Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

JERAHA LA MOYO - 3

 








Simulizi : Jeraha La Moyo

Sehemu Ya Tatu (3)







Tutudi miaka nane iliyopita. Kipindi ambacho Anita anahamia katika mtaa wa Mikanjuni akitokea kule alipokuwa akiishi na mume wake Ally kabla ya kifo chake. Kutokana na kufidia kiasi kadhaa cha pesa alichoacha mumewe. Aliamua amuhamishe binti yake Cecy kule alipokuwa akisoma shule ya kulipia na kumpeleka katika shule za serikali. Akiwa anatafakari ampeleke binti yake shule gani. Ndipo alipoona itakuwa vyema kama mwanae atasoma karibu na wanapoishi.



Shule ya msingi Mikanjuni aliona itafaa zaidi. Akafanya yote yanayotakiwa na Cecy akaanza kusoma katika shule hiyo akiwa darasa la tano. Ilikuwa ni ngumu kwake kuanzisha urafiki na wanafunzi wenzie. Lakini ikawa tofauti baada ya kupata mwanafunzi aliemzoea kwa muda mfupi ambae alikuwa ni Jenifa. Urafiki wao ukaanza siku hiyo ya kwanza Cecy kufika shuleni hapo.



Wakazoeana na kupendana. Wakawa wakishirikiana wote kwenye mambo mbalimbali. Urafiki wao ulikuwa zaidi mpaka kwa wazazi wao. Wakajikuta na wao wakizoeana kwa kuunganishwa na watoto wao. Kwenye mambo tofauti walishirikiana mpaka wakajihisi ni ndugu sasa na sio urafiki tena.



Miaka miwili mbele wakiwa darasa la saba kwenye miezi ya mwanzo mwanzo. Darasani kwao walipokea ugeni wa mwanafunzi mpya. Alitambulishwa na mwalimu wao kwao kwa jina la Rommy Antony Magasa. Wakasisitizwa kushirikiana nae kwenye masomo kama wafanyavyo wao. Kisha hapo Rommy akatafutiwa nafasi ya kukaa darasani humo. Dawati ambalo alipangwa. Lilikuwa jirani na dawati waliokuwa wakikaa Cecy na Jeni.

Tuendelee kuwamo kwenye kisa hiki huenda tukajua Rommy alitokea wapi na kwanini ahamishiwe hapo akiwa darasa la saba.



Kutokana na ukaribu wa madawati yao. Basi urafiki na mabinti wale ulijengeka haraka kuliko wanafunzi wengine. Rommy alikuwa ni muongeaji sana japokuwa alikuwa ni mgeni. Wiki chache alizokuwa hapo shule alijizolea marafiki wengi kutokana na tabia yake ya uongeaji.



Cecy alitokea kumhusudu sana kijana huyo. Mara nyingi alipenda kuwa karibu nae kiasi ambacho hata Jeni alionekana kumsahau. Hata hivyo Jeni hakuona tofauti yoyote kwasababu hata yeye alimhusudu pia kijana huyo. Wote wakawa karibu na kijana huyo.



“Huwezi amini Jeni. Sasa hivi najiona ninafuraha sana nikiwa karibu na Rommy hata sijui kwanini” Cecy aliongea hayo majira hayo wakiwa wanatoka shuleni kurudi makwao.



“Sio wewe tu. Mbona wengi hufurahi wakiwa karibu nae. Unajua Rommy ni mtu wa tofauti sana. Kwanza hapendi makuu, kila mmoja anazungumza nae, tena vyema tu. Kwasababu...”



“Sawa. Lakini kwangu ni tofauti. Sifurahii tu ukaribu wake. Pia najihisi kumpenda ati” Alimkatisha Jeni kwa kusema hayo. Jeni alimtazama usoni kwa mastaajabu..



“Unataka kuniambia na wewe unampenda? Mbona mtoto wa watu atakoma!.” Cecy alimtazama kwa mshangao. Akamuuliza ana maanisha nini kusema hivyo. Jeni akamjibu ni wanafunzi wengi wa kike wanasema kama asemavyo yeye kuwa wanampenda. Cecy akatulia kimya akifikiri hayo.



“Lakini mimi nampenda na nina imani na yeye ananipenda pia” Cecy aliongea.



“Sawa. Jitahidi” Waliachana hapo na kila mmoja akaelekea kwao.



Tangu siku hiyo alipoambiwa na Jeni kuwa wapo wengi wanaompenda kijana huyo. Cecy alihakikisha anakuwa karibu zaidi na Rommy ili kutowapa nafasi hao wengine wanaomtaka kijana huyo. Kila mahali anapokuwa Rommy alihakikisha Cecy nae alikuwapo. Kitendo ambacho Rommy hakukielewa mwanzo ila alipokuja kufanya uchunguzi wa chini chini. Akagundua kuwa Cecy alikuwa akimpenda.



“Mwanangu yule demu naona anakushobokea sana. Vipi demu wako nini?” Mwanafunzi mmoja wa kiume alimuuliza Rommy hayo walipokuwa darasani katika makundi waliyopangwa watatu watatu kwaajili ya kufanya kazi waliyoachiwa.



“Demu gani huyo?” Rommy nae aliongea huku akiacha kuandika na kumuangalia mtu huyo.



“Si Cecy bwana. Mbona unajifanya majinuni?” Rommy akacheka na kuwaambia kuwa mwanamke huyo hana mahusiano nae yoyote zaidi ya urafiki tu. Wakaguna huku wakimtazama Rommy kwa macho ya kumtahariza.



“Naona mwenetu sasa unatufanya sisi watoto. Hatupo hivyo bwana, sote wakubwa hapa, kwahiyo usitudanganye. Halafu chondechonde na demu wangu naona anakushobokea pia” Yule mwanafunzi anaekamilisha utatu wao nae aliongea.



“Abiria chunga mzigo wako. Yeyote yule atakaeingia kwenye kumi na nane zangu hatobaki salama. Kwahiyo lawama sipendi” Rommy aliongea na wote wakacheka.



Siku mbili mbele Rommy alijitoa kimasomaso kumtongoza Cecy. Halikuwa swala gumu sana kukubaliwa kwasababu hata Cecy alikuwa akisubiria hayo. Ukurasa wa mapenzi kwa wawili hao ukafunguliwa huku Rommy akimtaka Cecy awe msiri na jambo hilo. Kwanini awe msiri wa mapenzi hayo? Jibu ni jepesi tu ni kwamba Rommy alitaka kuwanasa wengine kama yeye. Cecy hakujua hilo, alichodhani yeye ni kwamba, pengine Rommy anahofia kujulikana mapema na walimu. Akawa msiri!.



Cecy alijitapa kwa Jeni kuwa ameshamnasa Rommy. Jeni alimpa hongera rafikie kwa kufikia hatua hiyo. Cecy alikuwa na wivu si mas'hara kwa Rommy. Kiasi ambacho muda mwingi aliutumia kuwa karibu nae ili kutowapa nafasi wengine. Kitendo hicho kilikuwa kikimkera sana Rommy. Hakupenda kubanwabanwa namna hiyo. Akampiga marufuku Cecy kuwa wasiwe karibu sana wawapo shuleni akitumia hila ya kutotaka kugundulikana. Cecy akakubali ila kwa shingo upande.



Ni tabia ya wakora kuwa na mwanamke kwa ajili ya kumjua kiundani kisha hapo anamtelekeza kama sio kumkataa kabisa. Rommy aliomba penzi kwa Cecy jambo ambalo lilikuwa gumu sana kwake. Maana hakuwahi kufanya kitendo hicho hata mara moja. Hata pale Rommy alipomuambia jambo hilo. Alimzungusha ikiwa anatafakari kuwa ni sahihi ama si sahihi kufanya kwa wakati huo.



Alimuelezea jambo hilo Jeni huku akimtaka ushauri juu ya hilo. Hata Jeni alikuwa ni mgeni huko, sasa ni vipi ampeushauri wa kukubali? Mwanzo alimshauri aachane na kitendo hicho ila baada ya Cecy kumsumbua sana. Alimuambia akili kichwani mwake kwasababu kwa umri aliokuwa nao. Alikuwa akijua walau baya na zuri. Kutokana na ushauri huo Cecy akapanga kutokukubali.



Rommy alipoona swala lake limepitishwa kushoto. Akatikisa kibiriti kwa kumuambia Cecy aachane nae maana hawezi kuwa na mpenzi asie na faida kwake. Mwanzo Cecy alidhani ni utani ila baada ya kupita kwa siku kadhaa na kuona Rommy hana shuhuli nae. Ndipo alipomaizi kuwa kijana huyo hakutania alipomuambia aachane nae. Sasa ni vipi aachane nae ilhali akiwa anampenda?? Akapitisha wazo la kukubali lakini iwe ni mara moja tu.



Akamtafuta Rommy na kumueleza kuwa amekubali lakini kwa sharti la kufanya mara moja tu. Huna kazi wewe. Rommy alijiwazia huku akimtazama binti huyo alieongea huku akiwa na aibu kuzungumza jambo hilo. Mipango ikapangwa ‘chap chap’ na Rommy ikiwa ni kutafuta geto la kufanya kitendo hicho. Alijua kivyovyote kwa umri waliokuwa nao, hawatoweza kuruhusiwa kuingia nyumba za wageni.



Harakati za kutafuta geto zilifanikiwa baada ya mchezo wao kudhaminiwa na rafiki yake aliempata hapo hapo shuleni. Geto likapatikana ikawa inasubiriwa siku husika. Rommy alimueleza Cecy kuwa siku ya tukio ni siku inayofuata. Hakuwa na la kupinga. Atapinga vipi ilhali amekubali mwenyewe? Akawa mpole!.







Siku ya tukio ilipofika. Cecy akahitajika magetoni. Alifika mahala hapo akiwa na uoga mwingi si kidogo. Hakuwahi kufanya. Hakufikiria kufanya kitendo hicho wakati huo. Mwanzo alitaka kughairi ila alipokumbuka kuwa hakulazimishwa na mtu. Akawa mpole na kufuata vyote Rommy alivyokuwa akitaka.



Mchezo ukaanzwa huku mgeni akiwa ni Cecy na mwenyeji akiwa ni Rommy. Cecy alileta usumbufu kiasi ambacho alimkera Rommy. Alikasirika na kutaka kumfukuza ndani humo. Cecy akawa mpole tena na mchezo ukaanzwa upya baada ya ule wa mwanzo kuvurugika.



Nusu saa mbele matokeo yalionekana baada ya shuka lililotandikwa kubadilika rangi na kuloa damu. Damu zilikuwa ni nyingi kiasi ambacho Cecy aliogopo. Si yeye tu. Hata Rommy pia aliingiwa na mchecheto baada ya kuona damu kwenye siri za Cecy ikizidi kutoka. Cecy alikuwa akilia huku akimlaumu Rommy kwa kitendo alichomfanyia. Ukweli ni kwamba. Pamoja na Rommy kutokuwa mgeni kwenye masuala hayo. Lakini hakuwahi kumtoa kigoli yoyote usichana wake.



Cecy ndio alikuwa wa kwanza na kwavile alishazoea kufanya na wale ambao walikuwa wenyeji kwenye mambo hayo. Hata kwa Cecy alifanya vivo hivyo na kupelekea kumpa maumivu mengi sana. Kilio cha Cecy kilimchanganya sana. Akamuambia asubiri hapo atarejea punde tu. Cecy akamuuliza huku akilia kuwa anaenda wapi. Rommy alimuambia asubiri kisha akatokomea nje.



Dakika kumi alirudi na vidonge fulani ambavyo vilikuwa ndani ya kipakti kidogo. Akamtaka anywe vidonge hivyo. Cecy akahoji ni vya nini na Rommy alijibu kuwa ni kwaajili ya kupunguza maumivu. Cecy akavichukua na kumeza akishushia na maji. Dakika ishirini mbele maumivu yalikata kabisa huku damu zikikoma kutoka. Uafadhali kwenye mwili wake aliusikia kwa kiasi fulani. Ikawa rasmi Cecy ameupoteza usichana wake!. Siku hiyo ikapita!.



Alivyosema atafanya siku moja alikuwa akijidanganya. Maumivu yalipokata kabisa. Rommy akamuomba warudie tena kwa mara ya pili na iwe ndio ya mwisho. Mwanzo alikataa ila baadae alikubali baada ya kulazimishwa. Mchezo ukaridiwa tena. Ikiwa uwanja ni ule ule badamu yake yalipomwagika mwanzo. Siku hiyo ikaisha na mazoea yakajengeka. Mara ya pili, ya tatu mpaka ya nne na kuendelea.



Rommy akanza kujitapa kwa marafiki zake. Jeuri ikamvaa na isijulikane ilipotekea. Dharau za chini chini Cecy alizivumilia huku akijitahidi kujinyenyekeza kwa kijana huyo. Matusi na kashfa zilimtoka kijana huyo kwa Cecy kuwa hajui kitu. Sasa atajuaje ikiwa ni yeye mwenyewe ndie aliemuingiza katika ulimwengu ule? Amakweli akufukuzae hakuambii toka!.



Cecy akawa ni mtu wa kulia kila mara huku kimbilio lake kuu ni kwa Jenifa. Jeni alimpoza kwa kumuambia atajaribu kumtafuta Rommy na kumueleza hayo. Akamuuliza hakuna pahali alipomkosea na Cecy akajibu kuwa hakuna. Alimuambia amejitahidi sana kujinyenyekeza kwake lakini imekuwa ni kazi bure tu. Jeni akamuambia asijali. Atamueleza Rommy na anaamini atamuelewa tu. Hata pale Jeni alipomtafuta Rommy na kumueleza maumivu ayapatayo rafiki yake juu yake. Chaajabu, Rommy alimtongoza na yeye!.



Hii sasa noma. Jeni aliwaza. Haki vile Rommy sio mtu. Yani ustaarabu wote ule kumbe ndivyo alivyo? Haya nimuambie nini huyu ni shosti? Aachane nae tu? Hapana! Cecy hawezi nielewa. Akarudisha majibu kwa Cecy kuwa Rommy hakutaka kumsikiliza huku akificha kile kitendo cha kutongozwa na yeye. Maana alijua atamzidishia maumivu rafikiye ama wagombane kabisa.



Cecy akajiahidi kupambana mwenyewe mpaka amuweke Rommy sawa. Hata hivyo nafasi ya kuzungumza na kijana huyo ikawa ni finyu kupatikana. Kila alipomtafuta alimbiwa kuwa hakuwa na muda wa kuzungumza nae labda amtafute muda mwengine ama siku nyengine. Cecy alivumilia lakini mambo yakawa yale yale. Uvumilivu ukamshinda, akamtafuta kijana huyo siku moja wakiwa darasani ikiwa ni muda wa mapumziko. Alitaka kujua nini hatma yake kwake maana amekuwa hamuelewi siku hizo.



“Bilashaka wewe ni mlemavu wa akili haki vile. Inamaana kusoma hujui hata maandishi huoni..?” Rommy alimvunjia uvivu na kumchana ukweli. “Muvi imefika mwisho ama huoni maandishi? Kwanza siwezi kuwa na mtu kama wewe kwasababu huna hadhi ya kuwa na mtu kaka mimi. Usinione nimekuja kusoma kwenye hii shule yenu ukadhani mimi ni maskini kama wewe pangupakavu tia mchuzi. Ugali wa dona mboga mbirimbi. Mi sio wa maisha ya chini kama unavyoniona ni hiyo mitihani tu tahira wewe. Kwanza sikukupenda hata kidogo ni shobo zako ndio zimekuponza. Halafu na uzuri wote uliokuwa nao kumbe kitandani hovyo tu kama gogo la buchani. Hutikisiki mpaka usogezwe. Sidhani kama wewe ni mzawa wa mji huu maana upo tofauti na wenzako. Jitahidi utaaibika” Rommy aliongea hayo kisha akampush kidogo Cecy na kuondoka hapo akiufuata mlango kwenda nje. Alipofika mlangoni. Akageuza na kurudi pale alipomuacha Cecy. Akamsogezea uso karibu kabisa na uso wake. “Usipende kujirahisisha kwa mwanaume hata kama unampenda kiasi gani. Vinginevyo utatafunwa na kutemwa kama Big G” Akatabasamu na kupotea ndani ya darasa hilo akimuacha Cecy akibung'aa.



Hivi kweli ni mimi? Alijiuliza. Akapepesa macho na kujaribu kuyafikiria maneno ya kejeli aliyoambiwa punde na Rommy. Hapana Rommy hawezi kunifanyia hivi mimi. Chozi la uchungu likamtoka. Hakuweza kulifuta maana hakuwa na ujasiri wa kunyanyua hata viganja vyake vya mikono. Akatikisa kichwa kuweka akili yake sawa na kuutazama mlango ambao Rommy alipita hapo.



“Kwanini iwe hivi? Kwanini Rommy anifanyie hivi mimi? Hata kama hanitaki lakini sio kunikashfu hivi? Aargh! Najuta. Najuta” Cecy alishindwa kuvumulia na kujikuta akilia kwa uchungu. Kamasi jepesi lilimtoka kwenye pua yake. Machozi yalimtiririka pasi na mfano. Akajilaza kwenye dawati lake na kuendelea kulia mwenyewe.



Jenifa aliingia humo darasani ambapo hapakuwa na yeyote zaidi ya Cecy ambae amejiinamia kwenye dawati akilia. Alimfuata mpaka pale na kumuinua kichwa. Hata hivyo Cecy alirudisha tena kichwa chake pale kwenye dawati. Ikabidi Jeni amuulize kulikoni. Huku akilia alimueleza yote yaliyomtokea. Jeni hasira zilimshika lakini hata hivyo hakuwa na chakufanya ikiwa alishamuonya kabla rafikiye juu ya kijana yule.



“Sasa Cecy huwezi kukaa hapa darasani ukiwa katika hali hiyo. Acha nikakuombee ruhusa kuwa unaumwa ili uende nyumbani ukatulize kwanza akili”



Jeni aliongea hivyo na kutoka nje. Alifika katika ofisi ya walimu na kumfuata mwalimu wao wa darasa na kumueleza kuwa Cecy alikuwa akiumwa sana. Bila kuhoji sana akatoka nae mpaka darasani. Mwalimu wao alishuhudia hali ya Cecy na kuamini ni kweli alikuwa akiumwa. Akawapa ruhusu wote wawili ikiwa Jeni amsindikize Cecy mpaka nyumbani kwao. Jeni akabeba mabegi yao wote na kumuongoza Cecy kutoka nje ya darasa hilo.



Huko nje kila mwanafunzi aliepishana nao aliuliza kulikoni na Jeni akawajibu kuwa Cecy alikuwa akiumwa. Pole zikatoka huku wakimsikitikia bila kujua ukweli wowote. Jeni alimpeleka Cecy mpaka nyumbani kwao ambapo Anita mama yake Cecy hakuwepo nyumbani hapo muda huo. Ikawa afadhali kwa Cecy maana hakujua angejibu nini ikiwa mama yake angemuuliza sababu ya kurudi shule mapema. Hata hivyo alipanga amuambie kuwa anaumwa kama alivyowaaminisha wanafunzi na mwalimu wake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Lakini Cecy nilikuambia rafiki yangu. Rommy sio mtu mzuri yule. Mi nilishamshuhudia mara kibao kule nyuma chooni akifanya uchafu na wanafunzi wakike. Nikikuletea taarifa zake unaniona mimi mbaya” Jeni aliongea hayo baada ya kuwa wameshaingia ndani ya nyumba hiyo na hapo walikuwa chumbani kwa Cecy.



“Japokuwa wanasema mapenzi upofu lakini wewe umezidi ndugu yangu. Jimtu ushaliona linatabia mbaya. Lina kudharau na kukukashfu kadri anavyojiskia, lakini ndio kwanza hukomi. Unazidi kujipendekeza kwake”



“Lakini mbona unanilaumu Jeni, kwani mi nilipenda iwe hivi?” Cecy aliongea kwa kulalamika huku vichozi vikitoka kwa mbali kwenye macho yake.



“Acha nikulaumu kwasababu nilishakuambia tangu mwanzo. Tena bahati nzuri sio mimi tu niliekuambia hayo. Sophi, Scola hata Minah wote walikuambia lakini ukatuona kama vile tunataka kukuingilia kwenye mambo yako. Haya sasa leo kimekukuta. Kashakufanya anavyotaka. Amekugeuza alivyoweza. Anakujua nje ndani, leo ndio kaamua akudhihirishie kwamba hakupendi. Kakukashfu sasa unalia kama mtoto. Hujui tu jinsi roho inavyoniuma. Yani naona kama nimefanyiwa mimi vile. Haya mapenzi gani hata mwezi hayajafikisha anakutaka kingono nawe hukushtuka tu. Mwenzangu unakuja kuniomba ushauri nakukataza kumbe ulikuwa tayari ushaamua na pale ulikuwa ukinichora tu. Mkafanya kimya kimya na sasa matokeo yake ndio haya. Dah! Cecy hujui tu ninavyoumia. Yani ningekuwa na uwezo sijui ningemfanya nini yule chakaramu” Akamalizia na msonyo kisha akabeba begi lake na kuondoka mahala hapo. Ukweli Jeni alikuwa amechukizwa na kitendo hicho. Chuki juu ya Rommy ikajengeka kwenye moyo wake. Cecy alikuwa akimuangalia tu Jeni jinsi anavyoondoka akiwa na hasira. Akalala chali kitandani na kuvuta mto akiufunika kwenye uso wake.



Siku zilikatika huku Cecy na Rommy wakiishi kama walikuwa hawajuani. Rommy hakuwa na haja tena na Cecy huku Cecy akiigiza kitu hicho ila ukweli ni kwamba, alikuwa akitamani hata walau amsemeshe kijana huyo. Roho ilikuwa ikimuuma kila akimuona Rommy na mwanafunzi yeyote wa kike nje ama ndani ya darasa.



Japo aliumizwa huku akitukanwa matusi na kashfa kibao. Lakini bado alikuwa akimpenda kijana huyo. Hata yeye hakujua ni kwanini alikuwa namna ile. Alitamani walau japo Rommy ampe salamu tu ili nafsi yake iridhike. Lakini ndio kwanza Rommy kama alilijua hilo. Alimfungia vioo binti huyo popote pale watakapoonana ama kupishana kwa bahati mbaya.



_________



Siku moja walichanganywa darasa lao na darasa jengine ambalo lilikuwa ni ‘B’ huku lao likiwa ni ‘A’. Waliambiwa waende darasa hilo ‘B’ kwaajili ya kwenda kufundishwa pamoja somo la Historia. Walifundishwa huko mpaka pale kipindi kilipoisha wakaruhusiwa kurudi darasani kwao ikiwa ni kwa yule aliemaliza kuandika. Rommy aliinuka pale alipokaa kwasababu yeye alishamaliza kuandika. Cecy alipomuona Rommy ameinuka kwaajili ya kurudi darasani kwao. Akamalizia kuandika haraka na kuinuka kwenda huko na yeye.



Kitendo cha kuingia kwenye darasa lao. Alimfuata Rommy aliekuwa akipanga madaftari yake vyema kwenye begi lake. Akamfuata kishari shari huku akimpigia siyahi za kumlaumu kwanini amemuharibia usichana wake kisha amkashfu na kumkejeli achilia mbali kumtusi. Rommy alimtazama kwa mshangao binti huyo. Kisha macho yake akayapeleka mlangoni ambapo kulikuwa kuna baadhi ya wanafunzi wengine walikuwa wakiingia humo. Suburi nimuonyeshe huyu. Akajisemea!.



“We demu vipi? Nikuambie mara ngapi kuwa sikutaki? Achana na mimi malaya mbovu. Mtoto wa kike kujirahisisha kwa wanaume. Unadhani stori zako sina kwamba ni hodari wa kutongoza wanaume. Umenikosa mama mimi sio kama hao. Halafu huenda ukawa na magonjwa yako unataka kushea na wengine. Unaonekana mpoole halafu kumbe machepere. Kwataarifa yako sichiziki na ‘body’ hilo. Halafu mi sitongozwi na wanawake bali mimi ndio natongoza wanawake. Fala wewe, tena nitokee mbele yangu nisije nikauchafua uso wako” Rommy aliongea hayo kisha akamsukuma Cecy na kwenda kuparamia dawati lililokuwa nyuma yake na kwenda chini moja kwa moja. Ebwana ee!.



Wanafunzi wote walioshuhudia kitendo hicho midomo yao ilibaki wazi kwa taharuki huku wakiwa hawaamini. Rommy akawapita pale mlangoni kwa hasira na kutokomea nje ya darasa hilo. Wanafunzi wale walimuangalia kisha wakarudisha macho yao kwa Cecy aliekuwa pale chini akijizoazoa huku akilia. Wooote wakaamini kwamba Cecy alimtongoza ama alikuwa anamtongoza Rommy pale. Maana hata uharaka wake kule darasa ‘B’ alioondoka nao waliuona baada ya Rommy kutoka tu.



Hata pale walipokuwa karibu na darasa hilo wakitaka kuingia ndani humo. Walisikia siyahi za Cecy ila hawakuelewa nini kinaendelea mpaka pale walipoingia na kushuhudia kwa macho yao. Hata Jeni aliwapo kwenye kundi lile. Pengine yeye ndie aliestaajabu sana kuliko hata wale wengine. Hakika roho ilimuuma sana baada ya kuona rafiki yake akidhalilishwa vile mbele za watu.



Akapiga hatua za haraka haraka mpaka pale alipo Cecy akijizoazoa kuinuka. Akamsaidia kuinuka na kutoka nae nje. Vifijo na vicheko vilisikika kutoka kwa wanafunzi wale wakati Cecy akitolewa nje na Jeni huku akilia. Wanafunzi walizidisha vicheko huku wakipiga kelele za shangwe huku wengine wakipiga madawati kwa furaha. Hata wale ambao walichelewa pia walipewa taarifa hizo na kushangaa sana. Mwisho wakacheka kwa dhihaka huku wahusika wenyewe wakiwa hawapo.







Jeni siku hiyo hakutaka kuaga kwa yoyote. Alimkokota hivyo hivyo Cecy mpaka nyumbani kwao ambapo waliingia chumbani kwake. Cecy alikuwa akilia sana kiasi ambacho ndio alikuwa akimzidishia uchungu Jeni aliekuwa akimtazama kwa hasira. Akataka kuongea kitu ila koo lake likagoma kutoa ushirikiano. Hakika hasira alizokuwa nazo hazikuwa na mfano. Akaja kuongea baada ya dakika moja alipopata afadhali kidogo.



“Sijawahi kukutukana ila leo acha tu nikutukane. Rafiki yangu wewe ni hovyo sana. Haya nikipi kimekuwasha ukamfuata yule shetani? Nilijua tu maana hata ile ondoka yako pale darasani ilikuwa inakitu. Haya ulikuwa unataka ukamuambie nini? Akakut**e tena ama? Haki leo umeniudhi sana. Mbona unakuwa limbukeni namna hiyo? Unajifanya kumpenda sana yule fala. Haya sasa amekudhalilisha kwa mara ya pili. Ya kwanza ilikuwa siri ukaona haitoshi ukatafuta nyengine ya dhahiri. Mbona unalia sasa? Kama unampenda sana kufa basi kwaajili yake. Kufa sasa, jinyonge tujue kwamba unampenda sana. Acha ujuha yule ni mwanaume akiamua kukudhalilisha hata dakika haiishi. Ona sasa umedhalilika hata sijui sura yako utaiweka wapi maskini. Haki vile umejidhalilisha sana ndugu yangu. Sio wewe tu hata mimi pia umenidhalilisha. Ikiwa amekusema kwa tabia ile aliyokuzushia si hata mimi pia nitaonekana natongoza wanaume? Eeee maana wanasema ukitembea na mwizi na wewe pia ni mwizi. Haya sasa wote kuanzia sasa tunaonekana tunadanga. Aargh Cecy umeniudhi hujui tu. Yani sijui nikudhihirishie vipi huu uchungu nilio nao. Umekuwa mpumbavu si kidogo. Na leo kakufanyia hivi kesho utamfuata tena ukamuambie nakupenda. Jinga sana wewe” Jeni alimaliza hivyo na kutoka ndani ya chumba hicho. Nia yake ni kurudi shule akalete vurumai kwa Rommy.



Hata pale alipoingia darasani alikuta wanafunzi wote wakiongelea jambo hilo lilotokea punde tu. Walipomuona akiingia wote wakakaa kimya huku wakimtazama. Jeni aliangaza macho yake darasa zima ila hakufanikiwa kumuona Rommy. Akasonya na kuliendea dawati lao. Akabeba begi lake na la Cecy na kuanza kutoka darasani humo. Minong'ono na vicheko vya chini chini vilimsindikiza mpaka pale alipopotea kabisa kwenye upeo wa macho yao.



Alifika nyumbani kwa kina Cecy kwania ya kumpelekea begi lake. Mlango wa chumba cha Cecy aliukuta ukiwa umefungwa kwa ndani. Hakujisumbua kugonga. Akaweka begi la Cecy mlangoni kisha akaondoka zake kuelekea kwao.



Tangu siku hiyo ikawa haziivi kati ya watatu wale. Yani Rommy na Cecy na Jeni. Jeni alikuwa akimchukia Rommy kuliko hata Cecy alivyomchukia. Hakumpenda na alimuombea mabaya popote pale alipomuona. Japo mwanzo walipata aibu sana kutazamana na wanafunzi wenzao. Lakini hakuna marefu yasio na ncha. Hata hivyo iligundulika ile ilikuwa ni hila tu ya Rommy ya kumtema Cecy ila si kweli kwamba Cecy alikuwa akimtongoza Rommy. Hata hivyo bado Cecy alipata aibu nyengine ya kuchezewa na kutemwa na kijana huyo.



Hiyo ilikuwa ni miezi ya mwisho mwisho ya kufikia mtihani wa mwisho wa darasa la saba. Siku za mitihani zilipokaribia. Rommy aliondoka na kwenda kufanya mitihani kwenye shule aliyotoka kama sheria inavyotaka huku akiacha jina na historia kubwa kwenye shule hiyo baada ya kutembea na wanafunzi kadhaa wa shule hiyo na hata wa shule ya jirani ambao walikuja kujijua mwisho kabisa wa mchezo.



___________



“Najua Cecy. Naelewa mtu anapopenda anakuwaje. Huwezi amini jana nilikaa nakufikiria wewe tu. Ishara mbaya niliziona tangu tulipoonana na Rommy kule Mkwabi. Kama si kuwaza kurudiana nae, basi ushampenda upya. Nakujua Cecy. Msingi nilikupokea mwenyewe. Na sio wewe tu hata yeye. Mwanzo wenu naujua vyema, kwahiyo hunidanganyi kitu”



“Lakini Jeni unanionea tu. Mi sikusema hivyo kwa nia yoyote ya tofauti” Cecy alijitetea.



“Ok. Umesema hivyo ili iweje? Si ili akupigie simu muendeleze kama sio kuanza upya yaleyaliotokea miaka ile? Cecy nakuona ukiingia pabaya ndugu yangu. Kwanza mtu mwenyewe amesema amekuja huku likizo sijui ni mwezi mmoja amba ni miwili. Sasa kama ukianzisha nae mapenzi huoni kama atakuacha tu vile vile? Kwanza kwanini uanzishe nae mapenzi. Kwani hukumbuki alichokufanyia? Unataka akufanyie tena kama alivyokufanyia miaka ile? Sikushauri kabisa umchanganye Ramah na yule mbwa” Jeni aliongea kwa hasira. Cecy akabaki kimya asijue aongee nini. Hata kumsuka Jeni aliacha mpaka pale alipokumbushwa.



Walipomaliza kusukana. Walihamia sebuleni ambapo waliweka muvi kwenye luninga na kuangalia. Muda wote Cecy alikuwa akiyakumbuka maneno aliyokuwa akitolewa na Jeni. Hata yeye hakujua ni kwanini alikuwa akimfikiria sana Rommy ilhali alikuwa akikumbuka yote aliyofanyiwa nyuma na kijana huyo. Lakini kwanini inakuwa hivi? Au ndio nampenda tena? Hapana siwezi kumpenda yule nakumbuka bado alichonifanyia. Cecy aliwaza.



Wakati wanaendelea kuangalia muvi ile. Simu ya Cecy ilitoa mlio wa kuingia ujumbe. Akaichukua na kutazama. Akakuta ni upande wa mtandao wa Whatsapp. Namba ilikuwa ni ngeni na kwenye ‘Profile’ kulikuwa na picha ya bendera ya Tanzania. Akaguna na kuufungua ule ujumbe.



‘Habar’ Ulisomeka hivyo. Salama tu’ Akajibu. ‘Rommy hapa. Ofcoz she's cute Cecilia??’ Cecy moyo ulimripuka na asijue kama ni hofu ama furaha. Akamtazama Jeni na kumuona akiwa bize na Luninga. Akatuma emoje zinazotaharuki ama kushangaa. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio na asijue ni kwanini. ‘Nini mrembo?” ‘Siamini kama ni wewe. Embu nitumie pic zako’ Akatuka ujumbe huo. Sekunde kadhaa picha za Rommy zikamiminika kwenye simu ya Cecy. Picha ambazo alizipiga katika sehemu tofauti. Jamani Rommy ni mzuri sana. Cecy aliwaza hayo akiwa anatazama picha hizo moja baada ya nyengine.



Upande Rommy alikuwa bize na simu yake ilhali jamaa zake kama yeye mwenyewe alivyopenda kuwaita wakiwa bize na Game pale sebuleni. Kipindi ambacho anamtumia picha zake Cecy baada ya kuziomba. Alikumbuka kuangalia ‘Profile’ ya Cecy. Aliibonyeza ile picha iliyokuwa eneo lile na kuitazama. “Mmmh!” Akaguna.



Akaisogeza simu yake karibu kabisa na macho yake. Akaitazama vizuri. Huyu mtu... Alijiuliza. Ni nani huyu? Mbona kama.... Akashtuliwa na sauti ya Paskali aliemuita huku akicheka. Akamtazama.



“Rommy nilikuambia huyu hana kitu ajuacho. Embu shika padi wewe tulisongeshe” Rommy aliinuka huku akicheka na kwenda pale kwenye vile viti ambapo mbele yake kulikuwa na ‘Screen’ inayoonyesha mchezo ule.



Upande wa Cecy aliona Rommy akiwa ametoka ‘Online’ ghafla tu. Akachukizwa na kitendo kile na kujikuta akisonya kwa nguvu. Jeni alishtuka na kumtazama. Akamuuliza kulikoni mbona anasonya? Akajibu kuwa kuna mtu amemuudhi. Jeni hakutaka kuhoji sana, akaachana nae na kuendelea kuangalia luninga.



Majira haya yalimkuta Ramah akitoka huko atokako akielekea maskani kwake anapopaki. Kufika tu akapata abiria mwengine alietaka apelekwe Mwahako. Akampakia na safari ya kwenda huko ikaanza. Dakika kumi na mbili ziliwatosha kufika huko. Ramah akalipwa na kugeuza pikipiki kurudi kule alipotoka.



Hata hivyo hakuona sawa kwenda tena maskani ilhali Mama yake alishamtaarifu kwenye simu kuwa chakula kilikuwa tayari. Moja kwa moja mpaka nyumbani kwao. Aliikuta pikipiki ya Jay nje akajua kivyovyote Jay lazima awepo hapo. Akapaki ya kwake na kuingia chumbani kwao ambapo alimkuta Jay akila chakula ambacho kilikuwa ni ugali na samaki mkubwa aliekaangwa vyema huku pembeni yake kukiwa na kibakuli chenye mchuzi wa samaki kama yule aliekaangwa lakini huyu aliungwa vizuri hadi pakapatikana rosti ya mchuzi.



Ramah hakumsemeza kitu badala yake alichukua bakuli la maji kwaajili ya kunawa. Akatoka nje kwenda kunawa. Akarudi na kuweka bakuli pembeni kisha yeye akakaa juu ya kitanda. Muda wote Jay alikuwa kimya akifuatilia akifanyacho Ramah mpaka pale alipotaka kupeleka mkono kwenye kisahani kilichokuwa na yule samaki. Jay aliunyaka mkono wake ukiwa bado unaelea na kumtazama usoni kisha akamuambia hakukuwa na shea yake hapo.



“Mjinga kumbe unaroho mbaya namna hii?” Ramah alimuuliza akiwa anamtazama usoni huku akitabasamu. Jay akakata kipande cha samaki kwa kutumia mkono wa kulia ikiwa wa kushoto bado umeushikilia mkono wa Ramah. Akabugia kile kipande na kumtazama Ramah usoni.



“Hakuna shea yako hapa. Tusivurugane saa hizi” Jay aliongea hayo na kuutupa mkono wa Ramah pembeni. Ramah aliinuka pale kitandani akiwa anasikitika. Akatoka nje huku akinung’unika kuwa anaishi na mtu mwenye roho mbaya. Akaongeza kuwa inaweza ikatokea siku akamuwekea sumu kwenye chakula. Jay alicheka baada ya kusikia maneno ya Ramah.



Muda kidogo Ramah alirudi akiwa amebeba sahani kubwa kiasi yenye sahani ndogo yenye ugali na kibakuli chenye mchuzi kama ule wa Jay. Pembeni kukiwa na kisahani kidogo chenye samaki mkubwa kama yule wa Jay. Ramah aliviweka pale pale mezani alipokuwa anakula Jay. Huku akipiga mluzi na usieleweke ni wa nyimbo gani. Akatoka nje na aliporudi alikuwa amebeba kifuko cheusi.



Akakiweka pale mezani na kukifungua. Harufu ya nyama za kukaanga ikazitesa pua za Jay. Kama Ramah alijua vile. Akazitoa zile nyama kwa madaha na kuziweka ndani ya lile sahani kubwa lililobeba vile vyakula vyake. Zilikuwa ni nyama nyingi za kukaanga za kuku wa nyama ambazo nyingi zilikuwa ni vipaja.



Taratibu alianza na kidali na kukibugia chote kinywani huku akimtazama Jay aliekuwa akimtazama yeye kwa jicho pembe. Nyama ile haikumpa shida kutafuna kwasababu haikuwa na mifupa migumu. Akaendelea kula taratibu na kwa maringo huku akiwa anaweka mifupa ya zile nyama karibu kabisa na upande aliokuwa akila Jay.



Hizi sasa kusudi. Jay aliwaza huku akimtazama Ramah kwa matamanio. Lakini nimejiharibia mwenyewe huenda kulikuwa na shea yangu hapa. Dah cheki mjinga anavyotafuna ile nyama. Jay alijiwazia huku akimtazama Ramah kwa macho ya matamanio. Ramah alimpiga jicho na kumuona Jay alikuwa akimtazama yeye. Kwa makusudi kabisa akachukua kwa mkono wa kushoto kipaja cha ile nyama huku wakulia ukiwa na kipande chengine. Akazila kwa zamu huku akizitazama kwa sifa zile nyama. Jay mate yalitaka kumtoka kinywani akawahi kuyameza.



Hawezi kuzimaliza zote zile nyama, lazima abakishe tu. Acha nile taratibu. Jay aliwaza huku akitazama mikono ya Ramah inavyopishana kupeleka zile nyama kinywani kwake. Ukisikia kula ugali kwa harufu ya samaki anaekaangwa jirani ndio huku sasa. Aliwaza kisha akameza funda kubwa la mate ya uchu.



Upande huu yakiendelea haya. Upande wa Cecy mambo hayakuwa mambo hata kidogo. Muda wote alikuwa akiwaza ni kwanini Rommy ametoka ‘Online’ ghafla namna ile. Kila mara alikuwa akiingia katika mtandao wa WhatsApp akiangalia kama atakuwa amerudi ama laa!. Baada ya kuwaza Rommy atakuwa ametoka kabisa ‘Online’. Akaona amtumie ujumbe kwa sms za kawaida. ‘Vipi? Mbon umetok Online?’.



Muda huo huo simu yake ikaita. Akatazama ni nani ampigiae na kukuta ni Rommy. Akajitoa mahala pale akimuacha Jeni akiangalia bado luninga. Akaenda chumbani kwake na kujifungia mlango. Akapokea simu huku akijilaza kitandani. Kwanza alianza kwa kuuliza kwanini Rommy ametoka ‘Online’. Rommy akamjibu kuwa kuna kazi alikuwa akiifanya muda ule.



“Unajua vyenye nimekumisi Cecy. Then nikitambo hatujaonana. So i have many things to talk with you. Kama itawezekana tukaonana leo itakuwa good sana” Rommy aliongea hayo kwa lafudhi ya ki Kenya. Haikujulikana kama alikuwa akiigiza ama ndio uongeaji wake. Lakini kama haigizi ni vipi siku mbili hizi tangu tumjue alikuwa akiongea vyema tu?. Cecy alitulia kimya akifikiria ombi la kijana huyo. Ilimchukua sekunde kadhaa kuwa kimya mpaka pale Rommy alipomgutusha tena.



“Vipi Cecy? Ama leo it can‘t be?”



“Unajua nini Rommy....”



“Subiri mara moja” Rommy alimkatisha Cecy alichokuwa anataka kusema na kuongea yeye. Kisha akakata simu. Dakika mbili simu ya Cecy iliingia ujumbe. Akaufungua na kukuta ni muamala wa pesa uliofanywa na Rommy. Kilikuwa ni kiasi cha shilingi Elfu Arobaini alizotumiwa. Papo hapo simu yake ikaita tena na kuipokea.



“Tumia kama nauli kiasi hicho na kama hakitoshi nijulishe. Nitakucheki baada ya nusu saa nikujuze where we will meet” Rommy aliongea hayo na Cecy hakuwa na budi kukubali. Simu ikakatwa na Cecy akashusha pumzi.









Mkono wa Cecy bado ulikuwa umeigandisha simu kwenye sikio lake japo ilishakatwa kitambo. Hakuelewa! Hakujielewa amekuaje. Alihisi kuchanganyikiwa na asijue chanzo ni nini. Pengine ni kukutana kwake na Rommy ndio kunapelekea kumchanganya. Lakini ni kwanini achanganywe na jambo hilo?. Kwani ni mara yake ya kwanza kukutana na kijana huyo?.



Simbiko haisimbuki ila kwa misukosuko. Hakika Cecy kuna kitu kilikuwa kikimsumbua kwenye nafsi yake. Upendo wake kwa Rommy ulianza kuchipua upya ndani ya mtima wake. Akasahau alichotendewa na jamali huyo miaka kadhaa nyuma hata kugeuza ule ubaya kuwa ni wema. Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.



Hata hivyo bado nafsi yake ilimsuta kwa kutaka kumsaliti Ramah. Sasa ni vipi amfikirie Rommy ilhali Ramah alikuwa akimpenda sana? Na hata yeye yuatambua hilo. Upendo kwa Rommy alikuwa nao kwa kusuasua. Ilihitajika mtu amjaze kichwa kidogo tu nae ajae huku akifutilia mbali kebehi na dhihaka zilizomtumbukiza kwenye kisima cha udhalili pasi na mdhalilishaji kujali lolote mpaka utengano wao.



Cecy alishusha simu taratibu kwenye sikio lake na kuitambaliza kwenye shavu akiipitisha upende wa kidevu mpaka kwenye paja lake. Tafakuri nzito zilipishana kwenye ubongo wake kiasi ambacho yalimpelekea maumivu ya kichwa yaliyokuwa yakianza taratibu. “Nimekuwaje mimi?” Alijiuliza kwa sauti. Hata yeye alijishangaa!.



Akiwa katika hali isiyoeleweka. Simu yake iliingia ujumbe kwa kutoa sauti ya alam aliyoiweka. Sauti ambayo ilimshtua kiasi kana kwamba ilikuwa ni ya ajabu ama yenye kuogofya na kuleta hofu nafsini. Akaitazama simu yake iliyokuwa kiganjani kwake kwa muda utadhani ilikuwa ni mpya na ndio mara yake ya kwanza kuishika. Kisha akaufungua ujumbe ule uliotoka kwa Rommy. ‘10 na nusu njoo Capchino Restaurant barbara ya 9 plz’ ujumbe ulisomeka hivyo.



Akaurudia kwa mara nyengine kuusoma kana kwamba hakuuelewa vyema. Akahamisha macho yake kutoka kwenye simu mpaka mahali ulipo mlango. Jeni alikuwa ameingia humo ndani. Walikuwa wakitazamana kama mahasimu wa siku nyingi wenye vita visivyoeleweka mwanzoni wala mwishoni.



“Haya mwanadada umenikimbia kule ukaja kujifungia huku. Vipi? Unaumwa?” Jeni alimuliza. Cecy aliekuwa akimtazama, aliacha kumtazama na kuitazama simu yake. Akazifuta zile jumbe zote alizotumiana na Rommy.



“Yeah! Kichwa nakisikia kinagonga kwa mbali. Ila itakuwa ni cha mpito tu” Cecy alijibu. Muongo huyu. Jeni aliwaza. Alikuwa akimtazama bado Cecy machoni. Kitendo ambacho kilimfanya Cecy ayaangalize macho yake kwenye simu.



“Pole bi dada. Acha nielekee home mama ameniita anataka kutoka. Naenda kuwa mlinzi wa nyumba”



“Ok. Mi nipo hapa napumzika kidogo pengine kinaweza kukoma”



“Mi nikadhani labda tunaenda wote”



“Acha nipumzike. Baadae nitakucheki, wangu” Jeni akajibu sawa na kuondoka.



Cecy akabaki mwenyewe akiendelea kutafakari yanayomuhusu. Kuna muda alijishauri asiende kule Rommy alipomtaka aende. Ila pia akaonelea aende akasikilize ni nini kijana huyo atamuambia. Ila kama atanitongoza nitamkatalia. Aliwaza. Akaangalia saa kwenye simu yake na kukuta ni saa kumi kamili. Acha nijiande muda huu. Alijisemea na kuinuka pale kitandani.



Saa kumi na dakika arobaini na mbili, alikuwa nje ya mgahawa huo baada ya kushuka kwenye usafiri uliomleta. Alikuwa akiangaza macho yake huku na huko mahala hapo. Kisha hapo akatoa simu yake na kumtumia ujumbe Rommy kumjuza kuwa ameshafika mahala hapo. Dakika moja majibu ya ujumbe wake yakarejeshwa ya kwamba. Aingie ndani ya mgahawa huo na aagize chochote akitakacho wakati akiendelea kumsubiri yeye aliekuwa njiani anaelekea mahala hapo.



Cecy alijibu sawa na kuingia ndani ya mgahawa huo. Alikuwa akishangaashangaa mandhari ya humo ndani maana hakuwahi kuingia ndani ya mgahawa huo zaidi ya kuuona kwa nje tu. Akatafuta sehemu na kukaa. Punde muhudumu alifika pale na kumtaka aagize anachotaka. Sekunde kadhaa ziliyeyuka akiwa anafikiria na mwisho alimtaka yule muhudumu amletee shurubati ya aina yoyote.



Nisije nikapoteza muda hapa halafu huyu mtu asitokee. Cecy aliwaza huku akiangalia mlangoni ambapo kulikuwa na watu wengine waliokuwa wakiingia hapo. Ila hao hawakuwa ni wale aliokuwa akiwasubiria yeye. Muhudumu alirudi tena akiwa amebeba shurubati ya embe iliyokuwa ndani ya glasi ya dongo. Akaweka juu ya meza kisha akamkaribisha mteja wake na kuondoka.



Cecy aliivutia karibu yake ile glasi na kuipiga pafu kidogo ile shurubati. Ladha tamu na safi ikatamalaki kwenye ulimi wake kabla kinywaji kile hakijapita taratibu kwenye koo lake na kuteremkia tumboni. Akaigida tena kinywani mwake shurubati ile huku akitazama mlangoni. Akawaona jamaa wawili wakiingizana ndani ya mgahawa huo. Mmmh! Hawa watu mbona kama nawafahamu? Akajiuliza huku akiinua shingo yake kuwatazama vizuri.



Kabla hajawafikiria vizuri, Rommy aliingia ndani ya mgahawa huo. Cecy akatabasamu na kusahau kabisa juu ya wale jamaa walioingia punde tu ndani humo. Walikuwa ni walinzi wa Rommy ndio ambao Cecy alihisi kuwafahamu. Rommy alipiga hatua fupi fupi mpaka pale kwenye ile meza aliyokuwa amekaa Cecy. Akasimama huku akitabasamu na asiongee chochote.



Cecy alianza yeye kusalimia maana Rommy alikuwa kimya akimuangalia yeye akiwa anatabasamu tu. Rommy aliikataa salamu ile kwa kutingisha kichwa kwenda kulia na kushoto. Cecy akatahamaki asielewe ni nini anamaanisha kijana huyo. Rommy akamuambia kuwa alitaka kumbato lake kama lile alilompatia siku iliyopita wakati wanaonana. Cecy alicheka huku akiangalia chini kwa aibu.



Rommy akapiga hatua moja mbele na kuuvuta mkono wa Cecy ambae nae alivutika bila shida mpaka akasimama na kumbato likafuata. Wazee walisema. Ukiona zinduna, ambari ipo nyuma. Rommy hakuona aibu kufanya kitendo hicho mahala hapo ambapo kulikuwa na watu wengi kiasi, ilhali aibu ilimvaa Cecy aliemkumbatia Rommy huku akiwa amefumba macho yake. Watu hoa waliokuwa mahali hapo waliwatazama kwa muda mfupi na kuendelea na yao. Ukitazamana na mwenye chongo, fumba lako jicho.



Cecy alijitoa kwenye kumbato la Rommy baada ya kuona kijana huyo hakuwa akifikiria kumuachia kwa wakati huo. Cecy akarudi alipokaa na Rommy akavuta kiti na kukaa. Macho yao yaligongana na Cecy akahamisha haraka na pembeni. Muhudumu alifika hapo na kumtaka Rommy aagize. Rommy akamuambia Cecy aagize chakula chochote akipendacho. Cecy aligoma kwa madai ya kuwa ameshiba na hakuhitaji kula tena.



Rommy alimgeukia muhudumu na kumtaka awapatie orodha ya vyakula vinavyopatikana hapo. Muhudumu akawataka subira na kuondoka. Aliporudi alikuwa na karatasi ngumu yenye orodha ya vyakula. Akawawekea mezani na kuwataka wachague. Rommy akamsogezea ile karatasi Cecy na kumuambia achague chakula akipendacho. Cecy hakuwa na jinsi, aliivuta ile karatasi na kuanza kusoma vyakula. Dakika moja akamuonyesha yule muhudumu. Rommy nae akasema aletewe chakula kama alichoagiza Cecy. Muhudumu akaondoka na kuwaacha wenyewe wawili.



Waliendelea na soga wakati wanasubiria oda yao. Mara kadhaa Cecy alipokuwa akinywa ile shurubati yake Rommy alikuwa akimtazama kiasi ambacho Cecy aliona aibu na kuamua kumuuliza ni kwanini alikuwa akimtazama vile. Rommy aliendelea kumtazama huku akitabasamu kama vile hakusikia kile alichoulizwa.



“Naionea wivu hiyo glasi inavyogusana na lips zako mpaka kupelekea mimi kusisimkwa na mwili kana kwamba ni mimi ndie nimepata bahati hiyo” Cecy alicheka huku akitazama pembeni kwa aibu. Akataka kusema kitu, ila alighairisha baada kuona muhudumu akirejea mahala hapo akiwa na vyakula walivyoagiza. Vyakula vikawekwa mezani na muhudumu yule akawakaribisha kisha akaondoka zake.



Waliinuka na kwenda sehemu ya kunawia mikono kwaajili ya kuvishambulia vyakula vile. Waliponawa wakarudi tena mezani kwao. Rommy alitulia mpaka pale Cecy alipoanza kula nae ndio akala. Muda wote Rommy alikuwa akila huku akimuangalia Cecy usoni kitendo ambacho kilimyima uhuru Cecy na kumfanya awe ni mwenye aibu muda wote.



“Unajua Cecy umebadilika sana ila kuna vichache havijabadilika” Rommy alianzisha soga baada ya kimya kirefu kupita.



“Vipi hivyo ambavyo sijabadilika?” Cecy aliuliza huku akimtazama kijana huyo muda huo alikuwa ameinamia sahani yake iliyo na chakula.



“Kama ulavyo, ama ukicheka na uongeaji pia vyote ni vile vile viuvutiavyo moyo wangu tangu kipindi kile” Cecy alicheka na kumfanya Rommy azidishe tabasamu zaidi usoni kwake.



“Mbona hata wewe kuna vitu hujabadilika zaidi umeongeza utashi tu” Cecy aliongea. Rommy alicheka cheko fupi kisha akachukua kipande cha ndizi kilichopikwa kwa ustadi mkubwa na kukitia kinywani.



“Oohhh! Nimekumbuka kitu. Kwenye ‘profile’ yako ya WhatsApp umeweka picha fulani. Hivi unaweza ukaniambia yule ni nani?” Rommy alibadili mada kwa kuingiza swali hilo. Cecy alimeza kile alichokuwa anatafuna muda huo na kujibu kuwa yule ni rafiki yake.



“Inaonekana ile picha ni ya kitambo sana eee?” Rommy alimuuliza na Cecy akaitikia kwa kichwa kukubali.



“Ok. Anaitwa nani?” Rommy alimuuliza. Cecy akataka kuhoji kwanini anauliza maswali yote hayo. Ila akaghairi na kuamua kumjibu tu.



“Anaitwa Ramah...” akaongeza akidhani ndio utakuwa mwisho wa maswali ya Rommy. “Ile picha aliipiga muda sana” Rommy akatingisha kichwa juu chini akimaanisha amemuelewa vyema Cecy.



“Yule wa kwenye ile picha kuna mtu amefanana nae sana anaitwa Rafael. Ni kitambo pia” Rommy aliongea hayo. Wakati anamaliza maneno yake alimuona Cecy akiwa ametaharuki si kidogo huku akimtazama yeye kwa mshangao.



“Mbona unanishangaa hivyo? Kunani?” Rommy alimuuliza hivyo baada ya kuona Cecy ameshtuka alipomtajia jina la yule aliekuwa akimfananisha yeye.



“Mbona hata yeye anaitwa Rafael. Hilo la Ramah amepewa tu kama ‘nickname’. Kwani unamfahamu?”



“Yeah! Na sio kumfahamu tu. Pia ni ndugu yangu. Ni muda sasa hatujaonana” Rommy aliongea hayo huku akimtazama Cecy aliekuwa amepagawa zaidi baada ya kumuambia hayo.



“Unataka kuniambia wewe na Ramah ni ndugu kabisa ama ndugu kivipi?” Cecy alimuuliza Rommy hayo akiwa ameacha kabisa kula akimtazama usoni akiwa na kiroho cha kutaka kujua undugu wa Rommy na Ramah ulivyo kama Rommy alivyosema.



“Yes! Ni ndugu kabisa. Ndugu kwa baba. Tumechangia baba. Ameanza yeye nikafuatia mimi. Kwahiyo ni kaka yangu yule” Cecy aliona dhahiri akichanganyikiwa huku akiwa haelewi ama haamini anachokisikia. “Kwani unapafahamu kwao? Maana nakumbuka walikuwa wakiishi mtaa flani unaitwa Duga” Cecy alishusha pumzi na kujibu kuwa ndio anapafahamu na anapoishi mtu huyo ni hapo hapo.



“Ok. Tuachane na hayo” Rommy alisema kisha akanywa kinywaji chake. Alipoitua glasi akamtazama Cecy na kumuona akiwa tofauti na vile akivyokuwa mwanzo. Cecy alipoona anatizamwa, akazuga kwa kutabasamu na kuendelea kula.



“Cecy..” Rommy aliita. Cecy akamtazama usoni huku akitafuna chakula kinywani kwake kwa madaha. Rommy akaendelea. “Usiku wa leo tunaweza kuwa wote?” Cecy akashtuka. Akamkazia macho Rommy huku akiacha kutafuna. Rommy akatabasamu na kukitazama chakula chake. Aibu!. Aliingiwa na aibu ndio kwa yale aliyomfanyia mnyange huyo miaka kadhaa nyuma. Na leo hii anamchombeza tena kimapenzi. Sasa aeleweke vipi?.



“Kivipi?” Cecy alimuuliza huku akiwa bado anamtazama Rommy usoni. Hakuwa akitabasamu wala kucheka. Na haikujulikana kama amechukizwa na maneno hayo ama vipi?. Rommy alikuwa akigonga gonga kijiko kwenye sahani taratibu huku akiwa anaangalia sehemu hiyo utafikiri kuna jambo ama miujiza yanaweza kutokea hapo. Baada ya sekunde kadhaa akaacha kugonga na kuinua kichwa kumtazama Cecy. Uso ulisawijika kwa haya na asijue aanze ama aongee lipi? Akashusha pumzi nzito na kusema.





http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Najua Cecy. Najua nimekukosea sana na bado unakumbukumbu ya yale yaliyotukia nyuma. Ila tambua kupotea njia ndio kujua njia. Nilipotea kipindi kile na nimekuja kugutuka nikiwa nishafika mbali zaidi. Natambua nilikosea sana kiasi ambacho naona haya sasa kukutazama usoni. Nimeamini ni heri kujikwaa kidole kuliko ulimi. Niliukwaa ulimi wangu mpaka sasa nashindwa kukuomba msamaha kwa haya iliyonivaa usoni. Naona haya hata kutazamana na mboni zako, naona zikinisuta kwa yale niliyoyafanya nyuma pasi na kufikiri yatakayotukia mbeleni. Wazee wetu walisema. Ukibomoa daraja, ujue kuogelea. Hakika nimebomoa daraja ilhali kupiga mbizi simjuvi. Thamani yako sikuiona kipindi kile nikakuchukulia kama tunda ndizi. Nimelivua maganda na kula kilicho ndani yake kisha nikatupa maganda kwenye jaa chafu bila ya kukumbuka kuwa bila ganda, ndizi isingekuwa na thamani yoyote. Nimekuja kutambua thamani yako pindi nilipokuwa mbali nawe. Nikajuta na kujilaumu huku nikiuchonyota moyo wangu kwa uchungu mithili ya mnyama apitishiwae kisu shingoni...” Rommy akafuta chozi lililokuwa likitoka kwenye jicho lake moja wakati akiyaongea hayo. Akaendelea. “Cecy funika kombe mwanaharamu apite. Naumia kila nikikumbuka yale mpaka nahisi sitahili kuketi meza moja na wewe kama hivi. Nimekuwa mdogo mithili ya mdudu chungu mbele yako, hata kunena vyema nashindwa nahisi kinywa kimekuwa kizito kwa soni iliyoigubika sura yangu. Hata ukinisamehe sidhani kama utarudisha wajihi na kuniamini tena kama mwanzo kiasi cha kunikabidhi usichana wako niutoe, tena kwa maumivu huku mimi nikichekelea kama mkufunzi Juha asiejua awafunze nini wanafunzi wake. Dah! Haki vile damu ya bikra yako ilinitesa na itaendelea kunisulubu kama usipopitisha msamaha juu yangu kwa niliyoyafanya kipindi cha nyuma. Hakika nilijizaini mwenyewe kukufanyia ubaya bila kujua kama utakuja kunitesa mwenyewe huku ukiniacha na maumivu makali ambayo hata nikipigi siyahi kubwa la namna gani kukuomba msamaha nitaonekana kama mwendawazimu fulani asiemaizi chochote hata mawio na machweo pindi yajiripo. Cecy muungwana akikosea huomba kusemehewa. Naomba unijumuishe kwenye kundi la waungwana kwa kuupokea msamaha wangu kwa mikono miwili na utambue bado nakupenda japo nilikufanyia ubaya zamani. Nisamehe Cecy wangu”



Rommy aliongea kwa taratibu mithili ya mtuhumiwa aombae msamaha mbele ya mahakama. Alikuwa akiongea huku akibubujikwa na machozi hali ambayo ili uteteresha moyo wa Cecy ambae hakuwa akijua mpaka muda huo achukue maamuzi gani. Alimtazama Rommy ambae alikuwa mnyonge kama kinda la ndege lililofiwa na wazazi wake huku akibubujikwa na machozi, viganja vyake amevifunganisha kwa mbele ishara ya kuomba msamaha.



“Hivi unajua Rommy kwamba ulinidhalilisha sana? Unajua kama uliniacha na maumivu makali zaidi ya yale niliyoyapata wakati ukinitoa usichana wangu? Unajua kwamba nilikuchukia sana kiasi ambacho nilikuombea mabaya? Unajua kama sikutaka kumuamini mwanaume mwengine yoyote kwa upumbavu wako ulionifanyia? Nadhani yote hayo huyatambui, na kama ni hivyo basi ndio nakuambia sasa. Haukufananiana kabisa na yale uliyoyafanya kipindi kile hata kidogo. Sura yako ya upole, maneno yako ya ucheshi na matendo yako mazuri uliyoyaonyesha mwanzo ndio ilikuwa kigezo kilichopelekea kukupenda na kukuamini. Lakini kumbe yote hayo yalikuwa ni maigizo tu ili kuziteka fikra za wengi na kuuteka moyo wangu dhalili ambao haukuwa ukijua nini maana ya kupenda kabla. Haukuwa ukijua maumivu ya kutendwa kabla. Ila kwa bahati mbaya nikakukabidhi wewe na bila kujali lolote ulipofanikisha uliyoyataka ukaniacha tena kwa udhalili mkubwa...”



“Najua Cecy na ndio maana nikaomba msamaha kwa yale niliyoyatenda kwako. Nakiri ilikuwa ni utoto tu ule ndio ulionisumbua kiasi cha kukufanyia vile. Ila now nimekuwa na nipo ithibati kiakili hata matendo pia na ndio maana nakiri kwako kwamba nimekosa na nahitaji msamaha wa dhati” Rommy alimkatisha na kumuambia hayo.



Cecy hakuwa na chakusema kwa wakati huo. Alikuwa kimya akitafakari hayo. Hakuwa na maamuzi sahihi kwa wakati huo. Akisema amsamehe Rommy ni dhahiri ndio mwanzo wa kufufuliwa lile penzi la miaka hiyo lililokufa kwa chuki. Sasa ni nini afanye? Akatae kusamehe? Hapana! Hata moyo wake ulishamsamehe muda mrefu lakini kutoa msamaha kwa kudhihirisha kwa mdomo ndio ilikuwa shida kwake.



Akataka kuomba muda afikirie swala hilo. Lakini ni swala gani la kuomba muda wa kufikiria? Kutoa msamaha? Hapana! Halikuwa la kufikiria hilo. Lilikuwa ni papo hapo adhihirishe kwamba amesamehe ama laa!. Rommy akauvunja ukimya kwa kumuomba tena msamaha Cecy na kumuomba ampe nafasi nyengine kwenye moyo wake.



“Rommy nimekusamehe. Lakini.....”



“Asante Cecelia kwa kunihurumia na kuamua kupitisha msamaha wa dhati juu yangu. Kwa kudhihirisha furaha niliyokuwa nayo. Twende kwenye gari kuna zawadi nikakupatie”



Rommy alimkatisha Cecy sentensi yake na kumueleza hayo. Cecy alitabasamu kisha akainuka baada ya kuona Rommy ameinuka kwaajili ya kwenda huko kwenye gari. Wakaanza piga hatua ndogo ndogo kutoka humo. Muhudumu aliewahudumia alipoona wateja wake wanatoka pasi na kufanya malipo. Akawafuata kwa mwendo wa haraka. Ila kabla hajawafikia, aliitwa na Paskali aliekuwa amekaa na Assu kwenye meza nyengine pembeni kidogo na ile waliyokuwa wamekaa wakina Rommy. Akajitambulisha kuwa amekuja na vijana wale na yeye ndie mwenye jukumu la kulipa vile walivyotumia. Akamtaka aeleze ni kiasi gani wametumia vijana wale na yule muhudumu akamtajia huku akishusha pumzi za hofu maana alidhani anaibiwa. Paskali akafanya malipo ya kina Ramah na yao vile walivyokuwa wakitumia wao pale kisha muhudumua akaondoka.



“Cecy wangu kukudhihirishia kuwa nimefurahi kwa kuutoa msamaha juu yangu na kuamua kusahau yote yaliyotokea nyuma. Nakupatia zawadi hii iwe kama ufunguo upya wa penzi letu. Naomba uipokee bila kujali udogo wake” Rommy aliongea hayo na Cecy hakuwa na cha kupinga wala kupangua. Akatulia kimya akisubiri aone ni zawadi ya aina gani atapatiwa.



Rommy alitoa ribbon kwenye mfuko wake wa jinzi aliyoivaa. Ilikuwa ni ya dhahabu inayomeremeta kwa upya wake, iliyochorwa herufi mbili ‘R $ C’ kwa upande wa juu. Rommy aliomba mkono wa kushoto wa banati huyo na kuivika. Akaipiga busu pale pale kwenye mkono wa Cecy kisha akamtazama. Cecy alikuwa akitabasamu tu.



Rommy akamsogelea taratibu Cecy mpaka alipofika karibu kabisa na uso wake. Akapeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Cecy na kilichofuata hapo kilikuwa ni kitendo cha kubadilishana mate ambacho Cecy alikipokea bila ubishi wala aibu kutokana na kuwa walikuwa ndani ya gari huku vioo vyote vikiwa vimefungwa. Ikawa hivyo!.



Iliwachukua dakika moja ndipo wakaachiana. Tabasamu kwa kila mmoja likaonekana kwenye nyuso zao. Rommy akasema anamapenda na Cecy akajibu anampenda pia. Ukurasa wa mapenzi kati ya wawili hao ukafunguliwa upya. Cecy akashukuru kwa zawadi aliyopatiwa huku Rommy akimuahidi kumpenda kwa dhati. Kisha hapo Cecy aliomba arudi kwao maana muda ulishakwenda sana. Rommy akatoa noti kumi za Elfu kumi kumi na kumkabidhi Cecy. Lakini Cecy alizikataa kata kata akidai zile alizomrushia mchana wa siku hiyo bado anazo na zinamtosha. Akamuambia akiwa na shida na pesa atamjuza. Rommy akawa mpole kisha akampiga busu la mdomoni na kumuambia washuke ndani ya gari. Waliposhuka Rommy akamtafutia usafiri wa bodaboda kwaajili ya kuwahishwa kwao. Baada ya kupanda na kuondoka. Rommy akageuza kurudi kule gari lake lilipo. Akawakuta Paskali na Assu wakiwa nje wakimsubiri. Kicheko kikali kikawatoka watu hao huku wakimpa heko Rommy na kugongeshana viganja vyao kwa furaha.



“Dogo wewe ni nyoko aisee!” Paskali aliongea hayo huku akiingia ndani ya gari upande wa dereva. Rommy nae aliingia ndani ya gari huku akitabasamu. Hata Assu nae aliingia upande wa nyuma.



“Kawaida tu. Lazima ujue mitego ya kuwanasa ndege washamba kama wale. Ni kujifanya mpole huku kulia kwingi na maneno mengi. Lazima ajae kingi tu” Paskali akacheka huku akiondoa gari mahala hapo. Mara hii dereva alikuwa yeye baada ya kumuacha Zuma akiendelea na kazi nyengine kule yalipo makazi yao.



“Ila pale ulikuwa ‘serious’ tofauti na vile ulivyosema utamuektia” Assu aliongea.



“Aaaa wewe tangu lini nikawa ‘serious’ na wajinga kama wale? Halafu unajua hawa wanawake ni mama zetu lakini muda mwengine acha tu tuwadharau. Mnajua yule manzi nilimdhalilisha sana mpaka sasa nikiangalia hakuna manzi niliemdhalilisha vibaya kama yeye. Ati leo namuomba msamaha kidogo tu huku nikitoa vichozi vya uongo na kweli basi ndio kalainiiika kama ng’ombe mwenye joto. Halafu usikute pale ana mtu wake lakini anakubali kumsaliti kwaajili ya ‘plyaboy’ Ethan” Paskali na Assu wakacheka huku Rommy ama Ethan akiwa anatabasamu.



“Ila mdogo wangu unawamaliza. Inamaana na uzuri wote ule pia utamtafuna na kumtema?” Assu alimuuliza. Rommy aligeuka nyuma kumtazama kisha akasema.



“Alaah! Unamuonaje Hanifa? Mtoto wa kisomali yule mkalii balaa mpaka mkanishauri nioe. Ila je nilimfanyaje?.. Hah hah hahaa majibu mnayo.” akageuka mbele kisha akasema. “Hadi mtoto anajinywesha sumu kwaajili yangu unadhani ni mchezo. Subiri kwanza niwadonyoe mpaka pale watakapokuja kutia akili”



“Dah! Mzee wa kisomali alikuwa anakuwinda na SMG utafikiri yupo vitani na angekupata yule sijui ungekuwa wapi saa hii. Maana wewe ndie muasisi wa kunywa sumu kwa mwanae na kama asingewaishwa hospitali halafu angekufa mtoto wa watu. Haki vile nakuapia mdogo wangu ungeihama ile nchi bila kupenda. Unajifanya mjuaji kwenye nchi za watu?..” Kicheko kikali kikawatoka. “Ila mdogo wangu achana na hayo mambo utakuja kuingia pabaya mwishoni ohooo!”



“We nawe kujifanya ‘tablikhi’ kila siku kunitolea mawaidha mi sipendi ujue. Hayo mambo yakuingia pabaya yana Mungu broo Assu”



Waliendele na soga zao mpaka pale walipofika kwenye makazi yao. Gari ikaingizwa ndani na wao wakashuka. Wakaingia wote mpaka sebuleni ambapo walimkuta Zuma akiwa amekaa yupo bize na simu yake. Aliwaangalia kwa sekunde moja na kurudisha macho yake kwenye simu yake kisha akawakaribisha. Kila mmoja akatwaa nafasi yake huku Rommy akiongoza mpaka kilipochumba chake.



Huko alivua nguo za juu na kubakiwa na nguo ya ndani. Kisha akatwa taulo na kuingia maliwatoni. Alienda kuoga ikiwa ni ‘hobi’ yake kuoga kila atakapojiskia. Hata anaweza fikisha mara tano kwa siku kuoga. Dakika kumi zilitosha kufanya jambo hilo kisha akatoka humo. Alipotua macho yake kwenye kitanda chake. Alimuona Siwema akiwa amekaa. Akatabasamu na kuendelea kwenda mbele zaidi.



“Vipi? Mbona kuna uvamizi usio na taarifa chumbani kwangu?” Ethan aliuliza hivyo huku akijifuta maji na taulo jengine alilolitungua kwenye henga.



“Kwani kuna ubaya? Mbona wewe jana ulifanya uvamizi chumbani kwangu na sikuwa na cha kusema?” Siwema alijibu kwa mtindo wa kuuliza. Rommy akacheka na kumgeukia kule alipo mwanadada huyo.



“Kwahiyo umelipiza?” Rommy alimuuliza. Siwema akatingisha kichwa kukubali. Rommy akapiga hatua mpaka pale alipo Siwema. Akamshika kidevu na kuiinua sura yake. Wakawa wanaangaliana. Rommy akasikitika huku akitabasamu na Siwema akataka kuhoji ni kwanini amesikitika. Lakini hakupata wasaha huo na badala yake alifumbwa mdomo na ‘romance’. Kitendo kilichopelekea wawili hao kulazana kitandani na kufanya zaidi ya yale ya kunyonyana midomo.



Cecy alikuwa amefika nyumbani kwao muda mwingi tu baada ya kuachana na Rommy. Muda wote hakuwa sawa kwa maamuzi aliyoyachukua. Nafsi ilimsuta kwa kumsaliti Ramah huku akianzisha uhusiano mpya na Rommy ikiwa anajua kabisa kwamba hao ni ndugu kama maelezo ya Rommy yalivyosema.



Lakini Ramah hatoweza kugundua, nitajitahidi kumficha naamini hatojua. Cecy aliwaza. Majira haya alikuwa chumbani kwake. Lakini ni ndugu sasa naweza vipi kuwachanganya? Inamaana ni kweli hawatoweza kujua? Mmmh! Hapana bwana hawatoweza kujua. Kwanza Rommy amekuja likizo tu huku ataondoka nitabaki na Ramah wangu.



Aliendelea na tafakuri zake zenye ufinyu wa maarifa na kupelekea kufanya maamuzi ya kijahili pasi na kufikiri matokeo yake yatakayokuja kutukia mbeleni. Ama kweli hila za mjinga hazimnasi mwerevu. Cecilia alijiona mwerevu kwa maamuzi hayo aliyoyaamua bila kufikiri mara mbili. Hakutaka kumshirikisha yoyote zaidi ya kuamua yeye mwenyewe na akili yake. Pema usijapo pema, ukipema si pema tena.



Muda huu walikuwa wameshamaliza starehe zao. Rommy alijiinua kitandani kwaajili ya kuingia chooni tena kwenda kuoga. Siwema akataka waongozane wote huko, Rommy akamzuia kwa kumuambia anacho chumba chake, akafanye yake huko. Siwema akatulia na kumuangalia kijana huyo anavyopotela kwenye mlango wa chooni ambacho kilikuwa humo humo. Kabla hajafunga mlango alisikia sauti ya Siwema aliesema kuwa muda wa kulala atarudi tena waendeleze kile walichokianzisha. Kisha Siwema akatoka baada ya kujua kuwa ujumbe wake umemfikia mlengwa.







Dakika ishirini Rommy alifika sebuleni ambapo wakina Zuma walikuwa hapo wakiendelea na soga zao. Rommy akalalamika njaa na kwenda kujipweteka kwenye viti vilivyokuwa vimeizunguka meza ya kulia chakula. Punde Siwema aliandaa chakula pale mezani na kila kitu kilipokamilika, Rommy akajipakulia kinachomtosha na kuendelea kula huku wakina Paskali wakijivuta mmoja mmoja pale mezani.



“Hivi Rommy. Hili jina la Ethan nilipata kumsikia mara nyingi bosi akikuita. Hii imekaaje kaaje. Rommy ama Ethan?” Assu aliuliza wakati wanaendelea kula. Rommy akameza kile anachotafuna kwa muda huo huku wote wakimuangalia yeye. Pengine na wao walitaka kusikia jibu la swali alilouliza Assu.



“Rommy, Ethan yote majina yangu. Hili jina la Rommy nilipewa na Mama tena aling'ang'aniza sana niitwe hivyo mpaka sasa ndilo ambalo nalitumia kila sehemu na ndilo linalojulikana sana na marafiki zangu. Na hili la Ethan nilipewa na Baba, lakini hili halijulikani na watu wengi sanaa kama hili la Rommy” Rommy aliwafafanulia.



“Ok. Hivi tangu tuwe huku bosi umewasiliana nae lini? Maana niliwahi kumsikia akisema kuna safari ya kwenda Zanzibar baada ya kutoka hapa Tanga” Paskal alimuuliza.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mchana wa leo nimewasiliana nae, pia akanikumbusha hayo ila nilimuambia sitoenda huko. Nataka likizo hii niimalize mji huu kisha nirudi masomoni. Kwenye likizo nyengine ndio naweza nikaenda huko”



“Watoto waki-Tanga wanakupagawisha” Zuma aliongea huku akicheka.



“Aaaah wapi! Kwani mimi mwenyewe si waki-Tanga vile vile?”



“We m-bara bwana, sio wa huku pwani” Zuma alizidi kumkomalia.



“Kumbuka mama yangu ni mzawa wa huku. Sasa utasemaje sio wa huku......? Halafu broo Zuma, kesho inabidi tuende kwakina Rafael aisee. Nimemkumbuka sana jamaa yangu yule... Hivi hajaacha utundu yule, maana nakumbuka kipindi kile alikuwa akinichukua mpaka kwenye ule mpera wa pale jirani. Tunapanda juu ya ule mti, tunakula mapera na tukirudi home ujue kuna fimbo. Tena hasa hasa yeye ndie aliekuwa akipokea kipigo maana mimi nilikuwa mgeni”



“Hivi sasa basi ukimuona utamjua? Amebadilika sana kama ulivyobadilika wewe. Ila mwenzako ana manywele kichwani Macelo haoni ndani. Ni mara chache sana nakutana nae mitaani ila yeye hanikumbuki kabisa” Zuma alisema.



“Yule kaka yake nae yupo. Yule aliekuwa akiitwa Jeremiah ama Jay?..” Zuma akamjibu kuwa hata yeye pia yupo. “Dah! Yule jamaa alikuwa mtata sana. Alikuwa hapendi kucheza na sisi wakati wote tulikuwa watoto....... Aisee kesho inabidi niende nimeimisi sana ile familia.”



Soga zao ziliendelea mpaka pale walipomaliza kula. Wakajinyanyua na kurudi tena sebuleni. Huko Paskali na Assu walicheza Game huku Zuma na Rommy kila mmoja akiwa bize na simu yake. Walikaa hapo kwa nusu saa kisha Rommy akaaga anaenda kupumzika. Akatoka akiwaacha watu hao wakiendelea na yale waliyokuwa wakiyafanya.



Rommy aliingia chumbani kwake kwa minijali ya kulala. Lakini dhamira hiyo ilikatishwa na Siwema alieingia humo akitaka waendeleze yale waliyoyakatisha saa moja nyuma. Rommy alikuwa amechoka sana muda huo. Alipinga jambo hilo huku akidai watafanya siku inayofuata lakini Siwema hakutaka kuelewa hilo. Alifanya vishawishi vyote mpaka Rommy akawa katika ‘mood’ ya kufanya tendo hilo. Uligemalo, utalinywa. Mchezo ukaanza kwa kasi zaidi ya ile ya mwanzo.



Majira hayo Ramah alikuwa chumbani kwake baada ya kutoka katika mizunguko yake ya siku hiyo. Hakuwa na sawa na uso wake ulidhihirisha hilo. Na hiyo ni kutokana na kitendo cha kutopokelewa simu yake na Cecy ambae alianza kumpigia tangu masaa mawili nyuma mpaka muda huo simu yake ilikuwa ikiita tu.



Hakumaizi ni kipi hasa kimemkuta mpenzi wake mpaka kusababisha kutopokea simu. Huenda ikawa kunatatizo limemkuta. Ramah aliwaza huku akiitazama simu yake ambayo kwa wakati huo alikuwa akimpigia Cecy. Tofauti na awazavyo yeye. Cecy muda huo hakuwa sawa pia kutokana na jambo lililotukia siku hiyo. Lilimchanganya sana na hakujua afanye nini. Kitendo cha kumkubalia Rommy ilhali yupo na Ramah, tena akithibitishiwa na Rommy kuwa yeye na Ramah ni ndugu kilimchanganya.



Hakuwa ameiona simu yake ilivyokuwa ikiita kwa uzito wa mawazo yaliyokuwa yakipishana kichwani kwake. Kichwa chake alikihisi ni kizito na kuamua kupumzika usingizini pengine atapunguza uzito wa mawazo. Akachukua simu yake kwaajili ya kutazama muda, ndipo alipokutana na simu za Ramah kumi na tano zilizopigwa pasi na yeye kuzipokea. Akiwa anatafakari ni vipi zipigwe simu zote hizo bila kuzisikia. Simu yake ikaita tena, aliekuwa anapiga ni Ramah. Akapokea.



“Nini tatizo mpenzi? Mbona muda mwingi napiga simu hupokei?” Ramah alianza na swali baada tu ya simu kupokelewa. Cecy aliingiwa na ubaridi ghafla moyoni mwake baada ya kusikia sauti ya Ramah hasa alipomuita ‘mpenzi’. Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa mpaka pale Ramah alipomuita jina lake.



“Oooh! Sorry mpenzi nilikuwa nimelala halafu simu niliiweka ‘silent’ kuepuka usumbufu ila sikujua kama utanitafuta. Nisamehe my” Cecilia alijitetea kwa uongo ambao Ramah aliuamini kwasababu alimuamini sana Cecy. Akamuuliza ni kipi hasa kilichomfanya akawa amelala muda huo nae akajibu ni maumivu ya kichwa anahisi kama ana homa. Ramah akampa pole nyingi huku akimsisitizia ameze dawa yoyote ya kutuliza maumivu muda huo kisha apumzike na ifikapo asubuhi ya siku inayofuata. Kama atakuwa anahisi homa zaidi, basi watajua wafanye nini. Cecy akashukuru kisha Ramah akamuacha apumzike akimuahidi kumtafuta asubuhi. Kisha akakata simu.



Ramah ananipenda sana na sijui ni kwanini namtendea hivi. Cecy aliwaza hayo huku akiitazama simu yake utafikiri inaweza kumpa ushauri wowote kwa hayo awazayo. Lakini hata Rommy najihisi kumpenda pia. Amekiri makosa yake na ameniomba msamaha wa dhati. Lakini nitawezaje kuishi nao wote wawili na wasijuane kama nawachanganya?. Akaguna. Kisha akatabasamu. Mi mtoto wa kike bwana siwezi shindwa na hili. Alijipa moyo kisha akajilaza kitandani tayari kuusaka usingizi.



* * * *



Shimo la ulimi, mkono haufutiki. Awazaye na kupitisha maamuzi pasi na mshauri hujiona sawa. Lakini mawazo yake akiyatanabaisha kwa watu kukosolewa ni lazima. Fikra ya mwanadamu awazapo jambo hutafuta kasoro kwa awazayo. Rabsha za fikra hufika ukingoni mwa bongo mapema. Wazee walisema, Natuone ndipo twambe, kusikia si kuona.



Majira ya saa sita mchana ikiwa ni siku mpya kabisa. Mama Ramah alikuwa akijiandaa majira hayo kupika chakula cha mchana kama ada yake ilivyo kupika mapema. Akiwa katika maandalizi hayo. Aliona ugeni ukiingia nyumbani kwake. Ugeni ambao hakuujua ni wanani ama kina nani zaidi ya kushuhudia gari la gharama kubwa kiasi likiingizana kwenye wigo wa nyumba yake. Akaacha kufanya afanyacho na kusimama macho kuutazama ugeni huo.



Gari ilipakiwa sehemu ambayo ilionwa ni sahihi kisha mlango wa dereva ukafunguliwa na Zuma alishuka. Mama Jay kiroho kikamvaa baada ya kumuona Zuma. Eee alikuwa akimfahamu ndio japo ni miaka mingi kidogo imepita. Punde alimuona mtu mwengine akishuka kwenye gari lile ambae alimtoa macho kwa mshangao. Ndie!?.. Alijiuliza. Ama sie?.



“Mama shikamoo” Zuma alimsalimia huku akiwa na bashasha usoni. Mama Jay akaitikia salamu hiyo na kumjulia hali yake. Zumo akajibu salama tu. Rommy akasogea karibu na hapo kisha akamsalimu mama huyo.



“Marahaba Ethan, za masiku tele?” Mama Jay aliitikia salamu hiyo huku akipokea mkono wa Rommy.



“Mama salama tu. Nimewakumbuka leo maana ni muda sana hatujaonana” Rommy alijibu huku na yeye akiwa na bashasha tele usoni mwake. Paskali na Assu walifika hapo na kumsalimia mama huyo. Akawaitikia salamu zao kisha akamgeukia tena Rommy.



“Za huko masomoni? Maana tangu utoweke mji huu baba yako aliposema unaenda kusoma Kenya ndio kimoja ati”



“Za huko salama tu, twashukuru Mungu masomo yanaenda... Nimekuja likizo tangu juzi, nikaona leo nije kuwasalimu maana ni muda sana. Vipi Rafael na Jeremiah wapo?” Rommy alijbu kisha akauliza.



“Hao tena! Wamejaa tele hapa kaya waende wapi unadhani?”



“Hah hah hahahaa! Nilijua basi wameoa na wanaishi kwenye kaya zao muda huu. Kumbe bado wanakula kwa mama kama mimi tu?” Rommy alileta utani huo uliomfanya mama Jay kucheka.



“Kuoa mwanangu bado. Ila kama nikuhama hapa wangeshahama muda tu. Ila ndio hivyo nawakatalia, unadhani wakiondoka wao nani atakuwa mlinzi wangu? Hata hivyo kaya itapwaya hii”



Mama Jay alipoona mazungumzo yanazidi. Akamkatisha na kuwakaribisha sebuleni. Wakajongea taratibu mpaka mahali hapo na kuweka makazi kwenye masofa yaliyo hapo. Wakati wakiendelea na soga za hapa na pale. Ulisikika muungurumo wa sauti ya pikipiki ikiingia mahala hapo. Mama Jay akawajuza kuwa huyo anaeingia hapo na chombo hicho. Huenda ni mmoja kati ya wanae. Akajaribu kuita jina la Ramah na sauti ya Ramah ikasikika. Akampazia tena sauti kumtaka afike mahala hapo.



Muda huo Rommy alikuwa na shauku ya kumuona nduguye huyo waliechangia kwa baba. Dakika moja mbele mlango wa sebuleni ukasukumwa na mwili uliobeba taswira ya Ramah au Rafael ukaonekana mahala hapo. Ramah akapitisha macho yake haraka haraka kwa wageni hao na mwisho yakatua kwenye uso wa Rommy ambae alikuwa akitabasamu muda wote. Akawa na mchechetu huku mshangao ukimvaa akiwa anamtumbulia macho Rommy.



“Ethan!?” Ramah aliita huku akiwa bado hajagandua macho yake kwenye taswira ya Rommy.



“Rafael?” Rommy nae akaita. Kisha hapo Rommy akainuka na kwenda kukumbatiana na Ramah aliekuwa bado haamini kama amuonae hapo ni yule aliepotezana nae miaka mingi nyuma.



MIAKA SABA ILIYOPITA.



TARATIBU za mazishi ya mzee Antony Magasa zilifanyika na kwenda kuzikwa huko kwao Mbeya. Baada ya mazishi kuisha. Ndugu walikaa kikao kwaajili ya kuzungumza swala la mirathi za mali alizoacha marehemu. Kwasababu marehemu mpaka anakutwa na mauti hakuwa ameoa mwanamke yoyote. Ikaonelewa mali hizo zirudi kwa ndugu.



Lakini mdogo wa marehemu Antony ambae alifahamika kwa jina la Kelvin. Aliwaambia kwamba, marehemu kaka yake Antony pamoja na kuwa hakuoa. Lakini alikuwa na watoto ambao alizaa na wanawake mbalimbali lakini aliokuwa akiwafahamu yeye ni wanawake wawili ambao mmoja hakuwa akiishi nae. Yani baada ya kumzalisha tu, akamtelekeza huku huyo mwengine akimfanya kama mkewe ambae walikuwa wakiishi wote pamoja na mtoto wao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baadhi ya ndugu waliposikia maelezo hayo walikuja juu kwa kufoka wakidai hawatambui wala hawakutaka kujua chochote kuhusu wanawake hao waliozalishwa wala watoto wao. Walichodai ni kwamba ndugu yao Antony wakati wa uhai wake hakuwa na mke wala hawakutambua kama ana watoto. Kwahiyo hawataki kusikia lolote kuhusu watu hao wa kando kwenye mirathi. Ila ukweli ni kwamba. Wote walitambua kama ndugu yao alikuwa na watoto ambao walikuwa sio wa ndoa, lakini walibisha ili mali za marehemu zisiende kwenye mikono mengine zaidi ya kwao.



Rabsha zilifurumuka kwa wanandugu hao ambao wengine walidai ni kweli marehemu alikuwa na watoto na ilihitajika mirathi iwafikie watoto hao na wazazi wao. Huku wengine hasa hasa wakubwa zake na marehemu wakidai hawalitambui hilo. Wanachotaka mali wagawane wenyewe.



Kikao kikavurugika pasi na kupatikana muafaka wowote huku ndugu hao wakiwekeana chuki na vinyongo kisa mali za marehemu. Kwakuwa kikao kilikatishwa pasi na kupatikana muafaka mzuri. Kelvin akarudi Tanga huku akiwasusia kaka zake wafanye watakavyo.



Aliporudi katika mji huo ambapo alikuwa akifanya shuhuli zake mbalimbali ikiwa aliwezeshwa na kaka yake Antony kipindi cha uhai wake na kupatiwa mtaji wa kuanza biashara yoyote aliyoiona inafaa. Moja kwa moja alienda katika nyumba aliyokuwa akiisha kaka yake akiwa na familia yake. Alimkuta mwanamke huyo akiwa mnyonge kwa kuondokewa na mwanaume ambae walikuwa wakiishi kama mke na mume mpaka kupata mototo mmoja wa kiume waliemuita majina mawili tofauti. Ethan likitoka kwa baba huku Rommy akilichagua mwanamke huyo.







Kelvin akamjuza yaliyotukia huko Mbeya kwenye kikao cha familia kilichokaliwa kwaajili ya kuzungumzia swala la mirathi. Akaongezea kuwa, huenda kaka zake wakafanya maamuzi mabaya ikiwa ni kumtoa yeye kwenye nyumba hiyo akiwa na mwanae maana walishasema hawatambui kama ndugu yao aliacha mwanamke na mtoto. Mwanamke huyo ambae alifahamika kwa jina la Maria, alihuzunika sana kiasi ambacho alidondosha machozi na kulia upya baada ya kufikishiwa taarifa hiyo.



Alikuwa akilalamika ataenda wapi ilhali nyumbani kwao walimfukuza baada ya kupata mimba angali yu shuleni bado. Ndipo Antony alipomchukua na kuamua kuishi nae mpaka akajifungua na mtoto wao muda huo akiwa mkubwa mwenye miaka kumi na miwili. Kelvini alimpa pole na kuahidi kumsaidia Maria. Akaaga na kuondoka. Maria akiwa na mawazo tele ya kuondokewa na mwanaume aliekuwa akishi nae na taarifa inakuja kuwa hatambuliki kwa ndugu wa mwanaume huyo. Hivyo anaweza kuja kufukuzwa kwenye nyumba hiyo.



Muda huo huo akaingia mwanae ambae alikuwa ni Rommy ama Ethan akitoka shule, ambapo alikuwa akisoma shule ya mtu binafsi yenye kulipiwa kiasi kingi cha pesa. Maria baada ya kumuona mwanae akiingia hapo alibadili sura na kuweka tabasamu ili asimtie hofu mwanae na kusababisha amuhoji maswali ambae yatazidi kumuongezea uchungu. Rommy alimsalimia mama yake kwa furaha na Maria alimpokea kwa tabasamu. Kisha hapo akamruhusu akabadili nguo kisha ajekupata chakula. Rommy alitoweka mahala hapo na kupotelea chumbani kwake.



Wiki moja ilipita huku hali ya Maria ikidhohofu. Hakujua ni nini hasa zaidi ya kuhisi ni mawazo ndio yanayomfanya kuwa katika hali hiyo. Alipoona maradhi yanazidi kumuandama. Akaonelea afike hospitali kwaajili ya uchunguzi zaidi. Hakika hatutarajia aliyoyasikia kwa daktari baada ya kupimwa. Majibu yalitoka kuwa, alikuwa ameathirika na ugonjwa mbaya wa UKIMWI.



Presha ilipanda ghafla huku mapigo yake ya moyo yakienda hovyo hovyo. Kizunguzungu kikamshika na kujikuta akidondoka chini baada ya kushindwa kukaa vyema kwenye kiti. Daktari aliwahi kumpa huduma ya kwanza kisha akamuwahisha wodini kwaajili ya matibabu zaidi. Lakini wazee walisema, kazi ya Mola haina makosa. Roho ya Maria iliachana na mwili majira ya usiku alipokuwa kitandani amepumzika. Ikawa rasmi sasa Rommy amebaki yatima na alihitaji msaada zaidi ili aweze kuishi vyema.



Kelvin alijitolea kuishi na Rommy baada ya kuhifadhiwa mwili wa mama yake Maria kwenye makazi yake ya milele. Kama alivyotabiri ndivyo ilivyokuwa. Kaka zake walifika jijini hapo wiki moja mbele kuja kuchukua mali za marehemu mdogo wao kinguvu baada ya kushindwa kuelewana. Kelvin aliwaacha wafanye watakavyo kama alivyojiahidi. Kaka zake wakagawana mali zote za marehemu mdogo wao Antony na kurudi tena Mbeya huku mmoja wao akiweka makazi katika mji huo.



Miaka mitatu ilipita huku Rommy akishi na Kelvin ambae alikuwa ni baba yake mdogo. Kipindi hiki hali ya iktisadi ya Kelvin haikuwa nzuri kutokana na biashara zake anazozitegemea kuenda ndivyo sivyo. Chengine kilichomchanganya zaidi ni kuhusu elimu ya Rommy. Shuleni ilihitajika pesa kwaajili ya ada ya mwaka huo ambao alikuwa akimaliza elimu ya msingi kabla ya kuendelea mbele.



Baada ya kuchekecha akili yake ndipo akapata wazo la kudai haki ya Rommy ambayo ilidhulumiwa na baba zake wakubwa. Baada ya kutafakari wapi aanzie jambo hilo. Ndipo alipokumbuka kuwa kulikuwa na mwanasheria ambae alikuwa akisimamia mali za Antony Magasa. Lakini mwanasheria huyo hakufanya lolote pindi mali hizo zilipokuwa zikigawanwa na ndugu wa marehemu maana yeye hakuwa na ‘saport’ yoyote ya kutetea mali hizo. Akatulia pembeni akiwaacha ndugu hao wafanye wanavyotaka ila hiyo ni baada ya kujiridhisha kuwa ni ndugu wa marehemu huyo.



Kelvin alipata wazo la kumtafuta mwanasheria huyo kwaajili ya kulizungumza vyema swala hilo. Muda huo Rommy alisitishwa shule kutokana na kuwa hakulipa ada ya mwaka huo. Kabla ya kumtafuta mwanasheria, Kelvin alihangaika kwanza na Rommy. Akafika katika uongozi wa shule aliyokuwa akisoma Rommy. Akawaeleza matatizo yake lakini hawakumuelewa zaidi walimpa ushauri wa kumuhamisha shule kwa muda asome shule za serikali kisha hapo ndipo arejee kufanya mtihani wa taifa katika shule hiyo.



Kelvin alilifikiria hilo na kuona linatija ndani yake. Akafanya utaratibu huo na baada ya siku tatu, Rommy akahama kwa muda shule aliyokuwa akisoma kwenda shule ya serikali ambapo huko ndipo alipokutana na Cecilia na Jenifa. Baada ya kulikamilisha hilo. Kelvin akaingia rasmi kudai haki ya Rommy. Alizungumza na mwanasheria kisha hapo wakaafikiana swala hilo walifikishe mahakamani ili itafutwe haki.



Mwanasheria alifikisha mahakamani faili aliloliandaa la kesi hiyo ya madai. Kisha hapo akapewa barua ambayo alitakiwa awapatie wahusika kwaajili ya kuhudhuria mahakamani siku pangwa ya kusomwa kesi hiyo. Alipotoka mahakamani, moja kwa moja alimtafuta Kelvin na kumkabidhi barua hizo. Moja akimuambia anatakiwa awapatie ndugu zake ili walitambue hilo. Kelvin akashukuru na kuahidi kulifanikisha hilo ndani ya siku hiyo hiyo.



Kama alivyosema ndivyo alivyofanya. Siku hiyo hiyo aliifikisha barua hiyo kwa mmoja wa ndugu zake ambae walishirikiana na wengine kugawana zile mali. Akatoweka akiacha taharuki kwa ndugu huyo. Ni vipi swala hili liibuke tena ilhali ilishapita miaka mitatu? Ndilo swali lililoundika kwenye fikra za ndugu huyo. Papo hapo akatwaa simu yake na kuwajuza wenzie. Viroho vya hasira viliwapanda ndugu hao huku wakimuahidi mwenzao kuwa ndani ya siku mbili watafika mjini hapo kwaajili ya kuitikia wito wa mahakama.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku mbili mbele. Ndugu hao ambao walikuwa ni wawili na yule mwenzao akiwa ni watatu. Walikutana sehemu moja na kujadili swala hilo. Wakaonelea wamuite Kelvin kwaajili ya kumuhoji vizuri kwanini ameamua kufufua mambo hayo ilhali yalishapita kitambo. Tena wanakumbukumbu ya maneno ya Kelvin kuwa hataki kujishuhulisha na ugawanaji wa mali hizo ambazo zilileta utata.



Kelvin aliitika wito wa ndugu zake na kukutana nao nyumbani kwa yule aliekuwa akiishi katika mji huo. Walianza kumuhoji maswali kama ni kwanini ameamua kulifufua swala hilo wakati lilishapita? Nae aliwajibu kwa utulivu kuwa, mtoto wa marehemu alikuwa akiteseka kwa shida ilhali mali za baba yake zipo. Walimjia juu huku wakisimamia msimamo wao wa kuwa marehemu hakuoa wala hakuacha mtoto yoyote.



Vurumai ilitokea hapo huku hali ya kutoelewana na rabsha zikitanabai. Hawakuwa wakielewana tena. Kaka zake walimtaka afute mashtaka hayo huku yeye akishikilia msimamo wake kuwa ni lazima jambo hilo likaongelewe mahakamani ili haki ipatikane. Kaka yao mkubwa hasira zilimpanda na kutaka kwenda kumvamia Kelvin. Ila aliwahiwa kuzuiwa na wadogo zake waliemtaka atulize munkari wayamalize.



“Mtoto mdogo kabisa wewe unataka kutuchanganya akili kaka zako? Ni nani hasa wewe mpaka unajifanya unajua vingi kuliko sisi. Kuna unaemfikia hapa? Eeee?... Jogoo yatima wewe na uifute hiyo kesi yako. Vinginevyo hii vita uliyoianzisha haitoisha hapa. Lazima tukushikishe adabu hayawani wewe. We unajifanya unajua sana uchungu. Kwanza mtoto mwenyewe sio wako lakini unashadadia mambo yasiokuhusu. Nakuambiaje. Usipoifuta hii kesi kabla hiyo siku ya kwenda mahakamani. Utanijua mimi ni nani. Mtoto mdogo wewe huwezi kuchanganya akili zetu. Alaaa!” Mzee huyo ambae ndie alikuwa kaka mkubwa wa familia hiyo. Aliongea kwa ghadhabu huku mate kinywani yakimtoka kama bomba la mvua na kusambaa hewani. Mishipa ya shingo ilimsimama huku macho akiyatoa utafikiri ni kipofu anaelazimishwa kuona kizani. Aling'aka kwa hasira huku akimtazama Kelvin kwa uchu baada ya kuzuiwa kwenda kumvamia akitaka kumshushia kipigo.



Kelvin nae hakutaka kuwa mnyonge kwa kaka zake. Nae pia alirudisha majibu kwa kuwadhihaki kaka zake kuwa ni madhalimu wa mali za watu. Aliwahakikishia kuwa hatoenda kufuta kesi na lazima wasimame mahakamani na haki ipatikane. Kisha akaondoka huku akiwaacha kaka zake wakipiga siyaha za hasira wakimuahidi kumtendea mabaya.



Kelvin alipotoka mahala pale. Moja kwa moja alirudi nyumbani kwake. Alijipweteka kwenye kochi na kuanza kutafakari yale maneno ya vitisho ya kaka zake. Ni kweli wanaweza kufanya kitu kibaya wale. Aliwaza. Inabidi niwe nao makini, hii vita ni kubwa sana. Chakufanya sasa ni kumhamisha Rommy kwenye nyumba hii mpaka mambo haya yatakapokwisha. Sasa ni wapi nimpeleke? Likawa ndio swali la kutafakari muda huo na kulipatia majibu haraka kabla mambo hajabadilika.



“Dorine..!” Akasema Kelvin kwa sauti ndogo. “Ndio.. Dorine naamini atanisaidi hili. Kwanza anautambua mchango wangu kwake. Nilimpigania sana kwa kaka yule. Hawezi kunikatalia hili” Tabasamu likachomoza kwenye uso wa Kelvin. Akainuka kwaajili ya kutoka nje. Wakati anafungua mlango kwa pupa, akakumbana na Rommy aliekuwa akiingia humo muda huo akitoka shule.



“Ethan..?” Kelvin alimuita Rommy wala asiitikie salamu aliyopewa. “Jiandae leo inabidi uhame hapa ukaishi sehemu kwa muda... Subiri narudi sasa hivi kwanza” Kelvin aliongea kwa pupa kiasi ambacho Rommy hakuwa amemuelewa hata kidogo. Akampisha pale mlangoni na Kelvin akapotelea nje. Rommy alitulia akijaribu kuyafikiri tena yale maneno aliyoyaongea baba yake mdogo. Akabetua mabega na kuingia chumbani kwake.



Safari ya Kelvin iliishia mtaa wa Duga kwenye nyumba fulani. Akagonga mlango na kusubiri baada ya kuitikiwa na aliekuwa ndani. Dakika moja akatoka mwanamke wa makamo aliekuwa katika mavazi ya kanga.



“Aaaa shemu karibu. Karibia ndani” Mwanamke huyo ambae sisi tunamtambua kama Mama Ramah au Jay. Akimkaribisha Kelvin na ndani. Kelvin aliingia na kwenda kukaa kwenye masofa yaliyokuwa sebuleni.



Walijuliana hali baada ya kutoonana kwa muda mrefu. Kisha hapo Kelvin akaeleza lililomleta hapo. Alianzia mbali sana ili apate kueleweka kwa urahisi na Dorine au Mama Jay apate kumuelewa na kumsaidia. Alimueleza mpaka nia yake ya kudai haki ya mirathi kwa watoto alioacha marehemu ikiwa ni pamoja na mtoto wa mama huyo aliezaa na marehemu kipindi cha uhai wake. Baada ya maelezo yaliyochukua dakika takribani saba ikiwa muda wote mama Jay akiwa kimya akimsikiliza. Akashusha pumzi ndefu na kumtazama Kelvin.



“Unajua wewe ni shemeji yangu. Na unatambua aliyoyafanya kaka yako mpaka kupelekea leo mimi niishi hivi niishivyo. Sikutaka kukumbuka ya nyuma. Ila sina budi kukumbusha ili utambue ni jinsi gani marehemu kaka yako alivyonifanya. Antony alinilaghai na kunipachika mimba nikiwa mke wa mtu. Tena si mke wa mtu tu. Pia ningali ninakichanga cha mwaka mmoja. Akanipatia mimba ilhali nina kitoto kidogo. Jambo hilo lilinifadhaisha sana na kunidhalilisha kwa ndugu zangu mpaka kwa mume wangu ambae mawazo yalisababisha kwa kiasi kikubwa kifo chake. Nikawa mjane huku ndugu zangu wakinitenga na nisijue nifanye nini. Nikamtafuta ili kumuomba msaada lakini alinifukuza na kunidhalilisha pasi na mfano. Kwa huruma yako shemeji yangu ukamshawishi mpaka akanijengea hiki kibanda lakini pia akinitaka nisimjue tena na wala nisiwaze kama nilishawahi kuzaa nae. Nashukuru Mungu kwa kiasi fulani niliiepuka ile aibu kule nilipokuwa nikiishi mwanzo na kuhamia hapa ambapo mpaka sasa naishi vyema na watoto wangu mpaka nimemkuza Rafael na kuwa mkubwa” Mama Jay aliongea hayo akiwa na majonzi lakini asindondoshe machozi zaidi ya kuhudhunika usoni. Pengine alishayasahau machungu hayo ya muda mrefu.



“Natambua yote shemeji. Na leo nimekuja na hilo unisaidie kumhifadh....”



“Hapana shemeji usiongee sana. Mlete huyo mototo, nitaishi nae kama mwanangu wa kumzaa hata ukitaka niishi nae milele. Hata hivyo kwa upande mwengine ni mwanangu pia maana ametoka katika kiuno cha aliewahi kunipa mtoto na mimi...” Akatulia kidogo kama anaekumbuka kitu. Kisha akasema. “ Mtoto mwenyewe ndie yule niliepata kusikia amezaa na mwanamke mwengine baada ya mimi kujifungua Rafael mwaka mmoja?”







“Ndio huyo huyo. Sasa nae mama yake alifariki miaka mitatu iliyopita ndio nikaamua niishi nae mimi maana hakuwa na msaada. Na leo hii nataka nimsaidie yeye na Rafael”



“Shemeji usiwe na shaka kabisa. Mlete nitaishi nae mpaka pale utakapoona inatosha”



Wakaafikiana na Kelvin akaondoka mahala hapo. Alirudi nyumbani kwake na kumtaka Rommy ajiandae amhamishe hapo. Kwakuwa Rommy bado yumdogo. Hakuwa na cha kupinga wala kuhoji chochote. Akakusanya nguo zake na kuongozana na Kelvin mpaka huko alipoambiwa anaenda kuishi kwa muda.



Akapokelewa kwa bashasha nyingi na Mama Ramah kisha hapo utambulisho ukafuata. Rommy alitambulishwa kwa jina la Ethan. Kelvin akiwa na maana kubwa kumtambulisha kwa jina hilo. Alihofu huenda kaka zake wakaamua kumtafuta Rommy ili wamfanyie ubaya nyumbani kwake. Sasa endapo watamkosa huko. Basi wanaweza kumtafuta popote pale na ndio maana hapo akamtambulisha kwa jina la Ethan ambalo halikuzoeleka sana.



Ethan na Rafael wakatambulishwa kuwa ni ndugu. Na Jeremiah akatambulishwa kwa Ethan kuwa ni kaka wa Rafael kwahiyo pia ni kaka yake na yeye. Kuanzia hapo wakafahamiana na Ethan ama Rommy akaanza kuishi rasmi katika familia hiyo. Kipindi hicho Rafaeli alikuwa kidato cha kwanza huku Jeremiah akiwa kidato cha pili ikiwa Ethan akiwa darasa la saba. Jina la Ramah alilipata akiwa kidato cha pili mwaka mmoja mbele baada ya Rommy kuondoka kwao. Ramah ni muunganiko wa majina mawili. Ikiwa ni lake Rafael, la baba yake mzazi Magasa na ‘H’ ya mwisho iliongezewa ili jina hilo liwe na ‘swaga’ pale litamkwapo kinywani. ‘RAMAH’.



Siku ya kesi ilifika na Kelvin pamoja na kaka zake wakiambatana na mwanasheria walihudhuria mahakamani. Mashtaka yao yalisomwa baada ya muda wao kufika. Kutokana na ushahidi wa maandishi na sahihi ya marehemu aliyoandika mwenyewe kipindi cha uhai wake akiwa na mwanasheria wake. Mali hizo alimrithisha mwanae ambae alitajwa ni mmoja tu Rommy. Pia kama haitoshi. Ipo sheria inayosema. Mwanaume akiishi na mwanamke zaidi ya miezi sita bila kumuoa, kisheria huesabika kama mume na mke. Na ikitokea wakatengana ama mwanaume kufa. Basi lazima mwanamke arithi ama agawiwe nusu ya zile mali.



Kutokana na sheria kuwabana pande zote kaka wa marehemu Antony. Hawakuwa na budi kuachia zile mali huku wakitakiwa kufunguliwa mashtaka mengine ya kudhulumu mali hizo. Ila walipojitetea kuwa hawakuwa wakijua kwamba mali hizo zilishaandikwa kuwa ni urithi wa mtoto wa marehemu na Antony mwenyewe. Mahakama ikasamehe hilo ila walitakiwa ndani ya siku mbili wawe wameshakabidhi mali zote bila kujali kama waliziendeleza ama laa!.



Pia Kelvin akaiambia mahakama, endapo akipatwa na tatizo lolote baya, basi waasisi ni hao ndugu zake maana walishamtishia hilo tangu anawapa barua ya kuhitajika mahakamani. Mahakama ikatoa onyo kali kwa watu hao kwa tishio walilotisha kwa mdogo wao Kelvin na kuwaambia ndugu hao, endapo ndugu yao akipatwa na tatizo lolote baya na ikajulikana ni wao ndio waasisi. Basi sheria kali itapita juu yao.



Mjadala ukafungwa na kesi ikaisha hapo. Ni dhahiri chuki ilishachipua mioyoni mwa ndugu hao kwa mdogo wao Kelvin. Walimuangalia kwa jicho baya kipindi wakitoka mahakamani hapo. Kelvin hakujali lolote zaidi ya kuendelea na shuhuli zake. Akapeana mkono na mwanasheria na kumuahidi atamuona baada ya hizo siku mbili ambapo nyaraka za mali hizo zilitakiwa zifikishwe mahakamani kabla ya kukabidhiwa Kelvin ambae ndie atakuwa msimamizi.



Siku ya kurejesha mali. Nyaraka mbalimbali za mali hizo walizokuwa wakimiliki ndugu wale waliziwasilisha mahakamani kisha kukabidhiwa Kelvin. Ndugu wale wakaondoka wakiwa hawana kitu huku Kelvin akiwa ndie msimamizi wa mali za Rommy kwa kipindi hicho mpaka pale atakapotimiza miaka kumi na nane ndipo anaweza kumkabidhi mwenyewe.



Kelvin alifanya jambo moja la kuzikusanya mali zote. Kisha akauza zile ambazo aliona hazina maana sana. Na kuamua kuanzisha biashara moja ambayo alihisi itaendeleza mali zile. Kisha hapo akatoa fadhila zake kwa Dorine Mama Ramah kwa kuikarabati vizuri ile nyumba yake. Baada ya hapo. Rommy alipomaliza elimu ya msingi. Akamhamisha nchini Kenya jijini Nairobi kwa ajili ya masomo.



Kipindi hiki Rommy aliishi kifahari kutokana na utajiri aliokuwa nao unaoendeshwa na baba yake mdogo. Alisomeshwa kwenye shule ghali jijini hapo huku Kelvin akimtafutia walinzi binafsi. Tangu amalize darasa la saba na kuondoka jijini Tanga. Hakuwahi kurudi tena mpaka mara hii aliporudi na kukutana na familia iliyomlea.



* *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Ramah na Rommy waliachiana na kila mmoja akachukua nafasi yake. Mazungumzo yenye kuamsha tabasamu kila sekunde kwa watu hao yaliendelea. Mama Ramah akatoka nje kwa ajili ya kupika chakula kwa ajili ya wageni na wao pia maana muda wa chakula ulikuwa ukikaribia.



“Dah! Ndugu yangu umebadilika sana mpaka nikahisi sio wewe ati” Ramah aliyanena hayo huku usoni akiwa na bashasha tele.



“Pengine ni kweli, lakini wewe umebadilika zaidi. Nilipata kusikia stori zako kwa broo Zuma hapa..” Ramah alimuangalia Zuma huku akitabasamu bado kisha akarudisha macho yake kwa Rommy..“ ....alikuwa akiniambia kuwa umebadilika sana kiasi ambacho kama ningekutana na wewe barabarani basi ningekupita bila salamu” Rommy aliongea na wote wakacheka.



Muda huo huo Jay aliingia humo kwa pupa, bilashaka kuna jambo alitaka kumuambia Ramah. Lakini akagwaya baada ya kuona ugeni. Akawatazama wote na macho yake yakaganda zaidi kwa Rommy. Kisha akaachia cheko dogo na kumfuata Rommy pale alipo. Rommy alisimama na kukumbatiana na Jay. Dakika mmoja wakakaa chini.



“Hii ni ajabu haki vile. Unajua juzi tu hapa nilikuwa namuuliza dogo kuhusu wewe. Na leo hii umetokea hapa. Dah! Kitambo sana Ethan, hivi ulipotelea wapi wewe?” Jay aliongea hayo na mwisho akamuuliza swali.



“Nilikuwa masomoni Nairobi na hapa nimekuja likizo tu kisha nitaondoka tena...”



Mazungumzo yaliendelea mpaka pale Mama Ramah alipoivisha chakula. Akatenga mezani kisha akawakaribisha watu hao. Hata pale walipokuwa wanakula, hawakuacha kuzungumza kuonyesha ni jinsi gani walikuwa wamekumbukana si kidogo.



Walipomaliza kula. Ethan akawataka ndugu zake wazungukezunguke mtaani hapo walau anaweza kukutana na marafiki zake wengine ambao aliwahi kufahamiana nao kipindi cha nyuma. Kuonyesha alikuwa na hamu na matembezi hayo na hakutaka bugudha yoyote. Aliwaruhusu walinzi wake wachukue gari wakatembee popote na kuwaambia kuwa atawatafuta atakapomaliza hamu zake. Paskal, Zumo na Assu hawakupinga hilo. Walipanda kwenye gari na kutimka maeneo hayo.



Majira ya saa tatu usiku. Rommy alimpigia simu Zuma kwaajili ya kumtaarifu kuwa, kwa siku hiyo atalala nyumbani hapo mpaka hapo kesho atakapo wapigia simu kwaajili ya kuja kumchukuwa. Zuma akaitikia sawa na simu ikakatwa. Usiku huo, Rommy aliupitisha nyumbani kwakina Ramah, nyumba ambayo alishawahi kuishi kwa muda miaka mingi nyuma.



Siku iliyofuata majira ya jioni. Rommy alikuwa tayari kuondoka hapo. Alikaa chini na Ramah kwaajili ya kuzungumza kama ndugu. Rommy alimueleza kuwa, huko jijini Nairobi, anasoma elimu ya chuo kikuu. Na hapo amebakisha miaka miwili ili ahitimu. Akamuahidi endapo atahitimu elimu ya chuo na kuanza maisha rasmi. Atahakikisha anamsaidia kimaisha nduguye kwa namna moja ama nyengine. Akamuachia kiasi cha laki nne ambacho alimtumia kwa njia ya mtandao akihamisha kutoka benki. Wakabadilishana namba za simu kisha hapo Rommy akaondoka baada ya kuaga familia hiyo huku Mama Ramah akimtaka kabla hajarudi Nairobi. Basi arejee tena hapo kwaajili ya kuwaaga.



“Yani siku ya leo ninafuraha sana mpenzi.” Ramah alinena hayo akiwa anaongea na Cecy kupitia simu. Majira hayo yakiwa ni usiku wa saa tano. Cecy akahoji ni furaha gani hiyo?. Ramah akamueleza yote kuhusiana na Rommy ambae yeye alimtaja kama Ethan. Pamoja na kuwa jina lilikuwa ni tofauti na lile analolijua Cecy. Lakini haikuwa ngumu kwake kumaizi kuwa anaeongelewa na Ramah ni yule Rommy anaemjua yeye. Ambae siku mbili zilizopita alimuambia kuwa ni ndugu na Ramah baada ya kuona picha yake ya utotoni aliyoiweka kwenye ‘WhatsApp profile ’.



Cecy akajidai kuhoji hoji maswali ikiwa ni geresha akizuga kutomfahamu kabisa huyo mtu anaemuongelea Ramah. Bila kujua, Ramah alimueleza vyema na kumuambia kuwa ipo siku atamkutanisha nae ili amjue. Cecy alikaa kimya akitafakari hayo anayoyaongea Ramah ya kutaka kumkutanisha na Rommy ilhali yeye anajua kila kitu kinachoendelea.



“Vipi Cecy? Mbona kimya?” Ramah alimuuliza baada ya kuona kimya kingi.



“Hakuna kitu..” akatulia tena kisha akasema. “Bilashaka mtakuwa mmefanana eee?” Ramah akajibu ndio lakini sio sana. Kisha yakafuata maongezi mengine.



Siku hii mpya ikiwa ni majira ya jioni. Katika hoteli ya kitalii iliyokaribu na ufukwe wa bahari ya Hindi almaarufu kama Mwambani Hotel. Katika meza mojawapo zilizopo katika mgahawa wa Hoteli hiyo. Ilikaliwa na Rommy pamoja na Cecy. Muda wote walikuwa wakiongea kwa furaha huku wakicheka kila mara.



“Unajua... Unajua Rommy siamini hata kidogo labda nishuhudie mwenyewe” Cecy aliongea hayo huku akicheka.



“Tatizo u'mbishi sana Cecy. Lakini siku moja nitakuchukua mpaka Mombasa ukashuhudie mwenyewe ili uamini... Kwani hapa Tanga pia mambo hayo si yapo huko Pangani. Tena kule ndio kuna mambo adimu ya zama za kale. Sasa sijui ni kipi kinachokufanya usiamini ya huko Mombasa” Rommy alinena hayo kisha akashushia na kinywaji chake.



“Basi inabidi siku moja kabla hujaondoka huku, unipelekea Pangani tukafanye ‘tour’ kule. Maana sijawahi kufika halafu watu wengi wananisimulia tu ya kule. Namini nataka niwasimulie wengine kama nisimuliwavyo mimi” Cecy alisema. Rommy akamuambia asijali, apange tu siku akiwa tayari amjulishe. Kimya kikatawala huku kila mmoja akiwa na bize chakula chake. Baada ya dakika tatu Rommy akauvunja ukimya huo.



“Cecy nimekumisi sana unajua?” Rommy aliongea akiwa anamuangalia Cecy usoni. Cecy akatabasamu na asijue ajibu vipi. Alishamaizi alichomaanisha kijana huyo.



“Bado mapema sana Rommy” Cecy akajibu hivyo na kugida kinywaji chake. Rommy akatabasamu kisha akaacha kutabasamu baada ya kuona Cecy akiinua macho yake kumtazama.



“Kwanini? Ama huniamini?” Rommy alihoji.



“Hapana! Sio hivyo my. Ila....”



“Ila nini Cecy? Eeeeh?” Cecy akabaki kimya asijue azungumze lipi. Akashusha pumzi baada ya kuona simu ya Rommy ikiita. Rommy aliitazama simu yake kisha akageuza macho huku na huko kama kuna kitu anatafuta hivi. Kisha akaipokea.







“Ok..” Alisema hivyo baada ya kusikiliza kwa dakika moja, kisha simu ikakatwa. Ilikuwa ni simu iliyotoka kwa Paskali aliemuomba wazunguke-zunguke maeneo hayo ili kufanya utalii mdogo. Nae akawaruhusu. Akamgeukia Cecy na kumuambia, simu hiyo imetoka kwa walinzi wake, wamemuomba watembeembee mahala hapo kung'aza macho. Cecilia ilikuepuka mazungumzo ya Rommy yanayoelekea kule asipotaka yeye, akamtaka na wao waende kutembea. Rommy akakubali!.



Wakati wao wakiendelea na ya huku. Upande wa Ramah mambo hayakuwa mazuri. Alishajaribu kuipiga namba ya Cecy mara kadhaa. Mwanzo ilikuwa ikiita kisha inakatwa. Lakini mara hii ilikuwa ikiita tu pasi na kupokelewa wala kukatwa kama ilivyokuwa mwanzo. Ana nini huyu? Ramah alijiuliza huku akiitazama namba ya Cecy kwenye simu yake. Akapiga tena!.



Ikawa vile vile, simu yake haikupokelewa. Ilikuwa ni hivi. Wakati yeye anampigia Cecy kwa mara ya kwanza. Cecy muda huo alikuwa na Rommy kule Mwambani Beach kabla hawajainuka kwenye viti walipokaa na kwenda kutembea. Aliiona simu ya Ramah ikiingia, akawahi kuikata kabla Rommy hajahoji chochote kuhusiana na simu hiyo. Kisha hapo akaitoa sauti, ikawa kila Ramah alivyopiga, iliita bila kutoa sauti. Mara hiyo sasa akawa huru.



‘Cecy unanini wewe? Pokea sim bas mara moja’ Ramah aliandika ujumbe huo na kuutuma. Cecy aliufungua na kuusoma, wakiwa wanatembea.



“Juzi na jana nilikuwa kwa kina Ramah...” Rommy aliikatisha sentensi yake baada ya kumuona Cecy akiwa ameshtuka na asijue kwanini ameshtuka. “Vipi?” Rommy alimuuliza huku anamtazama usoni.



“Hakuna kitu.. Ila hilo jina la Ramah umelijuaje wakati wewe unamjua kwa jina la Rafael?” Cecy alizuga na kupotezea kwa kuuliza swali. Ila ukweli ni kwamba, alishtuka ndio baada ya kusikia Rommy akimtaja Ramah ilhali yeye alikuwa akisoma ujumbe kutoka kwa Ramah. Alihisi huenda ikawa Rommy ameuona ule ujumbe.



“Ni kweli, sikuwa nalijua hilo jina. Lakini wewe uliponitajia hilo jina kwa mara ya kwanza wakati nakuuliza kuhusu yeye nilipomuona kwenye picha. Halafu nikalisikia kwa mara nyengine wakimuita hivyo pale kwao. Sikuwa na budi na mimi kulizoea na kumuita hivyo” Rommy alimuelezea.



Majira ya saa moja usiku. Walikuwa tayari kuondoka mahala hapo. Rommy na Cecy, waliingia kwenye gari jengine tofauti na lile alilokuwa akitembelea mara kwa mara. Muda huo Paskali alishatangulia kwaajili ya kuwaendesha wawili hao. Na kwenye lile gari jengine, aliingia Assu na Zumo. Msafara wa magari mawili ulianza kuondoka maeneo hayo taratibu.



Mwenye kudeka, hudekezwa bwama!. Cecy alikuwa huru kwa Rommy hata akahasau uwepo wa Paskali ndani humo. Pengine ni upendo ndio unaomsukuma kufanya hivyo bila kujali macho ya wengine. Wakiwa wamekaa kwenye siti za nyuma. Cecy alikuwa amemkumbatia Rommy utafikiri ni mwenye kuhisi baridi na alihitaji nguo nzito itakayo mkinga na hilo. Alideka si mas'hara!.



Rommy alitabasamu, Cecy nae alitabasamu. Rommy akacheka, Cecy nae akacheka. Walitazamana usoni kisha wakasogeleana nyuso zao taratibu kama wanaogopana. Nyuso zao zilipokaribiana kabisa vinywa vikapata urahisi wakugusana. Wakanyonyana mate mithili ya njiwa jike amlishapo kinda lake. Walipoachiana walitabasamu wote na Cecy akajificha kifuani mwa Rommy kwa aibu. Paskali aliekuwa akishuhudia vitendo hivyo kupitia kioo kilichokuwa juu yake alisikitika huku akitabasamu.



Dakika ishirini mbele magari yale yaliingizana kwenye viunga vya nyumba ya kina Cecy. Cecy alimuonyesha Rommy kuwa hapo ndio makazi yao yalipo. Rommy alipatazama kisha akatingisha kichwa juu chini kumaanisha kuwa ameelewa. Akamtazama Cecy usoni kisha Cecy nae akamtazama. Taratibu akapeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Rommy na kuachia busu safi kabisa. Kisha hapo akawa tayari kushuka ndani ya gari.



Gari zile zikaondolewa mahala hapo huku Cecy akizikodolea macho mpaka zilipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akatabasamu na kugeuka nyuma kwaajili ya kuingia nyumbani kwao. Akakutana macho kwa macho na mama yake aliekuwa amesimama akiwa ameshika ufyagio. Alionekana anataka kufanya usafi ama ameshafanya kabla.



“Haya! Mwenzangu usupastaa huo umeanza lini wa kutembea na magari mazuri namna ile?” Anita alimuuliza hayo huku akimtazama.



“Marafiki zangu mama wale, wamenipa lifti hapo njiani tu” Cecy alijibu.



“Ramah yupo wapi? Maana sio kawaida yako kurudi mwenyewe hapa unaponiaga unatoka nae” Anita alizidi kuhoji. Kitendo ambacho kilianza kumchukiza Cecy na kuona sasa hiyo ni kero.



“Tuliachana pahali, aliniambia mimi nitangulie yeye kunasehemu anaenda. Maana alipigiwa simu muda huo” Cecy alijibu hivyo kisha akaendelea kuingia ndani. Anita alimtazama tu kisha akaendelea kufanya usafi majira hayo ya jioni.



Mida ya saa nne usiku. Ramah alijaribu kumtafuta tena Cecy kwenye simu baada ya kumkosa jioni ya siku hiyo alipomtafuta. Alipiga namba ya Cecy na simu ikaita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa. Salamu ikafuata kwa wawili hao huku Ramah akifurahi zaidi baada ya kusikia Cecy hakuwa na tatizo lolote.



“Kuna muda nilikupigia simu sana lakini hukupokea. Ulikuwa na tatizo gani?” Ramah alimuuliza. Cecy akajibu kuwa, alikuwa mbali na simu hivyo hakuweza kupokea. Ramah akelewa na kumuuliza iwapo hakuziona ‘missedcall’ ama laa! Mpaka asimtafute?



“Ramah nini? Mbona maswali mengi hivyo?”



“Cecy maswali mawili tu ni mengi? Ama sipaswi kuuliza iwapo nina wasiwasi?” Ramah aliuliza katika hali ya kutaharuki.



“Ok. Niliziona lakini sikuwa na salio la kukupigia” Cecy alijibu. Ramah akamuuliza kuwa hakuwa na salio la kumpigia yeye ama hakuwa na salio la kupiga? Cecy akajibu hakuwa na salio la kupiga simu yoyote.



“Unajua Cecy sio rahisi kama wewe unavyofikiria. Haiwezekani ukute simu nyingi nilizokupigia halafu usinitafute ili ujue nina tatizo ama jambo gani nilitaka kukuambia. Sidhani kama ulikosa namna yoyote ya kunitafuta mpaka muda huu nilipoamua kukutafuta mimi tena. Na inaonyesha kama nisingekupigia muda huu, basi wewe usingenitafuta hata” Ramah alizungumza kwa upole akiwa ameficha hasira zilizoanza kumtawala juu ya majibu ya Cecy.



“Ndio namna nilikosa na nilijua kama utanitafuta tena ndio maana nikawa kimya” Cecy alijibu kwa dharau baada ya kuona Ramah akimletea kero.



“Haki vile Cecy unaumwa wewe. Embu pumzika, kesho nitakutafuta” Ramah alizungumza hayo akiwa na matarajio ya kuona Cecy akijirudi baada ya kuhisi alipokosea. Lakini Cecy alijibu Poa kisha akakata simu.



Ramah akabaki mdomo wazi huku akiitazama simu yake kwa mshangao. “Amekuaje huyu?” alijiuliza. Akampigia tena, lakini kabla haijaita akaikata. Akatabasamu na kuiweka simu pembeni. Akavuta gitaa lake na kuliweka sawa tayari kuliliza. “Nina siku nyingi sana sijakigusa hiki kifaa” akasema hivyo kisha akaanza kuvuta vyuzi moja moja kabla ya kuanza kuimba.



Cecy muda huu alikuwa amejilaza kitandani kwake. Alikuwa akiongea na Rommy kupitia simu. Ashukuriwe Mungu Ramah aliwahi kukata simu kabla haijaita kwa mara ya pili. Pengine angemaizi kama simu ya Cecy ilikuwa ikitumika majira hayo baada tu ya kukata simu yake. Huenda angeingiwa na mashaka zaidi.



Cecy alikata simu baada ya kuongea na Rommy takriban dakika kumi. Akaingia upande wa picha na kuangalia picha ambazo walizipiga siku hiyo walipokuwa kule Mwambani Beach. Kila alipokuwa akitazama picha hizo, ndipo tabasamu usoni mwake lilipozidi kuchanua. Akatulia kwenye picha moja ambayo iliwaonyesha wakiwa wamekumbatiana wakiwa kwenye maji mafupi ya bahari ile.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Haki vile hata nikiachana na Rafael nikabaki na Rommy sioni kama kuna ubaya. Japo wengi watanishangaa lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni mimi. Hawajui tu jinsi ninavyompenda huyu mtu...” Akazidi kutabasamu huku akiikuza taswira ya Rommy pale kwenye ile picha. “Ni kweli Ramah ananipenda lakini nami nampenda Rommy zaidi. Yeye ndie alieniingiza katika ulimwengu wa mapenzi. Akanionjesha kidogo utamu wa mapenzi kisha akaondoka. Leo hii amerejea nafasi yake bado ipo.... Dah! Ramah nitamuacha kwenye maumivu najua, lakini nimegundua sikuwa nikimpenda kwa dhati. Upweke na unyonge ndio ulinifanya niwe nae. Lakini hata hivyo siwezi nikamkataa mja kwa moja. Nampenda bado”



--------------







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog