Simulizi : Miss Tanzania
Sehemu Ya Nne (4)
***
Ngamao Kijambia aliingia ofisini kwa mkuu wake wa kazi wa muda pale makao makuu ya polisi na kuomba kuonana naye. Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa hatimaye alipata fursa ya kuonana naye.
“Mkuu, nadhani sasa kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kuhusu mtuhumiwa wangu kabla mambo hayajawa magumu zaidi…” Alimwambia, na yule mkuu akamtazama kwa macho ya kuuliza.
“Unataka tufanye juhudi za makusudi gani Ngamao?Tulikubaliana kuwa tutalifanyia kazi swala lako pindi mtuhumiwa akirudi nchini, sio?”
“Yaa, lakini sasa naona tayari ameshapitishwa kuwa kwenye ishirini bora…isije ikaleta taabu baadae mkuu, mi nadhani lingefanyika la kufanyika mapema tu iwezekanavyo!” Ngamao alisema kwa msisitizo.
“Sikuelewi Ngamao. Mpango unabaki vile vile kama ilivyokubaliwa awali…we wait!” Mkuu alimjibu.
Ngamao alitoka nje ya ofisi ya mkuu wake yule akiwa amefura kwa hasira.
***
GTZ alikuja mbogo.
“Hebu ona sasa mtoto ameingia kumi bora za Miss World Ngamao, Miss World! Kama tulishindwa kumshika wakati akiwa kidampa tu hapa bongo, na tukashindwa kumtaiti wakati akiwa miss chipsi kuku tu hapa TZ, haya nd’o tutamuweza akiwa miss world huko?”Alimaka akiwa sebuleni kwake kule masaki, mguu wake mbovu ukiwa umening’inizwa juu ya stuli.
Aliamua kutoka hospitali na kuwa anahudumiwa pale pale nyumbani kwake, masaki. Nesi mmoja aliwekwa pale nyumbani kwa ajili ya kumhudumia.
Ngamao alikunja nne pale sebuleni na kumtazama kwa macho yenye ghadhabu.
“Tangu lini ulisikia mtanzania akanyakua taji la miss world wewe? Hiyo itaishia kwenye riwaya zenu za kubakshiwa tu hizi mnazoandikiwa na hawa waandishi wenu hapa nchini…miss world mchezo? Hiyo kufika kumi bora tu mshukuru! Yule malaya atarudi tu hapa, na akirudi tunaye kama kawaida!” Ngamao alisema kwa jeuri.
GTZ alitikisakichwa kwa masikitiko.
“Yaani mtu mjinga kama yule ametuhenyesha namna hii sisi?” Alisema, na Ngamao akainuka.
“Mi’ naenda zangu…hamna jipya hapa!” Alisema.
Alishaamua kuhama nyumbani kwa GTZ mapema sana na kuchukua chumba kwenye hoteli moja nzuri tu maeneo ya sinza. Mwenendo wa GTZ wa kupenda kujichukulia sheria mikononi haukumpa amani kukaa naye nyumba moja akiwa ni afisa wa polisi. GTZ akikurupuka na kufanya lisilotarajiwa anaweza naye akajikuta akihusishwa bila hata ya kushiriki katika upuuzi wowote ambao GTZ angeufanya.
Alipoondoka, mtu mwingine mrefu na aliyejazia kimazoezi alijitokeza kutoka kwenye moja ya vyumba vya mle ndani na kuketi na GTZ pale sebuleni.
Jamaa alikuwa ameshabihiana sana na GTZ, tofauti yake ni kwamba yeye alikuwa mrefu na mweusi kidogo.
“Umesikia maneno ya Ngamao?” GTZ alimuuliza kaka yake wa kuchangia mama.
Jamaa aliguna tu.
“Hawezi kufanya vilivyo ndivyo huyu sasa nakwambia! Ndio maana toka mwanzo sikutaka kumuhusisha…” GTZ alimwambia kaka yake.
“Lakini bado hukuona kuwa ulipaswa unitafute mimi ukamtafuta yeye.” Jamaa alisema kwa kushutumu.
GTZ akagwaya.
“Ah, si unajua tena…hatukuwa katika mahusiano mazuri sana bwana. Ila mwisho wa siku damu ni nzito kuliko maji…nikakupigia!”Alijitetea.
Jamaa akaguna na kupiga kimya. Alikuwa na tabia za kijasusi-jasusi sana, na GTZ pamoja na ubabe wake, alikuwa akimuogopa sana.
“Tusubiri tu atie miguu hapa nchini huyo malaya GTZ…nitafanya litakiwalo halafu nitatoweka kama kawaida yangu. Sitahitaji chochote zaidi kutoka kwako!” Jamaa alimjibu.
***
Siku ilipotangazwa kuwa Candy Gamasala amepita na kuingia kwenye mchujo wa kumi bora katika shindano lile, nchi nzima iliingia kiwewe. Mrembo wa Tanzania kufikia kumi bora halikuwa jambo dogo. Maredio yakalinadi tukio la fainali zile kwa nguvu, vituo vya televisheni navyo havikuwa nyuma. Magazeti ndio usiseme!
Kamati ya Miss Tanzania ikaandaa mpango mkubwa wa kataifawa kutandaza ryuinga kubwa kabisa sehemu mbalimbali za nchi ambapo watu walishawishiwa kujitokeza kwa wingi kumtazama binti wa kitanzania akipambana kupeperusha bendera ya nchi yake kwenye kilele cha shindano lile kubwa la urembo duniani.
Upepo ulibadilika nchini.
Kila kona ukipita ilikuwa ni Candy Gamasala tu. Wajanja wa mjini nao wakatengeneza fulana maalum na kuanza kuziuza, zikiwana picha ya mrembo wa taifa na ujumbe wa kumtia moyo huko aliko.
“Tuko nawe Candy!”Baadhi ziliandikwa.
“Ni Candy Gamasala miss world mwaka huu!” Nyingine zilianzikwa.
“Go Candy, Go!” Na nyingine zilichagiza.
Alimuradi Candy Gamasala likaondokea kuwa jina maarufu sana nchini ndani ya siku chache kabisa kuelekea kwenye fainali za mpambano wa urembo wa dunia.
Kule Venezuela, Bishkuku alikuwa amefika katika kilele cha furaha wakati akimuona mwanafunzi wake akiwachachafya warembo wa duniani katika shindano lile, na Kokos Wandiba alijikuta akishukuru sana kwa kuunga kwake mkono bidii za Bishkuku na kumdhamini Candy katika shindano lile.
Candy mwenyewe ndio alikuwa akielea katika uwinguwa juu kabisa wa faraja kwa kupata nafasi ya kufanya kile ambachoalikuwa anakipenda kwa moyo wake wote.
Kwa wakati ule, siku mbili tu kabla ya shindalo la fainali za miss world, Candy alikuwa katika wakati bora kabisa wa maisha yake.
Ni wakati ambao ungembadilikia ghafla sana na kwa kishindo kikubwa, tena katika saa ambayo si yeye wala Bishkuku na Kokos waliitarajia…
***
Ukumbi wa matukio adhimu wa Poliedro de Caracas, ulioko jijini Caracas, nchini Venezuela ulikuwaumefurika kuliko ilivyowahi kutokea,pale watu kutoka pande zote za dunia walipokuwa wakisubuiri kushuhudia fainali za kumteua mrembo wa dunia.
Safari hii Bishkuku na mmoja wa watendaji wa kike wa kamati ya miss Tanzania walikuwa nyuma ya steji wakimsaidia mrembo wa Tanzania Candy Gamasala kwenye mavazi na itifaki mbalimbali za kiurembo, kama jinsi ilivyokuwa kwa wasimamizi wa warembo wengine wa shindano lile lililogusa mioyo ya mashabiki wengi duniani.
Kule kwa watazamaji, Kokos Wandiba alikuwa ameketi pamoja na watendaji wa kamati ya Miss Tanzania,pamoja na watanzania wengine waliokuwa wakiishi Venezuela na wale ambao walisafiri mahsusi kutoka Tanzania hadi Caracas kuhudhuria shindano lile, wakiwemo wawakilishi wa wadhamini wa shindano la Miss Tanzania pamoja na waandishi wa habari ambao wao pamoja na kwamba walikuwa wakiranda huku na huko ukumbini, kazi yao kubwa ilikuwa ni kupata kila tukio lililomhusisha mrembo wa kutoka nchini kwao, Candy Gamasala.
Balozi wa Tanzania nchini Venezuela, mkewe na wanawe wawili pia walikuwepo pale kwenye ukumbi ule usiku wa tukio, pamoja na akina Kokos.
Usiku uliopita balozi aliwaalika Candy na kamati nzima ya Miss Tanzania kwenda kwenye chakula cha jioni nyumbani kwake, na akatumia furs ile kumtia moyo Candy katika ushiriki wake kwenye shindano lile, hasa ikizingatiwa kuwa tayari alikwisha pita kwenye kumi bora na sasa alikuwa anaelekea kwenye kinyang’anyiro cha mwisho. Kinyang’anyiro nakulinyakua kabisa taji lile.
Msisimko wa kulinyakua taji lile ulikuwa hai mwilini kwa Candy Gamasala wakati akiwa nyuma ya jukwaa kusubiri kuanza kwa fainali zile.
Huku Tanzania, wananchi walikuwa wakiufuatilia mpambano ule mojakwa moja kutoka Caracas kwa kupitia kwenye runinga zao, na pale Mlimani City na maeneo mengine, runinga kubwa kabisa zilikuwa zikinadi kila kilichokuwa kikielekea kutokea kule Venezuela.
Kule Tarime kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ambacho Candy alitokea, watoto na wasimamizi wao walikuwa wamejirundika mbele ya runinga kwenye bwalo la kutazamia runinga pale kituoni, nao wakifuatilia kwa hamasa kubwa maendeleo ya mwenzao katika medani za kimataifa.
Homa ya kushuhudia kwa mara ya kwanza mtanzania akinyakuwa taji la urembo wa dunia ilitanda nchi nzima.
Jijini Dar, Ngamao Kijambia alikuwa ameketi ofisini kwa mkuu wake wa kazi wa muda akiwa jijini Dar, na walikuwa wakifuatilia shindano lile kwa makini.
“Imekuwa wazi kwa kila mtu niliyemshirikisha katika hili kuwa kutakuwa kuna madhara makubwa sana iwapo huyu binti atazidi kusonga mbele wakati huku nyumbani kuna shutuma nzito kama hizo ulizozileta dhidi yake…kwa nini ameachiwampaka imefikia hapa lakini?” Mkuu alisaili na Ngamao akajiuma mdomo na kubaki kimya, akijua kuwa sehemu kubwaya hali ile kufikiapale ni yeye kutaka kumkamata mwenyewe yule mwanadada kwa ajenda zake binafsi.
“Ah, nadhani hilo kwa sasa si muhimu…la muhimu ni kuchukua hatua muafaka saa hivi…tusisubiri zaidi, mkuu!” Ngamao alishadidia.
“Ah, hilo ni lamwisho kabisa Ngamao…kila kitu kiko stand by kwa sasa…!”
“Ah, haya! Lakini bado nasisitiza kuwa iwapo akitokea kuwa akatwaa hilo taji, na hilo ni iwapo…hana nafasi ya kuchukua taji yule, lakini iwapo itatokea hivyo, na shutuma kama hizi zikiwa zinamkabili huku nyumbani, basi tujue kuwa itakuwa ni bonge la skendo kwataifa, hilo!” Ngamao alisema.
Mkuu alisonya.
“Lazima kuna ka-uzembe fulani tu hapo Ngamao, na wewe uko katikati ya kauzembe hako…hii tuombee tu huyu binti aishie hapo na arudi nyumbani ili tumdhibiti…” Mkuu alisema.
“Hivyo ndivyo itavyokuwa tu…tangu lini binti wa kitanzania akafika zaidi ya kumi bora Miss world? Mi sina hata wasiwasi juu ya hilo...”
“Unajipa moyo Ngamao…huyu mtoto yuko vizuri sana…hivi ni nani aliyefikia kumi bora kabla yake kutoka hapa kwetu, eenh? Kama yupo basi ni zamani sana lakini naweza kukuwekea asilimia nyingi sana kuwa hakuna! Ombea tu mtoto ashindwe huko ama si hivyo akishinda itakuwa ni balaa kubwa sana!” Mkuu alisema, na Ngamao akaishia kujipapasa upara.
Kutokea kule nyumbani kwake Masaki, GTZ na kaka yake wa kambo, Greg Pasha, walikuwa wakifuatilia mashindano yale kwa makini, Greg akiwa anapiga kinywaji kikali taratibu, GTZ akiwa na kikombe cha chai.
“Yaani huyu mtoto anavyozidi kusonga mbele kwenye haya mashindano ndio anazidi kuniudhi kwa kweli! Ina maana ye’ ndo amekuwa bora kuliko warembo wengine wote walioenda kusindikiza mashindano haya miaka yote hii?Mi’ ananiudhi kweli kweli ujue!” GTZ alisema kwa hasira.
Greg Pasha alimtupia jicho la pembeni, kisha akanfyonza kinywaji chake na kubadili nne kutoka mguu mmoja kwenda mwingine.
“Unasahau msemo wa kwamba ukiwa juu zaidi ndio mweleka unakuwa mkali zaidi? Mwache apande tu hiyo chati…ndipo atakapoumia zaidi pale atakapoporomoka. Ye’ hata awe moja bora, wacha kumi bora…mwisho wa siku itabidi arudi tu hapa home…bongo. Na akirudi mi n’naye!” Greg alisema kwa utulivu uliotisha.
Jamaa alikuwa ni mtu wa kufurahia kuumiza watu.
Kutokea pale nyumbani kwa Bishkuku mtaa wa Aggrey, Morandi Gwaza na Nuru nao walikuwa wakifuatilia kwa makini mashindano yale.
“Mnh, mi’ moyo wangu umejaa wahka hata sijui kwa nini!” Nuru alisema huku akitafuna bisi, akifuatilia shindano lile.
Morandi akaguna.
“Hayo yatakuwa mashaka mengine tu Nuru…kwa kule alipo Candy yuko salama sana…balaa litaanza akirudi hapa. Au una wasiwasi kuwa atashindwa kulitwaa taji?” Alimwambia na kumuuliza.
“Ah, wala sio hilo la kukosa taji…nina wahka wa mashaka-mashaka tu, Mo…hata sijui ni nini kwa kweli!” Nuru alisema.
Morandi aliamua kumpotezea.
Kama wao, Sanura Kashogi na Tunis nao pia walikuwa wakifuatilia ule mpambano huku wakiwa na vijiba vya moyo…
***
Kule Caracas, kwenye ule ukumbi maridhawa wa Poliedro de Caracas, mashindano ya fainali za mrembo wa dunia yalianza na dunia nzima ikashuhudia.
Warembo kumi walioingia kumi bora walipita mbele ya majaji, wakaulizwa maswali, wakatakiwa kuonesha vipawa mbali mbali na kuulizwa maswali kwa mara nyingine tena.
Katikati ya matuko haya, tumbuizo za burudani kutoka kwa wasanii wakubwakabisa duniani zilikuwa zikiendelea kila baina ya tukio lililokuwa likitokea pale.
Hatimaye msema chochote ambaye alikuwa ni mcheza sinema maarufu wa Hollywood, alipanda jukwaani nakuita baadhi ya watu maarufu kwenda kutaja washindi wa vipengele mbalimbali kabla ya kutaja wale washindi watano ambao wangeingia hatua ya mchujo wa mwisho,mchujo ambao ndio ungemtoa mrembo wa dunia.
Hoihoi na nderemo zilitanda nchi nzima pale Candy alipoteuliwa kuwa “Miss Photogenic” wa shindano lile, yaani binti mwenye kupendeza zaidi akipigwa picha.
Si hoi hoi na mbija hizo kutoka pale kwenye kundi la watanzania waliohudhuria shindano lile pale ukumbini, Kokos Wandiba akikumbatiana na mratibu wa kamati ya miss Tanzania bila hata kujijua.
“Na sasa ni wakati wa majaji kututajia warembo watano ambao safari yao itaishi hapa, na kuwaacha watano wengine wakiendelea mbele na hatimaye kutufikisha kwa mrembo wetu wa dunia leo hii…” Msema chochote alinadi, na ukumbi ukabaki kimya, wakati wale warembo kumi wakijipanga kilimbwende pale mbele, Candy akiwa na shada lake la miss photogenic mkononi, moyo ukimpiga kwa nguvu sana.
Majina matano ya wale wanaoaga shindano yalipomaliza kutajwa, la Candy halikuwamo!
Heh!
Vurugu za shangwe zilirindima kutoka kila upande pale ukumbini, wakati Kokos na watendaji wa kamat ya Miss Tanzania wakibaki wakiwa wamepigwa butwaa kwakutoamini kile kilichokuwa kimetokea.Mratibu alimwaga chozi wazi wazi.
Haijawahi kutokea…lakin ndio ilikuwa inatokea!
Candy alibaki akibubujikwa na machozi ya furaha na kutoamini, Bishkuku akilia wazi wazi kule nyuma ya jukwaa akimsubiri mrembo wake arudi kutoka kule mbele. Wale warembo watano waliobaki walikuwa wakiwapungia watazamaji mikono kwa furaha, wote wakibubujikwa na machozi, wakijua kuwa yoyote kati yao alikuwa anaweza kuibuka mrembo wa dunia usiku ule.
Huku jijini Dar, Tunis aliangua kilio kikubwa cha wivu, na Sanura Kashogi akabaki akiwa amefinyanga sura kama aliyeramba ndimu gwadu, ilhali kule masaki, GTZ alibaki akiikodolea macho runinga bila ya kuamini kile alichokuwa akikiona.
Na kwa akina Ngamao, Mkuu wake wa kazi wa muda aliinua simu na kuipeleka sikioni kwake, huku uso wake ukiwa umefanya dhamira ya kile ambacho alikuwa akijitahidi kukiepuka muda wote…
***
Ilikuwa ni furaha ya hali ya juu kule Caracas. Msema chochote alipanda jukwaani na kunadi kuwa wale warembo watano waliopita hatua ya mwisho ya mchujo ule walikuwa wanarudi nyuma ya jukwaa kujiandaa na hatua ya mwisho, na kuwaalika watumbuizaji maarufu wa pale pale Venezuela kupanda jukwaani.
Ukumbi ulishangilia, msema chochote akajisogeza pembeni kuwapisha watumbuizaji, wakatiw ale warembo watano, Candy miongoni mwao, wakiondoka na kurudi kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo vilivyokuwa nyuma ya jukwaa.
“Aaah umetutoa kimasomaso Candy jamani…umetutoa mtoto!” Bishkuku alimrukia na kumkumbatia kwa furaha kule nyuma ya jukwaa, na yule binti kutoka kamati ya miss Tanzania naye akawafuata na kuwakumbatia wote kwa pamoja, mmoja wa waandishi wa habari waliosafiri na akina Candy kutoka Dar hadi pale Venezuela alifika hadi kule nyuma ya jukwaa na kuwapiga picha wakiwa wamekumbatiana namna ile.
“Ohh, Anti Bishi siamini kwa kweli…siamini!” Candy alisema kwa furaha, bado akibubujikwa na machozi.
“Ah, tumelitimiza mrembo wangu…tumelitimiza. Hapa piga ua…tukikosa taji basi mshindi wa pili hatukosi!” Bishkuku alisema kwa hamasa.
“Ah! Anti Bishi mpambano bado ni mkali sana huu…” Candy alimwambia huku wakielekea kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo, wakipishana na warembo wengine waliokuwa nao pale nyuma ya jukwa pamoja na wapambe wao.
“Hi Candy!” Miss Papua New Guinea alimwita huku akimpungia mkono.
“Hi!” Candy alimjibu huku naye akimpungia mkono.
“Good Luck on the finals, okay sweetie?” Miss Papua New Guinea, ambaye yeye alikuwa ni katika wale watano walioaga mashindano yale, alimtakia heri, na Candy akaguswa sana na hilo.
“Thank you dear!” Alimjibu.
“Come on…twendeni chumbani kwetu basi jamani…” Mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania aliwaambia.
“Okay. Yaani Bishkuku kwa kujitia matumaini!” Candy alisema huku wakielekea chumbani kwao.
“Ah, Candy! Hii picha mi’ nimeisoma kwa makini sana…kati yenu mliopita tano bora ni wewe tu na Miss Scotland ndio mliopata mataji ya ziada Candy…wewe umetwaa miss photogenic na yeye katwaa miss congeniality…na uzoefu unaniambia mara nyingi wanaotwaa mataji madogo ndio wanaoishia kutwa taji la mrembo wa dunia. Candy, u-miss world unakunukia mrembo wangu! Hii ni zaidi ya ndoto kutimia hii…hii ni historia kuandikwa…!” Bishkuku alimwambia na Candy akahisi mwili ukimsisimka.
Walikuwa wameufikia mlango wa kuingia kwenye chumba chao wakati walipoona kundi dogo la askari wa ki-Venezuela wakiongozana na baadhi ya watu wengine waliokuwa kwenye nguo za kiraia, pamoja na mratibu wa kamati ya miss world.
“Heh, hawa tena wamekuaje…?” Bishkuku aliuliza huku akiwa amesimama pale mlangoni, akistaajabu kuona wale askari wakiwa wanatembeza macho yao huku na huko eneo lile, na yule mratibu wa miss world akioneshea kidole pale walipokuwa wamesimama wao.
“Aka? Kuna nini…?”
Wale warembo wengine waliokuwa eneo lile nao wakawa makini na lile kundi dogo la wanausalama.
“Miss Candy Gamasala?” Mmoja wa wale askari aliita huku akiwafuata wao moja kwa moja, na moyo wa Bishkuku ukapiga mshindo.
“Yes…?” Candy aliitika huku akiwatazama kwa mshangao kidogo ila kwa udadisi mwingi.
Mmoja wa wale askari ambaye alikuwa mwanamke alimfikia na kumsimamia moja kwa moja mbele yake.
“Uko chini ya ulinzi kuanzia muda huu…” Yule askari alimwambia kwa kiingereza, na Candy akahisi dunia ikiyeyuka mbele ya macho yake.
“Whaaat?”
“Ati nini…?” Mwakilishi wa kamati ya Miss Tanzania alisaili na kujisogeza mbele ya yule askari, akimkinga Candy, warembo wengine pale nao wakamakinika na kile kilichokuwa kikitokea.
“Anti Bishi anasema nini huyu?” Candy aliuliza kwa kuchanganyikiwa, kisha akamgeukia yule askari wa ki-Venezuela.
Wale askari wengine wakamzingira.
“Inanibidi nikuweke chini ya ulinzi bibie, na nitataka uongozane nasi nje ya ukumb huu. Usitulazimishe tukutie pingu bure hapa!” Yule askari alimwambia kwa ukali, kwa kimombo.
“No! Nianchie! Msinishike mimi nyinyi…alla! Kuna kosa limetokea mahali…niwekwe chini ya ulinzi kwa vipi?” Candy alifoka, na Bishkuku aliyechanganyikiwa alimfuata yule askari na kujaribu kumshika bega ili amuulize vizuri, lakini hapo alivamiwa na wale askari wengine na kubanwa chini kama mtuhumiwa.
“Nooo! NIACHENI BWANA! Niacheni nasema…! Ni njama gani inafanyika hapaa?” Bishkuku alipiga kelele, na Candy akapiga hatua kumfuata pale alipokuwa, na hapo alikamatwa na wale askari. Akajaribu kujinasua, lakini askari wakamdhibiti.
Yule askari wa kike aliyekuwa akimsemesha awali alimfuata tena na kutoa pingu.
“Bi. Candy Gamasala…uko chini ya ulinzi kwa kuhusuka na mauaji ya…” Yule askari alimwambia na hapo akatoa kipande cha karatasi na kusoma jina la huyo mtu anayemtuhumu Candy kuwa amemuua.
“Mauaji???” Yule binti kutoka kamati ya miss Tanzania alimaka kwa kutoamini.
“…Bi. Shakira Swadafu!” Alimalizia yule askari, na Candy akatumbua macho kwa kutoamini.
“WHAAT??” Alimaka kwa sauti, halafu mwili wote ukamlegea, na akawa anaenda chini kama mzigo, lakini wale askari wakawahi kumdaka.
Candy Gamasala, Miss Tanzania, na Miss Photogenic kwenye shindano la miss world lililokuwa linaendela, alipoteza fahamu.
Tafrani!
Mtafaruku!
Hekaheka!
Alimuradi lile eneo la nyuma ya jukwaa likawa halitoshi ghafla.
Candy aliinuliwa na kupelekwa chumba cha huduma ya kwanza kule kule nyuma ya jukwaa, ilhali kule mbele tumbuizo ziliendelea, kilichokuwa kikitokea nyuma ya jukwaa hakikuwa kikijulikana isipokuwa kwa wachache tu.
Binti mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania alirudi mbio kule jukwaani na kupasua habari kwa akina Kokos na mratibu wa Miss Tanzania juu ya kilichotokea.
“Whaat?” Mratibu aliuliza na kumgeukia Kokos aliyesawajikwa uso ghafla, kumbukumbu ya mapingamizi aliyokuwa akimuwekea Bishkuku dhidi ya kumtumia yule binti wasiyemjua aa wala bee kwenye mashidano yale ya miss Tanzania…
Akatikisa kichwa kwa kustaajabu.
Alikumbuka maneno ya Morandi kuhusu Candy na mambo ya kisiri yaliyokuwa yamemuandama mrembo yule.
Na sasa nd’o yanatokea haya?
Katika hatua hii?
“Shit! Hapa kuna tatizo hapa…!” Kokos alisema kwa hamaniko huku akimfuata mratibu wa kamati ya miss Tanzania aliyechanganyikiwa kupita maelezo kule nyuma ya jukwaa.
Akili ilikuwa ikimzunguka vibaya sana.
Alikuwa na pingamizi kuhusu kumtumia Candy tangu mwanzo…lakini hiyo ilikuwa wakati ule, na sio sasa. Alipokubali kumdhamini na kuendelea kuwa karibu naye, moyo ulimbadilika.
Na alipokuwa akimfuata mratibu wa miss Tanzania kuelekea huko Candy alipokuwa nyuma ya jukwaa, Kokos Wandiba alijua kuwa atapigana kwa nguvu zake zote kumtetea Candy…mrembo wa nchi yake…mrembo wa moyo wake…
Balozi wa Tanzania nchini Venezuela alipigwa butwaa. Itifaki ilimtaka aendelee kubaki pale pale alipokuwa, ingawa naye ile habari ilikuwa imemchanganya vibaya sana.
Kokos na Mratibu walimkuta Bishkuku kwenye hali mbaya sana.
Alikuwa akilia kwa huzuni isiyo kifani, wakati wauguzi wa dharura wakijaribu kumzindua Candy kutoka pale alipokuwa amelazwa kwenye chumba cha huduma ya kwanza.
“Ni nini hasa kilichotokea hapa jamani...mshiriki wetu alikuwa anaendelea vizuri sana…kitu gani hiki mnachotueleza?” Mratibu wa miss Tanzania alihoji kwa wahka.
Mratibu wa kamati ya Miss World, ambaye sasa alikuwa ameungana na yule mwenyeji wao, mratibu wa kamati ya Miss Venezuela, walimvuta pembeni, na Kokos akajisogeza karibu yao.
“Imekuja taarifa kutoka nchini kwenu…huyu binti amekuwa akitafutwa huko kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji…”
“Akh! Sasa na nyie mnakubaliana na hilo?” Mratibu alikuja juu.
“Tukubaliane nalo au tusikubaliane nalo…hili haliko ndani ya mamlaka yetu! Hawa ni askari wa Interpol ofisi ya Caracas kaka…wanafanya kazi yao. Kinachonishangaza mimi…na sisi sote hapa…ni vipi nchi yako itakisa uzalendo kiasi hiki? Mtoto anafanya vizuri namna hii ndo mnapiga simu ya kumueleleza?” Mratibu wa kamati ya Miss Venezuela alimuuliza kwa mshangao mkubwa.
Mratibu wa Miss Tanzania Hakeem Labemba aliachia mguno na kumtupia jicho la kuuliza Kokos Wandiba.
“Jamani hii ni mistake kubwa sana! Siafiki kabisa kwa miss wetu kufanyiwa kitu kama hiki…!” Alisema.
“Huafiki vipi wakati nakwambia simu imekuja kutoka kwenu huko huko?” Mwenzake wa Venezuela alimjia juu.
“Sasa haiwezekani! Mtu kashiriki mashindano toka ngazi za vitongoji, wilaya, mkoa hadi taifa na hadi kutunukiwa taji la urembo wa nchi…hakujulikana tu kuwa ana kesi ya mauaji? Ije kujulikana leo hii siku ya fainali? Tena huku ughaibuni?” Mratibu alimaka, na Kokos akawa anatikisa kichwa kwa nguvu kuafikiana na hoja zake.
“Okay, sasa ni upi mtazamo wa taratibu za miss world katika hili? Ki-polisi ni sawa, wamemuweka chini ya ulinzi Candy kwa tuhuma za mauaji…Je miss world mnasemaje juu ya hili? Mnakubaliana nalo?” Kokos aliongea kwa mara ya kwanza, akili yake ya ki-anasheria ikisukuma hisia zote binafsi pembeni, na mantiki za kianasheria zikichukua nafasi.
“Yes…mtazamo wa miss world ukoje katika hili?” Hakeem Labemba, mratibu wa kamati ya miss Tanzania alishadidia hoja ya Kokos.
“Ah, katiba ya miss world iko wazi sana katika hili…kama mrembo akikutwa na tuhuma zozote za jinai au kimaadili, basi hastahili kushiriki. Kama ana taji na tuhuma zikaibuka basi anavuliwa taji, na….” Alianza kutoa maelezo.
“Kama akikutwa na tuhuma zilizothibitika kaka…zilizothibitika!” Bishkuku alidakia na kumkatisha yule mtendaji wa miss world, na wote pale wakamgeukia.
“Tuhuma zinazotolewa kwa mrembo wangu hazijathibitika popote! Si halali kumtoa mashindanoni kwa hili!” Bishkuku alizidi kutetea hoja.
Watendaji wakatazamana.
“Samahani…huyu ni nani?” Mratibu wa miss world alihoji, akimgeukia mratibu wa miss Tanzania.
“Huyu ndiye mkufunzi wa Candy, miss Tanzania…” Hakeem Labemba alisema.
“Na anazijua sana sheria na kanuni zote za mashidano ya urembo duniani!” Kokos alidakia, na mratibu wa miss world akatikisa kichwa kukubaliana naye.
“Ni kweli…ni vile tu huyu bibie alinikatisha. Nilikuwa nataka kusema kuwa na kama mrembo atakutwa na tuhuma ambazo hazijathibitishwa kama hili lililopo hapa, basi anashauriwa kuwa ataweza kuendelea na mashindano, lakini akishinda taji na zile tuhuma zikathibishwa, basi atavuliwa taji!” Mratibu wa Miss World alisema.
“Lakini pia huwa anashauriwa amue mwenyewe, kwa hiyari yake, kujitoa mashindanoni kutokana na kukutwa na tuhuma…halazimishwi, ila busara inasema ni vyema ajitoe kuliko kusubiri kushiriki hadi mwisho halafu kuja kuvuliwa taji!” Mratibu wa miss Venezuela aliongezea, na yule wa miss world akaunga mkono hoja ile.
Dah!
“Sasa hii inatuacha kwenye maamuzi gani hapa?” Kokos aliuliza.
“Hapa kama miss world hatukubali mrembo wetu kukamatwa namna hii…hawa polisi kama wana shida na Candy wamsubiri baada ya mashindano na sio hapa!” Mratibu wa miss world alisema.
“Lakini kama ni hivyo, kwa nini waliruhusiwa kufika mpaka huku na kumchanganya mrembo wetu namna hii?” Hakeem alikuja juu.
“Hawakuruhusiwa…waliingia tu. Hawa ni polisi ujue!” Mratibu wa miss Venezuela alisema.
“Kwa hiyo?” Kokos aliuliza.
“Nitaongea na hawa askari wamsubiri Candy baada ya mashindano…” Mratibu wa Miss world alisema, na kuendelea, “…na nyinyi itabidi mumsikilize mrembo wenu iwapo atataka kuendelea na mashindano pamoja na tuhuma zilizotajwa dhidi yake, au ataamua kujitoa mwenyewe kwa hiyari yake!”
Kokos, Bishkuku na Hakeem Lubemba wakatazamana….
Mratibu wa Miss World na yule mwenzake wa Venezuela waliondoka kurudi kule jukwaani kwenye meza ya majaji kueleza kilichojiri, na Hakeem akamgeukia Bishkuku.
“Yatupasa tuongee na Candy…kamcheki kama amezinduka…” Alimwambia huku akiwa amejawa mawazo. Kokos ndio alikuwa hasemekani, kwani akili ilikuwa ikimwenda kasi kuliko ilivyowahi huko nyuma, na wasiwasi wa dhahiri ulijionesha usoni kwake.
***
Bishkuku aliingia kwenye chumba cha huduma ya kwanza, na kukuta Candy ndio anazinduka. Alibaki akimtazama huku midomo ikimcheza kwa bidii ya kuyazuia machozi kumbubujika. Alitaka aonekane imara mbele ya mrembo wake atakapoongea naye ili ampe nguvu kwa hili lililomtokea. Kulia hakutasaidia lolote katika hilo.
Candy aligeukia kule alipokuwa, na akajaribu kuinuka kutoka pale kitandani, wale watoa huduma ya kwanza wakamzuia.
“Oh, Anti Bishi…” Candy alisema kwa unyonge, na Bishkuku alivuta pumzi ndefu na kujitutumiua, kisha akamuendea kwa hatua za haraka.
“Candy, mrembo wangu…”
“Oh, Anti! Ni nini alilokuwa anasema yule askari jamani…? Mimi nimemuua…Bi. Shakira?” Candy alibwabwaja kwa taabu na kutoamini, mchirizi wa machozi ukisafiri kutoka kwenye kona ya nje ya jicho lake kuelekea usawa wa sikio lake.
“Pole sana mrembo wangu…pole sana. Hivyo ndivyo alivyosema na…” Bishkuku alimwambia huku akipiga magoti kando ya kile kitanda kidogo cha huduma ya kwanza na akimfuta ule mchirizi wa chozi, bila hata ya kujitambua.
“Na…na wewe...nyinyi…mnaamini hilo?” Candy aliuliza huku akianza kulia waziwazi.
“Noo…of course not..! Hatukuamini pale tulipoyasikia yale maneno, na hatuamini sasa hivi Candy…nahisi hili ni kosa tu limetokea…” Bishkuku alisema, na muda huo Kokos na Hakeem waliingia mle ndani baada ya kuona kuwa Bishkuku amekawia kuwapelekea majibu iwapo Candy ameamka au la.
“Kokos…Kokos niambie kuwa huamini maneno yaliyosemwa juu yangu jamani…niambie huamini lolote katika hayo!” Candy alisema kwa maombolezo, machozi yakimmwagika wazi wazi kutoka machoni mwake, na Kokos Wandiba alijikuta akibanwa na donge kubwa kooni, macho yakimchonyota kwa kitu ambacho hakutaka kukubali kuwa ni machozi.
“Never, Candy…hata kidogo…siamini asilani!” Kokos alijibu.
Candy alilia wazi wazi.
“Er, Candy…pole sana. Kwa sasa tunalotakiwa kulishughulikia ni hili lililopo mbele yetu…swala la hizo tuhuma kwa kweli naomba tuliache mpaka baada ya hatima ya haya mashindano…” Hakeem Labemba alisema.
“Noo! Lazima kila kitu kieleweka kaka Hakeem…mi sikumuua huyo mtu jamani…mtu kuua mjusi tu kwangu mtihani…leo nije kuua mtu? Tena mtu mwenyewe mkubwa kama yule? N’taweza wapi miye?” Candy alisema kwa maombolezi na wote pale wakamakinika.
“Ina maana umanjua huyo Bi. Shakira?” Waliuliza kwa pamoja, maneno yao yakitofautiana kidogo lakini ujumbe wa swali lao ulikuwa ni huo huo.
Candy alilia kwa uchungu huku akitikisa kichwa kuafiki kuwa ni kweli alikuwa akimfahamu huyo mtu aliyeshutumiwa kumuua.
Kwa mara nyingine, akina Bishkuku walitazamana…
***
Huku mbele kamati nzima ya Miss World ilikutana kwa dharura kujadili swala lililotokea kwa mshindani kutoka Tanzania. Kufanyika kwa kikao kile cha dharura kulisababisha ratiba ya mashidano yale isogezwe mbele kidogo, na badala ya wale warembo watano waliotinga fainali kurudi jukwaani kutahiniwa kwa mara ya mwisho, ziliendelea burudani za mfululizo.
Maamuzi yakapitishwa.
Mrembo kutoka Tanzania apewe nafasi ya kujitoa mashindanoni na abaki na taji lake la Miss Photogenic…na iwapo hatataka kufanya hivyo, basi aendelee na mashindano kama kawaida ila kwanza asalimishe taji lake la miss Photogenic hadi baada ya mashindano. Na iwapo atatokea kuwa mshindi, basi kuna kifungu miongoni kwa vifungu vya katiba ya Miss World inayotoa mamlaka kwa kamati ya Miss world kulizuia taji mpaka hapo uhakika wa tuhuma zake utahapopatikana…kama ataonekana hana hatia atapewa taji lake, na kama akikutwa na hatia kwenye tuhuma hizo, taji linaenda kwa mshindi wa pili.
Ni utaratibu ambao wajumbe wote wa kamati ile hawakuupenda asilani, kwani ulikuwa unaliweka rehani taji la mrembo wa dunia mpaka hapo tuhuma za mrembo husika zitakapothibitika…nalo pia linaleta mashinikizo yasiyo na lazima. Iwapo mrembo atashinda kesi na upande wa mashitaka ukakata rufaa, ni kwamba taji bado litaendelea kuning’inia hewani tu mpaka hapo hukumu ya rufaa itakapopatikana.
Hakika ulikuwa ni utaratibu ambao si yeyote katika wajumbe wa kamati ile aliyeupenda. Lakini ndio katiba isemavyo na ilibidi ifuatwe.
Kwa kutaka kuleta haki na usawa katika maamuzi, wale majaji wote hawakushirikishwa katika kikao kile na wala hawakujulishwa juu ya kile kilichokuwa kimetokea kule nyuma ya jukwaa.
Majaji walipaswa wafanye kazi yao bila shinikizo wala kuwa na taarifa yoyote itakayoathiri maamuzi yao…
“Okay, na tukasikie basi maamuzi ya miss Candy juu ya hili!” Mwenyekiti wa ile kamati alisema na wajumbe wakarudi kwenye nafasi zao kule mbele ya jukwaa, wakati yule mratibu wa Miss World na yule wa Miss Venezuela wakirudi tena kule nyuma ya jukwaa kusikia maamuzi ya Candy…
***
“Ah, basi mi’ najitoa mashindanoni…siwezi kuendelea na hili jamani. Ni wazi kuwa tangu mwanzo nimekuwa nikukumbwa na vikwazo vya kila namna katika ushiriki wangu…I am sorry…siwezi kuendelea jamani…bora tu nijitoe!” Candy alisema kwa huzuni na simanzi na wote mle ndani wakabaki wameduwaa.
“Anasema nini huyo?” Mratibu wa Miss World aliuliza, kwani Candy aliongea kwa kiswahili, na Hakeem akamtafsiria.
Yeye na yule mwenzake wa kamati ya Miss Venezuela walitazamana.
“Okay, nadhani hivyo ndo itakavyokuwa…ni uamuzi wa busara kwa kweli…na unapunguza mashaka mengi kwenye shindano hili!” Mratibu wa Miss World alisema, na wawakilishi kutoka Tanzania walitazamana.
“No! Naomba tusubiri kwanza…Candy amehamanika tu. Nadhani tunahitaji kuongea naye zaidi juu ya hili!” Bishkuku aliwaambia.
“Kuna nini cha kuongea wakati tayari ameshaelezwa kila kitu, na amepewa maamuzi yaliyo wazi kwake…naye ameamua hivyo?” Mratibu wa Miss World alisema.
“Sawa…tunahitaji kujihakikishia kuwa hili ndilo hasa analotaka wazee…huyu ameogopa sana, sidhani kama ameamua kwa busara katika hili!” Bishkuku alisema. Mratibu wa Miss World alitaka kupingana naye zaidi, lakini akajizuia. Akabaki akitikisa kichwa.
“Jamani…haya mambo yana tabia ya kuja na madhara ya baadaye…” Kokos alidakia, na kuendelea, “…naamini hatuwezi kufanyia kazi maamuzi ya mdomo tu kutoka kwa Candy…vipi iwapo tutaamua kumtoa Candy kutokana na kauli yake hii, halafu baadaye akasema kuwa hakuwa katika akili timamu wakati anaamua hivi, na kwamba alipata shinikizo kutoka kwa waandaaji wa miss World kuwa ajitoe?”
Macho yaliwatembea waratibu wa mashindano yale waliokuwa pamoja nao mle ndani.
“Mi nadhani si busara kwangu kuendelea katika hali kwa hali kama hii jamani…” Candy alidakia.
“Hebu nyamanza kwanza wewe!” Bishkuku alimkemea.
Hakeem Labemba akawageukia wake waratibu wenzake.
“Jamani naomba tumpe muda Candy kama Bishkuku alivyoomba…”
“Muda kiasi gani? Tayari ratiba imeshachelewa kiasi cha kutosha!”
“Muda wa kutosha wewe kwenda kule na kuandaa maandishi kuwa Candy, kwa hiyari yake mwenyewe anajitoa kwenye mashindano haya…ukishamaliza kuandaa maandiko hayo na kuyaleta hapa, Candy atakuwa kishapitisha uamuzi. Na kama bado anataka kujitoa atasaini nanyi mtaendelea. Iwapo ataamua vinginevyo, maandishi yatachanwa na Candy atarudi jukwaani. Hapo vipi?” Kokos alidakia na kutoa pendekezo.
“Fair enough! Una muda mpaka nitakapokuletea hayo maandishi ya kusaini kufanya maamuzi!” Mratibu wa Miss World alimwambia Bishkuku, na kutoka nje ya chumba kile akifuatiwa na yule mwenzake wa Venezuela.
“Tupisheni humu ndani!” Bishkuku aliwaambia Hakeem na Kokos.
“Ah, sasa si sote tuko pamoja katika hili…?” Hakeem alipinga hoja.
“Tupisheni!” Bishkuku alifoka, Hakeem na Kokos wakatazamana. Kokos akamuashiria mwenzake kuwa waende nje kama walivyotakiwa.
Wakatoka.
Bishkuku akamgeukia Candy aliyekuwa amejiinamia.
“Candy, ntakubaliana na uamuzi wako huo iwapo utanijibu hili kwa ukweli…” Bishkuku alimwambia huku akiwa amemshika mabega na akimtazama moja kwa moja machoni.
“Ni kweli umemuua huyo mtu…Bi. Shakira?” Alimuuliza.
“No! Sijamuua mimi huyo mtu, na…”
“Basi hujitoi kwenye mashindano Candy! Endelea na mashindano upate kile ambacho Mungu amekuandalia katika hili...kama ni kutwaa taji, basi nenda kalitwae, kama ni ushindi wa pili, nenda kauchukue, na kama ni wa tatu pia nenda kauchulue…usijihalalishie ushindwaji kirahisi namna hii wakati we’ una kila kigezo cha kuwa mshindi Candy!”
“Hapana anti Bishi…nitawezaje kuendelea wakati kuna shutuma kama hizi dhidi yangu?”
“Na vipi ikija kuthibitika kuwa ulisingiziwa tu na tuhuma hizi si za kweli? Utaita tena shindano lirudiwe ili umalizie ushiriki wako? Usiwe mjinga Candy…hii ni nafasi yako pekee ya kuionesha dunia kuwa una uwezo wa kutwaa taji la urembo wa dunia, ni nafasi isiyorudi mara mbili duniani!” Bishkuku alizidi kumwambia.
“Lakini kwa mtindo huu Bishkuku? Nitakuwa mrembo gani mwenye tuhuma mbaya kama hizi?”
“Kuna warembo kibao waliokumbwa na kashfa na tuhuma mbali mbali kabla yako Candy, hivyo we’ huwezi kuwa wa kwanza…Marjorie Wallace, Miss World wa mwaka sabini na tatu, alikuja kuvuliwa taji hilo kwa kuwa na mahusiano na watu maarufu duniani kiasi cha kulitia doa taji alilopewa, alivuliwa taji lakini kwa umaarufu aliokwisha upata kutokana na taji lile, aliishia kuwa mtangazaji maarufu sana runinga huko kwao..” Bishkuku alimwambia.
“Ah Bishkuku, lakini…”
“Hamna cha lakini mdogo wangu! Pia kuna Vanessa Williams, ambaye najua unamfahamu sana. Yeye alivuliwa taji lake la Miss Amerika alilobeba mwaka themanini na tatu baada ya picha zake za utupu kutokea kwenye moja ya magazeti ya udaku huko kwao, lakini tazama alipo sasa…nyimbo ngapi kaimba, filamu ngapi kacheza, utajiri kiasi gani alio nao hivi sasa! Yote hayo ni kutokana na kushinda kwake taji lile la Miss Amerika, japo alikua kuvuliwa baadaye…sasa wewe unataka kujitoa kibwege tu hapa?”
“Dah ni kweli anti Bishi, lakini tuhuma za mauaji?”
“Ambazo si za kweli!” Bishkuku alimkatisha, na kuendelea, “Kuna warembo wengine wengi tu Candy waliokumbwa na tuhuma na kashfa mbalimbali…wenzako hao wote walishiriki na kushinda walichoshinda…na hata walipokuja kuvuliwa hayo mataji, tayari majina yao yalikuwa yameshaingia kwenye historia na yanabaki hapo! Usiwe mjinga Candy…tuhuma ni tuhuma tu mpaka zithibitishwe kwenye mahakama. Na ukiwa na taji ni kwamba unalo tu mpaka ithibitike kuwa hulistahili kutokana na tuhuma!”
Candy alibaki akilia kwa uchungu.
“Mbona ninakumbwa na majaribu mazito miye jamani…?” Aliomboleza kwa uchungu.
Muda huo mratibu wa Miss world aliingia na maandishi yaliyojieleza kuwa Candy Gamasala anajitoa kwa hiyari yake kwenye mashindano yale kutokana na tuhuma zilizowasilishwa dhidi yake kutoka nchini kwake, Tanzania.
“Okay, kama mko tayari, tunaomba Candy atusainie hapa ili shindano liendelee…” Aliwaambia huku akimkabidhi Bishkuku ile karatasi.
“Bado kidogo…” Bishluku alimwambia.
“Hatutakuwa na muda wa kusubiri zaidi…watu wameshaanza kuuliza kulikoni huko. Hatutaki skendo zisizo na msingi. Mi’ narudi jukwaani kutoa idhini warembo wapande jukwaani kumalizia shindano. Wakakarudi jukwani ndio hao hao watakaoshiriki, maelezo ya kwa nini Candy hakurudi jukwaani kuendelea yatatolewa huko huko!” Jamaa alimjibu na kutoka, akimwacha Bishkuku akiitazama ile karatasi ambayo Candy alitakiwa aisaini.
Kokos na Hakeem wakarudi mle ndani.
“Imekuwaje?” Waliuliza kwa wahka.
Bishkuku alitikisa kichwa huku akiwaonesha ile karatasi iliyoletwa kwa ajili ya saini ya Candy.
“Oh, shit!” Hakeem alilaani na kumgeikia Candy.
“Naiomba hiyo karatasi…” Candy alisema kwa unyonge.
Wote walitazamana, na kwa mashaka Bishkuku akampa ile karatasi…
***
Ukumbi ulilipuka kwa hoi hoi na nderemo pale warembo waliobakia kwenye fainali zile hatimaye walipojitokeza tena pale jukwaani kukabiliana na majaji kwamara ya mwisho. Walitoka mmoja baada ya mwingine, wakifuatisha midundo ya muziki maalum, na kwenda kusimama kilimbwende mbele ya majaji na watazamaji, kama ilivyo ada.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitoka wa kwanza hadi wanne na kubaki wakiwa wamesimama pale jukwaani ilhali mshindani wa tano akiwa hajatokea.
Candy hakurudi jukwaani.
Mdundo uliendelea kwa muda lakini mrembo wa tano hakutokea pale mbele. Watazamaji wakaanza kuulizana ilhali huku nyumbani watanzania waliokuwa wamekodolea runinga zao nao walianza kuulizana ni kwa nini mrembo wao alikuwa haonekani pale jukwaani.
Msema chochote alirudi jukwaani, na kuanza kumuita Candy jukwaani, wazi kuwa hakujua kilichokuwakimetokea, na alipokuwa hapati jibu alinadi kuwa atahitaji maelekezo kutoka kwa kamati ya miss world na majaji juu ya kutokuwepo kwa mshindani Candy pale jukwaani wakati ule.
Hapo ukumbi uliamka kwa kelele zisizoeleweka, baadhi wakipiga mbinja nyingi kulaani jambo lile, ikiwa ni namna yao ya kuonesha kutoridhika kwao na hali ile…
***
Jijini Dar, GTZ na nduguye wa kufikia wakatazamana.
“Mtoto kaingia mitini huko huko nini?” GTZ aliuliza kwamashaka.
“Mhn! Kwa ujanja gani…? Atakuwa ana tatizo jingine tu huyo ila hawezi kuwa amezamia huko!” Greg Pasha alimjibu.
Wakati huo huo Nuru naye kutokea sehemu nyingine ya jiji akamwita Morandi kwa wahka, ambaye alikuwa ameingia chumbani kufuatilia mechi ya mpira iliyokuwa ikiendelea kwa kutumia runinga ya huko chumbani.
“Nini wewe lakini?” Morandi aliitika kwa kukereka huku akirudipale sebuleni.
“Candy hajarudi ukumbini kumalizia shindano aisee…! Mi’ nakwambia moyo wangu una mashaka kweli kweli Mo!” Nuru alimwambia, na Morandi akawa makini na hali ile. Aliwatazama wale warembo wanne waliojipanga pale mbele ya jukwaa na wakati huo akimuona mratibu wa shindano la miss world akipanda pale jukwaani huku akiwa amenyoosha mkono kupokea kipaza sauti kutoka kwa msema chochote…
“Ah! Kuna nini tena huko kimejiri sasa?” Aliuliza kwamashaka, na Nuru akaishia kutikisa kichwa huku moyo ukimwenda mbio, akitazama kile kilichokuwakikiendelea kule ukumbini, kilometa nyingi sana kutoka pale walipokuwa usiku ule…
Sehemu nyingine ya jiji, Ngamao Kijambia na mkuu wake wa kazi wa muda wlaitazamana, uelewa wa kile walichokifanya ukipita baina yao bila ya kusema lolote.
***
Mwakilishi wa miss world alishika kipaza sauti.
“Er, samahani…nadhani natakiwa kutoa maelezo kidogo kuhusuana na…” Alianzakuongea, lakini alikatishwa namlipuko wa shangwe pale ukumbini huku baadhi ya watazamaji wakipigamakofi. Alishangaana kugeuka nyuma kwa uso uliojaa viulizo, na kumuona Candy Gamasala, mshindani kutoka Tanzania akiingia pale ukumbini kutokea kule nyuma ya jukwaa. Mara mojawatumbuizaji wakaanza kumpigia ule muziki ambao wenzake waliingia nao pale jukwaani, naye bila kulazimisha akaanza kunata na midundo ile huku akiwaendea wale wenzake waliokuwa wamesimama pale mbele ya majaji na watazamaji.
Na wakati akiwaendea wale wenzake pale jukwaani huku usoni akiwa ameweka lile tabasamu lake lililompatia sifa ya miss photogenic, hakuna yeyote miongoni mwa watazamaji pale ukumbini wakati ule, ambaye angeweza kujua kuwa muda mfupi tu uliopitayule binti alikuwa akilia kwa tumaini lililopotea, na uso ule uliojaa tabasamu liliwakongwa wengi katika safari yake ile ndefu ya kulisaka taji la urembo wa dunia, ilikuwa imesawajika kwa huzuni na masahibu mazito kabisa.
Makofi yalikuwa yakiambatana na Candy wakati akiwasogelea wale wenzake pale jukwaani.
“…kama nilivyokuwa nataka kusema…miss Candy kutoka Tanzania alipatwa na tatizo kidogo ambalo labda lingesababisha ashindwe kuendelea na mashindano…lakini sasa naona ameshakuwa sawa na tutakuwa naye kwenye fainali hizi za kipekee kabisa za urembo duniani!” Mwakilishi wa miss world alilazimika kuunga maneno pale pale jukwaani, na kwa mara nyingine ukumbi ukalipuka kwa shangwe na hoi hoi.
Ilikuwa ni kama kwamba Candy ndio katangazwa mshindi…
Nyuma ya jukwaa, Bishkuku alipiga magoti na kulia kwa uchungu, akikumbuka jinsi alivyolazimika kutumia nguvu za ziada kumshawishi yule binti kurudi jukwani, na jinsi walivyolazimika kumbadili nguo na kuremba mrembo wao haraka haraka kujaribu kuwahi kule jukwaani kabla shindano halijaendelea.
Kokos Wandiba na Hakeem Labemba waliachia mihemko ya ahueni kutokea kwenye viti vyao kule mbele, Labemba akijifuta chozi lililokuwa likimbubujika kwa siri akitumai kuwa Kokos hajamuona.
Kokos naye alikuwa bize kufuta machozi yake akitumai kuwa Labemba hajamuona.
Kule jukwaani hatua ya fainali iliaza kwa warembo kuanza kupigwa maswali mengine na majaji, na jijini Dar, Ngamao na yule bosi wake wa muda walibaki wakitumbuliana macho kwa kutoelewa…
***
Warembo walipigwa maswali mengine matatu, kisha wakatakiwa kutoa maelezo ya namna watakavyoziwakilisha nchi zao iwapo yeyote kati yao ataibuka kuwa mrembo wa dunia.
Hakuna aliyechemka, kwani ile ilikuwa ni hatua muhimu sana kwa kila mmoja wao, na wote walidhamiria kutofanya makosa. Lakini kati yao, ni Candy ndiye aliyekuwa kwenye wakati mgumu kwani alilazimika kujisahaulisha balaa lililokuwa likimsubiri baada ya shindano lile, na kinyume na kawaida aliyoionesha katika hatua za mwanzo za mashindano yale, mara mbili alilazimika kumuomba jaji aliyekuwa akimuuliza swali arudie swali ili alielewe vizuri kabla ya kulijibu, kwani wazo la kuwa ametuhumiwa kumuua Bi. Shakira Swadafu lilikuwa likimuwekea uzito mkubwa sana akilini mwake.
Burudani za matumbuizo zilipunguzwa sana, kwani tayari shindano lilikuwa limeshachelewa, hivyo baada ya washindani wote kutimiza hatua zilizohitajika waliruhusiwa kurudi nyuma ya jukwaa na kuwaachia majaji kazi ya kuchuja na kuchambua ili hatimaye mrembo wa dunia apatikane.
Warembo walirudi nyuma ya jukwaa, na huku nyumbani baadhi ya watu walikuwa wakisali mbele ya runinga zao ili mwakilishi wa taifa apite katika mchujo ule wa mwisho na aweze kuwaletea watanzania taji la urembo wa dunia kwa mara ya kwanza, pamoja nalo zikiwa ni fursa kemkem za kitalii kwa taifa kutokana na kufanikiwa kutoa mrembo wa dunia.
Kule Tarime kwenye ile nyumba ya kulelea watoto yatima, msimamizi wa kituo alikuwa amepiga magoti na watoto wake wakiomba kwa manani awatimizie ndoto yao ya kufanikiwa kupata mrembo sio tu wa taifa, bali pia wa dunia, kutoka miongoni mwao.
Ilikuwa ni wahka kila kona ya dunia wakati ule, hususan katika zile nchi tano ambazo wawakilishi wao walikuwa wamerudi nyuma ya jukwaa usiku ule kusuburi maamuzi ya majaji.
***
“Umefanya vizuri mpaka sasa mrembo wangu! Umefanya vizuri sana! Nakwambia huko majaji wafanye kazi ya ziada kukunyima taji leo!” Bishkuku alimpokea Candy kwa bashasha kule nyuma.
“Dah! Si mchezo Candy, we kichwa! Yaani sikutegemea kuwa baada ya yote haya ungeweza kutoa ushiriki hai namna ile!” Yule binti kutoka kamati ya Miss Tanzania naye alimpongeza huku akimpigapiga mgongoni.
“Lah! Jamani hakika sikuwa na umakini ambao ningeutaka kwa kweli…kwa upande wangu hata sijui nilikuwa naongea vitu gani kule mbele…” Candy aliwajibu kwa fadhaa.
“Wala usijiumize moyo Candy…ulifanya vilivyo ndivyo! Ulipoona hukuelewa swali uliuliza badala ya kukurupuka tu na jibu la ajabu –ajabu na hilo ni safi sana! Yaani mbona uko kwenye nafasi nzuri tu kisura?”Bishkuku alimwambia.
“Mnh! Hizi shutuma nilizopewa zimenikata maini sana Anti…yaani hata sina msisimko wa mashindano tena…”
“Acha hizo! Shutuma mahala pake ni baada ya mashindano Candy, na mashindano wakati wake ni sasa hivi! So, tukabiliane na hili la sasa hivi kwanza! Uko vizuri na utafanya vizuri ukiendelea kujiaminisha kama hivyo…”
“Hakuna tena cha kujiaminisha anti…sasa tunasubiri matokeo tu!Kama nimeboronga au vipi, ndio imeshakuwa tena…nimeshatupa karata zangu zote sasa!”Candy alimwambia.
“Na lazima nikwambie kuwa umezitupa vizuri sana, pamoja na masahibu yaliyotokea…” Binti wa kamati ya Miss Tanzania alisema.
“Ah, basi na tusubiri…” Candy alisema huku akijilaza kifuani kwa Bishkuku, ambaye alimkumbatia kwa upendo na majivuno ya hali ya juu.
Nilisema kuwa nitaingiza mrembo wa kweli miss World…nilisema!
Alijiwazia kwa faraja akiwa amemkumbatia mrembo wake namna ile.
Muda wa kusuburi ulionekana kuwa ni mrefu kuliko kawaida, lakini hatimaye warembo waliitwa tena kule jukwaani kusikia maamuzi ya majaji.
***
Candy alisimama kilimbwende pamoja na warembo wenzake wanne, tayari kusikia hatima ya mpambano ule. Ukumbi ulikuwa kimya sana, lakini kama bashasha ingekuwa inashikika, basi mtu angejikusanyia bashasha za kujaza malori na malori pale ukumbini usiku ule. Watazamaji walikuwa wana hamu ya kumjua mrembo wa dunia ajaye, wengi wao wakiwa tayari wameshampitisha ambaye wao walimuona kuwa anafaa kuwa mrembo, na sasa walikuwa na bashasha ya kujua iwapo na majaji nao watakuwa wameona kama walivyoona wao, au wamekuwa na maoni tofauti, ili wapate kuuliza sababu ni nini, kama kwamba watakuwa na fursa ya kufanya hivyo.
Mwakilishi wa Miss World alipanda juikwaani akiwa na mkuu wa sakafu wa shindano lile usiku ule, pamoja nao akiwa mmoja wa majaji wa shindano lile.
“Oh-oo…hii nini sasa? Sio kawaida hii!” Hakeem Labemba alimnong’oneza Kokos Wandiba huku akijiweka sawa pale kitini kwake.
“Kivipi tena…mbo’ un’taka kunipa presha tena saa hizi ‘aloo?” Kokos alimuuliza.
“Ah, wale sio watoaji matokeo ya urembo wale…sio itifaki ile bwana…hapa kuna kitu tu, lakini sio kututangazia…” Hakeem alimjibu, lakini hapo alikatishwa na msemaji kule jukwaani.
“Er, mabibi na mabwana. Tumekutwa na tukio ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi sana katika historia ya mashindano haya ya urembo wa dunia…” Mwakilishi wa miss world alinadi, na ukumbi ukaachia mguno wa pamoja, kila mtu akiwa hakutegemea kusikia maneno yale.
“…na kueleza kile kilichotokea, naomba nimkaribishe mwenyekiti wa jopo la majaji wa shindano hili ili aweke wazi…” Mwakilishi wa Miss World alisema na kumpisha yule mtu aliyetajwa kuwa ni mwenyekiti wa jopo la majaji. Alikuwa ni mwanamama mwenye asili ya ki-ethiopia ingawa mwenyewe alikuwa ana uraia wa Sweden.
“Er, mpaka sasa jopo la majaji limeshakubaliana kuhusu mshindi wa tatu wa mashindano haya…” Mwanamama aliongea, na ukumbi ukabaki ukiwa kimya kabisa, “…ila tunasikitika kusema kuwa tumeshindwa kukubaliana kwa pamoja kuhusu washindi wa pili na wa kwanza….kuna mfungano baina ya majaji ambapo kuna wanaodhani mmoja kati ya hawa mabinti walio mbele yetu hapa ndiye anayepaswa kuvalishwa taji usiku huu, na mwingine awe mshindi wa pili. Lakini pia kuna upande mwingine wa majaji unaodhani kuwa huyo anayesemekana kuwa awe namba mbili ndiye haswa anayepaswa kuwa namba moja!” Alimalizia maelezo yake na ukumbi ukaamka kwa minong’ono mingi ambayo haraka ilipanda na kuwa zogo la gumzo miongoni mwa watazamaji.
Kokos na Hakeem walitazamana, na kule nyuma ya jukwaa, Bishkuku na binti kutoka kamati ya Miss Tanzania nao wakatazamana.
“Candy kazua balaa huko nakwambia!” Bishkuku alisema kwa kutoamini.
Kule jukwaani msema chochote alijitajidi kuwatuliza watazamaji, na alipofanikiwa msemaji wa majaji akaendelea.
“Hivyo basi, majaji wanaomba nusu saa zaidi kupitia upya kumbukumbu zao za mashindano haya ili hatimaye wapate kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu ni nani awe miss world wetu mwaka huu, na nani awe mshindi wa pili. Narudia tena…kuhusu mshindi wa tatu hakuna mjadala. Ameshajulikana lakini hatotangazwa mpaka muafaka ufikiwe kuhusu namba moja na namba mbili. Ahsanteni!” Alimalizia na hapo hapo alianza kurudi kule alipotoka akifuatiwa na wale viongozi wengine wa mashindano yale, wakati ukumbi ukipoteza nidhamu kabisa kwa minong’ono ya sauti.
Kwa mara ya pili, warembo walirudi nyuma ya jukwaa wakiwa na wahka zaidi, sasa kila mmoja akijiuliza iwapo yeye ndiye huyo mshindi wa tatu, na akitamani isiwe hivyo.
Wakati warembo wakirudi nyuma ya jukwaa na burudani ya muziki ikianza kutumbuiza pale ukumbini, mwakilishi wa kamati ya miss world aliitwa kwenye chumba cha majaji. Mwakilishi aliingia ndani ya kile chumba na kuketi kwenye kiti alichoelekezwa na mwenyekiti wa jopo la majaji.
“Tumekwita hapa mwakilishi wa miss world ili utupatie taarifa ambazo tunadhani kwa sasa ni muhimu sana kwetu kutuwezesha kufanya kazi yetu…” Mwenyekiti wa jopo alimwambia, na wale majajiwengine wakawa wanatikisa vichwa kuafikiana na hoja ile.
Mwakilishi wa kamati ya miss world alizungusha macho yake kwa wale majaji huku akilini akihisi kuwa alikuwa anajua ni nini wale watu walikuwa wanataka kutoka kwake.
Alibaki kimya akisubiri kuambiwa hicho ambacho wale majaji waliobobea katika shughuli waliyoteuliwa kuifanya walikuwa wanataka kumuuliza.
“Ni kitu gani kilichosababisha mrembo Candy achelewe kurudi jukwaani kuendelea na shindano?” Mwenyekiti wa jopo alimuuliza, na mwakilishi wa miss world alifumba macho kwa kusikitishwa na lile swali alilokuwa akilihofia kutoka kwa wale majaji.
“Sidhani kama hilo ni la muhimu kwa sasa ndugu zangu, kwa sababu Candy ameshiriki shindano mpaka mwisho…kwa hiyo…”Alianza kuwajibu.Akakatishwa.
“Lakini alichelewa…alichelewesha shindano kuendelea kwa muda mrefu bila ya maelezo yoyote!”
“Bila ya maelezo kwa nani? Mimi mwakilishi wa miss world na mkuu wa sakafu tulikuwa tuna taarifa ya kuchelewa kwake, na tulitoa ruhusa asubiriwe kwa muda maalum.Aliwahi kurudi jukwaani ndani ya muda na hivyo kila kitu ambacho kingekuwa dhidi yake kwa kutorudi jukwani kwa wakati kilifutika!” Mwakilishi wa miss world, raia wa Uingereza, alijibu kwa kujiamini.
“Sasa hapa tunahitaji kufanya maamuzi baina ya watu wawili ambao tunaona wako sawa kwa takriban kila kitu…tunatafuta makosa kutoka kwakila mmoja ili tuweze angalau kupata mshindi…Candy tayari ameshatia doa…”
“Doa gani?Kivipi?”
“Si ndio tunataka utueleze kilichojiri kule nyuma ya jukwaa hadi ikawa almanusra ashindwe kurejea jukwaani?” Mmoja wa majaji alimjia juu.
“Na vipi kama alikuwa amepatwa na ugonjwa wa ghafla huko nyuma? Bado hilo linakuwa ni doa la kumpunguzia sifa na maksi?” Mwakilishi naye aliwajia juu majaji.
“Kwa hiyo unatuthibitishia kuwa alikumbwana ugonjwa kwa ndio maana akachelewa kurudi jukwaani?”Jaji mwingine akambana zaidi.
Mwakilishi alishindwa kusema uongo. Akabaki akitafuna midomo kwa hasira huku akitazama pembeni.
“Sisi sio wajinga bwana. Tumeona kundi la askari likienda nyuma ya jukwaa dakika chache kabla ya shindano kuendelea…na baada ya hapo ndio Candy akachelewa kurudi jukwaani…nini kilikuwa kinatokea huko nyuma?” Mwenyekiti wa jopo la majaji alizidi kumbana mwakilishi.
“Ninachojua ni kwamba chochote kilichotokea nyuma ya jukwaa hakina msingi wowote kwenye maamuzi yenu. Fanyeni maamuzi kwakufuata vigezo vya mashindano na kwa mujibu wa namna mabinti walivyojituma kule jukwaani…msitafute njia ya mkato hapa!”
“Bado tuna haki ya kutafuta taarifa za ziada katika maamuzi kwenye hali kama hii…na wewe unalijua hilo!” Jaji mwingine alimchachamalia.
“Sawa. Na kanuni inasema kama nikiona kuwa inastahili kutoa hiyo taarifa bila kumuathiri waziwazi mshiriki yeyote! Sasa mimi sioni kama ni sawa kueleza kile kilichotokea nyuma ya jukwaa huku nikijua wazi kuwa mnataka kukitumia kwa ajili ya kupitisha maamuzi ambayo bila ya kuwepo kwa hilo tukio la nyuma ya jukwaa ingewabidi muyapitishe tu. Ina maana kama Candy asingechelewa kurudi jukwaani mngesema kuwa mmeshindwa kupata mshindi kabisa?” Jamaa naye alichachamaa.
Majaji wakatazamana.
“Hutoi ushirikiano asilani wewe!” Mwenyekiti wa jopo alilalama.
“Ushirikiano wangu katika hali hii ni kushauri.Nashauri mfuate taratibu za ujaji katika hili!”Jamaa naye alisimamia msimamo wake.
“Tunaingiza kwenye kumbukumbu kuwa hukutoa ushirikiano utakiwao kwa majaji katika hili…na matokeo yoyote yatakayotoka, na kitakachofuata baada ya matokeo ni juu yako!” Mwenyekiti wa jopo alimjia juu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi najua taratibu zilivyo jamani. Matokeo yote ni dhima yenu majaji…msitake kunibebesha msalaba wenu!Taratibu na kanuni zetu za shindano la miss world zinanizuia kutoa taarifa iliyo nje ya vigezo vilivyokubalika katika mashindano…na ambayo najua wazi kuwa inataka kutumika kupitisha maamuzi muhimu kama haya!”
Dah!
Kimya kilitanda mle ndani.
“Sasa naweza kwenda? Shindano linazidi kuchelewa huko…” Mwakilishi wa Miss World aliuliza alipoona kimya kinazidi.
“Okay...unaweza kwenda. Tunaingiza kwenye kumbukumbu yote haya!” Mwenyekiti wa jopo la majaji alisema.
Mwakilishi alitoka nje ya chumba kile akiwa amefura kwa hasira.
***
Ukumbi ulikuwa umewiva karibu ya kutumbuka kwa wahka na bashasha wakati msafara wa walioteuliwa kunadi washindi wa shindano ukipanda jukwaani kiasi cha dakika kumi na tano baada ya mwakilishi wa miss world kutoka kwenye chumba cha majaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Miss World alipanda na kutoa hotuba yake, akiishukuru sana serikali ya Venezuela kwa kukubali kuendelea na uenyeji wa mashindano yale ilhali wakiwa kwenye kipindi kigumu kabisa cha kuuguliwa na raisi wa nchi yao, wanayempenda sana.
Kwisha kusema hayo, msema chochote aliwakaribisha wale mabinti watano waliotinga fainali, nao wakaingia ukumbini pale kwa mdundo maalum ambao walikuwa wakiufuata kwa namna ya shoo ya kukata kwa shoka. Ukumbi ulisimama kwa heshima huku wakiwapigia makofi wale mabinti kufuata midundo ya ule wimbo waliokuwa wakiingia nao, kisha mabinti wakajipanga kilimbwende mbele ya hadhira, kusubiri hatima yao.
Msema chochote akawakaribisha jukwaani mwigizaji sinema maarufu wa kike kutoka pale Venezuela, na mwimbaji maarufu zaidi wa kiume kwa miondoko ya R&B kutoka marekani ili kuwanadi washindi wa shindano lile lililoziweka juu roho sio tu za washindani wenyewe, bali pia za watazamaji na hata waandaaji wa shindano lile kubwa kabisa la urembo duniani.
Akiwa amesimama pale jukwaani mbele ya maelfu na maelfu ya watazamaji kutoka kila kona ya dunia, Candy Gamasala alikuwa amejawa na wahka uliotokana na mchanganyiko wa hisia…zile za kuwa hatimaye alikuwa amesimama kwenye kizingiti cha kunyakua taji la urembo wa dunia, na zile za fadhaa ya kadhia iliyokuwa ikimsubiri nyuma ya jukwaa usiku ule.
Hakika niko kwenye vizingiti viwili hapa Candy miye leo hii…cha mlango wa gereza, na cha mlango wa umalkia wa urembo wa dunia…n’taangukia mlango upi sasa? EeMungu nisaidie miye!
Alijiwazia huku moyo ukimwenda mbio, na bila kupenda alijikuta akipeleka macho kule kwa watazamaji. Alifarijika kuona kuwa sasa Bishkuku na yule binti kutoka kamati ya Miss Tanzania walikuwa pale mbele pamoja na akina Kokos…
Pale mbele, yule mwanadada wa ki-Venezuela alianza kuongea na ukumbi wote ukawa kimya kabisa.
Candy nawale warembo wenzake wakamakinika, wakiwa na wahka, kila mmoja akilia na hatima yake.
“Mabibi na mabwana…inanipa furaha kubwa kufungua bahasha yenye jina la mshindi wa tatu wamashindano haya…” Yule mwanadada alisema huku akiifungua bahasha aliyokabidhiwa na mmoja wa watendaji wa kamati ya miss world, alitazama kilichiandikwa ndani ya bahasha ile na kuachia mguno wa kishabiki.
“Woooh…na sasa naomba mwenzangu hapa atutangazie mshindi wa tatu wa shindano hili…” Alisema na kumkabidhi yule mwanamuziki maarufu kutoka marekani, ambaye aliipokea ile kadi yenye jina.
“Naye si mwingine bali ni…Miss India!” Jamaa alinadi na ukumbi ukalipuka kwa hoi hoi na nderemo, Candy akishusha pumzi za ahueni, huku muziki maaum ukisindikiza shangwe zile. Miss India alitoka mbele na kuvishwa utepe wake na kukabidhiwa shada la maua kisha akaenda kusimama pembeni ya kiti ambacho malkia wa urembo wa dunia atakaadakika chache tu ambazo zingefuata.
Shangwe zilirindima, zikafifia, na msema chochote akawakaribisha tena wale waalikwa maalum kwa shughuli ile wamtaje mshindi wa pili wa shindano lile. Ukumbi ukawa kimya kabisa, wakati Candy na wale warembo watatu aliobakia nao wakiwa wanajitahidi kuzuia moyo yao isichomoke nje ya vinywa vyao kwa wahka.
“Ni furaha kubwa kabisa kumtangaza mshindi wa pili wa mashindano haya mabibi na mabwana, naye si mwingine bali ni…” Yule mwimbaji R&B kutoka marekani alinadi na kumpatia kadi yule muigizajii kutoka Venezuela ili amnadi mshindi wa pili.
“Miss Tanzania, na miss photogenic… CANDY GAMASALAAA!”
Mguno wa pamoja ulizagaa ukumbini, ukiambataa na shangwe za haoa na pale, wakati Candy akiachia kilio cha furaha na mchanganyiko wa kutoamini pale alipojitokeza mbele akiwapungia watazamaji huku akipigiwa mdundo wa kumpongeza.
Makofi ya pongezi yalirindima ukumbini huku minong’ono pia ikisikika, mbinja za aidha kupongeza au kutofurahishwa na uteuzi yule zikizagaa ukumbini.
Bishkuku na Kokos walikumbatiana kule kwa watazamaji pamoja na wale watendaji wa kamati ya miss Tanzania.
“Ah, taji lilikuwa letu hili Kokos…lilikuwa letu kabisa nakwambia!” Bishkuku alisema kwa uchungu, kama jinsi ambavyo baadhi ya wasomaji wa kisa hiki watakavykuwa wanajihisi wakati huu.
“Aah, Bishi…ndio imeshakuwa hivi tena…Ushindi wa pili sio hatua ndogo…ni upinzani wa haja tumeuonesha…!” Kokos alimjibu dadaye huku akiwa amemkumbatia.
Kule jukwaani Candy alivikwa utepe wake wa mshindi wa pili na kwenda kusimama upande wa pili wa kile kiti cha malkia wa urembo wa dunia na kubaki akiwa anatabasamu kwa ushindi huku akilini akiwaza juu ya kadhia iliyokuwa ikimsubiri nyuma ya jukwaa.
Ni kwamba kila alichokuwa akikifanya na kukishuhudia pale ukumbini wakati ule kilikuwa kama ndoto fulani tu hivi.
Huku ukumbini minong’ono haikuisha. Msema chochote alifanya kila aliloweza kuwanyamazisha watazamaji, lakini ilikuwanikama kwamba kuna mjadala mzito uliokuwa ukiendelea.
“…na sasa kwa mrembo wa dunia kwa mwaka huu….” Muigizaji wa ki-Venezuela alikuwa ananadi kule mbele ilhali bado baadhi ya watazamaji wakionesha wazi kutokuwa na hamu tena ya kutaka kumjua mshindi, na hata pale walipofanikiwakumnadi Miss Scotland kuwa ndiye miss world, shamra shamra hazikuwa kama zile zilizokuwa kwa Candy, na kibaya zaidi, likatokea kundi la watazamaji ambalo liliamua kusimama na kuanza kupiga makofi huku likilinadi jina la mshindi wa pili…
Candy…Caaandy….CAAAANDDYYYYY….!
Kule alipokuwa amesima, Candy alianza kububujikwa namachozi ya uchungu, akijua wazi kuwa amelikosa taji kutokana na zile shutuma zilizotokea kwenye maisha yake ya awali, maisha aliyoyakimbia…sasa yamekwenda kumkamata katika wakati muhimu kabisa maishani mwake.
Kule kwa watazamaji, timu nzima kutoka Tanzania ilikuwa ikibubujikwa na machozi bila ya kificho sasa, kama jinsi ilivyokuwa sehemu mbalimbali nchini Tanzania…hususan kwenye ile nyumba ya watoto yatima kule Tarime.
***
Sehemu nyingine ya ukumbi ule, yule mwakilishi wa kamati ya Miss World raia wa Uingereza alikuwa akifinya uso wake na kutafuna midomo kwa hasira.
“Wapuuzi wameinyima Afrika nafasi ya kuchukua taji kipumbavu kabisa, shenzi zao!” Alinong’ona kwa hasira huku akimtazama miss Scotland akivikwa taji lake huku akiwa ametandaza tabasamu la ushindi usoni.
Mkuu wa sakafu aliyekuwa jirani naye aliafiki kwa kichwa huku akiwa ameweka mikono yake kwenye mifuko ya suruali yake, uso wake ukiwa umekunjamana kwa mawazo.
“Nakubaliana na wewe…nah ii ni kutokana na yale mazingira ya kule nyuma ya jukwaa…kwa nini uliwaambia juu ya hilo? Candy alikuwa anachukua hili taji pamoja na hizo shutuma ambazo hazijathibitishwa …hebu sikia watazamaji wanavyomnadi huko kama kwamba yeye ndiye aliyebeba taji! Huo ni ujumbe wa wazi kwa kamati yako mzee!” Alimwambia kwa simanzi na shutuma za wazi.
Mwakilishi wa kamati ya Miss World aliguna na kusonya.
“Sikuwaambia lolote kuhusu kilichotokea kule nyuma ya jukwaa…wao walitaka kujua kilichotokea…na mi’ sikuwaambia kwa sababu haikuwa sahihi! Washenzi wameenda kuamua kama kwamba wamethibitishiwa kuwa Candy aliua mtu huko kwao (akawatukania mama zao)! Naombea tu hii isije ikatuletea doa aisee!” Alisema kwa hasira.
“Doa limeshaingia kaka! Husikii watu wanavyomshangilia mshindi wa pili badala ya huyo malkia anayetawazwa hivi sasa huko? Unataka doa gani tena zaidi ya hilo?” Mwenzake alimwambia, kisha akaendelea kwa hasira, “…hivi hii mitanzania ikoje lakini? Haina akili, basi hata uzalendo pia inakosa? Kwa nini wamepiga simu kama ile wakati kama ule lakini, eenh?”
“Stupid individuals!!” Mwakilishi wa miss world alitema laana kwa hasira na kuondoka eneo lile huku akitikisa kichwa, akielekea kule kwenye shamrashamra za kumpongeza miss world mpya…mwanadada kutoka Scotland.
Kule jukwaani, matukio yote yaliyoambatana na kuvikwa taji la urembo wa dunia kwa yule m-scotland yalikuwa yakipita kama kama ndoto tu kwa Candy. Alishiriki kila hatua ya matukio yale kwa jithada kubwa…akilazimika kutabasamu na kumpongeza mrembo mwenzake pamoja na kupiga picha za pamoja na wale warembo wenzake kutoka Scotland na India, pamoja na wale wenzao wawili waliofika hatua ile ya fainali.
Hatimaye shamrashamra ziliisha na warembo wakarudi nyuma ya jukwaa kuchukua vilivyo vyao na kurejea kwenye nchi zao.
Naye akaenda kukabiliana na majanga yaliyokuwa yakimsubiri…
***
Bishkuku alimkumbatia kwa nguvu.
“Hongera sana mdogo wangu…Hongera! Umepata kile ulichopangiwa kukipata…umeweka historia duniani na kwa nchi yako pia!” Alimwambia huku akibubujikwa na machozi.
“Ah, Anti Bishi! Si umesikia watu walivyokuwa wakinishangilia lakini? Mi’ nimepokonywa tu hili taji anti yangu…nimepokonywa tu jamani…!” Candy alilalama kwa kilio.
Hakeem Labemba aliwafikia na kumkumbatia pia.
“Umetoa ushindani mkubwa kuliko mabinti wote niliowahi kuwafikisha kwenye mashindano haya Candy…si haba hatukupata taji, lakini ujumbe umeshafika duniani. Sasa Tanzania si kichwa cha mwendawazimu tena kwenye mashindano haya…!” Alimwambia kwa liwazo huku mwenyewe donge likimkaba kooni.
“Oh, kaka Hakeem…nahisi nimewaangusha watanzania jamani…nitawapelekea sura gani wale watoto yatima kule Tarime jamani! Hii ni hujuma tu…ni nani aliyenifanyia hivi lakini, eenh?” Candy alizidi kulalama.
“Hili ni pigo kwetu sote Candy…na elewa kuwa Miss Tanzania itakuwa nawe mpaka hatua ya mwisho!” Hakeem alimwambia kwa kutia moyo. Candy alizidi kulia.
Muda wote huo Kokos Wandiba alikuwa amesimama pembeni akitazama kile kilichokuwa kikitokea kwa hasira, kwani aliamini kabisa kuwa Candy amekosa taji kutokana na zile shutuma zisizoeleweka kutoka Tanzania. Sasa mashindano yameisha, akili yake ilirudi kwenye lile tatizo lililokuwa mbele yao. Na yale yaliyokuwa yanawasubiri kule nyumbani, ambako alijua kuwa Morandi angemnanga vibaya sana juu ya kujihusisha kwake na binti yule.
Pamoja na hayo, alijua kuwa hatorudi nyuma katika kumtetea binti yule.
Muda huo wale askari wa Interpol walifika pale walipokuwa.
“Er, Bi. Candy…naomba tuongozane tafadhali…kuanzia muda huu uko chini ya ulinzi!” Yule askari alimwambia Candy.
Candy akahamanika.
“Kwa hiyo ndio maana yake nini hii sasa, eenh? Niko chini ya ulinzi kivipi na mi’ nimeshasema kuwa sijaua mtu?” Alimaka kwa wahka, sauti ikimvunjika kwa kilio.
“Lolote utakalosema kuanzia sasa linatatumika kama ushahidi dhidi yako katika mahakama ya sheria, hivyo unashauriwa kukaa kimya…”
“Nooo! MI’ S’JAUA BWANAA!” Candy alimaka kwa wahka, akitembeza macho baina ya Hakeem Labemba, Bishkuku na Kokos.
“Mimi ni wakili wake…nitamuwakilisha kutokea hapa!” Kokos alijisogeza mbele huku akisema, na Bishkuku aliguna kwa mshangao. Hakeem halikadhalika.
Candy alimrukia na kumkumbatia kwa nguvu.
“Oh, Kokos…Kokos usiwaruhusu wanichukue hawa! Usiwaruhusu kabisa tafadhali!” Alilia huku akiwa amemng’ang’ania kwa nguvu. Kokos alimkumbatia kwa liwazo.
“Usiwe na wasiwasi Candy…niko kwa ajili yako katika hili…!”
“Mi’ s’jaua jamani!”
“Naamini hivyo…lakini sheria lazima ichukue nafasi yake kwanza…”
“Aaaaah Kokos unataka kuniambia niende nao wewe…unataka kuniambia nikawekwe mahabusu mimi!”
“Bibie! Hatuna muda wa kupoteza zaidi…yakupasa uongozane nasi sasa!” Yule askari alisema kwa ukali na hapo wasaidizi wake wakamng’atua Candy kutoka mwilini kwa Kokos na kumshikilia. Candy aliishiwa nguvu, hakuweza tena kuleta ushindani. Alibaki akiwa amesimama akimtazama Kokos kwa kuomboleza, machozi yakimbubujika.
Ni taswira iliyomkata maini na kumnyong’onyesha moyo vibaya sana Kokos. Alijitahidi kujikaza, akiuacha uwakili wake uchukue nafasi.
“Kokos! We’ si umenyang’anywaleseni ya uwakili wewe? Usije ukamletea matatizo zaidi!” Bishkuku alimsogelea na kumnong’oneza kwa ukali.
“Nimenyang’anywa leseni ya kufanya uwakili Tanzania, sio duniani…wale mafala hawakujua kuwa bado nina leseni yangu ya sheria ya kimataifa na nimekuwa nikiilipia kila mwaka…” Kokos alimjibu haraka, kisha akamgeukia yule askari.
“Okay afisa…mteja wangu hana ubishani wowote juu ya wewe kufanya kazi yako. Tuambie unajitaji nini kutoka kwetu.” Alimwambia.
“Kazi yangu ni kumuweka chini ya ulinzi na kumpandisha ndege ya kwanza kurudi Tanzania ambako huko ndipo atakapofunguliwa mashitaka yanayomstahili…” Askari wa Interpol alimjibu.
“Ndege yetu ya kurudi Tanzania inaondoka kesho saa tatu usiku, kwa hiyo unataka kusema kuwa Candy itabidi atafutiwe ndege nyingine ya mapema zaidi?” Hakeem Labemba aliingilia kati, akionekana wazi kuwa alikuwa amekorogwa sana akili na mambo yote yale.
“Hilo litafanyiwa maamuzi kituoni!” Askari alijibu.
Muda huo mwakilishi wa miss world alifika pale akiwa na watendaji wake wengine wawili.
“Pole sana Candy…naamini hili litaondokea kuwa ni mkanganyiko mdogo tu na sio zito kama lilivyowasilishwa hapa…” Alimwambia.
“Ah, utakuwa ni mkanganyiko ulioninyima taji la miss world mwakilishi…hauwezi kuwa mdogo hata kidogo! Moyo unaniuma sana mimi!” Candy alimjibu kwa simanzi huku akilia. Jamaa alitembeza macho na kulegeza koo.
“Er…ni masikitiko kwa kweli…na…kwa hili lililotokea basi, itabidi tuzuie zawadi yako ya mshindi wa pili ya paundi elfu thelathini, na tuizuie tuzo yako ya miss photogenic mpaka hapo mkanganyiko huo utakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu…sawa?” Mwakilishi alimwambia, na safari hii Candy akaishia kutikisa kichwa tu.
“Sisi tutakuwa tunafuatilia kwa karibu sana kila kinachoendelea huko kupitia kwa Hakeem na kamati nzima ya Miss Tanzania. Na itakapothibitika kuwa ulikuwa huna kosa lolote basi zawadi zako zitakabidhiwa kwako kama ipaswavyo. Pole sana.” Jamaa alizidi kumwambia.
Candy alikuwa akilia huku akitikisa kichwa tu.
Candy alikuwa akilia huku akitikisa kichwa tu.
“Lakini kutoka kwangu binafsi…hongera sana Candy.Nimevutiwa sana na ushiriki wako kwenye mashindano haya…ni ushiriki ambao Tanzania ilipaswa iuenzi kwa heshima zaidi ya hivi ilivyotokea…hongera sana!” Mwingereza alimwabia na kumpa mkono kwa heshima.
Candy aliupokea mkono ule huku akilia kwa uchungu, kwani yale maneno yalimchoma sana na yalizidi kumhakikishia kuwa hakika lile taji lilikuwa linaenda kwake, na likapindishwa kona katika hatua ya mwisho kabisa.
Ah, Mungu na amlaani aliyenifanyia mambo haya kwa kweli!
Ilikuwa ni vilio na simanzi wakati mrembo wa taifa la Tanzania, na mshindi wa pili wa shindano la urembo wa dunia na miss photogenic aliyewekwa kizuizini kwa muda, akiingizwa kwenye gari la polisi wa Venezuela akiwa na wakili wake Kokos Wandiba, na kupeleka kituo kikuu cha polisi cha Caracas. Hakeem Labemba na akina Bishkuku wakiwafuata nyuma kwa teksi hadi huko kituoni.
Nusu saa baadaye akina Kokos walirudi hotelini kwao kwa huzuni kubwa, na miss Tanzania alibaki mahabusu kule kituo cha polisi.
Ilikuwa ni simanzi kubwa sana.
Kule mahabusu, Candy alilia!
Alilia sana na kwa muda mrefu.
Alilia kwa uchungu na majuto dhidi ya nafsi yake iliyoandamwa na mikosi.
Akiwa pale mahabusu, hakuweza tena kukwepa kukumbuka kipindi cha maisha yake ambacho aliazimia na alishafanikiwa, kukifuta kabisa akilini mwake.
Kilikuwa ni kipindi kichungu na cha mateso makubwa. Machungu na mateso aliyoyapata akiwa mikononi mwa mwanamama aliyejulikana kama Shakira binti Swadafu…ambaye sasa anashutumiwa kumuua.
Ni kweli alikuwa akilala akimuombea kifo kibaya sana yule mwanamama…na alikuwa akimuombea kifo kibaya kutokana na mateso na machungu aliyoyapata ndani ya nyumba yake.
Ndani ya nyumba ya Bi. Shakira Swadafu.
Alikumbuka mambo yaliyotokea miaka miwili iliyopita akiwa nyumbani kwa Bi. Shakira Swadafu, huko Magu, kanda ya ziwa, nchini Tanzania…
Akiwa amefikisha kidato cha pili pale kwenye ile nyumba ya watoto yatima kule Tarime, walitokea wazazi ambao walijitolea kuchukua baadhi ya watoto na kuwalea katika mazingira ya nyumbani huku wakiendelea kuwapa matunzo yote ya muhimu yahitajikayo kwa watoto. Hili lilionekana kuwa ni jambo zuri sana kwa watoto wale kwani miaka yote wamekuwa wakitamani kuishi katika mazingira ya nyumbani, wakilelewa na wazazi kama watoto wengine.
Candy Gamasala alishashuhudia wenzake kadhaa wakiondoka pale kituoni na kwenda kuishi na wazazai wa kufikia.
Ilikuwa ni njozi wa kila mtoto pale kituoni kupata bahati kama ile, hivyo siku alipoitwa ofisini kwa mkuu wa kituo na kupewa taarifa kuwa ametokea mzazi ambaye waliona angeweza kuishi naye vizuri katika mazingira ya nyumbani, Candy alifurahi sana. Mkuu wa kituo alimjuza kuwa kwa kuwa alikuwa amekaribia umri wa miaka kumi na minane, ambapo baada ya umri ule angekuwa na uhuru wa kuamua kutoka nje ya nyumba ile ya watoto yatima, basi ile ingekuwa ni nafasi nzuri kwake kwenda kuanza maisha ya nje ya nyumba ile ya watoto yatima.
Lilikuwa ni wazo zuri sana lililopokewa kwa furaha tu na Candy aliyechoka kuishi kwenye yale mazingira ya kwenye kile kituo cha watoto yatima.
“Sa…sasa vipi na shule matron…si unajua mi’ natilia umuhimu sana shule?” Candy alimuuliza yule mkuu wakituo.
“Kila kitu kimewekwa wazi kwa huyo mlezi wako mpya, naye ameahidi kukupatia shule kwenye huo mji anaoishi nawe utasoma na kulelewa nyumbani kama kawaida…unaonaje?”
Candy alifurahi.
“Ahsante sana matron…naona ni vizuri sana hiyo!”
Matron alimpa karatasi yenye namba za simu za pale kituoni.
“Basi ikiwa kutatokea tatizo lolote kinyume na haya mwanangu, usisite kunijulisha, nami mwenyewe nitakuja kukuchukua, okay?” Alimwambia.
Candy aliipokea ile karatasi kwa mashaka.
“Kwa…kwani unadhani kutatokea nini…?”
“No. Hakuna kibaya ninachokitarajia huko…ila hiyo ni kwa tahadhari tu Candy…huwezi kujua…” Matron alimwambia, na Candy akaiweka kwenye mfuko wa shati lake la shule ile karatasi.
Siku ya pili alitoka nje ya nyumba ile akiwa na sanduku lake akiongozana na mlezi wake aliyetambulishwa kwake kuwa ni Bi. Shakira Swadafu, tajiri mkubwa kutokea maeneo ya Magu, na kuingia kwenye gari la kifahari aina ya Vogue…ingawa kwa wakati huo Candy hakujua kuwa lile gari lilikuwa ni aina ya Vogue. Yeye aliona ni gari la kifahari tu. Aliingia kwenye kiti cha nyuma pamoja na yule mama yake mpya mwenye mwili mkubwa, kule mbele dereva akawasha gari kuashiria mwanzo wa safari.
Candy aliwapungia mkono watoto wenzake waliojipanga nje ya geti la kile kituo pamoja na yule mkuu wao wa kituo, na safari ya saa tatu na nusu kuelekea Magu kutokea pale Tarime ikaanza.
Wakati ule Candy Gamasala alikuwa amejawa na matarajio makubwa kabisa kwenye maisha mapya aliyokuwa anaenda kuyaanza nyumbanikwa yule mama yake mpya, Bi. Shakira Swadafu.
Lakini aliyokutana nayo huko yalikuwa ni tofauti kabisa…
Magu, miaka miwili iliyopita:
Nyumba ya Bi. Shakira ilikuwa ni ya kifahari kweli kweli. Lakini kinyume na matarajio yake, Candy alishangaa kuona kuwa zaidi ya Bi. Shakira mwenyewe kwenye lile jumba, hakukuwa na mtoto mwingine yoyote zaidi ya mfanyakazi wa kusimamia mifugo ya yule mama na mwingine aliyekuwa akifanya kazi kwenye shamba kubwala yule mama lililokuwa nyuma ya jumba lile.
“Haya mtoto…wewe utakuwa unaishi humu ndani na mimi…na pia utakuwaunasaidia kazi ndogondogo za ndani…” Bi. Shakira alimwambia siku ile alipofikishwa ndani ya jumba lile.
“Sawa mama…na…vipi kuhusu shule? Utanipeleka kesho…?”
Alimjibu na kumuuliza.
“Yaaa, itabidi tusibiri kidogo kwa siku mbili tatu hivi, kisha nitakupeleka…” Bi. Swadafu alimjibu.
“Ah…sawa...na…hamna watoto wengine hapa? Watoto wako wako wapi?” Candy alimuuliza tena, na Bi. Shakira akamcheka kidogo.
“Wanangu mi’ ni wakubwa sasa…unadhani ni kwa nini nimekuja kukuchukua wewe kule? Ni kwa kuwa sina mtoto wa kuishi naye hapa. Wanangu wakubwa kabisa, na mume wangu alishafariki kitambo tu. Utamuona mwanangu mmoja...mwingine hayupo hapa mjini kwa sasa…haishi hapa kabisa!” Bi. Shakira alimjibu na kumuacha pale chumbani kwake.
Candy alijishughulisha kupanga vitu vyake kwenye kile chumba cha kifahari. Hakika yalikuwa ni mazingira tofauti sana nayale ya kule kwenye nyumba ya watoto yatima na siku ile alilala usingizi mororo sana.
Lakini ilimchukua wiki moja tu kubaini kuwa hakuwa amepelekwa pale kwa ajili ya kulelewa na kusomeshwa, bali kwaajili ya kufanyishwa kazi za ndani.
Hakika kule kulikuwa ni kusalitika kwa hali ya juu, na Candy aliumia sana.
Alikuwa akifanyishwa kazi za kupiga deki nyumba na kuandaa chakula kwa ajili ya Bi. Swadafu na vinywaji kwa ajili ya wageni wake ambao walikuwa hawaishi pale nyumbani kila mwisho wa wiki, wakinywa pombe na kulewa huku wakipiga kelele usiku kucha, naye akiwa ndiyo muhudumu wao.
Hali ile ilipoendelea aliamua kutafuta namna ya kumjulisha yule mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima. Alilifungua sanduku lake kuchukua kile kikaratasi kilichokuwa na namba ya simu ya yule mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima, lakini alipigwa na butwaa alipogungua kuwa hakikuwepo mle sandukuni alipokiweka.
Hah!
Alihaha kukitafuta kwa pupa, akipangua nguo zote kutoka mle sandukuni, lakini wapi!
“Unatafuta hiki?” Sauti ya Bi. Shakira ilimsemesha kutokea nyuma yake naye akaruka kwa mshituko huku akigeuka.
Naam, Bi. Swadafu alikuwa amekishika kile kipande cha karatasi kikiwa na namba za simu za kule kwenye nyumba ya watoto yatima.
Candy alibaki kinywa wazi.
“Aam…nakiomba kikaratasi changu…umekipataje…?”
Bi. Shakira alimsogelea na kumtazama kwa jeuri.
“Nimekipataje? Mi ndo Shakira binti Swadafu bwana! Nimesujudisha wahindi hadi wagiriki, itakuwa kisinoko kama wewe? Nimefungua hilo begi lako nikakichukua!” Bi. Shakira alimjibu, na Candy akabutwaika.
“Akh! Sa’ kwa nini umekichukua? Nikiomba kikaratasi changu mama!”
“Ili upige simu kwa walezi wako wa mayatima uwaambie nini?” Alimuuliza kwa jeuri, akiwa amembadilikia ghafla. Candy alizidi kumshangaa.
“Nataka kurudi kwetu ndiyo! Hapa sikuja kufanyishwa kazi…nilikuwa nasoma kule…hapa unajifanya mi’ mfany…”
Kibao!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hah!” Candy alimaka kwa mshangao huku akijishika shavu pale alipozabwa kofi na yule mama.
“Ng’waka nini, kisonoko mkubwa wee! Ulidhani mi nilikuja kukuchukua kule ili nije kukupa maraha tu hapa, eenh? Kwa kuwa nakuogopa sana, au? Hapa kazi tu! Serikali ya kijiji imezuia watoto wote hapa jirani kufanya kazi kwangu….eti wananyanyaswa! Sasa mi’ ndo nikaenda kukuchukua wewe wa mbali na usiye na jamaa yoyote hapa mjini. Utanifanyia kazi tu humu ndani! Kulala utalala pazuri, chakula utakula ninachokula mimi… na mshahara pia nitakupa, lakini swala la kukusomesha mi’ hata sikuwa nalo!” Bi. Shakira alimpasulia jipu bila kujali.
Candy hakuamini.
“Haah! Yaani mama ndio umeniharibia masomo yangu hivi hivi jamani?” Alimuuliza kwa kutoamini kile alichosikia.
“Na hutatoka nje ya uzio wa nyumba hii nakwambia! Kila kitu kitaletwa hapa!”
“Ah, Mi naondoka!” Candy alimaka na kujaribu kuuendea mlango. Bi. Shakira alimkamata mkono na kumtandika makofi mengine mawili makali sana, kisha akamsukumia kitandani.
“Hebu tulia humu wewe!” Alimkemea na kugeuka, akatoka nje ya chumba kile.
Candy alibaki akilia kwa uchungu pale kitandani.
Aliona dunia yote ikimgeuka bila ya huruma.
“Eee Mungu wangu! Hivi miye ndio umenileta hapa duniani kuja kuteseka tu jamani? Tangu naiingia hii dunia miye niwe ni mtu wa kutaabika na kunyanyasika tu kweli?” Alijisemea mwenyewe kwa kuomboleza.
Alilia!
Alilia sana siku ile.
Na ndio ulikuwa muendelezo wa machungu na madhila mengi ndani ya jumba la Bi. Shakira Swadafu…
***
Wiki mbili baada ya kuwasili kwake kwenye lile jumba, Candy alikuwa ameshakata tamaa ya kutoka kwenye jumba la yule mama ambaye alimwendea kule kwenye nyumba ya watoto yatima akiwa na sura ya tabasamu, na kumbadilishia sura baada ya kumfikisha pale kwenye jumba lake. Pamoja na hivyo, alikuwa akijitahidi kujiendeleza kwa kurudia madaftari yake ya shule kila alipopata wasaa. Na siku moja alikuwa amejifungia chumbani kwake akijisomea kitabu cha historia wakati mlango wake uliposukumwa kwa nguvu kutokea huko nje, na msukumaji alipoona kuwa ule mlango umefungwa kwa ndani alianza kuugonga kwa nguvu.
Haraka Candy alikimbilia pale mlangoni na kuufungua.
Alikutana uso kwa uso na jamaa mmoja aliyejengeka kimazoezi akiwa kidari wazi na bukta tu mwilini. Alikuwa maji ya kunde na alionekana mtanashati sana.
Walitazamana.
Jamaa alifunua kinywa lakini hakuna kilichotoka kinywani mle.
“Esh...sh’kamoo!” Candy alimsalimu kwa woga.
Hakuwa amepata kumuona hata siku moja mle ndani yule jamaa. Jamaa alizidi kumtazama kwa namna ya ajabu, na Candy akajikuta akiuchukia mtazammo aliopewa na yule jamaa na hapo hapo akajikuta hawezi kuendelea kutazamana naye. Akainamisha uso wake.
“Vipi wewe? Unalala tu mi napiga kelele huku nahitahji maji ya moto ya kuoga…we si ndo msaidizi mpya hapa, au si weye?” Jamaa alimkoromea hatimaye, na lile swali lilimkera Candy.
Alipotolewa kule kwenye nyumba ya watoto yatima hakuambiwa kuwa anakuja kufanywa msaidizi wa ndani!
“We…wewe ni nani kwani…?” Alimuuliza.
Jamaa akamkodolea macho kama kwamba alikuwa ameuliza swali la kijinga kuliko yote duniani. Kisha akaangusha kicheko kikubwa.
“Ee Bi Swadafu! Bi Swadafu eee…huyu mtoto umemtoa wapi lakini, eenh?” Alipiga kelele huku akigeuzia uso wake kwenye korido la nyumba ile.
“Haya kunani tena hukoo?” Bi Swadafu aliitika huku akija pale walipokuwa.
“Ana uduriki wa kuniuliza eti mimi ni nani…! Ama safari hii umetulea msomi humu ndani mama, eenh?” Jamaa alimwambia Bi, Swadafu, na Candy akanywea kwa matarajio ya makemeo mazito kutoka kwa Bi. Swadafu.
“Hap…hapana mama…sikumuuliza kwa ubaya! Mi’ nilikuwa…” Alianza kujieleza.
“Huyu ndiye mwanagu niliyekwambia sasa. we binti. Ndiye mfalme wa jumba hili…atakalo, alipata. Sasa nisisikie tena unahoji anachokwambia!” Bi. Swadafu alimwambia kwa ukali.
Heh! Ana mtoto mkubwa hivi!
Candy alijiwazia, na kama aliyesoma mawazo yake, Bi. Swadafu alimwambia, “Si nilikwambia kuwa nina watoto wakubwa miye? Sasa huyu ni wa pili…ana kaka yake huyu!”
“Ambaye hana haki ya chochote kwenye nyumba hii!” GTZ alidakia kwa hasira.
“Hebu nikelelee mimi na wewe huko! Hana haki kivipi?” Bi. Swadafu alimjia juu mwanaye.
“Baba hakumtambua na alisema wazi kuwa hataki aguse chochote katika mali zake!” Jamaa alimbishia mamaye, na Candy akabaki akiwatazama mama na mwana wakibishana namna ile kwa mshangao mkubwa.
“Na huyo babaako yuwapi sasa?”
“Hata kama amekufa…maagizo yake yanabaki!”
“Hebu acha kunichanganya mimi na wewe huko! Yule ni mwanangu mimi, kwa hivyo nawe ni nduguyo. Kuwa baba yake ni mwingine hilo si hoja. Kama hana haki na mali za marehemu babayo, basi ana kila haki na mali zangu mimi…” Bi. Swadafu alimjibu, na hapo akakumbuka kuwa walikuwa wakibishana mbele ya Candy.
“Hebu toka hapa na wewe kisonoko mkubwaa! Nenda kamchemshie maji ya kuoga huko!” Alimkemea, na Candy akaondoka haraka, ule mjadala baina ya mama na mwana ukiwa hai akilini mwake.
“Na kesho kutwa jioni kutakuwa kuna pati hapa ya kumpokea mwanangu…kwa hiyo uanze kufanya usafi mapema humu!” Alimtupia maneno.
“Ndio mama!” Candy alijibu huku akizidi kutokomea kutoka eneo lile.
Aliweka maji aliyoamriwa jikoni na kujiinamia nyuma ya nyumba ile huku akiwa amenyongea vibaya sana.
Ah! Yaani mi ndo nimekuwa mfanyakazi wa ndani jamani! Hapana. Lazima nitoroke hapa. Lakini nitaenda wapi? Hata sijui namna ya kurudi kule kwenye nyumba yetu ya watoto yatima na sina hata sen’tano!
“Hello, helloo mtoto shoo…! Vipi mbona umejiinamia hivyo chaurembo?” Sauti ilimsemesha kwa kubembeleza, naye akakurupuka kutoka kwenye mawazo yake.
Akamuona yule mchunga ng’ombe wa Bi. Swadafu akiwa amemsimia mbele yake.
“Ah, sh’kamoo…nilikuwa…”
“Achana na shikamoo mtoto shoo…mi ni blazameni flani tu mtafutaji…vipi wewe, unaitwa nani?” Jamaa lilimwambia na kumhoji.
“Er, Candy…wewe nakuonaga unachunga ng’ombe wa mama, sio?”
Jamaa akacheka.
“Nakuonaga ndio lugha ya wapi mrembo? Sema huwa unaniona nikichunga ng’ombe…” Jamaa alimwambia huku akimcheka. Alionekana mcheshi sana.
“Ah, okay…ndio hivyo…”
“Kwa hiyounataka niitwe mchunga ng’ombe?” Akacheka tena, kisha akaendelea,“Mi’ naitwa John, mrembo. Hapa naganga njaa tu mambo yakikaa sawa natambaa…”Yule jamaa aliyejitambulisha kwa jina la John alimwambia.
“Mi sio mrembo…naitwa Candy!”
“Okay…Candy. Lakini kwangu wewe ni mtoto shoo tu…!”
“Kwa nini? Ndio nini?”
“Allaaaa! Yaani hujioni ulivyokuwa mrembo we’ mtoto? Yaani we umekaa ki-shoo shoo tu! Umeangukiaje kwenye hili jumba la madhila lakini mtoto mzuri kama wewe?” John Koccho alimhoji.
“Ah, kaka John…we acha tu! Yaani hata sijui n’tafanyaje tu…”
“Caaanddddyy!” Bi. Swadafu aliita kutokea ndani ya jumba, na Candy akakaurupuka.
“Okay mtoto shoo nenda. Lakini jua kuwa ukihitaji rafiki…na kwa kweli utahitaji sana rafiki ukiwa humu ndani…jua mi’ nipo, okay?”
Candy alitabasamu.
“Okay!” Alijibu na kukimbia mbio ndani ya jumba lile.
Huku nyuma, John Koccho alibaki akiwa amesimama akitazama ule mlango aliopotelea yule binti huku tabasamu baya likiwa limejijenga usoni kwake.
Kisha akatundika fimbo yake ya kuchungia ng’ombe za Bi. Swadafu mabegani na kurudi kwa ng’ombe wake huku akipiga mbinja.
***
Jioni ya siku ya tatu Bi. Swadafu alifanya sherehe kubwa pale nyumbani kwake, ikiwa ni sherehe maalum kwa mwanaye wa kwanza aliyeitwa Greg Pasha ambaye alikuwa amerejea nchini kutoka nje ya nchi ambako alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya.
Ni katika sherehe ile ndipo Candy alipopata kumuona huyo mtoto mwimgine wa Bi. Swadafu. Yeye alikuwa mrefu kuliko yule mtoto wa pili wa Bi. Swadafu na alikuwa na weusi fulani ulioonesha mchanganyiko wadamu mbili tofauti mwilini mwake.
Greg Pasha, mtoto wa kwanza wa Bi. Swadafu aliyemzaa na bwana wa kihindi kabla hajaolewa na bwana wa kigiriki, alikuwa kimya muda wote wa sherehe ile, akiongea mara chache sana na akicheka au kutabasamu mara chache zaidi. Candy alikuwa akishughulika kugawa vinywaji kwa waalikwa akisaidiana na akina dada walioletwa pale na Bi. Swadafu kutoka mjini kwa shughuli ile.
Aliweza kuona kuwa hakukuwa na upendo wa dhatikati ya yule mtoto wa pili na huyu wa kwanza wa Bi. Swadafu, na baada ya kusikia yale majibizano kati ya mama na mwana asubuhi ile, alielewa ni kwa nini hakukuwa na upendo baina ya watoto wale.
Ilimfunukia kuwa huyo mume wa pili wa Bi. Swadafu ambaye ni marehemu, ndiye baba wa GTZ na ndiye aliyemwachia Bi. Swadafu utajiri aliokuwa nao pale Magu baada ya kifo chake.
Aligundua kitu kingine usiku ule.
Pamoja na kwamba alikuwa mjane tajiri, Bi.Shakira Swadafu hakuwa akikaa tu hivi hivi bila uhusiano. Katikati ya sherehe ya Greg usiku ule aliingia bwana mmoja mtu mzima aliyejengeka mwili vizuri. Aliingia kwenye ukumbi wa sherehe akiwa ndani ya suruali ya jeans na fulana nyekundu yenye lebo ya mavazi ghali sana huko nchi za nje, ambayo ilimshika misuli ya mikono yake na kuonesha jinsi alivyokuwa amejengeka kifua na misuli ile.
“Oooh my love umekuja…how nice!” Bi.Swadafu aliruka huku akimfuata yule bwana na kumkumbatia, na Candy alijikuta akitumbua macho pale alipomshuhudia yule mama mtu mzima akimpiga busu zito la kinywani yule bwana, ambaye bila hiyana wala kusita alilipokea vivyohivyo lile busu, watu waliokuwa pamoja nao pale wakicheka huku wengine wakiwapigia makofi.
Bila kupenda Candy alipeleka macho kwa wale watoto wa yule mama, na kuona kuwa GTZ alikuwa akilitazama lile tukio kwa furaha tu, ilhali Greg Pasha akibetua midomo kwa kutoridhishwa.
Bi. Swadafu alimshika mkono yule bwana na kumpeleka hadi kwa Greg.
“Greg…kutana na baba’ako wa kufikia mwanangu. Anaitwa Ngamao…yeye ni mkuu wa upelelezi katika jeshi la polisi hapa mjini!” Bi .Swadafu alimtabulisha yule bwana kwa Greg, ambaye bila kuonesha kupendezwa na hali ile aliinuka na kupeana mikono na yule bwana mwenye upara. Bi. Swadafu akamgeukia yule bwana wake aliyemtambulisha kwa jina la Ngamao.
“Waubani...huyu ndiye Greg, ambaye nilikuwa nakupa habari zake siku zote. Amerudi nyumbani hatimaye!” Alimwambia.
“Karibu tena nyumbani dogo...natumai mambo yaliyosababisha ukae mbali na mamayo kwa miaka yote hiyo hayatojitokeza tena sasa, no?” Ngamao alimwambia Greg huku akimtazama usoni.
“Sikujua kuwa uliolewa tena mama…” Greg Pasha alimwambia mama yake huku akimtupia jicho la kushutumu, akiipuzia ile kauli ya Ngamao.
“Ah! Achana na hayo sasa! Hatujaoana. Mi’ ni mpweke na Ngamao pia ni mpweke…tumeona tuwe pamoja tu.Umri huu tena ndoa za kazi gani?” Bi.Swadafu alimwambia mwanae kilevi, pombe zilikuwa zimempanda kichwani kwa kiasi fulani.
Greg aliguna tu, na kuuchomoa mkono wake kutoka kwa Ngamao na kuketi.
“Okay nimefurahi kuonana nawe…baba wa hiyari!” Alisema kwa kebehi, na Ngamao akaachia cheko ya kutojali.
“Nami hivyo hivyo bwana…” Alimwambia, na hapo hapo akamgeukia GTZ aliyekuwa pale jirani, “GTZ vipi wewe, uko poa lakini?” Alimuuliza, na Candy akajua kuwa GTZ alikuwa akijuana na Ngamao kitambo na hakuwa na taabu naye.
“Kama kawaida...tuko tu hapa tunasherekea ujio wa kipenzi cha mama!” GTZ alijibu kwa kitu kama kebehi Fulani hivi, na Candy akamuona Greg akimtupia jicho la pembeni.
“Candy!” Mmoja wa wale mabinti watoa huduma kwenye sherehe alimwita, na Candy akakurupuka kutoka kwenye kufuatilia kile kilichokuwa kikitokea pale kwenye ukaribisho wa yule muhibu wa Bi. Swadafu na kukimbilia jikoni alikoitwa.
Heh! Mama mtu mzima namna ile anajihusisha kwenye mapenzi bila ndoa! Aibu!
Sherehe iliendelea mpaka usiku wa manane. Candy alikuwa akimalizia kuondoa vyombo wakati alipomuona yule afisa wa polisi akiongozana na Bi. Swadafu kuelekea chumbani kwa yule mama, wakiwa wamekumbatiana kimahaba. Bi. Swadafu alikuwa akitoa sauti za deko mithili ya paka mdekaji afanyavyo akiwa kwa mmiliki wake amdekezaye.
Mwili ulimsisimka na akahisi kichefuchefu.
Mambo ya aibu kabisa haya!
***
Nusu saa baadaye alikuwa amelala kama pono chumbani kwake. Mchoko wa hekaheka za usiku ule ulimfanya awe legelelege kama mrenda. Ndipo ghafla aliposhitukia akiwa amelaliwa na mtu kifuani.
Heh!
Alikurupuka na kujaribu kujikwamua lakini wapi.
“Tulia kama ulivyo mtoto!” GTZ alimkoromea, harufu ya pombe kutoka kinywani mwake ikimzongaf ahamu zake.
“Ah! SITAK…SITAKI! Unanibaka…? Unan…”
Kofi kali la uso likamduwaza kwa sekunde kadhaa.
“Tulia! We motto hivi hujijui ulivyo mzuri wewe? Mi’ leo lazima niku…” GTZ alimnong’oneza kilevi.
“No! Tok…tokkaaa! Umeingiaje humu ndani…?”
“Funguo za akiba za vyumba vyote humu ndani najua zilipo mwanamwari…leo mimi na wewe lazima tumegeane tunda tuuu!” GTZ alimtambia kilevi huku akimtomasa sehemu ya uuke wake.
“AH! Ananibakaaaaa! JAMANI SAIDIAAAA! ANANIB…” Candy alianza kupiga kelele.
GTZ alimbana mdomo na kumtandika makofi makali sana.
Candy alikwa amezoea kulala na nguo ya ndani tu bila kitu chochote zaidi, na hii ilimpa yule jamaa mkware urahisi wa kufanya alitakalo. Kwa mvuto mmoja wa nguvu aliikatilia mbali ile chupi na kujizamisha mwilini mwake kwa nguvu.
Na hapo ndipo Candy alipopoteza usichana wake, kwani juhudi za kujikwamua ziligonga mwamba.
GTZ alimbaka.
Candy akatolewa bikira kwa kubakwa.
***
Akiwa pale mahabusu jijini Caracas, Candy Gamasala alishindwa kuendelea kukumbuka yale mambo ya kule Magu kutokana na uchungu wa mambo yale.
Kilio kilimkumba upya.
Uchungu wa kitedo alichofanyiwa na GTZ ndani ya jumba la Bi. Swadafu ulimjia upya. Ni uchungu alioamua kuusahau na kuufuta kabisa mawazoni mwake…Alitaka kusahau kila kilichotokea kule Magu ili awe mtu mpya mwenye maisha ya heshima na yasiyo na chembe za uchungu.
Lakini kinyume na hayo amekuwa ni mwenye maisha machungu yenye chembe chembe chache za furaha…chembe chembe ambazo zilianza kuyaangukia maisha yake pale alipokutana na Bishkuku mwenye upendo.
Akiziondoa hizo chembe chembe chache za furaha, maisha yake yamekuwa ni vikwazo na madhila tu. Kwanza kutoka kwa Jackie aliyempokea jijini na kutaka kumtumbukiza kwenye ukahaba…kisha kutoka kwa akina Tunis na bosi wake Sanura kwa kumfanyia vitimbi kadhaa wa kadhaa, na hatimaye kutoka kwa John Koccho, ambaye ndiye mpaka wakati ule ameshindwa kabisa kuelewa ni kwa nini amemuibukia akiwa na sura mbaya kabisa tofauti na ile aliyokuwa nayo kule Magu.
Alikuwa anaelekea kutimiza lengo lake maishani…kwa msaada wa Bishkuku na Kokos. Watu ambao hakuwajua kabisa hapo kabla, walioamua kumuamini na kumfikisha pale kwenye mashindano ya urembo wa dunia…
Ambako kwa mara nyingine tena maisha yake machungu ya huko nyuma yamemuibukia…safari hii yakimletea shutuma za kumuua Bi. Swadafu!
Ah! Jamani Candy miye! Hivi ni nini lakini?
Alibaki akilia usiku kucha…
Usiku ule si yeye tu ambaye hakulala. Kokos Wandiba, Bishkuku na timu nzima ya kamati ya Miss Tanzania pia ilikuwa kwenye mgogoro mkubwa kabisa na usingizi. Simu zilipigwa Tanzania na habari zikafika nchini kuwa mrembo wa Tanzania amewekwa chni ya ulinzi na askari wa Interpol jijini Caracas, muda mfupi tu baada ya kumalizika mashindano yale ambapo aliliwakilisha taifa kwa kiwango cha juu kabisa, akikabiliwa na tuhuma ziaminikazo kuwa ni za mauaji aliyofanya nchini Tanzania.
Waandishi wa habari waliosafiri na kamati ile walifanya kazi yao, na usiku ule kwa kule Caracas, ikiwa ni kama saa tatu za asubuhi kwa saa za Tanzania, vyombo vya habari vya redio na televisheni vilianza kurusha matangazo ya habari ile, wakati vile vya magazeti zilikuja kuandika habari ile usiku ule na kutoka kwenye magazeti ya siku iliyofuata.
Kilichofuatia kilikuwa ni mtafaruku mkubwa nchini.
Kabla habari zile hazijaenea nchini, Kokos Wandiba alimpigia simu Morandi Gwaza na kumpasha habari zile.
“Holy Shit, Kokos…Holly gaddem Sheeeeyyiiiiiiit! Haya ndio mambo niliyokuwanikikuasa juu ya huyu binti wakili wangu! Na sasa…” Morandi alianza kumjia juu baadaya kuelezwa kile kilichojiri kule Caracas.
“Na sasa unaweza kukaa huko uliko ukinisimanga kwa simu kwa kuwa bado uko hai na unapumua Morandi! Je, unataka nikukumbushe ni nani aliyefanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa unaendelea kuwa na pumzi na kukuwezesha kuwa hapo ulipo hivi sasa ukinisimanga kwenye simu, badala ya kuwa biriani ya mafunza ukiwa futi sita ndani ya tumbo la ardhi saa hizi?” Kokos naye alimjia juu na kumkatisha kwa ukali.
Huku Tanzania, Morandi akaachia mguno wa kukereka, huku Nuru akimtazama kwa macho ya kuuliza kando yake.
“Come on Kokos! Hivi huelewei ni nini maana yake hiyo? Ni kwamba sasa mimi na wewe tuko wazi mbele ya macho ya vyombo vya dola kwa mara nyingine Kokos! Na yote ni sababu ya huyo binti!” Morandi alifoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hebu niambie ni nini kilichotokea Mo, vipi wewe? Kuna nini kilichomtokea Candy huko?” Nuru alimuuliza mpenziwe kwa wahka, akiona kuwa tayari hali ilikuwa imeshabadilika.
“Ah! Candy yuko chini ya ulinzi huko Caracas…kumbe demu aliua mtu huku bongo!” Morandi alimjibu mpenziwe, na hapo hapo, wakati Nuru akiachia mguno wa kutoamini kwa taarifa ile, Morandi aliiweka ile simu kwenye mfumo wa spika, na sauti ya Kokos ikasikika kwao wote.
“…nilivyosema hapo awali Morandi. Nitakuwaupande wa huyu mtoto mwanzo mwisho…iwe ni kwa msaada wako au nisiwe nao. Lakini bado una deni na mimi ujue!”
Morandi akamtukania mama yake kwa hasira na kutupa mikono hewani.
“Tusi la kawaida hilo Morandi! Nimekupigia kukutaka unifanyie kazi moja tu kwa sasa Morandi, na kama baada ya hapo utaamua kuachana na hili kwakuwaunawaogopa hao mapolisi wenzako waliokutosa na kutaka kukutumbukiza kaburini huko nyuma poa tu…!”
“Siogopi mtu mimi! Lakini kwenye ukweli lazima nikwambie Kokos!” Morandi alikuja juu, na hapo hapo Nuru akadakia.
“Hakuachi mtu hapa Kokos. Tutakuwa nawe mpaka mwisho. Candy hajaua mtu bwana…achana na Morandi. Sema unataka nini kifanyike sasa?”
Morandi alimkata jicho la ghadhabu, na Nuru akamuamshiria akae kimya.
“Hayo ndio maneno ya kuambiana wakati kama huu! Sio kubebeshana lawama tu…” Kokos alimwambia, na Morandi alidakia.
“Sema unataka nini basi!”
“Nataka uende kwa wakili Abiyah Byabato Morandi. Ukifika huko unipigie simu niongee naye kuhusu utetezi wa Candy mara tukifika hapo nchini!” Kokos alisema, na Morandi akapiga kimya.
“Unadhani hilo ni wazo zuri? Unadhani atakubali?” Hatimaye alimuuliza.
“Na kwa nini usimpigie simu tu moja kwa moja kutoka huko, mpaka Morandi ndio aende kuongea naye? Huna namba yake?” Nuru alidakia.
“Alikuwa mpenzi wake zamani…wakagombana…sasa hawaongei kabisa!” Morandi alimjuza, na Nuru akaachia mguno.
“Kama kuna wakili anayeweza kumnasua Candy kwenye hili ni yeye tu, na wewe walijua hilo Morandi. Itabidi nimshawishi tu mpaka akubali. Nikimpigia mimi anaweza kukata simu akisikia tu sauti yangu!” Kokos alisema.
Kimya kilipita.
“Okay, tutaenda. Lini mnarudi?” Morandi hatimaye alisema na kumuuliza.
“Nitakufahamisha. Mpate Abiyah kwanza!”
“Poa!” Nuru alidakia.
“Na Kokos…” Morandi alimwita, na Kokos alipoitika, akamtukania tena mama yake, na kukata simu.
***
Saa mbili baadaye simu ya Kokos iliita kidogo na kukatwa, ikiwa ni saa tisa za usiku kwa kule Caracas. Alipoona kuwa ilikuwa ni namba ya Morandi akaenda hewani mara moja. Kufikia hapa Bishkuku alikuwa ameshasalimu amri kwenye usingizi wa mang’amung’amu, na Hakeem Labemba alikuwa ameshajisalimisha mwili, roho na akili pia kwenye usingizi mzito uliochagizwa na pombe nyingi alizojibugiza.
Kokos alibaki peke yake pale kwenye sehemu ya sebule ya chumba cha hoteli waliyopanga, chupa ya kahawa ikiwa mbele yake. Alijipiga marufuku kabisa kugusa pombe usiku ule, kwani alijua kuwa akigusa pombe tu, ndo hatoiacha kabisa, na Candy atazidi kuwa mashakani.
“Sema Mo, umempata Abiyah?” Aliuliza, na akajibiwa na sauti nyingine.
“Haya Chapombe…leo umenikumbuka,ewe mwana wa ibilisi? Mshukuru sana Morandi naongea nawe hivi sasa. Kama si yeye nisingepoteza pumzi zangu kuongea na bazazi, shetani na msaliti uliyetukuka kama wewe, shenzz taip!” Abiyah Byabato alimvurumishia shutuma simuni.
“Oh, Abiyah…nam…ahsante kwa kuongea nami. Nahitaji msaada wako…” Kokos alianza kuongea.
“Achana na hayo! Morandi ameshaniambia kwa ufupi. Na ushukuru kuwa huyo yatima wako hana dada mkubwa wala mdogo, ama si hivyo nina asilimia mia na moja kuwa ungemtafuna yeye halafu ungepitia na dada yake na ukamalizia na kwa mdogo wake pia, malaya mkubwa we!” Abiyah alimpasha na kule Caracas Kokos akauma meno na kufinya macho.
Akakosa la kusema.
“Vipi? The learned brother leo amekosa la kusema?” Abiyah alimuuliza na kupitisha kicheko cha kebehi, kisha akamwambia, “Elewa kuwa naongea nawe kikazi zaidi Kokos, na si vinginevyo. Usaliti ulionifanyia wa kutembea na mdogo wangu toka n’toke hautafutika moyoni mwangu milele, fala we!”
“Ilikuwani pombe tu Abiyah kipindi kile, na nimekuwa sorry ever since! Nisamehe bibie…” Kokos alirudia maneno aliyokiwisha yasema kwa Abiyah miaka miwili nyuma, na akapokewana sauti ya kukerekekakutoka upande wa pili wa simu ile.
“Sina haja na laghai zako! Najua unamnyemelea huyo mrembo na sasa ameingia kwenye matatizo unataka ujiineshe kuwa umekuwa naye bega kwa bega uli umpate vizuri fisi maji wewe...”
“Si hivyo Abiyah…hisia zangu kwake hazikuhitaji akutwe na matatizo ndio niziweke wazi, ila…” Kokos alianza kujitetea, lakini Abiyah akamkatisha.
“Gharama zangu kwa kazi hii ni milioni kumi Kokos. Sita sasa hivi, na nne baada ya kesi kuisha…vyovyote itakavyoisha. Najua sana kuwa unaweza kumudu gharama zangu hizo. Kwa hiyo napata six M, niko kazini. Vinginevyo tafuta wakili mwingine na kimada wako afie jela!” Abiyah alimjia juu, na Kokos akaachia mguno upande wa pili wa simu ile.
“Come on, Abiyah…kuwa mwenye staha. Unanikomoa kwayaliyotokea huko nyuma?”
“Sijakuomba unitafute kwenye kesi hii. Nakata simu!” Abiyah alimjia juu.
“Okay! Okay…milioni sita now…nne baada ya kushinda kesi. No problem!” Kokos alimaka.
“No, hatuendi hivyo chapombe! Nimesema sita now…nne baada ya kumaliza kesi, vyovyote ikatavyokwisha…sijasema swala la hizo nne kumaliziwa tukishinda kesi, mimi.Umelewa tayari?” Abiyah alimkoromea, na kule Caracas Kokos alitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
“Oh, okay…vyovyote kesi itakavyokwisha...lakini najua utamvua Candy kwenye kesi hii Abiyah…”
“Niite wakili! Sio Abiyah tenakwako kuanzia sasa Kokos…hii ni kazi zaidi…strictly business!”
“Okay mheshimiwa! Najua iwapo Candy ni wa kunusurika katika hili,basi hakuna wa kulifanikisha hilo ila wewe…” Kokos alimwambia.
“Lini napata hela yangu, au ndio mpaka mrudi bongo?” Abiyah aliuliza kibabe.
Kokos alitikisa kichwa kwa masikitiko. Alimfanyia mambo mabaya yule mwanadada na hajaweza kujisamehe kwa hilo. Alijitahidi kujisahaulisha, na Candy alikuwa anaelekea kumsahaulisha yote hayo. Sasa tena hili la Candy kuwa kwenye kesi ya mauaji lilielekea kumuondolea matumaini yake ya kujisahaulisha na kutokurudia makosa aliyofanya huko nyuma.
“Nadhani kesho sote tutarejea, ila kama ni lazima upate pesa yako kabisa basi nitumie akauti yako…dada yangu Bishkuku atakuhamishia kiasi hicho cha pesa kwa njia ya mtandao kutokea huku huku…si unajua kuna internet banking siku hizi?”
“Okay. Nitakutumia taarifa za akaunti yangu kwa sms baada ya kumaliza kuongea nawe hapa. Okay, umeongea naye chochote mteja wangu kuhusiana na kesi hii?” Abiyah alimuuliza.
“Ah, hapana…amewekwa mahabusu na hakuwa katika hali nzuri ya kuongea kipindi kile. Nadhani kesho atakuwa ametulia kiasi cha kuweza kumhoji…”
“Nitamhoji mwenyewe akifika hapa. Wewe utaleta mapenzi tu huko huwezi kuwa kikazi zaidi wewe!” Abiyah alimwambia.
“Oh, come on, Abiyah…mimi ni wakili wa kitaaluma bwana…naweza kutofautisha kazi na mambo binafsi!” Kokos alijitetea.
“Na bado ukaona unitafute mimi…” Abiyah akamsaili kikebehi.
“Aww, we nimekutafuta kwa kuwa mimi sina tena kibali cha kujishughulisha na kazi ya uwakili huko bongo Abiyah…lakini…”
“Okay, okoa muda. Nitakuja kumhoji mwenyewe akifika hapa bongo!”
“Sawa. Lakini si unajua kuwa kutakuwakuna jopo la wanausalama likitusubiri huko? Itabidi tuhakikishe kuwa hawaongei naye kabla ya…” Kokos alimwambia.
“Ndio maana inabidi nione hela imeingia kwenye akaunti yangu kabla sijaenda pale uwanja wa ndege kumsuburi Candy sasa! Hela hamna kwenye akaunti, siji airport…mtakutana na wanausalama…!” Abiyah alimwambia na kukata simu.
“Aaa-a, Abiyah…!” Kokos alimaka peke yake simuni.
Dakika tano baadaye ujumbe mfupi wenye jina la akaunti na namba ya akaunti za wakili Abiyah ukaingia kwenye simu yake.
***
Siku ile ile jijini Dar, GTZ alikuwa amejawa na wahka baada ya kusikia habari za Candy kukamatwa huko Caracas. Alimgeukia nduguye Gred Pasha.
“Ebwana Ngamao kafanya ndivyo hatimaye! Mshenzi yuko mbaroni sasa…sijui ataingia jijini lini tu sasa!” Alimwambia nduguye.
Greg Pasha aliguna.
“Ni Ngamao huyo huyo atakayetujuza ni lini anaingia nchini.Si ni lazima awasiliane na Interpol kujua ni muda gani mtuhumiwa amepanda ndege na muda gani ndege itatua jijini? Cha msingi tupate hizo habari mapema tu…” Alimwambia mdogo wake wa kufikia.
“Yeah…nadhani leo Ngamao atakuja tu.” GTZ alisema kwa hamasa, kisha akapiga kimya kidogo, halafu akamgeukia tena nduguye.
“Nashukuru sana Greg kwa kuja kuwa nami katika hili kaka…kwa hali ilivyo mimi sina namna ya kufanya tena…bado mguu wangu unaniweka kitini!”
Greg Pasha alimtupia jicho la pembeni.
“Ni mama yetu sote aliyeuawa GTZ…usisahau hilo hata siku moja. Nilidhamiria kulipiza kifo chake tangu awali, na hilo ndilo nitakalolifanya…sikuja hapa kwaajili yako na utajiri wa babaako…ni mama yangu tu ndiye aliyenileta hapa!” Alimwambia kwa msisitizo.
GTZ alimeza mate.
“Yah…nilikuwa na mtazamo mbaya kwako kwa choyo cha kijinga tu Greg…lakini ukweli ni kwamba sisi ni ndugu…na mama yetu ameuawa…na muuaji ndio huyo sasa anaangukia kwenye mikono ya sheria...kama jinsi Ngamao alivyotaka, ingawa mimi pia nilitaka nimuue kwamkono wangu shenzi zake!” Alimwambia nduguye kwa uchungu.
“Na kama ungenishirikisha tangu mwanzo Candy wangeshamzika saa hizi!” Greg alisema kwa hasira kidogo.
GTZ alitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
Greg alisonya na kuchukua miwani yake ya jua na kuuendea mlango wa kutokea nje ya nyumba ile.
“Mi natoka zangu kidogo…Ngamao akija hakikisha unapata dondoo zote za ujio wa muuaji wa mama!” Alimwambia nduguye.
“Unaenda wapi?”
“Kuna maandalizi yanipasa niyafanye!” Greg alimjibu na kutoka.
Geti la nyumba ya GTZ lilifunguliwa, na gari la kifahari aina ya porche likatoka na kuingia barabara kubwa, likichukua uelekeo wa katikati ya jiji. Hata wakati lile gari likikamata ile barabara kubwa, kioo chenye kiza cha upande wa dereva kilikuwa kikijipandisha na kumficha dereva wa gari lile.
Lakini sio kabla ya Nuru aliyekuwa amebana upande wa pili wa barabara akiitzama ile nyumba hajapata nafasi ya kuuona uso wa Greg uliokuwa umepachikwa miwani ya jua utosini.
Greg Pasha aliongeza kasi kuelekea mjini.
Hakuwa na sababu ya kuitilia maanani pikipiki kubwa iliyokuwa ikimfuata nyuma yake ikiwa imeacha magari mawili baina yao.
Nuru aliamua kumfuatilia yule mtu mgeni kabisamachoni mwake tangu sakata lile la Candy na GTZ lianze.
Akiwa amevaa kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki, haikuwarahisi kwa yeyote kubaini kuwa mtu aliyevaa suruali na koti vyote vikiwa ni vya kitambaa cha jinzi, aliyekuwa akiiendesha ile pikipiki alikuwa ni mwanamama…
Safari ya Greg Pasha iliishia maeneo ya gerezani jijini. Nuru aliiona ile Posrche ikisimama nje ya geti la gereji moja miongoni mwa mlolongo wa maregeji mengi yaliyozagaa eneo lile. Umakini wake ukiwa umezidi maradufu, aliiegesha pikipiki yake upande wa pili wa barabara na kubaki akiwa ameegemea usukani huku akitazama kule ambako lile gari lilipokuwa ilhali bado akiwa amevaa ile kofia yake ya kuendeshea pikipiki.
Kwa hali ilivyokuwa ni kwamba muda si muda geti la ile gereji lingefunguliwa na ile gari ingeingia mle ndani, naye asingeweza kumuona vizuri yule dereva wa ile gari.
Alimung’unya midomo yake ndani ya ile kofia ya kuendeshea pikipiki. Jamaa ndani ya Porsche alibamiza honi mara nyingine.
Kwa hali ya kawaida ingeonekana kuwa mwendesha Porsche alikuwa amepeleka gari gereji kutengenezwa. Kwa hali ya kawaida na kwa mtu wa kawaida, lakini Nuru hakuwa mtu wa kawaida. Alijua kuwa mtu mwenye kumiliki Porsche hawezi kupeleka gari kama lile kwenye gereji ya gerezani, hususan ile ambayo hata geti lake lilionekana kuwa ni la kubandika bandika tu.
Hii ilimwambia kuwa yule jamaa hakuwa ameenda pale kufuata huduma za gereji.
Sasa ni nini kilichompeleka pale?
Kule mbele geti lilifunguliwa na Porsche ikaingia ndani, kisha geti likafungwa.
Nuru aliachia dakika tano zipite, kisha akachomoa kikanyagio cha gia kwenye pikipikiyake na kukiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti lake la jinzi, kisha akaikokotea ile pikipiki hadi pale kwenye lile geti.
Akagonga lile geti kwa fujo kwa ubapa wa ngumi yake. Mara ya kwanza, ya pili na ya tatu kwa nguvu zaidi.
“Oyaaa! Nini palee…?” Sauti kutoka ndani ya lilegeti ilihoji kwa kukereka.
Nuru akagonga tena kwa nguvu zaidi, bila ya kujibu lolote.
Geti lilifunguliwa kwa ghadhabu, jamaa mfupi sana mwenye upara alijitokeza nje akiwa amekunja uso kwa hasira.
“Nini wewe…?” Aliuliza kwa hasira, na akaishia akiwa ameduwaa alipojikuta akikabiliana na sura ya mrembo aliyevalia jinzi tupu akiwa amekumbatia kofia ya kuendeshea pikipiki kwapani, akimtolea tabasamu la mvuto.
“Oh…!” Jamaa akagwaya.
“Kokotea ndani basi hii pikipiki kakaangu…imebuma ghafla tu…” Nuru alimwambia huku akimsukumia ile pikipiki naye akiingia mle ndani ya ile gereji.
“Hahh…ina tatizo gani…?” Upara aliuliza lakini Nuru tayari alikuwa ameshaingia mle ndani ya wigo mpana wa gereji ile akiangaza huku na huko. Ile Porsche ilikuwa imeegeshwa kwenye kona moja ya wigo ule, mlango wa dereva ukiwa wazi, dereva hakuwemo.
Nuru aliguna na kugeuka kule kwa yule jamaa aliyekuwa anakokota ile pikipiki mle ndani.
“Ina tatizo gani…?” Jamaa alimuuliza tena huku akiiegesha vizuri ile pikipiki.
“Bosi wenu yuko wapi hapa, eenh?” Nuru alimuuliza, akipuuzia lile swali lake.
“Ah, Mushi yuko na jamaa mwenye hilo gari baab kubwa pale…” Jamaa alimjibu huku akiielekezea ile gari aliyokuwa akiifuata.
“Okay, wako wapi…nataka kuonana na Mushi!” Nuru alimwambia, akielewa kuwa bosi waile gereji alikuwa anaitwa Mushi.
“Anti, usin’letee shobo…hili pikipiki lako lina shida gani? Kama una shida na Mushi subiri amalizane na huyo mgeni mwingine…”
“Kwani yule gari lake lina shida gani mpaka lihudumiwe na Mushi, na mimi pikipiki yangu ina upungufu gani hadi isihudumiwe na Mushi…?” Nuru aliuliza kwa kupoteza muda, akivizia kuona ni muda gani jamaa aliyekuwa akiendesha Porsche atatoka.
“Unaona ile gari inatengenezwa kitu pale? We fuata yako tu hapa dada, vipi wewe?” Jamaa alimkoromoea.
“Okay, poa. Nahitaji mtu wa kuishughulikia pikipiki yangu…”
“Mimi ndiye ninayeshughulikia mapikipiki yote hapa…kwa hiyo kama…”
“Okay. Mi nimeiona gea haipo kwenye pikipiki yangu…ghafla tu napekeka mguu siioni. Itakuwaje hapo?” Nuru alimwambia huku akizungushia jicho kule alipoambiwakuwa jamaa mwenye Porsche atakuwa ameelekea.
Upara akainama na kuitazamaile pikipiki.
“Oh, Una bahati sana…kitakuwa kimefyatuka na kuangukia huko barabarani…una elfu kumi na tano hapo nikuwekee kingine?” Upara alihoji na Nuru akamjia juu.
“Elfu kumi na tano? Una wazimu!”
Jamaa akamtumbulia macho, na muda huo Nuru aliona watu wawili wakitokea kwenye kijengo kidogo mwisho wa wigo ule, mmoja, ambaya ndiye yule aliyemfuata kutokea kule nyumbani kwa GTZ akiwa na mfuko mkubwa wa nailoni mkononi. Walitembea hadi jirani naile Porsche, wakapeana mikono, kisha jamaa akautupia ule mfuko wa rambo ndani ya lile gari na kuingia. Nuru alikuwa makini sana kumtazama yule jamaa wakati yule mwenzake akirudi ndani ya ile ofisi ndogo.
“Kwa hiyo ndo inakuwaje sasa anti?” Upara alimuuliza.
Nuru akaikamata pikipiki yake nakuikokota kwa nguvu.
“Naondoka nayo hivi hivi…sina hela hiyo mimi!” Alimjibu kwa hasira na kuisukuma kwa haraka kuelekea kule getini, kwa pembe ya jicho lake akiiona ile Porsche ikigeuza na kuanza kuelekea kule kule getini…
“Kwa hiyo ndo inakuwaje sasa anti?” Upara alimuuliza. Nuru akaikamata pikipiki yake na kuikokota kwa nguvu.
“Naondoka nayo hivihivi…sina hela hiyo mimi!” Alimjibu kwa hasira na kuisukuma kwa haraka kuelekea kule getini, kwa pembe ya jicho lake akiona ile Porsche ikigeuza na kuanza kuelekea kule kule getini…
Kufika getini akajitia kuelemewa na ile pikipiki. Muda huo lile gari la Greg Pasha likawa limefika nyuma yake kabisa pale mbele ya geti. Greg akasimamisha gari na kusubiri. Nuru akajitia kuhangaika na pikipiki yake, kisha kwa namna ya kukata tamaa, akaiegesha ile pikipiki pale pale mbele ya geti na kusimama pembeni huku akiwa amejishika kiuno.
Greg akampigia honi kwa hasira.
Nuru akamgeukia na kumtumbulia macho, kisha akamuashiria kwa mikono yake kwa namna ya kumuuliza anataka nini.
Ndani ya gari Greg akatukana na kubamiza honi nyingine.
Upara akamwendea mbio Nuru pale alipokuwa.
“Wewe dada vipi mbona unaleta usiku hapo? Ondoa mkweche wako hapo basi watu wapite…nini bwana!” Akamkoromea.
Nuru akamjia juu.
“Mkweche huu? Mkweche huu? Baba’ako analo hili, eenh? Analo?” Akajitia kumchachamalia huku akitupa tupa juu mikono, na kule kwenye gari Greg akakandamiza honi nyingine.
Nuru akamfuata pale kwenye gari na kumsimamia kando ya dirisha la dereva.
“Nini na wewe unapiga-piga mihoni hapa? Huoni kuwa tuna tatizo hapa?!” Akamfokea huku akimuoneshea mikono pale kwenye kioo kilichowekewa weusi. Greg akashusha kioo.
“Unasema nini wewe?” Akamkemea kwa hasira, usoni akiwa amevaa miwani yake ya jua. Nuru akamtazama kwa makini kisha akatupa jicho hadi pale kwenye kiti cha abiria mle garini ambako alimuona yule jamaa akiutupia ule mfuko wa nailoni aliotoka nao kule kwa yule mmiliki wa gereji aliyeitwa Mushi.
“Nasema nini? Si huyu upara hapa! Mi n’na matatizo na pikipiki yangu. Badala ya kunisaidia ananiambia eti mkweche…halafu na we’ badala ya kuja kumsaidia mtoto wa kike mwenye matatizo umekazana kupiga mihoni tu hapa! Nini bwana!” Nuru akamjia juu huku akizidi kumtazama kwa makini na akitupia jicho zaidi kwenye ule mfuko wa rambo pale kwenye kiti cha abiria mle garini.
Greg Pasha alimtazama kwa utulivu kwa sekunde kadhaa.
“Nenda kaondoe mkweche wako pale! Nataka kutoka mimi saa hizi we malaya, ala!” Akamkoromea huku akizidi kumtazama moja kwa moja usoni kutokea nyuma ya miwani yake. Nuru hakutarajia kabisa jibu lile na pamoja na uchakaramu aliojitia, alikosa jibu.
“Khah!?” Ndilo neno pekee lililomtoka, na Greg alibaki akimtazama vile vile.
“Mkweche ule...? Baba’ako ana…” Alianza kumjibu, lakini hapo akamuona Greg akimuoneshea kwa kidole chake kule mbele ilipokuwa ile pikipiki yake huku bado akiwa amemuelekezea uso wake. Nuru akageuka kufuata uelekeo wa kidole cha Greg,na akamuona yule upara akiivutia pembeni iIe pikipiki yake.
Shit!
Akamgeukia Greg kwa hasira, lakini akakuta ndio kile kioo chenye weusi kikimalizikia kujifunga, na hata pale alipokuwa akiona hali ile, lile gari lilichomoka mbele kwa kasi na kufunga breki kali karibu na geti ambalo yule upara bado alikuwa analifungua, na lilipofunguliwa, ile Porsche ikiwa na yule mtu aliyeokenekana kuwa ni chotara wa kihindi na Kiswahili ilichomoka kwa kasi nje ya wigo wagereji ile.
Nuru alibaki akiukodolea macho ule uwazi uliobakia pale mlangoni baada ya lile geti kufunguliwa huku uso wake ukiwa umejikunja kwa mawazo mengi.
Yule jamaa ni nani?
Kuja kwake huku kunahusiana vipi na sakata la GTZ na Candy?
Hakuwa amewahi kumuona hata siku moja yule mtu, lakini kila kitu kuhusu yule jamaa kilikuwa kinanuka ubaya-ubaya tu. Alionekana kuwa ni mtu mmoja katili sana. Ingawa Nuru alikuwa akifanya kazi yake tu pale alipokuwa akijibizana na yule jamaa, bado majibu ya yule jamaa yalimfanya ajione kama kwamba ni malaya kweli aliyekuwa akijirahisisha tu kwa yule mtu.
Alisonya.
“Poa tu. Unajifanya mjanja lakini mimi ni mjanja zaidi yako, mdosi koko wee!” Alisema kwa sauti ya chini huku akiiendea pikipiki yake na kuanza kuikokotea nje ya gereji ile iliyoficha maasi, akipuuzia maneno ya kejeli kutoka kwa yule upara.
Jamaa alikuwa amemfanyia dharau ya kutosha kisha akamfungia kioo ili asiweze kumjibu…lakini sio kabla Nuru hajaona kilichokuwa ndani ya ule mfuko wa nailoni uliokuwa umebwagwa pale kwenye kiti cha abiria ndani ya lile gari. Anaweza kuwa mbabe na mjanja, lakini ambalo Greg Pasha hakulijua ni kwamba Nuru alikuwa amefanikiwa sana katika alilokuwa akilitaka kwa kwenda kumsimamia pale kando ya dirisha la gari lake…
***
Jijini Caracas asubuhi ilifika na Candy akakutana tena na wenzake. Alionekana wazi kuwa hakuwa amepata hata lepe la usingizi usiku uliopita, kwani macho yalikuwa yamemvimba na yamemuwiva.
“Oh! Candy my princess! Hukulala kabisa wewe. Pole sana. Elewa hili ni letu sote na tutakuwa nawe mwanzo mwisho…!” Bishkuku alimwambia huku akimkumbatia.
Candy alijiachia akumbatiwe bila ya kusema lolote wala kujibidiisha kumkumbatia yule mwasisi wake katika urembo. Alikuwa amekata tama kabisa.
“Come on…inabidi ukajiweke safi kwa safari sasa. Tunarudi nyumba ni kwa ndege ya asubuhi hii, Candy…” Yule binti wa kamati ya Miss Tanzania alimwambia.
Mipango ilishaandaliwa na wale askari wa Interpol ya kumpa nafasi Miss Tanzania ya kujiweka safi kutokana na hadhi yake. Hivyo waliruhusiwa kwenda hotelini kwao wakiwa chini ya ulinzi ili Candy akaonge na akabidilishe nguo. Ndege yao ilikuwa inapaa ndani ya saa mbili kutoka muda ule waliokuwa wakikutana tena baada ya wote kupitisha usiku uliopita kwa mashaka makubwa kabisa.
Nusu saa baadaye Candy alikuwa ameshajiweka safi na tayari kwa safari ya uwanja wa ndege. Ndipo Kokos alipomwita pembeni, na kwa kuwa alikuwa wakili wake, wale askari wa Interpol walimruhusu.
“Tukifika Dar utakuwa chini ya uangalizi wa wakili mwingine…si miye tena. Ila ni wakili mzuri na makini…atakuvusha tu kwenye hili…” Alimwambia.
“Mi’ sikuua mtu Kokos…sikuua mtu kabisa!” Candy alimwambia kwa uchungu.
“Si neno. Utakapofika huko, utaongea na wakili wako na utamweleza kila kitu. Yeye atajua namna ya kukuvua kwenye hili. Mwambie ukweli wote kama ulivyo…usimfiche kitu!” Kokos alimsisitizia.
“Ina maana wewe hutakuwepo?”
“Nitakuwepo…ila sitakuwa wakili wako. Tukishuka tu Tanzania kutakuwa na maaskari ambao watataka wakuweke chini ya ulinzi hapo hapo. Akiwepo wakili wako atazuia usiulizwe maswali yoyote kabla hajaongea nawe. ...lakini ikitokea kuwa wamekuwahi maaskari kabla wakili wako hajafika, basi hata ukiulizwa nini, usijibu kitu. Sema kuwa unamsubiri wakili wako…tumeelewana?” Kokos alimwambia kwa makini.
Candy aliafiki kwa kichwa huku akihisi kutoamini kabisa kwamba amefikia hatua ya kupewa maelekezo kama yale.
Saa mbili na nusu baadaye wote walikuwa angani wakirejea nchini.
Ah! Ndio naenda kukabiliana na tuhuma za mauaji Candy miye tena!
Alijiwazia kwa simanzi akiwa kwenye kiti cha kati baina ya askari wawili wa Interpol, mmoja kila upande wake. Bishkuku na binti kutoka kamati ya Miss Tanzania walikuwa viti vya mbele yake, wakati Kokos na Hakeem walikuwa viti vya nyuma yake.
Akili yake ikamrudisha tena kule kwenye jumba la Bi. Shakira Swadafu…na kwenye ule usiku ambao GTZ alimfanyia kitu kibaya…
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alifanya fujo kubwa sana mle ndani siku ile, miaka miwili nyuma baada ya kujihakkikishia kuwa GTZ alikuwa amembaka. Alipiga kelele huku akimrukia kwa hasira na kumrarua usoni kwa kucha zake, na GTZ alibweka kama mbwa, na hapo hapo akamshindilia ngumi nzito ya tumbo iliyomtembezea maumivu makali na kumlegeza maungo.
“Mshenzi sana wewe…usilambwe we’ umekuwa nani? Kaa kimya hapo!” GTZ alimkemea huku akijifuta mchirizi wa damu uliokuwa ukichuruzika kutoka pale alipomkwaruza.
Candy alijikunja kwa uchungu na kubaki akitweta kwa maumivu huku machozi yakimbubujika.
“Naenda polisi! Naenda polisi usiku huu huu mshenzi mkubwa wewe!” Alimwambia kwa hasira, huku akijifunga upande wa khanga kwa mtindo wa lubega, na GTZ akamcheka kwa kebehi kisha akageuka na kutoka nje ya chumba kile huku akiendelea kucheka kilevi-levi.
Candy alimfuata mbio nje ya chumba kile akiwa ameinua kigoda kidogo kilichokuwa mle chumbani, na alikuwa anakishusha kwa nguvu kisogoni kwa GTZ aliyekuwa akiendelea kutembea kilevi kwenye korido yamle ndani wakati aliposhitukia akidakwa kwa nguvu kutokea nyuma yake na kunyanyuliwa juu mzima mzima, kile kigoda kikimtoka mkononi na kuvunjika sakafuni.
“Heeey! Tulia wewe nini hapo?” Greg Pasha alimkoromea kutokea nyuma yake huku akiwa amembana kwa nguvu kutokea nyuma yake.
“Niache! Niachie…niacch…”
Ngamao akafika mbio pale kwenye korido, macho yamemtoka pima.
“Nini kelele zote hizi hapa?” Alimaka, akitupa macho kwa GTZ aliyebaki ameduwaa akikikodolea macho kile kigoda kilichosambaratika pale sakafuni, kisha akamtupia macho Greg aliyekuwa amemkamata Candy kwa nguvu.
“Nimebakwa! GTZ kanibakk…..” Candy alilalama na kushindwa kumalizia na badala yake akaishia kulia.
Ngamao akamgeukia GTZ.
“Umem…what?” Ngamao alimkemea GTZ kwa hasira. GTZ akapiga mbwewe kilevi, kisha akatupa mikono juu kumaanisha kwamba hana muda wa kusumbuliwa na jambo lile tena. Ngamao alimwendea kwa hatua tatu kubwa na kumcharaza makofi matatu ya haraka haraka GTZ, kisha akamkwida na kumbabatiza ukutani kwa nguvu.
“Unafikiria nini wewe, eenh? Unajua hukumu ya kosa la kubaka ni miaka mingapi jela fala wewe?” Alimkemea, na kabla GTZ hajajibu akamalizia kwa kutoa jibu mwenyewe, “Miaka thelathini mkware mkubwa wewe! Thirty years! Nyie watoto vipi nyinyi? Huyu kaka’ako nd’o kwanza ametoka jela kwa mambo ya mihadarati, mama yenu anafanya sherehe ya mwanaye mmoja kurudi kutoka gerezani na wewe unaitafuta jela kwa jambo la kibwege tu kama hili…!”
“Niachie Ngamao!” GTZ alifoka.
“Na jela ataenda! N’tamshitaki na n’tahakiksha anafia jela mimi…sikubali! Sikubali!!!” Candy alimaka kwa hasira, bado akiwa ameshikiliwa na Greg.
Bi. Shakira akafika pale, usingizi ukiwa umempaa.
“Nini kelele hapa…?”
“Mwanao kanibaka mama! Kanibakaaaa!” Candy alipiga kelele kwa hasira.
Bi. Swadafu alimtazama kwa muda, kisha akamsogelea pale alipokuwa.
“Mwanangu yupi aliyekubaka kati ya hawa wawili?” Alimuuliza kwa hasira.
“Si huyo GTZ! Kanibb…”
Kofi!
“Hah!” Candy na Ngamao walimaka kwa pamoja, na hata pale Candy alipokuwa anapeleka mkono wake kujishika shavu pale alipochapwa kibao na Bi. Swadafu, yule mama akamtandika kofi la pili.
“Shakira! Sasa mbona unampiga tena huyu mtoto?” Ngamao alimaka kwa mshangao, akiifunika sauti ya malalamiko kutoka kwa Candy.
Bi. Swadafu alimsogelea Candy aliyeshikwa na Greg na kumbana taya.
“Mimi nimekuwa nikikuona we’ mtoto akimtingishia-tingishia GTZ vitako vyako siku nyingi!” Alimwambia kwa hasira, kisha akamgeukia Ngamao, “Huyu mtoto wa kiume anamfanyiavitimbi kama hivyo anatarajia nini? Anataka kumnasa mwanangu ili aingie kwenye familia tajiri sio? Basi hapa imekula kwake malaya mchanga huyu!”
“Hah! Mama...! Yaani kweli….?” Candy alimaka na Bi. Shakira akamkatisha.
“Kelele! Hili swala halitatoka nje ya nyumba hii! Nenda kalale huko!”
Candy alibaki akimtazama yule mama kwa kutoamini, na kwa hakika wakati ule, alitamani sana amuue yule mwanamke kwa mikono yake.
“No, Shakira…hii si sawa!” Ngamao alimlaumu mwenzi wake.
“Kwa hiyo unataka kumkamata GTZ sasa? Wewe si askari? Haya huyo hapo...mkamate basi ukamfungulie mashitaka!” Bi. Swadafu alimwambia mpenzie kwa nongwa.
Ngamao alitikisa kichwa na kubaki akiwa amejishika kiuno huku akimtazama GTZ kwa hasira.
“Oyaa…mi naenda zangu kulala…!” Greg Pasha alisema huku akimuachia Candy na kuanza kurudi chumbani kwake. Candy alijibweteka sakafuni kwa kuishiwa nguvu na kubaki akilia. Greg Pasha alisimama nje ya mlango wa chumba chake na kumgeukia GTZ.
“Kama ningekuwa wewe ningekuwa makini sana na huyu mtoto…anaonekana ni hatari sana…kigoda kingetawanyikia kisogoni kwako hicho kama sikuwahi kumzuia…!” Alimwambia, kisha akaingia chumbani kwake na kujifungia.
GTZ alimkodolea Candy macho ya hasira.
“Ulitaka kuniua mimi wewe?”
“Sasa na we’ uliyonifanyia ni mazuri? Nataka nikuue wewe na mama yako, wanyama wakubwa nyie!” Candy alifoka.
“Ah! Anasemaje kisonoko huyu…?” Bi. Swadafu alimaka huku akimfuata Candy pale alipokuwa, Ngamao akaruka mbele na kumkinga Candy.
“Okay, okay…tutulie…tutulie sote hapa!” Ngamao alidakia. Candy aliinuka na kwenda kujifungia chumbani kwake huku akilia kwa uchungu…
***
Bila ya kujijua kwikwi ya kilio cha uchungu ilimtoka akiwa ndani ya ndege baina ya wale askari wawili wa Interpol, machozi yakimbubujika kama kwamba ndio kwanza alikuwa anayapitia tena yale madhila aliyokumbana nayo ndani ya lile jumba la Bi. Swadafu.
Mmoja wa wale askari wa kike alimpigapiga pajani kwa namna ya kumliwaza.
Candy alijifuta machozi na kuegemeza kichwa chake kwenye mgingo wa kiti chake.
“Bado muda gani tufike Tanzania?” Aliuliza bila kumuangalia yeyote kati ya wale askari wawili, na mmoja wao alitazama saa yake na kumjibu kuwa bado walikuwa wana saa mbili za kusafiri angani kabla hawajatua Uwanja wa ndege wa KJ Nyerere, jijini Dar.
Candy alifinya macho na kumeza funda kubwa la mate.
Moyo uakaanza kumwenda mbio.
Bado saa mbili kabla sijaenda kukutana na macho ya watanzania waliosalitika na ushiriki wangu kwenye shindano la urembo wa dunia…nikiwa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji!
Eh Mungu wangu, usichoke kunisaidia mja wako…haya yanayonikuta hakika ni mazito kuliko uwezo wangu…
“Na kama ungenishirikisha tangu mwanzo Candy wangeshamzika saa hizi!” Greg alisema kwa hasira kidogo.
GTZ alitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
Greg alisonya na kuchukua miwani yake ya jua na kuuendea mlango wa kutokea nje ya nyumba ile.
“Mi natoka zangu kidogo…Ngamao akija hakikisha unapata dondoo zote za ujio wa muuaji wa mama!” Alimwambia nduguye.
“Unaenda wapi?”
“Kuna maandalizi yanipasa niyafanye!” Greg alimjibu na kutoka.
Geti la nyumba ya GTZ lilifunguliwa, na gari la kifahari aina ya porche likatoka na kuingia barabara kubwa, likichukua uelekeo wa katikati ya jiji. Hata wakati lile gari likikamata ile barabara kubwa, kioo chenye kiza cha upande wa dereva kilikuwa kikijipandisha na kumficha dereva wa gari lile.
Lakini sio kabla ya Nuru aliyekuwa amebana upande wa pili wa barabara akiitzama ile nyumba hajapata nafasi ya kuuona uso wa Greg uliokuwa umepachikwa miwani ya jua utosini.
Greg Pasha aliongeza kasi kuelekea mjini.
Hakuwa na sababu ya kuitilia maanani pikipiki kubwa iliyokuwa ikimfuata nyuma yake ikiwa imeacha magari mawili baina yao.
Nuru aliamua kumfuatilia yule mtu mgeni kabisamachoni mwake tangu sakata lile la Candy na GTZ lianze.
Akiwa amevaa kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki, haikuwarahisi kwa yeyote kubaini kuwa mtu aliyevaa suruali na koti vyote vikiwa ni vya kitambaa cha jinzi, aliyekuwa akiiendesha ile pikipiki alikuwa ni mwanamama…
Safari ya Greg Pasha iliishia maeneo ya gerezani jijini. Nuru aliiona ile Posrche ikisimama nje ya geti la gereji moja miongoni mwa mlolongo wa maregeji mengi yaliyozagaa eneo lile. Umakini wake ukiwa umezidi maradufu, aliiegesha pikipiki yake upande wa pili wa barabara na kubaki akiwa ameegemea usukani huku akitazama kule ambako lile gari lilipokuwa ilhali bado akiwa amevaa ile kofia yake ya kuendeshea pikipiki.
Kwa hali ilivyokuwa ni kwamba muda si muda geti la ile gereji lingefunguliwa na ile gari ingeingia mle ndani, naye asingeweza kumuona vizuri yule dereva wa ile gari.
Alimung’unya midomo yake ndani ya ile kofia ya kuendeshea pikipiki. Jamaa ndani ya Porsche alibamiza honi mara nyingine.
Kwa hali ya kawaida ingeonekana kuwa mwendesha Porsche alikuwa amepeleka gari gereji kutengenezwa. Kwa hali ya kawaida na kwa mtu wa kawaida, lakini Nuru hakuwa mtu wa kawaida. Alijua kuwa mtu mwenye kumiliki Porsche hawezi kupeleka gari kama lile kwenye gereji ya gerezani, hususan ile ambayo hata geti lake lilionekana kuwa ni la kubandika bandika tu.
Hii ilimwambia kuwa yule jamaa hakuwa ameenda pale kufuata huduma za gereji.
Sasa ni nini kilichompeleka pale?
Kule mbele geti lilifunguliwa na Porsche ikaingia ndani, kisha geti likafungwa.
Nuru aliachia dakika tano zipite, kisha akachomoa kikanyagio cha gia kwenye pikipikiyake na kukiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti lake la jinzi, kisha akaikokotea ile pikipiki hadi pale kwenye lile geti.
Akagonga lile geti kwa fujo kwa ubapa wa ngumi yake. Mara ya kwanza, ya pili na ya tatu kwa nguvu zaidi.
“Oyaaa! Nini palee…?” Sauti kutoka ndani ya lilegeti ilihoji kwa kukereka.
Nuru akagonga tena kwa nguvu zaidi, bila ya kujibu lolote.
Geti lilifunguliwa kwa ghadhabu, jamaa mfupi sana mwenye upara alijitokeza nje akiwa amekunja uso kwa hasira.
“Nini wewe…?” Aliuliza kwa hasira, na akaishia akiwa ameduwaa alipojikuta akikabiliana na sura ya mrembo aliyevalia jinzi tupu akiwa amekumbatia kofia ya kuendeshea pikipiki kwapani, akimtolea tabasamu la mvuto.
“Oh…!” Jamaa akagwaya.
“Kokotea ndani basi hii pikipiki kakaangu..imebuma ghafla tu…” Nuru alimwambia huku akimsukumia ile pikipiki naye akiingia mle ndani ya ile gereji.
“Hahh…ina tatizo gani…?” Upara aliuliza lakini Nuru tayari alikuwa ameshaingia mle ndani ya wigo mpana wa gereji ile akiangaza huku na huko. Ile Porsche ilikuwa imeegeshwa kwenye kona moja ya wigo ule, mlango wa dereva ukiwa wazi, dereva hakuwemo.
Bado saa mbili kabla sijaenda kukutana na macho ya watanzania waliosalitika na ushiriki wangu kwenye shindano la urembo wa dunia…nikiwa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji!
Eh Mungu wangu, usichoke kunisaidia mja wako…haya yanayonikuta hakika ni mazito kuliko uwezo wangu…
***
Jijini Dar Morandi alikuwa akiranda sebuleni kwa Bishkuku huku akijikuna kisogo na uso akiwa ameukunja kwa mawazo. Nuru alikuwa amekunja nne pale sebuleni akimtazama kwa utulivu. Alikuwa ameshamueleza yote yaliyojiri kule kwenye ile gereji maeneo ya gerezani, baina yake na Greg Pasha.
“Una hakika na ulichokiona kwenye ule mfuko wa rambo uliokua ndani ya lile gari?” Morandi alimuuliza tena swali ambalo alishamuuliza awali.
“Mo, nimekwambia hicho ndicho nilichokiona!Sasa hapo unataka nini tena? Mambo yako wazi…yule jamaa sio polisi …kwa hiyo naamini kabisa ana nia ya kumsaidia GTZ katika kumdhuru Candy…!” Nuru alimwambia kwa msisitizo.
Morandi aliketi kochini na kutazama saa yake.
“Na Candy nd’o anaingia usiku huu, bloody hell…inabidi tufanye kitu hapa Nuru…tena haraka!”Alisema.
“Hilo mbona liko wazi? Swala ni kwamba tunafanya nini? Najua maaskari watakuwa wanamsubiri Candy pale airport usiku wa leo…”
“Kama jinsi ambavyo watanzania lukuki watakavyokuwa wakimsubiri…pamoja na utata ulioibuka kwenye ushindi wake wa pili wa miss world…sasa na huyu mmanga koko wako aliyejitokeza leo….”
“Sio mmanga koko…ni muhindi koko!Halafu sio wangu, for your very good information!”Nuru alimjia juu.
“Poa sio ishu!Ila nadhani kama ingekuwa ni zile enzi zetu za uaskari tungevamia pale gereji na kumtia jamba-jamba yule mwenye gereji mpaka kieleweke!” Morandi alisema, na Nuru akatabasamu.
“Yaani mbona angekoma leo? Kwani hatuwezi kumuibukia na kumbana? Atajuaje kuwa sisi sio askari wa kweli?”
“No! Itatupotezea muda na itaweza kumfanya yule jamaa abadili mbinu…wacha ibaki hivyo hivyo. Wasijue kuwa tumewashtukia!”Moradi alitoa rai.
Kimya kikatawala.
“Sasa tunafanyaje juu ya usalama wa Candy dhidi ya hawa akina GTZ?” Nuru aliuliza.
Morandi alikaa kimya kwa muda, kisha akainuka.
“Nadhani najua cha kufanya sasa…mpigie simu wakili Abiyah…lazima tuongee naye haraka sana.Nahisi kuna mchezo mchafu unataka kuchezwa hapa.Bila shaka na wewe umeliona hilo!”
“Kabisa!”
“Basi huyu GTZ na muhidi koko wake lazima waelewe kuwa kuna upande wa pili wa hiyo shilingi wanayotaka kuitumia dhidi ya Candy, pumbavu zao!” Morandi alihitimisha.
“Okay!” Nuru alijibu huku akichukua simu na kumpigia wakili Abiyah Byabato.
***
Wakati Nuru na Morandi wanapanga mikakati yao, nyumbani kwa GTZ Ngamao Kijambia alikuwa akiongea na akina GTZ kwa wahka mkubwa sana.
“Ama hakika leo itakuwa ni siku muhimu sana kwangu…kwetu sote in fact!” Aliwaambia wale watoto wa marehemu Shakira Swadafu waliokuwa pamoja naye pale sebuleni.
“Kivipi, Ngamao? Kwa kuwa Candy atakuwa mikononi mwa polisi?” GTZ aliuliza kwa hasira.
“Exactly! Kifo cha mpenzi wangu…mama yenu…kitalipizwa ipaswavyo. Nitamtia pingu mimi mwenyewe, mshenzi mkubwa yule!” Ngamao alijibu.
“Mi nadhani ingekuwa siku nzuri sana kwetu kama hapa tungekuwa tunajiandaa kwenda kuhudhuria maziko yake…ili tuikebehi maiti yake!” Greg Pasha alimwambia kwa hasira nyepesi.
Ngamao akakunja uso.
“Hilo ndilo tatizo lenu nyote nyinyi! Mnadhani mkijichukulia sheria mikononi mwisho wa siku mnaishia wapi? Gerezani! Tena kwa kifungo cha maisha kama sio kuhukumiwa hukumu ya kifo! Sasa hiyo itakuwa ni faida ya nani?” Aliwakemea.
“Si mpaka nikamatwe? Kwani wangapi wanapotezwa tu humu nchini na wapotezaji tunapishana nao mitaani bwana? Candy kamuua mama yetu! Hii inapaswa iwe jicho kwa jicho!”GTZ alimjia juu.
“Mjadala huu tuliumaliza zamani!Wewe ulijaribu hilo…ona yaliyokukuta!”Ngamoa alimkemea.
“Si kwa kuwa mi sikushirikishwa tangu mwanzo?”Greg Pasha naye alidakia.
“Hebu acheni ubwege nyinyi! Nimeshasema kuwa hukumu ya kifo ataipata tu bila hata ya yeyote kati yenu kuingia kwenye maisha ya kuishi akigeika nyuma kila siku kwa kuhofia kukamwatwa na polisi kwa kosa la mauaji. Damu ya mtu nzito vijana...si mnamuona Candy? Kiko wapi…leo atakuwa mikononi mwa sheria baada ya kukimbia huku na huko kwa miaka miwili!” Ngamao aliwaambia.
Greg na GTZ walitazamana.
“Mnhu! Okay! Kama ndivyo uonavyo….kwani ni saa ngapi anaingia?” Greg alimwambia na kumuuliza huku moyo ukimwenda mbio.
“Leo saa nne usiku malaya anashuka hapa kwa Emirates! Na nitakuwa pale nikimsubiri in full uniform!”Ngamao alijigamba.
Hakuona jinisi Greg Pasha na mdogo wake walivyotupiana macho ya ushindi.
“Okay…kila la kheri katika hilo…ila ukishindwa haki ya mungu mi mamuua yule mtoto!” Greg alisema.
“Khah!Sasa nishindwe vipi?”
Greg aliguna.
“Unadhani hao watu waliokuwa wakimlinda huyu demu siku zote hizo hata wakamfanya GTZ namna hii wataacha kumuwekea mawakili waliobobea na hatimaye akaachiwa pamoja na kwamba ameua?Na hivi tayari ameshakuwa mtu maarufu duniani kwa huo ushindi wa pili wa miss world?” GTZ alimuuliza, na Ngamao akaachia kinywa wazi.
“Hilo halitatokea!” Hatimaye alisema kwa hasira.
Greg na GTZ walitazamana. Kisha Greg akainuka.
“Okay…liwalo na liwe..mi naenda kupiga usingizi wa mchana saa hizi…” Alisema huku akielekea chumbani kwake mle nyumbani kwa GTZ.
Usiku ule Candy Gamasala, mshindi wa pili wa shindano la Urembo wa Dunia, na mtuhumiwa namba moja katika kesi ya mauaji ya Bi. Shakira Swadafu, aliingia nchini akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa Interpol…
***
Uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar ulikuwa umefurika watanzania usiku ule. Wengi wao walikuwa wamebeba mabango yenye kutuma jumbe mbalimbali kuhusu mrembo wa Tanzania ambaye alikuwa anarejea nchini kwake akiwa amekamata nafasi ya juu kuliko warembo wengine wote nchini waliowahi kushiriki mashindano yale ya urembo ya dunia, lakini pia akirudi akiwa amebeba tuhuma nzito sana za mauaji.
Baadhi ya waliojirundika pale uwanjani usiku ule walikuwa wamevaa zile zile fulana zao walizovaa wakati Candy akipigania taji la urembo wa dunia kule Caracas, zenye maneno ya kumtia moyo mrembo yule, nao walikuwa wamebeba mabango yaliyonadi kuendelea kuwa naye mpaka mwisho, wakiamini kuwa alikuwa hana makosa na kwamba alikuwa amejengewa njama tu watu wachache wasio wazalendo.
Aidha kulikuwa na wengine ambao walikuwa wakilaani kitendo cha kamati ya Miss Tanzania kupeleka mrembo mpaka kwenye mashindano yale makubwa kabisa duniani bila ya kumchunguza na hatimaye amekwenda kuliaibisha taifa.
Mabango mbali yalinadi hisia za wananchi waliokuwa pale uwanjani.
Lamemba ajiuzulu!
Candy msaliti!
Muuaji Mkubwa!
Miss murderer 2013!
Tuko nawe mpaka mwisho mrembo wetu!
Ni Candy tu…hata iweje!
Ndio matatizo ya kutoa ma-miss kwa rushwa ya ngono haya!
Alimradi mabango yale yalieleza kila hisia za walioyabeba. Baadhi ya washabiki waliokuwa wakimtetea Candy wakawa wanatupiana vijembe na wale waliokuwa wakimponda Candy, mrembo Tunis akiwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakimponda Candy na kuimba nyimbo za kushinikiza adhabu ya kifo kwake, na kuvuliwa mataji yote ya urembo aliyokabidhiwa hapo awali.
Kwa waandishi wa habari waliomwagika pale usiku ule, uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere ulikuwandio eneo la mavuno kwao. Walikuwa wakijikusanyia habari na matukio kutokea kila upande. Tena ilikuwa ni waandishi wa aina zote, magazeti, redio na luninga pia. Mitandao ya kijamii pia haikuwa nyuma. Waliokuwa pale uwanjani usiku ule walikuwa wakituma picha za kilichokuwa kikiendelea pale kwenye mitandao ya Facebook, tweeter, YouTube na mingine kama hiyo. Ujio wa mrembo wa taifa muuaji ulikuwa unasubirikwa kwa kila namna ya hisia usiku ule.
Askari wengi walimwagwa pale uwanjani kujaribu kudhibiti hali ile na kudumisha amani, lakini ilikuwa ni kazi ngumu. Tafrani ilitanda kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K. Nyerere, na lile dege kubwa lilipoonekana likitua pale uwanjani, mayowe ya shangwe zilizochanganyika na sauti za kuzomea yalirindima eneo lote lile na askari wakawa makini maradufu.
Candy Gamasala alikuwa ameshuka jijini.
Katika hekaheka zote zilizokuwa zikiendelea pale uwanjani usiku ule, Inspekta Ngamao Kijambia akiwa ndani ya mavazi rasmi ya kiaskari aliingia ndani ya ule uwanja akiongozana na askari wengine wawili, mmoja wa kike.
Walipokewa na maafisa wa uwanja wa ndege na kuongozwa sehemu ya ndani kabisa mle uwanjani na kufikishwa kwenye lifti ambayo iliwapandisha hadi kwenye korido moja pweke na nyembamba.
“Hapa ndipo mtakapokabidhiana mtuhumiuwa na wale askari wa Interpol…subirini.” Mmoja wa wale maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege aliwaambia na kuondoka. Alikuwa amevaa mavazi ya kiaskari wa jeshi la polisi.
Akina Ngamao wakaketi kwenye viti vilivyokuwa kwenye eneo lile pweke na kusubiri, moyo ukimwenda mbio sana Ngamao.
***
Ndani ya ndege abiria walianza kuteremka, na wale askari wa Interpol wakamwambia Candy atulie pale pale kitini. Huku moyo ukimwenda mbio, Candy alijilazimisha kutulia.
Kokos na wenzake wote nao wakabaki wakisubiri pamoja naye. Hatimaye abiria wote walikuwa wameshatoka nje ya ndege ile, ndipo wale askari wa Interpol walipoamuru nao waanze kutoka nje.
Waliifuata korido maalum iliyounganishwa kutoka kwenye mlango wa ndege ile kuelekea kwenye sehemu ya mapokezi pale uwajani.
Msafara ule uliifuata korido ile na sehemu katikati yake akachomoza askari wa jeshi la polisi ambaye aliwaelekeza waingie kwenye mlango mwembamba kwenye ile korido na hivyo wakachepukia kwenye korido nyingine fupi zaidi.
Hii iliwafikisha kwenye ile sehemu ambayo Ngamao na wale askari wengine walikuwa wakiwasubiri.
Sehemu ya makabidhiano.
“Hello Candy…unanikumbuka mimi?” Ngamao alimuuliza Candy huku akimtazama moja kwa moja usoni.
“Hah! Anko Ngamao??” Candy alijukuta akipayuka bila kujijua, na Bishkuku na akina Labemba walitazamana.
“Usiongee lolote Candy!” Kokos alimkemea haraka.
“Yah, ni mimi yule yule. Ulidhani utakimbia milele, eeenh?” Ngamao alimsemesha Candy kwa kebehi.
“Lakini mbona sielewi??” Candy alimuuliza kwa hamaniko dhahiri.
“Shut-the-fuck up, Candy! Husikii wewe?” Kokos alimkemea.
Ngamao akawa ameshageukia kwa wale askari wa Interpol. Walipeana mikono na wakabadilishana makabrasha ya kukamatwa mtuhumiwa Candy Gamasala.
“Okay, komredi. Kuanzia hapa Candy Gamasala yuko mikononi mwako na mikononi mwa jamhuri ya Tanzania!” Mmoja wa wale askari wa Interpol alisema, na Ngamao akasaluti.
“Oh, yeah! Yuko kwenye mikono halali ya jamhuri huyu. Hatoki hapa!” Alisema kwa nongwa.
Wale askari wa Interpol wakageuza na kurudi kule walipotokea na kuifuata ile korido ya kwanza kuelekea sehemu ya mapokezi ya ule uwanja, wakionekana kuwa ni raia tu miongoni mwa raia wa kigeni walioingia nchini usiku ule.
Huku nyuma, Ngamao aliwageukia akina Kokos.
“Okay, nyie safari yenu inaishia hapa. Rudini kule kwenye korido ile mkapitie kule mapokezi kama wasafiri wengine. Sisi na Candy tutapitia huku…”
“No way! Candy anatakiwa awe na wakili wake…ambaye anamsubiri huko nje. Sasa atajuaje kuwa mko naye huku?” Kokos alihoji.
“Hilo si tatizo letu!” Ngamao alimjibu na kumuongoza Candy kwenye mlango wa ile lifti iliyowakifikisha pale mahala hapo awali.
“No! Nahitaji kuonana na watanzania jamani! I must meet them hata kama nina shutuma hizi!” Candy alipinga.
“Kimya wewe! Kuanzia sasa uko chini ya ulinzi!” Ngamaoalimkoromea wakati mmoja wa wale askari wenzake akibonyeza kitufe cha kuiita ile lifti ije iwashushe kule chini.
“Huko unataka kwenda kuzomewa tu mwanadada! Kaa kimya ufuate maelekezo hapa!” Yule askari wa kike aliyeandamana na Ngamao alimwambia. Muda wote huu Candy alikuwa amevaa ule utepe wake uliomnadi kuwa yeye ni mshindi wa pili wa shindano la miss world kifuani kwake, na alitaka wananchi wamuone akiwa ameuvaa ule utepe kwa macho yao, moja kwa moja pale uwanjani. Kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kwa utepe ule wa mashindano yale makubwa kabisa ya urembo duniani kuingia Tanzania, na ni yeye ndiye aliyeufikisha nchini utepe ule. Alitaka watu walione hilo na wasilisahau hilo, pamoja na zile shutuma nzito zilizomuangukia.
“Hilo si swala lako! Ni mimi ndiye nitakayezomewa…we’ shida yako nini?” Candy alimjia juu, na muda huo ule mlango wa lifti ulifunguka na askari mwingine mwenye sare za polisi alikuwa akiwasubiri mle ndani. Wote wakaingia ndani ya ile lifti, Candy akiwa amechanganyikiwa vibaya sana…
***
Muda Ngamao alipowazuia kuingia kwenye lifti pamoja nao na kuwarudisha kule kwenye ile korido ndefu iliyotokea kule kwenye mlango wa ile ndege, Kokos alitoa simu yake na kuiwasha. Akampigia Morandi.
“Oya! Sisi tumeshatua nchini. Candy amechukuliwa na maaskari huku huku kabla hata hatujafika huko mapokezi…”
“Wamempeleka wapi?” Morandi alihoji kwa wahka.
“Sijui…ila tumewaacha wanasubiri lifti ambayo bila shaka ndio itawashusha huko chini…sa’ sijui ile lifti inatokezea wapi huko chin…”
“Okay! Roger that! Nimekusoma…inabidi nitafute namna…tutawasiliana!” Morandi alimkatisha na kukata simu. Kokos alibaki akiikodolea macho ile simu kwa mshangao. Alijaribu kumpigia tena Morandi, lakini akapata jibu kuwa simu ya yule jamaa ilikuwa haipatikani. Akaachia sauti ya kukereka na kujaribu tena mara nyingine tatu, na zote jibu likawa ni lile lile.
Akamtukania Morandi mama yake, na kuiweka simu yake mfukoni.
***
Lifti iliwafikisha ghorofa ya pale mapokezi na milango ikafunguka. Wakatoka nje ya ile lifti na hapo Ngamao akatoa pingu na kumwambia Candy anyooshe mikono yake mbele.
“Una…unataka kunifanyaje sasa?” Candy aliuliza kwa mashaka.
“Nyoosha mikono upigwe pingu bibie…si unataka kwenda kuonana na wanachi wako wewe? Utawaona ukiwa na pingu mikononi…ready for that?” Ngamao alimkoromea kwa hasira.
Candy alimeza funda la mate.
“Kwa…kwani mi ’ n’takimbia jamani! Sitakiwi kuonana na wananchi katika hali hiyo! Utanifunga hizo pingu baada ya hapo, lakini kwa sasa…”
“Pingu mikononi, au huonani na mwananchi yoyote! Mi’ nakufanyia msaada tu hapa, hivyo amua upesi. Safari yetu bado ndefu mwanamke…so usin’potezee muda hapa!” Ngamao alimkoromea huku akimtazama kwa hasira.
Candy alimtazama kwa hasira vile vile, kisha akamnyooshea mikono kijeuri bila ya kusema neno zaidi.
“Good girl!”Ngamao alimwambia kwa kebehi huku akimpinga pingu mikono yake kwa mbele. Kisha akamshika kiwiko cha mkono wake na kumuongoza kuelekea ile sehemu ya ukaguzi wa pasipoti. Badala ya kupanga foleni kama wasafiri wengine, wao waliingia naye kwenye chumba kingine kidogo, na huko pasipoti yake ikagongwa mihuri itakiwayo kisha akarudishiwa. Kutoka hapo walielekea kwenye lango la kutokea nje ya uwanja ule, ambako raia wenye michanganyiko ya hisia walikuwa wakimsubiri.
Miss Tanzania na mshindi wa pili katika shindano la urembo wa dunia Candy Gamasala alitokeza nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K. Nyerere akiwa ameshikiliwa viwiko na askari wenye sare kila upande, Ngamao akiwa amemshika kiwiko cha mkono wa kulia na yuke askari mwingine wa kike akiwa amemshika kiwiko cha mkono wa kushoto.
Muda alipotokeza tu nje ya ule uwanja mlipuko wa mayowe ulisikika,ukiwa ni mchanganyiko wa shangwe, mizomeo na pia miguno ya fadhaa. Haijawahi kutokea mrembo wa taifa akarejea nchini akiwa na pingu mikononi hata siku moja katika historia ya taifa hili, na ile picha ilileta mchanganyiko wa hisia mpya kwa wananchi. Kamera za waandishi wa habari zilimpiga picha mfululizo akiwa katika hali ile, zikiwemo kamera za watu binafsi waliotumia simu zao kumpiga picha namna ile. Candy alijitikisa kwa nguvu na kuchomoa mkono wake kutoka kwenye himaya ya yule askari wa kike, lakini Ngamao alimng’ang’ania, lakini Candy akazidi kuuvuta kwa nguvu mkono wake na Ngamao akamuachia.
Akainua juu mikono yake yenye pingu na kuwafanyia watanzania ishara ya amani kwa mikono yake miwili huku akiwaameachia tabasamu la kweli usoni kwake, na pamoja na zile pingu, umma wa watanzania pale uwanjani ulijikuta ukibadili muelekeo na kuhamishia hisia zao kwake.
“Tuko pamoja nawe Candyyyyy!”
“Pole kwa yote mrembo wetu….mungu atakuvusha!”
“Malaya muuaji mkubwa wewe!”
“Alaaniwe aliyekubebesha shutuma hizi mrembo na mkombozi wetu!”
“Tunajua hiyo ni kazi ya ma-freemason tu! Washindwe na walegee!”
“Una nini la kuliambia taifa juu ya ushindi wako na shutunma hizi nzito dhidi yako?” Sauti na maswali ya baadhi ya waandishi wa habari vilivurumishwa kwake.
Yeye alibaki akiwa anatabasamu vile vile tu, akiwa ameinua mikono yake juu na ule utepe wa miss world uliomnadi kuwa ni mshindi wa pili ukionekana wazi wazi kwa kila mtu pale uwanjani ukiwa umelala kifuani kwake.
Mrembo wa taifa wa mwaka uliopita aliyekuwa ameandaliwa kuja kumlaki na kumvika shada la maua alisogea mbele na kutaka kumkumbatia, lakini wale askari walimzuia, na Ngamao akajisogeza mbele ya mmoja wa waandishi wa habari aliyekuwa pale uwanjani.
“Eenh! Tunawaomba radhi wananchi kuwa Bi. Candy Gamasala, kama wengi mlivyosikia kwenye vyombo vya habari anakabiliwa na tuhuma nzito za mauaji, na hivi sasa yuko chini ya ulinzi. Kwa sababu hii hatoweza kushiriki katika matukio yoyote yaliyoandaliwa kwa ajili yake hapa uwanjani. Aliomba aje kuonana nanyi kidogo tu nasi tumempa fursa hiyo…na sasa itabidi turudi naye ndani kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine za kipolisi!” Ngamao aliongea.
“Tungependa kusikia kauli kutoka kwa Candy kuhusu hili…”Mmoja wa waandishi wa habari alidakia, na kabla Ngamao hajajibu, yule mwandishi akamgeukia Candy, “Er, Candy… kwanza hongera sana kwa kushika nafasi ya pili katika shindano la Miss world lililokamilika hivi karubuni huko Venezuela…je nini mtazamo wako juu ya hizi tuhuma zinazikukabili…ni kweli umemuua Bi. Shakira Swadafu?”
Bila kusita wala kutetereka Candy akamjibu.
“Ahsante sana. Napenda watanzania wazingatie ushindi niliowaletea na kwamba hakuna mrembo yeyote aliyewahi kuwafikisha pale nilipowafikisha mimi katika mashindano haya ya urembo wa dunia. La pili ni kwamba nataka watanzania wote waelewe kuwa mimi sina makosa na sihusiki na kifo cha Bi. Swadafu. Mwisho wayote itajulikana kuwa sikumuua huyo mtu na hapo ndipo wale walioleta shutuma hizi dhidi yangu watakapokuwa na jukumu la kuwaeleza watanzania ni kwa nini walidiriki kuwanyima furaha niliyowaletea kwa kunibebesha tuhuma zisizo na ukweli. Ahsanteni sana wananchi na naomba dua zenu!”
Kwisha kusema hivyo akamgeukia Ngamao aliyebaki akiwa amepigwa bumbuwazi. Alikuwa ametarajia Candy aangue kilio mbele ya kadamnasi na azidi kumshusha hadhi mbele za watu, lakini kinyume na hayo Candy amemshangaza…kwa mara nyingine tena.
“Twende huko unipelekapo sasa!” Candy alimwambia huku akipuuzia maswali mengi ya mfululizo kutoka kwa waandishi wa habari waliozidi kutuma maswali ya kufuatilia ile kauli yake.
Ngamao alimkamata kiwiko na kuanza kumuongoza ndani ya ule uwanja.
“Subiri!” Sauti iliita kutokea kwenye kundi la wananchi waliojazana pale uwanjani, na haraka wale askari wengine wakatoka mbele kumzuia yule mwenye ile sauti asisogee karibu zaidi na alipokuwa Candy.
“Abiyah Byabato! Wakili wa Candy…nimekuwa nikimsubiri mteja wangu hapa, sasa naona mnamuingiza tena huko ndani. Natakiwa niwe naye na sheria inasisitiza hilo!” Mwanadada mrefu mweusi aliyekuwa amesuka rasta na akiwa ndani ya suti nyeusi safi ya kike alijisukuma mbele huku akimuonesha Ngamao kitambulisho, nyuma yake akifuatiwa na mwanadada mwingine aliyekuwa amevaa suti kama yake na akiwa amebeba mkoba wa kiofisi.
Candy alimtazama yule mwanadada aliyekuwa akiongea kwa lafudhi ya kihaya. Askari walitaka kuendelea kumzuia, lakini Ngamao akawazuia.
Alichukua kile kitambulisho na kukitazama, kisha akamrudishia kile kutambulisho.
“Na huyo?” Aliuliza huku akimuoneshea yule mwanadada mwingine aliyekuwa nyuma yake,
“Msaidizi wangu…paralegal huyo…yuko pamoja nami” Wakili Abiyah Byabato alimjibu, na hapo hapo yule msaidizi wake akajipenyeza na kusimama kando ya bosi wake.
“Candy…” Abiyah aliita huku akimpa Candy mkono. Candy akaupokea mkono wake kwa mikono miwili kutokana na kufungwa zile pingu.
“Umeulizwa maswali yoyote kabla ya ujio wangu?” Abiyah alimuuliza huku akimtazama moja kwa moja machoni. Candy kwa muda alikuwa amehamishia macho yake kwa yule msaidizi wa Abiyah Byabato, ambaye alikuwa ameinamia mkoba uliokuwa mkononi mwake wakati ule.
Akamgeukia Abiyah.
“Aam…hapana. Hakuna maswali yoyote niliyoulizwa kuhusiana na tuhuma hizi mpaka sasa…” Alimjibu, akili ikimzunguka.
“Good. Kuanzia sasa niko kwa ajili yako. Kila utakaloulizwa kuhusu kesi hii, utaulizwa mbele yanguna utajibu kwa maelekezo yangu. Kokos anakusalimia!” Abiyah alimwambia, na kumalizia kwa kauli iliyolenga kumfanya Candy aelewe kuwa alikuwa ametumwa kumwakilisha kwenye kesi ile na Kokos Wandiba. Candy alitikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa amemuelewa.
Abiyah akamgeukia Ngamao.
“Kulikuwa kuna haja yoyote ya kumfunga pingu mteja wangu namna hii?” Alimuuliza kwa hasira.
“Anakabiliwa na kesi ya mauaji...hiyo inamfanya awe mtu hatari sana. Pingu zinamhusu!” Ngamao alimjibu kwa hasira.
“Anakabiliwa na tuhuma za mauaji…hivyo mpaka tuhuma zitakapothibitishwa kwenye mahakama ya sheria…yeye hana makosa na pingu hazimhusu. Mfungue hizo pingu mteja wangu sasa hivi!” Abiyah akambadilikia.
Ngamao alimkodolea macho ya kutoamini. Akafunua kinywa kutaka kuongea akakosa la kusema.
“Nasema mteja wangu afunguliwe hizi pingu name sitaliingiza hili swala kama ukiukwaji wa haki za mtuhumiwa wakati wa kuwekwa chini ya ulinzi…je mteja wangu alitishia kukimbia au kutoroka hata mkalazimika kumtia pingu?” Abiyah alizidi kuhoji.
“Mfungue!” Ngamao alikoroma kwa hasira, na Candy akafunguliwa zile pingu.
“Good cop!” Abiyah alimwambia kwa kebehi, na pamoja na madhila yake, Candy alijikuta akiachia kicheko chepesi. Ngamao alimtumbulia macho kwa hasira.
“Twendeni!” Aliunguruma na kuwaongoza tena ndani ya ule uwanja.
Huku nje, makelele kutoka kwa wananchi yalizidi.
Ngamao aliouongoza ule msafara hadi pale kwenye ile lifti na wote wakaingia tena ndani yake.
“Tunaendelea na safari yetu sasa!” Aliwaambia wote mle kwenye lifti, na hapo hapo akabonyeza kitufe kilichoiamuru ile lifti ishuke chini zaidi ya ile sehemu ya mapokezi, na Candy akazidi kuchanganyikiwa.
“Mnatupeleka wapi?” Abiyah Byabato aliuliza.
“Mmetaka safari…so kaeni kimya mu-enjoy msafara!” Ngamao alimjibu kwa kiburi. Wale askari waliokuwa na Ngamao, na yule mwingine waliyemkuta mle kwenye ile lifti hapo awali walibaki kimya.
“Nina imani kuwa sasa Candy anajihisi kuwa kweli yuko kwenye mikono salama…!” Ngamao aliwakoromea huku akimtolea Candy tabasamu baya.
Lifti ilifika chini kabisa ambako milango yake ilifungukia kwenye korido iliyoelekea sehemu ya kuhifadhi mizigo ya wasafiri kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine ilikuwa ikielekea upande ambako ndege zilikuwa zinaegeshwa kwenye sehemu ya ule uwanja wa ndege.
***
Dakika tano tu baadaya akina Ngamao kurudi kwenye ile lifti, Kokosna wenzake wakafika eneo la mapokezi na kukuta bado kuna foleni ya ukaguzi wa pasi za kusafiria. Kutokea pale walipokuwa hawakuweza kuuona msongamano wa watu kule nje waliokuwa wamehamanishwa na kile kilichotokea pale uwanjani dakika chache zilizopita. Haikuwa mpaka walipokuwa wakisubiri mabegi yao pale kwenye mkanda wa kuleta mabegi kutokea sehemu ambako mizigo huwa inashushwa kutoka kwenye ndege, ndipo walipoweza kuona msongamano wa watu kule nje kupitia kwenye vioo vikubwa vilivyotenganisha eneo lile walilokuwepo na kule ambako wananchi huwa wanawasubiria wageni wao.
“Unadhani tutakutana na hali gani huko nje Kokos?” Bishkuku alimuuliza kwa mashaka makubwa.
“Huko ni balaa tupu ndugu zangu!” Mwanadada wa kamati ya Miss Tanzania aliwaambia huku akiendelea kutazama iPad yake iliyokuwa ikimpa habari za kulichokuwa kikijiri kule nje kupitia YouTube.
“What?” Bishkuku aliuliza kwa wahka. Mwanadada akamuonesha picha za YouTube zilizotumwa mtandaonikutokea pale pale uwanjani, na akina Kokos walipoona jinsi Candy alivyokuwa akijibishana na waandishi wa habari akiwa na pingu mikononi waliachia vinywa wazi.
“Oh, pumbavu! Ina maana yule jamaa ndio amemdhalilisha Candy namna hii? Where the hell alipo Abiyah sasa, for God’s Sake?” Kokos alilaani huku akiuliza ni wapi alipo wakili Abiyah. Kwani ile video iliyorushwa mtandaoni iliishia tu pale Candy alipomaliza kutoa kauli yake.
“Na kibaya zaidi…Tunis yuko mstari wa mbele kumkamdamiza Candy, bloody bitch!” Hakeem Labemba alikoroma kwa hasira huku akitupia macho kile kilichokuwa kikionekana pale kwenye iPad ya yule binti wa kamati ya Miss Tanzania.
“Mwana izaya mkubwa!” Bishkuku alilaani huku akiikodolea macho video nyingine ya YouTube iliyokuwa ikimuonesha Tunis akiwa na bango lisemalo “Avuliwe mataji yote!”.
“Anashinikiza hivyo kwa kuwa anajua iwapo Candy atavuliwa taji la Miss Tanzania kwa tuhuma hizi, ni yeye ndiye atakayevikwa…kama mshindi wa pili wa miss Tanzania, bloody, stupid, bitch yule!” Hakeem alizidi kumlaani, na Bishkuku akahisi msisisimko ukimtambaa mwilini.
“Hilo halitatokea! Au ni wao ndio waliopika fitna hizi?” Alimaka.
“Achana na hilo sasa. Madhali swala limeshafika mikononi mwa sheria, kila kitu kitakuwa wazi tu…haijalishi ni nani aliyepika hizi fitna…!” Kokos alimkoromea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dakika chache baadaye walitoka nje ya uwanja ule wakiwa na mabegi yao pamoja nayale ya Candy, na Hakeem Labemba akakutana na kundi la waandishi wa habari waliokuwa wanataka majibu ya kile kilichotokea kule Venezuela, na hatima ya Candy Gamasala.
“Nataka watanzania wote waelewe kuwa Candy Gamasala bado ni mrembo wa taifa hili kwa mwaka huu, na pia bado ni mshindi wa pili wa miss world kwa mwaka huu. Hali itabaki hivyo mpaka pale tuhuma dhidi yake zitakapothibitika au zinatakapofutwa katika mahakama ya sheria. Muda huo ukifika, kutegemea na hukumu itakayopitishwa dhidi yake, ndipo maamuzi ya kamati za Miss Tanzania na ile ya miss world yatakapowekwa wazi kwa wote.Kwa sasa nawaomba watanzania waendelee kumpongeza kwa matokeo mazuri aliyoliletea taifa na kuviachia vyombo vya sheria vifanye kazi yake. Ahsanteni!”
Kwisha kusema hivyo, yeye na msafara mzima wa akina Kokos wakaelekea kwenye magari yaliyokuwa yakiwasubiri pale uwanjani na kuondoka, wakiwaacha wananchi waliojazana pale uwanjani nao wakitawanyika na mabango yao…
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment