Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

JERAHA LA MOYO - 2

 








Simulizi : Jeraha La Moyo

Sehemu Ya Pili (2)







Ramah akajitoa pale ukutani na kumfuata Jay, akamsukuma na kuangukia kitandani huku akiwa na mshangao kwa kitendo hicho. Ramah akafika hadi pale mlangoni na kuweka pozi kama lile aliloliweka mama yake kipindi anawagombeza. Jay akamtazama kwa muda asielewe nduguye anataka kufanya nini. Ramah pale pale akanza kumuiga mama yake vile alivyokuwa akiongea hasa hasa pale alipokuwa akimkaripia Jay. Akaongeza na maneno mengine ya utani na kicheko kikali kikamtoka Jay huku akijilaza kitandani. Ramah nae akacheka!. Wote wakawa wanacheka!.



“Acha ujuha ndugu yangu. Embu tufanye haraka, tushachelewa saa hizi” Jay aliyaongea hayo huku akijiinua pale kitandani, kipindi hiki alikuwa ameacha kucheka.



“Sasa chombo nyengine tunaipata kwa nani?” Ramah alimuuliza na muda huu na yeye alikuwa hana mzaha tena.



“Nimeshaongea na Kidamu tayari. Ameniambia tuipitie home kwao. Oya tufanye chap mwanangu ili tuwahi kurudi. Leo nataka nijue kwanini huyu mtoto wa kike kanifanyia kusudi hizi asubuhi”



“Tatizo jamaa unafosi sana. Sema nikutafutie wa kuruka nae” Ramah aliongea. Jay akamtazama huku uso wake ukionyeasha kukasirishwa na maneno hayo. Ramah akatoka nje haraka huku akicheka.



Jay akatoka nje na kupanda pikipiki. Ramah nae akapanda nyuma. Sauti ya mama yao ikawagutusha na kufanya shingo zao zigeukie kule ambapo imesikika. Kwa haraka tu walijua kuwa mama yao alikuwa akitoka kwenda sokoni kutokana na kapu kubwa aliloshika mkononi. Wakamtazama kujua anataka kuwaambia nini.



“Mara hii mshakuwa marafiki?” Aliwauliza kwa dhihaka. Wakatabasamu lakini hawakuacha kumtazama. “Haya mnaenda wapi tena asubuhi yote hii? Mi nikajua basi nitapata lifti mpaka gulioni”



Jay aliposikia maneno hayo, alishuka kwenye pikipiki na kumfuata mama yake hadi pale mlangoni aliposimama. Akampatia noti ya shilingi Elfu Tano akimuambia kuwa wao kuna pahali muda huo wanawahi. Mama yao akawashukuru na Jay akarudi na kupanda tena pikipiki. Akaiwasha kisha wakaondoka huku mama yao akifunga mlango wake vizuri tayari na yeye kutoka.



Muda huu kila mmoja alikuwa juu ya pikipiki yake wakiwa maeneo ya Mabanda ya papa. Wakauzunguka mzunguko wa eneo hilo na kushika barabara ya ishirini. Wakaivuka bustani ya Madina na kuingia ndani kidogo mtaa wa Yebo yebo. Wakapaki pikipiki zao nje ya nyumba moja kubwa iliyokuwa eneo hilo. Kisha wakaingia kwenye nyumba hiyo. Walipokelewa na mlinzi wa nyumba hiyo na kuwaelekeza mahali alipo waliomfuata.



Hatua za miguu ziliwachukua mpaka nyuma ya nyumba hiyo ambapo kulikuwa na bustani nzuri. Kwenye bustani hiyo, kulikuwa na eneo la kupumzikia. Na eneo hilo kulikuwa na mtu ambae alikuwa amekaa huku mguu mmoja akiwa ameukunja nne na mbele yake kukiwa na shurubati ya ukwaju juu ya meza. Alipowaona vijana hao aliachia tabasamu la kuwakaribisha. Alikuwa Kaso mtu ambae siku iliyopita walionana kule Bahari Breeze na kuahidiana kukutana siku hiyo hapo.



Kwakuwa kiti kilikuwa ni kimoja tu. Jay na Ramah walisimama baada ya kupeana salamu na mtu huyo. Kabla hawaja ongea chochote. Simu ya Kaso ikaita. Akaitazama pale juu ya meza na kuachia tabasamu. Kisha akaipokea. Wakaongea kwa dakika tatu na huyo aliempigia kisha simu ikakatwa. Akawageukiwa wakina Jay.



“Maninja mbona mmechelewa wakati mliahidi saa mbili?” Kaso aliwauliza. Jay akaangalia saa yake ya mkononi na kukuta ni saa tatu na robo.



“Hata hivyo hatujachelewa sana” Jay alijibu. Kaso hakuongea kitu. Akainuka na kupotelea ndani ya nyumba hiyo. Baada ya dakika nne, alirudi hapo akiwa na mabegi ya mgongoni mawili. Akayaweka juu ya meza na kuwatazama vijana wale kwa zamu.



“Mzigo huu hapa. Unatakiwa ufike Maramba kabla ya jua halija kuchwa. Nitawapatia Shilingi Laki moja, kila mmoja atachukua nusu ya pesa hiyo. Hiyo ni kwaajili ya tatizo lolote dogo endapo mtalipata mkiwa safarini. Malipo yaliyobakia ni baada ya kurudi huku. Mzigo unapopelekwa Jay anapafahamu. Jay unajua masharti yetu. Hakuna ruhusa ya kufungua hayo mabegi mpaka mtakapo yakabidhi sehemu husika. Vinginevyo, mizigo ya watu ifike” Kaso aliwaambia hivyo. Kisha akawapatia kiasi hicho cha pesa alichowatajia. Akamalizia kwa kuwaambia kuwa. Endapo pakiwa na tatizo lolote, wasisite kumjulisha. Akawakabidhi mabegi na kuwaruhusu waende.



Safari ikaanzia hapo. Mwendo waliokuwa wakienda haukuwa mkubwa sana wala mdogo. Kuna pahali walienda mwendo mkubwa yote ikiwa ni kutaka kuwahi. Na kuna sehemu walikuwa wakienda mwendo wa kawaida. Tena walikuwa wakipiga stori. Mizigo yao mgongoni pasi na kujua wamebeba nini kwenye mabegi. Hata hivyo hawakutaka wala hawakuwa na mpango wa kujua hilo.



Pamoja na kwamba safari ilikuwa ni ndefu kiasi. Hawakutaka kusimama sehemu. Walikuwa wamejizatiti si kidogo. Makoti magumu waliyavaa kwaajili ya kuzuia upepo mkali upigao kifuani. Huku kichwani wakivaa kofia za usalama zenye vioo vya kuzuia vidudu na vitaka visiingie machoni. Safari bado ni ndefu. Mwendo mdogo. Saa ngapi watafika? Kasi ikaongezwa kila mmoja na uhodari wake wa kucheza na vyombo hivyo. Hapakuwa na maneno wala maongezi. Kila mmoja kimya akicheza na usukani.



Walichukua takribani saa moja na nusu tangu waianze safari. Sasa walikuwa Maramba mjini wakielekea huko wanapotakiwa waende. Kona hii, kona ile. Chochoro hii chochoro ile. Wakatokeza kwenye mtaa mmoja. Mtaa ambao ulionekana kuchangamka sana.



Kwenye baa moja iliyokuwapo eneo hilo ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuuchangamsha mtaa huo. Nje ya baa hiyo kulikuwa na gari moja la kisasa limepaki. Jay na Ramah walipaki pikipiki zao umbali mfupi na ilipo ile baa. Wakashuka na kuiendea ile baa wakiwa na mabegi yao mgongoni. Ile gari ambayo imepakiwa nje ya baa. Kioo kilishushwa na ikitokeza sura iliyowaashiria waifuate kama sio kuingia kabisa ndani ya gari ile. Kama ishara ya yule bwana ilivyowataka. Nao wakazama ndani ya gari.



Muda huo huo wakatoka wakiwa hawana mabegi. Wakawa wamesimama nje ya gari hilo huku wakiangalia huku na huko kuhakikisha usalama. Baada ya dakika tatu. Walipenyezewa mabegi yao na gari ile ikaanza kuondoka mdogo mdogo huku nao wakiondoka eneo hilo kuzifuata pikipiki zao. Wakazipanda na safari ya kurudi Tanga mjini ikaanza.



Saa saba kasoro wakawa wameingia mjini. Moja kwa moja walienda barabara ya kumi na tisa mtaa wa Yebo yebo kwenye ile nyumba ambayo mwanzo waliianzia safari hapo. Wakazama na mlinzi akawaelekeza kuwa wafikie sebuleni. Hatua kwa hatua hadi ndani ya nyumba hiyo. Sebuleni wakamkuta Kaso akiwa amekaa na yule jamaa mwengine ambae siku iliyopita walikuwa wote Bahari Breeze.



“Maninja mmerudi salama. Taarifa nimeshazipata kabla ya nyie kufika hapa. Sasa kilichobakia hapa si kuwapatia mtonyo wenu au sio?” Kaso aliongea na mwisho aliwauliza. Wakaitikia ndio. Akawaambia wasubiri na yeye akazama ndani. Dakika kadhaa akatoka mkononi akiwa ameshika fedha za noti za Shilingi Elfu Kumi kumi. Akazihesabu mbele ya macho ya zikatoka Shilingi Laki Moja. Akampatia Jay zile pesa.



“Nadhani tumeshamalizana kwa wema kabisa. Pesa hizo mkiongeza na zile nilizo wapatia mwanzo. Malipo yenu yanakuwa yamekamilika. Mnaweza kwenda” Jay na Ramah wakashukuru na kugeuka kuanza kuondoka ndani humo. Walipofika mlangoni. Wakashtuliwa na sauti ya Kaso.



“Dili jengine likitokea nitakustua Jay” Kaso aliwaambia huku akiwanyooshea dole gumba. Wakaitikia kwa vichwa na kutoka ndani ya nyumba hiyo.



Wakapanda pikipiki zao na kutokomea eneo hilo. Kwanza walirudisha pikipiki ya watu na kumpoza jamaa aliewaazima kwa shilingi kadhaa. Kisha wakapanda pikipiki ya Jay na wakashauriana kuwa muda huo waende nyumbani kwao wakaangalie masuala ya chakula kwanza kabla ya mambo mengine.



Walipofika nyumbani kwao. Mama yao aliwashangaa baada kuona kwenye miili ya wanae kote kumetapakaa vumbi la udongo mwekundu. Akawauliza kwa mashaka na wao wakamtoa hofu. “Au ndio mmeenda kutafuta uwanja kwaajili ya kukondana?” Mama yao aliwauliza na wao wakaangua kicheko. Kwakuwa matumbo yalikuwa yakitoa mlio wa alamu kumaanisha yalihitaji tiba. Wakamlalamikia mama yao njaa. Akawaeleza kuwa chakula kipo mezani na wao bila kusubiri chochote wakaenda kukivamia.



Wakati wanaendelea kula. Simu ya Ramah iliingia ujumbe kutoka kwa Cecy aliemjulisha kuwa muda si mrefu walikuwa wakienda kupewa ruhusa. Akamjibu kuwa ndani ya muda huo atakuwa hapo. Akamjuza Jay taarifa hiyo kisha akasema haendelei tena kula. Anachokifanya kwa muda huo ni kuwahi huko. Jay akamuambia wataelekea wote huko. Chakula kikaachwa na kufunikwa vizuri. Kisha wakaelekea chumbani kwao kubadili nguo bila kuoga ili tu wawahi hospitalini. Walipotoka, Ramah akamjuza mama yake taarifa hiyo na yeye akasema atakwenda kumuona nyumbani kwake hapo baadae.



Majira haya walikuwa ndani ya hospitali ya Makorora. Wakaingia kwenye chumba alicholazwa mama Cecy na kumkuta akiwa amekaa kitandani. Kwa kumuangalia tu. Alitangaza kuwa na siha njema. Afya yake ili tengemaa tofauti na siku zilizopita. Cecy akamjulisha tena kuwa muda si mrefu watapewa ruhusu. Kinachosubiriwa hapo ni Daktari tu ambae alienda kukamilisha mambo fulani.



Muda Daktari aliingia. Akawauliza yuwapi yule mwanamke ambae siku ya kwanza kuletwa Mama Cecy hapo alikuwa kama msimamizi wake. Wakamjibu kuwa kwa muda huo hakuwepo. Mwanamke huyo alikuwa ni Mama Jenifa. Basi akamtaka Jay na Ramah wamfuate ofisini kwake. Vijana wale wakatoka pamoja na Daktari hadi kwenye ofisi ya Daktari.



“Sasa vijana... Mgonjwa wetu tumemtibu vyema tangu mumlete hapa akiwa na hali mbaya mpaka sasa hali yake imetengemaa.” Akaacha kuwaangalia vijana wale na hivi sasa macho yake aliyahamisha juu ya kabrashi moja lililokuwa mikononi mwake. “Pamoja na hayo. Pia kuna malipo ambayo yule Mama aliyafanya mwanzo ikiwa ni kama ‘advance’ ya vitu vidogo vidogo. Sasa hapa inabidi mfanye malipo yote kabla hajaruhisiwa ili muondoke mkiwa hamna deni lolote”



“Tumekuelewa Dokta. Malipo ni kiasi gani?” Jay aliuliza.



“Aamm! Kutokana na huduma zote alizopatiwa tangu anakuja hapa mpaka sasa. Ni kiasi cha Shilingi Elfu Tisini na Nne ikiwa ni pamoja na malipo ya kitanda”



“Sawa Dokta. Malipo hayo yanafanyika wapi?” Ramah aliuliza.



“Nitawapatia karatasi mtaenda pale mapokezi. Mtaikabidhi pale pamoja na kiasi hicho cha fedha nilichowatajia. Kisha hapo mtakuwa huru kuondoka” Dokta aliwaambia na kuwakabidhi karatasi fulani. Wakashukuru na kutoka nje ya ofisi hiyo.



“Sasa Dogo. Shika hizi zitasaidia kwenye malipo” Jay aliongea hivyo huku akimkabidhi Ramah kiasi cha Shilingi Elfu Thelathini na Tano. Ramah akaipokea na kumshukuru nduguye. Kisha akaelekea mapokezi huku Jay akirudi tena kwenye chumba alicholazwa Mama Cecy. Cecy alipoona Jay anarudi pekeake ikabidi amuulize kuhusu Ramah. Jay akamjibu kuwa anakuja hivi punde, ameenda kufanya malipo.



Muda huo huo Ramah alirejea mkononi akiwa na lile faili ambalo mwanzo alikuwa nalo Daktari. Ramah baada ya kwenda kufanya malipo, aliambiwa arudi tena kwa Daktari ndipo akakabidhiwa lile faili. Akawajulisha kuwa ruhusu imeshatoka na wajiandae kabisa kwaajili ya kuondoka. Muda huo huo akaingia tena yule Daktari. Akawajuza kuwa wanaweza kwenda. Akawaaga kisha akaondoka zake.



Cecy na Mamae walichukua kilicho chao na kuanza kuondoka hapo. Nje ya hospitali hiyo. Ramah akaita Tax zilizokuwa zimejipanga karibu na hospitali. Waliingia watatu huku Jay akisema kuna mahali muda huo anaenda. Kwa shukurani za dhati kabisa, Mama Cecy alimshukuru Jay kwa msaada wake alioutoa kuanzia mwanzo mpaka hapo walipofikia. Jay akazipokea shukurani hizo kwa moyo mkunjufu na kuondoka hapo. Tax waliyoipanda ikaanza safari kufuata maelekezo ya wateja wake.







Dakika kumi na tano mbele. Wakawa wamefika katika mtaa anaoishi Mama Cecy, mtaa wa Mikanjuni. Wakashuka kwenye Tax na Ramah akafanya malipo kisha akaingia ndani ya nyumba hiyo. Majira hayo ikiwa ni saa kumi za jioni. Nyumba yao ikawapokea baada ya kuwakosa kwa siku mbili. Sebule nayo ikawakarimu kwa dhati kama walivyoiacha. Wakajibweteka kwenye masofa yaliyokua sehemu hiyo.



Wakawa wakipiga soga zisizo na maana sana hasa hasa walikuwa wakiongelea kuhusu hospitali ile waliyotoka. Katikati ya soga, Mama Cecy akataka kujuzwa ni kiasi gani wametumia kule hospitali kwa huduma alizopatiwa. Ramah akamjuza huku akimkabidhi lile faili. Mama Cecy alilipokea na kulipitishia macho. Kisha hapo akamshukuru sana Ramah kwa msaada aliuotoa.



Akataka hata kupiga magoti huku akilia kudhihirisha shukurani zake kwa kijana huyo. Ramah alimuwahi na kumkalisha kwenye sofa. Mama Cecy aliendelea kulia akiwa bado hajui amshukuru vipi kijana huyo. Cecy nae chozi lilimtoka baada ya kufikiria msaada alioutoa Ramah kwa mama yake.



“Mama usijali. Sijafanya hivi eti kwa vile namjua Cecy au nakujua wewe. Bali nimefanya kama jukumu langu kutoa msaada kwa yoyote anaehitaji msaada ilhali uwezo wa kumsaidia ninao.” Ramah aliyanena hayo huku akimtuliza Mama Cecy pale kwenye sofa.



“Asante sana baba. Asante mwanangu. Nashkuru sana na Mungu akuongoze kwenye mambo yako” Mama Cecy aliongea hivyo huku akifuta machozi.



Ramah akarudi sehemu alipokaa mwanzo na kutulia. Muda huo huo Mama Jenifa na Jenifa waliingia ndani humo. Mama Cecy alipowaona akawapatia shukurani zao kwa waliyomfanyia muda wote akiwa hospitali. Maana familia hiyo ndio ilijitwisha jukumu la kumpelekea chakula kila mara. Wakazipokea shukurani hizo bila kinyongo.



Mama Jay na Jay nao wakaingia ndani hapo. Mama Cecy hakuweza kuvumilia tena. Akaangua kilio huku akitoa shukurani zake kwa watu hao waliokuwapo ndani hapo kwa msaada waliotoa juu yake. Wanawake wale wawili watu wazima, wakachukua jukumu la kum'bembeleza mwanamke mwenzao mpaka pale aliponyamaza. Hali ya utulivu ikapatikana na soga zikaanza upya.



Wakamuuliza kuhusu hali yake nae akajibu kuwa anajiskia nafuu japo kichwa kinagonga kwa mbali. Hata hivyo hakuwa akisikia maumivu sana kama siku zilizopita. Wakampa pole na kuendelea na soga nyengine mpaka pale walipoaga. Ramah alimuomba Cecy amsindikize na Cecy akafanya hivyo. Wakiwa mbali kidogo na nyumba hiyo. Ramah alimpatia Cecy Shilingi Elfu Ishirini. Mwanzo Cecy alizikataa akidai msaada alioutoa unatosha sana. Ila baada ya Ramah kumlazimisha sana hakuwa na budi kukubali. Wakaagana na Cecy akarudi kwao huku Ramah akipotelea mitaani baada ya kuchwa na Jay ambae aliondoka na mama yao.



* * * *



Si kila leo itafanana na jana ama juzi. Kila iingiapo siku mpya hata matukio yanabadilika na kuwa tofauati na ya siku iliyopota. Japo saa, dakika na sekunde huwa ni zile zile. Wazee waliopata kuishi miongo mingi iliyopita walikuwa na maneno yao ambayo mpaka sasa tunaishi nayo. Mmoja wapo ukiwa ni ule unaosema, tenda wema nenda zako.



Siku zilibadilika, ikiwa ikitoka hii huja nyengine. Na hata nyengine huisha pia huja inayofuata huku majira ya mwaka yakizidi kubadilika nayo. Yote hii ni Muumba kuonyesha utukufu wake kwa viumbe wake kuwa hakuna kimshindacho ikiwa vyote ameviumba yeye mwenyewe.



Mwaka huo ukaisha na kufuata mwengine. Siku zote hizo hali ya Mama Cecy ilikuwa vyema kabisa baada ya kuzingatia masharti ya dawa aliyopewa Hospitalini. Siku zote hakuusahau wema aliotendewa na vijana wale wawili hasa hasa Ramah ambae sasa amekubali kwa moyo mmoja awe mkwe wake kwa mwanae kutokana na kumsoma tabia na kuona akiwa na tabia njema zilizompendezea.



Miezi ilisogea mbele kidogo tangu mwaka mpya uingie. Matokeo ya kidato cha nne yalitoka. Wahitimu wa kidato cha nne mwaka uliopita. Walikuwa na kiroho cha kuona kile walichokipanda miaka minne iliyopita kimeota nini? Hata Cecy na Jeni walikuwa kwenye mkumbo huo.



Kukuruka za hapa na pale waliweza kuyaona matokeo yao. Mioyo yao iliingiwa na ubaridi wa furaha baada ya kugundua kuwa wamefanikiwa kupita. Mioyo yao ilifurahika si mas'hara kiasi ambacho machozi yaliwatoka kwenye mboni zao kudhihirisha furaha yao.



Bila kupoteza muda akiwa bado ana kiroho cha wahka. Akataka kumjulisha Ramah kwa njia ya simu. Akampigia!. Pamoja na kumpigia simu lakini Ramah alimuambia kuwa kwa wakati huo hakuwa kwenye utulivu mzuri. Akamuomba wakutane pahali amjuze vyema hicho anachotaka kumjuza. Akamuuliza ni wapi watakutana. Ramah akamjibu kuwa asubiri kidogo atamjulisha. Cecy akakata simu. Kisha wakaanza kujitoa sehemu hiyo kurudi kule makazi yao yalipo.



Majira haya Cecy alikuwa pekeake baada ya Jenifa kuelekea kwao. Utulivu wa nyumbani kwao ulimshangaza sana. Tangu wahamie kwenye nyumba hiyo, hakuwahi kuona utulivu wa namna hiyo. Akapiga hatu za taratibu huku akiwa na wasiwasi kiasi. Akaufikia mlango wao mkubwa wa kuingia ndani. Akajaribu kuusukama na kukuta ukiwa umefungwa. Inamaana Mama hayupo? Alijiuliza.



Ile furaha aliyotoka nayo huko akitaka kumjulisha mamae kuwa amefaulu. Ilianza kupungua taratibu nafsini mwake. Hakuweza kuelewa atakuwa wapi kwa wakati huo ilhali alimuacha hapo kama nusu saa iliyopita na hakuwa na ratiba zozote za kutoka alizomuambia.



Kwakuwa na yeye alikuwa na funguo yake. Akafungua mlango na kuingia ndani. Huko alianza kumtafuta kila mahali huku akimuita akisahau kabisa kuwa yeye ndie aliefungua mlango huo na hakukuwa na dalili zozote kwa kuwapo kwa mama yake mahala hapo. Akaachana na zoezi la kuita na kujaribu kumpigia simu. Hata simu yake pia haikuwa ikipatikana. Akajipa imani ya kwamba atakuwa mahali na atarudi muda wowote.



Akaingia chumbani kwake na kufunga mlango wake. Moja kwa moja akaenda kujilaza kitandani kwake akifikiria maisha mapya atakayoenda kuyanza hivi karibu ya kidato cha tano. Muda huo hata yale mawazo ya mama yake hakuwa nayo tena. Alikuwa na furaha si kidogo kwa kufaulu vyema kwenye mitihani yake aliyoifanya mwaka uliopita alipokuwa kidato cha nne.



Simu yake iliita. Akaiotoa kwenye mkoba wake na kuiangalia kabla ya kuipokea. Akagundua kuwa Ramah ndie ambae alikuwa akimpigia. Akaunda tabasamu na kuipokea simu hiyo. Kabla hajaongea chochote. Ramah akamuwahi. Akamuambia kuwa majira ya saa moja jioni aende katika mgahawa fulani uliyokuwa maeneo ya barabara ya tisa. Akataka kuhoji kunanini maana sauti ya Ramah alionekana kama mtu mwenye wahka fulani. Bahati mbaya simu ikakatwa kabla hajahoji chochote.



Akajaribu kumpigia ila simu haikuwa ikipataikana tena. Nini hii? Akajiuliza. Akapuuza na kuamua kujilaza kitandani akivuta muda ili aende huko alipotakiwa kuenda. Majira hayo ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro za jioni.



Kwa wakati huo alitawaliwa na mawazo mengi. Hususan yale ya kufaulu. Hakupata nafasi nzuri ya kumfikiria Ramah wala Mamae ambae mpaka muda huo hakujua yuwapi. Mawazo yake yalimpeleka miezi mitatu mbeleni. Alijiona akiwa amevaa sare za shule. Mgongoni ana begi lake lililo na madaftari akiingia kwenye lango la shule atakayo pangiwa.



Tabasamu likaongezeka usoni kwake. Akamshukuru kimya kimya Mungu wake kwa kumpatia bahati ya kufaulu. Ni kweli alipenda sana kusoma, lakini tatizo linakuja. Je mama yake ataweza kumlipa ada ya shule? Alijiuliza. Lakini akikumbuka kuwa Mama yake ndie ambae alimsomesha tangu darasa la nne Baba yake alipofariki mpaka hapo alipomaliza mwaka uliopita kidato cha nne.



Akajipa imani ya kuwa Mama yake lazima afanye lolote ili yeye aendelee na masomo. Akamuombea Mama yake dua ili afanikishe swala la kumsomesha mpaka pale atakapomaliza masomo yake yote na kupata kazi. Mawazo yakampeleka mbali zaidi. Akajiona tayari ameshamaliza chuo na muda huo alikuwa akitoka kazini. Muda huo hawakuwa wakiishi tena kwenye nyumba hiyo. Walikuwa wakiishi nyumba nzuri. Akatabasamu na kujinyanyua pale kitandani baada ya kugundua muda umeenda sana na hapo anatakiwa ajiandae aelekee huko alipotakiwa aende.



Akajiandaa haraka. Pamoja na kuoga na kubadili nguo. Kisha hapo akahamia kwenye kioo na kuanza kujiremba. Si anaenda kuonana na baby wake bwana? Dakika kumi na tano ziliisha hapo. Akamaliza kufanya yote ya kufanywa na sasa akawa tayari kuondoka. Alitegemea akitoka nje anaweza kumkuta mama yake, lakini ikawa ni tofauti.



Nyumba ilikuwa vile vile kimya utafikiri hakukuwa na mtu. Sasa nitaondokaje ilhali mama hayupo? Akajiuliza. Akaguna. Ila akirudi na akikuta mimi sipo atanitafuta tu kwenye simu. Lakini ngoja nifanye kitu. Akawaza hivyo na kurudi tena chumbani kwake. Huko alichukua kalamu na karatasi. Akamuandikia mama yake ujumbe ambao utamtoa hofu pindi akirudi na kukuta yeye hayupo.



Kisha akatoka nao na kwenda kuuweka juu ya meza iliyokuwa pale Sebuleni. Akaiwekea na kijiko juu ili isipeperuke na upepo. Akatoka moyoni mwake akiwa na amani akijua hatomuweka mama yake na kiroho cha hofu. Akatafuta usafiri utakaomfikisha huko anapotaka kuenda. Majira hayo ikiwa ni saa moja kasoro za jioni.



* *



Muda huu alikuwa nje ya mgahawa huo akishuka kwenye usafiri uliomleta hapo. Akafanya malipo na kuanza kupiga hatua kuufuata mgahawa huo. Nje alimuona Ramah akiwa kwenye pozi la kumsubiri yeye. Akatabasamu na kwenda kumkumbatia. Wakaachiana na Ramah akatoa heko zake kwa Cecy kuwa amependeza sana.



Kisha akamuongoza kuingia ndani ya mgahawa huo. Alimpitisha mpaka nyuma ambapo kuna sehemu kama ‘Hall’ ndogo hivi. Lakini Cecy hakujua chochote kutokana na kuwa sehemu hiyo kuwa giza kiasi kwasababu hakukuwa na taa. Ama taa zilikuwapo lakini hazikuwashwa bado.



Cecy akahoji ni wapi wanaelekea maana yeye alidhani wataishia ndani ya mgahawa ule lakini anaona wanazidi kutokomea zaidi. Ramah akamtaka awe mtulivu. Cecy akawa kimya na kufuata vyote alivyombiwa na Ramah.



“Sasa unajua nini mpenzi. Nisubiri hapa nakuja sasa hivi kuna kitu nimesahau hapo nje” Ramaha alimuambia. Cecy akataka kuhoji lakini akatulizwa na busu lililotua juu ya lipsi zake. Akawa kimya kama maji mtungini. Sauti za viatu vya Ramah akiondoka zilisikika. Hakuweza kumuona vyema kutokana na sehemu hiyo kuwa na kiza kiasi.



Hapo ndio akagundua kitu chengine kuwa alikuwamo ndani ya chumba baada ya kusikia sauti la mlango ukifungwa. Hofu ikaanza kutanda moyoni mwake. Ramah amenileta wapi huku? Kufanya nini sasa mbona ameniacha mwenyewe? Akapiga hatua za kuotea kuufuata ule mlango ili walau atoke nje amsubirie huko. Lahaulaa!.



Mlango ulifungwa kwa nje. Ramah anataka kunifanya nini? Cecy alijiuliza kwa hofu. Akatoa simu yake na kuwasha tochi walau apate mwanga utakao mpunguzia hofu kidogo. Mwanga kidogo ukapatikana. Akaangaza huku na huko kwenye chumba hicho ili ajue kunanini chengine zaidi ya yeye. Katika kuangaza huko. Aliona swichi zilizokuwa ukutani. Akahisi kuwa huenda ikawa ndio zakuwashia taa za sehemu hiyo.



Akazifuata ili kujaribu kuwasha kama mawazo yake yalivyomtuma kuwa huenda ikawa ni za taa za hapo. Akaminya na ghafla mwanga ukatawala mahala hapo. Akageuka nyuma na hapo alipigwa na butwaa kiasi ambacho mkoba wake ulidondoka chini baada ya kutoushikilia vyema kwa mshtuko uliompata. Viganja vya mikono yake akavifumbata kinywani mwake huku akitazama mbele yake kwa hofu.



Jukwaa dogo lililokuwa karibu na pale aliposimama, liliwaka taa za rangi rangi huku taa nyengine zikiwaka kwa mtindo wa kuandika maneno. ‘Congratulation Cecilia To Pass You'r Examinations IV’. Yalikuwa yakisomeka hivyo. Akabaki kushangaa asielewe imekuwa kuwa vipi hivyo.







Akatazama umati uliokuwa mbele yake. Haukuwa umati mkubwaa. Walikuwa ni wachache tu. Ikiwa ni Mama yake mzazi, Mama yake na Ramah, Jay, Mama yake na Jenifa, Jenifa mwenyewe na baadhi ya marafiki zake wengine aliosoma nao shule ya upili. Nani kani Suprise hivi? Alijiuliza huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio na asijue kuwa ni hofu ama furaha.



Akiwa bado amesimama haelewi chakufanya. Maana watu wote waliokuwapo hapo walikuwa wakimuangalia huku wakitabasamu. Hakuna ambae aliongea chochote wala kufanya chochote. Mara kidogo mlango ukafunguliwa. Ramah akaingia ndani. Muda wote Cecy alikuwa amesahau kwamba Ramah ndie ambae amemleta hapo. Alipomuona kijana huyo akiingia hapo. Akaenda kumkumbatia bila kujali uwepo wa wakubwa zao waliokuwapo ndani hapo.



Ramah akamtoa kwenye kumbato hilo na kumuongoza mpaka pale juu ya lile jukwaa na kumkalisha kwenye kiti maalumu ambacho kilikuwa pale juu. Akamuokotea mkoba wake aliouangusha pale chini na kumpelekea mama yake Cecy. Kisha akarudi mbele na kusimama kama MC.



Kwanza alianza kuwasalimu kisha dua ikafuata. Hapakuwa na kipaza sauti, alikuwa akiongea ‘kavu kavu’ tu. Kipaza sauti cha nini ilhali hapakuwa na watu wengi mahala hapo? Akamgeukia Cecy na kuanza kumjuza kuwa shuhuli hiyo ni yake. Na imefanywa kwaajili yake. Cecy muda wote alikuwa akitabasamu tu kwa Suprise aliyofanyiwa.



Ipo hivi. Matokeo ya kidato cha nne yalitoka tangu siku iliyopita. Matokeo ambayo Ramah aliyaona kabla ya Cecy kwakuwa Cecy aliwahi kumuambia namba yake ya mtihani aliyofanya nayo. Ramah alifurahi baada ya kumaizi kuwa mpenzi wake amefaulu vyema kwenye mitahani yake. Nini amfanyie ili kudhihirisha furaha yake? Akapanga kum_Suprise kwa namna hiyo.



Akamjuza Jeni jambo hilo. Jeni aliliunga mkono. Ila pia akamuambia amuangalizie na yeye matokeo yake. Ramah akafanya hivyo na baada ya kumtazamia akamjuza kuwa na yeye amefaulu. Kisha Ramah akamjuza na ndugu yake jambo hilo, pia akaliunga mkono. Akawajuza wazazi wa pande zote mbili. Ikiwa ni mama yake na mama yake Cecy. Kisha akawakumbusha kuwa wasimuambie lolote binti huyo maana yeye amepanga iwe ni kumshtukiza.



Jambo la kumjuza mama Jeni alimuachia Jeni mwenyewe huku akimuambia kuwa awajulishe na baadhi ya wanafunzi wenzao waliosoma nao. Mishemishe zikaanza hapo kwa Ramah kutafuta sehemu hiyo. Mambo yote akayakamilisha siku iliyofuata ambayo ni siku hiyo. Kisha pakasubiriwa muda tu ili jambo hilo litendeke.



Kwakuwa jambo hilo lilipangwa lifanyike haraka haraka. Shuhuli ikaanzia hapo. Ramah alimpongeza kwa kufaulu mitihani yake na kumtakia mema kwenye safari yake ya masomo atakayoendelea nayo. Kisha hapo akampisha mama yake na Cecy aje kuongea chochote na yeye. Mama Cecy akainuka pale alipokaa na kwenda mbele. Aliongea machache na alipomaliza alirudi alipokaa.



Zoezi hilo likaendelea kwa wote waliokuwapo humo likiambatana na kutoa zawadi kwa kila anaeenda pale mbele. Lilipoisha. Ikawa ni zamu ya Ramah nae kutoa zawadi yake. Akamgeukia Cecy na kumuambia.



“Cecilia. Ninakupa nafasi ya upendeleo ya kunichagulia zawadi ambayo nitakupa usiku huu. Embu waambie nikupatie zawadi gani ya kwanza kabla sijakupatia ya pili ambayo itakuwa ni Suprise kwako” Cecy alikuwa kwenye tabasamu muda wote. Hakujua ni zawadi gani amuambie Ramah ampatie ambayo itakuwa ni ya haraka haraka. Baada ya muda kidogo kufikiria. Akasema zawadi ya haraka haraka aliyoiona yeye. Ni kuimbiwa na kijana huyo.



Ramah akashuka pale jukwaani na kuenda mwisho wa chumba hicho ambacho kilikuwa kama ni ukumbi fulani. Akarudi na gitaa lake. Ni dhahiri jambo hilo alilipanga pia ama alijua kwamba endapo akimuuliza Cecy ni zawadi gani ya haraka haraka ampatie basi angechagua kuimbiwa maana banati yule alikihusudu sana kitendo hicho cha kuimbiwa. Akarudi nalo pale jukwaani na kuchukua kiti chengine. Akakiweka sawa na kukikalia. Akapakata gitaa lake na kuwatazama watu waliokuwapo ndani humo. Wote walikuwa wakimtazama yeye huku wakitabasamu. Akamtazama na Cecy kisha macho yake akayahamishia kwenye nyuzi za kifaa hicho cha muziki. Akaanza kuvuta nyuzi kidogo kidogo zilizotoa ala nzuri kwenye masikio ya wote waliokuwapo hapo.



Baby ile siku nakuona, na nikakuomba, namba yakoooh. Hata siku sijaota, kwamba siku moja, nitakuwa wako wa milele eee. I wanna baby, mpaka leo hii, sijawahi kuwaza kukuachaaa. I wanna baby, mpaka leo hii, usiku na mchana ni wewe na kuwaazaaa. Na umenifuta mi machoozii, nilolia kwa mapenziii, oooh. Umenisahaulisha meengii, daima nitakueenziii.



We ni Malkiaa, we ni Malkiaa, kwenye Falme ya mapenzi yangu, Malkia. We ni Malkiaa, we ni Malkiaaaaa ooooh, Malkia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

You are my queen. Naomba mola abariki, maana, mitihani pia ni mingiii ooooh. Tukimaliza vigingiii baby, tutasherekea ushindiii. Yalopita sondwele yanayokuja yahusu mapenzi yetu. Kila siku nawaza kulilinda penzi letu. Kama unavyojuaa, moyo wangu umeamua, kutulia na penzi langu usijevua. My love, semagaa, nini kina kukwazaa, nataka tujenge lovee, oooh. Oooh mamaa, sometime huwa nakoseagaa, kama binadaamu nisamehee.



We ni Malkiaa, we ni Malkiaa, kwenye Falme ya mapenzi yangu, Malkia. We ni Malkiaa, we ni Malkiaaaaa ooooh, Malikia.



Makofi yalirindima ndani hapo baada ya Ramah kumaliza kuimba. Cecy aliinuka kwenda kumkumbatia Ramah. Wazazi wa watoto hao hawakuwa na la kusema wala kuongea kwa watoto hao walionekana kupendana sana. Walibaki kufurahia moyoni hasa hasa mama Cecy aliependa siku zote kumuona mwanae wa pekee akiwa na furaha na si huzuni kwasababu ndie mtoto huyo huyo alieachiwa na mumewe Ally kabla ya kufariki. Na alipanga kumlea kama mboni ya jicho lake.



Sekunde kumi na tano waliachiana. Cecy akarudi sehemu yake huku akiwa na furaha isiyokifani mtimani mwake. Aliwatazama waliokuwa mbele yake kwa muda kidogo. Akataka kuongea kitu ila Ramah akamuwahi.



“Hii ilikuwa ni zawadi ya kwanza alieichagua Cecilia. Na zawadi ya pili ambayo kwake itakuwa ni Suprise sana ndio ambayo inayofuatia sasa hivi ni hii”



Akashuka juu ya jukwaa na kumfuata Jay pale alipokaa yeye. Jay akampatia boksi kubwa kiasi la zawadi lililofungwa vyema. Akarudi nalo pale mbele. Akasimama sambamba na pale aliposimama Cecy. Akamkabidhi lile boksi kwa heshima fulani. Kisha akamtaka afungue mwenyewe. Cecy huku akitabasamu na shauku nyingi iliyomjaa nafsini mwake kutaka kumaizi kunani ndani ya boksi lile. Alianza kulifungua taratibu mpaka alipomaliza kabisa kulifungua.



Mshangao wa dhahiri ulimpata Cecy. Macho aliyatoa pima huku akiziba kinywa chake kwa kiganja chake cha mkono wa kushoto, mkono wa kulia ukiwa umeshikilia boksi lile la zawadi. Hakika hakuamini alichokiona. Chozi la furaha lilimtoka na kujikuta akimkumbatia Ramah kwa nguvu.



___________



Siku mbili zilizopita. Ramah na Cecy wakiwa katika matembezi yao. Walipitia katika duka fulani la nguo lililokuwa mkabala na uwanja wa mpira Mkwakwani. Cecy alimuambia Ramah kuwa kuna nguo aliiona katika duka hilo siku kadhaa nyuma na siku hiyo alipanga kuja kuipitia maana alishaweka oda kabla na kutoa kiasi kidogo cha pesa na kuahidi kuja kumalizia pesa iliyobaki ndipo aondoke nayo. Na siku hiyo ndio ameipitia akiwa na Ramah.



Wakaingia na Cecy alijitambulisha. Bahati nzuri yule muuzaji alikuwa akimfahamu bado kwahiyo haikuwa shida kujieleza. Cecy akalipa pesa anayodaiwa na kupewa nguo yake. Katika kuangaza macho huku na huko ndani humo. Akaona viatu vizuri vya kike, ambavyo vilishabihiana sana na ile nguo aliyoichukua muda huo. Akamueleza Ramah na hata yeye alivikubali kuwa ni vizuri. Akamtaka ajaribishe na yule muuzaji akamuonyesha chumba cha kujaribisha nguo. Cecy alionelea ajaribishe vyote ikiwa na ile nguo aliyonunua hapo na hivyo viatu alivyovioana muda huo.



Hakika alipotoka katika chumba cha kujaribisha alikuwa amependeza sana kiasi ambacho hata yule muhudumu alikiri kuwa mwanadada huyo alipendeza. Lakini ikawa tofauti kwa Ramah ambae alipinga na kusema kuwa viatu hivyo havikumpendeza hata. Cecy na yule muhudumu wakashangaa. Inakuaje aseme sijapendeza ilhali hata macho yangu yananionyesha kuwa nimependeza? Alijiuliza Cecy.



Ramah aliendelea kupinga kuwa havikumpendeza. Cecy akanyong'onyea kwa kuona Ramah amempinga. Tena akionekana yupo ‘Serious’ kabisa. Cecy hakuwa na budi kuviacha huku nafsi yake ikinung'unika. Wakatoka dukani humo na kupotelea kwenye njia za jiji hilo. Siku iliyofuata ikiwa ni siku ambayo Ramah aliyaona matokeo ya Cecy na kutafuta ni zawadi gani ampatie Cecy. Ndipo akakumbuka vile viatu kule dukani walipoviacha.



Akatoka na kwenda mpaka kule dukani. Bahati nzuri viatu alivikuta. Akavinunua na kuondoka navyo akiwa na dhamira ya kum_Suprise Cecy siku hiyo. Na hilo limetimia kwa asilimia mia. Cecy alijitoa kwenye kumbato la Ramah na kuvivaa viatu vile pale pale. Bahati ikawa kwake maana hata siku hiyo alivaa nguo ile ile aliyoinunua siku mbili zilizo pita.



Haki alipendeza mara mbili ya vile alivyopendeza mwanzo. Makofi yakarindima ndani humo kwa shangwe. Cecy baada ya kujiangalia na kujiona amependeza sana. Alienda kumkubatia tena Ramah na safari hii alijisahau kwamba hapo kuna wakubwa zao. Akapeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Ramah ambae na yeye ni kama pia alijisahau hivi na kumpokea Cecy vyema kabisa. Wanawake wale watatu watu wazima waliinamisha vichwa vyao chini. Hawakutaka kushuhudia kile kifanywacho na vijana wao.



Shwangwe na mbinja zilisikika hasa hasa Jay ambae ni kama alichanganyikiwa hivi. Dakika nzima ikapita, wakaachiana na hapo sasa soni zikawavaa kwenye nyuso zao. Shuhuli hiyo ikamalizika kwa kupata chakula kilicholetwa kutoka kwenye mgahawa huo. Wakala na walipomaliza ikiwa ni mida ya saa tatu na nusu usiku. Kila mmoja akashika njia yake. Hakika Ramah alijitoa kumfurahisha mpenzi wake bila kujali ingemgharimu kiasi gani cha fedha.



“Nauona uchizi mbele yako mwanangu” Mama Cecy alimuambia hivyo binti yake wakiwa ndani ya tax wakirudi nyumbani kwao.



“Kwanini Mama?” Cecy alimuuliza.



“Ramah anaenda kukuchanganya muda si mrefu. Ila ni vyema mkapendana kama hivyo. Inakuwa ni furaha kwenu nyote wawili kama ambavyo imekuwa muda mfupi uliopita” Mama Cecy alijibu.



Cecy akatabasamu na kumlalia mamae kwenye bega. Anita alimtazama Cecy aliekuwa akiliangakia boksi lile alilokabidhiwa na Ramah kama zawadi. Akatingisha kichwa huku akitabasamu. Chozi la huzuni lilimtoka kwenye jicho lake baada ya kumkumbuka mumewe Ally ambae aliuliwa kwa hila za mapenzi. Alikumbuka jinsi walivyopendana. Jinsi kila mmoja alivyojitoa kwa mwenzake akihakikisha tabasamu kwenye uso wa mwenzake halikauki.



“Lakini Cecy, unampenda kweli Ramah ama upo nae kwa muda tu?” Anita alimuuliza. Cecy akajitoa begani kwa mama yake na kumtazama usoni. Akakuta mama yake akiwa na shauku ya kutaka kuskia jibu lake. Akatabasamu na kujibu kuwa anampenda kweli na wala hayupo na Ramah kwaajili ya jambo fulani. Kisha akamuuliza ni kwanini amemuuliza swali hilo.



“Sina maana kubwa sana zaidi ya kujua tu. Nawajua nyie kizazi cha sasa mnakuwa na watu kwaajili ya jambo fulani na mkishafanikisha basi mnaachana. Ila tofauti sana na kwa Ramah. Yule mtoto ana upendo wa dhati unaonekana kwa yoyote anaeyajua mapenzi yenu. Kila siku nitakuambia haya maneno kuwa, siwezi kuingilia mapenzi yako hata kidogo kwasababu najua mtu akipenda anakuwaje. Kwasababu hata mimi nilishapenda kabla yako wewe. Ila maamuzi ya kuwa uwe na nani ni yako wewe mwenyewe hata ukiamua uachane na Ramah uwe na mwengine ni juu yako. Lakini unatakiwa upime mwenyewe. Je ukiachana na Ramah kwahuyo mwengine unaenda fuata nini? Kisha hapo ndio utachukua maamuzi ya busara” Anita alimaliza na kumvuta Cecy begani kwake. Safari ya kuelekea nyumbani kwao ikawa inaendelea.







Dakika chache mbele, wakawa wamefika. Wakashuka kwenye tax na kufanya malipo. Wakaingia ndani ya nyumba yao. Sebuleni juu ya meza. Anita aliona karatasi ikiwa imeshikizwa na kijiko. Akaifuata na kuichukukua. Alitabasamu baada ya kuisoma. Kisha akamfuata Cecy ambae alikuwa chumbani kwake muda huo.



“Naona uliniandikia ujumbe ili uende kwa jamaa yako” Anita aliongea hivyo huku akiionyesha ile karatasi. Cecy aligeuka baada ya kusikia sauti ya mama yake. Akamtazama usoni na kuutazama ule mkono wa mama yake ulioshika ile karatasi. Akaachia tabasamu kisha akanuna ghafla.



“Mama halafu kumbe ulikuwa unajua kila kitu lakini hata kuniambia hukutaka” Cecy aliongea kwa deko. Mama yake akamfuata mpaka pale kitandani na kwenda kukaa karibu yake.



“Nitakuambiaje wakati niliambiwa nisikuambie. Mbona hii ishu watu wote pale ndani tulikuwa tukiijua kasoro wewe tu”



“Haaa! Inamaana hata Jeni alikuwa pia akijua?” Aliuliza kwa mshangao. Anita akamuitikia kwa kichwa. Cecy akachukua simu yake ili ampigie Jeni kwa minijali ya kumlaumu kwa kutomjuza mapema jambo hilo.



Simu ilipopokelewa akaanza lawama. Alimlaumu rafiki yake utafikiri kilichotokea hakukipenda hata kidogo. Jeni muda wote alisikika akicheka tu. Mwisho alimuambia kuwa aliambiwa afanye siri asimuambie lolote. Cecy akakata simu akijifanya amekasirishwa na kitendo hicho. Akauvuta mdomo na kuangalia pembeni. Anita alicheka baada ya kushuhudia kitendo hicho kilichofanywa na mwanae.



Simu yake ikaingia ujumbe kutoka kwa Jeni ambao ulisomeka. ‘Ila tumekuweza hata ukinuna hahahahahaa’ Akaachia msunyo na kumtazama mama yake ambae alikuwa akicheka muda wote. Anita aliinuka huku akicheka na kutoka ndani ya chumba hicho akimuacha Cecy akimtazama. Baada ya mama yake kutoka chumbani kwake. Akaachia cheko dogo alipokumbuka ujumbe wa Jeni kuwa amewezwa. Ni kweli wameniweza. Alijisemea. Akachukua simu yake na kumpigia Ramah.



* * * *



Masaa yalisogea. Siku zikapita. Miezi ikasonga. Shule zikapangwa kwa wale waliobahatika kufaulu kidato cha nne. Cecy na Jeni walibahatika kupangwa shule moja. Usagara Secondary School ikawa tayari kuwapokea. Ikiwa zimebaki siku chache ili wanafunzi waripoti shuleni hapo. Maandalizi yalifanywa kwa Jenifa huku kwa Cecy yakiwa ni ya kusuasua.



Hali ya mama yake kwa kipindi hicho ilikuwa ni mbaya baada ya biashara zake alizokuwa akizitegemea kwenda kombo. Cecy aliuona ugumu wa yeye kwenda kuanza shule mwaka huo. Ila hakutaka kujikatisha tamaa haraka namna hiyo. Akajiapiza kivyovyote ni lazima asome. Je atasomaje ilhali hakuwa na kazi yoyote anayoifanya zaidi ya kumtegemea mama yake? Hapo sasa!.



Majira flani wakiwa sehemu flani yeye na Ramah. Baada ya maongezi mengi. Aliamua kumueleza wasiwasi wake. Ramah alikuna kichwa kwa tafakuri kisha akamuambia ampe siku mbili atampa mrejesho wa hayo waliyoayaongea. Furaha ya Cecy ikarudi japo kwa uchache baada ya kupewe moyo na mpenzi wake kuwa ni lazima asome.



Cecy aliyakumbuka maneno ya mama yake kuwa Ramah alikuwa akimpenda kweli na amejitoa sana kwaajili yake. Na hapo ndio alikuwa akiyathibitisha kwa mara nyengine maneno ya mama yake. Hivi ni kweli mimi nampenda Ramah kama yeye anipendavyo? Alijiuliza Cecy. Lakini mbona hata mimi nampenda sana... Eeee Mungu mjalie Ramah wangu.



Wakiwa bado wanaendelea kupiga soga mahala hapo. Simu ya Cecy ambayo muda huo alikuwa nayo Ramah iliingia ujumbe. Ramah akampatia Cecy simu yake ili asome mwenyewe ujumbe wake. Ila kwavile Cecy alikuwa akijiamini sana na mapenzi yake. Akamtaka tu Ramah amsomee ujumbe huo. Ramah bila ubishi wowote akaufungua ule ujumbe.



Na baada ya kuusoma. Sura yake ilisawijika kwa hasira. Kimya kimya akampatia Cecy simu yake bila kuongea chochote. Cecy aliyaona mabadiliko kwenye uso wa Ramah. Ana nini huyu? Alijiuliza huku akiipokea ile simu. Akausoma ule ujumbe na mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio mbio. Hivi kweli atanielewa? Ujumbe ule ulisomeka hivi. ‘ Mambo vp Cecy? Jana mbna umeniwka namn ile. Ama hukmaliz kaz kma ulivyniambia? Lakni kwanin usinijulishe kwa simu mpenzi?’



Ramah alikuwa amejiinamia akiangalia chini. Alihisi kuna kitu kikali kina uchoma moyo wake. Donge zito lilimkaba kwenye koo lake na kusababisha kutomeza mate kwa ufasaha. Usaliti!. Nasalitiwa!. Hivi ni nini anakikosa huyu mwanamke kutoka kwangu? Alijiuliza. Hapana hawezi kunifanyia hivi huyu. Wivu!.



Akainuka pasi na kuongea chochote. Cecy nae akainuka ili apate kumuelewesha vyema Ramah kuhusu mtu huyo alietuma sms hiyo. Unadhani Ramah alitakumsikiliza? Kusikiliza chochote kutoka kwa Cecy. Sasa asikilize nini wakati amethibitisha mwenyewe kuwa anasalitiwa? Tena inaonekana kuwa siku iliyopita Cecy na huyo mtu ambae namba yake haikuhifadhiwa kwenye kitabu cha simu cha majina walikuwa na miadi ya kukutana sehemu fulani ila kutokana na sababu ambazo hakuzijua mpaka muda huo. Cecy hakuweza kutokea!.



Akaanza kuondoka bila kujali sauti ya Cecy iliyomtaka asimame ili amueleze. Cecy alipoona hasikilizwi. Akatumia mkono wake kumzuia Ramah asiondoke. Akaguna huku akiutoa mkono wake kwenye mwili wa Ramah baada ya kukatwa jicho kali ambalo hakuwahi kuliona kwa kijana huyo hata kwa bahati mbaya. Akajirudisha nyuma huku akiwa amegwaya sana. Ramah akapotea kwenye upeo wa macho yake. Akibaki hajui afanye nini.



Ujumbe mwengine ukaingia kwenye simu yake kutoka kwenye namba ile ile iliyomtumia mwanzo ujumbe. Ujumbe ambao umevuruga amani iliyotawala kati yake na Ramah. ‘Mbon kimy?’ ulisomeka hivyo. Akasonya kwa hasira na kuamua kumpiga simu mtu huyo. Simu ilipopokelewa, bila kuchelewa alianza kumporomoshea matusi mtu huyo bila kujali mahali alipokuwa. Mwisho akamtaka aache mazoea na yeye ikiwezekana asijaraibu kumpigia simu achilia mbali kumtumia ujumbe na ikiwezekana zaidi namba yake aifute.



Bilashaka mtu huyo aligwaya kwa kitendo hicho cha ghafla kilichomtokea. Akakata simu yeye baada ya kuzidiwa na maneno hayo kama vile yeye ndie aliepiga. Cecy alipoona simu imekatwa. Akajaribu kumpigia Ramah lakini simu yake haikupokelewa. Akapiga tena na hivi sana ilikatwa kabisa na alipojaribu kupiga tena. Akajua Ramah amem_block tayari. Akapiga kite cha uchungu na kuondoka mahala hapo.



Siku hiyo haikuwa poa kwa Cecy kwa kile kilichotokea siku hiyo. Aliwaza sana atumie njia gani kumuelewesha Ramah ili amuelewe. Ni kweli hakuwa na hatia kwa jambo hilo. Ila usiri wake ndio uliomponza. Ni kweli kuna mtu alikuwa akimsumbua sana kwa kumtaka kimapenzi. Lakini yeye hakumkubalia. Kitendo cha kukaa kimya bila kumuambia Ramah jambo hilo akidhani labda nilamuda mfupi tu huku akihofia kumuweka na wasiwasi Ramah. Ndicho kilichosababisha mpaka siku hiyo kupelekea kutoelewana.



Sasa nini afanye ili kuyaweka sawa mambo? Hakujua!. Akawaza kumuambia mama yake jambo hilo huenda akapata msaada. Ila akaona ni mapema sana. Akaona bora atumie kwanza uwezo wake na ikishindikana basi ndio atajua nini cha kufanya. Ama nimueleze Jay? Alijiuliza. Lakini Jay hayupo Tanga mwezi sasa. Akajaribu kumpigia tena Ramah lakini yakaja yale yale kuwa simu hiyo ilikuwa ikitumika. Kwa maana kwamba namba yake iliblockiwa, maana haiwezekani simu itumike masaa mengi kiasi hicho.



Upande wa Ramah mambo yalikuwa machungu zaidi. Hakutaka kuamini kirahisirahisi kuwa Cecy amemsaliti. Sasa ni kipi amekikosa kwangu? Ama vile kujifanya mpole kwake ndio imekuwa kigezo cha kunichukulia mimi boya? Dah! Ama kweli mapenzi yanauma. Ramah alikuwa juu ya kitanda chake akiwaza hayo. Ni muda sasa tangu alipoingia ndani humo na hakutoka hata mara moja.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Chozi la uchungu likamtoka. Hakuwa akiamini bado kwamba mapenzi yote aliyokuwa akimuonyesha Cecy leo hii imekuwa ni maumivu moyoni mwake. Alijuta kupenda. Lakini nitamuhukumu vipi ikiwa sijasikiliza hoja zake? Alijiuliza. Akajiinua na kukaa kitandani. Hata hivyo angeniongopea tu, asingeniambia ukweli. Akajilaza tena. Akafuta machozi yaliyokuwa yakitoka kwenye macho yake baada ya kusikia sauti ya mama yake akimuita. Akajiinua kitandani na kutoka nje.



“Vipi wewe. Mbona ulijifungia ndani muda mwingi? Ama kwavile nduguyo hayupo ndio umekuwa mnyonge hivyo?” Mama yake alimuuliza hayo baada ya kuhisi kuwa Ramah kuna jambo linamtatiza. Ramah akajichekesha na kumtoa hofu kwa kusingizia uchovu.



“Haya nenda kachukue chakula. Mi nilipatwa na hofu ati, maana sikuona mishemishe zako nikajua kuna jambo limekupata ama ni kwavile nduguyo hayupo ndio umekuwa mnyonge hivyo. Hata sasa afadhali maana mlishaweka jadi kila kukicha lazima mzozane na kupiga masiyahi yasio maana” Ramah akacheka huku akielekea ndani ya nyumba yao kubwa ambapo kulikuwa na sebule.



Ni muda sasa Jay aliondoka katika mji huo kwa kile alichodai anaenda kutafuta maisha huko migodini. Japokuwa mama yake hakupenda mwanae aende huko lakini alipigwa kiswahili mpaka akaelewa na kutoa baraka zake na kumruhusu aende. Hata Ramah pia alitaka aende lakini mama yao akaweka mgomo akidai ni nani atakuwa mlinzi wake hapo ikiwa wote wataondoka? Jay akaondoka huku Ramah akibaki. Hata hivyo alitumia pikipiki ya Jay kujiingizia pesa kadhaa.



Siku hiyo ikapita bila kupatikana suluhisho lolote kwa wawili hao. Cecy alijitahidi kumtumia Ramah jumbe nyingi za kumtaka watafute sehemu walizungumze hilo. Lakini Ramah alizivalia miwani ya mbao akijifanya hazioni kabisa.



Siku iliyofuata. Jeni alimtafuta Ramah na kwaheshima aliyokuwanayo Ramah kwa Jeni. Hakuwa na budi kumsikiliza. Jeni alijitahidi kumtetea Cecy kuwa ni kweli huyo mtu alikuwa akimtaka Cecy lakini Cecy hakumkubalia na yote ni kutokana na mapenzi anayomuonyesha. Unadhani Ramah alitaka kuelewa chochote? Mazungumzo yakaisha bila kupatikana suluhisho lolote.



Siku hiyo ikaisha pia na kufuatia siku nyengine. Siku ambayo Cecy aliahidiwa na Ramah kabla hawajatofautiana kuwa atapewa mrejesho wa kile walichozungumza kuhusu ada ya Cecy ya kuanzia kidato cha tano. Cecy hakuwa na uhakika kama Ramah anaweza kumsaidia kwa hilo. Akawaza kumtafuta Ramah na siku hiyo pia ili wakae wazungumze tofauti zao lakini alisita kutokana na sababu zake anazozijua mwenyewe.



Akiwa anaendelea kutafakari hayo. Simu yake ikaingia ujumbe kutoka kwa Ramah. Moyo ukamlipuka kwa hofu. Shauku ikamjaa nafsini. Kiroho cha kutaka kujua Ramah amemtumia ujumbe gani kikamvaa na kumletea mchechetu usio wa kawaida. Akaufungua huku mikono ikimtetemeka na macho aliyakodoa juu ya kioo cha simu kusoma maandishi ya ujumbe huo. ‘Njoo Sizzler Corner saa 12 jioni’ Ujumbe ulisomeka hivyo.



Furaha ikatawala mtimani mwake. Akaangalia ni saa ngapi muda huo na kukuta ni saa kumi kasoro alasiri. Akatamani kusogeza saa mbele iliaende huko. Alipanga afanye lolote ili Ramah amuelewe na warudi kana zamani. Haraka haraka akampigia simu Jenifa na kumuelezea yote. Kisha akamtaka waende wote ili akatoe msaada wa kumuweka sawa Ramah. Jeni akamuambia asiwe na wasi, muda ukifika wataongozana wote.



Masaa yalisogea mpaka ilipotimu na saa kumi na moja jioni. Cecy akajiandaa haraka na kutoka. Nje alimkuta mama yake akipiga soga na wanawake wenzake ambao walikuwa ni majirani zao. Akamuaga kuwa anaenda kwa Ramah na Anita hakuwa na cha kumzuia. Cecy akaondoka na kupitia kwanza kwa kina Jeni ili safari waianzie huko.



Ndani ya mgahawa wa Sizzler Corner. Kulianza kuchangamka kutokana na kuwa watu wengi hupendelea kuwapo kuanzia majira hayo mpaka usiku mwingi. Ramah alikuwa amekaa kwenye meza iliyokuwa pembeni kabisa ya mgahawa huo. Alikuwa kimya akichezea simu yake. Cecilia na Jenifa majira hayo ndio walikuwa wakiingia mahala hapo.







Hawakuhitaji kuelekezwa Ramah alipo kwasababu hapakuwa na watu wengi sana kiasi ambacho wasiweze kumuona. Waliongoza kuelekea kwenye ile meza aliyokuwa Ramah. Walipofika wakamsalimia na kila mmoja akavuata kiti chake na kukaa. Ramah aliitikia salamu zao na kuwaangalia usoni mabanati hao. Kimya kifupi kikapita kisha Ramah pasi na kuongea chochote. Akaingiza mkono mfukoni mwake na kutoka na bahasha. Akaiweka juu ya meza na kumsogezea Cecilia karibu yake. Kisha akainuka tayari kuondoka mahala hapo.



Sauti ya uchungu ilisikika kwenye ngoma zake za maskio yake. Sauti ambayo ni nadra sana kuisikia kutoka kwa Cecy ambayo huiongea awapo na jambo ama tatizo kubwa linalomkabili. Cecy alimtaka asiondoke na amsikilize hata japo kwa dakika tano tu, kisha apime kama anavyomhisi ndivyo ama laa!. Aliongea huku akilia sasa.



“Ramah ungemsikiliza tu japo kidogo. Lakini sio kuhukumu bila ya kuwa na ushahidi kamili” Jeni nae alipigilia msumari maneno ya Cecy.



Ramah akageuka na kuwatazama mabinti hao. Akashusha pumzi nzito kisha akakaa kwenye kiti. Muda huo muhudumu wa mgahawa huo alifika na kuwataka waagize wanachotaka. Muda huo Cecy alikuwa amejiinamia akilia kimya kimya. Kwakuwa Ramah alikuwa na kinywaji chake. Jenifa akaagiza ziletwe ‘Juice’ mbili za matunda ya aina yoyote. Muhudumu akaondoka na baada ya dakika moja akarudi na vinywaji hivyo. Akawakabidhi na kutimua tena.



Kimya kifupi kilipita kabla ya Cecy kunyanyua tena kinywa chake. Uso mzima ulitapakaa machozi. Ramah alilishuhudia hilo, nafsi yake ikamuuma bila kutarajia. Akamuangalia Cecy kwa huruma na asijue ni kwanini amekuwa hivyo. Pengine ni hasira zake zilizosababisha asimsikilize mnyange huyo. Akakaa kimya akisubiri Cecy ataongea nini.



Cecy alianza kwa kuomba msamaha kwa Ramah kwa kutomjulisha mapema kuwa kuna mtu alikuwa akimsumbua akimtaka kuwa mpenzi wake. Cecy alikuwa akiongea huku akilia. Kitendo ambacho kilimfadhaisha sana Ramah. Akaendelea kwa kusema kuwa mtu huyo walikuwa wakisoma nae shule ya upili ambayo pia Ramah alisomea hapo hapo. Akamtaja jina na Ramah akakiri kimoyomoyo kumfahamu mtu huyo.



Cecy akaendelea kwa kusema kuwa. Pamoja na mtu huyo kumsumbua sana. Lakini yeye hakuwa akiwaza hata kidogo kumkubalia kwasababu alikuwa akimpenda yeye(Ramah) sana. Akaendelea kwa kusema kuwa, hata ile siku aliyotuma ujumbe uliofanya wakakosana. Siku ya nyuma yake alimtaka kweli wakutane na yeye akamchomolea kwasababu alishajua dhumuni lake.



Ramah hakutaka Cecy aendelee kuongea. Alimtaka anyamaze na kusema kuwa ameshamsamehe. Akaongezea kwa kusema hata yeye anaomba Cecy amsamehe kwa kuchukua maamuzi ya hasira pasi na kumsikiliza. Kisha hapo suluhisho likapatikana na amani ikarejea kwa wawili hao. Jenifa akatabasamu kisha akaaga anataka kuondoka kwa kisingizio kuwa nyumbani kwao hapakuwa na mtu. Mama yake ameenda mahali kwenye sherehe na hajui atarejea saa ngapi. Ila yote hiyo ni kuwapa nafasi wawili wale wa_enjoy pamoja. Wakamruhusu na Jenifa akaondoka baada ya kuimalizia ile shurubati yake.



Baada ya kuondoka kwa Jeni. Ramah na Cecy walibaki wakiangaliana. Iliwachukua kama dakika moja hivi. Kisha Ramah akainua mkono wake wa kuume. Akanyoosha kidole chake cha shahada huku vile vyengine vinne akivikunja. Kidole kile cha shahada alikipeleka taratibu mpaka kwenye pua ya Cecy. Kisha akakitambaza mpaka kwenye midomo na kushukia kwenye kidevu. Cecy alitabasamu na yeye akafanya kama vile Ramah alivyofanya kwake. Kisha wote wakacheka.



________



Wiki mbili zikapita. Kipindi hicho chote Cecy na yeye alijiandaa vilivyo kwaajili ya kuanza kidato cha tano baada ya kusaidiwa na Ramah kiasi kadhaa kwaajili ada japo haikutimia yote. Mama Cecy alizidi kumshukuru sana Ramah kwa kuisaidia familia yake kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa mwanae huku akimsihi kili siku binti yake kuwa Ramah ndio mtu wa kuwa nae.



Siku ya siku ilipowadia wanafunzi wapya wanaoanza kidato cha tano shule ya sekondari Usagara walienda katika shule hiyo. Cecy na Jeni wao pia walikuwa ni wamoja wapo. Taratibu zote walizifuata kama walivyotakiwa na baada ya hapo wakatakiwa wawepo madarasani ikiwa wanaendelea kusubiri wanafunzi wengine wanaokuja kwaajili ya kuanza kidato cha tano hapo.



Wiki hiyo ikapita ikaja wiki nyengine ambayo hii ndio masomo yalinza rasmi kwa wanafunzi hao. Ilikuwa ni furaha kwa Cecy baada kufufuliwa ndoto zake za kusoma baada ya kuwa zilififia kwa kukosa matumaini ya kusoma mwaka huo. Ni dhahiri asingesoma kweli maana mama yake hakuwa na jambo baada ya biashara zake azifanyazo kumuendea kombo kwa kipindi hicho.



Ramah alirejesha matumaini ya kusoma kwake baada ya kumpatia kiasi kidogo kama kianzio cha ada huku nyengine akimuahidi kumpatia siku za mbeleni. Hata hivyo Anita alishukuru kwa msaada alioutoa Ramah na kumuambia aache tu hicho kiasi kilichobakia atakimalizia mwenyewe. Cecy hakujua amshukuru vipi Ramah. Ila aliona shukurani ye pekee inayostahili kwa kijana huyo ni kumpatia upendo wa dhati.



* *



Sekunde zilisogea, dakika zikafuata. Masaa yakajiri, wiki zikakatika, miezi ikapita na mwaka ukaisha. Pamoja na vyote hivyo kubadilika. Hata mambo pia yalibadilika vivo hivyo. Majira ya mwaka na matukio. Hata elimu ya Cecy na wenzie ilibadilika na hivi sasa walikuwa kidato cha sita wakimalizia elimu ya sekondari.



Upande wa Ramah mambo yalikuwa mazuri kiasi baada ya kaka yake, ndugu yake wa pekee kurejea nyumbani akitokea migodini alipoenda kujaribu maisha. Hakurudi vizuri sana ila walau alipata chochote. Ile pikipiki aliyokuwa akiitumia yeye alimuachia rasmi Ramah huku yeye akinunua nyengine mpya. Hata hivyo alitaka kuhama pale nyumbani kwao akaanze maisha yake ya kujitegemea lakini mama yake alimkatalia kwa kumuambia. Yanini aharibu pesa ilhali hapo anaishi vyema. Maneno yake makubwa ni kwamba, nyumba hiyo ilikuwa ni urithi wao.



Jay hakuwa na budi kutii maneno ya mama yake lakini pia ndani ya fikra zake ni kukaa hapo kwa miaka kadhaa kisha aondoke. Maisha kidogo yalipata unafuu kwa upande wao. Jay alimfungulia mama yake biashara ya kuuza vitenge ambayo alitengeneza fremu pale pale nyumbani kwao.



Tangu kuingia kwa mwaka huo. Miezi sita ilipita na sasa wanafunzi waliokuwa wakisoma kidato cha sita walikuwa ndio wanahitimu elimu yao. Mitihani ikafanywa na walipomaliza wakarejea majumbani kwao kwaajili ya kusubiria matokeo yao.



MAJANI MAPANA. AIR PORT.



Ndege ndogo ya abiria ilitua katika uwanja wa ndege wa mji huo majira hayo ya jioni. Baada ya dakika kadhaa upande wa mapokezi. Alionekana kijana mdogo katika kundi la wasafiri walioshuka kwenye ndege hiyo. Kijana ambae kwa kumkadiria miaka yake ni kwenye ishirini hadi ishirini na mbili. Kijana huyo alikuwa amevalia kileo zaidi. Wenyewe huita‘Kibishoo’. Alikuwa amevalia flana laini na juu yake akiivika sweta dogo la kijivu. Suruali aina ya track ya bei ghali ilimsitiri kuanzia kiunoni mpaka chini kwenye vifundo vya miguu. Chini alivalia raba za bei mbaya aina ya NIKE zenye rangi nyeupe akimechisha na ile fulana nyepesi aliyoivalia ndani ya lile sweta. Kichwani alivaa kofia aina ya mvula ambao ulitaiti vyema kichwa chake likiwa la rangi ya kijivu pia. Mawani ya jua ya rangi nyeusi huku shingoni akining'iniza cheni ya dhahabu ‘pure’ vilizidi kumfanya aonekane wa kishua.



Alitembea kwa maringo huku pembeni yake pakiwa na jamaa wawili waliojazia miili yao kwa kufanya mazoezi mazito. Alikuwa akiangalia huku na huko kuangalia mazingira ya hapo huku nyuma yao wakifuatwa na muhudumu wa pale uwanjani ambae alibeba begi kwenye kimkokoteni. Walitembea mpaka walipofika mbele ya gari moja kali la bei mbaya la rangi nyeusi iliyometameta. Akafunguliwa mlango wa mbele upande wa kushoto na kuingia. Wale majamaa walionekana kuwa walinzi wake, wakampokea yule muhudumu lile begi na kumkabidhi kiasi kidogo cha pesa. Muhudumu akaondoka na lile begi likaingizwa kwenye buti la gari hilo. Kisha nawao wakaingia upande wa nyuma na safari ya kundoka hapo ikaanza.



Ndani ya gari hakuna ambae alieongea lolote mpaka walipofika kwenye nyumba moja ghali iliyokuwa maeneo ya Sahare ukuta wa mbolea. Gari likaingizwa kwenye mjengo na kwenda kupakia sehemu maalumu. Wale majamaa mmoja akashuka na kumfungulia mlango yule kijana mdogo huku yule mwengine akifungua buti na kutoa lile begi.



Dereva alieenda kuwachukua kule uwanjani alishuka na yeye na kumfuata yule kijana ambae muda huo alikuwa akishangaa shangaa mazingira ya nyumba hiyo. Akamfuata mbele yake kwa heshima kuu na kutoa tabasamu. Kisha akamuambia.



“Karibu nyumbani Rommy”



Yule kijana ambae ametambulishwa kwa jina la Rommy. Alivua mawani yake na kumtazama yule dereva. Kisha akaachia tabasamu na kutikisa kichwa juu chini kuashiria amekubali ukaribisho huo. Kisha hapo wakaanza kupiga hatua kuingia ndani zaidi ya nyumba hiyo.



“Ni muda sana tangu niondoke mji huu. Jiji naona limebadilika sana” Rommy aliyasema hayo huku akiwa nyuma ya yule dereva ambae muda huo alikuwa akifungua mlango mkubwa wa kuingia ndani ya nyumba hiyo.



“Sio sana Rommy. Ni kwavile umeondoka kitambo ndio maana unaona kumebadilika. Ila mbona kupo vile vile tu” Dereva aliongea huku akimpisha mlangoni Rommy aingie ndani. Rommy akaingia huku akitabasamu.



Akapokelewa na sebule safi yenye vitu vya samani. Masofa, Kabati, na vitu vyengine vikaavyo mahala kama hapo vilikuwapo vikiwa vya bei ghali sana. Rommy akatalii kwenye sebule hiyo huku akitabasamu. Alizunguka huku na huko mahala hapo huku wale majamaa na yule dereva wakimtazama tu.



Katika angaza yake. Macho yake yalitua ukutani ambapo kulikuwa na picha kubwa iliyoegeshwa hapo ikiwa na taswira ya watu watatu. Ikiwa na mwanaume na mwanamke huku katikati yao pakiwa na kitoto kidogo cha kiume wakiwa wamesimama pahali. Rommy aliishangaa kwa muda ile picha kisha akapiga hatua kadhaa mpaka pale ukutani.



Akaingalia kwa muda ikiwa pale pale juu kisha akanyoosha mkono akitaka kuitungua. Hakufikia!. Jamaa mmoja kati ya wale wawili akataka kwenda kumsaidia kuitungua ila Rommy akamzuia kwa kumnyooashea mkono. Jamaa akatulia na kurudi nyuma. Rommy akavuta meza ya kioo ambayo ilikuwa katikati ya sebule hiyo. Akaivuta mpaka pale ukutani na kupanda juu yake.



Hakuhofia kuvunja kioo. Alipanda juu yake na kuitungua ile picha. Akashuka juu ya ile meza na kwenda kukaa nayo kwenye sofa. Akaitazama ile picha kisha akatabasamu. Akawaangalia waliokuwapo hapo na kukuta wao wakimtazama yeye. Akayatoa macho yake na kuyahamisha pale kwenye ile picha.



Katika zile taswira za kwenye ile picha. Mbili hazikuwa na shaka kuzifahamu ikiwa ni ya yule mwanaume na yule mtoto. Yule mtoto alikuwa ni Rommy mwenyewe kipindi hicho alipokuwa mdogo. Huku ya yule mwanaume akiwa ni Antony Magasa. Ndio Antony Magasa huyu huyu tunaemfahamu ambae kipindi cha uhai wake alikuwa ni bosi wa Ally mume wake na Anita baba wa Cecilia.



Yule mwanamke hatukuweza kumfahamu ila pengine akawa ni mama mzazi wa Rommy. Na chengine ni kuwa. Hata hiyo nyumba waliyoingia hapo punde tu. Ilikuwa ni nyumba ya Antony Magasa ambayo tulimuona mara ya mwisho akimuulia bwana Ally hapo hapo sebuleni. Ila sebule ya kipindi kile ilitofautina na hii ya sasa baada ya thamani kubadilishwa.



“Nimewakumbuka sana wazazi wangu. Mungu awalaze pema peponi” Rommy aliongea hayo huku akiwa bado anaitazama ile picha. Hakuna yoyote aliyeongea wala kujibu chochote kati ya wale watatu waliosimama wakimtazama kijana huyo.



“Hivi humu ndani tunaishi wangapi broo Zuma?” Rommy aliacha kuitazama ile picha na kumuangalia yule dereva ambae alimuita kwa jina la Zuma.



“Tupo watatu ikiwa ni mimi na dada wa kazi na yule afande pale nje. Ila kwa sasa tupo sita tukiongeza na nyie” Zuma alijibu. Rommy alitingisha kichwa juu chini kisha akamtaka Zuma awaite hao wawili ili waje kutambuana. Zuma akatoka na kumfuata yule askari wa getini ambae alikuwa mlinzi kutoka katika shirika fulani linaloshuhulika na mambo hayo. Kisha akarudi tena ndani na aliporudi hapo sebuleni aliongozana na mwanadada ambae ilisemekana ni mfanyakazi wa ndani wa nyumba hiyo.





ENDELEA..



Rommy aliwatazama watu wale wawili kisha akainuka na kuwapa mkono. Zuma aliwatambulisha majina yao. Yule mlinzi wa getini alitambulishwa kama afande Koba huku yule mwanadada wa kazi akitambulishwa kama Siwema. Rommy alijitambulisha na yeye kisha akawatambulisha na wale walinzi wake. Ambapo ni Paskali na Assu. Kisha hapo akawaruhusu wakaendelee na kazi nyengine.



Majira hayo hayo ya jioni katika ufukwe wa Jetti Raskazone. Kwenye magahawa uliokuwa maeneo hayo. Kwenye meza moja, walikuwapo Ramah na Jeni wakiwa wamekaa wakipiga soga na kucheka. Muda kidogo Cecy alitokea kwenye meza hiyo akiwa amebeba vipakti vidogo vilivyo na karanga ndani yake na kuwasogezea kila mmoja chake watu wale. Kisha akakaa kwenye kiti kilichopo karibu kabisa na Ramah.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Umeenda kumpatia wapi?” Jeni alimuuliza huku akifungua na meno kile kipakti.



“Haki nimepata tabu. Nimekimbiza mpaka kule chini ndipo nilipoenda kumpatia” Cecy alijibu huku akimpatia Ramah kile kipakti chake amfungulie. Ramaha aliacha kile chake ambacho alikuwa akijiandaa kukifungua na kufungua kile cha Cecy. Kisha hapo akampatia mwenyewe na yeye akaendelea na kile chake.



“Mtoto unadeka wewe” Jeni alimuambia Cecy hivyo baada ya kuona akimpatia Ramah kile kipakti cha karanga amfungulie. Wote wakacheka.



“Hee! Kwani kuna ubaya?” Cecy aliuliza baada ya kuacha kucheka.



“Hapana ubaya si upo na bebebeibe bwana. Ila mara moja moja unatakiwa ujifunze kuishi mwenyewe bila uwepo wake” Cecy alicha kutafuna karanga baada ya kusikia maneno ya Jeni. Akamtazama na kumuuliza nini anamaanisha kusema hivyo.



“Sina maana kubwa. Ila pengine ikatokea Ramah ametoka nje ya mji huu kwenda mji mwengine huko kutafuta maisha na wewe ukabaki mwenyewe huku. Huoni kama itakuwia vigumu sana kuishi bila uwepo wake?” Jeni aliongea.



“Atakapoenda nipo nyuma yake” Cecy alijibu huku akitabasamu. Akamlalia Ramah begani. Ramah akamtazama Cecy kisha akamtazama Jeni. Wakajikuta wakicheka



Majira ya jioni yalipowadia. Walikuwa tayari kuondoka hapo maana muda ulishawatupa mkono. Walijinyanyua kwenye viti na kuanza kuodoka mahala hapo taratibu. Mwendo wao wa taratibu uliwafikisha Beach ya Raskazone ambapo kutoka hapo Jeti mpaka mahala hapo hapakuwa mbali. Huko walitafuta usafiri utakao wawahisha wanapotaka.



Nyumbani kwa kina Ramah yakiwa ni majira ya saa nne usiku. Baada ya kumaliza kula. Waliingia chumbani kwao. Huko walijitayarisha kulala. Ramah akapanda kitandani na kuchukua simu yake akawa bize nayo. Huku Jay yeye akiwa bize na Laptop yake akiwa amekaa kwenye pembe ya kitanda. Muda kidogo Jay alimgeukia Ramah pale kitandani huku akimuita jina lake. Ramah akaachana na simu na kumtazama yeye.



“Hivi yule ndugu yako alipotelea wapi yule?” Jay alimuuliza. Ramah alikunja paji lake la uso kwa tafakuri akifikiria swali hilo aliloulizwa na Jay. Kisha akamuuliza ni ndugu yake yupi huyo anaemzungumzia.



“Aaaaa Ramah inamaana humkumbuki yule dogo? Dogo flani hivi kipindi flani cha nyuma ulitambulishwa na bi maza kuwa ni ndugu yako mkawa mnatembeatembea pamoja. Unataka kuniambia bado hujampata tu?” Jay alimuelekeza na kumuuliza swali. Ramah alitoa ile mikunjo kwenye paji lake la uso kipindi anafikiria na kuachia tabasamu.



“Anhaa! Kumbe unamzungumzia Ethan?” Ramah akamuuliza. Jay akashadadia kwa kusema ndio huyo huyo. “Aaaa yule jamaa sijui yupo wapi, ila niliwahi kusikia kuwa ameenda kusoma sijui wapi huko. Dah kitambo sana asiee. Yani leo ndio umenikumbusha huyo mtu haki vile. Kwanza kwanini umemuongelea huyo mtu?” Ramah alimuuliza huku akijiweka sawa pale kitanda kwa kuinuka kidogo akiigamia ukuta.



“Sijui ila leo nimemkumbuka tu baada ya kuona hii picha yako ya utotoni. Mlikuwa mkifanana kiasi ila sema hayo manywele yako ndio yamekutoa kabisa kwenye ufanano wenu. Sidhani kama akikuona sasa atakukumbuka” Jay aliongea hayo. Ramah baada ya kusikia Jay ameona picha yake ya utotoni. Akajinyanya pale alipo na kumfuata Jay na kuikodolea macho ila Laptop ambayo kioo kizima ilitawaliwa na picha moja ya Ramah ya utotoni akiwa na miaka tisa.



Ramah aliomba aishike yeye ile Laptop ili apate nafasi nzuri ya kuitazama ile picha. Kisha akaachia tusi na isijulikane amemtukana nani huku akimuuliza Jay kuwa hiyo picha ameitoa wapi. Jay akacheka kisha akamuambia alikuwa nayo kwenye akaunti yake ya Facebook na ameitoa humo. Ramah akaomba aipate hiyo picha. Jay akamuambia kuwa afungue ‘bluetooth’ ya simu yake amrushie. Ramah akachukua simu yake na kufungua ‘bluetooth’ kisha Jay nae akafanya hivyo hivyo kwenye Laptop yake. Picha ikarushwa na sasa Ramah alikuwa nayo kwenye simu yake.



“Sasa Ramah si umuulize mama kuwa yule dogo alipotelea wapi. Huenda ikawa anafahamu” Jay alimuambia Ramah hayo aliekuwa bize na simu yake akiishangaa ile picha yake ya utotoni.



“Sidhani kama anafahamu. Tuachane nae kwanza kila mmoja anapamabana na hali yake sasa” Ramah akamjibu Jay pasi na kumtazama. Jay akageuza macho yake na kuendelea na shuhuli zake kwenye Laptop yake.



Ramah alikuwa akitabasamu kila mara. Aliingalia ile picha kwa kitambo sana. Akai_‘zoom’ na kuipeleka huku na huko kwa kidole chake pale kwenye kioo cha simu yake tamba. Alikuwa akiitazama vyema huku akikumbuka enzi hizo alivyokuwa mtoto. Alikumbuka mengi yaliyopita yaliyomfurahisha. Kisha akasikitika huku akitabasamu. Akaingia upande wa mtandao wa WhatsApp na kumtumia picha ile Cecy huku chini yake akiandika maneno. ‘Unaweza kumfahamu huyo kiumbe kwenye hiyo picha?’



Punde ujumbe ukaingia kutoka kwa Cecy aliejibu sms aliyotumiwa na Ramah. ‘(Aliweka emoje za kucheka) ni yule kiumbe alieutka moyo wa m2 fulan. Kumbe alikuwaga hiv kitambo hiyo? (Akamalizia na emoje za kucheka’



Ramah alitabasamu na kumtumia ujumbe mwengine. ‘Alikuwaje?’ Kabla Cecy hajajibu ule ujumbe. Kwenye ‘Profile picture’ yake akabadilisha picha na kuiweka ile picha aliyotumiwa na Ramah. Ramah baada ya kuona hivyo alitabasamu kisha na yeye akaisave ile picha kwenye ‘Profile’ yake. ‘So Handsome( akaweka na emoje ya kikatuni kinachopiga kiss)’. Ramah akatabasamu. Akawa anajiandaa kuandika ujumbe. Akaona Cecy aki_type. Akatulia aone ataandika nini. ‘Usku mwema beib naona mach yanafmba kwa usngizi. But 4give me’ Ramah akaishiwa pozi maana yeye ndio kwanza midadi ya kuchart ndio ilikuwa inapanda. Akamtakia na yeye usiku mwema kisha Cecy akashukuru na kutoka ‘Online’. Ramah akahamia katika mtandao wa Facebook katika page mbalimbali za Riwaya kwaajili ya kusoma ili walau avute muda wa kulala.



Siku iliyofuata majira ya asubuhi. Wakati ambao Ramah na Jay walishaamka. Walikuwa wakijiandaa kwaajili ya kwenda kutafuta riziki kwa kazi yao ya kupiga bodaboda. Ilikuwa ni tofauti kwa Jay maana yeye alikuwa na uwezo wa kufanya kazi yoyote nyengine kutoka na kiasi kadhaa cha pesa alichokuwa nacho baada ya kutoka migodini. Lakini alipenda kuendelea na kazi hiyo huku mwenyewe akidai anaiweka akili yake sawa ipate kutulia na kuchagua biashara nzuri atakayoianzisha ili aendeleze maisha yake.



Jay alikuwa amekaa kwenye sofa lililokuwa chumbani kwao akichezea simu yake. Mara kidogo akaachia cheko kubwa lililomshtua Ramah aliekuwa kwenye kioo akiweka sawa nywele zake zilizokuwa nyingi kichwani. Ramah alimtazama Jay kwa mshangao baada ya kusikia kicheko kutoka kwake. Jay alikuwa bado akicheka huku akiitazama simu yake.



“Kumbe kuna watu walikuwa wabaya namna hii walipokuwa watoto? Walikuwa na mavichwa kama mabibo” aliongea hayo na kucheka tena. Ramah alishatambua kuwa dongo hilo lilikuwa ni kwake. Akaachana nae na kuendelea na alichokuwa akifanya. Hata hivyo ilikuwa ni kweli Jay anaicheka picha ya Ramah aliyoiweka ‘Profile picture’ kwenye mtandao wa Whatsapp. Picha ambayo ni yeye mwenyewe ndio amei_donwload kwenye akaunti yake ya Facebook na kumrushia Ramah.



Alipoona Ramah hampatilizi. Akaendelea na kejeli zake. Kejeli ambazo zilianza kumkasirisha Ramah pamoja na kuwa ameshajisemeza kimoyomoyo kuwa kwa siku hiyo hataki maneno na Jay. Jay ni kama vile aliisoma akili ya Ramah. Kejeli na maneno ya kashfa alizidi kuyatoa kuhusiana na ile picha ya Ramah huku akicheka. Tena mara hii alikuwa akicheka mpaka machozi yalimtoka. Ramah alipoona anazidi kukasirishwa na maneno ya Jay. Akaonelea bora atoke nje ili amuepuke Jay.



“Jitu kumbe lilikuwa na mi_m'ba kama mti wa mpera halafu linapiga mapicha hovyo hovyo tu hahahahhah” Alizidi kukejeli Jay baada kuona Ramah akitaka kutoka ndani humo. Ramah aliekuwa ameushikilia mlango kwa minijali ya kutoka humo alighairisha na kumtazama Jay kwa hasira.



“Oya jamaa. Hii michezo ya kise**e tuiache. Tutakuja kuzinguana kweli siku moja halafu tusiongeleshane humu ndani. Tutakuwa kama sisimizi tunapishana bila kusemezana huku tunapigana vikumbo” Ramah alimuambia Jay hivyo ambae baada ya kusikia maneno hayo ndio kwanza aliongeza kicheko.



Mama yao aliekuwa nje akifanya usafi alikuwa akisikia kila kitu. Alisikitika kisha akapaza sauti yake.



“Mnadhani nitasema lolote japo tayari nishasema. Ila hiyo tabia yenu mtakuja kutoana ngeu siku moja maana mshaanza kutukanana tayari bado kukondana tu. Endeleeni tu na hiyo tabia yenu ila mwisho wenu mtauona” Mama yao aliwaambia hivyo kisha akaendelea na kazi aliyokuwa akiifanya.



Ramah akaacha kufungua mlango na kurudi mpaka kwenye meza. Akachukua funguo za pikipiki na kutoka nje ya chumba chao. Huko alimsalimu mama yake kisha akaingia kwenye chumba chengine ambacho walitumia kuwekea pikipiki zao. Akatoa ya kwake kisha akaidanda na kutokomea kusikojulikana.



Majira haya haya ya asubuhi. Rommy ndio alikuwa akiamka muda huu. Alikaa kitandani kwake kwa muda huku akipepesa macho yake kukitazama chumba hicho alichokuwamo. Kilikuwa ni chumba kizuri chenye vitu vya samani pia. Chumba hiki ndicho chumba alichokuwa akikitumia baba yake kipindi cha uhai wake.



Alijivuta na kuisogelea meza ndogo iliyokuwa karibu ya kitanda. Akachukua cheni yake ya dhahabu na kuivaa shingoni. Kisha akainuka na kwenda kujitazama kwenye kioo. Akayapikicha macho yake kwa viganja vyake vya mikono kisha akajitazama tena. Akaivua ile cheni na kuirusha pale kwenye kile kimeza. Akajitoa hapo na kuingia maliwatoni na baada ya muda alitoka akiwa ameshaufanyia mwili wake usafi.



Sauti ya kugongwa kwa mlango wake ikasikika. Akamkaribisha mgongaji kwa sauti huku akiuendea mlango. Akaufungua na kukuta ni Siwema ndie ambae alikuwa akibisha hodi. Siwema alimjuza kuwa kifungua kinywa kipo tayari mezani na anasubiriwa yeye tu. Akajibu kuwa anamalizia kuvaa atatokea muda si mwingi huko. Mwanadada yule akaaga na kuanza kupiga hatua kuondoka mahali hapo.



Huku nyuma macho ya Rommy yalikuwa yakimtazama sana mwanadada huyo. Hasa hasa chini kidogo ya kiuno jinsi kunavyotetemeka mithili ya tambara la mashine ya kusagia. Akameza mate ya uchu na kufunga mlango wake huku akitabasamu. Picha ya mwanadada Siwema alivyokuwa akitembea ilimrudia tena kichwani kwake na kumfanya agande kama vile alikuwa akimtazama ‘live’. Akaachana na mawazo hayo na kuiiende cheni yake na kuivaa. Kisha akaiendea tena ile meza ambayo juu yake kulikuwa na pakti ndogo la dawa. Akalifungua na kutoka na dawa, akachukua kidonge kimoja na kukitazama kwa muda kama ambae anajishauri jambo. Baada ya sekunde kadhaa akakimeza kisha akachukua na chupa ya maji ambayo ilikuwa pale pale juu ya meza. Akaifungua na kunywa kiasi yale maji asukumizie ile dawa. Kisha baada ya hapo akatoka na kwenda kujiunga na wenzake pale mezani kwaajili ya kupata staftah.



“Uchovu wa safari umekufanya uchelewe kuamka Rommy” Zuma alizungumza hayo baada ya kuwa mahala hapo pamepoa sana kila mmoja akiwa bize na chakula. Rommy alimtazama Zuma kisha akatingisha kichwa juu chini kukubaliana na maneno yake.



Kimya kikachukua tena nafasi huku kila mmoja akibugia na kushushia na chai ya maziwa vitafunwa hivyo. Mara kidogo Siwema alifika mezani hapo akiwa na sahani iliyojaa nyama za kuchoma. Akaiweka na kuondoka mahala hapo. Alipowapa mgongo watu hao. Rommy aliacha kula na kumtazama mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akarudisha macho yake taratibu na mbele. Huko aligongeshana macho na jamaa mmoja kati ya wale wawili ambao walikuwa ni walinzi wake. Jamama yule alitabasamu na kuendelea kula.



“Broo Zuma inabidi leo jioni tutoke tukazungukezunguke kidogo maana ni kitambo sana sijaliona jiji hili” Rommy aliongea.



“Hakuna shaka Rommy. Hata hivyo kukaa ndani sana haitopendeza. Umekuja huku likizo inabidi utembee ili ujionee mabadiliko ya mji huu kama mwenyewe unavyodai” Zuma nae aliunga mkono. Rommy aliwatazama wale walinzi wake na kuwaambia.







“Itakuwa ni ‘tour’ pia kwenu majamaa. Bilashaka hamkuwahi kufika mji huu. Au uongo kaka mkubwa Paskali?” Rommy aliwaambia majamaa hao. Kisha akamuuliza yule mmoja ambae mwanzo waligongeshana macho yao.



“Itakuwa vyema sana. Maana mwezi mzima kukaa ndani tu haitowezekana” Paskali alijibu.



Wakaendelea na soga zao huku wakijitahidi kumalizia vyakula hivyo vilivyokuwa juu ya meza. Huku ikiwa mada kuu ni juu ya matembezi watakayo yafanya siku hiyo majira ya jioni..



Majira ya saa tisa alasiri. Cecy alikuwa nyumbani kwao. Alionekana kama anataka kutoka hivi maana alikuwa akijiandaa kimtoko. Nusu saa mbele alikuwa tayari kutoka. Akamuaga mama yake na kutokomea nje ya nyumba yao. Safari yake ilikuwa ni kwenda nyumbani kwakina Jeni. Dakika kadhaa zilitosha kumfika nyumbani kwakina Jeni. Alipofika alimkuta Jeni na yeye ndio anajiandaa.



Hakuwa na budi kumsubiri. Akatumia nafasi hiyo kujipara upya mpaka pale Jeni alipomaliza kujiandaa. Wakatoka na kutafuta usafiri utakaowafikisha huko walipopanga waende. Walipopata usafiri wakapakia na kumuelekeza dereva ni wapi wanaenda. Dakika kumi na saba zilitosha kuwafikisha huko wanapotaka ambapo kulikuwa ni barabara ya kumi na tatu. Wakashuka kwenye usafiri ambao ulikuwa ni Bajaji na kufanya malipo. Kisha wakapiga hatua kuingia kwenye maduka ya nguo za kike yaliyokuwapo maeneo hayo.



Walifanya manunuzi ya nguo mpaka pale walipotosheka ama walipomaliza bajeti yao waliyoipanga kwa siku hiyo. Wakatoka nje ya duka hilo walilokuwamo.



“Tunarudi nyumbani ama?” Jeni alimuuliza Cecy. Cecy alitazama saa yake ya mkononi na kukuta ni saa kumi na moja kamili majira hayo.



“Tunarudi vipi nyumbani muda huu Jeni?”



“Ndo hapo sasa! Ok tunaelekea wapi sasa?” Jeni alijibu kisha akauliza. Cecy alifikiria kwa muda kisha akatoka na wazo kuwa waelekee Mkwabi SuperMarket kuna vitu anataka kwenda kuchukua. Jeni alimtazama kwa mshangao.



“Tutoke hapa mpaka Mkwabi. Na usafiri gani labda?”



“Kwa miguu tu. Kwani kuna umbali gani?” Jeni alizidi kumshangaa Cecy. Akamuuliza kuwa anaujua umbali kutoka hapo mpaka huko anaposema. Cecy alijibu anaufahamu vyema ila waende tu. Jeni akafikiri kwa muda na kukata shauri kuwa waende. Ukweli ni kwamba. Kutoka hapo mpaka huko walipopanga waende, hapakuwa na umbali wa kutisha. Ni mwendo wa dakika kama kumi mpaka kumi na tano tu.



“Ama tuchukue usafiri?” Jeni alimuambia Cecy wakiwa wanatembea kuelekea huko.



“Teh! Kwa nauli ya nani? Mi sina hela za mchezo” Cecy alijibu na kumfanya Jeni acheke.



* *



“Ama kweli mji umebadilika..” Rommy alinena hivyo huku akiangalia nje wakiwa ndani ya gari wakipita mitaa kadhaa ya jiji hilo.



“Sidhani pia kule ulipowahi kuishi kwa muda kama unapakumbuka” Zuma alimuambia hivyo huku akiwa bize na usukani wa gari. Rommy aliacha kuangalia nje na kumtazama yeye kisha akasema.



“Sio mahali tu hata jina pia limenitoka. Ila nakumbuka sijui panaitwa Du.. nini sijui. Aaa sikumbuki vyema”



“Duga”



“Yes i remember. Duga ndio. Hivi wewe unapajua pale sehemu?”



“Kwanini nisipajue wakati tulikuja kukuchukua wenyewe. Napakumbuka ndio”



“Itabidi tutafute siku tuende pale. Nimemkumbuka sana yule mama na yule mwanae sijui wanamuita nani hivi...”



“Rafaeli” Zuma alimkumbusha.



“Dah! Aisee unakumbuka vitu vingi sana broo. Tutafute siku tuende kweli” Rommy aliongea hivyo huku akiwa na furaha baada ya kukumbushwa jambo ambalo lililowahi kutokea miaka kadhaa nyuma. (Tuendelee kuwapo kwenye kisa hiki pengine tunaweza kumaizi yaliyojiri kipindi hicho.)



Soga ziliendelea kupigwa ndani ya gari huku wakipita mitaa hii na ile ya jiji hilo. Rommy alikuwa na furaha sana akifurahia safari hiyo. Akawatambia walinzi wake ambao yeye aliwachukulia kama kaka zake kwamba yeye ni mzawa wa jiji hilo ila kuna mambo ambayo yalitokea mpaka akahama mji huo. Hakutaka kujiona wafahari saana japo aliekuwa juu yake alitaka watu hao wamuoena kijana huyo wafahari.



Tembea yao iliwafikisha Mkwabi SuperMarket ambapo ilikuwa ni SuperMarket kubwa ya jiji hilo la Tanga. Rommy akashangaa sana mazingira hayo maana wakati yeye anaondoka katika mji huo jengo hilo halikuwapo bado. Akawaambia anataka kwenda kuangaza macho yake ndani ya Market hiyo. Zuma akaingiza gari kwenye jengo hilo na kwenda kulipaki sehemu husika. Kisha wote wakashuka.



Assu alibaki nje kwaajili ya usalama huku Rommy, Zuma na Paskali wakizama ndani ya jengo hilo. Huko walizunguka wakiangalia hiki na kile. Pamoja na kuangalia, pia Rommy alinunua kile alichoona kimempendeza.



Ndani ya jengo hilo hilo. Cecy na Jeni walikuwa wakilipia mapokezi kile walichochukua kwenye rafu zilizopangwa kwaajili ya kuwekea bidhaa. Walipomaliza kulipia. Walitoka kwaajili ya kutimka maeneo hayo. Rommy nae muda huo ndio alikuwa akilipia bidhaa kadhaa alizochukua na baada ya kukamilisha kila kitu akatoka nje ya jengo hilo.



“Oooh! Jeni nimesahau risiti” Cecy aliongea hivyo huku akisimama. Jeni nae alisimama na kugeuka kule ambapo Cecy yupo maana yeye alikuwa mbele ya Cecy kwa hatua kama mbili hivi.



“Cecy! Risiti ya nini tena... Hee! Yule mkaka..!” Jeni aliongea kwa kulalamika ila kabla hajamalizia sentensi yake. Akaganda kwa mshangao huku akitazama nyuma ya Cecy.



“Mkaka yupi...? Ananini?” Cecy alimuuliza huku akigeuka nyuma kule ambapo Jeni alikuwa akiangalia. Alikuwa ni Rommy ndie ambae walikuwa wakimshangaa. Alikuwa akitembea huku akichezea simu janja yake akielekea upande ambao walipaki gari lao.



“Yule si...Rommy ama?” Cecy aliuliza na asijue kuwa huyo anaemuuliza mwenyewe alikuwa pia akijiuliza swali hilo hilo.



“Itakuw ndie... Lakini mbona... Aaaa yule ndie bwana”



“Rooommy!?” Cecy aliita kwa sauti ndogo yenye mashaka ndani yake maana hakuwa na uhakika kama anaemuita ndie ama amemfananisha tu. Sauti ambayo ilimfikia Rommy mwenyewe na kunyanyua kichwa kuangaza mahala hapo.



Kitendo bila kuchelewa Cecy alichomoka mbio baadaa ya kujihakikishia kuwa amdhaniae ndie mwenyewe. Rommy akiwa bado anaangaza macho yake akishtukia akikumbatiwa kwa mbele. Hakufanya papara kujitoa kwenye kumbato hilo maana alijua kuwa huyo aliemkumbatia ndie huyo aliemuita. Na kama alimuita kwa jina lake basi alikuwa akimfahamu.



Cecy aliung'ang'ania mwili wa Rommy kitendo ambacho kilimuacha mdomo wazi Jeni. Sio tu kumshangaza Jeni. Hata watu alioongozana nao Rommy walistaajabishwa na kitendo hicho. Rommy mwenyewe alikuwa kimya huku mapigo yake ya moyo yakiwa mbio akiwa na shauku ya kutaka kujua ni nani hasa aliejitoa ufahamu na kwenda kumkumbatia bila kujali uwepo wa watu aliokuwa nao.



Dakika moja ilipita ndipo Cecy alipojitoa kwenye kumbato. Na Rommy ndipo alipopata kumjua huyo aliekuwa akimuita mpaka kumkumbatia. Akaachia tabasamu kuu usoni mwake kitendo ambacho kilimfanya Cecy amkumbatie tena. Kisha hapo akajitoa tena na kumtazama kijana huyo usoni. Haki amebadilika. Amekuwa mzuri zaidi tofauti na mwanzo. Cecy alijiwazia huku akimtazama Rommy usoni.



“Hivi ni wewe kweli Rommy?” Cecy alimuuliza huku bado akimtazama usoni kijana huyo. Rommy alizidi kutabasamu na kuzidi kumuacha hoi Cecy.



“Ni mimi Cecy. Hata mimi siamini kama kweli ni wewe. Umebadilika sana” Rommy alijibu.



“Nimekuweje?”



“So cute. More thane beuty i swea. I can't believe these miracle inayonitoke haki vile. Mbona umezidi kuwa mzuri hivyo?”



Cecy akajitoa mikoni mwa kijana huyo huku akichekacheka. Akamuita Jeni mahala hapo na Jeni akasogea kwa hatua ndogo ndogo huku akitabasamu. Rommy akazidi kutabasamu. Jeni alipofika akapeana mkono na Rommy. Salamu zikafuata huku wakikumbushia mambo kadhaa yaliyowahi kutokea nyuma.



Cecy alimuuliza kipindi chote hicho alikuwa wapi. Rommy akajibu kuwa alikuwa nchini Kenya katika mji wa Nairobi kimasomo na hapo amekuja likizo tu. Akamuuliza tena likizo yao inaisha lini naye akajibu ni mwezi mmoja tu kisha atatimka tena kurudi Nairobi. Cecy akanyongea ghafla. Jeni alishuhudia kitendo hicho hata Rommy pia. Ila akampoza kwa kumuambia kuwa wakati wote huo watakuwa pamoja. Kidogo furaha ya Cecy ikaonekana.



Majira hayo yalikuwa ni saa moja jioni. Rommy akawatambulisha mabinti hao kwa watu wake kuwa aliwahi kusoma nao shule ya msingi miaka hiyo. Pia aliwatambulisha watu wake kwa wanawake hao kuwa ni kaka zake wanaoshirikiana wote kwa mambo mbalimbali. Kwakuwa muda umeenda sana. Rommy akaomba namba ya Cecy na Cecy akampatia bila kinyongo. Kisha akazama mfukoni kwake na kutoka na kiasi cha shilingi Elfu Hamsini akiwaambia itawasaidia kwenye nauli ya kurudi. Ila akamuwekea ahadi ya kukutana nae siku nyengine. Wakaagana na Rommy akaingia kwenye gari na kutimka mahala hapo akimuacha Cecy akishangaa mpaka pale gari aliloingia Rommy lilipopotea kwenye upeo wa macho yake.



“Haki vile Rommy amebadilika sana” Cecy aliongea hivyo akiwa bado anaangalia kule gari aliloondoka nalo Rommy lilipoelekea. Jeni aliguna na kusikitika. Kisha akamtaka Cecy waondoke hapo wawahi nyumbani maana wote wanakazi za kuwasaidia wazazi wao kupika chakula cha usiku muda huo.



Wakatafuta usafiri wa Tax ambao utawafikisha haraka nyumbani kwao. Wakajitoma ndani baada ya kuelewana bei na dereva. Wakiwa ndani ya gari. Cecy alizitoa zile hela alizopatiwa na Rommy na kumpatia Jeni Elfu ishirini kisha yeye akabaki na Elfu ishirini huku ile Elfu kumi iliyobaki ikiwa ni ya usafiri waliochukua.



“Dah! Hii hela ningeipata mwanzo si ningechukua ile nguo niliyoiacha kule dukani” Jeni aliongea huku akizifutika zile pesa kwenye mkoba wake. “Inabidi kesho Cecy turudi tena kule nikaichukue ile nguo kabla haijawahiwa” Jeni alizidi kuongea. Alipoona hapati majibu yoyote kutoka kwa Cecy ikabidi amtazame. Akaona Cecy akitabasamu huku akitazama nje. Akasikitika na kumshtua. Cecy aligeuka kule alipo akiwa bado anatabasamu. Jeni alimtazama kwa muda huku akiwa na sura ya umakini.



“Dah! Kuna jambo baya naliona mbele yako. Ila kuliepuka usiruhusu Rommy akaingia kwenye akili yako. Ataharibu kila kitu”



“Kwanini unasema hivyo?” Cecy alimuuliza ila hakuacha bado kutabasamu.



“Kwasababu nakupenda rafiki yangu”



“Hapana. Usifikirie sana. Hakuna kitu kibaya kitakachotokea. Bado nakumbuka ya nyuma” Cecy mara hii aliongea akiwa tabasamu amelitoa kabisa na kuweka sura ya simanzi fulani. Jeni akamvuta kwake na kumpigapiga kwenye bega.



“Dogo naona unatabasamu tu muda wote” Zuma alimuambia Rommy aliekuwa kwenye siti ya pembeni yake.



“Sio kutabasamu tu. Pia ninafuraha kukutana na yule manzi maana kitambo sana”



“Kwani alikuwa demu wako yule ama?” Rommy akageuka kule alipo Zuma na kumtazama.



“Alikuwa demu wangu kweli halafu nikaja kumkataa kwenye mazingira ya ajabu kweli” Zuma alicheka baada ya kusikia kauli ya Rommy.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



ENDELEA...



“Nilijua tu. Haya ni mazingira yapi hayo ya ajabu uliyomkataa nayo?” Zuma aliuliza. Rommy akaachia cheko fupi na kuangalia tena nje.



“Tuachane na hayo broo. Tuendelee na safari”



“Huyu dogo mbona kawaida yake. Huko jijini kwa watu ameshaharibu sana” Paskali nae akitia neno na kicheko kifupi kikatawala kwa wote humo.



“Sasa kama wanajileta wenyewe mimi niwafanye nini? Siwezi kuvumilia upumbavu mimi” Rommy aliongea hivyo na sasa kicheko kikubwa kikafuata. Wote wakacheka.



“Kwahiyo na huyu manzi pia hatobaki salama?” Assu alimuuliza. Rommy akageuza shingo na kumtazama.



“Sikufunzwa kuacha mambo mazuri yanipitie mbali. Nacheza kama Ronaldo. Natikisa nyavu kisha nakimbia kushangilia ushindi nikiwa mbali na goli” Kicheko kikali kikafuata kwa wote wanne kiasi ambacho Zuma alibabaika kidogo na usukani.

“Broo Zuma angalia mbele yasije yakatokea makubwa tukajikuta tunazindukia hospital saa hizi” Rommy aliongea huku akicheka bado na kutazama mbele.



“Ok. Tumuhesabie siku ngapi huyu?” Paskali alimuuliza. Rommy akahesabu vidole vyake mpaka alipofikisha cha saba na kunyanyua mikono yote miwili juu. Kitanga cha mkono mmoja akiwa amevifungua vidole vyote huku ule mwengine akifungua viwili, vitatu akivikunja. Kisha akasema apewe wiki moja tu. Wakacheka tena!.



“Halafu leo nimekuona ukimcheki yule manzi wa pale home kwa matamanio. Vipi, nae yupo katika listi?” Paskali alimuuliza.



“Kwenye listi aliingia tangu namtia machoni kwa mara ya kwanza...” Akatikisa kichwa kama anasikitika. “Nae hana bahati, usiku wake ni ule uliopita ila waleo hachomoi”



“Ila dogo angalia magonjwa usije ukapotea ungali younk bado” Assu alimuonya huku akicheka.



“Magonjwa kitu gani bana! Yameumbwa kwaajili yetu” Rommy alisema huku akitazama nje.



Walifika mwisho wa safari yao na kuingiza gari ndani ya nyumba baada ya geti kufunguliwa. Kama kawaida Rommy hakushuka mpaka pale alipokuja kufunguliwa mlango na Assu. Wakaongozana kuingia ndani. Kama dhamira yake alivyopanga. Alianza kumtafuta Siwema ili aanze michakato ya kumnasa siku hiyo. Katika tafuta yake akagundua Siwema alikuwa jikoni akipika chakula ambacho kingekuwa ni cha usiku.



Akaelekea huko kwa mwendo wa taratibu huku akichezea simu yake. Akasimama upenuni mwa ukuta ambao paliachwa nafasi kubwa ya kupita ikiwa kama uwazi wa mlango. Akasimama hapo kwa muda akimuangalia jinsi Siwema alivyokuwa akihangaika jikoni. Mara huku mara kule. Alihisi rihi ya tofauti ambayo mwanzo haikuwa ikinukia. Akageuka nyuma kutazama ndipo alipogonganisha macho yake na ya Rommy. Akatabasamu na kurudisha sura yake mbele.



“Karibu bosi Rommy” Siwema alisema hayo huku akiendelea na mambo yake. Rommy alipiga hatua fupi fupi mpaka pale kwenye ile sehemu iliyojengewe kwaajili ya jiko. Akageuka kule alipotoka na kurudi nyuma kidogo. Kisha akajivuta juu na kudandia ile sehemu.



“Harufu ya mapishi yako ndio imenivuta mpaka hapa. Sitanii umeukosha moyo wangu kwa mapishi yako. Ni siku ya pili sasa lakini nikila chakula chako najihisi kutoshiba haraka kwa utamu wake. Hakika upo vyema sana. Kwani umesomea vitu hizi?” Rommy alisifia na kuuliza swali. Siwema alikuwa akitabasamu tu huku akiendelea na vitu vyake. Akajibu kuwa hakusomea ni mautundu tu hayo aliyorithi kutoka kwa mama yake.



“Aisee. Sipati picha mama anakuaje ikiwa mtoto ni balaa... Naruhusiwa kuonja ama nitakuwa nina kiherehere cha kula jikoni kama paka wa mjini?” Rommy alitania. Siwema alicheka kisha akamuambia kuwa asiwe na wasi kama anataka kuonja aonje tu. Akamtolea kipande kimoja cha nyama na jiko. Rommy alikichukua kwa viganja vyake na kukipeleka karibu kabisa na mdomo wake. Akaghairisha na kuushusha chini mkono.



“Nitakuamini vipi. Je kama umeniwekea dawa za usingizi? Onja wewe kwanza ndipo nifuatie”



Siwema alicheka baada ya kusikia maneno hayo. Bila kujua kwamba hizo ni hila tu za kijana yule. Akataka kuchukue kipande chengine. Lakini Rommy akamuambia kuwa huo ni uharibifu wa mboga. Akamkata aonje kile kile kipande alichomtolea yeye. Siwema aliona aibu, akacheka huku akitazama chini. Alipoinua sura yake, akakutana na mkono wa Rommy uliomnyooshea kile kipande karibu kabisa na mdomo wake. Akatabasamu huku akimuangalia kijana huyo usoni.



Rommy akatingisha kichwa juu chini akimaanisha afanye hivyo. Siwema akiwa na aibu alipeleka kinywa chake na kung'ata kipande kile sehemu ndogo. Kisha akakitafuna akiwa anacheka, akitazama pembeni huku kinywa chake akikiziba na viganja vyake. Rommy nae akakila kile kipande huku akitabasamu.



“Naweza nikajikuta nakula hapa hapa jikoni kabla ya mezani kutokana na utamu wa mapishi yako. Umfundi sana kwenye mapishi na unaonekana ni fundi pia kwenye mambo mengine” Rommy alizungumza hayo kisha akajiramba vidole vyake. Siwema alimtazama kijana huyo huku akiwa anatabasamu.



“Mambo mengine? Kama yepi?” Siwema alimuuliza. Rommy alitabasamu kisha akajishusha pale juu. Akamtazama mwanadada huyo kwa kitambo kidogo mpaka Siwema akaona aibu na kutazama pembeni.



“I will find you baada ya kula” aliongea hayo na kutoka akimuacha Siwema akimkodolea macho mpaka pale alipopotea kabisa.



Dakika Arobaini na tano mbele walijumuika wote wa nne mezani kwaajili ya kula. Siwema alikuwa akipishana muda wote akiandaa chakula mezani. Mara hii walaji waliwahi kukaa mezani kabla ya chakula kuandaliwa. Macho ya Rommy hayakuacha kumtazama mwanadada huyo kila mara mpaka Siwema akawa anajishtukia kila atazamwapo. Kila macho yao yanapokutana basi Rommy huachia tabasamu na Siwema nae hujikuta akitabasamu.



Baada ya kila kitu kukamilika. Chakula kilianza kuliwa taratibu huku soga zikiendelea. Muda huo Rommy alikuwa mkimya akipanga jinsi gani ya kumuingilia Siwema mpaka akubali. Hapana hawezi kunishinda yule. Alijiwazia mwenyewe. Lazima leo nimdonyoe kivyovyote vile. Paskali alishamsoma Rommy kuwa ana jambo analoliwaza. Hasa awazapo kuhusu wanawake. Ndio alilitambua hilo kwasababu huwa karibu nae kila mara hata awapo shuleni. Akatabasamu na kuendelea kula.



Majira ya saa nne na nusu usiku. Walikuwa wameshamaliza kula na sasa wapo hapo sebuleni wakipiga soga huku wakishushia na shurubati. Akili ya Rommy haikutulia hata kidogo. Alipanga na kupangua mipango yake mpaka pale alipoamua kunyanyuka na kuaga kuwa anenda kulala. Umri wa Siwema haukumpa uguma wa kufanya kama dhamira yake alivyotaka. Maana alishakutana na wenye umri mkubwa kumpita hata Siwema. Sasa iweje ashindwe kwa huyo ambae anaonekana wamepisha miaka minne kama sio mitatu tu?



Miguu yake ilimpeleka mpaka mlangoni kwenye chumba cha Siwema. Akagonga hodi na kusikilizia kwa sekunde kadhaa. Akagonga tena hodi na kuacha baada ya kusikia michakacho ya nyao zikijongea karibu na mlango huo kwa ndani. Mlango ukafunguliwa na Siwema aliekuwa ndani ya vazi jepesi la kulalia ambalo kuanzia kiunoni aliongezea na kanga baada ya kuona vazi hilo lisingemtosheleza kumsitiri kwenye macho ya huyo mgongaji.



Rommy alimtazama kuanzia juu mpaka chini kisha akarudisha tena macho yake juu kilipo kifua cha Siwema. Matiti ya wastani yalikuwa yakionekana kwa urahisi kutokana na vazi hilo kuonya. Akameza funda la mate na kumtazama usoni. Akamuomba kukaribia ndani na Siwema alimpisha. Moja kwa moja mpaka kitandani. Akakaa. Siwema alirudishia mlango wake na kwenda kukaa kwenye kiti cha mbao kilichokuwa humo.



“Bilashaka ulikuwa ukijiandaa kulala ama sivyo?” Rommy alianzisha maongezi baada ya kimya kifupi kupita. Siwema aliitikia kwa kichwa kukubali.



“Nilikuambia nitakutafuta baada ya kula. Ama ulisahau?” Rommy alimuuliza tena. Siwema alitabasamu na kuangalia pembeni. Akiwa bado ameangalia pembeni, akajibu kuwa hakusahau ila alidhani kuwa Rommy ameghairi kumtafuta. Rommy akatabasamu baada ya kuona kumbe ahadi yake Siwema alikuwa akiikumbuka muda wote.



“Mbona umekaa mbali hivyo? Umekisaliti kitanda chako. Ama mimi ndio nimeharibu pozi?” Rommy aliongea hayo. Siwema akajibu hapana. Rommy akasema kama ni hapana basi asogee pale kitandani. Siwema alitabasamu. Tabasamu ambalo lilielekea kucheka. Hakujua asogee ama aendelee kubaki pale pale. Rommy alijiongeza na kumfuata pale alipo. Akamshika mkono na kumvuta mpaka kitandani kama Ngamia apelekwae kisimani kwaajili ya kunywa maji.



Rommy akapenyeza mkono wake kwenye kiuno cha Siwema na Siwema asilipinge hilo. Hana kasheshe huyu. Alijiwazia. Akamvuta kwake na kupeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Siwema. Bila pingamizi. Bila ubishi. Wakanyonyana mate kwa sekunde kadhaa. Kisha hapo Rommy akamlaza Siwema kitandani na kufanya kile kilichotawala kwenye bongo zao. Walifanya nini?

Haijulikani!.



Majira hayo hayo upande wa Cecy alikuwa kitandani kwake. Alionekana kuwa na mkanganyiko wa mawazo yaliyotawala ubongoni mwake. Alikuwa yupo juu ya kitandani chake amejilaza chali huku akishikilia simu yake kwa mikono yote miwili. Alikuwa akiitazama kila mara kama imeingia ujumbe au hata japo ‘missed call’ Kutoka kwa Rommy.



Kitendo cha kukutana na Rommy kwa siku hiyo. Kilimchanganya sana kiasi ambacho fikra zote zilikuwa kwa kijana huyo. Hata yeye hakuelewa nini kimemkuta ama kinataka kumkuta. Au nataka kumpenda tena? Alijiuliza. Hapana! Haiwezekani. Na Ramah nae? Ramah ananipenda sana ila Rommy aliniumiza. Kweli simpendi. Tena simpendi. Atabaki kuwa rafiki tu. Lakini ni kwanini sasa mawazo mengi yapo juu yake. Au kwavile sikumuona kitambo. Pengine ni hivyo. Aliendelea kujiwazia mwenyewe. Kisha akaitazama tena simu yake. Nampenda sana Ramah na yeye ananipenda pia. Akaiweka simu pembeni na yeye akajilaza pembeni.



Mara kidogo simu yake ikaita. Akakurupuka na kuichukua haraka. Akatazama ni nani ampigiae na kukuta ni Ramah. Akashusha pumzi na kuipokea. Wakasalimiana na kujuliana hali. Kisha Ramah akamuuliza mbona tangu asubuhi alivyomtafuta na yeye hakumtafuta tena. Cecy akababaika kidogo kisha akajitetea kuwa amechoshwa na mizunguko aliyoifanya kwa siku hiyo.



Ramah akampa pole na kumuacha apumzike maana aliamini ni kweli huenda amechoshwa na mizunguko ya siku hiyo kama alivyomuaga asubuhi ya siku hiyo kuwa ataenda kufanya ‘Shopping’. Ukweli ni kwamba. Cecy hakuchoshwa na mizunguko ya aina yoyote kama alivyosema. Bali ni mawazo juu ya Rommy ndio yaliyomfanya hata asiyafurahie sana maongezi yake na Ramah. Alitaka muda mzuri wa kumfikiria Rommy bila kujua ni kwanini amekuwa hivyo.



Lakini Rommy aliniumiza, sasa kwanini namfikiria namna hii? Aliendelea kujiuliza. Alitamani walau angetumiwa tu ujumbe wa kutakiwa usiku mwema na kijana huyo ili aipate namba yake. Akajuta kwanini na yeye hakuchukua namba yake huenda asingepata tabu kumfikiria muda huo. Au nimekosea kumtajia namba? Alijuliza. Hapana bwana namba ni ile ile yangu ndio niliyomtajia. Sasa kwanini hanitafuti? Akaguna. Lakini mi simpendi.. Ndio, simpendi tena.



Akawaza kumpigia simu Jeni amuelezee hayo lakini aliona Jeni hatoweza kumpa ushauri wowote zaidi atamkera tu na kusababisha wagombane. Sasa ni nini afanye ili aache kumfikiria Rommy? Maana hata usingizi uligoma kumchukua muda huo. Akaonelea ampigie simu Ramah huenda mawazo ya Rommy yanaweza kumuondoka. Akampigia!.







ENDELEA..



Wakati ambao Cecy anamfikiria Rommy mpaka kukata shauri ya kumpigia simu Ramah. Upande wa Rommy ndio walikuwa wakimaliza kipindi cha kwanza. Walijinyanyua wote na kwenda kuoga pamoja kama mke na mume. Siwema hakujali ukubwa wake kwa Rommy. Wala Rommy hakuwaza umri wake kwa Siwema. Wote walionana sawa ilimradi watimize kile kilichoamuriwa na fikra zao. Walipotoka chooni. Wakarudi tena kitandani kwaajili ya kumpumzika kidogo kabla ya kuendelea tena.



________



Majira ya saa nne asubuhi. Ndio muda ambao Rommy alifumbua macho yake kutoka katika usingizi mzito. Mwili wote aliuhisi kuwa na uchovu. Alijiinua kiuvivu pale kitandani na kukaa. Akainuka na kuvuta nguo zake kisha akazivaa. Punde Siwema aliingia. Macho yao yalipogongana, Siwema aliwahi kuyapeleka pembeni maana alihisi aibu kutazamana na kijana huyo. Akamuambia kuwa chai ilikuwa tayari muda mrefu na hapo alikuwa akisubiriwa yeye tu.



Akashukuru na kutoka nje akimuacha Siwema akifanya usafi humo chumbani kwake. Rommy aliingia kwanza chumbani kwake kwenda kujifanyia usafi kabla hajaenda mezani kupata staftahi. Dakika kumi na tano mbele alitoka akiwa yupo safi. Aliwakuta wakina Paskali wakicheza game pale sebuleni. Akawasalimu na kukaa.



“Mbona hamkunywa chai hadi sasa?” Aliwauliza. Zuma akajibu kuwa walikuwa wakimsubiria yeye.



“Hapana bana. Hi nini sasa? Inamaana mi nisipokula na nyie hamtokula? Mambo haya siyapendi ila ndio hivyo tu Father anataka. Hata kile kitendo cha kufunguliwa mlango kwenye gari sikipendi hamjui tu. Ule ni utumwa usio na maana. Nyie ni kaka zangu na sio vijakazi wangu. Ila kwavile tupo mbali nae. Tuyaache kwanza yale mambo. Tuishini kama ndugu tu maana mi nd'o napenda iwe hivyo... Twendeni basi tukapate chai”



Rommy aliongea kwa hisia kudhihirisha kuwa amechukizwa na kitendo ambacho wakina Paskali walikifanya. Kitendo cha kumsubiria yeye mpaka aamke ndio wapate kifungua kinywa hakukipenda. Ama kile cha kufunguliwa mlango kwenye gari akitaka kuingia ama kushuka pia hakukipenda. Alidai maisha hayo yanatakiwa yafanyike huko Nairobi ambapo alikuwapo baba yake mdogo ambae ndie alikuwa akimlea na sio huku ambapo yupo mbali nae.



Wakaelekea wote mezani. Vyakula vyote vilikuwa tayari vipo mahala hapo vikisubiri walaji tu. Wakafunua ma_Hot Pot yaliyokuwa juu ya meza hiyo na kila mmoja alijipakulia alichoona kipo sawa na uwezo wake wa kula.



“Dogo leo umechelewa sana kuamka” Paskali alianzisha maongezi. Wote wakatabasamu.



“ Si unajua siku hazilingani” Rommy alisema.



“Dhamira imetimia. Naona umeamkia chumba cha jirani. Sijui jana usiku usingizi ulikulevya mpaka ukakosea chumba” Paskali alizungumza. Rommy aliacha kula na kucheka sana huku akisaidiwa na wenzake kucheka. Alipopunguza kucheka. Aliwaambia waache kwanza soga waendelee kula kisha mambo mengine yatafuata baadae. Maana anaweza akafa mtu kwa kupaliwa. Wakakaa kimya na kuendelea kula.



Majira ya mchana. Jeni alikuwa nyumbani kwa kina Cecy. Alienda hapo kwasababu ya kusukwa nywele zake. Wakati wanaendelea kusukana, pia walikuwa wakipoga soga zao. Muda wote Cecy alikuwa akiwaza kumuelezea Jeni yale yaliyomkuta usiku uliopita ya kumuwaza Rommy kwa kitambo kirefu. Hata hivyo hakupata nafasi ya kuongea kutokana Jeni alikuwa akiongea sana.



“Rommy hajanitafuta mpaka sasa tangu jana alipochukua namba yangu” Cecy aliongea hayo baada ya Jeni kutulia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Hivi Cecy. Si unampenda Ramah?” Jeni alimuuliza. Cecy akajibu kuwa anampenda tena sana.



“Sasa kwanini unataka kumuingiza tena Rommy. Ama hukumbuki alichokufanyia?”



“Jenii! Kwani nimesema nataka nirudiane na Rommy? Kwanza Rommy simpendi bado nakumbuka alichonitendea. Sasa nitamtaka vipi?”



“Najua Cecy. Naelewa mtu anapopenda anakuwaje. Huwezi amini jana nilikaa nakufikiria wewe tu. Ishara mbaya niliziona tangu tulipoonana na Rommy kule Mkwabi. Kama si kuwaza kurudiana nae, basi ushampenda upya. Nakujua Cecy. Msingi nilikupokea mwenyewe. Na sio wewe tu hata yeye. Mwanzo wenu naujua vyema, kwahiyo hunidanganyi kitu”



------------





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog