Simulizi : Je Haya Ni Mapenzi!!
Sehemu Ya Pili (2)
Sam alipotoka nyumbani kwa Sabrina, moja kwa moja akaamua kwenda kwao na wakina Sabrina ili kumuulizia kama Sabrina amefika kwao.
Alipofika aligonga mlango kwa muda kidogo kisha mama wa Sabrina akatoka na kumfungulia.
"Mbona usiku sana mwanangu? Vipi kuna tatizo gani?"
"Samahani mama, nimekuja kuulizia kama Sabrina kashafika huku"
"Sabrina!! Mbona huku ameondoka muda mrefu tu na wala hajaja tena, alisema atakuja kesho"
Sam akapumua kidogo na kuhisi kama vile haelewi haelewi kwavile hata akipiga simu ya Sabrina ilikuwa inaita tu bila ya kupokelewa.
Sam hakuwa na la kufanya wala la kuzidi kumwambia mama wa Sabrina badala yake aliaga na kuondoka zake huku akipanga kwenda asubuhi na mapema kwa Sabrina ili ajue alipoenda na kwanini alienda usiku ule.
Sam aliondoka huku mawazo yakitawala kichwa chake na kumkosesha raha ya maisha kabisa.
Sam alirudi kwake na kulala ila usingizi ulimjia kwa shida sana, kulipopambazuka tu akafunga safari hadi nyumbani kwa Sabrina ili kumuangalia kama tayari amerajea.
Ila alipofika kwa Sabrina, aligonga sana mlango wa nyumba ya Sabrina bila ya kufunguliwa na kumfanya Sam ajiulize,
"Au na kile kitoto nacho kimetoka? Mbona hawafungui mlango hawa?"
Aliendelea kugonga ila hakufunguliwa na kumfanya akate tamaa, kisha akaenda kukaa kwenye gari lake na kumngoja Sabrina pale nje.
Ila alikaa muda mrefu sana bila ya kumuona Sabrina wala Jeff.
Sabrina alishtuka na kuhisi macho mazito sana hata hayakutaka kufunguka, kichwa nacho kilikuwa kizito sana kama mtu aliyelewa sana usiku wa jana yake na kushindwa hata kuinuka ila pembeni yake akamuona mtu amelala na kumfanya ashtuke kuwa mtu yule ni nani na anatafuta nini kwenye chumba chake.
Sabrina akamuangalia vizuri na kugundua kuwa yule ni Jeff, na alipouona mkono wa Jeff upo juu ya kifua chake aakashtuka sana na kuutoa kwa nguvu kisha akakaa na kumfanya naye Jeff ashtuke toka kwenye usingizi aliokuwa nao.
Sabrina alimuangalia Jeff kwa hasira sana na kumuuliza kwa ukali,
"Unafanya nini chumbani kwangu?"
Jeff naye alimuangalia Sabrina bila ya kumjibu chochote, kisha Sabrina akamwambia Jeff kwa ukali,
"Toka chumbani kwangu mwehu wewe"
Jeff akainuka na kutoka chumbani kwa Sabrina.
Sabrina akajaribu kuinuka pale kitandani, akajihisi maumivu kwenye sehemu zake za siri na kumfanya ajiangalie vizuri,
"Mungu wangu, huyu mtoto kanibaka nini?"
Sabrina akatoka chumbani kwake hadi sebleni na kumuita Jeff, ambapo Jeff naye akaenda alipoitwa
"Umenifanya nini wewe mtoto, umenifanya nini mimi?"
"Nisamehe mapenzi"
"Nini!! Mbwa mkubwa wewe nani mpenzi wako?"
Sabrina akamvamia Jeff na kuanza kumpiga hovyo hovyo ila kwavile kichwa cha Sabrina bado kiliku wa kizito, akashindwa kusimama vizuri wakati wa kumpiga Jeff na kujikuta akianguka chini.
Jeff naye akainama kumuinua,
"Niache huko shetani mkubwa wewe"
Sabrina alikuwa na hasira sana juu ya Jeff na kumfanya atamani kumrushia chochote kile kilichokuwa mbele yake, Jeff kuona vile akaamua kwenda chumbani kwake ili kuepusha shari.
Sabrina alijikongoja hadi chumbani kwake na kwenda kuoga huku moyo wake ukiwa na maumivu makubwa sana, alitamani hata achimbe shimo ajifukie.
Alirudi kitandani kwake, na kugundua kuwa hata shuka alilokuwa amelitandika jana lilikuwa limetolewa, alipolichukua na kuangalia akaiona ile alama ya damu na kumfanya aumie zaidi na machozi kumtoka,
"Hivi ni kweli au naota mie Sabrina jamani? Mungu jamani nisaidie hii iwe ni ndoto tu jamani, kwanini mimi Jeff kanifanyia hivi jamani? Kumpenda kote huku, kumjali kote hajakuona hadi kuchukua uamuzi wa kunibaka jamani mimi! Nitaificha wapi sura yangu hii kwa aibu. Ni nani atanielewa katika hii dunia? Mtoto niliyemlea mwenyewe, niliyempa chochote alichokitaka eti leo kanibaka jamani mmh!!"
Sabrina alikosa raha kabisa na amani ya moyo, akachukua nguo zake na kuvaa.
Akatafuta mkoba wake ila hakuuona kabisa,
"Hili hili shetani litakuwa linajua mkoba wangu ulipo, hata sijui lilinipa kitu gani jamani hadi kutojua kama ananiingilia kimwili"
Sabrina hakuwa na raha kabisa.
Wakati anawaza mule chumbani kwake akasikia mtu akibisha hodi kwenye ile nyumba yake.
Sabrina akainuka na kwenda kufungua mlango, akakutana na Jeff sebleni akiwa ameshika mkoba wa Sabrina na viatu vyake na kumfanya Sabrina achukie zaidi.
Sabrina akasogea pale alipo Jeff na kumwambia,
"Haya weka vitu vyangu na upotee kwenye nyumba yangu, sitaki kukuona Jeff sitaki kabisa."
Jeff alisimama pale kama mtu aliyeganda na kumfanya Sabrina hasira zimzidie, akaamua kuchukua vile vitu na kutaka kumvuta Jeff ili amtoe mule ndani,
"Usihangaike kunivuta acha tu nitoke mwenyewe"
"Ndio toka shetani wewe"
Sabrina akafungua mlango ili Jeff atoke na kusahau kabisa kama kuna mtu alikuwa akigonga mlango.
Akamkuta Sam akiwa pale mlangoni huku akimshangaa Sabrina alivyovimba kwa hasira, Jeff naye akatoka tena bila hata ya kumsalimia Sam na kuondoka.
"Tena usirudi hapa kwangu mbwa mkubwa wewe"
Sam akamshika mkono Sabrina ili kumtuliza kwa ile hasira aliyokuwa nayo.
Alipoingia naye ndani walikaa ili kuzungumza,
"Kwani nini tatizo Sabrina mpenzi? Leo umemfukuza kizindiko chako hata siamini"
Sabrina aliinama na kuanza kulia, tena alilia kwa uchungu sana.
Sam alijitahidi kumbembeleza ila ilishindikana kwavile Sabrina alikuwa analia tu na mwisho wa siku Sabrina akamuomba Sam aondoke kwani uwepo wake ndio unaomzidishia uchungu.
Sam hakupinga na kuondoka zake kisha Sabrina akabaki mwenyewe ndani.
Sabrina alikuwa akivuta matukio toka muda alipokuwa na Sam hadi aliporudi nyumbani kwake.
Akili yake ikamwambia kuwa kuna kitu Jeff alimuwekea kwenye ile juisi aliyokunywa kwani tangia hapo hakukumbuka kilichoendelea hadi palipokucha.
Kilichomuuma zaidi ni pale alipokumbuka kuwa Sam alimuomba kuwa wakalale nyumbani kwake ila yeye aligoma kwa kuhofia muda bado, akatamani masaa yarudi nyuma ili amkubalie Sam na kuepukana na ile adha iliyompata kwani ilikuwa ni aibu kubwa sana mbele yake na mbele ya moyo wake.
"Kwanini mimi jamani, kwanini mimi! Bora hata ningelala na Sam kuliko Jeff jamani, aibu gani hii?"
Sabrina alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa kwani muda wote alikuwa akiongea mwenyewe tu.
Sam alipotoka kwa Sabrina, moja kwa moja alienda kwa mama yake na Sabrina ili kumpa habari ili aweze kwenda kumbembeleza mtoto wake kwani alihisi itakuwa vyema kama Sabrina akimueleza tatizo lake mama yake.
Joy alishangaa sana baada ya kupewa taarifa ya mtoto wake kuwa analia tu.
"Amepatwa na nini Sabrina mwanangu jamani!"
"Hata mimi mwenyewe sijui ndiomana nimekuita wewe, jana nilimrudisha vizuri tu na tuliongea mengi mazuri, hata mi nashangaa kuwa leo imekuwaje"
"Jamani, na mimi hapa nilipanga nae vizuri sana, nikakubaliana nae kuwa leo aje amuone wifi yake. Nimeshangaa hajafika mpaka muda huu kumbe mwanangu kapatwa na mengine huko"
Sam akamsubiri mama Sabrina ajiandae kisha akaondoka naye na kumpeleka hadi nyumbani kwa Sabrina.
Walipofika, Sabrina aliwafungulia mlango.
Ilibidi Sam aondoke na kumuacha Sabrina na mama yake ili wapate kuzungumza.
Joy akamkumbatia mwanae na kumuuliza kwa upole kabisa,
"Kwanza umekula mwanangu?"
Sabrina akatikisa kichwa kuashiria kuwa bado hajala.
"Jamani mwanangu mpaka saa kumi hii hujala?"
"Sijisikii kula mama, sijisikii kabisa"
"Hata chai jamani mwanangu?"
Sabrina alitikisa kichwa kuashiria kuwa hata hiyo chai haitaki.
Ikabidi Joy atumie uzoefu wa kimama kumbembeleza mtoto wake, na mwisho wa siku akaenda kumkorogea chai na kumpelekea anywe.
"Kunywa kikombe hiki kimoja tu ili tuzungumze vizuri mwanangu"
Sabrina alichukua kile kikombe na kunywa kidogo kisha akatulia kwanza.
"Mwanangu, niambie, nini tatizo? Tafadhari usinifiche mwanangu, kumbuka mimi ni mama yako wa pekee"
"Aibu kusema mama"
"Usinionee aibu mimi mwanangu, mimi ndio msiri wako. Niambie mimi tafadhari mwanangu"
Sabrina akafikiria kidogo, akawaza jinsi mama yake atakavyomuona kuwa ni mpumbavu kwa kulala na mtoto mdogo kama Jeff, mtoto ambaye amempita takribani miaka kumi, na licha ya hivyo ni mtoto ambaye amelea kama mtoto wake, leo aseme amembaka ni nani atakayemuelewa? Sabrina akajikuta akigubikwa na aibu kubwa sana na kushindwa kumwambia mama yake ukweli.
Ila Joy aliendelea kumbembeleza mwanae ili amwambie ukweli wa mambo yote.
"Mama, nikikwambia hutanifikiria vibaya kweli?"
"Usijali hilo mwanangu, ni bora uniambie mimi mama yako kuliko mtu mwingine yoyote"
Sabrina akapumua kidogo ili kujaribu kumwambia mama yake,
"Ilikuwa hivi mama......."
Kabla hajaendelea, simu ya Joy ikaita na kumfanya aitoe.
"Halafu ni bosi wako Sam anapiga sijui kuna nini!"
Joy akapokea ile simu na kuongea kwa mshangao na kumfanya Sabrina atamani kujua jambo ambalo Sam alikuwa akimwambia mama yake, simu ilipokatika tu Joy akapumua kwa nguvu sana halafu Sabrina naye akamuuliza,
"Kwani kuna nini mama?"
"Eti Jeff kapata ajali"
"Jeff!! Mungu wangu, Jeff kweli mama?"
"Ndio, Sam kasema Jeff kapata ajali na hali yake ni mbaya sana"
Sabrina alijikuta akipatwa na mshtuko wa gafla na kuanguka.
Sabrina alijikuta akipatwa na mshtuko wa gafla
na kuanguka.
Joy akaanza kumpa huduma ya kwanza binti yake kwani alianguka vibaya, alitoka pale kwenye kochi hadi kwenye sakafu na kutulia tuli.
Joy akampepea pale binti yake na kummwagia maji mpaka pale Sabrina alipozinduka na kumuuliza tena
"Kwani kuna nini mama?"
"Hakuna kitu mwanangu"
Sabrina akatulia kidogo na kuwa kama anavuta kumbukumbu pale.
Joy akaamua kumkatisha kwanza ili asiwaze sana waliyozungumza.
"Sabrina mwanangu, unaonaje tukaenda nyumbani!"
"Mmh mama, na wewe mara moja moja ukae hapa kwangu"
"Hilo sio tatizo, ila twende nyumbani ukamuone wifi yako"
"Basi sawa, ngoja nikachukue mkoba wangu chumbani"
Sabrina akainuka na kwenda chumbani, alipoingia akatazama mandhari ya chumba chake na kuliona lile shuka pembeni na kukumbuka kila kitu kumuhusu Jeff kisha moyo nao kuanza kumuuma upya kabisa, tena ukamuuma zaidi baada ya kukumbuka kuwa ameambiwa kwamba Jeff kapata ajali, kisha akatoka kule chumbani kwake na kurudi tena sebleni, mama yake akamwambia
"Twende basi Sabrina"
"Hapana mama, niache nimuombee Jeff apone"
Joy akamuangalia mwanae na kujua kuwa kumbukumbu zimemrudia, kisha akamwambia tena
"Twende basi huko hospitali ukamuone"
"Usijali mama, nimekwambia niache kwanza nimuombee sababu najua nini chanzo"
"Mmh makubwa haya, leo hadi mwanangu Sabrina naye anajua kuombea!"
Basi Joy akaona ni vyema yeye awasiliane na huyo Sam aliyewapa taarifa ili aende kumuona Jeff na kumfariji Sakina, kisha akamwambia mwanae
"Basi badae kidogo nitakuja kukupitia tena kidogo ili angalau Sakina akuone na wewe kidogo"
Kisha akamuaga na kuondoka, kwahiyo sasa mawazo yote yalikuwa juu ya ajali aliyoipata Jeff na si vinginevyo.
Sabrina alibaki pale ndani kwake mwenyewe akitafakari, akayakumbuka maisha yake ya zamani.
Maisha yale yaliyomfanya kuwa na kila mwanaume aliyemtamkia nakupenda, maisha yale yaliyomfanya aende rumande sababu ya mapenzi, yaliyofanya wanaume wale wale waliosema wanampenda na kuanza kumchukia, ila kati ya wote alibaki mtoto mdogo Jeff aliyemuombea mema muda wote, mtoto ambaye hakupenda kumuona Sabrina akiangamia, mtoto ambaye alimtahadharisha Sabrina kwenye kila aina ya majanga kwani aliweza hata kumng'ang'ania Sabrina alipokuwa shuleni na kumfanya achelewe ndege aliyotakiwa kupanda na kuponyeka na ajali iliyopangwa dhidi yake.
Ila leo mtoto huyo huyo kapata ajali sababu ya kitu kimoja tu, Sabrina akawaza na kusema,
"Tamaa na balehe ndio vimemchochea Jeff kufanya hivi na kumfanya aingie kwenye mlolongo wa matatizo yangu"
Sabrina akakumbuka ile kamba aliyofungwa kipindi kile kwenye kiuno chake, akakumbuka masharti aliyopewa mara ya mwisho kuwa haruhusiwi kuingiliwa kimwili na mwanaume yeyote yule. Na kama ikitokea kaingiliwa kimwili basi huyo mwanaume atakufa.
Sabrina aliinu a mikono yake juu na kushika kichwa chake huku akihofia maisha ya Jeff.
Muda huu Sabrina aliamua kupiga magoti chini na kuanza kumuombea Jeff.
Joy alimkuta Sakina akiwa pale nje ya hospitali huku machozi yakimtoka tu sababu ya hali mbaya aliyokuwa nayo mtoto wake.
Sakina akamkumbatia Joy kwa uchungu sana huku akilia,
"Sijui mwanangu atapona, mtoto mwenyewe huyo huyo mmoja kama jicho jamani. Mwanangu Jeff, uwiii sijui mimi jamani!"
Joy akajitahidi kumbembeleza Sakina kuwa wazidi kumuomba Mungu ili Jeff aweze kupona.
Sam ndiye aliyekuwa akishughulika na kila kitu kuhusu Jeff, ndiye aliyekuwa akihakikisha kuwa Jeff anapatiwa matibabu sahihi ili arudi katika hali yake ya kawaida.
Ingawa Sam naye hakuelewa mlolongo wa haya matukio kabisa.
Akakumbuka usiku alipokwenda kwa Sabrina na kujibiwa na Jeff kuwa Sabrina ametoka, akakumbuka asubuhi alipoenda tena na kugonga bila kufunguliwa, akakumbuka alipoenda tena mchana na kugonga ila akasikia majibishano kati ya Jeff na Sabrina na kisha pale Sabrina alipomfukuza Jeff.
Hakuelewa kwanini Jeff alifukuzwa, na pia hakutambua kuwa imekuwaje hadi Jeff akapata ajali ingawa yeye alikuwa wa kwanza kumshuhudia Jeff akivuja damu pale chini baada ya ajali.
"Hata sielewi kwakweli, sielewi kabisa kabisa kuwa kwanini inakuwa hivi"
Alitulia na kwenda kuwapa majibu ya daktari ndugu wa Jeff waliokuwepo pale hospitali.
Sam alikaa nao pale na kuzungumza nao kuhusu Jeff,
"Vipi lakini atapona?"
"Tumuombe Mungu jamani ili ainusuru hii hali"
Sakina alihisi kuchanganyikiwa muda wote na kujiona kama vile ni mtu asiyejielewa.
Muda kidogo, daktari naye akawafata na kufanya wote washtuke huku kila mmoja akifikiria yake kuhusu Jeff.
Daktari akawauliza,
"Jamani Samahanini, kuna yeyote anayeitwa Sabrina hapo kati yenu?"
Wakatazamani wote, kisha Sakina akajibu,
"Sabrina bado hajafika, kwani imekuwaje jamani! Sabrina wa nini?"
"Basi mwambieni huyo Sabrina aje, kwani tangu mwanzo huyu kijana amekuwa akimtaja sana, sasa kama madaktari tumeshauriana kuwa itakuwa vyema kama huyo Sabrina akija karibu."
Ikabidi Sam aamue kwenda kumfata Sabrina nyumbani kwake.
Sam alienda kwa Sabrina na kugonga, ila alipojaribu kufungua mlango aliukuta upo wazi na Sabrina akiwa bado amepiga magoti huku akiendelea na maombi yake.
Sam alikaa kwenye kochi huku akimsubiri Sabrina amalize maombi yake.
Baada ya muda kidogo, Sabrina akainuka na kukaa kwenye kochi kisha Sam akamueleza Sabrina yaliyojiri naye akakubali kwenda hospitali kumuona huyo Jeff ambaye muda wote alikuwa akimtaja Sabrina tu.
Sabrina alipofika hospitali, moja kwa moja Jeff akamuongoza kwenye chumba cha daktari
"Tuliona ni vyema tumchome sindano ya usingizi kwahiyo sahivi yupo kwenye usingizi wa sindano"
"Basi naomba hata nikamchungulie tu"
Daktari hakukataa zaidi ya kwenda na Sabrina kwenye chumba walichomlaza Jeff.
Sabrina alimwangalia Jeff na kumuhurumia sana hata akasahau yote yale ambayo Jeff alimtendea.
Sabrina alipotoka kwenye kile chumba, akaenda kwa ndugu wa Jeff kuwasalimia na hapo akakutana na Sakina ambaye alikuwa na majonzi tu na kumkumbatia Sabrina.
"Sabrina mtoto wetu jamani, sijui kama atapona"
"Usijali dada, Jeff atapona tu."
Sabrina akajitahidi kumpa moyo Sakina pale kwavile alionekana kukata tamaa kabisa.
Kisha Sakina akamuuliza Sabrina,
"Kwani alikuaga anaenda wapi leo?"
Sabrina akakaa kimya kwa muda na kumwambia Sakina,
"Tuachane na hizo khabari kwanza za kuaga au kutokuaga. Tuangalie kwanza hali ya Jeff"
"Nimekuuliza hivyo nikiwa na maana kabisa Sabrina, sababu nilimnenea mwanangu vibaya"
"Ulimnenea nini?"
"Jana usiku nilimnenea mwanangu hivi, akienda kwa huyo sugar mamy wake basi apatwe na majanga yeye pamoja na huyo mmama, sasa leo napewa taarifa kuwa mwanangu amepatwa na ajali kwakweli nimechanganyikiwa sana hata najuta kunena maneno ya ajabu kiasi kile. Ndiomana nikakuuliza kuwa alikuaga anaenda wapi? Namuomba Mola amnusuru mwanangu jamani"
"Pole sana dada, ila siku nyingine usimnenee mambo hayo mtoto wako, si unaona tabu tunayoipata? Maneno yako huwezi jua kuwa yatawaponza wangapi."
"Nimekoma mdogo wangu, yani sirudii tena mimi jamani. Mwanangu apone tu jamani, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo kama jicho."
Sabrina alijitahidi pale kumfariji Sakina na kumpa moyo kuwa Jeff atapona tu.
Usiku nao uliwakutia pale pale hospitali, ila kwavile Jeff alikuwa bado hajazinduka ikabidi warudi nyumbani kupumzika ili waende kesho yake.
Ila Sakina bado aliendelea kulalamika na kujiona kuwa yeye ndiye chanzo cha mambo yote yale.
"Bora ningemnenea yule jimama tu kuliko kumnenea na mwanangu"
"Acha maneno hayo dada, utapata laana kwa Mungu."
"Roho inaniuma Sabrina yani inaniuma sana, hata sijui nifanyeje!"
"Muombe Mungu akupe subira na uvumilivu na tuendelee kumuombea Jeff apone"
Basi sam alimpeleka Sakina hadi nyumbani kwake na kumuacha hapo kisha akampeleka Sabrina nyumbani kwake.
"Utaweza kulala mwenyewe nyumba yote mpenzi?"
"Usijali naweza"
"Nilitaka nibaki hapa nikupe kampani ya kulala pamoja"
"Hata usijali Sam"
Basi Sam akamuaga Sabrina na kuondoka, kisha Sabrina akaanza kufanya usafi wa nyumba yake usiku ule ule kwa kuyaloweka yale mashuka na usafi mwingine, alipomaliza ndio akalala.
Asubuhi na mapema, Sam akampitia Sabrina ili waende kazini ila Sabrina akamuomba Sam wapite kwanza hospitali.
Sam hakupinga na wakaenda hospitali kwanza.
Walipofika, walimkuta Jeff amefumbua macho na anaweza kuongea kwa mbali kidogo.
"Pole sana Jeff utapona"
"Asante mamdogo, ila nakuomba kitu kimoja"
Sabrina akashtuka na kumuuliza Jeff kwa sauti ya chini.
"Kitu gani?"
"Nakuomba usitembee peke yako"
Sam akadakia,
"Hilo halina shaka Jeff, yupo na mimi. Kwahiyo usijali"
Jeff akatikisa kichwa tu, kisha wakamuaga na kwenda kazini.
Sabrina alijifikiria sana alipokuwa kazini kuwa kwanini Jeff amemwambia kuwa asitembee peke yake,
"Au anahofia nitabakwa tena kama alivyonibaka yeye!"
Hapo akasita kidogo kwani moyo ulimuuma sana na kujiona kuwa atakuwa mjinga kuendelea kusikiliza maneno ya Jeff,
"Itabidi badae niende mwenyewe nikamuulize kuwa ana maana gani kuniambia mimi vile. Asiniletee ujinga wake kabisa."
Mara Sam akapita karibu na meza ya Sabrina na kumuona akinung'unika peke yake, kisha akamfata na kumuuliza kama kuna tatizo,
"Hakuna tatizo kwakweli"
"Basi mimi natoka kidogo, kuna watu wa kodo naenda kuzungumza nao ila nitawahi kurudi"
"Sawa boss"
Sam akatabasamu na kumuangalia Sabrina kisha akaondoka zake.
Sabrina aliendelea kufanya kazi yake ila mawazo yote ni kutaka kujua kuwa Jeff alikuwa na maana gani, hivyo akaona ni vyema aombe ruhusa hata ya saa moja akamuangalie Jeff hospitali na kujua kuwa alikuwa na maana gani.
Sakina alikuwa hospitali na mtoto wake, na alifurahi baada ya kuona hali ya mwanae ikiendelea vizuri leo.
Alizungumza na mwanae huku akimpa pole na kujutia maneno yake aliyotamka hapo kabla.
"Nisamehe sana mwanangu"
"Usijali mama"
"Ila hilo lijanamke hilo limama lililoitawala akili yako mwanangu, nataka mabaya yako yote yamfike yeye popote pale alipo"
"Jamani mama usiseme hivyo, au unataka mimi nife?"
"Hapana mwanangu, siwezi kutaka wewe ufe"
"Basi usiseme tena hayo maneno yako, utawaingiza hatiani watu wasio na hatia mama. Mimi sina mwanamke yeyote unayemsema wewe, mwisho wa siku hata watu wasiohusika nao utawaingiza humo. Mimi nipo kitandani hapa naumwa, wewe badala ya kunihurumia unaniambia maneno ya ajabu tu. Bora uende kama umechoka kuniona"
Sakina akajua wazi kuwa mtoto wake amechukizwa na yale maneno aliyokuwa akiyazungumza na kumlazimu kubadilisha ile mada yake ila Jeff alikuwa tayari ameshachukizwa na kumfanya asimsikilize tena mama yake.
"Jamani Jeff nisamehe mwanangu"
"Futa kwanza ile kauli yako"
"Naifuta mwanangu, huyo mwanamke asipatwe na baya lolote lile sababu ndio kipenzi cha mwanangu. Vipi sasa umenisamehe?"
Jeff akatikisa kichwa tu kama ishara ya kukubali ule msamaha.
Sabrina alitoka pale ofisini na kuianza safari ya kwenda hospitali ili akazungumze na Jeff.
Alipokuwa anatoka ofisini akakutana na Fredy, ambaye alimshtua na kupanda kwenye ile piki piki ya Fredy.
Muda huo huo Sam nae aliwasili pale ofisini na kumuona Sabrina akiishia na ile pikipiki.
Sam akachukia sana, kisha akaenda kuweka mafaili yake ofisini na kwenda kupanda gari lake ili aweze kufatilia Sabrina anapoenda.
Wakati Sam yupo njiani, akakuta ku na foleni ya gafla.
Ikabidi ashuke na kwenda kuulizia,
"Kwani kuna nini hapo mbele?"
"Kuna ajali, bodaboda mbili zimegongana na abiria mmoja mwanamke kafa pale pale"
Sam alihisi kuchanganyikiwa kabisa ukizingatia alimuona Sabrina akiondoka kwa bodaboda.
abiria mmoja mwanamke kafa pale pale"
Sam alihisi kuchanganyikiwa kabisa ukizingatia
alimuona Sabrina akiondoka kwa bodaboda.
Sam akaamua kusogea kabisa kwenye eneo lile la tukio ili aweze kushuhudia kwa macho yake mwenyewe bila ya kusimuliwa.
Akawapita watu wengi waliozingira eneo lile, akaona kuna mwanamke amefunikwa khanga huku damu nyingi zikiwa zimetapakaa eneo lile.
Akaona pikipiki mbili zikiwa pembeni, pikipiki moja wapo ilikuwa haitamaniki kabisa hata kuitazama na ilikuwa ni pikipiki ile ile aliyomuona Sabrina amepanda.
Muda huu Sam alihisi kurukwa na akili kabisa na kusogelea pale alipolala yule marehemu kwa lengo la kumfunua ili ahakikishe kuwa ni nani.
Ila askari nao, na wale wa gari la kubeba wagonjwa walikuwa wamewasili eneo lile na kumkataza Sam kumfunua yule mwanamke, kitendo ambacho kilizidi kumpa uchizi Sam.
"Tafadharini jamani, naomba nimuone kama ni yeye"
"Ameumia vibaya sana, hatuwezi kuruhusu afunuliwe"
Ila Sam aling'ang'aniza na kuwafanya wamfunulie yule mtu ili amuone.
Ila kabla hajamuangalia, kuna mtu alikuja na kumshika bega Sam na kumfanya ashtuke sana.
Alipogeuka alikuwa ni Sabrina ambaye alikuwa anatetemeka sana.
Sam hakujielewa kabisa, wale manesi walipoona kuwa mtu mwenyewe haeleweki wakaamua kumpakiza yule marehemu kwenye gari yao na kuondoka naye.
Sam aliganda kama barafu huku akihisi ubaridi ukipita kwenye mwili wake, akamshika mabega Sabrina na kumuuliza,
"Ni wewe kweli Sabrina?"
Sabrina akatikisa kichwa kama ishara ya kuitikia kuwa ni yeye.
Sam akaishika sura ya Sabrina, akamuangalia kwa makini na kumkumbatia kwa nguvu.
Sabrina akamwambia Sam,
"Ila mwenzangu ameumia"
"Nani huyo?"
"Fredy aliyekuwa amenibeba kwenye pikipiki"
"Yuko wapi?"
Sabrina akamshika Sam mkono na kumpeleka kwenye mtaro wa pembezoni mwa barabara, ambapo Sam akasaidiana na baadhi ya watu kumtoa Fredy kwenye mtaro na kumpakiza kwenye gari ili kumuwaisha hospitali.
Sam ingawa alikuwa na Sabrina pemb eni ila bado alikuwa hajiamini kabisa, na Sabrina nae muda wote alikuwa akitetemeka, Sam alimuangalia tena Sabrina na kumuuliza,
"Sabrina, ni wewe kweli?"
"Ndio ni mimi Sam, yani hata mimi mwenyewe sijiamini kama kweli nimepona. Siamini kabisa, mwili wote umejawa na uoga hapa yani siamini"
"Kwani ilikuwaje Sabrina?"
Sabrina hata hakuelewa ni wapi aanzie kuelezea na wapi aishie,
"Niambie tu Sabrina tafadhari"
"Yani ilikuwa hivi, nilipotoka pale ofisini nikakutana na Fredy na kumuomba anipeleke kumuona Jeff. Na kweli tumeondoka vizuri tu hapo, kufika mbele kidogo Fredy akasimamisha ile pikipiki yake kisha akaniambia kuwa nishuke, nikamuuliza kwanini akasema nishuke tu atanipa sababu. Basi mimi nikashuka, nilipomaliza tu kushuka. Uuh Mungu wangu hata ilipotokea ile pikipiki nyingine sijui, kwani ilikuja na kugonga ile pikipiki ya Fredy kisha nikamuona Fredy akiangukia mtaroni halafu ile pikipiki yake iliinu ka juu kabisa na kuja kuponda mtu wa nyuma ya ile pikipiki ambaye alikuwa ni mwanamke, yani kilikuwa ni kitendo cha sekunde tu. Masikini yule dada alipiga yowe moja tu na kuwa kimya pale pale. Kwakweli nguvu ziliniisha na kujiona kama vile nipo kwenye ndoto. Hadi muda huu sijielewi, yani sielewi kabisa sielewi"
Sam akamsogeza Sabrina karibu yake na kumkumbatia kwaajili ya kumtoa uoga alionao,
"Pole sana Sabrina, ila tumshukuru Mungu kwa kukuponya jamani yani hadi mimi mwenyewe siamini mpaka muda huu jamani."
Walitulia kwa muda wakingoja majibu ya daktari kuhusiana na hali ya Fredy.
Huku Sam akijiuliza kuwa inamaana Fredy alijua kuwa kuna ajali itatokea? Na kama alijua mbona yeye hakujiepusha? Alikosa jibu ila alitambua wazi kuwa majibu yote anayo muhusika ambaye ni Fredy.
Hali ya Fredy iliendelea vizuri, hata muda ambao Sam na Sabrina wanaondoka pale hospitali, Fredy alikuwa akiendelea vizuri.
Sam alimru disha Sabrina nyumbani kwao kwani akaona kwamba itakuwa salama zaidi kumuepusha na mawazo ya siku hiyo.
Kisha Sam akaondoka zake.
Sabrina akamsimulia mama yake kila kitu ambacho kilimtokea kwa siku hiyo na kumfanya mama yake naye ashangae sana.
"Ndiomana hukuja tena hospitali kumuona Jeff"
"Ndio majanga hayo mama ndiomana nikashindwa"
"Basi kuna kitu kati yako wewe na Jeff kimewaunganisha"
Sabrina akashtuka sana na kumuuliza mama yake kwa mshangao ulioambatana na uoga.
"Kwanini mama?"
"Unajua leo wakati tupo pale hospitali, kuna muda Jeff alishtuka sana na kupiga kelele akisema, 'Sabrina no usipande' kiukweli hakuna aliyemuelewa kabisa. Mara akasema, 'Eeh Mungu mnusuru Sabrina' mi nikajiuliza kuwa anamuongelea Sabrina yupi hata sikupata jibu ila tangia hapo Jeff hakutaka tena kuongea na mtu yeyote yule halafu akalala. Mi nikajaribu kumpigia simu Sam na kumuuliza mnaendeleaje sababu simu yako haikupa tikana ila akanijibu kuwa mnaendelea vizuri kumbe hakutaka kuniambia ukweli wa hayo mambo"
Sabrina akapumua kiasi na kumuangalia mama yake huku akijaribu kumsoma kama kuna chochote amegundua baina yake na Jeff, ila alijua wazi kuwa mama yake hajagundua chochote kile.
Kisha Joy akaendelea kumwambia mwanae,
"Nashukuru Mungu amekulinda mwanangu, nadhani maombi ya Jeff yamesaidia kwakweli"
"Ndio mama"
Kisha wakaenda kulala ili waweze kuwahi kesho kwenda kuendelea na mambo mengine.
Kulipokucha, kama kawaida Sam alimfata Sabrina kwao na safari ya kwanza ilikuwa kwenda kumuona Jeff na kisha kumuona Fredy.
Jeff leo alikuwa vizuri na aliweza hata kukaa na alifurahi sana kumuona Sabrina.
"Siamini kama nakuona tena mamy"
"Usijali nilipona"
Sabrina hakutaka Jeff azungumze zaidi kwa kuhofia kuwa atasema mengi na kumuharibia kwa Sam.
Kwahiyo wakaongea nae kidogo tu kisha wakamuaga na kuondoka.
Walipofika kwa Fredy hali yake ilikuwa ni nzuri pia.
"Leo wanaweza kuniruhusu nirudi nyumbani"
"Pole sana Fredy"
"Asante Sabrina"
"Najua umeumia kwa kuniokoa mimi Fredy"
"Usijali hilo Sabrina, cha muhimu ni kuwa hata mimi nimepona."
Wakaongea pale mawili matatu kisha Sabrina na Sam wakarudi ofisini.
Walipokuwa ofisini, Sam alimuita Sabrina kwenye ofisi yake na kumwambia,
"Kuanzia leo Sabrina, huruhusiwi kutoka kwenda sehemu yoyote bila ruhusa yangu. Ukitoka bila ruhusa usije ukanilaumu kwa nitakachokufanyia. Na hilo sio ombi bali ni amri Sabrina. Nimemaliza, nenda ukaendelee na kazi"
Sabrina alirudi kwenye ofisi yake akiwa kanyong'onyea huku akijilaumu kuwa yote ameyasababisha yeye mwenyewe maana kila akionywa huwa anajifanya asikii.
Zikapita wiki mbili, Jeff alikuwa kapona kabisa na alirudi nyumbani kwao. Hata Fredy nae alikuwa ni mzima kabisa hata aliweza yeye mwenyewe kwenda kwa kina Sabrina,
"Unajua Fredy, mi hadi leo huwa nakosa majibu ya ile ajali. Hivi ulijuaje kama kutatokea ajali hadi kuniambia kuwa nishuke.?"
"Kiukweli hata sikujua kama itatokea ajali, ila wakati nakuendesha gafla moyo wangu ukawa mzito, nikahisi kuna kitu kibaya kinataka kutokea ila sikujua kama ni ajali. Ndiomana nikakwambia ushuke Sabrina"
"Mmh basi ni khatari"
"Yote sababu nakupenda Sabrina ila wewe hujui tu, laiti kama ungeingia kwenye moyo wangu basi ungegundua kuwa mimi ndio mwanaume wa pekee unayepaswa kuwa naye. Jaribu wewe mwenyewe kuangalia, ni mambo mangapi mabaya yananipata mimi kwaajili yako? Kumbuka nishawahi kuwa kipofu mimi kwaajili yako Sabrina. Hivi nifanye kitu gani ili uelewe upendo uliopo ndani yangu juu yako Sabrina? Niambie tafadhari."
Sabrina alikuwa kimya tu akimsikiliza Fredy ila hata yeye hakujua la kumwambia kwavile alishakubaliana na Sam tayari.
"Ni kweli unanipenda Fredy, hata moyo wangu unatambua hilo. Ila siwezi kuwa nawe sababu nina mwingine tayari"
Fredy aliumia ila akamjibu Sabrina,
"Hakuna shaka, nitasubiri hadi siku utakayokubali kuwa wangu"
Sabrina aliona ni vyema kubadilisha mada ili kuweza kumkatisha Fredy na mwisho wa siku Fredy akaaga na kuondoka.
Sam alikaa na Sabrina na kuamua kupanga naye maswala muhimu,
"Sabrina, nataka kukuoa"
"Mmh Sam, ya kweli hayo?"
"Ndio ni kweli, kwanini nikuongopee mpenzi? Sitaki kukuharibia maisha mpenzi wangu, ndiomana nahitaji tufunge ndoa ili mambo mengine yote tufanye tukiwa ndani ya ndoa"
Sabrina akafurahi sana na kujilaumu kwa kuchelewa kumkubali mwanaume wa muhimu kama Sam, mwanaume anayejua thamani ya mwanamke, mwanaume ambaye haitaji ngono tu bali mapenzi ya dhati ndiomana yuko tayari kumuoa kwanza kabla ya mambo yote.
Moyo wa Sabrina ukamwambia kuwa huyu ndiye mwanaume ambaye amekuwa akimuhitaji siku zote za maisha yake, huyu ndiye mwanaume sahihi kwake.
Sabrina akainuka na kumkumbatia Sam kwa furaha ya hali ya juu kisha akamwambia,
"Nipo tayari kuolewa na wewe Sam, nakupenda kwakweli"
Sam naye akafurahi baada ya kuona kuwa Sabrina ameridhia ombi lake.
Sam alimzungusha Sabrina kwa ndugu zake wote ili wamtambue, na wote hawakuwa na pingamizi lolote kwani walimuona Sabrina ni mtu muelewa na mzuri pia.
Miezi miwili kupita hali ya Sabrina ilikuwa haieleweki kwani mara nyingi alikuwa mgonjwa na mara nyingine alijikuta akiwachukia watu bila sababu za msingi na kufanya wengi wamshangao na wao kuanza kumchukia pia.
Ila yeye aliona kuwa ile hali ni ya kawaida tu na wala haikumshtua na kitu chochote kile.
Siku moja walisafiri na kwenda Arusha kumsalimia mama wa Sam, ambapo alimuita mwanae pembeni na kumuuliza,
"Vipi mwanangu tayari nini?"
"Tayari nini mama?"
"Si huyo binti, tayari namaanisha ana mimba?"
Sam akamcheka mama yake,
"Ndivyo alivyo bhana mama, hana mimba wala nini"
"Mmh mwanangu hadi mimi mama yako unanificha?"
"Sikufichi mama, ila huo ndio ukweli"
"Haya, ila ile kitu huwa inaenda mbele hairudi nyuma basi tutaona tu"
Sam akataniana pale na mama yake na kumaliza maongezi yao kisha wakarudi alipo Sabrina na kuendelea na mazungumzo mengine ambapo mama wa Sam alimkaribisha sana Sabrina kwenye ukoo wao.
Sabrina na Sam wakafurahi sana kuwa pale Arusha,
"Yani huku Arusha pananikumbusha mbali sana Sam"
"Kwanini?"
"Nakumbuka ile siku ya kwanza mimi nafahamiana na wewe, mmh isingekuwa mimi kuja Arusha basi tusingefahamiana jamani"
"Sabrina, kila kitu hupangwa na Mungu kwahiyo labda tungekutana sehemu nyingine"
"Ila saivi naelewa ule usemi usemao kuwa kila jambo hutokea kwasababu"
Sabrina aliyafurahia sana mapenzi yake na Sam huku akingojea ndoa yake kwa hamu kubwa sana.
Muda wa kulala ulipofika, Sam alimpeleka Sabrina kwenye chumba cha kulala kisha na yeye akalala kwenye chumba kingine.
Kulipokucha wakafunga safari na kurudi jijini ili kuendelea na taratibu zao za kazi.
Walipokaribia mjini, Sabrina akamuona Jeff akikatisha njiani na kumwambia Sam,
"Si Jeff yule? Hebu simamisha"
Sam akasimamisha, kisha Sabrina akashuka na kumuita Jeff ambapo Jeff aliitika na kusogea alipo Sabrina,
"Unaenda wapi?"
"Kuna mdada fulani hivi mama kanituma nikamchukulie mzigo wake"
Sabrina alijikuta akimuangalia Jeff kwa hasira iliyotawaliwa na chuki, kisha akamwambia.
"Panda kwenye gari tukupeleke"
"Hapana, nimeshafika ni hapo tu"
"Unanisikiliza au hunisikilizi?"
"Nakusikiliza"
"Haya panda kwenye gari"
Ikabidi Jeff apande kwenye lile gari kisha Sabrina nae akapanda kwenye gari na kumwambia Sam,
"Haya sasa tuendelee na safari yetu"
Sam akawasha gari na kuendelea, Jeff akamuuliza Sabrina
"Inakuwaje na mimi safari yangu?"
"Huendi popote, nakurudisha kwenu. Kwa huyo mdada ataenda mwenyewe mama yako"
"Jamani mamdogo!"
"Tena usinilalamikie ng'ombe wewe"
Hata Sam akamshangaa Sabrina kuwa kwanini amekuwa na hasira kiasi kile.
Walimpeleka Jeff hadi kwao na kumshusha kisha Sam akampeleka Sabrina nyumbani kwake ili atulize akili.
Kesho yake, Sam kama kawaida alimfata Sabrina na kwenda naye kazini ila Sabrina alikuwa akijisikia vibaya na muda wote alikuwa akilalamika tu.
Walipokuwa ofisini, Sabrina akaona vyema kwenda kumuomba ruhusa Sam ili akaangalie afya yake.
"Najihisi vibaya kwakweli, nadhani nina malaria au typhodi"
"Basi ukapime ila uniletee majibu na mimi hapa"
Sabrina akakubaliana na Sam kisha Sam akampa Sabrina dereva wake ili ampeleke hospitali.
Alipofika hospitali, alipimwa vipimo vyote kisha daktari akamletea majibu.
"Hongera sana dada"
"Hongera ya nini?"
"Una ujauzito"
"Mungu wangu"
Sabrina alijishika kichwa na kuanguka chini.
Alipofika hospitali, alipimwa vipimo vyote kisha
daktari akamletea majibu.
"Hongera sana dada"
"Hongera ya nini?"
"Una ujauzito"
"Mungu wangu"
Sabrina alijishika kichwa na kuanguka chini.
Daktari akaamua kumuinua Sabrina na kuanza kumpa huduma ya kwanza, na moja kwa moja akagundua kwamba hii mimba itakuwa ni zile za bila ya kutarajia.
Akaendelea kumpa huduma Sabrina huku akiwaza jinsi ya kumsaidia.
Akili ya Sabrina ilipokaa sawa kidogo, akakaa pale ofisini na yule daktari ila hawakuweza kuongea chochote hivyobasi yule daktari akamwambia Sabrina kuwa aende nyumbani akapumzuke kwanza,
"Ila hakikisha kesho unakuja ili nikupe ushauri mzuri na unaokufaa"
Sabrina akaitikia na kutoka kwenye chumba cha daktari na kuelekea mahali lilipo gari lile la Sam lililompeleka pale hospitali.
Sabrina alipanda kwenye lile gari na kumuamuru yule dereva kuwa ampeleke nyumbani kwake,
"Lakini madam, bosi si amesema nikurudishe ofisini?"
"Tafadhari tusiharibiane siku, kama huwezi sema nishuke nichukue usafiri mwingine."
Yule dereva akaogopa na kuamua kumrudisha tu Sabrina nyumbani kwake.
Sabrina alipofika nyumbani kwake, aliingia ndani na kukaa huku akili yake ikiwa imechoka kabisa kimawazo,
"Hata sijui nifanyeje kwakweli, sijui Sam nitamweleza nini, sijui itakuwaje kwenye swala zima la ndoa baina yangu na Sam mmh!!"
Sabrina aliona kamavile dunia imemuelemea leo, alihisi akili yake kugoma kufanya kazi.
Akaona ni vyema achukue simu na kumpigia Jeff,
"Uje nyumbani kwangu haraka"
"Kwani kuna nini mamdogo?"
"Nimekwambia uje haraka sitaki maswali"
Sabrina akaikata ile simu na kuendelea kuwaza hatma yake na lile tumbo.
Jeff alijiandaa haraka haraka na kwenda nyumbani kwa Sabrina ili ajue ni kitu gani ameitiwa haraka vile.
Akamkuta Sabrina akiwa amejawa na hasira zisizopimika, na Sabrina alipomuona Jeff aliinuka na kumzaba kibao, Jeff akashika shavu lake na kuuliza,
"Mbona unanipiga lakini?"
"Ni haki yangu kukupiga, tena usiniulize maswali. Umenitia aibu sana wewe"
"Kwani ni vipi?"
"Nina......."
Sabrina akasita kuongea, huku akimuangalia Jeff kwa jicho kali.
"Una nini kwani?"
"Hayakuhusu, na pia uondoke mbele ya macho yangu upesi"
Jeff hakutaka kubishana pale na Sabrina, hivyo akaamua kuondoka tu.
Jeff alipoondoka, Sabrina alikaa kimya na kujifikiria jinsi gani ataweza kukabiliana na hali yake, hakuweza kumwambia Jeff moja kwa moja hali yake kwavile aliona kama ni kujidhalilisha kwa kijana huyo.
"Hata sijui nifanyeje kwakweli, au nikatoe? Naona vyema nikatoe, ni kheri Jeff asijue chochote hata Sam pia asijue. Mmh mie jamani, huyu Jeff huyu kanipa doa jamani"
Sabrina alikuwa akijilalamisha tu bila ya kuwa na muafaka wa majibu yake.
Sam alimshangaa dereva wake kurudi mwenyewe bila Sabrina,
"Mbona umerudi peke yako?"
"Madam kasema nimpeleke nyumbani"
"Kwani kazidiwa?"
"Hapana, ila amesema kuwa anahitaji kupumzika"
"Basi sawa"
Sam akaona kuwa ni vyema siku hiyo atoke mapema ili akamuangal ie Sabrina nyumbani kwake.
Na muda ulipofika, moja kwa moja akaianza safari ya kwenda kwa Sabrina, njiani akamuona Jeff na kusimamisha gari lake kisha akamuita, naye Jeff akasogea alipo Sam na moja kwa moja Sam akamuuliza Jeff
"Umetoka wapi?"
"Kwa mamdogo"
"Kufanya nini?"
Jeff akamuangalia tu Sam bila ya kusema chochote, kisha Sam akamwambia tena Jeff,
"Ulienda kufanya nini? Si alikwambia usiende tena wewe!"
"Hayo yalishapita tayari, hata hivyo aliniita mwenyewe"
Sam akamuangalia Jeff kwa chuki ya wazi wazi hata yeye mwenyewe hakujua ni kwanini anamchukia Jeff.
Kisha akarudi kwenye gari yake na kuondoka huku Jeff naye akiondoka huku na yeye akiwa na hasira za wazi kabisa dhidi ya Sam.
Sam alipofika kwa Sabrina alimkuta akitapika,
"Pole sana Sabrina mpenzi"
Kisha akaingia naye ndani,
"Kwani dokta kasema kuwa una tatizo gani?"
Sabrina akakaa kimya huku akifikiria kitu cha kumwambia Sam ili aridhike.
Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Dokta kasema majibu kamili nikachukue kesho"
"Nini? Kesho? Kwani ni vipimo gani hivyo hadi kesho?"
"Mi sijui ila dokta ndio kaniambia hivyo"
"Basi itabidi hiyo kesho twende wote mpenzi"
"Hapana bhana, haina haja ya kwenda wote. Nitaenda tu mwenyewe"
Sam akamuangalia Sabrina kisha akamwambia,
"Ila angekwambia Jeff muende wote ungekubali"
Sabrina akashtuka sana, kisha akachukia,
"Hivi Sam kwanini unapenda kujifananisha na Jeff jamani? Jeff ni mdogo sana kwako na pia hadhi yake ni tofauti na yako, wewe ni mume wangu mtarajiwa na yeye ni mwanangu"
"Wewe unaona hiyo tofauti ni ndogo sana ila bado ukweli utabaki pale pale kuwa yeye unampenda kuliko mimi"
Sabrina ikabidi amuonyeshe Sam kuwa amechukia sana ili Sam asiendelee kujilinganisha na Jeff.
Sam naye alipoona kuwa sura ya Sabrina imebadilika akaamua kubadilisha mada ili aweze kumridhisha Sabrina.
Jeff akiendelea na safari yake ya kurudi kwao akakutana na mwalimu wake njiani na kumsalimia,
"Mbona umepooza hivyo madam?"
"Najisikia vibaya, nahisi nina homa"
"Pole sana, unatakiwa uende hospitali madam"
"Nitaenda kesho, kuna daktari mmoja ni rafiki yangu sana"
"Basi sawa madam"
"Hivi yale mambo yako ulikamilisha?"
"Kiasi madam, ila bado naumia moyo. Nikipata muda, tutaongea vizuri madam"
Jeff akakubaliana na mwalimu wake ambaye ni Joy kuwa waonane nae siku ya kesho yake.
Jeff aliporudi nyumbani kwao alimkuta mama yake akiwa amekaa na binti fulani anayemfahamu. Binti ambaye aliyekuwa akisifiwa katika shule yao kwa uzuri wake, Jeff akashangaa kumuona pale kwao kuwa anahitaji kitu gani.
Alipofika akawasalimia na kuingia ndani, ila mama yake akamuita,
"Mbona hata hujamsalimia vizuri mwenzio?"
Jeff akamuangalia mama yake tena bila ya kujibu chochote kisha akaingia ndani kwao.
Sakina akamuangalia sana mwanae bila ya kummaliza.
"Yani hili toto hili kweli aliyemroga amekufa jamani mbna angekuwa hai angenionea huruma mimi"
Yule binti alikuwa kimya tu akimuangalia Sakina,
"Mwanangu Doris, msamehe bure huyu Jeff sio kosa lake kwakweli ni hajielewi tu"
"Usijali mama, nitakuja hata siku nyingine"
Yule binti akainuka kisha akamuaga Sakina na kuondoka.
Muda huo huo Sakina akamfata mwanae ndani,
"Ila wewe Jeff una matatizo gani mwanangu? Yani binti mzuri kama yule umeshindwa hata kumsalimia vizuri"
"Nisamehe mama kichwa kilikuwa kimevurugika"
"Hao wamama watu wazima ndio wanakuvuruga, na siku nikigundua Jeff! Yani nikimgundua huyo mwanamke nakwambia atataja jina langu kwa kilugha"
Jeff akamuangalia mama yake na kutabasamu, na kumfanya Sakina apandwe na hasira zaidi
"Wee cheka tu, unadhani ni mazuri haya! Yani nitamwambia Sabrina tusaidiane zaidi ili siku tukimgundua huyo jimama awe mboga yetu"
Jeff akacheka na kumfanya mama yake achukie na kuondoka kabisa.
Sam alimuaga Sabrina pale na kuondoka kuelekea nyumbani kwake.
Sabrina alitulia huku akiwaza cha kufanya kwa siku ya kesho.
Wakati akiwaza, simu yake ikaita. Moja kwa moja Sabrina akajua kuwa ni Sam anataka kumwambia kuwa ameshafika, ila alipoichukua ile simu akaona ni namba ngeni.
Sabrina akaipokea ile simu,
"Hallow"
"Kesho nakuja nyumbani kwako"
"Kwani nani wewe?"
Ile simu ikakatika na kumpa mashaka Sabrina kwani hakuelewa kuwa mpigaji ni nani na ile sauti ilikuwa ya kiume.
Ila aliamua kuachana na huyo mpigaji ili kujipunguzia mrundikano wa mawazo.
Kesho yake asubuhi na mapema, kama kawaida Sam alipita kumfata Sabrina ila siku hiyo Sabrina alichelewa sana kuamka na kushindwa kujiandaa upesi.
"Mbona leo umechelewa sana Sabrina?"
"Si unajua kuwa naumwa jamani Sam"
"Basi leo pumzika, nitakuagizia dereva ili akupeleke tena huko hospitali ukapewe majibu na uanze tiba mapema. Sawa mpenzi?"
"Sawa baba nimekuelewa"
Sam akaondoka pale na kumuacha Sabrina ajiandae.
Muda kidogo ulipofika, Sabrina akafatwa na dereva wa Sam kwaajili ya kwenda hospitali.
Sabrina alipofika pale hospitali, moja kwa moja akaenda kwa yule daktari ili aweze kuzungumza nae.
"Daktari, nina ombi moja"
"Ombi gani hilo?"
"Nataka kutoa hii mimba, lakini pia naomba kwenye cheti changu uandike kuwa nina typhoid"
"Hilo swala la kuandika kuwa una typhoid lipo kwenye uwezo wangu ila kutoa mimba hapana"
"Jamani daktari kwanini jamani, nisaidie tafadhari jamani"
"Kuna mwenzangu nitakupeleka, yeye ndio mtaalamu wa hayo mambo, sababu anakupima kwanza. Na uzuri wake hata mambo ya kienyeji anayajua"
Sabrina akaona kuwa ni vyema akakutane na huyo daktari ili aweze kutatua tatizo lake alilokuwa nalo.
Huyu daktari hakuwa na papara sana, hivyo akamtaka Sabrina asubiri kidogo ili akakutane na huyo dokta maarufu kwa kutoa mimba aliyejulikana kwa jina la Dr.Mambo, kutokana na hayo mambo yake.
Muda kidogo, Sabrina akaenda kukutanishwa na huyo Dr.Mambo ili aweze kumshughulikie lile swala la mimba.
Dr.Mambo akampima Sabrina, huku akiguna guna
"Vipi dokta, si itawezekana?"
Dokta akakaa kwanza na Sabrina kwaajili ya mazungumzo,
"Ni hivi Sabrina, mimi ni dokta maarufu sana wa kutoa mimba hapa mjini. Watu wengi wananifahamu, ila wewe nilipokuona kwanza kabisa nikashtuka sana. Na pia nilipokupima, inaonyesha kuwa mimba yako imekaa vibaya kwahiyo nikikutoa naweza kuhatarisha maisha yako. Ila kwa ushauri wangu kwako sasa, nakuomba uje na huyo jamaa mwenye hiyo mimba. Kuna kitu nataka nimuelekeze cha kufanya ili tuweze kuitoa"
Maelezo ya huyu daktari yalimvunja moyo kabisa Sabrina, alijikuta akikosa raha kabisa na kuamua kuondoka tu huku akiwaza jinsi ya kumleta Jeff mahali hapo.
Wakati Sabrina anatoka nje ya kile chumba cha Dr.Mambo, akamuona Joyce yule dada wa Sam akiwa kwenye benchi huku ikionyesha kuwa naye anangoja huduma toka kwa Dr.Mambo.
Sabrina alivyoona vile, akarudi kwa Dr.Mambo upesi,
"Dr, huyo dada wa nje huyo najua naye atakuwa amekuja kutoa mimba. Tafadhari mkatalie, ni mimba ya kaka yangu"
Dr.Mambo akacheka sana huku akimuangalia Sabrina na kumjibu,
"Usijali kitu Sabrina, nitakusaidia kwa hilo"
Sabrina akatoka, bila ya kumuangalia tena Joyce na kuondoka zake.
Sabrina, alirudi moja kwa moja nyumbani kwake huku akipanga namna ya kuzungumza na Jeff ili aweze kumkubalia yeye aitoe ile mimba.
"Naimani atakubali sababu hata yeye anajutia kitendo alichonifanyia mimi kipindi kile. Hii ni aibu jamani, hata sijui pa kuificha sura yangu."
Akachukua simu yake na kumpigia simu Jeff kuwa aende nyumbani kwake, naye Jeff alikubali bila kinyongo chochote.
Sam alitulia ofisini huku mawazo yake yote yakiwa juu ya Sabrina.
Alijiona wazi kuwa hawezi kufanya lolote bila ya uwepo wa Sabrina.
Hivyo akajipanga kutoka mapema ili kwenda kumuwahi Sabrina nyumbani kwake na ili waweze kupata muda muafaka wa kuzungumza.
Ila kabla Sam hajatoka pale ofisini, akapatwa na ugeni wa dada yake ambaye ni Joyce.
"Kaka kuna mambo nataka tuzungumze"
"Mambo gani hayo?"
"Kwani wewe hutaki mtoto?"
"Nataka sana, hata sasa hivi ningempata ningefurahi sana"
"Basi kuna kitu nimekusaidia leo, wewe mwenyewe utafurahi"
"Kitu gani hicho Joy?"
"Leo sitakwambia, ila utajua tu ni kitu gani. Nimekusaidia kaka yangu jamani, hata mi mwenyewe natamani kuitwa shangazi"
"Mbona sikuelewi Joy?"
"Ipo siku utanielewa tu"
Kisha Joy akamuaga Sam na kuondoka, na kumfanya Sam apatwe na maswali bila ya majibu kwani alifikiria mara mbili mbili ila hakuelewa kuwa ni mtoto gani anayezungumziwa hapo na ni kwa mantiki ipi.
Sam akaamua tu kuachana na hayo mawazo kwavile aliona kuwa yanamchanganya tu.
Alikamilisha kazi yake na kuanza kujikusanya ili kwenda nyumbani kwa Sabrina kumuona.
Jeff kama kawaida alifika kwa Sabrina kusikilizia wito wake, ila alimshangaa kumuona Sabrina leo akiwa mwanamke mpole kuliko siku zote.
"Jeff, nimekuita hapa kukwambia kuwa mimi nina mimba"
Jeff akashtuka sana kwani hakuamini, akajikuta akiropoka,
"Hatimaye ndoto zangu zimetimia"
Hapo ndipo alipomtibua Sabrina,
"Yani wewe kweli huna akili, mimi nimekuita hapa ili ukanisaidie kuitoa hii mimba halafu wewe unasemaje?"
"Namshukuru Mungu, ndoto zangu zimetimia"
Sabrina akazidi kupatwa na hasira,
"Mbwa mkubwa wewe, ndoto zako zimetimia kitu gani? Unafikiri mimi nafanyeje na hii mimba?"
Muda huo huo Sam naye aliwasili pale ndani na kuuliza kwa mshangao,
"Mimba?"
Sabrina na Jeff nao wakashtuka kumuona Sam pale ndani.
Muda huo huo Sam naye aliwasili pale ndani na
kuuliza kwa mshangao,
"Mimba?"
Sabrina na Jeff nao wakashtuka kumuona Sam pale
ndani.
Sam akawaangalia kwa makini na ule mshtuko wao kisha akawauliza tena,
"Nasikia kuhusu mimba hapa, haya niambieni ni mimba ipi na imefanyaje?"
Sabrina akachekecha akili yake na kutafuta jibu la kumpa Sam.
Wakati huo Jeff naye akaanza kujibu,
"Ni mimba yangu ipo kwa......."
Sabrina akamkatisha Jeff kwa kumpiga kibao,
"Yani wewe huna akili kabisa, unajua wazi una makosa halafu unataka kuelezea nini sasa? Huna akili wewe."
Kisha Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Yani hili litoto usilione hivi, limenipa kesi hapa balaa"
"Niambieni sasa ni kitu gani? Hivi unajua kama hapa mnazidi kunichanganya tu"
Jeff akataka kusema tena, ila Sabrina alimuangalia Jeff kwa jicho kali sana na kumuogopesha kisha akasema,
"Basi mwambie ukweli mwenyewe mamy"
Sam akiwa na hamu ya kujua kinachoendelea, akadakia
"Ndio niambieni ukweli"
"Unajua mimi naumwa Sam"
"Ndio unaumwa ila niambie ukweli kuhusu nilichokisikia hapa cha mimba"
Sabrina akapata maneno ya kujitetea muda huo huo,
"Ni hivi, unakumbuka kipindi kile nilipomfukuza huyu Jeff hapa kwangu?"
"Ndio nakumbuka, niambie sasa"
Kwa mawazo ya Jeff akajua kuwa Sabrina anataka kumwambia Sam ukweli, akaamua kuinuka kwa aibu na kwenda jikoni ili kama likitokea lolote la kutokea awe amejiandaa.
Sabrina akamuangalia Jeff alipokuwa akienda jikoni na kuendelea kumuhabarisha Sam,
"Basi huyu Jeff bhana kuna binti alikuwa ana mahusiano nae, nilipokuja kugundua nikaambiwa kuwa ni mtoto wa mwanajeshi, ili kuepuka matatizo nikaamua kumfukuza Jeff. Sasa jana nimegundua kuwa yule binti ana mimba ya Jeff. Yani huyu mtoto ananiletea balaa jamani"
"Mbona makubwa hayo, itakuwaje sasa?"
"Mie leo nilipoenda hospitali nimepitia kwa daktari mmoja hivi kumuuliza mlolongo wa kutoa mimba sababu yule binti amekubali kuitoa ila tatizo ndio kwa huyo Jeff namwambia hapa anakataa ndiomana nikawa nafoka"
Sam akamuangalia Sabrina na kuwa kama vile amemuelewa na kumuamini kiasi kisha akamuuliza,
"Na wewe je unaumwa nini? Si ulienda kuchukua majibu leo?"
Sabrina akachukua mkoba wake na kutoa kikadi kidogo na kumkabidhi Sam,
"Nimeambiwa nina typhoid, yani hapa nimechomwa sindano na kupewa dawa za kunywa"
"Yani typhoid ndio ugonjwa ambao jana ulishindikana kuonekana Sabrina?"
"Mi sijui mambo ya kidaktari"
Jeff akatoka kule jikoni na kuwapita pale sebleni na kuondoka.
Sabrina akapata mwanya zaidi wa kumueleza Sam,
"Si unamuona alivyo na kiburi mtoto mwenyewe!"
"Namuona ila ngoja mimi nipate nafasi ya kuzungumza naye ili tujue cha kufanya"
"Hata asikusumbue akili, mi najua cha kufanya hata usijali"
Sabrina akajitahidi kumpa maneno Sam yatakayomfanya asizungumze na Jeff kwani alihofia kuwa Jeff anaweza kumwambia ukweli Sam.
Siku hiyo hadi giza linaingia Sam alikuwa bado k wa Sabrina ingawa alitoka mapema ofisini lakini hadi usiku unaingia bado alikuwa kwa Sabrina, na muda mwingi alikuwa kimya huku akitafakari mambo mbali mbali kwenye akili yake.
Sabrina alitaka kwenda kupika,
"Hapana Sabrina unaumwa usiende kupika, sema unachojisikia kula nikakuletee"
"Labda chips mayai ila zikauke sana"
"Hakuna tatizo"
Sam akainuka na kwenda kumnunulia Sabrina chakula.
Wakati Sam ameondoka tu, mlango wa Sabrina ukagongwa.
Alipokwenda kufungua alimkuta Japhet pale mlangoni na kumfanya Sabrina achukie, ila Japhet aliingia moja kwa moja mpaka ndani.
"Hivi wewe Japhet wewe una shida gani na mimi jamani? Kwanini unapenda kunisumbua wewe jamani? Haya niambie umefata nini?"
"Jana si nilikupigia simu na kukwambia kuwa leo nakuja? Si ndio nimekuja sasa."
Hapa Sabrina akakumbuka kuwa simu aliyopigiwa jana yake na namba mpya ndio ilikuwa ya huyu Jeff.
"Sasa umekuja kufanya nini?"
"Nimekuja kulala hapa kwako leo mpaka ukubali kunisamehe na kurudiana na mimi Sabrina"
"Jamani Japhet, mi nilishakusamehe kitambo sana. Ila kurudiana na wewe sitaweza sababu nina mchumba tayari, sitaweza kuwa na wewe Japhet"
"Tafadhari Sabrina nihurumie, nakupenda sana. Nahitaji kuoa ila sijamuona mwanamke anayefaa kuwa mke wangu zaidi yako Sabrina, tafadhari kubali uwe wangu nakuomba"
"Siwezi Japhet, siwezi kabisa nawe nielewe tafadhari"
Japhet hakutaka kuondoka bado alimng'ang'aniza Sabrina juu ya swala la kumpenda sana.
Sabrina alijitahidi kwa kila njia kumfanya Japhet amuelewe ila bado alikuwa mgumu na aligoma kutoka mule ndani.
Muda Sam anarudi akasikia mzozo baina ya Sabrina na sauti ya kiume, akajikuta akitawaliwa na roho ya wivu katika moyo wake.
Alipoingia akamkuta Japhet amepiga magoti mbele ya Sabrina akimuomba msamaha, Sam kwa hasira akatoa bastora yake ambayo hupenda kutembea nayo siku zote.
Sabrina kuona vile akaamua kukaa mbele ya Japhet kumkinga huku akimsihi Sam airudishe ile bastora.
"Tafadhari Sam nakuomba, nakuomba sana mpenzi wangu usifanye chochote"
"Sabrina niache nimmalize huyo mjinga maana namuona tu akikusumbua kila siku"
"Nakuomba Sam, shusha hiyo chini tafadhari"
Sabrina akajaribu kumsogelea Sam ili kumzuia asimpige Japhet, na muda huo Jeff nae alifika na kufungua mlango, akapatwa na mshangao kwa lile tukio na kumfanya Japhet nae apate upenyo wa kukimbia.
Jeff aliendelea kushangaa huku akimuangalia jinsi Sam anavyotulizwa pale na Sabrina ili asifanye mambo ya ajabu.
"Ungeniachia yule ng'ombe nimmalize mie yani yule tena asirudie tena kuja hapa"
Halafu Sam akamuangalia Jeff na kumwambia,
"Tena ukimuona mtu yeyote anamsumbua mke wangu hapa unipe taarifa, mi nitamaliza watu mimi huwa sipendi ujinga"
Jeff hakujibu kitu ila alimuangalia Sabrina na kumwambia,
"Nimepita kukuaga mamdogo, kwahe ri"
Tena hata hakusubiri Sabrina ajibu kwani alitoka nje na kuondoka.
Sabrina alitulia huku akimuangalia Sam bila hata ya kumaliza kumtafakari alivyo.
"Chipsi ulizotaka hizo hapo, ule sasa"
Sabrina alichukua zile chipsi ili ale, ila alipokula kidogo tu akajihisi vibaya na kwenda kutapika.
Sam akamuonea huruma sana Sabrina,
"Pole sana, itabidi leo nibaki hapa kukuangalia mpenzi wangu jamani"
"Hapana Sam, usijali juu ya hilo. Mi nitakuwa sawa tu mpenzi wangu. Usiwe na shaka tafadhari"
"Hapana, siwezi kuondoka na kukuacha na hiyo hali. Au basi nikupeleke kwenu ili ukapate uangalizi wa karibu toka kwa mama yako"
Sabrina akafikiria na kukataa huku akiendelea kumsisitizia Sam kuwa atakuwa sawa tu huku akili yake ikiendelea kupanga mipango mingine.
"Kama ndio hivyo basi mimi leo siondoki kwakweli, nitalala hapa hapa hadi nihakikishe afya yako iko vizuri"
"Basi sawa, bora tu ulale hapa hapa"
Moyo wa Sabrina ukaridhia kuwa Sam alale pale ili ajaribu kufanya kitu cha kuokoa uchumba wao.
Muda wa kulala ulipofika, Sam akataka kulala pale kwenye kochi.
"Sio vizuri bhana Sam, utalalaje kwenye kochi wakati vitanda vipo"
"Kwahiyo nikalale kwenye chumba cha Jeff?"
"Hapana bhana, chumba chetu kipo twende tukalale chumbani"
"Kumbuka bado sijakuoa Sabrina!"
"Hilo sio tatizo Sam, si tunalala tu jamani kwani tatizo liko wapi wakati ni kulala tu?"
Ikabidi Sam akubaliane na Sabrina na kwenda chumbani kulala.
Walipofika kitandani, Sam akachukua shuka akajifunika na kulala.
Sabrina akamuangalia Sam bila kummaliza, akajiuliza kimoyomoyo
"Hivi huyu ni mwanaume kweli? Au ananitega tu? Mwanaume gani hata hajali kama amelala na mwanamke? Hata kama ndoa bado mbona wengine huwa wanafanya tu kwanini huyu jamani? Mbona ananitesa mie"
Sabrina alimuangalia Sam kwa jicho la hasira sana na kujaribu kulala ila hakupata usingizi.
Akaamua kuuchukua mkono wake na kuupitisha kwenye kiuno cha Sam ili ajaribu kumpapasa papasa, ila Sam akamgeukia Sabrina na kumwambia,
"Kumbuka bado sijakuoa"
"Kwani kuna tatizo jamani Sam! Wewe si mchumba wangu jamani!"
"Ndio mimi ni mchumba wako, kwani unataka nini Sabrina?"
Ikabidi Sabrina ajitoe aibu na kumwambia,
"Nataka tufanye Sam"
"Si unaumwa wewe? Na si uliniambia hujawahi kufanya? Mbona unataka kuniletea makubwa Sabrina jamani! Nakuheshimu sana, sitaki kukuchezea ndiomana nangoja tufunge ndoa kwanza"
Sabrina alitamani hata kulia kwa majibu ya Sam ila hakujua afanye nini, na kuendelea tena kumpapasa.
"Tafadhari Sam nakuomba tufanye leo tu tafadhari"
"Hapana Sabrina, usitake kunipa dhambi muda huu. Ni mengi niliyafanya hapo zamani ila siku hizi nimebadilika, nakuheshimu sana tena nakupenda sana"
Sam akainuka na kwenda sebleni kukaa kwenye kochi, Sabrina akajisikia aibu sana kwa kushindwa kumshawi shi Sam kulala naye.
Akajikuta akikaa tu pale pale chumbani kwa hasira.
Palipokucha, Sam akaingia kwenye chumba cha Sabrina na kumuaga.
Ingawa Sabrina alikuwa amenuna, ila Sam hakujali.
Alienda na kumbusu kwenye paji la uso kisha akamuaga na kuondoka kuelekea kwake kwaajili ya kujiandaa kwenda kazini kwake.
Sabrina alibaki na hasira sana huku akimchukia Sam waziwazi kabisa.
Naye akainuka na kujiandaa kwa lengo la kwenda kuzungumza na mama yake nyumbani kwao.
Alipokuwa kwenye daladala kuelekea kwao, alikuwa amekaa siti ya nyuma ambako alipakana na wadada watatu ambao mazungumzo yao yalimfanya Sabrina atege sana sikio kwao,
"Hivi jamani kuna mwanamke kweli anayeshindwa kumtega mwanaume hadi akaingia laini?"
"Mmh labda huyo mwanamke wa kijijini, watoto wa mjini sie hakuna mwanaume anayeweza kupingua"
"Umeona eeh! Sie wadada tuna vivutio vyote vya kuwapata wanaume. Yani hakuna mwanaume wa kupingua kama kwan gu nikiamua kumuweka mwanaume kwenye kumi na nane zangu hawezi kupindua"
Wote watatu wakacheka, kisha mwingine akaendelea,
"Mi si ndio nimelishangaa zoba moja hivi, mi nimelivutia jamaa hadi ndani eti limeshindwa kumseti. Mimi sasa nilichokifanya jana jamani hadi yule kaka alipagawa"
"Eeh ulifanyaje shoga?"
"Basi yule kaka alipokuja, nikamkaribisha ndani. Halafu nikaenda kuoga kwa makusudi na kujifunga khanga ili inishike, sasa wakati......"
Konda akataja kituo nao wakamwambia ashushe, gari ikasimama na wakashuka.
Yani Sabrina akatamani hata ashuke nao ili na yeye asikilize kilichoendelea ila ndiohivyo tena walikuwa ni watu asiowafahamu ikabidi atulie tu.
Sam alipokuwa ofisini alifikiria sana kuhusu Sabrina,
"Ila siwezi kufanya hivi, lazima nitimize ahadi yangu kwa Sabrina na pia sitaki Sabrina ajue madhaifu yangu mapema kiasi hiki. Acha anichukie kwasasa ila ni lazima nimuoe kwanza."
Muda huo Joy nae alifika kwenye ofisi ya Sam kumsalimia na kujua kinachoendelea baina ya Sam na Sabrina.
"Niambie kaka, wifi yangu Sabrina anaendeleaje?"
"Anaendelea vizuri tu, ila Joy huwa sikuelewi kwakweli. Au ulidhania kuwa Sabrina ana mimba?"
"Sio nilidhania, huo ndio ukweli kaka"
Sam akamcheka Joyce na kumwambia,
"Usilolijua litakusumbua, wee nenda zako tu dada yangu"
Joy alikaa kimya baada ya kushushuliwa na kuamua kubadilisha mada kisha akaaga na kuondoka.
Jeff akiwa nyumbani kwao alikuwa akiwaza tu jinsi ambavyo Sam akigundua ukweli kitu atakachokifanya.
"Sijui kama Sabrina anaweza akamuachia anipige mimi na kuniua. Najua kuwa naye ananipenda ila tu anashindwa kuwa na mimi kwavile mimi ni bado mdogo."
Mama yake akamsikia akiongea peke yake,
"Mbona unaongea peke yako Jeff?"
"Aaah hapana ni muingiliano wa mawazo tu"
"Basi naomba nikutume kidogo"
Jeff akakubali kisha Sakina akampa Jeff mzigo ambao alihitaji aupeleke kwa mama wa Sabrina.
Sabrina alipofika nyumbani kwao, alimkuta mama yake na kuamua kukaa naye ili kumueleza yanayomsibu.
"Yani mama, hivi unionavyo hapa mwanao nina mimba."
Joy akashtuka sana na kumuuliza kwa mshangao,
"Una mimba! Ya nani?"
Akatokea Jeff na kudakia,
"Ni yangu"
Joyce akamuangalia Jeff kwa mshangao.
Joy akashtuka sana na kumuuliza kwa mshangao,
"Una mimba! Ya nani?"
Akatokea Jeff na kudakia,
"Ni yangu"
Joyce akamuangalia Jeff kwa mshangao.
Sabrina akainuka kwa hasira na kumzaba Jeff kibao, na ili kupotezea maana kwa mama yake akaanza kumwambia Jeff kwa ukari,
"Unafikiri kila muda ni masikhara tu, muone. Tena tuondokee hapa nisije nikakuharibu bure."
Jeff hakusema kitu zaidi ya kukabidhi ule mzigo aliyopewa,
"Mama kanipa nikuletee"
Kisha akaondoka zake.
Joy akamuangalia Sabrina aliyekuwa kavimbwa na hasira na kumwambia,
"Achana nae yule ni utoto tu unamsumbua ukizingatia ulishamzoesha matani tangu siku nyingi"
"Kamenikera sana, watu tunaongea mambo ya maana hapa halafu yeye analeta maneno ya kipuuzi"
"Msamehe bure mwanangu"
"Nishamsamehe tayari"
Sabrina alimjibu hivyo mama yake ila moyoni mwake bado alikuwa na chuki juu ya Jeff ukizingatia anaona kuvurugiwa mambo yake mengi na huyu Jeff.
"Basi tuendelee na maongezi yetu mwanangu"
"Subiri mama, ngoja nipumzishe akili yangu kidogo"
Sabrina akaamua kwenda kulala.
Alishtuliwa na simu yake ya mkononi, alipomuangalia mpigaji alikuwa ni Sam akaipokea na kuongea naye
"Uko wapi mpenzi?"
"Nipo nyumbani"
"Nyumbani ya wapi? Mbona huku haupo?"
"Aah samahani sikukwambia, nimekuja huku kwa mama"
"Basi nakuja"
Kisha Sam akakata simu na kumfanya Sabrina ainuke sasa na kumfata mama yake, ila akamkuta mama yake akiongea na Sakina,
"Yani akili za Jeff jamani hata sijui zikoje labda Sabrina ataweza kunisaidia"
"Ndio Sabrina ataweza sababu wanapatana sana, yani leo Sabrina alivyomnasa kibao Jeff nikajua atalalamika, ila wala alikuwa kimya kama sio yeye vile. Ila angepigwa na mtu mwingine sasa loh hilo balaa lake nisingeingilia"
Sakina akacheka na kuuliza,
"Kwani alifanya nini?"
Ikabidi Sabrina aingilie kati yale mazungumzo ili yasije chimbua na mambo mengine yaliyojificha nyuma ya pazia.
"Mwanao ni mjinga tu yule, eeh niambie dada yangu za siku?"
"Kumbe ulikuwa unatusikia Sabrina jamani, nimekukumbuka sana mdogo wangu"
Wakafurahi pale na maongezi mengine yakaendelea.
Huku Sabrina akijitahidi kukwepesha mada ya awali.
"Badae au kesho nitakuja kwako dada, nina mengi ya kuzungumza na wewe"
"Hakuna tatizo uje tu Sabrina"
Sakina akaaga pale na kuondoka.
Baada ya muda kidogo Sam naye akawasili pale nyumbani kwa wakina Sabrina na kumkuta Sabrina na mama yake.
Alipomsalimia tu mama yake Sabrina, hapo hapo Sabrina akadakia ili mama yake asiingizie khabari za mimba.
"Ndio umekuja kunipitia eeh, basi twende"
Kisha Sabrina akamgeukia mama yake na kumuaga,
"Mama, nitarudi badae. Kuna mahali naenda na Sam"
Ikabidi Sam akubaliane na maneno ya Sabrina kisha naye akaaga na kuondoka pamoja.
Walipokuwa kwenye gari, Sam akayaanza mazungumzo
"Ila Sabrina umenitoa kwenu haraka sana, nilitaka kuzungumza kidogo na mama yako"
"Ulitaka kuzungumza naye kuhusu nini?"
"Kuhusu harusi yetu Sabrina, unajua kwenu ndio wanachelewesha mambo."
"Usijali, utazungumza nae siku nyingine"
"Au umechukia usiku wa jana Sabrina?"
"Hapana, achana na hayo mambo ya usiku yalisha pita tayari"
"Sawa mpenzi"
Sam alikuwa akifata kile anachokisema Sabrina ili kuepuka kumkera.
"Sasa twende wapi muda huu?"
"Twende hata baharini kupunga upepo"
Ikabidi Sam ampeleke Sabrina mahali alipopataka.
Sakina aliporudi nyumbani kwake akamtania mtoto wake,
"Nasikia leo Sabrina kakuzabua hata hujalalamika"
Jeff akacheka na kumuuliza mama yake,
"Kwani wamekwambia kuwa chanzo ni nini?"
"Hata hawajaniambia, kwani chanzo ni nini?"
"Aah mambo ya Sabrina na mimi yaache kama yalivyo mama, utachanganyikiwa bure"
"Una maana gani Jeff?"
Jeff akambadilishia mada mama yake,
"Kesho naenda kufanya usahili kuna kazi nimeomba"
"Na shule je? Yani hapo ndio huwa unanichosha mwanangu jamani, kwanini huwa unapenda kubishana na mimi jamani? Nenda shule kwanza, halafu hayo mengine yatafata. Yani huyo mwanamke aliyekushika masikio huyo nikimjua wallah atanitambua"
Jeff akamuangalia mama yake na kutabasamu tu.
Sabrina akiwa ufukweni na Sam, walimuona Joy akiwa maeneo hayo pamoja na kaka wa Sabrina yani James, wakaamua kuungana nao ili waweze kubadilishana mawazo.
Waliwafata na kuwasalimia,
"Kumbe na nyie mpo huku?"
"Ndio, tupo kubadilishana mawazo tu"
Sabrina akamuuliza kaka yake,
"Eeh ndoa lini?"
"Ni hivi karibuni tu, tunamngoja baba arudi ili niweze kuambatana naye pamoja na mama kwenda kutoa mahari na mshenga wangu"
"Basi vizuri, na sisi tunamngoja baba arudi ili Sam akanitolee mahari nyumbani. Si ndio hivyo Sam wangu!"
Sam akatikisa kichwa huku akitabasamu, muda huo wote Joy alikuwa kimya kabisa na hakuchangia chochote hadi wanaondoka eneo lile.
Ikabidi Sabrina amuulize Sam,
"Mbona vile dada yako, ana matatizo gani kwani?"
"Achana nae yule ana kisirani tu, nilimshushua alipokuja ofisini kwangu kuleta umbeya."
"Aaah kumbe!"
"Mi huwa sipendi maneno ya kuambiwa na watu, napenda kitu nikishuhudie mwenyewe ili hata kama nikichukua hatua basi nichukue hatua kihalali"
"Nimekuelewa"
"Kesho ni Jumamosi, ni siku fupi kwa kazi yetu. Je utaenda ofisini?"
"Naendelea vizuri kwasasa, kwahiyo nitaenda"
"Basi nitakupitia twende ila mi sitakaa ofisini, kuna mahali naenda kuwafanyia vijana usaili wa kazi"
Sabrina hakuwa na tatizo kwani anaelewa wazi kuwa Sam anamiliki vitengo mbali mbali na ndiomana ana pesa za kufanyia chochote atakacho.
Wakapanda kwenye gari kwaajili ya safari ya kurudi nyumbani kwa Sabrina kwanza.
Wakati wapo kwenye gari, Sam akamuuliza kitu Sabrina,
"Utajisikiaje siku ukiwa na mimba yangu?"
Sabrina akashtuka sana na kupumua kidogo kisha akamjibu Sam,
"Nitakuwa na furaha sana yani kupita maelezo ya kawaida"
"Kama ni hivyo basi itakuwa vizuri, naomba nikua hidi kitu Sabrina"
"Kitu gani hicho?"
"Siku utakapokuwa na mimba yangu napenda uniambie ni gari gani utapenda nikununulie ili iwe inakupeleka kliniki."
Sabrina alikuwa akimsikiliza Sam huku moyo wake ukiugua kwa maumivu makali na kumfanya hata atamani kurudisha siku nyuma ili awe salama.
"Ukiwa na mimba yangu, sitapenda uteseke na kazi. Sitapenda uwe na mawazo, ndiomana nataka nikuoe kwanza kabla ya mambo yote"
Sabrina alihisi kuchefuka tu na haya maneno ya Sam na kuamua kumbadilishia mada,
"Hivi bado hatujafika kwangu kweli!"
"Tunakaribia kufika usijari"
"Yani nimechoka halafu nina usingizi sana, nikifika tu ni kulala"
Sam akamuangalia Sabrina bila ya kusema chochote kile cha zaidi na kuendelea na safari.
Sabrina alipofika akamuaga Sam na kushuka huku akidai kuwa ana usingizi sana, hivyobasi alihitaji kwenda kupumzika.
Kwahiyo Sam akaamua kurudi nyumbani kwake tu na yeye.
Sabrina alikaa na kuilaumu sana ile mimba, alitamani kama isingekuwepo kwenye tumbo lake.
Ila ndio tayari ilishakuwa kwake.
Akaamua kulala tu kama alivyopanga kuwa amechoka, ila kabla hajalala akapigiwa simu, kuangalia mpigaji alikuwa ni Jeff,
"Sijui kanataka nini usiku huu"
Alipokea ile simu huku akiwa ameshapandwa na hasira tayari, ila iliongea sauti ya kike na alipoisikilizia ilikuwa ni sauti ya Sakina,
"Sabrina nakuomba kesho uje nyumbani kwangu kama utapata muda"
"Hakuna tatizo, nilishakuahidi kwahiyo lazima nitakuja"
"Sawa basi usiku mwema"
"Nawe pia"
Akakata simu na kuiweka pembeni, mara ikaita tena alipoiangalia ni namba ya Jeff akajua ni Sakina,
"Sijui kasahau kuniambia kitu gani"
Akaipokea ile simu ila sasa aliongea Jeff,
"Na mimi naomba nikutakie usiku mwema"
"Kwenda zako, usiniletee balaa mie"
"Sawa, ila kuna kitu nataka kukwambia"
"Kitu gani?"
"Mimi ndio yule Prince J niliyekuwa nakusumbua kipindi kile kwenye Facebook"
"Nyoko zako wewe"
Sabrina akaikata ile simu kwa hasira na kujisemea,
"Hivi huyu mtoto huyu ananitafutia kitu gani mimi jamani! Kwanini mimi, kwanini nikose raha sababu ya mtu mmoja? Aaaah, sijui kwakweli."
Sabrina akatafuta usingizi kwa lazima ila ukakawia kuja sababu ya mawazo aliyokuwa nayo kwa muda huo.
Usingizi ukampitia, akajiona anaolewa.
Amevaa shela zuri sana, na Sam nae kavaa suti nzuri sana.
Watu wengi wamejaa kushuhudia ndoa yao, ila wakati Mchungaji anataka kuwafungisha ndoa, akatokea Jeff na kusema,
"Ana mimba yangu huyu"
Sabrina akashtuka pale pale kutoka usingizini, alikaa chini na kujikuta akilia kwa uchungu huku roho yake ikimuuma sana na kuilaumu ile mimba pamoja na kiumbe alichonacho kwenye tumbo lake, akajikuta akisema
"Ewe mtoto uliye kwenye hili tumbo langu, tafadhari kama unanihurumia mama yako jitoe mwenyewe. Naumia mimi, sina raha, sina amani, sina furaha. Unafikiri nitakupenda kweli wakati umeharibu maisha yangu kiasi hiki? Tafadhari nihurumie ili niepukane na hii fedhea"
Alikuwa akiongea kamavile anaongea na mtu pembeni yake kumbe anaongea na mimba yake.
Na hakulala tena hadi palipokucha.
Kama kawaida, Sam alimfata Sabrina kwaajili ya kwenda kazini.
Walipokuwa kwenye gari Sabrina akampa hoja Sam,
"Baba anarudi wiki ijayo, unaonaje sasa wiki hiyo uje utoe mahali na tufunge ndoa kabisa"
"Ni jambo linalowezekana kabisa tena lipo ndani ya uwezo wangu. Ila kwanini tufanye haraka kiasi hicho? Ni kitu gani tunakimbilia?"
"Hivi wewe Sam hupendi kuishi nyumba moja na mimi? Hupendi kula na mimi? Kuoga pamoja na kulala wote hupendi?"
"Sabrina, yote haya nafanya kwa kufata ushauri wako. Unakumbuka siku ile niliyokuomba ukalale kwangu? Japo kwa maongezi tu? Ukagoma, nikakurudisha nyumbani ila ukaenda kulala unapopajua wewe ila kwavile nakupenda sijakuhoji hadi leo. Unadhani mimi sikuumia? Au unadhani nina moyo wa chuma ambao haupenyezi maumivu? Nataka tupate muda mzuri wa kufahamiana, swala la kutoa mahari sio tatizo kwangu, kwahiyo nitaitoa tu. Na swala la ndoa pia sio tatizo kwangu, kwahiyo nitakuoa tu ila sio kuharakisha kiasi hicho"
"Kwahiyo Sam umeamua kunilipizia eeh"
"Hapana, sio kukulipizia. Ila hatuwezi kuharakisha kiasi hicho kwakweli"
Sabrina alikaa kimya kwani alijua wazi kuwa hata kama akiendelea kuongea ni kazi bure.
Walifika ofisini, Sam akamuacha Sabrina pale ofisini na kuondoka zake mahali alipotakiwa.
Kisha Sabrina akaendelea na kazi, muda ulipofika tu wa kutoka, akaondoka kwaajili ya kwenda nyumbani kwa Sakina.
Njiani akakutana na Fredy ambaye alimpa taarifa ambayo hakuijua.
"Francis anaoa mwezi ujao"
"Nini? Francis anaoa?"
"Ndio anaoa"
"Mbona hakuniambia?"
"Atakuja tu kukwambia mwenyewe"
Wakaagana pale huku Sabrina akipata mawazo kuwa bora angekuwa na Francis labda ndio ungekuwa muda wake wa kuolewa.
Aliachana na Fredy pale huku akiwa na mawazo tu.
Alifika nyumbani kwa Sakina na kumkuta, wakasalimiana ila hoja kubwa ilikuwa ni kuhusu Jeff,
"Yani Sabrina, huyu mtoto Jeff hataki kusoma tena eti anataka kufanya kazi. Majibu ya kidato cha sita yalishatoka na amefanya vizuri tu ila hataki kusoma anataka kufanya kazi"
"Umejaribu kumuhoji kuwa kwanini anafanya hivyo?"
"Huwa haeleweki, sijui anataka kuoa na umri ule jamani si kuniletea mizigo tu mimi hapa, na wasichana wote ninaomletea mimi hawataki, hata sijui anamtaka nani"
"Sasa mimi nitajaribu kuongea nae, yuko wapi kwani?"
"Kaenda kwenye usaili wa kazi huko"
"Sehemu gani?"
Sakina akamtajia Sabrina na kumfanya moyo umlipuke kwani alijua wazi ndio huko ambako Sam alisema kuwa kuna watu anatakiwa akawafanyie usahili,
"Vipi Sabrina, unapajua eneo lenyewe?"
"Ndio napajua, ila ngoja kidogo niwasiliane na mtu fulani"
Sabrina akainuka na kwenda pembeni kisha akampigia simu Sam,
"Uko wapi?"
"Si ndio nipo huku kuwasahili watu bhana, ila nimekaona na kaJeff hapa na yeye anataka kazi"
Sabrina akapumua kidogo baada ya kugundua kuwa alikuwa anahisia kitu cha kweli.
"Ukitoka hapo unaenda wapi?"
"Nikitoka hapa, kuna baa pembeni nataka nikae na huyu bwana mdogo Jeff nizungumze nae mawili matatu"
"Vipi na mimi nije?"
"Hapana, usiwe na shaka nitakufata badae"
Kisha akakata simu, Sabrina akarudi kuongea na Sakina ila havikukalika akaamua kumuaga na kumuahidi kurudi badae.
"Mbona gafla hivyo Sabrina?"
"Kuna mtu nataka nikamuwahi kidogo"
Hakutaka hata kupoteza muda, akatoka na kuondoka.
Usahili ulivyoisha, Sam akamuita Jeff na kwenda naye kwenye baa ya pembeni ili kuzungumza naye kama alivyokuwa amepanga awali.
"Eeh Jeff, niambie kwanini umeamua kutafuta kazi"
"Nataka kupambana na maisha"
"Kwanini usingemaliza kusoma kwanza? Yani kama ungemaliza tu mi ningekuajili kwenye kampuni yangu moja kwa moja, kwanini sasa umeamua kutafuta kazi kwanza?"
"Nina majukumu tayari, kuna mwanamke anaujauzito wangu"
"Hivi kumbe alivyoniambia siku ile Sabrina ni kweli? Mwanamke gani huyo?"
"Tena huyo huyo Sabrina ndio ana........"
Sabrina akatokea mbele yao, na kufanya wote wawili wamuangalie.
"Hivi kumbe alivyoniambia siku ile Sabrina ni kweli?
Mwanamke gani huyo?"
"Tena huyo huyo Sabrina ndio ana........"
Sabrina akatokea mbele yao, na kufanya wote
wawili wamuangalie.
Jeff akainama chini kwa aibu, kisha Sam akamgeukia Jeff na kumuangalia, halafu akamwambia
"Endelea kusema, Sabrina ana nini?"
Jeff akainua kichwa na kumtazama Sabrina.
Akaiona sura ya Sabrina ilivyojawa na mashaka, Jeff akashikwa na kigugumizi kilichofanya ashindwe kuongea zaidi.
Sam akamshtua tena pale Jeff,
"Vipi mbona kimya cha gafla huongei tena?"
Sabrina nae akasogea karibu yao na kumfanya Jeff apate ujasiri wa kuongea kiasi ingawa aliongea pale alipoulizwa tena na Sam,
"Sema sasa, Sabrina ana nini?"
"Sabrina ndio huwa ananikataza nisiseme hovyo kwavile naweza kufungwa ukizingatia yule mtoto mwenyewe ni mtoto wa mwanajeshi"
Sabrina hakuamini kama Jeff angeweza kutunga maneno kiasi hicho, alitamani hata ampongeze ila alisita kwavile alihisi kuwa huenda Sam akagundua ukweli.
Akavuta kiti na kukaa, halafu Sam akamuuliza Sabrina,
"Si nilikwambia upumzike wewe! Sasa mbona umekuj a?"
"Nimekumiss sana ndiomana, sikuweza kuvumilia nyumbani nikikusubiri ndiomana nikaamua nikufate tu"
Sam akatabasamu na kuona sasa kazi kwake imepungua ukizingatia tayari Sabrina kampenda mwenyewe.
Kisha akamwambia Sabrina,
"Nilikuwa naongea na huyu mtoto hapa kuwa kwanini anatafuta kazi kwavile nimemkuta akiwa ni miongoni mwa watu niliokuwa nawasahili"
"Hata mi nimeambiwa na mama yake, ila sikujua kama yupo huku. Basi hili halina tatizo, nitazungumza nae mimi mwenyewe."
Kisha Sabrina akamwangalia Jeff na kutoa funguo kwenye mkoba wake na kumkabidhi,
"Shika hizo funguo uende nyumbani kwangu leo, ili nikirudi nije tuongee vizuri."
"Sawa mamdogo"
Jeff aliitikia bila hata kusita,
"Ila tafadhari sana kuwa makini na nyumba yangu, tena usitoke toke kabisa usije kuniletea balaa mie"
Jeff akaitikia kwa kichwa na kuondoka.
Sam akamuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Mbona umemuondoa huyu mtoto hata kabla sijamaliza mazungumzo naye?"
"Mwache aende bhana, mi nitazungumza nae nyumbani. Jamani Sam nimekumiss sasa huyu mtoto angefanya tushindwe kuzungumza vizuri mpenzi. Au hupendi uwepo wangu niondoke?"
Sabrina akatishia kama kuondoka,
"Hapana sio hivyo mpenzi, napenda sana uwepo wako tena nakupenda sana"
Kisha Sam akamkumbatia Sabrina na kumkalisha tena eneo lile huku wakiongea mawili matatu.
Baada ya muda kidogo, Sam akamshauri Sabrina kuwa akubali kubadilisha eneo naye Sabrina akakubali na wakaondoka pale kuelekea sehemu nyingine.
Walipofika eneo ambalo walipenda kukaa, walimuona Joy akiwa amekaa na kijana wa tofauti.
Kisha Sabrina akamuuliza Sam,
"Yule si dada yako Joy yule?"
"Ndio ni yeye"
"Na yule kijana ni nani?"
"Kwakweli simjui"
"Mmh! Huyu dada yako hajatulia Sam, yani hajatulia kabisa. Si amevishwa pete ya uchumba na kaka yangu juzi tu hapo halafu leo kakaa na mkaka mwingine!"
"Huwezi jua, labda wapo kwenye mazungumzo ya kibiashara"
"Mmh! Wewe mtetee tu ila nitaona mwisho wake leo, twende tukakae pale"
Sabrina alimuonyesha eneo Sam ambapo waliongozana na kwenda kukaa ila macho ya Sabrina muda wote yalikuwa kwa Joy na kijana aliyekuwa amekaa naye.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda kidogo Joy na yule kijana wakainuka huku wameshika mikono wakielekea mahali, Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Si umeona? Mi nilijua tu ni kibwana chake kile, si unaona wanapoelekea? Kule kuna nyumba za kulala wageni"
Sam alikuwa kimya tu huku akimtazama Sabrina na kumfanya Sabrina aendelee kuongea,
"Nahisi hata ile mimba sio ya kaka yangu ndiomana alikuwa anaenda kuitoa"
Sam akaongea na yeye sasa,
"Tatizo lenu nyie wanawake wengi hamjatulia, huwa mnaponzwa na tamaa zenu"
"Kwahiyo hata mimi sijatulia?"
"Siwezi jua nyuma ya pazia"
Sabrina akakaa kimya na kujitafakarisha moyoni huku akijua wazi kama Sam atagundua kuwa na yeye ana mimba basi lazima atamuwek a kwenye kundi la wanawake ambao hawajatulia.
Roho yake ikahudhunika na kusononeka, kisha akamwambia Sam
"Tuondoke turudi nyumbani"
"Mbona gafla hivyo Sabrina?"
"Mi dada yako kashaichefua roho yangu, bora twende tu"
"Unataka ukamwambie kaka yako?"
"Lazima nimwambie ndio, huu ni upuuzi kwakweli. Tusije poteza hela ya mahari bure kwa mtu asiyemaana"
"Sabrina mpenzi wangu, usipende kuingilia mambo ya watu. Kama kweli atayashuhudia mwenyewe kwa macho yake, usipende kuwa chanzo cha kuachana kwao"
"Mmh! Unamtetea sana wewe, ila kaka yangu lazima nimwambie"
Sam akamwangalia tu Sabrina bila ya kuongezea neno lolote, Sabrina nae alipoona Sam asemi chochote akainuka na kuanza kuelekea upande ule ambao Joy alielekea na yule kijana.
Sam akainuka na kuanza kumuita Sabrina ili arudi,
"Wee Sabrina, sasa wapi huko jamani. Njoo tuondoke sasa"
Sabrina hakugeuka nyuma, aliendelea kwenda huku akijisemea,
"Kama angetaka tuondoke basi muda ule ule niliomwambia angeinuka ili twende ila yeye kajifanya kiburi, na lazima nikamuharibie dada yake"
Sabrina aliendelea mbele huku Sam akimfata nyuma ili kumuwahi.
Sabrina alipofika kwenye ile nyumba ya kulala wageni na kuingia ndani moja kwa moja, akamuona Joy na yule kijana wakielekea kwenye chumba na kumuita Joy kwa nguvu,
"Eeh Joy nimekuona tena kwa macho yangu, sasa ngoja matokeo"
Joy akarudi nyuma na kumfata Sabrina,
"Jamani Sabrina mbona hivyo? Sina nia mbaya mimi na wala sina mahusiano na yuke kijana, tafadhari nakuomba usimwambie James"
Sabrina akayaiga yale maneno ya Joy kwa kubana pua moja juu,
"Eti tafadhari usimwambie James, nyooo namwambia kila kitu, la sivyo ondoka hapa sasa hivi"
Joy aliondoka bila hata kumuaga yule kijana aliyekwenda naye eneo lile.
Kisha Sam akamvuta mkono Sabrina ili waondoke eneo lile.
Alimvuta hadi kwenye gari yake kisha wakapanda na safari ya kumrudisha Sabrina nyumbani kwake ikawadia.
Walitembea kimya kimya kwenye gari hadi walipofika nyumbani kwa Sabrina.
Walifika, wakafungua mlango na kuingia ndani.
Sabrina akamuita Jeff ila Jeff hakuitika na kumfanya Sabrina atambue kwamba Jeff hakuwepo ndani,
"Umeona hili litoto sasa, limeondoka na kuacha mlango wangu wazi"
Sam akamwambia Sabrina,
"Ila wewe na huyo mtoto mnajuana wenyewe, ngoja nikuache upumzike"
"Haya mpenzi, kwaheri"
"Sawa, najua sasa moyo wako umeridhika"
Kisha Sam akambusu Sabrina kwenye paji la uso na kuondoka.
Kisha Sabrina akaendelea kujitafakarisha alipoenda Jeff,
"Sijui kaenda wapi kwakweli, yani huyu mtoto ananiumiza kichwa sijapata kuona maisha yangu yote."
Akainuka na kwenda kufunga mlango wake na funguo zilizokuwa zikining'inia pale mlangoni ili Jeff akirudi agonge mlango.
Alipomaliza kufunga na kurudi kukaa, akamuona Jeff nae amekaa kwenye kochi, ilibaki kidogo tu Sabrina aanze kupiga kelele.
Jeff akacheka na kumuomba Sabrina amsamehe,
"Inamaana ulijificha humu ndani?"
"Nilifanya hivyo ili yule bamdogo aamini yale maneno yako ambayo huwa unamwambia kuwa mimi situlii nyumbani"
Sabrina alitikisa tu kichwa chake na kusema,
"Kwakweli wewe Jeff wewe sijui hata akili zako zilivyo"
Kisha akakaa chini ili kuweza kuzungumza na Jeff.
"Jeff nakuomba unisikilize haya machache tu ninayotaka kuzungumza na wewe"
"Niambie tu hata usijali"
"Najua unatambua wazi kama umenikosea sana tena sana"
"Natambua hilo, na pia nakiri makosa yangu. Najua inakuwa ngumu kunisamehe ila nakuomba unisamehe"
"Nilishakusamehe Jeff najua ni akili ya balehe ndio iliyokutuma vile, ingawa moyo wangu uliumia sana na kufadhaika, hata sasa naumia ila nilishakusamehe. Lakini naomba unisaidie jambo moja tu"
"Jambo gani hilo?"
"Nakuomba hii mimba ibaki kuwa siri baina yako na yangu, sitaki mtu yeyote yule ajue kuhusu hii mimba. Mie tumbo likijitokeza kiasi hata cha mtoto mdogo kujua, nitawaambia nyumbani kuwa nilibakwa kwahiyo baba mtoto simjui. Tafadhari Jeff naomba iwe siri"
"Inamaana hata huyo mtoto asitambue kamwe kama mimi ni baba yake? Nitaweza kweli? Najua nimetenda dhambi kwako ila yote ni sababu nakupenda ingawa hutaki kukubaliana na upendo wangu kwako"
"Sasa hapo ndipo unaponichefua, tafadhari. Mambo ya kunipenda weka kando na unisaidie kwa hili"
"Mmmh!"
"Usigune Jeff tafadhari, hebu wewe jaribu kukaa katika nafasi yangu na uangalie maumivu niyapatayo. Angalia jinsi walimwengu wakijua ukweli aibu nitakayoipata! Angalia na utafakari Jeff, nimekulea kama mwanangu wa kuzaa kabisa, halafu leo hii jamii igundue nimezaa na wewe, hivi hii sura yangu mimi nitaiweka wapi? Tafadhari Jeff nihurumie, mimi nimekusamehe naomba na wewe unisaidie kwa hili"
Jeff aliamua kukubali ili aweze kumfurahisha Sabrina, na kufanya waingie katika makubaliano ya kufanya hiko kitu kiwe siri siku zote.
"Mimi nimekubali ila kwa sharti moja"
"Sharti gani hilo?"
"Naomba nikae kwako ili niwe nakuona kila siku maana mimi furaha yangu ni kukuona wewe"
"Basi sawa, hilo sio tatizo ila na mimi ombi langu jingine ni kuwa uachane na swala la kutafuta kazi na umalizie kwanza elimu yako sawa!"
"Sawa, ila ningependa kukusaidia katika kulea huyo mtoto"
"Usijali kuhusu hili, najua cha kufanya wala usipate tabu. Ila wewe usome"
Sabrina alimaliza kuongea na Jeff na kushukuru kueleweka kwake ili ile mimba yake na mtoto atakapojifungua ibaki kuwa siri yake na Jeff tu.
Siku ya leo Sabrina alilala akiwa ameridhika moyoni mwake, alijiona sasa anaweza panga mipango mingine kwa ufasaha zaidi ili kuepuka wasiwasi na mashaka yampatayo kila siku.
Kulipokucha siku hiyo, kwavile ilikuwa mwisho wa wiki, Sabrina akajiandaa na kwenda kumtembelea mama yake.
Kama kawaida alimkuta mama yake akiendelea na kazi zake za hapa na pale.
Sabrina akamsalimia mama yake na kuanza kumueleza shida zake,
"Halafu wewe Sabrina uliniambia kuwa una mimba, mbona hukuniambia kama ni ya Sam au la"
"Hicho ndio kitu kilichonileta mama, ni kweli nina mimba ila sitaki umwambie Sam sababu nataka nimfanyie surprise."
"Khee mwanangu kumbe una mimba kweli! Dah kweli Mungu mkubwa sana, na harusi inanukia"
"Ndio mama, ila naona baba anachelewa sana kurudi. Hivi mashangazi hawawezi kuja wao ili wawe na wewe mpokee hiyo mahari mama ili mimi nikaishi kwa mume wangu?"
"Inawezekana, ila inatakiwa baba yako akubali. Sasa kwa ushauri wangu, nenda kwa yule shangazi yako ambaye ni wajina wako, mshawishi yule. Yani yule akikubali tu mambo yametiki, kwakuwa yule anapatana sana na baba yenu"
Sabrina akaona wazi kuwa ushauri aliopewa na mama yake ni mzuri zaidi na akaona ni vyema afanye hivyo ili waweze kuharakisha mambo ya ndoa, ili yafanyike haraka.
"Basi mama naenda leo leo"
"Sawa mwanangu, hakuna tatizo"
Sabrina akamuaga mama yake na kuondoka kuelekea huko kwa shangazi yake.
Alipofika alimkuta shangazi yake akiwa mwenyewe tu na kuona ni afadhari ili aweze kumweleza aliyonayo kwa uhuru zaidi.
Alimsalimia na kuanza maongezi naye, alimwelezea lengo lake na shangazi yake akamuelewa ila akamuuliza,
"Mbona unataka kuharakisha hivyo hiyo ndoa?"
"Si unajua shangazi vijana mambo ni mengi, bora kuharakisha"
"Sabrina wewe una mimba"
Sabrina akashtuka na kumuuliza shangazi yake,
"Umejuaje?"
"Mimi ni mtu mzima Sabrina na nimepitia mambo mengi, nina utambuzi mkubwa sana"
"Ndio nina mimba shangazi ndiomana nataka kuolewa mapema ili nikazalie ndani ya ndoa"
Shangazi akatikisa kichwa kama ishara ya kusikitika na kusema,
"Kweli nimeamini maji hufata mkondo, Sabrina unataka kufanya kitendo alichofanyaga mama yako miaka ya nyuma iliyopita"
"Kitendo gani hicho?"
"Sabrina unataka kumbambika mimba mtu asiyehusika, unajua wazi kabisa kuwa huyo mwanaume anayetaka kukuoa sio muhusika wa hiyo mimba"
Sabrina akashtuka sana na kumuuliza shangazi yake,
"Inamaana wewe unamjua muhusika?"
Shangazi yake akaanza kucheka na kumfanya Sabrina kujawa na wasiwasi.
Sabrina akashtuka sana na kumuuliza shangazi
yake,
"Inamaana wewe unamjua muhusika?"
Shangazi yake akaanza kucheka na kumfanya
Sabrina kujawa na wasiwasi.
Sabrina akamuangalia shangazi yake kwa jicho la aibu huku akingoja jibu ambalo anahisi litamuondolea ujasiri wote, ila shangazi yake aliendelea kucheka tu.
"Sasa mbona unacheka shangazi?"
"Najua umepatwa na mshangao baada ya kujua kuwa mimi najua, natambua wazi unajiuliza kuwa nimejuaje"
"Ndio shangazi umejuaje?"
"Nimekwambia hapa Sabrina, mi ni mtu mzima na nimepitia mengi"
"Kwahiyo unajua hii mimba ni ya nani?"
"Sijui ila nikitaka kujua nitajua tu, napenda nikushauri Sabrina mwanangu"
Sabrina akapumua kidogo huku akimsikiliza shangazi yake,
"Sikia Sabrina, katika maisha kila unachokifanya kina madhara mbele huko. Ingawa huwezi kufikiria kuwa madhara yake ni kitu gani ila kina madhara. Mama yako nae aliwahi kufanya kitu cha namna hiyo huku akiamini kuwa itakuwa ni siri milele, ila siku ilipobumbuluka alitamani hata ajifiche kwenye uso wa ardhi."
Sabrina akapata wazo jipya sasa kuwa mama yake alipatwa na tatizo gani, akatamani sana kujua ingawa na yeye ana matatizo tayari.
"Kwani mama aliwahi kufanya nini?"
"Nenda umuulize yeye mwenyewe, akikataa ndio uje kwangu ila mkumbushe kuwa kila kitu kina madhara chini ya jua ila tu kuna madhara hasi na chanya. Sipendi tumuongelee mama yako hapa bali tuongee kuhusu wewe"
"Sasa shangazi nifanye kitu gani?"
"Mwambie ukweli huyo mwanaume"
"Kheee kila kitu shangazi?"
"Hapo utajua wewe mwenyewe utakavyoyapangilia maneno ila huyo mwanaume ajue wazi kuwa wewe una mimba ambayo sio yake, halafu uamuzi utakuwa juu yake. Kama anakupenda kweli basi atakuoa tu bila kujali chochote"
"Ila shangazi, huyo mwanaume ni mkari sana sijui kama nitaweza"
"Simba mkari lakini anazaa, ukari wake usikutishe sana. Ni kheri umwambie wewe mwenyewe kuliko aambiwe na watu, anaweza akafanya jambo la khatari zaidi. Jivike ujasiri umwambie ukweli"
"Sawa nimekuelewa shangazi, ila usiwaambie watu wengine kuhusu mimba yangu"
"Labda uwaambie mwenyewe, mie hayanihusu"
"Tafadhari usimwambie hata mama"
"Nimekwambia labda uwaambie mwenyewe"
Sabrina akakubaliana pale na shangazi yake kisha akamuaga na kuanza safari ya kuondoka.
Akiwa ndani ya daladala, Sabrina alikuwa na mawazo sana, alikuwa akiwaza namna ya kumwambia Sam huku akijiuliza kama Sam ataweza kumuelewa kweli.
Sabrina alifikiria sana, ila akashtuliwa na mtu wa pembeni kwenye lile gari, mtu ambaye alimuita Sabrina kwa mshangao,
"Sabrina!!"
Sabrina nae akashtuka na kumuangalia yule mtu huku akijaribu kuvuta kumbukumbu kuwa amewahi kumuona wapi, yule mtu akatabasamu na kumfanya Sabrina amgundue kuwa ni nani,
"Kheee kumbe John?"
"Ndio ni mimi, umepotelea wapi Sabrina?"
Wakaanza kupeana khabari mbili tatu huku John kama kawaida yake akitoa vichekesho na kumchekesha Sabrina,
"Khee hujaacha vituko vyako John?"
"Nitaachaje wakati hivi vituko ndio vilifanya nifahamiane na binti mrembo kama wewe"
Wakapeana mawasiliano na John, kisha Sabrina akashuka kuelekea kwao huku akijisemea,
"Yani hawa wanaume jamani uongo wameumbiwa kwakweli, yani huyu John alivyonifurahia leo utafikiri sio yeye aliyeniponda kipindi kile"
Wakati anatembea kuelekea nyumbani kwao akakutana na yule daktari ambaye alienda kwa lengo la kutoa mimba, wakasalimiana kisha yule daktari akamwambia Sabrina,
"Hiyo mimba yako ikifikia kipindi cha kujifungua uje kwenye zahanati yangu nikufungulishe mwenyewe"
"Kwanini umesema hivyo?"
"Nataka nikusaidie Sabrina, na ninakuhakikishia kuwa utajifungua vizuri kabisa"
Sabrina akamuangalia yule docta na kumuaga pale na kuendelea na safari yake huku akijiuliza,
"Kwani nikijifungulia sehemu nyingine nitajifungua vibaya au shobo tu za huyu docta!! Angejua nilivyo na mawazo hapa hata asingeniongelesha"
Sabrina alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake.
"Eeh nipe khabari za huko"
"Ni nzuri tu ila shangazi kanishauri kuwa tumngoje baba kwanza"
Mama yake hakuwa na tatizo kwavile hakujua chochote kinachoendelea, Sabrina akatamani kumuuliza mama yake alichoambiwa na shangazi yake ila akaona kuwa siri yake itakuwa peupe na kuamua kukaa kimya.
Kisha akamuaga mama yake na kuondoka kurudi nyumbani kwake.
Alimkuta Jeff akiwa ndani,
"Hujatoka leo?"
"Si tumekubaliana kuwa nitakuwa nakaa hapa siku hizi au umesahau?"
"Aah mambo mengi kwakweli, kichwa changu kimevurugika sana."
"Na nini tena?"
"Wee acha tu hata kuniuliza acha"
Sabrina akaenda chumbani kwake kupumzika.
Kulipokucha alijiandaa kama kawaida kwenda kazini, na Sam alikuja kumfata kama kawaida.
Walipokuwa ndani ya gari Sabrina akamuuliza Sam,
"Mbona jana hukunitafuta kutwa nzima?"
"Nilitaka na wewe unitafute, kwanini huwa nakutafuta mimi tu?"
"Tatizo ulishanizoe sha hivyo, ila nitaanza na mimi kukutafuta"
Walipofika ofisini, kila mmoja akaendelea na kazi zake kama kawaida.
Kitu pekee kilichomchanganya Sabrina ni ukaribu baina yake na Sam kwani haukuwa ule aliouzoea kawaida na kuanza kujiuliza moyoni,
"Mbona Sam kama amebadilika! Hivi nitaweza kumweleza kweli mmh!!"
Hakupata jibu na kuendelea na kazi zake.
Muda wa kutoka ulipofika, kama kawaida Sam akapanda kwenye gari na Sabrina kwaajili ya kumrudisha nyumbani kwake.
Walipokuwa ndani ya gari, Sabrina aliamua kumuuliza Sam maswali ya kumtega tu,
"Hivi Sam, kwa mfano mke wako akwambie kuwa ana mimba ya mtu mwingine utachukua hatua gani?"
"Una maana gani Sabrina?"
"Nijibu kwanza ndio nikwambie maana yangu"
"Kwakweli mimi nina wivu sana na huwa siwezi kustahimili kwa mtu ninayempenda, niambie kwanza unamaana gani?"
"Hapa nafikiria atakacho kifanya kaka yangu ikiwa ile mimba ya Joy sio yake"
"Kwani umemwambia?"
"Bado sijamwambia, ila nafikiria kwanza kama ikiwa hivyo sijui atachukua hatua gani"
"Inategemea na mtu ila kwa mimi ningechukia sana, tena sana sababu hakuna kitu nisichokipenda kama kusaritiwa kwakweli"
Sabrina akakaa kimya kwa muda kisha akauliza tena,
"Kwahiyo wewe utachukua hatua gani kwa huyo mwanamke?"
"Kwakweli sijui, ila inawezekana ukawa ndio mwisho wetu baina ya mimi na huyo mwanamke kwakuwa sitakuwa tayari kuona nimesaritiwa"
Sabrina alihisi kama moyo ukimuenda mbio hivi kwani uoga ulimjaa na kupitiliza, akaamua kukaa kimya hadi walipofika.
Sam akamuaga Sabrina, kisha Sabrina akashuka na kuingia ndani kwake.
Moja kwa moja alienda kukaa kwenye kochi huku akijiona mawazo kuzidi zaidi yani afadhari ya jana.
Jeff akasogea karibu yake na kumuuliza,
"Nini tena na leo?"
"Sidhani hata kama ndoa itakuwepo tena mbele yangu, najiona kabisa kutokuolewa jamani"
Jeff akamsogelea zaidi Sabrina na kuinua mkono wake na kuuweka kwenye bega la Sabrina, kisha akamwambia kama kwa kumnong'oneza,
"Usijali mamy, nitakuoa mimi"
Sabrina akautoa ule mkono wa Jeff kwenye bega lake na kumfokea,
"Unasemaje wewe? Nyoko weee, kwanza haya yote umeyasababisha wewe firauni mkubwa wewe"
Sabrina akainuka kwa hasira na kwenda chumbani kwake.
Sabrina alifika na kutafuta usingizi, alipokuwa amelala akajiwa na ndoto kuwa amejifungua mtoto wa kiume tena mtoto mwenyewe kafanana kila kitu na Jeff.
Akamuona Sakina pale hospitali akishangaa na kumuuliza,
"Mbona mtoto kafanana na Jeff?"
Sabrina akawa anajiuma uma bila ya kujibu chochote, kisha yule Sakina akamwambia tena,
"Au huyu mtoto ni wa Jeff? Inamaana Sabrina umezaa na Jeff!"
Sabrina akashtuka huku jasho likimtoka, na hakuweza kulala tena kwavile usingizi hakuupata tena.
Alikaa tu na kujitafakarisha kuwa ikiwa hivyo afanyeje ila hakupata jibu lolote.
Alikuwa macho pale kitanda ni hadi panakucha.
Aliinuka na kujiandaa, kama kawaida Sam alipita kwaajili ya kwenda nae kazini.
Siku hiyo ofisini Sabrina hakuwa na raha kabisa kwani muda mwingi alijikuta ni mtu mwenye mawazo na hakujua wa kumshirikisha mawazo yake kwasasa.
Siku zote mshauri wake na mtu wake wa karibu alikuwa ni Sakina, sasa leo hii ataweza kumwambia huyo Sakina kitu kinachomuhusu mtoto wake? Kwakweli hakuweza na ndiomana kichwa chake kilisongwa na mawazo muda wote.
Hadi muda ambao alikuwa anatoka kazini ilikuwa tayari kichwa chake kimechoka na msongo wa mawazo.
Kama kawaida Sam aliondoka na Sabrina na kumpeleka nyumbani kwake.
Sabrina akajifikiria kuwa huenda Sam kuna kitu anakihisi ndiomana amebadilika ila hakujua ni kitu gani.
Muda wote ambao Sabrina anakuwa na mawazo akiwa pale nyumbani kwake basi Jeff anakuwa pembeni yake.
Sabrina alimtazama sana Jeff kisha akamuuliza,
"Hivi kwanini unanitesa hivi?"
"Sikutesi, ila nakupenda"
"Na kwanini unanipenda?"
"Siwezi kumaliza kuelezea, ila nakupenda sana tena sana"
"Kwanini usipende wasichana wa rika yako jamani? Hata kama unapenda watu wazima mbona ni wengi sana huko nje?"
"Naelewa hilo, ila mapenzi ni kama majani huota popote. Mimi yameota kwako"
"Kwenda zako, lione vile"
Akainuka tena kwa hasira.
Akaingia chumbani na kuwaza sana kuhusu Jeff, kuhusu kupendwa na Jeff.
"Kwanini anipende mimi lakini? Kwani wasichana wa rika yake wameisha? Hivi huyu mtoto ana mashetani au ni kitu gani?"
Sabrina alijaribu kuwaza bila ya kupata majibu.
Akajaribu kutafuta usingizi ila hakupata usingizi kabisa kwa siku hiyo, alijikuta tu mawazo yakimrudia kichwani mwake muda wote.
Hadi panakucha yeye bado alikuwa macho tu, akajiandaa na kwenda kazini kama kawaida.
Sabrina alipokuwa ofisini siku hiyo alijikuta akilala kwenye meza ya ofisi na kushindwa kufanya kazi yoyote.
Sam alimuona Sabrina akiwa amelala pale kwenye meza na kumfata,
"Vipi unaumwa?"
Ikabidi Sabrina adanganye kuwa kweli anaumwa,
"Ndio, najisikia vibaya"
"Basi uende hospitali"
"Hapana"
"Basi nenda nyumbani ukapumzike"
Kisha Sam akaenda kumwambia dereva wake ampeleke Sabrina nyumbani,
"Nikitoka ofisini badae nitakuja kukuona"
Kisha yule dereva na Sabrina wakaondoka.
Sabrina alipokuwa nyumbani kwake moja kwa moja alienda kulala na usingizi ulimchukua kabisa.
Jeff alikuwepo mule ndani akiendelea na mambo yake mengine kama kawaida.
Sam naye alipata mawazo kuhusu Sabrina, alimuona kuwa amebadilika sana tofauti na ambavyo alikuwa akimfahamu mwanzoni.
Kwa mawazo yake ya haraka haraka akahisi kuwa lazima kuna mtu anayejua matatizo ya Sabrina na moja kwa moja akamuhisi mtu huyo kuwa Sakina kwavile ndiye msiri pekee wa Sabrina.
Akaamua kutoka pale ofisini na kwenda nyumbani kwa Sakina.
Sakina alishangaa kumuona Sam akifika pale nyumbani kwake na kumkaribisha.
"Vipi leo, kuna tatizo?"
"Hapana, ila kuna kitu nataka unisaidie"
"Kitu gani hicho?"
Sam akaanza kumueleza Sakina kuhusu Sabrina,
"Je kuna chochote unafahamu juu ya Sabrina?"
"Hapana, ila ninachofahamu mimi ni kuwa, Sabrina ni binti pekee kwa kipindi hiki anayeolewa akiwa bado bikra"
"Nalitambua hilo ila Sabrina ana mabadiliko ambayo siyaelewi kwakweli, sijui ana tatizo gani. Nampenda sana, nipo tayari kwa chochote juu yake"
Sam akamuelezea jinsi Sabrina anavyokuwaga na mawazo ofisini, pia akamuelezea jinsi alivyolala ofisini na kusema anajisikia vibaya na alivyokataa kwenda hospitali.
"Sasa mimi ninachokuomba ni kitu kimoja tu, naomba twende wote kwa Sabrina ili ukaongee nae"
Sakina hakukataa, na kwavile alikuwa hana kazi muda huo, akaweza kujiandaa na safari ikaanza.
Sabrina akiwa amelala hoi, akajiwa na njozi iliyomfanya aongee peke yake huku amelala,
" Naogopa mimi, peke yangu naogopa"
Jeff akamsikia Sabrina akilalamika peke yake na kuamua kwenda chumbani kwa Sabrina kumuangalia.
Akamkuta amelala hoi kabisa, Jeff akajisemea moyoni kuwa huenda leo Sabrina anaogopa kulala peke yake ingawa ni mchana.
Akajaribu kumgusa kuwa atashtuka ila Sabrina alikuwa amelala kabisa.
Jeff akakaa pale kitandani karibu na kichwa cha Sabrina na kukivutia kichwa cha Sabrina kwenye mapaja yake, na kwavile Sabrina alikuwa na usingizi sana alilala kama yupo juu mto vile.
Sakina na Sam walifika kwa Sabrina, na walipofungua mlango wakakuta uko wazi wakaingia ndani.
Sakina akamuuliza Sam,
"Sabrina atakuwa amelala eeh!"
"Ndio, aliniaga hivyo"
"Ngoja nikamuangalie kwenye chumba chake"
Sakina akaelekea chumbani kwa Sabrina.
Sakina na Sam walifika kwa Sabrina, na
walipofungua mlango wakakuta uko wazi wakaingia
ndani.
Sakina akamuuliza Sam,
"Sabrina atakuwa amelala eeh!"
"Ndio, aliniaga hivyo"
"Ngoja nikamuangalie kwenye chumba chake"
Sakina akaelekea chumbani kwa Sabrina.
Sakina akaingia moja kwa moja kwenye chumba cha Sabrina na kumkuta Jeff akiwa amesinzia huku kichwa cha Sabrina kikiwa kwenye miguu yake.
Sakina akashtuka kwa kumuita Jeff na kumfanya Jeff naye ashtuke,
"Wee Jeff wewe nini!!"
Jeff akainuka haraka pale kwenye kitanda cha Sabrina huku na yeye akijifanya kushangaa,
"Kwani nini mama? Umekuja saa ngapi?"
Sakina hakumjibu kitu bali aliendelea kumuuliza mwanae,
"Haya ndio maisha mnayoishi humu ndani?"
Jeff naye hakujibu zaidi ya kuendelea kumshangaa mama yake na kumuuliza pia,
"Kwani mama unashangaa nini?"
"Unawezaje kukaa chumbani kwa mama yako mdogo akiwa amelala tena kwa khanga moja na wewe pembeni?"
"Aaah mama na wewe acha zako, haya ni mambo ya kizungu"
"Mambo ya kizungu eeh! Haya niambie huo uzungu unafanya nini humu? Na kwanini umshikilie wakati amelala?"
"Unajua wazi mama kama mamdogo anaumwa, hata sijui unaniuliza vitu gani"
Kisha Jeff akatoka kwenye kile chumba na kumfanya mama yake abaki akiduwaa na kumuangalia hadi alipomalizia kutoka.
Macho ya Sakina yakatua kwa Sabrina sasa ambaye alikuwa yupo hoi na usingizi hata asijue kinachoendelea.
Sakina akakaa pembeni kwa Sabrina ili ajaribu kumuamsha.
Ila alipomuamsha, Sabrina alionekana kufumbua macho na kufumba tena na kumfanya Sakina agundue kuwa Sabrina ana usingizi mzito sana.
Hivyo basi Sakina akaamua kutoka tu nje ya chumba cha Sabrina.
Wakati Jeff anatoka kule chumbani akashangaa kumuona Sam akiwa pale sebleni, ambapo Sam naye alimshangaa Jeff kutokea kwenye chumba cha Sabrina na kumfanya amuulize,
"Kheee kumbe na wewe ulikuwa humo?"
"Ndio, mamdogo anaumwa hivyo anahitaji uangalizi wa karibu"
Halafu akaondoka kwani alijua wazi kama angeendelea kukaa basi kuna maswali ambayo angeshindwa kuyajibu kwa wakati huo.
Sam alitulia tu akimshangaa Jeff hadi muda ambao Sakina alitoka kwenye kile chumba cha Sabrina na kumkuta Sam akitikisa kichwa kama ishara ya kusikitika.
"Vipi tena?"
"Namshangaa huyu kijana wako, alikuwa anafanya nini chumbani kwa Sabrina?"
Sakina aliamua kumtetea mtoto wake,
"Sabrina anaumwa, huyu alimpelekea maji tu ila Sabrina mwenyewe kalala hoi sijui ndio homa hata sijui labda tumngoje usingizi ukimpungua"
"Sawa basi, mi nakuacha hapa nitarudi badae"
"Mmh! Hata mimi wacha niende, nadhani itakuwa vyema kama nikizungumza naye kesho"
Sakina akakubaliana na Sam, kisha Sakina akamuuliza Sam
"Ila nani atamuangalia, wakati anaumwa!"
Sam nae akamjibu,
"Hakuna tatizo Jeff yupo"
Kisha akainuka, na Sakina nae akamfata ili aweze kupata lifti ya kumrudisha nyumbani kwake.
Jeff alibaki mwenyewe sasa na kutoka chumbani kwake kisha kuelekea sebleni huku akiitafakari kauli ya Sam kuwa hakuna tatizo Jeff yupo,
"Huyu jamaa atakuwa ananitegeshea huyu, natakiwa kuwa makini . Sina hakika na kauli yake hii kama kweli imemtoka moyoni"
Jeff aliamua kujiandaa sasa, na umakini wake ukaanzia kwa kufunga milango ili wasiweze kuingia kinyemela.
Usiku ulipoingia, Jeff aliandaa chakula kisha akaenda chumbani kwa Sabrina na kulala pembeni yake ili atakaposhtuka aweze kumwimiza kwenda kula.
Sabrina alishtuka muda ukiwa umeenda sana.
Alikuwa amechoka sana na kuinuka ili ajinyooshe, akaona kuna mtu pembeni.
Alipomuangalia alikuwa ni Jeff, Sabrina akachukia sana na kumkurupusha kwa hasira,
"Hivi wewe Jeff wewe una matatizo gani jamani?"
Jeff akainuka pale kitandani na kusimama,
"Unataka kunitoa roho yangu ndio ufurahi? Hivi nini tatizo jamani? Kwanini wanifanyia hivi wewe?"
Jeff hakujibu kitu zaidi ya kutoka nje ya chumba cha Sabrina na kuelekea sebleni na kumuacha Sabrina akiwa na hasira sana.
Sabrina akainuka na kwenda kuoga kwenye bafu lake.
Jeff akaingia tena kwenye chumba cha Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa ametoka kuoga huku akijifuta futa maji.
Alisimama pale pale mlangoni huku akimuangalia Sabrina, haswaa kwenye maeneo ya tumbo lake huku akilithaminisha lile tumbo kuwa limeanza kukuwa tayari.
Sabrina naye akamuona na kumuangalia, kisha akamuuliza,
"Ushamaliza huo ufedhuli wako wewe mwanaharamu?"
Jeff alimuangalia tu Sabrina bila ya kujibu chochote, kisha Sabrina akamwambia tena,
"Haya ondoka wee mwana mwenye laana"
Jeff akatoka nje na kumuacha Sabrina akiendelea kufanya mambo yake huku akiwaza kuwa ni kitu gani afanye kwa Jeff ili aweze kumuheshimu kwani aliona wazi kuwa heshima baina yao imepotea kabisa.
Sabrina alipomaliza, alitoka chumbani kwake na kwenda sebleni na kumkuta Jeff akiwa amekaa, Jeff naye alipomuona Sabrina akamwambia moja kwa moja kuwa amemuandalia chakula tayari.
Sabrina hakusema chochote zaidi ya kuelekea mezani moja kwa moja ambapo alikaa na kuanza kula.
Kisha Jeff naye akainuka na kumfata Sabrina pale mezani, na yeye akakaa huku akimuangalia Sabrina wakati anakula, Sabrina naye hakuacha kumuuliza,
"Hivyo ndio unaona raha?"
"Ndio, napenda kukutazama"
Sabrina akayarudia yale maneno aliyoyasema Jeff kwa kubana pua, kisha akamwambia,
"Lione vile"
Halafu akachukua glasi ya maji iliyokuwepo pale mezani na kummwagia Jeff yale maji ya kwenye glasi usoni.
Jeff akasononeka sana ila aliendelea kukaa palepale,
"Si ukalale!"
Sabrina akamwambia Jeff, mara gafla wakasikia mtu akikohoa kwenye dirisha mojawapo la ile sebule na kugundua kuwa kuna mtu dirishani.
Jeff akainuka na kwenda kuchungulia dirishani ila hakuona chochote.
Sabrina akamuuliza,
"Ni nani?"
"Sijui, sijamuona mtu yeyote"
"Mmh nishaanza kuogopa tayari"
"Usiogope mamy, mi nipo nitakulinda wala usijali"
Sabrina akamuangalia Jeff kwa muda huku Jeff akimuashiria kuwa aendelee kula asiwe na shaka la aina yoyote ile.
Sabrina aliendelea kula huku moyo wake ukiwa umejawa na hofu kubwa sana.
Alipomaliza kula, alienda chumbani kwake na kufunga vizuri madirisha yake ya kioo na kufunika vizuri mapazia yake ili asiwe na wasiwasi, kisha akamuita Jeff na kumwambia,
"Ukisikia napiga makelele uje, Sawa eeh!"
"Sawa, hakuna tatizo"
Kisha Jeff akatoka mule chumbani kwa Sabrina na kuelekea chumbani kwake kujilaza.
Muda wote huo ni Sam ndiye alikuwa kwenye dirisha la sebleni kwa Sabrina, alitaka kujua kuwa ni mambo gani ambayo Sabrina hufanya na Jeff wakiwa peke yao wawili tu, ila kitendo cha kumuona Jeff akienda chumbani kwake kulala kirimridhisha na kuondoka eneo lile na yeye kurudi nyumbani kwake.
Huku akimtafakari Sabrina na Jeff, tena ikawa vyema yeye kwenda muda wapo sebleni sababu ingekuwa ni kule chumbani basi Sam angekuwa amepata khabari nyingine juu yao.
Jeff muda mwingi aliutumia kumfikiria Sabrina tu.
Ukaribu ule wa yeye na Sabrina ndio pekee aliokuwa akiuhitaji bila kujali kitu chochote hata kama Sabrina atamfanyia visa mbali mbali ila kwake aliona kuwa ule ukaribu unamtosha kabisa.
Kulipokucha, Sabrina aliamka kama kawaida na kujiandaa ili kwenda kazini ila akashangaa Sam akikawia kuja kumchukua.
Alitoka sebleni na kukaa, aliinuka na kufungua mlango ili kujaribu kuangaza ila hakuona dalili yoyote ile ya Sam.
Akarudi tena kukaa huku akijiongelesha,
"Sijui niende tu mwenyewe, dah mazoea yana tabu"
Akatokea Jeff na kudakia,
"Mazoea yana tabu kweli"
"Nini na wewe sasa?"
"Bora na mimi ningenunua gari tu ili niwe nakupeleka huko ka....."
Kabla hajamaliza, Sam naye akaingia muda huo huo na kusema,
"Sio kazini tu, bali kila sehemu atakayotaka kwenda"
Kisha akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Haya twende sasa"
Sabrina hakusema chochote cha ziada, zaidi ya kuinuka na kufatana na Sam kwa nyuma.
Walipokuwa ndani ya gari, Sam akayaanzisha maongezi kwa kumuuliza maswali Sabrina,
"Eeh niambie Sabrina, unampenda sana Jeff eeh!"
Sabrina akashtuka na yeye kuuliza,
"Kwanini umeniuliza hivyo?"
"Nimekuuliza sababu kuna kipindi ulimfukuza ila kwasasa umemrudisha tena nyumbani kwako"
"Nimemuonea huruma vile alivyokuwa akitafuta kazi, ndiomana nimemuweka kwangu ili asome"
"Kwani mtu akikaa kwako ndio anapata uwezo wa kusoma?"
Sabrina akakaa kimya na kumfanya Sam aongee tena,
"Nijibu Sabrina"
Simu ya Sabrina ikaita na kumfanya aipokee huku akishukuru kwani aliona ndio njia bora ya kukimbia maswali ya Sam.
Mpigaji alikuwa ni Sakina ambaye alimuulizia Sabrina hali yake kisha akamuomba kuwa badae waonane, Sabrina hakuwa na kinyongo na kukubali wito.
Simu ilipokatika, Sam akamuuliza Sabrina,
"Nani huyo uliyekuwa ukiongea naye?"
"Ni Sakina, anahitaji badae tuonane"
"Sawa hakuna tatizo, mimi nitakupeleka"
"Mmh"
"Sasa unaguna kitu gani?"
"Hamna kitu, nimekubali"
Safari ikaendelea hadi ofisini, na kufika huku kila mmoja akiendelea na shughuli zake za pale.
Kisha Sam akaenda kumuaga kidogo Sabrina kuwa anaenda kufatilia mambo yake huko nje na kumuacha pale ofisini.
Sabrina pale ofisini, akawasikia wale wafanyakazi wenzie wakiongea,
"Jamani, zamani bosi alikuwa hakai kwenye jiji hili, kidogo tu anasafiri. Maskani yake kubwa ilikuwa ni Arusha, sasa siku hizi kulikoni?"
"Mmh jamani, mambo ya Ngoswe hayo mwachieni Ngoswe"
Wote wakacheka, kisha mwingine akasema,
"Funika kombe jamani mwanaharamu apite, mi simo hapo"
Wa kwanza akadakia,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bwana eeh wangapi walikuwa kama yeye na kufanywa kama yeye na wamepita"
Wote wakacheka, Sabrina akachukia na kujua wazi anasemwa yeye.
Akainuka pale kwenye kiti na kutoka nje ya ofisi huku akiwa amejawa na hasira kifuani.
Alitamani hata asingefika ofisini siku hiyo kwani roho ilimuuma sana.
Sam aliporudi alimkuta Sabrina akiwa pale nje.
"Vipi tena, hapo nje"
"Nimeona nipigwe na jua kidogo"
"Halafu wewe Sabrina bado unaumwa ila ni mbishi tu kwenda tena hospitali kupima. Nikupe dereva akupeleke?"
"Hapana, nitakuwa sawa tu."
Kisha akarudi ofisini.
Sam nae hakumuelewa Sabrina kuwa ni kitu gani kinamsumbua zaidi ya kusikiliza anachosema yeye tu kuwa haumwi.
Muda ulipofika, kama kawaida Sam alitoka na Sabrina ila leo safari ilikuwa moja tu nayo ni kwenda nyumbani kwa Sakina.
Walipofika, walimkuta Sakina akiendelea na mambo ya hapa na pale, wakamsalimia kisha Sam akawaaga na kumuacha pale Sabrina na Sakina.
Sakina hakutaka kupoteza muda zaidi ya kuanza maongezi yake na Sabrina, akamuelezea kama jana yake alienda pale kwake na kumkuta akiwa amelala kabisa.
"Ila Sabrina naomba unieleze jambo hili kwanza"
"Jambo gani hilo?"
"Nyie mule ndani mnaishi vipi na Jeff?"
"Tunaishi kawaida tu, kwani vipi?"
Sakina akamueleza jinsi alivyowakuta chumbani na jinsi Jeff alivyomjibu, kisha Sabrina nae akacheka na kumwambia Sakina,
"Mbona ni mambo ya kawaida tu hayo dada, ndio uzungu huo"
"Mmh kuwa makini, mtoto kakua yule"
"Sio tatizo dada, Jeff hawezi kunifanya chochote mamake mdogo mie"
Sabrina aliongea huku akicheka na kuumia kwa lake moyoni kwani alijua wazi kama akisema basi atadharaulika.
Sakina hakuacha kumuuliza Sabrina kuhusu alichoagizwa na Sam,
"Kwani Sabrina una matatizo gani? Niambie mimi, kumbuka mimi ndio mtu wako wa karibu Sabrina"
"Mbona sina matatizo dada"
"Ya kweli hayo Sabrina? Unanificha hadi mimi! Utamwambia nani sasa?"
Sabrina alikaa kimya huku akimuangalia Sakina aliyeonyesha kuwa na hamu kubwa sana ya kujua kinachomsumbua Sabrina.
Alijitahidi kumbembeleza ila Sabrina hakutaka kusema ukweli na kumfanya Sakina akubaliane nae kuwa hana tatizo lolote lile.
Sakina akaongea mambo mengine na Sabrina kisha Sam akaenda kumfata Sabrina na kupita nae kwao kusalimia kidogo kisha wakaondoka.
Sabrina alikaa nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana, aliwaza kuhusu pale kazini na kuhisi kuwa mambo yataharibika endapo akigundulika kuwa ni mjamzito tena ujauzito ambao sio wa Sam.
Alijua wazi itakuwa ni kashfa nzito kwake na anaweza kufukuzwa kazi muda wowote ule na kufanya maneno ya wale wadada kutimia kuwa wengi walikuja na wamepita.
Akaamua kufanya mashauri katika kichwa chake.
Kesho yake alipokuwa ofisini, alienda moja kwa moja kwenye ofisi ya Sam na kumpa barua.
"Vipi tena Sabrina, barua ya nini hii?"
Sabrina akamwambia Sam,
"Isome tu utaona"
Sam akaisoma na kumshangaa Sabrina,
"Unataka kuacha kazi Sabrina? Kwanini?"
"Nimeamua tu"
Sam akamuangalia sana Sabrina, kisha akamwambia
"Mimi najua sababu"
Sabrina akamshangaa Sam na kumuangalia tu, kisha akamuuliza
"Sababu ipi hiyo?"
Sam akainuka na kuzunguka alipo Sabrina, kisha akainama na kushika tumbo la Sabrina kisha akamwambia,
"Hii ndio sababu"
Sabrina akashtuka na kushangaa.
Sam akainuka na kuzunguka alipo Sabrina, kisha
akainama na kushika tumbo la Sabrina kisha
akamwambia,
"Hii ndio sababu"
Sabrina akashtuka na kushangaa.
Sabrina akaogopa hata kumtazama Sam usoni kwa jinsi alivyokuwa akijihisi aibu na uoga, kwahiyo akainamisha kichwa chake chini na kumfanya Sam amuulize,
"Mbona hivyo Sabrina? Mbona umepooza gafla?"
Sabrina akaongea huku akitetemeka,
"Naomba ruhusa nikapumzike nyumbani kidogo"
"Ruhusa nakupa ila kazi huachi hapa, nenda ukapumzike nyumbani na ujifikirie kuhusu hili swala."
Sabrina akainuka na kuondoka, kisha Sam akamwambia dereva wake kuwa ampeleke Sabrina nyumbani.
Sabrina alipofikishwa nyumbani kwake alikuwa na wazo moja tu kwani alijua wazi kwa vyovyote vile Sam kaujua ukweli kuwa ana mimba na anaweza kumfanyia kitu kibaya kwa wakati wowote ule.
Akaingia chumbani kwake na kupakia baadhi ya nguo zake kwenye begi ili aondoke kabisa na asionane na Sam kwa kipindi hiko.
Alipomaliza kupakia nguo zake, akampigia simu dereva wa gari ya kukodi ili aende kumchukua.
Dereva alipofika nyumbani kwa Sabrina akamshtua kwenye simu ili aweze kutoka nje ya nyumba yake.
Wakati Sabrina anatoka ndani, akakutana mlangoni na Jeff,
"Vipi mamdogo unaenda wapi na mabegi?"
"Nitakupigia simu nikwambie"
Sabrina akatoka na kuifata ile gari na kumuacha Jeff akiwa mlangoni anamshangaa.
Sabrina akapanda kwenye gari na kumuacha Jeff akimuangalia tu huku akijiuliza kuwa anaenda wapi, na kwa mawazo ya haraka haraka akahisi kuwa kuna safari anaenda na safi,
"Ila mbona kaondoka na tax?"
Hofu ikamshika Jeff na kumfanya kukariri namba za ile gari.
Sabrina aliamua kwenda mbali ili kuepukana na janga lile, aliona kamavile dunia imemuelemea peke yake.
Aliumia moyoni ila alihisi yupo Sahihi kwa jambo aliloamua siku hiyo.
Kwavile alikuwa na pesa kidogo ya akiba akaamua kwenda kukaa hotelini kwanza.
Sam alipotoka ofisini moja kwa moja alienda nyumbani kwa Sabrina kumuangalia.
Alipofika alimkuta Jeff akiwa peke yake na kumuuliza alipo Sabrina.
"Hata mimi mwenyewe sielewi, nilijua umeondoka naye"
"Halafu wewe dogo usiniletee khabari zako, hebu niambie vizuri Sabrina yuko wapi?"
"Kiukweli sijui alipo"
"Siku ile uliniambia hivyo hivyo halafu kesho yake Sabrina nilimkuta akilia tu hapa, usifikirie sikumbuki ujinga wako na watu wako. Hadi leo Sabrina simuelewi, na unabahati sina hakika na ninachokihisi. Haya niambie upesi alipo Sabrina"
Jeff akamshangaa Sam na kukazia jibu lake kuwa hajui alipo Sabrina.
Gafla Sam akamkunja Jeff na kumpiga ngumi ya sura huku akikazana kuambiwa alipo Sabrina kwani alijua wazi Jeff anajua kila kitu kuhusu Sabrina.
"Unanionea tu brother, mi sijui alipo. Nilimuona tu akiwa amebeba begi lake na kuondoka, mi nikajua anasafiri na wewe"
"Unajua wewe dogo usinichanganye kabisa, yani wewe umuone Sabrina anaondoka na begi halafu asikwambie wewe!! Ni jambo ambalo haliniingii akilini kabis a"
Kisha Sam akiwa vilevile kamkunja Jeff, akachukua simu yake na kumpigia mama yake na Sabrina ili kujua kama yupo nyumbani kwao.
Ila mama wa Sabrina akamwambia kuwa Sabrina hajafika nyumbani kwao tangu walipopita jana kuwasalimia.
Sam akapatwa na mashaka zaidi na kuzidi kuhisi kuwa Jeff lazima anapajua alipo Sabrina.
"Siku ile mambo yalikuwa hivi hivi, wewe dogo lazima unajua alipo Sabrina wewe. Na leo usiponiambia alipo nafumua huo ubongo wako ili unijue vizuri mimi ni nani"
Jeff alikuwa akitetemeka tu kwani Sam alioneka kuwa na hasira na kumaanisha maneno aliyokuwa akiyasema na kumfanya ashindwe hata kujibu,
"Sema alipo alipo Sabrina wewe"
"Sijui"
Sam akazidi kuchukia na kumnasa kofi la nguvu Jeff hadi akajihisi kupepesuka huku akiombea muujiza wa Mungu utokee.
Ikabidi amtajie Sam aina ya gari ya kukodi aliyopanda Sabrina na namba ya ile gari.
"Kumbe ulikuwa unajua, sasa naenda kumtafuta huyo dereva ila na wewe ujipange kwani moyo wangu bado unaniambia kuwa unapajua alipo. Na siku nikigundua kuwa ulikuwa unapajua halafu unanificha, nakuapia siku hiyo utaisalimia ardhi"
Sam akamsukumia Jeff kwa chini na kuondoka zake.
Jeff alipoinuka pale akaona sio mahali sahihi tena kwa yeye kuendelea kuwepo.
Akaenda chumbani kwake, akapakia nguo zake baadhi kwenye begi lake la mgongoni na kuamua kuondoka pale nyumbani kwa Sabrina ili Sam akirudi tena akute tu milango imefungwa na hakuna watu.
Akapata wazo la kwenda nyumbani kwao ila bado akaona kuwa sio sehemu salama kwake kwani Sam anapafahamu mwanzo mwisho.
Akaona ni vyema kwa usiku huo akalale kwa rafiki yake kwanza ili kesho yake ajipange na kitu kingine cha kufanya.
"Dah huyu Sabrina kanipa mtihani mkubwa sana, ila hata hivyo na mimi nahusika kumpa yeye mitihani kwahiyo nijilaumu mwenyewe."
Akaendelea na safari yake.
Sabrina alienda Bagamoyo na kujich imbia mahali palipojificha kidogo ili kuwa huru na mambo yake na pia kuutuliza moyo wake.
Akatamani kumwambia mama yake alipo ila alijua wazi kwa vyovyote vile mama yake atamshauri kuwa arudi nyumbani, akaona ni vyema kutulia huko kwa siku kadhaa ili kupunguza mawazo aliyokuwa nayo.
Aliwaza pia kumwambia Sakina ila alijua wazi Sakina atamwambia ukweli Sam, pia aliogopa kumwambia Jeff kwani alijua wazi kwamba akibanwa lazima atasema ukweli wa mambo.
Sabrina aliamua kukaa pale bila ya mawasiliano na mtu yeyote yule huku akiamini kuwa hiyo ndio njia pekee ya yeye kuepukana na matatizo yanayomsonga kwa kipindi hiko.
Sam alipoona kuwa hata Jeff nae ameondoka akajua wazi ni mchezo wamemfanyia,
"Yani haka kajeff haka nikikashika katanieleza vizuri, haiwezekani nisumbuliwe akili na katoto kadogo kama kale"
Sam aliona kazi haifanyiki na kuamua kwenda tena kumtafuta gari aliyoelekezwa kuwa Sabrina alipanda wakati wa kuondoka.
Jeff aliona vyema asafiri kidogo na kwenda mji wa karibu ili kuepukana na hayo majanga hadi pale atakapowasiliana na Sabrina.
Akampata rafiki yake aliyekuwa Bagamoyo na kuona kuwa ni sehemu salama na isiyo na gharama kwa yeye kwenda.
Kwahiyo akaondoka na kwenda huko.
Sakina alienda nyumbani kwa mama yake na Sabrina kumuulizia vizuri.
"Hivi Sabrina yuko wapi maana nimeulizwa sana na kukosa jibu"
"Mi hata sielewi kwakweli, sijui ni kitu gani hadi mimi mama yake nisijue alipo"
"Khee makubwa, eti hadi Jeff anayekaa naye hajui alipo, jana nimemuuliza"
Wakabaki kushangaa na kumfanya Joy ajaribu kuwauliza baadhi ya ndugu zao kama Sabrina ameenda kwao ila hawakupata jibu lolote kwani kila mmoja hakujua alipo Sabrina.
"Kwakweli nachoka, sijui baba yake nikimwambia atachukua hatua gani."
"Ila ni bora umwambie tu kuliko kukaa kimya"
Joy akachukua simu yake ili ampigie mumewe, ila kabla hajapiga, ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake kutoka kwenye namba mpya, Joy akaufungua na kuusoma,
"Usiwe na wasiwasi mama, mimi nipo salama na sehemu salama. Nikipata muda wa kutosha nitakupigia ili tuongee vizuri. Sabrina."
Joy akamuangalia Sakina na kubaki kimya kwani hata cha kusema walikosa.
Sam alimtafuta yule dereva hadi akampata na kuamua kumuuliza, akamuelekeza kuhusu Sabrina na mahali alipoenda kumchukua
"Aaah huyo dada ni rafiki yangu sana"
"Eeh niambie ulimpeleka wapi?"
"Mi nilimpeleka stendi tu, aliniambia kuwa kuna mahali anataka kwenda"
"Ndio nataka kujua huko mahali ni wapi?"
"Mi sijui, ila kuna muda nilimsikia kuwa anataka kwenda Bagamoyo"
"Basi sawa, nashukuru kwa ushirikiano wako"
Kisha Sam akaondoka ili akajipange namna ya kumpata Sabrina kwani alihisi akili yake kuchanganyikiwa kabisa.
"Yani huyu Sabrina huyu, sijui hata kwanini ananitesa kiasi hiki"
Sam alikuwa akijisikitikia tu muda wote.
Jeff alifika salama nyumbani kwa rafiki yake ambaye aliamua kuanzisha maisha yake huko na alijulikana kwa jina la Shebby,
"Naona wewe kusoma tena basi"
"Nimeona akili za darasani sina ila za maisha ninazo ndiomana nikaona ni vyema nianzishe maisha tu. Msome nyie Jeff sababu akili hiyo unayo"
Jeff akacheka tu na kufurahia uamuzi wa rafiki yake kwani aliona kuwa ameamua vyema kuliko yeye anayezidi kujipotezea muda.
"Kesho nitaenda kukutembeza kwenye mashamba yangu ili uone jinsi kilimo kwanza kilivyofanya kazi juu yangu"
"Hongera sana"
Wakaongea mengi bila ya Jeff kumwambia rafiki yake kitu ambacho kimemkimbiza mjini.
Joy akiwa nyumbani kwake, akatembelewa na mkwe wake ambaye alikuwa wajina wake kwani na yeye aliitwa Joy.
Walisalimiana pale na kuongea mambo mbali mbali,
"Halafu wewe unaonekana una mimba wewe"
Joy akacheka na kumjibu mkwe wake,
"Ndio nina mimba, ndiomana nimek uja kukutembelea ili nikupe hii taarifa"
"Hongera sana mwanangu, najua utaniletea mtoto wa kike hapo, si unajua huku una wifi mmoja tu"
Joy akafurahi sana,
"Imebaki ndoa tu mama"
"Hilo swala halina tatizo, yani hivi karibuni mambo yote yatatimia na tutacheza chereko hapa"
Wakafurahiana pale kisha akaaga na kuondoka.
Sabrina alikuwa amejichimbia mahali ambako hapakuwa rahisi kwa mtu yoyote yule kupajua.
Alifika sehemu hiyo na kupanga chumba cha kuishi kwa muda mfupi kwani bado alikuwa na malengo yake mengine.
"Maisha yangu yameharibika, nayaona kabisa yakiteketea kwasababu ya kidudu mtu kimoja tu. Yani huyu Jeff huyu, ingekuwa amri yangu ningekapoteza kabisa kwenye macho yangu. Ila ubaya ni kuwa siwezi kumfanyia hivyo, namuhurumia sana. Siwezi kumfanyia vibaya ingawa ameharibu maisha yangu"
Sabrina alikosa raha na alikuwa akisikitika muda wote, aliona wazi kuhangaika na maisha.
Aliona wazi tabu atakazo zipata kwani hana kazi na mtu wa kumweka mjini ndio huyo Sam anayemuogopa.
Kulipopambazuka, Sam kama kawaida akajiandaa na kwenda ofisini ila hakukaa sana na kuwaaga kuwa atakuwa safarini kwa muda wa siku tatu na kuondoka.
Safari yake ilikuwa ni kwenda Bagamoyo ili akamtafute Sabrina kwa gharama yoyote ile,
"Na kama nikijua kuwa kuna mwanaume anayesumbua akili ya Sabrina au aliyemshauri Sabrina kuwa atoroke basi mwanaume huyo atakuwa halali yangu. Haiwezekani mtu mzima kama mimi kusumbuka kila siku usiku na mchana kuitafuta roho yangu halafu nilikute jamaa limetulia nae tu"
Sam alisafiri na gari yake huku kichwa chake kikimuwaza Sabrina tu.
Jeff alichukuliwa na rafiki yake Shebby na kwenda kumtembeza mashambani na kumfanya Jeff kuifurahia mandhari ya Bagamoyo.
"Ila Jeff hujaniambia mwana, ni madili gani yamekuleta huku?"
"Mi nimekuja kutembea tu sina cha madili wala kitu chochote"
Muda wote Jeff alikuwa na mawazo yake ila hakupenda kumuonyesha rafiki yake kama ana mawazo yoyote.
Sam alifika Bagamoyo na kuanza shughuli yake ya kumtafuta Sabrina siku hiyo hiyo ambapo aliwapa watu baadhi picha ya Sabrina ili wamsaidie kumtafuta Sabrina.
Ila siku hiyo ikapita bila ya kupatikana kwa Sabrina na kumfanya Sam kuanza kujipa imani kuwa kesho nayo ni siku.
Kulipopambazuka asubuhi na mapema, Sam akaianza kazi yake ya kumtafuta Sabrina.
Ila siku hiyo pia alitafuta hadi giza likaingia ila Sabrina hakupatikana na kumfanya Sam apandwe na hasira mara dufu kwani alimpenda sana Sabrina.
Ilikuwa ni hivyo hivyo kwake, kila kunapokucha anazama mtaani na picha za Sabrina huku akiwaahidi vijana kuwapa zawadi nono kwa yeyote atakayefanikisha kumpata Sabrina.
Jeff alizoea kiasi maisha ya pale Bagamoyo na siku hiyo akamuaga rafiki yake kuwa anaenda kutembea tembea kidogo.
Jeff alienda ufukweni kupunga upepo kidogo ili kupunguza mawazo yaliyokuwa yakimsonga.
Alipokuwa ufukweni, alimuona mwanamke akiwa amekaa chini na kuonyesha kuwa alikuwa na mawazo, alipomtazama vizuri akagundua kuwa ni Sabrina.
"Dah, Sabrina kumbe alikuja kujificha huku"
Jeff akaamua kumfata.
Sabrina alikuwa ametulia huku akiwaza, kubwa aliloliwaza kwa muda huo ni mimba yake. Akajikuta akijisemea,
"Mwanaume yoyote kati ya wale wanaosema wananipenda, akiwa wa kwanza kugundua mimi nilipo basi ni wazi ndiye atakuwa mume wangu"
Gafla akashikwa bega, kugeuka na kumuangalia alikuwa ni Jeff,
"Kheee Jeff!! Wewe mtoto mwanga nini?"
Jeff akaenda mbele ya Sabrina na kuchuchumaa pale huku akimuangalia Sabrina usoni.
Kabla hawajaongea chochote, Sabrina akamuona Sam akiwa nyuma ya Jeff tena na bastora mkononi.
Jeff akaenda mbele ya Sabrina na kuchuchumaa
pale huku akimuangalia Sabrina usoni.
Kabla hawajaongea chochote, Sabrina akamuona
Sam akiwa nyuma ya Jeff tena na bastora mkononi.
Sabrina akafanya kitendo kwa haraka kwa kwenda mbele ya Jeff na kumwambia Sam,
"Kabla hujafanya chochote kwa huyu, niue mimi tafadhari"
Sam hakujibu zaidi ya kushusha bastora yake chini, kisha bila ya kuongea chochote akaanza kuondoka eneo lile.
Sabrina akajua wazi kuwa amemchukiza Sam kwa kitendo chake cha kumtetea Jeff ila asingeweza kumuacha Jeff ateseke mbele ya macho yake ndiomana akafanya vile.
Akainuka pale mbele ya Jeff na kuanza kumfata Sam kwa nyuma huku akimuita, Jeff alijikuta tu akiduwaa kwani hakujielewa kabisa kwa wakati huo.
Sabrina alipozidi kumsogelea Sam kwa kumuita, ikabidi ageuke nyuma ili aweze kumtazama vizuri na kumsikiliza, kisha akamuuliza,
"Kwani unasemaje?"
"Usichukie hivyo Sam"
"Kwahiyo unataka nifurahie huu upuuzi wa wewe kukimbia na Jeff na kumuona Jeff ni wa muhimu sana kushinda mimi"
"Hapana Sam"
"Hapana nini? Unataka nikufanyie nini Sabrina?"
Sabrina akainama chini kwa aibu, kisha Sam akamuuliza tena
"Hivi ni mwanaume gani anayeweza kukubaliana na ujinga unaoufanya Sabrina? Ni mangapi nimekufanyia? Eti leo ndio unanilipa kwa stahili hii Sabrina!"
"Nisamehe Sam tafadhari"
"Hiyo nisamehe haina nguvu yoyote ile, labda utakapokubali turudi wote nyumbani tena nyumbani kwangu ndio nitakubaliana na hiyo nisamehe yako"
Sabrina akainama na kujifikiria kidogo, kisha akakubaliana na Sam huku akiuambia moyo wake kuwa liwalo na liwe,
"Sawa, nimekubali Sam"
Sam akatabasamu kidogo, kisha akamshika mkono Sabrina na kuondoka naye.
Jeff bado alikuwa eneo lile lile akiwatizama.
Sabrina alipofika mbele kidogo akasita na kumfanya Sam amuulize,
"Vipi mbona umesita?"
"Nina ombi moja Sam"
"Niambie, ni ombi gani hilo?"
"Naomba tuondoke na Jeff pia"
"Kwani huku alikuja na nani?"
"Peke yake"
"Basi na ataondoka peke yake"
"Mbona mimi nilikuja peke yangu ila naondoka na wewe!"
"Hivi Sabrina, akili yako ni nzuri kweli? Unajua wazi kuwa nilitaka kumfaya nini huyo Jeff halafu unaniomba tuondoke naye. Umejifikiria kweli hiko kitu?"
Sabrina akainawa tena chini, kisha akainua macho na kumtazama Jeff katika eneo alilomuacha na kumuona kuwa yupo pale pale, kisha akageuza tena macho na kumuangalia Sam na kumwambia,
"Tafadhari Sam tafadhari nakuomba"
Sam akaamua kukubali kwa shingo upande ili aweze kuwa karibu na Sabrina.
Kisha wakamuita Jeff ili waweze kuondoka.
Ila Jeff hakusogea walipo, ikabidi Sabrina amfate Jeff na kumuomba waondoke,
"Hapana, sitaki matatizo"
"Hawezi kukufanya chochote Jeff, tafadhari niamini mimi"
Sabrina akajitahidi kumbembeleza Jeff na mwisho wa siku Jeff akakubali kuondoka nao.
Wakiwa njiani, Sam akaamua kuuvunja ukimya na kuanza kumuuliza Jeff maswali,
"Mbona ulikuwa unanificha sasa wakati ulikuwa unajua Sabrina alipo?"
"Hapana, sijakuficha na wala nilikuwa sijui chochote"
"Kama ulikuwa hujui, mbona nimekukuta nae?"
Ikabidi Sabrina aingilie kati yale maswali.
"Ukweli wa mambo naujua mimi Sam na wala sio huyo Jeff, niulize mimi ndio nikueleze mambo yote"
Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Natambua kwamba ukweli wa mambo yote unao wewe Sabrina, ila nilikuwa na maana yangu kabisa kumuuliza Jeff"
Kimya kifupi kikatawala na safari ikaendelea.
Walipofika maeneo ya mjini, Sam akasimamisha gari mahali ili waweze kupata chakula kidogo kisha waendelee na safari.
Wakati wanasubiria chakula walichoagiza, Sabrina akamuaga Sam kuwa anaenda maliwatoni, ila Sam aliamua kumsindikiza Sabrina ila naye hakupinga chochote kile.
Alipokaribia kufika maeneo ya maliwatoni, akakutana na rafiki yake ambaye alikutana naye zamani sana, ambapo walishangaana na kusalimiana,
"Kheee Sabrina umenawiri kiasi hicho! Hongera sana"
Kisha akamgeukia Sam na kumwambia,
"Hongera sana , naona mambo mazuri"
Huku akimuangalia Sabrina tumboni na kumfanya Sabrina atambue moja kwa moja kuwa rafiki yake anamaanisha kitu gani.
Ikabidi akatishe yale maongezi kwa kujichekelesha na kumwambia rafiki yake,
"Mage, tutaongea vizuri badae. Ngoja tupeane namba"
Kisha akampa rafiki yake yule namba zake za simu na kumuaga, akamgeukia Sam na kumshika mkono ili waendelee na mambo mengine.
Jeff alikuwa ametulia pale kwenye meza huku akingoja huduma na pia akiwangoja wakina Sabrina warudi.
Akapita dada mmoja na kumtazama Jeff, akagundua kwamba wanafahamiana, kisha yule dada akasogea pale karibu ili kumsalimia Jeff,
"Khabari Jeff"
"Khee Dorry!"
Kisha Jeff akainuka pale alipo na kukumbatiana na Dorry.
Kile kitendo cha wao kukumbatiana kilionwa na Sabrina ambaye alikuwa akitoka maliwatoni na kujikuta akichukizwa na kile kitendo.
Yule Dorr akakaa kwenye moja ya viti vya pale huku akiendelea kuzungumza na Jeff bila wasiwasi wa aina yoyote.
Sabrina alipofika pale akamwambia Jeff,
"Tuondoke"
Jeff akashangaa kwavile Sabrina hata hakutaka kumsalimia yule binti aliyekuwa pale pembeni ya Jeff, hata Sam nae alionekana kumshangaa Sabrina kuwa imekuwaje kachukia vile tena gafla tu, Jeff akamuuliza Sabrina kwa mshangao,
"Kheee mamdogo, si tumeagiza chakula hapa au mmeahirisha?"
Huku Jeff akigeuza macho na kumtazama Sam ambaye alikuwa moja kwa moja akimtazama Sabrina,
"Haya, nyie kaeni mle mi naondoka"
Halafu akageuka na kuanza kuondoka. Ikabidi Sam amfate nyuma huku akimuita,
"Wee Sabrina"
Sabrina akageuka nyuma ila moja kwa moja macho yake yakatua kwenye ile meza aliyomuacha Jeff na kumuona bado yupo pale pale na yule binti na kumfanya Sabrina apandwe na hasira maradufu.
Sam alipomsogelea akamuuliza,
"Una matatizo gani Sabrina? Mbona sikuelewi jamani?"
"Niache Sam niondoke zangu"
"Uondoke zako uende wapi na chakula tumeshaagiza? Huoni kama unawatia hasara hawa wenye hoteli?"
"Basi cha kwangu kibebe nitaenda kula kwenye gari yako ila hapo siwezi kukaa tena"
"Basi hakuna tatizo, ngoja nikamwambie atufungie wote. Sipendi uwe mpweke Sabrina, kumbuka nakupenda sana"
Kisha Sam akamsogelea zaidi Sabrina na kumbusu kwenye paji la uso halafu akamuongoza hadi kwenye gari na kumuacha humo halafu yeye akarudi kwa wahudumu.
Alipotoka kwa wahudumu, akampitia Jeff na kumwambia waondoke ila Jeff nae hakupinga zaidi ya kuagana na yule binti kisha wakaondoka hadi kwenye gari.
Walipokuwa kwenye gari, Sam akamwambia Jeff,
"Mamako mmdogo katupa sharti moja la wote kula kwenye gari hata sijui ana matatizo gani. Vipi wewe Jeff unayajua matatizo yake?"
Jeff akatikisa kichwa kuwa hajui huku akicheka na kumfanya Sabrina achukie zaidi na kugoma kula kabisa,
"Mamdogo Samahani, si kwamba nakucheka wewe. Nisamehe tafadhari"
Ila Sabrina alikaa kimya na huku akionyesha hasira muda wote.
Ikabidi Sam aanze sasa kumbembeleza Sabrina ili aweze kula angalau kidogo tu.
Halafu safari ikaendelea kidogo kidogo.
Walipokuwa njiani, Sabrina alimuomba Jeff simu yake akidai kuwa anataka kuzungumza na Sakina, naye bila kusita akampatia.
Wakati Sabrina kaishika ile simu tena kabla hata hajafanya chochote ikaanza kuita, kuangalia mpigaji jina likatokea pale 'Dorry' Sabrina akawa anaiangalia tu ile simu hadi Sam akamgeukia na kumuuliza,
"Mbona humpi mwenyewe apokee simu yake, unaiangalia tu Sabrina"
"Nimeona mpigaji hapa si wa muhimu ndiomana sijampa"
"Mpe bhana, huwezi jua huyo mpigaji anataka nini"
Jeff alitulia kimya huku akisikilizia muafaka wao.
Ile simu iliita hadi kukatika, kisha ikaanza kuita tena.
Ikabidi tu Sabrina ampe Jeff aipokee.
Jeff aliongea na ile simu na alipomaliza akawaambia,
"Mamdogo, huyu aliyenipigia hapa ni yule dada ambaye mlinikuta nimekaa naye pale hotelini"
Sabrina akadakia kwa kumuuliza swali Jeff,
"Kwahiyo tukusaidiaje?"
"Sio mnisaidiaje mamdogo, huyu dada kasema kuwa umeangusha mtandio wako"
Kisha Sabrina akajipapasa mwilini na kuona kweli mtandio hakuwa nao, halafu akamwambia,
"Mwambie huyo dada anitunzie"
Sam akamuuliza Sabrina,
"Au tuufate?"
"Hapana, anitunzie tu"
Sam akamuangalia Sabrina na kuridhika na jibu lake kisha safari ikaendelea.
Muda wote tangu hilo tukio la simu kutokea Sabrina alikuwa kimya kabisa.
Walipoingia mjini, Sam akamuuliza Sabrina,
"Muda ule ulihitaji kuongea na Sakina, sasa mbona hukuongea nae tena?"
"Aah niliona hakuna umuhimu tena"
"Ila unajua kama leo utaenda kulala kwangu?"
"Natambua hilo Sam, ila kwanza nipeleke nyumbani nikamsalimie mama"
"Sawa, hakuna tatizo. Na huyu Jeff tunamuacha wapi?"
"Muache popote, huyo ni mtu mzima atajijua mwenyewe"
Sam akatabasamu kiasi na safari kuendelea.
Alipofika mjini kabisa akasimamisha gari na kumgeukia Jeff kisha akamwambia,
"Nadhani hapa patakuwa sahihi kwako kushuka"
Jeff naye hakupinga zaidi ya kumshukuru Sam na kushuka, na muda huo Sam nae akashuka huku akimwambia Sabrina kuwa anaelekea dukani ambako palikuwa karibu kabisa na aliposimamisha gari ili kununua maji.
Wakati Jeff anashuka, mbele akatokea mdada aliyeonyesha kumfahamu sana Jeff na kumsogelea kwa shauku yote huku akimuita,
"Jeff"
Jeff akageuka na kumtazama yule dada ambaye wazi alikuwa akifahamiana nae na kumsalimia.
Sabrina alizidi kupandwa na hasira mule ndani ya gari na kumuita Jeff,
"Wee Jeff njoo"
Muda Jeff anasogea tena kwenye gari ndio muda Sam naye alirudi kwenye gari na kumuuliza Sabrina,
"Mbona umemuita tena Jeff?"
"Huyu inabidi aende kwa mama yake maana hapa tulipomshusha si sahihi"
Kisha akamuangalia Jeff aliyekuwa bado pale nje na kumwambia,
"Panda kwenye gari twende."
Jeff hakubisha wala kupinga zaidi ya kumpungia yule dada mkono ambaye alikuwa amesimama mbali kidogo na kupanda kwenye gari kisha safari ikaendelea.
Sam alikuwa akitikisa kichwa tu.
Walipofika nyumbani kwa wakina Sabrina, wote walishuka kwenye gari na kuelekea ndani.
Baada ya salamu, Jeff akaondoka na kuelekea nyumbani kwao.
Walipokaa muda kidogo pale, akawasili kaka wa Sabrina ambaye ni James na mchumba wake Joyce ambaye ni dada wa Sam na kujikuta wote wakifurahi kwavile wamekutana mahali ambako hawakutarajia kukutana kwa siku hiyo.
James alianza kwa kuwaambia,
"Jamani, ndoa yangu na Joyce ndiyo itakayotangulia. Halafu nyie wenzetu mtasubiri"
Sam naye akachangia,
"Hapana, yangu na Sabrina ndiyo itatangulia"
Mama yao akawaomba watoe sababu naye James akasema,
"Sababu mimi ni kaka mkubwa wa Sabrina basi hainabudi kutangulia mimi"
Sam naye akajitetea,
"Hata mimi ni kaka mkubwa kwa Joyce, ukoo utashangaa akinitangulia yeye"
Mama wa Sabrina akacheka na kuwashauri kuwa kwanini wasifanye siku moja yani wafanye sherehe pamoja.
Sabrina akakubaliana na wazo la mama yake na kusema kuwa ni wazo zuri na kufanya wote walifurahie.
Maongezi yakaendelea pale, kisha Sam na Sabrina wakawa wa kwanza kuaga.
Walipotoka nje, Sabrina akamwambia Sam kuwa aende kwanza akamsalimie Sakina kisha ndio waondoke, Sam hakuwa na pingamizi zaidi ya kufatana na Sabrina.
Jeff alikuwa ndani kwao na mama yake, alijikuta akiinuka na kuchungulia dirishani kamavile kuna mtu alikuwa akimngoja, ndipo alipomuona Sabrina akiwa ameambatana na Sam wakija maeneo ya kwao.
Jeff akatoka pale dirishani kisha akamwambia mama yake,
"Kama mamdogo Sabrina akiniulizia mwambie kuwa nimetoka muda ule ule niliyorudi"
Kisha akaelekea chumbani kwake na kumfanya Sakina amshangae kuwa imekuwaje leo mwanae hataki kuonana na Sabrina.
Kisha muda huo Sam na Sabrina waliwasili pale kwa Sakina na kuanza kusalimiana nae, kisha wakamuaga ila kabla hawajaondoka Sabrina akamuulizia Jeff,
"Na Jeff yuko wapi?"
"Ametoka"
"Ametoka muda gani tena?"
"Aliporudi hata hakukaa, ameondoka muda huo huo aliorudi"
"Duh kweli mwanao ni kunguru hafugiki jamani"
Kisha wakaondoka.
Walipokuwa wanaondoka, wakati wapo kwenye gari wakielekea nyumbani kwa Sam, muda huo Sam akamuuliza Sabrina jambo moja,
"Ni kitu gani umewahi kunificha katika maisha yako na hadi sasa hutaki kukisema?"
Sabrina akafikiria kidogo na kumjibu Sam,
"Hakuna kitu chochote"
"Sawa, na mfano nikagundua kuna kitu?"
Sabrina akakaa kimya bila ya kujibu kitu chochote hadi walipofika nyumbani kwa Sam.
Akamkaribisha Sabrina hadi ndani.
Sabrina alikaa sebleni, ila Sam alienda kumshika Sabrina mkono hadi chumbani kisha akamwambia,
"Nataka leo tufanye jambo moja tu"
Mawazo ya Sabrina yakampelekea kuwa Sam anahitaji walale kwa siku hiyo ila Sam akamwambia.
"Usifikirie unachofikiria, ila mimi nataka utoe nguo yako ya juu tu niangalie tumbo lako"
Sabrina uoga ukamjaa moyoni.
Sabrina alikaa sebleni, ila Sam alienda kumshika
Sabrina mkono hadi chumbani kisha akamwambia,
"Nataka leo tufanye jambo moja tu"
Mawazo ya Sabrina yakampelekea kuwa Sam
anahitaji walale kwa siku hiyo ila Sam akamwambia.
"Usifikirie unachofikiria, ila mimi nataka utoe nguo
yako ya juu tu niangalie tumbo lako"
Sabrina uoga ukamjaa moyoni.
Akajishika tumbo kama mtu mwenye maumivu tumboni kwani hata sura yake aliikunja na kumfanya Sam amuulize,
"Nini Sabrina?"
"Tumbo linakata Sam, ooh tumbo langu mie"
Sam akaanza kumbembeleza huku akimsihi kuwa waende hospitali, ila kila Sam alipomshika Sabrina alilalamika kuwa anamaumivu sehemu hiyo,
"Tafadhari Sabrina, twende hospitali"
"Hapana Sam, acha nipumzike labda litapoa"
"Jamani Sabrina"
"Aaah naumia Sam, maumivu makali sana hasa chini ya kitovu. Naomba nipumzike kwanza"
Sam akamuwekea Sabrina vizuri pale kitandani na kumfanya apande na kuweza kulala huku akiendelea kufikiria cha kufanya.
Kisha Sam akatoka na kwenda kukaa sebleni kwake huku akijiuliza maswali mengi mengi.
Sabrina alitulia pale kitandani huku akiwaza kuwa Sam analengo gani hadi kutaka kuangalia tumbo lake? Na kwanini anamuuliza kama kuna chochote anamficha? Na kama amegundua ukweli wa hiki alichomficha siku zote atamfanya nini? Sabrina aliwaza bila ya kuwa na jibu kamili, huku akiendelea kujigalagaza pale kitandani.
Sam aliingia tena chumbani kwake ili amuangalie Sabrina hali yake,
"Vipi muda huu unaendeleaje?"
"Kidogo afadhari, ila itakuwa vyema kama ukinipeleka nyumbani kwetu ili niwe karibu na mama"
"Kwanini nisikupeleke hospitali jamani Sabrina?"
"Mi naomba niende tu nyumbani, tafadhari sana Sam"
Sam hakutaka kubishana zaidi na Sabrina zaidi ya kumsaidia kuinuka kisha kutoka nae nje tayari kwa safari ya kumrudisha nyumbani kwao.
Ambapo Sam aliondoka na Sabrina hadi nyumbani kwao kisha akamuaga pale na kumuahidi kwenda kesho kumuona.
"Sawa Sam nashukuru sana"
"Usijali Sabrina, ni wajibu wangu"
Kisha Sam akaondoka.
Jeff alipokuwa chumbani kwake alikuwa akifikiria kuhusu Sabrina, mawazo yake yote yalielekea juu ya Sabrina huku akijiuliza,
"Inamaana Sabrina nae ameanza kunipenda kiasi cha kuona wivu niongeapo na wasichana wengine? Amenipenda kiasi cha yeye kuhitaji na kutambua nilipo kila mahali? Au ni kitu gani hiki kama sio upendo?"
Jeff alijiuliza sana bila ya majibu, kisha akatoka ndani kwao na kumuaga mama yake kuwa anaenda kutembea kidogo.
Sabrina aliyepelekwa kwao na kudai kuwa ni mgonjwa sana, sasa akamuaga mama yake kuwa anaenda kumsalimia Sakina,
"Ila wewe Sabrina una vituko jamani, si umeletwa hapa kuwa unaumwa sana wewe? Haya sasa hivi unataka kwenda kumsalimia Sakina kivipi?"
"Jamani mama, si ninafanya mazoezi tu jamani kwani kuna ubaya gani?"
"Haya nenda, ila kiukweli mwanangu una makw azo"
Sabrina akainuka na kwenda nyumbani kwa Sakina ambako giza nalo lilishaingia na kumkuta Sakina akiwa peke yake.
Ila Sabrina alichofanya ni moja kwa moja kumuulizia Jeff,
"Ametoka tena"
"Inamaana alirudi na ametoka tena?"
"Ndio ametoka, tena hata sio muda mrefu"
Sabrina akakaa kimya kidogo kisha akamuaga Sakina,
"Mi naondoka"
"Inamaana nia yako ilikuwa ni kumuona Jeff tu?"
"Hapana, ila naona usiku nao umeingia sana"
Kisha akaondoka zake.
Wakati anatembea akasikia sauti akiitwa,
"Sabrina"
Akageuka na kumuangalia, akashangaa kumuona ni Jeff aliyemuita,
"Khee Jeff!"
"Ndio ni mimi"
Jeff akamsogelea zaidi Sabrina na kumkumbatia, kisha akamwambia,
"Najua umetoka kuniulizia mimi"
Sabrina akamuangalia tu Jeff bila ya kuongezea neno lolote, kisha Jeff akamuuliza tena
"Mbona kimya kimetawala?"
"Hapana, ila umeishusha sana heshima yangu hadi unafikia hatua ya kuniita kwa jina langu pekee!"
"Nisamehe mamy"
Sabrina akamtoa Jeff mikono ambayo ilikuwa juu yake kisha akamuaga,
"Kesho, naomba asubuhi na mapema uje unione"
Kisha akaondoka na kurudi kwao.
Sabrina alienda kulala moja kwa moja, akajiwa na njozi kuwa Sam amegundua kuhusu ule ujauzito na moja kwa moja amegundua kuwa ile mimba ni ya Jeff.
Sabrina akishtuka na kutamka kwa nguvu,
"Jeff nooooo....."
Mama yake akashtuka na kumfata chumbani,
"Nini tatizo Sabrina?"
Sabrina alikuwa anashangaa tu na kumjibu mama yake,
"Hakuna tatizo"
"Mbona umemtaja Jeff kwa nguvu hivyo?"
"Hapana mama, nilikuwa naota tu"
"Ndio umemuota Jeff?"
"Hapana mama, naomba nipumzike tafadhari"
Mama wa Sabrina ikabidi amuache Sabrina apumzike kisha akatoka nje.
Ila Sabrina hakulala usingizi tena kikamilifu kwani mawazo yalimjaa kupita kipimo na kumfanya ajiulize maswali bila ya majibu ya aina yoyote ile.
Kulipokucha, Sabrina aliamka na kwenda kukaa nje ya nyumba yao huku akijisemea moyoni,
"Atakayewahi kuja kuniona kati yao basi huyo ndiye mume wangu"
Mara kuna mtu akamziba macho kwa nyuma kwa kutumia viganja vya mikono, Sabrina akapapasa na kumuuliza,
"Nani wewe?"
Yule mtu akatoa vile viganja ili Sabrina apate kugeuka na kumuona, ila kabla Sabrina hajageuka, mbele yake alimuona Sam akisogea pale alipo na alipogeuka alimuona Jeff.
Sabrina alijihisi kuwa kama mtu mwenye mawenge kwani mambo mengi yalikuwa yakiingiliana na kumkosesha amani kabisa.
Kwavile Sam alikuwa mbele, Jeff akashindwa kukaa pale na kuzungumza zaidi ya kumuacha Sam aendelee na mazungumzo yake kwa Sabrina.
Sam akamuuliza Sabrina,
"Mbona dogo anaondoka?"
"Sijui kwakweli, labda tungemuuliza yeye mwenyewe"
"Naomba leo nikitoka kazini nije nikuchukue Sabrina, tafadhari usikatae. Kuna mambo ya muhimu sana nataka kuzungumza na wewe, haswaa kuhusu ndoa yetu"
"Sawa Sam, hakuna tatizo"
Kisha Sam akamuaga Sabrina na kuondoka zake.
Sabrina aliendelea na mawazo yake kuwa kwanini akiwaza kuhusu mume basi mara zote atatokea Jeff pamoja na Sam? Aliwaza pia kama inawezekana Jeff kumuoa yeye? Akajikuta akijijibu mwenyewe,
"Hapana haiwezekani, mimi ni mkubwa sana kwake na pia watu wananiheshimu kwahiyo nikifanya kitu cha namna hiyo lazima jamii nzima itanishangaa"
Akainuka na kuingia zake ndani.
Sam alipokuwa ofisini alikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza Sabrina na alipenda ajibiwe kiufasaha,
"Sijui huyu mwanamke nimfanye nini leo kama akinigelesha pia?"
Msaidizi wake alimsikia na kumuuliza,
"Nini tatizo bosi? Unamuongelea nani?"
"Natambua unaipenda kazi yako na unaihitaji sana, basi fanya kazi yako. Achana kabisa na mambo yasiyokuhusu"
Ilibidi yule dada akae kimya kwani anajua wazi Sam akichukia anakuwaje.
Sam aliendelea na kazi zake huku mawazo yake yote ya siku hiyo yalikuwa juu ya Sabrina.
Jeff nae kwao hapakukalika, alijikuta moyo wake ukipenda kuwa karibu zaidi na Sabrina kuliko mtu mwingine yeyote.
Akatoka tena kwao na kumuaga mama yake kuwa anaenda kumsalimia bibi ambaye ni mama wa Sabrina na nia yake ilikuwa ni kumuangalia Sabrina kama yupo au kama kashaondoka na Sam.
Kwa bahati alipofika alimkuta Sabrina akiwa pale ndani amepumzika huku akizungumza na mama yake.
Joy nae alipomuona Jeff akamwambia kwa shauku,
"Eeh Jeff, afadhari umekuja maana hapa Sabrina anakutaja hadi ndotoni nadhani hii mimba kakubebea wewe"
Jeff akatabasamu ila Sabrina akamuangalia mama yake kwa hasira kidogo na kumwambia,
"Mmh mama na wewe loh!"
Jeff akakaa pembeni ya Sabrina huku akiendelea kutabasamu na kuwa kama fisi aliyekabidhiwa bucha.
Sabrina akamuangalia Jeff na kumuuliza,
"Kilichokuleta muda huu?"
"Nimekuja kukuona tu"
"Haya ushaniona, unaweza kwenda"
Joy akamshangaa Sabrina kumwambia kwa hasira vile Jeff,
"Jamani Sabrina, mbona unamvunja moyo mtoto?"
"Si amekuja kuniona, basi ameshaniona na aende"
Jeff akainuka na kuaga kisha akaondoka, halafu Sabrina akamuuliza mama yake,
"Je umewahi kumwambia Sam kuwa mimi ni mjamzito?"
"Mmh hayo ni mambo yenu, mie hata hayanihusu"
"Na mbona hapo umeshadadia kuwa mimi mjamzito? Hivi mama kweli hujawahi kumwambia Sam wewe?"
"Kweli kabisa mwanangu, sijawahi. Ulinikatazaga nakumbuka, hayo mambo mtaongea wenyewe huko mimi hata hayanihusu"
Kimya kikatawala kidogo kisha Sabrina akainuka, mama yake akamuuliza,
"Unakwenda wapi?"
"Naenda kwa Sakina kidogo"
"Mmh! Si umemfukuza mwenyewe Jeff hapa, saivi ndio unahitaji kwenda kumuona?"
"Mmh mama na wewe, mi sina nia ya kumuona Jeff bhana, zaidi nina mambo yangu tu binafsi"
Kisha akaondoka zake.
Alipofika nyumbani kwa Sakina, alimkuta kakaa na binti mmoja mwenye asili ya uchotara pale nje kwake.
"Khee nani tena huyu?"
"Mkwe wetu huyu"
"Mkwe wetu? Kivipi?"
"Aaaah ni wa Jeff, kwahiyo sisi ni mkwe wetu"
Sabrina akajihisi kutapika muda huo huo na kumfanya akimbilie nyuma ya nyuma na kuanza kutapika.
Jeff aliyekuwa ndani alikuwa akimsikia Sabrina akitapika na kumfanya akimbilie nje kumuangalia.
Alipomkuta, akamsaidia kumkalisha na kumletea maji ili anawe.
Sabrina alinawa na kurudi katika hali yake ya kawaida kisha Jeff na Sakina wakamsaidia Sabrina kwa kumuingiza ndani ili apumzike kwenye kochi.
Sakina akaanza kuongea kwa kucheka,
"Kweli leo nimeamini kuwa mwanangu anakupenda Sabrina"
Sabrina akashtuka kisha akajigelesha kwa kucheka na kuuliza,
"Kwanini unasema hivyo?"
"Yani, nimetumia muda mwingi kumuita tangu huyu binti aje wala Jeff hakujitokeza ila aliposikia unatapika, kaja mbio kukusaidia. Yani Sabrina wewe nahisi utazaa mtoto wa kike kwaajili ya mwanangu na hapo tutaunga ukoo wetu vizuri"
Sabrina akacheka tu na kutania,
"Yani mwanangu akaolewe na mbabu loh! Maana kipindi hiko Jeff atakuwa ameshazeeka"
Wote wakacheka kumbe ukweli wa mambo alikuwa nao Sabrina na Jeff pekee.
Baada ya muda kidogo, Sabrina akamuaga Sakina kuwa anaondoka,
"Vipi utarudi badae?"
"Hapana, hivi ndio mpaka kesho au kesho kutwa kama Mungu akipenda"
"Sawa basi, mi nashukuru kwa kunitembelea"
Kisha Jeff akatoka na Sabrina huku akidai kuwa anaenda kumsindikiza.
Wakiwa wanatembea, Jeff akamvuta mkono Sabrina kamavile anataka kumrudisha nyuma, Sabrina akamuuliza,
"Nini tena Jeff"
"Hamna kitu"
"Sasa mbona umenivuta mkono"
"Nilitaka tu uongee"
"Yani wewe mtoto wewe, ingekuwa amri yangu sijui hata ningekufanya nini. Kwahiyo ndio umempelekea mama yako mchumba?"
"Kwani mamy, unapatwa na wivu?"
"Tahira wewe, nani awe na wivu juu yako? Haya rudi zako kwenu sitaki tena kusindikizwa na wewe, ushanichefua tayari"
"Jamani nisamehe, sikuwa na nia mbaya"
"Nimekwambia nenda zako"
Muda wanagombana pale njiani, akapita Sam na gari yake na kuwaona kisha akasimamisha ile gari na kuwaangalia, kisha akauliza,
"Vipi tena Sabrina na huyo dogo?"
"Hamna kitu, nimelituma hapa limenikatalia"
Kisha Sabrina akamuangalia tena Jeff na kumwambia,
"Haya rudi kwenu hata sitaki kukuona mtoto mbishi wewe"
Jeff hakutia neno zaidi ya kugeuza na kumuacha Sabrina akipanda katika ile gari ya Sam.
Moja kwa moja wakaenda kwakina Sabrina kuaga na kuondoka.
Sam alimpeleka Sabrina kwenye hoteli ili kufanya nae mazungumzo,
"Sabrina, kuna mambo makubwa manne nataka kukuuliza napenda jibu lako liwe ndiyo au hapana yani usiongeze neno lolote la zaidi katika jibu lako. Sawa"
"Sawa"
"Maswali yangu yataenda katika mtindo wa swali dogo kabisa kuelekea kubwa ila ni maswali manne tu. Narudia tena, jibu lako liwe ndiyo au Hapana."
Sabrina akaitikia huku akiwa tayari kuulizwa hayo maswali na kuyajibu, Sam nae akaanza kwa kumuuliza,
"Sabrina"
"Abeee"
"Najua unatamani sana kuolewa, tena unatamani hata uolewa muda huu. Je ni kweli?"
"Ndiyo"
"Sabrina, katika huko kuolewa huelewi moyo wako bado na wala hujui ni mwanaume gani sahihi kwako kati ya wawili wanaouzunguka moyo wako. Je ni kweli?"
Sabrina akasita kidogo kujibu hilo swali na kukaa kimya na kumfanya Sam aongee tena,
"Tafadhari Sabrina nijibu ili niendelee na swali la tatu"
Sabrina bado alikaa kimya, na kumfanya Sam amuulize,
"Au hili tuliruke kwanza twende swali la tatu?"
Sabrina akatikisa kichwa kuonyesha kwamba amekubaliana nae na kumfanya Sam aendelee kuuliza,
"Sabrina, hapo ulipo una mimba. Je ni kweli?"
Sabrina alihisi kuzimia muda huo.
Sabrina bado alikaa kimya, na kumfanya Sam
amuulize,
"Au hili tuliruke kwanza twende swali la tatu?"
Sabrina akatikisa kichwa kuonyesha kwamba
amekubaliana nae na kumfanya Sam aendelee
kuuliza,
"Sabrina, hapo ulipo una mimba. Je ni kweli?"
Sabrina alihisi kuzimia muda huo.
Sam nae alikazana kumuangalia kwa makini ili amjibu kiufasaha, Sabrina akakazana kujiuma uma na kumfanya Sam amwambie,
"Nijibu Sabrina, mbona kimya?"
Sabrina hakuwa na jibu zaidi ya kuinama na kuanza kulia, Sam akamsogelea na kukichukua kichwa cha Sabrina na kukiegesha kwenye bega lake, kisha akaanza kuongea nae kwa utaratibu kabisa,
"Niambie ukweli Sabrina, usiogope. Kumbuka nakupenda sana mpenzi"
Sabrina alitamani sana kumwambia Sam ukweli wote ulivyo ila aliogopa sana akifikiria hatua ambayo Sam ataichukua dhidi yake na kujikuta akizidi kulia bila kupumzika,
"Tafadhari Sabrina nyamaza, mie sitachukia Sabrina"
"Nisamehe Sam"
"Niambie ukweli mpenzi"
Machozi nayo yakazidi kumtoka Sabrina huku uoga nao ukimjaa ingawa Sam alisisitiza juu ya kuujua ukweli,
"Sam tafadhari usinichukie"
"Sitakuchukia Sabrina, wee niambie tu"
"Ni kweli nina mimba Sam"
Huku akiendelea kulia kuonyesh a kuwa anajutia mimba aliyobeba.
Sam alimkumbatia zaidi Sabrina, kisha akamuomba Sabrina kuwa waondoke eneo lile.
Walipanda kwenye gari kimya kimya, kisha Sam akaliendesha hadi nyumbani kwa Sabrina ambako toka kipindi ambacho Sabrina alienda Bagamoyo ndio siku hiyo akarudishwa nyumbani kwake.
Sam alimfikisha na kumuaga kisha yeye akaondoka zake na kumfanya Sabrina aendelee kuwa na mawazo yasiyo na muafaka.
"Inamaana anachukua uamuzi gani? Mbona sijamuelewa? Mbona hajanipa jibu lolote la moja kwa moja sasa sijui hatma yangu ni nini?"
Sabrina alitulia mule ndani huku akiwa na mawazo mengi sana.
Sam alienda moja kwa moja kwenye baa aliyozoea kwenda kunywa, aliagiza vile vinywaji vikali kabisa na kuanza kuvinywa, tena hakujali kwani alikunywa kamavile anakunywa maji.
Kwa bahati meneja wa ile ba alifahamiana sana na Sam na kwenda eneo lile ambalo Sam alikuwa amekaa kwani aliona wazi kuwa hali aliyokuwa nayo Sam kwa wakati huo haikuwa hali yake ya kawaida, akaamua kumsihi kuwa apunguze, na hapo akamfanya Sam kuzungumza ya moyoni.
"Kwakweli wanawake ni watu wapumbavu sana, wanawake hawafai hata uwafanye nini. Wanawake sio watu, tamaa inawaponza"
"Sam ndugu yangu, ni pombe hiyo imekuzidia ndugu, mi nakuomba nikusaidie ili uweze kurudi nyumbani kwako kupumzika."
Sam aliongea kilevi sasa,
"Niache Peter, nina akili zangu timamu kabisa. Nakwambia hivi, wanawake ni mashetani tena mashetani kabisa wenye pembe, hata huwabebe vipi huwa hawabebeki"
Moja kwa moja Peter akaelewa kuwa ni wazi mwenzie kachanganywa, na kikubwa kilichomchanganya ni mapenzi.
Akaona wazi kuwa Sam akiendelea kukaa mahali pale anaweza akajikuta akiropoka hata maneno ya ndani zaidi hivyobasi akapata kibarua cha kumbembeleza ili aweze kumpeleka nyumbani kwake.
Mwisho wa siku Sam alikuwa hajielewi kabisa na kukubali kuondoka na Peter ili aweze kumwendesha hadi nyumbani kwake naye Peter akafanya hivyo.
Muda Peter anamsaidia Sam kupanda kwenye gari ili ampeleke, Jeff nae alipita eneo lile na kuwaona ila hakutaka kuwafatilia.
Sam alipofika nyumbani moja kwa moja alienda kulala na hakuweza kusikia chochote kilichoendelea kwa muda huo.
Sabrina baada ya kuona muda umepita bila ya kupata mawasiliano yoyote kutoka kwa Sam, akaamua kumpigia simu ila ile simu iliita tu bila ya kupokelewa kabisa na kumfanya Sabrina aanze kupata wasiwasi.
Akapanga kwenda nyumbani kwa Sam kumuangalia, akainuka ili atoke na kuianza safari.
Alipokuwa anatoka akakutana na Jeff mlangoni,
"Vipi na wewe? Mi kuna mahali nataka kwenda."
"Ila kabla hujatoka kuna kitu nataka kukueleza"
Jeff akamshika Sabrina mkono kisha akarudi nae ndani na kuanza kumuelezea kuhusu Sam, jinsi alivyomuona
"Inaonyesha alikuwa kalewa sana, kwani kuna tatizo mamdogo?"
Sabrina akapumua kidogo na kuanza kumuelezea Jeff kuhusu Sam kugundua kuhusu ule ujauzito.
"Duh! Sasa itakuwaje hapo?"
"Kwakweli sijui, tena sijui kabisa Jeff. Yote haya umeyataka wewe"
"Kwani umemwambia kuwa mi ndio muhusika"
"Kwenda zako huko, tena usinikere"
Jeff akainuka na kumwambia Sabrina,
"Basi kwaheri, mi naenda"
Sabrina akamshika mkono Jeff na kumwambia,
"Ona sasa ambavyo huna akiki, unaenda wapi sasa? Hebu kaa hapo"
Jeff alijihisi kutabasamu kimoyo moyo kwani hali ile ilimuonyesha wazi kuwa anapendwa na Sabrina ila tu Sabrina hataki kuwa nae sababu ya aibu tu.
Jeff sasa akakaa karibu na Sabrina huku akimuangalia sana na kumfanya Sabrina amuulize,
"Mbona unaniangalia sana?"
"Si nakuangalia tu ulivyo mzuri"
"Lione vile, utaniudhi sasa hivi"
Huku Sabrina akitabasamu.
Sam alijikuta akiamka kesho yake tena pakiwa pamekucha kabisa, aliangaza huku na kule na kujiona kuwa alilala na zile nguo zake alizokuwa nazo siku nzima ya jana.
Alikaa na kujifikiria,
"Sasa nauona umuhimu wa kuoa, ila kwanini Sabrina kanifanyia hivi? Yani hapo bado hajayajua matatizo yangu, je akiyajua itakuwaje jamani? Huyu Sabrina huyu mbona kaniumiza sana? Nimsamehe kweli?"
Sam akawa anajipeleleza na moyo wake kwani kadri alivyofikiria ndivyo maumivu yalivyomjaa ndani ya moyo wake.
Ila aliamka na kuoga na kukoroga kahawa ili anywe na ili apate nguvu.
Sabrina nae kulipokucha, alikuwa wa kwanza kuamka siku hiyo na kwenda kukaa sebleni kwani alikuwa na mawazo sana ya kumuhusu Sam.
Ila alipokaa kidogo, Jeff nae akaenda kukaa pembezoni mwake, kisha akamsogelea karibu na kumshika begani.
Sabrina akamwambia,
"Una matatizo wewe, haya sasa unataka nini?"
"Sitaki chochote zaidi ya wewe"
"Acha hayo mazoea Jeff, mabinti wa rika zako wapo huko nje kibao. Wafate huko nje na uwe nao sio maswala ya kuning'ang'ania mimi tu"
"Sawa, nashukuru kwa kunipa ruhusa"
"Nyoo ruhusa ya nini?"
"Si ruhusa ya kuwa na hao mabinti wa nje"
"Lione vile, nitakutimua sasa hivi hapa"
Jeff akatabasamu na kuzidi kujipa matumaini kuwa Sabrina anampenda na ndiomana anapatwa na wivu akisikia kuwa yupo na wasichana.
Kisha akamwambia,
"Nakuomba usinitimue mamy, mi nataka leo nishinde na wewe siku nzima."
"Hilo sio tatizo ila cha muhimu ni kuangalia usinikere"
"Sitakukera, sipendi uchukie, sipendi kuwa mbali nawe"
"Taratibu wee mtoto, kumbuka mimi ni kama mama yako. Hayo yaliyopita tuyafumbue macho tu"
Jeff akakubaliana na Sabrina kuwa siku hiyo atashinda nae pale nyumbani kwa siku nzima.
Sam alichukua simu yake na kutaka kumpigia Sabrina, ila moyo wake ukasita kwavile bado alikuwa na maumivu huku akijiambia na kujiuliza,
"Ni kweli Sabrina ana mimba lakini je ile mimba ni ya nani? Mmh tafadhari Mungu isiwe ya mtu ninayemuhisi mimi maana nitazimia"
Alijiuliza kama ataweza kujizuia atakapoujua ukweli wa mambo.
Akaacha kumpigia simu Sabrina huku akingoja jibu sahihi kutoka kwenye moyo wake.
Ila badae akaona kuwa ni vyema aende tu mwenyewe kuongea na Sabrina ana kwa ana kuliko kuendelea kuutesa moyo wake kwa maumivu.
Akaona kuwa Sabrina pekee ndiye mwenye uwezo wa kumpa jibu la kumliwaza au kumuumiza zaidi, kwahiyo akainuka na kujiandaa kwa hiyo safari.
Sabrina akiwa amekaa ndani, Kuna muda alichoka, akaamua kujilaza kwenye kochi ili kujipumzisha kidogo. Wakati huo Jeff alikuwa jikoni, ila alipomuona Sabrina kajilaza pale kwenye kochi, naye akaenda na kukaa pale kisha akakiinua kichwa cha Sabrina na kukiweka kwenye miguu yake.
Alimfanya Sabrina acheke na kusema,
"Yani mtoto wewe una matatizo loh, kwahiyo hapo ndio umefurahi sasa?"
"Ndio nimefurahi mamy"
Wakajikuta wakitazamana na kucheka.
Muda huo hodi ikasikika na kumfanya Sabrina ainuke pale alipojilaza kisha Jeff akaenda kufungua mlango, na aliyeingia alikuwa ni Sam.
Moja kwa moja alienda kukaa pale alipokaa Sabrina na kumfanya Sabrina apatwe na uoga na aibu kwani hakujua jambo ambalo Sam amekuja nalo kwa siku ya leo.
Ila Sam alisalimia tu na kuwa kimya huku wakiangaliana bila ya kusema chochote, ikabidi Jeff auvunje ukimya ule kwa kumuaga Sabrina,
"Mamdogo, mi naenda nyumbani. Kwaheri"
Sam naye akauliza,
"Unaenda baada ya kuniona mimi au ilikuwa ni mpango wako kabla?"
"Ilikuwa ni mpango wangu wa muda tu"
"Na kilichokuleta wakati unataka kuondoka ni nini?"
"Nilikuja kumsaidia mamdogo tu kupika, na nishamaliza ndiomana nime...."
Simu ya Sabrina ikaita, mpigaji alikuwa ni Sakina,
"Jeff yupo huko kwako?"
"Ndio yupo"
"Tafadhari mwambie arudi nyumbani kuna mgeni wake"
Kisha ile simu ikakatika, Jeff akamtazama Sabrina kwani alijua wazi kuna ujumbe unaomuhusu,
"Mama yako kasema, usiende sasa hivi nyumbani kwenu. Kwahiyo cha kukushauri sasa ni ubakie hapa tu hadi hapo badae utakapoenda kwenu"
Jeff akamtazama Sabrina kisha akainuka na kwenda chumbani kwake.
Sam akamuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Mbona umempa ujumbe tofauti na uliopewa kwenye simu?"
"Kwani umesikia?"
"Nimesikia ndio"
"Aah, namjua mtu ambaye alikuwa akimuitia ndiomana nikamzuia"
"Ni nani? Na kwanini umemzuia?"
Sabrina akakaa kimya kwavile aliona wazi kuwa anaweza kujibu kitu ambacho kitakuwa ngumu kumuelewesha Sam, kwahiyo akakaa kimya kuepusha shari.
Sam nae akapata wazo jipya juu ya Sabrina, kisha akainuka na kutoka nje.
Akachukua simu yake na kumpigia Sakina, alipomsalimia akamuuliza,
"Eti kuna mgeni gani huyo anayemsubiria Jeff?"
"Ni mchumba wake, ila msimwambie sababu akijua basi hatokuja"
"Sawa basi kwaheri"
Sam akaikata ile simu, kisha akarudi tena ndani na kumwangalia Sabrina kisha akamwambia,
"Kwaheri Sabrina, nitakuja tena"
Hakutaka kungoja jibu la Sabrina kabisa kwani aliaga huku akiondoka.
Jeff alipogundua kuwa Sam ameondoka, naye akatoka ndani na kwenda kumuuliza Sabrina,
"Kwani imekuwaje?"
"Hata naelewa basi! Sielewi chochote"
Simu ya Sabrina ikaita tena, mpigaji alikuwa yule yule Sakina na kumuuliza Sabrina,
"Vipi huyo Jeff mnamleta nyie nini!"
"Kwanini?"
"Sam si kanipigia simu hapa kumuulizia huyo mgeni, mi nikajua...."
Sabrina alijikuta akiiachilia ile simu na kujisemea,
"Mungu wangu, sijui itakuwaje!"
Jeff akamuuliza, ikabidi Sabrina amsimulie ilivyokuwa.
"Sasa tutafanyeje Jeff"
"Tuipotezee tu, endelea na msimamo wako sababu ukibadilika anaweza akahisi mengine"
"Mmh! Mi naona vyema wewe ukirudi nyumbani kwenu kwanza halafu tufikirie mengine"
"Hapana, mi siendi popote. Acha tuangalie upepo utakavyokwenda"
Jeff alibisha kwavile moyoni mwake alishaamini wazi kuwa Sabrina anampenda ila hayupo wazi kwavile anamuona yeye kuwa mdogo.
Sam alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwani akili yake ilishindwa kufanya kazi kwa wepesi na kumfanya azidi kuamini anachokiwaza.
Alizunguka ndani ya nyumba yake na kujiona kamavile ni mtu anayeenda kupagawa,
"Hivi inawezekana kuwa Sabrina anatembea na Jeff? Inawezekana kweli? Aah kwakweli hainiingii akilini ila lazima niujue ukweli, na pindi nitakapoujua huo ukweli hapo ndio nitajua cha kufanya. Siwezi kukaa na kuchekelea upuuzi wa namna hii kila siku."
Sam akaingia chumbani kwake na kuchukua bastora yake huku akielekea tena kwa Sabrina ingawa usiku tayari ulikuwa umeingia.
Sabrina akiwa ametulia ndani kwake bila ya kujua kitakachoendelea, na wakati huo Jeff nae akiwa chumbani kwake, wakasikia mlango wa sebleni ukibamizwa kwa nguvu.
Kwavile Sabrina ndiye aliyekuwepo pale sebleni akashtuka sana.
Sam alikuwa mbele yake huku akionyesha kujawa na hasira, kisha akaitoa bastora yake na kuielekeza kwenye paji la uso wa Sabrina, kisha akamwambia
"Niambie ukweli Sabrina kama hiyo mimba ni ya Jeff"
Sabrina alitoa mimacho tu, na baada ya muda mfupi akaanguka.
Sam alikuwa mbele yake huku akionyesha kujawa
na hasira, kisha akaitoa bastora yake na kuielekeza
kwenye paji la uso wa Sabrina, kisha akamwambia
"Niambie ukweli Sabrina kama hiyo mimba ni ya
Jeff"
Sabrina alitoa mimacho tu, na baada ya muda mfupi
akaanguka.
Jeff alikuwa akichungulia na kumuona Sabrina alivyoanguka, akatamani kutoka ila akaona ni msala ukizingatia bwana mkubwa alikuwa na bastora.
Kwahiyo akajikausha tu mule mule ndani kuona kinachoendelea.
Akamuona Sam akielekea jikoni akajua wazi kuwa kuna kitu anaenda kufata kama huduma ya kwanza kwa Sabrina.
Jeff aliendelea kukaa mule mule akimchungulia.
Sam alirudi na maji kidogo na kummwagia kidogo kidogo Sabrina usoni ambapo Sabrina akashtuka na kukaa tena.
Sasa hivi Sam hakuishika tena ile bastora, badala yake akaiweka tu mahali anapoichomekaga kisha akamwambia Sabrina,
"Tafadhari nisamehe Sabrina, nilipatwa na hasira tu mwenzio"
Sabrina akatikisa kichwa huku akiashiria kuwa amemsamehe, ila moyoni mwake alikuwa akipanga majibu ya kumpa Sam.
Baada ya muda kidogo, Sam akaanza kumuuliza tena Sabrina ila kwa utaratibu kabisa,
"Niambie kwanza Jeff yuko wapi?"
"Hayupo, nilimwambi a aende kwao naye akaondoka."
"Haya nijibu basi Sabrina, hiyo mimba ni ya nani?"
"Sijui"
"Hujui kivipi wakati ipo kwako Sabrina?"
Sabrina akainama na kuanza kujiliza, kisha akamwambia Sam,
"Mimi nilibakwa tu, ila wewe hata huniulizi vizuri unanijia kwa jazba na kutaka kumuingiza Jeff mahali asipohusika. Hivi wewe unaweza kutembea na mamako mdogo hadi uje kusema hii mimba ni ya Jeff?"
"Nisamehe Sabrina, ukaribu wako na Jeff ndio uliofanya nitamke hayo"
"Ukaribu kitu gani? Mbona kunivunjia heshima yangu kiasi hiki Sam? Hivi mi nikikwambia kuwa umetembea na dada yako yule Joyce na kumpa mimba ungejisikiaje? Niambie Sam, kwakweli umeniumiza sana"
Sam akalazimika kuanza zoezi la kumbembeleza Sabrina ili aweze kurudi kwenye hali ya kawaida.
"Tafadhari Sabrina, nisamehe bure na ukumbuke kuwa hujawahi kuniambia kama ulibakwa"
"Hivi unadhani kubakwa ni jambo la kawaida kiasi hicho hadi nikuelezee? Hakuna mtu anayejua kama nilibakwa. Niliogopa kusema ili kuepuka aibu, halafu leo hii Sam unakuja kusema eti natembea na Jeff kweli? Yani hujui tu jinsi gani Jeff amekuwa muhimu kwangu kwa kuniliwaza mamake mdogo, yani Sam umenikosea heshima kabisa"
"Yaishe basi Sabrina"
Sabrina aliendelea kuongea na kuongea bila hata ya kunyamaza na kumfanya Sam aweze kumuacha ili apumzeke kwanza na kuamua kumuaga kuwa ataenda kesho ili waweze kuongea vizuri kisha Sam akaondoka zake.
Sabrina aliinuka pale na kwenda chumbani kwake, ambapo baada ya muda mchache Jeff naye alienda chumbani kwa Sabrina.
"Nisamehe na mimi mamy"
"Lione vile, wakati wewe ndio chanzo cha kila kitu hapa"
"Ila umejitahidi kumshawishi mamdogo"
Sabrina akatabasamu, kisha Jeff akamuuliza tena,
"Na mbona ulizimia mamy? Bastora ilikutisha nini?"
Sabrina akacheka na kusema,
"Wee unafikiri nilizimia kweli basi! Nilijifanyisha mwenzio maana ile bastora ya kutishiwa nayo kila siku nikaona isije bure kutua kwenye ubongo wangu jamani"
Jeff akacheka sana na kumwambia Sabrina,
"Kweli wewe msanii dah!"
"Na ukae kimya kabisa Jeff ili hii mimba ibaki kuwa siri yetu"
Jeff alikubali kwavile hakutaka kumuumiza moyo Sabrina, hakutaka kuharibu ukaribu uliopo baina yao.
Sam alikaa nyumbani kwake huku akijikuta akimuhurumia Sabrina.
"Hakuna jinsi, itabidi nimuoe hivyo hivyo tu kwani atatia huruma sana kwa kuzaa mtoto asiye na baba. Acha mimi nijitolee kuwa baba wa mtoto wake."
Sam alijisemea huku akijiandaa kwenda kulala.
Kulipokucha, asubuhi na mapema akaenda kwanza kwenye ofisi yake ili kuangalia hali inavyoendelea kwavile ni muda mrefu hakuwasili ofisini.
Na alipofika, baadhi ya wafanyakazi walianza kumuulizia kuhusu Sabrina,
"Bosi, vipi Sabrina atarudi au ndio basi tena?"
"Atarudi ndio, kwani tatizo lenu ni nini?"
"Hakuna tatizo, nilikuwa nauliza tu bosi"
"Haya kaendelee na kazi"
Yule binti akatoka ofisini kwa Sam, ambapo Sam nae hakuchukua muda mrefu akatoka mule ofisini na kuondoka huku safari yake ikiwa ni kwenda kwa Sabrina moja kwa moja.
Sabrina akiwa na Jeff pale nyumbani kwake akamuomba kuwa aondoke kwanza kwa siku hiyo ili hata kama Sam atakuja basi asimkute pale.
"Hakuna tatizo basi, ila ukipatwa na shida yoyote usisite kuniambia mamy"
"Hata usijali"
Jeff akaondoka na baada ya muda mfupi Sam nae akawasili.
Sam kwa siku ya leo alikuwa amejawa na tabasamu usoni, na alipomuona Sabrina moja kwa moja alienda kumkumbatia na kumfanya Sabrina ashtuke kwani ilikuwa maajabu kwake, kisha Sam akamwambia Sabrina,
"Nataka kukuoa mpenzi"
Sabrina hakuamini alichokisikia kwani aliona kama yupo ndotoni vile.
Sam alizidi kumkumbatia na kuendelea kumwambia kuwa anataka kumuoa.
"Yani Sabrina, sitaki hata huu mwezi upite. Nataka uwe mke wangu Sabrina"
Sabrina alitulia tu muda huu huku akiwaza kile anachoambiwa na Sam, kisha akamuuliza,
"Hutajali kuhusu hii mimba?"
"Sio tatizo Sabrina, tena kuanzia sasa nataka uanze kusema kuwa hiyo mimba ni yangu. Na mtoto utakapomzaa atakuwa jukumu langu, nitampa jina langu na atakuwa mwanangu. Tumeelewana Sabrina?"
Sabrina hakuwa na jibu la zaidi kwahiyo akakubali kila kitu ambacho aliambiwa na Sam, huku moyoni mwake akifurahi sana na kuona kamavile ni ndoto.
"Kwakweli nakupenda Sabrina mpenzi, sitaki kukupoteza kabisa katika maisha yangu. Nitakulea, nitakuhudumia na nitakuwa nawe muda wote"
"Sina la kusema Sam, nashukuru sana. Na pia nakuahidi kukupenda kwa dhati katika maisha yangu yote. Sitakusaliti mpenzi"
Sam akamkumbatia tena Sabrina na kumwambia,
"Sasa tufungue ukurasa wetu mpya wa mapenzi. Na kesho kama kawaida nitakuja kukufata ili angalau hata ukatembee tembee ofisini"
Sabrina alimfurahia Sam kwani aliona ndoto zake zikitimia kwa namna hiyo.
Sam alishinda hapo nyumbani kwa Sabrina kwa siku hiyo, huku akiendelea kuongea maneno ya kumliwaza Sabrina.
"Vipi mlinzi wako yuko wapi?"
"Mlinzi wangu! Nani huyo?"
"Si Jeff, au leo unamkana Jeff kuwa ni mlinzi wako?"
Sabrina akatabasamu na kujibu,
"Ameenda kwao"
"Yani hajarudi hadi leo! Mwambie aje bhana, mi sitaki mke wangu apate shida nikiondoka"
"Hata usijali, atakuja tu"
Kisha wakaendelea na maongezi mengine huku wakiwa na furaha tele usoni.
Jeff akiwa nyumbani kwao, mama yake akamuuliza maswali,
"Hivi ile mimba aliyokuwa nayo Sabrina ni ya Sam?"
"Mmh! Alikwambia kama ana mimba?"
"Hajaniambia, ila mimba si inaonekana tu unafikiri ni siri? Kwani wewe hujui kama Sabrina ana mimba?"
"Kiukweli sijui chochote mama, yani khabari kuwa Sabrina ana mimba ndio kwanza nazipata kwako"
Sakina hakuwa na cha kuongezea kwani alijua wazi kama mwanae hajui kuhusu Sabrina kuwa na mimba basi ni dhahiri kwamba kuna mengi hayajui.
Kisha akambadilishia mada na kumwambia,
"Leo usiondoke hapa, kuna mambo nataka kuzungumza nawe badae"
Jeff akakubaliana na mama yake.
Sam alikuwa na furaha sana siku hiyo na muda wote alijikuta akitazama tumbo la Sabrina na kutabasamu.
Hata yeye mwenyewe alijishangaa kuwa imekuwaje hadi kujikuta akifurahia ujauzito wa Sabrina kiasi hicho wakati hapo mwanzo alitamani hata kummaliza mtu sababu ya huo ujauzito.
Alishinda pale kwa Sabrina hata usiku ulimkutia pale pale ndipo akamuaga Sabrina na kuondoka.
"Ukipatwa na tatizo lolote lile, usisite kunipigia simu na kunipa taarifa Sabrina"
"Sawa, hakuna tatizo"
Kisha Sam akaondoka zake.
Sabrina alipobaki mwenyewe akampigia simu Jeff na kumuuliza kama ataenda,
"Hapana, nitakuja kesho mamdogo"
Sabrina akakata ile simu kwani hakutaka jibu la vile toka kwa Jeff hivyobasi akaenda kulala huku akiwa amechukia vya kutosha, hivyobasi akajikuta akichelewa kupata usingizi.
Kulipokucha Sam alimfata Sabrina nyumbani kwake ila alimkuta bado kalala,
"Umekuwa mvivu siku hizi ila sio kosa lako, uzuri ni kwamba najua tatizo"
Muda huo Sam anamwambia Sabrina maneno hayo, yeye alikuwa akijinyoosha tu kwa uchovu wa usingizi.
"Basi, malizia kidogo huo usingizi wako. Badae nitakuja"
Kisha Sam akaondoka.
Muda ulipita kidogo, Sabrina akaamka vizuri sasa na kuoga kabisa.
Wakati anamalizia kuvaa akasikia mtu akigonga mlango wake na kwenda kumuangalia na kumfungulia.
Alikuwa ni binti ambaye sura yake haikuwa ngeni sana machoni pa Sabrina kisha akamkaribisha ndani.
Naye binti yule alikaribia na kukaa.
Kisha akaanza kujitambulisha kwa Sabrina, na mtu aliyemuelekeza pale
"Kwahiyo wewe umeambiwa kuwa mimi ndio nitakupa msaada?"
"Mama wa Jeff kaniambia kuwa Jeff huwa anakusikiliza wewe. Tafadhari nisaidie mamdogo, nampenda sana Jeff yani hadi nahisi kuchanganyikiwa"
"Sasa unataka nikusaidiaje?"
"Nisaidie nimpate Jeff, nitafurahi sana kwani ndiye mwanaume pekee ninayempenda katika hii dunia"
Sabrina alimuangalia huyu binti na kumuona kama wale mabinti wanaochanganyikiwaga, kisha akampooza kwa kumwambia kuwa ataongea na Jeff,
"Basi usijali, mi nitazungumza nae"
"Dah nashukuru sana mama, nashukuru kwakweli. Mweleze jinsi gani nampenda, jinsi gani nahitaji kuwa na yeye"
"Nimekwambia usijali, na sasa unaweza kwenda."
Yule binti hakuweza kuongea ya zaidi kwani Sabrina alishaonyesha wazi kuwa hataki tena kusikia zile khabari.
Kwahiyo yule binti akaondoka na kumfanya Sabrina aweze kumpigia tena simu Jeff kuwa aende ingawa yake jana alimkera.
"Ila mamdogo mi huwa sikuelewi, nikiwa huko unanitimua, nikiwa huku unaniita. Ni kwanini inakuwa hivyo?"
"Usiniulize maswali, nimekwambia njoo na ndio hivyo uje"
Sabrina akaikata ile simu na kuendelea na mambo yake mengine.
Jeff hakutaka kumchukiza Sabrina hivyo akajiandaa ili aende.
Mama yake alipomuona akitoka alimuuliza,
"Vipi unaondoka"
"Ndio mama nataka"
"Si unajua kama bado hatujazungumza?"
"Si ulisema tutazungumza jana? Sasa jana ikapita, basi tutazungumza siku nyingine"
"Kwani huko unakoenda kunakokupa na kiburi ni wapi?"
Jeff hakutaka kumjibu mama yake, badala yake akampungia mkono na kuondoka zake.
Moja kwa Jeff alikuwa akielekea kwa Sabrina.
Njiani alikutana na mzee wa makamo aliyekuwa amezungukwa na watu sababu alikuwa akiwatabiria mambo yajayo.
Jeff naye akaamua kumsogelea na kumuuliza, ila yule mzee kabla hajajibu akamwambia Jeff,
"Tena wewe kijana, umemtia mimba mtu mkubwa kwako na ni mtu ambaye mnaheshimiana sana tena...."
Kabla yule mzee hajaendelea, Jeff akajikuta akipepesa macho kwenye eneo lile la karibu na kushtuka kumuona Joy ambaye amewahi kuwa mwalimu wake na pia ni mchumba wa kaka yake na Sabrina na pia ni dada wa Sam.
Jeff akaona hapo mambo yataharibika na kuamua kujiondoa taratibu na kuendelea na safari zake.
Joy naye aliyekuwa lile eneo la utabiri, alimshangaa yule mzee akimwambia
"Hapo ulipo unatarajia kuzaa na kaka yako"
Joy hakutaka kumsikiliza yule mzee kwani alijua wazi ni muongo kisha akajisemea,
"Ndiomana Jeff kaondoka, kumbe mzee muongo bhana"
Kisha na yeye akaondoka zake.
Jeff alimkuta Sabrina akiwa ametulia kabisa, na moja kwa moja akamsalimia na kukaa kwani alijua wazi lazima kuna ujumbe wake.
Kisha Sabrina akaanza kumueleza Jeff kuhusu maamuzi yaliyofanywa na Sam,
"Yani nimefurahi sana, Sam kasema atakuwa tayari kumlea mwanangu. Tena tutampa majina yake"
Jeff hapo akashtuka na kumuuliza Sabrina,
"Mtampa majina yake? Majina gani hayo?"
"Yani huyu mtoto atakuwa ni wa Sam, kwahiyo ataitwa kwa kutumia majina ya Sam"
Jeff akajikuta gafla akianza kufoka,
"Inamaana sitakuwa na haki yoyote juu ya mtoto wangu mwenyewe?"
Muda huo Sam nae alikuwa ameingia pale ndani kwa Sabrina na kujikuta naye akishangaa kufoka kwa Jeff.
Jeff akajikuta gafla akianza kufoka,
"Inamaana sitakuwa na haki yoyote juu ya mtoto
wangu mwenyewe?"
Muda huo Sam nae alikuwa ameingia pale ndani
kwa Sabrina na kujikuta naye akishangaa kufoka
kwa Jeff.
Sam aliamua kuuliza ili ajue kuwa wanazungumzia mtoto gani,
"Mtoto? Mtoto yupi huyo?"
Sabrina na Jeff wakajikuta wote kwa pamoja wakimuangalia Sam, kisha Sam akawauliza tena,
"Nasikia mnazungumzia mtoto, huyo mtoto ni yupi?"
Jeff akataka kuongea kitu, ila kabla Jeff hajasema chochote Sabrina alianza kuongea huku akihusisha na kumbukumbu za mwanzo za maneno yale aliyowahi kumueleza Sam kuhusu Jeff,
"Huyu Jeff ni mjinga kwakweli, eti anataka kwenda kudai mtoto kwa yule binti wa mwanajeshi aliyempa mimba"
"Sasa ndio afoke? Si aende zake tu"
Kisha Sam akamuangalia Jeff na kumwambia,
"Sipendi umsumbue mke wangu haswa katika hiyo hali aliyokuwa nayo, sitaki umsumbue kabisa. Kama una mambo yako nenda ukafoke huko huko"
Muda huu Jeff alijikuta akiwa na hasira sana ila alitambua wazi kama ataongea chochote basi ataweza kusababisha mambo mengine makubwa zaidi, kwahiyo akajiondokea taratib u tena bila ya kuaga wala kuongea chochote cha ziada.
Ukimya kidogo ukatawala, kisha Sam akauvunja ukimya ule kwa kumuuliza hali Sabrina,
"Unaendeleaje lakini?"
"Naendelea vizuri"
"Ila kila siku mimi nakwambia kuhusu huyu Jeff kuwa hafai kuwa karibu ila wewe unamtetea, si unaona sasa alivyokuwa anafoka hapa utafikiri anaongea na mdogo wake. Tatizo amekuzoea sana"
Sabrina aliamua kutetea zile hoja kidogo kwa Sam,
"Hamna bhana, tatizo Jeff bado mtoto. Akikua ataelewa tu."
"Bado mtoto!! Haya mama, sikubishii"
Ikabidi Sabrina aingize maongezi mengine ili kuepusha mzozo usiokuwa rasmi.
Jeff alijikuta akiwa na mawazo sana huku akilaumu utoto wake,
"Laiti kama ningekuwa mkubwa haya yote yasingetokea. Sijui kwanini mama yangu alichelewa kunizaa jamani. Mbona mimi nampenda sana Sabrina kwanini mapenzi haya yananifanya hivi?"
Jeff alijikuta akinung'unika tu, na ili kupunguza yale mawazo akaona ni vyema kama apate kilevi kidogo ili aweze kuchangamsha akili yake na kupunguza mawazo aliyokuwa nayo.
Kwahiyo akaenda baa na kuanza kuagizia pombe aina ya konyagi ili aweze kulewa kwa haraka zaidi.
Mama wa Sabrina akiwa nyumbani kwake huku akiendelea na shughuli zake zingine, akasikia kuna mtu akimuita, na ile sauti ilikuwa ikitokea nje,
"Joy"
Akajiuliza,
"Ni nani huyo tena ambaye hadi leo ananiita jina langu?"
Akaamua kuacha mambo yake na kutoka nje ili akaangalie, ila hakukuta mtu yeyote na kumfanya azunguke hadi nyuma ya nyumba ila bado hakuona mtu yeyote.
Akaamua kurudi zake ndani, akashangaa kumuona mumewe akiwa pale sebleni.
Joy akashangaa sana na kustaajabu kumbe mumewe ndiye aliyemuita ili kumpima akili tu.
Wakafurahi pale na kuanza kuongelea mambo tofauti tofauti kwani ilikuwa ni muda mrefu kidogo tangu mumewe aondoke na siku hii ya leo ndio alikuwa amerudi.
Joy akaona sasa harusi za wanae zikinukia kabisa kwani waliyekuwa wakimuombea na kumsubiria ndio tayari alishawasili, na kumfanya Joy apatwe na hamasa ya kuwataarifu watoto wake kuwa baba yao amerudi.
Sabrina alimtazama Sam kwa furaha baada ya kupokea simu kuwa baba yake amerudi,
"Sam ndoa yetu tayari, karibia tunafunga"
"Ndio ni kweli, karibia tunafunga. Hata mi nimefurahia ujio wa bamkwe wangu"
Ikawa ni furaha huku mipango ya ndoa yao ikiendelea kupangwa na wao wenyewe kwa taratibu kabisa.
Jeff alirudi kwao akiwa amelewa kiasi hata mama yake akamshangaa mwanae,
"Jeff, kumbe huwa unakunywa pombe mwanangu"
Jeff alikaa kwenye kochi, kisha akamtazama mama yake kwa dakika chache na kuinama kidogo, kisha akainua tena kichwa chake na kumuuliza mama yake,
"Mama, mfano wewe ni mwanaume, kwa bahati nzuri ukampa mimba mwanamke umpendae utafanyaje?"
"Yani wewe Jeff loh, nitafanyaje tena hapo zaidi ya kumuoa huyo mwanamke sababu ushasema nimpendae"
Jeff akamuangalia tena mama yake na kuendelea kumuuliza,
"Na mfano ukasikia kuwa mwanamke huyo anataka kuolewa na mwanaume mwingine halafu mtoto wako anamkabidhi huyo mwanaume utafanyaje?"
"Maswali gani haya leo Jeff? Au ndio pombe hizo mwanangu"
"Sio pombe mama, nijibu kwanza"
"Mie sitakuwa na tatizo juu ya huyo mwanamke kuolewa, huenda ameniona simfai ingawa itaniuma sana ila tatizo langu litakuwa ni juu ya mwanangu. Hapo lazima nipambane sababu natakiwa kupata haki ya kuwa na mwanangu kwani mtoto huyo atakuwa ukumbusho pekee kwangu juu ya upendo niliompenda mama yake"
"Kwahiyo mama unanishauri nini?"
"Nakushauri nini kuhusu nini?"
"Mapenzi mama, yanautesa moyo wangu"
"Inamaana kuna mwanamke uliyempa mimba mwanangu? Ni mwanamke gani huyo?"
Jeff alitamani kumueleza kila kitu mama yake, ila ilipomjia ile kauli ya Sabrina kuwa wafanye kuwa siri yao aliamua kukaa kimya,
"Mbona kimya mwanangu? Niambie ili nijue jinsi gani nitakusaidia mwanangu"
"Acha tu mama"
Kisha Jeff akainuka na kuelekea chumbani kwake kupumzika kwanza.
Kesho yake, Sabrina alienda nyumbani kwao kumsalimia baba yake na kuweza kuongea nae mawili matatu juu ya mambo yake ya ndoa.
Alifurahi kumuona tena baba yake, na alikutana na kaka yake nae akiwa na lengo kama lake.
Deo akawaambia watoto wake,
"Naona mlikuwa mkinisubiri kwa hamu maana kila mmoja anaongelea ndoa tu hapa. Ila ni jambo jema na nitasimamia vyema swala hili."
"Ndio baba, tena ukiharakisha itakuwa vizuri zaidi"
"Mie sina tatizo, labda nyie mcheleweshe"
Wakakubaliana na baba yao na kufurahi pamoja.
Wakati wakiendelea na mazungumzo, kuna mgeni alifika pale nyumbani kwakina Sabrina, na wote walimshangaa kwavile sura yake ilikuwa ni ngeni machoni pao.
Sabrina akatoka nje kwenda kumsikiliza.
Akamsogelea na kumsalimia,
"Samahani bibi, tukusaidie nini"
"Nisaidie maji tu mjukuu wangu, yani hapo utakuwa umenipa msaada mkubwa kupita yote duniani"
Sabrina akaona isiwe tatizo sana akaamua kwenda ndani kumchukulia huyo bibi maji.
Baada ya muda kidogo, Sabrina akatoka na kikombe cha maji na kumkabidhi yule bibi ambaye alikunywa yale maji na kumshukuru sana Sabrina, ila kabla Sabrina hajarudi tena ndani kwao yule bibi akamshika mkono na kumwambia Sabrina,
"Samahani mjukuu wangu, najua hunijui wala sikujui ila nimejisikia kukwambia jambo hili"
Sabrina akamsogelea tena karibu ili aweze kusikia kuwa ni jambo gani ambalo yule bibi anataka kumwambia,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Niambie tu bibi"
"Ni hivi, katika dunia hii kila jambo hutokea kwasababu fulani na hakuna siri itakayodumu milele"
"Mmh unamaana gani?"
"Sina maana yoyote ile mbaya ila moyo wangu umeona nikwambie hilo kwani ipo siku litakusaidia hapo badae"
Yule bibi akamuaga Sabrina bila ya kujua kuwa amemuacha Sabrina akiwa na mawazo kwa kiasi gani.
Sabrina alirudi ndani kwao huku akiwa amenyong'onyea mpaka baba yake akaamua kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
"Aah hamna tatizo baba"
Kisha akawaaga pale na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake ili aende akajiwazishe huko.
Akiwa njiani, akapigiwa simu na Sam,
"Uko wapi?"
"Nipo kwenye daladala narudi kwangu"
"Kwanini hukunisubiria nije kukufata?"
Sabrina akawa kimya, Sam akamwambia Sabrina kuwa ashuke na kumtajia Sam alipo kisha yeye atamfata mwenyewe.
Sabrina akafanya kamavile alivyoambiwa na Sam ili kuepuka swala la kumchukiza.
Alishuka na kukaa kwenye kituo huku akimngoja Sam aje kumfata.
Kuna mtu akatokea nyuma yake na kumgusa Sabrina, alipogeuka akakutana macho kwa macho na Francis,
"Khee Francis upo?"
"Nipo ndio, mwanaume pekee mwenye mapenzi ya dhati na wewe Sabrina"
"Saivi nimekuwa Francis, sio Sabrina yule wa zamani kwahiyo maneno yenu hata kidogo hayaingii katika akili yangu"
Francis akamuangalia Sabrina kwa makini huku akitaka kuongea neno lingine, ila muda huo huo Sam nae akawasili eneo lile na kumfata Sabrina pale kituoni alipokuwa amekaa.
Alipofika, akamshika mkono Sabrina na kuondoka nae bila hata ya kumsalimia Francis ambaye aliwaangalia hadi walipoondoka na gari kabisa.
Sam alimpeleka Sabrina moja kwa moja hadi nyumbani kwa Sabrina na kuingia ndani huku akihitaji kujua mushtakabali wa ndoa yao,
"Vipi baba anajua kama wewe ni mjamzito?"
"Hapana, ila kesho twende wote ili nimueleze pia kuhusu ujauzito na ukapange nae kila kitu"
"Yule mzee sina tatizo nae kwakweli, kwavile mambo yake ni kizungu tu. Mungu amlinde mzee wetu, kesho tutaenda pamoja"
Sabrina akakubaliana hivyo na Sam kisha Sam akamuaga na kuondoka kwenda nyumbani kwake.
Sabrina alipokuwa amebaki akapokea simu kutoka kwa Sakina, baada ya salamu, Sakina akaanza kumpa malalamiko yake aliyonayo kuhusu mtoto wake Jeff,
" Hebu niambie ukweli Sabrina, huko kuna mwanamke yeyote Jeff kampa mimba?"
Sabrina akafikiria jibu la kumpa Sakina, akahusisha na maelezo aliyowahi kumwambia Sam kuhusu Jeff, akaamua kumwambia Sakina kwa mtindo huo kuwa Jeff kuna binti wa mwanajeshi ndiye aliyempa mimba,
"Yani huyu mtoto wangu anamakubwa kwakweli, kumbe ni kweli? Nilitaka tu kuhakikisha"
"Ndio hivyo dada"
"Tena kesho nataka anipeleke huko kwao na huyo binti ili nikajue mbichi na mbivu"
"Dada mi nakushauri hayo mambo muachie tu Jeff mwenyewe, hata mimi yalishanishinda hapa"
"Kwakweli Sabrina, siwezi kuangalia upuuzi anaofanya Jeff kila siku huku, lazima nifatilie"
Sakina akakata ile simu na kumfanya Sabrina nae apatwe na mawazo tena kwa kiasi fulani kwani hakutegemea kama Sakina atahitaji kuingilia kati swala hilo.
Sabrina aliamua kwenda kulala, ila kabla hajalala alipigiwa simu na Jeff,
"Mamdogo umemwambia nini mama?"
"Sikuwa na la kufanya Jeff ikabidi tu nimdanganye"
"Sawa umemdanganya, sasa mi kesho nitampeleka wapi kumwonyesha? Maana mama amekazania kuwa nimpeleke kwa huyo mwanamke"
"Hapo utajijua mwenyewe utakachofanya ila mimi tu usinihusishe juu ya hilo"
"Mmmh mi nikishindwa namleta kwako"
Simu ile ikakatika na kumfanya Sabrina ajilalamishe peke yake,
"Toto halina akili kabisa hili, sijui hata limetokea wapi"
Sabrina alilala ila huku akiwa na hasira kiasi.
Wakati amelala, taswira ya yule bibi ambaye alienda muda wa mchana pale kwao ilimjia usoni tena na maneno yale yale yakajirudia na kumfanya Sabrina ashtuke na kuwa na mawazo mengi mengi huku akiendelea kujiuliza kuwa yule bibi alikuwa na maana gani ila hakupata jibu hadi panakucha.
Siku hii Sakina alimkazania mwanae ili akamuonyeshe kila kitu kilichojificha,
"Kwanza kabisa nataka unionyeshe huyo binti uliyempa mimba, nipeleke kwao nipajue hata kama wazazi wake ni wakali vipi wee nipeleke tu. Sipendi kukuona ukichanganyikiwa kwa mambo ambayo hata mimi mama yako naweza kuyashughulikia. Napenda kuona ukiwa na furaha tu muda wote"
Jeff hakujua ni uongo gani amwambie mama yake ili amridhishe, aliona mama yake kutaka kujua kila kitu kwa hali na mali.
Sam alimfata Sabrina, kisha wote kwa pamoja wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa wakina Sabrina ili kuweza kujadiliana kuhusu mipango ya ndoa na kumwambia Deo kuhusu ujauzito wa Sabrina.
Sam akamueleza baba mkwe wake,
"Napenda ndoa yangu na Sabrina iwe wiki ijayo kwavile nahitaji mtoto wetu azaliwe ndani ya ndoa"
Deo akafurahi, ila kabla hajasema jambo lolote wakamuona Jeff na Sakina wakiwa pamoja pale nyumbani kwa wakina Sabrina, ambapo Jeff akasema,
"Siwezi kabisa kukubaliana na jambo hili"
Wote waligeuka na kumuangalia.
Deo akafurahi, ila kabla hajasema jambo lolote
wakamuona Jeff na Sakina wakiwa pamoja pale
nyumbani kwa wakina Sabrina, ambapo Jeff
akasema,
"Siwezi kabisa kukubaliana na jambo hili"
Wote waligeuka na kumuangalia.
Sabrina akaona wazi kuwa ule ndio muda wa kufanya jambo fulani, akakumbuka na ule msemo kuwa ukicheka na nyani utavuna mabua.
Alijua wazi kuwa akijifanya kuzimia, Jeff ndio atajifanya muongeaji mzuri kwahiyo jambo jema ni kucheza na akili yake kwa haraka iwezekanavyo.
Sabrina alijivika ujasiri na kuinuka, akamfata Jeff na kumshika mkono huku akimvutia kwa nje.
Wote pale ndani walibaki kuduwaa kwani hawakuelewa kwanini Jeff alisema vile na kwanini Sabrina ameona ni vyema kumvutia nje ya nyumba.
Sabrina alimvuta Jeff nje kabisa ili hata akizungumza asiweze kusikiwa na mtu yeyote, Sabrina akajikuta akimuuliza Jeff kwa hasira,
"Hivi una akili wewe?"
Kisha akamnasa kibao, Jeff nae alikuwa ametulia tu ingawa Sabrina alimnasa vibao vitatu mfululizo,
"Unakaa kimya unaniletea kiburi eeh!"
"Tafadhari nisamehe, ila mimi sikuwa na lengo ambalo wewe unalifikilia kuwa ninalo. Siwezi kufanya lolote baya la kukukera wewe Sabrina. Sababu nakupenda"
Jeff alijikuta akimkumbatia kwa nguvu Sabrina.
Muda huo Sakina nae alikuwa ameshatoka nje akiwa ameelekezea macho yake kule alipo Jeff na Sabrina kwahiyo lile tukio la Jeff kumkumbatia sana Sabrina mama yake alikuwa ameliona na kuendelea kuwaangalia pale.
Sabrina akajitahidi kumtoa Jeff kwenye mwili wake, ila Jeff hakutaka kutoka na kumwambia Sabrina,
"Nakuomba jambo moja tu"
"Jambo lipi hilo?"
"Naomba kulala karibu yako kwa usiku mmoja tu, halafu mimi sitakusumbua tena"
"Ila wewe Jeff wewe kwanini unakosa akili kiasi hicho?"
Jeff alizidi kumkumbatia Sabrina bila ya kutaka kutoka kwenye mwili wa Sabrina, ikabidi Sabrina amkubalie ombi lake ili aweze kuganduka kwenye mwili wake.
Kisha Jeff akamuachia Sabrina, muda huo Sakina nae alianza kusogea pale walipo kisha Sabrina akamwambia Jeff
"Tafadhari ondoka, tena ikiwezekana nenda hata ukapumzike nyumbani kwangu ila usithubutu kumwambia chochote mama yako kuhusu yale mambo kabisa"
Jeff akaanza kuondoka, na Sakina alikuwa tayari amefika eneo lile,
"Imekuwaje tena? Mbona ananiona mimi ndio anakimbia?"
"Huyu mwanao huyu Sakina, itabidi siku tutulie na kuelezana vizuri kwavile anajielewa yeye mwenyewe kwakweli"
"Hadi nimechoka hapa mdogo wangu, ndio shida ya kuzaa katoto kamoja hii yani saivi najuta na kutamani nipate angalau mtoto mwingine wa ziada"
"Basi dada, wee kapumzike tu nyumbani, mi nikipata muda nitakuja tuongee vizuri ili tujue jinsi ya kumsaidia huyu Jeff"
Sakina akamuaga Sabrina pale na kuondoka, kisha Sabrina akaelekea ndani kwao ambapo kila mmoja alitaka kujua sababu ya Jeff kuja na kuwaongelea kiasi kile.
Wakawa wanasubiria jibu kutoka kwa Sabrina, ambapo Sabrina kama kawaida yake akaanza kuwachanganyia mada pale,
"Unajua yule Jeff akili yake sio nzuri, na kiukweli ni mimi tu ninayewe za kuisoma akili yake na kujua jinsi gani namtuliza ile akili"
Sam akaingilia kati na kuuliza,
"Ndio utuambie sasa, alikuwa na shida gani?"
"Jamani hayo mambo tuachane nayo na tuendelee kujadili mambo yetu, wale nishaongea nao na kama lingekuwa jambo la maana basi ningewaambia, ilimradi sijasema chochote basi mjue kwamba hapakuwa na lolote lile la maana. Naomba tuendelee na mambo yetu mengine"
Wakakubaliana na Sabrina ila bado Sam alikuwa na mashaka juu ya maneno ya Sabrina ingawa alikubaliana nae ili kuepusha mzozo tu.
Mipango ilipoisha, Sam alimuomba Sabrina kuwa waende nyumbani, kisha Sabrina akamuuliza Sam,
"Eeh tunaenda nyumbani kwangu au kwako?"
"Nataka twende kwako Sabrina, tena leo nataka nikalale huko huko"
Sabrina hakutaka kumpinga Sam kwani al ijua wazi kama akimpinga basi Sam anaweza kumuhisi vingine.
Alichokifanya Sabrina ni kumuandikia Jeff ujumbe mfupi kuwa aondoke kwahiyo akamuelezea hali halisi ilivyo ili Jeff apate kumuelewa.
Sabrina aliondoka na Sam mpaka nyumbani kwake, ambapo Sam alianza kuikagua nyumba ya Sabrina kila mahali utafikiri yeye ni mkaguzi mkuu wa nyumba za watu.
Sabrina alikuwa akimuangalia tu kwani alijua wazi kuwa hawezi kukutana na kitu chochote.
Sam alipojiridhisha sasa, akarudi na kukaa na Sabrina kisha akamwambia Sabrina,
"Leo tutaenda kula hotelini kisha tutarudi kulala"
"Hoteli gani leo?"
"Kuna hoteli nitakupeleka, huko bado sijawahi kwenda na wewe"
Kwahiyo Sam akamuomba Sabrina ajiandae sasa kwaajili ya kwenda huko hotelini, na alipomaliza kujiandaa Sabrina akatoka na kumfanya Sam acheke wakati wanaondoka,
"Unacheka nini sasa?"
"Khee tumbo lako linaonekana sana siku hizi"
Sabrina akajitazama na kuona kweli tumbo limesonga mbele, naye akajicheka na kuendelea na safari yao.
Walifika hapo hotelini na kuagiza chakula na vinywaji, baada ya muda kidogo Sam akamuaga Sabrina kuwa anaenda maliwatoni kidogo kwahiyo Sabrina alitulia pale alimsubiria.
Zilipita sekunde chache, akasogea muhudumu hadi pale alipo Sabrina na kumwambia,
"Naona siku hizi jamaa anajiweza, hadi kakupa mimba duh!"
Sabrina alimshangaa huyu muhudumu na kumuuliza,
"Unamaana gani wewe?"
"Sina maana mbaya, ila nampongeza tu kwa kumpa daktari wa magonjwa yote"
Sabrina bado hakumuelewa huyu dada, na wala hakujua kuwa alikuwa na maana gani na kujikuta akikazana kumuuliza,
"Unamuongelea nani wewe?"
Sam nae alikuwa amerudi na kumfanya yule dada aondoke, ikabidi Sam amuulize Sabrina,
"Kwani huyo dada alikuwa anataka nini?"
"Hata sijamuelewa, eti ananishangaa mimi kuwa mjamzito"
Hapo hapo Sam akaelewa mushtakabali wa mazungumzo ya yule dada, tena hakutaka kujua kama Sabrina ameelewa au hajaelewa kwani tayari alishakuwa na hasira.
Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Nisubiri kidogo tu"
"Unaenda wa pi tena jamani?"
"Wee nisubiri tu hata sikawii"
Sabrina hakujua ni kitu gani Sam anaenda kufanya huko.
Sabrina alibaki kuduwaa tu, baada ya muda mfupi Sam akarudi pale na kukaa.
Dakika mbili kupita, yule dada nae alifika pale huku akikazana kumuomba Sam msamaha, na baada ya muda kidogo wakaja walinzi kumvuta na kumwambia,
"Umeambiwa hutakiwi kuonekana katika hoteli hii kuanzia sasa"
Wakamvuta na kumfanya hata asiweze kushkia jibu la Sam.
Sabrina akamuuliza Sam,
"Vipi Sam? Inamaana umeenda kumshtaki?"
"Huwa sipendi ujinga kabisa mimi, yeye maisha ya watu yanamuhusu nini? Kama anataka kazi ya kutangaza maisha ya watu basi atoke hapa akayatangaze huko mbele ya safari. Anajua mimi ni nani kwenye hii hoteli au alikuwa anajiongelesha tu bila kujua! Ngoja akatangetange mtaani ndio ajue maisha, wambea huwa hawafanyi kazi kwahiyo asipokuwa na kazi ndio akasambaze vizuri umbea wake"
Sam aliongea kwa jazba kabisa na kumfanya Sabrina atambue wazi kuwa Sam amechukizwa sana na kitendo kile, ikabidi atulie tu ili kuepusha matatizo mengine huku akijilaumu yeye mwenyewe kwa kumueleza Sam.
Chakula kilifika pale, wakala kiasi kisha wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwao.
Usiku ulikuwa tayari umeingia, na muda wa kulala ulikuwa tayari umefika.
Sabrina alienda moja kwa moja chumbani kwake na kumvuta mkono Sam ili waweze kulala pamoja, ila Sam alikataa na kumwambia Sabrina kuwa muda wa wao kulala pamoja bado haujafika,
"Muda gani unaouzungumzia Sam? Harusi yetu ni wiki ijayo tu hapo, sasa kuna ubaya gani kama tukiamua kulala wote leo?"
"Sabrina, nakupenda sana. Hebu jaribu tufate sheria za dini, najua hata wewe hukufurahia kupata hiyo mimba kwa kubakwa. Nimeamua kuchukua hayo majukumu na kusema kuwa mimba ni yangu ila bado sitaweza kuivunja ile sheria ya tendo la ndoa"
Sabrina akamuangalia tena Sam na kumuuliza,
"Kwahiyo na leo utalala hapo sebleni?"
"Hapana, naenda nyumbani kwangu ila yote haya ni katika kukuonyesha tu kuwa jinsi gani nakupenda"
Sam akamsogelea Sabrina na kumbusu kwenye paji la uso kisha akamuaga na kuondoka zake.
Sabrina aliingia chumbani kwake na kukaa kitandani huku akimtafakari Sam,
"Hivi huyu mwanaume ni wa aina gani? Inamaana kweli anangoja ndoa? Yani hakuna chochote alichoshawishika kwangu? Mmh sijapata kuona mambo haya jamani. Huyu mwanaume mzima kweli huyu?"
Sabrina alijidadisi bila ya kupata jibu lolote la maana na kuamua kulala tu.
Asubuhi na mapema, mlango wa chumbani kwa Sabrina ulikuwa ukigongwa, moja kwa moja Sabrina akajua kwamba mgongaji ni Sam ila akajiuliza kuwa Sam amepata wapi funguo wa mbele wa ile nyumba? Jibu likamjia kuwa huenda Sam akawa na funguo hizo.
Akainuka pale kitandani na kwenda kumfungulia, mgongaji alikuwa ni Jeff ambaye alienda moja kwa moja na kumkumbatia kwanguvu Sabrina huku akimwambia,
"Nimekumiss sana mamy"
Sabrina alisimama tu akimshangaa Jeff kisha akamuuliza,
"Umelala wapi wewe?"
"Sikulala, mawazo yote yalikuwa juu yako"
"Kheee makubwa haya, ulikuwa unaniwaza mimi? Kuwa nimekufa au nimekuwaje?"
Jeff akazidi kumkumbatia Sabrina na kumwambia,
"Nakupenda sana, nakupenda sana, nakupenda sana"
Akawa kama mtu anayetaka kulia, Sabrina akamuhurumia na kumkumbatia pia kisha akamuomba airudishe akili yake kwani alimuona kamavile mtu aliyechanganyikiwa.
"Jeff, tulia na unisikilize nitakachokwambia"
"Tafadhari mamy, usiniambie neno lolote zaidi ya nakupenda. Nakuomba sana"
"Haya basi niambie unachotaka cha zaidi toka kwangu ni nini?"
"Nahitaji pendo lako, mapenzi yako. Nakuhitaji mamy, nakupenda sana labda uniue ndio itakuwa njia pekee ya kukuepusha na usumbufu wangu. Kwasasa nahitaji kuwa karibu na wewe kabla ya ndoa yako, tafadhari nikubalie nateseka sana mimi. Na kama kulaumu basi usinilaumu mimi, bali ulaumu moyo wangu ambao umekupenda wewe"
"Sawa, ila niahidi jambo moja tu. Baada ya ukaribu huo na mimi hautanisumbua tena kwenye ndoa yangu, niahidi hilo sasa"
"Nakuahidi sitakusumbua kabisa ingawa moyo wangu utaumia sana"
Sabrina akajaribu kuichekecha akili yake kwa maamuzi ambayo anataka kuyafanya ila hakupata jibu la haraka, na kuamua kutoa jibu la papo kwa hapo.
"Basi tutashinda wote siku nzima ya leo, ila kesho nitakuwa na majukumu yangu mengine"
"Asante mamy"
Jeff akamkumbatia tena Sabrina, kisha Sabrina akamuaga pale na kurudi kumalizia usingizi wake hadi pakuche kabisa.
Sam alikuwa akitafakari kama Sabrina ametilia maanani hayo maneno aliyoambiwa na yule muhudumu na kuanza kujiuliza kuwa huenda Sabrina ameanza kumuhisi kutokukamilika.
"Leo nitaenda usiku, bila ya kumwambia. Napenda nimfanyie surprise"
Akajipanga kwenye akili yake kitu cha kumfanyia Sabrina ili afurahi.
Kisha akainuka na kwenda kutembelea ofisi yake kwanza.
Sabrina alipoamka rasmi sasa akaenda kuoga na kutoka sebleni, akakuta Jeff ameshamuandalia chai ili anywe, kisha akamuuliza kwa masikhara tu,
"Hujaniwekea madude yako humu kweli na leo? Maana wewe mambo yako unayajua mwenyewe"
"Hapana mamy sijaweka chochote, siwezi kurudia tena makosa. Nimekuwa kijana mzuri sasa, na ningependa nikunyweshe hiyo chai"
"Khee, nitolee balaa mie. Umekuwa na maneno mengi kama muimba mashairi"
Sabrina akainywa ile chai.
Na alipomaliza, alikaa pamoja na Jeff, mara nyingi Jeff alionekana kumfanyia vituko vituko Sabrina ili kumfanya acheke na kufurahia uwepo wake.
Mara simu ya Sabrina ikaita, na mpigaji alikuwa Sakina ila kabla Sabrina hajaipokea Jeff akamwambia,
"Akiniulizia mimi mwambie sipo"
Na Sabrina alipoipokea ile simu, swali kutoka kwa Sakina lilikuwa ni hilo hilo la kumuulizia Jeff, naye Sabrina akamjibu kuwa Jeff hayupo, na simu ilipokatika wakajikuta wote wakicheka kwa pamoja.
Usiku ulipofika, Jeff akamuomba Sabrina,
"Nina ombi moja"
"Ombi gani hilo"
"Tafadhari nikubalie"
"Ndio nitakukubalia ila mpaka uliseme"
"Naomba usiku wa leo tu nikalale pembeni yako, tafadhari nakuomba"
Jeff alionyesha kama kulengwa na machozi na kumfanya Sabrina akubali kwavile amesema kuwa ataenda kulala pembeni yake.
Kisha wakainuka na kwenda kulala.
Sam alifika kwenye nyumba ya Sabrina kwenye mida ya saa tano usiku, kwavile alikuwa na funguo za geti akafungua bila ya kugonga.
Alipoingia, moyo wake ukamtuma kuwa akachungulie kwanza dirishani kwenye chumba cha Sabrina.
Ila aliposogea madirisha yote yalikuwa yamefungwa vizuri, ila aliposogeza sikio akasikia kuna miguno ya kimahaba kutoka kwenye kile chumba.
Sam alifika kwenye nyumba ya Sabrina kwenye
mida ya saa tano usiku, kwavile alikuwa na funguo
za geti akafungua bila ya kugonga.
Alipoingia, moyo wake ukamtuma kuwa
akachungulie kwanza dirishani kwenye chumba cha
Sabrina.
Ila aliposogea madirisha yote yalikuwa yamefungwa
vizuri, ila aliposogeza sikio akasikia kuna miguno ya
kimahaba kutoka kwenye kile chumba.
Sam akapatwa na wasiwasi juu ya kitu kinachoendelea ndani ya chumba cha Sabrina.
Akaenda kufungua mlango, akaona ni wazi umefungwa kwa ndani kwani hata haukufunguka.
Akaanza kujiuliza kuwa Sabrina yupo na nani, akajaribu kuipiga simu ya Sabrina ila iliita tu bila ya kupokelewa.
Sam akaona hapa sasa mambo yanakuwa magumu kwake.
Akaamua tena kwenda mlangoni huku akibamiza mlango huku akiita kwa nguvu jina la Sabrina.
"Sabrina, Sabrina"
Sabrina alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa sana tena kwa nguvu na moja kwa moja akaigundua ile sauti kuwa ni ya Sam.
Jeff akainuka na kwenda kumfungulia Sam mlango huku akifikicha fikicha macho yake kuonyesha kuwa ametoka usingizini, ambapo pale pale mlangoni alikula ngumi ya sura hadi chini, kisha Sam akamkwida Jeff na kuanza kumuuliza,
"Niambie ukweli sasa, mamako mdogo yupo na nani chumbani kwake?"
"Mi sijui"
Sam akampiga tena Jeff ngumi ya sura na kuzidi kumkunja huku akitaka amwambie ukweli wa mambo,
"Unanionea kaka, sijui chochote hapa unanionea tu"
"Nakuonea kitu gani wakati wewe ndio unaishi na Sabrina humu ndani"
"Ndio, ila sijui chochote. Mi nimetoka kulala, hata sijui nikwambie ukweli upi"
Sam akazidi kumsukumia Jeff chini kwa hasira, kisha akamuacha pale chini na yeye kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Sabrina.
Alipoufungua mlango wa Sabrina, ulifunguka bila ya tatizo lolote kwamaana kwamba hakuufunga kwa funguo ndani.
Sam alimuona Sabrina akiwa amelala huku akiweweseka kimahaba na kumshangaa kwani sauti aliyoitoa ilikuwa kamavile yupo na mwanaume.
Ikabidi amsogelee karibu zaidi na kumshtua kwa kumuamsha ambapo Sabrina alishtuka kamavile mtu aliyetoka kwenye usingizi mzito sana na kumfanya awe kama amepatwa na mshangao kwa kumuona Sam muda huo kwenye chumba chake.
Sam nae alikuwa akimshangaa tu kisha akamuuliza,
"Kwani una matatizo gani Sabrina?"
"Matatizo? Kivipi?"
Huku akijifikicha fikicha macho na kumfanya Sam aone aibu kumueleza kile alichomuhisi na alichokisikia.
Akaamua kumuuliza swali jingine,
"Mbona leo hukufunga mlango wakati umelala?"
"Kumbe sikufunga mlango? Hapa ndio nilitaka kukuuliza kuwa umeingiaje bila kugonga!"
Huku akipiga miyayo ya usingizi na kufanya Sam ampe pole sasa,
"Pole sana mpenzi kwa kushtua usingizini ila sijui nimekushtua wakati unaota!"
"Wakati naota? Kwanini unasema wakati naota?"
"Nimekuona ukiweweseka hapa"
"Mmh Sam jamani, mbona mi sikumbuki huko kuota! Umenikuta nikiweweseka kweli?"
"Ndio, tena hadi ulikuwa ukiongea peke yako"
"Mmh uongo huo Sam, maneno gani hayo nimeongea?"
"Mmh tuachane na hayo basi, hebu tuzungumze mengine au nikuache uendelee kupumzika na samahani kwa kukushtua"
Sabrina alimuangalia tu Sam akifululiza na maneno yake kisha akavuta shuka kuonyesha kwamba swala la kumuacha yeye apumzike ni la muhimu zaidi.
Sam nae alipoona vile akainuka na kuanza kutoka.
Ila kabla hajatoka akamwambia Sabrina,
"Ukumbuke kufunga mlango wako"
"Sawa hakuna tatizo"
Kisha Sam akatoka.
Alipofika sebleni alimkuta Jeff akiwa kakaa huku amejiinamia kwa mawazo.
Akamuinua kichwa na kumwambia,
"Samahani dogo"
Kisha akatoka nje na kuondoka.
Jeff akainuka na kufunga mlango, kisha akarudi kukaa pale kwenye kochi huku akitabasamu.
Baada ya muda mfupi, Sabrina alitoka chumbani kwake na kumfata Jeff pale sebleni,
"Uwii ndio amekuumiza hivyo?"
Jeff akatikisa kichwa kuitikia,
"Pole jamani, hatukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya hii"
Jeff akawa anatabasamu na kucheka, na kumfanya Sabrina amuulize,
"Unacheka nini sasa"
"Nimefurahi tu, yani siamini kama hili jambo limepita kwa amani kiasi hiki"
"Muone vile, yani leo dah sijui hata ingekuwaje jamani! Ila Jeff una akili sana, ngoja tukalale halafu asubuhi tujue nini kinaendelea"
Wakainuka na kwenda kulala.
Kulipokucha, Sam alifika tena nyumbani kwa Sabrina asubuhi na mapema na kwa muda huo alimkuta Sabrina akiwa bafuni kuoga.
Sam akaingia chumbani kwa Sabrina na kukaa kwenye kitanda.
Katika kuangaza angaza macho yake kwenye kile chumba, akaona shati ambalo huwa anamuona Jeff amevaa.
Akajiuliza maswali bila majibu huku akimngoja Sabrina atoke bafuni.
Sabrina alipotoka bafuni alishangaa kumuona Sam akiwa ameshikilia lile shati la Jeff, moja kwa moja akajiandaa kumpa majibu.
Na Sam alipomuona Sabrina moja kwa moja akamuuliza,
"Hii shati inafanya nini humu chumbani kwako?"
"Ooh ni shati ya Jeff hiyo, wakati naanua nguo nikasahau nayo nikaingiza ndani kwangu. Maskini Jeff najua hata nae hajui kama shati yake ipo humu"
Kisha Sabrina akaichukua ile shati toka mikononi mwa Sam na kumwambia,
"Ngoja nimpelekee huyo Jeff"
Sam hakusema kitu zaidi tu ya kumtazama tu na kumuangalia kile anachofanya.
Sabrina alitoka sebleni huku akiongea sauti kubwa ili Sam asikie,
"Wee Jeff shati lako hili, nilijisahau na kuingia nalo kwangu baada ya kulianua"
"Sawa asante"
Kisha Sabrina akarudi tena chumbani kwake, ambapo Sam alitoka na kumpisha Sabrina ili avae.
Sabrina alizidi kupatwa na mashaka juu ya tabia ya Sam.
Joy na James walijipanga sasa kwaajili ya kukutanisha familia zao ili kufanikisha ndoa yao.
Joy alianza kumwambia James kuhusu Sam,
"Unajua familia imefurahi sana kuona Sam amepata mwanamke na kumpa mimba"
"Inamaana Sam hajawahi kuwa na mwanamke?"
"Yani hatujawahi kumuona akiwa makini na mwanamke kiasi hiki, sijui Sabrina kampa nini Sam kwakweli"
James akatabasamu tu huku wakiwaza siku yao itakavyokuwa.
Baada ya Sabrina kumaliza kujiandaa, akatoka sebleni na kumkuta Jeff na Sam kamavile wakijadiliana kitu fulani ambacho yeye hakukifahamu kwa wakati huo ila hakuwa na mashaka kwani alijua wazi kuwa badae Jeff atamweleza kila kitu walichokuwa wakizungumza.
Kisha akamsogelea Sam ili kumuonyesha kwamba ameshajiandaa,
"Haya twende sasa"
"Ila hujaniambia kama tunaenda wapi Sam"
"Hata usijali, utaenda kupaona huko huko"
Wakaondoka pale nyumbani na kuelekea mahali ambako Sabrina hakupajua kwa wakati huo.
Walifika mahali Sam akasimamisha gari na kuingia kwenye eneo hilo.
"Sabrina, tunaenda hapo kuchagua nguo za harusi"
Sabrina alifurahi sana na kuona sasa ndoto yake ya kuolewa inatimia, tena ile ndoto ya kuolewa na mwanaume tajiri kama Sam.
"Yani Sam, hata siamini jamani"
"Ndio uamini sasa, harusi yetu tayari inanukia. Nataka mtoto wetu tumlee ndani ya ndoa"
Kwakweli moyo wa Sabrina ulimwambia wazi kuwa katika ulimwengu hakuna tena mwanaume kama Sam, mwanaume anayeweza kukubali mimba isiyoeleweka na kutaka kuharakisha ndoa ili mtoto ambaye ni haramu kwake azaliwe ndani ya ndoa na awe mtoto halali.
Sabrina hakujua cha kumwambia Sam zaidi ya kuonyesha tabasamu tu ili kudhihirisha kwamba amefurahi sana.
Waliingia kwenye hilo duka na kuanza kuchagua nguo zao za harusi.
Walichagua ngo na kujaribisha kisha wakazipenda na kuamua kwenda kuzilipia ili waondoke nazo.
Sabrina alipoangalia upande wa malipo wa duka hilo, alimuona mpokea pesa ambaye alikuwa ni rafiki yake mkubwa hapo kabla ila urafiki wao ukavunjika kwa mambo ambayo alifanyiwa.
Huyu si mwingine bali alikuwa Sia.
Sabrina alihisi moyo wake kujawa na ukungu kwa muda huo kwani hakutegemea kumuona huyo Sia mahali hapo.
Kisha akamgeukia Sam na kumwambia,
"Naomba tuondoke"
"Kwanini Sabrina?"
"Nguo za hapa sijazipenda"
"Jamani Sabrina, si ndio umesema mwenyewe kuwa umezipenda hizi tukazilipie!"
"Naomba unisikilize Sam, kama nilikwambia nimezipenda basi mimi mwenyewe nakwambia tena kuwa sijazipenda. Naomba tuondoke Sam"
Muhudumu wa lile duka kuona wanabishana, akaona ni vyema akamwambie yule mkubwa wake ili awabembeleze naye wapate kuchukua zile nguo.
Sia alipoambiwa, akasogea hadi eneo walilokuwepo wakina Sabrina ila alipomuona ni Sabrina akashindwa hata jinsi ya kumwambia na kujikuta akimuangalia tu huku akitamani hata kumuomba msamaha, ila muda huo Sam na Sabrina walishafikia muafaka na kuondoka kwenye duka lile.
Ambapo walienda kwenye duka lingine na kununua zile nguo.
Sia aliwaangalia na kurudi kwa yule muhudumu wake kisha akamwambia,
"Unajua, unaweza kufanya kitu leo ila madhara yake yakaja badae kabisa ingawa wakati unakifanya ulijua hakina madhara"
"Kwanini unasema hivyo?"
"Sasa najutia kosa nililolifanya miaka mingi iliyopita. Ila ndio hivyo tena. Ipo siku atanisamehe"
Kisha akarudi eneo lake na kuendelea na kazi.
Sam na Sabrina walipomaliza kununua mahitaji yao binafsi ya harusi wakarudi nyumbani sasa.
Kisha Sabrina akamuuliza swali Sam kama kumtega hivi,
"Vipi Sam, leo nikalale nyumbani kwako basi"
"Bado Sabrina, haraka ya nini mama! Pale ni kwako, utalala hadi kupachoka hata usiwe na wasiwasi mke wangu mtarajiwa"
Sabrina hakutaka kuhoji zaidi kwani aliona wazi kuwa hata akihoji ni kazi bure tu.
Muda kidogo Sam akaaga na kuondoka zake.
Kisha Sabrina akamuita Jeff ili apate kujua kuwa walikuwa wanajadili kitu gani muda ambao yeye alikuwa akijiandaa.
"Eeh niambie Sam alikuwa akikwambia vitu gani?"
Jeff akacheka kwanza na kuanza kuzungumza,
"Aaaah alikuwa ananiambia tu kuwa nikulinde eti asikusogelee mwanaume yeyote"
Halafu Jeff akacheka tena na kusema,
"Wakati fisi nipo hapa hapa"
"Lione vile, nitakufukuza"
"Mmh hutaniwi jamani! Usichukie, mi nilikuwa nakutania tu"
"Haya, ila kesho kuna kazi nataka nikupe"
"Sawa hakuna tatizo mamy"
Jeff aliitikia bila ya pingamizi la aina yoyote ile.
Sabrina akiwa anajiandaa kulala, akapigiwa simu na mama yake huku akipewa taarifa za harusi ya kaka yake.
"Wiki ijayo kabla ya harusi yenu tutaenda kulipa mahali kwa mke wa kaka yako kwahiyo na wewe unatakiwa kuwepo sawa"
"Hakuna tatizo mama nitakuwepo tu"
"Ndiomana nimeona nikupe taarifa mapema sababu wewe ni msumbufu na mbishi"
Sabrina alijikuta akicheka tu kwa maneno ya mama yake kisha akamuaga na kulala.
Kulipopambazaka, asubuhi na mapema Sabrina akatoka chumbani kwake na kwenda sebleni huku akitaka kumuita Jeff ila kabla hajamuita Jeff alisikia mtu akigonga mlango na kufanya ajiulize kuwa ni nani huyo kwa muda huo kwani angekuwa ni Sam basi angeita jina la Sabrina ili apate kufunguliwa.
Sabrina akajaribu kumuuliza yule mgongaji kuwa ni nani ila yule mgongaji hakujibu chochote na kumfanya Sabrina awe na wasiwasi na kumuita Jeff ambaye alitoka chumbani kwake na kwenda pale sebleni,
"Kuna mtu anagonga, nimejaribu kumuuliza kuwa ni nani hajatoa jibu. Labda ukamuangalie kuwa ni nani"
Jeff akaenda na kufungua mlango ila hakumuona mtu yeyote pale nje.
"Hakuna mtu, au umesikia vibaya?"
"Hapana bhana, nimesikia vizuri mtu akigonga labda kama ameamua kuondoka"
Kisha wakafunga milango na kuendelea na mambo mengine kama kawaida.
Mchana wa siku hiyo, Sabrina akapigiwa simu na Joy ambaye ni wifi yake kwa upande wa kaka yake James na kwa upande wa mchumba wake Sam,
"Sabrina, kuwa makini kuna ndoto mbaya nimeota kuhusu wewe"
"Ndoto gani hiyo? Na niwe makini kivipi?"
"Yani ninachokuomba ni uwe makini tu. Kwakweli nimeota ndoto mbaya, siku nikipata muda nitakuelezea nilivyoota ila tu kuwa makini"
"Sawa, nimekuelewa"
Wakaongea na mawili matatu kisha simu ikakatika na kila mmoja kuendelea na mambo yake.
Ilipofika jioni Jeff akamuaga Sabrina kuwa anaenda kwao kwavile mama yake alimwambia aende.
Kwahiyo Jeff akaondoka zake.
Muda kidogo simu ya Sabrina ikaita, akaipokea na mpigaji alikuwa ni Jeff,
"Nimesahau funguo za chumba changu cha nyumbani huko kwahiyo nitarudi kuzichukua"
"Na wewe kwa taarifa loh! Kama unarudi wewe rudi tu"
Kisha akakata simu na kuendelea na mambo mengine, akasikia mtu akigonga mlango, moja kwa moja akajua kuwa ni Jeff.
"Yani kasumbufu haka katoto"
Akawa anajisemea mwenyewe huku akienda kufungua mlango, na alipofungua tu waliingia watu wawili wakiwa wamevaa vitambaa vyeusi usoni na mmoja akakimbilia kumkaba Sabrina.
Akawa anajisemea mwenyewe huku akienda
kufungua mlango, na alipofungua tu waliingia watu
wawili wakiwa wamevaa vitambaa vyeusi usoni na
mmoja akakimbilia kumkaba Sabrina.
Sabrina akataka kupiga makelele ila yule mtu akamziba mdono, kisha wakamuangusha Sabrina chini na kumwambia,
"Achana na Sam mara moja, hili si ombi bali ni amri"
Sabrina hakuweza kujibu kitu kwavile walimziba mdomo.
Yule mwingine akainuka na kuanza kuelekea chumbani kwa Sabrina huku huyu wa mwanzo akizidi kumkandamiza Sabrina kwa pale chini.
Wakati Jeff anarudi nyumbani kwa Sabrina, njiani akakutana na rafiki yake na kujikuta wakianza kupiga story,
"Kwani unakaa wapi kwa mitaa hii Jeff"
"Hata sio mbali, ni hapo tu. Twende nikuonyeshe"
Wakaongozana kuelekea nyumbani kwa Sabrina.
Walipofika, Jeff akashangaa kwani alipaona kuwa kama tofauti vile hadi rafiki yake akamuuliza,
"Mbona unapashangaa au sio hapa?"
"Ndio hapa, ila napaona kama pako tofauti"
"Mmmh! Mi napaona kuwa sawa ila kwavile wewe ndiye unayepajua hebu angalia vizuri labda kuna matatizo"
Jeff akaanza kuongeza mwendo akielekea kwenye nyumba ya Sabrina.
Alipofika, akasukuma mlango, akamuona Sabrina akiwa chini na yule jamaa juu ikionyesha wazi anataka kumbaka.
Jeff akapandwa na hasira za ajabu na kujikuta akimvuta yule jamaa kwa nyuma na kumuangusha chini, kisha mpambano ukaanza kati yao.
Yule rafiki wa Jeff alianza kumsaidia Sabrina katika kuinuka kutoka pale chini.
Katika ule mpambano wa yule jamaa na Jeff, yule jamaa alifanikiwa kumponyoka Jeff na kukimbia.
Jeff akamsogelea Sabrina aliyeonekana kuwa bado anatetemeka, ila Sabrina hakuongea kitu ila akinyoosha kidole kuelekea chumbani kwake na kumfanya Jeff ahisi kuwa lazima kuna kitu au kuna mtu.
Jeff akachukua kisu na kuelekea chumbani kwa Sabrina, na kuanza kuangaza huku na huku kama ataona mtu ila hakuona chochote kile na kumfanya aanze kupekua kwa tahadhari kwani alihisi kuwa hata kama kutakuwa na mtu basi atakuwa amejificha kwa yale makelele aliyokuwa akigombana na yule wa mwanzo.
Kumbe yule mtu alikuwa kajificha nyuma ya mlango, kwahiyo Jeff alipotangulia mbele tu basi naye akapata upenyo wa kutoka.
Alipofika sebleni wakati anataka kukimbia akakutana na yule rafiki wa Jeff na kumkata mtama na kufanya aanguke chini huku akimwita Jeff atoke ndani.
Jeff alipotoka, walianza kwa pamoja kumshambulia yule mtu kwa kumpiga huku wakitaka awaambie kuwa ametumwa na nani na amekuja kufanya nini, ila yule mtu hakusema chochote ingawaje walimpiga sana.
Wakaamua kumtoa nje ili wakamfunze adabu vizuri na huko akawaponyoka na kuwakimbia.
Jeff alirudi ndani akiwa na hasira sana kwani hakujua lengo la wale vijana lilikuwa ni nini kwa Sabrina.
Alikaa karibu na Sabrina huku akimpa pole kwa kile kilichotokea,
"Ila imekuwaje? Na wameingia vipi ndani?"
"Kwakweli nimechanganyikiwa Jeff, unajua kuchanganyikiwa wewe? Mimi nimechanganyikiwa. Wakati wanagonga nilijua ni wewe. Ile kufungua tu wakanivamia. Nashukuru hata Mungu aliyekurudisha sababu hata sielewi ningekuwa na hali gani"
"Pole sana"
Simu ya Sabrina ikaita, na mpigaji alikuwa ni Sam.
Sabrina alipokea na kuanza kumueleza Sam kitu ambacho kimemtokea kwa siku hiyo.
"Kheee, nakuja sasa hivi"
Kisha akakata simu.
Jeff alikuwa akionekana bado kujawa na hasira dhidi ya wale watu kwani uoga wake mkubwa ulikuwa ni juu ya kukidhuru kiumbe cha kwenye tumbo la Sabrina.
Aliona wazi kuwa ni majanga iwapo wangembaka Sabrina.
Muda kidogo, Sam akafika mahali pale na kwenda moja kwa moja alipo Sabrina na kumkumbatia kwa kumpa pole.
"Pole sana mke wangu jamani, pole"
"Asante, hata sielewi kwakweli"
"Kwani walikuwa wanataka nini?"
"Wamesema niachane na wewe, tena wameniambia ni amri wala sio ombi"
Sam akafikiria kidogo, kisha ukimya ukatawala na kumfanya Jeff aulize,
"Kwani kuna watu unawahisi bamdogo?"
"Hapana, na wala sina maadui kiasi hiki cha kuja kumtishia maisha Sabrina, kwakweli nashangaa."
"Kwa mtindo huu, hatutakiwi kumuacha mamdogo hapa peke yake"
"Ila nitafanya upelelezi hadi nijue ni wakina nani na wametumwa na nani"
Sabrina nae alikuwa kimya kwa muda, kisha akamwangalia Sam na kumwambia.
"Nakuomba nipeleke kwetu"
"Hilo sio tatizo Sabrina, nipo kwaajili yako"
Kisha wakainuka wote na kufunga nyumba na kuondoka.
Walipokuwa ndani ya gari, Sabrina bado alionyesha kuwa na mawazo sana, inaonyesha wazi ni jinsi gani lile tukio lilivyoichanganya akili yake.
Sam aliligundua hilo kwa Sabrina na kujitahidi kumuongelesha ili kuweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida.
"Sabrina, harusi yetu inakaribia ungependa tuagize keki ya aina gani?"
Jeff alikuwa kimya akiwasikiliza ambapo Sabrina alimuangalia Sam na kutabasamu, kisha akamjibu,
"Iwe keki ya chocolate"
"Ukioza meno Sabrina mi simo"
Sabrina akacheka, na hiki ndicho alichokitaka Sam, kisha akaendelea kuongea nae,
"Eeh iwe na kazi ngapi?"
"Nne tu zinatosha"
"Nne tu kwani chache? Mi napenda iwe na ngazi kumi na mbili ili tukipanda tuchoke"
Sabrina akacheka tena na kumfanya Sam amuangalie Sabrina usoni na kusahau kuwa yupo barabarani anaendesha gari.
Kwa bahati mbaya akashukia akifunga breki mbele ya mtu kabisa kwahiyo ilibakia kidogo tu amgonge mtu huyo, ambaye alianza kutukana bila kituo akimtukana Sam kwa kutaka kumgonga,
"Nyie watu wenye magari mnajidai sana, kwahiyo ungenigonga ndio moyo wako ungeridhika. Unataka kunitoa kafara mimi kwa gari yako, thubutuu nimechanjiwa mimi huwa sitolewi kafara hovyo....."
Yule mtu aliongea mfululizo tena bila hata ya kumeza mate ila Sam alimuelewa na kumuomba msamaha ingawa yule mtu hakutaka ule msamaha na kuzidi kutukana,
"Na tutaona sasa kama...."
Sabrina kuona vile akaona kuwa itakuwa mzozo kwani yule mtu anaweza kujaza watu wengine eneo lile kwahiyo akamuomba Sam kuwa waondoke tu naye Sam akaondoa gari na kuondoka.
Walipofika kwa wakina Sabrina, alimkuta mama yake akiwa na wageni ndani kisha Sabrina nae akaingia na kufurahi kumuona mgeni mwenyewe kuwa ni shangazi yake.
Wakafurahiana pale na kusalimiana, kisha Sam akakaa kidogo na kuwaaga halafu yeye akaondoka na kuwaacha waendelee na mazungumzo yao.
Shangazi wa Sabrina alikuwa akimtazama tu Sabrina na lile tumbo lake kisha akamwambia,
"Ukweli humuweka mtu huru"
"Ni kweli shangazi, na ninashukuru sana kwakuwa sasa nipo huru kweli"
"Ingawa bado hujausema ukweli wote"
"Ila na wewe shangazi ni mtu wa aina gani? Mbona huwa unagundua mambo mengi?"
"Mimi ni mtu wa kawaida tu ila huwa nayasoma macho, sasa nikiyaangalia macho yako yananiambia kila kitu kuwa kuna mengine umeyaficha. Ila hakuna tatizo kwakuwa safari moja huanzisha nyingine, na taratibu ukweli utausema mwenyewe au la ukweli huo utakuumbua mwenyewe siku usiyoitarajia"
Sabrina akamtazama tu shangazi yake na kutabasamu kwani alionyesha sasa kuanza kuzoea maneno yake na kuwa kama mbuzi anayepigiwa gitaa na wakati hachezi wala nini.
"Eeh niambie shangazi, ndio umekuja kwaajili ya harusi zetu?"
"Ndio, ila hiyo sio sababu iliyonileta bali kuna jingine ambalo nimepatwa na hisia kwamba litaibuka ingawaje bado sijajua ni jambo gani"
"Nikuulize kitu shangazi?"
"Niulize tu"
"Hivi kuna siku umewahi kuota ktwa unataka kuwa mganga wa kienyeji?"
Shangazi akacheka kwani alijua wazi kuwa swali la Sabrina limeulizwa kwanini.
Ila kabla hajajibu, Jeff alikuwa amefika pale na kuwakatisha kwa maongezi kwa kumuitia nje kidogo sabrina. Kwahiyo Sabrina akainuka na kwenda kumsikiliza,
"Eeh niambie unasemaje?"
"Kwani mnafunga ndoa lini?"
"Wiki ijayo, mbona unapenda sana kuniuliza hilo swali Jeff?"
"Sababu naumia"
"Kinachokuumiza ni kitu gani?"
"Nakupenda Sabrina"
Huku akimsogelea zaidi na kutaka kumkumbatia, ila Sabrina akajikwepesha kidogo na kumwambia,
"Tafadhari Jeff, nakuomba sana usiyaweke haya mazoea kwenye kichwa chako. Mwisho wake utakuwa mbaya sana, tena kwangu na kwako. Nakuomba siri yetu ibakie kwetu, asijue mtu yeyeto. Na hayo mazoea unayotaka kuyaweka ndio yataharibu kabisa."
"Basi niambie, unanisaidiaje Sabrina?"
"Cha kukusaidia, tafuta msichana wa rika lako uwe nae. Huyo atakufanya usahau kuhusu mimi na pia angalia sana maisha yako"
"Ila maisha yangu bila wewe si kitu Sabrina, na hao wasichana kama ningewapenda basi ningekuwa nao ila kiukweli siwezi kumpenda tena msichana yeyote zaidi yako Sabrina"
Sabrina alimwangalia Jeff na kukosa cha kumjibu kabisa, kisha Jeff akaendelea kuongea,
"Nina ombi moja kwako"
"Ombi tena!! Ushafanya ni mchezo eeh!"
"Hapana, sio ombi hilo"
"Ila ni ombi gani?"
"Naomba utakapoolewa basi na mimi niishi nyumba moja na nyie"
"Je utaweza?"
"Ndio nitaweza, na nitaitunza siri yetu milele"
"Basi haina shida, nitazungumza na Sam"
Kisha Sabrina akamuacha Jeff pale nje na kuelekea ndani kwao.
Sabrina akamkuta shangazi yake ametulia kamavile alikuwa akimngoja yeye amalize maongezi yake, ila kabla Sabrina hajasema chochote kile, shangazi yake akamwambia.
"Yule mtoto inaelekea anakupenda sana Sabrina"
Sabrina akashtuka na kuuliza,
"Yupi huyo?"
"Si huyo uliyetoka kuongea nae, maskini angekuwa mkubwa angekuoa Sabrina"
Sabrina akacheka kwa kujigelesha,
"Jamani shangazi yule ni kama mwanangu"
"Kama mwanao! Basi sawa, ila mi nimemuona kuwa anakupenda sana."
Sabrina akaona jambo la muhimu ni kumbadilishia shangazi yake mada kwani alijua angeweza kufyukunyua na mengine bure.
"Eeh! Si ndio kesho tunaenda kumtolea mahali mchumba wa kaka James?"
"Ndio ni kesho, na ndiomana mimi nimekuja leo"
Wakaendelea na maongezi mengine kwa muda huo.
Sam alirudi moja kwa moja nyumbani kwake huku akifikiria watu waliokwenda kumteka Sabrina kuwa walikuwa na nia gani na nani aliwatuma.
Akili yake iliwaza watu baadhi na kuwatilia mashaka huku akijiweka kuanza kuwapeleleza kama ni wenyewe na walikuwa na lengo gani.
Wakati anafikiria, ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake,
"Ingawa vijana wangu hawajafanyikiwa leo, ila najua ipo siku watafanikiwa kwani nakujua Sam hujiwezi"
Sam alichukiza na ule ujumbe na kuamua moja kwa moja kuifuta ile meseji bila hata ya kufatilia kuwa ni nani aliyemtumia.
Ila akajisemea,
"Yani hawa wataumbuka tu siku Sabrina wangu akijifungua. Sina hata ya kukaa na meseji zao"
Kisha akaendelea na mambo yake mengine.
Usiku wa siku hiyo Sabrina alilala na shangazi yake, ambaye alishtuka usiku wa manane na kumwambia Sabrina,
"Nimeota umejifungua mtoto wa kike, halafu mtoto huyo anagombaniwa na baba yake mzazi na mwanaume mwingine asiye baba yake"
Sabrina akamuangalia shangazi yake na kuona kuwa anamletea mada zake zile zile za kila siku huku moyoni mwake akiwaza,
"Nikimfatilia huyu shangazi, si muda mrefu nami nitakuwa chizi kama yeye"
Kwahiyo alichokifanya ni kumuitikia kwa kumridhisha kisha wakaendelea kulala.
Kesho yake kama ambavyo walipanga, wakajiandaa na kufunga safari kwenda huko nyumbani kwa kina Joy kwa lengo la kujitambulisha na kutoa mahari.
Aliyeongoza msafara wao alikuwa ni James ambaye ndiye muhusika mkuu.
Walifika vizuri, na kupokelewa hadi ndani.
Mama wa Sabrina akashtuka kumuona Baba wa Joy yule mchumba wa mtoto wake James.
Baba wa Joy nae akashtuka kumuona mama wa Sabrina pamoja na Sabrina kwani akili yake ikamwambia wazi kuwa James atakuwa na undugu na hiyo familia.
Shangazi wa Sabrina, akamwangalia Sabrina na kumwambia,
"Umeona, mficha maradhi kifo humuumbua"
"Una maana gani shangazi?"
"Mama yako hapo ameshachanganyikiwa"
Sabrina akageuka na kumuangalia mama yake, mara gafla mama yake akaanguka chini.
Shangazi wa Sabrina, akamwangalia Sabrina na
kumwambia,
"Umeona, mficha maradhi kifo humuumbua"
"Una maana gani shangazi?"
"Mama yako hapo ameshachanganyikiwa"
Sabrina akageuka na kumuangalia mama yake, mara
gafla mama yake akaanguka chini.
Ikabidi Sabrina amkimbilie mama yake pale chini alipoanguka.
"Vipi mama?"
Huku akimsaidia kuinuka,
"Hata sielewi, yani nimepatwa na kizunguzungu cha gafla tu"
"Pole sana"
Na wengine wakasogea huku wakimpa pole na kumwambia kuwa huenda ikawa malaria.
Baada ya muda mfupi, baba wa Joyce aliwaaga kidogo pale ndani kuwa kuna mtu anamfata kwenye kituo cha daladala, Deo akamuuliza,
"Kwanini usiagize vijana?"
"Huyo mtu ni muhimu sana anione mimi"
Ikabidi tu wamruhusu aende ambapo walikaa na kumsubiri kwa muda mrefu bila ya kupatikana hadi mkewe akapatwa na wasiwasi,
"Hata sielewi amepatwa na kitu gani jamani, simu yake haipatikani, mambo ya hapa hatujayamaliza. Hata sielewi"
Deo akaamua kutoa maamuzi kuwa watarudi siku nyingine kwavile kisingefanyika kitu wakati baba mzazi wa binti wanaetaka kumchumbia hayupo.
Ikabidi waage na kuruhusiwa tu kuondoka kwa muda huo ili kuendelea na mambo yao mengine ingawa muda tayari ulikuwa umeenda sana.
Walipofika nyumbani, James akaamua kuondoka kwani alifadhaika kwa kitendo cha baba mkwe wake kuwaacha njiapanda.
Sabrina nae hakuwa na usemi zaidi ya yeye kubakia pale kwao kwa lengo la kumuangalia mama yake kwani alihisi kuwa huenda akawa na malaria.
Muda huo shangazi yao alikuwa naye ameshaondoka.
Sabrina alikaa na kuzungumza na mama yake kidogo,
"Kwani mama, shangazi anajua nini kuhusu wewe?"
"Tena mwanangu, ngoja nikwambie kitu. Huyo shangazi yako achana na maneno yake yatakuchanganya tu. Kwanza tambua hili, huyo shangazi yako aliugua sana kipindi cha ujana wake. Baba yako hupenda kumtumia kwenye mambo kama haya sababu anampenda tu ila akili za huyo shangazi yako si njema"
Sabrina alijidadisi na akili yake na kupata jibu kuwa huenda maneno ya mama yake yana ukweli ndani yake kwani hata yeye binafsi inakuwa ngumu sana kumuelewa shangazi yake huyo.
James alipokuwa ameenda kwa mtu aliyemuita, akaanza kuambiwa maneno ambayo yalimpa mashaka na kumfanya ashindwe kurudi nyumbani kwake,
"Hivi wewe hujiulizi kwanini unafanana na yule kijana kiasi kile? Au bado unajidanganya na ile kauli kuwa duniani wawili wawili? Hujiulizi kwanini yule kijana kapewa jina linalofanana na la kwako? Mi ukweli siujui ila kuna matukio ambayo nimeyafatilia na yakafanya nigundue kitu"
James ambaye ni baba wa Joyce alitafakari bila ya majibu ya haraka, ingawa huyu mtu aliyemuita alimruhusu kuondoka ila bado James hakuondoka kwavile moyo wake ulikuwa na maswali mengi bila ya majibu.
Mama wa Sabrina alipokuwa nyumbani na mumewe, aliamua kumueleza hali halisi kiunaga ubaga ili ajue jinsi gani watasaidiana,
"Ila Joyce, si tulikubaliana kuwa kuwa James ni mtoto wangu?"
"Ndio natambua hilo Deo"
"Sasa tatizo liko wapi?"
"Hatuja mtendea haki James, hebu jaribu wewe kufikiria kuwa leo hii watoto wako wanaoana, je utajisikiaje?"
"Ila huyo James hajui kama huyu ni mtoto wake"
"Ndio hilo kosa tulilolifanya Deo"
"Sidhani kama ni kosa, hebu tuangalie maisha yetu. Watoto wafunge ndoa mambo yaendelee"
"Ila dunia haina siri Deo"
"Ungetambua hilo basi toka mwanzoni usingetaka kunificha, ila ulinificha hadi pale ulipoumbuliwa na mdogo wangu"
Joy akaona sasa maneno yatakuwa makubwa na yatavuka mipaka hivyobasi akaamua kukaa kimya ili kuepusha mumewe kukumbushia yaliyopita.
Sabrina alienda nyumbani kwa Sam na kutulia ndani huku akimsubiria, na Sam aliporudi alimkuta Sabrina akiwa ndani,
"Nasikia eti imeshindikana kumtolea mahari dada yangu"
"Ndio imeshindikana sababu ya mjomba wako. Kaondoka na kutokomea halafu hajarudi tena, sijui na yeye vipi. Au hataki kaka yangu amuoe mwanae? Hata sijamuelewa kwakweli"
"Haya sasa, na wewe ulipotoka pale ndio ukaamua kuja hapa?"
"Nilivyotoka nikarudi nyumbani ila kuna mambo ambayo nimeyafikiria na ndio yamenileta hapa"
Sam akajiuliza kwa haraka haraka kuwa ni mambo gani ila hakupata jibu, na alipojaribu kumuuliza Sabrina naye hukumjibu zaidi ya kumwambia kuwa hayo mambo atayaona tu bila papara.
"Una maana gani Sabrina?"
"Usiwe na mashaka Sam, utaona tu"
Usiku ukaingia kabisa huku Sabrina akiwa hapo hapo nyumbani kwa Sam ambapo kila Sam alipombembeleza kuwa amrudishe nyumbani kwao, bado Sabrina aligoma kuondoka na kuendelea kuwepo mahali hapo.
James ambaye ni baba wa Joyce, alishindwa kuelewa kwani alitafakari sana bila ya kupata majibu ila upande mwingine wa moyo wake ulikuwa unamwambia kuwa ukweli wote ataupata kwa mama mzazi wa mtoto huyo, hivyobasi akapendekeza kuwa aweze kuonana nae na waweze kuzungumza juu ya hali halisi.
Usiku uliingia vizuri, na moja kwa moja Sabrina alienda kulala chumbani kwa Sam ambapo Sam akataka kulala sebleni ili kumpisha Sabrina kitandani.
Ila kabla hajaenda Sabrina akamshika mkono na kumzuia kisha akamuuliza,
"Utanikimbia hadi lini Sam?"
"Sikukimbii Sabrina kama unavyofikiria, ila napenda kutunza kiapo changu"
"Sawa, hata kama unatunza kiapo iweje ushindwe kulala na mimi kitanda kimoja? Kwani tukilala tu nini kinaharibika?"
Sabrina akajaribu pale kumshawishi Sam, na mwisho wa siku Sam akakubali na wakalala kitandani pamoja.
Usiku ulipofika, Sabrina akashtuka na kuamka ila alipomtazama Sam pembeni hakuwepo na kumfanya Sabrina apatwe na hasira sasa kuwa kwanini Sam anamkimbia kiasi hicho?
Akaamua kuinuka na kwenda kumchungulia sebleni, akamkuta amelala kwenye kochi na kumfanya Sabrina asikitike sana huku akizidi kujiuliza na kujiambia kuwa huenda anataka kuolewa na mwanaume ambaye si mzima ndiomana anamfanyia mambo hayo.
Hakutaka kumkurupusha pale zaidi ya kurudi chumbani na kulala.
Asubuhi kulipokucha, Sabrina alipoamka, alimkuta Sam akiwa amelala pale pembeni kisha na yeye akamkurupusha,
"Hivi wewe, kunikimbia usiku na kwenda kulala sebleni ndio nini?"
"Jamani Sabrina, sijakukimbia wala nini. Tena leo ndio hata kutoka hapa kitandani sijatoka"
"Sam, wakati nimekuona kwa macho yangu mwenyewe!"
"Labda uliota Sabrina ila kiukweli leo sijachomoka hapa kitandani"
"Haya bhana nikatalie, ila siandikii mate wakati wino upo"
"Una maana gani?"
"Najua nitakapo kukamata, tulia tu"
Sam akacheka, kisha akainuka na kwenda kuoga kwaajili ya kujiandaa na majukumu ya siku hiyo.
Sam alipomaliza kujiandaa, ikabidi amuage Sabrina kwavile Sabrina alisema hataki kutoka siku hiyo na anataka kushinda hapo hapo nyumbani kwa Sam.
James ambaye ni baba wa Joyce, siku hiyo aliamua kufunga safari na kwenda nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kuwaomba msamaha kwa kitendo chake cha kuondoka na bila ya kurudi tena ila lengo lake kuu lilikuwa ni kumuuliza mama wa Sabrina kuhusu maneno ambayo ameyasikia kwa siku ile.
Na alifika na kupokelewa vizuri tu na kijana mmoja aliyekuwa kaka wa Sabrina hadi ndani.
Alimkuta mama wa Sabrina akiwa sebleni huku akiendelea na mambo mbalimbali, ila alishtuka kumuona James mahali pale ingawa alimkaribisha,
"Karibu James, naona unamshangaa huyo ni mwanangu anaitwa Sam"
James akacheka na kumwambia,
"Watoto wako wote nilikuwa nawajua kwa sura na kwa majina. Ila mwanao mmoja tu ambaye nilikuwa namjua kwa jina tu, huyo mkubwa James. Sikuwahi kubahatika kukutana nae ingawa nilitamani sana kumuona, na kumbe ndio huyo mkwe wangu"
Mama Sabrina akaamua kujichekelesha hapo ili kuendelea kuukata mzizi wa mawazo kwa James, kisha yule Sam ambaye ni kaka wa Sabrina akainuka na kuwaacha waongee vizuri kwani aliona wazi kuwa wanafahamiana na itakuwa vyema kwao kama watakumbuka ya zamani kwani aliwasikia hata wakitaja khabari za kwaya.
"Kuna mambo mawili yaliyonileta hapa ila hili moja naomba kama utapata nafasi basi tupange siku tuonane na kuweza kuzungumza"
Mama Sabrina aliweza kuhisi kuwa ni jambo gani ila hakutaka Deo akirudi hapo amkute mtu huyo, hivyobasi akamuaga na kukubali kupanda siku ya kuzungumza.
James alipoondoka, akampa nafasi mama Sabrina kufikiria uongo wa kumwambia James ili akubali na aamini,
"Hata hivyo kuna mwingine wa ziada anayejua ukweli huu? Hata kama yupo basi atakuwa anakisia tu. Akisema kuhusu kufanana na mwanangu, nami nitamjibu kuwa duniani wawili wawili, nisipofanya kuongopa zaidi basi lazima nitaharibu tu"
Kwahiyo mama Sabrina akajipanga kwa mambo ya kuongea na James siku atakayo kutana naye.
Jeff alikuwa mpweke sana siku hiyo hadi mama yake alitambua hali ya mwanae,
"Mbona upo hivyo?"
"Nimemkumbuka sana Sabrina"
Sakina akamshangaa na kumuuliza kwa mshangao,
"Umemkumbuka Sabrina!! Kivipi?"
Hapo akamfanya Jeff naye ashtuke na kugundua kuwa ameropoka bila ya kutarajia.
Sasa akatafuta njia ya kumgelesha mama yake ili asielewe chochote na kujifanya akicheka,
"Unacheka nini sasa? Hebu niambie huyo Sabrina umemkumbuka kivipi? Unajua kama umenishangaza hapa, yani kumkumbuka Sabrina ndio mpaka uwe mpweke? Au una mengineyo wewe mtoto!"
"Mengineyo? Yapi hayo mama?"
Jeff alimuukiza mama yake kwa mshangao ili kujaribu kuona kwamba kama kuna chochote anachohisi,
"Una mengineyo huko kwa Sabrina wewe sio bure, maana ninavyohisi mtaa anaokaa Sabrina ndio huko kuna huyo mtu mzima anayekutoa akili wewe"
Jeff akagundua kuwa mama yake hajui chochote, hivyobasi na yeye akatumia nafasi hiyo kumuuliza mama yake maswali,
"Kwani mama mapenzi ni nini? Na je mapenzi yanachagua umri?"
"Halafu wewe Jeff usichefue, tena usinitibue kabisa na hayo maswali yako ya kijinga. Nilikutafutia binti mzuri hapa ila bado unang'ang' ania watu wazima. Kwakweli ipo siku yako utakayokumbuka maneno yangu yote wewe"
Jeff hakutaka kubishana na mama yake kwahiyo akaamua kuinuka na kwenda chumbani kwake ambapo moja kwa moja alimpigia simu Sabrina na kuanza kuongea nae,
"Wee mtoto, niache nipumue wewe. Huwa sipendi matatizo Jeff jamani"
"Ila mi natamani kukuona tu, yani hizi siku mbili kwangu imekuwa kama mwaka. Tafadhari nakuomba, yani nikuone tu"
"Sitaki, tena usithubutu kuja huku. Utaniona siku ya harusi yangu tu, nishafunga mkataba na wewe. Sitaki kumkera mume wangu"
Kisha akaikata ile simu na kumfanya Jeff apatwe na hasira, na kutaka kwenda nyumbani kwa Sam kumuona Sabrina kinguvu hata kama mwenyewe hataki ila akukumbuka kuwa Sam ana bastora, ikabidi awe mpole na kutafuta njia nyingine ya kumuona Sabrina kwa amani tu.
Sabrina alikuwa ameshachukizwa na simu ya Jeff,
"Haka katoto haka, katanipanda kichwani sasa. Natakiwa kuwa na msimamo wangu kwani mwisho wa siku nitaonekana malaya, sifai na majina yote mabaya nitapewa. Saivi nakuwa mkari tu ili niikomeshe tabia ya Jeff hata kama nina mimba yake. Kwanza nafuta kauli, sio mimba yake bali ni yangu"
Sabrina aliongea kwa hasira huku akimngoja Sam arudi nyumbani.
Kabla Sam hajarudi, kuna kijana aliyefika pale huku amebeba chakula kilichofungwa na kumkabidhi Sabrina kwa madai kuwa amepewa na Sam. Kisha naye Sam akampigia simu Sabrina katika kuthibitisha hilo.
Sam aliporudi, usiku nao ulikuwa umeingia na alionekana kama mtu aliyekunywa pombe.
"Kheee Sam! Ndio siku nyingine unakuwaga hivyo?"
"Jamani mama, unashangaa nini? Wewe si unataka tulale wote! Basi, mumeo nimesharudi na tayari kwa kwenda kulala sasa"
Sabrina alisikitika kiasi, kisha wakaenda chumbani na kujiandaa kulala ambapo Sam alijitupia tu kitandani na kulala fofofo, na kumfanya Sabrina naye alale tu.
Usiku sana Sabrina akashtuka, ila pale pembeni yake Sam hakuwepo na kujua wazi amefanya mchezo kama wa jana.
Sabrina akainuka na kwenda kumchungulia sebleni, akamuona mtu kwenye kochi akiwa amelala huku kajifunika shuka gubigubi, moja kwa moja Sabrina akajua ni Sam tu.
"Na leo lazima nimkomeshe, naenda kuchukua simu na kumpiga picha"
Kisha Sabrina akarudi tena chumbani.
Alipotazama kitandani, akamuona tena amelala akiwa amejifunika gubigubi kama sebleni.
Sabrina akajikuta akipiga kelele na kuanguka.
Kisha Sabrina akarudi tena chumbani.
Alipotazama kitandani, akamuona tena amelala
akiwa amejifunika gubigubi kama sebleni.
Sabrina akajikuta akipiga kelele na kuanguka.
Kelele za Sabrina zikamshtua Sam pale kitandani na kumfanya aamke kwa kukurupuka kisha akamfata Sabrina pale chini alipoanguka huku akijaribu kumpa huduma ya kwanza.
Sabrina alipozinduka akamuona Sam akimpepea, kwanza kabisa akapumua kwa uoga huku akimuangalia Sam kwa jicho la wasiwasi na kumfanya Sam amuulize,
"Kwani tatizo ni nini Sabrina?"
"Kwani wewe Sam ni mchawi?"
Sabrina akajikuta akiropoka na kumfanya Sam amshangae.
"Mchawi? Mchawi kivipi jamani Sabrina?"
"Kwakweli Sam hapana, mi siwezi kuendelea kulala humu ndani nataka nirudi kwetu sasa hivi"
"Mbona ni usiku sana Sabrina, una matatizo gani? Sikuelewi"
"Wewe mtu gani? Kwanza una mambo ya ajabu hueleweki, unajiweka sebleni na chumbani. Sam wewe utakuwa mchawi tu"
Sam akacheka na kuanza kuhisi kitu kinachomtatiza Sabrina, kisha akamuuliza,
"Hivi Sabrina unaweza kupata ujasiri wa kuzungumza na mchawi kiasi hiko? Hivi siku ukimuona huyo mchawi katika kazi yake, utaweza hata kujikaza na kumwambia maneno hayo? Na kama ningekuwa mchawi si ningeshafanya jambo la kukusahaulisha! Najua linalokutatiza, nenda tena sebleni ukamuone aliyelala pale."
Sabrina bado alikuwa na uoga huku akinyanyuka na kumuomba Mungu kimoyo moyo kuwa amsaidie kwa wakati huo.
Sabrina akainuka na kwenda sebleni ili kujiridhisha na moyo wake, akamkuta yule wa sebleni akiwa amelala vilevile huku kajifunika shuka gubigubi.
Sabrina akasimama tu huku akisita kumsogelea, Sam akamfata Sabrina kwa nyuma na kumsogeza mpaka kwa yule mtu,
"Mfunue mwenyewe uone kama ni mimi huyo"
Sabrina bado akasita kumfunua mtu yule, ikabidi Sam amsaidie mwenyewe kumfunua.
Sabrina akashangaa kumuona kuwa ni Jeff tena amelala fofofo.
Sabrina akamuangalia Sam na kumuuliza kwa mshangao,
"Jeff amefikaje hapa? Ameingia saa ngapi? Na mbona amelala hoi sana?"
"Hayo maswali Sabrina naomba kesho umuulize mwenyewe huyo Jeff ndio atakujibu kwa usahihi zaidi. Tafadhari turudi ndani tukalale"
Sabrina hakubisha muda huu zaidi ya kuwa mpole na kuanza kuelekea chumbani kwao.
Ila kiukweli Sabrina usingizi haukumjia kwa wakati kwani alijikuta akiwa na mawazo mengi sana.
Kulipokucha, kama kawaida Sam aliamka na kujiandaa kisha akamuaga Sabrina kuwa atarudi kwenye mida ya saa sita kumchukua kwaajili ya kwenda kanisani kwa mazoezi ya awali ya ndoa yao.
Sabrina alibaki mwenyewe sasa na kutoka tena sebleni, bado alimkuta Jeff akiwa amelala na wala hana habari.
Kwavile Sabrina alitamani sana kujua kuhusu Jeff kuwa hapo akaona ni vyema amuamshe tu.
"Wee Jeff, wewe, wewe hebu amka"
Huku akimtikisa tikisa ila bado Jeff alionekana kuwa na usingizi mzito sana na kumfanya Sabrina hata achukie kwavile lengo lake lilikuwa ni kujua kuwa imekuwaje hadi Jeff yupo pale nyumbani kwa Sam.
Baada ya muda kidogo, Jeff alimka akiwa na uchovu sana huku akijinyoosha na kukaa pale kwenye kochi, kisha akainama na kushika tama kamavile mtu mwenye mawazo mengi.
Muda wote Sabrina alikuwa akimuangalia tu, kisha akamshtua kwa kumuita,
"Wee Jeff"
Jeff naye akashtuka na kumuangalia Sabrina, kisha akainuka na kwenda kumkumbatia na kumfanya Sabrina amshangae,
"Kwani wewe Jeff una matatizo gani wewe?"
Jeff alizidi kumkumbatia Sabrina huku machozi yakimtoka, ikabidi Sabrina amwambie kwa ukali sasa,
"Wee Jeff nini?"
"Nakupenda Sabrina, nakupenda sana. Kwanini uninyanyase? Au umri wangu, au umbo langu? Nakupenda jamani"
Sabrina alimuangalia Jeff huku akitikisa kichwa kama ishara ya kumsikitikia,
"Yani wewe mtoto wewe, aliyekuroga alishakufa maana angekuwa hai angekuonea huruma kwa huu upuuzi wako unaouwaza kichwani mwako"
"Sio upuuzi Sabrina, jaribu kusoma hisia zangu. Bila wewe siwezi mimi, wewe ndio mwanamke wa maisha yangu. Nakuhitaji wewe, nataka kuwa na wewe, simtaki mwinginewe"
Sabrina akaona kama akiendekeza kumsikiliza Jeff basi atazidi kujiweka pabaya ukizingatia pale walipo ni nyumbani kwa Sam.
"Sasa Jeff sikia, hayo maneno yako si ya kuzungumza mahali hapa. Hebu jaribu kuelewa hapa upo kwa nani na anamahusiano gani na mimi. Tafadhari sana Jeff usiniharibie"
Jeff hakuongea muda huu ila alijiinamia tena kanakwamba anaendelea kuwaza alichokuwa anawaza.
Sabrina naye aliinuka na kwenda jikoni ili kuandaa chai.
Wakati Sabrina yupo jikoni, Jeff naye akaenda jikoni kumfata Sabrina ambapo alimfata kwa nyuma na kumkumbatia,
"Hivi wewe Jeff una matatizo gani? Na hii nyumba itakushinda muda sio mrefu nakwambia. Haya niachie"
"Sawa nakuachia, ila naomba nikubusu tu"
Sabrina aliona ni kero kwa uwepo wa Jeff pale, kisha akamuacha ambusu ili amuachie.
Naye Jeff akafanya hivyo, kisha akarudi sebleni na kumfanya Sabrina aongee peke yake pale jikoni,
"Yani huyu mtoto huyu, hata sijui nifanyeje mimi"
Sabrina alinung'unika sana kisha akaenda kuandaa chai yake na kuanza kunywa.
Muda sio mrefu Sam akawa amerudi, kisha akamwambia Sabrina ajiandae ili waende,
"Si ulisema saa sita wewe? Mbona muda bado?"
"Nimepigiwa simu kuwa tuwahi ndiomana nimekufata muda huu"
Sabrina akaenda kujiandaa na baada ya muda mfupi akawa amemaliza tayari kwa kuondoka.
"Vipi, huyu Jeff anabaki hapa ndani?"
Sabrina alimuuliza Sam, naye Sam akamjibu
"Muache tu, muda akijisikia kuondoka basi ataondoka mwenyewe"
Kisha Sam akamshika mkono Sabrina na kuondoka naye.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakiwa ndani ya gari, Sabrina akawaza sana kuwa ni kitu gani kimepelekea Sam kumkubali Jeff kiasi kile, akawa anawaza tu moyoni,
"Lazima kuna kitu hapa ambacho mimi sikijui. Kwani sio rahisi hivi kwa Sam kupatana na Jeff"
Muda wote mawazo yakamjaa huku akijaribu kutafakari kuwa ni kitu gani kimewapat anisha kiasi kile Sam na Jeff.
Kisha Sabrina akagundua kitu kuwa Sam amepanda gari ambayo huwa hata hatembei nayo mara kwa mara, kisha akamuuliza
"Vipi leo gari hii?"
"Aaah! Nimeikumbuka tu, nikaona ni vyema leo nayo ione mji"
"Sawa"
"Hii gari nitakupa wewe ukishajifungua"
Sabrina akatabasamu kwani kauli hiyo ilimfurahisha.
Walipokaribia kanisani, Sabrina akamuona mtu karibia na mlango wa kanisa na kuhisi wazi anamtambua mtu huyo tena si kumtambua kwa mema bali kwa mabaya,
"Sam tafadhari, pinda hii gari tukaingilie mlango ule mwingine"
"Ila mbona itakuwa kama tunazunguka sana?"
"Hapana, twende tukaingilie kule. Nina maana yangu"
Sam hakupinga zaidi ya kugeuza gari na kuelekea upande mwingine ambapo walienda kuingia kwenye geti la nyuma la kanisa hilo.
Moja kwa moja Sam na Sabrina wakaenda kwa mchungaji ili kupata muongozo.
Ambapo mchungaji alisalimiana nao na kuwauliza,
"Mbona mmewahi sana?"
"Nimepigiwa simu kuwa eti tunatakiwa kuwahi"
"Nani kakupigia simu? Maana hakuna mtu aliyepigiwa simu kuwa awahi kuja"
Sabrina akamwangalia Sam na kumwambia,
"Unaona Sam, yule mtu aliyesimama pale sio mtu mzuri pengine ndio wao wamekupigia simu. Hata sijui wana lengo gani na sisi"
"Kwani yule unamjua?"
"Mi simjui ila namkumbuka kuwa ni kati ya wale vijana wawili walionivamia pale kwangu siku ile"
Sam akashtuka, na kuamua kutoka ili akawafatilie ila Sabrina akamzuia,
"Niache Sabrina, nikashughulike nao"
Mchungaji akamuangalia Sam na kumwambia,
"Waache, Mungu ndiye atakaye shughulika nao"
Ingawa Sam alitulia kwa kufata maneno ya mchungaji ila moyoni mwake alimponda,
"Ndio shida ya walokole hii"
Ikabidi tu mchungaji awape muongozo kwavile wamewahi sana kwenda eneo la tukio kabla ya muda muafaka.
Akawaelekeza ya kufanya, kisha akawaruhusu kwaajili ya kuondoka.
Sam na Sabrina walitoka nje na kuingia kwenye gari yao kisha wakaianza safari ya kuondoka zao.
Walipofika nje, Sam bado akataka kupeleka gari eneo lile ambalo Sabrina alimuona yule mtu,
"Tafadhari Sam, twende nyumbani. Mi nakuomba, nihurumie mimi na mtoto wetu aliyetumboni, turudi nyumbani"
Sam kama kawaida yake huwa hapendi kumkwaza Sabrina, hivyobasi akafanya safari ya wao kurudi tu nyumbani.
Walitembea kimya njia nzima hadi walipofika nyumbani na kuingia ndani ambapo bado walimkuta Jeff akiwa pale pale ndani kwao.
Sabrina akamuuliza Jeff,
"Khee hujaondoka?"
Jeff akamuangalia Sabrina na kutabasamu na kumfanya Sabrina amuulize tena,
"Kinachokuchekesha sasa?"
Sam akaingilia kati,
"Sabrina acha kumfokea mtoto, muda wake wa kuondoka ukifika ataondoka tu"
Na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na mashaka zaidi kuwa kwanini Sam anafikia hatua hadi ya kumtetea Jeff.
Baada ya muda kidogo, Sam akamuaga tena Sabrina kuwa anatoka kidogo ila muda huu alitoka na Jeff na kumfanya Sabrina afurahi kiasi kwani uwepo wa Jeff huwa unamkosesha amani kabisa.
Nyumbani kwa wakina Sabrina hali haikuwa shwari sana kwani mama yake bado alikuwa na mawazo ya namna ya kuokoa jahazi la mtoto wake James, kwani ikiwa ukweli utakuwa wazi basi atamuharibu kisaikolojia mtoto wake huyo.
Kwahiyo aliona kuwa ni vyema ukweli usijulikane ili kuendelea kulinda heshima yake na heshima ya watoto wake wote watatu.
Wakati akifikiria mambo hayo, akapigiwa simu na wifi yake ambaye ni yeye anayeujua ukweli wa mambo kwa undani zaidi,
"Eeh wifi unaamuaje kuhusu kusema ukweli?"
"Tafadhari nakuomba hili swala niachie mwenyewe"
"Nakuachia ndio, uzuri ni kuwa nawajua fika wewe na mwanao kuwa mabingwa wa kudanganya. Mko radhi wenzenu waumie ili nyie mtunze siri"
Mama Sabrina akaona huyu wifi yake anamletea khabari za kumchanganya tu wakati kashamwambia kuwa amuachie yeye mwenyewe amalizane nao.
Kwahiyo akaamua kuikata ile simu bila ya kujua kuwa amemchukiza mpigaji.
Sabrina hakuwa na wasiwasi na pale nyumbani kwa Sam kwavile nyumba ile ilikuwa na ulinzi wa kutosha, kwahiyo Sabrina akakaa kwa uhuru zaidi, na kuendelea kufanya mambo yake mbali mbali.
Simu yake ya mkononi ikaita, na mpigaji alikuwa Sakina,
"Umewasiliana na Jeff kwa siku ya leo maana hata sielewi alipo"
"Nimetoka kuwasiliana nae muda sio mrefu, hebu kwanza nimpigie simu tena nimwambie awasiliane na wewe"
Sabrina hakutaka kumwambia Sakina moja kwa moja kama mtoto wake jana alilala hapo nyumbani kwa Sam.
Kwahiyo simu ilipokatika, Sabrina akajaribu kumpigia simu Jeff lakini hakupatikana na kuamua kumpigia simu Sam,
"Upo na Jeff hapo?"
"Ndio nipo nae"
"Naomba niongee nae"
Sam akampa simu Jeff kisha akaongea na Sabrina, na muda huo huo Jeff akamuaga Sam kuwa Sabrina kamuita kidogo kwahiyo anarudi nyumbani kumsikiliza.
Sam hakuwa na pingamizi lolote na kumruh usu kuwa aende tu.
Jeff alirudi nyumbani kwa Sam na kumkuta Sabrina,
"Kwani nimekwambia uje huku au uende kwa mama yako?"
"Huku nimekuja kukuaga tu, wala sikuja kwa ubaya"
Sabrina akamuangalia Jeff na kumwambia,
"Haya kwaheri"
Jeff akamsogelea Sabrina na kumkumbatia huku akimwambia kuwa anampenda,
"Wee Jeff nenda zako wewe usiniletee balaa mie"
"Hapana sina balaa, ila naomba unibusu"
Kisha Jeff akasogeza midomo yake karibu na midomo ya Sabrina.
Wakashtuliwa na mlio wa mlango ambapo aliyeingia alikuwa ni Sam.
Kisha Sam akawaambia,
"Msishtuke endeleeni tu nimeshajua kila kitu"
Wakajikuta wakitazamana kwa aibu.
Kisha Jeff akasogeza midomo yake karibu na
midomo ya Sabrina.
Wakashtuliwa na mlio wa mlango ambapo aliyeingia
alikuwa ni Sam.
Kisha Sam akawaambia,
"Msishtuke endeleeni tu nimeshajua kila kitu"
Wakajikuta wakitazamana kwa aibu.
Jeff akamuachia Sabrina na kubaki ameduwaa huku akimtazama Sam, ambapo Sam akawaambia,
"Nimesema endeleeni na mlichokuwa mnataka kufanya"
Jeff akaona utakuwa msala sasa, akataka kuondoka ila Sam akamzuia na kusema tena,
"Kwanini unataka kukimbia Jeff ikiwa kitu mlichokuwa mnataka kufanya ni kitu cha kheri?"
Sabrina hakuweza hata kumtazama Sam usoni kwani aibu ilimjaa tu huku wakisubiria hatma yao kwani wote walishindwa cha kusema.
"Kumbe mna ishara zenu siku hizi eeh!"
Wakaendelea kukaa kimya na kumfanya Sam aendelee kuongea,
"Jeff, uliponiambia kuwa Sabrina amekuita sikupata mashaka sana ila kuna kitu ambacho hukukigundua, mi katika simu yangu nimeweka huduma ya kurekodi mazungumzo yote yanayofanyika kwa kupitia simu yangu ili hata kama nimesahau basi nijaribu kusikiliza tena. Na ulipoondoka tu, nikaamua kusikiliza tena yale mazungumzo yenu na kumsikia Sabrina akikwambia kuwa uende nyumbani kwenu mama yako anakusubiri. Sasa kilichonishtua ni wewe kuniaga na kuniambia kuwa Sabrina anakuita na ndiomana nikaamua kurudi ili nikamate uongo wako. Haya sasa nataka kujua, je Sabrina ulimwambia Jeff kuwa mama yake anamuita kama ishara ya yeye kuja hapa? Au Jeff uliamua tu kuja kwa mazoea yako binafsi? Nijibuni sasa"
Sabrina alikuwa akitetemeka tu kwani hakuelewa hata ajieleze vipi ili aweze kueleweka kwa Sam,
"Inamaana leo mmekosa kabisa jibu la kunishawishi mimi?"
Jeff akaanza kujitetea,
"Hapana sio hivyo, mi nilikuja tu kumuaga mamdogo"
Sam akacheka sana na kusema,
"Kweli wewe mtoto hamnazo, yani katika kujitetea kote wewe umeona huo ndio utetezi mkubwa sana? Ok, kwa mfano nikakuuliza kwani asubuhi hukumuaga? Na kwanini usimuage kwenye simu? Na kwanini mimi usiniambie ukweli wakati unaondoka kule?"
Jeff alibaki kimya tu kwani kwa vyovyote vile alihisi kuwa ni wazi Sam ameshaujua ukwe li ila anawasanifu tu kwa maswali anayowauliza.
Kisha Sam akamuangalia Jeff kwa makini sasa na kumwambia,
"Haya nakuruhusu uende kwa mama yako, najua anakungoja"
Jeff hakuamini masikio yake na kujikuta akitoka kimya kimya bila ya kusema chochote.
Sabrina sasa, alibakia yeye na Sam mule ndani.
Alikuwa kasimama tu huku akingoja hatma yake.
Sam akamsogelea Sabrina na kumkumbatia vilevile ambavyo Sabrina alikuwa kasimama na kumwambia,
"Nakupenda sana mke wangu, eeh umeniandalia chakula gani leo?"
Sabrina alikuwa akijibu huku midomo ikimtetemeka kwani aliona wazi kuwa anaweza kutendewa jambo lolote baya na Sam kwa wakati ule.
Kisha Sam akaenda kukaa kamavile mtu anayengoja chakula kiandaliwe.
Naye Sabrina aliandaa kile chakula huku akiwa bado hana amani moyoni mwake.
"Chakula kitamu sana hiki Sabrina, asante kwa kuniandalia chakula kizuri kama hiki. Namshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema na mzuri anayejua mapi shi"
Sabrina alikuwa akimkodolea macho tu Sam,
"Tena kesho kutwa ndio harusi yetu, hivi hiyo mimba inamiezi mingapi mke wangu ili niandae nepi za mtoto?"
"Ina miezi sita unaenda wa saba"
"Ooh miezi mitatu imebaki, nina hamu sana ya kumuona mwanangu. Najua atakuwa wa kike tu"
"Hapana ni wa kiume"
"Kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Baada ya harusi, wiki ijayo nitakupeleka hospitali ukapige ultrasound hapo ndio tutamaliza utata wa jinsia ya huyo mtoto"
Sabrina akaitikia tu na kujichekelesha kiuongo uongo kwani furaha hakuwa nayo kabisa.
Muda kidogo kupita Sabrina akamuomba Sam kuwa aende nyumbani kwao ili siku ya harusi atokee nyumbani.
Sam nae hakuona kama lile ni jambo la kupinga, kwani aliona ni kheri tu tena italeta picha nzuri ingawa biharusi mwenyewe tayari alikuwa mjamzoto.
Kwahiyo Sam akajiandaa kwaajili ya kumpeleka Sabrina nyumbani kwao ingawa muda wote Sabrina alikuwa na mawazo tu.
Kwavile, waliondoka kwao jioni kwahiyo wakaingia kwakina Sabrina wakati muda nao umeshaenda ambapo mama wa Sabrina alifurahi na kuwaambia kuwa wamefanya vyema.
"Ni busara sana atokee hapa nyumbani kuliko mtoane huko huko"
Sam alikuwa akitabasamu tu muda wote ingawa Sabrina alikuwa kanyong'onyea.
Kisha Sam akawaaga na kuondoka.
Ila Sabrina hakukaa sana zaidi ya kujibeba na kwenda kulala, kwani aliona kichwa chake kuwa kizito kwa mawazo.
Wakati amelala, akajiwa na njozi kuwa wameshaenda kanisani kwaajili ya kufunga ndoa, ila watu wakaanza kuulizana,
"Jamani bwana harusi hayupo, hajafika mpaka saa hizi au haji tena?"
Akamuona shangazi yake akipayuka,
"Nilishayajua yote haya, kiburi chako kimekuponza Sabrina unaona sasa?"
Akajikuta akilia kwa uchungu, mama yake naye akamfata na kumwambia,
"Pole sana mwanangu, jikaze ndio ukubwa huo. Hata mimi mamako nimepitia hayo"
Akatokea na Jeff na kumwambia,
"Usijali Sabrina, ha ta wote wakutenge mimi nitakuwa pamoja nawe"
Ila Sabrina bado alikazana kulia, mara akamuona Sam kashika bastora na kuwaelekezea yeye na Jeff kisha akawaambia,
"Na mkapendane huko akhera, kwaheri"
Sabrina alishtuka huku jasho jingi likimtoka, hakutaka kuamini kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu.
"Lazima ina ukweli ndani yake, masikini Sabrina mimi. Nimekosa nini jamani? Mbona naonewa? Yani hii mimba hii inanitesa mimi, bora hata ingejitokea tu nijiepushe na aibu"
Sabrina alijikuta akibubujikwa na machozi tu na hakuweza kulala tena hadi panakucha.
Kulipokucha aliamka na kumfata mama yake kisha akamwambia,
"Sitaki tena kuolewa mimi mama"
"Wee Sabrina una kichaa au? Na hiyo mimba utaipeleka wapi? Mbona una mabalaa mwanangu?"
"Sina mabalaa mama ila tu sijisikii kuolewa"
"Yani harusi kesho halafu wewe unasemaje Sabrina? Huo upuuzi kamwambie baba yako mi sitaki hata kuusikia"
"Nina maana yangu mama"
"Maana gani hiyo? Tushakula hela za watu sie. Unataka utaolewa, hutaki utaolewa tu. Hizo sababu zako ukazitoe ndani ukiwa na mumeo"
Sabrina alimuangalia mama yake na kumuona kamavile ni mtu asiyemuhurumia ila alijilaumu mwenyewe kwakutokumwambia ukweli mama yake.
Akatoka na kujikalisha nje tu kwani mawazo yalimjaa.
Sam akiwa anamalizia mambo yake ya siku hiyo ili akajiandae kesho yake kwaajili ya harusi, njiani akakutana na kijana Francis ambaye alihitaji kuzungumza naye.
Kwanza kabisa Francis alimpongeza Sam kwa kumpata Sabrina,
"Hongera sana kaka, una bahati kwakweli. Sabrina ni dhahabu ambayo wengi wameitafuta bila mafanikio, ila wewe umebahatika hadi kumpa mimba dah hongera sana"
Sam alitabasamu kinafki kwani alijua wazi kuwa mimba ya Sabrina sio yake.
Kisha Sam akamuuliza Francis,
"Inamaana Sabrina ni binti aliyetulia sana eeh!"
"Tena sana, mimi nina mifano iliyohai kabisa kwani nina ndugu yangu aliwahi kuwa hadi kipofu kwaajili ya Sabrina lakini bado hakuweza kulala na Sabrina. Yani hakuna mwanaume aliyebahatika kulala na Sabrina, nakupongeza sana kaka."
Sam akamshukuru Francis kwa kufunguka kwake, tena akamkaribisha kesho yake kwenye harusi yao ambapo bila kinyongo Francis aliahidi kuwa ataudhuria tu.
Kisha Sam akarudi nyumbani kwake huku akiwa na tabasamu usoni ingawa moyoni alikuwa na mawazo kupita maelezo ya kawaida.
Jeff akiwa nyumbani kwao jioni ya siku hiyo alishangaa kupigiwa simu na Sam,
"Tafadhari Jeff nina mazungumzo na wewe. Naomba tuonane tafadhari"
Jeff aliogopa na kukataa ila Sam alimsisitiza kuwa hana nia mbaya na amemuita kuzungumza naye mambo mema tu.
Mwisho wa siku Jeff akakubali kwenda kuzungumza na Sam.
Kisha akamuaga mama yake,
"Haya wapi muda huu?"
"Jamani mama, yani hata nisiende kutembea"
"Haya nenda ila uwahi kurudi"
Jeff akakubaliana na mama yake ingawa mama yake alitambua wazi kuwa anadanganywa kwa muda ule kwani mwanae sio wa kurudi mapema wala nini.
Mida ile ya jioni pale kwakina Sabrina walianza kufika baadhi ya ndugu zao kwaajili ya kujiandaa na harusi ya kesho yake.
Sabrina akainuka na kumuaga mama yake kidogo,
"Nafika hapo kwa Sakina mara moja"
"Usiniletee balaa Sabrina, kesho mambo yananukia hapa. Kwa Sakina unaenda kufanya nini?"
"Kuna kitu naenda kumwambia"
"Kwanini asije yeye hapa? Kama unaenda uende na mtu"
Sabrina hakutaka kubishana sana na mama yake zaidi ya kuongozana na ndugu yake mmoja kwenda kwa Sakina.
Lengo kubwa la Sabrina lilikuwa ni kutaka kuzungumza na Jeff ila alijua wazi huyo nduguye atambania nafasi hiyo sema akaona ni vyema kama atumie ishara ya kuweza kuonana na Jeff hata badae wazungumze kwani hakutaka kumpigia simu wala kuzungumza nae kwenye simu akimuhofia Sam kuwa anaweza kufatilia mazungumzo yake.
Walipofika, walimkuta Sakina akiwa anamalizia kazi zake za hapa na pale, na alipowaona akaanza kuongea kwa kujishuku,
"Jamani biharusi hadi umenifata jamani, mi ndio nilikuwa namalizia hapa halafu nije angalau kusalimia wageni"
"Ndiomana nimekufata ili twende wote"
Wakaongea mawili matatu kisha Sabrina akamuulizia mtu aliyemfanya aende pale,
"Na Jeff naye yuko wapi?"
"Utamuweza yule? Yani wanawake watamponza mwanangu, hata hatulii hadi namuonea huruma. Hapa hayupo sijui kaenda kwa yupi leo."
Sakina aliongea bila ya kujua jinsi gani Sabrina ameumia, na muda huo huo Sabrina akaaga na kuondoka zao.
Na walipofika nyumbani moja kwa moja Sabrina alienda kulala kwani aliona kichwa chake kikichanganyika na mawazo.
Wakati yupo kitandani akitafuta usingizi, alijikuta akitafakari
"Hivi kwanini naumia nikiambiwa kuwa Jeff ameenda kwa wanawake? Inamaana namuonea wivu? Na kama namuonea wivu basi inamaanisha kuwa nampenda. Uwiii Mungu wangu, niepushe na hili janga tafadhari maana nahisi kuchanganyikiwa tu"
Sabrina alikuwa akiwaza na kuwazua pale kitandani mpaka pale usingizi ulipomchukua.
Kulipokucha, Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka kwani wengine walichelewa kidogo kutokana na mkesha ambao waliufanya usiku wake.
Na wao walipoamka ilikuwa ni maandalizi tu, amcpo Sabrina alipelekwa saluni kwaajili ya kupambwa na kuvaa shela.
Wakati anamalizia kupambwa, alitokea dada mmoja na kumfata Sabrina kisha akamsalimia na kujitambulisha,
"Naitwa Sara"
Sabrina naye akajitamburisha kwa jina ambapo yule dada akamwambia,
"Usijali Sabrina, mi nakufahamu tena sana tu na pia nafahamu kama unaolewa na Sam ila kilichonisogeza hapa kwako ni kuhusu jambo moja tu"
Sabrina akamuangalia kwa makini yule dada na kumuuliza,
"Jambo gani hilo?"
"Hivi unamfahamu vizuri huyu Sam anayetaka kukuoa?"
Sabrina akashtuka sasa na kumuuliza yule dada kwa makini,
"Kwanini unaniuliza hivyo dada?"
" Ninachotaka kukwambia mimi ni kuwa, unatakiwa uwe makini sana kwani huyo Sam kashawaliza wadada wengi sana hapa mjini. Kwaheri"
Sabrina alitaka kumuhoji vizuri huyu dada ila ndio hivyo alishainuka na kuondoka.
Sabrina alitamani kughairi kuvaa lile shela ila aliamua kuheshimu mawazo ya mama yake.
Muda wa kwenda kanisani ulifika, na karibia wote wakakutanika eneo la tukio ila Sabrina hakumuona Sam wala Jeff na kuanza kuhisi kuwa ndoto aliyoiota huenda ina ukweli ndani yake na kumfanya ajawe na uoga.
Ila muda haukupita sana, Sam na wapambe wake wakaingia pale kanisani na ndoa yao ikafungwa bila pingamizi kutoka kwa mtu yeyote yule.
Ndoa ilipomaliza kufungwa pale kanisani, kama kawaida wakaenda ukumbini kwa ajili ya kusherehekea kwa kula na kunywa na kupongezana kwa pamoja.
Hadi hatua hiyo ilipofika, Sabrina alikuwa na amani sasa moyoni ingawa mashaka kiasi bado yaliendelea kuutafuna moyo wake.
Baada ya tafrija kuisha, maharusi walitakiwa kusimama ili wawaage wageni waalikwa na waweze kwenda kupumzika.
Walipokuwa wamesimama, moja kwa moja Sabrina alifatwa na Jeff kisha yule Jeff akamkumbatia Sabrina kwa nguvu na kumfanya Sabrina amshangae kwani hakuonekana tangia harusi ile ianze ndio anaonekana muda huo.
Jeff akiwa kamkumbatia Sabrina, akaanza kumwambia,
"Kuwa makini Sabrina, Sam anaujua ukweli wote"
Muda huo huo Sabrina akaanguka chini na kuanza kutokwa na damu.
Walipokuwa wamesimama, moja kwa moja Sabrina
alifatwa na Jeff kisha yule Jeff akamkumbatia
Sabrina kwa nguvu na kumfanya Sabrina
amshangae kwani hakuonekana tangia harusi ile
ianze ndio anaonekana muda huo.
Jeff akiwa kamkumbatia Sabrina, akaanza
kumwambia,
"Kuwa makini Sabrina, Sam anaujua ukweli wote"
Muda huo huo Sabrina akaanguka chini na kuanza
kutokwa na damu.
Wote wakamkimbilia Sabrina pale chini bila kujali kuwa Jeff alikuwa akizungumza naye kitu gani.
Sam alimnyanyua Sabrina na kumkimbizia kwenye gari, tena bila hata ya kuwangoja wazazi wa Sabrina, alipanda kwenye gari na kuliendesha kwa kasi sana akimkimbizia Sabrina hospitali.
Wazazi wa Sabrina nao na baadhi ya ndugu walipanda kwenye gari jingine na kuanza kulifata gari la Sam.
Walipofika hospitali, Sabrina alipokelewa na kuanza kuhudumiwa kwa haraka sana kutokana na mumewe kujulikana sana katika hospitali hiyo.
Walimpeleka kwenye chumba cha huduma kisha, Sam alibaki nje kumngoja Sabrina.
Baada ya robo saa, daktari alitoka na kumfata Sam,
"Niambie docta nini tatizo?"
"Itabidi tumfanyie operesheni maana hali ni mbaya."
"Operesheni docta wakati mke wangu ni mjamzito?"
"Ndio, inabidi tumtoe kile kiumbe"
"Mungu wangu, kwahiyo mwanangu itakuwaje? Atapona kweli?"
"Tutajitahidi kuokoa maisha yao. Inabidi tu ukubali tuanze hiyo operesheni kwa haraka"
Sam hakuna na jinsi zaidi ya kukubali na kusaini karatasi kwaajili ya mkewe kufanyiwa operesheni.
Ndugu wa Sabrina walipotewa na Sam njiani kutokana na mwendo ambao Sam alikuwa akiuendesha, kwahiyo wakakosa uelekeo na kushindwa kuelewa pa kuelekea.
Waliamua kumpigia Sam simu ila iliita tu bila ya kupokelewa na kufanya wachanganyikiwe zaidi haswa mama wa Sabrina kwani alijihisi kamavile anaonewa kwa kutokujua hali ya mwanae wala kujua mahali alipo.
Ilibidi tu warudi nyumbani ili kusikilizia kama Sam atawapigia simu kwani walijaribu kuulizia kwa baadhi ya mahospitali ya karibu bila ya mafanikio yoyote.
Sam bado alikuwa na mawazo juu ya Sabrina, na kwavile alikuwa mwenyewe ndio akahisi kuchanganyikiwa zaidi.
Baada ya masaa mawili kupita, daktari alitoka kwenye chumba cha operesheni na kumkuta bado Sam akionekana kuwa na mawazo sana,
"Bwana Sam, punguza mawazo. Mkeo tunamshughulikia vizuri tu. Punguza mawazo"
"Niambie anaendeleaje mke wangu?"
"Bado amelala, ila anaendelea vizuri tu"
"Na mtoto je?"
"Usijali Bwana Sam, yote hayo tutakueleza vizuri tu ngoja mambo yakae sawa"
Sam alifarijika kidogo ila bado alikuwa na mawazo kwani furaha yake ni kusikia kuwa Sabrina amepona kabisa.
Kulipokucha, Sam alimfata tena daktari ili kupata majibu yake.
"Pole sana Mr.Sam"
Sam akashtuka na kuuliza,
"Pole ya nini tena?"
"Pole ya kumsubiria mkeo usiku wote, ila napenda kukupa na hongera pia"
Hapo Sam akatabasamu kwani alijua lazima ni khabari njema,
"Niambie daktari"
"Operesheni ilienda vizuri, ila sikutaka kukwambia usiku ule kwani nilijua wazi kuwa kwa vyovyote vile ningekuchanganya tu"
"Basi niambie daktari"
"Mkeo tulimfanyia ule operesheni na kumtoa yule mtoto akiwa hai kabisa, kwahiyo napenda kukutaarifu kuwa mkeo kajifungua mtoto wa kike ila tumemuweka kwenye uangalizi maalumu kwakuwa yule mtoto ni njiti"
Mwanzoni Sam alitabasamu ila aliposikia kuwa mtoto ni njiti akanywea gafla na kuuli za kwa upole,
"Njiti kivipi?"
"Njiti kwamaana kwamba amezaliwa kabla ya miezi na hata uzito wake upo chini sana kwahiyo anatakiwa akae katika uangalizi maalumu hadi pale afya yake itakapotengemaa" Sam akaridhika kiasi na kutaka kwenda kumuona mtoto wake ila daktari akamwambia kuwa itakuwa vyema kama ataenda kumwangalia badae kwa usalama wa mtoto huyo.
Sam alikubali kwani roho yake iliridhika sasa baada ya kusikia kuwa familia yake iko salama.
Kisha akaenda kwenye gari yake ili kuchukua simu kwaajili ya kuwataarifu ndugu zake hospitali aliyokuwepo.
Ila alipoichukua simu yake alikuta kuwa walimpigia sana simu bila kupokelewa.
Sasa alimua kumpigia kwanza mama wa Sabrina ambaye aliipokea kwa haraka sana kupita kawaida, tena hakutaka hata salamu zaidi ya kujua mwanae alipo.
Ikabidi Sam awaombe radhi kisha akawaelekeza hospitali ambayo yupo na Sabrina na kuwaambia kuwa Sabrina amejifungua.
Joy alikuwa nyumbani kwake pamoja na Sakina muda ambao Sam alikuwa akimpigia simu.
Muda anamaliza kuongea na simu hiyo, Jeff naye alikuwa mahali pale na kumsikia mama wa Sabrina akimwambia mama yake,
"Eti Sabrina kajifungua"
Jeff naye alishtuka na kufanya wamshangae pale,
"Sabrina kajifungua?"
Mama yake akamuuliza,
"Unachoshangaa ni kitu gani?"
"Mbona mimba yake ilikuwa bado ndogo?"
"Wee unajuaje kama ilikuwa ndogo? Mwingine tumbo dogo lakini mimba ishafikia wakati wake"
Jeff ikabidi anyamaza kwani alijua wazi akiongea zaidi anaweza kumwaga mchele kwenye kuku wengi.
Basi akawaacha pale mama yake na mama Sabrina wakiondoka kwenda hospitali kumuangalia Sabrina, alichofanya Jeff ni kuwauliza hospitali yenyewe kisha yeye akaanza kurudi kwao na kumfanya mama yake amuulize,
"Vipi, wewe huendi kumuona Sabrina?"
"Nitaenda wakati mwingine, nyie tangulieni tu"
Hawakutaka kumuhoji zaidi kwahiyo wakamuacha akiondoka nao kuondoka huku Joy akikazana kumpigia simu na mumewe ajue kwavile aliamkia mahospitalini kutafuta hospitali waliyoenda.
Jeff alirudi kwao na kumtafakari Sabrina,
"Kajifungua vipi wakati miezi tisa bado? Au tayari! Inamaana kama tayari basi ile mimba sio yangu mmh!! Na kama sio yangu mbona nilimkuta bado bikira? Haiwezekani, hata sielewi jamani"
Alitamani sana kwenda hospitali kumuona Sabrina ila bado mawazo yake yakamkwamisha kufanya hivyo kwani alijihisi vibaya kama itagundulika kuwa mimba ilifikisha miezi tisa wakati yeye tangia ambake Sabrina na kumpa hiyo mimba miezi tisa ilikuwa bado haijatimia.
Alikuwa na mawazo sana kwa muda huo.
Sam akaitwa na daktari ili aweze jambo kumtazama Sabrina ingawa bado alikuwa amelala.
Sam alishukuru na kwenda chumba walichomlaza Sabrina kumuangalia.
Na alipofika karibu alimuona kama Sabrina akijigeuza hivi na kujua wazi kuwa muda wowote anaweza kuzinduka.
Sam akawa karibu zaidi na Sabrina pale, ila Sabrina aliposhtuka akaita,
"Jeff"
Na kumfanya Sam ajisikie vibaya kwavile yeye ndio yupo nae karibu halafu anashtuka na kumtaja Jeff.
Alimshangaa kuwa anamaana gani, kwavile daktari alikuwa karibu akamsaidia kumuelewesha,
"Usichukie kwa mgonjwa hivyo, mwache akizinduka vizuri atatambua anachotaka kusema ila kwasasa ni kazi bure."
"Hata kama docta, kwanini amtaje Jeff?"
Daktari akamvuta Sam pembeni kidogo ili wasiweze kumsumbua mgonjwa, kisha akamuuliza,
"Kwani Jeff ndio nani?"
"Ni dogo mmoja hivi, tena yeye ndiye aliyesababisha mpaka mke wangu akaanguka"
"Basi hilo sio tatizo, kwanza kabisa ujue kuwa mkeo alianguka na kupoteza fahamu kwahiyo anapotaka kuzinduka picha inayomjia kichwani ni tukio lililompata kabla ya kuang uka na ndiomana akamtaja huyo Jeff"
Sam akamuelewa kidogo daktari na kurudi tena kumtazama Sabrina ambaye alikuwa amesharudi katika usingizi wake.
Kisha Sam akatoka nje kwaajili ya kuwaangalia ndugu wa Sabrina ambao watafika pale hospitali.
Joy na Sakina walifika pale hospitali na kumkuta Sam aliyewapa khabari zote juu ya maendeleo ya Sabrina.
Na wote wakatamani kwenda kumuona mtoto huyo aliyezaliwa kabla ya wakati ila daktari hakuweza kuwaruhusu kwa muda ule.
Jioni ya siku hiyo Sabrina aliweza kuzinduka na ndugu zake waliweza kumsalimia.
Na yeye pia aliweza kupewa taarifa kuhusu mtoto aliyejifungua.
Akamuuliza Sakina,
"Mbona Jeff hajaja kuniona?"
"Yule mtoto ni mwehu eti anashangaa umejifunguaje wakati mimba ilikuwa ndogo. Mi nikamshushua pale hadi akarudi nyumbani mwenyewe, ila atakuja tu yule"
Mama wa Sabrina naye akamsapoti Sakina,
"Ndio lazima aje yule, na anavyompenda Sabrina tena! Sie anafanya kutuchora tu kuwa tuondoke"
Sabrina akawasikiliza pale huku akijisifu kuwa hawajui vya moyoni mwake.
Ila walipoondoka, Sabrina nae alijikuta akitafakari kuwa kwanini Jeff asiende kumuona?
"Huwa Jeff hata wamseme vipi lazima aje, imekuwaje leo?"
Sabrina hakupata jibu ila bado alikuwa na matumaini kuwa Jeff ataenda tu kumuona kwa muda wowote ule.
Jeff akiwa nyumbani kwao, mama yake naye aliwasili kutoka hospitali ambapo moja kwa Jeff aliulizia kuhusu mtoto wa Sabrina,
"Eeh na vipi mtoto wake?"
!Mtoto hatujabahatika kumuona kwavile kazaliwa njiti kwahiyo hairuhusiwi watu kwenda kumuona ona hovyo"
Jeff naye alikuwa hajaelewa maana ya mtoto njiti na kumfanya mama yake apate kazi ya kumuelezea.
Kesho yake asubuhi na mapema, Jeff aliamka na kufunga safari ya kwenda kumuona Sabrina katika hospitali aliyoambiwa jana.
Na alipofika alimkuta Sam kwani Sam alikuwa anaenda nyumbani kidogo kwaajili ya kubadilisha nguo kisha kurudi tena hospitali.
Kwahiyo Sam alipomuona Jeff akamwambia akae hapo hospitali na Sabrina kwa muda huo wakati yeye anaenda kubadilisha nguo.
Jeff moja kwa moja alimfata Sabrina pale kitandani,
"Yani wewe mtoto ni mbaya sana, loh umeshindwa hata kuja jana?"
"Nisamehe bure mamy, kuna mambo nilikuwa nayaweka sawa kwanza halafu kuna kitu unatakiwa utambue"
"Kitu gani hicho?"
"Sam kashajua kuhusu mimi na wewe, kwahiyo anachofanya sasa ni kutafuta usahidi tu kwahiyo tunatakiwa kuwa makini kupita maelezo"
"Kwahiyo wewe ndio usipokuja kuniona Sam ndio hatojua?"
"Hapana sio kiivyo, ila natakiwa kupunguza ile kuja kukuona mara kwa mara ili asitugundue"
"Wewe umejuaje kama Sam ameshajua kila kitu?"
"Siku kabla ya harusi yenu Sam aliniita na nikaongea nae mambo mengi sana ila alinikatalia kuondoka na kunifanya nirudi nyumbani kesho yake. Ila kubwa zaidi ni kuwa aliniambia hivi..."
Kabla Jeff hajasema chochote tayari Sam alisharudi na tayari alishaingia mule wodini.
Ikabidi Jeff ajigeleshe na kuaga pale na kumfanya Sam amuulize,
"Mbona mapema sana?"
"Aah kuna vitu naenda kuvimalizia, naweza nikarudi badae kumuona"
Sam hakumbishia na kumuacha aende kisha yeye akaanza kumpa mazoezi Sabrina kama ya kumsaidia kukaa na hata kusimama ili waweze kwenda kumuona huyo mtoto wao.
Sam akamwambia Sabrina,
"Nampa jina mtoto"
"Khee hata kama bado njiti?"
"Ndio, nataka awe na jina lake kabisa mtoto wangu"
"Haya niambie, utamuita nani?"
"Nitamuita Cherry"
"Khee Cherry ndio jina gani?"
"Nina maana yangu kumpa jina hilo, hilo jina lina maana kubwa sana kwangu"
"Maana yake ni nini?"
"Muda ukifika nitakwambia maana yake, ila kuanzia sasa mtoto wetu ataitwa Cherry"
Sabrina hakuweza kubisha kwani ni yeye mwenyewe aliyempa Sam sifa ya ubaba kwa mtoto ambaye sio wake kwahiyo hakuwa na uwezo wa kukataa ukizingatia Sam tayari alishakuwa mume wake.
Ila akamuuliza,
"Kwa mfano angekuwa mtoto wa kiume ungemuitaje?"
"Ningempa hilo hilo jina la Cherry"
"Kwanini sasa?"
"Nimekwambia kuwa hilo jina lina maana sana kwangu, na ipo siku nitakwambia maana yake iwapo tu mtoto ataendana na jina lake"
Wakati wanazungumza hayo, daktari aliwafata na kuwapa taarifa kuwa mtoto anatakiwa kuongezewa damu.
"Sasa inakuwaje hapo docta?"
"Na sitaweza kuruhusu damu hiyo itoke kwa mama sababu huyo mama kashapoteza damu nyingi sana, kwahiyo itabidi tuchukue yako baba"
"Hakuna tatizo docta"
Moja kwa moja daktari akaenda maabara na Sam kwaajili ya vipimo vya damu.
Baada ya muda kidogo daktari akarudi na kumwambia kuwa damu yake na ya mtoto haviendani, daktari hakutaka kudadisi zaidi mambo ya kifamilia na kumuomba Sam atafute mtu wa kutoa damu itakayoendana na ya mtoto wao.
Sabrina alitamani ajitolee yeye ila daktari alikataa kutokana na usalama wake.
Sam akafikiria sana na kuamua kumpigia simu Jeff, na alipomwambia Jeff hakusita na kumfanya akubali kwenda hospitali kujitolea damu.
Wakati huo Sam akajiambia,
"Na leo, ndio nitajua ukweli wa mambo"
Jeff alifika hospitali na kupelekwa maabara, akapimwa damu ikaonekana inaendana kabisa na mtoto hivyo wakamtoa damu kwaajili ya kwenda kumuongezea mtoto.
Jeff alipotoka maabara akafatwa na Sam, kisha akamwambia
"Sikukuuliza wewe ukakataa?"
Jeff akashikwa na kigugumizi cha kujibu.
Jeff alifika hospitali na kupelekwa maabara,
akapimwa damu ikaonekana inaendana kabisa na
mtoto hivyo wakamtoa damu kwaajili ya kwenda
kumuongezea mtoto.
Jeff alipotoka maabara akafatwa na Sam, kisha
akamwambia
"Sikukuuliza wewe ukakataa?"
Jeff akashikwa na kigugumizi cha kujibu.
Sam akamuangalia Jeff kwa makini huku akingoja jibu ila bado Jeff hakuweza kutoa jibu kwani alikuwa akijiuma uma tu.
Wakati Sam akingoja jibu kutoka kwa Jeff, walifatwa na daktari pale walipokuwa wamesimama, kisha daktari akamwambia Sam,
"Samahani, mkeo anakuhitaji mara moja"
Sam hakupuuzia wito wa mkewe na kuamua kumuacha Jeff mahali pale kisha kwenda mahali alipo mkewe.
Alimkuta Sabrina akiwa amejitahidi na kukaa kitandani mwenyewe bila ya kusaidia na mtu.
"Kheee natumaini sasa umeanza kupata unafuu hadi unaweza kukaa mwenyewe!"
"Ndio, kwanza nina hamu na mwanangu, nimuone, nimnyonyeshe na kila kitu"
"Haya, imekuwa vyema damu ya kumuongezea mtoto imepatikana"
Sabrina akajifanya kushangaa,
"Khee jamani, nani kapatikana kujitolea hiyo damu!"
"Ni baba yake"
Sabrina akashtuka,
"Baba yake! Kivipi?"
"Ni Jeff ndio kajitolea, sasa Jeff nae si kama baba tu!"
"Hapana, Jeff hawezi kuwa na sifa ya ubaba kwa mtoto wetu, ila anaweza kuwa mjomba. Au kiswahili kinakupiga chenga mume wangu?"
Huku akijichekelesha na kumfanya Sam amuangalie tu, kisha na yeye akajiwa na hoja kwenye akili yake na kumuuliza Sabrina,
"Sawa, mimi sijui kiswahili ila vipi wewe unakijua? Jeff anakuita wewe mama mdogo, iweje sasa mwanao amuite Jeff mjomba? Kwani mjoba si kaka wa mama! Je wewe Jeff ni kaka yako?"
Sabrina akajiona wazi kuwa kachanganya mada, na ili kupotezea malengo ya Sam akajifanya ameanza kujisikia vibaya.
Akajishika kiuno na kujifanya kama anataka kujilaza huku akilalamika kwa Sam,
"Sam, nisaidie baba kiuno kinaniuma sana. Nisaidie, oooh kiuno mimi, kinaniuma jamani"
Ikabidi Sam aanze kumsaidia Sabrina, mpaka akaweza kumlaza kisha akamwambia,
"Ngoja nikamuite daktari"
"Hapana, usiende kumuita kwanza. Ngoja nijiangalie kwa muda kidogo"
"Pole sana mke wangu"
Kisha Sabrina alidai kuwa anataka kupumzika kidogo, hivyo Sam akaamua kumuacha ili angalau apate muda wa kupumzika.
Sam alikuwa na harakati sana ili kuhakikisha kuwa Sabrina na mtoto wao Cherry wanakuwa salama kabisa.
Alipotoka pale hospitali moja kwa moja alienda kwa mtaalamu wa kisaikolojia ili angalau ampe ushauri kidogo kwani hata akili yake ilikuwa ikifanya kazi ndivyo sivyo.
Alimkuta yule mtaalamu kama kawaida na kuanza kumueleza kinagaubaga tatizo lake ili ampe ushauri.
Mtaalamu huyo alijulikana kwa jina la Ayubu.
"Kwakweli naomba tu ushauri wako dokta"
"Bwana Sam, ngoja leo niongee jambo hili. Tangu nimekufahamu, kipindi hiki umekuwa ukija mara kwa mara kuomba ushauri ila tatizo ni moja, kwanini maelezo yako huwa yanapinda pinda?"
"Unamaana gani mtaalamu?"
"Hakuna siku uliyowahi kunieleza matatizo yako moja kwa moja nikakuelewa. Kiukweli Bwana Sam huwa unaniacha kwenye maswali pia, kwanini huwezi kuwa wazi katika kuelezea tatizo lako?"
Sam akainuka na kuondoka kwani aliona kuwa huyu mtaalamu anataka kuyapekenyua na matatizo yake ya ndani.
Tena aliondoka bila kuaga huku akijiambia,
"Nitakuwa najishauri mwenyewe, sio lazima wanishauri wao"
Alipanda gari yake na kuondoka.
Njiani alimuona Francis, kijana ambae alikutana nae kabla ya ndoa yake na kumpongeza sana kwa kumpata Sabrina.
Sam akasimamisha gari yake mbele ya Francis ili apate kumsalimia, ambapo alishuka na kumsalimia vizuri sana.
"Hongera kaka, nasikia mke wako kajifungua"
"Ndio, ila mtoto bado ni njiti"
"Aah, Mungu atamsaidia tu. Ila natumaini mwanao atakuwa mrembo kama mama yake"
Sam akatabasamu tu, na kumfanya Francis aendelee kuongea,
"Tena hongera kwa kuitimiza ndoto ya Sabrina. Natumaini wewe ni mwanaume wa pekee kwake, na tena umepata mwanamke wa pekee na muaminifu"
Sam akaitikia ila aliamua kuagana pale na Francis ili kuondoka na kuepusha kusongwa na mawazo zaidi juu ya Sabrina.
Ila hata alipokuwa anaendelea na safari yake bado sauti ya Francis ikimsifia Sabrina ilirudi katika akili yake na kumfanya ajiulize maswali na kujijibu mwenyewe,
"Sabrina ni mwanamke aliyetulia, mbona kabeba mimba nje ya ndoa tena kwa mwanaume asiye mumewe? Eti alibakwa, mbona kama anamfahamu mbakaji na kupatana nae? Inawezekana ndiye ampendaye? Ila kwanini asiwe naye? Na kwanini aseme alimbaka? Nadhani alitaka mwenyenye. Aaaaah!!!"
Alijikuta akipiga kelele na kufunga breki mbele ya mtu ambaye ilibaki kidogo tu amgonge.
Sam akashuka kumuomba msamaha, ambapo mtu mwenyewe alikuwa ni mdada.
"Samahani sana dada yangu, akili yangu haipo sawa"
"Nimekusamehe ila uwe makini maana ungenigonga hata sijui ningekuwa wapi muda huu"
Sam akaomba kumpa lifti yule dada na kumpeleka anapoelekea.
Ambapo alimpeleka hadi eneo husika kisha kumpa mawasiliano yake na kumuaga.
Ila kabla hajaondoka, yule dada akamuita tena Sam,
"Samahani kaka, hujanitajia jina lako na wala langu hulijui. Tumetembea kwenye gari kama mabubu, mimi naitwa Neema. Nani wewe mwenzangu?"
"Mimi naitwa Sam"
"Sawa Sam, tutazidi kuwasiliana"
Sam akamuaga yule dada tena na kuondoka ambapo yule dada alijikuta akimuangalia tu Sam hadi alipotokomea na gari yake.
Sabrina akiwa pale hospitali, ndugu zake walienda tena kumuona na kuondoka ila alishangaa kwa kutokumuona Sam na bila ya kupata simu yake.
"Mmh! Huyu Sam ananipa mashaka usiku na mchana. Kwanini asinipigie simu? Au bado anaendelea na kisirani chake?"
Ila hakupata jibu, hadi usiku sana unaingia Sam hakutokea pale hospitali na kumfanya Sabrina alale huku kichwani mawazo yamemtawala na kuumiza kichwa chake.
Asubuhi na mapema, alifika pale mama wa Sabrina ili kumpelekea mwanae uji.
"Nadhani leo nitatoka mama"
"Na mtoto je?"
"Mtoto hawezi kutoka, docta kasema eti afadhari afikishe hata mwezi kwenye kale kachumba ndio turudi nae nyumbani"
"Basi na wewe itakuwa ngumu, yani upo tayari wewe ukalale nyumbani halafu mwanao alale hospitali? Unaweza hayo Sabrina?"
"Mama, nimechoka kukaa hospitali. Naona watu wamenichoka"
Sabrina akainama na machozi yakamtoka na kumfanya mama yake amuulize,
"Nani amekuchoka mwanangu? Mimi nikuchoke? Hata dunia nzima ikukimbie mimi siwezi kukuacha mwanangu. Kuwa na roho ya umama, usimuache mwanao hapa. Natumaini baada ya wiki tu atakuwa anaendelea vizuri na tutaenda nae nyumbani. Hakuna wa kukuchoka mwanangu"
"Sam kanichoka mama, jana kaondoka hajaniaga na hadi leo hajaja"
"Usimlaumu mwanangu, Sam anakupenda sana. Na hata hivyo mimi ninakupenda mwanangu"
Ikamlazimu Joy siku hiyo ashinde hapo hospitali kumfariji mwanae.
Kwenye mida ya saa saba mchana, Sam alishtuka kutoka usingizini na kujishangaa.
Alipoangalia mida na kuona kuwa ni saa saba mchana ndio akajishangaa zaidi,
"Yani nimelala mpaka muda huu? Kwanini lakini?"
Akajaribu kuvuta kumbukumbu, akagundua wazi kuwa ni uchovu ndio uliomfanya alale mpaka muda huo.
Alikumbuka kuwa, alikesha sana hospitalini kama kwa siku tatu mfululizo bila ya kupata muda kamili wa kulala. Na vilevile jana yake baada ya matukio yote alijikuta akipita baa na kunywa pombe ili kupunguza mawazo na hiyo ndio imemfanya aamke kesho yake saa saba mchana.
Akakumbuka kuwa Sabrina yupo hospitali na anahitaji sana uwepo wake, hivyo akainuka na kwenda kuoga haraka haraka ili akamuwahi Sabrina hospitali.
Muda ulizidi kwenda na kumfanya Sabrina azidi kukosa raha huku akijiuliza maswali mengi mengi kuwa amemkosea nini Sam mpaka kutokwenda kumuona tena.
Ingawa mama yake alikuwa pale kumuangalia na kujaribu kumpotezea mawazo ila yeye alikuwa akifikiria tu kuhusu Sam ukizingatia hata Jeff alikuwa akienda hospitali hapo kwa machale kwani naye alikuwa akihofia uwepo wa Sam mahali pale.
Baada ya muda kidogo, Sam aliwasili kwenye ile wote aliyolazwa Sabrina.
Ila Sabrina alimuangalia tu bila ya kumfurahia kwani alishawaza hadi kuchoka.
"Samahani mke wangu, kuna mambo yaliingiliana kidogo"
Sabrina bado alimuangalia tu Sam bila ya kusema kitu,
"Tena ngoja nikamuangalie na mtoto kidogo"
Sam akainuka na kwenda kwa daktari ili ampeleke chumba alichowekwa mtoto wao akamuone.
Sabrina bado hakuwa na raha kwani hofu ilimzidia.
Muda kidogo Sam akarejea,
"Daktari kasema, kwa hali inayoendelea kwa mtoto wetu anaweza kuturuhusu wiki ijayo turudi naye nyumbani"
Sabrina akaitikia kwa kutikisa kichwa na kumfanya Sam amuulize,
"Vipi mbona hivyo, umechukia?"
"Hapana nimefurahia"
"Mbona unaongea kwa unyongea hivyo? Nakupenda Sabrina, nakupenda mke wangu. Kama kuna mahali nimekosea tafadhari nisamehe"
Sabrina akatabasamu kidogo baada ya kusikia kuwa anapendwa na kumfanya sasa aweze kupata nguvu ya ziada ya kuweza kuzungumza na Sam.
"Ila muda mwingine ukiondoka uwe unaniaga."
"Kama ni hilo hata usijari, nitakuwa nakuaga jana hata sijui nilipitiwa na kitu gani"
Mama wa Sabrina alipofika na kuwakuta wakitabasamu naye akafurahia hali ile.
Baada ya wiki kuisha, hali ya mtoto wao ilikuwa nzuri na wakaruhusiwa kurudi nae nyumbani na kupewa masharti ya namna ya kuishi naye ili wasiweze kumuathiri kwa chochote.
Sabrina alifurahi kwavile alishachoka kukaa pale hospitali.
Safari ilikuwa ni moja kwa moja hadi nyumbani kwakina Sabrina ili akaweze kupata uangalizi wa karibu zaidi kutoka kwa mama yake.
Walipofika nyumbani, shangazi wa Sabrina naye alikuwepo pale akingoja ujio wao na kumpokea mtoto wao na kwenda kumuweka ndani mahali walipo shauriwa na daktari.
Shangazi wa Sabrina alianza kumsifia mtoto yule,
"Aah umejifungua mtoto mzuri sana, mmempa jina gani?"
"Anaitwa Cherry"
"Nani kampa jina hilo?"
Akadakia mama wa Sabrina,
"Baba wa mtoto ndio kampa hilo jina"
"Mmh! Nikiwatajia jina ambalo baba wa mtoto alitaka kumpa huyu mtoto mtakaa nyie hapa? Ngoja ninyamaze tu"
Sabrina alikuwa kimya sasa huku akiwaza kimoyo moyo jinsi anavyochukizwa na maneno ya shangazi yake kwani mara zote anahisi kuwa anataka kumuharibia tu.
Sabrina aliendelea kumuhudumia mtoto wake huku akiwaza maisha yake pia yatakavyokuwa na huyo Sam kwani amejikuta mara nyingi akishindwa kumuelewa Sam na zaidi ni kuwa akishindwa kumuelewa kuwa anajua nini na anataka nini kutoka kwake.
Sam alipeleka vitu vingi sana vya mtoto ikionyesha wazi ni jinsi gani anavutiwa na mtoto huyo pia ni jinsi gani anampenda.
Muda mwingi kwa kipindi hiko Sam alikuwa akishinda pale nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kuwa karibu na familia yake.
Sam siku hiyo kama kawaida, alitoka nyumbani kwake na kufunga safari hadi kwenye duka la vitu vya watoto ili amnunulie mtoto wao baadhi ya vitu na kumpeleke.
Wakati yupo nje ya duka akitaka kuingia akasikia mtu akimuita,
"Sam"
Sam akageuka, akamuona mdada kwenye daladala akiwa amekaa kwenye kitu cha mbele.
Yule mdada akatabasamu na kumpungia mkono Sam wakati ile gari ikiondoka.
Sam alijaribu kuvuta kumbukumbu ya sura ya yule mdada kuwa alimuona wapi ila kumbukumbu hakuipata kabisa na kumfanya aingie mule dukani na kuendelea na mambo mengine.
Alichagua vitu vya kumchukulia mwanae kisha akavilipia na kuanza kuondoka navyo.
Wakati anatoka, akakutana na mtu ambaye hakumfahamu kwa wakati huo ila huyo mtu alionekana kumfahamu Sam na kumsalimia,
"Hebu nikumbushe, tumewahi kuonana wapi?"
"Hata nikikukumbusha huwezi kunikumbuka Mr. Sam ila kwa kifupi ni kuwa hunifahamu ila mimi nakufahamu"
Sam akamshangaa na kumuuliza tena,
"Unanifahamu kivipi?"
"Nitakwambia tu siku nikipata muda wa kutosha. Ila tunza jina langu kwenye akili yako, naitwa Musa"
Kisha yule mtu akaingia mule dukani na kumuacha Sam aende.
Sam alifika na kumfata Sabrina na kumkabidhi vile vitu vya mtoto, ila muda huo huo akapigiwa simu kuwa anahitajika ofisini.
Sam akamuaga Sabrina pale na kuisahau simu yake pale pale kwenye vitu vya mtoto, kisha akaondoka.
Sabrina akaisikia ile simu ya Sam ikiita, akaichukua na kuangalia, namba ilikuwa ni mpya na kumfanya Sabrina ashindwe kuipokea.
Ile simu iliita hadi kukatika, mara ukaingia ujumbe mfupi wa maneno.
Sabrina akafungua na kusoma.
Alipomaliza kusoma alihisi kubanwa na tumbo kwani ujumbe ulimtisha.
Ile simu iliita hadi kukatika, mara ukaingia ujumbe
mfupi wa maneno.
Sabrina akafungua na kusoma.
Alipomaliza kusoma alihisi kubanwa na tumbo
kwani ujumbe ulimtisha.
Sabrina akainuka na kwenda kujisaidia, kisha akarudi tena chumbani kwake na kushika ile simu, huku akirudia rudia ule ujumbe uliosema,
"Mpenzi Sam, nimefurahi sana kukuona leo. Mwaah"
Alikuwa akijiuliza mara mbili mbili,
"Inamaana Sam anamwanamke mwingine? Inamaana mimi hanipendi hadi anaenda kuonana na huyo mwanamke?"
Alijikuta wivu ukimjaa hadi kupitiliza na kuona kamavile amejiingiza kwenye shimo na kuanza kuwaza mambo mbali mbali,
"Ama kweli, aliyesema hakuna mwanaume wa peke yako duniani hakukosea"
Roho yake ilimuuma sana na kumfanya akose raha kabisa.
Muda kidogo, alifika Sakina kwa lengo la kumsalimia Sabrina,
"Mbona leo huna raha mdogo wangu?"
"Hamna dada, sijisikii vizuri tu"
"Acha kuwa na mawazo mdogo wangu, mume unae tena mzuri tu, anakupenda, anakujali na kila kitu. Angalia wenzio, mfano mimi, mume alishanikimbia tena bila hata sababu. Najitahidi kumuweka kwenye njia salama mwanangu Jeff ili asifate tabia za baba yake lakini naona kama juhudi zangu zinagonga mwamba"
"Kwanini dada?"
"Tabia ya Jeff haieleweki kabisa, sijui hata anataka mwanamke wa aina gani ili atulie nae. Nimeshaongea hadi mdomo kukauka ila huyu mtoto hanisikii kabisa"
Sabrina akategesha sikio vizuri ili kujua kama tabia ya Jeff imebadilika kutoka ile anayoijua yeye.
"Hebu niambie vizuri dada, kwani kafanyaje?"
"Leo alikuja yule binti wa kuitwa Dorry, yani mwanangu alivyomuacha pale nyumbani hadi huruma. Sijui hata ameenda wapi"
"Usijali dada, Jeff anasumbuliwa na ukuaji"
Kisha akambadilishia mada ili asije kuongea na mengineyo bure.
Sam alipokuwa ofisini, akagundua kuwa simu yake hakuwa nayo na kuanza kujiuliza kuwa ameiacha wapi,
"Au nimeiacha pamoja na vile vitu vya mtoto nilivyompa Sabrina?"
Aliamua kutumia simu yake ya mezani pale ofisini na kumpigia simu Sabrina ili kujua kama simu yake ipo kwa Sabrina, ila alipiga bila ya kupokelewa na kuamua kupiga simu yake mwenyewe ambayo nayo ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Akazidi kujipa jibu kuwa lazima itakuwa ameisahau kule kwa kina Sabrina.
Akaweka vitu sawa na kuamua kuondoka ofisini pale kwa lengo la kwenda kuifata simu yake.
Wakati ameondoka, njiani akagundua kuwa gari yake inakaribia kuisha mafuta na kuamua kwenda kwenye kituo cha mafuta cha karibu na pale kujaza kwanza gari lake.
Wakati yupo pale kwenye kituo cha mafuta, kuna mtu alimuita,
"Sam"
Na Kumfanya Sam ashuke kwenye gari yake na kumfata yule mtu,
"Mambo Sam"
"Salama tu"
"Mbona unaniangalia kama vile hunijui?"
"Samahani kwakweli, hebu nikumbushe nilipokuona"
"Mimi naitwa Neema, kuna siku ulitaka kunigonga na gari yako"
Sam akavuta kumbukumbu na kumkumbuka Neema,
"Aaah, nishakukumbuka tayari. Na si ndio wewe ulinipungia mkono ukiwa kwenye gari?"
"Ndio ni mimi Sam, nimefurahi sana kukuona."
"Basi vizuri Neema, tutazidi kuwasiliana"
Sam akaanza kuondoka akifata gari yake, naye Neema akamfata nyuma na kumwambia,
"Sam, tafadhari naomba unipe lifti na leo"
"Hilo halina tatizo, panda tu kwenye gari twende"
Neema alipanda kwenye gari ya Sam na safari ikaendelea.
Walipokuwa ndani ya gari Neema aliamua kuanzisha maongezi baada ya kuona kuwa Sam yupo kimya sana,
"Hivi Sam unaonaje tukapanga siku tukae pamoja na kubadilishana mawazo?"
"Hilo ni wazo jema, ila muda nao unabana sana"
"Basi hakuna tatizo, siku ukiwa na muda tu niambie halafu mimi nitakuja ulipo"
"Sawa nitakujuza, usihofu juu ya hilo"
"Asante Sam, unaonekana kuwa mkarimu sana. Hongera kwa hilo."
Sam akamfikisha Neema mahali alipokuwa anaenda kisha na yeye akaendelea na safari yake.
Sabrina alipomaliza maongezi na Sakina aliamua kurudi tena chumbani kwake, ambapo alikuta simu yake ikionyesha kuwa ilipigwa bila ya kupokelew a. Alipoiangalia ile namba ilikuwa ni namba ya ofisini kwa Sam ambapo aliamua kuipiga na yeye ila haikupokelewa pia.
Akaachana nayo huku kichwani akiwaza kuwa lazima Sam atakuwa na mwanamke na ndiomana hayupo ofisini.
Akaiweka ile simu pembeni, baada ya muda mfupi akasikia ujumbe mfupi ukiingia kwenye simu ya Sam.
Akaichukua na kuufungua ule ujumbe,
"Mpenzi Sam, asante kwa ukarimu wako. Nashukuru kwa kunifikisha nyumbani"
Roho ya Sabrina ikamuuma zaidi ya mara ya kwanza kwani ule ujumbe ndio ulimthibitishia wazi kuwa Sam alikuwa na mwanamke ambaye ndio huyo alikuwa akimshukuru kwa maneno matamu.
Sabrina akakosa raha zaidi na kumfanya azidi kuumwa na kichwa.
Sam alipokuwa anaendelea na safari yake, akaona eneo watu wamejaa sana na kuamua kusimamisha gari yake.
Na alipoangalia vizuri akagundua kuwa eneo lile kuna ajali imetokea.
Sam akashuka na kusogea eneo la tukio, alipomuangalia mtu yule aliyepata ajali aliona wazi kuwa ni mtu anayemfahamu kabisa, ikabidi asogee pale na kuamua kumsaidia.
Wakasaidiana na baadhi ya watu kumpakia yule mtu kwenye gari yake na kumuwaisha hospitali.
Walifika hospitali na moja kwa moja akapelekwa kwenye huduma.
Ikabidi Sam ajaribu kutafuta simu ya yule mtu kisha akamuomba daktari simu na kuanza kuangalia namba kwenye simu ya yule mgonjwa na kuwapigia ndugu wa mtu yule kwenye simu ya daktari.
Alipomaliza ikabidi akae sasa akingoja ndugu wa yule mtu wawasili.
Muda huo akaamua kumpigia simu Sabrina pia kwa kupitia ile simu ya daktari ili kumjulisha kuwa yupo hospitali,
"Sabrina, Sam anaongea hapa. Kuna tatizo limetokea na sasa nipo hospitali na sijui kama nitaweza kuja huko leo."
Sabrina akasonya na kukata ile simu, na kumfanya Sam atikise kichwa kama ishara ya kusikitika,
"Yani hawa wanawake bhana, basi hapo kashaniwazia mabaya wakati niliyemsaidia ni rafiki yake mwenyewe, ila upo muda ataelewa tu."
Sam alijisemea bila ya kujua kinachoendelea.
Kabla Sabrina hajapokea simu kutoka kwa Sam, alikuwa akiwaza sana na moyo kumuuma sana juu ya jumbe ambazo aliziona zikiingia kwenye simu ya Sam.
Hata hivyo aliona usiku ukijongea na kuona kuwa kuna uwezekano wa Sam kutokufika hapo kwa siku hiyo hadi kesho.
Wakati akitafakari hayo, kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Sam kwa namba ile ile,
"Mpenzi ni baridi sana leo, natamani uje ili uwe karibu yangu nipate joto lako"
Na baada ya muda mfupi ndio akapata ile simu kutoka kwa Sam kuwa hatoweza kwenda siku hiyo.
Sabrina akaoanisha matukio na kuweka kuwa tukio moja huku akiamini kuwa Sam lazima ameenda kulala na huyo mwanamke.
"Huyu Sam, ameishi na mimi siku zote, hajawahi kulala na mimi. Sijui huwa ananionaje? Leo hii ananidanganya mimi kuwa yupo hospitali kumbe yupo na mwanamke!!"
Sabrina akajikuta akitokwa na machozi ambayo hakuyatarajia ila yote ni kutokana na wivu ambao ulikuwa umeikamata roho yake kwa wakati huo.
Alijaribu kulala ila usingizi haukumjia, alikuwa akimtazama tu mtoto wake huku akiwaza maisha yake.
Ndugu wa yule aliyepata ajali walifika, wa kwanza kabisa alikuwa ni Francis ambaye alimshukuru Sam kwa kumsaidia ndugu yake,
"Kumbe huyu ni ndugu yako?"
"Ndio ni ndugu yangu, anaitwa Fredy"
"Niliwahi kumuona mara kadhaa akimleta Sabrina pale ofisini na ndiomana nikamkumbuka ila sikujua kama ni ndugu yako kwakweli"
"Sasa namba yangu ukaipata vipi na kuanza kunipigia?"
"Niliangalia simu yake nikaona jina kaka, ndiomana nikapiga na hata sikujua kama naongea na wewe"
Francis akamshukuru pale Sam kwani Fredy angeendelea kushangaliwa pale alipopata ajali basi angeweza kupoteza hata maisha.
Sam hakuweza kuondoka na kwenda kwakina Sabrina kwavile muda ulikuwa umeenda sana, hivyo akangoja pakuche ili aweze kwenda.
Na hakutaka kupoteza muda kwani kulipokucha tu akaamua kuianza safari ya kwenda kwakina Sabrina, hakutaka kupitia mahali popote zaidi ya kufika hapo.
Sabrina nae alikuwa akilala kidogo na kuamka hadi panakucha kwani mawazo yalimjaa sana kwenye akili yake.
Na muda kidogo akasikia mtu akigonga mlango.
Sabrina aliinuka na kwenda kufungua, mgongaji alikuwa ni Sam.
Sabrina alimuangalia kutoka juu hadi chini kisha akamuuliza,
"Umefata nini asubuhi yote hii?"
"Nimekuja kuwaona"
"Kuwaona wakina nani?"
"Wewe na mwanangu"
"Ili iweje?"
"Ndio maswali gani hayo Sabrina jamani?"
"Sio maswali gani, nisubiri hapo hapo"
Sabrina akafunga mlango na kumuacha Sam pale nje, baada ya muda kidogo akarudi kisha akamkabidhi Sam simu yake na kumwambia,
"Nenda kwako ukaoge kwanza ndio uje uongee na mimi, huwezi kuja kumshika mwanangu na mauchafu yako kutoka kwa mwanamke wako. Usije ukambemenda bure mwanangu. Kwaheri"
"Kivipi Sabrina?"
Sabrina aliingia ndani na kubamiza mlango na kumuacha Sam akiwa ameduwaa pale nje.
Sam akaamua kupanda gari lake na kuelekea nyumbani kwake huku akijiuliza kuwa kosa lake ni kitu gani hadi kufikia hatua ya kufungiwa mlango vile na Sabrina,
"Kwani nimemkosea nini huyu mwanamke jamani? Yani kutokwenda jana usiku tu? Si nilimwambia kama kuna matatizo na nipo hospitali, yani kashindwa hata kuniuliza ilikuwaje mmmh hapa mwanamke sina kwakweli."
Sam alijiwazia hadi anafika nyumbani kwake.
Akaamua kwenda kuoga ili akirudi tena kwakina Sabrina awe msafi ili asimkere tena.
Sabrina alitafakari na kuoanisha matukio vizuri sasa,
"Amekuja alfajiri na nguo zile zile za jana, inaonyesha wazi alilala kwa yule mwanamke kweli. Kwanini Sam ananifanyia hivi lakini, kama hanitaki si bora aniambie tu kuliko kunifanyia vituko namna hii"
Akaamua kumpigia simu Sakina ili aweze kuongea na Jeff,
"Hivi Jeff yupo?"
"Yupo ndio, ila jana karudi amechoka sana sijui hata alikuwa wapi. Yani huwezi amini hadi muda huu bado kalala"
"Sawa, akiamka basi mwambie aje maana nina shida naye sana"
Sakina alikubaliana na Sabrina lakini Sabrina alimuita Jeff si kwasababu alikuwa na shida naye kweli ila ni kwavile alitaka kumuona tu ili apunguze maumivu ya moyo wake kwa siku hiyo.
Jeff alipoamka, mama yake akampa ujumbe aliopewa na Sabrina na kumfanya Jeff atabasamu kwa kukumbukwa na Sabrina.
Kisha akaamka na kwenda kuoga ili aweze kwenda kumuona huyo Sabrina.
Sam naye alipomaliza tu kijiandaa akaianza safari ya kwenda kwa wakina Sabrina.
Njiani akamuona shangazi mkubwa wa Sabrina na kuamua kusimamisha gari,
"khee shangazi za siku"
Wakafurahiana pale na ikaonyesha wazi kuwa shangazi naye alikuwa akienda kumuona Sabrina na kumfanya Sam afurahie kuongozana nae kwani safari yao ilionekana kuwa ni moja tu.
Jeff alienda kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa chumbani kwake na mtoto.
Naye Jeff akaingia huko kumsalimia,
"Nimeambiwa kuwa una shida na mimi sana"
Sabrina akatabasamu, na kabla hajaongea kitu akasikia mama yake akiwakaribisha watu na kumfanya asikilizie vizuri.
Wale watu waliingia mpaka chumbani kwa Sabrina na kumfanya Sabrina afurahi kwavile aliyeingia alikuwa ni shangazi yake mkubwa.
"Jamani shangazi Penina, karibu sana"
Wakafurahi na kusalimiana, kisha Penina akakaa na kupewa mtoto ili amshike kidogo.
Penina alipomshika yule mtoto, alimuangalia kisha akamuangalia Jeff na kusema,
"Jamani huyu mtoto kafanana na huyo kijana kama mwanae vile"
Wote walimuangalia Jeff ili waone ufanano wake na mtoto.
Penina alipomshika yule mtoto, alimuangalia kisha
akamuangalia Jeff na kusema,
"Jamani huyu mtoto kafanana na huyo kijana kama
mwanae vile"
Wote walimuangalia Jeff ili waone ufanano wake na
mtoto.
Sabrina akaingizia maongezi mengine kati ili kuondoa maana,
"Huyu mtoto hataki kunyonya eti, mlete nimjaribu tena"
Penina akashangaa,
"Hataki kunyonya, kwanini?"
"Hata sijui kwanini shangazi"
Sabrina akamchukua yule mtoto na kufanya kama anataka kumnyonyesha, muda huo Jeff nae akaona bora aondoke ili kuepusha fikra za ziada kwa wengine.
Penina akamuangalia Sabrina alivyokuwa akimnyonyesha mtoto,
"Ila naona ananyonya tena anavuta vizuri sana"
Sabrina akatabasamu na kusema,
"Itakuwa kwavile amekuona wewe, bora shangazi umekuja kwakweli"
Penina nae akatabasamu na kusema,
"Mguu wangu una baraka ndiomana yote yanafanikiwa"
Muda wote huu Sam alikuwa kimya kabisa huku akiangalia matukio yanavyoenda.
Baada ya muda kidogo, mama wa Sabrina aliingia chumbani kwa Sabrina na kumuita Penina ili akazungumze nae kidogo.
Muda huo Sam nae akamsogelea Sabrina karibu ili asikie kuwa atamwambiaje tena.
Ila Sabrina alikuwa kimya tu huku akiendelea kumnyonyesha mtoto wake na kumfanya Sam aulize,
"Sabrina, mbona umekuwa hivyo?"
"Nimekuwaje kwani?"
"Sikuelewi Sabrina, kwani una tatizo gani?"
"Sina tatizo lolote, labda nikuulize wewe kuwa una tatizo gani"
Sam akamtazama Sabrina kwani hata majibu yake yalimpa mawazo pia.
"Mimi sina tatizo Sabrina, basi nipe mtoto angalau nimshike na kumsalimia"
"Weee thubutu yako, huyu mtoto utamshika baada ya kugundua kosa lako"
"Sasa kosa langu ni nini Sabrina?"
Penina nae akawa amerudi na kumfanya Sam kushindwa kuendelea kuuliza.
Alikaa kimya tu tena bila ya kumuelewa Sabrina kuwa anataka nini na kwanini alisema vile.
Muda kidogo, simu ya mkononi ya Sam ikaita na kumfanya ainuke na kwenda kuongelea nje ili asisumbue wengine pale ndani.
Na baada ya muda kidogo akarudi ndani na kumuaga Sabrina,
"Nitarudi badae kidogo Sabrina"
"Aah ndio unaenda kule kwa jana?"
Kwa mawazo ya Sam akajua kuwa anamuulizia kuhusu kule hospitali na kumjibu,
"Ndio kule kwa jana, ila nitawahi kurudi"
Kisha Sam akatoka na kuondoka bila ya kujua kuwa mwenza wake amemaanisha kitu gani.
Sabrina alikuwa akiongea na shangazi yake pale huku mawazo yake yakiwa mbali sana kwani aliwaza kuwa Sam ameenda tena kwa yule mwanamke.
Kisha akamuuliza shangazi yake,
"Hivi ukigundua kuwa mumeo anamwanamke mwingine, unachukua hatua gani shangazi?"
"Kwanini umeuliza hivyo Sabrina? Najua lazima utakuwa na sababu inayokupelekea wewe kuuliza hivyo. Je unamuhisi tofauti mumeo? Unahisi anakusaliti?"
Sabrina akaamua kugelesha pale,
"Hapana sio mimi shangazi ila ni rafiki yangu ndiye aliyekuwa akiniomba ushauri hapo"
Penina akacheka na kuanza kumuelekeza Sabrina.
Sam alienda moja kwa moja hospitali kama alivyopigiwa simu na Francis, ila lengo lake kuu ilikuwa ni kumuona Fredy kuwa anaendeleaje.
"Kwakweli wewe Sam ni mtu mwema sana, una roho njema. Fredy alipozinduka tu na nilipomueleza kuhusu wewe, kasema kuwa atapenda akuone mwenyewe"
Sam hakupinga na moja kwa moja akaenda alipolazwa Fredy ili kuzungumza nae kidogo.
Fredy nae alifurahi sana kumuona Sam kuwa ameenda kumtembelea pale hospitali,
"Nashukuru kaka, umenisaidia sana"
"Usijali Fredy, maisha ndivyo yalivyo"
Fredy alifurahi sana kuzungumza na Sam mahali pale ukizingatia siku zote alitamani kuzungumza na Sam na hakuweza kupata hiyo nafasi.
Sam alipokuwa anatoka pale hospitali, akapishana na mdada mmoja kwenye geti la kutokea hospitalini pale na akahisi wazi kuwa anafahamiana na yule dada, kwahiyo akasimamisha gari ili aweze kumsalimia.
"Dada"
Yule dada akasimama na kuangalia kama anayeitwa ni yeye, alipoona kuwa anayemuita ni Sam, yule dada akatabasamu na kumfata Sam alipo,
"Mambo Sam, naona leo umenikumbuka"
Sam nae akatabasamu na kusema,
"Nimekukumbuka ndio ingawa jina limenitoka kidogo"
"Mmh Sam, yani kila siku nijitambulishe jamani! Mi ni Neema, yule dada uliyetakaga kumgonga tena kila siku huwa nakutumia ujumbe"
"Yani uliposema kuwa wewe ni Neema hapo ndio nimekukumbuka dada"
Neema akamuangalia kidogo Sam na kutabasamu, kisha Sam akamuuliza,
"Vipi kuna mgonjwa umekuja kumuona?"
"Ndio, kuna ndugu yangu alipata ajali majuzi ndio leo nimekuja kumuona"
"Aah pole sana, anaitwa nani nduguyo?"
"Asante, anaitwa Fredy"
Sam akaamua kumdadisi na kugundua kuwa ni Fredy yule yule anayemfahamu yeye.
Kisha akamueleza Neema jinsi alivyomkuta Fredy na kumsaidia na kumfanya Neema amshukuru zaidi, kisha wakaagana pale huku Sam akielekea kwenye gari yake na Neema akielekea ndani ya hospitali.
Sam hakuwa na wazo kabisa juu ya jumbe za kwenye simu yake hivyo kumfanya asishughulike nazo kabisa.
Muda huu alikuwa akielekea tena kwa kina Sabrina ili akapate kuwaona kabla ya kwenda kwake kulala.
Alipofika alikuta yule shangazi wa Sabrina kashaondoka,
"Kheee shangazi hayupo!"
"Ndio hayupo, mama kaenda kumsindikiza. Muda sio mrefu wameondoka hapa"
Sam akamsogelea Sabrina ili ajaribu japo kumshika tu ila Sabrina akarudi nyuma kanakwamba hataki kuguswa na Sam.
"Vipi Sabrina mbona hivyo?"
"Unaniuliza mimi mbona hivyo kabla ya kujikagua mwenyewe na hayo marashi ya kike"
"Marashi ya kike? Kivipi mbona sikuelewi jamani?"
"Inamaana hujisikii kama una harufu ya marashi ya kike? Unanifanya mimi mtoto mdogo sio?"
Sam akaanza kujinusa ili aweze kusikia kama kweli ana harufu ya marashi ya kike, ila akakumbuka kuwa wakati Neema anamshukuru alimkumbatia na kupata jibu kuwa pengine marashi ya Neema yalibaki kwenye nguo yake.
Akamuangalia Sabrina bila ya kusema chochote, kisha Sabrina akamwambia,
"Umeona ulivyoduwaa, unajua makosa yako. Nipe simu yako, unadhani mi sijui mambo yenu"
Sam alichukua simu yake na kumpa Sabrina kwani alijua wazi hakuna lolote baya alilolifanya.
Sabrina aliishika ile simu huku akiwa bado na hasira ya wivu. Na muda huo huo kwenye ile simu ukaingia ujumbe na kumfanya Sabrina aufungue kwa haraka sana,
"Nashukuru kwa kumbatio lako mpenzi"
Sabrina alipomaliza kusoma huo ujumbe ndio akazidi kupatwa na hasira maradufu.
Akatamani hata aibwage chini ile simu, ila hakutaka kufanya maamuzi mabaya zaidi ya kumkabidhi Sam ile simu na kumwambia kwa hasira,
"Sam nakuomba uondoke nyumbani kwetu."
"Kwani kosa langu ni nini Sabrina?"
"Usinitibue Sam, nakuomba ondoka"
Sam hakumuelewa Sabrina kabisa na kwavile alikuwa hapendi shari, aliamua kujiondokea tu kwani Sam hakuwa mwanaume muongeaji.
Sam alipoondoka, Sabrina akajikuta akikaa chini na kulia sana huku akijilaumu kuolewa na Sam.
Uchungu ulimshika moyoni mwake kupita maelezo ya kawaida.
"Yani mimi, kwanini nimekubali kuolewa na Sam jamani? Mwanaume gani huyu? Halali na mimi ila analala na wanawake wengine, kama hanipendi si bora angeniambia tu. Mwanaume gani hata kubembeleza hajui? Yani anatambua kabisa kuwa anamakosa halafu anaondoka bila ya kunibembeleza. Kwanini mimi Sabrina mimi?"
Alilia sana huku akijigalagaza pale ndani.
Mara akasikia mtu akigonga mlango wa chumbani kwake, moja kwa moja akahisi kuwa ni Sam amerudi kumbembeleza, kisha akatabasamu kidogo na kuinuka ili akafungue mlango.
Alipofika mlangoni akanuna na kuvimbisha mdomo ili Sam ajue kuwa bado ana hasira na ambembeleze vizuri.
Ila alipofungua akakumbana na Jeff na kumshangaa,
"Kheee Jeff!!"
"Mbona umeshangaa hivyo? Najua hukutarajia ujio wangu"
"Na kweli sijakutarajia, haya karibu"
Jeff akaingia na kwenda kukaa moja kwa moja karibia na kitanda ambacho mtoto alikuwa amelazwa, kisha akamtazama yule mtoto na kumuangalia Sabrina.
Alifanya hivyo kama mara tatu na kumfanya Sabrina amuulize.
"Mbona unamuangalia mtoto na mimi mara zote?"
"Naangalia ni nani mwenye uhitaji wangu kwa muda huu kati yenu"
"Kivipi?"
"Nilikuwa nyumbani, gafla moyo ukaanza kuniuma sana halafu unaniambia nije huku kwenu, moja kwa moja nikatambua kuwa kati yenu kuna mmoja anauhitaji na mimi muda huu"
Sabrina alihisi kama damu ikitembea kwa kasi mwilini mwake kwa ujumbe wa Jeff.
Kisha akainuka na kusimama huku akigeukia mahali ambako Jeff alimuona mgongoni tu kwani hakutaka atazamane usoni na Jeff.
Kisha akamwambia,
"Najua umeshamtambua mwenye..."
Kabla hajamalizia, Jeff tayari alikuwa nyuma yake na kumkumbatia na kumfanya Sabrina ajikute akisisimka mwili mzima kwa kumbatio la Jeff.
Sabrina hakuendelea kuongea zaidi ya yeye kumkumbatia pia Jeff huku akijaribu kupunguza maumivu ya moyo wake.
Wakati wamekumbatiana, wazo likamjia tena kuwa Jeff ni mdogo sana kwake na kuamua kumuachia kisha yeye kwenda kukaa.
Jeff akamuangalia tena Sabrina na kumwambia,
"Nina ombi moja kwako"
"Ombi gani hilo?"
"Naomba kesho nipate muda kidogo nizungumze na wewe"
"Wapi?"
"Mahari pa utulivu ila sio hapa"
"Na mtoto je?"
"Tutamuacha sababu tutachukua muda mchache tu"
"Basi ngoja nifikirie halafu nitakupa jibu"
Jeff akatamani tena kumsogelea Sabrina ila kabla hajamsogelea akakumbuka kuwa kunamuda aliambia na mama yake kuwa Sabrina alimuita na alipofika ndio akakutana na yale majanga ya kufananishwa na mtoto.
Kwahiyo muda huu akaamua kumuuliza Sabrina ili amwambie kuwa ni kitu gani alimuitia,
"Hamna kitu ila nilikukumbuka tu"
Moyo wa Jeff ukajawa na furaha na kujikuta akimsogelea Sabrina kwa ujasiri zaidi na kumkumbatia.
Wakati kamkumbatia, mama wa Sabrina akaingia mule chumbani na kuwakuta,
"Eeeh nawaona mama na mwana mnaopendana"
Ile kauli ikawafanya kushtuka na kuachiana kwa aibu.
Sabrina akaamua kujichekesha pale ili kumfanya mama yake asiwe na maana ya ziada huku akijifanya kama anampa ujumbe Jeff,
"Sawa mwanangu Jeff, fanya kamavile nilivyokuagiza"
"Sawa mamy hakuna tatizo"
Kisha Jeff akajifanya kuaga pale na kuanza kuondoka.
Mama wa Sabrina akamuuliza,
"Kuniona mimi ndio unaondoka Jeff!"
Sabrina akaamua kujibu yeye,
"Hapana, alishaaga muda tu"
Kisha Jeff akaondoka na kumuacha Sabrina pale akizungumza na mama yake.
Sam alifika nyumbani kwake huku akijifikiria na kujiuliza,
"Ni kitu gani ambacho mwanaume unaweza kukifanya kumfurahisha mwanamke? Ni nini kitamfanya afurahie uwepo wako kila mara? Nampenda Sabrina, nahakikisha kila kitu anapata toka kwangu. Nimekuwa mwanaume wa pekee sana, mwaminifu nisiye na tamaa na wanawake wengine. Nimekubali kulea mimba isiyonihusu hadi mtoto nimechukua majukumu ya kumlea sababu tu ya upendo wangu kwa Sabrina. Nimemuoa, kila atakacho nampatia. Hivi nifanye nini tena aridhike huyu mwanamke!"
Sam aliwaza sana hadi kuhisi kichwa chake kikivurugika, na suluhisho pekee kwa wakati huo akaona ni bora akanywe pombe ili kupoteza mawazo yake.
Sabrina alikaa pale nyumbani kwao akitegemea kuwa labda Sam anaweza kupita pale mida ya usiku na kukiri makosa yake kwavile tayari angekuwa kashagundua kosa.
Ila usiku ulifika bila ya Sam kufika mahari pale na kumfanya Sabrina ahisi kuwa Sam amesusa.
Akajaribu kupiga simu ya Sam lakini iliita tu bila ya kupokelewa na mara ya mwisho akaambiwa kuwa haipatikani,
"Inamaana Sam ameamua kunizimia na simu kabisa!"
Moyo ukamuuma Sabrina aliona wazi kuwa Sam anamfanyia makusudi tu.
Akaamua kulala huku moyo wake ukiwa na maumivu ya kutosha.
Sam alipoenda kunywa, alijikuta akinywa sana hadi kulewa.
Akapita mdada aliyemfahamu Sam na kumkuta katika ile hali ya ulevi.
Akaamua kukaa nae karibu ili kumpa kampani asiboreke ingawa kalewa tayari.
Yule mdada akamuomba Sam kuwa amsaidie kumrudisha nyumbani kwake kwavile alikuwa na hali mbaya sana ya ulevi.
"Yani mchana ulikuwa vizuri tu Sam, muda huu kulewa hivyo hadi huruma"
Sam alikubali kupelekwa na yule dada kwavile walifahamiana na vilevile alishalewa kwahiyo asingeweza kuendesha.
Yule dada akapanda kwenye gari na Sam na kuanza kuendesha huku akifata maelekezo ya awali aliyopewa na Sam.
Wakati anaendesha simu ya Sam ikawa inaita, yule dada akaona ni usumbufu na kuamua kuizima kabisa hadi walipofika.
Na walipoingia ndani Sam hakutaka kulala, kwahiyo akafungulia mziki na kuanza kucheza pale sebleni.
Walicheza hadi kuchoka na mwisho wa siku wote wawili wakalala pale pale sebleni.
Kulipokucha, Sabrina akachukua simu yake na kumjaribisha tena Sam napo hakupatikana.
Sabrina akapatwa na uoga moyoni mwake kuwa pengine kuna jambo limempata Sam.
Kwahiyo akajiandaa na kumuaga mama yake kuwa anatoka kidogo na kumuacha mtoto na mama yake.
Mama yake hakutaka kumuhoji zaidi kwavile anamjua mwanae kama anapenda kuchukia kwa haraka, kwahiyo akamuacha aende tu.
Sabrina alifunga safari mpaka nyumbani kwa Sam.
Alipokuwa nje akasikia sauti ya mziki ikiimba.
Akampita mlinzi pale getini na kwenda ndani.
Kufika sebleni akamuona Sam amelala kwenye kochi na yule mwanamke akiwa juu yake.
Sabrina alifunga safari mpaka nyumbani kwa Sam.
Alipokuwa nje akasikia sauti ya mziki ikiimba.
Akampita mlinzi pale getini na kwenda ndani.
Kufika sebleni akamuona Sam amelala kwenye kochi
na yule mwanamke akiwa juu yake.
Sabrina akapatwa na hasira iliyopitiliza, kisha akaenda kwenye Friji na kuchukua maji yaliyokuwa kwenye jagi na kwenda kuwamwagia na kufanya washtuke kutokana na ubaridi wa yale maji.
Yule mwanamke ndio alishtuka zaidi baada ya kuona kuna mwanamke mbele yake.
Moja kwa moja, Sabrina bila ya kungoja neno toka kwa yeyote kati yao akaenda na kumkaba yule mwanamke hadi chini.
Muda huo Sam nae akiwa na uchovu wa usingizi na mlegezo wa pombe za usiku akaamua kwenda kuwagombelezea pale ila Sabrina alimpushi Sam na kumfanya aangukie upande wa pili kisha yeye akakazana kumkaba yule mwanamke.
Sam akaona bora amuite yule mlinzi wao ili awaamulizie.
Yule mlinzi kufika pale, akasimama kwanza akiwaangalia kisha akaenda kuwagombelezea kwavile aliona wazi itakavyoendelea lazima yule dada ataumizwa na Sabrina.
Alipomshika Sabrina, alimfanya Sabrina kuongea kwa hasira,
"Niache shetani wewe"
Ila yule mlinzi hakutaka kumuachia Sabrina kwani alijua wazi kikeendelea kitu kingine kwani Sabrina alikuwa na hasira sana.
Sam aliamua kumuamuru yule dada akimbie.
Yule mdada akatoka nje tu kwavile naye alikuwa na mlegezo wa pombe za jana yake, ikabidi Sam atoke nje na kumpa pesa ili akapande gari ya kukodi na kurudi nyumbani kwake kisha yule dada akaondoka.
Muda huo wote yule mlinzi alikuwa kamshikiria Sabrina ingawa alikuwa akihangaika nae kwavile Sabrina alitaka kuachiliwa.
Sam aliporudi ndani ndipo yule mlinzi alipomuachia Sabrina ambapo Sabrina alimfata Sam na kumnasa vibao vitatu mfululizo kisha akatoka nje kwa kukimbia.
Mlinzi akataka kumfata Sabrina ila Sam akamzuia kwani alijua wazi hasira za Sabrina zote zingeenda kumuishia yule mlinzi.
Sabrina alikuwa na hasira sana kwani yote yale aliyokuwa akiyawaza ameyaona kuwa ni kweli, kwahiyo akaamua kurudi kwao moja kwa moja ili kuepusha matatizo mengine ambayo yangeweza kumpata awapo njiani.
Ila wakati anarudi kwao, akiwa amesimama barabarani akasikia mtu akimuita nyuma yake,
"Sabrina"
Akageuka na kumuangalia, mtu huyo alikuwa ni Francis.
Sabrina akamtazama bila ya kwenda na kumfanya Francis amuite tena, hadi watu waliokuwa karibu yake wakamuangalia, mmoja wapo akamuuliza,
"Dada, si wewe ndiye unayeitwa?"
Sabrina kwa aibu akaamua kwenda alipo Francis.
Muda huo huo kabla hata hawajasalimiana likatokea tukio ambapo eneo lile lile alilokuwa amesimama Sabrina mwanzoni wakashuhudia kontena lililokuwa limebebwa juu ya lori likianguka pale na kuponda watu waliokuwa karibu.
Sabrina alijikuta akishika kichwa na kusema,
"Mungu wangu"
Eneo lile lilitapakaa damu tupu kwa muda mfupi.
Hata yule mtu aliyekuwa akimuuliza Sabrina kuwa anaitwa haendi hakuonekana kumbe alikuwa ameangukiwa na lile kontena.
Sabrina alipokumbuka hilo aliona machozi yakimtoka, Francis alimsogelea Sabrina na kumkumbatia kama kumfariji.
Sabrina alitokwa na machozi tu kwani alijikuta akifikiria mambo mengi sana, alifikiria kama ndio yeye angekuwa ameangukiwa na lile kontena pale, aliwaza hiyo khabari ingemfikia mama yake, akafikiria kuhusu mtoto wake na kujikuta akilia kwa uchungu sana na kumfanya Francis azidi kumbembeleze.
Francis hakutaka kuendelea kusimama eneo lile na Sabrina kwa ule uchungu aliomuona nao badala yake aliamua kukodi gari na kwenda naye sehemu nyingine.
Sam alitulia akijifikiria kuhusu Sabrina na kuona wazi kuwa amemkosea.
Akaona ni bora akamuombe msamaha kisha amuelezee vizuri jinsi ilivyokuwa.
Sam akaenda kuoga na kujiandaa kisha akaianza safari ya kwenda kwa wakina Sabrina.
Francis alifika mahali na kukaa na Sabrina ili kumfanya asipatwe na mawazo ila bado Sabrina alikuwa na uchungu na kumfanya Francis aone kuwa ni vyema ampeleke Sabrina nyumbani kwao akapumzike.
Sam alifika kwakina Sabrina na kumkuta mama mkwe wake akimbembeleza mtoto kwavile alikuwa akilia sana.
"Khee Sabrina yuko wapi mama?"
"Bado hajarudi, yani toka ameniaga asubuhi hadi saivi hajarudi na mtoto huku analia balaa"
Sam akajaribu kumchukua yeye mtoto na kumbembeleza ila bado mtoto hakunyamaza, ikabidi Sam amrudishe mtoto kwa mama mkwe wake, kisha akamwambia
"Ngoja nikajaribu kumuulizia kwa marafiki zake"
"Kwahiyo unaondoka?"
"Hapana ila natoka hapo nje ili nijaribu kuongea nao kwenye simu maana huyo Sabrina naona hata simu yake kaiacha humu"
Sam akatoka nje huku akijaribu kupekua namba za simu ili aangalie kama anaweza kupata namba ya mtu wa kumuuliza.
Akiwa pale nje akamuona Sabrina akiingia getini huku akiwa ameshikiliwa na Francis, akatamani hata kwenda kuwapokea ila akajua lazima Sabrina bado anakinyongo nae labda ndiomana kaenda kumfata yule kijana Francis.
Aliwaangalia tu hadi wakaingia ndani ingawa Sabrina hakumsalimia kabisa Sam lakini Francis alimsalimia na Sam akaitikia tu.
Moja kwa moja Sabrina akaenda kumchukua mtoto toka kwa mama yake na kujaribu kumtuliza kwa kumnyonyesha lakini bado mtoto alikazana kulia na hata kunyonya akakataa kwahiyo wote ndani wakawa wanahangaika namna ya kumbembeleza mtoto yule.
Muda kidogo akafika Jeff mule ndani na kuwakuta wakihangaika kumbembeleza mtoto, alimuona Sabrina akimbembeleza mwanae huku machozi yakimtoka kutokana na ajali aliyoiona.
Kila mmoja alikuwa akimshauri Sabrina anavyojua yeye, mama yake alimwambia,
"Nyamaza Sabrina ili mtoto nae atulie"
Ila Sabrina bado machozi yalimtoka tu.
Jeff akamsogelea Sabrina na mtoto, kisha akamuomba Sabrina ampatie yule mtoto.
Sam akadakia,
"Wote humu ndani tumeshindwa, ndio utaweza wewe kumbembeleza!"
Jeff hakuongeza neno kwani alingoja Sabrina ampatie yule mtoto.
Sabrina akakumbuka kauli ya jana ambayo Jeff aliiongea kuwa amefika kwavile kuna mmoja kati yao mwenye uhitaji na yeye.
Sabrina bila kinyongo akampa mtoto Jeff, sasa wote wakamtazama Jeff kuona atambembeleza vipi yule mtoto.
Jeff alipomchukua yule mtoto akaenda kukaa nae kitandani, kisha akamuangalia usoni kamavile anaongea nae bila hata kufungua mdomo ila muda huo huo yule mtoto naye akanyamaza na kutulia kisha Jeff akampa mtoto Sabrina na kumwambia,
"Mnyonyeshe mtoto"
Sabrina alimchukua na muda huu mtoto alinyonya bila ya matatizo yoyote.
Palikuwa na ukimya uliotawala ila Joy yani mama wa Sabrina ndiye aliyeukata ukimya ule,
"Naona damu ya Cherry na Jeff vimependana, yani katoto haka loh! Kamekataa kunyamaza kwetu wote eti kamenyamaza kwa Jeff"
Jeff akatabasamu tu, kisha akainuka na kuwaaga na kuondoka.
Sam nae akakaa huku akitafakari lile tukio kuwa linamaana gani, je lile tukio linamueleza nini? Hakupata jibu na kuona wazi kuwa akizidi kuwaza hayo basi ataiumiza akili yake kwa mawazo yasiyo na majibu.
Walipokuwa wamekaa ikabidi Francis awaelezee tukio ambalo limekuwa likimliza Sabrina muda aliorudi na kufanya wote kupata jibu kuwa kwanini Sabrina alikuwa akilia.
"Dah, kumuita kwako kumeokoa maisha ya mwanangu Sabrina hata sijui muda huu ningekuwaje mimi kama sio kuchanganyikiwa hapa jamani"
Sam nae akawa anamshukuru Francis kwa kumuokoa Sabrina,
"Hapana kaka, wakushukuriwa ni Mungu"
"Hata wewe pia Francis maana usingemuita Sabrina basi ingekuwa habari nyingine sasa"
"Ni kweli ila bado ni Mungu aliyefanya mimi niweze kumuita Sabrina mahari pale"
Wakaongea mambo mbali mbali kidogo, kisha mama wa Sabrina akauliza muda ambao ajali hiyo imetokea na kugundua kuwa ni muda huo huo ambao mtoto wa Sabrina alishtuka usingizini na kuanza kulia,
"Unajua hawa watoto ni malaika kwahiyo huwa wanaonyeshwa mambo mengi sana, ndiomana akaanza kulia ila kwavile sie wakubwa hatutambui ndiomana tukamshangaa tu na kuhangaika nae"
Sam akauliza,
"Mbona sasa hakutulia alivyomuona huyo mama yake kaja kutulia alivyomuona Jeff?"
"Unajua sisi hatukujua kuwa chanzo ni nini, tukawa tunambembeleza tu kwa njia zisizo sahihi. Huyu alitakiwa kubembelezwa kwa utaratibu kamavile alivyofanya Jeff"
Wote wakakubaliana na kilichosemwa na mama wa Sabrina.
Jeff akiwa nyumbani kwao, alijikuta akitafakari baadhi ya vitu ila alijipongeza kwa kuona kuwa mwanae amethamini uwepo wake na kutulia baada ya kumuona yeye.
"Kweli damu ni nzito kuliko maji, yule ni mwanangu tu hata wafanye vipi"
Alijikuta akiongea kwa sauti hayo maneno.
Mama yake akamsikia na kumuuliza,
"Jeff una mtoto?"
"Ndio ninae"
"Yani una mtoto kweli? Haya niambie umezaa na nani na huyo mtoto yuko wapi?"
Jeff akataka amueleze ukweli wa mambo yote mama yake kwa lile swali alilomuuliza ila alipotaka kumwambia akakumbuka kauli ya Sabrina kuwa alimuomba wafanye siri juu ya swala hilo na kuamua kujigelesha kwa mama yake.
"Hapana mama, sina mtoto nakutania tu"
"Mmh! Najua tu kuna kitu unanificha ila ipo siku nitagundua ukweli wote Jeff"
Kisha Sakina akaamua kwenda kufanya mambo yake mengine.
Sam alitulia mule ndani akingoja kuzungumza na Sabrina ili aweze kumuomba msamaha.
Sabrina alilitambua hilo na kumwambia Sam,
"Naomba uje badae, pale akili yangu itakapokuwa sawa ndio tuongee"
Kwavile Sam huwa hapendi kubishana na Sabrina, moja kwa moja aliinuka kisha kuondoka.
Pale ndani akabaki Francis ambaye naye aliamua kumuacha Sabrina apumzike na kumuaga ili kuondoka,
"Msalimie Fredy"
"Sawa nitamsalimia ingawa bado yupo hospitali"
"Vipi anaumwa?"
"Alipata ajali, kwahiyo bado yupo hospitali kwa matibabu"
"Ooh jamani mpe pole sana hata sikujua jamani, mpe pole sana"
"Usijali nitamwambia"
"Basi siku nikipata muda nitakuja kumuona"
Francis akakubaliana na Sabrina pale ili akiwa na muda ampigie simu ili aende kumchukua na kumpeleka huko hospitali.
Sam alirudi tena nyumbani kwake huku akiwa bado ametawaliwa na uchovu wa jana yake kwahiyo aliamua kwenda kulala moja kwa moja.
Akiwa amelala kwa usingizi mzito sana akashtuliwa na mlio wa simu yake na kumfanya aamke na kuipokea,
"Samahani nani mwenzangu?"
"Mimi Neema inamaana namba yangu hujaiandika jina hadi leo?"
Ile sauti na jina ikamfanya Sam ajue vizuri kuwa ni Neema gani na kuanza kumsikiliza kwa makini,
"Samahani nilikuwa nimelala"
"Yani Sam mkeo kaniumiza sana, shingo yote inauma hapa. Unajua alinikaba sana ile asubuhi"
"Pole sana Neema najua yote hayo ni makosa yangu mama"
Kitendo cha Sam kumbembeleza Neema na kumuita mama kilimpa nguvu ya ziada Neema na kumfanya kuongea kwa deko zaidi.
"Hata sijui nifanyaje na haya maumivu ya shingo Sam"
"Itabidi uende hospitali, ngoja nikutumie pesa kwenye simu yako ili uende hospitali"
Neema akamshukuru Sam pale, na muda huo huo Sam akamtumie Neema pesa kwenye simu yake kwaajili ya matibabu.
Baada ya Sam kumtumie Neema hiyo pesa, ukaingia ujumbe kwenye simu yake ukitokea kwa huyo Neema,
"Asante mpenzi kwa kunijali"
Sam akashtuka kuona Neema kamuita mpenzi na kumfanya acheke,
"Hawa wanawake bhana, kumsaidia kidogo tu eti kashanipa cheo cha upenzi tayari"
Alipokuwa anarudi nyuma kwenye jumbe zingine kwenye simu yake, akaona kuwa jumbe nyingi zikitokea kwenye hiyo namba ya Neema.
Sam akaamua kuzifungua na kuzisoma, akashtuka zaidi kwani karibia kila ujumbe uliotumwa na Neema kwenye simu yake ulionyesha kamavile ni watu waliokwenye mahusiano.
Akapata mashaka kuwa huenda Sabrina aliona zile meseji.
Aliamka pale kitandani na kuvaa tena na kuanza safari ya kwenda kwakina Sabrina kutatua lile tatizo,
"Safari hii sitaondoka hadi nihakikishe kuwa Sabrina amenielewa vya kutosha"
Sam sasa alikuwa akielekea kwakina Sabrina.
Jeff aliamua kwenda kwakina Sabrina pia kwavile jana yake alimuahidi kuwa watatoka nae kwa maongezi mafupi.
Jeff alimkuta ndani Sabrina kama kawaida, kisha akaenda kukaa kwenye kitanda karibu na mtoto.
Sabrina akamtania Jeff,
"Mzee wa kuotea, karibu sana"
Jeff akacheka, kisha Sabrina akamuuliza,
"Hivi ulijuaje kama mtoto analia huku muda ule?"
"Unajua nini?"
"Niambie, mi sijui"
"Mtoto wetu ni mzuri sana Sabrina na....."
Muda huo Sam nae alikuwa ameingia mule ndani na kuuliza kwa mshangao,
"Mtoto wenu?!"
"Mzee wa kuotea, karibu sana"
Jeff akacheka, kisha Sabrina akamuuliza,
"Hivi ulijuaje kama mtoto analia huku muda ule?"
"Unajua nini?"
"Niambie, mi sijui"
"Mtoto wetu ni mzuri sana Sabrina na....."
Muda huo Sam nae alikuwa ameingia mule ndani na
kuuliza kwa mshangao,
"Mtoto wenu?!"
Walikaa kimya wakimuangalia Sam, kisha akawauliza tena,
"Mtoto wenu kivipi?"
Sabrina akaanza kutafuta namna ya kujitetea bila ya kujua anajitetea vipi.
Jeff naye hakujua wajitetee kwa namna ipi na kufanya wazidi kukaa kimya.
Sam akawaangalia kwa zamu, kisha akamuangalia Jeff peke yake na kumwambia,
"Naomba uende, nataka kuongea na mke wangu."
Jeff akainuka na kumuangalia Sabrina, akawa kama anampa ishara kisha akaondoka bila ya kusema chochote cha ziada.
Sam akakaa sasa palepale alipokuwa amekaa Jeff mwanzoni, kisha akamuangalia Sabrina machoni na kumkabidhi simu yake.
Sabrina akamuuliza,
"Unanikabidhi simu yako ya nini?"
"Inamaana leo hutaki kuangalia simu yangu?"
"Niangalie ili iweje?"
"Kuuliza maswali Sabrina unajua sana ila kujibu unayoulizwa wewe ni ngumu. Sasa nataka uniulize maswali yote yaliyokutatiza kwenye hiyo simu yangu nami nitayajibu"
Sabrina akamuangalia Sam na kumuuliza tena,
"Kwanini umeamua hivi?"
"Nataka uridhike Sabrina, ulinìukumu kitu ambacho sikifahamu ndiomana nimekuja uniulize maswali nikujibu na kama hutoridhika basi nifanye chochote unachoona kuwa kitakuridhisha"
"Haya niambie, huyu mwanamke anayekutumiaga ujumbe wa kimapenzi anaitwa nani?"
"Anaitwa Neema"
"Na yule niliyekukuta nae ndani mkifanya mapenzi anaitwa nani?"
"Hapana Sabrina hatukuwa kufanya hivyo, ni huyo huyo Neema ila sina mahusiano na huyo mwanamke"
Ilikuwa ngumu kwa Sabrina kumuelewa Sam moja kwa moja ikabidi Sam amueleze Sabrina kuhusu pia hali ya Fredy na kufanya Sabrina apatwe na moyo wa huruma kwa Fredy na kusahau mambo yake.
Ila Sam alizidi kumsisitiza Sabrina kuwa hana mahusiano yoyote yale na yule mwanamke.
"Hata kufahamiana nae kwa mara ya kwanza ilikuwa ni ajali tu hata nashangaa anavyotuma jumbe za kimapenzi"
"Na hata kulala nae itakuwa ajali hivyo hivyo na utajishangaa na wewe mwenyewe ukimuita mpenzi"
"Hapana Sabrina, usinifikirie vibaya mke wangu"
Sabrina akakaa kimya kwanza na kuwa kamavile mtu aliyemuelewa kisha akaonekana kama mwenye mawazo ingawa Sam hakujua kuwa anawaza kitu gani.
Kisha ikawa kamavile anamshtua kwenye yale mawazo kwa kumwambia,
"Badae naomba tutoke kidogo mke wangu, tafadhari usiseme hapana. Nakuomba Sabrina"
Sabrina hakujua kama akubali au akatae ila akaamua kukataa kwavile alikumbuka kuwa Jeff alimwambia kuwa anahitaji kufanya mazungumzo na yeye.
"Hapana sitaweza Sam, siwezi kutoka na mwanangu na pia siwezi kutoka na kumuacha mwanangu"
"Mbona asubuhi ulikuja nyumbani bila mtoto? Hata hivyo muda huo mtoto atakuwa amelala"
"Tena usitake kunikumbusha yaliyopita Sam, tafadhari sana. Nishakwambia siwezi basi nielewe kwa hilo"
Sam hakutaka kumlazimisha zaidi ili kuepusha shari, kwahiyo akamuaga kuwa anaondoka.
Sabrina akamuuliza Sam ili kujiridhisha kabla hajaondoka.
"Kwahiyo ndio mpaka kesho?"
"Ndio mpaka kesho"
Kisha akamuaga tena na kuondoka.
Sam akiwa njiani kwenye gari yake, mawazo yakamjia kuhusu Sabrina na Jeff.
Aliona wazi kuwa hisia zake huenda kuwa ni za kweli,
"Ila huyu Sabrina anawezaje kutembea na kijana mdogo kiasi kile kama Jeff!! Anawezaje Sabrina jamani?"
Sam alikuwa akijiuliza huku akitafakari majibu ya maswali yake.
Akataka kwenda nyumbani kwake moja kwa moja ila aliona ni vyema apitie hotelini kula ndipo aelekee nyumbani kwake.
Na alipomaliza kula akapata wazo la kurudi tena kwakina Sabrina kuwa akamuone japo kidogo tu kwa usiku huo halafu ndio arudi kwake kulala.
Sabrina alipoona kuwa Sam ametoka, akaamua kujiandaa kwa haraka ili akaonane na Jeff kwani alitamani sana kujua kuwa Jeff anataka kuongea nae kitu gani.
Alipomaliza kujiandaa na kila kitu, akamuachia maagizo mama yake kisha akawasiliana na Jeff mahari pa kukutana nae. Kisha Sabrina akaondoka pale kwao na kwenda mahari alikopanga kuonana na Jeff.
Sabrina alifika mahari pale na kumkuta kuwa Jeff alishafika muda mrefu tu.
Jeff alipomuona Sabrina, moja kwa moja alienda kumkumbatia na kwavile ilikuwa ni usiku kwahiyo akaona kuwa hakuna tatizo lolote.
Sabrina alikuwa ametulia tu mpaka pale Jeff alipomvutia kiti na kukaa.
"Sabrina, wewe ni mwanamke mrembo sana"
"Ushaanza maneno yako Jeff"
Jeff akamuangalia Sabrina na kutabasamu na kumfanya Sabrina aongee tena,
"Ongea maneno ambayo umeniitia Jeff si unajua mtoto yupo nyumbani na bibi yake tu."
Jeff akasogeza kiti chake kidogo kwenye upande wa Sabrina na kufanya wawe karibu zaidi.
"Niambie basi Jeff"
"Kwanza kabisa napenda uwepo wako, nasikia raha sana kuwa karibu yako. Kwakweli nakupenda Sabrina tena nakupenda sana"
Moyo wa Sabrina ulijikuta ukifurahia na kufanya hata yeye binafsi kufurahia alichoambiwa na Jeff, na kumfanya aendelee kumsikiliza kwa umakini.
"Natamani kama mimi ndio ningekuwa na uwezo wa kuwa mume wako, kwakweli nisingekusariti maisha yote"
Sabrina akamuuliza Jeff,
"Unamaana gani kusema hivyo? Inamaana unawanawake wengi kwasasa?"
"Hapana, ila nimekuita hapa kama kukuomba ushauri tu. Sababu nimekuwa kijana nisiyejielewa kabisa, najua siwezi kuwa na wewe Sabrina kwavile tayari wewe ni mke wa mtu na pia huwezi kunikubali sababu ya umri wangu. Ila hata mimi siwezi kuwa na mwanamke yoyote yule zaidi yako na hili ndio tatizo kwangu"
Jeff akaishia hapo huku akingoja jibu ambalo atapewa na Sabrina ila Sabrina nae alimuangalia Jeff bila ya kumwambia chochote.
Jeff akachukua mkono wa Sabrina na kumshika kiganjani mwake, huku akimuangalia kama atasema chochote ila Sabrina hakusema kitu na kuutoa mkono wake kwa Jeff na hapo akaongea sasa,
"Tafadhari Jeff naomba tuondoke maana muda umeenda, hata mtoto anaweza kushtuka muda huu halafu mama asijue cha kufanya"
"Sasa mbona hujanipa ushauri wowote Sabrina? Tafadhari, niambie chochote cha kufanya ili moyo wangu uridhike"
"Tafuta msichana wa saizi yako uwe naye"
"Siwezi Sabrina siwezi"
"Kwanini usiweze?"
"Sababu nakupenda wewe, nakupenda sana"
Kila aliposikia hili neno nakupenda toka kwa Jeff alihisi kusisimka sana na kumfanya hata atamani kutoa maamuzi ila akimfikiria Sam na jinsi anavyompenda na kumjali anabaki kimya na kushindwa kusema chochote kwa Jeff.
Kisha Sabrina akainuka kama ishara ya kutaka kuondoka, Jeff nae akainuka na kwenda kusimama mbele yake, kisha akamshika viganja vya mikono yake na kumwambia,
"Niangalie machoni Sabrina"
Sabrina akamuangalia kidogo Jeff na kushusha macho yake kwavile kila anapomuangalia sana aliona wazi hisia za kimapenzi zikijaa na kwake pia.
Jeff akamwambia tena,
"Najua hata wewe wanipenda ila huna uhakika na hisia zako, mimi ni mwanaume sahihi kwako Sabrina. Nipo tayari kwa chochote ila si kukupoteza wewe. Tafadhari ona uwepo wangu kwako, angalia thamani yangu na mimi juu yako."
Sabrina akaangalia pembeni na kumwambia Jeff,
"Ila mimi naona ni vyema ukasome tu Jeff, tena utapata tu msichana wa rika lako na utampenda. Naomba mimi niende"
Sabrina akajitoa tena kwa Jeff na kumfanya Jeff aanze kumfata nyuma nyuma.
Sam alifika nyumbani kwakina Sabrina ili kuweza kumuaga kama alivyopanga hapo awali.
Ila alimkuta mama wa Sabrina tu bila ya Sabrina mwenyewe kuwepo.
"Kwani Sabrina yuko wapi mama?"
"Kwajinsi alivyoniaga nikajua amekuja kuonana na wewe. Vipi tena mbona wewe nakuona hapa?"
"Ilikuwa hivi mama, nilimwambia Sabrina kuwa badae tutoke kidogo akakataa kwa madai kuwa hawezi kumuacha mtoto na hawezi kutoka nae. Ndiomana mi nimerudi muda huu ili niwaage kuwa naenda kulala"
"Huwezi jua, labda alibadilisha maamuzi badae na kuona kuwa ni vyema aje muongee maana mi kaniaga kuwa anaenda kuonana na baba mtoto wake ambaye najua wazi ni wewe"
Sam kengele ya hatari ikagonga kwenye kichwa chake, kisha akamuaga pale mama wa Sabrina,
"Nitarudi badae kidogo, ngoja nikamuangalie mahali labda ameenda bila ya mimi kujua"
"Sawa mwanangu"
Kisha Sam akaondoka zake.
Moja kwa moja Sama akaenda hadi nyumbani kwa Sakina ili kumuulizia Jeff kwani aliona wazi akichezewa mchezo mchafu.
Alimkuta Sakina akiwa ametulia ndani kwake huku akiangalia kipindi kwenye luninga.
Ambapo Sakina alimkaribisha Sam vizuri sana, naye Sam akaingia na kukaa kisha akaanza kumuuliza,
"Samahani, nina shida na Jeff"
"Mmh Jeff alikuwa na harakati leo, jioni tu nimemuona akitoka hapa na bado hajarudi. Nahisi ameenda kwa wanawake zake watu wazima huko"
Sam akacheka kidogo na kuuliza,
"Wanawake watu wazima? Ndio wakina nani?"
"Mjini wanawaita masugar mamy maana mtoto wangu hata hasikii siku hizi, shule hataki wala chochote kile anawataka hao hao watu wazima tu. Namshangaa hata pesa anatoa wapi, najua wanamuhonga huko. Mwanangu kaharibikiwa kwakweli, naona hata Sabrina kashindwa kumrekebisha. Basi siku hizi namuangalia tu"
"Basi na mimi ngoja nijaribu kumrekebisha, yani mtoto mdogo kama yule awe na watu wazima! Kwanza ni aibu tena aibu sana, anaishusha thamani yake. Anaharibu maisha yake, mimi sisapoti huo upumbavu hata kidogo na nitakusaidia kumnyoosha"
"Utakuwa umenisaidia sana shemeji yangu, yani napata shida kwakweli. Najua Sabrina hawezi kwasasa kwani majukumu mengi na ya mtoto nayo yamezidi"
"Usijali, Jeff atanyooka tu shemeji"
Kisha Sam akamuaga Sakina naye Sakina akamshukuru sana Sam kwa ushauri wake aliompatia.
Halafu Sam akaondoka zake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akarudi kwakina Sabrina ila hakuingia ndani, bali alikaa pale nje akisubiri kuwa Sabrina ataletwa na nani na ataletwa muda gani.
"Yani Sabrina ananifanya mimi mtoto mdogo kwa kuniambia kuwa alibakwa. Hivi mtu aliyebakwa anawezaje kumjua baba wa mtoto wake? Na huyu Jeff leo nitamfundisha adabu maana siku zote huwa namchekea tu"
Sam alikuwa na hasira sana ukizingatia upendo ambao alikuwa nao kwa Sabrina ulikuwa ni mkubwa sana.
Sabrina alifika mbele na kuona gari ya kukodi akaisimamisha na kuingia mlango wa nyuma, wakati huo huo Jeff nae akaingia mlango wa nyuma.
Sabrina hakuwa na cha kusema zaidi ya kumwambia dereva kuwa aondoe gari ingawa alikuwa tayari amekaa kiti kimoja na Jeff.
Muda huu Jeff bado alikuwa akimtazama Sabrina huku lile gari likienda mahari ampapo dereva ameelekezwa.
Jeff alikuwa akimwambia Sabrina kamavile maneno ya kumnong'oneza,
"Tafadhari Sabrina, naomba nielewe nakuomba. Nisikie tafadhari napata shida sana"
Sabrina hakumjibu kitu, kisha Jeff akachukua mkono wake na kuuweka kwenye bega la Sabrina, hapo akafanya Sabrina ashindwe kumtoa mkono ule kwani aliona wazi kuwa utakuwa ni usumbufu kwa dereva kwani anaweza kuhisi kuwa watu hao wanaugomvi.
"Nakuomba Sabrina nionee huruma, napata shida sana. Nateswa na mapenzi niliyonayo juu yako. Nihurumie tafadhari"
Sabrina bado hakujibu kitu chochote.
Dereva naye alipofika pale alipoelekezwa akasimama na kuwaambia kuwa wameshafika.
Kabla Sabrina hajashuka, akampa yule dereva pesa yake ila muda huo Jeff naye alimuomba kuwa ambusu kwanza ndipo washuke.
Sabrina akakubali ili kumaliza shari, wakati Jeff anambusu Sabrina akashangaa kuona mlango wa nyuma wa lile gari ukifunguliwa kwa nje, na mtu aliyefungua mlango ule moja kwa moja akamvuta Jeff kwa nje.
Naye alipomtazama alikuwa ni Sam, na kabla hajafanya chochote, Jeff alishtukia akipigwa ngumi ya sura iliyompeleka hadi chini.
Naye alipomtazama alikuwa ni Sam, na kabla
hajafanya chochote, Jeff alishtukia akipigwa ngumi
ya sura iliyompeleka hadi chini.
Jeff hakuwa na utetezi wowote kwani Sam aliinama pale chini na kuzidi kumshindilia Jeff ngumi.
Yule dereva taxi kuona vile naye akaondoa gari yake akihofia kuhamishiwa yeye ule ugomvi.
Sabrina akajaribu kuamulizia lakini akashindwa, akaamua kukimbilia ndani kwao ili akamuite mama yake.
Ila kabla hajaingia ndani kwao, Sam akamvuta kwa nyuma Sabrina kisha akamwambia,
"Usimwambie chochote mama yako, Jeff nitampeleka mwenyewe nyumbani kwao"
Sabrina alikuwa akitetemeka tu kwa uoga kwani aliona wazi kuwa mambo yameharibika kwa pale.
Kisha Sam akamuinua Jeff pale chini huku akiwa ameumia vya kutosha tu na kuanza kuondoka naye huku akiongea naye kumpeleka kwao.
Alipokaribia nyumbani kwakina Jeff akamwambia,
"Nenda kwenu, mwambie mamako kuwa umefumaniwa leo na kupigwa ila usiseme kama ni mimi"
Kisha akamsukumia huko.
Wakati Jeff anapepesu ka, akamshika tena mkono na kwenda kugonga mlango wao ambapo Sakina alienda kufungua ule mlango na kufanya Sam aingie moja kwa moja ndani akiwa na Jeff.
Sakina akashtuka sana,
"Vipi tena? Nini kimempata mwanangu jamani?"
"Nimemkuta njiani kaumia hivyo nikaamua kumleta"
"Kwani kafanyaje jamani?"
"Eti kafumaniwa na mke wa mtu ndivyo alivyonieleza"
"Maskini mwanangu jamani, Jeff baba si unaona mwanangu? Nimekukataza mara ngapi hayo mambo jamani? Ona sasa ulivyoumizwa"
Sakina aliongea huku machozi yakimtoka ila Jeff hakuongea chochote kile zaidi ya kutazama chini tu, kisha akainuka na kwenda chumbani kwake, naye Sam alimuaga Sakina na kuondoka.
Sam akarudi kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina pale pale nje akitetemeka kwani alijua wazi kuwa ameshaumbuka kuhusu Jeff. Sam akamshika mkono Sabrina na kuingia nae ndani kwao ambapo alimkuta mama yake akiwa ameshikilia mtoto wao,
"Ulimpata Sabrina kumbe"
Sam akajibu,
"Ndio mama, kumbe Sabrina alikuwa akiningoja. Nimemkalisha sana pale mke wangu hadi nimemuonea huruma"
Mama wa Sabrina alikuwa akitabasamu tu kwani aliona kuwa Sabrina amepata mume bora kuliko watu wote ulimwenguni.
Ila Sabrina hakuongea chochote zaidi ya kumchukua mtoto wake kutoka kwa mama yake na kwenda naye chumbani kwake ambapo Sam naye aliingia na kumuaga Sabrina ambaye aliitikia kwa kichwa tu, kisha Sam akaondoka zake.
Sabrina hakuweza kulala usiku wa siku hiyo kwani alijikuta akitafakari tu namna ilivyo kati yake yeye na Jeff, alikuwa akiwaza kuwa siri ikibumbuluka aibu itakuwa ya nani? Aliona wazi kuwa aibu ni juu yake, atawezaje kumtazama Sakina ambaye ameishi naye siku zote kama dada yake wa damu.
Atawezaje kuwatazama watu wanaotambua ukaribu wa yeye na Jeff kuwa ni kama ndugu.
Sabrina alijiona yupo kwenye dimbwi la mawazo huku akiombea hii aibu isibumbuluke miongoni mwa watu wanaowa zunguka.
Wakati huo Sam nae alikuwa nyumbani kwake akitafakari namna ya kuwaweka mbali mbali Sabrina na Jeff,
"Sitaweza kukubali kwakweli, tena nakataa kabisa. Bora hata ningemfumania na mwanaume mwingine ila sio kale katoto ka Jeff. Siku zote nimekuwa nikipata hisia mbaya juu yao ila leo nimejionea kwa macho yangu. Kwakweli moyo umeniuma sana. Lazima nifanye kitu hata kwa gharama zozote zile"
Sam naye hakuweza kupata usingizi kwani mawazo yalimtawala sana.
Kulipokucha, Sam aliamka na kufunga safari hadi nyumbani kwa Sakina ambapo alifunguliwa mlango na Sakina mwenyewe.
"Eeh Jeff anaendeleaje?"
"Naona anaendelea vizuri, asante kwa kuijali hali ya mwanangu"
"Usijali shemeji, ila nimepata wazo la kumsaidia Jeff"
"Wazo gani hilo?"
"Kwanini Jeff tusimpeleke nchi za nje aende akasome? Tutakuwa tumemsaidia sana kwani kule atasoma vizuri"
"Wazo lako ni zuri shemeji, ila tatizo pesa. Yani sina uwezo huo kabisa. Mume mwenyewe alishanikimbia kitambo, kila kitu nafanya mwenyewe tu"
"Usijali kuhusu hilo shemeji kwani najitolea kwa gharama zote, ila tu mwambie mwenyewe akubali kwanza"
Kwakweli Sakina alifurahi sana, akatamani hata ambebe Sam juu juu kwa furaha aliyokuwa nayo,
"Jamani shemeji asante sana, nashukuru jamani. Jeff hawezi kukataa kabisa, kwanza anakataaje ofa kama hiyo, asante sana shemeji."
Sam hakutaka kupoteza muda pale badala yake akaaga na kuondoka.
Sakina alimuita Jeff na kumwambia zile khabari ambapo Jeff mwenyewe alionekana kutokufurahishwa nazo hata kidogo na hakumpa jibu lolote mama yake zaidi ya kurudi tena chumbani kwake.
Sam alienda kwakina Sabrina sasa kwa lengo la kumwambia kuhusu ofa aliyompa Jeff.
Alimkuta Sabrina chumbani kwake akiwa kajiinamia tu, akamshtua kwa salamu kisha akamueleza kuhusu ofa aliyompa Jeff.
Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Samahani Sam, nina ombi moja tu kwako kwa muda huu"
"Ombi gani hilo?"
"Naomba uniruhusu kuzungumza na Jeff kwani najua wazi kuwa hawezi kukubaliana na ofa yako. Tafadhari Sam naomba uniruhusu kuzungumza na Jeff"
"Unataka kwenda kuzungumza nae wapi?"
"Popote pale kwenye utulivu kwani najua wazi kuwa mimi ni mtu pekee ninayeweza kumshawishi juu ya hilo"
"Ngoja basi nitafikiria kuhusu hilo na nitakupa jibu"
Kisha muda huo huo Sam akamuaga Sabrina na kuondoka zake.
Jeff alikaa chumbani kwake na kufikiria sana, akajua wazi kuwa anafanyiwa vile ili kutenganishwa na Sabrina,
"Kwanini mimi wananifanyia hivi? Sababu ni umri kweli au kwavile sina pesa basi mwenye pesa anafanya chochote anachotaka. Kwani umri kwenye mapenzi unaingiaje? Mbona kuna wazee wanawapenda mabinti wadogo hadi wanawaoa ila watu hawasemi, ila mimi kumpenda mwanamke anayenizidi ndio tatizo. Kwanini duniani hakuna haki jamani, sina raha mimi nanyang'anywa nyama mdomoni huku naangalia! Kwakweli haiwezekani lazima na mimi nipambane"
Jeff alijiwazia kwani aliona kamavile anaonewa tu siku zote.
Mchana wa siku hiyo Sabrina akampigia simu Francis ili aende kumfata na waweze kwenda hospitali kumuona Fredy.
Francis alipofika, Sabrina akamuaga mama yake na kuondoka.
Walienda moja kwa moja mpaka hospitali aliyolazwa Fredy,
"Kwakweli Fredy atafurahi sana kukuona Sabrina"
"Ndiomana nimeona ni vyema nije kumuona, kwakweli sikujua kama amepata ajali. Nilishtuka sana nilipoambiwa."
Wakaenda moja kwa moja mpaka wodini, ambapo walimuona Fredy akiwa amekaa leo kuonyesha kwamba ameanza kupona.
Sabrina alimsogelea na kumkumbatia pale kitandani,
"Pole sana Fredy"
"Asante Sabrina, asante kwa kuja kuniona"
"Sikujua kama umepata ajali Fredy jamani, pole sana"
Fredy akaanza kumueleza Sabrina ilivyokuwa na jinsi ambavyo Sam alimsaidia, na kufanya Francis naye achangie hapo,
"Yani huwezi amini, ila Sam tulikuwa naye hapa usiku kucha siku hiyo tukiangalia hali ya Fredy tu, kwakweli ametusaidia sana"
Sabrina akatabasamu kuhusu hilo kwani akaona wazi kuwa mawazo yake juu ya Sam siku hiyo yalikuwa ni batili.
Muda kidogo wakati wapo pale, akawasili Neema naye alifika kwa lengo la kumuangalia Fredy.
Neema na Sabrina walijikuta wakitazamana kwa dakika kadhaa, mpaka pale Francis alipoamua kuwatambulisha.
"Huyu ni rafiki yetu anaitwa Sabrina, na huyu ni dada yetu anaitwa Neema"
Neema akanyoosha mkono kumpa Sabrina kama ishara ya kufahamiana, ila Sabrina hakupokea mkono ule badala yake akaaga na kuanza kuondoka ambapo Francis aliamua kumfata nyuma ili kumsindikiza.
Neema akaamua kujigelesha kwa Fredy kwa kumuuliza,
"Kwani huyo dada anamatatizo gani? Mbona yupo vile hata kusalimiana hataki?"
"Aaah yule huwa anajielewa mwenyewe hata asikuumize kichwa dada yangu"
Bila ya kujua kuwa Neema ana siri yake moyoni.
Sabrina alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake kama kawaida ambapo alikaa nae na kumsema.
"Mwanangu Sabrina, mwanao bado mdogo si vizuri wewe kutoka toka mara kwa mara maana siku hizi umeshafanya kama kamchezo mwanangu jamani. Nakuomba kama mama yako hayo mambo ya kutoka toka uache. Kaa nyumbani hapa ulee mtoto wako mwanangu"
Sabrina akamuitikia mama yake na kujiona wazi kuwa anafanya makosa kwavile anaondoka mara kwa mara na kumuacha mtoto wake mdogo ndani.
Kwahiyo akamuahidi mama yake kuwa atajitahidi kutokutoka toka hovyo.
Sakina alimuita tena Jeff ila bado Jeff hakumpa jibu lolote mama yake na kumfanya azidi kupatwa na mawazo.
Sakina nae akafikiria na kuona kuwa mtu pekee wa kuweza kuongea na Jeff hadi akubali ni Sabrina tu kwahiyo akapanga kesho yake kwenda kuongea na Sabrina kuhusu jambo hilo.
Usiku ulipofika, Sam kama kawaida akaenda kwa wakina Sabrina kuangalia familia yake.
Alimkuta Sabrina akiwa tayari amelala kutokana na uchovu aliokuwa nao kwahiyo Sam aliamua kuondoka bila ya kusema naye kitu chochote kile.
Kulipokucha kama kawaida, Sam alifika pale nyumbani kwakina Sabrina.
"Kheee kamavile umelala hapa hapa!"
Sabrina alimshangaa Sam na kumfanya Sam atabasamu na kusema,
"Hii yote ni mapenzi yangu kwako, kwavile jana sikuweza kuzungumza na wewe ndiomana leo nimewahi ili nizungumze na wewe japo kidogo kabla ya kwenda kazini"
"Haya nashukuru na nipo tayari kukusikiliza"
"Leo nina maombi mawili kwako"
"Yapi hayo?"
"La kwanza, nakuomba mwezi ujao tukakae nyumbani kwetu na mtoto wetu kwani namuona kuwa amechangamka kwa sasa. Sawa Sabrina?"
"Sawa nimekuelewa, eeh la pili!"
"La pili, sitaki uende kuzungumza na Jeff. Nitazungumza nae mwenyewe kwa muda wangu. Tafadhari Sabrina usiende nae popote kwa mazungumzo yoyote yale"
Sabrina akahema kiasi kisha akamuitikia Sam kuwa amekubaliana nae kwani alijua wazi kumkatalia ni kuzua mzozo mwingine usiokuwa na maana yoyote ile.
Kisha Sam akamuaga Sabrina na kuondoka.
Sabrina aliendelea na mambo yake mengine kama kawaida, muda kidogo akafika Sakina na kumsalimia.
Kisha akamueleza lengo la Sam kwa Jeff,
"Kwakweli shemeji ana lengo zuri sana juu ya mtoto wetu huyu. Tatizo lipo kwa Jeff tu, hataki hata kunisikia kuhusu swala hili, hataki hata kuelewa"
"Sasa tutafanyaje dada?"
"Ndiomana nimekufata wewe Sabrina kwavile natambua wazi kuwa mwanangu Jeff hakuna mtu anayemsikiliza kama wewe. Nakuomba Sabrina ukaongee na Jeff, tafadhari sana nakuomba"
Sabrina akafikiria, akakumbuka alichoambiwa na Sam muda mfupi uliopita, pia akawaza kuwa anawezaje kumkatalia Sakina wakati amemfata hadi pale sababu tu anamuamini, anawezaje kukataa kuwa hawezi kwenda? Akawa njiapanda.
"Basi dada nitakuja badae"
"Tafadhari Sana Sabrina, naamini kweli utakuja mdogo wangu"
Kisha Sakina akamuaga pale Sabrina na kuondoka.
Muda ulipita bila ya Sakina kumuona Sabrina akienda pale kwake.
Akaona ni vyema amfate tena na ikiwezekana basi aende nae kabisa.
Akaenda tena kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina akiwa hana hata khabari, Sakina akaamua kumuomba tena Sabrina ili akazungumze na Jeff,
"Yani leo toka asubuhi hajala chochote, najua akizungumza na wewe kwavile anakuelewa sana atarudi kwenye hali yake ya kawaida"
Sabrina moyo wa huruma ukamuingia na kuamua kumuaga mama yake kidogo kisha kutoka na Sakina kuelekea huko nyumbani kwa Sakina.
Sam nae alitoka ofisini kwa lengo la kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Sakina ili akaongee na Jeff kuhusu ofa yake aliyompa.
"Lazima akubali, lazima aende akasome huko nipunguze mzigo wa mawazo"
Akaingia kwenye gari na safari yake ilikuwa moja kwa moja nyumbani kwa Sakina.
Sabrina alifika pale na kukaa sebleni, moja kwa moja Sakina akaenda chumbani kwa Jeff ili kumuita aweze kuzungumza na Sabrina.
Alimkuta Jeff kajilaza kitandani tu,
"Tafadhari mwanangu, Sabrina yupo sebleni anahitaji kuzungumza na wewe"
"Mwambie aje huku chumbani, mi sebleni siji"
Basi Sakina akatoka na kumfata Sabrina sebleni na kumuomba kuwa akazungumze na Jeff chumbani, Sabrina nae hakutaka kusita ili kumuondoa wasiwasi Sakina.
Akainuka na kuongozana na Sakina hadi chumbani kwa Jeff,
"Jeff mwanangu, Sabrina huyu hapa atazungumza na wewe. Mi naenda kukuandalia chakula baba yangu"
Kisha Sakina akatoka nje ya chumba cha Jeff.
Muda huo Sabrina alikuwa amesimama tu akimtazama Jeff pale kitandani.
Jeff akainuka, moja kwa moja akaenda mlangoni na kufunga mlango kwa funguo na komeo kisha akarudi alipo Sabrina.
Akamuangalia kwa sekunde tano na kumkumbatia kwa nguvu sana.
Sam alifika kwa Sakina na kumkuta Sakina sebleni ambapo alimkaribisha vizuri sana,
"Karibu shemeji"
"Nimekuja ndio nataka kuzungumza na Jeff"
"Sawa subiri, ngoja nikamuite"
Sakina akainuka hadi mlango wa Jeff, akataka kufungua ili aingie ndani. Akashangaa kuona ni mgumu na kugundua kuwa umefungwa kwa ndani.
Akajiuliza kuwa kwanini mlango ufungwe.
Sakina akainuka hadi mlango wa Jeff, akataka
kufungua ili aingie ndani. Akashangaa kuona ni
mgumu na kugundua kuwa umefungwa kwa ndani.
Akajiuliza kuwa kwanini mlango ufungwe.
Sakina akasimama pale mlangoni kama dakika tano hivi akijaribu kujiuliza kinachoendelea mule ndani, ila hakuweka hisia mbaya kwavile anajua ni jinsi gani Jeff na Sabrina wanavyoheshimiana.
Akajaribu kusukuma ule mlango tena ila hakuona dalili yoyote ya kufunguliwa kwa ule mlango, akajaribu kumuita Jeff ila hakuitika.
Akaamua kumwambia Jeff pale pale mlangoni,
"Jeff, Mr.Sam anakungoja sebleni"
Ila bado hakujibiwa, ikabidi arudi sebleni huku akifikiria jibu la kumpa Sam.
Alimkuta Sam amekaa pale pale,
"Shemeji samahani, nilijua Jeff yupo ila kumbe ametoka kidogo"
"Kwani kaenda wapi?"
"Hata sijui, labda akirudi badae nitamwambia akufate"
"Hapana, mi ninahitaji kuongea nae leo. Ngoja tu nimsubiri kidogo"
Sakina akajiona kuwa ataonekana kuwa muongo kama Jeff atatokea pale sebleni.
Akaanza kufikiria maneno mengine ya kumwambia Sam ili aweze kumuelewa kuwa anamaanisha kitu gani, ila alishindwa kujieleza kwani hata yeye mwenyewe hakuelewa nini kinaendelea.
Sam naye akamuuliza swali Sakina,
"Umeongea na Sabrina leo muda mfupi uliopita?"
Sakina akaanza kujiumauma na kuhisi kamavile Sam kuna ukweli ameugundua.
Akataka kumwambia ukweli ili asionekane kuwa muongo sana.
Ila kabla hajamwambia ukweli, ujumbe ukaingia kwenye simu yake, akaufungua na kuusoma,
"Tafadhari usimwambie Sam kama nipo hapa.
Sabrina"
Ule ujumbe ulitumwa kwa namba ya Jeff ila ulionyesha kuwa umetumwa na Sabrina kwavile aliandika jina lake kwa chini.
Moja kwa moja Sakina akaelewa kuwa Jeff na Sabrina walimsikia vizuri ila tu walinyamaza kwa maana zao binafsi ambazo yeye hakuelewa kwa muda huo.
Wakati akifikiria, Sam akamshtua tena kwa swali lile lile na kumfanya Sakina ajigeleshe kwa kuuliza kwanza,
"Kwanini unaniuliza hivyo shemeji?"
Sam akatabasamu na kusema,
"Yani waswahili mna matatizo jamani, huwezi kujibu swali mpaka na wewe uulize swali mmh!!"
Akamfanya Sakina naye acheke sasa, kisha Sam akaendelea,
"Nimeuliza sababu nampigia simu haipokelewi"
Sakina akakb kimya huku akifikiria neno la kuchomekea hapo.
Jeff alikazana kumshika Sabrina ila ile sauti ya mama yake kuwa Sam amekuja ndio iliyomshtua ambapo Sabrina nae alishtuka pia,
"Unajua Sam alinikataza kuja kuzungumza na wewe Jeff, unafikiri itakuwaje kama akigundua kuwa nipo hapa na wewe?"
Wakaona wazi kuwa hapo itakuwa msala, ndipo Sabrina alipoamua kuchukua simu ya Jeff na kuandika ujumbe kwa Sakina.
Kisha akaanza kushauriana na Jeff pale ili wajue cha kufanya,
"Tafadhari Jeff hebu tuangalie jinsi ya kusaidiana, mi sitaki Sam ajue kama nipo na wewe hapa. Bora anikute popote pale nitatunga maneno ya kumwambia kuliko anikute hapa."
Jeff akakumbuka kuwa nyumba yao ina mlango mwingine wa ziada wa kutokea nje kwenye korido, ila akataka Sabrina amuhakikishie muda mwingine wa kuzungumza nae.
"Nakuahidi Jeff, nitatafuta muda mzuri wa kuzungumza na wewe hata kama itakuwa ni usiku sana. Ila kwasasa tujitahidi kuiondoa aibu hii."
Wakakubaliana kuonana tena usiku wa siku hiyo, kisha Jeff akamtoa Sabrina na kumpitisha mlango wa kutokea wa kwenye korido yao.
Wakati Sabrina anatoka pale, akasikia kama Sam akiaga kutoka mule ndani kwa Sakina.
Hapo Sabrina akajikuta akikimbia sana ili asiweze kuonekana kwa Sam kwani alijua wazi akimuona kutakuwa na balaa kubwa sana.
Sam aliona kumsubiria Jeff pale ni kupoteza muda, hivyobasi akaamua kuaga ili aondoke zake, ambapo Sakina nae akajigelesha kidogo,
"Shemeji jamani, hata kuvuta muda kidogo hutaki"
"Sio kwamba sitaki ila ngoja nikamuone Sabrina kwanza kwavile sijui hali yake muda huu ukizingatia nampigia simu halafu hapokei"
Sakina akaona ni vyema ili Sam asiweze kujua kama Sabrina yupo mahari pale, ingawa hakujua kuwa Sabrina angejitetea vipi kwa mumewe.
Kisha Sam akaondoka.
Sam alipofika kwa wakina Sabrina, akaingia chumbani kwa Sabrina moja kwa moja na kumkuta amelala hoi kuonyesha kwamba amechoka sana huku simu ikiwa kwenye chaji na kumfanya Sam aelewe kuwa kwanini Sabrina alikuwa hapokei simu na muda huo huo Sakina akampigia Sam simu kuwa Jeff amesharudi na kumfanya Sam aondoke tena na kuanza kurudi nyumbani kwa Sakina.
Kwakweli Sabrina hakuamini kama mchezo alioucheza umefanikiwa.
Alikuwa akihema tu juu kwa juu, kisha akachukua simu yake na kumpigia Jeff,
"Tafadhari Jeff nakuomba ukubali ofa ya Sam, tafadhari sana nakuomba"
"Nitakubali endapo utanihakikishia kuwa leo usiku tutaonana"
"Hilo sio tatizo Jeff, tutaonana ndio. Usijali kabisa kuhusu hilo nakuomba"
Jeff akakubali na kumfanya Sabrina atabasamu kwani alijua wazi kuwa kama Jeff akienda huko nje ya nchi itamsaidia pia yeye na ndoa yake itakuwa salama kabisa kwani alimuona Jeff kuwa kama kauzibe kwenye mambo yake.
Sam alifika kwa Sakina na kumkuta Jeff akiwa ametulia pale sebleni, akasalimiana nae pale na kuanza mazungumzo yao ambapo Jeff alikubali bila ya pingamizo lolote na kumfanya mama yake afurahi sana huku akimshukuru Sabrina kwani anajua wazi bila ya Sabrina basi wasingeweza kumshawishi Jeff kabisa.
Sam nae alifurahi kwani aliona wazi kuwa sasa tatizo lake lililokuwa likimtatiza limefika mwisho.
Akamshukuru sana pale Jeff, kisha akamwambia,
"Naomba kesho tuanze kushughulikia hati yako ya kusafiria"
Wakakubaliana na kupanga muda wa kukutana kesho yake ili aende naye kushughulikia hati ya kusafiria.
Baada ya hapo Sam akawaaga na kujiondokea zake.
Sakina akakaa na mwanae sasa na kuanza kumpongeza kwa uamuzi aliochukua,
"Asante sana mwanangu, umenisaidia mama yako yani siwezi kusimulia furaha niliyokuwa nayo"
"Usijali mama"
"Najua Sabrina amesaidia kwa namna moja au nyingine katika kukushauri mwanangu, kwakweli naye namshukuru sana"
Jeff akatabasamu tu kuonyesha kwamba anaelewa maneno ya mama yake, ila mama yake akamuuliza.
"Ila kwanini mlijifungia na Sabrina?"
"Hakutaka mumewe ajue kama yupo kwetu, kwahiyo alipoisikia sauti yake tu akafunga mlango"
"Ila kwanini hakutaka mumewe ajue kama yupo hapa?"
"Tafadhari mama, naomba hilo swali ukamuulize yeye mwenyewe"
"Mmh! Sawa nimekuelewa"
Kisha Jeff akamuaga mama yake na kuondoka pale kwao kwa muda huo.
Sam alirudi tena kwakina Sabrina, kwa bahati akamkuta Sabrina akiwa macho tofauti na mwanzoni.
Moja kwa moja alimfata Sabrina na kumkumbatia,
"Nakupenda sana mke wangu"
Kisha akambusu, Sabrina akamuuliza Sam,
"Mbona unafuraha hivyo?"
"Jeff kakubali kwenda nje kusoma"
"Wow, hongera sana mume wangu kwa kumshawishi Jeff akasome"
"Nashukuru Sabrina, najiona wazi leo nitakavyolala na tabasamu kwenye sura yangu."
Sabrina akatabasamu kwavile anaelewa ukweli wa mambo ulivyo.
Kisha Sam akaendelea kumuhabarisha Sabrina,
"Siku ya kurudi nyumbani kwetu utaikuta zawadi yako mke wangu, nimekuandalia kuonyesha mapenzi yangu ya kweli kwako"
Sabrina akafurahi sana na kumshukuru Sam kwa upendo wake kwake.
Kisha Sam akamuaga Sabrina kwa madai kuwa leo ataenda kupumzika mapema kwa furaha aliyokuwa nayo, halafu akaondoka.
Muda kidogo pale kwakina Sabrina akawasili Sakina na kumkuta Sabrina akinyonyesha mtoto wake, kwanza kabisa akacheka sana kumuona na kumfanya Sabrina naye acheke.
"Eeh niambie mdogo wangu uliwezaje kuondoka pale kwangu?"
Sabrina alicheka tena na kumueleza Sakina jinsi alivyoondoka mahali pale.
"Na kwanini uliogopa mumeo asikuone pale mdogo wangu?"
"Unajua Sam kanikataza kutoka toka humu ndani, sasa angenikuta kule ingekuwa khabari nyingine"
"Shemeji naye ndio mkoloni kiasi hicho loh"
Kisha wakaendelea na mazungumzo mengine na kumfanya Sabrina kufurahia vile alivyoaminika kwa Sakina.
Kisha akamuuliza,
"Vipi Jeff naye yupo?"
"Hata hayupo, alivyomaliza tu kuzungumza na Sam pale pale akaondoka"
"Sawa basi, nadhani atakuwa kuwatembelea rafiki zake"
"Itakuwa hivyo hivyo mdogo wangu"
Kisha wakaendelea na mazungumzo mengine halafu Sakina akaaga na kuondoka zake.
Sam alikuwa na furaha sana siku hiyo na alijua wazi siku atakayoondoka Jeff ndio itakuwa siku ya furaha zaidi katika moyo wake.
"Yani natamani hata akakae huko huko maisha yote maana huyu mtoto ananinyima raha kabisa kabisa"
Sam akaenda na kulala kwa furaha aliyokuwa nayo kwa siku hiyo.
Ulipofika muda wa kulala, Sabrina naye akalala na kusahau mihadi aliyopanga na Jeff kuwa watazungumza usiku huo.
Mida ya saa sita usiku, simu ya Sabrina ikakazana kuita.
Alipoitazama akakuta ni Jeff anapiga simu, ikabidi Sabrina aipokee simu ile,
"Nipo hapa nje kwenu"
Sabrina aliamua kuinuka na kwenda kumfungulia mlango Jeff ili akazungumze naye ndani tu.
Moja kwa moja akaingia naye chumbani kwake na kufunga mlango.
"Jeff sikiliza, wewe utakapoenda huko kwanza utaboresha maisha yako na ni wakati mzuri sana wa kukuwezesha wewe kuyajenga maisha yako ya badae"
"Tatizo nakupenda, najua wazi mmefanya yote haya ili kunitenganisha na wewe. Ila Sabrina, kamwe moyo wangu hautakuja wala kuweza kumpenda mwanamke yeyote yule zaidi yako. Mimi nakupenda wewe na siku zote nitaendelea kukupenda hadi naingia kaburini."
Sabrina akamtazama sana Jeff na haya maneno yake kwani aliona anaongea bila ya kufikiria ya mbele yake.
"Ila Jeff mimi sikufai, ni mkubwa sana kwako. Unatakiwa kuwapata mabinti wa rika lako ili uwe huru na ufurahie maisha ila sio mimi"
"Kwakweli siwezi, najua mnanitenganisha ila kamwe hamtaweza kutenganisha moyo wangu vile unavyojihisi juu yako."
Ikabidi Sabrina afanye kazi ya kumpa moyo kuwa atakuwa akiwasiliana nae kwa kipindi chote atakachokuwa huko nje ya nchi.
Jeff alifurahi ila alimuomba Sabrina kuwa kabla ya yeye kusafiri basi apate muda tena wa kuzungumza nae hata kwa usiku mmoja ili afirijike na moyo wake.
Sabrina alikubali kwani alitaka sana Jeff asafiri ili aweze kupumzika.
Alikubali kwavile anajua mazungumzo yao hayana madhara tena.
Kidogo Sabrina akamsikia mama yake akigonga chumbani kwake, Sabrina hakufungua mlango ila alikuwa akimsikilizia tu,
"Wee Sabrina unaongea na nani usiku huu?"
"Nilikuwa naongea na simu mama"
"Khee, utafikiri kuna mtu maana nimekusikia ukinong'ona nae"
"Hakuna mtu mama"
Kisha Joy akarudi chumbani kwake, ila kwa mawazo na sauti aliyoisikia ilikuwa kama sauti ya Jeff.
"Aaah ila isingewezekana kuwa ni Jeff kwa usiku huu, itakuwa tu alikuwa akiongea na simu kweli"
Kwa upande wa Sabrina nae akaona isije ikaleta tatizo lingine kwahiyo akaamua kumwambia Jeff kuwa aende.
"Sasa tutaonana wapi hiyo siku Sabrina"
"Usijali, tutaonana tu mbona leo tumeonana. Kwahiyo ondoa wasiwasi kabisa"
Kisha Sabrina akakazana kumsisitiza Jeff kuwa arudi kwao.
Ila Jeff akamuomba kuwa ambusu kwanza ndipo aondoke, ambapo Jeff alikutanisha kinywa chake na kinywa cha Sabrina kisha akambusu na kumuaga na kuondoka zake.
Sabrina alibaki akiwaza lile busu alilopewa na Jeff, akajikuta hata akitamani mambo mengine na kuamua kujilazimisha kulala ili kuyafunika mawazo yake.
Jeff naye aliporudi kwao, mawazo yake yake yalikuwa kwa Sabrina.
Aliona moyo wake ukiumia sana kuondoka mbali na Sabrina.
Kuna wakati alikaa na kujilaumu kuwa kwanini amechelewa kuzaliwa,
"Labda ningezaliwa mapema, leo hii Sabrina angenikubali kwavile ningekuwa mkubwa mwenzie. Ila Sabrina ananiona mimi mtoto, ananiona nimfai ingawa ninampenda kweli"
Roho yake ilikuwa ikimuuma sana na kujikuta hajalala usiku kucha kwa mawazo.
Kulipokucha Sam akampigia simu Jeff ili ajiandae na aweze kwenda naye mjini kwaajili ya kushughulikia maswala ya safari yake.
Na muda ulipofika, Sam akaenda kumpitia Jeff kisha wakaanza mizunguko yao ya hapa na pale.
Walipomaliza ile mizunguko, Jeff alijikuta akishikwa na usingizi na kulala ndani ya gari ya Sam.
Wakati Sam anaendesha gari kwa lengo la safari ya kurudi, akamsikia Jeff akiongea kutoka usingizini,
"Nakupenda sana Sabrina, siwezi kukuacha maisha yote."
Sam akashtuka sana kusikia kauli ile.
Walipomaliza ile mizunguko, Jeff alijikuta akishikwa
na usingizi na kulala ndani ya gari ya Sam.
Wakati Sam anaendesha gari kwa lengo la safari ya
kurudi, akamsikia Jeff akiongea kutoka usingizini,
"Nakupenda sana Sabrina, siwezi kukuacha maisha
yote."
Sam akashtuka sana kusikia kauli ile.
Kisha akamuangalia Jeff kwa makini na kungoja kama ataitoa tena ile kauli ili aweze kumrekodi, ila Jeff akaendelea kusinzia mule kwenye gari.
Sam akapaki gari pembeni na kumuamsha Jeff ambaye alikuwa mbali sana kwa usingizi,
"Jeff, Jeff"
Jeff akashtuka na kumuangalia Sam, kisha Sam akamuuliza,
"Mbona unalala mchana wote huu na kuongea peke yako?"
"Kuongea peke yangu?"
"Ndio ulikuwa unaongea peke yako, unayajua maneno uliyokuwa unaongea?"
Jeff akashangaa tena na kutikisha kichwa akiashiria kuwa hajui chochote, kisha Sam akamuuliza,
"Hukulala usiku nini?"
"Aah kichwa kimeniuma usiku kucha kwahiyo sikulala, nadhani ni mawazo tu"
"Basi ngoja tupite hapo baa ili tupate mbili tatu tuchangamshe damu"
Sam alikuwa na lengo lake kwani alijua Jeff akishakunywa ataweza kuropoka aliyonayo.
Wakaenda moja kwa moja kwenye baa, kisha Sam akaweka gari pembeni na kuwafanya washuke.
Wakaenda kukaa na kuagiza vinywaji.
"Kunywa tu Jeff hata usiniogope mimi"
Jeff akachezwa na kengele ya khatari kwenye kichwa chake, akakumbuka siku moja kabla ya harusi ya Sabrina, huyu huyu Sam alimpeleke tena baa na kumwambia anywe pombe na kumfanya aropoke baadhi ya mambo. Akaona hata leo hilo ndio litakuwa lengo lake.
Akajisemea kuwa leo atakunywa bia mbili tu,
"Kwavile kichwa kinanisumbua, sitaweza kunywa bia nyingi"
"Aah Jeff unaniangusha bhana, wewe ni mtoto wa kiume jiachie tu"
Ila Jeff aliendelea na msimamo wake ule ule kuwa hatoweza kunywa bia nyingi.
Basi Sam akaamua kumuuliza Jeff maswali kwa mitego tu kwavile Jeff amekataa kunywa pombe nyingi,
"Hivi Jeff uliniambiaga mpenzi wako anaitwa nani vile?"
"Aah! Mi kwasasa sina mpenzi bamdogo"
"Kwanini? Umeachana nae au ni nini?"
"Nimeachana nae ndio, nataka niangalie maisha yangu kwanza kwahiyo mambo ya wanawake nimeachana nayo kabisa"
Sam akaona kudanganywa ukizingatia muda mfupi uliopita, yeye mwenyewe kaongea ndotoni kuwa anampenda Sabrina.
"Niambie kwanini huwataki tena wanawake?"
"Wengi wao ni waongo"
Kisha Sam akambadilishia swali,
"Eeh niambie, unamuonaje Sabrina!"
"Nani? Mamdogo Sabrina au Sabrina gani?"
"Huyo huyo unayemjua wewe, je naye ni kati ya wanawake waongo?"
"Kwakweli kwa ninavyomjua mimi mamdogo alivyo, ni kati ya wanawake wachache tena wa kipekee katika hii dunia"
"Kwanini unasema hivyo?"
"Sababu mamdogo anaupendo, anajali na pia ana huruma"
"Mwanamke anayejali anawezaje kumuacha mtoto wake mdogo ndani na kwenda kumuangalia mumewe kama anamwanamke mwingine?"
Jeff akakaa kimya kwani hakuelewa ni kitu gani amjibu Sam kwa swali lake.
Sam naye alipoona Jeff yupo kimya akamgonga na swali jingine,
"Kwahiyo wewe ungependa mwanamke wa maisha yako awe Sabrina?"
Mara gafla Jeff akajishika tumbo na kudai kuwa linamuuma sana huku akihangaika na kujinyonganyonga.
Ikabidi Sam amsaidie kuinuka na kwenda naye kwenye gari ili amrudishe kwao.
Sabrina akiwa na shughuli zake za hapa na pale, akamuona Sam pale kwao na kumkaribisha.
"Nilikuja kumrudisha Jeff ndio nikaona ni vyema kupitia na hapa kuangalia familia yangu"
Sabrina akacheka na kumfanya Sam amuulize,
"Sasa unacheka kitu gani?"
"Nakucheka wewe kumrudisha Jeff"
"Kwanini?"
"Jeff na ukubwa ule unamrudisha! Si wa kurudi mwenyewe yule?"
"Aah kumbe Jeff ni mkubwa eeh! Kumbe mi naangalia vibaya sababu nilimuona ni mdogo kumbe kwako ni mkubwa"
Sabrina akajifanya kuchukia na kubadilisha mada ambapo Sam aliendelea na mada yake ile ile ya ukubwa wa Jeff.
"Ila Sam, hivi unamatatizo gani? Kwanini hunielewi ninachosema jamani? Haya ongea peke yako"
Kisha Sabrina akaingia ndani kwao na kumuacha Sam pale nje ambaye alikuwa akitikisa kichwa tu.
Sam hakuingia ndani kwakina Sabrina bali aliondokea pale pale nje na kurudi nyumbani kwake.
Sabrina akiwa ndani kwao akaulizwa na mama yake,
"Nimekusikia ukiongea na mtu hapo nje, ni nani?"
"Ni Sam mama"
"Sasa mbona haingii ndani?"
Ikabidi Sabrina ainuke na kwenda nje ili kumwambia Sam aingie ndani, ila akashangaa kuona gari ya Sam ikiishia.
"Yani huyu mwanaume ameondoka bila hata ya kuniaga jamani? Mapenzi gani haya? Sijapata kuona"
Kisha akarudi ndani kwao, na mama yake akamuuliza swali lile lile kuwa Sam yuko wapi.
"Alikuwa na haraka, kuna mahali anawahi kwahiyo ameshindwa kuingia ndani"
"Hata kunisalimia jamani ameshindwa! Nilikuwa na shida nae leo ila basi nitaongea nae hata kesho"
"Shida gani hiyo mama?"
"Inatakiwa nimwambie yeye mwenyewe kwahiyo wewe tulia tu"
Ikabidi tu Sabrina akubali kwavile hakutaka kumlazimisha mama yake kumwambia.
Jeff alitulia nyumbani kwao huku akiwaza kuwa ni kitu gani anachowaziwa na Sam.
"Inaonyesha wazi kuwa Sam anajua kila kitu ila kwanini anajifanya hajui? Na kwanini hupenda kuniuliza maswali ya mitego?"
Aliwaza bila ya kupata jibu, kisha akajiuliza tena,
"Nampenda sana Sabrina, wakati huo huo Sam anaonyesha kumpenda sana Sabrina pia. Ila Sabrina mwenyewe kuna wakati anaonyesha kunipenda mimi na wakati mwingine kumpenda Sam. Kwanini inakuwa hivi? Je haya ni mapenzi? Inamaana nikikaa mbali na Sabrina ndio sitampenda tena? Nawezaje kumtoa katika moyo wangu wakati yeye ndio damu yangu? Siwezi kumuacha, siwezi kabisa"
Jeff aliona wazi kichwa kikimuuma kutokana na mrundikano wa mawazo aliokuwa nao.
Sam nae alikaa ndani kwake akijifikiria, akiyapima mapenzi yake kwa Sabrina. Akipima kasoro yake, aliumia sana moyoni mwake kwani mali na utajiri aliokuwa nao havikutosha kumuonyesha Sabrina kuwa ni jinsi gani anampenda.
Alitamani kutoa hata machozi kwani yote aliyokuwa akiyafanya ni kumuonyesha Sabrina ni jinsi gani anampenda bila ya kujali gharama wala chochote kile.
Kesho yake kama kawaida, Sam akaendelea na harakati za kushughulikia safari ya Jeff.
Ikawa ndio shughuli yake kubwa ya kila siku.
Zikapita wiki mbili bila hata ya kwenda kwa wakina Sabrina kama ilivyokuwa kawaida yake hapo awali wala kuwasiliana na Sabrina.
Siku hiyo Sabrina alikaa na mama yake na kujikuta akiulizwa tena kuhusu Sam,
"Sabrina, kwani umegombana na Sam au ni kitu gani, maana sielewi toka siku ile uliyosema kuwa anaharaka hadi leo sijamuona"
Sabrina naye akaumia moyo kwa swali aliloulizwa na mama yake na kuamua kuingia ndani kwake kisha kumpigia simu Sam ili amsikie atamwambiaje,
"Nataka leo uje nyumbani"
Hakutaka hata kusikia jibu la Sam litakuwaje kwani muda huo huo akaikata ile simu huku akilalamika peke yake.
"Mtu kama hakupendi bora akwambie tu kuliko kukufanyia mambo ya ajabu kama haya. Mtu gani huyu kila siku haeleweki, najua anamuondoa Jeff ili kunijutisha mimi tu"
Alipofikia hapo akasita kidogo na kujiuliza tena,
"Hivi mimi naanzaje kumpenda kijana mdogo kama Jeff jamani? Tafadhari moyo wangu ondoa mawazo potofu juu yangu"
Kisha akaenda kuendelea na mambo mengine.
Muda kidogo Sam aliwasili kwakina Sabrina na kumkuta mama wa Sabrina akiwa nje ambapo alimsalimia na kuanza kuzungumza naye,
"Hujaonekana mwanangu, kwani nini tatizo?"
"Hakuna tatizo mama ila nilitingwa tu"
"Pole kwa majukumu mwanangu, nasikia unataka kumpeleka Jeff nje akaome"
Sam akatabasamu kidogo na kuongea,
"Asante mama, ila ndio swala hilo hilo la Jeff ndio linanifanya nitingwe na mambo mengi"
"Sawa, ila mi nilikuwa na ombi kidogo mwanangu. Ila tuingie ndani kwanza"
Ikabidi waingie ndani huku Sam akiwa na hamu ya kujua ombi la mkwewe ni nini kwa muda huo.
Walipokuwa ndani, Sabrina nae akatoka chumbani kwake na kuwafata pale sebleni ila alifika na kukaa bila hata ya kumsalimia Sam na kumfanya mama yake amshangae na kumuuliza,
"Mbona humsalimii mwenzio Sabrina?"
"Mmh mama, nishamsalimia kwenye simu tayari"
"Kwahiyo mkisalimiana kwenye simu ndiyo inatosha? Ndio uzungu huo au ni kitu gani?"
Sabrina akaona ni vyema aepushe shari kwa kumsalimia Sam, kisha mama yake akamuomba awapishe kwavile alihitaji kuzungumza na Sam, kwahiyo Sabrina akarudi tena chumbani kwake.
Sabrina alipokuwa chumbani kwake akatumiwa ujumbe na Jeff,
"Tafadhari naomba kesho tuonane"
Sabrina akaamua kumpigia simu Jeff ili amsikie kuwa ana shida gani,
"Kwani una tatizo gani Jeff"
"Sina tatizo ila naomba tuonane, kuna kitu nataka kukwambia"
"Si uniambie tu kwenye simu!"
"Hapana, haitakuwa poa nikikwambia kwenye simu ndiomana nikaomba tuonane"
"Kwahiyo tutaonana wapi?"
"Nitakuelekeza pa kukutania"
Sabrina akaamua tu kukubaliana na Jeff kwani alijua wazi kuwa ndio mwisho mwisho wa usumbufu toka kwa Jeff kwavile karibia atasafiri na kwenda huko masomoni kwahiyo atakuwa amempunguzia usumbufu.
Mama wa Sabrina nae alianza kuweka hoja zake kwa Sam,
"Mwanangu Sam si unamjua yule wajina wako?"
"Si unamaanisha yule shemeji yangu mdogo mama, yule Sam!"
"Ndio huyo huyo mwanangu"
"Kafanyaje kwani?"
"Anatamani kweli akamalizie masomo yake ulaya ila ndio hivyo mwanangu pesa ya kumpeleka huko imekuwa mtihani"
Sam alimuangalia mkwewe na kujiongeza kwani alielewa wazi kuwa mkwewe anamaanisha kitu gani ukizingatia alishapata taarifa kuwa Sam anamgharamikia Jeff kwenda kusoma nje ya nchi.
Sam akapumua kidogo na kuzungumza,
"Kwani inahitajika pesa kiasi gani mama"
Mama wa Sabrina akajichekelesha kidogo na kuendelea kuongea,
"Sijui mwanangu ila ndio hivyo, wajina wako anatamani sana"
"Sawa mama, basi ngoja nimalizane na hili swala la Jeff ndio nianze na la huyo Sam"
"Jamani nashukuru sana mwanangu, utakuwa umenisaidia sana jamani. Mungu akubariki sana mwanangu."
"Usijali mama"
Kisha Sam akamuaga mama mkwe wake huku akimuomba amuitie Sabrina.
"Nenda tu chumbani kwake mwanangu ukamuone na mtoto"
Sam nae akaona ni vyema kufanya hivyo, kisha akainuka na kwenda chumbani kwa Sabrina.
Akamkuta Sabrina kajilaza,
"Naomba unisindikize Sabrina mi naondoka"
Kisha akasogea kwenye kitanda cha mtoto na kumuangalia tu kwavile alikuwa amelala.
Akamuona yule mtoto akitabasamu ingawa alikuwa usingizini na kumfanya Sam amuulize Sabrina,
"Mbona mtoto kama anatabasamu?"
"Anaota huyo, hujawahi kukaa na watoto ndiomana unashangaa"
Kisha Sabrina akainuka na kumsindikiza Sam nje.
Walipofika nje Sam akamshika mikono Sabrina,
"Nashukuru kwa kunipigia simu leo, subiri haya mambo yapite utafurahi mwenyewe mke wangu"
Sabrina hakujibu kitu zaidi ya kumuangalia Sam tu, kisha Sam akambusu Sabrina kwenye paji lake la uso halafu akamuaga na kuingia kwenye gari yake na kuondoka.
Sabrina alipoingia ndani kwao, mama yake akamuita na kumwambia,
"Mwanangu, kwanini unakuwa na akili mbovu kiasi hiko!"
"Kwanini mama?"
"Yani wewe badala ya kumwambia Sam amsomeshe mdogo wako eti akamsomeshe Jeff wa kazi gani na atusaidie nini sasa? Mie leo nimemwambia mumeo kuwa amsomeshe na mdogo wako pia"
"Khee mama huna hata aibu jamani! Mambo mengine kujidhalilisha tu"
Kisha akainuka na kwenda chumbani kwake.
Kesho yake asubuhi na mapema, Sam akampigia simu Sabrina kumsalimia,
"Leo umekumbuka kunipigia simu asubuhi asubuhi?"
"Kuna mahari naenda, ila usiku nimekuota ndiomana nimekupigia simu asubuhi hii"
"Unaenda wapi kwani?"
"Naenda Bagamoyo ila nadhani nitarudi leo leo, ila nina ombi moja kwako"
"Ombi gani hilo?"
"Kutokana na ndoto niliyoota usiku, tafadhari Sabrina nakuomba leo usitoke. Usiende popote pale"
"Sawa mume wangu nimekuelewa"
Sam akatabasamu kwavile amemsikia Sabrina akimuita mume wangu kwa siku ya leo.
Kwahiyo akaona kuwa itakuwa siku ya furaha sana kwake.
Kisha wakaagana pale kwenye simu.
Jioni ya siku hiyo Jeff akampigia simu Sabrina na kumtajia mahali pa kuonana nae,
"Kheee Jeff mbona ni hotelini huko?"
"Ndio ni hotelini, na wala sina nia mbaya kukuita huku"
"Mmh! Ngoja nifikirie kwanza"
"Tafadhari Sabrina nakuomba, usikatae tafadhari. Sina nia mbaya, niamini ninachosema"
Sabrina akafikiria kidogo na kukubali kwenda kwani moyo wake ulimuhakikishia kuwa Jeff hawezi kumfanya chochote kibaya.
"Kipindi kile alinilewesha madawa ndiomana ila kwasasa hawezi nifanya chochote. Ngoja niende tu nikamsikilize"
Sabrina akajiandaa na kumuaga mama yake kuwa anatoka kidogo.
Sabrina alienda moja kwa moja alipoelekezwa na Jeff.
Alifika mpaka kwenye hoteli aliyoelekezwa na kuingia ndani.
Moja kwa moja akaelekea kwenye namba ya chumba alichoelekezwa.
Wakati anataka kufungua mlango, akasikia sauti ikiita kwa nyuma yake,
"Sabrina"
Sabrina akatetemeka kwani sauti aliyosikia ilikuwa ni sauti ile ile aliyoizoea ya Sam.
Wakati anataka kufungua mlango, akasikia sauti
ikiita kwa nyuma yake,
"Sabrina"
Sabrina akatetemeka kwani sauti aliyosikia ilikuwa
ni sauti ile ile aliyoizoea ya Sam.
Sabrina akaogopa kabisa kugeuka na kuganda pale pale mlangoni kwani hakuweza kwenda mbele wala kurudi nyuma kwa uoga aliokuwa nao.
Akahisi yule mtu akija nyuma yake na kumfanya Sabrina uoga umzidie.
Yule mtu akamshika Sabrina mabegani, kisha akanyoosha mkono wake mmoja na kufungua ule mlango halafu wakaingia ndani na Sabrina huku akiwa amemtanguliza Sabrina kwa mbele, muda wote huo Sabrina alikuwa akitetemeka tu.
Kisha yule mtu akazunguka ili Sabrina amuone, wakati huo Sabrina aliyafumba macho yake kwa uoga aliokuwa nao.
"Mbona umefumba macho Sabrina, hebu niangalie kwanza"
Sabrina akaitafakari tena ile sauti na kugundua kuwa ni sauti ya Jeff, alipumua kwa nguvu na kusema,
"Mungu wangu"
"Nini mamy, kwani kuna tatizo lolote"
Sabrina akajikuta akikaa kwenye kitanda kilichopo karibu akipumua tu kwani uoga aliokuwa nao mwanzoni ulikuwa mkubwa sana.
Ikabidi Jeff naye akae pembeni mwa Sabrina ili amuulize vizuri kuwa ana tatizo gani.
Sabrina alikuwa ameinama ila sasa akalala chali huku miguu yake ikining'inia kwenye kile kitanda.
Jeff naye akaenda juu kidogo ya Sabrina huku akimuuliza kwa sauti ya chini kabisa,
"Una tatizo gani mamy?"
Sabrina hakujibu kitu, muda huo Jeff naye akawa kama anambembeleza Sabrina kwa kumpapasa.
Sabrina akatulia akiisikilizia mikono ya Jeff ikitembea kwenye mwili wake.
Jeff naye alitumia muda huo kuzivuta hisia za Sabrina hata Sabrina akajishangaa kuwa ameshindwa vipi kumzuia Jeff asimpapase.
Jeff naye akaendelea kumuwekea Sabrina hali ya ushawishi na mwisho wa siku Sabrina akajikuta amelaghaiwa na Jeff na kulala nae akiwa na akili zake timamu tofauti na siku ya kwanza ambapo aliwekewa madawa ya kulevya na Jeff.
Baada ya mambo hayo kuisha, Sabrina alijikuta akikaa na kujiinamia bila kuamini kuwa ni yeye aliyelala tena na Jeff, alijikuta akijiuli za,
"Hivi ni kweli au naota?"
Jeff akamjibu kwa sauti ya taratibu,
"Ni kweli mamy, tafadhari nisamehe"
Sabrina akainua kichwa chake na kumtazama Jeff kisha akamwambia,
"Sio kosa lako Jeff"
Halafu akainuka na kuvaa nguo zake, hakutaka tena kumuangalia Jeff kwani aliondoka bila hata ya kugeuka nyuma, wakati huo Jeff naye hakuweza kumfata nyuma Sabrina kwani aliona wazi kuwa angemzidishia mawazo.
Sabrina alirudi nyumbani kwao, moja kwa moja akaenda kuoga kwanza.
Kisha akaenda chumbani kwake, na kumtazama mwanae ambaye alikuwa bado amelala, ila mtoto huyo alitabasamu akiwa usingizini na kumfanya Sabrina ajiulize,
"Inamaana huyu mtoto anafurahia au ananicheka?"
Mwishowe na yeye akajicheka kwani mtoto wao alikuwa bado mdogo na isingekuwa vyema kumuwazia mabaya.
Jeff naye alirudi nyumbani kwao huku sura yake ikiwa imejaa tabasamu na kumfanya hata mama yake amuulize kwa mshangao,
"Umefurahia safari yako nini!"
Jeff naye alijibu kwa shangwe sana,
"Nimeifurahia sana"
"Kwanini?"
"Sababu safari yangu imekuwa na matunda, imenipatia kitu nilichokuwa nakihitaji siku zote katika maisha yangu"
Mama yake akashangaa na kumuuliza tena,
"Mmh kitu gani hicho?"
Jeff akatabasamu tu tena na kwenda chumbani kwake.
Muda kidogo Sakina akamfata mwanae,
"Mwanangu, Dorry kaja kukuaga"
"Hivi mama ni mara ngapi nimekwambia kuwa siwataki hao wasichana?"
"Ila hujawahi kuniambia kuwa kwanini huwataki"
"Sababu siwapendi, yupo mwanamke mmoja tu katika ndoto zangu. Huyo peke yake ndio nahitaji awe mke wangu"
"Ni mwanamke gani huyo?"
"Ni........"
Kabla hajataja akaikumbuka kauli ya Sabrina kuwa ibaki kuwa siri yao, kisha akamtazama mama yake na kutoka nje kumuona huyo Dorry.
"Mbona umekuja usiku?"
"Nimekuja kukusalimia Jeff nasikia unakaribia kusafiri."
"Ndio nasafiri, nashukuru kwa kuja kuniaga"
"Basi tuwe tunawasiliana Jeff"
"Hakuna tatizo. Ila Dar umekuja lini maana mara ya mwisho nilikuona Bagamoyo. Na nani amekwambia khabari za kusafiri kwangu?"
"Dar nimekuja leo leo, nilikutana na yule kaka mliyekuwa naye siku ile na yeye ndiye aliyeniambia kuwa unataka kusafiri na hata hapa kanileta yeye"
Jeff akapata kumbukumbu kuwa huyo mtu lazima atakuwa Sam tu na kugundua kuwa Sam alienda Bagamoyo kwa siku hiyo.
Kisha akamuangalia tena Dorry na kumwambia,
"Nashukuru sana Dorry ila ni usiku sasa, itakuwa vyema kama nitakusindikiza"
"Hapana Jeff, kama uonavyo usiku tayari. Mi leo nitalala hapa kwenu halafu nitaondoka kesho. Au kuna ubaya?"
Kabla Jeff hajajibu, tayari mama yake alikuwa pale sebleni na kujibu lile swala.
"Hakuna tatizo Dorry, utalala tu hapahapa"
Kisha Jeff akamuangalia mama yake na kukosa cha kusema zaidi ya kwenda chumbani kwake tu, tena bila hata ya kuongea cha zaidi na Dorry.
Sabrina akiwa chumbani kwa mtoto wake, akasikia sauti ya Sam ikiongea na mama yake.
"Mmh isiwe tena ni sauti ya Jeff inanichanganya!"
Muda huo huo Sam nae akaingia mule chumbani kwa Sabrina, na kumkuta Sabrina akiwa amejiinamia kwa mawazo.
Akamfata na kumshika mgongoni,
"Nini tatizo mke wangu?"
Sabrina akainua macho yake na kumkumbatia Sam, hadi Sam akashangaa pia kisha na yeye akamkumbatia.
Halafu akamuuliza tena kwa sauti ya taratibu,
"Kuna tatizo lolote mke wangu?"
Sabrina akatikisa kichwa kuashiria kwamba hana tatizo lolote lile.
Kisha wakakaa na Sam akaanza kumuhabarisha Sabrina.
"Kesho kutakuwa na chakula cha jioni nyumbani kwa Sakina, tutakuwa tunamuaga Jeff anaondoka keshokutwa"
Sabrina akashangaa,
"Jeff anaondoka kesho kutwa!!"
"Ndio anaondoka keshokutwa ndiomana hata mimi nimeona bora nirudi leo leo. Kila kitu kwaajili ya safari yake ni tayari kwahiyo keshokutwa anaondoka"
"Mbona umeharakisha kiasi hicho?"
"Sasa si ndio vizuri ili akawahi masomo"
"Sawa nimekuelewa"
Sabrina hakuwa na nyongeza ya maneno zaidi ya kukubaliana na Sam tu.
Kisha Sam akaongea mengine na kumuaga Sabrina.
Sabrina alitafakari sana na kugundua sababu ya Jeff kumuita kule, aligundua kuwa lengo lilikuwa ni kumuaga sema ndio hivyo wakakumbana na mengineyo.
Sabrina aliwaza sana kuwa endapo Sam angegundua ukweli wa mambo ingekuwaje? Alishukuru kurudi kwani angechelewa basi pengine Sam asingemkuta na mwisho wa siku angezua makubwa zaidi.
Nyumbani kwakina Jeff, alibaki pale sebleni Sakina na Dorry muda huo Jeff alikuwa chumbani kwake.
Ingawa Sakina amekuwa akimshutumu mwanae kuwa na mahusiano na wanawake waliomzidi umri, ila bado alikuwa na mashaka kuwa huenda mwanae sio mzima.
Akaona huo ndio muda muafaka wa kujaribisha urijali wa mtoto wake, na akaona kuwa hakuna njia nyingine zaidi ya kumtumia huyo huyo Dorry.
Kwahiyo akamruhusu Dorry aende chumbani kwa mwanae ili akamshawishi awezavyo angalau ajipe moyo kuwa mwanae ni mwanaume rijali.
Dorry akainuka pale na kuanza kuelekea chumbani kwa Jeff kwani naye pia alifurahia nafasi hiyo ukizingatia ni muda mrefu tu anampenda Jeff.
Dorry alisukuma mlango wa Jeff nao ukafunguka kwavile Jeff hakufunga na funguo.
Akamkuta Jeff akiwa hoi amelala, moja kwa moja Dorry akaenda pale kitandani kwa Jeff na kuanza kumpapasa taratibu ili ampe muhemko.
Wakati anampapasa, akamsikia Jeff akinung'unika kimahaba,
"Aaah Sabrina, nakupenda mpenzi"
Dorry akasita kidogo na kujiuliza kuwa huyo Sabrina ndiyo nani, kisha akaendelea kumpapasa kwani lengo lake lilikuwa ni kulala na Jeff tu.
Dorry akatoa nguo zake zote na kulaza mwili wake laini juu ya mwili wa Jeff ili angalau joto lake limshtue na kumfanya afurahie uwepo wake.
Wakati huo Jeff naye alizidi kunung'unika kimahaba na kumfanya Dorry azidishe manjonjo yake.
Wakati Dorry akiwa kwenye hatua ya mwisho kufanikiwa kwani aliweza kumuondoa nguo Jeff, mara simu ya Jeff ikaanza kuita na kumfanya Jeff ashtuke.
Akashangaa kumuona Dorry mbele yake akiwa mtupu kabisa, akajishangaa na yeye kujiona yupo mtupu pia.
Akavuta haraka haraka shuka iliyokuwa karibu yake na kujifunika huku amekunja sura yake kwa kumtazama kwa mshangao yule Dorry.
Akachukua simu yake na kumuangalia mpigaji alikuwa ni Sabrina, ile hali ikamchanganya zaidi Jeff akajikuta akiinuka na kumsukumia Dorry nje ya chumba chake, kisha akarudi na kujiinamia huku akiwaza kuwa atamwambia nini Sabrina yani kamavile anahisi kuwa kuna kitu Sabrina amekigundua.
Ile simu iliita na kukatika kisha ikaanza kuita tena, akaamua kuipokea na moja kwa moja akapata swali kutoka kwa Sabrina,
"Umelala Jeff?"
"Ndio nilikuwa nimelala, simu yako ndio imeniamsha"
"Mi usingizi hauji ndiomana nimekupigia simu hata niongee nawe kidogo"
"Naomba unisamehe kwa yaliyotokea leo. Sikujua kama ingekuwa vile."
"Tafadhari achana na hayo, naomba tusahau kama yalitokea. Bado nakuomba jambo moja, hii iwe ni siri"
Jeff akakubali yote aliyoambiwa na Sabrina kisha akamuaga kwa kumbusu kwenye simu kitendo ambacho kilimsisimua sana Sabrina.
Jeff alipokata ile simu, bado alikuwa akijifikiria kuhusu Dorry.
Kisha akainuka na kuvaa nguo zake, muda huo Dorry nae akawa anamgongea Jeff mlango,
"Tafadhari Jeff naomba nguo zangu"
Jeff akazikusanya na kufungua mlango kisha akamrushia pale alipomtoa halafu yeye akafunga na funguo mlango wa chumbani kwake.
Dorry alirudi sebleni kwakina Jeff na kuwaza kuwa huenda Jeff ni mgonjwa kweli ila aliona ni vyema kama mama yake akimuuliza basi amtetee tu hivyo hivyo.
Asubuhi na mapema, Jeff aliamka na kuondoka pale kwao tena bila hata ya kumuaga mama yake.
Sakina alipotoka alimkuta Dorry sebleni,
"Eeh binti yangu, Jeff kaenda wapi tena asubuhi yote hii badala ya kukaa na wewe hapa!"
"Kaniambia kuna rafiki yake ameenda kumuona"
"Haya nipe khabari za usiku"
"Usiku ulikuwa mzuri sana mama"
"Vipi ulifanikiwa? Mwanangu mzima?"
"Ndio nilifanikiwa mama, ni mzima ndio"
Sakina akatabasamu na kumkumbatia Dorry.
"Karibu sana kwenye ukoo wetu Dorry"
"Asante mama"
Sakina alikuwa na furaha na kuona hata hiyo sherehe ya kumuaga mwanae angalau ataifanya kwa matumaini tofauti na mawazo aliyokuwa nayo mwanzoni.
Safari ya Jeff asubuhi ile ilikuwa ni moja kwa moja kwa wakina Sabrina.
Kama kawaida, alimkuta mama wa Sabrina akiwa nje tayari kwa kazi zake ndogo ndogo, akamsalimia pale,
"Kheee Jeff mbona leo asubuhi asubuhi! Umetuota nini?"
Jeff akacheka, kisha akasema,
"Nimekuja kumuona mamdogo na mtoto"
"Haya pita ndani utawakuta"
Jeff akaingia ndani na moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha Sabrina.
Hata Sabrina mwenyewe akamshangaa Jeff kuwa pale mapema vile. Kisha akamkaribisha,
"Najua mtanikumbuka sana, ila mtanisahau pia lakini mimi siwezi kuwasahau hata kidogo"
"Na wewe Jeff, ndio maneno gani hayo kamavile waenda kufa loh"
Jeff akatabasamu tu na kusema,
"Leo kwetu kuna chakula usiku kwaajili ya kuniaga mimi, umeniandalia zawadi gani?"
"Tulia utaiona tu, ila zawadi nitakayokuletea sitaki mtu yeyote aione. Nitakapokupa nakuomba uifungue ukiwa peke yako"
Jeff akatabasamu na kufurahi sana moyoni mwake kwani alijua wazi kuwa zawadi aliyoandaliwa na Sabrina itakuwa ya thamani sana mbele ya macho yake.
Kisha akamuaga na kuondoka zake.
Jeff alipotoka pale, moja kwa moja akarudi nyumbani kwao.
Akamkuta mama yake na Dorry wakiwa na furaha sana, hata yeye mwenyewe akawashangaa tu.
Sakina akamuuliza mwanae,
"Ungependa tukuandalie kitu gani kwa usiku wa leo mwanangu?"
"Chochote tu mama"
"Asante mwanangu"
Jeff akamshangaa mama yake kwa kumshukuru bila sababu bila ya kujua kuwa mama yake anamshukuru sababu ya Dorry.
Jioni ya siku hiyo Sabrina akiwa anafunga zawadi ya kumpelekea Jeff, mara mlango wa chumbani kwake ukafungulia na akaingia Sam.
Muda huo huo Sabrina akairushia ile zawadi uvunguni mwa kitanda.
Sam akamuuliza,
"Umerusha kitu gani?"
"Hamna kitu"
Sam akainama na kukiona, kisha akakivuta.
Muda huo huo Sabrina akairushia ile zawadi
uvunguni mwa kitanda.
Sam akamuuliza,
"Umerusha kitu gani?"
"Hamna kitu"
Sam akainama na kukiona, kisha akakivuta.
Sam akakiangalia na kumuangalia Sabrina, kisha akamuuliza
"Unamaana gani kufunga hivi? Na kwanini ufiche baada ya kuniona?"
Sabrina akajiuma uma kwani alikosa majibu ya kumpa Sam moja kwa moja.
Kwavile Sabrina alikuwa bado hajaifunga vizuri ile zawadi, Sam akaamua kufungua na kuangalia kilichomo ndani yake, kisha akamuuliza Sabrina,
"Mbona unaifunga nguo ya mtoto Sabrina? Kwanini ufanye hivi?"
Sabrina akapumua kidogo na kupata cha kuongea,
"Sasa usiwe unanikaripia Sam, niulize kwa utaratibu nikujibu"
"Hivi kwa mfano ungekuwa ni wewe halafu ukute mimi nafunga zawadi ambayo nikikuona naificha ungejifikiriaje?"
"Ila ni umenielewa vibaya tu Sam, na wala sikuwa na lengo baya kuificha. Hiyo ilikuwa ni surprise kwako"
"Surprise kwangu kivipi? Na iweje unifungie nguo ya mtoto?"
"Nilikuwa nataka kukwambia kwa mtindo wa zawadi kuwa mtoto wetu sasa amekua, ana miezi sita sasa."
Sam akamuangalia Sabrina na kuhisi ni wazi kuwa anadanganywa ila sasa atamuhukumu vipi wakati ukweli haujui.
Laiti kama angejua ukweli wa mahali ambako Sabrina anataka kwenda kuituma ile zawadi basi angejaribu kuhisi kuwa ni kitu gani kinaendelea.
Sam hakuwa na la ziada kwani alijua kwamba muda wowote ule kuanzia alipoiona ile zawadi basi ataujua ukweli tu.
Kisha akamwambia Sabrina kuwa ajiandae kwaajili ya kwenda kwenye chakula cha usiku kumuaga Jeff,
"Tangulia tu Sam, mi nitakuja"
Sam hakubisha kwani bado alikuwa kwenye harakati za uchunguzi wake, ukizingatia kuwa bado alihitaji kujua mbichi na mbivu.
Jeff aliona usiku umeanza kuingia, akbmua kumuuliza Dorry,
"Si ulisema unaondoka leo? Sasa mbona mpaka muda huu upo?"
"Jamani Jeff, leo si ndio wanakuaga! Sasa mimi naondokaje jamani!"
"Haya"
Kisha akaendelea na mambo mengine.
Muda huo Sam nae akawasili mahali pale na kuwakuta wakiwa wanaandaa andaa hiko chakula cha jioni kwaajili ya kumuaga Jeff kwa pamoja.
Muda ukafika na ndugu baadhi wa Jeff nao wakawasili.
Chakula kikaandaliwa na mawili matatu yakaongelewa kisha watu wakaanza kula ila Sabrina hakuonekana kabisa pale nyumbani kwa Sakina.
Sabrina akiwa nyumbani kwao, akaona ni vyema asiende kabisa kwenye hiyo tafrija fupi ya kumuaga Jeff kwani aliona wazi akimkera Sam ukizingatia na kitu alichokifanya jana yake.
Alitulia pale ndani kwao na mwisho wa siku akaenda kulala.
Muda kidogo Sam akafika pale kwakina Sabrina na kumgongea Sabrina mlango kwani alikuwa ameufunga siku hiyo.
Sabrina aliinuka na mausingizi yake kwenda kufungua ule mlango na moja kwa moja Sam akaingia mule ndani.
"Vipi Sabrina una matatizo gani? Unajua ulichofanya leo hakipo sawa kabisa, umeniahidi kuwa utakuja ila muda umepita pale bila ya wewe kutokea. Umemfanya Jeff asononeke sana kwavile hakukuona kwenye eneo la tukio."
"Naomba mnisamehe bure tu kwani sikutarajia kama nitapitiwa na usingizi kiasi hiki. Yani hata mimi mwenyewe ndio nashangaa hapa."
"Ila kitendo ulichokifanya sijakipenda kabisa"
"Kwani anaondoka kesho saa ngapi?"
"Anaondoka na ndege ya saa tatu asubuhi"
"Basi naomba nikamuage huko huko uwanja wa ndege, natumaini atanisamehe"
"Sawa, jiandae mapema kesho twende wote"
"Sawa, hakuna tatizo"
Sam akasogea kwenye kitanda cha mtoto kisha akambusu pale alipolala na kuwaaga na kisha kuondoka zake.
Jeff alishangaa pia kwakuto kumuona Sabrina pale nyumbani kwao, na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo ambavyo moyo wake ulizidi kumuuma kwani katika watu muhimu aliohitaji kuwaona kwa usiku ule basi alikuwa ni Sabrina.
Kwahiyo kitendo cha yeye kutokumuona Sabrina kilimsononesha sana na kumsikitisha.
Baada ya kuagana na ndugu zake pale, akaenda chumbani kwake na kujiinamia.
Aliona machozi yakimtoka kwa kumkosa Sabrina kwa muda kama ule. Akaiwaza zawadi ambayo aliahidiwa na Sabrina, akawaza mambo mengi sana na kuona kuwa hiyo ndio zawadi ambayo Sabrina amemuahidi kuwa hawezi kumsamehe na ndiomana hajatokea kwa siku ile ya muhimu kwake.
Wakati Jeff akiwa amejiinamia vile, akaingia Dorry mule chumbani kwavile alikuwa hajafunga mlango kwa funguo, moja kwa moja Dorry alienda kukaa karibu na Jeff pale kitandani kisha akazungusha mkono wake kwenye bega la Jeff, ambapo Jeff akaihisi vyema ile mikono ya Dorry kwenye mwili wake, kisha Jeff akaongea kwa sauti ya chini kabisa akimuuliza Dorry,
"Unataka nini Dorry?"
Naye Dorry akamjibu kwa sauti ya chini vile vile,
"Nakutaka wewe Jeff"
Jeff akainuka na kumuacha Dorry pale kitandani kisha yeye akatoka nje.
Alipofika nje akajifikiria sana, akaona wazi kuwa hamtendei haki Dorry ila upande mwingine wa moyo wake ukamwambia kuwa endapo atamtendea haki Dorry basi ajue kuwa hamtendei haki Sabrina.
Akajifikiria tena, kuwa je arudi ndani alipo Dorry au afanye kitu gani.
Akapatwa na wazo jipya kwenye akili yake kwa muda huo.
Sabrina akiwa amelala, akasikia mtu akigonga mlango.
Akaamka na kujiuliza, kisha akahisi kuwa huenda Sam amerudi tena.
Akainuka na kwenda kufungua mlango ule.
Akamkuta Jeff mlangoni ambapo aliingia moja kwa moja hadi chumbani kwa Sabrina.
Alienda na kukaa kitandani alipo mtoto, kisha akamnyanyua na kumshika.
Akambusu katika paji la uso, chozi likamtoka Jeff na moja kwa moja likamuangukia mtoto yule.
Jeff akamrudisha mtoto kitandani na kujifuta machozi yake.
Kisha akamtazama Sabrina na kuinuka pale kitandani, akamsogelea pale alipokuwa amesimama na kumkumbatia kwa nguvu sana kisha akamuachia na kumbusu kwenye kiganja cha mkono wake halafu akaondoka bila ya kusema kitu chochote.
Sabrina alikuwa kama ameganda vile akimtazama Jeff, hadi pale Jeff alipoishia kabisa ndipo Sabrina alipofunga mlango na kurudi chumbani kwake.
Alikaa na kujifikiria, aliona moyo wa Jeff uliojawa na mapenzi ya dhati juu yake.
"Kwanini Jeff unipende mimi? Kwani huwaona mabinti wa rika yako? Kwanini mimi? Nakuona umejaa penzi la dhati na la pekee juu yangu, je yupo wa kunipenda mimi kiasi hiki unipendacho? Kwanini Jeff?"
Sabrina nae alijiona akijiinamia na machozi kumtoka kwani aliweza kugundua ni jinsi gani Jeff anateseka na kuumia dhidi ya penzi lake.
Jeff alirudi kwao moja kwa moja na kuelekea chumbani kwake.
Akamkuta Dorry akiwa pale pale kitandani, ila muda huu alikuwa amelala kwa kujibidua.
Jeff alimtazama Dorry kwa huruma kwavile hakuwa na mapenzi naye kabisa.
Alisimama kwa muda kidogo akimtazama pale kitandani.
Dorry naye kamavile alihisi kuwa kuna mtu anamtazama kwani alizidisha manjonjo yake maradufu pale kitandani ili tu amvutie Jeff hata ashawishike kumgusa ila Jeff alisimama tu akimtazama na zile harakati zake.
Kama kuna watu huwa hawakati tamaa basi Dorry alikuwa namba moja kwani hakujali chochote kile zaidi ya kufanya mambo ya kumshawishi Jeff.
Jeff naye akasogea pale kitandani na kuwa kama anamshtua Dorry kutoka usingizini kwani alijifanya kuwa ameshalala.
Dorry alikaa sasa na kuanza kumpapasa Jeff kwa taratibu,
"Dorry, sijakwambia unipapase ila nimekuamsha ili unisikilize"
Dorry akatulia kwa taratibu na kuanza kumsikiliza, ambapo Jeff alimuuliza swali Dorry,
"Ushawahi kupenda Dorry?"
"Ndio na nimekupenda wewe"
"Sina kazi, sina pesa, sina chochote kile. Kwanini unipende mimi?"
"Upendo wa dhati hauangalii hayo, nakupenda wewe kama wewe bila ya kujali hali yako"
"Niambie kwanza, kwanini unipende mimi?"
"Wewe ni kijana mzuri Jeff, unavutia sana. Nina uhakika ni wengi wanatamani kuwa na wewe ila mimi nimekupenda"
"Kitu gani ambacho unaweza kukifanya ili kunidhihirishia mimi kuwa unanipenda?"
"Nataka kukupa mapenzi yangu Jeff, mapenzi ambayo hata utakapokuwa huko utanikumbuka kwa siku zote"
"Mapenzi hayo umewapa wangapi wanaokukumbuka hadi leo?"
Dorry akakaa kimya kidogo kisha akamjibu,
"Sijawahi kumpa yeyote mapenzi kama haya ninayotaka kukupa wewe, nataka uyapate wewe tu. Sababu nakupenda"
Jeff akamtazama Dorry kwa karibu zaidi, akainuka mkono wake na kumshika Dorry kwenye shavu, kitendo ambacho kilimfanya Dorry atazame chini, kisha Jeff akamuuliza,
"Kweli?"
"Ndio ni kweli Jeff"
Jeff akamkumbatia Dorry na kumwambia,
"Asante sana Dorry, nashukuru kwa majibu uliyonipatia"
Dorry sasa akajipa tumaini kuwa tayari amempata Jeff kwani alionyesha wazi kukubaliana na hisia zake.
Jeff alipomuachia Dorry pale, alikaa kama dakika mbili akimtazama kitu anachotaka kukifanya.
Akamuona Dorry akijisogeza kwenye mwili wake, kisha akalaza kichwa chake kwenye bega lake na kutoa sauti ya taratibu kabisa,
"Nakuomba Jeff, naomba leo hii nikutunuku zawadi hii"
Jeff akasimama na kusogea karibu na dirisha, kisha Dorry akanyanyuka na kwenda nyuma yake.
Akapitisha mikono yake nyenye kiuno cha Jeff kisha akalaza kichwa chake kwenye mgongo wa Jeff na kumwambia tena,
"Tafadhari mpenzi ikubali zawadi yangu"
"Tatizo nimeshatunukiwa tayari"
Dorry akashangaa, na kuzunguka mbele ya Jeff na kumuuliza kwa makini,
"Na nani?"
"Na mwanamke wa maisha yangu"
Dorry akapumua kidogo, kisha akaongea kwa utaratibu,
"Hawezi kuwa amekupa kama ambavyo nitakupa mimi, tafadhari Jeff na kamwe hutojutia siku ya leo katika maisha yako kwani itakuwa ni siku yenye kumbukumbu kubwa sana"
Jeff akageuka na kumpa mgongo tena Dorry na kumwambia,
"Nampenda sana huyo mwanamke, nampenda kuliko ninavyojipenda mwenyewe. Ni yeye pekee mwenye kumbukumbu tosha juu yangu"
Kisha akamgeukia tena Dorry na kumwambia,
"Pole Dorry kwa kumpenda mwanaume ambaye tayari anampenda mwanamke mwingine"
"Inamaana maswali yako yote yale juu yangu yalikuwa na maana gani?"
"Hayakuwa na maana kwako ila kwangu yalikuwa na maana kubwa sana. Nilikuuliza na ukanijibu, ingawa najua wazi kuwa majibu mengine umeyaweka ili kunivuta ila majibu yako hayo yamenipa moyo kwa yule nimpendae kwani yameendana na matendo yake. Pole sana Dorry"
Dorry alikaa kimya na kumuangalia Jeff huku akimuona kuwa ni mwanaume mwenye roho mbaya sana.
Kisha Jeff akatoka mule chumbani na kwenda kulala sebleni kwao.
Dorry aliumia sana moyo wake, akaona wazi yote hiyo ni kutokana na jina la mwanamke alilolisikia mwanzoni.
Jina hilo likamjia kuwa ni Sabrina.
Dorry akaona ni vyema amuachie Sam barua ya ukumbusho kwa yote aliyoyagundua kupitia yeye.
Sabrina hakuweza kulala tena tangu muda ule alipoondoka Jeff kwani alianza kuuona umuhimu wa Jeff katika maisha yake.
Aliweza kuona upendo wa Jeff alionao katika moyo wake.
Akachukua karatasi na peni na kuanza kuandika barua ambayo alijisemea kuwa lazima atamkabidhi Jeff pindi tu atakapokuwa uwanja wa ndege kumuaga.
Aliandika ile barua kwa uchungu sana, kwani aliwaza jinsi ambavyo Jeff amekuwa karibu yake kwa mara zote.
Jinsi alivyokuwa akimfukuza ila bado Jeff alirudi.
Sabrina aliandika pia vile anavyojihisi juu ya Jeff, kisha akaifunga vizuri kabisa ile barua tayari kwa kumkabidhi Jeff akimuaga.
Asubuhi na mapema, Jeff aliweka mizigo yake tayari kwaajili ya safari.
Wakiwa pale nyumbani, Dorry alienda karibu na kumkumbatia Jeff, kisha akaweka kitu kama barua kwenye koti alilovaa Jeff.
Kisha akamwambia,
"Nitakukumbuka sana Jeff, wewe ni mwanaume shujaa na jasiri. Nitakupenda siku zote, namuomba Mungu anisaidie nipate mume kama wewe"
Jeff naye akamkumbatia na kumshukuru kwa kumuelewa.
Muda ule Dorry naye akawaaga kwavile alikuwa anarudi Bagamoyo kwenye kazi yake, kwahiyo akaondoka pale bila hata ya kumwambia Jeff kama kuna barua ameiweka kwenye koti lake.
Sam alifika kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina ameshajiandaa tayari, kisha wakaondoka pale na kumfata Jeff na mama yake tayari kwa safari ya kwenda uwanja wa ndege.
Gari iliondoka pale wakiwa kimya kabisa, ilionyesha wazi kuwa kila mmoja alikuwa na mawazo yake binafsi.
Walipofika uwanja wa ndege wakashuka, muda nao ulikuwa umekaribia.
Moja kwa moja, Sabrina akaenda na kumkumbatia Jeff kama ishara ya kumuaga.
Alipokuwa amemkumbatia, akaichomeka ile barua yake kwenye koti la Jeff tena bila ya kumwambia chochote. Ila Jeff aliongea kwa sauti ya kunong'oneza kwenye sikio la Sabrina,
"Nakupenda sana Sabrina"
Kisha akambusu pale pale sikioni, busu ambalo lilisisimua mwili wote wa Sabrina.
Kile kitendo cha Sabrina kuchomeka barua kwenye koti la Jeff, kilionwa na Sam ila alitulia tu akiusoma ule mchezo.
Kisha Sakina nae akaenda kumkumbatia mtoto wake kama ishara ya kumuaga ila alijikuta akishikwa na mambo mawili kwa pamoja.
Kwanza furaha ya mwanae kwenda kusoma nje ya nchi na pili uchungu kwani atakuwa mbali na mwanae aliyemzoea.
Alijikuta akitokwa na machozi, hivyo Sabrina akamvutia kwa pembeni kumbembeleza kidogo.
Muda huo Sam nae akamkumbatia Jeff kumuaga, kisha akaichomoa ile barua kwenye lile koti la Jeff.
Walipomaliza kumuaga, Jeff aliingia kwenye uwanja sasa na kuwapungia mkono kuwaaga.
Hawakuwa na la kufanya pale nje, badala yake walipanda kwenye gari kisha Sawa akawarudisha wote nyumbani.
Alianza na Sakina kisha akamalizia na Sabrina, ila leo hakukaa kwa wakina Sabrina kwani muda huo huo aliaga na kuondoka.
Moja kwa moja Sam akaenda nyumbani kwake kwani alikuwa na hamu ya kujua kilichoandikwa na Sabrina kwenye ile barua.
Alitamani sana kujua kuwa Sabrina kamuandikia mambo gani Jeff.
Aliifungua ile barua na kuanza kuisoma, ila kila alipozidi kuisoma aliona wazi mapigo yake ya moyo yakienda kasi.
Alifungua ile barua na kuanza kuisoma, ila kila alipozidi kuisoma aliona wazi mapigo yake ya moyo yakienda kasi.
Sam alizidi kuisoma ile barua huku mapigo yake ya moyo yakiendelea kuwa na kasi ya ajabu.
Ikafikia kipindi hata akajiona kuwa anashindwa kupumua vizuri sasa mpaka pale alipofika mwisho wa ile barua ndio akaweza kuhema.
Barua ile iliandikwa,
"Kwako Jeff mpenzi,
Umekuwa ni mwanaume wa pekee sana kwangu.
Katika maisha yangu yote, nakiri wazi kukupenda wewe. Tena nakupenda sana hadi najishangaa, hakuna mwanaume yeyote nitakayeweza kumpenda katika dunia hii kama ninavyokupenda wewe.
Umekuwa ni mwanaume wa pekee sana, najua kwa mwanamke yeyote anayejielewa ni lazima atamani kuwa na mwanaume wa dizaini yako.
Napendwa na wengi ila moyo wangu umekuchagua wewe.
Nakumbuka ile siku niliyokuwa nakulazimisha tusex halafu ukakataa, niliumia sana ila umeweza kunidhihirishia kuwa huyo mwanamke uliyenaye ni kweli unampenda tena kwa dhati, napenda kukupongeza kwa hilo.
Kwa kifupi mimi ni mjamzito yani kuna jamaa amenipa mimba ila mimi simtaki, kwahiyo nilipokuwa nakulazimisha tusex nilitaka kukusingizia huu ujauzito.
Nimeamua kuwa mkweli baada ya wewe kunionyesha msimamo wako.
Mpende huyo Sabrina na pia huyo Sabrina akupende naye kwa kiasi kile kile.
Nakutakia safari njema na maisha mema.
Ni mimi mpenzi wako wa kudumu Dorry"
Sam ndio alikopumua kwenye jina la Dorry, kisha akairudia rudia kuisoma ile barua kanakwamba mwanzoni hakuielewa.
Akajiuliza mwaswali kuwa alimuona Sabrina akiweka ile barua kwenye koti la Jeff, sasa iweje hiyo barua kuwa imeandikwa na Dorry? Hakupata jibu kabisa, kisha akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Dorry ili waweze kuonana na kuzungumza.
Kisha akajiandaa kwaajili ya kumfata Dorry mahari alipomuelekezea.
Sabrina alikuwa ametulia chumbani kwake akimuangalia mtoto wake.
Mara kidogo akasikia simu yake inaita, Sabrina akaivuta na kuipokea
"Sabrina, uko wapi?"
"Nipo nyumbani, kwani kuna tatizo lolote?"
"Hamna tatizo nimeuliza tu"
Kisha Sabrina akashangaa na kujiuliza kuwa kwanini Sam amemuuliza vile?
Moja kwa moja akajiwa na mawazo mabaya kuhusu Sam, na kuhisi kuwa huenda anamwanake nyumbani kwake ndiomana anamuuliza kabisa alipo.
Sabrina akakaanza kufikiria mengine kwanza kabla ya kuchukua maamuzi yake ambayo hupenda kuyachukua.
Sam akaondoka pale nyumbani kwake na kwenda moja kwa moja mahari alipo Dorry.
Wakasalimiana, kisha akamuuliza Dorry maswali mawili matatu kabla ya kumuuliza kuhusu ile barua.
"Nilijua umeshaenda Bagamoyo, mbona bado upo?"
"Bagamoyo nitaenda kesho"
"Sasa mbona uliondoka mapema bila ya kumsindikiza Jeff uwanja wa ndege?"
"Roho ilikuwa inaniuma sana, sikuwa tayari kumuona Jeff akiondoka. Kwani nampenda sana"
Basi Sam akamuomba Dorry waende naye nyumbani kwake ili wapate kuzungumza kidogo.
Dorry akakubali, hivyobasi wakaanza safari ya kwenda nyumbani kwa Sam, ambapo njiani ndio Sam akampigia simu Sabrina ili kujua mahari alipo.
Sabrina naye akaendelea kuwa na mashaka kwa swali la Sam juu ya alipo, hivyobasi kama kawaida yake akapatwa na wazo la kujiandaa ili aende kwa Sam akajishuhudie mwenyewe kwa macho yake kile anachokihisi.
Sam alifika na Dorry nyumbani kwake na kuanza kuzungumza nae maswali mawili matatu,
"Hivi kweli unampenda Jeff wewe?"
"Ni kweli nampenda hata siku ile ulipokuja kunichukua kule Bagamoyo nilikwambia kuhusu hilo"
"Sasa kwanini hukuitumia ile nafasi kuonyesha upendo wako nilivyokupeleka kwao?"
Dorry akainama chini kwani alikuwa akifikiria kidogo kama amdanganye Sam au amwambie ukweli, ambapo Sam nae akamshtua kwa kumwambia,
"Niambie ukweli tu hata usiogope kwani nimekuita ili nikusaidie kama mdogo wangu"
Kisha akainua kichwa chake na kuanza kumuelezea,
"Ngoja nikwambie ukweli tu kaka yangu. Kwakweli Jeff nampenda sana, lakini sikubahatika kulala nae hata siku moja tangia ile siku uliyonipeleka pale kwao, ingawa mama yake anaamini kuwa nilikuwa nalala na mwanae"
Sam akamuuliza Dorry,
"Unamfahamu Sabrina?"
Dorry akashtuka na kumuangalia Sam kwa uoga, kisha akamjibu
"Hapana simfahamu"
Sam naye akamuangalia kwa jicho la udadisi kidogo, kisha akamuuliza tena,
"Nani ulimpa barua ili ampe Jeff wakati anaondoka?"
"Sikumpa mtu yeyote barua ila nilimuwekea Jeff barua kwenye koti lake kabla hajaondoka"
Sam akaitoa ile barua na kumuuliza kama ndio yenyewe,
"Ndio hii?"
Dorry akaichukua na kuisoma kidogo na kugundua kuwa ndiyo barua yake aliyomuwekea Jeff hata akashangaa kuwa imefikaje kwa yule Sam.
Na kutokana na kitu alichoandika akajikuta akiona aibu na kuinama chini, ambapo Sam alimwambia kuwa amweleze ukweli wote wa kuhusu ile barua kwani alitaka kujua pa kuanzia.
Dorry naye akaamua kuelezea ukweli tu kwani hakuwa na uwezo wa kuficha tena kitu ambacho kipo wazi kabisa.
Dorry alielezea huku akiwa na simanzi kabisa, alipomaliza kuelezea Sam akamwambia,
"Usijali Dorry nitakusaidia"
"Sasa utanisaidiaje?"
"Ilimradi hii barua haijafika kwa muhusika, basi ukweli tutabaki nayo siye wawili"
"Unamaana gani?"
Sam akampanga Dorry kusema kuwa anamimba ya Jeff, na kwavile mama wa Jeff anaamini kuwa Dorry alipatana na Jeff ingawa Jeff hakumtaka basi atumie nafasi hiyo kudanganya kuwa ile mimba ni ya Jeff.
"Unamaana gani kaka? Yani nimsingizie mwanaume ambaye sijawahi hata kulala nae?"
"Nani anayejua kama hujawahi kulala nae? Hiyo inabaki kuwa ni siri yako, si unajua Jeff kaenda nje kusoma yani si wa kurudi leo wala kesho sasa wasiwasi wako wewe wa nini ikiwa hata aliyekupa hiyo mimba kweli amekataa, wewe danganyishia huku ili upate msaada wa kulelewa mtoto wako.
Dorry akachekecha akili yake na kuona kuwa anaambiwa jambo la maana sana ukizingatia litamsaidia yeye na mtoto wake bila kujua kuwa Sam anamaana yake katika kumsaidia juu ya swala hilo.
Muda kidogo akawasili Sabrina pale nyumbani kwa Sam na kumfanya Sam ashangae,
"Khee mke wangu, me si nilitaka leo upumzike ili kesho nije nikuchukue na mtoto!"
Sabrina alikaa na kumuangalia Sam kisha akamuuliza kwa kumnyoshea mkono Dorry,
"Na huyo ni nani?"
"Kwani humjui kumbe! Huyu anaitwa Dorry, kuna kipindi tulikuwa Bagamoyo tukaonana nae hotelini, ni mpenzi wa Jeff"
Moyo wa Sabrina ukalia pa, kwani alianza kumkumbuka huyu mdada ila hakutaka kusema kingine zaidi ya kuuliza tu,
"Na mbona yupo hapa kwako?"
"Unajua huyu alikuwa pale kwakina Jeff kama siku tatu hizi, leo asubuhi akaagana na Jeff kwani alikuwa anarudi Bagamoyo ila akazidiwa njiani ndio wasamalia wema wakaona namba yake kwangu na kunipigia. Kufika pale nikamchukua na kumpeleka hospitali na kurudi nae hapa, kisha nataka nimpeleke kwa Sakina ndiomana nimekuuliza ulipo ili kama upo nyumbani nikitoka tu kwa Sakina nipitie"
Sabrina alimuangalia Sam na kuona kamavile anapigwa changa la macho ila alikubaliana nae tu kwani hakuwa na la kumbishia.
Kisha Sam akawaomba wainuke ili waende kwa Sakina kumpeleka huyo Dorry.
Sabrina alikubali ingawaje moyo wake bado ulikabiliana na maswali ya kila aina.
Safari ikawa moja kwa moja hadi nyumbani kwa Sakina ambapo jioni ilikuwa tayari imeshaingia ila Sakina aliwapokea na kushangaa ujio wa Dorry ambaye aliaga asubuhi kuwa anaondoka.
Sam akamuelezea Sakina kamavile alivyomuelezea Sabrina, na kumfanya Sakina aulize,
"Kwahiyo amekutwa na mgonjwa gani?"
"Walimpima juu juu tu, itabidi kesho au kesho kutwa uende nae hospitali wakampime vizuri maana walitoa majibu kuwa haumwi wakati mtu alianguka mbele za watu"
Sakina akampa pole sana Dorry na kumpeleka chumbani kwa Jeff ili akapumzike kwanza bila kujua kuwa ile ni mipango ya Sam tu akiwa na malengo yake binafsi.
Ila Dorry alimshukuru sana Sam kwa kumsaidia vile kwani ile barua kama ingefika kwa Jeff basi asingeweza kufanya vile kwani ukweli wote ungekuwa peupe.
Akamuona Sam kuwa ni mtu mwenye upeo upana sana kwani hata maneno yakf ni maneno yakiyopangiliwa vyema.
Kisha Sam na Sabrina nao wakamuaga Sakina na kuondoka hadi nyumbani kwa wakina Sabrina ambapo Sabrina alionekana kama kuwa na mawazo hivi,
"Mbona waonekana kuwa na mawazo Sabrina?"
"Hapana Sam, sina mawazo ila nafikiria tu kesho tunavyokuja na mwanangu kwenye makazi mapya"
"Sasa si ndio mawazo hayo, tena yale ni makazi mapya kwa mtoto na sio kwako kwavile wewe umeshapazoea tayari. Nyumba yako ile"
Sabrina alitabasamu kumuonyesha Sam kuwa amefurahia ingawaje moyoni mwake wala hana furaha.
Kisha Sam naye akamuaga na kuondoka.
Sabrina sasa akapata upenyo wa kufikiria, mawazo yake yote yalikuwa kwa yule binti aliyeitwa Dorry kwani alimuona kamavile ni kizuizi kati yake yeye na Jeff.
"Inakuwaje Jeff aseme hamtaki yeyote halafu awe na yule binti? Inawezekana kweli? Labda inawezekana kwamaana sijui nyuma ya pazia kuwa Jeff alikuwa na mawazo gani"
Sabrina alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.
Sam naye akiwa nyumbani kwake, akawaza jinsi mpango wake utakavyozaa matunda kwani ni dhahiri pale Dorry atakapotangaza kuwa na ujauzito wa Jeff basi Sabrina ataumia moyo na kumchukia Jeff, na hapo ndipo atakapoweza kufurahia mapenzi yao hata Jeff akirudi hatakuwa na nguvu tena dhidi ya Sabrina.
Sam alijiona kuwa ni mtu mwenye akili sana kwani ameweza kupanga mpango wenye matunda katika maisha yake, ila kitu pekee kilichomnyima raha ni ile barua aliyoona kuwa Sabrina kamuwekea Jeff, kisha akajipa matumaini kuwa itakuwa ni mawazo yake tu kwani barua aliyoipata ilikuwa ni msaada mkubwa kwake kushinda ile barua iliyoenda.
Kisha akaenda zake kulala ili kupoteza mawazo.
Wakati Sam amelala, akajiwa na ndoto.
Akajiona amekutana na mtu ambaye hakumfahamu, yule mtu alimuita kwa ishara na kumfanya aende.
Alipofika, yule mtu akamuuliza,
"Hadi lini utalea watoto ambao sio damu yako?"
Sam alikuwa amesimama tu, akaonyeshwa upande wa pili akaona damu nyingi sana kisha yule mtu akamuuliza,
"Je tuwatoe sadaka ya damu?"
Sam akawa kama anataka kukubali huku yule mtu akicheka.
Sam akashtuka usingizini na kusema kwa nguvu,
"Nooooo....."
Jasho jingi lilikuwa likimtoka, akakaa na kujiuliza kuwa ile ndoto inamaana gani hakupata jibu.
Alifumba macho yake kwa dakika mbili na kusema,
"Mungu nisaidie"
Kisha akavuta shuka lake na kulala tena.
Kulipokucha, asubuhi na mapema Sam aliamka na kujiandaa kwenda kwakina Sabrina kwanza ili waje waishi nae pale nyumbani.
Alipofika kwakina Sabrina alimkuta mama wa Sabrina akiwa nje kufanya usafi. Baada tu ya salamu, mama wa Sabrina akaanza kumueleza,
"Yani usiku wa jana bado kidogo tu tukupigie simu uje"
"Vipi tena mama, nini tatizo?"
"Yani mtoto alizidiwa jana usiku balaa ila ilikuwa ni kwa muda mfupi tu kwani sasa hivi anaendelea vizuri kabisa."
Sam akaenda moja kwa moja chumbani kwa Sabrina ili kuangalia hali ya mtoto wao, ambapo Sabrina naye akamwambia yale yale aliyoambiwa na mama mkwe wake.
"Kwani ilikuwaje hadi mtoto azidiwe?"
"Hata naelewa basi, ilikuwa ghafla tu yani na muda huo huo mimi pia nikaumwa na tumbo balaa"
Sam akawapa pole sana na kumtaka Sabrina afanye juu chini akapime,
"Huenda una malaria au typhoid, itabidi ukapime mke wangu na mtoto nae tukampime."
Wakakubaliana kwenda wote hospitali kupima kwanza kwani ile hali ya usiku hata Sabrina akajikuta akijihisi kuwa ana malaria.
Walienda moja kwa moja hospitali kupima, ambapo alipimwa mtoto kwanza na kukutwa akiwa hana tatizo lolote na kufanya hata wao wamuulize daktari,
"Sasa mbona alizidiwa sana usiku?"
"Inawezekana ni homa za mshtukizo tu"
Kisha akapimwa na Sabrina, naye akaonekana kuwa hana tatizo lolote.
Ila wakati wanaondoka daktari akamuita tena Sabrina na kumwambia,
"Ingawa vipimo vimeonyesha kuwa huna maradhi yoyote, ila pia tumeona kuwa wewe ni mjamzito"
Sabrina akashangaa,
"Mjamzito!!"
Sam nae akawasikia na kuwafata pale walipokuwa.
"Ingawa vipimo vimeonyesha kuwa huna maradhi
yoyote, ila pia tumeona kuwa wewe ni mjamzito"
Sabrina akashangaa,
"Mjamzito!!"
Sam nae akawasikia na kuwafata pale walipokuwa.
Kisha Sam akamuuliza daktari kamavile mtu ambaye hajasikia vizuri na anahitaji kujua kinachoendelea,
"Unasemaje daktari?"
Daktari akamuangalia Sam na kumwangalia Sabrina, lile jicho la Sam likamtisha daktari na kumfanya ajiume ume ukizingatia muda huo Sam alikuwa kambeba yule mtoto wao mdogo mikononi mwake.
Sam akazidi kumuangalia daktari kwa jicho la mshangao.
Daktari akbmua kujibu kwa kujiuma uma,
"Sikuwa na nia mbaya jamani ila nilikuwa namwambia mkeo hapa kuwa akija safari nyingine basi tujaribu kuangalia na swala la ujauzito"
"Unamaanisha kwamba mke wangu ni mjamzito?"
"Hapana simaanishi hivyo, ila kwakuwa hatujamkuta na ugonjwa wowote ndiomana nikamwambia kuwa inawezekana ikawa hivyo"
"Kwahiyo kwakuwa mtoto wetu naye hamjamkuta na ugonjwa wowote je inamaana naye ni mjamzito?"
"Hapana sina maana hiyo, itakuwa umenielewa vibaya tu mzee wangu. Sina maana mbaya, nawatakia safari njema"
Daktari akaanza kurudi ofisini kwake na kuwaacha pale Sam na Sabrina kisha nao wakaondoka.
Wakiwa ndani ya gari, Sam akaanza kuongea.
"Hivi yule daktari ana kichaa nini?"
"Hata mi mwenyewe namshangaa, lazima atakuwa na kichaa tu. Yani mimi nina mtoto mdogo tena bado nanyonyesha, halafu lenyewe linaibuka pa kuibukia eti utakuwa mjamzito. Yani kanichefua kweli natamani hata kumtapika"
"Achana nae chizi yule, wengine wapo mafunzoni tu yani sio madaktari wala nini, wapo wapo tu hata hawajielewi na pia hawatambui wanachokisema. Yani pale nilitamani hata kumnasa makofi"
Wakajikuta wakimlaani yule daktari tangia mwanzo wa safari yao hadi pale walipofika nyumbani kwa wakina Sabrina. Ambapo Sam akamuuliza Sabrina,
"Vipi tuondoke leo kwenda nyumbani au kesho?"
"Hata leo ni sawa"
"Hapana, acha iwe kesho. Asubuhi nitaenda ofisini halafu jioni nitakuja kuwafata ila uwe umeshajiandaa tayari na mtoto"
"Sawa hakuna tatizo basi juu ya hilo"
Wakakubaliana pale, kisha wakaingia ndani na muda huo huo Sam naye akaaga na kuondoka.
Sabrina akaitwa na mama yake, kisha akaanza kumuuliza kuhusu hali ya mtoto.
"Hata haumwi chochote, hawajamkuta na ugonjwa wowote"
"Mmh! Na wewe je?"
"Eti na mimi siumwi chochote"
"Sasa ile usiku ni ugonjwa gani ule mwanangu?"
"Hata mimi sielewi mama, ila nadhani daktari mwenyewe tuliyemkuta ni kimeo"
"Hapana mwanangu, inawezekana wamekuroga maana ugonjwa wa kurogwa huwa hauonekani hospitali"
"Mmh mama, huyo wa kuniroga kipindi hiki ni nani?"
"Dunia hii mwanangu, walimwengu wabaya unafikiri wanafurahia kuona umeolewa na unafurahia ndoa yako! Watu wabaya sana mwanangu"
Sabrina akakubaliana na mama yake kuwa yawezekana amerogwa kwani ugonjwa wa haraka vile uliwafanya waamini hivyo.
Sam alirudi nyumbani kwani na kuwa kama mtu anayetafakari kidogo juu ya Sabrina na mtoto wao.
Muda kidogo simu yake ya mkononi ikaanza kuita, kuangalia akaona ni namba ngeni na kuipokea,
"Nani mwenzangu?"
"Neema anaongea hapa"
"Neema! Neema yupi?"
"Mmh Sam, kila siku nafanya kazi ya kukuelekeza. Mi ni yule Neema niliyepigwa na mkeo hapo nyumbani kwako"
Sam alicheka kidogo kwavile alishamkumbuka tayari,
"Aah samahani, sikutunza namba yako ndiomana imekuwa ngumu kukutambua"
"Usijali Sam ila nina shida kidogo na wewe"
"Shida gani?"
"Kama hutojali naomba kesho tuonane"
Sam akakubali kwavile anapenda sana kusikiliza shida za watu.
Sakina alitulia na Dorry ndani kwake,
"Kwahiyo Bagamoyo utaenda lini?"
"Najiangalia tu hali halafu nitaondoka, inamaana hutaki kuniona tena mama!"
"Hapana, sina maana hiyo ila nakuhofia kwenye kazi yako"
"Usijali, nadhani kesho au kesho kutwa nitaondoka"
Muda kidogo Dorry akaenda jikoni, kama dakika tano kupita akaita kwa nguvu,
"Mamaaaaa......"
Sakina akakimbilia jikoni na kumku ta chini yani akiwa ameanguka.
Hivyo akaanza kumpepea na kumpa huduma ya kwanza pale chini.
Muda kidogo Dorry akainuka huku akilalamika kuwa kichwa kinamuuma sana,
"Itabidi twende hospitali Dorry"
Dorry alikubali pale, kisha Sakina akampigia simu dereva wa gari za kukodi ili awafuate pale na kuwapeleka hospitali.
Walifika hospitali na kisha Dorry akapimwa, wakati wa kusoma majibu daktari akamuuliza Dorry,
"Je nikupe majibu mbele ya huyu dada au atoke?"
Sakina akataka kutoka nje ila Dorry akamzuia, kisha akamwangalia daktari na kumwambia,
"Nipe tu hayo majibu, huyu ni mama mkwe wangu kwahiyo ni kama mama yangu. Yani ndio msaada wangu na mshauri wangu kwahiyo nipe tu hayo majibu kwani yeye ndio atanisaidia kwa hali yoyote ile"
Sakina alikaa na kuona kweli mkwe amepata, kwajinsi alivyomthamini hapo akaona kweli Dorry anastahili kuwa mke wa mtoto wake.
Basi daktari naye akatabasamu na kuwaambia,
"Basi hongereni"
Sakina na Dorry wakaangaliana, kisha Sakina akauliza kwa shauku,
"Hongera ya nini docta?"
"Mkweo ni mjamzito"
"Wow docta kweli?"
"Ndio ukweli huo, vipimo vimeonyesha hivyo"
Sakina alimuangalia Dorry na kumkumbatia kwa furaha huku akimpa asante za mfululizo.
"Asante Dorry, hatimaye nampata mrithi wa Jeff. Uuh Mungu mkubwa sana, natamani hata nipige kelele ili ulimwengu wote ujue furaha yangu."
Kisha wakamuaga daktari huku wakiondoka kwa furaha sana.
Sakina bado aliiendeleza furaha yake hadi nyumbani, akatamani ampate wa kwenda kumwambia furaha yake hiyo.
"Nitaenda kumwambia Sabrina, ila atanishushua tu najua"
"Kwani huyo Sabrina ni nani na kwanini akushushue mama?"
Dorry alimuuliza Sakina naye akamjibu,
"Sabrina ni kama ndugu yangu, ni mdogo wangu. Mambo mengi nashauriana nae, ndio yule mke wa Sam"
"Hapo nimemfahamu, na kwanini akushushue ukimwambia?"
"Kuna kipindi Sabrina aliniambia kuwa Jeff kampa mimba mtoto wa mwanajeshi ila sikufatilia. Kwanza nahisi mwanangu alisingiziwa tu. Ila hapa kwako sasa, yani mi namngoja mjukuu kwa hamu zote"
Dorry alikuwa akitabasamu tu kwani siri yake alikuwa nayo moyoni mwake mwenyewe.
Kulipokucha, Sam akajiandaa na kwenda ofisini kwake siku hiyo na kuwafanya wafanyakazi wake wafurahi na kupeleka malalamiko yao kwa urahisi kwani kwa siku za nyuma alionekana kuwa na mambo mengi sana yaliyomfanya wakati mwingine ashindwe hata kufika ofisini kwake.
Akapanga panga mambo yake ili aweze kumsikiliza mfanyakazi wake mmoja baada ya mwingine.
Muda kidogo akatumiwa ujumbe kwenye simu yake,
"Ule mpango umekamilika, jana tulienda hospitali na kupimwa. Mama kafurahi sana kusikia nina mimba ya Jeff.
Ni mimi Dorry"
Sam akatabasamu kisha akaiweka simu yake, ila kabla hajageuka upande wa pili ikaanza kuita.
Alipoangalia akaiona ile namba ya Neema, na kuipokea.
"Naomba tuonane basi Sam tafadhari sana nakuomba"
"Hakuna tatizo, tutaonana tu. Nisubiri baada ya masaa mawili"
Kisha akaikata ile simu na kuendelea na kazi yake.
Muda kidogo Sam akaenda kuonana na Neema kwaajili ya mazungumzo na kumkuta eneo lile lile walilopanga kuonana,
"Haya Neema nimeitikia wito"
"Kabla ya yote naomba nikuulize"
"Niulize tu"
"Eti Sabrina ameshawahi kuwa na mahusiano na Francis pamoja na Fredy kwa wakati mmoja?"
"Ndio ulichoniitia hapa Neema?"
"Hapana ila nimeuliza tu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Basi nenda kamuulize yeye mwenyewe"
"Samahani lakini, je amewahi kuwa na mahusiano na mkaka wa kuitwa Japhet na badae akawa na John?"
"Hivi wewe Neema una akili timamu kweli? Nimekwambiaje kuhusu hayo maswali?"
"Ila sina nia mbaya Sam, nina maana kubwa sana na haya maswali ambayo nimekuuliza"
"Laiti kama ningejua umeniitia huu upuuzi kwakweli nisingekuja kabisa"
Kisha Sam akainuka na kuondoka.
Akamuacha Neema pale akimuangalia tu anavyotokomea, kisha akajisemea.
"Hapo nimemuuliza maswali ya kumuhusu mkewe, je ningemuuliza ya kumuhusu yeye ingekuwaje? Nadhani asingeongea nami milele yote"
Kisha nae akainuka na kuondoka eneo lile.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment