Simulizi : Suprise
Sehemu Ya Tano (5)
Saa kumi na moja jioni, Victor anajitayarisha kutoka kwa ajili ya kwenda Airport, akasikia mlango wa chumbani kwake unagongwa, kumbe alikua ni Sarah, msaidizi wake.
"Samahani kaka, Mama Bill amekuja kitambo sana wakati uleule umeingia ndani, akasema nisikusumbue ataku..." Akamkata kauli kabla hata hajamaliza.
"Subiri kwanza, nani amekuja?" Aliuliza ili kupata uhakika kuhusu jina lile ambalo alilisikia,
"Mama Bill." Jibu la Sarah likamfanya Victor akasirike na kuongea huku akimnyooshea kidole,
"Nitakupiga Sarah! Mpumbavu wee, toka hapa!” Sarah akabaki amesimama akijiuliza kosa lake nini. Alipigwa na butwaa tu, maana anaona kama anakosewa tu, hajui lolote lililopo kati yao, akamuuliza
“Kaka mbona sikuelewi lakini? Mbona sasa unanitukana?” Aliuliza kwa upole mno kiasi ambacho jazba ya Victor ikapungua na kumwambia Sarah
“Mwambie huyo Mamam Bill atoke sasa hivi, nikitoka nisimkute hapo nje, akileta kiburi mwambie nitamuua." Alipomaliza kutoa amri ile akabamiza mlango na kurejea ndani kwake.
Kule chumbani aliita Taxi ili impeleke Airport, pamoja na kuwa na magari, lakini hakuwa na mtu wa kwenda nae ili aweze kurejea na gari, hivyo mara zote alilazimika kutumia Taxi kwenda Airport ama kituo cha basi. Kwa kuwa kituo cha Taxi hakikuwa mbali, Dereva Taxi alipofika akamjulisha kuwa yupo nje.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pale nje alishangaa kumkuta Eve akiwa amesimama akiwa na bandage kichwani, akamuuliza
"Wewe mwanamke bado upo tu? Sasa ngoja nikufundishe adabu na ndio utajua ni kwa nini Mbingu na ardhi ziliwekwa mbalimbali." Aliongea huku akimsogelea kwa kasi alipokuwa amesimama, Eve wala hakutetereka, kwani alikuwa tayari kwa lolote sasa.
Aliamini kila kinachomtokea sasa ni kile ambacho kinamstahili, kwani bila hivi alijua hatopata wokovu kwani inasemwa 'Mateso yakiongezeka jua wokovu umekaribia,' nae tangu awali aliisha amua kuwa kwa sasa yupo tayari kwa lolote, liwalo na liwe, bado alikuwa na upendo kwa Victor.
Lakini ujaji wa Victor ulimshitua kidogo akapiga magoti na kuficha sura yake, Victor alipofika akamnyanyua na kumpiga kelbu, wakati akianguka akamshindikiza na teke la mbavuni. Akamnyanyua tena na kumpiga kifuti, hali ikazidi kuwa mbaya, Sarah aliekuwa akishuhudia hali ile, akashindwa yeye binafsi kutoa msaada, hivyo akaanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Bahati mzuri dereva wa Taxi aliweza kumsikia na kuingia ndani kutoka kule nje alipokuwepo, muda wote huo Eve alikuwa akilia na kusema
"Wewe niue tu kabisa, lakini leo mimi sitoki humu ndani." Kwa msaada wa dereva Taxi na Sarah, waliweza kumuondoa Victor na kumchukua Eve aliekuwa sasa amepoteza fahamu kutokana na kipondo alichokuwa amekipata toka kwa Victor.
Eve aliekuwa hajitambui muda huo, wakamuingiza ndani ya Taxi, kisha Sarah na dereva Taxi wakaanza kujadiliana kidogo bila kusikika kile wanacho ongea, kisha Saraha akarejea kwa Victor aliekuwa akimtazama Eve kwa ghadhabu japo alikuwa mbali nae.
"Kaka tunaomba pesa tumuwahishe hospitali." Aliomba Sarah kwa nia njema tu
"We mjinga nini? Huyu ni ndugu yako wewe? Unamjua wewe, hebu achana nae."
Bila kuongeza neno lolote wala kutoa pesa, Victor akaingia ndani. Hakuna aliejua ni nini alikuwa akifuata, kumbe ni simu yake ilikuwa ndani kwenye charge alikuwa ameisahau, akasogea na briefcase yake hadi karibu na ilipo paki Taxi na kumsikia Eve akisema kwa sauti ya maumivu
"Victor hata kama utaniua, ni sawa tu, ila elewa mimi bado ninakupenda." Kwa muda huu Victor hakuwa Binadamu tena, aliisha poteza ile hali ya utu, sasa hivi alikuwa ni zaidi ya mnyama, tena mnyama mkali mwenye hasira ya kukoswa koswa na kifo.
Maneno yale ya Eve aliona kama vile yanamzidishia hasira, akamwambia akawapende wazazi wake kasha akashika vizuri simu yake na kupiga
"Hellow, mimi nitamuua huyu malaya, leo tangu asubuhi ananifuata fuata, amekuja ofisini, nikamuomba niondoke akanizuia, sasa amekuja na nyumbani, nitampiga risasi sasa hivi mimi," haikujulikana Victor kampigia nani simu ile, ila hata alie pokea simu ile ambae nae wala hakusalimiwa bali alianza kwa kukutana na tuhuma.
"Sasa hivi ninaingia ndani, nitakapotoka na kumkuta, ninampiga risasi, heri nifungwe."
"Kha Victor, ni nini? Mbona unaniambia maneno hayo nami nikiwa nipo mbali, ni nani huyo?" Kumbe Victor alikuwa amempigia simu Ommy ambae alikuwa kapigwa na butwaa kutokana na ukali wa maneno ya Victor, kwani hakuwa akijua chochote kilichokuwa kikiendelea
"Sijui yule bwege wake Ondiek kampiga chini sasa anadai amerudi kwangu, Ommy huyu mtu leo mie nitamuua!" Akakata simu.
Ommy akapata kazi nyingine, ikamlazimu yeye sasa ampigie simu Victor na kuongea nae. Kwa kuwa hakuna mtu ambae Victor anamsikiliza kuliko Ommy, alifanikiwa kumtuliza munkari, Victor akapoa na kumwambia Ommy awapigie simu wazazi wa Ommy wamfuate mtoto wao pale kwake, yeye anatoka kwa safari zake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kisha akamsogelea dereva Taxi na kumuuliza
"Unanipeleka mie ama unabaki na huyo changudoa garini mwako?"
"Kaka unasema?" swali lile likuwa ni kama mshangao kwa dereva, na hata kwenye kujibu jamaa alipata kigugumizi, Victor akarudia tena
"Mimi ndio nilie kuita unipeleke Airport, utanipeleka mimi ama utabaki na huyo malaya?" Dereva alipomtazama Eve huruma ikamuingia, akashindwa kujibu, ila akajikaza kisabuni
"Sasa kaka hebu angalia hali yake, tunapaswa kumuwahisha hospitali huyu kwanza."
"Mimi ningekuwa na haja ya kumuitia usafiri wa kumuwahisha hospitali, ningeita Ambulance, wala nisingeita Taxi, lakini nilikuita wewe ili uniwahishe mimi Airport, sasa kama huwezi, nitajua nitaendaje."
Victor nae akaona kuwa hawezi kuubadili ukweli kuwa dereva hayupo tayari kumshusha Eve na kumuacha ili ampeleke yeye Airport, akazama mfukoni huku akimsogelea Sarah, akatoa pesa kiasi na kumpatia huku akimwambia…
"Leo saa moja na nusu usiku huu mimi nasafiri, usiondoke hapa kwenda popote hadi nitakaporudi, hii ni pesa yako kwa ajili ya matumizi." Akaondoka kwa miguu tu huku akiwaacha Sarah na Dereva wakimtazama kwa jicho la mshangao. Mbele alisimamisha bodaboda iliyomuwahisha uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.
Kilichofuatia hapo ni Sarah ni kufunga milango mikuu ya pale nyumbani, kasha wakatoka kuelekea hospitali pasina Sarah kumjulisha mtu yeyote, maana hakuwa na namba ya mtu yeyote tofauti na Victor.
Kwa upande wake nae Ommy alitekeleza mazungumzo yake na Victor, akaongea na wazazi wa Eve na kuwajulisha juu ya kilichotokea kule nyumbani kwa Victor na baada ya dakika kadhaa wazazi wa Eve wakitumia Escudo ya Eve, waliwasili nyumbani kwa Victor na kukuta nyumba ni tupu tena ikiwa imefungwa na hakukuwa na hata mtu mmoja wa kumuuliza, ikalazimika wampigie simu Ommy awasaidie.
Nae akapiga simu kwa Victor ambae muda huo alikuwa hewani akiitafuta Uganda, hivyo simu yake haikuweza kupatikana. Sasa ikabidi wazazi wa Eve kukaa pale hadi saa nne usiku wakati Sarah aliporejea kutoka hospitali na kuwaeleza yote yaliyotokea.
Mwisho aliwaambia amemuacha Hospitali ya Amana, ward namba 7 kitanda C. Hadi siku ya pili hali ya Eve ilizidi kuwa mbaya maana bado alikuwa hata hajazinduka moja kwa moja, ilikuwa kila baada ya muda anapozinduka, anazima tena, ikamlazimu apewe rufaa kuelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kwa mara ya kwanza Mzee Dotto akampigia simu Ommy huku akilia na kumwambia
"Ni kweli Eve alimkosea mumewe, lakini hii wala haikuwa ni adhabu inayo mstahili," aliongea nae mengi sana na mwisho Ommy akaomba aachiwe lile tatizo atalishughulikia.
Ommy alimuhadithia Lidya mkewe ambae nae akashauri wawaambie wazazi wa Victor. Jukumu hilo akalichukua Lidya kuwasiliana na mama Victor. Bahati mzuri alipoongea nae alimwambia tayari anayo habari tangu siku iliyopita alipigiwa simu na Sarah na sasa wapo Muhimbili.
Mama Victor alimwambia Lidya kuwa hata Amana siku iliyopita, ni yeye ndio alilala na Eve. Lidya akashukuru ila kabla hajaaga, Mama Victor akamwambia Lidya wajaribu kuongea na Victor kwa alichokifanya sio kizuri na hawamuungi mkono hata kama alikosewa.
Wakati Lidya akiongea na mama Victor, Ommy nae alikuwa akiwasiliana na Victor. Upande huu hali haikuwa shwari kabisa, hasa baada ya Ommy kumueleza Victor hali halisi ya Eve, wala Victor hakushtuka bali akasema
"Waambie waende polisi kufungua kesi, tatizo lipo wapi? kama vipi mimi kesho jioni ninarudi, wanisubiri Airport wanitupe ndani, si basi? Tena hata nawe kuanzia sasa usinipigie tena simu za kunieleza mambo haya, tutakusana Ommy..." Akakata simu mara tu alipo maliza kusema maneno hayo, hata Ommy sasa nae akachanganyikiwa.
Alijaribu nae kumpigia tena kwa mara nyingine, lakini wala hakupatikana tena, akampigia simu Sabrina, akamjibu kuwa wameachana muda mrefu sana Victor akiwa ofisini yeye akawa amekwenda kwenye ofisi nyingine kushughulikia mambo mengine. Akamuomba akaongee na Victor awashe simu baadae waongee jambo la muhimu.
Siku hiyo Ondiek na dereva wao wa ofisini wakiwa sambamba na mpiga picha wao, baada ya kuona simu ya Eve haipatikani, wakaamua kwenda nyumbani kwa kina Eve ili kumuulizia kujua, huenda alizidiwa maana alijulikana kuwa naumwa tangu Rwanda.
Alishuka dereva tu kwani yeye alikuwa hatambuliki na pia ingekuwa ni rahisi kwake kujitambulisha, angeeleweka kwa muda mchache sana. Ondiek yeye hata kwa bahati mbaya asingeweza kuingia ndani ya nyumba ile tangu alipo haribu mara ile ya kwanza.
Ndani ya nyumba alibakia Msaidizi tu pekee, dereva baada ya kuingia na kujitambulisha na kumuulizia Eve, Msaidizi alimjibu kuwa hayupo na hawezi kurudi muda ule na kama ana shida nae muhimu kwa haraka aende Muhimbili hospitali kwani watu wote wapo huko, hivyo anaweza kupata habari zote huko.
Lidya na Ommy nao wakashauriana ni heri siku ifuatayo wapande ndege waende tena Tanzania, maana inaonekana Victor hatotoa msaada wowote kwa Eve, hivyo ni bora wao waende wakawafariji kidogo wazazi wa Eve na kuwapoza kwa kuwaambia vitendo alivyofanya Victor ni hasira tu, ambayo itafikia hatua itakwisha tu.
Lidya ndio alianza kuonekana kuchoshwa na safari za mara kwa mara. akamwambia mumewe kuwa yeye amechoka kabisa kusafiri, unakuta kila mwaka safari za nje ya nchi ni zaidi ya nne, akaomba safari hii yeye asiende, hasa ukizingatia aliisha muahidi Eve hawatoongea iwapo atarudiana na Ondiek na hakutaka kuvunja ahadi yake.
Ommy akambembeleza mkewe na kumwambia wanapaswa kwenda wote na wajitahidi kuwa ile ni safari ya mwisho kusafiri wakiwa pamoja, kwani atahakikisha mara tu baada ya kurejea, safari zote za matamasha hatoenda tena ila kwenye ile moja tu ya mwisho wa mwaka.
Hapo ndio Lidya akaridhia na Ommy akawasiliana na Wakala wao wa usafiri na kumuambia juu ya safari yao ya dharura ambayo wameipanga siku ifuatayo, wakala akawaambia wajitayarishe mapema tu saa 12 asubuhi kuna ndege ya moja kwa moja kuelekea Tanzania.
Kwa kuwa muda ulikuwa ukienda bure pasina Ondiek na kundi lake kutoa habari yoyote ya msingi wala yenye uzito mkubwa, Mkurugenzi wa Radio Kigezi, akamuamuru Ondiek na kundi lake lote lirejee nyumbani haraka, ikiwezekana waondoke siku ileile ama alfajiri ya siku ifuatayo.
Ile ilikuwa ni amri ambayo hakukuwa na wa kuipinga. Lakini Ondiek alimwambia Mkurugenzi wake kuwa hali ya Eve ni mbaya kutokana na kipigo alicho kipata toka kwa mpenzi wake, akauficha ukweli kwa kutokumwambia kuwa alipigwa na mumewe.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sababu iliyo mfanya aseme uongo ni kuwa, Eve kule Rwanda aliandika kwenye Mkataba wa ajira kuwa hajaolewa, sasa vipi tena aseme kapigwa na mumewe? ikalazimu hapo aseme uongo. Mkurugenzi akasema wao warudi peke yao na suala la Eve akipona watalishughulikia.
**********
Saa 3 asubuhi Ommy na Lidya wakiwa na watoto wao Bill na Jam waliwasili toka Kenya. Ommy alikwenda kwenye ubao wa taarifa za ndege ili kusoma ratiba ya ndege kutoka Uganda zitaanza kuwasili saa ngapi. Alikuta moja tayari iliwasili tangu saa 1 asubuhi.
Ratiba ilionesha ndege nyingine itawasili saa 5 na ya mwisho itaingia pale uwanjani saa 12 jioni. Walkaondoka kuelekea nyumbani kwa Victor, kwani walikuwa wameisha zoea kufikia kule, iwe Victor yupo ama hayupo, maana hata Sarah alikuwa akiwajua vema.
Nyumbani walimkuta Sarah peke yake ambae alikuwa mazingira hayo ya kuwa peke yake aliisha yazoea, aliwapokea na kuwakirimu sana, watoto wote walw wawili walikuwa wakimpenda sana Sarah. Lidya akamuuliza kama Victor amefika, akasema bado hajarudi.
Siku hii ya Jumapili, siku ambayo Lidya na mumewe wametua Tanzania, ni siku ambayo huwa ni kawaida kwa hospitali za serikali kuruhusu watu kuingia wodini kwa muda mrefu kutazama wagonjwa wao, hasa mida ya mchana, ambao kwa siku za kazi huwa hairuhusiwi.
Walioga na kuelekea mezani kupata chakula cha mchana, walipomaliza kula Ommy akawasha TV ili kuvuta muda kidogo. Muda ule alikuwa akitazama Classic TV, kulikuwa kuna kipindi cha Katuni alicho wawekea watoto wao wapendwa.
Ommy na Lidya pamoja na Sarah walikuwa wameketi kwenye sofa, Bill na Jam walikaa chini wakiwa makini wanatazama TV.
Ghafla ikatokea Habari MUHIMU. Katuni zikakatishwa ili kuipisha hiyo habari muhimu iliyo pewa uzito wa kipekee.
"Habari zilizo tufikia hivi punde, zinasema kuwa aliekuwa mtangazaji wa Classic FM na Classic TV, Mr. Ondiek, amefariki kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea wastani wa saa moja na nusu iliyopita.
Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika ila inahisiwa kutokana na ulevi kupita kiasi pia kuendesha gari kwa mwendo kasi. Ajali hiyo imetokea maeneo ya Chalinze walipokuwa wakielekea nchini Rwanda ambapo Mr. Ondiek alikuwa akifanya kazi huko.
Hali ya dereva wa gari hilo, ni mbaya na amekimbizwa hospitali ya Tumbi huko Kibaha, wakati mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, Amin!" na wote wakajikuta wakiitikia Amin wakiwa kama vile hawaamini kile kilicho tokea.
Hapo ndio ikawa ni mwisho wa habari ile Muhimu na vipindi vingine vikiendelea kama kawaida.
Wote bado akili zao zilikuwa zimezama kwenye habari ile muhimu, Ommy alikuwa akijisemea moyoni kuwa kumbe ni kweli Ondiek alikuwa Tanzania? Hawakuamini kabisa japo Mkurugenzi aliwaambia hivyo.
Lidya nae hata alikuwa kama hajielewi elewi, ghafla wakasikia sauti ikisema
"Mungu analipa hapa hapa duniani, wa kwanza huyo, bado na huyo mwingine." Ilikuwa ni sauti ya Victor akiunga mkono ajali iliotokea na kupelekea kifo cha Ondiek. Wote walipoisikia sauti ile walishindwa kuongea lolote, bali walitazamana tu.
Victor akawa tayari yupo usawa wa watu wote kumuona, akiwa na simu mkononi, akairejesha mfukoni na kusimama akiwatazama watoto kwanza akiwa na tabasamu usoni.
Jamillah alipoisikia sauti ile akageuka na kumuona Victor, akanyanyuka mbio na kumkimbilia kumlaki, tayari mzigo wake ulikuwa umepokelewa na Sarah aliuweka ndani.
"Ooh Uncle Vee Shikamoo!" Alizoea kumkatisha jina lake, Bill nae akafuatia
"Shikamoo Dad" akaitikia kwa furaha kubwa usoni kasha akawanyanyua wote na kuwaweka kifuani kwake huku akiwatania na kuwachekesha. kisha akawashusha na kuungana na wale wengine kwenye sofa.
Baada ya salamu Akamuuliza Lidya kuwa bado wanaendelea na Surprise tu? Wakacheka kasha akawaambia amewasiliana na mdau wao mmoja amemwambia kuwa Ondieka alikuwa hapa Dar kwa zaidi ya wiki sasa,
“Tena alitakiwa kutuhoji juu ya ajali yetu lakini akashindwa na hatimae kafa yeye,” aliongezea Victor huku akiwa na furaha kabisa moyoni. Akanyanyuka na kuekea ndani kubadili nguo.
Saa saba kamili ndio muda ambao walikuwa wamepanga watoke pale kuelekea hospitali, ulipowadia Lidya akamuomba Victor waongozane nae. Hilo jicho Victor alilomtazama, lilimfanya ajute kumuambia vile. Akazugazuga na kutoka nje, akimuacha na Ommy.
Ommy nae hakutaka makuu, akamuaga na kuekea nje pia, lakini alipokuwa akitoka akawa ni kama mtu anae jishauri kitu fulani hivi, akamrudia na kumwambia
"Victor ndugu yangu ni kweli Eve amekukosea, lakini hutakiwi kumtendea hivi unavyo mfanyia, yule ni mkeo pia ni mzazi mwenzio, naomba twende angalau ukamuone." Ommy akamtazama
"Ommy naamini unatambua ni kiasi gani nakuheshimu, wala haina kipimo, ila kwa hili sasa, samahani sana kaka yangu, nyie nendeni tu." Alisema huku akimkumbatia Jam na Bill akiwa kasimama mgongoni akaimchezea kola la shati yake.
"Haya bhana," kisha akawaita watoto ili waende nao, Victor akadakia
"Sasa si muende peke yenu tu? Watoto mie ninabaki nao hapa."
"We, we we, hapo sasa hata nami sikubali, watoto ni lazima waende." ukazuka mtafaruku
"Ommy watoto hawaendi popote ndugu yangu, yaani wapoteze muda kwenda kumuona yule shetani? Hiyo haiwezekani."
"Victor unakosea sana, yule ni mama yao tu na daima itabaki hivyo." Aliongea Ommy.
"Thubutuu, nani kasema? Unafikiri watoto watajifunza nini kwake yule kama sio upotevu tu." Jazba ilikuwa juu sana kwa Victor. Wakati akiongea wakiongea, Bill na Jam wakatoka wakiwa wameshikana mikono Victor akiwa hana habari, aliposhituka kuwa watoto hawapo, nae akatoka kuwafuata.
Macho yalikuwa ni mekundu kama koboko, akampita Ommy aliekuwa amesimama mlangoni na kuelekea nje hadi kwenye Baloon. Jinsi alivyokuwa akija, Lidya akaogopa na kumuuliza
"Vipi Shem?"
"Shusha watoto garini na mwende peke yenu, kama na nyie hamtaki rudini ndani tukakae." Aliongea kwa sauti nzito lakini kali. Lidya hakubisha wala kujishauri, palepale, akamshusha Bill ambae alikuwa yupo upande wake, Victor akazunguka upande wa pili na kumshusha Jam.
Akawashika mikono na kuanza kurejea ndani akakutana na Ommy aliekuwa akitoka, kwa ghadhabu nae sasa akampandishia Victor na kutaka hata kupigana nae, alichoka kubembeleza
"Hivi we Victor Umechanganyikiwa?" Victor akasimama na kumtazama Ommy huku akimuuliza
"Kwani hawa watoto ndio usafiri? Nyie si mwende tu peke yenu!" Lidya akaona leo... Kazi ipo, na kama asipokuwa makini, kunaweza kutokea tukio baya.
"Baba mbona sisi hatuendi na Uncle Ommy na Aunty Lidya?" Aliuliza Bill na swali hilo likakaziwa na Jam
"Eti uncle Vee?"
"Sisi tunakwenda kula Ice Cream pamoja na dada Sarah, sawa watoto wazuri?" wakaitika sawa huku wakifurahi.
Lidya akashuka garini na kwenda kumchukua Ommy ambae nae alikuwa amekasirika vibaya huku akimtazama Victor akiingia ndani na watoto. Akambembeleza mumewe na kumuomba aepushe shari, aingie garini waondoke. Ommy kwa shingo upande akakubali na kuingia garini. Lidya akawasha gari haoo wakaondoka zao kuelekea Muhimbili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya gari wote walikuwa kimya kabisa, hakuna aliekuwa akiongea, kila mmoja aliwaza lake. Lidya ndie alievunja ukimya kwa kuhoji tabia ya Victor
"Kumbe Victor ni mkorofi kiasi hiki?" Alimuuliza mumewe huku akimtazama kwa jicho la udadisi.
"Yaani sijawahi kumuonaVictor katika hali hii, huyu mwanamke ameleta tatizo ambalo hatma yake hata siijui." Alisema Ommy huku akitikisa kichwa.
"Hii ndio kama aliegundua pesa, kaisha kufa huku nyuma katuachia majanga matupu na maisha ya mashaka, ndio alicho kifanya Eve." Aliongezea Lidya.
"Umeona nawe, sasa mimi ninaamini iwapo Victor atalazimishwa chochote juu Evelyn, bila ya busara kutumika, basi kuna mmoja anaweza kudhurika, maana hata yeye mwenyewe haoni hatari kufanya chochote, amekuwa ni katili sana." Aliongea Ommy na kutoa fursa kwa Lidya kuhoji
"Hivi unafikiri ni kwa sababu gani?"
"Ujue Victor alimpenda sana Eve na kujitoa kabisa kimaisha kwake akiamini Eve ndio kila kitu kwake, sasa Eve amemlipa tofauti na Victor alivyokuwa akijua atalipwa." Alijibu kiurefu Ommy.
"Ndio maana Victor amekua sio yule tena ambae tunamjua hasa linapokuja suala la Eve."
"Alimpa moyo wake akiamini yule ni fungu lake, kumbe dah!"
"Ah! Eve amekuwa chanzo cha yote haya..." Aliongea Lidya
"Sio Eve, nyie wanawake ndio chanzo cha kila tatizo hapa duniani. Ni matatizo matupu, si basi tu, tunalazimika kuishi nanyi."
"Usiseme nyie wanawake, ni baadhi tu ndio wanao chafua sifa yetu, kwani hakuna wanaume wanaofanya kama haya aliyofanya Eve?" Aliuliza Lidya nae akionekana kukerwa na kauli ya mumewe Ommy.
"Kwani mna maana nyie?" Ommy hakujibu bali aliongea na kuzidi kumkera Lidya.
"Haya kama ni wanawake wote, niambie mimi nimekukosea nini?"
"Labda muda tu bado haujafika, nitajuaje mie?"
“Mapenzi yalimuua Romeo Julieth akabaki, pia ilitokea kwa Jack wa Titanic na Rose akabaki vilevile wengine kibao wanaume wanakufa kwa ajili ya mapenzi, akiwemo St. Valentine, nyie wanawake mpo tu…” Haya maongezi walipokuwa wakiongea hakuna aliekuwa akitania, kila mmoja alikuwa anamaanisha kile alichokuwa akikisema.
“Unakosea unapochanganya wanawake wote Ommy,” alisema huku akimtazama mumewe kwa jicho la kero
“Na hamjatofautiana sasa, kungekuwa na tofauti nisingewachanganya hivi…”
"Sasa mimi naona huu ugomvi utahamia kwetu, hebu tunyamaze na kukaa kimya." Lidya tayari alikuwa ameisha pandwa na jazba alisema na kuufunga mjadala. na kweli hawakuongea tena hadi walipoingia ndani ya wodi.
Jioni wamekaa maeneo ya Mnazi mmoja, wapo Victor, Bill, Jam na Sarah wakiwa wanakula Ice Cream, simu ya Victor ikaita kwa fujo sana. Akatoa simu yake na kuitazama, akakuta ni namba ya mzee wake aliekuwa akitaka kujua muda huo yupo wapi.
"Nipo Mnazi mmoja."
"Utakuja hospitali saa ngapi?"
"Nani? Mimi? Nije hospitali? Kufanya nini?" Aliuliza Victor kwa mshangao, kama hajui lolote.
"Wewe ni mwendawazimu eti? huji kumuona Eve?"
"Samahani Mzee kwa hilo, mimi siji na wala sitakuja." Baada ya jibu hilo Mzee Maganga alikasirika sana na kumfokea mno Victor
"Haya kama wewe hauji, mlete Bill aje kumuona mama yake."
"Baba mi siwezi kumleta Bill kumuona huyo, kwani huyo si mama yake."
"Hivi wewe Victor una kichaa? Hya huyo Bill mama yake ni nani?"
"Ninaamini alikufa tangu siku ile aliyomtelekeza," hiyo ilikuwa ni sehemu ya ya majibu ya maswali toka kwa baba na mwana.
Kutokana na Mzee Maganga kutumia sauti kali, ikawalazimu Ommy na Mzee Dotto waliokuwa pale jirani nao wasogee na kuhoji kulikoni.
"Mimi ninafikiri huyu mtoto amechanganyikiwa." Ikawa haina budi tena, Ommy kuingilia kati, akamuomba simu na kuikata kisha yeye akampigia Victor. Alikubali yeye kuwa mpole na kuongea nae kwa ufasaha na utaratibu wa hali yaa juu bila kukatiza.
Upole wa Ommy na maneno laini aliyo tumia yakamfanya Victor machozi yamtoke na kuridhia kumpeleka Bill akamuone mama yake, lakini akaapa hatoingia wodini. Akawasha gari na kuelekea Muhimbili na kumtaka Sarah awapeleke watoto ndani wakamuone Eve.
watu wote wakiwa wameketi wodini hawana hili wala lile, hali ya mgonjwa ilianza kuridhisha sasa. kwani alianza kupata nafuu na muda ule alikuwa akila kipande cha chungwa akiwa anatazama mlangoni, ghafla wakamsikia akisema
"Jamani Bill mwanangu," kama mtu alietaka kunyanyuka na kukosa nguvu, nao wakamzuia asinyanyuke, Bill ndio akamkimbilia mama yake. Pale pale kitandani akamkumbatia mwanae na kuanza kulia, kitendo ambacho kiliwahuzunisha wengi hadi Lidya alietokwa na machozi.
Wakamtuliza Eve na sasa akaanza kusalimiana na Jam ambae alianza kumuadhibu kwa maswali
"Aunty ulikuwa wapi? Halafu mbona umeumia hivi?" Yalikuwa ni mateso maswali yale.
"We Jam hebu muache Anti apumzike," Ommy ndio akaokoa jahazi baada ya kuona Eve akilengwa na machozi kutokana na maswali ya Jam.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Dotto akamuuliza Sarah kama wamekuja na daladala, Sarah akamjibu kwamba wamekuja na Kaka Victor. He! Si wote wakatazamana? Ina maana Victor amekuja hadi hospitali na hajaingia ndani?
Na kweli kama baada ya dakika 3 hivi, Ommy akapokea simu iliomtaka aende nje na watoto, Ommy akamwambia sawa, maana alikuwa ni Victor huyo aliepiga simu.
Kazi ikawa hapo, maana ilionekana dhahiri kuwa Eve bado ana hamu ya kukaa na mwanae, lakini ile simu ikamlazimu awaambie ni kipi kilichosemwa, akamwambia Eve kuwa Victor yupo nje anawataka watoto.
Kwa majonzi na huzuni tele na machozi yakimtoka, akambusu Bill na kumwambia wataonana kesho. kisha akaangusha kilio kikubwa sana wakati huo Jam alikuwa mikononi mwa Sarah na Bill ndio alikuwa anachukuliwa na Ommy na kuelekea nje alipo Victor.
Walitoka nje wakiwa wameongozana, mbele kabisa akiwa Sarah na Jam, kati alikuwepo Ommy aliembeba Bill na nyuma kabisa alifuatia Mzee Maganga hadi nje kabisa walipomkuta Victor akiwa amesimama mlango wa nyuma wa gari la kampuni.
Lilikuwa ni gari jipya kabisa aina ya Benzi la rangi nyekundu, alipowaona tu wamekaribia, akafungua ule mlango aliokuwa ameegamia, Jam alianza kuingia akifuatiwa na Sarah kisha mwisho akaingia Bill na kufunga mlango huku Victor akiwatazama watoto wao.
Sasa ndio akawageukia Ommy aliekuwa sambamba na baba yake Victor, akawasalimia lakini muitikio wa Mzee Maganga ulionesha kabisa kuwa ana kitu kinacho msumbua moyoni na alihitaji kukitoa, na hakuona muda tofauti na ule pale.
Waliongea kwa takribani dakika 10 pasina kufikia muafaka, hadi Mzee Maganga akatishia kumlaani Victor iwapo tu hatotaka angalau kwenda kumuona Eve mkewe. Pamoja na mkwara huo, bado Victor alisimika, akamuomba tena msamaha baba yake kuwa hatoweza kufanya hilo.
Kilichokuwa kikiendelea pale mbele ni kujaza watu tu, Ommy hakuwa tayari kwa hilo, hivyo alichokifanya ni kumuingiza Victor garini na kumtaka aondoke arejee nyumbani nae akabaki na Mzee Maganga akimpoza kwa ahadi ya kuendelea kuongea na Victor.
Alimfahamisha kuwa hatua ile ya kumleta mtoto leo ni hatua kubwa kwao, kwani hapo awali hakukubali hata kumuachia dakika moja kwenda kumuona mama yake, lakini jioni hii amemleta mwenyewe, wapunguze haraka kila kitu kitakaa sawa, muhimu subira.
Kidogo Mzee Maganga alionekana kuelewa sasa, wakarudi hadi ndani ya wodi na kumkuta Lidya akiwa anammenyea chungwa lingine Lidya ambae sura yake kidogo ilianza kuonesha matumaini na ile hali ya kukata tamaa ilianza kupungua taratibu.
* * * * *
Baada tu ya kupata taarifa ya ajali ya gari iliyopelekea kifo cha Ondiek, Mkurugenzi wa Radio Kigezi Mzee Kulwa Danga alikodi ndege ndogo akiwa na wawakilishi wawili kutoka kwenye radio yake ili kuja kuwahi taratibu za mazishi ambazo ni lazima zilikuwa zifanyike Tanzania.
Sabrina nae alipanda ndege huko Kampala mara tu baada ya kupata taarifa ya msiba ule na kuwasili siku hiyo hiyo ya Jumapili, siku ambayo Victor aliondoka kule Uganda. Wakiwa wamepishana muda tu wa kuwasili Tanzania.
Wote walirudi nyumbani kutoka hospitali na kumkuta Victor akiwa amelala, hawakutaka kumsumbua, walihisi atakuwa amechoka mno na safari zake za mara kwa mara.
Asubuhi mara tu baada ya kuamka, Victor alijitayarisha na kufungua kinywa ikiwa ni mapema zaidi, maana watu wote bado walikuwa wamelala isipokuwa Sarah peke yake. Akaelekea chumba cha watoto, akawaangalia na kutabasamu alipo waona wamelala.
Akafunga mlango na kutoka kuelekea kazini ili kupata mipango ya maendeleo ya tamasha la Kampala inavyokwenda ukizingatia Sabrina mwenyewe alikuwa katua Bongo kuhudhuria mazishi ya mume wake wa zamani.
Jambo la ajabu ni pale ilipotimia saa 5 Victor akamuona Sabrina katua ofisini kwake, hakutegemea kabisa kumuona muda ule ukizingatia ni kama saa moja iliopita ndio muda ambao ulitangazwa kuwa utafanyika mazishi ya Ondiek.
Walizungumza sana hadi Bina akajisahau kama amekuja msibani, matatizo yote akayaweka pembeni na kujiona ni kama mtu mwenye furaha tena. Victor alipomuuliza kuhusu mazishi, Bina akamwambia tayari wamezika saa 4 na walipoondoka kwenda Kisutu, nae akaondoka kuja ofisini kuendelea na majukumu mengine.
Baada ya saa moja kupita, yaani saa 6 mchana, wakaingia Ommy na Lidya na kuwakuta Victor na Sabrina wakiwa ni wenye furaha. Wakanyanyuka na kuwakaribisha kwa kuwapa mikono huku Lidya akimkumbatia Bina na kumpa pole kwa kufiwa na mumewe wa zamani.
Furaha iliendelea kutawala hadi ilipotimia wakati wa kula cha mchana. Victor akashauri kama vipi waagizie tu chakula wakiwa palepale, lakini Lidya alipinga na kusema kule nyumbani Sarah amepika chakula kingi ambacho kinawatosha wote pale, hivyo ni lazima kiliwe kile chakula.
Sabrina akamuunga mkono Lidya kuwa chakula kile ndio kinatakiwa kiliwe, hivyo wafanye mpango wa kuondoka ili kwenda kula nyumbani. Ommy aliekuwa kimya muda wote, akawaambia wenzie ni bora kifuatwe na kuja kuliwa pale. Nani wa kujitolea kukifuata.
Victor nae akawaunga mkono kukifuata ila akagoma mtu yeyote kutoka pale bali akampigia simu Dereva na kumtaka kwenda nyumbani kwake kuchukua chakula na kukileta pale ofisini, alishangaa kwani haijawahi kutokea, lakini leo ndio imekuwa hivyo.
Kauli ya Boss haipingwi, wakati dereva akiondoka, yeye akachukua simu yake na kumpigia simu Sarah na kumwambia amtayarishie chakula cha kutosha watu wanne kuna mtu anakifuata amemtuma. Sarah akaitika sawa na Victor akakata simu na kuendelea kupiga porojo.
Wakati wao wakijumuika kwa chakula cha mchana ofisini, Mzee Kulwa Danga, Mkurugenzi wa Radio Kigezi FM alikuwa nje ya majengo ya hospitali ya Muhimbili kama alivyokuwa ameelekezwa na Ondiek kabla ya kukutwa na mauti, nia yake ni kumuona Evelyn.
Bahati mbaya alikuta tayari kaisha ruhusiwa, hata hivyo alifanikiwa kupata ushirikiano wa kutosha, kwani alielekezwa kwao na mmoja wa manesi wa hospitali ile ambae alikuwa akimfahamu vema Eve kutokana na kuishi nae jirani na pia umaarufu wa Eve.
Kutokana na uenyeji kidogo alionao hapa jijini Dar Es Salaam, alioupata kipindi cha nyuma kidogo wakati alipokuwa yupo chuo akisoma, aliweza kupaelewa Victoria hapo Kijitonyama na kuamini kama ikitokea akapotea, basi haitokuwa mbali sana na nyumbani kwao.
Taratibu tu chakula kikawa kinalika huku porojo zikiendelea kwa furaha kubwa, wametawaliwa na amani tele kwenye mioyo yao, hakuna aliekumbuka kama kuna mtu anaitwa Eve, si Lidya, Ommy, Victor wala Bina…
Lidya akamkumbushia Victor baadhi ya maneno ambayo aliyatamka kwa ghadhabu mbele ya baba yake Mzee Maganga, walicheka kwa nguvu na Victor akitikisa kichwa akiwa na tabasamu usoni.
Akamwambia shemeji yake kuwa anapenda sana watu wale kwani wanasababisha afurahi wakati ambao hatamani hata tu kutabasamu.
“Nilifanya vile kwa sababu niliamini ni vigumu sana kufanya vile, hasa ukizingatia sijawahi kufanya hivyo mbele ya mtu yeyote seuze mzazi,” aliongeza Victor.
“Sasa kwanini ulifanya hivyo? Huoni kuwa ulionesha kiburi?” aliuliza Bina.
“Hapana! Ukifikiria hivyo Sabrina utakuwa umefeli, mimi nilifanya vile ili tu kuonesha hisia zangu na nikapenda nazo zithaminiwe, kwani name nina hisia zangu tofauti na za wengine wakiwemo wazazi wangu,”
Ommy akaona huu sasa ndio wakati muafaka kwa yeye kulianzisha lile suala la kuketi chini pamoja na wazazi na kuwakutanisha na Eve. Alipolianzisha tu, Victor akaonekana wala hayupo tayari kulizungumzia suala lile, maana alionekana kuchukia.
Akamtazama Bina na kumgeukia Lidya kisha akamuuliza
"Shem mnaondoka lini?"
"He! Shem, hata wewe wa kutuuliza sisi tunaondoka lini?"
"Ah! Unajua Shem, huyu ndugu hapa ananiudhi, bado anang'ang'ania tu kuzungumzia habari za yule Ibilisi." Haikujulikana kilichomkasirisha ni kipi, kulizungumzia jambo lile mbele ya Sabrina ama bado alikuwa na hasira zake.
Wakakubaliana jambo lile waliache kama lilivyo na waendelee na mambo mengine, Lakini Lidya hakuridhika na maamuzi yale, akamwambia Victor kuwa umefika wakati sasa Eve anatakiwa kusamehewa. Akamuelezea jinsi alivyokuwa wakati wao walipokwenda hospitali.
"Shem mimi ninajua ni kwa kiasi gani umeumia kutokana na kitendo alichokufanyia Eve, lakini sikia Victor..." Hapo akamuelezea ni vipi Eve aliwapokea wakati alipowaona wakiingia hospitali. Alimwambia Eve alilia sana na kuomba msamaha.
Zaidi alimuomba Lidya aongee na Victor, lakini pia alimuomba radhi Ommy kwa kuwadhalilisha Pamoja na kuwa hata yeye aliwahi kumuahidi kutokumsemsha wala kumsamehe iwapo watarudiana na Ondiek, lakini sasa alimsamehe tena bila sharti lolote.
"Hivyo Shemeji yangu Victor ninaomba umsamehe kama ambavyo sisi tumefanya, au sio Ommy?" Lidya alimuuliza mumewe huku akimtazama kuomba sapoti. Ommy akakazia
"Yeah! Ni kweli Victor, jaribu kufanya hivyo," alisema huku akimtazama vizuri Victor, lakini jibu sasa la Victor ndio liliwakatisha kabisa tamaa na wao kujihisi tayari wameshindwa, aliuliza
"Tayari mmemaliza? Kwa sababu mimi ninataka kumpeleka Bina kule Guest alipofikia." Ommy akanyanyuka na kumshika mkono Lidya bila kujibu lolote na kuanza kutoka nje hadi walipopaki gari lao aina ya Benzi jekundu na kuondoka.
Bina na Victor nao wakatoka na kuelekea nje ilipopaki gari nyingine ya ofisi aina ya VX ambayo waliitumia kwa safari za Rwanda na Burundi, nao wakaondoka kuelekea guest alipofikia Bina.
Mkurugenzi wa Radio Kigezi alifanikiwa kufika nyumbani kwa wazazi wa Eve, bahati aliwakuta na wazazi wa Eve. Eve alionekana kutokuamini mara tu alipomuona bosi wake kutoka Rwanda, hakutegemea kabisa kitu kama kile kutokea.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada tu ya kumfikisha hotelini alipofikia, Bina akasema anataka kuwaona watoto na lakini anapenda kutoka nao jioni ya siku ile wakiwa pamoja, hivyo akamuomba Victor aende nao wakati anakwenda kule jioni kulala, Victor akakubali na kumbusu na kutoka.
Eve Alimkaribisha na kumtambulisha kwa waliokuwepo na kuendelea kuongea nae kwa bashasha. Mzee Maganga akampigia simu Ommy na kumuuliza ni wapi alipo, Ommy akamjibu kwamba yupo nyumban muda ule akijitayarisha kwenda kumuona Eve, basi mzee Akaamuru Ommy asimuache Bill, aende nae ili akamuone mama yake.
* * * * *
"Nimefuata mtoto wangu tu humu ndani, nipeni niende!" Aliongea Victor na kuwaangalia watu wote waliomo mle ndani.
"Victor mtoto wangu, mbona umekuwa hivyo? Hata salamu hakuna?" Aliuliza Mzee Dotto na kufanya Victor akumbuke kuwa hajasalimia
"Wazee samahani sana, shikamooni nyote," wakaitikia huku wakimtaka akae chini.
Alikaa huku akitazama sa kama mtu ambae muda wa muhimu unamuacha kwa jambo lisilo na tija kwake, Mzee Danga akamkumbuka sura lakini hakusema lolote kutokana na mshangao alioupata mara alipomuona ameingia na jazba.
Lidya akatokea ndani akiimba kwa sauti ndogo na Jam, aliponyanyua sura yake mbele, akakutanisha macho na Victor aliekuwa amefura kwa hasira, akajitoakimasomaso kwa kumkaribisha
"Vip Shem, karibu huku ndani, mama Bill yupo huku na Bill."
"Ahsante sana hapahapa panatosha," Lidya akakaa kidogo na kuondoka tena kurudi chumbani na kumwambia Eve kwamba Victor yupo pale sebuleni.
Eve hakuamini masikio yake, wale wengine nao hawakutaka kuamini kile akisemacho Lidya.
Ommy akiwa mbele, alifuatiwa na Mama Victor na wengine walikuja nyuma yao, hata na Eve ambae alikuwa hawezi kutembea kwa sasa alikuwa anajikongoja kwa kushikwa upande wa kulia na Liya, huku kushoto kwake akiwa amemshika Bill.
Jamila sasa alikuwa kwenye mikono ya Victor wakati msururu wa waliokuwa ndani ukiikaribia sebuleni. Victor alipogeuza uso wake alipandwa na jazba, hali ambayo ilijionyesha kwa wote. Kama umeme alikwenda kumchukua Bill na bila kumsemesha Eve aliebaki amepigwa butwaa.
"Wazee mimi ninashukuru sana, ninatoka... Jamillah twende," Eve akajitoa kwenye mikono ya Lidya na kujipeleka mzima mzima kwenye mwili wa Victor na kusema
"Samahani mume wangu Victor, ninaomba niongee nawe japo kidogo tu." Machozi yakimtoka.
"Sina muda huo, tena toka mbele yangu, watoto wanasubiriwa huko," bado Eve hakubanduka.
Victor akajaribu kumchomoa lakini Eve alikua amemshika barabara mwilini mwake, akamuweka Bill chini na kumsukuma kabisa chini na bahati mbaya Eve akaangukia mezani na kujigonga kichwani, alitoa sauti kali mno ya maumivu na kisha kupoteza fahamu.
Watu wote wakaanza kumlaumu Victor kwa kitendo kile, mama yake akiwa ni mbogo zaidi
"We Victor ni kiumbe wa aina gani usie hata na chembe ya huruma hata kidogo?" akaondoka kwa ghadhabu na kumsogelea pale alipokuwa Eve, bahari nzuri alikuwa tayari ameanza kurejewa na fahamu. Kuna maneno alikuwa akiyasema kwa sauti ndogo
"Nisamehe Victor mume wangu, najua ni kosa langu."
Kutokana na kuzongwa na kila mtu pale sebuleni, Mzee Kulwa akamchukua Victor na kutoka nae nje ili wakaongee faragha. Ommy akawa ni mtu wa kwanza kuwafuata, waliongea kwa takriban dakika nne tu, wakashangaa kuona kundi lile lililokuwa sebuleni likihamia kule
"Anasema leo Victor ni bora tu umuue kama hutaki kumsamehe," Maneno ya Eve yalinukuliwa na Lidya mbele ya Victor aliekuwa akimtazama tu Lidya bila kuongeza kitu chochote.
Maneno ya mzee Kulwa yalimuingia mno, hasa pale alipomwambia
"Unajua Victor umeonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana leo? Hata kama alikuudhi vipi, bado hukupaswa kumsukuma vile na hasa ukizingatia hali ile aliyonayo, tambua yule anastahili kusamehewa bila kujali ukubwa wa kosa, kwani hakuna asiekosea, sisi binadamu ni dhaifu." Kauli ya Mzee Kulwa ilimfanya Ommy atikise kichwa kuikubali, Mzee akaendelea
"Ninaamini hata nawe uliwahi kuwakosea wazazi wako, lakini walikusamehe na hadi leo umefikia hatua hiyo. Hebu fikiria leo hii mtoto wenu ataishi katika mazingira gani ya kukaa mbalimbali na wazazi wake na hali wote wangali hai? Haya, maisha hayo yatakuwa hivyo hadi lini?" Maneno ya Mzee Kulwa yalikuwa ni kuntu, hakuacha, alimeza mate na kuendelea tena
"Sawa basi huenda huwezi kumsamehe Eve, basi angalia na kujali maisha ya mtoto wako Bill ambae anahitaji kuishi na wazazi wote wawili ili apate malezi yaliyo bora zaidi, fikiria hilo mara mbili, sawa Victor?" Alimaliza hotuba yake Mzee Kulwa na kuwataka warudi ndani.
walirejea ndani huku Victor akiwa anaendelea kufikiria maneno ya yule mzee, sauti ya Eve akaisikia kwa mbali ikilia na kuomboleza huku ikiomba msamaha
"Nisamehe baba Bill, ni kweli nilikukosea na adhabu uliyonipa, nakiri nimeipata na ninafikiri sasa imetosha, kama kuna nyingine naona sasa ni heri uniue tu kabisa kama hutanisamehe leo." Walikuwa tayari wameisha ingia sebuleni huku wakiwa kimya kabisa na wote wamesimama isipokuwa Eve aliekuwa amepiga magoti mbele ya Victor akiwa kazungusha mikono yake kwenye miguu ya mumewe.
Huruma ikaanza kumuingia Victor, ile hali ya ukatili ikaanza kutoweka polepole hasa ukizingatia maneno ya yule Mzee wa Kinyarwanda, yalimchoma sana moyo wake na kumkumbusha mengi tu mabaya aliyowahi kuyafanya siku za nyuma kwa wazazi wake.
Cha kwanza alichokikumbuka ni jinsi alivyokula karo ya shule, ada ilikuwa ni nyingi lakini akasamehewa japo kwa kelele nyingi, akalipiwa ada kwa mara nyingine na kuendelea na masomo.
Akamtoa mikono miguuni mwake na kumnyanyua taratibu, hadi aliposimama na kumwambia nimekusamehe Eve. Eve hakuamini, akamkumbatia na kulia sana, kilio kilicho sababisha na Victor kulia pia kama Eve.
Kilio kilichofuatana na makofi huku watu wakikumbatiana na wengine machozi yakiwatoka. Victor alipomuachia Eve akaenda na kumkumbatia Mzee Kulwa na kumshukuru kisha akawakumbatia wote na kuwashukuru pia.
Baada ya tukio lile, wakaketi kwenye masofa na kuanza kuongea, kila mmoja aliongea kile ambacho alikiona kama ni kitu ambacho kinastahili kuzungumziwa pale. Lakini karibu kila mtu alimshukuru na kumpongeza Victor kwa kuamua kumsamehe Eve.
“Katika maisha yangu ya sdhiki niliyopitia, kuna mengi sana nimejifunza, kwanza nimejifunza maisha yenyewe, pili nimejua thamani ya penzi huijui hadi ulikose, tatu nimejua kuwa kupoteza kitu ni rahisi sana tofauti na kukitafuta, maana kwenye kukitafuta kuna moja kati ya mawili, kukipata ama kukikosa…” Eve ndio alikuwa akiongea wote wakimsikiliza, kasha akaendelea
“Nilipoteza watu wangu muhimu wote ambao niliwapata kwa miaka kadhaa ila nikawapoteza kwa muda mchache mno, ila kwa hakika nilifanya kosa kubwa mno, lakini napenda mjue wote kuwa kosa hili limekuwa ni zaidi ya shule ama chuo kwangu, nimejifunza, nisamehe Victor mume wangu…” akaanza kulia tena.
Wakamtuliza na kasha mazungumzo yakaendelea, akaongea baba Eve na kusema
“Siku zote akili yako ndio rafiki yako na pia hiyo akili yako inaweza kuwa ni adui yako mkubwa, jambo la muhimu unaitumiaje akili hiyo,” kwa waliokuwa ni wanafalsafa kama Victor na baadhi yao wachache walielewa na kutikisa vichwa kumuunga mkono mzee.
Ilipofika zamu ya Mzee Kulwa, nae alimshukuru Victor kwa kumsikiliza na kisha akatoa offer kwa Evelyn kama atakuwa tayari kurudi kazini, yeye atakuwa tayari kumpokea na hata kuondoka nae siku ifuatayo.
Eve nae akamtazama mumewe Victor na kurudisha jibu kwa Mzee Kulwa na kusema kwamba yeye kwa sasa hana haki ya kufanya maamuzi yoyote, japo kuna kipindi alipokonya nafasi hiyo, lakini sasa ameirudisha kwa mumewe na ndie mwamuzi wa mwisho.
Victor akatabasamu na kumjibu Mzee Kulwa kwa kumwambia kuwa kwa sasa Eve hawezi kufanya kazi yoyote tofauti kazi za kampuni yao ya LOVE com, mwisho akamshukuru kwa offer yake.
Bado Mzee Kulwa akawa anapenda kuhoji kuhusu mwendelezo wa kampuni yao na walipofikia, Lidya akamkumbusha kuwa wakati wanakuja kule Rwanda si anakumbuka walimwambia kuhusu kujitoa kwa mtu mmoja? Akakubali haraka haraka,
“Ndio, ndio ndio, nakumbuka vizuri sana japo hata maana yake mlikataa kutuambia wapenzi wenu,” aliongea Mzee Kulwa kwa haraka huku akitikisa kichwa kukubali.
"Basi mtu mwenyewe ni huyu Eve ambae leo amerudi kundini, na leo ndio tunaweza kukueleza hata maana ya LOVE com, mkuu unaweza kuendelea,” Lidya akasema huku akimtazama Victor na wote wakamtazama, akasema;
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mzee wangu, kama ulivyosikia, neon lile limesimama badala ya majina yetu, huyo muongeaji sana huyo… (Huku akimnyooshea kidole Lidya, wote wakacheka na kujua ni sehemu tu ya utani) anaitwa Lidya na amesimama badala ya L, mumewe ni Ommy, hapo kuna O na mimi inahusika V kutokana na jina langu mwisho ni kipenzi hapa, Evelyn ambapo kuna kamilisha LOVE kwa herufi yake ya E,” alimaliza Victor na Mzee Danga akaingilia kati kwa mshangao
“Suprising! Nashindwa kuamini kama vijana mna akili nyingi kiasi hicho! Ubunifu tu wa jina lenu inavutia, naomba Mungu mfike mbali zaidi ya hapo kwa kweli,”
“Naam, ahsante na tunashukuru, nasi tunaamini tutafika mbali zaidi ya hapa tulipo na hivi karibuni tuna tamasha kubwa huko Kampala, hata nawe Mzee unakaribishwa.” Lidya alimtania na kucheka, wote wakacheka pia.
“Unajua vijana wa Kitanzania ni watundu sana, kila fursa wanayoiona wanakuwa wepesi sana kuitumia, sasa siku ile mlisema kuna mengine nje ya burudani?” Aliuliza Mzee Kulwa.
“Ndio mzee wangu, tuna mengi mengine nje ya burudani.” Alimjibu Ommy huku wengine wakimuunga mkono kwa kutikisa kichwa.
“Tuna jihusisha pia na mambo ya tiba za mifugo, afya za binadamu, kutafutia watu mbalimbali fursa na mfano huo,” alijibu Ommy kifupi tu.
"Amazing! Hakika nalazimika kuwaalika tena nchini kwetu Burundi ili kuja kutoa somo la ujasiria mali, maana akili mlionayo vijana nyie, inazidi akili ya maprofesa wa uchumi, safari hii nitaawaalika Rwanda kwa gharama zangu mimi kupitia kampuni yangu, naomba msinikatalie ombi langu."
"Usijali mzee wangu, jambo la msingi ni mawasiliano tu." Aliongezea Victor. Kikao kikavunjwa rasmi na kila mmoja akarejea kwake, ambapo mzee Maganga akarejeshwa na Ommy hadi kwake pamoja na mkewe.
Bill, Jam na mama zao waliingia gari moja na Victor aliekuwa akiendesha na kuelekea nyumbani kwao. Eve alikuwa bado ameketi kwenye sofa wakati watu wengine wakinyanyuka, alikuwa hajaelewa, anabaki kwao ama anakwenda kwake, nyumbani kwa Victor.
Victor akarudi ndani na kumnyanyua, akamwambia waende garini, ama bado ana mpango wa kubaki pale? Dah! Hukuwepo… alitamani tayari awe ndani ya gari, akaenda ndani na kuchukua nguo zake chache kwenye begi na kuelekea nje ambapo alikuta Lidya akiwa ameingia mlango wa nyuma akiwa na watoto.
Gari ikaondoka moja kwa moja hadi nyumbani kwa Victor, hatimae Eve akaingia tena ndani ya nyumba ambayo aliamini atafia ndani lakini akalikoroga mwenyewe na sasa ameingia kwa mara nyingine.
Hakuamini macho yake kutokana na mabadiliko aliyoyakuta, karibu kila kitu alichokicha mle ndani hakukikuta, asilia zaidi ya 90 ya vitu vya mle ndani vilikuwa ni tofauti na vile alivyoviacha.
Akampongeza mumewe kutokana na mabadiliko yale, akasahau hata kumsalimia Sarah ambae alionesha shauku ya kutaka kuongea nae. Alipogundua hilo akamgeukia na kusalimiana nae kwa bashasha huku wakiwa wamekumbatiana.
Muda sio mrefu baadae Ommy akawa amerejea na kuungana nao. Lidya kwa kushirikiana na Sarah wakaandaa mezani chakula cha usiku ambacho tayari kilikuwa jikoni kimeishapikwa.
Walikula na kufurahi hasa, huwezi kuamini kwa siku ile moja tu Eve na Victor waliweza kusahau kabisa tofauti zao, tena Eve akijitahidi kujiweka karibu zaidi na Victor mumewe.
Victor akakumbuka kuwa alimuahidi Bina kuwa atawapeleka watoto hotelini jioni na watalala huko, lakini akajikuta anashindwa hata baada ya kukumbuka, akajipa moyo kuwa atawapeleka siku ifuatayo.
Kutokana na furaha aliyokuwa nayo Ommy, akawaambia Eve na Victor watoke muda ule waende kujirusha kidogo ili kuweka sawa akili yao na angalau wapate cha kusimulia wao wakirudi Jijini Nairobi.
Wanawake ndio wakapewa nafasi ya kwanza ya kujiandaa na kukumbushwa kuwa muda ni mchache wajitahidi kufanya haraka. Wakapotelea vyumbani mwao kujiandaa wakiwaacha waume zao wakiongea.
“Kaka, katika maisha yangu sistahili kuwa sawa wakati wote, kwa kuwa mimi ni binadamu, lakini katika maisha yangu mimi ninahitaji kuwa na furaha tu hasa itokane na kile ninachokiamini mimi,” aliongea Victor na Ommy akaongezea
“Furaha inatokana na faraja, faraja huipati kwa kuifikiri tu, bali kwa kuitengeneza, safi sana mdogo wangu kwa kujua mapungufu ya kibinadamu,”
“Nafurahi kwa kuwa zamani za enzi tayari niliisha tengeneza faraja kwa kuwa na marafiki wachache ambao wananijua na kunikubali kwa jinsi nilivyo,” aliongea Victor na kumfanya Ommy acheke na kusema
“Kumbe unajijua kuwa wewe ni mtata eti?”
“Mi mtata kweli hasa pale kwenye kitu ambacho mimi ninaona kina maslahi halafu hatuelewani? Hahahaaa!” wakamaliza maongezi kwa kuwa tayari wanawake wa LOVE com walikuwa wametoka wameisha pendeza, wao nao wakajiandaa haraka.
Walitoka wote kwa kutumia gari la ofis na kuanza kujiuliza ni wapi kwa kwenda. Lidya akawashauri waende Dar Live, moja ya ukumbi ambao alikuwa akiusikia tu, hivyo alikuwa ana hamu ya kufika huko. Muda huo wanaongea walikuwa maeneo ya Tazara, safari ikaanza kuelekea Mbagala Zakhem.
Waliwasili na kuingia ndani, walikutana na Surprise nyingine ambayo hata wao wote hawakuweza kuiwaza hata dakika thumni, walitazamana na wote wakaanza kumuangalia Victor ambae wala hakuwa na habari, akashangaa kivipi wote wanamuangalia yeye, akahoji vipi?
“Ujue mimi tayari nimechoka na Surprise? Kwa kweli nimezichoka na sitamani hata kuiona kwa jirani akifanyiwa, imekuwa too much sasa!” aliongea Ommy akivuta kiti ili kukaa.
“Hata name shemeji yangu sasa hapana, wewe tu kila siku kuwafanyia wenzako?” aliongezea Lidya na kufanya Victor na Eve watazamane wakiwa hawajui lolote linaloendelea, Victor akasema
“Haya Eve nawe ongea kitu kama wenzako, maana hata siwaelewi, nawe utasema lipi?” masikini Eve yeye hakuwa na lolote kichwani mwake, Lidya akagundua na kusema
“Shem unajua kuwa Classic band inapiga hapa umetuleta tu bila hata kutujulisha?” Victor akatabasamu na kusema kwa kujiamini kabisa
“Ah! Sasa mi ningefanyaje na nyie ndio wageni wangu na mmetaka kuja huku? Ningewakatalia? Isingewezekana bhana,” akajitetea kisha akaendelea
“Kila siku ya wiki kma leo, bendi yetu hupiga hapa, na hapa tunaweza sema ni sehemu yetu ya Ng’ombe wa maziwa, tunakamua tu…” wote wakacheka na
kujumuika kuanza kufurahi.
Walikunywa vinywaji mchanganyiko hadi kufikia saa 10 alfajiri, wakati ambao Ommy alipotazama saa na kugundua wanakaribia kuimaliza siku ile wakiwa wamekesha, akawashtua wenzie na kunyanyuka, wakarejea nyumbani.
Kila mmoja alikielea kilipo chumba anacho paswa kulala na kukitafuta kitanda ikiwa ni alfajiri kabisa. Walipoingia ndani kutokana na kulewa kupita kiasi, Victor na Eve wakajikuta wakiwa wamefanya mapenzi bila kutarajia na kuvunja ahadi waliyo kubaliana kuwa wasifanye hivyo hadi wapime afya zao kwanza.
Ajabu walipoamka, Eve akamwambia Victor kuwa ile ni Suprise kwake, Victor akamwambia mbona hajamuelewa?
"Ni Suprise ipi?"
"Unakumbuka kabla ya safari yako uliyo elekea Uganda, ambayo huku nyuma mie niliondoka?"
"Ndio ninakumbuka, ina nini?"
"Kabla hujaondoka, usiku ule mimi nawe tulifanya mapenzi."
"Ndio nakumbuka."
"Basi tangu siku ile, sijafanya chochote na mwanaume yeyote hadi leo hii tena, Victor mume wangu."
"Kwenda zako huko wewe," Alisema Victor huku kiroho kikimdunda, kama haamini vile
"Huo ndio ukweli, ndio maana niliamua kuwa mkimya, hakuna ambae angeweza kunielewa kwa jambo hilo."
"Kivipi wakati wewe muda wote ulikuwa na mtu mnaishi nae?"
"Mume wangu hiyo raha ya kufikiria mapenzi ningeitoa wapi? na isitoshe kufika kule kila mtu akawa anajitegemea japo kuna muda tulikuwa tunakuwa pamoja, lakini mapenzi hayakuwepo tena, niamini."
"Basi tuliache hilo, nitahakikisha baada ya kufanya vipimo mke wangu." Wakanyanyuka na kwenda kuoga huku kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani.
Wa kwanza kutoka chumbani alikuwa ni Eve akakuta Lidya akiongea na Sarah ambae kwa siku zote hizi amekuwa akilala na watoto, alipomuona Eve akafurahi na kumsalimia kwa furaha zote akiwa na sura ya matumaini ya kwamba bosi wake amerudi rasmi nyumbani.
Asubuhi ile walipokea simu kutoka kila sehemu za wazazi wao ambao walikuwa wakitaka kujua hali zao. Walikunywa chai na kutoka kuelekea ofisini kwao wakiwa leo wamekamilisha jina lao la Kampuni ambalo ni LOVE.
Wakiwa njiani, Victor aliekuwa akiendesha gari lao aina ya VX, akanyoosha gari hadi maabara ya LOVE com na kuwaambia waanzie pale. Wakati wanazunguka zunguka mle ndani, Victor akamchukua Eve na kwenda kupima, majibu nayo hata hayakucheleweshwa.
Yalikuwa ni majibu mazuri kwa upande wao, wakarejea garini wote na kuondoka wakielekea zilipo ofisi za shirika la ndege la Kenya na kukata tiketi, walipomaliza hapo, Victor ndio akawapa majibu ya vipimo vya damu zao.
Wote walibaki wakiwa na mshangao na kuhoji walipima muda gani, Victor alicheka tu huku akimtazama Eve alieonekana akiwa na furaha zaidi ya wote, ndio alijibu kwa kuwaambia wakati wao wakitazama ile mashine mpya ya kupima Malaria, wao ndio wakaenda kupima.
Lidya akawapongeza kwa kukutwa afya zao zikiwa ni salama, kisha Ommy akapendekeza
"Jamani samahanini, mimi ninaombi moja, kuna kitu cha mwisho kinatakiwa tukifanye kabla sisi hatujaondoka." Wote wakamtazama, akaendelea
"Japo Ondiek alitukosea, lakini ninapendekeza twende tukazuru kaburi lake kwa sababu sote tayari tumesameheana na kwa kuwa hatukushiriki kwenye mazishi yake, ni bora sasa tuutumie muda huu kwa kwenda kuweka hata maua, au mnasemaje?" Wazo lake lilipita bila kupingwa japo Eve alionekana kama vile kanyongea.
Safari yao ikaanza na kuelekea duka la maua na kununua kisha moja kwa moja hadi makaburi ya Kisutu alipozikwa Ondiek. Haikuwa taabu sana kulipata kwani lilikuwa bado ni jipya na jina lilionekana. Wakaweka maua na kumuombea kwa Mungu.
Baada ya kukamilisha zoezi lile, wakarejea nyumbani ili kuwapa nafasi Ommy na mkewe ya kujitayarisha kwa safari ya kwenda kwao Kenya. Furaha ikazidi kutawala baada ya maafikiano kuwa Bill atabaki pale na wazazi wake.
Sasa ndio Victor akaanza kujifanyia tathmini na kujiuliza
"ina maana kiuhalisia mimi ndio niliekosa? maana ni mimi nimekuwa na mpenzi mwingine wakati yeye mke wangu akiwa aeondoka nyumbani kwa woga?Ama kweli binadamu hatupaswi kuongozwa na hisia...
Hiyo ndio ilikuwa ni Suprise ya mwisho kwa Victor, suprise iliyorudisha penzi lililopotea na kufanya Victor nae kujihic ni mkosaji na kushusha pumzi kwa nguvu.
Victor baada ya kutulia sasa, ndio akachukua simu na kumpigia Sabrina,
"Hellow Bina," Lidya na Ommy wakatazamana, japo walitambua Bina ni kama mtendaji mwenzao, lakini walikuwa wakitambua kuwa kuna kingine zaidi kipo kati yao.
"Nimefurahi kukupata hewani muda huu ambao nipo pamoja na Ommy, Lidya na mke wangu Eve, nashukuru tumerudiana na mam watoto wangu, ndio sababu jana sikukuletea watoto, naomba unisamehe sana kwa kutokukujulisha hilo."
Upande wa pili yaani Sabrina hakuipokea vizuri ile simu, kwani taarifa ile ilimchoma sana moyo wake lakini ilikuwa ndio habari na pia ni lakini ililazimika aikubali, maana ndio tayari imeisha tokea na haikuwa na uongo wowote bali ukweli mtupu.
Nae akajitutumua na kumwambia Victor kuwa habari ile imekuwa kama ni Surprise kwake, lakini si Surprise ya kufurahisha bali ni Surprise ya kuumiza, lakina akatumia nafasi ile kumwambia anamuaga muda ule yupo kwa wakala wa ndege kwani anatarajia kuondoka jioni kurudi Uganda.
Basi wakaagana na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja japo mapenzi ndio wameyazika rasmi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jioni ya siku hiyohiyo, familia ya Ommy Bazo nayo ikaondoka Bongo kuelekea kwao wakiwa wameacha simanzi kubwa kwa familia ile ya Victor na mwathirika mkubwa akiwa ni Bill ambae karibu muda wote alikuwa karibu na Jam na familia nzima ya Ommy.
Ukweli haupingiki, ikifika hatua fulani ama muda fulani, ni lazima watu fulani mtengane, muda huo ulikuwa ndio sasa. Bill na Jam sasa wakatenganishwa, kila mmoja akienda kuishi na wazazi wake. Maisha ya Eve na mumewe yakaanza upya sasa yakiwa kwenye hatua nyingine ya kujali kupita awali, huku kampuni nayo ikizidi kukua.
Zilikuwa ni Surprise, Surprise ambazo kamwe hakuna kati yao atakaekuja kuzisahau, Surprise ndio zimefanikisha uwepo wa LOVE com…
***** MWISHO. *****
0 comments:
Post a Comment