IMEANDIKWA NA : RAMADHANI K KAONEKA
*********************************************************************************
Simulizi : Jeraha La Moyo
Sehemu Ya Kwanza (1)
Jua angavu liliangaza mji huo huku likisindikizwa na upepo mkali ambao uliwafanya wakazi baadhi wa mji huo kugadhibika kutokana na kero ya upepo. Mara kadha ulileta purukushani kusambaratisha vitu huku na huko. Mtaa wa Mikanjuni katika mji huo wa Tanga. Vurumai lile la upepo liliukumba mtaa huo. Mara kwa mara wakazi wa mtaa huo. Walionekana wakiziba nyuso zao kwa mikono au hata kwa vitambaa au kanga kutokana na vumbi lililotimuliwa na upepo huo. Lakini hiyo haikufanya shuhuli zisiendelee.
Nguo zilizofuliwa na kuanikwa kwenye kamba pasi na kuchomekwa vishikizo. Zilianguka huku na huko na kuleta kero kwa dobi ambae alikuwa akizifanyia usafi. Hadi muda huo alishazirudia mara kadhaa baada ya kuanguka kwenye kamba. Upepo ulimletea kero si mchezo.
“Jamaniii! Aargh!...” aling'aka kwa ghadhabu huku akiitupilia ndani ya beseni nguo ambayo alikuwa akiifua baada ya nguo alizoanika kuanguka tena. Akainuka pale alipo na kuliruka lundo la nguo lililokuwa limejikusanya pembeni ya beseni.
“..........mara ya sita sasa hii kila mara nazirudia rudia hizi nguo kuzifua. Sa'ntamaliza saa ngapi mimi....” aliongea kwa hasira huku akiziweka vizuri zile ambazo zilining'inia vibaya juu ya kamba zikitaka kuangaku muda wowote kama zilivyoanguka zile nyengine. Akaziokota zile ambazo zimeanguka na kuanza kupiga hatua kurudi nazo pale alipokuwa akifua huku sura yake ikitangaza hasira za wazi wazi.
“Mama Ashuraa!” aliita kwa sauti huku akiztupilia ndani ya beseni jengine zile nguo alizotoka kuziokota baada ya kuanguka.
“Abeee” sauti ilisikika ikiitika kutokea nyumba ya pili pasi na mwenyewe kuonekana.
“Embu niazime vibanio vyako maana naona huu upepo unataka kunichezea....sijui umetumwa” akaomba anachokihitaji na kukaa kwenye kiti chake. Akalisogeza pembeni lile beseni la mwanzo na kulivuta lile jengine lenye nguo zilizoanguka kwenye kamba. Baada ya dakika moja. Kukaonekana kitoto kidogo chenye miaka yapata mi'nne kikija hapo na lundo la vibanio kikiwa kimeviweka kwenye gauni lake kwa mbele. Kilipofika pale kikaambiwa kiweke vibanio chini na yeye akaliachia gauni lake na vibanio vile vikaanguka na kusambaa pale chini. Kisha kikatimua mbio huku kikirukaruka na kuimba nyimbo anayoijua yeye.
Mara kidogo palisikika kelele za muuza samaki aliekuwa mbali na nyumba hiyo. Mwanamke huyo mtu mzima akaacha kufua na kurudisha mgongo wake nyuma mikono akiwa ameiweka juu ya mapaja yake. Alionekana kutafakari kitu. Akaziangalia zile nguo kwa sekunde kadha kisha macho yake akayapeleka kule barabarani ambako muuza samaki aliekuwa akinadi samaki zake alikuwa tayari ameshafika karibu na nyumba hiyo.
“Aargh! Sina namna nyengine sasa...” akamtazama yule muuza samaki aliekuwa kwa wakati huu ameshafika nje ya nyumba yake. “Samakiiii!” aliita kwa sauti huku akiinuka kwenye kiti alichokalia. Muuza samaki alisimama lakini hakusimama kuzinadi samaki zake kwa sauti kuu iliyochagizwa kwa mbwembwe kuzisifia samaki zake.
“ Nianao samaki watamu kushinda nyama ya kuku. Kula samaki uondoe magonjwa yako kama ugomvi na jirani, ugomvi na mume na pia wanaondoa madeni, nuksi, uchawi na mabalaa. Kula samaki ujione kama upo ulaya na Kanumba mkila raha. Kula samaki weeeeee” aliendelea kuzinadi samaki zake huku akifukuza nzi kwa majani yaliyokuwa mule mule ndani ya tenga. Mama yule alikuja na sufuria huku akiwa na tabasamu lililoelekea kucheka baada ya kusikia maneno ya kijana yule muuza samaki.
“Mdigo unatabu sana. Haya hao samaki wako wanaondoa vipi madeni” aliongea hivyo na wakati huo alikuwa tayari ameshamfikia.
“Embu acha maneno yako Msambaa sema unataka samaki wa shin'ngapi” Wakafanya biashara ya haraka haraka huku kila mmoja akizungumza lake. Mdigo au muuza samaki aliondoka huku akiendelea kuzinadi samaki zake baada ya kulipwa hela zake. Na mama mtu mzima aliondoka huku akiwapetapeta wale samaki waliokuwa ndani ya sufuria. Alipofika pale kwenye lile lundo la nguo. Akasimama. Akaziangalia zile nguo kisha macho yake akayapeleka kwenye lile sufuria lililokuwa na samaki ndani yake. Akachoka ghafla. Mkono wake wa kulia akaupeleka kiunoni kwake huku ile sufuria yenye samaki ambayo ameishika kwa mkono wa kushoto akiibananisha kwenye mbavu zake.
“Mmmgh!...” akaguna na kuliangalia tena lile lundo la nguo kisha macho yake akayarudisha tena kwenye ile sufuria.“ Haya huku ninakufua huku nako nina kutengeneza hawa samaki. Haya kazi zote hizi nitazifanya vipi kwa wakati mmoja?....aagh kufua hata kesho nitafua ila sio hawa samaki...lakini mwanangu angenisaidia mimi, sijui ni lini hali ile itamuondoka. Dah! Eee MUNGU naomba umnyooshee mkono wako mwanangu mimi. Mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja tu”
Mama huyo aliongea kwa masikitiko huku uso wake ukisawijika kwa huzuni zaidi ya ile mara ya kwanza. Akaziangalia tena zile nguo kisha akaaza kupiga hatua kuingia ndani ya nyumba hiyo. Huko moja kwa moja alienda jikoni na kuwaweka samaki wale aliotoka kuwanunua muda mfupi uliopita. Kisha akatoka na kupiga hatua kukifuata chumba kimoja kati ya vi'nne vilivyokuwa kwenye nyumba hiyo. Alipofika mlangoni. Akanyonga kitasa na kuzama ndani.
Huko alimkuta msichana mdogo mwenye umri usiovuka miaka ishirini na mbili akiwa amekaa juu ya kitanda kwa mtindo wa kuikunja miguu yake( kama mkao wa kula) huku mikono yake akiwa ameilaza juu ya mapaja yake, uso wake ukiangalia mbele na wala hakuonekana kujali au kujua kama kuna mtu ameingia mule ndani. Akiwa sura ameiangaliza mbele huku macho yake yasiopepesa yakiangalia mbele pasi na kuangalia sehemu yoyote.
Alionekana ni mrembo haswa ila urembo huo ulifichwa kwa hali aliyokuwa nayo. Nywele kichwani ziko timtim huku mashavu yake yakiwa na michirizi ya machozi yaliyogandiana. Macho mekundu yaliyoonekana kulia muda mwingi. Alikuwa kimyaa kama sanamu. Hadi sasa hakikujulikana ni kipi hasa kilichomfanya kuwa katika hali hiyo.
Mama huyo alionekana kuwa na sura ya huzuni sana baada ya kumuona binti huyo akiwa katika hali hiyo. Aliganda pale pale mlangoni huku akiendelea kumuangalia kwa masikitiko makubwa sana binti huyo. Akapiga hatua za kinyonge kumfuata pale kitandani alipokaa binti yule akiwa kimya vile vile. Akakaa na kumuangalia kwa dakika kadhaa usoni. Kisha mkono wake akaupeleka hadi kwenye mkono wa binti huyo. Akaushika mkono huo huku akiupapasapapasa. Kwa mara ya kwanza binti alitingisha kope zake lakini asitingishike mwili wala kichwa. Alikuwa vile vile.
“Cecilia mwanangu...” akaita mama huyo kwa sauti ya upole huku akimuangalia binti huyo aliemuita kwa jina la Cecilia. Lakini binti hakujisumbua kumuangalia mama huyo wala hata kutikisika. Mama huyo akaendelea.
“.....utaendelea kuwa katika hali hii mpaka lini binti yangu? Mbona unaniweka na hali ya mawazo kila mara. Mbona hutaki kunipa furaha mama yako? Mbona hutaki kuyasahau yaliyopita nyuma? usiwe hivyo binti yangu. Chukulia kama mtihani tu aliokupa Mungu. Sasa utakuwa katika hali hii mpaka lini? Ona mwili wako unavyoporomoka kwa kujiweka katika hali hiyo. Ona unavyokonda kwa mawazo. Ona unavyoteseka mwenyewe. Embu ona basi!.. Hunipi furaha hata kidogo mwanangu. Wewe ndio mtoto wangu wa pekee tangu baba yako alipofariki. Ameniachia nikulee mwenyewe na wala halikuwa tatizo. Nimekulea tangu ukiwa binti mdogo sana na hadi sasa umekuwa. Unajua lipi baya lipi zuri. Sasa kwanini hutaki kuyasahau yaliyopita. Acha kuwa hivyo mwanangu” Mama huyo aliongea kwa upole na kubembeleza. Akanyamaza kidogo. Kisha akaendelea.
“Cecilia yaache ya nyuma yapite. Yaache yaliyopita yabaki kama historia. Kama ingekuwa kila mtu anayapa nafasi ya kuyakumbuka yaliyomuumiza nyuma, basi kusingekuwa na mtu mwenye akili timamu hata mmoja. Wengi walishaumia kama ulivyoumia wewe lakini walilia na wakayasahau. Sasa wewe nashangaa una mwezi wa tatu sasa mambo yale bado yapo kwenye kumbukumbu zako. Embu acha hizo binti yangu. Ukiwa katika hali hiyo mi moyo wangu unakosa amani kabisa. Nahofia kukupoteza mwanangu. Nahofia kukupoteza binti yangu. Aargh!...” akashindwa kuendelea kuongea. Akabaki akilia tu kilio cha kwikwi huku machozi yakikipamba kilio hicho. Lakini hiyo haikua sababu iliyomfanya binti huyo hata kutikisika. Alibaki vile vile akiwa ameangalia mbele bila kupepesa macho yake sehemu yoyote ile. Kumbukumbu ya miaka kumi na mbili iliyopita ikamjia kichwani mwake wakati analia.
Miaka kumi na mbili nyuma.
“Hah hah hahah! Hapa ndio kwangu bwana jisikie huru na siku yoyote utakayoamua kuja wewe njoo tu bosi wangu” Mwanaume mmoja aliekadiriwa kuwa na miaka thelathini hadi thelathini na tano, alimuambia hivyo mtu mwengine alieonekana kuwa mkubwa kwake kiumri. Nae alikadiriwa kuwa na miaka arobaini hadi araobaini na tano. Alimuambia hivyo kumkaribisha bosi wake kama mwenyewe alivyomuita nyumbani kwake kwa bashasha kuu.
“Usijali Mr Ally nimeshakaribia” mtu huyo aliongea kwa sauti nzito yenye tambo za majivuni ndani yake. Wakaingia ndani ya nyumba hiyo na kumkaribisha kwenye masofa yaliyokuwa ndani humo.
“Sasa Mr Ally mi sikuja kukaa sana hapa kwako. Naomba unipatie zile Docoment niende nazo nikawapatie sasa hivi wale.....” mtu huyo alieitwa kwa jina la bosi alikomea hapo baada ya kutokea mwanamke mrembo alionekana ni mwenye uchovu mwingi wa usingizi. Bilashaka alikuwa ametoka kulala mchana hiyo. Macho yake yakaganda kwenye uso wa mwanamke huyo na wala asijali hamaniko lililomkumba bwana Ally baada ya kuona bosi wake amegandisha macho yake kwa mwanamke yule.
“Bo...bosi huyo apo ni mke wangu kipenzi changu mwanamke pekee aliechaguliwa na moyo wangu” Mr Ally aliongea kwa kujiumauma kupoteza hiyo hali iliyo gubika ndani humo ghafla.
“Hah hah hahah! Mr una mke mzuri sana bilashaka atakuwa ni Msambaa huyu” Bwana huyo aliongea huku akiwa bado macho yake hayaja ganduka kwenye uso wa mwanadada yule aliekuwa amesimama pale pale upenuni mwa ukuta. Muda huo huo pakaingia mtoto mdogo aliekuwa katika mavazi ya shule. Aliingia kwa furaha humo ndani na kwenda kumkumbatia Ally aliekuwa amekaa kwenye sofa tofauti na lile alilokaa yule bwana majivuni. Akasalimia kwa kumuita baba kisha akafanya vile vile na kwa yule mwanamke aliekuwa amesimama pale ukutani. Yule nae alimuita mama.
“Cecilia binti yangu mbona hujamsalimia anko hapa” Ally alimuambia mtoto yule aliemuita kwa jina hilo baada ya kumuona amemng'ang'ania mama yake. Mtoto yule ndipo alipogeuka na kutazama kwenye lile sofa jengine na kukuta kuna mtu amekaa akiwa anajichekeshachekesha mwenyewe. Akajongea kwa hatua za kivivu hadi pale alipokaa yule bwana. Akamsalimia na yule bwana akaitikia na kumuhoji hoji maswali mawili matatu kuhusiana na shule. Kisha akamuweka katikati ya miguu yake.
“Mama Cecilia, embu nenda kwenye ile droo kule chumbani kuna bahasha kubwa naomba uniletee” Ally aliongea hivyo na yule mwanamke akageuka kwaajili ya kwenda alipoagiziwa. Cecilia nae alichomoka kwenye miguu ya yule bwana na kumkimbilia mama yake wakaingia wote ndani. Baada ya dakika moja mama Cecilia alirudi na bahasha na kumkabidhi Ally. Kisha Ally akaiangalia ndani kwa kuichungulia halafu akampatia yule bwana.
“Sasa Mr Ally acha mimi niende niwahi mara moja nyumbani” Aliongea yule bwana huku akiinuka kwenye lile sofa. Ally nae akainuka.
“Acha nikutoe hadi hapo nje bosi”
“Shemeji mimi naenda tutakutana siku nyengine na kuanzia sasa mimi nishakuwa mgeni wako kwahiyo usishangae nikija siku yoyote hapa” Yule bwana aliongea hivyo na mwisho kabisa akamalizia na kumbania jicho mke wa Ally. Kitendo hicho Ally hakupata kukishuhudia kwasababu yeye alikuwa tayari yupo karibu na mlango wa kutokea huku yule bwana akiwa bado nyuma yake. Kwa mshangao uliompata mke wa Ally wala hakuweza kujibu chochote baada ya kushuhudia kitendo hicho. Akabaki kutumbua macho na asijue kuwa bwana huyo alimaanisha nini kumfanyia hivyo.
Wakatoka hadi nje na bwana yule akaondoka akimuacha Ally akirudi zake ndani. Sebuleni alimkuta mke wake amekaa kwenye sofa na wala asiwe na sura yoyote ya furaha. Akamfuata taratibu na kupiga magoti mbele yake huku uso wa umakini ukiwa nae. Viganja vyake vya mikono akaviweka kwenye mapaja ya mke wake.
“Unanini mke wangu kipenzi mbona huna furaha kama nilivyokuzoea? Au kuna jambo lolote haliko sawa?” Ally aliongea kwa upole na sauti ya kubembeleza huku akiwa anamuangalia mke wake kwa uso wa mashaka.
“Hapana mume wangu kawaida tu. Halafu si unajua nimetoka kulala muda si mrefu. Kwahiyo bado nina uchovu kidogo” Hapo Ally akatabasamu na kuinuka taratibu. Kisha akampiga busu la kwenye paji la uso mke wake.
“Pole kwa uchovu mke wangu, nilidhani labda unatatizo lolote ila kama ni uchovu basi endelea kupumzika acha niingie ndani nikabadili nguo nije kukusaidia baadhi ya kazi za hapa”
“Usijali mume wangu wewe pumzika tu, umechoka na kazi za huko kwahiyo haina haja tena ya kujichosha na kazi za hapa. Mi'ntazifanya hata hivyo sio nyingi kivile” aliongea mwanamke huyo huku tabasamu la upendo likiwa usoni mwake. Tabasamu la kweli na wala sio la kuigiza. Tabasamu ambalo lilimfanya Ally kumpiga tena busu la kwenye papi za mdomo kisha akaondoka hapo na kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Akiachana na uchovu aliokuwa nao. Pia kule kukonyezwa na yule bwana ambae ametambulishwa kuwa ni bosi wa mume wake. Ndio kitu kikubwa kilichomfanya akose raha ghafla. Maana alijua nini maana ya kile kitendo. Akajua kivyovyote vile yule bwana ana lake jambo. Akaona ndoa yake inaenda kuvurugika muda si mrefu kama bwana yule atakuwa amekusudia kama vile alivyo waza yeye. Akamuomba mungu kimya kimya ainusuru ndoa yake dhidi ya shetani mtu alieanza kuonyesha makucha yake.
Na kilichomnyima raha zaidi ni vile bwana yule alivyo ahidi kuja kumtembelea kama alivyodai. Akawaza kumuambia mume wake hofu yake. Lakini akaona huenda ikawa ataonekana ni mshamba kwa jambo hilo hata hivyo bwana yule ndio mara ya kwanza kuja kwenye nyumba hiyo. Akapuuzia kumuambia mume wake akidhani ataleta uchonganishi kati ya mume wake na bosi wa mume wake. Akakaa kimya akipuuzia jambao hilo.
Lakini hakujua. Hakujua yepi yangekuja kutokea huko mbele kwa kulipuuzia jambo hilo. Ni bora angemuambia huenda ikawa angeweza kuepuka kwa namna moja au nyengine matatizo yaliyokuwa mbele yake.
Akainuka pale alipokaa na kwenda jikoni. Huko alichukua mabakuli ya chakula na kuyapeleka kwenye meza ya chakula. Akaanda kila kitu kilichopaswa kuwa juu ya meza hiyo. Baada ya hapo akaingia chumbani na kumkuta mumewe ndio anatoka kuoga. Tabasamu kwenye nyuso zao likaonekana dhahiri baada ya kuangaliana.
Upendo.
Mapenzi ya kweli ama upendo wa kweli unaweza ukawafanya wapendanao wafurahikiane kila mara waonanapo. Tabasamu ni kitu cha kwanza kwenye nyuso za wapendanao. Tabasamu huongeza theluthi kadhaa za mapenzi kwenye mioyo iliyofanana kwa upendo. Huweza kuondoa hata hasira ama mnuno kama utakuwa umemuuzi mwenza wako. Jaribu kutabasamu kabla ya kuomba msamaha kisha tumia sauti nzuri ya kubembeleza kwa hisia za kweli. Kama ni kweli mwenza wako anakupenda kwa dhati. Basi mioyo yenu itazungumza hilo.
“Mume wangu twende tukale chakula tayari kipo mezani” Mama Cecilia aliongea kwa sauti ya mahaba ambayo ilimfamfanya Ally au baba Cecilia kuongeza tabasamu zaidi usoni mwake. Hakuongea kitu zaidi ya kutabasamu vile vile. Akaiendea henga na kuchomoa bukta ndefu iliyokuwa inaning'inia juu yake. Akaivaa kisha akavuta na fulana ya mpira nayo pia akaivaa. Wakaongozana hadi kwenye meza huko walimkuta Cecilia tayari ameshakaa kwenye kiti akiwasubiri wao. Hapakuwa na maongezi yoyote zaidi ya kula tu..
Siku iliyofuata wakati bwana Ally akijiandaa kutoka kazini kwake. Akashtukia akiitwa na mfanyakazi mwenzake kuwa alikuwa akihitajika na bosi wao. Akapiga hatua kuiende ofisi ya bosi wake. Alipofika akamkuta bosi wake akiwa na tabasamu kuu. Akampa ishara ya kukaa na yeye akakaa. Bwana yule ambae anajulikana kwa jina la Antony Magasa. Akapekuwa droo yake na kutoka na kiboksi kidogo kisha akampatia Ally.
“Hiyo ni zawadi kwa shemeji. Ukifika utampatia zawadi yangu” Antony Magasa aliongea huku akiwa anatabasamu. Ally alikipokea kiboksi hicho huku akiwa na mshangao wa dhahiri. Ila akapotezea kwa kutabasamu. Kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo akiwa na maswali kibao yaliyokisumbua kichwa chake. Akaingia ndani ya gari lake na kutulia humo.
“Yani kumkaribisha jana tu nyumbani kwangu leo hii ananipa zawadi eti nimpelekee mke wangu?” alijiuliza kwa sauti ndogo huku akikiangalia angalia kiboksi hicho. Akakifungua na kukuta ilikuwa ni cheni ya dhahabu ‘pure’. Ilikuwa ikiwakawaka si mchezo. Akaguna baada ya kuona kitu chengine kilichomshtua zaidi. Cheni ile kwa chini ilikuwa na herufi ‘A’. Akaguna tena na kuiangalia vizuri cheni hiyo hasa hasa kwenye ile herufi.
“Hii ‘A’ ina maanisha nini? Inamaanisha jina la bosi wangu Antony, au inamaanisha jina langu Ally. Au au... Inamaanisha jina la mke wangu Anitha? Lakini kalijuaje wakati sikuwahi kumuambia wala jana mke wangu hakuwa na dalili hata za kumuambia jina lake?...” akaguna tena kwa mara ya tatu.
“Au labda alimaanisha jina langu?.... Lakini atamaanisha vipi jina langu wakati zawadi hii ameitoa yeye?.... Bilashaka hii zawadi alimaanisha jina lake.... Sasa jina lake lina husiana vipi na mke wangu? Mbona bosi anataka kunichanganya sasa huyu... Aargh!..” akapiga kite cha ghadhabu na kuirudisha cheni ile ndani ya kile kiboksi. Akaondoa gari mdogo mdogo akiwa amepitisha wazo la kutompatia mke wake ile zawadi aliyopewa.
Safari yake iliishia kwenye baa moja iliyopo katika mtaa wa Chumbageni. Hapo alishuka kwenye gari na kuingia ndani humo. Akatafuta meza moja iliyokuwa pweke na kukaa hapo huku mkononi mwake akiwa na kile kiboksi. Akatoa simu yake na kuiminyaminya kisha akaiweka sikioni. Akaongea maneno mawili matatu na simu akaiweka mfukoni baada ya kuikata.
Punde tu akaja muhudumu na kumtaka aagizie anachotaka. Akaagizia maji baridi na kutulia. Yule muhudumu akarudi tena na kumletea maji hayo yaliyokuwa yakitiririka kijasho cha ubaridi. Akamimina kwenye glasi na kuanza kunywa taratibu. Mawazo kibao yalimpitia kichwani mwake. Bosi wake alimchanganya sana sio mchezo. Baada ya dakika saba akaja mtu mwengine hapo na kukaa. Wakasalimiana, na huyo mtu mwengine yeye aliagizia kilevi baada ya muhudumu kumtaka aagizie anachotaka.
Muhudumu alirudi na kinywaji hicho nae akampatia na kukifungua. Akaanza kukinywa taratibu huku wakianzisha maoengezi ya kawaida. Baada ya muda. Ally akaona amuelezee kile ambacho alichomuitia huyo rafiki yake. Baada ya kuelezwa hicho kitu alikuna kichwa huku akitafakari sana. Mwisho akainua sura yake na kumuuliza Ally swali.
“Kwanza ilikuaje bosi akaenda nyumbani kwako?”
“Kulikuwa kuna docoment alizihitaji kwa haraka. Sasa ndio nikaongozana nae hadi nyumbani. Hadi hapo ndipo huo mkasa ulipoanzia” Ally alilijibu swali hilo.
“Dah! Ndugu yangu hapo kuna namna. Haiwezekani eti umuangalie mtu tu namna hiyo hata ule uoga kwamba huyu ni mke wa mtu pia huna. Halafu leo hii anakuja kuleta mazawadi. Hicho kitu ndugu yangu mi kinanitia mashaka sana”
“Kwahiyo wewe unahisi nini?” Ally alimuuliza huku akinywa kinywaji chake.
“Mi nahisi bosi atakuwa ameshaanza kumtamani mke wako na kuanzia sasa uchunge sana na hiyo zawadi pia usimpelekee kwasababu utamchanganya mkeo”
“Hata mimi pia nimefikiria hivyo. Lakini je kesho akiniuliza kuwa nimeifikisha ile zawadi yake sasa nitamjibu nini?”
“Aaaaa! Ally mke wako yule na Antony Magasa ni bosi wako. Kwani hata kama ukimjibu kuwa hujamfikishia atakufanya nini? Au unahisi atakufukuza kazi? Acha hizo bwana mke wako una mamlaka nae kuliko mtu mwengine yoyote. Sasa ukianza uoga hapa mi nakushangaa eti”
“Ila kweli...” akakitoa kile kiboksi na kukishika shika tena.“.....zawadi yenyewe ni hii hapa” akampatia yule jamaa na kuiangalia na yeye.
“Sasa hii ‘A’ inamaanisha nini? Jina lako au jina lake?”
“Ajabu sasa ndio iko hapo maana hata mke wangu pia jina lake linaanza na ‘A’” yule jamaa macho yakamtoka pima huku akimuangalia Ally kwa mshangao.
“Kwahiyo mke wako pia jina lake linaanzia na ‘A’? Sasa kalijuaje? Au ulimuambia?”
“Hapana sikufikiria hata kumuambia na wala mke wangu jana hakuongea chochote zaidi ya salamu tu”
“Basi huenda ikawa alimaanisha jina lake yeye au jina lako wewe” Jamaa huyo aliongea huku akimrudishia kiboksi kile. Wakazungumza kidogo na mwisho wakaagana huku Ally akilipitisha wazo la kutompelekea mke wake ile zawadi aliyopewa na bosi wake.
* * * *
Ilipita wiki moja ikiwa bado Antony Magasa haishiwi kumuuliza Ally chochote kuhusiana na mke wake. Mara vizawadi vya hapa na pale huku akimsisitiza amuambie kuwa ipo siku atakuja kumtembelea. Kauli hiyo ilimuacha hoi sana Ally kila aambiwapo, akabaki kujiuliza. Inamana ni kumtembelea na wala sio kuwatembelea. Akajua kivyovyote bosi wake ana lake jambo.
Lakini nae hakufanya jitihada zozote zile za kumjulisha mke wake juu ya vituko vya bosi wake. Akawa ni mkimya pasi na kujua kuwa ukimya wake unaweza kuja kumgharimu huko mbele.
Mara kadhaa alishawahi kujaribu kumdodosadodosa mke wake juu ya bosi wake. Lakini alionekana kama anamuonelea tu maana hakukaribia kujua chochote kuhusina na bosi wake. Alichojibu yeye ni kuwa alimuona mara moja tu tena ni ile siku aliyokuja nyumbani hapo na wala hakuwahi kuiona tena sura ile.
Akajaribu kumgusia kuwa bosi wake anamsalimia sana, lakini alikutana na sura iliyoonyesha kuchukia habari za mtu huyo. Yani hakutaka kwenye maongezi hayo atajwe mtu huyo. Na alikasirika kiasi ambacho alinuna kabisa na kumpa kazi Ally ya kumbembeleza. Hapo Ally akajihakikishia kuwa hata mke wake pia alikuwa hana habari na bosi wake.
Siku moja majira ya mchana. Anita alisikia geti lao likigongwa hodi. Akajua kama sio mume wake amerudi kutoka kazini, basi atakuwa ni mtoto wake amerudi kutoka shule. Akainuka na kwenda kufungua geti. Anita alichukizwa baada ya kumuona aliekuwa akigonga hodi. Lakini punde alibadili na kuweka tabasamu bandia kumkirimu huyo mgeni. Hata yeye hakujua ni kwanini anamchukia mtu huyo na wakati ni mara ya pili tu kumuona mpaka muda huo.
Antony Magasa ndie ambae aliekuwa hapo majira hayo. Tabasamu usoni mwake halikukauka na ndio lilizidi muda hadi muda. Alishamsalimu mara tatu Anita lakini alionekana kuwa mbali kimawazo. Ikabidi hivi sasa aongeze kidogo sauti ndipo Anita alipogutuka na kuitikia salamu hiyo, hata hivyo pia hakuonekana kutaka kumkaribisha ndani mgeni huyo hadi pale Antony alipoomba kuingia ndani ndipo Anita alipompisha mlangoni alipokuwa amesimama.
Wakaingia ndani huku Anita akiwa na wasiwasi mwingi mno. Hakumuamini mtu huyo hata kidogo na wala asijue ni kwani hataki kumuamini. Kilichomtia uoga zaidi ni vile kuwa peke yao ndani ya nyumba hiyo. Tabasamu la hofu bado liliendelea kuwa usoni mwake hata pale walipokuwa wamekaa sebuleni akiwa tayari ameshampatia kinywaji cha maji mgeni huyo alichokiomba.
Kimya kilitawala hapo sebuleni ikiwa macho ya Antony yakiwa hayaganduki usoni mwa Anita. Jambo hilo lilimnyima raha sana Anita, hakupenda aangaliwe namna hiyo na mtu huyo. Na sio huyo tu, ni mtu yoyote yule hakupenda amuangalie usoni kwa muda mrefu isipokuwa mume wake Ally tu. Na hicho ndicho kilichompa ‘pont’ Antony Magasa kuongea alichopanga kuongea. Akajikohoza kiumbea kisha akasema.
“Bilashaka ulizifurahia zawadi zangu?” Antony aliongea hivyo huku akitabasamu. Anita aliinua uso wake ukiwa na umakini na mshangao ndani yake baada ya kusikia kauli hiyo. Alimuangalia kwa muda Antony na asijue amjibu nini. Alibaki kujiuliza mwenyewe. Zawadi? Zawadi zipi hizo anazozizungumzia mtu huyu ikiwa ndio mara ya pili kuonana?..
“Zawadi zipi?” Anita akauliza kwa mshangao.
“Kwahiyo hukuwahi kupokea zawadi zozote kutoka kwangu?” Antony alimuuliza huku akitabasamu tabasamu la mshangao. Alishajua kuwa Ally hakuwa akizileta zile zawadi alizokuwa akimpatia amletee mkewe. Anita akataka kuongea kitu. Ila akawahiwa na sauti ya Antony.
“Usifikirie sana mrembo nilikuwa nakutania tu..." akatulia kidogo na kunywa yale maji. Kisha akamuambia. “....naweza nikakutoa sehemu mchana huu?”
“Hapana siwezi. Na siwezi kutoka bila ruhusa ya mume wangu” Anita aliongea.
“Basi mpigie simu na umuambie kuwa unatoka na mimi mchana huu”
“Sina simu” alijibu lakini alionekana kuchoshwa na maongezi hayo. Na sio kama ni kweli hakuwa na simu. Alikuwa nayo lakini hakutaka maongezi na mtu huyo yaendelee.
“Ok. Shika simu hii wasiliana nae na umuombe kutoka na mimi” Antony aliongea huku akimyooshea mkono wenye simu Anita. Ila Anita hakujisumbua kuipokea ile simu.
“Hata hivyo sijisikii kutoka. Sijisikii kutoka na mtu yoyote isipokuwa mume wangu tu” Anita sasa alijibu kwa jeuri hafifu baada ya kuchoshwa zaidi na maongezi hayo. Antony alirudisha simu yake mfukoni.
“Sawa... Kuna jambo nataka nikueleze” akanywa maji yaliyokuwa nusu kwenye glasi. Kisha akainua sura yake na kuuangalia uso wa Anita usiokuwa na tabasamu hata la kuchongesha. Lakini bado uzuri wake ulibaki nae, tena pengine labda ungesema ni bora abaki hivyo hivyo ndio anakuwa mzuri zaidi. Na anapotabasamu pia utasema ni bora awe hivyo kila muda achilia mbali akicheka. Alikuwa na uzuri wa asili.
“Nataka niyabadilishe maisha yako kutoka kwenye huu ufukara hadi kuwa mtu mwenye heshima kuliko mwanamke yoyote katika jiji hili...” akatulia kidogo na kuiangalia ile glasi ambayo kwa sasa haikua na kitu ndani. Anita nae macho yake akayapeleka pale kwenye ile glasi na ndipo alipogundua kuwa haikuwa na maji kwa wakati ule. Hakujishuhulisha nayo. Macho yake akayapeleka kwenye uso wa bwana yule. Wakati huu hata ile aibu aliyokuwa nayo pindi aangaliwapo usoni na mwanaume kwa muda mrefu hakuwa nayo. Hiyo ilitokana na kuchoshwa na uwepo wa mtu huyo hapo ndani.
“Nakupenda na ninataka nikuoe....” akayaongea hayo na kutulia kimya akiuona mshangao wa Anita baada ya kusikia kauli hiyo. Anita alikerekwa zaidi baada ya kusikia maneno hayo. Chuki ya waziwazi ilionekana usoni mwake. Kifua kilipanda na kushuka kwa hasira. Akataka apige mayowe lakini asijue apige mayowe kwa ajili gani. Akatamani ampige vibao mtu huyo lakini akaona uwezo huo hakuwa nao. Wazo lililomjia kwa wakati huo ni kumtoa ndani humo. Akainuka pasi na kusema chochote na kuuendea mlango wa kutoke humo. Akaufungua kwa pupa na macho yalimtoka pima baada ya kuishuhudia sura ya mume wake mlangoni hapo aliekuwa akijianda kuufungua mlango huo kutaka kuingia ndani.
“Oooh! Karibu mume wangu” Sura ya chuki aliiyondoa na kuweka tabasamu. Akampokea mkoba aliokuwa ameubeba mumewe.
Ally akapigwa na butwaa baada ya kuingia sebuleni na kumkuta bosi wake akiwa amejipweteka kwenye masofa. Hata Antony aliingiwa na haya baada ya kumuona baba mwenye nyumba akiingia. Ukweli ni kwamba. Antony siku hiyo alimpatia Ally kazi nyingi za kufanya ofisini. Na mpango huo aliuandaa siku chache nyuma ili itakapofika siku hiyo. Ampatie kazi nyingi Ally ofisini ili yeye apate muda mzuri wa kukaa na mke wake.
Mwanzo alidhani Ally ameziacha kazi alizompatia na kuamua kurudi nyumbani. Lakini alipoangalia saa yake ya mkononi. Akamaizi ni saa moja na nusu imepita sasa baada ya kumuachia kazi hizo. Kivyovyote Ally amezimaliza kazi zile na muda huo ndio alikuwa akirudi nyumbani kwake. Akaujutia uchelewaji wake kwa kupitia nyumbani kwake kwanza kabla ya kuja nyumbani kwa Ally.
“Aaaa! Bosi kumbe upo? Karibu bwana” Ally alisema hayo baada ya kumuona bosi wake. Mara hii aliuficha ule uso wa taharuki uliomkuta mwanzo wakati anaingia. Sasa alikuwa na mashaka na bosi wake na asijue ni kwanini muda huo awepo nyumbani kwake ilhali yeye hakuwepo.
“Ni mimi ndie napaswa kukukaribisha Mr. We si umetukuta?” Antony aliongea kwa utani ili aondoe mashaka yaliyojionyesha dhahiri kwa Ally kipindi anaingia.
“Hahaha haya bwana nimekaribia tayari” Ally aliongea huku akikaa kwenye sofa jengine.
Mara hii Anita alieingia ndani kuupeleka mkoba wa mumewe alirudi. Akaenda kukaa kwenye lile sofa alilokaa Ally. Akamuegamia kimahaba huku akimtupia jicho pembe Antony. Wivu ulimshika utafikiri alikuwa ni mke wake. Akamakazia jicho Anita kipindi ambacho Ally alikuwa bize na simu yake.
“Mmependezana” Antony aliyasema hayo huku akijichekesha_chekesha kama zuzu. Ally aliinua kichwa na kumuangalia bosi wake huku akiwa anatabasamu. Kisha macho yake akayahamisha kwa mke wake.
“Vipi. Mbona humuwekei mgeni chakula?” Ally alihoji.
“Si amekataa. Nimemkaribisha mara nyingi kweli” Anita alijibu huku akimuangalia Antony usoni.
“Usijali Mr nipo vizuri hapa maana nilipotoka kazini nilipitia nyumbani. Na hapa naelekea Kwaminchi ndio nikaona nipitie hapa kwa shem wangu maana ni muda sasa sijafika kumsalimu....” Antony aliongea huku akichekacheka. “......acha mi niwahi nitarudi siku nyengine kuwasalimu”
“Sawa Mr. Mi sikutoi maana nimechoka sana na zile kazi nimezimaliza bado saini yako tu ziwetayari kuwapatia wale mabwana”
“Hakuna shaka Mr mambo yote tutayamaliza kesho”
Antony aliaga na kuondoka. Ally na Anita wakabaki wenyewe. Kimya kilichukua nafasi kama dakika mbili. Kila mmoja hajui amuanze mwenzake vipi. Anita alivunja ukimya huo kwa kumuambia mume wake anahitajika akaoge ili apate kula. Ally alishukuru kwa kukumbushwa na kuingia ndani akimuacha mkewe akiandaa chakula. Na mara hiyo hiyo Cecilia nae akarudi kutoka shule.
Chakula kilitengwa mezani na wote watatu wakachukua nafasi. Kimya kilitawala wakati wanaendelea kula. Kila mmoja alikuwa akiwaza lake. Ally aliwaza amuulize mkewe kuwa bosi wake amefuata nini hapo nyumbani, maana alishaanza kumtilia shaka tangu siku ya kwanza kumkaribisha hapo. Huku Anita akiwaza kumuambia mumewe kuwa, hataki kumuona bosi wake akija hapo nyumbani kwake. Lakini kikwazo kikaja ni vipi atajibu pindi akiulizwa kwanini anaamuzi hilo? Cecilia nae aliwaza michezo yake baada ya kumaliza kula.
“Mume wangu...” Anita aliita wakati wanaendelea kula. Ally akamuangalia ishara ya kumtaka aendelee. Akaendelea. “.....tafadhali sana. Naomba yule bosi wako asifike hapa nyumbani” Ally alimkazia macho Anita kwa mshangao huku chakula alichokuwa akikitafuna alikituliza kwanza mdomoni. Sio kwamba alishangaa kuambiwa kuwa bosi asifike hapo? La hashaa! Bali aliishangazwa na kauli hiyo. Akameza kile chakula kwa tabu maana hakuwa amekitafuna vyema na kusababisha kipite kwa tabu kidogo kooni. Kisha akahoji kwanini amesema hivyo.
Anita alijing'atang'ata kwasababu hakuwa na jibu la kueleweka la kumpa mumewe. Akatulia kimya akiendelea kula huku sura yake ameinamisha chini. Muda wote Ally alikuwa akimkazia macho akisubiri jibu. Mashaka yaliongezeka mtimani kwake kwa kuhisi kuwa kuna mchezo unaendelea kati ya mkewe na bosiwe. Hasira zikampanda ghafla baada ya kuona ukimya wa Anita unazidi kuchukua nafasi bila kutoa jibu lolote.
Akakema kwa hasira kiasi ambacho Anita alishtuka. Hapana. Si Anita pekee alieshtuka. Hata Cecilia mtoto wao pia alishtuka. Akamuangalia baba yake kwa macho ya mshangao na kuhamisha kwa mama yake. Hakuelewa chochote!. Ally baada kumaizi amefanya kosa kumkaripia mkewe mbele ya mwanae. Akajichekesha huku akimuangalia Cecilia. Cecilia nae akacheka!.
Ally baada ya kuona furaha ya mwanae ameirudisha. Akamkata jicho la chuki Anita, kisha akainuka na kupotelea ndani bila kunawa mikono. Anita akazuga sekunde kadhaa ili amuache mwanae akiwa hana viulizo kwa yale yaliyotokea punde tu hapo. Akanawa mikono na kumfuata mumewe kule chumbani alipoelekea. Huko alimkuta Ally akiwa amevimba kwa hasira mithili ya chura wa mtoni.
“Naomba uniambie nini kinaendelea kati yako na bosi wangu, la sivyo.....” Akanena maneno hayo na kuikatisha sentensi yake kwa kutilia mkazo aliyoyasema.
“Hakuna chochote kinachoendelea mume wangu. Ila bosi wako mi simuelewi...” Akaikatisha sentensi yake na kuangalia chini akishindwa kumalizia. Ally akamuambia kwa sauti kali kuwa amalizie huku macho yakimtoka mithili ya fundi saa aliepoteza nati.
“Ananitaka!” Anita aliongea kwa uoga huku akitetemeka kama amemwagiwa maji kipindi cha baridi kali.
“Anakutaka!? Kivipi” Ally alihoji. Anita alishindwa afafanue vipi. Alijua mumewe alimuelewa ila alitaka kumtia shuhuli ya kujieleza. Siku hiyo ikaisha bila maelewano yoyote kati ya wawili hao. Hata pale Anita alipomuambia kuwa bosi wake alikuwa akimtongoza lakini bado Ally aling'ang'ania kwa kusema kwamba wanamzunguka.
“Ipo siku nitaujua ukweli tu. Na hiyo siku ikifika....” Akaacha sentensi yake ining'inie hewani na kupotelea nje isijulikane ameenda wapi. Anita alibaki akilia huku akimuomba mungu wake ainusuru ndoa yake dhidi ya shetani mtu aliejitokeza kwaajili ya kuwatenganisha.
* *
Ally alirudi nyumbani kwake asubuhi. Alimkuta Anita akiwa sebuleni amekaa kinyonge huku usoni michirizi ya machozi ikionekana. Ukweli ni kwamba. Usiku wa siku iliyopita tangu mumewe alipoondoka nyumbani. Hakupata hata lepe la usingizi kutokana na kutojua ni wapi mumewe alipo kwa muda huo. Je huko alipo yuhali gani? Akabaki sebuleni akimuombea mungu arudi salama na afanye hima kuirejesha amani kwenye ndoa yake.
Hakuzoea kutokuwa na maelewano mazuri na mume wake kwa muda mrefu mpaka ifikie kulala nje ya nyumba yake. Alifikiria ni lini mumewe aliwahi kulala nje ya nyumba na kukumbuka ni mara moja tu, tena siku hiyo alienda kijijini kwao baada ya kusikia mamaye anaumwa, na hata siku ya pili ilipofika alirejea nyumbani huku akisema hali ya mzazi wake ipo vizuri tofauti na yeye alivyodhani. Ni siku hiyo tu ndio alilala nje ya nyumba yake. Na hii ya leo ni ya pili lakini hakujua ni wapi amelala.
Akamsalimu mumewe kwa heshima zote na wala Ally asijali hata kidogo salamu hiyo. Papo hapo Anita alianguka miguuni kwa mumewe akidai anaomba asikilizwe. Na sio asikilizwe tu. Pia aaminiwe kwa atakachoongea. Maana hata siku iliyopita aliongea lakini hakuaminiwa. Ally alimuangalia kwa hasira, fikra zake zikimtuma kuwa anataka kudanganywa tena kama siku iliyopita alivyodanganywa. Sasa nani anamakosa kati ya hao wawili? Anita anaehisiwa kuwa anatoka kimapenzi na bosi wa mumewe. Ama Ally anaehisi mkewe anatoka kimapenzi na bosi wake? Duh!!.
Huruma zimuendee Anita aliepitwa bila kuambiwa chochote na Ally. Alibaki akilia kwa uchungu huku akimlalamikia Mungu wake ya kuwa kwanini usiku mzima alikesha kumuomba ainusuru ndoa yake na majibu yake yamekuja tofauti. Alilia huku akirusha rusha mito ya kwenye masofa.
Muda huo huo Ally alitoka akiwa tayari kwenda kazini. Anita alimfuata na kupiga magoti huku akiwa amemshika miguu yake akimuomba walau sekunde moja tu amsikilize na amuamini. Ally alimkemea kwa ghadhabu kuwa amuachie anataka kuwahi kazini na hana muda wa kukaa chini na kusikiliza maneno ambayo alijua dhahiri atadanganywa. Anita aliendelea kumshikilia vile vile huku akimsihi amsililize tu. La haulaa!!.
Ally alifanya kitendo ambacho tangu amuoe Anita hakuwahi kukifanya. Na sio tu hakuwahi. Pia hakufikiria kama atakuja kukifanya kwa mke wake mpendwa. Sauti kali ya kofi lililotua shavuni kwa Anita ilisikika na Anita aliachia haraka miguu ya Ally na kushika shavu lake huku akilia kwa uchungu zaidi baada ya kuadhibiwa na mumewe bila makosa. Ally alisonya na kupotelea nje akimuacha Anita amejilalisha chini huku akilia kwa uchungu. Bado aliendelea kulia na mungu wake.
Ally alifika kazini kwake huku akiwa kama amechanganyikiwa. Hata pale wafanyakazi wenzake walipompa salamu hakuweza kuzijibu. Aliifuata meza yake na kukaa kwenye kiti kisha akalaliza kichwa chake juu ya meza. Eddy rafiki yake mkubwa ambae walikuwa wakifanyakazi wote hapo. Alimfuata pale alipo na kumjulia hali. Ally alijibu kuwa kwa siku hiyo hakuwa vizuri kiakili. Eddy alimaizi kinachomsumbua Ally tangu siku chache nyuma alipomueleza utata wa bosi wake juu ya mke wake.
Kutokana na kumaizi mapema kinachomsumbua rafikiye. Alimuomba ampatie kazi zake amfanyie maana haitokuwa vyema kuwa kazini na aondoke hajafanya chochote cha maana. Hata hivyo kazi alizobakiwa nazo Ally hazikuwa nyingi. Ilikuwa ni kazi moja tu nayo akampatia Eddy na yeye akaendelea kulala pale kwenye meza. Eddy aliichukua ile kazi na kurudi nayo kwenye meza yake apate kumsaidia.
Muda wa kula mchana ulipofika. Ally na Eddy walitoka kwenda kula. Tena hiyo ni baada ya Eddy kumlazimisha sana Ally waende kula. Lakini Ally alikuwa akigoma akidai ati ya kuwa hana njaa ilhali asubuhi hakula chochote na Eddy alishuhudia hilo. Walienda kwenye mgahawa uliokuwa karibu na ofisi yao. Wakaagiza wanachotaka na kuanza kula. Katikati ya mlo, Ally alisema.
“Eddy ndugu yangu. Ukisikia nimeua mtu wala usishangae maana kuna watu wameumbwa kwaajili ya kuharibu maisha ya wengine” Eddy alistaajabu maneno hayo kiasi ambacho aliacha kula na kumtazama Ally kwa mshangao.
“Kwanini?” Eddy alimuuliza.
“Ndugu yangu huyu bosi wetu naona ananitafuta..” Ally alizungumza kwa uchungu sana kiasi ambacho, hata Eddy alikaa vyema kumsikiliza. Akataka kuuliza kwanini. Ila sauti ya Ally ikamuwahi. “Jana si nilikuambia kuwa ameniachia kazi nizimalizie.. Sasa baada ya kumaliza mi niliondoka mpaka nyumba. Ndugu yangu huwezi amini nilimkuta yule bwana amekaa kwenye masofa yangu kama yake..” Hapo mdomo wa Eddy ukafunguka kwa mastaajabu. Hamu ya kutaka kujua kilichoendelea ikamjaa zaidi. Akaweka kijiko kwenye sahani na kumtazama vizuri Ally. Ally akaendelea. “.....lakini wakati naingia, kidogo nipamiane na mke wangu mlangoni aliekuwa akifungua mlango huku akiwa amekasirika. Sijui wenyewe ilikuwaje kabla hadi kuwa hivyo. Basi aliponiona alibadili sura na kujifanya akitabasamu. Lakini mimi nilihisi tu kutakuwa na tatizo. Nilipoingia ndani nikasalimiana nae yule bwana kisha baada ya muda fulani akatuaga na kuondoka zake.....” Ally aliendelea kumueleza kila kitu kilichotokea siku iliyopita na hata asubuhi ya siku hiyo. Eddy alisikitika kwa kutingisha kichwa kulia na kurudisha kushoto. Kisha akamuambia.
“Ndugu yangu mbona umechukua maamuzi hayo ya haraka pasi na uchunguzi yakinifu?” Eddy alimuuliza.
“Kivipi?” Ally nae akauliza.
“Kwasababu kwa maelezo yako ni kwamba. Wakati wewe unaingia kwako na kidogo mpamiane na mkeo aliekuwa amekasirika. Na baada ya kukuona wewe tu akatabasamu. Mi nahisi bwana mkubwa alikuwa akimuambia jambo shemu kama mwenyewe alivyokuambia kuwa alikuwa akimtongoza. Kwahiyo pale alichukia kitendo kile na bilashaka alikuwa akitaka kutoka nje ili amuache bwana mkubwa ndani mwenyewe kwasababu walikuwa wao wawili tu. Sasa wewe ulipoingia ndipo ukahisi kwamba kuna jambo lilikuwa likiendelea kati yao lakini mimi naamini sivyo. Jaribu kukaa na mkeo na umsikilize vizuri halafu ndio utaujua ukweli upo wapi ndugu. Lakini sio kuchukua maamuzi ya haraka namna hiyo”
Ally maneno ya Eddy yalimuingia vyema. Akabaki kwenye tafakuri ya maneno hayo. Akafikiria ni jinsi gani walikuwa wakiishi kwa upendo mkubwa yeye na mkewe. Upendo ambao hata mzazi wake alikiri kuwa mwanae amepata mke bora. Na aliyakumbuka vyema maneno ya mamae kuwa asijaribu kufikiria kumuacha Anita. Akakumbuka ni mara kadhaa Anita alikuja kumletea kesi ya kuwa fulani na fulani walikuwa wakijaribu kumrubuni. Na kitendo hicho kilimuongezea imani ya kuwa alikuwa akipendwa sana na mkewe. Tabasamu la furaha likajiunda usoni kwake.
“Hakika mungu hakukosea hata kidogo kunipatia rafiki mwema kama wewe. Wewe ni zaidi ya ndugu Eddy namuomba mungu urafiki wetu udumu kaka. Umenieleza jambo ambalo mwanzo sikuliwaza hata kidogo kutokana na hasira nilizokuwa nazo” Ally aliyanena hayo kisha akainuka na kwenda kumkumbatia Eddy. Wakafurahi kwa pamoja na kuendelea kula.
Hata Ally alipotoka kazini. Alipitia SuperMarket na kumnunulia mkewe zawadi kadhaa. Ili hata kama atakapofika nyumbani. Amuombe mkewe msamaha na kuirejesha tena amani iliyotoweka ndani ya siku hizo mbili. Alinunua vitu kadhaa kwaajili ya mkewe na mwanawao. Kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani kwake.
Alipofika. Alimkuta mkewe akiwa amekaa na mchungaji wakimsubiri yeye. Akawasalimu na kuchukua nafasi na yeye. Kisha hapo mchungaji akaeleza malalamiko aliyoyapata kutoka kwa Anita mkewe. Ally alitubu ni kweli palitokea mgogoro kati yao. Lakini akasema kuwa ni hasira tu zile na ndio zilizomfanya kuwa katika hali ile. Yakazungumzwa na mwisho muafaka ukapatikana. Kabla ya kuondoka. Mchungaji alishusha maombi kuibariki ndoa hiyo dhidi ya pepo wachafu wanaoinyemelea.
Furaha ikarejea tena baada ya Ally kumpatia zile zawadi mkewe. Anita alifurahi si mas'hara kwa kuona mume wake amekubali yapite. Alimkumbatia huku akidondosha machozi ya furaha na mara kadhaa akimtaja Mungu kwa kuirejesha amani kwenye nyumba yao.
“Niliteseka sana baada ya amani kutoweka kwenye nyumba hii. Ila sasa ninafuraha baada ya kuona Mungu amejibu maombi yangu ambayo nilikuwa nikimuomba usiku kucha. Nakupenda sana mume wangu hata Mungu baba analijua hilo” Anita aliongea kwa hisia kali akiwa bado kwenye kumbato la Ally.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuachiana. Anita aliandaa haraka haraka chakula kwaajili ya mumewe. Siku hiyo alipika kile chakula ambacho mumewe alikuwa akikihusudu sana. Kilikuwa ni ndizi za nyama almaarufu kama mtori. Furaha ikaongezeka zaidi baada ya Cecilia kurudi kutoka shule akiwa na ripoti yenye matokeo yake. Alikuwa ameshika nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi wote aliokuwa akisoma nao. Ally papo hapo akainuka kwenye kiti alichokuwa amekaa kwaajili ya kula. Akampatia zawadi mwanawao na Cecilia akafurahi zaidi na kuifanya familia hiyo iwe katika furaha kuu kwa siku hiyo.
Majira ya usiku wakiwa kitandani wamejilaza. Kichwa cha Anita alikuwa amekilaza kwenye kifua cha Ally huku Ally akichezea nywele za Anita. Mara kadhaa alipitisha kidole kwenye sikio la Anita na kumfanya asisimke mwili. Walikuwa wakiongea hili na lile ikiwa ni pamoja na kuuvuta usingizi ambao kwa siku hiyo ulionekana ukiwa mbali nao.
“Mke wangu mpendwa. Nimeamini kuna watu wameumbwa kwaajili ya kuharibu maisha ya wengine. Na endapo ukiwapa nafasi ya kuwasikiliza achilia mbali kuwa karibu nao tu. Lazima utapotea. Najua wajua ni kiasi gani nikupendavyo. Na siku zote ili upendo udhihirike ni lazima wivu uonekane. Hakuna mapenzi ya kweli bila wivu mke wangu. Na wivu ukizidi sana hubomoa. Kidogo tu niivunje ndoa yangu kwaajili ya wivu na Mungu ameliepusha mbali hilo. Amani imerejea kwenye kasri aishilo mfalme na malkia wake baada ya kupotezwa bwana majivuni alietaka kumpendua mfalme ili ammiliki malkia wake...” Ally aliyanena hayo akiwa na tabasamu huku akiusawili mwili wa Anita kila pahali. Maelezo yake yakakatishwa na swali kutoka kwa Anita aliemuuliza ni nini maana ya maneno hayo?
“Maana yangu ni kwamba. Nakupenda sana Malkia wangu ulienizalia princess kwenye ufalme wangu” Alijibu hivyo kisha akampiga busu la kwenye paji la uso. Na Anita akatulia kimya akilihisi busu hilo limegusa mpaka kwenye moyo wake. Kisha akafumbua macho na kujibu kuwa. Na yeye anampenda sana mumewe. Kisha hapo kikafuatia kile ambacho sio sahihi kuandikwa hapa. Labda kwenye simulizi za machombezo.
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumamosi. Siku ambayo walikuwa wakitoka mapema kazini. Siku hiyo Ally alitaka kuitoa familia yake ‘out’ ila kuna jambo likajitokeza lililosababisha wasitoke siku hiyo. Akawahidi siku inayofuata lazima afanye hivyo. Wakakubaliana nae na shuhuli nyengine zikaendelea. Siku iliyofuata walitoka wote na kwenda huko walipopanga waende siku iliyopita. Huko wakafurahi kwa kila namna. Na siku ilipoisha, wakarudi nyumbani.
* *
Alfajiri ya siku ya Jumatatu ilisawili. Wingu lilikuwa ni lenye rangi la dhahabu lililopendezesha anga. Ndege walisikika wakinena kwa lugha zao kwa sauti zao nzuri laini. Jogoo nao walichagiza kuipendezesha siku hiyo kwa kuwika kwa sauti kubwa mithili ya waimbaji wa muziki wa bendi. Sauti za honi za magari na pikipiki zilisikika kwa wingi kumaanisha kuwa kumeshakucha.
Majira haya ya asubuhi Anita alimuamsha Ally kwaajili ya kujiandaa kwenda kazini. Ally alijibiringisha huku na huko huku akitoa sauti za puani kama kuitika vile anavyoitwa na mkewe. Anita alibaki akicheka huku akimuangalia Ally pale kitandani anavyojibingirisha kama nyoka.
Baada ya dakika moja. Ally alifumbua macho na kumkuta mkewe akiwa anacheka. Naye akacheka. Anita akamjulisha kuwa ni muda wa kwenda kazini. Ally aliangalia saa iliyokuwa ukutani na kukuta ni saa kumi na mbili na nusu sasa. Akainuka kiuvivu na kukaa kitandani. Akamuangalia mkewe na Anita akamuambia basi afanye haraka kujiandaa kisha yeye akatoka nje kwenda kuandaa kifungua kinywa kwaajili ya mumewe na mwanawo ambae kwa siku hiyo hakuwa ameenda shule baada ya kufunga kwa muda mfupi.
Baada ya nusu saa walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa hicho. Kisha hapo Ally aliaga na kwenda kazini baada ya kuwa ameshapata staftah. Siku hiyo aliingia kazini akiwa na furaha sana hata kuwashangaza wafanyakazi wenzake. Alikuwa mchangamfu sana kiasi ambacho kazi zilikuwa zikifanyika taratibu mno kwasababu Ally alikuwa akileta mizaha kila baada ya muda na kuwafanya wenzake wacheke kila mara.
Majira ya jioni muda ambao ndio walikuwa wakijiandaa kutoka kazini. Ally alipokea wito ya kuwa anahitajika na bosi wake. Akainuka kuiendea ofisi ya bosi wake huku akiwa anachukizwa sana na bwana huyo. Alifika na kuitika kwa heshima wito wa bosi wake. Antony alimuashiria kwa mkono kuwa akae kwenye kiti. Nae akakaa.
“Ndio Mr. Kwanza kabla ya yote, ile kazi niliyokupatia leo uliimaliza?” Antony alimuuliza. Ally akajibu kuwa amebakisha pa chache sana kuimalizia na anaamini kuwa siku inayofuata atakuwa ameshamaliza tayari.
Hapo Antony alinyamaza kimya kwa muda kabla hajamuuliza Ally kuhusu hali ya Anita. Ally alichukizwa sana na swali hilo. Ila alitumia busara yake kujibu kuwa anaendelea vizuri tu na hakuna shida yoyote. Antony alimuuliza ni kwanini hakuwa akimpatia Anita zawadi ambazo alikuwa akimpatia kwaajili ya kumpa yeye. Ally alishikwa na gadhabu kiasi ambacho alitetemekwa na mikono. Kwanini huyu bwana ananiuliza maswali ya kuudhi? Alijiuliza.
Uvumulivu ukatwaa taji kwenye moyo wake na subiri ikachukuwa nafasi. Akajibu kuwa ni kweli hakuwa akimpatia kwasababu hakutaka kumchanganya mkewe. Antony alitabasamu kwa majivuno. Kisha akasema.
“Ally Mr. Kila nikikuangalia jinsi ulivyo na nikimuangalia na yule unaemuita mkeo. Naona utofauti mkubwa sana kati yenu. Kiufupi hamuendani. Na unamtesa tu mtoto mzuri kama yule. Yule anapaswa kuwa na mtu kama mimi ambae atakae weza kumtunza kwa kila hali. Sasa labda nikuambie kitu. Embu chagua chochote ukitakacho ili uniachie mwanamke yule na wewe utafute mwanamke wa hadhi yako. Maana hata nikikuangalia kwa haraka haraka. Huonyeshi kabisa kumfikish......”
Haijulikani hadi sasa Ally alitumia sekunde ngapi kwenda kumchomoa bosi wake pale kwenye kiti alichokalia na kwenda kumning'iniza ukutani. Antony alikuwa amekidwa shati lake maeneo ya kifuani na Ally ambae alikuwa akimuangalia kigahabu sana. Alimtikisa kama mtu atikisavyo mti wa mpapai kwaajili ya kushusha mapapai yaliyoiva mtini.
Alimning'iniza huku akimkemea kwa hasira kuwa aache mazoea na mke wake. Muda wote huo Antony alikuwa akitabasamu tu na isijulikanae iwapo amekifurahia kitendo hicho cha kuning'inizwa ukutani ama laa! Kutokana na zile purukushani huku Ally akiongea kwa sauti kubwa ya gadhabu. Wafanyakazi wenzie walikuja na kuwaachanisha watu hao.
Ally alikuwa akiwaomba wampe dakika moja tu ya kumfunza adabu ili akome kuwazoea wake za watu. Hawakutaka kusikiliza maneno yake, badala yake walimuondoa hapo na kumtoa nje. Kwenye ofisi ile. Alibaki Antony pekee. Alirekebisha shati lake mahali ambapo alikuwa amekwidwa na Ally kisha akasikitika. Akakaa kwenye kiti chake na kuchukua simu yake ya mkononi. Akabofya bofya na kuiweka sikioni.
Kule nje. Eddy alimpeleka Ally hadi kwenye gari lake na kumuingiza humo. Majira hayo Ally alikuwa amefura kwa hasira. Mwili mzima wamtetemeka kama kifaranga kilichomwagiwa maji. Eddy akamuuliza kunani tena mbona vurumai limetokea ofisini kwa bosi wao? Kwa zile hasira alizokuwa nazo wakati huo. Hakuweza hata kuzungumza.
Akatulia kwa dakika tano nzima ndipo alipomuelezea yote Eddy. Eddy alisikitika na kushindwa aseme nini. Hadi hapo alishajua fariki yake hana kazi tena. Sasa ni kipi atamsaidia rafiki yake? Hakujua!. Akawasha gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa Ally ikaanza.
Gari ikaingizwa ndani ya uzio wa nyumba ya Ally, kisha wakashuka wote. Eddy akamuambia kwa siku hiyo hatoweza kuingia ndani kwasababu kuna mahali anapaswa kuwepo na anapaswa kuwahi muda huo. Ally kwa hali aliyokuwa nayo. Wala hakuweza kumlazimisha kuingia ndani. Akamuacha aende zake na yeye akaingia ndani.
Hapo alimkuta Anita na mwanawao Cecilia wakiwa sebuleni wanaangalia luninga. Akawapita bila kusalimia na kuingia chumbani. Anita aliinuka na kumfuata mumewe kule chumbani. Alimkuta akiwa amekaa kitandani, mikono akiilaliza juu ya mapaja yake na kichwa amekilaza juu ya mikono. Aliomuona akiwa na mawazo mengi sana.
Akamfuata pale kitandani na kukaa karibu yake. Mkono wake wa kulia akaupitisha nyuma ya shingo ya Ally na kutokezea bega la kulia. Akamuita kwa taratibu. Ally aliinua kichwa na kumtazama mkewe kisha macho yake akayaelekeza mbele. Anita alimuuliza ni kipi kimsumbuacho na Ally alishusha pumzi nzito na kusema.
“Ukiona kesho narudi mapema nyumbani mkononi nikiwa na barua, basi usishtuke, jua nishaachishwa kazi”
“Kwanini?? Sijakuelewa bado” Anita aliuliza.
“Kwasababu. Bosi nimemning'iniza ukutani” Akanita akaguna na kuuliza amemning'iza kivipi? Ally alimueleza yote yaliyotukia ofisini. Anita akabaki kuliwazia tukio hilo. Kisha Anita akaongea baada ya kimya cha muda mfupi.
“Inabidi umuombe msamaha sasa, maana.....”
Walizungumza swala hilo huku Anita akimsihi mumewe amuombe msamaha bosi wake. Lakini Ally aligoma kwa kusema hawezi kuomba msamaha. Na yupo tayari kwa lolote litakalo tokea. Anita ikabidi atulie tu maana hakuwa na chengine cha kumshauri mumewe. Wote wakasubiri waone nini kitafuata.
Majira ya saa kumi na mbili za jioni. Ally akiwa amepumzika chumbani kwake. Alikuja kushtuliwa na Anita aliekuwa akimuambia kuwa kuna wageni wanamsubiria sebuleni. Akainuka kivivu na kuvuta fulana yake iliyokuwa imening'inia kwenye henga, kisha akaivaa. Akatoka na kwenda sebuleni.
Huko aliwakuta vijana wawili wakiwa wamekaa kwenye masofa. Bilashaka hao ndio walikuwa wageni wake. Sura za watu wale hazikuwa ngeni sana machoni kwake. Mara kadhaa aliwahi kuwaona watu wale wakija kazini kwao na kuingia kwenye ofisi ya bosi wao. Akawasalimu na kukaa kwenye sofa jengine.
Hawakuwa na mengi ya kusema hapo. Zaidi walimtaka Ally aongozane nao waende sehemu bosi wake anamuita kwaajili ya kuyasuluhisha yaliyotukia siku hiyo. Kivipi? Kwani hatuwezi tukayasuluhisha kazini hadi tuende sehemu nyengine? Ally alijiuliza. Akamuangalia mkewe na mkewe akamtaka aende wakayasuluhishe maana haifai kuishi kwa Uhasama na watu. Hasa hasa huyo bosi wake.
Akawaomba watu wale wampe dakika kadhaa za kujiandaa. Wakamruhusu na Ally akamtaka mkewe waingie wote chumbani. Wote wakaingia. Huko Ally alibadili nguo na kuvaa nyengine. Kisha hapo akakaa kitandani mahali ambapo alikuwa amekaa mkewe akimuangalia yeye. Kwanza alimjulisha mkewe kuwa wale watu wana ukaribu na bosi wake na huenda hata pale wametumwa kweli kwaajili yake.
“Ila mke wangu mpenzi. Nisiporudi nyumbani. Usihangaike kunitafuta. Labda uhangaike kuitafuta maiti yangu...” Akavuta pumzi na kutazama mbele. Kisha akaendelea. “Kwenye akaunti yangu ya benki, kuna milioni kumi. Naamini zitawasaidia kwa lolote wewe na mwanangu. Nyumba hii sio yangu ni ya ofisi. Ila nina nyumba yangu kama ujuavyo maeneo ya Mikanjuni. Mtahamia huko baada ya kufukuzwa hapa. Kama nisiporudi. Basi nilelee mwanangu katika misingi mizuri. Usimsimulie sababu ya kifo changu ila mdanganye vyovyote vile ujuavyo. Mke wangu kipenzi. Nisiporudi. Basi nakuomba usijaribu kushiriki chochote na bosi wangu. Na kama utataka kuolewa. Basi olewe na yoyote lakini si yeye. Mwisho niombee nirudi salama”
Alihitimisha maelezo yake. Maelezo ambayo yalimuacha Anita katika sintofahamu asielewe kwanini mumewe ameongea maneno hayo? Ikabidi amuulize. Ally alimtazama usoni mkewe na kutabasamu. Kisha akampiga busu la mdomo na kumuambia kuwa anampenda sana. Hata Anita pia alijibu kuwa anampenda na yeye, lakini hajajua ni sababu ipi iliyomfanya akayanena yote hayo. Ally akamtoa hofu kwa kumuambia asijali kila kitu kitakuwa sawa.
Baada ya hapo wakatoka wote nje. Huko Ally alipitia kwenye chumba cha mtoto wao. Akamkuta Cecilia akiwa amelala. Akamfuata pale kitandani na kumpiga busu la kwenye paji la uso. Kisha akatoka nje. Akawakuta wale vijana wakimsubiri. Akawaambia yupo tayari na safari. Wakatoka huku Ally akimtahadharisha mkewe asisahau aliyomuambia.
Wakatoka nje na kuingia kwenye gari walilokuja nalo wale vijana. Baada ya kuingia tu. Ally akashangaa akifungwa mikono kwa nyuma na kamba ngumu. Akahoji kunani mbona tena anaona mambo yasiyoeleweka? Akatahadharishwa kuwa, Aache kelele vinginevyo watammaliza kabla hawajamfikisha huko wanapotakiwa kwenda. Akatulia kimya huku roho ikimuenda mbio. Gari ikawasha na safari ya kwenda kusikojulikana ikaanza.
Safafi yao ikashia Sahare ukuta wa mbole. Wakakunja kushoto na kwenda mbele kidogo. Na gari ikaingizwa kwenye nyumba moja ghali iliyokuwa eneo hilo. Wakamshusha Ally vile vile wakiwa wamemfunga na kumkokota mpaka ndani ya nyumba hiyo. Sebuleni walimkuta Antony Magasa akiwa amekaa akivuta sigara aina ya ‘Shisha’. Antony alipomuona Ally aliachia cheko kubwa huku moshi wa sigara hiyo ukimtoka mdomoni. Akapaliwa baada ya moshi ule kumtoka na puani bila ya kuupangilia. Akakohoa na kusema.
“Nafurahi sana kumuona hayawani anaejishindanisha na binadamu mara hii akiwa mnyonge kama kijidege kijidogo dogo kilichofiwa na wazazi wake. Karibu Mr Ally kwenye himaya yangu” Aliongea hivyo Antony na kuvuta tena ile sigara. Ally muda wote alikuwa akitetemeka na isijulikane ni hofu ama ni hasira. Alimtazama bosi wake usoni kwa kitambo kama ndio kwanza anamuona. Kisha akasema.
“Najua kilichokufanya utume vijakazi wako wanichukue nyumbani kwangu na kunileta...”
“Hah hah hahahah! Bwana mdogo unachekesha sana. Unaujeuri wa kumiliki nyumba wewe hapa mjini? Kama sio kumilikishwa nyumba za watu ambazo muda wowote unapokonywa. Sasa ni hivi. Wewe unafia humu. Na yule uliekuwa ukimuita ati ni mkeo anakuja kuishi humu pia. Namtumia nikishamaliza hamu zangu namtimua kama nilivyowatimua wengine...” Akawageukia vijana wake. “Embu leta manati ya mzungu nimuonyeshe huyu fala kuwa mimi ni nani” Akaongea maneno hayo. Jamaa mmoja kati ya wale wawili. Akachomoa bastola yake na kumkabidhi Antony Magasa. Kisha antony akasema.
“Siwezi nikakupa hata walau sekunde moja ya kutubu dhambi zako. Na kama hujafanya hivyo kabla, basi umechelewa. Wewe si bingwa wa kudhalilisha wakubwa zako. Sasa idhalilishe na hii risasi itakayozama kwenye bichwa lako hivi punde” Kisha hapo akamnyooshea Ally aliekuwa amesimamishwa mbele yake. Ghafla tu. Mlio mkubwa wa risasi ukasikika huku mwili wa Ally mara hii wenye kichwa kisichoeleweka kwa haraka kama ni kichwa ukidondoka chini.
Antony alicheka sana huku akipigapiga kifua chake kwa majivuno aliyonayo utafikiri kile alichokifanya ni jambo zuri sana. Akawaamrisha vijana wale wauondoe ule mwili na wakautupe katika ufukwe wa Sahare. Kwakuwa majira hayo bado giza halijatanda vizuri. Wakashauri wasubiri giza litande ndipo wakautupe huko. Antony aliwaambia ni wao tu ila yeye anachotaka kwa muda huo asiuone mbele yake.
Vijana wale wakafanya haraka haraka kuutuo ule mwili. Wakaenda kuuhifadhi pahali kabla ya kwenda kuutupa ufukweni. Kisha wakarudi pale ndani na kusafisha vizuri. Pakawa safi kama vile hapakumwagika ubongo uliochnganyikana na damu muda mfupi uliopita. Na giza lilipoingia. Wakaenda kuutupa mwili wa Ally.
* *
Sebuleni hapakukalika, chumbani ndio kabisa. Alikuwa akihangaika huku na huko. Mara aingie chumbani. Atoke hadi sebuleni. Mara atoke nje kabisa na kwenda kuchungulia huko akidhani labda anaweza kumuona Mumewe akirejea. Hadi muda huo alishamuomba Mungu wake sana. Alishalia sana. Alishanung'unika sana. Lakini mumewe hakutokea.
Hata pale aliposhika simu na kumpigia mumewe amuulize yuwapi. Simu ilikuwa ikiita tu pasi na kupokelewa. Akajipa moyo kuwa huenda atarudi muda wowote. Akakaa sebuleni akiangalia luninga lakini asielewe chochote kinachoendelea pale. Sauti ya mwanae ikimuulizia babaye ilizidi kumchanganya sana kiasi ambacho moyo wake ulizidi kumuuma huku hofu ikiongezeka mara dufu.
Jibu alilokuwa akimpa ni kuwa. Baba kuna sehemu ameenda na atarudi muda si mrefu. Cecilia akatulia na kuendelea na mambo yake. Saa mbili, saa tatu, hadi sasa ni saa tano usiku lakini Ally asitokee. Ebwana wee! Ikambidi atoke na kwenda kituo cha polisi Chumbageni kwenda kutoa taarifa. Alihojiwa hili na lile na yeye akaeleza yote anayoyajua. Akaambiwa aondoke na uchunguzi utafanyika juu ya upotevu wa mume wake.
Akarudi nyumbani kwake akiwa mnyonge sana. Akiwa njiani, alikuwa akimuomba mungu wake amfanyie miujiza akifika amkute mumewe akiwa salama. Lakini alipofika. Hakukuta kama alichokuwa akiomba. Machungu yalimzidi moyoni. Hofu ikazidi kutanda nafsini. Wasiwasi ukamuandama usoni. Hakujua mumewe atakuwa katika hali gani muda huo. Je ni kweli kuna jambo baya limemkuta kama alivyoniambia wakati anaondoka? Alijiuliza!.
Siku iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi. Anita alipigiwa simu kuwa anatakiwa kituo cha polisi muda huo. Aliambiwa kuwa kuna mwili umepatikana ukiwa mfu kwenye ufukwe wa Sahare, kwahiyo anahitajika kituoni akathibitishe kama huyo mtu ndio huyo aliekuwa akimtafuta ama laa!. Taarifa hizo alizipewa kwasababu siku iliyopita wakati alipoenda kutoa taarifa hiyo, aliacha namba za simu ili kama kutakuwa na taarifa yoyote ajulishwe.
Hofu!. Uoga!. Wasiwasi!. Pengine na kiroho cha mshtuko wa taarifa hiyo, vyote vilimpata Anita. Je ikiwa ni yeye kweli itakuaje jamani? Alijiuliza. Kisha akajiandaa haraka haraka na kutaka kutoka. Cecilia ambae muda huo alikuwa amesimama upenuni mwa mlango wa chumba chake anacholala. Alimsalimia mamae kisha alipoitikiwa salamu yake na Anita ambae alikuwa akitaka kutoka. Alimuuliza kuhusu babae kuwa yuwapi maana ni siku nyengine sasa hii hakumuona.
Anita akaghairisha kufungua mlango na kumsogelea Cecilia pale alipo huku akiwa na tabasamu usoni ili kumuondoa wasiwasi mwanae. Alipofika. Alichutama mbele yake na kumshika mashavu yake kama anayapangusa hivi. Kisha akamuambia.
“Usijali mwanangu. Baba yupo ndio naenda kumpokea sasa huko alipoenda. Na muda si mrefu atarudi. Umesikia mwanangu?” Cecilia akatingisha kichwa ishara ya kuwa amemuelewa mamae. Kisha akauliza.
“Kwani ameenda wapi?” Anita alibaki akimtazama machoni na asijue amuambie nini? Baada ya kimya kifupi akamuambia kuwa alienda kwa bibi na atarudi tu.
“Mbona mimi nilimuambia akienda kwa bibi tuende sote. Halafu sasa hivi tumefunga shule na mimi nataka kwenda kwa bibi”
“Usijali mwanangu. Akirudi tutaenda wote. Wewe, mimi na baba yako. Sawa binti yangu?” Cecilia akatingisha kichwa kukubali. Kisha Anita akamtaka akajiandae haraka ili atakaporudi wapate staftah wote. Cecilia akarudi ndani kwenda kufanya usafi wa mwili.
Anita alifika kituoni Chumbageni. Akapokelewa na yule askari alietoa maelezo kwake siku iliyopita. Askari yule akamuambia amsubiri mara moja ndipo waongozane wote kwenda hospitali ya Bombo kuthibitisha kama huyo anaemtafuta ndio huyo alieokotwa Sahare ufukweni na wavuvi ama laa! Anita akasubiri huku bado moyo wake ukienda mbio kwa hofu. Baada ya dakika tano, yule askari alirejea. Wakatoka na safari ya kwenda Bombo ikaanza.
Walipofika walifanya taratibu zote na hivi sasa walikuwa wakiongozwa na daktari kuelekea Monchwari kuenda kuthibitisha walilolitaka. Anita alilia kwa uchungu baada ya kuthibitisha kwa macho yake kuwa huyo mtu alikuwa ni Ally mume wake. Alilia sana kiasi ambacho alipoteza na fahamu kabisa. ‘Chap chap’ akawahishwa wodini kwaajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.
Taratibu za mazishi ya bwana Ally zilifanyika siku mbili baada ya kifo chake. Mwili wake ulihifadhiwa katika makaburi ya Mzingani. Hakika Anita hakuweza kuamini kuwa ni kweli siku hiyo ndio alikuwa anafukiwa mwanaume anaempenda kuliko yoyote. Alilia sana kwa uchungu. Ni nani atambembeleza pindi adekapo?. Ni nani atakae muita baba Cecilia? Ni nani tena atakae muita mume wake kwa mahaba. Hakika ni lazima umuonee huruma wakati akiwa analalamika. Kiasi ambacho muda mwengine alikuwa akikufuru sasa.
Muda huu hata Cecilia alielewa nini kinaendelea. Umri wa miaka kumi na mbili aliokuwa nao, ulitosha kabisa kumjulisha kuwa hakuwa na baba tena duniani. Hata yeye alikuwa katika ukiwa mzito. Muda wote alimsaidia mamae kulia. Kumlilia Ally ambae alikuwa ndio kichwa cha familia hiyo.
Hata wafanyakazi wenzake pia walihuzunika sana baada ya kupata taarifa ya kifo cha mwenzao. Walikuwa hawaamini kwamba ni kweli Ally aliwatoka kama utani tu. Japokuwa Eddy alijikaza kiume. Lakini machozi alishindwa kuyakaza. Yalimporomoka kutoka machoni taratibu hadi mashavuni na kuangukia chini kisha kupotelea ardhini. Kila aliepata taarifa za kifo cha Ally alihuzunika si mas'hara.
Inakuaje siku aliyotoka kutofautiana na bosi. Siku ya pili yake zije taarifa ya kifo chake?. Kifo ambacho hajulikani muhusika hadi muda huo. Hapana!. Bosi atakuwa anahusika kwa namna moja ama nyengine. Hayo yalikuwa ni mawazo ya wafanyakazi wenzie walioshuhudia kisanga kilichotoke siku tatu nyuma kati ya bosi wao na Ally. Lakini ni nani anyanyue kinywa chake na kujifanya akitangaza. Ati ya kuwa bosi wao anahusika kwa namna moja ama nyengine?. Hakuna!.
Kila mmoja alikuwa kimya kama vile ajahisi chochote. Na ili kujitahadharisha zaidi. Wakaambiana siri hiyo ibaki kwao wenyewe wasije wakaizungumza kwa yoyote. Pamoja na hivyo. Pia hawakuwa na ushahidi wa kutosha. Wakiwa na huzuni tele. Wakamzika mwenzao huku wakibaki na walichokitiliashaka.
* *
Wiki tatu sasa zimepita tangu wamzike Ally. Pamoja na kuwa ni muda mrefu kiasi umepita tangu afiwe na mumewe. Lakini machungu hayakumuisha hata kidogo mtimani mwake. Huzuni ilimtwala kila mara amfikiriapo mumewe. Alitamani walau arudi waendelee kuishi kwa furaha kama mwanzo. Ila hiyo ilikuwa ni kama ndoto ya kuhuzunisha aiotae mkiwa usiku wa giza. Haitoweza kutokea kamwe.
Kwa masiku hayo yaliyopita. Antony alikuwa akijifanya kuja nyumbani hapo na kumpa pole Anita kwa kufiwa na mumewe. Hata mudaa huu Anita alishamaizi kuwa muasisi wa kifo cha mumewe ni huyo huyo mnafiki anaekuja kumpa pole. Lakini yeye ni kama wale wafanyakazi wenzie na marehemu mume wake. Alikuwa kimya hakutaka kusema chochote. Popote kwa mtu yoyote. Alibaki kumuachia mungu huku akiushikilia vizuri ule msemo usemao ‘Funika kombe mwanaharamu apite’.
Kutokana na kero zilizozidi kutoka kwa Antony. Anita akapanga aondoke kimya kimya kwenye nyumba hiyo. Ahamie kwenye hiyo nyumba yao iliyoko Mikanjuni. Na kwavile haikuwa bado imemalizika. Akatoa milioni tano kwenye akaunti ya mume wake na kuimalizia japo kidogo ili wapate walau pa kuishi. Na zile milioni tano zilizobaki. Akapanga kufungua biashara yoyote ili apate kuiendeleza familia yake.
Mipango yake ilipokamilika. Kimya kimya. Akiwa yeye na mwanae huku anaejua siri hiyo ni Eddy tu rafiki mkubwa wa mume wake kipindi cha uhai wake. Walihamia rasmi katika mtaa huo wa Mikanjuni ambapo pia aliona amuhamishe mwanae shule ampeleke shule za kawaida ili kubana matumizi ya pesa. Wakayaanza rasmi maisha mapya katika mtaa huo mgeni machoni mwao. Cecilia akahamia shule ya msingi Ukombozi ambayo haikuwa mbali na wanapoishi. Kipindi hicho alikuwa darasa la nne.
Mtaa huo wakaishi vizuri tu bila bugudha yoyote kutoka kwa Antony. Pengine huenda hakujua walipo. Hata hivyo alipokea taarifa kutoka kwa Eddy ya kuwa Antony alikuwa akimtafuta sana. Baada ya kuishi kwa mwaka mmoja mtaa huo. Eddy akawajia na taarifa ya kuwa bosi wao Antony amekufa kwa gonjwa hatari la Ukimwi. Anita hakuweza kuhuzunika wala kufurahika baada ya kupokea taarifa hiyo. Aliona hayo ndio malipo yaliyokuwa yakimfaa bwana yule. Kisha akamshukuru Mungu kwa kumuepusha nae. Huenda hivi sasa na yeye angekuwa muathirika wa Ukimwi endapo angekubaliana na vishawishi vyake.
MWISHO WA KUMBUKUMBU..
Mwanamke yule mtu mzima ambae kwa sasa tumemjua kuwa akiitwa Anita. Alimtazama mwanae kwa huruma. Cecilia alikuwa vile vile ametulia kimya akitazama mbele. Hivi sasa alikuwa akitokwa na machozi na isijulikane kimlizacho. Anita aliuvuta upande wa kanga aliyoivaa na kuipitisha kwenye macho ya Cecilia na kumfuta machozi. Akaishusha na kumtazama tena.
Akajifuta machozi na yeye yaliyokuwa yakimtoka baada ya kuikumbuka kumbukizi hiyo ya kifo cha mumewe. Tangu Ally alipofariki. Hakutaka kuolewa na yoyote pamoja na kuwa wengi walishamfuata wakiwa na nia ya dhati kabisa ya kumuoa. Ila yeye aliwakatalia akitaka aishi pekeake huku akimlea mwanae alieachiwa na mumewe ambae kwa sasa bilashaka alishageuka mchanga ndani ya ardhi.
Akainuka kimya kimya na kutoka nje. Huko alienda kuziingiza na ndani zile nguo ambazo mwanzo alitaka kuzifua. Baada ya hapo akashika kazi ya kuwapaa wale samaki ambao kwa sasa walikuwa wakitoa harufu kwa mbali kuashiria kuwa walikuwa wakienda kuharibika. Akafanya hima hima kuwaandaa kisha akaandaa na chakula ambacho kitasindikizwa na mboga ile.
Raskazone Beach majira haya ya jioni. Kulikuwa na watu wengi walioenda kubarizi katika beach hiyo siku hiyo ya mwisho kabla ya kuanza wiki nyengine. Vitoto vidogo na watu wakubwa walionekana wakiogelea kila mmoja kwa nafasi yake kwenye bahari hiyo. Kelele za hapa na pale zilisikika wakiyafurahia maji hayo. Watu wengine wengi walikuwa juu sehemu hiyo wakiwaangalia kwa chini wale waliokuwa wakiogelea huku wakionekana wakifurahia zaidi kuwaangalia watu wale wanaoyakata maji kila mmoja kwa mtindo wake kuliko wao kwenda kujiunga kuogelea.
Kule kule juu upande wenye miti miti na mawe makubwa yaliyokuwa eneo hilo. Kulikuwa na watu wawili wa jinsia tofauti. Walionekana katika mkao wa kimahaba zaidi huku yule wakiume akipiga gitaa taratibu huku akiimba nyimbo ya mapenzi akimuimbia yule mwenza wake aliekuwa amejilaza begani kwake akisikiliza mashairi matamu yaliyotoka kwenye beti za nyimbo hiyo aliyokuwa akiimba mpenziwe.
“Mpenzi...” Yule binti alimkatisha yule mwanaume aliekuwa akimuimbia. Alipoona yule mwanaume ameacha kupiga gitaa na kuimba, muda huu akiwa anamuangalia yeye. Akaendelea. “Unaonaje kesho tukienda nyumbani kwakina Cecilia tukamtazame. Maana ni muda sasa hatukufika” Aliongea yule binti huku akimuangalia yule kijana kwa jicho la mahaba.
“Siwezi kwenda kumuangalia” Yule mwanaume alijibu huku akiangalia mbele ambapo kuna watu waliokuwa wakiogelea.
“Ramah! Kwanini sasa?” Binti aliongea kwa mashangao huku akijitoa begani kwa yule mwanaume ambae amemuita kwa jina la Ramah na mara hii alikuwa akimuangalia machoni.
“Jenifa. Hivi umesahau alichonifanyia? Unadhani labda nimesahau? Sio rahisi kama unavyodhani. Siwezi kwenda kumuangalia hata kidogo hata nisikie amekuf.....”
“Mlaani shetani Ramah. Usiseme hivyo. Kumbuka yule alikuwa nani kwako kabla yangu na istosh....” Jenifa kama alivyoitwa na yule mwanaume ambae tulipata kuona akiitwa Ramah. Alimkatisha Ramah na kunena maneno hayo. Na yeye kabla hajamaliza, alikatishwa na Ramah.
“Sikiliza Jeni. Hali ambayo yeye anayo kwa sasa. Hata mimi ilinitokea nawe watambua hilo. Tena mimi ilikuwa zaidi yake. Japokuwa sikuwa sawa kiakili. Lakini sikuweza kuhisi hata kidogo uwepo wake karibu yangu. Sasa ni vipi leo mimi niende kumjulia hali ilhali yeye hakuwahi kuja kunijulia hali? Wewe kama unaenda, nenda mwenyewe tu hata hivyo yule ni rafiki yako bado”
“Hata kama. Lakini ukumbuke mlivyokuwa kipindi cha nyuma kabla ya kutoke....” Jenifa alikatishwa na sauti kali ya Ramah aliemtaka aache kuzungumzia mambo hayo. Na akamuonya ya kuwa. Kama ataendelea kulizungumzia hilo. Basi watagombana muda si mrefu. Jenifa akatulia!.
“Basi babaa nimekuelewa. Si unajua vyenye nakupenda?” Jeni aliikatisha mada.
“We haya tu. Nitakubeba sasa hivi nikakutupe kwenye maji kule. Ohooo” Ramah nae akachomekea utani. Wakacheka pamoja.
Waliendelea na maongezi yao hadi pale muda ulipowatupa mkono. Wakaondoka kabla hapajaanza vuruga za watu kuondoka. Walitafuta usafiri wa kuwarudisha walipotoka na wakaupata. Dereva wa bajaji aliwauliza ni wapi waendapo na Ramah akajibu kuwa mwisho wa safari hiyo ni Duga Mwembeni lakini watamshusha Jenifa Komesho ndipo waimalizie safari hiyo. Dereva akawatajia kiasi chake cha pesa alichokihitaji na walipokubaliana nae. Safari ikaanza.
Nini Kilitokea Kipindi Cha Nyuma. Turudi Miaka Miwili iliyopita.
Katika ukumbi wa Polisi Mecy. Shangwe, nderemo na vifijo zilitawala humo. Ndani ya ukumbi huo kulikuwa na sherehe ya maafali ambayo waliokuwa wakiifanya ni vijana wahitimu wa kidato cha nne mwaka huo. Ilikuwa ni furaha mno kwa vijana hao wa Shule ya Sekondari Mikanjuni.
Wanafunzi wa kidato hicho. Walikuwa wamevaa sare zao za shule huku wageni wengine waalikwa wakiwa na mavazi ya kawaida. Shuhuli ziliendelea humo kwa ufasaha zaidi. Kila kitu kilichokuwa kwenye ratiba. Kilienda bilashaka yoyote.
“Jeni mpenzi. Ramah umemuona wapi. Maana ni muda sasa namtafuta tupige picha lakini simuoni” Cecilia aliyaongea hayo kumuambia Jenifa huku akiwa anaangalia huku na huko kumtafuta huyo aliemtaja kama Ramah.
“Ramah nilimuona akielekea nje. I think atakuwa ameenda toi... Aaaa yule pale anakuja” Jenifa aliongea huku akimuonyeshea kidole Ramah aliekuwa akija upande huo. Cecilia nae akageuka na upande ule. Alipomuona Ramah akija hapo. Akajifanya kununa kimapozi.
“Vipi nyie, mbona mnanishangaa?” Ramah aliekuwa katika mavazi ya kawaida ya T_shirt na jinzi huku kichwani nywele zake nyingi zikiwa katika mtindo mzuri. Na chini akiwa amevalia raba kali aina ya Nike. Aliwafikia banati wale waliokuwa katika mavazi ya shule na kuwauliza swali hilo.
Ipo hivi. Ramah yeye alimaliza kidato cha nne mwaka uliopita shule hiyo hiyo waliyomaliza ma binti hao. Na hapo alikuja kama mgeni mualikwa. Ikiwa pia alikuwa hapo kumpa ‘Suport’ mpenziwe Cecilia na rafiki yake Jenifa waliokuwa wakisherekea mahafali yao.
“Nini tena mpenzi? Mbona umenuna hivyo?” Ramah alimuuliza Cecilia huku akimshika kidevu.
“We umeondoka hata sijui umeenda wapi. Mi nakutafuta muda wote sikuoni. Kwanza ulienda wapi?” Cecilia aliongea kwa deko na mwisho akamuuliza swali hilo.
“Mpenzi nilikuwa toi mara moja” Ramah alijibu.
“Kwahiyo ndio usiniage?” Cecilia alilalamika.
“Hapana mpenzi. Sikukusudia kukuweka roho juu namna hii. Bali nilikutafuta na nikakuona ukiwa na shuhuli nyingi. Nikaona niende mara moja. Hata hivyo sijachelewa sana Eti?” Ramah aliongea huku akimuangalia machoni binti huyo mwenye uzuri wa pekee. Cecilia akadengua kidogo kisha akamuambia kuwa. Alikuwa akihitajika na mama yake kwaajili ya kupiga picha za ukumbusho. Ramah na Jenifa walicheka baada ya kuona Cecilia akideka sana utafikiri ni mtoto mdogo. Cecilia akajifanya amenuna na kuanza kupiga hatua kuondoka hapo. Huku nyuma Ramah na Jenifa waligongesha viganja vyao. Kisha wakaanza kumfuta nyuma Cecilia.
Huko walipiga picha nyingi za ukumbusho. Anita alikuwa akitabasamu muda wote kila amuonapo mwanae akiwa na furaha. Hasa hasa awapo karibu na Ramah. Alijua vyote vilivyokuwa vikiendelea kati ya mwanae na kijana huyo. Na yeye kwavile alijua mtu akipenda anakuaje. Alimuacha mwanae awe na Ramah ambae alionekana kumhusudu sana kijana huyo.
Baada ya kuisha sherehe hiyo. Watu wakaondoka hapo kuelekea majumbani kwao. Anita, Cecilia, Ramah na Familia ya Jenifa. Walionelea wakaimalizie sherehe hiyo katika ufukwe wa bahari ya Jeti. Ila kabla ya kwenda huko. Cecilia na Jenifa. Walibadili nguo za shule walizokuwa wamezivaa. Na hivi sasa walikuwa wamevaa nguo za kawaida ambazo ziliwatoa bomba si mas'hara. Kisha hapo. Safari ya kwenda Jeti ikaanza.
Huko walisherehekea kwa kila namna. Walikula vyakula na vinywaji walivyoenda navyo. Wakafurahi kwa kila namna waliyoipenda. Na wazazi wa watoto wale wakike. Walikuwa kwenye furaha baada ya kuwaona mabinti zao wakifurahi. Saa kumi na mbili jioni. Ndipo wakafunga safari kurudi majumbani kwao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama leo si utaniruhusu niende kwakina Ramah?” Cecilia alimuuliza hivyo mama yake wakati wakipanda juu walipoacha ufasiri uliowaleta.
“Embu acha ujinga wako. Twende nyumbani” Anita alimkoromea na Cecilia akanuna. Lakini nuna yake haikumfanya Anita abadili maamuzi yake. Walipofika karibu na usafiri. Cecilia alichomoka na kumfuata Ramah ambae yeye alikuja kuchukuliwa na usafiri wa pikipiki na ndugu yake ambae walikuwa wamefanana kila kitu, unaweza sema ni mapacha. Ila ukweli ni kwamba. Walipishana mwaka mmoja tu katika uzao wao. Alianza huyo kaka yake aliefahamika kwa jina la Jeremiah. Lakini walimkatisha kwa kumuita Jay. Kisha ndio akafuatia yeye. Na katika familia yao walikuwa wao wawili tu huku kila mmoja akiwa na baba yake.
“Sasa mpenzi mama anenikatalia leo kuja kwenu. Na sijui itakuaje” Cecilia aliongea baada ya kuwafikia vijana wale.
“Usijali mpenzi. Nenda kapumzike. Hata hivyo pia umechoka sana na mishemishe za leo. Usiku nitakucheki kwenye simu” Ramah aliongea.
“Haya bwana. Sionekani kabisa, macho yote umeyagandisha kwa baba chanja wako” Jay aliongea kwa mzaha na kumfanya Cecilia atahayari. Alimkumbatia Ramah huku akicheka kwa aibu.
“Sorry shem wangu. Nilikuona ila ndio hivyo mama kanichanganya sana baada ya kunikatalia kuja kwenu. Ila sijafanya kusudi kutokukusalimia”
“Ila siku nyengine uwe makini shem. Ramah asije akakuchanganya” Jay alisema.
“Hahhaha. Hata sasa nimeshachanganyikiwa kwake. Halafu mbona hukuja kwenye sherehe yetu wakati nilikualika? Au mdogo wako amekuzuia kuja?” Cecilia aliongea.
“Umeona wapi mkubwa akapangiwa na mdogo? Mishe nyingi tu ndio maana sikutokea. Ila nilimtaarifu braza hapa akujulishe”
“Ooooh! Nimekumbuka tayari. Ok acheni basi mimi niwaache” Akamgeukia Ramah na kumpiga busu la mdomo. “Bye” Akamalizia hivyo na kuondoka zake. Ramah aligongesha mkono na Jay huku wakicheka. Kisha Ramah akadanda pikipiki na safari ya kuondoka hapo, ikaanza.
Majira ya usiku. Ramah alimpigia simu Cecy. Kisha wakaanza mazungumzo yao baada ya Cecy kupokea simu. Waliongea sana wapenzi hao maneno ya mapenzi. Mara Cecilia alitaka aimbiwe nyimbo na Ramah akamuimbia. Alipotosheka. Wakawa wakizungumza. Ikafikia muda wakaishiwa na maneno. Sasa wakawa wakitaniania tu. Utani ambao kama ungepata kusikiwa na mtu mwengine anaweza sema watu hao hawakuwa na shuhuli za kufanya. Ama pengine walitaka kuupitisha usiku huo wakiwa wakavu wa macho.
Waliongea hadi majira ya saa tisa usiku. Sasa ikawa kila mmoja amechoka lakini bado anatamani kuendelea kuongea. Hata hivyo. Pia hawakuwa na mada yoyote muhimu ya kuiongelea. Mwisho wakawa wakifanya mchezo. Kila mmoja akitaka mwenzake ndio akate simu. Wakabaki wakizozana hadi pale salio lilipoisha. Simu ikajikata na kila mmoja akavuta shuka kwaajili ya kumalizia masaa machache yaliyobaki kutimia Alfajiri.
________
Majira ya saa mbili asubuhi. Cecy alifumbua macho asubuhi hiyo akiwa bado ameulaza mwili kwenye kitanda chake. Tabasamu likajiunda usoni kwake. Akaupeleka mkono wake kiuvivu hadi kwenye meza ndogo iliyokuwa karibu na kitanda. Akavuta simu yake na kuiangalia. Kisha akaingia sehemu ya kuhifadhia majina na kutafuta jina alilolisevu ‘Dear Ramah’. Kisha akapiga.
Simu ikaita kwa dakika chache na kupokelewa. Wakajuliana hali asubuhi hiyo. Kisha wakaahidiana majira ya jioni waende sehemu kwaajili ya maongezi zaidi. Kisha hapo simu ikakatwa. Sauti ya mamae ilisikika ikimuita huku akikaribia chumba hicho. Cecy alitabasamu na kujifunika shuka mwanzo mwisho. Anita alifungua mlango na kuzama ndani. Alimuona mwanae akiwa amejifunika shuka gubigubi. Akatabasamu na kumuita tena.
“Mmmmh” Cecy aliitikia kwa mguno. Mama yake akamuiga kisha akasema.
“Nyoo. Hadi muda huu umelala. Usiku kucha nakusikia ukizungumza na simu tu. Utakuja kuugua magonjwa ya ajabu kwa kutolala vizuri. Haya inuka, chai tayari” Cecy alifunua shuka haraka usoni kwake na kumtazama mamae kwa macho ya mashangao.
“Chai tayari saa hizi?”
“Kwani unajua saa hii ni saa ngapi?” Anita nae alirudisha swali huku akitabasamu. Cecy alichukua simu yake na kutazama saa. Kisha akahamaki huku akiufumba mdomo wake kwa viganja vya mkono wake. “Saa tatu kasoro!”
“Kwani ulijua saa ngapi? Embu twende huko” Anita aliongea huku akipiga hatua kuondoka chumbani humo. Alipofika mlangoni. Alishtuliwa na sauti ya Cecy.
“Mama...” Alimuita. Kisha alipoona mama yake amegeuka kumtazama. Akaendelea. “Leo jioni naomba kutoka” Aliongea huku akiigiza huruma.
“N'shajua unapotaka kwenda. Huendi mpaka umalize kazi za hapa” Anita aliongea hivyo na kupotelea nje. Cecy aliinuka huku akiwa na tabasamu. Akaliendea kabati ambalo lilikuwa na kioo kikubwa. Akajiangalia mwanzo mwisho akiwa na vazi la kulalia ambalo liliuacha mwili wake sehemu kubwa wazi. Hakika hata yeye mwenyewe alikiri kuwa alikuwa ni mzuri haswa. Akajigeuza geuza huku na huko huku akitabasamu. Mwisho akacheka na kwenda kujitupa kitandani. Akachukua tena simu yake na kuingia uwanja wa meseji. ‘Nitakucheki baadae kipenzi. Love U my lovely bae’ Akaituma kwa Ramah na kuitupa simu kwenye kitanda.
Akajifunga kanga kuanzia kiunoni hadi chini. Kisha akatoka nje kwaajili ya kwenda kuufanyia mwili wake usafi. Alitumia nusu saa na aliporudi. Akabadili nguo na kuichukua simu yake. Akakuta kuna ujumbe umeingia kwenye simu yake. Akaufungua. ‘Poa. I wish hata ingekuwa sasa’ ulisomeka hivyo ujumbe kutoka kwa Ramah.
Akatabasamu na kwenda chumbani kwa mama yake. Akachukua chaji na kurudi nayo chumbani kwake. Akachomeka simu yake chaji na kwenda sebuleni ambapo alimkuta mama yake amekaa akifumua nywele zake. Anita alipomuona Cecy. Akavuta kitambara chake cha kichwa na kukivaa. Kisha akaiendea meza ambayo juu yake kulikuwa na mabakuli kadhaa.
Wakaandaa staftah haraka. Kisha wakaanza kunywa taratibu. Muda wote walikuwa wakiongea na kucheka. Furaha ya Anita ilikuwa ni kumuona mwanae akiwa na furaha. Na mara zote alihakikisha anafanya kila awezalo ilimradi Cecy awe katika furaha. Kila akimuangalia usoni aliiona sura ya Ally mumewe. Alimkumbuka sana mumewe ambae aliuliwa kwasababu ya mapenzi.
“Cecy...” Anita alimuita na kumalizia kutafuna kipande cha chapati ambacho kilikuwa mdomoni kwake. Kisha akaendelea. “Shule umeshamaliza. Sasa nataka kujua. Unampango wa kuendelea ama vipi?”
“Mama mi lazima nisome kivyovyote vile. Hata kama nikifeli kidato cha nne. Najua unaouwezo wa kuniendeleza mama yangu. Mi nataka nisome tu kwa muda huu”
“Naijua shauku yako ya kutaka kusoma. Ila nilikuuliza tu maana si unajua watu mawazo huwabadilika. Ila pia nakuaminia sana binti yangu, kwenye masomo upo vizuri sana. Naamini hutofeli”
Waliendelea na maongezi yao. Hata pale walipomaliza kunywa chai. Anita alimtaka binti yake amsuke. Wakatoa mkeka na nje tayari kusukana. Wakati wakiendelea kusukana. Anita alikuwa akimnasihi binti yake kuhusiana na maisha. Alimtahadharisha achunge na maisha. Hasa hasa maisha ya mapenzi. Hadi muda huo hakutaka kumuambia ukweli mwanae ni kipi chanzo cha kifo cha baba yake. Muda wote Cecy alijua kuwa baba yake alikufa kwa ajali.
________
Majira ya jioni Jubilee Garden. Ramah na Cecilia walikuwa hapo wakiwa wamekaa chini kwenye majani ya ukoka yaliopandwa katika hali nzuri ya kupendeza. Ramah muda huu alikuwa akicharaza gitaa lake taratibu huku akiimba nyimbo tamu ya mapenzi. Nyimbo ambayo ilimfanya Cecy atulie kimya, akiskilizia utamu wa mashairi hayo yakigota hadi kwenye mtima wake.
Sehemu hiyo hapakuwa na watu wengi majira hayo. Na sio majira wala siku hiyo. Ni siku zote huwezi kukuta watu wakiwa wengi kwenye Garden hiyo. Muda mwingi panakuwa tulivu licha ya mazingira yake kuwa mazuri machoni kwa yoyote ayaonayo. Mara kadhaa Garden hiyo ilitumiwa kufanyiwa sherehe kama ‘birthday’ na nyenginezo ndogo ndogo kama hizo.
Hata siku hiyo. Pia hapakuwa na watu wengi waliokuwa hapo. Ni watu wachache tu huku baadhi yao wakionekana na wapenzi wao na wengine walikuwa hapo kama mahali walipopanga kukutaniana kwaajili ya kuzungumza yao. Magari yaliyokuwa yakipita kwenye barabara iliyokuwa karibu na bustani hiyo. Hayakuweza kuwa ni kero badala yake yalikuwa ni kivutio cha macho kwa waliokuwa wamekaa kwenye bustani hiyo.
Muda huu Cecy aliomba na yeye apige gitaa. Ramah alimpatia huku akitabasamu maana alijua kuwa Cecy hakuwahi na wala hawezi kukitumia kifaa hicho. Cecy alikamata gitaa na kuliangalia kwa muda ikiwa tayari ameshaliweka katika mkao wa kulicharaza. Akainua macho yake na kumtazama Ramah ambae muda huo alikuwa akitabasamu. Wote wakajikuta wakicheka!.
Ramah akamtaka apige gitaa, na Cecy akarudisha macho yake kwenye kifaa kile. Akaanza kuvuta nyuzi za kifaa kile lakini katika mtindo ambao haukuwa sahihi. Ramah akacheka kwa nguvu na hapo hapo Cecy akanuna na kuliweka gitaa pembeni. Yeye nae akageuka na upande mwengine muda huo Ramah alikuwa bado akicheka.
Alipoacha kucheka. Alichukua gitaa ambalo lilikuwa chini baada ya kususwa na Cecy. Akalivutia kwake na kuliweka katika mkao wa kulicharaza. Taratibu alianza kuvuta nyuzi na ‘Code’ za nyimbo ya Beka Ibrozama, Nikukunda zikaanza kusikika.
Sikupendi kwasababu huja nidanganya hata siku moooja. Nakupenda kwasababu tumeshakuwa kitu kimoooja. Fikra zangu ndo za kwako, wewe wajuaa. Fikra zako wewee, na za kwangu tambuaa.
We ndo wangu wathamani, sitakutupa nakuthaminii. We ndo wangu unathamaaniii iiii. Nikukunda mama wee, nitakupenda milelee. Nikukunda mama mama wee, mama mama wee eee.
Ramah aliendelea kumuimbia nyimbo hiyo hata pale Cecilia alipogeuka na upande ule akiwa vile vile amenuna kimapozi. Alimzuia kuendelea kupiga gitaa na kumtazama machoni. Ramah na yeye alimtazama huku akiwa anatabasamu. Akalikumbatia gitaa kwenye mapaja yake na kumuuliza Cecy mbona amemkatisha starehe yake.
“Mi siwezi halafu wewe unanicheka” Cecy aliongea kwa deko huku sauti yake akiibana kiasi na kuifanya isikike kama inatokea puani na kufananiana na ya kitoto kidogo kiongeapo kinapokuwa kimenuna mbele ya mamae. Ramah akaliweka gitaa pembeni na kumsogelea Cecy. Akamkumbatia kwa kupitisha mkono wake kwenye shingo yake na kumtazama usoni.
“Cecy wangu kipenzi. Hujui tu ni kiasi gani nafurahia uwepo wako karibu yangu..” Akautoa mkono wake kwenye shingo ya Cecy na hivi sasa akawa amemgeukia ule upande aliokuwepo. “ Wapo wanaotamani wangepata bahati ya kupewa upendo unipao wewe. Lakini nashkuru bahati hiyo nimeipata mimi mnyonge nisie na mali wala hali. Bado sijang'amua ni kipi hasa unipendeacho ilhali sina chochote. Wengi walishakufuata na kukutamkia waziwazi kuwa wanakupenda na wapo tayari kukupatia chochote ukihitajicho. Lakini sijui ni kipi hasa kilichokufanya uzibe maskio yako na kufumba macho yako, usiwatazame wala usiwasikie. Na kuthubutu kunisogelea na kunieleza jinsi wanavyokurubuni kwa maneno yao huku unalia begani kwangu. Hata ukatamani tuhame sayari hii na kwenda sayari ya mbali tukaishi pekeetu ili tu tusipate usumbufu wowote. Ni matumaini yangu hutokuja kunigeuka na kuziacha ahadi zako zipotelee angani kama moshi wa magunzi yaliyochomwa kuchochea moto.” Alipeleka mkono wake na kukishika kidevu cha Cecy. Kisha akaendelea.
“Umzuri sana Cecy wangu. Uzuri wako ni kama wingu la asubuhi lenye rangi ya dhahabu litandalo kwenye anga la Muumba. Kama nchi yetu ingekuwa na Malkia. Basi ningejaribu kumshawishi hata kwa uchache raisi akuweke wewe. Naamini ungeitendea haki nafasi hiyo na sifa zako zingefika dunia nzima kwa mastaajabu ya uzuri wako. Siwezi elezea ni jinsi gani uzuri wako umezichota akili zangu na kuzifumba mboni zangu. Hadi inafikia kipindi sasa kila mwanamke nimuonae namuona kama mwanaume mwenzangu ispokuwa wewe tu. Siwezi kukuelezea hisia nizipatazo kila niwazapo pindi ukiniacha. Hivi unadhani labda nitaweza kustahimili maumivu nitakayoyapata? Hakika sintoweza. Nakuomba uuokoe uhai wangu uliokuwa kwenye viganja vya mikono yako. Sitoweza vumilia ukiniacha halafu nikikumbuka kuwa ladha tamu niipatayo kinywani mwako mara hiyo utakuwa ukimpatia mwengine. Mwili wako unisisimuao kila niugusapo mara hiyo atakuwa akiusawili mwengine. Kila kitu chako ambacho ninakifurahikia sasa mara hiyo atakuwa akikifurahikia mwengine. Hivi Cecy endapo mimi nikikusaliti kama sio kukuacha, wewe utakuwa katika hali gani?” Akamuuliza swali hilo.
“Hakika mpenzi sitoweza vumilia. Na kwanini unisaliti uwende kwa mwengine. Kwani min'nakasoro gani? Ila kiukweli utakuwa umenifanyia ukatili ambao siwazi kama utakuja kunitokea maishani kwangu” Cecy alijibu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi hivyo ndivyo ambavyo nitakavyokuwa pindi ukiniacha. Nakupenda Cecy hata wewe watambua hilo. Sitaki kurudia tena na tena kukuelezea jinsi ulivyouteka moyo wangu. Ila ipo sababu ya kukukumbusha kila mara nijiskiavyo niwapo karibu na wewe. Uwepo wako karibu yangu hata nikiwa na shida nazisahau. Najihisi kama ni Mfalme ninaye miliki Kasri kubwa huku Malkia wangu ukiwa ni wewe. Najaribu kukulinda kama nilindavyo mboni zangu na husda ya upepo wenye vitaka. Kila iwapo mawio na machweo ya siku. Namuomba Mungu wangu akuepushe na mashetani watu wanao liangalia pendo letu kwa jicho la tatu. Pia sisahau kumuomba akukumbushe kila mara ahadi zako ulizokuwa ukiniahidi. Nakupenda Cecy na sitochoka kukuambia neno hilo. Na hata kama lingakuwepo zaidi ya hilo. Pia ningekuambia ili tu niudhihirishe dhahiri upendo wangu juu yako” Ramah aliyanena hayo na muda wote Cecy alikuwa kimya akimtazama yeye. Ramah aliangalia saa yake ya mkononi kisha akamtazama Cecy.
“Muda umeshatutupa mkono. Ni vyema tukianza kuondoka eneo hili” Ramah aliongea na Cecy akakubaliana nae. Wakachukua kila kilicho chao na kuanza kuondoka hapo.
“Si tunaelekea nyumbani, ama vipi?” Ramah alimuuliza.
“Yeah leo tupo wote hadi unichoke mwenyewe” Cecy alijibu huku akimkumbatia.
“Kivipi? Na nyumbani napo?”
“Nyumbani hakuna shaka. Mama nimemuaga na sharti lake kubwa aliniambia nimalize kazi zote ndipo niondoke”
“Kwahiyo unaniambia tunaweza tukalala mpaka asubuhi?” Ramah alimuuliza.
“Mmmh! Kwenda zako huko. Kwani umenioa” Kicheko kikazuka kati yao huku Cecy akiziba wajihi wake na viganja vyake.
Ramah akasimamisha bajaji na wote wakapanda. Safari ya kwenda nyumbani kwa kina Ramah ikaanza.
Walifika na Ramah akafanya malipo. Kisha wakaongozana kuifuata nyumba moja iliyokuwa mtaa huo. Ambayo ilikuwa na hadhi ya kawaida tu. Kwakuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi familia tu. Yani hapakuwa na mpangaji yoyote. Ilisababisha kutokuwa na rabsha za watu wengi mahala hapo. Nje ya nyumba hiyo. Walimkuta mwanamke wa makano akiwa anawasha moto kwenye jiko la mkaa. Alipowaona vijana hao aliacha kuupulizia ule moto na kuwatazama wao huku akitabasamu.
“Mama shikamoo” Cecy alisimama kumsalimia mwanamke yule ambae alikuwa ni mzazi pekee wa Ramah. Muda huo Ramah alimpita yule mama na kupotelea katika chumba kimoja ambacho kilikuwa ni cha nje.
“Marhaba mama. Haya za siku?” Mama alijibu salamu hiyo huku akimtazama Cecy usoni huku akiwa na tabasamu. Cecy akajibu kuwa ni salama. Mama huyo akamuuliza hali ya huko atokako na Cecy akajibu ni nzuri. Mama Ramah akampongeza kwa kumaliza salama kidato cha nne na Cecy akashukuru na kuingia kwenye kile chumba ambacho aliingia Ramah.
“Subiri nikamsaidie mama kupika” Cecy alisema na Ramah hakuwa na cha kupinga.
Cecy akapunguza baadhi ya nguo alizokuwa amevaa na kutoka nje. Huko alimkuta Mama Ramah akibandika sufuria kwenye lile jiko ambalo kwa sasa moto ulikuwa umeshika. Cecy akataka kumsaidia lakini Mama Ramah akamkatalia. Lakini baada ya muda alikubali baada ya Cecy kumlazimisha sana. Ikabidi aingie ndani kwenda kumtolea kanga ambayo Cecy alijifunga nayo kiunoni. Cecy akaendelea kupika chakula kile huku Mama Ramah akiwasha jiko jengine kwaajili ya kupika mboga ili mambo yaende haraka haraka. Shuhuli za kupika zikaendelea.
Saa moja ilitosha kukamilisha chakula ambacho kilikuwa kikipikwa. Chakula ambacho kilikuwa ni wali na nyama ya ng'ombe. Muda huo huo Jay aliingia hapo. Wakasalimiana na Cecy kwa furaha kisha akaingia ndani kwenye kile chumba ambacho Ramah alikuwamo.
“Naona manzi katia maguu home” Jay aliongea huku akivua koti kubwa ambalo alikuwa amelivaa mwanzo kwajili ya kuzuia upepo mkali kwenye pikipiki upigao kifuani.
“We ulikuwa wapi nakupigia simu muda wote hupokei?” Ramah akauliza swali akisahau alichoambiwa na Jay wakati anaingia.
“Kaka mkubwa nilienda Muheza kuna mzigo niliupeleka kule. Halafu kale kakidemu kakule Muheza kana kusalimia. Alitaka nimpe namba yako ila nikamzuga nikamuambia huna simu. Basi akachukua yakwangu kwaajili ya kuwasiliana na wewe”
“Achana nae mshamba tu yule. Tena umefanya vizuri kutompa namba yangu angenisumbua sana yule”
Mara hiyo walisikia mlango ukigongwa. Wakamkaribisha mgongaji na Cecy akaingia ndani akiwa na sahani kubwa ambalo juu yake kulikuwa na sahani mbili zilizokuwa na chakula ndani yake. Akaweka kwenye meza iliyokuwa ndani humo. Kisha akatoka nje huku akisindikizwa na maneno ya utani kutoka kwa Jay.
Akarudi tena na mara hii alikuwa ameshika jagi na bakuli ambalo pia aliviweka juu ya ile meza. Kisha akawakaribisha. Wakati akiwa anatoka. Ramah alimuita, Cecy akarudi. Ramah alinawa mkono na kuchukua kipande cha nyama kisha akamlisha Cecy. Akakila huku akiona aibu. Ramah na yeye akadai anataka alishwe kama yeye alivyomlisha. Huku akiwa na aibu bado. Alichukua kipande cha nyama na kumlisha Ramah. Ghafla zilisikika kelele za shangwe kutoka kwa Jay aliekuwa akifurahia kitendo hicho. Aibu ilimvaa Cecy mpaka kupelekea kuziba wajihi wake kwa viganja.
Cecy nae alicheka huku akiangalia chini kwa aibu. Akatoka nje akimuacha Jay akiwa bado anaendelea kupiga kelele. Ila mara hii hazikuwa kubwa kama alizopiga mwanzo. Cecy alienda sebuleni ambapo Mama wa watoto hao alikuwapo hapo akiandaandaa maaukuli mezani.
“Wana nini hao. Mbona wanapiga kelele kama vichaa?” Mama Ramah alimuuliza huku akichukua vyombo kabatini. Cecy alishindwa kujibu kwasababu ya aibu. Akabaki akicheka tu mwenyewe. Wakaa mezani na kuanza kula.
Majira ya saa mbili na nusu usiku. Cecy alikuwa akijiandaa kwaajili ya kurudi kwao. Alipomaliza akatoka yeye na Ramah. Kisha akamuaga Mama Ramah na kuanza kuondoka hapo. Kwakua Duga na Mikanjuni sio mbali sana. Ni kama mwendo wa dakika kumi na tano tu. Lakini kwa utembeaji wao. Iliwachukua nusu saa kufika Mikanjuni.
“Wakati tuna kula, Mama ameniuliza eti na wewe unanipenda ama mimi najipendekeza tu kwako” Cecy aliongea hivyo muda huo wakiwa tayari wameshafika karibu na nyumbani kwao. Na hapo walikuwa wakitembea kama wamelazimishwa ili kutofika haraka nyumbani kwakina Cecy.
“Na wewe ukamjibuje?” Ramah alimuuliza.
“Mi nikamjibu kwamba na wewe pia unanipenda. Basi hapo akatutakia baraka huku akinisihi nisome kwanza ndipo mambo mengine yafuate”
Hata kama wangepiga hatua fupi kiasi gani. Lakini wangefika tu kivyovyote. Hata kinyonga hutembea polepole lakini hufika aendapo. Muda huu walikuwa wakikanyaga miguu kwenye ardhi ya nyumba hiyo. Walimkuta Anita akiwa amekaa kwenye mkeka nje kwenye kibaraza cha nyumba hiyo.
Walimsalimu na kuingia ndani wote watatu. Walizungumza machache kisha Ramah akaaga anaondoka. Lakini Anita alipinga na kumtaka ale kwanza ndipo aondoke. Cecy na Ramah wakajikuta wakicheka pamoja baada ya kukumbuka kuwa ni muda mfupi tu wametoka kula. Ikabidi Ramah ajitetee lakini Anita hakumuelewa hata kidogo. Alishikilia msimamo wake kuwa ni lazima ale ndipo aondoke.
Ramah hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali. Chakula kikatengwa kisha wakaanza kula. Dakika chache tu. Ramah na Cecy walidai kuwa wameshiba. Anita akalalama kuwa wanamtenga. Maana muda wote alikuwa akiwasubiri wao. Wakajitetea kuwa huko watokapo. Wamekula sana na wala hawakukumbuka kuacha nafasi ya kuja kula na hapo. Anita hakuwa na namna, akakubalina nao.
Ramah aliaga na Cecy akamsindikiza kwa umbali mfupi kisha wakaagana na Cecy akarudi nyumbani kwao na Ramah akarudi kwao huku wakiahidiana kuwasiliana baadae.
* *
Ikiwa ni siku mpya tena. Siku ambayo Ramah aliinuka na uchovu mwingi kutokana na kuwa usiku mzima alikuwa akiongea na Cecy kwenye simu. Majira haya ya asubuhi alipoinuka hakumkuta Jay kitandani. Hata hivyo hakujishuhulisha nae kwasababu alijua pengine ameenda kwenye mambo yake. Ramah yeye hakuwa na kazi maalumu kutokana na kuwa alimaliza kidato cha nne mwaka uliopita na baada ya hapo alianza kujishuhulisha na kazi yoyote itakayomjia mbele yake.
Akiwa na uchovu mwingi wa usingizi. Aliivuta simu yake juu ya meza ndogo iliyokuwa karibu na kitanda kwaajili ya kutazama saa. Hata hivyo alisahau jambo hilo baada ya kukuta simu nyingi za Cecy alizompigia wakati yeye akiwa amelala. Akaipiga namba ya Cecy na kuiweka simu sikioni. Simu ile ikapokelewa kisha wakasalimiana kidogo. Lakini Ramah aligundua kitu kwenye sauti ya Cecy. Hakuwa ni mwenye furaha kama alivyomzoea. Akamuuliza ni nini tatizo na Cecy akajibu kuwa mama yake yumgonjwa.
Ramah akajiinua pale kitandani alipojilaza ili asikilize vizuri kuwa Mama Cecy alikuwa akiumwa nini ilhali ni jana tu ametoka huko na alimkuta akiwa na siha njema kabisa. Cecy alimuambia Mamae analalamika kuwa mwili mzima ulikuwa ukimuuma na kujihisi homa.
Ramah akamuambia kuwa muda si mrefu atafika hapo. Akakata simu na kuinuka pale kitandani. Akatoka nje kwenda kujifanyia usafi kabla hajaenda huko. Alipomaliza kila kitu, akamjuza mamae taarifa aliyopewa na Cecy kuwa mama yake alikuwa akiumwa. Mama yake akamuambia ampe pole na kama akipata muda ataenda kumjulia hali. Kisha Ramah akaondoka.
Muda huu alikuwa nyumbani kwa kina Cecy. Alimkuta Cecy akiwa amekaa na mamae sebuleni na Jenifa akiwapo mahala hapo pia. Akawasalimu na kuchukua nafasi na yeye. Akamjulia hali Anita. Na Anita alijibu kuwa kwa muda huo hajambo kidogo baada ya kutumia dawa aliyonunua kwenye dula la dawa. Akaongezea kwa kusema kuwa. Usiku wa siku hiyo ndipo homa hilo lilipomuanza.
Alikuwa akitetemeka huku mwili mzima akiuhisi kufa ganzi. Na ilipofika majira ya asubuhi. Ndipo alipomuagizia Cecy akamchukulie dawa dukani na baada ya kuzitumia, kidogo hali yake ipo sawa kwa wakati huo. Ramah alimpa pole na kumuambia kuwa hata mamae alimpa taarifa hiyo na yeye amesikitishwa na amesema atakapopata muda mzuri, atakuja kumuangalia.
Anita alishukuru kwa kuona mwanamke mwenzake amesikitishwa na hali iliyompata. Ramah baada ya muda kidogo aliaga na kusema kuwa muda huo kuna pahali anataka kwenda. Anita alishukuru kwa kuja kumjulia hali. Ramah aliondoka na kupotelea mitaani.
* *
Majira ya saa kumi na moja alfajiri ikiwa ni mwanzo wa siku nyengine. Ramah muda huu akiwa amelala. Alishtuliwa na simu yake iliyokuwa ikiita. Aliamka kiuvivu na kutazama ni nani anaepiga muda huo? Akakuta ni Cecy ndie anaempigia. Akajiweka vizuri huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio mbio na asijue ni kwanini. Akaipokea na kupokelewa na sauti ya kilio kutoka kwa Cecy.
Akajaribu kumtuliza huku akimuuliza ni nini tatizo. Lakini Cecy hakuongea ya kueleweka zaidi ya kumtaja mama yake huku akitaja na neno hospitali. Kwavile Cecy hakunyoosha maelezo ya kile anachokisema. Ikabidi Ramah amuulize ni hospitali ipi walikuwapo ili aende huko akajue kulikoni. Cecy akamuambia kuwa wapo hospitali ya Makorora. Ramah alikata simu na kumuamsha Jay. Kisha akamjuza taarifa hiyo na hapo likatoka shauri kuwa waende huko. Kabla ya kuondoka. Walimpa taarifa hiyo mama yao na kwavile giza bado lilikuwapo. Akasema yeye atatokea pindi giza likifunikwa na nuru ya jua. Wakapanda pikipiki na kuwahi huko.
MUDA kidogo, wakawa wamefika nje ya hospitali hiyo. Wakapaki pikipiki yao sehemu maalumu na kuzama zaidi ndani ya hospitali. Kwa maelekezo ya Cecy wakafanikiwa kufika ambapo walimkuta Cecy akiwa amekaa kwenye benchi, akiwa na Jenifa na Mama yake. Akatoa salamu na Cecy ambae muda wote alikuwa amejiinamia akilia kimya kimya kila akifikiria hali ya mamae ilivyobadilika ghafla.
Alikuwa na uchungu usio mithilika. Alikuwa akifikiria ni vipi mzazi wake huyo wa pekekee endapo ataondoka duniani. Ni nani atakaemlea ilhali yeye ni mtoto na bado anahitaji malezi ya mama yake. Muda wote alikuwa akilia na Mungu wake amnusuru mamae na ugonjwa ambao hadi muda huo hawajapata kumaizi ni kipi hasa kinachomsumbua mgonjwa wao.
Cecy aliposkia sauti ya Ramah akitoa salamu hapo. Akainua haraka na kwenda kumkumbatia huku akizidisha kilio. “Rafael mama yangu mimiii iii!” Cecy alilia huku akizidi kumkumbatia Ramah kiasi ambacho Ramah moyoni mwake alihisi uchungu kwa kuona kipenzi chake akiwa katika uchungu wa kumlilia mama yake bila kumaizi hali aliyokuwa nayo.
Ramah ikabidi achukue jukumu la kum'bembeleza kwa kumpa moyo kuwa mama yake atakuwa sawa tu cha muhimu ni kumuombea kwa Mungu amfanyie miujiza ili hali yake irudi kama kawaida. Baada ya kumbembelezwa kidogo. Alipunguza kulia na Ramah alimkokota hadi kwenye benchi na kwenda kukaa nae hapo. Cecy aliacha kulia na sasa alikuwa akigumia huku akiwa amelaza kichwa chake kwenye bega la Ramah.
Daktari aliwafuata na kuwauliza ni nani hasa ambae anapaswa kupokea majibu ya mgonjwa wao. Cecy akataka aende yeye. Mama Jenifa akamzuia. Akaondoka yeye na Jay ambao kidogo walikuwa sawa kwa muda huo. Cecy akawa mpole na kusubiri majibu ya mamae huku akimuombea mungu.
“Nam... Nadhani sasa ni muda wa kuwapa majibu ya ugonjwa unaomsumbua mgonjwa wetu. Kwanza kabla ya yote, ningependa mnijulishe majina yenu na undugu wenu kwa huyu mgonjwa” Daktari aliwaeleza hayo. Mama Jenifa akajitambulisha kama jirani huku Jay akijitambulisha kama mtoto wa hiyari wa mama huyo.
“Hana mume yule mama?” Daktari akawauliza swali hilo. Wakaangaliana machoni kisha Mama Jeni akajibu kuwa hana, mume wake alishafariki kitambo. Daktari akajikohoza kidogo na kuvuta faili moja lililokuwa juu ya meza.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mgonjwa wetu anasumbuliwa na maradhi ya Moyo. Presha yeke ipo juu sana. Halafu chengine anaupungufu wa damu mwilini mwake, inahitajika aongezewe damu haraka iwezekanavyo kisha ndio tuendelee na haya magonjwa mengine...” Mama Jeni na Jay waliangaliana tena. Sauti ya Dakta ikawagutusha na kumtazama tena yeye. “Na kwa bahati mbaya kwenye stoko yetu tumeishiwa damu. Sasa inabidi wapatikane watu wawili watakaoweza kumtolea damu.”
“Kwani ni chupa ngapi zinahitajika Dokta?” Mama Jeni alimuuliza.
“Ni chupa mbili Mama na zinahitajika haraka ili tukishamuongezea damu ndipo tuendelee na haya magonjwa mengine” Dokta aliwaeleza.
Wakakuna vichwa kutafakari. Ni nani atakae mtolea damu mgonjwa? Hawakujua!. Ikabidi wamuombe Dokta wakajadiliane na wenzao hapo nje ili zoezi hilo lifanyike haraka. Dokta aliwakubalia na kuongezea ya kwamba. Kama kati yao hatopatikana wa kutoa damu. Basi anaouwezo wa kuwatafutia watu ambao watakao toa damu lakini kwa malipo. Wakakubaliana nae na kutoka nje.
Cecy alipowaona wakitoka ofisini kwa Dokta huku sura zao zikitangaza mashaka fulani. Moja kwa moja alijua mamae kuna kubwa limempata. Akaanza kulia upya huku akimtaja mama yake. Hata Mama Ramah muda huu alikuwa ameshafika tayari hapo. Ikabidi wambembeleze huku wakimtoa hofu kuhusu hali ya mama yake. Utulivu ukapatikana na Mama Jeni akawa tayari kuwaeleza waliyoambiwa na Dokta.
Akawaeleza yote na hata zoezi la kutoa damu kwa mgonjwa likitakiwa lifanyike haraka. Wakauliza ni damu kiasi gani inatakiwa na yeye akajibu ni chupa mbili. Katika hali ya kushangaza. Ramah alijitolea kutoa damu chupa zote mbili. Wote walitaharuki na kumuangalia usoni kwa mshangao. Ila yeye wala hakujali hilo. Alisimamia msimamo wake kuwa atatoa chupa zote yeye.
Mama Jeni alirudi ofisini kwa Dokta kumueleza. Lakini Dokta alipinga kwa kusema ni hatari sana kwa mtu mmoja kutoa damu chupa mbili na ndio maana yeye akataka watu wawili. Mama Jeni akatoka na kwenda kuwaeleza hayo. Kutokana na huruma aliyokuwa nayo kwa ndugu yake wa pekee na kwa Mama Cecy. Jay alijitolea kutoa chupa moja na yeye.
Baada ya majadiliano kukamilika na kupatikana watu watakao toa damu. Mama Jeni alifikisha taarifa hizo kwa Dokta na Dokta akamuambia wamsubiri kwa dakika kadhaa atakwenda kuwachukua vijana hao kwaajili ya vipimo kabla ya kutoa damu. Ili ifahamike kwamba wanaouwezo wa kutoa damu ama laa!.
Baada ya dakika kumi na tano. Dokta alitoka na kuwataka vijana hao wanaojitolea damu kumfuata nyuma. Ramah na Jay waliinuka na kuongozana na Daktari. Kabla ya kutoa damu kwanza walipimwa uzito na vitu vyengine vipimwavyo kabla ya zoezi hilo. Wakaonekana wapo sawa na wakaaingizwa katika chumba fulani kwaajili ya zoezi hilo.
Nusu saa mbele. Zoezi la kutoa damu likakamilika na vijana hao wakatakiwa wapumzike kwa muda kwanza kabla ya kufanya chochote. Muda wote waliokuwa kwenye mabenchi wakisubiri. Walikuwa wakiomba Mungu mazoezi hayo yakamilike yakinifu ili hali ya kawaida irejee. Ramah na Jay walitoka kule walipochukuliwa damu zao na kwenda kuungana na wenzao pale kwenye mabenchi ili wasubiri matokeo ya Daktari.
Muda kidogo. Daktari alitoka na kuwaeleza hali ya mgonjwa wao. Mara hii aliwaeleza wote pale pale walipokuwa wamekaa. Wakumuuliza kwamba kuna ruhusa ya kwenda kumuona mgonjwa wao kwa muda huo. Na Daktari aliwajibu kuwa kwa muda huo wanaweza kwenda kumuona lakini wasimbugudhi kwa chochote. Wakainuka wote na kuingia kwenye chumba alicholazwa Anita au Mama Cecy.
Walimkuta akiwa amejilaza kitandani akiwa macho. Damu inayopita kwenye mrija kutokea kwenye drip iliingia taratibu kwenye mishipa yake. Cecy alipomuona mamae. Alitaka kuangusha kilio lakini akakatizwa na sauti ya Mama Jeni akimkumbusha maneno ya Daktari kuwa wasimbughuzi mgonjwa. Akafumba mdomo wake na kubaki akigugumia kimya kimya.
Anita alimuita na kumtaka akae karibu yake. Hapo wakamjulia hali na yeye akajibu kuwa kwa muda huo anajihisi afadhali tofauti na vile ilivyokuwa masaa kadhaa nyuma. Wakampa pole huku wakimfariji kuwa atapona tu cha muhimu ni kumtumaini Muumba. Maana yeye ndio muweza wa kila kitu. Baada ya muda walimuaga huku wakimuambia kuwa watakuja kumuona tena muda mwengine.
Cecy alibaki na mama yake huku Ramah akitoka kwaajili ya kwenda kutafuta chakula cha mgonjwa na cha Cecy. Baada ya muda alirudi na chakula hicho. Akawapatia na kuondoka akiahidi kurudi tena baadae. Nje ya hospitali Jay alikuwa akimsubiria. Alipofika, wakapanda pikipiki na kurudi nyumbani kwao.
“Duh! Kaka ile sindano ni nzito balaa. Cheki nilivyovimba hapa” Jay alikuwa akimueleza hayo Ramah muda huo wakiwa wamefika nyumbani kwao na hapo walikuwa wakikiendea chumba chao. Ramah akatazama kisha akacheka.
“Ila sema dogo pale umeonyesha ushujaa wa ajabu. Hata Sharukhan mwenyewe sidhani kama angeweza kuuonyesha. Kutoa damu chupa mbili pekeako..! Hahaha Hapana bwana” Jay aliongea. Ramah alikuwa kimya huku akitabasamu.
“Au ulikuwa unataka kujionyesha kwamba wewe ni zaidi ya muhindi ukipenda” Jay alizidi kuzungumza hayo. Mara hii sasa Ramah alikuwa anaanza kuchukizwa na maneno hayo. Lakini alijizuia tu asimjibu chochote Jay.
Jay baada ya kuona Ramah yupo kimya. Akaendeleza maneno yake. Ambayo safari hii Ramah hakuweza kuyavulimia na kujikuta akifungua mdomo na kumkoromea Jay kuwa aache kumtafuta asubuhi hiyo.
“Jamani..Jamani. Lakini kwanini nyie watoto hamkui? Eeeeh! Kila ifikapo mawio lazima muanzishe vurumai. Na hilo mshajizoesha nalo tayari. Embu acheni ujuha wenu huko” Ilisikika sauti ya Mama yao kwa nje akiwakaripia waache kuzozana. Ilikuwa ni jadi ya watoto hao. Kila ifikapo asubuhi lazima wazozane kwa jambo lolote lile na mara nyingi ni Jay ndie muanzilishi wa mizozano hio huku mara chache sana Ramah akiwa muanzilishi. Wote wakawa kimya baada ya mama yao kuwakaripia.
___________
Majira ya mchana. Nyumbani kwa kina Jeni. Alikuwa akijiandaa muda huo kufungasha chakula kwaajili ya kupeleka kwa mgonjwa ambae ni Mama Cecy. Mama yake alimuachia maagizo kuwa akifika amuambie Mama Cecy kuwa, mchana huo hakuweza kutokea kwasababu alikuwa na shuhuli nyingi, hivyo jioni anaweza kwenda. Jeni akajibu sawa na kupotelea nje ya nyumba yao.
Muda huu alikuwa anafika hospitali na nje alikutana na Ramah ambae nae alikuwa akienda huko huko. Waliungana na safari ikawa moja. Kwenye mabenchi, walimkuta Cecy amekaa ni kama vile kuna jambo alikuwa akilisubiri hivi. Wakamsalimia na kumuuliza kulikoni. Akawajibu kuwa. Mama yake kwa muda huo alikuwa akipatiwa tiba ya magonjwa yanayomsumbua. Hivyo alitakiwa atoke nje ili awapishe madaktari wafanye yao.
Nao wakaungana nae pale kwenye benchi. Wakamuuliza vipi kuhusu hali ya mgonjwa wao. Nae akajibu ipo salama ni kama vile walivyomuacha tu asubuhi ya siku hiyo.
“Basi ungekula kwanza wakati huu tuna subiri matibabu yapite” Ramah alishauri.
“Hapana. Tusubirini tu, nitaenda kula nae. Hata hivyo wameniambia hawachelewi sana” Cecy alijibu. Wakakubaliana nae na kusubiri.
Dakika kadhaa mbele. Daktari aliwaruhusu waende wakamuone mgonjwa wao. Wakainuka na kukifuata chumba hicho. Huko walimkuta Anita akifyonza kipande cha chungwa. Alipowaona alitabasamu na kujiinua pale kitandani akakaa. Ramah na Jeni walimsalimu na kumjulia hali. Aliwajibu kuwa. Hivi sasa anajiskia afadhali na hata Madaktari wamemuambia, ikiwa ataendelea na hali hiyo hadi hapo siku inayofuata. Basi watatoa ruhusu ya kurudi nyumbani.
Walishukuru Mungu kwa hiyo hatua aliyofikia. Ila akasema mwili bado unamuuma kila pahali lakini sio kama vile ulivyokuwa ukimuuma mwanzo. Anita aliwauliza kuhusu wazazi wao. Na wao wakajibu kuwa kwa muda huo walikuwa na udhuru lakini wamesema jioni watatokea. Baada ya kukaa kwa muda mrefu hapo. Wakaaga ikiwa pia muda wa kuona wagonjwa umeisha. Ramah na Jeni walitoka nje ya hospitali hiyo.
“We unaelekea wapi muda huu?” Ramah alimuhoji Jeni wakiwa wamesimama nje ya hospitali.
“Naelekea Nguvumali kwa Shangazi” Jeni alijibu. Ramah akasema yeye anaelekea Donge kabla ya kwenda nyumbani kwao. Ikawa ni hivyo. Wakaagana na kila mmoja akashika njia yake.
“Dokta amekuambiaje mama?” Cecy alimuuliza mama yake, kipindi hicho akiwa anaandaa chakula walicholetewa.
“Walichoniambia kwamba, presha imekaa sawa na hata moyo pia upo sawa. Lakini inabidi leo nibaki hapa ili waendelee kuicheki hali yangu kama itakuwa na mabadiliko au laa!”
“Dawa wamekuongezea ama ndio hizo hizo?” Cecy alimuuliza.
“Heee! Si wataniua sasa. Madawa yote haya halafu waniongezee mengine”
Anita aliyanena hayo akiwa amechangamka sana kiasi ambacho alimpa furaha Cecy kwa kuona mamae amerudi katika hali yake ya kawaida. Hakujua ni kwa kiasi gani amshukuru Ramah kwa msaada aliompatia mamae. Kila akifikiria ni kwa kiasi gani Ramah alivyojitoa kwake kwa hali yoyote inayompata. Hakujua amuweke kwenye fungu gani la watu wake wema waliopata kumtokea kwenye maisha yake.
Chozi la furaha lilimdondoka huku mamae akilishuhudia waziwazi. Cecy alidondosha chozi la furaha alipomfikiria Ramah. Sio kwamba hakuuona wema wa rafiki yake kipenzi Jeni au Jay ndugu yake na Ramah. Hapana. Ila ilikuwa ni tofauti kwasababu Jenifa alikuwa ni rafiki yake tangu walipokuwa shule ya msingi na Jay alikuwa ni shemeji yake kwa mdogo wake. Ilhali Ramah ni mpenzi wake na wamekutana Sekondari. Mamae akamvutia kwake na kumkumbatia.
“Cecilia binti yangu. Najua kikulizacho ni juu ya Ramah. Binti yangu, maisha ya mapenzi yanatafsiri nyingi sana ukiyafikiria. Mpaka sasa haijapatikana tafsiri yakinifu kuhusu mpenzi. Sijui kwenu nyie vijana, ila kwetu sisi tuliyatambua ama tunayatambua kama ni kifungo cha moyo anachojiwekea mtu juu ya mtu mwengine. Nikisema hivyo namaanisha kwamba. Endapo utaamua kupenda, basi hutoangalia huyo umpendae ana mapungufu gani, ana hali gani, ana kipi cha thamani kwenye maisha yako, nini watu wanasema juu yake. Wakimsema kwa mabaya nafsi itakuuma, na hicho ni kipimo kimojawapo kuthibitisha kwamba unampenda mtu fulani. Wakimsema kwa wema utazidi kumfurahikia na kumuongezea thamani kwenye moyo wako kwa kuona kumbe hata watu wanaokuzunguka wanamuona ni wathamani. Cecy binti yangu. Umeshakuwa na nijuavyo unamiliki miongo mingi kiasi cha kukufanya utambue hili baya hili zuri. Na mimi kama mzazi wako wa pekee niliebaki, siwezi nikakuchagulia mtu wa kuwa nae. Maamuzi hayo yapo ndani yako mwenyewe kwasababu siwezi jua ni wapi mmekutana na ni vipi mmeonana. Au hata kama nikiyajua hayo, pia haitokuwa ndio chanzo cha kukuchagulia mtu wa kuwa nae. Najua wajua ni kwa kiasi gani Ramah akupendavyo. Ni mara nyingi sana amejitoa kwako sio kwa hili tu. Lakini Ramah huyo huyo anaejitoa kwako unaouwezo wa kumtoa kwa hii nafasi aliyonayo kwako na kumfanya rafiki.”
“Kwanini mama unasema hivyo?” Cecy alimuuliza mamae baada ya kusikia maneno hayo ya mwisho. Ni mara nyingi sana anakuwa mtulivu pindi asikiapo mamae akiongea chochote. Alipenda sana kumsikiliza maana alijua kinywa cha mtu mzima ni dawa.
“Nasema hivyo nikiwa na maana kubwa sana binti yangu. Tumeumbwa na nafsi zenye kubadilika. Kubadili maamuzi ambayo wakati huu tunayaona ni ya muhimu na kuyaweka katika hali nyengine baadae. Na huko kubadilika kwa nafsi kunatokana na tamaa za moyo. Binti yangu, binti yangu usikubali kuendeshwa na tamaa za moyo wako maana itafikia wakati utaijutia tamaa yako. Nijuavyo nafsi imeumbwa kupenda moja kwa moja huku moyo ukiumbwa na viwili. Ikiwa ni kupenda na kutamani. Tamaa ya moyo inaweza ikakuweka matatizoni. Unachotakiwa ni kuipinga kabla hujapatwa na Jereha la Moyo. Binti yangu, tuliza moyo wako na ukubali mapungufu yenu. Dhaifu la mwenzako usilifanye kuwa ndio kigezo cha kumuadhibu kwa maumivu ikiwa yeye dhaifu lako analitumia kama kigezo cha kukuongoza panapostahili.”
“Lakini mama mi bado sijakuelewa nini unanimaanishia japokuwa nimekuwa mlevi wa maneno yako mama yangu. Lakini ya leo, mmh! naona yamezidi sana maana na mafumbo. Embu jaribu kupunguza mafumbo ili niielewe maana yako” Cecy aliyanena hayo akimtazama mamae usoni. Anita alitabasamu kisha akafumbua kinywa chake tayari kuendelea na nasaha yake.
“Hutonielewa kwa sasa binti yangu, maana hata mie nilipoelezewa na mama yangu kipindi kile ningali binti kigoli kama uwavyo wewe kipindi hiki sikumuelewa. Na hata nilipohoji zaidi hakutaka kunifafanulia zaidi alinimbia nitaelewa nikikuwa. Na hata mimi sipaswi kukujulisha maana ya maneno haya. Unachotakiwa ni wewe kuyapa nafasi kwenye bongo lako na kuyafikiria kwakina ili upate maana. Wewe bado ni binti mdogo sana na huo umri ulionao sasa ni pevu ambao unapitia changamoto nyingi. Kwaakili ulizonazo sasa usikubali kuongozwa na tamaa za moyo. Ramah anakupenda na wewe mpende kwa hali yoyote atakayokuwa nayo. Binti yangu, wahenga walisema. Usiache mbachao kwa msala upitao.” Anita alimaliza nasaha yake hivyo kisha akamtaka Cecy aweke chakula wale.
“Nimekuelewa Mama yangu” Cecy aliongea hivyo na kujiinua pale kitandani. Akakifuata chakula ambacho alikuwa tayari amekiweka kwenye sahani na kukifunika wakati mama yake alipomtaka asogee karibu yake. Alikianda na kuanza kula taratibu huku wakiongea hili na lile. Kilikuwa ni viazi mbatata ambavyo vimeungwa utamu kiasi ambacho harufu yake tu ilithibitisha hilo.
Walikula kiasi tu kisha hapo wakaacha chakula kile kikiwa bado ni kingi. Wakakiweka vizuri kwenye bakuli. Anita alimtaka bintie watoke nje wakapunge upepo na kubadili hewa, maana ndani humo kulitawaliwa na harufu ya madawa tu. Cecy alimsaidia mamae kushuka kwenye kitanda, kisha wakaanza kutembea taratibu kutoka nje. Walitafuta sehemu nzuri na kukaa.
* * * *
Majira ya saa kumi na moja jioni. Mama Jeni, Mama Ramah, Ramah na Jay walikuwa wakitoka nje ya hospitali aliyolazwa Anita au Mama Cecy. Majira hayo walikuwa wakitoka ndani ya hospitali hiyo kumjulia hali Anita. Na muda huo walikuwa wakitoka kwenda majumbani kwao.
“Sasa dogo inabidi turuke time hii kule juu kabla jamaa haja ghairisha, au vipi?” Jay alimuambia Ramah hayo huku akiwa anaikokota pikipiki yake kuitafutia sehemu nzuri kabla ya kuipanda.
“Kwani jamaa alitaka muda gani? Maana muda huu nataka niruke home mara mo....”
“We vipi wewe? Kila mara unataka kuwa home tu? Acha hizo bwana, twenzetu saa hii. Kwanza mida flani ya saa moja kuna sehemu nataka niende. Sasa ukileta habari za kuchelewa hapa min'takuacha” Jay alikoroma. Ramah akawa mpole na kundandia pikipiki. Safari ya kwenda huko wanapobishaniana muda wa kwenda ikaanza.
Dakika kadhaa wakawa wamefika Bahari Breeze. Wakapaki pikipiki yao sehemu maalumu na kuzama ndani ya baa hiyo iliyoko kandokando ya Bahari ya Hindi. Huko walikuta watu wengi wamekaa kwenye viti kuzizunguka meza zilizokuwa mbali mbali. Jay akatoa simu yake na kuiminya minya kisha akaiweka sikioni huku akiangaza hu
Muda kidogo. Daktari alitoka na kuwaeleza hali ya mgonjwa wao. Mara hii aliwaeleza wote pale pale walipokuwa wamekaa. Wakumuuliza kwamba kuna ruhusa ya kwenda kumuona mgonjwa wao kwa muda huo. Na Daktari aliwajibu kuwa kwa muda huo wanaweza kwenda kumuona lakini wasimbugudhi kwa chochote. Wakainuka wote na kuingia kwenye chumba alicholazwa Anita au Mama Cecy.
Walimkuta akiwa amejilaza kitandani akiwa macho. Damu inayopita kwenye mrija kutokea kwenye drip iliingia taratibu kwenye mishipa yake. Cecy alipomuona mamae. Alitaka kuangusha kilio lakini akakatizwa na sauti ya Mama Jeni akimkumbusha maneno ya Daktari kuwa wasimbughuzi mgonjwa. Akafumba mdomo wake na kubaki akigugumia kimya kimya.
Anita alimuita na kumtaka akae karibu yake. Hapo wakamjulia hali na yeye akajibu kuwa kwa muda huo anajihisi afadhali tofauti na vile ilivyokuwa masaa kadhaa nyuma. Wakampa pole huku wakimfariji kuwa atapona tu cha muhimu ni kumtumaini Muumba. Maana yeye ndio muweza wa kila kitu. Baada ya muda walimuaga huku wakimuambia kuwa watakuja kumuona tena muda mwengine.
Cecy alibaki na mama yake huku Ramah akitoka kwaajili ya kwenda kutafuta chakula cha mgonjwa na cha Cecy. Baada ya muda alirudi na chakula hicho. Akawapatia na kuondoka akiahidi kurudi tena baadae. Nje ya hospitali Jay alikuwa akimsubiria. Alipofika, wakapanda pikipiki na kurudi nyumbani kwao.
“Duh! Kaka ile sindano ni nzito balaa. Cheki nilivyovimba hapa” Jay alikuwa akimueleza hayo Ramah muda huo wakiwa wamefika nyumbani kwao na hapo walikuwa wakikiendea chumba chao. Ramah akatazama kisha akacheka.
“Ila sema dogo pale umeonyesha ushujaa wa ajabu. Hata Sharukhan mwenyewe sidhani kama angeweza kuuonyesha. Kutoa damu chupa mbili pekeako..! Hahaha Hapana bwana” Jay aliongea. Ramah alikuwa kimya huku akitabasamu.
“Au ulikuwa unataka kujionyesha kwamba wewe ni zaidi ya muhindi ukipenda” Jay alizidi kuzungumza hayo. Mara hii sasa Ramah alikuwa anaanza kuchukizwa na maneno hayo. Lakini alijizuia tu asimjibu chochote Jay.
Jay baada ya kuona Ramah yupo kimya. Akaendeleza maneno yake. Ambayo safari hii Ramah hakuweza kuyavulimia na kujikuta akifungua mdomo na kumkoromea Jay kuwa aache kumtafuta asubuhi hiyo.
“Jamani..Jamani. Lakini kwanini nyie watoto hamkui? Eeeeh! Kila ifikapo mawio lazima muanzishe vurumai. Na hilo mshajizoesha nalo tayari. Embu acheni ujuha wenu huko” Ilisikika sauti ya Mama yao kwa nje akiwakaripia waache kuzozana. Ilikuwa ni jadi ya watoto hao. Kila ifikapo asubuhi lazima wazozane kwa jambo lolote lile na mara nyingi ni Jay ndie muanzilishi wa mizozano hio huku mara chache sana Ramah akiwa muanzilishi. Wote wakawa kimya baada ya mama yao kuwakaripia.
___________
Majira ya mchana. Nyumbani kwa kina Jeni. Alikuwa akijiandaa muda huo kufungasha chakula kwaajili ya kupeleka kwa mgonjwa ambae ni Mama Cecy. Mama yake alimuachia maagizo kuwa akifika amuambie Mama Cecy kuwa, mchana huo hakuweza kutokea kwasababu alikuwa na shuhuli nyingi, hivyo jioni anaweza kwenda. Jeni akajibu sawa na kupotelea nje ya nyumba yao.
Muda huu alikuwa anafika hospitali na nje alikutana na Ramah ambae nae alikuwa akienda huko huko. Waliungana na safari ikawa moja. Kwenye mabenchi, walimkuta Cecy amekaa ni kama vile kuna jambo alikuwa akilisubiri hivi. Wakamsalimia na kumuuliza kulikoni. Akawajibu kuwa. Mama yake kwa muda huo alikuwa akipatiwa tiba ya magonjwa yanayomsumbua. Hivyo alitakiwa atoke nje ili awapishe madaktari wafanye yao.
Nao wakaungana nae pale kwenye benchi. Wakamuuliza vipi kuhusu hali ya mgonjwa wao. Nae akajibu ipo salama ni kama vile walivyomuacha tu asubuhi ya siku hiyo.
“Basi ungekula kwanza wakati huu tuna subiri matibabu yapite” Ramah alishauri.
“Hapana. Tusubirini tu, nitaenda kula nae. Hata hivyo wameniambia hawachelewi sana” Cecy alijibu. Wakakubaliana nae na kusubiri.
Dakika kadhaa mbele. Daktari aliwaruhusu waende wakamuone mgonjwa wao. Wakainuka na kukifuata chumba hicho. Huko walimkuta Anita akifyonza kipande cha chungwa. Alipowaona alitabasamu na kujiinua pale kitandani akakaa. Ramah na Jeni walimsalimu na kumjulia hali. Aliwajibu kuwa. Hivi sasa anajiskia afadhali na hata Madaktari wamemuambia, ikiwa ataendelea na hali hiyo hadi hapo siku inayofuata. Basi watatoa ruhusu ya kurudi nyumbani.
Walishukuru Mungu kwa hiyo hatua aliyofikia. Ila akasema mwili bado unamuuma kila pahali lakini sio kama vile ulivyokuwa ukimuuma mwanzo. Anita aliwauliza kuhusu wazazi wao. Na wao wakajibu kuwa kwa muda huo walikuwa na udhuru lakini wamesema jioni watatokea. Baada ya kukaa kwa muda mrefu hapo. Wakaaga ikiwa pia muda wa kuona wagonjwa umeisha. Ramah na Jeni walitoka nje ya hospitali hiyo.
“We unaelekea wapi muda huu?” Ramah alimuhoji Jeni wakiwa wamesimama nje ya hospitali.
“Naelekea Nguvumali kwa Shangazi” Jeni alijibu. Ramah akasema yeye anaelekea Donge kabla ya kwenda nyumbani kwao. Ikawa ni hivyo. Wakaagana na kila mmoja akashika njia yake.
“Dokta amekuambiaje mama?” Cecy alimuuliza mama yake, kipindi hicho akiwa anaandaa chakula walicholetewa.
“Walichoniambia kwamba, presha imekaa sawa na hata moyo pia upo sawa. Lakini inabidi leo nibaki hapa ili waendelee kuicheki hali yangu kama itakuwa na mabadiliko au laa!”
“Dawa wamekuongezea ama ndio hizo hizo?” Cecy alimuuliza.
“Heee! Si wataniua sasa. Madawa yote haya halafu waniongezee mengine”
Anita aliyanena hayo akiwa amechangamka sana kiasi ambacho alimpa furaha Cecy kwa kuona mamae amerudi katika hali yake ya kawaida. Hakujua ni kwa kiasi gani amshukuru Ramah kwa msaada aliompatia mamae. Kila akifikiria ni kwa kiasi gani Ramah alivyojitoa kwake kwa hali yoyote inayompata. Hakujua amuweke kwenye fungu gani la watu wake wema waliopata kumtokea kwenye maisha yake.
Chozi la furaha lilimdondoka huku mamae akilishuhudia waziwazi. Cecy alidondosha chozi la furaha alipomfikiria Ramah. Sio kwamba hakuuona wema wa rafiki yake kipenzi Jeni au Jay ndugu yake na Ramah. Hapana. Ila ilikuwa ni tofauti kwasababu Jenifa alikuwa ni rafiki yake tangu walipokuwa shule ya msingi na Jay alikuwa ni shemeji yake kwa mdogo wake. Ilhali Ramah ni mpenzi wake na wamekutana Sekondari. Mamae akamvutia kwake na kumkumbatia.
“Cecilia binti yangu. Najua kikulizacho ni juu ya Ramah. Binti yangu, maisha ya mapenzi yanatafsiri nyingi sana ukiyafikiria. Mpaka sasa haijapatikana tafsiri yakinifu kuhusu mpenzi. Sijui kwenu nyie vijana, ila kwetu sisi tuliyatambua ama tunayatambua kama ni kifungo cha moyo anachojiwekea mtu juu ya mtu mwengine. Nikisema hivyo namaanisha kwamba. Endapo utaamua kupenda, basi hutoangalia huyo umpendae ana mapungufu gani, ana hali gani, ana kipi cha thamani kwenye maisha yako, nini watu wanasema juu yake. Wakimsema kwa mabaya nafsi itakuuma, na hicho ni kipimo kimojawapo kuthibitisha kwamba unampenda mtu fulani. Wakimsema kwa wema utazidi kumfurahikia na kumuongezea thamani kwenye moyo wako kwa kuona kumbe hata watu wanaokuzunguka wanamuona ni wathamani. Cecy binti yangu. Umeshakuwa na nijuavyo unamiliki miongo mingi kiasi cha kukufanya utambue hili baya hili zuri. Na mimi kama mzazi wako wa pekee niliebaki, siwezi nikakuchagulia mtu wa kuwa nae. Maamuzi hayo yapo ndani yako mwenyewe kwasababu siwezi jua ni wapi mmekutana na ni vipi mmeonana. Au hata kama nikiyajua hayo, pia haitokuwa ndio chanzo cha kukuchagulia mtu wa kuwa nae. Najua wajua ni kwa kiasi gani Ramah akupendavyo. Ni mara nyingi sana amejitoa kwako sio kwa hili tu. Lakini Ramah huyo huyo anaejitoa kwako unaouwezo wa kumtoa kwa hii nafasi aliyonayo kwako na kumfanya rafiki.”
“Kwanini mama unasema hivyo?” Cecy alimuuliza mamae baada ya kusikia maneno hayo ya mwisho. Ni mara nyingi sana anakuwa mtulivu pindi asikiapo mamae akiongea chochote. Alipenda sana kumsikiliza maana alijua kinywa cha mtu mzima ni dawa.
“Nasema hivyo nikiwa na maana kubwa sana binti yangu. Tumeumbwa na nafsi zenye kubadilika. Kubadili maamuzi ambayo wakati huu tunayaona ni ya muhimu na kuyaweka katika hali nyengine baadae. Na huko kubadilika kwa nafsi kunatokana na tamaa za moyo. Binti yangu, binti yangu usikubali kuendeshwa na tamaa za moyo wako maana itafikia wakati utaijutia tamaa yako. Nijuavyo nafsi imeumbwa kupenda moja kwa moja huku moyo ukiumbwa na viwili. Ikiwa ni kupenda na kutamani. Tamaa ya moyo inaweza ikakuweka matatizoni. Unachotakiwa ni kuipinga kabla hujapatwa na Jereha la Moyo. Binti yangu, tuliza moyo wako na ukubali mapungufu yenu. Dhaifu la mwenzako usilifanye kuwa ndio kigezo cha kumuadhibu kwa maumivu ikiwa yeye dhaifu lako analitumia kama kigezo cha kukuongoza panapostahili.”
“Lakini mama mi bado sijakuelewa nini unanimaanishia japokuwa nimekuwa mlevi wa maneno yako mama yangu. Lakini ya leo, mmh! naona yamezidi sana maana na mafumbo. Embu jaribu kupunguza mafumbo ili niielewe maana yako” Cecy aliyanena hayo akimtazama mamae usoni. Anita alitabasamu kisha akafumbua kinywa chake tayari kuendelea na nasaha yake.
“Hutonielewa kwa sasa binti yangu, maana hata mie nilipoelezewa na mama yangu kipindi kile ningali binti kigoli kama uwavyo wewe kipindi hiki sikumuelewa. Na hata nilipohoji zaidi hakutaka kunifafanulia zaidi alinimbia nitaelewa nikikuwa. Na hata mimi sipaswi kukujulisha maana ya maneno haya. Unachotakiwa ni wewe kuyapa nafasi kwenye bongo lako na kuyafikiria kwakina ili upate maana. Wewe bado ni binti mdogo sana na huo umri ulionao sasa ni pevu ambao unapitia changamoto nyingi. Kwaakili ulizonazo sasa usikubali kuongozwa na tamaa za moyo. Ramah anakupenda na wewe mpende kwa hali yoyote atakayokuwa nayo. Binti yangu, wahenga walisema. Usiache mbachao kwa msala upitao.” Anita alimaliza nasaha yake hivyo kisha akamtaka Cecy aweke chakula wale.
“Nimekuelewa Mama yangu” Cecy aliongea hivyo na kujiinua pale kitandani. Akakifuata chakula ambacho alikuwa tayari amekiweka kwenye sahani na kukifunika wakati mama yake alipomtaka asogee karibu yake. Alikianda na kuanza kula taratibu huku wakiongea hili na lile. Kilikuwa ni viazi mbatata ambavyo vimeungwa utamu kiasi ambacho harufu yake tu ilithibitisha hilo.
Walikula kiasi tu kisha hapo wakaacha chakula kile kikiwa bado ni kingi. Wakakiweka vizuri kwenye bakuli. Anita alimtaka bintie watoke nje wakapunge upepo na kubadili hewa, maana ndani humo kulitawaliwa na harufu ya madawa tu. Cecy alimsaidia mamae kushuka kwenye kitanda, kisha wakaanza kutembea taratibu kutoka nje. Walitafuta sehemu nzuri na kukaa.
* * * *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majira ya saa kumi na moja jioni. Mama Jeni, Mama Ramah, Ramah na Jay walikuwa wakitoka nje ya hospitali aliyolazwa Anita au Mama Cecy. Majira hayo walikuwa wakitoka ndani ya hospitali hiyo kumjulia hali Anita. Na muda huo walikuwa wakitoka kwenda majumbani kwao.
“Sasa dogo inabidi turuke time hii kule juu kabla jamaa haja ghairisha, au vipi?” Jay alimuambia Ramah hayo huku akiwa anaikokota pikipiki yake kuitafutia sehemu nzuri kabla ya kuipanda.
“Kwani jamaa alitaka muda gani? Maana muda huu nataka niruke home mara mo....”
“We vipi wewe? Kila mara unataka kuwa home tu? Acha hizo bwana, twenzetu saa hii. Kwanza mida flani ya saa moja kuna sehemu nataka niende. Sasa ukileta habari za kuchelewa hapa min'takuacha” Jay alikoroma. Ramah akawa mpole na kundandia pikipiki. Safari ya kwenda huko wanapobishaniana muda wa kwenda ikaanza.
Dakika kadhaa wakawa wamefika Bahari Breeze. Wakapaki pikipiki yao sehemu maalumu na kuzama ndani ya baa hiyo iliyoko kandokando ya Bahari ya Hindi. Huko walikuta watu wengi wamekaa kwenye viti kuzizunguka meza zilizokuwa mbali mbali. Jay akatoa simu yake na kuiminya minya kisha akaiweka sikioni huku akiangaza huku na huko eneo hilo.neo hilo.
Simu ikapokelewa kisha akaomba uelekeo wa huyo aliyokuwa akiongea nae. Akaelekezwa. Akakata simu na kumtaka Ramah amfuate. Kwenye meza iliyojitenga mbali kidogo. Palikuwa na mabwana wawili wakiwa wamekaa kwa kuangaliana. Jay na Ramah walipofika pale. Wakatoa salamu ya kugongesha mikono huku Jay akiwachangamkia sana mabwana wale na bilashaka alikuwa akiwafahamu kabla.
“Dogo naona umemleta na pacha wako” Jamaa mmoja kati ya wale wawili aliyasema hayo. Jay akacheka na kumjibu kuwa kizuri kula na ndugu yako. Majamaa wale wakacheka kisha wakawakaribisha Jay na Ramah wajiunge kwenye ile meza yao. ‘Chap chap’ wakakaa na muhudumu akafika pale na wao wakaagiza soda tu huku majamaa wale wakiwaambia waagize vilevi. Lakini vijana wale walikataa huku wakidai kuwa hawatumii vitu hivyo.
“Hawa bado watoto wa Mama, wakikuwa watatumia tu” Jamaa mwengine aliyaongea hayo. Sasa hapo ikawa mada ni kuhusiana na vilevi. Jamaa wakaongea, na kina Jay wakajibu huku wakicheka. Dakika kadhaa mbele wakaingia kwenye mada iliyowaleta hapo.
“Sasa madogo, mzigo unatakiwa upelekwe Maramba. Je mtaweza?” Jamaa yule wakwanza kuongea, aliwaambia.
“Braza Kaso, nadhani mwenyewe unanijua. Hakuna haja ya kujieleza sana” Jay aliongea. Akainua glasi iliyokuwa na kinywaji na kuipiga pafu dogo. Akaishusha na kumtazama yule jamaa aliemuita kwa jina la Kaso.
“Dogo Jay nakuaminia sana. Hofu yetu ni kwa huyu mwanao maana ndio kwanza unamleta kwetu na sina shaka kwamba hii ndio kazi yake ya kwanza. Nadhani nilishakuambia sana kuhusu bosi wetu alivyo. Anatabu sana. Dah! Halafu nikijana mdogo makamo yenu tu lakini haoni haya kutuzingua wakubwa zake. Ila tutafanyaje, si tunataka pesa bwana” Kaso aliongea.
“Wakubwa hata msiwaze, hii ishu inapigika kwa uangalifu sana. Kila kitu kitaenda safi tu” Jay aliongea.
“Ok. Saa ngapi nyie mtaruka huko? Ila mi nashauri mtembee usiku maana hakuna wadudu wa taa wengi” Kaso aliongea.
“Usiku tukikutana na wazee njiani lazima watie shaka. Ila kweupe hata kama tukitinga mabegi yetu mgongoni halafu tukitembea mdogo mdogo hakuna atakaetia shaka” Jay nae alito shauri lake.
“Aaaa! Ni nyie tu bora mzigo wetu ufike panapostahili... Kwahiyo hapa si kesho ndio mnaenda au vipi?” Kaso aliwauliza na wao wakajibu ndio. Muda ukapangwa kuwa ni saa mbili asubuhi na walichagua muda huo kwasababu watakuwa tayari wameshatoka hospitalini kumjulia hali Mama Cecy.
“Mzigo mtaufuata kule maskani. Jay wewe unapajua. Mtakuja kule na kuuchukua. Mtaupeleka na mkirudi ndio tutawapatia pesa zenu” Baada ya mazungumzo kuisha. Jay na Ramah wakaaga na kuondoka zao.
Majira ya saa tatu na nusu usiku. Walikuwa wapo sebuleni wakipata chakula cha usiku kabla ya kwenda kulala. Walikula mpaka pale walipotosheka kisha kila mmoja akanawa mikono kwa wakati wake na kutokomea nje ndani ya chumba chao.
“Oya bado mapema sana. Acha mimi nikalambaze-lambaze haya masaa mawili ndipo nitarudi kulala” Jay alimuambia Ramah. Muda huu wakiwa chumbani kwao.
“Lakini mzee si unakumbuka kama kesho tuna safari? Kwanini tusiutumie muda huu kupumzika tujiandae na safari ya kesho?”
“Saa tano ndio muda mzuri wa kuanza kuutafuta usingizi. Najua hata kama nikisema nilale saa hii, wala sitopata usingizi mpaka sita huko. Kwahiyo acha niende tu kwanza” Jay aliyaongea hayo. Ramah aliekuwa akimuangalia muda wote. Alihamisha macho yake kwenye simu na kuendelea na kile kilichokuwa kimemuweka bize. Jay akatoka na kupotelea nje.
Ramah baada ya kuona nduguye ametoka. Akainuka pale kitandani na kuliendea gitaa lake lililokuwa limeegemea ukuta karibu na mlangoni. Akalichukua na kurudi nalo kitandani. Akaliweka sawa na kuanza kucharaza nyuzi taratibu huku akiiamba nyimbo za hisia.
Mwanzo alikuwa akiimba huku akiliangalia gitaa lake. Lakini sasa alikuwa akiimba huku amefumba macho. Gitaa lilitoa sauti nzuri iliyochagizwa na mashairi matamu kutoka kinywani mwa Ramah. Hakuwa akiimba nyimbo ya mapenzi wala siasa. Bali mashairi hayo yaliegemea sana kwenye maisha ya mapenzi. Mlio wa simu yake ulimgutusha na kuacha kile alichokuwa akikifanya. Akaitazama simu yake na kumaizi kuwa kipenzi cha moyo wake amem-beep.
Tabasamu lilichanua usoni mwake. Akaweka gitaa lake pembeni na kuichukua simu yake. Hapo hapo ukaingia ujumbe kutoka kwa Cecy alietaka kupigiwa. Ramah akampigia!. Wakazungumza hili na lile, hiki na kile. Ramah akamuuliza hali ya mgonjwa inaeendeleaje kwa wakati huo. Cecy akajibu kuwa matumaini yapo ni kumuomba Mungu tu amponye zaidi.
Waliyaongea ya kuongea na mwisho wakaagana. Ramah akarudisha gitaa pale ukutani alipolichukua na kuliendea redio kubwa. Akawasha na muziki ukapiga kwenye spika za redio hiyo. Akapunguza nguo mwilini mwake na kujilaza kitandani. Hakuwa na wasiwasi wa kupitiwa na usingizi akiiacha redio ile ikizungumza pekeake. Alijua pindi Jay atakaporudi, ataizima tu.
Dakika kumi mbele. Jay alirudi. Ramah ambae bado hakuwa amelala, alimuuliza ni vipi amerudi muda huo ilhali alisema angerudi saa tano? Jay akajibu kuwa kuna mtu ametaka wawasiliane muda huo, kwahiyo ameamua arudi nyumbani ili kuepusha usumbufu wa kijiweni kwao. Ramah akavuta shuka na kugeukia upande wake.
Majira ya saa kumi na mbili asubuhi. Jay alidamka kitandani. Muayo mrefu ukamtoka kinywani. Akajinyoosha kisha akamtazama Ramah aliekuwa bado amelala wakati huo. Akamuamsha kwa kumtingisha na Ramah akaamka. Jay aliivuta simu yake na kupiga namba fulani. Majibu yakaja kuwa mmliki wa namba hiyo hakuwa akipatikana. Atakuwa bado amelala huyu. Akajiwazia. Akaiweka simu pembeni na kushuka kitandani.
Walijiandaa haraka na walipomaliza wakapanda pikipiki safari ya kuwahi hospitali ikaanza. Walipofika hospitali moja kwa moja hadi katika chumba alicholazwa mama Cecy. Wakamsabahi na kumjulia hali. Aliwajibu kuwa hali yake dhahiri anaona imetengemaa. Kinachosubiriwa ni ruhusa ya Daktari tu iliwaondoke.
Muda kidogo Jenifa alifika hapo akiwa na chakula cha mgonjwa na muuguzi wake. Jay na Ramah waliaga kwa kusema kuwa muda huo kuna pahali wanaenda na endapo itatoka ruhusu, basi Cecy awajulishe kwa njia ya simu. Wakaaga na kuondoka. Wakiwa nje hospotali, Jay alimuuliza Ramah kwamba muda huo ungefaa wao kuenda hiyo safari? Ramah akajibu kuwa muda wa miadi ilikuwa ni saa mbili, sasa ni vipi wao waende muda huo. Wakakubaliana warudi nyumbani kwao kwanza wakavute muda ndipo waende huko walipotaka kuenda. Wakadanda pikipiki kurudi nyumbani.
Dakika kadhaa wakawa wamefika. Walimkuta mama yao akiandaa chai jikoni. Akaacha kile alichokuwa akikifanya na kuwauliza hali ya mama Cecy. Ramah alimjibu kuwa hali yake kwa siku hiyo ipo vyema na wanachosubiria kwa muda huo ni ruhusa tu kutoka kwa Dokta. Baada ya kutoa majibu hayo. Ramah nae aliingia chumbani kwao.
Jay alijaribu kuipiga ile namba ambayo mara ya kwanza aliletewa majibu kuwa haipatikani. Lakini sasa ilikuwa ikipatikana lakini haikuwa ikipokelewa. Alipiga karibia mara tatu lakini hakuna majibu yoyote zaidi ya kuita tu. Akaiweka simu pembeni na kujilaza kitandani. Muda kidogo mama yao aliwaita kwaajili ya kupata staftah. Walitoka kwenda kuungana nae.
Baada ya kumaliza kupata staftah iliyoandaliwa na mama yao asubuhi hiyo. Waliingia chumbani kwao kwaajili ya kujiandaa na safari ya kwenda Maramba. Jay alichukua tena simu yake na kuipiga ile namba lakini ikawa kama mwanzo. Haikupokelewa!. Akaachana nayo na kupiga namba nyengine. Hii muda huo huo ilipokelewa. Wakasalimiana na huyo mtu kisha Jay akamueleza shida yake. Alikuwa na shida ya pikipiki na amempigia huyo kwaajili ya kumjuza hilo.
“Usijali Jay. Kwanza leo sitoki popote njooni tu mje kuichukua najua sitokosa chochote kitu” Mtu huyo alijibu hivyo na Jay akakata simu.
Mara hii akajaribu kuipiga tena ile namba ya mwanzo ambayo haikuwa ikipokelewa. Hata sasa ikawa kama mwanzo. Akajaribu kupiga tena lakini haikupokelewa. Akang'aka kwa ghadhabu huku akiitazama simu yake utafikiri ilikuwa ikimfanyia makusudi kutopokelewa na huyo aliekuwa akimpigia. Ramah aliangua kicheko cha haja huku akijilaza kitandani. Jay akaacha kutazama simu yake na kumtazama yeye.
“Usifosi kama hutakiwi hahahahah!” Ramah aliyaongea hayo na kuchukua simu yake. Akawa anaiminya minya. Jay alimtazama kwa muda na kuachana nae.
“Watu hamna bahati lakini bado mnalazimisha tu” Ramah aliongea tena. Jay aliyapuuza maneno hayo na kuipiga tena ile namba. Safari hii hakutaka kuweka sauti kubwa akihofia Ramah anaweza akasikia simu ikiita tu pasi na kupokelewa. Lakini ikawa ni vile vile tu. Simu haikupokelewa!. Kicheko chengine kikamtoka Ramah mara hii macho yake yakawa yanatoa machozi kwa kucheka sana.
“Kwani si uache tu, lazima za nini? Haya muandikie barua kwamba umekasirika kwa kutopekea simu yako. Watu tangu jana usiku maongezi yenu yalikuwa ni kufosiana tu hasa hasa wewe jamaa yangu. Achana nae baba tafuta mwengine hata kama unagundu” Ramah aliyanena hayo huku akiwa bado anacheka.
Jay alimtazama huku akiwa anatabasamu. Lakini halikuwa tabasamu la furaha kwamba amefurahishwa na maneno ya Ramah. Dhahiri alikuwa amechukizwa na maneno hayo. Chuki ambayo ilichagizwa kwa kutopokelewa simu yake. Alizuga kuwa hakubabaishwa na maneno ya kejeli kutoka kwa Ramah kwa kutabasamu. Lakini ikawa kama vile Ramah alijua kuwa nduguye amechukia lakini aliificha chuki yake chini ya mwamvuli wa tabasamu. Akaendelea kukejeli!.
Baada ya maneno ya kejeli na vicheko vya dhihaka kutoka kwa Ramah kuzidi kumchonyota mtimani mwake. Akashindwa kuvumilia na kumpa onyo kuwa akiendelea na hicho alichokuwa akikifanya anaweza kumfanya kitu chochote. Ramah akamtazama kwa mshangao kisha akaachia kicheko chengine kikali zaidi akichagiza na maneno mengine ya kejeli yenye kuudhi.
Jay alitoka kwa gadhabu na kwenda kumnyanyua Ramah pale kitandani kwa kumkwida fulana yake kwenye kifua na kwenda kumning'iniza ukutani huku akimtolea maneno ya gadhabu.
“Haaa! Jamaa ishakuwa ni vita tayari?” Ramah alimuuliza na mara hii hakuwa akifanya utani tena baada ya kujua amepitiliza kiwango cha matani. Walikurupushwa na sauti ya mlango wao na wote wakageukia upande mlango ulipo. Wakamkuta mama yao amesimama akiwa na hasira za waziwazi.
“Endeleeni. Si vidume nyie mmekuwa tayari mnataka kupimishana ubavu. Piganeni sasa” Mama yao aliwaambia huku akiwa anawaangalia kwa hasira. Walitahayari si mas'hara!. Jay akamuachia Ramah na kujirudisha nyuma hadi kitandani. Akakaa, akamuangalia mama yake kwa jicho pembe na akafanya hivyo kwa Ramah pia. Akarudisha macho yake na kutazama chini.
“Yaone vile yalivyo tahayari! Mitoto mikubwa lakini kama vitoto vidogo. Kila mawio lazima muanzishe vurumai. Mnatupigia siyahi zisizo na maana. Mbona hamuendi kufanya rabsha zenu huko mitaani mkaonekana mabondia mpewe heko na wenzenu. Acheni ujuha wenu mmekuwa nyie, mnatakiwa muangalie ni jinsi gani mtasaidiana na sio kuzozana hadi mkafikia kushikana matai kama walevi wa gongo kilabuni” Mama yao aliongea kwa hasira kiasi ambacho wote walikuwa kimya kila mmoja ameinamisha macho chini akiona haya hata kumtazama mama yao usoni.
“Na wewe ni kipi kilichokufanya ukamning'iniza mwenzio ukutani?” Alimgeukia Jay. “We si ndo mwanzilishi wa mzozano kila siku? Haya iweje leo ujifanye una hasira kumshinda mtetea aliechukuliwa kitoto chake na mwewe hadi ukataka kumtengua mwenzako shingo?” Jay kimyaa!. “Lione vile lilivyo tahayari. Minywele mibaya kama mateja wa kumi na tano” Akamalizia na msonyo na kutokomea zake nje.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakatazamana watoto wale. Kicheko kikafuata kwa wote wawili. Kisha hapo Ramah akaendelea na kejeli zake. Mara hii hazikuwa kama zile za mwanzo za kutopokelewa kwa simu ya Jay. Mara hii zilikuwa juu ya kutahayari kwa Jay kwa maneno ya mama yao. Jay akamtazama kwa uso wa hasira. Kisha akaachia kicheko na kuinuka pale kitandani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment