IMEANDIKWA NA : ATUGANILE MWAKALILE
*********************************************************************************
Simulizi : Mume Gaidi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ilikuwa ni kipindi cha mvua za masika, na siku hiyo mvua ilikuwa inanyesha. Kijana Patrick alikuwa ndani na mama yake bi. Deborah, hoja ya Patrick ilikuwa ni moja tu kuhusu baba yake mzazi.
PATRICK: Mama, hivi kwanini hutaki kuniambia ukweli kuhusu baba yangu.
DEBORAH: Mwanangu ni historia ndefu sana, tafadhari usinikumbushe.
PATRICK: Mama, mimi ni kijana mkubwa sasa. Niambie ukweli, baba yangu ni nani? Hayo machungu yako, machungu gani? Ninachotaka mimi ni kumjua baba yangu tu.
DEBORAH: Hii ndio tabu yenu watoto wa kiume.
Mara Patric akainuka na kuelekea nje.
DEBORAH: Jamani mwanangu, unaenda wapi na mvua hii?
PATRICK: Kutembea.
DEBORAH: Kutembea na mvua utalowa mwanangu, halafu humu ndani hakuna hata mwamvuli.
PATRICK: Unanijali eeh!!
DEBORAH: Ndio nakujali mwanangu.
PATRICK: Kama kweli unanijali, ungenitajia baba yangu ni nani.
DEBORAH: Siwezi mwanangu siwezi.
PATRICK: Ndio hapo unaponikera mama, haya bhana badae.
DEBORAH: Jamani Patrick.
Patrick hakujali chochote, alitoka nje na kuondoka.
Deborah alikuwa na siri nzito juu ya mtoto wake Patrick, hakutaka kuusema ukweli kwa kipindi hicho, alijua wazi ukweli huo utamsononesha sana Patrick.
Deborah akiwa amesimama mlangoni na kumuangalia mwanae akitokomea kwenye mvua, mara akamuona dada yake aliyeitwa Marium akiwa anakuja na mwamvuli.
MARIUM: Vipi? Mbona umesimama mlangoni halafu namuona Patrick akitokomea mvuani.
DEBORAH: Dada we acha tu, karibu ndani kwanza.
Akamkaribisha dada yake ndani na kuzungumza nae hili na lile. Akamueleza na nia ya Patrick hadi kuondoka vile kwa hasira.
MARIUM: Debo, hunabudi kumueleza Patrick ukweli. Watoto wa kiume na baba zao mdogo wangu.
DEBORAH: Mmmh!!
MARIUM: Mbona unaguna sasa? Si umwambie tu Patrick kama baba yake ni Jumanne, na aende akamtafute huko Dar.
DEBORAH: Dada, hujui chochote kuhusu mimi na Patrick.
MARIUM: Inamaana hata Jumanne si baba yake? Ulizaa na mwanaume mwingine Deborah, sasa nimeelewa sababu kubwa ya Jumanne kukuacha wewe.
DEBORAH: Dada, usilolijua ni sawa na usiku wa giza.
MARIUM: Sawa, endelea kukaa na siri yako moyoni, nadhani utaitoa kaburini siku utapokufa.
DEBORAH: Jamani dada!!
MARIUM: Ndio hivyo Deborah.
Wakaongea mambo mengine ila Deborah akaendelea kubaki na siri yake moyoni.
Badae, mwanae Patrick alirudi akiwa amelewa sana kwahiyo akapitiliza kulala.
Kesho yake asubuhi, Patrick alikuta mama yake akiwa amemuandalia supu, baada ya kunywa alirudi na kukaa tena na mama yake kumuuliza vizuri.
PATRICK: Mama ni kweli unanijali sana, tena unanipenda sana ila ingekuwa vyema kama ningemjua na baba yangu.
DEBORAH: Patrick mwanangu, ni historia ndefu sana kuhusu baba yako.
PATRICK: Jana nilienda kwa mamdogo Anna, nae ameniambia kuwa inawezekana baba yangu akawa Jumanne. Je huyo Jumanne ni nani? Na je ni kweli ndiye baba yangu?
DEBORAH: Hapana Patrick, Jumanne si baba yako mwanangu.
PATRICK: Jamani mama, sasa baba yangu ni nani? Je ni yule tuliyekuwa tunaishi nae Arusha bwana Maiko?
DEBORAH: Hata Maiko si baba yako.
PATRICK: Sasa baba yangu mimi ni nani? Nahitaji kujua mama, nahitaji kutambua. Hata kama ulibakwa hadi kunipata mimi, niambie tu mama.
DEBORAH: Unapofikia ni pabaya huko Patrick, mi sijawahi kubakwa.
PATRICK: Sasa mbona baba yangu humjui?
DEBORAH: Ipo siku nitakwambia ukweli wote, ila sio sasa.
PATRICK: Mama, ni kweli umenisomesha. Umenilea vyema ila kumbuka kwamba kumjua baba yangu ni haki yangu, haijalishi alikutenda mambo gani mama ila nina haki ya kumjua.
DEBORAH: Sawa mwanangu, nitakueleza tu. Ipo siku utaujua ukweli wote Patrick.
Patrick alijiona hana umuhimu wa kuendelea kuishi nyumbani tu bila ya kufanya kazi maalum. Ikabidi atafute kazi na kuamua kupanga safari ya kwenda kwani alipata kazi kwenye mkoa wa Morogoro.
Patrick akasafiri bila ya kumuaga mama yake, kwa madai yake kuwa amempa adhabu mama yake ya kutomtajia baba yake.
Wakiwa njiani, basi lao likapata ajali kwani liligongwa na lori na kupinduka. Watu waliumia sana, haikuwezekana kuendelea na safari tena.
Majeruhi wakabebwa na kupelekwa hospitali, baada ya matibabu Patrick akaamua kurudi kwa mama yake. Kwakweli Deborah alimuhurumia sana mwanae.
PATRICK: Naomba unisamehe mama, najua yote hii ni laana ya kuondoka bila ya kukuaga mama yangu.
DEBORAH: Usijari mwanangu, cha muhimu hapa ni uzima wako tu mwanangu.
Patrick aliendelea kujiuguza mpaka pale alipopona kabisa. Ila ile kazi ya Morogoro haikuwepo tena kwani muda mrefu uliku umepita.
Patrick akaamua kutafuta kazi tena, na safari hii akapata kazi mkoani Arusha. Akahitajika kwenda huko, akaamua kumuaga mama yake.
DEBORAH: Ila mwanangu, huko Arusha mi sikuamini kabisa.
PATRICK: Kwanini mama?
DEBORAH: Sababu ya Maiko.
PATRICK: Mama usijali, kwanza hata sipakumbuki anapoishi huyo bwana. Siwezi kwenda mama.
DEBORAH: Najua ulimzoea Maiko kama baba yako, ila Maiko ni mtu asiyefaa kabisa mwanangu.
PATRICK: Mama, tumeondoka Arusha tangia nikiwa na miaka sita. Siwezi kumjua tena huyo Maiko, wala yeye hawezi kunikumbuka mama.
DEBORAH: Nakuhurumia mwanangu, ukimuona mkimbie kabisa. Atakufundisha tabia mbaya. Ila nakuombea kheri mwanangu.
PATRICK: Sawa mama usijali, huko Arusha nitafanya kilichonipeleka tu. Na pia nitakuwa nakuja huku Mwanza kukuona mama yangu.
DEBORAH: Sawa mwanangu, ila kuwa makini sana na Maiko, ni mtu hatari sana huyo.
PATRICK: Sawa mama, ingawa nae sijui alikufanya nini?
DEBORAH: Hiyo ni siri yangu mwanangu, ila jitenge nae.
PATRICK: Sawa mama nimekuelewa.
DEBORAH: Nakupa baraka zangu zote mwanangu.
PATRICK: Asante mama, najua nitakaporudi utakuwa tayari kunitajia baba yangu.
DEBORAH: Mmh na wewe, kila mara baba baba kama wimbo wa Taifa!
PATRICK: Ni wajibu wangu kumjua mama.
DEBORAH: Sawa mwanangu, ipo siku nitakwambia ukweli.
Deborah na mwanae wakaongea mengi kwani kesho yake asubuhi ndio ilikuwa siku ya safari, siku ya Patrick kuiacha Mwanza na kwenda Arusha kikazi.
Alfajiri na mapema, Patrick akasindikizwa na mama yake hadi kituo cha mabasi na kumuacha Patrick akiwa ndani ya basi akielekea Arusha.
Safari ilikuwa ni ndefu sana, hadi muda ambao Patrick alifika Arusha alijihisi akiwa na uchovu mwingi. Wazo pekee alilopata kichwani kwa muda huo ni kutafuta nyumba ya wageni ambayo atapumzikia siku hiyo.
Akiwa pale stendi, mara kuna mtu akamshika bega, Patrick alipogeuka akapatwa na kitu cha ajabu sana.
Akiwa pale stendi, mara kuna mtu nyuma yake akamshika bega. Patrick alipogeuka akapatwa na kitu cha ajabu sana, kwani alishtukia akishindikwa ngumi usoni kitu kilichofanya aone kizunguzungu na kabla hajajitetea alijikuta akisokomezwa ndani ya gari, akiwa anafurukuta wakampulizia kitu cha ungaunga usoni na kujikuta akilala bila ya kubisha zaidi.
Patrick alipozinduka alijikuta kwenye kiti akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi.
Patrick akakumbuka tukio la mwisho baada ya kupigwa ngumi ni kuwa alipakiwa kwenye gari na kupuliziwa unga usoni. Akiwa anayatafakari hayo, mara akaingia mtu mule ndani na kuita huku akicheka.
"Patrick, Patrick"
PATRICK: Kwanini mnanitenda hivi jamani?
Yule mtu wa nyuma akazunguka mbele na kumuangalia usoni Patrick huku akisema.
"Mimi ni Maiko"
PATRICK: Maiko baba yangu.
MAIKO: (Akacheka sana), Patrick mimi si baba yako. Na vile vile mimi sina mtoto yeyote hapa duniani. Kama Deborah alikwambia kuwa mi ni baba yako basi amekudanganya.
PATRICK: Sasa mbona umenifunga hivi?
MAIKO: Kama utaongea na mimi kwa ustaarabu basi nitakufungua. Najua wewe Patrick ni mtoto mtukutu sana.
PATRICK: Ila mimi Sina tatizo na wewe na tutaongea vizuri tu.
Basi Maiko akaita vijana wake ambao walimfungua kamba Patrick na kwenda nae sebleni. Na hapo ndipo Maiko akaanza kumwambia Patrick kusudio lake.
MAIKO: Nahitaji kufanya kazi pamoja na wewe.
PATRICK: Lakini mimi nimekuja huku Arusha kwenye kazi nyingine, sio kazi yako baba.
MAIKO: Patrick, umesomeshwa kwa pesa yangu. Ni halali yako kuniita baba, na lazima unipe fadhila kwa kufanya kazi yangu.
PATRICK: Ila mimi nimesomeshwa na mama.
MAIKO: Hahahaha, mama yako ni mshenzi sana. Aliniibia pesa yule, kwahiyo ni pesa yangu ndio iliyokusomesha Patrick. Deborah alidhani amenikimbia milele kwa kuishi Mwanza, hakujua kama nina mtandao mkubwa. Kwa kipindi chote hiki nilikuwa namuangalia tu.
PATRICK: Hata kama alikuibia ni yeye, na hata hivyo mimi nitakapofanya kazi zangu nitakulipa. Tafadhari niachie niende nilipoitwa.
MAIKO: Hujui kama hapa ndipo ulipoitwa? Hukushangaa kupata kazi kwenye kampuni ambayo hujaomba? Au ulidhani ni mchezo wa bahati nasibu!! Patrick umesoma, ila umeshindwa kutafakari. Unafikiri kuna unarihisi wa kupata kazi namna hiyo? Tumia akili Patrick, jua kuchanganua mambo.
Patrick hakujua kama Arusha aliitwa na Maiko, akakumbuka matukio ya nyuma kuwa ameitwa kuanza kazi Arusha. Patrick akajiona mpumbavu sana kwa kutokufikiria mapema kuwa anapata vipi kazi kwenye kampuni asiyoomba.
PATRICK: Sasa hapa nitafanya kazi gani?
MAIKO: Kazi zipo nyingi tena zinalipa kupita maelezo, utakapofanya kwa kujitoa unaweza kuwa tajiri kunipita mimi. Patrick, tangia ukiwa mdogo nimekuona kuwa wewe ni kijana jasiri najua hii kazi utaiweza na utafika mbali Patrick.
PATRICK: Kazi gani sasa?
MAIKO: Kazi yenyewe unatakiwa ule kiapo kwanza kabla ya kuifanya.
PATRICK: Mmmh!! Kazi ya kula kiapo kwanza!! Dah!! Sasa kama wewe si baba yangu, baba yangu mimi ni nani?
MAIKO: Hilo swali muulize mama yako Deborah, maana kwangu alikuja akiwa na mtoto mchanga ambaye ndio wewe, alikuwa akikunyonyesha huku akilia muda wote. Kuna mengi nitakwambia ila ufanye kazi yangu kwanza.
Patrick hakuwa na la kusema wala la kuongezea, akawa anajiwazia tu kuhusu hiyo kazi ambayo atapewa na Maiko. Na pia alimuwaza huyo baba yake aliyemfanya mama yake alie muda wote wakati yeye akiwa mtoto mdogo.
Deborah akiwa amelala akamuota mwanae Patrick, akajikuta akishtuka na kusema kwa nguvu "Patrick"
Mara akamsikia mtu akigonga mlango wake, alipoinuka na kwenda kufungua alikuwa ni mdogo wake Anna. Akamkaribisha ndani,
ANNA: Dada mbona nimesikia ukiita Patrick kwa nguvu?
DEBORAH: Kuna ndoto mbaya imenijia kumuhusu Patrick.
ANNA: Kwani Patrick mwenyewe yuko wapi?
DEBORAH: Ameenda Arusha kikazi.
ANNA: Mmh!! Hata kuaga jamani! Hivi huyu mtoto wako baba yake ni nani?
DEBORAH: Jamani, kwani haiwezekani kuwa na mtoto bila ya baba?
ANNA: Acha maneno yako hayo, kila mtoto ana baba yake tatizo ni kuwa wengine wanawatambua baba zao na wengine hawawatambui.
DEBORAH: Sasa wewe unataka nini?
ANNA: Nataka kumtambua baba yake Patrick.
DEBORAH: Hakuna anayeweza kumtambua baba yake na Patrick hata mimi mwenyewe.
ANNA: Khaaaa, inamaana ulibakwa dada!!
DEBORAH: Ndio kitu pekee unachowaza, sijawahi kubakwa. Siri ya mwanangu Patrick ninayo mwenyewe moyoni mwangu.
ANNA: Au Joseph ndio baba yake na Patrick?
DEBORAH: Hayakuhusu.
Joseph alikuwa ni mwanaume aliyempenda sana Deborah na amekuwa akimfatilia mara kwa mara jambo ambalo linamfanya Anna ahisi kuwa huenda Joseph ndio baba mzazi wa Patrick.
Deborah hakutaka kabisa kuulizwa chochote kuhusu Patrick, kwani ni siri kubwa sana aliyoiweka moyoni mwake miaka na miaka, hakutaka mtu yeyote kuijua siri hiyo. Akawa anajisemea tu,
"Ila muda ukifika nitamwambia ukweli Patrick, nadhani atanielewa kwanini nimekaa na siri hii miaka yote"
Siku zote tangu Patrick akiwa mtoto mdogo, Deborah hakutaka kabisa kuulizwa kuhusu baba yake na Patrick.
Patrick akaitwa na Maiko ili aweze kula kiapo cha hiyo kazi.
PATRICK: Nitakulaje kiapo cha kazi nisiyoijua?
MAIKO: Ni lazima ule kiapo kwanza, kazi utaijua hapo baadae.
PATRICK: Hapana siwezi, kama kazi ya kuua watu je? Siwezi.
MAIKO: Inamaana mimi ni muuaji? Kama ningekuwa hivyo ningemuua mama yako na wewe mwenyewe kipindi kile.
PATRICK: Kwanini usinitajie hiyo kazi kwanza?
MAIKO: Lazima ule kiapo kwanza.
PATRICK: kwakweli siwezi kula kiapo kwa kazi ambayo siijui.
MAIKO: Unakataa kula kiapo Patrick!!
PATRICK: Siwezi kabisa kula kiapo kwa kazi nisiyoijua.
Maiko akabadilika gafla kitendo ambacho kilimtetemesha Patrick.
Maiko akabadilika gafla kitendo ambacho kilimtetemesha Patrick.
MAIKO: (akaongea kwa ukali), Sema tena Patrick.
Patrick akawa anajiuma uma tu kwani hakujua kitakachompata, akakumbuka maneno ya mama yake kuwa Maiko ni mtu hatari sana.
PATRICK: Nakuomba basi hata nimuulize mama aniruhusu kwanza.
MAIKO: Wewe ni mtoto wa kiume Patrick, mama kitu gani?? Wajibu wako kwa mama yako kwa sasa ni kumpelekea pesa tu.
PATRICK: Hata kumuomba ushauri pia.
MAIKO: Akupe ushauri gani mwanamke?? Nishakwambia mpelekee pesa tu uone atakavyochekelea hadi jino la mwisho tena atakupenda zaidi.
PATRICK: Ila mama ananipenda siku zote hata nilipokuwa nyumbani bila kazi.
MAIKO: Acha kujidanganya Patrick, nitakueleza mambo ambayo yataufumbua ubongo wako na kukuelewesha kwanini mwanamke akawa mama.
PATRICK: Mambo gani hayo?
MAIKO: Utajua vingi baada ya kukubali kula kiapo na kuanza kazi, jambo ni moja tu sitakuruhusu kutoka kwangu bila ya kula kiapo.
Patrick hakuwa na la kufanya, alishindwa namna ya kumkwepa Maiko. Na ubaya wa kazi ya Maiko ukiianza huwezi kuiacha, akawaza vitu vingi sana Patrick, akawaza pale mama yake atakapojua ukweli kuwa yuko na Maiko. Akajisemea kuwa atafanya kuwa kama siri ili mama yake asigundue.
Hatimaye Patrick akaamua kula kiapo, kitendo ambacho kilimfurahisha sana Maiko.
MAIKO: Sasa Patrick utajiri unanukia katika maisha yako.
Patrick alifurahi machoni ila moyoni alihudhunika kwa kumsaliti mama yake.
Deborah alikuwa na mawazo sana, mawazo ya kukosa mawasiliano kutoka kwa mtoto wake Patrick.
Alikuwa amekaa na dada yake Marium akimlalamikia.
DEBORAH: Tangia Patrick aondoke ni mwaka sasa umepita, hakuna cha simu wala nini sijui mwanangu amepatwa na kitu gani!
MARIUM: Usiwaze sana dada, muombee tu kwa mwenyezi Mungu.
Wakasikia muungurumo wa gari ukiishia kwao, ila hawakufikiria kama gari hiyo inakuja kwao.
Mara mtu akaanza kugonga mlango, kwenda kufungua ni Patrick, kwakweli Deborah alifurahi sana, alimkumbatia mwanae kwa furaha na kumshangaa jinsi alivyobadilika.
Patrick alimbebea zawadi nyingi sana mama yake na akaongea nae mambo mengi ila hakumwambia ukweli kama anafanya kazi kwa Maiko, hilo jambo alimficha kabisa hakutaka mama yake ajue.
PATRICK: Mama, nitakaa hapa wiki mbili.
DEBORAH: Kweli mwanangu?
PATRICK: Ndio mama, yani nilikukumbuka sana mama yangu.
DEBORAH: Na mbona hata simu ulikuwa hupigi?
PATRICK: Mama swala la kuwapigia majirani kukuulizia nilichoka, ndiomana nimeamua kukununulia simu yako.
MARIUM: Inaelekea kazi uliyopata inalipa sana Patrick, yani ndani ya mwaka ndio umebadilika hivyo!!
PATRICK: Aaah! Mambo madogo tu haya mamkubwa.
DEBORAH: Ila ni kazi gani hiyo mwanangu?
PATRICK: Nipo mgodini mama.
MARIUM: Hongera sana Patrick.
Walikuwa wakiongea mambo mengi ya hapa na pale, ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Deborah.
Tusa alikuwa ni binti mrembo na wa kupendeza machoni mwa watu. Mwanaume yeyote rijali lazima akimuona Tusa ajihisi tamaa ya kuwa naye.
Sura yake ya mviringo, mashavu yenye vibonyeo, meno meupe na yaliyokwenye mpangilio mzuri na mwanya. Ukimuona Tusa amecheka utatamani muda wote uyatazame meno yake yalivyo. Kwakweli alipendeza sana, hakuwa mrefu wala mfupi, umbo lake la wastani na rangi yake ya machungwa vilimfanya avutie zaidi. Tusa alizoea sana kudeka labda kwa vile alikuwa ndio mtoto wa kwanza wa bwana Adam na mkewe Pamela, na pia alikuwa ndio mtoto pekee wa kike kwenye familia yao ya watoto watatu.
Tusa alipenda sana kutumia mitandao ya kijamii hasa hasa facebook, tangu amalize kidato cha sita hadi alipoenda chuo muda wake mwingi aliutumia kwenye facebook, akiweka picha nyingi na kuandika jumbe mbali mbali kila leo, alikuwa na mpenzi wake aliyeitwa Sele ambaye aliichukia sana ile tabia ya Tusa kuwa facebook muda wote.
SELE: Kwakweli Tusa hiyo tabia yako siipendi, hakuna muda tunaoongea vizuri muda wote wewe na simu tu.
TUSA: Jamani nachat na rafiki zangu.
SELE: Huo mtandao siupendi Tusa, au unanidharau kwavile sijasoma kama wewe.
Tusa alikuwa hapendi kusemwa kuhusiana na swala la facebook, mara nyingi alikuwa anaenda kulalamika kwa dada yake aliyeitwa Tina ambaye alikuwa ni mtoto wa mama yake mkubwa.
TUSA: Ila Sele anakera sana dada.
TINA: Tatizo lako Tusa hutaki kuachana na huyo Sele, mwanaume gani huyo hata aendani na wewe.
TUSA: Sasa unataka niwe na nani? Hata hivyo Sele nampenda.
TINA: Nitakutafutia pedeshee mdogo wangu, kwa jinsi ulivyo na mvuto ni wakati wa kutengeneza pesa sio kukalia uzuri wako kwa mtu kama Sele.
TUSA: Simtaki yeyote zaidi ya Sele tu.
Siku zote Tusa alikuwa anajazwa ujinga na Tina.
Patrick aliamua kutembelea ndugu, jamaa na marafiki wa pale Mwanza ambao wote walimshangaa Patrick jinsi alivyobadilika.
Akiwa kwa rafiki yake John wanaongea.
PATRICK: John, yani wewe na simu tu muda wote.
JOHN: Nyie wenzetu mshatoka kimaisha, wenzenu tunajiliwaza tu humu.
PATRICK: Acha vituko John, unajiliwaza vipi na simu?
JOHN: Nipo facebook, kuna binti flani hivi anaitwa Tusa namfukuzia kinoma.
PATRICK: Hahaha, kweli John wewe ni domo zege, yani mademu wote mtaani huwaoni hadi uwafukuzie wa huko facebook?
JOHN: Hujui tu Patrick kuna mademu wana mvuto humu balaa.
PATRICK: Aah!! Huwa naisikia tu hiyo facebook, basi na mi niungie niwe nawaona hao mademu.
JOHN: Poa, ngoja nikufungulie sasa hivi kwa namba yako ya simu. Na wewe ulivyo kicheche nadhani utataka kuwalamba wote wewe.
Wakaanza kucheka, huku John akimuunganisha Patrick na facebook.
PATRICK: Ila mi sio kicheche bhana, nitajiunga ili kuwaangalia tu ila sina hata haja nao.
Patrick alirudi nyumbani kwao huku jina la Tusa likitembea kwenye fikra zake.
Patrick alirudi nyumbani huku jina la Tusa likitembea kwenye fikra zake.
Alipokuwa nyumbani kwao, akajaribu kuingia facebook ili amuone huyo Tusa. Alipoandika jina, wakaja Tusa wengi wengi, akashindwa kutambua Tusa aliyetajwa na John ni yupi, akaingia kwa John napo akakuta John ana marafiki watatu wenye jina hilo la Tusa. Akakuta,
=> Tusa Adam
=> Tusa the cute baby
=> Tusa the daughter of P&A.
Na akaona kuwa wote watatu wanaufanano. Nia kubwa ya Patrick ni kumjua huyo Tusa aliyetajwa na John. Ikabidi apange kesho yake kwenda tena kwa John ili akapate maelezo ya kutosha kumuhusu huyo Tusa, alitaka kujua ni kwanini John amepagawa na binti huyo.
Patrick alimfata John kama alivyopanga, alipofika wakapiga story za hapa na pale.
PATRICK: Jana nilikusikia ukimtaja binti mmoja hivi wa kwenye facebook, je ndio demu wako?
JOHN: Unamsema Tusa? Hapana si demu wangu ila narusha ndoano ni mgumu kweli.
PATRICK: Hebu nione picha yake.
John akaifungua picha ya Tusa na kumpa Patrick aiangalie, nia kubwa ya Patrick ni kuona Tusa anatumia jina lipi mbele zaidi ya Tusa. Akaona imeandikwa Tusa the cute baby. Akalishika hilo jina vilivyo.
PATRICK: Ni mkali kweli John.
JOHN: Umeona alivyo kifaa, yani siachi hadi anikubali.
PATRICK: Nipe namba zake za simu nikusaidie kumwaga swaga.
JOHN: Ninazo basi!! Amenigomea kunipa. Hata kama ningekuwa nazo nisingekupa sela.
Wakawa wanacheka ila Patrick akawa ameshamjua huyo Tusa anayemuhitaji.
Akarudi kwao na kumsikia mama yake akizungumza na Anna.
DEBORAH: Namshukuru Mungu kwakweli tangu Patrick arudi sijamsikia kabisa habari ya baba.
ANNA: Labda ameshamjua.
DEBORAH: Hakuna anayemjua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara Patrick akaingia ndani na kuwafanya wote washtuke, akawasalimia na kuingia chumbani. Jina la Tusa liliendelea kucheza kwenye akili yake, alienda moja kwa moja na kuingia facebook, akatafuta jina na kumuona kwakweli akavutiwa nae sana, picha nyingi za Tusa ziliendelea kumvuta Patrick, akaamua kumuomba urafiki. Ila hakukubaliwa ombi lake kwa siku hiyo, aliendelea kuangalia tu picha za Tusa. Akakumbuka kuwa muda wake wa kukaa Mwanza umeisha, inambidi apange safari ya kurudi tena Arusha.
Wazo lingine likamjia kuwa amtumie ujumbe Tusa ili ajaribu kama atamjibu.
Tusa akiwa na Tina kama kawaida yao.
TUSA: Sipendi watu wanaoomba urafiki bila ya picha.
TINA: Mwingine tena amekutumia?
TUSA: Ndio anaitwa Patrick, tena inaonyesha ni mgeni kwenye huu mtandao maana limenitumia na meseji eti unaitwa nani.
TINA: Hahaha, Mkubalie tu umfundishe mji Tusa, inakuwaga mijinga hiyo, inamaana hajaona jina lako hapo juu!
TUSA: Labda ni account fake.
TINA: Kama fake si utamblock tu, wee mkubalie kwanza, litakuwa jinga hilo.
Tusa akaamua kukubali ombi la urafiki toka kwa Patrick.
TUSA: Nishalikubalia.
TINA: Hiyo ndio mimbulula Tusa, unaweza ukalidanganya chochote humo.
Waliongea mengi bila kujua furaha ya Patrick ya kukubaliwa urafiki na Tusa, akajisemea kuwa atahakikisha anampata huyo Tusa hata awe mgumu wa kiasi gani.
Patrick alianza kutumiana ujumbe na Tusa na kufanya nae mazungumzo ya mara kwa mara kwenye mtandao ila kila akijaribu kumuomba namba ya simu Tusa alionyesha kuwa mgumu kutoa namba yake.
Siku ikafika ya Patrick kurudi Arusha, akaamua kumuaga mama yake na kumauachia pesa kiasi za kumsaidia hapo nyumbani. Halafu akamkataza mama yake kufanya kazi aliyokuwa anaifanya, kazi ya usafi kiwandani.
DEBORAH: Kwanini mwanangu umenikataza kwenda kwenye kazi?
PATRICK: Ile kazi haikufai mama yangu, naomba upumzike kwa sasa. Nitakuwa nakutumia pesa kila mwezi, na ukiwa na shida yoyote niambie.
DEBORAH: Ila mwanangu, ile kazi nimeifanya miaka na miaka.
PATRICK: Naelewa mama, ila haikufai tena. Nitakutumia pesa nyingine ya biashara ila sitaki uende tena kwenye ile kazi mama.
DEBORAH: Sawa mwanangu.
PATRICK: Ila kitu kimoja nakuomba mama yangu.
DEBORAH: Kitu gani tena Patrick.
PATRICK: Nikirudi tena niandalie maelezo ya kutosha kuhusu baba yangu na Maiko.
DEBORAH: Mmh mwanangu!!
PATRICK: Ndio hivyo mama, nataka kujua ukweli.
Akili ya Patrick iliwaza vitu vingi sana, maneno ya Maiko kuwa mama yake alimuibia pesa yalimjia mara kwa mara. Nyumba aliyoishi na mama yake ilikuwa ni nzuri ukilinganisha na kazi, na akajiuliza sana kama mama yake aliiba pesa na kwanini akafanya kazi ya usafi, na pia kwanini Maiko hakumtafuta Deborah siku zote hadi alipomnasa yeye Arusha. Kwakweli Patrick aligubikwa na maswali mengi ambayo alijua wazi majibu ya maswali hayo anayo mama yake bi. Deborah na bwana Maiko, alihitaji kufanya uchunguzi kwa siri na kuwauliza taratibu labda aweze kupata majibu ya maswali yake.
Safari ya Patrick ikakamilika na kumuaga mama yake na kuondoka zake kurudi Arusha.
Alipokuwa Arusha hakuacha kuendelea kuwasiliana na Tusa kwenye facebook.
Siku moja Maiko alimkuta Patrick akiwa na mawazo sana, alipomuuliza Patrick akamueleza kuhusu Tusa.
MAIKO: Sasa tatizo ni nini?
PATRICK: Hataki kunipa namba zake za simu.
MAIKO: Tatizo dogo sana hilo, nitakufundisha njia rahisi ya kupata namba zake na atakupa mwenyewe bila hata ya kumlazimisha.
PATRICK: Njia gani hiyo?
Patrick alihitaji sana kujua njia ambayo Maiko angempa ili aweze kumpata Tusa.
PATRICK: Niambie hiyo njia basi.
MAIKO: Patrick, Patrick. Unajua mtu mwenye pesa yu tofauti kabisa na mtu asiye na pesa?
PATRICK: Niambie basi.
MAIKO: Hakuna mwanamke anayeweza kukubabaisha ukiwa na pesa, Patrick wewe ni level nyingine sasa na unauwezo wa kumpata mwanamke yeyote umtakaye. Kwahiyo swala la huyo Tusa ni dogo sana, halafu umesema ni binti mrembo eeh!!
PATRICK: Ndio ni mrembo, tena ni mrembo sana.
MAIKO: Oooh!! Kama ndio hivyo nitakusaidia kumpata pale utaposhindwa niambie maana huyo anaweza kuwa msaada tosha kwenye kazi yetu.
PATRICK: Atatusaidiaje sasa?
MAIKO: Usijali, ukishampata nitakwambia. Ngoja nikupe njia za kumpata huyo mrembo wako.
Maiko akamfundisha Patrick njia kadhaa za kupata namba za Tusa na hatimaye kumpata kabisa na kumuweka katika himaya yake.
Patrick akaanza kutumia njia hizo kwa kasi ya ajabu.
Tusa akiwa amekaa nyumbani kwao, huku simu yake ikiwa kiganjani akifanya mawasiliano na Patrick kwa njia ya facebook.
PATRICK: Nikufanyie kitu gani Tusa ili unipatie namba yako?
TUSA: Sijui.
PATRICK: Naomba nifanye deal na wewe.
TUSA: Deal gani?
PATRICK: Nitakutumia namba za vocha uingize kwenye simu yako, halafu ukizipata unitumie namba zako ili nimalizie nusu ya vocha hiyo kwa kukurushia.
TUSA: Hebu tuma nione.
PATRICK: Unatumia mtandao gani?
TUSA: Natumia tigo.
PATRICK: Basi ingiza, 4262 6698 2898 195.
TUSA: Poa.
Tusa akaichukua hiyo namba ya vocha na kuingiza kwenye simu yake, mara gafla akapiga ukelele wa kicheko uliomshtua mama yake.
PAMELA: Jamani, laiti kama huyo mwanzilishi wa facebook angejua shida ninayopata huku nyumbani angeufunga kabisa huo mtandao, maana mwanangu unakaribia kuwehuka, unaongea mwenyewe na kucheka mwenyewe nikiuliza nini najibiwa facebook loh!!
TUSA: Sio hivyo mama.
PAMELA: Ila ni nini?
TUSA: Kuna rafiki mpya nimempata humu facebook ameniomba namba zangu nimegoma kumpa, amenitumia namba ya vocha. Nikajua utani mama kumbe ni kweli, maana nimeingiza imesoma elfu tano.
PAMELA: Jamani mwanangu hebu nirushie buku na mimi maana simu yangu haina hata hela.
TUSA: Mama nawe tamaa tu, tena ameniambia kuwa nikimtumia namba atanimalizia nusu ya vocha kwa kurusha kwahiyo atanitumia elfu tano nyingine.
PAMELA: Kheee mwanangu hebu mtumie na mie unirushie elfu mbili.
TUSA: Kheee mama!! Unapenda vya bure wewe, mi sitaki kutoa namba yangu.
PAMELA: Kama wewe hutaki mtumie yangu basi.
TUSA: Hahahaha, utapigwa na baba wewe. Namtumia yangu bhana.
PAMELA: Mtumie tu, kwani namba kitu gani Tusa? Unaogopa nini? Mtu mwenyewe hakujui mwanangu.
TUSA: Namuogopa Sele mama.
PAMELA: Hebu usiniletee hicho kichefuchefu chako cha huyo mlanda mbao, sitaki hata kumsikia.
Pamela alikuwa ni mmoja kati ya watu waliopinga mapenzi ya Tusa na Sele, kwavile Tusa na mama yake walikuwa kama marafiki kwahiyo mambo mengi ya Tusa, Pamela aliyajua.
Alimpinga sana Tusa kuwa na Sele kwasababu moja tu, nayo ni kuwa Sele hakusoma kama Tusa.
Tina nae alifikia kwenye mazungumzo hayo,
TINA: Nimesikia yote Tusa, na mimi nirushie jero basi.
TUSA: Mmh!! Wewe Tina na huyu mamako mdogo mnaweza kumteketeza mtu kwaajili ya pesa nyie.
TINA: Acha maneno mengi Tusa, mtumie hiyo namba na mimi unipunguzie vocha.
Tusa akamtumia Patrick namba yake ya simu na Patrick akafanya kama alivyomuahidi ili kuzidi kumvuta Tusa na fikra zake.
Patrick akampigia simu Tusa na kuzungumza nae mawili matatu na hiyo ikawa furaha yake.
Mawasiliano ya Tusa na Patrick yakawa ya mara kwa mara.
Patrick alifurahi sana na kuisifu pesa kuwa kweli inaweza kununua kila kitu.
MAIKO: Umefanikisha eeh!! Chezea mwanamke na pesa wewe.
PATRICK: Dah!! Kweli wanawake wananunulika kirahisi baba.
MAIKO: Ukiwa na pesa kila kitu kinakuwa kwenye mstari Patrick.
PATRICK: Na kwanini unaona kuwa ni vyema kutumia pesa katika kumpata mwanamke?
MAIKO: Sikia Patrick, tamaa ya mwanamke ipo kwenye pesa. Halafu kitu kingine ni kuwa unapompa pesa mwanamke kuna kitu unajenga juu yake?
PATRICK: Kitu gani?
MAIKO: Unajenga hasira juu yake, na hiyo ni kwamaana kwamba akikukataa wakati ushatupa pesa yako nyingi kwake, unakuwa tayari kufanya chochote ili kumpata. Hata kumdhuru unaweza.
PATRICK: Mmh!! Kumdhuru mtu umpendaye tena?
MAIKO: Patrick, vyote hufanywa kwa nguvu ya pesa. Pesa inauma sana, kwahiyo akikuzingua unakuwa na hasira naye vilivyo na hapo ndipo mwanamke anaanza kujutia tamaa yake.
PATRICK: Ila mi sitaki yafikie huko.
MAIKO: Nakushauri uendelee kumvuta kwa pesa Patrick, halafu akikuzingua utaona nguvu ya pesa itakachofanya.
PATRICK: Na vipi kuhusu wewe na mama yangu?
MAIKO: Deborah ni mwanamke mrembo sana, ila mambo ya mimi na yeye ni siri yetu.
Maiko alimwambia mambo mengi sana Patrick, ila mambo yake yeye na Deborah aliendelea kuyafanya kama siri.
PATRICK: Ila nitahakikisha mpaka nampata.
MAIKO: Ukishindwa nitakupa msaada wa ziada Patrick.
PATRICK: Nitampata bhana, na huyo mwanaume wake nikimjua atanikoma.
MAIKO: Hahahaha, ushammiliki tayari duh!! Ila usijari ukishindwa nipo mimi kukusaidia Patrick.
Maiko alikuwa akifanya mambo ya ajabu zaidi ambayo Patrick hakuyajua.
Patrick alitamani sana kujua vitu zaidi alivyofanya Maiko ndiomana alipenda kuwa nae karibu mara kwa mara.
Sele hakuacha kumlaumu Tusa kwa kuiendekeza facebook.
SELE: Laiti kama ningeweza, ningeufunga huo mtandao wa facebook. Tusa hunisikilizi wala nini.
TUSA: Jamani Sele!!
SELE: Jamani nini Tusa? Kiukweli unanikera tena unanikera sana.
Mara simu ya Tusa ikaanza kuita, Sele akampora Tusa ile simu, kuangalia mpigaji akaona jina "Patrick fb" ile simu iliita hadi ikakatika.
SELE: Patrick ndio nani Tusa?
TUSA: Ni rafiki yangu kwenye facebook.
SELE: Aaaargh, hiki ndio kitu nilichokuwa nakipinga Tusa.
Mara simu ikaanza kuita tena na mpigaji ni yuleyule, Sele akaamua kuipokea ile simu.
Mara simu ikaanza kuita tena na mpigaji ni yuleyule. Sele akaamua kuipokea ile simu.
SELE: (kwa ukali), Nani wewe?
PATRICK: (huku akicheka), Mpe mwenye simu ananijua.
SELE: Anakujua nini? Sema wewe ni nani?
PATRICK: Kama ulivyo wewe kwake na mimi ndio hivyo hivyo.
SELE: Aaaarghh!!
Akakata ile simu kwa hasira na kuizima kabisa. Akataka kuitupa chini, Tusa akaiwahi.
TUSA: Tafadhari Sele mpenzi usifanye hivyo.
SELE: (Akiongea kwa hasira), kwanini Tusa, kwanini unanitenda hivi? Kwanini unanidharau Tusa?
TUSA: Nisamehe mpenzi tafadhari.
SELE: Kukupenda imekuwa shida Tusa? Au kwavile wewe ni binti mrembo Tusa? Kwanini unifanyie hivi Tusa?
TUSA: Jamani Sele, nisamehe.
SELE: Natamani kuivunja hii simu yako au kuikatakata kabisa line yako kwa upumbavu wako.
TUSA: (kwa sauti ya upole na kubembeleza), Nisamehe mpenzi, haitajirudia tena. Niamini baby.
Kwakweli Sele alichukizwa sana kwani Tusa ni mwanamke aliyemuamini. Ila ikambidi amsamehe kwavile alikuwa akimpenda sana.
Tusa akiwa nyumbani kwao, akamwambia Tina mambo yaliyomsibu kwa Sele.
TUSA: Yani ilibakia kidogo tu Sele avunje simu yangu.
TINA: Huyo Sele wako nae ni fala sana, avunje simu kwani ameinunua yeye? Janaume lenyewe randambao bora uachane nae tu Tusa.
TUSA: Siwezi fanya hivyo Tina, nampenda sana Sele. Yeye ndiye mwanaume nimpendae.
TINA: Fikiria na future yako Tusa, utakula mapenzi ndani? Pesa ndio kila kitu, kama mwanaume hana pesa ujue hakufai.
TUSA: Ila tunapendana dada, na niko tayari kula chochote ambacho tutapata na Sele.
TINA: Mtakula na uchafu nyie, shule yenyewe la saba, kazi mranda mbao. Atakupeleka wapi huyo Tusa? Utaishia kuhongwa elfu tano na elfu kumi tu na yeye wakati wenzio wanapata mihela.
Mara simu ya Tusa ikaita, kuangalia ni Patrick alikuwa anapiga.
TUSA: Umenisababishia makubwa sana Patrick, si nilishakwambia nina mtu wangu?
PATRICK: Ooh!! Samahani Tusa, ngoja nikutumie samahani yangu.
Halafu akakata simu, Tusa akamgeukia Tina na kumwambia.
TUSA: Hata sijamuelewa huyo Patrick, eti anasema ananitumia samahani yake.
Mara meseji ikaingia kwenye simu ya Tusa, alipoiangalia ilikuwa inatoka kwenye Tigopesa.
TUSA: Ona Tina, sijui Tigo wamenitumia mimeseji yao.
Tina akaichukua ile simu na kufungua ule ujumbe.
TINA: Khaaaa!!
TUSA: Nini Tina?
TINA: Umetumiwa laki moja na Patrick.
Tusa akachukua ile simu ili aweze kuhakikisha, akaona ni kweli.
TUSA: Mmh!! Patrick ni mtu wa ajabu sana, hata hanijui kanitumia pesa yote hii!!
TINA: Patrick anakufaa Tusa, yani kakutumia pesa nyingi hivi hujamuomba, ukimuomba je? Itabidi na mimi unipe ya bia mbili tatu.
Mama yake na Tusa akawasikia na yeye akadakia.
PAMELA: Na kwenye huo mgao msimsahau mama mzaa chema.
Wote wakaanza kucheka.
TINA: Mamdogo nawe hupitwi!!
TUSA: Alivyo na tamaa atapitwa wapi?
PAMELA: Wajinga kweli nyie, tena mgao huo mie ndo nipate pakubwa.
Tusa akawa amepunguza jazba yote aliyonayo juu ya Patrick, na hapo akampigia simu na kumshukuru.
PATRICK: Usijari Tusa, mambo madogo hayo.
Tusa akawa kama mtu aliyewekwa kwenye mtego kwani Sele anampenda, na pesa ya Patrick anaipenda pia.
Patrick akajivunia kweli nguvu ya pesa inavyofanya kazi.
PATRICK: Dah, kweli bhana nimeamini kuwa pesa ndo kila kitu. Unaweza nunua vyote vya hapa ulimwenguni.
MAIKO: Umeona Patrick, pesa ndo kila kitu. Na kitu kinachouma ni kupoteza pesa, usione mtu anakamata mwizi na kumpiga hadi kumuua yote hiyo ni pesa, pesa inauma Patrick.
PATRICK: Maneno yako huwa yana mafumbo ndani yake, unamaana gani?
MAIKO: Mpe Tusa pesa afurahi na aridhike ila asithubutu kukukataa kwamaana atajuta.
PATRICK: Sitegemei kama Tusa atanikataa milele, Tusa ndio mke wangu na lazima nimuoe Tusa iwe isiwe.
MAIKO: Hapo ndipo ninapoyapendea mapenzi, ila mwanamke huwa haeleweki Patrick. Ni lazima umdhibiti vilivyo.
PATRICK: Nimekuelewa, ila nitafanya kila njia ili Tusa awe wangu.
Wazo kubwa la Patrick kwa kipindi hicho ni kumpata Tusa tu, alitaka ampate Tusa kwanza ndio aanze kufatilia mambo mengine.
Tusa akiwa katulia nyumbani kwao, akaona ujumbe mwingine toka Tigopesa kuwa katumiwa laki moja na nusu toka kwa Patrick. Na mara akapokea ujumbe toka kwa Patrick kuwa amemtumia pesa hiyo kwa matumizi madogo madogo.
Hela ikawa inamchanganya akili Tusa, akaweka mawazo mengi akilini mwake na kumwambia Tina.
TUSA: Kuna kitu nimefikilia kuhusu Patrick.
TINA: Kitu gani?
TUSA: Nimeamua kumbadili jina Patrick kwenye simu yangu ili Sele asimgundue tena.
TINA: Sawa sawa Tusa, tena umsave jina la kike ili Sele akiona ajue ni shoga yako.
TUSA: Jina gani sasa?
TINA: Andika Maria.
TUSA: Ila Sele hamjui rafiki yangu mwenye jina hilo.
TINA: Kwani Sele atawajua rafiki zako wote bhana!! Mwandike hivyo au utasahau kama ni yeye? Basi kama vipi muandike Patricia.
TUSA: Ndio, nadhani Patricia itakuwa rahisi kumkumbuka kuwa ni nani.
Tusa akabadili jina la Patrick kwenye simu na kuandika Patricia, huku yeye na nduguye Tina wakicheka kwa furaha.
Kesho yake Tusa akaitwa na Sele na kwenda kumtembelea, wakaongea mambo mengi kuhusu mapenzi yao.
Sele akachukua simu ya Tusa na kuikagua kama kawaida yake, ila Tusa alikuwa mjanja siku hiyo kwani simu yake haikuwa na meseji hata moja, alikuwa amefuta meseji zote, kwani aliona uvivu kufuta moja moja na anajua wazi kuwa Sele anapenda kuikagua simu hiyo.
Wakati Sele ameishika ile simu mara ikaingia meseji, kuangalia imetoka kwa Patricia, Sele akaifungua na kuisoma.
"kama ukiwa na tatizo lolote mpenzi niambie, na kumbuka kwamba nakupenda sana"
Wakati Sele ameishika ile simu, mara ikaingia meseji, kuangalia imetoka kwa Patricia. Sele akaifungua na kuisoma,
"kama ukiwa na tatizo lolote mpenzi niambie, na kumbuka kwamba nakupenda sana"
Sele akamuangalia Tusa kwa makini na kumuuliza.
SELE: Patricia ndio nani Tusa?
TUSA: Ni rafiki yangu.
SELE: Kwanini akutumie meseji kama hii?
Tusa akachukua ile simu yake na kuangalia meseji iliyotumwa.
TUSA: Jamani Sele!! Wivu gani huo hadi kwa wasichana wenzangu?
SELE: Kwahiyo huyo ni msichana?
TUSA: Tangu lini umesikia Patricia akiitwa mvulana? Hili ni jina la kike Sele.
SELE: Mbona akuite mpenzi na akwambie kuwa anakupenda sana?
TUSA: Usitake kunichekesha Sele, jina mpenzi kwa wasichana ni kitu cha kawaida sana. Na je kuna ubaya gani mimi kupendwa na msichana mwenzangu? Acha wivu wa kijinga Sele.
SELE: Nimekuelewa Tusa, ila yote sababu nakupenda na pia naichunga mali yangu, naogopa wajanja wa mjini wasije wakakuiba Tusa wangu.
TUSA: Usijali Sele, wewe ndie mwanaume nikupendae.
SELE: Natumai huwezi kushawishika mpenzi.
TUSA: Siwezi mpenzi.
Mara meseji kutoka Tigopesa ikaingia kwenye simu ya Tusa kuwa katumiwa laki tatu na Patrick Mwamba. Baada ya Tusa kuisoma, Sele nae akataka kuiona ikabidi amkabidhi ili aweze kuisoma.
SELE: Na huyu Patrick Mwamba ndio nani Tusa?
TUSA: Atakuwa wakala wa Tigopesa, maana baba alisema atanitumia pesa nadhani ndio kamtumia huyo wakala.
SELE: Sasa pesa hii babako kakutumia ya nini mpenzi?
TUSA: Ni ya matumizi nyumbani maana baba hayupo kasafiri.
Sele hakuwa na budi zaidi ya kukubaliana na maneno ya Tusa kwasababu alimpenda sana.
Tusa alirudi kwao akiwa na furaha sana, alijikuta akitabasamu muda wote ama kweli pesa ni tamu sana. Mama yake akaamua amuulize maswali mawili matatu.
PAMELA: Mwanangu nakuona siku hizi mambo sio mabaya, nani anafanya yote hayo?
TUSA: Si yule kijana wa Arusha mama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
PAMELA: Ila kweli watu wa Arusha wana pesa sana mwanangu, mng'ang'anie huyo kijana.
TUSA: Ila nampenda Sele mama.
PAMELA: Tusa acha ujinga mwanangu, unadhani Sele ataweza kukuoa? Ataweza kutoa mahari tutakayomtajia? Sele hajiwezi mwanangu, achana nae, angalia maisha bora na yanayofaa nadhani huyo kijana wa Arusha atakufanya uwe mwanamke wa kuvutia siku zote na sio Sele, atakuzeesha mwanangu.
TUSA: Kwani wewe ulimpenda baba sababu ya pesa?
PAMELA: Mimi na baba yako historia yetu ni ndefu sana nikikuelezea naweza kumaliza kitabu.
TUSA: Mmh!! Mama niambie kidogo.
PAMELA: Kwanza kabisa baba yako alikuwa mume wa mtu na huyo mkewe alikuwa ni rafiki yangu kipenzi nadhani hadi leo hajui kama mimi ndio nilimchukua mumewe, ni kitambo sana, baba yako alikuwa na pesa kiasi ila tamaa ilimtawala sana. Ipo siku nitakwambia mwanangu, usijari.
TUSA: Mmh!! Mama yangu na wewe ni kiboko ila najua kuwa uliolewa nae kwakuwa mnapendana.
PAMELA: Mwanangu, weka hili akilini mwako, si kila anayeamua kuoa au kuolewa basi amependana na mwenza wake, mara nyingine huwa tunafanya ili kutimiza wajibu ila mkifika ndani mnajifunza kupendana na ndoa yenu inadumu. Kijana wa Arusha anakufaa mwanangu, hata kama humpendi, utajifunza taratibu kumpenda ukiwa nae.
TUSA: Ila mama siwezi kumuacha Sele.
PAMELA: Mwanangu, Sele hakufai. Sijui nitumie lugha gani upate kunielewa.
Kwakweli Tusa alimpenda sana Sele, ila tamaa ya pesa na maneno ya watu ndio vinavyoichanganya akili yake ili iwe inatoka taratibu kwa Sele. Furaha ya Tusa ni kuwa karibu na Sele, alipenda sana Sele ndio awe mume wake.
Patrick aliona sasa mambo yake yakiwa kwenye mstari ulionyooka, mstari alioutaka yeye.
PATRICK: Sijui niende dar kumfata Tusa?
MAIKO: Hapana Patrick, ukienda dar kazi hapa italala cha muhimu mwambie Tusa aje Arusha.
PATRICK: Unadhani itakuwa rahisi kwa Tusa kuja Arusha?
MAIKO: Atakuja Arusha tu kwa nguvu ya pesa.
PATRICK: Inawezekana kweli?
MAIKO: Inawezekana Patrick, nitakupa maneno ya kumshawishi. Atakuja mwenyewe nakwambia.
PATRICK: Nitafurahi sana akija.
MAIKO: Usijali Patrick.
Patrick akaona ni vyema afate mawazo ya Maiko na kumuomba Tusa aende Arusha kwani Maiko alimpa maneno mazuri na ya kumteka mtu kimawazo.
Patrick akampigia simu Tusa na kumwambia nia yake.
TUSA: Mmh!! Patrick sidhani kama ni vyema mimi kuja huko.
PATRICK: Tafadhari Tusa nakuomba uje, nia yangu ni kuonana tu mimi na wewe.
TUSA: Halafu nini kitaendelea?
PATRICK: Hakuna chochote kitakachoendelea sababu tukishaonana unaweza kurudi kesho yake dar.
TUSA: Halafu nitalala wapi?
PATRICK: Nitakukodia hotel Tusa, sina nia mbaya na wewe. Shida yangu ni kuonana tu.
TUSA: Na wewe utalala wapi?
PATRICK: Mimi nitalala nyumbani kwangu Tusa, nitafanya hivyo ili uwe huru zaidi.
TUSA: Mmh!! Ila naogopa kuja huko!!
PATRICK: Usijali Tusa, nitakutumia tiketi ya ndege ya go and return kwahiyo usiwe na shaka kabisa.
TUSA: Sawa nimekubali, nitakuja Arusha.
Simu ilipokatika tu, Tusa akatumiwa meseji ya pesa na Patrick, akatumiwa shilingi laki tano kitu ambacho kilizidi kumpagawisha Tusa.
Halafu akapokea meseji toka kwa Patrick,
"Hiyo pesa ni kwaajili ya maandalizi yako na mahitaji yako kadhaa ya kuja Arusha."
Kiukweli pesa ilichanganya kabisa akili ya Tusa, aliona ikihamia upande mwingine kabisa.
Ilikuwa ni furaha sana kwa Patrick,
PATRICK: Dah!! Kwakweli wewe bosi ni noma jamani, unawajua vipi hawa wanawake na udhaifu wao?
MAIKO: Patrick, mimi niliweza kuwa na mama yako, ukiona mwanaume amefanikiwa kuwa na Deborah ujue huyo mwanaume ni balaa, mama yako ni mgumu sana Patrick.
PATRICK: Bado najiuliza ulimfanya nini mama mpaka anakuchukia kiasi hicho?
MAIKO: Ni historia ndefu sana Patrick, ila ipo siku najua utaijua. Na mbona hutaki kunipa mawasiliano ya mama yako?
PATRICK: Wee, sitaki kabisa ajue kama nafanya kazi kwako. Anaweza kufa kwa presha jinsi anavyokuchukia.
Patrick akainuka na kwenda kuangalia mambo mengine, ila alisahau simu yake kwa Maiko.
Wakati Maiko yupo na simu ya Patrick, mara ikaanza kuita, kuiangalia jina la mpigaji limeandikwa "mama".
Maiko akapata shauku na kuipokea kwakuwa alijua kwa vyovyote vile mpigaji yule atakuwa Deborah tu.
Wakati Maiko yupo na simu ya Patrick, mara ikaanza kuita, kuangalia jina la mpigaji limeandikwa "mama".
Maiko akapata shauku ya kuipokea kwakuwa alijua kwa vyovyote vile mpigaji yule atakuwa Deborah tu.
Akaitazama ile simu na kuipokea, ile kusema "hallow Deborah" akatokea Patrick kwa nyuma na kumnyang'anya ile simu na kuiangalia kisha akaikata.
PATRICK: Jamani Maiko kwanini hupendi kunielewa? Kwanini upokee simu yangu?
MAIKO: Nilitaka kuisikia sauti ya Deborah tu.
PATRICK: Utaniulia mama yangu bhana, sitaki huo mchezo. Umeamua kunitumikisha mimi basi inatosha achana na mama yangu kabisa.
MAIKO: Patrick, Patrick. Mimi sikutumikishi bali nakuonyesha raha ya utajiri.
Simu ya Patrick ikaita tena, ikabidi Patrick asogee mbali kuongea nayo.
DEBORAH: Nani alipokea mwanzo?
PATRICK: Ni mimi mwenyewe mama.
DEBORAH: Na mbona ukaikata?
PATRICK: Ni network mama.
DEBORAH: Patrick, usinifanye mjinga. Kuna sauti nimeisikia tena ni ya mtu ninayemfahamu.
PATRICK: Niamini mama, ilikuwa ni mimi.
DEBORAH: Na mbona ukaniita Deborah? Toka lini umeanza kuniita hivyo?
PATRICK: Mama itakuwa umesikia vibaya sababu ya mawimbi, niamini mama yangu.
DEBORAH: Natumai unaongea ukweli Patrick, napenda kukukumbusha kwamba kaa mbali na Maiko. Maiko si mtu mzuri.
PATRICK: Sawa mama nimekuelewa.
Patrick alikuwa anajiuliza maswali mengi sana juu ya Maiko ila alikosa majibu ya maswali yake.
Tusa alikuwa akijipanga kwaajili ya safari ya kwenda Arusha, ikabidi aende kumuaga Sele ili asiwe na wasiwasi.
Katika kumuaga Sele alimuongopea kuwa anaenda Bagamoyo kwa shangazi yake.
SELE: Kwahiyo unategemea kurudi lini?
TUSA: Sitakawia sana, kama siku mbili tatu.
SELE: Vipi mawasiliano huko?
TUSA: Mmh!! Sehemu yenyewe ni huko Bagamoyo ndanindani ni Kijijini sana sijui hata kama kuna network.
SELE: Nitakumiss sana mpenzi wangu.
TUSA: Usijari mpenzi, nikirudi nitakubebea na zawadi za huko.
Mara Tusa akafungua mkoba wake na kumpa Sele pesa kama laki mbili hivi.
SELE: Umenipa za nini sasa hizi?
TUSA: Baba amenitumia pesa nyingi ya matumizi, ndio nimeamua kukupa na wewe kidogo.
SELE: Hivi Tusa, baba yako anakupa pesa nyingi hivi kwa misingi gani?
TUSA: Jamani mimi ndio mtoto wake wa kwanza halafu nimekubali kwenda kwa dada yake huko kijijini ndiomana akanitumia pesa kama kunifurahisha.
SELE: Je huwezi kufurahi bila ya pesa? Na hii pesa uliyonipa mimi nifanyie nini?
TUSA: Ni matumizi tu mpenzi wangu.
SELE: Ili badae useme mwanaume mwenyewe suruali hadi nimuhonge mie? Baba yako amekupa pesa ili usipatwe na vishawishi, nenda tu kaitumie mwenyewe mpenzi wangu.
TUSA: Hapana Sele, mimi nimekupa wewe bhana.
SELE: Hii pesa sitaitumia Tusa bali nitaiweka, siku ukiishiwa njoo uichukue.
TUSA: Mmh!! Sele!!
Mawazo ya Tusa kwa muda huo ilikuwa ni juu ya safari ya kwenda Arusha tu.
Aliporudi kwao ikabidi apange na mama yake mpango murua wa yeye kuwa Arusha.
Akampatia kiasi cha shilingi laki mbili mama yake ili apate kumdanganya mumewe pindi atakaporudi.
TUSA: Sasa mama utamwambia baba kuwa nimeenda wapi?
PAMELA: Mambo ya baba yako niachie mimi tu, nitayarekebisha hata usijari.
TUSA: Maana akigundua atagomba huyo.
PAMELA: Usijari, nikimnunulia bia mbili tatu yule hana usemi tena.
Tusa akapokea meseji toka Tigopesa kuwa amepokea laki tano nyingine toka kwa Patrick, na ikafata meseji toka kwa Patrick mwenyewe.
"Mpenzi ongezea pesa hiyo kwenye maandalizi yako"
TUSA: Mama amenitumia pesa nyingine.
PAMELA: Dah!! Huyo mwanaume kweli anakupenda mwanangu.
TUSA: Nitakupunguzia laki mbili nyingine na wewe upate ya kuumia mama.
PAMELA: Ooh!! Ndio raha ya kuzaa mtoto wa kike hii. Upo mmoja lakini nafaidi, ingekuwa na wale wadogo zako ni wakike ningekuwa tajiri jamani.
TUSA: Mama nawe loh!!
PAMELA: Ndio hivyo mwanangu, hii ndio faida yangu kama mzazi. Najivunia kuwa nawe.
Tusa akawa anafanya maandalizi ya safari ya kesho kwenda Arusha kuonana na Patrick.
Deborah akiwa nyumbani kwake, alijikuta akiwa na mashaka sana juu ya Patrick huko Arusha, akawa anamwambia na dada yake Marium.
MARIUM: Kwani wasiwasi wako nini na huko Arusha?
DEBORAH: Maiko dada, kwakweli Maiko anayatesa mawazo yangu. Namuwazia vibaya Patrick kuwa yuko na Maiko.
MARIUM: Kwani kuna ubaya gani akiwa na Maiko?
DEBORAH: Maiko ni mtu mbaya sana dada yangu, Maiko hafai, hafai kabisa duniani. Ooh!! Mwanangu jamani? (huku machozi yakimlengalenga).
MARIUM: Jamani, Patrick ni mzima halafu unamlilia Deborah, kwanini?
DEBORAH: Namlilia marehemu mwanangu, dada hujui chochote. Roho inaniuma kila nikikumbuka kifo chake, najua ni Maiko tu ndiye alisababisha.
MARIUM: Deborah, kwakweli hata sikuelewi. Umetoka kwa Patrick, umeenda kwa marehemu mwanao. Kwani umewahi kufiwa na mtoto?
DEBORAH: Ndio kipindi nikiwa Dar, nahofia Maiko atamfundisha mambo mabaya Patrick. Maiko ataniharibia mwanangu, najua hiyo ndio itakuwa nia yake.
MARIUM: Basi acha mawazo mabaya mdogo wangu, hebu nisimulie kwanza ilikuwaje hadi ukafiwa na mtoto halafu ndugu zako tusijue?
DEBORAH: Ni historia ndefu, yote yalifanyika nikiwa Dar wakati naishi na Jumanne. Ipo siku nitakwambia.
MARIUM: Kwahiyo Patrick baba yake ni nani? Jumanne au Maiko? Au yupo ambaye sisi hatumjui?
DEBORAH: Ipo siku nitakusimulia mkasa mzima na utaelewa kwanini nimekaa na siri hii miaka yote, lengo kubwa ni kujikinga mimi na mwanangu Patrick.
MARIUM: Sawa, endelea kubaki na siri yako.
Deborah alikuwa akiumia moyo sana kila akikumbuka mambo ya nyuma, alijikuta akitokwa na machozi na siri yake ilimuumiza sana maishani mwake.
Tusa alisindikizwa hadi uwanja wa ndege na mama yake pamoja na Tina.
Kwa mara ya kwanza Tusa alipanda ndege na kuelekea kwenye mji wa Arusha.
Alipotua na kushuka alifata yale maelekezo aliyopewa na mwenyeji wake, alimkuta kijana mdogo ambaye walisalimiana na kutambulishana majina kisha kuingia kwenye gari na safari ikaanza, safari ya kwenda kukutana na Patrick.
Tusa alianza kupatwa na hofu kwani sehemu walizopita zilikuwa kimya sana na ukizingatia Tusa haufahamu mji wa Arusha.
Tusa ikabidi amuulize yule kijana aliyeitwa Rashidi.
TUSA: Tunaelekea wapi?
RASHIDI: Nyumbani kwa boss.
TUSA: Nani? Patrick?
RASHIDI: Ndio boss Patrick.
TUSA: Ila makubaliano yetu haikuwa nyumbani kwake.
RASHIDI: Tulia mama, kwanza tumeshafika.
Tusa ikabidi amuulize yule kijana aliyeitwa Rashidi.
TUSA: Tunaelekea wapi?
RASHIDI: Nyumbani kwa boss.
TUSA: Nani? Patrick?
RASHIDI: Ndio boss Patrick.
TUSA: Ila makubaliano yetu haikuwa nyumbani kwake.
RASHIDI: Tulia mama kwanza tumeshafika.
Tusa akaona geti likifunguliwa na gari ikiingia ndani, hofu kubwa ikatanda moyoni mwaka.
Gari iliposimama, Rashidi akashuka na kwenda kumfungulia mlango Tusa ili ashuke, kwakweli Tusa aliona kuwa kapatikana.
Aliposhuka akawa anashangaa tu yale mazingira, palikuwa ni mahari pazuri ila palipotulia sana, akatamani hata kukimbia ila hakuwa na pa kukimbilia zaidi ya kumfata Rashidi. Wakaingia kwenye hiyo nyumba, Tusa akagomea mlangoni kuwa hawezi kuingia zaidi bila kumuona huyo Patrick, ikabidi Patrick aitwe, ambapo Patrick alifika pale mlangoni na kumtazama Tusa, aliutazama uzuri wa Tusa, kwakweli alikubali kuwa Tusa ni binti mrembo.
PATRICK: Wow Tusa, karibu ndani.
TUSA: Ila haya si makubaliano yetu Patrick.
PATRICK: Usijali Tusa, yote tutayazungumza pamoja.
Tusa akakaribishwa mule ndani, ambako kulikuwa na vitu vingi vya thamani. Tusa alikuwa bado hajiamini wala hajielewi, yule Rashidi aliyempeleka pale akatoka nje na kuondoka, kwahiyo ndani akabaki Tusa na Patrick.
TUSA: Kwahiyo wewe ndio Patrick?
PATRICK: Ndio mimi Tusa mpenzi, na hapa ni kwangu usiwe na shaka.
TUSA: Kwanini nije hapa wakati tulikubaliana kuwa nitalala hotelini?
PATRICK: Na kwanini ulale hotelini wakati hapa kwangu kupo na ni pazuri tu!!
TUSA: Ila mi sijapenda, haikuwa kwenye mpango wetu hii. Sasa mimi nitalala wapi?
PATRICK: Utalala pale ninapolala mimi.
TUSA: Kivipi?
PATRICK: Si utalala na mimi mpenzi?
TUSA: Nitalalaje na wewe wakati mimi nina mpenzi wangu?
PATRICK: Nadhani ungelijua hilo la kuwa na mpenzi usingekuja huku, mimi nakupenda nawe walijua hilo, wewe mwenyewe umenifata huku halafu unaniletea swaga za kuwa na mpenzi. Unadhani ni mwanaume gani atakayekimbia kulala na mrembo kama wewe Tusa? Umekuja mwenyewe kwangu na utalala na mimi kama mpenzi wako.
TUSA: Jamani Patrick, hayo si makubaliano yetu.
PATRICK: Ila makubaliano yetu ni kukupa pesa tu? Tusa wewe ni wangu, na utaolewa na mimi maana baada ya hapa nina mpango wa kuja kutoa mahari kwenu na kukuchukua jumla.
TUSA: Hapana Patrick, mimi nina mpenzi wangu na siko tayari kuolewa na wewe.
PATRICK: Ili mradi upo kwangu itakubidi ukubaliane nami tu.
Kwakweli Tusa alijiona kuwa mwanamke mpumbavu na mjinga, akajilaumu kwa tamaa ya pesa aliyopata toka kwa Patrick kwani alikuwa mikononi mwa Patrick na kujinasua hawezi.
Wakati wa kulala Tusa alijitahidi sana kujinasua toka mikononi mwa Patrick ila haikuwezekana kwani Patrick alitumia nguvu na kumuingilia kimwili bila kutaka yani alimbaka na alikuwa anamfanyia hivyo kila anapojisikia. Kwakweli Tusa alijawa na kilio na majonzi kwani hakuwa na la kufanya.
Palipokucha Patrick alitoka na kufunga mlango kwahiyo Tusa hakuweza kutoka hata nje ya nyumba hiyo, Tusa alikuwa analia tu. Alitamani apige simu nyumbani kwao ila hakuweza kufanya hivyo kwani Patrick aliondoka na simu zote za Tusa.
Patrick aliporudi, Tusa akajaribu kumuomba kuwa awasiliane na kwao.
PATRICK: Usijali nimeshawasiliana na mama yako kwahiyo anajua kuwa uko salama.
TUSA: Sasa kwanini unifungie ndani Patrick? Na mie ungeniacha japo nitembeetembee na kuuona vizuri mji wa Arusha.
PATRICK: Yani binti mrembo kama wewe nikuache utembee!! Unataka vijana wa Arusha waniibie? Kwakweli sikujua kama facebook kuna mabinti warembo na watamu kama wewe Tusa.
Patrick alikuwa akicheka tu ila Tusa alikuwa akilia kwani siku moja tu ilishamchosha kukaa hapo Arusha kwa Patrick.
TUSA: Nitaondoka lini sasa?
PATRICK: Utaondoka pale nitakapopenda mimi.
Tusa alikuwa akilia huku huyo huyo Patrick akimbembeleza.
Patrick akiwa na Maiko kwenye kazi zao.
MAIKO: Yani Patrick hutaki kabisa nimuone huyo Tusa?
PATRICK: Utamuona tu, ila kwasasa muda bado.
MAIKO: Nitafutie basi na mie kidemu kwenye hiyo facebook ila awe mzuri kama Tusa.
PATRICK: Hujamuona huyo Tusa unamsifia ukimuona je!! Ila inaonyesha yule jamaa wa Tusa anazingua sana.
MAIKO: Sikia Patrick, ukitaka usimpoteze tena Tusa, anaporudi Dar mtume mtu awe anafatilia nyendo zake ngazi kwa ngazi, hapo itakuwa ngumu kwa Tusa kuchomoka mikononi mwako, na ukishamuoa nitakuonyesha jinsi Tusa atakavyotusaidia kwenye biashara yetu.
PATRICK: Hilo swala la kumfatilia ni zuri sana, ila kuhusu biashara mbona unaongea kama vile mtu unayemjua vizuri Tusa?
MAIKO: Simjui, ila kwavile wewe umesema ni binti mrembo. Na hadi wewe kukiri kwa kinywa chako kuwa Tusa ni binti mrembo, ndiomana nakwambia kuwa anatufaa kwenye biashara.
PATRICK: Ni kweli ni binti mrembo ila sijui atatufaa vipi?
MAIKO: Wewe ngoja tu ukishamuoa.
Patrick alikuwa akijiuliza maswali bila majibu, ni kweli Tusa ni binti mrembo ila watamtumia vipi kwenye biashara yao hapo hakujua kwakweli.
Baada ya kimya kirefu kupita na kama wiki mbili kukatiza bila ya kupata habari yoyote kuhusu Tusa, Sele alipatwa na mashaka kuhusu mpenzi wake akaamua kwenda kwao kumuulizia.
PAMELA: Tusa yupo kwa shangazi yake, kwani wewe wasiwasi wako ni nini?
SELE: Mama, Tusa ni rafiki yangu na muda mrefu sijapata mawasiliano nae.
PAMELA: Ndio hivyo yupo kwa shangazi yake.
SELE: Atarudi lini mama?
PAMELA: Sijui.
Pamela alikuwa anamjibu Sele kwa mkato kwavile ni kijana asiyempenda na pia anaona kuwa haendani kuwa na binti yake ila laiti kama angeyajua anayokumbana nayo binti yake huko Arusha labda na yeye angekuwa na hofu kama aliyokuwa nayo Sele.
Kwakweli Sele aliendelea kuumia moyo juu ya Tusa, mambo mengi yalizitesa fikra za Sele kwani alihisi kuwa Tusa hayupo salama sehemu aliyokuwepo.
Maiko akafanya kila hira kwa Patrick na kufanikiwa kuipata namba ya Deborah.
Maiko akiwa kwake ametulia akaamua kumpigia simu Deborah.
MAIKO: Hallow Deborah.
DEBORAH: Maiko!!
MAIKO: Ndio ni mimi Maiko.
DEBORAH: Unataka nini?
MAIKO: Deborah, nimekumiss sana mpenzi wangu.
DEBORAH: Tena unikome shetani mkubwa wewe, nani amekupa namba yangu?
MAIKO: Deborah, kamwe hutaweza kunikimbia mimi.
DEBORAH: Sina haja ya kukukimbia ila ipo siku utajikimbia mwenyewe kwa mambo yako unayoyatenda.
MAIKO: Sema yote mama ila mimi ndio Maiko bhana.
DEBORAH: Tafadhari Maiko usiniharibie mwanangu Patrick.
MAIKO: Umechelewa Deborah.
Kwakweli Deborah alihisi kuumia moyo sana na kuamua kuikata ile simu huku machozi yakimlengalenga.
Maisha ya kuishi kama mfungwa yalimchosha sana Tusa, kwakweli alichoka na alitamani sana kurudi nyumbani kwao. Ikabidi amuombe tena Patrick ili aweze kumkubalia yeye kuondoka.
TUSA: Nakuomba Patrick, naomba nirudi nyumbani.
PATRICK: Ni kweli unataka kurudi kwenu?
TUSA: Ndio nataka kurudi kwa mama.
PATRICK: Basi ukubaliane nami jambo moja.
TUSA: Jambo gani?
PATRICK: Kubali kuolewa na mimi.
TUSA: Mmmh!!
PATRICK: Ndio, kama unataka kurudi kwenu basi unatakiwa ukubali kwa hiyari yako kuwa utaolewa na mimi. Je uko tayari kuolewa na mimi?
Tusa akawa amekodoa macho tu huku lile swali likimuingia vilivyo.
PATRICK: Nijibu sasa. Je, uko tayari kuolewa na mimi?
Tusa alikuwa mtegoni tena mtego aliojinasisha mwenyewe.
Tusa akawa amekodoa macho tu huku lile swali likimuingia vilivyo.
PATRICK: Nijibu sasa, je uko tayari kuolewa na mimi?
Tusa alikuwa mtegoni tena mtego aliojinasisha mwenyewe.
Machozi yalikuwa yakimtoka tu Tusa.
PATRICK: Nijibu Tusa, hata ukilia haisaidii.
TUSA: Jamani Patrick nihurumie, mateso yako yamenitosha.
PATRICK: Hakuna mateso yoyote niliyokupa Tusa zaidi ya mapenzi ya dhati, naomba ukubali kuolewa nami.
TUSA: Kwakweli siko tayari kuolewa nawe Patrick.
PATRICK: Nini? (aliongea kwa ukali hadi Tusa akatetemeka), sema tena Tusa.
TUSA: Sijui (huku akitetemeka)
PATRICK: Hujui nini sasa? Nimekwambia kuwa, ukitaka kurudi kwenu ni lazima ukubali kuolewa na mimi, halafu kile kibwana chako uachane nacho kabisa. Umenielewa?
TUSA: Ndio nimekuelewa.
PATRICK: Haya niambie kuwa unanipenda.
TUSA: Abee.
PATRICK: Abee nini? Nimekuita kwani? Niambie kuwa unanipenda.
TUSA: Nakupenda
PATRICK: Unanipenda nani?
TUSA: Patrick.
PATRICK: Una akili wewe? Sema neno zima kuwa unanipenda Patrick. Na nitakuuliza tena, ole wako unikwepeshee majibu. Haya anza kusema kuwa unanipenda Patrick.
TUSA: Nakupenda Patrick.
PATRICK: Haya, upo tayari kuolewa na mimi?
TUSA: Ndio.
PATRICK: Je hautawasiliana tena na kibwana chako?
TUSA: Ndio.
PATRICK: Je unanipenda?
TUSA: Ndio.
PATRICK: Unanipenda nani?
TUSA: Nakupenda Patrick.
PATRICK: Haya, kesho nitaenda kushughulikia tiketi yako ya kurudi Dar.
Kwakweli Tusa alijisikia vibaya sana, alikosa raha kabisa alijikuta akilia tu muda wote.
Patrick akaandaa vijana wawili wa Maiko ambao alitaka wasafiri na Tusa ili waweze kumchunguze mambo yote ambayo Tusa angeyafanya akiwa Dar es salaam. Ila Tusa mwenyewe asijue kama kuna watu wanamchunguza.
Asubuhi na mapema, Tusa aliamshwa na safari ikaanza, alipelekwa kituo cha mabasi ya mkoani na si uwanja wa ndege tena.
Alipakizwa kwenye basi alilokatiwa tiketi halafu Patrick akampa Tusa kiasi cha shilingi elfu ishirini na tano tu kwaajili ya kula njiani, kwakweli Tusa alishangaa sana kuona Patrick aliyezoea kumpa pesa nyingi amempa pesa hiyo tu kwa safari nzima. Ila moyoni mwake alifurahi kuwa anarudi kwao, alifurahi kuondoka kwenye mikono ya Patrick.
Muda wote Tusa alikuwa amejiinamia tu kwenye siti akikumbuka matukio yote yaliyompata, aliilaumu sana tamaa yake ya pesa. Hakuwa na hamu ya kufanya chochote zaidi ya kungoja muda ambao basi lile litaingia Ubungo ili aweze kushuka na kwenda nyumbani kwao.
Deborah aliumia sana moyo kutokana na maneno ya Maiko, alitafakari sana na kukosa jibu. Siku hiyo akaamua kumpigia simu Patrick ili kujua kama kweli yuko na Maiko au la.
DEBORAH: Patrick mwanangu, usiwe na Maiko ni mtu mbaya sana.
PATRICK: Mbona mama sipo na Maiko na hata simkumbuki.
DEBORAH: Usinidanganye mwanangu Patrick, Maiko alinipigia simu na akasema kuwa mpo wote.
PATRICK: Amekudanganya tu mama, mimi siko nae kwakweli.
DEBORAH: Patrick, kumbuka nimekulea katika njia nzuri na maadili mema. Tafadhari usiache njia ambayo nimekufundisha, usipende kutenda mabaya.
PATRICK: Mama, mimi ni mtu mzima sasa najua baya na jema kwahiyo usijari.
DEBORAH: Sipendi uwe kama Maiko mwanangu.
PATRICK: Usijari mama.
Patrick alimpa moyo mama yake ila ukweli wote aliujua, Patrick anazidi kuwa na mashaka na kazi zaidi zifanywazo na Maiko, anajua tu kuna wakati Maiko atamshilikisha kazi hizo, anangojea huo muda ili apate kuzitambua na aweze kujua kwanini mama yake anamuogopa sana Maiko.
Tusa alifika kwao na kupokelewa na mama yake akiwa amechoka sana hata Pamela alimshangaa mwanae alivyopungua, ule mwili wake wenye unene kiasi ulikuwa umesinyaa na kunyorodoka, alijaa machozi tu usoni.
Mama yake alimpokea na kumfariji mtoto wake, alimuwekea maji ya kuoga na kumuandalia chakula apate kula.
Tusa alipokuwa amepumzika sasa, mama yake akaamua kumuuliza maswali mawili matatu.
PAMELA: Mbona umepungua hivyo mwanangu? Huko ulipokuwa huli?
TUSA: Mama, wee acha tu, ni makubwa sana. Nitakueleza vizuri kesho mama yangu.
PAMELA: Sawa mwanangu, ila je ulikosa chakula?
TUSA: Chakula kilikuwepo mama ila ni mambo mengine tu yaliyonikondesha. Nitakwambia vizuri kesho mama.
Kesho yake asubuhi, Tusa alitoka na kwenda duka la madawa na baada ya muda akarudi nyumbani kwao.
Ilipofika jioni Pamela alimuona mwanae kajiinamia huku analia.
PAMELA: Jamani mwanangu nini tatizo?
TUSA: (Huku akilia), sitaki kuolewa na Patrick sitaki mama.
PAMELA: Jamani mwanangu, mbona mimi sijakulazimisha kuolewa naye.
TUSA: Ndio hivyo sitaki mama, sitaki kabisa kuolewa na Patrick.
PAMELA: Kwani nini Tatizo?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tusa akainama na kuzidi kulia tena alilia kile kilio cha kwikwi. Kwakweli Tusa aliumia sana moyoni mwake.
TUSA: Nina mimba mama.
PAMELA: Una mimba yake?
Tusa akainama na kuzidi kulia tena kile kilio cha kwikwi. Kwakweli Tusa aliumia sana moyoni mwake.
TUSA: Nina mimba mama.
PAMELA: Una mimba yake?
TUSA: Ndio mama, nina mimba ya Patrick.
PAMELA: Sasa itakuwaje mwanangu?
TUSA: Mama, mimi simtaki Patrick na mimba yake siitaki.
PAMELA: Jamani mwanangu, kwahiyo unataka kufanyaje?
TUSA: (Akiendelea kutokwa na machozi), nataka kuitoa mama.
PAMELA: Hapana Tusa mwanangu, usitoe mimba mwanangu. Kuna madhara mengi halafu utajutia siku zote za maisha yako.
TUSA: Siwezi kujutia kitendo cha mimi kutoa mimba ya Patrick, kwanza simpendi halafu alinibaka.
PAMELA: Jamani mwanangu, usitake kufanya kama mimi nilivyofanya. Najutia hadi leo.
TUSA: Kwani ulifanyaje mama?
PAMELA: Niliwahi kutoa mimba, tena mimba kubwa sana. Kwa bahati mbaya akatoka mtoto kabisa, najutia hadi leo.
TUSA: Loh!! Mama ulikuwa muuaji, yani mtoto mkubwa ukamtoa!
PAMELA: Hata wewe unachotaka kufanya ni uuaji, mi sikutoa kwa kupenda ila ni baba yako ndio alinilazimisha nitoe mwanangu. Ningekuwa na mtoto mkubwa kupita wewe sasa, najutia sana kile kitendo. Tafadhari mwanangu usiende kutoa mimba.
TUSA: Mama, nitaenda tu kutoa. Sitaki kabisa kuendelea kubaki na mimba ya Patrick. Namngoja Tina anielekeze kwa madaktari wake.
PAMELA: Na hiyo pesa ya kutolea utaipata wapi?
TUSA: Hata sijui, yani Patrick ni mwanaume mshenzi sana. Alitoa pesa yangu yote ya kwenye Tigopesa, na kuondoka akanipa elfu ishirini tu. Hata hiyo pesa ya kutolea sijui nitaipata wapi. Mama inamaana hujabakiwa na pesa hata kidogo?
PAMELA: Sina mwanangu, nilitumia yote. Labda jaribu kumuomba tena huyo Patrick.
TUSA: Sitaki pesa yoyote ya Patrick, simtaki yeye wala pesa zake kwani ndio zilizoniponza.
Tusa akawa anajadili tu na ubongo wake mahari ambako atapatia pesa ya kwenda kuitoa mimba aliyokuwa nayo. Akaona njia rahisi ni kwenda kumuomba Sele.
Kesho yake Tusa akaenda nyumbani kwa Sele. Kwakweli Sele alifurahi sana kumuona Tusa bila ya kujua kilichomsibu.
SELE: Jamani mpenzi wangu, nilikukumbuka sana. Vipi za huko, wote wazima? Na mbona umepungua sana mpenzi?
Tusa alimuangalia Sele kwa jicho la masononeko kwani alishindwa kumjibu swali hata moja.
SELE: Tusa, una tatizo gani mpenzi?
TUSA: Nahitaji pesa Sele, sina hela kabisa halafu nina matatizo.
SELE: Matatizo gani? Niambie kwanza mpenzi.
TUSA: Kama una pesa kiasi nisaidie Sele, nikirudi nitakuja kukwambia.
SELE: Pesa ipo, si nilikwambia kuwa ile laki mbili sitaitumia! Ngoja nikupatie basi Tusa.
Sele akamtolea Tusa ile laki mbili na muda ule ule Tusa akamuaga Sele na kumuahidi kurudi badae au kesho.
Tusa aliondoka pale na kwenda kwa Tina, ambaye walichukuzana moja kwa moja hadi kwa daktari.
Tina akaongea na daktari huyo na baada ya muda Tusa aliingia kwenye chumba ambacho alifanyiwa operesheni ndogo hiyo ya kutoa mimba, Tusa alipata maumivu ila alivumilia kwavile ni kitendo alichokidhamiria.
Walipotoka pale Tusa akaamua kuagana na Tina.
TUSA: Asante Tina kwa kunileta huku.
TINA: Usijari Tusa, yule ni daktari professional kwahiyo usiwe na shaka. Wewe meza tu hizo dawa ili ukae sawa kabisa.
TUSA: Nashukuru, umenisaidia sana ndugu yangu.
Tusa alipomaliza kuagana na Tina akaamua kurudi kwao kupumzika huku mama yake akiwa hajui kama Tusa tayari ameshatoa mimba ya Patrick.
Deborah akiwa ametulia nyumbani kwake kwa mawazo, dada yake akamtembelea na kumshtua akiwa na mawazo ya hali ya juu.
MARIUM: Wallah, utakufa kwa mawazo mdogo wangu.
DEBORAH: Dada wee acha tu.
MARIUM: Yanakutesa kwavile hupendi kushirikisha wenzio.
DEBORAH: Dada, nilikuwa nangoja muda muafaka ufike ili niweze kusema.
MARIUM: Inamaana hadi sasa muda haujafika?
DEBORAH: Namngoja Patrick arudi safari hii nitamwambia kila kitu, kwanza nimechoka kukaa na siri hii moyoni.
MARIUM: Ni bora useme ili upate kupumua mdogo wangu, nikikumbuka siku ile umekuja kwa shangazi na Patrick akiwa mtoto mchanga loh nilikuonea huruma sana, najua ulipata shida sana mdogo wangu na huyo mwanao.
DEBORAH: Yani dada, shida niliyopata mmh!! Hata siamini kama Patrick wangu amekua mkubwa vile, kwakweli umefika wakati wa kumwambia ukweli tu.
MARIUM: Hapo ni sawa mdogo wangu na nitakupongeza sana, unaweza muona mtoto ana kiburi kumbe sababu hajui magumu uliyopitia mdogo wangu.
DEBORAH: Kweli dada, lazima nimwambie Patrick ukweli wa mambo yote.
Deborah aliamua haswa kumueleza Patrick ukweli alikuwa anangoja tu muda atakaorudi tena.
Tusa akaamua tena kwenda kwa Sele kwani alijikuta akikosa amani kwa kitendo alichofanya.
SELE: Hebu niambie yaliyokusibu Tusa, kulia hakusaidii mpenzi.
TUSA: Nimekutenda dhambi Sele, sijui kama unaweza kunisamehe ila wewe ndie mwanaume pekee nikupendae.
SELE: Nieleze Tusa, usijari chochote. Hata wewe ndie mwanamke nikupendae.
Tusa akitokwa na machozi akaamua kumueleza kila kitu kilichomsibu kwa Patrick.
TUSA: Najua itakuwa ngumu kunisamehe Sele, mimi ni mwanamke nisiyefaa. Nilisema kwamba sitakusaliti ila nimekusaliti, mimi sikufai tena Sele ila nakupenda sana.
SELE: Kwakweli imeniuma sana Tusa, nilikukataza mpenzi hayo mambo ya facebook ona sasa. Hapa ni balaa juu ya balaa, ulienda kutoa mimba ungekufa je, nani angelaumiwa kama sio mimi niliyekupa zile pesa Tusa?
TUSA: Nisamehe Sele ila sikuweza kuvumilia kukaa na mimba ya Patrick, nimeamua nikwambie ukweli wa mambo yote, ingawa najua maji yakishamwagika hayazoleki.
SELE: Sasa unadhani tufanyeje?
TUSA: Sijui Sele, kwakweli sina la kufanya natamani hata kufa.
SELE: Usiseme hivyo Tusa, kama vipi tutoroke twende mbali kabisa sehemu ambayo hawawezi kukupata tena.
TUSA: Wapi huko Sele?
SELE: Twende kijijini kwetu Tusa, tutaenda kijiji alichokulia mama yangu.
Tusa na Sele wakakubaliana kutoroka ili waweze kwenda mbali na Dar es salaam.
Tusa akarudi kwao ili kukamilisha mipango yake, wakati anajipanga mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake kutoka kwa Patrick.
"Kwanini umetoa mimba yangu Tusa?"
Tusa akarudi kwao ili kukamilisha mipango yake, wakati anajipanga mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake kutoka kwa Patrick.
"kwanini umetoa mimba yangu Tusa?"
Tusa akajikuta akitetemeka na akili yake ikikosa muelekeo kabisa. Hakujua afanye kitu gani kwa muda huo, simu yake ikaita, kuangalia ni Patrick, akaipokea huku akitetemeka.
PATRICK: Nijibu Tusa, kwanini umetoa mimba yangu?
Tusa hakuwa na jibu zaidi ya kutetemeka tu.
PATRICK: Vizuri sana kukaa kimya, na vizuri sana kutoa mimba yangu.
Tusa alizidi kutetemeka na kuamua kufanya uamuzi muda ule ule.
PAMELA: Unataka kwenda wapi Tusa?
TUSA: Mama, nimetoa mimba na Patrick mwenyewe amegundua kwakweli sitaweza kuendelea kuishi hapa nyumbani.
PAMELA: Kumbe umeshatoa mimba yake? Sasa unataka kwenda kuishi wapi Tusa? Na je huyo Patrick amejuaje?
TUSA: Hata sijui amejuaje mama, naondoka na Sele naenda nae Songea nikifika huko nitakwambia mama yangu.
PAMELA: Jamani mwanangu Tusu, unadhani baba yako nitamwambia nini mimi?
TUSA: Mama usijari ila ni muhimu mimi kufanya hivi.
Tusa akabeba mkoba wake wenye nguo kiasi na kumuacha mama yake akiwa mwenye majonzi.
Tusa na Sele walikuwa pamoja katika kukamilisha mpango wao, na alfajiri wakafanya safari ya kwenda Ubungo na kuianza safari yao ya kwenda mkoani Ruvuma.
TUSA: Hivi Sele, huko Songea tutaenda kuishi wapi?
SELE: Tutaenda Mbinga, huko kuna bibi yangu mzaa baba ni mpole sana, najua atatupokea vizuri.
TUSA: Bora niepukane na janga hili kwakweli, nimechoka sana na pia najutia.
SELE: Usijari Tusa, cha muhimu tuko pamoja mpenzi.
Wakaingia Songea wakiwa wamechoka sana kwa safari ndefu, ikawabidi walale nyumba ya kulala wageni ili kesho yake wafanye safari ya kwenda Mbinga.
Walifanya hivyo na kufika Mbinga salama kabisa, na wakapokelewa vizuri sana na bibi yake Sele aliyeitwa Asha.
Sele akamtambulisha Tusa kama mkewe ambapo ameenda nae huko ili waweze kumtambua na kuyajaribu maisha ya kule, hakumwambia ukweli wowote bibi yake.
ASHA: Msijali wajukuu zangu, hapa ni pazuri tu. Mtakula, mtalala na kuishi vizuri.
SELE: Sawa bibi ila hapa tutaishi kwa muda mfupi tu. Nia yangu ni nyie mpate kumfahamu mke wangu.
ASHA: Naelewa mjukuu wangu, ila huku ni kuzuri sana kushinda huo mji wenu mnaoung'ang'ania.
SELE: Aaah!! Bibi mazoea tu.
Bibi akawapa chumba ambacho Sele na Tusa watakuwa wakipumzika.
Tusa alifurahi na kujiona kuwa ataishi kwa amani sasa, akaamua kumpigia simu mama yake kuwa yuko salama.
TUSA: Mama niko salama na hiyo ndio namba yangu mpya.
PAMELA: Kumbe umebadilisha namba mwanangu!! Ila ni vizuri, kwahiyo mko wapi?
TUSA: Tuko Songea mama, sehemu moja hivi inaitwa Mbinga. Ni ndanindani na pazuri mama.
PAMELA: Mmh mwanangu, maisha ya kijijini utayaweza kweli?
TUSA: Sio kijijini sana mama, ni pazuri kwakweli. Ila hata hivyo tukizoea, Sele amesema kuwa tutahamia Songea mjini, sehemu moja hivi inaitwa Majengo.
PAMELA: Bora ya mjini mwanangu, ila huko nakuhurumia kwakweli.
TUSA: Usijari mama, ilimradi nipo na Sele jua kwamba nitakuwa salama muda wote.
Kwahiyo Sele na Tusa wakaishi kama mke na mume huko Mbinga. Tusa alifurahia maisha yale ingawa yalikuwa ya hali ya chini sana.
Pamela akiwa nyumbani kwake hajui hili wala lile, mara akavamiwa na vijana wawili wakiwa wamejifunika sura zao, walimkaba Pamela na kumuuliza mahali alipoenda Tusa.
Pamela alitetemeka sana kwani ni kitu ambacho hakuwahi kufikiria katika maisha yake, mambo yale huwa anayaona kwenye filamu tu, leo hii aliingiliwa yeye, hakuweza kuficha chochote akaeleza kila kitu hadi na namba za simu ambazo Tusa alimpigia, kweli kifo ni kiboko maana mtu anajikuta akiropoka kila kitu.
Wale vijana wakamwambia.
"Na ole wako umwambie Tusa kama kuna watu wamemuulizia, tutakuchinja wewe pamoja na mwanao"
PAMELA: Jamani sitamwambia, sitamwambia kabisa.
Wale vijana wakaondoka na kumuacha Pamela akitetemeka hovyo hovyo.
Walikuwa ni vijana wa Patrick waliotumwa kuchunguza nyendo zote za Tusa, walichanganya mabasi ya kusafiri pindi walipofika mahali ambapo abiria upumzika kwa muda, badala ya kuingia basi la Songea wakajikuta wameingia basi la kwenda Mbeya na ndio hapo lile basi la kwenda Songea likawaacha.
Wakafika njiani na kushuka, wakakosa usafiri wa kwenda huko hadi kesho yake. Walipofika Songea hawakujua pa kuelekea, baada ya siku mbili wakaamua kurudi Dar ili waweze kutafiti, hawakujua wamuulize nani ila wakaona vyema wamfate mama yake na Tusa ndipo siku hiyo walipoamua kumvamia Pamela.
Ingawa wale vijana walikuwa wameshaondoka ila bado Pamela alikuwa akitetemeka, hadi Tina anafika hapo alimkuta mamake mdogo huyo akitetemeka.
TINA: Mamdogo, nini tatizo?
PAMELA: Tina, haya yaliyonipata ni mabalaa. Kwakweli Tusa ametuletea balaa.
TINA: Vipi tena jamani?
PAMELA: We acha tu naomba nikae kimya wasije wakanirudia tena.
TINA: Wakina nani hao mamdogo?
PAMELA: Hakuna kitu mwanangu, tuyaache kama yalivyo tu.
Pamela aliogopa kumwambia ukweli Tina akihofia kurudiwa tena na wale watu waliomkaba.
Deborah alikuwa akifikiria tu kuwa kwanini Patrick harudi Mwanza, kwakweli Debora alikuwa anaumia moyoni mwake, alipokuwa amekaa na dada zake akaamua kulizungumzia.
DEBORAH: Kwakweli simuelewi Patrick, sijui ameng'ang'ania nini huko Arusha, hata kuja kunitembelea jamani!
MARIUM: Ndio watoto walivyo mdogo wangu, ona mwanangu mie tangu ameenda Dar kutafuta maisha hadi leo hajarudi sijui hata huwa wanakumbwa na nini hadi wanatusahau.
ANNA: Jamani yote huwa ni mapenzi tu, hawa watoto wetu wakishaanza kuwa na wenza wao basi inakuwa tabu tupu.
DEBORAH: Ina maana na Patrick atakuwa na mpenzi?
ANNA: Kwanini asiwe nae wakati amekamilika?
DEBORAH: Jamani nimekaa na Patrick kwa kipindi chote, sijawahi kumuona na msichana yeyote. Hata yeye mwenyewe huwa anasema kuwa hata kutongoza hawezi.
ANNA: Deborah, mtu husema hivyo pale anapokosa mwandani ila akimpata sasa mmh!! Anasahau yote hayo.
DEBORAH: Ila Patrick ni mpole sana, ulevi yes, ila wanawake sidhani.
ANNA: Usimkanie mtoto Deborah, ngoja akija umuulize vizuri kuhusu mkweo.
Mawazo ya Deborah ni kuwa kuna jambo kubwa linalomzuia Patrick kurudi ila si mapenzi kwani alimjua mwanae kuwa si mtu wa kuchanganywa akili sababu ya mapenzi.
Tusa na Sele waliona kuwa sasa wapo sehemu salama na maisha yao yakaendelea kama kawaida.
Siku hiyo Tusa akiwa ametoka kuichaji simu yake, ikaingia meseji, kuangalia namba ni ya Patrick.
Tusa akashtuka sana huku akitetemeka, akaamua kuifungua.
"Huwezi kunikimbia Tusa, yani umeenda kuishi Mbinga na kibwana chako? Rudi Dar mwenyewe kabla sijakufata mimi huko"
Tusa alishtuka sana huku akitetemeka, akaamua kuifungua.
"Huwezi kunikimbia Tusa, yani umeenda kuishi Mbina na kibwana chako? Rudi Dar mwenyewe kabla sijakufuata mimi huko."
Tusa akaingiwa na uoga, akaamua kumfata Sele na kwenda kumuelezea.
SELE: Amejuaje sasa kama tupo huku?
TUSA: Hata sijui, pengine Patrick ni jini.
SELE: Mmh!! Tusa mbona tumekwisha kama ndio hivyo. Ila natumai si jini.
TUSA: Tamaa yangu imeniponza Sele, hata sijui cha kufanya jamani.
SELE: Si wakati wa kujipa lawama huu Tusa, tunatakiwa tuondoke huku mara moja.
TUSA: Tutaenda wapi sasa?
SELE: Bado sijajua ila itajulikana tu maana hapa pesa hatuna kwahiyo hatuwezi panga safari bila ya pesa.
Mara meseji ya M-pesa ikaingia kwenye simu ya Tusa maana alikuwa anatumia mtandao wa Vodacom kipindi hiki, meseji ilimjulisha kuwa amepokea shilingi laki mbili kutoka kwa Patrick.
Na ujumbe mfupi wa maneno ukafatia.
"fanya pesa hiyo kama nauli ya kurudi Dar"
Tusa alijikuta akiibwaga ile simu chini, bahati nzuri ilikuwa ni simu imara kwani Sele alipoiokota ilikuwa bado inawaka.
Sele alimshangaa Tusa kutupa ile simu na ndiomana akaiokota na kuangalia ujumbe uliotumwa.
TUSA: Sitaki hela ya Patrick, sitaki pesa yake kabisa.
SELE: Sasa tutafanyaje Tusa?
TUSA: Kwakweli sijui cha kufanya Sele.
SELE: Unaonaje kama tukienda kwa wazazi wangu Mwanza?
TUSA: Nauli tutapata wapi? Maana Mwanza ni mbali sana.
SELE: Dah!! Hata sijui, labda tukakope.
TUSA: Au basi tuumie hii pesa aliyotuma kutorokea.
Tusa na Sele wakapanga mpango wa kuondoka hapo Songea na kwenda Mwanza, ila wakakubaliana kuwa wasifike Dar kwani mashaka yao ni kuwa Patrick anaweza kuwa kule Dar na kuwafatilia, kwahiyo wakaona bora kuishia Morogoro na kutafuta usafiri wa kwenda Mwanza.
Wakajiandaa kwa safari na kumuaga bibi yao, kwakweli bi.Asha alishangaa sana kwa ile safari ya gafla ambayo wajukuu zake waliipanga, hawakumwambia ukweli ila walimwambia kuwa wamepatwa na dharura tu.
Sele akawasiliana na ndugu zake wa Mwanza na kuona kuwa ni vyema yeye na Tusa wakajifiche huko.
Kesho yake wakiwa Songea mjini wakapata usafiri wa kwenda Dar, ambapo walikata tiketi za kuishia Morogoro tu.
Wakiwa ndani ya basi, Tusa akamtaarifu kitu Sele ambacho kilimshngaza pia.
TUSA: Sele, ujue mwenzio nimepata ujauzito wako.
SELE: Acha masikhara Tusa, si umetoa mimba wewe wiki tatu tu zilizopita iweje leo uwe mjamzito?
TUSA: Unajua daktari aliniambia kuwa baada ya kutoa mimba via vya uzazi vinakuwa wazi na uwezekano wa kupata mimba kwa muda huo ni mkubwa sana. Daktari alinishauri kuwa baada ya siku tano nikachome sindano za uzazi wa mpango, mi sikufanya hivyo kwaajili ya safari yetu. Tangu jana nimejihisi kuwa nina ujauzito, nikaenda kununua kipimo nacho kikanihakikishia kuwa ni kweli.
SELE: Labda Mungu amesikia kilio changu kwa wewe kutoa ile mimba ya Patrick.
TUSA: Nimefurahi sana kuwa na mimba yako Sele, ingawa tulikuwa tunaepuka kipindi kile ila huu ndio wakati muafaka.
Tusa na Sele walikuwa wanaongea kwa furaha bila ya kujua kuwa ni watu wanaofatiliwa.
Basi lilipokaribia kufika kitonga, Tusa akalala, walipofika mahali pa kujinunulia chakula, Tusa alikuwa bado yupo usingizini kwahiyo Sele akaamua kuteremka bila kumuamsha Tusa ili kuepuka kumsumbua.
Sele alienda kununua chakula ili Tusa atakaposhtuka apate chochote cha kutafuna.
Ila Sele aliposhuka ndio ikawa kashuka moja kwa moja kwani hakurudi tena kwenye basi, hadi basi linaondoka ile sehemu Sele hakuwemo ndani.
Tusa alishtuka basi likiwa maeneo ya Mikumi, akashangaa kwa kutokumuona Sele pembeni yake. Akajaribu kuangaza macho huku na kule kwenye lile basi lakini hakumuona Sele kabisa.
Walipokaribia Morogoro, Tusa ikabidi amuulize Konda, naye konda akasema kuwa hajui akabakia tu kukisia kuwa labda wamemuacha pale pa kulia chakula.
Basi lilipofika Morogoro, Tusa akaamua kushuka na kujaribu kuangaza huku na kule kuwa labda atamuona Sele lakini hakumuona, akaamua kumngoja pale stendi, akangoja na kungoja na kungoja ila Sele hakutokea, Tusa akahisi kuumia moyo, mawazo mengi yakamtawala hakujua mpenzi wake amekwenda wapi.
Alingoja sana pale stendi, kesho yake akaamua kupanda gari ya kwenda Dar ili arudi kwao ili akajaribu kumuulizia Sele sehemu mbalimbali.
Tusa aliingia nyumbani kwao akiwa analia, macho yake yalijaa machozi. Pamela alimpokea mwanae kwa uchungu sana.
Tusa akamsimulia mama yake yote yaliyotokea na kupotea kwa Sele.
TUSA: Hata sijui Patrick alijuaje nilipo, sijui ni jini yule mmh!!
PAMELA: Nilaumu mimi mwanangu, nadhani wale vijana walitumwa na Patrick.
Pamela akamsimulia mwanae ilivyokuwa.
TUSA: Mmh mama kama ndio hivyo tupo hatarini, inaonyesha Patrick ni mtu hatari sana.
PAMELA: Sijui hata cha kufanya mwanangu, hata najutia tu kukuruhusu wewe kumpa namba.
TUSA: Hata mimi najutia tamaa yangu mama kwani ndio iliyoniponza.
Tusa alijikuta akilia tu na hata hakuelewa aanzie wapi kumtafuta mpenzi wake Sele.
Deborah akiwa kwa dada yake Marium, wakajikuta wakiongelea habari za watoto wao kutokomea mjini.
MARIUM: Mwanangu alisema ameamua kurudi Mwanza cha kushangaza hadi leo kimyaa.
DEBORAH: Mjini mambo mengi dada, hata Patrick alivyonipenda vile mwanangu ni wa kunisahau kweli? Kila siku ukimpigia simu neno lake nitakuja mama usijari, ila imekuwa kama wimbo wa Taifa.
MARIUM: Ila bora Patrick kuliko huyu mwenzie, anataka hadi tumsahau jamani.
DEBORAH: Wanajua kwamba mzazi hawezi kusahau mtoto ndiomana wanaturingia, ila watarudi tu. Mi mwenyewe nimemkumbuka sana huyo mwanampotevu.
MARIUM: Sijui hata amekuwaje sasa? Sijui kabadilika? Mweeeh! Watoto hawa balaa.
Kila mmoja anagumia mtoto wake maana vijana wakizamia mjini kutafuta maisha ndio wanasahau kabisa kurudi makwao.
Tusa akiwa na mawazo juu ya Sele, mara akapokea simu kutoka kwa Patrick.
PATRICK: Je unakipenda kile kibwana chako?
TUSA: Ndio nampenda tena sana.
PATRICK: Kama unampenda na unapenda awe mzima basi swala ni moja tu, unatakiwa ukubali kuolewa na mimi. Kumbuka, maisha ya kibwana chako yapo mikononi mwangu.
Tusa akakosa jibu na kujikuta akitetemeka hadi kuangusha ile simu.
Tusa akakosa jibu na kujikuta anatetemeka hadi kuangusha ile simu.
Tusa hakujielewa kabisa, mama yake akamfata na kumuuliza.
PAMELA: Nini tena mwanangu?
TUSA: Patrick ameniambia kuwa natakiwa kuolewa nae lasivyo atamdhuru Sele. Nadhani atakuwa amemteka mama.
PAMELA: Mweeeh mweeh mweh, mbona huyo Patrick ni wa ajabu? Hadi anafikia hatua ya utekaji loh! Sasa itakuwaje mwanangu?
TUSA: Hata sijui cha kufanya mama yangu, naona Patrick amedhamiria kunitesa jamani.
PAMELA: Basi kataa kuolewa nae.
TUSA: Atamdhuru Sele mama, halafu huyu Patrick anaweza kututeka hata sisi itabidi nikubali tu kuokoa maisha ya Sele.
PAMELA: Mmh! Mwanangu, usiyatoe maisha yako kwajili ya mwanaume. Yani umuokoe Sele halafu wewe uteseke jamani!
TUSA: Mama kumbuka kwamba Sele nampenda, halafu mimi ndio chanzo cha yote haya. Bora niteseke mimi ila Sele apone.
Pamela akasikitika sana kwa maamuzi ambayo mwanae anataka kuyafanya.
Ikambidi Pamela awasiliane na Tina ili ambembeleze Tusa juu ya maamuzi yake.
TINA: Mamdogo mwache tu aolewe nae.
PAMELA: Ila ni khatari mwanangu, inaonyesha Patrick si mtu wa kawaida.
TINA: Patrick anampenda Tusa kwahiyo inaonyesha kuwa atafanya vyovyote kumpata, cha msingi mkubali tu ili na nyie mnufaike.
PAMELA: Kunufaika kivipi?
TINA: Mtajieni Patrick mahali kubwa, akishindwa kulipa basi kakosa mke na akiweza basi na nyie mtakuwa mmefaidika.
PAMELA: Unachosema Tina ni kweli, ngoja nitakifanyia kazi. Ila natumai Patrick hatomtenda mwanangu vibaya.
TINA: Hawezi kumtenda vibaya sababu anampenda sana mamdogo, Patrick anampenda sana Tusa.
Maneno ya Tina yalimuingia Pamela vizuri sana kwenye akili yake na akapanga kuyafanyia kazi.
Tusa alipopigiwa tena simu na Patrick ikabidi amwambie kuwa amekubali kuolewa nae, na Patrick akamwambia Tusa kuwa hatomfungulia Sele mpaka pale watakapofunga ndoa kwahiyo harusi yao ilitakiwa kuharakishwa sana ili kumuokoa Sele.
Patrick akatuma watu wa kwenda kujitambulisha kwa kina Tusa ili wapate kutajiwa mahali ambayo Patrick angeenda kuilipa.
Walikuwa vijana wawili na mzee mmoja walioenda kujitambulisha, wakamuomba baba yake Tusa awatajie na mahari kabisa, jambo hilo lilimshtua Adamu, ila binti yake akamwambia kuwa awatajie tu.
Ikabidi Adamu na mkewe waende kujadili kwanza, Adamu akashangaa kiasi ambacho alitajiwa na mkewe.
ADAMU: Mbona kubwa sana?
PAMELA: Kwani inaendana na binti yetu? Hiyo ni mahali tu.
ADAMU: Je huyo muoaji akishindwa kuitoa.
PAMELA: Akishindwa basi amekosa mke.
Adamu akaamua kukubaliana na mawazo ya mke wake, kwahiyo wakaenda kuwatajia wale watu mahari waliyoipanga, hata wao wakashtuka kwa hiyo mahari waliyotajiwa, ila na wao ikawabidi waondoke ili waweze kuwasiliana na Patrick kuhusu hiyo posa.
Patrick alipopata ile habari akaamua kuwasiliana na Maiko kwa ushauri kama kawaida.
MAIKO: Kwani wamepanga kiasi gani?
PATRICK: Milioni kumi na tano.
MAIKO: Itoe tu si unataka mke wewe!
PATRICK: Ila ni nyingi sana, kama wanamuuza binti yao loh!
MAIKO: Patrick, hiyo pesa ndio itakayokupa uchungu zaidi kwa mkeo, wewe itoe tu.
PATRICK: Dah, nitafikiria kwanza.
MAIKO: Hakuna cha kufikiria, swala hapa ni kutoa hiyo posa. Ok, wewe toa milioni tano halafu kumi nitatoa mimi.
PATRICK: Ooh!! Utakuwa umenisaidia sana baba, maana nishapoteza hela nyingi sana kwa wale vijana wangu.
MAIKO: Usijari Patrick, pesa yetu itarudi tu.
PATRICK: Itarudije?
MAIKO: Wewe utaona tu baada ya kumuoa Tusa.
Patrick akafanya mpango wa kwenda Dar kwaajili kukamilisha swala la posa na kumchukua Tusa kwaajili ya kumuoa.
Patrick alifika na watu wake kwakina Tusa na kukamilisha swala la mahali ambapo wakawakabidhi pesa na kila kilichohitajika.
Tusa akashtuka sana kuona pesa nyingi kiasi kile ikitolewa kwaajili ya posa yake, ikabidi amuite mama yake pembeni.
TUSA: Kwanini mama? Kwanini mnapokea pesa nyingi kiasi kile kwaajili yangu mama? Inamaana mmeniuza? Je mtaweza kurudisha hiyo pesa nikiamua kurudi nyumbani?
PAMELA: Mwanangu, niliweka pesa nyingi ili Patrick ashindwe kutoa.
TUSA: Patrick ana hela mama na nilishakwambia, unaona sasa ameshalipa pesa yote. Nitatetewa na nini mimi jamani?
PAMELA: Nisamehe mwanangu ila hakuna jinsi, hata sijui cha kufanya kwakweli mmh!
Tusa akaitwa ili kuweza kuvishwa pete ya uchumba na mwenza wake.
Patrick akaomba kuruhusiwa kuondoka na mwenza wake wakati wanaandaa mambo ya harusi.
Wazazi hawakuwa na pingamizi zaidi ya kumruhusu tu.
Tusa alikuwa na mawazo mengi sana kichwani mwake ikiwa ni pamoja na swala la kumtoroka Patrick, wakati huo Patrick alikuwa na mawazo pia haswa posa aliyoitoa kwaajili ya Tusa.
Patrick akaamua kufanya maamuzi ya haraka kichwani mwake. Akaamua kuanza kuitangaza ndoa yake na Tusa.
Tusa alimshangaa sana Patrick kwani alikuwa kijana mpole kwa muda mfupi, hadi siku ya harusi yao ilipofika.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wachache sana kwavile ilikuwa ni harusi iliyoharakishwa.
Tusa alishangaa sana kwani hakuweza hata kuwagundua ndugu wa Patrick, alijiuliza maswali mengi kuwa je Patrick ana ndugu? Kwani hakumuona yeyote kwenye harusi zaidi ya marafiki wa Patrick tu. Hata wazazi wa Tusa wakajaribu kumdadisi Patrick kuhusu wazazi wake ila akawadanganya kuwa wana udhuru, ukweli ni kwamba Patrick aliogopa kumwambia mama yake sababu mama yake alimwambia kuwa kabla ya kuoa anatakiwa akamtambulishe kwake huyo mwanamke ili amchunguze mwenyewe. Patrick akaona kuwa itachukua mlolongo mrefu wakati yeye alitaka kuharakisha ndiomana hakumwambia mama yake wala ndugu zake.
Baada ya ndoa ya Tusa na Patrick, ndipo Patrick alipowaruhusu vijana wake kumuachia Sele ambaye alitoka akiwa amekonda sana.
Alikuwa na masononeko yaliyopitiliza, akaenda nyumbani kwa kina Tusa japo aelezee uchungu wake.
SELE: Mama, umemtupa mwanao kwakweli. Patrick si mtu mzuri.
PAMELA: Mbona ni kijana mstaarabu sana, umewahi kumuona?
SELE: Hapana ila ndiye aliyetuma watu wanitese.
PAMELA: Pole sana ila ndio hivyo Tusa kashaolewa.
SELE: Nampenda sana Tusa, naye ananipenda. Patrick ametumia uwezo wake kumpata Tusa ila Mungu atanilipia tu.
PAMELA: Mmh! Pole Sele ila cha kukusaidia nitakupa pesa kidogo ili urudi kijijini kwenu, hapa mjini hapakufai tena.
Pamela akaingia ndani na kumtolea Sele kiasi kidogo cha pesa na kumkabidhi.
SELE: Asante mama ila najua ipo siku nitakutana tena na Tusa wangu, ngoja nikajipange sasa.
Sele akaondoka na kusafiri kabisa kurudi kwao Mwanza, aliona mji ukiwa mchungu sana kwake.
Patrick akagundua kuwa Tusa ni mjamzito tena ujauzito huo ni wa Sele, kwakweli akachukiza sana na kumuuliza Tusa kwa ukali.
PATRICK: Tusa una mimba?
Tusa akawa anatetemeka huku akiogopa kujibu swali aliloulizwa.
Tusa akawa anatetemeka huku akiogopa kujibu swali aliloulizwa.
Patrick akarudia tena kumuuliza Tusa lile swali.
PATRICK: Una mimba Tusa?
Tusa bado akawa anaogopa kujibu.
PATRICK: Najua kama una mimba, ninachotaka ni kuwa ukubali mwenyewe kuwa unayo kweli. Nakuuliza tena, je una mimba?
Tusa akatikisa kichwa kama ishara ya kuitikia.
PATRICK: Hivi wewe mwanamke una akili kweli? Pesa yote ya mahari niliyotoa kwenu bado unanijia na mimba. Unajua nimetoa pesa ngapi wewe?
TUSA: Ndio najua ila nisamehe.
PATRICK: Kweli wanawake ni watu mlionyimwa akili jamani, mimba yangu ulienda kuitoa ila huku unakuja na mimba ya mwingine. Umeshindwa nini kuitoa na hiyo? Nijibu Tusa!
TUSA: Tafadhari Patrick nihurumie.
PATRICK: Nikuhurumie nini Tusa? Kiumbe changu hukukihurumia, ulikiona hakina faida. Sasa hicho ulichobeba kina faida gani kwangu? Na hiyo mimba uliyobeba lazima ukatoe na ubebe yangu.
TUSA: Jamani Patrick usinifanyie hivyo, kutoa mimba ni dhambi.
PATRICK: Ungelijua hilo usingeitoa mimba yangu, lazima nikutoe hiyo mimba.
TUSA: Patrick, Patrick tafadhari nionee huruma. Najua nilifanya makosa makubwa sana kuitoa mimba yako ila niliapa kuwa sitarudia tena. Kutoa mimba ni maumivu sana Patrick, naomba unisamehe.
PATRICK: Hata kuzaa ni maumivu pia, hiyo mimba lazima itolewe utake usitake. Nimekuoa kwa gharama sana wewe, usiniletee mchezo kabisa.
Tusa alibaki analia wakati Patrick ametoka, laiti kama Tusa angeweza basi angetoroka ila Patrick alimfanyia Tusa kama vile alivyofanya mwanzo kwa kumfungua ndani ya nyumba.
Tusa alikuwa akilia tu akifikiria hiyo shughuli ya kutolewa mimba.
Kesho yake Patrick alitoka asubuhi sana na baada ya muda akarudi na daktari ndio hapo Tusa akaona kuwa kazi yake itaanza, Tusa akawa analia pale ambapo aliitwa.
Akapelekwa kwenye chumba kingine humo ndani, akaambiwa alale kwenye kitanda ili afanyiwe ile operesheni ndogo ya kutolewa mimba, Tusa akagoma ikabidi yule na daktari na Patrick wamfanyie kinguvu.
Wakatumia nguvu kumlaza Tusa kitandani, akafungwa kamba mikono na miguu yaani kila mguu upande wake na mikono hivyohivyo akiwa amelazwa chali.
Yule daktari alifanya kazi yake bila hata ya huruma na Tusa akapata maumivu makali sana kwani mimba yake ilikuwa kubwa kubwa.
Tusa alipiga kelele na kulia hadi akazimia.
Hata alipozinduka Tusa aliendelea kulia akiyajutia maisha yake.
PATRICK: Pole sana Tusa ila sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya vile.
Tusa alikuwa analia tu, hakuona raha kabisa ingawa Patrick alikuwa akimuongelesha vizuri kama vile ni mtu mwema.
Tusa alitamani kufa, alikuwa akimuomba Mungu tu amchukue ili apumzike na yale mateso anayoyapata kwa Patrick.
Baada ya siku mbili kabla hata Tusa kupona vizuri, Patrick alikuwa akimuingilia Tusa kimwili kwa kasi ya ajabu ili tu kuhakikisha kuwa Tusa anapata mimba nyingine.
Siku zote Tusa alikuwa akilia na kujutia maisha yake.
Sele alirudi kwao Mwanza ambako walimzoea kwa jina lake la kuzaliwa la Sulemani, ambapo alipofika mjini alisikia wengine wakiitwa Selemani na kufupishwa majina na kuitwa Sele, akaona kuwa akifupisha jina lake la Sulemani na kuitwa Sule haitanoga na ndiomana akaamua kujiita Sele na watu wote mjini wakamjua kama Sele ila nyumbani kwao kabisa walimzoea kama Sulemani.
Mama yake bi.Marium alisikitika sana kumuona mwanae jinsi alivyokonda, kwakweli alimuhurumia.
MARIUM: Jamani mwanangu nini kilikupata huko mjini?
SELE: Nilitekwa mama.
MARIUM: Pole sana mwanangu, kumbe huko kuna utekaji loh! Halafu ulisema utaniletea mkamwana wangu, yukn wapi?
SELE: Mama, wee acha tu. Yani yaliyonipata dah!! Siku nikikaa na kutuliza akili yangu nitakusimulia vizuri mama.
MARIUM: Pole sana mwanangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SELE: Usijari mama, haya ni mapito tu ya dunia.
Marium akaenda kumwambia mdogo wake kuwa mwanae amerudi, kwakweli Deborah akafurahi sana.
MARIUM: Ila amekonda huyo, huwezi amini kama ndio yule Sulemani tuliyemzoea. Mwenyewe anajiita Sele siku hizi.
DEBORAH: Kumbe anajiita Sele, vijana bhana ila hilo jina linaendana na jina lake halafu linapendeza tu. Mwambie aje na huku basi.
MARIUM: Atakuja tu, nimemwambia akae kae kidogo nyumbani arudishe mwili.
DEBORAH: Basi nitakuja mimi dada, tena ikiwezekana aje akae huku si unajua mi nipo mwenyewe tena! Hakuna hata mtu wa kukaa nae.
MARIUM: Basi itakuwa vyema, uje umshawishi mwenyewe kuja huku.
DEBORAH: Hawezi kukataa bhana, sema rafiki yake kipenzi Patrick hayupo nadhani atakuwa amemkumbuka sana.
MARIUM: Na huyo Patrick atarudi lini?
DEBORAH: Mwenzangu hata simuelewi, kila siku nitakuja nitakuja hadi leo kimya.
MARIUM: Tumuombee mema tu mdogo wangu, natumaini atarudi.
Walimkumbuka Patrick walipomuongelea Sele, maana Patrick na Sele licha ya kuwa ndugu walikuwa ni marafiki waliokaribu sana. Na walipatana kupita kiasi kipindi wapo wote huko Mwanza.
Maiko akiwa na Patrick kwenye mipango yao.
MAIKO: Sasa Tusa yupo mikononi mwetu ila ni binti mrembo sana, nimeona picha zenu za harusi kwakweli pesa yetu imeenda kihalali.
PATRICK: Huwa sikosei kabisa katika kuchagua mimi, nachagua vilivyo bomba.
MAIKO: Nakuaminia Patrick, ila kuna kazi moja kubwa sana nataka ukaifanye wewe.
PATRICK: Kazi gani hiyo?
MAIKO: Ni kazi ya khatari halafu inahitaji tahadhari kubwa sana. Najua wewe utaiweza.
PATRICK: Mmh! Itachukua siku ngapi?
MAIKO: Kama siku tatu tu, vijana wangu watakuelekeza.
PATRICK: Mke wangu nitamuacha na nani? Si unajua kuwa ndoa yangu bado ni changa!
MAIKO: Naelewa Patrick, usijali kuhusu mkeo. Mimi nipo na nitamlinda, atakuwa salama kabisa. Wala usiwe na shaka.
PATRICK: Sawa nakuamini.
Patrick akajipanga kwaajili ya kufanya kazi aliyotumwa, kazi hiyo ilitakiwa kufanywa kwenye mkoa wa Morogoro.
Walifika Morogoro, Patrick akiwa na vijana watatu wa Maiko.
Patrick alipotajiwa kazi yenyewe alitaka kukataa kabisa kuifanya ila akatishiwa kuwa ameshakula kiapo kwahiyo kukataa kwake kutahatarisha maisha yake.
Patrick na kundi lake wakajiandaa kuifanye hiyo kazi hatari.
Patrick na kundi lake wakajiandaa kuifanya hiyo kazi hatari.
Kazi yenyewe ilikuwa ni kumteka mzee mmoja mwenye upara aliyeita Ayubu, mzee huyu alikuwa ni mlevi na alisifika kwa ulevi wake ila alikuwa ni mtu makini sana.
Wakamtumia Patrick kuweza kumshawishi mzee huyo ili afatane nae na wakammalize wanapopajua wao, kwavile Patrick alikuwa ni mtu aliyesoma na mwenye muonekano wa ukarimu na upole, ukimuona huwezi kumfikiria kama anaweza kutenda jambo lolote baya.
Patrick akatumia kama siku mbili kumzoea mzee huyo kwenye duka la pombe.
Tusa akiwa ndani ametulia kwani hakuweza kwenda popote kwavile alifungiwa ndani na Patrick, alishangaa siku nzima imepita bila ya Patrick kurudi.
Tusa akajiuliza kuwa Patrick yuko wapi ila hakuwa na jibu wala hakuwa na wa kumuuliza, kwa upande mwingine alishukuru kwa kutokumuona Patrick kwani alikuwa ni mateso mbele ya macho yake.
Siku ya pili jioni tangia Patrick aondoke, Tusa akasikia mlango ukifunguliwa naye akajua kwavyovyote vile atakuwa ni Patrick tu ila ukweli ni kwamba hakuwa Patrick bali ni Maiko.
Maiko aliingia hadi sebleni na kuita 'Tusa'
kwavile Tusa alijua ni Patrick, akaitikia tu kule kule jikoni alipokuwa. Maiko akamfata Tusa hadi jikoni, Tusa akashtuka kuona sura ngeni ambayo hajawahi kuiona kabisa.
MAIKO: Mbona umeshtuka Tusa?
TUSA: Kwasababu sikujui.
MAIKO: Usiwe na wasiwasi, mimi naitwa Maiko ni kama baba mkwe wako. Njoo basi sebleni tuzungumze.
Tusa akatoka jikoni na kumfata Maiko pale sebleni, kwa upande mwingine Tusa alihisi kuwa labda ukombozi wake umefika.
TUSA: Abee.
MAIKO: Usiniogope Tusa, Patrick ni kama kijana wangu hata mahari yako nimemchangia.
Tusa alikuwa anakodoa mimacho tu, wala hakujua cha kujitetea.
MAIKO: Nimekuja tu kukusalimia na kujua unaendeleaje, vipi hali yako lakini?
TUSA: Niko salama, je Patrick yuko wapi?
MAIKO: Patrick ameenda kuchukua mzigo Nairobi, kwahiyo usijari.
TUSA: Atarudi lini?
MAIKO: Siku mbili tu zimepita ndio umemkumbuka hivyo!
TUSA: Hapana, nimeuliza tu.
Muda wote Maiko alikuwa akimuangalia Tusa kwa macho makali sana, macho hayo yalimuogopesha sana Tusa kiasi cha kuingiwa na uoga.
Maiko kuona vile kuwa Tusa anaogopa akaamua kuaga.
MAIKO: Kesho nitakuja tena kukuangalia kwahiyo usijari.
TUSA: Sawa nashukuru.
Maiko akainuka na kutoka, akafunga milango kama ambavyo aliikuta, kwahiyo Tusa akafungiwa ndani vile vile kama kawaida.
Maiko akiwa anaelekea nyumbani kwake sura ya Tusa ilimkaa kichwani bila kutoka, mara akapigiwa simu na Patrick.
PATRICK: Nadhani hii kazi itachukua kama siku tano na sio tatu tena, maana huyu mzee ni mtata sana.
MAIKO: Hakuna tatizo, nyie fanyeni kazi tu.
Maiko alifurahi kusikia hivyo ili na yeye apate wasaa mzuri wa kuzungumza na Tusa.
Kama ambavyo Deborah alihitaji, alimuomba Sele na kwenda kuishi nae nyumbani kwake.
SELE: Nimemkumbuka sana Patrick, hivi yuko wapi?
DEBORAH: Yupo huko kwenye miji ya watu, amepata kazi huko. Na yeye amekukumbuka sana.
SELE: Dah! Bora arudi anifanyie na mimi mpango wa kazi.
DEBORAH: Hilo ondoa shaka, Patrick na wewe mmh!! Lazima atakufanyia tu.
SELE: Ndio mamdogo najua Patrick hawezi kunitupa mimi. Nikikumbuka wakati tuko wadogo ilikuwa raha sana.
DEBORAH: Utoto raha, hata mimi namtamani Patrick wangu arudi utoto ili nikae nae muda wote ila ujana ukifikia mara kutafuta kazi mara kuoa ndio kunikimbia kabisa hapo.
SELE: Hivi Patrick ana mchumba mama?
DEBORAH: Awe nae wapi? Angekuwa nae angeniambia, Patrick anatafuta maisha kwanza si unajua wanawake wanavyofilisi mwanangu.
SELE: Kweli kabisa, ila lazima atakuwa nae wa kuzugia. Mmh ila Patrick na mambo ya mademu yuko mbali nayo kabisa, labda kama atampatia huko kazini.
DEBORAH: Hata kutongoza kwenyewe mwanangu yule hawezi.
SELE: Hahaha, mamdogo nawe loh!
Sele alitamani sana kumuona nduguye Patrick, alikuwa amemkumbuka sana.
Alikuwa akipiga stori nyingi na mamake mdogo za kumuhusu Patrick.
Sele alikuwa anaishi na Deborah kama ambavyo alizoea ila kwasasa hakuwepo Patrick, alingoja zipite siku mbili tatu ili aanze kuzunguka mitaani na kuwasalimia vijana wenzie aliowaacha.
Patrick alitumia lugha nzuri sana kumshawishi mzee Ayubu ili aweze kufatana nae.
PATRICK: Mzee kuna bia mpya imezinduliwa ila tulikuwa tunahitaji watu wa kuonja na kwavile nimekuona mzee wangu hapa ni mkarimu nimependelea uwe mmoja wapo kati ya watu watakaoionja na kutuambia ladha yake.
AYUBU: Hayo ndio mambo ninayopenda kijana, inaitwaje hiyo bia na je kuna malipo?
PATRICK: Hiyo bia bado haijapewa jina ila waonjaji ndio mtakaopendekeza jina la pombe hiyo. Ndio mtalipwa elfu ishirini ila leo nitakupa elfu kumi kama advance.
Mzee Ayubu alifurahi sana alipokabidhiwa hiyo pesa na kuambiwa kuwa atafuatwa badae kwaajili ya hilo zoezi.
Muda ulipofika Patrick alimfata mzee Ayubu na kuondoka nae.
Akampeleka huko kwa wenzake, wenzee huyo alidhania kuwa na wale wapo kwaajili ya kuonja hiyo bia mpya.
Mzee Ayubu akapewa glasi moja tu na kulala hapohapo, wakamfanya watakavyo na kuondoka.
Kwakweli kwa Patrick ilikuwa ndio mara yake ya kwanza maishani kuua mtu, siku zote alijua kuwa kazi haramu afanyayo yeye na Maiko ni madawa ya kulevya tu kumbe kuna kazi mbaya zaidi ya kuchukua baadhi ya viungo vya mwili wa binadamu na kuua kabisa, alitetemeka sana kuuangalia ule mzoga wa mzee Ayubu. Roho ya Patrick ikasinyaa, huruma ikamjaa ila hakuwa na jinsi zaidi ya kulikimbia hilo eneo la tukio.
Walirudi Arusha, na kwenda kwenye hilo jumba ila Patrick hakuweza kuingia kwani mawazo yake yalikuwa kwa Tusa, alihitaji kumuona Tusa, ingawa ilikuwa usiku ila Patrick alishaamua kurudi kwake ili akamuangalie Tusa.
Tusa akiwa katulia ndani kama ambavyo Maiko alimuahidi, na kweli siku hiyo akaenda tena kumuona Tusa. Mida ya jioni mlango ulifunguliwa na Maiko akaingia, Tusa akajiuliza kuwa iweje tena huyo Maiko kuja jioni vile, na hakutaka kuondoka wala nini.
Muda kidogo Maiko akaanza kumsifia Tusa.
MAIKO: Tusa, kweli wewe ni binti mrembo tena unayevutia machoni. Kweli pesa yetu imeenda kihalali kabisa.
Mara Maiko akaanza kumsogelea Tusa, Tusa akawa analia huku akipiga kelele na kumsihi Maiko asimfanye chochote.
MAIKO: Tusa, hata mimi ni halali kuwa na wewe kwani nimekulipia mahari kubwa sana. Kwahiyo hutakiwi kuninyima.
Tusa akawa anakimbia hovyo hovyo mule ndani, ila mwanaume ni mwanaume tu.
Maiko alimkamata Tusa na kumuingilia kimwili kwa nguvu, Tusa akawa analia na kuomboleza.
Mara mlango unafunguliwa, Patrick alikuwa anaingia ndani.
Maiko alimkamata Tusa na kumuingilia kimwili kwa nguvu, Tusa akawa analia na kuomboleza.
Mara mlango unafunguliwa, Patrick alikuwa anaingia ndani.
Maiko hakuweza kusikia mlango unavyofunguliwa kutokana na kelele za Tusa na pia hakufikiria kama Patrick anaweza kuja muda huo, aliendelea na yake mpaka pale alipohisi amejiridhisha.
Patrick alishangaa kumsikia Tusa akilia na kujiuliza maswali "Hivi huyu Tusa ni chizi nini? Yani anajiliza hata kama sipo." akaanza kufatilia sauti ya Tusa inapotokea na akagundua kuwa ni chumba cha mwisho kabisa, kile chumba ambacho walitumia kumtoa Tusa ujauzito aliobeba.
Patrick alipofika kwenye kile chumba alimuona Maiko kasimama na Tusa amejikunyata chini, Patrick akaelewa kuwa kwa vyovyote Maiko alikuwa amemuingilia kimwili Tusa, Patrick akachukia sana, kwa ghadhabu akamsukumia Maiko pembeni ambapo alikuwa hajafunga suruali vizuri, ile Maiko anainuka akashtukia anapigwa ngumi ya uso, kabla hajajiweka sawa akapigwa ngumi nyingine.
Maiko akaiona kuwa ishakuwa cheche, akaamua kukimbia.
Patrick alikuwa na hasira hadi mishipa ikamtoka usoni, hakuweza kuzungumza zaidi ya kutetemeka tu, alikuwa akimuangalia Tusa kwa macho makali na ya ghadhabu.
Maiko akafanikiwa kutoka na kupanda gari yake na kuondoka.
Sele alikuwa akimuwaza sana Tusa, alikosa raha kila alipomfikiria Tusa. Alijiuliza maswali mengi sana kuhusu Tusa.
"kwanini ulikubali kuolewa Tusa? Inamaana hukunipenda tena? Na vipi mimba yangu uliyobeba Tusa? Natamani nikuone mpenzi wangu ili moyo wangu uridhike"
Deborah akamuangalia Sele aliyejawa na msononeko machoni.
DEBORAH: Tatizo nini jamani? Eti Sulemani, una nini wewe? Kila siku mawazo.
SELE: Mamdogo, nilikuwa na msichana mzuri sana. Niliyempenda kwa dhati ila mapedeshee wamemuiba mpenzi wangu.
DEBORAH: Mmh pole sana, tatizo la mabinti si waaminifu.
SELE: Alikuwa mwaminifu ila wamemlaghai kwa pesa na mali. Mamdogo nikimfikiria moyo wangu unaniuma sana, sijui kama atatokea msichana yeyote nikampenda kama yeye.
DEBORAH: Usiwe na shaka mwanangu, kama ni wako basi ni wako tu. Tambua ipo siku atarudi kwako.
SELE: Natamani hiyo siku hata iwe leo, kwakweli tunanyanyasika sana maskini katika mapenzi.
DEBORAH: Usijari mwanangu, kila kitu kitakuwa sawa.
SELE: Asante mama.
DEBORAH: Uwe unaenda na kuzungukazunguka huko mtaani ukutane na wenzio, wakina Juma, John labda upunguze kidogo mawazo.
SELE: Sawa mamdogo.
Sele akaamua kwenda kutembea tembea kidogo pale mtaani kama alivyoshauriwa na Deborah ili aweze kupunguza mawazo kiasi.
Patrick akiwa na ghadhabu juu ya Maiko na Tusa.
PATRICK: Kwanini Tusa umelala na Maiko?
TUSA: (Huku akitetemeka), alinilazimisha, amenibaka.
PATRICK: Kwanini akubake Tusa? Umeshindwa kujizuia? Nadhani nawe ulipenda.
TUSA: Hapana Patrick, sijapenda.
PATRICK: Unataka na mimi nikuingilie wapi? Huko kwenye uchafu wa Maiko? Nijibu Tusa.
TUSA: Hapana Patrick.
PATRICK: Kiukweli nimekereka sana Tusa, umeichefua roho yangu.
Tusa akawa anatetemeka tu huku machozi yakimtoka.
Kwavile ulikuwa usiku ikabidi waende kulala, Tusa alilala kwa uoga na mashaka yaliyopitiliza.
Patrick akainuka na kumuingilia Tusa kinyume na maumbile, Tusa alitapatapa na kulia sana ila Patrick hakumuacha hadi pale alipojiridhisha.
Tusa hakuweza kulala hadi panakucha, alikuwa akilia tu. Siku hiyo alipatwa na ugonjwa wa kuhara gafla, alikuwa akiendesha tu na tumbo likimsokota.
Patrick alimuacha Tusa akiwa analia na kuondoka zake ile asubuhi.
Sele akiwa mtaani alikutana na marafiki wengi sana na kupiga story za hapa na pale, na ndipo alipotokea John na kukumbushana mambo yao ya zamani na kuambiana ya sasa.
JOHN: Mwenzio Patrick kaukata, maisha yamemnyookea ile mbaya. Ila wewe umechakaa balaa, vipi hata demu bongo hukuopoa?
SELE: Wee nilikuwa na msichana wangu mzuri sana John, yani huwezi amini.
JOHN: Nilitaka nishangae, kukaa kote bongo usiwe na demu. Labda kama uliwataka wa huku Mwanza.
SELE: Wewe, sijaona huku msichana mrembo kama Tusa wangu.
JOHN: Anaitwa Tusa? Ngoja nikuonyeshe mrembo mwingine mwenye jina hilo kwenye facebook.
John akafungua picha ya Tusa na kumuonyesha Sele.
Sele akashtuka kuiona picha ya Tusa.
SELE: Ndio huyuhuyu Tusa wangu, naye alikuwa anaipenda sana facebook.
JOHN: Mmh! Kaka, yani wewe ndio ulikuwa na huyu mrembo? Aliwahi kuniambia kuwa mpenzi wake anaitwa Sele, sasa wewe Sulemani na Sele wapi na wapi?
SELE: Mimi ndio huyo Sele, kule Dar wamezoea kuniita Sele jamani.
JOHN: Basi una bahati sana kama huyu mrembo ni wako.
SELE: Sipo nae tena, kuna pedeshee mmoja ameniibia mrembo wangu.
JOHN: Kivipi? Au ndomana siku hizi simuoni facebook.?
Sele akaamua kumueleza John kinagaubaga ilivyokuwa kwake na Tusa hadi pale alipokuta Tusa kaolewa na huyo pedeshee Patrick.
Stori hiyo ikafungua akili ya John na kumfanya afikirie kwa kina kama awazacho ndicho au sicho.
Safari ya Patrick asubuhi hiyo ilikuwa ni moja kwa moja kwa Maiko.
PATRICK: Kwanini umenifanyia hivi Maiko?
MAIKO: Mmh! Hata ubaba umekufa sababu ya mwanamke!
PATRICK: Sina baba kama wewe, na bora wewe si baba yangu wala ndugu yangu. Binadamu mwenye roho mbaya kama ya simba.
MAIKO: Jamani Patrick, tusameheane tu ni mambo ya kupitiwa.
PATRICK: Unayajua maumivu ya mke wewe? Umenituma kufanya kazi ya kinyama na bado unanisaliti na mke wangu, kwanini Maiko?
Patrick alikuwa na hasira sana, wakati anaongea alimsogelea Maiko na kumkunja.
MAIKO: Tafadhari Patrick usinitende vibaya, najua wewe ni kijana jasiri. Usiniumize tafadhari, ila kumbuka hata mimi mahari ya Tusa nimechangia tena nimetoa pesa nyingi kushinda wewe.
PATRICK: Kwani nilikuomba unichangie pesa? Kumbe ulikuwa unatoa kwa shingo upande? Dah najuta kukufahamu Maiko.
MAIKO: Niachie Patrick, tuzungumzie kazi niliyokutuma.
PATRICK: Sina muda huo.
Akatoka nje na kuingia kwenye gari yake na kuondoka.
Maiko akawa anajisemea,
"alitaka afaidi peke yake yule binti mrembo! Hajui kuwa kizuri kula na nduguyo, toto choyo kama mama yake loh! Mke kitu gani wakati nimechangia mahari!!"
Maiko kazi yake ni kuharibu tu, kwanza huwa hapendi kuona mtu anaishi kwa furaha mwanzo mwisho.
Akajiandaa na yeye ili akaone kazi yake aliyowatuma wakina Patrick.
Nyumbani kwa kina Tusa, mama yake bi.Pamela akiwa anafua, mara akamuona Tina akija mbio mbio huku anahema kwa kasi ya ajabu.
PAMELA: Tina kuna nini?
TINA: Kuna tatizo mama.
PAMELA: Tatizo gani?
TINA: Tumepatwa na msiba mama.
Pamela alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwani hakujua ni msiba wa nani.
Pamela alihisi kuchanganyikiwa kwani hakujua ni msiba wa nani.
PAMELA: Jamani Tina, nani tena?
TINA: Mamdogo, ni babu yao na wakina Tusa.
PAMELA: Wee Tina wewe, unamaanisha mzee Ayubu? Nani amekupa taarifa?
TINA: Ndio mzee Ayubu, nimeona kwenye taarifa ya habari. Tena amekufa kifo cha kusikitisha sana.
Pamela alishapagawa kusikia habari za huyo mkwe wake, ikabidi aende kumtaarifu mumewe na wajaribu kuwapigia ndugu zao ili kujua ukweli wa habari hiyo.
Pamela akaamua kumpigia simu wifi yake aliyeitwa Amina, ambaye naye alimwambia kuwa ndio wamepata habari muda huo.
Ilikuwa ni huzuni sana kumpoteza mtu mcheshi kama mzee Ayubu.
Patrick alirudi nyumbani kwake na kumkuta Tusa yupo palepale alipomuacha asubuhi.
Patrick akamuangalia Tusa na kukaa kwenye kochi, Tusa akamtazama Patrick na kumfata pale alipokaa, Tusa akaanza kuongea kwa maombolezo na kwa uchungu.
TUSA: Hivi Patrick, wewe ni mume wa aina gani? Mume usiyemjali mkeo na unasema unampenda? Hivi ulinioa ili unitese? Nimekukosea nini mimi jamani?
Patrick alimuangalia Tusa kwa jicho kali ila lililojaa huruma.
TUSA: Nasema ya moyoni, kiukweli natamani kufa kuliko kuishi na wewe Patrick. Kukupa namba yangu ndio kosa kubwa la kunifanya niteseke hivi? Unanifanya kama mbwa jike nisiye na thamani, kila anayetaka anachukua tu. Patrick umeniharibia maisha yangu, pesa zako ndio za kunitesa kiasi hiki!! Nimewahi kukuomba pesa mimi?
Tusa akainama na kuendelea kulia.
PATRICK: Nisamehe Tusa mke wangu, kiukweli nimejaribu kufanya mambo mengi ili unipende cha kushangaza huna mapenzi nami kabisa, kama vile sio mumeo. Hata mimi inaniuma Tusa, lini utajifunza kunipenda?
TUSA: Sikupendi na sitakupenda kamwe hadi naingia kaburini.
PATRICK: Kwani Tusa nina kasoro gani mimi? Kwanini usinipende kama yule bwanako?
TUSA: Siwezi kukupenda Patrick, wewe ni gaidi uliyejificha. Nampenda Sele na sikuzote nitaendelea kumpenda, najua sitaweza kuwa nae tena ila nitampenda milele. Nani akupende wewe Patrick? Mwanaume mwenye roho mbaya, usiyejali wengine, mtu mwenye roho ya shetani.
PATRICK: Ni kweli nina roho mbaya ndiomana nimeua.
TUSA: (Akashtuka sana) umeua?
Patrick hakumjibu Tusa ila akaenda chumbani, Tusa akaona maisha yake hapo ni ya mashaka, akabaki anajisemea.
"Eeh Mungu, naomba unitetee katika maisha haya"
Baada ya kutafakari sana, John akaamua kumfata Sele ili amwambie anachofikiria yeye.
JOHN: si uliniambia kuwa huyo pedeshee aliyemchukua Tusa anaitwa Patrick?
SELE: Ndio anaitwa Patrick.
JOHN: Mmh! Hivi sio Patrick ndugu yako kweli?
SELE: Acha masikhara bhana John, kwanini umuhisi yeye?
JOHN: Sikia nikwambie, Patrick ana hela sana kwa sasa halafu anaishi Arusha.
SELE: Hata kama, hawezi kuwa yeye.
John akaamua kumueleza Sele kuwa kwanini amemuhisi Patrick.
JOHN: Sikia nikwambie, kipindi Patrick amerudi hapa alinishangaa kuona nashinda facebook.
SELE: Kwani kukushangaa kuna tatizo John?
John akamueleza Sele ilivyokuwa, na jinsi Patrick alivyotaka kufunguliwa akaunti ya facebook na jinsi alivyomuulizia Tusa.
JOHN: Aliniuliza kwa makini jina analotua Tusa, nikagoma kumtajia ila akaomba kuona picha yake nadhani hapo ndipo alipojua jina lake na kumuomba urafiki.
SELE: Hayo uyasemayo John yananiingia sana halafu inaonyesha kama kuna uhusiano, ila kiukweli nakataa. Patrick hawezi kufanya vile, majina yanafanana John tena hayo majina ya Patrick wako wengi sana duniani.
JOHN: Kwahiyo haiwezekani kuwa ni yeye ingawa alimuulizia Tusa?
SELE: Kumuulizia mtu ni jambo la kawaida John, sidhani kama anaweza kuwa Patrick huyu.
Sele alipinga kabisa hisia za John za kudhania kwamba Patrick wanaemjua ndio muhusika.
Wakiwa msibani, hadi wanazika kila mmoja alisikitishwa na kifo cha mzee Ayubu, kwani kilikuwa ni kifo cha kusikitisha sana.
Mzee Ayubu alikutwa ametolewa upara na kunyofolewa sehemu za siri, kila mtu alihuzunika kwa kifo cha mzee huyo.
Hata baada ya mazishi habari ilikuwa ni hiyo hiyo ya juu ya kifo cha mzee Ayubu, hakuna aliyetambua mtu aliyemfanyia unyama mzee huyo, watu walikuwa wakisikitika tu.
Amina kama mtoto mkubwa wa kike wa mzee Ayubu akaamua kumuulizia Tusa kwani Tusa ndie mjukuu mkubwa wa mzee huyo na hakuonekana msibani.
AMINA: Wifi, Tusa yuko wapi?
PAMELA: Tusa yupo kwa mumewe, ameolewa.
AMINA: Yani mnamuoza mtoto bila ya kutushirikisha na wengine?
PAMELA: Ilikuwa ni haraka wifi, naomba utusamehe.
AMINA: Na mbona hajaja msibani au hamjampa taarifa? Unajua Tusa ni mtu muhimu sana kwa babu yake, angepaswa kuwepo mahali hapa.
PAMELA: Kwakweli Tusa hapatikani kwenye simu, huwa tunawasiliana na mumewe tu. Ila tangu msiba utokee naye hapatikani.
AMINA: Mmh! Wifi mmeuza mtoto nyie, yani hapatikani na hata kumfatilia hamumfatilii?
PAMELA: Mumewe kasema wanaendelea vizuri, hata hivyo mtu mwenyewe ana pesa.
AMINA: kupenda pesa uache wifi dada, ila mfanye juu Tusa apate habari na aje kutembelea kaburi la babu yake.
PAMELA: Sawa tutafanya hivyo.
Baadhi ya maneno yalimuingia vizuri Pamela, akawaza sana moyoni kuhusu mtoto wake Tusa kwani ilikuwa kama amemtupa vile.
Patrick alikuwa nyumbani kwake kama vile mtu aliyepagawa.
Akaitazama simu yake na kugundua kuwa alibadilisha laini ya simu, aliweka laini inayojulikana na watu wachache ili kuepuka usumbufu, wakati anatazama simu yake, ilianza kuita muda huo na mpigaji alikuwa Maiko.
PATRICK: Sema.
MAIKO: Mbona umekuwa hivyo Patrick? Unataka kuharibu kazi mwishoni? Uje kufanya kazi, kesho asubuhi nakuhitaji kuna mpango flani wa pesa uje tupange.
PATRICK: Poa.
Bado Patrick hakujisikia raha kuzungumza na Maiko ni kwavile tu ameshakula kiapo cha kufanya kazi ya Maiko hadi mwisho.
Tangia Patrick aropoke kwa Tusa kuwa aliua, Tusa alijikuta akimuogopa zaidi Patrick.
PATRICK: (Kwa ukali), una nini wewe Tusa? Unaniogopa mimi nimekuwa jini? Nakusemesha hujibu, umekaa kama sanamu. Nina hasira zangu hapa naweza nikakubutua ukiendelea kuwa kimya.
Tusa hakuweza kujibu zaidi ya kujipeleka kulala tu, ndipo Patrick nae alipoamua kulala.
Patrick akiwa usingizini, akamuona mzee Ayubu akimjia kwa sura ya huruma, na kuanza kuongea.
"kwanini umeniua Patrick?"
Patrick akiwa usingizini, akamuona mzee Ayubu akimjia kwa sura ya huruma, na kuanza kuongea.
"kwanini umeniua Patrick?"
Patrick akabaki akimtazama na kukosa jibu, mzee Ayubu akasema tena,
"Laiti ungelijua mimi ni nani yako! Usingethubutu kuniua."
Patrick akashtuka na kupiga kelele, "mzee Ayubuuu..."
Tusa nae akashtuka na kujisemea.
TUSA: Mzee Ayubu!!
PATRICK: (Huku akihema sana), nilikuwa naota Tusa.
TUSA: Huyo mzee Ayubu ni nani na ana mahusiano gani na wewe?
PATRICK: Ni rafiki yangu tu.
TUSA: Kivipi?
PATRICK: Aaargh, hayo mengine hayakuhusu bhana. We endelea kulala tu, nishakwambia ni rafiki yangu inatosha.
TUSA: Sawa bhana.
Tusa akaamua kujilaza tena, ila muda ule ule Patrick akaanza kumlazimisha Tusa kuwa anataka kumuingilia kimwili, kwakweli kile kitendo kilikuwa ni kero kwa Tusa kwani hakuwa na la kufanya, na siku zote Patrick huwa anamuingilia Tusa kwa kumlazimisha tu kitu kinachomfanya Tusa aumie na kulia sana kwani hakupewa maandalizi yoyote.
Kulipokucha Patrick aliwaza sana juu ya mzee Ayubu, na akajiuliza kuwa ana mahusiano yapi na mzee huyo kwani ile sauti kuwa angejua ni nani yake asingemuua ilimrudia mara kwa mara.
Alipoamua kwenda kwa Maiko alihitaji kumuuliza baadhi ya maswali ili apate kujua kwanini Maiko alimtuma kwenda kumuua mzee Ayubu, na pia aweze kujua kuwa yeye na mzee Ayubu wana mahusiano gani.
Sele aliendelea kuichuja kauli ya John katika akili yake, alishindwa kuamini kabisa kuwa inawezekana akawa ni Patrick ingawa kuna uthibitisho wa kutosha kuwa ni yeye.
Sele aliwaza sana bila ya kupata majibu, akawa anajiuliza tu,
"Hivi ni kweli Patrick anaweza kunitenda vile? Mmh!! Hapana, hata kama angekuwa mtu mwingine Patrick hawezi kuwa na roho mbaya ya kiasi kile"
Akamfata alipokaa Deborah ili amuulize maswali mawili matatu kuhusu Patrick.
SELE: Hivi mamdogo, ulisema kuwa Patrick yupo mkoa gani?
DEBORAH: Patrick yupo Arusha.
SELE: Anafanya kazi gani?
DEBORAH: Alisema yupo mgodini.
SELE: Ana pesa sana eeh!
DEBORAH: Mbona leo maswali mengi kama polisi? Ana hela ndio, nadhani kazi yake ina kipato sana.
SELE: Maswali kawaida tu mamdogo, mpigie basi nimsalimie.
DEBORAH: Yani ni kama wiki mbili sasa simu yake haipatikani, ngoja nimjaribishe.
Deborah akaamua kuchukua simu na kumpigia Patrick ila napo hakupatikana.
SELE: Vipi hapatikani?
DEBORAH: Ndio hapatikani, hata sijui amepatwa na matatizo gani maana sio kawaida kabisa.
SELE: Basi tungoje siku atapiga mwenyewe.
DEBORAH: Ndio ila nitaendelea kumjaribisha mara kwa mara kama nitampata hewani.
Sele hakuweza kumwambia mamake mdogo juu ya maneno ya John kuwa uenda Patrick ndio muhusika kwani aliona ni kumpa presha mamake mdogo na pia hakuwa na uhakika bado.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Patrick alienda kwa Maiko na kufanya nae shughuli za hapa na pale, baada ya hapo akaamua kutulia nae na kumuuliza maswali aliyoyakusudia.
PATRICK: Hivi kwanini ulinituma kumuua mzee Ayubu? Kwani unamfahamu au unamahusiano naye?
MAIKO: Kiukweli simfahamu kabisa huyo mzee Ayubu, ila haya ni mambo ya biashara. Kuna mtu alitoa oda ya kufanya hivyo na tumeingiza pesa nyingi sana.
PATRICK: Huyo mtu ni nani na ana mahusiano gani na wewe?
MAIKO: Huyo mtu ni ndugu yangu ila haishi hapa, yupo nje ya nchi ni huko hufanya hiyo biashara ya viungo vya wanadamu. Hapa anakujaga mara moja moja sana.
PATRICK: Viungo vya wanadamu vina kazi gani?
MAIKO: Akija tena nitakutambulisha kwake umjue halafu utamuuliza hayo maswali yako.
PATRICK: Je, kuna uhusiano wowote kati ya mimi na mzee Ayubu?
MAIKO: Acha kuota Patrick, wewe mtu wa Mwanza, mzee Ayubu wa Morogoro huo uhusiano wenu unatokea wapi? Una ndugu Morogoro wewe?
PATRICK: Hapana.
MAIKO: Ndugu zako wako Mwanza, mzee Ayubu hakuhusu wewe wala mimi.
PATRICK: Unajua nini? Mi najiuliza, kwanini iwe mzee Ayubu na si mwingine yeyote?
MAIKO: Hayo maswali utamuuliza mwenye kazi, labda ana kisasi nae.
Patrick aliondoka kwa Maiko na kutambua kwamba mtandao wa Maiko ni mkubwa sana kwani hata yeye ana bosi wake, yote hayo yalimchanganya Patrick.
Walipomaliza matanga ya kwenye msiba, Pamela na mumewe walirudi kwao wakiwa na mwanamke mmoja wa makamo akidai kuwa yeye ni mama mzazi wa Adamu.
Mwanamke huyo aliitwa Rehema, hata Adamu alimshangaa kwani hakuweza kumuona tangia alipokuwa mdogo na yote hayo ilitokana na kwamba Adamu aliachwa na mama huyo akiwa na miaka miwili.
PAMELA: Mama, kwanini ulimuacha mwanao akiwa mdogo hivyo?
REHEMA: Nilijifungua mapacha, wazazi wangu hawakutaka niolewe na Ayubu ila Ayubu alihitaji watoto wake ikabidi tugawane mmoja nikawa nae na mwingine akaondoka na Ayubu. Kwa kipindi kirefu nimemtafuta Ayubu bila mafanikio mpaka pale nilipoona taarifa ya kifo chake kwenye luninga. Kwakweli nimesikitishwa sana, nikaamua kufunga safari hadi Morogoro.
PAMELA: Kwahiyo umetokea mkoa gani?
REHEMA: Kigoma mwanangu, kwakweli ilikuwa safari ndefu sana.
PAMELA: Pole sana mama.
REHEMA: Asante, na mbona kule wanapenda kukuita wifi dada?
PAMELA: Mama, kuna kaundugu flani hivi kapo kati yangu na Adamu ila mwanzo hatukugundua hadi tumeoana na kufunga ndoa. Ila undugu wenyewe hauna nguvu sana, ni undugu wa mbali.
REHEMA: Undugu gani tena?
PAMELA: Nitakwambia tu mama usijari ila kwanza turekebishe tofauti yako wewe na Adamu. Natumaini kuna muda atakuelewa mama yetu, hata usijari.
Pamela alipatana sana na huyu bi.Rehema kutokana na ucheshi wa bibi huyo hata akashangaa kwanini hakuweza kuishi na mzee Ayubu.
Patrick kabla ya kurudi nyumbani kwake alipitia baa kwanza ambako alikunywa pombe hadi akaridhika.
Aliporudi kwake alimkuta Tusa amelala, akaanza kumuamsha kwa nguvu, tofauti na walevi wengine ambao wakilewa wanakuwa legelege ila Patrick alikuwa na nguvu sana.
Akawa anamsumbua Tusa hadi akafanikiwa kumuingilia anakokutaka yani kinyume na maumbile, Tusa hakuweza kulala tena zaidi ya kulia tu.
Patrick akaanza kumwambia Tusa.
PATRICK: Unajua ile siku ya kwanza nimekufaidi sana huko nyuma na nimeona kutamu zaidi, siku hizi itakuwa hukohuko na safari hii hadi utapata mimba ya mgongo.
Halafu akalala, Tusa alilia sana na kuombea ukombozi wake ufike.
Kulipokucha Patrick aliamka kama kawaida ila alijikuta akimkumbuka sana mama yake, akaamua kuchukua simu yake na kumpigia ila iliita kama mara tatu bila ya kupokelewa.
Patrick akaweka simu mezani na kwenda kuoga, kwakweli siku hiyo alijisahau kwani huwa haachi simu yake, kila mahali anakuwa nayo.
Patrick akiwa bafuni ile simu yake ikaanza kuita, Tusa aliposikia akasogea kuitazama akaona jina 'mama' Tusa akaona kuwa kwa vyovyote vile huyo lazima atakuwa mama yake na Patrick, akaamua kuipokea ili amueleze matatizo yake.
Patrick akiwa bafuni ile simu yake ikaanza kuita, Tusa aliposikia akasogea kuitazama akaona jina 'mama' Tusa akaona kuwa kwavyovyote vile huyo lazima atakuwa mama yake na Patrick, akaamua kuipokea ili amueleze matatizo yake.
Tusa akaipokea ile simu na kuisikia sauti iliyosema 'hallow' kuwa ni ya mwanamke wa makamo.
TUSA: Mama, mimi ni mke wa Patrick. Ananitesa na kuninyanyasa sana.
DEBORAH: Patrick kaoa?
TUSA: Ndio na mimi ndiye mkewe.
DEBORAH: Unaitwa nani binti?
Mara Patrick akatoka bafuni na kumkuta Tusa yupo na ile simu sikioni, akaenda na kumpokonya halafu akaiweka sikioni mwake.
Deborah aliendelea kuongea kwani kilio cha Tusa kilimuingia masikioni mwake vilivyo.
DEBORAH: Niambie binti, halafu niambie anachokufanya hadi ulie hivyo.
Patrick akaikata ile simu na kumgeukia Tusa.
PATRICK: Nani kakutuma upokee simu yangu? Hujui mama yangu ana presha, akifa je? Nijibu, nani kakutuma?
Tusa aliendelea kulia bila ya kutoa jibu, Patrick akamuuliza tena.
PATRICK: Kitu gani kinakuliza sasa wakati umeshafanya makosa?
TUSA: Unanionea Patrick, unaninyanyasa, unanitesa. Nini kosa langu jamani?
PATRICK: Kosa lako ni kupokea simu isiyo kuhusu.
Patrick akamsogelea Tusa akiwa anahitaji la kumzabua kibao, mara simu yake ikaita tena. Patrick akashindwa kupokea kwani hakujua cha kumjibu mama yake kwa muda huo.
PATRICK: Unaona sasa Tusa, mimi namwambia nini mama? Unadhani atanielewa? Yani we Tusa una akili mbovu sana.
Patrick alikuwa na hasira sana akaona kuwa akiendelea kukaa hapo atamuumiza huyo Tusa, akaamua kuvaa na kuondoka zake.
Tina alimkumbuka sana ndugu yake na rafiki yake kipenzi Tusa, kama kawaida yake alikuwa mara kwa mara nyumbani kwa kina Tusa ili kujua kama kuna taarifa yoyote kuhusu Tusa.
Akiwa amekaa na mamake mdogo wanaongea.
PAMELA: Hivi Tina dadangu bado hajarudi?
TINA: Anarudi leo mamdogo, halafu amesikitishwa sana na kifo cha babu. Kama angewezaa kupaa kutoka china basi angekuja msibani.
PAMELA: Kwakweli kifo chake kimetushtua wengi.
TINA: Vipi kuna taarifa yoyote kuhusu Tusa?
PAMELA: Hakuna mwanangu, tuzidi kumuombea tu.
TINA: Sawa mamdogo, mi naenda ila akija mjomba msalimie.
PAMELA: Sawa usijari.
Bi. Rehema akajikuta akiwa na maswali mengi kichwani.
REHEMA: Huyo mjomba wa Tina hapa kwako ni yupi?
PAMELA: Adamu mama ndio mjomba ake.
REHEMA: Adamu si mumeo na Tina wewe ni mamake mdogo iweje mumeo awe mjomba ake?
PAMELA: Utajua tu mama kwanini imekuwa hivyo, hata usijari.
Bi. Rehema alikuwa akishangaa tu bila kuelewa.
Deborah alishindwa kuelewa kabisa, akabaki anajisemea mwenyewe.
"Hivi kweli Patrick anaoa bila hata ya kunitaarifu? Dharau gani hii?"
Sele alimuona mamake mdogo huyo akiwa anajisemesha mwenyewe.
SELE: Nini tena mamdogo?
DEBORAH: Kwakweli nashindwa kumuelewa Patrick.
SELE: Kafanyaje tena?
DEBORAH: Asubuhi nilipotoka kuoga nikakuta kwenye simu yangu kuna missed call tatu, ile kupiga sasa mmh.
SELE: Kwani ikawaje?
Deborah akamsimulia Sele alichoambiwa kwenye simu.
SELE: Mmh! Yani Patrick kaoa? Kamuoa nani? Na kwanini hakusema?
DEBORAH: Hayo yote sijui, najaribu kumtafuta kwenye simu hapatikani halafu ile namba haipokelewi, nadhani ni namba yake anaogopa kupokea kwavile mimi nimeshajua ukweli.
SELE: Sasa itakuwaje mamdogo?
DEBORAH: Usijari Sele, mimi namjua Patrick. Natambua wapi pa kumkamatia, atanitafuta mwenyewe.
SELE: Sawa mamdogo.
Akili ya Sele ikawaza mengi sana, akaanza kuhisia kuwa huenda huyo binti akawa Tusa ila tu hakuwa na uhakika.
Deborah hakuacha kumtafuta Patrick kwenye simu ila simu yake haikupokelewa. Akaamua kumtumia ujumbe, alijua utafika na atausoma tu.
Mama yake na Tina aliyeitwa Fausta alienda nyumbani kwa mdogo wake Pamela ili kumsalimia bi. Rehema.
FAUSTA: Karibu sana mama.
REHEMA: Asante ingawa nimefika kipindi cha majonzi.
FAUSTA: Kwakweli huu msiba wa baba umetugusa sana, ingawa sijaishi nae sana ila namkumbuka sana baba alikuwa mcheshi na mpenda watu. Yeyote aliyemfanyia hivi baba na alaaniwe milele.
REHEMA: Inaonyesha unamjua sana mzee Ayubu.
FAUSTA: Ndio namjua, ni baba yangu mzazi kwakweli nimeumia sana.
REHEMA: Mmh!! Baba yako mzazi? Wewe na Pamela si mtu na mdogo wake? Iweje mzee Ayubu awe baba yako mzazi?
FAUSTA: Mama, sijui kama utanielewa.
REHEMA: Nieleweshe tu nitakuelewa.
FAUSTA: Mama, mimi na Pamela tumechangia mama halafu mimi na Adamu tumechangia baba kwahiyo Pamela ni ndugu yangu na Adamu ni ndugu yangu.
REHEMA: Mmh! Ndiomana Pamela wanamuita wifi dada!! Sasa nimeanza kuelewa, kwamaana hiyo Adamu na Pamela ni kama ndugu.?
FAUSTA: Wenyewe wanakataa kuwa si ndugu, ila walioana bila kujua. Hata hivyo undugu wao hauna nguvu sana.
REHEMA: Yani umenielewesha kwakweli, ndomana mwanao anamuita Adamu mjomba. Mmh! Kazi ipo. Eeh na wewe ulikuwa wapi kwani hadi msiba umeisha?
FAUSTA: Nilikuwa China, huwa naenda mara kwa mara kuna mizigo naitoaga kule naileta huku.
REHEMA: Hongera kwa hiyo kazi, kila siku namngoja Adamu kumwambia kuhusu pacha wake ili aende akamtafute huko Mombasa.
FAUSTA: Mombasa? Alienda kutafuta nini huko?
REHEMA: Aliondoka na kaka yangu ila hawajarudi hadi leo halafu huyo kaka yangu mwenyewe ana akili mbovu huyo balaa hadi kuna kipindi alipelekwa Milembe halafu akatoroka.
FAUSTA: Mmh! Kazi ipo, ila hakuna tatizo mama tutampata tu.
REHEMA: Eeh! Na huyo mama yenu yuko wapi?
FAUSTA: Alishakufa na hivi baba nae amekufa basi tumebaki yatima.
Rehema na Fausta wakaongea mambo mengi ya maisha na kuweza kutambuana kwa undani zaidi.
Patrick akiwa kwa Maiko huku akiendelea kuzipotezea simu anazopiga mama yake.
Mara akaona meseji imeingia kwenye simu yake kutoka kwa mama yake.
"Patrick mwanangu, hutaki kunitafuta, simu zangu hupokei! Nashukuru sana najua hiyo ndiyo fadhira yako kwa malezi yote niliyokupa. Umeona maisha ya huko Arusha ni bora kuliko mimi, basi endelea na maisha hayo ila usahau kabisa kama una mama anayeitwa Deborah"
Patrick alisoma ujumbe huo mara mbili mbili, neno la mwisho likawa linamrudia mara kwa mara kuwa asahau kabisa kama ana mama anayeitwa Deborah. Patrick akajihisi ni mkosaji, akatambua alichofanya hapo hakipendezi, akaamua kwenda sehemu iliyotulia na kumpigia simu mama yake ili amwombe msamaha.
Patrick aliongea kwa kutubu kwa mama yake ambapo Debora alimpa chaguo moja tu.
DEBORAH: Ukitaka nikusamehe basi chagua moja kati ya haya.
PATRICK: Yapi hayo mama? Niko tayari kwa chochote ilimradi tu nipate msamaha wako mama.
DEBORAH: Mlete huyo binti uliyemuoa Mwanza aje nimuone au mimi nije huko Arusha kumuona.
Patrick akajikuta anawaza jibu la kumpa mama yake.
Patrick akajikuta anawaza jibu la kumpa mama yake.
Deborah akamuuliza tena Patrick na kumsisitiza ampe jibu.
PATRICK: Mama, naomba kama masaa mawili nifikirie majibu ya kukupa.
DEBORAH: Kwani ni mtihani huo?
PATRICK: Hapana mama ila nahitaji muda kidogo.
DEBORAH: Kwahiyo utanipa jibu saa ngapi?
PATRICK: Nimekwambia baada ya masaa mawili mama.
Patrick akajikuta akiwaza sana na kujiuliza maswali mengi, kuwa akimwambia mama yake aende Arusha itakuwa msala kwa Maiko na akiamua kwenda yeye Mwanza atamuagaje Maiko kipindi hicho wakati walikuwa na kazi nyingi za kufanya, akajikuta akijiuliza sana. Akaamua kurudi kwake ili akatafakari kwa kina.
Bi. Rehema alikuwa akitafakari mara kwa mara juu ya mtoto wake Adamu na mkewe Pamela.
REHEMA: Hivi Pamela mwanangu hukujua kabisa kama una undugu wa mbali na Adamu?
PAMELA: Tulijua wakati tumeshapendana sana ila hata hivyo undugu wetu hauna nguvu sana.
REHEMA: Hata kama, nyie ni sawa na dada na kaka ila ndo hivyo maji yashamwagika. Vipi huyo binti yenu atarudi lini?
PAMELA: Hata sijui mama, maana tangu ameolewa huko Arusha hatujapata kuzungumza na yeye hadi leo. Mwanzoni tulikuwa tunazungumza na mumewe ila sasa kimya.
REHEMA: Hivi mnajua kama Arusha kuna ujangili sana? Mnajua wanapoishi?
Akatokea Adamu nae na kuchangia.
ADAMU: Na huko Mombasa alipoenda mwanao je? Unadhani atakuwa mzima? Kama akiwa mzima basi shoga.
REHEMA: Sina maana mbaya, ila nyie kama wazazi mlipaswa kutambua kwanza anapoenda mtoto wenu kabla hajaenda. Mlipaswa kuwatambua ndugu wa mkwe wenu, mlipaswa kuwa na mawasiliano nao. Ila hapo mlipo hamjui chochote.
PAMELA: Usemayo mama ni kweli kabisa, tumefanya makosa sana kumuozesha mwanetu kwa mtu tusiyemfahamu vizuri. Ila hakuna la kufanya sasa, labda tungoje arudi tu.
REHEMA: Cha msingi ni kumuomba Mungu arudi salama, sinamaana kwamba mji wa Arusha ni mbaya hapana. Ila Arusha ina watu flani ambao hupenda sana kufanya mambo ya ajabu.
ADAMU: Sio Arusha tu, hata Mbeya kuna wachuna ngozi. Shinyanga kuna machinjachinja.
PAMELA: Mmh!! Na wewe Adamu unataka kuleta mada zako za mikoa hapa.
Adamu alipenda sana kumpinga mama yake huyu kwani alimuona ni mwenye upendeleo, kwa kumchukua pacha mmoja kumlea yeye na kumuacha yeye kwa baba yake ambapo alilelewa na mashangazi.
REHEMA: Unanichukia bure mwanangu, ila ni baba yako aliyetaka tugawane watoto. Sio kwamba sikukupenda mwanangu.
Pamela alimuhurumia bi. Rehema aliyejaribu kumuelekeza Adamu kila leo japo amuelewe.
Patrick akiwa nyumbani kwake na kuendelea kutafakari, akamuita Tusa, naye Tusa alishajiandaa kwa majibu yaliyonyooka iwapo akiulizwa chochote na huyo mumewe.
PATRICK: Hivi siku ile ulipopokea simu yangu ulimwambia nini mama?
TUSA: Sijamwambia chochote zaidi ya kujitambulisha tu kuwa mimi ni mkeo.
PATRICK: Na kwanini ulipokea Tusa?
TUSA: Kwanza sikujua kama ni mama yako, nilihisi ni mwanamke wako ndomana nikapokea nisikie atasemaje.
PATRICK: Inamaana Tusa umeanza kuwa na wivu na mimi?
TUSA: Ndio ninao, wewe ni mume wangu lazima nikuonee wivu.
Kauli ya Tusa ilimfanya Patrick ajisikie vizuri sana.
PATRICK: Vipi ukionana na mama yangu utamwambiaje?
TUSA: Sitamwambia chochote zaidi ya kufurahi kumuona.
PATRICK: Eeh ungependa mama yangu aje hapa umuone au nikupeleke alipo ukamuone?
TUSA: Nadhani itakuwa vizuri tukimfata yeye, kwani itanifanya hata mimi kutambua miji mingine.
PATRICK: Sawa sawa Tusa, naona leo umekuwa mke mwema. Usijari tutapanga safari hivi karibuni.
TUSA: Sawa mume wangu.
PATRICK: Aaaah! Umeniitaje Tusa?
TUSA: Mume wangu.
PATRICK: Umenifurahisha sana, siku zote ungekuwa hivi ningenenepa jamani.
Patrick aliona kuwa ameanza kupendwa na Tusa na hiyo ndio ikawa furaha yake.
Deborah bado alitafakari kwa kina mambo ya Patrick. Alimuona Patrick kuwa mtoto wa ajabu tofauti na malezi aliyompa.
Alipoona muda umepita sana akaamua kumpigia simu tena Patrick ili ajue jibu lake.
PATRICK: Mama usijari, nitakuja nae Mwanza.
DEBORAH: Kweli Patrick?
PATRICK: Kweli mama, nitakutajia siku ya kuja. Ni hivi karibuni kati ya siku mbili tatu mama.
DEBORAH: Mungu akutangulie mwanangu ili muweze kufika salama huku wewe na mkeo.
PATRICK: Asante mama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Deborah akafurahi kwani akahisi ni yule Patrick aliyemzoea kwani amejirudi sasa.
Sele akatokea na kumuuliza mama yake mdogo.
SELE: Mama, Patrick amekutajia jina la mkewe?
DEBORAH: Hapana ila anakuja nae huku Mwanza.
SELE: Lini hiyo?
DEBORAH: Kasema ataniambia hiyo siku.
Sele akabaki na lindi la mawazo huku maswali lukuki yakimuelemea kuwa je kama huyo mwanamke akiwa Tusa wake atafanyaje. Alikosa jibu kabisa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment