Simulizi : Michirizi Ya Damu
Sehemu Ya Pili (2)
ILIPOISHIA
Akaanza kuwaangalia wote wawili kwa macho yaliyokuwa na shari, kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwani hata mwili wake ulianza kutetemeka kwa hasira kali.
****
“What can I help you, sir?” (nikusaidie nini bwana mkubwa?) aliuliza Keith huku akimwangalia Godfrey aliyekuwa na hasira kali.
“I want my bae,” (namtaka mpenzi wangu)
“Your bae? Who the hell is she?” (mpenzi wako? Ndiye nani huyo?) aliuliza Keith huku akimwangalia mwanaume huyo machoni.
Godfrey akayahamisha macho yake na kumwangalia Fareed ambaye alikuwa akitetemeka tu. Kwa kitendo kile cha kumwangalia Fareed, Keith akajua mtu aliyekuwa akizungumziwa na hivyo kumuuliza Fareed kama alikuwa akimfahamu mwanaume huyo.
“I don’t know him,” (wala simfahamu) alisema Fareed huku akimwangalia Godfrey kwa macho yaliyojaa mshangao, alionekana kama kweli hamfahamu mwanaume huyo.
“Fareed, look at my eyes! Don’t you know me? Look at my eyes bastard,” Fareed, yaangalie macho yangu! Hunifahamu? Yaangalia macho yangu mwanaharamu weee) alisema Godfrey huku akionekana kuwa na hasira kali zaidi.
Bado Fareed aling’ang’ania kwamba hakuwa akimfahamu mwanaume huyo na hiyo ndiyo siku ya kwanza kumuona machoni mwake. Keith hakutaka maswali zaidi, alichokifanya ni kumwambia dereva wake aliondoe gari mahali hapo na kufanya hivyo.
Godfrey alibaki akiwa amelowa, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea, kukataliwa na Fareed mchana kweupe namna ile kulimuumiza mno moyoni mwake. Watu wote walikuwa wakimwangalia, wengine walimpigia honi kumaanisha kwamba walimtaka aondoke mahali pale ili waendelee na safari yao.
Akarudi ndani ya gari, akaingia na kutulia kwenye usukuni, alikuwa na wazo tele na muda mwingine alikuwa akitokwa na machozi, kwa kile kilichokuwa kimetokea kwake kilionekana kuwa kama ndoto ya mchana. Hakukaa sana mahali hapo, akaondoka zake huku akiwa na hasira kifuani.
Moyo wake ukajaa ghadhabu, hakufikiria kitu kingine kama kumuua Fareed. Aliutesa moyo wake, hakuwa radhi kumuona mwanaume tata huyo akiendelea kuishi na wakati aliuumiza moyo wake kupita kawaida.
“Ni lazima nimuue, nitatumia gharama zangu zote kumuua huyu mpumbavu,” alisema Godfrey huku akionekana kuwa na hasira sana. Moyo wake ukapanga kumuua Fareed kama kumlipizia kisasi kwa kile alichokifanya.
****
Wanaume wote waliokuwa wakitembea na Fareed walichanganyikiwa, hawakuamini kama alikuwa akijua sana kitandani. Mioyo yao iliuchanganyikiwa, walipokutana naye, hawakutaka kumuacha, waliendelea kumtafuta zaidi na zaidi.
Kitendo cha kuwa na Keith kwake yalikuwa mateso makubwa, alibanwa sana kwani mwanaume huyo hakutaka kumuona akiondoka kuelekea sehemu yoyote ile.
Alipokea simu kutoka kwa matajiri wengi ambao walimuahidi kumpa kiasi kikubwa cha fedha lakini kuonana nao suala hilo lilikuwa gumu sana. Aliwasiliana nao kwenye simu, aliwatumia picha zilizokuwa zikionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa mzuri.
Hakuzoea kuwa na mwanaume mmoja, tangu alipompata wakala wake, Asteria, alikuwa akitoka na wanaume mbalimbali, hayo ndiyo yalikuwa maisha yake na hata alipoambiwa na Keith kwamba hakutakiwa kutoka, kwake yalikuwa mateso makubwa.
“Haiwezekani! Siwezi kukaa na mwanaume mmoja, kwani kanioa? Yeye mbona ana familia yake, lazima nitoke,” alisema Fareed huku akionekana kutokukubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea.
Ndivyo alivyofanya, baada ya wiki moja huku akiwa amempa Godfrey mahaba mazito akaamua kuondoka na kuelekea Dubai. Hakuwa ameaga, alimtoroka kwani kitu alichokuwa akikiangalia ni kwa namna gani angeweza kuifurahisha roho yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huko Dubai alikwenda kuonana na bilionea mwingine, Saed ambaye alikuwa akimsumbua sana kwenye simu. Walipoonana kwa mara nyingine, wakaelekea kitandani ambapo huko wakafanya mambo yote na kukumbushiana siku ya kwanza walipokuwa wameonana.
Hakutaka kuwasiliana na Keith, mwanaume huyo alimpigia sana simu kutaka kuzungumza naye lakini hakupokea, alinyamaza kimya na hata zile meseji alizokuwa akitumiwa, nazo hakuzijibu japokuwa aliziona na kuzisoma.
Akili na mawazo yake yalikuwa kwa Bilionea Saed tu ambaye hakuwa msiri, alimchukua Fareed na kumtamulisha kwa baadhi ya marafiki zake na kuwaambia kwamba alikuwa mpenzi wake wa kufa na kuzikana. Hilo lilimpa furaha Fareed kwa kuamini kwamba angeishi milele na mwanaume huyo.
Marafiki wa Saed nao hawakutaka kukubali, kwa kuwa Fareed alionekana kuwavutia tena huku kwa nyuma akianza kutuna na kifua kuonekana, hawakutaka kumuacha, walichokifanya ni kuanza kummendea kitu ambacho kilimfurahisha kwani akili yake ilifikiria fedha kuliko mapenzi.
Alipokea meseji nyingi kutoka kwa wanaume mbalimbali, wote walimtaka kimapenzi. Hakuwa mchoyo, alikubali kufanya nao na hivyo kukutana nao sehemu yoyote waliyotaka na kuwaridhisha.
Ndani ya mwezi mmoja akatembea na marafiki kumi wa Saed, hakuwa akijua, alipokuwa naye alikuwa akimsifia kwa marafiki zake kumbe ndiyo haohao waliokuwa wakimbadilikia kila alipowapa kisogo.
Wakati mwezi wa pili ulipokatika, ndipo akaingia kwenye umbo rasmi la kike, alikuwa na muonekano kama wa wanawake wengine, alikuwa na kifua kikubwa, wowowo, mavazi ya kile, alijitahidi kuibadilisha sura yake kwa kuipaka sana poda, akaseti nywele zake, kwa kifupi alikuwa mwanamke kamili isipokuwa sehemu za siri ambapo alishindwa kuibadilisha.
“Hivi huyu mpumbavu Keith anaendelea kunisubiri au? Asahau! Mimi siwezi kuwa na bwana mmoja. Kwanza ukila ugali kila siku utachoka, siku nyingine kula wali, ukiuchoka, kula pilau, nalo ukilichoka, nyonya koni,” alijisemea huku akiirambaramba midomo yake kama mwanamke aliyepewa ahadi ya kukutana na mwanaume kwenye nyumba ya wageni.
Wakati yeye akifikiria hayo yote, upande wa pili Keith alikuwa na hasira kali, hakuamini kama kweli Fareed alikuwa amemtenda kiasi hicho na wakati alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kumgharamia.
Hakukubali, moyo wake ulijaza ghadhabu nzito na alikuwa tayari kufanya lolote lile kumshughulikia mwanaume huyo.
Alimtafuta, aliwaagiza vijana wake kila kona hapo Los Angeles kumtafuta na kumleta kwake. Vijana hao wakafanya kazi usiku na mchana, wakazunguka katika Cassino mbalimbali lakini hawakuweza kumuona. Hawakuishia hapo, wakazunguka kwenye miji mingine lakini napo hawakuweza kumuona kitu kilichowapa maswali mtu huyo alikuwa wapi.
“Tumemtafuta sana! Hatujamuona!” alisema kijana mmoja.
“Sawa. Ngoja nimpigie wakala wake,” alisema Keith na kumpigia simu Asteria, alitaka kufahamu mahali alipokuwa Fareed ili amuue, hata mapenzi aliyokuwa akiyataka, yakamtoka, hakuwa radhi kuona mtu aliyemgharamia akimchukua mwanaume mwingine.
“Na akisema yupo Tanzania tu, namfuata na kumuua hukohuko!” alisema Keith na kumpigia simu mwanamke huyo. Kwa kuwa Fareed hakumwambia kuhusu kumtoroka Keith, wala kumwambia kwamba alikuwa bwana wake mpya, mwanamke huyo akamwambia kwamba alikuwa Dubai akila maisha na bilionea Saed, maneno yaliyomchoma mno Keith.
“Yaani anakula maisha na mwanaume mwingine. Sasa atanitambua,” alisema Keith! Hapohapo akawapigia simu vijana wake. Alitaka kuzungumza nao, mezani kulikuwa na jambo moja tu. Kumteka Fareed na kumuua.
Huko Dubai maisha yalikuwa ni ya raha kabisa, Fareed hakuishia kwa wanaume hao tu, alichokuwa akikiangalia kilikuwa pesa tu. Siku zikakatika huku akiendelea kupata fedha, alilala katika mahoteli makubwa na ya kifahari ambayo alipangiwa na mabwana zake.
Alisahau kabisa kama kulikuwa na shida katika dunia hii, alifurahia kwa kuwa aliona kwamba hakukuwa na kitu alichoshindwa kukifanya kwa sababu alikuwa na pesa ya kufanya kitu chochote kile.
Baada ya wiki mbili akapigiwa simu na mwanaume mmoja, alikuwa mwanaume wa Kizungu aliyemwambia kwamba alitaka kuonana naye, mwanaume huyo alijitambulisha kwa jina la Mickey Downford.
Kwanza Fareed hakutaka kukubali, lilikuwa jambo gumu kukutana na mwanaume huyo, alihisi kwamba hakuwa na fedha za kumpa kwani yeye aliwazoea mabwana wa Kiarabu ambao walikuwa radhi kutoa kiasi chochote cha pesa ili kupata wanachokihitaji.
Kwa kipindi cha wiki nzima Mickey alikuwa akiomba kuonana na Fareed lakini alikuwa akikataa na wakati mwingine alimwambia kwamba hakuzoea kutembea na Wazungu, yeye aliwapenda Waarabu tu.
“Lakini nina pesa!” alisema Mickey kwenye simu.
“Nitaamini vipi?”
“Subiri! Nipe namba yako ya benki,” alisema Mickey na hivyo kupewa namba hiyo.
Ndani ya dakika kumi, simu ya Fareed ikalia kuonyesha kwamba kulikuwa na ujumbe, haraka sana akaichukua na kuangalia, ilikuwa ni meseji kutoka katika huduma ya kibenki ambayo ilimwambia kwamba alikuwa amepokea kiasi cha dola elfu hamsini, zaidi ya milioni mia moja na nusu kwa fedha za Kitanzania.
Akakaa chini, hakuamini kile alichokuwa amekiona, hakujua kama alitumiwa na mwanaume ambaye alimpuuzia kila alipomwambia kwamba walitakiwa kuonana. Kiasi hicho kilikuwa kikubwa sana kwake, kwa kawaida aliwatoza wanaume kiasi cha dola elfu moja mpaka elfu mbili, kitendo cha kupewa kiasi kikubwa cha fedha kilimchanganya. Wakati akiwa kwenye hali ya furaha, Mickey akampigia simu.
“Nadhani umeona mabadiliko kwenye akaunti yako!” alisema Mickey.
“Nimeona mpenzi!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huo ni mwanzo. Na nimekupa kiasi kidogo kwa sababu tu huniamini!” alisema Mickey.
Kichwa cha Fareed kilichanganyikiwa, hakuamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa amemtumia kiasi kikubwa cha fedha. Hapo ni kwamba hawakuwa wamekutana na kuzungumza, hawakulala kitandani alimgawia kiasi hicho cha fedha, kama angemfanyia kama wengine angepata kiasi gani?
Alipojiuliza, akajikuta akianza kuvutiwa na Mickey. Hakutaka kubaki hotelini, haraka sana anawasiliana na mwanaume huyo kwa miadi ya kuonana na kumwambia kwamba walitakiwa kuonana sehemu tulivu, katika ufukwe wa Kite uliokuwa Magharibi mwa mji huo.
Ndani ya saa moja, tayari Fareed alifika mahali hapo. Alikuwa akiangalia huku na kule akimtafuta mwanaume aliyekuwa amepanga naye miadi ya kuonana.
Baada ya dakika kadhaa, akaliona gari la kifahari, Bugatti la watu wawili likifika mahali hapo. Alilikodolea macho, lilikuwa gari la gharama kubwa na ilionyesha kwamba mtu aliyekuwa humo ndani hakuwa wa mchezomchezo kuhusu masuala ya pesa.
Mlango ukafunguliwa, ukafunguka kwa kwenda juu na mwanaume mmoja aliyevalia suti kuteremka. Watu wote waliokuwa katika ufukwe huo walikuwa wakimwangalia, hawakuamini kama kijana mdogo aliyeteremka ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo la kifahari.
“Mmh! Kuna watu wana hela bwana!” alijisemea Fareed, hakuwa amejua kwamba mwanaume huyo ndiye alikuwa Mickey aliyekuwa akimsubiri.
Moja kwa moja Mickey akaifuata meza ya chakula iliyokuwa katika eneo la kulia chakula, akachukua simu yake na kumpigia Fareed kwa ajili ya kumpa taarifa kwamba alikuwa amefika.
“Mbona sikuoni?” aliuliza Fareed.
“Unaliona hilo gari lililosimama hapo ufukweni?”
“Ndiyo! Hili la kifahari?”
“Yaap!”
“Sasa wewe upo wapi?”
“Umemuona dereva aliyeteremka?”
“Ndiyo!”
“Huyo ndiye mimi!”
“Ndiye wewe? Unaendesha Bugatti?”
“Yeah! Naomba unifuate! Bila shaka unajua hapa nilipokuja kukaa,” alisema Mickey na kisha kukata simu.
Fareed hakuamini, alimdharau mwanaume huyo lakini kumbe alikuwa bilionea mkubwa tu. Wakati anapiga hatua kuelekea kule kulipokuwa na meza ile, macho yake hayakuacha kuliangalia gari lile, lilimpagawisha na kujiona kama yeye ndiye mmiliki halali.
Alipofika katika meza hiyo, kitu cha kwanza Mickey akasimama na kumkumbatia. Ilikuwa vigumu kuamini kama mtu huyo alikuwa mwanaume kwani alivalia gauni refu, kilemba na nyuma alijazia kwani zile sindano alizokuwa amechomwa zilifanya kazi vizuri na hata kifua chake kilijaa.
“U mzuri sana,” alisema Mickey huku akimkumbatia Fareed.
“Nashukuru sana mpenzi!” alisema Fareed, akatoa tabasamu la kike na kutulia kwenye kiti.
Walizungumza mambo mengi huku Mickey akimwambia kwamba alikuwa bilionea kutoka nchini Australia na alifika hapo kwa ajili ya mambo yake ya biashara ila alipomuona klabu siku za nyuma ndizo zilimpagawisha na kuitafuta namba yake ambayo kwa maelezo yake alimwambia kwamba aliinunua kutoka kwa mtu kwa dola elfu mbili.
“Jamaniiiii!”
“Ndiyo ukweli!”
Walizungumza mambo mengi mno huku muda wote Mickey akizungumza kama bilionea mkubwa. Walichukua saa moja, walipomaliza, wakaelekea katika Bugatti ile, wakaingia na kuondoka mahali hapo.
Njiani, Fareed alipagawa mno, moyo wake ulijuta kutofahamiana na mwanaume huyo tangu kitambo kwani alikuwa mzuri wa sura na kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na pesa kitu kilichokuwa ugonjwa wake mkubwa kama mtu aliyezaliwa benki.
Wakafika hotelini, Mickey hakutaka kuwa na haraka, aliamini kwamba huyo alikuwa wake hivyo alichokiifanya ni kumuacha huku akimpa dola elfu mbili na kuondoka zake pasipo kufanya kitu chochote kile.
Fareed alichanganyikiwa, alipoingia hotelini, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mwanaume huyo tu. Hakuamini kama kweli alikuwa amefanikiwa kuwa na mtu aliyekuwa na pesa, ambaye hakuwa mchoyo kama alivyokuwa Mickey.
Akaanza kuwa msumbufu, kila wakati alikuwa akimpigia simu mwanaume huyo na kumuuliza alikuwa akiendeleaje, alitaka kuonana naye na kumpa haki yake na si kutumia pesa zake tu.
“Tutaonana tu mpenzi kabla sijarudi Australia! Utakuwa na nafasi usiku wa leo nikufuate twende klabu?” aliuliza Mickey.
“Yeah! Tena nitakuwa mpweke sana. Naomba uje kunichukua mpenzi!” alisema Fareed.
“Sawa. Nitakuja!” alisema Mickey na kukata simu.
Usiku huohuo Mickey akafika hotelini hapo, hakutaka kuchelewa, akamchukua Fareed na kuondoka naye. Walizungumza kama wapenzi, aliongea kama mwanamke na hata mapozi aliyokuwa akiyafanya pale kitini alipokaa alikuwa kama mwanamke.
Saa 8:12 usiku Mickey akamrudisha Fareed hotelini na kisha kuondoka zake. Njiani, hata kabla hajafika katika hoteli aliyochukua chumba, akachukua simu yake na kupiga upande wa pili ambapo baada ya sekunde kadhaa, ikapokelewa.
“Umefikia wapi?” iliuliza sauti ya upande wa pili.
“Kila kitu kipo poa. Kama itawezekana basi kesho tumuue,” alisema Mickey.
“Haina shida. Waambie wenzako kesho mfanye hayo mauaji! Au subiri mpaka nije. Kesho jioni nitaingia, nitahakikisha namuua kwa mkono wangu,” alisema mwanaume upande wa pili na kisha kukata simu.
Keith hakutaka kubaki nchini Marekani, aliamini kwamba kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima Fareed afe kama alivyokuwa amepanga hivyo ilikuwa ni lazima aondoke na kuelekea Dubai.
Njiani, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mwanaume huyo, aliuumiza moyo wake vilivyo, alitumia kiasi kikubwa cha fedha kumlea lakini kama kunguru vile alishindwa kufugika kabisa.
Aliamua kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumuua ili kuupa furaha moyo wake. Wakati mwingine aliiona ndege ikienda taratibu sana, alitamani hata kuiongezea kasi kwani ilikuwa ni lazima afike mapema, amuue Fareed na kurudi zake nchini MArekani.
Baada ya saa zaidi ya ishirini, ndege ikatua uwanja wa ndege ambapo moja kwa moja akaondoka na kuelekea hotelini. Akawasiliana na Mickey, kijana wake aliyempa kazi ya kufanya mauaji na kumwambia kwamba ilikuwa ni lazima waonane hotelini na vijana wenzake kwa ajili ya kupanga ni kwa namba gani wangeweza kufanya mauaji hayo.
Ndani ya dakika ishirini, vijana wote walikuwa hotelini humo. Akazungumza nao na kuwaambia mipango iliyokuwepo, wakajadili ni kifo cha namna gani mwanaume tata huyo alitakiwa kufa, wakakubaliana kwamba ilikuwa ni lazima abakwe, aingizwe kwenye boti, iende katikati ya bahari huku akiwa amefungwa miguu kwa jiwe kubwa kisha kufa hukohuko.
“Sawa. Wewe endelea kuwasiliana naye,” alisema Keith.
Hapo akawa na amani moyoni mwake, Mickey hakuwa na hofu alijua kwamba Fareed hawezi kutoka mikononi mwake hivyo ilikuwa ni lazima kufanya kama alichoambiwa.
Ili kumtia mshawasha Fareed, siku hiyo alizima simu siku nzima kitu kilichomnyima raha Fareed na kumpigia kila wakati lakini simu haikuweza kupatikana.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilipofika saa moja usiku na Fareed kupiga simu, ikawa inaita, mapigo yake ya moyo yakawa juu, hakuamini kama kweli simu hiyo ilikuwa hewani. Alikumbuka Mickey, hakujua kama mwanaume huyo alikuwa mtu mbaya aliyetaka kumuua baada ya kumbaka yeye na wenzake.
Kitendo cha Mickey kupokea simu, Fareed akaanza kuongea kwa sauti ya kulialia kwani alitaka abembelezwe sana, apozwe kama mwanamke aliyekuwa akihitaji faraja kutoka kwa mwanaume aliyekuwa akimpenda kwa dhati.
“Nisamehe mpenzi! Nilikuwa sehemu fulani hivi,” alisikika Mickey kwenye simu.
“Nimekukumbuka jamani! Mpaka nikataka nijiue kwa ajili yako,” alisema Fareed kwa sauti yake ya kuwapagawisha wanaume.
Wakazungumza mengi na mwisho wa siku wakakubaliana kwamba lingekuwa jambo jema kama wangekutaka katika Klabu ya Dubai Night kwa ajili ya kuburudika na kuzungumza mengi. Hiyo ilikuwa furaha kwa Fareed kwani kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa kipindi hicho ni kuonana na mwanaume huyo tu.
“Nakuja bebi!”
“Sawa.”
Akakata simu. Akaelekea bafuni na kujiandaa. Siku hiyo alijiapiza kwamba ni lazima alale na Mickey kwani kama asingefanya hivyo basi kungekuwa na watu ambao wangemfuata na kulala naye kisha kumsahau yeye.
HAkutaka kuona hilo likitokea. Alichukua dakika kumi kuoga, akatoka bafuni na kisha kuanza kujipaka losheni na kujipulizia marashi yake ya Kizenji, alipomaliza, akavaa taiti iliyombana hasa iliyokuwa na rangi nyeusi, akakibusti kifua chake na kisha kupaka wanja sehemu nyusi zake alizokuwa amezinyoa na kumalizia na kujipata lipstiki mdomoni.
Alipojiangalia kwenye kioo, yeye mwenyewe akajitamani, siku hiyo alitoka chicha, alikuwa akivutia na aliamini kwa kila mwanaume ambaye angemuona, kusingekuwa hata na mtu mmoja ambaye angegundua kwamba alikuwa mwanaume kwani alikuwa na muionekano wa kike kwa asilimia mia moja.
Akatoka mpaka nje ya hoteli ambapo ndani ya dakika chache, Mickey akafika mahali hapo na kumchukua. Ndani ya gari kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele. Ilikuwa vigumu kumgundua Mickey kwamba alikuwa na mpango mchafu kwani kwa jinsi alivyokuwa akitabasamu, ilionekana kabisa hakukuwa na tatizo lolote lile.
HAwakuchukua muda mrefu wakafika klabu ambapo wakateremka na kuelekea ndani. Humo, Fareed alionekana kama kuchanganyikiwa, alikuwa akicheza kila wimbo uliokuwa ukipigwa na kila alipotaka kunywa, alikwenda sehemu ya kununulia vinywaji na kunywa kwani alikuwa na mtu mwenye pesa.
Wakati hayo yote yakiendelea, vijana wa Keith walikuwa humo ndani, walikuwa wakifuatilia kila kitu, walimwangalia, wao wenyewe walihisi kwamba alikuwa mwanamke kwa jinsi alivyokuwa amejiremba na kuonekana mrembo kupita kawaida.
Muziki uliendelea mpaka iipofika saa tisa ambapo wakatoka huku Fareed akiwa amechoka kupita kawaida. Wakaingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo.
Wala hawakuchukua mwendo mrefu, Mickey akasimamisha gari pembezoni mwa barabara ambapo hakukuwa na mwanga mkali na kisha kuteremka, Fareed alishangaa, naye akateremka kwa kuhisi kulikuwa na kitu lakini hata kabla hajafanya kitu chochote kile, gari moja likasimama, wanaume wawili waliokuwa na miili mikubwa wakateremka, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumfuata, wakamkamata na kumziba mdomo kisha kumuingiza ndani ya gari lao na kuondoka.
Fareed aliogopa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendela, hakujua wale watu walikuwa wakina nani na kwa sababu gani walikuwa wamemteka kama walivyofanya.
Wakati akijiuliza hilo, mwanaume aliyekaa pembeni ya dereva akageukia kule nyuma na kumwangalia Fareed, walipogonganisha macho, akashtuka baada ya kugundua kwamba alikuwa Keith.
“Keith…” aliita Fareed.
“Yes my love!” (ndiyo mpenzi wangu) alisema Keith huku akitoa tabasamu.
“What are you doing?” (unafanya nini?)
“I just want to play a game! A nice one, it is Flecks of Blood,” (ninataka tucheze mchezo! Mchezo mzuri, unaitwa Michirizi ya Damu) alijibu Keith huku akiwa kwenye tabasamu pana.
Safari iliendelea, Fareed alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake, alijua kabisa kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, hakutegemea kuona mwanaume huyo akimfuatilia mpaka huko.
Akaanza kuomba msamaha kwa kuamini kwamba angesamehewa lakini hicho hakikuwa kipindi cha kusamehewa bali kilikuwa kipindi cha kuuawa kwa kile alichokuwa amekifanya.
Gari likaondoka na kuelekea katika ufukwe wa Kite, huko, tayari kulikuwa na boti waliyokuwa wameiandaa ambayo ingewapeleka mpaka mbali kabisa kwa ajili ya kumtosa baharini, na hawakutaka kabisa mwili wake uonekane, hivyo walikuwa na jiwe ndani ya boti ile kubwa.
Wakateremka na kuingia ndani ya boti na safari ya kuelekea katikati ya bahati kuanza. Njiani, kila mtu alikuwa akimwangalia Fareed kwa macho yaliyojaa tamaa, kwani kwa jinsi alivyokuwa, ilikuwa vigumu sana kumuacha hivihivi.
Hapo ndipo walipoanza kumbaka kama walivyokubaliana. Fareed alisikia maumivu makali, alikuwa akilia huku akitaka kuachwa lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuachia.
Aliendelea kubakwa mpaka akahisi mwili ukikosa nguvu, macho yake yakaanza kujaa giza, na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
“Tayari! Mfungeni jiwe,” aliagiza Keith, Fareed akafungwa jiwe kubwa na kisha kutupwa baharini. Akaanza kuzama huku akiwa amepoteza fahamu. Walichokifanya wanaue hao, kwa haraka sana wakaondoka mahali hapo huku kila mmoja akiwa na furaha kwani waliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angeuona mwili wa Fareed.
****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asteria alichanganyikiwa, hakujua mahali alipokuwa Fareed, alijaribu kumtafuta katika simu yake kwa kuona kwamba angempata na kuwasiliana naye kwa ajili ya biashara lakini mwanaume huyo hakupatikana.
Hakujua alikuwa wapi, aliangalia kwenye WhatsApp yake, ilionyesha kwamba mara ya mwisho kwa mwanaume huyo kuwa katika mtandao huo ilikuwa ni wiki moja iliyopita.
Hakujua ni kwa jinsi gani angempata, akajaribu kuwasiliana na Keith na kumuuliza kuhusu Fareed lakini bilionea huyo alimwambia kwamba yeye mwenyewe alikuwa akimtafuta kwani alimuaga kwamba anakwenda Dubai, baada ya hapo hakumuona tena.
Hakumwambia ukweli kwamba alimuua Fareed, alimficha kwa kuhisi kwamba siri hiyo ingedumu milele. Moyoni mwake hakuwa na huruma, kwa kile alichokifanya kwake kilionekana kuwa sahihi kwani kama kuumizwa moyo wake na mwanaume huyo, aliumizwa sana na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumuua bila huruma.
Asteria hakutaka kukubali kuendelea kubaki nchini Tanzania, Fareed ndiye alikuwa biashara yake kubwa, japokuwa alikuwa na wanawake wengine waliokuwa wakijiuza lakini kwa mwanaume huyo ndiye alikuwa soko, aliyempa pesa na kuishi katika maisha ya raha kupita kawaida.
“Nakwenda Dubai!” alisema Asteria.
“Kufanya nini?”
“Kumtafuta Fareed.”
“Kwani bado hujampata?”
“Ndiyo! Wewe umempata?”
“Hapana!”
Alikuwa akizungumza na mmoja wa wasichana waliokuwa wakimfanyia kazi. SIku iliyofuata, hakutaka kubaki nchini Tanzania, akapanga safari na kupaa kuelekea Dubai kwa kuamini kwamba angeweza kumuona huko.
Moyo wake ukaanza kuingiwa na hofu, akahisi kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa na mwili wake kutupwa kwani kwa mtu kama Fareed, jinsi alivyokuwa akipenda mitandao ya kijamii lingekuwa suala gumu sana kukaa hata saa moja pasipo kuingia Facebook, WhatsApp, Beashare au mtandao mwingine wowote ule.
Alipofika Dubai, akaelekea hotelini. Siiku hiyo hakuwa sawa, alipanga kuonana na wanawake wengine ambao walikuwa chini yake, akaonana nao na kuzungumza nao pamoja na kuwauliza kuhusu Fareed lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akifahamu mahali alipokuwa, kila mmoja alisema kwamba mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kabla hajakwenda Ubelgiji, baada ya hapo hawakujua alikuwa wapi.
Alikaa Dubai kwa mwezi mzima, hakumuona Fareed na wala hakujua mahali alipokuwa. Akakata tamaa na kuona kwamba tayari mwanaume huyo alikuwa marehemu hivyo kitu pekee alichokuwa akikitaka ni kuiona maiti yake ili ajiridhishe tu.
“Hata nikiiona maiti yake nitashukuru Mungu! Yaani Fareed amekufa? Amekufaje? Mbona hata taarifa sikupewa?” alijiuliza huku akiwa amechanganyikiwa, hakujua kabisa mahali alipokuwa mtu huyo.
Alichokifanya ni kuwasiliana na marafiki zake wengine waliokuwa wakiishi nchini humo na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba kulikuwa na ndugu yake ambaye hakujua mahali alipokuwa mpaka muda huo, hao ndiyo waliomshauri kwamba alitakiwa kutembelea katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya kumtafuta kwani inawezekana alikuwa amekufa ila mwili wake ulihifadhiwa mochwari.
Hilo lilikuwa wazo zuri, alichokifanya siku iliyofuata ni kwenda katika hospitali mbalimbali lakini kote huko hakuweza kuukuta mwili wa Fareed kitu kilichomfanya kumalizia katika hospitali ya mwisho ya Sultan Idris Medical Center iliyokuwa pembezoni mwa Dubai ambapo haikuwa mbali kutoka baharini.
Alipofika huko akajitambulisha na kitu kilichomfanya kufika mahali hapo. Kwa jinsi alivyokuwa akijielezea, kila mmoja alimuonea huruma hivyo kumchukua na kuondoka naye kuelekea mochwari kwa ajili ya kuitambua maiti ya ndugu yake aliyokuwa akiitafuta.
“Ni tangu lini?” aliuliza daktari.
“Mwezi mmoja sasa umepita sijaweza kumuona.”
“Una uhakika kwamba alikuja Dubai?”
“Ndiyo! Mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuja huku,” alijibu Asteria.
Hawakuchukua mwendo mrefu wakafika katika mochwari ya hospitali hiyo na hivyo kuingia ndani. Humo ndani kulikuwa na masanduku mengi ambayo ndani yake kulikuwa na maiti kadhaa huku kukiwa na baridi kali ambalo muda mwingi Asteria alikuwa akitetemeka tu. Wakaanza kuzunguka huku na kule, wakayafungua madroo makubwa na kuangalia ndani kama kulikuwa na maiti ya Fareed.
Walizunguka kwenye madroo mengi lakini hawakufanikiwa kuiona maiti ya Fareed kitendo kilichomfanya kuhisi kwamba mwanaume huyo hakuwa amekufa lakini wakati akijiandaa kutoka ndipo akaambiwa kwamba kulikuwa na sehemu nyingine ya madroo hawakuwa wameangalia hivyo wakaelekea huko.
Walipofika, yakafunguliwa na kuanza kuangalia maiti moja baada ya nyingine. Muda wote mapigo ya moyo wake yalikuwa juu, kila alipopiga hatua alikuwa akitetemeka mno.
Baada ya dakika kadhaa, wakafika katika droo moja kubwa, ndani yake kulikuwa na maiti ya mtu mmoja, ilikuwa imefunikwa, haraka sana msimamizi aliyekuwa ndani ya mochwari ile akaifungua maiti ile, macho ya Asteria yalipotua katika sura ya maiti ile, miguu yake ikamlegea, hakuamini kile alichokiona, akashindwa kuvumilia, hapohapo akaanza kulia kama mtoto.
Maria alikichanganya kichwa cha Keith, hakutaka kukubali hata mara moja, kwake, msichana huyo alionekana kuwa na uzuri wa ajabu na alipanga kuwa naye maisha yake yote, hata kama ingemgharimu kiasi cha fedha kikubwa namna gani lakini ilikuwa ni lazima amchukue.
Walipoondoka Malaysia safari ya kwanza ilikuwa ni kwenda nchini Marekani. Hakutaka kumuacha msichana huyo, alizungumza naye sana, alimtongoza, kwa kutumia uwezo wake kifedha, akafanikiwa kumpata msichana huyo ambaye alikubaliana naye kwenda nchini Marekani kula raha kama kawaida yake.
Huko, walifanya kila kitu kilichotakiwa kufanywa kwa wapenzi, akatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya Maria. Akamtambulisha kwa marafiki zake, kwa kuwa alikuwa kwenye makwaruzano na mkewe kwa muda mrefu, akawaambia kwamba huyo ndiye ambaye angeziba pengo la mkewe kama tu wangetengana.
Maisha yaliendelea kama kawaida, hakutaka kumkumbuka Fareed, aliamini kwamba msichana huyo alifariki dunia nchini Dubai, moyo wake ulijisikia amani tele, kuua, halikuwa jambo la kushangaza kwake, kama walivyokuwa mabilionea wengine, hata kwake kuua ilikuwa ni sawa na kumuua panzi.
Uhusiano wao haukuwa siri hata kidogo, waandishi wa habari wakazipata taarifa hizo, wakaanza kuwapiga picha na kuziweka kwenye mitandao huku wengine wakizitumia picha hizo kuziweka katika magazeti yao.
Kila mmoja alishtuka, hakukuwa na aliyeamini kama mzee huyo angemchukua msichana kama Maria. Si kwamba hakuwa mzuri bali alikuwa msichana wa Kiafrika, na mabilionea wengi nchini Marekani walipenda kuwa na Wazungu wenzao.
Safari hazikukoma, mara kwa mara walikuwa wakisafiri huku na kule wakila bata, hakutaka kuona akitulia, kwa sababu alimpenda Maria kwa mapenzi ya dhati aliamini kwamba kama angekwenda naye sehemu mbalimbali kula raha basi ingemfanya kufanikiwa kuliteka penzi la msichana huyo moja kwa moja.
Kwa kuwa alijua kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na bilionea mkubwa duniani, Maria hakutaka kuona mwanaume huyo akiondoka mikononi mwake, alijitahidi kumfanyai utundu mkubwa kitandani kiasi kwamba mzee wa watu alichanganyikiwa kabisa.
Alimfanyia utundu mithili ya mwanamke aliyetoka kuchezwa siku za karibuni, alijua kummiliki mwanaume, alimfanyia mambo mengi ambayo mengine mzee huyo hakuwahi kufanyiwa, alibaki akistaajabu kwamba msichana kama Maria aliwezaje kumfanyia mambo yote hayo.
“How did you know all these things?” (umejuaje mambo yote haya?) aliuliza Keith huku akiwa amelala pembeni mtupu, kijasho kilikuwa kikitoka, kwa shughuli aliyokuwa ameonyeshewa, hata kuendelea alishindwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“I was taught to take care of men like you!” (nilifundishwa kuwashughulikia wanaume kama wewe) alisema Maria.
“Ooh! Maria, I will never leave you, just be with me forever,” (Ooh! Maria, sitokuacha kamwe, naomba uwe nami milele yote) alisema Keith.
“No problem! Give me some more sweetie,” (hakuna tatizo! Naomba tena mpenzi) alisema Maria, wakati akiyazungumza hayo tayari alikuwa juu ya Keith na kumkalia, akaanza kumminyaminya mwili wake.
“I can’t! You will kill me,” (siwezi! Utaniua) alisema mzee huyo.
“You rather die. Give me some more,” (Bora ufe. Naomba tena) alisema Maria, kilichofuata ni kushika maiki na kuanza kuimba.
Hiyo ndiyo ilikuwa njia sahihi ya kumteka mzee huyo, kwa kufanya hivyo, alizidi kupendwa, alipewa kiasi kikubwa cha fedha kilichomchanganya kupita kawaida, hakutaka kuona akimuacha mwanaume huyo, kwake, alikuwa kila kitu na alitaka kuhakikisha anazichuma pesa zake kadiri anavtyoweza.
Mzee wa watu alizidi kupagawa, alikuwa radhi kugombana na kila mtu lakini si Maria. Alimpenda kwa penzi la dhati na kila siku alikuwa akipewa mambo mapya kitandani ambayo yaliuchanganya moyo wake kupita kawaida. Hakutaka kuwaambia marafiki zake kuhusu Maria, alijua fika kwamba kulikuwa na kugeukana, siri ya ujuzi wa Maria kitandani ukabaki moyoni mwake, aliendelea kulala naye na kufanyiwa vituko vya kimahaba kila siku.
“Nitampa kila kitu! Hakika ameniondoa ukungu katika mapenzi kitandani! Mwanamke anajua utadhani nini! Ni lazima nitangaze ndoa,” alisema Keith huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikiongea.
***
Fareed alikuwa safari akielekea nchini Kuwait, tayari aliwasiliana na bilionea Sadiq Rahman kutoka nchini humo ambaye alikuwa akimuhitaji kimapenzi kuliko kitu chochote kile. Moyo wake ulikuwa na furaha na muda wote alikuwa akimshukuru Asteria kwani yeye ndiye alikuwa mchakarikaji katika kuwatafutia mabwana waliokuwa na pesa katika nchi za Kiarabu.
Njiani, huku akiwa ndani ya ndege moyo wake ulikuwa na hofu tele, hakujua nu kitu gani ambacho kingetokea huko. Hakutaka kuona Keith akigundua kwamba alikuwa hai, alitaka mwanaume huyo ajue kwamba alikuwa amekufa mpaka siku ambayoo angeamua kumuua kama kulipa kisasi.
Akiwa ndani ya ndege, akachukua Gazeti la The Mirror na kuanza kulisoma. Humo ndania akakutana na habari iliyomshtua ambayo ilimuhusu bilionea Keith ambaye alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msichana wa Kinigeria aliyeitwa Maria.
Moyo wake ulimuuma sana, wivu ukamkamata, japokuwa alifanyiwa mambo mengi mabaya na mwanaume huyo lakini bado sehemu ya moyo wake ulikuwa ukimpenda. Akakunja sura yake na kuliweka pembeni gazeti lile.
Safari ilikuwa ndefu lakini walifika salama ambapo akateremka na nje akakutana na mwanaume mmoja aliyekuwa na boksi kubwa kiasi lililoandikwa jina lake alilokuwa akijulikana sana kipindi hicho, Farida.
Akamsogelea mwanaume huyo na kisha kumsalimia. Kwa kuwangalia, ilikuwa vigumu kugundua kwamba mtu huyo alikuwa mwanaume, alijipamba, alijiwekea wigi kichwani, alivalia gauni huku midomo yake ikiwa imepakwa shedo iliyokolea na nyusi alizinyoa kisha kupaka wanja.
Alivutia, kwa nyuma, alikuwa na mzigo wa maana, kifua kilituna, alikuwa na muonekano wa kike kwa asilimia mia moja na kila mwanaume aliyemwangalia, alimtamani.
Akachukuliwa na mwanaume huyo na kuelekea ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea katika jumba alilotakiwa kulala kwa siku hiyo. Njiani, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule, moyo wake ulichanganyikiwa kwa furaha, haikuwa mara yake ya kwanza kufika nchini humo ila kilichomfanya kuwa na furaha ni kwamba alirudi kwenye chati baada ya kupotea.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika jumba moja kubwa ambapo gari likaingizwa ndani. Akabaki akiliangalia jumba hilo, lilikuwa kubwa, lenye mapambo yaliyonakishiwa kwa rangi ya dhahabu, bwawa kubwa la kuogelea na vitu vingine vingi, kwa kifupi, kwa kuliangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua kwamba hilo lilikuwa jumba la bilionea mkubwa nchini hapo.
Akaingia ndani, macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule, lilipendeza sana, aliliguata kochi na kutulia, lilibonyea na kuyafanya makalio yake kuhisi yamekalia kitu kilichokuwa na thamani kubwa.
Wakati akiwa hapo, mlango mwingine ukafunguliwa na mwanaume mmoja aliyevalia msuli kutokea sebuleni hapo. Alikuwa mwanaume mwenye kitambi kikubwa, ndevu nyingi alizozipaka hina, alionekana kabisa kwamba alikuwa ndama, akamfuata Fareed kochini pale, akamuinua kisha kumkumbatia.
“Wewe ndiye mwenyewe?” aliuliza Mzee Sadiq.
“Ndiyo!”
“Aisee! Unaonekana kama mwanamke mbichi,” alisema Mzee Sadiq huku akiachia tabasamu.
Kwa mwendo wa madaha akamchukua na kumpeleka katika chumba walichotakiwa kulala usiku huo. Walipofika, akamuweka kitandani na kumwambia amsubiri kwani kulikuwa na mambo alitaka kukamilisha kabla ya kushinda naye chumbani.
“Haina shiida.”
Mzee huyo akatoka chumbani humo. Fareed alibaki akikishangaa chumba hicho, kilimstaajabu sana, na kila alipokuwa akikiangalia, aliona kabisa hakikuwa kikistahili kukaliwa na mtu kama yeye.
Wakati akiwa hapo, mara simu yake ikatoa mlio kumaanisha kulikuwa na ujumbe mfupi wa simu umeingia. Haraka sana akaichukua simu yake na kuufungua ujumbe huo ambao haukuandikwa maneno mengi, ulisomeka: ‘Nimekuona ukiingia Kuwait. Naomba nikuone ukitoka kwa huyo babu’ ulisomeka ujumbe huo, akashtuka.
“Wewe nani?” aliuliza.
“Naitwa Belleck Peter.”
“Ndiye nani?”
“Huwezi kunijua. Ila nilipata mawasiliano yako kutoka kwa Asteria. Amenipatia namba yako. Naomba nikuone ukitoka kwa huyo mzee,” aliandika mwanaume huyo.
“Mmh! Sawa.”
Hapohapo bila kuchelewa Fareed akampigia simu Asteria na kumuuliza kuhusu mwanaume huyo. Asteria alikiri kumpa namba kwa kuwa alikuwa mteja mkubwa wa wanaume tata. Alikuwa Mmarekani bilionea ambaye kwake, pesa hazikuwa tatizo hata kidogo.
“Ila hajuani na Keith! Asije kuniletea shida!”
“Hilo ondoa shaka. Hawajuani kabisa.”
“Sawa,” alisema Fareed na kukata simu. Hapohapo akapiga magoti, akamshukuru Mungu kwa kumuumba mwanaume, kwani kama angekuwa mwanamke, hakika asingeweza kukutana na mabilionea hao.
“Mungu! Nashukuru sana kwa kuniumba mwanaume. Ungeniumba mwanamke, sijui kama ningepata mazali kama haya,” alisema Fareed huku akitoa tabasamu pana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda huo ulikuwa zamu ya Mzee Sadiq, alilala na Fareed usiku kucha, haikuishia siku hiyo, huo ulikuwa muda wake wa kuwa na mwanaume tata huyo. Maisha ya Fareed yaliendelea kubadilika, alikaribia kuwa milionea kwa sababu tu alijiuza kwa wanaume matajiri ambao walikuwa tayari kutoa kiasi chochote cha fedha mpaka kufanikisha kile walichokuwa wakikihitaji.
Siku ziliendelea kukatika, waliendelea kuwa pamoja. Japokuwa maisha yalikuwa mazuri, alipata kila kitu alichokuwa akikihitaji lakini hakuacha kuwasiliana na wanaume wengine, wote hao alitaka kulala naye na mwanaume ambaye alikuwa na hamu naye kwa kipindi hicho alikuwa Belleck.
Aliendelea kuwasiliana na mwanaume huyo, hakutaka kuonana naye kwa muda huo, alitaka kumuweka kiporo, alale naye katika siku za mwisho za kutaka kuondoka nchini humo.
Kwa kuwa mwanaume huyo alimuhitaji sana, alijitahidi kumtumia kiasi kikubwa cha fedha, kila shida ambayo Fareed alikuwa akiililia, alitumiwa fedha na mwanaume huyo ingawa hawakuwa wameonana.
Baada ya kukaa na Mzee Sadiq kwa siku kadhaa hatimaye akaamua kuondoka nyumbani kwa mzee huyo na kwenda kuonana na Belleck ambaye alionekana kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.
Macho yake yalipotua kwa mwanaume huyo, moyo wake ulimlegea, alikuwa mwanaume mwenye sura nzuri, ya kitoto ambapo mwili wake ulikuwa umejazia kidogo. Alipomuona tu, moyo wake ukatokea kumpenda, alikuwa ana mvuto wa ajabu, zaidi ya wanaume wote ambao aliwahi kukutana nao.
Belleck alivalia suti iliyotengenezwa na Kampuni ya Pollo, alivalia saa nzuri, ya thamani iliyotengenezwa na Kampuni ya Solex, kwa kifupi, muonekano wake ulikuwa ni wa kitajiri.
“Fareed…” aliita Belleck huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Nimekuja kukuona mpenzi!” alisema Fareed.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuonana na mwanauume huyo, kilichofuata baada ya hapo ni kula maisha kwa kutembea sehemu mbalimbali. Fareed alijisikia amani moyoni, hakuuacha kumshukuru Mungu kwa kumuumba mwanaume.
Alijua kwamba kuulikuwa na wanawake wengi waliotamani nafasi kama ile aliyokuwa nayo lakini hakukuwa na yeyote aliywahi kuipata. Alifarijika na muda wote alijiona kuwa mtu mpya, aliyebarikiwa na Mungu, mtu msafi ambaye hata kama angekufa basi angekwenda peponi.
“Nakupenda sana Fareed,” alisema Belleck huku wakiwa kitandani.
“Nakupenda pia!” alijibu Fareed na kumbusu shavuni.
***
Belleck Peter alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa waliokuwa na kampuni nyingi nchini Marekani. Alikuwa miongoni mwa watu waliojitengenezea utajiri mkubwa huku ukiendelea kuongezeka kila siku iliyoitwa leo.
Alikuwa miongoni mwa mabilionea ambao waliheshimika nchini Marekani kutokana na mchango mkubwa aliokuwa akiutoa katika jamii. Utajiri wake wa dola bilioni kumi na tano ulikuwa ukitikisa kila kona. Alikuwa mtu wa watu, bilionea asiyekuwa na sifa, bilionea ambaye siku zote alitaka kuishi katika maisha ya chini kwa ajili ya kuwafanya hata wale masikini kuona wapo sawa naye.
Japokuwa alikuwa na kampuni nyingi lakini nyuma ya pazia utajiri wa mwanaume huyo ulikuwa ukisaidiwa na biashara kubwa ya madawa ya kulevya aliyokuwa akiifanya. Hiyo ilikuwa siri kubwa, aliwaandaa vijana wake ambao walikuwa wakizunguka dunia nzima kwa ajili ya kumfanyia kazi hiyo.
Alijificha kwa kutumia kivuli cha serikali, hakukuwa na mtu aliyehisi kama mwanaume huyo alikuwa akishughulika na biashara hiyo. Alikuwa na vijana wa Kimexico ambao walikuwa na kazi kubwa ya kusambaza mizigo yake Marekani ya Kati na Kusini, alikuwa na vija abarani Afrika ambao nao alikuwa akiwatumia kumsafirishia biashara yake.
Alitisha, utajiri wake uliongezeka. Kwa kuwatumia vijana wake, akawatafuta watu wengine ambao walikuwa na kazi ya kumeza dawa hizo na kuzipeleka sehemu husika. Wanaume wengi waliogopa kumeza kwa kuwa walipata tabu muda wa kutoa madawa hayo chooni kupitia sehemu ya haja ndogo na ndiyo ikawa sababu ya kuwatafuta wanaume waliokuwa wakijihusisha na mapenzi ya jinsi moja.
Kwenye kutafuta watu hao, aliwapata wengi, aliwatumia, hakutaka kuacha, aliendelea kujificha kwa mwamvuli wa serikali. Kwenye kuendelea kutafuta wanaume hao, ndipo akafanikiwa kumpata Fareed.
Hakumpenda mwanaume huyo, aliamua kuwa naye kwa kuwa alitaka kuona biashara yake ikiendelea kusonga mbele, alitaka kumtumia katika kusafirisha biashara zake kama walivyofanya wenzake.
Alitumia kiasi kikubwa cha fedha kumuhonga lakini alijua kwamba mwisho wa siku angepata kile alichokuwa akikihitaji. Alimuonyeshea mapenzi ya dhati, Fareed hakujua kwamba mwanaume huyo hakuwa tofauti na Keith, aliendelea kumwamini kila siku.
Aliwapanga vijana wake kama kawaida, ilikuwa ni lazima kumtumia mwanaume huyo kusafirisha madawa yake kupeleka nchini Ufaransa na baada ya kufika huko, vijana wake wangempokea na kumlazimisha kuyatoa kisha kumuua.
Hilo halikuwa tatizo, akajipanga kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Kabla ya kumsafirisha ilibidi kwanza amleweshe na kisha kumywesha kete za madawa ya kulevya na kisha kumlazimisha kusafiri kuelekea nchini Ufaransa.
“Ushawahi kunywa Kemikal Boom?” aliuliza Belleck huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Hapana!”
“Hahaha! Unakosa utamu mkubwa sana. Ni pombe nzuri yenye kulewesha kidogo,” alisema Belleck huku akiifuata chupa moja iliyokuwa mezani ambayo iliandikwa Kemical Boom ambayo ilikuwa na kilevi cha 70%.
“Mmh! Nitaiweza?”
“Kwa nini uishindwe mpenzi! Ni tamu sana,” alisema Belleck huku akichukua glasi na kuimimina pombe ile katika glasi ile aliyokuwa nayo.
Ilikuwa vigumu kwa Fareed kugundua kwamba mwanaume huyo alikuwa mtu mbaya katika maisha yake, alichokiona, kilikuwa ni mapenzi ya dhati, kila alichokuwa akifanyiwa, kwake kilionekana kuwa sahihi kwa kuwa tu alipewa fedha nyingi na mwanaume huyo.
Akaifakamia pombe hiyo na kuanza kunywa kwa kasi. Hakuchukua dakika nyingi, akahisi viungo vya mwili wake vikianza kuuma, akaanza kusikia kizunguzungu, ilikuwa pombe kali na hakutakiwa kunywa nyingi kiasi hicho. Wakati akiwa kwenye hali hiyo, ndiyo kwanza Belleck alikuwa akicheka tu.
“Nimelewa…..” alisema Fareed. Hakukaa kwenye hali hiyo kwa muda mrefu, akaona giza, akajilaza kitandani, alionekana kama mtu aliyepoteza fahamu.
“Safi sana! Ngoja niwaite vijana,” alisema Belleck, hapohapo akachukua simu na kuwapigia vijana wake wa kazi.
Ndani ya dakika kadhaa wanaume watatu wakafika mahali hapo, walikuwa wamejiandaa vilivyo, kwa jinsi walivyoonekana, walikuwa tayari kufanya kazi muda wowote ule. Belleck akawakaribisha huku akionekana kuwa na furaha tele, katika maisha yake yote, hakukuwa na kitu kilichokuwa kikimuingizia fedha kama biashara ya madawa ya kulevya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitaka kumtumia Fareed katika biashara zake, alitaka kumpa mzigo wa madawa ya kulevya na kuyasafirisha maka nchini Ufaransa. Hilo kwake halikuwa tatizo, usiku huohuo wakamnywesha kete kumi na mbili za madawa ya kulevya na kumsubiri aamke ndipo wamwambie kuhusu safari hiyo kwani tayari walimuandalia tiketi yake.
Fareed aliamka baada ya saa moja kupita. Alijisikia uchovu, hakujua alikuwa mahali gani. Pale alipokuwa kulikuwa na kitanda kikubwa, chumba kizuri, akaamka na kuanza kuangalia huku na kule na ndipo kumbukumbu zake zikaanza kurudi na kukumbuka kwamba mara ya mwisho alikunywa pombe kali na baada ya hapo hakujua ni kitu gani kiliendelea.
“Nipo wapi? Belleck kanileta wapi?’ alijiuliza huku akisimama kutoka pale alipokuwa.
Akaelekea dirishani, akachungulia, alikuwa kwenye ghorofa ya nne, aliogopa, ile haikuwa hoteli aliyokuwa amefikia, ilikuwa nyingine kabisa. Alipoangalia kwenye kimeza kidogo akakutana na kitabu kidogo kilichoandikwa ‘King Caspian Hotel’.
“Nimefikaje King Caspian?” alijiuliza.
Aliijua hoteli hiyo, ilikuwa hapohapo Kuwait, haikuwa hoteli ile aliyofikia, alijiuliza sana lakini mwisho wa siku akajua kwamba Belleck ndiye aliyekuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Alijaribu kutoka ndani ya chumba hicho, mlango ulikuwa umefungwa kwa nje, moyo wake ukajawa na hofu kwa kuhisi kwamba Belleck alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa Keith ambao walijua kwamba hakuwa amekufa baharini hivyo kutaka kumuua tena.
“Mungu! Huyu Keith ananitakia nini lakini?” alijiuliza huku akionekana kuwa na hasira kali.
Akaliangalia begi lake lililokuwa pembeni, zipu ilikuwa wazi kuonyesha kwamba kulikuwa na mtu alilifungua, alipoangalia ndani, akakuta kukiwa kumepekuliwa, hakukuwa na vitambulisho vyake, hakukuwa na hati ya kusafiria.
Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Moyo wake ukaingiwa na hofu kwa kuona kwamba alipoteza kila kitu, akakifuata kitanda, akakaa na kuanza kulia.
Wakati akiendelea kulia, mara mlango ukafunguliwa na wanaume watatu kuingia ndani ya chumba hicho. Hawakuzungumza kitu, walibaki wakimwangalia. Harakaharaka Fareed akasimama na kuwaangalia, akajua kwamba watu hao ndiyo waliokuwa wamefungua begi lake na kupekua.
“Naomba mnisamehe! Hivi kwa nini Keith anataka kuniua? Nimemfanya nini? Kama ni gharama za pesa yake nitamrudishia,” alisema Fareed huku akiendelea kulia.
“Keith ndiye nani?”
“Bosi wenu aliyewatuma!”
“Hatumfahamu huyo. Tumekuja kukupa ujumbe mmoja.”
“Upi?”
“Unatakiwa kusafiri leo kuelekea Ufaransa,” alisema mwanaume mmoja.
“Kuelekea Ufaransa?”
“Ndiyo!”
“Kufanya nini?”
“Una mzigo wetu tumboni mwako, utatakiwa kufika nchini humo. Utakapofika katika Jiji la Marseille, ukitoka nje utakuta kuna mtu anakusubiri huku akiwa na bango lililokuwa na jina lako, mfuate huyo, ukipinga na kufanya kitu cha tofauti, tutakuua!” alisema mwanaume huyo huku akimwangalia Fareed kwa macho yaliyomaanisha kile alichokuwa akikisema.
“Sawa,” alijibu Fareed huku akitetemeka.
Muda ulipofika, akakabidhiwa kila kitu na kuanza kuelekea uwanja wa ndege. Moyo wake ulijuta, wakati mwingine alijiapiza kutokurudia kufanya ukahaba kwa Wazungu kwani wao ndiyo waliokuwa wakimuingiza kwenye matatizo tofauti na Waarabu ambao wao walichokuwa wakikihitaji ni mapenzi tu.
Njia nzima alilia, hakunyamaza, mpaka alipoingia ndani ya ndege bado aliendelea kulia kama kawaida. Moyo wake ukaanza kuifikiria safari hiyo, hakujua kama angevuka salama uwanja wa ndege kwani kwa nchi za Ulaya na Marekani kulikuwa na ulinzi mkali viwanjani kuliko hata katika nchi za Afrika na Asia.
Alitumia saa thelathini kwenye ndege, tena kwa kubadilishabadilisha mpaka alipofika nchini Ufaransa katika Jiji la Marseille. Akateremka na abiria wengine, mabegi yakapita sehemu ya uchunguzi na wao kuruhusiwa.
Hakushtukiwa na mtu yeyote yule, akatoka na kwenda sehemu ya watu waliokuja kuwasubiri watu wengine, hapo akamuona kijana mmoja akiwa amesimama huku akiwa na bango dogo lililoandikwa jina lake ambapo akamfuata na kujitambulisha kwamba yeye ndiye alikuwa Fareed.
“Are you Fareed?” (wewe ndiye Fareed?) aliuliza jamaa huyo huku akishangaa.
“Yes!” (ndiyo)
“How? Are you a boy or girl?” (Kivipi? Wewe ni mvulana au msichana?)
“Hey! You are wasting my time. Take me where Am suppose to be,” (Hey! Unanipotezea muda. Nipeleke ninapotakiwa kuwa) alisema Fareed huku akionekana kuanza kukasirika.
Mwanaume huyo hakuongea kitu chochote lakini alionekana kuwa na maswali mengi kichwani mwake. Alikuwa akijiuliza kuhusu mtu aliyekwenda kumpokea, ilikuwa awe na jina la kiume na wakati alikuwa na muonekano wa kike? Alivalia gauni refu, kichwani alikuwa na wigi, alipaka wanja na lipstic, sasa ilikuwaje awe mwanaume?
Hakutaka kujiuliza maswali zaidi bali ni kukaa kimya na kuendelea kuendesha gari kuelekea katika sehemu ambayo alitakiwa kumpeleka mgeni huyo. Akiwa hapo njiani akamtumia meseji Belleck kwamba mgeni aliyetakiwa kufika, tayari alikuwa ndani ya gari
***
Belleck aliwaanda vijana wake kwa ajili ya kazi ya kuyatoa madawa ya kulevya kutoka tumboni mwa Fareed. Yalikuwa ni madawa yenye thamani kubwa ambayo yangemuingizia kiasi kikubwa cha fedha.
Kete za madawa hayo zilikuwa tumboni mwa Fareed, kwa kawaida alitakiwa kwenda kujisaidia ili kutoa kete hizo lakini Bellck hakutaka kuona hilo likifanyika na badala yake alihitaji mtu huyo apasuliwe tumbo na kutolewa madawa hayo.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, waliwahi kufanya kazi kama hiyo kipindi cha nyuma kwa watu wengi, kuua, kwa vijana hao lilionekana kuwa jambo dogo sana ambalo lilikuwa ni kama kumuua sisimizi kwa kumkanyaga.
Walijiandaa nyumbani, walimtuma mwenzao kwenda kumpokea Fareed uwanja wa ndege ili atakapofika basi kazi ya kumpasua tumbo ianze mara moja.
Belleck alivyotumiwa meseji kuambiwa kwamba mtu huyo aliwasili na alikuwa ndani ya gari, naye akawapigia simu vijana wake na kuwaambia kwamba mtu waliyeta kumpasua tumbo na kumtoa madawa hayo alikuwa garini akielekea hapo nyumbani.
“Hakikisheni mnamuua na kutoa huo mzigo. Ni wa gharama sana, kama ukipotea nitapata sana hasara,” alisema Belleck kwenye simu.
“Hakuna shida mkuu! Wapo njiani wanakuja.”
“Basi haina shida. Kazi njema.”
“Nawe pia.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawakuchukua muda mrefu wakafika ndani ya jumba hilo la kifahari. Moyo wa Fareed ulikuwa ukitetemeka, hakuamini kama kweli alikuwa amenusurika katika mdomo wa kifo kwa bilionea Keith lakini mwisho wa siku alikuwa kwenye mdomo wa kifo kwa bilionea mwingine.
Aliumia na wakati mwingine alikuwa akijutia kazi yake ya kujiuza aliyokuwa akiifanya kwa moyo mmoja. Aliwachukia Wazungu, hakutaka uswahiba nao tena, kila alipoifikiria safari ya maisha yake mpaka kunasa kwa watu hao, moyo wake uliumia kupita kawaida.
Gari likasimama katika eneo la kupaki magari na wanaume wawili waliokuwa na bastola kutokea mahali hapo. Wakaufungua mlango na kumshusha Fareed kinguvu kisha kuanza kumpeleka ndani.
Walimshangaa mwanaume huyo, muonekano wake ukawatia hofu kwa kuhisi kwamba huyo hakuwa mwanaume kama walivyoambiwa, walihisi kwamba alikuwa mwanamke kutokana na muonekano wake wa kike aliokuwa nao.
Wakamchukua na kumpeleka katika chumba kimoja kilichokuwa na meza kubwa pamoja na vifaa vya kumfanyia mtu upasuaji. Fareed alipoviona vifaa hivyo na chumba hicho, moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama siku hiyo na yeye alibebeshwa madawa ya kulevya kama walivyokuwa wakifanyishwa watu wengine.
“Call Dr. Watson,” (mpigie simu daktari Watson) alisema mwanaume mmoja.
Bonny Watson alikuwa daktari kutoka katika Hospitali ya St. Napoleon iliyokuwa hapohapo Marseille nchini Ufaransa. Daktari huyu ndiye aliyekuwa akitumiwa sana na Bilionea Belleck kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji watu wote waliokuwa wakimeza kete za madawa ya kulevya nchini Ufaransa.
Hakukuwa na mtu aliyepona, wote waliokuwa wakipelekwa huko, walichomwa sindano ya usingizi na kufanyiwa upasuaji huo ambao uliwapelekea vifo vyao.
Alizoea kazi hiyo, alilipwa kiasi kikubwa cha fedha na hakutaka kuiacha. Mara kwa mara Bilionea Belleck alipokuwa akiwatuma watu, alipigiwa simu na kuambiwa aelekee nyumbani kwa bilionea huyo kisha kufanya kazi hiyo au kama alibanwa sana basi ilikuwa ni lazima mtu huyo apelekwe katika hospitali yake na kumfanyia upasuaji.
Muda huo alipigiwa simu na kijana wa Belleck na kumwambia kwamba kulikuwa na kazi alitakiwa kuifanya. Hakushtuka lakini kwa siku hiyo kulikuwa na ugumu kwani hospitalini hapo alikuwa na wagonjwa ambao walihitaji sana kufanyiwa upasuaji.
“Mleteni lakini nitamfanyia baada ya saa tano,” alisema Dk. Watson.
“Haina shida.”
Hawakutaka kubaki nyumbani hapo, haraka sana akachukuliwa na kupelekwa katika hospitali hiyo. Muda wote huo Fareed alikuwa na hofu moyoni mwake, alihisi kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake.
Alikuwa na mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya tumboni mwake, wakati mwingine alihisi kwamba kete zile zingeweza kupasuka na madawa hayo kusambaa mwilini mwake na kumuua.
Hakutaka kuona hilo likitokea, alilia kimyakimya, kwake, Belleck alionekana kuwa mwanaume katili aliyeithamini fedha yake kuliko hata uhai wa watu wengine. Huyo hakuwa mwanaume aliyestahili kuwa hai, alitakiwa kuuawa kwani kwa kutumia fedha zake alipata nafasi ya kuwafanyia watu wengine matendo mabaya ya kikatili.
“Mungu nisaidie! Nikitoka katika hili, nitakukabidhi maisha yangu!” alisema Fareed huku gari likiwa safarini kuelekea hospitalini huko.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika hospitalini hapo ambapo moja kwa moja akachukuliwa na kupelekwa katika chumba maalumu kwa ajili ya mapumziko. Hapo alipokuwa, muda wote mwili wake ulikuwa ukimtetemeka, aliogopa, mbele yake alikiona kifo kitu ambacho hakutaka kukiona kikitokea mpaka pale atakapokamilisha ndoto zake.
“Mbona unakuwa na hofu sana?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Hapana! Sina hofu!”
“Usiogope. Ni suala la kuchukua mzigo wetu na wewe tutakuruhusu kuondoka,” alisema mwanaume huyo, japokuwa alijitahidi kumuondoa hofu Fareed lakini hakuonekana kuwa na amani hata kidogo.
Baada ya dakika kadhaa, daktari huyo akafika mahali hapo, akamwangalia fareed, uso wake ulikuwa na maswali mengi juu ya jinsi aliyokuwa nayo mtu aliyeletwa hospitalini kwake siku hiyo.
“Huyu ni mwanamke au mwanaume?” aliuliza Dk. Watson.
“Mwanaume!”
“Hapana! Mbona kama mwanamke?”
“Ni mwanaume tata!”
“Hapo sawa. Tena kwa sababu ana tabia chafu hivyo, nitamfanyia upasuaji bila ganzi,” alisema daktari huyo.
Baada ya dakika kadhaa, akamwambia Fareed aingie katika chumba kingine kabisa. Akasimama na kuelekea katika chumba hicho ambacho kwa kukiangalia tu wala usingejiuliza maswali mengi juu ya kazi iliyokuwa ikifanyika ndani ya chumba hicho.
Kulikuwa na vifaa vingi vya kufanyia upasuaji, kilitisha na kila wakati Fareed alipokuwa akikiangalia mapigo yake ya moyo yalidunda kwa nguvu, aliogopa mno na kuuona mwisho wake ukiwa umekaribia.
“Usiwe na hofu, chukua maji kwanza unywe,” alisema daktari huyo huku akimpa maji ambayo aliyawekea dawa ya usingizi. Fareed hakujua, akayapokea maji hayo na kunywa harakaharaka, baada ya dakika mbili tu, macho yake yakawa mazito na hapohapo kulala kwenye kiti alichokuwepo. Akanyanyuliwa na kulazwa kwenye kitanda cha kufanyia upasuaji tayari kwa kufanya kazi hiyo.
****
“Mchungaji! Mimi ni mkosaji! Nimekuja kutubu dhambi zangu! Nimekuwa nikimtumikia shetani kwa kipindi kirefu katika maisha yangu. Nimemtenda Mungu wangu dhambi! Nimekuja kutubu mchungaji,” alisikika mtu mmoja akimwambia padri aliyekuwa kwenye chumba kidogo cha kuungama dhambi.
“Umefanya nini mtoto wa Mungu?” aliuliza padri huyo.
“Nimezini kwa kipindi chote cha maisha yangu, nimekuwa na tamaa ya fedha, nimekuwa nikimtumikia shetani kwa kila aina ya uchafu. Nimechoka, ninataka kuokoka mchungaji, sitaki kumtumikia tena shetani,” alisikika mtu huyo akizungumza na padri huyo ambaye muda wote alikuwa akionyesha ishara ya msalaba.
“Mungu atakusamehe dhambi zako. Amesema kwamba hata kama dhambi zako zinakuwa nyekundu kama damu, atazisafisha na kuwa nyeupe kama theluji,” alisema padri huyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment