku iliyofuata baada ya siku iliyopita kumtafuta sana na kumkosa. Taarifa ambazo zilimuumiza sana mpaka kupelekea akili yake kuvurugika na kuwa kichaa kabisa. Majirani zake walipozipata taarifa zile walisikitika na kufanya msaada mmoja wa kumkamata Anita na kumpeleka hospitalini kwaajili ya matibabu kwasababu pia alikuwa akileta fujo mtaani.



    Mama yake na Jeni, alichanganyikiwa baada ya kupata taarifa za kifo cha mwanae. Siku ya tukio hilo hakuwapo nyumbani kwake. Na hata pale alipopata taarifa hizo ikambidi kuwahi hospitalini kwenda kuthibitisha mwenyewe kama ni kweli mwanae amefariki baada ya kushambuliwa na bastola na mtu ambae mpaka sasa hakujulikana na uchunguzi wa kipolisi ulikuwa bado ukiendelea.



    Upande wa kina Paskali wao baada ya kurudi kwenye mizunguko yao na kushuhudio mwili wa Rommy ukiwa chini damu zikivuja kichwani. Na mashaka hayo walianza kuyapata kwa mlinzi walipomkuta chini amezimia huku bega lake likivuja damu, ndipo walipoingia ndani kwa uangalifu huku wakiwa wameshika vyema bastola zao. Chumbani kwa Rommy ulikuwapo mwili wake pekee huku yule mwanamke aliekuwa nae akiwa ameshakimbia baada ya kupata fahamu. Nini wafanye baada ya kukuta tukio hilo baya limeshatendeka? Kila mmoja alikimbilia anapopajua yeye kuiokoa roho yake dhidi ya mlezi wa kijana huyo ambae walimtambua kwa utata wake.



    Siku mbili mbele mazishi ya vijana wale waliokufa chanzo kikuu kikiwa ni mpenzi walizikwa. Cecy alizikwa kwa msaada wa Eddu rafiki ya baba yake kipindi cha uhai wake huku majirani wakifanikisha hilo pia. Anita alikuwa hospitali ya vichaa akiuguzwa huko baada ya kugundulika kuwa akili yake ilivurugika baada ya kusikia kifo cha mwanae na kupata mshtuko uliyomsababishia ukichaa. Uchunguzi wa kidaktari ulisema kwamba akili yake itarudi vyema lakini hiyo ni baada ya kuchukua muda mrefu kidogo. Eddu akajitoa kwa hilo na kuhakikisha mke wa aliekuwa rafiki yake anarudi katika hali ya kawaida.



    Siku hiyo hiyo pia yalifanyika mazishi ya Jenifa. Mama yake alikuwa taabani kwa kilio kila mara alipokumbuka kuwa mwanae wa pekee hanae tena. Iliwasikitisha wengine baada ya kutojulikana muuaji ni nani hasa. Wapo walioowanisha ajali iliyotokea na kifo cha Cecy. Huku wengine wakidai mambo hayo hayana uwiano wowote. Swali likabaki vichwani mwao. Muuaji ni nani? Na alikuwa na dhamira gani mpaka kuuondoa uhai wa binti mdogo? Mpaka kesho hakuna ambae aling'amua lolote.



    Kelvin yeye baada ya kusikia taarifa za kifo cha mwanae Rommy ambae alikuwa ni mtoto wa kaka yake Antony Magasa. Alifika jijini hapo huku akiwa amechanganyikiwa si kidogo. Aliwatafuta sana wakina Paskali lakini hakuwaona. Kichwani kwake kukapita wazo moja kwamba. Wauaji wa mwanae ni hao hao vijana aliowapa kujukumu la kumlinda. Akaapa kimya kimya kuwa ni lazima awatafute na alipe kwa hilo kipindi ambacho analitazama kaburi la Rommy.



    Siku mbili baada ya mazishi ya Jeni pamoja na rafiki yake Cecilia. Ramah alionekana katika ufukwe wa bahari ya Jeti akiwa amekaa kwenye jiwe moja kubwa mkononi mwake ameshika gitaa lake akivuta nyuzi na kuimba kwa hisia huku machozi yakimtoka sana. Baada ya dakika nne akaacha kupiga gitaa na kutazama mbele ilipo bahari. Pamoja na kuacha kuimba na kutopiga gitaa, lakini bado machozi hayakuacha kumtoka machoni mwake.



    “Maumivu niyahisiyo sasa hakuna ambae anaweza kuyatafsiri hata nikimuelezea kwa upana. Jeraha lililopo Moyoni mwangu sidhani kama litapona tena baada ya kutoneshwa upya kidonda ambacho kilianza kukauka. Cecilia ulinifanya nilie kwaajili yako. Mungu akasaidia nikapata wakunifuta machozi. Sasa kwanini umenifanya nilie tena kwaajili yako? Anhaaa! Nimegundua kitu. Kumbe ulikuwa unapenda kuniona kila mara nikiwa sina furaha. Ndio, kwasababu kama si wewe uliesababisha mauti ya Jenifa ni nani tena? Kama si wewe uliesababisha mauti ya ndugu yangu ni nani sasa? Ni wewe Cecy haiwezekani ukakutwa na ajali karibu kabisa na nyumbani kwa rafiki yako ambae mimi alikuwa ni mpenzi wangu baada ya wewe. Ndio ni wewe Cecy na Mungu hakutaka ufike mbali baada ya kusababisha mauti ya rafiki yako na kutaka kukimbia... Basi sawa... Sawa, nisalimie mpenzi wangu mwambie nampenda sana hata kama hayupo tena nami. Pia usiache kumsalimia na ndugu yangu mwambie nimemsamehe pengine ni kweli hakuwa akijua chochote. Hakika umeniachia JERAHA LA MOYO ambalo katu haliwezi kupona...”



    Ramah alikomea hapo. Akatabasamu ingali bado machozi yakimtoka. Akahamisha macho yake kutoka kule baharini na kulitazama gitaa lake. Alilitazama kwa muda kama ambae aliekuwa akilishangaa. Akaliinua kwa mkono mmoja huku akilitazama, mara hii hakuwa tena na tabasamu usoni mwake zaidi ya kuonyesha mshangao. Kisha akaachia cheko kubwa na refu lenye sauti kali lililowashtua baadhi ya watu waliokuwa hapo kwaajili ya kubarizi.



    Akiwa anacheka bado, aliinuka pale alipokaa. Akaliigamiza gitaa lake kwenye jiwe na kulipiga_piga kidogo kama kulipoza hivi. Kisha akajitoa mahala pale huku akicheka sana na kuliacha gitaa lake pale pale kwenye jiwe huku yeye akipandisha na juu. Ni dhahiri Ramah akili yake ilivurugika yote na kuwa mithili ya kichaa. Alipofika juu alipotelea huko na isijulikane ni wapi ameelekea.



    Ni siku ya tatu sasa familia yake ilikuwa ikimtafuta ndugu yao aliekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Walizunguka kote kuanzia mahospitalini mpaka vituo vyote vya polisi wakihangaika kumtafuta. Siku hii ya tatu baada ya kupotea kwake. Walipata taarifa kwamba ndugu yao ameonekana katika jalala fulani akizurura huko. Walienda huko walipoelekezwa wakiwa hawaamini kwamba yanaukweli hayo. Lakini walisibitisha baada ya kufika na kushuhudia wenyewe kwa macho yao.



    Iliwaumiza kwenye mioyo yao na mwisho walimkamata na kumfikisha moja kwa moja hospitalini kwaajili ya kumtibu. Hata baada ya vipimo Daktari aliwahakikishia kwamba mgonjwa wao hatoweza tena kupona kutoka katika ukichaa mpaka kifo chake. Lakini pia aliwapa moyo kwa kuwaambia wamuombee kwa Mungu pengine anaweza fanya miujiza yake na hali ya mgonjwa wao ikarudi sawa.



    Dorine Mama mzazi wa Ramah alizimia baada ya kupata taarifa hiyo iliyoushtua moyo wake. Lakini kuzimia huko ilikuwa ndio chanzo cha kifo chake. Alifariki huku akimlilia mwanae. Jay alilia kwa uchungu kwa kuondokewa na mzazi wake ilhali Ramah alikuwa akicheka kwa furaha. Maskini hakuwa na ufahamu wowote wa kuweza kujua kwamba Mama yake amefariki kwaajili yake.



    Hata pale Daktari alipomshauri Jay kwamba ampeleke Ramah kwenye hospitali ya vichaa. Jay aligoma akidai atakaa nae mwenyewe nduguye. Akarudi nyumbani kwao na kwenda kutoa taarifa kwa ndugu na majirani zake. Tatatibu za mazishi zikafanyika na Dorine alienda kuzikwa kwa wazazi wake huko kijiji walipomfukuza baada ya kuwatia aibu kwa kupata mimba ya Ramah ilhali alikuwa ni mke wa mtu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya wiki moja kupita. Jay anaonekana chumbani kwao akifunga kamba za viatu vyake alivyovivaa. Ramah alikuwa pembeni akiongea maneno yasiyoeleweka huku mara kadhaa akicheka_cheka mwenyewe. Jay baada ya kumaliza kufunga kamba za viatu. Alisimama na kumgeukia Ramah. Alimtazama kisha akatabasamu.



    “Sasa dogo unajua hapa nyumbani tupo wenyewe. Kwahiyo wewe nisubiri hapa nikatafute chakula tuje kula..” Akamtazama kichwani na kuziangalia zile nywele zake zilizokuwa hovyo baada ya kukosa matunzo. “Inabidi nikirudi nikunyoe hizo nywele kwasababu hazikupendezi kwa sasa” Alimaliza hivyo kisha akatabasamu. Akamshika Ramah kichwani kisha akatoka nje ya chumba chao akimuacha Ramah akicheka mwenyewe utafikiri aliyaelewa yale aliyoyaongea Jay. Jay aliufunga mlango wake kwa komeo kule nje na kupotelea mtaani.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog