Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MISS TANZANIA - 2

 








Simulizi : Miss Tanzania

Sehemu Ya Pili (2)







Candy alishirikiana na mabinti wa urembo wenzake katika kuwafariji watoto yatima walioenda kuwatembelea pale kwenye kituo cha kulelea mayatima kilichokuwa huko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar. Ingawa alionana tena na Tunis, hakukuwa na kituko chochote kilichojiri baina yao.Hiyo ilitokana na Candy kujiweka mbali naye kadiri alivyoweza, huku akijichanganya na warembo wengine. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari walihudhuria na kupiga picha kadhaa za matukio ya warembo wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa uongozi wa kituo kile, na pia wakicheza na wale watoto yatima.

Akiwa katika harakati za kuwasukuma baadhi ya wale watoto kwenye bembea huku wakiimba, Candy alishtushwa na mmoja wa wale watoto yatima aliyekuja na kumpa kipande cha karatasi. Alipokea kile kipande cha karatasi huku akitabasamu akiamni kuwa ni yule mtoto apataye miaka minne hivi ndiye aliyekiandika, lakini uso wake ulibadilika ghafla na akawa makini maradufu pale alipoona kile kilichoandikwa kwenye ile karatasi. Kwanza muandiko haukuwa wa mtoto wa miaka minne, bali ni wa mtu mzima, na pili kile kilichoandikwa kwenye ile karatasi kilikuwa kimekusudia na kufanikiwa kumkosesha amani kabisa.

“Na..nani kakupa hii karatasi, mtoto?” Alimuinamia na kumuuliza yule binti mdogo huku macho yakimtembea na moyo ukimwenda mbio.

“Yule anko paleeee!” Binti alimjibu huku akigeuka na kuoneshea kwa kidole, lakini hapo naye uso wake ukasajili butwaa la kitoto.

Candy alipotazama kule alipoelekezwa na yule mtoto hakuona mtu yeyote.

“Al…alikuwa pale…” Mtoto alisema kwa mashaka.

Candy aliinuka na kuelekea kule alipoelekezwa na kuona watoto tu wakiwa na baadhi ya ma-miss wenzake, lakini hakukuwa na mtu mwingine asiyetakiwa kuwa pale.

Alihamanika.

Akageuka kule kwenye mkusanyiko wa waandishi wa habari, wake kwa waume, ambao walikuwa wakijiandaa kuondoka kuwahi kutoa machapisho yao.

Mwanadada wa urembo alichanganyikiwa na kumrudia yule binti.

“Ni mwanaume au mwanamke aliyekupa hii karatasi?” Alimuuliza.

“Mwanaume…” Mtoto alimjibu, na Candy akamshika mkono na kuongozana naye kuelekea kule kwenye kundi ma waandishi wa habari.

“Ukimuona tena si utamkumbuka?” Alimuuliza yule mtoto, naye akaafiki kwa kichwa.

“Okay, mtoto mzuri...hebu nioneshe ni nani basi katika hawa…” Alimwambia huku akitembea naye taratibu miongoni mwa wale waandishi wa habari waliokuwa katika harakati za kukusanya mabegi yao na kuondoka. Hapo mmoja wa wale waandishi wa habari alimpiga picha akiwa na yule mtoto.

“Hayupo…!” Mtoto alimwambia, na Candy akachanganyinyiwa.

Akachutama kilimbwende na kumuuliza yule mtoto huku akimtazama kwa makini usoni hali amefanya tabasamu la kumtia moyo ili mtoto asiogope, na hapo yule mwandishi akampiga picha nyingine.

“Una hakika mtoto mzuri? Hebu watazame tena, eenh?” Alimwambia kwa kubembeleza kisha akainuka.

Mtoto aliwatazama tena wale watu wazima waliokuwa pale, wengine wakiingia kwenye magari tayari kuondoka, na kutikisa kichwa.

“Hata hayupo tena!” Alisema huku akicheka kwa aibu.

Candy akazidi kuhamanika.

“Okay, mtoto mzuri…labda ameenda nyumbani kwao, eeenh?” Alimwambia huku akimnyanyua na kumbeba yule mtoto. Mwandishi akampiga picha nyingine, ambayo pia Candy hakuitilia maanani wala kuizingatia. Alirudi na yule mtoto hadi pale kwenye bembea na kumwacha na watoto wenzake, naye akarudi kujichanganya na warembo wenzake huku akili ikizidi kumzunguka kuhusu ule ujumbe alioletewa na yule mtoto kutoka kwa mtu asiyejulikana.



Ninajua kila kitu kilichotokea Magu, bibie.

Wasiliana nami kwa namba hii kama unataka niendelee kukutunzia siri yako.



Chini ya ujumbe ule kulikuwa kuna namba ya simu ya kiganjani ambayo hakuwa amepata kuiona kabla.

Magu!

Alichanganyikiwa.

Ni kweli aliwahi kuishi Magu, lakini ni lipi hilo alilolifanya huko hata liwe la siri?

Je huyu ndio yule jamaa mwenye pikipiki? Alijiuliza na akashindwa kujithibitishia hilo.

Sasa kama si yeye, ina maana kuna mtu mwingine tena zaidi yake na Jackie anayenisakama kwa mambo ambayo hata mimi mwenyewe siyajui?

Hakika mlimbwende alichanganyikiwa, na ni kwa neema za manani tu ndivyo alivyoweza kuikamilisha ile siku pale kwenye kile kituo cha watoto yatima.



***

Hatimaye mabinti walimaliza shughuli iliyowapeleka pale kwenye ile nyumba ya kulelea mayatima na kuingia kwenye basi kubwa la kifahari la Miss Tanzania ili kuanza safari ya kurejeshwa mjini.

Kutokea kwenye kimgahawa kimoja cha kienyeji kilichokuwa nje ya nyumba ile ya kulelea watoto yatima kule Chamazi, John Koccho alilitazama lile gari likiondoka taratibu eneo lile huku wale mabinti wa urembo, Candy miongoni mwao, wakiwapungia mikono ya kuwaaga wale watoto yatima waliojirundika nje ya geti la kituo kile.

Okay mrembo wangu…nasubiri simu yako sasa!

Alijiwazia huku akinywa soda aliyonunua kwenye ule mgahawa wa kienyeji.

Candy hakuipiga ile namba ya simu na aliazimia kutofanya hivyo asilani, liwalo na liwe. Alirudi nyumbani kwa Kokos akiwa mwingi wa mawazo na wasiwasi. Sasa alitamani kabisa kumweka wazi Bishkuku kuhusu yale mambo yaliyokuwa yakimtokea, lakini kwa namna moja kuna kitu kilikuwa kinamzuia kufanya hivyo.

Akidai kuwa amechoka, alipitiliza chumbani kwake na kujibwaga kitandani. Akiwa pale kitandani, alijaribu kuvuta kumbukumbu za maisha aliyokumbana nayo alipokuwa huko Magu kulipotajwa kwenye ule ujumbe wa kukanganya kutoka kwa mtu asiyemjua.

Kabla mawazo yake hayajafika mbali, Bishkuku alimgongea mlango na kumwambia kuwa kulikuwa kuna mgeni wake.

Candy alishangaa.

“Mgeni wangu?” Aliuliza.

“Khaswa!” Bishkuku alimjibu naye akazidi kushangaa.

Ni mgeni gani tena huyo aliyekuja kumfuata mpaka huku?

“Ni nani…na kapajuaje huku?” Aliuliza.

Badala ya kumjibu, Bishkuku aligeuka na kuondoka, na Candy aliinuka kumfuata huku akili ikimzunguka.

Alipofika sebuleni alimkuta binti mmoja mrembo akiwa ameketi na Bishkuku.

“Kutana na Juttie K, mwandishi wa habari maarufu wa maswala ya mitindo na urembo nchini, naye alikuwa anataka kukuhoji kidogo kuhusiana na kinyang’anyiro hiki cha Miss Ti-Zedi ulichokuwamo.” Bishkuku alimwambia huku akiachia tabasamu pana, na Candy akashusha pumzi za ahueni.



***

Siku mbili baadaye makala ya mahojiano yale yalitoka gazetini na kumnadi Candy kama yatima mwenye moyo wa upendo aliyeazimia kutwaa taji la Miss Tanzania. Zile picha alizopigwa na yule mwandishi wa habari kule kwenye kituo cha kulelea watoto akiwa amembeba yule mtoto zilitumika sana kuinadi azma yake ile.

“Heh Bishkuku…hizi picha nilipigwa saa ngapi?” Alimuuliza Bishkuku huku akiwa meshika gazeti lenye ile makala ya Juttie K.

“Yeah…nilihakikisha kunapatikana picha muafaka, na jamaa naona alifanya kazi nzuri sana.” Bishkuku alimjibu, na Candy akishangaa.

“Ina maana ulimtuma mtu aje kunipga picha?”

“Sasa kumbe ulidhani nini…hivi hivi tu mdogo wangu utakuwa huandikwi magazetini wala picha zako hazitoki magazetini…!”

“Heh!”

“Hizo ndio mbinu za mchezo hapa mjini mwanadada…! Mambo mengine tena unawachia majaji, lakini huku chini mbinu muhimu!” Bishkuku alimjuza na Candy akabaki akitikisa kichwa kwa mastaajabu huku akitabasamu.

Makala yale yalipokewa kwa mitazamo tofauti na Sanura Kashogi na GTZ, mahasimu wakubwa wa Bishkuku na Candy.

Kule Masaki, GTZ alilifinyanga like gazeti kwa hasira na kulitupia kwenye kapu la taka lililokuwa sebuleni kwake.

“Eti yatima mwenye moyo wa upendo…moyo wa upendo?” Alisema kwa hasira na kuachia msonyo mkali.

“Mnafiki mkubwa! Moyo wa upendo unaujua wewe? Basi subiri nikutie mikononi Kisonoko mkubwa we!” Alibwata na kubamiza meza pale sebuleni.



***



Siku mbili baadaye GTZ alikuwa ameegesha gari lake mtaani kwa akina Bishkuku naye akawa amesimama hatua chache mbele ya gari lile akiitupia macho ile nyumba ya akina Candy kwa hasira. Muda ulikuwa ni saa kumi za alfajiri, na alikuwa na imani kuwa kile kituko cha siku kadhaa zilizopita kilikuwa kimesahaulika. Ingawa hakuwa akitarajia kumuona tena yule binti akitoka nje peke yake muda ule, alikuwa ameenda tu ili angalau aweze kumuona yule hasimu wake muda atakaotoka. Safari hii aliamua kummaliza kwa namna yoyote ile hata ikibidi kumgonga gari.

Hivi anavyoendelea kujinadi magazetini namna hii, kuna uwezekano kuwa hata wale ambao hawakumuona hapo mwanzo nao wakamuona… na kuja kuniharibia azma yangu.

Alijiwazia kwa hasira.

Hakuamini kabisa pale ilipofika saa kumi na mbili kasoro alipomuona yule mrembo akitoka nje ya lango la ile nyumba aliyokuwa akiishi na kuanza kukimbia kimazoezi kuelekea kule alipokuwa, tena akiwa na nguo zile zile alizokuwa amevaa siku ile alipojaribu kumteka, akiwa amefunika kichwa chake na ile kofia iliyoungana na ile fulana yake ya mazoezi.

“Hah! Huyu binti kumbe mjinga sana, eenh? Leo sifanyi makosa…!” Alijisemea huku akirudi na kuingia kwenye gari lake. Kupitia kwenye kioo cha kuonea nyuma cha gari lile aliweza kumuona yule binti akizidi kulikaribia gari lake, akikimbia kimazoezi.

Alipoona yule binti amelifikia kabisa gari lake aliufungua kwa nguvu na ghafla mlago wa dereva na yule binti akajipamia vibaya, yowe likimtoka na akinguka chini. Haraka GTZ aliruka nje ya gari na kumkwida kwa nguvu kwa lengo la kumuinua na kumtupia ndani ya gari atimke naye, Lakini hapo akabaki amepigwa na butwaa.

“Hah! Nani wewe…?” Alijikuta akipayuka kwa mshangao pale alipojikuta akimtazama mwanadada mwingine kabisa, na akajua kuwa alikuwa amecheza pata potea.

Alimsukuma chini kwa nguvu yule mwanadada na kugeuka haraka kurudi kwenye gari lake, lakini hapo alijikuta akidakwa koo kwa mikono yenye nguvu, na akikabiliana na mtu mrefu mweusi aliyekuwa kwenye mavazi ya kimichezo kama yule dada.

“Tulia hivyo hivyo wewe!” Sauti nzito ilimwambia kwa ukali, na GTZ akamakinika kimakabiliano.

Haraka sana alitupa juu mikono yake kwa nguvu kwa lengo la kuipangua kutoka shingoni kwake ile mikono iliyomkaba, lakini Morandi alitaraji na alikuwa akisubiri tendo hilo, hivyo aliiachia ile shingo na mikono ya GTZ ikaambulia patupu naye akabaki akiwa amenyoosha juu mikono yake.

Morandi alimtandika ngumi nne nzito na za haraka haraka sana zilizotua kwenye solar plexus, sehemu ambapo kifua chake kilikuwa kinaishia na tumbo lake linaanzia. Hii ni sehemu nyeti sana na pigo lolote zito sehemu hii huwa lina uwezo wa kumkata mtu yeyote pumzi zote mwilini kwa muda na kumpumbaza kiasi cha kumfanya asiweze kabisa kujihami na pigo lolote litakalofuata, kwani hapo ndipo mishipa mingi ya fahamu za binadamu inakupotana, na Morandi Gwaza alilijua hili.

Bila ya kupenda GTZ alijikuta akijipinda huku akigumia kwa uchungu, lakini hapo hapo akili yake ikamwambia kuwa lile lilikuwa ni kosa kubwa na haraka akajitahidi kuinuka wima huku akiwa amejikinga uso kwa mikono yake hali amekunja ngumi katika ile staili maarufu ya kibondia iitwayo honour stance.

Morandi aliruka pembeni haraka huku akimstaajabia yule jamaa kwa kuweza kusimama tena wima hata baada ya mapigo yale mazito katika sehemu ile nyeti.

Huku akiwa amelewa mapigo, GTZ alitupa ngumi mbele yake bila kuangalia lakini tayari Morandi alikuwa ameshajiepusha kutoka pale alipokuwa hapo awali na kumtandika teke kali la mbavu na GTZ akajibamiza kwenye boneti la gari lake na kurudi tena alipotokea huku akipepesuka kibwege.

Wapita njia waliokuwa eneo lile walianza kupiga mayowe huku wakikimbilia pale walipokuwa, na Morandi akajua muda wa yeye kuendelea kuwepo eneo lile ulikuwa umekwisha.





Alimdaka kabali kali GTZ aliyekuwa bado akipepesuka bila kujielewa na kumbana kichwa chake mbele ya kifua chake na kumwekea mdomo wake sikioni.

“Hiyo ni trela tu we fala! Kaa mbali kabisa na Candy Gamasala! Kiyume cha hapo picha kamili litaanza,nawe utakufa kabla hata ya mapumziko, umesikia we’ khanithi?” Alimkoromea kwa sauti ya kuogofya, na wakati huo huo GTZ alimwona yule binti aliyemkwida hapo awali akidhani kuwa ni Candy akimpiga picha haraka haraka kwa kutumia kamera aliyokuwa nayo na kutoweka.

Lah!

Sasa watu walikuwa wameshawazonga huku wakihoji kulikoni, na GTZ alitaka kuanza kupiga kelele za mwizi ili aonekane kuwa alikuwa anakabwa kwa lengo la kuporwa, wakati Morandi alipomsukuma pembeni GTZ na kuanza kuondoka.

“Huyu fala anadhani kuwa na gari kunampa uhalali wa kutongoza wake za watu (akamtukania mama yake)…n’tamtoa nishai mimi!” Alijisemesha kwa sauti na kusonya.

Watu kusikia hivyo wakaanza kushangilia huku wakimzomea GTZ.

GTZ alirukia ndani ya gari lake na kuondoka kasi eneo lile akiwa amechanganyikiwa vibaya sana, maumivu makali yakimmaliza nguvu za miguu yake.



***

Dakika arobaini na tano baadaye, mlango wa sebule ya Bishkuku pale mtaa wa Aggrey ulifunguliwa kutokea nje na binti aliyekuwa katika nguo za mazoezi aliingia mle ndani na kushusha pumzi ndefu.

“Niambie habari njema kisura!” Morandi Gwaza alimwambia yule binti aliyejivalisha nguo za Candy kwa lengo la kumtega GTZ.

Binti alienda hadi kwenye meza iliyokuwa pale sebuleni na kuketi juu yake huku akimrushia Morandi simu aliyotoa mfukoni mwa ile suruali yake ya mazoezi. Morandi aliidaka kirahisi ile simu na kuzidi kumtupia macho ya kuuliza yule binti. Binti alimrushia funguo zilizokuwa mkononi mwake ambazo nazo Morandi alizidaka kwa mkono wake mwingine bila papara na kuzitupia kando yake pale kwenye kochi alilokuwa amekalia.

“Ongea maneno mazuri kwangu, mrembo…vipi wewe?” Morandi alimkoromea tena yule binti, ambaye alijifuta kijasho chembamba kilichokuwa kikimtoka kwa kutumia mkono wa ile fulana ya Candy aliyokuwa ameivaa, kisha akamtazama moja kwa moja usoni huku uso wake ukiwa makini na usio na masikhara hata kidogo.

“Tunaye mwanaharamu…nimeshajua anapoishi sasa!” Hatimaye alimjibu, na hapo uso wake ukaachia tabasamu pana na zuri sana, na Morandialiruka kutoka kwenye lile kochi na kumnyanyua mzima mzima kutoka pale kwenye meza huku akimzungusha hewani kama baba ambebavyo mwanaye.

“That’s my girl! Safi sana! Yuu-Huuu!” Alisema kwa furaha, na binti alicheka kwa furaha huku akimsisitizia amteremshe.

Morandi alimweka chini na kukaa juu ya ile meza aliyokuwa amekalia yule binti hapo mwanzo.

“Kwa hiyo mpango wetu umefanikiwa eenh?”Alimuuliza.

“Oh, yeah! Jamaa amebabaika vibaya sana yule, kama ulivyotaraji! Kutoka pale alienda moja kwa moja hadi nyumbani ambako nahisi kuwa ndio kwake huko masaki na kujitoma ndani ya geti na gari lake!” Binti alimwambia, na Morandi akachanua tabasamu jingine pana.

“Na wala hakuonesha kuwa amejua kuwa alikuwa akifuatwa?”Alimuuliza.

“Yaani hata kidogo. Nimemfuata kwa pikipiki yako mpaka anafika pale kwake naye wala hakuonesha kujua kuwa alikuwa anafuatwa…”

Morandi akacheka kwa sauti maridhawa.

“Mjinga alikuwa amehamanika ipaswavyo, pumbavu zake”.

Nuru alitabasamu kwa furaha.

“Na uliipata vizuri picha yake, sio?”Morandi alimuuliza.

“Yap.Naamini hivyo…utaziona mwenyewe picha kwenye simu yako hiyo!”Binti alimjibu.

“Safi sana Nuru, nadhani sasa kazi yako imekwisha.Nikikuhitaji nitakufahamisha okay?” Morandi alimwambia yule binti aliyewahi kuwa askari katika siku za nyuma, naambaye aliamua kuacha kazi baada ya kuona madhila aliyopambana nayo Morandi wakati huo, na kuamua kujishughulisha na biashara ya kuendesha kituo cha kufanyia mazoezi, yaani Gym.

“Hah,yaani unanikatisha stimu wakati ndo kwanza msisimko unakuja?”Nuru alimuuliza, na Morandi alitikisa kichwa.

“No Nuru. Hili ni swala binafsi sana kwangu…na we’ unajua hilo. Nakushukuru kwa msaada wako hata hivyo…” Alimwambia.

Nuru alipiga kimya kwa muda, kisha akamtazama usoni.

“Okay Mo…kama hivyo ndo utakavyo.”Alimwambia.

“Yes Nuru…hivi ndivyo nitakavyo.”

Walitazamana kwa muda.

“Okay, wacha nikabadilishe hizi nguo za miss Dar City Center basi…” Nuru alisema nakuingia chumbani kwa Candy.

Muda mfupi baadaye alitoka akiwa amevaa nguo zake binafsi, suruali ya jeans, blauzi nyeupena kofia ya kepu.

“Okay, sasa nipe maelekezo ya huko nyumbani kwayule shaitwani.” Morandi alimwambia.

Nuru alimwandikia maelekezo kwenye kipande cha karatasi na kumkabidhi.

Walitazamana tena, kisha wapenzi wale wa muda mrefu wakakumbatiana kwa muda mrefu. Nuru alimbusu shavuni haraka mpenzi wake yule mwenye misimamo, na kutoka nje ya sebule na nyumba ile.

Morandi Gwaza alibaki kimya peke yake mle ndani akiwa na ile karatasi yenye maelekezo ya namna ya kufika nyumbani kwa yule mtu aliyeenda kwa utambulisho wa GTZ…



***

Wakati Nuru na mpenzi wake wa muda mrefu Morandi, au Mo, kama mwenyewe alivyopenda kumwita wakipongezana juu ya kufanikiwa kwa ule mtego waliomtegea mtu ambaye mpaka muda ule walikuwa wakimtambua kama “mwendesha pikipiki”, muathirika wa mtego ule GTZ alikuwa akifurumia kwa ghadhabu isiyo kifani kule nyumbani kwake maeneo ya Masaki.

Njia nzima alipokuwa akitimua mabio kwa gari lake kutokea kule mtaa wa Aggrey amekuwa akizungukwa na akili juu ya kile kituko alichokumbana nacho pale nje ya nyumba aliyokuwa akiishi Candy Gamasala.

Na njia nzima wakati akiisumbua akili yake ili angalau iweze kumuelewesha kile kilichomkumba asubuhi ile, hakuweza kabisa kuiona pikipiki iliyokuwa ikimfuata nyuma kwa uangalifu mkubwa, muda wote ikiwa imeacha gari moja baina yake na lile gari alilokuwa akitorokea GTZ.

Yule jamaa ni nani?

Na yule mwanadada naye ni nani?

Ni wazi kuwa wakati yeye ameenda pale akijua kuwa anamvizia Candy, wale watu wawili walikuwa wakimsubiri kwa muda mrefu tu…walikuwa wamemtega.

Naye kama bwege akaingia mzima mzima kwenye mtego wao!

Ina maana Candy huyu huyu amjuaye yeye ndiye amekuwa na uwezo wa kumkodia watu wa kumdhibiti yeye, Gino Tzaspaparos?

Candy? Kisonoko wake mwenyewe?

Alitikisa kichwa kuipinga hali ile na kusonya.

Haiwezekani!

Lakini ndivyo ilivyotokea, na hivyo imewezekana!

Na kibaya zaidi ni kwamba wamenipiga picha…kwa nini?

Alikumbuka maneno ya yule jamaa mweusi aliyemjaza masumbwi mazito asubuhi ile.

Huyu fala anadhani kuwa na gari kunampa uhalali wa kutongoza wake za watu (akamtukania mama yake)…n’tamtoa nishai mimi!

“Lile jamaa lilisema vile ili kujipa uhalali tu mbele za watu wa kunishambulia namna pale barabarani…na limefanikiwa bloody fool!”

“Aaaargh!” GTZ aliunguruma kwa ghadhabu na bilauri ya maji baridi aliyokuwa ameishika ikapasuka mkononi mwake na akahisi maumivu makali pale vipande vya bilauri ile vilipomkata kiganjani.

Alipiga ukelele mwingine wa ghadhabu huku akiruka kutoka kwenye sofa alilokuwa amekalia, maji yaliyokuwa kwenye bilauri ile ya kioo yakimmwagikia na kumlowesha suruali yake.

Bi. Mwana, msaidizi wake wa kazi mle ndani akaja mbio pale sebuleni huku akiuliza kulikoni. GTZ alimtazama kwa ghadhabu na kuondoka pale sebuleni bila kumjibu, akiwa amejishika kiganja chake kuelekea chumbani kwake ambako pia kulikuwa na bafu ili akajisafishe lile jeraha.

Alizidi kupandwa ghadhabu pale alijikuta akishindwa kutembea wima na badala yake akalazimika kujikunja kidogo kuinamia mbele kutokana na maumivu aliyokuwa akiyahisi kutokea sehemu baina ya tumbo lake na kifua, pale ambapo yule jamaa alimjaza makonde mazito ya mfululizo. Zile ngumi za chembe alizotwishwa na yule jamaa zilikuwa nzito sana.

Dah! Yule jamaa ni nani lakini?

“Ila tutakapokutana tena sitakupa nafasi ya kunishtukiza kama ulivyonishtukiza leo rafiki yangu…nitakuwa nimejiandaa!” Alisema kwa sauti huku akijiosha lile jeraha dogo pale kiganjani kwake.

Alikumbuka jinsi yule jamaa alivyombana kabali na kumkoromea sikioni kuwa akae mbali na Candy…

Halafu akaniita mi’ khanithi!

Ghadhabu zake dhidi ya Candy Gamasala ziliongezeka maradufu.



***





Sehemu nyingine ya jiji Sanura Kashogi naye alikuwa mbogo kwa hasira. Alilitikisa gazeti la siku mbili zilizopita lililoandika yale makala ya mwandishi maarufu wa habari za mitindo na urembo Jutti K mbele ya uso wa Tunis huku uso wake wa ki-sariyama ukiwa umemuwiva na kuwa mwekundu.

“Hii ni mbinu ya Bishkuku tu nakwambia!” Alipayuka.

“Bishkuku?” Tunis akamtolea macho na kumuuliza pasi kuelewa, lakini bado Sanura alikuwa na mengi ya kusema.

“Hivi we’ ulikuwa unajua kuwa yule Candy wa Dar City Center ni yatima?” Alimuuliza, na Tunis akamakinika.

“Candy? Yatima …? Hapana, kwani…?”

“Huyu ni Bishkuku tu nakwambia, conniving bastard! Yaani ye’ anataka kutumia huo uyatima wa huyo mrembo wake kama mbinu ya kujipatia kura za huruma kutoka kwa majaji ili mrembo wake ashinde? Stinking bitch, mi’ n’naye leo!” Alisema kwa jazba, na kabla Tunis aliyepigwa butwaa hajasema neno, akachukua simu yake na kumpigia Bishkuku.

Kule Mbezi beach, Bishkuku aliitazama simu yake ikiita huku uso wake ukiwa umefanya tabasamu la kejeli, na Candy aliyekuwa ameketi kando yake nyuma ya jumba kubwa la Kokos lililozungushiwa uzio madhubuti ambako kulikuwa na bustani mwanana, alimgeukia kwa uso wa kuuliza.

“Sa’ mbona hupokei hiyo simu, Anti Bishi?”

Huku akitabasamu, Bishkuku aliichukua ile simu na kumuonesha jina lililokuwa likionekana kwenye uso wa simu ile, na hapo Candy akamuinulia nyusi kwa udadisi.

“Oww…atakuwa anataka nini sasa?” Aliuliza, na Bishkuku akacheka huku ile simu ikiendelea kuita.

“Tutajua muda si mrefu mrembo wangu, poa moyo.” Alimjibu na kubonyeza kitufe cha kupokea simu ile na kisha akabonyeza kutufe kilichowawezesha wote kumsikia muongeaji wa upande wa pili.

“Unasemaje Sanura Kashogi?” Aliongea kuielekea ile simu.

“Unadhani huo ndio ujanja? Yaani umeshaanza kucheza mchezo mchafu hata kabla shindano halijafika mbali? Basi ujue umeshapoteza mwelekeo Bishkuku, na kwa hilo umenisikitisha sana!” Sauti yenye wahka ya Sanura Kashogi ilisikika kutokea kwenye simu ile.

“He he he heeee, haloooo!” Bishkuku alimcheka kwa bezo, na upande wa pili Sanura akamjia juu.

“Unacheka unafikiri mazuri hayo?”

“Nacheka kwa kuwa wan’chekesha bibi, heh! Haya ni lipi hilo nilolifanya hata unipigie simu na kunijia juu ka’a moshi wa kifuu namna hiyo?” Alimuuliza kwa mtindo wa mipasho motomoto na Sanura alitoa sauti ya kukereka kutokea kule alikokuwa.

“We’ unajitia kumnadi huyo mwanasesere wako kwa uyatima magazetini ili apate kura za huruma kutoka kwa majaji sio?” Sanura alimuuliza kwa ukali, na Candy akaachia kinywa wazi na kutumbua macho aliposikia akiitwa mwanasesere.

“Ama! Yaani kumbe mayowe yote hayo kisa ni hicho tu?” Bishkuku alimuuliza kwa kejeli huku akicheka.

“Basi elewa kuwa mi’ nimeshaigundua hiyo mbinu yako…” Sanura alizidi kushadidia hoja yake.

“Mi’ hata sijui unachoongelea Sanura! Hakuna mbinu yoyote hapo, Candy ni yatima kweli. Hakuomba wala hakutaka…imetokea hivyo, sasa kwa nini jamii isijue juu ya hilo?”

“Hamna lolote!”

“Aka! Sa’ hamna lolote kitu gani Sanura? Yaani we kila kitu wakitaka wewe…nimemfunda Tunis, ukamtaka na ukampata…sasa wautaka na uyatima wa Candy pia? Makubwa haya!” Bishkuku alimpasha vikali, na kidogo Sanura akagwaya.

“Upo bibie? Au nikate simu miye?” Ilibidi Bishkuku amuulize, huku akionekana kufurahia kila sekunde ya mkabala ule wa maneno.

“Hiyo ni mbinu yako tu ya kutafuta kura za huruma kutoka kwa majaji wewe!” Sanura alimkoromea.

“Na aliyekwambia u-miss huwa unapatikana kwa kura kama ubunge na urais wa chaneta nani wewe? Mtu mambo huyajui unataka kuyaparamia tu, hebu nipishe mimi huko!” Bishkuku alimjia juu na hapo hapo akakata simu.

Muda huo huo ile simu iliita tena, na wala hakujishughulisha kuipokea. Alibaki akiitazama huku akiwa ametandaza tabasamu la ushindi usoni kwake.

“Heh! Anti Bishi…ndio imeshakuwa hivi tena?” Candy alimuuliza kwa mshangao.

“Hiyo ni mojawapo ya mbinu za kumshusha imani adui mrembo…hebu twende ndani kwanza. Iache hiyo simu iite hapo mpaka betri iishe chaji!”

Waliinuka na kuingia ndani wakiiacha ile simu ikiendelea kuita pale nje. Si yeyote kati yao aliyejua kilichokuwa kimetokea kule mtaa wa Aggrey asubuhi ile.



***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kinyume na GTZ aliyejawa ghadhabu dhidi ya Candy, John Koccho alikuwa amejawa na udadisi juu ya tabia aliyoonesha Candy baada ya kupata ule ujumbe mfupi uliokusudiwa kumkangaya yule mrembo.

Candy hakuwa amempigia simu kama ambavyo yeye alivyotarajia, na hili, ikiwa ni siku nne tangu auwasilishe ule ujumbe kwa yule mrembo, lilimfanya adadisike maradufu.

Ina maana Candy hakuona umuhimu wa ule ujumbe?

Au hakujua uzito wa mambo yaliyotokea kule Magu, na athari za mambo yale kwake iwapo yatawekwa wazi mbele ya jamii katika kipindi hiki?

Ni nini kinampa kujiamini namna hii?

Kwamba ujumbe ameupata hilo alikuwa na hakika nalo kabisa, kwa alimshuhudia yule mtoto akimkabidhi kile kipande cha karatasi pale ndani ya eneo la kile kituo cha kulelea yatima, na akamshuhudia jinsi alivyokuwa akihaha kumsaka mtu aliyemtumia ule ujumbe kupitia kwa yule mtoto…

Sasa kwa nini hakuwa amempigia simu mpaka muda ule?

Hili lilimjaza udadisi mkubwa sana, na ili kukidhi kiu ya udadisi ule, aliazimia kuonana uso kwa uso na yule mrembo wa Dar City Center mara atakapoenda kwenye tujkio lake lijalo katika safari yake kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha Miss Tanzania wiki chache zijazo.

Aliitoa ile karatasi yenye ratiba ya matukio yajayo katika haratati za kuelekea kwenye shindano lile kubwa kabisa la urembo nchini, na kutazama tukio lililokuwa linafuatia lile la pale kwenye kituo cha watoto yatima.

Baada ya kujiridhisha juu ya tukio lifuatalo, alibaki akiwa amejiegemeza kwenye mto pale kitandani kwenye chumba cha nyumba ya wageni aliyopanga, tabasamu likiwa limeganda usoni kwake.



***

Simu mpya ya Morandi Gwaza illita, na mara moja alijua kuwa mpigaji wa simu hiyo angekuwa aidha Kokos au mpenzi wake Nuru, kwani hao ndio watu pekee wanaoijua ile namba.

Alibonyezakupokeleokwenyesimuilenakuipelekeasikioni.

“Candy!” SautiyaKokosWandibailivumasikionimwake, naye akaachia tabasamu dogo baada ya kuona kuwa Kokos amekumbuka kufuata maelekezo aliyompa hapo awali juu ya kuwasiliana naye kwa simu ile mpya.

“Sema wakili wangu, nilikuwa naisubiri sana simu yako!” Alimwambia.

“Haya ndo nimepiga sasa…vipi kuna maendeleo yoyote kwenye kondarasi niliyokupa, Morandi?” Kokos alisaili.

“Bado naifanyia kazi…naamini iko kwenye hali nzuri. Una jipya?”

“Yaa!Inabidi tuonane…kuna mambo yanatokea huku ambayo hayanipi amani hata kidogo!” Kokos alimjibu.

“Okay. Njoo kwenye makazi yangu ya muda…tutaongelea hapa.”

“Okay, saa ngapi?”

“Hata sasa hivi!”

“Okay…niko njiani!”

Nusu saa baadaye Kokos aliingia sebuleni kwa Bishkuku na kusita akiwa mlangoni. Ile sebule ilikuwa imegeuzwa mpangilio. Ile meza kubwa iliyokuwa katikati ya sebule ilikuwa imesogezwa ukutani, na juu yake kulikuwa kuna kompyuta mpakato mbili, hali ukutani kukiwa kumebadikwa picha kubwa ya GTZ aliyekodoa macho kwa woga hali mkono mmoja ukionekana ukiwa umembana sehemu ya paji lake la uso na mwingine ukiwa umepitishwa shingoni kwake kwa kilichoonekana wazi kuwa ni kabali.

Kando ya picha ile kulikuwa kuna ramani kubwa ya jiji la Dar, na pini kubwa za virungu zenye rangi tatu tofauti zikiwa zimebadikwa kwenye ramani ile kuonesha sehemu tatu tofauti za jiji.

“Ebwana we!What…huyu ni nani huyu?” Kokos aliuliza huku akiiendea ile picha kubwa pale ukutani.

“Humjui huyo jamaa?”Kokos alimuuliza huku akitabasamu.

Kokos aliitazama ile picha, kisha akamgeukia Morandi.

“Unataka kuniambia kuwa huyu ndiye yule jamaa mwendesha pikipiki…?”

“The one and only!”Morandi alimjibu kumaanisha kuwa ndiye, huku akizidi kutabasamu, na Kokos aliguna kwa mshangao.

“Sasa…umeipataje hii picha…?”

“Kaa chini nikupe habari za huyo jamaa yako…” Morandi alimwambia, na kuendelea kumsimulia mkasa wote jinsi ulivyokuwa siku ile GTZ alivyoingia kwenye mtego wake.

Kokos alifurahi kweli kweli.

“Yes! Sasa atajuakuwa Candy hatakiwi kusumbuliwa (akamtukania mama yake), alla!” Alipayuka, na Morandi akatikisa kichwa.

“Yule jamaa anaonekana matata sana yule. Nahisi atarudi tena tu…hasa baadaya mimi kumzidi kete namna ile.” Alimwambia.

“Kwa nini unasema hivyo?”

Morandi aliiendea ile picha ya GTZ pale ukutani.

“Hebu angalia haya macho…yamejaa wazimu wa wazi kabisa! Huyu mtu ana nia moja mbaya sana na mrembo wako, na mpaka nitakapojua ni kitu gani anachomtafutia, sitakuwa na amani kuwa ataacha kumfuatilia.” Alimwambia.

“Na hilo ndilo haswa lililonifanya nikupigie simu leo hii…” Kokos alimwambia.

“Ni nini, maana ulisema kuna mambo yanayotokea ambayo…”

“Yaa! Ni kwamba sasa Candy anatakiwa aende mikumi na warembo wenzake…kutembelea zile mbuga za wanyama.”

“Na hilo ni tatizo?”

“Yes, hilo ni tatizo, kwani huko si mimi wala dadaangu Bishkuku anayeweza kwenda naye…atakuwa peke yake. Sasa itakuwaje kama huyu jamaa ataamua kumuibukia huko?” Kokos alisema, na Morandi akatikisa kichwa kuafikiana naye.

“Ni kweli usemalo wakili wangu…hilo litakuwa gumu.Na kibaya zaidi ni kwamba hata mimi sitaweza kuambatana naye huko bila kujianika wazi mbele ya mabinti wa urembo”

“See? Sasa tunafanyaje? Mi’ nilitaraji ungekuwa umemdhibiti yule ms--ge by now, bwana!” Kokos alinung’unika.

Morandi aliachia tabasamu la upande mmoja.

“Yule jamaa nimemdhibiti, alright. Hana namna tena…ila kwa uhakika zaidi, nadhani sasa nitahitaji msaada wako zaidi”

“Oh! Utamdibiti kivipi…? Na msaada gani unaouhitaji kwangu?”

Morandi alienda kwenye ile ramani kubwa ya jiji la Dar.

“Si nimekwambia kuwa sasa nimeshajua anapoishi?”Alimuuliza huku akioneshea ile pini yenye kirungu chekundu iliyochomekwa eneo la Masaki kwenye ile ramani.

“Yes…”

“Na sisi tuko hapa…” Akaoneshea pini yenye kirungu cha njano ambayo ilikuwa imechomekwa eneo la kariakoo jijini, pale mtaa wa Aggrey, na kuendelea, “Na kwa sasa Candy yuko hapa!” Akaoneshea pini yenye kirungu cha kijani, ambayo ilikuwa imechomekwa kwenye eneo la Mbezi Beach kwenye ile ramani.

“Kwa hiyo?”

“Kwa hiyo kwa sasa huyu jamaa ana sehemu moja tu ya kujionesha, nayo ni kule nyumbani kwake Masaki. Hapa hawezi kuja tena maana mziki aliokutana nao hapa keshauona kuwa ni mnene. ..”

“Kweli!”

“Ya! Na kule kwa Candy Mbezi Beach hakujui hata kidogo,so hamna shaka kuwa huko Candy atakuwa salama tu.”

“Sawa, lakini bado sielewi hiyo inakuwa imemdhibiti vipi?” Kokos alimuuliza.

“Ina maana sasa atabaki akiwamejifungia kule masaki, na hawezi kumsumbua tena Candy.Najua ataona kwenye vyombo vya habari kuwa sasa Candy anaenda Mikumi, lakini hawezi kwenda mikumi bila kutoka nje ya nyumba yake kule Masaki!”Morandi alizidi kutoa mkakati wake.

“Kwa hiyo…?”

“Kwa hiyo akitoka tu nje ya nyumba yake, mi n’takuwa namsubiri. Mikumi hafiki yule!”

Kokos aliachia tabasamu pana.

“Now you are talking!” Alisema kwa sauti iliyoonesha ahueni ya hali ya juu, kisha akaendelea, “Na ulisema utahitaji msaada wangu…ni upi huo?”

“Nitahitaji hela Kokos…”

“Hilo limepita…sema kiasi gani unahitaji!” Kokos alimuuliza, na Morandi akamwambia kiasi alichokuwa anahitaji. Kokos hakupepesa wala kuuliza zaidi.

“Okay, nitakupatia hiyo pesa leo hii hii.” Alimwambia, kisha akampigia simu Bishkuku na kumwambia aende Benki akamtolee kiasi kile cha pesa. Baada ya hapo akamgeukia Morandi.

“Okay…sasa huyu jamaa umeshamfahamu ni nani?”

“Hilo bado nalifanyia kazi…nitamjua ndani ya muda mfupi tu. Kwanza nina namba za gari lake, na kwa kutumia hilo nitaweza kujua jina la mmiliki wa gari lile…”

“Ambalo sio lazima liwe nd’o la yule jamaa…anaweza kuwa alitumia gari mtu mwingine!”

“True! Lakini pia njia nyingine ni kumwonesha Candy picha ya huyu jamaa. Nina hakika yeye atakuwa anamfahamu…”

Kokos alilitafakari hili kwa muda.

“Kweli…lakini pia huenda ikawa yule jamaa ametumwa tu na mtu mwingine amfanyie ubaya Candy…kwa hiyo Candy anaweza asimjue!” Alitoa hoja.



“Basi na tumwachie Candy atufahamishe hilo…ni muda gani unadhani tutaweza kumpata Candy na kumwonesha hii picha?” Morandi alisema na kumuuliza.

“Anytime. Nipe hiyo picha nitaenda kumwonesha kabla hawajaondoka kwenda huko Mikumi.”

“Nataka niwepo wakati anaiona hiyo picha…”

“Oh, basi itabidi twende sote?”

“Not now. Kwanza wacha nimkabili huyu jamaa kabla ya safari ya Candy. Kama nitashindwa kupata taarifa nizitakazo kutoka kwake, basi tutamkabili Candy pamoja na picha ya huyu mjinga.” Morandi alisema, na Kokos aliafikiana naye kwa kichwa huku uso wake ukisajili fikra nzito.

“Je habari za safari ya mabinti wa urembo kwenda Mikumi imeshatangazwa kwa wananchi?” Morandi aliuliza.

“Nadhani leo ndio itatangawa rasmi, ila mabinti wao walishapewa taarifa hiyo tangu jana jioni…”

“Okay, niache nifanye kazi ya kukulipa deni lako sasa Kokos…” Morandi alisema, na wakaagana.



***

Saa mbili baadaye GTZ alikuwa anaangalia kwa utulivu wakati mratibu wa mashindano ya kugombea taji la Miss Tanzania nchini akiwafahamisha waandishi wa habari juu ya safari ya mabinti wa urembo kuelekea kwenye mbuga za wanyama za Mikumi kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea kwenye mpambano mkuu wa kugombea taji la malkia wa urembo nchini.

Mara baada ya kumaliza kuangalia habari ile, alizima runinga yake na kuelekea chumbani kwake huku uso wake ukiwa na dhamira ya wazi.

Dakika chache baadaye alitoka nje ya chumba chake akiwa amevaa suti nzuri ya kijivu na mkononi alikuwa ameshika kibegi kidogo kilichobeba zana zake muhimu.

“Bi. Mwana mi’ natoka…nitakuwa safarini nje ya mji kwa kama siku mbili hivi…” Alimuaga msaidizi wake wa kazi za ndani huku akielekea mlangoni.

“Hewalla baba!” Bi. Mwana alimjibu naye akatoka nje ya nyumba ile.



***

Kutokea upande wa pili barabara, Morandi alilishuhudia geti la nyumba aliyoelekezwa na Nuru kuwa yule mtu waliyembandika jina la “mwendesha pikipiki” likijifungua taratibu naye akawa makini.

Alikuwa amekaa nje ya saluni ya kiume iliyokuwa upande wa pili wa barabara ikitazamana na ile nyumba. Pamoja naye kulikuwa kuna vijana wachache waliokuwa wakisubiri kunyolewa huku wakibishana kuhusu maswala ya mapenzi kati ya Rihanna na Chris Brown. Kutokea pale alipokuwa amekaa aliona gari aina ya Toyota Harrier jeusi likitoka nje ya lile geti, na macho yake makali yaliweza kuona kuwa dereva alikuwa amevaa kofia kubwa ya pama ingawa hakuweza kuona vizuri iwapo alikuwa ndiye mtu aliyemkusdia au la. Baada ya lile gari kutoka alilishuhudia lile geti likijifunga lenyewe nyuma yake na ile Harrier ikakamata barabara ikichukua uelekeo wa mjini.

Ingawa alitarajia kuona gari aina ya Toyota Caldina jeusi badala ya ile Harrier, hakuwa na shaka kuwa yule dereva angeweza kuwa ndiye yule mtu aliyekuja kumvizia.

Aliinuka na kwenda kuiparamia pikipiki yake kubwa aliyokuwa ameiegesha pembeni ya ile saluni, akiwaacha wale vijana wakiendelea na ubishani wao juu ya wale wanamuziki wa huko ughaibuni, naye akaanza kulifuata lile gari lililotoka nyumbani kwa yule hasimu wao kwa uangalifu mkubwa.

Huyu jamaa anaonekana ni mwenye uwezo mkubwa tu kifedha…sasa anamtafutia nini huyu binti?

Alijiwazia.

Na kama ana uwezo namna hii, inawezekana kweli akawa ametumwa tu na mtu kumdhuru huyu binti naye akakubali? Kwa malipo gani sasa? Hapana. Lolote alitakalo kwa Candy, litakuwa ni lake binafsi na si la kutumwa…na mi’ nataka nilijue hilo leo!

Alizidi kuwaza huku akiwa makini kutolipoteza lile gari kutoka kwenye upeo wa macho yake.

Walipofika Mbezi mwisho na bado ile Harrier ilikuwa imekaza mwendo kuelekea usawa wa Kibaha, Morandi alijihakikishia kuwa hakika dereva wa ile Harrier alikuwa ni yule mbaya wao, na kwamba alikuwa akielekea Mikumi kumsubiri Candy ili amfanyie hilo alilokuwa akitaka kumfanyia mara zote alizojaribu kumtia mikononi yule binti. Aliegesha pikipiki yake kando ya barabara na kumpigia simu mtu aliyekuwa amemuandaa tangu awali. Yule mtu alipopokea simu, alimtajia namba za lile gari alililokuwa akiendesha yule hasimu wao, na kumpa aina ya gari lenyewe na rangi yake.

Kwisha kufanya hivyo, aliingiza kwa kasi zaidi pikipiki yake barabarani na kuelekea kule alipojua kuwa ile Harrier ilikuwa imeelekea.



***



GTZ alikuwa akiendesha kwa kasi ya kilometa hamsini kwa saa, akizingatia sheria za barabarani ili kuepuka kusimamishwa na askari wa usalama barabarani, waliozagaa njia nzima kutokea Dar es salaam kuelekea Mikumi. Kilometa chache baada ya kulipita eneo la Chalinze kulikuwa kuna eneo refu lililokuwa pweke na hivyo akakanyaga mafuta zaidi na kufikisha kilometa sitini kwa saa.

Safari hii sifanyi makosa, na nikimaliza mchezo natimkia huku huku…Dar sitarudi tena kwa sasa…Bi. Mwana n’tamtumia tu mshahara wake…

Aliwaza huku akizidi kuongeza kasi na kufikia kilometa sitini na tano kwa saa na hapo akaona askari wa usalama barabarani akichomoza kutoka kando ya barabara, akimnyooshea mkono kumsimamisha.

“Aww, Sheeeeyiit! Sasa huyu katokea wapi tena jamani??” Alibwata peke yake mle garini huku akipunguza kasi na akijua kuwa tayari alikuwa ameshakiuka sheria ya barabara ile.

Aliegesha gari kando ya barabara na kusubiri.

Yule askari wa usalama alimsogelea hadi pale kwenye gari lake, naye akashusha kioo cha gari. Askari akamuonesha tochi maalum ya kusoma kasi ya magari aliyokuwa nayo na GTZ akaona kasi ya gari lake ikisoma kuwa alikuwa akiendesha kwa kilometa sitini na tano nukta 6 kwa saa.

“We’ bwana vipi…mbona unaendesha kasi namna hiyo…hujui kanuna za barabara wewe?” Yule askari alimuuliza huku akimtazama usoni.

GTZ alijikuta akijitazama yeye mwenyewe kutoka kwenye vioo vya miwani ya jua aliyokuwa amevaa yule askari mrefu mwenye rangi ya kunde.

“Aah, yaaa…ni kwamba nina msiba Morogoro afande, so nilikuwa najaribu kuwahi maziko…samahani sana!” Alimjibu huku mkono wake ukichomoza na noti ya elfu kumi na kuuacha ukielea na ile hela juu ya usukani wake ili yule afande aione.

Jamaa aliitazama ile hela kwa muda.

“Naomba leseni yako na kadi ya gari…” Alimwambia, na GTZ akaguna.

“Afande! Mambo haya si yanaisha fasta tu? Mi’ nina haraka nakwambia!” Alisema, na mkono wake wa pili ukaungana na ule wa kwanza pale kwenye usukani wake, nao ukiwa na noti nyingine ya elfu kumi, hivyo yule askari akawa anatazama elfu ishirini zilizokuwa mikononi mwa GTZ. Alibaki akizitazama zile hela kwa muda.

“Teremka garini!” Askari alimwamuru, na GTZ akaduwaa kwa muda.

“Ebbo? Sa’ nishuke kwa nini? Mtu nakwambia n’na msiba na nakuonesha mshiko huu halafu we…” Alianza kumjia juu huku akikunja uso, na hapo akasikia mvumo wa pikipiki nyingine ukifika eneo lile na alitaharuki kuona mwendesha pikipiki mwingine akiegesha pikipiki ubavuni kwa gari lake, ule upande wa abiria.

“Hah, hii ni nini…?” Alimaka huku akigeukia ule upande wa pili wa gari lake ambako aliona mtu aliyekuwa amevaa suruali ya jeans na koti la jeans likiwa juu ya fulana nyekundu akiteremka kwenye ile pikipiki nyingine. Hapo hapo akasikia ule mlango wake wa dereva ukifunguliwa na kengele za hatari zikagonga kichwani mwake.

Aligeuka haraka kutaka kumzuia yule askari huku mkono wake ukienda chini ya kiti chake kutoa bastola aliyoificha pale, na hapo akasikia ule mlango wa abiria nao ukifunguliwa na mdomo wa bastola ukitulia ubavuni mwake.

“Tulia hivyo hivyo wewe!” Sauti nzito ilimkoromea na akageuka tena kule upande wa dirisha la abiria na kujikuta akitazama na yule jamaa aliyemshindilia magumi ya chembe siku chache zilizopita, sasa akiwa ameketi kwenye kiti cha abiria pamoja naye mle garini na akiwa amemdidimizia bastola ubavuni.

E bwana we!

“Wewe!” Alimaka kwa hamaniko.

“Tunakutana tena it seems, my friend!” Morandi Gwaza alimwambia huku akimtazama kwa macho ya kuongofya, na GTZ aliishiwa namna.

Yaani wakati yeye anageuka kuitazama ile pikipiki iliyokuwa ikiegeshwa ubavuni mwa gari lake, yule askari alifyatua loki za milango yake kupitia pale dirishani kwake na kufungua mlango. Alipogundua kosa hilo na kuanza kumgeukia yule askari huku akijaribu kuchomoa bastola yake, yule jamaa mwenye ngumi nzito akawahi kufungua mlango wa abiria na kuingia ndani huku akimwekea bastola ubavuni.

Alimgeukia yule askari kwa hasira, lakini akaona jamaa ameshaufunga tena ule mlango wake na amesimama hatua zipatazo tatu kutoka kwenye lile gari huku akimtazama kutokea nyuma ya miwani yake ya jua.

Dah!

GTZ alichanganyikiwa. Akamgeukia yule jamaa aliyekuwa naye mle garini.

“Wewe ni nani…na unataka nini kwangu lakini?” Alimuuliza kwa ghadhabu zilizokithiri, akilini akijua kuwa mpango wake dhidi ya Candy ulikuwa umeharibika.

Kwa mara nyingine!

Badala ya kumjibu, Morandi alimuongelesha yule askari huku bado akimtazama GTZ kwa macho ya kuogofya na akiwa amemkandamizia bastola ubavuni.

“Kazi nzuri kamarade wangu. Sasa we’ kazi yako imeisha. Utarudi na hiyo pikipiki yangu kama nilivyokuelekeza. Bahasha yako utaikuta kwenye mfuko wa hilo kava la tanki hapo…”

“Laki moja?” Askari alimuuliza.

“Kama tulivyokubaliana kamarade…laki moja cash!” Morandi alimjibu, na kwa mara ya kwanza yule askari aliachia tabasamu. Akasogea pale dirishani na kupitisha mkono wake na kuzichukua zile elfu ishirini ambazo bado zilikuwa mkononi mwa GTZ.

“Naamini na hizi pia zilikuwa zimetolewa kwa ajili yangu!” Alisema huku akimtazama GTZ kutokea nyuma ya miwani yake, na GTZ alifura kwa hasira. Mguno wa cheko ulimtoka Morandi.

Yule askari aliiparamia pikipiki ya Morandi na kuondoka kwa kasi kutoka eneo lile, akichukua elekeo wa Dar es Salaam.

“Okay…ni nini kinafuata sasa?” GTZ aliuliza kwa hasira.

“Kwa upole zaidi…toa hiyo bastola hapo chini ya kiti na unikabidhi…” Morandi alimkoromea, na GTZ alisita kidogo, akili ikimcheza kujaribu kutafuta namna ya kumzidi kete yule jamaa aliyeondokea kumchukia kwa kiwango kilichokaribia sana kile cha Candy. Lakini kabla hajapata namna, Morandi alimkoromea tena, “…na kumbuka kuwa nina bastola aina ya Luger9 mm ya Mrusi mwenyewe! Kwa hapa ilipo, ina uwezo wa kuchana mbavu zako, ikachabanga matumbo yako na kutokea ubavu wako wa pili na kuendelea kuunyofoa kabisa na mlango wa gari lako hili, hivyo usijitie kuleta usteringi wa kwenye picha za kidosi hapa…ntakuua!” Morandi alimkoromea na GTZ ajua alikuwa amezidiwa.

“Unataka nini kwangu wewe nakuuliza?” Alimkoromea huku akiwa ameuma meno na akimkabidhi ile bastola yake. Morandi aliishindilia ile bastola ya GTZ kwenye mfuko wa jaketi lake la jeans.

“Nilikwambia ukae mbali na Candy wewe…umekaidi. Sasa utakiona cha mtema kuni!”

“Huyu Candy we’ ni nani kwako? Na una uhakika gani kama ninamfuata yeye?” GTZ aliuliza kwa hasira.

“Washa gari hilo huko! Maongezi tutayafanya njiani, pusi we!” Morandi alimkoromea tena.

“Tunaenda wapi?” GTZ alijitia kutoa jeuri.

Morandi alimzaba lofi kali la uso kwa mkono wake wa kushoto, na hapo hapo akamdidimizia ile bastola ubavuni kwa nguvu.

“Waaargh!” GTZ alipiga ukelele bila kujijua huku akijipigiza kichwa kwenye kiegemeo cha kiti chake.





“Fanya nikwambiavyo wewe. Ebo!”

GTZ aliwasha gari huku akitikisa kichwa kwa aidha masikitiko au kwa ajili ya kuweka akili sawa.

“Un…nan’peleka wapi sasa?”

“Tunarudi Dar es Salaam!” Morandi alimwambia, na GTZ aliachia msonyo mkali kwa hasira.

“Nini? Unataka kofi jingine?” Morandi alimkoromoea.

“No sweat…uneshinda hili pambano, lakini sio vita! Utaingia tu kwenye anga zangu wewe, bloody fool!” GTZ alimkoromoea kwa uchungu.

“Endesha gari wewe!”

Toyota Harrier iligeuza na kuchukua uelekeo wa kurejea Dar es Salaam.

Wakati wakiendela na safari kurejea Dar, Morandi alianza kumhoji.

“We bwana unaitwa nani?”

“Sijui!”

Kimya kikachukua nafasi kwa muda mle garini, kisha Morandi akaendelea.

“Okay, jina lako si muhimu sana, kwani hata we’ mwenyewe si muhimu sana. Unamtakia nini huyu mwanadada Candy?”

“Hilo pia sijui!” GTZ alijibu kwa jeuri, akili yake ikimwenda kasi kujaribu kutafuta namna ya kujikwamua, lakini ile bastola kubwa iliyokuwa ubavuni kwake ilimnyima amani.

“Unajitia hamnazo eenh? Basi si neno (akamtukania mama yake) …nikikufikisha ninapopataka utasema tu wewe!” Morandi alimkoromea.

“Usin’tishe! Hata mimi nataka sana kujua kuhusu wewe na ni jinsi gani hata ukajihusisha na huyu malaya anayedaiwa kuwa eti ni Miss Dar City center…lakini sina haraka!” GTZ alimjibu huku akiwa ameuma meno na akiendesha gari kwa kasi ya wastani.

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha kuwa na mimi nitakapokugeuzia kibao utasema yote hayo! Sina haraka…”

Morandi alimzaba kofi jingine kali na uso, na GTZ alijipigiza tena kisogo kwenye kiegemeo cha kiti chake. Gari liliyumba kidogo naye akajitahidi kuliweka sawa.

“Tusubiri hapo utakaponigeuzia hicho kibao basi, fisi we!” Morandi alimkoromea kwa hasira.

GTZ alijiramba mchirizi wa damu iliyomtoka mdomoni baada ya kujing’ata pale alipopigwa lile kofi la pili. Hakuongea kitu, ila ghadhabu za hali ya juu zilijidhihirisha usoni kwake.

Kabla ya kufika Mbezi walipishana na basi la kifahari la Miss Tanzania likiwa limewabeba wale mabinti wa urembo kuelekea Mikumi.

“Candy huyoo anaenda zake Mikumi…vipi hapo?” Morandi alimuuliza GTZ kwa kebehi huku akiwa ameachia tabasamu la upande mmoja. Jamaa alizidi kufurumia kwa hasira huku akilitupia jicho la pembeni lile basi la warembo, mishipa ya kichwa ikimpiga kwa jazba.

Walipofika Mbezi mwisho Morandi alimwamuru akate kushoto kufuata barabara ya vumbi iliyokuwa na mashimo-mashimo kiasi kwamba mwendo haukuwa wa utulivu.

“Huku wapi sasa?” GTZ aliuliza, akilini akiwa ameingiwa na mashaka mazito.

“Sijui...endesha gari!” Morandi alimkaripia.

Ulikuwa ni mwendo wa kama saa nzima kwenye ile barabara mbovu iliyowapitisha kwenye makazi ya watu na hatimaye kwenye eneo la msitu mwepesi. Mbele zaidi walifika kwenye eneo pweke lililokuwa limezingirwa na msitu mnene wenye miti mirefu. Morandi alimwamuru asimamishe gari.

GTZ alitii na kumgeukia kwa mashaka.

“Hapa ni wapi wewe… na unataka kufanya nini?”

Kwa muda Morandi alimtazama kwa macho yake makali bila ya kumjibu, kisha akaongea.

“Hapa tuko katikati ya msitu ambao kiasi cha kama kilometa mbili huko mbele ndio kuna eneo maarufu la Mabwepande…nadhani unajua watu huwa wanafanywa nini kwenye huo msitu, sio?”

GTZ alimtazama kwa hasira.

“Kwa hiyo umekuja kuniua na kuuacha mwili wangu ukioza huku porini.” Halikuwa swali.

“Hiyo itategemea na wewe…kama utatoa ushirikiano, basi naweza kukubakishia huo uhai wako potofu. Lakini ukijitia machinoo, haki ya Mungu fisi watapata kitoweo leo! Watatafuna mzoga wako tu!” Morandi alimjibu kwa sauti ya kuogofya.

GTZ alizungusha uso wake na kutazama huko nje. Msitu ulikuwa umetanda, na upande mmoja wa barabara ile kulikuwa kuna kijimporomoko kidogo.

“Zima gari, chomoa ufunguo na uurushie kiti cha nyuma huko,upesi!” Morandi alimkemea.

GTZ alifanya alivyoambiwa na kubaki akimtazama kwa hasira.

“Fanya ufanyalo ndugu yangu, lakini la kukwambia kuhusu Candy sitakuwa nalo, maana…” Alianza kumwambia, lakini hapo hapo Morandi akampiga na mdomo wa ile bastola usoni kisha akaielekeza usawa wa kichwa chake.

GTZ alilia kwa uchungu, lakini Morandi hakumpa muda zaidi, akamkoromoea.

“Fungua mlango na uteremke kwa upole zaidi…tena kumbuka kuwa hii bastola itakuwa imekuelekea muda wote na ukijitia ujanja nakupa njugu za kichwa fala wewe, umes’kia hiyo?”

“Ah, sasa kama kweli unataka kuniua kwa nini usiniue tu humu humu garini?” GTZ alimtolea ubishi, na Morandi akaikoki ile bastola.

“Halafu nirudi mjini na gari lililotapaka mi-damu yako? Shuka huko!” Morandi alimkaripia, na GTZ akajua kuwa alikuwa amefikwa. Alimtazama kwa hasira, kisha alianza kuufungua mlango taratibu bila ya kuondoa macho yake usoni kwa adui yake. Morandi naye alikuwa anafungua mlango wake kwa mkono wake wa kushoto ilhali kwa ule wa kulia akiwa amemuelekezea bastola yule jamaa. Alianza kushusha mguu wake mmoja nje ya gari akiwa makini na GTZ naye alishusha wa kwake, lakini mara aliruka nje huku akiubamiza ule mlango. Morandi aliona kile kitendo na alimpigia ukelele huku akimfyatulia risasi.

Mlipuko wa ile bastola kubwa ulirindima msituni na ile risasi ikapiga kioo cha lile gari mahala ambapo muda mfupi uliopita uso wa GTZ ulikuwapo.

Vitu viwili vilijidhihirisha akilini kwa Morandi kwa wakati mmoja.

Kwanza kile kioo hakikupasuliwa na ile risasi yake, na pili alimuona GTZ akipotelea nyuma ya ubavu wa upande wa pili wa lile gari.

Ah, kumbe vioo vya hile gari ni bullet proof!

Mara moja alijua kuwa yule adui yake alikuwa anataka amzungukie hadi pale alipokuwa na amkabili, ila hakujua iwapo angemzungukia kutokea mbele ya lile gari au nyuma, na hivyo alipoteza nukta chache sana kabla hajapitisha uamuzi.

Na zile nukta chache za kutokuwa na maamuzi ya haraka ndizo GTZ alizokuwa anazitarajia.

“Nini? Unataka kofi jingine?” Morandi alimkoromoea.

“No sweat…uneshinda hili pambano, lakini sio vita! Utaingia tu kwenye anga zangu wewe, bloody fool!” GTZ alimkoromoea kwa uchungu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Endesha gari wewe!”

Toyota Harrier iligeuza na kuchukua uelekeo wa kurejea Dar es Salaam.

Wakati wakiendela na safari kurejea Dar, Morandi alianza kumhoji.

“We bwana unaitwa nani?”

“Sijui!”

Kimya kikachukua nafasi kwa muda mle garini, kisha Morandi akaendelea.

“Okay, jina lako si muhimu sana, kwani hata we’ mwenyewe si muhimu sana. Unamtakia nini huyu mwanadada Candy?”

“Hilo pia sijui!” GTZ alijibu kwa jeuri, akili yake ikimwenda kasi kujaribu kutafuta namna ya kujikwamua, lakini ile bastola kubwa iliyokuwa ubavuni kwake ilimnyima amani.

“Unajitia hamnazo eenh? Basi si neno (akamtukania mama yake) …nikikufikisha ninapopataka utasema tu wewe!” Morandi alimkoromea.

“Usin’tishe! Hata mimi nataka sana kujua kuhusu wewe na ni jinsi gani hata ukajihusisha na huyu malaya anayedaiwa kuwa eti ni Miss Dar City center…lakini sina haraka!” GTZ alimjibu huku akiwa ameuma meno na akiendesha gari kwa kasi ya wastani.

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha kuwa na mimi nitakapokugeuzia kibao utasema yote hayo! Sina haraka…”

Morandi alimzaba kofi jingine kali na uso, na GTZ alijipigiza tena kisogo kwenye kiegemeo cha kiti chake. Gari liliyumba kidogo naye akajitahidi kuliweka sawa.

“Tusubiri hapo utakaponigeuzia hicho kibao basi, fisi we!” Morandi alimkoromea kwa hasira.

GTZ alijiramba mchirizi wa damu iliyomtoka mdomoni baada ya kujing’ata pale alipopigwa lile kofi la pili. Hakuongea kitu, ila ghadhabu za hali ya juu zilijidhihirisha usoni kwake.

Kabla ya kufika Mbezi walipishana na basi la kifahari la Miss Tanzania likiwa limewabeba wale mabinti wa urembo kuelekea Mikumi.

“Candy huyoo anaenda zake Mikumi…vipi hapo?” Morandi alimuuliza GTZ kwa kebehi huku akiwa ameachia tabasamu la upande mmoja. Jamaa alizidi kufurumia kwa hasira huku akilitupia jicho la pembeni lile basi la warembo, mishipa ya kichwa ikimpiga kwa jazba.

Walipofika Mbezi mwisho Morandi alimwamuru akate kushoto kufuata barabara ya vumbi iliyokuwa na mashimo-mashimo kiasi kwamba mwendo haukuwa wa utulivu.

“Huku wapi sasa?” GTZ aliuliza, akilini akiwa ameingiwa na mashaka mazito.

“Sijui...endesha gari!” Morandi alimkaripia.

Ulikuwa ni mwendo wa kama saa nzima kwenye ile barabara mbovu iliyowapitisha kwenye makazi ya watu na hatimaye kwenye eneo la msitu mwepesi. Mbele zaidi walifika kwenye eneo pweke lililokuwa limezingirwa na msitu mnene wenye miti mirefu. Morandi alimwamuru asimamishe gari.

GTZ alitii na kumgeukia kwa mashaka.

“Hapa ni wapi wewe… na unataka kufanya nini?”

Kwa muda Morandi alimtazama kwa macho yake makali bila ya kumjibu, kisha akaongea.

“Hapa tuko katikati ya msitu ambao kiasi cha kama kilometa mbili huko mbele ndio kuna eneo maarufu la Mabwepande…nadhani unajua watu huwa wanafanywa nini kwenye huo msitu, sio?”

GTZ alimtazama kwa hasira.

“Kwa hiyo umekuja kuniua na kuuacha mwili wangu ukioza huku porini.” Halikuwa swali.

“Hiyo itategemea na wewe…kama utatoa ushirikiano, basi naweza kukubakishia huo uhai wako potofu. Lakini ukijitia machinoo, haki ya Mungu fisi watapata kitoweo leo! Watatafuna mzoga wako tu!” Morandi alimjibu kwa sauti ya kuogofya.

GTZ alizungusha uso wake na kutazama huko nje. Msitu ulikuwa umetanda, na upande mmoja wa barabara ile kulikuwa kuna kijimporomoko kidogo.

“Zima gari, chomoa ufunguo na uurushie kiti cha nyuma huko,upesi!” Morandi alimkemea.

GTZ alifanya alivyoambiwa na kubaki akimtazama kwa hasira.

“Fanya ufanyalo ndugu yangu, lakini la kukwambia kuhusu Candy sitakuwa nalo, maana…” Alianza kumwambia, lakini hapo hapo Morandi akampiga na mdomo wa ile bastola usoni kisha akaielekeza usawa wa kichwa chake.

GTZ alilia kwa uchungu, lakini Morandi hakumpa muda zaidi, akamkoromoea.





Ah, kumbe vioo vya lile gari ni bullet proof!

Mara moja alijua kuwa yule adui yake alikuwa anataka amzungukie hadi pale alipokuwa na amkabili, ila hakujua iwapo angemzungukia kutokea mbele ya lile gari au nyuma, na hivyo alipoteza nukta chache sana kabla hajapitisha uamuzi.

Na zile nukta chache za kutokuwa na maamuzi ya haraka ndizo GTZ alizokuwa anazitarajia.

Morandi alijitupa chini na kuchungulia uvunguni mwa lile gari ili kuona uelekeo wa miguu yake. Kule upande wa pili wa lile gari GTZ alijirusha haraka juu ya paa la lile gari na kujisereresha kuelekea ule upande ambao Morandi alikuwapo.

Akiwa ametanguliza bastola yake kule uvunguni tayari kumkongoroa miguu GTZ kwa risasi, Morandi alishangaa kutoiona miguu ya yule adui yake kule upande wa pili wa lile gari. Alijigeuza haraka huku akianza kujiinua, lakini hapo alishtukia teke zito la kichwa kutokea juu ya paa na lile gari na akapigiza uso wake kwenye kioo kigumu cha mlango wa nyuma wa lile gari naye akapepesuka vibaya.

GTZ alimshukia haraka kutoka kule juu na kuutandika teke kali ule mkono wake uliokuwa umeshika bastola, nayo ikatupwa pembeni, kisha hapo hapo akaurudisha nyuma kwa nguvu ule mguu na kumshindilia kisigino kwa nguvu kifuani, na Morandi akaenda chini kama mzigo.

GTZ hakutaka kumpa muda wa kujiweka sawa. Huku akiunguruma kwa ghadhabu, alimrukia pale chini huku akiwa ametanguliza mikono yake aliyoielekeza kooni kwa yule jamaa aliyekuwa amemuwekea kinyongo kikali, lakini sasa Morandi naye alikuwa ameshaelewa kilichomtokea.

Alimdaka ile mikono huku akigotesha soli za viatu vyake tumboni kwa GTZ na kumtupa hewani kwa nguvu katika mtindo wa judo maridadi. Muungurumo wa ghadhabu wa GTZ ukabadilika na kuwa ukelele wa fadhaa wakati akielea hewani. Aliangukia mgongo kwa kishindo nyuma ya Morandi, kisha akaserereka vibaya kwenye ule mporomoko mdogo, na kubingirikia upande wa pili wa ile barabara, akijivuruga kwenye majani na mawe.

Morandi aliruka wima na kumfuata mbio kule kwenye mporomoko. Alimuona yule adui yake akijishikilia kwenye mti na kujiinua, naye akaenda hewani kwa flying kick, na kumbabatiza kifuani kwa soli ya kiatu chake. GTZ akatupwa tena hewani na kujibwaga chini kwa kishindo na kubingirika vibaya kule bondeni kama tairi la gari, huku Morandi akimfuata mbio.

GTZ alijikita kwenye shina la mti mwingine kule bondeni na kuhangaika kujiinua kwa kujishikilia kwenye ule mti huku akiwa amegeuzia mgongo wake kule barabarani walipotokea. Alijigeuza kutaka kujua ni wapi yule adui yake alipokuwa, na hapo alishituka alipomuona Morandi akiwa amesimama akimtazama anavyohangaika.

Walibaki wakitazamana, GTZ alitweta vibaya sana.

Yule jamaa alikuwa na nafasi nzuri ya kumvamia na kumpiga vibaya wakati alipokuwa amemgeuzia mgongo akihangaika kujiinua, lakini badala ya kumvamia, alibaki akiwa amesimama namna ile akimsubiri.

Anajiamini nini huyu?

“Unataka kuniletea usteringi wa kidosi mimi, eenh??” Morandi alimkoromea kwa hasira. Alikuwa amesimama hatua kama mbili mbele yake, mguu wake wa kulia akiwa ameutanguliza mbele kidogo, mikono yake ikining’inia kila upande wa mwili wake bila kujali, ilhali uzito wa mwili wake wote akiwa ameuegemeza kwenye mguu wake wa kushoto.

GTZ alighadhibika.

Aliachia ukelele huku akimrukia kwa konde zito alilokuwa amelielekeza usoni kwa yule jamaa, na hakuelewa kilichompata.

Morandi Gwaza alijisukuma hewani kwa mguu wake wa kushoto huku ule wa kulia akiwa ameuinua juu, na akiwa hewani aliuinua kwa nguvu ule mguu wake wa kushoto na kumfumua teke zito sana la kidevu yule jamaa kwa kisigino cha mguu ule, na kutua tena ardhini akitanguliza ule mguu wake wa kulia.

Ebwana we!

Yowe fupi sana lilimtoka GTZ huku miguu yake akiiacha ardhi na kutangulia mbele hali kiwiliwili chake kikisukumwa nyuma na teke lile, naye akaelea hewani na kujibwaga chini kama mzigo.

Hakuinuka.

Lilikuwa ni pigo la mtindo wa “Karate Kid” lililokadiriwa kwa umakini na wepesi wa hali ya juu, na Morandi alibaki akiwa amesimama akimtazama yule jamaa aliyelala chali bila fahamu pale chini, damu ikimchuruzika kutoka mdomoni, bila shaka kutokana na kujing’ata mdomo au ulimi wakati akipokea pigo lile.

Alisonya, na kugeuka kurudi kule barabarani. Aliiokota ile bastola na kuiweka mfukoni. Akaliegesha pembeni zaidi ya barabara lile gari na kukomea milango yote, kisha akarudi tena kule bondeni ambako alijua kuwa bado yule jamaa atakuwa amepoteza fahamu. Alimshika mguu na kumkokotea ndani zaidi ya lile pori nene.



***

GTZ alifumbua macho ghafla na kubaki akimkodolea macho Morandi aliyekuwa amechutama mbele yake, kama kwamba ndio anamuona kwa mara ya kwanza. Alikuwa ameegemezwa kwenye mti huku mikono yake yote miwili ikiwa umefungwa kwa nyuma kwenye mti ule kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

Morandi alimchapa kofi jingine kwa mkono uliokuwa ndani ya glovu laini za mpira, na kuongeza idadi ya makofi aliyomtandika yule jamaa kwa lengo la kumzindua na kumrejeshea fahamu zilizomhama baada ya kufumuliwa lile teke zito.

“Amka bibie… amka!Nahitaji kunena nawe kidogo hapa!”Alimwambia huku akimtikisa kichwa chake akiwa amemshika kidevu.

GTZ alijikurupusha huku akigumia kwa hasira baada ya kusikia akiitwa “bibie”, lakini alikuwa amedhibitiwa kwenye ule mti.

Alijaribu kumpiga teke kwa hasira, na ndipo alipogundua kuwa na miguu yake iliyonyooshwa mbele nayo ilikuwa imefungwa pamoja kwa kutumia tai iliyokuwa shingoni kwake hapo awali.

Alibaki akimkodolea macho ya ghadhabu yule jamaa.

“Sasa uamuzi ni wako bibie…aidha utoe ushirikiano kwa kujibu maswali yangu, au niwaachie fisi kitoweo leo huku porini!” Morandi alimwambia kwa sauti yake nzito iliyojaa vitisho.

“Sio bibie mimi wewe…fala nini? Kama unajiamini mbona umenifunga hapa?” GTZ alimkoromea, na Morandi akamcheka.

“Najua kuwa wewe ni Gino Tzaspaparos…lakini kwangu mi we’ mchumba tu, nd’o maana nakwita bibie…na nd’o maana hata sikupata taabu kukufunga hapo kwenye mti!” Morandi alimjibu huku akimtazama usoni kwa makini, na akatabasamu alipoona GTZ akitumbua macho kwa mshangao.

“Un…unan’juaje mimi wewe,eenh?” GTZ alimuuliza kwa wahka, kwani hakutegemea kabisa kumsikia jamaa akimtaja jina.

Badala ya kumjibu Morandi akamtolea leseni yake ya kuendeshea gari kutoka kwenye mfuko wa ndani wa lile koti lake la jeans, na kumuonesha.

GTZ alifinya uso kwa hasira na kusonya huku akitazama pembeni.

“Si nimekwambia mi’ kwangu we’ mchumba tu? Ninaweza kukufanya lolote na usiwe na ujanja. Nimekuburura mpaka hapa, nimekufunga kwenye mti, nimekugeuza nitakavyo, nimekusachi na kuchukua leseni yako, nawe huna habari…sasa kama si uchumba ni nini tena huo?” Morandi alimuuliza kwa kebehi, na GTZ alijikukurusha kwa nguvu pale kwenye mti huku akiunguruma kwa hasira, na hapo hapo mkono mwepesi wa Morandi ukachomoka na kumtandika kofi kali la kelbu.

“Tulia mchumba!Sasa nataka unijibu maswali yangu yote wewe!Na swali langu la msingi ni kuhusu Candy Gamasala…una kisa gani naye?” Alimkoromea kwa vitisho, yale maskhara yote yakifutika usoni kwake.

“We’ waandalie tu hao fisi kitoweo cha mzoga wangu aisee…mi’ sisemi kitu hapa!” GTZ alimjibu kwa kiburi na Morandi akamzaba makofi mawili kwa wakati mmoja kwa kumbabatiza kwa nguvu kichwa chake baina ya viganja vyake vilivyokuwa ndani ya glovu, na GTZ aliachia yowe la maumivu.

“Unajitia mgumu sio? Basi leo utagundua kuwa we’ si mgumu si lolote (akamtukamia mama yake)”

GTZ naye akamtukania mama yake na kumtemea mate usoni. Morandi alimtazama kwa hasira bila kujifuta yale mate.

Kisha kwa upole sana akachomoa kisu kutoka kwenye ala iliyokuwa imefungwa kwa mikanda maalum mguuni kwake na kufichwa na ile suruali yake ya jeans. GTZ alimtazama kwa macho yenye hasira huku akiwa ametutumua midomo yake kwa kiburi. Morandi aliikwida suruali ya GTZ kwenye eneo la uume wake na kwa kitendo cha haraka sana akakipitisha kile kisu kikali na kuchana kipande cha suruali ile na kuacha tundu kubwa sehemu ile, na bila kupenda GTZ aliachia mguno wa woga.

Huku akiendelea kumtazama kwamacho ya yaliyokuwa yakizidi kuwiva kwa ghadhabu, alijifuta yale mate kwa kutumia kile kipande cha suruali na kukitupia pembeni.

“Mara ya pili nakukata huyo mjusi wako hapo, pumbavu mkubwa wewe!Unamtakia nini Candy Gamasala nakuuliza?” Alimwambia kwa hasira na kumuuliza.

Badala ya kumjibu GTZ akamtukania mama yake.

“Okay, naona hunijui wewe…subiri basi!” Morandi alimwambia na kuanza kumporomoshea kipondo cha mbwa mwizi pale alipofungwa.

Mateso aliyopewa na Morandi pale msituni yalitosha kwa mtu mwingine yeyote kumtoa rehani hata mama yake mzazi ili apunguziwe mateso.

Lakini si GTZ.

Jamaa alikuwa anagumia kwa maumivu huku akimvurumishia Morandi matusi mazito mazito, lakini hakumjibu hata kidogo maswali yake.

Hatimaye Morandi alibaki akimtazama kwa kukereka yule jamaa aliyetapakaa damu usoni na mwilini, huku akiwa na manundu sehemu kadhaa za mwili wake mkakamavu.

“Okay, kama umehakikisha hutoi majibu, basi nami nitahakikisha kuwa hukipati ukitakacho kutoka kwa Candy, nyau we!” Alimwambia, na GTZ akaanza kumcheka huku akibubujikwa na damu nyingi kinywani.

“Nilitakalo kwake nitalipata tu…yule malaya tayari ni marehemu hivi niongeavyo, bado kuzikwa tu!” Alimwambia kwa kebehi huku akitweta kwa kipigo alichopokea, na Morandi akamakinika.

“Kwa hiyo shida yako ni kumuua Candy?”Alimuuliza.

GTZ alizidi kucheka huku akilaza kidevu chake kifuani kwake kwa mchoko wa kipondo alichopokea, na Morandi akamkwida na kumtikisa kwa nguvu.

“Hebu nijibu wewe! Unataka kuniambia kuwa shida yako ni kumuua Candy? Kwa nini?”

“Sina la kuongea zaidi kaka…kama unaniua niue tu, lakini ujue nikitoka hapa namuua tu!” GTZ aimjibu kwa taabu, sasa akipumua kwa taabu kutokana na kujitia kucheka wakati akiwa ameshapokea kipigo na mateso mazito.

“Sa’ nikikuua utamuuaje?”

“Hiyo ndiyo salama yake pekee, lakini mi najua huwezi kuniua wewe! Huna ubavu huo!”

Moradi alimbabatiza kwa nguvu kisogo chake kwenye ule mti na kumkaba koo kwa nguvu.

“Sikia wewe mpumbavu…kuua ni kazi yangu! Usidhani kukuua wewe ni jambo zito sana kwangu…ni jepesi sana, paka we! Ukiona nakuacha hai ni kwamba bado kuna kitu nahitaji kutoka kwako…”

“Na hutokipata!”

Morandi aliinuka na kumtazama kwa muda, kisha akatoa bastola yake kubwa huku akimtazama kwa macho yenye dhamira mbaya.

“Ni nani aliyekutuma umuue huyu binti…na amekuahidi nini?” Alimuuliza kama namna ya kutaka kujihakikishia hisia yake ya hapo awali.

“Unaona hii ni shepu ya kutumwa ujinga kama huo na mtu hii? Nina sababu zangu za msingi za kutaka kumuua…”

“Kwa hiyo una kisa binafsi na yeye?”

Badala ya kumjibu GTZ akamtukana.

Morandi alichutama tena na kumtazama moja kwa moja machoni.

“Sikiliza vizuri bibie…”

“Sio bibie mimi!”

“Tena sikiliza kwa makini maana sitarudia tena. Wewe ni mgonjwa wa akili…lolote unalodhani linakupa uhalali wa kumuua yule binti, litakuwa ni zao la wazimu ulio kichwani mwako. Kazi yangu ni kumlinda Candy dhidi ya hila zako, na njia ya mkato kulifanya hilo ni kukuua hapa hapa na kukuacha ukioza huku…”

“Huna jeuri hiyo!”

“Lakini sitofanya hivyo. Sitokuua, kwa sababu nataka nikuone jinsi unavyoendelea kuumia kwa kushindwa kutimiza hiyo azma yako potofu wakati mrembo Candy akiendelea kung’aa mbele ya jamii, fala we! Hilo litakuwa ni pigo kubwa kwako kuliko hata hicho kifo!”

GTZ alimcheka kwa kebehi.

“Suit yourself!” Alimwambia kwa kimombo, akimaanisha kuwa kama ameamua hivyo, basi ni juu yake mwenyewe.

Morando alimkamata mguu wake na kuanza kumbonda-bonda gotini kwa kitako kizito cha ile bastola yake kama jinsi mtu anavyovunja kokoto kwa nyundo, na GTZ alilia kama mtoto.

Alimbonda-bonda kwa nguvu sana bila ya kujali vilio vya uchungu kutoka kwa GTZ, hadi akasikia kokwa la goti lile likivunjika na kusambaratika, damu ikibubujika vibaya sana kutoka kwenye eneo lile.

“Haya sasa na tuone umfuatilie Candy na kumuua, fala we!” Alisema huku akihema kwa hasira na kuinuka.

“Aaaaagh! Nitakuua wewe na Candy wako pumbavu, weee!” GTZ alibwata kwa hasira huku akilia wazi wazi.

Morandi alimkata ule mkanda uliomfunga mikono yake nyuma mti na kumwacha akilia kwa hasira na uchungu pale chini.

“Hilo goti litakuweka hospitali si chini ya miezi minne, bibie. Na hiyo ni kama utaweza kupata msaada kutoka huku porini na kufikishwa hospitali mapema!” Alimwambia huku akiondoka.

“Usiniache huku wewe! Usiniache nakwambia, usiniacheee, usiniacccheeeee!” GTZ alimpigia kelele huku akijisotesha kwa mikono yake kutambaa, mguu wake wa kulia ukiwa hauna msaada wowote kwake.

Morandi aligeuka na kumtazama akihangaika kusota kwa taabu pale chini.

“Hii bado ni trela tu bibie…kama kwa majaaliwa yake muumba utatoka salama huku porini, nitakuwekea picha kamili! Vinginevyo…rest in peace!” Alimwambia na kugeuka kuelekea kule kwenye gari.

Kelele na matusi ya GTZ vilimfikia hadi pale kwenye gari. Aliingia kwenye lile gari na kuondoka kwa kasi eneo lile, akichukua uelekeo wa Mabwepande.



***

Dakika arobaini na tano baadaye alichomozea eneo la Bunju mwisho na kukata kulia kwenye ile barabara kuu ya Bagamoyo kuchukua uelekeo wa kurudi Mwenge. Alipofika maeneo ya Boko aliegesha lile gari kwenye baa moja iliyokuwa kando ya barabara, miongoni kwa magari mengine mengi yaliyokuwa yamejazana nje ya baa ile. Akiwa mle ndani ya gari, alilifuta kwa kitambaa lile gari maeneo yote aliyohisi kuwa aliyashika kabla hajavaa zile glovu. Alivua zile glovu na kuzishindilia mfukoni mwake, kisha akafungua mlango kwa kuushika kwa kile kitambaa chake na kuteremka.

Alitazama saa na ikamwambia kuwa ilikuwa ni saa kumi na mbili za jioni.

Hakuona mtu yeyote aliyeonekana kumtilia maanani pale kwenye eneo la maegesho la baa ile. Alizunguka ubavuni mwa ile baa na kutokea upande wa pili, na kusimama kwa muda akiangaza kwa makini eneo lile. Bado hakuna aliyeonekana kumtilia maanani. Alimsimamisha mwendesha bodaboda aliyekuwa anapita pale barabarani.

“Nipeleke Tegeta!” Alimwamuru na jamaa akageuza ile pikipiki huku akimtajia bei.

“Sio tatizo…twen’zetu!”Alimwambia.

Aliondoka na dereva wa bodaboda akiliacha gari la GTZ pale baa.Njia nzima alikuwa akijiuliza ni kwa nini yule jamaa anayeenda kwa jina la Gino Tzaspaparos, alikuwa akitaka kumuua Candy kwa udi na uvumba namna ile.

Usiku ule ule Kokos Wandiba alikuwa akisikiliza sehemu ya mahojiano yale ya kibabe kati ya Morandi na GTZ kupitia kwenye spika za simu ya Morandi. Ilipofika sehemu ambapo Morandi alianza kumbondabonda goti yule jamaa, Morandi aliizima ile spika ya simu, kisha akakifuta kabisa kile kipande kilichorekodi mjadala ule.

Kokos alibaki akimtazama kwa mshangao.

“Kwa…kwa hiyo umemfanyaje yule jamaa…umemuua?” Aliuliza, na Morandi akaguna.

“Hilo sio la msingi kwa sasa. La msingi ni kwamba umemsikia mwenyewe huyu jamaa akitangaza nia ya kumuondoa duniani mrembo wako…swali linakuja, kwa nini?” Alimwambia.

“Hatujui! Ila ni wazi kuwa jamaa kadhamiria, ndo maana hakusema kabisa pamoja na mateso uliyompa. Lakini umemuachaje sasa? Huja…”

“Sijamuua bwana! Ila hali ndio hiyo kaka, jamaa ni mwehu, na amewehuka na hiyo nia yake mbaya kwa huyo mrembo wako. Sasa hapa ni lazima tuongee na Candy. Tujue ana kisa gani na huyu mjinga!”

“Kweli. Akirudi itabidi tuongee naye kwa undani sana aisee!” Kokos aliafiki huku akiwa amekunja uso kwa mawazo.

“Na ujiandae kwa mshituko kaka…” Morandi aimwambia, na Kokos akamtazama kwa uso wa kuuliza.

“Unaweza kugundua vitu usivyovitarajia kutoka kwa huyo mrembo wako. Usijenge imani kuwa yeye ni mwema tu na mwenye kuonewa katika hili. Huenda kuna zito alilolifanya huko nyuma linalosababisha huyu Gino Tzaspaparos amwekee azma ya maangamizo namna ile!” Morandi alimwambia huku akimtazama kwa macho makavu, na Kokos akaguna.

“Ah! Najua hilo linawezekana Morandi, lakini pia huyu jamaa tusiache kumfuatilia. Nashangaa umemuachaje huko msituni!” Kokos akamwambia.

Morandi akamweleza jinsi alivyomuacha kule msituni, na Kokos akaingiwa wasiwasi.

“Unadhani ataweza kutoka kule?”

“Atatoka tu yule. Jamaa ni mgumu kwelikweli ujue! Asipotoka pia ni sawa tu. Lakini akitoka atarudi mjini, hatoenda tena Mikumi. Si nilikwambia kuwa Mikumi hafiki!”Morandi alimjibu na kimya kikachukua nafasi baina yao. Hawakuwa na la zaidi la kuongelea tena.



***

Safari ya Mikumi hakuwa na tukio lolote lisilo muafaka, hivyo wale mabinti wa urembo, Candy miongoni mwao, walifika huko salama usalimini. Walifikia kwenye hoteli nzuri kwenye eneo la mbuga na kwa kuwa walifika katika robo ya mwisho ya mchana, hawakuweza kutembea sana mbugani.

Badala yake warembo walioneshwa vyumba vyao na kujipumzisha, ilhali baadhi waliotaka kuzurura mbugani waliruhusiwa kufanya hivyo, ingawa matembezi rasmi ya mbugani yalipangwa kufanyika siku iliyofuata.

Candy aliamua kutembea ndani ya eneo la ile hoteli waliyofikia huku akifurahia kuwa mahala pale. Baadhi ya warembo wenzake walikuwa wakijiburudisha kwa vinywaji baridi kwenye eneo la mapumziko la hoteli ile, na baada ya muda naye akajumuika nao.

Akiwa na warembo wenzake pale kwenye eneo la mapumziko la hoteli ile ya kitalii, simu yake ikaita, na akaona kuwa ni Bishkuku ndiye aliyekuwa akimpigia. Aliinuka na kupokea simu ile huku akijitenga pembeni na wale wenzake.

Bishkuku alitaka kujua iwapo alifika salama, na waliongea kwa muda, kisha wakakata simu. Candy alibaki akiwa amesimama kwenye veranda pweke nje ya lile eneo la mapumziko ya ile hoteli, ambayo ilikuwa ghorofa ya kwanza. Kutokea pale alipokuwa aliweza kusikia sauti na vicheko vya wale warembo wenzake waliokuwa kule ndani kwenye eneo la mapumziko.

Aliegemea ukingo wa veranda ile na kubaki akitazama nyota zilizokuwa zimetapakaa angani katika kiza kile cha mwamzo wa usiku.

“Helloo mtoto shoo, hujambo eeenh?” Sauti aliyoifahamu ilimsemesha kutokea kando yake na akajikuta akiganda kwa muda.

Mtoto shoo!

Ni mtu mmoja tu ndiye aliyezoea kumwita hivyo…sasa naye yuko hapa?

Aligeuka taratibu huku moyo ukimwenda mbio, kutazama kule ile sauti ilipotokea.





John Koccho alikuwa amesimama kando yake na badala ya kumtazama yeye alikuwa akiangalia moja kwa moja mbele.

Uso wa Candy ukachanua kwa tabasamu pana.

“Hah! Kaka John! Za miaka? Vipi mbona uko hapa? Jamaani, yani hata siamini!” Candy alisema huku akimtazama, na hapo John Koccho akamgeukia, akimtazama kwa macho yake madogo na makali.

Kinyume na matarajio yake, John Koccho hakuonesha bashasha ya kuonana naye kama jinsi yeye alivyokuwa, na Candy akabutwaika.

“Kaka John, mbona hivyo…”

“Ujumbe wangu hukuupata mtoto shoo?” Koccho alimuuliza huku akimtazama moja kwa moja usoni, na Candy akazidi kuchanganyikiwa.

“Ujumbe…?”

“Sina muda wa kupoteza sana hapa mtoto shoo! Ujumbe wangu kuhusu mambo yaliyotokea Magu…kwa nini hukunipigia simu kama nilivyokuangiza?” Koccho alimkoromea na Candy akahisi kama kwamba ile sakafu aliyokuwa amesimama juu yake ikididimia naye akibaki akielea hewani.

“Ni wewe!” Alimaka huku akipiga hatua moja nyuma, na hapo mkono mwepesi wa John Koccho ulichomoka na kumdaka mkono.

“Yes, ni mie mrembo! Tulia hapa nikupe maelekezo mapya sasa!” Koccho alimkoromea.

“Mi’ s’kuelewi, k’ka John, una maana…?”

“Shut up! Nataka hizo hela ulizopewa zawadi ya miss Dar City Centre kabla hazijaisha. Halafu nataka hela zaidi ya hapo, ama si hivyo nakupoteza!” Koccho alimkoromea tena na Candy akachanganyikiwa maradufu.

Heh! Na yeye pia? Kwanza Jackie…na sasa John?

Aliuvuta mkono wake kwa nguvu kutaka kujikwamua kutoka kwenye himaya ya yule jamaa aliyemjia kwa sura nyingine kabisa na ile aliyokuwa akiijua miaka kadhaa iliyopita, lakini Koccho naye akamvuta kwa nguvu huku akitembeza macho huku na huko kuona iwapo bado walikuwa peke yao pale kwenye ile veranda.

“Niacche! Kwa nini unafanya hivi?” Candy aliuliza kwa hamaniko lililokithiri.

“Kuna zawadi ya milioni tano kwa yeyote atakayetaja ulipo, nawe utapotea. Sina haja ya kukuchomea, kwa kuwa nakupenda, lakini pia hela naitaka, hivyo utaanza kwa kunipa hizo na utamalizia nyingine kadiri tuendeleavyo!”

Hah!

“Kadiri tuendeleavyo? Hebu niachie huko! N’takupigia mayowe sasa hivi!” Candy alimkaripia huku akiuvuta tena mkono wake,lakini John Koccho alizidi kuung’ang’ania ule mkono na hakumuona mtu aliyetokeza ghafla nyuma yake na kumtandika teke zito la mbavu.

Koccho na Candy walipiga mayowe kwa pamoja, kila mmoja kwa sababu tofauti, na Koccho akalazimika kumwachia Candy na kugeuka kule lilipotokea lile pigo.

Akakutana na teke jingine zito zaidi la ubavu wa pili nayowe jingine likamtoka huku akijipinda na kumtazama kwa mshangao yule mshambuliaji.

Candy aliachia ukelele mkubwa wa woga, na wale warembo wenzake kule ndani nao wakaitika kwa kelele na kuanza kukimbilia kule kwenye ile veranda.

Akiwa pale nje, Candy alimuona mwanadada akirudi nyuma na Koccho akimwendea kwa hasira huku ametanguliza mikono yake kimakabiliano. Na hata pale alipokuwa akitazama tukio lile, alimwona yule dada akiruka juu na kujigeuza hewani, pigo la John Koccho likimkosa, naye akamshushia pigozito kwa ubapa wa kiganja chake shingoni, na John Koccho akatupwa mbele na kuangukia uso pale sakafuni.

Yule dada alitua tena sakafuni wakati wale warembo wengine nao wakifika pale nje. Nuru akamgeukia Candy.

“Nenda chumbani kwako wewe!” Alimwambia kwa msisitizo, kishaakamgeukia John Koccho.

Koccho alijiinua na kujirusha juu ya ukingo wa ile veranda na kuangukia kule chini kutoka pale juu. Nuru naye akaruka kumfuata, akatua chini na kujiviringisha kiufundi kutuliza kishindo, akainuka wima.

John Koccho alikuwa akitimua mbio kupotelea kizani, naye akamtimkia mbio kumfuata.

Huku juu Candy alibaki akichungulia kule chini kwakutoamini, akiwaona wale watu wawili wakifukuzana kimya kimya kizani.

“Ni nini Candy!” Mmoja wa wale warembo wenzake aliuliza kwa hamaniko, na wenzao wengine nao wakafika pale huku wakiuliza kulikoni kwa wahka.

“Mwi-mwizi!” Candy aliropoka bila kufikiri.

“Hah! Kaiba nini?”

“Mwizi katokea wapi huku?”

“Amekuibia?”

Msururu wa maswali ulimwangukia, na Candy akazidi kuchanganyikiwa.

“A…alitaka kunipora simu!” Ndilo jibu lililochomoka kinywani mwake.

“Hah! Sasa…?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ametokea mtu…wanakimbizana huko!” Candy alisema kwa wahka huku akioneshea kwa kidole kule walipokimbilia John Koccho na yule mkombozi wake ambaye hakuwa akimjua hata kidogo.

Wahudumu wa ile hoteli walifika na kusaili kulikoni. Candy akarudia maelezo yake na hapo hekaheka ikapamba moto. Meneja wa hoteli na mratibu wa Miss Tanzania na baadhi ya watendaji wake nao walifika. Candy akaeleza tena maelezo yake yale yale huku kichwa kikimzunguka.

“Sasa huyu ni nani aliyekuja kumfukuza huyo mwizi?” Mratibu wa Miss TZ alisaili kwa wahka.

Wahudumu walitazamana na meneja wao, kisha meneja wa ile hoteli akajibu.

“Eh, ni mmoja wa wana usalama wetu mheshimiwa…tulipojua kuwa mnaleta warembo wa Miss TZ hapa, tulichukua hatua za tahadhari za ziada…na…na, naona zimekuwa muafaka!” Jamaa alisema uongo uliotukuka ili kuficha kashfa iliyokuwa ikielekea kuikumba hoteli yao, huku akilini akijiuliza ni nani huyo aliyemuokoa yule mrembo.

“Dah, safi sana! Mmefanya jambo la busara mno!” Mratibu wa shindano la Miss Tanzania alipongeza, kisha akawageukia wale warembo, “haya mabinti…sasa nadhani nyote mngetulia tu ndani ya hoteli…msitoke nje, nashauri sote tukapumzike vyumbani mwetu, muda wa mlo ukifika tutaarifiwa, okay?”

Mabinti walianza kurejea vyumbani mwao.

“Nimeona yule aliyekuwa akishambuliana na yule mwizi wako alikuwa mwanamke, Candy!” Tunis alimfuata na kumwambia huku akiongozana naye kuelekea vyumbani, na Candy akamshangaa.

“Kwa…kwa hiyo?”

“Ah, kwa hiyo najiuliza iwapo hiyo stori yako kuwa yule jamaa alikuwa mwizi ina ukweli wowote…” Tunis alimjibu huku akiendelea kutazama mbele, na mdomo wake ukiwa umefanya tabasamu la uchokozi.

“Khah! Unataka kusema kuwa nasema uongo? Ili iweje? Na kwanza we’ inakuhusu nini?” Candy alimuuliza, akili ikimzunguka.

Huyu Tunis naye ananiletea habari gani tena hizi sasa?

Walifika chumbani kwa Tunis naye akasimama nje ya mlango wa chumba chake.

“Mi’ imenikalia kama kwamba ni fumanizi fulani hivi…” Alimwambia huku akimtazama kwa jicho la uchokozi, na Candy hakuamini.

“Ah! Fumanizi??”

“Yap! Umekutwa na mume wa mtu, na mke na mume wakaanza kuzichapa…sa’ s’jui itakuwaje waandishi wa habari wakiipata habari hiyo!” Tunis alimjibu na kuingia chumbani kwake, akimwacha Candy akiwa ameduwaa pale nje



***

Wakati Candy akijieleza kwa mara ya pili mbele ya uongozi wa ile hoteli na wa kamati ya Miss Tanzania kule hotelini, kule nje Nuru alikuwa akiongeza kasi kumkimbiza yule jamaa aliyemkurupusha akimpa Candy wakati mgumu kule hotelini.

Alimwona jamaa naye akiongeza kasi huku akijaribu kugeuka nyuma kuona iwapo bado alikuwa akifukuzwa, na Nuru akajua kuwa muda si muda atamtia mkononi tu.

Alikuwa akimkimbiza jamaa kimya kimya makusudi, kwani alijua mtu akikimbizwa hutaraji kusikia mayowe kutoka kwa wakimbizaji wake, nayo yalimpa picha kuwa wakimbizaji wake walikuwa umbali gani kutoka kwake. Lakini akikimbizwa kimya kimya, wahka humfanya ajaribu kugeuka kuona mtu au watu wanaomkimbiza wako umbali gani. Na mtu akikimbia huku akigeuka-geuka nyuma lazima atapoteza muelekeo, na yumkini akajichanganya na kuanguka mwenyewe.

Nuru aliyajua yote haya, na akazidisha kasi huku akijipinda kutokea kiunoni tayari kumrukia yule jamaa pindi atakapojichanganya.

John Koccho alikuwa amechanganikiwa vibaya sana.

Iweje avamiwe na mwanamke namna ile? Kwanza yule mwanamke ni nani? Polisi…?

Ina maana Candy kawekewa mlinzi maalum?

Au ni warembo wote ndio huwekewa walinzi namna ile?

Sasa mbona tangu wale warembo wamefika pale hotelini amekuwa akimfuatilia kwa makini na hakuona dalili yoyote ya mlinzi miongoni mwa wale warembo, na hususan kwa Candy?

Ingawa alikuwa akisikia vishindo vya miguu ya yule mwanadada hatari aliyekuwa akimkimbiza, hakuweza kujizuia kugeuka tena nyuma na kuona bado kivuli cha yule mwanamke kikiwa nyuma yake, na nusura ajipamie kwenye mti uliokuwa mbele yake.

Aliachia ukelele wa mshituko na kuukwepa ule mti, akatupa jicho mbele yake na kuuona uzio uliokuwa ukiitenganisha sehemu ile ya mbuga na barabara ya wapitao nje ya mbuga zile ukiwa hatua chache tu kutoka pale alipofika.

Akapiga hatua moja kubwa kuuwahi uzio ule, na hapo akashitukia akikumbwa kwa nguvu kutokea nyuma na akapiga mweleka mzito, akihisi mikono imara ikiwa imemkamata kiunoni.Yeye pamoja na yule mwanadada aliyekuwa akimkimbia walibingirika vibaya kwenye majani na vumbi.

Nuru alimng’ang’ania kwa nguvu yule jamaa, lakini katika kubingirika namna ile mikono yake ikaachia naye akasererekea upande mmoja ilhali yule adui yake akipitiliza na kujikita kwenye ule uzio wa senyenge uliokuwa ukiitenganisha mbuga ile na barabara iliyokuwa nje ya mbuga.

Nuru alilaani huku akijitupa wima na kuangaza huku na huko kumtafuta adui yake, na hapo akasikia mtikisiko wa nguvu wa zile senyenge. Aligukia kule ule mtikisiko ulipotokea, na ndipo apomuona yule jamaa akiziparamia zile senyenge kwa pupa.

“Pummmbaaavvv!!” Alipiga ukelele huku akimtokea kasi na kwenda hewani kujaribu kumdaka miguu yule jamaa kabla hajapotelea upande wa pili wa zile senyenge, lakini alichelewa na akaishia kujibabatiza kwenye zile senyenge huku akimwona yule jamaa akiangukia barabarani nje ya ule uzio na kupotelea kwenye mwitu uliokuwa upande wa pili wa ile barabara.

Alibaki akiwa amezikamata zile senyenge huku akiweta kwa hasira na uchovu.

Alikaa chini taratibu na kujiegemeza kwenye zile senyenge huku bado pumzi zikimtoka kwa kasi. Alitulia kwa muda mpaka pumzi zake ziliporudia hali ya kawaida, ndipo alipotoa simu yake na kumpigia Morandi.



***



Candy aliingia chumbani kwake na kujibwaga kitandani. Mambo yaliyomtokea usiku ule yalimchanganya akili vibaya sana. Mtungo wa maswali uliokuwa ukizunguka akilini mwake ulionekana kutokuwa na mwisho.

Kwanza Jackie, halafu akatokea yule mtu asiye jina aliyejaribu kumteka kule Kariakoo siku kadhaa nyuma, halafu tena na John Koccho naye ameibuka na kumgeuka kabisa, akimkumbusha mambo ya Magu.

Magu ambayo aliamua kuifuta kabisa katika kumbukumbu zake kutokana na uchungu wa madhila aliyokumbana nayo huko…

Na alipochanganya yote hayo na lile la mwisho aliloangushiwa na Tunis usiku ule, aliishiwa namna kabisa.

Hakika hii ilikuwa imezidi viwango na hakuona kama aliweza kuendelea kuyabeba tena mambo yote yale yaliyoazimia kumwandama bila kikomo maishani mwake.

Ni vyema angebaki yatima tu asiye na mbele wala nyuma, kuliko kujitia matarajio ya kujitengenezea jina na maisha bora kuliko yale ambayo bila shaka muumba ndiyo alikuwa amemuandalia hapa duniani.

Kufikia hapo, mwanadada aliangua kilio kikubwa na cha kukata tamaa.







Alilia sana!

Alilia huku akikumbuka madhila aliyokumbana nayo Magu, na alilia kutokana na mambo yaliyokuwa yakimtokea wakati ule aliokuwa nao. Kila aliyemjua alionekana kuwa anafanya kila liwezekanalo kumzamisha kwenye matatizo makubwa ambayo kiukweli hata yeye mwenyewe alikuwa hayaelewi.

Sasa John Koccho anasema eti kuna zawadi ya milioni tano kwa yeyote atakayetaja nilipo…kwa nini?

Na kama kuna hiyo zawadi, baada ya kuwa ameshajua nilipo, kwa nini yeye asiwatajie hao walioahidi hiyo zawadi mahala nilipo ili achukue hiyo million tano?

Badala yake eti anataka nimpe mimi hela zilizobaki kwenye zawadi yangu ya Miss Dar City Center, halafu hela nyingine nitakuwa nampa kadiri tunavyoendelea!

Tunavyoendelea?

Ina maana anataka mi’niwe bomba lake la hela!

Yale yale ya Jackie!

Yaani kweli hela ndiyo inawatoa watu imani kiasi hiki? Kwanini?

Kwa kuwa kuna mambo yaliyotokea Magu ambayo yakijulikana nitakuwa kwenye wakati mgumu!

Akh, mambo gani hayo mabaya kiasi hicho?

Hakuna lililomjia akilini, kwa kweli, na kwikwi za kilio zikazidi kumkwida.

Na wakati akilia, alishtushwa na wimbo wa hayati Tupak Shakur, Me against the World, kutoka kwenye simu yake.

Kokos!

Aliinyakua ile simu na kuona ni kweli kuwa Kokos alikuwa akimpigia.

Kutokana na yule jamaa kupenda sana kusikiliza nyimbo za hayati Tupak, yeye akaweka muito wa wimbo ule ili uwe unaita kila anapopigiwa simu na Kokos, na Bishkuku alimwekea wimbo wa Celine Dion, A new day has come.

Alijifuta machozi na kupokea ile simu.

“Eh, hello….”

“Ah, Candy vipi…uko poa?” Kokos alimuuliza kwenye simu na Candy akashangaa.

Je ameshajua yaliyonikuta? Au ni yeye ndiye aliyemtuma yule dada aje kunilinda huku?

“Ah, Yaa, niko vizuri tu…vipi kwani?”Alijikakamua kujibu.

“Ah, safi. Sina jipya…nilitaka kukusalimu tu na kujua hali yako…kwa hiyo mmefika salama na kila kitu kiko okay?”

Hajui kilichotokea?Au ananitega?

“Ya, all is okay. Ahsante kwa kunipigia….kuna lolote ?”

“No, no…nili…nilitaka kujua hilo tu Candy. Ukirudi itabidi tuongee kuhusu yule mtu anayekufuatilia, sawa?”

Hajui.

“Er, sawa tu. Kwani…kuna jipya?”

“Hakuna ambalo unahitaji kujitia mashaka kwalo kwa sasa. Fanya mambo yako tu huko, ila ukirudi tutaongea zaidi, okay?”

“Sawa, Kokos…thanks for calling, eenh?”

“No problem.”

Wakakata simu na Candy akabaki akiwa amekunja uso kwa tafakuri, ule wimbo wa Tupak bado ukirindima akilini mwake.

Alikaa katika hali ile kwa muda, kisha akapitisha uamuzi na kutoka nje ya chumba kile.



***

Jijini Dar Morandi alikuwa akifuatilia habari za mtu aitwaye Gino Tzaspaparos kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia kompyuta mpakato yake akiwa pale sebuleni kwa Bishkuku, ambako ndio alikuwa amefanya makazi yake ya muda wakati akina Bishkuku wakiwa wamehamia kule nyumbani kwa Kokos.

Kwa kupitia mtandao wa Facebook alipata habari za yule jamaa na kuona baadhi ya picha zake mbalimbali; na kwa mara nyingine akajithibitishia kuwa yule jamaa alikuwa anajiweza sana tu kifedha, kwani picha zake nyingi zilimuonesha akiwa kwenye magari mbali mbali ya kifahari, au akiwa ndani ya sebule na nyumba za kifahari, ilhali nyingine zikimuonesha akiwa nje ya nchi, na hizi zilikuwa nyingi sana. Hii ilimpa imani kuwa lolote lililokuwa likimsukuma yule jamaa kutaka kumdhuru Candy na kumuondoa kabisa hapa duniani lilitokana na kisa binafsi na binti yule.

Sasa ni kitu gani hicho?

Ilimfunukia kwa mara nyingine kuwa Candy alikuwa ameficha siri kubwa ambayo hakuwa amewaambia hata wale wafadhili wake, na hii ilimtia wasiwasi sana. Ni moja kati ya sababu zilizomfanya amuache hai yule jamaa ambaye kutokana na ule mtandao wa Facebook, aligundua kuwa hupenda kujitambulisha kama GTZ.

Simu yake iliita.

Akaipokea na sauti ya Nuru aliyejaa wahka ikavuma sikioni mwake.

“Ah, Mo we kichwa! Kweli jeshi la polisi limepata hasara sana kwa wewe kutokuwa upande wake hivi sasa aisee, Dah!”

“Ni nini Nuru, kumetokea nini huko?”

“Ulikuwa sahihi Mo. Huyo jamaa anayemfuatilia Candy alikuwa na mshirika wake aliyemtanguliza huku Mikumi kumshughulikia Candy!”

“Whaat?”

“Kabbisa bwana!”

“E bwana we!” Morandi alistaajabu, na Nuru akaendelea kumuelezea juu ya ule mkabala baina yake na John Koccho kule Mikumi.

“Kwa hiyo ulifanya la maana sana kunitanguliza huku kumfuatilia Candy, Mo!” Nuru alimalizia.

“Sasa ulipata kumuona vizuri sura yake huyo mjinga wa huko?” Morandi aliuliza huku akili ikimzunguka.

“Bahati mbaya sijaweza kuiona sura yake vizuri, ila nikimuona tena namna anavyotembea, nadhani nitamjua tu!”

“Okay, na ulifanikiwa kusikia walikuwa wakibishania nini na Candy kabla hujaanza kumpa madochi huyo jamaa?”

“Not really. Nilisikia tu Candy akimwambia amuachie ama si hivyo atapiga kelele…ila kwa namna fulani nahisi wanajuana wale!” Nuru alijibu, na Morandi akamakinika.

“Kwa nini wasema hivyo, kisura?”

“Kwa sababu nilimsikia Candy akimwita yule jamaa kwa jina…nahisi lilikuwa John…au Jonas…au kitu kama hicho. Sikuweza kusikia kwa yakini sana.” Nuru alimjibu kutokea Mikumi.

Huku Dar, Morandi alifinya uso kwa tafakuri.

Alikumbuka kauli ya GTZ kule porini alipokuwa akimtesa.

…yule malaya tayari ni marehemu hivi niongeavyo, bado kuzikwa tu!

Ah! Ina maana alisema vile akijua kuwa kuna mwenzake keshatangulia Mikumi, au ni mambo tu yamegongana?

Akamwelezea Nuru juu ya mkasa wake na yule jamaa aitwaye GTZ.

“Ah! Huyo na huyu jamaa niliyemkurupusha huku wote lao moja hawa!” Nuru akahitimisha baada ya kusikia maelezo ya Morandi.

“Basi bora na iwe hivyo!” Morandi alisema huku sauti yake ikionesha mashaka mazito, na Nuru akashindwa kumuelewa.

“Ni bora iwe hivyo…?”

Morandi aliguna kidogo na kupitisha kimya kabla ya kufafanua.

“Yap, kisura wangu, ni bora iwe hivyo. Kwa maana kama si hivyo, itamaanisha kuwa kuna watu wawili tofauti wanaomsaka huyo binti kwa nia mbaya. Sasa huoni kuwa huo utakuwa ni mtafaruku mkubwa zaidi?”

“Duh, kweli aisee!”

“Yaa, na hilo linazidi kuniletea maswali mengi kuhusu huyu Candy, Nuru. Yumkini kuna mazito aliyoyafanya huko nyuma…”

“Au kuna mazito aliyoyaona, au anayoyajua, ambayo hawa jamaa hawataki ayaseme kwa wengine! Umeshafikiria kitu kama hicho?” Nuru alitoa hoja yake na kusaili.

“Lah!” Morandi aliishia kuguna, kisha akasema, “Yaweza kuwa hivyo pia, ingawa moyo wangu haunitumi kuwa ni hivyo…”

“Sasa inakuwaje?”

“Sikia mrembo wangu. Usimwache kabisa mbali na upeo wa macho yako huyo binti. Najua huyo jamaa hatorudi tena, ila hakikisha unafuatilia kila nyendo za Candy. Nataka Candy arudi Dar akiwa hai ili niweze kujuasiri zake!” Morandi alitoa maelekezo.

“Roger that, Mo!” Nuru alimjibu, akitumia lugha ya kipolisi kumaanisha kuwa amemuelewa vilivyo.



***



Tunis alisikia mlango wa chumba chake ukigongwa. Akijua kuwa atakuwa ni mmoja wa warembo wenzake hakufanya ajizi kwenda kufungua ule mlango, na alipomuona mgongaji wa hodi ile, aliachia tabasamu pana.

“Karibu Miss Dar City Center…nikusaidie nini sasa?” Alimuuliza.

Candy alimsukumia ndani kwa nguvu huku naye akimfuata mle ndani. Tunis alitoa yowe dogo la mshituko huku akimtazama kwa mshangao. Candy aliukomea ule mlango kwa ndani na kumgeukia Tunis aliyekuwa akijiweka kitandani huku akimtazama kwa woga.

“Wewe na mimi tunahitaji kuongea Tunis, na tukishaongea, hutarudia tena kuniletea hivyo vichokochoko vyako vya kijinga wewe, umenisikia?” Candy alimwambia kwa sauti iliyojaa hasira, na uso wake ukiidhihirisha hasira aliyokuwa nayo.

Tunis aligwaya vibaya sana.

“Un…unataka kufanyaje sasa wewe?” Alimuuliza kwa mashaka.

Candy aliketi kwenye kochi lililokuwa kando ya kile kitanda alichokalia na kubaki akimtazama kwa hasira.

“Nataka ufute kabisa huo uzushi unaotaka kuueneza juu yangu akilini mwako Tunis, kwa sababu hautakusaidia lolote.” Alimwambia, na Tunis akaachia kicheko kidogo cha mashaka.

“Hah, uzushi? Mi’ si nimesema nilichokielewa kwenye tukio lile? Na nisipoacha utanifanya nini?”

“Umeelewa vibaya Tunis, na unajua kuwa umeelewa vibaya. Unataka kueneza uzushi huo ili iweje lakini Tunis?”

“Hah! Ili iweje? Si ili nikupake choo ukose mvuto kwa watu na uukose ubingwa wa Miss Ti-zedi! We’ vipi? Hii ni vita, kila mtu anatumia mbinu zake kushinda…kama wewe ulivyojitia kujinadi uyatima ili upate huruma za wananchi. Sasa wananchi inabidi waone kuwa yatima wao si lolote bali ni mvunja ndoa za watu tu!” Tunis alimchachamalia.

Candy alitikisa kichwa kwa masikitiko.

“Uyatima sikujisingizia Tunis, mimi ni yatima kweli. Na Bishkuku alishamweleza bosi wako Sanura juu ya hilo.”

“Mi’ sijali! Hiyo mmeitumia kama mbinu, na mi’ naamua kutumia hili tukio la leo kuwa ndiyo mbinu yangu!”

“Basina iwe ni mbinu yenye ukweli ndani yake wewe! Sio uzushi na upotoshaji! Mi’ siwezi kukubali!” Candy alimjibu.

“Hiyo mi’ hainishughulishi. Utajijua!”

“Sikia Tunis. Mimi sina ubaya na wewe. Lakini ukitaka niwe mbaya kwako nitakuwa mbaya kweli kweli ujue! Kuna mtu wangu wa karibu naye alijaribu kunifanyia kitu kama hicho unachotaka kunifanyia wewe…naamini hivi sasa anajuta sana huko aliko na haamini kuwa ningeweza kumfanyia kile nilichomuonesha kuwa naweza kumfanyia…”

“Usinitishe wewe!”

“Wala sikutishi. Nakwambia. Nimelia sana kwa kitendo ulichotaka kunifanyia leo hii. Lakini nikaona kuwa kulia hakutanisaidia, ila kuja kukukanya kutanisaidia. Achana na hilo wazo lako Tunis!”

“Kwa nini?”

“Kwa sababu halina tija. Hapa tulipo hatujui nani atanyakua ubingwa, hivyo hata ukinifitini na kunitoa kwenye kinyang’anyiro hiki, bado kuna warembo wengine kibao tayari wenye nafasi sawa ya kutwa ubingwa…sasa utawafitinisha wote ili ubaki peke yako? Haiwezekani…achana na hilo!”

“Ah! Hivi we’ unaona kuna mtu wa kunyakua taji katika hawa wadada wengine? Hapa wanyakuaji taji ni mimi na wewe tu! Na nikikutoa wewe basi taji ni langu!”

Candy akamshangaa.

“Khah! Unapata wapi mawazo hayo wewe lakini, eenh? Kwa nini ni mimi na wewe tu ndio tustahili kunyakua…”

“Si sote tumefundwa na Bishkuku!Bishkuku ni mkufunzi mzuri sana ati, na nd’o maana najua kuwa kama si mimi basi ni wewe…mi’ nataka niwe mimi!”

“Ama! Sasa kama unalijua hilo kwa nini basi ulimhama Bishkuku ukaenda kwa Sanura? Unajua we’ ni mpuuzi sana!”

“Ah, hiyo si kazi yako! Bishkuku hana pesa na hajuani na watu wengi wenye hadhi ya kuweza kumpaisha mrembo wake kuwa zaidi ya Miss Ti-zedi bhana, ndo maana nikaenda kwa Sanura!” Tunis alimjibu, na Candy akazidi kumshangaa.

“Basi bora tukachuane jukwaani Tunis. Achana na huo mpango wako mchafu, yule ni kibaka aliyetaka kunipora simu nasi vinginevyo. Umesikia maelezo ya meneja wa hoteli pale.Yule mwanamke aliyemfukuza yule kibaka ni afisa wao wa usalama hapa hotelini na alikuwa akifanya kazi yake. Hizo porojo zako za fumanizi ni uzushi na achana nazo…”

“Yote hayo sio muhimu kwangu, bibi eenh, upo? La muhimu ni kwamba magazeti yataandika kuwa umefumaniwa, na hilo linatosha kukupaka choo mbele ya jamii…”







“Basi sasa sote tutatoka kwenye kinyang’anyiro hiki Tunis, tuwaachie hao madada wengine wapambane na sisi tutakuwa tukishuhudia tu pembeni kama watanzania wengine!” Candy alimkemea na hapo hapo akamrukia na kumkandamiza pale kitandani.

Tunis alipiga kelele za woga

“Ahh, we vipi niachie! Unataka kufanya nini sasa?” Alipayuka.

“Sikiliza wewe. Kama huachi huo ujinga wako basi sote tutaaga mashindano haya, upo?”

Tunis alijikurupusha na Candy akazidi kumdhibiti kwa kumlalia huku akimbana mikono yake pale kitandani.

“Ahh, sikuelewi m’mi bhana…niache!” Tunis alilalama.

“Labda umesahau. Kanuni kuu ya shindano la Miss Ti-zed inasema nimarufuku warembo kutukanana, kupigana au kuzozana wakiwa katika shindano au maandalizi ya shindano. Na warembo watakaofanya hivyo wataondolewa mashindanoni mara moja.Tena bila kujali nani kaanzisha ugomvi au mabishano hayo. Unaikumbuka hiyo?” Candy alimkoromea huku akitweta, na Tunis akagwaya.

Ile habari ilikuwa ni kweli tupu naye hakuwa ametarajia kuwa Candy angeweza kufikiria kuchuka hatua ile.

“Kwa hiyo…?”

Candy akamuachia na kurudi kuketi kwenye kochi.

“Kwa hiyo usipoacha huo ujinga wako nakuanzishia vurumai usiku huu huu wakati wa mlo wa jioni, mbele ya kila mtu hapa hotelini. Amini usiamini bila kujali nani kaanzisha ugomvi sote tutatupwa nje ya mashindano mjinga wewe! Sasa tuone nani kati yetu atachukua ubingwa tukiwa nje ya mashindano. Upo?”

Dah, Tunis alichanganyikiwa.

“Huwezi kufanya hivyo!”

“Nijaribu uone fala wewe! Utaacha huo mpango au huachi?” Candy alichachamalia, na Tunis aliona kuwa hakika Candy alikuwa amemmbadiliakia vibaya sana.

“Sasa unajuaje kama bado sijapiga simu kwa wadaku kuwapa habari hiyo?” Aliuliza kwa mashaka.

“Basi na litote tugawane mbao bibi. Mi’ nalianziasha tu Tunis, na sote tutaaga mashindano!” Candy alijibu na kuinuka kuanza kutoka nje ya chumba kile.

“No! Usiondoke! Bado sijasema bhana, haki ya Mungu tena s’jasema!” Tunis alipayuka.

Candy alisimama huku akiwa ameshikilia kitasa cha mlango na kumgeukia.

“Kwa hiyo tumekubaliana juu ya hilo? Hutaendelea na huo ujinga wako Tunis?”

Tunis alimtazama kwa hasira ya kushindwa.

“We’ unajitia mjanja sana wewe!”

“Tumekubaliana, hatujakubaliana?”

“Mi’ ntakubwaga tu kwenye mashindano wewe!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Tumekubaliana, hatujakubaliana Tunis?”

“Ya! Poa, sio ishu. Ipotezee, lakini ujue huu ni mchuano kati yangu na wewe Candy, na mi’ n’tatoka kidedea tu…kwa vyovyote vile!” Tunis alimwambia kwa hamasa.

Candy alimtulizia macho kwa muda mrefu, kisha akamuuliza tena.

“Tumekubaliana juu ya hili Tunis?”

“Ndiyo bhana! Si nimeshasema? Tumekubaliana. Sitaeneza huo uvumi!” Tunis alimpayukia na kumsonya.

“Good girl! Sasa nikisikia popote habari hiyo, jua nakuvamia na kulianzaisha, na sote tunatupwa nje ya mashindano. Have a bad night!” Alimjibu na kutoka nje ya chumba kile.

Ilikuwa ni zamu ya Tunis kubaki akiwa amechanganyikiwa vibaya sana.

Aliporudi chumbani kwake, Candy alimpigia simu Bishkuku na kumjuza juu ya lile tukio la kutaka kuvamiwa na John Kochho, ingawa kidogo hadithi yake aliipindisha na kumwambia kuwa alikuwa ni kibaka aliyetaka kumpora simu.

Bishkuku hakushtuka sana kwa kuwa aliipokea kuwa ni habari ya kibaka tu wa kawaida na Candy hakukutwa na madhara yoyote. Naye aliinua simu na kumpigia Kokos kumjuza juu ya hilo. Tatizo simu ya Kokos ilikuwa ikiita tu bila majibu, naye akalisahau kabisa swala hilo.

Kokos alikuwa akipiga ulabu muda huo.



***

Siku mbili baadaye warembo walikuwa njiani kurudi jijini bila ya tukio lolote la ajabu kutokea. Ingawa Candy alijitahidi sana kumsaka yule mwanadada aliyemuokoa kutoka mikononi mwa John Koccho usiku ule wa tukio, hakufanikiwa kabisa kumuona.Bila ya yeye kujua, Nuru alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu sana muda wote aliokuwa kule Mikumi baada ya lile tukio la John Koccho.

Jijini Dar Morandi Gwaza aliona habari ya GTZ kuokotwa na wasamaria wema huko msitu wa jirani na Mabwepande kwenye gazeti, na uso wake ukafanya tabasamu pale aliposoma kuwa alipohojiwa na polisi, GTZ alisema kuwa hawakumbuki kabisa watu waliomteka na kumtesa na kumpora baadhi ya vitu vyake vya thamani ikiwamo pochi lake la pesa na gari.

Habari ile pia iliandika kuwa gari lake lilikutwa likiwa limeegeshwa kwenye baa moja maeneo ya Boko, na hakuna aliyejua ni nani aliyelifikisha gari lile mahala pale, ingawa muandishi wa habari ile aliandika kuwa bila shaka ni hao watu waliomteka na kumpora yule jamaa.

Habari ilianisha kuwa GTZ alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan, jijini Dar.

Morandi alitabasamu na kulitupa kando lile gazeti huku akijiegemeza vizuri kitini pale sebuleni kwa Bishkuku, akisubiri kuwasili kwa Candy kutoka Mikumi ili amhoji kinaga ubaga.

Lakini hilo halikuwa.

Kwani habari iliingia katika ofisi za kamati ya Miss Tanzania kuwa hali ya rais wa Venezuela, ambako ndiko mashindano ya Miss World, yaani mrembo wa dunia, yalikuwa yamepangwa kufanyika ilikuwa ni mbaya sana. Kamati ya Miss World ilikuwa kwenye wakati mgumu kwani serikali ya Venezuela iliweka bayana kuwa iwapo hali ya rais wao itaendelea kuwa mbaya, itabidi waahirishe uenyeji wao wa shindano lile, na kamati ya Miss World ikaingia taharuki. Ni nchi gani itakubali kubeba jukumu hilo ndani ya muda mfupi namna ile? Maandalizi yote ya likuwa yamekamilika kule Venezuela, sasa iweje tena waanze kutafuta nchi nyingine?

Maamuzi yalipitishwa kuwa shindalo la Miss World lifanyike haraka iwezekanavyo, kulekule Venezuela, kabla hali ya rais wa nchi hiyo kuwa mbaya zaidi.

Ikapitishwa kuwa shindano lifanyike miezi miwili kabla ya muda uliopangwa awali.

Na huku Tanzania, shindano la Miss Tanzania ikabidi lifanyike miezi mitatu kabla ya muda uliopangwa awali.

Hii ilibadilisha mipango ya Morandi kwa kiasi kikubwa sana.



***

Baada ya Candy kuwasili jijini alikutana na habari ya shindano kuu la kumchagua mrembo wa taifa kwa mwaka husika kufanyika ndani ya wiki mbili tu baada ya ile safari yao ya Mikumi.

“Heh, Bishkuku! Sasa mbona imekuwa ghafla sana? Kuna ratiba kadhaa bado hazijafanyika…si tulitakiwa twende kutembelea mlima Kilimanjaro na maeneo mengine ambayo yanasemekana kuwa ni vivutio vya utalii wa nchi yetu?” Candy alisaili kwa hamaniko.

“Ndiyo hivyo bi mdogo! Mambo yameharibika na inabidi twende na hali iliyopo. Kamati ya Miss Tizedi imeahirisha ratiba nyingine zote. Sasa kilichopo ni kujiwinda kwa ajili ya mchuano mkuu tu, na hilo halina masihara!” Bishkuku alimjuza.

“Dah, sasa kuna mambo ambayo inatupasa tuyafanyie kazi jamani kuhusu yule jamaa anayemfuatilia Candy! Kuna matukio yaliyotokea hapa kati, na nadhani ni muda wa kuliweka hilo nyuma yetu kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha miss tizedi!” Kokos alidakia, na Bishkuku hakukubali.

“Hapana Kokos. Kwa sasa nataka Candy ashughulike na mtihani ulio mbele yake tu na si kinginecho! Maandalizi na taabu zote tulizopata miezi yote hiyo iliyopita yalikuwa ni kwa ajili ya shindano hili, na sasa…”

“Ah, Bishi! Unadhani bila usalama wake ataweza kushiriki kikamilifu? Kuna mtu nataka nimkutanishe naye ili atoe habari za kutuwezesha kumjua kiundani yule mwendesha pikipiki!”Kokos alidakia.

“Si umesema kishadhibitiwa na huyo mtu wako?” Bishkuku alisaili, na Candy akamakinika.

“Kadhibitiwa? Kivipi?” Alihoji.

Kokos na Bishkuku walitazamana. Kokos akamweleza kuwa walifanikiwa kumdhibiti asimfuate Mikumi lakini bado walikuwa wanataka kujua sababu za yule mtu kumkamia namna ile, naye alitakiwa awape maelezo fulani kutekeleza hilo.

“Sasa mmemdhibiti kivipi…amekamatwa?”

“Hapana, ila tunadhani kwa muda wote ambao utakuwa kwenye mashindano yako, hatoweza kutusumbua tena.Tunachotaka kujua ni nini akitakacho kwako?”

“Hilo tutalijua tukijaaliwa baada ya shindano Kokos, na si kabla ya hapo. Sitaki Candy achanganyiwe habari za kumpotezea umakini muda huu!”Bishkuku alidakia. Candy bado alikuwa na hamu ya kujua zaidi ni kivipi yule mtu alidhibitiwa na Kokos, na muda ule alikuwa wapi, lakinini wazi Bishkuku hakutoa nafasi ya hilo.

Kufikia hapo mjadalaukachukua picha ya kilichojiri kule Mikumi kati yake, JohnKoccho, na Nuru.

“Ah, how come sijaambiwa juu ya hili jamani? Si nd’o mambo ninayoyasema haya?Sasa kumbe kuna mtu mwingine aliyekufuata huko?Ni nani huyo?Candy inabidi tuwekane wazi hapa.Kuna nini kinachoendelea?”

“Sio kumfuatilia Kokos…ni kibaka tu aliyetaka kumpora simu…lakini hakufanikiwa!” Bishkuku aimwambia, akielezea kile alichoelezewa na Candy, na Candy akajisikia vibaya sana.

Nadhani itabidi niseme ukweli sasa…hii hali inaelekea kubaya!

“Dah!Lakini ningepaswa kujua!”Kokos alilalama.

“Wewe nimekupigia simu sana kutaka kukujuza juu ya hili na hukupokea! Ulikuwa kwenye ulabu na kwa machangudoa yako huko mtizame kwanza!”Bishkuku alimjia juu.

“Hebu acha hizo Bishi, machangudoa kitu gani?” Kokos alijitetea, kisha akamgeukia Candy, “Sikuwa kwa changudoa Candy, usimsikilize huyu. Labda nilikunywa tu lakini…”

“Ah, sasa hiyo mi’ inanihusu vipi Kokos? We’ endelea tu na mambo yako!” Candy alimjibu kwa tahayari kiasi.

Bishkukua aliwatazama na akataka kusema kitu, akaghairi.

Kokos akajibalaguza na kujikohoza huku akijikunakuna kichwa.

“Er, okay…sawa…lakini Bishkuku, si tuko nyumba moja hapa?Ina maana uliponikosa kwenye simu hatukuonana tena mpaka leo hii?”

“Nilipitiwa tena Kokos. Hii habari ya kufanyika shindano wiki mbili kabla imenichanganya sana.”

Kimya kikatandakwa muda.

“Okay…sasa tunafanyaje kuhusu Candy na huyu mwendesha pikipiki kwa sasa jamani? Mi’ nataka tupate maelezo tu ya Candy, halafu mi’ na mtu wangu tutaendelea na ufuatiliaji wetu na nyi’ mtaendelea na harakati zenu!” Kokos alitupa karata yake ya mwisho.

“Kwa sasa siruhusu Candy kufikiria lolote zaidi ya mpambano wa wiki mbili zijazo Kokos. Fanya ufanyalo ili aendelee kuwa salama, baada ya kujua mbivu na mbichi mpambano ukiisha she is all yours, lakini kwa sasa, yeye ni wangu na ni wangu tu!” Bishkuku alisisitiza.

“Ah, okay sista…itabidi nikaongee na mtu wangu sasa. Lakini nina hakika hatopendezewa…” Kokos aliafiki kwamashaka.

Bishkuku alipiga kimya, mdomo wake akiwa ameubana kwa dhamira ya kile alichokiamua.

“Er, lakini nadhani kuna kitu inabidi niwajulishe kuhusu lile tukio la kule Mikumi jamani…” Candy alisema kwa mashaka, na wote wakamgeukia, naye akawaeleza juu ya kitisho alichopewa na Tunis baada ya lile tukio la John Koccho.

“Ah! Yaani Tunis amekuwa hivyo? Ama kweli ukikaa na nyoka nawe utachukua tabia za kinyoka-nyoka tu! Huyo ni Sanura huyo anayemjaza ujinga namna hiyo!”Bishkuku alikuja juu.

“Hilo ni wazi kabisa! Sasa ikawaje?” Kokos aliuliza kwa udadisi.

“Ah, mi nikamtishia kumfanyia fujo na kumuanzishia ugomvi ili sote tutupwe nje ya mashindano…ndio akaacha.”

Bishkuku alimtazama kwa kutoamini.

“Umefanya hivyo?” Hatimaye aliuliza.

“Sasa kumbe ningefanyaje Anti Bishi!Mtu anataka kuniharibia nafasi hivi hivi tu?”

“Shabbash! Umefanya safi sana! Ama kweli ukikaa na nyoka na we’ lazima uchukue tabia za kinyoka tu. Kwani naamini hata kama ningekuwa mimi nisingekubali, ningetafuta namna tu ya kumnyamazisha!” Bishkuku alisema huku akimpigapiga pajani yule mrembo, na Candy akashusha pumzi za ahueni.

Kokos alibaki akimtazama kwa mastaajabu, mawazo mengi yakipita kichwani mwake.



***





Morandi Gwaza alikuja juu vibaya sana.

“Sasa hii ndio nini? Mi’ nataka kumaliza hili swala nishike hamsini zangu Kokos! Sasa unaponiambia kuwa tusuburi mpaka shindano la Miss Tanzania liishe ndio tupate kuongea na Candy sikuelewi, ujue!” Alisema kwa hamasa.

Kokos alimtazama tu bila ya kusema kitu, wakiwa sebuleni kwa Bishkuku pale mtaa wa Aggrey. Alishampasha habari juu ya uamuzi wa Bishkuku kuhusu swala lile na sasa alikuwa akishuhudia matokeo ya habari ile.

Kutoka kwenye kochi lililokuwa upande wa pili wa sebule ile, Nuru alijiweka sawa na kukohoa kidogo. Akijua kuwa Nuru naye alitaka kuongea, Morandiakamgeukia kwa macho ya kuuliza.

“Mo, nadhani bwana Kokos anapaswa ajue juu ya tukio la kule Mikumi.Labda hapo ataona umuhimu wa kulifanyia kazi hili swala sasa hivi na si baadaye.” Nuru alisema, na Kokos akamgeukia.

“Kuhusu nini tena huko Mikumi? Msiniambie na nyie mnajua juu ya yule kibaka aliyetaka kumpora simu Candy!” Alisema, na akina Morandi wakatazamana, uelewa wa aina fulani ukipita baina yao. Kokos akaona namna walivyotazamana, na akataka kujua kulikoni.

“Candy kawadanganya Kokos.Yule hakuwa kibaka.” Morandi alimwambia, na Kokos akafunua kinywa tu bila sauti yoyote kumtoka.

“Ndio, Kokos. Mrembo kaongopa…sasa swali linakuja…kwa nini?”Morandi alimthibitishia.Kokos alimtazama, akamgeukia Nuru, na kumrudia tena Morandi.

“Kwa nini mnasema kuwa yulehakuwa kibaka…nyie mnajuaje?”

“Kokos, nilipokuomba pesa wakati ule nilizihitaji kwa ajili ya kumtanguliza mshirika wangu Nuru hapa huko Mikumi, kwa kuwa mimi nilijua sitaenda. Hiyo ilikuwa ni kama tahadhari tu, na kwa hakika imelipa!” Morandi alimwambia, kisha akamwacha Nuru asimulie kisa chote kilichotokea kule Mikumi.Nuru alipomaliza kusimulia Kokos alibaki hoi.

“Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa Candy anajuana na huyo mtu aliyetuambia kuwa ni kibaka?”

“Ndiyo tunakwambia hivyo kaka! Candy anajuana na yule mtu, na sitashangaa iwapo hata huyu ambaye sasa tumeambiwa na Morandi kuwa kalazwa Aga Khan, pia anajuana naye!” Nuru alimjibu.

Kimya kizito kilichukua nafasi wakati wakili wa zamani Kokos Wandiba akiranda-randa pale sebuleni huku akimung’unya midomo na akichezea-chezea ndevu zake za kidevuni, uso akiwa ameukunja kwa tafakuri nzito.

Morandi na Nuru walibaki wakimtazama kwa utulivu.

Baada ya muda Kokos aliketi kitini na kuwatazama wale maaskari wa zamani huku akionekana kuwa amepitisha uamuzi fulani.

“Okay. Tutaendelea kumlinda Candy mpaka amalize mashindano yake kwa sasa kama dada yangu alivyopendekeza…” Aliwaambia.

“Aww come on, Kokos! Whats the matter with you? Mtoto anakudanganya hivi hivi halafu we’ bado tu…” Morandi alilaani kwa fadhaa huku akitupa mikono hewani, ilhali Nuru akiachia mguno wa kushangazwa na maamuzi yale.

“Relax Morandi! Haya ni maamuzi ya busara kwa sasa. Tuongee naye baada ya mashindano. Wiki mbili sio nyingi kivile. Hii itanipunguzia mashinikizo yasiyo na msingi kutoka kwa Bishkuku…”

“Kwa nini unaruhusu hali hii?”

“Kwa sababu ukweli ni kwamba tayari mpaka sasa nimeshatumia pesa nyingi kwenye maandalizi ya ushiriki wake kwenye shindano hili, hivyo sitaki mimi mwenyewe tena ndio niwe sababu ya yeye kushindwa shindano hili. Akishindwa ashindwe kwa mengine lakini sio hili!” Kokos aliwajibu. Nuru na Morandi walitazamana.

“Haya, na katika wiki mbili hizo siye tutakuwa tunafanya nini sasa?” Morandi alisaili.

“Kama nilivyosema. Tuendelee kulinda usalama wake tu…Si ndio kazi niliyokupa tangu mwanzo Morandi? Wakati ukifika tutaongea sote na Candy na bila shaka kila kitu kitakuwa wazi.” Kokos alijibu, uso wake ukionesha dhamira halisi ya kile alichokuwa akikisema.

“GTZ hawezi kutoka hospitali leo wala kesho, sasa unadhani mrembo wako atahitaji usalama dhidi ya nani?”

“Yoyote awaye…hata yule jamaa wa Mikumi!” Kokos alijibu kimkato.

Morandi alimtazama kwa muda.

“Na baada ya shindano tunamweka mtu kati mrembo wako?” Hatimaye aliuliza.

“Tena mimi mwenyewe nitamleta kwako kwa ajili ya hilo!”



***

Sanura Kashogi naye alikuwa akiranda kutoka pembe moja ya ofisi yake maridhawa kwenda nyingine.

“Lazima tunyakue hili taji Tunis, lazima! Nina ahadi za mikataba minono na makampuni mawili makubwa ya mavazi iwapo tutanyakua hili taji mdogo wangu, na wewe ndio utakuwa kinara wa nguo zao zote duniani, mimi nikiwa wakala wao wa hapa nchini. Ni mikataba itakayotuweka kwenye anga tofauti kabisa!” Alisema kwa hamasa.

“Ulishaniambia hilo siku nyingi tu Anti Sanura.” Tunis alimjibu huku akitabasamu.

“Na sasa nakwambia tena, maana sasa mashindano ndio yameshawadia…”

“Na mimi niko tayari kabisa!” Tunis alithibitisha.

“Najua. Ila natafuta namna ya kujihakikishia hilo kwa asilimia mia moja. Hilo ndilo ambalo linanitatiza kwa sasa!” Sanura alisema, na Tunis akakunja uso.

“Ah, shaka ondoa…sijaona mrembo wa kunipa ushindani pale zaidi ya Candy…”

“Na huyo ndio kabisa hatakiwi kutushinda! Bora ashinde mwingine lakini si yeye…!”

“Hakuna mwingine pale anti Sanura nakwambia! Pale ni aidha mimi au Candy, si vinginevyo!”

“Basi lazima Candy ashindwe!”

“Yaa…” Tunis aliafiki kwa mashaka, na Sanura akashtushwa na hali ile.

“Mbona unaonekana kuwa na mashaka tena?”

Tunis alisita kidogo, kisha akajibu.

“Ah, ile njama yake ya kujinadi uyatima hainipi amani kabisa Anti Sanura…naona magazeti yanaendelea kumnadi kama ‘yatima mwenye upendo’, nahii inanipa mashaka mimi!”

Sanura alikaa kitini taratibu huku uso wake ukionesha kulitafakari lile swala kwa umakini.

“Kwa hiyo inamaanisha kuwa hata Candy atakuw amejipanga kutumia hiyo kama ndio kauli mbiu yake kwenye mashindano, sio?” Aliuliza.

“Yaani hilo sina shaka nalo kabisa!”

“Basi kitu pekee cha kufanya ni kumkosesha la kusema pale kwenye shindano, iwapo mtafika wote hatua ya kumi bora!” Alisema huku uso wake ukichanua kwa tabasamu.

“Na sasa hilo litawezekanaje?” Tunis aliuliza kwa kutoelewa.

“Rahisi sana…utasema wewe swala la mayatima kwenye shindano Tunis, na hiyo itamchanganya Candy kiasi cha aidha kumkosesha cha kusema hivyo ataonekana bwege mbele ya kadamnasi…” Sanura alimjibu huku uso wake ukizidi kuchanua kwa kile alichokuwa akikipanga. Tunis alikunja uso na kumtazama kwa macho ya kutoelewa kabisa, na Sanura akamalizia kauli yake, “…au naye aseme tu yale aliyojipanga kusema kuhusu mayatima, kitu ambacho kitamfanya aonekane amekuiga wewe, na hivyo kupoteza pointi!”

Tunis alicheka kwa sauti.

“Anti Sanura unan’chekesha. Sasa utajuaje kama mimi ndiye nitakayeitwa kwanza kujieleza kabla ya Candy? Vipi akianza kuitwa yeye? Hiyo mbinu yako siyo, Anti!” Alimwambia.

Sasa ilikuwa zamu ya Sanura kumcheka kwa sauti.

“Hilo niachie mimi binti. Tayari nimeshamjua mmoja wa majaji na nitamweka sawa tu. Hatuwezi kukosa namna ya kufanya ili uitwe wewe kabla ya Candy. Kuanzia sasa anza kusoma kila kilichopo kuhusu mayatima, na tazama video za mashidano yaliyopita tuone warembo wengine waliwahi kusema nini kuhusu jitihada za kusaidia mayatima…halafu sisi tutaboresha zaidi kwa mujibu wa nyakati za sasa, upo?”

Tunis alimkodolea macho.

“Un…una hakika Anti…?”

“Fanya nikwambiavyo Tunis! Hayo mengine niachie mimi!”

Tunis alibaki akimtazama kwa muda, kisha naye uso wake ukachanua kwa tabasamu pana.

“Yes!”



***



Candy alikuwa akifanya mazoezi ya kutembea kilimbwende huku akiwa ameachia lile tabasamu lake ambalo siku zote lilionekana kuwa ni sehemu ya umbile lake na si la kulazimishwa au la kufundishwa kama jinsi baadhi ya warembo waonekanavyo, hasa wakiwa kwenye mashindano ya urembo.

Bishkuku na Kokos walikuwa wakimtazama kwa makini wakati akifanya mazoezi yale, na hapo Bishkuku alimgeukia Kokos.

“Ah, mi nakwambia huyu mtoto asiponitoa kimaso-maso mwaka huu basi Bishkuku sitaingiza tena mrembo wa taifa maishani mwangu, Kokos! Yaani Candy ni chata ya Miss Tizedi kabisa nakwambia!” Alisema kwa hamasa kumwambia Kokos aliyekuwa ameketi kando yake pale uwani kwao kule Mbezi Beach.

Kokos alitabasamu.

“Usemayo ni kweli Bishi, ila mi kinachoniua kwa Candy ni lile tabasamu lake tu dadaangu…mtoto ana tabasamu utaf’ki’i Cameron Diaz, bwana? Dah!”Alisema kwa msisitizo wa hamasiko la kweli na Bishkuku akaachia cheko kali ya kimbea.

“Mnh! Ila kweli Kokos, lile tabasamu ni la Cameron Diaz kabisa! Na sijaona tabasamu kama lile likakosa kumvutia mtu duniani. Ama hakika Muumba kamuongoza huyu binti kwangu kwa sababu maalum, na kama sababu yenyewe ni kuutwaa ulimbwende wa Tanzania, basi nitahakikisha nafanya kila niwezalo kumwezesha Candy katika hilo…kwa msaada wako of course!”

“Yaaa, mtoto kakamilika kila idara huyu. Hata kichwani kuko vizuri sana. Ni hayo madhila tu ya kidunia yaliyomkuta.Mi’ n’na mipango mingi sana naye kichwani mwangu huyu!” Kokos alijiweka bayana mbele ya dadaye, na Bishi akaachia cheko nyingine ya kimbea.

“Kakaangu mi’ najua sana kuwa unammezea mate huyu mtoto, lakini kwanza ujue kuwa Candy sio daraja lako, na pili huu sio wakati wa kuanza kumtupia ndoana zako!”

“Ama! Sio daraja langu kivipi na wewe?”

“Sio Changudoa yule wewe, vipi? We’ zako si machangudoa tu siku hizi?”

“Sasa kama si miye kumuopoa ile siku yake ya kwanza alivyokuwa anataka kuuanza Uchangudoa unadhani ingekuwaje?” Kokos alihoji.

“Yaani hilo halina mjadala, mtoto angepotea! Lakini Mungu hakutaka, ndio akakupa wewe nafasi moja ya kufanya jambo jema hapa duniani, ingawa mwenyewe nia yako ilikuwa chafu tu wakati unamuopoa!”

Kokos alitaka kumjibu, lakini hapo Candy akawaendea pale walipokuwahuku akitabasamu.

“Enhe? Umeonaje Anti Bishi miondoko ile?” Aliuliza, na Bishi akatabasamu.

“Yaani katika idara hiyo uko vizuri sana mwanangu. Sasa kilichobaki ni namna utakavyojiuza kwa majaji kwa kujieleza…” Alimwambia, na Candy akaafiki kwa kichwa huku akiketi kwenye kiti cha kibwanyenye kilichokuwa pale bustanini kwa Kokos.

“Si tulishakubaliana kuwa nijielezee kuhusu kutaka kutoa misaada kwa watoto yatima?”Candy alimwambia.

“Haswa! Sasa hivi magazeti mengi yameshakunadi kuwa wewe ni yatima mwenye upendo, mwenye ndoto za kutwaa urembo wa taifa. Na sisi tutatashididia hapo hapo! Si mlishaelekezana na Kokos namna utakavyojieleza kwa majaji juu ya hilo?” Bishi alimwambia.

“Iwapo nitafika kumi bora…” Candy alikumbusha.

“Of course ukifika kumi bora…si Kokos alishakupa maelekezo muafaka juu ya hilo mrembo?”

“Mimi hiyo kazi nilishamaliza.Kilichobaki ni yeye tu kuyaweka akilini maelezo yake kwa ajili ya siku ya tukio.” Kokos aliingilia kati huku akimchanulia Candy tabasamu pana.

“Nitataka kuona kuwa mayatima wote wanapewa nafasi ya kuinuka katika jamii na kutimiza ndoto zao maishani bila ya uyatima wao kuwa kipingamizi katika hilo.” Candy alirudia maneno waliyokubaliana na Kokos kuyatumia kama kauli mbiu yake kwenye mashindano yale, na wote Kokos na Bishkuku walifurahi kwakumpigia makofi kwa jinsi alivyoitamka kauli mbiu yake ile kwa ithibati bila kusita.

“Shabbash!Safi sana mrembo wangu…haya bado nini teba hapo?” Bishkuku alisema kwa furaha huku akiuliza lile swali lililoomanisha kuwa hakukuwa na lolote lililopungua kwa mrembo wao yule.

Kokos na Candy walibaki wakicheka kwa furaha.

Si yeyote kati yao aliyejua kuwa tayari Sanura Kashogi alikuwa ameshaanza mikakati ya kuhakikisha kuwa lile walilolipanga halitokei.



***





GTZ alikuwa amefura kwa hasira pale kitandani kwake katika wodi maalum ndani ya hospitali ya Aga Khan, na alikuwa amefura kwa kuwa luninga iliyokuwa mbele yake ndani ya ile wodi ya wagonjwa wanaopewa hadhi ya umahsusi, yaani V.I.P, ilikuwa ikionesha tangazo la kulinadi shindano la Miss Tanzania lililokuwa likifanyika ndani ya wiki moja na nusutu kutoka siku ile.

Kitendo cha yeye kuwa majeruhi pale kitandani, na hapo hapo akimuona Candy Gamasala akijinadi namba yake ya shindano na kuwaomba watanzania wamuombee anyakue ubingwa ule kilikuwa hakivumiliki kabisa.

Alibadilisha stesheni ya televishe ni kuhamia chaneli nyingine, nako akakuta tangazo lile lile ndio linaanza. Aliunguruma kwa hasira na kuizima ile luninga na kubaki akiwa amejilaza chali pale kitandani huku akigeukia pembeni.Maneno ya yule bazazi aliyemkomgoroa goti kule msituni bila huruma yakimrudia akilini mwake.



…Lakini sitofanya hivyo. Sitokuua, kwa sababu nataka nikuone jinsi unavyoendelea kuumia kwa kushindwa kutimiza hiyo azma yako potofu wakati mrembo Candy akiendelea kung’aa mbele ya jamii, fala we! Hilo litakuwa ni pigo kubwa kwako kuliko hata hicho kifo!



GTZ alibubujikwa machozi waziwazi kwa hasira na kukata tamaa.

“Pole sana kaka…mguu unauma sana eenh?”

Sauti laini ya kike ilimwambia kwa upole, na GTZ alijikurupusha huku akijifuta machozi kumgeukia mmiliki wa sauti ile.

Hakusikia kabisa wakati yule muuguzi alipoingia mle wodini, bila shaka kutokana na mawazo aliyokuwa nayo na alivyokuwa amegeuzia uso wake pembeni. Alimuona muuguzi wa kike akiwaakimsogezea kijimeza chenye sahani maalum ya hospitali, huku ameinamisha uso. Juu ya kijimeza kile chenye matairili kulikuwa kuna juisi na bakuli la supu.

“Ah, yaa …ni…ni maumivu makali kidogo anti!” GTZ alijisemesha kwa aibu huku akimtazama yule nesi aliyevaa koti jeupe la kitabibu juu ya nguo zake za kawaida, usoni akiwaamevaa miwani ya macho na kichwani akiwa amejitanda mtandio maridhwawa.

“Pole sana…jaribu kunywa supu na juisi basi kaka…” Nesi alimjibu huku akigeuka na kutoka nje ya wodi ile.

GTZ alibaki akiwa amekodolea macho ule mlango aliotokea yule nesi muungwana, akilini akijilaumu kwakuruhusu yule mwanadada kumuona akilia, na hapo ghadhabu zake dhidi ya Candy na yule jamaa mbaya aliyemlaza kitandani muda ule zikaongezeka maradufu.



Nifanyaje sasa?

Ukweli ni kwamba sitaweza kumuwahi Candy kabla hajaingia kwenye hayo mashindano yake…daktari kasema nitakuwa hapa kwa karibu miezi sita! Ina maana ndio nimeshindwa kabisa kutimiza azma yangu kweli mimi?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Akiwa amechanganyikiwa, aliliinua lile bakuli la supu huku kwa mkono mwigine akichukua kijiko cha kunywea supu ile, na hapo akaganda kama aliyeiona mzimu.

Pale kwenye ile sahani pana, au “tray” maalum ya kubebea vyakula kulikuwa kunaile leseni yake ya kuendeshea gari ikiwa juu ya kipande kidogo cha karatasi. Hakuwa ameiona kabla ile leseni yake kwa kuwa ilikuwa imewekwa chini ya lile bakuli la supu.

Mwili ulimfa ganzi na kijiko kilichokuwa mkono wake wa kulia kikamuanguka hali akihisi kuliangusha lile bakuli la supu lililokuwa mkono wake wa kushoto.

Taratibu aliliweka pale kwenye ile meza ndogo lile bakuli na kuichukua ile leseni yake kwa mkono uliojaa kitetemeshi.

Ilikuwa ni leseni yake kabisa!

Mara ya mwiso kuiona ile leseni yake ilikuwa ni kule msituni alipoteswa vibaya, wakati leseni ile ikipotelea ndani ya mfuko wa koti la yule jamaa mwenye roho mbaya.

Sasa imekuwaje tena iko hapa?

Huku akiwa amehamanika pasina kiwango na moyo wake ukicheza kiduku ndani ya kifua chake, alikichukua kile kijikaratasi kidogo kilichokuwa pamoja na ile leseni yake pale chini ya bakuli la supu nakusoma ujumbe ulioandikwa juu yake.



I AM STILL WATCHING YOU!



Ni maneno yaliyokimaanisha kuwa yeyote ambaye alimuandikia ujumbe ule, bado alikuwa akimfuatilia kwa karibu sana.

Mara moja GTZ alijua kuwa ujumbe ule ulitoka kwa yule yule mtu mbaya aliyempa kifinyo cha maana kule msituni siku kadhaa zilizopita. Sasa akiwa amefikia hatua ya juu kabisa ya hamaniko, alianza kutembeza kichwa na macho yake huku na huko mle wodini na kujiona akiwa peke yake mle ndani.

Ah, yule nesi! Ni yule nesi! Hakutaka kuniletea supu bali huu ujumbe tu (akamtukania mama yake)…why?

Katumwa na yule jamaa!

Ukelele wa ghadhabu ukamtoka GTZ na hapo hapo akaanza kupiga kelele kumwita yule nesi aliyetoka mle ndani muda mfupi tu uliopita.

Nje ya ile wodi, Nuru aliyejitanda mtandio maridhawa aliachia tabasamu la ushindi wakati akiondoka kwa kujiamini kutoka eneo lile, akipishana na manesi wawili waliokuwa wakikimbilia kule wodini kwa GTZ.



***



Ukumbi wa Mlimani City ulikuwa umefurika kuliko kawaida, kutokana na umma wa watanzania kutaka kushuhudia mrembo wa taifa lao atakavyopatikana. Ni mrembo ambaye angeliwakilisha taifa kwenye shindano kubwa zaidi la urembo duniani, shindano la mrembo wa dunia.

Miss World.

Hali ilikuwa ni wahka kwa kwenda mbele kwa warembo waliobahatika kushiriki shindano lile kubwa la urembo usiku ule. Kila mmoja kati yao alikuwa akijiona ana nafasi kubwa ya kuchukua umalkia ule wa urembo nchini.Kilichokuwa kikisubiriwa ni kile kipindi ambacho mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania atakapopanda jukwaani na kutangaza warembo watakaokuwa wameshika zile nafasi tatu za juu, kila mmoja akijitamani yeye ndiye atajwe kuwa mshindi wa kwanza na hivyo kutawazwa taji lile adhimu katika medani za urembo nchini.

Lakini hilo peke yake silo lililosababisha warembo wote waliokuwa wakishiriki shindano lile kuwa na wahka uliokithiri. Kilichowaongezea wahka ni zawadi iliyotangazwa kwa mrembo atakayetoka kidedea kwenye shindano la usiku ule, kwani kutokana na mkataba maalum na benki kubwa kabisa nchini, Kamati ya Miss Tanzania ilikabidhiwa nyumba kubwa ya kifahari iliyokuwa imeshehenezwa samani zote muhimu zihitajikazo kwenye nyumba ya hadhi ile, na mshindi ndiye atakayekabidhiwa jumba lile. Na hii ni pamoja na gari la kisasa, fedha taslimu milioni ishirini na tano, na mkataba wa uanamitindo wa mwaka mmoja.

Haijawahi kutokea nchini kwa mrembo wa taji la Miss Tanzania kupatiwa zawadi kubwa kama ile, na mabinti walijawa wahka si kidogo. Kila mmoja akitaka kukabidhiwa funguo za nyumba na za gari, pamoja na hizo zawadi nyingine. Fukuto la kutafuta ushindi lilikuwa limetanda kila kona katika vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya ukumbi ule maarufu kwa matukio ya kukata na shoka jijini Dar.

GTZ alikuwa akishuhudia matangazo ya shindano lile yakirushwa kwa vipande vipande kutokea kwenye luninga ya wodi yake pale hospitali ya Aga Khan, na roho ilizidi kumuuma.

Alikumbuka jinsi alivyoaibika siku ile alipopokea ule ujumbe wa kukera kutoka kwa yule jamaa aliyemvunja goti, hususan jinsi wale manesi wawili walivyomshangaa kwa kupiga kelele namna ile kama mwehu. Hakika hakuwa na la kuwaambia zaidi ya kubaki akiwa amepiga kimya huku akibubujikwa machozi ya hasira. Aliona jinsi wale manesi walivyotazamana kama kwamba wakiambiana kwa macho yao kuwa jamaa alikuwa amechanganyikiwa, naye akawafukuza kwa hasira kutoka mle wodini.

Tangu siku ile amekuwa akihudumiwa na manesi wa kiume.

Alipokuwa akitazama matangazo yale yaliyokuwa yakionesha maandalizi ya shindano lile usiku ule, alijua kuwa alikuwa ameshindwa kutimiza azma yake dhidi ya Candy Gamasala, na hivyo kwa moyo mzito sana alitoa simu yake na kuamua kumpigia mtu ambaye siku zote hakutaka ajue kuwa alikuwa ameshamuona Candy.

“Sina jinsi sasa…itabidi nimwambie ili afanye alitakalo yeye, maana nilitakalo mimi limeshashindikana!” Alijisemea peke yake mle wodini.

Alimpigia mtu aliyekuwa amemkusudia, lakini simu yake ilikuwa haipatikani.

GTZ aliunguruma kwa ghadhabu na kujaribu tena, na tena na tena. Mara zote hizo simu ya yule mtu ilikuwa haipatikani.

Mwishowe aliamua kumtumia ujumbe mfupi.



***

Shindano la miss Tanzania lilianza kwa muda uliopangwa usiku ule. Warembo walipita jukwaani wakiwa katika mavazi mbalimbali, kuanzia mavazi ya ufukweni, jioni, kitamaduni na yale ya kiubunifu. Pamoja na harakati hizo, wanamuziki wa kizazi kipya walikuwa wakitumbuiza kila baada ya aina fulani ya vazi kupita, na wananchi walipata burudani safi sana.

Hatimaye ilifika wakati wa mchujo kwa warembo kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa majaji. Kipengele hicho kilipopita warembo wote walijipanga jukwaani kusubiri hukumu ya nani kati yao angekuwa miongoni mwa wale warembo kumi watakaoingia nusu fainali.

Shangwe na hoi hoi zilitawala ukumbini pale walipopatikana wale warembo kumi. Miongoni mwao walikuwamo Candy Gamasala na Tunis.

Bishkuku alimgeukia Sanura Kashogi aliyekuwa upande wa pili kutoka pale alipokuwa amekaa, na Sanura alimtolea tabasamu la kebehi huku akimuashiria ishara ya dole gumba lililoinamishwa chini.

Bishkuku alimkazia jicho la ghadhabu, na Sanura akazidi kumcheka.

“Achana naye Bishi…huu mpambano ndio kwanza unaanza. Candy na Tunis wote wameingia kumi bora, so sasa tungalie nani kati yao ataishia njiani.” Kokos alimwambia, na Bishkuku alipiga kimya.

Moyo ulikuwa ukimdunda vibaya sana.

Kutokea kwenye kona tofauti za ukumbi ule, Morandi Gwaza na Nuru nao walikuwa wakifuatilia kwamakini shindano lile, ingawa wao akili yao ilikuwa imeelekzwa zaidi kwa Candy Gamasala.

Hatua ya nusu fainali ilihusisha warembo kuonesha ubunifu wao binafsi mbele ya majaji na majaji ndio wangeamua wepi wapite kwenda hatua ya fainali na wepi waishie pale. Kuna warembo waliokuja na vipaji vya uimbaji, wako waliokwenda na vipaji cha kucheza ngoma za kienyeji na wengine vipaji vya kazi za mikono na mitindo.

Tunis yeye aliingia na kipaji cha uimbaji ambapo aliimba vizuri sana wimbo wa muimbaji maarufu wa kike nchini na ukumbi mzima ulirindima kwa hoi hoi na vifijo kumpongeza.

Candy naye aliwakonga nyoyo watazamaji kwa kuonesha kipaji cha kupiga gitaa kwaufundi mkubwa sana, kipaji alichojengewa akiwa katika nyumba ya watoto yatima miaka mingi huko nyuma. Alipiga gitaa kwa utulivu na umahiri uliosababisha watazamaji wasimame huku wakimpigia makofi.

Ilipofika hatua ya kutangaza washindi watano watakaoingia fainali, Candy na Tunis pia walikuwa miongoni mwa watano wale.

Si hoi hoi na nderemo hizo kutoka kwa watazamaji!

“Mnh, ama hakika sasa mpambano umekolea Bishkuku!” Kokos alimwambia dada yake.

Bishkuku aliafiki kwa kichwa huku uso wake ukionesha mashaka mazito.

Baada ya burudani kadhaa, msemaji alipanda jukwaani na kutangaza kuwa hatua ya fainali itahusisha majaji kuwaita wale warembo watano mmoja baada ya mwingine na kumtaka kila mmoja ajinadi mbele yao juu ya jambo au mambo atakayofanya iwapo atachaguliwa kuwa mshindi wa mchuano ule, na kwamba baada ya kujinadi, kila mshiriki angetakiwa kujibu kwa ufasaha swali moja kutoka kwa majaji. Baada ya hapo ndipo majaji wangefanyia tathmini maelezo na majibu ya kila mshiriki na hatimaye kutangaza mshindi.





Baada ya maelezo hayo shangwe zilirindima ukumbini, wakati majaji wakionekana kujadiliana baina yao juu ya nani waanze kumuita kutoa maelezo ya kwanza. Muda si muda, taarifa ikatolewa kuwa majaji wako tayari kuendesha hatua ya fainali, na wale warembo watano wakajitokeza tena jukwaani na kusimama kilimbwende mbele ya majaji na mashuhuda waliojazana ukumbini pale.

Saa ya ukweli ndio imewadia sasa…ee Mungu naomba unisaidie…

Candy alijiwazia huku akiwa amesimama na warembo wenzake pale mbele.



***

Kule hospitali, ujumbe mfupi uliingia kwenye simu ya GTZ, naye akaikwapua simu yake kwa wahka mkubwa, akijua kuwa ujumbe wake aliotuma ulikuwa umefika kwa aliyemkusudia, lakini alikata tamaa pale alipoona kuwa ilikuwa ni ripoti iliyomfahamisha kuwa ule ujumbe alioutuma hapo awali ulikuwa umeshindwa kupelekwa kwa aliyemkusudia.

Aliunguruma kwa hasira na nusura aibamize ile simu ukutani, lakini alijizuia kwa kujua kuwa hiyo ingekuwa ni hasara zaidi kwake.Alibaki akifura pale kitandani kwa hasira, kisha akautuma tena ule ujumbe kwa yule mtu aliyemkusudiakabla ya kuirudisha ile simu kwenye kijimeza kilichokuwa pale kando ya kitanda.

Kwa nini ujumbe hauendi? Kapoteza simu? Kabadilisha namba?

GTZ alizidi kuchanganyikiwa.



***

Kule Mlimani City, ukumbi ulikuwa umejawa kiherehere cha kujua ni yupi kati ya wale warembo watano waliosimama pale jukwaani angeibuka mshindi na kuvikwa taji la Miss Tanzania…na hivyo kuliwakilisha taifa kwenye mpambano mkubwa kuliko yote ya urembo duniani, Miss World.

Wakiwa kule kwa watazamaji, Kokos na Bishkuku walitazamana, kila mmoja akiona wahka uliojaa kwenye uso wa mwenzake, na bila ya kusema neno waligeukia kule jukwaani ambako mmoja wa majaji aliinuka na kujiandaa kuteua mrembo wa kwanza atakayetakiwa kujiuza kisera mbele ya majaji na watazamaji.

“Haya…nafasi ya kwanza inakwenda kwa mrembo mwenye namba ishirini na saba…Tunisizye Mwakabaga, maarufu kama Tunis!” Jaji alitangaza na kuketi. Matabasamu ya ushindi yalipita kwenye nyuso za Tunis na mfadhili wake Sanura, kila mmoja kutokea mahala alipokuwa.

Mkakati wao dhidi ya Candy ulikuwa umefanikiwa.

Tunis alisogea mbele kilimbwende huku akitabasamu na kutulia kwa muda mbele ya kipaza sauti. Alipoanza kutangaza sera zake juu ya atakayoyafanya iwapo atachaguliwa kuwa mshindi wa shindano lile, moyo wa Candy ulipiga sarakasi ndani ya kifua chake, na akahisi dunia yake ikisambaratika mbele ya uso wake.

“Khah! Sasa yule tena na mambo ya kusaidia watoto yatima inahusu nini, Kokos?” Bishkuku aliuliza kwa hamaniko lililokithiri huku akiinuka kutoka kwenye kiti. Kokos alimdaka mkono na kumkalisha tena kitini.

“Tulia Bishkuku, picha limeshaharibika hili…!” Alikoroma kwa hasira huku akiwa ameuma meno akimtazama Tunis akijinadi kwa sera ambazo wao ndio walikuwa wamemuandalia Candy kuzitumia.

Bishkuku alijikuta akigeukia kule kwa Sanura kwa uso uliohamanika, nako akakutana uso kwa uso na Sanura aliyejaa tabasamu pana la ushindi. Bishkuku alikunja uso na kumtazama kwamakini zaidi Sanura, ambaye alimfanyia ishara ya kifo kwa kupitisha kiganja chake akikifananisha na kisu, shingoni kwake.

Ah!

Bishkuku aligeuka na kutazama chini kwa muda, akili ikimchemka, kisha akamgeukia Kokos.

“Yule khabithi amefanya kusudi (akamtukania bibi yake) nakwambia…Kusudi!” Aliropoka kwa hasira, na Kokos akamshangaa.

“Nani tena Bishkuku wakati Tunis keshatuharibia pozi kule na wewe?” Kokos alimjia juu.

“Si Sanura bwana? Sanura kafanya kusudi hii, kwa sababu alijua kuwa by all means Candy angeongelea swala la mayatima! Akamfunda Tunis aongee yeye juu ya hilo!” Bishkuku alimjibu na kumalizia kwa kumtukania Sanura mama yake.

Kokos alitaka kuhoji, lakini kule mbele Tunis alimaliza kujieleza na makofi yakarindima ukumbini kumpogeza.

“Oh, Mungu wangu…sasa Candy ataongea nini tena kule jamani?” Bishkuku alilalama kwa hamaniko kubwa, na Kokos akakunja uso kwa kuchanganyikiwa.

“Akh! Tulia Bishkuku…huna lolote la kufanya sasa. Ni Candy pekee ndiye atakayejua la kufanya pale…ni yeye na Mungu wake tu!”

Kule jukwaani, Tunis aliwapungia wananchi mkono na kugeuka kurudi kusimama na wenzake, akihakikisha kuwa amegonganisha macho na Candy, na alipoona macho yao yamekutana, akambania jicho moja kwa kumkejeli.

Candy akahisi miguu ikimwisha nguvu.

Eee Mungu wangu…hebu nipe ujasiri wa kuvuka kikwazo hiki Yarabi!

Kwa muda ilikuwa kama aliyepigwa ganzi kwenye ubongo. Hakusikia kabisa wakati mabinti wengine wawili wakiitwa kwenda kujieleza pale mbele, na wala hakusikia walikuwa wamejieleza juu ya nini.

Candy Gamasala alikuwa amechanganyikiwa, na hakuwa na la kufanya juu ya hilo.

“Na sasa ni zamu ya Candy Gamasala!” Jaji mwingine alinadi kutokea pale kwenyemeza ya majaji, na Candy hakumsikia mpaka mrembo mwenzake alipomgonga kwa kiwiko ndipo alipozinduka.

Oh, My God nimeitwa! Nitaenda kuongea nini sasa kule!

Kama mbwa anayejipeleka kwenye mdomo wa mamba, Candy alianza kukisogelea kipaza sauti.

“Come on Candy…fungua hilo tabasamu lako basi mwanangu, eenh?” Bishkuku alimsemesha kutokea kule ukumbini kama kwamba Candy angeweza kumsikia. Na kama aliyesikia, Candy alijikuta akiachia tabasamu lake lenye mvuto alipofika pale kwenye kipaza sauti. Aliinua uso kuikabili hadhira huku akili ikiwa bado imemfa ganzi.

Mungu wangu! Niseme nini sasa Candy miye…?

Ukimya uliotanda pale ukumbini ulikuwa ni wa kuweza kuisikia pini ikianguka, wakati kila mwananchi aliyekuwepo akisubiri kumsikia ‘yatima kwenye upendo’ akijinadi mbele ya hadhira.

Hakuna kilichomjia akilini, na woga mkubwa ukamtawala.

“Okay, Candy Gamasala…tueleze sera zako. Utafanya nini uwapo utachaguliwa kuwa mrembo wa taifa letu adhimu la Tanzania?” Msema chochote alirudia swali aliloulizwa na jaji baada ya kuona Candy amekuwa kimya kwa muda mrefu.

Donge zito likamkaba Candy. Hakuwa na la kusema na alijiona kuwa alikuwa anaelekea kuangua kilio mbele ya kadamnasi.

Aibu gani hii?

Kushindwa gani huku?

Woga ukamwelemea.

Kilio kilizidi kumkabili naye akashindwa kukizuia, na alipoona kuwa kilio kilikuwa kinaelekea kumchomoka, alifunua kinywa na kuanza kuongea.

Akawaliza watu ukumbini.



***

Ngamao Kijambia alifumbua macho na kujinyoosha huku mwayo mrefu ukimtoka. Aliinuka kutoka kitandani alipokuwa amelala kama mfu kwa zaidi ya saa kumi na mbili mfululizo, na sasa usingizi ule wa uchovu ulikuwa umemuisha. Aliinua mkono wake na kutazama saa yake, nayo ikamjuza kuwa muda ulikuwa ni saa nne na nusu za usiku.

Aliguna huku akifinya uso na kuubana mwayo mwingine uliokuwa ukimtoka, akibaini kuwa alikuwa akihisi njaa kali sana.

Amekuwa kijijini kwa mama yake kwa muda wa wiki zipatazo mbili, ambako alikuwa ameenda kwa ajili ya maziko ya mama yake huyo. Na muda wote alipokuwa huko amekuwa nje ya mawasiliano yoyote ya simu kutokana na mtandao wa simu kutofika kule kijijini alipokuwa.

“Shit, nimebaki mwenyewe sasa!” Alijisemea huku akipitisha mkono wake kwenye kichwa chake chenye upara, halafu akainuka na kujiburuza kuelekea jikoni kutafuta chochote cha kupunguza njaa. Inspekta Ngamao Kijambia hakuwa na mke wala mtoto, na hakuwa na ndugu yoyote. Kifo cha mama yake kimemfanya abaki peke yake hapa duniani na hilo lilikuwa ni jambo zito sana kwake.

Alikuwa ni mtu mzima apataye miaka hamsini hivi, lakini kutokana na kazi yake ya u-askari, bado alikuwa ni mwenye nguvu na imara. Mtu pekee aliyekuwa karibu naye zaidi ya mama yake, na ambaye alitaraji labda angetengeneza naye familia alishafariki miaka kadhaa huko nyuma, na tangu kifo cha muhibu wake huyo, Ngamao hakutaka tena kujiingiza kwenye mahusiano mapya.

Alifungua jokofu jikoni kwake na kuchukua boksi la juisi, kisha akaenda kupekua kwenye makabati ya pale jikoni na kufanikiwa kuibuka na kifurushi cha korosho.Akarudi navyo sebuleni na kuanza kupooza njaa yake taratibu.

Wakati akiendelea kula vitu vyake vile, aliikumbuka simu yake ambayo ilikuwa imezima kwa kukosa chaji wakati yuko kule kijijini. Aliichomoa kutoka kwenye chaji na kuiwasha, na muda si muda meseji ya GTZ ikaingia.

Aliisoma ile meseji na hapo hapo aliinuka huku uso wake ukiwa mgumu ghafla.

Nimemuona mbaya wetu jijini Dar. Tuwasiliane haraka sana!

Alipousoma kwa mara ya tatu ule ujumbe akaelewa ni mbaya gani ambaye GTZ alikuwa anamuongelea. Hapo hapo alimpigia simu GTZ, na nusu saa baadaye, Inspekta Ngamao Kijambia alikuwa kwenye gari lake aina ya Nissan Patrol akisafiri kutokea Mwanza kuelea Dar es Salaam.

Hatimaye mtu aliyekuwa akimsaka kwa muda mrefu na ambaye aliamini kuwa labda amepotelea nje ya mipaka ya nchi hii, alikuwa amepatikana.

Hatimaye sasa atamtia mbaroni…



***



Jijini Dar, Candy Gamasala aliporomosha maneno kutoka kinywani kwake huku akili ikimtembea.

“Jambo kubwa nitakalolifanya ni kupigania kumaliza migogoro kati ya jamii za wakulima na za wafugaji nchini…na nitafanya kila niliwezalo kuishawishi serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa jamii hizi mbili zinaishi bila uhasama wala kuingiliana…

“Kuna akina mama na watoto wengi wanaoishi maisha ya dhiki na taabu kutokana na akina baba na waume zao kuuawa katika mapambano baina ya jamii hizi mbili, na mimi kama mhanga wa hali hiyo…”

Hapo kilio kilimzidia na sauti ikamvunjika kwa kilio, machozi yakambubujika. Sio kwa ajili ya kile alichokuwa akikiongea, bali ni kwa namna ambavyo alivyokuwa anapata taabu kujieleza mbele ya umma kwa kuwa yale sio maelezo ambayo alikuwa amejiandaa kuyatoa pale ukumbini usiku ule.

Lakini waliokuwa kule ukumbini hawakulijua hilo. Walijua analia kutokana na kuguswa na ile hali aliyokuwa akiielezea.

“Mimi nikiwa kama mhanga wa mauaji hayo, sitakuwa na uhalali wa kuendelea kuwa hai leo iwapo nitapata nafasi ya kutwaa taji la miss Tanzania halafu nisipiganie kumaliza hali hiyo kwa kadiri niwezavyo…”

Eh Mungu wangu, ndio maelezo ya kunipa ushindi haya kweli?

Alijikuta akishindwa kuendelea na kubaki akibubujikwa machozi.

Kule ukumbini, Bishkuku alijikuta akiinuka huku naye akibubujikwa machozi, na Kokos alitaka kimvuta ili akaechini, lakini akasita pale alipoona akina mama wengine wawili nao wakisimama huku nao wakibubujikwa na machozi.

Alizungusha kichwa pale ukumbini, nakuona akina mama wengine watatu nao wakibubujikwa na machozi huku wameketi.

Akajiweka sawa kitini na kutulia.

Kule jukwaani Candy alimuona Bishkuku akimuashiria kwa kichwa kuwa aendelee kuongea huku akibubujikwa na machozi.

“Nadhani…nadhani kama nikiweza kufanya hivyo, nitakuwa nimechangia kutatua chanzo cha tatizo la watoto wa mitaani na mayatima, na hivyo kupunguza idadi ya watoto hao nchini kwetu. Naona hili ni bora zaidi kuliko kusubiri mpaka mayatima wawepo ndio nije niwasaidie kwa kuwapelekea miche ya sabuni, magunia ya mchele na nguo…” Candy alimaliza na kubana midomo kwa nguvu, akijizuoa asiendelee kuongea zaidi kwani hakuwa na hakika iwpao angeweza kumalizia vizuri maelezo yale aliyoyakokotoa pale pale, akihusisha kisa cha maisha yake.

Shangwe na mbinja vilizagaa pale ukumbini, huku wale akina mama wakianza kumpigia makofi na muda si muda watu wengi pale ukumbini walisimama huku wakimpigia makofi.







Candy hakuamini, na mbubujiko mpya wa machozi ya faraja ukammwagika huku akitabasamu. Aliinama kidogo kutoa heshima kwa watazamaji na majaji na kurudi tena kusimama na warembo wenzake, mrindimo wa makofi ukimsindikiza nyuma yake.

Hatua ya warembo wale kujieleza iliisha, na baada ya burudani kadhaa ilifika hatua ya kila mmoja wa wale warembo kujibu swali moja kutoka kwa majaji, ambapo kila mmoja wao alitakiwa kuchagua swali kutoka kwenye bakuli kubwa la kioo lililokuwa limesheheni vijikaratasi vyenye namba mbalimbali zilizoshabihiana na maswali kadhaa yaliyoandaliwa na majaji wa shindano lile.

Candy Gamasala alimtazama Tunis akichomoa kijikaratasi na kuwatajia majaji namba iliyoandikwa juu ya kijikaratasi alichoibua.

Namba tano.

Mmoja wa majaji akamuuliza swali namba tano kutoka kwenye mlolongo wa maswali kadhaa waliyokuwa nayo. Lilikuwa ni swali lililohusu ni nini kilichomfanya aamue kuingia kwenye mashindano yale ya urembo. Ukumbi mzima ulilipuka kwa hoi hoi na Candy alijikuta akitamani kuwa yeye ndiye angepata swali lile.

Binti akajieleza kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kuwa aliamua kuingia kwenye mashindano yale kwa kuwa alitaka kutokea kwenye runinga na magazeti, kisha akabaki akimtolea jaji aliyemuuliza swali lile tabasamu pana la ushindi.

Ukumbi uliachia mguno wa pamoja, na Candy Gamasala alijikuta akipigwa butwaa kwa kutoamini kama kweli yule mrembo mwenzake ameona kuwa lile ndio jibu muafaka kwa swali jepesi kama lile.

Kule kwa watazamaji Bishkuku alimuinamia Kokos na kumnong’oneza.

“One down, three to go!”

Kokos aliachia kicheko cha mashaka lakini hakujibu kitu, kwani hakika alikuwa na wasi wasi mkubwa.

Mrembo wa pili aliulizwa swali kuhusu namna ambavyo angeweza kuutangaza utajiri wa Tanzania kimataifa, iwapo angepewa nafasi ya kufanya hivyo. Yeye alijieleza namna ambavyo angeutangaza mlima Kilimanjaro, mbuga kadhaa za wanyama, utajiri wa madini yaliyopo sehemu kadhaa za Tanzania, na kabla hajamaliza ukumbi ulilipuka kwa shangwe, vifijo na hoi hoi kama kwamba tayari ameshatangazwa mshindi. Binti akaishia hapo hapo huku akitabasamu kwa furaha kubwa.

Bishkuku alishitushwa na mtu aliyekuwa kando yake akimgusa bega. Alipomgeukia yule mtu alimuoneshea kwa kidole chake kwenye viti vilivyokuwa kulia kwake kwa mbele, ambako alimuona Sanura Kashogi akimpungia mkono. Na alipohakikisha kuwa Bishkuku ameshamuona, Sanura alijiwekea kidole chake shingoni na kumfanyia ishara ya kuichinja shingo yake huku akimtolea tabasamu la kejeli. Bishkuku alimuinulia kidole chake cha kati, na alifarijika alipoona Sanura akitumbua macho kwa kutoamini huku uso ukimuanguka. Aliachana naye na kugeukia kule ukumbini ambako alisikia namba ya Candy ikiitwa na alimuona Candy akienda kuchagua swali kutoka kwenye lile bakuli la kioo.

“Oooh, hapa ndio pa kujua kati ya kusuka au kunyoa sasa…!” Kokos alinong’ona kwa mashaka huku akitazama kule jukwaani.

“Yeah…”

Alichagua swali namba kumi na mbili, na jaji mwenye swali alicheka kidogo kisha akamuuliza, “Candy Gamasala…utachukua hatua gani iwapo hutaibuka mshindi katika shindano hili?”

Candy, kama jinsi ambavyo ukumbi wote ulivyokuwa, alitulia kimya kwa swali lile.

“Akh, sasa hili ndio swali gani sasa!” Kokos alinong’ona kwa hasira.

Lilikuwa ni swali ambalo hajawahi kuulizwa mgombea yoyote wa urembo nchini, labda hata duniani. Mara nyingi swali huwa ni nini mgombea angefanya iwapo angeshinda, sio iwapo angeshindwa.

“Tulia Kokos, mwache mtoto ajibu swali kule!”

“Hatukumuandaa kwa swali kama hili kabisa, Bishi! Unadhani…”

“Ahsante sana kwa swali lako mheshimiwa…” Kule mbele Candy alianza kuongea, na Kokos na Bishkuku walikatisha mazungumzo na kubaki wakimsikiliza mrembo wao akijinadi.

“…awali ya yote napenda kuwafahamisha kuwa naelewa kwamba sote tuliokuja kwenye

shindano hili tumekuja kwa nia ya kutwaa taji la miss Tanzania, kwa hiyo hakuna aliyekuja kushindwa.”

Watu kadhaa walipiga makofi kwa jibu lile, ingawa sehemu kubwa ya ukumbi ule, wakiwemo akina Kokos bado waliona kuwa lile halikuwa jibu kamili.

Na Candy alikuwa hajamaliza kujieleza.

“Lakini pia kwa kuelewa kuwa mwisho wa shindano hili ni mrembo mmoja tu ndiye atakayeondoka na taji, napenda kujibu swali lako kwa kunukuu maneno ya mwanamuziki mmoja mwenye falsafa za hali ya juu katika maisha, na ambaye hatunaye tena hapa duniani hivi sasa…yeye alisema, na nanukuu,‘through every dark night, there’s a bright day after that. So no matter how hard it get, stick your chest out, keep your head up, and handle it.…”

“Ah, mtoto kamnukuu Tupak bwana, DAH!” Kokos Wandiba aliropoka kwa mastaajabu huku bashasha ikimzidi nguvu.

Kufikia hapo ukumbi ulikuwa kama umemwagiwa pilipili kwa mayowe. Si hoihoi, nderemo na vifijo hivyo. Kokos alijikuta akiwa wima juu ya kiti chake hali akibweka kama mbwa huku akipiga mbinja kila alipopata nafasi.

Bishkuku alikuwa ametulia kwenye kiti chake akitazama jinsi Candy alivyoipagawisha hadhira, tabasamu pana likiwa limemtanda usoni huku akipiga makofi.

Upepo ulikuwa umegeuka ghafla kwa Candy, ambaye alibaki akiwa ametulia na tabasamu lake maridhawa usoni, macho yake yakitoa mng’aro wa furaha, na alipoona watu hawanyamazi, aliwainulia mkono kuwaashiria wanyamaze, jambo ambalo lilizua mlipuko mpya wa hoi hoi na nderemo. Ukumbi ulizidi kupagawishwa na jinsi alivyoonekana kulitawala jukwaa pale mbele.

“…kwa hiyo ingawa najiamini kuwa nina uwezo mkubwa wa kulibeba vyema taji la miss Tanzania, iwapo sitatangazwa mshindi, nitainua uso wangu na nitasimama kifua mbele na kukubaliana na hali hiyo huku nikiamini kuwa kutakuwa na neema nyingine tu mbele yangu. Ahsante.” Candy alimalizia pale alipoona shangwe zimepungua, na kuamsha shangwe nyingine kubwa zaidi.

Kwa dakika tano mfululizo ukumbi ulikuwa ukirindima kwa vifijo, mshereheshaji akijaribu mara kadhaa kuingilia kati kuutuliza ukumbi bila mafanikio.

“Mtoto kafanya kweli Kokos…hii ni ndoto kuelekea kutimia sasa!” Bishkuku alimnong’oneza Kokos kwa bashasha.

“Aaah, sio siri mtoto kanikosha kweli kweli leo Bishi…lakini bado hatuwajasikia hao washindani wawili waliobakia…”

“Hao saa hizi watakuwa wameshahamanishwa na nderemo alizopigiwa mwenzao! Hili picha limeishia kwa Candy nakwambia, hakuna cha Tunis wala nani hapa! Wafuatao wote ni kutimiza wajibu tu!”

Kule jukwaani binti wa nne alikuwa anaenda kuchagua swali lake.

“We’ unajiamini sana Bishkuku…unasahau kuwa hawa majaji huwa hawaaminiki…wanaweza kutuacha vinywa wazi hapa mpaka tu-bloo!”

Kule mbele binti aliulizwa swali gumu kiasi, naye akaboronga vibaya sana kiasi Bishkuku akamgeukia Kokos.

“Sasa utasema pale kuna mtu wa kumpiku Candy pale?”

“Yeah…three down, one to go…” Kokos alikubaliana naye wakati binti wa mwisho akichagua swali na kusogea kwenye kipaza sauti. Binti alitakiwa aieleze hadhira ni mwanamke gani duniani ambaye angependa kujifananisha naye na kwa sababu gani.

Binti alipenda kujifananisha na Winnie Mandela, kwa sababu angepata fursa ya kuwa mke wa kwanza wa mzee Nelson Mandela. Kisha akabaki akitabasamu kwa kujiamini kabisa. Ukumbi uliachia mchanganyiko wa miguno na makofi ya hapa na pale, lakini zaidi ya hapo sehemu kubwa ya wananchi waliokuwepo walibaki wakiwa wamepigwa butwaa.

“Hah! Sa’ ndo jibu gani lile!”Kokos alimaka huku akimgeukia Bishkuku.

“Hilo ndo jibu linalotuthibitishia ushindi Kokos, usiwe mjinga!Kwa mtaji huu Candy kachukua taji nakwambia!” Bishkuku alimwambia.

“Duh, e bwana eee!” Kokos alisema kwa bashasha huku akisugua viganja vya mikono yake kwa mchecheto wa kile walichokuwa wanakitarajia kutokea pale ukumbini usiku ule.

Kule mbele wale warembo walikuwa wamejipanga kwa mbwembwe mbele ya hadhira, nyuso zao zikiwa zimepambwa na yale matabasamu yao ya kilimbwende. Muda huo msema chochote aliihabarisha hadhira kuwa mabinti watarudi nyuma ya pazia kujipumzisha wakati majaji wakifanya tathmini ya mwisho kabla ya kumnadi mshindi.

Mabinti walisindikizwa kwa mdundo wa muziki maridhawa nao wakapotelea nyuma ya jukwaa kwa miondoko iliyorandana na mdundo ule, na burudani ya muziki ikafuata.



***

Muda wote wakati matukio ya pale ukumbini yalipokwa yanatokea, Nuru alikuwa akitembeza macho kila kona ya ukumbi ule kwa utulivu na umakini mkubwa. Na muda wote alikuwa akipata wasaa wa kumfuatilia Candy na yeyote ambaye angeonekana kuonesha kumfuatilia Candy kwa namna isiyo ya kawaida, lakini hakuna kilichotokea.

Alikuwa amevaa gauni refu la jioni la rangi ya zambarau lililopigwa mpasuowa kukata na shoka, mpasuo ulioishia sehemu katikati ya paja lake, na chini alikuwa amevaa viatu virefu vya usiku.

Alikuwa ameketi kwenye kiti kilichokuwa nyuma kabisa pale ukumbini na kando ya lango kuu la la kuingilia ndani ya ule ukumbi, hivyo kuweza kuwaona kila waliokuwa wakiingia na kutoka mle ukumbini.

Alitupa jicho kwenye kona ya moja iliyokuwa mshazari na pale alipokuwa ameketi ila kwa mbele ya ukumbi ule ambako kulikuwa kuna lango jingine la kuingilia mle ukumbini, na huko akamuona Morandi Gwaza aliyekuwa ndani ya suti moja kali sana akiwa amejiegemeza kwenye nguzo iliyokuwa kando ya kiti alichokalia ilhali usoni akiwa amevaa miwani iliyoonekana kuwa ni ya macho ambayo ilimfanya aonekane tofauti sana.

Bado moyo wake ulikuwa ukimchonyota kama kwamba kuna kitu kilikuwa kinaelekea kutokea, na siku zote apatapo hali kama ile ni kweli huwa kuna kitu kinatokea.

Lakini nini?

Aliinuka na kutembea taratibu kama anayetaka kuelekea msalani huku akizungusha macho mle ukumbini na moyo ukimwenda mbio. Simu yake ikaita sikioni kwake naye moja kwa moja akaanza kuongea nayo kwa kutumia kisikilizio cha Bluetooth alichokuwa amekipachika sikioni kwake ilhali ile simu ikiwa ndani ya kipochi chake ghali kilichokuwa mkononi mwake.

“Vipi wewe?” Sauti ya Morandi ilivuma sikioni mwake.

“Ah, hamna kitu…bado napata hisia kuwa kuna kitu kitatokea hapa, ila sijaona chochote au yeyote wa kunithibitishia hilo!” Alilalama kwa mpenziwe.

“Okay, sa’ unaelekea wapi?”

“Ah, nazurura tu humu ndani kwa muda niangaze-angaze…yaani pale nilipokaa naona kabisa kuwa utulivu wangu ni ziro chini ya ziro…”

“Okay, stay in touch!” Morandi alimjibu na kukata simu.

Nuru alichukua uelekeo wa msalani, na hapo moyo wake ukafunga breki ghafla na kuanza kwenda kwa kasi ya mtelezo. Mbele yake alimuona jamaa akitokea sehemu za maliwato ya wanaume na mara moja akajua kuwa alishapata kumuona mahala.

Lakini wapi?

Alipishana na yule jamaa ambaye alikuwa amevaa kapelo kichwani ilhali chini akiwa amevaa suruali safi ya jeans na shati zito, jeupe, la mikono mirefu. Aligeuka kumtazama yule jamaa akizidi kuambaa kwenye ile korido ndefu ya kutokea maliwatoni kuelekea kule ukumbini na hapo kitu kikafyatuka kichwani mwake.

Ule mwendo! Ni yule jamaa wa mikumi,bloody shit, nilijua tu kuwa kuna kitu hapa!

Alisimama na kumtazama yule jamaa akipotelea nje ya ile korido.

Kule ukumbini simu ya Morandi iliita naye akaipokea.

“Kuna jamaa ameingia hapo sasa hivi kutokea maeneo ya msalani!Shati jeupe la mikoni mirefu, kapelo na jeans!” Alimwambia, lakini Morandi hakumsikia vizuri, kwani kule ukumbini muziki ulikuwa umepamba moto, na watazamaji nao walikuwa wakishangilia hovyo.

“Nini? Nyati mweupe?” Aliuliza kwa mshangao.

“Shati jeupe wewe! Nyati vipi tena? Mfuate huyo jamaa Mo, ndiye yule wa Mikumi!” Nuru alisema huku akikata simu na kurudi pale ukumbini.

Aliangaza macho huku na huko, lakini jamaa hakuwepo! Alitupa macho kule kwa Morandi, naye hakumuona.

Akh!

Alihamanika.

Hakika ni yule jamaa wa mikumi!

Sasa yuko wapi tena?

Kwanza kaja kufanya nini huku?

Ni wazi alikuwa anamfuatilia Candy…lakini anategemea kumfanya nini kwenye kadamnasi kama hii?







“Ni nini?” Morandi alimkoromea kutokea nyuma yake na kidogo aliruka kwa mshituko. Aligeuka na kumjuza alichokiona. Morandi alimakinika. Alimshika mkono na kutembea naye kuelekea kwenye lango la kutokea nje ya ukumbi ule.

“Umesema shati jeupe na kapelo?” Alimuuliza tena, na Nuru akathibitisha hilo.

“Mi’ nimekuwa nikikufatilia wakati ukiingia kule usawa wa msalani…na nilimuona huyo mtu akitokea maeneo hayo…” Alisema kwa utulivu.

“Sasa kaenda wapi?” Nuru aliuliza huku akimfuata Morandi.

“Ameelekea usawa wa vile viti vya nyuma kabisa upande wa pili wa hili lango la kuingilia ukumbini” Morandi alimjibu.

Kwenye kiti kilichokuwa kwenye kona kabisa ya ukumbi ule katika msururu wa viti vilivyokuwa nyuma kabisa pale ukumbini, John Koccho alikuwa ameketi kwa utulivu akisubiri kushuhudia iwapo Candy ataibuka kidedea ili ampandishie dau. Alikuwa amekwenda pale ukumbini usiku ule makusudi kabisa kwa lengo la kuhakikisha kuwa anaonana tena uso kwa uso na binti yule, ili kumdhihirishia kuwa bado yuko na haogopi lolote kutoka kwake. Baada ya hapo aliamini kuwa ingekuwa rahisi kumbana tena yule binti na kumdai mrungula.

“Akiutwaa u-miss mtoto hatakuwa na namna ila kunikubalia matakwa yangu, akihofia kashfa itakayomuangukia wakati tayari ni miss Tizedi!” Alijiwazia kwa matumaini huku akijiweka sawa pale kitini.

Hapo aliona mtu akimsimamia mbele yake, naye akadhani kuwa jamaa alikuwa anataka kupita, lakini hapo hapo akaona hilo haliwezekani kwani yeye alikuwa kwenye kiti cha kwenye kona kabisa, kushoto kwake kukiwa na ukuta. Aliinua uso kumtazama yule mtu aliyemsimamia mbele yake kwa macho ya kuuliza.

“Ndugu naomba tuongozane nje bila ya vurugu, tafadhali” Morandi alimwambia huku akimwonesha kitambulisho kilichoonekana kama kwamba ni cha askari, kisha haraka sana jamaa akakirudisha mfukoni kile kitambulisho na kubaki akimtazama kwa macho makali.

Mwili ulimfa ganzi John Koccho na hakuelewa kilichokuwa kinaelekea kumtokea.

Nakamatwa na polisi! Wamenijuaje?

“Er, sikuelewi mzee….una…tuongozane nje kivipi?”Alimuuliza, akiwa makini kuona kuwa watu waliokuwa jirani nao pale ukumbini walikuwa wameanza kufuatilia mjadala ule.

“Nimekwambia tuongozane nje.Tutaongea huko, au unataka nikupige pingu hapa hapa?” Morandi alimkoromea, na mwanadada aliyekuwa kando ya Koccho pale ukumbini aliachia mguno wa woga.

“Kwa kosa gani lakini…?” Koccho alihoji huku akili ikimzunguka.

Candy kaniuza,malaya mkubwa…lakini kivipi?

Morandi alisonya na kumkwida shati kibabe. Akamuinua kwa nguvu kutoka pale kitini, mayowe ya wahka yakiwatoka baadhi ya wahudhuriaji waliokuwa pale jirani, na kumbana mkono wake kwa nyuma kisha akamuongoza nje ya ukumbi ule huku akitembeza macho yake huku na huko kutazama iwapo maaskari wa kweli waliokuwapale ukumbini walikuwa wakiona tukio lile.

“Okay, okay…twende bwana…twende!” Koccho alisema huku akiongozana naye.

Nuru alikuwa amesimama kando ya mlango wa kutokea nje ya ukumbi ule akiwa anacheza na simu yake, na muda yule jamaa alipokuwa anakaribia pale mlangoni akiongozana na Morandi, alimuweka kwenye taswira ya kamera ya ile simu yake na kumfyatua picha nne za haraka haraka, halafu akaungana na Morandi kumuongoza nje yule jamaa.

Nje ya ukumbi walimuweka katikati yao, kila mmoja akiwa amemshika kiwiko cha mkono wake.

“Ah, we…wewe!”Koccho alimaka alipomuona Nuru.

“Alaa, umenikumbuka eenh?Ulidhani ulivyonitoroka kule mikumi kizani sitaweza kukutambua tena?”

“Jamani hapa kuna kutokuelewana kudogo tu, wala hamna tatizo…”Koccho alianza kujieleza.

“Twende wewe! Tutaongea kwa kituo sana tu tukifika tukupelekapo…” Morandi alimkoromea huku akimuongozea sehemu yenye maegesho ya magari yaliyoko karibu na eneo la benki ya TIB pale mlimani City.

“Nako ni wapi?”Koccho aliuliza.

“Hebu kelele wew…” Nuru alianza kumkoromea, lakini ghafla Koccho aliwageukana kuwaamshia kizaazaa kikubwa.

“Nako ni wapi?”Koccho aliuliza.

“Hebu kelele wew…” Nuru alianza kumkoromea, lakini ghafla Koccho aliwageukana kuwaamshia kizaazaa kikubwa.

Alijilegeza mwili mzima, na ghafla akina Morandi wakamhisi mateka wao akiwawia mzito mikononi mwao. Nuru akawa wa kwanza kumwachia huku akimaka kwa mshituko na Koccho akawa anaenda chini. Morandi aliguna huku akijitahidi kumdhibiti lakini hakuweza na yule jamaa akajidondosha moja kwa moja mpaka chini.

“Nini huyu!” Morandi alilaani huku akianza kumuinamia pale chini, na hapo Koccho alikurupuka ghafla. Alizungusha mguu wake na kumchota ngwara kali. Morandi alishtukia kitendo kile akiwa amechelewa, hivyo aliwahi kuinua mguu wake kuikwepa ngwara ile lakini ngwara ya koccho ikaukumba mguu wake uliobaki naye akawa anaenda chini mzima mzima huku akijitahidi kujizuia asianguke, tusi kubwa likimtoka, akimsikia Nuru akipayuka kwa mshituko.

Koccho hakushughulika naye tena, na badala yake alijizungusha pale chini na kujiinua kumkabili Nuru ambaye naye ndio alikuwa anazinduka na kuelewa kilichokuwa kimetokea. Aliruka nyuma hatua moja huku akiwa ametanua miguu yake kwa lengo la kujidhibiti asichotwe ngwara kama mwenzake, ule mpasuo maridhawa wa kwenye lile gauni lake ukimwezesha kufanya hivyo bila shida yoyote.

Lakini badala ya kumtupia ngwara, Koccho alimrukia mzima mzima na kupigiza bega lake tumboni kwa yule mwanadada, akimkumba na kwenda naye mpaka chini, wakati huku nyuma yake bidii za Morandi kujizuia asiangushwe na ile ngwara ziligonga mwamba naye akajibwaga chini kama mzigo, yowe la ghadhabu likimtoka na hapo hapo akijirusha wima kutoka pale chini.

Nuru alipiga mweleka kwa mgongo wake pale chini huku akihisi pumzi zikimhama kutokana na kushindiliwa bega tumboni kwa nguvu na yule jamaa, na hapo hapo Koccho alijikurupusha na kutimua mbio.

“WEWWEE!” Morandi alimpigia kelele huku akianza kumtimulia mbio, na hapo Nuru alijigeuza na kutupa mkono wake kwa lengo la kumdaka mguu yule jamaa huku naye akijiinua. Mkono wake ukamparaza tu Koccho mguuni, lakini hiyo ilitosha kumpoteza mwelekeo yule jamaa naye akaanza kupepesuka huku akikimbia.

“WEZIIIII!” Koccho alipiga kelele huku akipepesuka wakati Nuru akiwa ameshainuka na kumkaribia. Koccho alijiweka sawa na kuanza kukimbia tena, lakini hapo alimhisi yule mwanadada akiwa karibu naye sana, hivyo aligeuka na kofi kali sana la kubahatisha, na lile kofi likampata Nuru sawia usoni naye akamaka kwa kilio cha mshituko zaidi kuliko maumivu, muda huo akisikia mayowe ya askari wa ulinzi wa pale Mlimani City yakiitikia kile kilio cha mwizi, filimbi zikipigwa kutokea kona tofauti za eneo lile.

Koccho alizidi kutimua mbio kuelekea kwenye geti la kutokea nje ya lile eneo la Mlimani City, Morandi akimtokea mbio nyuma yake.

Nuru alitikisa kichwa kuweka akili sawa na kuangaza huku na huko kutafuta walikoelekea akina Morandi na hapo alishtushwa na mmoja wa wale walinzi pale mlimani city.

“Mwizi wapi?” Jamaa alibwata, na Nuru alimuoneshea kule walipokimbilia akina Morandi, na yule mlinzi akatimua mbio kuelekea kule alipoelekezwa ilhali mwingine akimzuia Nuru pale alipokuwa.

Oh, shiit!

Koccho alizidi kulikaribia geti pweke la kutokea na kuingilia pale mlimani city huku akizidi kupiga kelele za mwizi. Mlinzi wa pale getini alimfikia mbio, na Koccho akazidi kutumbua macho.

“Wezi kulee…wanapigana na walinzi wenzako…walitaka kunikaba!” Alibwata huku akioneshea kule alipotokea, ambako Morandi ndio alikuwa akitokea.

“Kaa hapa!” Mlinzi aliamuru naye akasimama imara kusubiri kukabiliana na huyo mwizi aliyekuwa anakuja. Morandi alisikia vishindo vya askari nyuma yake huku akipigiwa kelele kuwa asimame, na pia aliona na kusikia alichokuwa akikifanya na kukisema Koccho kule kwa yule mlinzi wa pale getini, na akajua kuwa jamaa alikuwa amekoroga mambo kusudi.

“Huyo ndiye mwizi wewee, ama!” Alimpigia kelele yule mlinzi wa getini.

“Simama nakwambia wewe, ama sivyo nakuwasha!” Mlinzi aliyekuwa akimkimbiza nyuma yake naye alimbwakia, na Morandi Gwaza akajua kuwa hakuwa na jinsi.

Alisimama.

Kule getini, yule mlinzi alimsikia Morandi, na akamgeukia Koccho kwa macho ya kuuliza, na hapo akakumbana na kofi kali la uso. Alibwaka kwa mshituko, na Koccho akamdidimiza teke la korodani na mlinzi alipiga ukelele wa maumivu huku akienda chini bila kupenda. Koccho akatimua mbio kutoka nje ya geti lile na kupotelea nje ya eneo lile, akiamuacha yule mlinzi akigaragara pale chini huku yule mwenzake akimfikia na kumuinamia.

Morandi alitazama kule alipokimbilia yule jamaa na akamuona akivuka barabara kwa kasi ya ajabu, akikoswa-koswa kugongwa na gari ambalo liliburuza matairi kwenye lami kwa breki kali za ghafla huku honi zikirindima kila upande.

Son of a bitch!

Alilaani na kugeuza kurudi kule kwa Nuru, akipuuzia maswali ya wale walinzi waliokuwa wakitaka kujua kulikoni. Muda huo Nuru alifika pale walipokuwa, akiongozana na yule mlinzi mwingine.

“Ah, kumbe hawa jamaa ni askari bwana! Yule jamaa ndiye alikuwa mwizi, aisee!” Yule mlinzi aliyekuja na Nuru aliwaambia wenzake, wazi kuwa hivyo ndivyo alivyoelezwa na Nuru.

“Twenzetu!” Morandi alikoroma kwa hasira, na waliondoka wakiwaacha wale walinzi wakijadiliana juu ya kile kilichotokea.

“Uko sawa?” Morandi alimuuliza Nuru.

“Ah, mshenzi kanizaba kofi la uso nahisi uso wangu utakuwa umeumuka vibaya sana…hata sijui nitauweka wapi uso wangu humo ukumbini sasa…” Nuru alisema kwa malalamiko, na Morandi akawa makini.

“Kofi la uso? Umejishika hapo alipokupiga?” Alimuuliza.

“Ah, sasa na we’ swali gani hilo bwana? Mtu akuzabe kofi la uso a’fu usijishike? Of course nimejishika, ila sijataka kujikuna sana usije uso ukazidi kuumuka, pumbavu zake!” Nuru alimjibu kwa kisirani.

“Okay,basi kuna kitu inabidi tufanye…” Morandi alisema na kumuongoza hadi kwenye gari lao lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya pale Mlimani City.

Ndani ya gari Morandi aliwasha taa ya mle ndani na kumtazama ile sehemu aliyopigwa kofi, na kweli, alama za vidole vya John Koccho zilibakia pale shavuni kwake.

“Oh, safi sana!” Morandi alisema na Nuru akamjia juu.

“Safi sana? Yaani mi napigwa bao namna hii we’ unasema safi sana Mo?”

“Oh, no. Sorry…sikumaanisha safi kuwa umepigwa…nadhani hapa tunaweza kupata alama za vidole vya yule jamaa na kuweza kumfuatilia ki-intelijensia zaidi…” Morandi alimjibu.

“Aah, kivipi…?”

Hapo Morandi akamwomba kishubaka cha poda maalum aina ya mascara ambacho alijua kuwa huwa anatembea nacho kwenye pochi yake. Alimpaka ile poda nyepesi yenye rangi ya kahawia kwa umakini sana kwenye lile eneo lililoachwa alama za vidole na yule jamaa. Kisha akachukua karatasi laini, yaani tissue paper kutoka kwenye boksi maalum la karatasi zile lililokuwa mle garini na kuiweka kwa ufundi juu ya ile poda iliyokuwa juu ya ile alama ya kofi pale shavuni kwa Nuru. Aliididimiza kwa umakini ile karatasi pale shavuni, kisha akaitoa na kuitazama.

Alama za vidole vya yule jamaa zilibaki kwenye ile karatasi laini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Safi sana! Sasa tumeshamjua huyu jamaa…ni swala la muda tu pumbavu zake!” Alisema kwa ushindi, na Nuru akatabasamu.

“Duh, ama kweli we kiboko Mo…mi’ sikufikiria kabisa kitu kama hicho.” Alisema huku akijifuta ile makeup kutoka usoni kwake.

“Yaa, ukikaa ndani ya idara ya upelelezi kwa muda mrefu kama mimi unakuwa unajua vitu kama hivi!” Morandi alimjibu huku akiiweka kwa uangalifu ile karatasi kwenye droo ya mle garini.

“Sasa turudi kule ukumbini tuone mtoto Candy anaendeleaje…maana nina hamu sana ya kuongea naye, na leo ndio mwisho wa mashindano yake haya!”









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog