IMEANDIKWA NA : ATUGANILE MWAKALILE
*********************************************************************************
Simulizi : Je Haya Ni Mapenzi!!
Sehemu Ya Kwanza (1)
Mimba yake ndio iliyosumbua wengi sababu alijikuta akimchukia kila mtu aliyemuona mbele yake, hata mume wake alimchukia kasoro binti mmoja mdogo ambaye ni mtoto wa mwenye nyumba anayoishi Sakina.
Alimpenda sana huyu binti aliyekuwa na umri wa miaka kumi kwa kipindi hicho na alijulikana kwa jina la Sabrina.
Kila kitu ambacho Sakina alikitaka alipenda achaguliwe na Sabrina.
Kitendo cha Sakina kuwa karibu sana na Sabrina kilikuwa kinamkera sana mzazi wa Sabrina aliyeitwa Joyce, hakupenda kabisa mwanae awe karibu vile na Sakina kwani alijua wazi kuwa Sakina atamfanya mwanae kama mtumwa wake ila hakutaka kusema sana kwavile alimuhurumia Sakina kwa ule ujauzito aliokuwa nao kwani mimba zingine huwa zinafanya mtu awe vile kama alivyo Sakina.
Mume wa Sakina nae alikerwa sana na tabia ya mkewe kwani kila alichokifanya yeye mkewe hakukitaka, hata kama akimletea kitu alikuwa anakikataa hadi amuite Sabrina na kumuomba amkabidhi hiko kitu kwa niaba yake, kwakweli hii hali ilimkera na kumfanya aombe usiku na mchana mkewe ajifungue mapema ili awewe kuepukana na hiyo hali.
Bwana huyu alijulikana sana kutokana na tabia yake ya ucheshi, mtaa mzima walimjua Juma kwahiyo tabia ya mkewe pia ikajulikana mtaa mzima na kufanya watu wengi kumsema kwa mazuri na mabaya.
Sakina alikuwa na imani kuwa atajifungua mtoto wa kike kutokana na mapenzi yake kwa Sabrina hivyobasi akaahidi kwamba atakapojifungua huyo mtoto atamuita Sabrina ili tu iwe kama kumbukumbu katika maisha yake.
Sabrina nae alifurahi kwani hata yeye alimpenda sana huyu dada.
Wakati Sakina na Sabrina wakizungumza kwa furaha, Joyce ambaye ni mama wa Sabrina alimuita mwanae kwa nguvu sana ikabidi Sabrina aende kwa mama yake
"Hivi siku hizi huna masomo ya ziada ya shule?"
"Ninayo mama ila nishafanya na kumaliza"
"Kwahiyo ukimaliza ndio unapata muda wa kwenda kuongea na wajawazito! Yani wewe mtoto hata sijui una matatizo gani jamani"
Wakati akiongea hayo, simu yake ikaita na kufanya aache kuzungumza tena na Sabrina hivyo kumfanya huyu mtoto nae arudi kule kwa Sakina.
Sakina alimuomba Sabrina waende mahali, naye Sabrina hakuweza kukataa kwani alikuwa bado mdogo na hakuwa na uelewa wa mambo mengi yanavyokuwa kwahiyo alikubali na kwenda kujiandaa kimya kimya kisha akaondoka bila ya kumuaga mama yake kwani anajua kwa vyovyote vile akimuaga tu lazima atamkataza wakati yeye safari anaitaka.
Kisha yeye na Sakina wakaondoka na kutokomea.
Simu ambayo Joyce aliipokea ilikatika bila mpigaji kuongea chochote kitu hicho kilimfanya Joyce ampigie mumewe na kumuomba amrushie muda wa maongezi ili aweze kuzungumza na huyo mpigaji.
Alipotumiwa, akaipiga ile namba na akapokea mtu ambaye alimfahamu,
"Wifi habari!"
"Kumbe ni wewe! Mbona umetumia namba mpya?"
"Maelezo ni marefu hapo, je Sabrina yuko wapi?"
"Nadhani atakuwa nje, umemkumbuka wajina leo?"
"Nakuomba usimruhusu aende mahali popote wifi"
Kisha akakata simu na kumfanya Joyce amshangae, huyu aliyepiga aliitwa Sabrina na ndiomana alipomuulizia Sabrina mama yake akamuuliza kama amemkumbuka wajina wake.
Huyu alikuwa ni wifi wa Joyce yani ni dada wa mumewe.
Kutokana na ile siku kakatwa bila ya kumaliza maongezi ikabidi Joy atoke kwanza na kwenda kumtafuta mwanae ili ajue kama yupo au vipi ingawa mwanzo aliamini kuwa yupo.
Alipofika nje alimuita bila ya kuitikiwa ikabidi amfata jirani yake mmoja na kumuuliza
"Umemuona Sabrina?"
"Ndio nimemuona, kapita hapa muda sio mrefu na yule mpangaji wako"
"Wameelekea wapi?"
"Nadhani wameelekea stand"
"Jamani huyu mtoto ataniua mimi mwaka huu, mbona amekuwa wa ajabu kiasi hiki jamani! Yani aondoke bila kuaga! Ameanza lini hiyo tabia jamani!"
"Labda hawajaenda mbali sana, usiwe na mawazo sana jirani atarudi tu si yupo na mtu mzima"
"Mtu mzima gani? Yule Sakina hajielewi kabisa na ile mimba yake, asije akamuacha mwanangu njiani sijui nitamueleza nini baba yake"
Joyce alirudi ndani huku akiwa na mawazo sana kuhusu binti yake, akaamua kuchukua tena simu na kumpigia wifi yake ila safari hii akampigia kwa simu yake tofauti na ile namba ya mwanzo.
Ile simu ilipokelewa na mume wa Sabrina, moja kwa moja Joyce alimueleza mume wa Sabrina alivyoambiwa na wifi yake huyo kuhusu mwanae na huyo mwanae ameshatoka bila hata ya kuaga.
Mume wa wifi yake akamjibu,
" Usiumizwe akili na ulichoambiwa na wifi yako kwani hata mimi simuelewi sijui akili yake imekuwaje lakini usishangae sana, si unajua huyu wifi yako ni wa mauzauza tangia zamani!"
"Natambua hilo, ila inabidi kumsikiliza mara nyingine kwani huwezi jua kwanini kasema hivyo"
"Asikuumize akili nakwambia, mimi ndio mumewe namjua huyu vizuri najua hata wewe wamjua sijui umeshasahau mauzauza yake? Ana mwezi mchanga huyu, usijali mwanao atarudi tu tena salama kabisa"
Wakaongea na kuagana ila wazo la kuambiwa kuwa ni mauza uza ya wifi yake bado lilimpa mashaka kwani hakufikiria kama mauza uza hayo yangemfanya apige hadi simu na kumueleza yaliyopo ila bado alikuwa na mashaka na wifi yake huyo kwani kuna kipindi aliwahi kuisumbua sana familia yake kwa mauzauza aliyokuwa nayo kwahiyo alimuamini nusu kwa nusu sababu mengi aliyokuwa akisema kwa kipindi hiko cha nyuma yalikuwa na ya kweli.
Joy alifikiria sana ila hakuwa na jibu la moja kwa moja huku akilalamikia majina ya kurithi
"Ndiyo tabu ya kurithisha watoto majina hii, yani huyu mwanangu akili zake zimekuwa waruwaru kama shangazi yake ila yeye uwaruwaru umemuanza mapema jamani. Mmmh sijui nimbadilishe jina! Ila hawatanielewa hawa, ngoja nitulie nione itakavyokuwa"
Joy alitulia kwa muda ila Sakina hakurejea wala Sabrina na kuzidi kumpa mashaka, akataka kumpigia simu Sakina lakini akakumbuka kwamba Sakina hana simu kwani aliwahi kuivunja kipindi anagombana na mumewe
"Huyu Sakina akili yake sio nzuri kabisa yani sijui kama mwanangu atakuwa salama jamani, mbona ni majanga haya!"
Aliendelea kusubiri na kusubiri lakini hawakurejea na kuzidi kumpa mawazo yasiyo na kikomo.
Mume wa Sakina alirejea nyumbani kwake lakini Sakina hakuwepo na kumfanya huyu bwana apatwe na maswali kuwa mkewe amekwenda wapi. Moja kwa moja alienda kwa mama mwenye nyumba yao kumuuliza,
"Samahani mama James"
"Bila samahani"
"Eti Sakina umeelekea wapi?"
"Hata sijui, tena ameondoka na binti yangu jamani mwanangu akipotea sitakuwa na utu na nyie. Mtoto mwenyewe wa kike ninaye mmoja tu halafu mkeo anaondoka naye tena bila hata ya kuaga, tutaonana wabaya hapa jamani"
Juma alimuangalia tu huyu mama na kubwabwaja kwake kwani alitakiwa kumjibu mara moja ila aliweka maelezo mengi sana, ikabidi Juma aage ili aende kumtafuta mkewe.
"Ndio nishakwambia hivyo, nataka mwanangu arudi akiwa salama kabisa msiniletee mie hayo mabalaa yenu jamani msiniletee kabisa"
Joy aliongea sana kwa uchungu wa mwanae na pia hakujua atamueleza nini mumewe atakaporudi na kumuulizia binti yake huyo maana alimpenda sana na hakuweza kufanya chochote bila kumuulizia binti yake, hilo ndio jambo pekee lililompa mashaka mama wa Sabrina.
Juma hakutaka kupoteza muda, hivyo akajiandaa na kwenda kumtafuta mkewe kwani kwa ndugu zao wote alikupiga simu aliambia kuwa mkewe hajafika hivyobasi akaamua kwenda kumtafuta mwenyewe ingawa hakuwa na uelekeo sahihi wa mahari alipo.
"Yani huyu mwanamke asingekuwa na ujauzito wangu hata nisingejisumbua kumtafuta, bahati yake ana ile mimba sijui mimwanamke mingine ikoje jamani laiti ningejua hii adha ya huyu mwanamke nisingemuoa jamani. Ila dawa yake inakuja, akijifungua tu namuolea mke mwenza ili akili imkae sawa"
Juma alikuwa akiongea kwa hasira sana kwani hakupendezwa na tabia aliyokuwa nayo mkewe kwa hiki kipindi cha mimba yake.
Aliondoka bila uelekeo wa maana kumtafuta mke wake.
Huku Joy naye hakuwa na raha kabisa, akaamua kumpigia tena wifi yake simu kwa ile namba mpya naye akapokea ile simu
"Hebu niambie vizuri kuhusu mwanangu Sabrina"
"Kwani yuko wapi?"
"Ameondoka"
"Ameondoka!!" Akauliza kwa mshangao.
"Ndio ameondoka tena bila hata ya kuniaga jamani"
"Umemuacheje wifi hadi aondoke jamani wakati nilishakupa tahadhari!"
"Jamani wifi yangu hakuniaga jamani"
"Ulitakiwa kuwa makini, unadhani itakuwaje sasa?"
Halafu akakata simu na kumfanya Joy apatwe na mawazo zaidi, wazo likamjia na yeye na kumfanya ajiandae na kwenda kumtafuta mwanae ingawa hakujua pia kama aanzie wapi na aishie wapi kwani hakuelewa kabisa kuwa wameelekea sehemu gani.
Sakina na Sabrina walielekea sehemu moja kulikuwa na miti mingi sana kisha Sakina akamwambia Sabrina dhumuni la yeye kwenda naye huko
"Sikia Sabrina, najua wewe ni mtoto mdogo sana na hujui chochote kuhusu maswala ya uzazi. Umeona hili tumbo lilivyokubwa!"
Huku akilishikashika tumbo lake, Sabrina akaitikia kwa kutingisha kichwa kuwa ameliona.
"Basi hii inaitwa mimba au ujauzito, nimebeba mtoto humu tumboni. Nimekaa kwa muda kidogo nikiwachukia watu wote na kukupenda wewe tu, wengi hawapendezwi na tabia yangu ila mimi nimejikuta tu nikiwachukia"
"Ila mbona zamani kabla ya kuwa na hilo tumbo uliwapenda?"
"Ni kweli, kwamaana hiyo hili tumbo ndio limefanya niwe hivi. Nimekuja huku sababu marehemu bibi yangu alipenda sana kuja huku pindi anapokuwa na tatizo la aina yoyote ile, aliamini akija huku atapata suluhu la tatizo lake. Nami nimekuja huku kujiombea niweze kujifungua mapema ili niepukane na haya mambo ya kuchukizana na majirani na watu wengine. Nahitaji huyu mtoto atoke, awe mtoto mzuri kama wewe na awe na upendo kama mama yake hapa"
Sabrina akacheka kwa furaha baada ya kusikia kuwa mtoto atoke akiwa mzuri kama yeye huku akijipa sifa moyoni mwake kuwa kumbe yeye ni mzuri hadi anasifiwa na watu akatamani hata aletewe kioo ajitazame tena ila ndio hivyo walikuwa kwenye kipori kidogo.
Wakaongea mambo mengi sana wakiwa huko hata kusahau kama wanatakiwa kurudi, kuja kutahamaki muda nao ulikuwa umekwenda sana hivyo ikabidi Sakina amshtue Sabrina na kuanza safari ya kurudi nyumbani.
Wakati wapo njiani gafla wakaona kitu cha kustaajabisha sana na kufanya washtuke.
Kuangalia vizuri kile kitu lilikuwa ni lile joka kubwa ambayo hujulikana kwa jina la chatu.
Uoga ukawajaa wote wawili, Sabrina kukimbia angeweza ila je angeelekea wapi maana walipokuwa wanaenda mbele yake ndio alikuwepo huko chatu. Huyu Sakina ndio kabisa angewezaje kukimbia na lile tumbo lilivyokuwa kubwa, ila wakaamua kukimbia hivyo hivyo.
Kugeuka nyuma yule chatu alikuwa akiwakimbiza, kitendo hicho kilimfanya Sakina aanguke vibaya sana na ubaya zaidi ni kuwa alimuangukia Sabrina
Kugeuka nyuma yule chatu alikuwa akiwakimbiza, kitendo hicho kilimfanya Sakina aanguke vibaya sana na ubaya zaidi ni kuwa alimuangukia Sabrina.
Sabrina alipiga kelele ya maumivu kutokana na uzito aliokuwa nao Sakina, kelele ambazo zilisikika kwa nguvu na kukatika gafla kwani alikuwa amezimia pale pale.
Kitendo kile kilimtoa jasho Sakina na kuzidi kummaliza nguvu, alijisogeza kwa shida na kumuangalia Sabrina ambaye alikuwa hajitambui kabisa.
Sakina akasahau hali yake na kuanza kuwaza kuhusu huyu mtoto wa watu kuwa itakuwaje, alipomtazama yule chatu aliyekuwa akiwafuata hakuonekana tena na kumfanya Sakina ajiulize kuwa ni kitu gani hiki au ni mauzauza tu kati yao bado hakujielewa.
Wakati anajitahidi kuinuka pale chini ili aweze kumuinua na Sabrina, alijikuta amelowa damu na kufanya azidi kuogopa huku mawazo mabaya yakimjia kuhusu kiumbe chake tumboni. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujaribu kujikongoja ili tu yeye na Sabrina watoke eneo lile na waweze kufika eneo ambalo watapata msaada ila atambebaje Sabrina aliyezimia huku na yeye ana mimba kubwa ya kujifungua! Hapo ndio ikawa kazi kubwa sana kwa Sakina huku akiomba Mungu awapatie msaada wowote ule pale walipo ili waweze kupona.
Joyce alitafuta hadi kuchoka na kuamua kurudi nyumbani huku akiwa na mawazo mengi sana kuhusu binti yake na kujisemea
"Yani wakirudi tu nawapa notes wahame kwenye nyumba yangu siwezi kuvumilia huu upuuzi kwakweli. Sijui nitamueleza nini baba yake mimi jamani mmh!"
Wakati akiyawaza hayo, mumewe nae alirudi muda huo huo na kumkuta mkewe akiwa kajiinamia tu.
Alimuulizia kilichomsibu ila Joyce hakutoa jibu la maana lakini mumewe hakusumbuliwa na jibu la mkewe kwani alikuwa na nia ya kumuona binti yake kwakuwa haikuwa kawaida kwa yeye kurudi na kukuta nyumba kimya kiasi kile ikabidi aulize kwanza
"Yuko wapi Sabrina?"
Hapo ndio palimfanya bi.Joyce ajiume vizuri zaidi kwani hakujua hata amjibu nini ila mwisho wa siku aliamua kumueleza tu mumewe ukweli.
"Unasemaje wewe?"
"Sabrina hayupo"
"Unajua ni saa ngapi saizi?"
Joyce akainua macho na kutazama mida, ilikuwa ni saa mbili usiku. Akashindwa hata kumjibu mumewe kuhusu muda
"Hivi unaakili kweli wewe mwanamke? Yani mwanangu hayupo nyumbani na usiku ushaingia halafu wewe umekaa umejiinamia bila kufanya chochote!"
Joy alijaribu kumueleza hali halisi mume wake lakini huyu mwanaume aliyeitwa Deo hakutaka kabisa kumsikiliza mkewe kwa chochote alichokisema badala yake alimpa kauli moja tu
"Naomba upotee kwenye nyumba yangu hadi pale utakapomrejesha binti yangu, usitake kufanya nikatenda dhambi bure. Tafadhari sana potea kwenye macho yangu"
Aliongea kwa ukali sana na kufanya Joy atetemeke na kuondoka kwenda kumtafuta Sabrina ambaye hata hakujua aanzie wapi na aishie wapi.
Joyce alikuwa na mawazo sana ya binti yake na jinsi mumewe alivyompenda mtoto huyo kwa vyovyote vile kama asipopatikana basi ndoa yake itakuwa imefika mwisho kwani mumewe alimuona kamavile ni mwanamke mzembe asiyejua kuitunza familia yake.
Joyce alitembea tu huku mawazo mengi yakiichanganya akili yake na kujihisi kamavile akili yake imetoweka kwani haikuwa sawa kabisa.
Akitembea huku na kule bila ya kujielewa, akamuona mtu mmoja upande wa pili wa barabara na kujihisi kuwa anamfahamu mtu huyo, akajaribu kuvuka barabara ili kumuwahi mtu huyo ila kabla hajamaliza kuvuke ile barabara alijikuta akipitiwa na pikipiki kisha akaanguka na kupoteza fahamu.
Wasamalia wema wakamuwahi na kumkimbiza hospitali.
Deo alitulia nyumbani kwake huku akilaumu akili za mke wake kwa kumuacha mwanae aende mahali pasipoeleweka
"Na akirudi hapa bila mwanangu ajue talaka itamfata kwao"
Kwakweli hali haikuwa shwari kabisa.
Muda nao ulizidi kwenda na kumfanya Deo azidi kupatwa na mawazo dhidi ya mwanae ingawa alikuwa na watoto wengine ila huyu alimpenda zaidi, labda kwavile mtoto huyu alifanana na mdogo wake aliyempenda pia hata jina la mtoto huyu lilikuwa ni jina la mdogo wake mpendwa na kumfanya Deo azidi kumpenda binti yake huyu.
Swala la binti yake kutokujulikana alipo lilimpa mashaka sana na kumfanya apate maswali bila ya majibu, alitamani binti yake arudi ili apate furaha ya moyo ila hakurejea binti yake wala mke wake na muda nao ulizidi kuyoyoma bila ya taarifa yoyote.
Akaamua kumpigia mkewe simu lakini hakupatikana na kumfanya Deo wasiwasi umdhidi kwa kumfikiria binti yake mpendwa.
Alitulia akitafakari cha kufanya kwa muda huo maana naye alihisi kuchanganyikiwa.
Juma naye aliendelea na swala la kumsaka mke wake bila ya tumaini lolote la kumpata.
Aliendelea kumsaka mkewe kila mahari huku akiwaza usalama wa kiumbe chake kwenye tumbo la mke wake.
"Najuta kuoa mwanamke mwenye akili fupi kama Sakina, ona ambavyo ninapata shida hapa"
Alimsaka kila mahali bila ya mafanikio ya kumpata wala ya kujua mahali alipo.
Wakati alipokuwa akikatisha barabarani ndipo aliposhangazwa na lile tukio la ajali, aliposogea karibu akagundua kuwa ni mama mwenye nyumba wake kagongwa na pikipiki, ni hapo aliposaidiana na wasamalia wema wengine kumpeleka hospitali kwani hali yake ilikuwa mbaya sana.
Juma naye hakujielewa kabisa kwani ile hali ilizidi kumchanganya akili yake, mambo ambayo yalikuwa yakimtokea sasa alikuwa akiyahisi kamavile ni ndoto na hakujua kwanini imekuwa kama ilivyokuwa.
Hakupata jibu kwa mawazo yake yote aliyoyawaza ikabidi ampigie simu baba mwenye nyumba wake ambaye ni mume wa Joyce yani yule mwanamke aliyepata ajali.
Deo akiwa bado na mawazo, alishtuliwa na simu aliyopigiwa na Juma na kumfanya azidi kuchanganyikiwa kwa ule ujumbe kuwa mkewe kapata ajali.
Alijilaumu sana kwa kitendo chake cha kumtimua mke wake kuwa akamtafute mtoto wao, alihisi kuchanganyikiwa sasa ikabidi aende huko hospitali ili kujua hali ya mkewe kuwa anaendeleaje.
Bado hali ilikuwa tete kwa upande wa Sabrina na Sakina kwani Sabrina alikuwa bado hajitambui kutokana na kuangukiwa na Sakina aliyekuwa na uzito mkubwa hata msaada nao haukupatikana na kumfanya Sakina azidi kuchanganyikiwa kwani giza lilitawala kila mahari, kwakweli Sakina alihisi kuwa anaenda kufa yeye na Sabrina wake.
Ingawa alijitahidi kujikongoja ila bado alishindwa kutoka kwenye kile kichaka kutokana na maumivu aliyokuwa nayo na vilevile hakuweza kumuacha Sabrina, aliamua kukaa chini huku akimuomba Mungu tu amsaidie yani alijitoa kwa jambo lolote lile kwa muda huo.
Alitulia huku machozi yakimtoka, lakini sala zake zilimsaidia kwani walitokea wawili na kupita njia hiyo kwakweli halikuwa jambo la kawaida ila ndio hivyo wakapata msaada na safari ikawa ni moja tu yani kukimbizwa hospitali.
Walipofika hospitali moja kwa moja Sakina alikimbizwa kwenye wodi ya wazazi kwani ilionyesha kuwa angejifungua muda sio mrefu.
Sabrina naye akafanyiwa huduma na kuzinduka huku akijishangaa tu kwani hakujielewa kabisa.
Manesi walitafuta mawasiliano ya watu wa karibu na hawa na moja kwa moja wakampata Juma na kumpa taarifa kuhusu mkewe na huyu binti mdogo Sabrina.
Juma alishukuru kwa taarifa na moja kwa moja akazifikisha kwa Deo pia yani baba mwenye nyumba yake ili ajue alipo binti yake Sabrina, kwahiyo wakamuacha Joyce pale hospitali akiendelea kuhudumiwa na kwenda kuwaona hawa wengine ambao hawakuelewa hali zao.
Sabrina alifurahi sana kumuona baba yake, ikabidi akae nae pale hadi alipomalizwa kuhudumiwa ila muda nao ulikuwa umekwenda sana na haikuwa rahisi kurudi kwenye ile hospitali ya mwanzo ambako Joy alilazwa kwahiyo wakangoja iwe alfajiri kidogo ndio waondoke ili kuepusha majanga mengine.
Hali ya Sakina kwenye chumba cha uzazi haikuwa nzuri kabisa kwani hakujifungua muda ule waliofikiria wala nini na aliendelea kutokwa na damu tu.
Hali ile iliwapa mashaka manesi wa pale kwani muda nao ulipita hadi pakakucha bila Sakina kujifungua, na kila wakipima wanaona mtoto yupo mlangoni huku mama mtu akizidi kuvuja damu tu.
Madaktari wakakaa na kushauriana kuwa ili kuokoa maisha ya mama na mtoto itabidi operesheni ihusike mahali hapo kwani imeshashindikana kwa mwanamke huyu kujifungua kwa njia ya kawaida.
Wakamuita Juma na kumuelezea hali halisi ambapo alikubali tu mkewe afanyiwe operesheni kwani hata yeye aliweza kushuhudia jinsi hali ya mke wake ilivyokuwa mbaya.
Madaktari wakamfata muhusika sasa ili akubali na harakati za operesheni zifanyike, lakini Sakina alikataa kabisa kufanyiwa operesheni kwani moyo wake ulimwambia kuwa bado ana nafasi ya kutosha ili ajifungue kwa njia ya kawaida. Madaktari wakamshangaa sana na kujiuliza kuwa labda hapatwi na maumivu
"Sikia dada, tunapenda tukusaidie wewe na hiko kiumbe chako tumboni. Kubali tukufanyie operesheni na utasalimia dada yangu"
Sakina nae aliwajibu kwa maumivu makali sana
"Kama mnapenda kunisaidia basi naomba mnisaidie kitu kimoja tu"
"Kitu gani hicho?"
"Naomba mniitie yule binti niliyeletwa naye hapa usiku wa jana"
"Yule binti mdogo!!"
"Ndio, huyo huyo anaitwa Sabrina"
Madaktari wakaangaliana kwa hamaki na kumuuliza Sakina
"Sasa yule binti atakusaidia nini?"
"Mimi najua atakachonisaidia, nawaomba mniletee tu yule binti"
"Ila hii ni wodi ya wazazi, watoto hawaruhusiwi humu dada yangu"
"Jamani nawaomba jamani, kama kweli mnahitaji kuninusuru nawaomba mniitie huyo Sabrina"
Madaktari hawakutaka kusema zaidi, wakaamua kufanya alivyotaka Sakina ingawa ilikuwa nje ya utaratibu.
Deo alishaagana na Juma kuwa anaondoka na binti yake baada ya hali yake kuwa nzuri ili akamuone mkewe. Ila wakati anataka kuondoka alishangazwa na daktari mmoja aliyemfata na kumwambia kuwa binti yake anahitajika kwenye wodi ya wazazi, kwakweli Deo alikataa sana
"Mtamfanya mwanangu aote jamani, mambo gani hayo!"
Yule daktari akamuomba sana na kumsihi awaruhusu waende na huyo binti yake, mwisho wa siku Deo akakubali na kumuacha Sabrina chini ya uangalizi wa Juma huku yeye akienda hospitali aliyolazwa mkewe.
Sabrina alipelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha uzazi, moja kwa moja alipo Sakina kisha akamsogelea Sakina na kumshika mkono.
Muda huo huo Sakina akajifungua, na muda huo huo huyo Sakina akapoteza fahamu.
Deo alienda hadi hospitali aliyolazwa mkewe, akaenda hadi wodi aliyomuacha.
Alipokaribia kitanda alichokuwa amelazwa mkewe alishtushwa kuona pamezungushwa pazia la kijani.
Deo alienda hadi hospitali aliyolazwa mkewe, akaenda hadi wodi aliyomuacha.
Alipokaribia kitanda alichokuwa amelazwa mkewe alishtushwa kuona pamezungushwa pazia la kijani.
Nguvu zilimuisha Bwana Deo na mawazo yake yakavutika mbali kabisa na kuhisi kuwa mkewe amekufa.
Akaanza kusogea taratibu kwenye kile kitanda chenye pazia la kijani kisha akafunua ila hapakuwa na mtu, akamuona nesi akija eneo hilo na kumuuliza kwa masikitiko
"Eti mgonjwa aliyelazwa hapa yuko wapi?"
Yule nesi alimuangalia kwa huruma na kumuuliza tena
"Ni ndugu yako"
Deo alijibu kwa kutikisa kichwa, kisha yule nesi akamsogelea karibu na kumwambia
"Kaza moyo baba, huyu mama wa hapa ametutoka"
Deo alihisi kuchanganyikiwa kwani hata machozi nayo yalishindikana kutoka, ikabidi yule nesi amuombe awasiliane na ndugu zake wengine kwani yeye mwenyewe hataweza kukabiliana na ile hali.
Bwana Deo akatoka nje ya wodi akiwa amechanganyikiwa kabisa, hakujielewa hata kidogo na alijihisi kuwa yeye ndio chanzo cha kifo hiko cha mkewe.
Sabrina aliogopa sana kumuona mtoto mchanga akiwa kajaa damu, ilibidi manesi wamtoe nje Sabrina ili waweze kuendelea na taratibu zingine za pale kwenye chumba cha wazazi.
Juma alimchukua Sabrina na kumuweka mahali ili kumfanya akili imkae sawa.
Manesi nao walimfata Juma na kumpongeza kwa kupata mtoto.
"Hongera sana kaka"
"Hivi ni mtoto gani?"
"Umepata dume kaka yangu, hongera sana"
Juma akafurahi sana kwani ndio kitu alichokuwa anakihitaji siku zote na kusahau hata kuuliza hali ya mke wake, hadi nesi aliyemletea habari akamuuliza kwa mshangao
"Inamaana hata hali ya mke wako hutaki kuijua?"
"Aaah furaha ilipitiliza, eeh anaendeleaje na mwanangu je yupoje?"
"Utamuona tu ila mkeo amepoteza fahamu, ila usijali atazinduka tu"
Swala la mke wake kupoteza fahamu halikumpa wasiwasi sana kwani alichotaka yeye ni kumuona mtoto wake tu na si vinginevyo.
Sakina alipozinduka alikabidhiwa mtoto wake naye pia akafurahi sana.
Kisha yeye na Juma pamoja na Sabrina na mtoto wao wakaruhusiwa kurudi nyumbani na moja kwa moja walifika ndani kwao huku wakisemezana hili na lile.
Sakina akamuomba jambo moja tu mumewe kuwa aruhusu yule mtoto apewe jina na Sabrina, Juma naye hakuwa na pingamizi dhidi ya hilo na kuruhusu tu Sabrina ampe jina mtoto.
Sakina akamwambia Sabrina,
"Kwavile nilikuahidi kwamba nikipata mtoto wa kike basi ataitwa jina lako, sasa nimepata mtoto wa kiume basi ningependa wewe umpe jina. Sawa Sabrina!"
Sabrina akatingisha kichwa akiashiria kuwa amemuelewa, kisha akaulizwa tena
"Nitajie basi jina utakalompa mtoto"
"Aitwe Jeff"
"Jeff!!"
Juma na Sakina walijikuta wakisema pamoja kwa hamaki kisha wakaangaliana, wala Sabrina hakujua kuwa kwanini wameshangaa kwa kiasi kile. Ikabidi awaulize,
"Mbona mmeshangaa au hamjalipenda?"
"Hapana, ila kwanini umechagua hilo jina?"
"Mi nalipenda tu na ningependa huyu mtoto aitwe hivyo"
Basi Juma alimwambia Sabrina kuwa watajadili kuhusu hilo jina na kuona kama linafaa au halifai kwa mtoto wao.
Hali ya Deo haikuwa sawa kabisa kwani alihisi kuwa chini, akatafuta mahali na kukaa kisha akitafakari cha kufanya kwani hakujielewa kabisa, hakujua aanzie wapi na aishie wapi. Hakuweza kupata majibu kwa yote aliyoyawaza, ikabidi aamue kurudi tu nyumbani ili awaambie ndugu wote mambo ambayo yametokea kuhusu mke wake na taratibu za mazishi ziweze kuendelea hata akasahau kama kuna hospitali nyingine aliacha watu wanaomuhusu.
Alipokaribia kwake hakutaka kuingia ndani na badala yake ni moja kwa moja akaenda kwa mpangaji wake ambaye alikuwa ni Juma kwani aliona uwepo wa watu kwenye nyumba hiyo.
Juma alimkaribisha Bwana Deo kwa uzuri sana ila akamshangaa Bwana Deo alivyokuwa amenyong'onyea na hapo hapo akaelezwa habari za msiba uliowafanya wote wakose raha pale ndani kwani ilikuwa kamavile wamemwagiwa pilipili.
Sabrina ndiye aliyetia huruma zaidi kwani hakuamini kuwa mama yake kamtoka kwa mtindo huo ukizingatia aliondoka kwao bila kuaga kwahiyo ikawa simanzi kubwa sana kwake.
Deo akawapigia simu ndugu zake na kuwapa habari za msiba huo, akapiga simu na shuleni kwa watoto zake ili warudishwe kwakweli Deo alikuwa kapatwa na pigo kubwa sana kwenye maisha yake.
Haikuchukua muda sana kwa ndugu na majirani kuanza kukusanyika katika nyumba ya Deo huku kila mmoja akisema lake
"Yani ni jana tu nilikuwa nikitaniana nae eti leo katutoka jamani!"
Wengi waliingiwa na simanzi na walikuwa na majonzi sana kwa msiba huo ambao haukutarajiwa wala kutegemewa.
Sabrina mkubwa alifika kwa kaka yake na kuwapita wale ndugu kisha akamfata kaka yake na kumuuliza
"Huyo marehemu yuko wapi?"
"Maswali gani hayo Sabrina bila hata ya salamu?"
Sabrina akacheka na kumuuliza tena kaka yake
"Marehemu yuko wapi?"
"Hospitali, amepelekwa monchwari"
"Sawa kaka yangu"
Kisha akacheka tena na kuondoka pale msibani na kufanya baadhi ya ndugu waamini kwamba huyu mdada anamatatizo kwenye akili yake au anamambo ya kishirikina kwani kwenye swala la msiba kwa mtu mwenye akili timamu hawezi akacheka.
Deo akazidi kupatwa na mawazo kwa akili fupi za mdogo wake ingawa anampenda sana mdogo wake huyo.
Ndugu waliokuwepo hapo kwenye msiba wakaanza mipango kwaajili ya huyo marehemu kuwa wengine wataenda hospitali kushughulika na mwili wa marehemu huku wengine wakibaki nyumbani kwa mipango na shughuli zingine za mazishi.
Binti mdogo Sabrina hakutaka kuamini ukweli kuwa mama yake amekufa, akaenda kwa baba yake na kumuomba kuwa ampeleke hospitali akamuone mwenyewe mama yake kabla hata hajaletwa nyumbani
"Hawaruhusiwi watoto kule mwanangu"
"Naomba waniruhusu mimi tu baba kwani siamini kama amekufa kweli"
"Akiletwa utamuona mwanangu"
Deo alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani kila alipoitazama familia yake hakuweza kuamini kama mkewe ndio kashamuachia watoto wale tayari, alitamani hata siku zirudishwe nyuma ili mambo yaweze kubadilika na mkasa huu uweze kupotea pia ila hali haikubadilika kwake.
Yule dada wa Deo aliyeitwa Sabrina ilikuwa kamavile kuna kitu anakijua kuhusu huyu wifi yake ambaye inasemekana kwamba amekufa.
Na alipotoka pale huku akicheka alikuwa na nia ya kwenda moja kwa moja hospitali ili akahakikishe kama ni kweli au la kwani mawazo yake yalimtuma kwamba sio kweli na ndiomana akacheka na kuondoka.
Ila wakati anaondoka hakuweza kugundua kitu kimoja kuwa kuna mtu kutoka pale msibani alikuwa akimfatilia kwa nyuma na baada ya dakika chache yule mtu aliyekuwa akimfatilia Sabrina kwa nyuma alionekana akiwa kwenye nyumba yake iliyokuwa njiani na ni njia hiyo hiyo ambayo Sabrina alitakiwa kupita.
Sabrina alipokaribia kwenye hiyo nyumba alishangaa kuona ukungu mbele yake na gafla macho yakamuwasha kamavile mtu aliyemwagiwa pilipili, muda huo huo akahisi kizunguzungu na kuanguka.
Watu wakajaa eneo hilo huku wakimshangaa kuwa amepatwa na kitu cha aina gani.
Yule mtu ambaye alikuwa akimfatilia naye alitoka kwenye nyumba yake huku akionekana kama mtu aliyestaajabishwa na alichokiona kisha akawaomba wamuingize ndani kwake ili ampatie huduma ya kwanza.
Watu waliomzunguka Sabrina hawakusita bali walifanya kama walivyoshauriwa na huyo mwenye nyumba kisha wakaondoka bila hata ya kuhoji kitu chochote.
Sabrina alipobaki na yule mtu akazinduka ila hakuweza kuona kitu chochote kwani alikuwa kama kipofu kisha yule mtu akamuuliza
"Kilichokuwa kinakuchekesha kwenye msiba?"
Sabrina akashangaa na kuuliza pia
"Kwani wewe ni nani?"
"Huna mamlaka ya kunijua ila unatakiwa kujibu unachoulizwa"
"Kwasababu siamini kama kweli amekufa"
"Kwanini huamini? Kuna kitu chochote unajua?"
"Sijui chochote"
"Kama hujui chochote kwanini ulicheka? Na kwanini huamini?"
"Nilijikuta nikicheka tu ila ukweli ni kwamba siamini kama alikufa"
"Basi unatakiwa uamini na usipende kufanya masikhara kwenye mambo kama haya"
Kisha yule mtu akamshika macho Sabrina, naye akaona kilichotokea hospitali.
Kuwa Deo alipoenda hospitali kumuangalia Joyce alikuwa akifatwa na mtu nyuma bila kujua na walipofika hospitali kisha kuhamia hospitali nyingine kwaajili ya kumuona Sabrina mdogo, yule mtu aliyekuwa akimfatilia naye aliondoka, na muda kidogo likatumwa jeshi la watu watatu na kummaliza yule mgonjwa pale kitandani.
Sabrina akatokwa na chozi moja la uchungu kwani alitamani afanye kitu kisha akajisemea
"Nilijua yote haya ndiomana nikamkataza mwanae asitoke"
"Ulijua nini?"
Ila Sabrina hakujibu na wala hakujielewa kuwa ajibu kitu gani kwani aliona ni mambo ya ajabu na kujiambia kimoyomoyo kuwa akipona moja linakuja la pili.
Muda huo huo alijiona yupo pale njiani tena, kwakweli hakuweza kuendelea na safari badala yake alijikuta akikimbia na kurudi nyumbani kwa kaka yake huku amenyong'onyea sana hadi kaka yake akashtuka kuwa mtu aliyeondoka huku anacheka ndio huyo amerudi huku kanywea, kisha akamuuliza
"Ni nini tena muda huu mdogo wangu"
"Sijui"
"Hujui nini?"
"Nitakwambia"
Alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana kwa muda huo na hakuna ambaye alimuelewa kuwa alikuwa anamawazo gani.
Ndugu nao waliongezeka pale nyumbani kwa Deo huku wakilia na kuomboleza kuwa wamempotea Joyce aliyekuwa mtu wa watu, kipenzi cha watu yani sifa zote alizipata hapo hata sifa ambazo hakuwahi kuambiwa kuwa anazo ila hapo walizisema huku wakilia na kuomboleza.
Kama ambavyo ilipangwa, ndugu wengine wakajiandaa na kwenda hospitali kwaajili ya kuandaa mwili wa marehemu na wengine walibaki pale nyumbani huku ratiba ya mazishi ikipangwa.
Deo alikuwa bado hajielewi kwakweli, dada yake mdogo akamfata tena na kumwambia
"Nikwambie kitu kaka!"
"Niambie tu"
"Wifi hajafa"
"Mmh Sabrina mdogo wangu umechanganyikiwa au?"
"Sijachanganyikiwa, ila huo ndio ukweli"
Deo alimuangalia Sabrina kwa makini sana bila ya kumuelewa, kisha Sabrina akamwambia tena
"Utaamini maneno yangu wakirudi hao wa hospitali"
Wakati wakiongea hayo wakasikia watu wakipiga kelele nje na kuwa kama wakikimbizana.
Ikabidi watoke ndani na kwenda kushuhudia kuwa kuna nini, walishangaa kumuona Joyce akitembea huku anachechemea akiwa anarudi pale nyumbani.
Ikabidi watoke ndani na kwenda kushuhudia kuwa kuna nini, walishangaa kumuona Joyce akitembea huku anachechemea akiwa anarudi pale nyumbani.
Watu pale nje walitawanyika wote, Deo aliganda mlangoni kama barafu huku macho yamemtoka kwani hakuamini kitu ambacho alikiona mbele yake.
Ilikuwa kama mauzauza tu.
Kati ya wote waliokuwemo mule ndani ni Sabrina pekee aliyepata ujasiri wa kwenda na kumsogelea Joy kisha akamshika mkono na kumsaidia kuingia ndani.
Deo hakuwa na ujasiri zaidi ya kumtazama tu mkewe, hata watoto wa Joy nao hawakuwa na ujasiri zaidi ya kumkodolea macho tu mama yao.
Baada ya Joyce kukaa, naye alikuwa akiwashangaa kuwa kwanini wanamkwepa, akaanza kwa kuwaita majina watoto wake na kuwauliza
"Mbona mpo mbali na mimi wanangu? Inamaana hamjafurahi kuniona?"
Watoto wake wote walikuwa kimya na ilionyesha dhahiri walimuogopa mama yao baada ya kusikia kuwa amekufa.
Ni Sabrina mdogo tu aliyeweza kumsogelea tena mama yake na kumwambia kwa upole
"Tumeambiwa kuwa umekufa mama"
Joyce naye akauliza kwa mshangao,
"Nimekufa!!"
"Ndio"
"Nani kasema kuwa nimekufa?"
"Baba ndio katuambia hivyo"
Joyce akasikitika sana na kumuangalia mumewe, kisha akamwambia
"Hata kama hunipendi tena, si vizuri kuwatangazia watu nimekufa Deo! Kufa wewe uone kama kufa ni kuzuri"
Muda huo huo Deo akaanguka chini na kufanya wote washtuke, watoto wake walikuwa ni wa kwanza kumfata baba yao pale chini huku wakimtingisha na kulaumu maneno ya mama yao kuwa ndio yamesababisha.
Joy nae aliinama kumuangalia mume wake aliyekuwa hajitambui kwa muda huo ila na yeye hakuelewa kwanini imekuwa hivyo.
Sabrina mkubwa alitulia pembeni huku amesimama, kisha akawaacha pale wakimtingisha Deo na kutoka nje.
Alipofika nje akamuona mtu mmoja aliyekuwa amemgeuzia mgongo, mawazo ya Sabrina yakamtuma kuwa yule mtu ndio yuleyule aliyempa kizunguzungu muda ambao na yeye alianguka njini alipokuwa anaenda hospitali kushuhudia.
Kengele ya hatari ikagonga kwenye kichwa chake, kwa haraka akarudi ndani na kuwazui wote waliomzunguka kaka yake kuwa waende pembeni nao wakatii na kusogea halafu Deo akabaki mwenyewe pale katikati alipoanguka.
Joy akauliza,
"Mbona sielewi mambo ya hapa?"
Sabrina mkubwa akamfanyia ishara ya kidole kuwa anyamaza kimya, naye akatii na kunyamaza kama ilivyotakiwa.
Kimya kile kilitanda kwa dakika kama tano hivi kisha Deo mwenyewe akazinduka alipokuwa ameanguka na kuinuka, kisha akajisogeza kwenye kiti kwani hakuelewa hata ni kitu gani kilichotokea kwake.
Ila bado wote waliendelea kuwa kimya mpaka pale ambapo walisikia kuna mtu akigonga mlango wa pale ndani kisha Sabrina mkubwa akainuka na kwenda kufungua mlango, walikuwa ni watu waliotoka hospitali nao wakashtuka kumuona Joy pale nyumbani
"Mambo gani haya jamani?"
Sabrina akawatuliza na kuwaingiza ndani ili waweze kuzungumza vizuri zaidi.
"Mmetutuma hospitali, mmefanya tuzunguke kila jokofu kumtafuta huyo marehemu. Mambo gani haya kumbe mtu mwenyewe ni mzima kabisa"
Sabrina akajaribu kumtetea kaka yake kwa ndugu hawa
"Jamani naomba mtuwie radhi kidogo kwani kaka yangu alichanganyikiwa tayari ndiomana ikawa kama ilivyokuwa, naomba mtusamehe"
Wengi waliongea sana ila mwisho wa siku wakaelewana na kuondoka.
Sabrina mkubwa alitamani sana kujua kilichomtokea wifi yake kwani hata yeye hakuelewa kitu, moja kwa moja akiwa na kaka yake waliamua kukaa na Joyce na kumuhoji imekuwaje kuwaje hadi kufikia hatua ya kudhaniwa kuwa amekufa. Naye Joy akawaelezea ilivyokuwa,
"Nilitoka hapa nyumbani nikiwa na mawazo sana baada ya Deo kunitimua kuwa nikamtafute mtoto, njiani nikamuona Juma. Sasa ile kuvuka ili nimfate si ndio nikagongwa na pikipiki.
Waliniwaisha hospitali kwakweli na kuanza kupewa huduma vizuri tu ila tatizo likawa nilipozinduka sikumuona ndugu hata mmoja, nikamuuliza nesi akaniambia kuwa mume wangu alikuwepo ila ameondoka kwakweli roho iliniuma sana.
Yule nesi alipoondoka aliletwa mgonjwa mwingine, naye alikuwa kagongwa na pikipiki ila kwavile kitanda nilichokuwa mimi ilikuwa ni sehemu nzuri kwa yule mgonjwa ni hapo nilipoamua kumpisha kisha ndugu zake wakaanza kumtafutia huduma.
Ni muda huo nikapigiwa simu na rafiki yangu ambapo nilishangaa kuona vitu vyangu vyote nilikuwa navyo pembeni ingawa nilikuwa nimepata ajali.
Yule rafiki yangu nilipomwambia nilipo na hali halisi ilivyo aliamua kuja kunifuata, kwavile ana zahanati, moja kwa moja akanipeleka kwenye zahanati yake ili nikaendelee kutibiwa huko.
Hata nilivyorudi hapa ni baada ya kuona kuwa hali yangu ina unafuu sasa."
Sabrina akamuangalia kaka yake Deo kama naye yupo makini katika kusikiliza maelezo ya Joyce, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kukubaliana na huo ukweli. Deo akajiuliza kwa mshangao
"Inamaana aliyekufa ni yule uliyemuacha mwanzoni"
Sasa akapata picha kwa kilichotokea kwa mkewe bila kujua kama kule kuondoka kwa mkewe pale hospitali palimsaidia sana kwani kifo chote kilikuwa juu yake kwahiyo yule aliyekufa ilikuwa ni badili yake lakini hakuna hata mmoja aliyejua hilo zaidi ni kushukuru tu kwa kurudi kwa Joy.
Siku hiyo ikapita kwa mtindo huo huku kila mmoja akiwa na mawazo sana.
Sabrina mkubwa aliondoka ila alihitaji sana kumjua yule mtu ambaye alikuwa akiwafatilia na akasema kuwa lazima atamjua na akishamjua ndio ataamua ni kitu gani afanye.
Nyumba yao ilirudi katika hali ya kawaida baada ya mambo yote kupita na kufanya wajisikie amani kidogo bila kujua kama adui bado hajajulikana kuwa ni nani na analengo gani kwao.
Sabrina mtoto wa Joyce kuna mambo yaliyomchanganya sana na kuhisi kuwa kuna kitu anakijua ila haelewi kuwa hicho kitu ni kitu gani na kina mpango gani katika maisha yake.
Baada ya hali kuwa shwari kabisa hata wale watoto wao wawili kurudi shuleni ambao walikuwa wakisoma shule ya bweni.
Sasa ndio Joyce alipoamua kwenda kumtazama Sakina kwani hakuweza kuonana nae tangia siku amejifungua.
Alimkuta Sakina akiendelea kupata huduma ya uzazi kama kawaida ya wanaojifungua na huduma wanazopatiwa.
Joy alitamani sana kujua ni kitu gani kilitokea wakati ambao aliondoka na Sabrina, aliona ni vizuri akielezwa muda huo kwani mtoto wa Sakina alikuwa amelala
"Kwani Sabrina hajakueleza?"
"Kwakweli sijui hata nikwambie nini kuhusu huyu mwanangu ila kwa kifupi ni kama amechanganyikiwa hivi maana hata mimi simuelewi na kila ninapomuuliza huwa hasemi chochote"
Ikabidi Sakina amsimulie kwa kifupi ilivyokuwa na kumfanya Joyce ashtuke sana
"Mmmh mbona hayo mambo ni kama ushirikina?"
"Hata mimi nahisi hivyo kuwa kuna ushirikina unaendelea hapa kati yetu ila nitajua tu hata usijali mama James"
Ila kilichomsikitisha zaidi Joyce ni kile kitendo cha kumpeleka mwanae kwenye chumba cha uzazi kwani alijua lazima mwanae kaenda kuona mambo makubwa ambayo hakupaswa kuyaona ila ndio hivyo ilivyotokea.
Joy aliondoka pale akiwa na maswali mengi sana dhidi ya mwanae ambaye alionekana dhahiri kutokuwa sawa.
Joy alipofika ndani kwake alijaribu tena kumuuliza Sabrina maswali mawili matatu ambayo yote hakupata majibu yanayoeleweka toka kwa mwanae
"Ni kitu gani ulikiona wakati Sakina anajifungua?"
"Sikuona chochote"
Alijaribu hata kumbembeleza ila mtoto hakusema kitu chochote kile na kumfanya Joy azidi kupatwa na mawazo kwani alihitaji kujua kuwa mwanae anajua nini ili ajue jinsi ya kumsaidia ila tatizo la mwanae hakutaka kusema ukweli wowote na kila alichoulizwa alidai kuwa hajui kitu wakati hata mama yake alihisi kuwa kuna kitu mwanae anakijua ila hataki kukisema kuwa ni kitu gani.
Joy akajisemea kuwa atakijua tu kinachomsumbua mtoto wake.
Kuna siku Joy alikaa tena na mwanae akamsikia akisema
"Mimi sitaki kuolewa wala kuzaa"
Joy akamshangaa sana mwanae na kumuuliza kwa makini ila hakujibu chochote kuwa amesema kitu gani
"Ila nimekusikia Sabrina, hebu niambie kwanini unasema hivyo"
Sabrina aliendelea kuwa kimya.
"Hivi umemuona tena mtoto wa Sakina alivyopendeza?"
"Anaitwa Jeff"
"Kumbe anaitwa Jeff!! Sikujua jina lake mwanangu. Umemuona tena alivyokuwa mzuri?"
Sabrina akatingisha kichwa kuwa hajamuona tena
"Basi badae tutaenda pamoja kumuangalia mwanangu. Sawa mama!"
"Sawa"
Joy alitamani sana kujua anachojua mtoto wake ila hakuweza kukijua kabisa kwani mtoto wake hakuwa muwazi kwa anachokifikiria muda wote.
Sakina hakuwa na tatizo kwa jina ambalo Sabrina alimpa mtoto wao ila Juma bado hilo jina hakulitaka kutokana na mambo ambayo yalimtokea nyuma.
Aliwahi kuwa na urafiki na mtu mmoja aliyekuwa akiita hivyo kisha yule mtu wakagombana nae na kuweka chuki za milele kwani yule mtu naye alikuwa akimuhitaji Sakina na kufanya ugomvi wao uwe mkubwa kupita wa kwanza.
Hivyo Juma hakutaka mwanae aitwe jina la adui yake, Sakina akamuuliza mumewe
"Sasa huyu mtoto tumuite nani?"
"Tumuite tu mtoto hadi pale nitakapompatia jina ninalolitaka"
"Mpaka lini sasa?"
"Leo leo nitampa jina kama umechoka kumuita mtoto"
Sakina hakutaka kugombana na mumewe hivyobasi akafanya kama alivyotaka.
Sakina akatembelewa na jirani yao mmoja kwa lengo la kumuona mtoto ila nae alimkuta mtoto amelala, huyu jirani alimshangaza Sakina kwa maswali ambayo alimuuliza kwani yalikuwa ni maswali ya mshangao
"Hivi ulijifunguaje Sakina?"
"Nilijifungua kawaida tu"
"Kawaida kabisaa!!"
"Ndio kawaida kwani wewe ulijua ni nini"
"Basi"
Akainuka na kuondoka bila hata ya kuaga na kumfanya Sakina apate maswali mengi sana kwenye kichwa chake kwani hakuelewa yule jirani alimaanisha nini.
Joyce alipokuwa anajiandaa kwenda kwa Sakina akapigiwa simu na wifi yake kisha akaambiwa
"Kuna jirani yenu hapo si mtu mzuri, kwahiyo kuwa makini na watoto wifi"
"Jirani gani huyo?"
"Simjui ila ndio hivyo"
Kisha akakata simu na kumfanya Joy ajiulize maswali na kujisemea
"Simu za huyu huwa sio za kheri kwakweli bora hata asiwe ananipigia jamani kwani ananitisha tu"
Kisha akamuita mwanae na kumwambia kuwa waende kwa Sakina kumuona kwani ndivyo alivyopanga nae mwanzo kuwa wataenda kumuona ukizingatia Sabrina hakumuona tena toka siku wametoka hospitali ingawa nyumba wanayoishi ndio hapo hapo.
Walimkuta Sakina akiwa na mtoto wake kama kawaida na mume wake naye alikuwepo.
Sakina aliwaeleza kuhusu yule jirani aliyekuja kumuona na maswali ambayo alikuwa akimuuliza, ikabidi Joyce aulize vizuri kuhusu huyo jirani
"Ni nani huyo?"
"Si yule mama jembe"
Sabrina akashtuka sana na kufanya wamuulize vizuri kuwa kwanini ameshtuka vile.
"Wakati ulipokuwa mule ndani kabla ya kuniita mimi, nilimuona huyo mama jembe kwenye mlango wa kule mlipokuwa"
Wote wakamshangaa na kumuuliza kama anauhakika, Sabrina naye aliwahakikishia kabisa ila Sakina akasema kuwa atafanya kitu ili ajue ni wapi kuna huo mzizi wa fitina.
Wakati wanazungumza, Juma nae akasogea na kuwatajia jina aliloamua mwanae aitwe.
"Kuanzia sasa mwanangu ataitwa Jabali"
Sabrina akachukia sana kuona yule mtoto amebalishwa jina.
Sakina hakuwa na neno, ila kwavile mwanae alikuwa nae mkononi akajaribu kumuita hilo jina aone kama litampendeza mtoto wao.
"Jabali"
Gafla hali ya hewa ilibadilika mule ndani kisha giza likatanda, na yule mtoto alianza kulia kwa nguvu kama ameangushwa chini.
Gafla hali ya hewa ilibadilika mule ndani kisha giza
likatanda, na yule mtoto alianza kulia kwa nguvu
kama ameangushwa chini.
Sakina alishtuka sana na kutetemeka kwani hakuelewa tatizo ni jina au ni kitu gani.
Giza lilitanda kwenye nyumba yao na kufanya wote waanze kuogopa, na ile sauti ya mtoto kulia iliwafanya wazidi kupatwa na mashaka.
Sakina alijikuta akimbadilisha mwanae jina pale pale.
"Basi nyamaza mwanangu Jeff"
Ni kweli yule mtoto alinyamaza ila giza nalo lilizidi kutanda.
Mtu wa kwanza kufanikiwa kushika mlango alikuwa ni Sabrina na kuwafanya wote watoke nje huku wanashangaa kuwa ni kitu gani kile, yani nyumba ipatwe na giza la gafla kama vile kwakweli ilikuwa ni hali ya ajabu kwani haikuwahi kuwatokea.
Ikabidi wote waelekee ndani kwa Deo ambaye aliwashangaa na kuuliza
"Kwani mtoto ameshaanza kutoka nje?"
"Maajabu ya mule ndani leo imetubidi tu tutoke nae"
"Maajabu gani?"
"Yani mule ndani mmeingia giza la gafla"
"Nyumba yangu mimi inaingiaje giza la gafla?"
Deo akataka kwenda kushuhudia ila mkewe akamzuia lakini Deo hakutaka kusikiliza kisha akatoka na kwenda kuangalia, Joy hakuwa na jinsi zaidi ya kumfata nyuma mumewe.
Deo alipofika aliingia ndani ila hali ilikuwa kawaida tu wala hakuona hilo giza walilolesema, Deo akatoka huku anacheka kwa kusikitika na kurudi ndani kwake huku Joy akimfata nyuma.
Deo kufika ndani akawa anawauliza kwa kucheka
"Haya hilo giza liko wapi?"
"Lilikuwepo mule ndani"
"Kweli nimeamini mna mashetani nyie sio bure kabisa"
Akainuka na kwenda chumbani kwake.
Wakaishia kuulizana pale
"Inamaana sisi wote tuna mashetani? mmmh!"
Sakina alisema hawezi kukubaliana na ile hali hivyobasi alipanga kuwa lazima arudi kwao kabisa na huko ataenda kujua mbivu na mbichi za kwanini imewatokea vile.
Joy akamuuliza Sakina
"Kwahiyo wewe unaamini ni ushirikina?"
"Ni ushirikina ndio kwasababu hiki sio kitu cha kawaida"
"Mmh waswahili mnamambo jamani, haya nenda ukachunguze mama"
Juma alikuwa katulia tu huku akifikiria kitu cha kufanya.
Baada ya hali kuwa shwari ndipo Juma akamuomba mkewe warudi ndani kwao, naye akakubali na kurudi ila kesho yake Juma na familia yake wakasafiri na kuondoka mahali hapo.
Bado Joy hakuwa na furaha na maendeleo ya mtoto wake Sabrina, ndipo alipomuomba mumewe kuwa wampeleke shule za bweni mtoto wao huyo ambapo Deo aliamua kukubali kwani maendeleo ya mtoto wake kielimu yalirudi nyuma sana hivyobasi akaona ni vyema kwenda kujaribisha shule za bweni ili kuona kama atabadilika au vipi.
Makubaliano yalipokamilika, Sabrina akatafutiwa shule na kupelekwa huko ambako palikuwa mbali kidogo na nyumbani kwao kwahiyo haikuwa rahisi kwa yeye kurudi tena nyumbani kama ilivyokuwa awali.
Sabrina alipooza sana alipokuwa shuleni na alikuwa ni mtoto mwenye mawazo kwa muda mwingi na kufanya hata walimu wajiulize kuwa ana tatizo gani na kujaribu kuwa nae karibu kwa muda mwingi ili kumuweka sawa na ili aweze kufanana na watoto wengine.
Sakina alirudi nyumbani kwake baada ya mwaka mmoja na mtoto wake Jeff alikuwa amekuwa kwasasa na aliweza kutembea hata kuzungumza baadhi ya maneno.
Sakina alikawia sana kurudi nyumbani kwake kutokana na mila alizozikuta kwao, kwahiyo aliyerudi alikuwa ni mumewe na aliishi mwenyewe kwa kipindi chote hicho ambacho mkewe alikuwa kwao.
Joy alimpokea vizuri sana Sakina kwani ilikuwa ni kipindi kirefu tangia aondoke.
"Kheee, ndio ulienda kuzamia moja kwa moja!!"
"Kutokana na mambo nilivyoyakuta ilinibidi nifanye hivyo ila sasa nimerudi na nguvu mpya na kasi mpya"
Joyce alicheka, mengi yaliyofanyika nyuma yalikuwa yameshasahaulika kabisa kwani mambo mengi yalikuwa ni mapya ila Sakina alirudi na majibu karibia yote ya mambo ambayo yalifanyika nyuma kati yao na kumfanya Joy apate hamu ya kujua tena kuwa ni kitu gani na kwanini kilitokea kama ilivyokuwa Kwanza kabisa alianza kumuuliza Joy
"Hivi mama Jembe bado yupo?"
"Hapana, alihama"
"Nilijua tu kuwa lazima ahame, mimi kwetu Tanga na niliaga kamwe siwezi kusumbuliwa akili kiasi kile"
"Hebu niambie vizuri Sakina maana hata sikuelewi"
Basi Sakina akaanza kumueleza ilivyokuwa.
"Nilipoondaka hapa nilienda nyumbani kisha nikaenda kwa mtaalamu mmoja huko kwetu na akanieleza kila kitu.
Kumbe mimi nilifungwa ile mimba ili nisijifungue ndiomana miezi ilipitiliza bila hata ya kuwa na dalili yoyote ya kujifungua, kwakweli nilichoka ndiomana nikaamua kwenda kule msituni na Sabrina.
Moyo wangu ulikuwa unaniambia kuwa Sabrina ndio mtu pekee wa kunisaidia hata nikipatwa chochote huko porini sababu ya upendo niliokuwa nao kwake hata yeye pia alinipenda.
Wakati tunarudi kutoka kwenye kale kapori tukakutana na chatu, kumbe hakuwa chatu bali alikuwa ni huyo huyo mama Jembe hadi mimi nikamuangukia Sabrina na hapo akajua kuwa amemaliza kazi. Nia yake ni kuvunja mahusiano yetu ndiomana kuna kipindi hata wewe ulikuwa unanichukia bila sababu yoyote ile.
Ila Mungu mkubwa kwani tulipata msaada na kuwaishwa hospitali na mie nikapelekwa leba ili nikajifungue sababu mtoto alikuwa mlangoni kabisa ila hakutoka kumbe muda wote huo, huyu mwanamke mbaya alikuwa anazuia ili nisijifungue.
Nilipoomba waniitie Sabrina ndio hapo alipochukia na kuja kumalizia kwako hasira zake zote.
Nia yake ilikuwa ufe ila Mungu amekusaidia kwakweli sababu kile kitendo cha wewe kuondoka pale hospitali ndio ilikuwa pona yako badala yake watu aliowatuma wakammaliza mtu waliyemkuta amelazwa pale.
Na uliporudi nyumbani alitaka amalizie hasira zake kwa mumeo ila yule wifi yako aligundua kitu ndiomana mumeo akapona.
Yule mama Jembe alikuwa mbaya sana, na mimi nimemfanyia yangu hadi amehama"
Joy alikuwa kimya akisikiliza huku akisikitika sana kwani hakujua kama yule jirani angemfanyia vile kama alivyosimuliwa na Sakina kwahiyo akaishia kushangaa tu.
Baada ya yote hayo, Sakina akamuomba Joy kusahau yaliyopita na kuanza ukurasa mpya wa maisha bila kubughuziwa na mtu yeyote yule. Na maisha yakaendelea kama kawaida, ingawa Sakina aligundua kuwa mumewe ana mwanamke mwingine.
Siku hiyo Joy akiwa ametulia ndani kwake akapigiwa simu na wifi yake na hiyo ni baada ya muda mrefu kupita bila ya mawasiliano yoyote kati yao.
Wakasalimiana vizuri sana na kufurahiana
"Ila wifi kuna jambo moja ningependa ulifahamu"
"Jambo gani hilo?"
"Bado hamjafika mwisho na yule mtu kwahiyo kuweni makini sana"
"Mtu gani huyo?"
Ni yule niliyewahi kukwambia kuwa anaifatilia familia yako, kuwa makini sana wifi yangu"
Joy alishaelewa moja kwa moja kuwa ni mtu gani anayezungumziwa hapo kwahiyo haikumpa shida sana, tofauti na pale mwanzoni wakati haelewi chochote.
Likizo ilifika na wakina Sabrina wakarudi, safari hii Sabrina alifurahi sana kumkuta Sakina nae amerudi na kufanya wawe marafiki kamavile wapo rika moja.
Ila mapenzi ya Sabrina yalihamia kwa mtoto wa Sakina sasa kwani likizo yote Sabrina alikuwa karibu na huyu mtoto, kila alichofanya alipenda kufanya na huyu mtoto.
Huyu mtoto nae alifurahia sana uwepo wa Sabrina hadi kipindi likizo ikiisha huyu mtoto Jeff alikuwa ananyong'onyea sana kwa kukosa uwepo wa Sabrina.
Kitu kimoja kilichomsononesha Sabrina ni kumkuta Sakina hakuwa na raha na ile furaha kama zamani na alipokuja kuchunguza akagundua kwamba mume wa Sakina alikuwa na nyumba ndogo yani alikuwa na mwanamke mwingine.
Sabrina na udogo wake lakini aliumia sana kamavile ni yeye aliyefanyiwa yale na kumfanya azidi kujiapia moyoni mwake kuwa hatokuja kuolewa kamwe katika maisha yake kwani alichokiona kwa watu kilitosha kabisa kumuonyesha kuwa ndoa ni mbaya.
Maisha nayo yaliendelea kama kawaida.
Sabrina akakua sasa na kuwa binti mkubwa kabisa ila hakutaka kujihusisha na mahusiano huku akiamini kuwa ni kitu kibaya na kisichofaa katika maisha yake kwahiyo wote waliokuwa wakimfata na kumtongoza aliwakataa kwamadai kuwa watakuwa sio waaminifu.
Sakina akagundua kuwa Sabrina ameathirika kisaikolojia kutokana na mambo ambayo yalikuwa yakimtokea wakati akiwa binti mdogo, akajaribu kukaa nae ili kumuweka sawa lakini Sabrina hakukubaliana na hali halisi.
Kuna siku Sakina alipewa ujumbe na kaka yake, moja kwa moja aliufikisha ule ujumbe kwa mama wa Sabrina.
"Kaka yangu anahitaji kumuoa binti yako"
"Unajua ulipokuja hapa na kusema kuwa una khabari njema nilijua ni njema kweli kumbe ni upuuzi tu"
"Upuuzi kwa habari ya kuolewa binti yako!!"
"Mwanangu ndio kwanza ana miaka ishirini, subirini akue kwanza msitake kuniharibia mtoto"
"Laiti ungeyajua hayo mawazo ya mtoto wako hata ungetamani kujaribu hili ili kidogo uone ingekusaidiaje"
"Tafadhari, usiniletee khabari kama hizo Sakina"
Ikabidi Sakina atulie na Khabari zake ingawa mdogo wake alimsumbua sana kuhusu Sabrina.
Muda mwingi Sabrina alikuwa akiutumia kuongea na huyu mtoto mdogo Jeff ambaye alisikia mambo mengi ya kumuhusu Sabrina toka kwa mama yake na kujaribu kuyauliza mengine kwa muhusika kama ni kweli au la,
"Eti Anti Sabrina, nasikia hutaki kuolewa eti ni kwanini?"
"Hayo ni mambo ya kikubwa, subiri ukue utayajua tu"
Hakutaka kumuweka wazi kwani bado aligundua kuwa ni mtoto sana na hakupaswa kujua.
Siku moja Sabrina akiwa njiani ameongozana na Jeff huku wakizungumza wanayoyajua wao, likatokea kundi la vijana watatu na kuwavamia na nia yao kubwa ilikuwa ni kwa Sabrina, na lengo lao lilikuwa ni kumbaka.
Walimshika kwa nguvu sana na kutaka kumuingilia, walipomfunua walikuta ana kitu cha ajabu mwilini mwake na kitu hicho kilikuwa ni tofauti kwa mwanamke wa kawaida.
Hivyo wale wabakaji wakamuacha Sabrina na kukimbia hata Sabrina mwenyewe alishangaa ila alishukuru walivyokimbia bila kumfanya chochote ila hakujua ni kwanini walikimbia.
Jeff alimfata Sabrina pale chini na kumsaidia kuinuka huku akimpa pole kwa yaliyomkuta huku wakiondoka.
Walifuka nyumbani wakiwa wamechoka sana kutokana na ile purukushani waliyokutana nayo kwa wale wabakaji, Sabrina alimsimulia mama yake na kumfanya mama yake aumie sana kwa hao wabakaji kutaka kumbaka mwanae
"Ila afadhari hawajakudhuru mwanangu"
"Yani mama, ni Mungu tu kanisaidia maana sijui ingekuwaje"
Sabrina hakujua ni kitu gani kilichowakimbiza wale wabakaji ila alishukuru kwa kutodhurika na kuwa makini sana katika safari zake zingine.
Sakina akasikia kitu cha tofauti kutoka mtu wake wa karibu kuhusu Sabrina ila hakuamini na alijiuliza kuwa hata kama ni kweli huyo mtu kajuaje kuhusu Sabrina!!
Mwanae alipokuja kumueleza kuhusu kilichowatokea yeye na Sabrina wakati wanarudi kwa siku mbili zilizopita ndipo Sakina alipogundua kuwa huenda yule ndugu yake anahusika.
Yule kaka yake aliyetaka kumuoa Sabrina ndiye aliyetuma vibaka wambake ili kumkomesha kwavile alimkataa, ila hao vibaka ndio waliompa taarifa kuhusu utofauti wa Sabrina na wanawake wengine na kuwafanya waogope kumbaka.
Sakina alichukizwa sana na hiyo tabia ya nduguye aliyoifanya kwa binti aliyempenda na kumuheshimu sana, hata hivyo hakuamini kama yale aliyoambiwa yalikuwa ni ya kweli.
Siku moja Sabrina akiwa kwenye matembezi yake akamuona kijana mmoja aliyemvutia sana, ikawa ni mara ya kwanza katika maisha yake kuvutiwa na mwanaume na hakujua aanze vipi kuongea nae ila uzuri ni kwamba yule kijana alimsogelea mwenyewe Sabrina na kumsalimia
"Mambo dada"
"Poa tu, mambo"
"Safi, samahani kuna kitu nataka kukuuliza"
Ila kabla hajamuuliza, Sabrina alijishtukia akibanwa na haja ndogo ya gafla na kumfanya ashindwe kuendelea kuongea na yule kijana wala kumsikiliza zaidi.
Hivyo basi akaondoka kwa yule kijana na kukimbilia kwenye kakichaka kidogo ili kujisaidia, gafla ikasikika sauti yake ikipiga kelele kwa nguvu.
Yule kijana kwa hofu akakimbilia mahali ambako Sabrina alielekea ili kujua nini kimemtokea.
Akamkuta Sabrina kasimama huku anapiga kelele, yule kaka akamfata na kumshikilia kisha akamuuliza
"Nini kimekupata dada?"
Lile swali likaonekana kama kumshtua Sabrina na kumfanya aone aibu gafla kwa zile kelele alizokuwa anapiga, akajikuta akimuacha yule kijana pale tena bila ya kumjibu na kutoka kwenye kile kichaka.
Yule kaka naye alitoka kwenye kile kichaka na kumfata tena Sabrina ila Sabrina hakutaka kabisa kumuangalia yule kijana, badala yake alikimbilia kwenye kituo cha madaladala na kupanda daladala moja wapo kisha akaondoka zake na kumuacha yule kijana akiwa na maswali mengi sana dhidi ya Sabrina.
Sabrina alipofika kwao alikuwa na mawazo sana dhidi ya yule kijana, kila mara alikuwa akijiuliza swali moja tu
"Sijui ameniona nilivyo!!"
Na kila alipojiuliza swali hilo alijisikia vibaya sana, alitamani wakati urudishwe nyuma kisha yeye akutane na yule kijana kwa namna nyingine lakini isiwe kama ilivyokuwa.
Aliwaza sana Sabrina bila ya kupata jibu ila mwisho wa siku aliamua kufanya kama hajawahi kukutana na yule kijana na wala hajaona alichoona ili aweze kutuliza moyo wake wenye mawazo.
Sabrina akiwa chumbani kwake na mawazo, akaitwa na mama yake na kuambiwa kuwa anahitajika nyumbani kwa Sakina.
Hivyobasi Sabrina akajiandaa na kwenda nyumbani kwa Sakina ambako palikuwa sio mbali sana kutoka kwao, na nyumba hiyo waliuziwa na baba wa Sabrina ambaye ni bwana Deo.
Sakina alishukuru kwa Sabrina kuitikia wito wake,
"Jambo nililokuitia hapa Sabrina ni moja tu kama jingine likiongezeka basi ni ziada"
"Jambo gani hilo?"
"Nakuomba uzungumze na mwanangu Jeff, nahitaji kumpeleka shule ya bweni ili asome vizuri lakini hataki. Nakuomba ujaribu kumshawishi ili akubali, tafadhari Sabrina nakuomba"
Sabrina akacheka kidogo, kisha akamuuliza Sakina
"Ikiwa mama yake mzazi kakukatalia je kwangu atakubali?"
"Mwanangu anapatana sana na wewe Sabrina, halafu anakusikiliza sana najua kwa vyovyote vile atakubali tu kwako"
"Basi ngoja nikajaribu"
Sakina akafurahi sana, kisha Sabrina akamfata Jeff ili aweze kumshawishi juu ya hilo.
Mtoto huyu Jeff alimpenda sana Sabrina na hakuna jambo ambalo aliambiwa na Sabrina halafu akakataa ndiomana mama yake aliona kuwa Sabrina ndio mtu pekee wa kumshawishi mwanae.
Sabrina aliongea na Jeff halafu mwisho wa siku mtoto huyu akakubali kwenda hiyo shule aliyotafutiwa na mama yake.
Sabrina akaenda kumueleza Sakina ambapo naye alifurahi sana, kisha akamuuliza
"Umewezaje kumshawishi?"
"Nimemwambia nitakuwa namtembelea mara kwa mara"
Sakina akacheka na kusema,
"Yani mwanangu huyu mmh! Tena shida yake ni akuone tu ndio aridhike"
"Tena amesema huko shule nimpeleke mie"
"Sasa itakuwaje?"
"Usijali nitampeleka"
Sakina akafurahi zaidi na kumshukuru sana Sabrina kwa kumsaidia kwa hilo.
Siku waliyopanga kumpeleka mtoto huyo shuleni, Sabrina alijiandaa na kumuaga mama yake.
"Unajua Sabrina huwa unanishangaza sana mwanangu, yani huyo mtoto majukumu yote juu yako halafu unajisikia raha tu!"
"Jamani mama!!"
"Jamani nini? Nenda zako huko usije kusema nimekuzuia bure"
"Haya mama nashukuru"
Sabrina akaondoka na kumfata Jeff kisha safari ya kuelekea shule ikaanza.
Siku hiyo Jeff aliongea maneno mengi sana kwa Sabrina na kumfanya Sabrina ashangae yale maneno ya Jeff ila alielewa wazi kuwa mtoto yule aliongea yote yale kutokana na mambo aliyoyaona.
"Anti, mimi nikiwa mkubwa nitaoa mke mzuri sana ila sitathubutu kumpiga mke wangu wala kumtesa. Sitaki alie kama mama"
Sabrina huruma ikamjaa kwa maneno hayo,
"Usemayo yawe ya kweli mtoto mzuri, usije badae ukabadilika"
"Utaniona tu anti, nampenda
sana mama yangu. Sipendi alie na ndiomana nilikuwa sitaki kuja hii shule ya mbali ila kwavile umenihakikishia kuwa mama hatalia tena ndiomana nikakubali, ila uwe unakuja kweli kuniona huko shuleni"
"Usijali Jeff"
Sabrina hakupendezwa pia na tabia aliyokuwa nayo Juma, ilimfanya hata achukie wanaume kwaajili ya tabia hiyo na akajua wazi hata Sakina kuamua kwake kumpeleka mtoto wake shule ya bweni ni kutokana kwamba hakupenda kuona mwanae akiyaona yale mambo ya aibu kila siku.
Sabrina akamuhurumia sana mtoto wao huyu mdogo aliyeonekana kuongea kwa uchungu sana na kuumizwa kwa matendo ya baba yake, hivyo basi Sabrina alijiapia kufanya chochote awezacho ili kudhibiti tabia ya Juma haswa ile tabia ya kumpiga mke wake.
Sabrina alifika shuleni na kumkabidhi Jeff kwa walimu wake kisha akamuaga ili aanze safari ya kurudi
"Bye Anti"
"Bye Jeff"
"Nakupenda Anti"
"Nakupenda Jeff"
Kisha akampungia mkono na kuondoka huku akili yake inawaza kitu cha kufanya ili kuikomesha tabia ya Juma.
Akiwa njiani akamuona mtu mbele yake ambapo mawazo yake yaliwaza kuwa kuna mahali amewahi kuonana na mtu huyo ila hakuweza kukumbuka kuwa ni wapi alionana nae.
Ila wakati anawaza hayo, yule mtu naye alimfata na kuanza kumsalimia
"Habari yako dada!"
"Nzuri tu habari!"
"Nzuri, naitwa Francis. Vipi mwenzangu waitwa nani?"
Sabrina akajiuliza kimoyomoyo, "nimekuuliza kwani!"
Kisha akamjibu,
"Naitwa Sabrina"
"Nashukuru kukufahamu dada yangu, unakumbuka siku ile tuliyoonana kwa mara ya kwanza pale stendi!!"
Kisha yule kijana akatoa kapelo aliyokuwa ameivaa kichwani na kumfanya Sabrina kumbukumbu zimjie kichwani na kukumbuka kuwa ni yule kijana aliyekutana nae siku ile aliyoenda kichakani kujisaidia.
Aibu ikamjaa Sabrina na kumfanya aangalie chini kwani hakutegemea tena kukutana na yule kijana.
Sabrina alikuwa kimya kabisa na kumfanya yule kijana ndio aendeleze maongezi
"Vipi dada unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri"
"Basi itakuwa vizuri kama tukipeana mawasiliano"
Sabrina akaona ampatie tu hayo mawasiliano ili aende zake kuliko kuendelea kumpa wasiwasi wa moyo mahali hapo.
Kisha akamuaga na kuendelea na safari ya kurudi kwao, ila mawazo yake sasa yalihama kutoka kitu cha kumfanyia Juma ili amkomeshe kuja kwa huyu kijana alikutana naye tena kwani taswira ya sura yake ilibaki kwenye mawazo ya Sabrina.
Alihisi kabisa kitu tofauti kati yake na yule kijana, kwahiyo akajikuta safari nzima akimuwaza yule kijana hadi wakati anapanda kwenye daladala, bado mawazo yake yalikuwa ni kwa yule kijana tu na si vinginevyo.
Alipokaribia maeneo ya kwao alimuona Juma akitokea kwenye nyumba fulani huku ameongozana na mwanamke ambaye hakumjua ni nani ila kwa mawazo yake ya haraka haraka alihisi kuwa huyo mwanamke ndiye anayempa kiburi Juma na kumfanya asirudi kwake na anaporudi agombane na mke wake.
Sabrina akatulia pembeni ili kuwaona wanapoelekea, ila walifika mahali wakasimama na kukumbatiana kama ishara ya kuagana, mambo yote hayo Sabrina alikuwa akiyashuhudia tu pale alipokuwa.
Kisha Juma akaondoka zake na yule mwanamke akawa anarudi nyumbani kwake .
Sabrina sasa ikawa kama wale watu wanaonunua ugomvi tena ugomvi usiowahusu kabisa kwani alimfata yule mwanamke hadi nyumbani kwake tena bila hodi wala karibu akaingia ndani.
"Kheee mbona umeingia hivyo!! Kuna kheri kweli hapa"
"Hakuna kheri"
"Kheee, umekuja kwa shari?"
"Ndio"
"Haya niambie hiyo shari yako"
"Kwanini unatembea na mume wa mtu?"
"Ni mume wako wewe?"
"Hapana"
"Sasa wewe tatizo lako nini? Pilipili iko shamba wewe inakuwasha huku loh! Tena nitolee balaa mtoto wa kike nisije nikakuharibu bure"
"Thubutuuu! Jaribu uone cha mtemakuni"
Yule mama alimuangalia Sabrina kwa hasira sana kwani alikuwa ni mdogo sana kwake na angeweza kumfanya chochote atakacho ila aliona wazi kuwa atamuumiza binti huyo, wakati huo Sabrina naye kajitunisha mbele ya yule mama kamavile ni binti mwenye nguvu sana tena anayejiamini.
"Ila wewe mtoto dawa yako ni ndogo sana na nitakukomesha nakwambia"
"Unikomeshe kwa lipi!! Huniwezi nakwambia. Tena uachane na huyo mume wa mtu"
Kisha akasogea mezani kwa yule mama na kuchukua glasi iliyokuwepo juu ya meza na kuibwaga chini, yule mama akataka kumfata ila Sabrina akashika moja ya chupa iliyovunjika na kumtishia huku akielekea nje
"Wewe mtoto wewe! Umejifanya mjanja eeeh! Nitakukomesha, najua pa kukupata na cha kukufanya. Utajuta kunifahamu wewe mtoto"
Sabrina hakujali kitu chochote zaidi ya kuondoka, na safari yake ya kwanza haikuwa tena nyumbani kwao bali alienda moja kwa moja kwa Sakina.
Alimkuta Sakina akiwa na mawazo sana kama kawaida yake ila alipomuona Sabrina alifurahi
"Asante Sabrina kwa kunipelekea mwanangu shule"
"Usijali kuhusu hilo dada yangu, nina habari nyingine hapa"
"Ipi hiyo?"
Sabrina akaanza kumsimulia Sakina kile alichokifanya kwa yule mwanamke huku akijua kwamba Sakina atafurahishwa na zile khabari ila ilikuwa kinyume na matarajio yake.
"Nimemkomesha yule mwanamke dada"
"Mungu wangu Sabrina kwanini umefanya hivyo?"
"Basi akawa anajitamba eti atanikomesha mimi, nikamwambia thubutu yake! Nimemchamba hadi amekoma"
Sakina alisikitika sana
"Jamani Sabrina jamani"
"Kwani nini dada?"
"Yule mwanamke ni khatari Sabrina, ninapokwambia khatari ni khatari kweli. Mtaa mzima huu wanamuogopa jamani halafu wewe mmmh!! Hadi naogopa hapa"
"Unaogopa nini sasa?"
"Yule mwanamke ni mshirikina, yani ni mchawi hakuna mfano. Mtaa mzima wanamuogopa, hakuna anayeweza hata kumwambia chochote. Sabrina umeharibu mdogo wangu, nakuomba uende ukamuombe msamaha tafadhari"
Sabrina akanywea muda huo huo na kumfanya akose raha gafla.
"Nitaanzaje kumuomba msamaha sasa?"
"Fanya vyovyote Sabrina ila nenda ukamuombe msamaha tafadhari, sitaki matatizo mie Sabrina. Yale ya zamani yamepita, sitaki kuzua mengine. Usijali kuhusu baba Jeff atarudi mwenyewe kwangu wala yule mwanamke hawezi kunifanya mimi kitu chochote, mie nimeaga kwetu mdogo wangu. Ila wewe umeenda mwenyewe kuyafata, tafadhari rudi ukamuombe msamaha"
Sabrina akajifikiria sana, mwisho wa siku akaamua kuwa mpole na kwenda tena kwa yule mwanamke ili akamuombe msamaha.
Alipofika alimkuta yule mwanamke akifagia vile vipande vya chupa kutokana na zile glasi ambazo Sabrina alivunja.
Kwanza kabisa Sabrina alishangaa kuona anafagia muda huo sababu ni muda umepita tayari tangia azivunje, ila hayo hayakumuhusu sana kwahiyo akaamua kufanya kilichompeleka
"Samahani mama"
"Nilijua tu utarudi"
"Naomba unisamehe"
"Ushachelewa tayari, mdomo wako umekuponza rudi kwenu ukajionee kwa macho"
"Naomba unisamehe tafadhari!"
"Nimekwambia umeshachelewa"
Kisha akaingia ndani kwake na kufunga mlango.
Sabrina aliondoka kwa unyonge sana eneo hilo.
Alielekea moja kwa moja nyumbani kwao huku mawazo mengi yakiwa yamemtawala kichwani.
Akaingia ndani na kumuita mama yake, ambaye alitoka chumbani akiwa amechoka sana na moja kwa moja alimuuliza swali moja tu mtoto wake
"Mwanangu Sabrina kwanini unanifanyia hivi?"
"Nimekufanyia nini mama?"
Muda huo huo mama yake akaanguka na kuanza kutokwa na damu puani na mdomoni.
Alielekea moja kwa moja nyumbani kwao huku
mawazo mengi yakiwa yamemtawala kichwani.
Akaingia ndani na kumuita mama yake, ambaye
alitoka chumbani akiwa amechoka sana na moja kwa
moja alimuuliza swali moja tu mtoto wake
"Mwanangu Sabrina kwanini unanifanyia hivi?"
"Nimekufanyia nini mama?"
Muda huo huo mama yake akaanguka na kuanza
kutokwa na damu puani na mdomoni.
Uoga ukamshika Sabrina, akatamani kupiga kelele ila moyo wake ukasita kufanya hivyo.
Alijikuta akichanganyikiwa kwakweli ila muda huo huo likamjia wazo la kumpigia simu shangazi yake kwanza na kumueleza kuhusu mama yake
"Kwani umemfanyeje hadi imekuwa hivyo?"
Ikabidi Sabrina amuelezee shangazi yake hali halisi ilivyokuwa
"Nimekuelewa sasa,ila nakuomba utumie ujasiri wako. Usipige kelele wala usifanye chochote, mie nakuja huko. Umenielewa!"
Sabrina alimuitikia shangazi yake na kutulia ndani huku akimngoja aje, wakati huo moyo wake umegubikwa na mawazo ya kila aina.
Alitamani hata akamuite Sakina, ila aliamua kufata ushauri wa shangazi yake na kutulia pale ndani.
Hali ya mama yake ndiyo iliyomfanya azidi kutetemeka, alitamani kufanya kitu chochote cha kumsaidia mama yake ila maneno ya shangazi yake bado yalimrudia kuwa asifanye kitu.
Baada ya muda kidogo akapigiwa simu na shangazi yake,
"Haya toka humo ndani kwenu, rudisha mlango kama ulivyoukuta mwanzo halafu njoo kama unakuja stendi ili tukutane katikati halafu ndio tutarudi wote hapo nyumbani. Fanya kama ninavyokwambia tena upesi"
Sabrina akashangaa kuwa kwanini amfate na wakutane njiani wakati huyo shangazi yake anakuja huku nyumbani kwao? Ila alifanya kama alivyoambiwa na shangazi yake kisha akatoka na kuanza kumfata ili wakutane njiani.
Walikutana njiani kweli, Sabrina akatamani alie mbele ya shangazi yake wajina ila shangazi mtu alikuwa na sura kavu sana.
Kabla hata hawajaongea chochote, alitokea yule mwanamke toka upande mwingine na kujikuta akiwashangaa Sabrina na shangazi yake na kwa bahati mbaya akajikwaa na kuanguka.
Kitendo hicho kilimchekesha shangazi wa Sabrina na kujikuta akicheka sana.
Sabrina akamuangalia shangazi yake na kumwambia
"Usicheke shangazi"
"Usijali wajina, haya turudi nyumbani huko"
Yani muda huo huyu shangazi wa Sabrina alikuwa amechangamka sana na hakuwa na mashaka yoyote, kisha akamwambia Sabrina
"Ondoa hofu yote inayokutawala, uliyoyaona kuwa yalimtokea mama yako fanya kamavile hukuyaona. Usiweke kwenye akili yako, na tukifika utulie usifanye hizo papara zako"
Sabrina alikuwa akishangazwa tu na maneno ya shangazi yake muda wote.
Walipofika waliingia ndani, jambo la kwanza ambalo Sabrina alilifanya ni kumuangalia mama yake ambaye hakumuona tena pale chini na kumfanya uoga uzidi kumtawala sasa kuwa mama yake amepelekwa wapi.
Akataka kumuuliza shangazi yake ila shangazi mtu akamuonyesha ishara ya kimya na badala yake, Sabrina alijikuta akiulizwa maswali mengine kabisa na shangazi yake
"Nipe khabari za chuo"
Sabrina alimuangalia tu shangazi yake bila hata ya kumjibu kitu chochote.
Muda huo huo, bi. Joyce ambaye ni mama wa Sabrina alitokea chumbani huku akiwa anajinyoosha nyoosha na alionekana kuchoka sana.
Na moja kwa moja aliushangaa uwepo wa wifi yake
"Kheee wifi umekuja muda gani? Na wewe Sabrina kumbe umerudi!"
Sabrina alikuwa akimshangaa tu mama yake kwani ile hali hakuielewa kwakweli, shangazi mtu ndiye aliyeweza kujibishana na mama wa Sabrina hata Joy aliushangaa ukimya wa gafla kwa mtoto wake
"Una matatiz o gani leo! Mbona umepooza hivyo mwanangu?"
"Hakuna kitu mama"
"Haya kamletee shangazi yako juisi"
"Hapana hata asihangaike"
Wakaendelea kuongea maongezi mengine, ndipo Joy alipoanza kuwaeleza kuwa ameota ndoto mbaya sana
"Yani hizi ndoto za jioni hazifai jamani, eti nimeota kuwa nimekufa halafu watu wanalia kweli. Basi mkaanza kupanga mipango ya mazishi, eti hapo hapo nikashtuka kutoka usingizini. Basi hapa nimechokaje jamani!"
Sabrina aliendelea tu kumuangalia mama yake kwani yeye bado aliona ni mambo ya ajabu na kuzidi kujiuliza kuwa shangazi yake ana mahusiano yapi na mambo hayo? Alihisi kuwa huenda hata shangazi yake naye akawa mchawi kwamaana hakuelewa kabisa yale mambo ambayo shangazi yake aliyafanya, hivyo kujikuta akiwa na maswali mengi sana bila ya majibu kamili ya maswali yale.
Akajiandaa kumuuliza maswali yake kwavile alikuwa akiongea na mama yake akaamua kumvizia atakapomaliza kuongea na mama yake.
Muda ulifika na Shangazi wa Sabrina akajitoa kumsindikiza huku akitarajia kumuuliza yale maswali lakini mama yake aliambatana naye katika kumsindikiza na kumfanya Sabrina ashindwe tena kumuuliza maswali shangazi yake kwahiyo akajipanga kufanya hivyo atakapoenda kumtembelea.
Waliporudi nyumba ilikuwa kawaida kabisa yani kamavile hakuna kilichotokea mahali hapo na maisha yakaendelea kama kawaida.
Siku zilipita bila Sabrina kupata mawasiliano yoyote toka kwa yule kijana aliyempa namba zake, na alipofikiria vizuri zaidi akagundua kuwa kuna namba moja alikosea wakati anampa yule kijana namba
"Ila ndio basi tena sababu sitaweza kuonana nae tena"
Aliishia kujisemea hayo huku akijiandaa kwenda nyumbani kwa shangazi yake kwaajili ya maswali yake ambayo alishindwa kumuuliza siku ile alipokuwa kwao.
Sabrina aliianza safari hadi kwa shangazi yake, na alimkuta akiendelea na shughuli zake zingine
"Nimekuja shangazi, nina maswali yangu nataka unijibu"
"Niulize tu hayo maswali"
"Unajuaje hayo mambo ya kichawi?"
"Ni historia ndefu sana, ipo siku nitakuelezea kwahiyo usijali sana."
Sabrina akakosa majibu aliyoyatarajia hivyobasi akajiandaa kuondoka ili aweze kurudi kwao.
Akiwa njiani alimsikia mtu akimuita kwa jina lake, akageuka nyuma na kumuona yule kijana na hapa ndipo aliposhangaa kwani anajikuta akikutana na huyu katika maeneo ambayo hakuyatarajia.
"Vipi dada yangu za tangu siku ile"
"Nzuri tu, mambo"
"Poa, mbona ukanipa namba ambayo haipatikani!!"
Sabrina akaanza kujitetea pale kwa yule kijana ili asionekane kama ana mambo ya kiswahili, kisha akampa tena namba yake ambayo alikuwa na uhakika nayo sasa
"Nina ujumbe wako Sabrina, nitakutumia"
Sabrina alijiuliza kuwa ni ujumbe gani! Wakati mwingine mawazo yake yalimrudisha siku ile ya kwanza aliyokutana na yule kijana na kujikuta akijiuliza
"Au aliniona nilivyo!!"
Yule kijana alimsikia na kumuuliza kwa makini
"Ulivyo nini?"
"Hamna kitu, kuna jambo nimekumbuka tu hapa"
"Basi hakuna tatizo, nitakutafuta Sabrina"
Kisha wakaagana na kuondoka.
Alipofika nyumbani kwao akajikuta akijiuliza kuhusu yule kijana tu kama alimuona alivyo au la.
Ila kila alipoyawaza hayo alikosa raha.
Kuna kitu kilimsumbua Sabrina kwenye maumbile yake, kitu hicho huwa kinamtokea na kupotea na ndiomana alipiga kelele kule porini kwavile ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kukiona ingawa hakujua kama wale wabakaji walikiona na ndiomana wakakimbia ile siku waliyotaka kumfanyia vibaya.
Alijiuliza sana kuwa kinatokana na nini ila hakujua chochote na hakujua kuwa ni kwanini kipo kwenye mwili wake yeye.
Alitamani kumwambia mama yake kuhusu jambo hilo ila aliogopa huku akihisi kuwa pengine mama yake atamfikiria vibaya.
Kwakweli hakuona wa kumwambia kuhusu hilo tatizo lake na ndioma na alijisikia vibaya kila alipohisi kuwa yule kijana alimuona alivyo.
Wakati anawaza hayo, simu yake ikaita
"Hallow, nani mwenzangu!"
"Francis anaongea hapa"
"Francis!! Francis yupi?"
Ikabidi aanze kumueleza walipokutana,
"Ooh nimekukumbuka tayari, eeh nipe huo ujumbe wangu"
"Nakupenda Sabrina"
Sabrina alijihisi kama amepigwa shoti ya umeme kwa lile neno moja tu aliloambiwa na yule kijana na kujikuta akikata ile simu na kuanza kujiuliza
"Atanipendaje mimi wakati kaniona nilivyo!! Au ananitania ila mimi nimechukulia kwa maana nyingine?"
Ile simu yake ikaita tena,
"Mbona umenikatia simu Sabrina?"
Sabrina hakuwa na jibu zaidi ya kukaa kimya tu kwani hakuelewa amjibu kitu gani.
"Nakupenda Sabrina, tena nakupenda sana"
"Uliniona nilivyo?"
"Haijalishi Sabrina, mimi nakupenda kwa vyovyote vile ulivyo"
Sabrina akajipa jibu la moja kwa moja kuwa ameonekana jinsi alivyo na kumfanya ajisikie vibaya zaidi, akamuaga yule kijana kwenye simu na kujikalia kitandani kwake huku machozi yakimtoka kuwa kwanini ameonekana vile alivyo wakati hakutaka kuonekana vile kwa mtu yoyote yule. Akajisikia vibaya sana ila hakuweza kufanya chochote kwani tayari alijua kuwa ameshaonekana na mtu mwingine.
Akiwa nyumbani kwao ametulia, alikuja Sakina kuwatembelea pale nyumbani na nia yake ilikuwa ni moja tu nayo ni kuzungumza na Sabrina.
"Eti mdogo wangu Sabrina una matatizo gani kwenye maumbile yako?"
Leo Sakina alijitoa muhanga na kuamua kumuuliza Sabrina ila Sabrina alishangazwa zaidi kuona kuwa hata Sakina anajua kasoro alizokuwa nazo, na kumfanya azidi kujisikia vibaya zaidi.
"Sina tatizo lolote"
"Niambie ukweli Sabrina, nipo tayari kukusaidia"
"Utanisaidia kweli?"
"Ndio nitakusaidia, ukweli wako ndio utakaokuweka huru"
"Ni kweli nina matatizo dada tena makubwa tu"
"Pole sana na usijali kitu nitakusaidia. Ngoja niongee na mtu halaf u nitakupa majibu yanayoeleweka mdogo wangu hata usijali"
"Ila usimwambie mama"
"Usijali sitamwambia chochote"
Sabrina akakubaliana na huyu Sakina jinsi atakavyoweza kusaidika kutokana na tatizo alilokuwa nalo kwenye maumbile yake.
Wakapanga siku ya kupelekana mahali ambako ataenda kupata msaada wa tatizo alilokuwa nalo.
Siku hiyo wakajiandaa kisha Sakina akamfata Sabrina na kuelekea kwa huyo mtu waliyekubaliana nae.
Ilikuwa ni safari ya mbali kiasi, ambayo ilichukua takribani masaa matano kufika huko.
Walipofika walikaribishwa na bibi mmoja aliyekuwa mzee sana ila alisifika kwa kujua dawa za kila aina na kila mtu aliyemtibia ilikuwa lazima apone kutokana na dawa zake kuwa kali na zenye nguvu.
Wakamueleza yule bibi tatizo la Sabrina, naye akawapa imani kuwa lile tatizo ni dogo tena ni la kawaida tu wala haliwezi kuwa kikwazo kwake na lazima atamsaidia hadi atapona kabisa.
Kwakweli hilo lilikuwa wazo la matumaini kwa Sabrina.
Yule bibi alichuma dawa na kumchanja Sabrina kwenye kiuno, halafu nyingine alimfunga kiunoni ikawa kama shanga kisha akamwambia.
"Kesho mje ili nikutoe hiyo kamba hapo kiunoni, msisahau kuja kwakuwa hiyo kamba natakiwa nikutoe mimi mwenyewe. Tena mje mapema"
"Sawa tumekuelewa"
Sakina naye akauliza,
"Kwahiyo baada ya hapo atakuwa amepona?"
"Ndio, atakuwa amepona. Yani hiyo kamba ndio itabeba huo ugonjwa wake, na itatakiwa itolewe kesho saa saba mchana tena itolewe na mimi mwenyewe niliyoifunga ndiomana nawaambia kuwa muwahi kwamaana isipotolewa madhara yake ni makubwa sana"
Wakakubaliana na yule bibi kisha wakamshukuru na kuanza safari ya kurudi nyumbani.
Wakiwa kwenye daladala, Sabrina akasikia wimbo ukiimba kwenye redio ya mule kwenye daladala na maneno yake yakamchoma kwakweli. Akausikiliza kwa makini, ulisema
"Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa ni kinga yake....."
Sabrina alijiuliza kuwa kwanini yale maneno yamemchoma sana! Ila aliamua kuyapuuzia na kujifanya kamavile hakuyasikia.
Walifika nyumbani na giza kabisa huku wakijiandaa kwaajili ya safari ya kesho yake.
Ila leo Sabrina hakuulizwa chochote na mama yake kuhusu alipokuwa, ila aliona ni vyema kutokuulizwa kwakuwa mama yake ana asili ya mdomo sana.
Kesho yake ilipofika, asubuhi na mapema akapitiwa na Sakina na kuianza safari yao ya kuelekea kwa yule bibi wa kuwatibia huku wakiwa na imani kuwa lile tatizo linaenda kuisha leo.
Wakiwa njiani lile basi walilopanda likapata pancha, ikabidi wasubiri ila Sabrina alichukia sana kwani aliona wanacheleshwa tu, ingawa konda aligoma kuwarudishia nauli zao ili wasiondoke ila wao hawakujali na wakaenda kupanda gari jingine.
Walipokaribia kufika ile gari nayo ikapata pancha na kufanya wajiulize
"Kuna tatizo gani huko?"
"Hadi nimeanza kuingiwa na uoga dada"
"Ngoja tuchukue bodaboda basi"
Wakaamua kuchukua bodaboda ili iwapeleke kwa haraka.
Walipofika kwenye nyumba ya bibi walishangaa kukuta kimetawala kilio kwenye eneo lile.
Walipofika kwenye nyumba ya bibi, walishangaa kukuta kimetawala kilio kwenye eneo lile.
Wote wawili wakajikuta wakitazamana kwa mshangao, ikabidi Sakina aende kuulizia vizuri ili wajue kuna nini.
Alimfata binti mmoja na kumuuliza,
"Eti kuna nini hapa?"
"Bibi ametutoka"
"Eti nini!!"
Sakina alijihisi kuchanganyikiwa kwakweli,
"Hebu niambie vizuri, bibi madawa ndio amekufa?"
"Ndio amekufa leo saa nne asubuhi yani kila mmoja umuonaye hapa amechanganyikiwa na wala hatujui itakuwaje"
Sakina alinywea sana na kujikuta akifikiria mambo mengi bila ya majibu yanayojitosheleza.
Alihisi ni mkosi wa kujitakia wenyewe.
Akamuita Sabrina pembeni ili wajaribu kujadili cha kufanya kutokana na ile hali.
Sabrina akawa analia tu,
"Usilie Sabrina, ngoja tufikirie kitu cha kufanya kwa sasa"
"Tutafanya kitu gani wakati anayejua amekufa tayari"
Machozi hayakuacha kumtoka Sabrina huku akiwaza kuwa ataishije na atafanyaje ili aeleweke kwenye jamii.
"Usijali Sabrina, tutapata utatuzi tu wa swala hili kwahiyo usijali sana."
Wakakaa chini huku wakitafakari cha kufanya.
Wakamuona mwanamke flani akija pale kwa yule bibi ila baada ya kupewa taarifa za msiba alijitupa chini akijigalagaza huku akilia kilio kikubwa.
Wakaamua kumfata yule mwanamke na kuanza kumpooza
"Niacheni nilie jamani labda itapunguza uchungu nilionao, hata sijui nitafanya kitu gani mimi"
Yule mwanamke aliendelea kulia kwa uchungu sana huku akiendelea kusema
"Kuna dawa hapa ilitakiwa itolewe leo na huyu bibi na ikifika saa kumi na mbili kama haijatolewa basi nakuwa kichaa. Uwiiii jamani ukichaa unanikaribia jamani, nani atanisaidia mimi!"
Sabrina alimuangalia huyu mwanamke kwa huruma sana huku akijiuliza na yeye kuwa atapatwa na tatizo gani? Maana yeye hakuelezwa moja kwa moja kuwa ile dawa isipotolewa au ikitolewa na mtu mwingine, atapata matatizo gani?
Alitamani siku zirudi nyuma ili asikubali ushauri wa Sakina wa kuja kwa huyo bibi.
Sabrina alikuwa na mawazo sana na eneo lile watu walizidi kuongezeka huku wakilia na kujitupa tupa kwani kila mmoja alikuwa na tatizo lake na mtu pekee wa kuwasaidia ni huyo bibi aliyekufa.
Kwakweli kila mmoja ile hali ilimuwia vigumu sana kwani hakuna aliyejua cha kufanya kwa wakati huo kila mmoja alikuwa njiapanda na mawazo yake.
Sakina akamuomba Sabrina kuwa warudi nyumbani ili wakafikirie cha kufanya.
Sabrina akagoma kwani alitamani hata alale hapo hapo ili ajue mbivu na mbichi, ila Sakina akatumi a uwezo wake wote wa kushawishi hadi Sabrina alipokubali kuwa warudi nyumbani.
Nao wakaianza safari ya kurudi nyumbani.
Sabrina alipofika kwao alikimbilia chumbani kwake huku akijiangalia ile kamba kiunoni na kujikuta akilia sana na kujiona kuwa ni mjinga na mpumbavu kwa kufanya vitu bila kufikiria.
Wakati analia, mama yake akamuita ila Sabrina hakuitika na kumfanya mama yake amfate kule alipo ili ajue kuwa mwanae ana matatizo gani
"Ulikuwa wapi Sabrina? Na huo mchezo wa kuondoka bila kuaga umeuanza lini?"
Sabrina alikuwa akilia tu na kumfanya mama yake atake kujua kitu kinachomliza mwanae.
"Niambie una tatizo gani kwani?"
"Sijui mama"
"Hujui nini? Niambie mwanangu, mimi ndio mama yako ninayeweza kukusaidia"
Lakini Sabrina hakuweza kumwambia chochote mama yake na badala yake akadai kuwa kichwa kinamuuma kwahiyo anahitaji muda wa kupumzika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama yake hakuwa na tatizo, kisha akamruhusu mwanae apumzike halafu yeye akaenda kuendelea na shughuli zake zingine.
Sabrina hakupata usingizi hadi panakucha na palivyokucha tu akajihimu tena na kuanza safari ya kwenda kwa yule bibi tena bila ya kumwambia Sakina wala nani.
Alifika mapema sana kwa yule bibi na kukuta msiba ndio umenoga vizuri siku hiyo kwani mikeka ilitandikwa na maturubai ya kutosha yaliwekwa.
Sabrina akaamini vizuri sasa kuwa ni kweli yule bibi amekufa ila je hitimisho la yeye na ile kamba kiunoni ni nini?
Akajaribu kufatilia wagonjwa baadhi waliokuwa wakihudumiwa na yule bibi, akawaona wengine wakiwa wamezimia, wengine hawajitambui yani kila mmoja alikuwa na hali yake ya kusikitisha.
Akamkuta yule mwanamke wa jana akiwa anaongea peke yake kwamaana kwamba kichaa ndio kimeshampata tayari.
Sabrina alihisi kuchanganyikiwa kwani hapakuwa na msaada wowote wa kusaidiwa wagonjwa wale wa bibi.
Mpaka muda wa mazishi unafika bado Sabrina alikuwa eneo lile lile hadi walipoenda kuzika, akatazama kwa makini sana kaburi alilozikwa bibi yule huku mawazo yakimtawala kichwa chake.
Ila hakuwa na la kufanya zaidi ya kuamua kurudi kwao ingawa bado alikuwa akisita kwani hakuelewa kuwa ni kwa jinsi gani angeweza kumueleza mama yake na akamuelewa juu ya hayo mambo ambayo mama yake huwa anapingana nayo kila siku.
Wakati anarudi kwao alifika mahali na kukaa chini ya mti huku akitafakari cha kufanya.
Akiwa kwenye mawazo mazito, akatokea yule kijana ambaye huwa wanaonana mara kwa mara.
Akafika hadi pale alipo Sabrina na kumuuliza,
"Sabrina, mbona upo hivyo! Una matatizo gani mama? Niambie, pengine naweza nikakusaidia"
Sabrina akawaza sana kuwa je amwambie ukweli? Na je atamsaidia au atamtangaza? Akasita kumwambia ukweli, ila yule kijana alimuomba na kumsihi sana kuwa amwambie ukweli ulivyo.
Kwavile Sabrina maji yalishamfika shingoni aliamua kumueleza ukweli ili apate kupumua kidogo.
"Pole sana Sabrina, ila usijali kwani nitakuwa nawe bega kwa bega hadi pale tutakapopata ufumbuzi wa tatizo lako"
Kwavile muda ulikuwa umekwenda, yule kijana akaona kuwa ni vyema kama atamrudisha kwanza nyumbani halafu ndio harakati za kushughulika na hilo swala zianze.
Sabrina akakubali kurudi kwao, kisha yule kijana akamsindikiza Sabrina hadi kwao.
Akamkuta mama yake akiwa kavimba kwa hasira, tena bila hata ya salamu wala kuitikia salamu zao moja kwa moja alimuuliza swali Sabrina
"Unaweza kuniambia kuwa huyo kijana ni nani?"
"Ni rafiki yangu mama, anaitwa Francis"
"Haya wewe kijana nenda zako, na wewe Sabrina ingia ndani"
Yule kijana akaondoka kisha Sabrina akaingia ndani kwao, na kufuatwa na maswali kutoka kwa mama yake
"Unaweza kuniambia ulipokuwa?"
Sabrina alikaa kimya tu
"Hivi unatambua kwamba unatakiwa kuwa chuoni wiki ijayo?"
Sabrina akaitikia kwa kutikisha kichwa
"Kwanini unape nda kunivuruga wewe mtoto jamani! Kwanini lakini?"
"Nisamehe mama"
"Kwakweli sipendezwi na tabia yako, nakwambia tena huo uchizi wako peleka huko kwa shangazi yako mwenye jina lako. Sipendi matatizo mtoto wa kike, usinivuruge kabisa. Kaka zako wametulia zao huko ila wewe kichwa maji, sitaki ujinga"
Aliong ea kwa hasira sana na kuondoka zake.
Sabrina alitulia kimya kwani bado mambo yake yalimsumbua.
Usiku aliongea sana na yule rafiki yake kwenye simu na kukubaliana na ushauri aliopewa. Akaona ni vyema aanze kuufanyia kazi na wakapanga kesho yake kutimiza kile walichoongea kwenye simu.
Sabrina akamshukuru sana kwa kumfariji na kumtia moyo.
Kulipokucha, Sabrina akajiandaa asubuhi na mapema kama alivyopanga na rafiki yake kisha akamuaga mama yake kuwa anaenda kwa shangazi yake.
Aliondoka moja kwa moja na kwenda kukutana na yule rafiki kisha wakaianza safari ambayo waliipanga usiku wakati wanaongea kwenye simu.
Safari yenyewe ilikuwa ni moja kwa moja kwenye makaburi, na lengo lao ni kwenda kwenye kaburi ambalo yule bibi alizikwa.
Nao wakaenda kama walivyopanga, kisha Sabrina akaanza kumuomba yule bibi juu ya ile kamba ambayo amefungwa kiunoni.
Wakati akiomba hayo, matone ya mvua yakawaangukia na kuhisi kuwa mvua itaanza muda wowote katika eneo lile.
Francis akamuomba Sabrina kuwa waondoke ila Sabrina hakutaka kutokana kwamba alihitaji kwanza kuona ile kamba ikitoka hata kama kwa miujiza ila iweze kutoka.
Mvua ya ukweli ikaanza sasa na kuwafanya waweze kushtuka kwani eneo lenyewe halikuwa na mahali popote pa kujikinga na mvua ya aina yoyote ile.
Ikabidi Francis amshike mkono Sabrina na kuanza kukimbia ila mvua nayo ilikazana na kuwafanya waloe chapachapa.
Kwa bahati nzuri walipata kibanda na kujibanza hapo, Francis alimkumbatia vizuri sana Sabrina na kumfanya ajisikie vizuri hata akasahau tatizo linalomkabili kwa muda huo.
Hadi pale mvua ilipoisha walianza kukauka pole pole, Sabrina alijihisi wazi kuwa anampenda huyu kijana tena anampenda sana ila kwavile huyu kijana alishamwambia kuwa anampenda, akawa anangoja siku atakayomwambia tena kuwa anampenda naye ndio amjibu kwamba anampenda pia.
Ila huyu kijana alikuwa kimya tu kwa wakati huu kwani hakuwaza kabisa swala la kumsumbua tena Sabrina kwa kumtongoza wakati bado anamuona kuwa ana matatizo yanayomkabili kwahiyo kumwambia habari za mapenzi ni kama kumuongezea matatizo tu.
Walitoka eneo lile huku wakiendelea na safari ya kurudi nyumbani.
Francis alimpeleka Sabrina hadi nyumbani kwao kisha akamuaga na kuondoka, ila Sabrina alihitaji kuagwa zaidi ya ile ya kwaheri sema yule Francis alishaondoka kwani alihofia kuonana tena na mama wa Sabrina aliyemfokea sana jana yake.
Sabrina aliingia ndani ila mawazo yote yalikuwa ni juu ya Francis hata akasahau matatizo yanayomkabili kwa kipindi hicho.
Alichokuwa anawaza yeye ni kwanini huyu Francis hamwambii tena kuwa anampenda?
"Au kanichukia kutokana na hizi kasoro nilizonazo? Ila mbona bado ananisaidia sana! Au ananihurumia tu ili nisijisikie vibaya!!"
Moyo wake ulishampenda kijana huyo na alishangaa kuwa ni kwanini hamwambii tena kuwa anampenda.
Siku hiyo alilala vizuri sana hadi kunakucha kwani mawazo yake yote yalikuwa ni kwa rafiki yake mpenzi aliyejiona wazi kuwa anampenda tena sana.
Kulipokucha, alimtumia ujumbe yule kijana ili kujua hali yake naye alimjibu kuwa yupo salama na hiyo ndio ikawa furaha kwake.
Akajiandaa na kwenda nyumbani kwa Sakina ili amweleze yaliyojiri wakati wa jana na juzi ambazo hawakuonana ila hakumkuta Sakina nyumbani kwake, na ile nyumba ilikuwa kimya sana na kuonyesha kwamba hapakuwa na mtu yeyote ndani yake.
Ikabidi ajitoe na kuanza kurudi kwao, ila wakati anageuka akagongana macho na yule mwanamke aliyewahi kumfanyia fujo nyumbani kwake, mwanamke anayesifika kwa uchawi mtaa mzima.
Yule mwanamke alimuangalia Sabrina kwa jicho kali sana kisha akamsonya na kumwambia
"Utakoma leo, lazima nikukomeshe"
Sabrina alimshangaa tu huyu mwanamke kwani hakumuelewa kuwa anazungumzia vitu gani wakati alijua kuwa yale yameshapita.
Yule mwanamke aliendelea kuongea
"Siku ile mlijifanya wajanja eti mmeniweza mimi, thubutu yenu! Hii namba mbaya na hakuna anayeiweza, leo nitakufunza adabu"
Halafu akaondoka na kumuacha Sabrina akiwa na maswali mengi bila majibu ila aliamua kuachana na hayo mambo na kuendelea na vitu vingine kisha akarudi nyumbani kwao na kufanya mambo mengine kama kawaida.
Usiku akaenda kulala, ila katikati ya usiku wa manane alihisi akitekenywa na ile kamba yake ya kiunoni na kumfanya aamke kwa nguvu na kuwasha taa bila hata kufikiri zaidi akamuona yule mwanamke wa mchana akiwa mtup u kabisa mbele yake.
Usiku akaenda kulala, ila katikati ya usiku wa manane
alihisi akitekenywa na ile kamba yake ya kiunoni na
kumfanya aamke kwa nguvu na kuwasha taa bila
hata kufikiri zaidi akamuona yule mwanamke wa
mchana akiwa mtup u kabisa mbele yake.
Sabrina akashtuka kumuona yule mwanamke ila pia yule mwanamke akashtuka kumuona Sabrina ameshtuka halafu wakatazamana kisha yule mwanamke akapotea.
Sabrina akapiga kelele huku akitoka chumbani kwake na kumuita mama yake ambapo mama yake alishtuka kwa hofu kubwa na kumfata mwanae ukizingatia kipindi hiko mumewe bwana Deo hakuwepo kwavile alisafiri.
Joy akamuuliza mwanae ni kitu gani naye akamueleza ilivyokuwa huku anatetemeka sana
"Usijali mwanangu, ngoja tuombe"
Joy akamshika mwanae na kuomba kisha akamwambia akalale bila uoga wala hofu kwavile haitatokea tena.
Sabrina alirudi kulala huku mawazo mengi yakiwa yameizunguka akili yake na kumfanya ashindwe kupata usingizi kabisa hadi palipokucha.
Asubuhi ilipofika, Joyce aliamua kumuuliza kwa makini mtoto wake
"Hivi yale ya usiku yalikuwa kweli au mauzauza yako tu mwanangu?"
"Kweli kabisa mama wala sio mauzauza, nimeona kwa macho yangu"
"Mmh umeanza matatizo kama ya shangazi yako nini? Mmh isiwe hivyo kwakweli tusije kukimbia nyumba bure"
"Kwani shangazi alikuwa na matatizo gani?"
"Ni historia ndefu sana ila cha msingi ni kuwa makini mwanangu haswaa na hao wanaume"
Alimaliza hivyo Joy na kwenda kuendelea na mambo yake mengine na kumfanya mwanae azidi kubakiwa na viulizo bila majibu ya kutosha.
Mchana wa siku hiyo Sabrina alitoka nyumbani kwao na kwenda kuonana na Francis, kisha akamueleza yale mambo yaliyomkuta usiku
"Pole sana Sabrina, ila usijali tutapata tu suluhisho la tatizo lako"
"Unadhani naweza kupata ufumbuzi?"
"Hata usijali"
Leo Sabrina akaamua kuvunja ukimya wa neno aliloambiwa na Francis kwa siku za mwanzoni kuwa anampenda ila kwavile hakupata kulisikia tena ikabidi aulize kwa namna nyingine
"Hivi Francis unanipenda kweli na matatizo yangu haya?"
Hakujua kama amempa urahisi sasa kijana huyo kuweza kuelezea hisia zake kwa upana zaidi
"Kwakweli nakupenda sana Sabrina, nangoja tu siku utakayosema ndio"
Sabrina akatabasamu na kufurahi sana moyoni mwake kuona kuwa kijana huyu ni kweli anampenda ila akavunga kujibu ndio kwa wakati huo ili kuonyesha kwamba ni binti mwenye msimamo.
Alipokuwa anarudi, moja kwa moja akapita nyumbani kwa Sakina ili kuona kama naye amerudi.
Alifurahi kumkuta kwani alikuwa na hamu ya kumueleza mambo yaliyojili usiku uliopita.
Sakina nae alifurahi kumuona Sabrina
"Afadhali umekuja mdogo wangu maana nina ujumbe mzito juu yako"
"Upi tena? Mbona wanitisha!"
"Usijali, ngoja nikikueleza ndio utaelewa
"
Sabrina akayaacha ya usiku na kuanza kumsikiliza Sakina
"Kamba hiyo mdogo wangu"
"Kamba gani?"
"Si hiyo ya kiunoni mwako"
"Imefanyaje dada? Umempata mtu wa kunitoa?"
"Mmmh nimpate wapi? Ila nilichokipata ni kuwa hiyo kamba yako ina mambo"
"Kivipi? Mbona sikuelewi dada?"
"Kamba hiyo inaonyesha wachawi"
Sabrina akashtuka na kumuangalia Sakina kwa makini kamavile mtu ambaye hajaelewa vizuri, Sakina akaendelea kuongea
"Unashangaa nini sasa? Ona mimacho ulivyoitoa! Hiyo kamba yako inaonyesha wachawi"
"Kivipi dada sijakuelewa"
"Yani mtu akija kukuchawia, lazima ushtuke na umuone sababu ya hiyo kamba"
Sabrina ikawa kama mtu aliyeelewa kitu fulani kisha akaanza kumueleza Sakina mambo yaliyomtokea usiku
"Umeona sasa eeh!! Yote ni sababu ya hiyo kamba, sasa mimi nitakufundisha kitu kisha ukifanyie kazi kwani ndio kinaweza kuwa uponyaji wako"
"Sawa, nimekuelewa dada. Wewe niambie tu ili niondokane na hili janga"
Sakina alimwambia Sabrina mambo ambayo hakupaswa kumwambia yeyote hata mama yake ili iwe rahisi kufanya kile anachoambiwa.
"Usijali dada, nakuahidi itakuwa ni siri yangu kwani sitamwambia yeyote yule. Nataka kupona dada yangu, nimeshachoka kuwa hivi mwenzio"
"Usijali, ukifatilia kwa makini utapona tu mdogo wangu"
Wakaongea mengi kisha Sabrina akaaga na kurudi kwao.
Moyo wa kijana Francis uliumia sana kwa kushindwa kupata jibu la uhakika kutoka kwa Sabrina na kumfanya ajiulize maswali mengi
"Au hanipendi jamani! Ila kama hanipendi ndio angependa kuwa karibu nami kiasi hiki!! Lazima nifanye kitu ili nimpate"
Alijiona akimpenda sana Sabrina, na lihitaji sana upendo wake bila kujali matatizo yake.
Sabrina alikuwa akijifikiria tu kwao juu ya yale mambo ambayo aliambiwa na Sakina kuhusu kamba yake ya kiunoni ila hakutaka kuitoa siri hiyo kwa mama yake ili aweze kufanikisha kile ambacho aliambiwa na Sakina kuwa kitaweza kumsaidia.
Hakutaka kumwambia mtu yeyote siri hiyo na kumfanya ashukuru kwa kutomkuta mama yake nyumbani kwa muda huo kwani angeweza kumgundua kwa yale mawazo aliyokuwa nayo siku hiyo.
Sabrina alikuwa akifikiria tu namna ya kukabiliana na kitu alichoambiwa na Sakina.
Joyce ambaye ni mama wa Sabrina akiwa njiani na yeye kwenye harakati za kurudi nyumbani kwake, akakutana na mmama wa makamo ambaye kwake angeweza kuwa hata mama yake.
Yule mmama alimsimamisha Joy njiani na kumsalimia kisha akamwambia
"Nina ujumbe kuhusu mwanao"
Joy akaguna na kuuliza kwa makini
"Mmmh ujumbe gani?"
"Kuhusu kijana anayempenda"
"Kijana anayempenda? Mmh kijana gani huyo? Yani kuna kijana mwanangu anampenda?"
"Yupo ndio ila mwambie mwanao, wake yupo atampata tu muda ukifika"
Yule mama akawa anaondoka, Joy akamfata na kumuuliza zaidi lakini hakujibiwa wala nini na kumfanya apatwe na mawazo huku akibaki na mshangao tu kuwa yule mama amewaza vitu gani hadi kumwambia vile. Ila hapakuwa na la kufanya zaidi ya yeye kuendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake tu.
Alimkuta mtoto wake akiwa ametulia tu na mawazo yake yakimsonga, akamuita kuzungumza nae bila ya kujua kwamba anampa mawazo juu ya mawazo kwani mwanae alishakuwa na mawazo tayari yanayomtatiza kwa siku hiyo
"Eti Sabrina una mwanaume?"
"Mwanaume? Mimi nina mwanaume! Nani kakwambia hayo maneno mama?"
"Wewe nijibu tu, una mwanaume?"
"Hapana mama, mi sina"
"Na yule kijana unayekujaga nae hapa?"
"Nani unamsema? Francis! Aaah yule ni rafiki yangu tu"
"Rafiki eeeh! Kuwa makini sana"
Kisha akaenda kuendelea na mambo mengine yaliyokuwepo na kumfanya Sabrina apatwe na wazo jipya na kujiuliza
"Kwanini mama kaniuliza hivyo? Au mimi sitakiwi kuwa na mwanaume jamani? Au muda wangu bado? Ila mimi ni mkubwa tayari na Francis nampenda, itabidi mapenzi yetu yawe siri ili mama asije akaleta longolongo bure"
Naye akaenda kufanya mambo yake mengine.
Usiku wa siku hiyo, aliongea mambo mengi sana kwenye simu na Francis na kujikuta wakikubaliana kwenye maongezi na kuwa wapenzi kwa urasmi kabisa.
Moyo wa Sabrina ulifurahi sana na kumfanya amuwaze tu huyo kijana kwa muda huo kwani aliona kamavile ameshatua mzigo kwa kumkubali na pia aliona moyo wake ukiwa umeshinda kwa kile kitendo cha yeye kuwa na mpenzi anayependana nae.
Alijiona ameshashinda kwenye swala la mapenzi, kilichobaki ni kamba yake ya kiunoni tu ambayo alikuwa akikazana kujipigania ili ile kamba iweze kutoka kwenye kiuno chake na kumuacha akiwa huru kama wanawake wengine.
Hilo ndio jambo pekee lililobaki katika akili yake.
Kesho yake Sabrina alienda tena kwa Sakina kwaajili ya ushauri kwa yale waliyopanga
"Mbona hakijanitokea chochote usiku dada jamani"
"Usijali Sabrina, itatokea tu halafu utafanya kama tulivyopanga sawa"
"Ni sawa ila mi nimechoka kwakweli, hii kamba siitaki dada"
"Usijali, ila kumbuka kitu kimoja tu kuwa mama yako hatakiwi kujua kitu chochote wala kuona kitu chochote kile"
"Usijali kwa hilo dada, mama hajui chochote na hatojua. Hii ni siri yetu wawili tu dada"
"Basi ni vizuri ili tusiharibu"
Kisha Sabrina akamueleza Sakina kuhusu Francis
"Una uhakika kuwa unampenda kweli?"
"Ndio nampenda dada, tena sana tu"
"Mapenzi huwa hayatabiriki mdogo wangu ila kuwa makini sana, na uniletee nimuone huyo kijana"
"Nitakuletea dada usijali"
Kisha Sakina akamtania Sabrina
"Mwanangu Jeff angekuwa mkubwa angekuoa Sabrina maana anavyokupenda mmmh!"
Sabrina na Sakina wakacheka, kisha Sabrina akasema
"Mi mamake mdogo ila Jeff ataoa mwanangu sababu mwanangu wa kwanza lazima atakuwa wa kike"
Wote wakafurahi huku wakiendelea kutaniana na kufanya wote wawili wasahau matatizo yao kwa muda kidogo.
Sabrina alirudi kwao na jambo alilolifanya muda huo ni kuzungumza kwenye simu na kijana wake kwani penzi lao lilikuwa changa na kuwafanya wapendane na wakumbukane kila dakika na kujiona kuwa dunia nzima ni wao tu wanaopendana na kujua mapenzi ni nini.
Muda huo wakati Sabrina akiongea na simu, aliitwa na mama yake lakini hata hakupenda kuitika kwani aliona akikatishwa kwenye maongozi yake hadi pale mama yake alipoamua kumfata mwenyewe
"Inamaana hunisikii Sabrina?"
"Samahani mama"
"Hizo simu wenzio tulishatumia hadi kusahau halafu wewe ndio unajiona upo kwenye matumizi, nikikwambia una mwanaume hutaki kukubali ukweli, ila upo muda nitagundua tu. Haya njoo uone mambo uliyoyafanya"
Alimvuta mkono na kukuta mboga yote waliyobandika ikiwa imeungua, kisha Joy akamwambia mwanae
"Furahi sasa, na tutakula simu humu ndani leo. Ndiyo furaha yako hiyo"
Joy alikerwa na hiyo tabia ya binti yake ingawa ndio kwanza aliifanya kwa mara moja ila alimfanya mama yake amchukie huyo kijana anayemsumbua binti yake kabla hata ya kumjua.
Siku hiyo Sabrina aliwahi kwenda kulala huku akiwaza yale aliyopanga na Sakina kuwa akiyatimiza ndio uzima wake kwahiyo akatamani sana yaweze kutimia ili awe huru.
Alipokuwa kwenye usingizi akapata ndoto kuwa yale mambo ameshayatimiza tayari na kumfanya acheke na kufurahi huku akiwa ndotoni bila ya kujua kama kicheko chake kilisikika hadi kwa mama yake.
Ni muda huo Sabrina nae akashtuka na kujiona kuwa alikuwa amelala, kwahiyo yote aliyodhani yamefanikiwa ilikuwa ni ndoto tu na kumfanya akunje sura yake kwa hasira.
Wakati akichukia vile, akahisi kuna kitu sio cha kawaida kwenye chumba chake na kumfanya arudi kulala ili aweze kukabiliana nacho.
Akamuona mwanamke wa makamo akiwa mtupu kabisa mbele yake.
Mwanzoni Sabrina aliogopa sana ila badae akajipa ujasiri na kuinuka, kisha akamshika yule mwanamke mkono na kabla hajafanya chochote, mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa kisha akaingia mama yake na kushangaa alichokiona mbele yake.
Mwanzoni Sabrina aliogopa sana ila badae akajipa
ujasiri na kuinuka, kisha akamshika yule mwanamke
mkono na kabla hajafanya chochote, mlango wa
chumbani kwake ulifunguliwa kisha akaingia mama
yake na kushangaa alichokiona mbele yake.
Sabrina nae akashtuka kumuona mama yake akiwa mule chumbani kwake na kumfanya ashindwe kufanya alichokikusudia.
Muda huo Joy nae alikuwa akimshangaa yule mtu aliyeshikwa mkono na Sabrina tena akiwa mtupu kabisa, Joy akashtuka sana na kuuliza
"Kitu gani kinaendelea hapa?"
Sabrina akashtuka zaidi baada ya lile swali la mama yake na kufanya amwachie mkono yule mama.
Kitendo kile kilimfanya yule mmama ashtuke na kutoweka kwenye macho yao na kumpa uoga Sabrina ambaye alikimbilia mwilini kwa mama yake kwa uoga na kumkumbatia.
Joy bado alikuwa akishangaa kwani yale mambo yalikuwa ni ajabu kwake na kumuuliza binti yake.
"Kwani ni nini Sabrina mwanangu, mbona sielewi?"
Sabrina alikuwa akitoa machozi tu kwa uoga, ikabidi Joy aende na mtoto wake huyo sebleni na kuanza kuomba kwa kukemea yale waliyoyaona na mwanae.
Baada ya hapo akamchukua mwanae na kwenda kulala nae kwani mtoto wake hakuweza tena kulala peke yake kwani ujasiri ulishampotea.
Kulipokucha, Joy hakutaka kupoteza muda bali alihitaji kujua kile kinachomsumbua mtoto wake.
Pia alichanganywa na kitu kimoja haswa taswira ya mtu aliyekuwa mtupu kwa ule usiku kwani alikuwa ni mtu yuleyule aliyemuonya kuhusu mwanae na mwanaume.
Hapo Joy hakuelewa kabisa kuwa ni kwanini bila kujua kama mtoto wake ana kitu kinachomfanya aweze kuona wachawi wanaomfata kumuwangia usiku.
Joy akamuuliza mwanae
"Hebu niambie vizuri Sabrina, unajua sielewi"
Sabrina anashindwa kumwambia mama yake ingawa ameshaona kila kitu cha usiku wake na kumfanya mama yake azidi kujihoji kwa kukosa majibu toka kwa mtoto wake.
Kisha Sabrina akainuka na kwenda kujiandaa ili aende kwa Sakina kumueleza, yani yeye alikuwa anaona kuwa ni vyema kwenda kumueleza Sakina kuliko kumwambia mama yake.
Kitendo kile kilimuumiza sana Joy na kujikuta akimwambia mwanae
"Kumbuka mimi ni mama yako. Nakujua wewe vizuri tena vizuri sana, wewe endelea tu kuwaambia matatizo yako watu wengine ukidhani utasaidika. Nenda tu ila kwangu utarudi"
Joy alikuwa akiongea kwa hasira kwavile mwanae hakutaka kumwambia ukweli, hiko kitu ndio kilimuuma zaidi.
Ila Sabrina hakuyajali sana maneno ya mama yake na badala yake aliondoka.
Alipofika kwa Sakina, alimkuta nae akiwa na mawazo yake ila alifurahi kumkuta ili aweze kumweleza kilichotokea na waweze kushauriana cha kufanya.
Akamueleza kila kitu hadi jinsi mama yake alivyomkuta na kumuuliza.
"Vipi umemwambia chochote?"
"Sijamwambia, na amechukia huyo balaa"
"Usijali, hawezi kuchukia hivyo kwa siku zote. Hapa tupange cha kufanya sasa. Ila vipi, aliyekuja usiku unamfahamu?"
"Nimfahamie wapi? Yani sura yake ilikuwa ngeni kabisa kwenye macho yangu, sijawahi hata kumuona yani usiku wa jana ndio ilikuwa mara ya kwanza kumuona"
"Na kama ukimuona mchana unaweza kumkumbuka?"
"Nitamkumbuka ndio, sababu nilimuangalia sana usiku. Yani mama ndio aliharibu kila kitu, jana ningefanikiwa kabisa ingawa alikuwa ni mgeni kwenye macho yangu"
Sakina akampa matumaini Sabrina kuwa watafanikiwa tu muda ukifika kwahiyo asijali. Kisha akamuuliza
"Vipi kuhusu kamba yako ya kiunoni je mama yako anajua?"
"Mama hajui chochote, ila nimechoka kwakweli. Wale watu wanatisha sana sijui kama nitaendelea kuwa na ujasiri wa kukabiliana nao"
Sakina akamfundisha Sabrina mbinu nyingine dhidi ya hao wachawi aliokuwa akiwaongelea, mbinu hiyo Sabrina akaiona kuwa ni mbinu bora zaidi kwake na pia ni bora katika kuwakomesha hao wachawi waliokuwa wanamsumbua.
Wakaongea mengi sana, kisha akarudi nyumbani kwao.
Alimkuta mama yake nae akiwa na mawazo kwani mambo ya mtoto wake yalishamchanganya tayari
"Kwahiyo sasa unafuraha baada ya kuyapeleka mambo yako kwa watu wa nje na kuacha kumwambia mama yako eeh!"
"Jamani mama"
"Jamani nini sasa, unadhani nafurahia? Ila yakikushinda utayasema mwenyewe tena bila hata ya kuulizwa"
Sabrina alijua kama mama yake kachukia ila je atawezaje kumwambia wakati kaambiwa wafanye siri ili aweze kupona kwa yale matatizo aliyokuwa nayo.
Hakuna na la kufanya zaidi ya kuendelea kumficha mama yake.
Jioni ya siku hiyo alitoka nyumbani kwao na kwenda kuonana na Francis, kijana wa kwanza kumpenda katika maisha yake.
Alifurahi kuonana nae, na kuzungumza mengi kuhusu mahusiano yako.
"Eeeh Sabrina, lini utanitambulisha kwenu wanijue?"
"Usijali, ngoja niweke mambo sawa na mama yangu kisha nitakupeleka nyumbani kukutambulisha rasmi. Ila wewe kwetu unapafahamu, mama yangu unamfahamu pia wakati mimi sipafahamu kwenu wala simfahamu ndugu yako hata mmoja"
Francis akacheka kwavile ni kweli Sabrina hakufahamu anapoishi huyu kijana,
"Usijali Sabrina, kesho nitakupeleka kwa bibi yangu kukutambulisha. Yani huyo bibi yangu ni wa pekee, ni bibi aliyenilea mimi yani namuona kama mama yangu vile. Ananipenda sana, nauhakika hata wewe atakupenda pia. Basi kesho nitakupeleka"
Sabrina alifurahi sana na kujiona kuwa ni binti mwenye bahati kuliko mabinti zote.
Alijiona kuwa yeye ni wa pekee na kumfanya aiombee hiyo kesho kuwa ifike mapema ili yeye aweze kwenda huko kutambulika.
Alipokuwa anarudi kwao akapitia kwa Sakina kwaajili ya kuchukua vya kukamilishia zoezi walilopanga iwapo itatokea kama jana yake.
Sakina akamkabidhi fimbo ambayo alitakiwa aitumie kwa makini sana, kisha akampatia na dawa ya unga.
"Tumia kwa uangalifu Sabrina, nimeenda kuvitoa mbali sana hivyo"
"Usijali dada"
"Hakikisha unamchapa fimbo tatu usizidishe sababu ukizidisha unaweza kumfanya asiamke"
"Hakuna tatizo dada, maelekezo yote nimeyaelewa na ninakuhakikishia kuwa safari hii sitokosea hata kidogo"
"Vizuri sana, tukikamilisha hili tutakuwa tumebakiwa na jambo kubwa moja tu, kwahiyo jitahidi tufanikiwe halafu mama yako asivione hivi vitu. Sawa!"
"Sawa dada, ila kwanini hutaki mama ajue?"
"Nitakwambia sababu, ila ngoja tukamilishe haya mambo kwanza"
Sabrina akakubaliana na mpango wa Sakina bila kujua kuwa Sakina anamuwazia nani katika mpango wake huo.
Baada ya kukamilisha yote, Sabrina akarudi nyumbani kwao.
Kama kawaida, alimkuta mama yake akiwa amechukia tu
"Siku hizi pana misumari hapa nyumbani mwanangu, najua huwezi kukaa"
"Jamani mama!"
"Endelea na jamani zako ila yakikushinda utasema hivyo hivyo jamani mama, umeku a mkubwa sasa kwahiyo na wewe unajiona ni mama tayari"
Sabrina alimkodolea macho tu mama yake huku akili yake ikiwaza kufanikisha kile alichotakiwa kukifanikisha.
Moja kwa moja alienda kuviweka vile vitu kitandani kwake na kwenda kumsaidia kazi mama yake huku akiwaza ya kufanya tu.
Muda wa kulala ulipofika, Joy alimuita mwanae
"Tena leo uje tuombe wote ili yale mambo yanayokufataga yasije"
"Aaah mama, mi nina usingizi bhana. Wee niombee tu"
"Hivi wewe mtoto una mashetani au una nini wewe jamani!!"
Alimsikitikia sana mtoto wake kwani hakuelewa mwenendo wake na mawazo yake yalivyo.
Sabrina alienda chumban i kwake na kupaka ile dawa ya unga unga aliyopewa na Sakina kisha akalala.
Wakati wa usiku wa manane, akahisi ile kamba ya kwenye kiuno chake ikitingishika na kumfanya ashtuke tena.
Alipoangalia pembezoni mwa chumba chake, akamuona yule mwanamke wa jana tena ila leo alikuwa akiwa amejisiliba madawa yaliyoonekana kama masizi kwenye mwili wake.
Sabrina, akachukua ile dawa ya unga iliyobaki na kumpulizia yule mmama ambapo yule mmama alijikuta akiganda pale pale.
Sabrina akainuka vizuri na kile kiboko sasa, akamchapa vitatu kama alivyoambiwa na Sakina kisha akajisemea kuwa ampe cha nyongeza na kumpiga cha nne .
Halafu akamwambia
"Hiko nimekuchapa cha ziada na......"
Kabla hajamaliza yule mmama akatoweka na kufanya Sabrina ashtuke na ujasiri wote kumuisha, alichofanya ni kukimbilia chumbani kwa mama yake na kumfanya mama yake amshangae
"Nini sasa na leo?"
Joy akawasha taa ili kumuangalia vizuri mtoto wake.
"Kheee, mbona una maunga usoni?"
Sabrina akakumbuka kuwa ni ile dawa aliyojipaka wakati wa kulala.
"Niambie Sabrina, mambo gani hayo?"
"Sijui mama"
"Kwakweli kesho lazima nikupeleke kanisani wewe mtoto, acha kuniletea mauzauza ya shangazi yako kwenye nyumba yangu jamani"
Sabrina alimshikilia tu mama yake huku uoga umejaa, kwanza hakujiamini kama ni yeye aliyeweza kumchapa viboko yule mchawi.
Kulipokucha, Sabrina ndiye alikuwa wa kwanza kuamka na alichofanya ni kwenda kukichukua kile kiboko ili kukirudisha kwa Sakina kabla ya mama yake kukiona.
Alipofika kwa Sakina alimkuta nae ndio ametoka kuamka na kuanza kumueleza yaliyojiri usiku
"Ile dawa kweli ni khatari dada maana hadi nimejishangaa kupata ule ujasiri jamani"
"Ile dawa ilikuwa inakuwa wewe ujasiri halafu inamzubaisha yule mchawi. Ila usingemsemesha, ningekuja kumuona na mimi"
"Kumbe nisingemsemesha asingeondoka eeeh!"
"Ndio, ila ulipomsemesha ndio ukamzindua na kumfanya aweze kuondoka. Na je umemchapa viboko vingapi?"
"Vitatu kama ulivyosema"
"Vizuri sana Sabrina"
Hakutaka kusema ukweli kama kamchapa viboko vinne ili Sakina asichukie kwavile amekiuka masharti waliyokubaliana nae.
Baada ya hapo alirudi kwao ili kujiandaa kwaajili ya safari aliyopanga na Francis.
Alitafuta ile nguo yake nzuri kabisa tena ya heshima ili akionekana aweze kukubalika ukweni bila ya tatizo lolote.
Hadi muda anapigiwa simu alikuwa tayari ameshajiandaa vya kutosha na kwenda kuonana na Francis.
Kwanza kabisa akaenda nae kwa Sakina ili aweze kuwasaminisha
"Mmh Sabrina mdogo wangu umependeza sana"
"Asante dada"
"Na wewe Francis angalia bhana, tena tafadhari sana usimuumize mdogo wangu. Nampenda sana huyu"
"Usijali dada, nakuahidi sitokuja kumuumiza kamwe katika maisha yake. Nampenda sana na ndiomana leo nimejitoa ili nimpeleke kwa ndugu zangu wamjue"
Sabrina alikuwa akifurahi tu muda wote kwani aliona fahari kila aliposikia neno nakupenda toka kwa Francis.
Sakina aliwapa baraka zake kisha nao wakaendelea na safari zao.
Njiani, walikutana na yule mwanamke ambaye Sabrina aliwahi kumfanyia fujo.
Walipopishana nae, yule mwanamke alimsonya Sabrina kisha akamwambia
"Dawa yak o inachemka wewe"
Na kuwapita pale, Francis alimuangalia Sabrina na kumuuliza
"Kwani vipi na huyo mwanamke?"
"Ni mchawi huyo"
"Unawezaje kuwekeana visasi na wachawi Sabrina?"
"Ni historia ndefu sana ila tuachane nayo kwanza"
Wakaendelea na safari yao.
Walipofika kwa bibi yake na Francis waliwakuta watu wakiwa kimya sana, kisha wakakaribishwa vizuri sana na kumfanya Sabrina azidi kupata furaha ya moyo.
Kisha Francis akamuuliza nduguye mmoja alipo bibi yake ili aweze kumtambulisha Sabrina
"Eti bibi yuko wapi?"
Akijibu huku amenyong'onyea,
"Bibi anaumwa"
"Anaumwa? Tangu lini? Na mbona hamkuniambia?"
"Ni leo tu ndio ameamka vibaya, tena tulitaka tukupigie simu. Afadhari umekuja mwenyewe"
"Kwahiyo yuko wapi?"
"Kalala tu chumbani kwake, hajiwezi kwakweli"
Francis akainuka na kwenda kumuangalia bibi yake kipenzi, akamuhurumia sana kwani bibi yake hakuweza hata kuzungumza.
"Pole sana bibi yangu"
Aliongea huku machozi yakimlengalenga kwani alimpenda sana, bibi nae aliitikia kwa kichwa tu pale pale kitandani.
Kisha Francis akamuomba bibi yake kuwa amletee mchumba wake japo amuone tu, bibi akaitikia kwa kichwa kisha Francis akaenda kumchukua Sabrina.
Akaenda nae chumbani kwa bibi yake, Sabrina kufika pale macho yake yakagongana na macho ya yule bibi na kufanya ashtuke kwani alikuwa ni yule yule mmama aliyempiga usiku.
Akaenda nae chumbani kwa bibi yake, Sabrina kufika
pale macho yake yakagongana na macho ya yule bibi
na kufanya ashtuke kwani alikuwa ni yule yule
mmama aliyempiga usiku.
Sabrina akaogopa sana na hakuweza kuzuia uoga wake kwani yule bibi alimkazia sana macho na kumfanya atetemeke na kutoka nje huku anakimbia.
Francis akamfata nyuma na kumuuliza,
"Kwani nini Sabrina?"
Kama kawaida yake ya kuropoka akajikuta akimwambia Francis
"Yule bibi ni mchawi"
Bila kujua kama kauli hiyo ingewezaje kumbadilisha Francis
"Unasemaje Sabrina?"
Sabrina akaongea kwa kujiumauma sasa na kujilaumu kuwa kwanini ameropoka vile
"Samahani Francis"
"Yani unamuita bibi yangu mchawi halafu unaniomba samahani kirahisi tu!"
"Naomba unisamehe Francis"
Francis alikuwa amechukia sana kwa kile kitendo cha bibi yake mpenzi kuitwa mchawi
"Yani siamini kabisa kama wewe Sabrina unaweza kumuita bibi yangu mchawi, siamini kwakweli"
"Nisamehe jamani"
"Usitake nitende dhambi Sabrina, tafadhari naomba uende. Kwa usalama wako nenda"
Kwa jinsi Francis alivyokuwa akiongea kwa ukali ilimbidi Sabrina aondoke huku moyo ukimuuma sana na kujilaumu kwa kuropoka kwake ingawa ilikuwa ni kweli ila ndio ilishamponza tayari.
Wakati Sabrina anatoka kwenye ile nyumba, akakutana na kijana aliyekuwa anataka kuingia mule ila alipomuona Sabrina akitoka huku machozi yakimbubujika alimuonea huruma na kumfata.
"Nini tatizo dada?"
"Hamna kitu"
"Mbona unalia sasa?"
Sabrina alizidi kutokwa na machozi tu, yule kijana akamshika Sabrina mkono na kumrudisha ndani ya geti la ile nyumba ili amuhoji vizuri kinachomliza.
Alipomrudisha tu, Francis nae alitoka nje na kuchukizwa kwa kuendelea kumuona Sabrina eneo lile, kisha akamwambia nduguye aliyemshika Sabrina mkono
"Fredy, mwache huyo malaya aende zake"
"Kwani amefanyaje?"
"Achana nae bhana"
Kile kitendo cha Sabrina kusikia kuwa yeye akiitwa malaya kilimuuma sana tena zaidi hata alivyoumia mwanzo kwani hakuamini kama Francis huyu aliyemwambia kuwa anampenda kwa vyovyote vile leo hii anamfukuza na kumuita malaya kisa tu kaongea ukweli, roho ilimuuma sana na kuondoka huku akilia zaidi ila Francis hakujali chochote.
Fredy, alimfata Francis ili kumuuliza vizuri
"Kwani kafanyeje yule?"
"Mwanamke fala sana yule, ndio kwanza leo namleta halafu anamuita bibi yangu mchawi! Na akafie mbele huko"
"Kwahiyo ni sababu hiyo tu iliyokufanya umfukuze?"
"Tena sio kumfukuza tu, yani hata kumuona sitaki yani sitaki kabisa"
"Mmh ulimpenda kweli yule mwanamke wewe?"
"Nilimpenda ndio ila siwezi kuvumilia upuuzi kama huu kwakweli"
Francis alionekana kuwa na hasira sana kupita maelezo ya kawaida na kuingia tena ndani.
Moyo wa Fredy bado ukamtuma kuwa amfate yule binti, kisha akatoka na kuanza kumfatilia.
Kwavile Sabrina alijihisi kuchanganyikiwa hadi akasahau njia waliyokuja nayo mwanzo na kujikuta akipita njia nyingine.
Isingekuwa Fredy kumfata basi angepotea leo.
Fredy alimuuliza,
"Kwani unaenda wapi?"
"Nataka kwenda kupanda daladala nirudi nyumbani"
"Dah huko uendako unapotea dada, twende nikupeleke stendi"
Kisha Sabrina akaanza kufatana pamoja na Fredy ambaye alipanda nae daladala hadi akamfikisha kwao kabisa.
"Asante sana"
"Usijali, mimi ni kati ya wanaume walioumbwa na moyo wa huruma katika dunia hii. Nimekuhurumia sana ndiomana nikafanya haya"
"Nashukuru sana kaka"
"Naitwa Fredy, vipi wewe jina lako!"
"Naitwa Sabrina"
"Sawa Sabrina tutawasiliana basi"
Kisha Fredy akampa namba zake Sabrina na kumuaga pale halafu akaondoka.
Sabrina aliingia ndani kwao ila mama yake hakuwepo na kumfanya apate muda muafaka wa kuwaza yanayomsibu.
"Mmh sijui nikamuhadithie dada Sakina! Lakini ataniona ni mpumbavu. Ngoja nijaribu kukaa nalo moyoni huku nikiombea Francis anisamehe jamani"
Alikuwa akiwaza sana huku akiumia moyoni mwake.
Baada ya masaa kupita akajaribu kumpigia simu Francis lakini simu yake haikupokelewa na kumfanya aumie zaidi na zaidi.
Muda kidogo alifika mgeni nyumbani kwao na mgeni huyo alikuwa ni Sakina
"Kheee Sabrina, umerudi saa ngapi?"
"Muda tu, karibu"
"Mi nimemfata mama yako"
"Na hata hayupo"
Ila Sakina alimgundua Sabrina kuwa hayupo sawa ingawa kila alipomdadisi kuhusu alipotoka hakusema ukweli na kuishia kujibu kuwa ni nzuri tu.
"Niambie ukweli Sabrina, najua una matatizo niambie tafadhari"
Baada ya kumbana sana, Sabrina akaamua kusema ukweli kwa Sakina kwa yale yaliyojiri
"Mungu wangu Sabrina, kheee kwani wewe ulimchapa viboko vingapi jana"
Napo ilibidi aseme ukweli kuwa alimchapa viboko vinne tofauti na alivyoambiwa
"Hayo majanga mdogo wangu, kwanini ulifanya tofauti na nilivyokwambia? Haya swali jingine sasa, kama huyo bibi ni bibi yake huyo Francis kwanini alikufata wewe kukuwangia?"
"Hata mi mwenyewe sielewi dada yani sielewi kabisa na hata sijui cha kufanya maana Francis nampenda ila sijui itakuwaje. Sijui kama ataendelea na mimi kwa jinsi alivyonifukuza"
Sakina alimuhurumia sana Sabrina na kumpa moyo
"Usijali, atakusamehe tu wala usiwe na wasiwasi"
Muda mwingi Sabrina alijilaumu mdomo wake kwa kuropoka mambo yasiyotakiwa kuropokwa kama hili linalompa mawazo kwasasa na kumkosesha raha ya maisha na kumfanya akose furaha.
Usiku ulipofika alimkumbuka sana Francis lakini kila alipojaribu kumpigia simu, simu yake haikupokelewa. Hata alipojaribu kumtumia ujumbe, jumbe zake hazikujibiwa na kumfanya azidi kupatwa na mawazo yasiyo rasmi.
Akaamua kuitafuta ile namba aliyopewa na Fredy ili amuulizie Francis kwa Fredy
"Unaongea na Sabrina hapa"
"Ooh! Kumbe Sabrina, nipe khabari"
"Namuulizia Francis, anaendeleaje?"
"Yuko poa, ila acha kujiumiza kichwa kwa hayo mambo wangu. Utaumia bure, kesho kama unamuda basi tuonane. Sawa?"
"Hakuna tatizo basi"
Akamuaga na kukata simu huku akiamini kuwa huyu Fredy ndiye atakayemsaidia yeye kuwa na mahusiano tena na Francis.
Kesho yake alimuaga mama yake na kwenda kuonana na Fredy kama ambavyo walipanga kwenye simu.
"Kwani Francis mlifahamiana vipi?"
Sabrina alimueleza Fredy kwa kifupi tu.
"Nimekuelewa, sasa una mpango upi baada ya yote"
"Nampenda Francis, nahitaji anisamehe ili niwe nae tena"
"Poa usijali, ila kama akikataa kukusamehe usiwe na shaka. Wengine tupo hapa"
Aliongea kwa utani lakini ndio alikuwa akimaanisha hivyo kwani nae alijikuta akimpenda Sabrina na kuvutiwa nae.
Waliongea mambo mengi sana, kisha wakaagana na kuondoka.
Sabrina alirudi kwao huku akiwa na imani kwamba atasaidiwa na Fredy kuweza kurudiana na Francis bila kujua kwamba Fredy nae kashampenda tayari na hatoweza kufanya kitu hiko cha kumsaidia.
Maisha yao nayo yakaendelea kwa mtindo huo huku Fredy akidumisha mawasiliano na Sabrina.
Toka lile sakata la Sabrina kumpiga yule mchawi usiku, hakuweza tena kufatwa na hao wachawi kwa kipindi hiko na bado hakujua kwanini bibi yake Francis alimfata.
Alitamani sana kujua ni kwanini ila hakuweza kujua kabisa.
Mawasiliano baina yake na Fredy yalishamiri sana.
"Naomba kesho nikutembelee kwenu hapo Sabrina"
"Karibu tu hata usijali, wee njoo tu"
Fredy alifurahi kwani alijua ndio sehemu ya kwenda kubwaga ya moyo wake.
Kesho yake Fredy alienda kwa wakina Sabrina na kumkuta, ile leo hakumkuta mama yake na Sabrina kwavile alitoka.
"Eeh niambie Francis anaendeleaje, maana hapokei simu zangu wala hajibu meseji zangu"
"Francis kanipa ujumbe kuwa usimsumbue tena, na hivi ninavyokwambia ana mwanamke mwingine. Kwakweli nimekuhurumia sana Sabrina kwa kung'ang'ania sehemu usiyotakiwa wakati wapo watu wa maana tu wanaokuhitaji kushinda hata huyo Francis"
"Wakina nani hao?"
"Mimi hapa, kwakweli nakupenda sana Sabrina. Siku zote hizi nimekuwa nikikupenda sema tu sikujua nianzie wapi kukwambia"
"Mmmh Fredy!"
"Sikutanii Sabrina, mi ni msema kweli na huo ndio ukweli kutoka moyoni mwangu"
"Wewe si ndugu yake na Francis! Halafu si unamwanamke wewe!"
"Sina mwanamke mie, nakupenda wewe Sabrina. Ni kweli Francis ni ndugu yangu ila yeye alikutamani, mimi ndiye ninayekupenda. Mungu alifanya makusudi kukukutanisha wewe na Francis ili uweze kukutana na mimi mwenye mapenzi ya dhati na wewe. Sina nia mbaya naye zaidi ya upendo wa dhati"
Maneno ambayo Fredy alikuwa akiyaongea yalimuingia akilini Sabrina na kujikuta akivutiwa nae huku akiwaza kuwa anayoyasema yanaweza kuwa yana ukweli ndani yake.
"Basi tutaongea vizuri kwenye simu badae"
Hakutaka kumjibu kwa muda huo kwavile bado alimpenda Francis ingawa maneno ya Fredy nayo yalimuingia kichwani.
Wakaongea mengi kisha Fredy akaaga na kuondoka halafu Sabrina akamsindikiza.
Wakati Sabrina anarudi kutoka kituoni alipotoka kumsindikiza Fredy.
Njiani alijikwaa kwenye jiwe na kuanguka, alipojitahidi kuinuka aliona damu zikimtoka kwenye kidole, alikuwa amechunika ngozi kwenye dole gumba la mguu wa kushoto na damu kiasi zilimwagika pale.
Alijikongoja hadi nyumbani kwa Sakina kwavile hapakuwa mbali sana na alipojikwaa.
Sakina alipomuona alimshangaa
"Vipi mbona unachechemea Sabrina?"
Sabrina akamuonyesha kile kidole na kumueleza alivyojikwaa.
Sakina akachukua pamba na kumfuta Sabrina kisha akamfunga pale kwenye kidole.
Wakati anamalizia kumfunga ikawa kama mtu aliyekumbuka kitu na kumuuliza
"Umejikwaa sehemu gani?"
"Pale karibia na kiwanja, pale kwenye njiapanda"
"Mmmh!!"
"Mbona unaguna?"
Akamfunga haraka haraka na kumwambia
"Hebu twende ukanionyeshe"
Wakainuka na kwenda mahali alipojikwaa Sabrina.
Kufika pale, walikuta ile sehemu ambayo damu ya kwenye kidole cha Sabrina imemwagika ikawa kama mtu kaja kuichota na mchanga wake na kuacha kijishimo.
"Umeona Sabrina?"
"Nimeona"
"Inamaana hapa kuna mtu kaichota damu yako"
"Sasa kwanini kaichota?"
"Unafatiliwa Sabrina, yani ni bora tungekumbuka muda ule ule ila bado hatujachelewa sana. Nisubiri kidogo tena hapa hapa usiondoke"
Sakina akaondoka na kumuacha Sabrina mahali pale.
Baada ya muda kidogo akarejea na kimfuko kidogo, ndani yake alibeba majivu na kipande cha mkaa, kisha akamwambia Sabrina
"Kwavile yeye alisahau kufukia hiki kishimo wakati anachukua damu yako basi tutakifukia sie"
Akachukua kale kamkaa kadogo na kuweka kwenye kale kashimo halafu akaweka majivu juu yake kisha akasawazisha na mchanga pale juu na kumwambia Sabrina kuwa waondoke.
Waliporudi nyumbani, Sakina akamuonya tena Sabrina
"Usimwambie mama yako"
"Ila dada leo hebu niambie kwanini hutaki nimwambie mama?"
"Mama yako yule ni mtu wa maombi kwahiyo ataharibu kila kitu ndiomana sipendi umwambie"
"Hapo nimekuelewa sasa"
Kisha akarudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake akiwa ndani.
"Haya niambie, pale njiani mlikuwa mnafanya nini na Sakina wako?"
Sabrina akashtuka kugundua kwamba mama yake aliwaona, ikabidi amdanganye
"Tulikuwa tunaongea tu mama, kuna mgeni tulimsindikiza"
"Endelea kunificha mwanangu ila ipo siku kila kitu kitakuwa peupe"
Joy alihisi tu kuwa kuna vitu mtoto wake anamficha ila hakutaka kumlazimisha sana kuwa amwambie kwani alijua ipo siku lazima atasema yeye mwenyewe bila hata ya kushurutishwa.
Siku hiyo ikapita, hata usiku wake ukapita vizuri kabisa bila ya tatizo lolote.
Kitu kimoja tu kilichomtatiza Sabrina ni kamba yake ya kiunoni na ilikuwa ni siri yake yeye na Sakina, hakutaka mtu mwingine ajue hiyo siri haswaa Fredy.
Wakati akiwaza kuhusu huyo Fredy na kukiambia kichwa chake kiamue moja kama kumsubiri Francis arudishe moyo au kuwa na Fredy.
Muda huo huo akapigiwa simu na huyo Fredy
"Naomba tuonane Sabrina"
Sabrina hakukataa na wakapanga mahali pa kwenda kukutana, ambapo waliona kuwa sehemu nzuri ni ufukweni ili waweze kufikia muafaka wa swala lao.
Muda wa kuonana ulifika, wote wawili waliwahi kufika eneo la tukio.
Walikaa kwenye mchanga na kupeana habari mbalimbali.
Wakati wakizungumza, Fredy alijikuta akipatwa na matamanio zaidi juu ya Sabrina na kumfanya awe nae karibu zaidi hata aweze kumshikashika ili aridhike.
Wakati yupo karibu vile, akazungusha mkono wake kwenye kiuno cha Sabrina na kujikuta akiishika ile kamba.
Bila uvumilivu akamuuliza Sabrina
"Unavaaga shanga?"
Sabrina nae akashtuka na kujibu
"Hapana, sivaagi"
"Sasa hii naishika kwenye kiuno chako ni nini"
Sabrina akaogopa kujibu na kuutoa mkono wa Fredy kwenye kiuno chake.
"Niambie Sabrina, kitu gani hicho?"
"Sio kitu"
Fredy alitamani sana kujua kuwa ni kitu gani, wakati wanaendelea na maongezi, Fredy akamfunua Sabrina blauzi kwa kumshtukiza ili aone kile cha kiunoni.
Muda anakitazama tu ni muda huohuo Sabrina akashtuka na ni muda huohuo Fredy nae akaanguka chini kwenye mchanga huku damu zikimtoka machoni.
Fredy alitamani sana kujua kuwa ni kitu gani, wakati
wanaendelea na maongezi, Fredy akamfunua Sabrina
blauzi kwa kumshtukiza ili aone kile cha kiunoni.
Muda anakitazama tu ni muda huohuo Sabrina
akashtuka na ni muda huohuo Fredy nae akaanguka
chini kwenye mchanga huku damu zikimtoka
machoni.
Hofu ikampata Sabrina, alihisi kuchanganyikiwa kwa muda huo na hakujua ni kitu gani afanye ili kukabiliana na ile hali.
Aliangalia watu pale ufukweni kama kuna yeyote anayewatizama ila kila mmoja alikuwa akiendelea na mambo yake kanakwamba hawaoni kinachoendelea.
Sabrina alitamani hata akimbie na kumuacha Fredy pale ila moyo wake ulimsuta.
Akapata wazo la kumpigia simu Sakina, na hakutaka kupoteza muda kisha akachukua simu na kumpigia.
Wakati Sakina anapokea ile simu tena kabla hata ya Sabrina kuongea nae kitu chochote kile alishangaa kumuona Fredy akiinuka pale chini tena akiwa hana hata tone la damu kwenye macho wakati mwanzoni macho yake yalikuwa yakitoa damu.
Sabrina akashtuka sana na kushindwa kuongea chochote na Sakina hata Sakina mwenyewe alishangaa kwani alikazana kusema "Hallow, hallow" bila ya majibu ya aina yoyote ile hadi akaamua kuikata ile simu tu.
Sabrina alikuwa kama mtu aliyepigwa na butwaa, hakuelewa chochote kwa wakati ule.
Fredy nae alipoinuka pale akaanza kulalamika kuwa kichwa kinamuuma hivyobasi akamuomba Sabrina waondoke. Sabrina hakukataa kwani naye alishachanganyikiwa tayari na akaona kuwa labda waondoke mahali hapo na kurudi makwao tu.
Sabrina alirudi nyumbani kwao huku akiona akili yake kuwa imepagawa.
Moja kwa moja alienda kulala kwani alijihisi kuumwa kichwa pia kwa kutafakari kitu asichokielewa.
Usiku kwenye mida ya saa mbili alimsikia mama yake akimuita, alipotoka nje alishangaa kumuona baba yake.
Alifurahi sana ingawa baba yake alirudi bila ya kuwapa taarifa.
"Jamani baba, hata bila ya kusema!!"
"Nilitaka kuwafanyia surprise kama hivi mwanangu"
Wote walikuwa na furaha kwa ujio wa baba wa mwenye nyumba.
Hata Sabrina aliporudi kulala akawa amesahau yote yaliyomtokea kutokana na furaha aliyokuwa nayo kwa wakati huo wa usiku.
Kesho yake, asubuhi na mapema, Sabrina alipigiwa simu na Fredy
"Sabrina, kwanini umenifanyia hivi?"
"Nimekufanyia nini Fredy?"
"Inamaana hujui ulichokifanya!"
"Niambie Fredy, sijui chochote"
Fredy akakata ile simu na kumfanya Sabrina apatwe na mawazo kwavile hakujua kuwa ni kitu gani kimemtokea Fredy mpaka akasema vile tena asubuhi kabla bila hata ya salamu.
Sabrina akapata wazo la kwenda kwa Sakina ili amwambie yaliyojiri na pia aweze kupata ushauri kutoka kwake.
Alifika kwa Sakina na kumkuta kama kawaida yake, naye akamkaribisha vizuri sana na kama kawaida ya Sabrina hakutaka kupoteza wakati hivyobasi akamsimulia Sakina mambo yote yaliyojiri juu yake.
"Kheee mbona makubwa hivyo Sabrina!!"
"Ndio hivyo dada, yani hapa hata sijui cha kufanya dada yangu"
"Hayo mambo ni makubwa sana Sabrina, itabidi nimtafute mtu akakuulizie kuwa ni kitu gani"
"Itakuwa vizuri sana dada"
"Haya niambie, na huyo mwanaume kwani umemfanya nini hadi akakulalamikia?"
"Hata sielewi dada yangu, mi mwenyewe nimeshangaa tu akinilalamikia. Sijui ni kitu gani, itabidi nimuulize vizuri"
Sabrina akaongea mambo mengi sana na kushauriana vitu vingi sana huku wakipanga namna ya kukabiliana na matatizo yanayomzunguka Sabrina.
Baada ya kuridhika na mazungumzo yale, Sabrina aliamua kurudi kwao sasa.
Alipofika kwao, moja kwa moja akamkuta mama yake na baba yake wakiongea.
Ile alipotokea tu, mama yake akasema
"Umemuona mtoto wako! Basi ndio tabia yake siku hizi, pakikucha tu mwanao anaona miguu inamuwasha. Basi yuleee kiguu na njia kwa majirani"
"Anaendaga wapi kwani?"
"Wapi kwingine zaidi ya kwa Sakina! Yani huyo Sakina ndio amekuwa mama yake na baba yake hapo unapomuona, kila kitu anamueleza Sakina tu"
Bwana Deo akasikitika sana na kumuita Sabrina ili ajaribu kumuuliza vizuri, ila kama kawaida ya Sabrina maelezo yake yalipindapinda na kumfanya baba yake apate wazo la kufanya dhidi yake.
"Nenda tu, najua cha kufanya"
Sabrina akainuka na kwenda kuendelea na mambo yake mengine bila ya kujua kuwa baba yake ameamua kufanya kitu gani dhidi yake.
Usiku ulipofika aliamua kuwasiliana na Fredy ili kujua kuwa ni kitu gani alichomfanyia
"Ni kweli unataka kujua?"
"Ndio, nahitaji kujua Fredy"
"Kujua unajua ila tu unajipumbaza, ila kama unahitaji kujua kwa undani zaidi nakuomba kesho tuonane"
"Hilo halina tatizo Fredy, tutaonana tu"
Fredy akakubaliana na Sabrina mahali pa kukutaniana siku ya kesho ingawa hakumtajia kuwa wataenda kufanya kitu gani, na kumfanya Sabrina kuwa mgumu sana kuelewa juu ya hilo.
Sabrina alipokuwa amelala usiku, ikamjia njozi.
Alihisi kuna watu watatu wameingia kwenye chumba chake tena kwa staili zilezile ambazo wachawi huwa wanaingia, wale watu wakamnyanyua Sabrina pale kitandani kwa madawa yao kisha Sabrina akaanza kuwafata kama wanavyomuelekeza.
Yani ilikuwa kama roboti zinavyopelekwa na mashine ndivyo ilivyokuwa kwa Sabrina, akafikishwa mahali halafu akafanywa kama meza.
Wale watu walikuwa wakicheza na kula nyama, mara nyingine walimkalia kwa juu kama kiti, mara nyingine walimuwekea chakula juu yake kama meza na mara nyingine walimfanya kama punda au farasi, kwamaana kwamba walipanda juu yake kisha Sabrina akawa anawatembeza kama ambavyo farasi hufanya.
Mambo mengi yalifanyika ila kwa Sabrina ilikuwa kama njozi tu.
Muda ulifika wakaanza kumpa maelekezo mengine kama ya kumrudisha kwao, wakampeleka tena hadi chumbani kwake kitandani ila wakasahau kumuosha miguu.
Ila walipotaka kumchukua tena ili wakamnawishe, ndio hapo hapo Sabrina akashtuka kutoka kwenye ile njozi na ilikuwa ni alfajiri tayari.
Sabrina aliinuka kutoka usingizini na kukaa huku akiwaza ile ndoto kuwa ni ya aina gani! Ila alijihisi kuchoka sana kwa viungo vyake, haswaa mgongo ambao ulikuwa ukimuuma sana kwa wakati huo.
Akajaribu kujinyoosha lakini bado maumivu aliyasikia mwilini na kumfanya atafakari vizuri zaidi kuwa ile ni ndoto au ni kweli.
"Mbona sijielewi sasa! Hivi nilikuwa naota au ni kweli ilikuwa vile usiku!!"
Hakupata jibu, ila alipojitazama miguuni alishtuka zaidi baada ya kuona miguu yake imejaa vumbi
"Mungu wangu, inamaana ni kweli? Inamaana wachawi walikuja kunibeba usiku!"
Hofu ikamjaa na kumfanya palipokucha vizuri tu aende kwa Sakina kumuelezea yale mambo.
Alipofika kwa Sakina hakumkuta na kumfanya ajiulize kuwa asubuhi ile amekwenda wapi, na alipojaribu kupiga simu yake haikupatikana. Ilikuwa ni ajabu sana kwa Sabrina na kumfanya apatwe na mawazo zaidi na kuamua kurudi kwao tu.
Alimkuta baba yake akiwa amekaa sebleni na kumsalimia
"Kumbe ni kweli mwanangu kuwa ikifika asubuhi miguu inakuwasha!"
"Hapana baba, nilikuwa hapo nje tu"
"Hapo nje kwetu ndio siku hizi kuna vumbi kiasi hicho mwanangu!!"
Sabrina akajitazama tena miguuni, akatamani kumwambia baba yake ukweli kuhusu mambo yaliyojiri na ndoto aliyoota usiku lakini midomo yake ilikuwa mizito kusema na kujikuta akimuangalia tu baba yake bila ya kumwambia kitu cha aina yoyote ile.
Deo alimtazama sana binti yake na kujaribu kuitafakari akili ya mwanae bila ya majibu yoyote yale, kisha akamruhusu kuwa aende akaendelee na shughuli nyingine.
Sabrina alienda kuoga moja kwa moja.
Alipokuwa anaoga alijishika kiunoni na kuona hali sio ya kawaida kwani ile kamba haikuwepo tena kwenye kiuno chake.
Sabrina alijaribu kutafakari bila majibu,
"Imeenda wapi ile kamba? Mbona maajabu haya! Au yule bibi alinihurumia akaitoa?"
Sabrina hakupata jibu zaidi ya kujiongezea maswali na mawazo katika kichwa chake.
"Sijielewi kwakweli, kitu gani kimetokea kwangu? Na kimetokeaje? Na kwanini kimetokea? Mbona sipati jibu?"
Hakuwa na raha kabisa, hata alipomaliza kuoga bado alikuwa na mawazo na kumfanya ashindwe kufanya kitu cha aina yoyote ile.
Mchana akapigiwa simu na Fredy
"Sabrina, kama tulivyoongea usiku. Tukutane pale Mitini guest house"
"Sawa hakuna tatizo ila hujaniambia kuwa tunaenda kufanya nini hapo"
"Nimekwambia utajua huko huko"
"Poa, hakuna tatizo"
Fredy akashangaa kwa Sabrina kuitikia haraka hivyo wakati usiku wa jana yake tu alikuwa akipinga swala hilo ingawa badae alikubali kwa kusitasita ila leo alikubali moja kwa moja bila mashaka ya aina yoyote ile.
Mawazo ya Sabrina yalimpelekea kwamba Fredy anahitaji kulala nae na ndiomana kamwambia wakutane huko kwenye nyumba za kulala wageni.
"Mmh nitaweza kweli kulala na mwanaume? Sijui itakuwaje, nitajua hukohuko ila bora kamba imetoka"
Sabrina hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote yule na ile kamba ndiyo iliyokuwa ikimpa mashaka zaidi kuwa hakuna mwanaume atakayeweza kumuelewa ukizingatia kamba yenyewe ilikuwa na muonekano wa hirizi.
Kwavile sasa ile kamba haikuwepo tena kiunoni mwake, akaona sasa ni wakati muafaka kwake kwenda kujaribu ukizingatia Fredy mwenyewe ndiye aliyetaka na kumuita.
Mida ilipofika, Sabrina alijiandaa na kwenda kumuaga mama yake
"Haya wapi sasa?"
"Naenda kwa rafiki yangu mama"
"Sabrina, Sabrina. Kuwa makini mwanangu na hizo safari zako zisizoeleweka"
"Usijali mama, niko makini"
Kisha akamuaga na kuondoka.
Safari ilikuwa ni moja kwa moja alikopanga kukutana na Fredy.
Njiani akakutana na mmama mmoja, yule mmama alipita karibu na Sabrina kisha akacheka.
Sabrina akamuangalia yule mmama na kumshangaa kuwa kilichomchekesha ni kitu gani, kisha yule mmama akamwambia Sabrina
"Na bado"
Halafu akaondoka, Sabrina alikuwa na mshangao tu pale aliposimama kwani hakumuelewa kabisa yule mmama.
Wakati anaendelea na safari, wazo likamjia. Taswira ya yule mmama ikamji kuwa ni kati ya wale watatu aliowaona ndotoni ambapo bado anamashaka kuwa ni ndoto au ni ukweli. Ila kwa ile hali ilivyoonekana akapata jibu kuwa ile haikuwa ndoto tu bali ni ukweli mtupu.
Akaamua kuendelea na safari yake ingawa mawazo yaliendelea kuitafuna akili yake.
Alifika mahali walikopanga kukutana na Fredy, kisha Sabrina akampigia simu Fredy ili ajue alipo
"Nishafika Fredy uko wapi?"
"Ingia moja kwa moja ndani, chumba namba tano"
Sabrina hakujishauri sana, alipokata simu tu akaelekea ndani hadi kwenye chumba alichoelekezwa na Fredy.
Alipofika alifungua mlango na kumkuta Fredy amejilaza kitandani.
Moja kwa moja Sabrina alimuuliza Fredy,
"Mbona umejilaza hivyo?"
"Wee njoo tu"
Sabrina akasogea hadi alipo Fredy na kukaa huku mapigo yake ya moyo yakienda kwa kasi sana, hata Fredy aligundua hiko kitu kutoka kwa Sabrina.
Fredy akainuka na kwenda mlangoni kisha akafunga vizuri ule mlango kwa funguo na kurudi kukaa karibu na Sabrina, kila alipomsogelea ndivyo mapigo ya moyo ya Sabrina yalivyozidi kwenda kwa kasi ya ajabu.
Fredy akainua mkono wake na kumshika Sabrina kwenye kifua chake, karibia na mapigo ya moyo.
"Mbona moyo wako unadundadunda sana?"
Sabrina hakujibu chochote zaidi ya kumtazama tu Fredy.
Kisha Fredy akajilaza tena chali na kumwambia Sabrina
"Jilaze kama mimi"
Sabrina bila kubisha nae akajilaza chali, halafu Fredy akakaa na kumfunua Sabrina blauzi yake na kuanza kushika kiuno chake, Sabrina alijihisi kusisimka mwili mzima kwavile alivyokuwa akishikwa.
Gafla Fredy aliacha kumshika Sabrina na kumuuliza
"Kamba yako ya kiunoni iko wapi?"
Sabrina akashtuka baada ya kugundua kwamba Fredy anakumbukumbu juu ya ile kamba ya kiunoni mwake.
Sabrina alikaa na kumuangalia Fredy kisha akamjibu
"Sijui"
Fredy nae akamwambia Sabrina
"Ila mi najua"
Kisha Fredy akajilaza chali na kumwambia tena Sabrina
"Nifanye kama nilivyokufanya wewe"
Sabrina akaogopa, ila akajaribu na kumfunua shati Fredy.
Hapo Sabrina alishtuka sana kwani ile kamba ilionekana kwenye kiuno cha Fredy.
Ila kabla Sabrina hajafanya chochote cha zaidi, yule bibi ambaye alimfunga kamba hiyo Sabrina alitokea mbele yao.
Ila kabla Sabrina hajafanya chochote cha zaidi, yule
bibi ambaye alimfunga kamba hiyo Sabrina alitokea
mbele yao.
Sabrina akashtuka sana kumuona yule bibi sababu alishakufa kwa muda mrefu.
Muda huo, Fredy alikuwa kama mtu aliyepitiwa na usingizi mzito kwani alikuwa hadi akikoroma kwa muda mfupi tu.
Yule bibi alikuwa akimtazama tu Sabrina, kisha akainua mkono wake na kunyoosha kidole chake mpaka kwenye kiuno cha Fredy kisha ile kamba ikatoka kwenye kiuno cha Fredy na kuhamia kwenye kiuno cha Sabrina.
Muda huo Sabrina alijikuta akiongea kwa nguvu
"Naomba unitoe hii kamba"
Yule bibi akajibu,
"Siwezi kukutoa kwani ukiitoa hiyo kamba utateseka sana kama usiku wa jana. Ila kuna sharti moja sikukupa"
"Lipi hilo?"
"Hutakiwi kukutana kimwili na kijana yoyote yule"
Kisha yule bibi akatoweka na kumfanya Sabrina ashtuke sana.
Sabrina akajishika kiunoni na kujikuta na ile kamba ambayo hakuitaka siku zote.
Akamuangalia Fredy pale kitandani ambaye aliamka na kuwa kama mtu anayeshangaa kisha akamuuliza Sabrina
"Kwani kimetokea nini Sabrina?"
"Sijui na siwezi kuelezea"
Sabrina akatoka nje na kuondoka kwavile hakujielewa kabisa, hakuielewa akili yake kabisa.
Alipofika kwao, alimkuta mama yake akiongea na Sakina.
Akawasalimia, kisha akataka kumuuliza kuhusu kutokupatikana kwake ila alijiona akisita kuongea chochote, na badala yake akajikuta akiamua kwenda chumbani kwake tu.
Fredy akiwa kwenye kile chumba cha kulala wageni bado alijishangaa na kujiuliza maswali mengi bila ya majibu yoyote, akakumbuka maneno ya bibi yao alipokuwa akimwambia Francis kuwa yule Sabrina sio mwanamke wa kuwa naye
"Inawezekana bibi aliongea maneno ya ukweli, najuta kumfahamu huyu mwanamke kwakweli ingawa moyo wangu bado unampenda sana"
Fredy aliinuka naye na kutoka kwenye kile chumba walichokuwa na Sabrina.
Wakati Fredy anaondoka, akashangaa gafla akiitwa na yule muhudumu wa ile nyumba ya kulala wageni
"Kaka samahani, nakuomba mara moja"
Ikabidi Fredy arudi na kusikiliza wanachomuitia.
Alipofika karibu, yule muhudumu alikuwa amebeba mkoba wa kike na kumkabidhi Fredy
"Mmesahau mkoba wenu kaka"
Fredy akauangalia kwa makini na kugundua kuwa ule ni mkoba wa Sabrina, hivyobasi akauchukua na kwenda nao kwao ili ajipange siku ya kuupeleka huo mkoba kwa muhusika.
"Nitampelekea kesho huu mkoba"
Ila Fredy hakuelewa imekuwaje hadi Sabrina asahau mkoba wako.
Sabrina alipokuwa chumbani kwake, akakumbuka kuhusu mkoba wake na kuamua kumpigia simu Fredy ili kujua kama aliuacha kule au ni vipi.
"Fredy, eti niliacha mkoba wangu kule"
"Ndio, ila nitakuletea kesho Sabrina usijari"
"Naomba unitunzie Fredy, huo mkoba ni wa muhimu sana kwangu"
"Usijali Sabrina nitautunza"
Walipomaliza mazungumzo, bibi yake Fredy alikuwa pembeni na alisikia kila kitu ambacho Fredy alikuwa akikizungumza.
"Mkoaa gani huo Fredy?"
"Ni mkoba wa Sabrina, kuna mahali aliusahau"
"Basi nipe mie niutunze mpaka hiyo kesho kwamaana nyie wanaume huwa hampo makini sana"
Fredy akampa bibi yake ule mkoba na kuondoka.
Sabrina hakujisikia hata kula kwa siku hiyo zaidi ya kulala tu ili aweze kupunguza mawazo aliyokuwa nayo juu ya mambo yaliyomtokea na kile alichoambiwa na na yule bibi alipowatokea.
Muda mwingi taswira ya yule bibi ilicheza katika akili yake, akatamani hata siku zirudishwe nyuma ili iwe ile siku aliyopelekwa kwa yule bibi na kufungwa kamba kiunoni ili aweze kuikataa siku hiyo katika maisha yake. Ila kama ilivyo, maji yakishamwagika hayazoleki. Siku nayo ikipita imepita, ndiyo iliyomtesa katika maisha yake ya sasa.
Usingizi ulimpata kwa shida sana kwani muda mwingi alikuwa na mawazo.
Kulipokucha, Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka katika nyumba yao na moja kwa moja alienda kukaa sebleni na kujiinamia kwa mawazo aliyokuwa nayo.
Mama yake alimkuta na kujaribu kumuuliza tena
"Una tatizo gani mwanangu?"
"Sina tatizo mama"
"Hivi kwanini huwa hutaki kusema? Unajua kukaa na mawazo sana ni dhambi? Kwanini hutaki kuniambia mama yako ili niweze kukushauri mwanangu jamani!"
Sabrina alimuangalia mama yake kwa huruma, huku akitamani kumwambia ukweli wa mambo ila mara zote alihisi kama atasema ukweli basi mama yake anaweza kumfikiria kwa mabaya.
Bibi yao na wakina Fredy, alimuita Francis na kumwambia
"Mkoba huu ni wa Sabrina"
"Umeutoa wapi bibi?"
"Alikuwa nao Fredy, kuna mahali Sabrina aliusahau. Sasa mimi nataka wewe ndio ukampelekee Sabrina"
"Kwanini mimi bibi? Na mbona umemjua Sabrina kiasi hicho wakati ulimuona mara moja tu tena ukiwa mgonjwa!"
"Wewe mpelekee huu mkoba, ukirudi nitakwambia kila kitu. Ila ufate nitakacho kwambia wakati unaenda"
Francis akakubali, kwani cdo alikuwa anampenda Sabrina ingawa mara ya mwisho alimfukuza kama mbwa na ubaya ni kwamba hakujua chochote kilichoendelea kati ya Fredy na Sabrina.
Hakujua kama walifahamiana zaidi kwa siku zote hizi ambazo yeye ameshindwa kuwasiliana na Sabrina.
Francis alijiandaa na kuianza safari ya kwenda kwa wakina Sabrina kwa lengo la kumpelekea ule mkoba na vilevile kwa lengo la kumuona kuwa anaendeleaje ingawa alishaambiwa na bibi yake kuwa mwanamke huyo hafai kuwa naye, na ndiomana Francis huwa anamshangaa bibi yake kuwa anamjua vipi Sabrina.
Francis alienda mpaka kwakina Sabrina, na mtu wa kwanza kuonana naye ilikuwa ni mama wa Sabrina.
Alishangaa kuona yule mama akimkumbuka
"Khee mbona ulipotea wewe kijana?"
"Majukumu mama, je Sabrina nimemkuta?"
"Yupo ndani ndio, ngoja nikuitie"
Joy alimuita binti yake, na moja kwa moja Sabrina akatoka nje ili tu kujua ni kwanini anaitwa.
Sabrina akashangaa kumuona Francis mbele ya macho yake, akajikuta akitamani kumkumbatia.
Wakati yeye akitamani hivyo, hata Francis naye alikuwa akitamani hivyo hivyo na kujikuta wamekaribiana na kukumbatiana, kisha maongezi mengine yakaendelea
"Nimekuletea mkoba wako Sabrina"
Sabrina akashtuka kwani hakujua kama Fredy angempa Francis ule mkoba aulete.
Francis alimpa Sabrina mkoba ukiwa ndani ya mfuko wa plastick, Sabrina alipokea na kumshukuru Francis
"Asante sana"
"Ila unajua nilipoutoa?"
Sabrina alinyamaza kimya kwa muda, kisha akamjibu
"Sijui, niambie umeutoa wapi?"
Francis akacheka na kusema
"Najua unanizuga tu hapa, ngoja niende ila badae nitakutafuta Sabrina nina shida sana na wewe"
"Poa, hakuna tatizo karibu sana"
Kisha wakaagana na Francis akaondoka.
Sabrina alienda chumbani kwake na kuweka ule mkoba, mawazo yakamuhama sasa.
Yakahamia kwa Francis, alijiona wazi akimpenda Francis zaidi ya alivyojihisi kumpenda Fredy.
Alikaa na kujiuliza,
"Hivi ni nani nimpendaye kati ya Francis na Fredy? Inawezekana hawa ni ndugu, itakuwaje sasa? Ila kama Francis akiamua kuwa na mimi tena basi ni bora nikawa mbali na Fredy kwavile Fredy alishanikuta nikiwa na mahusiano na Francis tayari."
Mapenzi yalionekana kumchanganya sasa baina ya watu hawa wawili, ila kila alipoikumbuka ile sauti ya yule bibi kuwa haruhusiwi kulala na mwanaume yeyote yule, alinyong'onyea.
Jioni ya siku hiyo alienda mahali na kukutana na Francis ambaye alimuomba msamaha kwa yale aliyomwambia.
"Nisamehe Sabrina, bado nakupenda"
"Hata na mimi nisamehe, kwani bado nakupenda"
Wakakumbatiana kwa furaha bila ya kujali ni kwanini waligombana.
Kisha wakaagana huku wakiwa na nyuso za furaha, ambazo zimejaa mapenzi.
Sabrina alirudi nyumbani kwao, alipofika nje alikutana na mama yake aliyemwambia
"Tena afadhari, kuna mgeni wako ndani huko"
"Mgeni gani? Kwani baba yupo?"
"Baba yako hayupo, kasafiri tena ila kwavile wewe una mambo mengi akashindwa kukuaga. Kuhusu mgeni, ingia mwenyewe ndani utamuona"
Sabrina alisononeka kuona baba yake ameondoka bila ya kumuaga, kwahiyo akaingia ndani kwa msononeko.
Akamkuta Fredy akiwa ndani kwao, na kumshangaa
"Kheee Fredy!"
"Nini sasa Sabrina jamani!"
"Huogopi kuja kwetu bila taarifa?"
"Niogope nini kwa mkwe wangu?"
Sabrina akamuangalia tu Fredy, kisha akamfata alipokaa.
Akatamani kumwambia ukweli kuhusu yeye na Francis, ila alishindwa kwani alijua lazima Fredy angejisikia vibaya.
"Sabrina, unafanya mambo mengi sana yasiyoeleweka. Ila mi sijali sababu nakupenda sana Sabrina, jana uliondoka bila hata ya kuniaga hadi ukasahau mkoba wako mule ndani. Ila kwa mapenzi yangu, nikauchukua na kwenda kukutunzia nyumbani....."
Sabrina akamkatisha Fredy hapo na kumwambia
"Na kwa mapenzi yako, ukaamua kumpa Francis aniletee"
Fredy akashangaa sana, ila akili yake ikamwambia kuwa ni bibi yao tu ndio aliyefanya hivyo.
"Kwahiyo, Francis ndiye aliyekuletea mkoba?"
"Inamaana hujui au?"
"Sijui ndio"
"Hebu niambie kwanza, je kuna undugu kati yako wewe na Francis?"
"Hayo nitakwambia tu, ila naomba uniletee huo mkoba wako mara moja nione"
Sabrina hakusita, moja kwa moja akaenda chumbani kwake kwa lengo la kuutoa ule mkoba ili akampe Fredy aweze kuuona.
Francis nae aliporudi kwao ile jioni, moja kwa moja bibi yake alimuita na kumuuliza
"Ule mkoba uliufikisha kwa Sabrina?"
"Ndio bibi"
"Hukuufungua kweli wewe!"
"Siwezi kufanya kitu ambacho umenikataza tayari, siwezi kabisa bibi yangu. Ila nimerudiana na Sabrina"
"Kwanini umerudiana nae? Yani ndio hapo unaponikera wewe mtoto"
"Bibi, nampenda sana Sabrina. Alikosea ndio ila nimemsamehe, nampenda kwakweli"
"Hakuna shida, je unaweza kuwa na mahusiano na mwanamke asiyeona?"
"Kivipi bibi?"
"Namaanisha kipofu"
"Mmmh! Mie sitaki mwanamke asiyeona bibi, na ndiomana nikampenda Sabrina"
"Kwasababu anaona, si ndio!"
"Ndio bibi, na macho yake yanavutia sana"
"Ila weka akilini jambo hili, hata binadamu anayeona anaweza kuwa kipofu kwa sekunde chache tu"
"Mbona sijakuelewa bibi?"
"Ndiomana nikakutuma wewe, kwavile ningemtuma Fredy angeharibu kila kitu yule na huwa hajielewi kabisa"
"Kwani angefanyaje?"
"Angechungulia ule mkoba wa Sabrina"
"Kwani ulikuwa na nini?"
"Ulikuwa na vitu vya kike ambavyo hairuhusiwi mwanaume kuviona. Usipende sana kudadisi mambo, unaweza ukawa kichaa bure"
Francis alichukua muda mrefu kuyatafakari maneno ya bibi yake bila ya jibu la aina yoyote ile.
Mwisho wa siku aliacha kama mambo yalivyo na kuendelea na mambo yake mengine.
Sabrina, alichukua ule mkoba wake na kwenda kumpa Fredy.
"Kheee ndio alikuwekea kwenye rambo kabisa!"
"Ndio, hivyo hivyo alivyouleta"
Fredy akautoa ule mkoba kwenye rambo na kuupakata, kisha akataka kuufungua.
Sabrina akamzuia,
"Sasa unataka kitu gani humo Fredy?"
"Lazima nione, labda Francis kakuwekea vibarua vyake humu"
"Mmmh Fredy acha wivu bhana"
"Siwezi hadi nione kilichopo ndani"
Ikabidi Sabrina amuachie Fredy ule mkoba aangalie sababu alijua wazi kuwa hakuna chochote cha ajabu kwenye mkoba wake.
Fredy akafungua ule mkoba, kikatoka kitu kama moshi na kuyakumbuka macho ya Fredy.
Fredy akaachia ule mkoba na kupiga ukelele wa nguvu kisha akaanguka chini.
Fredy akafungua ule mkoba, kikatoka kitu kama
moshi na kuyakumba macho ya Fredy.
Fredy akaachia ule mkoba na kupiga ukelele wa
nguvu kisha akaanguka chini.
Sabrina akamuita mama yake aliyekuja mbio sana kutokana na ile kelele aliyoisikia kutoka ndani kwake.
Alipoingia alishangaa kumuona Fredy akiwa chini
"Imekuwaje Sabrina?"
"Sijui mama, ni gafla tu"
Mama huyu akaenda kuleta maji na kuanza kumwagia Fredy, hadi Fredy akazinduka.
Ila alipozinduka, alikuwa akifikicha macho yake na kudai kuwa yanamuwasha sana.
Joyce alichukua yale maji na kujaribu kumnawisha Fredy kwenye macho, lakini bado Fredy alilalamika kuwa macho yanamuwasha tena sana tu.
Aliyafikicha kwa muda, huku nao wakijaribu kuendelea kumpa huduma ya kwanza ambayo kwao ilikuwa ni kumuosha kwa maji.
Baada ya muda kidogo, muwasho ulipungua kwenye macho ya Fredy, naye akajaribu kuyafumbua ili aone lakini hakuona kitu chochote kile.
"Jamani sioni, sioni jamani"
Wakajaribu kufanya kila kitu walichoweza lakini bado Fredy aliendelea kulalamika kuwa hawezi kuona chochote.
Joyce aliamua kumbembeleza Fredy ili atulie na wajue cha kufanya kwa wakati huo.
Fredy akatulia kiasi na kumpa mama Sabrina nafasi ya kuongea
"Kwani imekuwaje Sabrina?"
"Hata mi mwenyewe sielewi mama, yani nashangaa tu hapa"
"Hebu nipe mlolongo mzuri wa matukio nikuelewe"
Sabrina akamwambia mama yake kuhusu ilivyokuwa muda mfupi uliopita.
"Mbona sielewi? Kwani hiyo pochi ina nini?"
"Haina kitu mama"
Kisha Sabrina akachukua ile pochi na kubwaga vyote vilivyokuwemo ndani yake.
"Si unaona mwenyewe mama, hii pochi haina chochote yani hata mi mwenyewe nimeshangaa tu hapa"
"Mmh makubwa haya mwanangu"
Wakaanza kujadiliana jinsi ya kumrudisha Fredy kwao na jinsi ya kuwataarifu ndugu zake kuhusu yaliyotokea.
Basi Joy akainuka na kumuacha mwanae Sabrina ili amuulize vizuri namna watakavyomrudisha kwao.
"Kwakweli Fredy mi nimechanganyikiwa hapa, sasa tutakupelekaje kwenu?"
"Mpigie simu Francis ili aje kunichukua"
Sabrina akakubaliana na hilo kwa Fredy, kisha akaenda kumwambia mama yake ambaye pia aliafikiana kuhusu hilo na kuamua kumpigia simu Francis ili aje kumfata ndugu yake.
"Kwani kuna nini Sabrina?"
"Njoo tu utaona hukuhuku, tafadhari njoo upesi"
Ingawa Francis hakujua anaitiwa kitu gani ila ile kauli ya kumwambia aende upesi ilimpa wasiwasi na kumfanya ajiandae haraka na kuianza safari.
Francis alipofika kwakina Sabrina, alikaribishwa ndani na kushangaa kumuona Fredy akiwa pale ndani.
Moja kwa moja Francis akauliza
"Vipi jamani!"
Fredy akajibu,
"Sioni Francis, sioni mwenzio"
"Imekuwaje kwani Fredy?"
"Nipeleke nyumbani tafadhari, nitakueleza tukifika nyumbani"
Ikabidi Francis asaidiane na Sabrina katika kumpeleka Fredy nyumbani kwao.
Walipofika, walimpeleka Fredy chumbani akapumzike.
Ikabidi Sabrina amuage Fredy,
"Tafadhari usiniache Sabrina"
"Usijali Fredy, sitakuacha kamwe"
"Nakupenda sana Sabrina, tena sana"
Kisha Francis akamfata Sabrina kuwa watoke ili amsindikize.
Francis akamsikia Fredy akimwambia Sabrina
"Tafadhari Sabrina, nibusu kabla hujaenda"
Sabrina akainama na kumbusu Fredy, kisha akamuaga na kutoka nje na Francis.
Ila kile kitendo cha Sabrina kumbusu Fredy kilimuumiza sana na kujikuta akipatwa na wivu juu yao.
Walipotoka nje akamuuliza
"Kwani kuna nini kinaendelea kati yako na Fredy?"
Sabrina alishindwa kujibu kwavile hakuelewa ni kitu gani atamwambia Francis ili aweze kumuelewa.
"Naomba umuulize Fredy mwenyewe"
"Niambie vizuri Sabrina, si unajua kama nakupenda! Halafu Fredy ni ndugu yangu, ila kwanini unataka kunifanyia hivi Sabrina?"
Sabrina hakuwa na jibu na akajua wazi kama ataendelea kuongea kuhusu hilo na Francis basi lazima kuna ugomvi utatokea tu, hivyobasi alipoona gari inapita alisimamisha na kupanda ili tu kuweza kuepukana na marumbano na Francis ukizingatia usiku ulishakuwa mkubwa.
Sabrina akiwa kwenye lile gari, alikaa na kijana mmoja aliyemsikia kwa jina moja ambalo wenzie walikuwa wakimuita.
Kijana huyo alikuwa akiongea sana kwenye lile gari, na kila alipoongea aliwafurahisha watu wengi akiwemo na yeye mwenyewe Sabrina.
Na walipofika kwenye kituo, Sabrina alijikuta akishuka pamoja na yule kaka. Ikabidi amuongeleshe tu,
"John!"
"Kheee dada umenijuaje?"
"Nimesikia watu wakikuita hivyo kwenye gari, nimeyapenda sana maongezi yako"
"Kumbe eeh! Nipe namba zako basi"
Sabrina hakuona tatizo kumpa huyu kijana namba zake ili waweze kujadiliana zaidi na zaidi.
Kisha wakaagana na kuondoka.
Sabrina alipofika nyumbani kwao alimsikia mama yake akifanya maombi, haswaa alimsikia akimuombea pia na yeye kuwa arudi salama.
Alikaa pale nje na kumsikiliza mama yake kwa makini zaidi hadi alipomaliza yale maombi ndipo naye akaingia ndani.
"Sabrina, mgonjwa anaendeleaje?"
"Nimemuacha pale kwao amelala mama"
"Amegoma tena kuhusu hospitali?"
"Amekataa kabisa, anaamini kuwa atapona tu"
"Ndio, Mungu mkubwa hata mi naamini kuwa atapona tu"
"Basi vizuri mama, ngoja niende chumbani kwangu"
Sabrina aliingia chumbani kwake, ila kabla hajafanya chochote alipigiwa simu na yule John aliyekutana nae kwenye basi.
"Hivi jina lako unaitwa nani?"
"Naitwa Sabrina"
Basi John akaanza kumwambia Sabrina vitu vingi vya masikhara na kumfanya Sabrina acheke sana kutokana na kile ambacho John alikuwa anamwambia hadi pale alipokata simu, Sabrina alikuwa ameshacheka sana hadi machozi yakamtoka kwa kucheka na kujikuta akiongea peke yake
"Yani huyu kijana ana vituko sana dah, nimecheka hadi raha"
Kisha akaenda kuoga na kurudi kulala.
Akiwa usingizini, akamuona yule bibi wa wakina Francis akiwa ameushika ule mkoba wake aliousahau katika nyumba ya kulala wageni.
Kisha akaifungua na kuweka vitu vyenye asili ya ungaunga halafu akawa kama ananenea vitu fulani kwenye ule mkoba.
Kisha Sabrina akajiona akishika ule mkoba, vikatoka vitu kama moshi kwenye ule mkoba na kuelekea kwenye macho yake, kisha akahisi macho yakimuwasha sana na alipokuja kufumbua alikuwa ni kipofu tayari.
Sabrina akanza kulia bila ya kujua kama anaota, hadi mama yake akakimbilia chumbani kwa Sabrina huku akijua kuwa binti yake kapatwa na matatizo.
Alimkuta akiwa kalala chali huku machozi yakimbubujika
"Wee Sabrina, wee Sabrina"
Sabrina akashtuka na kujifikicha macho,
"Una matatizo gani wewe mtoto?"
"Kumbe naona mama!"
"Kwani ulikuwa huoni! Mbona una mambo ya ajabu wewe mtoto?"
Alitafakari ndio akagundua kwamba alikuwa anaota.
"Samahani mama, ni ndoto tu"
"Aaah! Una kichaa sana wewe mtoto wangu, muone na akili zake zilivyofupi. Ngoja nikamalizie usingizi wangu mie"
Akatoka na kwenda chumbani kwake huku akijisemea
"Najuta kumpa mwanangu jina la shangazi yake"
Kulipokucha, Sabrina akaamka na mawazo mapya kichwani mwake kwani ile ndoto aliona kama vile imempa mjibu ya maswali kadhaa katika akili yake.
"Inawezekana ule mkoba wangu ulifika kwa yule bibi na ndiomana nimeletewa na Francis, ni lazima yule bibi alifanya kitu kibaya kwenye ule mkoba ili aweze kunidhuru mimi, sasa kamdhuru mjukuu wake mwenyewe! Mmh sijui itakuwaje sasa. Inamaana Fredy kawa kipofu badala yangu! Lazima nifanye kitu cha kumsaidia"
Sabrina alijiona kuwa yupo njiapanda kwasasa na haya mambo kwani hakuyatarajia.
Mchana wake alienda kwa Sakina, alikuwa na mengi ya kumueleza ukizingatia ni siku kadhaa zimepita bila ya wao kuongea chochote.
"Bora umekuja Sabrina mdogo wangu"
"Kuna nini dada?"
"Nina khabari mbaya kuhusu hiyo kamba yako ya kiunoni"
"Mmh! Hebu niambie vizuri dada, maana hata sielewi kitu hapa."
"Ni hivi, mimi niliondoka hapa kwenda kuulizia kuhusu hiyo kamba yako kwa watu wenye uzoefu nazo"
"Eeh wamesemaje?"
"Ni hivi mdogo wangu, kwavile aliyekufunga hiyo kamba alishakufa na hakuna wa kukufungua tena basi lazima wewe uliyefungwa hiyo kamba upate madhara"
"Mmh yapi hayo, niambie dada jamani"
Huku moyo wa Sabrina ukienda kwa kasi sana, Sakina aliendelea kumueleza
"Kwanza kabisa, hutakiwi kukutana kimwili na mwanaume yoyote yule. Hairuhusiwi mwanaume yoyote kuiona hiyo kamba yako, na siku ile yule mkaka aliamka ni kwa bahati tu. Pia, hiyo kamba haitakiwi kukatwa na mtu yeyote yule labda kama itatokea siku ikakatika yenyewe huo ndio utakuwa uzima "
"Jamani dada, naishije mimi sasa kwa mtindo huo? Kwahiyo sitakiwi kuwa na mchumba? Kwahiyo mimi sitaolewa wala kuwa na watoto?"
"Ndio hivyo Sabrina, kwahiyo kuwa makini sana. Na ikitokea mtu akakukata hiyo kamba jua kwamba mtu huyo atapata madhara makubwa sana, vilevile kila mwanaume utakayelala nae atakufa na ukibeba mimba lazima itatoka"
Sabrina aliogopa sana na kutetemeka huku machozi yakimtoka, hakutaka kuwa na hali ya namna hiyo katika maisha yake kwani alipenda kuwa kama wanawake wengine duniani.
"Sasa nitafanyaje dada?"
"Cha msingi ni kuombea hiyo kamba ikatike yenyewe ili uwe huru"
"Itabidi niende tena kwenye lile kaburi la yule bibi ili nimuombe anipunguzie adhabu hii au hata aikate kimiujiza"
"Labda tufanye hivyo mdogo wangu, basi kesho asubuhi na mapema twende huko"
"Sawa dada"
"Ila kuwa makini sana na hiyo kamba, jihadhari mtu yeyote asije akaiona hiyo kamba Sabrina. Sawa eeh!"
"Hata hivyo nipo makini sana, hata mama tu ndani kwetu hajui kama nipo hivi"
Sabrina akakubaliana na Sakina juu ya mpango wao wa siku ya kesho wa kwenda kwenye kaburi la yule bibi.
Sabrina alirudi nyumbani kwao akiwa amepunguza kiasi kidogo cha mawazo na kuongeza kiasi kingine ambacho hakujua kitaishia wapi.
Hakujua hatma yake na ile kamba yake ya kiunoni, kwavile alikuwa na mawazo mengi sana, akama ni vyema ampigie simu yule John mwenye vituko ili aweze kucheka na kufurahi.
Akaipiga ile simu, ila haikupokelewa na John kama alivyotarajia bali ilipokelewa na sauti ya kike
"Samahani, John yupo?"
"Unamuulizia John wewe kama nani?"
Sabrina akaona kuwa itazuka shari pale na kuamua kukata ile simu huku akijisemea
"Kumbe huyu John ana mwanamke, kwanini hakuniambia sasa?"
Alihisi kama moyo ukimuuma vile na kujigundua kuwa ameingiliwa na mdudu wivu kwa John wakati si mpenzi wake.
"Ngoja niachane na mawazo ya kijinga ilihali najua wazi kwamba siwezi kuwa na mpenzi kutokana na matatizo niliyonayo, hata najishangaa kuwa naanzaje kupenda jamani"
Hali ya kuwa hivi ilimsumbua sana Sabrina na kujikuta akitamani kesho yake ifike na waweze kwenda huko makaburini na pengine ukawa ndio ukombozi wake kwenye maisha.
Usiku wa siku hiyo alikuwa akiwaza tu kuhusu kamba yake ya kiunoni
"Ni kweli inanisaidia kuona wachawi, na pia inanisaidia kupambana nao lakini kwanini initese hivi!! Na mbona kabla sijawa nayo hao wachawi hawakunisumbua?"
Alikuwa akiwaza tu muda wote huku akiamini kwamba akienda kule makaburini kulia na kumuomba yule bibi basi atasalimika na kusahau kwamba ameshawahi kufanya hivyo kabla lakini tatizo bado liliendelea tena kwa makubwa zaidi kila kukicha.
Usingizi ulimpitia akiwa bado na mawazo.
Wakati yupo usingizini, alikuja yule mmama waliyekutana nae mchana. Kama kawaida Sabrina alishtuka na kuanza kuangaliana nae,
"Kwani mnataka nini kwangu nyie?"
"Tunataka uwe mshirika mwenzetu"
"Sitaki, na muondoke"
"Nimekuja peke yangu leo, sina nia mbaya ila nataka uwe mshirika mwenzetu"
Sabrina akainuka huku akitetemeka, akachukua maji yaliyokuwepo pembeni yake na kumwagia yule mchawi, muda huo huo yule mchawi akatoweka.
Sabrina akashangaa kuona kuwa hata maji nayo ni dawa, ila hakuweza kulala tena hadi palipokucha.
Aliamka na kwenda kuoga ili kujiandaa kwaajili ya safari aliyopanga na Sakina.
Wakati anaanza kujiandaa tu, mama yake akaingia gafla chumbani kwake bila ya hodi na moja kwa moja alimshangaa Sabrina kiunoni
"Nini hiko cheusi kwenye kiuno chako Sabrina?"
Sabrina akashtuka sana na kuchukua khanga ili kujifunika.
Kama kawaida ya Joy, hakutaka kukubaliana na kujifunika kwa mwanae.
Hivyo basi akamfata na kuitoa ile khanga kwa nguvu,
"Khee una kamba kiunoni Sabrina! Tena nyeusi! Mambo gani hayo ya kishirikina Unayaleta ndani kwangu!"
Akamfata karibu, kisha akachukua mkasi uliokuwepo kwenye meza ya Sabrina na kuikata ile kamba.
Akamfata karibu, kisha akachukua mkasi
uliokuwepo kwenye meza ya Sabrina na kuikata
ile kamba.
Sabrina akapigwa na butwaa kwani kilikuwa ni kitendo cha gafla kwa mama yake kuikata ile kamba.
Alitamani apige makelele kwa kulia kwani aliona mambo yake yote yakiharibika, hakutegemea kama mama yake angefanya vile alivyofanya.
Sabrina alikaa chini huku machozi yakimtoka
"Yani unalia sababu ya hii kamba Sabrina? Mbona unaniletea mambo ya ajabu wewe mtoto jamani!"
Sabrina alikuwa kimya kabisa huku machozi yakimtoka, ila Joy hakujua ni kwanini mtoto wake alikuwa akitokwa na machozi kiasi kile, hakujua kama ile kamba ilikuwa na maana kubwa sana kwenye kiuno cha mwanae.
"Sabrina, hivi wewe mtoto una kichaa au ni kitu gani jamani? Unajua sikuelewi! Yani sikuelewi kabisa. Eti unalia na kulia sababu ya huo uchafu nilioukata, mtoto mwehu kweli wewe"
Joy akatoka chumbani kwa mwanae na kwenda kuendelea na kazi zake zingine.
Sakina alipoona muda unapita tu bila ya Sabrina kutokezea, akaamua kwenda kumfata mwenyewe.
Na alipofika alikaribishwa na Joy, wakasalimiana na kumuulizia Sabrina.
"Asubuhi yote hii Sabrina wa nini?"
"Kuna mahali nilipanga nae kwenda ila sijamuona hadi sasa"
"Wewe si ndio msiri wake! Nenda huko chumbani kwake ukamuangalie anavyolia lia"
Sakina akashangaa kumuona Joy akiongea kwa jazba kiasi kile, akajua kwa vyovyote vile lazima kuna kitu Joy amekijua kuhusu Sabrina.
Akaongoza moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Sabrina, alimkuta kajifunga khanga huku amejiinamia na machozi kumtoka.
"Nini tatizo Sabrina mdogo wangu jamani?"
Sabrina akamuonyesha Sakina ile kamba pale chini na kumfanya Sakina nae ashtuke kisha akamuuliza kuwa imekuwaje.
"Mama kaikata na mkasi"
"Ameionaje?"
Sabrina akamuelekeza Sakina ilivyokuwa
"Nilijua tu kuwa mama yako akijua itakuwa balaa kama hivi, yani mamako kaongeza tatizo juu ya tatizo hata sijui itakuwaje jamani!"
"Nisaidie dada, nitafanyaje mimi jamani!"
"Basi ngoja tufanye kitu, najua wewe haupo sawa kwasasa. Hivyobasi ngoja mimi niende mahali kuulizia vizuri kuwa tufanyaje kisha nitakwambia kila kitu mdogo wangu. Punguza mawazo, mimi nipo kukusaidia Sabrina"
"Basi nitashukuru dada"
Sakina akampooza pale Sabrina kisha akamuaga na kuondoka.
Kufika nje, akamuaga na Joy ili aende zake
"Nenda mama, ya kiunoni nimeikata. Nenda ukamletee ya shingoni sasa ili niione vizuri na nitaichoma moto"
Sakina alimuangalia tu Joy kwani alielewa wazi kama akiamua kubishana nae basi atabishana nae hadi siku ya pili.
Akamuaga tena na kuondoka.
John baada ya kusikia mkasa alioufanya mpenzi wake kwa Sabrina akajihisi vibaya na kuamua kumpigia simu Sabrina ili aweze kumuomba msamaha.
Ila ile simu iliita tu bilawake na ndiomana hakutaka kuwasiliana nae tena bila kujua kwamba Sabrina alikuwa na matatizo mengine yaliyomsumbua akili yake tayari.
Sabrina hakujisikia vizuri kabisa siku ya leo, kila alipofikiria masharti ya ile kamba ya kiunoni iliyokatwa hakujua itakuwaje. Hakujua mama yake atapatwa na janga gani baada ya kumkata ile kamba.
Alijihisi vibaya na moyo kumuuma sana kwa mawazo.
Aliisikia simu yake ikiita ila hakujisikia kuzungumza na mtu yeyote wala kumjibu ujumbe mtu yeyote kwahiyo alikuwa akiitazama tu simu yake wakati inaita.
Joy alikaa na kujifikiria sana, alihisi kuwa mwanae ana mapepo na ndiomana amekuwa akifanya mambo ya ajabu.
Akaamua kumpigia simu mchungaji wao na kumueleza matatizo ya mtoto wake.
"Nimekuelewa mama James, nadhani jioni nitafika hapo na nitapenda kuzungumza na huyo binti yako"
"Hakuna tatizo mchungaji, utamkuta tu hapa nyumbani"
"Ila kuna huduma nafanya, kwahiyo itakuwa ni jioni sana"
"Hakuna tatizo, cha muhimu ni ufike tu"
Joy akaona itakuwa afadhari kwa binti yake kuzungumza na huyo mtumishi wa Mungu, kwakuwa matendo yake yalimdhihirishia wazi kuwa mwanae ana mapepo kwani yale mambo ya kujifunga kamba za kichawi kiunoni hayakuwa ya kawaida.
"Yani mtoto wangu ni wa ajabu huyu mmh! Maombi kwake mwiko, yeye na ushirikina tu hata sijui kajifunzia wapi!"
Joy alikuwa akijilalamisha mwenyewe tu bila ya muafaka wa anachokilalamikia kwa muda huo.
Sabrina akaona kujifungia ndani ni kuzidi kujipa mawazo tu, kwahiyo akaona ni vyema hata atoke na kutembea tembea kidogo ili kupoteza mawazo mpaka pale Sakina atakaporudi.
Alitoka na kumuaga mama yake kuwa anaenda kutembea tembea kidogo
"Umepata nguvu ya kuzurulia sasa eeeh!"
"Sio hivyo mama"
"Nini sasa?"
"Siendi mbali mama, nafika hapo kwa rafiki yangu Sia tu"
"Haya wee nenda tu, naona leo hata wakina Sia wamekumbukwa ila uwahi kurudi tu"
"Sawa mama"
Sabrina akaondoka na kwenda kwa huyo rafiki yake.
Alipofika alimkuta rafiki yake na kufurahi sana, walikaa na kuongea mambo mengi sana.
"Sabrina, hivi yule kaka yangu Japhet unamjua?"
"Ndio namjua, kafanyaje kwani?"
"Jamani Sabrina, kaka yangu anakupenda yule yani kafa kaoza kwako"
"Mmh Sia ya kweli hayo!"
"Mie nitakudanganyaje wewe shoga yangu jamani! Kaka yangu anakupenda, tena anakupenda sana Sabrina"
Sabrina alijikuta akitabasamu kwa furaha kwani alikuwa na tatizo kubwa moja, yani yeye akisikia kuwa anapendwa alijihisi kama kupagawa wakati zamani alikuwa hataki hata kusikia kuhusu mapenzi ila siku hizi akiambiwa anapendwa basi anajihisi kama ni malkia pekee kwenye dunia.
Kwahiyo swala la Sia kumwambia kuwa anapendwa na kaka yake lilimfanya asahau matatizo yake kwa muda na kujisikia vizuri,
"Nimpe namba zako? Maana aliniomba mawasiliano yako ili akwambie mwenyewe"
"Mpe tu namba zangu, hakuna tatizo"
"Mmh Sabrina! Je na wewe utampenda?"
"Sijui"
Na kuanza kucheka, Sia akapata jibu kuwa lazima Sabrina nae atakuwa anampenda kaka yake huyo ila tu hakuweza kusema.
Wakaongea mengi sana, na mwisho wa siku Sabrina akaaga na kuanza safari ya kurudi kwao.
Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwao, alipita karibu na mti wa mbuyu.
Mti ule ulikuwa umefungwa kwa pembeni kitambaa chekundu na cheusi, halafu chini yake kulikuwa na kiwembe kimoja na yai ambalo lilikuwa limechorwa chorwa kwa maandishi mekundu.
Sabrina akaogopa sana kupita na kuanza kurudi nyuma nyuma, alipofanikiwa kufika nyuma akaanza kukimbia kwa uoga kwani hakutegemea ile hali kwakweli, hakutegemea kukutana na vitu vya aina ile pale njiani.
Alipofika mbele alisimama na kuhema sana, mara akapita mmama mmoja ambaye hakuwahi kumuona yani ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona.
Yule mmama akamwambia Sabrina,
"Kilichokukimbiza ni nini wakati wewe ni jasiri!"
Sabrina akamuangalia huyu mmama bila ya kumjibu kitu chochote na kuendelea na safari yake, ila yule mmama akamuita Sabrina kwa nguvu
"Wee Sabrina!"
Sabrina akaogopa kuona huyu mama kamuita kiasi hicho, inamaana anamjua. Na kama anamjua basi anamjuaje!
Sabrina akasita kugeuka na kuendelea kutembea kwa nguvu, akaisikia sauti ya yule mmama ikisema
"Unajifanya kiburi eeh!! Utaona sasa"
Sabrina akaogopa sana na kumfanya aanze kukimbia ili aweze kupotea kwenye eneo hilo aliloona kuwa linampa maajabu tu.
Akakimbia sana na kutokea katika mitaa ya kwao, moja kwa moja alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake akiwa ametulia tu
"Leo umewahi kurudi kweli!"
"Ndio mama, nimekuwa mtoto mzuri"
"Haya, mmbea mwenzio katoka hapa sasa hivi anakutafuta"
"Nani huyo mama?"
"Nani mwingine zaidi ya Sakina! Kasema uende kwake haraka uwezavyo"
Basi Sabrina alivyoambiwa hivyo hakutaka kupoteza muda na kugeuka ili aende ila kabla hajaondoka mama yake akamwambia
"Na nilijua tu baada ya ujumbe huo hutotoka hata kuingia ndani na kunywa maji tu, basi uwahi kurudi sababu kuna mtu wa muhimu sana anakuja leo kuzungumza na wewe"
"Sawa mama"
Sabrina alimuitikia mama yake ila bado alikuwa na kinyongo kikubwa sana dhidi yake kutokana na ile kamba ambayo aliikata siku hiyo na kumfanya akose raha ya maisha kwa siku nzima.
Alipofika kwa Sakina, alimkuta nyumbani kwake kama kawaida.
Na moja kwa moja Sakina alianza kumuelezea Sabrina aliyoenda kuyakuta huko alipotoka
"Mwenzangu Sabrina kuna makubwa"
"Niambie dada, si unajua nina matatizo! Sasa unaponiambia hivyo unazidi kunitisha jamani"
"Yani ile kamba haikutakiwa kukatwa na mtu yoyote yule, kwavile mama yako kaikata basi kuna majanga yatampata"
"Mmh majanga gani hayo?"
"Tena kuna mawili, anaweza akapona au asipone kabisa na kama atapona basi kunatatizo litajitokeza kwani anaweza akapararaizi"
Hii habari ilimuumiza sana Sabrina, alijihisi atanywea sasa
"Sasa nitafanyaje dada katika kumnusuru mama yangu?"
"Mmh hata mi mwenyewe sielewi ila..."
Kabla hajaendelea, simu ya Sakina ikaita na kumfanya apokee simu ile na kukatisha yale maongezi huku Sabrina akiwa na hamu ya kujua kitu kwani ile ila ya Sakina ilimfanya ahisi kuwa kuna njia ya wao kukomboka na yale majanga.
Sakina alipomaliza kuongea na ile simu, akamuangalia Sabrina kwa makini sana na kumuuliza swali moja tu
"Ulikuwa wapi leo?"
"Nilikuwa kwa rafiki yangu Sia"
"Ni kitu gani kimekutokea?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku akimuangalia Sabrina kwa makini sana na kumfanya aanze kuingiwa na uoga huku akimuelezea yaliyomtokea wakati anatoka kuonana na Sia.
"Kwahiyo huyo mama aliyekuita hukuweza kumsikiliza?"
"Hata kama ungekuwa wewe dada usingeweza, alikuwa akiniita kwa ukari sana na kuniambia maneno ya kejeli"
"Sasa kwa taarifa yako tu ni kuwa yule mmama ndio alikuwa mtu pekee wa kukusaidia wewe na hilo tatizo lako"
Sabrina akashtuka na kushangaa kuwa mtoa msaada gani anakuwa mkali kiasi kile!
"Mmmh dada, mbona leo unanipa maajabu zaidi?"
"Sio maajabu ila wewe umeshindwa kupata msaada kwa ujinga wako mwenyewe. Kwanini hukutaka kumsikiliza?"
"Basi tena dada, hakuna la kufanya nimeshakosea tayari"
"Kwahiyo kirahisi tu hivyo unaitikia kuwa huna la kufanya kwavile umeshakosea tayari! Hivi unajua matatizo vizuri wewe Sabrina? Angalia jinsi ya kumuokoa mama yako, maana hapa muathirika sio wewe tu bali na mama yako pia"
Sabrina alihisi kichwa chake kuvurugika kwani hakujua ni vipi anapata msaada ikiwa wazi huyo mmama alimkimbia, alijua ni wale washirikina waliokuwa wakimsumbua.
Wakaongea mengi sana na Sakina ila hawakupata muafaka wa jambo lolote lile zaidi ya kuongea tu.
Sabrina alitulia kimya akitafakari cha kufanya na hali ya mama yake pia.
Simu ya Sabrina ikaita, na akaipokea kwa unyonge sana kwani alishakuwa na mawazo tayari
"Japhet naongea hapa"
"Aaah! Mambo vipi?"
"Poa tu, je tunaweza kuonana muda huu?"
Sabrina akajifikiria kidogo kumjibu, kisha akakubali kuonana nae na kupanga pa kukutana na huyo Japhet, kisha akakata simu.
Akamuangalia Sakina na kumuaga
"Unaenda wapi sasa Sabrina?"
"Kuna mahali nataka kwenda nikatulize akili yangu"
"Ila kwa ushauri wangu mie ni bora uka...."
Kabla hajamaliza, simu ya Sabrina iliita tena, naye akapokea
"Francis anaongea hapa"
Akajua moja kwa moja kuwa anataka kumpa hali ya Fredy tu,
"Eeh niambie"
"Nipo hapa kwenu naomba uje haraka"
Halafu akakata ile simu, Sabrina akamuangalia Sakina na kumwambia
"Huyu mwanaume ana wazimu nini? Eti uje haraka, halafu anipe nini! Ngoja nikaonane na huyo Japhet kwanza"
"Ila si yupo kwenu huyo!"
"Ndio yupo nyumbani"
"Basi nakuomba uende nyumbani kwenu kwanza kwani kuna kitu nahisi kuwa hakipo sawa huko"
Sabrina akajiona kama yupo njiapanda, na kuamua kurudi kwao huku akiwa amenuna kabisa.
Alipofika kwao, alimkuta Francis akiwa nje ya nyumba yao, naye alipomuona tu akamkimbilia Sabrina na kumwambia
"Siielewi hali ya mama yako"
Sabrina hakutaka kusikiliza zaidi na kukimbilia ndani kwao ambapo alimkuta mama yake amekaa huku ametambaliza miguu yake na kurudia rudia maneno
"Kamba, kamba, kamba, kamba...."
Sabrina alishtuka kwani mama yake alikuwa kamavile mtu aliyewehuka na alipomuona tu Sabrina, akaacha kusema na kuanguka chini huku akitapatapa.
Sabrina alishtuka kwani mama yake alikuwa
kamavile mtu aliyewehuka na alipomuona tu
Sabrina, akaacha kusema na kuanguka chini huku
akitapatapa.
Sabrina akashtuka zaidi na uoga kumjaa, akaanza kupiga makelele na yeye ili aweze kupata msaada zaidi ila mwisho wa siku akagundua kuwa kelele zake hazisaidii kitu kwani atajaza watu bure tu.
Akaona njiabora ni kwenda kwa yule mmama wa njiani aliyemkimbia ili akamuombe msaada kwani hakujielewa kitu.
Akamuangalia Francis na kumuomba abakie pale na mama yake ili yeye akachukue msaada
"Sabrina, sasa utaondokaje na kumuacha mama yako katika hali kama hii?"
"Ningoje tu Francis, acha niende kwani nimfataye ndio uzima wa mama yangu"
Kisha akatoka nje na kujaribu kukimbia ili aweze kuwahi lile eneo ambalo alikutana na yule mmama.
Sabrina alikuwa anahema sana na giza nalo lilishaanza kuingia ila Sabrina hakuacha kukimbilia eneo la tukio ili aweze kuwahi.
Alipofika lile eneo, akauona ule mbuyu ila hakuona vitambaa vile alivyoviona jana yake.
Akajihisi kuchanganyikiwa, akakaa chini ya ule mbuyu huku akili yake ikikosa muelekeo.
Akiwa amejiinamia vile, akapita mtu mmoja na kumshika kichwa Sabrina, kisha Sabrina akainua kichwa na kumuangalia mtu huyo ni nani.
Alikutana na mzee wa makamo aliyekuwa amevaa nguo ndefu mpaka chini aina ya kanzu na kikofia kidogo kichwani.
Yule mzee akamuuliza "Unafanya nini hapo na giza hili binti?"
"Kuna kitu nangoja"
"Unangoja nini? Mashetani au?"
"Kuna mtu namngoja"
"Unamngoja mtu chini ya mbuyu binti yangu? Hivi unajua kama mibuyu ni nyumba za majini?"
Sabrina akashtuka sana kusikia ni nyumba za majini na kuanza kuogopa.
Yule mzee akamwambia tena Sabrina,
"Mtumainie mwenyezi Mungu, hayo mambo ya kukaa chini ya mibuyu hayatakusaidia"
Kisha yule mzee akaondoka na kumfanya Sabrina ainuke kwenye eneo lile alilokuwa amekaa.
Sabrina akaanza kuondoka taratibu huku akiangalia lile eneo labda apate kumuona tena yule mmama ili aweze kupata msaada.
Akafika mbele na kusimama huku macho yake yakiwa katika eneo lile la mbuyu na akiamini kuwa yule mmama atatokea kumpa msaada.
Wakati amesimama vile, ni kweli yule mmama akatokea ila alikuwa amekasirika sana, lakini Sabrina alishukuru huku akiamini kuwa mama yake atakuwa mzima.
Sabrina akaanza kumfata yule mmama, ila yule mmama alianza kuongea kwa hasira sana,
"Mmeniudhi sana nyumbani kwenu nyie"
Sabrina alimuangalia tu yule mmama kwani hakuelewa ni kitu gani kingendelea
"Nakwambia kwenu mmeniudhi sana, rudi nyumbani kwenu na ukawazuie yote wanayoyafanya"
"Kwani ni nini?"
"Tena uwazuie uwezavyo lasivyo mimi nammaliza mama yako"
Sabrina akaogopa sana kwani hakujua ni kitu gani kinaendelea nyumbani kwao.
Akiwa bado amesimama kwa kusitasita, yule mmama akampazia sauti
"Nammaliza mama yako, nenda wee mwanakwenda"
Ile kauli ya nammaliza mama yako ikamtisha zaidi Sabrina na kumfanya Sabrina apige magoti kwa yule mmama na kuanza kumuomba kuwa asimdhuru mama yake
"Hivi wewe mtoto una akili kweli? Watakaomdhuru mama yako ni hao waliopo nyumbani kwenu, nenda ukawazuie ili mama yako nimuachie lasivyo nammaliza leo leo"
Sabrina aliwaza kuwa ni watu gani hao wanaozuia uponyaji wa mama yake na kuamua kuanza kukimbilia maeneo ya nyumbani kwao ili akawawahi watu hao na kuwazuia ila hakujua kuwa ni watu wa aina gani.
Wakati Sabrina ameondoka kwaajili ya kumfata yule mmama kule kwenye mbuyu, huku nyumbani kwao alifika yule mchungaji ambaye alipigiwa simu asubuhi ili aweze kuja kuongea na Sabrina.
Na muda huo, Francis nae alikuwa amempigia simu mchungaji aliyekuwa anamfahamu na kuomba afike eneo hilo. Kwahiyo wale wachungaji walijikuta wamefika wote wawili kwa muda mmoja, na kwavile hali ya Joy ilikuwa mbaya waliamua kuingia kwenye maombi moja kwa moja na kuanza kukemea roho ya mapepo wakati huo Joy alikuwa hajitambui kabisa, kwani alikuwa akitapatata tu huku na kule.
Ila kadri walivyokuwa wakiomba ilionyesha Joy akipatwa na unafuu fulani.
Sabrina alipofika nyumbani kwao aliwakuta wale wachungaji wakiendelea kufanya maombi, moja kwa moja alienda kati yao na kuanza kuwazuia
"Muacheni mama yangu, hakuna anayehitaji maombi hapa"
Ila wale wachungaji waligundua wazi kuwa Sabrina anaendeshwa na mapepo kwahiyo sio akili yake inayomfanya awazuie na kufanya wazidi kufanya maombi.
Francis alibaki kushangaa kuwa kwanini Sabrina amekuwa vile na kumfata pale alipokuwa akiwazuia wale wachungaji, ila Sabrina hakuelewa wala kusikia na kumfanya apatwe na wazo lingine la kwenda kumuita yule mmama tena.
Sabrina akatoka pale kama chizi kwani alikuwa akikimbia na kumfanya Francis atake kumkimbiza ili aweze kumrudisha lakini wale wachungaji walimzuia Francis na kumwambia
"Mwache tu atarudi, Mungu ni mwaminifu"
Francis alimuacha Sabrina huku roho ikimuuma sana.
Ila wale wachungaji waliendelea na maombi ya kumuombea Joy.
Sabrina alipokaribia kufika alipokuwa anakimbilia, aliona giza zito sana yani giza ambalo huwezi hata kuona chochote kile na kumfanya aanze kuogopa.
Kisha akasikia sauti ikimkaripia kwa nguvu,
"Toka Sabrina tokaaaaaa.... Na kamwe hutokuja kupata mtoto kamwe katika maisha yako, na kila mwanaume utakayelala nae lazima afe na wewe upate kesi ya mauaji. Tokaaa Sabrinaaa....!"
Ile sauti ya mwisho ikagongana na mwangwi na kumfanya Sabrina aogope zaidi.
Ila alipiga magoti eneo lile huku machozi yakimtoka kamavile anaomba kupunguziwa ile adhabu kwani ilikuwa ni kubwa sana.
Ile sauti ikasema tena,
"Na mama yako lazima nimmalize na ba......"
Kabla hajamalizia kusema, mara ukimya ukatanda na gafla ilisikika ile sauti ikipiga ukelele wa nguvu,
"Aaaaaaaaaaaaaahhhhh.........!!!!!"
Na ikakatika gafla na kumfanya Sabrina ashtuke pale alipopiga
magoti na kuanza kuangaza macho yake ambapo yalikutana na mwanga mkali wa ajabu na kumfanya ashindwe kustahimili kuuangalia kwani alihisi ule mwanga ukimchoma choma.
Sabrina alipata nguvu ya ajabu na kuanza kukimbia huku akielekea kwao, ila kila alipokimbia ule mwanga ulizidi kumfata.
Alipofika kwao alikuwa anahema sana na moja kwa moja akaanguka mlangoni na kuzimia.
Wakambeba na kumuingiza ndani kwani hali yake haikuwa sawa, na muda huo mama yake alikuwa mzima kabisa huku akisimulia aliyokuwa akiyaona wakati ule aliokuwa akitapatapa.
Francis alikuwepo muda wote akisikiliza yaliyojiri ila walimshukuru sana Mungu kwa kuwasaidia kwa hilo na kwa kuweza kumponya mama huyo.
Ingawa muda ulikuwa umekwenda ila hakutamani kuondoka na kumuacha Sabrina akiwa amezimia vile.
Wale wachungaji walimuhakikishia kuwa hapatakuwa na tatizo lolote kwani Mungu amewakomboa tayari.
"Hapana, mi nitakuwa nao hapa hadi kesho ili niendelee kuona hali zao kwani hapa walipo wapo wenyewe"
Basi wakakubaliana na Francis kisha wale wachungaji wakaaga na kuondoka na kuahidi kuendelea kufanya maombi hata watakapokuwa makwao.
Francis alisaidiana na Joy kumkokota Sabrina na kumpeleka chumbani kwake ili akapumzike kwani wameambiwa kuwa ataamka mwenyewe tu muda ukifika kwahiyo wasiwe na wasiwasi.
Kisha Francis akaenda kulala sebleni.
Kulipokucha, Sabrina aliamka akiwa amechoka sana hata asielewe kilichokuwa kimetokea.
Alijiona akiwa na uchovu mwili mzima, hivyobasi akaenda kuoga na huko ndipo alipokumbuka swala la kamba yake ya kiunoni na kumfanya ajiulize maswali,
"Kamba yangu iko wapi? Inamaana imeyeyuka au ni kitu gani?"
Ni wazi Sabrina alijihisi kusahau kila kitu kilichomtokea.
Alipotoka kuoga, alienda na kukaa kitandani kwake huku akitafakari na kukosa jibu.
Akavaa na kwenda sebleni kwao, alishangaa kumuona Francis pale kwao na kumuuliza kwa mshangao,
"Francis, asubuhi yote hii unafanya nini hapa kwetu?"
"Khee, Sabrina kwanza niambie unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri, kwani nilikuwa naumwa?"
Mama yake nae akatoka ndani na kumfanya Francis aage kwani usiku ulishapita na tayari palishakucha.
"Mama, mimi naenda ila kama kutatokea tatizo lolote msisite kunipigia simu na badae nitakuja kuwatembelea tena"
"Asante sana mwanangu, umetusaidia sana hapa. Mungu akubariki"
Kisha akaaga na kuondoka, na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na maswali kuwa ukaribu wa hivyo wa Francis na mama yake umetoka wapi? Ila hakuwa na kumbukumbu kabisa kwa yaliyotokea siku ya jana.
Katika akili yake alijua wa kumpa majibu yote ni Sakina tu, hivyo akataka kwenda kwa Sakina.
Mama yake alikuwa akiingia chumbani kwake na kwake na kumwambia Sabrina,
"Nisubiri hapo mwanangu nikupe ushuhuda"
Kisha akaingia chumbani ila Sabrina hakutaka kujua hizo khabari za ushuhuda, kwani alichotaka kujua kwa wakati huo ni juu ya kamba yake ya kiunoni kuwa imekwenda wapi.
Pale pale aliinuka na kufanya safari ya kwenda nyumbani kawa Sakina.
Alimkuta Sakina akiwa amelala kwenye kochi ndani kwake, tena alionekana kuwa ni mtu aliyechoka sana.
Kisha Sabrina akamuamsha Sakina na kumfanya ashtuke sana kutoka kwenye ule usingizi.
"Utaniua kwa presha Sabrina, mambo gani hayo ya kushtuana kiasi hicho?"
"Sio hivyo dada ila nimepatwa na maajabu"
"Maajabu gani hayo?"
"Ile kamba yangu ya kiunoni imeyeyuka"
"Imeyeyuka! Kivipi?"
"Leo nimeamka asubuhi sijaikuta kwenye kiuno changu"
"Hebu acha uwehu Sabrina, wakati ile kamba jana ulikatwa na mama yako"
Sabrina akashtuka sana na kumfanya Sakina amkumbushe jinsi ilivyokuwa na kumfanya Sabrina akumbuke kila tukio ambalo lilitokea siku ya jana na kumfanya atetemeke,
"Hivi nilikuwa ni mimi au ni nani?"
"Mbona sikuelewi Sabrina?"
Ilikuwa ngumu kwa Sakina kumuelewa Sabrina kwavile matukio mengine hakujua kama yalitokea.
Sabrina aliinuka na kumwambia Sakina,
"Ngoja nikamuulize mama vizuri kama atakuwa na kumbukumbu na kuweza kunieleza"
"Hebu ningoje twende wote"
Sakina nae aliinuka akiwa na hamu ya kujua kwani hakumuelewa Sabrina hata kidogo.
Walimkuta Joy akiwa ametulia huku akisikiliza nyimbo tu.
"Yani hapa mtoto kweli sina, sikuamini kama nikitoka ndani sitakukuta mwanangu!"
"Nisamehe mama, ila kuna mambo ambayo yalinichanganya ndiomana"
Kisha akasalimiana na Sakina huku Sakina akiwa na hamu ya kujua kuwa ni mambo gani yalitokea.
Joy aliamua kuwapa ushuhuda wake juu ya mambo ambayo yalimtokea kwa siku ya jana.
"Unajua kile kitendo cha mimi kuona kamba kwenye kiuno cha mwanangu kilinisikitisha sana na ndiomana nilipatwa na hasira na kuikata, ninachoshukuru ni kuwa baada ya tukio hilo nikapata wazo la kuwapigia simu watu wa Mungu"
Sabrina akdakia kabla hata mama yake hajamaliza,
"Na ndio hapo ulipoharibu mama"
"Sijaharibu chochote, hujui tu ni jinsi gani wameifanya kazi kubwa hapa sababu ya hayo mashetani yako."
Hapo Sakina na Sabrina walitulia kumsikiliza ataongea vitu gani, Sabrina akashangaa kuona mama yake akimsimulia mambo aliyokuwa akikumbana nayo kule kwenye mbuyu, kumbe mama yake alikuwa akiyaona yote wakati ameanguka na kutapatapa,
"Ile kamba ilikuwa inakupa mwanangu uwezo wa kuwaona wachawi na kumbe ilitaka pia uwe mchawi, kule kwenye mbuyu ambako ulikimbia mara ya kwanza, walitaka wakupe uchawi ila machale yakakucheza mwanzoni na kukimbia. Ila uliponikuta mimi nikihangaika ndipo ujinga wa kwenda kumsujudia pepo ulipokupata mwanangu na kusahau kuwa Mungu ndio kila kitu"
Joy pia akasimulia jinsi Francis alivyomsimulia kwa hali aliyomkuta nayo na jinsi alivyowasiliana na yule mchungaji mwingine.
Sabrina akamuuliza mama yake,
"Inamaana Francis anajua kila kitu?"
"Ndio anajua, na yeye amesaidia kumuita mchungaji"
"Mmmh huyo Francis bibi yake ni mkubwa wa wachawi, eti leo ndio amekuitia mchungaji mama mmh!"
"Hata kama bibi yake ni mchawi wa kuzimu, kumbuka yeye yupo tofauti"
Kwa upande mwingine Sabrina alijisikia vibaya kwani akiyafikiria mambo aliyoyafanya jana na kuambiwa kuwa Francis alikuwepo alijionea aibu sana na kuhisi kamavile Francis atakuwa akimfikiria vibaya.
Joy alifanya kazi ya ziada ya kumtaka Sabrina na Sakina wamtumainie Mungu kwani aliona wazi kuwa wanaamini ushirikina zaidi ya Mungu.
"Mungu amekuokoa mwanangu, unatakiwa uanze kufanya ibada sasa"
Sabrina alikubaliana na mama yake nusu nusu kwani kwa fikra zake alihisi kuwa yale mambo yatajirudia tu.
Jioni ya siku hiyo, Sabrina akapigiwa simu tena na Japhet.
"Kuniweka jana ndio nini?"
"Naomba unisamehe tafadhari"
"Basi naomba leo nije nikufate hapo kwenu, kuna mahali ningependa twende wote"
Sabrina akakubali na kukata simu, kisha akaanza kujiandaa kwaajili ya hiyo safari.
Alipomaliza tu kujiandaa, akasikia mtu akibisha hodi pale kwao. Moja kwa moja akahisi ni huyo Japhet kaja kumpitia, ila alipoto kufungua alimkuta Francis na Fredy, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuwakaribisha tu.
Ile wanaingia ndani tu, Japhet naye akawasili.
Alipomaliza tu kujiandaa, akasikia mtu akibisha
hodi pale kwao. Moja kwa moja akahisi ni huyo
Japhet kaja kumpitia, ila alipoto kufungua alimkuta
Francis na Fredy, hakuwa na cha kufanya zaidi ya
kuwakaribisha tu.
Ile wanaingia ndani tu, Japhet naye akawasili.
Sabrina akamtazama Japhet na kujiuliza kama aondoke na Japhet na kuwaacha pale Francis na Fredy au abakie nao na kumuacha Japhet aende zake.
Yote akayaona si mazuri kuyatenda kwa muda huo ukizingatia Fredy aliletwa na Francis pale akiwa vilevile haoni, ni wazi alihitaji sana kuongea na Sabrina baada ya kusikia yote yaliyompata. Japhet nae alimkawiza sana siku ya nyuma, ila leo alimwambia ni ahadi ya kweli na ndio amekuja kumfata.
Ilibidi akili ya Sabrina ifanye kazi kwa haraka sana, akamvuta mkono Japhet na kutoka nae nje kisha akamwambia kitu
"Nisubiri hapo nje ya geti dakika mbili, natoka sasa hivi"
Kwavile Japhet hakujua kinachoendelea ikambidi tu akubaliane na Sabrina na kwenda nje ya geti kumngoja.
Kisha Sabrina akaingia ndani na kuwafata Francis na Fredy kisha akawaambia
"Natoka kidogo tu, naenda hapo duka la mbele kidogo ila nitarudi muda sio mrefu"
Na kutaka kuondoka ila Fredy akamshika mkono Sabrina na kumwambia
"Unatuongopea Sabrina, najua kama huendi dukani"
"Siwadanganyi, huo ndio ukweli"
Francis nae akamuuliza
"Na mbona umependeza sana?"
"Kupendeza ni kawaida yangu kwahiyo usiwe na shaka, narudi sasa hivi"
Ila Fredy hakutaka kuuachia mkono wa Sabrina na kuzidi kumuomba kuwa asiende
"Nakuomba usiende huko unapotaka kwenda Sabrina"
"Usijali Fredy, ni hapo dukani tu"
"Si salama kwako Sabrina, sipendi ujutie badae. Uendako si dukani, uendako napajua sababu usiku nimeota juu yako. Tafadhari Sabrina usiende huko kwani si salama kwako tafadhari nakuomba"
Sabrina akaona Fredy anamletea longolongo na vitisho tu ingawa Fredy alionekana akiongea kwa uchungu sana.
Ila mwisho wa siku Sabrina aling'ang'ania na kuamua kumuacha aende tu kisha Fredy akasema
"Mtoto akililia wembe mpe, nenda Sabrina, nenda mama, sie tuache hapa ila ukirudi tutakuwa tumeshaondoka"
Sabrina hakujali hilo na kujitokea zake nje.
Akamkuta Japhet akiwa na sura ya hasira kiasi,
"Umeniuzisha sura sana hapa Sabrina"
"Naomba unisamehe Japhet, nipo tayari sasa tunaweza tukaondoka"
Japhet akamuangalia vizuri Sabrina kisha akapanda kwende pikipiki yake aliyokuja nayo halafu Sabrina akapanda nyuma yake na safari yao ikaanza.
Moja kwa moja walienda ufukweni kupunga upepo na kubadilishana maongezi kwanza.
Huku nyumbani kwao mama wa Sabrina alirudi na kuwakuta Francis na Fredy tu mule ndani kwake.
Baada ya salamu ilibidi awaulize,
"Kwani huyu Sabrina yuko wapi?"
Wakamueleza alivyowaaga kuwa anaenda dukani, Joy akachukia sana,
"Yani hapa mtoto sina jamani, sina kabisa yani. Kavizia nimetoka kidogo tu naye akatokomea pa kutokomea. Mmh hapa mtoto sina."
Fredy na Francis nao hawakutaka kukaa zaidi hivyo basi wakaaga ili waweze kuondoka na kurudi kwao ukizingatia Fredy bado alikuwa haoni kitu, yani macho yake bado yalikuwa na upofu.
Wakati wanaondoka, Fredy akamwambia Joy,
"Ila mama, kuwa makini sana na Sabrina"
"Usijali mwanangu, huyu Sabrina ni kiburi tu kinamsumbua. Ila msijali nipo makini naye, na ngoja arudi leo ili anieleze alipokuwa mtoto huyu loh"
Francis na Fredy wakaaga tena na kuanza safari ya kurudi kwao
Sabrina na Japhet waliongea mambo mengi sana kule ufukweni, na ni dhahiri kila mmoja alifurahia maongezi ya mwenzie kwani nyuso zao zilijawa na furaha kweli kweli.
"Ila Japhet kweli huna mwanamke wewe!!"
"Nimpeleke wapi huyo mwanamke wakati nakupenda wewe Sabrina jamani!! Kisura wangu nakupenda sana"
Sabrina alikuwa akitabasamu tu muda wote na ukizingatia ni mtu anayependa kusifiwa na kusikia kuwa anapendwa.
Japhet aliendelea kumwambia Sabrina,
"Na ili kukudhihirishia kuwa kwangu upo peke yako, naomba leo leo nikupeleke ninapoishi. Tafadhari Sabrina usikatae nakuomba"
Sabrina akaendelea kutabasamu tu na kuwa kama wale watu wa sitaki nataka, ila mwisho wa siku akakubali na kusahau kuwa hata mama yake hakumuaga siku hiyo na pia nyumbani kwao aliacha wageni.
Wakaendelea na maongezi kidogo kisha wakanyanyuka na kuanza safari ya kwenda kwa Japhet.
Japhet alimpeleka Sabrina mpaka nyumbani kwake, kisha wakaingia ndani huku sura ya Sabrina ikiwa imejawa na furaha tu
"Karibu Sabrina, hapa ndio nyumbani kwangu na kwako pia kwani mimi lazima nikuoe kwahiyo utakuwa mke wangu na changu kitakuwa chako"
"Kweli nimeamini Japhet unanipenda jamani"
"Ndio, nakupenda sana naomba ujisikie huru tafadhari"
Wakati wanaendelea kubadilishana mawazo huku Japhet akiwa na hamu kubwa ya kuwa karibu na Sabrina, mara simu ya Japhet ikaita na kisha akaipokea na kusikika akijibu
"Nani?..... Unataka nini?...... Usije tafadhari...... Mbona unakuwa hivyo bhana...... Poa ningoje hapo hapo dakika sifuri."
Kisha akaikata ile simu na kumuangalia Sabrina, ila kabla hajasema chochote Sabrina akamwambia,
"Unataka kutoka?"
"Aaah kuna mtu mmoja namfata hapo tu ila sasa hivi narudi"
"Basi usichelewe"
"Sitachelewa, ila akija mtu na kugonga mlango hapa kwangu usimfungulie hadi nirudi"
Kisha Japhet akatoka na kwenda alikopigiwa ile simu.
Sabrina akiwa kabaki mwenyewe mule ndani ya nyumba ya Japhet, akawa anajisemea sasa,
"Huyu ndio mwanaume bhana anaishi kwake, sio Francis na Fredy wanaoishi kwao bado"
Wakati akijisemea hayo, kuna mtu akabisha hodi kwenye nyumba ile ya Japhet.
Ila kwakuwa Sabrina huwa anapenda kujua mambo akaona akamfungulie tu ingawa alikatazwa na mwenye nyumba.
Waliingia wadada watatu walioonekana kuwa na jazba sana ila mmoja kati yao alikuwa na tumbo kubwa, inaonyesha wazi alikuwa na ujauzito.
Sabrina alikuwa akiwashangaa tu kwani hakuelewa walitaka kitu gani, mmoja akamuuliza Sabrina
"Upo humu ndani kama nani?"
"Kwani vipi jamani?"
"Tueleze tujue, upo hapa kama dada wa Japhet au kitu gani!"
"Hapana, mi ni mpenzi wake....."
Hawakutaka Sabrina amalizie maneno kwani walimvamia mwilini gafla na kuanza kumpiga hovyohovyo, huku wakisema
"Umetusumbua sana wee mbwa, ngoja leo tukufunze adabu ili usirudie tena"
Sabrina alipiga kelele lakini hazikusaidia kwani wale wadada walimpiga sana na kumuacha akiwa ameumia sana kisha wakaondoka zao.
Sabrina alibaki na maumivu pale chini huku akilia kwani hakujua kosa lake kuwa ni kitu gani hadi wale wadada kumshambulia kiasi kile.
Sabrina hasira ikampata na kumfanya ajikongoje kuinuka pale kisha akafanya uamuzi wa kuondoka kwa hasira tena bila hata ya kumuaga Japhet.
Akatoka nje na kuanza kuondoka huku amejawa na hasira tupu moyoni mwake.
Akiwa anajaribu kutafuta usafiri huku anaenda hovyohovyo, ikatokea baiskeli upande mwingine na kumvamia, kisha akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Wasamalia wema wakamzingira ili kumsaidia, kwa bahati Japhet nae alikuwa anakatisha eneo lile. Alishangaa kuona watu wamezingira kwenye lile eneo, akaamua naye kwenda kushuhudia.
Alishangaa sana na kustaajabu kuwa ni Sabrina pale chini.
Wakasaidiana na baadhi ya watu na kumuwaisha Sabrina hospitali. Hata mwendesha baskeli mwenyewe alishangaa kuwa amemgonga vipi Sabrina hadi kuzimia vile.
Japhet ikabidi ampigie simu mama wa Sabrina na kumjulisha kuhusu ajali aliyoipata binti yake.
Joy alihisi kuchanganyikiwa kabisa, bahati nzuri kwa muda huo Sakina naye alikuwepo pale kwa Joy na kumsaidia kumpa matumaini kisha kufunga hospitali na kwenda alipolazwa Sabrina.
Walipofika walimkuta Sabrina bado amezimia, ila baada ya muda kidogo akazinduka na kuanza kulia.
Mama yake alikuwa pembeni akimbembeleza huku akishangaa kuwa ni kitu gani kinamliza.
Japhet nae akasogea karibu, ila Sabrina alipomuona Japhet akazidisha kulia hadi daktari akaamua kumtoa Japhet nje. Kisha yule daktari akamchoma Sabrina sindano ya usingizi ili alale kwanza na kupotezea lengo la kulia kwake.
Walipotoka nje ya wodi, Joy alimfata Japhet na kwenda kumuuliza
"Hivi umemfanya nini mwanangu wee kijana?"
"Mi sijui mama"
"Hujui nini na wakati alilia zaidi kukuona wewe!!"
Ikabidi Sakina asogee karibu na kumtuliza Joy aliyemuona kuwa na jazba ya haswaa dhidi ya mwanae.
Wakati Francis na Fredy wamerudi nyumbani kwao, kuna mtu alimpigia simu Francis na kujitambulisha kwa jina la Sabrina kisha akaomba kuzungumza na Fredy.
Francis hakusita kwa hilo na kumkabidhi Fredy ile simu, upande wa pili ukaongea
"Najua huoni"
"Ndio, kwani wewe ni nani?"
"Nishajitambulisha tayari, mimi naitwa Sabrina pia napenda kukusaidia. Je upo tayari?"
Fredy akasita kidogo, kisha akakubali
"Ndio nipo tayari"
Yule dada akampa maelekezo Fredy, akamwambia mambo ya kufanya kisha akakata simu.
Fredy aliishikilia ile simu na kumuuliza Francis
"Eti ni Sabrina gani huyu?"
"Hata mi simjui kwakweli, kwani sauti yake ni ngeni masikioni mwangu. Hata sio Sabrina tuliyemzoea, haya niambie alichokwambia"
Fredy akaanza kumwambia Francis kile alichoambiwa na huyo mdada kuhusu kupona kwake.
"Usijali Fredy nitakusaidia"
Fredy akafurahi na kumshukuru nduguye Francis.
Baada ya siku mbili Sabrina alikuwa katika hali nzuri na kuruhusiwa kurudi kwao, kwahiyo wakarudi naye nyumbani huku akiwa na hali nzuri kiasi.
Joy hakutaka kumsema mtoto wake kuhusu kitu chochote kile kwani hakutaka kumkumbusha yaliyopita na hakutaka hali yake iwe mbaya zaidi.
Sabrina alitulia tu nyumbani kwao bila ya kuwasiliana na mtu yeyote yule hata Fredy na Francis nao hawakuja kumuona na kumfanya ajihisi vibaya,
"Najua walichukia siku ile nilipoondoka na kuwaacha hapa ndani peke yao"
Mama yake alimsikia akijilalamisha na kumuuliza,
"Ni wakina nani hao?"
"Sio kitu mama"
Kisha Sabrina akaenda kupumzika.
Usiku wa siku hiyo alijikuta akipatwa na njozi za kila aina ambazo hakuelewa zinamaana gani katika maisha yake.
Aliota kuwa ana mtoto mchanga anamnyonyesha, ila baba wa mtoto huyo hakumfahamu na kushtuka toka kwenye ule usingizi kisha akajiangalia kwa makini na kujiuliza kuwa ile ndoto inamaana gani kwake! Kisha akakumbuka maneno ya yule bibi kuwa ile kamba ikikatwa basi hatobeba mimba wala hatoweza kuzaa, sasa ndoto ya kuwa na mtoto mchanga ilikuwa na maana gani kwake, hakuelewa kabisa.
Kulipokucha bado alikuwa na mawazo ya ndoto aliyoota usiku wake bila ya majibu.
Alianza kuwawaza wanaume waliowahi kumwambia kuwa wanampenda na mapungufu yao, kisha akajiambia
"Kati ya wote, nadhani Fredy ndiye anayenipenda kiukweli. Najua yeye atanivumilia katika hii hali niliyokuwa nayo, natakiwa kuwa na Fredy tu"
Moyo wake sasa uliona kuwa umefanya maamuzi sahihi ya kuwa na Fredy, akangoja apone vizuri ili aende kumuona Fredy na kumwambia ya moyoni.
Mchana wa siku hiyo, Sabrina alitembelewa na watu wawili ambao aliwaona ni wa muhimu sana katika maisha yake.
Alikuwa ni Francis na Fredy, Sabrina alifurahi sana kuwaona ingawa hawakwenda hospitali kumuona.
Baada ya muda kidogo, Fredy akamuomba Sabrina kuwa anahitaji kuzungumza naye.
Hivyobasi Francis akawaachia nafasi ili waweze kuzungumza.
"Sabrina, kuna jambo la muhimu sana nahitaji kuzungumza na wewe"
"Niambie tu, Fredy hata usiwe na shaka"
"Ila nakuomba unisamehe kwa haya nitakayokwambia"
"Mbona unanitisha Fredy, niambie tu"
"Kuanzia leo Sabrina, sitakuwa na wewe"
"Mbona sikuelewi Fredy!!"
"Yani sikutaki tena"
Kimya kikatawala kwa muda huo, Fredy akajaribu kumuita Sabrina ili ajue kama yupo anamsikiliza ila kimya kikatawala.
Fredy akaamua kupapasa pale alipokaa Sabrina ila hakugusa mtu, akashangaa kusikia mshindo na kuashiria kuwa kuna mtu kaanguka.
Fredy akaamua kupapasa pale alipokaa Sabrina
ila hakugusa mtu, akashangaa kusikia mshindo na
kuashiria kuwa kuna mtu kaanguka.
Fredy akaamua kumuita Francis kwavile yeye alikuwa haoni chochote kile kinachoendelea mahali pale.
Francis alipofika akashangaa kumuona Sabrina akiwa chini ameanguka na kumfata pale chini huku akimtingisha na kumuita
"Sabrina, Sabrina"
Ila Sabrina hakutingishika wala kuitika.
Francis akamuuliza Fredy kwa mshangao,
"Kwani umemfanya nini huyu!!"
"Nimfanye kitu gani mie!! Hata mwenyewe nashangaa tu hapa, sielewi nini kinaendelea"
Francis akahisi huenda Sabrina amezimia na kuanza kumpepea ila hakuamka wala nini na kufanya Francis na Fredy wasiwasi uwapate vizuri sasa.
Baada ya muda kidogo Joy naye akaingia ndani kwake na kukutana na yale maswahibu yaliyompata binti yake.
"Nini tatizo hapa tamani!!"
"Hata sisi wenyewe tunashangaa maana ameanguka gafla tu"
Joy aliinama pale chini na kumuangalia vizuri mtoto wake huku na yeye akijaribu kumtingisha tingisha ili aweze kuzinduka.
Wali muamsha sana na kujikuta wakikata tamaa juu ya hilo.
Kabla Joy hajaendelea na kitu chochote cha zaidi, wakapatwa na ugeni mahali pale.
Kumuangalia vivuri yule mgeni akagundua kuwa ni wifi yake na kujikututa akimuita pale chini ili apate kumsaidia ila alipewa jibu ambalo huwa anapenda kulitoa iwapo akikutana na hali kama hiyo
"Inuka hapo na umuache kwanza"
"Jamani wifi!!"
"Hakuna cha jamani, nakuomba umuache hapo. Kisha wote tutoke nje"
Ikabidi wamsikilize alichosema, kisha wakatoka nje.
Walipotoka nje, baada ya kama dakika mbili hivi, Fredy alianza kulalamika kuwa macho yake yanawasha.
Fredy akawaomba maji kuwa labda ajaribu kunawa, ila mgeni huyu aliyejulikana kwa jina la Sabrina alimkataza Francis kwenda kumchukulia maji Fredy
"Ila macho yananiwasha sana jamani"
"Acha yakuwashe, ndio uzima wako huo"
Fredy aliendelea kulalamika kuwa macho yanamuwasha hadi machozi yakaanza kumtoka, akapewa ushauri kuwa aende kulala kidogo tu hata kwa dakika tano, naye hakupinga kisha Joy akamuongoza hadi chumbani kwa Sabrina kitandani na kumuacha huko.
Akakatisha pale sebleni na kumwangalia mtoto wake na kusikitika sana, kisha akatoka tena nje.
Hali hii iliyokuwa ikiendelea ilimfanya Francis ahisi kuwa huyu ndiye mdada aliyewapigia simu siku ile kwa madai kwamba anataka kumsaidia Fredy kwani jina alilojitambulisha siku ile ndio lilikuwa jina lile lile walilotambulishwa pale.
Akajiuliza kuwa kwanini yule dada anaongea vitu kama mganga wa jadi! Ila hakupata jibu kabisa.
Wakiwa pale nje wakaisikia sauti ya Sabrina ikikohoa ndani na kutambua kwamba Sabrina atakuwa amezinduka, kisha wakaamua kuingia ndani ambapo walimkuta Sabrina akiwa amekaa kwenye kiti, na alipomuona shangazi yake alifurahi sana na kuinuka kumsalimia
"Umekuja saa ngapi shangazi?"
"Muda sana, wewe si hutaki kuja kwangu"
"Nitakuja tu shangazi"
Sabrina alionekana kuwa sawa kabisa na hata hakuwa na kumbukumbu kama alikuwa ameanguka muda mfupi uliopita.
Baada ya muda kidogo, Fredy alitoka kwenye chumba cha Sabrina na wote wakamshangaa pale sebleni ila yeye alimfata nduguye Francis moja kwa moja na kumwambia
"Kaka, kaka naona mwenzio. Siamini kabisa eti naona jamani"
Francis alifurahi sana na kumfanya azidi kuamini kuwa huyu mdada ndiye aliyewapigia simu ingawa masharti aliyowapa leo ni tofauti na aliyowaambia kwenye simu.
Wote pale walifurahi kuona kuwa Fredy anaona tena, haswaa Sabrina alifurahi sana kwani siku zote alijilaumu kuwa yeye ndio chanzo cha Fredy kutokuona.
Wakafurahi na kuongea mambo mengi sana.
Francis uzalendo ukamshinda na kumfanya aulize kwanza kwani bado alijiuliza bila ya kupata majibu,
"Samahanini jamani, kuna kitu kinanitatiza sana hapo. Naomba kuuliza, haswaa nahitaji nikuulize shangazi"
"Uliza tu hakuna tatizo"
Francis akaanza kuelezea jinsi alivyopigiwa simu na yule mtu na jinsi alivyojitambulisha kwao na kuwapa maelezo ya kupona kwa Fredy,
"Ninachotaka kujua sasa, je mtu huyo ndio wewe shangazi? Na kama ndio wewe mbona masharti uliyotupa hapa ni tofauti na ulichotuambia kwenye simu?"
"Kwani kwenye simu mliambiwaje?"
Ikabidi Fredy aelezee kwavile yeye ndiye aliyeongea na yule dada kwenye simu
"Kwanza kabisa alisema kuwa, tukitoka nyumbani tupite karibu na mbuyu na kuchota mchanga, kisha tukifika hapa kwa wakina Sabrina tuumwage ule mchanga chini ili uchanganyike na ule wa kwenye mbuyu, kisha mimi nizungumze na Sabrina kuwa simtaki tena. Halafu wakati tunaondoka, tuchote mchanga hapo nje kwa wakina Sabrina na kwenda kuumwaga pale kwenye mbuyu aliotuelekeza halafu hapo hapo ndio ningeona. Na hayo mambo ilitakiwa tufanye kwa haraka, kwahiyo hapa hatukutakiwa kukaa sana"
"Eeeh na nyie mmeyafanya yote hayo?"
"Hapana, tulipotoka nyumbani tulisahau kupita kwenye ule mbuyu na kuchota mchanga hivyobasi tukaja moja kwa moja huku na hatukutaka kupoteza muda ndiomana nikamwambia Sabrina kuwa simtaki tena na mambo yakaharibikia hapo"
Sabrina mkubwa aliwasikiliza sana na kuamua kuwapa majibu ya maswali yao,
"Jamani aliyewapigia simu hakuwa mie kabisa kabisa kwanza namba zenu sina na hata nilikuwa siwajui"
Joy naye alishangaa kwa yale maelezo na kuuliza,
"Sasa alikuwa ni nani? Ana lengo gani? Na wewe umejuaje kuwa leo tuna matatizo huku?"
"Unajua jana usiku nimeota vibaya sana kuhusu huku na ndiomana nikaja moja kwa moja, ila hata sikujua chochote. Ila nilipomkuta Sabrina yupo chini huku wewe ukilia lia nikajua tu ni mambo yale yale kama kipindi kile na ndiomana nikawaambia twende nje na kumuacha mwenyewe ndani. Ila mtakuja kumjua tu kuwa ni nani na alikuwa ana lengo gani kwani hakuna kitu ambacho huwa kinajificha milele"
Walibaki kimya huku maswali kadhaa yakitembea kwenye vichwa vyao, tena maswali yasiyokuwa na majibu kabisa kwa wakati huo.
Wakaongea mambo mbali mbali kisha Francis na Fredy wakaaga kwani usiku ulishatawala ila siku hiyo Sabrina mkubwa hakuondoka na kulala hapohapo.
Kesho yake, walipoamka hakutaka kupoteza muda kisha Sabrina akamsindikiza shangazi yake, shangazi yake akamtahadharisha sana Sabrina
"Kuwa makini wee mtoto, mama yako alinisimulia mambo mengi sana juu yako. Wewe bado mtoto mdogo sana, mambo ya kishirikina ya nini? Hata sijui ulianzaje kwenda huko kwa waganga jamani! Wenzio hatukuwa hivyo, na hao
wanaume jamani hebu tulia usome mwanangu, mbona mi shangazi yako sikuwa hivyo jamani! Shauri yako, utapata mimba bure na usijue ni ya nani. Unatakiwa kwenda chuo, tulia uende chuo ukamalizie masomo yako sio kutangatanga tu na wanaume. Pata mmoja utulie naye"
"Sawa shangazi nimekuelewa"
Sabrina alikuwa makini sana kumsikiliza shangazi yake hadi pale alipopanda gari na kuondoka, kisha Sabrina akaanza safari ya kurudi kwao.
Njiani akakutana na John, kisha akasimama kwaajili ya kusalimiana nae
"Za siku nyingi Sabrina"
"Nzuri tu"
"Yani tangu siku ile ndiyo hukutaka tena kupokea simu yangu jamani! Lakini sio kosa langu Sabrina"
"Sio hivyo ila nilikuwa na matatizo tu"
"Hapana Sabrina, najua ulichukizwa sana. Ila yule mwanamke nimemuacha"
Sabrina akashangaa,
"Umemuacha! Kwanini umemuacha?"
"Kwasababu yako Sabrina, sikupenda alivyokujibu"
"Acha masikhara John, yani umemuacha kweli kwasababu yangu!!"
"Ndio Sabrina, sikupenda ule ujinga aliokufanyia. Hajui jinsi gani wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu"
"Khee wa muhimu kushinda yeye!!"
"Yeye kitu gani bhana, yani nilichukia sana. Nisamehe Sabrina, naomba usinichukie wewe ni mtu muhimu sana kwangu, bila wewe mimi si chochote"
Maneno hayo yakaingia kwenye akili ya Sabrina na kufanya kazi yake ipasavyo.
"Usijali John, mi nilishakusamehe kitambo sana"
"Asante sana Sabrina"
Kisha John akamkumbatia Sabrina na kuzidi kuichanganya akili yake, akaomba wapange siku ili wapate muda wa kuongea zaidi.
Sabrina akakubali na kupanga siku ya kukutana tena kisha wakaagana na Sabrina kuendelea na safari yake ya kurudi kwao.
Sabrina aliingia ndani kwao huku akiwa amejawa na tabasamu usoni na kujiambia,
"Huyu John atakuwa ananipenda sana yani hadi kafikia hatua ya kumuacha mpenzi wake kwasababu yangu! Mmh huyu ndio ananipenda huyu"
Alikuwa anatabasamu tu hadi mama yake akamuuliza
"Shangazi yako amekwambia maneno mazuri nini huko?"
"Ndio mama, Shangazi ana vituko sana. Leo nimemfaidi na maneno yake kwakweli"
"Na pia uyasikie na maonyo yake na kuyatendea kazi"
"Hapana shaka mama, mimi tena! Lazima niyatendee kazi"
Aliingia chumbani kwake huku mawazo yake yote yakiwa juu ya John, hakumuwaza mwanaume mwingine yeyote kwa wakati huo zaidi ya John tu aliyetawala akili yake.
Usiku ulipofika, John akampigia simu Sabrina na kuzungumza nae mawili matatu na kumfanya Sabrina azidi kufurahia kupendwa na kijana John.
Mchana aliokutana na John walipanga kuonana keshokutwa ila kwa maongezi yao ya kwenye simu kwa usiku huo, waliona keshokutwa ni mbali sana na kuamua kupanga kukutana kesho yake ili waweze kuzungumza.
Wote wawili waliafikiana juu ya maamuzi hayo ya kukutana kesho yake badala ya keshokutwa.
Sabrina alilala huku sura yake ikiwa imetawaliwa na tabasamu tu usoni mwake.
Kulipokucha, Sabrina aliamka na kufanya kazi zake kwa haraka zaidi ili aweze kwenda kwenye safari yake bila ya kipingamizi cha aina yoyote ile kutoka kwa mama yake.
"Leo umekuwa mtoto mzuri kweli mwanangu Sabrina jamani"
"Sipendi kukuchukiza mama yangu, nataka ufurahie mimi kuwa mtoto wako mama"
"Kweli kabisa"
Joy alifurahi sana kuona mwanae kabadilika kwani kupigishana nae kelele kila siku alishachoka kwakweli.
Jioni ilipofika, Sabrina alijiandaa na kumuaga mama yake.
Joy hakuwa na kipingamizi kwakweli ukizingatia mtoto wake alishafanya kazi zake zote tayari.
Sabrina akaianza safari yake ya kwenda kuonana na John.
Alipofika eneo alilopanga kukutana na John, alimkuta John amewasili kitambo tu na akafurahi kumuona Sabrina.
"Yani Sabrina, nina furaha hapa kupita maelezo ya kawaida kwa kukuona tu. Halafu umependeza sana, yani kama malkia vile"
Sabrina akajitazama na kutabasamu kisha akakaa na kuanza kumsikiliza John.
Mwanaume huyu alijua sana kumsifia mwanamke, na kutokana na hilo ikawa rahisi sana kuiteka akili ya Sabrina ambaye muda mwingi alipenda kusifiwa.
"Kwakweli Sabrina nakupenda, sijui nikueleze vipi ila nakupenda jamani. Mimi bila wewe Sabrina sijiwezi, tafadhari nielewe Sabrina. Nikikukosa wewe nitampata wapi tena binti mrembo kama wewe! Hakuna Sabrina, niamini kwa hilo"
Sabrina alikuwa makini kabisa kumsikiliza John, kwakweli maneno ya John yalijua kuiteka akili ya Sabrina na kumfanya awe kimya kabisa katika kumsikiliza,
"Napenda uwe malkia wangu, nitafanya chochote juu yako Sabrina. Simtaki mwingine mimi, nakutaka wewe tu ndio wa kupoza mtima wangu"
Sabrina akatabasamu kuashiria kwamba yale maneno ameyaelewa na yamemuingia vizuri.
Kisha John akamwambia,
"Napenda upate muda wa kutosha kuyatafakari maneno yangu Sabrina ili tuwe pamoja kwa mapenzi ya dhati"
Halafu John akamuomba Sabrina amsindikize nyumbani kwao, Sabrina akamzuia John na kumwambia kuwa asijali ataenda tu mwenyewe.
Ingawa John alisisitiza kumsindikiza ila bado Sabrina alisisitiza kwenda mwenyewe.
John hakuwa na budi zaidi ya kumruhusu kwenda mwenyewe.
Sabrina alipokuwa anarudi kwao, njiani akakutana na mdada mjamzito.
Sura ya yule mdada ikamjia Sabrina kichwani na kumjulisha kuwa ni mdada yuleyule ambaye alikuja na wenzie kule kwa Japhet na kumpiga Sabrina.
Wakati Sabrina akiwaza hayo, mara akatokea mtu nyuma na kumsukuma Sabrina na kufanya amwangukie yule dada mwenye mimba.
Wakati Sabrina akiwaza hayo, mara akatokea mtu
nyuma na kumsukuma Sabrina na kufanya
amwangukie yule dada mwenye mimba.
Sabrina alijishangaa tu akiwa juu ya tumbo la yule dada mjamzito huku yule dada akilalamika kuwa anaumia.
Sabrina akainuka upesi, akashangaa kuona watu wamejaa eneo lile kwa ule muda mfupi tu.
Wakatokea wadada wawili waliokuwa na jazba sana, tena walikuwa ni wadada wale wale waliopiga Sabrina alipokuwa kule kwa Japhet.
Akaona hapo akiendelea kusimama atapigwa hadi kufa, Sabrina alitumia sekunde tu kupata wazo la kukimbia.
Muda huo huo akawachoropoka wale watu na kuanza kukimbia, huku nyuma walikuwa wakimkimbiza pia.
Bahati nzuri ilitokea gari na kusimama, kisha mlango wa nyuma wa lile gari ukafunguliwa ili Sabrina aweze kuingia.
Naye Sabrina akaona wazi kuwa ule ndio utakuwa usalama wake na kuingia kwenye lile gari kisha dereva akaondoa lile gari.
Sabrina alikuwa anahema sana kwani hakuamini kama amesalimika eneo lile la tukio, na kuanza kuwashukuru wale watu wa kwenye lile gari,
"Asanteni jamani, asanteni sana hata siamini kama nimesalimika"
Alikuwa akitetemeka kabisa, akamsikia mmoja wa watu mule kwenye lile gari tena ni yule wa pembeni yake akimwambia,
"Nilikwambia Sabrina nikupeleke kwenu ukakataa, umeona faida ya ubishi sasa?"
Sabrina akamuangalia kwa makini, kumbe alikuwa ni John,
"Khee kumbe ni wewe John!!"
"Ndio ni mimi, pole sana kwani imekuwaje?"
"Hata sielewi, yani sielewi kabisa kabisa sielewi"
Sabrina alijihisi kama kuchanganyikiwa kabisa na hakuelewa kitu kingine zaidi ya kujishangaa tu.
Wakamuacha akili imtulie kwanza huku wakimpeleka kwao.
Walipofika kwao, John alishuka na kumfungulia mlango Sabrina.
"Pole sana Sabrina, hao wawili mbele ya gari ni rafiki zangu. Nimeshindwa hata kukutambulisha vizuri, ila nenda ukapumzike kisha nitapanga siku ya wewe kufahamiana nao"
Sabrina akaitikia na kuingia kwenye nyumba yao akiwa kajichokea kabisa, mama yake alimshangaa kwa ile hali aliyorudi nayo nyumbani,
"Mbona umenywea hivyo wakati uliondoka na furaha mwanangu?"
"Majanga yamenikuta njiani wakati narudi mama yangu"
"Majanga gani hayo mwanangu"
Sabrina akamsimulia alivyomuangukia yule dada mjamzito ila hakuthubutu kusema kama alishawahi kuonana nao kabla.
"Pole mwanangu, ila sio kosa lako. Ni kosa la huyo aliyekusukuma, usiwaze sana mwanangu. Sawa eeh!! Nenda ukapumzike tu kwasasa"
Kwavile kigiza kilishaingia, Sabrina akaenda kuoga na kulala kwani mawazo yalishamjaa tayari.
Akiwa usingizini, ikamjia ndoto akiwa amezungukwa na rafiki zake huku wakimsema kwa kupokezana maneno
"Yani Sabrina umeua! Tena umeua kiumbe cha Mungu kisichokuwa na hatia!"
"Nakwambia ukweli Sabrina, kwa kosa hili kamwe huwezi kusamehewa na Mungu"
"Umetia aibu Sabrina, yani mambo ya mapenzi unayapeleka kwenye mimba aliyobeba mwanamke mwenzio!"
"Unadhani huyo mwanaume atakuwa na wewe kwa mtindo huo? Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke muuaji, hata kama alikupenda vipi hawezi kukutaka tena kwa kumuulia mtoto wake"
Wote walikuwa wakimshambulia kwa maneno, mara akatokea rafiki yake Sia na kuwaambia,
"Jamani, dawa ya mtu muuaji ni kuwa naye auawe tu. Kwahiyo huyu Sabrina tusimwache hivi hivi kwani ataendelea kusumbua watu"
Halafu likatokea kundi la watu wakiwa wamebeba silaha mbali mbali, wengine mawe, visu, mapanga, fimbo na wote wakitaka kumpiga Sabrina.
Akashtuka kwenye ile ndoto huku jasho jingi likimtoka, alikaa na kujiuliza maswali bila majibu.
"Inamaana mimba ya yule dada ikitoka, muhusika ni mimi? Lakini mimi kosa langu hapo ni lipi jamani? Eeh Mungu nisaidie mja wako"
Kisha akainuka na kwenda kujimwagia maji kwani joto kali lilitembea mwilini mwake na jasho jingi kumtoka.
Aliporudi kulala hakuweza kupata usingizi hadi panakucha, kwani mawazo yalimuandama zaidi na kumkosesha usingizi kabisa na kumfanya auone usiku ni mrefu.
Asubuhi alimuuliza mama yake kuhusu masomo yake.
"Hivi mama, mlisema nitaenda lini chuo?"
"Usiniambie umeshachoka kuwa hapa nyumbani!"
"Nimechoka ndio mama, nataka nikasome"
"Kama umeamua hivyo basi ni vizuri sana, nitamwambia baba yako kuwa upo tayari sasa"
"Ila mama, mfano yule dada niliyemuangukia jana, mimba yake ikatoka je wa kulaumiwa nitakuwa mimi?"
"Hakuna wa kulaumiwa hapo mwanangu, laiti kama ungemjua aliyekusukuma basi yeye ndiye aliyepaswa kulaumiwa ila sio wewe. Usiwaze sana mwanangu, yote muachie Mungu tu"
Sabrina alikubaliana na mama yake ila bado alikuwa na mawazo mengi sana.
Sabrina akiwa ametulia sasa, simu yake iliita. Alipoichukua na kuangalia akashtuka sana na moyo wake ukafanya paaa, kwani mpigaji alikuwa ni Japhet.
Moja kwa moja Sabrina alijiuliza kuwa Japhet alikuwa na nia gani.
Akapokea simu huku anatetemeka kwani ni muda mrefu hakuwasiliana na Japhet,
"Uko wapi Sabrina?"
"Nipo nyumbani"
"Nakuja"
Kisha akakata simu na kumfanya Sabrina apatwe na maswali mengi bila ya majibu ya kueleweka.
"Mmh anakuja kufanya nini? Au kuniuliza? Mmh naogopa"
Mawazo yakamzidi sasa.
Muda kidogo, mama wa Sabrina akamuaga Sabrina kuwa anatoka,
"Unaenda wapi kwani mama?"
"Naenda kwenye vikoba vya kinamama ila sitakawia sana kurudi"
Joy akaondoka na kumuacha binti yake mwenyewe pale nyumbani kwao.
Alipotoka tu, zikapita dakika chache Japhet nae akawasili pale kwakina Sabrina.
Sabrina akamkaribisha Japhet ndani kwao ila Japhet alionekana wazi kutokuwa na furaha. Na swali la kwanza kumuuliza Sabrina lilikuwa,
"Kwanini umenifanyia hivi Sabrina?"
"Kwani nimekufanyia nini Japhet?"
"Usiulize wakati unajua, umeniulia mwanangu Sabrina. Nilikupenda sana ila umeniumiza sana dah!"
Sabrina akajiona akikosa raha kabisa, akajaribu kumuelezea Japhet ilivyokuwa ila Japhet alikuwa akimpinga ukizingatia tayari kuna watu walishamueleza wanavyojua wao.
"Sasa unanituhumu bure Japhet, mi nimejulia wapi kama huyo ni mwanamke wako? Walikuja kweli siku ile kwako na kunipiga"
Japhet akasimama na kuanza kufoka,
"Hebu acha uongo Sabrina, siku ile ulipatwa na alama za kugongwa unasema ulipigwa eti! Na aliyekugonga nampongeza sana, sababu wewe ni mwanamke malaya na ni wazi ulikuwa unakimbilia kwa bwana zako"
Sabrina akaumizwa sana na hayo maneno, naye akaamua kuinuka kisha akafungua mlango na kumwambia Japhet
"Nakuomba uende"
"Kwenda nitaenda ila umeniumiza sana kwa kuniulia kiumbe changu"
Sabrina alikuwa na hasira kwa muda huu na kumfanya aongee vitu kwa hasira,
"Usinibabaishe bhana, kiumbe kiumbe hata panya nae ni kiumbe"
"Unasemaje Sabrina?"
"Kama ulivyosikia"
Japhet akajikuta akipandwa na hasira na kuanza kumpiga Sabrina mule ndani, kwa bahati nzuri Fredy na Francis walitokea na kumsaidia Sabrina kisha Japhet akaondoka zake.
Sabrina alikuwa analia tu kwani Japhet alimpiga vya kutosha, kwahiyo Francis na Fredy wakapata kazi ya kumbembeleza.
Ila Sabrina bado alikuwa na hasira sana na hata hakujisikia kubembelezwa alitamani tu nao waondoke mahali hapo ili alie na moyo wake tu kwani kuzungukwa na watu wa aina ile hakutaka kabisa.
Francis na Fredy walijitahidi kumtuliza ila ilishindikana, Francis akamwambia Sabrina
"Ila na wewe Sabrina mambo mengine haya unajitakia mwenyewe"
Huyu ndio alikuwa anamzidishia hasira zaidi,
"Najitakia kitu gani? Kitu gani najitakia?"
Francis naye akatoa yake ya moyoni,
"Mwanamke gani bhana wewe hujui kukataa, kila mwanaume unamkubali tu. Ona sasa, mimi ulinikubali na Fredy pia ukamkubali. Haya ukiulizwa mpenzi wako ni nani kati yetu utajibu nini, uwe unajifikiria wakati mwingine. Inamaana wewe una moyo wa penda penda, yani kila mtu wewe unampenda. Mwanamke wa aina gani wewe? Ndiomana unapigwa hivyo, wote tukitaka haki yetu itakuwaje! Si utakuwa na shimo wewe! Mwanamke gani hujiheshimu bhana!"
Sabrina hakuamini masikio yake kama yale maneno yote yanatokea kwenye kinywa cha Francis, hakuamini kabisa na kumfanya azidi kulia zaidi na zaidi.
"Naomba na nyie muondoke, ondokeni kwetu tafadhari"
"Kuondoka tunaondoka ndio ila niliyokwambia yaweke kwenye akili yako. Na kwa mtindo huo kitu ndoa utakuwa ukisikia kwa wenzio tu kwani hakuna mwanaume hata mmoja anayependa kuwa na uchafu"
Kisha Francis akamwambia Fredy kuwa waondoke na kumuacha Sabrina akilia sana na kujiuliza maswali bila ya majibu ya aina yoyote.
Joy aliporudi alishangaa kumkuta mwanae akiwa analia kiasi kile tena akiwa na alama za kupigwa kwenye mwili wake.
"Sabrina mwanangu nini tatizo?"
Sabrina hakuweza kuelezea kwa wakati huo na kujikuta akizidi kulia tu,
"Nyamaza mwanangu, kichwa kitakuuma jamani. Nyamaza dada"
Joy alijitahidi pale kumtuliza mwanae na kumbembeleza hadi Sabrina akatulia kabisa ila bado alishindwa kuelezea anavyojisikia kwenye moyo wake kwani alihisi kama kuna kitu kimemkaa kooni na kumfanya ashindwe kusema.
Macho yake yalivimba sababu ya kulia sana.
Kisha Joy akamshauri mwanae kwenda kupumzika ili kuweza kupoteza yale mawazo ambayo yanamsumbua na kumtesa kwa wakati huo.
Sabrina akainuka na kwenda kulala.
Kwenye mida ya saa tatu usiku alienda kuamshwa na mama yake ili aweze kwenda kula.
Alitoka ndio na kula kwa kiasi kidogo sana kwani mawazo bado yalimsumbua.
Aliporudi chumbani kwake ili alale, alikuta ujumbe mfupi umetumwa kwenye simu yake kutoka kwa John,
"Kumbe yule mwanamke wa jana alikuwa ni mwanamke wa mpenzi wako, nasikia mimba yake imetoka. Najua utakuwa na mawazo kama hukukusudia ila kama ulikusudia utakuwa na furaha ila hukufanya vyema kwakweli. Kumbuka yule hana kosa lolote, ni mwanamke tu kama wewe. Yakupasa ukamuombe msamaha, yangu ni hayo tu Sabrina. Usiku mwema, ila ulivyo na mambo uliyoyafanya havifanani"
Sabrina aliumia tena kuona kila mtu akimpa lawama kwa jambo ambalo sio kosa lake kabisa, alijisikia vibaya sana.
Hakuweza kulala tena, na alikuwa akijizungusha tu usiku kucha kwani kila upande aliogeuka alijiwa na mawazo yale yale ukizingatia hakutaka mama yake aujue ukweli kuhusu Japhet wala yule mwanamke ambaye mimba ilitoka.
Kulipokucha, Sabrina aliamka na kuoga huku akili yake bado ikiwa na mawazo yasiyo na majibu wala mwisho.
Akapigiwa simu na rafiki yake Sia, akajua wazi kuwa mambo ni yale yale tu. Akatamani asipokee ila aliamua kupokea ili asikie naye atakavyomponda,
"Pole sana Sabrina, nimesikia yaliyotokea. Ila sijaamini kwakweli, na siwezi kuamini kabisa. Sabrina nakufahamu rafiki yangu, najua wazi huwezi kufanya haya niliyoyasikia"
"Ndio hivyo Sia, hata mi mwenyewe sielewi. Kila mtu ananichukia kwa kosa ambalo sio langu"
"Usijali, nitakuja ili tuongee vizuri. Najua wazi huwezi kufanya hivyo Sabrina, utakuwepo kwenu lini ili nije?"
"Nipo Sia, saa yoyote ile ukija utanikuta"
"Sawa nakuja kwenye mida ya saa kumi rafiki yangu"
Huyu akamfanya Sabrina ajisikie vizuri kiasi kwni hali yake ilikuwa mbaya sana mwanzoni,
"Nashukuru Mungu, rafiki yangu Sia ananielewa jamani"
Kidogo muda huu Sabrina akapata nguvu ya kufanya baadhi ya mambo yake huku akimngoja huyo Sia ili aweze kumueleza yote yaliyopo kwenye moyo wake.
Sabrina alikaa na mama yake kuzungumza mawili matatu,
"Nimeongea na baba yako kasema amechelewa kutupa taarifa, ila wiki ijayo unatakiwa kuanza chuo. Kwahiyo mwishoni mwa wiki hii utasafiri mwanangu. Sawa!"
"Sawa mama, hiyo ni khabari njema kwangu na nimefurahi sana mama"
"Usijali mwanangu, kwahiyo hao mashoga zako sijui wakina nani nani huko uwaage kabisa. Sio siku inafika, nawe uanze porojo zako"
"Hakuna tatizo mama"
Mara mlango wao ukagongwa, moja kwa moja Sabrina akajua kuwa ni Sia tu anayegonga mlango na kwenda kumfungulia.
Ni kweli Sia alikuwa mbele, nyuma yake walikuwepo wale wadada wawili waliompiga Sabrina na yule aliyekuwa mjamzito siku mbili zilizopita.
Sabrina akashtuka sana baada ya kumuona mtu mwingine aliyekuja na hao watu akiwa amevalia mavazi ya kipolisi.
Sabrina akashtuka sana baada ya kumuona mtu mwingine aliyekuja na hao watu akiwa amevalia mavazi ya kipolisi.
Sabrina alikuwa kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi kwani hakuelewa kabisa kuwa kwanini Sia aje na hao watu, na kwanini aje na polisi!
Wakati Sabrina akistaajabu hayo, Sia akasogea karibu na kuwaambia wale wenzie
"Sabrina ndio huyo hapo"
Yule polisi akamsogelea Sabrina na kumuuliza yule binti ambaye mimba ilitoka
"Msichana mwenyewe ndio huyu?"
Yule binti akajibu huku akiwa kama machozi yanamlenga lenga,
"Ndio huyo huyo"
Yule askari, akamshika Sabrina na kumwambia,
"Upo chini ya ulinzi, unahitajika kituoni"
Sabrina hakuelewa kitu kawani alikuwa anashangaa tu na kuona mambo yale kama ni ndoto tu kwake.
Alijikuta akiuliza,
"Kwani nimefanyaje jamani!"
Yule askari akamjibu kwa ukari,
"Utajua huko huko kituoni"
Joy nae muda wote alikuwa akishangaa tu kwani hakuelewa kabisa kuwa ni kitu gani kinaendelea, akazuia mwanae asipelekwe kituoni lakini ilishindikana.
Alihisi kuchanganyikiwa kwakweli, akamuangalia Sia na kumuuliza
"Yani wewe ndio unamfanyia hivi rafiki yako?"
Ila Sia hakumjibu chochote mama huyu na safari ya kwenda kituoni iliendelea.
Walipofika, moja kwa moja wakampeleka Sabrina rumande na kumfanya Joy azidi kuchanganyikiwa.
Akamfata askari mmoja na kumuuliza,
"Kwani binti yangu amefanya nini jamani?"
"Inamaana hujui kama mwanao ameua!"
"Ameua? Kamuua nani?"
Yule askari akacheka, kisha akanyoosha kidole huku akimuonyesha Joy yule msichana ambaye alikuwa mjamzito,
"Umemuona yule binti pale! Alikuwa na mimba yule, sasa inasemekana mwanao alikuwa na mahusiano na mchumba wa yule binti. Mwanao asivyokuwa na akili sasa, alimuibia mwenzie mwanaume halafu siku hiyo kamkuta mwenzie njiani nasikia akamsukuma na kumponda na kitu kizito tumboni kisha akakimbia. Ndio hapo mimba ya huyo binti ikatoka, je sio uuaji huo?"
Joy alitulia kimya huku machozi yakimlengalenga, alijisikia vibaya sana kusikia hivyo vitu ambavyo ni tofauti kabisa na alivyosimuliwa na mwanae kabla.
Joy akainuka pale na kuomba kuzungumza kidogo na mwanae, kwa bahati wakampa nafasi hiyo.
Sabrina alipoitwa kwa mama yake alikuwa akilia tu na kufanya ashindwe kabisa kuzungumza na mama yake hata pale walipomrudisha tena rumande alikuwa akilia tu.
Joy ilibidi ajikaze na kujipa moyo ili aweze kufanya kitu cha kumsaidia mtoto wake.
Akamfata yule binti inayesemekana kuwa mimba imetoka.
"Mwanangu, unauhakika kweli Sabrina alikusukuma na kukupiga na kitu kizito tumboni?"
"Ndio, Sabrina kaniulia mwanangu"
Huku akijiliza liza pale.
Joy alimuangalia tu huyu binti kisha akamwambia,
"Kama uyasemayo yana uongo ndani yake basi jua kwamba Mungu anatambua hilo naye ndiye atakayetoa hukumu"
Kisha Joy akaondoka eneo lile, akatafuta eneo la utulivu ili aweze kumpigia simu mumewe na kumwambia yaliyojiri.
Sabrina alikuwa akilia tu huku akiwaza yote yaliyotokea nyuma, hakuelewa kwanini rafiki yake Sia amegeuka kiasi kile na kuamini maneno ya watu kuwa rafiki anaweza kugeuka na kuwa adui kwa dakika moja tu.
Sabrina hakuweza kukaukwa na machozi, alikumbuka hadi jinsi Fredy alivyokuwa akimzuia kuwa asiende ila kwa kiburi chake akaenda na kukutana na hayo yaliyomkuta sasa.
Alitamani siku zirudishwe nyuma ili awe Sabrina mpya ila ndio hivyo tena alikuwa rumande tena kwa kosa asilohusika nalo.
Alijikuta akiyachukia mapenzi, na kujiapia kule rumande kuwa hatokuja kupenda tena katika maisha yake yote yaliyobaki.
Khabari ya mwanae kupelekwa rumande ilimsikitisha sana Deo, na vile alivyoambiwa kuwa dhamana imeshindikana kwahiyo mtoto wake atalala rumande kulimfanya aombe likizo ya dharura ili aweze kwenda kumsaidia mtoto wake aliyejua wazi kuwa hana hatia.
Sakina nae alisikitishwa sana na khabari hii, alijua wazi kuwa Sabrina amesingiziwa tu.
Alikuwa akijisemea tu,
"Maskini Sabrina sijui ana damu ya kuchukiwa jamani!! Wachawi wamemfatilia wee hadi basi, saivi kaanza kufatiliwa na watu wa kawaida hadi kufikia hatua ya kumsingizia mmh!"
Kumbe Joy alikuwa akimsikiliza Sakina kwa makini na kujikuta akisema,
"Umeona eeh! Mwanangu anaonewa jamani hata sijui amewakosea nini watu hawa hadi wanafikia kumfanyia hivi mtoto wangu!!"
Wote wakajikuta wakisikitika kwa pamoja kwani jitihada zote walizokuwa wakizifanya kwaajili ya dhamana ziligonga mwamba na kufanya siku hiyo Sabrina alale rumande.
Joy aliumia sana tena sana hata hakutamani kurudi nyumbani kwake, alitaka alale pale pale polisi ila Sakina ndiye aliyefanya kazi ya kumpooza na kumbembeleza.
Sabrina alizidi kuumia kuona vile anakandamizwa kwa kosa ambalo hakulitenda hata kidogo na wakizidi kumwambia kuwa amelitenda.
"Ila ni Mungu pekee anayejua hatma yangu, ni Mungu pekee atakayenihukumu kwa haki juu ya hili"
Moyo ulimuuma zaidi pale alipogundua kwamba siku hiyo atapaswa kulala hapo rumande sababu dhamana yake imekataliwa.
Sabrina alilia muda wote, hakujisikia kunyamaza kwani moyo ulikuwa ukimuuma tu na kujiona kama mtu mwenye mkosi katika maisha yake, ukizingatia kile chumba kilikuwa na mbu na harufu ya mikojo ndiyo ilitawala mule ndani na kumfanya Sabrina ajisikie vibaya zaidi.
Deo hakutaka kupoteza muda na kuamua kuchukua gari yake na kusafiri siku hiyo hiyo ili aweze kuwahi hata kwa kesho na kumsaidia mtoto wake.
Wakati yupo njiani, kuna jamaa mmoja alionekana kupatwa na matatizo kwenye gari yake njiani na kuliweka pembeni, alionekana kusimamisha kila gari inayopita ili kuweza kupata msaada ila gari zote zilimpita kwenye eneo lile, kwahiyo lilipopita gari la Deo nalo akalisimamisha.
Deo alitamani kutokusimama kwani aliona kuwa anacheleweshwa tu, ila huruma ikampata na kusimama, kisha akamuuliza yule mtu
"Nini shida hapo kaka?"
"Nina tatizo bhana na gari yangu hapa, sijui kama utaweza kunisaidia"
"Tatizo ni kitu gani?"
"Tairi langu la mbele limepata pancha, ubaya ni kuwa sina hata tairi la ziada"
Deo akaenda kwenye buti la gari yake na kutoa tairi, kisha akamwambia yule bibi
"Mimi ninalo, chukua hili"
Kwakweli yule baba hakuamini kupata msaada kiurahisi kiasi kile,
"Dah, nashukuru sana na Mungu akubariki. Ngoja nijaribu kuliweka, ila unaweza kwenda sasa usije ukachelewa zaidi"
"Usijali, ngoja tusaidiane kuliweka ili tuondoke kwa pamoja. Eneo sio zuri hili, nisije nikafika mbele na kusikia mengine bure"
Kisha Deo akaanza kumsaidia yule jamaa, yani alijikuta tu akipatwa na moyo wa kumsaidia.
Walipomaliza pale, ikabidi wafahamiane na kupeana mawasiliano yao
"Naitwa Deo"
"Nami naitwa James, itabidi unipe namba zako Deo yani hapa hata simu yangu haipo hewani sababu haina chaji na namba zake sijazishika"
Ikabidi Deo amuandikie yule James namba zake kwaajili ya kufahamiana zaidi.
Kisha kila mmoja akapanda kwenye gari yake na safari kuendelea.
Hali ya Sabrina kwenye kale kachumba haikuwa nzuri kwakweli, bado alikuwa na matatizo mule ndani na kila kilichoendelea hadi palipokucha.
Alimsikia mama yake akizungumza nje ya kile kituo cha polisi na kugundua kwamba mama yake alikuwa mtu wa kwanza kufika pale kushinda hata watu wote.
"Naombeni jamani hata nimuone mtoto wangu"
"Hairuhusiwi mama, subiri muda ufike"
"Msinifanyie hivyo jamani, mwanangu anahitaji uwepo wangu kwasasa. Naomba nimuone tu"
Malalamiko hayo ya mama yake yalimfanya Sabrina azidi kuumia moyo mule kwenye kile kichumba.
Joy alizidi kuwaomba lakini walimkatalia kabisa, yote hayo yalifanywa kwa lengo la kumtesa Sabrina tu ukizingatia ndugu wa yule binti ambaye mimba ilitoka walishafanya mambo yao pale kwenye kituo na Kuhonga baadhi ya askari ili kumfanya Sabrina ateseke na ndiomana Joy hakusikilizwa kabisa.
Joy aliona itakuwa vyema kama ataenda kumtafutia mwanae chakula kwanza, kwa kifupi Joy alikuwa amechanganyikiwa kabisa.
Njiani wakati anaenda kumtafutia mwanae chakula akakutana na Sakina.
"Najua umeshachanganyikiwa dada yangu, ila usijali chakula mie nimekibeba"
"Ni kweli nimechanganyikiwa, tena nimechanganyikiwa kabisa kabisa"
Wakaenda tena pale kwenye kituo cha polisi na kuanza kumuomba askari ili awatolee Sabrina waweze kumpa kile chakula,
"Hairuhusiwi, labda mnipe hiko chakula nimpelekee. Kesi ya mtoto wenu ni kubwa sana. Sitaki kufanya makosa tena"
Wakamuomba sana, ila yule askari alikataa na kuamua kumpa kile chakula ili akampe Sabrina.
Yule askari akachukua kile chakula na kumpelekea Sabrina kwenye kale kachumba ambapo alikuwa na watuhumiwa wengine kama watatu hivi, hao watuhumiwa wengine ndio waliokula kile chakula.
Joy na Sakina wakajaribu kufatilia ili wajue hatma ya ile kesi ya Sabrina,
"Mtoto wenu ana hatia sana, na ushahidi upo wa kutosha. Kwanza kabisa alikimbia eneo la tukio baada ya kulitenda, huo ni ushahidi tosha kuwa alitenda. Halafu kila tukitaka kumuhoji analia tu, inaonyesha wazi anajutia kosa alilolifanya ila tu hataki kukubali ukweli kuwa amelifanya"
Ndivyo walivyojibiwa na yule askari, akaendelea kuongea
"Hapa ni moja kwa moja segerea, tena kesi ya mauaji hiyo ataenda kufungwa huko maisha"
Joy alihisi kama moyo wake ukitaka kupasuka kabisa, ikiwa ameshindwa kukabiliana na hali ya mwanae kulala pale polisi kwa usiku mmoja je ataweza kukabiliana na hiko kifungo cha maisha kwa mwanae!!
Joy alihisi kama hiyo hukumu itatolewa kwa mtoto wake basi na yeye ndio itakuwa mwisho wa maisha yake.
Walishinda pale pale kituo cha polisi huku wakiwangoja ndugu wa yule dada ambaye mimba ilitoka kujua hitimisho la ile kesi inayomkabili Sabrina.
Deo alirudi nyumbani kwake na kushangaa kukuta hakuna mtu ila milango yote iko wazi,
"Kweli huyu mke wangu ameshachanganyikiwa jamani mmh!"
Na yeye hakutaka kupoteza muda, nia yake ilikuwa ni kujiandaa kidogo na kwenda huko kituoni.
Wakati anajiandaa, akapigiwa simu na namba ngeni. Akaipokea,
"James anaongea hapa, yule mtu uleyemsaidia njiani"
"Aah kumbe ni wewe, nipe khabari ndugu yangu"
"Salama tu, nishafika nyumbani kwangu. Najiandaa hapa kwenda kazini kidogo ila naomba jioni nikutafute"
"Sawa hakuna tatizo"
Kisha akakata ile simu na kumalizia mambo yake kisha kuanza safari ya kwenda kwenye kituo cha polisi alichoambiwa na mkewe jana.
Alipofika hakuwakuta, ikabidi aulize.
Akajaribu kumpigia mkewe simu lakini hakupatikana, ikabidi awafate askari wa pale na kuwaeleza kisha wakamwambia,
"Ile kesi imehamishwa na kupelekwa kituo cha kati kule"
Deo, akaondoka eneo lile na kwenda alipoelekezwa.
Alipofika, aliwaona Joy na Sakina wakiwa wamekaa chini ya mti pale kituoni, ikabidi awafate.
Joy alipomuona mume wake, akapata nguvu kiasi huku machozi yakiendelea kumtoka.
"Hebu nielezeni kwanza ili nijue pa kuanzia"
Joy akamuelezea mume wake kila kitu hadi vile alivyoelezewa na mwanae wakati wapo nyumbani.
Deo akawa amepata picha kichwani kuwa ni wapi waanzie na wapi waishie.
"Ngoja nikamuulizie mkubwa wa kituo kwanza"
"Mkubwa wao hayupo, kuna msaidizi tu. Ila huyo naye hataki hata kutusikiliza"
"Na ilikuwaje mkaamishiwa huku?"
"Nahisi ni njama tu Deo, yani kule hata hatukukaa sana ile jana wakatuhamishia huku utafikiri mwanangu ndio muharifu wa kwanza duniani. Hata dhamana wakatukatalia"
Deo kuna kitu kikawa kinajengeka katika akili yake, alijua wazi kuwa mkewe alisahau kumwambia kama walihamishwa kituo ile jana sababu ya kuchanganyikiwa.
Deo akawaacha pale na kuanza kushughulikia kesi ya mwanae, alitaka kuhakikisha kwamba siku hiyo mwanae anapata mdhamana hata kama siku inakaribia kuisha sababu alichelewa kufika.
Alienda kwenye ofisi ya mkuu wa kituo na kuambiwa angoje nje, baada ya muda aliruhusiwa kuingia.
Alishtuka sana kumuona mkuu wa kituo ni mtu waliyeonana naye kabla,
"Kheee bwana Deo, umejuaje kuwa nipo huku? Maana hapa nikakumbuka ile ahadi yangu na kutaka nimalize nikupigie"
"Tatizo mwanangu bhan"
"Kafanyaje!!"
Deo akamuelezea vile alivyoelezewa na mke wake.
"Dah! Vijana wetu hawa wanamatatizo kwakweli, ni ujana tu unawasumbua. Ngoja waniitie hapa huyo binti yako nimuhoji mwenyewe. Sababu maelezo unayonipa na niliyopewa ni tofauti kabisa"
Yule mkuu wa kituo akaamuru Sabrina apelekwe ofisini kwake, kwahiyo askari akaenda kumtoa Sabrina.
Sabrina alikutwa hajitambui kwenye kile kichumba, inaonyesha wazi kuwa alilia sana hadi kupoteza fahamu kwahiyo walimtoa kama mzoga.
Sabrina alikutwa hajitambui kwenye kile
kichumba, inaonyesha wazi kuwa alilia sana hadi
kupoteza fahamu kwahiyo walimtoa kama mzoga.
Deo alishtuka sana kumuona mwanae katika hali ile, ikabidi mkuu wa kituo atoe amri kuwa Sabrina awahishwe kwenye kituo cha afya, nao wakafanya hivyo.
Joy alihisi kuchanganyikiwa zaidi kwa ile hali ya mtoto wake, hata alipopelekwa hospitali bado hakuwa na matumaini juu yake.
Sabrina aliendelea kupewa huduma huku akiwa chini ya uangalizi kwa wafanywavyo watuhumiwa wengine.
Yule mkuu wa kituo akamuita Deo na Joy pembeni ili kuweza kuwahoji vizuri kuhusu mtoto wao.
"Kwani hii kesi imekuwaje hadi kufikia huku?"
"Kwakweli, labda mke wangu ndio anaweza kueleza"
"Sasa, ngoja niwape kazi ndogo ya kufanya"
"Ipi hiyo? Inamaana mwanangu akitoka hospitali mtamrudisha tena rumande?"
"Hapana, siwezi kukufanyia hivyo Deo. Ila ningependa mjaribu kuchunguza kidogo kwa upande ule wa pili, sababu naona kama kuna mchezo unachezeka hapa"
Wakatulia na kumsikiliza kwa makini yule mkuu wa kituo ambaye alimuhurumia sana Deo ingawa walifahamiana kwa siku moja tu.
Kesho yake, hali ya Sabrina ilirejea na kuwa katika hali yake ya kawaida, hata yeye mwenyewe akajishangaa kujikuta pale hospitali.
Wazazi wake waliruhusiwa kurudi naye nyumbani ila kwa masharti ya dhamana iliyopitishwa na yule mkuu wa kituo.
Joy alifurahi sana kurudi na mwanae nyumbani ingawa kesi ilikuwa bado haijaisha.
"Nashukuru Deo mume wangu kwa kujuana na watu"
"Kwani unafikiri mtu mwenyewe nimejuana nae siku nyingi basi!! Nimejuana nae wakati narudi, najua Mungu ndiye aliyepanga yote haya. Hii kesi itaisha tu, hata usiwe na shaka"
"Naamini itaisha kwakweli"
Sabrina alikuwa amenywea sana, tofauti na jinsi anavyokuwaga siku zote. Ile kesi ilionyesha wazi kuichanganya akili ya Sabrina vilivyo.
Siku waliyoambiwa kwenda tena kwaajili ya ile kesi wakajiandaa ili kwenda huko.
Joy alikaa kidogo na mwanae ili kumpa nguvu na hali ya kujiamini pindi atakapokuwa anahojiwa na askari.
"Usiogope mwanangu, haya ni mambo ya kawaida tu. Babako saivi yupo basi hakuna baya litakalo kupata. Umenielewa?"
"Ndio mama, nakuelewa"
"Na ukiulizwa kitu elezea vile kilivyo, hakuna atakayekudhuru mwanangu"
Sabrina akaelewa aliyoambiwa na mama yake na kujiamini, ukizingatia hakuna alichohusika nacho kati ya vyote walivyomsingizia ingawa hakuwa na shahidi.
"Ila mimi sina shahidi mama"
"Usijali mwanangu, shahidi wako ni Mungu peke yake ambaye hana upendeleo"
Kisha wakatoka hapo nyumbani kwao na kuelekea kwenye kituo cha polisi.
Sakina alikuwepo kwenye kile kituo cha polisi tena hata kabla wakina Sabrina hawajawasili.
Hata walipowasili alikuwepo pale pale nje kwani ilimuuma sana kwa rafiki yake kipenzi na mdogo wake kupewa kesi kama ile aliyopewa.
Wakati yupo pale nje alikuwa amekaa nyuma ya mabinti watatu ambao hakuwafahamu kwa muda huo ila aliwasikia wakizungumza,
"Kheee Sia wewe ni noma, hata sikujua kama ungemkomesha hivi Sabrina"
Mwingine akacheka na kujibu,
"Yani nimemkomesha haswaaa na aache tabia ya kutaka bwana za watu, kazidi. Yani nilivyoona meseji zake kwa John wangu, halafu John akaniacha kwaajili yake. Eti na yeye akajileta mwenyewe kwetu, nikasema hapo hapo ndio pa kumkomesha"
"Ila ameyataka mwenyewe, inamaana hakujua kama mwanamke wa John ni wewe!"
"Atajijua mwenyewe, nimemfatilia nyendo zake mwanzo mwisho halafu lenyewe kama zoba hata halikujua. Na nimemkomesha, hadi kaonja tamu ya rumande. Kanywea kawa mdogo kama piritoni"
Wote watatu wakawa wanacheka bila kujua kama kuna mtu wanamuumiza na maneno yao ambayo wanayaongea kumuhusu Sabrina.
Waliendelea kuongea huku wakifurahi na kugongeana viganja vya mikono yao.
"Na pale angejua kama ni mimi nilimsukuma wee angechukia balaa"
"Angejulia wapi? Mi nakuaminia Manka ndiomana nikakupa kazi, huyo Bi. Shoga naye anavyojua kujiliza utadhani mimba imetoka jana kumbe kitambo tu, ila nimewakubali jamani kazi mnaiweza"
Wenyewe walikuwa wakifurahia maneno yao ila Sakina alipata kitu kutoka kwao tena bila hata ya wao kujua chochote kile.
Sabrina alikuwa akihojiwa na kuamua kuelezea kila kitu jinsi kilivyokuwa ila kama watamuamini basi na wamuamini, na kama ikishindikana kumuamini basi wasimuamini lakini ukweli akiwa kashausema wote jinsi ulivyo.
"Inamaana huyo mdada unajuana nae kwa muda mrefu?"
"Sio kwa muda mrefu, ni kama nilivyowaelezea kuwa mara ya kwanza nilikutana nao kwa kaka wa rafiki yangu"
Sabrina hakutaka kuwaficha kitu kwa wakati huo, aliwaelezea mlolongo mzima wa tangia mara ya kwanza alipoonana na yule mdada ambaye mimba imetoka na wenzio hivyobasi akafanya waweze kumuelewa kwa urahisi zaidi tena kushinda hata alivyoelewa yeye.
"Kuna picha fulani naipata kwenye kichwa changu"
Aliongea yule askari ambaye alikuwa akifanya kazi ya kumuhoji Sabrina, kisha Sabrina na wazazi wake wakaruhusiwa kurudi nyumbani na kutakiwa kuja tena kesho kwaajili ya hitimisho la ile kesi.
Sakina aliendelea kuwasikiliza wale mabinti waliokuwa wakibwabwaja bila hata ya kuangalia pembeni,
"Hivi Sia, yule kaka yako Japhet naye yupo katika mlolongo huu wa mchezo?"
Huyo Sia akacheka,
"Awepo wapi? Hata yeye haujui ukweli, na yeye nilimfanyia kusudi sababu kazidi na tabia yake ya kupenda penda"
"Kwahiyo alikuwa anampenda kweli?"
"Ndio, kaka yangu ni penda penda yule"
Wakawa wanacheka, wakamuona Sabrina akitoka na wazazi wake kwenye kile chumba cha mahojiano wakatulia kimya kama wamemwagiwa maji.
Kisha wakamuona yule dada wa nyuma yao akiinuka na kuwafata wakina Sabrina kisha akaondoka nao.
Wakajikuta wakishangaa kwa pamoja,
"Inamaana yule dada anajuana na wakina Sabrina!"
"Na inamaana maongezi yetu yote ameyasikia! "
"Mmh pameshanuka hapa jamani, tuondokeni tu"
Kuna askari alitoka kwenye kile chumba cha mahojiano, kisha Sia akamfata yule askari kuongea nae
"Imekuwaje kwani?"
"Naona hii kesi inataka kuwa kubwa, maana yule mzee wa yule muhalifu kasema anaenda kutafuta mwanasheria"
"Mmh kugumu huko, au tuje tuifute?"
"Ni nyie tu na makubaliano yenu, sie tunafanya kazi yetu tu"
Sia akamuaga yule askari na kwenda kuwafatilia wale wenzie ili wapange cha kufanya kwa wakati huo.
"Nadhani itakuwa vyema tukimwambia Vicky awaambie ndugu zake waje kufuta hii kesi jamani, maana yule dada ameshatusikia kila kitu, yanaweza yakatugeuka haya jamani"
Wakakubaliana na kuondoka eneo lile.
Sabrina na wazazi wake walifika kwenye nyumba yao, Sakina alitamani kuwaambia kile alichokisikia toka kwa wale wasichana ila akasita na kuona kwamba ni vyema angoje Sabrina awe peke yake ndio amwambie.
Wakaongelea mambo mengine kabisa, hakuthubutu kuongelea chochote kati ya alivyovisikia.
Kesho yake waliporudi pale polisi walishangaa kuambiwa kuwa ile kesi imefutwa.
"Imefutwa!!"
"Ndio imefutwa, kwahiyo hakuna kesi tena labda mfungue kesi nyingine"
Wakapewa maelekezo kuwa yule mdada ambaye mimba ilitoka ameamua kufuta kesi kwani ameamua Kusamehe.
Sakina akaongea kidogo na yeye,
"Sijapata kuona eti kesi ya mauaji inafutwa kirahisi kiasi hiki"
Joy akamuangalia Sakina na kumshangaa,
"Unamaana gani Sakina?"
"Sina maana mbaya, ila nilitaka kujua hatma ya hii kesi eti imefutwa mmh! Na sie tufungue yetu ya usumbufu"
Sabrina akapinga swala hilo na kwenda kusaini karatasi zilizomuhusu kisha akaruhusiwa rasmi na familia yake kurudi nyumbani.
Sabrina alifurahi sana kufika nyumbani kwao na kuwaomba wazazi wake wafanye haraka ili aweze kwenda chuo kwni alishachoshwa na khabari za hapo.
Kwavile Sabrina sasa alikuwa na furaha, Sakina aliamua kutumia muda huo katika kumwambia Sabrina kile ambacho alikisikia kikizungumza.
Sabrina aliishia kushangaa tu,
"Inamaana Sia ndio alikuwa mwanamke wa John?"
"Sasa mbona hakuniambia?"
"Mi sijui ila hapa nimekwambia tu kile ambacho nilisikia."
"Kumbe yote haya ni njama juu yangu! Ila nimejifunza kitu dada"
"Kitu gani hivyo?"
"Sitaki tena kuwa kwenye mahusiano, yaliyonipata yanatosha tayari"
"Usiseme hivyo Sabrina, huwezi jua mambo ya mbele"
"Hata kama siwezi jua, ila ndio hivyo sitaki tena"
Sakina hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na kile ambacho Sabrina mwenyewe alikiamua kwaajili ya maisha yake yanayoendelea.
"Ila kama ungekuwa umemkubali yule kaka yangu haya yote yasingekukuta, maana yule angekuoa tu ila...."
Sakina akakumbuka kitu na kuamua kunyamaza,
"Ila kitu gani?"
"Hapana, nilitaka kuchangany maneno tu hapo"
Hakutaka kumwambia Sabrina ukweli kuwa hata alivyotaka kubakwa ni kaka wa Sakina ndiye aliyepanga mpango ule.
Wakaongea mengi kisha Sakina akaamua kuaga na kuondoka.
Sabrina akiwa ndani kwake ametulia, akaisikia simu yake ikiita kwa mara ya kwanza tangia apatwe na ule msukosuko.
Alipoitazama aliona mpigaji ni Fredy, akaiacha ile simu iite hadi ilipokata na kuchukua simu yake kisha akaizima na kuichomoa ile laini na kuivunja, kisha akajisemea
"Kuanzia leo nataka niwe Sabrina mpya, sitaki rafiki wala kitu gani. Nitakuwa mwenyewe siku zote."
Alitulia na kuyatuliza mawazo yake kisha akamfata mama yake.
"Mama, kumbe marafiki ni wabaya sana eeh!"
"Ulikuwa hujui mwanangu? Urafiki na mwanadamu yataka umakini sana kwakuwa huwezi jua kilichopo moyoni mwake"
"Sasa mama wewe huna marafiki?"
"Wa kazi gani? Rafiki mkweli na wa pekee ni Mungu tu anayetuwazia yaliyo mema siku zote. Wengine hawa salimiana nao tu, cheka nao ila kamwe huwezi jua anakuwazia kitu gani"
Maneno ya mama yake yalimfanya Sabrina kushikilia maamuzi yake ya kutokuwa na rafiki tena.
Kesho yake, Sabrina akaletewa taarifa na baba yake kuwa anatakiwa kusafiri kwaajili ya kwenda kwenye masomo yake.
"Una siku mbili tu hapa mwanangu, unatakiwa kwenda kwenye masomo yako"
Khabari ile ilimfurahisha sana Sabrina kwani alihitaji sana kusahau mambo yote yaliyomtokea katika maisha yake, mambo yote yaliyomfanya aone kwamba maisha ni kitu kibaya.
Sabrina akamfata mama yake na kumwambia,
"Mama, ila kabla sijaenda huko kwenye masomo yangu naomba nikamuage mtu mmoja muhimu sana kwangu"
"Umeanza tena Sabrina, juzi tu hapa umesema kuwa hutaki marafiki, eti leo ukamuage mtu muhimu sana. Ni nani huyo? Kama ndugu zako wote wamesema leo watakuja hapa kukuaga"
"Ndio mama, ila nitapenda nikamuage na huyo mtu pia. Laiti kama nitaondoka bila kumuaga, moyo wangu utaniuma sana"
"Basi kwa huyo mtu tutaenda wote. Kwanza niambie ni nani?"
"Si tutaenda wote mama! Basi usijali, utamjua huko huko"
Joy hakutaka kubishana sana na mwanae kwani anamjua mwanae kama ana tabia ya ubishi.
Badae walifika ndugu baadhi kwaajili ya kumuaga Sabrina ambaye alikuwa anaenda masomoni kwenye nchi ya mbali. Wengi waliumia kwakuwa Sabrina alikuwa ni mtu pekee anayewakumbuka ndugu zake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kaka zake pia walikuwepo, na wote kwa pamoja wakafanya tafrija ya kuagana na Sabrina.
Sakina akamfata Joy na kumwambia,
"Ila hawa ndugu zenu ni kituko, kwenye tafrija wote wamekuja ila kule polisi hakuna hata mmoja aliyekuja"
"Sio hivyo ila hatukuwaambia, kipindi kile nilikuwa nimechanganyikiwa kwakweli"
Sakina akaona Joy anajitetea tu hana lolote la maana.
Tafrija ilipoisha wote wakasambaratika na kuagana.
Kesho yake kabla ya safari, Sabrina akamkumbusha mama yake kuwa waende kwa mtu wake muhimu ambaye anahitaji kumuaga.
Mama yake akajiandaa na kuanza safari yao.
Walienda hadi shuleni, shule ambayo Sabrina alimpeleka Jeff. Nia na madhumuni yake ni kwenda kumuaga Jeff.
"Kumbe mtu muhimu huyo ndio Jeff! Si ungeniambia mapema mwanangu hata nisingesumbuka kuja huku"
Sabrina akacheka, na kuingia lile eneo la shule.
Walipotazama pembeni waliona kuna wanafunzi wengi wamezunguka huku wakipiga kelele, Sabrina akajikuta akikimbilia eneo lile ili kujua kuna tatizo gani.
Alipopita kwenye lile kundi, alimuona mwanafunzi mmoja wa kiume akiwa yupo chini, inaonyesha wazi alikuwa amezirai.
Alipomsogelea na kumuangalia vyema mwanafunzi huyo alikuwa ni Jeff.
Alipopita kwenye lile kundi, alimuona mwanafunzi
mmoja wa kiume akiwa yupo chini, inaonyesha
wazi alikuwa amezirai.
Alipomsogelea na kumuangalia vyema
mwanafunzi huyo alikuwa ni Jeff.
Sabrina akashtuka na kuinama pale chini kumuangalia Jeff, muda huo huo walimu watatu nao wakawasili eneo lile kisha wakawasambaratisha wanafunzi waliokuwa wamemzingira Jeff.
Walimu wale wakasaidiana kumuondoa Jeff eneo lile na kumsogeza katika sehemu nzuri, Sabrina aliamua kuwauliza wale walimu
"Kwani amepatwa na nini?"
"Hata sisi tunamshangaa siku hizi, yani leo ni mara ya tatu ameanguka hivi"
"Mara zote hizo ameanguka leo?"
"Hapana, ila kumuona leo ameanguka ni mara ya tatu. Siku mbili zilizopita nazo alianguka, ila huwa anazinduka mwenyewe. Ila akizinduka huwa hana kumbukumbu "
"Mmewahi kumpigia mzazi wake simu kumjulisha?"
"Tulijaribu ndio ila huwa hapatikani"
Sabrina akakumbuka kuwa pale shuleni aliweka namba zake yeye kwaajili ya lolote lile litakalo muhusu Jeff, na hapo akajua wazi kosa ni lake.
Muda kidogo, Jeff akazinduka. Akamuona Sabrina mbele yake, akainuka na kwenda kumkumbatia Sabrina huku machozi yakimtoka.
Sabrina akamuuliza,
"Nini tatizo Jeff baba?"
"Ulinidanganya wewe"
"Nilikudanganya nini mtoto mzuri?"
"Uliniambia utakuwa unakuja mara kwa mara kuniona ila hujaja hata mara moja tangia uliponileta"
"Ila mama yako si alikuwa anakuja jamani Jeff!!"
"Ndio mama alikuwa anakuja ila nilitaka na wewe uje"
Sabrina alitulia akimsikiliza Jeff huku akitafakari maneno ya mwalimu kuwa Jeff akizinduka huwa kumbukumbu zinapotea, sasa amewezaje kukumbuka ahadi za uongo za Sabrina kwa muda mfupi.
Sabrina akamuangalia mwalimu na kumuuliza,
"Si mmesema huwa anapoteza kumbukumbu, mbona!!"
"Hata sie wenyewe tumemshangaa leo, maana huwa anakaa masaa kama mawili kurejesha kumbukumbu zake"
"Mlimpeleka hospitali?"
"Ndio, na wakampima kila kitu na wakasema ni mzima kabisa hana ugonjwa wowote ule"
"Basi nitawaomba leo niende naye halafu kesho tutamrudisha"
Walimu hawakuwa na pingamizi lolote juu ya swala la Sabrina kuondoka na mtoto Jeff.
Sabrina aliamua kuondoka na Jeff ili kuweza kumuhoji na kumuacha katika hali nzuri.
Joy alimuuliza Sabrina,
"Si unajua kama safari yako ni kesho?"
Nalijua hilo mama"
"Na huyu mtoto sasa utamrudisha muda gani?"
"Nitamrudisha kwanza kabla ya kuondoka, ila hata hivyo mama yake naye yupo"
Walipofika nyumbani, ikabidi Sabrina ampeleke Jeff moja kwa moja kwa mama yake ili waweze kuonana.
Walimkuta Sakina akiendelea na mambo yake, naye alipowaona akashangaa ila alifurahi kumuona mwanae.
"Mbona umemrudisha huyo?"
"Kasema amekumiss mama yake ndiomana nikamleta"
"Na walimu wamekukubalia tu?"
"Ndio wamekubali"
"Mmh mna ajenda zenu nyie, haya mwanangu njoo"
Jeff akamsogelea mama yake, ikabidi Sabrina amueleze Sakina kuhusu hali aliyomkuta nayo Jeff shuleni na jinsi alivyoelezewa na walimu wake.
"Mmh lazima kuna kitu hapa, ngoja nimtafute mtaalamu nimuulize"
"Ushaanza mambo yako ya kishirikina dada"
"Sio ushirikina Sabrina, hili jambo sio la kawaida nakwambia. Lazima kuna kitu hapa, mwanangu hawezi kuanguka hovyo kama mgonjwa wa kifafa"
Sakina akachukua simu yake na kuanza kuwapigia watu wake, Sabrina akamwambia
"Wewe wapigie tu ila hayo mambo usinishirikishe kwakweli"
"Sio tatizo ila lazima nijue"
Sabrina akatulia na Jeff ili kumuhoji maswali mawili matatu na yeye apate kuelewa kilichojificha kwa mtoto huyo.
Ila Jeff naye alijibu kuwa haelewi chochote kile, hata yeye mwenyewe anajishangaa tu kuwa kwanini inamtokea hivyo.
Sabrina hakupata jambo la maana kutoka kwa Jeff zaidi ya kujizidishia maswali yasiyo na majibu.
Sakina akarudi na majibu aliyopewa na watu wake,
"Wewe Sabrina ndio unamtesa mwanangu"
Sabrina akashangaa,
"Namtesa mwanao! Kivipi? Si ile kamba yako ya kipindi kile, ndio inayomtesa"
Jeff naye akashtuka na
kumuuliza mama yake,
"Umesema kamba mama! Kamba nyeusi?"
"Ndio kamba nyeusi, umekumbuka kitu gani hapo?"
"Huwa kabla sijaanguka naona kitu kama kamba nyeusi mbele yangu, huwa kinanizingira usoni na mwisho wa siku nakuja kuambiwa kuwa nilianguka"
Sakina akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Umeona sasa? Umeona mambo yako hayo Sabrina!"
"Huu sio wakati wa kulaumiana dada"
Kisha Sabrina akamuangalia Jeff na kumuuliza,
"Na mbona hukuniambia hayo yote wakati nakuuliza?"
"Nilisahau kukwambia"
Sakina sasa alikuwa anaongea tu tena bila nukta,
"Sijui hata una nini Sabrina kwa huyu mwanangu, yani majanga yako wewe umeenda kumuhamishia mwanangu halafu huku mnajifanya mmepona na mama yako"
"Usinilaumu bure, hata wewe una husika pia hapa sababu yule mtu aliyenifunga kamba sikwenda mwenyewe. Tena ni wewe uliyenishauri kuwa twende hadi leo nimekuwa na matatizo ya milele, tena mimi ndio napaswa kukulaumu wewe ila sio wewe kunilaumu mimi"
Wakajikuta wakibishana muda huo hadi Jeff akawa analia kwa mabishano yao.
Joy akiwa nyumbani kwake aliona kuwa mwanae anakawia sana kurudi nyumbani, na Deo nae alishaanza kumuulizia,
"Umemuacha wapi Sabrina wakati mliondoka wote?"
"Hata kurudi tumerudi wote ila yeye akaenda kwa Sakina mara moja kumpeleka mtoto wa Sakina. Nashangaa hadi sasa hajarudi"
"Hebu nenda kamfate, yule mtoto hatakiwi kukaa mbali na nyumbani kwa muda mrefu kwasasa"
Ikabidi Joy ajihimu kwenda kumfata binti yake.
Alipofika aliukuta ule mzozo baina ya Sakina na Sabrina,
"Kuna nini hapa? Eeh! Mnarumbana nini nyie maswahiba wawili?"
Sabrina akamjibu mama yake,
"Hakuna kitu mama"
Sakina akadakia,
"Hakuna kitu nini? Hebu mwambie ukweli mama yako naye ajue. Si ulikuwa naye katika kuiteketeza ile kamba"
Joy akawashangaa sana,
"Kamba gani mnayoizungumzia hapa?"
"Eti ile uliyoikata"
"Kwahiyo muda wote mnabishania huo upuuzi wa kishetani! Hebu tumieni akili wakati mwingine jamani, haya mambo mengine ni ya kijinga tena hayafai hata kurumbana. Kwani tatizo ni nini?"
Ikabidi Sabrina amueleze mama yake kuwa yale matatizo waliyomkuta naye Jeff, chanzo chake ni ile kamba.
"Sasa hapo ndio hayo mambo yenu ya kishirikina yanaponishangaza, sasa kamba ile ilikuwa kwenye kiuno cha Sabrina mmefungana na waganga wenu wa kitapeli huko, halafu hiyo kamba eti imeruka na kwenda kumtesa mtoto mdogo huyu Jeff asiye na hatia. Inamaana hiyo kamba mliifunga kwaajili ya Jeff au kulikuwa na kitu gani hapo?"
Sakina akataka kusema chanzo kizima cha kufunga ile kamba lakini Sabrina akamzuia hivyobasi wote wawili wakawa kimya tu.
"Kama hamtaki kusema basi. Sabrina nenda nyumbani baba yako anakungoja, nawe Jeff mtoto mzuri twende kwenye maombi."
Kisha Joy akamshika mkono Jeff na kuondoka naye.
Sabrina na Sakina walibaki wakiangaliana, kisha Sakina akamwambia Sabrina
"Nenda kwenu sasa baba yako anakungoja"
"Naenda ila usije ukamwambia mama bhana kile kitu"
"Haya simwambii, ila wewe mtoto mjinga sana huwa unaniona mimi kama rika lako vile wakati nimekupita miaka kibao. Haya nenda kwenu, na huyo mamako kajishauwa kumpeleka mwanangu kwenye maombi sasa ole wake asipone"
Sabrina akaondoka eneo lile na kurudi nyumbani kwao.
Joy alirudi nyumbani kwake kwenye mida ya saa tatu usiku na kuwakuta wote wakiwa pale kwake hata Sakina alikuwepo pale kwa lengo la kumfata mwanae.
"Jamani, mapambano yalikuwa makali sana ila Mungu ni mwaminifu ametusaidia"
Sabrina alikuwa na hamu ya kujua kilichotokea huko, ila kwasababu ya usiku Joy hakuona vyema kuwaelezea na kuamua kumruhusu Sakina amchukue mtoto wake ili akalale, ila Jeff aligoma.
"Kwanini hutaki kwenda nyumbani mwanangu?"
"Nataka kulala na anti Sabrina leo sababu nimesikia kuwa anaondoka kesho"
Sakina akajaribu kumshawishi mwanae ila ikashindikana kumfanya akubali kurudi nyumbani hivyobasi akaamua kumruhusu tu alale pale na Sabrina kisha yeye akaaga na kurudi nyumbani kwake.
Muda wa kulala ulipofika, Sabrina akamchukua Jeff na kwenda kulala nae chumbani kwake ila muda mwingi Jeff alionekana kutokulala kwa haraka ikabidi Sabrina amuulize,
"Mbona hulali toto?"
"Usingizi hauji mama"
"Fumba macho usingizi utakuja"
Jeff akafumba macho yake, naye Sabrina akamkumbatia mtoto yule ili kumfanya alale.
Baada ya masaa mawili, Jeff akashtuka huku jasho jingi likimtoka.
Sabrina nae akainuka na kukaa pale kitandani na kumuuliza Jeff kuwa anatatizo gani,
"Nini tatizo toto?"
"Nimeota ndoto mbaya"
"Ndoto gani hiyo?"
"Nimeota umepata ajari na umekufa"
"Jeff tafadhari usiniotee vibaya toto. Lala tena ila angalia upande wangu ili usiote tena"
Wakalala tena ila baada ya masaa mawili mambo yakawa yale yale, hadi panakucha Jeff alimuelezea Sabrina ndoto moja tu.
Sabrina alijiandaa vizuri, ila kama ambavyo alipanga ni kuwa atampeleka kwanza Jeff shuleni kwao kisha ataelekea uwanja wa ndege kwaajili ya safari yake kimasomo.
Akamwambia mama yake,
"Mi nitawahi kuondoka hapa na Jeff shuleni kwao kisha ndio nitaenda huko uwanja wa ndege"
"Hayo mambo yako ya kuchelewa ndio ambayo baba yako ameyakataa mwanangu. Yeye kasema atatoka moja kwa moja kazini kuelekea uwanja wa ndege kukuaga halafu wewe unaanza mambo yako mengine, Jeff atarudishwa shule na mama yake"
"Nilimuahidi mama, kumbuka ahadi ni deni acha nifanye hivi tafadhari"
"Basi ngoja nimpigie yule dereva aliyesema baba yako ili uwahi, halafu mie nikimaliza kujiandaa nitamshtua baba yako anipitie hapa"
Sabrina alishukuru kuruhusiwa na mama yake.
Dereva alipofika, Sabrina akapikia mizigo yake kisha yeye na Jeff wakaingia kwenye ile gari.
Wakakatisha kidogo kwa Sakina ili Jeff aweze kumuaga mama yake kisha safari ikaendelea hadi walipofika shuleni kwa Jeff.
Sabrina akamuomba Jeff ashuke ili akamkabidhi kwa walimu wake, ila Jeff akagoma na kuanza kulia
"Mbona hivyo Jeff jamani!"
"Sitaki uondoke"
"Naenda masomoni Jeff usijali mtoto mzuri"
"Ndio unaenda masomoni ila sitaki uondoke leo"
"Kwanini jamani Jeff!"
"Sitaki ufe"
"Sitakufa Jeff, niachie tafadhari uende shule na wewe"
Ila bado Jeff hakutaka kumuachia Sabrina, bado alikuwa akilia sana.
Sabrina akajaribu kumpa vishawishi vyote ila mtoto huyu hakutaka kuelewa kabisa, bado alikuwa analia na kumng'ang'ania Sabrina asiondoke.
Ikabidi Sabrina afanye ujasiri tu na kwenda kumuita mwalimu mkali wa Jeff ili Jeff aende darasani kwa wenzie.
Mwalimu yule kama kawaida yake, yeye ni bakora tu kwa mtoto mbishi.
Jeff alipomuona yule mwalimu yeye mwenyewe akashuka kwenye gari na kumwambia mwalimu,
"Tafadhari usinichape, ila niruhusu niongee neno moja tu na anti yangu hapa"
Yule mwalimu akampa dakika mbili za kuongea na Sabrina,
"Nenda salama mama, ila naenda kumuomba Mungu uikute hiyo ndege imeshaondoka"
Sabrina alijua Jeff anasumbuliwa na utoto, kisha akamuaga pale na kuondoka.
Njiani kulikuwa na foleni sana, na kila walipoangalia mida, masaa yalikuwa yameenda sana.
Sabrina akamwambia yule dereva,
"Naona hapa tutazidi kuchelewa, nadhani itakuwa vyema kama nikichukua bodaboda na kuwahi"
Yule dereva alimuhakikishia kuwahi ila Sabrina alihisi kuchelewa na kuamua kushuka kisha akaita bodaboda na kupakia mizigo yake halafu safari ikaendelea hadi uwanja wa ndege.
Akawakuta mama na baba yake wakimngoja,
"Yani wewe mtoto una matatizo sana, haya fanya upesi usije kuchelewa maana imesalia robo saa tu"
Sabrina hakutaka kupoteza muda, moja kwa moja alipeleka mizigo yake kukaguliwa, kisha wakampekua na kuangalia tiketi yake na kuruhusiwa kuingia uwanjani.
Kwavile ilikuwa ni mara yake ya kwanza Sabrina kuingia kwenye uwanja wa ndege, alijikuta akishangaa shangaa tu kisha akaenda kupanda ndani ya ndege.
Wazazi wake walikuwa pale nje wakitaka kushuhudia mtoto wao anapoiacha ardhi ya Tanzania.
Waliondoka eneo lile hadi pale waliposhuhudia ndege ikipaa angani, na kuamua kurudi kwao kwa furaha.
Walipofika nyumbani, waliendelea na mambo mengine kama kawaida.
Mara wakamuona Sakina akiwa amekuja huku jasho jingi likimtoka, Joy akamuuliza
"Una tatizo gani leo?"
Sakina hakujibu, ila alienda moja kwa moja kuwasha luninga iliyokuwepo mule ndani kwao.
Wakakutana na habari iliyoandikwa
"Taarifa zilizotufikia hivi punde"
Habari ile ilihusiana na ndege ile ile aliyopanda Sabrina kuwa imeanguka.
Wakakutana na habari iliyoandikwa
"Taarifa zilizotufikia hivi punde"
Habari ile ilihusiana na ndege ile ile aliyopanda
Sabrina kuwa imeanguka.
Joy alijikuta akiinuka kwenye kiti na kusema,
"Uwiiiii!!! Mungu wangu!"
Na kujikuta akianguka chini na kupoteza fahamu.
Deo nae alihisi kuchanganyikiwa, alijihisi kamavile yupo ndotoni kwani hakuamini kile alichokiona na kukisikia.
Sakina ndiye aliyetakiwa kufanya kazi ya ziada kuwambembeleza ili waweze kuwa katika hali ya kawaida.
"Jamani tusipanic sana, tufatilie kwanza taarifa yenyewe"
Sakina akainama pale alipoanguka Joy na kujaribu kumpa huduma ya kwanza hadi pale Joy alipozinduka.
Deo akawaambia,
"Ngoja mi nijikaze niende huko uwanja wa ndege nikaangalie, yani siamini"
Deo hakutaka tena kupoteza muda pale nyumbani kwake kwani alihisi kuchanganyikiwa tayari, wakati anataka kutoka akakutana mlangoni na dada yake mwenye jina la mwanaye yani Sabrina mkubwa ambapo Sabrina huyo alimzuia kaka na kumuuliza,
"Unaenda wapi sasa?"
"Naenda uwanja wa ndege, kuna khabari mbaya imetokea"
"Ndiomana nimekuja kaka, tafadhari nakuomba urudi ndani"
"Hapana Sabrina, mwanangu yupo kwenye matatizo"
"Sasa wewe ukienda huko uwanja wa ndege utasaidia nini? Au na wewe unajitafutia matatizo tu kaka yangu! Tafadhari nakuomba turudi ndani tukajadili"
Deo alikuwa mbishi kwa hilo kwani muda huo
mawazo yake yalikuwa kwa mtoto Sabrina, ila dada yake alijitahidi kumsihi mpaka akakubali kurudi ndani.
Ila hakuwa na raha kabisa na alihisi kuchanganyikiwa na maisha yale, aliona kama maisha yake yanaonewa kwa wakati huo haswaa maisha ya binti yangu,
"Yani majuzi tu hapo tumetoka kwenye kesi, leo ndio kama haya yaliyotokea. Mwanangu jamani, eeh Mungu baba mnusuru mwanangu na majanga haya"
"Ndiomana nimekuja kaka, ila roho yangu inaniambia kuwa Sabrina ni mzima kabisa. Kwahiyo tungoje kwanza, tungoje miujiza ya Mungu kwakuwa anaweza kufanya chochote kwaajili yetu"
Deo alimsikiliza mdogo wake huyu kwa makini lakini hakuna alichokuwa anaelewa kwani mawazo yake yalikuwa yanampeleka mbali kabisa.
Wakati wanaongea, simu ya Deo ikaanza kuita.
Alipoipokea, habari ilikuwa ni ile ile ya ajari ya ndege huku aliyempigia simu akimpa pole.
Deo alipomaliza kuongea na simu akamwambia dada yake,
"Tafadhari, nakuomba twende uwanja wa ndege ili nikashuhudie kwa macho yangu"
"Hapana kaka, wewe ushachanganyikiwa tayari tunaweza tukasababisha mambo mengine bure"
"Hapana, sitaweza kukaa hapa ilihali sielewi chochote. Sielewi mwanangu mie jamani, sijui amekufa!!"
Deo aliinama kwa muda na kunyanyuka, ikabidi mdogo wake naye ainuke na kumfata kaka yake ili aweze kumsaidia kwa lolote lile litakalo tokea.
Walitoka na kumuacha Joy akiwa hajielewi kabisa pale chini kwahiyo ni Sakina tu aliyebaki naye kumuangalia.
Deo alifika nje na kupanda kwenye gari yake, kisha Sabrina naye akaingia kwenye lile gari la kaka yake na safari ya kwenda uwanja wa ndege ikaanza huku akili ya Deo ikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
Deo alikuwa anaendesha gari kwa haraka ili aweze kuwahi hadi mdogo wake alikuwa akijaribu kumsihi aweze kupunguza mwendo.
Walipokaribia uwanja wa ndege, palikuwa na watu wengi kiasi kwani wengi walitaka kujua mustakabali wa ile ajali waliyosikia kuwa imetokea.
Sabrina akamshauri kaka yake kuwa aweke gari yake pembeni.
Wakati anaendelea kumshauri kaka yake, mara akashtuka hadi kumfanya kaka yake naye ashtuke kutokakana na ule mshtuko alioufanya mdogo mtu, kisha akamuuliza
"Kuna nini kwani?"
"Kuna kitu nimeona, subiri"
Deo hakumuelewa dada yake huyu kuwa anamaanisha kitu gani na kujikuta akimuangalia tu bila ya kummaliza.
Kisha yule Sabrina akashuka na kuelekea mahali ambapo alisema kuwa kuna kitu amekiona.
Deo naye akajikuta akishuka na kumfatilia dada yake.
Alifika mahali akasita kidogo kwenda mbele, na kumfanya Deo naye asite na kuzidi kumshangaa mdogo wake, kisha akamuuliza tena
"Kwani kuna nini?"
"Angalia pale"
Sabrina akanyooshea kidole mahali ambako alitaka kaka yake apaone, ila ni dhahiri kwamba kaka yake hakuona chochote na kumwambia mdogo wake,
"Sioni kitu, kwani kuna nini?"
"Basi kama huoni, nisubirie hapo hapo hata usiende popote pale"
Kisha akaongoza kwenda mahali alipokuwa anamuonyeshea kaka yake kuwa apaone.
Deo alisimama palepale huku akimuangalia mdogo wake mahali alipokuwa anaelekea na kusahau kabisa kilichowapeleka kule uwanja wa ndege.
Alimuona dada yake akiinama na kuokota kitu kama jiwe, Deo hakuelewa ila alikuwa akimuangalia kila kitu ambacho mdogo wake alikuwa akikifanya.
Mara akamuona akiinuka na kwenda mbele kidogo, kisha akainama tena na kuokota kitu kama jiwe halafu akainuka na kuanza kurudi mahali alipomuacha kaka yake.
Deo alikuwa ameduwaa tu eneo lile na kumshangaa mdogo wake mpaka alipofika eneo alilosimama.
"Vitu gani hivyo Sabrina?"
"Watu hawa"
Deo akashtuka, na kumuuliza mdogo wake kwa makini
"Watu!! Kivipi?"
"Twende hivi kaka nikakuonyeshe"
Deo aliongozana na mdogo wake mpaka mahali palipoonyesha kuwa ni kiwanja cha
watoto kucheza mpira wa miguu.
Ikabidi Deo amuulize mdogo wake tena,
"Mbona sikuelewi Sabrina?"
"Hata mi mwenyewe sielewi ila tutaelewa tu hapa hapa"
Sabrina akachukua moja wapo ya yale mawe mawili aliyoyaokota kisha akalipuliza na kulituma chini, lile jiwe lilipotua chini tu liligeuka kuwa mtu aliyekuwa amevaa shuka jekundu huku amejipaka masizi usoni na kumfanya Sabrina na kaka yake washtuke na kuogopa ingawa lile jiwe alilitupa mwenyewe.
Deo akamuangalia tena mdogo wake na kumuuliza kwa mshangao
"Mbona maajabu haya Sabrina?"
Sabrina naye akavuta pumzi kwani hakuelewa kama itakuwa vile, akajikuta akipata ujasiri wa gafla na kuanza kumuuliza yule mtu aliyekuwa mbele yao.
"Ni nani wewe na una shida gani?"
Yule mtu alianza kujibu tena bila uoga wa aina yoyote ile,
"Nimetumwa"
"Umetumwa na nani?"
"Na mkubwa wangu, siwezi kumtaja"
"Umetumwa kitu gani?"
"Nimetumwa nisababishe ajari kwaajili ya mtu mmoja tu tunayemuhitaji"
"Mtu gani huyo?"
"Sabrina"
Sabrina akashtuka ila moja kwa moja akajua Sabrina anayetajwa pale ni mtoto wa kaka yake, kisha akamuuliza tena yule mtu,
"Unamuhitaji huyo Sabrina wa kazi gani?"
"Tunataka kumtoa kafara kwakuwa alikiuka masharti yetu na kumuumiza mkubwa wetu"
"Masharti yenu? Masharti gani hayo?"
"Mwenzangu ndio anayajua"
"Mwenzako yupi?"
"Huyo uliyemshika kwenye mikono yako"
Sabrina akajikuta akishtuka na kuliachia lile jiwe chini bila kufanya kama alivyofanya kwenye jiwe la kwanza yani kulipuliza kwanza.
Lile jiwe la pili nalo lilipoanguka tu chini liligeuka kuwa mtu aliyekuwa amevaa shuka yenye rangi nyeusi na kujipaka masizi usoni.
Ila yeye hakuonesha kuganda kama mwenzie bali alishika shuka la mwenzie na wote wawili wakayeyuka kabisa wala yale mawe mawili hayakuwepo tena pale chini, Sabrina alijikuta akishtuka sana na kuanza kukimbia huku kaka yake akimfata kwa nyuma.
Walifika mahali Sabrina akiwa anahema sana utafikiri kakimbia mrefu.
Deo alimuangalia kwa makini tena mdogo wake na kumwambia,
"Yani leo nimeamini maneno yote niliyokuwa naambiwa kuhusu wewe mdogo wangu, kwakweli wewe sio mtu wa kawaida"
Kisha akaanza kuondoka na kumfanya Sabrina amfate nyuma ili ajaribu kumueleza,
"Tafadhari kaka usinifikirie vibaya"
"Unajua siku zote nilijua watu wanatunga maneno kuhusu wewe kumbe ni kweli ndivyo ulivyo"
"Hapana kaka, nisikilize kwanza"
"Nitakusikiliza endapo utaniambia ukweli, wewe wale watu uliwaonaje? Na uliwezaje kuyabeba yale mawe mawili wakati unajua ni watu? Na ujasiri wa kuwahoji watu wa ajabu kiasi kile umeutoa wapi?"
Muda huo Deo alikuwa amesahau kabisa kuhusu ajari ya mtoto wake kwani haya mambo yalimtisha na kumchanganya zaidi.
"Ngoja nikueleze kaka yangu"
"Ndio nieleze tena kwa umakini kabisa"
Ikabidi Sabrina amueleze kaka yake kwa kifupi jinsi alivyowaona wale watu,
"Sikia nikwambie, wakati tunakuja hivi nilikuwa nahisi kuwa kuna kitu si cha kawaida. Pale nilipokwambia uweke gari pembeni nilihisi nywele zikinisimama na kuona kuwa kuna kitu si cha kawaida, ndipo nilipoangalia kule mbele na kuwaona wale watu, nikakuonyesha ukasema huoni kitu hapo ndio nikagundua kuwa wewe huna uwezo wa kuona kile ambacho mie nilikuwa nakiona.
Ikabidi niwafate mwenyewe, ila waliponigundua kuwa nimewaona wakajigeuza kuwa vile vijiwe, hata mimi mwenyewe sijui nilipata ujasiri wapi na kujikuta nikiweza kuviokota vile vijiwe viwili, kuna kipindi niliwahi kupatwa na matatizo na kujikuta nikijua vitu vingi kuhusu wachawi na ndiomana nikakuomba kuwa tuonde kwenye kile kiwanja.
Lile jiwe la kwanza nililitupa kwa ujasiri sababu nililipuliza kwanza yani pale nilipuliza nguvu zake na ndiomana aliweza kusema kila kitu nilichomuuliza, nilichokosea ni kwenye lile jiwe la pili sababu nilipatwa na uoga na kulitupa bila kulipuliza na kufanya wao pia wapate nguvu za kupotea eneo lile, ila kama ningepuliza majiwe yote mawili basi wale wangesema kila kitu"
Deo akamuuliza swali moja mdogo wake,
"Wewe ni mshirikina?"
"Hapana mie hata ushirikina wenyewe siupendi"
"Kwahiyo wewe ni nani?"
"Mimi ni mdogo wako"
Deo akaongoza kwenda mahali alipoacha gari yake.
Alipofika pale akajikuta akijiuliza,
"Hivi huku tumefata nini?"
Hakupata jibu na kupanda kwenye gari yake, Sabrina akamfata nyuma naye akapanda kwenye lile gari na kumuuliza kaka yake
"Inamaana umeshalizika sasa na majibu ya kitu kilichokuleta huku!"
"Hivi ni kitu gani kilichonileta huku?"
Sabrina akatambua kuwa akili ya kaka yake imeshachanganyikana na kuona ni bora warudi tu nyumbani kuliko kuendelea kuwa katika eneo hilo na kusababisha mambo mengine wakati anaona wazi akili ya kaka yake imechanganyikana.
Walipokuwa njiani, Sabrina alimuona mtu ambaye alimstua sana na kumuuliza kaka yake
"Si yule mama aliyekuwaga jirani yenu yule!"
Deo akamuangalia kwa makini na kumjibu mdogo wake,
"Ndio ni yeye, kwani vipi tena?"
"Muangalie vizuri halafu ujijibu mwenyewe"
"Namuona kawaida tu"
"Mie nahisi kitu juu yake"
Wakati Sabrina akiongea hayo, muda huo huo Deo akajiwa na kumbukumbu za binti yake na kujikuta akisema,
"Jamani mwanangu!"
Sabrina akajua kuwa kaka yake amekumbuka kila kitu, na muda huo huo akafunga breki gafla kwani ilibaki kidogo tu asababishe ajari.
Ikabidi Sabrina amuombe kaka yake na kwenda kukaa eneo la kuendeshea na kuanza kuendesha yeye mpaka nyumbani.
Walipofika, Joy alikuwa pale pale chini na alipowaona jambo la kwanza aliwauliza
"Yu wapi mwanangu Sabrina?"
Deo na mdogo wake wakaangaliana bila ya kutoa majibu na kumfanya Joy azidi kuchanganyikiwa na kuwa kamavile mtu mwenye kichaa, kwani akainuka pale chini na kwenda kumuuliza Deo huku akipiga makelele ya kilio
"Yuko wapi mwanangu? Mwanangu mimi yuko wapi jamani? Sina tena mtoto wa kike mimi jamani, namtaka mwanangu, namtaka Sabrina wangu"
Machozi mengi yalikuwa yakimtoka Joy hata Deo hakuwa na jibu la moja kwa moja kumpa mkewe na kujikuta naye akilia na kuwafanya Sabrina na Sakina nao walie.
Joy alikuwa akilia huku akiongea,
"Niitieni Sabrina wangu jamani, Sabrina wangu hayupo tena, muiteni jamani"
Huku akipaza sauti ya kilio na kuita,
"Weee Sabrina weee, Sabrina mwanangu nakuita mama yako jamani...."
Wakati akiendelea kulia huku akitamka maneno akasikia sauti,
"Mimi hapa mama nimekuja"
Kuangalia mlangoni wakamuona Sabrina akiwa amesimama.
Kuangalia mlangoni wakamuona Sabrina akiwa
amesimama.
Wote wakajikuta wakimshangaa Sabrina huku Sabrina naye akiwashangaa wao.
Ikabidi Deo ainuke na kumfata Sabrina pale mlangoni kwavile ni yeye tu aliyekuwa na ujasiri huo, kisha akamshika mkono na kumvutia kwa ndani.
Sabrina hakusita na kuingia ndani kwao.
Joy hakuamini kwakweli, alimfata mtoto wake na kumshika vizuri ili kuweza kugundua kama ni yeye kweli.
"Sabrina mwanangu ni wewe au naota?"
"Ni mimi mama, mbona hivyo mnalia kwani kuna kitu gani?"
Sabrina hakutambua chochote kilichoendelea kwao na kujikut akiwauliza kuwa wanalia nini.
Deo alimuangalia binti yake kwa makini na kuwa kama mtu anayeshangaa na kustaajabu lile tukio la Sabrina.
Deo akamuuliza mwanae,
"Hebu tuambie mwanetu, umeokokaje kwenye ile ajari!"
Sabrina akalishangaa swali la baba yake kisha na yeye akajikuta akiulza
"Ajari gani hiyo?"
Wote ndani wakaangaliana baada ya kugundua kuwa Sabrina hata hajui kama kuna ajari iliyotokea, ikabidi Deo amuulize tena binti yake
"Si tulikuacha unasafiri wewe!!"
Sabrina akawaangalia wazazi wake kwa jicho la uoga kwani alishajua kuwa ana makosa tayari kisha akaanza kuwaomba msamaha,
"Baba na mama naomba mnisamehe sana. Najua nishapoteza pesa zenu tayari, ila sio kosa langu"
"Kivipi Sabrina? Na je ni kosa la nani?"
"Ni kosa la ushamba wangu na kale katoto kadogo Jeff"
Sakina naye akashangaa kusikia kuwa mtoto wake naye anahusika na kuamua kuuliza kwa upana zaidi,
"Jeff!! Jeff kafanyaje tena mtoto wangu?"
Sabrina aliamua kuwaeleza kuhusu Jeff, kwanza kabisa aliwaeleza jinsi Jeff alivyokuwa anashtuka usiku na kumwambia Sabrina kuwa amemuotea kapata ajari na jinsi kesho yake alivyokuwa akimzuia kuwa asiende, na maneno aliyomwambia wakati anataka kusafiri.
Walimsikiliza Sabrina kwa makini, na kujiuliza kuwa mtoto Jeff alijuaje na vipi Sabrina aliweza kupona wakati alikuwa akibishia maneno ya huyo mtoto na hadi akafika uwanja wa ndege kwaajili ya safari yake, Deo akamuuliza mwanae
"Halafu ikawaje mwanangu?"
Sabrina akaendelea kuwaeleza,
"Kwanza kabisa kale katoto kalinichelewesha sana pale uwanja wa ndege yani nilichelewa sababu yake, hadi kuchukua bodaboda chanzo ni yeye. Sasa nilipoingia pale uwanja wa ndege, dah kumbe ni pazuri, si nikajikuta nashangaa ila nikaona watu wanaenda kupanda ndege nami nikawafata na kupanda, nilikaa kama dakika tano hivi kuna mtu akanifata na kuniuliza nilipomwambia ndege ninayotakiwa kupanda akaniambia kuwa nishachelewa na ndege imeshaondoka.
Kwakweli nilijisikia vibaya sana na kushuka, nilitamani kulia lakini nilijua haitasaidia, nikaogopa kurudi nyumbani kwanza kwani najua mngenisema sana.
Nilipotoka pale uwanja wa ndege, moja kwa moja nikaenda shuleni kwakina Jeff kumsema ila na kumsema kote yeye alikuwa akifurahi tu na nimekaambia sitaenda tena kukaona. Jamani wazazi wangu nawaomba mnisamehe sana mtoto wenu kwa kuwatia hasara, hapa hata sijui itakuwaje tena"
Maelezo yale ya Sabrina yalifanya waone kwamba mtoto wao kuna nguvu kubwa inayomzunguka na ndiomana inakuwa vile, kwanza walifurahi zaidi ya mwanzo.
Joy aliwatuliza na kuanza kumshukuru Mungu kwa hayo aliyowatendea.
Baada ya hapo wakamsimulia Sabrina tukio lililotokea kuhusu ile ndege aliyotakiwa kupanda kuwa imelipuka
"Kheee kwahiyo na mimi ningekuwa nimekufa!!"
"Ndio mwanangu, ndiomana ulitukuta tunalia hapa"
"Ooh asante Mungu kwa kumtumia mtoto Jeff kuyakomboa maisha yangu"
Sabrina alijisikia furaha sasa, ikabidi Deo awaambie na mengine,
"Tena kuna mambo mengine ya ajabu tuliyoyakuta huko na huyo shangazi mtu"
"Mambo gani tena?"
"Ngoja awaeleze mwenyewe, mi hata sielewi na kuelezea siwezi"
Ikabidi Sabrina mkubwa awaeleze kila kitu alichokiona uwanja wa ndege akiwa na kaka yake huyo na kuwafanya wote wazidi kushangaa maajabu yale.
Joy akajikuta akitahamaki,
"Mungu wangu, kumbe ile ajari ilipangwa kwaajili ya mwanangu tu! Lakini kwanini wanamuonea mwanangu kiasi hiki! Hivi ni lini mwanangu ataachiwa na hawa watu jamani!! Mwanangu kawakosea nini!"
Joy alijikuta akilalamika kwa uchungu sana kwani moyo ulimuuma kutokana na yale mambo aliyoyasikia juu ya binti yake.
Waliongea mengi sana na kushauriana vitu vingi, ila Sakina akawapa wazo lingine
"Jamani hapa si pa kupoteza muda, kwavile wale watu wanajua kuwa Sabrina amekufa basi asikae hapa kwanza, ikiwezekana hata asafiri na kwenda mkoa hata wa jirani kwanza kubadilisha mazingira yake. Au mnaonaje jamani juu ya hilo?"
"Ni wazo jema kabisa hilo, basi tusipoteze wakati. Mimi shangazi yake nitaenda naye"
Joy akajikuta akiguna kwanza,
"Mmh nyie wote wawili ni majanga tu, bora aende na Sakina halafu sisi tutamfataga tu"
Basi wakakubaliana juu ya hilo, kisha Sakina akaenda nyumbani kwake na kujiandaa kidogo halafu safari ya kwenda kituo cha mabasi ya kwenda mkoani ikaanza.
Walipofika kituoni kwa bahati wakapata basi la kwenda Arusha na kupanda kwavile Sakina aliwaambia kuwa Arusha ana ndugu zake.
Kisha Sakina na Sabrina wakaondoka halafu wengine wakarudi nyumbani huku wakiwa hawaamini amini kitu ambacho kimetokea kwao kwa siku hiyo.
Waliporudi nyumbani sasa wakapumua na kupumzika kwani yale mambo yaliwapa hofu na kuwachanganya tu.
Sabrina mkubwa aliwaambia kuwa siku hiyo hatoondoka hapo kwahiyo atalala hapo hapo kwaajili ya kuangalia mambo yanavyokwenda tu kwenye hiyo familia yao.
Wakiwa wamekaa pale sebleni wakapatwa na mgeni, huyo mgeni alikuwa ni yule mmama ambaye walimuona njiani wakati Deo anarudi nyumbani kwake na mdogo wake.
Wakaamua kumkaribisha yule mmama ili kujua kuwa ni kitu gani kimemleta mahali pale.
Yule mmama alianza kwa kuwapo pole,
"Poleni sana jamani, nimesikia hayo mambo yaliyowapata na kushtuka sana."
Joy akamuuliza huyu mmama,
"Kitu gani hicho kilichokushtua?"
"Si nimesikia kuwa mtoto wenu alikuwa anasafiri kwenda nje na ndege aliyopanda imeanguka"
Joy alijikuta akipatwa na hasira sana moyoni mwake, akamjibu huyu mama kwa dharau
"Sasa kama imeanguka sie tufanyeje!"
"Khee mfanyeje wakati binti yenu naye yumo?"
"Hayo hayakuhusu, nakuomba uende"
Joy aliongea kwa hasira sasa kuonyesha kwamba maswali ya huyu mama yalimchosha tayari na kuhisi kuwa huenda ana husika na kitu kilichokuwa kinataka kumpata binti yake
"Nimekwambia uende zako, unangoja nini sasa?"
Yule mmama akainuka na kuanza kutoka,
"Muone kwanza, mchawi mkubwa wewe"
Ikabidi Deo aanze kumtuliza mke wake, ila yule mama baada ya kusikia kuwa kaitwa mchawi akageuka na kuuliza tena
"Umeniita nani mimi?"
Joy hakuacha kumwambia kwavile alikuwa na hasira sana kwa wakati huo,
"Nimekwambia wewe ni mchawi tena mchawi mkubwa, ondoka nyumbani kwangu"
"Naondoka ndio ila utauona huo uchawi wangu vizuri"
Yule mama akaondoka na kumuacha Joy akiwa amevimba kwa hasira huku mumewe akikazana kumbembeleza pale.
Walipotulia kwa muda, wakajikuta wakimshangaa Sabrina mkubwa aliyekuwa amekaa kimya muda wote tangia yule mmama alipofika pale ndani, Joy akamuuliza
"Wifi, mbona hujaongea chochote?"
"Kuna kitu nakitafakari"
"Kitu gani hicho?"
"Huyu mama si mtu mzuri jamani, kwa ushauri wangu mdogo tu hebu tuondoke hapa kwa muda"
"Twende wapi sasa?"
"Nyie twendeni, halafu nitawaambia pa kwenda, najua kaka una pesa bora ufanye haya mambo sasa kisha tuendelee na vitu vingine"
Deo alikuwa akimshangaa mdogo wake kwa muda mwingi sana kwani alikuwa akimuma kama ni mtu wa ajabu
"Mbona una mambo ya ajabu kiasi hicho mdogo wangu? Unajua huwa sikuelewi kabisa?"
"Ni ngumu kunielewa kwa sasa ila ipo siku utanielewa kaka. Nawaomba tufanye ninavyosema ili tuwe na amani kwa muda na kujua jinsi ya kupambana na haya mambo"
Ikabidi wamsikilize na kuamua kufanya walichopanga kisha wakajiandaa na kuianza safari.
Moja kwa moja wakampeleka Sabrina mkubwa nyumbani kwake na wao kuanza safari ya kwenda Arusha kumfata Sabrina mdogo ili kuweza kuendana na mawazo waliyopewa na Sabrina mkubwa.
Sakina na Sabrina walifika salama kwenye mji wa Arusha na moja kwa moja wakaelekea hotelini kwanza ili waweze kupumzika hapo na kesho yake wafikirie kuianza safari ya kwenda kwa mojawapo za ndugu wa Sakina.
Sabrina alikuwa na mawazo sana na kujiona kuwa binti mwenye mkosi katika maisha yake, alijihisi vibaya sana.
Baada ya muda kidogo akamuomba Sakina kuwa aweze kwenda kukaa nje pale mbele ya hoteli ili apate kidogo upepo wa Arusha.
Sakina hakuna na pingamizi, kisha akatoka naye nje na kumuacha apumzike halafu yeye akarudi ndani kuweza kuendelea kuwasiliana na ndugu zake.
Sabrina alipokuwa amekaa pale na mawazo yake, akatokea kijana wa makamo kiasi na kumsalimia pale kisha akamwambia,
"Samahani dada, naweza kukaa hapa karibu na wewe!"
Sabrina akamuitikia kwa kichwa na kumfanya yule kijana akae mahali pale, kisha akaanza kujitambulisha pale,
"Samahani dada, mi naitwa Sam. Je wewe mwenzangu unaitwa nani?"
"Naitwa Sabrina"
"Nashukuru kukufahamu, mbona umejiinamia hapo una matatizo gani Sabrina?"
"Matatizo ya kimaisha tu"
"Niambie basi hata kidogo tu kama hutojali"
Sabrina alimuangalia huyu kijana kwa makini huku akitamani kumueleza na huku akisita, ila moyo wake ukaamua kumwambia kwa kifupi tu kuwa alitakiwa kwenda masomoni ila ndege ikamuacha ila hakusema kama hiyo ndege ilipata ajari, yule kijana akamuhurumia Sabrina na kumwambia,
"Pole sana Sabrina, ila usiwaze sana hilo sio tatizo kubwa"
"Sio tatizo kubwa !! Unadhani mi nitapata wapi tena pesa ya nauli kwenda huko?"
"Usijali, nitakusaidia"
Sabrina akashangaa na kushtuka
"Utanisaidia kivipi?"
"Si hiyo pesa ya nauli nitakusaidia"
"Khee wewe utaitoa wapi?"
Yule kijana akacheka na kumuangalia tena Sabrina,
"Unanidharau! Hata hii hoteli ni yangu pia"
Sabrina akashangaa sana kumuona yule kijana mdogo kuwa na uwezo kiasi kile.
"Mbona unaonekana bado mdogo?"
"Ni mwili wangu tu ila mimi ni kijana mkubwa tu"
Sabrina akaongea mengi sana na yule kijana na kujikuta akifarijika moyo wake kwani yule kijana alikuwa akimwambia mengi ya kumtia moyo na kumpa amani kwenye ro ho yake.
Deo na mkewe waliwasili Arusha usiku sana na kuamua kutafuta hoteli ya karibu ili wapumzike halafu kesho yake waanze kuwatafuta Sabrina na Sakina hewani kwakuwa muda huo hawakupatikana.
Kulipokucha waliwapata hewani na kujishangaa kuwa wote wapo hoteli ya aina moja.
Ikabidi wakutane pamoja na kujadiliana mawili matatu ya kitu cha kufanya, Deo alienda pembeni na binti yake kuongea
"Nahitaji uende mwanangu ukaendelee na hayo masomo ila kuna mtu nangoja anitumie pesa kiasi nikakate tiketi nyingine"
"Usijali baba, kuna mtu amesema kuwa atanisaidia"
"Mtu gani huyo?"
Sabrina akamueleza baba yake kila kitu kuhusu kijana aliyekutana naye, Deo naye akapenda kuonana na huyo mtu.
Mchana wa siku hiyo, wote wakakutanishwa na huyo kijana naye akakiri mbele ya wazazi wa Sabrina kuwa yupo tayari kumsaidia.
Wote wakafurahi na kukubaliana juu ya hilo.
Joy akamuita pembeni mwanae na kumwambia,
"Kuwa makini mwanangu, hata shangazi yako aliolewa na mtu anaiwa Sam"
"Sio tatizo mama, huyu hata kunitongoza hajanitongoza yani tofauti kabisa na wengine"
Mama yake akakubaliana nae.
Baada ya siku mbili Sabrina alifanikiwa kusafiri na kwenda kwenye nchi aliyotakiwa kusoma kisha wazazi wake na Sakina wote wakarudi mjini kwao huku wakiwa na amani baada ya Sabrina kuwapa majibu kuwa amefika salama.
Walipokuwa nyumbani kwao, Sakina akaamua kumueleza Joy ukweli kuhusu kitu kilichokuwa kinamsumbua binti yake Sabrina.
"Ni kitu gani hicho?"
"Alikuwa na kinyama fulani kimeota huku kwenye sehemu....."
Kabla hajamaliza kuongea, wakashtuka na mshindo mkubwa uliotokea nje ya nyumba ile.
Kabla hajamaliza kuongea, wakashtuka na
mshindo mkubwa uliotokea nje ya nyumba ile.
Ule mshindo uliwafanya wajikute wakiulizana kwa pamoja kuwa,
"Kuna nini?"
Wakatazamana, kisha wote wawili wakainuka ili waweze kwenda kuangalia nje wajue kuna kitu gani kinaendelea.
Ila wakati wanataka kutoka nje Sakina kuna kitu kikamzuia na kujikuta naye akimshika mkono Joy na kumzuia kwenda nje.
"Kwani vipi Sakina?"
"Kuna kitu kimenizuia, nahisi huko nje si kwema hebu tungoje kwanza"
Joy akatulia kimya huku akimtafakari Sakina na ule mshindo.
Kimya kikatawala kabisa hata wao walikuwa kimya kabisa kamavile kuna mtu aliyewakataza kuongea jambo lolote lile.
Muda kidogo ukapita, kisha Joy akauvunja ukimya ule uliokuwa umetawala pale ndani.
"Mbona hivi Sakina!!"
Sakina alikuwa kimya kamavile kuna kitu anakisikilizia, gafla wakasikia mshindo mwingine na muda huo huo ikasikika sauti ya paka kama ambavyo huwa wanali, ile sauti ilikuwa kama inalilia mule ndani kwa Joy na kumfanya Joy ahamaki,
"Ndani kwangu sina paka wala kiumbe chochote chenye umbo la mnyama, sasa hiyo sauti ya paka inatokea wapi? Lazima ni nguvu za giza tu"
Joy akaanza kukemea ile hali na ile sauti ya paka aliyoisikia kuwa ishindwe.
Sakina alikuwa kimya tu huku akimuangalia Joy akiendelea na maombi yake.
Baada ya muda kidogo hali ikawa shwari kabisa na hakikusikika kitu chochote tena.
Wakiwa wametulia mule ndani, wakasikia mtu akibisha hodi.
Ikabidi Joy ainuke ili kuweza kumkaribisha, alikuwa ni Fredy yule rafiki wa Sabrina.
"Karibu sana Fredy, za siku nyingi!"
"Nzuri tu za hapa"
"Nzuri kabisa, mbona leo hujachangamka kama unavyokuwaga siku zingine?"
Joy alimuuliza Fredy kwani hakuwa kawaida kama anavyokuwaga siku zote haswaa kwa kipindi cha nyuma ambacho alikuwa anakuja kuwatembelea, ila Fredy hakujibu swali kuwa kwanini hajachangamka na badala yake akauliza swali jingine
"Kwani Sabrina yuko wapi?"
"Si amesafiri kwani hujui?"
"Amesafiri kwenda wapi?"
Joy akaona anaulizwa maswali kama polisi yani kamavile huyu muulizaji ana haki ya kujua alipo Sabrina.
Ingawa Joy anaelewa wazi kuwa Sabrina hakuwaaga wale rafiki zake ila bado hawakuwa na haki ya kuuliza kwa jazba kiasi kile ambacho yule Fredy alikuwa akiuliza.
Ikabidi Joy ajaribu tena kumkaribisha hata akakae kwanza.
"Karibu basi ukae kwanza"
Yule Fredy alijivuta na kwenda kukaa kwenye mojawapo ya makochi pale ndani, kisha Joy akaenda mlangoni ili aurudishie vizuri.
Alipoona kuwa geti lake nalo lipowazi akaamua kwenda kulifunga kwanza.
Alipofika getini akapata wazo la kuangalia pale nje kwake.
Alipoangalia kwa mbali akamuona mtu kama Fredy na kujiuliza mwenyewe,
"Sio Fredy yule!!"
Akamuangalia kwa makini na kugundua kuwa ni yeye kwavile macho yao yalipogongana alitabasamu na kisha Fredy akaanza kuja pale alipo Joy.
Wakati huo Joy alikuwa ameganda kama sanamu huku akijiuliza kuwa je yule aliyeingia ndani kwake ni nani kama Fredy yupo huku nje.
Yule Fredy alipokaribia tu Joy akamuuliza bila salamu,
"Mpo mapacha?"
"Hapana mama, shikamoo"
Joy hakuitikia kwani akili yake ilianza kuvurugika na kujikuta akimuuliza yule yule Fredy,
"Sasa aliyekuwepo humu ndani kwangu ni nani?"
Fredy naye akashangaa na kumuuliza,
"Kivipi mama?"
"Twende ukaone"
Joy akamshika Fredy mkono na kuanza kumvutia kwenye nyumba yake ili akaone na aseme mwenyewe.
Walipoingia ndani wakapatwa na mshangao kwavile Sakina alikuwa chini amezirai na wala yule Fredy aliyeingia mwanzo hakuwepo mule ndani.
Joy alitahamaki sana na kujiuliza kuwa ni kitu gani kinaendelea, waliinama na kuanza kumpa huduma Sakina ambaye alikuwa ameanguka pale chini.
Sakina naye alipozinduka akashtuka kumuona yule Fredy na kutamani kupiga makelele, ila Joy ndio akajaribu kumtuliza ili awe sawa kwanza.
Baada ya muda kidogo Sakina akatulia na kurudi katika hali ya kawaida kabisa.
Fredy alikuwa pembeni akishangaa kuwa aliambiwa kuna mwingine yupo ndani akamuone ila hakumuona na badala yake ndio kumkuta yule Sakina akiwa amezimia.
Walipotulia ikabidi naye aulize kuwa kuna kitu gani, wakamueleza kuwa kuna mtu alifika pale mwenye muonekano kama wake na kumfanya azidi kushangaa
"Nilipotoka kufunga geti ndio nikashangaa kukuona wewe sasa"
Fredy alishangaa sana na kuuliza,
"Huyo mtu yuko wapi sasa?"
"Ndio hapo cha kushangaza kuwa ndani hatujamkuta tena"
"Mmh mambo ya kutisha hayo jamani"
Walikaa pale ndani ila wote walijawa na uoga kwenye mioyo yao tu.
Muda kidogo Sakina naye akapata ujasiri wa kuzungumza,
"Unajua yule mtu alibadilika na kuwa yule mmama wa siku ile, nikataka kupiga kelele lakini kabla sijapiga kelele akageuka na kuwa paka mweusi kwakweli sijui ni nini kiliendelea baada ya hapo"
"Kheee makubwa haya jamani, mbona mambo ya ajabu kutokea kwenye nyumba yangu mie Joy! Bora nimpigie simu mchungaji aje leo"
Joy hakutaka kupoteza wakati, aliamua kuchukua simu yake na kumpigia mchungaji wao.
Fredy naye aliamua kuaga kwani aliona ile nyumba kuwa na mauzauza tu, kwahiyo aliaga na kuondoka.
Jioni mchungaji na watu wengine wa maombi wakafika pale nyumbani kwa Joy na kufanya ibada kwa pamoja.
Baada ya ibada kila mtu akarudi nyumbani kwake, hata Deo aliporudi na kusimuliwa kilichotokea hakuamini kabisa kama ni kweli yametokea kwenye nyumba yake mwenyewe.
Kesho yake Joy alimfata Sakina ila kumuuliza vizuri kuhusu binti yake.
"Uliniambia mwanangu Sabrina alikuwa na kitu gani?"
"Mmh yasije yakatokea ya jana bure, mie sipo tayari kukabiliana na matatizo dada kwahiyo sitaweza kukwambia tena"
"Sasa mimi nitajuaje ukweli?"
"Utaujua tu, ipo siku binti yako atakueleza kila kitu kinachohusiana naye na kila kitu kinachomsumbua katika mwili wake, kwahiyo usijali chochote"
"Hivi unajua kama Sabrina huwa hasemi?"
"Najua ndio, ila ipo siku atakwambia mwenyewe, yani hakuna hata haja ya mimi kukwambia. Ila uamuzi wenu wa kumpeleka kwenda kusoma mbali mlitumia busara sana kwamaana hapa asingeweza kusoma kamwe"
Joy alielewa vizuri kauli ya Sakina ila aliona ni mbali sana kumngoja mtoto wake mpaka arudi, alitamani sana kuambiwa kila kitu na Sakina ila Skina alikataa kumwambia ukweli huku akisisitiza kwamba anajikwepesha na matatizo ya kujitakia.
Ikabidi Joy aache mambo kama yalivyo na kumuaga Sakina kisha kurudi nyumbani kwake ili kuendelea na mambo mengine ya umuhimu.
Maisha yaliendelea bila ya chochote kile kibaya kuwapata kwa kipindi hicho.
Miaka ilipita na maisha nayo yaliendelea, Sabrina hakuacha kuendelea kuwasiliana na yule kijana Sam aliyemsaidia.
Alimfanya kuwa rafiki yake mkubwa sana na wala Sabrina hakutaka tena kujiingiza kwenye maswala ya kimapenzi kwani kila alipofikiria alikopita alijikuta akiumia sana na kutokutaka tena kuwa na mpenzi.
Kwajinsi alivyokuwa akiwasiliana na Sam tena bila ya kumtaka kimapenzi aliona ndiye mwanaume pekee wa tofauti duniani kwani wengine wote walishamfanyia mambo ya ajabu ambayo yalimfanya alie muda wote, ila sasa anaishi kwa furaha na amani huku akiwasiliana na kijana Sam kama ndugu yake au rafiki yake wa karibu.
Jeff aliporudi kwao alimkuta mama yake kama kawaida, kwa kipindi hiki alikuwa amekua kiasi cha kuweza kwenda mwenyewe shule na kurudi mwenyewe kwenye likizo ikifika.
Kwavile ilikuwa ni kipindi kirefu tangu Sabrina aondoke akajikuta akimkumbuka sana Sabrina na kuamua kumuulizia kwa mama yake,
"Hivi mamdogo Sabrina atarudi lini?"
"Khee! Miaka yote hiyo bado unamkumbuka Sabrina! Kweli ameitawala akili yako"
Jeff akacheka na kumuuliza tena mama yake,
"Niambie bhana mama, atarudi lini?"
"Kwakweli sijui atarudi lini, ila nikisikia kuwa anataka kurudi nitakwambia. Kwani nimemkumbuka sana pia, ila unataka nini?"
"Yeye ndio mshauri wangu"
"Kaone vile, lini umeshauriwa na Sabrina? Au ndio zile story zenu za kudanganyana za sungura na fisi"
Jeff akacheka sana na kuonekana kuwa amekumbuka mambo ya mbali sana. Na kumwambia mama yake,
"Ila nashangaa yeye hata hanikumbuki tangia ameondoka hadi roho inaniuma"
"Usijali mwanangu, atakuwa anatingwa tu si unajua mambo mengi kule alipo"
Akaongea mambo mengi na mama yake pale kisha akamuaga na kurudi shuleni kwao.
Sabrina aliendelea kufurahia maisha ya nchi aliyokuwepo huku akiendelea kuwasiliana na kijana Sam.
"Karibia nitarudi Sam, hata sijui nitapata kazi wapi!"
"Hilo sio tatizo Sabrina, ila bora urudi ni miaka mingi sasa imepita"
"Basi nikutumie cv zangu uanze kusambaza kwenye sehemu tofauti ili nipate kazi Sam"
"Usijali Sabrina, niamini mimi, kazi umeshapata tayari"
Maneno ya Sam yalikuwa yanampa sana moyo Sabrina na kumfanya ajilaumu kwa kuchelewa kwake kufahamiana na mtu kama Sam kwani alikuwa akimpa furaha na faraja kwa muda wote aliokuwa akiwasiliana naye.
Wakaongea mambo mengi na kupanga mambo mbali mbali, hakuna aliyechoka kuongea na mwenzie na hakuna aliyewahi kumtamkia mwenzie kuwa anamuhitaji kimapenzi.
Fredy alimkumbuka sana Sabrina ila hakujua ni jinsi gani ataweza kumpata kwani hakujua hata alipo kwa wakati huo, aliamua kumwambia ukweli nduguye Francis
"Kwakweli miaka yote hii nimejaribu kumsahau Sabrina ila nimeshindwa, nisaidie cha kufanya"
"Sasa mie nitakusaidia kitu gani? Labda uende kwao"
"Itabidi nifanye hivyo ili nijue kuwa atarudi lini, kwakweli nimemkumbuka sana yani hadi nakosa raha nikimfikiria"
Francis alitulia kimya huku akimsikiliza kwa makini nduguye, na muda huo huo yeye mwenyewe alijihisi akimpenda sana Sabrina na kujiona wazi kuwa Sabrina ndio mwanamke anayemuhitaji katika maisha yake ila hakuelewa kuwa ni kwanini yeye na nduguye wamejikuta wakiwa na hisia zinazofanana na kujiuliza kuwa ni nani anayempenda Sabrina kiukweli kati yao kwakuwa alijiona yeye na nduguye wakiwa na upendo unaofanana kwa Sabrina.
Kila mmoja kwa wakati wake akajipanga kwenda kwakina Sabrina ili kuulizia ujio wa Sabrina.
Siku zilipita na Sabrina akamaliza masomo yake na kuanza kujipanga kurudi nyumbani kwao.
Alitoa taarifa kwao na wote walifurahi na kuona vyema Sabrina arejee kwao, kwahiyo wote walioenda kumuulizia Sabrina waliambiwa siku atakayorudi na kufanya wamngoje kwa hamu.
Siku ilipofika, Sam alijipanga vyema kwenda kumpokea Sabrina uwanja wa ndege.
Alishangaa kuwaona na wengine pale akajua wote walikuwa wakingojea ndugu zao.
Sabrina alitokea mbele ya macho yake na kumfanya Sam ajawe na tabasamu mbele yake huku akitegemea kuwa Sabrina ataenda na kumkumbatia.
Akamshangaa Sabrina akienda kwa kijana mwingine aliyekuwa amesimama peke yake na kumkumbatia kwa furaha.
Akamshangaa Sabrina akienda kwa kijana mwingine aliyekuwa amesimama peke yake na kumkumbatia kwa furaha.
Sabrina alimkumbatia yule kijana kwa shauku sana na kumfanya Sam ahisi kupatwa na wivu juu yao.
Akatamani hata aende kuwatoa pale walipokuwa wamekumbatiana ila alijiona wazi kuwa hatakiwi kufanya vile hata watu watamshangaa.
Sabrina aliendelea kumkumbatia yule kijana bila hata ya kujua kama kumbatio lake kwa yule kijana kuna watu waliumia haswaa Sam ingawa alivumilia.
Sabrina alionekana kumfurahia sana yule kijana,
"Siamini kama umekuwa mkubwa kiasi hiki jamani, yani sura yako haibadiliki mwanangu. Sikutegemea kama ungekuja kunipokea na wewe jamani"
Sabrina aliongea sana kwani alifurahi na hakutegemea, kisha akaenda alipo Sam na kumfanya Sam agundue wazi kuwa Sabrina alimuona sema alimuanza mtu muhimu zaidi kupita yeye.
Akamkumbatia pale Sam na kumsalimia huku akipepesa macho yake kuwatafuta wazazi wake,
"Inamaana hawajaja?"
"Wakina nani?"
"Wazazi wangu"
"Wapo hapo nyuma kidogo wanakungoja"
Kisha Sabrina akaongozana na Sam kuwafata wazazi wake, baada ya hatua chache akasita na kugeuka nyuma kisha akamuita mtu kwa jina.
Muda huo Fredy na Francis nao walikuwa pembeni, na Sabrina aliposita na kugeuka walijua wazi wataitwa wao ila akaitwa yule kijana ambaye Sabrina alimkumbatia mwanzo,
"Jeff twende"
Jeff naye hakusita na kuanza kumfata Sabrina.
Wazazi wa Sabrina walifurahi sana na kumpokea mtoto wao kwa shangwe, kisha safari ya kwenda nyumbani ikaanza.
Sabrina alifurahi sana kurudi tena nyumbani kwao kwani ni miaka mingi ilipita bila ya yeye kuwa kwao, akafurahi kuwaona kaka zake ambao nao walikuwa wakimngoja kwa hamu.
Wakafanya tafrija ndogo ya kumpokea Sabrina na wote walikuwa na furaha siku hiyo.
Sam alitulia kabisa huku akiweka matukio yote kwenye kichwa chake, hakuweza kuacha tukio hata moja kwani yote aliona kuwa na maana kubwa sana katika maisha yake.
Muda huu, Sabrina alienda kukaa karibu na Sam kwani alimuona kama mtu aliyepooza kabisa na hakuwa na raha.
Sabrina alipokaa tu akaulizwa swali na Sam,
"Ushamaliza kupiga picha?"
"Aah na yule mtoto!! Nishamaliza tayari"
"Naona umemzoea sana huyo kijana"
"Tena sana, yani ni mtu muhimu sana maishani mwangu"
Sam alimuangalia tu alivyowahi kujibu bila kujua ni kwa jinsi gani yalimuumiza kwenye moyo wake.
Walifurahi pale mpaka muda ulipokwisha na kuagana.
Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana nyumbani kwao hata Sabrina alipokuwa amelala alikuwa akitabasamu na kuonyesha kuwa alikuwa na furaha sana siku hiyo.
Alipopitiwa na usingizi, akajiwa na ndoto, hiyo ndoto ilimuonyesha kuwa anaolewa na watu wengi walijaa ila alipotaka kumgundua mume wake kwenye ile ndoto akajikuta akishtuka sana na kuamka, kisha akakaa na kujisemea,
"Sitaki kuolewa, najua hakuna wa kunipenda mimi kiukweli zaidi ya ndugu zangu wanao nizunguka, ila kwanini niote kuwa naolewa!! Sitaki kuolewa kwakweli"
Sabrina alitulia huku akiilaumu ndoto yake aliyoiota, kisha akaendelea kulala hadi palipokucha.
Sam alijiona vyema kumpenda Sabrina ila Sam alikuwa na tatizo ambalo hakupenda hata mtu mmoja alijue tatizo lake hata wazazi wake hakuwaambia na wala hawakujua kama ana hilo tatizo.
Akawaza sana kama ataweza kumwambia Sabrina tatizo lake na akaeleweka, akawaza kama Sabrina akiamua kumtangaza itakuwaje, akawaza pia swala la kumwambia Sabrina kuwa anampenda wakati alimzoea kama rafiki tu!!
Sam alijikuta akiwaza mambo mengi sana kichwani mwake ila akili yake ilimwambia wazi kuwa anampenda Sabrina tatizo alilokabiliana nalo ni namna ya kumueleza Sabrina huyo.
Francis na Fredy kila mmoja alirudi kwao kwa muda wake na kujikuta wote wawili wakijiuliza,
"Inamaana Sabrina hakutuona au ni dharau?"
"Pale imeonyesha wazi kuwa hatuna umuhimu tena kwake"
"Ila me siwezi kukubali Francis"
"Kama huwezi kukubali inamaana unataka kufanya kitu gani?"
"Najua nitakacho kifanya ila siwezi kukubaliana na hili swala kamwe"
Francis alimuangalia tu Fredy huku akijaribu kusoma mawazo yake kuwa ni kitu gani amepanga kukifanya, kisha akamshauri nduguye,
"Ila kuwa makini usije kufanya mambo ya ajabu sababu ya mapenzi ndugu yangu wakati hata mimi mwenyewe uliyenikuta nimeachia ngazi."
"Ni wewe ila sio mimi"
Francis hakuwa na jinsi, zaidi ya kumuacha nduguye aamue kufanya kile kitu anachotaka mwenyewe.
Baada ya siku mbili tatu kupita, Sakina alienda nyumbani kwa Joy kwa lengo la kuongea na Sabrina kuhusu mtoto wake.
"Unajua simuelewi Jeff mwanangu, sijui hata amekumbwa na nini kwa siku mbili hizi amenyong'onyea sana"
"Kwani umemuuliza mwenyewe anasemaje?"
"Ukimuuliza anasema yupo sawa tu"
"Basi usijali"
"Nisijali nini sasa?"
"Ndio kukuwa huko, usiwe na mashaka naye"
"Kukuwa ndio anyong'onyee vile!!"
"Si unajua kama mwanao yupo kwenye kipindi cha balehe!! Kwahiyo usijali sana"
"Kipindi cha balehe ndio mtu ananyong'onyea?"
"Usikute mapenzi nayo yameanza kumpa mawazo, kwahiyo usijali atakuwa sawa tu"
Sakina ikabidi akubaliane na Sabrina kuwa mtoto wake amenyong'onyea kutokana na kipindi hicho cha ukuaji kwake.
Kisha Sakina akaaga na kurudi nyumbani kwake.
Baada ya wiki kupita, Sabrina akaletewa khabari njema na Sam kuwa anahitajika kwenda kufanya kazi kwenye shirika lao haraka iwezekanavyo.
Sabrina alifurahi sana kwani hapakuwa na mambo ya usahili wala nini, alichotakiwa yeye ni kwenda kazini tu.
Yote hiyo ni kutokana na ukaribu wake na Sam ukizingatia Sam ndiye aliyekuwa na mamlaka makubwa na shirika hilo.
Sabrina alimshukuru sana Mungu kwa kumkutanisha na Sam na kuanza kuamini kuwa kila kitu katika maisha hutokea kwa sababu fulani, kwani mambo yaliyotaka kumpata kipindi kile ndiyo yalimfanya kukimbilia jijini Arusha na kukutana na kijana huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa sana katika maisha yake.
Sabrina alijiandaa kwaajili ya kwenda kuripoti kazini kwa siku ya kwanza.
Mama yake akamuita pembeni na kumuuliza,
"Hivi hakuna chochote kinachoendelea kati yako wewe na Sam kweli?"
"Hakuna chochote mama"
"Mmh Sabrina mwanangu, mimi ni mtu mzima usinifiche"
"Huo ndio ukweli mama, yani huwezi amini hata kunitongoza Sam hajawahi mama"
"Mmh makubwa haya jamani, hata siamini tena siamini kabisa. Ila mficha maradhi kifo kitamuumbua"
Huku akionyesha ishara ya kama mwanamke mjamzito na kumfanya Sabrina acheke kwavile aliyokuwa akimwambia mama yake yalikuwa ya kweli ila mama yake hakutaka kuamini kabisa kama kuna ukweli wowote ndani yake. Kisha Sabrina akamuaga mama yake na kuondoka zake.
Alipofika kwenye ofisi alizoelekezwa alipelekwa moja kwa moja kwenye ofisi ya Sam kisha Sam akaenda kumuonyesha Sabrina ofisi atakayokuwa na kumfanya Sabrina afurahi zaidi.
Kwakweli Sabrina alishangaa kuwa na bahati kiasi kile, wakati wenzie wanahangaika mitaani na mavyeti yao kutafuta kazi hadi soli za viatu kuisha yeye kapata kazi kiulaini kabisa tena bila jasho, hapo akaamini ule msemo wa ongea na watu uvae viatu kwani hakutegemea kabisa.
Sam akamwambia Sabrina,
"Usijali Sabrina utakuwa unaelekezwa taratibu hadi utazoea mwenyewe, usiwe na wasiwasi kabisa"
"Asante sana Sam, sijui hata nitakulipa nini"
"Hata usijali, wewe fanya kazi yako tu. Mimi nipo kwaajili yako"
Sabrina alijisikia fahari sana huku akitunza ya kumsimulia mama yake nyumbani.
Baada ya kazi, Sam akamrudisha Sabrina nyumbani kwao kisha akamuaga na yeye kwenda nyumbani kwake.
Moja kwa moja Sabrina alikaa na mama yake kuulizwa habari za kazi aliyoitiwa
"Kwakweli mama ni jambo la kumshukuru Mungu sana, Sam ni kijana mwenye roho nzuri na mkweli."
"Niambie khabari za hiyo kazi mwanangu, na siku hizi umebadirika yani tangu uliporudi kila unachosema lazima uweke kumshukuru Mungu na pia unakumbuka sana kusali"
"Ni mambo ya Sam hayo mama, wakati nipo uingereza alikuwa akinikumbusha sana kusali, pia anapenda sana kumshukuru Mungu ndiomana amebarikiwa kiasi kile. Kwakweli mama, Sam ana hela, kwa kifupi ni tajiri"
Sabrina alianza kumueleza mama yake kuhusu vitu vichache tu ambavyo Sam anamiliki na kumfanya mama yake tamaa imshike na shauku pia.
"Huyo ndio mwanaume mwanangu, mng'ang'anie, mshikilie, usimuache aende kwa wengine usije kula wa chuya kwa uvivu wa kupembua. Mwanangu, mng'ang'anie huyo Sam ng'ang'ani ili uwe mke wake"
"Jamani mama, yote hayo yanakutoka bure tu. Huyo Sam mwenyewe hajawahi kunitongoza hata mara moja, na mimi kumtaka siwezi kwanza nalinda heshima yangu na pili sitaki kuumia kama kipindi kile. Nimekuwa Sabrina mpya mimi, sina mchumba wala mpenzi. Mama, kama Sam ananipenda basi ataniambia na kiukweli sitaweza kusema hapana ingawa sijapanga kuwa na mpenzi"
Joy alimsikiliza mwanae huku akiombea muda wowote Sam aweze kumtongoza mtoto wake, hata yeye mwenyewe alishangaa kuwa kwanini Sam hamwambii Sabrina kuhusu kuwa naye wakati dalili zote za kuwa anamuhitaji zinaonekana,
"Kwanini hakwambii mwanangu?"
"Muda utaamua mama, labda muda wake bado"
Kisha Sabrina akaenda kuendelea na mambo mengine.
Kesho yake asubuhi, Sam alifika kwakina Sabrina kumpitia kisha safari ya kuelekea ofisini ukaanza.
"Usiwe unajisumbua hivi Sam jamani, kunipitia kila siku utaweza!!"
"Jana yenyewe sababu ulikataa tu nisikupitie ila usingekataa ningekuja, kila kitu naweza kufanya kwako wewe Sabrina"
Sabrina alitulia kimya kidogo na kuendelea kuongea,
"Ila mimi naona unasumbuka sana jamani"
"Nimekwambia usijali Sabrina, tena wiki ijayo kuna nyumba nitakupeleka ukaishi huko, huwa tunawapangishia wafanyakazi wetu ili na wewe uache kuwategemea wazazi sasa na uanze maisha yako mwenyewe. Wao wamekusomesha na kazi yao imeishia hapo, kwasasa ni wewe kujiendeleza na maisha yako"
Sabrina akakubaliana na Sam na kuona kuwa amepewa ushauri unaofaa kwenye maisha.
Safari ya ofisini iliendelea na walipofika kazi nayo iliendelea.
Baada ya wiki moja, Sabrina alipelekwa kuangalia nyumba aliyotafutiwa na ikamvutia sana, aliipenda na kuifurahia.
"Asante Sam"
"Usijali Sabrina, hivi vitu ni vya kawaida tu"
"Yani nimefurahi sana hata sijui niseme vipi furaha yangu ilivyo hapa"
Muda wote Sabrina alikuwa akitabasamu tu, alijisikia raha sana na kuona anapendwa na Sam ingawa Sam hakumtamkia kuwa anampenda.
Kesho yake Sabrina alienda kwao na kumpeleka mama yake kwenye nyumba aliyotafutiwa.
"Mmh mwanangu, yani juzi tu ndio umetafutiwa nyumba ya aina hii!! Huyu kijana anakupenda sana mwanangu"
Sabrina alikuwa akitabasamu tu na kufurahi.
"Sina cha kusema mama yangu, ila nina furaha sana"
"Lazima ufurahi mwanangu, na uendelee kuwa na utulivu huo huo ili huyu kijana azidi kukupenda mwanangu"
Sabrina alikuwa akipendezewa tu na maneno ya mama yake, kisha siku hiyo Joy akalala kwenye nyumba ya mwanae ili kuweka baraka kwenye nyumba hiyo.
Maisha yaliendelea kuwa ya furaha kwa upande wa Sabrina, huku akipelekwa ofisini na kurudishwa kila siku na Sam tena bila ya kuambiwa chochote kinachohusu mapenzi na kumfanya Sabrina ahisi kuwa huenda Sam aliamua tu kumsaidia ila sio mapenzi wala nini.
Siku moja wakati Sabrina anarudishwa nyumbani na Sam, simu yake iliita. Kuangalia ilikuwa ni namba ngeni, Sabrina akaipokea na kuongea nayo.
Sam alimsikia Sabrina akimuelekeza yule mtu kuwa afike nyumbani kwake, Sam akajikuta wivu ukimjaa moyoni na kutamani kumjua huyo mtu ambaye Sabrina alikuwa akiongea naye kwenye simu.
Sam alimfikisha Sabrina kwake na kuondoka, ila hakuwa mbali na nyumba ya Sabrina.
Sabrina aliingia ndani, na kuweka mkoba kisha akatoka nje kama dakika tano kumngoja mgeni wake.
Akafika Jeff mahali pale na moja kwa moja alienda kumkumbatia Sabrina kwa nguvu huku machozi yakimtoka.
Sabrina aliingia ndani, na kuweka mkoba kisha
akatoka nje kama dakika tano kumngoja mgeni
wake.
Akafika Jeff mahali pale na moja kwa moja
alienda kumkumbatia Sabrina kwa nguvu huku
machozi yakimtoka.
Sabrina akamshangaa Jeff kuona akitokwa na machozi, moja kwa moja akamshika mkono na kuingia naye ndani, bila kujua kama Sam alikuwa akiwaangalia na moyo kumuuma sana ila hakutaka kufanya chochote kwa siku hiyo zaidi ya kurudi kwenye gari yake na kuondoka zake kwenda nyumbani kwake.
Sabrina alimfikisha Jeff ndani na kumkalisha kwenye kochi ili amueleze matatizo yake na ajue kitu gani kinamliza.
"Una tatizo gani Jeff? Niambie mwanangu"
"Sijui hata nina tatizo gani"
"Kwanini hujui? Na mbona unalia?"
"Najihurumia mamy, sijielewi kwakweli, sijitambui kabisa"
"Nieleze basi tatizo lako"
Muda huu Sabrina alikuwa karibu sana na Jeff huku akimbembeleza, Jeff naye aliinama bila ya kusema chochote kile. Kisha Sabrina akamuuliza Jeff,
"Inamaana unanificha? Hutaki kuniambia ukweli?"
"Nashindwa kusema mamdogo"
"Sasa ukishindwa kusema kwangu utaweza kwa nani? Mimi ndio mtu pekee ninayekuelewa Jeff, tafadhari niambie"
Jeff bado aliendelea na msimamo wake wa kushindwa kusema na kumfanya Sabrina achukie sasa,
"Kama kusema hutaki umekuja kwangu kufanya nini? Haya jilize hapo ukichoka utaniita"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani kwake na kumuacha Jeff akiwa pale sebleni amejiinamia.
Sabrina alipoingia chumbani kwake, moja kwa moja akachukua simu yake na kumtumia ujumbe mfupi Sakina,
"Toto lako lipo huku linajiliza peke yake, naliuliza tatizo nini halitaki kusema"
Kisha akajilaza kwenye kitanda chake, muda kidogo ule ujumbe ukajibiwa na kumfanya Sabrina afungue haraka simu yake kuangalia kitu alichojibiwa na Sakina.
"Achana nalo hilo halijielewi"
Sabrina akacheka sana na kuandika,
"Na kweli halijielewi, ndiomana nimeliacha sebleni lijilizee wee hadi lichoke. Mitoto ya siku hizi bhana kama mitahira yani na kukua kote kule eti bado linajiliza"
Kisha akautuma ule ujumbe kwa Sakina na kuendelea kujilaza pale kitandani kwake huku akijishauri kwenda kuoga.
Muda wote Sabrina anamtumia ujumbe Sakina kwenye ile namba bila kujua kuwa simu ya Sakina alikuwa nayo Jeff kwa siku hiyo.
Jeff aliumia sana kwa zile jumbe alizozituma Sabrina kwenye simu ya mama yake, na ndiomana ujumbe wa kwanza akamjibu ili aone kuwa ataendelea kutuma ujumbe gani, ila ujumbe wa pili ukamuuma zaidi na kumfanya ainuke na kuondoka tena bila hata ya kumuaga Sabrina ambaye alikuwa ndani huku akijua amemtumia ujumbe Sakina kumbe simu ipo kwa Jeff.
Sabrina akiwa bado anajishauri, simu yake ikaingia ujumbe. Moja kwa moja akajua utakuwa umetoka kwa Sakina, alipochukua simu kuangalia akakuta ujumbe umetoka kwa Sam
"Naomba ujiandae, nakuja kukupitia twende wote kula chakula cha usiku leo"
Sabrina alisoma ule ujumbe huku akitabasamu na kuinuka pale kitandani na kwenda kuoga, hapakuwa na tatizo sana kwavile chumba chake kilikuwa na choo na bafu pia.
Akaoga na kuanza kuvaa kwaajili ya huo mtoko kwani hata muda nao ulienda kiasi.
Alipomaliza kuvaa akatoka chumbani kwake huku akiongea,
"Wee Jeff bado unajiliza hapo, mi mwenzio nataka ku...."
Akanyamaza baada ya kuona anaongea mwenyewe wakati muhusika hayupo, akajaribu kuangalia na kuita ila hakuitikiwa, ikaonyesha wazi kuwa Jeff alishaondoka muda mfupi uliopita.
"Khee huyu mtoto kweli ni mwehu, yani kaondoka bila hata ya kuniaga mmh!"
Akaamua kukaa na kumngoja Sam, muda mfupi ukapita na Sam akawasili mahali pale kwa lengo la kumchukua Sabrina na kwenda naye kwenye chakula cha usiku.
Wakaondoka pale huku Sabrina akiwa na wazo kwamba leo ataambiwa na Sam kama anampenda na kumuhitaji kimapenzi.
Walifika hotelini na kwenda kukaa eneo moja zuri sana kisha wakaagiza vitu wanavyotaka na maongezi ya hapa na pale yakaendelea.
Sam alitamani kumuuliza Sabrina kuhusu Jeff ila alisita na kuona kama vile Sabrina ataona kuwa anamfatilia mambo yake, akatamani pia kumwambia kama anampenda ila akasita pia na kuona kuwa Sabrina atahisi kufanyiwa yote yale sababu ya mapenzi tu na si vinginevyo.
Wakati yeye akifikiria hayo, Sabrina naye alikuwa akijiuliza kuwa kwanini Sam hamwambii ukweli kama anampenda huku wakiendelea na maongezi mengine.
Sam akajitahidi kuziba hisia zake kwa Sabrina ila mwisho wa siku alianza kumwambia kimafumbo,
"Nikwambie kitu Sabrina!"
"Niambie Sam"
Muda huu Sabrina alijawa na tabasamu usoni kwani aliamini kuwa kitu anachotaka kuambiwa na Sam ni kuwa anapendwa tu.
Sam akaanza kwa kumuuliza Sabrina swali
"Hivi kama mtu unampenda, utafanyaje ili ajue unampenda na asiweze kuwafikiria wengine?"
Sabrina akapumua kidogo na kujibu,
"Inatakiwa umwambie kuwa unampenda ili ajue"
"Kwani vitendo haviwezi kumuonyesha kuwa unampenda?"
"Vitendo vinamuonyesha ndio, ila unapomwambia ndio inakuwa vizuri kwake na atafurahi kufahamu hilo"
"Sawa basi nitamwambia"
Sabrina akashtuka na kumuuliza Sam,
"Kwani kuna mtu unampenda?"
"Ndio, tena nampenda sana. Natamani siku moja awe mke wangu"
Sabrina akajibu kwa kunyong'onyea,
"Basi mwambie"
"Nitamwambia tu siku ikifika, nikipata muda nitamwambia ukweli wote ulivyo ili ajue"
Sabrina akatulia kwa muda na kuamua kubadilisha mada kwani aliona mada ile kutompendeza tena.
Walipomaliza kula, Sabrina akadai kuwa amechoka sana, ikabidi Sam amrudishe Sabrina nyumbani kwake.
Sabrina alitulia nyumbani kwake na kuyatafakari maneno ya Sam aliyokuwa akiyaongea,
"Inamaana yupo mwingine anayempenda na sio mimi? Kwanini isingekuwa mimi jamani! Yani huyu Sam na kunifanyia mambo yote haya kumbe kuna mwingine anayempenda!"
Aliwaza sana Sabrina na kujikuta furaha yake ikitoweka kwani alidhani kuwa ni yeye anayependwa na Sam ila maneno ya Sam ya kumueleza kuwa kuna mtu anampenda yalimkosesha raha kabisa.
Akawaza na mwisho wa siku akaamua kulala ili awahi kazini.
Kulipokucha kama kawaida, Sam alienda kumpitia Sabrina na kwenda naye kazini. Ila Sabrina alipotoka kazini siku hiyo alipotoka saluni hakutaka kwenda nyumbani kwake na wala hakutaka kupelekwa na Sam.
Alichukua usafiri na kwenda moja kwa moja nyumbani kwao ili kumueleza mama yake yaliyojiri kwa jana yake,
"Basi ndio akaniambia hivyo mama, yani roho iliniuma kweli yani"
"Huwezi jua mwanangu, labda huyo ampendae anamaanisha ni wewe""
"Hapana mama, ingekuwa ni mimi lazima angeniambia tu. Yani ndio nishamkosa tayari"
"Usijali sana mwanangu, huwezi jua Mungu amekupangia nini"
"Ni kweli mama, ila sitaki mwanaume mie niliyopitia yanatosha tayari"
Joy akampa moyo pale mwanae na kuanza maongezi mengine.
"Hivi wale watu wa ajabu wameishia wapi kutufatilia mama?"
Joy akacheka sana na kumjibu mwanae,
"Wale walikuwa wakikufatilia wewe mwanangu, sasa ulipoondoka nao wakaacha na vile hawakujua ulipo ndio kabisa. Ila sielewi walikuwa na lengo gani kwakweli"
"Ila bora yalipita mama, leo nitalala hapa hapa"
Kwahiyo siku hiyo Sabrina akalala nyumbani kwao na kesho yake asubuhi akaenda moja kwa moja kazini.
Sam aliumia sana na kuhisi kuwa Sabrina kuna mahali alikuwa na mtu mwingine.
Aliingia ofisini kisha akatoka nje ili kumuona Sabrina atakavyokuja ofisini.
Sabrina naye wakati yupo njiani akielekea ofisini, akakutana na foleni.
Akaamua kushuka kwenye ile daladala na kujaribu kutafuta usafiri wa bodaboda ili aweze kuwahi.
Wakati anang'aa ng'aa macho kutafuta usafiri wa haraka, kuna pikipiki ilifika na kusimama mbele yake.
Kumuangalia vizuri alikuwa ni Fredy.
Sabrina alifurahi kuona kuwa usafiri umepatikana kirahisi vile, akamsalimia na kumwambia ilivyo kisha Fredy akamwambia Sabrina apande kwenye ile pikipiki ampeleke.
Sabrina akapanda na safari ikaanza.
Alipofika karibu na mlango wa ofisi, Fredy akasimama kisha Sabrina akashuka na kumuaga pale Fredy.
"Asante sana Fredy kwa msaada wako"
"Usijali Sabrina, ila naomba nikuombe kitu"
"Niombe tu Fredy"
"Naomba badae nije kukupitia, nina maongezi na wewe kidogo Sabrina"
Sabrina hakuwa na pingamizi sana kwani alishika lile neno la kata neno sio wito, kwahiyo akamwambia muda wa kutoka na kuingia ofisini.
Mambo yote hayo yalikuwa yakishuhudiwa na Sam na kumuumiza sana, na kutambua kuwa Sabrina hisia zake zipo kwa mtu mwingine na sio kwake.
Kisha naye akarudi ofisini kwake kuendelea na kazi zake za kawaida.
Jioni ilipofika alijua itakuwa kama kawaida, yani yeye kumchukua Sabrina na kumrudisha kwake.
Ila akashangaa kumuona Sabrina akiondoka bila hata ya kwenda kumuaga kama ilivyokuwa kawaida yake.
Ikabidi aangalie kwenye camera zao kuwa Sabrina anawahi kitu gani nje, akamuma Sabrina akitoka na kupanda ile pikipiki iliyomleta asubuhi.
Sam akazidi kupatwa na wivu na kuumia moyoni mwake, akaamua afanye kitu cha kumkomesha Sabrina.
Fredy akampeleka Sabrina hadi mahali alipotaka kufanya naye mazungumzo kwanza.
"Kwanza kabisa naomba msamaha kwa kukupotezea muda Sabrina"
"Bila samahani Fredy"
"Nina ujumbe mzito sana juu yako"
"Ujumbe gani huo, hebu niambie"
"Yani huwezi amini Sabrina, nimeonyeshwa kuwa....."
Kabla hajasema, simu ya Sabrina ikaita. Alipoiangalia, mpigaji alikuwa ni Sam.
Sabrina akaipokea ili kusikiliza alichokuwa akipigiwa simu,
"Mbona umeondoka bila kuaga?"
"Nilimuaga secretary jamani Sam"
"Mie ni bosi wako unatakiwa uwe na heshima, kuzoeana isiwe tabu. Huyo secretry sio muajiri wako na hajui majukumu yako, sasa unatakiwa urudi upesi kuna nyaraka zinatakiwa hapa"
Kisha akakata simu na kumfanya Sabrina astaajabu na kushangaa kwani hakutegemea kama ipo siku Sam ataongea kwa ukali kiasi kile.
Sabrina akamuangalia Fredy kwa unyonge na kumwambia
"Natakiwa nirudi tena ofisini Fredy"
"Kheee si ushatoka tayari!!"
"Ndio nishatoka, ila nimeambiwa eti kuna kazi sijaimalizia"
Fredy hakuwa na jinsi zaidi ya kumrudisha Sabrina tena ofisini na kumuaga,
"Nije kukuchukua ukitoka tena au?"
"Muda utakuwa umeenda Fredy kwahiyo usijali"
"Hapana Sabrina, nipo tayari kufanya chochote kwaajili yako"
"Usijali Fredy, tafadhari nit aenda mwenyewe"
"Basi naomba kesho tuonane ili nikupe ujumbe ambao nilitakiwa kukupa leo"
"Hakuna tatizo tutaonana tu Fredy"
Kisha Sabrina akaenda ofisini kwa Sam moja kwa moja.
"Nimekuja bosi"
"Kaa hapo kwenye kiti"
Sabrina akakaa na kuanza kumsikiliza Sam kuwa amemuitia nyaraka zipi.
"Una bahati nyaraka zimeonekana, ila siku nyingine usifanye ujinga kama wa leo. Uwe unaaga kwanza kabla ya kuondoka"
Sabrina alichukia kimoyo moyo ila tu hakuweza kuonyesha jinsi gani amechukia muda huo.
"Basi naomba ruhusa niende nyumbani bosi"
"Usijali, tutaondoka pamoja na nitakupeleka"
Sabrina akatulia kimya kwani hakuweza kubishana na bosi wake.
Fredy alipotoka pale ofisini kwakina Sabrina aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwakina Sabrina.
Alimkuta Joy akiwa na shughuli zake.
"Khee Fredy karibu, za siku nyingi! Umepotea sana"
Fredy alimsalimia mama wa Sabrina na kuanza kumwambia kilichompeleka mahali pale.
"Nina shida mama"
"Shida gani hiyo? Niambie"
"Shida yangu ni moja tu, mwambie Sabrina awe makini sana"
"Kivipi Fredy?"
"Kuna mtu anamfatilia Sabrina, na asipokuwa makini atampeleka mahali pabaya. Mwambie awe makini"
"Mbona unanitisha Fredy, mtu gani huyo?"
"Mi simjui mama ila ndio hivyo, kwaheri"
Fredy akaaga na kumuacha Joy na viulizo vingi kichwani bila hata ya majibu.
Sabrina alimngoja Sam na kisha wakaianza safari ya kurudi nyumbani kwa Sabrina kwanza.
Walipofika pale nyumbani kwa Sabrina walishangaa kuona kuna mtu amelala kwenye mlango wa Sabrina.
Wakashtuka kwani hawakumuelewa mtu yule, Sabrina akataka amsogelee ili amjue kuwa ni nani ila Sam akamzuia Sabrina kuwa asisogee.
Wakati wakibishana, simu ya Sabrina ikaanza kuita, ikabidi aichukue na kuipokea.
Mpigaji alikuwa ni mama yake,
"Sabrina mwanangu, nina ujumbe wako"
"Ujumbe gani mama wakati huku mwenzio nimekutwa na makubwa"
"Makubwa!! Makubwa gani hayo?"
"Yani ndio kwanza nimerudi nyumbani, hapa nashangaa kwani nimemkuta mtu amelala kwenye mlango wangu"
"Kheee mwanangu, isije ikawa ndio mtu niliyeambiwa huku"
"Mtu gani tena? Mbona unanitisha mama?"
"Kuwa makini mwanangu, nasikia kuna mtu anakufatilia na mtu mwenyewe si mzuri kwako kwahiyo kuwa makini"
"Sawa mama"
"Lolote litakalotokea unijulishe Sabrina, sawa eeeh!!"
"Usijali mama angu"
Ile simu ilipokatika ikabidi Sabrina amueleze Sam alichoambiwa na mama yake ili aweze kuona ni jinsi gani atamsaidia.
"Basi tutoe taarifa polisi Sabrina, au unaonaje?"
"Hapana Sam, ngoja tumuone kwanza kuwa ni mtu gani yule ndio tutoe taarifa"
Sam akamuangalia Sabrina na kumkubalia wazo lake, wakaanza kusogea karibu ili wajue ni nani.
Yule mtu akajigeuza pale mlangoni na kufanya sura yake igeukie upande wao, hapo Sabrina akashtuka na kumuangalia Sam kisha akamwambia,
"Si Jeff yule!!"
Sam akamuangalia tu Sabrina bila ya kumjibu chochote, Sabrina akamuacha Sam akiwa amesimama na kumkimbilia Jeff pale mlangoni, akainama na kuanza kumtikisha
"Jeff, wee Jeff wewe!!"
Jeff akashtuka na kumuangalia Sabrina,
"Mbona umelala hapa mlangoni, una matatizo gani?"
Jeff alikuwa kimya tu, ikabidi Sabrina afungue mlango wake na kumwambia Jeff aingie ndani kisha yeye akatoka nje na kumfata Sam mahali alipokuwa amesimama ili amuage.
"Sam, yani umesimama hapo hapo tu!! Asante kwa kunileta nyumbani"
"Aah usijali kwa hilo, ila yule kijana huwa ana matatizo gani?"
"Akili za kitoto huwa zinamsumbua yule, ila nitakwambia vizuri kesho"
Sam akaamua kumuaga Sabrina na kuondoka zake.
Sabrina akarudi ndani ili kuyajua matatizo ya Jeff,
"Eeh Jeff niambie una matatizo gani?"
"Sina matatizo"
"Unamaana gani kusema hivyo?"
"Muulize mama"
Ikabidi Sabrina ampigie simu Sakina ili amuulize,
"Dada, Jeff yupo huku kwani ana matatizo gani?"
"Mwache huyo, njoo kesho nyumbani nikuelezee vizuri"
"Kheee makubwa haya, basi sawa dada"
Kisha akamgeukia Jeff na kumwambia,
"Siku nyingine ukiwa unakuja kwangu uwe unasema Jeff sio kulala kwenye mlango, na kama una usingizi sana, chumba kile pale nenda ukalale."
Jeff hakumjibu chochote Sabrina zaidi ya kuinuka na kwenda kwenye chumba ambacho alionyeshwa na Sabrina.
Alipofika kwenye kile chumba akajilaza, Sabrina akainuka na kumchungulia akamuona amelala.
Sabrina akatikisa kichwa kama ishara ya kusikitika na kuanza kuongoza kwenda chumbani kwake,
"Yani watoto hawa akili zao loh!"
Alipofika chumbani akapigiwa tena simu na mama yake,
"Vipi huyo mtu uliyesema yupo mlangoni kwako ametoka?"
Sabrina akacheka na kumjibu mama yake,
"Yani mama ni kichekesho tu, eti mtu mwenyewe alikuwa ni Jeff huyo mtoto wa Sakina"
Joy naye akacheka na kumjibu mwanaye,
"Saivi ndio umenikumbusha kitu hapa, huyo Jeff kabla hajaondoka kuja huko alikuja kwangu na kuniaga kuwa anakuja huko, nimesahau kukwambia kutokana na yale maneno niliyoambiwa"
"Hebu mama nieleze vizuri kuhusu yale maneno"
Joy akamueleza Sabrina vile ambavyo aliambiwa na Francis,
"Sasa mwanangu, inabidi uwe makini. Bora urudi ukae hapa nyumbani au huko kwako utafute mtu wa kukaa naye"
"Kweli mama, ila kuna wazo nimelipata hapa"
"Wazo gani hilo?"
"Kwanini nisimuombe Sakina kuwa nikae na mwanae kwa siku mbili tatu ili niangalie mambo yatakavyokuwa!"
"Wazo lako ni zuri mwanangu, hebu lifanyie kazi hilo wazo kwakweli"
Sabrina akaendelea kuongea na mama yake mawili matatu, kisha wakaagana na kukata simu.
Sabrina akafikiria sana kuwa ni mtu gani anayemfatilia ila hakupata jibu kabisa.
Sabrina alipolala akajiwa na njozi tena kuwa ana mtoto na ameolewa, akashtuka na kujiuliza
"Huyo baba watoto na mume wangu ni nani? Mbona napata maswali bila ya majibu? Ila inawezekana akawa Sam, lakini mbona haniambii chochote? Na vipi na hali yangu nitaweza kweli kuzaa? Mwanaume nitakayelala naye atapona kweli? Mmmh naogopa, hapa dawa ni moja tu kama ikatokea mtu akanitongoza nitamwambia sitaki kufanya naye chochote hadi ndoa. Nadhani hiyo itasaidia"
Sabrina alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe huku akiendelea kujipa matumaini ya aina tofauti tofauti, na moyo wake ukimwambia wazi kuwa Sam ndiye mwanaume pekee ambaye ni sahihi kwake.
Kulipokucha, kama kawaida. Sabrina alijiandaa kwaajili ya kwenda kazini.
Akaenda kumgongea Sam na kumuaga,
"Kama utatoka basi funguo zangu nizikute kule kwa mama"
Na alipotoka tu nje akamkuta Sam na gari yake akimsubiri kwaajili ya kwenda naye kazini.
Wakasalimiana na kuendelea na safari hadi walipofika ofisini na kila mmoja kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Kwasababu siku hiyo ilikuwa ni siku za mwisho wa wiki, ilikuwa ni Jumamosi Sabrina akaona itakuwa vyema kama ataenda kumuaga mapema Sam ili awahi kwenda kuzungumza na Sakina.
Akafika kwa utaratibu kabisa kwa Sam,
"Samahani bosi, naomba uniruhusu niende nina dharula kidogo"
"Dharula gani hiyo?"
"Mama ameniita nyumbani, anataka kuzungumza na mimi"
"Kwasababu ni mama yako basi nakuruhusu uende, ila nakuomba badae nije mimi kukuchukua hapo kwenu na kukurudisha kwako"
Sabrina hakuwa na pingamizi juu ya hilo, ikabidi tu amkubalie Sam na kuianza safari yake.
Alipokuwa njiani kurudi kwao, kuna baba alikuja karibu yake na kumsalimia,
"Hujambo Sabrina!"
"Sijambo, shikamoo"
Sabrina alimtolea macho yule baba sababu sura ilikuwa ngeni kwenye macho yake, yule baba akaitikia na kumwambia Sabrina
"Marhaba, najua ni vigumu sana kwa wewe kunifahamu mimi ila mimi nafahamiana sana na mama yako. Ukifika nyumbani mwambie, anko James yule mwalimu wa kwaya anakusalimia sana"
Sabrina akauliza,
"Mwalimu wa kwaya? Kwaya gani?"
"Wewe mwambie tu mama yako hivyo atakuelewa"
Kisha yule baba akaondoka na kumfanya Sabrina apate maswali juu ya taswira ya huyu mwalimu wa kwaya na kama mama yake amewahi kuimba kwaya.
Sabrina aliendelea na safari yake hadi kwao, na hapo akamkuta mama yake akiendelea na shughuli zake.
Akamsalimia na kuendelea na maongezi mengine,
"Kilichonileta huku leo ilikuwa ni kukusalimia tu ila nia yangu kubwa ilikuwa ni kuongea na Sakina, ila kwa mtu niliyekutana naye njiani amefanya nipate maswali ya kukuuliza leo mama"
"Maswali gani hayo?"
"Kwanza kabisa, je umewahi kuimba kwaya mama?"
"Ndio, ila ni zamani sana. Kwanini umeniuliza?"
"Mbona hujawahi kutuambia mama? Leo nimekutana na mwalimu wako wa kwaya"
Joy akashtuka na kumuuliza mwanaye,
"Umekutana naye wapi? Na je amekufahamu vipi?"
Sabrina akamueleza mama yake jinsi alivyokutana na mwalimu huyo wa kwaya.
"Tena kasema nikusalimie sana"
"Haya nashukuru mwanangu kwa salamu"
"Kwani mama, una undugu na yule mwalimu wa kwaya?"
"Kwanini?"
"Kafanana sana na kaka James, halafu naye kasema kuwa anaitwa James"
Joy akacheka na kumbadilishia mada binti yake,
"Hebu nenda kwa Sakina huko mkajadiliane mambo yenu, duniani wawili wawili bwana"
Ikabidi Sabrina acheke naye na kumuaga kidogo mama yake na kuelekea kwa Sakina.
Alimkuta Sakina akiwa ametulia ndani kwake na kumsalimia,
"Nimekuja sasa uniambie matatizo ya mtoto wetu Jeff"
"Bora umekuja, kuna siku Jeff aliondoka na simu yangu halafu mi mwenyewe hata sikujua, aliporudi hapa alikuwa na hasira sana. Nilipomuuliza akaniambia kuwa nitajisikiaje kuona mwanangu akiitwa litoto litahira, mi nikamwambia kuwa nitajisikia vibaya. Jeff akasema kuwa kuna mtu amemuita hivyo na ananitaka mimi nimpe adhabu kama kweli ningejisikia vibaya, nilipomuuliza ni nani. Akanipa simu na kunionyesha ujumbe, nikaona kuwa wewe umetuma. Hata cha kusema sikuwa nacho ila Jeff akasema nikupe adhabu, kwavile ndio amemaliza kidato cha sita anangoja matokeo nimeona adhabu yake ni aje kukaa kwako"
Sabrina akacheka sana,
"Kweli mwanao hamnazo dada, sasa yeye kaona hiyo ndio adhabu kubwa kwangu?"
Sakina naye akacheka,
"Ndio ni adhabu hiyo ili akusumbue kama anavyonisumbua mimi hapa. Anatoka haagi, mida ya kurudi anajua mwenyewe. Ndio ukome kumuita litoto"
"Ndiomana siku ile aliondoka bila ya kuniaga, kumbe simu yako ilikuwa kwake mmh! Nitamuomba msamaha basi"
Kwa upande wa Sabrina ilikuwa ni kheri kwani hata yeye alitaka kumuomba Sakina ili akakae na Jeff kwa muda kwahiyo akaona wamemrahisishia kazi.
"Ngoja nimpigie aje achukue na baadhi ya nguo zake"
"Hapana usihangaike, wee zifunge tu baadhi kisha nipe nimpelekee tu hakuna tatizo"
Sakina akaandaa nguo za Jeff na kumpa Sabrina aende nazo kisha Sabrina akaaga na kuondoka.
Alipofika tu kwao, alikuta gari ya Sam ikiwa nje ya nyumba yao na kugundua kuwa Sam ameshakuja kumfata.
Akaingia ndani kwao na kumkuta Sam akiongea na mama yake, moja kwa moja Joy alimuuliza mwanae
"Na huo mzigo vipi?"
"Nguo za Jeff hizi mama"
"Aaah sawa, mwenzio amekufata"
Kisha Sabrina akasalimiana tena na Sam na kuongea kidogo kisha wakaaga na kuondoka.
Wakiwa ndani ya gari, Sam akaanza kumwambia Sabrina
"Unajua mimi nikimpenda mtu nampenda kweli"
"Mmh basi mwanamke unayempenda atakuwa na furaha sana duniani"
"Ila, mwanamke ninayempenda mimi sitaki awe na mwanaume mwingine yoyote na laiti kama nikigundua basi naweza kumfanyia kitu kibaya sana"
Sabrina akaguna na kujiuliza kimoyo moyo, "kwanini asinipende mimi huyu kijana jamani?"
Sam akamuuliza Sabrina,
"Mbona umeguna halafu umekaa kimya?"
"Aah! Hamna kitu, natafakari tu huyo mwanamke unayempenda wewe ni wa aina gani!"
"Inamaana haiwezekani nikawa na mwanamke wa kwangu peke yangu?"
"Inawezekana, na wala sikuwa na maana mbaya na kutafakari kwangu"
"Yani mimi nikigundua kuwa kuna mwanaume anamnyemelea mwanamke ninayempenda, basi niko radhi kummaliza mwanaume huyo"
"Upo sahihi Sam, mapenzi yanaumiza sana"
Sabrina akajikuta akikumbuka matukio ambayo yaliwahi kumpata hapo zamani na kumfanya hata afungwe, alijiona akitokwa na machozi hadi Sam akamuuliza
"Mbona unalia?"
"Hapana, macho yananiwasha tu"
Kwa muda huo alitamani afike nyumbani kwake haraka na kujifungia chumbani ili alie kwa uhuru zaidi.
Walipofika, alimshukuru Sam na kumuaga kisha akaingia ndani kwake.
Alimkuta Jeff ametulia huku akitazama video, alimkabidhi ule mzigo wa nguo zake na kuingia chumbani kwake.
Jeff aligundua wazi kuwa Sabrina hakuwa sawa kwa wakati huo.
Sabrina alikaa kitandani kwake na kujikuta machozi yakimtoka na kuanza kujiuliza
"Hivi ni nani mimi atanipenda kwa dhati? Ni nani atanipenda kiukweli? Natamani kupendwa na mimi jamani, eeh moyo wangu tafadhari nakuomba uache kumpenda Sam kwani ana mtu wake tayari anayempenda, yasije kunipata kama yaliyonipata kipindi kile. Ni mwanaume gani yuko pekee? Wote wana wao tayari, rafiki zangu karibia wote wameolewa na wengine wana wachumba zao kasoro mimi tu. Kwani nina kasoro gani mimi?"
Sabrina alijikuta akiumia na kulia sana, alilia hadi usingizi ukampitia.
Alipoamka ilikuwa ni saa tano usiku, alienda sebleni na kumkuta Jeff akiwa macho bado na kumuuliza,
"Jeff huendi kulala?"
"Sina usingizi"
"Huna usingizi kwanini?"
"Na mbona wewe macho yako yamevimba?"
"Sababu nililala"
"Mmh! Nahisi ulikuwa unalia wewe, au hutaki mi nikae hapa kwako mamy?"
"Hapana, sio hivyo usinielewe vibaya"
Jeff akakaa kimya na kumuangalia Sabrina,
"Khee mbona unaniangalia sana?"
"Yani mamdogo, licha ya macho yako kuvimba ila bado u mzuri, kwakweli Mungu alikupendelea sana"
Sabrina akacheka sana,
"Haya, asante toto yangu. Ila ni wewe tu unayeuona huo uzuri"
Sabrina akainuka ili arudi chumbani kwake kulala, ila Jeff akamshika mkono Sabrina na kumfanya Sabrina amshangae.
Sabrina akainuka ili arudi chumbani kwake kulala,
ila Jeff akamshika mkono Sabrina na kumfanya
Sabrina amshangae.
Sabrina akamuangalia Jeff na kumuuliza,
"Nini tatizo Jeff?"
Jeff akamuangalia tu Sabrina bila kusema chochote,
"Hebu niache nikalale mie"
"Nataka tukae wote hapa"
"Kheee! Una wazimu nini, mie nikae hapa kuangalia hayo mapicha yako!! Naenda kulala mie"
Jeff akamuachia mkono Sabrina na kumfanya aende chumbani kwake.
Jeff naye hakuchukua muda pale sebleni na kwenda chumbani pia.
Kuna hisia kali ambazo zilikuwa zikimsumbua Jeff, hisia ambazo hakupenda mtu yeyote azijue.
Zilikuwa zikimsumbua sana na kumpa mawazo muda wote, hisia hizo ndio zilizomfanya Jeff aonekane kama mwehu wakati ana akili zake timamu.
Hakuweza kuzitoa hisia zake na ndiomana alikuwa akiumia muda wote.
Kitendo cha Sabrina kumfokea na kumwambia kuwa ana wazimu kilimuuma ila hakuwa na la kufanya ndiomana akaamua kwenda kulala tu, ila hakulala kwavile hakuwa na usingizi na kuamua kuchezea simu tu.
Sabrina hakupatwa na usingizi kwavile alishalala kabla, akatamani hata angepata mtu wa kuwasiliana nae kwa usiku ule
"Sijui nizame kwenye mitandao ya kijamii ili nipate watu wa kupoteza nao muda usiku huu!"
Wazo hilo likamkaa na kumfanya achukue simu yake na kuzama kwenye mtandao wa facebook, huku akijisemea
"Ila humu wanajaaga watoto tu, basi nitakutana na ujinga mtupu ila kwavile nahitaji kupoteza muda basi si mbaya sana"
Akaanza kuperuzi ule mtandao, akaona kunamtu kamtumia ombi la urafiki muda ule. Alipoangalia jina hakulifahamu kwani liliandikwa 'Prince J'
Pia hapakuwa na picha yoyote, ila kwavile alitaka mtu wa kupoteza naye muda, akaamua kukubali lile ombi la urafiki na kuanza kuzungumza na yule mtu kwa njia ya maandishi.
Sabrina alikuwa akiandika huku akitabasamu sana, kisha akajisemea
"Kweli facebook kuna watu wa ajabu, yani mtu hata hanifahamu ndio kwanza kaiona picha yangu leo eti ananisifia mi mzuri na kunitongoza eti ananipenda. Kheee, kweli watu wengine ni vichaa humu"
Sabrina alipochoka akamuaga yule mtu na kulala.
Kulipokucha, akachukua simu yake kuangalia kwenye mtandao, moja kwa moja akakutana na ujumbe kutoka kwa Prince J
"Umeamkaje mpenzi"
Sabrina akacheka na kujisemea tena,
"Eti mara hii nishakuwa mpenzi wake, khee makubwa haya jamani"
Hakujibu ule ujumbe bali aliinuka na kwenda kuoga ili ajiandae kufanya mambo mengine.
Alipotoka kuoga, akaangalia tena simu yake na kukutana na ujumbe
"Ungeniambia kama unaenda kuoga ili nije nikuogeshe mpenzi"
Sabrina akashtuka na kumuuliza,
"Umejuaje kama nilienda kuoga?"
"Kwasababu nakupenda, najikuta nikijua vitu vingi kuhusu wewe"
Sabrina akaona analetewa mauzauza sasa, ikabidi akae kimya na kuendelea na mambo mengine.
Alipotoka sebleni, alimkuta Jeff akiwa tayari ameandaa chai na vitafunio mezani
"Mamdogo, karibu chai mezani"
"Khee kweli umekuwa mwanaume wa shoka toto yangu, yani umeandaa mwenyewe duh!"
Sabrina akaenda kunywa chai aliyoandaliwa na Jeff.
Alipomaliza alirudi kukaa huku akijiongelesha
"Naona uvivu, sijui leo mchana kama nitaweza kupika"
Jeff akamwambia,
"Usijali madogo, leo kila kitu nitafanya mimi"
"Kheee kweli mtoto nimepata jamani"
Jeff akacheka tu na kwenda kuendelea na mambo yake mengine.
Huku Sabrina akiendelea kuperuzi simu yake kwenye mitandao ya kijamii, ujumbe ukaingia kwenye simu yake
"Unaonaje kama nikiwa karibu yako hapo mpenzi"
Sabrina akatabasamu na kumjibu,
"Itakuwa vizuri sana"
Yule kijana naye akaandika,
"Napenda nikutoe upweke ulionao na kukufanya uwe mwanamke mwenye furaha duniani"
Sabrina akatabasamu tena, na kumjibu
"Una maneno ya ushawishi sana wewe, ila asante"
"Niruhusu nije mpenzi, niwe karibu yako nikuliwaze"
Sabrina akapumua kidogo na kujisemea, "Yani huyu mtu loh! Kuja aje wapi ananijua mie mmh kweli facebook ina mambo jamani"
Muda anajiongelesha mwenyewe, Jeff alikuja na kukaa karibu yake huku akimuangalia na kumuuliza,
"Mbona unacheka mwenyewe?"
"Mambo ya mitandao haya mwanangu loh ni vituko"
Jeff naye akacheka na kumuuliza,
"Kwani unatumia mtandao gani hapo?"
"Facebook hiyo mwanangu"
"Kumbe huwa unaingia huko na wewe duh!"
"Kwani tatizo nini? Huku sio kwa watoto peke yao, hata watu wazima kama mimi wapo"
"Sina maana hiyo mamy, umenielewa vibaya"
Kisha Jeff akainuka na kumuacha Sabrina akiendelea na simu yake pale.
Alipoangalia tena kwenye ule mtandao akakuta ujumbe kutoka kwa yule mtu,
"Mbona kimya mpenzi? Au ombi langu kwako limekukera?"
"Hapana, sio hivyo"
"Mi napenda niwe karibu na wewe, nikuliwaze, nikubembeleze na kukufanyia kitu chochote unachokitaka. Tafadhari nakuomba unikubalie ombi langu mpenzi"
Wakati akifikiria kujibu, simu yake ikaita na mpigaji alikuwa ni Sam
"Naomba nije nikuchukue leo tukatembee Sabrina"
"Hakuna tatizo Sam"
Wakapanga muda wao utakaowafaa kutoka.
Alipomaliza kuongea na simu ikabidi aende kujiandaa kwaajili ya hiyo safari.
Muda ulipofika, Sabrina akapigiwa simu na Sam kuwa atoke nje kwani yeye yupo nje anamngoja.
Sabrina akamuita Jeff na kumuaga,
"Mi natoka Jeff , nadhani nitarudi badae sana kwahiyo kuwa makini tu hapa ndani"
Jeff hakuwa na pingamizi zaidi ya kukubaliana na mwenye nyumba.
Sabrina akatoka nje, Jeff naye akasogea kumchungulia Sabrina, hadi alipopanda gari na ile gari kuondoka kabisa.
Akajikuta akijiuliza,
"Sijui ndio mchumba ake!! Silipendi lile likaka basi tu sina la kufanya"
Sabrina alipokuwa kwenye gari ya Sam akamuuliza,
"Mbona leo hukutaka hata kuingia ndani kwangu?"
"Si kapo kale katoto kako! "
"Nani? Jeff au?"
"Ndio huyo huyo bhana"
"Kafanyaje kwani?"
"Simpendi tu, nadhani damu yake na yangu haziendani"
"Jamani Sam usiseme hivyo, Jeff ni mtoto mpole sana tena asiye na makuu, usimseme hivyo bhana"
"Haya tubadilishe mada, usije ukalia bure hapa maana unavyokapenda ni balaa"
Safari yao ikaendelea na kukomea kwenye nyumba moja kwa nje.
"Vipi Sam, mbona tumekuja hapa?"
"Nataka nikutambulishe kwa mjomba wangu, jana alikuja ofisini ila hakukukuta"
"Sawa, hakuna tatizo"
Wakaingia kwenye ile nyumba na kukaribishwa vizuri sana.
"Sabrina, huyu ni Shangazi yangu. Anaitwa Betty ni mke wa mjomba"
Sabrina akatabasamu na kusalimiana vizuri na huyo shangazi mtu.
Kisha Sam akamuuliza shangazi yake,
"Mjomba yuko wapi?"
"Bado hajarudi kutoka kanisani ila msijali, atarudi muda sio mrefu"
Wakaendelea kuongea mawili matatu huku wakimngoja mjomba huyo arudi na Sabrina apate kumfahamu.
Kwenye mida ya jioni, huyo mjomba aliwasili na kuwakuta Sabrina na Sam wakiwa ndani kwake.
Akafurahi sana na kuwasalimia kwa shangwe, kisha Sam akaanza utambulisho
"Mjomba, huyu anaitwa Sabrina ni....."
Kabla hajamaliza mjomba akadakia,
"Namjua huyu, ni mtoto wa Joyce hata jana nilikutana naye"
Sabrina akacheka na wote wakacheka na kuendelea na mazungumzo mengine, ila Sabrina alijisikia kumuuliza maswali yule mjomba haswaa kuhusu mama yake na uimbaji wa kwaya.
"Eti mjomba, mama yangu alikuwa anaimba kwaya vizuri eeeh!!"
"Tena alikuwa anaimba vizuri sana, sijui ni kitu gani kilimpelekea mama yako kuacha kuimba kwaya wakati alikuwa ni muimbaji mzuri sana. Yani angeendelea hadi leo basi angekuwa ni kati ya waimbaji wakubwa nchini"
"Unajua nini mjomba, mi kila nikimuuliza mama kuhusu kuimba kwaya huwa hanijibu vizuri. Hebu nieleze kwa kifupi, na kwanini hamkumfatilia tena baada ya kuacha kuimba kwaya ili arudi?"
Mjomba akaamua kumueleza Sabrina kwa kifupi kama ambavyo yeye alikuwa akielewa.
"Hakuna anayejua sababu halisi ya Joyce kuacha kuimba kwaya, ila tetesi za watu wengi ni kuwa mumewe alimkataza kuimba sababu haijulikani. Ila Joy alikuwa ni muimbaji mzuri sana, alijua kuipangilia vizuri sauti yake, aliweza kuimba hata alipokuwa mjamzito tena mimba kubwa kabisa lakini Joy bado alimudu kuimba vizuri kwa sauti yenye mvuto. Mambo yalibadilika alipojifungua tu, kwani aliacha kuja kwenye kwaya kabisa"
"Mlijaribu kumfatilia ili kujua nini tatizo?"
"Tumemfatilia sana, kama mimi ndio sikuchoka kumfatilia hata nikawajua nyie watoto wake wote . Ila mwisho wa siku Joy na mumewe wakahama kule walipokuwa wanakaa hadi leo"
"Kumbe!! Mama alikuwa anaimba na mimba ya mtoto gani huyo?"
"Mtoto wake wa kwanza, yule kaka yenu James"
"Aaah ndiomana kaka James naye anapenda sana kuimba, leo umenijulisha kitu mjomba"
"Ndio hivyo, mama yako alikuwa muimbaji mzuri sana, ndiomana hata mimi mtoto wangu wa kwanza nimemuita Joyce kwa ukumbusho wa uimbaji wa mama yako"
Kisha mjomba akamuita huyo Joy ili wapate kumsalimia vizuri.
Joy akasalimiana na wakina Sabrina pale na kufurahi nao.
Wakaongea mengi sana na mwisho wa siku, Sam na Sabrina wakaaga na kuondoka.
Wakiwa ndani ya gari, Sabrina alikuwa akijiuliza maswali mengi kuwa Sam alikuwa na maana gani kwenda kumtambulisha kwa mjomba wake, na je alikuwa akitaka kumtambulisha kama nani yake? Lakini hakupata jibu na kuendelea kujiwazia moyoni tu.
Sam naye alikuwa na mawazo yake ambayo hakupenda kumshirikisha Sabrina kwa muda huo kwani yeye aliona bado muda, alihitaji muda muafaka kuweza kulifikisha wazo lake hilo.
Kwahiyo wote wawili walijikuta wakiwa kimya tu ndani ya lile gari.
Kufika mbele, Sam akaamua kuuvunja ukimya ule
"Unaonaje kama tukienda kula kwanza chakula cha usiku halafu ndio nikupeleke nyumbani?"
"Hakuna tatizo Sam"
Wakaenda mahali palipotulia kiasi na kuagiza chakula na vinywaji, baada ya muda kidogo Sam akainuka na kwenda msalani.
Sabrina akiwa amekaa kwenye eneo lile, mara akafatwa na muhudumu mmoja wa kike kwa karibu kisha muhudumu huyo akamwambia Sabrina,
"Hongera dada, umempata huyu jamaa ana hela sana. Mng'ang'anie leo hadi asubuhi ila hakikisha....."
Kabla hajamaliza kuongea, Sam alikuwa amerudi kwenye ile meza yake na yule muhudumu kuondoka.
Kisha Sam akamuuliza Sabrina,
"Mlikuwa mnaongea nini na yule?"
"Aaah aaah aaa alikuwa anauliza kama naongeza vinywaji"
"Hayo maneno umetunga ndiomana ulikuwa unasita kuongea, kwakweli hii ndio sababu ya mimi kuchukia vibaa vya uswahilini yani ni umbea mtupu"
Sabrina akagundua wazi kuwa Sam amechukia na kubadilisha mada muda ule.
Walipomaliza kula, Sam akamrudisha Sabrina nyumbani kwake na kumuaga kisha naye akaondoka zake.
Sabrina akaingia ndani na kumkuta Jeff amekaa ila alipomuona tu Sabrina mlangoni, akainuka na kwenda kumkumbatia kwa nguvu.
Sabrina akajaribu kumtoa Jeff mikono ila bado Jeff hakutaka kuacha na kuendelea kumkumbatia tu.
Sabrina akaingia ndani na kumkuta Jeff amekaa
ila alipomuona tu Sabrina mlangoni, akainuka na
kwenda kumkumbatia kwa nguvu.
Sabrina akajaribu kumtoa Jeff mikono ila bado
Jeff hakutaka kuacha na kuendelea kumkumbatia
tu.
Sabrina akachukizwa na kile kitendo na kumwambia Jeff kwa ukari,
"Wee mtoto hebu niache huko"
Jeff akamuachia Sabrina, wakati huo Sabrina aliendelea kufoka
"Kunikumbatia gani huko?"
"Nisamehe mamy"
"Wewe umeshakuwa mkubwa saivi Jeff, mambo ya kitoto uache sasa"
"Inamaana hunipendi siku hizi mamy?"
"Hapana, kukupenda nakupenda tena sana tu ila michezo ya kitoto uache. Si vizuri kunikumbatia kiasi kile"
"Sawa mamy nimekuelewa"
Kisha Sabrina akaenda chumbani kwake akiwa amejichokea kutokana na mizunguko ya siku hiyo.
Moja kwa moja akaenda kulala na kupitiwa na usingizi pale pale.
Aliposhtuka ilikuwa tayari ni usiku sana, akakumbuka kuwa alilala bila hata ya kuoga na kuinuka kwenda kuoga.
Alipotoka kuoga, akajihisi usingizi umekatika na kichwa chake kutawaliwa na mawazo tena, akajikuta akiwaza kuwa yule muhudumu wa pale baa alitaka kumueleza kitu gani kuhusu Sam. Akakosa jibu kabisa, kwavile kichwa chake kilizungukwa na mawazo, akaamua kuchukua simu yake tena na kuzama kwenye mtandao wa kijamii ili kupoteza mawazo yake.
Alipoingia tu kwenye mtandao wa facebook, akakutana na jumbe tano kutoka kwa Prince J na tena akamuma huyo Prince J hewani, ikabidi amuulize,
"Hulali wewe?"
Prince J naye akawa haraka sana kumjibu Sabrina,
"Nalala vipi wakati nakuwaza wewe"
"Kheee! Unaniwaza mimi? Kwanini?"
"Kwasababu nakupenda tena nakupenda sana"
"Unawezaje kumpenda mtu ambaye hujawahi kumuona?"
"Hisia ndio zinazoniongoza Sabrina, nipe nafasi tafadhari. Niruhusu nije nikukumbatie na kukubusu, niwe shuka lako unapolala. Niwe joto lako unapohisi baridi, tafadhari Sabrina sikia kilio changu"
"Khee una mashairi wewe!"
"Sio mashairi Sabrina, ni hisia zangu juu yako"
"Ila mimi ninaye wangu tayari"
"Sabrina, hilo sio tatizo kwangu sababu nakupenda. Nipo tayari kupanga foleni kwaajili yako malkia wa moyo
wangu"
Sabrina alikuwa akitabasamu tu kwani maneno ya Prince J yalimvutia sana, kisha akamuandikia tena,
"Ila mimi sikufahamu, sitaweza kukupenda kwakweli"
"Hakuna tatizo Sabrina, nitasubiri tu sababu nakupenda sana na sitaki nikukose malkia wa maisha yangu"
Sabrina hakuishiwa na tabasamu usoni na kusahau hata kama ule ni usiku tayari.
Alijikuta akijisemea tu,
"Yani huyu mtu ningekuwa namjua ningefurahi sana, ila tatizo simjui mmh! Anavyoongea kwa hisia hadi raha"
Akaendelea kuwasiliana nae na mwisho wa siku usingizi ukampitia na kulala.
Asubuhi aliamshwa na hodi ya Jeff kwenye chumba chake,
alipotahamaki, muda ulikuwa umekwenda sana.
Akainuka haraka pale kitandani na kufungua mlango wake,
"Vipi mamdogo, leo huendi kazini?"
"Hata me mwenyewe najishangaa nilivyochelewa kiasi hiki"
Muda huo huo Sam naye alikuwa akibisha hodi kwenye nyumba ya Sabrina kisha Jeff akaenda kumfungulia na kumkaribisha,
"Sabrina mbona nakupigia simu hupokei?"
"Sikuisikia Sam nisamehe, hata hivyo nimechelewa kuamka. Ngoja nijiandae upesi, ila wewe ungetangulia tu"
"Hapana, nakungoja"
Sabrina akaingia chumbani kujiandaa haraka haraka halafu Sam akakaa kwenye kochi kumngoja.
Jeff akamwambia Sam,
"Si umeambiwa utangulie, huoni kama na wewe unachelewa?"
"Kwani wewe shida yako ni nini?"
"Sio shida yangu ni nini, nilikuwa najaribu kukushauri tu"
"Asante, lakini sihitaji ushauri wako"
Jeff akainuka na kwenda kwenye mambo yake.
Baada ya muda kidogo Sabrina akatoka akiwa tayari amejiandaa na kuondoka na Sam kuelekea ofisini.
Jeff alitulia pale kidogo kisha naye akatoka kwenda kwenye matembezi kidogo kupoteza muda.
Alipokuwa njiani kwenye matembezi yake akakutana na mwalimu wake aliyekuwa akipatana naye sana,
"Jeff huji kututembelea siku hizi!"
"Mambo mengi madam ila nitakuja tu"
"Uje bhana"
"Nitakuja madam"
Jeff akaagana na mwalimu wake huyo kisha kila mmoja kuendelea na safari yake.
Sabrina akiwa kazini kwake akapigiwa simu na namba mpya, akapokea ile simu na kuongea nayo.
Ilikuwa ni sauti ya kiume,
"Sabrina, nakuomba hapa nje mara moja"
"Kwani wewe ni nani?"
Ile simu ikakatika na kumshangaza Sabrina, akainuka na kutoka nje ya ofisi.
Alishangaa kumuona Japhet akiwa mbele yake,
"Khee Japhet! Una shida gani?"
"Mmh jamani Sabrina! Hata salamu mama!"
Japhet akasogea na kutaka kumpa mkono Sabrina, ila Sabrina akaukwepa mkono ule,
"Tafadhari Japhet, nakuomba uende"
"Kwani tatizo ni nini Sabrina jamani? Sioni kosa langu"
Sabrina hakutaka kuendelea kumsikiliza Japhet, badala yake alirudi zake ofisini na kumuacha Japhet pale nje.
Sabrina alikaa pale ofisini na kujikuta akiongea peke yake,
"Mijitu mingine kuharibiana siku tu, sijui hata limetokea wapi na ushetani wake"
Alichukia sana muda huo huku akiendelea na mambo yake mengine.
Muda kidogo, simu ya mezani kwake pale ofisini ikaita na mpigaji alikuwa ni Sam
"Njoo ofisini kwangu"
Sabrina akainuka na kwenda ofisini kwa Sam ili kumsikiliza kuwa Sam anataka nini.
Sam akaanza kuongea,
"Unajua huwa sipendi masikhara katika kazi Sabrina"
"Masikhara gani nimefanya tena bosi?"
"Ulienda kuongea na nani pale nje?"
"Aaah mmh ni mtu aah mi simjui"
"Unaona unavyojiuma uma eeh! Haya nenda ukaendelee na kazi yako"
Sabrina akarudi kwenye ofisi yake na kujiuliza,
"Kwanini Sam anapenda sana kunifatilia? Yani nisijambe loh!"
Muda wa kuondoka ulipofika, Sam alimshtua Sabrina na kuondoka naye.
Wakiwa ndani ya gari, Sam akaanza kumwambia Sabrina,
"Yani mimi nikimpenda mwanamke huwa namfatilia sana hadi ataona kero ila ni kwavile nampenda"
Sabrina akajiuliza kuwa ni mwanamke gani huyo, na hapo akaamua kuuvunja ukimya na kumuuliza Sam,
"Ni mwanamke gani huyo umpendaye?"
"Unataka kumjua?"
"Ndio nataka kumjua, kwani kila siku nakusikia tu ukisema, nami nataka kumfahamu huyo mwanamke mwenye bahati"
Sam akatabasamu na kumwambia Sabrina,
"Usijari, utamfahamu hivi karibuni"
"Kwanini unanificha huyo mwanamke jamani?"
"Nakuahidi Sabrina, siku ya Jumamosi ya wiki hii utamjua mwanamke ninayempenda kwani nitakufanyia Surprise"
Sabrina akakaa kimya kwani hakuweza kuyasoma vizuri mawazo ya Sam, hadi pale alipofika nyumbani kwake na kushuka.
"Asante Sam"
"Usijali Sabrina"
Sabrina akaingia ndani kwake na kumkuta Jeff akiwa ametulia huku akichezea simu yake.
Sabrina akamsalimia Jeff na kuingia chumbani kwake.
Ila alipokuwa chumbani alimfikiria Jeff na kugundua kuwa hajachangamka kama siku zote anavyokuwaga, ikabidi atoke sebleni ili akamuulize kuwa tatizo ni nini.
Alimkuta Jeff akiwa ametulia vile vile,
"Mbona leo hujachangamka toto yangu jamani!"
"Kuna mtu amenikera tu leo"
"Mtu gani huyo jamani"
"Mtu mmoja hivi, na mbona na wewe leo umeniuliza?"
"Lazima nipende kujua maendeleo yako Jeff ila na mie leo kuna mtu kanikera sana"
"Mtu gani huyo? Na amekufanyeje?"
Sabrina akamueleza kwa kifupi Jeff kuhusu Japhet.
"Pole sana mamy, nikuulize kitu!"
"Niulize tu"
"Wewe ungependa mwanaume wa aina gani awe mume wako?"
Sabrina akacheka sana na kumuuliza Jeff,
"Ndio swali gani hilo?"
"Si nimekuuliza tu"
"Nitapenda nimpate mume mwenye mapenzi ya dhati na mimi, yani anipende, anijali na kunithamini"
"Ni hivyo tu basi!"
"Ndio ni hivyo"
"Hata kama akiwa hana pesa?"
Sabrina akacheka tena na kumwambia Jeff,
"Bwana maswali yako yamenishinda, ngoja nikapumzike mie"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani kwake kupumzika.
Ila kabla hajafanya chochote, akachukua simu yake na kuingia kwenye mtandao huku akijisemea,
"Tayari nishammiss huyu mtu wa kuitwa Prince J, sijui naye atakuwa hewani!"
Ila alipoingia tu akamuona Prince J akiwa hewani na muda huo huo ujumbe ukaingia kwa Sabrina,
"Najua umechoka muda huu mpenzi, natamani nije nikukande kande hapo"
Sabrina akajigunisha kidogo na kujisemea,
"Yani huyu mtu ana maneno ya kiuchochezi loh! Sijui hata nimjibu kitu gani"
Ila kabla hajajibu, ujumbe mwingine ukaingia,
"Nakupenda Sabrina, wewe ni kama mboni ya jicho langu. Sitaki nikupoteze, napenda uwe kwenye himaya yangu ili nikumiliki milele"
Sabrina akatabasamu na kumjibu Prince J,
"Naenda kuoga kwanza, nitakutafuta badae"
Kisha akainuka na kwenda kuoga.
Alipotoka kuoga, alichukua tena simu yake na kukutana na ujumbe wa Prince J,
"Kwanini hutaki nije kukuogesha mpenzi wangu?"
Sabrina akatabasamu, ujumbe mwingine ukaingia,
"Natamani nikuandalie chakula mpenzi"
Sabrina akacheka sasa na kumjibu,
"Hiko chakula utaniandalia hewani au?"
"Kama unahitaji sema nikuandalie, mi nakupenda sana Sabrina"
Sabrina naye akajibu kimasikhara,
"Haya niandalie sasa"
"Nipe dakika kumi mpenzi, nakupenda sana. Mmwaaah!"
Kisha Prince J akapotea hewani na kumfanya Sabrina acheke na kuendelea na mambo yake mengine.
Baada ya muda kidogo, Sabrina aligongewa mlango na Jeff. Alipotoka, Jeff akamwambia,
"Chakula tayari mama, twende tukale"
Sabrina hakupinga kwavile njaa ilishamshika kweli ila aliona uvivu kupika ndiomana akaenda kujilaza.
Sam alipokuwa nyumbani kwake alihisi kutaka kuwa karibu na Sabrina, akaone ni vyema kama akienda nyumbani kwa Sabrina.
"Tena leo hata simwambii kama naenda, na nikifika kwake hata sitagonga yani kama mlango nitaukuta wazi basi atashangaa tu nipo ndani kwake, nikamwambie tu usiku mwema"
Sam akatoka pale nyumbani kwake na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa Sabrina ambako hapakuwa mbali sana na nyumbani kwake.
Wakati Sabrina anakula, chakula kidogo kikamuangukia kwenye blauzi yake lakini yeye hakukiona.
Jeff alikiona na kumwambia Sabrina,
"Naomba nije nikutoe uchafu huo kidogo mamy"
"Uko wapi kwani?"
"Wewe huwezi kuuona, ngoja nije nikutoe mimi mwenyewe"
"Sawa, njoo unitoe"
Jeff akainuka na kuzunguka nyuma ya Sabrina, kisha akamuinamia pale alipokuwa amekaa na kuinua mkono wake kwa lengo la kutaka kumtoa Sabrina ule uchafu.
Ila gafla akajikuta akikilaza kichwa chake kwenye shingo ya Sabrina, wakati Sabrina akitahamaki hilo alimuona Sam akiwa mbele yao.
Jeff akainuka na kuzunguka nyuma ya Sabrina,
kisha akamuinamia pale alipokuwa amekaa na
kuinua mkono wake kwa lengo la kutaka kumtoa
Sabrina ule uchafu.
Ila gafla akajikuta akikilaza kichwa chake kwenye
shingo ya Sabrina, wakati Sabrina akitahamaki
hilo alimuona Sam akiwa mbele yao.
Sam akamwita Sabrina kwa nguvu na kwa mshangao,
"Sabrina!!"
Jeff akashtuka na kuinuka kwenye bega la Sabrina, wakati huo Sabrina nae alikuwa kama akijipukuta kwenye nguo yake ili kuweza kukipoteza kile kilichotokea.
Kisha Sabrina akainuka na kumfata Sam alipo ambapo Sam alimvuta mkono Sabrina na kutoka naye nje,
"Unaweza kuniambia chochote?"
"Chochote kuhusu nini? Na mbona umepaniki hivyo?"
"Unajua Sabrina mi simuelewi huyu mtoto unayeishi naye humo ndani! Ni kitu gani kinaendelea kati yenu?"
"Unamaana gani Sam?"
"Sio nina maana gani, nataka kujua kinachoendelea kati yako na huyo kijana wako hapo ndani"
"Kwani wewe unaona nini kinaendelea?"
"Sijawaelewa kwakweli, mnakaa kama wa...."
Sabrina akaingilia kati yale maneno tena hata kabla Sam hajamaliza kusema,
"Naona unataka kunivunjia heshima Sam, inamaana hujui kuwa Jeff ni nani yangu hadi uanze kunihisi vibaya!!"
Sam alikaa kimya akimuangalia Sabrina tu anavyoongea kwa hasisa huku Sabrina naye akiongea kwa ukali kuonyesha kama amekerwa na jinsi alivyohisiwa vibaya na Sam.
"Kwakweli Sam sijapenda ulivyonihisi vibaya"
"Basi yaishe Sabrina, acha kupaniki ila nakuomba uwe makini"
"Makini na nini? Unataka kunivuruga tu"
"Usivurugike, ila ipo siku utayakumbuka maneno yangu"
"Ila kiukweli hata sikuelewi Sam, yule Jeff ni kama mwanangu tafadhari usinihisi nae vibaya"
"Ok, yaishe basi"
Sabrina akaamua kuweka mazungumzo mengine ili waweze kukatisha yale ya awali.
Muda wote Jeff alikuwa dirishani akiwachungulia Sabrina na Sam huku akitamani kurudisha wakati nyuma na kufanya kama vile Sam hakutokea ni nini kingeendelea na je Sabrina angechukua hatua gani.
Alijikuta akiwaza sana, mara nyingine alijilaumu ila moyo wake ndio uliomsumbua na kumfanya afanye vitu bila ya kufikiria.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akawaangalia Sam na Sabrina, akawaona wakikumbatiana na kuagana kisha akamuona Sabrina akija maeneo ya kuingia ndani.
Jeff akatoka pale dirishani na kuingia chumbani kwake.
Sabrina alipoingia ndani akajua kuwa Jeff ameshalala, akamuita
"Jeff, wee Jeff wee hebu njoo"
Jeff akatoka kama mtu aliyetoka kulala kweli,
"Yani muda huu umeshalala!"
"Usingizi huo mamdogo"
"Sasa utoto wako uache, utakosa baba wadogo shauri yako"
Kisha Sabrina akaelekea chumbani kwake na kumuacha Jeff akiwa kasimama huku akimuangalia tu, huku akijiuliza moyoni,
"Eti nitakosa baba wadogo mmmh! Inamaana wapo wengi!!"
Kisha akaenda chumbani kwake.
Sabrina alikaa kitandani kwake na kuanza kujiuliza kuhusu Sam kuwa anampenda kweli au hampendi
"Mbona simuelewi jamani!Huyu Sam ananipenda mimi au kuna mtu anayempenda? Na kama hanipendi usiku huu alikuja kufanya nini kwangu? Eti kunisalimia tu mmmh! Na kama ananipenda mbona hajaniambia sasa? Kwanini inakuwa hivi!"
Sabrina alijifikiria sana bila ya jibu la aina yoyote ile.
Akaamua kulala ila bado wazo moja likamjia kichwani na kumfanya kujiuliza swali,
"Kwani Jeff alikuwa na maana gani kunishika vile mpaka Sam kutuona na kuchukia? Ila mi sijaona kama kuna tatizo sababu Jeff ni kama mtoto wangu tu"
Alijiuliza maswali ambayo alijijibu mwenyewe, wakati akiendelea kujiuliza, simu yake ikaita.
Kuangalia ilikuwa ni namba ngeni, kuipokea tu ikakatika pale pale na kumfanya Sabrina ajiulize kuwa ni nani alikuwa akimpigia.
Alipojaribisha tena ile namba ilikuwa haipatikani, ikabidi Sabrina aachane nayo na kuamua kuendelea na mambo mengine kwenye simu yake.
Moja kwa moja akaingia kwenye mtandao wa kijamii, facebook na kukutana na jumbe zaidi ya kumi toka kwa Prince J, Sabrina akatabasamu na kuzifungua kisha naye akamtumia ujumbe Prince J kama kumshtua hivi.
Ila leo ilikuwa tofauti na siku zote kwani Sabrina alishangaa kutokujibiwa ujumbe wake na kuhisi kuwa Prince J amechukia kwani alimuona hewani ila hakujibiwa kitu.
Sabrina akajikuta akimuandikia Prince J,
"Naomba namba yako tafadhari"
Sabrina akautuma ujumbe huo, na muda huo huo akajibiwa na Prince J
"Unahitaji kweli namba zangu?"
"Yeah, mbona jumbe zangu za kwanza hujazijibu?"
"Ulinikera Sabrina"
"Kukukera nini kwani? Mbona sikuelewi!"
"Kwani mi siwezi kuwa mume wako?"
Sabrina akakaa kimya na kuuliza,
"Kivipi na kwanini?"
"Nijibu kwanza, je siwezi kuwa mume wako?"
Sabrina akakaa kimya, kisha Prince J akatuma ujumbe mwingine
"Nakupenda Sabrina, unavyonikalia kimya unaniumiza sana"
"Pole"
"Pole haisaidii"
"Nini sasa itasaidia?"
"Kuonana na wewe ndio itasaidia"
Sabrina akatulia kwanza na kujiuliza kama ataweza kuonana nae, ila alipofikiria sana akaona ni vyema kama ataweza kuonana na huyu Prince J ili awe na uamuzi mzuri juu yake.
Sabrina akaamua kumpa Prince J namba yake ili aweze kumtafuta kwa muda wake wa ziada na kupanga naye ni wapi wataweza kuonana na ni lini siku yenyewe.
Kisha Sabrina akamuaga Prince J na kulala.
Kesho yake asubuhi na mapema, Sabrina akashtuliwa na mlio wa simu yake.
Kuangalia mpigaji alikuwa ni Sam,
"Tafadhari Sabrina nakuomba leo tutoke"
"Sawa haina tatizo"
Kisha Sabrina akakata ile simu na kuanza kujilalamisha,
"Yani huyu Sam hana cha weekend wala nini, hajui hata kama leo ni Jumapili natakiwa kupumzika yani yeye asubuhi asubuhi kunipigia simu eti nakuomba tutoke. Dah! Ana bahati sana nampenda lasivyo ningekuwa namkatalia, kunitongoza kwenyewe hanitongozi yani mwanaume huyu loh"
Ikabidi Sabrina ainuke tu kitandani na kwenda kuoga ili aweze kujiandaa mapema.
Alipotoka sebleni akamkuta Jeff akiandaa chai, na kumuuliza
"Mbona mapema sana mamdogo wakati leo Jumapili?"
"Namngoja Sam, kasema twende tukatembee"
"Mmmh!"
"Nini sasa unaguna?"
"Umtambulishe kabisa basi kwangu mamy"
" Nenda zako na wewe, nimtambulishe nini"
Sabrina akaona kuwa Jeff anamletea mada zisizokuwa na msingi kwa wakati huo.
Alipokaa muda kidogo Sam akawasili, wakasalimiana tena na kutoka.
Jeff akawaangalia tu huku moyo wake ukimuuma.
Sabrina na Sam wakiwa njiani, wakamuona Joy ambaye ni ndugu wa Sam akiwa ameongozana na rafiki yake.
Ikabidi Sam asimamishe gari kuwasalimia.
Sam na Sabrina wakashuka na kuwasimamisha Joy na rafiki yake, kisha wakasalimiana halafu Joy akamtambulisha rafiki yake kwa Sam,
"Huyu ndio yule rafiki yangu uliyekuwa ukimsikiaga nikimtaja, anaitwa Agness"
"Aaah! Kumbe Agness ndio wewe, nashukuru sana kukufahamu"
Kisha wakapeana mikono, ila Agness naye akasema
"Usijali Sam, mi nakufahamu kitambo sana"
Wakaendelea kufurahiana, muda wote huo Sabrina alikuwa kimya tu ila yule Agness alimuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Wewe sio Sabrina kweli?"
Sabrina akashangaa na kujiuliza kuwa huyu dada amemfahamia wapi,
"Ndio ni mimi, kuna mahali umewahi kuniona?"
"Nahisi ila sikumbuki ni wapi, lakini ni vyema kufahamiana nafurahi kukuona"
"Nafurahi pia"
Kisha Sam na Sabrina wakawaaga Joy na rafiki yake na kupanda gari na kuondoka.
Ndani ya gari Sabrina akamuuliza Sam,
"Kwani yule mtoto wa mjomba wako yule Joy anafanya kazi gani?"
"Mwalimu yule, tena ni mwalimu mzuri sana. Hutoa pia ushauri nasaha kwa wanafunzi"
"Basi ni vizuri, nimemuona amechangamka sana. Yani alinifahamu kwa siku moja tu ila ameshanizoea"
"Ni mwepesi sana kuzoea watu yule ila ukikaa nae hutaipenda tabia yake moja tu"
"Tabia gani hiyo?"
"Ni mmbea sana, na marafiki zake wote wambea kwahiyo ni wakumzoea tu"
Sabrina akacheka na kuendelea na maongezi mengine huku safari yao ikiendelea.
Joy na rafiki yake Agness wakajikuta wakiwajadili Sabrina na Sam, alianza Agness kwa kumuuliza Joy
"Kwani yule Sabrina ndio mwanamke wa Sam?"
"Nahisi maana kila sehemu wako wote. Kwanza niambie yule Sabrina umemjulia wapi?"
"Mmh shoga yangu, kama kaka yako ana mahusiano na yule binti basi kaumia"
"Kheee! Kaumia! Kivipi?"
"Yule binti si amesoma nje yule!!"
"Ndio, niambie vizuri basi ameumia kivipi?"
"Yule binti ni muathirika shoga yangu, chuo alichokuwa anasoma wote wanamjua"
"Mmh! Wewe umepata wapi hiyo khabari wakati nje hujawahi kwenda? Mipakani tu hujawahi kufika lakini eti una khabari ya chuo alichosoma Sabrina mmh!"
"Umbea si kazi shoga yangu, kazi ni kusutwa. Kuna mtu ana picha za huyo Sabrina na ndiye aliyenipa khabari zake. Usimuone na uzuri huo ni mgonjwa huyo."
Joy akaishia kushangaa na kumsikitikia kaka yake kuwa ameangamia.
Sam alimpeleka Sabrina kwenye hoteli ambayo ilikuwa ufukweni ili waweze kupumzika hapo.
Sabrina alitulia huku akiamini kuwa leo ameletwa huku na Sam ili kumwambia anavyompenda, wakati wanazungumza simu ya Sabrina ikaita.
Kuangalia mpigaji alikuwa ni Sakina, na kumfanya Sabrina apokee kwa tabasamu
"Jamani mdogo wangu nimekukumbuka sana"
"Usijali dada, nitakuja kukutembelea"
"Vipi huyo mwanangu naye hajambo? Hebu mwambie aje anitembelee mama yake"
"Sawa dada, ngoja nimwambie"
Sabrina akakata simu na kutaka kumpigia Jeff ila kabla hajapiga Sam akamkatisha na kumuuliza,
"Unataka kumpigia nani?"
"Nampigia Jeff ili umwambie nini?"
"Nimwambie kama mama yake kamkumbuka na anamtaka aende kwao kumsalimia"
"Tena umwambie akakae huko huko kwao"
Sabrina akacheka na kumpigia simu Jeff na kumwambia kuhusu kwenda kwao kusalimia, urahi sana,
"Kwakweli nafurahi kuonana na wewe, ila naomba nikutafute ili tuweze kuongea vizuri zaidi"
"Usijali Jeff, wee nitafute tu"
Kisha akaagana nae , na kuondoka zake.
Alipoondoka tu, akafika rafiki wa mwalimu yule
"Nani yule ulikuwa unaongea naye hapo?"
"Anaitwa Jeff, ni mwanafunzi wangu. Nilikuwa mwalimu wake kipindi anasoma"
"Ni kazuri hako"
"Mmh na wewe kwa kupenda watoto hujambo, hebu acha mambo yako. Yule ni kijana mdogo sana, yani urefu tu ule unamzuzua"
"Hata kama, ila ni mzuri acha nimpe sifa yake. Mabinti walikuwa hawajigongi kwake kweli!"
"Yule kijana katulia sana yani huwezi amini, mabinti wengi alikuwa akiwapotezea"
Walijikuta wakimjadili tu Jeff kwa muda huo, hata Sam hakukosea kusema kama wanatabia ya umbea kwani hawa walikuwa ni Joy na mwenzie Agness.
Jeff alipofika kwao alimkuta mama yake akiwa ametulia kabisa na kumsalimia kisha kuongea nae mawili matatu.
"Mwanangu, kale kabinti kazuri kale kanakokupendaga kalikuja hapa jana"
"Nani huyo?"
"Yule Zuwena mwanangu"
"Mi hata simtaki mama"
"Kwanini sasa mwanangu? Yule binti ni mzuri sana tena ana heshima zake, tafadhari mwanangu usikatae bahati ya kuwa naye"
"Sasa mi simpendi, nitakuwaje naye sasa? Yupo mwanamke ninayempenda mama"
"Nani huyo? Ni mwanamke gani huyo? Kuwa makini mwanangu, magonjwa ni mengi ila Zuwena ni binti mzuri kwako"
"Jamani mama, simpendi huyo Zuwena kwakweli. Nampenda....."
"Nani huyo? Mtaje"
"Nitakutajia tu usijali, ila leo naenda kuonana nae. Kwahiyo badae nitaondoka"
"Mmh sikuwezi wewe mtoto"
Sakina alitamani kujua mwanamke ambaye anapendwa na mtoto wake ila hakufanikiwa kumjua.
Sam na Sabrina wakaendelea na maongezi, Sabrina akamuomba Sam simu yake na kuingia nayo kwenye mtandao wa kijamii ili kuona kama kuna ujumbe wowote aliotumiwa ila hakukuta ujumbe wowote ule, akajisemea kimoyo moyo
"Mmh leo Prince J hata hajanikumbuka"
Kisha akamrudishia Sam simu yake, wakaendelea kuongea na kuagana.
Sam akamrudisha Sabrina nyumbani kwake.
Sabrina alipokuwa nyumbani kwake akaamua kuingia tena kwenye mtandao wa kijamii, moja kwa moja akakutana na ujumbe kutoka kwa Prince J
"Tafadhari naomba tuonane leo mpenzi"
Sabrina hakuwa na pingamizi kabisa kwavile alihitaji kumfahamu kwa sura na kumjua ni nani.
Kwahiyo akapanga naye muda wa kuonana.
Muda ulipofika Sabrina alijiandaa ili kwenda kuonana na Prince J.
Alipofika eneo la tukio, akaangaza macho ili aweze kumuona Prince J.
Macho yake yakagongana na watu wawili mbele yake, Sam na Jeff.
Muda ulipofika Sabrina alijiandaa ili kwenda
kuonana na Prince J.
Alipofika eneo la tukio, akaangaza macho ili
aweze kumuona Prince J.
Macho yake yakagongana na watu wawili mbele
yake, Sam na Jeff.
Sabrina akawashangaa na kujiuliza kuwa ni nani anayemchezea akili kati yao, alihisi labda kuna mchezo unaendelea pale
"Inawezekana Prince J ni Jeff kweli! Hapana Jeff hawezi kunichezea mchezo kama huo, na je inawezekana ni Sam kweli! Mmh inamaana Sam ameshindwa kunitongoza kawaida hadi atumie njia ya facebook kweli! Hapana, ila nitajua ukweli tu"
Alisimama kamavile anayengoja kuwaona wote wawili wakisogea eneo alilokuwepo, na kweli wote wawili wakasogea eneo lile.
Sabrina alianza kwa kumuhoji Jeff,
"Umefata nini huku?"
"Nina maagizo yako toka kwa mama na ndiomana nimekufata"
Sabrina akamuangalia Jeff kwa jicho kali sana na kumuuliza tena,
"Eeh umejuaje kama nipo huku?"
"Ulinitumia ujumbe kuwa unatoka kidogo na kusema unakuja huku, kwahiyo mi nikaja kukubahatisha tu"
"Kwanini usingenisubiria nyumbani?"
"Jamani mamdogo, kama nimekosea kukufata basi unisamehe kisha Jeff akaondoka zake"
Sabrina alimuangalia Jeff hadi alipoishia, na kujisemea
"Haka katoto hakana akili kwakweli"
Akamuangalia Sam sasa na kumuuliza,
"Eeh nawe umejuaje kama nipo hapa?"
Ila Sam alikuwa na hasira sana, alimuangalia Sabrina kwa jicho kali na kumwambia,
"Nimekuja kumuona huyo Prince J wako"
Sabrina akashtuka na kumuangalia vizuri Sam, kisha akamuuliza
"Umejuaje kuhusu Prince J?"
"Kwakweli sikuweza kuamini kama wewe Sabrina ungeweza kufanya upuuzi wa namna hii, yani unachat na watu kwenye facebook! Aah umenisononesha sana"
Sabrina bado hakumuelewa Sam na kuendelea kumuangalia tu,
"Sam, sikuelewi lakini"
"Hunielewi eeh!! Angalia uchafu wako sasa"
Sam akamfungulia Sabrina mtandao wa facebook kwenye simu yake na kumfanya Sabrina atambue kosa alilolifanya ni kuwa alisahau kutoka kwenye mtandao alipotumia simu ya Sam.
"Angalia sasa, na huyo mpuuzi wako wa kuitwa Prince J amekutumia ujumbe tena angalia vizuri"
Sabrina akaona ujumbe toka kwa Prince J uliosema,
"Samahani mpenzi, nimepatwa na dharura kidogo kwahiyo sitaweza kufika eneo la tukio ila nakupenda sana Sabrina mpenzi wangu"
Sam alikuwa akimuangalia Sabrina kwa jicho la hasira sana huku akifoka,
"Nilikuthamini Sabrina, nilikuheshimu na kukuona ni mwanamke wa pekee kwenye hii sayari. Sikuamini wala kufikiria kama ungeweza kufanya upuuzi wa namna hii na ndiomana nikaamua kuja ili niweze kujionea mwenyewe kwa macho. Na huyo Prince J wako ana bahati sana kwamaana ningemkuta ningemfumua ubongo wake, na leo nimetembea na bastola kabisa kwaajili yake"
Akainua shati lake vizuri na kumfanya Sabrina aione ile bastola na kutetemeka.
"Haya twende kwenye gari nikurudishe kwako"
Sabrina hakuweza kusema chochote kwani uoga ulimshika na alikuwa akitetemeka tu.
Alienda kupanda gari na safari ya kurudishwa nyumbani kwake ilianza.
Alipofika kwake, moja kwa moja Sabrina akaenda chumbani kwake na kuiona siku hiyo kuwa mbaya sana kwake.
Alijiuliza maswali mengi sana,
"Mbona huyu Sam simuelewi jamani, ana lengo gani na mimi? Ndio kusema ananipenda au ni kitu gani? Mbona simuelewi, na kwanini achukie kiasi kile?"
Sabrina hakupata jibu, akatamani aingie facebook ili amseme Prince J ila alishindwa kwani alijua wazi atakapoingia tu basi Sam ataona tena kila kitu, ikabidi atulie na kutafuta usingizi tu ili apoteze yale mawazo yanayomtatiza.
Kesho yake asubuhi na mapema Sabrina akajiandaa kwaajili ya kwenda kazini, na kwajinsi Sam alivyochukia jana yake Sabrina akajua kuwa hawezi kuja kumchukua tena kwenda nae kazini.
Ila Sabrina alipotoka, alimkuta Sam akiwa nje anamngoja.
Akamsalimia na kupanda kwenye gari halafu safari ikaendelea.
Sabrina akatamani kumuuliza Sam swali moja tu kuwa "je unanipenda!"
Ila kila alipotaka kumuuliza mdomo wake ukasita na kuona kamavile atajibiwa vibaya kwahiyo akakaa kimya hadi walipofika ofisini.
Sabrina alipokuwa ndani ya ofisi, na leo akapata ugeni pia.
Mgeni wake alikuwa ni kaka yake James.
Sabrina akafurahi sana kutembelewa na ndugu yake pale ofisini.
Wakaongea kiasi kisha James akaaga na kumfanya Sabrina amtoe kidogo kaka yake hadi nje ya ofisi.
Kufika pale nje wakakutana na ndugu wa Sam ambaye naye alikuwa anakuja pale ofisini, Sabrina akamkaribisha kwa furaha kabisa
"Karibu Joy"
Joy naye akatabasamu kiasi na kuendelea kwenda kwenye ofisi ya Sam.
Kisha Sabrina akamuangalia kaka yake na kumwambia,
"Kaka umemuona yule mdada?"
"Si yule uliyemuita Joy hapa"
"Ndio huyo huyo"
"Kafanyaje kwani?"
"Yani yule mdada, ana baba yake unafanana nae huyo balaa halafu na yeye anaitwa James, nitawakutanisha siku moja"
"Itakuwa vizuri, si unajua duniani wawili wawili tena"
Kisha James akamuaga Sabrina na kuondoka zake.
Walivyotoka ofisini kama kawaida Sam alimrudisha Sabrina nyumbani kwake, ila leo Sabrina leo hakutaka kukaa ndani kwake bali alitaka kujua ukweli japo kwa kifupi tu kumuhusu Sam, na aliona mtu pekee wa kumwambia ni yule muhudumu wa baa ambaye amewahi kumdokeza Sabrina kuhusu Sam.
Kwahiyo Sam alipoondoka, Sabrina akaitumia nafasi hiyo kwenda kwenye ile baa ili amuhoji yule muhudumu kiasi.
Sabrina alipofika kwenye ile baa aliangaza kila mahali ili aweze kumuona yule muhudumu na kwa bahati akamuona.
"Samahani dada, unanikumbuka?"
"Mmh! Sura yako sio ngeni sana ila sikumbuki nimekuona wapi"
Sabrina akaamua kumuelezea kuhusu siku aliyoenda kwenye ile baa na Sam, na jinsi huyu dada alivyomwambia mwanzo.
"Aah! Nimekukumbuka dada, si ndio ulikuja na yule kibosile"
"Ndio, niambie ulichokuwa unataka kuniambia"
Yule muhudumu akawa anasita sita, Sabrina akagundua anachotaka yule dada.
Kisha akafungua pochi yake na kutoa elfu tano na kumpa ili amueleze vizuri.
"Ni hivi dada yangu, yule kaka huwa ana michezo michafu"
"Michezo michafu! kivipi?"
"Yani akikuchukua na kukupeleka ndani kulala naye, atakachokufanyia humo ndani hakifai"
"Anakufanyia mambo gani kwani?"
Yule dada akaitwa na kuamua kumuaga Sabrina,
"Umekuja muda mbaya, siku ukiwahi mapema nitakusimulia vizuri"
Kisha akaondoka na kumfanya Sabrina atafakari bila hata ya majibu na kuamua kurudi nyumbani kwake.
Alipoingia ndani kwake alimkuta Jeff akiangalia video, moja kwa moja Sabrina akamwambia Jeff
"Najua wewe ni mtundu sana, nataka unisaidie kitu"
"Kitu gani hiko?"
"Mfano niliingia facebook kwa simu ya mtu mwingine na nikasahau kutoka, halafu sitaki yule mtu aone meseji zangu. Je nifanyeje?"
"Kitu kidogo sana hicho, nipe simu yako"
Sabrina akampa Jeff simu ili aweze kumrekebishia, baada ya dakika mbili Jeff alimrudishia Sabrina simu
"Tatizo lako limeshaisha hapo"
"Yani bila hata kubadili neno la siri?"
"Wewe usijali, tatizo hapo limeisha niamini mimi"
Sabrina akaingia chumbani kwake na kumtumia ujumbe Prince J huku akingoja kuona kama Sam naye atazipata.
Baada ya muda kidogo simu yake ikaita, mpigaji alikuwa ni Sam na kumfanya Sabrina aogope kwani alihisi Sam kaona huku akimlaumu Jeff kuwa amemdanganya.
Ila alipopokea simu ya Sam aliulizwa swali moja tu,
"Kwanini umeifunga facebook yako kwangu nisiione?"
"Sijaifunga mbona, labda matatizo ya mtandao tu"
Sam hakujibu kitu zaidi ya kukata simu na kumfanya Sabrina acheke na kufurahia ushindi wake.
Wakati akifurahia hayo, ujumbe ukaingia toka kwa Prince J
"Mpenzi umekula?"
Sabrina akafurahi kwani aliona kuwa Prince J ni mtu anayemjali sana,
"Bado sijala, ila sijisikii kula leo"
"Tafadhari mpenzi nakuomba ule, usipokula wewe unaniumiza mimi. Nakuomba mpenzi wangu, au nikuandalie chakula mpenzi?"
Sabrina akatabasamu na kujikuta akiinuka pale kitandani na kwenda sebleni ambako alimkuta Jeff akiwa makini na simu yake tu.
Sabrina akapitiliza moja kwa moja jikoni ambako Jeff alimfata na kumuuliza
"Unataka kufanya nini mamy?"
"Nataka kupika chai"
"Acha nikupikie mie mamy"
Sabrina akamuangalia Jeff kisha akamuacha mule jikoni na kurudi sebleni.
Jeff alipomaliza, alimuandalia Sabrina ile chai ili aweze kunywa kama alivyohitaji.
Alipomaliza kunywa alirudi chumbani kwake, na moja kwa moja aliingia kwenye mtandao apate kumuaga Price J, akakutana na ujumbe toka kwake
"Uwe unaniambia mapema mpenzi ili nikuandalie chukula kizuri zaidi"
"Usijali, nina mwanangu hapa naye ananiandalia vizuri sana"
"Kuna kitu hujui Sabrina"
"Kitu gani?"
Prince J akatoweka hewani na kumfanya Sabrina akose jibu na kuamua kulala tu.
Kulipokucha, Sabrina aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazini.
Kama kawaida Sam alikuwa pale kwaajili ya kwenda nae kazini.
Walisalimiana na kuianza safari, lakini Sabrina hakuthubutu kumuuliza Sam kuhusiana na yote aliyoyasikia.
Sam akavunja ukimya na kumwambia kitu Sabrina,
"Nimepata safari ya gafla Sabrina kwahiyo kesho natarajia kusafiri, naenda Nairobi"
"Sawa bosi, ila kweli ni safari ya gafla hiyo"
Wakaendelea na maongezi mengine mpaka pale walipofika ofisini. Halafu kila mmoja akaendelea na kazi zake.
Mchana wa siku hiyo, Sabrina alijihisi vibaya na kuomba ruhusa ya kurudi nyumbani kwake.
Ingawa Sam hakuwepo mchana huo lakini Sabrina hakukataliwa kuondoka na kwenda kupumzika.
Alifika nyumbani kwake na kujilaza kwenye kiti, Jeff akamfata pale karibu
"Nini tatizo mamy?"
"Kichwa kinaniuma sana"
"Punguza mawazo mama angu, ni mawazo hayo ndio yanakuumiza kichwa hiko"
Kisha Jeff akainuka na kwenda kumletea maji Sabrina ili apate kutuliza maumivu kiasi.
Sabrina alikunywa yale maji na kwenda kulala.
Muda kidogo akafika mgeni wa Sabrina pale nyumbani na kumkuta Jeff,
"Samahani, eti Sabrina yupo?"
"Hata hayupo"
"Mmh mbona nimeongea nae muda si mrefu akasema yupo nyumbani na yeye ndio kanielekeza hapa"
"Basi alichanganya mada tu ila hata hayupo"
Yule mgeni alisita kidogo na kuondoka zake.
Jioni ilipofika Sabrina alitoka ndani na kumuuliza Jeff,
"Hakuna mtu wa kuitwa Fredy aliyekuja hapa kuniulizia leo?"
"Mmh hata sijamuona mtu yeyote"
"Basi kanidanganya, alisema atakuja kumbe hana lolote. Kashanikera tayari"
Jeff alikaa kimya tu na kuendelea na mambo mengine mpaka pale usiku ulipoingia na kila mmoja kwenda kulala akiwa na mawazo anayoyajua yeye.
Siku ya leo Sabrina aliamka asubuhi na mapema ili kuwahi kujiandaa kwani alijua wazi kuwa siku hiyo lifti haipo kwavile Sam alimwambia jana kuwa atasafiri.
Alipomaliza kujiandaa akatoka nje, akashangaa kuona kuna gari imepaki pale nje kwake, halafu dereva akashuka baada ya kumuona.
"Nimetumwa na Bosi Sam kuwa nije nikuchukue nikupeleke kazini"
Sabrina alifurahi sana na kupanda kwenye lile gari na safari kuanza.
Wakiwa wanaendelea na safari, Sabrina akashangaa kuona lile gari halielekei njia ya ofisini kwao.
Akamshtua yule dereva na kumuuliza,
"Mbona hunipeleli huko ofisini?"
"Hatuendi ofisini ndio, kuna mahali nakupeleka"
"Ni wapi huko?"
Yule dereva hakujibu ila alianza kucheka.
Akamshtua yule dereva na kumuuliza,
"Mbona hunipeleli huko ofisini?"
"Hatuendi ofisini ndio, kuna mahali nakupeleka"
"Ni wapi huko?"
Yule dereva hakujibu ila alianza kucheka.
Sabrina akamuangalia na kumshangaa yule dereva kisha akamuuliza tena,
"Mbona unacheka wakati mi niko serious nakuuliza jamani!"
Ila bado yule dereva hakumjibu kitu Sabrina na kumfanya aweze mambo mengi zaidi bila ya jibu.
Ile gari ikafika mahali furani na kusimama kisha yule dereva akashuka na kwenda kumfungulia mlango wa gari Sabrina ili naye ashuke,
"Tumefika mama, teremka"
Kwa uoga Sabrina akashuka ili kujua kitu ambacho ameletwa huko, yule dereva akamwambia Sabrina
"Kwa kifupi Sabrina nimekuleta hapa kwa jambo moja kubwa muhimu ila sio kama Sam amenituma kweli ila nilikwambia vile ili uweze kukubali kuja nami hapa"
"Sasa kwanini ukanidanganya kuwa Sam amekutuma?"
"Nimesha kujibu hilo Sabrina, unajua wazi kuwa ningekwambia ukweli usingekubali wewe. Nakuomba ufatane nami sasa, ni jambo la muhimu sana Sabrina"
Kwakweli Sabrina alijisikia vibaya kwa kuongopewa na hakujua kuwa yule kijana ana lengo nae lipi.
Yule kijana akamwambia Sabrina kuwa amngoje pale nje ili waingie wote.
Sabrina akaona kuwa ni kheri aondoke eneo lile.
Sabrina akatoka pale kwenye gari na kuongoza kwenye barabara kisha akasimamisha bodaboda na kuelekea kazini huku akiwa na mawazo mengi kichwani mwake.
Alipofika ofisini akamlipa yule wa bodaboda na kuingia ofisini ingawa alikuwa tayari ameshachelewa.
Sabrina aliingia ofisini huku mawazo mengi yakimtawala hata kujieleza kuwa kwanini amechelewa hakuwa na jibu la kuandika.
Sabrina alikaa ofisini ila mawazo yake yote hayakuwepo pale na kumfanya afanye kazi za pale ofisini kinyume na utaratibu uliopo.
Akafatwa na bosi msaidizi na kuulizwa,
"Mbona umechelewa sana leo, na kwanini umeharibu kazi kiasi hiki?"
Yule bosi msaidizi akamtolea Sabrina zile faili alizoharibu na kumfanya Sabrina kukaa kimya na kujiona wazi kuwa ana makosa kweli na hakuwa na cha kujitetea kwahiyo akabaki kimya tu na kumchukiza yule dada ambaye alikuwa ndiye bosi wake msaidizi.
"Huwa unafanya ujinga sababu unajua wazi Sam atakutetea ila leo hayupo huyo Sam wako, na haya makosa lazima niyafikishe mbali ndio nadhani utaelewa umuhimu wa kazi"
Sabrina aliendelea kuwa kimya tu huku akimuangalia huyu dada na kumfanya huyu dada achukie na kuondoka.
Sabrina akaona kuendelea kwake kubaki pale ofisini ni sawa na kujiongezea matatizo kwahiyo akaenda kuomba ruhusa ili arudi nyumbani ila walimkatalia kuondoka na kumfanya achukie zaidi.
Jeff aliamua kwenda kwa yule mwalimu wake ili kuweza kupata ushauri, uzuri ni kwamba alimkuta akiwa hana watu wengi na kuona kuwa hapo atapata nafasi ya yeye kuzungumza na mwalimu wake huyo kama alivyomuahidi,
"Eeh Jeff niambie tatizo lako"
"Tatizo langu madam ni mapenzi"
"Mapenzi!! Yamefanyaje kwani?"
"Kwanza madam niambie mapenzi ni nini?"
Joy akacheka kwanza kisha akamjibu Jeff,
"Mapenzi ni kama mti au majani, huota popote"
"Kwamaana hiyo mtu yeyote anaweza akapendwa na kupendwa?"
"Ndio maana yake hiyo Jeff"
"Je mapenzi yanajali umri, kabila, pesa na kiwango cha elimu?"
"Nimekwambia mapenzi ni kama mti huota popote, kwamaana hiyo mapenzi ya kweli hayajali umri, kabila, elimu, pesa wala muonekano ila yanajali moyo unavyohisi na kuumia kwa yule umpendae. Vipi Jeff je kuna mtu umempenda?"
"Tena sana ila nashindwa kumwambia sababu yeye ni mkubwa kwangu, natamani angetambua hisia zangu, angejua ninavyoumia na kuteseka juu yake. Natamani angejua upendo uliopo ndani yangu kwake"
"Mmmh ni nani huyo aliyepata bahati hiyo Jeff?"
"Yupo mdada madam, ni mzuri, anavutia na kupendeza. Huwa siwezi kusahau siku aliyorudi nchini na kunikumbatia!"
Jeff alitulia na kuwa kama mtu anayevuta hisia na kukumbuka kitu fulani, Joy alikuwa akimuangalia tu na kugundua kuwa kweli huyu kijana kuna mtu anampenda kweli.
"Alinikumbatia vizuri sana sijapata kuona, huwa sisahau kabisa. Mimi ndiye nilikuwa mtu wa kwanza kukumbatiwa naye siku hiyo kabla ya watu wote. Alinifurahia sana, hajui tu jinsi kumbatio lake linavyonipa hisia kali hadi leo. Siwezi kumsahau kwakweli, sitaki kumpoteza jamani. Nisaidie madam, nifanye nini ili aweze kuzisoma hisia zangu?"
"Hebu nitajie kwanza kuwa huyo mwanamke ni nani?"
"Hapana madam, sitaweza kukutajia jina lake kwa sasa ila muda ukifika nitamtaja"
Joy akajaribu kumwambia Jeff njia ambazo aliona kuwa itakuwa rahisi kwa huyo mtu kumuelewa Jeff, kisha Jeff akamuaga mwalimu wake huyo na kuondoka.
Sabrina bado alikuwa na kisirani pale kazini, alitamani muda wa kazi uishe mapema aondoke kwani alihisi wazi kuwa watu wa ofisini ndio waliofanya ule mpango wa kumdanganya kuwa yule dereva katumwa na Sam kumfuata kumbe ni njama zao za kumchelewesha kazini tu siku hiyo ili wapate sababu ya kugombana nae.
Sabrina hakuwa na raha siku hiyo na aliona ni vyema akitoka hapo basi aende nyumbani kwao akatulize mawazo yake.
Muda wa kutoka ulipofika, Sabrina hata hakuaga siku hiyo bali alitoka na kuondoka zake, na moja kwa moja alienda nyumbani kwao.
Alimkuta mama yake kama kawaida na kumsalimia, moja kwa moja Sabrina alianza kumueleza mama yake jinsi alivyochukizwa siku hiyo
"Yani leo kazini wamenikera balaa"
"Nini tena mwanangu?"
Sabrina akamuelezea mama yake kilichomtokea siku ya leo tangu alipotoka nyumbani kwake,
"Mwanangu ndio mambo yalivyo katika dunia, kuwekeana wivu na kinyongo ndio kawaida katika kazi. Vumilia tu mwanangu"
Joy akampa moyo binti yake na kumfanya kurudi katika hali ya kawaida na kuwa na furaha tena.
"Ngoja nikamuone na dada Sakina mama"
"Sawa mwanangu"
Sabrina akainuka na kwenda nyumbani kwa Sakina.
Alipofika alimkuta Sakina akiwa amelala na kumuamsha pale alipolala,
"Dada, dada"
Sakina akashtuka sana kutoka usingizini,
"Kheee Sabrina utaniua mwenzio, umenishtua halafu nilikuwa naota ndoto mbaya sana"
"Ndoto gani hiyo dada?"
"Yani sijawahi kuota ndoto ya namna hii kwakweli, eti nimeota Jeff ameoa"
Sabrina akacheka na kumshangaa Sakina,
"Sasa hiyo ndio ndoto mbaya? Kwahiyo hutaki wakwe wewe! Hutaki mwanao aoe?"
"Sio hivyo Sabrina, tatizo ni kwa mwanamke niliyeota kuwa ameolewa na mtoto wangu"
"Mwanamke gani huyo hadi useme ni tatizo?"
"Ni mtu mzima, yani nimeota kuwa Jeff kamuoa mwanamke ambaye ni mkubwa kwake, kwakweli sijaipenda hii ndoto jamani"
Sabrina akacheka tena na kumuuliza Sakina,
"Inamaana Jeff kaanza mahusiano na masugar mamy? Mbona hiyo ndoto yako siielewi dada!"
"Yani nikigundua kuwa kuna mwanamke mtu mzima anaisumbua akili ya mwanangu hadi anawakataa watoto wenzie huyo mwanamke atanitambua nakwambia, atataja majina yangu ya utoto nakwambia."
"Ila una uhakika kama Jeff anatoka na mwanamke mtu mzima?"
"Sina uhakika ila mbona anakataa wasichana wazuri wanaomtaka? Hebu niambie vizuri huko kwako anatulia kweli nyumbani?"
"Anatulia ndio ila sijui muda ambao sipo nyumbani kama anafanyaga upuuzi"
"Basi nakupa kazi Sabrina, tafadhari mchunguze mwanangu. Ongea nae kwa ukaribu ili ujue kama kuna kitu kinamsumbua, najua wewe hawezi kukuficha"
"Usijali kwa hilo dada yangu"
Wakaongea vitu mbali mbali na kujikuta wakikumbuka mambo yaliyopita hapo nyuma,
"Tena umenikumbusha Sabrina, hivi yale matatizo yako yaliisha mdogo wangu?"
"Yapi hayo dada?"
"Yale ya kipindi kile, si unakumbuka ulikatazwa kulala na mwanaume yeyote yule, si unakumbuka!"
"Nakumbuka ndio"
"Vipi umewahi kulala na wanaume wangapi? Na kile kinyama kilichokuotaga vipi kilitoka?"
"Dah ni historia ndefu dada yangu, ila kwa kifupi sijawahi kulala na mwanaume yeyote yule"
"Hebu nieleze vizuri, imekuwaje hadi leo usilale na mtu kweli!"
"Naogopa kuwaua watu wasio na hatia dada yangu. Ngoja nikusimulie kidogo ilivyokuwa. Wakati nipo chuo nilienda hospitali na kufanyiwa operesheni kile kinyama kikatolewa. Nimeogopa kulala na mwanaume yeyote tangia kipindi kile, ni kweli wakati nipo chuo nilifatwa na vijana wengi sana ila kuna kitu nilifanya ambacho kimekuwa ni doa kwangu hadi leo"
"Kitu gani hicho mdogo wangu?"
"Pale chuoni nilijitangazia kuwa nimeathirika kwa virusi vya ukimwi kwahiyo watu wote waliosoma pale wanajua mimi nimeathirika na kufanya vijana wengi wanikwepe kama ukoma"
Sakina alimsikiliza sana Sabrina na kumuonea huruma kwa tatizo lake,
"Sasa itakuwaje kwa kijana Sam?"
"Sijui kwakweli ila nampenda, najua Mungu atanisaidia kwa hili. Hata hivyo Sam ni kijana mwenye pesa labda ataweza kunipeleka mahali pazuri kuweza kutibiwa"
Wakaongea mengi sana, mwisho wa siku Sabrina akamuaga Sakina na kuondoka kisha akapita nyumbani kwao na kumuaga mama yake ili kuianza safari ya kurudi kwake,
"Ila mbona muda umeenda sana mwanangu! Leo si ungelala hapa hapa tu jamani"
"Acha tu nirudi kwangu mama, hata usijali kitu"
Joy akambembeleza mwanaye ila ikashindikana na kuamua kumpa tu ruhusa ya kuondoka halafu Sabrina akaondoka na kwenda nyumbani kwake.
Alipofika muda ulikuwa umeenda sana, Jeff alimfungulia mlango Sabrina
"Mbona leo umechelewa sana mamy?"
Sabrina akamueleza alikopita baada ya kutoka kazini, na kwenda kukaa kwenye kochi. Kisha akamwambia,
"Mama yako leo kanichekesha sana, eti amekuotea wewe umemuoa mtu mzima basi akachukiaje huyo"
Sabrina aliongea hayo huku akicheka na kumfanya Jeff naye atabasamu na kumuuliza,
"Kwani kuna ubaya gani mi nikimuoa mtu aliyenizidi umri ikiwa nampenda?"
"Weee usitake kumuua mama yako kwa presha, hataki kabisa kusikia huo upuuzi"
"Kwani kuna ubaya gani mamy? Mbona kuna wanaume wazee kabisa na wanaoa mabinti wadogo! Kwani mi nikioa mtu mkubwa kuna ubaya gani jamani!"
"Kwamaana hiyo ndio unanihakikishia hapa kuwa ndoto ya mama yako ni ya kweli, na wewe umepata sugar mamy! Eeh hebu niambie vizuri nikuelewe Jeff"
Jeff alimuangalia Sabrina na kutamani kumwambia ukweli ila akasita na kubakiwa na kigugumizi, wakati huo Sabrina nae aliendelea kumdadisi
"Niambie mwanangu, mi ndio msiri wako jamani. Au kuna mwingine?"
"Hakuna mwingine zaidi yako mamy"
"Basi niambie ukweli toto yangu jamani"
Jeff akatabasamu tu na kumuangalia Sabrina kisha akambadilishia mada
"Nikuwekee chakula mamy?"
"Najua unaipotezea mada tu huna lolote"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani kwake kwaajili ya kupumzika.
Kesho yake Sabrina akajiandaa kwaajili ya kwenda kazini, na alipofika kazini akakutana na barua kwenye meza yake na kushangaa kuwa ile barua kawekewa ya nini.
Akakaa kwenye kiti na kuifungua, akashangaa kukuta barua ikiwa imeandikwa kuwa amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana
"Mungu wangu, hivi wananifanyia yote haya sababu Sam hayupo au ni nini? Mbona haya kwangu ni mambo ya ajabu jamani!"
Sabrina hakutaka kubishana na mtu kwa muda huo kwahiyo akabeba mkoba wake na kuondoka huku kichwa chake kikiwa kimejaa mawazo.
Jeff akiwa nyumbani kwa Sabrina, alitawaliwa na wazo moja tu, wazo la kutaka kumwambia Sabrina ukweli ila hakujua ni kwa jinsi gani ataweza kumwambia ukweli huo.
Wakati Jeff akiwaza hayo akashangaa kumuona Sabrina amerudi nyumbani kwa muda wa mapema kiasi kile.
"Mbona leo mapema mamy?"
"Ofisini kwetu kimenuka, yote hii sababu Sam hayupo tu"
Jeff akamuangalia Sabrina alivyokuwa akilalamika hadi pale alipoenda kukaa.
"Ila mamy, mi nina ujumbe wako"
"Ujumbe gani huo?"
"Nakupenda sana, tena sana"
Sabrina akamuangalia Jeff na kucheka.
Jeff akamuangalia Sabrina alivyokuwa akilalamika
hadi pale alipoenda kukaa.
"Ila mamy, mi nina ujumbe wako"
"Ujumbe gani huo?"
"Nakupenda sana, tena sana"
Sabrina akamuangalia Jeff na kucheka.
Jeff alitulia na kutaka kumsikiliza Sabrina kuwa atasema kitu gani ila Sabrina hakusema chochote zaidi ya kucheka na kufanya Jeff aulize
"Mbona unacheka mamy?"
"Hivi wewe Jeff asiyejua kama unanipenda nani? Ndiomana umetafuta kisingizio cha kutoka kwenu na kuja kwangu"
Jeff akajiuliza moyoni kama kweli Sabrina amemuelewa vyema upendo anaouzungumzia yeye na kufanya amuangalie tu, kisha akamuuliza
"Kwahiyo unajua kama nakupenda?"
"Ndio najua, tena wewe kunipenda mimi hujaanza leo wala jana. Yani toka upo tumboni mwa mama yako ulikuwa unanipenda mimi, hakuna kitu ambacho mama yako aliweza kufanya bila ya mimi kwahiyo natambua vyema kama wanipenda mwanangu ndiomana jukumu la kukulea sioni kama ni gumu kwangu. Hivi umekula leo?"
Sabrina alikuwa tayari ameshabadili mada muda huo huo na kumfanya Jeff ashindwe kuendelea na pia ashindwe kuelewa kama ameeleweka alichokuwa anakisema au la.
Sabrina aliendelea na habari zingine tena hata kabla Jeff hajamjibu kama amekula au la,
"Yani ile ofisi, ngoja Sam arudi wataipata. Yani wamenitegeshea mtego ili nichelewa kazini halafu wamenitafutia vijisababu vya uongo na kweli ili wanisimamishe kazi dah"
Ikabidi Jeff nae aendane na mazungumzo ya Sabrina tu,
"Si ungemtafuta huyo Sam kwenye simu umwambie"
"Sam hapatikani, angepatikana mbona ningekuwa nimemwambia kila kitu tayari! Yani sina hata raha jamani"
"Pole mamy, mi nipo kwaajili yako"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani kwake ambapo alikuwa amejichokea kwa mawazo tu.
Sabrina alikaa sana chumbani kwake akiwaza na kuwazua, mlango wake ukagongwa naye akaenda kufungua alikuwa ni Jeff,
"Chakula tayari, twende ukale upunguze mawazo"
"Kheee Jeff na wewe unakuwa kama mfanyakazi wa ndani, uwe unajipikia chakula chako tu sitaki mama yako akija hapa aseme nakunyanyasa. Na hata kama unaona kazi zako binafsi ni nyingi niambie niajili housegirl, sawa!"
"Hapana tatizo, mie kazi naziweza mamdogo hata usilete huyo housegirl"
Sabrina akatoka chumbani kwake na kwenda sebleni kula.
Wakati Sabrina anakula, Jeff akapigiwa simu na kuongea nayo
"Poa nakuja, nipe kama dakika tano hivi"
Kisha akamgeukia Sabrina na kumuaga,
"Natoka kidogo mamdogo, nitarudi muda sio mrefu"
"Mmmh wapi saivi?"
"Hapo juu kidogo"
"Kufanya nini?"
"Kuna rafiki yangu naenda kuonana nae"
"Kwanini yeye asije hapa?"
"Aaah atakuja siku nyingine"
Jeff akainuka na kuondoka, Sabrina akahisi vitu vingine kabisa juu ya Jeff
"Huyu mtoto huyu, atakuwa ameenda kwa hilo sugar mamy lake na tukiligundua litatutambua maana mtoto mawenge yamemjaa balaa"
Akatamani hata ampigie simu Sakina na kumueleza ila alisubiri apate uhakika kwanza ndio amwambie Sakina.
Akaamua kutulia pale na kuwasha luninga ili kupunguza mawazo.
Wakati ametulia pale sebleni, akapigiwa simu kwa namba ngeni kabisa, Sabrina aliipokea ile simu kwa haraka huku akifikiria kuwa mpigaji atakuwa ni Sam, ila hakuwa Sam bali alikuwa ni Fredy ambaye alimuulizia Sabrina alipo ili akamtembelee
"Nipo nyumbani, karibu tu utanikuta"
"Poa nakuja"
Ile simu ilikatika huku Sabrina akitarajia ujio wa Fredy pale nyumbani kwake.
Sam alirudi kutoka katika safari yake na kuwaza jambo kubwa moja, nalo ni kumwambia ukweli Sabrina kuwa anampenda na anataka kumuoa.
Alikaa na rafiki yake mkubwa aliyeitwa Jose na kushauriana nae juu ya jambo hilo,
"Nataka nimfanyie Sabrina surplise ndiomana nikawaambia wampe ile barua ya kusimamishwa kazi mapema ili arudi nyumbani kwake"
"Sam kwa mipango nakukubali sana"
"Yeah, mimi ndio Sam bhana huwa sibabaishwi na kitu. Nataka pale kwa Sabrina leo tuwe wawili tu ndiomana nikakwambia tuchonge lile dili la kumuondoa yule dogo mahali pale maana ni king'ang'anizi balaa"
Wakafurahi na Jose huku wakipanga namna ya Sam atakavyoingia pale kwa Sabrina na kumfanyia ule mshtukizo ambao Sam amepanga kuufanya kwaajili ya Sabrina.
"Leo lazima lengo langu litimie"
"Usijali Sam, kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa"
Sam akajiandaa vizuri ili aende kwa Sabrina, mwanamke pekee aliyeona akimpenda kuliko wote.
Sabrina aliendelea kuungoja ujio wa Fredy ili amsikilize kuwa kaja na jambo gani jipya.
Muda kidogo mtu akabisha hodi, moja kwa moja Sabrina akajua kuwa mtu huyo lazima atakuwa ni Fredy ila alipofungua tu macho yake yakagongana na Japhet
"Kheee Japhet, nini kwangu muda huu?"
"Nimekuja kukutembelea Sabrina"
"Ni nani huyo aliyekuonyesha hapa kwangu?"
"Nilienda ofisini kwenu kuna mtu amenielekeza"
"Haya nakuomba uende, sitaki hata kukuona kwenye macho yangu. Tafadhari Japhet nakuomba uende"
"Naomba unihurumie Sabrina, nahitaji msamaha wako tafadhari. Najua nilikukosea sana"
"Naomba uende"
Sabrina akataka kufunga mlango ila Japhet akauzuia ule mlango na kumfanya Sabrina ashindwe kuufunga.
Japhet alikuwa kama mtu anayeng'ang'aniza kufanya kitu fulani ambacho Sabrina hakukitaka.
Wakati Japhet aking'ang'aniza hivyo, Fredy nae aliwasili mahali pale na kwajinsi alivyomuona Japhet alijua wazi kuwa anataka kumdhuru Sabrina, alijikuta akimrukia Fredy na kumpiga ngumi ya sura kitendo kilichomfanya Japhet aanguke kwavile hakujipanga.
Kuanguka kwa Japhet kukampa Fredy nafasi kubwa ya kumshambulia, ni Sabrina sasa aliyemtaka Fredy kupunguza hasira zake
"Basi Fredy inatosha"
Fredy alionyesha kuwa na hasira sana kanakwamba ule ugomvi unamuhusu yeye kabisa.
Fredy alisikiliza kauli ya Sabrina na kumuachia Japhet, muda huo Japhet nae akainuka kutoka pale chini na kumuangalia Fredy kisha akamwambia,
"Kumbe ni wewe! Nitakupata tu sehemu"
"Nenda zako, na bado picha itaendelea"
Fredy alijibu kwa jazba sana na kumfanya Sabrina ahisi kuwa Fredy na Japhet wanajuana kutokana na vile vitisho ambavyo walikuwa wakipeana.
Japhet akaondoka kwa hasira kisha Fredy na Sabrina wakaingia ndani, ikabidi Sabrina aende kumletea Fredy maji ili kumtuliza zile hasira kidogo
"Kunywa maji basi Fredy"
"Usijali Sabrina"
Fredy akanywa yale maji kidogo na kupunguza hasira ili aweze kuzungumza kile kilichomleta kwa Sabrina.
"Pole Fredy, nimekuingiza kwenye matatizo hata usiyo husika nayo"
"Usijali Sabrina, yule jamaa ni bwege sana"
"Kwani unamjua?"
"Ndio namfahamu vizuri sana"
"Khee umemfahamia wapi?"
"Nitakwambia tu ila ngoja nipumue kidogo"
Fredy alitulia kwa muda kidogo, Sabrina nae akatulia huku akitafakari mambo mawili matatu.
Wakati Fredy ametulia pale, usingizi nao ukampitia pale pale na kujikuta akilala pale sebleni kwa.
Sabrina akatamani kumuamsha ila akaona kwamba itakuwa ni kumuharibia usingizi wake na kumuacha aendelee tu kulala
pale kwenye kochi.
Huku Sabrina akiendelea na mambo mengine.
Wakati Sabrina akiwa jikoni kwake akasikia mtu akibisha hodi, akajiuliza kuwa atakuwa ni nani maana kama angekuwa ni Jeff basi angefungua tu sababu ana funguo yake.
Yule mtu naye akazidi kugonga na kumfanya Sabrina awaze kuwa Japhet amerudi tena kutokana na kile kipigo alichopewa akahisi kuwa amekuja kulipiza kisasi kwake.
Hofu ikamjaa Sabrina kuwa inawezekana akapigwa.
Akatoka jikoni na kwenda sebleni hadi mlangoni na kuuliza,
"Nani wewe?"
Yule mtu hakujibu bali aliendelea kugonga tu na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na hofu. Hivyobasi akaenda hadi alipolala Fredy na kumuamsha,
"Kuna mtu anagonga mlango wangu hata sijui ni nani halafu naogopa kwenda kufungua"
"Usijali, twende wote"
Sabrina akaongozana na Fredy hadi mlangoni, muda huo Fredy alikuwa nyuma ya Sabrina na kujikuta akipatwa na tamaa ya kumshika Sabrina kiunoni.
Wakati Sabrina anafungua mlango, mikono ya Fredy ilikuwa tayari imezunguka kwenye kiuno cha Sabrina, na aliyeingia ndani alikuwa ni Sam.
Alipoona sura ya Sabrina alitabasamu ila alipoona mikono ya Fredy kwenye kiuno cha Sabrina alichukia sana na badala ya kuingia ndani vizuri, alitoka nje na kuanza kuondoka na kumfanya Sabrina amfate kwa nyuma,
"Sam, Sam. Tatizo nini jamani"
"No, siwezi kuzungumza kwasasa."
Sam akaenda na kupanda gari yake na kuiondoka, Sabrina alibaki kaduwaa tu kwani hakumuelewa kabisa Sam na hakuelewa kuwa ni kwanini achukie kiasi kile.
Aliangalia gari ya Sam ikiishia tu,
"Halafu kaja na gari mpya ile, nadhani kanunua nyingine. Dah hata sijui kachukia nini, yani amerudi bila kuniambia na amekuja nyumbani kwangu na kuondoka kwa hasira."
Sabrina akaamua kurudi ndani tu ambapo Fredy alikuwa bado mlangoni huku naye akishangaa kuwa kwanini yule Sam kaondoka tena bila ya salamu wala kuaga.
Sabrina alipofika pale mlangoni akaingia ndani na Fredy huku akiendelea kujiongelesha mwenyewe,
"Hata sijui kwanini Sam amechukia kiasi kile"
Fredy akamuuliza Sabrina,
"Kwani una mahusiano nae?"
"Hapana, yule ni bosi wangu na rafiki yangu"
"Sasa mbona amechukia vile?"
"Hata sijui ni kwanini"
Sabrina akachukua simu yake na kujaribisha kama namba za Sam zinapatikana ila bado hazikupatikana na kumfanya Sabrina awe na mawazo zaidi.
Fredy akaanza tena kwa kumuongelesha Sabrina,
"Kuna jambo moja tu lililonileta hapa kwako Sabrina"
"Tafadhari Fredy, nakuomba usiniambie kitu chochote kile. Maana akili yangu haipo sawa kabisa hapa."
Fredy hakuwa na la kusema zaidi wala la kufanya na kuamua kumuaga Sabrina ili aende.
"Basi ngoja niende Sabrina, ila kumbuka nakupenda sana. Na hakuna mwanaume anayekupenda kama mimi ninavyokupenda yani hakuna kabisa. Nakupenda Sabrina tena sana"
Sabrina hakumjibu kitu chochote Fredy zaidi ya kumuangalia tu.
Fredy akatoka zake nje na kuondoka.
Sabrina akiwa amebaki mwenyewe ndani, aliwaza sana.
"Huenda Sam naye ananipenda ndiomana kachukia kunikuta na Fredy. Inawezekana ikawa hivyo tu, au ana mambo yake mengine yaliyomfanya achukie. Kwanini jamani, kwanini haniambii ukweli huyu Sam jamani mmh"
Sabrina aliwaza sana bila ya kupata jibu, muda kidogo akawasili Jeff akiwa amechoka sana na kumfanya Sabrina amuulize.
"Vipi tena na wewe?"
"Yani hapa nimechoka mamy balaa, huwezi amini. Mtu aliyenipigia simu amenizungusha mji mzima na mwisho wa siku sijaonana nae wala nini"
"Pole sana, basi mwenzio hapa yamenikuta makubwa leo"
"Makubwa!! Mambo gani hayo?"
Sabrina akaanza kumueleza Jeff tangia ujio wa Japhet, Fredy na Sam ambapo Jeff nae akaonyesha kuchukizwa
"Na bahati yao hawajanikuta haswa huyo wakuitwa Japhet ningemfunza adabu"
"Mmh Jeff wakubwa zako wale"
"Mi mdogo ila nitawashinda"
"Mmmh kivipi"
Jeff akacheka bila ya kumjibu Sabrina na kumuingizia habari zingine.
Ila Sabrina akaendeleza khabari zilezile,
"Sijui kesho niende ofisini ili nikamwambie Sam kuwa nimesimamishwa kazi!"
"Usijisumbue mamdogo, kumbuka huyo Sam ndio bosi mwenyewe kwahiyo wale hawawezi kufanya chochote bila ya maamuzi yake."
"Unamaanisha kuwa Sam ndio kakubaliana nao kuwa mi nisimamishwe kazi?"
"Hiyo ndiomaana yake, wewe tulia kwanza uone kitakachoendelea"
"Mmh wee mtoto, kazi naitaka mie. Unataka nirudi tena kukaa nyumbani! Niombe hela ya mafuta na vipodozi kwa mama! Hapana kwakweli, lazima nibembeleze kazi"
"Sasa utafanyaje"
"Ilimradi Sam amerudi, basi kesho kwenye mida ya saa nne nitaenda ofisini ili nikajaribu tena bahati yangu"
Jeff hakuwa na pingamizi juu ya hilo zaidi ya kukubaliana nae tu.
Sam alikuwa amejawa na hasira, kile kitendo cha kumkuta Sabrina ameshikwa kiuno na mwanaume mwingine kilimuumiza sana.
Alijaribu kukaa na rafiki yake Jose ili kuweza kupata ushauri.
"Kwakweli sijui cha kufanya, roho inaniuma sana."
"Ila Sam, wewe ndiye unayechelewesha mambo. Kwanini usimwambie ukweli yule mtoto?"
"Nina matatizo Jose, sitaki kumchukua tu Sabrina bila ya yeye kujua matatizo yangu. Leo nilijipanga kabisa kumueleza Sabrina kila kitu kuhusu mimi, najua asingekataa ndiomana nikataka kumpa hata lile gari kama zawadi tu"
"Pole sana, najua jinsi gani unaumia ingawa hata mi mwenyewe huwa sijui una matatizo gani ila la msingi ni kumwambia Sabrina ukweli tu. Kuchukia sio suruhisho baina yenu"
"Naona kamavile Sabrina hajatulia, nami nahitaji mwanamke aliyetulia ili aweze kunielewa ni kitu gani nakitaka kutoka kwake"
Jose akajaribu kumuelekeza rafiki yake na kumtuliza zile hasira alizokuwa nazo.
Usiku ulipofika Sabrina alienda kulala, ila akajiwa na ndoto kuwa ameolewa na kumfanya ashtuke na kujiuliza
"Hivi hii ndoto inanijia mara kwa mara kwani mume wangu ni nani?"
Akasikia sauti ya Jeff ikijibu kutoka mlangoni,
"Mimi hapa"
Sabrina akashtuka na kuuliza tena,
"Nani?"
Jeff akajibu tena,
"Mimi hapa Jeff"
Sabrina akainuka ili kuangalia kama kweli anayemjibu ni Jeff.
"Hivi hii ndoto inanijia mara kwa mara kwani
mume wangu ni nani?"
Akasikia sauti ya Jeff ikijibu kutoka mlangoni,
"Mimi hapa"
Sabrina akashtuka na kuuliza tena,
"Nani?"
Jeff akajibu tena,
"Mimi hapa Jeff"
Sabrina akainuka ili kuangalia kama kweli
anayemjibu ni Jeff.
Sabrina alipofungua mlango alimkuta ni Jeff kweli na kumshangaa kuwa kwanini ajibu kwamba yeye ndiye mumewe.
Akamuangalia kwa makini sana na kumuuliza,
"Ni wewe Jeff!!"
"Ndio ni mimi, kwani vipi?"
Sabrina akamzaba kibao Jeff na kumfanya Jeff ashangae na kumuuliza,
"Mbona unanipiga mamdogo! Kwani kosa langu ni lipi?"
"Ulikuwa unaniitikia nini hapa mlangoni? Je mimi ni mtani wako?"
"Sikuelewi mamdogo, kwani ni nini?"
"Inamaana hujui ulichokuwa unajibu hapa mlangoni au kiburi?"
"Kwakweli nakushangaa mamdogo, mi nilikuja mlangoni kwako kukugongea kuwa muda umeisha uamke uende kazini, ukauliza nani nikakujibu mimi, ukauliza tena nani nikakujibu ni mimi Jeff. Sasa hapo kosa langu ni lipi jamani?"
Sabrina alimuangalia Jeff kwa jicho la huruma na kumuomba msamaha, akajiona wazi kuwa mwenye makosa ni yeye na ndoto zake zisizoeleweka lakini yeye alichukua jukumu tu la kumpiga Jeff kibao bila hata ya kujiuliza au kumuuliza kwanza.
"Nisamehe sana Jeff toto yangu"
"Usijali mamy"
Jeff akaondoka na kumuacha Sabrina akiwa amesimama pale pale mlangoni.
Akasikia mtu akigonga mlango wao wa nje na kwenda kumfungulia, akashangaa kumuona kuwa ni Sam,
"Nimekupitia twende kazini"
"Nimesimamishwa kazi Sam"
"Mwenye uwezo huo pale ni mimi tu, haya kajiandae nakungoja twende"
Sabrina hakuamini masikio yake na kuamua kwenda kujiandaa haraka haraka ili aweze kuwahi kuondoka na huyo Sam.
Alipomaliza alitoka na kumkuta Sam akiwa bado anamngoja kwahiyo akatoka naye nje na kuondoka zao.
Ndani ya gari Sabrina akatamani sana kumwambia Sam kila kilichojiri juu yake wakati hayupo ila akajikuta akisita kwavile Sam alikuwa kimya sana hata tabasamu lake tu halikuonekana siku hiyo na kumfanya Sabrina nae akae kimya ili kuhofia kuharibu siku yake kabisa.
Walipofika ofisini, kila mmoja alikodoa macho kwa Sabrina huku wakiongea chini kwa chini, wakati huo Sabrina aliongoza moja kwa moja kwenye ofisi ya Sam.
"Nilijua tu kuwa atarudishwa"
"Ulidhani kuna mtu mwenye uwezo wa kumfukuzisha Sabrina kazi kwenye ofisi hii! Hakuna hata mmoja, na sie tukionekana tunachonga basi tutafukuzwa sisi"
Wakaangaliana na kugonga kwa mbali mbali kisha wakakaa kimya.
Sabrina alipokuwa kwenye ofisi ya Sam,
"Hebu nipe hiyo barua ya maelezo kuwa usimamishwe kazi"
Sabrina akatoa ile barua na kumkabidhi Sam, ambapo Sam aliisoma huku akitikisa kichwa na kumwambia Sabrina,
"Huwa simpendi mtu anayefanya kitu kinyume na maelezo yangu, sasa huyu atanijua vizuri kuwa Sam ni nani. Haya nenda ukaendelee na kazi zako"
Sabrina alikuwa kimya tu kwani hakuelewa hata kuwa Sam alitoa maelezo gani na kwanini waliopewa maelekezo walifanya kinyume.
Akatoka na kwenda kwenye ofisi yake, na kufanya baadhi ya watu kwenye zile ofisi kuishia kununa tu.
Wakati Sam yupo ofisini akifikiria namna ya kufanya na msaidizi wake ambaye alimpa barua hiyo Sabrina akapatwa na ugeni.
Alikuwa ni Joyce dada yake, mtoto wa mjomba ake.
Baada ya salamu, Joy akamwambia kaka yake
"Bora umerudi kaka, nina ujumbe wako mzito sana."
"Naomba badae tuonane nikwambie, maana nimejaribu simu zako hazipatikani ndiomana nikaona ni vyema nije moja kwa moja kama hivi"
Sam hakuwa na pingamizi na kumpa dada yake namba zingine alizokuwa anazitumia na kuagana nae huku wakipanga pa kuonana baada ya kazi.
"Basi usijali dada yangu nitakutafuta"
Joy akatoka kwenye ile ofisi na kupita kwenye ofisi ya Sabrina na kumsalimia kwa kugelesha kisha akamuaga na kuondoka.
Jioni yake Sam alimchukua Sabrina na kumrudisha nyumbani kwake kisha yeye akaamua kwenda kuonana na dada yake ili aweze kupewa ule ujumbe uliokusudiwa.
Walionana kama walivyopanga huku Sam akiwa na hamu ya kupata huo ujumbe.
Joy alianza kuongea kwa utulivu kabisa,
"Kwanza kaka samahani kwa nitakayo kwambia. Nimejitahidi kuvumilia lakini nimeshindwa na nimeona bora tu nikwambie halafu wewe mwenyewe ndio utaamua kula mbichi au iliyoiva"
"Usijali dada yangu, wee niambie tu"
"Ni kuhusu Sabrina"
Sam akashtuka sana na kumuuliza dada yake kwa mshangao,
"Kwani Sabrina kafanyeje!!"
Joy akapumua kwanza na kumuuliza kaka yake,
"Je! Una mahusiano yoyote ya kimapenzi na Sabrina?"
"Hapana, ila nampenda sana"
"Basi tahadhari kaka yangu, ule ni waya wa umeme. Ukikanyaga tu unanasa"
"Kivipi Joy? Mbona sikuelewi?"
Joy akaamua kumwambia Sam yale aliyoyasikia kumuhusu Sabrina kuwa ameathirika na chuo alichosoma wote wanatambua hilo na kumfanya Sam aishie kushangaa kwani hakufikiria hata kidogo kitu cha namna hiyo.
"Hivi Joy una uhakika na unayoyasema?"
"Ndio, nina uhakika kwa asilimia tisini na tisa pointi tisa kasoro sifuri pointi moja."
Sam akamuangalia sana Joy huku akijaribu kuyasoma mawazo yake na maneno yake, kisha akamwambia
"Asante kwa taarifa dada yangu, ila nitafanyia kazi hiyo taarifa yako ili niweze kujiridhisha na mimi mwenyewe"
"Sawa kaka, hakuna tatizo ila mi nimekupa ujumbe tu na kukuachia kazi wewe mwenyewe"
Wakaongea mawili matatu na kuagana.
Sam akiwa nyumbani kwake alijifikiria sana kuhusu Sabrina kama yale aliyoyasikia ni ya ukweli au la
"Kama ni kweli, basi Sabrina atakuwa amewaambukiza watu wengi sana kwa ule mtindo wake. Au ndiomana wakati mwingine anasema kuwa hataki mchumba! Mmh ananipa mashaka sasa"
Sam aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile.
Sabrina alipokuwa nyumbani kwake, akagundua kuwa ana siku kama mbili tatu hajaingia kwenye mtandao wa kijamii
"Itakuwa kale kajamaa kamenimiss sana ila tatizo lake uongo mwingi, siku ile kamenigandisha pale hadi nikakutana na watu nisiowatarajia"
Ila akaamua kuingia kwenye mtandao ili kuona kama kweli Prince J amemkumbuka.
Alikutana na jumbe nyingi sana kutoka kwa Prince J za kumkumbuka, ila ujumbe uliomshtua ulikuwa ni mmoja tu toka kwa huyo huyo,
"Ipo siku nitakuja na tutalala wote, siku hiyo itakuwa ya furaha kwako kwani utaburudika kwa penzi ambalo nitakupa. Ila kesho yake najua utachukia sana, ila penzi langu lazima liache doa kwako na kukufanya unikumbuke siku zote za maisha yako"
Sabrina akashtushwa sana na ujumbe huo, kwanza alimshangaa huyo Prince J kwani alijua kuwa hatoweza kuonana nae tena hata iweje.
Akajiuliza sana bila ya majibu,
"Ila kwanini aseme hivi? Kwanini aandike ujumbe kama huu? Anamaana gani huyu mtu? Eti ataniachia doa, doa gani hilo? Yani mijitu mingine hata sijui kwanini nilikuwa nikichat nalo shetani hili, ndiomana watu husema kuna majini humu"
Sabrina akafanya kitu kimoja juu ya Prince J, akamfuta kwenye orodha ya marafiki zake facebook ili awe huru sasa na kusahau kuwa alishawahi kumpa namba ya simu kwa mawasiliano.
Sabrina aliamua kulala kwani alijua hata kama ataamua kuwaza sana hawezi kupata jibu la kumridhisha au la moja kwa moja.
Kulipokucha kama kawaida Sabrina alijiandaa kwenda kazini na akapitiwa na Sam na kuondoka naye.
Ila kwenye gari kila mmoja alikuwa kimya, hakuna aliyemuongelesha mwenzie hadi wanafika ofisini.
Ila walipofika kwenye mlango wa ofisi, Sam akamwambia Sabrina
"Badae nina maongezi na wewe"
"Sawa, hakuna tatizo"
Sam akaingia kwenye ofisi yake na Sabrina pia akaingia ofisini.
Sabrina akatulia kwenye meza yake na kupatwa na ugeni asubuhi ile ile, ugeni ambao ulimshangaza sana kwani alikuwa ni binti mdogo na moja kwa moja alimuulizia Sabrina na kupelekwa kwenye meza ya Sabrina,
"Karibu, niambie shida yako nikusaidie"
"Asante, kuna mtu kanituma na kanipa ujumbe huu"
Yule binti akamuachia karatasi Sabrina kisha akamuaga na kuondoka.
Sabrina akafungua lile karatasi na kukutana na maandishi ya mtu kuwa anaomba waonane nae baada ya kazi kwakuwa ana ujumbe wake.
Sabrina hakujua pa kuanzia wala kuishia ukizingatia Sam ameshamwambia kuwa badae aonane nae, na vipi huyu mtu aliyemtumia ujumbe je itakuwaje! Alitamani kumjua kuwa ni nani ila alikuwa njiapanda.
Jioni ilipofika, akaona ni vyema kuanza kuonana na yule aliyemtumia barua kwanza kwahiyo aliamua kwenda kwa Sam ili amuage,
"Naomba ruhusa bosi kuna mahali nataka kwenda kidogo"
"Si nimekwambia nina maongezi na wewe!"
Sabrina akakaa kimya kwa muda na kumjibu,
"Natambua hilo, ila naomba nikaonane na huyu kwanza"
"Haya nenda"
Sam alijibu kama mtu mwenye hasira sana ila aliyezificha hasira zake.
Sabrina akaondoka pale ofisini na kwenda mahali ambako alielekezwa kwa ile barua kuwa aende.
Alipofika pale, akaangalia kushoto na kulia ili kujua ni nani aliyemuita ila alitokea mtu kwa nyuma na kumziba Sabrina kwa viganja vya mikono yake, Sabrina akauliza
"Nani wewe?"
Yule mtu akamjibu,
"Otea "
"Mmh! Kuotea siwezi kwakweli, wee niambie tu kuwa ni nani"
Akacheka na kumuacha Sabrina amuangalie mwenyewe,
"Kheee kumbe ni Francis!"
"Ndio ni mimi mpenzi, mwanaume nikupendaye kupita wote duniani"
Sabrina akamuangalia Francis, kisha Francis akamuomba Sabrina kuwa wakae na waweze kuzungumza mawili matatu.
Sabrina hakukataa zaidi ya kukaa na kumsikiliza Francis,
"Siku zote nilikuwa natafuta siku nzuri na muda muafaka wa kuzungumza na wewe Sabrina, kiukweli bado nakupenda tena nakupenda sana"
Sabrina alimuangalia Francis bila ya kumjibu chochote kwavile alikuwa anajiuliza kuwa kati ya Francis na Fredy ni nani aliyekuwa anampenda kweli? Kwavile hakuelewa kwanini wote wanamwambia kuwa wanampenda sana.
Francis aliendelea kuongea tena kwa hisia kabisa,
"Sema chochote juu ya penzi letu Sabrina. Mi mwenzio bado nakupenda sana, nakuhitaji katika maisha yangu. Napenda uwe nami siku zote."
"Sawa Francis nimekuelewa tena sana tu ila tafadhari nipe muda ili niweze kutafakari"
"Kumbuka Sabrina, mi ni mwanaume pekee ninayekupenda toka kipindi kile. Yale yote niliyokuwa nikiongea zamani ilikuwa ni sababu ya hasira tu mpenzi. Tena usipende kumsikiliza Fredy, hana lengo zuri na wewe ila nia yake ni kuona kuwa penzi letu linaporomoka"
Francis aliongea mambo mengi sana na kumfanya Sabrina awe kimya kabisa akimsikikiza hoja zake.
"Natumaini una nielewa Sabrina, nakuombea yaliyo mema. Fanya uchaguzi sahihi katika maisha yako, wakati ni huu na hakuna wakati mwingine usije kujutia badae. Ushakuwa mtu mzima sasa, unatakiwa kuolewa na kuwa na familia yako. Najua majibu yanakuwa magumu kwangu kwavile ni wengi wanaokwambia kuwa wanakupenda, ila angalia kwa makini ni nani anayekupenda kweli ili badae usijutie tena"
"Nashukuru Francis, nimekuelewa sana tena sana hakuna haja ya kurudia maelezo"
Kisha wakaongea mengine kati ya yale, na muda nao ulikuwa umeenda hivyo Francis akamuomba Sabrina ampeleke nyumbani kwake kwa usafiri wake wa pikipiki ili aweze na kupafahamu pia.
Sabrina akakubali kwavile muda ulishaenda tayari.
Francis alimfikisha Sabrina nyumbani kwake na kumuaga kwavile muda ulikuwa tayari umeshaenda sana.
Aliingia ndani na kwenda kukaa karibu na Jeff ambapo akabambana na maswali ya Jeff.
"Mbona umechelewa sana leo mamy?"
"Kuna mtu nilikuwa nazungumza naye, yani mwanangu mapenzi haya mi yataniua jamani"
"Kwanini unasema hivyo mamy?"
"Kwakweli sielewi yani sielewi kabisa, sijui nani ananipenda kweli sijui nani ananidanganya. Yani wale wale waliofanya niyachukie mapenzi eti leo wanakuja na kusema kuwa wananipenda sana. Hata sijui ni nani wa kuwa nae kati yao!"
"Nikwambie kitu mamdogo?"
"Niambie mwanangu."
"Kati ya hao watu usimkubali hata mmoja mamy"
"Kwanini unasema hivyo?"
"Watakuona mjinga halafu wao ndio washindi wakati washakuumiza sana. Huu ni muda wa wewe kuwaumiza wao"
"Kuwaumiza wao kivipi?"
"Unatakiwa uwe na mtu mwingine kabisa, mtu ambaye atakusahaulisha kila kitu kuhusu wao. Unatakiwa kuanza upya maisha yako, sitapenda kuona ukilia au ukiteseka sababu ya mapenzi mama angu"
"Sasa nitafanyeje hapo?"
"Unatakiwa uwe na mtu mwingine"
"Mwingine yupi?"
"Kesho nitakuonyesha mamy"
"Aaah sitaki kesho, nataka uniambie leo"
"Kweli unataka leo?"
"Ndio niambie leo"
"Haya inuka nikakuonyeshe"
Jeff alimshika mkono Sabrina mpaka chumbani kwa Sabrina, kisha akamwambia
"Nenda ukakae pale kwenye kitanda chako nikuonyeshe"
Sabrina akamuangalia Jeff kwa mshangao na jicho la hasira.
Jeff alimshika mkono Sabrina mpaka chumbani
kwa Sabrina, kisha akamwambia
"Nenda ukakae pale kwenye kitanda chako
nikuonyeshe"
Sabrina akamuangalia Jeff kwa mshangao na
jicho la hasira.
Halafu akamuuliza kwa mshangao,
"Hivi wewe mtoto una akili!!"
Sam akamuangalia Sabrina na kutabasamu kitendo ambacho kilimkera sana Sabrina,
"Hivi wewe mtoto una kichaa? Yani unaniambia vitu visivyoeleweka halafu nakuuliza jambo unashindwa kunijibu kwanini huku unatabasamu tu. Haya nionyeshe na ukiniletea ujinga wako leo tutaonana wabaya nakwambia. Haya nionyeshe"
Jeff akamuangalia Sabrina kwa upole kisha akaongea kwa utaratibu.
"Sina maana mbaya mamdogo, ila nimekuona ukiwa umechoka sana halafu nakwambia nitakuonyesha kesho wewe unang'ang'ania leo, ndiomana nimekuleta humu chumbani kwako na kukwambia ukakae pale kitandani kwako ili upumzike mamdogo"
Sabrina akacheka na kusema,
"Yani wewe mtoto wewe akili zako sijui huwa zinafikiria vitu gani. Haya nipishe nilale mie"
Jeff akatoka, ila kabla hajafika mbali Sabrina akamuita tena
"Jeff njoo"
Jeff akarudi kwa shauku huku akitamani kujua kuwa kaitiwa kitu gani.
"Na leo kweli nimechoka jamani, naomba unitolee viatu vyangu nimeviacha pale nje"
"Sawa"
Akaitikia kiunyonge na kutoka nje.
Sabrina akiwa chumbani kwake usiku huo, akapigiwa simu na Sam hadi yeye mwenyewe akashtuka kwani akakumbuka wazi kuwa waliahidiana kufanya mazungumzo.
"Mmmh sijui nitamjibu nini jamani!"
Akaiangalia ile simu ambayo iliita hadi kukatika na kuanza kuita tena.
Sabrina akaamua kuipokea, na swali la kwanza toka kwa Sam lilikuwa
"Uko wapi?"
"Nipo nyumbani"
"Unafanya nini?"
"Nimelala"
"Na nani?"
"Mmmh peke yangu"
"Una uhakika?"
"Ndio"
"Haya, usiku mwema"
Kisha akakata simu na kumfanya Sabrina aishie kumshangaa tu,
"Maswali kama polisi, inahusu! Kuwa bosi ndio mpaka kujua njia zangu! Akha! Anipishe mie asinipe shida, yani hata simuelewagi kwakweli maana kama angekuwa ananipenda basi angekuwa ameshaniambia kitambo sana ila anachojua yeye ni kunifatilia tu loh nishamchoka mie"
Sabrina alikuwa akijiongelea mwenyewe pale kitandani na kulala.
Akajiwa na ndoto kumuhusu Jeff, ndoto iliyomuonyesha kuwa Jeff ana mahusiano na mwanamke aliyemzidi umri.
Aliwaona wakiwa wameongozana, ila Sabrina aliweza kumuona huyo mwanamke mgongoni tu, wakati yule mwanamke anataka kugeuka Sabrina akashtuka na kuanza kujilaumu,
"Kwanini nimeamka bila kuijui sura ya huyo mwanamke? Haiwezekani, mi ndoto zangu mara nyingi huwa ni za kweli. Lazima nikamwambie Da Sakina ili tupambane kuhusu hili janga"
Muda wa kwenda kazini ulikuwa umefika na kumfanya Sabrina ainuke na kujiandaa kabisa.
Alipotoka, alimkuta Jeff akiwa sebleni
"Basi siku hizi hulali wala nini, unamuwaza sugar mamy tu. Hiyo mimama itakutokea puani mtoto wewe"
Sam alifika na kumsikia Sabrina akifoka kwa Jeff kisha akatoka na Sabrina kwaajili ya kwenda kazini.
Wakati wapo ndani ya gari, Sam aliamua kumuuliza Sabrina,
"Mbona ulikuwa unamfokea yule dogo, kafanyaje kwani?"
"Usimuone vile yule mtoto, anatembea na mimama mikubwa"
"Kwanini sasa kijana mdogo vile anajiharibu?"
"Ndio pakumshangaa hapo, yani kuna mabinti wazuri kweli yeye anakazana na masugar mamy, yani leo nikitoka tu ofisini naenda kwa mama yake kumpa habari"
"Ila Sabrina unajipa mizigo mikubwa bure tu, huyo dogo angerudi kwao ili mama yake awe nae karibu na aweze kumchunguza"
"Ngoja nikashauriane nae juu ya hilo kwanza"
Waliongea mambo mengi ya kumuhusu Jeff hadi pale walipofika ofisini.
Sabrina alifanya kazi yake, na alipomaliza akaona ni vyema aende kupata ruhusa sababu alikuwa na hamu sana ya kuongea na Sakina.
Kwavile ilikuwa ni mwisho wa wiki, hawakushindwa kumpa ruhusa ukizingatia kazi alishazikamilisha.
Sabrina akaondoka pale na kufanya safari ya kwenda kwao.
Moja kwa moja alianza na nyumbani kwao kwanza, na kumkuta mama yake na kaka yake mkubwa.
"Kheee leo kaka James umekumbuka nyumbani!!"
Mama yao akadakia,
"Kaja kunipa khabari kuwa amepata mchumba, kwahiyo Sabrina mwanangu umepata wifi"
"Mmh! Nani huyooo?"
James akacheka, kisha mama yao akajibu tena,
"Kasema atamleta kesho, tena anajina kama langu"
"Joyce!!"
"Ndio, anaitwa Joyce"
Sabrina akamuangalia kaka yake na kumuuliza,
"Mmh sio Joy yule kweli!!"
James akatabasamu na kumjibu dada yake,
"Na wewe acha papara, utamjua kesho"
"Basi kesho nitakuja mapema jamani kumuona wifi"
Huku akitabasamu na kufurahia na wote wakafurahia.
Kisha Sabrina akawaaga kuwa anaenda kuonana na Sakina.
Siku ya leo, Jeff akiwa nyumbani kwa Sabrina akachekecha kichwa chake na kuwaza cha kufanya juu ya Sabrina.
Akapata wazo la haraka, tena la bila kutumia nguvu wala maneno mengi na kuona kuwa wazo hilo ndio litakalomfaa katika mpango wake wa kumpata Sabrina.
"Mungu atanisamehe tu, kwakweli nampenda Sabrina tena nampenda sana sitaki kumkosa wala sitaki mtu yeyote wa kuyaingilia mapenzi yangu kwake. Mimi ndiye mwanaume pekee nimpendaye kwa dhati, hata kama ni mkubwa kwangu ila nampenda na siwezi kumpenda mwingine zaidi yake"
Aliendelea kupanga mipango yake ili aweze kumpata Sabrina kwani alijua wazi hata kama aseme vipi Sabrina hawezi kumuelewa ukizingatia anamuona kama mtoto wake.
Sabrina alimkuta Sakina na kuanza kuongea nae mawili matatu, kisha akamsimulia ndoto aliyoota kuhusu Jeff na kumfanya Sakina azidi kuchukia kuhusu huyo mama mtu mzima mwenye mahusiano na Jeff bila hata ya kumuona.
"Kwakweli nikimfahamu huyo mwanamke, nakuapia Sabrina nitammeza mzima mzima. Yani wanawake wengine sijui vipi, hawana hata huruma na wanawake wenzao. Kuniharibia katoto kangu Jeff ndio nini? Mtoto mwenyewe ndio huyu huyu kama jicho jamani!"
"Dada, tufanye uchunguzi na tukimjua lazima ajue sisi ni akina nani. Hata kama watu wanasema haifai kumchagulia mtu mchumba sio kwa mtindo huu jamani. Mi nahisi huyo mmama kampa Jeff madawa"
"Itakuwa hivyo tu, ila kumbuka Sabrina mi ni mtoto wa kitanga siogopi kitu na nitamkomesha hilo jimama"
Sakina alikuwa akiongea kwa jazba sana na hasira.
"Ila dada, mi nina wazo"
"Wazo gani hilo?"
"Naona ni vyema Jeff arudi kukaa hapa na wewe ili uweze kumchunguza vizuri sababu mimi muda mwingi nakuwa kazini dada"
"Kweli ni wazo zuri mdogo wangu, ila kama wewe umeshindwa mi nitaweza kweli! Unajua Jeff anakusikiliza sana wewe, kwahiyo mi nakuomba ujaribu kumbana ili akutajie huyo mjaalaana asojua vibaya maana hata nikimfikiria huyo mwanamke kutembea na katoto kangu nahisi kichefuchefu"
"Basi dada mi nitajaribu kumbana nimuulize ila kama ikishindikana basi itabidi tu arudi huku kwako sababu mi sitaweza zaidi kwakweli"
"Hakuna tatizo, ndio kujaribu huko ndugu yangu. Ila lazima tushirikiane kumjua huyo mwanamke."
Sakin a akakubaliana na Sabrina juu ya swala hilo.
Kisha Sabrina akamuaga Sakina na kuelekea tena nyumbani kwao.
"Mi nataka kuondoka mama!"
"Si ungelala hapa hapa leo! Kwanza kesho hakuna kazi, pili ungesubiri tu hadi hiyo kesho umuone wifi yako"
"Usijali mama, Sam alihitaji kuongea na mimi tangia jana ila ratiba zikaingiliana. Ndio leo naenda kuzungumza nae, halafu kuhusu wifi hakuna tatizo kwani kesho asubuhi na mapema nitafika hapa na kumngoja wifi yangu"
Basi Joy hakuwa na jinsi zaidi ya kumruhusu binti yake aende tu huko alikopanga.
Sabrina akaenda kuonana na Sam kwaajili ya mazungumzo ambayo walipanga kuongea jana yake.
Ila alijikuta akiwa eneo la tukio peke yake bila ya Sam kutokea,
"Inamaana ananilipizia ya jana au ni kitu gani? Si angeniambia tu kuliko kunifanyia hivi!"
Ila aliendelea kusubiria na kujipa moyo wa subira kuwa Sam atatokea tu.
Mida iliendelea kupita bila ya Sam kutokea na kumfanya Sabrina ajawe na hasira kwenye moyo wake.
"Kwanini kanifanyia hivi jamani, kwanini Sam lakini!"
Wakati akilalamika hivyo ujumbe ukaingia kwenye simu yake, ulionyesha kuwa umetoka kwa Sam na kumfanya Sabrina aufungue kwa shauku kubwa,
"Samahani Sabrina, ratiba zimeingiliana. Kuna watu muhimu sana natakiwa kuonana nao leo, kwahiyo tutapanga siku nyingine ya kuongea"
Sabrina akavimba kwa hasira, akatamani hata aipasue ile simu yake.
Akainuka kwenye kiti huku moyo wake umejaa hasira na kuanza kuondoka, simu yake ikaita. Sabrina hakutamani hata kuipokea kwakuwa mpigaji alikuwa ni Sam, ila aliona ni vyema aipokee tu
"Geuka nyuma Sabrina"
Sabrina akageuka na kumuona Sam akitabasamu, Sabrina alimuangalia Sam kwa jicho la hasira huku likicheza cheza na kutamani kucheka na kulia kwa pamoja.
Sam alisogea pale alipokuwa Sabrina huku akiendelea kutabasamu,
"Sabrina, twende tukakae tufanye mazungumzo yetu"
"Kwanini Sam umenifanyia hivi jamani!"
"Nilitaka kupima uvumilivu wako Sabrina"
"Ili iweje?"
"Twende tukakae basi kwanza tuzungumze"
Sam akamshika mkono Sabrina na kumpeleka mahali ambako kulikuwa na kiti na kumsihi akae, kisha wakaagiza vinywaji na kuendelea na maongezi.
"Nimegundua kitu kutoka kwako Sabrina"
"Kitu gani hicho?"
"Nimegundua kuwa wewe ni mwanamke mvumilivu sana, una hasira za karibu lakini pia ni mvumilivu"
"Haya, nashukuru kwa hilo ila umenikera sana"
"Nisamehe Sabrina, tena unisamehe sana"
"Poa usijali"
"Nisijali ndio umenisamehe au!"
"Nimekusamehe ndio"
"Sasa Sabrina mi kuna jambo moja kubwa nataka kukuuliza"
"Jambo gani hilo?"
"Nilitaka kukuuliza kuhusu maisha yako Sabrina ila kuna jambo lingine linataka kuingilia kati hapa"
"Niambie basi ni ja mbo gani hilo!"
"Leo ngoja niseme ukweli wa moyo wangu, kwakweli Sabrina nakupenda sana, nakuhitaji, napenda uje kuwa mke wangu. Nakupenda Sabrina jamani nakupenda sana."
Sabrina hakuamini macho yake wala masikio kwa kile alichokisikia kutoka kwa Sam na kujikuta akiwa kama mtu anayehitaji kusikia zaidi.
"Hivi Sam upo serious kweli?"
"Sabrina, unadhani yote haya nayafanya kwaajili ya nini jamani? Ni sababu ya upendo wangu juu yako Sabrina, nakupenda wewe, sitaki kukukosa. Sitaki uwe mbali na mimi, nakupenda sana Sabrina"
Sabrina hakujua amjibu nini Sam kwa muda huo kwani alihisi akili yake kamavile ikipaa angani, alihisi kama yupo ndotoni vile kwani hakuamini kuwa Sam ndiye aliyekuwa akimtamkia maneno yale.
Sabrina akaamua kumjibu Sam kwa tabasamu kubwa usoni,
"Hata mimi nakupenda Sam, siku zote nilikuwa nikingoja kwa hamu siku ambayo utanitamkia wazi kuwa unanipenda. Sikutaka kuanza kusema kwavile ungenielewa vingine, nashukuru Mungu aliyekufunulia kuniambia ukweli huo Sam. Nami nafurahi sana na kukwambia kuwa nakupenda pia"
Sam aliinuka pale alipokuwa amekaa, kisha akamshika mkono Sabrina na kumuinua halafu akamkumbatia kwa furaha.
Kisha akamnong'oneza sikioni,
"Naomba leo ukalale kwangu Sabrina maana nina mengi ya kuzungumza na wewe"
Sabrina akasita kidogo na kuacha kumkumbatia Sam, kisha akamuomba kwenda msalani.
Alipokuwa maeneo ya msalani, Sabrina akafikiria sana.
"Nikikubali kwenda kulala kwake leo lazima atataka kufanya mapenzi na mimi. Mmh! Siku ya kwanza tu ya kukubaliana nitaonekana malaya ni bora nikatae halafu tutapanga siku nyingine. Na vipi kuhusu matatizo yangu yale je! Nitamdhuru kijana wa watu, bora nikatae halafu nitamuelewesha siku zijazo"
Sabrina akakubaliana na moyo wake na kisha kurudi eneo alilomuacha Sam ili kuendelea na mazungumzo.
"Unasemaje sasa mpenzi, twende ukalale kwangu leo"
"Hapana Sam, nitalala kwako siku nyingine ila sio leo"
"Nina mengi ya kuzungumza nawe Sabrina, nina mengi ya kukwambia. Yani usiku wa leo nilitaka uwe ni usiku wa mazungumzo tu baina yetu Sabrina, nakupenda jamani"
"Naelewa Sam, ila tupange siku nyingine tafadhari. Hata mi nakupenda"
Sam hakutaka kubishana sana na Sabrina badala yake akamwambia kuwa atamrudisha nyumbani kwake ila kesho atampitia kwaajili ya matembezi.
"Tena kesho naenda nyumbani sababu kaka yangu kapata mchumba anataka atutambulishe"
"Basi itakuwa ni vyema, tutaenda wote ili nami kwenu wakanitambue"
Waliongea kiasi kisha Sam akamrudisha Sabrina nyumbani kwake na kumuaga kwa kumbusu kwenye paji la uso.
Sabrina alipoingia ndani kwake alianza kwa kumuita Jeff,
"Jeff mwanangu leo nina habari njema sana"
Jeff alitoka chumbani kwake ili kumsikiliza Sabrina hiyo habari yake njema,
"Kuanzia leo, Sam ni baba yako mdogo"
Sam alijibu kwa unyonge, ila nae akamwambia kitu kingine Sabrina
"Hongera mamy, ila na mimi nina surprise yako leo"
"Surprise gani hiyo?"
"Leo nimekutengene zea juisi unayopenda kuliko zote duniani"
"Ipi hiyo?"
Jeff akaenda kwenye jokofu na kutoka na glasi yenye juisi na kumpa Sabrina,
"Jeff na wewe, nimeshiba sana leo"
"Jamani mamdogo, ndio hutaki kunywa wakati mi nimepoteza muda wangu wote hapo!"
"Haya lete ninywe kidogo"
Jeff alimkabidhi Sabrina ile juisi kwa furaha.
Sabrina naye aliipokea na kuinywa, muda huo huo Sabrina alijikuta akikaa kwenye kochi na kulala pale pale.
Jeff alimkabidhi Sabrina ile juisi kwa furaha.
Sabrina naye aliipokea na kuinywa, muda huo
huo Sabrina alijikuta akikaa kwenye kochi na
kulala pale pale.
Jeff akamuangalia Sabrina pale alipojilaza na kutabasamu.
Akainama ili kumbeba ila moyo wake ukasita kidogo na kuona kuwa anafanya makosa.
Aliulaumu sana moyo wake wa matamanio ila bado hakuweza kupingana na matamanio yake.
Alimnyanyua na kumbeba mpaka kwenye chumba chake na kumlaza kitandani.
Wakati yupo chumbani kwa Sabrina tena kabla hajafanya chochote alisikia mtu akibisha hodi, hofu ikamjaa Jeff ila aliamua kutumia akili ya haraka sana.
Alitoka chumbani kwa Sabrina na kufunga mlango kwa funguo kisha akaenda kufungua mlango, ila kabla hajafungua akakumbuka vitu vya Sabrina kama mkoba, simu na viatu vipo pale sebleni.
Akbmua kuvichukua na kwenda kuviweka chumbani kwake, kisha akaenda kufungua mlango.
Mgongaji alikuwa ni Sam, ambapo alipofunguliwa tu alipitiliza ndani moja kwa moja na kumuuliza Jeff,
"Mbona umekawia sana kunifungulia mlango?"
Huku Jeff akifikichafikicha macho akamjibu Sam,
"Nilikuwa nimelala bamdogo"
"Khee leo ndio umeamua kuniita hivyo?"
"Mamdogo kasema, kuanzia leo wewe nikuite bamdogo"
Sam akatabasamu na kumuulizia Sabrina,
"Eeh yuko wapi sasa mamako mdogo?"
"Katoka"
"Kaenda wapi?"
"Kasema anaenda kulala kwa bibi"
"Yani kaondoka usiku huu!! Mbona hatukukubaliana hivyo? Huyu Sabrina jamani mbona anataka kunipa matatizo!"
Sam akaondoka akiwa amechukia kabisa hata kumuaga Jeff hakutaka.
Jeff akafurahi na kufunga mlango baada ya kuona kuwa amemuweza Sam kwa uongo aliomwambia.
Akarudi chumbani kwa Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa bado hajitambui.
Sam alianza kumpapasa Sabrina na kumtoa nguo taratibu, kisha akajikuta amemuingilia kimwili Sabrina, na kuhamia kwenye ulimwengu mwingine kabisa hata akasahau kuwa Sabrina alikuwa hajitambui.
Alipomaliza alishangaa kuona damu kitandani na kumfanya ashtuke na kujiuliza,
"Mungu wangu, inamaana nimemuingilia akiwa kwenye siku zake?"
Jeff akajaribu kumkagua Sabrina na kujiuliza tena,
"Au mimi ndiye mwanaume wa kwanza kumuingilia kimwili?"
Akakaa chini na kushika tama huku akisema,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nimeutoa usichana wake, ndiomana nilikuwa napata shida kuingiza! Jamani mimi sijui kwanini nimemfanyia hivi mamy wangu, ila yote sababu nampenda sana na kumwambia nilikuwa siwezi. Sijui akishtuka itakuwaje"
Jeff alijikuta akinyong'onyea gafla kwani moyo wake ulimsuta kwa kile kitendo alichokifanya kwa Sabrina na kumfanya atoke mule chumbani kwa Sabrina huku moyo wa aibu na huruma ya kumuhurumia Sabrina ukimjaa.
Jeff akiwa chumbani kwake, akajaribu kutafuta usingizi ila hakupata usingizi ingawa alisharidhika na moyo wake kwa alichomfanyia Sabrina na kuhisi kuwa anastahili kutenda alichokitenda lakini bado kupata usingizi ilikuwa ni shida, na mwisho wa siku akaamua kurudi chumbani kwa Sabrina na kulala nae karibu yake ili ajue hali ya Sabrina itakavyoendelea.
Jeff alimuwekea Sabrina mkono kifuani na usingizi ukampitia pale pale.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment