Simulizi : Jestina
Sehemu Ya Pili (2)
Namimi nikaona kwanini nisikuapatie zawadi hii kama fadhila za msaada wako mkubwa katika masomo yangu. Ndipo nikaipiga picha pamoja na vifaa vyote ulivovichora kisha nikampelekea baba yangu na kumwambia anitengenezee, aliponiuliza ni kwanini nataka itengezwe nikamjibu kuwa hii itakuwa zawadi kwa mtu aliefanikisha mimi kupasi japo nilikuwa mzito kwenye masomo. Hapo akanambia nimueleze wewe ni nani na mimi nikamwambia kila kitu, basi alisafiri kuelekea ujerumani kwa ajili ya kazi hii tu. Kwa vile wewe ni genius akaamua kutengeneza kiboxi hichi na kuweka funguo na kunambia kuwa mwenye uwezo wa kufungua kiboxi hichi ni mtu mwenye IQ kati kati ya 165 na kuendelea juu. Na ameweza kukidizaini hicho kibox kwa mfumo wa hesabu" aliongea Miryam na kumshangaza Alwin, "basi kama baba yako ndie aliekitengeneza koboxi hici bila shaka na yeye ni kama mimi" Alwin aliongea.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hujakosea mwanangu ila mimi nimekuzidi sana" iliskiaka sauti ikitokea nyuma yao. Alikuwa ni baba yake Miryam " mimi nina 197 IQ capacity na ndie niliendaa mashindano ya magenius" alijib Mr Alexander Harison, hilo ndio jina lake nainasemekana ndie mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani. "mimi na wewe tutaonana kwenye fainali za mashindano haya na nakutakia siku njema" alimaliza kuongea na hapo hapo ikaja gari, aliingia na kuondoka. Alwin hakuamini macho yake kama mtu aliemuona mbele yake ndie mtu ambae alikuwa akimkubali tokea udogoni kwake. Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwa Alwin alijikuta kwa muda akisahau machungu yote na maumivu aliyoyapata kutoka kwa Jestina.
Alwin alijikuta akimkumbatia Miryam kumbatio ambalo kwa wengi lilitafsiri kuwa ni upendo. Kwa mara ya kwanza Miryam alijikuta akilihisi joto la mwanaume huyo ambae alitokea kumpenda kupita maelezo. Mkumbatio huo ulidumu kwa dakika kama mbili hivi, kisha wakaachiana huku Miryam akiangalia chini kwwa aibu. "asante sana Miryam kwa zawadi yako nzuri" Aliongea Alwin huku machozi kwa mbali yakilowanisha macho yake. "usijali Alwin hivyo ndivyo marafiki wanavotakiwa kuwa" alijibu Miryam na kutoa kitambaa chake na kumfuta machozi ambayo tayari yalishaanza kulowanisha mashavu ya Alwin.
Yote hayo yalifanyika huku Jestina akishuhudia kila kitu, lakini hata hivyo alipotezea na kuondoka eneo hilo. "ah halafu nimesahau subri na mimi nikupe zawadi yako" Alwin aliongea na kufungua begi lake na kutoa kitu mfano kama wa simu. "hiki kifaa nimekiteneza mwenyewe na nimekiprogram na maswali mengi sana ambayo yatakusaidia ikiwa utahitaji msaada na sitokuwa karibu" Aliongea na kumkabidhi kifaa kile. Miryam alirukaruka kama kidege huku meno yote thalathini na mbili yakiwa nje. Baada ya hapo kila mtu aliondoka na Alwin aliltafuta Jestina ili ampe zawadi ya siku ya marafiki duniani lakini alichokutana nacho huko kilikuwa kinyume maana Jestina alitoa maneno machafu huku akimwita Miryam malaya. Hakumaliza kuongea alichezea kibao kizito kutoka kwa Alwin na kumfanya ayumbe kidogo kabla ya kuzuiwa na bwana wake Matt "umeniacha bila chaguo Jestina ila kukufunga mdomo na nikwambie kitu huna haki ya kumuita Miryam majina machafu kama hayo. Nimejaribu sana kukueleza lakini inaonekana Matt anakutia kiburi sana" Alwin aliongea na wakati huu alivimba kwa hasira.
"We dogo sikia nikwambie, kama unataka kupimana uzito pimana na saizi yako na sio kukimbilia waschana" Matt aliongea huku akimsukuma Alwin. "Na wewe mwanaume mpumbavu usie na akili, kwa muonekano tu hata kurusha jiwe huwezi achilia mbali kukunja ngumi. Kama unadhani kuwashusha sketi wanawake ni uanaume basi umebugi na nikwambie kitu kama kweli unaweza ndondi tuzame uwanjani nikuonesha kama mwanaume hasifiwi kuchungulia wanawake" yalitoka maneno hayo kinywani mwa Alwin na kushangza umati mzima maana huyo hakuwa Alwin aliezoeleka hapo college. Basi Matt alitaka kumjaribu Alwin japo Jestina alijaribu kumzuia lakini ilishindakana.
Jestina alimfahamu vizuri sana Alwin anakuaje hasa pale anapojaribu kuwalinda wale anaowajali sana. Basi kwa kutaka kuonyesha kama yeye ni kidume alianza kumsukum Alwin ambae kwa wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hasira, alipomsukuma mara ya tatu Alwin alijibu mashambulizi kwa kumpiga ngumi mbili kwa wakati mmoja kwenye mabega yote mawili. Bila kutaka Matt alijikuta akikibetua kifua chake huku mikono ikikosa ushirikiano na mwili, hapo Alwin alimtandika ngumi nzito ya kifua iliotuwa kwenye chembe na kumfanya Acheuke damu na bila kutarajia alidondoka chini na kupoteza fahamu. "huu ni mfano tu, nikuskie unamtovukia tena adabu Miryam na akiinuka huyo basha wako mwambie akae mbali na mimi" aliongea Alwin na kugeuka, alikwenda mpaka lipo Miryam na kumwambia waondoke.
Siku ya mashindano ya magenius kwa ngazi ya kitaifa ilifika na matokeo yalikuwa kama yalivotarajiwa na wengi. Alwin na Jestina waliiwakilisha shule yao vizuri huku wakiibuka na alama nyingi sana. Walirudi college na kupokewa kwa shangwe "mashindano ya kimataifa yatakuwa mwezi ujao hivo naomba mujiandae vizuri ili mtusaidie kurudisha sifa ya college yetu" mwalimu mkuu aliongea wakati alipowaita ofisini kwaaajili ya kuwapongeza. "usijali mwalimu, tutajitahidi na kuhakikisha jina la college hii linakuwa zuri kama la zamani. Baada ya maongezi hayo walitoka na kuelekea nje, huko Jestina alipokewa na MAtt na Alwin alipokewa na mtoto Miryam. Maisha yalindelea huku maandalizi kwa ajili ya fainali yakipamba moto. Hatimae siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu ilifika, Jestina na Alwin walisafiri kuelekea nchini England maana huko ndipo fainali zilipokuwa zinafanyika. Watu wote wa Mashvile walikusanyika katika nyumba za ibada kuwaombea makinda hao ushindi wa kishindo..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"habari zenu mabibi na mabwana, karibuni katika THE WORLD ULTIMATE GENIUS CHALLENGE. Mgeni rasmi atakuwa profesa Alexander Harison mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani mpaka sasa. Kwa ujumla mwaka huu timu zitakuwa hamsini na mchezo utakuwa na jumla ya mizunguko mitatu" MC alindelea kutangaza huku akiwekwa mbwembwe nyingi. "Jestina, huu ndio wakati tulikuwa tukijiandaa nao" Alwin alimwambia Jestina huku akimuangalia kwa makini. Wakati huu walizieka pembeni tafauti zao, "lakini mi naogopa" Jestina alijibu kwa sauti ya kutetemeka. "sasa unaogopa nini, usiwe na hofu kombe mara hii linakwenda nyumbani" Alwin alimjibu huku akimshika mkono.
Mashindano yalianza huku kila timu ikijitahidi kubakia mpaka mzunguko wa pili, lakini ni kawaida ya mchezo wengine kuwa wasindikizaji tu. Maunguko wa kwanza uliisha zikiwa zimebakia timu ishirini na tano tu na nafasi ya kina Alwin ilikuwa ni ya ishirini jambo ambalo lilimtia wasiwasi Alwin. "Jestina una nini lakini mbona ulikuwa unakosa maswali kizembe" Alwin alimwambia wakiwa mapumziko. "hata sijui kwa kweli" alijibu, "sasa ukiendelea kuwa hivyo tutatolewa mzunguko wa pili" Alwin aliongea na kumsisitiza arudi katika hali yake ya kawaida.
Kengele ya mzunguko wa pili ililia na washindani wote wakaingia ulingoni, mzunguko huo ulikuwa na maswali magumu sana na yalihitaji uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Kwa upande wa Alwin kazi haikuwa ngumu sana kwa sababu alitrain akili yake katika kiwango kikubwa cha kufikiri. Lakini kwa upande wa Jestina mambo yalikuwa magumu sana, hii ilitokana kila alipojaribu kufikiri mawazo ya Matt yaliingilia kati. Mzunguko wa pili ulikwesha na kwa bahati walipenya japo waliponea chupuchupu kutoka. Walikuwa katika nafasi ya tano katika timu tano zilizopita, kiufupi walishika mkia.
"Jestina, Jestina una nini lakini" Alwin alimlalamikia, "ukiendele kuwa hivo basi ushindi utatupitia mbali" aliendelea kuongea. Mapumziko yalikwisha na muda wa kurudi uwanjani ulifikia lakini hali ya Jestina ilibadlika ghafla na wakati wanatoka alidondoka chini na kupoteza fahamu. Watu wa huduma ya kwanza walimuwahi na kumpeleka katika chumba cha huduma ya kwanza. Na kwa bahati mbaya sana majibu yalikuja vibaya, Jestina asingeweza kushiriki mzunguko huo kutokana na kuwa akili yake imechoka sana. Sasa maamuzi yalibakia kwa Alwin ima aendelee kupambana peke yake au akubali kuachia mzunguko huo. "yaani nitoke kote huko mpaka hapa halafu niachie kirahirahisi hivi" alijsemea moyoni "litakalokuwa na liwe kombe linakwenda Mashvile".
Aliingia uwanjani akiwa peke yake. "sasa ni ule mzunguko wa akili nyingi, mabibi mabwana si mwengine bali ni THE ULTIMATE BRAIN STORMING CHALLENGE, mzunguko huu ni wa hatari hivyo tunaomba machela ziwe karibu na watu wa huduma ya kwanza msiwe mbali na ukumbi maana ni shiiiiida" MC alizidi kuweka vikombwelezo vingi. "mzunguko huu utakuwa na swali moja tu na kila timu itakuwa na nusu saa tu kumaliza mchezo, itaanza timu kutoka London" waliingia vijana hao walikuwa wamevaa miwani mikubwa, honi ililia na kuanza mchezo huo. Mchezo ulindelea "na sasa timu ya mwisho kuingia uwanjani ni kutoka Mashvile" Alwin aliingia peke yake na kuwafanya watu wote washangae.
********************
Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa, "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema"
Upande wa Alwin watu walizidi kushangaa maana walielewa kuwa jaribio hilo la mwisho mtu mmoja hawezi hata siku moja kushinda akiwa peke yake. "Alwin Kelvin inabidi uingie makubaliano kwamba lolote litakalotokea jumuiya ilioandaa mashindano haya haitahusika", "ndio nimekubali lolote litakalotokea litakuwa ni juu yangu" Alijibu Alwin kwa kujiamini. "Una dakika thalathni kuipanga ramani hii na muda wako unaanza sasa", honi ililia na dakika zikaanza.
Alwin aliangalia fumbo hilo ambalo kwa akili ya kawaida tu ungedhani michoro tu ya kitoto, "ikiwa watu wawili wanatumia dakika ishirini na tano zaidi kutatu fumbo kama hili, mimi natakiwa nitumie chini ya hapo kwa sababu niko peke yangu na hakuna wa kupingana na mawazo yangu" alijisemea mwenyewe huku akiendelea kuliangalia fumbo hilo. Baada kuridhika alitoa kalamu na karatasi na kuanza kazi, tayari dakika tatu zilishakatika. Kitu kimoja ambacho wengi hawakukijua juu yake ni kwamba ameifanya akili yake kufanya kazi kasi mara tatu zaidi kuliko computer, alianza kuandika namba namba nyingi huku akizikata kwa kuzipiga michoro. kila baada sekunde tano aliandika namba na kukata namba, wengi walimuona kama kijana anaepoteza muda kjaribu kutafuta umaarufu kwa kujaribu kujibu fumbo hilo peke yake wakati anajua kuwa hatoshinda..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"profesa mi naona anapoteza muda huyu kijana" mmoja kati ya watu waliokaa karibu na profesa Alexander Harison aliropokwa. "Huyu kijana atashinda tena atatumia dakika ishirini tu" Alijibu profesa huku akiwa hamuangalii mtu huyo, lakini ukweli alichukizwa na swali hilo. Dakika saba zilishakata huku Alwin akiendelea kuandika namba tu, kumbuka hapo yuko peke yake. Zilipotimia dakika kumi alibadilisha mfumo na kutumia mfumo wa matrix, kazi iliendelea huku watu wengi wakitegemea atashindwa kumaliza. Kutokana na kufikiria sana mishipa ya fahamu iliopita pembeni ya kichwa ilianza kuvimba na haukupita muda alianza kutoka damu za pua. Lakini wala alikuwa hajui hasa kama anachuruzika damu, MC alitaka kumwambia ache lakini Prof Alexander Harison alimpa ishara amuache kwani kumshtua pale kungepelekea kupasuka kwa mishipa hiyo.
Dakika kumi na tano zilikata na Alwin alianz kutabasamu baada hesabu zake kwenda kama alivyotaka. Alianza kuipanga ramani hiyo huku akiangalia saa iliokuwa ikimwambia kuwa zilibaki dakika kumi na tatu.
Aliongeza kasi ya kupanga ramani hiyo huku akihisi maumivu makali ya kichwa, Prof Alexander aliligundua hilo baada kumuangalia usoni. Aliinuka alipo kaa na kushuka kuelekea kwenye jukwaa alipo Alwin huku akiangalia saa yake ambayo ilimwabia bado dakika moja tu kutimia dakika ishirini. Alifika na kusimama nyuma yake na ilipotimia tu dakika ishirini Alwin aliinua mikono kuashiria alishamliza kupanga na hapo hapo Profesa akamgusa kwenye shingo kidogo na kumminya, alianguka na kupoteza fahamu. Kisha akatoa ishara watu wa huduma ya kwanza wafanye kazi yao na kuwaambia wamtundukie dripu ya damu pamoja na maji ya glucose, pia aliwaambia baada dakika tano atazinduka. Alirudi kwenye kiti chake na kutulia, dakika tano baadae Alwin alizinduka na kuruka kwa furaha. Watoa huduma wote walishangaa kumuona vile, walimtuliza na baada ya dripu kuisha alinyanyuka na kurudi ukumbini. "jamani makofi kwa mshindi wetu wa shindano hili gumu ALWIN KELVIN" MC alitangaza na watu wote walipiga makofi. "ndugu Alwin umepata nafasi ya kufanya mawasiliano na profesa Alexander Harison hapahapa ukumbini" aliendelea kutangaza na kumuelekeza kwenye kiti na majadiliano yakaanza.
Prof : Pole kijana kwa kazi nzito
Alwin: asante profesa
Prof: Tunaomba utuambie uwezo wako wa akili
Alwin: 176 IQ capacity
Prof: unajua kama leo umevunja rikodi ya mtu mkubwa sana
Alwin: hapana sijui
Prof: Hongera Alwin kwa kuvunja rikodi yangu, mimi nilimaliza ndani ya dakika ishirin na sekunde moja.
Alwin: Ah asante lakini wewe utabaki kuwa kama ulivo
Prof: na pia hongera kwa kujinyakulia cheo cha uprofesa katika hesabu hasa kwenye Matrix
Ukumbi mzima walishangaa kusikia maneno hayo kutoka kwa profesa huyo, mjadala ulikwisha kwa namna hiyo huku Alwin akinyakua tuzo tatu moja kama mshindi, ya pili ya kuvunja rikodi na ya tatu cheo cha uprofesa. Katika vyombo vyote vya habari, habari ilikuwa ni hiyo tu "KIJANA ALIEVUNJA RIKODI YA PROFESA ALEXANDER HARISON". Walipumzika siku hiyo na siku ya pili walipamnda ndege na kurudi Mashvile, walipokewa kwa shangwe hasa Alwin ambae alionekana shujaa wa sehemu hiyo.
Kama njia ya kutoa shukrani college iliamua kupanga safari kwa ajili ya Alwin na Jestina, ilikuwa ni safari ya kuelekea Mashvile National Park. Wanafunzi walifurahi sana kwa sababu kwa mwaka huo ilikuwa ni safari ya kwanza.
****************************
"hawezi kunifanya mimi nionekane bwege kiasi chote hichi, tokea tuingie katika mahusiano hajawahi kunipa penzi" Matt alikuwa akiongea peke yake huku akionekana mwenye hasira sana "lakini subiri atatoa tu, anadhani mi kaka yake". Siku ya safari ilifika na mapema asubuhi wanafunzi waliondoka na kuelekea Mashvile National Park (M.N.P), walifka saa sita mchana kwa sababu kulikuwa mbali sana. Muda mwingi Alwin alikuwa na Miryam na walionekana kufurahi sana, upande wa Jestina alikuwa hana amani kabisa hasa baada kugundua kuwa aliingia woga na kukubali kudhalilishwa na Alwin ambae kwa alivyotafsiri yeye ni kwamba "sina haja ya kuwa na mwenza kama wewe hata peke yangu naweza kushinda". Hivyo ndivyo alivokuwa akitafisiri Jestina, basi walindelea kufurahia safari hiyo huku wakitembezwa maeneo mbali mbali, jioni lipofika walikwenda kuogelea katika mto..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usiku uliingia na wote waliambiwa wapumzike katika mahema yao. "Jestina....Jestina amka mpenzi" Matt alikuwa akimuamsha Jestna, "unataka nini bwana" Jestina aliongea kwa uvivu "twende nje tukaangalie mwezi". Basi waliinuka na kutoka lakini wakati wanatoka Alwin aliwoana na alihisi kuna kitu hakipo sawa kwa jinsi Matt alivyokuwa akimvuta Jestina, Hivyo aliamua kufwatilia kimyakimya. "Jestina kwa kweli nimevumilia muda mrefu na sasa nimechoka, naomba unipe penzi" Matt aliongea kwa macho makavu. "si nimekwambia tusubiri nikishakutambulisha nyumbani nitakupa" Jestina alijibu huku akijaribu kujitoa mikononi mwa Matt. "we nipe saa hivi ukishanitambulisha ndio itakuwa kawaida yetu" Matt aliendelea kusisitiza na alipoona Jestina hakubaliani nae alipiga mruzi wakatokea wenzake wengi wakiwemo waschana, kwa haraka idadi yao ilifika kama ishirini hivi.
Basi akatoa ishara watu wanne wakamvamia Jestina na kumlaza chini "mpumbavu wewe unajifanya unajua kubana si ndio sasa leo nataka nikuoneyeshe mimi ni nani" Matt aliongea huku akivua mkanda. Baada Alwin kuona vile alichomoka alipokaa na kutaka kutoa msaada lakini aliwahiwa na kupigwa gongo la kichwa lilimfanya aanguke chini. "we boya shuhudia ninavokata utepe wa genius mwenzako" Matt aliongea bila kuchelewa alimuinamia Jestina na kuanza kufanya uchafu mbele ya Alwin Jestina alijaribu kupiga kelele lakini mschana mmoja alimuwahi na kumtia kitambaa cha mdomo. Damu nyingi zilianza kumtoka lakini Matt hakujali hilo aliendelea kufanya yake mpaka aliporidhika alimuacha na kunyanyuka "oya anaetaka kujisevia na ajisevie tu mimi nishaafungua dimba" baada kutamka hivo vijana kadha walitaka nao kuonja utamu wa genius, jambo hilo lilimuumiza sana Alwin lakini hakuwa na la kufanya kwa sababu alikuwa ameshikwa kisawasawa.
Waliendelea kupokezana lakini waliingia wasiwasi baada kuona kuwa Jestina alitulia kimya chini huku damu nyingi ikimtoka sehemu za siri. Mmoja alijaribu kumtikisa lakini hakushtuka "toba kashakufa" mmoja wao aliropokwa na kila mmoja alitimua upande wake wakamuacha Alwin peke yake ambae alijivuta mpaka alipokuwa amelala Jestina. Alimuinua na kumuweka mapajani kwake. "Jestina... Jestina amka nakuomba" Alwin aliita huku akimpiga vibao vidogo vidogo mashavuni, "Alwin najua kama unanichukie sana kwa nilokufanyia" Jestina aliongea kwa sauti ya chini yenye maumivu makali ndani yake, "hapana sijawahi kukuchukia hata kidogo, nilikuwa nakupa muda tu ugundue tu njia ulochagua sio salama lakini ukweli nakupenda sana kuliko kitu chchote kile katika maisha yangu" Alwin alijibu huku machozi yakimtoka. "we unadhani kwanini nimeenedelea na mashindano hata baada ya wewe kutofanikiwa kushiriki, nilitaka ujue tu kama sikuwa tayari kukubebesha lawama za kushindwa, nilitaka ujue tu kama bado nakujali japo mengi yametokea" aliendelea kuongea kwa kwikwi.
"Alwin kwanini unanipenda kiasi chote hicho na wakatii nilishaakwambia zamani kuwa sina hisia za kimapenzi juu yako" Jestina aliongea japo kwa tabu sana. "Jestina kukupenda mimi haikuwa na maana na wewe unipende, penzi la upande mmoja lilitosha kabisa kuishi na wewe" Alwin aliendelea kuongea huku machozi yakimchuruzika ka maji machoni mwake. "Alwin nakuomba unyamaze na uniache nipumzike kwa amani, nakuahidi kuwa nitazaliwa tena kwa ajili yako iwe katika maisha haya au yoyote yale..... tafadhali niache niende kwa amani" alimaliza kuongea maneno hayo na kukaa kimya, Alwin alijaribu kumtingisha lakini hakushtuka, alipeleka kidole kwenye pua na hapo ndio akagundua kuwa tayari Jestina alishaamuacha peke yake duniani. "no...n.o...no ple...ase Jestina...Jestina... Jestinaaaaaa" alipiga kelele na papo hapo akapoteza fahamu.
*************************************************************
(miaka kumi baadae)
"Jestina amka" iliskika sauti laini ikimuamsha Jestina, alikurupuka kutoka kwenye usingizi huo akihema. "karibu katika ulimwengu wa waliodhulumiwa" alisikia tena sauti ikiongea lakini aliongea hakumuona. Na alipoangalia vizuri aligundua kuwa alikuwemo ndani ya jeneza, alitoka mbio huku akijaribu kutafuta njia lakini hakuiona kutokana na kiza kizito kilichokuwepo katika macho yake. "niko wapi" aliuliza, "khah! kwani hujui uko wapi" alijibiwa ,"sasa ningekuwa najua ningeuliza" alijibu Jestina kwa hasira kidogo. "wewe upo katika dunia ya wafu kwa maana nyingine tayari umeshakufa" alijibiwa lakini alionekana kutokubaliana na jibu hilo "haiwezekani mara ya mwisho nilikuwa mikononi mwa..." hakumalizia picha za tukio la yeye kubakwa na Matt halafu akaruhusu wenzake wajisevie zilianza kurudi kichwani mwaka. Akajikuta anaanza kupiga kelele huku machozi yakianza kumotoka lakini alipojaribu kuyafuta aligundua kuwa hayakuwa machozi bali ilikuwa ni damu iliokuwa ikitiririka machoni mwake..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kweli Matt ni wa kunifanyia vile, kumpenda kote kule ameamua kunifanyia unyama wa aina ile" alijikuta akijesemea mwenyewe huku hasira zikianza kumpanda. "usijali hapa upo kwa sababu wewe umedhulumiwa na hukupaswa kufa siku ile lakini Matt na wenzake wamekuhujumu na kusababisha kifo chako na matatizo mengine mengi sana ambayo ukiyaona lazima machozi yatakutoka". Ghafla mandhari ilianza kubadilika, muangaza mkali ulitokea mbele yake na kumfanya afunge macho yake. Alipoyafungua alijikuta yuko mbele ya watu wengi sana tena walikuwa wanatisha sana. Wapo waliokuwa hawana vichwa na wengine walikuwa wakivuja damu mwili mzima. "karibu katika ullimwengu wa mpito wa watu waliodhulumiwa" aliongea mwanamke mmoja alionekana kama kiongozi wa sehemu hiyo. "hapa upo kwa ajili ya kuwalipa wale waliosababisha kifo chako na kusababisha watu wako wa karibu kufarakana, kifo chako kimeacha utata mkubwa sana duniani na haki haiwezi kutendeka kwa sababu mtu mmoja tu ndie anaujua ukweli juu ya kifo chako lakini hawezi kutoa ushahidi kwa sababu amepata matatizo ya akili" alizidi kufafanua mwanamke huyo ambae alionekana ni Malikia.
"oh samahani Jina langu naitwa Malkia Alina" aliongea mwanamkwe huyo baada kugundua kuwa hakujitambulisha. "na utakaa katika ulimwengu huu mpaka pale kazi yako itakapo kamilika" aliendelea kuongea. Jestina alianza kujiangalia kwa makini sana na kugundua kuwa kucha zake zilikuwa kubwa sana tena ngumu huku macho yake yakiwa meupe bila kuonesha kiini, nguo alioivaa ilikuwa imetapakaa damu iliokuwa ikiendelea kutoka katika sehemu zake za siri. Sura yake ilikuwa imeharibika kabisa na ilikuwa ni vigumu hata yeye mwenyewe kujitambua. "najua utakuwa na maswali mengi sana, lakini ukiachilia damu inayokutoka sehemu zako za siri mabadiliko mengine yametokea kwa sababu hata wewe ulimdhulumu mtu haki yake wakati ukiwa hai na si mwingine bali ni Alwin" aliongea mwanamke huyo na kumfanya Jestina atoe macho akijiuliza amemjuaje Alwin.
"mimi mbona sijamdhulumu Alwin" alijaribu kujitetea lakini ghafla aliskia maumivu makali sana sehemu zake za majeraha, alipiga kelele akiomba msaada lakini yule malkia akamwambia "huku hakuna kusema uongo, na ukifanya hivo maumivu yatakuwa yanazidi kila saa". "kwani mi nilimdhulumu vipi Alwin" aliuliza kwa sauti iliojaa maumivu, "kwanza inabidi ukubali kama ulikuwa ukimpenda Alwin lakini kutokana na kuwa alikuzidi kiuwezo wa akili uliapa kutokuwa nae kama mpenzi wako, unakumbuka siku ya kwanza kukutana na Alwin nyumbani kwenu". "Ndio nakumbuka" alijibu Jestina. "siku ile Alwin alikushunda katika kitu ambacho uliamini hakuna anaekuweza hivyo tokea siku hiyo uliacha wivu wako wa kimasomo ukutawale lakini unajua alichijisemea Alwin baada kukuona unalia siku ile". "hapana sijui" alijibu Jestina, "sasa ni hivi baada Alwin kugundua kuwa ulikuwa ukilia kwa sababu amekushinda, aliapa kutokukuliza tena na kuahidi kuwa daima atakupa furaha". Jestina baada kusikia hivo alihisi maumivu makali sana moyoni mwake, huku akijisemea "kwanini Alwin".
**************************************
Kelele ziliendelea kusikika huku kila kichaa akiongea na kuimba anachokijua yeye isipokuwa mmoja tu ambae alikuwa kimya huku akiuwangalia ukuta alioandikwa kwa maandishi fulani kwa damu, maandishi hayo hayakufahamika kabisa isipokuwa jina moja tu ambalo lilikuwa juu kabisa na jina lenyewe lilikuwa ni JESTINA. Naam chizi huyo hakuwa mwingine bali ni Alwin ambae ubongo wake uliingia ufa baada ya kifo cha mwanamke aliempenda. Yeye pekee ndie aliewajuwa wahusika lakini alishindwa kusema kutokana na kuwa hakukuwa na mawasiliano kati ya akili na mdomo wake hivo hakuweza kuongea chochote kile. "inspecta Hans hapo utajisumbua tu, huyo hawezi kuongea" dokta alikuwa akimwambia inspecta huyo ambae ameifufua kesi ya mauaji ya Jestina iliotokea miaka kumi iliopita. "Asante dokta mimi sitaki kuongea nae bali nataka kujua tu kile alichokiandika kwenye ukuta, kivipi kinahusiana na kifo cha Jestina".
Alitoa camera ndogo na kupiga picha yale maneno, aliporidhika aliondoka na kurudi kituoni kwa ajili ya kuendelea na upelelezi. Inspector Hans ni afande machachari sana na ni kawaida yake kuona kila mtu anapata haki yake. Hivyo baada kuhamishiwa Mashvile alikutana na kesi hiyo ambayo ilishaafungwa muda mrefu. Lakini kutokana na ukaribu wake na profesa Alexander Harison aliombwa aifungue upya kwa kile alichoambiwa na profesa huyo kuwa "ili kumrudisha Alwin kama alivyokuwa zamani ni lazima kesi hii itatuliwe". Aliayakumbuka maneno hayo alioambiwa na rafiki yake huyo. Profesa Alexander alifanya kwa sababu ya mwanae Miryam ambae ilibidi amhamishe mji baada matatizo yaliotokea lakini pia alihofia mwanae kuchizika. Hivyo akaamua kuvalia njuga kesi hiyo ambayo ni ngumu kupita maelezo kutokana na kuwa mwenye ushahidi hawezi kuutoa..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa Jestina, "Jestina utarudi duniani kama mzimu, lakini jambo la kwanza ukifika ni kwenda kumwambia ukweli Alwin ili arudi katika hali yake ya kawaida ila kwa sasa huwezi kuonekana mpaka pale Alwin atakapokusamehe na kukubali kuwa wewe umekufa maana mpaka sasa ni mtu pekee ambae anaamini hujafa" Malkia Alina aliongea na kumueleza kila kitu Jestina. "Baada ya hapo muombe akupe damu yake kidogo kwa sababu damu yake itakufanya uweze kuonekana na kutoonekana na pia jitambue kuwa wewe si binaadamu tena" aliendelea kuongea, "sasa kama unasema siwezi kuonekana mpaka nipate damu yake, nitaongea nae vipi" aliuliza Jestina. "Njia pekee ni kuongea nae ni akiwa usingizini" Alijibiwa na papo hapo mwanga mkali ukatokea. Ulipotoweka alijikuta yuko pembeni ya mtu mwenye manywele mengi sana huku akionekana kama kichaa lakini alipomuangalia vizuri akagundua kuwa alikuwa Alwin. Basi alisogea mpaka pembeni ya kitanda na kupiga magoti, Alwin nae alianza kuota na katika ndoto yake alimuona mschana analia. Taratibu alimsogelea ili kjua nini kilichomsibu.
Alwin: mbona unalia, (lakini alipouangalia vizuri akagundua kuwa mschana huyo si mwengine bali ni Jestina, bila mategemeo alimkumbatia kwa ngvu huku machozi yakimtoka) mi nilijua tu kama hujafa.
Jestina: Alwin naomba unisamehe kwa yote nlokutndea, ukweli ni kwamba nilikuwa nakupenda lakini wivu wangu wa kimasomo ulinifanya nisikubali kuingia katika mapenzi na wewe. mambo yote nilioyafanya nilitaka nikuchanganye ili japo mara moja na mimi nikupite darasani lakini nikajikuta nimejichanganya mwenyewe.
Alwin: mi nilishaakwambia kama nishaakusamehe kwa kila kitu kilichotokea, sasa naomba tuinuke nikupeleke kwenu maana wazazi wako wanakusubiri kwa hamu.
Jestina: Haiwezekani Alwin mimi tayari nilishakufa muda mrefu sana, saa hivi nimepata nafasi ya kuja kulipa kisasi changu kwa wale ambao ndio chanzo cha kifo changu, lakini kwa sasa unaeniona ni wewe tu hivyo ntahitaji damu yako kidogo ili niweze kurudi katika hali yangu ya kawaida na kweza kuonekana pale nnapotaka mtu anione.
Alwin: (kwa hasira) damu yangu nitakupa lakini nakuomba uniahidi kitu kimoja, wale wote waliohusika na kifo chako na wao wafe vifo vibaya sana.
Aliokota kama chupa pembeni na kujikata mkononi, kisha akamzogezea mkono Jestina ambae aliushika mkono huo na kuanza kunya damu. Alwin akiwa usingizini alianza kupiga kelele kutokana na maumivu makali ya kichwa alioyaskia. Wale madakatari waliokuwepo zamu walifika katika chumba chake na kumuwahisha hospitali. Hali ya hewa ilibadilika ghafla na radi pamoja na ngurumo zikaanza kupiga zikiamabatana na mvua kali sana yenye upepo ambao si wa kawaida. Katika kaburi alilozikwa Jestina ilipiga radi kali sana na papo hapo Jestina akatokea juu ya kaburi lake huku macho yakiwa mekundu mithili ya damu. "Matt na wenzako jiandaeni kwani hata mungu hawezi wasaidia sasa, mtalipa kwa kile mlicho nitendea" alijisemea hayo kishaa akacheka kicheko kikali sana na kutoweka eneo hilo.
Harakati za kuokoa maisha ya Alwin zilianza punde tu alipofika hospitali huku madaktari wakijitahi kadri ya uwezo wao. Habari zilimfikia profesa Alexander Harison na bila kuchelewa alitoka kuelekea hospitali, dakika kumi baadae aliwasili hospitali na kutokana na cheo chake aliruhusiwa kuingia katika chumba ambacho matibabu ya Aklwin yalikuwa yakiendelea. Wakati huo daktari alikuwa na sindano ya usingizi mkononi, nia ilikuwa ni kumchoma Alwin ili alale kwa sababu ingemsaidia kukabiliana na maumivu lakini Profesa Alexander alipiga kelele kumzuia "usijaribu kumchoma hiyo sindano utamuua kabisa" aliongea profesa. Kisha akasogea mpaka pembeni yake na kuanza kumgusa sehemu mbali mbali za mwili wake "muacheni hivohivo, yupo katika wakati mgumu sana, akifanikiwa kupita wakati huu basi huenda akapona lakini pia kuna uwezekano kupoteza maisha kwa sababu anazinduka kutoka katika usingizi wa kifo" aliongea Profesa na kuwafanya madaktri wote wamshagae na swali kubwa lilikuwa anajuaje vile bila hata kufanya uchunguzi wa kitaalamu. Lakin hakuna aliemuuliza swali lolotea na waliamua kutoka hasaa katika chumba hicho na kumuacha peke yake akiwa na Alwin..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Leo nataka nikuoneshe nina uwezo gani katika sita kwa sita" kijana Frank akiwa na mpenzi wake kwenye gari. Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana bila kuchukua tahadhari kama huo ulikuwa ni usiku na barabara ilikuwa imepita katikati kijipori kidogo. Wakati anaendesha alifungua zipu na kutoa uume wake "oyaa fanya huduma ya kwanza basi" alimwambia mpenzi wake, "we huoni kama ni hatari hiyo" alijibiwa. "acha uboya wewe sasa dereva si mimi, we utakuwa unaramba pipi mi ntakuwa naendesha" alijibu huku akimshika kichwa na kumuinamisha, kuona mpenzi wake kakomaa ilibidi amridhishe. Kutokana na raha kuna wakati Frank alifunga macho, lahaula alipoyafungua aliona mschana kasimama katikati ya barabara na katika harakati za kumkwepa gari ilimzidi na kuacha njia na kupinduka. Ilipotulia Franka alimuangalia mpenzi wake ambae muda mrefu alikuwa ameshakata roho, wakati akihangaika kujitoa akaona miguu kwa nje huku ikichuruzika damu nyingi sana tena yenye kutoa harufu mbaya sana.
Alipepesa macho ma alipoyafungua hakuiona tena, alijitahidi na kufanikiwa kutoka kwenye gari huku damu zikimtoka kichwani. Alianza kutembea taratibu huku akiskilizia maumivu lakini alihisi kama kitu kikimfata kwa nyuma, alipogeuka hakukuta kitu lakini apogeuka tena mbele uso kwa uso na mschana . "wewe ni nani" aliuliza huku akirudi nyuma maana kwa muonekano tu hakuwa mtu wa kawaida, "leo umenisahau" alijibiwa kwa sauti yenye kujirudia. Aliiskiliza kwa makini na ndipo sauti hiyo ikagonga vizuri kwenye ubongo wake "hapana, haiwezekani Jestina kashakufa" aliongea huku haja ndogo ikianza kumtoka. Na ndipo Jestina akaziondoa nywele zake usoni na kumfanya Frank atoe macho kama mjusi aliebanwa na mlango. "Utalipa kwa ulichokitenda, kifo" aliongea Jestina na kupotea, kushuhudia vile Frank alitoka nduki.
"Jestinaaaa...." Alwin alizinduka kutoka usingizini kupiga kelele huku akiliita jina la Jestina, kwa bahati nzuri Profesa Alexander alikuwepo hivyo alimuwahi na kumwambia atulie. Alwin alianza kulia kama mtoto mdogo "kweli Jestina wakufanyiwa vile", "tulia Alwin mimi nipo kwa ajili yako" aliongea Profesa huku akimbembelea. "kwanza nataka kumuona Jestina" aliongea Alwin huku akijaribu kusimama. "mwanangu huwezi kumuona tena", "kwanini" "Jestina ameshafariki na huu ni mwaka wa kumi tokea kifo chake" alijibu Profesa. Machozi yalizidi kumtoka Alwin huku akijilaumu kwanini aliruhusu Jestina wake afanyiwe unyama kama ule. Ilibidi profesa atumie njia za ziada kumtuliza mpaka alipohakikisha ameshaanyamaza, "sasa pumzika kesho utakwenda nyumbani kwani wazazi wako wanakusubiri kwa hamu" aliongea profesa na Alwin alikubali. Baada ya hapo profesa aliondoka na kuwaambia madaktari kuwa keshi atakuja kumchukua Alwin.
Wakati Alwin akiwa amepumzika huku machozi yakilowanisha mashavu yake, ghafla umeme ulizimika na papo hapo Jestina akatokea lakini alikuwa katika umbile lake la kibinaadamu "Jestina" Alwin aliita kwa uoga. "usiogope Alwin mimi siko hapa kukudhuru" Jestina alijibu. Alwin alijaribu kumgusa lakini mwili wa Jestina ulikuwa wa baridi sana. "wewe si ushakufa" aliongea Alwin, "ndio" alijibu Jestina "sasa kama umeshakufa hapa unafanya nini" Alwin aliuliza tena. "ndio hilo nnalotaka kukwambia, mimi nimepewa nafasi ya kuja kuwalipa wale wote walionifanyia ubaya kwa hivyo nakuomba uvumilie kwani wote watalipa vilivyo" aliongea Jestina huku machozi yakimtoka lakini hayakuwa ya kawaida zilikuwa ni damu zilizokuwa zikitoka machoni. Alwin alimshika mkono na kumwabia "mimi niko pamoja nawe na sito pumzika mpaka nihakikishe wamemalizika" kisha akamvuta ili amkubatie lakini Jestina alipotea na kujikuta akikumbatia hewa.
***************************
Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa. "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema". Kijana huyo hakuwa mwengine isipokuwa Frank ambae alionekana kuchanganyikiwa, "oyaa tuambie basi nani huyo anaetaka kukuua". "Jestina jamani" aliongea Frank na kuwafanya wenzake waanze kucheka, "wee hebu tuambie leo umekunywa ngapi" Jay aliuliza. "washkaji mimi sijalewa, amini msiamini nimemuona tena anatisha si mchezo" alijaribu kujitetea Frank lakini wenzake walizidi kumcheka. "oya hebu msindikize geto akalale kwanza labda pombe imepanda kichwani" Jay aliongea na watu wawili wakamchukua Frank mkukumkuku na kumpeleka chumbani. "oya dogo pumzika kwanza kesho asubuhi tutaongea fresh" James aliongea na kutoka, kwa bahati mbaya aliufunga mlango kwa nje..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Frank alijaribu kutafuta usingizi huku akijipa moyo labda kweli atakuwa kalewa lakini ghafla hali ya hewa ndani ya chumba hicho ilianza kubadilika. "ah hahahahahah......" sauti kali ya kicheko iliskika, "nisamehe Jestina, ujinga tu ulikuwa ukinisumbua" alianza kuomba msamaha. "hahahaha msamaha wako haukubaliki na leo utakiona cha moto" Jestina aliongea huku alizidi kutisha na kuanza kuangua kilio ambacho kilimbana na mruzi mkali uliopenya kisawasawa kwenye maskio ya Frank. Alianza kusikia maumivu makali sana, na damu ziianza kumtoka kwa wingi sana masikioni. "Jestina nakuomba unisamehe niko chini ya miguu yako" aliomba lakini ni kama alikuwa akiomba azidishiwe adhabu. Kwa makucha makubwa katika mikono ya Jestina alianza kumchanachana bila huruma, Frank alipiga sana kelele lakini hazikuskilikana kutokana na chumba hicho kuwa katika nyumba nyingine tafauti na ile waliokuwepo wenzake. Alikimbilia mlangoni kujaribu kujiokoa lakini wapi mlango ulikuwa umetiwa loki kwa nje. "unakwenda wapi unadhani" Jestina aliuliza kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, wakati huu alikuwa kashaabadilika na kuwa katika mwili uliokuwa ukitoka funza wengi na wenye harufu kali sana ya kuoza. Harufu hio ilimfanya Frank anze kutapika, mpaka aliishiwa nguvu. Jestina alimsogelea alipo na kumshika koo na kuanza kuliminya mpaka kulinyofoa kutoka shingoni. Frank aliaga dunia huku mwili wake ukiwa hautaminiki, kabla ya kutoweka aliandika ukutani kwa damu "AMELIPA".
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment