Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

SUPRISE - 3

 








Simulizi : Suprise

Sehemu Ya Tatu (3)







Aliingia jikoni Eve kumuandalia Victor chakulakizuri na tena kile akipendacho, alikipika kwa ustadi wa hali ya juu. wakati kikiendelea kukamilika akawa anamuandaa na Bill kimavazi. Chakula kilipokuwa tayari, Bill nae alikuwa yupo tayari. Akampa Bill chakula na kingine kukiweka kinapo stahili.

Huku chozi likimtoka, Eve akashika kalamu na karatasi na kuandika maneno yafuatayo;

'Victor sikustahili kukutendea hiki nilicho kutendea, lakini kwa sababu ndio tayari nimeisha tenda, ina maana inakuwa nimekukosea, hivyo ninastahili adhabu. Umekuwa ni mwema sana kwangu, umenipa kila ninachotaka, tena kwa wakati niutakao, lakini bado nimekusaliti, hujawahi kunipiga, lakini ninahofia adhabu nitakayoipata kutokana na maswali utakayo niuliza.'

'Ninajua fika kwamba sitakuwa na majibu kutokana na maswali utakayo niuliza, hivyo ninaona ni vema nijiadhibu mimi mwenyewe. Victor bado ninakupenda sana na ndio maana sipendi kuonana nawe ana kwa ana. Nikikumbuka upweke wangu wewe ndio uliutoa, ukanivusha kwenye bahari ya matatizo iliyokuwa na kina kirefu.'

'Ajabu sasa eti mimi mwenyewe nimejipeleka kwenye msitu wa majonzi wenye wanyama wakali wenye uchu wa nyama kutokana na usaliti wangu, hakika sistahili hata kidogo kuitwa mpenzio japo naongeza kosa jingine la kuondoka bila kukuaga mume wangu, najuta Victor, ninaomba unisamehe baba mtoto wangu.'

'Ninakupenda kwa dhati Victor wangu lakini hata nafsi yangu inanilazimu kukuambia ni heri utafute mwanamke mwingine ambae atakupenda zaidi yangu na kutokukusaliti ili umuoe na kuziba pengo langu.'

'Ni zaidi ya mwaka mzima sasa Victor nimekuwa nikikusaliti, hakuna chochote zaidi ya ujinga tu ndio ulionipelekea kukusaliti, amini sikufai, niache niende, wala usihangaike kunitafuta bali tu ninaomba unisamehe.'

Mume wangu nina ondoka na mtoto wetu wa pekee Bill, usiwe na shaka nae, atapata matunzo yote yanayo mstahili, kwani yeye hahusiki na lolote kati ya matendo ya kiovu niliyoyafanya. Pia ninaamini hata dada Lidya na Shem Ommy hawatafurahi juu ya jambo hilo, hivyo nimeona ni heri mimi niende kule kusikojulikana.'

'Baba Bill nitakujulisha nitakapokuwa, amini bado nakupenda sana na milele itakuwa hivyo. Nakutakia mafanikio katika kila nyanja ya maisha yako, kuanzia kwenye kwenye kampuni ya LOVE.com hadi kwenye Romantic love'

Akupendae kwa dhati lakini akakusaliti,

Mama Bill - Evelyn.

Akairudia kuisoma tena kuanzia mwanzo hadi mwisho, aliporidhika kuwa ipo sawa, akaibusu na kuiweka katika CD ya Aurus Mabele ile album ya Evelyn ambayo Victor hupenda kuisikiliza kila mara. Akatoa begi lake na kuliingiza ndani ya gari lake, yaani ile Escudo, akarudi ndani ya nyumba yao na kukiangalia chumba chao kwa mayonzi.

taratibu machozi yakawa yanashuka shavuni huku akisema kwa sauti ya ndani ya nafsi ambayo haisikiki

"Kwa heri nyumba ambayo niliamini nitafia ndani yake, kumbe nilijidanganya, kwaheri ya kuonana." akaziangalia picha zao ukutani.

Akahisi hakuna kipya anachokipata zaidi ya machungu, akamnyanyua Bill aliekuwa kakaa kwenye sofa akicheza, akatoka akiwa amemshika mkono na kufunga mlango wa nje.

Wakaingia garini na kugeuza ili watoke kuelekea asipo pajua. Bill akauliza ni wapi wana kwenda, mama yake aamjibu kuwa wanakwenda kumtembelea bibi yake. Bill akahoji tena mbona baba Bill hawaendi nae.

Lilikuwa ni swali gumu mno kwa Eve, maana ni kweli, ilikuwa ni kawaida kila wakitaka kwenda kwa bibi yake Bill, iwe kwa Mama Eve au kwa Mama Victor, basi ilikuwa ni lazima waende wote. Akalazimika kumdanganya kuwa baba Bill ametangulia huko nao watamkuta kule akiwasubiri.

*******



"Hallow Ondiek upo wapi?" lilikuwa ni swali la Eve bila hata salamu akiwa amepaki pembeni ya barabara ndio akili ikamuijia ya kumtafuta hewani Ondiek.

"Nipo Studio, nawe upo wapi Eve?"

"Mimi nipo njiani naelekea wapi sijui, naweza kukuona sasa hivi?"

"He mbona sasa sikuelewi?" Baada ya swali lile la Ondiek, ambae kiukweli alikuwa hamuelewi hasa pale aliposema hajui anaelekea wapi, Eve akawa ni mkali na kuuliza kwa hasira

"Nasema hivi nahitaji kukuona sasa hivi, tutaonana wapi muda huu huu?"

"Ok! sasa basi kama ni kitu cha haraka sana basi njoo hapa hapa Studio tukutan..." akamkata

"Sitaki kufika hapo Studio, sasa kama nawe hutaki kuonana nami niambie." Masikini Eve alikuwa kama mtu alie changanyikiwa, alikua mkali kwa kila kitu hata ambacho hakikupaswa kuwa mkali, hata Ondiek akishangaa

Kha! Eve, mbona hivyo, leo umekuwaje..." Hata kabla Ondiek hajamaliza kauli yake, Eve alikata simu na kuanza kulia huku akiilaumu nafsi yake

'Maisha gani haya? Hii adhabu ninayoipata leo, siku hii moja, nafikiri ninaistahili...' Mlio wa simu yake ukapeperusha mawazo yake. Aliitazama na kukuta ni Ondiek ambae sasa alikuwa amempigia kumjulisha ni wapi wakutane. wakafikia pia muafaka kuwa tangu muda ule Eve azime simu, hadi watakapo onana jioni ndio watafikia muafaka ni nini cha kufanya.

Saa 9 na nusu alasiri, kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar Es Salaam, Victor aliteremka akiwa na hamu ya kumuona mkewe na mwanae. Alipita sehemu zote husika na kumaliza taratibu zote za pale uwanjani kama inavyotakiwa, akiamini kule nje atalakiwa na mkewe Eve na mwanae Bill.

Ajabu alipotoka nje hakuona gari yoyote katika gari zao mbili, akahisi huenda amekwamishwa na msongamano wa jiji la Dar ama huenda amejisahau. Kwa mapenzi makubwa alio kuwa nayo kwa mkewe, akapanga amuachie kama robo saa akiona kimya ampigie.

Lakini basi ilifika? Maana aliona karibu kila mtu anaondoka, akatoa simu na kumpigia mkewe, jibu alilolisikia ikamlazimu tu kuita Taxi na kuingia, akamuelekeza dereva hadi nyumbani kwake. Alipofika akamlipa na kushuka. Kwa funguo yake ambayo huwa anatembea nayo, akafungua na kuingia ndani.

Hakuona badiliko lolote mle ndani, ila ukimya tu ndio ulikuwa umetawala, na sababu ilikuwa wazi, patakuwaje na mishemishe ilihali hakuna mtu? Lakini kutokuwepo kwa msaidizi wao ndio kuliko mpa shaka, lakini akajipa moyo tu huenda mkewe ametoka nao wote na hawatochelewa kurejea.

Alielekea chumbani kwake na na kuingia bafuni kuoga huku akisikia harufu nzuri ya Pilau ikinukia, akajua kabisa kwamba mkewe mama Bill amemuandalia chakula kile yeye. Akaoga harahka haraka, kisha akaenda kula mbiombio, baaada ya kushiba tu akarudi chumbani kujipumzisha.

kitandani alipokuwa kajipumzisha, alikuwa akimsubiri Eve arudi, sasa alijenga imani kuwa Eve atakuwa Studio ndio maana kazima simu na Bill atakuwa ametoka na Sarah na huenda watakuwa yupo kwa mmoja wa babu zake, akageuka upande wa pili na kuchapa usingizi.





Baada ya kutoka studio, Ondiek alimfuata Eve sehemu aliyo mwambia amkute. Alimkuta na kumchukua pale kisha akampeleka maeneoya Tabata kwenye hotel ya Wallet na kuanza kuongea nae. Pale waliongea kwa muda mrefu sana na muda wote huo Eve hakuwa ni mwenye furaha hata kidogo.

Muda wote machozi yalikuwa yakimtoka, majuto yalikuwa yamemtawala na kila wakati alikuwa akimlaumu Ondiek kwa kuyeyusha furaha yake kutokana na kumlaghai na kusababisha matatizo yote yale yaliyo tokea sasa. Ondiek alijitahidi sana kumshawishi Eve arudi kwa mumewe lakini ilishindikana.

Aligoma kabisa na mwishoni wakaamua ni heri wakatafute nyumba ya wageni walale kwa usiku ule mmoja kisha mengine yatajulikana kesho pindi kutakapo kucha.

Saa 12 na nusu jioni ndio Victor alishtuka kutoka kwenye usingizi mzito aliokuwa amejilaza. Akanyanyuka kitandani na kuchukua simu yake kuangalia kama labda hata kuna ujumbe ama missed call toka kwa mkewe, lakini kukawa hakuna kitu.

Akapiga tena namba ya mama Bill, jibu likawa ni lile lile tu kwamba hapatikani, akabadili upepo, sasa akapiga ofisini, akajibiwa kuwa Eve aliomba ruhusa tangu jana kuwa anaumwa na hatofika kazini kwa siku 3. Hakutaka kujua zaidi ya hapo, akakata simu na kupiga kwao na Eve.

Mzee Dotto ndio alipokea simu, na baada ya salamu alipomuuliziamkewe akaambiwa kule hajafika tangu siku ile waliyokwenda wote pamoja na mtoto wao. Akashusha pumzi kwa nguvu na kuiangalia simu yake kama kwamba ni mpya ndio kainunua leo ama tuseme sasa hivi.

Akapiga namba zingine sasa, ila safari hii alipiga Victoria kwa wazazi wake yeye Victor, kule alimpigia mama yake. Jibu la huko halikupishana na jibu la Mzee Dotto, lilikuwa ni lile lile, kwamba hajaonekana kule tangu walipotoa miguu wakiwa pamoja na Bill.

Victor akahisi akikaa ndani atachanganyikiwa, akaona ni heri atoke na kwenda kujichanganya sehemu yoyote ile. Yaani aondoke ile sehemu ya upweke na aende akatafute angalau mapumziko ya moyo wake. kwani aliamini hawezi kupata faraja akiwa mpweke.

Wazo la kwanza lilikuwa ni kwenda Studio, kule aliamini ndio patakapo mpa faraja, kwani kuna mambo mengi hufanya na Eve, hayo aliamini ndio yatakayo rudisha amani na furaha kwenye mtima na hatimae anakuwa na faraja, hivyo ndivyo alivyo amini ndani ya nafsi yake.

Mlango aliufunga na kuingia garini kuanza safari ya kuelekea Classic House zilipo ofisi za Classic FM, ambapo alijua pindi akikutana na Ondiek huenda akapata habari yoyote kuhusu Eve, ukizingatia yeye ndio Radio Manager wa Classic FM.

Alipowasili Studio alishuka garini na kupanda ngazi kwa kasi akiwa ni mwenye furaha 2 kama kawaida. Macho yake yakakutana na msichana ambae anajua fika kuwa anamfahamu, alimtazama kwa makini, lakini katu hakumkumbuka jina.

Msichana yule nae alikuwa akimtazama Victor, na ndio akawa wa kwanza kumsemesha

"Samahani kaka, habari ya saa hizi?" Victor akamjibu kifupi tu kuwa mzuri huku akimtazama kwa shauku ya kutaka kumjua mtu huyu ni nani, japo alianza kuitambua sauti.





Na yule binti kama vile alikuwa akiisoma akili ya Victor, akaendelea



"Samahani kaka, ninakufananisha na mkaka mmoja hivi ninae mfahamu, sijui nimekosea?"



"Hata nami sina uhakika, ila ninakufananisha na msichana mmoja aitwae Sabrina, sijui nimepatia?"



"Aah! Victor... Una kumbukumbu nzuri." Alisema Sabrina huku akimkumbatia Victor, walifurahi



"Habari za siku nyingi?" Aliuliza Victor akijihisi kupoteza kumbukumbu ya matatizo yake yote na kujihisi kama vile kawa mpya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"Ni nzuri tu upande wangu, sijui wewe huko?" tabasamu ziliwatawala wote nyusoni mwao. Waliongea kwa takriban dakika kama 5 hivi wakiwa wamesimama pale pale kwenye ngazi, ngazi ambazo Victor alimuona Eve kwa mara ya kwanza, leo amekutana na mtu aliepotezana nae kwa muda mrefu eneo lile lile.



Mwishoni wakaamua kutoka na kwenda kuongelea ndani ya gari ya Victor. Wakiwa ndani ya gari walikumbushana mengi sana, ikiwepo hata vile Sabrina alivyo wakimbiza shuleni kutokana na uzuri wake na kuwa ni mtoto wa ghorofani. Sabrina alicheka sana, maana alikumbushwa mbali sana, maana ilikuwa ni miaka ya 2000 hiyo wakiwa sekondari.



"Sina haja ya kuuliza, najua ni lazima sasa utakuwa na familia, vipi haijambo?" Aliuliza Sabrina.



"Eenh, familia yangu haijambo, wewe kwa sasa upo wapi Bina?" Wakiwa shule walikuwa wamezoea kumfupisha jina badala ya Sabrina, walimuita Bina. Alijibu kuwa kwa sasa anaishi Kampala na anafanya biashara mbalimbali.



Hata ile safari ya kuwepo pale, kuna mzigo alikuwa amefuata. Victor alipomdadisi ni mzigo gani, akamwambia amekuja kufuata samaki aina ya Kamba ambao yeye huwanunua na kuwauza kwenye mahoteli makubwa makubwa hukohuko Kampala. Victor aliridhika na kuona hapa kwa huyu msichana kuna fursa ya kuunganisha nguvu.



Victor akatazama saa na kumuuliza Bina kama wanaweza kupata muda na wakakaa na kuongea zaidi, maana ni siku moja tu iliyopita nae alikuwa Kampala alipokwenda kutafuta mtu ambae anaweza kuwa ni mwenyeji wao kwa ajili ya kampuni yao iitwayo LOVE. com, alimueleza wazo la kuisambaza Afrika Mashariki yote na kufungua matawi kila mji mkubwa.



"Hiyo ndio ilikuwa ni sababu ya kukuomba muda wa kuongea nawe Bina kama hutajali," alimueleza Victor huku akimtazama usoni, Sabrina akajibu amekubali lakini pia



"Unajua Victor pamoja na kuletwa na biashara, lakini kuna jambo lingine tofauti limenileta, napaswa kulishughulikia pia kipindi hiki hiki." Akakunja sura na kuangalia chini, akaendelea



"Jana asubuhi nilipata gazeti moja la hapa Bongo liitwalo 'HABARI ndio hiyo' likiwa na habari inayo muhusu mume wangu, ambae ni mfanyakazi wa hapa Classic FM, kama Meneja..." Victor akashtuka na kuhoji hata kabla Sabrina hajamaliza



"Ondiek ndio mumeo?"



"Ndio, yule ni mume wangu na tulizaa nae mtoto mmoja ila kwa bahati mbaya mwaka jana alifariki." Alisema Sabrina kwa huzuni, Victor akampa pole na kumwambia hayo ni mapenzi ya Mola, ni lazima yatimie.



Kufikia hapo sasa ndio Victor akaelewa kuwa muhusika wa habari ile aliyoiona kwenye gazeti la ‘HABARI ndio hiyo’ ni Ondiek, akajilaumu sana kwa kutokulisoma vizuri gazeti lile na kutokuwaangalia vizuri wahusika, huenda nae angeweza kuwajua na hata ingekuwa ni rahisi kuwatambua.



Akiwa bado anatafakari ni hatua gani achukue muda ule, simu yake iliita na katika kioo cha simu likatokea jina la Evelyn, akamuomba radhi Sabrina kwa mumwambia anaomba apokee simu ya mkewe, Bina akatikisa kichwa na Victor akasogea pembeni kidogo na kupokea.



“Hellow baby…”



“Samahani Victor, mimi kwa sasa nipo Mwananyamala, ninamuacha motto hapa nyumbani kwetu, ila kesho nitaondoka kuelekea pasipo julikana. Ukihitaji gari uliyo ninunulia, nayo pia nitaiacha hapa, kwani aibu niliyoipata, inatosha kabisa kuwa ni adhabu tosha…” Victor akamkatisha na kumtaka aongee taratibu, lakini Eve akaendelea kuongea kwa kasi ileile



“Kama ulivyosikia kwa watu na kusoma gazetini, nilikusaliti. Matokeo ya usaliti huo ni aibu kubwa kwangu mimi binafsi na kwa jamii nzima inayo nizunguka, ukiwemo na wewe Victor…”



“Eve mbona sikuele…” Nae Victor hata kabla hajamaliza, Eve akamkata kauli kwa kumwambia kuwa anatambua vizuri kwamba yeye Victor anajua kila kitu, ila kwa maelezo zaidi akamwambia aangalie katika ile CD ya Aurlus Mabele. Kasha akaendelea



“Victor mume wangu,ninakupenda sana, lakini ninaondoka katika maisha yako, suala la muhimu ni moja tu, ninaomba unisamehe kwa yote niliyokutendea.” Akamaliza Eve kwa kilio kikubwa na kukata simu akimuacha Victor hata hajielewi na pia haelewi kabisa ni nini ambacho Eve anazungumzia.



Baada ya hapo Eve hakupatikana tena hewani, Victor akachanganyikiwa, hapo hata ofisini hajaingia, anaambiwa Eve yupo nyumbani kwao pamoja na mwanae, na kesho anaondoka kuelekea pasipo julikana, sababu hadi sasa hajaielewa. Akapiga ngumi mkononi mwake.



Sabrina akamuuliza kuna tatizo gani, Victor akamtoa mchezoni kwa kumwambia hakuna tatizo lolote huku akitabasamu na kumjuza kuwa ni mambo ya kifamilia tu yamemchanganya kidogo. Bado akiwa kwenye dimbwi la mawazo, simu yake ikaita tena.



Safari hii alikuwa ni Mzee Dotto aliepiga kutaka kujua kuna nini, maana jinsi alivyomuona Eve pale ndani ni dhahiri alijua kuna tatizo, kama sio ni ugomvi, basi anaumwa, tena akiwa ni mwenye haraka na analia.



Mshangao alio uonesha Victor hasa baada tu ya kusikia kauli ile ya Mzee wake Yule, ikamlazimu amueleze ukweli mkwewe ya kwamba tangu afike kutoka safari yake hadi muda ule hata hawajaonana nae, hivyo nae akaomba wamzuie pale hadi yeye atakapo fika kule.



Kabla hata hajamaliza, Mzee Dotto akamueleza ya kwamba, Eve tayari ameisha toka pale nyumbani muda mchache uliopita, akamwambia pia ya kuwa Bill amemuacha pale na kuahidi kwamba wewe utamfuata, sasa yeye kapiga simu ili tu kujua tatizo ni nini.



Bado Victor hakuwa na jibu la kumpa mkwewe, ila ili tu kumpa amani, akamwambia yeye anaelekea huko muda si mrefu ujao na kukata simu. Akashusha pumzi kwa nguvu na kuegemea gari yake huku akimtazama Sabrina alikuwa nae akimtazama na ambae alisikia kiasi cha maongezi yao.



Kwa mara nyingine tena Bina akamuuliza Victor ana tatizo gani. Jibu lake likawa ni mapema mno kwa yeye Bina kufahamu, avute subira hadi pale muda wa kufahamu utakapofika, atajua kila kitu kinachomsumbua. Kasha sasa ndio akakumbuka kumuuliza kama tayari ameisha onana na Ondiek.



Bina akamjibu bado, kwani wakati alipokwenda kumuulizia aliambiwa yupo chumba cha uzalishaji wa habari ‘Productin room’ basi Victor akamwambia angoje yeye akamuitie. Victor haraka haraka akazielekea ngazi za Classic House na kumuacha Bina akimtazama kwa jicho la mshangao kutokana na jinsi anavyopanda ngazi zile kwa kasi.



Moyo wa Ondiek ulilipuka kwa wasiwasi mara tu baada ya kumuona Victor pale.





Tena moja kwa moja Production room, wakati yeye alikuwa akitambua kuwa Victor ataingia kazini siku ifuatayo, sasa imekuwaje aingie leo tena usiku hivi? Ama ndio tayari ameisha jua kila kitu na sasa ndio kaja kuvamia ili wapambane? Ni mawazo tu yalimtawala ghafla.



Akiwa na wasiwasi tele akasimama pale alipokaa na kumuhoji Victor haraka haraka



“Kamanda vipi?” Alihoji akiwa hajiamini kabisa kwa kuhisi huenda likachomoka konde



“Poa Ondiek…” baada ya salamu, ndio Victor akamuuliza kuhusu Eve



“Wakati anaomba ruhusa aliaga anakwenda wapi?” Swali lile alililenga kwa Ondiek kama Meneja wao, hivyo alitambua matatizo mengi sana ya wafanyakazi wake.



“Hapana Mzee, yeye hakusema ni wapi anakwenda bali alisema anaumwa na kuomba kupumzika kwa siku 3, yaani jana leo na kesho.” Aliongea sasa akiwa anahisi Victor hajajua ama lah anambana taratibu.



“Ok! Pia ndani ya gari langu kuna mgeni wako anakusubiri, mimi ninaongea na jamaa hapa kwanza kasha ninakuja, nina shida nawe muhimu sana, ninahitaji kuonana nawe tukiwa wawili tu, yaani mimi na wewe basi,” Ondiek alitikisa kichwa kuonesha kukubali, sasa aliamini Victor kajua, ndio kuna kitu anataka kufanya wakiwa wawili.



Kwa woga aliokuwa nao, hakusubiri wala kuuliza mgeni huyo ni nani, bali alitoka mle chumba cha habari kwa haraka kwa kuhofia huenda Victor akamuwahi na kuanzisha ugomvi, kwani walikuwa wawili tu mle chumbani.



Hakutambua kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi walikuwa tayari wamesogea kwenye mlango wa kile chumba cha habari mara tu baada ya kumuona Victor akielekea kule. Karibu wote walikua wakijuakwamba tayari Victor amejua kila kitu na sasa ndio kaja kuwasha moto.



Kumbe masikini Victor alikuwa hajapata picha kamili, hata ile kumwambia Ondiek kuwa nataka wakutane baadae wakiwa wao wawili tu ili waongee faragha, lilikuwa ni suala la kuhusu Sabrina kumshirikisha kwenye biashara zao kama ni mwaminifu, maana ni yeye ndio amjuae.



Lakini kichwani kwa Ondiek akili yake ilikuwa imeamini kabisa kuwa anachotaka Victor ni kumbana ama kupambana nae kuhusu suala lake na Eve. Hata nae sasa nafsi yake ilianza kujuta ni kwa nini alitoka na mke wa mtu na hali tayari ana wake wawili japo huyo mmoja amemuacha.



Ndani ya gari Ondiek alimkuta Sabrina, mtu ambae wala hakumtegemea kuwepo pale, hivyo alimtaka atoke garini lakini Sabrina alimgomea kabisa na kumwambia yeye ndio aingie garini ili waongee na kama hataki ajue Sabrina akishuka anaanzisha vurugu kubwa.



Victor aliingia kila chumba pale ofisini na kila alipopita alishangaa kuona wanavyo mtazama kwa jicho la mshangao, maana alionekana kama vile ana tabasamu tu usoni. Mshangao wao wala haukumfanya ahoji lolote linalo watatiza, bali aliwasalimia kwa bashasha kama alivyo kawaida yake kasha akaga na kuondoka.



Aliteremka na kurejea garini kwake, aliwakuta Ondiek na Sabrina wakiwa ni kama watu wanao kwaruzana kuhusu jambo Fulani. Aliweza kuona hata kwa mbali kuwa Ondiek amezidiwa na Sabrina, akajua leo mtu mzima anaumbuka.



Victor alipo wakaribia zaidi, Ondiek akajidai kutabasamu na kumuuliza Victor



“Vipi bosi?” Victor akatabasamu na kujibu



“Safi, mimi ninakwenda, nilikuja hapa ili tu kujua suala hilo nililo kuuliza, nafikiri mambo mengine muhimu zaidi, tutaongea kesho kwani ninaamini tutakuwa pamoja.” Ondiek akatikisa kichwa kukubali na kumpa nafasi Victor kumeza mate kasha akaendelea



“Leo ngoja nimuache Sabrina aongee nawe kiurefu.” Ondiek sasa akawa anajibu kwa haraka haraka ili Victor aondoke



“Sawa Mheshimiwa,” bado hiyo haikumfanya Victor aondoke haraka, bali alimgeukia Sabrina aliekuwa ameshika kitambaa cha mkononi, maarufu kama ‘Handkerchief’ akijifuta machozi kwa mbali, japo hakutaka kujionesha kama kuna kitunkinaendelea.



Akamsemesha na kumpa Business Card kasha akawaaga na kuondoka akiwaacha kama walivyo bila kuulizia ni nini kilichokuwa kikimliza Sabrina, maana tayari kitambo Bina mwenyewe alikuwa ameisha mueleza ni nini kipo kati yao na Ondiek.



Moyoni mwake Victor alijisemea kuwa Ondiek ana bahati sana ya kuwa na wana wake warembo, lakini utulivu wake ndio unakuja na kuharibu, maana ni sifuri. Akatikisa kichwa akikata kona ya barabara ya Msimbazi kuingia Morogoro Road akielekea Mwananyamala, nyumbani kwa kina Eve.



Lengo la kwenda huko kwa kina Eve ni kutaka kwenda kupata habari na kusikiliza chochote kilichopatikana juu ya Eve na pia amchukue mwanae ambae hajamuona tangu atue Bongo mchana wa siku ile.



Nyumbani kwa Mzee Dotto, Mwananyamala walikuwa bado hawajala wala kufanya chochote wakimsubiri mkwe wao Victor afike ili kuja kuwapa habari kwa kudhani kwamba huenda yeye akawa na taarifa mpya aliyoipata upande wake huko ama kueleza ni nini kilichotokea baina yake na Eve, kumbe wala hawakuwa sahihi.



Aliwasili na kuwasalimia kasha akaketi na kumuulizia Bill kabla ya jambo lolote lile, akajulishwa kuwa mwanae tayari ameisha lala. Mama Eve akawa nae ndio wa kwanza kuulizia kwa Victor juu ya Eve. Hakuna walicho kipata wazazi wa Eve zaidi ya mshangao wa Victor ambae alijua huku ndio atapata mwanga.



Victor aliwaambia kuwa tangu afike Dar hajamuona mkewe zaidi ya kuongea nae kwenye simu na kumwambia motto wao kamuacha pale nyumbani lakini wala hakumueleza sababu yoyote ya kutokuwepo nyumbani, na alitegemea kuwa pale atapata maelezo zaidi mara atakapofika pale nyumbani lakini imekuwa sivyo ndivyo.



Bado waakiwa hawajui ni wapi alipo Eve na sababu gani iliyomfanya kuto onekana, Mzee Maganga, baba yake Victor alipiga simu kwa mwanae kumuuliza kama kuna chochote kinacho endelea ama tayri ameisha muona mkewe Eve.



Akamjibu kuwa hawajamuona na wala hakuna habari yoyote mpya na muda ule yupo Mwananyamala, kwani Eve alimpigia simu na kumwambia Bill atamuacha pale. Akamueleza tu kwa kifupi kasha akapanga kuonana nao siku ifuatayo.



Baada ya maongezi na wazazi wa Eve, Victor aliaga na kusema atakuja kumchukua Bill siku ifuatayo asubuhi, kwani tangu aje hadi sasa hajamuona. Wakakubaliana hivyo na kasha akatoka kurejea nyumbani sasa akili yake ikahamia kwenye ile CD ambayo Eve amemwambia ameacha barua ndani.



Ulikuwa ni usiku mrefu mno kwa Victor, hasa baada ya kuipata ile barua iliyo kuwepo ndani ya CD na kuisoma, hakika alikuwa yupo nyuma sana ya muda. Mwanzo hakuwa amejua chochote, lakini sasa alipata mwanga kuwa Eve amemsaliti na usaliti wake umetambulika na sasa ameumbuka.



Lakini ni nani amenisaliti pamoja nae? Alijiuliza kama ni Ondiek? Moyo wake ulikataa na kusema Yule ni rafiki yake sana wala hawezi kumsaliti kwa kumtenda vile. Akaamua kumpigia simu Ommy usiku uleule.



Muda wote wa siku ile, kitu hiki cha kupigiwa simu na Victor wao walikitegemea, tena walijua itakuwa ni mapema kuliko muda ule ambao Victor alipiga simu ile.





Endelea;



Walitazamana Ommy na mkewe kila mmoja akimsakizia mwenzie apokee, mwisho Ommy akapokea yeye.



Ommy aliongea na Victor kwa marefu na mapana, Victor alimueleza mambo yote tangu kufika kwake nyumbani Tanzania hadi kuiona barua ile. Ommy hakuwa na msaada kwa usiku ule zaidi tu ya kumshauri alale na siku ifuatayo ndio walishughulikie jambo lile, Victor akakubaliana na kauli ya Ommy ambae yeye humchukulia ni kama zaidi ya rafiki.



Tatizo likawa ni moja tu… Je atapata usingizi? Lakini jambo la kumshukuru Mungu, alipata usingizi japo ulikuwa ni usingizi wa mang’amu ng’amu na pia si kwa wakati alioutaka yeye, lakini alilala.



Kabla ya kulala, alilazimika kulichukua gazeti la ‘HABARI ndio hiyo’ na kulisoma sasa kwa umakini ikiwepo suala la kuziangalia picha vizuri, ndio akajiona ni mpumbavu wa mwisho kushindwa kumjua mkewe japo sura haikuoneshwa. Lakini sasa baada ya kuangalia vizuri, aliweza kumgundua mkewe na pia aliweza kumuona vema kabisa Ondiek.



Hasira ilimpanda sana, akanyanyuka na kwenda kunywa majim kasha akafungulia muziki laini japo kwa kipindi kile ulikuwa haupandi, lakini alijilazimisha tu kufanya vile ili tu aweze kuuvuta usingizi ambao ulikuwa ukionekana upo mbali sana.



Binadamu kwa usingizi hatuna ujanja, hatimae kufikia saa 10 alfajiri, alifanikiwa kupata usingizi akiwa amekaa kwenye sofa.

* * * * *



Asubuhi ya siku iliyofuata, pigo kubwa sana lilitokea Classic FM pale walipokuta barua ya Eve iliyo andikwa kwa mkono ikisema kuwa yeye tangu siku ile, kazi basi. Kwa kuhakikisha kile alicho kiandika, mwisho kabisa alisaini. Lakini hakusema sababu ni ipi ya kuacha kazi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Haraka sana Victor akaitwa na Mkurugenzi wa Radio na kumtaka afike ofisini muda uleule, kumbe hakujua tu, kuwa hata nae alikuwa tayari kaisha jiandaa kuelekea kulekule ofisini tena akiwa anaelekea huko sio kwa kheri, bali leo alitaka kwenda huko kwa shari, alidhamiria shari.



Alifika na kuelekea moja kwa moja kwenye ofisi ya Mkurugenzi na kumkuta akiwa na watu wengine ambao aliwatambua kama viongozi wa Radio ile na kuambiwa aketi kitini. Walimuhoji juu ya suala lile la Eve kuacha kazi na ni mtu gani alieleta barua ile.



Victor alikana kutambua suala lile na kuwaambia ni jambo jipya kabisa kwake lile, yeye binafsi haelewi lolote na akatumia nafasi ile kuwaeleza hali halisi tangu safari yake akiwa Kenya na makubaliano yake na mkewe, lakini hayakutimia. Viongozi sasa wakawa wameijua hali halisi.



Mkurugenzi kwa kuwa yeye hakuwa ni mtu wa kukaa sana pale ofisini, hakuwa anajua lolote linalo endelea, hivyo aliposikia juu ya jambo lile, lilimshangaza sana na kuahidi kulifuatilia kwa haraka sana na kumwambia Victor kuwa hata ile barua yeye hatoitambua, huenda haopo kukawa kuna kitu hapo kati ama imeandikwa kwa shinikizo.



Victor akanyanyuka na kuanza kumtafuta Ondiek kila sehemu pale ofisini, kwa kuwa ilikuwa ni siku fupi ya Jumamosi, wafanyakazi walikuwa wachache, lakini hata wale waliokuwepo, waliweza kuona tofauti kubwa sana ya Victor wa leo na Yule wanae mjua.



Ondiek alikosekana kila sehemu na hata namba yake nayo ikawa haipatikani, alipo muulizia kwa watu wa Production room, walimwambia leo alifika alfajiri na kuandaa vipindi vyake vya mchana na kuondoka akiahidi wataonana baadae, Victor akatoka akiwa yupo tofauti sana kuelekea Mwananyamala.



Msaidizi wa Mama Eve alipokuwa akifua nguo chafu alizokuwa amezivua Bill, zile nguo alizovaa siku iliyopita, alikuta kiasi kidogo cha pesa na ujumbemdogo kwenye karatasi, pesa akaficha na karatasi akaipeleka ndani baada ya kuona haijaandikwa kama kuna pesa ndani yake.



Alimkuta mama Eve akiwa anasoma gazeti la siku kadhaa zilizo pita, gazeti lililokuwa na habari ya tukio lililo sababisha matatizo kwenye maisha ya mwanae wa pekee Eve, lakini bila kujua kama ni mwanae ndio muhusika.



Msaidizi akampatia barua ile aliyo ikuta kwenye suruali ya Bill na kumwambia alipoipata. Mama Bill mwanzo alichukulia kuwa ni makaratasi tu ya kitoto ambayo Bill kachezea na kuweka mfukoni, lakini akaamua aisome kidogo baada ya kuona ni karatasi nyeupe kabisa lakini ikiwa na mwandiko wa mkono.



Akaisoma mwanzo mwisho huku akiguna guna, kasha akanyanyuka harakaharaka na kuelekea chumbani kwake na kumpelekea mumewe na kumwambia asome mambo ya motto wake. Yaliyokuwa yameandikwa mle ndani ya barua ile ni haya;



‘Wazazi wangu, Shikamooni!



Kwanza kabisa ninaomba sana msamaha kwa kuwadhalilisha kwa kitendo changu hiki nilicho kifanya sasa, kawaida ya malipo ya dhambi huwa ni mauti, lakini mimi ninaona mauti si adhabu tosha, adhabu inayonifaa ni kuondoka hapa kwenu na kwa Victor kwenye mikono salama na kwenda kuishi huko kusiko julikana.



Wazee wangu nilipata kila nitakacho kutoka kwa mume wangu Victor, lakini bado nimemsaliti, naona kabisa sistahili kuishi nae hivyo nimeamua kuondoka. Sipendi kumuona tena, sio kwa sababu simpendi, lah hasha, ninampenda sana.



Sipendi kumuona kwa sababu ninajiona mimi ni mjinga kupita kiasi kutokana na hayo niliyo yatenda na kwa yakini kabisa ninajutia makosa yangu na sidhani kama ninapaswa kusamehewa, hasa nanyi wazazi wangu, kwani ni mara nyingine nawakosea.



Baba na mama yangu, ninawaachieni mwanangu Bill, motto halali kabisa wa Victor, ninawaomba kwa kushirikiana nae, mumtunze kwani huyo ni mjukuu wenu, mimi ninakwenda kusiko julikana ili kuikwepa aibu hii kubwa niliyompa Victor



Hakika ninajuta mno, sijui ninapokwenda kwa sasa, ila baada ya mwezi mmoja hivi, ninajua tayri nitakuwa sehemu na hapo nitawaambia. Nawapenda sana wazazi wangu, ila aibu niliyo wapa, ninaomba mnisamehe kwa mara nyingine mwanenu.



Wazazi wangu naomba mnifikishie ujumbe huu kwa Victor mumwambie kwamba ninampenda zaidi ya maisha yangu, lakini tatizo ni usaliti… Mtu aitwae Ondiek, ndio alie haribu ndoa yangu, najuta sana wazee wangu…!



Kwa herini ya kuonana wazee wangu,



Evelyn (Mama Bill)’



Wakiwa wanajadiliana baba na mama Eve baba Eve akasema kwa hasira



“Huyu Hayawani kumbe alirudiana na Yule punguani mwenzie? Haya matoto mengine hayana akili hata moja, yeye anajua kabisa kuwa huyo nani sijui… Ondiek, aliwahi kumtorosha mara ya kwanza, akarudi hapa nasi tukamsamehe kwa kuficha aibu ya wazazi ambao ni sisi, leo tena anarudia kosa lilelile tena na mtu yuleyule na aibu zaidi akiwa ameolewa. Ameona aibu aliyotutia hapo mwanzo haitoshi, sasa ataniona siku atakayo rudi hapa, labda asitie miguu yake humu ndani…” Aliongea maneno makali Mzee Dotto na kumuacha Mama Eve akiwa kimya tu.



Muda sio mrefu akaingia Victor na kuungana nao. Waliongea mengi mno ila hawakutaka kumgusia juu ya upatikanaji wa ile barua yenye ujumbe tata, bali wakamuuliza tu kama ana taarifa yoyote mpya.





Akawaambia hana taarifa yoyote mpya nae pia hakuwaambia kuhusu Eve kuandika barua ya kuacha kazi.



Alikaa na wakwe zake na mto wake hadi baada ya kula chakula cha mchana, ndio akaondoka akiwa na Bill hadi Victoria nyumbani kwa wazazi wake, pale napo alikaa hadi jioni ulipowadia muda wa kwenda Studio , akawaaga wazazi wake na kumuaga Bill pia, kasha akaelekea sehemu yake ya kuwajibika.



Kule Studio sasa ndio alipata picha kamili kuthibitisha kile alicho andikiwa na Eve na kuelezwa kila kitu kilicho tokea wakati yeye akiwa hayupo.



Kuna mfanyakazi mwenzie ambae ni DJ maarufu kwa jina la Meddy, ambae huongoza kipindi chao cha Romantic Love ndio akafunguka.



Alifunguka kila kitu na kibaya zaidi alimwambia wao pale ofisini karibu kila mtu anajua kuhusu uhusiano uliopo baina ya mkewe Eve na Ondiek jamaa yake, lakini hakuna hata mmoja aliekuwa na ujasiri wa kumwambia, walikuwa na hofu, wataanzaje kumwambia?



Victor alishukuru kwa kumweleza ukweli ambao alikuwa anaufahamu bila ushahidi, na hapohapo bila hata ya kusubiri, akiwa tayari kaisha kiandaa kipindi, akampigia simu Mkurugenzi wa Radio Classic na kumwambia ana shida ya dharula na anataka waonanae muda uleule.



Mkurugenzi akahisi huenda Victor ameisha jua kilichoendelea ama amepata fununu kuhusu Eve, hivyo anataka amueleze kwani aliahidi kufuatilia suala lilena kujua kila kitu, kitu ambacho hakukifanya, hivyo hata nae sasa alikuwa akimuonea aibu Victor.



Ikamlazimu Mkurugenzi aseme uongo ili kujitetea, akamdanganya kuwa muda ule kidogo yupo na shughuli nyingi, hivyo waonane baadae ama siku ifuatayo. Victor akamwambia kama yupo na kazi nyingi, basi haina haja ya kuonana, wanaweza kumaliza maongezi yao hata kwenye simu tu.



“Kwani kuna nini Victor?” aliuliza Mkurugenzi, Victor akamjibu



“Tangu muda huu name sitaki kazi tena, na muda huu ninapoongea nawe, ndio ninatoka Studio na hutonisikia milele.” Aliongea kwa sauti ya kawaida lakini yenye kufiicha jazba kubwa moyoni



“Victor, unaongea taratibu sana, lakini nyuma ya pazia nasikia pumzi zako zikiniambia kuna kitu kikubwa unakificha.”



“Mkuu, ukweli wote ninaujua sasa, hapo awali sikuwa nikijua lolote, nilichukulia kuwa ni kitu rahisi sana, lakini kifupi ni kwamba, siwezi kufanya kazi na adui yangu.”



“Adui yako ni nani hapo ofisini?”



“Kama unafanya kazi na watu na kinatokea kitu wewe unashindwa kukifahamu, inaonesha mahusiano sio mazuri, sasa kama mahusiano sio mazuri na wafanyakazi wenzangu, sioni kama ni sahihi kwa mimi kuendelea kufanya kazi hapa.”



“Lakini hilo Victor ni suala ambalo linazungumzika, hupaswi kufanya maamuzi hayo magumu.”



“Bosi muda huo haupo tena, nimedhalilika sana baada ya kujua ukweli leo.”



“Kijana, maisha yetu mara chache sana kukwepa baadhi ya mambo, lakini kama utachu…” Victor akamkatisha kauli kwa kumwambia



“Siku zote unapojua kuwa mpenzi wako anatoka na mtu Fulani, iwe kazini ama nyumbani, ilimradi pawe na watu wengine, basi tambua hata kama utahisi wewe ndio wa kwanza kujua, bali wewe ndio wa mwisho wa kujua.” Alisema Victor ili kumpa nafasi bosi wake aseme kitu.



“Ni kweli, na ndio maana nimekuambia kwamba jambo hilo bado lina nafasi ya kuzungumzika.”



“Bosi nimekuwa nikifanya kazi kwenye radio yako kama ni mali yangu vile, nimejitolea muda wangu na elimu yangu, nikaacha kazi serikalini ambapo kulikuwa kuna kazi yenye fani yangu, haikutosha nikajitolea kila kitu change, ili kufanya tufike mbali zaidi ya pale nilipoikuta radio hii, kumbe malipo yamekuwa ni tofauti na nilivyotegemea.” Victor alifika mbali sana.



Kauli yake ilimgusa hadi Mkurugenzi na kukosa cha kuongea hasa alipofikiria na kuona ni ukweli mtupu alio uongea. Sasa radio yake ina wadhamini wengi sana hasa kwenye kipindi cha Romantic love na ndio kipindi kinacho sikilizwa sana hapa nchini.



“Umenisikia Victor, ninaomba suala hilo uniachie mimi sasa nilishughulikie, sawa kijana?”



“Nashukuru sana kwa kipindi chote nilicho fanya kazi hapa, kuna mengi nimejifunza, nashukuru kwa kila aina ya msaada niliopata nikiwa hapa, na mwisho kabisa napenda kutoa shukrani za kipekee kwako wewe Mkurugenzi, Ahsante sana, ila mwambie Ondiek, ama zake, ama zangu.” Victor akakata simu na kumuacha Mkurugenzi akiwa na masikitiko makubwa kwa kupoteza watu wawili muhimu kwenye kipindi kimoja.



Kibaya zaidi wote kawapoteza kwa siku moja na aliamini hata huyo mtu wa tatu, nae hawezi kudumu tena kazini, hana muda mrefu ni lazima aondoke tu siku chache zijazo. Mtu huyo alikuwa ni Ondiek, Mkurugenzi Kichwa kikawa kizito.



Akachukua simu na kumpigia Victor akiwa na nia ya kumwambia waonane usiku uleule kabla hajalala, lakini haikupokelewa.Simu ilipokata tu, Victor akaizima kabisa. Huo ndio ukawa ni mwisho wa kufanya kazi kwa Victor pale Classic Radio, alipita na kuwaaga wachache waliokuwepo Studio na kuwatakia kazi njema.



Wapo walio sikitika na wapo walio ona uamuzi wake ni sahihi japo walijua kuwa watatetereka sana hasa kipindi kile cha Romantic love. Yeye hakujali lolote, akatoka pale ofisini na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa Ondiek kwa nia moja tu… Kuwasaka hadi kuwapata, aliamini watakuwa huko pamoja.



Bahati mbaya hadi anafika pale hakufanikiwa kumuona mtu yeyote na hata nyumba ilionekana kama vile haina mtu, maana taa zote zilionekana kuzimwa na giza lilitawala kuanzia ndani ya nyumba hadi nje akajipa moyo kwamba huenda hawajarejea, akakaa na kuwasubiri kwa dakika 30 lakini hawakutokea, akakata tama na kuondoka kurejea kwake.



Victor alifika na kuingia ndani kwake kiuvivu akajitupia kwenye sofa, akashika Remote na kuwasha music huku mawazo kedekede yakiwa yamemtawala. Taswira ya kwanza kumuijia kichwani mwake ni ile mara ya kwanza kukutana na Eve kwenye ngazi za Classic House, alikumbuka mambo waliyoyafanya wakiwa pamoja.



Kumbukumbu nyingi sana zikamuijia kama maji ya bahari. Chozi lilimtoka pale alipogungua sehemu ileile aliyokutana na Eve kwa mara ya kwanza imekuwa ndio sehemu uliyo sababisha tena sasa wametengana, nafsi yake iliumia sana.



Baada ya hapo ikamuijia picha ya Ondiek tangu wakiwa shuleni kasha kazini. Baadae akakumbuka wema ambao Ondiek amekuwa akimfanyia pale Studio na hadi kufikia kumuamini kutokana na historia zao za nyuma na muendelezo wa ukaribu walio nao sasa. Kumbe haukuwa urafiki, ulikuwa ni unafiki ambao sasa umewapeleka kwenye uadui wa kudumu.



Aliwaza sijui ni kitu gani awafanyie pindi siku ambayo atakayo wakamata. Akili moja ilimtuma awaue tu ili kufanya iwe fundisho, lakini moyo ukamwambia kuna gereza, na Bill je? Ama atapata faida gani akiwaua? Akaahirisha wazo hilo na kusema atajua siku hiyo ikitokea.



Huku akinyanyuka kuelekea chumbani lilipo bafu ili akaoge, Victor akajisemea moyoni



“Ni heri kuishi na shetani unae mjua kuliko kuishi na Malaika usiemtambua, nimekuwa nikimchukulia Ondiek kama Malaika ninae mtambua, kumbe ni shetani nisie mtambua, tena basi huyu ni Zimwi anae nitambua, amenila na kunimaliza, japo wahenga walisema Zimwi likujualo halikuli likakwisha, lakini mie alichonifanyia Ondiek, mh! Ipo siku yao.”





Eve alikaa guest kwa siku mbili akiwa hatoki nje hata kwa bahati mbaya, akimtegemea Ondiek kwa kila kitu, alikuwa akiogopa sana kukutana na waandishi wa habari kuliko hata mumewe Victor, sababu ya kukaa guest pia ilikuwa ni hiyo, kwani kila mtu alipajua nyumbani kwa Ondiek na waliamini Victor anaweza kwenda kumtafuta mkewe kule.



Asubuhi ya siku hiyo, gazeti la ‘HABARI ndio hiyo’ lilitoka na habari nyingine kubwa ukurasa wa mbele kabisa isemayo



‘NDOA YA KIBOPA yasambaratika’ kasha ikaendelea kwa habari ndogondogo ‘Ni baada ya gazeti hili kuandika maovu ya mwanamke, njemba yakana kuhusika na kashfa hiyo, kibosile hadi sasa hajapatikana kuelezea undani wa sakata lenyewe’ Mwisho wakaonesha habari ile inapatikana ukurasa wa pili.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kichwa kile cha habari kikamfanya Eve alie sana na kumtaka Ondiek ambae muda ule alikuwa nae pale, afanye chochote aweacho, ili yeye aondoke pale kwa gharama yoyote siku ileile, au lah sivyo, ikifika jioni hajaondoka Dar Es Salaam, basi anajiua. Ondiek aliekuwa natazama gazeti lile akamgeukia Eve na kumtazama kwa jicho la mshangao.



Eve alipokuwa akimtazama Ondiek, akasisitiza kwa kumwambia kwamba kuanzia sasa hayupo tayari tena kuendelea kuona maovu yake yakiandikwa na kuwekwa hadharani. Muda wote huo, Ondiek alikuwa hajalipitia gazeti lile, lakini sasa nae baada ya kulipitia, pozi zilimuisha.



Akakumbuka kuwa jana mchana akiwa ofisini kuna kijana mmoja alikuja na kutaka kuongea nae faragha. Alikubali na kusogea pembeni kuongea nae. Kijana alijitambulisha kuwa yeye ni mwandishi wa habari wa gazeti la ‘HABARI ndio hiyo’



Ondiek alitumia nafasi hiyo kukanusha habari ile kwa kudhani kuwa huenda jamaa ataenda kumsafisha, lakini mwandishi hakupindisha chochote, aliandika na kutoa habari vilevile kama alivyo muhoji na alivyo njibu yeye.



Sasa Ondiek alianza kuwa mdogomdogo, akaona dawa ya kupunguza kadhia hii ni heri amsafirishe, japo hakujua ni wapi ampeleke kwa ghafla vile, lakini akamwambia ajitayarishe kwenda popote, Eve akasema sawa, yupo tayari kwenda popote kuliko kuwepo pale.



Akatoka Ondiek na kuahidi atarudi baada ya masaa mawili akiwa na tiketi ili aondoke, akamuomba passport yake, Eve bahati nzuri alikuwa ametoka nayo, akampa. Wakaachana kwa ahadi ya kukutana baada ya masaa mawili kwa ajili ya safari.



Juhudi za kumshawishi Victor arudi kazini zikagonga mwamba, kipindi kikaonekana mapema kwamba kitayumba siku chache zijazo. Upande wapili Victor alijaribu sana kumtafuta Ondiek kwa siri na dhahiri, lakini hakufanikiwa kumuona. Alikuwa akimtafura si kwa heri, bali alidhamiria shari.



Gazeti la siku hiyo ndio likamchanganya kabisa mara tu alipoliona na kulinunua. Alirudi nyumbani na kukaa kasha akaanza kulisoma kwa kituo. Akakumbuka Ni kweli kuna namba mpya zimekuwa zikimpigia mara kadhaa, lakini amekuwa hazipokei, bila kujua kuwa ni waandishi wa habari.



Akaazimia kubadili namba zake zote za simu. Moja ya sababu aliyo waambia ni kukwepa usumbufu wa waandishi wa habari, watu wake wa muhimu wote aliwajulisha. Kasha akatoka kuelekea ofisini Classic kuendelea kumtafuta Ondiek, bahati mbaya akamkosa tena.



Jioni aliwasiliana na familia ya Ommy Bazzo na kuwaeleza hali halisi ya matukio yanayo endelea kule Bongo. Nafsi ilimuuma sana Lidya, lakini angefanya nini? Hakuwa na cha kufanya, alimuonea huruma sana Victor, kwani alijua ni kiasi gani alikuwa akimpenda mkewe.



Alichokiamua tena peke yake bila hata kumshirikisha mumewe Ommy ni kumuomba Victor awape motto wakae nae wao kwa kipindi kile wakati hawajajua ni nini kitafuata hapo baadae. Hakukataa, ukizingatia hakupenda kuwasumbua tena wazazi wake ambao umri ulikuwa umesogea sana.



Kingine kilicho mpa nguvu ni kwamba Lidya alikuwa na motto mwingine, hivyo isingekuwa ngumu kwa yeye kumlea na huyu pia kwani hawakupishana sana. Hivyo akamwambia atafanya mpango ndani ya wiki ileile kumpeleka Nairobi.



Kama alivyo ahidi, masaa mawili mbele, Ondiek alirejea akiwa na tiketi na kumchukua Eve hadi Airport, akampandisha ndege na kumwambia kule aendapo, tayari kuna mtu wa kumpokea na mipango yote imeandaliwa, akifika atamjulisha. Eve akakwea pipa kuelekea nchi ya ugenini.



Ondiek nae aliendelea kufanya kazi pale radioni kwa siku 3 lakini katika mazingira magumu mno, alikwisha pata habari kuwa Victor anamtafuta kwa hasira zote, ikamlazimu aweke watu wawe wanamjulisha kila anapo onekana Victor wanamuambia, lakini Victor yeye alimtafuta peke yake.



Taarifa zilipokuwa zikimfikia Ondiek kuwa Victor kaonekana sehemu Fulani, basi kama yeye alikuwa maeneo ya jirani na pale, ikawa inamlazimu kuhama eneo. Studio akawa hasomi tena taarifa ya habari ya moja kwa moja kwa kumuhofia Victor. Vipindi vya moja kwa moja kwake ikawa ni kesi, akakaa navyo mbali kabisa.



Hayo sasa ndio yakawa maisha ya Ondiek, yakatoka kwenye furaha na kwenda kwenye mashaka. Nae namba yake ya simu akaibadili, gari yake akawa haitumii tena, muda wote aliokuwa na shida na gari, basi alitumia gari za marafiki zake.



Hata gari ya ofisi nayo aliiogopa, kwani alijua Victor anajuana na madereva wote, ina maana akiwasimamisha popote hawawezi kukataa na anaweza hata kuwaambia wakiwa nae wamjulishe, kumbe hizo zote zilikuwa ni hisia zake, wala Victor hakuwahi kufikiri hivyo.



Nyumbani kwake akiwa na shida akawa anamtuma kijana mmoja ambae ni msaidizi wake wa pale nyumbani, anamuagiza kitu na kumtaka ampelekee sehemu. Lakini baada ya zile siku siku 3, uzalendo ukamshinda, sasa nae akaomba poo! Akanyoosha mikono kusalimu amri.



Vita ya Victor ilikuwa ni kubwa sana, akakubali kushindwa. Ikambidi aombe likizo fupi ya dharula, tena bila malipo yoyote. Akiamini huenda sasa akapata nafuu iwapo nae ataondoka pale nchini na kuelekea kwanza Kenya kupumzika.





Baada tu ya kuwasilisha barua ile ya maombi, hata kabla ya kusubiri majibu ya Mkurugenzi, ambae tayari alikuwa akijua kutokea kwa jambo lile tangu mapema, akamruhusu. Hakuona umuhimu wowote wa kumzuia, maana hata akiwepo hakuna chochote kinacho fanyika.



Kimyakimya akafunga safari kuelekea pasipo julikana, alihofu kwenda Kenya, kwani tayari kule wapo kina Ommy ambao tayari ana hakika watakuwa wanajua kinacho endelea huku, hivyo nae akaamua kumfuata Eve kule alipoelekea. Mkewe Yasmin muda huu alikuwa amerudi kwao kutokana na kashfa ya Ondiek aliyoisoma kupitia vyombo vya habari.



Kabla ya kuondoka akauza gari na kuwaomba madalali wapangishe nyumba yake na kumpigia simu mkewe Yasmin akachukue vitu vyote vya ndani. Yote yalipo kamilika, akavunja chip yake ya simu na kuchukua pesa za nyumba na gari, kasha akaondoka na pesa ile kama nauli na pia kama kianzio kule aendapo.

**********



Miezi 9 sasa imekatika, Victor amezoea kuishi mpweke. Isipokuwa mara moja moja alipokuwa akija Ommy kwenye masuala yao ya kibiashara.

Ndani ya kipindi hicho walifanikiwa kufungua tawi moja jipya la LOVE.com nchini Uganda na kuonyesha mafanikio makubwa chini ya Mkurugenzi wa tawi hilo, Bi Sabrina Munnabhai.



Safari za Victor za mara kwa mara nchini Uganda kufuatilia maendeleo ya kampuni yao na pia safari mfululizo za Bina hapa Tanzania, kufuata biashara zake na wakati mwingine safari kwa maslahi ya kampuni, zikafungua ukurasa mpya wa mapenzi kati ya hawa watu wawili, lakini hakukuwa na hata mmoja wao aliekuwa tayari kusema kwamba waishi pamoja.



Kila mtu kati yao alikuwa akijua kabisa raha na chungu ya ndoa, Victor alikuwa na mme wa ndoa kabisa ya kikristo na Eve na Bina alikuwa mke wa ndoa kabisa kwa Ondiek lakini ndoa yao wao ikiwa ni ya kiislamu ambayo kwa sasa haikuwepo kabisa baada ya Ondiek kutoa talaka 3.



Penzi lao halikuwa na kificho kwa Lidya na Ommy, bali huku Bongo hakuna alielitambua yoyote. Na hicho ndio walichokuwa wakikitaka. Upepo wa wanahabari waliokuwa wakifuatilia suala lile sasa ulitulia, Victor akairudia namba yake ya awali kwani aliiacha ili kuwakwepa wana habari.



Victor akiwa ametokea nchini Uganda kuadhimisha mwaka mmoja wa kuanzishwa tawi la huko, akapita Kenya kumuangalia mwanae, maana walikutana na Ommy huko, lakini Lidya na watoto walishindwa kuuungana nao kutokana na watoto kuwa masomoni.



Siku ya pili akiwa huko akaongea na wadau wenzie kwa kuwaambia wanapaswa kufungua tawi jingine nchini Burundi. Daima anapoanzisha majadiliano Victor, huwa amejiandaa, na wale wengine hujua hilo, hivyo huwa wala hawataki kubishana nae bali humuuliza mipango ikoje.



Lidya alitaka kujua kama tayari kuna mtu wa kuwasaidia kuandaa michakato yote ya nchi ile ambayo ni ngeni kwao. Victor akawaambia tayari kuna mtu amemuandaa na yupo tayari kufanya nao kazi bega kwa bega ni Mtanzania mwenzao mwenye asili ya kiarabu, jina lake Harbush, ameishi kule kwa miaka zaidi ya 20, hivyo ni mwenyeji kabisa.



Kuwadhihirishia hilo, akamtafuta kwa simu mbele yao na kuongea nae akimuambia kuwa tayari huku wao wamekutana na wamejipanga kuja huko, sasa yeye anasemaje? Harbush akamwambia kuwa yeye yupo tayari kuwapokea kwa mikono miwili na kuahidi kuwasaidia kwa hali na mali.



Wakajipanga na kuamua safari hii ya Burundi, aende Ommy kurekebisha wakati huo Victor yeye arudi nyumbani Tanzania ili kwenda kufanya usaili kupata Meneja wa tawi la Burundi na nafasi ya Ukurugenzi wampe Harbush. Wakakubaliana hivyo na siku mbili mbele wakaachana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, Victor akielea Tanzania, Ommy akaenda zake Burundi.



Mambo yalikwenda vema, Ommy ambae alikwenda peke yake, na kwa msaada mkubwa wa Harbush, walili shughulikia suala lile kwa kasi ya ajabu na ndani ya wiki moja tu, kila kitu kikawa tayari.

Walikamilisha usajili na katikati ya Jiji la Bujumbura, sehemu iitwayo Buyenzi, barabara ya pili, ndio hapo Harbush alifanikisha wakapata nyumba nzima kwa ajili ya ofisi.



Ofisi iliandaliwa hasa na kuwa ni moja kati ya ofisi mzuri sana pale Bujumbura, kila alie iona ilimvutia. Ommy alikaa kwa siku 3 zaidi hadi pale Victor alipompeleka Meneja wa muda wa tawi lile Jipya, ndio hapo sasa Ommy akapata nafasi ya kuondoka kurejea kwwke kupitia Bongo.

* * * * *



Kutoroka kwa Evelyn na Ondiek nchini Tanzania, kuliwapeleka moja kwa moja nchini Rwanda, kule wakapata kazi Radio Kigezi FM, kila mmoja kaipatiwa usafiri na nyumba ya makazi, kwani wakiwa kule wao walijitangaza kama ni watu wa karibu tu na si wapenzi.



Hawakupenda kabisa watu waelewe uhusiano wao ulivyo. Sababu walioitoa mara zote walipoulizwa ukaribu wao, walisema kwamba wamezoeana sana na ndio maana hata kuja pale wamekuja pamoja. Watu wakaelewa hivyo, hawakuujua ukweli zaidi, waliridhika.



Mwezi wa 9 mashule mengi sana hufungwa nchini Kenya, hivyo familia ya Mr. Ommy Bazzo ikiwa pamoja na Bill ilirejea nyumbani Tanzania kutembea. Na katika kipindi hichohicho mara tu baada ya Victor kumuona Ommy, akamuomba wautumia muda ule kutembelea tawi lao la Burundi, Ommy alikubaliana nae, wakaondoka wao wawili tu.



Lidya akabaki na watoto palepale Dar Es Salaam, wakaanza safari yao wakitumia gari jipya la kampuni yao aina ya VX, kutoka pale Dar walielekea Kahama na kasha Ushirombo, wakaelekea Biharamulo na Kibondo hadi Kasulu na kukatisha kuitafuta Manyovu, iliyo waingiza ndani ya nchi ya Burundi.



Safari ilikuwa ni ndefu sana, lakini waliipenda na kuifurahia sana tangu awali. Hivyo walipowasili Burundi, walifurahishwa na mafanikio ambayo sasa walianza kuyaona, hivyo yakawa ni chachu ya kutafuta sehemu nyingine kwa ajili ya kufungua tawi jipya kwenye nchi nyingine iliyomo ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.



Eve na Ondiek, kazi yao iliendelea kuwa vizuri sokoni na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuliteka soko la muziki wa Kibongo huko Rwanda hasa wale walio tokea kukipenda sana kipindi cha Bongo Hits ambacho walikiendesha kwa pamoja.





Siri kubwa sana ya kipindi kile kupendwa ni kwa vile watangazaji husika wa kipindi kile, yaani Eve na Ondiek, nao walikuwa ni Watanzania na hata huku Tanzania walikuwa ni watangazaji pia, hivyo historia ya wanamuziki wa Bongo flavor, walikuwa wakiijua vema, kwa hali hiyo ilikuwa ni lazima wawakimbize mno Wanyarwanda.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jioni ya siku hiyo baada ya matembezi kwenye maduka ya LOVE com na labalatory yao, wakarejea na kuketi kwenye bustani ya maua iliyopo mbele ya nyumba ya Harbush na kuanza mikakati ya kufungua tawi jingine, na sehemu walio ona muafaka ni Rwanda.



Kwa kuwa siku zote kujipanga huwa ni kuzuri, Harbushi akawasaidia tena, maana hata nae sasa aliona umuhimu wa kampuni ile ya LOVE com ambayo imempa jina kubwa Burundi, alitamani na nduguye aliepo Rwanda nae afanikiwe pia. Ndugu yake aliitwa Kihuna, aliishi Kigali.



Akampigia Kihuna na kuongea nae akiwa amemuweka kwenye sauti ya nje (Loud speaker) na wote waliweza kumsikia akikubali kwa roho nyeupe na kuomba waende hata siku ileile. Walicheka mna kumwambia wataondoka siku ya pili kuelekea huko. Kihuna alisisitiza sana wasiache kwenda siku ifuatayo.



Walimuhakikishia kuwa watafanya hivyo haraka iwezekanavyo, sasa yeye ndio akawa na shauku kubwa sana, akawaambia ili aamini kuwa wanakwenda siku ifuatayo, wamtumie baadhi ya Document ili yeye akiamka siku ifuatayo tu aanze mambo ya usajili, japo nchi yao ndio ambayo inachukua muda mfupi zaidi kusajili kampuni.



Walitazamana na kumkubalia, wakasema wanaenda kumpa Harbush muda uleule amtumie wala asihofu, akaanza kuongea Kirundi na Harbush ambae alikuwa akicheka tu na kuwaacha Ommy na Victor hawaelewi ni nini kinacho zungumzwa.



Alipokata simu akawaambia huku akicheka na kusema kuwa Kihuna anaomba sana niwasisitize kesho alfajiri muondoke hapa kuelekea huko kwake, mtamkuta akiwasubiri kwa hamu sana, maana wao wanapata taabu sana kuwapata wasanii wa kibongo, sasa kama kampuni ile ikiweka ofisi na kule, watakuwa na uhakika wa kuwapata.



Hivyo kamtuma kusisitiza kuwa yeye yupo tayari kufanya lolote ili wafanikiwe kwa hilo. Wakampa document zote Harbush akazituma kwa Fax na wakatoka kwenda kutembea wakitembezwa huku na kule wakiwa na Meneja wa LOVE com wa pale Burundi.



Siku ya pili wakaanza safri kuelekea Rwanda ili kukamilisha ndoto za kuwa na kampuni kubwa afrika na Dunia na waweze kuliteka na soko la Burudani kwa ukanda mzima huu wa Afrika mashariki na baadae iwe Afrika nzima.



Safari ilikuwa ni nzuri, hadi wanaingia Rwanda, hawakupata tatizo lolote, wakafikia Hotel Rwanda ambapo walikuta tayari Kihuna amewapangia vyumba pale. Waliingia kuoga na kula kasha wakatoka kwa gari ya Kihuna ili kuzunguka zunguka kutazama mandhari ya Jiji la Kigali.



Waliliona Jiji lile safi kuliko majiji yote kwa ukanda huu wa Afrika mashariki, nao wakathibitisha hilo na kumaliza mizungukio yao kwa kurejea hotelini. Wakiwa wapo garini ndio Kihuna akawaambia kuwa amefikia hatua za mwisho za usajili na hadi kufikia kesho muda wa saa 5 asubuhi, watakuwa wamekamilisha utaratibu wote wa usajili.



Walishangaa sana kwa kasi kubwa aliyoitumia kuweza kusajili kampuni kwa siku moja. Ajabu yeye ndio akawashangaa, maana hata hivyo alishindwa kukamilisha siku ile kwa kukosa document muhimu kama ofisi na mfano wake. Lah sivyo, angekuwa amekamilisha.



Walimuelewa na kuahidi siku ya pili watakamilisha iwapo yeye atajitahidi kutafuta nyumba kwa ajili ya ofisi. Akawaambia nyumba tayari amepata, hakuwa tu na uwezo wa kuilipia, lakini kwa kuwa wamekuja, atawaijia asubuhi na mapema wakaione na kufanya maamuzi, wakaagana.



Siku ya pili walikamilisha kila kitu kabla ya mchana, walishangaa sana, hawakutegemea kabisa hali ile. Walimshukuru sana Kihuna kwa kufanikisha lile na kumwambia yeye atakuwa ndio Mkurugenzi wa tawi, wao wataleta Meneja siku chache zijazo.



Walikaa siku moja tu na kurejea Tanzania kwa nia ya kwenda kufanya michakato ya kumpata meneja mpya wa tawi atakae shika nafasi ile ya Rwanda. Wakaagana na Kihuna na kasha wakaingia hotelini na kwenda kukaa kwanza chumbani kwa Ommy kupiga story, maana ilikuwa bado ni mapema sana kwa wao kulala.



Wakiwa wamekaa chumbani story zimenoga, Victor akamwambia Ommy kuwa anahamu ya kusikia sauti ya Kinyarwanda, hivyo akasimama na kuweka FM station. Bahati nzuri wakaipata radio moja ambayo ilikuwa ikicheza muziki wa kibongo uitwao ‘Nakupenda’ ulioimbwa na msanii chipukizi wa Kibongo aitwae JRam.



Ommy akamshauri aache hapohapo, baada ya muda kidogo wakasikia Jingo likiitangaza ile ni Radio Kigezi FM. Papo hapo wakasikia sauti wanayo ifahamu, wakatazamana kasha Ommy akauliza



“Victor huyo sio Ondiek?” Victor alikaa kimya bila kujibu bali akaongeza tu umakini kwenye kuisikiliza sauti inayo dhaniwa kuwa ni ya Ondiek;



“Baada ya matangazo mafupi, tutarudi kuendelea na burudani hadi mwisho wa kipindi, au sio DJ Elyn?” sasa ndio alipata uhakika kuwa Yule ni Ondiek aliekuwa akiuliza, sauti ikasikika ikijibu



“Yeah!” Sauti ile hata ukiwaamsha wanaume wale wawili usiku wa manane wataitambua vema na bila hata ya kusita, watakwambia Yule ni nani.



“Mh! Ommy, kumbe Ondiek yupo pamoja na Eve? Si umesikia sauti yake?” Victor akamuuliza swali Ommy na hali anajua fika alicho uliza ndio jibu alilotakiwa kupewa.



“Nimeisikia ila ngoja tuendelee kuisikia huenda si yeye, labda tumeifananisha.” Hata Victor alijua fika kuwa Ommy ameongea vile ili kumtuliza tu lakini alikuwa na hakika kabisa kuwa ile ni sauti ya Eve mkewe.



Dakika chache mbele, ikasikika tena sauti ya Eve. Ambayo sasa kwa asilimia 100 wote wakaitambua kuwa ni sauti ya Eve. Victor akakurupuka na kusimama akisema huku akitoa simu





“Washenzi hawa, leo watanitambua, lazima niwakomeshe…” Ommy akamuuliza huku nae akisimama



“Sasa unataka kufanyeje dogo?”



“Nampigia simu Kihuna aniambie wanapo ishi hao mbwa ama anielekeze wapi ilipo Studio ili niende nikawaoneshe mimi ni nani, pumbavu zao.”



“Acha utoto bhana, wewe unajua fika kuwa kilichotuleta huku sio hicho unachotaka kufanya.”



“Ni kweli Ommy, lakini si unajua kabisa kuwa Eve ni mke wangu halali?” Aliongea Victor kwa ghadhabu, Ommy akajaribu kumpoza. Alifanikiwa baada ya kutumia nguvu nyingi sana ya ushawishi na Victor akakubali kuachana nao.



Walisikiliza kipindi kile hadi mwisho wakati wale waliopo Studio walipo aga na kutoka ikiwa ni saa 3 usiku. Nao wakashauriana watoke kwenda kutembea mjini ili kuvuta usingizi, kwani walijiona kama hawana usingizi na walitamani kuendelea kutembea kwenye Jiji lile zuri.



Waliamua wasiende mbali sana, hivyo watembee kwa miguu tu, sehemu ya chini ya jingo lile la Hotel Rwanda kuna Restaurant, wakapitia vinywaji vya kopo. Victor alipitia Bavaria wakati Ommy aliagiza Amstel. Taratibu wakaanza kukata mitaa wakiwa ni wenye amani tele na furaha.



Hata kabla hawajakatiza barabara hata moja, Victor alimuona Evelyn akiwa amesimama dukani, akamuonesha Ommy ambae alikuwa bado hajamuona. Wakajificha kutokana na ushauri wa Ommy ili waweze kuwafuatilia, japo jazba kwa Victor ilikuwa ipo juu, lakini aliukubali ushauri wa Ommy kwa shingo upande.



Jirani na pale walipokuwa wamejificha wao, hatua kadhaa mbele yao waliweza kuiona Taxi iliyokuwa imesimama, wakapanga kuitumia ile kama itawalazimu, lakini wakashangaa kuona Ondiek anatoka ndani ya Taxi ile na kulipia baada ya kufuata kitu kama change dukani pale alipokuwa amesimama Eve.



Waliichunguza kwa umakini taxi ile na kuziona namba zake za ubavuni zilizo someka 1280, tena ikiwa inaonesha Parking yake kuwa ni Hotel Rwanda, Victor alijisemea moyoni kuwa atawapata tu, midhali kaijua namba ile ya gari.



Ile Taxi iliondoka na kuwapita kina Ommy mbele yao wakiitazama. Hiyo iliwapa nafasi mzuri zaidi ya kuzisoma tena vizuri. Baada ya hapo Eve na Ondiek wakaingia kwenye ile nyumba yenye duka. Nao wakakaa pale kwa takriban robo saa. Walipoona hawatokei, nao wakaamua kuondoka kurejea hotelini.



Kitu cha kwanza walicho kifanya mara tu baada ya kufika hotelini, walimtafuta Yule dereva Taxi mwenye # 1280 lakini wakamkosa, kwani waliambiwa ametoka. Wakaacha maagizo kuwa muda wowote atakao rudi usiku ule awatafute, kwani wana shida nae muhimu awapeleke sehemu asubuhi na mapema.



Wakaacha namba za vyumba vyote viwili, maana hawakujua muda atakaorudi wao watakuwa kwenye chumba kipi, wakaelekea tena chumbani kwa Ommy. Walipoingia mle ndani na kuwasha TV walikuta kuna mechi ya mpira wa miguu, fainali ya wanawake.



Kwa kuwa wote walikuwa ni wapenzi wakubwa wa mpira wa miguu, wakaamua wakae na kutazama mechi ile. Wakiwa mzuka umewapanda kwenye mechi ile, wakasikia simu ikiita, wakaanza kusakizizana kila mtu anaona kama vile atapitwa na sehemu ya mchezo.



Ommy akajitosa na kuipokea, akasikia sauti nzuri ya kike ikimuuliza;



“Please Sir, may I talk with Mr. Ommy or Mr. Victor?

(“Samahanibwana mkubwa, Naweza kuongea na Bwana Ommy ama Victor?”)



“Yeah! Right now, U speak with Mr. Ommy.”

(“Ndio, hapa sasa hivi unaongea na Ommy.”)



“Ahaa! Ok… There are Taxi driver here, held # 1280, waiting for U at reception on ground floor Mr.”

(“Anhaa! Sawa bwana… kuna dereva wa Taxi mwenye namba 1280 anawasubiri hapa maulizo sehemu ya chini ya ghorofa hili.”)



“Ok! Give us 3 minutes we will be there.”

(“Sawa, tupe dakika 3 tu tutakuwa hapo.”)



“Right, You are most welcome.”

(“Haina shida, karibuni sana.”)



“Thanks!”



(“Ahsante!”) Alimaliza Ommy na kukuta Victor akiwa anamuangalia kwa umakini akiwa amepunguza sauti ya TV, hakumwambia kitu zaidi ya kumpa ishara ya kuwa watoke nje.



Waliteremka na kumkuta Yule dereva taxi akiwa amependeza mno kwenye suti yake ya rangi nyeupe safi. Aliwakaribisha kwenye gari yake kwani ile ndio ilikuwa ni sehemu ya ofisi yake na hasa baada ya kumwambia maneno yenyewe wanayotaka kuongea ni ya siri, walikubali na kuingia garini.



Ommy akachukua nafasi ile kujitambulisha na kumwambia wao hawana safari yoyote, ila tu wana maongezi nae nyeti ambayo yanahitaji muda wake. Wakamdanganya kuwa wao ni wafanya biashara wanaotaka kuwekeza pale Rwanda, hasa kwenye habari.



“Sasa kaka sisi hapa tunataka watangazaji wazuri, wanao kubalika mbele ya wasikilizaji, na kwa kuanzia tu, tumeambiwa kwamba kuna watangazaji wawili wa Kitanzania na tumekuona nao leo wewe usiku huu, sasa tunahitaji msaada wako.” Aliongea Victor kama vile alikuwa kajipanga.



“Ok! Sasa ni msaada gani mnaoutaka?” aliuliza Yule dereva Taxi huku akiwatazama kwa zamu

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Tunajuia kuwa wao ni wageni, lakini tunaomba historia yao japo kidogo tangu wafike hapa Rwanda.” Aliongea Ommy kasha Victor akaongezea ili tu kumkoleza Yule dereva Taxi



“Unajua ni vema saana kumuajiri mtu ambae unamjua hata kidogo, kuliko kumchukua mtu usie mjua kabisa.” Ommy akawa anatikisa kichwa kuonesha kukubaliana na maneno asemayo Victor, dereva akaingia Kingi moja kwa moja



“mimi ninawajua hawa tangu nilipokuwa nyumbani kwetu Tanzania, nilikuwa nikifanya kazi hii hii wakati huo nilikuwa nikipaki pale Kilimanjaro Kempiski.” Wakashangaa kusikia hata nae ni Mtanzania japo Kiswahili chake kilijionesha kabisa kuwa yeye ni Mtanzania wa kuzaliwa na wala si ule wa kujifunza.



Dereva akaendelea kufunguka;





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog