Simulizi : Mji Tulivu Ulionipa Ugonjwa Wa Milele
Sehemu Ya Pili (2)
MASHAKA yakiingia katika ndoa yoyote ile iliyokuwa imara hapo awali… huu ni mwanzo wa ndoa kugeuka kuwa kama bomu lililotegeshwa na lisijulikane ni lini litalipuka!
HATIMAYE
ikawa kama nilivyopambana kwa udina uvumba iwe. Nyambura akawa mke wangu halali
kabisa aliyetambulika kwa kila mtu.
Tuliendelea kufanya kazi katika kampuni yangu….lakinihatukudumu sana, Nyambura akanieleza kuwa anajiona utendaji kazi wake unashuka kwa kasi kubwa sana, akaniweka chini na kunishauri kuwa kama sitajali basi yeye ashughulike na biashara nyingine na mimi niendelee kuwa mkurugenzi wa ile kampuni.
Wazo la Nyambura halikuwa baya, niliridhika kabisa na maelezo yake na nikampa uwanja wa kuamua ni kitu gani tunaweza kufanya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimpa nafasi ya kutulia na kuandika mchanganuo wa chochote chenye manufaa ambacho anadhani ni sahihi kufanya.
Wakati akiwa katika kuunda wazo lake la biashara, mama yangu alipatwa na maradhi yaliyochangiwa na utu uzima, sasa alikuwa analalamika kuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Taarifa za ugonjwa wa mama nilimshirikisha Nyambura pia, huku nikiacha kuzipa uzito mkubwa sana.
Usiku tukiwa mezani kwa ajili ya kuupitia mchanganuo wa Nyambura, badala atoe makaratasi aliyoyatumia kuandika mchanganuo ule, Nyambura alizungumza maneno machache tu.
“Nitaenda kumuuguza mama kwanza!”
Sikutarajia hata kidogo kauli ile kutoka kwa Nyambura, nilistaajabu.
Nikacheka nikijua anatania lakini alikuwa anamaanisha kile alichokuwa anakisema.
Hakutaka biashara wala kitu kingine kile alisema kuwa suala la afya ya mama lianze kwanza!
Ndugu msikilizaji kama mapenzi huwa yanaongezeka uzito na yanaweza kupimika, basi Nyambura alikuwa ameongeza kilo tano za mahaba yangu kwake.
Nikaukumbuka usemi usemao kuwa ukimpata mwanamke ambaye anaweza kuwa mama kwako, mama kwa watoto wako na mama kwa familia yako basi mkamate kwa mikono miwili kamwe usimwache aende zake.
Nami nikakiri kuwa Nyambura alikuwa na sifa hizi, alinipenda mimi na familia yangu!!

Siku
mbili baadaye alifunga safari kuelekea kijijini alipokuwa akiishi mama
yangu!
Nikabaki mjini peke yangu.
Nikabaki mjini peke yangu.
______
Sifa
za Nyambura kutoka kwa mama zilinifanya nizidi kuvimba kichwa na kila mara
nikitabasamu na kujisifu kuwa nilichagua mke ambaye wengi hawana!
Kwanza nilimkuta akiwa ni msichana bado, pili ana akili sana na ni msikivu!
Hakika nilikuwa na kila sababu za kujisikia kuwa mimi ni wa pekee zaidi.

moja asubuhi niliamka kama kawaida, si unajua tena mazoea hujenga tabia. Ilikuwa
kawaida ya mke wangu kuniandalia nguo za kuvaa, yaani ni yeye aliamua leo navaa
hiki na kesho kile. Alikuwa ananyoosha nguo zangtu vyema na kuniwekea juu kabisa
ya nguo nyingine ama wakati mwingine alikuwa akiziweka katika kochi, nikitoka
kuoga nazivaa.
Siku hii hakuwepo basi kila kitu nikalazimika kufanya mimi mwenyewe.
Nilipatwa na uvivu na kutamani hata kuvaa nguo ambazo si za kunyoosha ila ofisini nilikuwa nimekabiliwa na ugeni wa heshima sana nisingeweza.
Upesi nikaitafuta pasi ilipo, na baada ya kuiwasha nikaliendea kabati la nguo, nikaanza kutafuta nguo, nilivuruga hovyo!
Badala ya kupata nguo nikakutanana kitu kigeni kabisa katika macho yangu ambacho sikutarajia kukutana nacho.
Nilikutana an akaratasi jeupe sana huku likiwa limeandikwa jina langu kwa kalamu nyekundu.
Hapakuwa na maelezo yoyote zaidi ya jina langu kamili. Nilitumia dakika tano nzima kuitazama karatasi ile ambayo haikuwa pale bahati mbaya bali ilikuwa imehifadhiowa.
Sasa ni karatasi ya nini? Nilijiuliza…..
Na kwanini nimeandikwa jina langu kwa kalamu nyekundu.
Nilitamani kumpigia simu mke wangu Nyambura ili nimuulize nini maana ya karatasi ile lakini nikahofia kuwa kinaweza kuzuka kizaaazaa wakati akiwa na mama kule kisha nikaonekana kama mtu nisiyejua kutafakari mambo kwa kina.
Nikalimezea lile jambo sikumgusia Nyambura kabisa.
Nikanyoosha nguo niliyoichagua nikavaa na kwenda kazini, kinyonge kabisa huku akili yangu ikiwa inahangaika kujiuliza ni nini kinaendelea.
Au ameniendea kwa mganga? Nilijiuliza punde tu baada ya kuingia ofisini. Wazo hilo lililonipitia ghafla kichwani lilinifanya nijisikie vibaya sana kwa sababu katu maishani sijawahi kufanya mambo ya kishirikina japokuwa siwezi kuapa kuwa kamwe sitashiriki.
Wakati nafikiria juu ya jambo lile mara ghafla moyo wangu ukapiga kwa nguvu sana nikajikuta nimesimama, mwili wangu ukikumbwa na joto kali licha ya uwepo wa kiyoyozi.
Nilikuwa nimekumbuka kuwa nimeona kitu kingine cha ziada katika lile karatasi ambacho sio cha kawaida kabisa.
Katika yale majina yaliyoandikwa pale lilikuwa limeambatanishwa pia jina langu la utotoni!!
Jina ambalo niliacha kulitumia miaka mingi sana huko nyuma, jina ambalo lilisahaulika kabisa.
Fantom!!
Jina hili mke wangu alilitoa wapi, na aliliandika kwa kalamu nyekundu ili iweje.
Niliumia sana kichwa, nikawaza na kuwazua.
Mwisho wa siku nikanyanyua simu na kumpigia katibu muhtasi.
“Waambie sitaweza kushiriki mkutano leo, nitafutie muwakilishi tafadhali!” nilimweleza na sikungoja majibu, nikakata simu na kujilaza katika meza yangu ya ofisi, nikishindwa kabisa kupata maana ya ile karatasi katika kabati yangu!
“Au sio Nyambura aliyeiweka mle ndani…” nilijiuliza, lakini nikalipuuza wazo lile, mle ndani tuliishi wawili tu. Sasa iweje lile karatasi liingie biola kuingizwa?
Na kama sikuliingiza mimi basi ni Nyambura!
Sasa kwa nini?
Niliomba kimoyomoyo jambo lile liwe katika namna zozote zile lakini isiwe mambo ya kishirikina, sikutaka hata kidogo kuamini kuwa yawezekana Nyambura amenipika na kunifanya anavyotaka.

hii sikuweza kulala nyumbani, sikuwa na amani kabisa nikaamua kulala nyumba ya
kulala wageni, Nyambura aliponipigia simu niliongea naye na kumweleza kuwa
nilikuwa nyumbani.
Nilipokata simu nafsi ilinisuta, kwa mara ya kwanza nilikuwa nimemdanganya mke wangu!
Sikuupata usingizi siku hii, hadi majira ya saa nane usiku bado nilikuwa macho tu.
Hakika lile karatasi lilikuwa limenichanganya sana na sikujua nitaanza vipi kumueleza mke wangu ilimradi tu tusigombane.
Nililala nikiwa nasumbuliwa na kisa kimoja…. Asubuhi mambo yakapamba moto!

*****************
ASUBUHI
majira ya saa nne nilikabidhi chumba kisha nikaongoza njia kuelekea nyumbani,
nia ikiwa kubadili nguo kisha nielekee ofisini.
Nilianza kupuuzia juu ya karatasi lile lililoandikwa kwa wino mwekundu majina yangu matatu, moja kati ya jina hilo nikiwa nimeacha kulitumia kiwa miaka mingi sana.
Nilipanga kuwa nitakapotoka kazini nitaenda nyumbani kwa Revo rafiki yangu kumgusia juu ya jambo lililotokea nyumbani kwangu, lakini nilipanga kuyapanga maneno ili asije akapata pa kusemea eti alinieleza kuwa nisiwe na papara katika kuoa na sikutaka kabisa arejee lile swali aliloniuliza ikiwa ninamjua vizuri Nyambura.
Nilifika nyumbani na kuingiza funguo mlangoni.
Ajabu! Mlango ulikuwa wazi tayari.
Ina maana nilisahau kuufunga au? Nilijiuliza huku nikiingia ndani kwa tahadhari kubwa kabisa.
Nilianza kusikia dalili ya uwepo wa kiumbe hai pale ndani. Upesi nikawahi kuchukua chupa tupu ya soda pale sebuleni tayari kwa kukabiliana na yeyote atakayethubutu kunikabili.
Nilienda hadi nikakifikia chumba, sasa nikasikia sauti ya kike ikiwa katika kilio cha kwikwi.
Nyambura mke wangu yuko safarini, huyu ni nani ndani ya nyumba yangu!
Nikaufungua mlango upesi huku nikitanguliza ile chupa mbele.
Lahaula! Alikuwa ni Nyambura, akanitazama kwa jicho kali jekundu lililoiva haswa kwa hasira.
Nilijikuta ile chupa inanitoka huku ikipasuka vipande.
“Ulikuwa na nani huko ulipolala?” aliniuliza huku akisimama. Mikono yake ilikuwa inatetemeka sana, alikuwa amevaa nguo ya kulalia pekee.
Michirizi ya machozi ilijionyesha dhahiri katika mashavu yake.
Alikuwa ananisogelea, mimi nilikuwa katika pumbazo nisijue nini cha kujibu.
Sikutarajia kabisa shambulizi lile la ghafla kiasi kile.
“Joshua ulilala na nani, hadi kufikia hatua unaniongopea kuwa upo nyumbani kumbe unalala kwa hawara zako, Joshua ni nini hiki unanifanyia eeh! Ni nini Joshu….” Alilalama huku akibubujikwa na machozi. Akashindwa kumalizia akanitazama kidoleni….CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Na pete ya ndoa ukaona uivue kabisa, ukamwambia kuwa hauna mke….wanaume sijui mnataka nini katika maisha ya wanawake. Au Mungu alifanya makosa kutuumba? Au kwa sababu tulitoka katika mbavu zenu” Alizungumza huku akinitazama kidole changu ambacho kilitakiwa kuwa na pete.
Aisee! Nilijisikia aibu sana, si kweli kwamba nilikuwa nimeivua pete kwa sababu za kumsaliti mke wangu lakini niliivua ili kuisafisha na nikasahau kuivaa tena.
Sasa ile bahati mbaya imegeuka kuwa kesi inayohitaji majibu. Ningeyatoa wapi majibu!!
Mdomo ulikuwa mzito sana kana kwamba umedungwa sindano ya ganzi.
“Umekuja lini?.” Nilijitutumua nikamuuliza huku nikiwa sijiamini. Lilikuwa swali la kizembe sana
“Ulitaka nikueleze siku ambayo ninakuja ili uvae pete na kuja kunipokea uwanja wa ndege na maneno matamu kuwa unanipenda sana eeh!” alisema kwa uchungu Nyambura, nikajaribu kumshika ili nimsihi, akajitoa katika mikono yangu na palepale akaninasa kofi kali usoni.
Niliumia lakini kwa hali aliyokuwanayo Nyambura sikuwa na chochote cha kumfanya. Nilikuwa upande wa mashtaka na yeye akiwa ni mshtaki.
Alizungumza mengi sana mwanamke yule kiasi kwamba nikajikuta nikikosa walau doti ya ujasiri kuweza kumshutumu juu ya kile kikaratasi chenye jina langu katika wino mwekundu.

_____
KESI
ile iliisha lakini Nyambura akiwa mnyonge kabisa. Lakini hakuwa na budi
kukubaliana na utetezi wangu, maisha yakaendelea.
Ili kuyajenga tena upya mazoea ya kusahau kile kilichotokea nililazimika kumpa mke wangu likizo fupi kidogo ili aende nyumbani kwao kusalimia ndugu zake.
Licha ya kwamba alipoondoka nilimweleza kuwa natamani abaki lakini kwa uhakika nilitamani sana aondoke, sikuwa nikiishi kwa amani kabisa huku Nyambura akiwa ameninunia.

Kuondoka
kwa Nyambura kukairejesha amani yangu lakini kukinifanya niwe mtu ninayeishi kwa
tahadhari sana ili nisije kufanya makosa katika hatua ninazopita kisha
nikamkwaza mke wangu kwa kitu ambacho si kweli kabisa.
Napenda kukiri mbele yenu tena kuwa nilimpenda Nyambura kwa dhati kiasi kwamba sikuwa napatwa na msisimko wowote ule nikianza kumfikiria msichana mwingine.
Labda hili ndo kosa kubwa zaidi ambalo niliwahi kufanya katika maisha yangu, kupenda kwa dhati!!
Sijui kama maamuzi haya yalinifanya kuwa mjinga, ama zezeta!

Baada
ya likizo ile fupi kuisha Nyambura alirejea tena nyumbani tukiwa tumesahau
kabisa yaliyopita… tukaanzia tulipoishia nikampatia pesa ya mtaji na yeye
akaongezea akiba yake yake.
Wazo lililopitishwa ni biashara ya nguo za wanawake na watoto kutoka China kuja Tanzania.
Hata sikuwa na mashaka juu ya mke wangu katika suala la uelewa. Alikuwa mjanja sana na mwepesi kuelewa hivyo nilijua kuwa safari ya kwanza na ya pili pekee ndo atakuwa mikono nyuma lakini baada ya hapo atakuwa mjuzi maraduhu.
Naam! Nyambura wangu akaanza kwenda China.
China ikawa China…… mimi sioni mabadiliko zaidi ya kusifia kila nilichokuwa nakiona kuwa mke wangu anapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
Mara zikapenyezwa habari kuwa Nyambura ana mwanaume mwingine asiyekuwa mimi!
Yaani ananisaliti.
Nilijikuta nacheka tu, kwa sababu hayo maneno nilishayazoea kila kukicha na kila nilipojaribu kufuatilia majibu yalikuwa ni uongo mkubwa.
Kabla sijaendelea kukusimulia mkasa huu mpenzi msikilizaji hapa nikugusie neno kidogo, katika maisha yako kuna vitu hutakiwi kuviamini kwa asilimia nyingi.
Kimojawapo ni mwanamke mwenye hasira ama aliyewahi kujeruhiwa!
Anaweza kufanya jambo ambalo wewe na halmashauri ya kichwa chako nyote mkabaki kuduwaa.
Tetesi zilivyozidi nikaamua kufanya utafiti wa chini kwa chini….
Nyambura alikuwa hachunguziki jama!
Sikuambulia kitu chochote, niliishia kuwa upande wake na kuwacheka wale wanaosema kuwa ananisaliti.
Waswahili wanasema kuwa lisemwalo lipo njiani linakuja. Nilijipa tahadhari na hapa nikajipa tahadhari, na kwa mara ya kwanza nikatambua kuwa namna nzuri ya kukabiliana na hali hii ya sintofahamu ni kupata mtoto na Nyambura.
Hili litaleta heshima.

Alipotoka
katika safari zake nikamsihi juu ya jambo hili, mke wangu msikivu akalipokea kwa
mikono miwili na yeye akasema kuwa anatamani kupata mtoto na
mimi.
Wakati mimi nilidhani kuwa itakuwa ngumu sana imekuwa nyepesi kuliko kawaida.
Nyambura akasitisha safari zake ili tutafute mtoto.
Hapa ndipo nilipoanza kupungua uzito siku kwa siku.
Jaribio la kwanza likashindikana, Nyambura akaingia katika siku zake kama kawaida kumaanisha kuwa nimegonga mwamba, jaribio la pili pia vilevile.
Tukajaribu tena mwezi wa tatu, hali ikawa vilevile.
Kuna shida mahali!
Nilijisemea huku nikiomba sana hiyo shida isijekuwa ipo upande wangu. Kwa sababu ningedharaulika sana na ikiwa Nyambura ataamua kusimulia kila mtu basi nisingekuwa na uwezo tena wa kusimama mbele ya watu na kuzungumza.
Tulipojaribu mwezi wa nne na shida kubaki palepale, tulikubaliana kuwa iwe siwe tutalazimika kwenda hospitali ili tujue kuna shida gani hadi inakuwa hivi??
Niliunga mkono jambo hili lakini bado maombi yangu yalikuwa yakimsihi Mungu, lile tatizo lisijekuwa upande wangu.
Vipimo vikachukulia, tukiwa kama wanandoa tukakubaliana kuwa tutayachukua majibu yetu tukiwa pamoja.
Muda ukawadia ndani ya chumba cha daktari, alitutazama machoni kisha akalitazama faili aliloshikiria akatuuliza majina yetu upya, kisha akauliza ikiwa mmoja wetu amewahi kupata mtoto katika maisha yake ya ujanani…
Sote hatukuwa tumewahi walau kuhusika katika kusingiziwa walau mtoto hata kwa bahati mbaya.
“Ok! Mmesema kuwa ni wanandoa eeh!” alihoji tena.
Swali lake likanifanya nione kuwa anachelewa sana kutoa majibu yake ambayo bila shaka sio mazuri hata kidogo!
Alipomaliza swali lie akaanza kutoa majibu akianza na Nyambura, ambaye hakuwa na mashaka kabisa……

JIFUNZE
NDOA… zione wakati zinafungwa, waone waliofunga ndoa kwa nje, furahia kuwaita bibi na bwana fulani, lakini ingia katika NDOA uijue NDOA vizuri!

*******************
Baada
ya vipimo vile daktari alianza kuzungumza mambo mengi sana kuhusiana na afya ya
uzazi, na mwisho ndipo akatoa majibu yetu.
Ndugu msikilizaji, Nyambura hakuwa na tatizo lakini mimi nilionekana kuwa na tatizo.
Daktari alinifariji sana na kuelezea kuwa tatizo nililonalo si kubwa kiasi cha kutisha na linatibika.
Sikuamiani maneno ya daktari kwa sababu niliwatambua vyema kuwa nia yao siku zote si kumkatisha tamaa mgonjwa bali kumpa moyo ili awe imara zaidi.
Jasho lilinitoka sana, mawazo lukuki yakaniandama na pepo la hofu likaniingia.
Hofu kubwa ikiwa kumpoteza Nyambura wangu, angweza vipi kuishi na mimi bila ndoto ya kupata mtoto?
Niliondoka pale nikiwa sijiwezi kabisa, nilimsihi Nyambura aendeshe gari kwani mimi sikuwa sawa hata kidogo.
Nyambura alinielewa, akaendesha gari tukafika nyumbani akiwa hajasema neno lolote lile bado.
Ukimya wa Nyambura uliniumiza sana, nilijitahidi kuwaza badala yake na nikaona kuwa anachowaza ni kuanzisha maisha mengine bila kuwa na mimi.
Aliniandalia maji nikaoga, akaingia jikoni na kuniandalia chakula nikipendacho.
Ugali dagaa na mboga za majani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tofauti na siku nyingine, siku hii chakula hakikulika, nilikiona kichungu huku nikihisi hata harufu yake ni mbaya.
Mawazo yalikuwa yamenikabili sana, yaani jitihada zangu zote hizo nikose wa kurithi jasho langu kweli?
Iliniuma sana jama!
“Joshua mume wangu…. Nakupenda sana. Sijawahi kukueleza ni kwanini nakupenda na kamwe sitakueleza kwa sababu nakupenda kama ulivyo bna utakavyokuwa hapo baadaye.” Hatimaye Nyambura alizungumza. Sasa tulikuwa chumbani alikuwa ameniegemea huku akizisukasuka ndevu zangu.
Nilifarijiwa sana na maneno yake yale ya kutia nguvu.
Nikapata faraja kwa mara ya kwanza lakini haikumaanisha kuwa hofu yangu ilikuwa imeisha.

Tofauti
na matarjio yangu kuwa itafikia wakati ambao Nyambura atahitaji tena majadiliano
juu ya jambo lile, haikuwa hivyo.
Maisha yakaendelea kama kawaida, huku upendo wake wa dhati nao ukizidi kuichukua nafasi yake.
Lakini katu sikuacha kuwaza juu ya lile jambo, nilifahamu fika kuwa miaka itasogea marafiki wataulizia mtoto lini, mama ataulizia mjukuu lini, nitawajibu nini?
Hili nalo liliniumiza sana. Nikajiuliza ni kitu gani nitafanya kukabiliana na jambo hili.
Sikupata majibu, nikajitoa muhanga na kurejea kwa rafiki yangu Revo ambaye alikuwa ndoani nikamshirikisha kiuwazi kabisa juu ya jambo hili linalonitokea.
Alinisikitikia sana lakini zaidi ya kunisihi nisikate tamaa hakuwa na ushauri zaidi.
Na zaidi alinikanya nisimshirikishe kila mtu maana si kila mtu anayependa kuonamambo mazuri yakitokea upande wangu.
Nikapokea ushauri wake.

Nilipotoka
pale nilipita mahali na kupima uzito, nikagundua kuwa nilikuwa nimepoteza jumla
ya kilo tano ndani ya majuma mawili tu.
Nilijisikitikia na kujiona mtu nisiyekuwa na bahati kabisa. Lakini nilipoyasema haya mbele ya Nyambura alinikumbusha kuwa nimejaliwa mengi ambayo wengine hawajawahi kuyapata kabisa, akanielezea juu ya pesa nilizokuwa namiliki pamoja na vitega uchumi, kisha akanieleza kuwa nina bahati wazazi wangu bado wanaishi wengine ni yatima tangu wana siku moja duniani.
Maneno yake yaliniimarisha sana, na hapa akawa ameichota akili yangu zaidi na kuona huyu ndiye mwanamke wa maisha yangu yaani akitoka mama yangu basi ni huyu anayefuatia.

Miezi
ilikatika, takribani miezi miwili…. Nyambura akarejea tenakatika zile biashara
zake za kusafiri huku na kule kama alivyokuwa amenieleza.
Nilimkubalia bila mashaka kabisa.
Nyambura akaanza kuishi mbali na mimi siku akisafiri, upweke unanitawala na mawazo tele nikitamani kuwa na mtoto.
Siku moja Nyambura akiwa safarini, nilitembelewa na Revo yule rafiki yangu, aliniahidi kuwa atanitembelea hivyo haikuwa jambo la kushtukiza.
Revo alinileza kwamba siku ile alishindwa kuzungumza na mimi vizuri kwa sababu mkewe alikuwa amemvuruga hivyo hakuwa sawa.
Na alikuwa amekuja hapo ili tujadiliane juu ya tatizo linalonikabili.
Revo akaniuliza ikiwa nimejaribu tiba za jadi, nikamweleza kuwa sijawahi kujaribu hata siku moja.
“Hizo tiba za hospitali zimekusaidia lolote?” aliniuliza, nikatikisa kichwa na kumweleza kuwa hakuna nilichofanikiwa hadi wakati huu.
Akanitazama kwa muda kisha akanieleza kuwa nijaribu huko.
“Ujue kaka, unaweza kumwona Nyambura ni mvumilivu, lakini elewa kuwa hawezi kuvumilia mkaisha yote. Kaka pambana upate mtoto, hapa umefungwa tu na mjinga mmoja asiyependa kuona unja furaha… najisikia vibaya kwa haya yanayokutokea. Wewe ni rafiki yangu tafadhali….” Alinisihi sana Revo, maneno yake yalikuwa kweli tupu.
Ndoa ni mtoto… na Nyambura hawezi kuvumilia miaka yote bila mtoto.
Kama hawezi kuvumilia basi hii inamaanisha kuwa atatafuta njia nyingine kumpata.
Mwanaume mwingine!! Jibu hili likanijia kwa kasi kubwa sana na kukiyumbisha kichwa changu, nikafumba macho yangu na kumwona Nyambura wangu akiingia kwenye mahusiano na mtu mwingine.
Hakuna kitu kinaumiza ndugu msikilizaji katika mahusiano kumwona yule mpenzi wako ambaye moyo wako unafarijika kuwa naye eti anaingia kwenye mahusiano na mtu mwingine.
Sikuwa tayari kuupa fedheha kiasi hicho moyo wangu, nikajikuta kwa mara ya kwanza natamani kufanya jambo lolote lile ilimradi tu kumtunza Nyambura wangu.
Nikamuuliza Revo juu ya huyo tabibu wa jadi ni wapi nitakapompata. Akaniambia kuwa anaye rafiki yake ambaye anafahamu wataalamu wazuri kabisa ambao wanaweza kunifungua na kufanikiwa kupata mtoto.
“Kaka asijekuwa mtoto wa masharti halafu baadaye wakaja kumdai!!” nilimpa tahadhari Revo huku nikikumbuka filamu nyingi ambazo nimewahi kuzitazama zikiwa na matukio kama hayo.
Akaniondoa hofu huku akinieleza kuwa kabla ya yote tutamuuliza huyo tabibu atuhakikishie kabisa kuwa mtoto atakuwa salama asiyekuwa wa masharti hata kidogo.
Revo akaniaga huku akiniacha nikiwa nimekubali kabisa kwenda kwa tabibu wa jadi ili niweze kuiokoa ndoa yangu.
Punde tu baada ya Revo kuondoka, mama yangu alinipigia simu na katika maongezi hayo aliulizia ni lini aje mjini kulea mjukuu, nikajichekesha tu na kumwambia kuwa ajiandae na nepi na kanga za kumbembe mjukuu mgongoni.
Akanipa hongera!
Hongera ya mama iliniumiza sana kwa sababu alikuwa anampa hongera mtu asiyekuwa na uwezo wa kuleta mtoto duniani!
Chozi likanitoka!
Na hii ikaniongezea ujasiri wa kuzifuata tiba za jadi.
Nikatamani hiyo siku ya kwenda huko ifike.
Nikanyanyua simu na kumpigia Revo, nikamsisitiza awasiliane na huyo rafiki yake upesi ikiwezekana twende kabla Nyambura hajarejea. Akanijibu kuwa tayari amemtumia ujumbe na anangoja majibu tu!
“Mama amenipigia simu Revo, nimejisikia vibaya sana ameniuliza kuhusu mjukuu. Nimeumia sana Revo”
“Relax Joshua…. Mambo yote yanaenda kuwa sawa muda si mrefu!” alinijibu kwa upole Revo. Kisha tukaagana na kukata simu.

NAKUSIHI
Mtoto ni majaliwa katika ndoa, ikitokea haujajaliwa kumpata mtoto katika ndoa usijione kama umelaaniwa. Itulize akili yako usije kuingiza mguu wako katika kaa la moto!!

CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****************
SIKU
mbili baadaye Revo alinipigia simu kunieleza kuwa rafiki yake yupo tayari ni
sisi tu kwenda kwa huyo mganga kumsikiliza.
Nilijiandaa upesi na kwenda nyumbani kwa Revo, tukatumia gari lake kumpitia huyo rafiki yake.
Awali nidhani kuwa atakuwa ni mwanaume lakini ajabu nilikutana na mwanamke.
Niliona aibu sana kwa sababu nilihisi kichwani mwake ananing’ong’a kuwa ‘tazama mwanaume suruali huyu hawezi kuzaa’.
Nilijisikia hovyo sana lakini kwa sababu hiyo ilikuwa tafsiri sahihi ya mficha maradhi kifo humuumbua, nilikubaliana na ile hali.
Ilimradi ilikuwa ni njia ya kuelekea kupona na kurejesha tena heshima.
Mwanadada yule alinisalimia kwa furaha, akaingia na kuketi siti ya mbele pamoja na Revo aliyekuwa anaendesha tukaondoka hadi kwa huyo tabibu wa jadi.
Tulipokaribia yule dada alimsihi Revo asimamishe kwanza gari.
“Kaka, tafadhali usijiruhusu kumweleza tatizo lako. Acha aseme mwenyewe tu….. maana ukimpa mwongozo naye atapitia humohumo… ma ukiona anaenda ndivyosivyo usimwonee haya muulize. Kumbuka tunaenda kumpa pesa kwa huduma hii” alinipa angalizo nami nikalipokea ipasavyo.
Tulipofika na kupokelewa ilikuwa hivyo, akaniuliza majina yangu hapo nikiwa nimebaki naye ndani mimi mwenyewe, akaliandika jina langu kisha akaanza kuandika vitu ambavyo alivijua yeye mwenyewe kwa lugha nisiyoielewa.
Mwishowe akanitajia mambo takribani manne ambayo aliyagundua kutoka katika jina langu.
Akanitajia kuwa ninasumbuliwa sana na hasira za hovyo, pili nina msongo wa mawazo kwa sababu nawaza kitu nisichokijua, tatu nyota yangu imewekwa ki-zani hivyo sina tofauti na mtu asiyekuwa na nyota, nne akanieleza kuwa ninatafuta kitu ambacho watu wamekishikilia na hawataki kukiachia, na kwa nguvu zangu pekee siwezi kukichukua.
Hapo ndipo alipokazia zaidi akaanza kunihoji, na mwishowe akanitajia kuwa ninahitaji mtoto kwa udi na uvumba.
Niliposikia neno lile nilisisimka sana, kwea sababu alikuwa amegusa kile nilichokuwa nakihitaji kwa dhati
Nikakiri kuwa pale nilikuwa nimefikishwa kwa mganga haswa asiyekuwa na longolongo.
Akanieleza kuwa anatakiwa kujipanga vyema ili kukabiliana na watu walioushika uzazi wangu. Alidai kuwa wana nguvu kali sana na hawezi kwenda kichwakichwa.
Akataja vifaa vya kununua na kama siwezi kununua basi natakiwa kumpatia shilingi laki tano za kununua vifaa hivyo.
Mchezo ukaanzia hapa rasmi nah ii ngoma nikabaki kuicheza mwenyewe.
Sasa sikuwa nasindikizwa tena na Revo wala yule dada, badala yake nilikuwa naenda peke yangu kwenye tiba, ninapewa maagizo na kuyafanyia utekelezaji, napangiwa siku za kufanya tendo la ndoa na mke wangu kipenzi, napangiwa rangi ya nguo ya ndani ninayotakiwa kuvaa na mambo kedekede lakini kila juma nilijikuta shilingi laki moja hadi laki mbili ikiishia kwa mganga.
Kutokana na wingi wa masharti na safari za kwenda kwa mganga nikajikuta hata utendaji kazi wangu ofisini ukawa unashuka kwa kasi kubwa sana, yaani sikujali kuhusu kampuni yangu badala yake nilikuwa nawaza kuhusu kupata mtoto kwa namna yoyote ile.
Ndugu msomaji hali niliyokuwanayo hakuna anayeweza kuipa tafsiri zaidi ya mwanaume kama mimi mwenye nia ya dhati ya kupata mtoto na asimpate.
Ama sijui kuhusu uchungu wa mwanamke kukosa mtoto ingali mawuifi wanamsimanga unavyokuwa, labda hali ile nd’o kama niliyokuwanayo mimi.
Nilikuwa kama mpumbavu anayejijua kuwa ni mpumbavu lakini akiwa hana namna ya kuukwepa upumbavu ule.

mitatu ikakatika bila Nyambura kubeba ujauzito huku mganga naye akizidi kunipa
ahadi kedekede kuwa mambo yameiva na muda wowote ule nitaitwa baba
kijacho.
Ahadi za mganga zikaanza kunichosha na hapo nilikuwa nimetumia pesa nyingi sana kwa ajili ya kutatua jambo hili.
Miezi sita ya mahangaiko ya hapa na pale ikapita na hapa nikaamua kuyafikiria upya maisha yangu.
Nikakumbuka juu ya kulazwa juu ya makaburi, kunywa damu mbichi ya mbuzi, kuishi mwezi mmoja bila kuvaa nguo ya ndani, juma moja bila kuoga, na mengineyo lukuki.
Nikapiga goti na kumuomba msamaha Mungu wangu huku nikimsihi kuwa kama kuninyima mtoto ni adhabu katika maisha yangu basi amtume malaika wake walau anieleze nilikosa nini. Nitubu kwa dhati na aitengue adhabu ile.
Nilijichukia mpenzi msomajina msikilizaji wa mkasa huu, nilijiona kama niliyeukosea sana mwili wangu kwa kuupeleka kwa mganga ambapo sikupata mafaniko kabisa.
Nilikuwa nimechanjwa, nilikuwa nimepakwa unga nisioujua, nilikuwa nimenyweshwa vinywaji tele nisivyovifahamu huku vikiwa na ladha mbaya.

Lakini
akili ya mwanadamu inabaki kuwa ya mwanadamu, tunawahi sana kusahau….. yaani ni
rahisi sana kudanganywa upya.
Miezi miwili baada ya kuachana na mambo ya yule mganga, nilipokea simu… simu kutoka kwa yuleyule mganga. Akadai kuwa ananihitaji sana kuna jambo zito sana ameonyeshwa na mizimu.
Nilijiuliza kama niende ama nisiende baadaye nikakata shauri la kwenda huku nikijiapiza kuwa sitafanya lolote ambalo atahitaji na badala yake nitamwambia kuwa sihitaji huduma zake zaidi.
Kichwani nilijua wazi kuwa ni njaa zinamsmbua yule mganga na sasa anataka tena kunichuna pesa zangu. Nami nilikuwa nimejanjaruka tayari

Nilifunga
safari hadi nyumbani kwake, akaniweka kitako kisha akanieleza kuwa amepata
ujumbe kutoka kwa mizimu, mizimu haina kingine cha kusema zaidi ya kuwa imeleta
majibu mazuri kabisa ya mimi kupata mtoto.
Lakini mizimu inataka ahadi ikiwa nitapata mtoto ni zawadi gani nitaipatia.
Kwa sababu nilikuwa nimechoshwa na bla bla za huyu mganga nilimjibu kuwa zawadi yoyote ambayo watahitaji mimi nitatoa.
Akaniuliza mara ya pili “Una uhakika utatoa zawadi yoyote?”
“Nitatoa lakini kama nilivyosema awali sipo tayari kumwaga damu…” nilimjibu.
“Mizimu haiitaji damu, sina urafiki na mizimu inayotaka damu.” Alisema tena huku akinishika kichwa changu na kunitikisa tikisa akazungumza lugha ambazo sijui hata tafsiri yake kisha akaniruhusu niondoke.
Nilijiondokea huku nikijisikia karaha na kujiona nimerejea enzi za utoto, enzi za kudanganywa kuwa naletewa pipi ninanyamaza na siletewi.
Sasa nadanganyishiwa mtoto katika utu uzima huu!
Na bado sipewi…
Niliumia mno.
Majuma kadhaa yakakatika, nikasahau ule wito wa mganga na ahadi zake kem kem, nikaendelea na maisha yangu ya kukubaliana na hali.
Siku moja jioni tukiwa mezani tunapata chakula, mke wangu hakuwa sawa kabisa. Hakutabasamu!
Niliongea sana lakini yeye hakuongea, nilijaribu kukisifia chakula lakini hakuonyesha ushirikiano ule niliouzoea.
Ana nini huyu? Nilijiuliza huku nami hamu ya kula ikipotea.
Nilimuuliza kuna nini akasema kuna kitu nimemkosea sana.
Mungu wangu! Nikawaza kuwa amegundua tayari kuwa nilienda kwa waganga wa jadi kusaka mtoto.
Nitamjibu nini sasa!! Nilitaharuki.
“Nyambura mke wangu, ni lini mimi nimekukosea ukanuna badala ya kunieleza??” nilimuhoji huku nikiacha kula.
Hakunijibu badala yake akasimama akiwa na kisirani na kukimbilia chumbani.
Doh! Kupenda! Acha tu… labda kama wewe hujawahi kupenda, ila mwenzenu kwa Nyambura nilikuwa mateka.
Niliacha kila nilichokuwa nafanya nikakimbia kule chumbani.
He! Alikuwa amejifungia ndani. Nilibisha hodi hakufungua, nikaita jina lake hakujibu.
Nilipagawa!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara nikasikia mlango unafunguliwa, nikawahi kitasa nikakishusha.
Nikaingia ndani!
Asalaleee!! Nyambura akanikumbatia kwa nguvu na kutua nami kitandani, kwa fujo. Akanigalagaza huku na kule kisha akaniachia na kukaa juu yangu.
Akanitupia kikaratasi kifuani mwangu.
Nikiwa bado nina mawenge, akaniacha na kusimama akinipa uwanja wa kusoma kile kilichoandikwa. Nilisoma lakini sikuelewa kwa sababu ya mawenge…
“Ehee! Anza kuandaa jina kabisa, akiwa wa kume, akiwa wa kike ama wakiwa mapacha!” alizungumza huku akijishika tumbo lake.
Ndugu!! Nilisikia shoti ikipiga kuanzia katika unyayo wa mguu hadi katika mizizi ya nywele.
“Nyambura we Nyambura ni nini unasema eeh! Kwamba… eh! Kuna nini” nilihoji maswali mfululizo katika hali halisi ya kupagawa.
Akacheka kwa sauti ya juu, huku ile nguo nyepesi aliyovaa ikiruhusu matiti yake kurukaruka vizuri kifuani.
Nyambura alikuwa mrembo jama!
Baada ya kucheka akanieleza kwa kina sasa.
Alinieleza huku machozi ya furaha yakimtoka. Nilitamani kusema neno lakini nilikosa neno sahihi la kuelezea juu ya furaha yangu.
Nilijikuta namkumbatia kwa nguvu Nyambura nami nikajikuta nikitokwa machozi huku nikilia kama mtoto.
Nilitamani dunia yote iingie katika moyo wangu Joshua mimi nha kuipima ile furaha iliyokuwa moyoni mwangu.
Baada ya furaha hii nikamkumbuka yule mganga na ahadi yake ya ghafla ambayo sasa imezaa matunda.
Mizimu! Nikaikumbuka.
Nikakumbuka pia nilikubali kuwa nitakuwa tayari kutoa kitu chochote kile.
Baada ya siku tatu nilimtembelea mganga na kumweleza kuwa nipo tayari kuiskiliza mizimu iseme itakacho.
“Umepata mtoto tayari?” alinihoji bila kunitazama.
“Hapana mke wangu ameshika ujauzito!”
“Ikiharibika je? Mizimu wanataka upate mtoto ndo wachague ni kitu gani utawapatia….” Alijibu yule mganga kwa utulivu bila kushtushwa na ile habari.
Jibu lake lilimaanisha kuwa mizimu pamoja na yeye mwenyewe walikuwa wamenipigania kweli kwa dhati na wala hawakuwa na tamaa ya pesa.
Nikamwachia yule mganga shilingi laki mbili kama shukurani.
Nikaondoka kurejea nyumbani.
Asikuambiaemtu jama, mawazo yanakondesha na kukosesha raha.
Baada ya mke wangu kupata ujauzito niliona mimi ni mwanaume kamili sasa, nikawa na furaha tele, mwili wangu ukarejea kwa kasi utendaji kazi wangu ofisini ukarudi katika kiwango cha juu.
Kila aliyenifahamu alikiri kuwa nilikuwa nimebadilika.
Ni mwanandoa gani asingefurahia taarifa hii?? Mtoto ana thamani kubwa sana katika ndoa, akikosekana tunasema ni mipango ya Mungu lakini mioyo yetu husononeka pindi tunapotoa kauli hiyo.
Hakika nilikuwa mmoja kati ya watu wenye furaha duniani. Furaha ambayo nilihisi itakuwa furaha ya kudumu.
Kumbe usilolijua ni sawa na usiku wa giza….
Kuna kiza kinene kilikuwa kinanivizia…..

JIFUNZE!!CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
FURAHA ya kweli huja ukiwa na amani ya moyo, ikiwa huna amani ya moyo na unatabasamu pana usoni wewe hauna furaha bali unapambana kuificha hofu yako. Hii ni vita kuu sana kujaribu kuficha hofu kwa kutumia tabasamu……
Furaha ya kweli hudumu lakini vita ya kuficha hofu itakuangusha tu wakati ukifika……
Na wakati huo huja mapema kuliko ulivyojipanga

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment